annuur 1178

20
ISSN 0856 - 3861 Na. 1178 SHAABAN 1436, IJUMAA , MEI 22-28, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu facebook: [email protected] AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST Masheikh wasilimisha Segerea Aliingia Emanuel, anatoka Nassor 'Atiwa Suna' huko huko Gerezani Kasema kweli Mh. Lowassa Ndivyo tulivyo Watanzania Wa chai ya rangi, ya maziwa, lakini… Wote wanaambiwa wapo hotelini Tukimeza chambo tumeumia Al-Shabab wa Nkurunziza watatubamiza Bendera nyeusi, akina ‘Kaisi’, mtego tu… Kutuingiza katika kundi la Wajinga ndio… Waheshimiwa ‘Wakubwa’, Sheikh huyu aelekea kuwa gaidi! Jiulize mwenyewe. Hivi picha hii inaonyesha ‘mtu gaidi’, aliyetakabari, asiyejua kuwa kuuwa, ni dhambi? Je, hii ni sura inayowakilisha ‘jitu katili’, jahili lisilojua kuwa Uislamu unakataza kabisa kusababisha madhara kwa wanawake, watoto na watu wengine wasio na hatia! (Soma zaidi uk. 2, 3 na 10) MAKAMU wa kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad. Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein. Mh. Edward Lowassa wakati wa Harambee ya kuchangia Msikiti wa Patandi Arusha hivi karibuni. SHEIKH Msellem Ali. Allah Ameonya mwenye kwenda kuhiji asivunjiwe heshima, yaani atukuzwe(Al-Maaidah:2). Kwa mapenzi ya Allah, huyu amepewa cheo maalum cha "Al-Hajj au HAJJAT". Waislamu hatuna budi tuipende sana Hijja Muda unakwisha! Gharama zote kwa Hijja ni Dola 4,500. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,300. Karibuni Ahlu Sunna Wal Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0765462022;0782804480; 0717224437. Zanzibar:0777468018;0777458075;0777845010. (11) "MWENYE KUHIJI" NI KIPENZI CHA ALLAH!

Upload: zanzibariyetu

Post on 24-Sep-2015

1.275 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • ISSN 0856 - 3861 Na. 1178 SHAABAN 1436, IJUMAA , MEI 22-28, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

    Sauti ya Waislamufacebook: [email protected]

    AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST

    Masheikh wasilimisha SegereaAliingia Emanuel, anatoka Nassor'Atiwa Suna' huko huko Gerezani Kasema kweli Mh. Lowassa

    Ndivyo tulivyo WatanzaniaWa chai ya rangi, ya maziwa, lakiniWote wanaambiwa wapo hotelini

    Tukimeza chambo tumeumiaAl-Shabab wa Nkurunziza watatubamizaBendera nyeusi, akina Kaisi, mtego tuKutuingiza katika kundi la Wajinga ndio

    Waheshimiwa Wakubwa, Sheikh huyu aelekea kuwa gaidi!

    Jiulize mwenyewe. Hivi picha hii i n a o n y e s h a m t u g a i d i , a l iyetakabar i , asiyejua kuwa kuuwa, ni dhambi?

    Je, hii ni sura inayowakilisha j i t u k a t i l i , jahili lisilojua kuwa Uislamu unakataza kabisa k u s a b a b i s h a m a d h a r a k wa w a n a w a k e , watoto na watu wengine wasio na hatia! (Soma zaidi uk. 2, 3 na 10)

    MAKAMU wa kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.

    Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein.

    Mh. Edward Lowassa wakati wa Harambee ya kuchangia Msikiti wa Patandi Arusha hivi karibuni.

    SHEIKH Msellem Ali.

    Allah Ameonya mwenye kwenda kuhiji asivunjiwe heshima, yaani atukuzwe(Al-Maaidah:2). Kwa mapenzi ya Allah, huyu amepewa cheo maalum cha "Al-Hajj au HAJJAT". Waislamu hatuna budi tuipende sana Hijja Muda unakwisha! Gharama zote kwa Hijja ni Dola 4,500. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,300. Karibuni Ahlu Sunna Wal Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0765462022;0782804480; 0717224437.Zanzibar:0777468018;0777458075;0777845010.

    (11) "MWENYE KUHIJI" NI KIPENZI CHA ALLAH!

  • 2 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 22-28, 2015AN-NUUR

    S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.

    www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected] zetu zipo: Manzese Tip Top

    Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

    Tahariri/Habari

    Kasema kweli Mh. Lowassa Ndivyo tulivyo WatanzaniaKWA hakika kasema kweli Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Edward Lowassa. Hivi ndivyo t u l i v y o Wa t a n z a n i a . Hatubaguani kwa hali zetu, dini zetu wala kabila zetu. Ila tu, tunayatambua madaraja yetu.

    Ukiingia katika hoteli zetu za mitaani, utakuta mtu anakunywa chai ya rangi na zege (maandazi yamekatiwa katiwa ndani ya maharage), mwingine chai ya maziwa, omleti na maini au supu ya kuku wa kienyeji na chapati. Kama ni mchana, yupo kaagiza wali wake na m c h i c h a , m w i n g i n e anakula pilau kwa kuku. Lakini wote wanaambiwa wapo hotelini. Wala yule aliyeagiza wali mchuzi juu, hajioni mnyonge. Anakula na kujisikia vyema akamshukuru Mola wake akaendelea na shughuli zake.

    S h a m r a s h a m r a n a shukrani zi l izotolewa A r u s h a b a a d a y a Mheshimiwa Edward L o w a s s a k u s h i r i k i harambee ya uchangiaji fedha za ujenzi wa Msikiti wa Pa t a n d i , a m b a p o z i l ipat ikana za idi ya shilingi milioni 200, inataka kurasimisha hali hii hata katika nyanja za kisiasa na haki za raia wa nchi hii wa dini tofauti.

    Kama vile yule anayeingia hotelini akala ugali wake dagaa akaridhika huku wengine wakila wali maini wakishushia na juisi ya karoti, basi isije ikawa sasa bei ya Waislamu ni michango ya harambee, wakat i wengine , k i la mwaka wanatengewa fungu katika bajeti ya nchi kuendesha miradi yao ya kimaendeleo.

    Kwa mujibu wa hotuba ya Mheshimiwa Ra is Kikwete aliyotoa katika Misa ya kusimikwa Askofu wa Jimbo la Dodoma, Gervas Nyaisonga, Machi 2011, serikali imekuwa i k i t o a m a b i l i o n i y a shilingi kutoka Hazina

    ya Taifa kuzipa taasisi za Kikristo kuendesha miradi yao ya elimu na afya (kupitia Memorandum of Understanding).

    Katika hotuba hiyo Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete alisema kuwa kwa mwaka 2010 serikali iliwapa Wakristo ruzuku ya shilingi bilioni 61 .9 (61 ,900 ,000 ,000) . Ambapo kwa mwaka 2009/2010 walipewa bilioni 50.

    L a k i n i k a m a v i l e kuonyesha kuwa bei ya Waislamu sio kuwekewa M o U , i l i p o t o k e a Waislamu kuhoji kwa nini wao hawapewi pesa hizo na hakuna MoU ya Waislamu na serikali, jibu la serikali lilikuwa kwamba Waislamu hawakuomba. Lakini ni serikali hiyo hiyo, wakati huo Waziri Mkuu akiwa Mheshimiwa S a m w e l M a l e c e l a , Waislamu walipoomba kukutana naye kuwasilisha malalamiko na maombi yao juu ya MoU, serikali haikujali hata kujibu barua yao ya maombi.

    Sasa yote haya, tunadhani ni katika vielelezo vya kutufahamisha kuwa wapo watu wa MoU, wa kula biryani kwa kuku hotelini na wale wa wali mchuzi juu. Tunadhani kisiasa hii haikukaa vizuri.

    S a s a m a a d h a l i Mheshimiwa Edward Lowassa amewaal ika Masheikh na Waislamu waje kumuunga mokono atakapotangaza Safari yake ya Matumani pale Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha, Mei 24, tunadhani itakuwa busara k wa M a s h e i k h we t u kulisema hili.

    Tarehe 24 mwezi huu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid siku hiyo nitasema neno ambalo nitahitaji mniunge mkono.

    "Ukiulizwa unaenda wa p i , s e m a u n a k u j a kuniunga mkono katika safari yangu ya matumaini".

    Hiyo ilikuwa kauli na wito wa Mheshimiwa

    Lowassa kwa Masheikh, Waislamu na watu wote waliokuwa wamehudhuria harambee ya uchangiaji Msikiti wa Patandi.

    Sasa kat ika Safar i h i i y a M a t u m a i n i , tukumbushane kuwa kule hotelini, hakuna shida. Ni kila mmoja na alicho nacho mfukoni mwake. Lakini inapokuja kwa Hazina ya Taifa inayochangiwa na kodi za Watanzania wote, Waislamu na Wakristo, pasiwe tena na wananchi wa MoU wa kupewa zaidi ya bilioni 61 kila mwaka, huku wengine wakiwa bei yao ni harambee ya siku moja.

    Waheshimiwa Wakubwa,huyu aelekea kuwa gaidi!

    Mwaka 1989 Profesa Noam Chomsky alitoa m u h a d h a r a ( l e c t u r e ) ambao ulikuja kurekodiwa na kusambazwa Machi 1990 ukipewa anuwani: Propaganda Terms in the Media and What They Mean: "peace process" has two meanings.

    K a t i k a m u h a d h a r a huo Profesa Chomsky alisema kuwa hutaona au kusikia, hata mara moja katika vyombo vya habari ndani ya nchi hiyo, Marekani ik i laumiwa kuwa inahatarisha amani au inapinga mazungumzo ya kuleta amani, japo kwa vitendo vya wazi kabisa, Marekani inahatarisha amani na kuchafua kabisa amani Mashariki ya Kati na Amerika ya Kusini. Akatoa mifano mingi tu.

    K a t i k a k u f a f a n u a akasema kuwa hutasikia

    wanasiasa wa nchi hiyo wakizungumzia serikali ya Marekani kupinga mazungumzo ya amani au kuhatarisha amani ya nchi yoyote , kwa sababu kila wanalolifanya wao, wanaamini kuwa ndio sah ih i . I l a k i la anayepingana nao, ndio waovu, wavunja amani na magaidi.

    Ndio pale akasema, "peace process" has two meanings.

    Kwamba, kuna tafsiri za kwenye kamusi, ambazo hazifanyi kazi katika siasa za Marekani . Profesa Chomsky anasema kuwa kwa serikali ya Marekani, kila inachofanya kukidhi maslahi yake ya kibeberu, basi hiyo ndiyo amani, ndio ustaarabu na ndio demokrasia, hata kama itakuwa ni kuhatarisha m a i s h a ya we n g i n e , kuvunja haki zao, uhuru w a o n a k u w a p o r a demokrasia yao. Na katika hiki kinachoitwa Vita Dhidi ya Ugaidi, ilitangaza wazi, kwamba kama hupo pamoja na Marekani, basi upo na magaidi. Huna uhuru wa kuchagua.

    Sasa inavyoelekea, na sisi tunaelekea kushika njia hiyo hiyo. Ni zaidi ya mwaka sasa kuna Masheikh, viongozi wa Kiislamu wapo rumande wakipachikwa tuhuma za ugaidi. Mengi yamesemwa juu ya kuvunjwa haki z a o z a k i b i n a d a m u , kiraia na kisheria. Lakini, haionekani kuwa kuna kujali. Kile wanachosema, w a n a o w a t u h u m u , kinaonekana ndio sahihi, huku vikitumika vipengele

    vya kisheria na kauli za kisiasa kuzidi kuwashikilia Masheikh hao, bila kujali hali zao kiafya na hata bila kujali iwapo kuna sababu za kutosha kuwashikilia kwa tuhuma nzito kama hizo.

    Ukisikiliza, maneno y a P r o f . C h o m s k y unachojifunza ni kuwa, ubinadamu ukishakuwa bidhaa adimu, basi lolote linaweza kufanyika na likahalalishwa hata kama lingekuwa jambo ovu kiasi cha kumfanya hata shetani kuona vibaya kulisogelea.

    Yupo Bwana mmoja aliwahi kufika nyumbani k w a M t u m e ( s . a . w ) akamkuta Mtume akiwa kawapakata na kucheza na wajukuu zake. Yule Bwana akashangaa sana. Akasema, yeye ana watoto wengi, lakini hajawahi kucheza n a o , k u w a k u m b a t i a hata kuwabusu kama a n a v y o f a n ya M t u m e (s.a.w). Jibu la Mtume (s.a.w) kwa Bwana yule lilikuwa kwamba, kama ameondokewa (kama hana) mapenzi ndani ya moyo wake wa kuwapenda watoto wake, hana la kumsaidia.

    S i s i t u n a d h a n i jambo hili kuna haja ya kutizamwa kibinaadamu. La kama viongozi wetu na wanaowangangania M a s h e i k h h a o , wameondokewa na hata ile chembe ya ubinadamu, sasa hapo la kufanya ni kumlilia Mwenyewe Allah Mtenza Nguvu kwa Dua, Itqaaf na Swaumu. Tunaamini Yeye, hadhulumu mtu na hakuna pazia baina Yake na Dua ya mwenye kudhulumiwa.

    KILIO cha Masheikh wanaoshikiliwa bila ya kesi zao kuzungumzwa h u k u w a k i n y i m w a dhamana, kimepiga hodi Bungeni baada ya mbunge kuhoji, hatma yao.

    Alikuwa Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Mheshimiwa Maryamu Salum Msabaha kutoka Pemba, aliyetaka kujua nini hatma ya Masheikh hao ambao wanashikiliwa kwa zaidi ya mwaka sasa.

    Mheshimiwa Maryam alisema kuwa ukiacha k u w a w a m e t o l e w a

    Mbunge ahoji kulikoni Masheikh wa UAMSHOVipi ingekuwa ni MaaskofuSpika Makinda aingilia kati

    Na Mwandishi Wetu Zanzibar, ambayo ni nchi na kuletwa Bara, lakini bado kumekuwa na kushikiliwa huku wakinyimwa haki ya dhamana.

    Alisema, kama wana kesi ya kujibu, basi kesi i n g e z u n g u m z w a n a kuhukumiwa ikajulikana kuwa ni wakosa.

    L a k i n i w a m e k u w a w a k i s h i k i l i w a b i l a kesi kumalizika huku wakinyimwa dhamana.

    Maryam alihoji, hebu ifikiriwe kama ingekuwa ni Maaskofu na Mapadiri, nao wangefanyiwa hivyo. Na kama wangefanyiwa, hali ingekuwaje.

    Hata hivyo, kabla ya kumaliza hoja yake mbunge huyo, Spika Mheshimiwa Anne Makinda alimkatisha kuwa alikuwa akiongea mambo yaliyo nje ya mada.

