annuur 1036

16
ISSN 0856 - 3861 Na. 1036 Dhuul-Qaad 1434, IJUMAA SEPTEMBA 28-OKTOBA 4, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu Kweli imedhihiri…. Salim, Butiku wakiri kuwepo udini nchini Kilichodhaniwa utaifa ilikuwa hewa Bila kufumuliwa mfumokristo, balaa Wakristo hawataki Benki za Kiislamu Mufti wa Bakwata akwama Barua yake kwa Obama yadoda Waislamu wavunja ngome ya Polisi Usheha sio hati miliki ya CCM DKT. Salim Ahmed Salim JOSEPH Butiku Maalim Seif akerwa na ubaguzi katika ajira Maimam wamtupia lawama Rais Shein [BAADHI ya Waislamu wakiwa katika viwanja vya Kidongo Chekundu, jijini Dar es Salaam wakiwa katika mkutano wa kulaani filamu iliyomkashifu Mtume (s.a.w.) Ijumaa iliyopita. (Picha na Bakar Mwakangwale] Uk. 3 Uk. 4 Uk. 2 Kisonge sasa wamelewa Wasema tujadili mkataba wa Pemba, Unguja Halafu, muungano wa Tanganyika na Zanzibar Uk. 5

Upload: hassan-mussa-khamis

Post on 19-Feb-2015

4.327 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: ANNUUR 1036

ISSN 0856 - 3861 Na. 1036 Dhuul-Qaad 1434, IJUMAA SEPTEMBA 28-OKTOBA 4, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamu

Kweli imedhihiri….

Salim, Butiku wakirikuwepo udini nchini

Kilichodhaniwa utaifa ilikuwa hewaBila kufumuliwa mfumokristo, balaaWakristo hawataki Benki za Kiislamu

Mufti wa Bakwata akwama Barua yake kwa Obama yadodaWaislamu wavunja ngome ya Polisi

Usheha sio hati miliki ya CCM

DKT. Salim Ahmed Salim JOSEPH Butiku

Maalim Seif akerwa na ubaguzi katika ajira

Maimam wamtupia lawama Rais Shein

[BAADHI ya Waislamu wakiwa katika viwanja vya Kidongo Chekundu, jijini Dar es Salaam wakiwa katika mkutano wa kulaani filamu iliyomkashifu Mtume (s.a.w.) Ijumaa iliyopita. (Picha na Bakar Mwakangwale]

Uk. 3

Uk. 4Uk. 2

Kisonge sasa wamelewa

Wasema tujadili mkataba wa Pemba, Unguja Halafu, muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Uk. 5

Page 2: ANNUUR 1036

2 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 28 - OKTOBA 4, 2012

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 0713 110148, DSM. www.ipctz.org E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

MAONI YETU

Tahariri/Tangazo

P.O. Box 55105, Tel: 2450069, 0754 260241 Fax: 2450822 Dar es Salaam

E-mail: [email protected]

UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL

Maandalizi ya Kidato cha Kwanza 2013

Shule ya Kiislamu ya Ubungo (Ubungo Islamic High School) inatangaza PROGRAMU maalum ya maandalizi ya kujiandaa na Kidato cha Kwanza 2013 kwa wanafunzi Waislamu.Programu hii itaanza tarehe 15/09/2012 hadi tarehe 10/12/2012 Jumatatu hadi Jumamosi saa 3:00 asubuhi hadi saa 8:30 mchana.Masomo yatakayofundishwa katika programu hii ni:1. Elimu ya Dini ya Kiislamu2. English Language3. Arabic Language4. Mathematics6. Introduction to ComputerNi programu maalumu ya miezi mitatu (15/09/20212 hadi 10/12/2012)Ada ya masomo kwa programu yote ni Tshs 50,000/= inalipwa yote mwanzoni mwa programu.

Fomu za kujiunga zinapatikana Shuleni - BURE

Kwa mawasiliano zaidi: 0714 888557, 0659 204013, 0717 295107

MLETE MWANAO APATE ELIMU BORA NA MALEZI MEMA YA KIISLAMU

Wabillah TawfiiqMKUU WA SHULE

Bismillahir Rahmaanir Rahiim

Mufti wa Bakwata akwama JUHUDi za Muft i wa Bakwata za kumnusuru Obama kutokana na hasira za Waislamu zimekwama.

K u k w a m b a h u k o kumetokana na Waislamu k u p u u z a w i t o w a k e n a k u m i m i n i k a M n a z i Mmoja kupasa sauti ya kulani watengeza filamu i n a y o m k a s h i f u M t u m e (s.a.w).

WAISLAMU Jijini Dar es Salaam, walifanya mkutano huo wa kulaani f i lamu iliyomkashifu Mtume (s a w), chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi liliweka msimamo huo kufuatia amri ya Kamanda Suleiman Kova, kupiga marufuku mkutano huo, kufanyika popote baada ya kutengua amri ya awali ya kuruhusu mkutano huo kufanyika katika viwanja vya Jangwani.

Amri hiyo ya Jeshi la Polisi, ya kupiga marufuku mkutano wa Waislamu ilianza kusikika kupitia vyombo vya habari (radio) majira ya jioni Alhamisi na usiku wa kuamkia Ijumaa, wiki iliyopita.

Amri hiyo ilichagizwa zaidi na kauli ya Mufti wa Bakwata, Sheikh Shaaban Simba, aliyenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari, akisema hakuna haja ya mkutano kwa kuwa Bakwata, imesha mwandikia barua Rais wa Marekani, Barack Obama.

Amri hizo hazikurudisha nyuma Umma wa Waislamu, kwani waliitikia wito wa Masheikh wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, ambapo ilipotimu majira ya saa saba adhuhuri, uwanja huo ulikuwa umezungukwa na askali wa FFU, ambao walikuwa wakizuia Waislamu kuingia.

Kufuatia hali hiyo, Waislamu walianza kujikusanya katika mitaa ya Kariakoo, wakiwa katika mitaa hiyo, walikata shauri kuingia katika viwanja hivyo huku wakitoa shahada na kuashiria kuwa tayari kwa lolote sambamba na kupaza sauti ya Takbir.

Bi la hofu wakisonga wakiwakabili askari, katika mshikamano, walitoka katika mitaa hiyo na kuelekea katika viwanja hivyo, ambako jeshi la Polisi lilikuwa limetanda kwa kuuzunguuka uwanja, sambamba na magari yao likiwamo gari la kumwaga maji ya kuwasha.

Katika hali iliyostaajabisha ni pale kundi la kinamama wa Kiislamu ambalo lilikuwa la mwanzo kuwakabili askali hao kabla ya wanaume, ambao walifika na kukata utepe uliokuwa umezungushwa

Na Bakari Mwakangwale katika uwanja huo, kisha kumiminika katika viwanja hivyo.

Awali Jeshi la Polisi majira ya asubuhi lilifika katika viwanja hivyo na kuwakuta vijana wa Kiislamu wakiwa katika maandalizi ya kufunga majukwaa, na vipaza sauti.

Maafande hao, katika harakati zao za kuhakikisha mkutano huo haufanyiki, waliwanyang’anya vijana hao vipaza sauti na spika na kuliweka eneo hilo chini ya ulinzi mkali.

Wakizungumzia tukio hilo Masheikh wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu katika viwanja hivyo, walisema huo ni uonevu, ambao kama Serikali haitokuwa makini, huenda ikaleta matatizo katika jamii.

Maalim Ally Bassaleh, a l i s e m a W a i s l a m u w a m e k u s u d i a k u f a n y a mkutano wa dini, wa amani tena wa kutetea dini yao na wala si wa kisiasa, lakini Polisi wamewanyang’anya vyombo vyao.

A l i s e m a , Wa i s l a m u wanadhalilishwa katika nchi yao jambo ambalo alilifafanua kuwa ni hatari kubwa kwa mustakabali wa nchi yao.

Maalima Bassaleh, aliasa kwamba kwa mwenendo huo wanako kwenda ni kubaya, kwani alidai awali Waislamu walizuiliwa kukutana katika uwanja wa Jangwani, kwa mae lezo kuwa wenzao (Wakriso) wameuomba.

Lakini a l i sema kama haitoshi, waliamua kuhamishia mkutano huo katika viwanja v y a K i d o n g o c h e k u n d u lakini bila sababu za msingi wakazuiwa kwa maelezo pasifanyike mkutano wa dini.

Alisema, asubuhi vijana wao wakiwa katika maandalizi ya mkutano huo, Polisi walifika katika viwanja hivyo na kuchukua vifaa hivyo kisha kuzuia maandalizi, kwa ujumla.

Maalima Bassaleh, alisema k w a Wa i s l a m u M t u m e Muhammad ni bora kuliko nafsi zao na kitu kingine chocho te , nd io sababu waliamua kuingia huku wakitamka shahada.

“Leo kama sio moyo wenu wa kujitolea tusingeingia k a t i k a h a d h a r a h i i . Tumekuja hapa tumekuta pamezungushwa utepe hakuna

Inaendelea Uk. 4

NI ukweli ulio wazi kwamba dawa bandia zimekithiri nchini. Hivi sasa kuna sakata la kusambazwa sehemu mbalimbali nchini dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi za ARV ambazo zimegunduliwa kuwa ni ‘feki’.

Jambo la kushangaza na kushtua zaidi ni kwamba, dawa hizo zisizokuwa na viwango, z imesambazwa ziki tokea katika hospitali za serikali na tayari maelfu ya wagonjwa wameshazitumia.

Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa Tanzania kwa muda mrefu imekuwa jalala la bidhaa mbovu zisizokidhi viwango. Kuanzia dawa za binadamu na mifugo, vifaa vya ujenzi, vifaa vya umeme, samani za ndani, vyakula, vifaa vya elekroniki, magari mabovu nk.

Tunaamini kuwa bidhaa zote hizi hazi ingizwi na kusambazwa nchini kwa miujiza au kimazingaombwe. Bali kuna udhaifu makubwa kwa mamlaka husika katika kudhibiti hujuma hizi. Rushwa, ufisadi, tamaa za kutaka kutajirika ghafla, yote haya yanachangia kukithiri tatizo hili la bidhaa feki.

Ni wazi kwamba sehemu kubwa ya bidhaa hizi mbovu zinaingizwa nchini kwa njia za kawaida hususana bandarini na kwa njia ya ndege, zikiwa kwenye makontena na kwenye makasha rasmi ya kuhifadhia mizigo, lakini kutokana na kukosekana uaminifu na uadilifu kwa wale wanaopewa jukumu la kusimamia uingizaji na utoaji wa bidhaa nchini, matokeo yake ni nchi kuwa jalala la vitu vibovu visivyofaa kwa matumizi ya binadamu.

Tunasema hivyo kutokana na ushahidi kadhaa wa kimazingira a m b a o u p o w a z i . K w a mfano, hivi karibuni Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe, alitoa amri kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwakamata mara moja polisi wanaoshiriki katika wizi wa mafuta Bandarini Kurasini jijini Dar es Salaam. Kauli hii ya Waziri inadhihirisha wazi kwamba wizi wa mafuta umekuwa ukifanyika kwa muda mrefu bandari ya Dar es Salaam na kuna uwezekano mkubwa kwamba watendaji wa juu wa Bandari wanajua siri hii.

H iv i s a sa tunae lezwa kwamba hizi dawa feki za ARV, nazo zimekuwa zikisambazwa kutokea hospitali za serikali na kuonyesha kwamba zimetolewa

Uhodari wa Dola kudhibiti raia utumike kudhibiti dawa bandia

na mamlaka halali za dawa za serikali. Huu ni ushahidi mwingine kwamba dawa hizi mbovu ni mradi unaojumuisha vigogo kadhaa ama kutoka Wizara ya Afya au MSD.

Sisi tunaona kwamba pamoja na juhudi zinazofanywa na mamlaka za kulinda afya za watu nchini kama TFDA na TBS, bado taasisi hizi haziwezi kuzuia kikamil i fu uhuni unaofanywa kwa makusudi na watu wenye tamaa ya fedha kuhatarisha maisha ya Watanzania.

Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa ni vyombo ambavyo kama vingetekeleza wajibu wake ipasavyo, basi hali hii isingekithiri kwa kiwango kilichofikiwa hivi sasa.

Ni jambo la ajabu kabisa kuwaona Polisi wakionyesha uhodari wao kuwakong’ota raia wasio na hatia katika mikutano ya hadhara ya Waislamu au ile ya CHADEMA . Wakifikia hatua hata ya kuua na kujeruhi.

Lakini uhodari huo hatuuoni katika kukabiliana na wahuni wachache wanaotumia nyadhifa zao serikalini kushirikiana na wafanyabiashara wenye uchuku kuhatarisha maisha ya Watanzania kwa maslahi yao binafsi.

Ni dhahiri kwamba hata huko mipakani wao ndio vinara wa kuruhusu wafanyabiashara haramu kupenya na bidhaa zao mbovu ilimradi kuna kitu kidogo.

Tumesikia yale ya Uhamiaji mipakani. Wametuhumiwa kuchukua chochote na kuruhusu wahamiaji haramu kuingia nchini. Vivyo hivyo na bidhaa feki nazo hupenyezwa.

M a i s h a y a u m m a w a Watanzania yana thamani kubwa ka t i ka uha l i wa Taifa lolote lile. Kuwaacha Watanzania wahatarishiwe maisha yao na walafi wachache wanaojali fedha kuliko maisha ya watu, ni uhalifu na usaliti ulio mkubwa.

Tunaona kuwa sasa ipo haja kwa serikali kuwa na mkakati wa makusudi kwa kushirikisha vyombo hivi vya dola kudhibiti kikamilifu uhalifu huu wa kuzagaa vitu feki nchini ili kuyanusuru maisha ya Watanzania na vizazi vijavyo.

Kuonyesha nguvu kubwa ya dola kwenye mikusanyiko ya kiraia, kisiasa au za kidini na kuonyesha uhodari wa kubamiza watu, haina maana yoyote wakati nguvu hizo walitakiwa kuzielekeza kwa wahalifu kama hawa wanaosambaza ARV feki mahospitalini.

Hii ni aibu kubwa.

Page 3: ANNUUR 1036

3 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 28 - OKTOBA 4, 2012Habari

Salim, Butiku wakiri kuwepo udini nchiniIMEJISEMEA Qur’an, “Sema ukweli umefika na uwongo umetoweka. Uwongo mwishowe huwa ndio wenye kuondoka.”

Vigogo wakuu wa Serikali Wastaafu, Salim Ahmed Salim na Joseph Butiku wamekiri kuwa nchi sasa imegawika vipande kwa misingi ya dini.

Sasa ni dhahiri kuwa hakuna kitu tena kinaitwa utaifa, hakuna tena watu wanaitwa Watanzania, bali tunao Waislamu Watanzania na Wakristo Watanzania.

Hiyo ndiyo hali inayojitokea katika kukusanya maoni ya Katiba ambapo Salim Ahmed Salim amesema kuwa toka wameanza kukusanya maoni, hakuna maoni ya kitaifa yanayotolewa ila ya Waislamu na Wakristo.

Akihitimisha zoezi la ukusanyaji maoni katika Kata ya Kitangiri Mwanza juzi, Salim Ahmed Salim amesema kuwa kila walipopita nchini, akisimama Muislamu atazungumzia masuala ya Kiislamu kama kutaka OIC, Hijabu, Mahkama ya Kadhi na mambo kama hayo.

Na kwamba akisimama Mkristo pamoja na kupinga Mahkama ya Kadhi, OIC na masuala ya Hijabu na Uislamu kwa ujumla, atazungumzia masuala ya Kikristo badala ya kitaifa.

Kwa mtizamo huo ndio akasema kuwa hivi sasa ni dhahiri nchi imegawika.

Tathmini inaonyesha kuwa toka zoezi hili la kukusanya maoni lilipoanza, Wakristo wanataka au kupinga mambo matano.

Moja, wanataka Katiba itamke kuwa nao ni halali kuchinja na Muislamu akala.

Pili, katiba ipige marufuku uvaaji wa Hijabu mashuleni na vyuoni.

Tatu, katiba iseme wazi marufuku OIC na Mahkama ya Kadhi.

Lakini zaidi ya hapo hawataki kuona Benki za Kiislamu.

Kwa hiyo wanataka Katiba iseme kuwa ni marufuku kuwepo Benki za Kiislamu Tanzania.

Katika kuonyesha kuwa watu wamelishwa maoni na viongozi wao wa kidini na ndiyo wanayosema katika mikutano, katika tukio mmoja Tume ilipokuwa Usagara, Mkoani Mwanza, alisimama mzee wa Kisukuma Mkristo kutoka vijini na kusema kuwa hataki kuwepo kile chama cha Waislamu.

Na Mwandishi Wetu Alipotakiwa na watu wa Tume kueleza ni chama gani hicho, akabaki akisema i le . .O. .O. .OC. .OC, hal i iliyoonyesha kuwa alikuwa akimaanisha OIC.

N a k w a m b a h a y o kafundishwa kanisani japo yeye mwenyewe hajui hata hiyo OIC ni nini.

Akitilia makazo hoja hiyo ya nchi kugawika, Mzee Joseph Butiku amesema kuwa, imef ik ia maha l i akisimama mtoa maoni na kujitaja kuwa ni Muislamu, wanatamani kumwambia akae chini kwa sababu washajua atakayozungumza.

Ni hivyo hivyo akisimama mwenye jina la Kikristo, hawategemei kupata maoni ya kitaifa, ila yale ya Kikristo na kupinga ya Waislamu.

Haya siyo tuliyoachiwa na waasisi wa Taifa letu, akiwemo Baba wa Taifa; yalikuwa maoni ya Mzee Butiku katika kuonyesha ukubwa wa tatizo na kwamba nchi inakwenda kombo.

Hata hivyo, baadhi ya watu waliokuwepo katika mkutano wa Kitangiri wakitoa maoni yao wamesema kuwa anachosema Mzee Butiku si sahihi kwani kama ni udini, ul ias is iwa na Mwalimu Nyerere i la u l i funikwa kwa ulaghai ambao sasa umefichuka.

