annuur 1148

16
ISSN 0856 - 3861 Na. 1148 DHUL-HIJJA, IJUMAA , OKTOBA 24-30, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz Katiba inayopendekezwa koti linalobana zaidi-Seif Imekiuka hata misingi ya Muungano Kutoka mtuhumiwa Victor hadi kuuawa Yahya Sensei Afande Liberatus Soma Biblia John 8:32 "Intelligence Assets” watatusumbua kama… Hatupo tayari kusema kweli ili kuwa huru Madaktari wachunguza afya za watuhumiwa Keko, DSM Sheikh Msellem anaendelea vizuri Jumuia ya Maimamu yawafariji Watendaji wa gazeti la AN-NNUR wanawatakia Waislamu wote kheri ya Mwaka Mpya wa Kiislamu 1436 Hijiria. VICTOR Ambrose Calist. Uk. 3 Uk. 5 Uk. 8 KAMANDA wa Polisi Arusha, Liberatus Sabas. MWILI wa mtuhumiwa wa ugaidi, Marehemu Yahaya Hassan Omar (Sensei) anayedaiwa kufariki baada ya kupigwa risasi na polisi mguuni na makalioni. Inadaiwa kuwa alitaka kuwakimbia polisi kwa kutumia ujuzi wake wa karate na Judo.

Upload: zanzibariyetu

Post on 07-Feb-2016

1.016 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: ANNUUR 1148

ISSN 0856 - 3861 Na. 1148 DHUL-HIJJA, IJUMAA , OKTOBA 24-30, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz

Katiba inayopendekezwa koti linalobana zaidi-Seif

Imekiuka hata misingi ya Muungano

Kutoka mtuhumiwa Victorhadi kuuawa Yahya Sensei

Afande Liberatus Soma Biblia John 8:32"Intelligence Assets” watatusumbua kama…Hatupo tayari kusema kweli ili kuwa huru

Madaktari wachunguza afya za watuhumiwa Keko, DSM Sheikh Msellem anaendelea vizuri Jumuia ya Maimamu yawafariji

Watendaji wa gazeti la AN-NNUR

wanawatakia Waislamu wote kheri ya Mwaka

Mpya wa Kiislamu 1436 Hijiria.

VICTOR Ambrose Calist.

Uk. 3 Uk. 5

Uk. 8

KAMANDA wa Polisi Arusha, Liberatus Sabas.

MWILI wa mtuhumiwa wa ugaidi, Marehemu Yahaya Hassan Omar (Sensei) anayedaiwa kufariki baada ya kupigwa risasi na polisi mguuni na makalioni. Inadaiwa kuwa alitaka kuwakimbia polisi kwa kutumia ujuzi wake wa karate na Judo.

Page 2: ANNUUR 1148

2 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 24-30, 2014

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Tangazo

NIMELAZIMIKA kuanza makala haya kwa hoja, hivi kwanini maradhi angamizi ya virusi yanaibukia katika bara la Afrika zaidi kuliko mabara mengine? Kila ninapojaribu kutafakari, swali hili limekuwa likija kila mara katika hisia zangu, bila kupata majibu. Nimejaribu kutafuta kwenye mitandao, kama labda kuna mtaalam yeyote aliyejaribu kupata harufu ya kiini cha sababu za maradhi haya angamizi kujitokeza na kukolea zaidi katika bara la Afrika na si kwingineko, sijafanikiwa kumpata.

K a r n e z a n y u m a , yamewahi kutokea maradhi yanayoadhiri idadi kubwa ya watu, kama vile kipindupindu (cholera) , surua, pol io , homa ya manjano, mafua ya ndege (sars) nk. Hata hivyo, taarifa zinaonyesha kuwa maradhi haya pamoja na kwamba yalionekana kuwa

Kuna haja ya kujiuliza kwanini maradhi haya chanzo ni Afrika

Watu milioni 30 wameangamia kwa UKIMWINa Shaban Rajab ni hatari na angamizi kwa

wakati wake, lakini kamwe hayajaweza kufua dafu dhidi ya maradhi yanayoenezwa kwa virusi ya Ukimwi na huu unaoutetemesha ulimwengu kwa sasa, yaani ugonjwa wa ebola.

Maambukizi ya virusi vya ukosefu wa kinga mwilini (VVU/UKIMWI) ni ugonjwa wa mfumo wa kingamwili wa binadamu unaosababishwa na virusi vya ukosefu wa kinga mwilini (VVU).

Baada ya kuambukizwa, mtu anaweza kukumbwa na kipindi cha maradhi ya aina mbalimbali kwa kuwa kinga za kupambana na maradhi zinakuwa zinaharibiwa na virusi hivi, jambo ambalo kusababisha mtu hatimaye kupoteza maisha.

Ukimwi huambukizwa zaidi kwa kufanya ngono z i s izo sa lama au watu kushirikiana vifaa vyenye ncha kali.

Watafiti wameonyesha kuwa VVU viligunduliwa huko Afrika Magharibi ya kati

katika karne ya ishirini.Tangu kugundulika kwa

maradhi hayo , hakuna tiba wala chanjo hadi sasa. Hata hivyo, tahadhari ya k u a m b u k i z wa i n a we z a kupunguza mwendo wa ugonjwa huu.

H a t a h i v y o b a a d a e kuligunduliwa dawa za kujaribu kupunguza kasi ya ushambuliaji ya VVU, ambavyo husababisha urefu wa maisha ya mgonjwa.

UKIMWI uligunduliwa k wa m a r a ya k wa n z a na Vituo vya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa mnamo mwaka wa 1981, na kirusi (VVU) tunaelezwa kuwa kiligunduliwa mwanzoni mwa muongo huo.

VVU/UKIMWI umekuwa na madhara makubwa katika jamii, kama ugonjwa na chanzo cha ubaguzi. Ugonjwa huu pia una madhara ya kiuchumi.

Ta n g u k u g u n d u l i wa , U K I M W I u n a d a i w a kusababisha vifo vya watu

Inaendelea Uk. 3

HIVI silaha za kutumia v i u m b e z i n a j a r i b i w a kwa Waafrika? Taarifa zimehusisha kufumuka wa virusi vya Ebola na majaribio ya kupunguza idadi ya watu barani Afrika. Liberia pia ndiyo nchi ambayo idadi yake ya watu inaongezeka kwa kasi kuliko kwingineko barani Afrika.

Wapendwa wananchi wa dunia:

Nimesoma makala kadhaa katika ukurasa wenu wa mtandao pamoja na makala kutoka vianzio vingine kuhusu vifo vilivyotokea Liberia na nchi nyingine za Afrika Magharibi kuhusiana na uharibifu uliotokana na virusi vya Ebola. Yapata wiki moja iliyopita, nilisoma makala iliyochapishwa katika muhtasari wa habari kutoka

Ebola imetengenezwa na makampuni ya madawa, Wizara ya Ulinzi ya Marekani? Wanasayansi wanadaiNa Dk. Cyril Broderick, Profesa wa Mifumo ya Uhai ya MimeaOktoba 19, 2014 ‘Mtandao wa Kupashana Habari’ na ‘Liberian Observer’

BILA shaka Waislamu nchini wana taarifa za kuwekwa mahabusu v i o n g o z i w a o mbal imbal i ka t ika gereza la Keko jijini Dar es Salaam.

A i d h a w e n g i wa n a f a h a m u k u wa v i o n g o z i h a o n a Wais lamu wengine , wamo gerezani humo kutokana na kutuhumiwa kwa makosa kadhaa, lakini zaidi ni ya ugaidi na uchochezi. Miongoni mwao ni pamoja na Sheikh Ponda Issa Ponda, baadhi ya Masheikh wa Jumuiya ya Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar w a k i w e m o S h e i k h Msellem Ali Msellem na Farid Hadd.

Tunatambua kwamba kesi za Waislamu hawa b a d o z i n a e n d e l e a m a k a h a m a n i . H a t a hivyo, kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya watuhumiwa katika muendelezo wa kesi hizo, na hata mawakili wao wanaowatetea , wamesema kuwa tangu walipoingizwa katika mahabusu, wamekuwa wa k i s u m b u l i wa n a maradhi huku wakikosa matibabu stahiki.

Wa m e s e m a k u wa s e h e m u k u b wa ya maumivu wanayopata ni kutokana na mateso waliyopewa na baadhi ya askari wa jeshi la polisi, hasa wakati wakihojiwa. Ilifikia hata kusema kuwa baadhi ya unyama waliofanyiwa hawawezi kuueleza hadharani. Bila shaka ni kwa kuwa ni wa aibu, hasa kwa mtu wa kaliba ya kiongozi wa dini.

Pamoja na maumivu na maradhi yanayowakabili, Masheikh hao walikosa kupatiwa hata ile hati ya matibabu kutoka polisi (PF3), licha ya amri ya mahakama ya kutaka wapatiwe hati hizo.

Hata hivyo, baada ya

Tuwasaidie Masheikh wetukuzirai Sheikh Mselem w i k i i l i y o p i t a n a baadhi ya watuhumiwa kuonyesha alama za usaha katika mavazi yao mbele ya mahakama, tunafarikijika kusikia kwamba madaktar i w a m e w e z a k u f i k a gerezani Keko na kuanza kuwafanyia uchunguzi wa afya Masheikh hao na kuwapatia matibabu.

Ifahamike tu kwamba, suala la matibabu ni haki ya msingi ya kila b i n a d a m u , a w e n i mfungwa au mahabusu. Kwa hiyo, wito wetu kwa Waislamu nchini, hususan wa jijini Dar es Salaam, ni kutoa kila aina ya msaada unaohitajika k u h a k i k i s h a k u wa w a t u h u m i w a h a o wanapata haki yao ya matibabu na haki nyingine za msingi ambazo haziondolewi na tuhuma zinazowakabili.

Wa n a h i t a j i s a n a huduma za kijamii kama vile dawa kukabiliana na maradhi yanayowakabili, vyakula bora, kuchangia k a t i k a k u w a p a t i a msaada wa kisheria na hata kuwatembelea kuwafariji.

P ia n i wa j ibu wa Waislamu kuzisaidia familia zao, ambazo zilikuwa zikitegemea mahitaji yao kutoka kwa watuhumiwa.

Waislamu wafanye hivyo wakitambua kuwa hao ni ndugu zao na waumini wenzao.

Shura ya Maimamu w a m e o n y e s h a n j i a . K u w a s a i d i a watuhumiwa hawa, mtakuwa mnatekeleza na kudhihirisha udugu na mshikamano wa Kiislamu.

Tu s i m a m e k a t i k a mafundisho ya Uislamu kuwa tumsaidie ndugu yetu akiwa kadhulumiwa au kadhulumu. Tutizame ubinadamu.

mtandaoni unaochapishwa na ‘Marafiki wa Liberia’ iliyosema kuwa kulikuwa na uelewano kuwa kufumuka kwa Ebola huko Afr ika Magharibi kulitokana na kugusana mtoto wa miaka miwili na popo ambaye aliletwa kwa ndege kutoka Congo. Taarifa hiyo ilinisikitisha kwa na utoaji taarifa kuhusu Ebola, na ikasukuma kutolewa jibu kwa ‘Marafiki wa Liberia,’ kusema watu wa Afrika siyo wajinga wanaodanganyika tu, kama inayoainishwa. Jibu kutoka kwa Dk. Verlon Stone lilisema kuwa makala hiyo haikuwa yao, na kuwa ‘Marafiki wa Liberia’ walikuwa tu wanatoa huduma. Halafu akauliza kama anaweza kuchapisha barua yangu katika jukwaa lao la mtandao. Nilitoa ruhusa hiyo, lakini sijaiona imechapishwa. Kutokana na vifo vingi, woga, dhoruba z a k i h i s i a n a k u k a t a tamaa kwa wa-Liberia na wananchi wengine wa Afrika Magharibi, inahitaji kuwa nitoe mchango katika kufikia utatuzi wa hali hii ya kutisha,

ambayo inaweza kutokea tena, kama haitakabiliwa inavyopasa na kwa ukamilifu . Nitazungumzia hali hii katika maeneo matano muhimu:

1 . E b o l a n i k i u m b e kilichobadilishwa vinasaba (GMO)

Horowitz (1998) alikuwa muwazi bila kificho alipoelezea hatari ya magonjwa mapya katika chapisho lake, ‘Virusi v i n a v y o z u k a : U k i m w i n a E b o l a - M a u m b i l e , ajali au dhamira.’ Katika mahojiano na Dk. Robert Strecker katika Sura ya 7, mjadala, katika miaka ya 1970 mapema, uliweka wazi kuwa vita ilikuwa ni kati ya nchi zinazolea KGB na CIA, na kuwa ‘utengenezaji’ wa virusi vinavyofanana na Ukimwi ulikuwa unamlenga mwingine. Katika mahali fulani wakati wa mahojiano, il iainishwa kuhusu Fort Detrick, ‘jengo la Ebola,’ na “matat izo makubwa na magonjwa yasiyo ya kawaida.” Hadi kufikia Sura ya 12 katika chapisho

Inaendelea Uk. 13

Page 3: ANNUUR 1148

3 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 24-30, 2014Habari

Katiba inayopendekezwa koti linalobana zaidi-SeifKATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema Katiba inayopendekezwa ni koti linalozidi kuibana Zanzibar, badala ya kuipa nafuu na kamwe Wazanzibari hawawezi kuikubali.

Maalim Seif ameyasema hayo wakati alipokuwa akihutubia katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha Gombani ya Kale, Chake chake Pemba.

Alisema Katiba hiyo ina mambo mengi ambayo yanainyang’anya Mamlaka yake Zanzibar, na wale wanaopita kusema kuwa Zanzibar imepata kila inachokitaka kwenye Katiba hiyo ni waongo.

Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar alisema Katiba hiyo imekiuka hata ile misingi mikuu ya mkataba wa Muungano ambayo inatambua Mamlaka ya Zanzibar ndani ya Muungano.

Akitoa mfano, Maalim Seif alisema CCM anapita na kusema kuwa Katiba hiyo imeyatoa mafuta na gesi asilia sasa kuwa ya Muungano, jambo hilo ni sawa na kuipaka mafuta Zanzibar, kwa sababu ardhi sasa imefanywa ni jambo la Muungano.

Alisema sheria za Zanzibar ziko wazi kabisa juu ya ardhi kumilikiwa na Wazanzibari, lakini kwenye Katiba inayopendekezwa suala hilo sasa ni la Muungano, licha ya kuwa ardhi ya Zanzibar ni ndogo sana na haitoshi hata kwa Wazanzibari wenyewe.

Maalim Seif alisema kuwa si kweli kwamba kuna msururu wa makampuni ya kuchimba mafuta na gesi asilia, baada ya kusikia sekta hiyo imetolewa kwenye Muungano.

Alisema kwamba Zanzibar haiwezi kuruhusu kuchimbwa mafuta na gesi asilia, kabla kwanza haijawa na sheria na Sera juu ya mafuta hayo ambazo ni nzuri zinazotamka wazi wazi ni vipi Wazanzibari watanufaika na mafuta na gesi hiyo.

“ L a z i m a t u we n a c h o m b o chetu wenyewe Wazanzibari cha kushughulikia uchimbaji wa mafuta, ambacho kitakuwa na usimamizi m z u r i u t a k a o h a k i k i s h a k i l a Mzanzibari ananufaika na mafuta na gesi, ikiwemo suala la ajira”, alisema Maalim Seif.

Katika hatua nyengine, Maalim Seif alisema katika uchaguzi mkuu ujao mwakani hakuna wa kukizuia chama cha Wananchi CUF kushinda na kuingia Ikulu ya Zanzibar.

A l i s e m a k wa m b a m a t u k i o yaliyojiri Dodoma juu ya mchakato wa Katiba yatawafanya Wazanzibari kushikamana na kuitetea Zanzibar, jambo ambalo wanajua litaweza kufanikiwa iwapo chama cha CUF kitakamata Serikali.

“ H a w a w a m e s h a m a l i z i k a , wameshamalizika kabisa namwambia rafiki yangu Rais Kikwete wasiwaletee Katiba hiyo Wazanzibari wataikataa”, alisema.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CUF, Ismail Jusa Ladhu amewapongeza wananchi wa kisiwa cha Pemba kwa kuwa imara miaka yote na kuonesha ukomavu mkubwa na msimamo usio yumba

Na Khamis Haji

katika kuhakikisha hadhi ya Zanzibar ina baki na wao wamekuwa ngome imara ya kuitetea Zanzibar na maslahi yake.

Alisema kwa wananchi wa Pemba hakuna kituko au kitimbi ambacho hawajafanyiwa, lakini hilo kamwe halikuwatoa kwenye mstari na wameweza kuhimili dhoruba hizo na hivi sasa kuna kila dalili chama cha CUF kitashika serikali katika uchaguzi mkuu hapo mwakani.

“Hakuna wa kuzuia wakati , wakati ni ukuta. Wakati sasa umefika, kila wanalolifanya CCM hivi sasa linawageukia wenyewe, na Inshallah ushindi wa CUF mwakani hauna mjadala na Maalim Seif anaingia Ikulu ya Zanzibar”, alisema Jusa.

Al ie leza kwamba uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa upande wa Zanzibar utakuwa ni kati ya wanaotaka Mamlaka kamili na wale madalali wa Zanzibar waliokwenda

kuiuza Dodoma.Jusa alisema kuwa katika hali

hiyo upande unaotaka Mamlaka kamili lazima utashinda kwa sababu unaungwa mkono na Wazanzibari walio wengi, wakiwemo viongozi mashuhuri ambao baadhi yao ni viongozi mashuhuri wa CCM.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui amesema mambo ya l iyokuwa yakifanyika Dodoma si mambo ya kufanywa na watu waungwana, hasa kitendo cha baadhi ya wajumbe kuuza nchi yao ya Zanzibar kwa kujali maslahi yao wachache.

Al ie leza kuwa Wazanzibar i wanachotaka sasa ni kuwa na Mamlaka ya kujiamulia mambo yao katika kuimarisha uchumi na hali za wananchi, na wala hawataki kuona baadhi ya wachache wakipigania matumbo yao na kuwaacha wananchi walio wengi wakisumbuliwa na hali

ngumu ya maisha. Mkurugenzi wa Habari na Uenezi

wa CUF, Salum Bimani amesema dalili ya kuwa katiba iliyopendekezwa Dodoma haina maslahi kwa Zanzibar, wa j u m b e we n g i wa l i o h u s i k a kuipitisha hivi sasa wanaona shida kutembea Zanzibar kutokana na usaliti walioufanya.

M k u t a n o h u o u l i o f a n y i k a Gombani ya Kale Pemba ni wa pili mkubwa kufanywa na CUF tangu Bunge Maalum kutoa Katiba inayopendekezwa na kukabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar huko Dodoma.

Mkutano wa kwanza ambao pia ulihutubiwa na Maalim Seif na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wanachama, wafuasi na wananchi mbali mbali wa Zanzibar ulifanyika Oktoba 16 katika viwanja vya Kibandamaiti.

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

Kuna haja ya kujiuliza kwanini maradhi haya chanzo ni AfrikaInatoka Uk. 2takriban milioni 30 (kufikia mwaka wa 2009).

Hadi mwaka 2010, takriban watu milioni 34 wameambukizwa UKIMWI kote duniani. UKIMWI umechukuliwa kama janga, yaani mlipuko wa ugonjwa katika eneo kubwa, na ambao ungali unaendelea kuenea sehemu mbalimbali duniani kote,lakini zaidi barani Afrika.

K u n a s i n t o f a h a m u k u h u s u UKIMWI kama vile kwamba unaweza kusambazwa kwa kugusana tu bila ngono.

