annuur 1112

16
ISSN 0856 - 3861 Na. 1112 RABIUL THAN 1435, IJUMAA , FEBRUARI 14-20, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz Facebook:[email protected] Mauwaji Msikitini: Makubwa yafichuka Usiombe kuingia anga ya polisi wa ugaidi Sheikh aling’olea macho, sehemu za siri Mchezo wa danganya toto jinga waendelea JUMUIYA na Taasisi za Kiislamu (T) chini ya Ha-y-at Ulamaa, imewataka Waislamu Baraza Kuu, Ulamaa kuteuwa Makadhi Waislamu wenye taaluma ya Shariah waitwa Na Bakari Mwakangwale Profesa Jeffrey-kutoka Ukatoliki hadi Uislamu Wizara ya Elimu yatakiwa kuwa na sera ya madrasa Wito wa Maalim Seif maulidini Alabama Hazina ya maadili, historia itiliwe mkazo waliohitimu Digrii ya Sharia za Kiislamu, kuwasilisha wasifu wao (CV), ili kuingizwa katika mchakato wa kuwapata Makadhi. Akiongea na An nuur, Jumatano wiki hii, Amiri wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Alhaj Mussa Yusuph Uk. 16 Inaendelea Uk. 3 Balozi mdogo wa Marekani nchini Sudan, Joseph D. Stafford (mwenye kilemba cha kijani na picha ndogo chini) akiwa nchini Sudan. PROFESA Jeffrey Lang. Soma habari yake Uk. 6. DHULKIFLI A. Rogo. Habari Uk. 8 RAHMA Hassan mke Sheikh Said Mohammed Njiro.

Upload: zanzibariyetu

Post on 21-Oct-2015

914 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1: ANNUUR 1112

ISSN 0856 - 3861 Na. 1112 RABIUL THAN 1435, IJUMAA , FEBRUARI 14-20, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs

Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz Facebook:[email protected]

Mauwaji Msikitini: Makubwa yafichukaUsiombe kuingia anga ya polisi wa ugaidiSheikh aling’olea macho, sehemu za siriMchezo wa danganya toto jinga waendelea

JUMUIYA na Taasisi za Kiislamu (T) chini ya H a - y - a t U l a m a a , imewataka Waislamu

Baraza Kuu, Ulamaakuteuwa Makadhi

Waislamu wenye taaluma ya Shariah waitwaNa Bakari Mwakangwale

Profesa Jeffrey-kutoka Ukatoliki hadi Uislamu

Wizara ya Elimu yatakiwa kuwa na sera ya madrasa

Wito wa Maalim Seif maulidini AlabamaHazina ya maadili, historia itiliwe mkazo

w a l i o h i t i m u D i g r i i ya Sharia za Kiislamu, kuwasilisha wasifu wao (CV), ili kuingizwa katika mchakato wa kuwapata Makadhi.

Akiongea na An nuur, Jumatano wiki hii, Amiri wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Alha j Mussa Yusuph

Uk. 16

Inaendelea Uk. 3

Balozi mdogo wa Marekani nchini Sudan, Joseph D. Stafford (mwenye kilemba cha kijani na picha ndogo chini) akiwa nchini Sudan.

PROFESA Jeffrey Lang. Soma habari yake Uk. 6.

DHULKIFLI A. Rogo. Habari Uk. 8

RAHMA Hassan mke Sheikh Said Mohammed Njiro.

Page 2: ANNUUR 1112

2 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 14-20, 2014

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Makala

KUTOKANA na tafiti mbalimbali za wataalamu na wanazuoni mahiri na hata kutoka katika ndimi za mabeberu wenyewe, vita dhidi ya ugaidi ni vita bandia. Ni vita ya kupanga iliyolenga kutafuta adui ili kuhalalisha mambo kadhaa.

Tafiti hizo zinasema k u w a m a k u n d i y a kigaidi yal iundwa na asasi za mabeberu na k w a m b a h a d i s a s a yanasaidiwa na kufanywa yaendeleekuwepo na asasi hizo.

A i d h a i n a e l e z w a kuwa kundi la Al Qaeda liliundwa na mabeberu hao toka kipindi cha vita ya kiitikadi kati ya Marekani na Urusi na linaendelea kupewa misaada kwa siri.

'Vita ya kimataifa dhidi ya ugaid i ' inae lezwa kuwa ni mkakati wenye miingi l iano mingi na ya kijasusi na kwamba ni nyenzo ya kueneza ukoloni ambao unaelekeza kuhujumu mataifa huru.

Makundi ya kigaidi y a k i s h a u n d w a , hutumikishwa kat ika kuleta ghasia na machafuko katika nchi lengwa na hatimaye kuidhoofisha.

