annuur 1114

16
ISSN 0856 - 3861 Na. 1114 RABIUL THAN 1435, IJUMAA , FEBRUARI 28-MACHI 6, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz Facebook:[email protected] Acheni kuuwa Waislamu Wanajeshi nao washiriki kuuwa Mustaadhafiina wakimbilie wapi? Masheikh UAMSHO wapata dhamana Inaendelea Uk. 4 WILLIAM Boykin, Jenerali mwenye sifa, ndiye mkereketwa wa Kikristo anayejulikana zaidi katika jeshi la Marekani. Alipokuwa kamanda wa Delta Force, brigedi maalum ya kusaka walengwa maalum, alikuwa akielezea vita yake binafsi dhidi ya Uislamu. Akisema ‘Mungu wangu ni mkubwa kuliko wenu (Waislamu). Pia alisema Mungu wa Uislamu ni ‘sanamu.’ Katika mikusanyiko kadhaa ya kanisa, Boykin alikuwa akitoa picha iliyopigwa Mogadishu ambayo, alidai, ilikuwa ni pamoja na kivuli cha ajabu alichokielezea kama ‘uwepo wa jinni. Akaongeza kuwa “maadui wa kiimani watashindwa tu kama tunakuja dhidi yao kwa jina la Yesu.” Hivi sasa Boykin ni mtetezi wa sera ya ‘Kataa Misikiti Marekani’. (Soma zaidi uk. 8) ‘Bunduki za Yesu’ zitashinda-Boykin Vita ya Msalaba sasa kurejea upya Salamu za Kamanda wa Delta Force Inawatanganzia safari ya Hijja mwaka 2014 sawa 1435 kwa gharama ya USD 4,500 kwa mawasiliano piga simu 0715 746 578/ 0716 749 474 au fika katika ofisi zetu Mwenge kituo cha mabasi. Jamarati Hajj huduma zaidi kwa ibada sahihi. Jamarat Hajj and Umra Travellers KWA mara nyingine tena kesi inayomkabili Katibu Mkuu wa Jumuia na Taasisi za Kiislam nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda, imesogezwa mbele hadi Machi 3 mwaka huu, baada ya wakili wa upande wa Jamhuri kuweka pingamizi la awali dhidi ya upande wa utetezi. Kufuatia hatua hiyo Wakili wa Sheikh Ponda, Juma Nassor, naye aliiomba Mahakama Kuu kupanga tarehe nyingine ya kusikiliza shauri hilo ili kupata muda wa kupitia pingamizi hilo la upande wa Mashtaka. Jaji Augustino Mwalija alikubali maombi ya wakili wa Kesi ya Ponda Jamhuri yaweka tena pingamizi Na A. Msengakamba Inaendelea Uk. 3 MWANAJESHI akitenda unyama dhidi ya Muislamu katika vurugu zinazoendelea Afrika ya Kati. Habari kamili Uk. 3 MAHAKAMA KUU Zanzibar jana ilipunguza masharti ya dhamana kwa Masheikh wa Jumuia ya Na Shaban Rajab Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar, (JUMIKI), hali iliyowawezesha Masheikh hao kutimiza masharti ya dhamana na mahakama kuwaachia huru kutoka mahabusu. Taarifa zinaeleza kuwa Masheikh waliopewa dhamana na Mahakama Kuu Zanzibar jana ni Farid Hadi, Mselem Ali, Mussa Juma, Azan

Upload: zanzibariyetu

Post on 26-Nov-2015

611 views

Category:

Documents


19 download

TRANSCRIPT

Page 1: ANNUUR 1114

ISSN 0856 - 3861 Na. 1114 RABIUL THAN 1435, IJUMAA , FEBRUARI 28-MACHI 6, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz Facebook:[email protected]

Acheni kuuwa WaislamuWanajeshi nao washiriki kuuwaMustaadhafiina wakimbilie wapi?

Masheikh UAMSHO wapata dhamana

Inaendelea Uk. 4

WILLIAM Boykin, Jenerali mwenye sifa, ndiye mkereketwa wa Kikristo anayejulikana zaidi katika jeshi la Marekani.

Alipokuwa kamanda wa Delta Force, brigedi maalum ya kusaka walengwa maalum, alikuwa akielezea vita yake binafsi dhidi ya Uislamu.

Akisema ‘Mungu wangu ni mkubwa kuliko wenu (Waislamu).

Pia alisema Mungu wa Uislamu ni ‘sanamu.’ Katika mikusanyiko kadhaa ya kanisa, Boykin alikuwa akitoa picha iliyopigwa Mogadishu ambayo, alidai, ilikuwa ni pamoja na kivuli cha ajabu alichokielezea kama ‘uwepo wa jinni.

Akaongeza kuwa “maadui wa kiimani watashindwa tu kama tunakuja dhidi yao kwa jina la Yesu.”

Hivi sasa Boykin ni mtetezi wa sera ya ‘Kataa Misikiti Marekani’. (Soma zaidi uk. 8)

‘Bunduki za Yesu’zitashinda-Boykin

Vita ya Msalaba sasa kurejea upyaSalamu za Kamanda wa Delta Force

Inawatanganzia safari ya Hijja mwaka 2014 sawa 1435 kwa gharama ya USD 4,500 kwa mawasiliano piga simu 0715 746 578/ 0716 749 474 au fika katika ofisi zetu Mwenge kituo cha mabasi. Jamarati Hajj huduma zaidi kwa ibada sahihi.

Jamarat Hajj and Umra Travellers

KWA mara nyingine tena kesi inayomkabili Katibu Mkuu wa Jumuia na Taasisi za Kiislam nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda, imesogezwa mbele hadi Machi 3 mwaka huu, baada ya wakili wa upande wa Jamhuri kuweka pingamizi la awali dhidi ya upande wa utetezi.

Kufuatia hatua hiyo Wakili wa Sheikh Ponda, Juma Nassor, naye aliiomba Mahakama Kuu kupanga tarehe nyingine ya kusikiliza shauri hilo ili kupata muda wa kupitia pingamizi hilo la upande wa Mashtaka.

Jaji Augustino Mwalija alikubali maombi ya wakili wa

Kesi ya Ponda Jamhuri yaweka tena pingamizi

Na A. Msengakamba

Inaendelea Uk. 3

MWANAJESHI akitenda unyama dhidi ya Muislamu katika vurugu zinazoendelea Afrika ya Kati. Habari kamili Uk. 3

M A H A K A M A KUU Zanzibar jana ilipunguza masharti y a d h a m a n a k w a Masheikh wa Jumuia ya

Na Shaban Rajab Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar, ( JUMIKI), hali iliyowawezesha Masheikh hao kutimiza masharti ya dhamana na mahakama kuwaachia huru kutoka mahabusu.

Taarifa zinaeleza kuwa Masheikh waliopewa dhamana na Mahakama Kuu Zanzibar jana ni Farid Hadi, Mselem Ali, Mussa Juma, Azan

Page 2: ANNUUR 1114

2 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 28-MACHI 6, 2014

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Habari

Ushoga wa Obama wakwama UgandaKAMPALARAIS Yoweri Museveni wa Uganda ametoa kauli nzito dhidi ya Rais wa Marekani Barack O b a m a , a k i m t a k a a k o m e k u i n g i l i a masuala ya ndani ya Uganda.

Kauli hiyo kali ya Rais Museven imekuja baada ya Rais Obama kutishia kuwa uhusiano wa nchi yake na Uganda unaweza kuharibika iwapo Rais Museveni atasaini na kuufanya kuwa sheria muswada wa kupinga vitendo vichafu vya kujamiiana watu wa jinsia moja.

R a i s M u s e v e n i amesema, atashirikiana na Urusi iwapo Marekani itaendelea kuingilia masuala ya ndani ya Uganda na kuongeza kuwa Urusi imekuwa ikifanya shughuli zake barani Afrika tangu mwaka 1917, ikiwa ni zaidi ya miaka 100.

H i v y o a n a t a k a kushirikiana na Urusi k w a s a b a b u w a o hawachanganyi siasa zao na siasa za nchi nyingine.

R a i s M u s e v e n aliongeza kuwa ukiona mtu anaingia ndani ya nyumba ya mtu mwingine, basi jua kuna tatizo.

“Hapa ni nyumbani k w e t u . H u w e z i kumuona mtu mwenye upara kama mimi hivi ndani ya nyumba yake na kuanza kumpangia a f a n ye u n a v y o t a k a wewe. Rudi kwenu!" Alinukuliwa akisema Rais Museveni.

Rais Barrack Obama hivi karibuni alimwonya Rais Yoweri Musuveni, kwamba ikiwa atasaini muswada wa sheria i n a y o h a r a m i s h a mapenzi ya jinsia moja,

basi uhusiano kati ya Uganda na Marekani utatatizika.

Chini ya sheria hiyo, watu watakao patikana na hatia ya kujihusisha na vitendo vya kishoga, w a t a k a b i l i w a n a hukumu kali ikiwemo kifungo cha maisha jela.

Marekani imekuwa moja ya mataifa ya nje yanayotoa misaada zaidi Uganda.

Itakumbukwa kuwa mwaka 2011 wanajeshi kadhaa wa Marekani walitumwa kulisaidia j e s h i l a U g a n d a kupambana na kundi l a wa a s i wa Lo r ds Resistance Army (LRA).

Mbali na Uganda, Rais Obama pia alilalamika vitendo vya kupigwa marufuku vitendo vya kishoga katika mataifa ya Urusi na Nigeria.

Rais Museveni alisema anasaini mswada huo kufuatia maelezo ya kisayansi yaliyotolewa na wataalamu kwamba, ushoga s i jambo la kuzaliwa nalo.

Msimamo wa Marekani k u h u s u k u s i m a m i a haki za mashoga pia unakosolewa vikal i na baadhi ya viongozi wa dini nchini Kenya, wakidai kuwa Wakenya h a w a h i t a j i k u p a t a mafunzo kutoka jamii iliyoharibikiwa.

A l i p o z u r u n c h i n i Senegal mwaka jana, Rais Obama al i taka mashoga wathaminiwe kama watu wengine chini ya sheria za Afrika.

“Maoni yangu ya msingi ni kwamba bila ya kujali rangi, bila kujali dini, bila kujali jinsia, bila kujali hisia za kimapenzi, linapokuja sheria, watu wanapaswa kutendewa kwa usawa,” alinukuliwa Rais Obama

alipokuwa Senegal.H a t a h i v y o R a i s

Macky Sall wa Senegal, amesema nchi yake haiko tayari kuruhusu ushoga na maingiliano ya ngono kati ya watu wenye jinsia moja.

Rais Sall alimjibu Rais Obama akisema japo Senegal imeonyesha ustahamilivu mkubwa, lak in i ha iko tayar i kuruhusu maingiliano ya ngono kati ya watu wenye jinsia moja.

Ukiacha Uganda na Nigeria, katika miaka ya hivi karibuni nchi za Burundi na Sudan Kusini, zilipitisha sheria zinazozuia maingiliano ya jinsia moja na kuyataja kuwa ni ‘ushetani’ na kosa la jinai.

Tayari Rais Yoweri K a g u t a M u s e v e n i , Jumatatu ya wiki hii, Februari 25, 2014 ametia s a i n i n a k u u f a n ya kuwa sheria muswada wa kupiga marufuku mahusiano haramu ya watu wa jinsia moja.

Serikali ya Uganda imepitisha sheria hiyo huku ikisisitiza kwamba haiyumbishwi na kelele za madola ya Magharibi ya n a y o o n g o z wa n a Marekani.

Rais Museveni wa Uganda.

Rais Museveni ambwatukia KUNA haja ya busara kutumika katika Bunge Maalum la Katiba kutenga siku ya Ijumaa, kwa ajili ya kuwapa nafasi Waislamu kwenda miskitini kutekeleza ibada muhimu ya Ijumaa.

Tunashukuru kwamba hata baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo, akiwemo Sheikh Musa Kundecha, wametambua mapema kasoro hiyo na akalishauri Bunge hilo maalum, kutenga siku hiyo, ili kuwapa nafasi wajumbe Waislamu kutekeleza ibada ya swala ya Ijumaa bila kuadhirika na vikao vinavyoendelea.

Hatuna sababu ya kuhoji kama kosa hilo lilifanyika kwa makusudi au kwa kusahau. Madhali ndio kwanza wabunge wanajadili kanuni za kuliongoza Bunge hilo maalum, bado kuna nafasi ya kufanya marekebisho na hatua zikachukuliwa na Ijumaa iakawa siku ya mapuymziko ili kutoa nafasi ya wajumbe kutekeleza ibada ya swala ya Ijumaa.

Hatudhani kama hoja hiyo itapuuzwa. itoshe tu kusema kwamba, Bunge la Katiba ni kwa maslahi ya watanzania wote. Ni Bunge lionalokusudiwa kuwa huru, la wazi na la haki kwa watanzania wote bila kufungamana na upande wowote.

Kwa msingi huo, kwa kuwa wajumbe wengi wa Bunge hilo wana imani zao, na kwa kuwa imani kuu za wajumbe walio wqengi ni Waislamu na Wakristo, basi hakuna budi maamuzi ya kistaarabu na kiadilifu kuchukua nafasi yake, kwa kuweka uwiano mzuri wa kupumzisha shughuli za Bunge hilo siku ya Ijumaa ili kuwapa wajumbe Waislamu nao kumkurubia Muumba wao.

Haitafaa kuona baadhi ya wajumbe wanapata wasaa wa kuabudu bila kuingiliwa na shughuli za Bunge, huku wengine wakilazimika kukosa mijadala ya bunge hilo maalum, ili kwenda kuswali swala ya Ijumaa.

Kwa mtizamo wetu, tunaona ni vyema Bunge likazingatia hoja za wajumbe waliotaka kutengwa siku ya Ijumaa kama ilivyo kwa Jumapili kwa Wakristo, ili kutoa nafasi kwa ajili ya wajumbe Waislamu nao kuhudhuria katika ibada muhimu ya mjumuiko. Kwa kutimizwa hili tuna imani kwamba itakuwa ni kielelezo muhimu cha kujenga hali ya umoja, kuthaminiana, kuheshimiana.

Bunge la Katiba litenge Ijumaa ya swala

Page 3: ANNUUR 1114

3 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 28-MACHI 6, 2014Habari

Acheni kuuwa WaislamuNa Mwandhishi Wetu

“STOP killing muslims in Central African Republic”. “ G e n o c i d e a g a i n s t Muslims Central Africa.” “Threa tening Musl im genocide in Central Africa.”

Baada ya vichwa hivyo vya habari, aya nyingi za kufungua habari zinasema:

“ M a s s s l a u g h t e r committed by the Christian militia against Muslims in Central Africa, st i l l continues.”