Kwa miaka mingi , wataf i t i wamekuwa wakijaribu kutafuta chanzo cha HIV, ambao hadi sasa tunaelezwa kuwa zaidi ya watu milioni 36 wameshapoteza maisha kwa ugonjwa huo dunia kote, zaidi katika nchi karibu na jangwa la Sahara.

Kwa sasa timu ya watafiti ya Kimataifa (International research team) imesema wamepata jibu la asili ya ugonjwa huo. Wamesema kuwa wamegundua kuwa maradhi hayo yalianzia katika jiji la Kinshasa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika miaka ya 1920s.

"Our genetic data tells us that HIV very quickly spread across the DRC, traveling with people along railways and waterways to reach Mbuji-Mayi and Lubumbashi in the extreme South and Kisangani in the far North by the end of the 1930s and early 1950s," amenukuliwa akisema Dk. Nuno Faria wa timu ya watafiti hao.

Timu hiyo ya watafiti iliyoongozwa na wachunguzi kutoka Chuo Kikuu cha Oxford cha Uingereza na wale wa Chuo Kikuu cha Leuven (KU Leuven) cha Ubelgiji, walichapisha majibu ya utafiti wao katika jarida la Science.

Kwa mujibu wa watafiti hao,

ilibainishawa kwamba virusi vya HIV vilihamishwa kutoka kwa nyani hadi kwa binadamu kwa si chini ya mara kumi na tatu.

Mwandishi maarufu, Prof. Oliver Pybus, wa Idara ya Zoology katika Chuo Kikuu cha Oxford, alisema kuwa kufuatia utafiti wa uhakika wa HIV, timu yao ya watafiti ilifuatilia asili ya Ukimwi huko Kinshasa – zamani ikiitwa Léopoldville, katika miaka ya 1920s nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Prof. Pybus, alisema walitambua sababu kadhaa ambazo zilisababisha virusi vya Ukimwi kusambaa kutoka Kinshasa hadi Katika nchi za karibu na jangwa la Sahara kati ya miaka ya1920s na 1950s.

"Ilipogundulika asili ya ugonjwa, walishabihisha na vielelezo vya kihistoria na kuthibitika kwamba

Inaendelea Uk. 13

Page 4: ANNUUR 1148

4 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 24-30, 2014Makala

Sifa na masharti ya kujiunga Muombaji atimize sifa na masharti yafuatayo:(i) Awe Muislamu aliye tayari kuishi Kiislamu(ii) Awe anajua kusoma Qur’an kwa ufasaha.(iii) Awe amemaliza juzuu ya 1 na 2 ya Maarifa ya

Uislamu, Darasa la Watu Wazima kabla ya kujiunga.(iv) Awe na uwezo wa kusoma na kuandika lugha ya

Kiswahili kwa ufasaha.(v) Awe amehitimu darasa la saba au kidato cha nne

na awe anafundisha madrasa au kipindi cha dini katika shule za Msingi au Sekondari.• Patakuwanausaili namtihani siku ya tarehe

29/11/2014 saa 2:00 asubuhi katika chuo cha Ubungo na Kirinjiko na katika vituo mbalimbali vya mitihani kote nchini.• Mwishowakuchukuafomunitarehe28/11/2014.• Fomuinalipiwashilingi5,000/-tu.

Fomuzinapatikana katika vituo vilivyoorodheshwaukurasawa15wagazetihili.

MKURUGENZI

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

NAFASI ZA KUJIUNGA NA KOZI FUPI YA UALIMU KATIKA VYUO VYA UBUNGO NA KIRINJIKO-2015

VUGUVUGU la kisiasa lililopita kwenye nchi za Kiarabu, maarufu kama 'Arab Spring', na makundi yaliyokamata madaraka baada ya vuguvugu hilo, yameonyesha mapungufu makubwa ya kisiasa. Kulikuwa na matumaini kwamba siasa za zamani kwenye nchi hizo, zingetupwa kwenye jalala la historia na siasa mpya kuibuka. Hata hivyo, vikundi vya Kiislamu vilivyokamata madaraka, vikafanya kila linalowezekana kuhifadhi mfumo ule ule uliokuwepo, hatua ambayo imekwaza siasa za Kiislamu kuibuka kwenye nchi hizo.

Kabla ya kuingia ndani sana, ni vyema wasomaji wangu wakaelewa kwanza, fikra ya kisiasa ya Kiislamu ni nini? Umma wa Kiislamu unapaswa kufahamu s iasa na Uis lamu. Waislamu lazima wafahamu kwamba Uislamu unawapa mchepuo maalumu (angle), wakati wanapoyaangalia matukio mbalimbali yanayotokea ulimwenguni.

Na yale matukio ambayo hayaakisi siasa za Kiislamu katika namna iliyo wazi na isiyo tatanishi, kwa hakika hayapaswi kuungwa mkono na Waislamu. Mwenyezi Mungu anasema:

"Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo katika nafsi zao" Qur(13:11).

Kujenga wanasiasa: Mwanasiasa aliye makini lazima awe na fikra iliyo wazi kabisa kuhusu mwelekeo wa siasa zake. Hii ina maana kwamba anatakiwa kuweka mchepuo (angle) kuhusu jinsi anavyoyaangalia mambo au matukio yanayotokea. Mwanasiasa anapokuwa hana mchepuo huu, lazima atachanganyikiwa kwenye mseto wa matukio yanayokinzana, ambayo hutokea nchini mwake na duniani kwa ujumla.

Kwa hiyo atakuwa hana ufanisi katika kufikia malengo yake na siasa anazosimamia zitakuwa vurugu mechi iliyokosa mwelekeo. Katika Ulimwengu wa Magharibi, wanasiasa wa kikafiri wana mchepuo sahihi sana, (kwa mujibu wa itikadi yao), wa kuyaangalia mambo na matukio yanayotokea duniani.

Wanayaangalia mambo kutoka kwenye msingi wa Ubeberu na fikra zake kama usekula, misingi ya k i d e m o k r a s i a , d h a n a z a uhuru na kuendeleza maslahi binafsi. Wanapojiingiza kwenye siasa, wanasiasa wa Kimagharibi wanafahamu vizuri kwamba sera ya Mambo ya Nje ya nchi zao, inalenga kuhakikisha maslahi ya mataifa yao. Wanafahamu jinsi ya kuyatazama mataifa mengine, na nini cha kutafuta kutoka kwenye mataifa hayo, katika uhusiano wa aina yoyote watakaokuwa nao.

Katika siasa za ndani,wanafahamu maana ya jukumu la dola kuhudumia masuala ya wananchi. Wanazo fikra kuhusu jinsi gani raia waishi, na haki za wananchi zinapaswa kuwa nini. Wanaijua vizuri itikadi yao na wanaikumbatia kikamilifu, ikiwa ni pamoja na kuutazama ulimwengu kupitia misingi iliyowekwa na itikadi hiyo.

Wanasiasa hawa wa Magharibi pia wanaendeleza dhana zile zile

Mtazamo wa kisiasa wa KiislamuSaid Rajab za kisiasa, wakipata uzoefu kupitia

mila ya kisiasa iliyopo kwenye nchi zao. Wanajifunza ubinafsi, ulaghai, hadaa, usanii, kuhalalisha uovu, na kusema uongo ili kuficha kashfa zinazowahusu. Wanajifunza kwamba namna ya kuhukumu jambo, siyo ukweli wake au uongo wake, bali namna gani itaendana na maslahi yao. Wanajenga uwezo wa kutumia matukio yanayojiri kwa faida yao na hasara ya wengine. Wanasiasa hawa wanatambua kwamba kuna taswira ya umma, ambayo lazima waionyeshe hadharani, bila ya kuzingatia ukweli halisi wa kile wanachohisi na kufikiria. Wanasiasa hawa wa Kimagharibi wanajifunza pia kwamba katika siasa zao, ni sheria ya mwituni (mwenye nguvu humtafuna mnyonge), na kwamba mtu anaweza akawa rafiki leo siku inayofuata akawa adui. Ni kupitia njia hii ndipo wanasiasa wa Magharibi wanavyoweza kujenga mchepuo wao wa jinsi ya kuyaangalia mambo na matukio yanayojiri. Misingi hiyo ndiyo inayoongoza hatua zao za kisiasa, ambazo ni muhimu kwa mwanasiasa binafsi na kwa nchi yake.

Uislamu unapinga vikali tabia zote hizo zinazofanywa na wanasiasa wa Kimagharibi . Uislamu pia unapingana vikali na misingi na itikadi inayotumiwa na wanasiasa hao kujenga mchepuo wao wa kisiasa. Uislamu unawajenga wanasiasa kwenye msingi wake wa kipekee wa maadili na uadilifu.

Kwa mfano, badala ya ubinafsi, Uislamu unajenga ukarimu, badala ya kutumia mbinu chafu kukamilisha ajenda, Uislamu unasisitiza ukweli, uwazi, uadilifu na hofu ya Mwenyezi Mungu. Uislamu unafundisha kwamba kile ambacho Muislamu anachotaka kwa ajili yake, basi humtakia pia Muislamu mwenzake. Lakini ulimwengu wa Magharibi unafundisha kwamba maslahi binafsi yanatangulia maslahi mengine yote. Kwa Waislamu, wanasiasa wanaobeba mtazamo halisi wa siasa za Kiislamu, karibu wote walipotea wakati dola ya Kiislamu ya Uthmaniyya ilipoanguka mwaka 1924. Maadui wa Uislamu walifanikiwa kuitia sumu fikra ya kisiasa ya Waislamu na hivyo kuvuruga kabisa mchepuo wao wa kisiasa. Maadui hawa walipandikiza fikra tofauti za kisiasa kwenye nchi za Waislamu - kama vile utaifa ambapo Waislamu kutoka Arabuni wakaanza kujiona ni tofauti na ndugu zao wa Istanbul.

Baada ya dola ya Kiislamu kusambaratika kabisa mwaka 1924, siasa katika nchi za Waislamu zikadhibitiwa na fikra za Kisoshalisti na Kibeberu. Harakati za kisiasa ambazo ziliendeshwa ndani ya miundo ya dola iliyobadilika kutoka kwenye utawala wa Kiislamu, zikawa hazina ufanisi kabisa na zilitumiwa tu na maadui kama daraja la kufikia malengo yao.

Mchepuo wa wanasiasa katika nchi za Waislamu, ukawa siyo wa Kiislamu tena, kama tunavyoshuhudia mpaka leo, ambapo lengo lao kuu ni kuendelea kubaki madarakani. Orodha ya baadhi ya wanasiasa wa ulimwengu wa Kiislamu katika karne iliyopita ni pamoja na Mustafa Kemal, Muhammad Ali Jinnah, Gamal Abdul Nasser, Anwar Sadat, Mfalme Hussein wa Jordan, Saddam Hussein,

Nawaz Sharif, Pervez Musharraf, Benazir Bhutto na wengine wengi. Hao wote walikuwa mbali kabisa na siasa za Uislamu na wote walitumikia maslahi ya mataifa ya Magharibi kuliko ya watu wao.

Wale ambao walijaribu kujenga mataifa yao, walifanya hivyo kwa kutumia msingi dhaifu wa kisiasa - mfano Gamal Abdul Nasser alikuwa na msingi dhaifu sana wa Utaifa wa Kiarabu (Arab Nationalism) katika kujenga siasa zake. Wote hao walitumia mfumo wa kisiasa u l i o p a n d i k i z wa n a wa t u wa Magharibi, ambao umejengwa kwa kuzingatia dhana za Kimagharibi. Kwa sababu hiyo, haikuwezekana kabisa kwa mtu yeyote ndani ya serikali au vyama, kufanyakazi ndani ya mfumo huo na kuleta manufaa kwa Waislamu.

Kama mchepuo wa k is iasa ulioshikwa na Waislamu katika nchi za Waislamu siyo wa Kiislamu, basi maadui wa Uislamu wanafurahi zaidi kwa sababu hilo linawahakikishia kuziburuza nchi za Waislamu hata miaka elfu moja ijayo!

Sasa hiyo ni changamoto kwa Waislamu wote popote walipo duniani. Katika mazingira kama haya, Waislamu wanatakiwa kujipamba katika utamaduni wa Kiislamu kama itikadi na mfumo wa maisha, ili kwa mara nyingine tena kuwe na 'block' ya kisiasa miongoni mwa Waislamu, ambayo itaurudisha umma wa Kiislamu mahali pake.

Mchepuo Maalumu: Tunapoingia

kwenye siasa, lazima Waislamu tufahamu mtazamo na mchepuo wetu kwa usahihi. Kama hatujui, basi kuna uwezekano mkubwa watu wengine wakawatumia Waislamu kukamilisha ajenda zao. Iwapo mchepuo na mtazamo havitakuwa wazi kichwani, basi hii inaweza kusababisha mwanasiasa Muislamu kuwa na msingi dhaifu wa kisiasa, unaoweza kumfanya atupilie mbali malengo yake.

Mchepuo wa kisiasa unaozingatia misingi ya Kiislamu ni tofauti na wa kipekee sana. Mchepuo huu unatumika kama dira kwa wanasiasa Waislamu, ambao utawafanya wachukue hatua sahihi za kisiasa na kuwapeleka kwenye mwelekeo sahihi. Mchepuo huo maalumu ambao Wais lamu wanapaswa kuyaangalia mambo, hautokani na matamanio ya nafsi zao, bali unatoka kwenye Aqida ya Kiislamu.

Kutoka kwenye maandiko ya Kiislamu, inafahamika vyema kwamba Uislamu umekuja kwa wanadamu kama Dini, na mchepuo wa 'La illaha ila Llah' ndiyo unaopaswa kuwa miwani ya kuangalia mambo yote na matukio yanayojiri. Hii maana yake ni kwamba 'hukmu sharia' na ufahamu wa itikadi ya Kiislamu ndiyo lenzi za wanasiasa Waislamu katika kuyaangalia mambo.

Mchepuo wa Muislamu katika kuyaangalia matukio na masuala yanayotokea kwenye maisha, lazima

Inaendelea Uk. 11

Page 5: ANNUUR 1148

5 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 24-30, 2014Habari

JAMII ya Waislamu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imelaani vikali mashambulizi ya waasi wa Uganda dhidi ya yao.

Mjumbe wa Jumuiya hiyo ya Waislamu Musa Angwandi, ameonyesha masikitiko makubwa kuhusu mauaji ya Waislamu 80 raia wa nchi hiyo katika kipindi cha wiki mbili zilizopita kwenye eneo hilo.

Waislamu hao wa mji wa

NAIBU Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk. Marie Paule Kieny, amesema J u m a n n e w i k i h i i k u wa majaribio ya dawa ya chanjo ya Ebola yanaendelea huko Ulaya Marekani na Afrika na kwamba, kama chanjo hizo zikionekana kuwa salama, yanaweza kufanyika majaribio yake Afrika Magharibi Januari mwakani.

H a t a h i v y o D k . K i e n y , hakusema ni lini chanjo ya Ebola inaweza kupatikana duniani kote,

MOMBASAMaelfu ya wakazi wa Mombasa wakiongozwa na viongozi wao wamehudhuria mazishi ya msomi maarufu nchini Kenya, Profesa Ali Mazrui, aliyezikwa katika makaburi ya familia yake mjini Mombasa, karibu na jengo la makumbusho la Fort Jesus, siku ya Jumapili.

Mwili wa Profesa Mazrui uliwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mombasa alfajiri na kupokelewa kwa heshima za kitaifa na wakuu wote wa kisiasa wa County ya

Profesa Ali Mazrui azikwa Mombasa

Mombasa, wakiongozwa na Gavana Ali Hassan Joho akiwemo pia Mwanasheria Mkuu wa Kenya, Willy Mutunga.

Baadae ulisindikizwa kutoka New York nchini Marekani na binamu yake Profesa Al Amin Mazrui, mjane wake Pauline Uti, mwanae Farid na wenzake wawili wa Chuo Kikuu cha Binghamton New York.

Profesa Mazrui alifariki Oktoba 12, 2014 nyumbani kwake Vestal, New York, baada ya kuugua kwa muda akiwa na umri wa miaka 81. (VOA).

WHO yasema chanjo Ebola kuanza Januariwakati alipokuwa akiongea na waandishi jijini Geneva Uswisi.

Hata hivyo wakati Naibu Mkurugenzi huyo akitoa kauli yake hiyo ya matumiani, bado mpaka sasa hakuna dawa wala chanjo ya ugonjwa huo, ambao umeuwa zaidi ya watu 4,500 huko Afrika Magharibi mwaka huu.

Jumatatu shirika hilo lilitangaza kuwa taifa la Nigeria halina tena ugonjwa wa Ebola, baada ya siku 42 kupita bila ripoti za kesi mpya a ugonjwa huo.(VOA).

Waislamu wa DRC walaani kuuawa na waasiBeni walisema kuwa licha ya kufahamika kuwa Qur’ani Tukufu inapinga kuua watu wasio na hatia, lakini waasi hao wa Uganda wamekuwa wakizidi kuwafanyia ukatili na ukandamizaji Waislamu.

K w a m u j i b u w a r i p o t i iliyotolewa na Jumuiya za kiraia katika mkoa wa Kivu Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo, imewataja waasi hao wa Uganda kuwa ndio waliofanya mauaji hayo ya hivi karibuni.

Madrasa Hijjatul Wadaa. Iliyopo Nangurukuru, Kilwa. Inaomba msaada wa ujenzi wa Jengo la Madrasa. Kwa sasa madrasa hiyo yenye watoto wa Kiislamu 75, inaendeshwa nje ya nyumba ya Muislamu na kushindwa kuendelea na masomo katika kipindi cha mvua au cha jua kali. Msaada unaohitajika ni pesa au vifaa vya ujenzi. Toa kwa ajili ya Allah (sw).

Ka maelezo zaidi piga namba:- 0682 40 65 75.

Waislamu wa Kata ya Mzenga, Wilayani Kisarawe, wanatoa wito kwa Taasisi za Kiislamu na Waislamu kujitokeza kwao ili wawauzie eneo/Ardhi yenye heka 200, kwa ajili ya maendeleo ya Uislamu na Waislamu. Ardhi inafaa kwa Kilimo na ujenzi wa Shule. Ardhi ipo Km 35, Kutoka Mlandizi, Barabara ya Morogoro (Highway).

Kwa maelezo zaidi wasiliana kwa namaba:- 0787/0767 40 81 10 au 0714 111 669.

Msaada wa ujenzi wa Madrasa

Kiwanja kinauzwa

Madaktari wachunguza afya za watuhumiwa Keko, DSM

Hali ya Afya ya Sheikh Mselem Ali Mselem inaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu na hatimaye ameweza kuhudhuria mahakamani juzi Jumatano kusikiliza kesi inayomkabili.

Wa k i l i w a m t u h u m i w a al i thibi t ishiwa juu hal i za w a t u h u m i w a w a g o n j w a gerezani na kwamba, madakitari walipelekwa na kuchukua vipimo kwa ajili ya uchunguzi wa afya za watuhumiwa hao.

Kwa mujibu wa maelezo ya Wakili wa upande wa utetezi, Abdalah Juma Mohammed, alisema kuwa Sheikh Mselem, alikuwa akisumbuliwa na malaria tangu alipoletwa gerezani Keko.

Akizungumzia upande wa watuhumiwa wengine, wakili huyo alisema hali zao zinaendelea vizuri tofauti na ilivyokuwa awali, baada ya jopo la madaktari kufika gerezani na kuwapatia huduma.

Sheikh Farid Hadi na wenzake 22 walithibitisha kuwa ni kweli jopo hilo la madaktarii walifika na wal i shachukua v ip imo kwa uchunguzi zaidi wa afya za watuhumiwa, kwa hiyo wanasubiri majibu ili waweze kupatiwa tiba kamili, na kwamba huduma za awali zilishaanza kutolewa.