    Wiki iliyopita, gazeti hili liliarifu kuwa hali za watuhumiwa wa ugaidi ni mbaya na baadhi yao walikuwa wamegoma kula.

    S h e i k h F a r i d H a d Ahmed akizungumzia hali hiyo, mbele ya Hakimu wa Mahakama anayesikiliza kesi yao, Renatus Rutta, alisema kuwa kumekuwa na udhalilishaji mkubwa

    Inaendelea Uk. 4

  • 3 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 22-28, 2015Habari

    Masheikh wasilimisha SegereaW A F U N G W A n a Mahabusu katika Gereza la Segerea, Jijini Dar es Salaam, wameendelea kupata Daawa gerezani humo na kusilimu kwa nyakati tofauti.

    Kazi hiyo imekuwa ikifanywa na Waislamu walio katika gereza hilo walio nyimwa dhamana takriban mwaka mmoja sasa, kwa tuhuma za ugaidi, akiwemo Sheikh Mselem.

    A k i o n g e a n a A n nuur katikati ya wiki h i i , mfungwa mmoja aliyemaliza kifungo chake katika gereza hilo na kurejea uraiani, amesema aliingia gerezani akiitwa Solo Emanuel Malaja, akiwa Mkristo, muimba kwaya, na sasa anatoka akijulikana kwa jina la Nassoro Emanuel Malaja.

    A l i s e m a , b a a d a ya kusilimu alibaini kasoro aliyodumu nayo akiwa M k r i s t o , n a i l i a w e Muislamu safi, alilazimika k u h i t a j i h u d u m a ya k u f a n y i w a T o h a r a (kutahiriwa) kwa Masheikh gerezani humo.

    Baada ya kusil imu nilibaini bado sijakamilika kutokana na mafundisho ya Uislamu niliyokuwa nikiyasoma kupitia vitabu vidogo vya Ki is lamu walivyokuwa wakinipa Masheikh, kabla sijasilimu.

    Sikutaka nifiche kitu, niliwaambia kutokana na mila ya kwetu (Usukumani) na dini niliyotoka kutokuwa na muongozo wa jambo hilo, hivyo nilikuwa bado sijafanyiwa suna. Alisema Bw. Malaja.

    Alisema, katika vitabu alivyosoma akiwa gerezani, kabla hajasilimu, alijifunza kuwa kufanya sunna (tohara) ni katika hatua ya usafi kwa Muislamu na ukamilifu.

    Bw. Malaja (27) alisema, wapo wengi wanapata m a f u n d i s h o h u m o gerezani na wengine w a n a s i l i m u k w a n i Masheikh wanatumia v i t a b u m b a l i m b a l i wanavyopelekewa na Waislamu katika kufikisha mafundisho ya Uislamu gerezani humo.

    Bw. Malaja amesilimu Januar i 1 , 2015 , kwa usimaizi wa Ustadh Salum, kisha kuchagua jina la Nassor.

    Mimi nimefuata dini sahihi, sijafuata ushabiki au maslahi, kuwa kwangu gerezani nimepata fursa ya kujifunza upande wa pili wa Dini ya Kiislamu baada ya kukutana na Masheikh na Waislamu waliopo gerezani. Alisema

    Na Bakari Mwakangwale Bw. Malaja.Alisema, katika maisha

    yake ndani ya Ukristo, a m e s h a w a h i k u w a m wa n a k wa ya k a t i k a v i k u n d i m b a l i m b a l i hususani katika Mji wa Kahama.

    N i k i w a K a h a m a , niliimba katika kwaya m b a l i m b a l i n i k i w a kiongozi na mtungaji na mara ya mwisho nilikuwa katika kwaya moja inaitwa AIC iliyopo katika kijiji cha Bufuko, nje kidogo ya Mji wa Kahama. Alisema.

    Alisema, mara baada ya kufanya maamuzi ya kusilimu, alipata lawama kutoka kwa baadhi ya Wakristo wenzake gerezani humo, wakimueleza kuwa atakuwa gaidi , huku akiwajibu kuwa amesilimu kwa kue lewa ukwel i kuhusu imani ya dini ya Uislamu.

    A l i s e m a , w a t u w a m e k u w a wakiwaaminisha kuwa ndani ya Uislamu kuna ugaidi, lakini akasema kwa jinsi alivyosoma baadhi ya v i tabu kwa muda mchache, hajaona mahala ambapo kuna chembe ya mafundisho ya Ugaidi, zaidi ya kubaini kuwa Uislamu ni dini nzuri na ustaarabu.

    Kwa kawaida mt i wowote ukiwa na matunda mazuri na matamu ni lazima utapigwa mawe na kushambuliwa na kila mtu au wadudu, pengine hata kabla hayo matunda hayajaiva. Alisema Bw. Malaja.

    Akielezea sababu ya kuwa karibu na Masheikh gerezani humo kabla ya kusilimu, alisema ni baada ya kukutana na Sheikh Mohammed Isyaka Yusufu, (Mshatakiwa namba sita) ambaye aliwahi kuwa bosi wake mwaka 2007, Sumbawanga katika duka la vyakula.

    A l i s e m a , b a a d a ya kumuona alimfuata na kusalimiana naye, kisha naye aliwatambulisha kwa Masheikh wenzake, kwamba alikuwa kijana wake katika biashara zake Sumbawanga, lakini yeye ni Mkristo na kwamba w a l i m l i n g a n i a , b i l a mafanikio.

    A l i s e m a , w e n z a k e w a l i m u e l e z a k u w a huwa halazimishwi mtu kufuata haki, ila akizidi kulinganiwa na akiujua u k w e l i , m w e n y e w e ataufuta tu, na haipaswi kumkatia tama.

    B w . M a l a j a aliyehukumiwa kifungo kwa kosa la kununua pikipiki ya wizi, alisema awali alikuwa mahabusu, na baada ya kuhukumiwa

    kifungo alipewa kitengo cha kusaidia jikoni, jambo ambalo lilimfanya awe karibu zaidi na Masheikh hao kwa mahitaji yao mbalimbali, hususani maji kutokana na shida ya maji gerezani humo.

    Zaidi alisema, alipewa jukumu la kumuhudumia Ustadh Salumu baada ya kurejea kutoka katika m a t i b a b u a l i y o p a t a hospitali ya Muhimbili, hatua iliyomfanya kuwa karibu zaidi na Waislamu wengine walio katika kundi la Sheikh Mselem na wenzake.

    A l i s e m a , k u t o k a n a n a m a r a d h i ya U s t . Salumu, aliwekwa katika selo maalumu ambayo h u w e k wa wa g o n j wa na raia wa mataifa ya nje ambapo humo pia alikuwemo Mzungu, raia wa Uingereza, ambaye ni Muislamu.

    A l i s e m a , M z u n g u huyo aliyemtaja kwa jina la Hassan, pia alikuwa ni rafiki yake wa karibu kwa muda mrefu gerezani h u m o , h i v y o k w a kushirikiana na Masheikh, naye alitumia ukaribu wao kumuelimisha kuhusu dini kwa ujumla.

    Baada ya mimi kuwa mgumu kwa Masheikh, wao walimtumia Mzungu (Hassan) kunielimisha zaidi ambaye yeye alikuwa akinifuata hadi j ikoni akiwa na shida. Alisema.

    Alisema, awali Masheikh w a l i k u w a w a n a m p a vitabu vidogo vidogo vya Kiislamu, vilivyo andikwa Kiswahili, Kiingereza na Kiarabu lakini alikuwa

    akivikataa.Hata hivyo alisema,

    walipomtumia Mzungu ( H a s s a n ) , a l i a n z a kuvipokea na kuvisoma usiku na mchana.

    K u n a s i k u m o j a walinipa vitabu viwili, k i m o j a k i k u b wa c h a K i i s l a m u ( M s a h a f u ) pamoja na Biblia, (Agano la Kale na Jipya) ambapo waliniandikia sehemu maalum za kusoma katika Msahafu na Biblia.

    Ni l i soma k ipande kwa k ipande kutoka katika vitabu hivyo, kweli nilipata mambo mapya ya kujifunza na nilitafakari zaidi kuhusiana na imani za dini hizi mbili katika kumuabudu Mungu. Alisema.

    Hata hivyo akasema, matukio na matendo machafu, kuingi l iana kinyume cha maumbile, gerezani humo, nayo yalimfanya atafakari sana kiimani, kwani alidai mambo hayo yamekithiri sana, lakini kwa wafungwa Wa i s l a m u n i n a d r a kuyaona.

    Maana wale rafiki zangu wa kiimani kabla sijasilimu (Wakristo) walikuwa na mambo hayo ilifika kipindi mpaka niliamua kuachana nao na nilikuwa naona tabu hata kula nao pamoja, lakini nikiwa na Waislamu mambo hayo huyakuti wala huyasikii.

    Ha l i h i i i l i chang ia k u i n g i a k w a n g u katika Uislamu ambao mafundisho yake yamejaa ustarabu na inakemea wazi wazi tofauti na upande

    niliotoka. Alisema Bw. Malaja.

    Alisema, Desemba 29, 2014, alipopeleka maji ya moto kwa Ust. Salumu, aliwakuta Shekh Nondo, A b u b a k a r M g o n d o , pamoja na Jihadi Jaribuni, ambapo walimpa darsa zito na kumfafanulia zaidi yale aliyo yasoma.

    Baada ya hapo ilipofika, Januari 1, 2015, nilipo peleka maji kwa Ust. Salumu, akiwa na Hassan (Mzungu) niliwaeleza kuwa sasa n ipo tayar i kus i l imu baada ya kujiridhisha na mafundisho ya Uislamu pamoja na nasaha zenu.

    Walienda kuwaita Sheikh Jihadi, Abubakari pamoja na Nondo, ambao kwa pamoja walifika pale na kunisilimisha rasmi, kisha waliniambia nichague jina, nikachagua jina la Nassoro. alibainisha Bw. Nassoro Malaja.

    A l i s e m a , b a a d a ya kusilimu alikabidhiwa kwa Mzungu (Hassan) ili amfundishe hatua za awali za kuiendea ibada (Kuswali) ambaye alianza kunifundisha mambo mbali mbali ya awali ya Uislamu.

    Alisema, hapo ndipo l i l i p o k u j a s u a l a l a kufanyiwa Tohara, baada ya kuwaeleza, ambapo alisema Ust. Jihadi na Hassan walisema wao wana pesa ambazo walizikabidhi wakati wakiingiia gerezani, h i v y o wa t a o n g e a n a uongozi ili kiasi fulani kitumike katika gharama za kumshughulikia.

    Alisema, jukumu hilo alikabidhiwa Daktari wa hapo Segerea, aliyemtaja kwa jina la Hamisa, ambaye naye alilisimamia kwa kumletea Daktari kutoka Gereza la Ukonga, ambaye alimfanyia Suna humo humo gerezani.

    Bw. Nassoro (Solo) kwa sasa yupo J i j in i Dar es Salaam, chini ya Kamati ya Maafa ya Shura ya Maimamu, ambayo inafanya mchakato wa kumtafutia Chuo cha mafunzo ya Dini, ikiwa ni ombi lake la kusaidiwa kuusoma Uislamu.

    Katibu wa Kamati hiyo, Ustadhi Ally Mbaruku, ametoa wito kwa Wadau wa elimu katika vyuo vya Dini, kuwasiliana na Kamati, (0655/0784 816 040) ili kuweza kumsaidia kielimu Muislamu huyo mpya, aliyesilimu akiwa Gerezani.

    NASSOR Emmanuel Malaja (Solo)

  • 4 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 22-28, 2015Makala

    Mbunge ahoji kulikoni Masheikh wa UAMSHOInatoka Uk. 2waliofanyhiwa.S h e i k h F a r i d H a d akimpa Hakimu historia fupi ya kesi yao iliyopo mbele yake, alisema kuwa, wamebambikiziwa kesi ya ugaidi kwa kudai nchi yao huru ya Zanzibar na kusema mfumo wa M u u n g a n o u l i o p o hawautaki.

    Alisema, kesi yao ni ya kisiasa na si vinginevyo na kwamba, walikamatwa na kuletwa bara kuja kudhalilishwa tu na polisi wa kike na wakiume.

    S h e i k h F a r i d alimtambulisha Hakimu h u y o k u w a w a o n i Viongoz i wa Taas i s i mbalimbali na yeye akiwa ni kiongozi Umoja wa Mihadhara na Sheikh Mselem Ali Mselem ni kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho, zote za Zanzibar.

    Sheikh Kama huyu ( M s e l e m ) k a f a n y i wa udhalilishaji mkubwa wa kuachwa uchi wa mnyama huku amening'inizwa kwa p ingu, huyu n i Sheikh anayesoma kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu, akisikika akisoma Qur'an tukufu katika R e d i o n y i n g i k a t i k a Afrika ya Mashariki, lakini anafanyiwa ushenzi kama huo Alisema Sheikh Farid mbele ya hakimu huyo.

    Naye mshitakiwa Salum alimkumbusha Hakimu Rut ta kuwa a l i ah id i kuwa atafuatilia hali zao gerezani na kuhoji mbona hawakumuona?.

    Alisema yeye ni moja wa wal iodhal i l i shwa na Polisi kwa kutiwa chupa na majiti, lakini

    Ile kesi yao mpaka leo inazunguushwa, ni kwa nini kesi ile isiwekwe wazi ikaamulia mbivu na mbichi. Kama kweli Masheikh wale wana m a t a t i z o a u k a m a wameenda kinyume ama wana kitu gani, basi wahukumiwe wajue kama wamefungwa.

    L a k i n i

    Alichosema Mhe. Maryam Msabaham a n a w a z u n g u s h a , l e o h i i wa m e g o m a kula mnaipeleka wapi S e r i k a l i . M n a s e m a hakuna mgawanyo wa dini. Leo nataka niseme tena kwa kinywa kipana, ingekuwa ni Mapadri na Maaskofu, wamo mle ndani leo kungekuwa na amani Tanzania Bara?

    L e o m n a s e m a ,

    MBUNGE wa Viti Maalum (CHADEMA) Maryam Msabaha toka Pemba.

    Zanzibar ni nchi, sasa ikiwa Zanzibar ni nchi, kwa nini wale Masheikh waliletwa huku.

    Mh. Spika, haya ni masuala ya kuishauri Serikali, ni masuala ya amani. Tunataka amani na utulivu. Zanzibar tunasema Zanzibar njema atakae na aje.

    alisikitishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe ambaye alisema hawajatendewa chochote huku akijua sio kweli.

    Kulingana hali hiyo Sheikh Farid, aliiomba Mahakama kufika katika gereza hilo kuangalia hali halisi ya watuhumiwa hao i l i hatua stahiki zichukuliwe.