“Amnesty International on Wednesday ( 12.02.2014 ), issued a warning that there is currently a genocide against Muslims in the Central African Republic.”

Ndivyo yanavyoandika baadhi ya magazeti ya kanda ya Afrika na hata Ulaya, Asia na Marekani yakimaanisha kuwa mauwaji yanayokaribia kuwa ya hilaki yanaendelea huko Afrika ya Kati.

Wahanga wanaokabiliwa na mauwaji haya ya kimbari, ni Waislamu wakiuliwa na wanamgambo wa Kikristo.

W i t o u n a o t o l e w a kwa ser ika l i ya muda inayoongozwa na Catherine Samba-Panza, ni kuwa zichukuliwe hatua za haraka kukomesha mauwaji hayo.

Wito huo unafuatia mauaji yanayokaribia kuwa ya kimbari sasa wanayofanyiwa Waislamu chini ya serikali hiyo.

A wa l i wa l i k u wa n i magaidi wa anti-balaka, a m b a o n i wa p i g a n a j i wa Kikristo waliokuwa wakifanya mauwaji hayo, lakini sasa jeshi la serikali nalo limeungana na magaidi hao katika kampeni ya kuwaangamiza Waislamu.

“Terrorist group “Anti-Balaka” has killed hundreds of Muslims in Central Africa and ruined their homes and mosques, plus robbing all their properties.”

N d i v y o i n a v y o s e m a taarifa moja inayopatikana katika mtandao ikiandamana na picha za mauaji na uhalifu huo dhidi ya binadamu.

Hata hivyo taarifa hiyo inasema kuwa la kutisha zaidi ni kuwa mauwaji hayo sasa yanafanywa na jeshi mbele ya macho ya Rais wa muda.

K a t i k a t u k i o m o j a inasimuliwa kuwa Rais wa muda Catherine Samba-Pa n z a , a l i wa h u t u b i a w a n a j e s h i a k i s e m a

anawapongeza kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuzima machafuko na mauwaji , lakini mara tu alipomaliza na kuondoa askari hao wakamkamata mtu mmoja waliyemdhania Muslamu akiitwa Idriss, na kumuuwa kwa kumchoma visu.

“What happened next was swift and brutal. The soldiers seized the man and repeatedly stabbed him. He was dead within two minutes.”

Anasema Peter Bouckaert wa Human Rights Watch, ambaye alishuhudia mauwaji hayo.

Bouckaert anaongeza kuwa matukio ya askari kushiriki mauwaji ya Waislamu na hata kuwachoma moto, ni ya kawaida katika mji wa Bangui.

Katika tukio moja anasema al ishuhudia askar i hao wakikusanya matairi ya magari kuzunguka mwili wa Muislamu kisha wakawa wanashangilia wakitazama anavyoungua.

“The soldiers piled tires on the body and set it alight. One leg protruded awkwardly from the ashes. Soldiers celebrated as the flames rose.” Anasema.

K a m a a n a v y o r i p o t i mwandishi wa Associated Press (AP), tukio hilo la kinyama lililofanywa na askari wa jeshi la taifa, ni kielelezo cha chuki ya kidini dhidi ya Waislamu iliyojikita Afrika ya Kati na kiashiria kuwa hatma ya Waislamu katika nchi hiyo ni kiza kitupu.

“Central African Republic soldiers join chaotic violence.” Anaripoti Jerome Delay na Andrew Drake wa Associated Press, wakionyesha kuwa maadhal i wal iotara j iwa kuwa walinzi wa usalama wamejiunga katika mauwaji dhidi ya Waislamu, hakuna salama tena inayotarajiwa kama hakutachukuliwa hatua nyingine.

“Jeshi lajiunga kushiriki mauwaji ya Waislamu Afrika ya Kati”, anasema mwandishi mwingine akitahadharisha kuwa kama hakutakuwa na hatua za makusudi na za haraka zikazochukuliwa, huenda nchi hiyo ikatumbukia katika mauwaji ya kimbari mabaya zaidi kuliko yale ya Rwanda.

Ukiacha mauwaji hayo holela, makundi ya Kikristo, anti-balaka na wengine, wa m e k u wa wa k i v u n j a Misikiti, kuvamia na kupora na kuharibu makazi ya

Waislamu.Hata wale wanaodaiwa

kuwa askari wa kulinda amani, baadhi yao ama wamekuwa wakishiriki mauwaji hayo au wakibaki wakitizama anti-balaka, polisi na wanajeshi wa nchi wanapouwa Waislamu.

Pamoja na ahadi ambayo amekuwa akiikariri Rais Catherine Samba-Panza, lakini hali inazidi kuwa mbaya kwa Waislamu ambapo hata wale wanaotaka kukimbia nchi hiyo, huzuiwa na wanajeshi na kurejeshwa kukabili kifo.

A l i y e k u w a R a i s w a muda hapo awali baada ya Rais Mkristo Francois Bozize kupinduliwa, Bwana Michel Djotodia alilazimika kujiuzulu akituhumiwa kuwa alikuwa ameshindwa kuzuiya mauwaji baina ya Waislamu na Wakristo.

Hata hivyo, baada ya Michel kuondoka na sasa kushika Rais wa muda Mkristo Catherine Samba-Panza, inaonekana ndio mauwaji yamezidi ila sasa wanaouliwa zaidi ni Waislamu kwa sababu ya kuingia jeshi.

Hadi sasa inaaminika kuwa zaidi ya watu 1,000 washauliwa katika mji wa Bangui pekee toka machafuko yaliyoanzia Desemba mwaka jana katika nchi hiyo yenye idadi kubwa ya Wakristo. Waislamu wakiwa kiasi cha asilimia 15 tu.

Kinachoonekana sasa ni ulipizaji kisasi uliovuka mipaka yakiwepo madai kuwa kisasi hicho kinatokana na mauwaji yaliyofanywa na askari wa Seleka waliosaidia k u m u w e k a M u i s l a m u madarakani.

Hivi sasa kuna askari wa kulinda amani wapatao 5,000 kutoka nchi za Afrika na wengine 1,600 kutoka Ufaransa.

Hata hivyo, askari hao wanaonekana kutokuchukua hatua madhubuti kuzuiya mauwaji dhidi ya Waislamu.

Kwa upande mwingine, uk iacha hatua h iyo ya kupeleka jeshi la kulinda amani, hakuonekani juhudi zozote kuchukuliwa na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kukomesha hali hiyo.

Kinachoonekana kwa sasa ni kuwa hali hiyo imeachwa ijiendeshe yenyewe mpaka hapo anti-balaka na wauwaji w e n g i n e w a K i k r i s t o itakapokoma kiu yao ya kuuwa Waislamu.

Hai jul ikani hapo kiu hiyo itakapokatika kama

atakuwa amesalia Muislamu tena katika nchi hiyo yenye Waislamu wapatao 4,500,000 (milioni nne na laki tano tu).

Hal i inaelezwa kuwa mbaya zaidi katika miji ya Kaskazini na hasa ile yenye utajiri mkubwa wa dhahabu kama Yaloke.

Awali mji wa Yaloke, wenye utajiri mkubwa wa dhahabu ulikuwa na Waislamu 30,000 na misikiti minane (8).

H i v i s a s a wa m e b a k i Waislamu 500 tu na Msikiti mmoja baada ya mingine saba kubomolewa na anti-balaka.

Waislamu wengi katika mj i huo wameuliwa na waliobahatika wamekimbia, wakikimbilia nchi jirani za Chad na Cameroon.

Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa ya Peter Bouckaert wa Human Rights Watch.

Kesi ya Ponda Jamhuri yaweka tena pingamizi

Inatoka Uk. 1Sheikh ponda, Juma Nassor kuahirishwa kwa kesi hiyo ili kuweza kupitia sheria na vifungu mbalimbali v i n a v y o h u s i a n a n a pingamizi hilo.

Kesi hiyo ya Sheikh Ponda Issa Ponda iliendelea kusikilizwa Jumatano wiki hii katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ikitarajiwa kusikilizwa kwa kesi ya msingi ambapo awali upande wa utetezi uliomba kufanyika marejeo ya uamuzi wa makahama y a h a k i m u m k a z i Morogoro, ambako Sheikh Ponda anakabiliwa na kesi ya uchochezi na kukiuka amri ya Mahakama ya Kisutu iliyotolewa mwaka jana, ambayo ilimtaka kutumikia kifungo cha nje.

Awali Sheikh Ponda aliiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kufuta shitaka la kukaidi amri ya Mahakama ya Kisutu lakini mahakama hiyo ilimkatalia hivyo k u wa s i l i s h a m a o m b i Mahakama Kuu Dar ili kufanya marejeo ya kesi hiyo ya uamuzi huo.

Wakili Mkuu wa Serikali, Benard Kongola aliweka p i n g a m i z i l a k u t a k a kesi hiyo isihamishiwe Morogoro.

Wa k i l i w a S h e i k h Ponda a l i sema kuwa pingamizi hilo ni sehemu tu ya changamoto za kimahakama kwa kuwa upande wa Jamhuri , hautaki maombi yao ya kuhamisha kesi kutoka Morogoro yasikil izwe

katika Mahakama Kuu.Msimamo wa upande

wa Jamhuri ni kutaka kesi hiyo irudi Morogoro hadi hukumu itakapotolewa.

A k i z u n g u m z a n a mwandishi wetu mara baada ya kuahirishwa keshi hiyo, wakili wa upnde wa utetezi, Juma Nassoro, alisema kuwa walipokuja mahakamani hapo Februari 19, Jaji aliagiza upande wa Jamhuri kuambatanisha m a j i b u y a o k w e n y e maombi ya upande wa utetezi kuhusu kurejewa uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro katika Mahakama Kuu.

Alisema hadi kufika terehe 24 Februari upande wa Jamhuri ulitakiwa uwe umeshaambatanisha majibu yao.

A l i s e m a b a d a l a ya kuambatanisha majibu yao, yaliletwa majibu pamoja na pingamizi la awali.

“Siku ile ya tarehe 19 Februari tulipanga leo (26 Februari) tusikilize maombi ya msingi, yaani kesi ya msingi.

Kwasababu wameleta pingamizi la awali kisheria, inabidi kwanza lisikilizwe hilo pingamizi la awali kabla ya kwenda kwenye m a o m b i y a m s i n g i . Wameweka pingamizi l a k i s h e r i a a m b a l o halikupaswa kuletwa hapa Mahakama Kuu. Tunahitaji muda wa kupitia vifungu mbalimbali vya sheria kuhusiana na suala hili”. Alisema wakili Nassor.

Baada ya hoja za pande zote mbili kusikilizwa mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Machi 3 saa 3:00 asubuhi itakapotajwa tena.

Page 4: ANNUUR 1114

4 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 28-MACHI 6, 2014Makala

S H U K U R A N I z o t e anastahiki Mwenyezi Mungu na rehema na amani zimfikie mtume wa mwenyezi mungu n a j a m a a z a k e n a masahaba zake na wote wanaomfuata, ama baada ya utangulizi huu mfupi kwa Uislamu na kutilia mkazo juu ya udugu wao na umeamrisha kila jambo ambalo ndani yake kuna mshikamano wa kimoyo na kukataza kila sababu za uadui na bugudha na kila jambo ambalo ndani yake kuna faraka kwa jamii na kuziparaganya safu na kufanya vitendo vya kukata ukoo na kuondoa mapenzi na huruma na mshikamano wa waislamu baadhi yao na wengine au kati yao na wasio waislamu na kwa kuwa tofauti zinatokea kwa watu na kuzusha ugomvi kati ya makundi ya jamii kama vile tofauti kati ya mume na mke na kati ya rafiki na rafiki yake na kati ya jirani na jirani yake na kati ya mshirika na mshirika mwenzie na kati ya mtu na mwengine baadhi yao na baadhi na hili ni jambo la kawaida na yanaonekana hayapingiki na sababu zake ni nyingi hazidhibitiki.

N a k a w a i d a zinazopelekea tofauti h i z i z a k u p a n g u a sa fu na kuutawanya umoja na kuwagawa w a l i o k u s a n y i k a n a k u t a t u a u g o m b i n a misongamano baada ya mapenzi na maelewano na kushikamana na kuunga.

H i v y o U i s l a m u unatuamrisha kusuluhisha k a t i y a w a t u k i a s i ametuamrisha mwenyezi Mungu ni jambo la papo k w a p a p o a k a s e m a m w e n y e z i M u n g u “Wanakuuliza juu ya mali iliyotekwa yaani ngawira igawiwe vipi? Sema mali iliyotekwa ni ya mwenyezi Mungu na mtume yafuate ni watakavyokugawieni

Kupatanisha kati ya mataifa mbalimbali

Na Sheikh Ahmad Ragab Shestawi

basi muogopeni mwenyezi Mungu na suluhisheni m a m b o b a i n a y e n u na mtii ni mwenyezi Mungu na Mtume wake ikiwa nyinyi ni katika wanaoamini kweli” Surat Anfaki aya ya kwanza na akasema tena “Na ikiwa makundi mawili katika waislamu yanapigana b a s i f a n ye n i s u l u h u baina yao na likiwa moja la hayo linamdhulumu mwenziwe basi lipigeni lile linalooneka mpaka lirudie katika amri ya mwenyezi Mungu kipande cha aya ya hujurat i . Na akasema tena kwa waumini wote ni ndugu basi wasuluhishe ni kati ya udugu wao na muogopeni M w e n y e z i m u n g u hakika mtarehemewa aya ya 10. Na maneno yote anayoyaongea mtu a t a l i p wa n a h a k u n a maneno mazuri isipokuwa ya aina tatu ambayo yamekusanyika katika aya hii:-

“Hakuna kheri katika mengi wanayoshauriana kwa siri isipokuwa mahauri ya wale wanaoamrisha kutoa sadaka au kufanya mema au kupajanisha kati ya watu na atakayefanya hivi kwa kutaka radhi ya mwenyezi Mungu basi tutampa ujira mkubwa Nisai (114) na amefanya Mtume (SAW) kwenda kusuluhisha baina ya watu dara ja yake n i ya juu kuliko daraja la mfungaji na mtoaji sadaka na mswaliji. Na ameitoa imamu Abu Daydu na tirmidhi katika sunani zake kwamba mtume (SAW) “Jee ni kujulisheni lililobora kuliko mfungaji na mswaliji na mtoaji sadaka? Wakasema ndiyo:-

Akasema “kusuluhisha m i g o g o r o k w a n i kuharibika kwa mambo ndio kuhabika kwa dini na sisemi kunyoa nywele lakini ni kuharibika kwa dini” ameitoa Abuu daudi na tirmidai. Na akafanya mtume (SAW) kwenda kusuluhisha kati ya watu ni sadaka anayoitoa yeye mja mwenyewe pa le anaposhindwa kutoa pesa. Ameitoa Imamu Bukhari katika sahihi yake kwamba mtume (SAW) amesema “salam zangu kwa watu sadaka kila siku ya kutoka jua na kusuluhisha kati ya wawili ni sadaka” kusuluhisha wagomvi wawi l i kwa uadi l i fu (usawa) ameitoa Imamu Bukhari na wasuluhishaji ni watu walio katika mapenzi ya mwenyezi Mungu amesema Mtume (SAW) “Hakika Mwenyezi m u n g u a n a p e n d a unapouza unasamehe

na unapouza unasamehe n a u n a p o d a i d e n i unasamehe”

Vi jana vya su luhu na namana ya suluhu kusuluhisha kati ya mtu na mtu na kundi na kundi ameitoa Imamu Bukhari toka kwa sahli bin saidi Ra kwamba watu wa kubaa sehemu ya madini wanauana na wanagombana hadi w a n a t u p i a n a m a w e wakamwambia mtume (SAW) naye akasema “Twendeni tukasuluhishe” ameitoa Imamu Bukhari.