Sheikh Farid aliongeza kuwa wiki iliyopita walitembelewa na Jopo la Masheikh wa Jumuiya ya Maimamu Tanzania, jambo ambalo liliwafariji sana.

Hakimu anayesimamia kesi hiyo, Hellen Liwa, alisema kuwa uamuzi wa shauri hilo hauwezi kutolewa kwa sababu jalada la kesi hiyo bado lipo Mahakama Kuu.

Aliwataka waumini kuzidisha

Na Seif Msengakamba

dua kwa watuhumiwa hao, kwani dua zao zinahitajika ili Masheikh hao na Waislamu wengine waweze kuwa huru na kuendelea na shughuli zao za kumtumikia MwenyeziMungu.

Kesi hiyo iliahirishwa na itatajwa tena Novemba 4 mwaka huu.

Sheikh Mselem Ali Mselem.

Jeneza la Profesa Mazrui likipelekwa makaburini Kibokoni Mombasa, Kenya.

Page 6: ANNUUR 1148

6 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 24-30, 2014Makala

J U M A M O S I i l i y o p i t a n i l i p a t a b a h a t i y a kuhudhuria katika mahafali ya kuwaaga wanafunzi wal iohi t imu darasa la saba wa shule ya msingi ya Kiislamu Thaaqibu, iliyopo mtaa wa Kiloleli, Kata ya Nyamanoro, Tarafa ya Ilemela wilayani Ilemela Mwanza.

Mahafali hayo yalikuwa ya kuwaaga wanafunzi wa shule hiyo waliohitimu elimu ya msingi mapema mwezi Septemba mwaka huu, na yalifanyika katika viwanja vya shule hiyo kuanzia saa mbili asubuhi hadi majira ya saa tisa alasiri.

Mahafal i hiyo, mbali n a k u h u d h u r i w a n a Waislamu kwa ujumla wao, yalijumuisha pia wanafunzi, walimu, wazazi, walezi, wadau wa elimu pamoja na viongozi mbalimbali wa dini.

M g e n i R a s m i k a t i k a mahafali hiyo alikuwa ni Mratibu wa Elimu wa Kata (MEK) ya Nyasaka Bw. Mussa Ramadhani Khamisi, ambaye pia aliwahi kuwa Mratibu wa Elimu wa Kata (MEK) ya Nyamanoro, Kata ambayo ndipo shule hiyo ya msingi ya Kiislamu ilipo.

Pamoja na kuvut iwa n a m a m b o c h u n g u niliyoyashuhudia katika mahafali hiyo, yakiwemo m a o n ye s h o a n u wa i ya kinadharia na ya kivitendo ya masomo mbalimbali katika elimu ya mazingira na ya mwongozo, mvuto wangu kwa yaliyokuwa yakiendelea kujiri katika mahafali hiyo, ulishtadi zaidi kutokana na uwasilishwaji wa taarifa ya shule.

Taarifa hiyo iliyosomwa mbele ya mgeni rasmi na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Mwl. Khamisi Kambi, kwa hadhirina wote, iliainisha na kubainisha pamoja na mambo mengine, mintaarafu ya shule hiyo, mafanikio ya kitaaluma yaliyofikiwa na wahitimu wa kwanza kabisa wa shule hiyo mnamo 2012, pamoja na wahitimu waliowafuatia watangulizi wao mnamo 2013.

Akifafanua mafanikio hayo kupitia taarifa ya shule, Mkuu wa shule hiyo alianza kwa kubainisha matokeo ya wahitimu wa mwaka 2012, ambapo aliainisha kwamba wa n a f u n z i wa l i o f a n ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka huo walikuwa ni arobaini na sita (46). Kati ya hao, waliopata daraja 'A' ni mwanafunzi mmoja (1), daraja 'B' ni wanafunzi ishirini (20), na wanafunzi ishirini na watano (25) waliosalia walipata daraja 'C'.

Hakukuwa na mwanafunzi yeyote aliyepata daraja 'D', 'E'

Kila la kheri wahitimu ThaaqibuNa Abuu Nyamkomogi

wala 'F' kwa mwaka huo. Kwa upande wa matokeo

ya m wa k a 2 0 1 3 , M wl . Khamisi Kambi, alibainisha k w a m b a w a n a f u n z i waliofanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka jana walikuwa ni wanafunzi arobaini na watatu (43), ambapo mwanafunzi mmoja (1) alipata daraja 'A', wanafunzi ishirini na watano (25) walipata daraja 'B' na wanafunzi kumi na saba (17) walipata daraja 'C'.

Kadhalika katika matokeo hayo ya mwaka jana hakuna mwanafunzi yeyote wa shule hiyo aliyepata daraja 'D', 'E' wala 'F' kama ilivyokuwa kwa matokeo ya mwaka 2012.

N d u g u m s o m a j i , ukilinganisha matokeo hayo ya mwaka juzi na ya mwaka jana unaweza kubaini mambo makuu matatu ambayo ni uwiano, ongezeko pamoja na punguzo.

Kwa kuanza na kipengele cha uwiano wa madaraja ya ufaulu, matokeo ya mwaka juzi na ya mwaka jana yanawiana kwa idadi ya wanafunzi waliofaulu kwa daraja hilo, ambapo mwaka 2012 ni mwanafunzi mmoja (1) tu aliyepata daraja 'A' kama ilivyokuwa kwa matokeo ya mwaka 2013.

Kwa upande wa kipengele cha ongezeko , idadi ya wanafunzi waliopata daraja 'B' imeongezeka kutoka wanafunzi ishirini (20) kwa mwaka juzi hadi kufikia wanafunzi ishirini na watano (25) kwa mwaka jana.

K w a u p a n d e w a kipengele cha punguzo, idadi ya waliopata daraja 'C ' imepungua kutoka wanafunzi ishirini na watano (25) kwa mwaka juzi hadi kufikia wanafunzi kumi na saba (17) kwa mwaka jana.

M a f a n i k i o h a y a y a

kitaaluma ya vijana wetu hawa yanapaswa, si tu kuungwa mkono kwa hali na mali na kila Muislamu mwenye raghba na maendeleo ya Uislamu na ya Waislamu kwa upande mmoja, bali pia na kila mwananchi mwenye nia njema na maendeleo ya nchi hii na ya wananchi wake kwa ujumla kwa upande mwingine.

Kwa mantiki hii, kwanza nashawishika kama (nikiwa) Muislamu na pili kama (nikiwa) mwananchi mwenye raghba na maendeleo ya dini yangu pamoja na nia njema ya ustawi wa taifa langu, kuunga mkono mafanikio haya ya kitaaluma ya vijana hawa wa Kiislaamu kwa upande wa kwanza na ya wananchi wenzetu kwa upande wa pili, japo kwa kuwaombea dua na kuwatakia kheri katika maendeleo yao ya kitaaluma kwa mustakbali wa maendeleo ya dini yao na ustawi wa taifa lao, na hususan katika matokeo yao tarajiwa ya mtihani wao wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka huu.

Alhamduli l lah, kama w a l i v y o p a t a k u n e n a wahenga kwamba "nyota njema huonekana asubuhi". Matokeo ya mtihani wa somo la maarifa ya dini ya Kiislamu kwa kuhitimu elimu ya msingi ya vijana wetu hawa mwaka huu ambayo tayari yalishatoka, yanatoa ishara njema na taswira chanya na tumainishi pamoja na farijishi kwa mustakbali wa matokeo ya wahitimu hao, kwa masomo ya elimu ya mazingira yanayotarajiwa k u t o k a s i k u z a u s o n i Inshaallah.

Kwa matokeo ya somo la maarifa ya dini ya Kiislamu ya m wa k a h u u 2 0 1 4 , wanafunzi wa shule hiyo

waliofanya mtihani wa somo hilo walikuwa ni hamsini na watano (55) ijapokuwa walipaswa kuwa hamsini na sita (56), ila mmoja wao hakujaliwa kufanya mtihani huo kutokana na dharura iliyokuwa nje ya uwezo wake.

Kati ya hao, waliopata daraja ‘A’ ni wanafunzi thelathini na t isa (39) , w a l i o p a t a d a r a j a ‘ B ’ ni wanafunzi kumi na watano (15) na daraja ‘C’ ni mwanafunzi mmoja (1) tu. Halikadhalika hakukuwa na mwanafunzi yeyote aliyepata daraja 'D', 'E' wala 'F' kwa mwaka huu kama ilivyokuwa kwa matokeo ya masomo ya mazingira kwa mwaka 2012 na 2013.

Kwa jumla, wanafunzi waliohitimu elimu ya msingi katika shule ya Kiislaamu Thaaqibu mwaka huu ni hamsini na sita (56) ambapo wavulana wal ikuwa ni ishirini na wanane (28) na wasichana walikuwa ni idadi hiyo hiyo, yaani ishirini na wanane pia (28).

Tunamuomba Allah (S.W.) awajaalie wahitimu wote hawa wafuzu mtihani wao huo wa kuhitimu elimu ya msingi na waweze kuendelea na masomo ya elimu ya sekondari, pasi na kusahau lengo la kuumbwa kwao na dhima ya kuletwa kwao hapa ulimwenguni. Allaahumma aamiin.

Kama ilivyo ada, kila penye mafanikio ni nadra kutokuwapo changamoto. K w a m u k t a d h a h u o , pamoja na mafanikio hayo ya kitaaluma ya shule hii kama ilivyodokezwa hapo nyuma, shule hii inakabiliwa na changamoto kadhaa kama zilivyodokezwa na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo kupitia taarifa ya shule kwa mgeni rasmi na hadhirina wote katika mahafali hiyo.

Baadhi ya changamoto zilizodokezwa na Mkuu huyo katika mahafali hayo

ni pamoja na ukosefu wa Msikiti wa kudumu wa shule, ukinzani baina ya malezi yatolewayo shuleni kwa mwanafunzi na yale yatolewayo nyumbani kwa mwanafunzi, pamoja na uchelewaji wa kulipa ada kwa baadhi ya wazazi au/ walezi, jambo ambalo husababisha pia kuchelewa au kukwama na wakati mwingine hata kutokutekelezwa kwa baadhi ya mambo yaliyo katika mpango-kazi wa shule, kutokana na ufinyu wa bajeti inayotokana na nakisi ya fedha.

A k i s h a d i d i a k u h u s u namna ya kukabiliana na changamoto ya suala la ulipaji ada, kama ilivyodokezwa hapo juu mbele ya wazazi na walezi na wote waliohudhuria katika mahafali hiyo, mgeni rasmi aliwakumbusha na kuwahimiza wazazi na walezi wajitahidi na kujizatiti kadri wawezavyo kuwalipia watoto wao ada ya shule kwa wakati, ili kurahisisha suala la uendeshaji wa shule.

Ving inevyo sua la l a uendeshaji wa shule pasi na kuwa na fedha litakuwa gumu kwa kuwa shule haina chanzo kingine cha kutegemewa cha mapato, zaidi ya ada ya wanafunzi kama ilivyobainishwa awali kat ika taari fa ya shule iliyowasilishwa kadamnasi na Mwalimu Mkuu wa shule ya Thaaqibu.

K w a k u z i n g a t i a c h a n g a m o t o z o t e zilizodokezwa zinazoikabili shule yetu hii, ni dhahiri shahiri kuwa nguvu za binafsi na za pamoja za kihali na za kimali zinahitajika ili kukabiliana na changamoto zilizoelezwa.

Kwa upande wa mikakati ya shule, Mwalimu Mkuu a l i b a i n i s h a b a a d h i ya mikakati ya baadaye waliyo nayo shuleni hapo kuwa ni pamoja na ujenzi wa maktaba, uendeshaji wa semina za malezi kwa wazazi na walezi, ufundishaji wa madarasa ya mitihani wakati wa likizo pamoja na uandaaji wa ziara za kitaaluma za kuzuru maeneo mbalimbali, kwa lengo la kupanua wigo wa ufahamu na uelewa wa mambo mbalimbali pamoja na kuwajengea ta j i r iba wanafunzi husika kupitia mazingira halisi na kutokana na mambo mbal imbal i wa j i f u n z a y o d a r a s a n i kinadharia.

Nihitimishe makala hii kwa kuradidi kauli ya anuwani ya maudhui ya makala hii kama usuli wa makala husika, kwa kuwatakia wahitimu wa darasa la saba katika shule ya msingi ya Kiislamu Thaaqibu kheri na fanaka katika matokeo yao tarajiwa, kwa kauli za tumaini na za faraja kwa vijana wetu hao.

“Kila la kheri wahitimu thaaqibu-2014”.

(Abuu Nyamkomogi ni msomaji wa muda mrefu wa gazeti la AN-NUUR anayeishi jijini Mwanza).

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Suleiman Rashid (Wa tatu kutoka kushoto )akiwa na Masheikh na watoa mada katika semina ya Maimamu wa mkoa wa Dar es salaam, iliyozungumzia nafasi ya Imamu na mlinganiaji katika kuoingoza jamii. iliyofanyika katika kituo cha Kiislamu Markazi Chang'ombe, jijini Dar es salaam wiki iliyopita.

Page 7: ANNUUR 1148

7 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 24-30, 2014Makala

ULIMWENGU wa leo ni ulimwengu wa Sayansi na Teknologia. Watoto michezo yao imejikita kwenye gemu za kompyuta, watu wazima usomaji wao wa magazeti na habari, wanatumia blogi za jamii, nazo pia ni kwa kutumia kompyuta. Wengine wanasoma hizo makala kwa kupitia simu zao, ambazo kitaalam pia zinakubalika kuwa kompyuta za mkononi.

Ni mtu mmoja mmoja ambae anatoka nje kwenda kurusha vishada. Kwa maana hiyo, si wengi watakaonielewa nikisema “Zanzibar Arijojo”. Kwa wasionielewa na wanaotaka kujikumbusha, arijojo, ni ile hali ambayo kishada ambacho kilikuwa kimedhibitiwa kwa umakini kwa kutumia uzi mwembamba, kinapigwa na upepo mkali au kamba inakatika na udhibiti wa kishada kupotea, hapo ndipo kishada kinakwenda arijojo. Na mara nyingi hupotea na hakionekani tena.

Hali ya nchi ya Zanzibar ambayo ni kipenzi cha wengi hasa wale ambao vitovu vyao vimezikwa huko inaonekana kwenda arijojo. Hali hiyo inazidi kuendelea hasa wakati wa mchakato wa kutunga Kat iba Mpya ya Jamhur i ya Muungano wa zilizokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika, ambazo kwa sasa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, unavyoendelea.

Wazanzibari walioko ughaibuni wanajaribu kufuatilia na kuchambua mambo yanayotokea. Kwenye makala hii, nitaweka baadhi ya mambo ambayo wataalam na wasiokuwa wataalam wa Kizanzibari wanavyosema kuhusiana na yaliyojiri kwenye mchakato wa katiba mpaka hapa tulipofikia.

Ikumbukwe kwamba, hali ya Zanzibar kisiasa na kimaendeleo imepitia hatua kadha. Nyingi ya hizo ni hatua nzito sana. Kwa muda wote huo, Zanzibar imeweza kuhimili mikiki na dhoruba nzito zilizotokea. Dhoruba ya mara hii inakuja kwa nguvu kubwa mno, na hatujui ni jinsi gani Zanzibar itasalimika kwenda arijojo.

Inaaminika lakini kwamba, wananchi wa Zanzibar wana historia ya kuwalaghai wakorofi wengi. Waliweza kuwashinda Wareno, ambao walikuwa na jeshi kubwa sana. Walishirikiana na Waoman, kuwaondoa Wareno. Waliwashinda Waingereza, pamoja na nguvu zote walizokuwa nazo, baada ya muda ilibidi waitowe Zanzibar. Ingawa sio kwa utulivu, walifanya Mapinduzi, yaliyokusudiwa kuleta usawa baina ya watu. Bahati mbaya kwa watu wa kawaida hawaamini kwamba Mapinduzi hayo yalifikia malengo yaliyokusudiwa.

Na katika kipindi hichi cha karibuni, walitoka kuanzia kutokuwa na Katiba, Bunge wala Bendera. Mpaka wamefikia kuwa na vyote hivyo, ilhali wanaamuliwa mengi ya mambo yao Tanganyika. Kwa mambo yanavyokwenda, inaashiria kana kwamba Zanzibar ni Koloni la Tanganyika. Ukitaka ujue undani wa haya, angalia bendera ya Tanganyika ilivyokuwa Koloni la Uingereza na bendera ya Uingereza ilivyo. Na jinsi bendera ya Zanzibar na ilivyo Bendera inayoitwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini hasa inayosimamia mambo ya Tanganyika. Hapo utaona udhahiri wa Zanzibar

Zanzibar ArijojoNa O. Ali

ni nini mbele ya Tanganyika. Bila kutafuna maneno inakimu maana ya KOLONI (chambilicho rafiki yangu).

Mchakato wa Katiba Mpya, i l ikuwa ni ndoto ya mchana ambayo Wazanzibari walikuwa wanaota na wanaona ni nafasi pekee ya kujikwamua kutokana na hali wanayoiona inaikandamiza nchi yao waipendayo ya Zanzibar. Waliingiwa na hamu ya kuona jinsi gani wanaweza kushiriki kwa salama na amani katika hatua za kuboresha maslahi ya Wazanzibari na kuufanya Muungano ambao una manufaa kama ungekarabatiwa vizuri.

Matokeo yake, wametoa mawazo, wamekutana , wamejadi l iana , wametoa maoni na kufuatilia hayo maoni ambayo kwa mujibu wa Tume ya ukusanyaji wa hayo maoni ambayo iliyawakilisha kwa Bunge Maalum la Katiba kama Rasimu ya Pili, hayakusikilizwa na yamebezwa.

Baya zaidi kwa wananchi wa Zanzibar, wametumiliwa viongozi wao ambao walitarajia wawatetee, kuwazamisha. Hii ni hasara kubwa kwa Zanzibar na ukorofi kwa jamii iliyostaarabika. Hebu jiweke kwenye nguo (maana viatu vitakavyokufaa ni adimu kwa Wazanzibari) ya mtu wa kawaida wa Zanzibar halafu uangalie hali hii anaifikiriaje.

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anatangaza kwamba kutokana na hali ya kisiasa na kiuchumi ya chi hiyo ya Muungano wa nchi mbili kwamba ni wakati muafaka wa kutengeneza katiba mpya itakayokidhi mahitaji ya Wananchi kwa wakati huu. Anawatuma wapambe wake wapeleke Muswada Bungeni kutunga sheria ya kusimamia mabadiliko hayo ya Katiba.

Ingawa mpango huo haukuwa mpango wa Rais wala Chama anachokiongoza, ulikuwa ni mpango wa wale walioitwa wapinzani hasa Chadema ambao waliupigia Debe kwa kipindi kikubwa. Wananchi wanaupokea kwa furaha kubwa baada ya kuutathmini na kuupigia kelele na kwa pamoja wanaamini kwamba utaleta Manufaa. Hasa kwa upande wa Zanzibar.

Bahati mbaya kati ya masharti yaliyowekwa kwenye mchakato wa kukusanya maoni, eti, Muungano usizungumzwe. Inajulikana lakini kwamba, kiini cha malalamiko ya Wazanzibari ni jinsi Muungano ulivyo na wanavyohisi unaikandamiza

Zanzibar kufurukuta. Hatua za mwanzo kabisa , Wazanzibar i wanapiga kelele kubwa sana, mpaka inasikilika kwamba Muungano Ulivyo hauwafai na hivyo inabidi uzungumzwe na upatiwe ufumbuzi.

