annuur 1176b.pdf

20
ISSN 0856 - 3861 Na. 1176 RAJAB 1436, IJUMAA , MEI 8-14, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu facebook: [email protected] AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST Soma Uk. 6 MWAKA 1984 katika kuunusuru Muungano, ilibidi Serikali nzima ya Zanzibar iondolewe madarakani. Aliondolewa Rais Aboud Jumbe Mwinyi, Waziri Kiongozi wake Ramadhan Haji Faki na Baraza lake lote la Mawaziri. WATANZANIA wamekwama, na wale ambao wanawategemea kuwakwamua nao wamekwama. Hii ndiyo hali Tanzania, sasa kondoo anayesubiri kuchinjwa Magazeti yanalitoa Jini katika chupa… Polisi, JWTZ hawamuwezi subiani huyu Serikali yetu inasikitisha! Imezoeya kulea matatizo Wananchi wakikwama, nayo… Inakwama katika namna mbaya inayowakabili Watanzania kwa sasa. Maisha yamezidi kuwa magumu kwao. Umeme ambao ndio nyenzo muhimu angalau ya kuwaongezea pumzi ya kuishi, nao hivi sasa umekuwa wa katakata, hauwasadii. Shilingi ambayo wanaifukuzia kula uchao, nayo imezidi kuporomoka thamani yake. Mfumuko wa bei umeshapiga hodi. (Soma Uk.12.) Hoja ni afya ya muungano sio umri wake- Awadh Said Mwanasheria Mkuu wa Serikali hiyo aliyekuwa Raia wa Ghana,Bashir Swanzy alitimuliwa nchini na kurejeshwa kwao. Orodha ya waliopata majeraha katika harakati za kuudumisha Muungano ni ndefu. (Soma Uk. 9) Watoto wetu wanafundishwa Historia ya kughushi shuleni Ni kutokana na chuki za kidini Mzungu ageuzwa kuwa Muarabu Mtume(saw) amesema, “Mwenye kuja kunizuru mimi kwa kutaraji ujira kwa Allah, basi mimi nitakuwa muombezi na shahidi wake (siku ya Kiama)”. Wahi sasa kuja kulipa ujihakikishie kuombewa na Mtume wako(saw). Muda unakwisha! Gharama zote kwa Hijja ni Dola 4,500. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,300. Karibuni Ahlu Sunna Wal Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0765462022;0782804480; 0717224437. Zanzibar:0777468018;0777458075;0777845010. (9) UOMBEZI WA MTUME(SAW) AWADH Said ZBIGNIEW Brzezinski. Soma Uk. 11

Upload: annurtanzania

Post on 18-Dec-2015

1.014 views

Category:

Documents


3 download

TRANSCRIPT

  • ISSN 0856 - 3861 Na. 1176 RAJAB 1436, IJUMAA , MEI 8-14, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

    Sauti ya Waislamufacebook: [email protected]

    AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST

    Soma Uk. 6

    MWAKA 1984 katika kuunusuru Muungano, ilibidi Serikali nzima ya Zanzibar iondolewe madarakani.

    Aliondolewa Rais Aboud Jumbe Mwinyi, Waziri Kiongozi wake Ramadhan Haji Faki na Baraza lake lote la Mawaziri.

    W A T A N Z A N I A wamekwama, na wale ambao wanawategemea k u w a k w a m u a n a o wamekwama.

    H i i n d i y o h a l i

    Tanzania, sasa kondoo anayesubiri kuchinjwa

    Magazeti yanalitoa Jini katika chupaPolisi, JWTZ hawamuwezi subiani huyu

    Serikali yetu inasikitisha!Imezoeya kulea matatizo

    Wananchi wakikwama, nayoInakwama katika namna mbaya

    inayowakabili Watanzania kwa sasa.

    M a i s h a y a m e z i d i kuwa magumu kwao. U m e m e a m b a o n d i o nyenzo muhimu angalau

    ya kuwaongezea pumzi ya kuishi, nao hivi sasa umekuwa wa katakata, hauwasadii.

    S h i l i n g i a m b a y o wanaifukuzia kula uchao, nayo imezidi kuporomoka thamani yake. Mfumuko wa bei umeshapiga hodi. (Soma Uk.12.)

    Hoja ni afya ya muunganosio umri wake- Awadh Said

    Mwanasheria Mkuu wa Serikali hiyo aliyekuwa Raia wa Ghana,Bashir Swanzy alitimuliwa nchini na kurejeshwa kwao.

    Orodha ya waliopata majeraha katika harakati za kuudumisha Muungano ni ndefu.

    (Soma Uk. 9)

    Watoto wetu wanafundishwa Historia ya kughushi shuleni

    Ni kutokana na chuki za kidiniMzungu ageuzwa kuwa Muarabu

    Mtume(saw) amesema, Mwenye kuja kunizuru mimi kwa kutaraji ujira kwa Allah, basi mimi nitakuwa muombezi na shahidi wake (siku ya Kiama). Wahi sasa kuja kulipa ujihakikishie kuombewa na Mtume wako(saw). Muda unakwisha! Gharama zote kwa Hijja ni Dola 4,500. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,300. Karibuni Ahlu Sunna Wal Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0765462022;0782804480; 0717224437.

    Zanzibar:0777468018;0777458075;0777845010.

    (9) UOMBEZI WA MTUME(SAW)

    AWADH Said

    ZBIGNIEW Brzezinski. Soma Uk. 11

  • 2 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 8-14, 2015AN-NUUR

    S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.

    www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected] zetu zipo: Manzese Tip Top

    Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

    Tahariri/Habari

    K W A h a k i k a , tukiyaangalia mambo kwa kina kirefu, zama za leo siyo tofauti sana na zile zilizotajwa katika Hadithi Tukufu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu. Dini ya Uislamu imekuwa ngeni, ufisadi na vurumai kila mahali. Sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu imepotoshwa na Uislamu umefungiwa ndani ya Misikiti. Kweli kabisa, hata mimbari nyingi za Misikiti yetu haziwakilishi Uislamu. Kwa upande mwingine, nguvu za mabeberu kwa kushirikiana na watawala wa nchi zetu, zimeendesha vita kali dhidi ya Uislamu.

    Katika kipindi cha miongo kadhaa iliyopita, mikakati ya vita hii ilianza kwa kuipaka matope dhana ya Kiislamu ya Jihad. Na sasa wanajaribu kuifuta kabisa dhana ya Dola ya Kiislamu kwenye vichwa vya Waislamu. Mtume wa Mwenyezi M u n g u a m e s e m a : "Uislamu ulianza kama mgeni, na utarudi ukiwa mgeni kama ulivyoanza..."

    K w a h a k i k a , t u k i z i a n g a l i a z a m a za leo, hazina tofauti sana na zile zilizotajwa kwenye Hadithi Tukufu ya M t u m e . U i s l a m u

    "Allah amewaridhia, nao wamemridhia.."Said Rajab l e o u m e k u wa m g e n i

    kabisaa duniani! Lakini hata hivyo, Mwenyezi M u n g u a s h u k u r i w e sana! Hisia miongoni mwa Waislamu kwamba Uislamu unashambuliwa, k w a m a r a n y i n g i n e tena, imewaunganisha Waislamu na kuwafanya wajitambue zaidi.

    W a i s l a m u s a s a wanajaribu kuuhuisha tena Uislamu na kusafisha m a t o p e ya l i y o p a k wa kwenye fikra zake karne nyingi zilizopita. Wanataka k u u r e j e s h a m t i w a Uislamu kwenye heshima yake ya awali. Waislamu wako nj iani kuelekea tena kuwa Umma bora, ambao utaifanya Itikadi ya Kiislamu kuwa juu ya Itikadi zote.

    Hata hivyo, hii siyo kazi rahisi. Kwenye njia hii, kuna ugumu na mitihani mingi. Vipi Makafiri wanaweza kuvumilia kusimamishwa tena Uislamu duniani, a m b a o wa l i f a n i k i wa kuusambaratisha kwa gharama kubwa? Leo, M u i s l a m u y e y o t e duniani, anayesimamia wito huo, mahali popote alipo, nguvu ya Makafiri itamuandama na hatimaye atafungwa mdomo kabisa. Kama kuzungumza, basi azungumzie udhu, talaka, kuoga janaba, kufanyia watoto Hakika, Khitma, Maulid, kuosha maiti,

    umuhimu wa kupiga m s w a k i , b a s i ! K w a hiyo, Muislamu yeyote anayejaribu kuutekeleza Uislamu kama Itikadi na Mfumo wa Utawala, basi atakuwa mgeni katika ulimwengu huu, kama alivyosema Mtume wa Mwenyezi Mungu. Leo hii, mwanaharakati wa kweli wa Kiislamu lazima a j i a n d a e n a u k w e l i k wa m b a a n a h i t a j i k a kwenda kinyume kabisa na mwelekeo wa jamii yake.

    Yale masuala ambayo siyo muhimu mbele ya M w e n y e z i M u n g u , ndiyo yamefanywa kuwa muhimu. Tena ndiyo hasa msingi wenyewe wa maisha yetu. Lakini yale masuala ambayo ndiyo ya kufa na kupona yanachukuliwa kuwa siyo muhimu. Hiyo ndiyo athari ya Mfumo wa Kibeberu ambao umetekelezwa kwenye Ulimwengu wa Waislamu kwa miongo mingi i l iyopita. Hiyo ndiyo sababu utawakuta Waislamu katika nchi za Waislamu wanahangaikia d u n i a t u . W a t u wanaonekana kufanikiwa ni wale wenye maisha mazuri ya hapa duniani.

    Wanaharakati halisi wa K i i s l a m u , a m b a o walifanikiwa kusimamisha Sheria ya Mwenyezi Mungu katika ardhi, waliipa kisogo

    NDANI ya Katiba ya Mtume (s.a.w) akiwa mtawala wa City State ya Madina, moja ya mambo yaliyoelezwa, k u f a f a n u l i w a n a kuwekewa misingi na kanuni, ni mahusiano ya waumini na wasio kuwa Waislamu, hasa Mayahudi. Nini haki zao na nini wajibu wao katika Dola ya Kiislamu. I l i k u wa n i K a t i b a iliyoweka mazingira ya kuishi kwa amani baina ya Waislamu wa kabila mbalimbali h a l i k a d h a l i k a mazingira ya kuishi kwa amani baina ya Waislamu na Mayahudi. Haikuwa Katiba ya kuwatangazia ukafiri na azimio la kuchinjwa makafiri, muda wa kuwa hawajawashikia silaha waumini.

    I l i k u w a K a t i b a i l iyotambua uwepo wa makundi yote na kuweka utaratibu wa namna yatakavyoishi kwa amani, pamoja na tofauti zao za kiimani (lakum diinu waliyadiin na i le kanuni kuwa hakuna kulazimishana katika dini).

    Hii ndiyo hoja ya msingi t u n a v y o z u n g u m z i a tunapojibu madai ya wanaosema kuwa kuwa na Katiba ni ukafiri.

    Kwa bahati mbaya kabisa, wengi wa watu wetu ile tu kutambua hoja inayozungumziwa, i m e k u w a m t i h a n i kidogo. Yupo msomaji wetu mmoja, kama ni kutajirisha kampuni za simu za mkononi, inawezekana anaongoza kwa wiki hii. Katutumia ujumbe wa kutosha, z inapishana mese j i kila baada ya sekunde akijitahidi kuonyesha ukafiri wa Katiba na

    Tunahitaji wasomi wenye kuutambua ulimwengu wa leo

    Demokrasia . Lakini u k a f i r i w e n y e w e anaonyesha madhaifu yaliyomo katika Katiba ya Tanzania. Kama kwa mfano Katiba ya Tanzania itasema kuwa inatambua ushoga kuwa ni haki ya mtu, huwezi kusema kuwa, Katiba yenyewe n i h a r a m u , h a i f a i kuwa nayo. Huko ni kuchanganya mambo.

    Tu n a c h o s e m a n i kuwa kama ambavyo Mtume (s.a.w) alitambua umuhimu wa kuwa na kanuni za msingi kuongoza jamii, Quran i k i w a p a l e k a m a Mwongozo, ndivyo ambavyo jamii yoyote duniani, lazima iwe na Sheria Mama ya kuongoza nchi.

    Sasa kama Waislamu wameshindwa kuwa makini , wamekuwa w a z e m b e , w a o g a na dhaifu, kiasi cha kuruhusu mambo yaliyo kinyume na Uislamu kuingizwa katika Katiba ya Tanzania, haifanyi kuwa dhana ya kuwa na Katiba ni jambo h a r a m u . Wa i s l a m u n d i o w a n a t a k i w a wajiulize, walikuwa wapi Katiba ikaingiza mambo yaliyo kinyume na Dini yao. Mbona Wakristo walichachamaa wakazuiya suala la Mahakama ya Kadhi kuingizwa katika Katiba. Mbona walichachamaa na kuzuiya OIC! Sasa k a m a n i h a r a m u , basi haramu itakuwa u d h a i f u w e t u Waislamu.

    Jambo la pili ambalo tungependa kulikariri mara kwa mara ni kuwa ulimwengu wa sasa hivi ni wa utandawazi. Ukafiri umekuwa ni wa kidunia kama ambavyo Uislamu unatakiwa uwe

    ni wa kidunia. Wakati makafiri wamejizatiti na kuwa wamoja katika ukafiri wao, Waislamu wametupwa mbali sana katika hilo. Na kwa bahati mbaya, l inapoibuka jambo la Wais lamu ambalo linatakiwa kuwa na msimamo wa pamoja, hata zinazoitwa nchi za Waislamu huwa katika kundi la makafiri na kujumuishwa katika, kwa mfamo kuipiga nchi ya Kiislamu.

    Kat ika ha l i h iyo , h u w e z i l e o w e w e ukadhani utapambana katika jiji chako, mji wako au nchi yako usimamishe Dola ya Kijiji cha Kiislamu, Dola ya Mji wa Kiislamu au Dola ya Nchi ya Kiislamu halafu ulimwengu wa kikafiri ukutizame tu.

    Sasa unapozungumzia Jihad ya kusimamisha Uis lamu, ni laz ima uyazingatie yote hayo. Je, umewekeza kiasi gani katika kuandaa umma wa kupigania na kuihami hiyo Dola ya Kiislamu?

    Tunavyoona sisi, kuna mambo mengi ya msingi ambayo kama umma wa Kiislamu tunatakiwa kuyafanya, lakini hatupo tayari. Tunajidanganya kuwa umma upo tayari na Mujahidina wapo tayar i , tuk i tangaza tu, Dola itasimama. Tu n a t a k a k u v u n a tusichopanda.