(5 ) Suluhu kat i ya mume na mke kama itatokea tofauti kati yao watu wa familia moja na yakatokea matatizo kati ya mume na mke kwa umuhimu wa usalama wa familia iepukane na chokochoko ya kutengana na kuwatelekeza watoto na familia ambayo ni moja ya jiwe la msingi la jamii kwa kubomoka kwake hubomoka jamii kwa hivyo kwa ajili ya umuhimu wa kuitetea familia.

Umepupia uis lamu katika kusuluhisha kati ya mume na mke na kama mkijua kuwa kuna ugomvi baina ya mke na mume basi pelekeni mwamuzi mmoja jamaa wa mwanamke na mmoja katika jamaa wa manamume kama w a k i t a k a m a p a t a n o m w e n y e z i M u n g u atawawezesha hakika mwenyezi Mungu ni mjuzi wa habari za siri na habari za dhahiri “Surat Nnisai aya ya (35) ikiwa hofu kubwa ipo upande wa mume na pakahofiwa kuzuka kwa ugumbi basi pafanywe haraka kusuluhisha kwa usalama wa fami l ia amesema mwenyezi mungu “na kama mke akiona kwa mume wake kugombana gombana na kutengana tengana basi si vibaya kwao waki tenganeza baina yao sulhu njema wakastahmiliana vivyo hivyo bila kuachana maana sulhuni kitu bora surat Nnisaai aya ya (128) na amebashiri mtume (SAW) juu ya sulhu kati ya mke na mume katika sehemu kati ya mke na mume katika sehemu nyingi tunapa dalili kama vile suhuhu ya Imam Ally Bin Abii Kama vile suluhu ya imam Ally Bin Abii twalibi na bi Fatwima Binti Thaa laba na bwana Ausi bin swamit (RS) na sehemu za mtume nyingi.

(3) S u l u h u b a i n a ya mataifa na makabila kwani kazi ya kwanza aliyoifanya Mtume (SAW) baada ya kuhamia madina

yeye nuru baada ya kujenga msikiti mtukufu alisimamia suluhu baina yamaka bila mawili ausi na khazaraji kwa kuwa walikuwa na ugomvi kati yao mkuu wa uliopelekea v i t a n a k u u w a n a akasimamia suluhu hiyo mtume (SAW) na kuondoa vyanzo vya ugomvi wao a m e s e m a m w e n y e z i mungu Mtukufu. (Na akaziunga nyoyo zao wakapendana wote hao masahaba zake hata kama ungalitoa vyote vilivyopo ardhini usingaliweza kuziunga nyonyo zao lakini mwenyezi Mungu ndiye aliyewaunganyisha

hakika yeye ni mbora na mwenye hekima” surat Anfali aya ya (63).

(4) Suluhu baina ya ugomvi wa wanasiasa w a l e w a n a o g o m b e a uongozi inapofikia hatua ya kugombana na kuuana ni wajibu wa wlainganiaji (wana daawa) na watu wema waingilie ili kufanya suluhu kati ya pande mbili ili jahazi lokoke pamoja na abiria wake kama ilivyo tokea kati ya imamu Hassan Bin Ally (RA) na bwana muawia bin Abii sufiani ilitokea tofauti kati yao kwa kugomba uongiz wakaungana waislamu wote.

Masheikh UAMSHO wapata dhamana

Inatoka Uk. 1Khalid, Seleiman Juma, Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakar Suleiman, Gharib Ahmada Juma, Abdallah Said na Salum Haji.

Hata hivyo Naibu wa Shura ya Maiman Zanzibar, Sheikh Khamis Yusuf, alisema wakati akizungumza na An-nuur majira ya saa 8:00 mchana kwamba, hadi wakati huo watuhumiwa saba walikuwa tayari wako nje kwa dhamana na kwamba, watatu walikuwakatika hatua za mwisho za kupatiwa dhama hiyo, akiwame Mzee Suleiman Haji.

Kufuatia kutolewa d h a m a n a h i y o , Sheikh Yusuf alisema kuanzia sasa zoezi la kuchangisha fedha lililokuwa likiendeshwa n a Wa i s l a m u b a r a n a v i s i w a n i s a s a linasitishwa.

A l i s e m a f e d h a zilizopatikana hadi sasa, watakaa kujadili namna na kuzitumia dhidi ya walengwa na kwamba, wa l e wa l i u o k o p wa fedha zao kwa ajili ya zoezi hilo la kusaka dhamana watarejeshewa fedha zao.

Awal i Mahakama Kuu Zanzibar iliweka m a s h a r t i m a g u m u ya kupata dhamana

kwa Masheikh hao wa UAMSHO, ha l i iliyowafanya kuendelea kubaki rumande hadi jana.

M a s h a r t i h a y o y a l i k u w a n i k i l a mtuhumiwa kuwa na mdhamana ya shilingi milioni 25, wadhamini watatu wanaofanya kazi ya kuajiriwa serikalini.

M a h a k a m a K u u Zanzibar jana ilipunguza masharti hayo ambapo k i l a m t u h u m i w a a l i tak iwa kuwa na m d h a m i n i m m o j a ambaye ni mwajiriwa serikalini badala ya watatu, dhamana ya shilingi milioni 25 kila moja kwa ahadi ya maandishi tu bila kuwa na fedha taslim, badala ya kulipa fedha taslim.

Aidha Mahakama hiyo iliona kwamba hata mtu binafsi asiye mwajiriwa serikalini, anaweza kumdhamini mtuhumiwa, ilimradi tu ana mali isiyohamishika hapo Zanzibar.

A w a l i M a s h e i k h wa JUMIKI Zanzibar waliwekwa mahabusu k a t i k a g e r e z a l a Kiinua Mguu baada y a k u k a m a t w a n a k u s h t a k i w a m a h a k a m a n i k w a makosa ya kuharibu mali, uchochezi, kushawishi na kuhamasisha fujo, na kula njama ya kutenda kosa.

Page 5: ANNUUR 1114

5 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 28-MACHI 6, 2014Habari za Kimataifa

BRUSSELSB A R A Z A l a K u p a m b a n a n a Ubaguzi ya Baraza la Ulaya imeelezea kusikitishwa kwake na mipango ya chuki na ubaguzi katika televisheni nchini Ubelgiji.

B a r a z a h i l o limesema katika ripoti yake ya tano kuwa, kumeongezeka sana kurasa za Intaneti a m b a z o z i m e j a a masuala ya kibaguzi dhidi ya Waislamu nchini ya Ubegiji.

Kufuatia kukithiri hali hiyo Tume hiyo imeitaka serikali ya Ubelg i j i , kufanya j i t i h a d a i k i wa n i pamoja na kushirikiana na nchi ny ingine katika kupambana na vitendo vya kibaguzi n a k u e n e z a h o f u na woga dhidi ya Uislamu.

K a t i k a s e h e m u nyingine ya ripoti ya k e , Tu m e h i y o ya Kupambana na Ubaguzi ya Baraza la Ulaya imeelezea wasiwasi mkubwa w a v i t e n d o v y a makundi ya kidini na kimadhehebu dhidi ya Waislamu nchini Ubelgiji.

Kamati ya Kuondoa U b a g u z i a m b a y o inafanya kazi zake c h i n i y a U m o j a wa Matai fa , nayo imeikosoa serikali ya Brussels kwa mwendo wake wa kinyonga k a t i k a k u a n z i s h a taasisi ya kitaifa ya haki za binadamu.

Pamoja na kukosoa utendaji wa kibaguzi n a w a u t u m i a j i mabavu wa polisi ya Ubelgiji, Kamati hiyo imelalamikia m a a n d a m a n o y a kibaguzi dhidi ya U i s l a m u n c h i n i Ubelgiji na uzembe katika kushughulikiwa mashtaka.

Ulaya wakosoa ubaguzi dhidi ya Waislamu Ubelgiji Ripoti ya Kamati

ya Kufuta Ubaguzi ilibainisha kwamba, wahamiaji wamekuwa wakifanyiwa vitendo vibaya na kutimuliwa nchini humo. Wimbi jipya la kueneza chuki dhidi ya Uislamu liliibuka nchini Ubelgiji baada ya kuchaguliwa Wa i s l a m u wa w i l i katika uchaguzi wa Mabaraza ya Miji mjini Brussels.

Utafiti uliofanywa kuhusiana na vitendo vya kueneza chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya, unaonesha kuongezeka vitendo hivyo hususan nchini Ubelgiji.

Taas i s i ya Haki z a B i n a d a m u y a Wa i s l a m u n c h i n i Ubelgiji hivi karibuni ilitoa ripoti ya utafiti wake kuhusiana na vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu, ambayo i n a o n e s h a k u wa , takriban Waislamu laki sita nchini Ubelgiji wa n a k a b i l i wa n a vitendo mbalimbali vya kibaguzi, hususan katika maeneo ya kazi, katika sekta ya elimu na huduma za jamii.

Ripoti pia inaonesha k w a m b a , n j a m a dhidi ya Uislamu n a W a i s l a m u zimeongezeka sana mwaka 2013. Zaidi ya mashtaka 700 ya vitendo vya kibaguzi na kueneza chuki dhidi ya Uislamu yal iwasi l ishwa na kuandikishwa katika v i t u o v ya p o l i s i , ambapo asilimia 27 kati ya vitendo hivyo vilihusiana na sekta ya elimu, asilimia 24 katika maeneo ya kazi na asilimia 15 ilihusiana na ubaguzi katika vyombo vya habari na magazeti.

Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International mara kadhaa limekosoa na

kulalamikia vitendo vya kibaguzi dhidi ya Waislamu barani Ulaya. Wachambuzi wa mambo wanaamini kwamba, l icha ya k u w e k o w i m b i kubwa la hujuma

na propaganda za vyombo vya habari vya Magharibi dhidi ya matukufu ya Kiislamu, lakini Uislamu ndio dini yenye wafuasi wengi zaidi barani U l a y a b a a d a y a

Ukristo, na idadi ya watu wanaosilimu na kuingia katika dini hii tukufu imekuwa ikiongezeka kila siku katika nchi za Ulaya na Marekani.

KAMPALANchi tatu za Jumuia ya Afrika Mashariki zimezindua Viza ya Pamoja ya Utalii kwa nchi hizo ambapo kuanzia sasa, watalii w a n a o t e m b e l e a nchi za Uganda, Kenya na Rwanda watahitaji viza moja tu badala ya viza ya kila nchi wakati wa kuzitembelea nchi hizo tatu za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Uzinduzi wa Visa ya Pamoja ya Utalii Afrika Mashariki umefanyika Alhamisi i l i y o p i t a m j i n i Kampala Uganda n a k u h u d h u r i wa na Marais Yoweri Museveni wa Uganda,

Uganda, Kenya, Rwandazazindua viza ya pamoja

Uhuru Kenyatta wa Kenya na Paul Kagame wa Rwanda.

R a i s M u s e v e n i a l i e l e z a k u w a kuanzishwa kwa visa hiyo kutaimarisha zaidi ushirikiano wa kisiasa baina ya nchi wanachama, huku Rais Kenyatta wa Kenya akisema viza hiyo ni mwanzo wa usafiri huru wa watu na bidhaa.

K w a u p a n d e wake Rais Kagame wa Rwanda alisema kuzindul iwa v iza hiyo ni ishara ya azma ya kuimarisha u s h i r i k i a n o w a Jumuiya ya Afrika Mashariki.

V i z a h i y o

inayotumika kwa siku 90, itagharimu dola za Kimarekani 100 na watalii wanaweza kuomba viza hiyo katika ofisi yoyote ya uhamiaji ya nchi hizo tatu au kwenye mtandao wa internet.

Pamoja na matamshi ya baadhi ya viongozi wa nchi zilizokubaliana kuanzisha visa hiyo kudai kwamba uamuzi w a k u a n z i s h w a visa hiyo ni ishara y a k u i m a r i s h w a Jumuia ya Afr ika Mashariki, Burundi na Tanzania zinaonekana k u t o h u s i s h wa n a m p a n g o h u o n a hai jul ikani iwapo zitaunga mkono hatua hiyo au la.

RAIS Yoweri Museven wa Uganda (kulia).

Page 6: ANNUUR 1114

6 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 28-MACHI 6, 2014Makala

Inaendelea Uk. 7

J A M H U R I y a M u u n g a n o w a zilizokuwa Jamhuri y a W a t u w a Zanzibar na Jamhuri y a T a n g a n y i k a z i l i z o u n g a n a n a k u u n d a J a m h u r i ya Muungano wa T a n g a n y i k a n a Zanzibar ; baadae k u i t w a J a m h u r i ya Muungano wa Tanzania na wengi w a n a i j u a k a m a Tanzania; imeamua kutengeneza katiba mpya.

Kwenye katiba hiyo, kuna makundi ya aina kwa aina, yanayotaka m a m b o t o f a u t i yafanyike. Maarufu kati ya makundi hayo ni yale yanayotaka mabadiliko ya muundo wa Muungano wa hizo Jamhuri zilizokuwepo kabla, ambapo Tume iliyokusanya maoni i n a s e m a z a i d i ya a s i l i m i a 6 0 k w a Z a n z i b a r n a k wa Tanganyika asilimia 61 wanataka mfumo wa Muungano uliopo ubadilike.