“Mwalimu ndiye muasisi wa udini huu, yeye ndiye aliyesimika mfumokristo nchini hapa pale alipotangaza kulipa Kanisa Katoliki nafasi ya upendeleo na kuweka mawakala wa mfumo huo ndani ya serikali waliokuwa wakiwahujumu Waislamu k a t i k a k i l a N y a n j a , kinachotokea hivi sasa ni kuwa ile hadaa imeondoka Wais lamu wametambua ukweli wanapinga dhulma, na Wakristo nao wanataka udumu mfumokristo ili waendelee kufaidi.”

Amesema mzee mmoja na kuongeza kuwa “njia pekee ya kuinusuru nchi hii ni kufumua mfumokristo na kurejesha nchi katika maadili ya kitaifa.”

Jambo jingine ambalo limejitokeza na kuonyesha hatari ya mgawanyiko huu ni kuwa kila aliposimama Muislamu, kulikuwa na uzomeaj i mkubwa ha l i iliyokuwa ikiwafanya watu wa Tume kuingilia kati mara kwa mara kutuliza munkari.

Lakini hata watu wa Tume wenyewe katika baadhi ya maeneo wameshutumiwa kuwa wamekuwa hawatoi nafasi kwa Waislamu hali iliyofanya watu wavue kofia

na kanzu zao ili wasitambulike kuwa ni Wasilamu.

Kwa mujibu wa maoni ya baadhi ya wajumbe wa Tume ya kukusanya maoni

ya Katiba, japo bado zoezi lina muda zaidi mbele, lakini hawadhani kuwa yatakuwepo maoni mengine zaidi ya haya ambayo washakusanya.

Muelekeo ni huo wa kujirudia Waislamu kutaka mambo yao na Wakristo nao halikadhalika kutaka yao.

Usheha sio hati miliki ya CCMMAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad ameonyesha k u k e r w a n a u b a g u z i unaodaiwa kuwepo katika kutoa ajira za Masheha.

Katika kukemea ubaguzi huo, amezitaka Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na Wilaya kuzitangia uwezo wa mtu badala ya itikadi au chama cha siasa anachotoka wakati wa kupendekeza majina ya watu wanaotakiwa kuteuliwa kuwa Masheha.

Maalim Seif amesema hayo alipokuwa akizungumza katika semina maalum kwa ajili ya Masheha na Madiwani kuhusu uhusiano baina ya viongozi wa kisiasa na utendaji katika serikali za mitaa Zanzibar huko Wesha, Mkoa wa Kusini Pemba.

Maalim amesema, yapo malalamiko mengi kuwa Masheha wote wanatoka chama kimoja, jambo ambalo huwafanya wananchi kuhisi kuna ubaguzi dhana ambayo haifai wakati huu wa serikali yenye muundo wa umoja wa kitaifa.

Japo hakufafanua lakini malalamiko yaliyopo ni kuwa Masheha kwa kiwango kikubwa ni kutoka CCM na imekuwa ikidaiwa kuwa huwabagua

Alghaithiyyah, Zanzibar wanachama wa CUF ikiwa ni pamoja na kuwanyima vitambulisho vya ukaazi na kadi za kupigia kura.

Akasema, ili kuondoa dhana hiyo mbaya, Kamati za Ulinzi na Usalama ambazo ndizo zenye jukumu la kupendekeza majina ya Masheha zinapaswa kufanya uadilifu na kuzingatia uwezo wa mtu kiutendaji katika kutumikia wananchi.

“Malalamiko hayo ni kweli yapo, inasemwa hata nafasi za ajira ya kupuliza dawa za kuulia mbu wa malaria majumbani, hupewi mtu hadi uwe unatoka chama fulani”, alisema Maalim Seif.

A l i e l eza kuwa Sheha a n a t a k i w a a w e m t u anayeheshimika miongoni mwa jamii na wananchi anaowaongoza na lazima wawe hawana shaka na uadilifu wake.

Maalim Seif alisema hayo baada ya Madiwani kutoka Wadi mbali mbali kisiwani Pemba kulalamika juu ya kuwepo ubaguzi katika uteuzi wa Masheha na Kamati zao za wajumbe 10, hali ambayo inachang ia kuporomoka utendaji na ushirikiano kati yao na Madiwani.

Madiwani hao walitupa lawama hizo kwa wakuu wa Wilaya na Mikoa kuhusika na uteuzi huo na kukielezea kitendo hicho kuwa kimekuwa

kikiwakosesha haki wananchi wenye itikadi tafauti na Mashha hao, ikiwemo suala la kupatiwa vitambulisho vya Wazanzibari Wakaazi.

Akijibu hoja za Madiwani hao, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Meja Mstaafu, Juma Kassim Tindwa alisema kuwa Wakuu wa Mikoa hufanya uteuzi wa Masheha baada ya kupewa majina matatu yanayopendekezwa na Kamati za Ulinzi na Usalama katika Mikoa yao.

Al isema kuwa hakuna upendeleo wowote unaofanywa katika kupata viongozi hao wa serikali za mitaa, kwa vile kamati hizo za ulinzi na usalama haziainishi watu waliopendekezwa wanatoka chama gani cha siasa.

Tindwa alisema yeye binafsi katika mkoa wake hafahamu Masheha wake wanatoka katika chama gani, kwa sababu hata hao waliopo baadhi yao wanalalamikiwa kuwa hawafai kwa sababu wanatoka chama cha upinzani.

Awali akifungua semina hiyo, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein alisema mafunzo hayo kwa viongozi wa serikali za mitaa yanalenga kujenga misingi bora ya uongozi, maadili mema katika utendaji na kutekelezaji wa dhana ya utawala bora.

JAJI Joseph Sinde Warioba (kushoto) akiwa na Dkt. Salim Ahmed Salim wakitafakari jambo.

Page 4: ANNUUR 1036

4 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 28 - OKTOBA 4, 2012Habari/Tangazo

1. Algebra ni shule ya BWENI na KUTWA kwa WAVULANA NA WASICHANA2. Inaongozwa kwa maadili ya Kiislamu na Iko Kigamboni - Kibada3. MAHALI PENGINE ZINAKOPATIKANA FOMU Mtambani (0715 – 866 887), UBUNGO ISLAMIC (0712 - 033 556) na ANNUR (0713 -110148)4. Maabara, Kompyuta na Maktaba vimeongezwa ili kuongeza ubora 5. Tumesajiliwa kwa namba S.4198 Tunajua tunakoenda na namna ya kufika huko

CHAGUA ALGEBRA ISLAMIC SEMINARY, INSHAALLAH HUTAJUTIA UAMUZI WAKO

ALGEBRA ISLAMIC SEMINARYP.O. BOX 36262 KIGAMBONI, DAR ES SALAAM

TEL: 0715 – 299 945, 0714 – 112 083, 0655 – 260 241, 0714 - 593 897

NAFASI ZA MASOMO 2013Kidato cha Kwanza

Mufti wa Bakwata akwama Inatoka Uk. 2

ruhusa Waislamu kuingia lakini tumeingia, waelewe kuwa tupo tayari kufa kwa ajili ya Mtume wetu.” Alisema Maalim Bassaleh.

K w a u p a n d e w a k e Sheikh Mohammed Issa, alisema hatua ya jeshi la Polisi, kuzuia mkutanio huo, ni kuwatafuta Waislamu muhali kwani hapakuwa na sababu za msingi za kuwazuia Waislamu kulaani Mtume wao kutukanwa na kudhalilishwa.

“Tumeomba kongamano la amani tukutane Waislamu tuzungumze hisia zetu, lakini tunazuiwa tusizungumze kwa madai kuwa tutavunja amani. Kuletewa mambo ya namna hii kuna siku Waislamu tutashindwa kuvumilia na itakuwa balaa.” Alisema Shkh. Issa.

Alisema, bila ya kutokuwa na mapenzi kwa Mtume wao, Waislamu wasingeweza kuingia katika viwanja hivyo kwa kuhofia askari Polisi.

Alisema, zuio la kuwepo kwa mkutano huo, ambao ulikuwa ni wa kuonyesha hisia za Waislamu kupinga kudhalilishwa Mtume wao, li l ianza kutolewa tokea usiku wa kuamkia Ijumaa (iliyopita).

A l i sema , pamoja na katazo hilo, lakini Waislamu waliweka mapenzi yao mbele na kujitokeza kwa wingi bila kujali vitisho wakiashiria kuwa wapo tayari kufa kwa ajili ya Mtume wao.

Alisema, wanaotoa ushauri kama huo kwa vyombo vya dola ili kuwanyima Waislamu haki zao k ikat iba kwa chuki zao binafsi ni wazi wanawashauri vibaya.

Akihitimisha mkutano huo, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema wanatoa

wito kwa Umoja wa nchi za Kiislamu OIC, kutoa msimamo utakaokomesha kejeli na udhalili dhidi ya Mtume Muhammad (s a w), unaojirudia mara kwa mara.

Wito huo ni moja ya m a j u m u i s h o y a l i y o m o katika tamko la Waislamu, kupitia Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T) la kupinga filamu inayomkashifu Mtume wao.

Akisoma tamko hilo mbele ya maelfu ya Waislamu waliojitokeza kulani filamu hiyo, katika viwanja vya Kidongochekundu, Ponda, aliye Katibu wa Jumuiya hizo, amesema hatua yoyote ya kumkejeli, kumkashifu au kumtusi Mtume, haiwezi kuvumiliwa na Umma wa Kislamu popote duniani.

Kup i t i a t amko h i lo , Ponda, amesema wanaitaka Serikali ya Marekani kwa pamoja kuzuia filamu hiyo kuonyeshwa kwa njia yoyote ile, iwe katika runinga, Intanenti au DVD.

A l i s e m a , k u p u u z a na kuiachia filamu hiyo inaweza kuwa ni chanzo na muendelezo wa uhasama ba ina ya Wais lamu na nchi zinazohusishwa na utengenezaji wa filamu hiyo.

Ponda aliwataka wafuasi wa dini nyingine kuiga mfano wa mafundisho ya Uislamu, kwa kuheshimu dini nyingine na kwamba dunia haijawahi kusikia Muislamu, kasababisha vurugu kwa kukejeli au kutusi imani ya dini zingine.

“Ni vyema wafuasi wa dini zingine zikaiga mfano wa Uislamu, kwani hauruhusu mtu kuchupa mipaka na kutumia mwanya wa uhuru wa kuamua kujieleza na kutukana.” Alisema Ponda.

Maimam wamtupia lawama Rais SheinNa Mwandhsi Wetu

JUMUIYA ya Maimamu Z a n z i b a r ( J U M A Z A ) imelani vikali matumizi ya nguvu kupita kiasi kulikofanywa na vikosi vya SMZ hususan KMKM katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Bububu.

Vurugu hizo zilijumuisha kuwapiga ra ia na hata kuwafyatulia risasi za moto katika kile kiichodawaiwa kuwatisha wananchi wapishe mamluki waipigie kura CCM.

Aidha JUMAZA inalani vitendo vilivyofanywa na watu wasiojulikana waliofunika nyuso zao na kubeba silaha kuwashambulia raia.

“ N d u g u Wa z a n z i b a r wapendwa vurugu na vitendo vya uvunjifu wa amani na utulivu vilivyotokea katika uchaguzi mdogo katika jimbo la Bububu vimeleta maafa makubwa yakiwemo kuwajeruhi watu, kuleta khofu ndani ya jamii, kuharibu mali za watu, kuvunja heshima za watu na kusadikiwa kupotea kwa maisha ya kijana wa Kizanzibari asiye na hatia kwa kupigwa risasi. Matukio haya kwa hakika yametia doa kubwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyopatikana kwa

gharama kubwa na taufiq ya Allah (S.W)”.

Imesema sehemu ya barua hiyo ya JUMAZA ikionyesha wazi kulaumu serikali ya Dr. Shein kwa kushindwa kusimamia amani ya nchi.

“ J U M A Z A i n a a m i n i kuwa vitendo vya vurugu na uvunjifu wa amani na utulivu vilivyotokea katika uchaguzi huo n i miongoni mwa mikakati inayotekelezwa na kikundi cha watu wanaopinga Serikali ya Umoja wa Kitaifa pamoja na kupa t ikana mamlaka kamili ya Dola ya Zanzibar.”

Imeongeza barua hiyo na kuidokeza kuwa waliohusika na vurugu hizo ni watu ndani ya serikali ambao hawataki kuwepo kwa serikali ya maridhiano.

H i y o n i s a w a n a kumshutumu Rais Shein moja kwa moja kwa sababu yeye ndiye Mkuu wa Vikosi vya SMZ na hakuna namna yoyote ambayo vikosi hivyo vingevuruga uchaguzi bila ya ridhaa au maagizo yake.

“Kutokana na vitendo hivi, JUMAZA inaiomba SMZ kumuwajibisha Kamanda Mkuu wa KMKM pamoja

na Afisa wa Operesheni kwa kuliingiza jeshi hilo katika kadhia ya kuvuruga uchaguzi katika jimbo la Bububu.”

Wamesema JUMAZA huku wakimtaka Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dr Ali Muhamed Shein na Makamo wake Seif Sharif Hamad watekeleze ahadi yao waliyoichukua pale Bwawani wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita.

“ K w a n i a n j e m a tunawakumbusha viongozi wetu hawa wawe na yakini wataulizwa siku ya malipo kwa kiasi gani wameitekeleza ahadi hiyo.”

Kwa upande mwingine J U M A Z A i n a w a o m b a Wazanzibari wote “wasikubali kurejeshwa walikotoka bali wawe na subra na kudumisha mapenzi na mshikamano wao ili kufikia malengo makubwa waliyojipangia.”

Aidha Jumuiya h iyo imewaomba Wazanzibari wote kuiunga mkono Serikali ya Umoja wa Kitaifa pamoja na kuwaunga mkono viongozi wa ngazi za juu wa serikali muda wa kuwa wanasimama katika haki na katika masilahi ya Zanzibar.

WAISLAMU wakiingia wakiwa viwanja vya Kidongo Chekundu na mabango ya kulaani Marekani na Israel.

Page 5: ANNUUR 1036

5 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 28 - OKTOBA 4, 2012Habari za Kimataifa

Kisonge sasa wamelewa M A S K A N I y a C C M Kisonge imeibuka na mpya ambayo pengine yaweza kuitwa ya mwaka.

Katika bango lao sasa wameandika kuwa ujadiliwe kwanza mkataba wa Pemba na Unguja kabla ya kujadili muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Wakitoa maoni yao jana katika mitaa mbalimbali mjini hapa, baadhi ya wananchi wa l iosoma bango h i lo wametuhumu kuwa huenda kuna watu wanaotumiwa kuhujumu mas i lah i ya Zanzibar.

“Mi nadhani wanaoandika u jumbe kama huu s io Wazanzibari, inawezekana ndio wale aliowaita Mwalimu Nyerere kuwa ni Wazanzibara, unapozungumzia mkataba wa Pemba na Unguja, ni laz ima useme kwanza , visiwa hivi viliungana lini, lini viliandikiana mkataba wa kuungana , na nan i aliviunganisha ili leo kuwe na mantiki ya kujadili muungano baina yao, mbona watu wetu hawana akili? Mbona hatuoni

Na Mwandishi Wetu wala kusikia mfano watu wa Songea wakihoji mkataba wao na Musoma au Bukoba, mbona hatusikii Wachagga wak i sema Wamakonde wahame Moshi, mbona ujinga huu unaonekana tu huku Kisonge? Mi nadhani hawa wanatumiwa sio Wazanzibari, ni Wazanzibara”.

Alisema Mzee mmoja wa makamo akionyesha kukerwa na ujumbe huo wa Kisonge.

“Bara kule tunasikia m c h u a n o w a C C M n a C h a d e m a , l a k i n i w o t e h u s i m a m a k a m a ‘Watanganyika’ (Tanzania Bara) wakiipigania Tanzania Bara, hutawasikia iwe ni CCM au Chadema wakizungumzia s i a s a z a k u w a g a w a Watanganyika, upuuzi huu unaonekana huku kwetu tu, kwa nini? Mbona tunajiabisha Wazanzibari?” Alisema Mzee huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Suleiman.

“Hivi sasa wakati ambapo Wazanzibari wanaonekana kuungana katika kupigania mas i lah i ya nch i ye tu katika muungano, wanataka k u t u r e j e s h a n y u m a , wanatusaliti, wanatuletea

siasa za Upemba na Uunguja, hivi hatuna akili? Hatutambui? Hatufahamu?” Aliongeza na kuhoji.

Kwa upande mwingine baadhi ya watu wamesema kuwa inawezekana wapo viongozi wa ngazi za juu wa CCM na ser ika l in i wanaofadhili na kuzipenda siasa hizo za farka, chuki, ubaguzi na fitna.

Hoja yao ni kuwa Kisonge ni maskani ya CCM, tena iliyopo jirani na Makao Makuu ya CCM Zanzibar, Kisiwandui, haiwezekani Kisonge wakatoa ujumbe na miito iliyo kinyume na maadili ya CCM yenyewe kama hakuna wakubwa serikalini na ndani ya CCM wanaozipenda f i tna na kuzipalilia faraka hizo.

Hata hivyo ikasemwa kuwa, wanaopenda siasa hizo watakuwa ni wale wanasiasa walioghafilika wakathamini masilahi yao haba binafsi na wakawa tayari kuuza nchi.

Kwa lugha ny ing ine watu hao wametafsiriwa kama wasaliti walio tayari kuona Zanzibar ikiangamia ilimuradi tu kama wao binafsi watashiba.