    L a k i n i b a y a zaidi , pengine kwa makafiri kujua kuwa kuna ujinga mwingi miongoni mwetu, sasa wanatutumia katika yao, huku sisi tukijiaminisha

    (tukijidanganya) kuwa tunapigania Dini.

    Hili nalo limekuwa msiba mkubwa kwa Waislamu kwa sababu ndio kafiri analitumia hivi sasa kuwatangazia Waislamu ugaidi na kuwa sababu ya kuwapiga na kuwafitinisha kuuwana wenyewe kwa wenyewe kama inavyotokea Syria hivi sasa.

    Kwa hakika kuna haja kwa wasomi wa Kiislamu kukaa kitako na kutafakari kwa kina hali ya ulimwengu ilivyo hivi sasa na kuweka mipango inayoweza kuleta manufaa kwa Waislamu.

    Vinginevyo tukienda hovyo kama ilivyo hivi sasa, tutabaki kupiga porojo za kuwatangazia wengine ukafiri , na haitatusaidia kitu.

    Inaendelea Uk. 3

  • 3 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 8-14, 2015Habari

    Wanaokwenda hija wachache Ni ikilinganishwa na kiwango kinachotolewa na Saudia

    Na Bakari Mwakangwale

    IMEELEZWA kuwa, Tanzania imekuwa na idadi ndogo ya Mahujaji wanaojisajili kwenda kufanya Ibada ya Hijja nchini Saudia Arabia, i k i l i n g a n i s h wa n a idadi waliyopangiwa ya Mahujaji 25,000 mwaka 2014.

    Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Taasisi z a H i j j a Ta n z a n i a (TAHAFE) Dk. Ahmed Twaha, akiongea na An nuur mapema wiki hii na kuzungumzia yaliyojiri katika kikao chao na Wizara ya Hijja nchini Saudia Arabia, Februari 8-21, 2015.

    Dk. Twaha, alisema lengo la mkutano huo lilikuwa ni kutathmini kwa pamoja mafanikio n a c h a n g a m o t o z a utekelezaji wa ibada ya Hijja kwa mwaka 2014 (1435 Hijiria), sambamba na kupata utaratibu wa maandalizi ya Hij ja ya Mwaka 2015 (1436 Hijiria).

    Changamoto kwa upande wa Tanzania ni kwamba tumekuwa na idadi ndogo ya Mahujaji wanaojisajili ikilinganishwa na idadi tuliyopangiwa (HISA), ambayo ni takriban Mahujaji 25,000. Kwa h i v i s a sa Ta n z a n i a hatujafikia zaidi ya asilimia ishirini (20%) ya HISA tulizopangiwa. Hata hivyo mwaka huu tumepewa idadi ya HISA 3,000 kwa Tanzania nzima. Alisema Dk. Twaha.

    Aidha alisema, katika Hijja ya mwaka huu 2015 (1436 Hijiria), jambo la kuzingatia kwa Mahujaji watarajiwa ni kuhakikisha wanaanza kujiandikisha mapema i w e z e k a n a v y o k a t i k a t a a s i s i z a o wanazoz ipenda , i l i wasishindwe kufanya ibada kwa sababu ya kuchelewa kujiandikisha.

    Natoa wi to kwa M a h u j j a j i w o t e watarajiwa, tujisalili

    mapema katika Taasisi zetu kwa kila mmoja ile anayoipenda kabla ya Mfungo wa mwezi wa Shaaban 20, sawa na Tarehe 10, 2015, ili kufanikisha hijja kama i l i v y o k u s u d i w a . Alishauri Dk. Twaha.

    A l i w a t a n a b a s h a Mahujaji hao watarajiwa kuwa wanatilia mkazo k u w a u t a r a t i b u n a m p a n g o w a kujiandikisha kupitia kimtandao ni endelevu kwa kila mwaka, kwani nchi za Asia na za Magharibi, wanaendelea na utaratibu huo kwa siku nyingi.

    Akitoa mwongozo kwa Taasisi mbalimbali zenye jukumu la kusafirisha Mahujaji humu nchini, alisema kila Taasisi ni lazima Mahujaji wake wasajiliwe na kuingiza t a a r i f a z a H u j a j i kulingana na Hati zao za Kusafiria kupitia Mtandao, kabla ya Juni 10, 2015 ( Shaaban 20, 1436).

    Alisema, hatua hiyo inalengo la kuwawezesha Mahujaji kupata huduma stahili ikiwemo VIZA, na kwamba mal ipo

    ya h u d u m a s t a h i l i yanapaswa kupitia Benki zilizoanishwa na Wizara ya HIJJA, Saudia Arabia.

    Taasisi zote zinatakiwa k u f u n g a m i k a t a b a rasmi ya huduma zote za Makazi, Chakula

    n a U s a f i r i k u p i t i a mtandao kwa Mawakala, Mashirika na Makampuni yaliyosajiliwa na Wizara ya Hijja nchini Saudia Arabia. Alisema.

    Dr. Twaha, alisema Taasisi i takayoweza kutekeleza hayo na kuthibitishwa ndiyo i t a k a y o r u h u s i w a k u p e l e k a M a h u j a j i k w a m w a k a h u u , 2015, ambapo alisema kwamba safari za Hijja zinatarajiwa kuanza rasmi, Agosti 16,2015.

    A l i s e m a , Ta a s i s i hizo pia zinatakiwa kuwapima afya Mahujaji wataraj iwa mapema mwanzoni mwa mwezi Agost, 2015 au kabla ya hapo sambamba na kujaza fomu maalum z i t a k a z o t o l e wa n a BIITHA kisha kuingizwa kwenye mtandao.

    Alisema, ni jukumu la Taasisi kuhamasishaji na kuelimisha Waislamu n c h i n i k u f a h a m u umuhimu wa Ibada ya Hijja na Umra ikiwa ni moja ya nguzo 5 za Kiislamu.

    "Allah amewaridhia, nao wamemridhia.."Inatoka Uk. 2dunia na raha zake. Wao zaidi waliangalia malipo ya Akhirah. Waislamu kama hawa ukiwaambia kuhusu dunia na raha zake, wanahisi hukumu za Kiislamu, mahitaj i yake, Sunna ya Mtume na mwenendo wa masahaba, vyote vimekuwa vigeni! Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu w a l i p o k u w a k a t i k a mazingira ya kuchagua kati ya Dini na dunia, basi wakati wote walichagua D i n i y a M w e n y e z i Mungu. Mujahidina hawa walichukulia suala la kueneza na kusimamisha Uislamu kama lengo la maisha yao hapa duniani. Insha-Allah, Waislamu waliochagua kuishi kama wageni katika hii ardhi n a wa k a z i p a k i s o g o raha za dunia, ikiwa ni pamoja na kufanya juhudi za kusimamisha Dini ya Allah, Mwenyezi Mungu atawalipa. Lakini malipo haya yana vigezo vyake

    ambavyo visipopatikana, b a s i m a l i p o h a ya p o . I n a h i t a j i k a k u j i t o a , umakini, Ikhlasi na 'focus' k a m a w a l i v y o k u w a Masahaba wa Mtume.

    Tabia na mwenendo wa Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, lazima vizingatiwe kikamilifu kwa kuwa hili ni kundi la watu ambao Mwenyezi Mungu mwenyewe amelithibitisha ndani ya Qur'an kutokana na Imani yao, Ikhlasi, Subira na Uvumilivu. Mwenyezi Mungu anasema:

    "Na wale waliotangulia wa k a wa wa k wa n z a k a t i k a ( U i s l a m u ) - Muhajiri na Ansari, na wale waliowafuata kwa mwendo mzuri - Mwenyezi Mungu atawapa radhi nao wamridhie (kwa hayo mazuri atakayowapa) na amewaandalia Mabustani yapitayo mito mbele yake, wakakae humo milele. H u k u n d i k o k u f u z u kukubwa" Qur(9:100)

    Ni muhimu sana kwetu k u s o m a k wa m a k i n i maisha ya Masahaba ambao pamoja na Mtume waliweza kusimamisha

    Dini ya Mwenyezi Mungu, i l i n a s i t u k a m i l i s h e j u k u m u h i l o k u p i t i a mfano na mwenendo wao. Mara zote Masahaba waliuelekea Uislamu na wala hawakujiweka nyuma kwa sababu ya kuogopa changamoto na mitihani kutoka kwa maadui.

    Jambo la msingi kwa wanaharakat i wa leo k u t a m b u a n i u k we l i kwamba mazingira ya sasa ni tofauti sana. Kwa mtu muaminifu na muadilifu, kujipatia kipato kwa njia za halali inazidi kuwa jambo gumu. Mifumo iliyowekwa imefungua milango kwa tarat ibu ambazo mtu unalazimishwa kujipatia riziki kwa njia za haramu! Watawala wa nchi zetu wanatekeleza sera za Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, ili kufanya maisha ya wananchi yawe magumu zaidi. Lakini hata hivyo, mipango yao isiwafanye wanaharakati wapoteze msimamo wao. Shetani asibadili vipaumbele vyao vya Kiislamu na kuwafanya waisujudie dunia.

    MSIKITI wa Mtume (s.a.w.) Masjid Nabawwi, Madina Saudi Arabia.

  • 4 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 8-14, 2015Makala

    M A N E N O y a n g u ni kama mwango. Mwango ni sauti ya pili baada ya sauti ya kwanza ambayo ni halisi kutoka na kusikika, sasa ukisikia sauti ya kwanza imeshatoka lakini kuna sauti ya pili ambayo inafanya kurudia ile sauti ya kwanza, basi huo ndio m w a n g o . M a n e n o ya n g u n i m wa n g o kwani narudia tu yale ambayo yameshasemwa na yanasemwa, na wanasiasa, viongozi wa kidini, wananchi wa kawaida na kila mtu anayejua ubaya wa muungano huu. Tuendelee!

    Wacha moshi ufuke, harufi itande, ongeza na ubani, kisha waalike w a z e e w a p a n d e z o t e z a Z a n z i b a r , tunataka tusome dua i l i maadhimisho ya Muungano wa aina hii yawe ndio mwaka wake wa mwisho huu.

    Tukiwa tunaikumbuka siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, pia tunaikumbuka kuwa ni siku ambayo Zanzibar i l i t iwa k i tanz i cha roho na ndio ulikuwa mwanzo wa kutojiweza, hadi leo kamba za kukosa uhuru kamili zimekaza bara`bara.

    S a s a u p o u g u m u wa kujinasua, kwani wanaotaka mamlaka kamili inaonekana ni kana kwamba ghafla wamekuwa wahaini!

    Sasa kuna kila hali ya kutetea mfumo wa M u u n g a n o u l i o p o , hata wakati mwengine wanatumia njia haramu kuhakikisha muungano unaendelea kubaki kama

    Ni nchi ya Wazanzibarisio ya wana-CCM, CUF

    Na Rashid Abdallah

    ulivyo. Na malengo yao hasa ni kuelekea serekali moja. Huko ni kuelekea kubanwa zaidi.

    C C M b a d o w a o wanataka serekali mbili kuelekea moja, maana yake tunatoka kwenye umasikini tunaingia hatua nyengine ya kuwa mafukara. Ikiwa hapa tulipo hali ni mbaya kwenye serekali mbili, vipi tukielekea serekali moja, hali si itazidi kuwa mbaya?

    Ulevi wa madaraka si mwema, inaumiza kiongozi au viongozi w a n a p o l e w a h a t a w a k a d h a n i k u w a kuna mtu aliwauzia nchi wanayoiyongoza na wala s i mali ya wananchi waliowaweka madarakani.

    Baada ya kuamini h i v y o w a n a a n z a kuamua kana kwamba wako peke yao, na maamuzi yao ndio ya mwisho na wala hakuna anayepaswa kule ta fikra mpya. Viongozi wa k i f i k i a k u a m i n i hivyo, huo unakuwa ni wakati mgumu sana kwa waongozwaji.

    B a a d h i y a n c h i zinaonekana ni kama mali za urithi, viongozi walirithishwa kutoka kwa wakoloni, hawana hata nia ya kuondoka sio kwa nguvu lakini hata kwa kutumia katiba

    RAIS wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein.

    MAKAMU wa kwanza wa Rais Zanzibar, Seif Sharif Hamad.

    ambayo walishir iki wenyiwao kuiweka, hilo halipo hapa petu lakini lipo Afrika, lililopo kwetu n i v iongoz i kupuuza matakwa ya wananchi na kuhesabu sera ya chama chao kuwa ndio muhimu zaidi.

    S e r a z a C h a m a zinapokwenda kinyume na matakwa ya msigi ya wananchi, unadhani kwel i chama h ich i kitakuwa kipo kwa sababu ya wanachi? Unajua kuwa mfumo huo hauna faida lakini bado tu umo umo kwa kuwa unapata tonge.

    Matatizo ya Zanzibar mengi yanajulikana, na matatizo ya Zanzibar anayeyajua hasa ni wananchi wa nchi hiyo. Wao ndio wanajua kwa siku wanapata pato gani, mlo wao unakuwaje, lipi ni tatizo la kudumu kat ika maisha yao, k i u f u p i wa o n d i o wanapitia hali hizo zote.

    Iwapo utawakatalia lile ambalo wao wanahisi dio l i ta leta unafuu katika maisha yao huko kutakuwa ni kuwaonea. Na wala haitokuwa ndio munawapenda na kuwatendea haki. Sera za nyumbani kwako zitofautiane na za kazini, pia sera za Chama chako zisikinzane na matakwa ya watu wote.

    Muungano huu wa

    sasa umepigiwa kelele nyingi mno, wasomi na wasiokuwa wasomi pia, hata hali ya kimaisha tu inamuonesha mtu kuwa kuna mapungufu katika jambo fulani.

    Sera za CCM Zanzibar zinakinzana kwa kiasi kikubwa na matakwa ya msingi ya watu wa nchi hiyo. Na ndio tatizo linalowakabili Wazanzibari wanaotaka m a m l a k a k a m i l i , k wa C C M h a k u n a m a b a d i l i k o a m b a o wao wanayataka. Hata ukiwaeleza kwamba tuwe huru zaidi ya hapa tulipo kwao wao haliingii akilini.

    CCM kama chama tawala bado hawajataka Zanzibar kuwa huru, wao ndio wameshika m p i n i m u k i z i n g u a wanawaweka ndani, au vigongo vya kutosha kutoka kwa vyombo vyao vya dola.