    Tunaiomba mahakama k u j a k u l e g e r e z a n i mjionee hali halisi, ili hatua stahiki z iweze kuchukuliwa, vinginevyo subirini kupokea maiti na muingie katika historia ya Zanzibar. Alisema Sheikh Farid Mahakani hapo bila kufafanua zaidi.

    A s k a r i M a g e r e z a a m b a y e h a k u w e z a kufahamika jina lake mara moja, alikiri kuwepo kwa hali hiyo kwa watuhumiwa hao wa ugaidi baada ya Hakimu wa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam anayesikiliza kesi hiyo Renatus Rutta, kupokea maelezo na taarifa hiyo ya Amir Hadi na kumuhoji askari huyo.

    Hakimu alimtaka Ofisa wa Magereza aeleze ni kwa nini watuhumiwa hao watatu hawakufika mahakamani.

    Afisa huyo aliieleza m a h a k a m a k u w a wameshindwa kufika kutokana mgomo na wametoa masharti kuwa wanahitaji Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Zanzibar na wa Tanzania bara pamoja na Jaji Mkuu, wa wa t e m b e l e e h u k o gerezani.

    Watuhumiwa ambao hawakuweza kufika ni Said Amour, Salum na Said Shehe, Sharifu na Abdallah Hassani Hassani.

    Serikali ya Zanzibar imeombwa kutoa ulinzi na kutunza usalama wa Masheikh kuhubiri amani pale wanapotekeleza majukumu yao kutokana na usalama wa Masheikh hao kuwa hatarini muda wote wanapohubiri.

    Khofu hiyo imeoneshwa juzi kwenye semina ya siku moja ya kuhamisisha v iongozi wa dini ya Kiislamu katika kusimamia amani wakati wa uchaguzi mkuu iliyofanyika katika ukumbi wa Shirika la Bima Zanzibar.

    Akisoma majumuisho hayo mbele ya washiriki hao, Ustadh Masoud Hemed amesema wajumbe

    Serikali itoe ulinzi kwa Masheikh wa ZanzibarNa Salma Al

    Ghaithiyyah, Zanzibarhao wameanzimia hayo kutokana na hali ilivyo ya khofu na wasiwasi kwa watu ambao wanahubiri amani na mambo mengine ambapo bado baadhi ya Masheikh wapo ndani kwa kutoa maoni, huku wengine hawajui khatima yao.

    Serikali iwe tayari k u w a p a M a s h e i k h u l i n z i n a k u t u n z a usa lama wao wakat i Masheikh watakapokuwa wanatekeleza Jukumu la kuhubiri amani kama walivyotakiwa na Semina hii . amesema Ustadh Hemed.

    K a t i k a m i c h a n g o y a o , w a m e s e m a wanashangazwa na hali ilivyo tete, ambapo wakati mambo ya l ivyokuwa

    yameharibika, walilitwa Masheikh kutuliza hali ya nchi kuzungumza na wananchi misikitini na katika mikusanyiko jambo lililosaidia kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, lakini sasa ndio wanateseka magerezani bila ya kuhukumiwa.

    Sisi tunashangaa kwa nini tul iweza kuitwa kuhubiri amani wakati ule nchi ilipochafuka tukatakia kufanya sala ya pamoja na kuomba dua lakini kwa nini ishindikane sasa hivi kuna nini? Alihoji Ustadh Hamad.

    Amesema, sio tabia nzuri inayotendeka kuwanyima uhuru Masheikh kutoa m i h a d h a r a h u k u wakiogopa kukamatwa n a p o l i s i k a m a

    walivyofanyiwa wenzi wao zaidi ya 20 ambao wapo ndani zaidi ya mwaka sasa wakikabiliwa na kesi ya ugaidi huko Tanzania Bara.

    W a s h i r i k i h a o w a m e s e m a k a t i b a imeruhusu watu kutoa maoni yao, lakini baada ya kukamatwa watu na kuwekwa ndani, baadhi ya masheikh wamerudi n y u m a k u h u b i r i wakiogopa kwa kuwa hawajui wakati gani na wao watafuatwa na wao na kusingiziwa kesi.

    Aidha katika maazimio Masheikh na viongozi wa Taasisi za Kiislamu watumie hafla mbalimbali za k idini pamoja na mikusanyiko ya kiibada ikiwemo khotuba za Ijumaa

    kuhimiza na kuhamasisha amani na utulivu wakati wa uchaguzi mkuu.

    K a t i k a m a a z i m i o mengine, Masheikh hao wamesema kwa kuwa chanzo k ikubwa cha machafuko Zanzibar ni uchaguzi, basi Tume ya Uchaguzi Zanzibar iwajibike katika kusimamia na kuendesha uchaguzi ulio huru, haki na uadilifu ili kuepusha visababishi vya uvunjaji wa amani katika nchi.

    A i d h a , M a s h e i k h washirikiane na viongozi wa Taasisi za Kiislamu kuandaa Dua ya Kitaifa ya kuiombea nchi amani, u t u l i v u n a u s a l a m a kuelekea uchaguzi Mkuu.

    Wamesema, Semina Inaendelea Uk. 5

  • 5 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 22-28, 2015Habari/Matangazo

    WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MASOMO, CHUO KIKUU CHA INTERNATIONAL UNIVERSITY OF AFRICA, KHARTOUM SUDAN 2015/2016.

    Munazzat Al- Daawa Al- Islamiyya (MDI) ofisi ya Tanzania inayofuraha kuwatangazia wafuatao kuwa wamechaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha INTERNATIONAL UNIVERSITY OF AFRICA kilichopo Khartoum, Sudan kwa mwaka wa masomo 2015/2016. Usajili utaanza tarehe 01/09/2015 masomo yataanza tarehe 13/09/2015.

    SN NAME OF APPLICANT FACULTY1 KHADIJA HIJJA KANDEGE MEDICINE2 AMOUR ISSA SULEIMAN MEDICINE3 NUSURA ABDALLAH SAIDI NURSING4 FAT-HIYA FAKIH ABDALLAH NURSING5 AMINA MOHAMED MAKAME NURSING6 SAFIA ALI HAMAD NURSING 7 ZULEKHA MUDHIHIRI AHMAD PHARMACY8 SULEIMAN SAID SULEIMAN PHARMACY9 AISHA OMARI SAID DENTIST

    10 MUHAMMED SALIM MUHAMMED DENTIST11 AMAN MOHAMED AMAN PETROLEUM12 SALUM ABDALLAH PETROLEUM13 TAKIYU MIKIDADI PETROLEUM14 HARUNA BURHANI PETROLEUM15 ALI ABDULLA KHAMIS PETROLEUM16 HUSSEIN ABOUD HASSAN PETROLEUM17 ALI MASOUD RASHID PETROLEUM18 ALI MIRAJI MSOMI PETROLEUM 19 ABDULRAHMAN MWINYIPEMBE MTORO ENGINEERING20 SALUM KHAMIS NGWALI ENGINEERING21 MARIAM SULEIMAN MZEE LAB SCIENCE22 HAMIDA JUMA HAJI LAB SCIENCE23 SAIDE OMAR AHMED LAB SCIENCE24 AMINA ABOUD DARWESH LAB SCIENCE25 MARYAM ALLIY KILIMA COMP SCIENCE26 ACKRAM S. KIBONAJORO COMP SCIENCE27 JABIR DAUDA AHMAD PURE SCIENCE28 SAMIRA MBARAKA HEMED ECONOMY29 MALIK SHAAME KAI ECONOMY30 AHMED SALIM ALI ECONOMY31 FAHMI ABASI SULEIMAN LAW & SHARIA32 YUSUFU ABDALLAH ISSA LAW & SHARIA33 OMARI SWALEHE OMARI LAW & SHARIA34 KHERI JUMA NASSOR LAW & SHARIA35 SWAALIHINA SAIDI GELLEKO LAW & SHARIA36 YAHYA MUSTAFA NGALAWA LAW & SHARIA37 AULA NUHU HUSSEIN LAW & SHARIA38 HUSSEIN JUMANNE SAADY LAW & SHARIA39 SHABANI LUJAMA MWIZARUBI LAW & SHARIA40 MARYAM SEIF KHAMIS LAW & SHARIA41 WILDAT SULEIMAN MOHAMED LAW & SHARIA42 MAULIDI BAKAR ALI LAW & SHARIA43 AHMED YUSUPH KAISI ISLAMIC STUDIES44 ISSA MASOUD RASHID ISLAMIC STUDIES45 SALMIN RASHID HASSAN ISLAMIC STUDIES46 OMARI ATHUMAN SULEIMAN ISLAMIC STUDIES47 RASHIDI HAMADI YASINI ISLAMIC STUDIES48 ASNALI MUDATHIR MACHEYA ISLAMIC STUDIES49 HASSAN AHMED MFAUME ISLAMIC STUDIES50 DHULKHAIR SULEIMAN ISSA ISLAMIC STUDIES

    KWA MAELEZO ZAIDI FIKA KITUO ULICHOFANYIA MTIHANI AU PIGA SIMU 0786 806662.

    KHAMIS M.A. LIYENIKEIDARA YA DAWA

    WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MASOMO, CHUO KIKUU CHA INTERNATIONAL UNIVERSITY OF AFRICA, KHARTOUM SUDAN 2015/2016.

    Munazzat Al- Daawa Al- Islamiyya (MDI) ofisi ya Tanzania inayofuraha kuwatangazia wafuatao kuwa wamechaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha INTERNATIONAL UNIVERSITY OF AFRICA kilichopo Khartoum, Sudan kwa mwaka wa masomo 2015/2016. Usajili utaanza tarehe 01/09/2015 masomo yataanza tarehe 13/09/2015.

    SN NAME OF APPLICANT SEX FACULTY EXAMINATION CENTRE 1 KHADIJA HIJJA KANDEGE F MEDICINE DAR ES SALAAM 2 AMOUR ISSA SULEIMAN M MEDICINE ZANZIBAR 3 NUSURA ABDALLAH SAIDI F NURSING IRINGA 4 FAT-HIYA FAKIH ABDALLAH F NURSING ZANZIBAR 5 AMINA MOHAMED MAKAME F NURSING ZANZIBAR 6 SAFIA ALI HAMAD F NURSING ZANZIBAR 7 ZULEKHA MUDHIHIRI AHMAD F PHARMACY DAR ES SALAAM 8 SULEIMAN SAID SULEIMAN M PHARMACY ZANZIBAR 9 AISHA OMARI SAID F DENTIST DAR ES SALAAM

    10 MUHAMMED SALIM MUHAMMED M DENTIST ZANZIBAR 11 AMAN MOHAMED AMAN M PETROLEUM DAR ES SALAAM 12 SALUM ABDALLAH M PETROLEUM MWANZA 13 TAKIYU MIKIDADI M PETROLEUM MWANZA 14 HARUNA BURHANI M PETROLEUM MWANZA 15 ALI ABDULLA KHAMIS M PETROLEUM ZANZIBAR 16 HUSSEIN ABOUD HASSAN M PETROLEUM ZANZIBAR 17 ALI MASOUD RASHID M PETROLEUM ZANZIBAR 18 ALI MIRAJI MSOMI M PETROLEUM ZANZIBAR 19 ABDULRAHMAN MWINYIPEMBE MTORO M ENGINEERING DAR ES SALAAM 20 SALUM KHAMIS NGWALI M ENGINEERING ZANZIBAR 21 MARIAM SULEIMAN MZEE F LAB SCIENCE DAR ES SALAAM 22 HAMIDA JUMA HAJI F LAB SCIENCE ZANZIBAR 23 SAIDE OMAR AHMED M LAB SCIENCE ZANZIBAR 24 AMINA ABOUD DARWESH F LAB SCIENCE ZANZIBAR 25 MARYAM ALLIY KILIMA F COMP SCIENCE DAR ES SALAAM 26 ACKRAM S. KIBONAJORO M COMP SCIENCE MWANZA 27 JABIR DAUDA AHMAD M PURE SCIENCE MWANZA 28 SAMIRA MBARAKA HEMED F ECONOMY DAR ES SALAAM 29 MALIK SHAAME KAI M ECONOMY ZANZIBAR 30 AHMED SALIM ALI M ECONOMY ZANZIBAR 31 FAHMI ABASI SULEIMAN M LAW & SHARIA DAR ES SALAAM 32 YUSUFU ABDALLAH ISSA M LAW & SHARIA DAR ES SALAAM 33 OMARI SWALEHE OMARI M LAW & SHARIA DAR ES SALAAM 34 KHERI JUMA NASSOR M LAW & SHARIA IRINGA 35 SWAALIHINA SAIDI GELLEKO M LAW & SHARIA IRINGA 36 YAHYA MUSTAFA NGALAWA M LAW & SHARIA IRINGA 37 AULA NUHU HUSSEIN M LAW & SHARIA IRINGA 38 HUSSEIN JUMANNE SAADY M LAW & SHARIA MWANZA 39 SHABANI LUJAMA MWIZARUBI M LAW & SHARIA MWANZA 40 MARYAM SEIF KHAMIS F LAW & SHARIA ZANZIBAR 41 WILDAT SULEIMAN MOHAMED F LAW & SHARIA ZANZIBAR 42 MAULIDI BAKAR ALI M LAW & SHARIA ZANZIBAR 43 AHMED YUSUPH KAISI M ISLAMIC STUDIES DAR ES SALAAM 44 ISSA MASOUD RASHID M ISLAMIC STUDIES IRINGA 45 SALMIN RASHID HASSAN M ISLAMIC STUDIES IRINGA 46 OMARI ATHUMAN SULEIMAN M ISLAMIC STUDIES IRINGA 47 RASHIDI HAMADI YASINI M ISLAMIC STUDIES IRINGA 48 ASNALI MUDATHIR MACHEYA M ISLAMIC STUDIES IRINGA 49 HASSAN AHMED MFAUME M ISLAMIC STUDIES IRINGA 50 DHULKHAIR SULEIMAN ISSA M ISLAMIC STUDIES IRINGA KWA MAELEZO ZAIDI FIKA KITUO ULICHOFANYIA MTIHANI AU PIGA SIMU 0786 806662.

    KHAMIS M.A. LIYENIKE IDARA YA DAWA

    Serikali itoe ulinziInatoka Uk. 4za aina hii ziendelee kufanyika kwa wadau wengine muhimu wa uchaguzi wakiiwemo watumshi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Polisi, Viongozi wa Vyama vya Siasa na Watumishi wakuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalumu.

    H a t a h i v y o , Vyombo vya Ulinzi na Usalama visijihusishe kwa namna yoyote n a m a s u a l a y a kisiasa, badala yake vitekeleze shughuli zao kwa uadilifu zaidi

    ili kulinda maslahi ya wananchi nay a Taifa kwa ujumla.