Waliocheza filamu ya kumkashfu Mtume SAW wafikishana mahakamaniLOS ANGELESCINDY Lee Garcia, msanii aliyecheza filamu ya “Innocence of Muslims” ambayo imemtusi na kumvunjia heshima Bwana Mtume Muhammad (SAW) amefungua kesi katika mahakama ya shirikisho nchini Marekani dhidi ya mtayarishaji wa filamu hiyo Nakoula Basseley Nakoula, akisema kwamba alimhadaa kucheza filamu ambayo sasa inahatarisha maisha yake.

Wakili wa msanii huyo Cris Armenta, amesema mashitaka katika kesi hiyo ambayo ni ya madai ya haki mi l ik i yanaihusisha pia mitandao ya YouTube na Google kwa kitendo chao cha kuonyesha sehemu ya filamu hiyo katika mitandao.

Katika kesi hiyo Bi. Garcia ambaye ni mkazi wa California amedai kuwa amemshitaki Nakoula anayetumia lebo ya Sam Bacile kwa kumhadaa kucheza filamu aliyoeleza kuwa ni ya “kueneza chuki”.

Wakili wa msanii huyo amesema mitandao ya Youtube na Google imekiuka kanuni na taratibu zao zinazopiga marufuku kuonyesha mambo yanayoeneza chuki.

Maandamano ya Waislamu wenye mapenzi makubwa na

Mtume na uchungu na dini yao, bado yanaendelea kufanyika katika kila pembe ya dunia kulaani filamu ya Kimarekani inayomtusi na kumvunjia heshima Nabii Muhammad (SAW).

Nakoula Basseley Nakoula, mtengeneza filamu mwenye itikadi kali ya Kikristo, amezua tafrani kubwa hivi sasa kwa umma wa Kiislamu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Dai ly Beast , mtengeneza f i l a m u h u y o a l i w a h i kufungwa kwa kutengeneza methamphetamine.

Nakoula aliwahi kukamatwa

mwaka 1997 na kuhukumiwa kwenda jela mwaka mmoja na kutumikia miaka mitatu kifungo cha nje.

Alifungwa tena mwaka mmoja kwa kuvunja masharti ya kifungo cha nje.

Baada ya maandamano ya kulaani filamu hiyo kulipuka, N a k o u l a i l i e l e z a k u w a alitengeneza filamu hiyo kwa msaada wa kampuni ya Kiisraeli ya kuendeleza dhamana ya Sam Bacile ya California, akieleza kuwa ametengeneza filamu hiyo kwa msaada wa wadhamini 100 wa Kiisrael.

Sheikh al Azhar aitaka UN kupitisha sheria ya kuzuia kashfa dhidi ya WaislamuCAIROSheikh wa al Azhar, Ahmad Tayyib, ameutaka Umoja wa Mataifa –UN kupitisha sheria za kupambana na vitendo vinavyovunjia heshima matukufu ya Kiislamu.

Baada ya kutengenezwa na kuoneshwa filamu ya “Innocence of Muslims” huko Marekani, Sheikh Tayyib amemwandikia barua ya wazi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, akisisitiza juu ya udharura wa kubuniwa sheria za kimataifa za kupiga marufuku kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu.

Sehemu moja ya barua hiyo imesema kuwa, sheria hizo zinapaswa kuainisha adhabu kwa watu wanaovunjia heshima na kuwakebehi Waislamu na matukufu ya

kidini, kwani vitendo kama hivyo vinahatarisha amani na usalama wa kimataifa.

Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa unawajibika kulinda amani na usalama wa dunia na kukabiliana na aina zote za ukatili na utumiaji mabavu.

A m e s e m a , i w a p o sheria hizo zitapasishwa, haku ta shuhud iwa t ena m a t u k i o y a h a t a r i y a kukashfiana kiimani kama haya ya sasa.

Sheikh Ahmad Tayyib, amelaani tena filamu ya Kimarekani inayovunjia h e s h i m a m a t u k u f u y a Ki i s lamu na kuwataka Waislamu kuwa watulivu na kutohatarisha maisha ya watu wasiokuwa na hatia.

Baada ya filamu ya kashfa…

Vitabu vya Kiislamu vyauzwa kwa wingi UingerezaLONDONBAADA ya kutoka filamu inayomvunjia heshima Mtume (saw) na kuibua kadhia kubwa duniani, Wananchi wa Uingereza wanaelekea kwa wingi katika maduka ya kuuza vitabu vya Kiislamu kwa lengo la kutaka kuijua vyema dini tukufu ya Uislamu.

Baadhi ya watumishi wa maduka ya kuuza vitabu nchini Uingereza yameleza kuwa, uuzaji vitabu vya Kiislamu umeongezeka

kwa asil imia 30 nchini humo baada ya kutolewa filamu ya Innocence of Muslims inayomtusi Mtume Muhammad (saw).

Ripoti zinasema kuwa baada ya kutazama filamu hiyo ya Kimarekani, Waingereza wasio Waislamu wamekuwa na hamu kubwa ya kuujua Uislamu na wamekuwa wakinunua kwa wingi vitabu vinavyohusiana na dini hiyo ya Mwenyezi Mungu.

Tar jumi ya lugha ya Ki ingereza ya Qur ’ani Tukufu ni miongoni mwa vitabu vinavyouzwa kwa wingi nchini humo.

CINDY Lee Garcia, msanii aliyecheza filamu ya “Innocence of Muslims

MTAYARISHAJI wa filamu ya kumkashifu Mtume (s.a.w.) Nakoula Basseley Nakoula.

Page 6: ANNUUR 1036

6 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 28 - OKTOBA 4, 2012Makala/Matangazo

Inawatangazia Mahujaji wake wote kuwa Safari ya kuondoka ni tarehe 09/ 10/2012 na 11/10/2012Kurudi ni tarehe 03/ 11/2012 na 05/11/2012Mahujaji wote wamalize kuchanja haraka iwezekanavyoPaspoti zipelekwe ofisini kwa ajili ya Viza na SafariSemina Dar es salaam siku ya Jumapili tarehe 30/ 09/ 2012 Madrasatul Jabalhira Magomeni karibu na ofisiniZanzibar ni Suni Madrasa Mkunazini tarehe 08/09/2012.Wamalize malipo na taratibu zote za safari.Nafasi bado zipo bei zetu ni USD 3,375 tu kwa huduma zote pamoja na mahema maalumu ( VIP). Kwa mawasiliano zaidi piga simu.FOMU ZINAPA TIKANA A. Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es salaam Mtaa wa Dosi na Mkadini Nyumba Namba 26 Mkabala na Showroom ya Magari Tel- 0713 730444 au 0773 804 101 AU 0785 930 444 AU 0773 930444.B. Ofisi ya Ahlul Daawa Zanzibar Raha leo Tel- 0777 484 982 0777 413987C. Abubakari Maulana wa Markaz wa Kiwalani Dar es salaam Tel- 0784 453 838D. Abdallah Salehe Mazrui (Hoko) Dar es Salaam Tel-0715724444E. Salim Is-Haq Dar es Salaam Tel-0754 286010 au 0774 786101F. Dukani kwa Abdalla Hafidh Mazrui Wete-Pemba Tel-0777482665G. Dukani kwa Mohammed Hafidh Mazrui Mkoani Pemba Tel-0777456911H. Sheikh Daud Hamis Sheha Tel-0777 679692I. Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar Tel-0777 417736

Wahi kulipiaUsisahau kikundi cha Ahlul Daawa ni cha bei nafuu kuliko vingine na huduma bora kuliko wengi

Wabillah Tawfiq

AHLUDAAWA HAJJ AND TRAVEL AGENCY

BIA ni ulevi ambao ni maarufu hapa nchini na duniani kote. Pamoja na bia, pia baadhi ya Watanzania wamekuwa watumiaji ‘wazuri’ wa pombe kali.

Madereva wa pikipiki za kubeba abiria maarufu kama ‘boda boda’ na wale wa daladala siku hizi wamekuwa wateja wakubwa wa pombe kali zinazofungashwa kwenye vifuko maarufu kama ‘viroba’, ambavyo vimekuwa vikiuzwa kiholela mitaani.

Wote hawa wanatumia sehemu kubwa ya fedha wanazopata kunywa vileo hivyo bila kujua athari zake kiafya na kijamii kwa ujumla. Matokeo yake ajali za pikipiki haziiishi, watu wanapoteza maisha, mali zinaharibika, wamekuwa wateja wa maradhi. Wakati wanywaji wakiongezeka na afya zao kudhoofu, serikali kwa upande wake imekuwa ikineemeka na kujivunia pato kubwa.

Bei kwa wanywaji kwa kila chupa ya bia ni kati ya shilingi 1,500 na shilingi 1,700 na faida kwa kila chupa inayonyweka ni kati ya sh 250 na sh 400.

Biashara ‘huchangamka’ zaidi nyakati za sikukuu ambapo watu wengi hutumia zaidi vilevi pengine kuliko vipindi vingine.

Kwa kukimbiza pato la ulevi, leo kila mahali kumezagaa bar na grocery, ambazo zimeanzishwa kama uyoga kutokana na kuongezeka wanywaji wa pombe. Wenyewe wanasema kuwa biashara ya vileo ndio biashara yenye faida kubwa na ya uhakika isiyopungukiwa wateja.

M o j a w a p o y a v y a n z o vikubwa vinavyolipatia taifa mapato kupitia makusanyo ya kodi ni pombe. Pamoja na kodi kubwa inayolipwa serikalini na makampuni yanayotengeneza pombe nchini, hasara kubwa za kiafya na kiuchumi zimekuwa zikisababishwa na ulevi. Pamoja na kuonekana kuwepo faida kwa serikali kupitia kodi, ukweli umeendelea kubaki palepale kwamba pombe imekuwa na athari kubwa katika maisha ya binadamu.

Kwa kipindi cha mwaka 2011/2012, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ilipata faida kwa asilimia 30 na kufikia Shilingi bilioni 239 ikilinganishwa na faida ya Shilingi bilioni 219 mwaka juzi.

Akizungumza katika kikao cha wanahisa wa kampuni hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TBL, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya, alisema kufuatia mafanikio hayo walifanikiwa kulipa shilingi bilioni 312 serikalini na kuongeza kodi zilizolipwa na kampuni hiyo kufikia asilimia 32.

Kampuni tanzu ya TBL, Tanzania Dist i l ler ies Ltd yenyewe ilielezwa kuongeza mapato kwa asilimia 26 na

Raha ya kodi inatuletea Taifa la waleviNa Shaaban Rajab kufikia shilingi bilioni 801 kwa

mwaka uliopita, ikilinganisha na shilingi bilioni 528 kwa mwaka juzi.

Kwa sasa kampuni za vileo ndizo zinazoingiza faida na kulipa kodi kubwa serikalini. Kati ya mwaka 2005 hadi 2011 moja ya viwanda hivyo kililipa shilingi bilioni 165.4, kingine kililipa shilingi bilioni 13.4 huku kile cha sigara kikichangia shilingi bilioni 92.1.

Kati ya makampuni kumi na tano yanayoongoza kwa kulipa kodi, makampuni matatu ya vileo yameshika nafasi za juu ambapo yamechangia takriban asilimia 30 ya kodi serikalini sawa na shilingi bilioni 270.9.

Wakati serikali ikijivunia kodi kubwa kutokana na pato la vileo, watu wake wanaendelea kuathirika kila uchao. Hasara kubwa zimedhihiri katika kaya na familia za Watanzania ikilinganishwa na faida ya kodi inayokusanywa. Kutokana na kukithiri kwa kiwango cha watu kulewa au kunywa pombe, imefikia hatua serikali ikalazimika kupiga marufuku unywaji wa pombe nyakati za asubuhi na mchana.

Hatua hiyo ya serikali bila shaka imetokana na kukithiri kiwango cha unywaji pombe kiasi kwamba watu hawana muda maalum wa kulewa au kunywa. Hali hii bila shaka huzaa Taifa la watu wazembe, wavivu na wapenda starehe zaidi kuliko wachapakazi.

Wiki iliyopita, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Seif Rashid alisema kuwa serikali ipo mbioni kutengeneza sera madhubuti itakayohusu kudhibiti tatizo la unywaji wa pombe ambao umekithiri nchini na kuathiri jamii hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

K a d h a l i k a a l i s e m a k u w a m a g o n j w a m e n g i yanayo igha r imu se r ika l i yametokana na unywaji pombe. Amebainisha kuwepo athari za kuvunjika ndoa na kuongezeka ajali mbalimbali zikiwemo za barabarani, ambazo ni matokeo ya vileo.

Dkt. Rashid alisema hayo wakati akifungua mkutano wa sera ya matumizi ya vileo katika nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki, ulioandaliwa na taasisi ya IOGT-NTO, Movement International Institute ya watu wa Sweden na uliofanyika mjini Arusha. Mkutano huo ulibebwa na kauli mbiu ya ‘Kilevi si bidhaa ya kawaida na ni kikwazo katika maendeleo.’

Pamoja na serikali kuonekana kuja na mikakati ya kudhibiti (si kuzuia ) unywaji pombe, lakini hatua hizo ni dhahiri hazikusudiwi kuleta athari iliyokusudiwa kwa kuwa ni serikali hiyo inayoneemeka na watu wake kuwa wanywaji wazuri wa pombe.

Madhara ya moja kwa moja anayopata mnywaji wa pombe ni makubwa kuliko faida inayopata serikali kwa watu

wake kuwa walevi. Licha ya kuwepo madhara ya kijamii kama kuvunjika ndoa, wanywaji kutokuwa na tabia ya kuwa na lishe bora, kutumia mapato kwa ulevi, mfarakano katika familia, ajali za barabarani, kupotea hadhi na heshma ya mtu, uzembe, uvivu, gharama zisizo za msingi n.k, lakini imedhihirika kuwepo madhara ya kiafya kwa jamii japo hakuna takwimu sahihi zinazoweza kuonyesha kiwango halisi cha madhara yanayopatikana.

Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa kuna jumla ya magonjwa 60 yanayosababishwa na unywaji wa pombe. Baadhi ya magonjwa hayo yametajwa kuwa ni saratani, maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi, unene kupita kiasi, utapiamlo, mimba kuharibika na kisukari, kuathirika kwa mishipa ya fahamu mwilini kote kwa kupunguzwa uwezo na kuungua baadhi ya viungo vya mwili hasa tumbo pindi mtu anapokunywa.

Wataalam wanaeleza kwamba katika kuathirika mishipa ya fahamu kumetizamwa kwa hatua nne kwa wanywaji. Hatua ya kwanza ni ile ya kuchangamka. Hapa mtu hujisikia mzima kuliko kawaida, moyo unapiga haraka, tumbo linameng’enya chakula haraka na hamu ya chakula kuongezeka. Hatua y a p i l i , m t u a k i e n d e l e a kunywa anachanganyikiwa na

kuzungumza sana, kukosa aibu, utu kubadilika, kutawala tabia za kimwili, hamu ya chakula kuongezeka na hapa ndipo watu wanaagiza nyama choma kwa wingi.

Mnywaji akiendelea kunywa pombe hucharuka kutokana na mishipa yake ya ubongo kushindwa kumiliki mwili. Mambo yote anayoyafanya hayana utaratibu kwani huwa mkorofi.

Mnywaji huwa mkorofi na anaongea maneno yasiyo na maana, baadhi ya wanywaji huchukulia hatua hii kama raha yao. Hapa kitu kinachojitokeza ni kupoteza hamu ya kula. Hatua ya nne mtu akilewa kupita kiasi huwa hajijui na analala fofofo kutokana na kupoteza fahamu. Huenda akajikojolea au kutapika, inategemea na kiasi cha pombe alichokunywa.

Wakati kwa upande wa viungo, pombe huathiri zaidi viungo vinavyopata pombe nyingi kila wakati mtu akiwa anakunywa. Mdomo, koo na tumbo, ni viungo ambavyo vyenyewe hufikiwa na pombe nyingi mara mtu anapomeza. Tumbo likiumia inaonekana kama maumivu ya tumbo, pengine kutapika na kuharisha. Lakini kutokana na utaratibu wa tumboni, lazima chakula chote pamoja na sumu au dawa vinavyonyonywa tumboni vipitie katika ini kuondoa sumu

na vyakula visivyohitajika.Na kwa sababu hii, pombe

yote mtu anayokunywa hupita katika seli za ini na zinajaribu kuiondoa, lakini nazo zinalewa chakari na baadhi zinakufa.

Ie leweke kwamba mtu akinywa kidogo seli chache zinakufa na akinywa sana zinakufa nyingi na nafasi yake inajazwa nyuzi nyuzi za makovu. Ini huwa na mabilioni ya seli ambazo ni imara, hata mtu akinywa pombe nusu, seli zake bado zitaendelea na maisha mpaka inafikia kikomo ini linashindwa kufanya kazi na kujikuta njia za nyongo na mishipa ya damu inaziba.

Kila kiungo mwilini kinaumia kwa wakati wake, lakini tumbo na ini ni mifano dhahiri . Kwa sehemu kubwa pombe husababisha utegemezi kuanzia ngazi ya familia hadi taifa. Baadhi ya maradhi yamethibitika kuwa husababishwa na pombe kwa wanaume. Baadhi yake ni uhanithi, kuharibu kongosho, saratani ya mdomo, njia ya haja kubwa na moyo kusinyaa.

Wataalam wamethibitisha kwamba nguvu kazi kubwa ya taifa ambayo ni vijana, hupotea kutokana na matumizi ya pombe ambapo huwa ndio kichocheo cha kupata maradhi ya ukimwi.

Nchi za Afrika Kusini , Zambia na Malawi zinatajwa kuwa zinaongoza kwa unywaji

Inaendelea Uk. 7

Page 7: ANNUUR 1036

7 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 28 - OKTOBA 4, 2012Makala/Tangazo

wa pombe. Hali hii imetokana na hulka za watu wa mataifa hayo kukubali kurithi tamaduni z a K i z u n g u w a u n y w a j i pombe. Wataalam wanasema kuwa asilimia 50 ya raia wa Afrika Kusini hutumia kilevi. Ni Afrika Kusini hiyo hiyo ambayo inaongoza kwa watu wake kuathirika kwa maradhi ya ukimwi.