Bahati nzuri, tume ya kukusanya maoni ya wananchi inaundwa ikiwa na nusu kwa nusu ya Wajumbe. Yaani nusu kutoka Zanzibar na nusu kutoka Tanganyika. Maoni yanakusanywa na inaonekana dhahiri kwamba, Wazanzibari hawaridhiki na hali iliyopo ya Muungano. Wanatoa maoni ambayo yanaashiria wanataka Zanzibar ipate mamlaka Kamili na baadae kuwe na maelewano ya kuifanya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Shirikisho la Mkataba baina ya Tanganyika na Zanzibar.

Nyuso za Wazanzibari ziling’ara na nyoyo ziliingiwa na tamaa pale tarehe 30 Desemba mwaka 2013 wakati Rais Kikwete alipokabidhiwa Rasimu ya Pili ya Katiba kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Kukusanya maoni Jaji Warioba. Wazanzibari waliposikia kiliochao kimesikilizwa, wakafurahi kutarajia kwamba, sasa Zanzibar itapata hadhi na thamani ambayo vizazi vingi hawajapata kuiona wala kuisikia. Thamani hiyo ingetokana na sababu kadhaa.

Kwanza udogo wa Zanzibar kama nchi na watu wake, ni rasilimali kubwa inayowezesha kusimamia na kuendesha mambo kiurahisi, kama itakuwa na uwezo wa kujumuika na nchi nyengine duniani katika kila inalotaka kulifanya. Pili, mazingira na maeneo Zanzibar ilipo, ni rasilimali kubwa pia kwa vile inaweza kutumia ardhi ndogo iliyonayo na Bahari kubwa iliyoizunguka.

Kinachohitajika ni kuwa na uhuru wa kujiamulia mambo yake inayotaka yenyewe bila ya kuingiliwa na wengine kwa kisingizio chochote kile. Kiwe kisingizio cha usalama. Kisingizio cha udugu au kisingizio cha kusaidia. Zanzibar inahitaji ipewe hadhi yake kama nchi na ipewe nafasi ya kujiwakilisha bila kukabwa roho na yeyote yule. Kulitokea mbinu fulani ya kuwanyamazisha Wazanzibari na Watanganyika waishio nje kwa kuwaambia kwamba wao wasifuatilie masuali mengine, wafuatilie Uraia pacha tu. Wengi wa Wazanzibari waliling’amua hilo na wakasema Kama tukiambiwa tuchague kati ya kupata Uraia pacha wa Tanzania na kuipatia Zanzibar adhi na tusipate

Uraia pacha wa Tanzania. Basi tutachagua hilo la kuipatia Zanzibar hadhi, kwani Zanzibar kwetu ni muhimu zaidi kuliko jambo lolote lile. Hiyo ilikuwa inaonyesha jinsi gani Wazanzibari wanavyoitakia mema Zanzibar waipendayo.

Hizo ni hisia za Wazanzibari walio wengi na ilikuwa inaonekana dhahiri. Kwa kusikiliza wasia wa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar baada ya Mapinduzi, Marehemu Abeid Amani Karume ambae alisema enzi ya uhai wake, kuwataka wananchi wa Zanzibar washiriki katika siasa. Aliwaambia watu, “Siasa ndio Utu”.

Wazanzibari wakafuatilia hatua kwa hatua jinsi mchakato wa kupata kat iba mpya unavyokwenda. Wazanzibari waliomo ndani ya Zanzibar na walio nje ya Zanzibar walifuatil ia kwa moyo mmoja wakiamini kwamba mara hii haki i tatendeka na Zanzibar kama Tanganyika itasimama na kuwa nchi na heshima zake na zote mbili Zanzibar na Tanganyika zitapata heshima kwenye katiba hii mpya ambayo wananchi wametoa maoni yao ya dhati ya nyoyo zao.

Afanaaleki, maneno ya waimbaji “Mzoea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi”. Mara tu lilipoanzishwa bunge la katiba. Tamaa bado ilikuwepo ya kupata Katiba yenye maoni ya wananchi na iliyoboreshwa na wabunge wa Bunge Maalum la Katiba. Akachaguliwa kiongozi wa muda wa kuliongoza Bunge hilo. Mh. Pandu Ameir Kificho.

Baadhi ya watu wakaingia tamaa kwamba, mambo huenda yakaenda vizuri na yakasimamia usawa kwa wote na kupata katiba iliyo bora na ambayo ina kila sifa wanazozitaka Wananchi. Ushahidi wa hayo ni timu aliyoichagua wakatia anatayarisha Kanuni za Bunge Maalum la Katiba. Matokeo yake akashambuliwa mpaka akatakiwa ajiuzulu. Maskini kuanzia hapo, kimyaa.

Mara haijafika hatua yeyote, u p e p o u k a a n z a k u b a d i l i k a . Utaratibu uliokuwa umepangwa wa kumleta Rais kufungua Bunge hilo maalum na baadae Mwenyekiti wa Tume iliyotengeza Rasimu ya pili, kuwasilisha rasimu, ukabadilishwa eti Rais ana majukumu mengine, wakati ni dhahiri kwamba umuhimu huo kulikuwa na sababu nyengine.

Kuanzia hapo tuliona hatua ambazo zilikuwa zinaonyesha dhahiri kwamba lengo halikuwa kuwasikiliza wananchi kilio chao. Hasa Wanachi wa Zanzibar. Badala yake, lengo ilikuwa ni kuvuruga mpango mzima. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambae alikuwa tayari ameshajikusanyia sifa kemkem kutoka kwa Wazanzibari aligeuka, kama kwamba sie yeye aliyepokea Rasimu ya pili ya mabadiliko ya Katiba.

Rais al ikuja kwa mshangao mkubwa, badala ya kulitakia heri Bunge la Katiba na kuondoka na heshima alizopewa, akawaambia waliopo wasiikubali Rasimu ya pili kama ilivyo, hasa ukizingatia masuala ya mfumo wa Muungano kama ulivyo. Wengi walisikitika na Wazanzibari waliona kama wamemwagiwa maji ya baridi na wakawa hawana la kufanya. Kuanzia hapo ile hali ya furaha iliyokuwa imetanda Zanzibar na kuwa na Wazanzibari wengi walioshikamana iliingia dosari kubwa.

Hali ilizidi kuyoyoma. Ama kwa

Inaendelea Uk. 12

ALIYEKUWA Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud.

Page 8: ANNUUR 1148

8 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 24-30, 2014Makala

NINGEPENDA nianze na kusema mambo mawili. Moja ni kuwa kama nilivyosema katika makala yangu wiki iliyopita, wanasiasa wetu wakitaka kujua ukweli juu ya tuhuma zinazomkabili Sheikh Msellem na wenzake, wanaweza kujua tena kwa uhakika kabisa. La, kama wataona ni vyema kuacha wadhulumike , hata kama hawana hatia, hiyo ni hiyari yao pia. Lakini jambo moja tu wazingatie: ipo siku ya Hukumu. Yupo Mfalme wa Siku ya Malipo.

J a m b o l a p i l i n i k u wa , y a w e z e k a n a w a p o w a t u waliokamatwa na zipo sababu za msingi zinazo halalisha kukamatwa kwao na kupewa tuhuma zinazowakabili. Lakini pamoja na ukweli huo, kama lengo ni nchi, kama lengo ni kuangalia usalama wa nchi, basi kuna haja ya kutizama kwa undani, ni nani hawa watuhumiwa, wanayafanya haya wao wenyewe tu au yupo mtu (wa nje) nyuma yao na kwa lengo gani.

Biblia John 8:32, inasema: “Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika Neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli. Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.”

Uhuru unaozungumziwa hapa, ni uhuru kutokana na dhambi. Na utumwa unaozungumziwa ni utumwa wa dhambi unaotokana na kutokuijua kweli.

Wiki il iyopita tuliarifiwa kuwa mtuhumiwa mmoja wa ugaidi alipigwa risasi na kufariki alipojaribu kuwatoroka polisi. Likiarifu juu ya habari hizo, gazeti moja la kila siku lilisema:

“Mtuhumiwa wa matukio ya ugaidi auwawa Arusha.”

Likieleza habari hizo gazeti hilo likasema kuwa “Mtu anayedaiwa kuwa kiongozi mkuu wa kundi la watu wanaohusika na matukio ya milipuko ya mabomu na umwagiaji tindikali viongozi wa dini ameuawa kwa kupigwa risasi na jeshi la polisi.”

Likiendelea likasema kuwa “mtuhumiwa huyo Yahya Hassan Omar Hela (31), maarufu kwa jina la Yahya Sensei, mkazi wa Mianzini jijini Arusha, aliuwawa kwa kupigwa risasi mguuni na makalioni.

L i k i m n u k u u K a m a n d a wa Polisi Arusha Liberatus Sabas, likasema kuwa, kabla ya kupigwa risasi mtuhumiwa huyo alikwishakiri kuhusika na matukio ya ugaidi yakiwemo lile la Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi mwaka jana ambapo watu watatu walipoteza maisha.

Kisa cha kupigwa r isas i ikadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akijaribu kuwatoroka polisi kwa kutumia uzoefu wake wa judo na karate.

Bila shaka tutakumbuka vizuri habari za bomu la Kanisani kwa Mtakatifu Joseph ambapo

Kutoka mtuhumiwa Victorhadi kuuawa Yahya Sensei

Afande Liberatus Soma Biblia John 8:32"Intelligence Assets” watatusumbua kama…Hatupo tayari kusema kweli ili kuwa huruTunapigana Vita Feki. Itatuangamiza sote.

Na Omar Msangi

mtuhumiwa kijana Victor Ambrose Calist alikamatwa katika eneo la tukio na kufikishwa mahakamani. Hakuna anayejua hadi hii leo kesi ile iliishia wapi. Bila shaka tutakuwa tunakumbuka pia lile sakata la kukamatwa Waarabu wakidaiwa kuwa ni watuhumiwa na yaliyojiri. Wakati tuliambiwa kuwa unafanyika uchunguzi wa kina ili kuweli ufahamike, hakuna kilichoendelea katika kesi ile wala kufahamishwa lolote juu ya uchunguzi uliofanyika. Sasa ghafla tunaambiwa kuwa ‘ M a r e h e m u Ya h ya ’ a l i k i r i kuhusika! Na maiti hawezi kuwa na haki maana hawezi kujitetea. Lakini kinachoonekana hapa dhahiri ni kusajili kuwa wahusika wa ugaidi ni akina Yahya na sio wale waliokamatwa akina Victor! Watakuwa washaweka katika rekodi zao. Kila wakizungumzia kitisho cha ugaidi nchini, kielelezo ni shambulio lililofanywa na ‘Marehemu Yahya Sensei’ katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi! Victor atakuwa amefutwa. Itakuwa ndio Septemba 11 yao.

Lakini hata ikiwa hivyo, kwamba hao akina “Yahya’ ndio watuhumiwa wakubwa wa ugaidi, bado yapo mambo ya kutafakari.

Tuwe karibu na Mungu kwa kusema yaliyo kweliAfisa mmoja aliyekuwa na

cheo cha juu katika vyombo vya dola katika nchi moja ya kibeberu, aliwahi kusema maneno yafuatayo:

“Licha ya kuwa kwa kawaida sipendi-kama ambavyo mtu yeyote wa kawaida (hapendi), kizunguzungu cha kujisikia vibaya katika bahari zilizochafuka za maisha, ilikuwa ni uadilifu wa kuchagua. Hivyo, kwa heshima ya familia yangu na bila kusitasita mno na kwa vile kusalimu amri katu siyo chaguo mojawapo pale ukweli unapohusika, nilichagua Odysseus (janga la kutangatanga baharini) na kuivaa tufani inayokuja. Kwani ni katika taabu nyingi ndipo tunapoletwa karibu zaidi na Mungu, na ubinadamu wetu ghafi kuchujwa. Wakati ni katika ulaini wa raha na uvivu ambako nguvu yetu ya maisha inasambaratika na kuoza kwa uchangamfu wa kiakili kulipo.”

Afisa huyu aliyasema maneno haya baada ya kugundua kuwa inayoitwa Vita dhidi ya ugaidi, ni vita feki na kwamba wanaodaiwa k u w a n i m a g a i d i , h u w a wanatengenezwa na kupewa pesa na serikali za kibeberu zilizojinadi kuwa vinara wa kupambana na

ugaidi. Kwamba serikali hizo zinatengeneza adui, ambaye atafanya mauwaji ya kutisha. Watu wasio na hatia watauliwa, wa t a t i wa v i l e m a n a m a l i kuharibiwa katika harakati hizo za kuwaunda hao magaidi. Lakini anasema pia askari wazalendo ambao kwa nia na moyo mmoja wanajiona wanapigania nchi yao kuilinda na kitisho cha ugaidi ili kuwe na amani, nao watauwa watu wasio na hatia, lakini na hata wao kuuliwa na kutiwa vilema. Kumbe wanaopambana nao ni watu walioandaliwa kama wao walivyoandaliwa na serikali zao na wanapewa pesa kama wao wanavyopewa na serikali,

Inaendelea Uk. 9

MAREHEMU Yahaya Sensei .ila hawa ‘magaidi’ wao pesa zao zinawafikia kupitia mlango wa nyuma na kwa siri Ukisoma makala, “Gangster Bankers: Too Big to Jail: How HSBC hooked up with drug traffickers and terrorists. And got away with it (By Matt Taibbi | February 14, 2013), utaona kile alichokiita Usama Bin Laden, “Golden Chain”.

Huo n i mtandao ambao hutumika kupitishia pesa kutoka mabenki ya Marekani na Ulaya na kuingia katika akaunti za watu au taasisi zenye majina ya Kiislamu ili hata ikigundulika ionekane kuwa hao Waarabu/Waislamu ndio wafadhili wa magaidi. Lakini uchambuzi mwingine kama huo umeweka wazi kuwa fedha hizo hutokea huko huko kwa hao wanaojidai kupambana na magaidi ambao ndio hao wanaotupa maelekezo na kutupa misaada ya kikachero, kipolisi na kijeshi katika vita dhidi ya ugaidi.

Prof Michel Chossudovsky ameandika makala aliyoipa jina, “Going After” the Islamic State. Guess Who is Behind the Caliphate Project? (Global Research, September 12, 2014) na nyingine akaipa jina “The Islamic State, the “Caliphate Project” and the “Global War on

Page 9: ANNUUR 1148

9 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 24-30, 2014Makala

Inatoka Uk. 8 Kutoka mtuhumiwa Victorhadi kuuawa Yahya Sensei

Terrorism.”Katika uchambuzi, mwandishi

anaeleza jinsi magaidi wa zama zote, toka ilivyokuwa Al-qaidah, Al-Shababa, Al-Nusra, na sasa ISIS, walivyoandaliwa, kupewa mafunzo, fedha, kulelewa na kulindwa au kupata hifadhi kutoka vyombo vya kikachero vya nchi za kibeberu kwa malengo ya kibeberu. Akifafanua anasema:

“The US-led Global War on Terrorism (GWOT) constitutes the cornerstone of US military doctrine. “Going after Islamic terrorists” is part and parcel of non-conventional warfare. The underlying objective is to justify the conduct of counter-terrorism operations Worldwide, which enables the US and its allies to intervene in the affairs of sovereign countries.”

Kwa hiyo kupitia GWOT, mabeberu wanapata mwanya wa kuzivuruga nchi zetu na kupata kisingizio cha kuingia na kuingilia mambo yetu ya ndani wakidai kusaidia kupambana na ugaidi kumbe wanalo lao. Kutukalia, kutandaza makucha yao ya kijeshi na kuvuna watakavyo.

Na haya ndiyo aliyosema Rais wa Argentina, Cristina Elisabet Fernández de Kirchner, katika Umoja wa Mataifa akizishutumu nchi za k ibeberu kwamba zinawachukua akina Shimon Elliot na kuwatengeneza kuwa magaidi, halafu wanakuja kusimama bila ya kuona vibaya wala aibu mbele ya jumuiya ya kimataifa kwamba zinataka washirika wa kupambana na akina ‘Shimon’ wao.

Prof Michel Chossudovsky akifafanua zaidi anauliza, “What is the ISIS mission?” Na kisha kujibu akisema kuwa:

“The declaration by ISIS to restore the Islamic Caliphate under their new caliph Abu Bakr al- Baghdadi is one of the silliest stories that have ever been sold to the gullible western public. This story sounds like a cheaply produced Hollywood movie that targets Islam and Arabs and attempts again to dehumanize them by portraying them as evil killers.”

Kwamba madai kuwa hawa ISIS Ni Mujahidina wanaopigania k u s i m a m i s h a u t a wa l a wa Kiislamu, Khilafah ukiwa na Khalifa aitwaye Abu Bakr al-Baghdadi, ni katika moja ya hadithi za kipumbafu walizolishwa watu kupitia vyombo vya habari vinavyoongozwa na waandishi wasiojitambua au wanaotumika bila kujali heshma zao. Ni kama muvi ya Hollywood (Hollywood movie) iliyochezwa kwa ajili ya kuwahujumu Waislamu na Waarabu ikiwaonyesha kuwa sio binadamu bali mazimwi waovu na wauwaji katili.

Hiyo ni kwa ISIS, lakini waweza pia kuchukua ile muvi ya ‘Westgate

Nairobi’ au tamthilia ya ‘Bring Back Our Girls” kule Nigeria na visa vyote vya Boko Haram. Hivi kuna mtu yeyote mwenye akili yake timamu anayeamini juu yaliyojiri katika ile Muvi ya Nairobi ambapo tuliambiwa kuwa magaidi kutoka Mogadishu waliingia na magari ya silaha ndani ya maduka ya Nakumati, Westgate wakafanya mauwaji mbele ya kamera za CCCTV, walinzi wa maduka hayo, polisi, vikosi maalum, jeshi la Kenya, Idara ya Usalama ya Kenya na makachero wa CIA, Mossad na wale wa kutoka Uingereza, na hawakukamatwa wala kuuliwa. Ukimsikia mtu anazungumzia Muvi hii ya ki-Hollywood kuwa ni tukio la kweli, basi ama akili yake ina mushkeli kidogo au ni katika hao hao wanaotumiwa kama hao magaidi waliodaiwa kuingia Nakumati.

Kinachotafutwa nini?Labda swali la msingi ni hili:

Mabeberu wanafanya yote haya ili wapate nini?

Prof Michel Chossudovsky akijibu swali hilo kupitia mada yake ya hivi karibuni, “Globalization of War” anasema kuwa wanachotafuta mabeberu ni “Global Hegemony” kwa masilahi yao ya kibeberu. Kwamba watu hawa kwanza hutafuta “pretext” na “justification” ya kuingia mahali na kuvuruga nchi na wanaowapa “pretext” na “justification” hiyo ni hawa al-Shabab, al Qaida, ISIS, Boko Haram, na wengine ambao wote hawa amesema kuwa ni “Intelligence Assets” na “Foot Soldiers” wa mabeberu.

“Intelligence Assets” hawa ndio hutumika kuleta vurugu na machafuko katika nchi

mbalimbali bila kujali mamia kwa maelfu ya watu wasio na hatia wanaouliwa. Anatoa mfano akisema kuwa hivi sasa Marekani na washirika wake inajifanya kuwashambulia ISIS, lakini anasema huo ni uwongo mtupu. Kwanza, ni Marekani na washirika wake NATO na Mossad waliowaunda ISIS lakini na sasa inapojidai kupambana nao sio kweli. Ingekuwa lengo ni kuipiga ISIS, hiyo ingechukua sekunde chache tu kwa kuangamiza misafara ya askari wa ISIS wakiwa katika Toyota Hilux zao. Lakini inachofanya ni kushambulia m i u n d o m b i n u - b a r a b a r a , madaraja, viwanda, visima vya mafuta na mitambo ya kusafisha mafuta katika Syria na Iraq. Lengo kuidhoofisha Syria ili kufikia lile lengo la “Regime Change.”