U f u p i w a m a n e n o na kwa lugha nyepesi tunafahamishwa kuwa “magaidi” ni adui wa kuundwa kuhalal isha utoaji misaada ya kikachero n a k i j e s h i , n a h i v y o kuwezesha nchi kukaliwa kijeshi na mabeberu.

Nchi ik ishaingizwa katika mchezo huu mchafu, itakuwa ikiandamwa na mashambulizi ya kigaidi kila uchao. Watu wake wakiuliwa na magaidi na polisi/jeshi la nchi nalo likiuwa watu kwa mtizamo wa kupambana na magaidi. H a l i h i i i t a k u wa ya kuendelea ili kuhalalisha wito wa kupewa msaada wa kikachero na hata jeshi.

Matokeo yake ni kuwa m n a j i k u t a , k w a n z a m n a u wa n a we n ye we kwa wenyewe. Pili, nchi inakuwa katika machafuko, hakuna maendeleo na

Vita dhidi ya ugaidi:

Tusijidharaulishe wenyewewala tusilaumu mabeberu

h a t i m a y e m n a j i k u t a mmekaliwa na mtandao wa kikachero na kijeshi kutoka kwa mabeberu. Hamfanyi jambo mpaka muelekezwe la kufanya. Rasilimali zenu zinaporwa na mnakuwa hamna kauli ila kwa yale mnayoruhusiwa kufanya.

K wa n c h i z e t u z a A f r i k a M a s h a r i k i , ukiacha Al Qaidah, hivi sasa tumeletewa adui mwingine, Al Shabab. Wote hawa ni katika ule mkakati kwamba “adui anahitajiwa kuwezesha agenda ya kijeshi ifaulu a m b a y o i n a k u wa n i kuwafuata Al Qaida na Al Shabab.”

Katika mchezo huu, tunahadaiwa ‘tunaletewa’ maga id i , wanatuuwa na kuharibu mali. Kisha tunapewa mafunzo (polisi) ya kupambana na magaidi. Tunajazwa ukati l i wa kutuwezesha kumlaza mwananchi mwenzetu kitandani na kumpiga risasi kichwani tukiwa t u m e m f u n g a p i n g u . Tunajazwa mafunzo ya kututoa ubinadamu wetu kuwa baada ya kumuua mwananchi mwenzetu asiye na hatia kwa kumpiga r i s a s i s i t a k i c h wa n i , tunakosa soni bali tunavaa u s o w a k i h a y a w a n i kumsingizia kuwa ni gaidi hatari tuliloliuwa baada ya kutushambulia kwa risasi. Alipotukosa, tukamuwahi.

H a y a n d i y o y a n a y o w a k u t a wanaotuhumiwa kwa uga id i nch in i Kenya hivi sasa. Haya ndiyo wanayofanya askari wa ATPU Kenya.

Hatima ya yote haya, ni vurugu na kuuwana Wakenya kwa Wakenya. Analohakikisha beberu ni kuwa watuhumiwa wa ugaidi hawakosekani kila uchao, na askari katili wa ATPU wanazidi kupewa mafunzo na posho zao k u p i t i a m s a a d a w a mamilioni ya dola kutoka kwa mabeberu kila mwaka.

Ya p o m a m b o m t u unaweza kufanya kwa uj inga. Lakini hi l i la

v i ta dhidi ya ugaid i lishafanyiwa kazi sana. Hakuna kiongozi wa nchi leo anaweza kuwa na udhuru wa kusema kuwa alikuwa hajui.

U k i a c h a h a y a yanayoelezwa hivi sasa juu ya Al Qaida na Al Shabab, wanaweza kurejea katika historia waone wenzao walivyofanyiwa katika nchi za Nicaragua, Guaetamala, El Salvador, Chile, Cuba na Panama. Nchi zilivurugwa ‘magaidi wa kuundwa’ wakifanya mauwaji ya

kutisha huku vikosi vya serikali navyo vikiuwa. Nchi zikawa taabani huku mabeberu wakipora mali.

Kwa nini hatujifunzi katika historia hiyo? Hivi kama tunaridhia kutumiwa kijinga na kirahisi namna hii, tunachowaeleza hao wa n a o t u t u m i a n i n i ? Ujumbe gani tunawapa? Kwamba sisi si binadamu kamili na wenye akili kama wao?

Sisi tunaamini kuwa Mungu katuumba sote katika hali ya usawa kiakili

na uwezo wa kufikiri. Ndio maana tunao maprofesa wa taaluma mbalimbali walioko Marekani na Ulaya wakisomesha katika vyuo vikuu na hata kutumikia taasisi nyeti na muhimu za nchi hizo. Kama ni kuzidiana, inatokana n a m t u m w e n y e w e anavyoitumia akili yake.

Hebu tutumie aki l i zetu vizuri tuepukane na mabalaa haya ya kuletwa na binadamu wenzetu kwa tamaa zao za kupora na

SHUKRANI zote anastahiki Mwenyezi Mungu ambaye amemuumba Binadamu na akamfundisha ubainifu (Uwazi) na akainyanyua mbingu na akaweka mizani.