Jambo la kushangaza ni kwamba imefikia hatua hapa nchini watu wamediriki kuanzisha hadi chama cha wanywa pombe! Wenyewe wamekiita chama cha wanywa pombe kwa staha Tanzania (TRBDA).

Pamoja na mambo mengine, chama hiki kazi yake imetajwa kuwa ni kuhakikisha wanywaji wanapata mahali pa kupaza sauti zao na tayari wameweka mikakakati ya kudai haki zao dhidi ya serikali kwa kile walichokiita ni kuongezeka bei ya vi leo ki la mwaka, kufuatia serikali kuongeza kodi za vileo. Wanadai hali hiyo inawaongezea wanywaji mzigo hivyo kulazimika kuzama zaidi mifukoni mwao ili kugharimia vileo hivyo.

Inashangaza zaidi serikali

Raha ya kodi inatuletea Taifa la waleviInatoka Uk. 6 kukikubali chama hiki na

kukipatia usajili kabisa Mei 22 mwaka huu. Bila shaka serikali ilikisajili kwa kuamini kuwa wanywaji ndio wanaoiwezesha serikali kupatikana pato kubwa la kodi.

Kazi za chama hiki zimetajwa kuwa ni kupigania bei nafuu ya bia ili wanywaji wamudu kulewa. Wakitaka serikali ikome kuongeza kodi katika ulevi huo ili na wao wamudu kunywa.

Nyingine ni kutoa ushauri kwa wale wanaokunywa pombe kupindukia, wanaofanya vitendo visivyofaa wanapokunywa na wale wasiotunza familia zao kutokana na ulevi.

Kwa sababu hiyo chama pia kitapokea malalamiko kutoka kwa watu mbalimbali, wakiwepo wanawake, wanaume ambao wanaona familia zinaathiriwa kutokana na mmoja wa wazazi kuendekeza ulevi.

Kwa hatua hii waliyofikia Watanzania kuongezeka idadi ya wanywaji na walevi, huku serikali ikifumba macho kwa kuchelea kupungua donge nono la kodi za vileo, basi lisubiriwe taifa la wagonjwa na watu walevi siku za usoni.

KITUO CHA MAFUNZO NA AJIRA CHA TAMPRO

MAFUNZO YA JINSI YA KUANZISHA KUSIMAMIA NA KUKUZA BIASHARA KWA

KUMLENGA MTEJA NA SOKO

Kutokana na maombi ya wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati, Jumuiya ya wataalam wa kiislam Tanzania (TAMPRO) kupitia kitengo chake cha Ajira na Mafunzo kinawatangazia wafanyabiashara na wajasiriamali wote kuwa kitaendesha mafunzo maalum ya Kuanzisha, kusimamia na kukuza biashara kwa kumlenga mteja na soko. Mafunzo yatakuwa kama ifuatavyo:-

Lengo: kuwapa mbinu na kuwajengea uwezo wajasiriamali juu ya kuanzisha, kusimamia na kukuza biashara kwa kumlenga mteja na soko.

Mahali: Ukumbi wa mikutano TAMPRO makao makuu

Muda: Jumamosi tarehe 29/09/2012 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni

Mada zitakazo wasilishwa: Ujasiriamali na taratibu za kuanzisha biashara, kukuza biashara kwa kumlenga mteja, kuunda mikakati ya kufanikisha biashara, kukuza biashara kwa umahiri wa kuuza, Namna ya kuweka kumbukumbu za biashara.

Gharama: Shilingi 20,000/= kwa mtu mmoja. (Kwa ajili ya cheti cha ushiriki, vitini vya mafunzo, na chakula) Kujisajili: Ili kujisajili tuma SMS yenye jina lako kwenye namba 0714 151532, 0767151532, 0719988919 au fika TAMPRO Makao Makuu, Magomeni Usalama, jirani na Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni.

TANBIHI: Ili kufikia lengo la mafunzo TAMPRO itatumia Wataalamu wenye uwezo na uzowefu katika nyanja ya biashara

Wahi kuijiandikisha kwani nafasi ni chache.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia 0714 151532, 0767151532, 0719988919, 0767989909, 0688988919 au [email protected]

Imetolewa na

MRATIBU MAFUNZO TAMPRO MAKAO MAKUU

Ndugu Mhariri,Naomba nami niungane na Waislamu wenzangu kutoa maoni yangu katika gazeti letu tukufu na tegemeo la wengi An-nuur.

Hapo zamani Waislamu walipokuwa wakilalamika dhidi ya NECTA nilikuwa nikidhani kuwa hawana uwezo wa kuingia kidato cha tano au hata kwenda Chuo Kikuu lakini nimethibitisha kuwa NECTA ni Machinjio ya Waislamu fuatilia Mkasa ulionikuta mimi mwenyewe.

Nilifanya mtihani wa kidato cha sita 2009 katika School ya binafsi ya Lumumba Zanzibar na nikapewa barua ya kuniruhusu kufanya mtihani bila ya tabu nashukuru nilifanikiwa nikaufanya huo mtihani wangu, baada ya hapo niliendelea kusubiri matokeo yangu mwisho wa siku yakatoka matokeo.

Muda si mrefu zikatolewa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa kuna majina ya wanafunzi yamezuiliwa nikiwamo mimi kat ika kituo cha Lumumba kwa sababu ya kusajiliwa mara mbili baada ya kuonekana tumefaulu mtihani wetu na kama kweli kwa nini musitoe ushahidi wa kuthibitisha usajili wetu katika vituo vyote tulivyosajiliwa ikiwa umekamilika kikamilifu kwa nini niruhusiwe kufanya

NECTA machinjio ya Waislamumtihani wakati sina sifa ya kufanya mtihani.

Nilienda NECTA katika kujua hali hii watu wa Baraza walinithibitishia kuwa ni kweli yamezuiliwa, vipi nitapata matokeo yangu ni suala liliwachanganya watu wa Baraza. Nilituma barua za maombi kama tano lakini sikujibiwa hata moja na mimi wenyewe nikaenda Baraza ikawa kazi ya kwenda na kurudi bila ya majibu zaidi ya kwenda na kurudi bila ya majibu zaidi ya mara tano ilipata wasiwasi mkubwa n i n a o n d o l e w a b i l a y a kuunganishwa na wahusika.

Wa l i n i t a k a n i p e l e k e vyeti vyangu vya kumalizia masomo Peter Lubimbi ndiye aliyehakiki vyeti vyangu na baadae aliniita na kunithibitishia wewe huna tatizo na utapata matokeo yako sasa hapa niko barazani Peter alipiga simu watu w a n a o h u s i k a m a t o k e o pale pale hakupewa jibu aliitwa ndani sikufahamu alichoambiwa na wenzake alipotoka alikuja na jibu jengine na akinicheka na kusema utatumiwa matokeo yako.

Nilipo muuliza sakata hili alimjibu kazi yangu mimi ni kuhakiki vyeti tu, lakini alishindwa kuniunganisha na wahusika. Nil ikuwa

nikiwasiliana nae kwa simu yake ya mkononi aliyonipa mwenyewe 0717 151 962 kila nilipokuwa nikimpigia simu alisikitika na kusema mimi sielewi wapi matokeo yako yamekwama lakini wewe humo katika kundi la wanafunzi waliozuiliwa matokeo yao. Rohoni nikisema k a m a h a y a k u z u i l i w a , basi itakuwa yamefutwa inawezekana kikundi cha watu wachache hujifungia chumbani na kuamua nani ach in jwe rohon i , nan i mkononi na nani miguuni.

Baada ya muda mrefu kupita bila kupata taarifa kutoka NECTA niliamua kuandika barua ya kutishia kwenda Mahakamani. Mara moja nilijibiwa kwa simu ya Mkononi 0652 088148 na alijitambulisha kwa jina la Mheza akijibu kwa upole kwa tumefanya mabadiliko

ya matokeo yako, cheti chako bado picha tutumie kwa Njia yoyote ile.

Wanafunzi wote katika kituo nilichofanyia mtihani taarifa wameshapewa mimi tu nikijiuliza hii nchi ya kusadikika? Au mzuri bado

hajazaliwa? Jee? Mauaji haya yanatokana na MfumoKristo? Kuwanyima Waislamu Pass (Credit) za kuingia chuoni.

Zubeir Machano0778 422 002Zanzibar

DKT. Shukuru Kawambwa DKT. Joyce Ndalichako

Page 8: ANNUUR 1036

8 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 28 - OKTOBA 4, 2012Makala

KWA mara nyingine tena, filamu mpya ya kupinga Uislamu inayoitwa ‘The Innocence of Muslims’ i m e t o l e w a n c h i n i Marekani. Wakishindwa kabisa kudhibiti sumu na chuki waliyonayo dhidi ya Uis lamu, makafir i w a m e r u s h a k o m b o r a lingine zito dhidi ya kipenzi chetu Mtume wa Mwenyezi Mungu. Kafiri Sam Bacile, mtunzi wa filamu hiyo, siyo wa kwanza kutayarisha maigizo ya kumtukana Mtume, na wala hawezi kuwa wa mwisho.

Baada ya kushindwa kabisa kuubomoa Uislamu na maadili yake mema kwa hoja za kitaalamu (Intellectual Argument), sasa ulimwengu wa Magharibi umebaki na matusi, uongo, propaganda na ghushi. Mashambulizi kama hayo mwisho wake ni kushindwa tu. Kwanza yanazidi kuwaimarisha Waislamu duniani kote na yanaleta hamasa kubwa zaidi ya Uislamu kwa wasio Waislamu. Uislamu ni dini inayokua kwa kasi zaidi barani Ulaya na Marekani:

“ Wa n a t a k a k u z i m a nuru ya Mwenyezi Mungu (Uislamu) kwa vinywa v y a o ; n a M w e n y e z i Mungu atakamilisha nuru yake ijapokuwa makafiri watachukia” Qur(61:8).

Kwa matusi mazito kama hayo anayotukanwa Mtume wa Mwenyez i Mungu , Waislamu wote duniani wanapaswa kuunganisha nguvu zao za k i s iasa , kiuchumi, kielimu na hata za kijeshi ili kulinda heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu. Mtume amedhali l ishwa kupitia filamu iliyowekwa kwenye mtandao wa Internet. Kama ilivyotokea siku za nyuma, hasira za Waislamu kutokana na kitendo hicho kiovu, hususan katika miji ya Cairo, Benghazi, Khartoum, Tunis, Rabat, Sanaa na Tehran zimetikisa Ikulu ya Marekani na maeneo mengine ya dunia.

Hasira hizo za Waislamu, kama ilivyo kawaida, pia zimekutana na shutuma nyingi kutoka kwa watoa m a o n i w a k i s e k u l a , wakiupaka matope Uislamu kuwa ni dini isiyovumilia kukosolewa. Wanashangaa k w a n i n i M t u m e w a Mwenyezi Mungu kuguswa kidogo tu, inaleta ghasia na machafuko ulimwengu mzima wa Kiislamu! Katika kujibu hoja hizo, ningependa kuwapitisha wasomaji wangu katika nukta kadhaa muhimu za kuzingatia.

Kwanza , kumtukana Mtume wa Mwenyezi Mungu, limekuwa na litaendelea kuwa ni jambo lisilokubalika kabisa kwa Waislamu. Hili ni jambo lisilo na mjadala kwetu duniani kote. Hakuna namna ya kuzungumza. Katika

Tulinde heshima ya MtumeNa Said Rajab

medani ya kidiplomasia inaitwa ‘Non-Negotiable Point’.

Pili, vitendo kama hivi vya watu wa Magharibi, ni maadili yaliyojengeka juu ya msingi wa kutenganisha dini na siasa. Yaani kuondoa dini katika uendeshaji wa kila siku wa maisha ya binadamu. Katika jamii kama hizi, wanawake hudhalilishwa kwa mujibu wa sheria, watoto hawako salama na hakuna kuheshimiana. Hawaheshimu sheria, hawaheshimu walimu na hata watu watukufu kama mitume.

K w a s a b a b u j a m i i imepoteza heshima kwa

Mwenyezi Mungu, basi inaona kuwatukana Mitume wake ni jambo jema na sehemu ya uhuru wa kutoa maoni . Kama kawaida, Waislamu wanatarajiwa kuvumilia “uhuru” wa watu wengine kuwatukana na kuwadhalilisha! Utaratibu huu wa kuwaacha watu watoe maoni bila mipaka, umeshaleta maafa makubwa barani Ulaya na Marekani. Tumeshuhudia mauaji ya kimbari Bosnia, watu weusi wali teswa Marekani na Mayahudi kuangamizwa Ujerumani.

Ta t u , m a s h a m b u l i z i kama haya dhidi ya Mtume

w a M w e n y e z i M u n g u hayatokei kwa bahati mbaya, isipokuwa ni propaganda katika ulimwengu ambao Marekani na washir ika wake, kama Uingereza na Ufaransa hutumia kuzivamia nchi za Waislamu. Wanasiasa wakubwa wa nchi hizo hujaribu kujenga mtaji wa kisiasa kwa kudhalilisha Uislamu na Waislamu.

Janga kubwa linalowakabili Waislamu duniani leo ni kukosekana kwa Mamlaka kamili au dola ya Kiislamu a m b a y o i n a s e r i k a l i inayoendeshwa Kiislamu. Wananch i wa nch i z a Waislamu, kama Misri, Libya,

Sudan, Tunisia, Yemen na nyinginezo wameumia mno Mtume wao kudhalilishwa na makafiri. Kwa ujasiri m k u b w a , w a m e v a m i a balozi za Marekani, ambazo zina ulinzi mkali zaidi kuliko balozi zote duniani. Hawawezi kuvumilia kuona Mtume wa Mwenyezi Mungu akitukanwa!

Kwa sababu ya kulinda heshima ya Mtume, Waislamu nchini Libya wameua balozi wa Marekani na maafisa wengine kadhaa wa ubalozi huo. Katika mazingira ya kawaida ungetarajia viongozi wa nchi za Waislamu kama Dk. Mohammed Mursi wa Misri, Mohammed el-Magariaf wa Pakistan, Abdullah al Saud wa Saud Arabia, Hassan al Bashir wa Sudan, kuvunja uhusiano wa kibalozi na nchi yeyote inayoruhusu matusi kama hayo, ikiwa ni pamoja na kuacha kabisa kuziuzia hata tone la mafuta. Lakini viongozi hawa wameshapigwa ganzi la Obama na Clinton na wameahidi kushirikiana na Marekani kuwasaka Waislamu. Katika kadhia hii, wao na wananchi wao wametofautiana.

Nne, Uislamu haukukataza mdahalo kuhusu imani zake. Uislamu haujakataza mfumo wake wa maisha kukosolewa na viogozi wake watukufu kuchunguzwa kiuadilifu. U i s l a m u u m e a m r i s h a subira kwa waumini wake kuvumilia matusi ya wajinga. Umetoa haki kwa watu wote, Waislamu na wasio Waislamu - haki zao za kuishi, kuabudu, kuheshimiwa, mali zao kulindwa na kutoa maoni. Hakuna mfumo wowote duniani ulioweza kufika hatua hiyo.

Lakini pamoja na hayo, Uislamu pia umechunga haki ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake kuheshimiwa n a k u t o t u k a n w a w a l a kudhalilishwa na mtu yeyote yule. Uislamu ni dini ya kweli na nguvu yake ya hoja (Intellectual Strength) imeifanya udumu kwa karne nyingi na itaendelea kudumu mpaka s iku ya k iama. Mifumo yote iliyobuniwa na binadamu ambayo msingi wake ni upotofu itatoweka tu. La msingi zaidi, Waislamu tus ikubal i hata k idogo kulegeza msimamo wa dini yetu. Mwenyezi Mungu anatuonya:

“Wanataka lau mngekufuru kama walivyokufuru wao ili muwe sawa sawa”Qur(4:89)

Nimalizie tu kwa kutoa wito kwa Waislamu kukabiliana na udhalilishaji huu dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa kusambaza ujumbe sahihi wa Uislamu, ikiwa ni pamoja na kuonyesha sifa njema za Mtume wa Mwenyezi Mungu kama binadamu, mume, baba, kiongozi wa dola, kiongozi wa kisiasa na kamanda wa jeshi.

WAISLAMU wakiwa katika mkusanyiko uliofanyika katika viwanja vya Kidongo Chekundu wiki iliyopita, Jijini Dar es Salaam. [Picha zote na Bakar Mwakangwale]

Page 9: ANNUUR 1036

9 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 28 - OKTOBA 4, 2012Makala

SENSA ya mwaka 2012 i m e a c h a m a j e r a h a m a k u b w a s a n a k w a Waislamu nchini Tanzania. Taar i fa toka s ehemu mbal imbal i mij in i na vijijini zinaeleza Waislamu kukamatwa na askari wa jeshi la polisi, kupigwa mabomu ya machoz i , wanawake kudhalilishwa, kuzabwa vibao na polisi wa kiume.

Kuna tukio moja mjini Muleba-Kagera, Mama alitiwa selo ya polisi na mwanae mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 2 kuanzi saa 5 asubuhi hadi saa moja jioni. Mtoto mwingine mwenye umri wa mwaka 1 na miezi michache alikaa selo zaidi ya masaa 24, hadi pale mama yake alipoachiwa huru tena bila masharti yoyote ingawa Mama mtoto hakubadili msimamo, aliendelea kugoma kuhesabiwa.