Hivi sasa, pamoja na kuwatia doa Waislamu wao wenyewe na dini yao, lakini linalolengwa ni kutimiza malengo ya mabeberu, yakiwemo kutandaza makucha yao ya kijeshi kudhibiti rasilimali na kuwatia kitanzi viongozi wa serikali mbalimbali duniani wawe wanatumikia masilahi yao, ambapo kinachotakiwa Syria na Iraq kwa sasa ni kuzigawa nchi hizo katika vinchi vidogo vidogo-“Sunni state, Shiite state, and Kurdistan”.

Na hiyo itakuja baada ya kufanyika mauwaji ya kutisha baina ya Wasuni, Washia na Wakurdi ambapo inayoitwa jumuiya ya kimataifa itatakiwa kuingilia kati na kusemwa kuwa ufumbuzi pekee ni kwa mahasimu hao kila mmoja kuwa na nchi yake.

Hawa ndio mabeberu na vita yao dhidi ya ugaidi waliyoisambaza mpaka huku kwetu. Ambacho kinasisitizwa hapa ni kuwa kama tutaelewa ukweli huu, tutafahamu kuwa mchezo huu wa kuandaa

magaidi na kisha kutangaza vita dhidi ya magaidi unahusisha sehemu mbili. Moja, ni mamluki na wasaliti wanaopewa kazi ya kufanya vitendo vya kigaidi, na pili, ni serikali, jeshi na polisi wa nchi mbalimbali wanaopewa kazi ya kupambana na magaidi hawa-walio vifaa vya mabeberu. Wote

hawa wakifanya kazi yao vizuri (kwa maana ya magaidi na polisi wanaopambana na magaidi), lengo la mabeberu linatimia. Na wala inayodaiwa kuwa amani na usalama haitapatikana kamwe kama ambavyo haijapatikana Afghanistan, Pakistan, Yemen, Iraq, Kenya, Somalia na nchi nyingine zilizotutangulia katika vita hii.

Kuwauwa tunaowatuhumu kwa ugaidi, haitatusaidia sana. Kitakachotusaidia ni kujua ukweli na kuwa tayari kuukubali. Na tukiukubali, h a t u t a h a n g a i k a t u n a ‘mtuhumiwa wa ugaidi’, bali na yule aliyemtuma kwa namna tunayoona itasaidia kufikisha ujumbe na kukomesha uovu na dhulma hii.

Ukweli utakaotuweka huru ni huu:

“The world is at a dangerous crossroads. The United States and its allies have launched a military adventure which threatens the future of humanity.” (Prof Michel Chossudovsky)

Al-Shabab, Al-Qaida, na wote wanaodaiwa kuwa ni magaidi, ni zao la mabeberu na “Intelligence Assets” zao katika kufikia lengo lao la Global Hegemony. Kadiri tunavyopokea na kukubali kutekeleza maelekezo yao, ndivyo tunavyosababisha ghasia na machafuko katika nchi zetu na hivyo kuwapa kisingizio cha kutuzinga na mtandao wao wa kikachero na kijeshi.

Salama yetu haipo katika kukaza buti kuwauwa watuhumiwa wa ugaidi, bali kujitolea kufichua uwongo ambao umefanywa k u w a k w e l i . U w o n g o ufichuliwe, ukweli udhihiri. Hapo ndio tutakuwa huru na salama.

Page 10: ANNUUR 1148

10 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 24-30, 2014Makala

OKTOBA, 14, 2014, Watanzania wameadhimisha miaka 15, toka kufariki kwa Rais wa kwanza wa Tanganyika na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pale alipoiga dunia Oktoba 14, mwaka 1999.

Katika maadhimisho hayo kila mmoja ameweza kumkumbuka kwa namna yake anavyomkumbuka kulingana ama alivyomsikia, kupitia vyombo vya habari, alivyoona mwenendo wake au alivyoshirikiana naye enzi za uhai wake katika harakati na matukio mbalimbali.

Mzee Bilali Rehani Waikela, kutoka Tabora, ni mmoja wa watu waliokuwa karibu na Mwalimu Julius Nyerere, akimfahamu kabla ya Uhuru na katika harakati za kupigania Uhuru na badaa ya kupatikana Uhuru. Mzee Waikela, kwa masiku ya hivi karibuni anaweza kukumbukwa na Waislamu pale aliposimama katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam, akiwa shahidi katika kesi iliyomuhukumu Sheikh Ponda Issa Ponda, kifungo cha mwaka mmoja nje. Kesi iliyohusuana na madai ya uvamizi uwanja wa Markazi Chang’ombe Jijini Dar es salaam.

Mzee Waikela, aliye mwanachama wa tatu kupokea kadi ya TANU, kwa mkoa wa Tabora, katika maelezo yake kwa nyakati tofauti kuhusu Mwl. Nyerere, anasema, pamoja na kumsitiri, kumpokea na kumfanyia ihsani za kila aina katika harakati za kutafuta Uhuru, lakini baada ya kupatikana Uhuru aliishia kuekwa gerezani.

“Nimekaa gerezani kwa muda aliotaka Nyerere, wenzangu wote wakatoka. Mimi nilipotoka nikapewa masharti, ndani ya miaka miwili niripoti Polisi, kila mwezi mara mbili na faili langu limetembezwa mikoa yote, sikuwa na ruhusa ya kukutana na watu kumi, na sikuwa na ruhusa ya kutoka umbali wa maili tano ndani ya mji wa Tabora, mpaka nikamaliza muda huo”. Anasema Mzee Waikela.

Mzee Waikela, akizungumzia kisa cha kuwekwa gerezani (kizuizini) katika utawala wa Nyerere, anasema wakati huo alikuwa Katibu Mkuu wa Waislamu kupitia Jumuiya ya Waislamu ya Afrika Mashariki (EAMWS),na alikuwa mstari wa mbele kupinga mipango ya kuwahujumu Waislamu na kuwaeleza ukweli viongozi Serikalini.

Mbali ya kuwa kiongozi wa Jumuiya hiyo ya Waislamu, lakini pia Mzee Waikela, alikuwa ni miongoni mwa wanaharakati wa kutafuta uhuru tokea enzi za Chama cha TAA, wakati huo Nyerere, akiwa chuoni Makerere nchini Uganda.

Kisa na mkasa wa Mzee Waikela, anauelezea kuwa umeambatana na kuikingia kifua Jumuiya ya Waislamu ya EAMWS, wakati huo yeye akiwa Katibu Mkuu wa Mkoa wa Tabora, kati ya miaka ya 1958.

Anasema, EAMWS, wakati huo ilikuwa ni chombo ambacho kinawapeleka vizuri Waislamu, chini ya uongozi wa Tewa Saidi Tewa, na kuwafanya Waislamu kuwa kitu kimoja nchi nzima tofauti na ilivyo sasa.

“Majukumu ya EAMWS, yalikuwa yanafurahisha kwa sababu ilibaini kwamba, kelele hazifai bali kinachofaa ni vitendo, hivyo ilianziasha mashule ya Waislamu. Na ilikuwa na utaratibu mzuri, kwamba ikiwa Waislamu wenyewe mmechanga kiasi chochote kama ni milioni kumi, Jumuiya

Yaliyomkuta Mzee Waikela mikononi mwa J. K. Nyerere

Na Bakari Mwakangwale

inaongeza kiasi hicho kwa ajili ya maendeleo ya Waislamu”. Anasema Mzee Waikela.

Mzee Waikela, anaeleza kuwa Jumuiya hiyo, ilikuwa ipo mikoa yote, na kutokana na mtandao huo ilileta tabu sana katika kuiondoa kwake baada ya Nyerere, kutengeneza kamati na kupita nchi nzima kwa viongozi ili watangaze kuihujumu Jumuiya hiyo ya Waislamu, kwamba wamejitenga nayo.

Alisema, pamoja na juhudi hizo ni mikoa minane kati ya mikoa 20 kwa wakati huo ndio iliyokubali fitina ya Mwl. Nyerere, kutangaza kujitenga na EAMWS, lakini mikoa mingine yote, ukiwemo wa Tabora, ilikataa kukubaliana na fitna hizo.

Mzee Waikela, anasema, kwa kuwa yeye kama kiongozi wa mkoa wa Tabora, alishawishiwa kukubali mipango hiyo kwa kupewa pesa, inawezekana pia viongozi waliokubali nao walipewa pesa ndio maana walikubali kuihujumu EAMWS.

“Si jui kama mikoa mingine walipewa pesa, lakini mimi kama Katibu wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Tabora, niliahidiwa 40,000/- ( Elfu Arobaini) ilinitangaze kuwa mkoa umejitoa katika Jumuiya. Lakini sikukubali kupokea pesa hiyo.” Alisema Mzee Waikela.

Kwa maana hiyo, Nyerere na wenzake wakawa wamefeli, baada ya kufeli sasa ikatumika nguvu kuiwa EAMWS, wakati huo Bw. Said Maswanya, ndiye alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi.

Hata hivyo, anaeleza Mzee Waikela, kwamba alipobaki na msimamo wake huo Ofisi zao za EAMWS, Mkoani Tabora zikatiwa kufuli na kulindwa na askari wakiwa na bunduki, na pale walipokwenda katika ofisi hizo

walirudishwa na askari hao.Anasema, hata pale alipohojiwa

na wale aliowaita vibaraka wa Nyerere, katika kuihujumu Jumuiya ya Waislamu, na kumshangaa kwa nini akatae pesa ile, aliwajibu na kuwahoji kwamba, ‘Uislamu hauna Baitul Mali, lakini wao katika kazi hiyo wanasafiri kwa ndege na magari ya kifahari (Benzi) na kulala katika mahoteli makubwa, ‘hizi fedha, manazipata wapi’.?

Anaeleza Mzee Waikela, kuwa msimamo na maswali yake kama hayo ndio ulianza kuwa mvurugano baina yake na Nyerere, pamoja na hao vibaraka wake, baada ya kumpelekea taarifa na msimamo wake.

Mzee Waikela, anaeleza kwamba ili kufanikisha azima yake, Nyerere alimrubuni Rais wa Zanzibar, Bw. Abed Karume, kwamba nchi yake inataka kupinduliwa ili warudishwe Waarabu. Karume, akaingia katika fitina hiyo, anasema, hali hiyo ilimlazimu kwa mdomo wake, kumkabili Karume, na kumtamkia kwamba anatumika.

“Akaniambia ‘Bilali unanitukana, unanimbia mie natumiwa na Nyerere, hujui mimi ni nani’, nikamwambia najua wewe ni Rais, lakini nakujulisha kile ninachokijua mimi, ambacho pengine wewe hukijui.” Anaeleza Mzee Waikela.

Akasema, alimtanabaisha kwamba huyo (Nyerere) anayemtumia katika shauri hilo la kutafuta vibaraka anamtumia kwa lengo lingine ili atimize malengo yake si kwa malengo aliyomuelezea na kwamba hakuna kitu kama hicho cha kutaka kupinduliwa.

Akiwa gerezani, Mzee Waikela, a l i k u wa a k i t u m i wa u j u m b e wakimtaka aandike maelezo ya kumwomba radhi Nyerere, ili atolewe

gerezani, jambo ambalo Mzee huyo hakuliafiki.

“Mimi nikawa nakataa kuomba radhi, Mkuu wa Gereza akawa ananinasihi kwamba niombe radhi kwa maandishi kwa sababu alikuwa anabughudhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora”. Anaeleza Mzee Waikela.

B a a d a ya k u o n a s h i n i k i z o hilo linazidi, alimuuliza kama atakachoandika kitapelekwa kwa Nyerere, alijibiwa kuwa atapelekewa bila shaka, “Nikamwandikia, kama mtu mwadilifu, Nyerere, fanya moja katika matatu haya:- Mosi, nifanye niwe huru nikaishi na wenzangu, Pili kama hapana, nipeleke Mahakamani nijue kosa langu, yote haya huyawezi basi, nipeleke popote unapojua wewe”. Alirejesha ujumbe huo ambao anasema kopi yake anayo mpaka sasa.

Hata hivyo, hayo hayakufanyika, na baada ya siku tatu kupita, akafikiwa na ujembe tena wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, aliyemueleza kuwa jeuri imenizidi kutokana na maelezo yake yale kwa Nyerere, na kumueleza bila kuandika kinachotakikana haoni atatokea wapi.

Kwa maelezo hayo ya Mkuu wa Mkoa, mzee Waikela, alimjibu kwamba alidhani kuwa raia wakiwa nje wanatishwa kwa maneno kama hayo ili waliogope gereza, lakini yeye tayari yupo gerezani haoni cha kuhofia kwa hayo aliyoelezwa.

“Akaniambia kwa jeuri yangu sitotoka humo, nami nika mwambi tatoka tu, nikamtaka aangalie mle gerezani, kama ameona kuna kaburi, nikamwambia kama hakuna basi namimi tatoka kupitia mlango huo huo, nikiwa mzima au mfu lakini tatoka tu”.

Anaeleza aliendelea kukaa kwa muda aliotaka Nyerere, huku wenzake wakiachiwa mapema na wakati walipoamua kumtoa walimpa masharti ya kuripoti polisi na hakuwa na ruhusa ya kukutana na watu kumi, wala kutoka nje ya Mji wa Tabora.

Tena Nilitoka katika siasa na kuamua kushughulika na EAMWS.

Anasema, Nyerere, aliwageuka Waislamu kwani Anakumbukwa kuwa mwaka 1958, katika nyumba waliyomuandalia Nyerere kufikia Mjini Tabora, majira ya saa nane usiku alimweleza kwamba Waislamu wanamuunga mkono nini itakuwa matokeo yake baada ya Uhuru.

“Alinijibu akisema, ‘Bilali unaleta shauri gumu hi lo , nakuomba usi l i tamke tena……, tukianza kuzungumza haya tutashindwa kupata Uhuru’, akaniambia ‘niachie mimi nakunyamazisha, wacha tupate Uhuru, tukishapata uhuru wetu, mimi nitakuwa wa kwanza kuwasogeza Waislamu’”.

Lakini Mzee Waikela, anasimulia kuwa baada ya kupata uhuru, mwaka huo huo wa 1961, kukaanza matusi kwa watu wa TANU kuutukana Uislamu na Waislamu na haswa Jumuiya ya Waislamu ya EAMWS.

Akasema, ilipofika mwaka 1963, EAMWS iliandaa mkutano Jijini Dar es Salaam, wakati huo ilikuwa imeshajitenga mbali na kuipigia kelele Serikali ya Nyerere, kutona ya yaliyokuwa yakiendelea.

Anasema, akiwa mjumbe kutoka Tabora, katika mkutano ule, kabla ya mkutano alifatwa na Sheikh Hassan bin Amir na Shkh Ally Komorian na kuelezwa kwamba wenzake wote (Wajumbe wa EAMWS) wamealikwa katika chakula kwa Nyerere, lakini

Inaendelea Uk. 11

HAYATI Mwalimu Julius K. Nyerere.

Page 11: ANNUUR 1148

11 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 24-30, 2014Makala

Yaliyomkuta Mzee Waikela mikononi mwa J. K. Nyerere

Inatoka Uk. 10hakuitwa yeye na wenzie wawili, kwa sababu walijulikana kuwa na misimamo wa kutokukubali kurubuniwa na kutafsiriwa kuwa ni wakorofi.

“Walinieleza kuwa wamealikwa k wa l e n g o l a k u wa s h a w i s h i iliwakubali kuiuwa EAMWS, na tayari ananieleza hivi nikakumbuka usiku alinifuta Adamu Nassibu, nikiwa pale Anatoglo, aliniambia habari kama hii, akinishawishi niache ukorofi wangu kwa sababu yanakuja mapesa ili tukubali kuifuta EAMWS”. Anaeleza Mzee Waikela.

Masheih Hassan Bin Amir na Komorian, walinituma na kunitaka nikiwa ndani ya kikao hicho nifanye kila linalowezekana kuzuia hili shauri la kuiua Jumuiya ya Waislamu, kweli anasema mkutano ulipoanza lililetwa shauri hilo kama ilivyotazamiwa, ndani ya kikao niliwaeleza wajumbe maongezi yangu na Nyerere, mwaka 1958 na kuwaambia hizi ni fitana zake, za kuwapiga teke Waislamu badala ya kuwasogeza kama alivyowaahidi.

Akasema, kwa kuwa aliongea h a k i M u n g u a k a s a i d i a , n a kuwabadilisha fikra wajumbe wale, aliyoongea yeye katika kikako hicho ndio yaliyochukuliwa na wale waliokwenda kula wali kwa Nyerere, wote walibadilika, na katika maazimio ya kikao kile, waliazimia kwamba Nyerere, aitwe katika kikao hicho.

W a l i a f i k i a n a n a k a t i k a kutengeneza maazimio chini ya wa j u m b e s a b a wa l i o t e u l i wa walimteuwa yeye (Waikela) awe Mwenyekiti, na waliporudi katika Baraza maazimio yao yalikubalika wakawa wanamsubiri Nyerere, afike katika kikao hicho, ambapo wajumbe wakamtaka awe msemaji mkuu mbele ya Nyerere.

“Alipokuja kat ika kikao na kutusikiliza baada ya maelezo ya maazimio ya kikao lakini pia katika maelezo yangu nikamtaka Nyerere, akomeshe kwa kutangaza tabia ya kutukanwa Waislamu kwani ndio walioleta uhuru wa nchi hii”.

yao.Anasema, ni busara ndio ilitumika

wakakubali ombo la Fundikira na alipofika, Nyerere, alikuwa ni mtu wa kawaida hakuwa na chochote na alifanywa kuwa sekretari (Katibu) wa Duka la klabu ya vijana wa Tabora.

Anafafanua kuwa Nyerere , ameingia Tabora hana chama si mwanachama wa chama chochote, kwani aliingia katika mji huo kama kama mwalimu.

“Na atokee mtu mashuhuri kwa anayemjua Nyerere katika kipindi cha miaka ya 1950 mpaka 1952, atamke kuwa Nyerere, alikuwa mwanachama wa Chama gani”. Anatilia mkazo maelezo yake Mzee Waikela.

Nyerere, aliondoka Tabora, na kwenda kufundisha Dar es Salaam, huko alikutana na Kasela Bantu, ambaye a l imtambul i sha kwa Kiongozi wa TAA, Bw. Abdulwahid Sykes, na yeye alimtambulisha kwa wazee wa Dar es Salaam.

Mzee Waikela, anatoa maelezo kwambamMwaka 1953, ndipo Nyerere, alichukua kadi ya TAA, na mwaka 1954, kulifanyika mkutano kuibadilisha TAA kuwa TANU, kabla ya hapo tayari katika harakati za Waislamu walishatuma wajumbe mara kadhaa umoja wa Mataifa (UNO).

Katika hatua hizo za awali walielezwa vipi wanakwenda Waislamu watupu wakati kuna makundi mawili ya Waislamu na Wakristo, ndipo busara ilipotumika kwa Sykes, kumuachia Uongozi wa TAA, Nyerere.

“Sio kama Nyerere, alimshinda Sykes. Katika uchaguzi ule uwezo wa

kumshinda haukuwepo, bali ilikuwa ni mipango na makubaliano baada ya wanachama kuelimishwa. Bila hivyo ilikuwa ngumu Nyerere, kushinda kwani alikuwa mgeni kwenye siasa, mgeni katika mji lakini pia alikuwa Mkristo, kwa kuwa Waislamu wengi wakati huo ndio walijishughulisha na siasa kudai uhuru”. Anafafanua Mzee Waikela.