Lenye nguvu ni kundi la chama tawala C C M , wa n a o t a k a mfumo wa Muungano na Serikali uliopo sasa hivi ubakie. Kuna wengine wanaotaka m a b a d i l i k o y a ushiriki wa mambo ya nje kwa kila nchi. Wote wanakubaliana k w a m b a s h e r i a za nchi za kikatiba zilizokuwepo kabla

Uibuliwe mjadala wa uraiya wa nchi mbiliDiaspora ya Wazanzibari ikubaliwe Katiba Mpya.Kuwa wale wenye uraia wa Oman, Uingereza n.kNi Watan wa Zanzibar wenye uchungu na Zanzibar

Na Omar Ali.Mwenyekiti wa ZADIA.

ambazo ni muafaka na matakwa ya wananchi ziendelee kuwepo kwenye katiba mpya.

Kuna kundi kubwa la raia waliokuwa raia wa hizo nchi mbili kabla ya Muungano na baadaae kwa sababu na awamu moja au nyengine, walihamia kwenye nchi tofauti, nje ya hizo nchi mbili z a a wa l i . B a a d h i ya o wa l i l a z i m i k a kuchukua uraia wa nchi walizohamia. Kwa mujibu wa sheria ambazo zinaaminika zilihofia enzi za vita baridi. Sheria za uraia za Tanzania zinasema kwamba, mtu yeyote a k i c h u k u a u r a i a wa nchi nyengine anapoteza uraia wa Tanzania. Kundi hilo l a wa t u wa p a t a o milioni mbili, linapiga k e l e l e k u j a r i b u k u wa t a n a b a h i s h a w a h u s i k a w o t e wanaotengeza katiba m p y a k w a m b a , kwenye katiba hiyo kuwe na k i fungu rasmi kinachoeleza wazi wazi kwamba, mtu yeyote mwenye as i l i ya Tanzania ama kwa upande wa baba, au wa mama, au pande zote, basi ana haki ya kuwa raia wa Tanzania hata kama amechukuwa uraia wa nchi nyengine.

K w a m a a n a n y e n g i n e , m t u akipenda kuwa na uraia wa nchi mbili a u u r a i a p a c h a aruhusiwe. Bahati mbaya mpaka sasa haijaonekana kwamba;

sua l i h i l i ingawa l i n a w a u n g a n i s h a watu wa mirengo yote, kwenye Jamhuri zote za iliyokuwa ya Watu wa Zanzibar na Tanganyika. Watu hao wanajihisi kama kwamba hawatakiwi nchini kwao. Hapa nataka kutoa ufafanuzi wa hisia hizo kwa ufupi.

Tukiangalia hali ya wanaoishi nje ya Tanzania na kuamua kuchukua uraia wa nch i h izo u taona kwamba, walilazimika kufanya hivyo kwa lengo la kurahisisha maisha yao na ndugu z a o wa l i o wa a c h a huko nyuma. Ama w a m e c h u k u a u r a i a m p ya k wa k u t a k a k u p a t a e l i m u , m a t i b a b u ,

huduma za j ami i au kutosumbuliwa tu na sheria za nchi w a n a z o i s h i s a s a hivi. Kwa lugha ya mkato wengi husema tunatafuta maisha. Kwa vile wengi wao wamehamia kwenye nchi zilizoendelea zaidi kuliko Tanzania, watu hao wamejiendeleza kielimu na kimaisha na wakati wote huo wanagawana faida ya h a t u a z a o n a ndugu zao na Taifa wal i lo toka . Kama ambavyo Muungano u l i v y o u n d w a kurahisisha baadhi y a m a m b o k w a wananchi wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar na nchi zenyewe, ndio vivyo hivyo watu hawa walivyoamua kutafuta mazingira bora ya maisha ili kurahisisha mambo kwa watu wao.

M u u n g a n o uliopo umewafanya

Wazanzibari kuwa w a t u w a n c h i mbili , Tanganyika n a Z a n z i b a r n a Watanganyika kuwa watu wa nchi mbili, yaani Zanzibar na Tanganyika. Jambo hili liliwezekana kwa makubaliano tu ya aliyekuwa Raisi wa Jamhuri ya watu wa Z a n z i b a r , S h e i k h Abeid Amani Karume na Raisi wa Jamhuri ya Tanganyika Mwalimu Jul ius Kambarage Nyerere.

Kwenye kundi hilo la watu milioni mbili walioko ughaibuni, utaona kuna wengi wa watoto, ndugu jamaa na marafiki wa viongozi wakuu wa serikali zote mbili za Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa Ta n z a n i a . N i t a j i e k i o n g o z i y e y o t e maarufu wa Tanzania ambaye hana ndugu, jamaa au rafiki wa

BAADHI ya Majaji na Mahakimu kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliokutana Zanzibar hivi karibuni.

Page 7: ANNUUR 1114

7 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 28-MACHI 6, 2014Makala

Uibuliwe mjadala wa uraiya wa nchi mbiliInatoka Uk. 6karibu sana ambae a m e h a m i a n c h i nyengine, hasa ya m b a l i . K u n a p i a watoto wa wavuja jasho ambao, wao ndio hasa waliohamia kwenye nchi zao za sasa hivi ili kupata manufaa na faida ya kuhamia kwenye nchi zilizoendelea ili kusaidia ndugu zao, lakini mioyoni mwao, siku zote wanajisikia na kuumiya kukosa kuwa makwao wote Wa z a n z i b a r i n a Watanganyika.

Huo ni upande wa hisia na mahusiano.

Tu k i j a k w e n y e upande wa mapato. Zaidi ya watu husika, T a n z a n i a n d i o inayofaidika zaidi kwa kuwa na watu wake nje ya nchi. Inafaidika kwa kukusanya fedha za kigeni ambazo wahajiri hao walio nje wanatuma kwa n d u g u n a j a m a a z a o . I n a f a i d i k a w a k a t i w a h a j i r i hao wakitembelea Tanzania. Inafaidika k w a w a h a j i r i hao, kutokana na u z a l e n d o w a o , kuwaunganisha watu wa nchi wanazoishi na Tanzania na hatimae watu hao kuwekeza nchini na inafaidika kwa mambo mengine mengi ambayo si moja kwa moja.

Ili kuelezea faida zinazopatikana na kuzitia sura, nitatoa mfano mmoja hapa. Kikawaida Watanzania n a Wa z a n z i b a r i wakiumwa na kukawa hakuna mat ibabu nchini wanapelekwa nchi za nje kutibiwa. B i la shaka wengi wanaopata huduma hiyo ni wale walio kwenye tabaka la ama kuwa na kitu au kujua mtu wa juu kama sio m we n ye we k u wa kiongozi wa ngazi za juu. Ikitokezea h i v y o , S e r i k a l i a m a ya Z a n z i b a r a u ya M u u n g a n o

hulazimika kutowa zaidi ya shillingi za Kitanzania milioni 60 kwa kila mtu mmoja.

Watanzania wenye ndugu zao nchini ambao wanaumwa na kuwa na uwezo, wanawapokea ndugu zao hao na kuwatafutia matibabu na serikali haigharimiki hata shilingi moja. Hiyo ni faida ya moja kwa moja kwa Tanzania k w a n i w a n a n c h i wal iokuwa wake , wamepata uraia wa nchi nyengine na wana haki ya kuwasaidia ndugu zao watibiwe.

H i v i k a r i b u n i n i l i a n g a l i a v i d e o m o j a a m b a m o R a i s wa J a m h u r i ya Muungano wa Tanzania, ambae kwa mujibu wa maelezo mengi niliyosoma, inaonyesha kwamba hana tatizo na suala la Watanzania kuwa na uraia pacha. Alisema kumjibu Daktari wa fani ya urojo wa ndani ya mifupa aliyeuliza suali kuhusiana na u r a i a p a c h a . D r . Kikwete alijibu kwa kusema kwamba suala hilo litaangaliwa. Na akatania kwa kusema kwamba yeye haoni tatizo na alimuamuru Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Bernad Membe aliweke hili s u a l a h a d h a r a n i . Akasema lilipokewa, lakini Watanzania wanasema “Sasa hawa mbona wanataka huku na huku. Si walihama kwa hiari yao?” Na akaongezea, “Profesa mmoja wa pale chuo k ikuu a l ikuwa ni mmoja wa wapinzani hasa.” Nilivyoelewa a n a m a a n i s h a kwamba wasomi ndio wapinzani wa suala la uraia pacha. Kulikoni?

Nimefuatilia video hii kwenye Michuzi Blog, Kuna baadhi y a w a c h a n g i a j i wanadiriki kusema eti “TANZANIA NI NCHI YA PASSPOTI

MOJA”. Huu ni ufinyu na mawazo mgando, kwani haulinganishi f a i d a n a h a s a r a zilizopo kwa Tanzania kuwa na uraia pacha. Kwanza kwa kuanza kufikiria ni kuangalia, kwani hiyo Tanzania imekujaje? Jee kama waasisi wa Tanzania w a n g e k u w a n a mawazo mgando, i n g e k u w a p o . Au t u n g e k u wa b a d o t u n a Ta n g a n y i k a na Zanzibar kama zamani?

K w a m u j i b u w a m a e l e z o y a n a y o p a t i k a n a kwenye mtandao, kuna nchi kama 23 za Afrika ambazo z inakuba l l i ura ia pacha kwa njia moja au nyengine. Nchi hizo kwa majina ni: Angola, Benin, Burundi, Cote d’Ivoire (bila ya uwezo wa k u s h i k a v ye o vitatu vya juu kabisa), Djibouti, Egypt (kwa r u h u s a m a a l u m ) , Eritrea (kwa ruhusa na imetayarisha njia ya mpito), Gabon,

Gambia, Ghana (Raia pacha hawezi kuwa na cheo cha juu ), Kenya, Lesotho, Morocco, M o z a m b i q u e , Namibia, Nigeria, Rwanda, Sao Tome & Principie , Sierra Leone, South Africa (kwa ruhusa maalum kwenye Wizara ya Mambo ya Ndani), Togo, Tunisia, Uganda. [ K u t o k a h a p a ] . Tanzania, Zambia na Zimbabwe zinatajwa kwamba utayarishaji w a s h e r i a u k o kikaangoni. Najiuliza suali hapa, kwa nini Tanzania inayokuwa m s t a r i wa m b e l e kwenye ukombozi na masuali mengine yote iwe imeachwa nyuma na hizi nchi 23? Natarajia pia kwamba haitabaki nyuma zaidi ya hapa na Uraia pacha utawekwa kwenye katiba kama Diaspora inavyopendekeza.

Makala h i i fupi n a i a n d i k a k a m a c h a n g a m o t o k wa j a m i i k u e n d e l e z a mjadala, ambao kama

ukieleweka na kutumia fursa hii ili kuwapatia wale wote waliozaliwa ama Tanganyika, au Zanzibar au Tanzania uwezo wa kuwa raia wa Nchi zaidi ya moja. Kwa kufanya hivyo, Tanzania itakuwa tena imeshinda wengine kwa fikira endelevu k w a k u a n z i s h a Muungano wa nchi m b i l i z i l i z o k u wa huru za Tanganyika na Zanzibar, baadae k w e n y e k a t i b a m p y a , b a a d a y a kuyatafakar i ya le yote yenye uzito wa hali ya juu, wahusika h a w a k u s a h a u kwamba, pamoja na watu milioni arubaini waliomo nchini, kuna ndugu zao milioni mbili , ambao kwa sasa wanajihisi kama “watu wasiotakiwa kwao”, lakini katiba mpya imewafungulia milango na kujiona na wao ni sehemu ya Jungu kuu liitwalo Tanzania.

Balozi wa Uturuki nchini Bw. Ali Davutoclu na Bi. Canan Koru wakifungua koki za bomba za maji baada ya taasisi ya Rehema Friendship and Solidarity Trust, kuchimba kisima katika shule ya msingi Vingunguti na kuondoa kero ya muda mrefu ya maji safi shuleni hapo juzi. Na A. Msengakamba.

Page 8: ANNUUR 1114

8 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 28-MACHI 6, 2014Makala

Inaendelea Uk. 9

F e b r u a r i 1 7 , 2 0 1 4 ‘ M t a n d a o w a Kupashana Habari’ n a ‘ A m e r i c a n Conservative’

Uhusiano kati ya v i ta vya Marekani huko Mashariki ya Kati – na vita vyake kwa jumla – na baadhi ya mifumo ya kikereketwa ya U k r i s t o n c h i n i Marekani inako lea kihisia. Tafiti za maoni z i n a o n ye s h a k u wa jinsi mtu anavyokuwa mkereketwa kidini , ndiyo atakavyounga mkono vita katika nchi mbalimbali au hata kile ambacho unaweza kuita uhalifu wa kivita. Kiasi cha asilimia 60 kamili ya wanaojiita wahamasishaji Injili, waliunga mkono utesaji wa waliodhaniwa ni magaidi mwaka 2009 kwa mfano.

H i k i n d i c h o k i n a c h o s h a n g a z a , k wa n i U k r i s t o n i , k a m a u n a u j u m b e wowote, dini ya amani ambayo ilijilazimisha tu kukubali dhana ya ‘vita ya haki’ ambayo iliundwa kwa dhamira na uangalifu kuwezesha Wakristo – katika hali finyu ya hatari ya wazi – kupigana kujilinda.

Kwa uhakika, baadhi y a w a k e r e k e t w a ( w a h a f i d h i n a ) w a K i k r i s t o a m b a o w a n a w e z a k u i t w a wafuasi wa dhana ya Armageddon, wanaona vita vya Marekani barani Asia kama sehemu mahsusi ya matukio a m b a y o y a t a f i k i a kurudi kwa mara ya pili kwa Kristo, ambako wanakutazamia kwa shauku kubwa. Pia, rafiki yangu mmoja mpinzani wa s iasa za kuingilia ki jeshi nchi za nje ambaye anatoka katika familia ya kikereketwa kidini alinieleza jinsi ukinzani huo unavyoanzia kwa kiasi fulani katika hali kuwa wengi kati ya Wakristo wahamasishaji Injili ni nadra kujikita katika Agano Jipya,

Majeshi ya Agano la Kale Ukereketwa wa dini umeenea katika jeshi la Marekani, na kati ya wale wanaotaka kulitumia

Na Philip Giraldi

hata kidogo. Wakati wanaweza kunukuu maandiko na mistari kutoka Agano Jipya, wanakuwa hawana u f a h a m u w a k i n a kuhusu kinachotajwa na kuonyeshwa katika Agano Jipya inayohusu Ye s u k u s i f u v i p a j i vya kupatanisha na kumpenda jirani yako. Kama ni kweli , ina maana kuwa wengi wa wahamishaji Injili wamebobea zaidi katika maadili ya jicho kwa jicho au kuwakatilia mbali Wafilisti zaidi y a w a n a v y o e l e w a kilichosemwa katika Mlima wa Mizeituni. Kumekuwa hata hivyo na ukinzani kutoka kwa viongozi wa kiinjili k a d h a a p a m o j a n a baadhi ya wakereketwa wa dini vijana zaidi, dhidi ya fikra kongwe ya vita ilipakwa mafuta na Mungu. Lakini kwa vile wale wanaojiitaWakristo wahamishaji wa Injili, wanaelekea kwa ujumla

wao kuunga mkono vita vinavyopiganwa na Marekani. Labda s i y o a j a b u k u w a fikra za kikereketwa zimesheheni kat ika ngazi tofauti za jeshi.