    Huenda kunahitajika w a t a a l a m u w a saikolojia, ili waende kutoa matibabu kwa wahafidhina kuwa zama za kutawaliwa zimepita. Pengine kutawaliwa na Muingereza na Mreno kumeleta athari hata za kisaikoloj ia kwa baadhi ya watu ndani ya Zanzibar.

    M t u h a w e z i tena kuishi bi la ya kutawaliwa, ni kama

    mvuta sigara asiyeweza kuacha tena. Ikifikia hatua mvuta sigara hawezi kuiacha, basi tunaweza kuwatafuta wataalam wakatusaidia. Nadhani pia tupate wataalam wa kueleza athari za kutawaliwa, wapo watu wamelala, akili zao zimeathirika na ukoloni wa Muigereza.

    M u a n d i s h i w a mashairi na hadithi, Michael Bassey Johnson anasema usizungumze uwongo ili upendwe, ni bora kusema ukweli na ukachukiwa

    Hata wale ambao wanazungumza ukweli kuhusu kanuni mbovu za chama cha CCM wanaishia kufukuzwa, lakini ni ubora kama alivyosema Michael kuwa bora tu useme ukweli, na ndio jambo la msingi, usijali na wala usiumie kipi kitatokea kwa kusema ukweli la msingi ni kuuweka wazi.

    Faida zi l izopo za Muungano kwa Zanzibar ni kama kuuza nazi za elfu kumi, ukakosa hata mtaji. Hasara ni nyingi kuliko faida, lakini kwa wale ambao unawapa faida, hasara zake kwa wananchi wa kawaida wanajifanya hawazioni.

    Naamini uchaguzi mkuu huenda ukawa n d i o s u l u h i s h o l a Muungano kwa upande wa Zanzibar, naamini huu ndio u takuwa mwaka wa mwisho kusherehekea aina hii ya Muungano.

    Upepo wa mabadiliko unavuma kila kona ya visiwa vya Zanzibar, na kengele pia zimeshalia. Ni nchi ya watu wa Zanzibar na wala si nchi ya chama chochote kile. Nafsi zinazoamini kuwa utumwa ndio uhuru basi waamke na waungane na wenzi wao kudai mamlaka huru ya Zanzibar.

    Sogeza kietezo cha udongo, weka na makaa ya moto ya kutosha, m w a g a n a u b a n i tunyanyue mikono juu, wacha moshi utande na hewa unukie. Insh-allah wa Jangombe, M i c h e w e n i , We t e , Kizimkazi na maeneo mengine tumuombe A l l a h a z i f a n y e kumbukumbu hizi za Muungano wa aina hii ziwe ndio za mwisho, tena kwa amani kabisa.

    MAKAMU wa pili wa Rais Zanzibar, Balozi Idd Seif.

  • 5 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 8-14, 2015Habari za Kimataifa

    WANAMGAMBO wa Chama cha Hizbullah n c h i n i L e b a n o n w a m e f a n i k i w a k u d h i b i t i e n e o l a a l - Q a l a m u n i linalotenganisha nchi ya Syria na Lebanon, kutoka kwa wanachama wa kundi la Kiwahabi.

    Taarifa iliyotolewa na Hizbullah imesema w a n a h a r a k a t i h a o wamedhibiti eneo hilo bila mapigano yoyote kutoka upande wa pili uliokuwa katika eneo hilo.

    K w a m u j i b u w a Shirika la habari la Reuters , imeelezwa kwamba wiki iliyopita j e s h i l a L e b a n o n l i l i tangaza kuhusu mpango wa kuanzisha operesheni ka l i ya jeshi kwa kushirikiana na wanamgambo wa Hizbullah, dhidi ya magaidi waliopo katika maeneo ya mpakani kati Syria na Lebanon.

    Taar i fa z inae leza kuwa kufuatia kuenea taarifa za mpango huo, hatimaye magaidi hao walipata wasiwasi na kuondoka eneo hilo la al-Qalamuni na kukimbilia maeneo mengine usiku wa kuamia Jumamosi

    Hizbullah wahakikisha usalama wa LebanonWadhibiti eneo la al-Qalamuni

    WANAMGAMBO wa Chama cha Hizbullah ambao wamekuwa ni ngome ya Lebanon.

    W A K A T I mashambulizi ya ndege za kivi ta za Saudi Arabia n a w a s h i r i k a w a k e i k i w e m o Marekani na Israel yakiendelea nchini Yemen, vyombo vya habari vimefichua kuwa Washington ilificha siri kwa miaka mingi juu ya kuwepo kisima kikubwa zaidi cha m a f u t a d u n i a n i nchini Yemen.

    Televisheni ya Sky News imethibitisha t a a r i f a h i y o n a kuongeza kuwa, serikali ya Marekani i l i s h i r i k i a n a n a serikali zilizopita nchini Yemen katika

    Siri kubwa ya vita Yemen yafichuka

    Mabeberu wamezea mate kisima cha mafuta Ni kikubwa zaidi duniani. Hakuna mfano wakeKiligunduliwa siku nyingi ikawa siri ya Marekani Rais kibaraka akaambiwa asiseme kwa wananchi

    kuficha siri hiyo. K w a m u j i b u

    wa habar i h iyo , Washington iliitaka s e r i k a l i y a A l i Abdullah Saleh na ile ya Abd Rabbuh M a n s u r H a d i , kutotangaza kwa wananchi taarifa ya

    kuwepo hazina hiyo kubwa ya mafuta duniani.

    Inaelezwa kuwa kisima hicho cha mafuta kinaanzia Saudia na baadhi ya sehemu za Iraq huku sehemu kubwa zaidi ikiweko nchini

    Yemen na kwamba, Washington ilifanya n j a m a k u b w a kuhakikisha kuwa wananchi wa Yemen hawapati taari fa hiyo.

    Imeelezwa kuwa kufuatia kubainika kwa siri hiyo, Weledi

    wa mambo mbali na kukosoa hatua hiyo, imeleta shaka kubwa kwamba hata mashambulizi y a S a u d i a n a Marekani dhidi ya taifa hilo ni njama za kujaribu kuwazuia Wayemen kufaidika na utajiri huo wa mafuta.

    Hii ni katika hali a m b a y o n d e g e za utawala wa al Saud, zikiendeleza mauaji ya umati nchini Yemen huku raia wasio na hatia wakiathirika zaidi na mashambuklizi hayo katika maeneo tofauti ya nchi hiyo.

    wiki iliyopita. H a b a r i z i n a e l e z a

    k u w a , v i k o s i v y a Hizbullah vimechukua udhibiti wa eneo hilo baada ya waasi hao kutoroka usiku wa

    kuamkia Jumamosi wili iliyopita.

    Chama cha Hizbullah kimesisitiza azma yake ya kudhibiti maeneo yote muhimu ya nchi kutoka kwa makundi

    ya Jabhatu Nusra na Daesh.

    K w a u p a n d e mwingine, jeshi la Syria nalo limepeleka askari wengi katika maeneo muhimu ya miinuko

    ya mji wa al-Zabadan, karibu na mpaka wa Lebanon kwa lengo la kuwaangamiza wale i l iyowaita kuwa ni magaidi katika maeneo hayo.

  • 6 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 8-14, 2015Makala

    TA N Z A N I A n i nchi iliyojaaliwa kuwa na utaj i r i mkubwa wa maliasilia n a h a l i ya h e wa ya wastani yenye kupendeza, mvua zinazonyesha na kustawisha miti, mito na maziwa ya maji safi, ardhi pana za kulimia zenye rutuba, misitu mikubwa, mbuga zenye wanyama mwitu wengi na bahari yenye samaki wa kila aina. Katika maliasilia kuna migodi ya maadini kutoka dhahabu hadi almasi na tanzanite . Hali kadhalika ni nchi inayosifika duniani kwa usalama na kwa Serikali inayojinata ulimwenguni kuwa haina dini na kuwa inazihishimu dini zote bila ya mapendeleo.

    Lakini, kwa sababu ya nguvu na saut i kubwa walizonazo Wakristo wenye msimamo mkali wa udini, tunashuhudia kuwa Serikali imelazimishwa kuwa na mapendeleo makubwa kwa watu hawa na msimamo wao mkali dhidi ya Uislamu na Waislamu. Hii ni khatari k u b w a i n a y o i s u k u m a Tanzania mahala pabaya sana.

    K a t i k a k i t a b u h i k i tutaonesha waziwazi kadiri gani Serikali ya Tanzania imeachilia siasa za huo msimamo mkali wa udini dhidi ya wananchi wa Ki i s lamu kutapakazwa mpaka katika shule bila ya kizuwizi chochote. Tokea Wa i s l a m u wa l i p o k u wa wananungunika pembeni mpaka imefika hadi ya kulalamika hadharani.

    Kama hawa wachache wenye nguvu za dola wenye msimamo mkali wa udini wataachiliwa waendelee kutapakaza sumu za siasa zao dhidi ya Waislamu, na Serikali itaendelea na mwendo wa mbuni wa kuyafumbia macho

    Tanzania na Propaganda za Udinimambo haya ambayo ni ya khatari iliyoikabili nchi, basi tusistaajabu tukija kushtukia vita vya maneno kugeuka ghafla na kuwa hali mbaya baina ya wananchi wa dini hizi mbili kubwa kama ilivyokwisha kutokea na vinavyoendelea kutokea katika nchi mbalimbali u l i m w e n g u n i . M a m b o y a d h u l m a h a y a w e z i kuendelea, lazima patatokea mripuko iwapo hapatatokea wenye busara na uadilifu watakaoyaondosha haya kwa upesi sana; na kama haya niliyoyaelezea kwa mukhtasari juu ya hali ya udini iliyotanda Tanzania na khatari zake hayakutwangi akilini mwako, basi endelea kusoma asaa ukaelewa.

    Kwa muda mrefu sana nimekuwa nasikiliza na k u s o m a m a d u k u d u k u ya Wais lamu Tanzania na mijadala baina yao na Wakristo, na kutokana na haya nikawa ninajadiliana baina yangu mimi na nafsi yangu nini cha kufanya. Mimi nilikuwa najiambia kuwa hii khatari unayoiona i l i y o i k a b i l i Ta n z a n i a isikushughulishe kwani huna uwezo wa kubadilisha chochote, maana Watanzania wameshaingia katika vita vya maneno na hawana budi mwishowe watoane roho. Kwa upande mwingine, nafsi yangu inaniambia kuwa ni dhambi kubwa kumwona mtu anaelekea kutumbukia shimoni na ukanyamaza kimya usimtahadharishe n a k h a t a r i n a m a a f a yaliyomkabili , na kama utasikilizwa au utapuuzwa hayo si yako wewe tena maana umeshatimiza wajibu wako wa kutahadharisha. Wala kuwa katika watakaokusoma wa k o wa t a k a o k u p i g i a makofi na kutaka upewe tunza kubwa na pia kuna watakaokushambulia vikali sana na kutaka utokomee, haya pia si yako tena na yasikushughulishe. Iwapo Yesu aliyekuja na ujumbe wa salama na amani walimtenda waliyomtenda, wewe ni nani mbele yake? Basi timiza wajibu wako.

    K a t i k a k i t a b u h i k i tutaonesha wazi kabisa mifano ya propaganda za siasa kali za udini zenye mwelekeo wa Vi t a v ya M s a l a b a zilipoanzia na kupaliliwa, lakini hatutayajadili sana maandishi ya kipropaganda y a l i o m o v i t a b u n i n a kwingineko, kwani haya yatahitajia kuandikwa kitabu kingine. Tutazungumzia zaidi kukhusu picha ambazo nyingi si za kamera bali ni za ubunifu wa kuchora. Picha ambazo zimo katika vitabu vya shule za Tanzania zinazotumiwa kusomeshea

    v i j a n a h i s t o r i a y e n y e ukweli f inyu na mengi yasiyokuwa ya kweli kwa lengo la kupalilia fitina dhidi ya Waislamu na dini yao. Wavyele wetu hawakukosea wa l i p o t u a c h i a m s e m o usemao, kuona si kusikia kwani picha aghlabu huacha athari kubwa zaidi katika bongo za watazamaji kuliko maelezo ya jambo hilohilo, khasa picha hizo zikionesha waziwazi ukhabithi hata ukiwa unatokana na ubunifu w a k i p r o p a g a n d a w a mchoraji na hauna msingi katika matokeo ya kweli. Na hivi ndivyo propaganda zinavyofanya kazi kubwa khasa kat ika bongo za vi jana wadogo shuleni. Halikadhalika, hawakukosea wavyele wetu waliponena, udongo upatilize uli maji.

    Mimi binafsi nashindwa k u e l e wa v i p i S e r i k a l i ya Ta n z a n i a , a m b a y o ina j inata u l imwenguni kuwa haipendele i d ini yoyote bali inazihishimu dini zote sawasawa bila ya mapendeleo, ikafika hadi ya kuwaachilia wachache wenye msimamo mkali wa udini kutapakaza sumu zao kali za kipropaganda mpaka shuleni! Hii ndiyo sababu moja ya kukiandika kitabu hiki. Natumai baada ya wahishimiwa wakhusika k u n i s o m a k wa m a k i n i niliyoyaandika watachukua khatua za busara, haki na uadilifu na kuyaondosha yote yale yasiyokuwa na ukweli pamoja na yale yaliyokuwa na ukweli finyu na uwongo mwingi na pia yenye fitina za kipropaganda zilizotopea dhulma na khatari. Tuombe k u w a w a k h u s i k a h a o hawatakuwa katika washiriki a m b a o wa n a i p e n d e l e a Tanzania izidi kutekwa na wenye siasa kali za udini zinazoitokomeza Tanzania kubaya.

    Ninaelewa fika kuwa wenye siasa kali za udini hawatakubali kwa urakhisi kuuwacha mwendo wao muovu na tusistaa jabu w a k i f i k a h a d i y a kunishambulia mimi binafsi. Mkiyaona haya yanatokea, basi juweni kuwa hiyo ni alama kubwa ya kuwa watu hao ni muflis wa hoja na kweli hawaitakii amani Tanzania, kwani ni wapungufu wa akili na hawana mapenzi ya kweli na Tanzania.