Ama baada ya utangulizi huu mfupi, kwa hakika u l i m we n g u u m e u we k a Uislamu kwenye mizani ili wauhukumu lakini mizani i n a t o f a u t i a n a n a k a u l i zinazogongana tunaikuta hukumu juu ya Uislamu ni kinyume na ni kuuludhumu na ni kuvuka mipaka ya haki. Uhakika wa mambo ya Dini ya Kiislamu imeepukana na hayo yote. Kwani dini ya Kiislamu ni Dini ya Amani na Usalama Dini ya upole na utulivu. Dini ya ukati na kati, uwastani na uadilifu (Usawa) na Dini iliyompa kila mtu haki yake na ni Dini ya kimaumbile ya binadamu na Dini nyepesi na tabia njema na mwenendo mzuri. Na wenye kudhibitika na ni Dini ya Elimu na utamaduni na bidii na kufanya kazi na ni Dini ya maendeleo na ni Dini ya ushindi na utukufu na ni dini ya afya na usafi. Nayo ndio Dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na ni Dini ya kila nabii na mitume (a.s)

SUALI moja ninajiuliza mimi Mwenyewe, kwanini dini hii tukufu inatuhumiwa kwa tuhuma hizi zote ambazo ni uongo mtupu?

NA JIBU: Kwa hakika wao sababu na wao kuuweka Uis lamu kat ika mizani mbovu na ya dhuluma kwani baadhi yao wana uhukumu Uislamu kwa kuwatazama baadhi ya “Waislamu ambao wanajinasibisha na Dini hii

Na Dr. Ahmed Abdulatif

Uislamu katika mizanikatika zama hizi wakawakuta baadhi yao watu wa dhuluma wengine masikini wengine wanatengana na wengine maadui na wengine wanatisha kwa tabia zao za kinyama isipokuwa waliorehemewa ujinga tu walionao kwamba dini yao ya Kiislamu ndio sababu ya hayo yote.

Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, Uislamu yaliyotajwa katika matusi yao kwa yale wanayoyaona kwa baadhi ya hali ya waumini wake kwani hawa wanakwenda kinyume na mafunzo ya U i s l a m u n a wa m e a c h a vyanzo vya Diini na misingi yake na hawakuyafanyia kazi kwa upande wa maisha yao na muamala wao wengine wanauweka Uislamu katika m i z a n i ya u p a n d e wa ugaidi pale walipowaona wa n a o l i u n g a h i l o k wa ujinga wao upande wa Dini pamoja na kujinasibisha na Dini hiyo kwa ujinga wao wanajiingiza katika kazi ya ugaidi kwa kuwaua wasio na hatia wala makosa. Kwa wanayoyafanya watu hawa makosa watu hawa kwani Uislamu unaamrisha Amani amesema Mwenyezi Mungu “Enyi mlioamini ingieni katika sheria za Uislamu zote na wala msifuate nyayo za shetani kwani yeye kwenu ni adui wawazi.” Surat Al-Bakarat aya ya (208).

Na miongoni mwao wapo wanaochuma makosa ya makusudi na kuuzushia Uislamu hayo yote kwa dhuluma na kwa uadui kama kwamba wanataka kuizibia njia ya Mwenyezi Mungu na wakaweka ushahidi juu ya madai yao kwamba Uislamu unahimiza jihadi pale unapofanyiwa uadui kwa kuchukua dalili kauli yake Mwenyezi Mungu “Na atakayekufanyieni uadui, basi wafanyieni uadui.” Al-bakarat (194)

Na tunajiuliza na kukaa pembeni ni kujibu uadui? Na ajabu jambo hilo lakini sisi tunajisifu kwa kuwa dini yetu inatuamrisha tulipize Uadui

vile vile na hii nikuonyesha wazi uadilifu na utukufu wa dini hii amesema Mwenyezi Mungu “(na piganeni katika njia ya Mwenyezi Mungu wale ambao wanaopigeni nyinyi na wala msivuke mipaka hakika mwenyezi Mungu hawapendi wavukao mipAka).” Surat Al-bakarat aya ya (190)

Jee, hapo kuna ugaidi? Bali wengine wanaotaka kujibu uadui kwa kuuweka Uislamu kwenye ncha ya ugaidi basi mizani yao imegeuka kwani magaidi ni wale ambao wanaovuka mipaka duniani kwa kuzifanyia uadu ardhi nafsi na rasilimali bila ya haki.

N a m i o n g o n i m wa o wapo wanaoiga ambao wanawasikiliza wanaoutaka Uislamu bila ya kuilazimisha nafsi yake kutafuta uhakika wa Uislamu na wanakiri na kujitambulisha kutokana na vyanzo vya asili na wala hawazigeukii kauli za wana chuoni wasio Waislamu katika Elimu nyingi na matunda ya elimu toka katika Qur – ani na suna na wanatosheka na wanayoyasikia toka kwa wanaotukana dini wale ambao wana malengo yao na maslahi katika kuupakazia Uislamu mabaya.