Taarifa nyingine zinasema askari polisi wanaume wa kituo cha Bukoba mjini tarehe 26 Septemba 2012 waliwapiga picha [moving camera] wakina mama wa Kiislamu wakiwa uchi chini ya ulinzi wa polisi katika kituo cha kati mjini Bukoba usiku wa terehe 26 Septemba 2012 na kuwakejeli. Taarifa k u t o k a M u l e b a m j i n i zinaaeleza kuwa polisi wa kiume waliwatomasatomasa wanawake wa Kiislamu nywele zao na kuwakejeli. Pia taarifa zaidi zinaeleza kuwa askari polisi mjini Muleba na Kyaka walivamia na kuvunja milango ya nyumba za Waislamu kadhaa, kuwanasa vibao wanawake kuwavua, Hijaab na kuwapeleka vituo vya polisi. Ripoti kutoka Zanzibar pia zinaeleza kuwa askari polisi walimnasa vibao Sheikh mmoja na kumfunga pingu huku wakimuelekezea mkewe mtutu wa bunduki na kumlazimisha kujibu maswali ya karani wa sensa. Kwa ujumla matukio yote haya ni ya kuudhi kwani yamewadhaalilisha Waislamu na kuwaachia simanzi.

Hata hivyo, pamoja na yote hayo, sensa hii imeleta faida kubwa kwa Waislamu. Kwanza imepelekea Waislamu wengi kupata Sunna ya Mtume Yusuf ya kukaa jela kwa ajili ya kutafuta radhi za Mola wao sambamba na kupinga dhulma dhidi ya mfumokristo.

Pili, kuna matumaini kuwa mtihani wa kutiwa ndani kwa ajili ya kupinga dhulma umewapandisha dara ja Waislamu na kuwaweka tayari kwa mtihani mwingine, kwani kawaida mitihani huwa na malengo ya kukuza Imani za waja. Tunamuomba Allaah [SW] ajaalie waliofuzu mtihani huu wafuzu na itakayofuatia na mwisho aje awalipe Pepo.

Pia mitihani huwa na malengo ya kuwapambanua

Faida iliyotokana na sensa 2012Abaa Swaaliha

[kuwachuja] waja katika harakati zao za kuuendea ukombozi, “…bila shaka tuliwatia katika taabu wale waliokuwa kabla kabla yao ili , na kwa yakini Mwenywzi Mungu atawatambulisha wale walioku wakweli na atawatambulisha wale walio waongo” [29:3].

Katika sensa ya mwaka huu, awali Waislamu wote waliungana katika msimamo wa kupinga kushiriki wakiwa na hoja za msingi, lakini kwa mshangao mkubwa baadhi ya taasisi zikajitoa kundini na kuwa upande wa dhalimu.

Sensa pia imeleta mwamko mkubwa miongoni mwa Waislamu. Kwa mfano, nimepata kutembelea wilaya kadhaa za mkoa wa Kagera, Waislam wengi hata waliomo ndani ya Bakwata, walikuwa hawaungani na msimamo wa viongozi wao wakuu, wakawa na msimamo wa kupinga sensa ya kidhalimu. Nilipata bahati ya kusikiliza maongezi ya baadhi yao, hawakuwa na hoja za kukinaisha juu ya kwa nini wanagomea sensa nadhani kwa sababu ya mtandao tuliona Waislam katika kupashana habari, lakini bado walishikilia msimamo, taarifa za juujuu kwamba sensa ni muendelezo wa dhulma dhidi ya Waislamu ziliwatosha kugomea zoezi la sensa.

Sensa hii pia imedhihirisha

kuwa kila kona katika serikali, hata katika ofisi ya takwimu, kumejaa mawakala wa mfumokristo wenye malengo ya kuendeleza dhulma, kwa mfano ni akili gani ya kuweka dodoso la kuhesabu nyumba za watu, kisha usione umuhimu wa kutaka kujua wakaazi wa nyumba hizo! Unataka kuhesabu Misikiti na makanisa, unagoma kuhesabu idadi ya watumiaji wake! Bw. Matimbwa na Sheikh Barahiyani wameeleza kwa kina malengo ya kutaka kuhesabu nyumba za ibada na kugomea hitajio la kujua watumiaji wake. Kumbuka walioweka kipengele hiki ni watumishi wa serikali ambao ni mawakala wa kanisa.

Faida nyingine ni kuwa maamuzi ya serikali pale yanapokutana na maslahi ya kanisa na ya wananchi wengine, kinachozingatiwa ni msimamo wa kanisa wala si hoja. Rejea mkutano wa maofisa wa takwimu na viongozi wa Dini mjini Dodoma tarehe 11 Juni 2012, Waislam walidhoofisha hoja za serikali, na kujenga hoja kinaifu juu ya msimamo wao, viongozi wa Kikristo hawakutoa hoja, bali “hatutaki kipengele cha dini kiwepo katika dodoso la sensa” kwa nini? Hatutaki tu! Kimantiki wenye hoja ndio walitakiwa k u s i k i l i z w a , m a m b o yakakiuka mantiki! Kanuni

ya “hoja ya nguvu” ikafanya kazi na si “nguvu ya hoja”, kwa nini? Ndio msimamo wa kanisa. Waislamu wanapata funzo kuwa wanapokuwa na mjadala utakaopelekea maamuzi fulani na wao wakawa na maoni kinzani na kanisa hata kama wana hoja madhubuti, waende mezani wakiwa na namna mbadala ya kushinikiza matakwa yao kwa sababu kanisa na serikali huwa hawatizami hoja. Rejea uzoefu katika malalamiko ya maaskofu na kesi zote za kuukashifu ukristo, pamefanyika vikao kadhaa kati ya serikali na viongozi wa Dini, Wakristo wakiwa walalamikaji na Waislam walalamikiwa, wakristo walishindwa kutetea hoja , lakini mwishowe Masheikh na Wahadhiri wa Kiislam waliishia jela, na damu ya Waislam kumwagwa Mwembechai.

Jengine ni namna sensa imevyokuwa ik i tumika kuhujumu maeneo ambayo Waislam ni wengi, kumbe hata maafisa wa Takwimu hutumika kutoa takwimu potofu ili kuhalalisha hujuma dhidi ya Uislam na Waislam. Kwa mfano, binafsi nimekuwa napata taabu kufahamu ni kwa namna gani mikoa yenye Waislam wengi ambayo i l ikuwa imepiga ha tua kubwa kimaendeleo miaka ya mwanzoni ya uhuru, leo hii iko nyuma imeandamwa na umasikini kiasi cha kutisha, ina bandari ambazo kitaalam ni moja ya vitu muhimu sana katika kukuza uchumi wa eneo husika na kuwaendeleza wananchi wake, kumbe moja ya mbinu ni kuchakachua takwimu za idadi ya watu, ili pasiwepo na vipaumbele katika kuelekeza hudumu muhimu za kuwaendeleza wanachi wake.

Kadhalika ni ule ujasiri waliouonyesha Waislam, m f a n o m j i n i B u k o b a , Muleba, Tanga, Zanzibar na kwingineko, pale ambapo polisi waliwakamata Waislam wachache kwa tuhuma za kugoma kuhesabiwa, mamia ya Waislam walijikusanya vituo vya polisi na kuwaambia maofisa wa polisi wafungue milango kisha wawaweke wote ndani [wawatie jela] kwani hawakuwa tayari kuhesabiwa.

Vitisho hivi viliwazidishia Iman i Wa i s l am “Wale waliomwitikia Allaah na Mtume wake baada ya majeraha yaliyowapata, kwa wale waliofanya wema…wale ambao watu waliokodishwa waliwaambia Waislam .Watu wamekukusanyikieni kwa hivyo waogopeni. Lakini maneno hayo yakawazidishia imani [Waislam] wakasema “Mwenyezi MwenyeziMungu

Anatutosha Naye ni Mlinzi bora kwetu” [3:172-173].

K w a m f a n o , k a t i k a harakati za kumshurutisha Sheikh Muhammad Swiddiiq Mudiir wa AMYC-Kyaka, mkoani Kagera, mkuu wa wilaya ya Misenyi kanali mstaafu Issa Njiku akiwa na maafisa wengine wa polisi huku wamemuelekezea mitutu ya bunduki kituo cha polisi Kyaka, Kanali Njiku alimwambia Mudiir kuwa haoni fedheha kulazimishwa kwenda polisi kwa ajili ya kakataa kuhesabiwa na baadae kumwabia kuwa kanzu yake imechafuliwa katika harakati za kumpeleka polisi kwa sababu askari polisi walikosa ustaarabu hadi kufikia hatua ya kumchafulia Sheikh kanzu yake?

kwa ujasiri na bila chembe ya woga Mudiir alimjibu mkuu wa wilaya “Kuna wengine Kanzu zao huchafuliwa na damu katika kutafuta Radhi za Mola wao na kutetea haki zao, zeuze vumbi”

Hapa naomba pia niunganishe na tukio lililomkuta Marehemu H a s s a n w a k a t i Wa i s l a m wakifuatilia hatma ya kesi ya kuchanwa Qur’an mahakama kuu mjini Mwanza, askari polisi walimchoma na singe Marehemu Hassan mguuni na kumjeruhi, wakati anavuja damu, alimwambia askari polisi asipate taabu, akamtegea kifua na kumwambia “nipige risasi nife lakini sitorudi nyuma katika kutetea haki na kuuhami Uislam”. Maneno haya pia yamebeba ujumbe mzito na muhimu kwa Waislam na kwa upande wa dhalimu pia.

Kanisa na serikali wanatakiwa wafikir ie sana, binaadam akidhulumiwa sana, hufika hatua akachoshwa na akaona kufa ni bora kuliko kuishi, kwa kuwa kuna aliyemsababishia hali hiyo, ni vigumu kutabiri mdhulumiwa ataamua kufa kwa staili gani, huenda akaamua kuondoka na aliyemfikisha hatua hii, na Waislam wanapokufa katika harakati za kutetea haki zao na kulinda heshima ya Dini yao huwa hawana cha kupoteza, tena hutamani kifo cha namna hiyo kwani kwao kina heshima kuliko kifo chochote kile.

Faida nyingine ni ule umoja na mshikamano waliounyesha Waislam wakaweka mbali tofauti zao za kimadhehebu, kwa mfano, mkoani Kagera Viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam walitoa agizo kuwa yeyote atakayekamatwa kwa kosa la kugoma kuhesabiwa, suala litakuwa ni la Waislam wote, na hili lilidhihirishwa na Waislam kwa vitendo.

Ukizingati nukta hizi, basi pamoja na madhila, udhalili na manyanyaso waliyoyapata Waislam katika sakata la sensa ya Watu na makaazi nchini Tanzania 2012, kuna faida kubwa na nyingi kwa Waislamu wenye kutafakari.

Allaah [SW] Anatuambia Waislam “Na msilegee wala msihuzunike, maana nyinyi ndio mtakaokuwa juu ikiwa mnaamini kweli” [3:139]

MMOJA wa Waislamu mlemavu jijini Arusha aliyepata usumbufu katika zoezi la sensa lililomalizika hivi karibuni.

Page 10: ANNUUR 1036

10 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 28 - OKTOBA 4, 2012Makala/Tangazo

SHUKRANI zote anastahiki Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote na rehema na amani zimfikie mtukufu wa mitume (S.A.W).

Kwa hakika mada hii ni miongoni mwa mada muhimu kwa sehemu kubwa na kwa hivyo sisi tunaona baadhi ya nyakati tofauti ya maoni hupelekea watu kutengana na kugombana kwa muda mrefu au mfupi.

Tunaz inga t i a juu ya hayo mambo mawili : - Kutofautiana ni mwenendo wa kimaumbile. Kutofautiana hakukimbiliki.

K w a n z a : - H a k i k a ku tofau t iana maoni n i

Kutofautiana maoni katika Uislam hakuharibu upendo kwa Waislam

Na Sheikh Waheed Mansour Mohamed

mwenendo wa kimaumbile na pia upo tangu kuumbwa viumbe kwani ni tabia ya viumbe na wala haiwezekani kuwakusanya watu kwa neno moja na kwa maoni aina moja na kwa hivyo amesema Mwenyezi Mungu mtukufu, “Na lau angetaka Mola wako angewafanya watu wote umma mmoja (kundi moja) lakini hawaachi kutofautiana”.

Surat Huudi aya ya 118, kwa hakika kutofautiana wa tu na kugawany ika makundi yaki – taifa, ki – maumbile, ki – dini na kuongezea mgawanyiko wa kimadaraka na vyeo huu ndio msingi wa maisha na jamii na mwenendo wake na kusababisha Dunia isisimame mahala pamoja.

Amesema Mwenyez i M u n g u m t u k u f u , “ N a miongoni mwa milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbali mbali na mingine myeusi sana” Surat Fatir aya ya 27.

Na kwa hakika kutofautiana kwa rangi na viumbe na

lugha zao na imani zao hivi ni kuthibitsha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu na uwezo wake kama inavyowakilisha kutofautiana rangi kwa maua na tabia za viumbe ni dalili ya kustarehe kwa mtu isipokuwa sio kwa kustarehe kwa kutofautiana kwa maua yenyewe tuu bali hata katika nafsi yake mwenyewe pia.

Amesema Mwenyez i Mungu, “Na katika nafsi zenu hamuoni” na masomo ya elimu ya nafsi na jamii imesimama misingi hii na kwa hekima amehukumu Mola Mtukufu akasema, “Enyi watu sisi tumewaumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke na tukakufanyieni mataifa na makabila ili mjuane hakika mbora wenu kwa Mwenyezi Mungu ni yule amchae sana hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi na mwenye habari”. Surat Al hujurati aya ya 113.

Pili:- Popote ulipo tofauti haikwepeki kwa uhakika mara ngapi tunashitaki kuwepo na matatizo, mizozo na ugomvi kwa mambo madogo au makubwa au yenye nguvu

kubwa na hii ni sehemu kubwa ya mahusiano ya kibinadamu na kijamii ikiwa ni ndugu wa karibu au marafiki na tofauti zote hutokana na kuteleza kwa ulimi na dhana mbaya na kutokuheshimiana na hili linakuwa ndio fungu lake tosha kwa ulimi na uadui wake ambao ni ujanja na wasiwasi ambao upo kwa njia ya kujificha kwa mtu.

Amesema Mtume (S.A.W), “Kwa hakika shetani amekata tamaa kuabudiwa na watu wanaoswali katika kisiwa cha Uarabu lakini kuwatia wasiwasi kati yao”.

Ameitoa hadithi hii Imamu Muslimu na hapa tutasimama kisimamo kirefu kati ya neno letu kwa tofauti ya maoni hayaharibu mapenzi katika jambo lolote.

Ni kwa nini tunatengana pale tunapotofautiana? Sisi tunatengana wakat i wa kutofautiana na kwa sababu sisi tumekosa uwezo wa kuelewa juu ya makusudio ya watu wengine na kuacha kupokea muelekeo wa muono wao.

Na hakuna vitendea k a z i v y a k u v u n j a mijadala inayokuja. Pia kutokuheshimu lugha ya midahalo na kung’ang’ania maoni yako na kukataa kuiachia hata kama itakuwa ina makosa.

N a i t a k a p o k u w a kutofautiana kunapelekea hadi kutengana, hapo mapenzi yanakwenda wapi? Ikiwa kutofautiana kunahitaji hadi miaka ili kurudisha upya mapenzi, bas i upo wapi ubora wa hadithi ya Mtume (S.A.W) na itakapokuwa kutofautiana kunapelekea hadi kukimbiana mapenzi yanakwenda wapi? Na ikiwa kutofautiana kunapelekea hadi kuchukiana, basi unakwenda wapi urafiki.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atupe Elimu ya Dini yetu na atuonyeshe kwa macho yetu na azizoeshe nafsi zetu katika kuelewa.

WA I S L A M U k a t i k a m j i w a S u m b a w a n g a wameusalimisha mji huo na machafuko baada ya kuzuiya wahadhiri wa Kikristo kufanya mhadhara wa kumkashifu Mtume (s.a.w).

Awali, Waislamu walitoa onyo kuwa endapo Polisi hawatazuiya mhadhara huo, basi wajue watabeba lawama kwani yaliyomkuta Balozi wa Marekani pale Benghazi, L i b y a , n d i y o i t a k u w a hatma ya wahadhiri hao wa Kikatoliki.

Kufuatia tangazo hilo, na kufuatia hatua ya polisi na serikali kutokujali, ‘rijali’ katika wanaume wa Kiislamu waliuzunguka mhadhara huo hali iliyowatisha wahadhari wakabadili mada.

Awali gari la matangazo la Kanisa Katoliki lilipita k a t i k a M a n i s p a a y a Sumbawanga wakitangaza kuwa kutakuwa na mkutano wa Injili na mojawapo ya mada itakayokuwapo ni k u m c h a m b u a M t u m e Muhammad (SAW).

H i v y o W a i s l a m u walitangaziwa katika misikiti kuwa huo ni uchokozi wa Wakristo.

Kwa mara ya mwisho mapema mwaka huu kulikuwa na mdahalo mkubwa wa Wakristo na Waislamu na ulikuwa wa amani bila ya

Waislam Sumbawanga wafanya kazi ya Polisi

Waliosusia sensa Rukwa wanusurika kifungo

Na Mwandishi Wetu

fujo.Katika mdahalo huo,

timu ya Waislamu ilikuwa imekamilika kwa wahadhiri maarufu wakiwemo Ust Mazinge, Ust Juma Kinyogoli, Ust Ally Kadogoo, Ust Shafii Omary, Ust Muarobaini, Ust Ibrahim na wengine wengi.

Hata hivyo, baada ya siku 3 za mdahalo, Mkuu wa Wilaya (DC) Mkatoliki a l ipoona wanaelemewa akapiga marufuku na mdahalo ukaishia kabla ya wiki nzima mbele.

S a s a w a l i c h o s e m a W a i s l a m u n i k u w a haiwezekani wamchambue Mtume kwenye mhadhara wao pekee.

Kama ni kumzungumzia Mtume, basi wawaite na wahadhiri wa Kiislamu uwe mdahalo kama wa awali.

Ndio katika kuepusha shari, barua ilipelekwa polisi na ilitaarifiwa kuwa kama polisi hawatazuia mada hiyo kutajwa, basi Waislamu

watazuia na yatakayotokea basi wasilaumiwe.