Kumekuwepo kwa kiasi fulani taarifa katika magazeti kuhusu athari z a u k e r e k e t wa wa Kikristo katika jeshi, ikiwa ni pamoja na maelezo ya kutatanisha ya mlenga shabaha wa jeshi la Marekani kuandika mistari ya Biblia katika bomba la kulengea , h ivyo kumfanya mchambuzi mmoja kusema askari wanapewa ‘bunduki za Yesu.’ Jenerali mmoja mwenye sifa, William Boykin,ambaye hadi hadi h iv i kar ibuni a l i k u w a n d i y e mkereketwa wa Kikristo anayejulikana zaidi katika jeshi la Marekani, alikuwa akifanya sala za wakati wa kifungua k i n y wa a l i p o k u wa kamanda wa Del ta Force, brigedi maalum

ya kusaka walengwa maalum, na alipokuwa Naibu Waziri Mdogo wa Ulinzi wa shughuli za Ujasusi chini ya Rais George W. Bush, alikutana na ukinzani mkali kwa kuonekana katika makanisa na hadhara nyinginezo akiwa amevaa kijeshi, na medali zake zote. A l i k u wa a k i e l e z e a v i t a y a k e b i n a f s i d h i d i ya U i s l a m u , a k i s e m a ‘ M u n g u wangu n i mkubwa kuliko wenu,’ huenda akiwa anamaanisha k u wa u k u b wa u n a u m u h i m u f u l a n i , kwa mfano miongoni mwa wakereketwa na wana-dini wenzake. Pia alisema Mungu wa Uislamu ni ‘sanamu.’ Katika mikusanyiko kadhaa ya kanisa, Boykin alikuwa akitoa picha iliyopigwa Mogadishu ambayo, alidai, ilikuwa ni pamoja na kivuli cha ajabu alichokielezea k a m a ‘ u w e p o w a jinni,’ akaongeza kuwa

“maadui wa kiimani watashindwa tu kama tunakuja dhidi yao kwa jina la Yesu.” Boykin ambaye anatetea sera ya ‘ K a t a a M i s i k i t i Marekani’ hivi sasa ni Makamu wa Rais mtendaji wa Family R e s e a r c h C o u n c i l , a m b a y o i n a f a n y a kampeni katika makao makuu ya Jesh i l a Marekani kulalamika kuwa kuna ‘vita dhidi ya Ukristo’ katika jeshi.

Boykin hakuwa mtu wa aina ya peke yake. Majenerali wengine kadhaa na maof isa wengine wa ngazi za juu wameonekana katika matukio yaliyoratibiwa n a k a n i s a a u kutengeneza mikanda ya video ya shughuli hizo wakiwa wamevalia sare zao rasmi, mara k a d h a a w a k i s i f u undani wa kidini wa v i t a vya Mare k a ni katika Mashariki ya Kati. Walikuwa labda wa m e p a t a h a m a s a kutoka juu, kwa mlokole Rais George W. Bush aliyekuwa na uelekeo wa wazi wa kidini , akimzungumzia Yesu Kristo kama ‘mtoa falsafa anayempenda zaidi.’ Iwe ilivyo, mshtuko wa matukio ya 9/11 ulitoa jinni la ukereketwa wa injili kutoka kwenye chupa kuelekea katika mgogoro wa kitamaduni duniani ambao baadhi ya wafuasi wa dhana y a A r m a g e d d o n waliipokea vyema, huku Pentagon (makao makuu ya jeshi la Marekani) katika taarifa zake za kila siku za kiusalama kote duniani ikitumia aya za Biblia kama maelezo ya picha za vita. Bush mwenyewe hapo awali aliita vita ya kimataifa dhidi ya ugaidi kama ‘vita vya imani,’ lakini akaeleza masikitiko yake kwa hisia hizo alipokumbushwa kuwa wengi kati ya washirika tarajiwa wa Marekani katika vita dhidi ya ugaidi hasa ni Waislamu.

Jeshi la Marekani, l i k i wa l i n a f a h a m u vizuizi vya kikatiba vya

MWANAJESHI akitenda unyama dhidi ya Muislamu katika vurugu zinazoendelea Afrika ya Kati.

Page 9: ANNUUR 1114

9 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 28-MACHI 6, 2014Makala

Majeshi ya Agano la KaleInatoka Uk. 8kuendekeza dini yoyote, huwa linajitahidi kuzuia majigambo ya wazi ya kidini miongoni mwa maofisa wake, lakini kupuuziwa waziwazi k w a j u h u d i h i z o kumeongezeka huku wakereketwa wakiwa na madai zaidi , na wanao wawaki l ishi wengi katika ngazi za juu za maofisa wa jeshi. Theluthi nzima ya wasaidizi wa kidini jeshini hivi sasa ni wahamasishaji Injili na idadi yao inaongezeka.

Wakereketwa wengi wanaamini kuwa ili mtu awe ofisa mzuri wa jeshi lazima, awe na ‘maadili,’ ambayo ina maana kuwa na mwelekeo wa ‘kidini,’ kwa hisia kuwa haiwezekani kuwa na maadili bila kuwa na uhusiano na Mungu. Kwa vile wengi kati ya wahamasishaji wa Injili pia wanaamini wameshikilia ukweli mtupu kuhusiana na wanavyoelezea kuwa na uelekeo wa dini, hakuna mwanya wa mawazo tofauti.

Askari wanaoeneza hisia zao za kiimani wanakwepa vizuizi vya jeshi kuhusu vitendo vyao kudai kuwa nia yao ni ‘kuwainjilisha wasiokuwa kanisani,’ na siyo kueneza udini. Wanapotoa nakala ya

Biblia kwa Waafghani wanasema ni kutoa ‘ z a w a d i . ’ J e n e r a l i D a v i d P e t r a e u s , alipokuwa mkuu wa makao makuu ya jeshi, alikuwa akifahamika kwa msimamo wake wa n g u v u k u h u s u ‘ukakamavu kiimani’ kama hitaji muhimu kwa maofisa wake, hali iliyotoa mwanya kutoka juu kuingiza dini katika maendeleo ya maofisa kitaaluma

na kiufanisi. Mwaka 2007 Petraeus aliruhusu matamasha ya muziki wa bendi ya nyimbo za Injili katika makambi ya jeshi. Mwaka mmoja baadaye, msimamizi mwandamizi wa mambo ya dini jeshini William McCoy aliinua hoja ya uelekeo kidini hatua moja zaidi, akielezea jinsi askari asiyekuwa na mwelekeo wa dini, hana ulinzi dhidi ya dhambi, anaweza kusababisha

kushindwa kwa kikundi chake. Petraeus aliandika utangulizi wa kitabu cha McCoy kiitwacho ‘Chini ya Amri: Mwongozo wa kiroho kwa Wanajeshi,’ akitoa rai kiwepo katika kila begi la kubeba mgongoni katika nyakati ambazo askari anahitaji ‘nguvu za kiimani.’

M s i m a m i z i mwandamizi wa kijeshi aliyekuwa Afghanistan pia alifurahia kuonyesha j insi kuongoza kwa

vitendo kunavyoleta m a t o k e o m a z u r i , ambako asilimia 85 ya maofisa 22 waliokuwa wanawajibika kwa Petraeus wakishiriki ‘masomo endelevu ya Biblia,’ ingawa kuna haja ya kuuliza kama wali fanya hivyo i l i kuinua uwezekano wa kupandishwa vyeo.

U k i n z a n i n a usumbufu wa muda mrefu katika chuo cha jeshi la anga la Marekani kuhusu nafasi halisi ya uelekeo wa dini kwa jumla haukubadilisha lolote katika kueneza uhamasishaji Ukristo wa kikereketwa katika ngazi nyingi, mwenendo ambao ulisaidiwa na kuungwa mkono na wasimamizi kadhaa ambao wenyewe ni wakereketwa. Hata t i m u ya m p i r a wa miguu ya Jeshi la Anga haikuachwa, kukiwa na bango kubwa katika chumba cha kubadilisha nguo linalosema, ‘Mimi ni mmoja wa Timu ya Yesu Kristo.’ Kapteni M e L i n d a M o r t o n , msimamizi imani jeshini wa Kilutheri, ambaye a l i f ik ia kula lamika k u h u s u u e n e z a j i wa h is ia za k id in i kwanza alipuuzwa na halafu akahamishiwa kwingine.

(Imefasiriwa kwa Kiswahi l i na Ani l Kija kutoka makala iliyokuwa ya Kiingereza ya mwandishi Philip Giraldi.)

K U N A z a i d i y a Waislamu billioni 1.5 ulimwenguni kote, l a k i n i j a m i i z e t u zinaonekana kuwa katika hali mbaya na migogoro isiyokwisha. Kupitia makala hii, n i t a j a r i b u k i d o g o kuangalia kwa ujumla, k wa n i n i j a m i i z a Waislamu duniani ziko katika hali mbaya na ufumbuzi wake ni nini.

N i j a m b o linalofahamika vizuri

Maradhi ya umma, utambuzi na tiba yakeSaid Rajab kwamba watu bilioni

1.5 duniani wanaoitwa Waislamu, wako katika migogoro mikubwa k w e n y e t a k r i b a n nyanja zote za maisha. Ufafanuzi unaotolewa k u h u s u Wa i s l a m u kuwa katika hali mbaya k i s i a s a , k i u c h u m i , kielimu, kiutamaduni na kijamii, mara nyingi hutofautiana kutegemea na mtazamo unaotumika kufanya uchambuzi huo.

L a k i n i m w i s h o wake , ma j ibu yote y a n a y o p a t i k a n a hudondokea kwenye

m a e n e o m a k u b w a m a w i l i . E n e o l a kwanza, ni ule ufafanuzi unaoulaumu Uislamu wenyewe kwa Waislamu kuwa katika hali mbaya. Na mwingine, ni ule unaodhani kwamba Wa i s l a m u k u a c h a Uislamu, ndiyo sababu k u u y a m a d h i l a yanayowakuta sasa.

Ufafanuzi wa kwanza unauangalia Uislamu kama dini mgando (static dogma), ambayo inapinga maendeleo; na ufafanuzi wa pili unauona Uislamu kuwa

ni mfumo wa maisha ulio nyumbulifu (dynamic s y s t e m ) , a m b a o umekusudiwa kwa zama zote na mahali popote. Mtazamo wa kwanza umeanzia ulimwengu wa Magharibi yapata miaka 300 iliyopita, na umeingia kwa kina ndani ya ulimwengu wa Waislamu. Mtazamo huu sasa umechukua sura mpya, ambapo badala ya kuulaumu Uis lamu moja kwa moja, njia ya kuzunguka hutumiwa kuutia dosari U i s l a m u . U t a s i k i a

wanasema: "Tatizo siyo Uislamu, bali tafsiri yake mgando, ndiyo kikwazo kwa Waislamu". Na t iba inayoshauriwa na watu hawa ni wito wa kuleta tafsiri mpya i l i y o " b o r a z a i d i " ya Uislamu, ambayo i taendana na usasa (modernity), halafu baadaye huilinganisha na maendeleo.

Ufafanuzi wowote unaotolewa kuhusu madhila yao, unakubali k wa m b a Wa i s l a m u wako katika mgogoro

Inaendelea Uk. 10

KIJANA wa Kikristo mwenye kisu akimvizia Mzee wa Kiislamu huku naye akionekana kujihami Afrika ya Kati.

Page 10: ANNUUR 1114

10 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 28-MACHI 6, 2014Makala

DVD, inayozungumzia umuhimu wa El imu ya kumjua ALLAH (SWT), sasa zinapatikana. Mwasilishaji wa mada hiyo ni Sheikh Fahad Ibrahim kutoka Shule ya Alfurqaan, Buguruni-Malapa.

Kwa mahitaji na mawasiliano zaidi piga Simu No:- 0773 032 328, 0712 232 328, 0768 816 040.

DVD DVD DVD

Maradhi ya umma, utambuzi na tiba yakeInatoka Uk. 9mzito. Hii ikiwa ni kweli kwa upande mmoja, hata hivyo, ushahidi unaotolewa unahitaji kuthibitishwa kwanza. Kipimo kinachotumika h a p a k u o n y e s h a k wa m b a Wa i s l a m u w a k o k a t i k a h a l i mbaya ni mtazamo tu. Ni kulinganisha hali ya Waislamu na ile ya jamii za Magharibi. Ulinganisho huu wa hali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi ya Waislamu na watu wa Magharibi, au ustaarabu mwingine w o w o t e d u n i a n i , u l i o s a l i m u a m r i kwa ulimwengu wa Magharibi, unazingatia vigezo fulani. Kama ilivyo mizani, ambayo imeundwa kwa ajili ya kupima uzito, vile vile vipimo vingine vinatumiwa kupima ' k u p o r o m o k a ' a u 'kuendelea' kwa jamii za watu.

B i l a s h a k a , h i l i linahusisha kuanishwa kwa mambo ya msingi, kama maendeleo, ubora wa maisha, na ustawi. Ulinganisho huo pia unachukua mambo ya msingi kama maadili, a ina ya maisha na miundo ya kijamii na kiuchumi kama msingi wa ulinganisho.

V i p e n g e l e h i v i vilivyojificha ni muhimu sana katika kufanya u l i n g a n i s h o h u u . Vigezo vinavyotumika k a t i k a u l i m w e n g u wa Magharibi , bi la shaka, vitazingatia vile ambavyo ulimwengu h u o u n a v i t h a m i n i . Havitazingatia vile ambavyo Waislamu wanaviona muhimu, ingawa havina thamani katika ulimwengu wa Magharibi.