Bali hakika Dini ya Uislamu nayo ni Dini ambao amekuja nayo nabii wote nabii Nuhu amesema (Na nimeamrishwa n i w e m i o n g o n i m w a Wais lamu) na Ibahimu amesema (nimenyeyekea kwa Mola wa Ulimwengu) amesema Nabii Yakubu kuwambia watoto wake (hakika Mweneyezi Mungu amekuchagulieni Dini musife isipokuwa mufe Waislamu) amesema Suleimani (na nijilieni mimi Waislamu) na Issa (Wamesema (na shuhudilieni kwamba mimi ni Muislamu) na akasema Mussa (na kwa Mwenyezi Mungu tegemeeni ikiwa nyinyi ni Waislamu) na aya nyingine za Qur-an zinashuhudia juu ya hilo.

Mwenyezi Mungu ndiye muwezeshaji.

Page 3: ANNUUR 1112

3 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 14-20, 2014Habari

KUNA mfuko wa Rais Bush wa Kupambana na Ugaidi Afrika Mashariki (President Bush’s East African Counter-t e r r o r i s m I n i t i a t i v e ) . Pia kuna Scholarship za Balozi kwa wasichana (The Ambassador’s Girls’ Scholarship Program) . U s i s a h a h u p i a M f u k o wa elimu Afrika (African education initiative).

Unajua misaada na mifuko hii inavyowaathiri Waislamu na Dini yao? Wanazitumia pesa hizo kuwasomeshea Waal imu wa Ki i s lamu, kuandaa mitaala na vitabu, kuwalipa mishahara waalimu, na viongozi wa jamii, na kusaidia pia kipesa watoto wa masikini. Wameanzisha pia Kituo cha Vitabu vya rejea vya madrasa Zanzibar (The Zanzibar Madrasa Resource Centre). Misaada hiyo Marekani kwa kupitia mradi wa MKEZA (Mradi wa Kuendeleza Elimu Zanzibar) imekwisha kujenga madrasa 16 (mpaka mwaka 2007) m o j a ya m a d r a s a h i z o aliyotembelea mke wa Bush, Laura, Julai 2005. Na kwa mujibu wa USAID wenyewe M a r e k a n i n i wa f a d h i l i wakubwa kwenye nyanda ya elimu huko Zanzibar.

Kwa upande wa Tanzania bara, USAID kwa kushirikiana na BAKWATA wametoa kitabu cha Mwongozo wa kufundishia walimu wa Kiislamu. USAID pia imetoa mafunzo kwa walimu 54 wa madrasa ya kuwafundisha watoto wa Kiislamu namna ya kupambana na UKIMWI. Mwongozo huo wa vitabu 2,500 uligawanywa kwa walimu wa madarasa Dar es Salaam na Iringa. (Taarifa hizi zote zimepatikana kutoka katika tovuti ya USAID/

Baraza Kuu, Ulamaa kuteuwa MakadhiInatoka Uk. 1K u n d e c h a , a m e s e m a mchakato huo utawahusu Makadhi watakaofanya kazi chini ya Jumuiya na Taasisi za Kiialamu.

“Tunawaomba wale wote waliohitimu masomo ya Shariya (Digrii ya Sharia) katika vyuo mbalimbali kuwasilisha vyeti na wasifu (CV) katika Ofisi za Baraza Kuu na Ha-y-at, wakati tukielekea katika mchakato wa kuanzisha vituo vya Kadhi kwa mujibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu”. Amesema Amir Kundecha.

Alisema, hatua hiyo imefikiwa katika kikao k i l i c h o wa k u t a n i s h a viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu pamoja na wale wa Ha-y-at Ulamaa, Jumamosi ya wiki iliyopita Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Amir Kundecha, alisema kwamba baada ya zoezi la kupokea wasifu wa wanataaluma hao katika fani ya Sharia ya Kiislamu, watawaita tayari kwa usaili (Interview).

Alisema, zoezi hilo la kupokea wasifu kutoka kwa Waislamu litakoma

Februari 28, 2014, hivyo aliwataka wale wote wenye sifa na vigezo vinavyo kidhi haja kuwahi kuwasiolisha vyeti vyao katika ofisi za Hay-at Ulamaa na Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T).

Al i sema, wamef ika maamuzi hayo kutokana n a k wa m b a S e r i k a l i i m e s h a w a r u h u s u Waislamu kuendelea na zoezi hilo katika Taasisi zao juu ya jambo hilo.