Baada ya kuona kuwa Polisi hawakujali, Jumapili ya tarehe 9/9/2012 Waislamu wali tangaziana waende kwenye mhadhara huo

uliofanyika katika viwanja vya wazi nyuma ya Maktaba ya Mkoa na Ofisi ya OTTU, lengo likiwa moja tu: ikitokea matusi yameanza, bas i watafute namna nzuri ya kushughulika nao.

Hata hivyo, baada ya wahadhiri kuona kundi la Waislamu l imeuzingira mkutano, hawakuthubutu kugusa mada ya Mtume, wakaongea mambo mengine mwanzo hadi mwisho.

W a k a t i h u o h u o , wale Waislamu watano waliokamatwa katika kijiji cha Muze –Rukwa kwa kugomea sensa , wamehukumiwa kifungo cha miezi 6 au kulipa faini ya Shilingi 50,000 kila mmoja.

Waislamu kwa umoja wao wamechanga fedha hivyo na kulipa faini na kuwafanya ndugu zao Waislamu kuwa huru.

JESHI la polisi jijini Arusha wakiwa katika nyumba ya Bi Khadija wakimlazimisha kuandikisha Sensa.

Page 11: ANNUUR 1036

11 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 28 - OKTOBA 4, 2012Tangazo

Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za kidato cha Kwanza kwa shule zifuatazo:• Mkuzo Islamic High School - (Songea) - BWENI TU.• Kirinjiko Islamic Sec. School – (Same) - BWENI TU• Nyasaka Islamic Sec.School – (Mwanza) - BWENI TU.• Ubungo Islamic High School –(Dar es Salaam) - KUTWA NA BWENI

1. Shule hizi ni za Kiislamu, zenye lengo la kuwapa watoto elimu bora na kuwalea kwa malezi ya Kiislamu.2. Masomo yanayofundishwa ni haya yafuatayo: Elimu ya Dini ya Kiislamu, Usomaji Qur’an na mafunzo yake, Lugha ya Kiarabu, Kiswahili, English, Basic Mathematics, Physics,

Chemistry, Biology, Geography, History, Civics, Book – keeping na Commerce.3. Patakuwa na mtihani tarehe 01/12/2012 saa 2:00 asubuhi katika vituo vilivyoorodheshwa kwenye fomu ya maombi. Muombaji anaweza kufanyia mtihani katika kituo chochote.4. Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 30/11 /20125. Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini.6. Pia, fomu zinapatikana kwenye Tovuti: www.ipctz.org. Ikumbukwe kuwa atakayepata fomu kupitia tovuti (download) atatakiwa kulipia wakati wa kurejesha siku ya mtihani.

• Arusha - Ofisi ya Islamic Education Panel Jambo Plastic Ghorofa ya 2 mkabala na msikiti Mkuu Bondeni -0763 282 371/ 0784 406 610• Kilimanjaro - Moshi: Msikiti wa Riadha – 0654 723 418 - Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0655 697 075• Tanga - Uongofu Bookshop: - 0784 982525/ - Mandia Shop - Lushoto: 0782257533• Mwanza - Nyasaka Islamic Secondary School 0717 417685/0786 417685 - Ofisi ya Islamic Education Panel - Mwanza -Mtaa wa Rufiji mkabala na Msikiti Al-Amin – 0785 086 770• Musoma - Duka la Kansolele -Stendi ya zamani sokoni-0714587193• Kagera - Bukoba: Alhuda Café Kwa mzee Kinobe karibu na ofisi za TRA.-0688 479 667

• Shinyanga - Msiikiti wa Majengo-0718866869 - Kahama ofisi ya AN –NUUR Karibu na msikiti wa Ibadhi: 0753 993930 • Dar es Salaam - Ubungo Islamic High School 0754 260 241/0712033556 - Ofisi ya Islamic Ed.Panel –Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin-0655144474• Morogoro - Wasiliana na Ramadhani Chale :0715704380• Dodoma - Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0712 325086• Singida - Ofisis ya Islamic Ed. Panel –karibu Nuru snack Hotel-0714285465• Manyara - Babati: Shule ya Msingi Hangoni: 0784 667575• Kigoma - Msikiti wa mwanga Kigoma: 0753 355224 - Kibondo – Islamic Nursery School: 0784 442860 - Kasulu: Murubona Isl.ss 0714710802• Lindi - Wapemba Store: 0784 974041/0786 959663• Mtwara - Amana Islamic S.S 0786 729 973• Songea - Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU—0715 68 1 701/0716791113 - Mkuzo Islamic High School. 0716 791113• Mbeya - Duka la vifaa vya Kiislamu nje ya Msikiti wa Uyole-0713 200209 - Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209

• Rukwa - Sumbawanga: Masjid TAQWA 0717082 073

• Tabora - Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566

• Iringa - Madrastun – Najah: 0714 522 122

• Pemba - Wete: Wete Islamic Education Center: 0777 432331

• Unguja - Madrasatul –Fallah: 0777125074- • Mafia - Ofisi ya ust.Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu – 0653705627

USIKOSE NAFASI HII ADHIMU – WAHI KUCHUKUA FOMU SASA!

MKURUGENZI

WABILLAH TAWFIIQ

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

NAFASI ZA KIDATO CHA KWANZA – 2013

Page 12: ANNUUR 1036

12 AN-NUURBarua/Shairi Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 28 - OKTOBA 4, 2012

Je! Una maoni, barua au Mashairi? Tuandikie:Mhariri AN-NUUR,

S.L.P. 55105, Dar es Salaam au tutumie kwa Barua pepe

E-mail: [email protected]

Kwa mahitaji ya viroba bora vipya kabisa kwa matumizi mbalimbali sasa unaweza kupata kwa bei ya jumla na rejareja kwa saizi zote kwa bei nafuu zaidi, kwa BANDO.

Tupo mtaa wa Likoma na Pemba Kariakoo, Dar es Salaam (nyuma ya Msikiti wa Idrisa).

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana kwa simu: 0657 800999/0683 800999.

VIROBA MURUA

Na Wanachuoni: Imaam Ibn Baaz (Rahimuhu A l l a a h ) ´ A l l a a m a h Swaalih bin Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

S w a l i : B a a d h i y a Waislamu wanasherehekea sikukuu ya kuzaliwa Yesu - yaani Christmas kama wanavyoiita, tunaomba nasaha?

I m a a m I b n B a a z : Haijuzu kwa Muislamu mwanamme na mwanamke kushirikiana na Manaswara au Mayahudi au makundi mengine katika sikukuu zao. Ni wajibu kuacha hilo kwa kuwa [Mtume yu wasema]:

“Mwenye kujifananisha na watu, basi yeye ni miongoni mwao.”

Na Mtume (Swal la Allaahu ́ alayhi wa sallam) katukataza kushirikiana nao , kuchukua t ab ia zao. Ni juu ya muumini mwanamme na mwanamke kujiepusha na hilo wala was ihudhu r i e ka t i ka sikukuu zao kwa chochote. Kwa kuwa sikukuu zao zinakhalifu Shari´ah ya Allaah isitoshe ni maadui wa Allaah. Kwa hiyo haijuzu kushiriki humo wala kusaidizana nao wala kuwasaidia kwa lolote; si kwa [kunywa] hata chai, kahawa nakadhalika. P i a Anasema Al l aah (Subhaanahu wa Ta´ala):

“Na saidianeni katika wema na ucha Mungu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui.” (05:02)

Kushirikiana na makafiri kunako sikukuu zao ni aina ya kusaidiana katika dhambi na uadui. Ni wajibu kwa Waislamu wote wanaume na wanawake kuacha hilo. Wala mtu asidanganyike na wayafanyayo watu; bali ni wajibu aangalie alifanyalo - Uislamu na yale iliyokuja nayo na atekeleza amri za Allaah na Mtume Wake wala asidanganyike na mambo ya watu. Hakika watu wengi hawajali na Shari´ah ya Allaah, kama alivyosema Allaah (´Azza wa Jall) katika kitabu Chake kitukufu:

“Na ukiwatii wengi katika hawa waliomo duniani watakupoteza na Njia ya Allaah.” (06:116)

“Na wengi wa watu si wenye kuamini hata

Kusherehekea Kirisimasiukijitahidi vipi.” (12:103)

Ni wajibu kutekeleza S h a r i ´ a h , h a i j u z u k u i c h u k u l i a s a h a l i . Muislamu hufanya vitendo na kauli zake na za watu kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ikiwa yataafikiana nayo (Qur-aan na Sunnah), b a s i y a t a k u b a l i w a hata watu wakiyaacha. N a w a k i y a k h a l i f u a u w a k a y a c h u k i a w a t u , y a t a r u d i s h w a (hayatokubaliwa) hata watu wakiyafanya.

Swali: Ipi hukumu ya kuwapa pongezi (hongera) makafiri kwa sikukuu zao na kushiriki katika sikukuu zao?

´Allaamah al-Fawzaan:

Ha i juzu kush i r ik i na manaswara katika sikukuu zao wala kuwapa pongezi wala kuhudhuria.

(Allaah Anasema): “Na wale wambao hawatoi ushahidi wa uongo.” (25:72)

Na uongo ni sikukuu za mashirikina, kushudia na kuhudhuria. Hakuna kuhudhuria, kuwasaidia na wala kuwapa pongezi. Haijuzu kwa mtu kushiriki wala kuhudhuria wala kuwapa pongezi wala kuwasaidia wala asile katika chakula ambacho wametayarisha khaswa kwa ajili ya hizo sherehe.

( C h a n z o : h t t p : / /w w w. y o u t u b e . c o m /watch?v=O7jikWCbou0)

Ndugu mhariri,Semantiki ni fani inayohusika na maneno na matumizi Msamiati nyumba Kisementiki ni tatanishi ( AMBIQOUS WORLD) hivyo una sifa ya kumiliki maana zaidi ya moja kimatumizi.

Mwanamke wa Kiswahili anapotakiwa na mumewe nyumba hufahamu kilichokusudiwa aidha kungwi anapomfunda bi. Harusi ajenge tabia ya kusafisha nyumba, kauli hiyo humfunda mengi saana.

Nyumba linaponyambuliwa kuwa UNYUMBA huficha faragha ya siri ya mwanamke. UNYUMBA ni UKE au UTUPU wa mwanamke. Mwanamke pekee ndie aliyepambwa kumiliki UNYUMBA mwilini mwake.

Mwanaume na matao na maguvu yake hakuruzukiwa ubavu wa kumiliki Unyumba mwilini mwake.

Wataalamu wetu wa katiba nadhani walipitikiwa namna walivyoutumia msamiati Unyumba katika katiba yetu tukufu.

Kifungu cha 16- ( 1) kimeandikwa.“Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa

nafasi yake, binafsi na familia yake naUNYUMBA wake………………………………Kama kweli hilo limetumika kimakosa nashauri

marekebisho wakati wa katiba yetu mpya aidha wataalamu wetu wa Kiswahili wa BAKIZA na BAKITA washirikishwe kikamilifu katika uandikaji wa katiba mpya. Mbona kwa hapa kwetu Zanzibar tunao wataalamu wengi ambao kisima cha taaluma waliyonayo bado haijachotwa? Kwa nini hatujawatumia kikamilifu?

Lengo letu liwe ni kuwa na katiba yenye ufasaha wa ladha ya lugha tamu isiyokwisha hamu. Kiswahili lugha ya taifa letu, KUINANGA (kuiharibu) huvukuta jamani!!!

Hitimisho: Sote tuwe mabalozi wa kuilinda lugha yetu hii adhimu, iliyo sharifu na nadhifu.

Tuelekeze na tufahamishane na tuelimishane ili tukilinde Kiswahili chetu. Nyonyo ya mama nitamu haikwishi hamu!!!.

Mzee Hassan Mkwende Hassan.Zanzibar.

Tulia nikuarifu

So kwamba nafurahika,moyoni ninamajonziHaya sio ya kucheka,ni ya kutoa machoziMlojipa madaraka,mwogopeni AZYZIWatendaji wa BAKWATA,hebu someni nyakati

Umsemapo mwenzako,hebu nawe jitazameUkilitoa tamko,kaa chini uchutameUsitoke utokako,ukatusi WANAUMEWatendaji wa BAKWATA,hebu someni nyakati

Hayo mnayoyasema,mwatafuta masilahiMwalinda yenu nidhama,kwa kuacha ya ILAHIMwokopeni KARIMA,mtaja juta Wallahi !Watendaji wa BAKWATA,hebu someni nyakati

Tarekhe yatuonesha,chombo hicho ni cha naniNi nani alotonesha,donda hilo kuwa ndaniNyerere kaianzisha,BAKWATA iwe nchiniWatendaji wa BAKWATA,hebu someni nyakati

Malengo yake hakika,si kujenga wauminiNi kujenga vibaraka,kudhofisha yao diniNi kweli haya hakika,BAKWATA mu hatianiWatendaji wa BAKWATA,hebu someni nyakati

Kwa nini mwawa wabishi,kuleta mabadiliko?Panakuwa hapatoshi,mwaleta misukosukoMwazijenga kashikashi,ili kupata ujikoWatendaji wa BAKWATA,hebu someni nyakati

Lipi mmepigania,kwa kutukanwa RASULI?Sensa mlipigania,leo mwafunga kauliZawasisia Media,zile zilo wakubaliWatendaji wa BAKWATA,hebu someni nyakati

Wamefika waumini,pale kidongo chekunduIkawavuka Imani,mkaanzisha majunguBAKWATA ikumbukeni,siku ya kwenda kwa

MUNGUWatendaji wa BAKWATA,hebu someni nyakati

Ninyi kinachowasibu,masilahi ya duniaSerikali mwaiihibbu,dini mwaitupiliaTayarisheni majibu,kwenda mjibu JALIAWatendaji wa BAKWATA,hebu someni nyakati

Hautoshi ukurasa,wengine wauhitajiVisa vyenu na mikasa,mwisho wenu ni khurujiKama mtajitakasa,haitakuja kharajiHEKIMA ya kufikiri,BUSARA ya maamuzi

Mwl.Mohammed MakimuUITC-Dar es SalaamP.O.BOX [email protected]

BAKWATA SOMENI NYAKATI

Page 13: ANNUUR 1036

13 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 28 - OKTOBA 4, 2012Makala

M A K A L A i n a y o f u a t a iliandikwa kwa ajili ya Jarida la tafiti kuhusu 9/11 kwa kumbukumbu ya 11 ya matukio ya Septemba 11 2001, s iku ambayo ilifikisha mwisho wa serikali inayowajibika na uhuru wa raia wa Marekani.

Ili kuelewa ukinzani wa maelezo ya serikali kuhusu 9/11, haihitaji kujua chochote kuhusu nguvu gani ilitumika au zilitumika katika kuangusha majengo matatu ya Kituo cha Biashara cha Kimataifa, nini kiliipiga Pentagon au k u s a b a b i s h a m l i p u k o , uwezo wa kurusha ndege au vinginevyo wa waliosemekana walizikamata, kama ndege iliyoanguka Pennsylvania ilipigwa risasi au hapana, kama simu za mikononi zilizopigwa urefu ule kutoka chini zingeweza kupokelewa, au eneo lolote lingine la tukio hilo linalobishaniwa.

I n a b i d i t u u f a h a m u vitu viwili: Moja ni kuwa kulingana na maelezo rasmi, kundi dogo la Waarabu, hasa Wasaudi, wakifanya shughuli hiyo nje ya mtandao wowote wa kigaidi wa kiserikali au mwingine wenye ufanisi, watu wasio na James Bond na V (cheo cha kijeshi) cha uwezo wa vendetta – ulipaji kisasi – waliigaragaza siyo tu Shirika la Ujasusi la CIA na Shirika la Upelelezi la FBI, na Mamlaka ya Usalama wa Taifa, ila mashirika yote 16 ya ujasusi, pamoja na mashirika ya ujasusi ya washirika wa Marekani katika NATO na Mossad ya Israel. Siyo tu kwamba mashirika yote ya ujasusi nchi za Magharibi yalishindwa, lakini asubuhi hiyo ya mashambulio mfumo mzima wa usalama wa taifa ulishindwa kwa pamoja. Waongoza ndege walishindwa. Jeshi la Anga la Marekani l i l i s h i n d w a . B a r a z a l a Usalama la Taifa lilishindwa. Makamu wa Rais Dick Cheney alishindwa. Hakuna hata kitu kilichoweza kufanya kazi siku hiyo. Taifa lenye nguvu kuliko yote duniani, tena kwa mbali, likawa halina jinsi mbele ya fadhaa iliyoletwa na Waarabu wachache wasiojulikana.

N i v i g u m u k u f i k i r i a riwaya isiyo na mashiko zaidi ya hiyo – ila kuna kitu kingine inabidi ukifahamu: Kushindwa na kudhalilishwa kwa Usalama wa Taifa wa Marekani hakufikia uhitaji wa lazima kutoka kwa Rais wa Marekani, Bunge, wakuu wa majeshi, na vyombo vya habari kufanya uchunguzi wa jinsi kushindwa kabisa huko kwa ajabu kungeweza kutokea. Hakuna aliyewajibishwa kuhusiana na kushindwa kwa usalama wa taifa kusiko na mfano wake katika historia ya dunia. Badala yake, Ikulu ya Marekani ikajibaraguza kwa mwaka mmoja kukataa uchunguzi wowote hadi madai ya waathirika wa 9/11 kutaka uwajibikaji yalimlazimisha

Kuteketeza dunia katika vitaMadhimisho ya 11 ya 9/11

Na Paul Craig Roberts

BARACK Obama, Rais wa Marekani

Rais George W. Bush kuunda tume ya kisiasa, isiyo na wataalamu wowote, kujifanya inafanya uchunguzi.

Siku ya 9/11 shaka ilizuka ghafla

Hapo Septemba 11, 2001 jirani alipiga simu na kusema, “fungua TV yako.” Nikadhani kuwa kuna kimbunga, labda kibaya sana kutokana na sauti ya jirani yangu, kinachoelekea kwetu, na kufungua TV kuona kama tulikuwa tunahitaji k u f u n g a m a d i r i s h a n a kuondoka.