    Tanzania haikukumbwa na siasa kali za udini tu peke yake, bali imekabiliwa pia na siasa chafu za ugozi, yaani kumbagua mtu kwa sababu ya asili yake. Tutaelezea na kuyanakili maneno yao wenyewe magogo wa siasa wa Tanganyika ambao hutapakaza chuki za ugozi zinazopalilia fitina baina

    ya Wazanzibari ili wapate k u e n d e l e a k u i t a w a l a Zanzibar vizuri ili, hatimaye, waimeze kabisakabisa na kuigeuza Zanzibar mkoa wa Tanganyika; na kwa mujibu wa kauli zao wenyewe, sababu yao kubwa ni kuwa Zanzibar ina Waislamu wengi sana; na ni huo Uislamu wao Wazanzibari ndilo jambo kubwa l inaowachukiza wenye siasa kali za udini. Kwa hivyo tutaigusia mada hii na kuonesha kadiri ya athari zake zilivyokuwa mbaya kwa watu wa Zanzibar na nchi yao.

    Kwa dasturi yangu huwa sipendi kuzungumza juu ya ukabila ila pale ninapoona kuwa haki za watu fulani zinadhulumiwa kwa siasa chafu za ubaguzi. Tutaonesha humu vipi uonevu huu na dhulma za siasa za kigozi z i l i v y o t u m i wa v i b a ya Z a n z i b a r h a t a i k a f i k a kuuwawa bure watu wengi sana wasiokuwa na hatia yoyote kwa sababu ya kutokana na asili fulani; pia watu wengi wameuwawa k wa s a b a b u wa l i k u wa wanachama wa vyama vya Zanzibar Nationalist Party (ZNP) na Zanzibar and Pemba Peoples Party (ZPPP) . Hiv i kar ibuni tumeshuhudia maradhi haya yalivyomwagwa hata katika Bunge Maalumu la Katiba. Yale ya wananchi kubaguliwa, ambayo ni wajibu yakemewe vikali sana, yamekuwa yanapaliliwa na kupigiwa makofi na wanasiasa waovu.

    P e n g i n e k u n a watakaopendelea kuujua msimamo wangu wa imani umeelekea wapi? Mimi n i M w i s l a m u m we n ye kuamini Mungu Mmoja na tokea utotoni mwangu, waalimu wangu vyuoni na skuli na wazee nyumbani w a m e n i f u n z a k u w a Wakris to na Mayahudi wameteremshiwa Vitabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu huyo huyo Mmoja, na wameteremshiwa Mitume wa kuwafundisha watu maagizo yake; hivyo basi, wote wanaofuata maagizo ya Mwenyezi Mungu sawasawa ni ndugu wa kiimani, na huu ni udugu mkubwa zaidi kuliko wa kidamu au hata wa kudai wanafuata dini moja huku hawafuati amri na maagizo yake Mola Mkwasi. Kuna watu wema wanaofuata dini zao sawasawa na pia kuna watu waovu ambao hudhania kuwa wanafuata amri zake Mola wetu, lakini kwa kweli ni wafuasi wa mafunzo ya Sheitani. Watu wema ni watu wema wawe wa dini yoyote na watu waovu ni waovu wawe wa dini yoyote ile. Kama watu

    wema wenye kupendelea v iumbe wenzao mema hawashikamani, basi waovu wenye kumfuata Shetani watashinda na watatawala.

    Pili, nimekulia na kuishi zaidi Shangani, Unguja a m b a k o t u l i k u w a n a majirani wengi wa Kigoa ambao walikuwa Wakristo na pia Wahindu na Maparisi na Wasiloni (Wasrilanka) na wengineo wenye dini mbal imbal i . Tukicheza pamoja na kuingia nyumbani mwetu na nyumbani mwao bila ya ubaguzi. Wengine mpaka leo tunaandikiana kidugu kabisa. Pia nilikuwa na marafiki wa kila kabila Ngambo ambao tukisoma pamoja na tukitembeleana sana. Pia nimeishi na kusoma skuli Wete Pemba na shambani Donge Unguja. Nimeishi na kusoma Uganda pia na nimefanya kazi Kenya na Marekani na kujuana na watu wengi na kuishi nao kirafiki. Lakini lililonisaidia sana ni msingi nilioupata utotoni kwa wazee na vyuoni kwa waalimu unaopendelea haki sawasawa kwa binadamu wote na kukataza maovu na ubaguzi na dhulma.

    Kwa hivyo sina chuki na mtu yoyote ambaye ana imani yoyote yenye kufuata maamrisho mema yenye kuwatakia watu wote mema, na sina udugu na wale wenye siasa za ubaguzi na za udini. Naamini hivi sasa Tanzania i p o h a j a k u b wa s a n a , khususan kwa Waislamu na Wakristo wema wenye kufuata maagizo mema ya dini zao, kuungana na kupinga propaganda za udini na za ubaguzi. Bila ya shaka yoyote ile, wanayoyakhubiri na kuyatapakaza wenye siasa kali za udini yanakwenda k i n y u m e n a k i i n i c h a Maamrisho ya Mwenyezi Mungu na mafunzo ya Yesu Kristo na Mtume Muhammad (s.a.w).

    (Huu ni utangulizi wa Kitabu cha Profesa Ibrahim Noor Shariff alichokipa jina Tanzania na Propaganda za Udini. Kinapatikana Ibn Hazm Media Centre Msikiti wa Mtoro na Manyema. Phone: 0773777707, Tanzania Publishing House (TPH) Dar es Salaam, Phone 0222130669, TAMPRO, Magomeni Area along Morogoro Road, Adjascent to Kinondoni Municipal, Plot no. 169 block R, Kinondoni Dar es Salaam. Phone: 0222172182, KEF Kalamu Education Foundation, Magomeni Kinondoni District, Dar es Salaam. Phone: 0776525268 na Masomo Bookshop, b e h i n d t h e C e n t r a l Market, Zanzibar. Phone: 0242232652)

    Profesa Ibrahim Noor Shariff

  • 7 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 8-14, 2015Makala

    Inawajibika kitabu hiki kisomwe na kila Mtanzania hasa wakubwa wa serikali na wanasiasa na mapadri na mashekhe wa dini zote. Makusudio ya kitabu hiki ni kuihifadhi nchi yetu na sumu za chuki za udini zinazopaliliwa kwenye masomo ya vijana wa leo ambao ni viongozi wa kesho. Inatakiwa k i l a w e n y e u w e z o wafanye juhudi kuondoa p r o p a g a n d a s h u l e n i mwetu na washiki l ie kusomeshwa historia ya ukweli.

    Kitabu Tanzania na Propaganda za Udini kina milango mitatu na sahifa 152. Mlango wa Kwanza unahusu Taarikh Ya Kuwasili Kwa Wabantu, Washirazi Na Waarabu P wa n i Ya A f r i k a Ya Mashariki. Hapa anaeleza kwa ushahidi wa taarikh usiokatal ika kwamba Waarabu wamefika Pwani ya Afr ika Mashar ik i maelfu ya miaka iliopita na Wabantu wamefika Pwani hiyo katika Karne ya 16 B.K. Makusudio ya mlango huu ni kuonesha kwamba Waarabu s i wageni, bali ni wenyeji wenye haki hapa sawasasa na wenyeji wengineo.

    M l a n g o w a P i l i u n a z u n g u m z i a Propaganda Za Siasa Za Chuki Na Athari Zake. Humo tunaona uovu wa propaganda za udini zilizowatuhumu Waarabu na Waswahili Waislamu peke yao kukamata , k u u z a n a k u m i l i k i watumwa. Propaganda hizo zimepelekea kuuliwa maelfu ya Waislamu bure bila ya sababu ilipovamiwa Zanzibar, nchi yenye Wais lamu wengi , na kumezwa na Tanganyika 1964.

    Kat ika Mlango wa Ta t u Ta n z a n i a N a Propaganda Za Udini

    Sumu za Chuki za Udini-1Watu wema ni watu wema wawe wa dini yoyote na watu waovu ni waovu; wawe wa dini yoyote ile. Kama watu wema wenye kupendelea viumbe wenzao mema hawashikamani, basi waovu wenye kumfuata Shetani watashinda na watatawala.

    Ibrahim Noor Shariff

    PROFESA Ibrahim N o o r S h a r i f f ametunga kitabu kipya cha Kiswahili kuhusu udini na ugozi Tanzania. Mtungaji kakusudia kutunga ki tabu chake kwa Kiswahili ili ukweli uwafikie wale watu wengi ambao kila siku wanatiwa sumu za udini Tanazania.

    Picha hii iliyochapishwa 1861 inaonesha waziwazi kuwa wakamataji wa Waafrika na kuwatia utumwani ni Wazungu.

    Shuleni mtungaji, ambae ni Profesa wa Sanaa, a n a o n e s h a u b i n g wa wake wa kuchambua picha. Anatunakilia picha za kuchorwa kutokana na vitabu vya shule za Tanzania zinazoonesha Waarabu na Waswahili Waislamu wanawakamata na kuwapiga na kuwauwa wanyonge wa Kiafrika ili kuwafanya watumwa. Hapo hapo Profesa Ibrahim anaonyesha uzushi wa

    picha hizo zilizokopiwa na kubadilishwa kutoka picha za wauzaji watumwa wa Kizungu huko Amerika. Pia ameonesha kwamba b i l a ya s h a k a p i c h a nyingine zimebuniwa na wachoraji na hazina ukweli.

    Profesa Ibrahim Noor anakazia katika kitabu chake hiki kuyapitia na kuyatengeneza masomo ya taarikh (historia) katika shule za Tanzania. Anataka

    masomo haya yajengwe kwenye misingi ya taarikh ya kweli, sio misingi ya uongo wa siasa za udini unaotokana na ukoloni.

    I b r a h i m N o o r a n a h a d h a r i s h a Watanzania wote na hatari ya kuendelea kupanda mbegu za chuki dhidi ya Waarabu, Wahindi na Waswahili na khasa Waislamu katika mipango ya masomo Tanzania. Hizi chuki za udini zitaleta

    b a l a a k u b wa k u l i k o mauwaji ya Zanzibar ya 1964. Na watakaoumia na chuki hizi, ni wafuasi wa kila dini na kila kabila nchini Tanzania.

    Kitabu hiki kinahitajia kimfikie kila mwenye uwezo wa kubadilisha mambo Tanzania, kwa mfano: Wahishimiwa m e m b a w a B u n g e Tanzania, memba wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mawaziri wa serikali ya Muungano na wa Zanzibar, wakubwa wa makanisa na wakubwa wa vyama vya Kiislamu, wak ub wa wa vyama vya siasa, wakubwa wa magazeti nchini Tanzania, wakubwa wa TV na radio zote, na kabla ya wote hao waliotangulia ni mimi na wewe, wananchi ambao tunapiga kura kuwachagua viongozi wema.

    Tanzania na Propaganda za Udini ShuleniK a t i k a s e h e m u

    h i i t u t a o n e s h a n a kuzungumzia baadhi ya picha za propaganda k u k h u s u u t u m w a zilizochorwa khasa katika v i tabu vya shule za Tanzania na athari zake. Kwa muda mrefu sana mabingwa wa saikologia wameelewa kuwa picha za michoro na za kamera zinaweza kuwa na taathira kubwa katika kuufikisha ujumbe uliokusudiwa kwani picha haikwepeki jichoni. Picha inahifadhika haraka katika akili na ni kigezo kikubwa cha kuamsha hisia.

    Baada ya kufahamu nguvu ya picha katika kufikisha ujumbe, vikundi au watu mbal imbal i wamekuwa wakizitumia picha kwa malengo na makusudio tafauti kwa maslaha yao. Lakini, lililo muhimu ni kuwa sio kila picha inaelezea ukweli wa matokeo. Picha nyingine zinakusudia kupotosha ukweli na kubadilisha fikra za walengwa zikubaliane na fikra au propaganda zao. Hali kadhalika picha nyingi aghlabu hutokana na tasnifa zake mwenyewe mpiga j i au mchora j i picha na jinsi anavyotaka kufikisha ujumbe wake.

    Tokea Karne ya Kumi

    Picha hii iliyochorwa 1866 inaonesha kuwa ni Waafrika na Wazungu waliowakamata Waafrika dhaifu na kuwatia utumwani

    Inaendelea Uk. 8

  • 8 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 8-14, 2015Makala

    Sumu za Chuki za Udini-1Inatoka Uk. 7

    BAADA ya miaka 140 wanapropaganda wa Tanzania wenye siasa kali za udini wameona wazibadilishe picha za zamani zinazowalaumu Wazungu na Waafrika kwa ukamataji wa watumwa na badala yake kumpachika Mwarabu kuwa ndiye aliyefanya uovu huo. Ukiangalia vizuri utaona picha ni ileile, lakini wachoraji ndio waliobadilika na kubadilisha muundo wa uchoraji.

    na Tisa lengo la Wazungu wakoloni wenye siasa kali za udini lilikuwa kuwapiga vita Waislamu na kuwaonesha katika maandishi na michoro yao kama kwamba Waislamu ni sawa na masheitani weusi. Angalia tena mfano wa picha tuliyoionesha i l i y o c h o r w a k a t i k a gazeti la Punch, or The L o n d o n C h a r i o v a r i tarehe 30 November 1889, wakati mataifa ya Ulaya walipoamua kuupiga vita Uislamu wakiamini kuwa Uislamu ndio sababu ya kuwazuia wao kutimiza malengo yao ya kikoloni na kidini katika Afrika ya Kati na Mashariki. Katika mazingaombwe yao walitumia kigezo cha utumwa, na ili kuufikisha ujumbe wao kwa jamii na kupata kuungwa mkono, waliuchora Uislamu kwa sura ya shetani mweusi m w e n y e p e m b e n a manyoya kama mnyama ambaye lazima auwawe na Wakristo.

    H a p o h a p o , d o l a za Ulaya za Kikristo zimechorwa kwa sura n z u r i n a m a u m b i l e m a z u r i , w a m e s h i k a panga zao za misalaba tayari kuzishindilia na kuuwa Uislamu. Michoro inayotokana katika ndoto za akili ya mchoraji wao. Sidhani kama panahitajia hapa kuelezea maana ya Mtu Mweusi tena mwenye manyoya kama kima katika karne hizo ambazo Wa z u n g u wa l i z i o n a rangi zao ni bora kuliko za wengineo na naamini mtazamaji mahiri hana haja ya kuele-zewa dharau ya kumwotesha pembe binadamu. Ishara hizo ziko wazi katika akili, batra na ubora waliojiona wanao Wazungu hao pamoja na dini yao.