    Ustadh Hemed amesema Waislamu w a n a t a k i w a wadumishe amani, utulivu na udugu wao katika kipindi hiki cha kuelekea u c h a g u z i m k u u , bila ya kujali tofauti zao za kivyama na misimamo ya kisiasa.

    L a k i n i p i a wamesema Serikali k u p i t i a W i z a r a y a E l i m u n a Mafunzo ya Amali i i n g i z e m a f u n z o ya amani , udugu n a m s h i k a m a n o

    katika mitaala ya ngazi zote za Elimu n a k u w e p o n a Mkutano wa pamoja kati ya Masheikh na Viongozi wakuu wa Nchi ili kuzungumzia m u s t a k a b a l i Ta i f a kuelekea uchaguzi M k u u h u k u l e n g o likiwa ni kudumisha hali ya amani.

    M a d a m b i l i zimewasilishwa katika semina hiyo ikiwemo k u s i m a m i a a m a n i wakati uchaguzi mkuu iliyowasilishwa na Abdallah Talib na nafasi ya Uislamu katika kujenga amani katika jamii.

    Waislamu wote nchini mnaalikwa kuhudhuria Tamasha la Ujenzi wa Kituo cha Kiislamu Ilongo Mbeya litakalofanyika kuanzia tarehe 05, 12 Juni, 2015.

    Shime Waislamu tujitahidi kuhudhuria kwa wingi. Wasio na wasaa wa kuhudhuria wachangie fedha na vifaa vya ujenzi.

    Tukumbuke, tukifanya hivyo tutakuwa tumefanya biashara na Allah (s.w) kwa mafanikio ya hapa duniani na malipo ya Pepo Quran (61:10-13)

    Usafiri / Gharama: Kutokana na Miundombinu ya barabara kwa sasa kila mkoa utaratibu safari ya Mbeya kupitia Maamir wa Mikoa

    Kwa kupitia Dar es Salaam nauli ni Tshs. 70,000/- kwenda na kurudi Dar. Kuripoti Dar es Salam ni tarehe 04/06/2015 (0689665045/0713 992395).

    Kipindi hiki Mkoa wa Mbeya una baridi, hivyo wanatamasha waje na nguo za kuzuia baridi.

    Wabillah TawfiiqAMIR TAIFA

    TAMASHA LA KITAIFAILONGO MBEYA

    05 12 JUNI , 2015

  • 6 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 22-28, 2015TANGAZO

    Inaendelea Uk. 7

    ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

    Muda wa Kozi ni miaka miwili

    SIFA ZA MUOMBAJI:(a) Awe Muislamu.(b) Awe amefaulu masomo manne (4) au zaidi kwa kiwango cha D au zaidi katika Mtihani wa Kidato cha 4.(c) Atakayekuwa na ufaulu wa kiwango cha D au zaidi katika Lugha ya Kiarabu, Kiingereza, Kiswahili na Elimu ya Dini ya Kiislamu atapewa kipaumbele zaidi.

    Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 15 JULAI, 2015.Fomu za maombi zinapatikana kwa gharama ya Shilingi 5,000/= (elfu tano) katika Tovuti:www.ipcorg.tz na katika vituo vifuatavyo:

    KOZI YA UALIMU WA LUGHA YA KIARABU, KIINGEREZA, KISWAHILI NA ELIMU YA DINI YA KIISLAMU NGAZI YA CHETI

    USIKOSE NAFASI HII ADHIMU - WAHI KUCHUKUA FOMU SASA!

    Bismillahir Rahmaanir Rahiim

    KIRINJIKO ISLAMIC TEACHERS COLLEGE - SAME, KILIMANJARO

    ARUSHA: Ofisi a Islamic Education Panel, Jambo Plastic, Ghorofa ya 2 mkabala na Msikiti Mkuu wa Bondeni, Simu: 0783 552414/0762 817640.KILIMANJARO-Moshi: Msikiti wa Riadha: 0712216490 Same Juhudi Studio mkabala naBenki ya NBC Same: 0757013344.Same: Kirinjiko Islamic Secondary School: 0784 296424/0655 676075.

    Usangi: Falhum Kibakaya: 0787 142054.

    Ugweno: Kifula shopping Centre: Yusuph Shanga: 0784 585776.

    TANGA: Twalut Islamic Centre - Mabovu Darajani: 0715 894111Uongofu Bookshop: 0784 982525.Korogwe: SHEMEA SHOP: 0754 690007.Lushoto: Mandia Shop: 0782 257533Handeni: Mafiga - 0782 105735/0657 093983.MWANZA: Nyasaka Islamic Secondary School: 0717 417685/0786 417685.Ofisi ya Islamic Education Panel, Mtaa wa Rufiji mkabala na Msikiti wa Al-Amin: 0785086770/0714 097362.MUSOMA: Ofisi ya Islamic Education Panel Mtaa wa Karume, Nyumba Na. 05: 0765024623.

    SHINYANGA: Msikiti wa Majengo karibu na Manispaa ya Shinyanga Mjini: 0752 180426.Kahama: Ofisi ya AN-NUUR na Msikiti wa Ibadhi: 0753 993930/0688 794040.

    DAR ES SALAAM: Ubungo Islamic High School: 0756584625/0657 350172.Ofisi ya Islamic Education Panel, Temeke - Msikiti wa Nurul Yakin: 0655144474, 0787119531.

    MOROGORO: Ramadhani Chale-0715704380

    DODOMA: Hijra Islamic Primary School: 0716 544757/0718661992.

    SINGIDA: Ofisi ya Islamic Education Panel, karibu na Nuru Snack Hotel:0786425838/0784 928039.

    MANYARA: Ofisi ya Islamic Education Panel-Masjid Rahma: 0784 491196.

    KIGOMA: Msikiti wa Mwandiga: 0714 717727Kibondo: Marubona Isl. SS. 0714 710802.

    LINDI: Wapemba Store: 0784 974041/0783 488444/0653 705627.

    MTWARA: Amana Islamic S.S. 0715 465158/0787 231007.

    SONGEA: Kwa Kawanga karibu na Msikiti wa Nuru - 0713 249264/0683 670772.

    Mkuzo Islamic High School: 0717 348375.

    MBEYA: Ofisi za Islamic Education Panel Uhindini- 0785 425319.

    Rexona Video mkabala na Mbeya RETCO, 0713 200209/0785 425319.

    RUKWA: Sumbawanga: Jengo la Haji Said - Shule ya Msingi Kizwike 0717 082072.

    TABORA: Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566, 0787 237342.Nzega: Dk. Mbaga 0754 576922/0784 576922.

    IRINGA: Madrastun-Najah: 0714 522 122

    PEMBA: Wete Islamic Sch. 0777 432331/0712772326

    UNGUJA: Madrasatul - Fallah: 0777 125074

    Pandu Bookshop: 0777 462056 karibu na uwanja wa Lumumba.

    MAFIA: Ofisi ya Ust. Yusufu Ally jirani na Msikiti Mkuu: 0773 580703.

    Kwa maelezo zaidi piga simu: 0787 188964, 0784 267762 na 0654 613080

  • 7 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 22-28, 2015Makala

    Profesa Ibrahim Noor Shariff

    Propaganda za udini shuleni Tanzania-3

    KATIKA toleo lililopita, kuna maelezo ambayo hayakuwa yameambatana na picha zilizokusudiwa hivyo, kutokufahamika kama il ivyotarajiwa. Tunakirejea kipande hicho pamoja na picha zake.

    N a h i i ya j u u p i a inamshirikisha Mwarabu

    Nini lengo la wachoraji picha kuficha ukweli?

    katika ukamataj i . Na inayofuata inawashirikisha

    Picha hii imechorwa kuonesha kuwa hakuna wa kulaumiwa katika ukamataji wa watumwa ila Waarabu Waislamu.

    Na katika picha hii pia, wenye kulaumiwa kwa ukamataji wa wanyonge wa Kiafrika ni Waarabu na Waswahili Waislamu.

    Waarabu na Waswahili k a t i k a k i t e n d o kilichofanywa na Waafrika wa Bara. Dhahiri kuwa ukhabithi wa wakamataji wa kweli, yaani makabila ya Waafrika wa Bara yaliyokuwa na nguvu wanatupiwa Waarabu na Waswahili. Kisa ni kwa kuwa ni Waislamu.

    N a h i z i p i c h a zinazofuata kutokana na vitabu vya kusomeshea historia Tanzania hali ndiyo hiyohiyo. Mtwike Mwarabu lawama zote za ukamataji wa wanyonge wa Kiafrika na kuwatia utumwani na kwa kufanya hivyo lengo khasa la kuichukiza dini yao ya Kiislamu litafikiwa katika bongo za watoto vijana katika shule za Tanzania. Lakini hilo halitafikiwa kwa sababu kila kukicha

    wengi wenye kutumia akili zao wanazidi kuuona

    Mwarabu hajulikani wa wapi! Wanawake wa Kiafrika katika zama hizo kweli walikuwa wakivaa vitambaa

    ukweli. Lakini wenye lengo lao la siasa kali za udini ni sawa kwao

    wanaona kuwa haidhuru kitu wakija Waislamu na Wakristo kuuwana siku za mbele, na Tanzania ikawa nchi isiyokalika. Siasa zao kali za udini ni masikitiko makubwa kwa nchi nzima.

    Na hii inayofuata ndiyo naipa nishani kubwa kabisa. Maelezo yanasema, kwa tafsiri: Watumwa wakiwa kazini katika mashamba ya miwa katika West Indies.

    West Indies ni visiwa vilioko Amerika ambako Waarabu hawakuweko huko. Sasa inakhusu nini nokoa achorwe Mwarabu? H a wa wa a n d i s h i n a wachoraji wenye siasa kali za propaganda za udini dhidi ya Waislamu

    Angalia na picha inayofuata. Tena na tena picha za kuchora zinamlaumu Mwarabu kwa ukamataji wanyonge wa Kiafrika na kuwatia utumwani.

    wamefikaje kuidhibiti manhaji (karikulamu) ya kusomeshea historia

    Hata katika mashamba ya miwa ya West Indies ambako Waarabu hawakuweko, wanawalaumu Waarabu kuwa ndio waliokuwa manokowa!

    Ta n z a n i a n a h u k u tunaambiwa Tanzania haina dini?

    Hapana ubaya kufikisha ujumbe, ikiwa ujumbe wenyewe ni sahihi, lakini ikiwa ujumbe si sahihi au umekusudia kupotosha ukweli au kuleta chuki au kuigawa jamii, basi ujumbe huo utakuwa ni wa khatari sana, na kila mpenda haki na usalama wa nchi na jamii zake anatakiwa aupinge kwa kupaza sauti yake, khasa ikiwa wanaofikishiwa ujumbe ni wanafunzi wadogo ambao watakuwa viongozi wetu kesho, na wao ndio watakuwa wanatuamulia mambo yetu na kutuongoza.

    Angalia pia na picha hii ya wafanyabiashara wa Kiafrika. Jaribu utambue propaganda iliomo ndani yake:

    Propaganda si lazima iwemo katika yaliyosemwa a u y a l i y o c h o r w a . I n a w e z a k u w e m o k a t i k a y a l i y o k u w a hayakuzungumzwa au yaliyokuwa hayakuchorwa pia. Katika picha hii tunawaona Waafr ika kutoka Bara wamechukua v i t u v i c h a c h e k a m a ngoma, mikeka, pembe za ndovu (na mmoja katika watu wawili hao,

    Inaendelea Uk. 18

  • 8 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 22-28, 2015Makala

    LINI kilikuwa Kipindi cha Israa na Miiraaj? Tarehe hasa ya tukio la Israa na Miiraaj haifahamiki kwa uhakika. Ibn Kathiyr amenukuu kutoka kwa wanachuoni mbali mbali katika kitabu chake Al-Bidaayatu wan-Nihaayah (3/108) juu ya terehe ya tukio hilo. Wanachuoni wengi wanaona kuwa tarehe hiyo ilikuwa kati ya miezi 12 na 16 kabla ya Hijra yake kwenda Madiynah. Na wa zaidi ya hapo wamekhitilafiana juu ya siku na hata huo mwezi.

    K a b l a y a S a f a r i : Malaika Jibriyl (Alayhis-Salaam) alifungua kifua cha Mtume Muhammad (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam), akatoa moyo wake na kuuosha kwa maji ya Zam Zam. Anasema Anas Bin Maalik (Radhiya Allaahu anhu): RasuluLlaah (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) alichukuliwa katika Israa na Miiraaj kutoka Msikiti Mtukufu wa (Makkah) Kaabah. Watu watatu walimjia (ndotoni) akiwa amelala ndani ya Msikiti wa Makkah kabla Wahyi haujaletwa kwake. Mmoja wao akasema: Ni yupi kati ya hawa watu? Malaika wa kati akasema Yule ambaye ni mbora kuliko wote na Malaika wa Mwisho akasema, Chukueni aliye mbora wao. Mambo haya yalitokea katika usiku huo huo. Usiku huo hakuwaona, lakini aliwaona usiku mwingine ambapo tayari wahyi ulikuwa umeletwa kwake na alikuwa macho amelala lakini alikuwa hadhiri (Ni kawaida ya Mitume wote kulala macho wakati wako hadhiri). Wale Malaika h a w a k u m s e m e s h a bal i wal imbeba hadi wakamfikisha kat ika kisima cha Zam Zam. Miongoni mwao Jibriyl (Alayhis-Salaam) alikuwa akiongoza na kuelekeza kifanyike nini. Alipasua sehemu kati ya koo na kati ya kifua na akatoa vyote vilivyokuwemo kifuani na kuviosha kwa maji ya Zam Zam kwa mikono yake mwenyewe na pia kusuuza sehemu za ndani za mwili na kisha kikaletwa chano cha dhahabu kikiwa na bakuli la dhahabu

    kililetwa ndani ya bakuli mkiwa mkajazwa imani na busara. Jibriyl (Alayhis-Salaam) akachukua vitu hivyo kutoka ndani ya bakuli na kuvijaza kifuani m w a M t u m e k i s h a akachukua viungo vya Mtume pamoja na mishipa ya damu akavijaza kifuani kwa Mtume na kukifunga k i f u a S wa h i y h A l -Bukhaariy Juzuu 9 Namba 608, na Juzuu 5 Namba 227).

    Israa maana yake ni safari ya Mtume (Swalla A l l a a h u a l a y h i wa aalihi wa sallam) yeye akiwa ni mwili wake na akili zake na roho yake kutoka Kaabah huko Makkah mpaka Msikiti wa Al -Aqswaa huko Quds (Jerusalem) akiwa amebebwa na mnyama wa ajabu mwenye kuvutia umbo lake anayeitwa Buraaq na kisha safari ya kurejea kwake Makkah.