Nilichokiona ni moshi mweusi ukitokea ghorofa za juu za moja ya majengo ya Kituo cha Biashara cha Kimataifa. Haikuonekana kwangu kama ni moto mkubwa” na ripoti zilikuwa zinasema kuwa moto ulikuwa umedhibitiwa. Wakati nikijaribu kufikiria kwanini kila kituo cha televisheni kinaonyesha habari hizo za kuzuka kwa moto katika ofisi, kamera za televisheni zikaonyesha ndege ikipiga mnara ule mwingine. Ndipo nikatambua kuwa minara yote miwili imegongwa na ndege.

Kamera zilionyesha watu wakiwa katika shimo kwa ndani ya mnara wakiangalia nje. Hii haikunishangaza. Ndege hiyo ilikuwa ndogo sana ukilinganisha na ukubwa wa jengo. Lakini nini kilikuwa kinaendelea? Ni ajali mbili, moja juu ya nyingine?

Minara hiyo – robo tatu au asilimia 80 ya majengo chini ya ndege zilipogonga – yalikuwa yames imama, inae lekea yakiwa hayajahar ib iwa. Hapakuwa na dalili ya moto isipokuwa maeneo karibu na ndege zilipogonga. Kufumba na kufumbua, mnara mmoja ukalipuka, ukasambaratika, na kupotea katika vumbi laini. Kabla mtu hajaweza kuelewa nini kimetokea, jambo hilo likatokea kwa mnara wa pili, nao pia unapotea katika vumbi laini.

Watangazaji wa televisheni walilinganisha kusambaratika kwa minara na kuvunjwa kimpangilio kwa majumba. Kulikuwa na taarifa nyingi za milipuko kote katika minara hiyo kutoka za chini ya usawa wa kuingilia jengo, hadi ghorofa za juu kabisa. (Mara serikali ilipotoa habari ya shambulizi za kigaidi, uainishaji wa kuvunjwa kimpangilio na milipuko iliondoka katika magazeti na televisheni). Hii ilikidhi mantiki. Kuna mtu ameyabomoa majengo hayo. Ilikuwa wazi kabisa k u w a m a j e n g o h a y o hayakuanguka kutokana na kuharibika kimfumo. Yalikuwa yamelipuka.

P i cha za ndege h i zo zikigonga minara na minara ikilipuka zilirudiwa tena na tena. Ndege ziligonga sehemu za juu za minara, na si muda mrefu baadaye minara ikalipuka. Nilifunga

televisheni nikiwa nashangaa ni vipi kamera zilikuwa ziko tayari kudaka tukio hilo lisilo la kawaida kama ndege kuingia katika jengo refu.

Sikumbuki muda wenyewe, lakini haikuwa ki tambo kabla habari haijatua kuwa Osama bin Laden na genge lake la Al Qaeda walikuwa wameishambulia Marekani. Hat i ya usaf i r i i l ikuwa imekutwa katika mabaki ya minara. Ndege nyingine ilikuwa imeruka hadi Pentagon, na ndege ya nne ilianguka au ilipigwa ikaanguka. Ndege nne zilikuwa zimetekwa, ikimaanisha kuwa usalama katika viwanja vya ndege ulishindwa mara nne asubuhi hiyo. Magaidi walikuwa wameipiga Marekani bila kipingamizi.

Niliposikia taarifa hizi, nilijiuliza (juu ya usanii huu). Ni vipi ki-hati kidogo cha kusafiria kinaweza kugunduliwa katika mabaki ya majengo mawili yaliyokuwa na zaidi ya ghorofa 100 kila moja, wakati miili, fenicha za ofisi na kompyuta hazikuweza kuonekana? Inawezekanaje kuwa usalama wa v iwan j a vya ndege ushindwe kikamilifu kiasi hicho na ndege nne zitekwe ndani ya saa moja? Ingekuwaje watawala kufahamu kwa haraka na papo hapo majina ya wahusika ambao walifanikisha shambulio hilo kubwa dhidi ya nchi yenye nguvu kuliko zote duniani, wakati watawala hao hawakuwa na ufahamu wowote kuwa shambulio kama hilo lilikuwa limepangwa au hata kuwa linawezekana?

Haya maswali yalinisumbua, kwa sababu kama msaidizi wa zamani wa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na mteuliwa wa Rais kwa ofisi za juu, nilikuwa na uthibitishaji wa kina wa usalama. Pamoja na kazi yangu kama Naibu Waziri wa Fedha, nilikuwa na majukumu ya ziada ya jopo la usimamizi ikiwa nchi itashambuliwa kwa nuklia. Kulikuwa na maficho ya mlimani ambako nilitegemewa kufika ikiwa kuna shambulio la nuklia na ambako nilitakiwa kushika hatamu za serikali ya Marekani kama hapakuwa na ofisa wa ngazi ya juu zaidi aliyepona shambulio hilo.

J i n s i h a b a r i z a 9 / 11 zi l ivyokuwa zikiendelea kuwekwa katika vyombo vya habari, ndivyo zilivyozidi kuwa za ajabu. Haiwezekani kuwa siyo tu CIA na FBI walishindwa kugundua mpango huo, lakini mashirika yote 16 ya ujasusi ya serikali, ikiwa ni pamoja na Mamlaka ya Usalama wa Taifa, ambayo inamchunguza kila mtu katika sayari, na Mamlaka ya Ujasusi ya Jeshi, Mossad ya Israel na mashirika ya kijasusi ya washirika wa Marekani katika NATO. Kimsingi ni kuwa wako walinzi wengi mno na kuingiliwa kwingi sana miongoni mwa makundi ya

kijasusi kufanikisha shambulio lenye ugumu kama hi lo litayarishwe na kutekelezwa bila kizuizi.

Maelezo ya Washington kuhusu shambulio yaliainisha kushindwa kwa usalama kwa kiwango kikubwa mno i s i v y o w e z a k u a m i n i k a . Mporomoko huo wa usalama wa taifa unamaanisha kuwa Marekani na Ulaya Magharibi hawakuwa sa l ama ha t a sekunde moja wakati wa Vita Baridi, kuwa Urusi ingeweza kuteketeza Magharibi yote katika pigo moja kubwa lisilokuwa na tahadhari.

K a m a m t u a m b a y e w a s h i r i k a w a k e k a t i k a Taasisi ya Mifumo ya Ulinzi na Usalama ya Kimataifa jijini Washington walikuwa ni Mawaziri wa Mambo ya Nje waliopita, Washauri wa Zamani wa Usalama wa Taifa, Wakurugenzi wa Zamani wa CIA, Wenyeviti wa Zamani wa Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi, nilipata taabu kuamini riwaya kuwa kundi dogo la watu wasiokuwa na mtandao wa kijasusi kuwawezesha walikuwa wameleta tukio la 9/11.

K a m a m t u m w e n y e uzoefu wa juu wa utumishi serikalini, nilifahamu fika kuwa operesheni iliyofaulu kama 9/11 ingeleta madai ya haraka kutoka Ikulu, Bunge, na vyombo vya habari kuwajibika wanaohusika. Kungekuwa na uchunguzi kuhusu kila eneo la usalama wa taifa Marekani lingeweza kushindwa kabisa kwa pamoja asubuhi hiyo moja. Mkasa huo wa kuaibisha wa kushindwa kwa taasisi za usalama wa nchi kusingeachwa bila kuchunguzwa.

NORAD ilishindwa. Jeshi la Anga la Marekani halikuweza kupeleka ndege za kivita hewani. Wasimamizi njia za ndege viwanjani walipoteza dira ya ndege zilizotekwa. Hata hivyo, badala ya kuanza uchunguzi, Ikulu ilizuia kwa mwaka mmoja madai ya familia za waathirika wa 9/11 ya kufanyika uchunguzi. Si wananchi, vyombo vya habari au Bunge waliodhani kuwa uchunguzi ulikuwa lazima. Mwelekeo ulikuwa katika kulipa kisasi, ambako utawala hafidhina wa Bush ulisema ina maana kuvamia Afghanistan ambayo ilituhumiwa kumficha mtekelezaji wa mpango huo, Osama bin Laden.

Kwa kawaida, magaidi wanajivunia ushindi wao na kutangaza kuhusika. Ni njia ya kujenga harakati. Mara kadhaa vikundi tofauti vya magaidi vitashindana kutambuliwa ndiyo walifanikiwa operesheni fulani. Lakini Osama bin Laden katika video ya mwisho ambayo imehakikishwa na wataalamu huru alisema alikuwa hana mamlaka yoyote kuhusu 9/11, kuwa hakuwa na lolote dhidi ya wananchi wa Marekani, kuwa upinzani wake ni kuhusu sera za kikoloni za serikali ya Marekani na kuzibana serikali za Kiislamu, basi.

Inaendelea Uk. 14

Page 14: ANNUUR 1036

14 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 28 - OKTOBA 4, 2012Makala

W A A T H I R I K A w a matukio ya September 11 2011 hawaonekani tu New York. Waathirika wa 9/11 walikuwa wanaishi Afghanistan, Iraq, Libya na leo, Syria, kampeni ambazo zilianzishwa na vita kupigwa nyuma ya tukio la kustusha zaidi la kutumia woga katika historia ya binadamu. 9/11 ilikuwa ni tusi kwa kumbukumbu za waliokufa, na dhihaka kwa familia zao.

Yas ioe leweka ka t ika m a s h a m b u l i o y a 9 / 11 yameanikwa kwa undani na watafiti katika miaka 11 iliyopita, tangu ndege zile mbili kujibamiza katika Minara Miwili kabla kidogo haijavunjiliwa mbali katika mlipuko maalum wa ndani, wakati ndege moja iliigeuza Pentagon kuwa Quadragon, licha ya kuacha nguzo za taa za barabarani ambako ilibidi ipitie zimesimama, na kabla ndege nyingine haijasemekana kuwa imepotea… tani 200 zote, pamoja na injini.

(Hebu fikiria kiroja na usanii huu kwamba) Kama mabaki ya Air France 747 y a l i p a t i k a n a b a h a r i n i , basi haiwezekani kabisa kuwa ndege ya aina hiyo inayoanguka ardhini ipotee hivi hivi tu. (Usaniu huu) Kuwa mbili na mbili haziwi nne katika mashambulio ya 9/11 hakupunguzi mateso waliyopata wale waliopoteza waume zao, wake, wana, familia, wapendwa wao na marafiki, waliochukuliwa katika nukta moja, kufanya kuwapoteza kuwe kwa mshtuko mkubwa zaidi na mgumu kustahimili.

Hapo ndipo fikra zetu zinatakiwa kuwa leo, miaka 11 baada ya Marekani na washirika wake kupewa ‘cheki nyeupe’ kuparamia kote duniani nyumba ya wimbi la mapinduzi ya kihisia, kuhalalisha uvamizi, kuhalalisha mauaji ya watu wengi, kuhalalisha uhalifu usiopimika dhidi ya haki za binadamu na sheria ya k imata i fa . Hayo ndiyo matokeo ya 9/11.

Matokeo ya 9/11 ni kuundwa kwa zimwi la mahusiano ya kimataifa, kwa vile FUKUS (Ufaransa, Uingereza na Marekani) walipata nafasi murua ya kutumia sarakasi hiyo kuhalalisha vita vyao wakitimiza matakwa ya makundi ya washikadau,

9/11: Zimwi la mahusiano ya kimataifaSeptember 11, 2012 “Jukwaa la Kupashana Habari”Na Timothy Bancroft-

Hincheyyanayomzunguka rais yeyote wa Marekani, na kuwaondoa wachache ambao wanakataa kukubali wanayotaka.

Kwa mgongo wa 9/11 i l i k u j a A f g h a n i s t a n , upotezaji muda na fedha usio na manufaa na muhimu zaidi , maisha ya watu, mustakabali unaoendelea hadi leo, mustakabali ambao umeendelea kuvuruga nchi ambayo zamani ilikuwa tulivu na endelevu kwa kutumia Mujahiddin, waliopelekwa huko na Shirika la Ujasusi l a Marekan i , CIA, na waendesha Madrassah wa Pakistan dhidi ya serikali halali. Taliban ni mkakati wa CIA uliowaharibikia. 9/11 ilikuwa ndiyo salamu yao ya ‘asante.’

Kwa mgongo wa 9/11 ilikuja Irak, uvamizi usio halali dhidi ya taifa huru nje ya ridhaa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kuwafanya Bush na Blair wahitaji kushitakiwa kwa uhalifu wa kivita, mkakati ambao unaendelea na ambao kuna matumaini siku moja watajikuta wakitumia muda usio haba gerezani, hata hivyo bila kuwa hatarini kupata kadhia ambazo majeshi yao yaliwapa wafungwa katika kambi za mateso na vituo vya kuweka watu kizuzini, hata ingekuwa kuna raha mtu angepata kuwaingiza

kifudifudi majini.Kwa mgongo wa 9/11

ilikuja Libya, nchi ambayo mipaka yake ya Magharibi na Mashariki ilifungwa kutokana

na mapinduzi, nchi ambayo Ukanda wake wa Mashariki ulikuwa umeshasimamiwa kikamilifu mapema, nchi iliyovamiwa kinyume cha

sheria na Vikosi Maalum vya Mfungamano wa FUKUS, ambako mfungamano wa FUKUS uliosaidia kinyume cha sheria kundi mojawapo katika mgogoro wa ndani ya nchi, ambako uhalifu wa kivita ulifanyika, ambako silaha za kijeshi zilielekezwa dhidi ya raia, na ambako wajukuu wa Gaddafi waliuawa wakiwa nyumbani kwao.

Kwanini? Kwa sababu mipango ya Muammar al-Qadhafi kwa

Afrika ambayo ilikuwa t i s h i o k w a m a k u n d i yanayodhibiti mfungamano wa FUKUS. Haikuwa bila sababu kuwa kiongozi huyo wa Libya alikuwa apewe Nishani ya Umoja wa Mataifa ya Ubinadamu mwaka 2011.

Matokeo ya 9/11 hivyo ni madhara yake: utesaji, ubakaji, mauaji, kuweka watu kizuizini kinyume cha sheria, uhalifu wa kivita, mateso, ulawiti, kukojolea chakula, kuzuia usingizi, kufungulia mbwa kwa wafungwa , ugaidi, mauwaji ya kimbari, ubaguzi… orodha inaendelea na zaidi inaonekana kama orodha ya anavyoenda kununua dukani Shetani.

Na hili, mabibi na mabwana, ni tusi kwa waathirika wa 9/11 na familia zao.

(Imetafsiriwa na Anil Kija)

Kuteketeza dunia katika vitaInatoka Uk. 13

Haile t i maana yoyote kuwa “mbunifu mkuu” wa pigo la kuaibisha kuliko yote katika historia ya dunia ambalo limewahi kufanywa dhidi ya himaya yenye nguvu kuliko yote ya wakati huo asingedai kutambuliwa kwa kufaulu huko. Kwa Septemba 11, 2001,Osama bin Laden alikuwa anajua kuwa ana ugonjwa wa kufisha. Kwa mujibu wa taarifa za habari alifanyiwa upasuaji wa figo mwezi uliofuata. Taarifa za uhakika zaidi tulizo nazo ni kuwa alifariki Desemba 2001. Haingii akilini kabisa kuwa bin Laden alikataa kuhusika kwa sababu alikuwa anaiogopa Washington.

Lakini Osama bin Laden alikuwa anafaa sana kama mtu wa kutwishwa lawama, na Washington na vyombo mfumo vya habari vilimweka hai kwa muongo mwinginen hadi Obama alipoamua kumwua mfu

ili kuinua viwango vyake duni vya kuungwa mkono katika kura za maoni ili wafuasi wa chama cha Democrat wasianze kumunga mkono mshindani mwingine katika uteuzi wa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama hicho.

Video maridhawa za bin Laden, kila moja ikitangazwa kuwa feki na wataalamu, zilitolewa wakati wowote ule ambako Washington iliona zinahitajiwa. Hakuna hata mmoja katika vyombo vya habari vya Magharibi au katika Bunge la Marekani au mabunge ya Ulaya au Uingereza aliyekuwa na udadisi wa kutambua kuwa video ya bin Laden ilikuwa inatokea ghafla pale Washington inapoihitaji. “Kwanini huyu ‘mbunifu mkuu’ awe msikivu hivyo kwa Washington?” ndilo swali ambalo lilipita akilini mwangu kila mara moja ya video hizo feki ilipoonyeshwa.

‘Uchunguzi’ wa 9/11 ambao hatimaye ulifanyika ulikuwa wa

kisiasa ulioendeshwa kutoka Ikulu. Mmoja wa wajumbe wa kamati alijiuzulu, akitangaza uchunguzi huo kuwa ni feki, na wenyeviti wote wawili na mshauri wa kisheria wa Tume ya 9/11 walijitenga na ripoti yao kwa taarifa kuwa Tume ya 9/11 ‘iliundwa ishindwe,’ kuwa viwezeshaji vilizuiwa kwa tume, kuwa wawakilishi wa jeshi la Marekani walisema uwongo mbele ya tume na tume ikafikiria kupeleka suala la ushahidi wa uwongo kushitakiwa kama jinai.

U n g e t a z a m i a k u w a kufichua mambo kwa njia hii kungesababisha watu kujitafuta, lakini vyombo vya habari, Bunge, Ikulu na wananchi walikuwa kimya.

Yote haya yalinihangaisha kwa k iwango k ikubwa . Marekani ilikuwa imevamia nchi mbi l i za Ki is lamu k u t o k a n a n a m a d a i yasiyohakikishwa kuhusisha nchi hizo na 9/11, ambayo pia imebaki bila kuchunguzwa.

Wahafidhina waliojaza utawala wa George W. Bush walikuwa wanahamasisha uvamizi wa nchi nyingine za Kiislamu. Paul O’Neill, Waziri wa Fedha wa kwanza wa Rais Bush, alisema wazi kuwa utawala wa Bush ulikuwa unapanga kuivamia Irak kabla ya 9/11. O’Neill alisema kuwa hakuna mtu katika Baraza la Usalama la Taifa al iyekuwa hata akiuliza swali la ‘kwanini’ kuivamia Irak? “Ilikuwa tu ni jinsi ya kupata njia ya kufanya hivyo.”