    H a l i k a d h a l i k a , miongoni mwa waandishi wa vitabu vya historia v i n a v y o - f u n d i s h w a s h u l e n i T a n z a n i a , wamefahamu nguvu na uwezo wa picha katika kuf ikisha u jumbe na kuelewa taathira kubwa iliyonayo picha katika kuba-dilisha fikra, na watungaj i wa vi tabu wameitumia fursa hiyo kuingiza agenda zao za

    siri ambazo zimelenga kuzipandikiza chuki z a o k a t i k a j a m i i . K wa n z a u k i v i p i t i a vitabu vya historia v i n a v y o f u n d i s h wa shuleni utaona picha nyingi zilizochorwa za biashara ya utumwa zinawaonesha Waarabu au Waswahili kuwa ndio wafanya biashara hiyo. Iko haja mtu aiulize nafsi yake: Jee utumwa Afrika Mashariki na Kati ulifanywa na Waarabu na Waswahili tu? Au kuna jamii nyingine pia zinakhusika? Na kama zipo, kwa nini basi michoro yenye kuonesha jamii hizi hazimo? Jee hawa waandishi wa vitabu vya historia v i n a v y o f u n d i s h wa s h u l e n i Ta n z a n i a , w a m e i p a t a w a p i dhamana na haki hii ya kuwafunza wanafunzi wa Tanzania historia yenye ukweli finyu na uwongo mwingi? Na kama hawana haki hiyo, kwa nini wasiwajibishwe k u u e l e z e a u k w e l i m t u p u wa m a m b o yalivyokuwa?

    A n g a l i a m i f a n o hii miwili ya picha z i l i z o c h o r w a n a Wazungu. Picha ya kwanza imechapishwa 1861 na inaonesha w a z i w a z i k u w a w a k a m a t a j i w a wanyonge wa Kiafrika

    ni Wazungu wenyewe. Wameonesha bila ya kificho:

    Picha ya pili inayofuata imechorwa na Mzungu mwingine miaka mitano tu baadaye, yaani 1866. Mchoraji ameichora tena picha ileile iliyotangulia na kuibadilisha kidogo, badala ya mkamataji kuwa ni Mzungu peke ya k e wa m e m c h o r a Mzungu Mreno (kavaa heti na surual i ) na Mwafrika kuwa wote walikuwa ni wakamataji:

    Historia ya kweli inatuambia waziwazi kuwa wote Wazungu Wakristo na Waafrika walishiriki pakubwa sana katika kuwasaka, k u w a u w a k w a idadi kubwa sana , kuwakamata wengineo na kuwatia wanyonge wa Kiafrika utumwani na kuwasafirisha kwa mamilioni wanyonge hao katika makoloni yao Wazungu. Picha hii imeitwa Kikundi cha mateka [watumwa] waliokutwa Mbambe wakielekea Tete. Haya matokeo yametokea Msumbiji na wala sio Afrika Kaskazini na yalifanywa na Mzungu Mreno.

    Sasa angalia katika ukurasa wa 24 wa kitabu cha History for Secondary Schools, Form Two, kilichoandikwa na Parazia Kaloli na Felix Kiruthu na kuchapishwa

    2 0 0 9 n a O x f o r d University Press, utaona propaganda za siasa kali za udini zilivyofanya k a z i k w a n a m n a zilivyobirua ukweli huu. Utaiona picha hiyo hiyo imechorwa tena baada ya miaka 138. Katika picha hii tunaona waziwazi kuwa mkamataji, kwa ishara ya mavazi yake, ni Mwarabu Mwislamu:

    Baada ya miaka 140 wanapropaganda wa Tanzania wenye siasa kali za udini wameona wazibadilishe picha za zamani zinazowalaumu Wazungu na Waafrika k wa u k a m a t a j i wa watumwa na badala yake kumpachika Mwarabu kuwa ndiye aliyefanya uovu huo. Ukiangalia vizuri utaona picha ni ileile, lakini wachoraji ndio waliobadilika na kubadilisha muundo wa uchoraji.

    Kimsingi, picha zote tatu ni ileile. Jee mchoraji wa picha iliyomo katika kitabu cha kusomeshea h i s t o r i a Ta n z a n i a a l iyekopi p icha za zamani alidhani, katika wakati huu tulionao wa utandawazi na kuwa n i m a r a m o j a m t u kutambulikana wapi amenyakuwa fikra au picha zisizokuwa zake, kuwa kujepa kwake na kubadilisha ukweli ndiyo hatatambulikana?

    Jiulize mwenyewe, n i kwa makusudio gani mchoraji wa leo akabadilisha wakamataji waliokuwa ni Wazungu Wakristo na Waafrika na kumweka Mwarabu M w i s l a m u b a d a l a yake katika kitabu cha kuwasomeshea historia wanafunzi wa Tanzania leo?

    Asili ya mchoro huo unatokana na masimulizi ya David na Charles L iv ings tone kat ika safari yake ya Zambezi na sehemu nyingine, na katika ugunduzi wa Ziwa Shirwa na Nyasa. Inakhusu kikundi cha wanaume watumwa waliounganishwa kwa magogo ya miti , na watoto na wanawake wamefungwa pamoja k w a k a m b a n a minyororo, wakiwa pamoja na walinzi wao Waafrika. Watumwa h a w a w a l i k u w a wakipelekwa Afrika Mashariki. Tukio hili lilishuhudiwa July 1861. Kwa mara ya kwanza picha hii ilichapishwa katika gazeti la Harper`s New Monthly Magazine (vol: 32, Dec 1865 May 1866).

    I n a s i k i t i s h a mwandishi wa kitabu cha Historia cha Form Tw o c h a Ta n z a n i a ya leo, kughushi na badala ya picha ya mtu unayemuona aliyekuwa akiusindikiza msafara huo ambae alikuwa Mzungu, kaweka picha ya mtu anaefanana na Mwarabu au Mswahili, na badala ya kusema watumwa hawa ni wa Tete ilioko mto Zambezi k a s e m a n i A f r i k a Kaskazini.

    Kwa nini kafanya hivi? Kwa nini uongo huu? Nini faida yake? Na nini anapata kwa kuleta fitina hii? Nini sababu ya chuki hii? Kwa nini anataka kuwasafisha Wazungu Wakr is to k wa k u wa o n d o s h a pichani wasiwemo na kupotosha historia? Nini alichopata mchoraji wa Kitanzania hata akauza hadhi , heshima na utu wake? Wangapi wamedhulumika na kudhal i l i shwa kwa uongo huu na kwa mifano mingi mingineyo ya kama huu?

  • 9 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 8-14, 2015Makala

    FAKHARI iliyozoeleka katika maadhimisho ya kila mwaka ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar u l i o a s i s i w a m w a k a 1964 kwa kusainiwa Hati za Makubaliano ya Muungano kulikofanywa na Marais wa Mataifa huru ya Tanganyika na Zanzibar, ni kuhisabu umri wa Muungano wenyewe na kujipa maliwazo kuwa Muungano umeendelea k u d u m u . H a t u n a mazowea ya kutathmini afya na uimara wa kweli wa Muungano wenyewe.

    Pengine kufanya hivyo kunaweza kuhesabiwa k u w a n i s a w a n a kuunyanyapaa Muungano. Lakini ukweli mchungu ni kuwa Muungano huu u m e d u m i s h w a k w a gharama kubwa katika muktadha wa maendeleo ya kisiasa katika Tanzania na khususan kwa upande wa Z a n z i b a r . T o k e a kuasisiwa kwake hadi leo, ikiwa sasa ni zaidi ya nusu karne, Muungano na khasakhasa muundo wake, umebaki kuwa ndio ajenda kuu ya kitaifa katika siasa za Zanzibar. Muungano u n a e n d e l e a k u d u m u ukiwa unalindwa kwa nguvu kubwa za kisiasa na kidola pengine kuliko jambo lolote katika uwanja wa kisiasa hapa Tanzania.

    Kat ika umri wake , Muungano huu umepitia misukosuko mingi. Mwaka 1984 katika kuunusuru Muungano ilibidi Serikali n z i m a y a Z a n z i b a r iondolewe madarakani. Aliondolewa Rais Aboud Jumbe Mwinyi, Waziri Kiongozi wake Ramadhan H a j i F a k i n a Ba r a z a lake lote la Mawaziri. Mwanasheria Mkuu wa Serikali hiyo aliyekuwa Raia wa Ghana,Bashir Swanzy alitimuliwa nchini na kurejeshwa kwao. Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Zanzibar baada ya Mapinduzi, Marehemu W o l f g a n g D o u r a d o alikamatwa Zanzibar na kupelekwa magereza ya Tanzania Bara kwa kile kilichodaiwa ukosoaji wake wa Muungano. Orodha ya waliopata majeraha katika harakati za kuudumisha Muungano ni ndefu.

    H i v i k a r i b u n i tumeshuhudia kufutwa kazi kwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na kufukuzwa uanachama kwa aliyekuwa Waziri k a t i k a S e r i k a l i y a Mapinduzi ya Zanzibar Mansour Yussuf Himid na hivyo kupoteza nafasi zake zote za k i s iasa

    Miaka 51 ya shuruti la muungano wa Tanganyika dhidi Zanzibar

    AWADH Ali Saidkutokana na misimamo yao ya kutokukubaliana na mambo mbalimbali katika Muungano wakati wa Mchakato wa Katiba Mpya. Viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Uamsho t a k r i b a n 2 0 a m b a o wamekamatwa Zanzibar na kushitakiwa katika Mahkama za Tanzania Bara na kuzuiliwa katika magereza ya Tanzania Bara kwa makosa ya ugaidi, nao kabla ya kukamatwa k w a o w a l i e n d e s h a harakati kubwa ambazo z i l iungwa mkono na wafuasi wengi zilizolenga kuukosoa Muungano. Hata yale maeneo ambayo t u n a j i v u n i a k u wa n i mafanikio ya Muungano, kama kukua kwa biashara baina ya pande mbili hizi, nako kila uchao tunasoma ripoti za vikwazo katika uendeshaji wake. Mathalan vilio vya kila leo vya utozwaji kodi mara mbili kwa bidhaa zinazotokea Zanzibar na kuingia kat ika soko la Tanzania Bara. Biashara inaendelea kwa mtindo wa kila kilema kina mwendo wake

    Yote hayo ni matokeo ya Muundo wa Muungano a m b a o k wa m a u m b i l e yake, muundo huo milele hauwezi kujenga Muungano unaotoa haki, hadhi na fursa sawa baina ya washirika wa Muungano. Huu ni muundo wa Muungano wa Nchi mbili unaoendeshwa na Serikali mbili. Serikali moja, ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imebeba na kuyachanganya kwa pamoja mambo ya Tanzania Bara na yale mambo ya Muungano ambayo kimsingi ni mambo ya ushirika wa pamoja baina ya pande mbili za Muungano; na Serikali ya pili , Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imebakishiwa yale mambo ambayo si ya Muungano.

    Muundo huu uliobuniwa kama muundo maalum wa kipindi cha mpito cha mwaka

    mmoja kutokea 1964 hadi 1965 kama ilivyoelezwa kwa ufasaha ndani ya Hati ya Makubaliano ya Muungano ukafanywa kuwa Muundo wa Kudumu. Kila muda unavyokwenda, Muungano ulikuwa UNADUMISHWA kwa kuongeza orodha ya Mambo ya Muungano, ilianza yakiwa mambo 11 na sasa yako 22; na hii maana yake ni kuyamega mamlaka ya Zanzibar katika eneo fulani. Mathalan suala la fedha na sarafu (1965) na mafuta na gesi (1969) na kuyaingiza katika himaya ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo kimsingi ni Serikali ya Tanganyika iliyobaki na mambo yake yote na ikaongezewa mamlaka juu ya baadhi ya mambo ya Zanzibar na baada ya ongezeko hilo ikabadilishwa jina na kuitwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

    Kiuhalisia Tanganyika ili j ibakisha kama ilivyo na ikajiongezea mambo ya Zanzibar. Haikumega chochote kutoka kwenye mamlaka yake na kuyapeleka kwengine. Aliyeuita muundo huu kuwa ni kiinimacho alikuwa amefikiri vyema. Muundo huu utadumisha misukosuko daima. Mfano chukua eneo la mapato na matumizi ndani ya muundo huu wa Serikali mbili. Baada ya miaka 50 ya Muungano huu, eneo hili linafukuta mgogoro. Na utata uko wazi.

    Na msingi wa utata huu ni muundo wenyewe wa Muungano. J iul ize uko wapi mfuko wa mapato na matumizi kwa ajili ya mambo ya Tanzania Bara yasiyohusu Muungano (ambayo hayo Zanzibar haihusiki asilani), na uko wapi mfuko wa mapato na matumizi wa mambo ya muungano (ambao katika mfuko huo Zanzibar

    inahusika kikamilifu na ingestahiki kuchangia na kupata gawio kama kuna bakaa).

    L a k i n i n i wa z i k wa m u u n d o h u u k a m w e huwezi kutofautisha kuwa mapato haya yametokana na vyanzo vya Tanzania Bara au yametokana na vyanzo vya Muungano. Yote yamo mfuko mmoja tu. Pia huwezi kutofautisha kuwa matumizi haya ni kwa ajili ya shughuli za Tanzania Bara au kwa ajili ya shughuli za Muungano tu. Yote yanatumiwa kwa pamoja tu. Katika hali hii, huwezi kutegemea utulivu k wa s a b a b u u wa z i n a utambuzi wa maeneo na mipaka katika mapato na matumizi ni jambo nyeti katika ushirikiano wowote.

    T u c h u k u e m f a n o mwengine, uchumi si jambo la Muungano, Zanzibar ina uchumi wake na Tanzania Bara ina uchumi wake na kiukweli hizi ni chumi mbili tofauti , mmoja ni uchumi mkubwa na mwengine ni uchumi mdogo LAKINI n i c h u m i s h i n d a n i (competing economies na ushahidi wa hilo ni utozaji kodi mara mbili kwa bidhaa za Zanzibar) h a s a k a t i k a m a e n e o ya biashara ya bidhaa, uwekezaji na utalii . Kwa upande wa Zanzibar uchumi huu ambao ndio unaopaswa kuiendeleza na kuihudumia Zanzibar N Y E N Z O K U U z a u c h u m i , a m b a z o n i S E R A Z A F E D H A (monetary policies) na SERA ZA KODI (fiscal policies) zimeondoshwa na kufanywa ni mambo ya muungano na hivyo Z a n z i b a r h a i w e z i kusarifu uchumi wake b i l a m i s u k o s u k o . Wakuu wa Benki Kuu na Mamlaka ya Mapato Tanzania, Taasisi ambazo kimsingi zinasimamia uchumi wa Tanzania Bara hawawezi kuandaa sera zi tazoendesha chumi

    mbili zenye mgongano wa kimaslahi na kwa vile huwezi kuokoa chungu cha mwenzako wakati chako kinawaka pia , Taasisi hizi zinatumika kuimarisha uchumi wa Tanzania Bara.