K w a m a a n a h i y o Amir Kundecha, alisema wanaimani kwamba hata Ofisi za Ha-y-at na Baraza

Kuu nazo pia zinawajibika kuwa na jambo la namna hiyo, kwani aliongeza kusema huduma hiyo inatakiwa itolewe kwa kiwango cha kutosha na haitoshi kuwa katika eneo moja tu.

A m i r K u n d e c h a , alifafanua kuwa kwa muda wote huo tokea Serikali itoe amri hiyo, walikuwa k a t i k a m c h a k a t o wa kujipanga kwa kuandaa Ofisi na vituo katika Mikoa na Wilaya, jambo ambalo tayari limekamilika na hatua inayofuata ni kutafuta wenye sifa na

watakaokidhi haja katika taaluma hiyo.

“Sasa kinachofuata ni kutafuta Makadhi katika utaratibu unaokubalika kisheria kasha tutafanya nao semina tayari kwa kuanza kazi rasmi kwa mujibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiis lamu”. Alisema.

Alisema, zoezi hi lo litasimamiwa na Msheikh kutoka Hay-at Ulamaa k a t i k a m c h a k a t o wa k u wa c h u j a M a k a d h i hao, ambao watakuwa wakifanya kazi chini ya Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T).

Tunavurugwa bila kujuaNa Hassan Kombo

Tanzania).Kwa mujibu wa hotuba ya

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali (SMZ) kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa mwaka wa fedha 2013/2014: Elimu ya madrasa na vyuo vya Quran

Anasema, “Mheshimiwa Spika, Idara hii inashughulikia jumla ya madrasa/vyuo vya Kur- ani 2,251. Aidha zipo skuli za maandalizi za madrasa 84, Unguja na Pemba zinazosimamiwa na kuhudumiwa kupitia Kituo cha Zanzibar Madrasa Resource Centre (ZMRC), ambazo ufundishaji wake unafuata misingi ya dini ya Kiislamu.”

“Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Wizara kwa kushirikiana na Shirika la UNICEF inakusudia kutoa mafunzo kwa walimu wa madrasa/vyuo vya Kur-ani 350, Unguja 200 na Pemba 150. Pia itaendelea kufanya ziara mbali mbali za kikazi katika madrasa na vyuo vya Kur-ani pamoja na kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili p a m o j a n a k u s h a j i i s h a kufanya ziara za pamoja za kubadilishana uzoefu.”

Je, unadhani watu hawa, wafadhi l i hawa kutoka Marekani, wana jema lolote kwa misaada yao hii kwa madrasa zetu?

Wakoloni wa Kiingereza n a m a e n e o m e n g i n e o h a wa k u k a t a t a m a a n a k u w a a c h i a Wa i s l a m u w a e n d e l e e k u j i t a w a l a wenyewe katika maeneo yao wala hawakukusanya misahafu na kuitia moto, bali waliweka mikakati ya

kuitoa Qur’an katika maisha ya Waislamu. Waliweka Mitaala katika mifumo yao ya elimu iliyo wahakikishia kuwa k izaz i k i takacho elimishwa kupitia mitaala hiyo kitatoa Waislamu wengi wasio na haja hata ya kuisoma Qur’an, wachache watakao penda kuisoma wasielewe, watakaoielewa wasiingize katika maisha yao ya jamii bali iishie katika kuiendea kwenye ibada maalumu za swala, zakat, swaumu hija nk.k na wale wachache watakaoingiza Qur’an katika maisha ya jamii wapigwe vita na kusalitiswa na Waislamu wenzao na kuitwa wazushi, siasa kali, magaidi n.k.

Kwa marejeo haya ya historia itoshe kuona kuwa hali waliyonayo Waislamu, takribani ulimwenguni kote, katika suala la kuiendea Qur’an sio jambo lililotokea kwa bahati nasibu, bali ni mikakati ya makusudi i l iyofanywa na nchi za kitwaaghuut katika harakati za kuitawala dunia kinyume na Mwongozo wa Allah (Subhaanahu wa Ta’ala).

Matatizo yote tuliyokuwa nayo tumeyapata baadaya kuiacha Qur’an na kuwafuata maadui zetu (Matwaaghuut) na “hawaa” za nafsi zetu. Iweje leo tuweze kuwa na matatizo hali kuwa tunao muongozo wa kutuwezesha kupata suluhisho la matatizo yetu, ni baada ya kuiacha kuingiza Qur’ani katika mfumo wa maisha yetu.

A m e s e m a M we n y e z i Mungu,

“Kwa hakika wanayo yakataa mawaidha haya yanapo wajia (wataangamia), na haya bila ya shaka ni Kitabu

chenye nguvu na utukufu” (Fuss'ilat 41:41)

“Hautakifikia upotovu mbele yake wala nyuma yake. Kimeteremshwa na Mwenye hikima, Msifiwa” (Fuss'ilat 41:42)

Hii Qur’an tumeletewa ili tuweze kuisoma kwa kuizingatia na kuitekeleza kwa kile ambacho imetuelekeza.