    A l - B u r a a q : M t u m e (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) a l i chukul iwa kutoka M s i k i t i w a H a r a m , Makkah mpaka Msikiti wa Al -Aqswaa mj in i Quds juu ya mnyama aitwaye Al-Buraaq akiwa ameambatana na Malaika Jibriyl (Alayhis-Salaam) Mtume (Swalla Allaahu a layhi wa aal ihi wa sallam) alimwelezea Al-Buraaq kuwa, Nililetewa Al-Buraaq, mnyama mrefu wa umbo na mweupe, ni mkubwa kiasi zaidi ya punda lakini ni mdogo kuliko nyumba, ambaye a n a p o k w e n d a m b i o hatua yake ni upeo wa

    macho yake. Nilimpanda mnyama huyo mpaka nikafika Msikiti wa Al-Aqswaa huko Al-Quds ( J e r u s a l e m ) . H a p o nilimfunga pale mahali ambapo Mitume wengine wal ikuwa waki funga wanyama wao. (Swahiyh Al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim)

    A n a s B i n M a a l i k alisema, Katika usiku ambao Mtume alipelekwa mbinguni , Al-Buraaq aliletwa kwake akiwa amefungwa vikuku na ana matandiko, lakini alileta ujeuri kidogo, na ndipo Jibriyl alipomwambia Al-Buraaq Je unafanya haya kwa Muhammad? Hakuna mtu mtukufu aliyewahi kukupanda ambaye ni mtukufu zaidi ya huyu mbele ya Macho ya Allaah. Kisha akatoa jasho. (At- Tirmidhiy na Musnad Ahmad)

    Maana Ya Al-Buraaq Kwa Kiarabu Ni Mwale Unaotoka Katika Mwanga. Leo hii , Wanasayansi w a n a t u a m b i a k u w a mwanga una mwendo kasi zaidi ya vitu vyote duniani. Huenda masafa ya maili 700 milioni kwa saa moja. Miaka 1400 iliyopita wakati ambapo kulikuwa hapajatokea uta f i t i na uvumbuzi palikuwa hakuna mtu ambaye al iweza hata kukisia mwendo kasi wa mwanga wala ukweli wake ukoje. Allaah (Subhaanahu wa Taala) na Mtume Wake (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) w a l i m w i t a m n y a m a huyo kama Al-Buraaq

    kwa msingi wa mwendo wake ulivyo na kasi kali.. Huu ni ukweli ambao unathibitisha ukweli wa Uislamu na ukweli wa Utume wa Muhammad (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) k a m a A l i v y o s e m a Allaah ndani ya Qur-aan, Tutawaonyesha ishara Zetu katika upeo wa mbali na katika nafsi zao wenyewe mpaka iwabain ik ie kwamba haya ni kweli. (Fusswilat 41:53).

    H a p o k a l e w a t u walipinga na kusema mnyama huyo katokea w a p i t e n a a m b a y e a l i m c h u k u a M t u m e (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) kutoka sehemu moja ya dunia mpaka nyingine na kisha kapita naye katika anga za mbingu na tena katika usiku mmoja? Leo hii tunaona vipando ambavyo vimeundwa na binadamu, roketi na misali vikisafiri maelfu ya maili kwa muda dakika chache tu. Iwapo mtu ambaye ni kiumbe cha Allaah Muumba wa Ulimwengu, Je, Allaah kwa nini asiumbe mnyama mwenye uwezo wa kukata masafa ya mamilioni ya maili kwa muda mfupi.

    Kituo cha kwanza cha Safari - Al-Aqswaa: Mtume alisema: Kisha niliingia Msikiti wa Al-Aqswaa, nikaswali Rakaah mbili (Swahiyh Muslim)

    Kuna riwaya nyingine

    ambazo zinaeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu a layhi wa aal ihi wa sallam) aliswali na Mitume wengine hapo msikitini na yeye akiwa Imaam. Msikiti wa Al-Aqswaa umekuwa na sifa ya kuwa ni kituo cha Mitume wote. Toka siku ya Al-Khaliyl Ibraahiym ( Alayhis -Salaam) hivyo Mitume wote walikusanyika hapo na Mtume Muhammad (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) akawa Imaam wao. Hii ni dalili ya nafasi kubwa aliyo nayo Muhammad ambaye ni Mtume wa mwisho miongoni mwa Mitume wengine (Alayhimus- Salaam). [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

    K i s a c h a I s r a a n a M i i r a a j k i m e e l e z wa ndani ya Qur-aan (Al-Israa 17:1) Aayah inayofuatia inaeleza matendo ya aibu na makosa ya Mayahudi na kufuatia juu ya hayo makemeo makali ya Qur-aan. Mpangilio huo si kwa bahati tu, Al-Quds ( J e r u s a l e m ) i l i k u wa ni ki tuo cha kwanza cha safari hii ya Usiku na hapa kuna ujumbe a m b a o u n a e l e k e z wa k w a M a y a h u d i n a kupewa ujumbe kuwa hadhi waliyokuwa nayo ya kuongoza dunia na binadamu kwa ujumla imetanguliwa. Utenguzi wa uongozi kwa mayahudi ulitokana na mabaya yao waliyokuwa wakiyafanya n a y a l e a m b a y o wanaendelea kuyafanya.

    U j u m b e h u o unathibitisha wazi wazi k u w a u o n g o z i h u o umehamia kwa Mtume M u h a m m a d ( S wa l l a Allaahu alayhi wa aalihi wa s a l l a m ) a c h u k u e u o n g o z i w a m a k a o makuu ya Aqiydah ya Baba Ibraahiym na pia kuwa makao hayo sasa ni Makkah na Msikiti wa Mbali (Al-Aqswaa) huko Al-Quds ( Jerusalem). Hivyo mamlaka hayo yalihamishwa kwenda kwenye tai fa ambalo ni la Wacha Mungu na lenye utii kwa Allaah p a m o j a n a M t u m e ambaye amependelewa kubeba Qur-aan ambayo inaongoza watu kuelekea kwenye ukweli. [Ibara imechukuliwa kutoka katika kitabu Ar-Rahiyqul-Makhtuum].

    Safari ya Israa na Miiraaj

    Inaendelea toleo lijalo

    MASJID Nabawi Madina.

  • 9 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 22-28, 2015Makala

    WEWE tu tunakuabudu. (Al-Fatiha:5)Kama tunavyojuwa sote na kama ilivyokuja katika tafsiri zote kwa hakika madhumuni ya undani hapa kutokana na kumtanguliza mtendwa, madhumuni hayo kwa ufupi: Ee Mola wa h a k i , h a k i k a s i s i tunakiri na hatuukubali isipokuwa uungu wako na hatunyenyekei kwa yeyote asiyekuwa wewe na hatupati utulivu na upole na kuliwazika isipokuwa mbele zako.

    Na undani mwengine, ambao unastahiki kuandikwa hapa undani huo ni kwamba badala ya kutumiwa tamko l i l i lop i ta Ameabudu limekuja tamko la muda wa sasa wa kitendo hicho hicho Tunaabudu kwa sababu tamko la kitendo kilichopita linakusanya maana mengi, mifano ya tumeabudu tumeswali tumefanya hivi na vile. Maana kuna baadhi ya maana ya kudanganyika ambayo hayakubaliani na moyo wa ibada na uja.

    A m a k a t i k a t a m k o : Tunaabudu haipatikani ishara yoyote, kwa mfano wa ubaya wa kufahamu h u k u , k w a k i t e n d o tunaabudu kinaashiria kwenye kushindwa kwa binadamu na uhitaji wake m b e l e z a h a d h a r a ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuendelea kuuelewa ushindwaji huo na tunaweza kuyafupisha yale ambayo anayataka binadamu hapa kama hivi:

    Ee Bwana wangu, kwa hakika nimeifunga azma yangu juu ya kutoyatoa muhanga uhuru wangu wala kuidhalilisha nafsi yangu kwa yeyote as iyekuwa Wewe. Kwa sababu hiyo, mimi ninaelekea kwako na kwenye mlango wako kwa ujio wa nafsi yangu, kwa niya ya utumwa na udhalili, na ninaelekea kwenye ibada yako na twaa yako, kwa nafsi iliyojaa shauku na mapenzi, hali ya kuifunga azma juu ya kujiepusha na maasia yako na yote usiyoyapenda na usiyoyaridhia, niya yangu ni kubwa sana na bora kuliko

    Mafundisho ya Quran

    matendo yangu na mimi nina nyenyekea kwako, ninakuomba nikubali niya yangu kutokana na kutenda mbele zako kwa kukifanyia k a z i k i p i m o c h a ya l e ninayonuiya kuyatenda, na si kwa kipimo cha yale ambayo nimekwisha kuyafanya. Ee Bwana wangu.

    K i s h a h a k i k a y e y e anasisitiza kwamba yeye hakuwa peke yake katika uwanja wa matara j iwa na kunyenyekea huku, bali anasema, kwa hakika ndugu zake wanashirikiana naye katika matarajiwa na unyenyekevu huu maana anaonyesha hapa uzuri wa dhana pana yenye kuenea. Na wakati huo huo anakusanya kuunga mkono kwao na kushiriki kwao kwenye upande wake, kwa hiyo anadhamiria muafaka na makubaliano ambayo hawezi kuyatia kasoro na yaliyokuwa yeye anaelekea kwenye mlango wa mwenye kukidhi mahitaji kwa hiyo anajiepusha na wasiwasi wa shetani na anatoa sura kamili ya uja uliyokamilika mbele za Mungu uliyokamilika ambao hauna mpaka.

    (1) Alif Lam Mym. (2) Kitabu hicho hapana shaka ndani yake, ni mwongozo kwa wenye kumcha Mwenyezi Mungu [Al-Baqarah 1-2]

    Tamko (HUDAN) ambalo limekuja katika aya tukufu, tamko hilo limo katika mfano wa Masdar chembuko la neno na linabeba maana ya k wa m b a b i n a d a m u hawezi kufikia kwenye uongofu na kwenye lengo linalotazamiwa nyuma ya tamko hilo pasi na juhudi yake iliyotakata na kwa maelezo mengine kwa hakika sisi vile vile tukichunguza kwa mazingatio TANWIN-

    tutajuwa kwamba kitabu hiki ambacho haipatikani ndani yake chembe yoyote ya shaka, ndilo chimbuko la uongofu kwa wenye kumcha Mwenyezi Mungu. Kwa wenye kumcha Mwenyezi Mungu tu, kwa sababu nafsi zao zimeepukana na shaka na matatizo na nyoyo zao na roho zao zimeelekea kwenye kuukubali ukweli na kuzichunga kanuni za maumbile za Mwenyezi Mungu na sharia yake tukufu na nafsi zao zimetakata na z imej iandaa kuukubal i uongofu na kufaidika nao na sina kuwazuia na jambo hilo fikra yoyote au hukumu iliyotangulia.

    Isipokuwa ni kwamba tamko HUDAN l i l i lo mwishoni mwa aya wako juu ya uongofu kutoka kwa Bwana wao. [Al-Baqarah 5] limetajwa kwa mfuo wa Masdar chembuko la tamko, maana ni kwamba Mwenyezi Mungu mtukufu huenda akawafanyia ukarimu waja wake kwa uongofu pasi na kupatikana uhusiano wa sababu na matokeo ambayo ameyaumba na akayafanya ni katika sababu za uongofu. Na mlango wa kumcha Mwenyezi Mungu ndiyo mlango ambao unafikisha na unafunguka juu ya ukarimu huu na utoaji. Na daraja la kwanza la mfano wa uchaji huu ni imani na maarifa ya kweli na daraja la mwisho ni kufika kwenye kupata radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kama ilivyokuja katika maelezo ya wazi yaliyopitishwa ya aya kwamba, hatafika na hatapata nja ya kuokoka isipokuwa yule aliyefika k we n ye k i wa n g o h i k i cha uongofu. Kisha kwa hakika pamoja na mtiririko

    wa aya na kuwa uongofu umefungamana na kupatisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa huo uongofu, kwa hakika kufika kwa binadamu kwenye amani na usalama na kwenye utulivu katika dunia na kwenye kufuzu siku ya Kiyama na kunarejea kwenye kipimo kikubwa kwenye mwenendo wake na matendo yake ambayo anayadhihirisha kwa matakwa yake yaliyo huru.

    K w a m s i n g i h u o , kunawezekana na kusema kwa ufupi: Kwamba tamko (HUDAN) la kwanza ni sababu na tamko (HUDAN) la pili yakiwa matokeo, likiwa limepakwa manukato ya upole na wema na matamko yote mawili ni majibu ya maombi ya ( tuongoze) ambayo limekuja katika Surat Al-Fatiha na ni ufafanuzi vile vile wa namna ya mwenendo wa wale wenye kupatikana juu ya njia.

    Ndani ya nyoyo zao pana ugonjwa akawazidishia Mwenyezi Mungu ugonjwa, [Al-Baqarah 10]

    Imekuja katika baadhi y a t a f s i r i k w a m b a : Akawazidishia Mwenyezi Mungu ugonjwa maneno hayo ni katika mlango wa malipo na katika j insi ya matendo. Isipokuwa ni kwamba mimi naona k wa m b a n i b o r a s a n a kukaribia kwenye maana ya aya kama hivi:

    Hakika Mwenyezi Mungu amewaongezea ugonjwa katika nyoyo zao kwa sababu wao wamejichafua k wa s h a r i n a m a a s i a mbalimbali katika kiwango cha niya na kila wanapokuta kuwa fursa iko tayar i , wanajitahidi kuzihakikisha niya zao mbaya hizo, na kwa sababu zinapozidi, huzidi

    matokeo na hili linamaanisha kuingia kwao ndani ya duara ambayo hana mahala pa kutokea. Maana yake ni kwamba wao hawakuweza kuziokoa nyoyo zao na niya hizi mbaya, bali ni kwamba hawakufikiria kabisa jambo hilo, na niya hizi mbaya zimejaa nia mbaya nyingine juu ya nia hizi yamezaa matendo mengine na kwa sababu ya kuingia katika hii duara ambayo haina mahali pa kutokea, kumepatikana kuangamia kwa wanafiki.

    Mambo yakiwa hivyo, wakati tunapoifasiri aya hii, Akawaongezea Mwenyezi Mungu ugonjwa, ni juu yetu kuyachunguza maana yake kama matokeo ya kitabia ya kuingia katika hii duara isiyokuwa na mahali pa kutokea.