    Katika jambo pekee lililo kwenye orodha ya mambo ya Muungano na Zanzibar ikaliwekea Wizara na Waziri basi ni suala la fedha lakini ni wazi Waziri huyu hana uwezo wowote katika maamuzi ya sera za fedha na kodi. Athari za kiuchumi zinazotokana na muundo huu zipo za kila aina. Hivi karibuni kuliibuka kashfa ya ESCROW ambayo kimsingi imetokana na mambo yasio na uhusiano wowote na mambo ya Muungano, ni mambo ya Tanzania Bara. Kufuatia mzozo huo, wafadhili wakazuia misaada ya fedha na hii ikapelekea kuadimika kwa fedha za kigeni katika soko la ndani. Kwa vile mahitaji ya fedha za kigeni yalibaki palepale au yaliongezeka thamani ya fedha za kigeni ikapanda. Wakati wa f a d h i l i wa n a z u i a misaada tunaambiwa thamani ya dola moja ilikuwa ni tshs 1635 hivi sasa thamani ya dola ni tshs 1900 ikiwa ni ongezeko la thamani kwa asilimia zaidi ya 15. Hii maana yake ni kuwa thamani ya sarafu ya Tanzania ambayo n i j ambo la Muungano imeporomoka kwa asilimiaa 15 kutokana na matendo ya upande mmoja wa Muungano na kupelekea kuyumba kwa uchumi sio tu wa upande huo, bali na wa upande wa Zanzibar kwa kosa lisiloihusu. Na katika mtanziko kama huu wa kiuchumi haijawahi Taasisi za kifedha na kiuchumi za Tanzania kuinusuru (bail out) Zanzibar.

    Kwa hali ya mwenendo wa M u u n g a n o we t u ni sahihi a l ivyowahi k u s e m a P r o f . Ya s h G h a i , m w a n a s h e r i a mashuhuri wa mambo ya Katiba aliyeongoza Mchakato wa Kat iba Mpya ya Kenya aliposema k u w a h a i s h a n g a z i kuwa Muungano huu unakumbwa na matatizo, bali kinachoshangaza ni kuwa umeweza kudumu

    ( the surprise is not that the Union has run into difficulties, but that it has survived at all )

    (Issa G. Shivji,Tanzania The Legal Foundations of the Union, Second Expanded Edition, 2009, pg xviii, Foreword by Yash Ghai)

  • 10 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 8-14, 2015

    Na Mohamed Said

    Makala

    Mjue Abdurahman Ali Msham

    Ali Msham aliyekaa katikati katika moja ya mikutano ya ndani ya TANU aliyokuwa

    akifanya uani nyumbani kwake Mtaa wa Jaribu, Magomeni Mapipa

    Picha inamwonyesha Mwalimu Nyerere akipokea samani hiyo iliyotengezewa na Mzee Ali Msham. Aliyesimama wa kwanza kulia ni Mzee Ali Msham mwenyekiti wa tawi la TANU Magomeni Mapipa wakati TANU inawaunganisha wananchi kupigania uhuru wa Tanganyika.

    ABDULRAHMAN Ali Msham sasa ni mtu mzima na ana umri wa miaka 65. Wakati TANU inaasisiwa Dar es Salaam mwaka 1954 yeye alikuwa mtoto w a m i a k a m i n n e . M a j u m a m a c h a c h e yaliyopita, alikisikia kipindi kilichorushwa na Radio Kheri 104.10 FM kuhusu safari ya M wa l i m u N ye r e r e UNO mwaka 1955. Kwa kauli yake mwenyewe anasema kipindi kile kilimrudisha nyuma sana akamkumbuka marehemu baba yake Ali Msham ambaye a l i k u w a m o j a w a wazalendo waliokuwa mstari wa mbele katika kupambana na ukoloni. A b d u l r a h m a n A l i Msham akawa na hamu kubwa ya kukutana na aliyekuwa akieleza safari ile ya kihistoria. A l i k u wa n a h a m u kwa kuwa na yeye alikuwa na machache angependa kueleza nini baba yake Mzee Ali Msham alifanya katika TANU katika ile miaka ya 1950.

    Abdulrahman alianza kwa kueleza kuwa baba yake alikuja Dar es Salaam kutoka Kilwa katika miaka ya 1950 akiwa fundi seremala na alikuwa akifanya s h u g h u l i z a k e z a kutengezeza samani M t a a wa K a r i a k o o n a C o n g o . TA N U ilipoasisiwa mwaka wa 1954 baba yake alijiunga na kuwa mwanachama kwa kukata kadi ya TANU. Makazi yake ya l i k u wa M t a a wa J a r i b u M a g o m e n i Mapipa ambako alikuwa akiishi kwenye nyumba y a k e m w e n y e w e . Kat ika hamasa zi le z a k u p a m b a n a n a ukoloni , baba yake alitoa chumba kimoja katika nyumba yake akafungua tawi la TANU na yeye mwenyewe ak iwa mwenyeki t i . Katika harakati zile za kupambana na ukoloni alisikitishwa na hali ya ofisi ya Mwalimu

    Ofisi ya TANU Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa kama ilivyokuwa ikionekana katika miaka ya 1950 ikiwa imezungikwa na wanachama wake.

    Kushoto: John Rupia, Julius Nyerere, Zuberi Mtemvu Waliosimama nyuma yao ni BANTU Group Vijana Walinzi wa Viongozi wa TANU

    Ali Msham aliyekaa katikati katika moja ya mikutano ya ndani ya TANU aliyokuwa akifanya uani nyumbani kwake Mtaa wa Jaribu, Magomeni Mapipa

    Nyerere pale New Street kwa kuwa hakuwa na samani za maana katika i le ofisi yake. Baba yake alirejea kwenye kiwanda chake pale Mtaa wa Kariakoo na Congo akatengeneza meza ya ofisi ya hadhi ya rais wa TANU pamoja na viti kadhaa. Mzee Ali Msham alimwalika M wa l i m u N y e r e r e kwenye tawi la TANU la Magomeni Mapipa i l i akabidhi samani mpya kwa ajili ya ofisi yake. Mwalimu Nyerere alifika pale kwenye

    tawi la TANU na katika sherehe fupi Mwalimu Nyerere akakabidhiwa samani ile.

    K u m a l i z a m a z u n g u m z o ye t u Abdulrahman Msham alikabidhi picha za baba yake za wakati ule wa kupigania uhuru. Picha hizo nami naziweka hapa kwa ajili ya kuhifadhi na kuthamini mchango wa wazee wetu mashujaa waliopigania uhuru wa Tanganyika lakini kwa bahati mbaya michango yao haijathaminiwa.

  • 11 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 8-14, 201511 AN-NUURMakala

    KATIKA Filamu, Mzee wa Swaga , JB kuna m a h a l i a n a m p a s h a mshirika wake katika utapeli kwamba, ashapata kondoo ambaye yupo tayari kwa kuchinjwa. K o n d o o m w e n ye w e n i m w a n a d a d a mwenye pesa ambaye ashawekewa mazingira ya kuingia katika mtego wa kutapeliwa. Na kweli alitapeliwa.

    Ndiyo hali tuliyo nayo Watanzania hivi sasa. Kama hatutatanabahi, tukasema hapana, kwa hakika ni Mwenyezi Mungu peke yake anaweza kutunusuru. Kwa hapa tulipofikishwa, yale ya Garissa, Mpeleketoni na ya Boko Haram, wala hayana muda mrefu. Na lazima tuseme na mapema k w a m b a M C H AW I WETU MKUU, ni vyombo vya habar i . Mchawi namba mbili tutakuwa sis i wenyewe ambao t u l i v i f u m b i a m a c h o vyombo vyetu vya habari vikitulisha propaganda za kitisho cha ugaidi mpaka tukaziamini, tukatishika na wakatupora akil i , fahamu na uwezo wetu wa kuyatafakari mambo.

    Terrorized by 'War on Terror', ni makala na uchambuzi ulioandikwa mwaka 2007 na Kachero Zbigniew Brzezinski, ambaye aliwahi kuwa Mshauri wa Mambo ya Usalama (National Security Adviser) wa Rais Jimmy Carter. Lakini pia alikuwa mtu muhimu sana katika vita ya Afghanistan wakati ikipigana na mvamizi Urusi. Huyu alifanya kazi kubwa katika kuandaa j e s h i l a M u j a h i d i n a waliopigana na Mrusi kwa niaba ya Marekani. Kwa hiyo anasema kitu anachokijua.

    Katika uchambuzi wake huo, Zbigniew Brzezinski, anasema kuwa, magaidi na inayoitwa vita dhidi ya ugaidi ("war on terror"), imebuniwa ili kujenga utamaduni wa hofu na kutafuta adui wa kubuni i l i kut imiza maslahi ya wanasiasa (siasa za ubeberu) kama ilivyokuwa katika vita baridi.

    Hebu msikilize katika moja ya maneno yake. Anasema:

    The phrase itself (war on terror) is meaningless. It defines neither a geographic context nor our presumed enemies. Terrorism is not an enemy but a technique

    Tanzania, sasa kondoo anayesubiri kuchinjwaMagazeti yanalitoa Jini katika chupaPolisi, JWTZ hawamuwezi subiani huyu

    Na Omar Msangi

    o f war fare - - po l i t i ca l intimidation through the killing of unarmed non-combatants.

    K w a h i y o k a m a anavyosema Zbigniew Brzezinski, ugaidi sio adui lakini mbinu, njama chafu za kufikia malengo fulani ambapo watu wasio na hatia huuliwa.

    Z a i d i a n a s e m a k u w a m s e m o h u o umefanywa usiwe na maana inayoeleweka sio kwa bahati mbaya, bali umefanywa hivyo makusudi na walioubuni na wanaoendeleza vita hiyo ili kufikia malengo yao ya kusimika kitisho (culture of fear).

    Kwa nini imekuwa ni laz ima kuwat isha watu? Kachero Zbigniew Brzezinski anafafanua akisema kuwa:

    Fear obscures reason, intensifies emotions and makes it easier for demagogic politicians to mobilize the public on behalf of the policies they want to pursue.

    Kwamba ukishawatisha watu, unaondoa uwezo w a o w a k u f i k i r i , unawaburuza unavyotaka kwa sababu, badala ya kuyatizama mambo kwa akili na kutafakari na kuhoji, wanaongozwa na

    mihemko (emotions).Nilikuwa napata tabu

    sana, inakuwaje watu wenye akili zao timamu, wakiwemo Wahariri wetu katika vyumba vyetu vya habari , wanashindwa kuona kuwa tukio kama lile la Westgate na hata hili la juzi la Garissa, hakuna namna ya kuwa limefanywa na wanaoitwa magaidi kutoka Somalia. L a k i n i j i b u n i h i l i ana losema Zbigniew Brzezinski.

    Wa t u wa m e t i s h wa kuhusu magaidi wa Al-Qaida na Al-Shabaab, sasa akili hazifanyi kazi tena. Wakiambiwa kuna magaidi wamepiga mahali fulani na jeshi nzima la nchi limeshindwa kuwapata, wala hawapigi mahesabu mepesi ya uwezekano wa kufanyika hilo. Emotions huwapelekea kuamini tu moja kwa moja na kama ndio katika vyumba vya habari , basi hugeuka vipaza sauti.

    A k i e l e z e a u b a y a wa utamaduni huu wa k u wa t i a wa t u h o f u , Zbigniew Brzez inski anasema kuwa:

    The culture of fear is like a genie that has been let out of its bottle. It acquires a life of its own -- and can become

    MKUU wa Majeshi, Jenerali Devis

    Mwamunyange.

    MKUU wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali

    Ernest Mangu.

    demoralizing.Kwamba ukiwekeza

    katika kuwatia watu hofu, basi ujue kuwa hofu hiyo ni kama jini. Ukishalitoa katika chupa, linajipatia uhai wa kivyake vyake. Hutaliweza tena. Ndio unaona hi i leo Boko Haram, inakuwa jinamizi linaloshinda polisi, jeshi na vyombo vyote vya usalama vya nchi kubwa (The Giant of Africa) Nigeria.

    Leo Kenya, pamoja na kuuwa Mashe ikh kikatili wakituhumiwa kwa ugaidi, na pamoja na kuwa na vikosi katili vya mauwaji vinavyopewa mafunzo na Marekani na Israel, ikidaiwa ni vya kupambana na magaidi, lakini wanapata kipigo Westgate, Mepeleketoni, Mandera na Garissa juzi.

    P e n g i n e a m b a l o hakul i fa fanua vizur i Zbigniew Brzez inski katika uchambuzi wake ni kuwa hiki KITISHO C H A U G A I D I n d i o m t a j i w e n y e w e w a mabeberu. Mkishatishwa na mkaaminishwa kuwa miongoni mwenu kuna magaidi wenye uwezo wa kufanya hili na lile, basi yatakayofuatia wala hamtakuwa na uwezo nayo, wala atakayefanya hamtamjua ila nyinyi mtabaki mkiimba tu Al-Shabaab, magaidi, Al-Qaida na mambo kama hayo. Litakuwa ni jinni ambalo, si Afande Mangu wala JWTZ watakaoweza kupambana nalo. Tutabaki tukiwalaumu bure, kama ambavyo hivi sasa Uhuru Kenyatta na serikali yake wanalaumiwa au kama ambavyo Jeshi na vyombo vya usalama vya Nigeria vinalaumiwa kuhusu Boko Haram.

    Tunalotakiwa kufahamu hapa ni kuwa ukishafanya kosa la kwanza, mengine y a n a j i e n d e a t u . N i J i n i a m b a l o k a m w e hamtaliweza. Ni lenyewe tu liamue kurejea baharini au msituni lilikotokea.

    U k i r e j e a ya l i y o j i r i k a t i k a n c h i a m b a z o zimetutangulia katika k u i n g i z w a k a t i k a m c h e z o h u u m b a ya , kinachotangulia kinakuwa ni matukio ambayo kila ukiyatizama yanakuwa na sura ni mambo ya kupangwa (staged, false flag), lakini kana kwamba vyombo vya habari ni

    sehemu ya mkakati huo, hufanya kazi ya kupiga propaganda kuwa hayo ni matukio ya kwel i ya ugaidi . Vyenyewe vinaweza kujifanya kuwa vinatoa tahadhari na kuhimiza vyombo vya dola kuchukua tahadhari, lakini kwa hakika kazi w a n a y o f a n y a n d i o ile ya kusimika kitisho kisichokuwepo.