Amesema Allah (Sw),“ N a h i k i K i t a b u ,

tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili.” ( S’aad 38:29)

“Ama mimi nimeamrishwa nimuabudu Mola Mlezi wa mji huu aliye ufanya ni mtakatifu; na ni vyake Yeye tu vitu vyote. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu, wenye kunyenyekea.”(Naml 27:91 )

“Na niisome Qur'ani. Na mwenye kuongoka, basi ameongoka kwa faida ya nafsi yake; na aliye potea - basi sema: Hakika mimi ni miongoni mwa waonyaji.” .(Naml 27:92 )

Kwa kutoifuata Qur’an na kuwafuata matwaaghuut na “Hawaa” za nafsi zetu, Wais lamu ndio sababu inayotufanya kuweza kupata tabu na mateso katika mfumo mzima wa maisha yetu ya kibinafsi na kijamii, na hili ni angalizo ambalo tumepewa kwenye Qur’an.

Amesema Allaah (Sw):“Akasema: Ondokeni

humu nyote, hali ya kuwa ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Na ukikufikieni uwongofu kutoka kwangu basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika” (Ta’Ha 20:123)

“Na atakaye jiepusha na

mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu. ” (Ta’Ha 20:124)

Amesema Allah (Sw):“ N a M t u m e a l i k u wa

akisema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wameifanya hii Qur'ani ni kihame.” (Al Furqan25:30)

Baadhi ya maswahaba wal i shanga au kuul iza vipi wameihama (Kuipa mgongo) Qur’an hali yakuwa wanaisoma?

Alisema Mtume (Saw) “…Umekuwa mzigo kwa mama yako ewe! Ziad, nilikuwa ninakuona kuwa ni mtu mwenye ufahamu zaidi katika Maddina (Je, Nyinyi sio kama)… Mayahud na Manasara ambao mkononi mwao wana Tourati na Injili wala hawanufaiki navyo nachochote.” (Ahmad)

Kwahivyo pamoja na kuwa nayo Qur’an lakini hatunufaiki nayo kibinafsi wala kijamii, kama sawa na Mayahud na Manasara.

K a t i k a h a l i h a l i s i tuliyo nayo viongozi wa kitwaaghuut ambao hawana ufunuo kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) ndio ambao ambao wanaotuundia mfumo wa maisha yetu vile wao wanavyoataka tuwe.

P a m o j a n a k w a m b a matwaaghuut wana mchango mkubwa wa kutufanya tuweze kuipa mgongo Qur’an, lakini sisi wenyewe kwa sehemu kubwa pia tunao mchango wetu kwa kufuata “hawaa” za nafsi zetu kwa kuisaliti Qur’an. Hivyo inatupasa kujiuza na kupatia majibu mambo yafuatayo;

Je, pale tunapoisoma au kuisikiliza Qur’an kwenye swala nk. Tunakuwa tupo hadhiri na kufahamu kile

Inaendelea Uk. 7

Page 4: ANNUUR 1112

4 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 14-20, 2014Makala

AMA kweli Mwenyezi Mungu humjaalia amtakaye neema zake, kwa vigezo a m ba vy o ni s i r i ya ke mwenyewe muumba.

Wakati mwingine utajiri si kwa uhodari, akili nyingi au ujanja wa mtu, bali ni kwa hiari yake mwenyewe Allah (sw).

Hata hivyo lililo dhahiri k wa m wa n a d a m u k wa mujibu wa mafundisho ya Mwenyezi Mungi, ni kwamba utajiri au ukwasi, ni mtihani mkubwa kwa mwanadamu.

Kwamba rizki za watu wengine kwa namna moja au nyingine, zimehifadhiwa ndani ya utajiri wa mtu.

Hata hivyo, rizki na haki za wengine zilizohifadhiwa kwa mkwasi , z inaweza z i k a p a t i k a n a i w a p o aliyepewa dhamana hiyo n a M we n ye z i M u n g u , atatambua hadhi ya aliyempa utajiri huo, yaani Mwenyezi Mungu, akawa mwadilifu na mwenye busara katika kuutendea haki ukwasi aliojaaliwa, ili na wengine waweze kupata rizki zao wal izopangiwa kupit ia ukwasi huo.

K i n y u m e c h a t a j i r i kushindwa kufanya uadilifu katika mali yake, basi ni kuangukia katika majaribu na mi t ihan i mikubwa, ikiongozwa na kibri, fahari, israafu, ria, dhulma, dharau nk.

Alhaj Aliko Dangote, alizaliwa April 10, 1957 katika jimbo la Kano lililopo Kaskazini mwa Nigeria.

Dkt. Dangote ambaye maskani yake yapo jijini Lagos, alipata taaluma ya biashara katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar cha jijini Cairo nchini Misri.