    Kwa hakika afya ya mwili ndiyo msingi na ugonjwa ni jambo l i l i lozuka. Ni hivyo hivyo, maumbile yaliyosalimika ndiyo msingi, n a u g o n j wa wa m o y o ndicho kitu kipya. Kwa sababu hiyo yule ambaye hashughuliki na afya ya moyo wake na kuulinda na kuyashika mashart i yote ya kihali kwa ajili ya kuukinga, atakiacha hiki kitu muhimu kilichowekwa na Mwenyezi Mungu mtukufu kuwa ni tonge nyepesi na laini kwa virusi na bacteria mbalimbali. Ijulikane kuwa pamoja na kuwa mwanzo huenda ukawa ni kitu kidogo sana, kwa hakika kuhama kutoka katika makosa na kwenda kwenye makosa mengine na kutoka katika dhambi na kwenda kwenye dhambi nyingine na kutoka katika maasia na kwenda kwenye maasia mengine, hayo yatapelekea mwishoni kwenye kuchanika ile sehemu na kuingia kwenye maasia makubwa sana ambayo yanapita kiwango cha kutia akilini maana itapelekea kwenye kubwa la maasia yote, nalo ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, kwa sababu kuna njia nyingi sana zinazopelekea kwenye ukafiri.

    Ukiwa uharibifu wa itikadi au kupinduka kati ya mambo yenye kutatiza na shaka ndiyo ugonjwa wa wanafiki, hili linamaanisha wakati huo huo kupatikana kwa hali ya kukubali ambayo imejificha ya ukafiri na upingaji. Iwapo msaada wa Mwenyezi Mungu haukuuwahi ugonjwa huu na havikuvunjika vile vikuku vyenye kufikisha kutoka maasia, na kwenda kwenye ukafiri, kwa hakika maasia kwa sababu ya kuongezeka kwake maradufu, hupelekea k w e n y e k u m k u f u r u Mwenyezi Mungu mtukufu. Bali huzuka mara nyingi kwamba binadamu wakati inapomzunguka shaka, huenda zikawa na sababu ya k u i k a t a n j i a ye n ye kuunganisha kati yake na Mwenyezi Mungu Mtukufu.

    Fethullah-Gulen

  • 10 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 22-28, 2015Makala/Tangazo

    K I A S I w i k i m b i l i zilizopita, vyombo vya habari viliripoti kuwa w a n a o d a i w a k u w a magaidi wa kundi la The Islamic State, wamekiri kuhusika na shambulio k u l e D a l l a s , Te x a s , Marekani. Watu wawili, ambao baadae waliuliwa na Polisi, wanadaiwa kumshambulia askari aliyekuwa katika lindo nje ya ukumbi uliokuwa ukionyesha vikaragosi (cartoons) vikifananishwa na Mtume Muhammad (s.a.w).

    I n a y o d a i w a k u w a Redio ya IS, ikitajwa kwa jina la Al Bayan radio station, inadaiwa kutoa taarifa i l iyodai kuwa washambuliaji wawili wa Dola ya Kiislamu, Elton Simpson na Nadir Soofi, wali fanya shambul io h i l o k u wa t i a a d a b u wanaomkashifu Mtume na Uislamu.

    "We tell ... America that what is coming will be more grievous and more bitter and you will see from the soldiers of the Caliphate what will harm you, God willing".

    Inadaiwa kusema taarifa ya IS kupitia Al Bayan radio, ikitoa kitisho kwa Marekani kuwa shambulio hilo ni mwanzo tu, lakini mashambulio makubwa na ya kutisha zaidi yanakuja kutoka kwa askari wa Khilafah.

    Hata hivyo, ukisoma taarifa hiyo, unachogundua na kilicho wazi ni kuwa ni katika zile zile propaganda za kuteka akili za raia wa Marekani wawe tayari kuunga mkono hatua za serikali yao kupelekea askari Iraq na Syria kwa kisingizio cha kupambana na magaidi hatari wa IS (sio Osama Bin Laden wala Al-Qaida tena).

    K w a m b a h i y o n i sehemu ya propaganda, inathibitishwa na taarifa n a u j u m b e m w i n g i u l i o m i m i n i k a k a t i k a mi tandao ya k i j ami i ikiwapongeza waliofanya shambulio hilo na kutoa vitisho zaidi. Moja ya ujumbe huo katika Twitter unasema

    "How are you (Americans) going to live when we create our lone wolves to be nuclear bombs ... by God, you can't match us and in the heart of your homes you will see".

    Wana mipango mikakati na waandaa propaganda hizi, Wanachowaambia wananchi wa Marekani ni

    Tukimeza Chambo TumeumiaAl-Shabab wa Nkurunziza watatubamizaBendera nyeusi, akina Kaisi, mtego tuKutuingiza katika kundi la Wajinga ndio

    Na Omar Msangi kuwa kama hawataunga mkono mipango ya serikali yao kwenda kuwapiga magaidi wa IS huko huko Syria na Iraq walipo, basi wajue kuwa watakujieni na kukupigeni huku huku Dallas na New York!

    Al-Shabaab wa Nkurunziza

    US warns of al-Shabaab attacks in Burundi ni k i c h w a c h a h a b a r i kilichokuwa kimebeba tahadhari iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Oktoba 2014 ikitahadharisha kuwa Burundi watapigwa na Al-Shabaab. Taarifa hiyo iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ( S t a t e D e p a r t m e n t ) , iliitaka serikali ya Burundi kuchukua tahadhari kwani kulikuwa na taarifa za ki-intelijensia kwamba kundi la al-Shabaab wanaweza kuipiga Burundi.

    W a s w a h i l i w a n a msemo wao, waj inga ndio waliwao. Burundi imefanywa upawa wa kukorogea uji wa moto, m a b e b e r u w a n y w e kwa raha zao. Serikali ya Burundi, kama ilivyo kwa Uganda, Tanzania na Kenya, haikuhusika kwa namna yoyote kuchochea ghasia na kuibuka kwa wapiganaji wa Al-Shabaab. Ni mabebru, wakiitumia E t h i o p i a a m b a o waliivurumisha serikali ya Umoja wa Mahakama za Kiislamu iliyokuwa imeleta amani katika nchi hiyo. Baada ya kuivuruga nchi hiyo, sasa wanaitwa Burundi, Kenya, Uganda, wakapigane kwa niaba ya Beberu aliyetoka maelfu ya maili kutoka huko atokako kuja kuivuruga Somalia kwa masilahi yake. Ili msifike mahali m k a c h o k a , m k a t a k a kurejesha majeshi yenu nyumbani, lazima mtiwe kitanzi na motisha ya kuendelea kuweka majeshi yenu Somalia. Motisha yenyewe ni kutishwa kila wakati kuwa Al-Shabaab wanakuwindeni. Ni magaidi kat i l i na hatari. Kama wanaweza kwenda kupiga Dallas, Te x a s , h a wa s h i n d w i kuja kukubamizeni hapo Bujumbura na Mwanza.

    Kwa hiyo mnapigiwa n g o m a y a k i t i s h o c h a k u s h a m b u l i w a n a A l - S h a b a a b k i l a wakati. Mkikaa kidogo mnakumbushwa kutoka Department of State

    Inaendelea Uk. 11

    TA N G U S e p t e m b a 11 , 2001 , Bin Laden amekuwa zaidi mtajwa asiyekuwepo. Video zake chache au mikanda ya video ilikuwa haiaminiki, na wasiwasi kuhusu kifo chake umesikika mara kadhaa. Hapo Julai 11, 2002, Amir Taberi aliandika katika gazeti la New York Times, "Osama bin Laden amekufa. Habari hiyo kwanza ilikuja kutoka vianzio nchini Afghanistan na Pakistan karibu miezi sita iliyopita: mkimbia sheria huyo al ikufa mwezi wa Desemba na alizikwa katika milima ya kaskazini mashariki ya Afghanistan."

    Akiwa na his ia ya kujisikia inayofanana na Mlima Everest, Osama bin Laden asingeweza kubaki kimya kwa muda wote huo kama bado angekuwa hai (alisema mwandishi huyo. Wakati wote alipenda kutangaza kuhusika na vitu ambavyo hakuwa na uhusiano navyo. Iweje

    Bin Laden: Hivi kweli tunajua nini?Na Linh Dinh

    May 16, 2015 - 'Mtandao wa Kupashana Habari, na 'Lew Rockwell'

    Osama bin Laden

    akae kimya kwa miezi tisa na asijisifu kwa kushinda hatari zote?

    Lakini nje ya video moja yenye utata, Bin Laden hata siku moja hakudai kuhusika na 9/11. Kinyume chake, alikataa mara kadhaa kuhusika kwa njia yoyote kwa mauaji hayo ya watu wengi. Hapo Septemba 28, 2001, alihojiwa na gazeti la Karachi Ummat, gazeti la lugha ya ki-Urdu. Shirika la habari za nchi za nje la Marekani, kitengo cha CIA, lilitafsiri: (Osama alisema yafuatayo:)

    " N i m e s h a s e m a kuwa mini sihusiki na mashambulio ya Septemba 11 nch in i Marekani . Kama Muislamu, najaribu niwezavyo kutosema uwongo. Wala sikuwa na ufahamu wowote wa mashambulio hayo na sioni mauaji ya wanawake, watoto na binadamu wengine wasio na hatia kuwa ni jambo adilifu. U i s l a m u u n a k a t a z a k a b i s a k u s a b a b i s h a madhara kwa wanawake, watoto na watu wengine wasio na hatia. Kufanya

    Inaendelea Uk. 11

    Rais Nkurunziza (katikati)

  • 11 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 22-28, 201511 AN-NUURMakala

    Tukimeza Chambo TumeumiaInatoka Uk. 10au Ubalozini kwamba, jamanae.. Al-shabaab wanakuja! Na hivyo nchi kama Burundi, Uganda na Kenya ambazo tayari zina majeshi kule, lazima zikumbushwe mara kwa mara kwamba mkiacha Al-Shabaab wakishinda, b a s i w a t a k u f u a t e n i huko nyumbani kwenu Bujumbura na Garissa.

    A l i j i s e m a M z e e Al l i Hassan Mwingi kuwa mtoto akibebwa hutizama kichogo cha mamaye, wakati ule yeye akimaanisha kuwa kama Rais atakuwa akitizama mapito ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Sasa Rais Pierre Nkurunziza n a y e a n a t i z a m a kichogo cha mabeberu a n a o wa t u m i k i a k u l e Somalia. Wakati tatizo lililopo ni wananchi wake kumkatalia kugombea urais kwa muhula wa tatu, yeye anageuza mada inakuwa ni ugaidi wa Al-Shabaab.

    Kwa kweli ukichukua msemo huu kuwa Wajinga ndio waliwao, unatukaa vizuri sana. Katika taarifa hiyo ya tahadhari ya kushambuliwa Burundi mwaka jana, ilielezwa kuwa sababu ni kutokana na Burundi kuwa na majeshi Somalia. Taarifa ilisema:

    It is believed that al-Shabaab wish to attack the country because Burundian troops are part of a coalition of African Union (AU) forces which are battling the groups insurgency in Somalia.

    The al-Qaida linked al-Shabab insurgents have claimed recent attacks in Kenya,Uganda and Djibouti, who also sent peacekeepers to Somalia.

    Labda tujiulize, Burundi, au hata Tanzania yetu, na kwa maana hiyo AU iliyo na vikosi vya kulinda amani Somalia, inahusika vipi na kuibuka hao al-Shabaab insurgents? Hivi viongozi wetu hawajui nani alilikoroga Somalia? Hivi hawajui kwa nini al-Shabaab? Nani kaleta huu u-alQaidah katika al-Shabaab na Somalia? Kwa nini hawamwambii aliyelikoroga alinywe m w e n y e w e ! K a m a hoja ni kuwa Burundi itapigwa kwa sababu ina majeshi Somalia, kwa nini Bujumbura isijiulize inafanya nini kule?

    La kusikitisha ni kuwa hao hao wanaotugeuza

    mkakati mwingine wa kuwafanya wananchi wa Ufaransa na Ujerumani waunge mkono uwepo wa majeshi ya nchi zao Afghanistan.

    Moja ya mikakati hiyo imetajwa kuwa ni ku-D r a m a t i z e u n ya m a wa Tal iban dhidi ya wanawake kupitia vyombo vya habar i . Kwamba yakionyeshwa matukio ya kikatili wanayofanyiwa wanawake na kwamba ukatili huo unafanywa na Taliban, basi wananchi wa nchi hizo wataona b o r a wa n a j e s h i wa o wa z i d i k u k a a h u k o wawatokomeze magaidi katili wa Taliban. Lakini v y o m b o v ya h a b a r i vitatumika pia kuonyesha kuwa kama wananchi wa Ulaya wataacha Taliban ishinde, wajue itawafuata huko huko katika miji ya Ulaya. (Soma: Why Counting on Apathy May Not Be Enough)

    Unaposoma taar i fa kama hizi, lazima uwe na wasiwasi kuwa hata yale matukuo ya msichana M a l a l a a l i y e d a i w a kupigwa risasi na Taliban kwa sababu eti anataka kusoma shule, huenda ni katika mambo ya kupanga k a t i k a k u k a m i l i s h a mikakati hii.

    Lakini pia ukitizama jinsi baadhi ya vyumba vyetu vya habari hapa nchini vinavyopigia debe kitisho cha ugaidi, ukirejea matukio ya akina Kaisi na michango yao ya pesa za kununulia tasbih (risasi), ukija na yale ya kukutwa vijana msikitini wakiwa na mi l ipuko pamoja na bendera ya ki-Al Shabaab, Lazima wasiwasi uwe mkubwa k u w a t u m e t u p i w a chambo. Na kwa bahati mbaya baadhi ya vyombo vyetu vya habari, ama kwa ujinga tu au kununuliwa na usal i t i , vimemeza chambo hicho. Vinafanya kazi kwa juhudi kubwa kusimika kit isho cha ugaidi. Wao watanufaika vipi, hata ukiwauliza wenyewe hawajui. Lakini la uhakika ni kuwa kama ni kuangamia, itakayohiliki ni nchi, si watu wa dini fulani pekee.

    Hata hivyo, matarajio yetu ni kuwa ndani ya jamii yetu, ndani ya vyombo vyetu vya usama na ndani ya serikali, tuna watu wazalendo wenye akili zilizofunga vizuri na mambo haya wanayaona kwa mtizamo sahihi.

    k u w a u p a w a w a kuwapoozea uji wa moto, ndio wanaotoa kaul i kuwa tupo katika hatari ya kupigwa kwa sababu tuna vikosi kule. Lakini ndio hao hao wanapotupa mikakati yao ya kutuundia v ikos i vya Counter Terrorism, kama i le ATPU ya Kenya . Na ndio hao hao hutugeuka n a k u t u s h u t u m u kuwa tunakiuka haki z a b i n a d a m u , AT P U wanapotesa na kuuwa watu kikat i l i ! Lakini baya zaidi, mikakati yao inatutumbukiza katika machafuko na maafa zaidi.