    S i k u ya M e i M o s i i l i d a i wa k u wa k u n a w a t u w a l i j e r u h i w a huko Morogoro baada y a k u r u s h i w a k i t u kinachodhaniwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono. Sasa soma kichwa hiki cha habari: Ugaidi tena Moro. (Mtanzania Toleo Na. 7810 la Jumapili Mei 3, 2015)

    H a b a r i y e n y e w e inasema, Watu watano wamejeruhiwa vibaya katika tukio lenye sura ya k iga id i baada ya k u l i p u l i w a n a k i t u kinachohisiwa kuwa ni bomu lililorushwa kwa mkono wakiwa katika sherehe za maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi)

    M t u u n a j i u l i z a , kinacholifanya tukio hilo liwe la kigaidi ni nini?

    Habari inasema Ugaidi tena Moro. Maana yake n i k u wa u l i s h a wa h i kufanyika tena ugaidi Morogoro. Ugaidi huo ni upi?

    Mtanzania likielezea ugaidi huo l inasema: Tukio hilo limetokea karibu kabisa na eneo a m b a l o w i k i m b i l i zilizopita Jeshi la Polisi l i l iwakamata watu 10 wanaodhaniwa kuwa ni magaidi wakiwa na milipuko 30 ndani ya Msikiti wa Sunni uliopo katika Tarafa ya Kidatu wilayani Kilombero.

    Watu wamekamatwa wakiwa na milipuko, nini kinafanya wadhaniwe kuwa ni magaidi? Kwa nini wasidhaniwe kuwa ni wahalifu na kwamba pengine milipuko hiyo ni ya kufanyia uvuvi haramu wa samaki! Lakini, je, ni Polisi waliowakamata waliodai kuwa huenda ni magaidi au ni mwandishi?

    Ukisoma uchambuzi huu wa Kachero Zbigniew Brzezinski na ule wa mwandishi Arda Bilgen, aliouita Terrorism and the Media: A Dangerous Symbiosis, na wengine wengi walioandika juu ya mada hii, inaelezwa wazi kuwa vyombo vya habari

    Inaendelea Uk. 12

  • 12 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 8-14, 201512 MAKALA/MASHAIRI

    W A T A N Z A N I A wamekwama, na wale ambao wanawategemea k u w a k w a m u a n a o wamekwama. Hii ndio h a l i i n a y o wa k a b i l i Watanzania kwa sasa.

    Maisha yamezidi kuwa magumu kwao, usafiri hakuna, umeme ambao ndio nyenzo muhimu angalau ya kuwaongezea pumzi ya kuishi nao hivi sasa umekuwa wa katakata, hauwasadii.

    S h i l i n g i a m b a y o wanaifukuzia kula uchao ili kuganga hayo maisha japo ni duni, nayo imezidi kuporomoka thamani yake ikilinganishwa na thamani ya sarafu za kigeni. Mfumuko wa bei umeshapiga hodi.

    Wakati watanzania walio wengi wakiendelea kugugumia maumivu m a k a l i ya k i m a i s h a wanayopata kutokana n a m a t a t i z o h a y a , a m b a y o k w a k w e l i yamekosa mtatuzi, mvua zinazoendelea kunyesha nazo zimewazawadia janga la mafuriko katika m a e n e o m b a l i m b a l i y a n c h i . N y u m b a z imeezul iwa, mazao yamezolewa, chakula hakuna , msaada wa uhakika hakuna.

    S e r i k a l i n i t a a s i s i k u u i n a y o s i m a m i a maslahi ya wananchi k i m a i s h a . N d i c h o chombo kilichosimikwa kisheria na kimamlaka k u w a s h u g h u l i k i a wananchi, ili kuhakikisha maisha yao yanastawi.

    Iwapo chombo hicho kitashindwa kusimamia na kuwahakikishia wananchi ustawi wao wa kimaisha, ina maana chombo hicho kimekwama. Waliopewa mamlaka ya kukiendesha wamekosa mbinu yakinifu za kuendesha chombo na matokeo yake kila janga linaloibuka linawatesa watu kwa kuwa hakuna kinga yeyote iliyoandaliwa ya kuzuia majanga hayo.

    Ninaelewa kwamba yapo majanga au matatizio a m b a y o n i v i g u m u kuyazuia kirahisi pale ayanapotokea. Na sehemu kubwa ya majanga hayo ni ya asili kama vile mafuriko kama yale yaliyotokea

    Ni mazoea mabaya kulea matatizoTukikwama, wa kutukwana nao hukwama

    Na Shaban Rajab M s u m b i j i , u k a m e , k imbunga kama cha Tsunami kule Indonesia, tetemeko la ardhi kama lililoikumba Nepal siku za hivi karibuni, magonjwa kama ebola kule Liberia na Sierra Leone nk.

    H a y a n i m a j a n g a ambayo hayatokani na nguvu au uwezo wa watu bali ni kwa uwezo wa Muumba wa mbingu na ardhi. Hata kuyakabili kwake ni kugumu kwa kuwa yanadhuru sehemu kubwa kwa wakati mmoja na kwa nguvu kubwa zaidi.

    Lakini yapo majanga ambayo kwa serikali yenye watendaji makini, wanaotimiza wajibu wao kulingana na dhamana waliyopewa, wanaweza kujipanga na kujiandaa vizuri kuzuia majanga a m b a y o k w a k i a s i kikubwa husababishwa na binadamu wachache wenye kibri.

    Tena wanaweza kufanya hivyo kwa muda mfupi na kwa gharama ndogo alimuradi wanawajibika kwa wananchi, wakiamini h u o n i wa j i b u wa o kusimamia ustawi wa watu chini ya mwavuli wa serikali.

    Serikali au dola yeyote kushindwa kuyakabili m a j a n g a y a n a m n a h i i , ( h a y a m a d o g o y a n a y o s a b a b i s h w a na watu wachache) ni kipimo tosha kwamba serikali imekwama na haina utaratibu wa kuzuia kabla ya tatizo kutokea na kusababisha madhara.

    Nimelazimika kuanza n a m u h t a s a r h u o kidogo tu, kuonyesha p icha ha l i s i n i kwa namna gani Watanzania hivi sasa wanateseka kutokana na serikali kushindwa kuchukua hatua mapema kudhibiti matatizo yanayowakabili Watanzania kwa sasa hasa hili la usafiri.

    K u a n z i a J u m a t a t u hadi Jumanne wiki hii, madereva wa magari ya abiria nchi nzima waligoma kusafirisha ab i r ia . Hakuna bas i linalosafiri kuanzia yale yanayofanya safari za mikoani na nchi jirani na yale ya safari fupi yaani daladala.

    Wa t a n z a i a w e n g i ambao kipato chao ni cha kikabwela, waliteseka kwenda na kurejea katika shughuli zao mbalimbali za kujikimu.

    Uwezo wao kimapato ni mdogo, hawawezi k u p a n d a n d e g e , h a w a w e z i k u k o d i taksi, hawawezi kukodi boda boda wala bajaji kutokana na gharama kubwa ya nauli, sehemu ya kwenda kwa shilingi 400, mtu analazimika kulipa shil ingi 2000. S h u g h u l i z a w e n g i zilisimama, wakashinda majumbani kwa kukosa nyenzo ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine, uchumi wao umeanguka. Wanafunzi hawaendi shule, tena wale wa kidato cha sita wakiwa katika kipindi cha mitihani ya mwisho ya kuhitimu.

    Hali hiyo inatokea huku kukiwa hakuna usafiri mbadala na wa uhakika kama wa gari moshi, ambao kwa muda mrefu umekuwa ni haba na usiokidhi, lakini pia unaishia mikoa na maeneo machache. Kwa ujumla wananchi walikwama na hakuna aliyeweza kuwakwamua.

    Ni jambo linalofahamika k w a m b a s e k t a y a usafirishaji ni miongoni mwa sekta muhimu sana kwa uchumi wa Taifa lolote lile. Lakini ni sekta ambayo inahitaji jitihada za ziada kuhakikisha usalama wa maisha.

    Kupuuza au kudharau matatizo yaliyopo au ya n a y o i b u k a k a t i k a sekta hii, ni kuchangia kuporomosha uchumi wa mtu mmoja mmoja na uchumi wa ta i fa kwa ujumla, lakini pia k u d h a r a u m a t a t i z o yanayoweza kugharimu maisha.

    Mzozo uliopo katika sekta ya usafirishaji kiasi cha kusababisha madhara na hasara iliyopatikana k wa k i a s i k i k u b wa u m e s a b a b i s h w a n a serikali yenyewe kutojali.

    Katika sekta hii mara kwa mara kwa nyakati tofauti kumekuwa na matatizo kati ya madareva n a s e r i k a l i , wa k a t i mwingine tatizo kati ya wamiliki wa vyombo

    Inaendelea Uk. 16

    Tanzania, sasa kondoo anayesubiri kuchinjwaInatoka Uk. 11vimetumika vibaya mno katika kusimika kitisho hewa cha ugaidi kiaminike kuwa kipo i l i wenye malengo yao wafanye yao. Na inaelezwa wazi p i a k u wa ya n a we z a kufanyika mambo mengi (staged) ili kuthibitisha kuwa ugaidi upo.

    K w a h i y o t a a r i f a kama hizi za gazeti letu Mtanzania, ndio katika yale anayosema Zbigniew Brzezinski, their task is to convince the public that it faces new threats. Kwamba waiaminishe jamii kuwa wanakabiliwa na kitisho cha ugaidi.

    Na matukio kama yale tuliyoambiwa kule Msikiti wa Suni, Kidatu kwamba watu wamekamatwa na milipuko, kombati za jeshi na bendera ya Al-Shabaab, ni vitu Brzezinski alivyoita kuwa ni v iwaki l i sh i vinavyotoa salamu kuwa matukio ya kutisha ya kigaidi yanakuja. Halafu likitokea (kwa kupangwa) hao hao wa magazeti watasema tulisema, t u l i t a h a d h a r i s h a . N i k a n a k w a m b a walikuwa wamepewa kazi ya kuwatayarisha Watanzania kisaikolojia kupokea kipigo.

    Akizungumzia jamii ya Kimarekani, Brzezinski anasema kuwa kwa bahati mbaya Amerika kumekuwa na mambo ya kipuuzi ya kuwapachika Waarabu na Waislamu ugaidi wa kupandikiza, hali inayofanya jami i kugawanyika na kujengeana chuki zisizo na maana wala faida kwa taifa.

    Vitu kama bendera hizo zinazodaiwa kukutwa M s i k i t i wa S u n i n a kwamba katika matukio hayo hutumiwa watu wenye kuvaa kanzu na vibandiko, bendera h i z o n a v i b a n d i k o hivyo hutumiwa kama alama kwamba likitokea shambulio baya, tayari ishajengwa picha kuwa wafanyaji ni Waislamu. Kwa namna hiyo anasema kuwa hivi sasa Marekani kuna chuki kubwa dhidi ya Waislamu na Waarabu, jambo ambalo anadhani kuwa halina faida na nchi.

    Lakini kwa upande m w i n g i n e a n a s e m a kuwa upumbafu huu wa kujitisha kupitia vyombo vya habari, kumezalisha upumbafu mwingine wa hofu na kuweka taratibu nyingi za kiusalama ambazo na zenyewe ni upumbafu mtupu. Ni upumbafu kwa sababu, ni matokeo ya upumbafu wa kujitisha wenyewe mkaj i t ia wazimu wa kudhania kuwa kila kona kuna gaidi lililo tayari kuwapiga. Ni upumbafu

    pia kwa sababu gaidi la kweli haliwezi kuzuiwa na njia hizo. Anatolea mfano kuwa alikuwa akienda katika ofisi moja kule New York City, ambapo ilibidi apitie katika alichoita absurd security checks".

    Anasema ni "absurd security checks" kwa sababu, wewe unaweka machine ya kukagua watu wakiingia ofisini, kama lengo ni kuzuiya gaidi asiingie na bomu, je wale wanaopanda daladala unawakagua? Je, wanaoingia sokoni Kariakoo!

    Ukienda Zanzibar, pale bandarini unakuta kuna machine ya kupekuliwa. Unajiuliza, hivi walioweka mashine hii, lengo lao nini? Hata wale wanaofanya kazi pale, unawatizama, unabaki tu kujinyamazia. Unajua kuwa ndio kile alichosema Z b i g n i e w B r z e z i n s k i kwamba:

    "Security" procedures have become routine, wasting hundreds of millions of dollars and further contributing to a siege mentality.

    Kama tunaona starehe na kwamba labda ndio biashara itanoga ya magazeti kila uchao kuibuka na habari ya watu wenye madevu, wavaa kanzu wenye bendera nyeusi kuwa ndio magadi wauwaji, tujue pia kuwa tukishalitoa jinni hilo katika chupa, linaweza pia kuanza na kunyonya damu za wavaa tai na misalaba shingoni kama tulivyoaminishwa kuwa ndio ilivyotokea Garissa.

    Na kama alivyosema Dr. Preston James, Ph.D, katika uchambuzi wake WAR ON TERROR: The Worlds Biggest New Business , Ugaidi ni zimwi lenye njaa (hungry monster ) wala msidhani kuwa mnaweza kulishibisha au kuliuwa kwa polisi na jeshi lenu. Undeni vikosi hivi na vile vya kupambana na ugaidi, lakini mkishajikubalisha kuwa lipo, kosa. Ni jinni subiani mmelitoa katika chupa. Mtauwa watu wenu kama walivyouliwa akina Sheikh Roggo na Sheikh Makaburi, lakini lenyewe lipo tu linaendelea na Westgate na Garissa zake.

    Imefika mahali tuseme basi kwa mpagao huu wa wazimu wa kuona magaidi kila kona na kuyapepea. Hata kama ni kuchukua tahadhari, basi tuonyeshe kutumia akili japo kidogo tu.

    Tuyatizame mambo kwa usahihi wake. Tusitumike tu kijinga. Hakuna nchi iliyolifungulia jini hili ugaidi ikasalimika.

    Kwanza wenye jinni l a o n d i o wa t a k u p a silaha, pesa na mbinu za kupambana nalo ambazo zitakuwa kama 'damu' ya kulishibisha 'subiani' na kulifanya litishe zaidi na kuwa hatari zaidi.

  • 13 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 8-14, 2015Habari

    Mimi ni Binti wa Kiislamu HAMIDA RASHIDI. Pia ni yatima, ambaye ninasoma Chuo cha Ualimu Ununio (Ununio Teachers College) mwaka wa pili.