Lengo la kufanya hivyo lilikuwa yeye (Nyerere) aongozane na mjumbe mwingine kutoaka Tanga, kurudi Umoja wa Mataifa na kueleza kuwa Waislamu na Wakristo wapo pamoja katika kudai Uhuru wa Tanganyika.

Chama kilipobadilika kutoka TAA kua TANU, wanachama wa Tabora waliandaa mkutano, klabu yao ya mpira ambayo Mzee Waikela, alikuwa Katibu masaidizi, Katibu Mkuu akiwa Shabani Mohamed Silabu (Kichwa), iliandaa mkutano na kumwalika Mwl. Nyerere.

Akiwa Tabora, walimweleza Nyerere, walimweleza kwamba huko Dar es Salaam, wajitahidini wapate makundi ya hamasa, tuna kumweleza wajitahidini kuifanya klabu ya mpira ya Yanga, kuwa mwanachama wao naklabu ya samba, pia vikundi vya akina mama vya burudini wawe upande wao ili wapate mafanikio ya Chama kuungwa mkono.

Anasema, Nyerere, al ikuwa akiingia Tabora, kwa heshima ilikuwa mahala atakapo lala anapishwa analalia katika kitanda cha Samadari, na wao wanalala chini.

Lakini pia anasema Mzee waikela kuwa mwl. Nyerere, alikuwa akiingia Tabora ni gari za watu watatu ndio alikuwa akitembelea, yakwake (Waikela) ya Juma Shabani Ambari au gari ya Mohammed Ikunji (wawili hao sasa ni marehemu).

Aeleza kuwa yeye (Waikela), hata kabla ya siasa alikuwa na afadhali kiuchumi na kimaisha, kwani alikuwa akitembelea gari na hata wakati wa siasa alikuwa anakwenda nayo katika mikutano Dar es Saalam na kurudi Tabora, lakini Nyerere, alikuwa hana hata baiskeli, hivyo anasema alikuwa si Kiongozi wa kurubuniwa kirahisi.

Anabainisha Mzee Waikela, aliye mwanachama wa 264, kitaifa baada ya kuundwa TANU.

Anasema, baada ya hapo na ukirejea ile hali ya kumkabili Rais Karume kwa kumeleza kuwa anatumiwa na Nyerere, na mengine mengi, mwisho wake ikawa ni kuwekwa gerezani.

Akizungumzi harakati zake za kisiasa katika harakati za Uhuru akiwa na Mwl. Nyerere, Mzee Waikela, anasema alianza siasa kabla ya Nyerere, akiwa Diwani wa kwanza wa Tabora, wakati huo ikiitwa Town Ship Authority.

Anamtaja Abdallah Fundikira, kuwa ndie a l iyemtambul isha Nyerere, kwa vijana wa Tabora, ambao walikuwa wanaendesha harakati zao za kisiasa kupitia Klabu zao za burudani.

Anasema, Fundikira, alikutana na Nyerere, Chuo Kikuu Makerere Uganda, na alimtangulia kumaliza n a a l i p o r u d i Ta b o r a , n d i p o alipomuelezea Nyerere, katika Klabu za vijana katika mambo ya mipira na burudani.

Fundikira, aliyemzawa wa Tabora na mtoto wa Chifu Said Fundikila, aliwaeleza vijana kuwa amemwacha Nyerere, Chuoni (Makerere), hapo akiwaeleza akina Maulidi Kivuruga, na wengine. Akaomba kwamba baada ya masomo yake wampokee katika kombaini ya klabu yao.

Hata hivyo imeelezwa ombi hilo, halikupita kirahisi kwani walitaka kujua ulazima na sababu haswa za kumkaribisha Nyerere, katika klabu yao, Fundikila, aliwajibu kuwa ataweza kuwa mwalimu katika Klabu

Mtazamo wa kisiasa wa KiislamuInatoka Uk. 4ujengwe juu ya msingi wa Uislamu na hukumu zake. Haupaswi kujengwa juu ya vipengele vya faida au manufaa kama ilivyo kwenye ubeberu. Kufahamu tu kwanini, wapi au ajenda za wanasiasa mbalimbali, haitoshi kwa Waislamu kujiingiza kwa ufanisi kwenye siasa.

Kujenga Mchepuo wa Kisiasa wa Kiislamu: Katika mazingira ya kawaida, kujenga mchepuo maalumu ni jambo rahisi kwa Wais lamu. Iwapo Uis lamu ungekuwa unatekelezwa katika kiwango cha dola na jamii, dhana za itikadi ya Kiislamu, zingejikita vizuri katika jamii na kwa mtu mmoja mmoja.

B a h a t i m b a y a a m b a y o imezikumba jamii za Waislamu duniani leo, ni kwamba jamii zao z imeundwa kwa f ikra mchanganyiko badala ya Uislamu. Wanasiasa Waislamu wamepoteza mchepuo wa Kiislamu katika

siasa.Siasa mara nyingi huainishwa

kama kushughulikia masuala yanayowahusu wananchi. Maana yake ni kwamba wanasiasa wanachukua hatua za jinsi gani matatizo, mahitaji na changamoto za wananchi vishughulikiwe.

Katika zama za leo, umma wa Waislamu duniani unakabiliana na masuala mengi. Katika ardhi za Waslamu, kuna ukaliaji kimabavu wa kijeshi, kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Kwa ufupi, hali ya Waislamu ni mbaya. Katika mazingira hayo, lazima kuna Waislamu walio sawa sawa, ambao wanataka kubadili hali hiyo na kuleta ukombozi halisi wa Waislamu.

We n g i m i o n g o n i m w a Waislamu, wanaotaka kuleta mabadiliko hayo kupitia mifumo iliyopo, wanaanza vizuri harakati zao, lakini baadaye wanaishia kuwa vifaa muhimu vya watawala madhalimu dhidi ya Waislamu

wenzao. Katika baadhi ya nchi, kuwatetea Waislamu ni kinyume cha sheria.

B a a d h i ya M a s h e i k h n a viongozi wa dini ya Kiislamu wametupwa magerezani kwa sababu tu ya kubainisha ukweli kuhusu udhalimu wanaofanyiwa Waislamu na watawala wa nchi zao. Harakati mbalimbali za Waislamu kujikomboa zimekuwa zikija na kuondoka, na nyingine zimepoteza kabisa mwelekeo. Hali ya Waislamu imezidi kuwa taabani.

Kabla Waislamu hawajaingia kwenye harakati za kuleta mabadiliko ya kijamii, wanahitaji kwanza ku jenga mchepuo sahihi na ulio wazi ambao ndiyo utakaokuwa msingi wa kazi wanayotaka kuifanya. Mchepuo wa Kisiasa wa Kiislamu lazima ujengwe juu ya Itikadi ya Kiislamu. Itikadi ya Kiislamu ndiyo msingi ambao Muislamu anaendesha maisha yake yote ikiwemo siasa.

Iwapo misingi ya ufahamu wa I t i k a d i ya K i i s l a m u itakuwa dhaifu kwenye akili za wanaharakati wanaotaka kuleta mabadiliko ya kisiasa katika jamii zao, basi itakuwa rahisi mno kwao kugeuzwa na kuhamishwa kwenye ajenda hiyo. Atashidwa mwanzo tu! Harakati zote za Kiislamu, iwe za kijamii au kisiasa, lazima ziwe ndani ya wigo wa Itikadi ya Kiislamu.

Muislamu kwanza lazima ajenge dhana (concept) sahihi, ambazo atazitumia kama miwani ya kuonea mambo. Kisha lazima ajenge ufahamu wake kuhusu ulimwengu unaomzunguka, yaani masuala na matukio yanayotokea duniani . Kisha anaweza kujua harakati gani ya kisiasa inayopaswa kufanyika kwa wakati husika na mazingira yaliyopo.

Page 12: ANNUUR 1148

12 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 24-30, 201412 Barua/Mashair

Nina swali mtimani, naliweka hadharani,Naomba mniauni, kujibu kwa tamakuni, Kuhusu wanazuoni, wasomao mavyuoni,Tuwete wanazuoni, au nao majahili ?

Wasomi wetu vyuoni, maadili mtihani,Hulkayo kimizani, sawia na hayawani,Si nao mimi imani, hata chembe mtimani,Tuwete wanazuoni, au nao majahili ?

Mabanati wa vyuoni, ebu jama washufuni,Libasizo chunguzeni, wajivikazo mwilini,Ndipo mtajabaini, cha swali langu kiini,Tuwete wanazuoni, au nao majahili ?

Kukicha vyao vimini, nusu uchi mitaani,Kukichwa libasi gani, watovaa nijuzeni,Fasheni eti vimini, 'machangu' wavae nini,Tuwete wanazuoni, au nao majahili ?

Wajiacha vitovuni, tupu pasi hata soni,Mithili ya majununi, punguani nadharini,Zi wapi za vitabuni, akilizo za matendoni,Tuwete wanazuoni, au nao majahili ?

Wajivika vibikini, si 'bichi' bali vyuoni,Vinowacha migongoni, wazi hata makwapani,Wajidhani huriani, kumbe wako uryani,Tuwete wanazuoni, au nao majahili ?

Na titizo sudurini, wazanika hadharani,'Machangu' wako kazini, hivyo 'waweza kudhani, Kama hilo huamini, kavinjari 'mlimani',Tuwete wanazuoni, au nao majahili ?

Hazina tena thamani, yumkini kwa wahuni,Wenye nia ya kuzini, nao si kuwa ndoani,Wao 'sipojithamini, wa kuwathamini nani,Tuwete wanazuoni, au nao majahili ?

Vijijinzi vya kihuni, vya kubana juu-chini,Wavitinga hadharani, vyuoni na mitaani,Vyawadhiki maungoni, kwa ghururi ya fasheni,Tuwete wanazuoni, au nao majahili ?

Navyo vyao visikini, 'taiti' si jina geni,Virasimuvyo ramani, na kukashifu vya ndani,Tofautiye jamani, na stokingi ni nini,Tuwete wanazuoni, au nao majahili ?

Bandia nywele kichwani, za kushtari dukani,Na 'kalikiti' saluni, wetwe wazungu kwa nduni,Amini usiamini, josholo nusu bafuni,Tuwete wanazuoni, au nao majahili ?

Mabarobaro vyuoni, ninyi nao kulikoni,Mwaiga Ughaibuni, hata yaso na maani,Vipuli masikioni, mwavaa kwa lengo gani,Tuwete wanazuoni, au nanyi majahili ?

Mwalabisi mikononi, mabangili bila soni,Na vya dhahabu vidani, mwajirembesha shingoni,Si yenu kufu jamani, ya dada zenu nyumbani,Tuwete wanazuoni, au nanyi majahili ?

Nywele mwasuka kwanini, kama si ulimbukeni,Ujuha au fasheni, wenyewe jihukumuni,Ujike mwautamani, madume ninyi kwanini,Tuwete wanazuoni, au nanyi majahili ?

Sarawili kulikoni, mwashusha makalioni,Kiunoni kuna nini, hasa kinokukwazeni,'Andaweya' zenu ndani, mwazikashifu kwanini,Tuwete wanazuoni, au nanyi majahili ?

Mwagezageza kwanini, msoyajua kiini,Mwatutaka tuamini, ushoga mwautamani,Kama la kulikoni, mwaiga ya ushogani,Tuwete wanazuoni, au nanyi majahili ?Kama si ujuha nini, wa wetu wanazuoni,Kugeza yaso thamani, kisa ya Ughaibuni,Pamoja tuketi chini, tutafakari kiini,Tuwete wanazuoni, au nao majahili ?Hofu yangu mtimani, kwa hawa wanazuoni,Wenye tengefu uoni, wangali bado vyuoni,Kesho kufanywa kifani, hapo mwatarajiani,Tuwete wanazuoni, au nao majahili ?

Mwisho nakudhukuruni, swali langu nijibuni,Mlo humo mavyuoni, kadhalika mitaani,Kikoa mniauni, wa Bara na Visiwani,Tuwete wanazuoni, au nao majahili ?

Kaditama ishirini, zangu beti shairini,Timilifu themanini, mishororo mwake ndani,Pamwe vina na mizani, tamamu vyote si guni,Tuweteje nambieni, kwa yenu ninyi mizani?

Na Abuu Nyamkomogi

Wasomi au majahili ?

Ndugu Mhariri,N a p e n d a k u t o a

nasaha na kuonya juu ya tabia chafu ya kusambaza picha chafu k we n ye m i t a n d a o . Kwa hakika hil i ni kosa kubwa kwani watu husambaza kwa kutumia simu, picha za uchi, na picha za aibu za watu, baadhi ya wakati picha hizi hubuniwa, na watu husingiziwa maovu, ukisambaza utakuwa umemzulia mtu, na ikiwa ni picha za aibu lakini ni za kweli utakuwa umefanya kosa kubwa zaidi kuliko kumsengenya, yaani utakuwa umemkashifu na umemdhalilisha.

Ik iwa kwel i mtu amefanya kosa, basi taratibu za Uislamu ni kwenda kuzungumza aliyefanya kosa hilo na ukamkataza. Ama mtindo wa kuwakashifu Masheikh na watu wengine kwa kuwazulia mabalaa na kurusha picha zao za aibu, hizi ni tabia za kikafiri.

Amesimul ia Abu Mussa Ashary (R.A) k w a m b a , M t u m e ( S .A.W) a l iul izwa yupi Muislamu bora? A k i s e m a , “At a k a e msalimisha Muislamu mwenzake na shari ya ulimi wake, mkono wake (SB10 N5009 T 2628).

Amesimul ia Abi i H u r a y r a ( R . A ) , a m e s e m a M t u m e (S.A.W), “Msihusudiane wala msizidishiane b e i m i n a d a n i , m s i b u g h u d h i a n e , m s i h a m a n e , w a l a mtu asinunue juu ya b e i ya m we n z a k e , kuweni waja wa Allah (S .W) mlio ndugu. Muislamu ni ndugu wa Muislamu mwenzake a s i m d h u l u m u , a s i m wa c h e k a t i k a shida bila ya kumsaidia, a s i m d h a r a u , u c h a M u n g u u p o h a p a , a k a a s h i r i a M t u m e (S.A.W) kifuani pake mara tatu. Inatosha kwa mtu kupata shari kamili k w a k u m d o g o s h a ndugu yake Muislamu!.

Kusafirisha picha chafu kwenye mitandao (whatsapp)

Kila Muislamu kwa Muislamu mwenzake, ni haramu damu yake ( a s i i m wa g e ) , m a l i yake (asimdulumu) n a h e s h i m a y a k e (asimvunjie) ”. (SM 2564).

Kwa hivyo ni haramu na dhambi kubwa, kutizama picha chafu k w e n y e m i t a n d a o na kuziweka pia ni haramu, na ni katika makatazo makubwa.

K w a v i l e s u a l a l a k u p i g a p i c h a l i n a k u b a l i wa k wa udhuru tu, ni makosa kwa wanawake kuweka p i c h a z a o k we n ye mitandao ya facebook na mitandao myengine, au kuweka picha chafu kwenye simu.

Wanawake wengi Waislamu, wameiga mila za kikafiri na kuweka p icha zao wakiwa wamejipamba k we n ye m i t a n d a o , wengine wameweka picha za uchi kabisa, picha hizo hutazamwa na watu zaidi ya milioni ishirini, maana yake ikiwa umeweka picha na hali umejipamba, a u u k o u c h i k wa mujibu wa sheria, basi utapata dhambi kwa kila anayekutizama, hapo utajua kwamba u m e s h a t a n g u l i z a dhambi ngapi.

Wakati wa Mtume (S.A.W) , Mayahudi wa kabila la Banii Qaynuqa, wal ikula n jama za kumvua mwanamke wa Kiislamu nguo na wamuone uchi wake, mwanamke alikataa na wakamvua kwa ujanja, mmoja kati ya Mayahudi hao aliibana nguo ya mwanamke huyo ukutani kwa pini, bila ya yule mwanamke kujua wakati alipokuwa k w e n y e d u k a l a sonara wa Kiyahudi, a l i p o o n d o k a n g u o ilimvuka na Mayahudi wakacheka. Na ujanja huu pia unatumika l e o , m i t a n d a o

amewekwa mabinti wa Kiislamu, watakaa uchi wadhalilike na mitandao hii ni ya hao hao Mayahudi na wamekashifika wengi sana.

Kwa hiyo nawashauri a m a k u w a s i h i wanawake watukufu wa Kiislamu kuondoa picha zao kama hakuna dharura yeyote kwenye facebook, twitter, na mitandao mingine, ili ulinde hadhi yako na hadhi ya dini yako.

P i a n i h a r a m u kuwasiliana (kuchat) na wanaume kwenye mitandao bila udhuru, na udhuru ni kuumwa au biashara na mengine munasaba na hayo, lakini kuchat i b i la dharura ni haramu.

Hata hivyo ikiwa mwanamke amevaa h i j ab v izur i , hapo anaweza kuweka picha yake katika mitandao i n a y o a m i n i k a y a Kiislamu, ikiwa kuna udhuru maalum kama kutafuta mume nk.

Wa l e w a n a w a k e w a l i o w e k a p i c h a h a l i wa m e j i p a m b a a u wa m e k a a u c h i (yaani hawakujistiri ipasavyo), wazitoe na waache ‘kuchat’ hovyo na wanaume kwani huko ni kuikaribia z i n a a . M wa n a m k e anatakiwa azungumze na mwanamme pale tu itakapobidi, aidha kwa biashara au hukmu au maslahi ya maisha, si ‘kuchat’ hovyo na wanaweza ‘kuchat’ na wanawake wenzao na wanaume ‘wachat’ na wanaume wenzao, i s ipokuwa mtu na mkewe na maharimu zake.

Na kwa hivyo ni haramu kuwatizama wanawake kwenye m i t a n d a o i l a k wa yule anayetaka kuoa atatizama uso wa yule anayetaka kumuoa tu basi.MUSSA AME MUSSA 0773834795

Page 13: ANNUUR 1148

13 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 24-30, 2014MAKALA

Kuna haja ya kujiuliza kwanini maradhi haya chanzo ni Afrika

Inatoka Uk. 3kuaenea kwa awali kwa virusi vya ukimwi (HIV-1) kutoka Kinshasa hadi katika maeneo mengine yenye wakazi wengi," alisema Prof. Phillippe Lemey, wa Chuo Kikuu cha Leuven.

Ilielezwa kuwa usafirishaji na mabadiliko ya kijamii kunaweza kusababisha mtandao wa Ukimwi kuenea sehemu nyingine kutoka Kinshasa hadi nchi za Afrika ya Kati, hususan usafirishaji kwa njia ya reli, unaonekana kuchangia sana kuenea kwa HIV.

Mtafiti huyo aliongeza kuwa, zaidi watu milioni moja walikuwa wakitumia usafiri wa reli kwa mwaka kueleka mwishoni mwa miaka ya 1940s.

"Vielelezo vyetu (Our genetic data) vinatueleza kuwa HIV vilisambaa haraka sana nchi nzima ya DRC, vikisaf ir ishwa na watu maeneo ya usafiri wa reli na majini hadi kufika Mbuji-Mayi na Lubumbashi na maeneo ya kusini zaidi na Kisangani kaskazini hadi kufikia mwishoni mwa miaka ya 1930s na mapema miaka ya 1950s. Hali hii ilisaidia kuanza kuambukiza virusi vya HIV-1 katika ukanda huo ambao uliunganishwa barabara na nchi za kusini na mashariki mwa Afrika," alielezea Dk. Nuno Faria, wa Idara ya Zoology ya Chuo Kikuu cha Oxford.