Kwa sasa ndiye mmiliki, Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Dangote Group.

Inaelezwa kwamba utajiri wa Dkt . Dangote hadi kufikia Novemba mwaka jana (2013) ulikuwa ni dola za Kimarekani bilioni 20.8, kiasi kilichomfanya kuwa tajiri namba moja Afrika kwa muda wa miaka mitatu mfululizo, kwa mujibu wa jarida maarufu la Fobes.

Alhaj Dangote ni mtoto wa mzee Mohammed Dangote na mama Mariya Sanusi Dantata.

Amelelewa na wazazi wake katika maadili kamili ya Kiislamu. Familia ya Dangote ni miongoni mwa familia zilizokuwa na uwezo huko Kano.

Kampuni ya Dangote Group iliyoanzishwa mwaka 1977, shughuli zake zikiwa ni kuuza bidhaa mbalimbali nchini Nigeria, hususan bidhaa za vyakula.

Leo kampuni hiyo si ya kuuza bidhaa tu, bali ni kampuni inayomiliki

Mkwasi namba moja Afrika Alhaj Dkt. Aliko Dangote

Utajiri ulianza kwa kuuza pipi

Na Shaban Rajab

na kuendesha viwanda vya kutengeneza bidhaa mbalimbali katika nchi kadhaa za Afrika, hususan k a t i k a n c h i z a B e n i n , Cameroon, Togo, Ghana, Afrika Kusini na Zambia.

Alhaji Dangote, ambaye mwaka jana alizuru nchini, hivi sasa kampuni yake ndiyo inajenga kiwanda kikubwa cha saruji nchini mkoani Mtwara, kiwanda ambacho kitakuwa kikubwa zaidi cha kuzalisha saruji kwa Afrika Mashariki na Kati.

Kwa mujibu wa viwango vya utajiri vya jarida la Forbes, Dangote anashika nafasi ya kwanza ya utajiri barani Afrika huku akiwa tajiri wa 43 katika matajiri wakubwa kabisa duniani.

Tangu awali akiwa kijana mdogo kabisa, inaelezwa kwamba Alhaj Dangote a l i k u wa n a m v u t o wa kibiashara. Labda kutokana na historia ya wazazi wake kuwa watu wa biashara.

Mwenyewe alinukuliwa na gazeti la The Nation la Nigeria akisema, "I can remember when I was in primary school, I would go and buy cartons of sweets

and I would start selling them just to make money. I was so interested in business, even at that time."

Yaani anasema, “Naweza kukukumbuka nilipokuwa nasoma shule ya msingi, nilimudu kununua katoni ya pipi na kuanza kuziuza ilimradi tu nipate pesa. Nilikuwa ninavutiwa sana na kufanya biashara tangu kipindi hicho”.

Baada ya kumaliza shahada yake ya biashara katika chuo kikuu cha Al-Azhar Cairo, Misri, alirejea nyumbani Nigeria na kuomba mkopo kutoka kwa mjomba wake aliyeitwa Sanusi Abdulkadir Dantata. Naye alimpatia mtoto wa dada yake huyo kiasi cha fedha za Nigeria Naira 500,000 na kuanza shughuli za biashara, wakati huo Dangote alikuwa na umri wa miaka 21.

Kwa sasa Dangote Group imepanua zaidi shughuli zake za biashara kuanzaia viwanda vya kusindika vyakula (food processing), kutengeneza saruji, kusafirisha shehena (freights) , kutengeneza n a k u s a m b a z a s u k a r i , kutengeneza na kusambaza

vinywaji baridi, mikate, biashara ya mafuta na gesi, usafirishaji wafanyakazi huko Nigeria nk.

Kwa ujumla kampuni hiyo inashika karibu asilimia 70 ya soko la bidhaa na huduma zake nchini Nigeria.

Inaelezwa kuwa Dangote Group ndio kampuni kubwa zaidi ya kutengeneza na k u s a m b a z a b i d h a a z a vyakula bara la Afrika na inashika nafasi ya tatu katika huduma hizo kwa dunia nzima, ikizalisha jumla ya tani 800,000 za sukari kila mwaka.

Mbali na hilo Dangote Group inamiliki viwanda vya kutengeneza chumvi, unga na ndio kampuni kubwa ya kuingiza mchele, samaki, tambi, mbolea na saruji nchini Nigeria.

K a m p u n i h i y o p i a husafirisha pamba, korosho, cocoa, mbegu za sesame, tangawizi katika nchi kadhaa za nje.

Pia kampuni imewekeza katika sekta ya fedha na ardhi na viwanda vya nguo. Kampuni yake imeaj ir i watu 11,000 na kuifanya kuwa kampuni iliyoajiri

watu wengi zaidi Afrika Magharibi.