    K a t i k a m a k a l a

    E x p l o i t i n g S o c i a l Issues for Mili tarism a n d I m p e r i a l i s m , m w a n d i s h i G l e n n Greenwald ananukua n ya r a k a m b a l i m b a l i akionyesha jinsi mabeberu wanavyohangaika katika mikakati yao ya kushikilia akili za wajinga ndio wal iwao i l i waweze kushiriki katika mikakati yao. Akielezea juu ya Afghanistan, anasema kuwa wasiwasi uliopo ni kuwa washirika wa Marekani kwa maana ya nchi za Ulaya kama Ufaransa na Ujerumani, huenda zikaondoa majeshi yao katika muungano

    unaoikal ia kibamavu nchi hiyo- International Security Assistance Force ( ISAF) . Anasema, i le kusema tu kuwa kuna kitisho cha ugaidi/Osama, Taliban n.k, haitasaidia. Wa n a h i t a j i k u t a f u t a m k a k a t i m w i n g i n e . Waweka mikakati wa mabebrru wanasema, ile kwamba awali, nchi hizo zi l i tegemea kile wal i choki i ta Publ i c A p a t h y , k w a m b a wa n a n c h i wa l i k u wa hawajal i inachofanya serikali na jeshi lao kule A f g h a n i s t a n , i t a f i k a mahali isifanye kazi. Kwa hiyo lazima utengenezwe

    Bin Laden: Hivi kweli tunajua nini?Inatoka Uk. 10

    h i v y o k u n a k a t a z w a katika mwenendo wa mapambano. Ni Marekani ambayo inaendeleza kila ubaya dhidi ya wanawake, watoto na watu wa kawaida wa imani nyingine, hasa wafuasi wa Uislamu. K i l e k i n a c h o e n d e l e a huko Palestina kwa miezi 11 iliyopita kinatosha kuitisha ghadhabu ya Mungu kwa Marekani na Israel. Kuna onyo pia kwa zile nchi za Kiislamu, ambazo zimeshuhudia yote haya zikabaki kimya. Nini kilifanyika hapo kabla kwa watu wasio na hatia wa Irak, Chechnya na Bosnia? Ni jumuisho moja tu linaweza kufikiwa kwa

    kutojali kwa Marekani na nchi za Magharibi kwa matendo haya ya uharamia na kuwafadhili madhalimu kwa nchi hizi kuwa Marekani ni nchi inayopigana na Uislamu na inafadhili harakati za kuupinga Uislamu. Urafiki wake na nchi za Kiislamu ni onyesho tu, au udanganyifu. Kwa kuzivuta au kuzitisha n c h i h i z i , M a r e k a n i inazilazimisha kuchukua nafasi inayotaka. Tupa jicho kuangalia dunia utaona kuwa watumwa wa Marekani ni watawala au maadui (wa Waislamu). Marekani haina marafiki, wala haitaki kuwa nao kwani hitaji la kwanza la urafiki ni kufika katika

    h a t u a ya u r a f i k i n a kumwona kuwa ni sawa na wewe. Inatazamia utumwa kutoka kwa wengine. Hivyo, nchi nyingine ni watumwa wake au wasaidizi wake. (............) Yeyote aliyefanya matendo ya Septemba 11 siyo rafiki wa watu wa Marekani.

    Nimeshasema kuwa tunapinga mfumo wa Marekani, siyo dhidi ya watu wake, wakati ambapo k a t i k a m a s h a m b u l i o hayo, watu wa kawaida wa Marekani wameuawa. (.....) Marekani ingejaribu kuwatafuta waliofanya mashambulio hayo ndani ya nchi yake yenyewe;

    Inaendelea Uk. 12

    WANANCHI wa Burundi wakiandamana kumpinga Rais Nkurunziza

  • 12 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 22-28, 201512 MAKALA/MASHAIRI

    1. Kwa jina lake Jalali, Mola mwenye MiujizaMuumbaji wa awali, dunia kaitandazaYote kwake ni sahali, gumu hakulibakizaAsiyejua maana, kwani haambiwi mana

    2. Kisha swala kwa Rasuli, Mtumewe mpendezaMaswahabaze Rijali, Tumwa walo mtukuzaWalotoa zao mali, elimu kuisambazaAsiyejua maana, kwani haambiwi mana

    3. Sasa nianze suali, wenzangu kuwaulizaLanisumbua akili, macho yanaona kizaNiwaambie ukweli, hili limenitatizaAsiyejua maana, kwani haambiwi mana

    4. Ni semi za Kiswahili, Babu yangu kanifunzaAu sijui methali, vyema hakunielezaZinafika mia mbili , ninazo nimezitunzaAsiyejua maana, kwani haambiwi mana

    5. Nyenginezo afadhali, kufafanua nawezaHazinipi mushkeli , japo ni za kuchokozaIla hii nimefeli, ingali ikinikwazaAsiyejua maana, kwani haambiwi mana

    6. Jambo tunalokubali, kawaida ni la kwanzaAnoshindwa tafaswili, vizuri kumwelekezaMimi naona muhali, asojua kumtwezaAsiyejua maana, kwani haambiwi mana

    7. Shida ilonikabili, Babu nimeshapotezaNikimjulia hali, haya tukizungumzaSasa sinae batwali, walobaki ni vilazaAsiyejua maana, kwani haambiwi mana

    8. Enyi malenga wakweli, nini mtanielezaKuwapuuzia mbali, wasojua ni ruwazaAu la kuwabadili, mtazamo kugeuzaAsiyejua maana, kwani haambiwi mana

    9. Mimi natoa kauli, kabla sijamalizaNakataa jambo hili, Babu alinipotezaItapokuwa halali, msimamo taregezaAsiyejua maana, kwani haambiwi mana

    Mtunzi: Ukht. Zainab MtimaMbweni, Zanzibar - 0717 165 602

    SHAIRI LA ASIYEJUA MAANA

    Naianza simulizi, kwa jina lake KarimaMola wetu U mjuzi, mfano huwezi pimaSifa zako zote hizi, za kuumba na uzimaMwili raha yake kazi.

    Zote hizi zako sifa, za kuumba na uzimaUkazipa maarifa, ili mwali kujitumaKiungo kimoja kifa, mwili zote huzizimaMwili raha yake kazi.

    Ndugu mwana mhimili, isikilize kalmiaKwa kuushangaa mwili, Zainab wa MtimaViungo hujihimili, hadi kazi kusimamaMwili raha yake kazi.

    Kama kazi zikizidi, mwili nao hulalamaHuuleta ukaidi, na kufikia kugomaAkili yajitahidi, mwili wazidi kuzamaMwili raha yake kazi.

    Hapa ninapiga mbizi, pembeni ninayoyomaNinafunga simulizi, shairi langu kukomaMajibu ukimaizi, nambie ulipokwamaMwali raha yake kazi.

    SHAABAN AYOUB-Mjukuu wa KabongoDar es Salaam.

    Raha ya mwili kazi

    Bin Laden: Hivi kweli tunajua nini?Inatoka Uk. 11watu ambao ni sehemu ya mfumo wa Marekani, lakini wana dukuduku dhidi yake, au wale ambao wanatumik ia mfumo mwingine; watu wanaotaka kui fanya karne hii iwe ni karne ya mapambano ili ustaarabu wao, taifa, nchi au itikadi yao iweze kudumu. (....).

    Halafu kuna mashirika y a k i j a s u s i n c h i n i M a r e k a n i , a m b a y o yanahitaji mabilioni ya fedha za Marekani kutoka Bunge na serikali kila mwaka. Suala hili (la kutoa fedha) halikuwa t a t i z o ( w a k a t i w a ) uwepo wa Urusi lakini baada ya hapo bajeti za mashirika haya zimekuwa hatarini. Wanahitaji adui. Hivyo walianza kwanza propaganda dhidi ya Usama na Taliban halafu tukio hi l i l ikatokea . Unaona, utawala wa Bush ulipitisha bajeti ya d o l a b i l i o n i 4 0 . K i a s i h i k i k i k u b wa cha fedha kitakwenda wapi? Kitatolewa kwa mashirika hayo hayo ambayo yanahitaji fedha nyingi na kuonyesha umuhimu wake. Sasa yatatumia fedha hizo kwa kujipanua na kuongeza umuhimu wao. Nitakupa mfano. Wauza madawa ya kulevya kutoka kote duniani wanawasiliana na mashirika ya kijasusi ya Marekani. Mashirika haya hayataki kufutilia mbali ulimaji wa bhangi na usafirishaji wa unga kwa sababu umuhimu wao utapungua. Maofisa wa Shirika la Kupambana na Madawa ya Kulevya (DEA) wanahamasisha biashara hiyo ili waweze kuonyesha wanachofanya na kupata mamilioni ya dola katika bajeti. Jenerali Noriega (mtawala wa z a m a n i wa Pa n a m a ukanda wa Amerika ya Kati) alifanywa kuwa m u u z a u n g a n a ilipohitajika, akafanywa mbuzi wa kafara.

    Kwa njia hiyo hiyo, kama ni Rais Bush au rais mwingine yeyote, hawawezi kuif ikisha Israel mbele ya sheria kwa uvunjaji wake wa haki za binadamu au kuiwajibisha kwa uhalifu huo. Haya yote ni kitu gani? Hivi si inaonyesha kuwa kuna serikali ndani ya serikali ya Marekani? Serikali hiyo

    ya siri lazima iulizwe nani aliyefanya mashambulio hayo. (Hiyo ni kauli ya Osama Bin Laden)

    J iul ize mwenyewe. Hiv i h i i inaonyesha mzungumzaj i kichaa anayetamka chochote k i le , anaye j i s ik ia n i mkubwa kama Mlima Everest? Anaelekea kuwa mtulivu, kwa uhakika, na ana uelewa unaopenya akilini kuliko wanasiasa wote na wasomi wote wa Marekani. Kwa hali yoyote, mahojiano haya yalikuwa mazungumzo ya mwisho yenye uzito kutoka kwa Bin Laden. Baada ya hapa, ni kama vile alipotea.

    L i c h a y a k u w a h a k u o n e k a n a w a l a k u s i k i k a , a l i k u w a a n a k u m b u s h i w a k u h a l a l i s h a u h a l i f u ambao Marekani ilikuwa ikiwafanyia wengine, na hata raia wake yenyewe. Bin Laden alidhihirisha c h o c h o t e a m b a c h o viongozi wetu waliamua kufanya. Lakini miaka kumi ni mingi kutupa kivuli hiki katika kuta zetu. Mtu huyu mwenye m a d e v u a l i k u w a amekuwa kama mzaha hivi, kusema kweli. Katika onyesho la katuni, wakazi wa South Park jimbo la Colorado walifikia mahali wakamtaka Bin Laden awasaidie kupambana na kundi la maharamia l i n a l o va m i a k u t o k a New Jersey. (Ni kama kusaidia kupambana na maharamia wanaovamia Tabora, kutoka Tanga)!

    Hapo Mei 2 , 2011 serikali yetu ikaamua kumalizika mbali mzuka wa Bin Laden. Kwa vile Marekani inasemekana ilikuwa inamtafuta tangu mwaka 1998 (milipuko katika balozi za Marekani A f r i k a M a s h a r i k i ) ungedhania wangebaki naye kirefu zaidi baada ya kumpata, endapo walimpata, lakini ndani ya masaa kadhaa ya kumpata adui yao namba moja, Marekani ikamfutilia mbali Bin Laden.

    Hola, kama huwezi kunionyesha chochote, labda hunacho, hasa kama wewe ni mwongo a l iyekubuhu na upo katika biashara ya bisu lililofichwa chini ya koti. Kwa kesi za mauaji kwa nchi zinazotumia lugha ya Kiingereza tangu kupotea

    kwa William Harrison mwaka 1660, kumekuwa na kanuni ya 'bila maiti hakuna mauaji ' (mtu kuhukumiwa kwa shitaka hilo), lakini hapa kuna mtu anayesema kuwa ameua, akatangaza kila mahali, lakini hakuna mwili , kitu ambacho ni sawa na kuteketeza ushahidi, ushahidi wowote ule.

    K w a h i y o C I A inachotuambia hasa ni "mbwa al ikula mait i hiyo." Kusema kweli mzaha huu uliundwa bila ustadi wowote, maelezo yake yakiwa hayaingii ak i l in i kabisa , k ias i kwamba wanaotutawala l a z i m a w a n a d h a n i kuwa sisi ni mataahira, t u m e f a g i l i wa b o n g o zetu kwa propaganda tangu kuzaliwa hadi kufa inayotolewa kwa kuchapishwa au kwa m w a n g a n a s a u t i . Nachelea kufikiria kuwa wanaweza kuwa sahihi.

    Katika picha iliyobezwa sana, Bush anaonyeshwa akiwa katika koti la Jeshi, m k o n o wa k e u k i wa umeshika sahani yenye kanga al iyekaangwa, amefunikwa na zabibu. Amezungukwa na askari wa Marekani, wengi wao wakiwa hawamwangalii. Hii ina nia ya kuonyesha k u w a p i c h a h i y o ilichukuliwa kikawaida, bila urasimu, kusimama kwa kupiga picha. Hivyo ni ya uhakika.

    Katika picha nyingine, ambayo mara moja ilitajwa kama ya kukumbukwa na ya kuhifadhiwa kwani inabadili tunachofahamu akilini mwetu, Obama a n a o n ye s h wa a k i wa k a t i k a c h u m b a c h a mikutano cha Ikulu ya Marekani, amezungukwa na washauri wake wakuu wa masuala ya usalama. Wanaangalia kitu fulani. Kati ya watu hao 13, hakuna anayeangalia kamera. Hii pia ni kuonyesha kuwa picha hiyo ilikuwa ya kawaida, ya kiasili na siyo ya kuundwa kwa ajili ya tukio. Obama a n a o n ye s h wa a k i wa amevalia koti la kawaida, Biden amevaa shati ya mikono mifupi, vianzio vinavyoonyesha kuwa wako kazini, na siyo wanachukua picha ya propaganda. Monekano h u o u m e k u w a w a u h a k i k a k i a s i c h a

    Inaendelea Uk. 17

  • 13 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 22-28, 2015MAKALA/TANGAZO

    K WA wa l e wa l a j i wa mikate ya kiasili y a K i z a n z i b a r i maarufu kama boflo, wanafahamu ambacho hutokea pale mkate huo unapovamiwa na umma wa sisimizi. M l a j i w a m k a t e huo hususan pale anapokuwa na njaa kali, hujaribu kukata kipande cha mkate huo na kukipigapiga chini mara kadhaa ili sisimizi watoke ndani ya mkate huo, lakini wapi, huwa hawatoki bali huzidi kujificha ndani kwa ndani . Mara nyengine mlaji hujaribu kuupasha moto mkate huo ili kuona kama athari ya sisimizi hao itapungua ili aweze kuula, lakini hata hivyo hakuna k i n a c h o b a d i l i k a . Badala ya sisimizi hao kubaki ndani ya mkate wakiwa hai, sasa hubaki wakiwa wafu. Ni yale yale, mkate umezidiwa na sisimizi, hauliki.