Watafiti hao walisema kuwa mabadiliko ya kijamii yaliyozunguka upatikanaji wa uhuru katika miaka ya 1960s yanaonekana

kusababisha kuenea kwa maambukizi kutoka idadi ndogo hadi idadi kubwa ya watu, na baadae maambukizi kufikia dunia nzima.

Walisema kulikuwa na idadi kubwa ya maambukizi kutokana na kampeni za afya za maradhi mengine zilizokuwepo wakati huo, a m b a z o z i l i s a b a b i s h a matumizi na yasiyo salama ya sindano zenye maambukizi,

sababu zote hizo zilisababisha kuenea kwa kasi kwa HIV.

Prof. Pybus aliongeza kuwa utafiti wao ulibainisha kuwa kufuatia maambukizi ya virusi kutoka mnyama wa awali hadi kwa binadamu (yanawezekana kwa njia ya uwindaji au utumiaji wa nyama pori) yalikuwa na nafasi ndogo ya kueneoa HIV wakati wa utawala wa Ubelgiji huko DRC.

Kwa upande wa ugonjwa hatari wa ebola, unaonezwa kwa virusi, umezidi kutikisa dunia huku bado kukiwa hakuna uhakika wa tiba wala chanjo ya uhakika ya maradhi haya.

Kama ilivyokuwa kwa virusi vya ukimwi, virusi vya Ebola navyo pia watafiti wamedai kuwa asili yake au chanzo chake ni huko huko DRC (zamani ikiitwa

Zaire), ambako imedaiwa kwamba ndiko virusi hivyo vilipogunduliwa kwa mara ya kwanza.

Maisha ya watu katika nchi za Liberia, Siera Leone, Guinea na nchi jirani na hizo katika Afrika magharibi, yanazidi kuteketea kila uchao huku hofu ikitawala zaidi bara Ulaya na Amerika.

I m e f i k i a b a a d h i y a watu kuamini kwamba ugonjwa huo ni mahsusi kwa Waafrika, kwa kuwa umeonekana katika bara hili huku ukiteketeza zaidi Waafrika.

virusi vya ebola vimedaiwa k u wa n i h a t a r i z a i d i , ambavyo husababisha homa kali na za mara kwa mara kwa binadamu na wanyama wengine aina ya mamalia na mtu huchukua muda mfupi kupoteza uhai, tofauti kidogo na ukimwi.

Virusi hivyo vimeitwa E b o l a m wa k a 2 0 1 0 i l i kuepuka mkanganyiko. Wataalam wanasema kuwa aina hiyo ya virusi ni virological taxon species ikijumuisha Ebolavirus, familia ya Filoviridae.

U g o n j w a h u o p i a umeelezwa kuwa umetokana na maambukizi kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu kwa njia ya mafua.

Kutokana na kuwa na madhara makubwa, ebola imewekwa katika orodha ya magonjwa hatari zaidi (Risk Group 4) na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Shirika hilo limesema kuwa mlipuko wa homa ya ebola ulioziathiri baadhi

Inaendelea Uk. 15

Ebola imetengenezwa na makampuni ya madawa, Wizara ya Ulinzi ya Marekani? Wanasayansi wanadai

Inatoka Uk. 2lake, alikuwa ameyakinisha kuwepo kwa kiwanda cha kijeshi cha dawa za binadamu ambacho kinafanya majaribio ya silaha za vijidudu chini ya kinachodaiwa ni kutoa chanjo kudhibiti magonjwa na kuinua afya ya ‘Waafrika weusi ng’ambo.’ Kitabu hicho ni kizuri sana, na viongozi wote na yeyote mwenye ari na sayansi, afya, watu, na njama akisome. Ninashangaa kuwa viongozi wa Afrika hawatoi shukrani au kuzungumzia machapisho haya.

2. Ebola ina historia chafu, na majaribio yamekuwa yakifanyika kwa siri barani Afrika: Sasa hivi ninasoma ‘The Hot Zone,’ riwaya ya Richard Preston (hatimiliki ya mwaka 1989 na 1994); kinaumiza moyo. Mwandishi mahiri na maarufu, Steven King, ananukuliwa akisema kuwa “kitabu hicho ni moja ya vitabu vya kutisha zaidi ambavyo nimewahi kusoma. Ni kazi ya kushangaza sana.” Kama kitabu kilichovunja rekodi za mauzo kwa mujibu wa gazeti la New York Times, ‘The Hot Zone’ inaelezwa kuwa ni hadithi ya kuogofya ya kweli. Inatisha kwa sababu undani wa maumbile ya k i l i c h o o n e k a n a k a t i k a wanyama waliouawa kwa virusi vya Ebola ndicho a m b a c h o v i r u s i h i v y o vimekuwa vikifanya kwa

raia wa Guinea, Sierra Leone na Liberia katika kuzuka kwa Ebola hivi karibuni: Virusi vya Ebola vimeteketeza mifumo ya ndani ya mwili n a m w i l i u n a h a r i b i k a k wa h a r a k a b a a d a ya kifo. Inalainisha misuli na kuifanya kuwa mgando, hata kama imewekwa katika jokofu kuifanya iwe na baridi. Kubadilika mwili uwe wa majimaji ndicho kinatokea kwa watu wanaokufa kwa virusi vya Ebola! Mwandishi aliainisha katika kitabu Point 1, kuwa Dk. Horowitz anambeza mwandishi wa Hot Zone kuwa aliandika ili aonekane mwema kisiasa; naelewa kwa sababu kitabu chake kimefanyiwa kila juhudi kuwa sahihi. Tukio la Ebola la mwaka 1976 nchini Zaire, wakati wa utawala wa Rais Mobutu Seseseko, ilikuwa ni kuingizwa kwa virusi vya Ebola barani Afrika.

3. Vituo vilivyoundwa Afrika, na Afrika Magharibi, v i m e k u wa v i k i t u m i wa kujaribisha magonjwa mapya.

hasa Ebola: Shirika la Afya Duniani (WHO) na mashirika mengine kadhaa ya Umoja wa Mataifa, yamehusishwa katika kuteua na kuzua nchi za Afrika kushiriki katika matukio hayo ya majaribio, yakihamasisha chanjo, lakini yakiwa na mikakati kadhaa ya majaribio. Makala ya August 2, 2014, “Afrika Magharibi: Watafiti wa silaha za vijidudu wa Marekani wanafanya nini katika eneo la Ebola?” ya John Rappoport wa Global Research (mtandao wa kupashana habari) inaainisha tatizo linalozikabili serikali za nchi za Afrika.

Kilicho wazi katika hili na taarifa zingine ni, pamoja na mengineyo” (a) Taasisi ya Jeshi la Marekani ya Magonjwa ya Kuambukiza, kituo kinachofahamika kwa utafiti wa silaha za vijidudu, iliyoko Fort Detrick, jimbo la Maryland; (b)Chuo Kikuu cha Tulane, jimbo la New Orleans nchini Marekani, kinahopata ruzuku (kubwa) za utafiti, ikiwa ni pamoja na dola milioni saba kupitia

Taasisi ya Taifa ya Afya (NHI) kufanya utafiti kuhusu homa ya kupoteza damu ya virusi vya Lassa; (c) Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa (CDC); (d) Madaktari Wasio na Mipaka (wanaojulikana zaidi kwa jina lao la Kifaransa, Medecins Sans Frontiers); (e) Tekmira, kampuni ya dawa ya Canada; (f ) Kampuni ya GlaxoSmithKline ya Uingereza, na (g) Hospitali ya Serikali ya Kenema mjini Kenema, Sierra Leone.

Taarifa zinaelezea habari za Wizara ya Ulinzi ya Marekani ikitoa fedha za kufanyika kwa majaribio ya Ebola kwa binadamu, majaribio ambayo yalichukua wiki kadhaa tu kabla ya kufumuka kwa gonjwa la Ebola huko Guinea na Sierra Leone. Taarifa hizo zinaendelea na kuyakinisha kuwa Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilitoa kandarasi (tenda) ya thamani ya dola milioni 140 kwa Tekmira, kampuni ya dawa ya Canada, kufanya utafit i kuhusu Ebola. Utafiti huo ulikuwa ni pamoja na kupiga sindano

na kuingiza katika mwili wa mtu mwenye afya virusi hatari vya Ebola. Hivyo, Wizara ya Ulinzi ya Marekani i n a o r o d h e s h w a k a m a mshirika katika “Kwanza kwa mtu - Majaribio ya Ebola katika maabara za hospitali (NCT02041715 iliyoanza hapo Januari 2014 mara tu kabla gonjwa la Ebola halijatangazwa katika Afrika Magharibi mwezi Machi. Cha kuchukuza zaidi ni kuwa taarifa nyingi zinafikia tamati kuwa serikali ya Marekani ina maabara ya kufanya utafiti wa vita ya kigaidi ya vijidudu huko Kenema, mji ulio katikati ya wimbi la kuzuka gonjwa la Ebola huko Afrika Magharibi. Tawi pekee la kijani lililoonekana katika kusoma taarifa hizi ni kuwa Theguardian.com iliripoti. “Kutoa fedha kwa majaribio ya Ebola kwa binadamu w e n y e a f ya k u n a k u j a wakati tahadhari zimesikika kutoka wanasayansi wenye hadhi katika vyuo vikuu vya Harvard na Yale kuwa majaribio ya virusi kama hayo yanaweza kule ta mfumuko wa gonjwa hilo duniani kote.” Hatari hiyo bado inadumu.

4. Hitaji la hatua za kisheria za kupata fidia kwa hasara kutokana na kuendelezwa kwa ukandamizaji katika vifo, kuumia na mishtuko

Inaendelea Uk. 15

Page 14: ANNUUR 1148

14 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 24-30, 2014Habari

Zanzibar ArijojoInatoka Uk. 7

mmoja ilikuwa ni mbinu na hatua hatua ya kuzidisha mapambano ya kuwatisha Wazanzibari. Walisimama k i d e t e n a w a k a a m u a liwalo naliwe. Ama kwa kwenye haki, basi rasimu ile ingeambiwa haikupita, kwani Ulimwengu wote uliona kwamba Wazanzibari hawakutimia theluthi mbili ya walioikubali rasimu na haki haikutendeka.

Kwa wafuat i l i a j i na kama nilivyosema hapo mwanzo, Wazanzibari kwa kusikiliza sauti ya Muasisi wao kufuatilia mambo ya siasa, walikuwa wanafuatilia k we l i k we l i . Wa l i o n a dhahiri shahiri yaliyokuwa yanatokea. Kati ya mambo yaliyotokea ambayo kwa yeyote mwenye akili timamu angejiuliza ni:

1. Wakati Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba anawasilisha idadi ya wapiga kura alisema, Wazanzibari ni 210 na akasema waliomo ni 142, hivyo akidi imetimia.

2. Wakati matokeo ya kupiga kura yalipoangazwa, basi Wazanzibari walitajwa kuwa 219 na akidi ya theluthi mbilki ni 146. Hiyo inatosha kubatilisha matokeo hayo. Hesabu na namba zinakuwa s i kama his ia ambazo unaweza kuzi wasilisha huku umeibabaisha.

3. Mwanasheria Mkuu wa Zanziabr ambae ni Mzanzibari kindakindaki alipopiga kura za Hapana juu ya Rasimu hiyo ya Katiba, ambayo yeye kwa ueledi wake haina faida na Zanzibar. Seuze mambumbumbu wanaojifanya wanajua zaidi kuliko bingwa wa Sheria wa Zanzibar. Hebu jiulize?! Lakini tena, mzoea vya kunyonga, vya kuchinja haviwezi.

H i v i k a r i b u n i k u n a m u a n d i s h i m m o j a a l iyewaki l i sha makala il iyochapishwa kwenye gazeti la Mtanzania, inayo chambua kwa kina jinsi gani kwa utafiti wake anaona theluthi mbili za Zanzibar hazikupatikana. Anataja kati ya mambo mengine, mmoja wa Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Zanzibar alihesabiwa kama ni Mbunge kutoka Tanganyika. Pia alifafanua ni jinsi gani isingewezekana kuwapata Wabunge wa Bunge hilo waliokuwa Hijja na yule aliyekuwa India kwa matibabu. Yote hayo ametoa ushahidi wa kuonesha utata mkubwa uliokuwepo.

Baada ya maelezo hayo, sasa tuangalie ni vipi na kwanini tunasema Zanzibar itakwenda arijojo kama hali haitabadilika na Mchakato huu ukazimwa na baadae

ukarekebishwa ili ipatikane katiba ambayo itaridhiwa na wengi wa Wananchi, hasa Wazanzibari?

A m a k i u s t a r a b u inajulikana kabisa kwamba iwapo haki i tafanyika, basi kura ya maoni juu ya Katiba haiwezi kupita Z a n z i b a r . I n a e l e we k a lakini kutokana na uzoefu uliopo kuanzia 1995-2010 k wa m b a , h i v y o s i v y o mambo yanavyofanyika Zanzibar. Hasa kwa vile viongozi walikubaliana kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa, lakini wakashindwa k u k u b a l i a n a k u wa n a msimamo mmoja wenye manufaa kwa Wazanzibari. Hapo ndio kama ule msemo wa k i s wa h i l i u s e m a o “Wakipigana kuku, afaidiye ni mwewe”.

Wazanzibar hawaonekani kupata dalili ya kushikamana kwa jambo hili. Ni dhahiri lakini wengi wa Wazanzibari juu ya Jambo hili wanataka Nchi yao yenye mamlaka Zaidi kuliko ilivyo kwenye Katiba ya sasa na hiyo i l iyopendekezwa. Kwa namna hiyo, watataka waipigie kura ya hapana Katiba iliyopendekezwa. I n a s i k i t i s h a l a k i n i , W a z a n z i b a r i s a s a wamekuwa kwenye hali kama aliyoisema muimbaji mmoja, kwamba mbele yao kuna simba, nyuma yao kuna chatu, kulia kwao kuna faru na kushoto kwao kuna tembo. Hawajui waleekee upande gani wasalimike.

Wazanzibari walikuwa tayari wanaona kunonooka na kupata tamaa ya kuipata na kuijenga Zanziabr yao.

Hali ilivyo si shuari, ingawa walioshika hatamu wanataka tuelewe vyengine. Wakipiga K u r a k u i k a t a a K a t i b a i l iyopendekezwa, kuna mambo kadhaa yanayoweza kutokea:

1. La kwanza, itapitishwa tu kwa hali yeyote. Na hapo ndio patakapokuwa n a m a t a t i z o , k w a n i Wazanzibari hawatakubali kutulia, kama walivyokataa kutulia, mwapotawaliwa na Mreno, walipotawaliwa na Muingereza na walipoona w a n a h i t a j i k u f a n y a Mapinduzi. historia ina tabia ya kujirudia. Nafasi adhaimu iliyokuwepo imevurugwa kwa woga au utashi tu.

2. Jengine linaloweza kutokea ni kukubaliwa isipitishwe hiyo Katiba i l iyopendekezwa. Kwa n a m n a h i y o , k a t i b a itakayotumika itakuwa ni ile iliyopo sasa hivi. Na kwa wakati huo itakuwa tatizo juu ya tatizo.

3. Walioutengeneza huu mtego watakuwa wamepata n o n g w a n a k u s e m a Wazanzibari wanakubaliana na hali yao ya sasa na h a wa t a k i m a b a d i l i k o . Kabla hujanishambulia, naelewa hali na hisia halisi za Wazanzibari , lakini Mchakato huu wa kupata Katiba Mpya ya Wananchi, umegeuka kuwa mta j i kwa baadhi na jukwaa la kujiimarisha kisiasa kwa we n g i n e n a wa t a t a k a kufanya hivyo hivyo huko mbele.

Sasa nini la kufanya? Wengi wa Wazanzibari

RAIS Jakaya Kikwete

maksudi au kwa mbinu, Wabunge waliojiita watetezi wa Katiba ya Wananchi, wakatoka Bungeni. Kwa kweli, kama hiyo ilikuwa ni kwa makusudi, walipatikana na mitego i l iyowekwa. Inawezekana k ihesabu walidhani Bunge Maalum la Katiba halitaendelea, kwa vile wao hawamo Bungeni. Walifikiria, wapinzani wao watakuwa wastaarabu na wawasikilize. Bahati mbaya hilo halikutokea, na matokeo yake kukawa na wapenzi hasa wa Zanzibar wachache tu.

K w e n y e m e d a n i z a mitandao ya Jamii, wengi wa Wazanzibari walisema w a l i o m o B u n g e n i n i Wa s a l i t i wa Z a n z i b a r . Kwani walitakiwa watoke na warudi Zanzibar kwa vile Bunge hilo halikuwa na faida tena na Zanzibar. Mitandaoni wal iobakia bungeni waliambiwa ni woga na wanafiki. Kulikuwa na kikundi kidogo cha Wazanzibari ambao wao walitaka kuitetea Zanzibar wakiwa kwenye hilo Bunge Maalum la Katiba. Hawa waliendelea mpaka karibu sana au karibu na mwisho.

Kwa kweli kama Bunge maalum la Katiba ingekuwa ni Kombe la Dunia la mpira wa miguu, basi wapenzi na watazamaji walikuwa wamevunjika moyo kama ambavyo wapenzi wa kombe la dunia walioipendelea Brazil kuvunjika moyo pale walipofungwa mabao 7 bila kuona mlango. Wananchi hasa wa Zanzibar walijisikia vibaya, wakawa wanaumia n a wa n a t o a h i s i a z a o kwenye mikutano, lakini hawakupendelea yaliyokuwa yanaendelea, kwani ile hamu yao ya kuiona Zanzibar iliyojikomboa na kuanza kunawiri ilififia.

Kwa vile Bunge maalum la Katiba, lilikuwa kama timu ya mpira wa miguu inayoshindana na mpinzani wake. Ikawa na muamuzi katika mmoja wa wachezaji wake, upande wa pili wa wa p i n z a n i wa m e b a k i a wa s h a b i k i t u , h a k u n a wachezaji, na hao washabiki ni wachache sio timu kamili ambayo haina hata golikipa. Hapo ndio Bunge Maalum lilipokosa muelekeo na Katiba ikawa inapitisha kama vile timu inayocheza uwanjani kwake wakati wapinzani wamo wawili au watatu na hawana golikipa. Wakawa wanayafunga tu magoli.

Pamoja na hali hiyo, hao wachezaji wawili watatu w a l i o k u w a u w a n j a n i walimudu kuichukua mechi mpaka muda wa majeruhi, wakati wa penalty walijaribu kufunga goli la ushindi. Haikuwezekana, kwani, timu kubwa ilikuwa ina refa wao na washabiki wao. Hivyo waliokuwa upande wa pili wakatishwa, mpaka kutishiwa maisha yao.

Hali hiyo kwa upande

wanaona, kutokana na Katiba iliyopendekezwa iwe kama ilivyo, itakuwa ni kama kujipeleka mbele ya simba ukitarajia atakuacha upite. Kwa kweli haitaridhisha hata kidogo, Zanzibar ikifanywa koloni la Tanganyika na kuendelea kukandamizwa kama ilivyo sasa hivi na kuvifanya vizazi vijavyo viwe kama wageni nchini kwao wenyewe. Kwa nini tumebahatika kupata furusa tunaichezea? Wengi wa Wazanzibari wanajiuliza!

Ukiangalia kwa undani, hakuna faida kubwa ambayo Tanganyika inapata kuikaba Zanzibar, zaidi ya kuwa na Koloni ambalo inasema ni Muungano. Kama Zanzibar ingekuwa ni mshirika sawa kwa Tanganyika. Nchi zote mbi l i z ingekuwa fa ida kubwa sana.Faida nyengine kubwa zaidi, sasa hivi nchi nyengine nyingi zingekuwa zimeshajiunga na Muungano huu na kuifanya ndoto ya kuiunganisha Afrika kuwa rahisi.