    Nimesimamishwa masomo kwa kutolipa ada na kushindwa kuendelea na masomo. Mpaka sasa nipo nyumbani. Mlezi aliyekuwa ananilipia ada ameshindwa kufanya hivyo kutokana na hali yake kuwa mbaya kiuchumi.

    Naomba kila atakae guswa na habari hii anisaidie kwa kile atakacho jaaliwa na Muumba wake kwani kutoa ni moyo. Toa kile alicho kuruzuku Allah (S.w) hakika hutopoteza utayakuta malipo yako mbele ya muumba wako.

    Kiasi cha ada ambayo nadaiwa ni Shilingi laki Nane (800,000). Unaweza ukatuma kwa namba ya mlezi wangu Yassin M. Mwagamile 0783 723312 au unaweza wasiliana na uongozi wa chuo 0715 822332, 0687 505 292 au unaweza lipia Benki ya KCB Account Namba 3300627761 kwa jina la Ununio Teachers' College kwa jina la Mwanachuo HAMIDA RASHIDI. Ukituma kwa akaunti ya chuo ni vyema ukatujulisha kwa namba ya mlezi wangu.

    MSAADA WA KULIPIWA ADA

    SAUDI Arabia imesema w a n a j e s h i w a k e wamewauwa na waasi wa Yemen waliofanya s h a m b u l i z i l a o l a kwanza kubwa dhidi ya nchi hiyo tangu kuanza mashambulizi ya angani yanayoongozwa na Saudia nchini Yemen mwezi uliopita

    Wizara ya ulinzi ya Saudi Arabia imesema kuwa wanajeshi wake watatu wameuliwa katika mapambano hayo baada ya waasi wa Houthi kuvilenga vituo vyao vya uangalizi, ambapo jeshi lilijaribu kuzuia shambulizi hilo.

    K w a m u d a s a s a kumekuwa na mapambano makali kati ya wanajeshi wa Saudia na washirika wake na wapiganaji wa Kihouthi nchini Yemen lakini hii ni mara ya kwanza kwa jeshi la Saudi Arabia kuripoti kuhusu shambulizi la waasi wa Houthi katika mipaka yake.

    K a t i k a m j i m k u u Sanaa, mashambulizi mapya kutoka angani yanayoongozwa na Saudia yalifanywa katika uwanja wa ndege, ikiwa ni siku chache tu baada ya ndege za kivita kuilipua njia ya ndege katika uwanja huo ili kuzuia ndege moja ya Iran kutua.

    Wa k a t i h u o h u o , mawaziri wa mataifa ya Ghuba Jumatatu wiki hii walipinga pendekezo la kuandaa mazungumzo katika nchi isiyounga mkono upande wowote katika mzozo wa kisiasa nchini Yemen.

    U m o j a wa M a t a i f a u n a j a r i b u k u m a l i z a operesheni ya angani iliyodumu wiki kadhaa, na kuzirejesha pande zote mbili katika meza ya mazungumzo.

    Baada ya mkutano wa mjini Riyadh, mawaziri wa nchi za Ghuba walisisitiza kuwa mazungumzo baina ya makundi hasimu ya kisiasa nchini Yemen yaandaliwe nchini Saudi Arabia, ambayo ndiyo inayoongoza muungano wa nchi za Kiarabu dhidi ya waasi wa Kishia Yemen tangu Machi.

    I r a n k w a u p a n d e w a k e i n a p e n d e k e z a kuandaa mazungumzo ya Umoja wa Mataifa katika taifa lisiloegemea upande wowote, ambalo

    Shambulio la Wahouthi laua askari wa SaudiaTofauti Iran na Waarabu kuathiri mazungumzo

    haliwakilishwi katika muungano unaoongozwa na Saudia ili kumaliza vita nchini Yemen.

    Hata hivyo Baraza la Ushirikiano wa Ghuba lenye nchi sita wanachama limesisitiza kuunga mkono juhudi kali zinazofanywa na serikali halali ya Yemen za kuandaa mkutano chini ya mwamvuli wa Baraza hilo mjini Riyadh.

    K a t i b u M k u u w a Baraza hilo Abdullatif al-Zyani, amesema mkutano huo utahudhuriwa na pande zote za Yemen na zinazounga mkono uhalali na usalama na uimara wa Yemen.

    Mkutano wa nchi za Ghuba ambazo ni Bahrain, Kuwait, Oman, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu, ulilenga kuweka msingi wa mkutano mkuu wa viongozi wa Baraza hilo utakaoandaliwa Jumanne wiki ijayo, na ambao pia utahudhuriwa na Rais wa Ufaransa Francois Hollande.

    M g o g o r o h u o umeongeza mivutano katika kanda hilo. Iran i n a y o t u h u m i wa k wa kuwapa silaha waasi wa Houthi, imesema meli zake mbili zilizotumwa katika Ghuba ya Aden zimefika mlango wa Bab al-Mandab, njia muhimu ya bahari baina ya Yemen

    ASKARI wa Saudi Arabia wakiwa wamebeba mwili wa mwenzao aliyeuawa kutokana na vita vinavyoendelea nchini Yemen.

    na Djibouti. Iran inasisitiza kuwa meli zake hizo hazitafika katika mipaka ya bahari ya nchi nyingine.

    Umoja wa nchi za K i a r a b u u m e k u w a ukiishutumu Iran kuwa imekuwa ikiwapa silaha waasi wa Houthi tangu mwaka wa 2009. (DW)

    M w e z i u l i o p i t a , wapiganaji wa makabila ya Yemeni yaliwaua makumi ya wanajeshi wa Saudia na kuwakamata wengine mateka walipoishambulia kambi ya kijeshi iliyopo jirani na mpaka wa Yemeni na Saudia.

    Ripoti kutoka Yemen zilieleza kuwa muungano w a w a p i g a n a j i w a Makabila ya

    Ta k h ya n a H o u t h i walifanya shambulio la kushtukiza katika kambi ya Saudia ya al-Minare iliyopo jirani na mji wa Saada siku ya Jumapili.

    S h a m b u l i o h i l o l i m e 4 e l e z w a k u w a n i kul ipa k i sas i cha mashambulio ya anga ya jeshi la Saudia dhidi ya makabila hayo na kuua.

    Wapiganaji hao pia walikamata idadi kubwa ya silaha na magari kadhaa kutoka kambi hiyo.

    Siku ya Ijumaa askari w a t a t u w a S a u d i a waliuliwa kwa roketi n a w e n g i n e w a w i l i kujeruhiwa na wapiganaji

    wa Kihouthi katika jimbo la Najran lililopo Kusini mpakani mwa nchi hizo.

    April 3, askari wengine wawili wa Saudi waliuliwa katika kutupiana risasi mpakani kati ya askari wa Saudia na wapiganaji wa kikundi cha Ansarullah, ikiwa I siku moja baada ya askari mwinginwe kupoteza maisha na wengine kumi kujeruhiwa katika mapigano mpakani hapo.

    Mashambulizi ya anga ya Saudi Arabia dhidi ya wapiganaji wanaopinga serikali ya Yemen yalianza

    Machi 26 mwaka huu. Hata hivyo mashambulizi hayo yanafanyika bila idhini ya bila idhini ya UN yakiwa ni jitihada za kurejesha mamlaka ya Rais Abd Rabbuh Mansur Hadi, ambaye amekimbilia Saudia na rafiki mkubwa wa serikali ya Riyadh.

    Ingawa idadi kamili bado haijatolewa, lakini mpaka sasa mamia ya raia wa Yemen, wakiwemo wanawake na watoto w a m e u l i w a k a t i k a m a s h a m b u l i z i h a y o aya anga, huku maelfu wakijeruhiwa.

  • 14 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 8-14, 2015Makala

    Na Ben Rijal

    Na Ben Rijal

    Mchango wa Waislmau katika maendeleo ya Dunia - 10

    UWANJA WA VIJANA - JIONGEZEE MAARIFACHEMSHA BONGO namba 4

    MAJIBU CHEMSHA BONGO NO:41.Taja katika Quran Sahaba aliyotajwa kwa jina

    katika Sura ipi? Al-Ahzab 33:37, Al-Baqara 2:50, Al-Kahf 18:33. Jawabu: Al-Ahzab 33:37

    2. Siku ipi iliokaririwa sana katika Quran? Ijumaa, Qiyama, Ramadhani. Jawabu: Qiyama

    3. Surah ya kwanza iliteremshwa katika mji gani? Jawabu: Mji wa Makka.

    4. Inakisiwa Quran imetafsiriwa kwa lugha ngapi ikiwa Kiswahili ni lugha mojawapo? 50, 103, 85, Jawabu: 103,

    5. Neno Allah limekaririwa mara ngapi katika Quran? 2,698, 11, 585 Jawabu: 2,698

    6. Mwezi gani wa mwaka uliotajwa katika Quran? Ramadhan, DhulQada, Jamadul Thani. Jawabu: Ramadhan

    7. Katika Surah Rahman ni mara ngapi kalima 'fabi ayye aalahi rabbikuma tukazziban' limekaririwa? Mara 50, 125, 31 Jawabu: 31

    8. Ni nani aliozaliwa pasi kuwa na mama? Jawabu : Bibi Hawa

    9. Mtume yupi alikuwa na ujuzi wa Usaremala? Idriss, Ebrahim, Nuh. Jawabu: Mtume Nuh

    10. Mtume gani alikuwa akisarifu vyuma? Suleiman, Daud, Yahya. Jawabu: Mtume Daud

    I B N Z u h r anatafautiana kidogo na wasomi wenzake w a l i o m t a n g u l i a katika ilimu. Ibn Zuhr alijishughulisha zaidi na taaluma ya utibabu ingawa haimanishi alikuwa mbumbumbu katika taaluma kama hesabati , i l imu ya nyota n.k.

    Ibn Zuhr jina lake kamili ni Abu Marwan Abdal Malik Ibn Zuhr n a k a t i k a n c h i z a Ulaya alibatizwa jina la Avenzoar. Msomi huyu wa el imu ya utabibu aliozama katika upasua j i a l iza l iwa katika mji wa Seville nchini Uspaini (Spain) k a t i k a m wa k a wa 1094. Alifuzu somo la utabibu katika Chuo wa Cordoba na kutakhasus na elimu ya utibabu.

    I b n Z u h r a n a t a f a u t i a n a n a w a s o m i w e n z a k e w a n y a k a t i h i z o k w a n i a l i z a l i w a kutokana na ukoo wa watu waliokuwa wakijiweza na kuweza kusomeshwa yeye na dada zake wawili katika Chuo cha Cordoba na hao dada zake wawili baadaye wakawa ndio madaktari katika kasri ya mtawala Almohad.

    Baada ya kuhitimu m a s o m o y a k e y a utibabu huko Seville na kuwa anafanya kazi ya utabibu, alitokea kuwa s io wenye kupewa uso na mtawala hilo lilimfanya kuikimbia nchi yake na kuangukia M o r o c c o l a k i n i al i fwatwa huko na kuwekwa korokoroni kwa muda mrefu.

    K u k a a k w a k e kifungoni kulimpanua m a wa z o n a b a a d a ya utawala Almohad k u a n g u k a k a t i k a mwaka wa 1162 Ibn Zuhr alifunguliwa jela

    Ibn Zuhrna kufunga virago na kurudi Seville; hapo moto uliwaka kwani alikuwa akisomesha akifanya utaf i t i na a k i f a n y a k a z i y a upasuaji kwa wagonjwa.

    U p e o w a k e w a k u f a h a m u n a k u m u a n g a l i a m w a n a d a m u kat ika mwil i wake kulimpelekea kuikataa n a d h a r i a y a h a l i ya k iak i l i ambayo magwiji wa Kiyunani Hippocrates na Galen walishikamana nayo na hata Ibn Sina naye alikuja kuikumbatia na badaye kuiwacha. Akiwa kama daktari a l i k u wa a n a f a n ya m a j a r i b i o y a k e mengi kwanza kwa wanyama kisha ndio huwafanyia wanadamu na kuaminika kuwa ndio mtu wa mwanzo kuanzisha jambo hili katika fani ya udaktari. Aliweza kugundua mengi kati yaliokuwa yakiwasibu wanadamu kat ika ta f i t i zake . Alikuwa ni mtu wa mwanzo kuelewa upele kuwa unasababishwa na vimelea na kuelezwa kuwa ndio mtu wa mwanzo kukubalika kama Parasitologist. Aliweza kutumia mbinu ya kumlisha mgonjwa k w a n j i a a m b a y o kinyume na i le ya kawaida ya kula kupitia mdomoni. Alifanya kazi ya kuweza kuelewa uvimbe unaotokana na saratani, uvimbe katikati ya mashikio na matatizo mbalimbali ya m a g o n j wa k wa mwanadamu.

    Ibn Zuhr alifika kusema yafwatayo Y o y o t e Y u l e atakayejishughulisha na somo la ndani ya maumbile ya viumbe (anatomy) basi imani yake kwa Allah itazidi.

    Kazi nzito na ilioleta t i j a kubwa ni k i le kitabu alichokiandika kwa anuwani Kitab al-Taisir fi al-Mudawat wa al-Tadbir. Kitabu hiki kiliwafanya Sarton, Guthrie na Ulman wote hao ni watu wa Ulaya ya Magharibi kusema kitabu hicho kilikuwa ni kitabu kilichokamilika katika fani ya utabibu. Kitabu hichi kilifanyiwa tafsiri haraka baada ya kukiandika kwa lugha

    Gwiji la Utibabu Ibn Zuhr

    ya Kiyahudi na ya Kilatino. Kitabu hichi kilifanyiwa tafsiri kwa mara 8 baina ya mwaka wa 1490 na 1554. Tafsiri zake hizi za Al Taysir zilikuwa zinachapishwa sambamba na kazi za Ibn Rushd.

    Ibn Zuhr katika kazi ya usomeshaji alisisitiza kuwa somo la upasuaji l i w e s o m o l e n y e kujitegemea kuweza kuwasaidia madaktari watakaotaka kufanya takhasus katika somo hilo. Siku zote Ibn Zuhr hakuwa anafanya majaribio ya upasuaji wala wa matumizi ya dawa moja kwa mojawa binadamu, bali alikuwa akifanya utafiti kupitia wanyama na kuangalia matokeo yake, akiona kuwa majaribio yake yameleta mafanikio k w a w a n y a m a ndipo anapotumia k wa m wa n a d a m u . Akipendelea kuwatibu wagonjwa wake kwa kuwashauri kutumia vyakula aina maalumu na aliweza kufanikiwa kwa hili ambalo hivi sasa kuna madaktari ambao fani yao ni kushauri malaj i i l i