Hebu tuchukue mfano wa "nyumbani", eneo ambalo lina nafasi ya msingi na ya kipekee katika Uislamu. Nyumba ambayo imejaal iwa k u m k u m b u k a M we n ye z i M u n g u , ndipo mahali ambapo malezi ya awali ya

watoto huanzia. Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema ma jumba ambayo Qur'an tukufu husomwa, ni kama nyota z inazong'ara mbinguni. Hii maana yake Malaika wa kheri wanaiangalia nyumba hiyo. Kwa hiyo, kigezo ambacho kinazingatia vipimo vya Kiislamu, k ingetoa umuhimu wa kipekee kwa eneo hi l i la "nyumbani" . Lakini kinyume chake, hali haiko hivyo pale vigezo vya Kimagharibi v i n a p o t u m i k a . K u t o k a n a n a h i l o , tunafikia mahitimisho tofauti kuhusu hali ya ' m a e n d e l e o ' a u ' k u p o r o m o k a ' k wa jamii fulani, kutegemea na vigezo au vipimo vinavyotumika. Isitoshe, kipengele kingine, ni hili suala la "maadili". Kile ambacho kinaweza kuonekana ni maadili k a t i k a j a m i i m o j a , kinaweza kisionekane k u w a n i m a a d i l i katika jamii nyingine. Katika karne iliyopita, mambo mengi maovu ya m e f a n y wa k u wa maadili ya kawaida katika ulimwengu wa Magharibi. Mchakato huo wa "kuadilisha"

u m e g e u z a m a o v u k u wa m e m a . K wa mfano, talaka, ambayo awali i l ionekana ni jambo linalochukiza kwenye ndoa, sasa "imeadilishwa" kwa k i a s i k i k u b w a n a i m e k u b a l i k a k a m a maadili ya kawaida Ulaya na Marekani. Kule ndoa kuvunjika ni rahisi kama kupiga mluzi tu! Ndoa zinavunjika sana Marekani, lakini hilo halitazamwi kama kero kwa sababu taasisi y e n y e w e y a n d o a imeshapoteza thamani. Ainisho lake kongwe l i m e b a d i l i s h wa n a kuwa kibali cha kisheria kufanya uasherati! Huu ni mfano mmoja tu. Mambo mengi maovu k a t i k a u l i m w e n g u w a M a g h a r i b i y a m e b a d i l i s h w a kwa mtindo huo na kuwa utarat ibu wa maisha ya kawaida, ha l i i l iyosababisha kuzaliwa kwa jamii ambayo maadili mema hayachukuliwi tena kuwa ni jambo muhimu.

(Familia) Nyumbani k u m e p o t e z a k a z i yake ya msingi kama i l i v y o k u wa a wa l i . Matokeo yake majumba m e n g i y a m e k u w a

mahali pabaya ambapo, badala ya kuwa chachu ya mapenzi na malezi bora ya watoto, ndiyo kumekuwa kichaka cha uovu, vurugu, chuki, tabia mbaya, udhalilishaji na mateso kwa watoto. Ukweli

k w a m b a k a t i y a watoto milioni 60 wa Marekani, watano kati yao, wanachukuliwa kuwa wako katika hatari "children at risk", ni ushahidi tosha wa janga kubwa lililoukumba u l i m w e n g u w a Magharibi. Ukiangalia k w a m t a z a m o w a Kimaghar ib i , j ami i inafikiriwa kuwa katika hali mbaya, kwa sababu tu inashindwa kufikia viwango fulani vya kiidadi (quantitative s tandards) , b i la ya k u z i n g a t i a m a m b o yasiyopimika kama vile mapenzi, malezi, maadili mema na uchamungu. Isitoshe, hata vipimo vinavyotumika kupimia nyanja mbalimbali za kiidadi (quantitative a s p e c t s ) , p i a s i y o sahihi. Kwa sababu wanapima ukuaji wa uchumi, uzalishaji na mgawanyo wa mali, w a k i t u m i a d h a n a nyingi (assumptions), ambazo kimsingi hazina mashiko katika jamii zisizo za Kimagharibi.

Inaendelea Uk. 11

BAADHI ya Waislamu wakiwa katika Msikiti wa Makukura, Buguruni Jijini Dar es Salaam February 24, 2014 katika kongamano lililofanyika Msikiti hapo.

Page 11: ANNUUR 1114

11 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 21-27, 2014Makala

Maradhi ya umma, utambuzi na tiba yakeInatoka Uk. 10Mfumo wa familia

p a n a , k wa m f a n o , unabadilisha vipimo v y a k i u c h u m i v i n a v y o t u m i k a kwenye ulimwengu wa Maghar ib i kwa kiasi kikubwa. Mtu anayelipwa dola 1000 k wa m we z i n c h i n i Marekani, ambaye hana mtandao wa kifamilia unaomsaidia; kiuchumi hayuko kwenye hali sawa kama mwingine anayelipwa kiasi hicho cha fedha nchini Iran, ambaye ana mtandao mpana wa kifamilia unaomsaidia.

Sasa v ip imo hiv i " v i s i v y o s a h i h i " vinapotumika, jamii za Waislamu zinaonekana kuwa mwishoni mwa orodha na Uislamu u n a l a u m i w a k w a Waislamu kuwa katika hali hiyo mbaya. Lakini h a o w a n a o l a u m u Uislamu, wanashindwa kufafanua vipi Uislamu n i k i k w a z o k w a maendeleo, wakati dini hii imeleta ustaarabu uliong'ara kimaendeleo kwa karne nyingi?

Wanadai kwamba Mapinduzi ya Kisayansi

yasingeweza kutokea kwenye Ustaarabu wa Kiislamu, kwa sababu k u n a k i t u k a t i k a Uislamu, kinachokwaza maendeleo kama hayo. Hao wenye mtazamo h u o wa n a s h i n d wa kufafanua, kwanini

Uislamu ndiyo uliokuwa msingi wa kuibuka kwa utamaduni wa kisayansi, uliodumu kwa takriban miaka 800.

Si lengo langu hasa kuleta masahihisho haya ya kimtazamo, ili kukanusha ukweli

kwamba Umma wa Kiislamu duniani una hali mbaya. Nia hasa ni kuleta mtazamo sahihi, kwa sababu bila ya mtazamo huo, mtu anaweza kutoa hukumu ya jumla dhidi ya jamii za Kiislamu, wakati

ukweli wenyewe hauko hivyo.

Masahihisho hayo ya k i m t a z a m o p i a yatatusaidia mahali pa kuanzia, wakati wa kuzijenga upya jamii za Wais lamu. Kwa sababu, kabla kazi hiyo ya ujenzi haijaanza, lazima tufahamu kwa kina , as i l i hasa ya maradhi yanayoukabili Umma wetu, ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya madhara yaliyopatikana.

H i l i , b i l a s h a k a , hal iwezi kufanyika kwa kutumia vipimo na vigezo vya Kimagharibi. Utambuzi wa maradhi haya, lazima ujikite kwenye Qur'an, ambayo inatuambia kwamba, M w e n y e z i M u n g u Mtukufu, ana Sunna yake, njia yake, ambayo kamwe haibadiliki:

"Hii ni kawaida ya M w e n y e z i M u n g u iliyokuwa kwa wale waliopita zamani; wala hutapata mabadiliko k a t i k a k a wa i da ya Mwenyez i Mungu" Qur(33:62).

(Itaendelea)

UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL inatangaza program maalum ya maandalizi ya kurudia mtihani wa Kidato cha nne 2014.

Program hii itaanza tarehe 10/03/2014. Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 2:00 kamili asubuhi hadi saa 9:00 Alasir.

Masomo yatakayofundishwa ni:-Masomo yote atakayohitaji mwanafunzi kuyafanyia mtihani.

Fomu za Kujiunga zinapatikana shuleni BURE baada ya kulipa ada.Mlete mwanao apate Elimu yenye tija itakayomwezesha kufikia malengo yake kielimu.

Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba:0712 974428

Wabllah tawfiq MKUU WA SHULE

Ubungo Islamic high SchoolP.o. Box 55105 Tel: 2450069, 0712 974428, fax: 2450822 Dar es salaam.

E-mail: [email protected]

MAANDALIZI YA KUJIANDAA KURUDIA MTIHANI WA TAIFA KIDATO CHA NNE 2014

BAADHI ya Waislamu wakiwa katika Msikiti wa Makukura, Buguruni Jijini Dar es Salaam February 24, 2014 katika kongamano lililofanyika Msikiti hapo.

Page 12: ANNUUR 1114

12 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 28-MACHI 6, 2014Mashairi/Makala

Nimeishika malenga, kalamu yangu ya ngisi, Beti naanza kupanga, zisomwe kadamnasi, Si choza wala si kunga, ya ndanimwe mdurusi, Lengolo si ya Taifa, bali yao maslahi.

Nabtadi nganganga, dailo kuliakisi, Poshoyo waloipanga, si toshelezi kuhisi, Bilhaki ni majanga, kwa kina ukiandisi, Lengolo si ya Taifa, bali yao maslahi.

Mtima unanigonga, kwa hofu na wasiwasi, Pamwe kichwa kuniwanga, na kukosa taanusi, Kwa wanodai 'faranga', ya mazidi si nakisi, Lengolo si ya Taifa, bali yao maslahi.

Baadhiyo walolonga, waongezewe fulusi, Mkono ningewaunga, wangehitaji nakisi, Kwa nyongeza nawapinga, waso na kite unasi, Lengolo si ya Taifa, bali yao maslahi.

Tafakari hili janga, machungu utayahisi, Poshoyo wanoipinga, kwa mwalimu na polisi, Mwezi mzima wafunga, chini ya hicho kiasi, Lengolo si ya Taifa, bali yao maslahi.

Mafisadi waizonga, nchi yetu kufanisi, Kwa kutaka 'kuinyonga', ishindwe kutanafusi, Kwalo dai zimenonga, za watu tumbi nufusi, Lengolo si ya Taifa, bali yao maslahi.

Hadhi wameitabanga, yao kwa 'kujinajisi', Pamwe na kuibananga, ya bunge lao nemsi, Wasimtafute mwanga, mwanga ni zao nufusi,Lengolo si ya Taifa, bali yao maslahi.

Adhimu wachokilenga, ni kuusaka ukwasi, Kwa kuanza kuujenga, kayaya ubinafsi, Nikosani nikilonga, si "Wazalendo halisi?", Lengolo si ya Taifa, bali yao maslahi.

Wasitutishe kwa ngenga, kwalo dai lao hasi, Si wa kuwaengenga, nchi wataifilisi, Kwa mimi ninokienga, ebu kando wajulusi, Lengolo si ya Taifa, bali yao maslahi.

Aula ni 'kuwatenga', na wa kwao ugigisi, Si watu wa kuwakenga, 'tuwambie' sasa "Basi!", Tumwone atayeringa, 'huyo kweli ni mkwasi !',Lengolo si ya Taifa, bali yao maslahi.

Hawa si wa kuwanyenga, Muhtaramu Raisi, kuna haja kuwagunga, kwalo dailo tatasi, Dawayo ni kuwashunga, bungeni hawa 'waasi', Lengolo si ya Taifa, bali yao maslahi.

Asaa wakanizonga, kwa hilo kuliramisi, Ama kwa hisi kujenga, ya kwamba nimewatusi, Au hata kwa kulonga, 'vyomboni' mimi "sabasi", Lengolo si ya Taifa, bali yao maslahi.

ALIMU wa yangu kunga, ya fuadi ni QUDUSI, Yu pweke wa kunikinga, na shururi za unasi, Sina haja ya mganga, wa 'north' au wa kusi, Lengolo si ya Taifa, bali yao maslahi.

Mikoba yangu nafunga, ya hoja ya udadisi, Wachokinena wahenga, hoja kinaiakisi, Kalamu yatia nanga, bandari ya udodosi, Kaditamati nafunga, kidau changu cha ngisi.

ABUU NYAMKOMOG - MWANZA.

Bunge la Katiba (ukistaajabu ya Musa,...!)

Page 13: ANNUUR 1114

13 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 28-MACHI 6, 2014Makala

N a m s o m a M h e s h i m i wa Z i t t o Kabwe hapa na nafikiri kuna nukta muhimu haifahamu. Anasema “Zanzibar iwe na Waziri Mkuu Mtendaji kwa masuala yote ambayo s i o ya M u u n g a n o . Tanganyika iwe na Waziri Mkuu Mtendaji kwa masuala yote ambayo s i o ya M u u n g a n o . Hawa watateuliwa na Rais wa Muungano kutoka chama chenye Wawaki l i shi wengi k a t i k a B a r a z a l a Wawakilishi Tanganyika na Baraza la Wawakilishi Z a n z i b a r . W o t e watakuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa utaratibu kwamba iwapo Rais anatoka Zanzibar, basi Waziri Mkuu wa Tanganyika atakuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na wa Zanzibar atakuwa Makamu wa Pili wa Rais. Kule kule kwenye misingi haswa ya Muungano. Hawa wataongoza Mabaraza yao ya Mawaziri na watakuwa na nguvu ya kuteua na kufukuza Mawaziri wanavyotaka. Hawatakuwa Wabunge k a t i k a B u n g e l a Muungano.”

Naona kuna nukta m u h i m u a m b a y o a n a i p u u z a a u kutoifahamu. Kwanza kwa n in i Zanzibar t u d u n i s h w e k w a kuwa na Waziri Mkuu badala ya Rais? Mbona Mwalimu aliuondosha m f u m o wa Wa z i r i Mkuu kama mkuu wa serikali na kuiweka Tanganyika kama ni jamhuri huku akiwa Rais mwenye mamlaka kamili? Jee, Wazanzibari watakubali kuifanyia tena marekebisho katiba yao kumuondosha Rais wa kupigiwa kura na wenyewe wakabakiwa na Waziri Mkuu wa kuteul iwa sawa na mfumo wa mfalme anapomteua Waziri Mkuu wake?

Tulikuwa na Waziri M k u u wa k wa n z a

Kutoka Facebook

Zanzibar baada ya u h u r u , t e n a k w a mfumo huo huo wa wingi wa Wawakilishi, akapinduliwa na ikawa ndio msingi wa kuwa na mfumo wa Jamhuri inayoongozwa na Rais mwenye mamlaka yake. Ukiwasikiliza hoja ya mwanzo hawa ndugu zetu wa “Panafricanism Movement”, hukwambia hawaitambui siku ya uhuru wa Zanzibar. Sababu kuu ni mfumo h u o u l i o k u w a n a Wa z i r i M k u u j a p o kuwa hakuchaguliwa n a m f a l m e l a k i n i watakwambia uhuru b a n d i a . H a l a f u w a t u r e j e s h e k u l e kule tena. Basi Waziri Mkuu mwenyewe wa kuteuliwa, kama si ufalme tuliouondosha ni nini?

H e b u t u f i k i r i u w e z e k a n o k w a M z a n z i b a r i k u w a Rais wa muungano k a t i k a m f u m o w a n a o u p e n d e k e z a hasa kwa kutegemea k u r a z a b a i n a y a Watanganyika milioni 44 na Wazanzibar i m i l i o n i 1 . 5 ! U p o kweli? Hawakueleza n a m n a g a n i h u y o Rais atapatikana kwa mfano wa mzunguko wa m g o m b e a k wa a w a m u b a i n a y a Zanzibar na Tanganyika. Kinachodhaniwa, au tuseme, kinachotakiwa

ni kwamba Rais atatoka Tanganyika kupit ia wingi wa idadi yao, na ndiye atakayekuwa na uwezo wa kututeulia Wazanzibari Waziri Mkuu. Sasa tukitazame k i p a n d e h i c h o n a hali halisi ilivyo sasa hasa tukirudi nyuma kidogo pale Naibu Kat ibu Mkuu CCM Zanzibar aliposema wanataka nafasi ya R a i s wa Z a n z i b a r kumchaguwa wenyewe bi la kupit ishwa na NEC ya muungano na akaiorodhoresha kama kero nyengine ya mfumo wa sasa. Jee, kuna tafauti?