B a h a t i m b a y a , k w a Muungano huu, kwa vile wasiokuwemo wanaona madhila inayopata Zanzibar, hakuna nch i nyengine inayotaka ku j iunga na M u u n g a n o h u u , k a m a ulivyo. Linaloendelea ni kaka mkubwa, Tanganyika kujivalisha koti la Muungano na kuifanya Zanzibar kama kitoto kidogo ili ikubali kwa kuwatumia wanaoitwa na wana mtandao Wanafiki. Hali hii haitaendelea kuwa nzuri na salama, ikiwa itaendelea hivi hivi kuifanya Zanzibar Koloni la Tanganyika.

Inawezekana kuwaziba midomo wachache sasa hivi, kama alivyofanyiwa Mh. Mansour Yussuf Himid na Mh. Othman Massoud Othman, kwa kupiga kelele kwao kuitetea Zanzibar. Lakini ieleweke kwamba kizazi kipya hakitakubaliana n a u n a f i k i p a m o j a n a ukandamizaji.

Kizazi kipya kinajua jinsi Kompyuta zinavyofanyakazi, kwa hivyo kitataka kila kitu kifanye kazi bila mizengwe ya kinafiki na kuoneana. Hapo ndio, ingawa Zanzibar inakwenda arijojo sasa hivi, utafika wakati itatoka kwenye hali hiyo na wakandamizaji wa t a i t o a we n ye we n a watabakia kusema Laitani t u n g e j u a ! Tu s i n g e i t i a Zanzibar Arijojo. Na hapo itakuwa vigumu kuulinda na kuuhifadhi Muungano, ambao kwa sasa bado Wazanzibari wanautaka, lakini wanautaka uwe wa haki na heshima kwa pande

zote mbili.(mwandishi:[email protected])

Page 15: ANNUUR 1148

15 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 24-30, 2014Makala

Kuna haja ya kujiuliza kwanini maradhi haya chanzo ni Afrika

Inatoka Uk. 13ya nchi huko magharibi mwa Afrika, umeua watu zaidi ya 4,400 hadi hivi sasa huku wengine zaidi ya 7000 wakiambukizwa virusi hatari vya maradhi hayo.

N a i b u M k u r u g e n z i Mkuu wa Shirika hilo Bruce Aylward, amenukuliwa akisema mlipuko wa virusi vya ebola uliojitokeza mwezi Machi mwaka huu huko magharibi mwa Afrika.

H a t a h i v y o , w a p o wanaoitaja Marekani kuwa inahusika na kuzalisha na kueneza virusi vya Ebola.

Gazeti la Daily Observer la mjini Monrovia nchini Liberia, lilitoa nyaraka na ushahidi unaothibitisha k u wa M a r e k a n i n d i y o iliyotengeneza na kusambaza virusi vya ugonjwa wa Ebola.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, Marekani imekuwa ikifanya operesheni mbalimbali za siri barani Afrika, likatolea mfano wa ile iliyopewa jina la siri la "Hati ya Maelewano ya 200", ambayo ilielezwa kuwa kazi yake ilikuwa ni kuzalisha virusi hatari vya Ebola.

Profesa Siele Brodrick, mtaalamu wa maradhi ya kuambukiza na mwandishi wa makala hiyo anaamini kwamba, virusi angamizi ya Ebola ni moja ya virusi vilivyozalishwa na viwanda vya kijeshi vya Marekani kwa kushirikiana na utawala wa zamani wa makaburu nchini Afrika Kusini mwaka 1975.

Kwamba tangu wakati huo, Wizara ya Ulinzi ya Marekani imekuwa ikitumia virusi hivyo kama silaha ya kibiolojia. Kwa mtazamo wa profesa huyo, mwaka 1975, Marekani kwa kushirikiana na utawala wa ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini, ulifanya operesheni ya siri nchini Zaire (sasa Jamhuri

Mkurugenzi wa WHO Margaret Chan

ya Kidemokrasia ya Kongo) na kupandikiza nchini humo kwa mara ya kwanza virusi hatari sana vya Ebola.

Alisema jambo lisilo na shaka ni kwamba, operesheni ya siri iliyopewa jina la siri la "Hati ya Maelewano ya 200" ilianzishwa kwa lengo la kupunguza idadi ya watu katika bara la Afrika.

Imedaiwa kuwa Marekani imeeneza balaa hilo la virusi barani Afrika, ili kupunguza idadi ya Waafrika duniani.

Katika moja ya vitabu vyake vilivyozungumzia ugonjwa huo, Profesa Siele Brodrick, alisema kuwa Marekani kwa kushirikiana na baadhi ya nchi washirika wake, ilianzisha operesheni za siri za kueneza maradhi barani Afrika.

K a t i k a r i p o t i h i y o imeelezwa kuwa kwa mara ya kwanza virusi vya Ebola viligunduliwa pembezoni mwa mto Kongo Agosti 26, 1976 katika kijiji kidogo cha Yambuku, Wilaya ya Mongala huko Jamhuri ya Kongo mwaka 1976.

Kuanzia mwezi Desemba mwaka jana, virusi hatari vya Ebola vilianza kuenea magharibi mwa Afrika. Mtaalam huyo amesema kuwa kuna vituo vingi sana vya tiba vimeanzishwa katika eneo hilo, ili kupambana na ugonjwa huo na kutafuta dawa za kutibu maradhi hayo, lakini vyote viko chini ya usimamizi wa Marekani na mashirika yenye mfungano

na Washington. Ni dhahiri kuwa kituo

cha kudhibiti magonjwa ya kuambukiza cha Marekani (CSD) kimeshindwa kupata chanjo ya ugonjwa huo. Hata hivyo ugonjwa huo umeshafika hadi Marekani k w e n y e w e b a a d a y a mwandishi mmoja wa habari wa Kimarekani, Thomas Eric Duncan, kuambukizwa ugonjwa huo hatari.

Tunaweza kusema kuwa Marekani ambayo shutuma zote zinaelekezwa kwake kuwa ndiyo iliyotengeneza

na kusambaza virusi hivyo barani Afrika, yenyewe nayo imekumbwa na ugonjwa huo angamizi.

Nako huko Ujerumani w a l i t a n g a z a k u w a watauchoma moto mwili wa raia wa Sudan aliyekuwa akihudumia wagonjwa wa Ebola huko Afrika Magharibi aliyekufa kwa ugonjwa huo wakati akitibiwa nchini humo, ili kuzuia kuenea virusi vya ugonjwa huo nchini humo.

Aidha WHO ilieleza kuwa, kuna maambuki mapya zaidi

ya 10,000 ya Ebola hadi sasa.Hadi sasa tiba ya Ebola

b a d o h a i j a g u n d u l i wa . Dalili za homa ya Ebola ni kuharisha, kutapika na kutokwa damu katika sehemu mbalimbali mwilini.

Wa k a t i t u k i j i s h a u r i j u u ya m a r a d h i h a ya yanayosababisha vifo vya halaiki kwa Waafrika tu, ikumbukwe kuwa kuna wakati tuliambiwa kuwa magaidi wa al-Qaeda chini ya Osama bin Laden, baada ya shambulio la Septemba11 katika majengo ya World Trade Centre (WTC) na kule Makao Makuu ya Jeshi-Pentagon, waliendeleza mashambulizi yao dhidi ya Marekani kwa kutumia kemikali za kimeta (anthrax) na kuendeleza mauaji.

Madai haya yalikolezwa sana na Marekani kiasi cha kusababisha mataifa n a u l i m we n g u m z i m a kuingia woga kwa kuamini tuhuma za anthrax ni tishio jingine kutoka kwa Osama na al-Qaeda. Wamarekani wa l i e n d e l e a k u p o t e z a maisha kwa kusoma barua zilizopandikizwa vimeta.

H a t a h i v y o k a m a i l i v y o k u w a k a t i k a mashambulio ya Septemba 11 yalivyozua mashaka na maswali mengi kwa watu wa Marekani na ulimwengu kwa ujumla, baadae ilikuja kugundulika kuwa vimeta hivyo ni aina maalum ya virusi vya kutengenezwa tu na katika maabara katika jeshi la Marekani.

Kuna haja ya Wataala wa Afya wa nchi za Kiafrika kukaa na kutafakari kwa kina juu ya maradhi haya ya U k i m w i n a E b o l a . Inawezekana kuna ‘siri kubw’a ndani yake.

Inaendelea…

Ebola imetengenezwa na makampuni ya madawa, Wizara ya Ulinzi ya Marekani? Wanasayansi wanadai

Inatoka Uk. 13i l i y o b e b e s h w a w a t u wa Liberia na wa-Afrika wengine kutokana na Ebola na njia nyingine za kuzua m a g o n j w a : M a r e k a n i , C a n a d a , U f a r a n s a n a Uingereza wote wanahusika katika vitendo vya kuchukiza na vya kishetani ambavyo ndiyo haya majaribio ya Ebola. Kuna haja ya kufungua kesi za jinai na madai ya fidia, na nchi za Afrika na watu wapate uwakilishi wa kisheria kuhitaji fidia kutoka nchi hizi, mashirika kadhaa, na Umoja wa Mata i fa . Ushahidi ni mwingi dhidi ya Chuo Kikuu cha Tulane, na kesi zinaweza kufunguliwa kuanzia hapo. Makala ya Yoichi Shimatsu, “Kuzuka k wa g o n j wa l a E b o l a kuliambatana na kampeni za chanjo,” iliyochapishwa Agosti 18, 2014 katika Liberty Beacon, ni kielelezo.

5. Viongozi wa Afrika na nchi za Afrika wanahitaji kuchukua nafasi ya mbele katika kuwalinda watoto wachanga, watoto wadogo, wanawake wa Kiafrika, wanaume wa Kiafrika na wazee. Wananchi hawa hawastahili kutumika kama panya wa maabara! Afrika

isidunishe bara hili kuwa ni pahala pa kulundika na kuondoa kemikali na madawa ya hatari, pamoja na na vianzio vya kikemikali au vijidudu vya magonjwa yanayozuka. Kuna haja ya haraka ya mkakati wa kuwalinda wasio na uwezo katika nchi maskini, hasa wananchi wa Afrika, ambao nchi zao hazina uwezo wa kisayansi na viwanda kama Marekani na nchi zilizobaki za Magharibi, ambazo ni chanzo cha virusi au vijidudu vilivyobadilishwa vinasaba na kuundwa kama silaha za kutumia viumbe hai. Inasikit isha sana kuwa serikali ya Marekani imekuwa ikiendesha maabara ya homa ya virusi ya kupoteza damu kwa ajili ya silaha za kigaidi za viumbehai nchini Sierra Leone. Hakuna nyinginezo? Kokote zilipo,

ni wakati wa kuziteketeza. Kama kuna vituo vingine kama hicho, inafaa kufuata n j i a i l i y o c h e l e we s h wa lak in i muhimu: S ie r ra Leone ilifunga maabara ya Marekani ya silaha za viumbehai na kuzuia Chuo Kikuu cha Tulane kuendelea na majaribio.

Dunia inahitaji kuchukua tahadhari. Waafrika wote, Wa m a r e k a n i , U l a y a , Mashariki ya Kati, Waasia, na watu kutoka maeneo yote katika sayari ya Dunia wanatakiwa kushangaa. Wa t u wa A f r i k a , h a s a wananchi wa Liberia, Guinea na Sierra Leone wanatumiwa na kufa kila siku. Wasikilize w a t u w a s i o z i a m i n i hospitali, ambao hawawezi kusalimiana kwa kupeana mikono, kukumbatia nasaba na marafiki zao. Watu wasio na hat ia wanakufa , na

wanahitaji msaada wetu. Nchi hizi ni maskini na haziwezi kununua vifaa maalum vya kujikinga ambavyo hali halisi inahitaji. Hatari ni ya kweli,, na ni kubwa zaidi kuliko nchi kadhaa za Afrika. Changamoto ni ya dunia nzima, na tunaomba msaada kutoka kila mahali, ikiwemo China, Japan, Australia, India, Ujerumani, Italia na hata watu wenye huruma nchini Marekani, Ufaransa, Uingereza, Russia, Korea, Saudi Arabia na kokote kwingine ambako azma yao ni kusaidia. Hali ni mbaya kuliko sisi tulio nje tunavyoweza kufikiria, na ni lazima tutoe misaada kwa kiwango tunachoweza.

Kuhakik i sha ha l i ya baadaye isiyo na ina hii ya matukio, ni muhimu kutaka sasa kuwa viongozi wetu na serikali wawe wakweli,

wawazi, wenye haki na kuhusika kwa njia chanya ipasavyo. Lazima wajibu kilio cha watu. Tafadhali simama na kuzuia haya majaribio ya Ebola na kuenea kwa gonjwa hili la kutisha.

Asanteni sana.

Wakatabahu,

Dk. Cyril E. Broderick, Sr

(Kuhusu mwandishi: Dk. Broderick ni Profesa wa zamani wa Mifumo ya Mimea katika Chuo cha Kil imo na Misi tu cha Chuo Kikuu cha Liberia. Amekuwa akiandika safu ya mausala ya kilimo katika gazeti la Observer katika miaka ya 1980. Ilikuwa ni katika safu hiyo katika gazeti letu la Daily Observer a m b a k o k a m p u n i y a Firestone (yenye miradi mikubwa nchini Liberia) i l imgundua na kumpa nafasi ya kuwa Mkurugenzi wa Utafiti kuelekea mwisho wa miaka ya 1980. Na zaidi, ni mwanasayansi, ambaye amefundisha kwa miaka mingi katika Chuo cha Kilimo cha Chuo Kikuu cha Delawere.)

Page 16: ANNUUR 1148

16 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 24-30, 201416 MAKALA

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works Limited, S.L.P. 4605 Dar es Salaam.

AN-NUUR16 DHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 24-30, 2014

Soma gazeti la

AN-NUUR kila Ijumaa

S H E I K H M s e l e m A l l y M s e l e m , a m e s e m a u d h a i f u wa afya yake akiwa gerezani unatokana na kusumbuliwa na maleria na kipigo cha Polisi alipokamatwa.

Amesisitiza kuwa hakupata madhara yoyote akiwa gerezani isipokuwa ni kutokana na kipigo cha polisi na homa aliyoingia nayo.

K w a u p a n d e mwingine amesema kuwa haoni kuwa ana kosa bal i hupigwa propaganda tu wakati uhakika wa mambo ni msimamo wake na wenzake kupinga mfumo wa muungano uliopo.

Z a i d i a k a s e m a kuwa, ni jambo la kusikitisha kuwa kuna watu wanapalilia na kupigia chapuo kitisho cha ugaidi usiokuwepo nchini bila ya kujua madhara yake.

Mwanazuoni huyo wa Dini ya Kiislamu, a m e t o a u f a f a n u z i huo baada ya wiki iliyopita kushindwa kufika Mahakamani na kuelezwa kuwa alipoteza fahamu akiwa gerezani.

Sheikh Mselem alitoa maelezo hayo Oktoba 18, 2014, mbele ya Kamati ya Maafa ya Shura ya Maimam (T), iliyolazimika kufika gerezani hapo ili kujua hali yake kiundani zaidi pamoja na Waislamu wengine 20 , wal io m a h a b u s u k a t i k a gereza la Segerea, Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Katibu wa kamati hiyo, Ust. Ally Mbaruku Seboy, al isema wameweza

Mselem aliumizwa na PolisiAsisitiza kosa lao ni kukataa muungano wa 2Wanapakwa matope jamii iwachukie Alia na wanaopalilia ugaidi, hao ndio maadui

Na Bakari Mwakangwale

kuonana na Sheikh Mselem, na kuongea nae baada ya kufuata taratibu za Magereza na kupatiwa kibali maalum, Jumamosi ya wiki iliyopita.

U s t . M b a r u k u , alisema, Sheikh Mselem, a m e wa e l e z a k u wa alikuwa anasumbuliwa n a m a l e r i a , k a b l a ya k u k a m a t wa n a alipokamatwa na Polisi alipigwa sana jambo ambalo limesababisha udhaifu zaidi kiafya.

A l i s e m a , b a a d a ya kuingia gerezani, alipatiwa matibabu y a m a l e r i a , k w a kupewa dozi ya Mseto, m a r a m b i l i l a k i n i haikusaidia na ndipo alipobadilishiwa na kupewa Qunini.

Alisema, kutokana na mabadiliko hayo ya dawa kutoka Mseto hadi Qunini, yaliyofanywa na Daktari wake, siku ya kusikilizwa kwa kesi yake Oktoba 15, 2014, ilisababisha tatizo la presha ya kushuka.

H a l i h i y o n d i y o iliyosababisha Sheikh Mse lem, kuanguka ghaf la , ha ta h ivyo a l i s e m a b a a d a ya kutokea ha l i h iyo , a l ipat iwa matibabu chini ya uongozi wa gereza na daktari wake na hatimaye afya yake ikarudi katika hali ya kawaida.

“Sheikh anaomba ieleweke kuwa kipigo n a m a r a d h i h a y o hakuyapata gerezani ba l i a l i ing ia humo

a k i w a m b o v u w a afya kwa maleria na kipigo cha Polisi wakati akikamatwa.” Alisema Ust. Mbaruku.

K w a u p a n d e m w i n g i n e , S h e i k h Mselem, ameonyesha m a s i k i t i k o y a k e kwa jinsi kadhia yao i n a v y o c h u k u l i w a kwani amedai limejaa proganda za idi ya uhalisia wa kadhia husika, na kupelekea hata jamii kuwaweka katika kundi baya.

Alisema, kosa lao halielezwi wazi ambalo ni kutumia haki yao ya kikatiba ya kutoa maoni yao, ambayo ni kukataa mfumo wa Muungano uliopo sasa na hilo sio kosa bali ni kutumia uhuru wa mtu kujieleza.

“Hii ni siasa chafu ambayo ni mchezo m c h a f u k w a n i unapanda mbegu mbaya na kama ikichepua sijui itakuwaje, lakini inatakiwa tuzibe ufa tusije kupata kazi ya kujenga ukuta, angalia Somali, Rwanda na Siria”. Alisema Ust. Mbaruku, akimnukuu Sheikh Mselem.

Katika hatua nyingine, Ust. Mbaruku, ametoa wito kwa Waislamu kutoa ushirikiano wao na michango katika kuwasaidia Masheikh h a o n a Wa i s l a m u wengine wanaokabiliwa na tuhuma za ugaidi.

A l i s e m a , b a a d a ya kupata fursa ya kwenda kuonana na Waislamu hao pia wameweza kusikia sh ida na mata t izo yanayowakabili.

Alisema, siku hiyo w a l i p o o n a n a n a Waislamu hao walipewa o r o d h a y a d a w a zilizokuwa zinahitajika a m b a z o z i l i k u w a zinagharimu kiasi cha Shilingi 59,000/-.

A l i u t a j a M a s j i d Rahma Makangira , Namanga Msasani , k u w a w a l i w e z a kuchangia kiasi cha pesa na kuwezesha kununuliwa Dawa hizo kwa ajili ya Waislamu hao waliopo gerezani, ambazo zilipelekwa Jumatatu wiki hii.

U s t . M b a r u k u , a l i s e m a , J u m a n n e , w i k i h i i a l i w e z a kupeleka Misahafu, m i t a n o , v i t a b u 1 0 Soksi jozi tatu, ikiwa ni sehemu ya mahitajio wa l i y o h i t a j i , h a t a hivyo alisema, alipewa vyeti vya Waislamu watatu vinavyohitaji k u n u n u l i wa d a wa baada ya kuonana na Daktari wa Gereza.

SHEIKH Msellem Ally Msellem (anayetabasamu katikati).