Dokezo la s ir i kubwa lililovuja kutoka Downing Street lililoandikwa na Mkuu wa Idara ya Ujasusi ya Uingereza (MI6) linathibitisha ushuhuda wa Paul O’Neill. Dokezo hilo, linalojulikana kama ‘Dokezo la Bunduki Inayotoa Moshi,’ ambalo usahihi wake umehakikishwa, linasema kuwa “Rais George W. Bush anataka kumwondoa Saddam Hussein, kwa nguvu za kijeshi,

Inaendelea Uk. 15

GEORGE W. Bush, Rais wa zamani wa Marekani.

Page 15: ANNUUR 1036

15 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 28 - OKTOBA 4, 2012MAKALA

Kuteketeza dunia katika vitaInatoka Uk. 13ikihalalishwa na kuunganisha ugaidi na silaha za maangamizi. Lakini taarifa za kijasusi na kinachojulikana bayana vinakitishwa kuzunguka sera hiyo.” Kwa maneno mengine, uvamizi wa Marekani nchini Irak haukutokana na chochote ila uwongo wa kutungwa.

Kama mwanafunzi wa uhandisi niliwahi kuangalia usambaratishaji wa jumba kwa mpangilio. Pale mikanda ya kuanguka kwa jengo la saba la Kituo cha Biashara cha Kimataifa ilipotolewa, ilikuwa wazi kuwa jengo la saba lilikuwa limeangushwa kwa usambaratishaji wa mpangilio. Wakati mwalimu wa fizikia David Chandler alipopima kuanguka kwa jengo na kuainisha kuwa lilianguka katika kasi inayolingana na nguvu ya uvutano (bila kizuizi chochote), suala hilo lilikuwa limefungwa. Majengo hayawezi kuanguka wima bila ya uangushaji wa mpangilio kuondoa uzuiaji wote wa ghorofa zinazoanguka.

Kama ndege ziliangusha majengo hayo mawili ya ghorofa nyingi, kwanini uangushaji wa mpangilio utumike kuangusha jumba la tatu?

Nilihisi kuwa wataalamu wa mifumo ya uchoraji, wahandisi mifumo, na wanafizikia wangepiga filimbi kuhusu habari hiyo ambayo kwa wazi ni potofu. Kama nilikuwa naweza kuona kuwa kuna kitu kinakanganya, lazima watu wengi wenye elimu zaidi wangeona.

Mwanafizikia wa kwanza aliyetoa hoja yenye ncha na ushawishi alikuwa Steven Jones wa BYU. Jones alisema kuwa milipuko iliiangusha minara miwili. Alitoa mada nzuri. Kwa juhudi zake zote, alisukumwa ajiuzulu nafasi yake ambayo ilishahakikishwa ni ya maisha. Nilijiuliza kama serikali kuu ilikuwa imetishia ruzuku za utafiti za BYU au wadhamini wazalendo na waliohitimu hapo zamani walikuwa ndiyo chanzo cha kufukuzwa kwa Jones. Liwalo liwe, ila ujumbe ulikuwa umefika kwa wataalamu wengine wa vyuo vikuu: “Nyamaza au tutakupata.”

Steven Jones alidhihirika kuwa alisema ukweli pale Mkemia Niels Harrit wa Chuo Kikuu cha Copenhagen nchini Denmark aliyetoa taarifa isiyo na utata wowote kuwa timu ya kisayansi ambayo alishiriki ilikuta nano-thermite katika mabaki ya minara miwili. Ugunduzi huu haukutajwa katika magazeti na televisheni za Marekani, kwa ufahamu wangu.

Miaka kadhaa baada ya 9/11 msanifu majengo Richard Gage aliunda kundi la Wasanifu na Wahandisi wa Ukweli kuhusu 9/11, asasi ambayo imekua na kujumuisha wataalamu 1,700. Michoro ya minara imechunguzwa. I l ikuwa imara sana, Ilitengenezwa

ASKARI wa Marekani wakiendesha operesheni ya mauaji jijini Fallujah nchini Iraqkustahimili kugongwa na ndege na mioto. Hakuna maelezo yanayoingia akilini ya kushindwa kustahimili isipokuwa kuangushwa kwa makusudi.

Niliona pia karaha uharaka wa kuelewa wa wananchi, vyombo vya habari, na Bunge katika kukubali bila maswali maelezo rasmi kuhusu njama za mbeba bomu katika viatu, mbeba bomu katika mafuta ya nywele na mbeba bomu wa maji ya chupa ya plastiki, na mbeba bomu lililofichwa katika nguo za ndani kulipua ndege zikiwa zinaruka. Mipango hii ni upuuzi. Tunawezaje kuamini kuwa Al Qaeda, yenye uwezo wa kutekeleza tukio la ugaidi la kushangaza kuliko yote katika historia na lenye uwezo wa kutengeneza vifaa vya kulipua ambayo vinaua na kujeruhi askari wa Marekani na kuharibu magari ya kijeshi ya Marekani ingetegemea kitu ambacho inabidi kiwashwe kwa kiberiti? Wabeba mabomu wa kiatu na nguo ya ndani wangehitaji tu kubonyeza kitufe katika simu zao za mikono au kompyuta za mfukoni, na bomu hilo la majimaji lisingehitaji muda wa ziada katika choo kuchanganywa (yote bila matokeo).

Hakuna kinachoingia akilini katika yote hayo. Isitoshe, wataalamu walihoji mengi kati ya madai ya serikali, ambayo hayakuwahi kuthibitishwa kwa chochote ila maelezo tu ya serikali. Hakuna ushahidi huru kuwa kulihusika chochote i la baruti za kusambaza milipuko.

Suala la mbeba bomu katika nguo ya ndani hasa ni gumu kulikubali. Kwa mujibu wa mashahidi, mbeba bomu katika

nguo ya ndani hakuruhisiwa kuingia kwenye ndege, kwa sababu hakuwa na hati ya kusafiria. Hivyo anatokea ofisa ambaye anampeleka ndani ya ndege inayoelekea Detroit, siku ya Krismasi. Ni ofisa gani mwenye uwezo wa kuweka pembeni kanuni zinazofahamika, na ofisa huyo alikuwa anafikiria nini kitatokea kwa msafiri huyo alipojipeleka kwa maofisa wa Idara ya Forodha ya Marekani bila hati ya kusafiria? Ofisa yeyote mwenye mamlaka ya kuweka pembeni kanuni za kawaida za uendeshaji atakuwa anajua kuwa hapakuwa na haja ya kumpeleka msafiri katika nchi ambayo kuingia kwake kungekataliwa.

Ushahidi wa kimazingira unaonyesha kuwa haya y a l i k u w a n i m a t u k i o yaliyoandaliwa kwa lengo la kuhakikisha woga unaendelea kuwepo, kuongeza uwezo zaidi wa kuingilia kwa mamlaka mpya ya kipolisi ya kitaifa, kuwazoesha wananchi wa Marekani kufanyiwa upekuzi wakati wowote na jeshi la polisi la kufanya hivyo, na kuuza vifaa ghali vya kubaini kilicho ndani ya utupu wa mtu na vifaa vingine vya teknolojia ya juu kwa Mamlaka ya Usalama wa Usafirishaji. Inaelekea mkusanyo huo wa vifaa vya teknolojia za juu hakutoshi kutulinda na magaidi, na Agosti 2012 Idara ya Usalama wa Ndani ikaagiza rasasi milioni 750, zinazotosha kumpiga risasi kila mtu nchini Marekani mara 2.5 takriban.

R a i a w a M a r e k a n i wasiotumia akili zao wanadai kuwa kama sehemu moja ya serikali ya Marekani ingehusika na 9/11, “kuna mtu

angekwishaongea hadi sasa.” Ni wazo linalotuliza, labda, lakini siyo zaidi. Chukua, kwa mfano, kufunika kwa serikali ya Marekani kwa shambulio la Israeli mwaka 1967 dhidi ya Meli ya Kijeshi ya USS Liberty ambalo liliua au kujeruhi wanamaji wengi zaidi katika meli hiyo lakini likashindwa kuizamisha. Kama manusura walivyosema, waliamrishwa kwa njia ya vitisho kutosema kuhusu tukio hilo. Ilikuwa miaka 12 baadaye ndipo mmoja wa maofisa wa USS Libery, James Ennes, alielezea kikamilifu tukio hilo katika kitabu chake, Shambulio dhidi ya Liberty. Naendelea kujiuliza jinsi wataalamu katika Taasisi ya Taifa ya Viwango na Teknolojia wanavyojisikia kuhusu kutumiwa na serikali kuu kuchukua msimamo usio wa kisayansi kuhusu kuanguka kwa minara ya Kituo cha Kimataifa cha Biashara.

Nini kitatokea kuhusu shaka inayozunguka maelezo rasmi iliyotolewa na wataalamu? N i n a w a s i w a s i k u w a Wamarekani ni wadhaifu mno kimawazo na kihisia kuweza kukabiliana na ukweli. Wameridhika mno na habari kuwa maadui waliishambulia Marekani kwa ustadi licha ya mitandao mikubwa ya usalama wa taifa iliyopo. Raia wa Marekani wameonyesha uoga kiasi cha kukubali, bila kuguna, kutoa kafara uhuru wa kiraia na ulinzi wa kisheria vinavyohakikishwa na Katiba ili wawe ‘salama.’

Bunge la Marekani haliko t aya r i ku j iumbua kuwa limetumia trilioni za dola kwa vita visivyo na sababu vilivyotokana na ‘Pearl Harbour mpya’ ya kutengenezwa.

Wakati wahafidhina mamboleo waliposema kuwa ‘Pearl Harbour mpya’ ndiyo ilikuwa inahitajiwa kwa vita vyao kuimarisha ubabe wa Marekani na Israel, waliweka jukwaa la vita vya karne ya 21 ambavyo Washington imeanzisha. Kama Syria itaanguka, kuna Iran tu iliyobaki, na hapo Washington itakuwa inakabiliana ana kwa ana na Russia na China.

Isipokuwa kama Russia na China zinaweza kupinduliwa kwa “mapinduzi ya maua,” dola hizi mbili zenye silaha za nuklia hazielekei kukubali ubabe wa Marekani. Dunia tunavyoifahamu sasa inaweza kuwa inakaribia kumalizika.

Kama Wamarekani wa kutosha na hata watu wengine duniani wangekuwa na akili ya kutambua kuwa mifumo mizito ya chuma cha pua haivurugiki na kuwa vumbi laini kwa sababu ndege nyepesi imezigonga na mioto ya muda mfupi iendelee kwa masaa kadhaa, Washington ingejikuta na tuhuma inazostahili.

Kama 9/11 ilikuwa kweli ni kushindwa kwa mtandao wa usalama wa taifa kuzuia shambulio, kukataa kwa serikali kufanya uchunguzi halisi ni kupogoka zaidi ya hapo. Imebakia kwa watalamu wanaojali na wenye ustadi wa suala hilo kufanya uchunguzi uliotelekezwa na serikali. Mada zilizowasilishwa katika Jopo la Toronto, pamoja na maainisho ya wanajopo, sasa zinapatikana, kama ulivyo mkanda wa tukio hilo, “Ushahidi unaolipua: Wataalamu Wazungumza,” u l io to lewa na Wasanifu Majengo na Wahandisi wa Ukweli wa 9/11.

Mawakala wa serikal i na wate tez i wana ja r ibu kukwepesha mwelekeo kutoka vielelezo vinavyosumbua kwa kuchuja ushahidi halisi uliotolewa na wataalamu kuwa unatokana na ‘utamaduni wa kuamini njama.’

K a m a w a t u l i c h a y a kupakwa chokaa akili zao na kutokuwa na elimu ya kitaaluma wanaweza kupokea taarifa zilizowasilishwa kwao, labda Katiba ya Marekani na amani vinaweza vyote kurudia kawaida. Ni pale tu watu wenye ufahamu wanapoweza kuizuia Washington na kukwepa ubabe wa kiwazimu wa serikali ya Marekani kuteketeza dunia katika vita.

(Paul Craig Roberts alikuwa Naibu Waziri wa Fedha akihusika na Sera za Uchumi na Mhariri Mshiriki wa Jarida ya Wall Street. Alikuwa mwanasafu katika jarida la Business Week, asasi ya kutawanya habari ya Scripps Howard, na Creators Syndicate. Amepata kuteuliwa mara nyingi kama mhadhiri vyuo vikuu. Safu zake katika internet zimepata ufuatiliaji mkubwa kote duniani.) Makala hii imefasiriwa na Anil Kija.

Page 16: ANNUUR 1036

16 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 28 - OKTOBA 4, 2012

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

AN-NUUR16 Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 28 - OKTOBA 4, 2012

AMIR wa Baraza Kuu la Jumiya na Taasisi za Kiislamu (T), Sheikh Mussa Kundecha , amesema kuwa amani ya dunia itadumu kama kutakuwa na kuheshimiana.

Katika mtizamo huo akasema kuwa serikali mbalimbali duniani ndio z i tahar ibu amani kwa kuruhusu vi tendo vya kukashifu na kuvunjia heshma dini za watu.

Akazitaka mamlaka za Mataifa mbalimbali Duniani kudhibiti maeneo ambayo ni msingi wa amani na utulivu katika nchi zao.

A m i r K u n d e c h a , ameyasema hayo akihutubia m a e l f u y a Wa i s l a m u waliofurika katika viwanja vya Kidongochekundu, Jijini Dar es Salam, Ijumaa ya wiki iliyopita waliokutana kulaani f i lamu yenye maudhu ya kumdhalilisha Mutume Muhammad na Uislamu.

Alisema, mamlaka yoyote Duniani ni lazima itambue kwamba, chokochoko na dharau za kidini, dhidi ya dini nyingine ni mbaya lakini pia kuchezea maeneo ya dini za watu hilo ni baya zaidi.

“Tumekusanyika hapa, sasa tunapaza sauti zetu kwa kuwataka wenye mamlaka kote duniani wajitahidi kuwa makini, kisha wadhibiti maeneo ambayo ndiyo yanayo lenga kuwa msingi wa amani na utulivu wa nchi zao.” Alisema Amir Kundecha.

Akasema, mbali ya kuiambia Dunia juu ya suala hili lakini pia alisema, wanaiambia Serikali ya T a n z a n i a , k w a m b a wakimsikia mtu yoyote anamchezea ama kumkejeli Mtume Muhammad (s a w), wasisubiri Waislamu wachukue hatua.

Alisema, ili kudumisha hali ya amani na utulivu, ni vyema mamlaka husika k u w a c h u k u l i a h a t u a haraka wachokozi kabla

Tuheshimiane amani idumuAsema Sheikh KundechaNa Bakari Mwakangwale ya Waislamu hawajaamua

kuchukua hatua wenyewe, ili kuweka heshima ya dini na imani yao.

Alisema, thamani ya Waislamu ni Uislamu wao na kipimo chao ni Mtume Muhammad , na ik iwa watashindwa kumtetea maana yake ni kuwa wameshindwa kuulinda Uislamu wao.

Alisema, katika Uislamu huwezi kuwa Muislamu kamili kama hukumtaja na kumthamini Mtume Muhammad ( s a w).

Alisema, vita na chuki dhidi ya Mtume ilikuwapo tokea enzi za uhai wake, kwani Mayahudi na Manaswara, walipenda Mtume aige mila zao na kuacha mila za Allah (sw).

A m i r K u n d e c h a alisema kufatia hali hiyo, ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Mtume wake (s a w) kwamba hawawezi kuridhika naye Mayahudi na Manaswara, mpaka afuate mila zao.(Mfumo wao wa Kimaisha).

Amiri Kundecha, alisema maneno hayo yanahamia kwa Muislamu wa sasa, kwamba Mayahudi hawezi kuridhika na Waislamu kiakili, kiroho na kiuhalisi ila uwe umefuata mwenendo wao.

Alisema, analazimika kusema hayo kwani alidai kwa sasa wapo baadhi ya Wais lamu wanaodhani kwamba wanapendwa na Makafiri.

A l i s e m a , w a t u h a o w a n a p a s w a k u e l e w a k w a m b a , m a a d a m u w a m e t a m k a s h a h a d a Mayahudi , Manaswara hawezi kuridhika nawe katika mwenendo huo.

“Ukifikiria kuwafurahisha kwa maneno ndiyo sababu ya kuishi vizuri nao na kudhani kuwa watakulinda milele kwa kuwa tu unawafurahisha huku ukiwarahishia mambo yao na kuwasaliti ndugu zako Waislamu, utakuwa umekosea sana.” Alisema Amir Kundecha.

Hata hivyo, alisema, anavyo fahamu yeye kwa mujibu wa lugha ya Qur an ni kuwa kila nafsi itaonja mauti, sawa inamlinzi au

SHEIKH Ponda Issa Ponda (kushoto) akiwa katika viwanja Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam Ijumaa ya wiki iliyopita waliokutana kulaani filamu yenye maudhu ya kumdhalilisha Mutume Muhammad na Uislamu. Picha chini baadhi ya Waislamu wakiingia katika viwanja hivyo. [Picha zote na Bakar Mwakangwale]

Uandikishaji unaendelea. Gharama za Hijja ni kama Hijja iliyopita mwaka jana, USD 3850. Tarehe za safari ni 19 Oktoba, 2012 na kurudi tarehe 11 Novemba, 2012. Wahi kujiandikisha sasa. Kumhijia mtu ni $900. Semina zitaanza Oktoba 7-16, 2012Kwa mawasiliano:+255 22 2181577, +25 22 2182370, 0754 498888, 0786383820, 0754 261910E-mail: [email protected], [email protected] Website: wwwhajjtrusttz.org

Safari ya Hijja Hijiria 1433