Wa k a t i w e n z e t u waki fanya chaguzi hata kwa magavana wa States zao (Majimbo), sisi tunaota ndoto za kuteuliana “under the umbrella ya pseudo democracy” ya uchaguzi wa wawakilishi ambao u n a w e z a k u l e t a ush indi wa vyama katika majimbo yao ya kura huku mwenye “popular vote” akabaki kuwa mshindi wa pili. Mfano halisi ni uchaguzi Zanzibar 1963 ambapo chama kilichoshinda kilikuwa na viti vingi, lakini “popular vote” ilikwenda kwa chama cha pili na ndio sababu za mapinduzi. Sasa w a t u r e j e s h e k u l e kule? Au misingi gani ya demokrasia kwa

Mzanzibari mwenye wingi wa kura 1.5M k u w a c h a g u l i a Watanganyika milioni 44 Waziri Mkuu wao hata ikiwa urais ni wa kupokezana.

A n a c h o k i t a m a n i Mheshimiwa Zitto na kukificha kwa ustadi mdogo tu, ni serikali m o j a . U s h a h i d i n i kwamba anakuba l i mwisho wa maandishi yake kwamba kuwe na dola moja na mkuu wa nchi mmoja chini ya serikali mbili zenye hadhi sawa na serikali za mitaa. Madai ya wanamabadiliko sio serikali ni mamlaka kamili nje na ndani ya nchi, na sio jina tu la serikali kwani hata mitaani kuna serikali za mitaa na mabaraza yao ya wawakil ishi s a wa n a m a b a r a z a ya madiwani ambao nao pia huchaguliwa n a wa n a n c h i . H i l i halikubaliki. Anasema m w i s h o k w a m b a kutakuwa na Hotuba ya Rais kama ile ya State of The Union ya Marekani, huku akisahau kwamba Wazanzibari tumeuona muungano wa States za Marekani na haukuwa rahisi maana civil war (vita ya wenyewe kwa wenyewe) peke yake iwe somo kwa hawa waj i i tao “unionist” kwa vi le ta fs i r i ya “unionist” kwao ni

serikali moja. wengine tunaamini mfumo wa kweli wa union wenye maendeleo ni wa mfano wa European Union uliojikweza ndani ya mipaka yao kwa chachu ya maendeleo. Miaka 50 tumezubaa kwa kuwa tuliambiwa tuna serikali huku tukisahau serikali na mamlaka ni vitu viwili tafauti.

N i m a l i z i e kuwakumbusha Pan-Africanists kwanini hawaweki msisitizo mkubwa katika EAC na hii “coalit ion of willing” inayokwenda mbele zaidi na agenda z a “ i n t e g r a t i o n ” kubwa EAC badala ya kutuhadaa kwa mifumo itakayomeza utambulisho wa nchi husika bila hata ya idhini ya wananchi we n ye we . N a s e m a hivi kwa sababu kipo kielelezo kwa upande wa Zanzibar pale wananchi walipoiptisha kura ya maoni kwa wingi wa aslimia 60 kwa kauli moja ya kwamba ni nchi, sio jimbo, chochoro wala mkoa na udogo wetu isiwe kielelezo c h a k u m e z wa k wa hamasa za propaganda za “panafricansim” zisioeleweka.

Hatuna haja yakuwa na mfumo wa nchi yenye “quens speech” kwani hio pekee ndio sababu ya mapinduzi yaliotoa roho za watu na kuleta fitna kubwa kwa miaka 50 sasa.

N i w a k u m b u s h e zaidi viongozi kwamba maoni yalishatolewa na tume ilishayabeba, asilimia 60 Zanzibar kwa pamoja maoni yao ni mfumo utakaotoa mamlaka kamili. Na kwa upande wa Tanganyika asilimia 60 wametaka serikali tatu. Vile vile mukumbuke kwamba kuna kura ya maoni, wadau wa mwisho ni wananchi, na hakuna haja kwa Wazanzibari kubadili tena katiba yao mbichi ya 2010 ilioweka “blueprint” ya mamlaka yao. Tuende mbele badala ya kurudi nyuma.

Page 14: ANNUUR 1114

14 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 28-MACHI 6, 2014Makala

K WA m i a k a m i n g i Watanzania wamekuwa wakijadili mengi, lakini hawakupata fursa pana ya kujadili Mkataba wa Muungano yaani ‘Articles of Union’, uliosainiwa n a M wa l i m u J u l i u s Kambarage Nyerere na Mzee Sheikh Abeid Aman Karume.

H a i j a p i t a m i a k a mitatu tangu baadhi y a W a z a n z i b a r i walipojaribu kuupata m k a t a b a h u u k a t i k a mamlaka zinazohusika, wakaambiwa hauonekani.

R a i s wa Z a n z i b a r , Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza kwa hasira katika mkutano mmoja wa hadhara mjini Zanzibar, alisema:

“ M k a t a b a w a Muungano upo kwenye makabati ya Ikulu. Hapo hapo, akasema wanaotaka kuuona mkataba huo wajaribu kuupata kutoka United Nations”.

M w a n a s h e r i a w a CHADEMA, Mheshimiwa Tundu Lissu (MB) mwaka jana alipowasilisha Hotuba ya Kambi ya Upinzani Bungeni, alielezea dai la Serikali ya Tanganyika, lakini akatamka wazi kuwa:

“Hatutaki kuona picha za (Mwalimu) Nyerere n a ( M e e K a r u m e ) wakichanganya udongo..tunataka Mkataba wa Muungano”.

Ikumbukwe, miaka m i w i l i n y u m a , k u l e ‘Jamii Forums’ walitafuta k i tabu cha Mwal imu Julius Nyerere, kiitwacho ‘Uongozi wetu na Hatima y a Ta n g a n y i k a ’ . I l i kujiridhisha.

Leo tena, tunawaletea Mkataba wa Muungano ‘Articles of Union’. Wapo wanaosema Mkataba huu ndiyo mama wa Katiba zote mbili yaani ya Muungano na ya Zanzibar.

Wapo wanaosema yale mambo 11 ya Muungano yameongezwa kadhaa, sasa Mkataba huu hapa, tuangalie ukweli wake.

M K A T A B A W A MUUNGANO BAINA Y A J A M H U R I Y A T A N G A N Y I K A N A JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR

Kwa kuwa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa

Huu ndiyo mkataba wa Muungano (?)

Zanzibar zinafahamu u h u s i a n o w a m u d a mrefu (wa) watu wake n a m s h i k a m a n o n a kukuza uhusiano huo na kuimarisha mshikamano na kukuza umoja wa watu wa Afrika, zimekutana na kutafakari Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar.

Na kwa kuwa Serikali za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar, zinapendelea ya kwamba Jamhuri hizi mbili ziungane kuwa Jamhuri m o j a h u r u . M o j a ya masharti ya makubaliano yafuatayo:

K w a h i y o IMEKUBALIWA baina ya Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na ya Jamhuri ya watu wa Zanzibar, kama ifuatavyo:-

I) Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar zitaungana na kuwa Jamhuri huru moja.

II) Katika kipindi cha kuanza kwa Muungano mpaka Baraza la Kutunga katiba lililotajwa katika ibara ya (vii) litakapokutana

na kupitisha katiba ya Jamhuri ya Muungano (Kuanzia hapa kitaitwa k i p i n d i c h a m p i t o ) , Jamhuri ya Muungano itaongozwa kwa masharti ya ibara ya (iii) mpaka ya (vi).

III) Katika kipindi cha mpito katiba ya Jamhuri ya Muungano itakuwa katiba ya Tanganyika i l i y o r e k e b i s h w a i l i kuweka:

a) Chombo tofauti cha kutunga sheria na Serikali kwa ajili ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria zilizopo za Zanzibar na vitakuwa na mamlaka ya mwisho kat ika Zanzibar kwa mambo yote isipokuwa yale tu yaliyo chini ya bunge na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

b) Nafasi ya makamo wawili wa Rais mmoja kati yao akiwa ni mkaazi wa Zanzibar atakuwa ndiye kiongozi wa Serikali iliyotajwa kwa ajili ya Zanzibar na atakuwa ndiye msaidizi mkuu wa rais wa Jamhuri ya Muungano katika utekelezaji wa kazi za Serikali kwa upande wa

Zanzibar.c ) U w a k i l i s h i w a

Zanzibar katika bunge la Jamhuri ya Muungano.

d) Mambo mengine yatayofaa au kuhitajika ili kuipa nguvu Jamhuri ya Muungano na mkataba huu.

IV) Mambo yafuatayo yatakuwa chini ya Bunge na Serikali ya Jamhuri ya Muungano:-

a) Katiba na Serikali ya Jamhuri ya Muungano

b) Mambo ya nchi za njec) Ulinzid) Polisie ) M a m l a k a

yanayohusika na hali ya hatari

f) Uraiag) Uhamiajih) Mikopo na biashara

ya nchi za njei ) Utumishi kat ika

Jamhuri ya Muungano.j ) Kodi ya mapato

inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini na kusimamiwa na idara ya forodha

k) Bandari , mambo yanayohusu usafiri wa anga, Posta na Simu.

V) Bunge na Serikali vilivyotajwa vitakuwa na mamlaka ya mwisho juu ya mambo yote yahusuyo Jamhuri ya Muungano na kuongezea mamlaka juu ya mambo yote yahusuyo Tanganyika.

Sheria zote zilizopo za Tanganyika na za Zanzibar zitaendelea kutumika katika maeneo yao bila kuathiri:-

a) Mashart i yoyote y a t a k a y o w e k w a n a chombo chenye mamlaka ya kutunga sheria.

b ) M a s h a r t i yatakayowekwa kwa amri ya Rais wa Zanzibar juu ya sheria yoyote inayohusu jambo lolote lililotajwa kwenye ibara ya (iv), na kufuta sheria yoyote inayolingana Zanzibar.

c) Mabadiliko yoyote k a m a y a t a o n e k a n a yanafaa au kuhitajika ili kufanikisha Muungano na mkataba huu.

a) Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano atakuwa ni Mwalimu J.

K. Nyerere na ataongoza Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kufuata masharti ya mkataba huu na kwa kusaidiwa n a m a o f i s a we n g i n e a takaowateuwa toka Tanganyika na Zanzibar na watumishi wa Serikali zao.

b) Makamu wa Kwanza wa Rais atakuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa BLM kutoka Zanzibar aliyeteuliwa kwa kufuata m a r e k e b i s h o k a m a yalivyoelezwa na ibara ya 3, atakuwa Sheikh Abeid Amani Karume.

VI) Rais wa Jamhuri y a M u u n g a n o k w a kukubaliana na Makamu wa R a i s a m b a y e n i kiongozi wa serikali ya Zanzibar.

a) Atateua tume kwa ajili ya kutoa mapendekezo kwa ajili ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

b) Atait isha Baraza l a k u t u n g a K a t i b a ikiwa na wawakilishi kutoka Tanganyika na Zanzibar katika idadi itakayoamuliwa likutane katika kipindi cha mwaka mmoja tokea kuanza k wa m u u n g a n o k wa madhumuni ya kutafakari mapendekezo ya tume iliyotajwa juu na kupitisha Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

V I I ) M k a t a b a h u u utahitaji kuthibitishwa kwa kutungiwa sheria na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kwa kushirikiana na Baraza lake la Mawaziri, na mkataba kupitishwa na kuundwa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibar kwa kufuata masharti yaliyokubaliwa.

KWA KUSHUHUDIA HAPA: Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Jamhuri ya Tanganyika na Abeid Amani Karume, Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, wametia saini nakala mbili za mkataba huu, hapa Zanzibar siku ya tarehe ishirini na mbili ya mwezi Aprili, 1964

HAYATI Mwalimu J.K. Nyerere

Page 15: ANNUUR 1114

15 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 28-MACHI 6, 2014Makala

N I N A T A R A J I A k u y a j u m l i s h a k w a msomaji maisha ya Nabii Muhammad na nafsi yake iliyokwezwa juu sana na yenye heshma kubwa. M t u h u y u a m b a ye ndiye “Maji ya maisha” kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu sharti ajulishwe kwa kila mtu.

Nabii Muhammad ( s.a.w) ni majivunio ya wanadamu. Kwa karne kumi na nne zilizopita, wengi wa watalaamu, wanafalsafa, wanasayansi, na wanazuoni, kila mmoja wao a k iwa n i n y ot a angavu katika dunia yetu iliyoelimika, wamesimama nyuma yake kwa heshima upendo, na wamejivunia kule kuwamo kat ika umma wake.

Inatosha kuelewa na kutathimini ukubwa wake kiasi kwamba, hata baada ya mashambulizi mengi sana, bado tunasikia maneno ya “Nashuhudia kwa moyo na kutamka kwa ulimi kuwa yupo Mwenyezi Mungu Mmoja tu na Muhammad ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu”, yakitangazwa kwenye minara ya misikiti mara tano kila siku.

Tunafurahi wakati j i n a l a k e l i n a t a j w a kwenye minara, kama wa n a v y o f a n ya wa t u na viumbe wengine wa kiroho. Juu ya juhudi nyingi za kuwapotosha vijana wetu na kuwapeleka kwenye njia mbaya, vijana wanaendelea kukimbilia kwake, ingawa hawawezi kuuona ukweli kamili wa Muhammad.

Wakati haujatufanya tusahau ukweli kumhusu mtu huyu. Kumbukumbu yangu ya mtu huyu akilini mwangu ni mbichi au dhahiri mno kiasi kwamba nikilitaja jina lake tukufu nakuwa kama ninakaribia kumwona. Wakati mmoja, nilipokuwa nikihiji katika jiji lake tukufu la Madina, nilihisi kuwa yu karibu kujitokeza atukaribishe.

K a d r i w a k a t i unavyopita, fikra zingine hufutika, lakini yeye hubakia mbichi kama ua la waridi myoyoni mwetu. Kwa hivyo kila tusikiapo jina lake likitajwa kutoka katika minara ya misikiti, huwa tunasitisha kazi zetu, na tukiwa tunaitikia wito huo, huanza kuelekea

Mtume Muhammad (s.a.w)misikitini.