    H e b u s a s a tuufananishe mkate huu wa boflo uliojaa sisimizi na Chama kikongwe c h a s i a s a , C C M , upande wa Zanzibar. Chama hichi badala ya kutekeleza kazi na urithi kilioachiwa na mtangulizi wake A S P , a m b a y o n i kukamilisha malengo ya kupigania uhuru wa visiwa hivi, chama hicho kimeukengeuka kabisa wajibu huo. ASP ilipigania uhuru w a W a z a n z i b a r i i k i m a a n i s h a k u m k o m b o a mwananchi kutokana na kila aina ya idhlali na unyonge ili wana wa visiwa hivi vitukufu waweze kuishi katika maisha bora, na yenye heshima.

    ASP il ipigana na h a t i m a e k u u n g o a utawala uliohodhiwa n a w a c h a c h e n a hatimae mamlaka ya nchi yakawa ndani ya mikono ya wengi. Ilifanikiwa kuondoa kila aina ya ubaguzi wa rangi, kabila, asili na kadhalika, hatimae Wa z a n z i b a r i w o t e wakawa na haki sawa, heshma sawa na hadhi sawa. Ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuondoa umasikini wa kipato, chakula, mavazi na makaazi na Wazanzibari kuwa watu wenye kuheshimika ndani ya nchi yao.

    C C M Z a n z i b a r , m r i t h i w a A S P imesaliti wajibu wake w a k u y a e n z i n a kuyaendeleza mazuri hayo ya ASP. Badala yake imekuja kujengea

    CCM Zanzibar mkate wenu umejaa sisimiziNa Ahmed Omar Khamis misingi mipya miovu

    na kuweka mazingira mapya ya kuyaendeleza yale yote yaliyopigwa vita na ASP. Utawala wa nchi hii umetolewa n d a n i y a m i k o n o y a W a z a n z i b a r i n a u m e k a b i d h i wa kwa majirani zetu, k w a k i s i n g i z i o c h a M u u n g a n o . W a t a n g a n y i k a wanautumia vyema Muungano huo na fursa zake kuijenga nchi yao na kuiimarisha kiuchumi na kisiasa h u k u Z a n z i b a r i k i d h a l i l i k a n a ikitokomea pole pole kutoka katika ramani ya ulimwengu.

    CCM imere jesha upya ubaguzi miongoni m wa Wa z a n z i b a r i wenyewe kwa wenyewe kwa misingi ya rangi zao, makabila yao na asili zao na kuifanya kazi kubwa ya ASP ya kufuta laana hiyo ya ubaguzi kuwa ni bure. Nyimbo zile za zama zile za Uarabu, U a f r i k a , u b w a n a , utwana, na kadhalika ambazo sisi vijana wa leo tumezikuta vitabuni na katika masimulizi ya walimu wetu maskulini, sasa tunazisikia zikitoka ndani ya midomoya viongozi wa CCM na katika mabango ya maskani za CCM. Ni jambo la kushangaza sana.

    ASP iliikomboa ardhi na kuweka sera na sheria ambazo ziliwezesha wanyonge wa nchi hii kuweza kuitumia na kuimiliki ardhi ya nchi yao pamoja na udogo wake. CCM imerejesha tena kadhia hi i ya laana ya kuimilikisha ardhi katika mikono y a w a c h a c h e n a kuipora kutoka kwa masikini na mafukara walio wengi. Ardhi ni raslimali muhimu kwa nchi ndogo ya Zanzibar ambayo wananchi wake wanaongezeka kila siku. Badala ya kuwekewa sera na sheria nzuri na madhubuti za umiliki na matumizi yake. Sehemu nyengine ya ardhi inauzwa kifisadi kwa matajiri na wawekezaji na kuwawacha raia masikini wakikosa hata sehemu ya kuzikiwa. Nchi yetu inanuka migogoro ya ardhi kila upande kuanzia Nungwi hadi Mkoani Pemba.

    W a n a n c h i w a Zanzibar wanaishi bila matumaini. Njaa itokanayo na ukosefu wa kazi za kufanya na kipato kisichokidhi mahitaji, ndio kilio kikubwa kinachosikika k a t i k a k i l a k o n a ya nchi. Visiwa hivi vilivyojaaliwa wingi w a r a s l i m a l i n a

    utajiri wa kila aina havionekani kuwa na mvuto na utulivu kwa wananchi wake. Watu wanaishi kwa rehma za Mwenyezi Mungu. Hakuna anaethubutu kula ak ipendacho, kuvaa nguo aipendayo au kuishi ndani ya nyumba aipendayo. Yote hayo sasa kwa Wazanzibari yamekuwa n i n d o t o . C C M imewapiga Wazanzibari wamepigika.

    Matokeo ya usaliti huu, CCM Zanzibar imepata pigo kubwa. Nguo ya umaarufu na heshma ambayo ilijivalisha kutoka kwa mri thi wake, ASP, sasa inavuliwa maana haistahiki tena kuivaa. Inainukisha kupuu na vundo. Ngome zake z o t e z i n a b o m o k a . I k i j a r i b u k w e n d a kujenga palipobomoka kidogo jana, kesho ya k e k u n a b o m o k a kwengine zaidi ya jana. CCM inahamwa kama mji uliokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Haina tena hata i le kauli mbiu ya kujifakharisha n a k u j i p a m b a n a historia ya uombozi ambapo Mapinduzi daima! sasa husikika katika majukwaa ya C U F . Wa a s i s i n a w a n a m a p i n d u z i wanaonyesha wazi wazi kuwa Chama hicho kinawaaibisha na hivyo wanakikimbia.

    B a d a l a ya C C M k u j i t a t h m i n i n a kufahamu kwamba imekwisha k i s iasa mbele ya Wazanzibari na haina pakushika ili ijizoezoe kunyanyua u p ya m g u u wa k e na kujaribu kupiga h a t u a m b e l e , i m e a m u a k u f a n ya m a i g i z o i k i d h a n i itasalimika. Inaona kitakachoinusuru ni rafu katika uchaguzi.

    H i v i s a s a kunafanyika zoezi la kupitia upya mipaka ya wilaya, wadi na shehia na kutangazwa mipaka na majina ya wilaya, wadi na shehia hizo katika gazeti la serikali. Ukataji huo wa wilaya, wadi na shehia uliotangazwa unaakisi vyema wazi wazi ramani ya kisiasa na sio kijeografia wala kidemografia. Ukataji h u o u m e p u n g u z a j u m l a ya wa d i 3 0 kutoka katika wadi zilizokuwepo huku wadi 25 zikipunguzwa kutoka k is iwa cha Pemba peke yake . Ukataji umezichukua shehia zisizooana au zisizolingana kijeografia na kuzifanya wadi moja, huku katikati

    yao zikitenganishwa na shehia za wadi n ye n g i n e . L e n g o la ukata j i huo ni k u w e k a r a m a n i i t a k a y o i o n g o z a Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kupitia na kukata upya majimbo ya Uchaguzi kwa upendeleo wa kisiasa (gerrymandering).

    I n a s e m e k a n a Tume ya Uchaguzi y a Z a n z i b a r ilikwishakamilisha kazi ya kupitia na kukata upya majimbo ya Uchaguzi mapema sana lakini hata hivyo ukataji huo ulipingwa v i k a l i n a C C M wakidhani hautakuwa na faida na chama chao. Badala yake Tume ya Uchaguzi ikalazimika kusubiri ukataji wa mipaka ya wilaya, wadi na shehia utakaofanywa ili iwe kigezo na muongozo

    kwa ajili ya ukataji wa majimbo ya uchaguzi.

    K wa m u j i b u wa sheria inayofuatwa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC), ukataji wa majimbo hautafanyika katika kipindi kilicho chini ya miezi sita kabla ya Uchaguzi Mkuu. Ikizingatiwa pia Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ni wakala wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, majimbo ya Zanzibar pia ni majimbo ya Uchaguzi katika uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano, hivyo basi nayo hayapaswi k u g u s wa c h i n i ya kipindi cha miezi sita. Mpango wowote au jaribio lolote la Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kupitia na kukata upya mipaka ya majimbo ya Zanzibar bila shaka ni kinyume na sheria, kwa sababu moja tu, Tume ya Uchaguzi

    ya Zanzibar inashea majimbo hayo hayo na Tume ya Uchaguzi ya Taifa.

    H a t a C C M ikifanikiwa kukata u p ya m a j i m b o ya Zanz ibar k inyume n a s h e r i a n a k wa kutumia ramani yake ya upendeleo wa kisiasa ishayoitengeneza, bado haitapata nusura na h a i t a o k o k a . M i m i n a h i s i h a i t a s a i d i a kwani hakuna tena n g o m e y a C C M , hakuna tena pakukata wala pakuacha. CCM haipo tena popote. Hakuna il ipobakia, s i o K a s k a z i n i , s i o Kusini, sio mawioni wala machweoni. Ndio maana tunasema CCM Zanzibar mkate wenu umeshajaa s is imizi wote. Hauna pakukata tena, kilichobaki ni kufumba macho na kuumeza.

  • 14 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 22-28, 2015Makala

    Na Ben Rijal

    Na Ben Rijal

    Mchango wa Waislmau katika maendeleo ya Dunia - 11

    UWANJA WA VIJANA - JIONGEZEE MAARIFACHEMSHA BONGO namba 6

    1. Majina ya Mwenye-enzi- Mungu katika Quran yametajwa majina mangapi? Jawabu: 99

    2. Surah gani na aya ipi katika Quran inayosmea Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. 2:256, 43:22, 2:222. Jawabu: 2:256

    3. Waislamu wanavikubali vitabu vingapi vilioteremshiwa Mitume? Jawabu: Tawrat, Injil, Zabur, Quran.

    4. Mwaka wa Kiislamu una siku pungufu ngapi ukilinganisha na mwaka wa Kizungu? Jawabu: 11

    5. Kinywaji gani kimeharamishwa na mnyama yupi ameharamishwa kula kwa Waislamu? Jawabu: Ulevi, Nguruwe.

    6. Jina gani limechukua nafasi kubwa kwa Waislamu kuwaita watoto wao? Jawabu: Mohammad

    7. Kiongozi gani maarufu kazikwa katika kisiwa cha St. Helena? Napolon, Colombus, Vasco Dagama. Jawabu: Napolon

    8. Zambia na Zimbabwe kwa pamoja zikiitwa kwa jina gani? Jawabu: Rhodesia

    9. Jimbo gani la Marekani lilio karibu na Urusi? Alaska, Hawai, New York Jawabu: Alaska

    10. Kikawaida moyo wa mwanadamu hupiga mara ngapi kwa nukta (minutes)? 72-80, 70-75, 82-87 Jawabu: , 72-80

    N G U R U W E N A M

    1 2 A Q I U 7 A L O 1 A B U N L 2 P A H

    9 C V R J E 8 O S A 9 R T A I V 0 L K M

    U P P N L I P E A M

    Z A B U R X C O G A

    2: 2 5 6 2: 2 2 N M D

    R H O D E S I A I O

    T A W R A T 43: 2 2 N

    K a t i k a m a k a l a i l iopi ta , n i l i j a r ibu k u m u e l e z e a I b n Khaldun kwa kuweza k u m t a m b u a n a mchango wake katika maendeleo ya dunia yetu hii. Makala hii n i t a k i z u n g u m z i a k i t a b u c h a k e c h a M u q a d d i m a h n a mchango aliochangia katika suala zima la somo la elimu ya jamii.

    Watu wengine wa nchi za Magharibi husema kuwa Ibn Khaldun hakuandika yeye h icho k i tabu cha Muqaddimah na kuna wasemao kuwa kaiba kazi za wengine na kuandika kitabu hicho. Hoja hizo hazina mashiko kwani hakuna m m o j a a l i o w e z a kuthibitisha kuwa Ibn Khaldun kazi yake kubwa ya Muqaddimah amedokoa katika kazi za watu wengine.

    M w a n d i s h i m a s h u h u r i w a Kiingereza katika karne ya 20, Toynnbee, yeye bila kuchelea kuitwa mtu wa ajabu, amesema kuwa Muqaddima ni kazi kubwa ya aina yake ambayo haijawahi kubuniwa na akili ya mtu yeyote yule, wakati wowote ule na mahali popote pale, ikiwa ni uchambuzi mpana na angavu wa maisha ya mwanadamu ambao haujafanyika popote pale.

    K a z i k u b w a y a Muqaddimah ya Ibn Khaldun al iandika katika mwaka wa 1377 na alijizatiti kuandika tarekhe yaani historia ya mwanadamu ikiwa ni Kitab al-akbar na jina kamili la kitabu hicho ndani ya Muqaddimah ni Kitbu l-ibar wa Diwnu l-Mubtada' wa l-Habar f tarikhi l-arab wa l-Barbar

    Ibn Khaldun-2wa man sarahum m i n D a w A s h -Sha'n l-Akbr, katika utangulizi huu alikuwa analinganisha tarehe ya Waarabu na Wabarbar kazi ambayo iliojaa utafiti na kutayarishwa na yeye Ibn Khaldun.

    A l i a n z a M u q a d d i m a h k wa k u w a t o a m a k o s a w a t a n g u l z i w a k e walioandika historia na katika migawanyiko y a u a n d i s h i n a kuayaangalia maeneo 7 kwa kina juu ya maelezo yake. Maeneo hayo ni: Ushirikiaono, imani na mawazo, kujiamini mtu katika kuandika na kuelezea historia, kushindwa kwa mtu kufahamu alichokikusudia katika kuiandika historia, makosa ya kuamini u k we l i wa j a m b o , kutokuwa na uwezo wa mwandishi wa historia kuelezea eneo lilotokea tokea kwa kulinukulu i t a k i wa v y o , h a m u ya waandishi katika kujipendekeza kwa watawala kwa kuwasifu katika maandishi na ujuhula wa wandishi wa kutojuwa sheria ziliopo katika mabadiliko ya jamii ya mwanadamu inayomzunguka. Katika nukta 7 hizo ndipo alipoweza kuziratibu na kuandika nadharia ya jamii ya Mwanadamu inayomzunguka katika Muqaddimah.

    Utangulizi huu wa Muqaddimah kama alivyoandika Sati al-Husri kwa kusema kazi yake ya ilimu ya jamii aliinukulu ndani ya kitabu kimoja kwa kutoa vitabu 6 ikiwa ilimu ya jamii kwa jumla, ilimu ya jamii katika maisha ya mijini, ilimu ya ja