T u n g e r u h u s i w a k u m f a f a n u a a u k u m u a i n i s h a y e y e k a m a wa t u we n g i n e w a l i v y o f a f a n u l i w a , tungetumia taasisi za kielimu na za kijamii, basi huenda vijana wetu wangekuwa wanaifuata n j i a y a k e . J u u y a mapungufu yetu, wengi hutwaa “bilauri” zao na kukimbilia kuzijaza kutoka kwenye “chemchemi nadhifu” hii. Katika kila sehemu ya duniani pamoja na Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, uamsho wa Uis lamu unatokea.

Waislamu wanazipanda n c h i h i z i m b e g u z a mustaqabali wa furaha. Ki la pahala Uis lamu u n a s h a m i r i k a m a ulivyofanya wakati wa furaha. Ki la pahala U i s l a m u u n a s h a m i r i kama ulivyofanya wakati w a f u r a h a - w a k a t i wa Muhammad, s.a.w mwenyewe.

H u t o k e a v i v y o hivyo katika nchi zenye Waislamu wengi. Wale Waislamu ambao upendo na kujitolea kwao katika Uislamu kulikuwa kwa mazoea tu na hakukuwa na mtizamo wala utafiti wa kina, wamewapisha kizazi kipya ambacho kinamfuata Muhammad kwa ridhaa na ufahamu kamili, huku wakimulikwa na mwanga wa sayansi na maendeleo ya elimu. Wale waliokuwa wakizitumia shule na vyuo vikuu kwa niaba ya kutoamini, sasa wanamkimbil ia yeye. Hata watu maarufu kama Maurice Bucaille na Roger Graudy waliona uongo wa mifumo yao na wakamkimbilia yeye.

M U H A M M A D ( S .A.W) KAMA MTU ANAYEPENDWA ZAIDI NA NYOYO NYINGI K U L I K O W A T U WENGINE.

S i j u i k a m a tumemtambua kikamilifu mtu mpendwa wa nyoyo kuliko wote. Hata mie a m b a e n i m e k u w a nikidumisha swala tano kila siku tangu niwe na umri wa miaka mitano

na ninaendelea kuwa mtumishi mlangoni pake, sielewi kama ninaweza kumtambua yeye. Je! Tu m e w e z a k u u j a z a upendo katika nyoyo za vizazi vya hivi karibuni kwa kumfafanua huyo chimbuko la mwisho la upendo wote na shauku kubwa?

Laiti kama wanadamu wangemjua Muhammad (s.a.w), wangempenda y e y e k a m a M a j n u n al ivyompenda Layla . (Majnuni na Layla, ni watu wa kingano (hadithi) ambao walipendana sana.) Na kila jina lake linapotajwa, h a o w a n a a d a m wa n g e t e t e m e k a k wa furaha kwa mategemeo ya kuingia katika utamaduni unaomzunguka yeye na wafuasi wake kwa moyo wote.

Tunaweza kumpenda yule tu ambae tunamjua, tena kwa kadiri ya upeo w a k u m j u a k w e t u . Maadui zetu wamejitahidi kutufanya sie tumsahau, kuhakikisha kuwa jina lake halitajwi. Lakini kwa kuwa anaungwa mkono na Mwenyezi Mungu (S.W.T) mwenyewe, v ikwazo vyote huvunjiliwa mbali na vijana wanajisalimisha kwake kwa furaha kama mtu anayekaribia kufa kwa k iu a fanyavyo anapoyagundua maji . Ulaini wake wenye nguvu sana na huruma na upendo alio nao, humkumbatia k i l a “ m w e n y e k i u ” anayemwendea yeye.

L a z i m a u t a k u w a u m e o n a k w a m b a , unapokwenda kuswali Ijumaa, wengi wa waumini wanaokuja kuswali siku hizi ni vijana wadogo wadogo. Je! Umewahi k u j i u l i z a k w a n i n i inakuwa hivi, kuwa juu ya uongezekaji wa upotoshaji na uasi, vijana wadogo wadogo huja misikitini na wanakaa kuswal i misikitini bila kujali hali ya hewa kama baridi na magumu mengine? Jibu au kivutio ni kimoja tu, nacho ni: Muhammad (s.a.w.). Tuelewe hivyo au tusielewe, roho na n y o y o h u m k i m b i l i a M u h a m m a d ( s . a . w . )

kama nondo (wadudu) w a n a v y o u k i m b i l i a mshumaa au taa.

Na hata wale "wadudu wa majira ya baridi" ambao hawajabahatika, punde si punde watamkimbilia yeye. Wanasayansi na wataalamu wabunifu watamtafiti. Wale ambao hadi sasa bado ni maadui, hivi watakuwa marafiki wapenzi na watakimbilia makaribisho yake mazuri kabisa. Wakati Muhammad (s.a.w.) alipokuwa hai, h a t a m a a d u i w e n g i walimtamani.

Safari moja alihadithia n d o t o y a k e k a m a ifuatavyo:

“Walinipima mie katika mizani dhidi ya watu kumi wa umma wangu, nikawazidi uzito. Kisha wakanipima mie dhidi ya watu mia, kisha elfu moja, name nikawazidi wote uzito. Pia akatoa hadithi nyingine: “Nilipimwa dhidi ya umma wangu wote, name nikawazidi uzani.” Muhammad s.a.w anawazidi uzito watu wote wenye akili, uchamungu, hali ya kiroho, imani, elimu na ujuzi, kwani viumbe wote wengine wameumbwa kwa sababu yake. Imeripotiwa kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) a l i m wa m b i a M t u m e (s.a.w): “Isingekuwa kwa ajili yako nisingeyaumba matufe.”

M U H A M M A D (S.A.W.) AFAFANUA MAANA YA UUMBAJI

Ulimwengu ni kitabu. M u h a m m a d ( s . a . w . ) asingeumbwa, kitabu hiki kisinge eleweka. Kukiumba kitabu kisichoeleweka ni kupoteza wakati na j u h u d i . K w a k u w a Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Ametakasika na mambo ya upungufu kama haya (ya kupoteza juhudi, n.k.), Alimuumba Muhammad (s.a.w.) i l i kuiainisha maana ya uumbaji kwa wanadamu. Allah (s.w.t.) Akawa Mwalimu wake, na dunia, anga na mbingu vikawajibishwa kwake. Akajibu maswali yote ya umilele kwa mfano: -

“Mie ni nani? Niko wapi? Kwa nini nimeumbwa? Hatima yangu ya mwisho ni nini? Ni nani kiongozi

wangu katika safari hii?" Muhammad (s.a.w.)

ndiye aliyeupa uumbaji m a a n a n a a k a w a p a wanadamu majibu ya maswali kama hayo.

A n g e t a m b u l i k a kikamilifu, angependwa sana tena sana. Lakini ingawa tunamfahamu k i d o g o , s i e b a d o tunampenda sana yeye.

Hebu nisimulie tukio lililotokea nilipoizuru Madina.

"Mazingira ya kule yalinizidi nguvu. Kitu kikanitanabahisha: Mimi huswali mbele ya Allah (s.w.t.) kila asubuhi, na kutamka mara saba:

"Ee Mwenyezi Mungu wangu (s.w.t.), niepushe na Moto wa Jahannan na Uniingize Peponi pamoja na wacha-Mungu."

H a k u n a m u u m i n i ambaye hapendi kuingia Peponi. Hata hivyo, katika mazingira haya, nilijiuliza mimi mwenyewe swali hili:

Ungelialikwa wewe uingie Peponi kupitia l ango lo lo te ka t i ya milango yake saba, wapi utapenda kwenda, rawdha (eneo ndani ya msikiti wake linalopakana na kaburi la Mtume ( s.a.w)) au ungependa kuingia Peponi?

Niamini ninavyokuapia kwa Jina la Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwamba nilijijibu mie mwenyewe kuwa: 'Mahala hapa pananipendeza zaidi mie. Nimeweza kuugusisha uso wangu katika udongo wa bwana wangu ambaye m i e n a p e n d a n i w e mtumwa niliyefungiwa kwa mnyororo mlangoni pake, kuliko kitu chochote kingine duniani. Sitaki kuikosa fursa hiyo.'

N i n a a m i n i k u w a hili ndilo takwa la kila muumini. Nilipobarikiwa n a f u r s a h i i k u b wa (ya kwenda Madina), nilikuwa na Mbunge wa Bunge la Uturuki, Bwana Arif Hikmet. Aliniambia kuwa yeye alijiahidi kuwa atagalagala katika udongo kama punda atakapouvuka mpaka na kuingia ardhi ya Madina. Mtu huyu mkubwa a l i i teke leza ahadi yake biyo. Kila n i n a p o l i k u m b u k a tukio hili , nashindwa kuyazuia machozi yangu kumiminika.

(Hii ni sehemu ya mwanzo ya utangulizi k u t o k a k i t a b u Muhammad mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kilichoandikiwa na M. Fethullah Gulen)

Page 16: ANNUUR 1114

16 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 28-MACHI 6, 201416 MAKALA

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works LTD, S.L.P. 4605, Dar es Salaam.

AN-NUUR16 RABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 28 - MACHI 6, 2014

Soma AN-NUUR

kila Ijumaa

ILIKUWA ni kama ‘Jahanamu’ ya aina yake , ambayo s i rahisi kuamini kuwa binadamu anaweza kumfanyia binadamu mwenzake.

N i m a t e s o n a udhalilishaji ambao hata hivyo Masheikh w a l i o k u t w a n a mkasa huo hawataki kusimulia sana, bali k u i s h i a k u s e m a “Inshaallah ipo siku ya hukumu”.

“Ipo siku hakimu w a m a h a k i m u a t a h u k u m u k w a h a k i a m b a p o wa l i o d h u l u m i wa n a k u o n e w a watalipiziwa kisasi.”

Hayo yameelezwa n a S h e i k h S a i d Kassim, akidai kuwa siku arobaini za awali za maisha ya gerezani kwa viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO, w a n a o s h i k i l i w a k a t i k a g e r e z a l a K i i n u a M i g u u Zanzibar, zilikithiri kwa udhalilishaji na mateso.

S h e i k h h u y o k u t o k a Z a n z i b a r a l i y a s e m a h a y o katika Kongamano lililofanyika katika Msikiti wa Makukula, Buguruni Jijini Dar es Salaam, Jumapili wiki iliyopita, alipokuwa a k i z u n g u m z i a m u s t a k a b a l i w a Masheikh hao tangu kukamatwa kwao hadi sasa na kusema wanahitaji nusra.

“ M a s h e i k h wamepata mateso makubwa gerezani, hususan katika siku arobaini za mwanzo, walikuwa wakilazwa katika sakafu (chini), s u a l a l a c h a k u l a l i l ikuwa ni tatizo

Jahanam siku arobaini ndani ya Kiinua Miguu

Na Bakari Mwakangwale

kwao hali i l ikuwa ni mashaka juu ya mashaka.

“ K a t i k a s i k u h i z o M a s h e i k h hawakuruhusiwa hata kutoka nje, kama si juhudi za mawakili w e t u b a s i a m a wangepoteza maisha au kupata ki lema cha milele, ukiachilia mbali kitendo cha kunyolewa ndevu kwa nguvu”. Alisema Sheikh Kassimu.

She ikh Kass im al isema Mawaki l i hao ambao a l idai wanafanya kazi hiyo kwa ajili ya Allah (s.w) walipambana na baada ya hizo siku arobaini, hali i l ibadilika na kulegezewa masharti kisha waliruhusiwa kuonana na familia

zao na watu wengine sambamba na kupata c h a k u l a k u t o k a majumbani mwao.

Alisema suala kubwa na la kusikitisha zaidi ni pale Sheikh Mselem Bin Ally, alipozuiliwa k we n d a k u m z i k a mtoto wake baada ya kufariki wakati yeye akiwa gerezani na kueleza kwamba hiyo ni dhulma kubwa.

Sheikh Kassimu, ambaye ndiye mtendaji mkuu katika zoezi la kukusanya michango kwa ajili ya dhamana, a l isema hal i h iyo imetafsiriwa kuwa ni moja ya muendelezo w a d h u l m a k w a viongozi hao wakiwa gerezani kwani alidai mtu akiwa mahabusu

a u m f u n g w a anaruhusiwa kwenda kuzika mtu wake wa karibu.

“Haya na mengine mengi sisi tulio karibu huko tunayashuhudia ndiyo waliyoyapata siku za mwanzo baada ya kukamatwa na kuingizwa gerezani n a m w i n g i n e m m e s h u h u d i a kulazimika kwenda kutibiwa nje ya nchi.” Alisema Kassimu.

A l i t a n a b a h i s h a k u w a w a t a w a l a w a n a o s i m a m i a dhulma hizo waelewe kwamba Allah (sw) yupo na siku ya malipo ipo.

Aliwataka watawala wa sasa kujifunza kutoka kwa kiongozi

mmoja wa ngazi ya juu Zanzibar, ambaye katika utawala wake aliwafanyia dhulma kwa kuweka kizuizini viongozi wa kisiasa na sasa yanamkuta, kwani alidai Allah (s w) anaanza kumlipa hapa hapa duniani kwa dhulma alizofanya.

“Ya akhera hatujui, anajua Subhana wa taalah juu ya kiongozi huyo, mimi naamini kuwa yanayomfika sasa ni kichapo Mungu anampa hapa hapa duniani. Watawala wa sasa wajifunze kupitia kwa mtawala huyu, wanaona ni mambo ya kawaida na hawahofu kwamba yupo hakimu w a m a h a k i m u ” . Alisema Kassimu.

A l i s e m a b a a d a ya Mahakama Kuu Z a n z i b a r k u t o a masharti ya dhamana k w a M a s h e i k h w a n a o s h i k i l i w a gerezani, walikaa na kutafakari ni namna g a n i w a t a w e z a kutekeleza mashariti y a d h a m a n a n a w a k a a f i k i a n a kuwaeleza Waislamu.

Naye Sheikh Khamisi H a m a d k u t o k a Zanzibar , a l isema Masheikh waliopo gerezani wamepata changamato nyingi t o k a k u i n g i z w a gerezani ukiachilia m a d h i l a y a o binafsi , lakini pia z i p o c h a n g a m o t o zinazozikabili familia zao.

A k a w a t a k a Waislamu kutorudi nyuma katika kudai haki zao kwa kuwa M a s h e i k h w a o wapo kizuizini, bali wa e n d e l e e k u d a i haki zao na kupinga d h u l m a d h i d i ya Waislamu kwa kuwa hilo ni jukumu la kila M u i s l a m u m p a k a atakapoingia kaburini.

SHEIKH Khamis Yusuph (kushoto) anayefuata ni Sheikh Khamis Hamad wakipokea mchango kutoka kwa mmoja wa Maimamu wa Msikiti Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya dhamana ya Masheikh wa Uamsho Zanzibar.(Picha Na Bakari Mwakangwale).