Pamoja na kujishughulisha n a b i a s h a r a h i z o , p i a k a m p u n i y a D a n g o t e imeingia katika biashara ya sekata ya mawasiliano na imeshaanza ujenzi wa njia za mawasiliano (fibre optic cables) kilometa 14,000 ili kukidhi mawasiliano kwa nchi nzima ya Nigeria.

Matokeo yake, Dangote Group ilitunukiwa tuzo Januari 2009 kwa kuongoza kwa kutoa ajira katika sekta ya ujenzi nchini Nigeria.

"Let me tell you this and I want to really emphasize it...nothing is going to help Niger ia l ike Niger ians bringing back their money. If you give me $5 billion today, I will invest everything here in Nigeria. Let us put our heads together and work."

Amenukuliwa akisema Alhaj Dangote, akisisitiza falsafa yake kuwekeza zaidi nchini mwake na kuwataka Wanigeria kuingiza zaidi mita j i nchini humo na kushirikiana kufanya kazi pamoja.

Itakumbukwa 23 Mei 2010, gazeti la Daily Mirror la Uingereza liliripoti kuwa Alhaji Dangote alikuwa akitaka kununua asilimia 16 za hisa za klabu ya soka ya Arsenal z i l izokuwa zinamilikiwa na Lady Nina Bracewell-Smith.

Hata hivyo Alhaji Dangote alikana tetesi hizo.

Novemba 14, 2011, Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan alimtunukiwa Alhaj tuzo maarufu heshma ya juu nchini Nigeria ya Grand Commander of the Order of the Niger (GCON).

Alhaj Dangote amekuwa akijitolea sehemu ya mali yake kusadia wasiojiweza, waliothiriwa na majanga kama mafuriko, ukame nk.

A i d h a i m e k u w a i k i r i p o t i w a k w a m b a amekuwa kishiriki katika hafla za kugawa zaka nchini Nigeria.

Hata hivyo kuna mashaka iwapo mali yake inatolewa zaka kama inavyotakikana, maana hata hapa kwetu hatujawahi kusikia wakwasi wakishiriki katika kutoa zaka kwa kiasi cha mali zao, zaidi ya misaada isiyokidhi katika jamii, hususan siku za Ijumaa.

A i d h a k u n a h a j a ya Taasisi za Kiislamu zinazoaminika, kuwa na utaratibu rasmi wa k u t o a z a k a , a m b a o u t a wa s h i r i k i s h a p i a wa k wa s i i l i k u f i k i a malengo yanayotakikana.

Tukirejea katika enzi za Khal i fa Umar (ra) kuhusu suala la zaka, hakika tutafika pale kila Muislamu anapopatamani kuf ika, kuikomboa jami ya Kiislamu dhidi ya umaskini na ufukara.

Alhaj Dkt. Aliko Dangote,

Page 5: ANNUUR 1112

5 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 14-20, 2014Habari za Kimataifa

BANGUIMashirika ya kutoa misaada Jamhuri ya Afrika ya Kati yameonya kuwa endapo Waislamu nchini humo wataendelea kulihama taifa hilo, njaa itawamaliza raia wa Taifa hilo.

Taarifa kutoka Bangui zinaeleza kwamba tayari m a s o k o n c h i n i h u m o yameanza kuwa matupu na bidhaa za vyakula kuwa haba.

M a s h i r i k a ya k u t o a misaada ya Oxfam na lile la Action Against Hunger, yamesema kuwa ni chini ya maduka kumi ya jumla ndiyo yaliyosalia katika mji mkuu wa nchi hiyo huku wafanyabiashara wengi wakiendelea kutoroka taifa hilo.

U m o j a w a M a t a i f a umekadiria kwamba watu milioni 1.3, ikiwa ni zaidi ya robo ya idadi ya watu nchini humo wanahitaji msaada wa haraka wa chakula kufuatia machafuko ambayo jamii ya kimataifa nayo imeonekana kushindwa kudhibiti hali na wafanyabiashara wakiwa wameondoka na biashara zao.

I m m e e l e z w a k u w a Waislamu ndio wanaomiliki sehemu kubwa ya biashara katika nchi hiyo kutoka nchi za jirani, na ndio ambao wamekuwa wakisambaza huduma muhimu za bidhaa za vyakula kama sukari, unga wa mahindi na ngano, sabuni, mafuta ya kupikia na vitoweo kwa watu zaidi ya 800,000 wa mji wa Bangui na miji mingine nchini humo.

Bei za bidhaa za vyakula zimepanda kwa asilimia ishirini tangu Novemba, huku bei ya nyama ikiwa imepanda zaidi ya mara mbili ya bei iliyokuwepo awali kufuatia wafugaji kukimbilia porini na mifugo yao.

Katika soko la Petevo, lililopo karibu na ukingo wa mto Oubangui Kusini m w a m j i w a B a n g u i , limebaki tupu huku huduma ya kitoweo ikififia tangu kuondoka Waislamu, ambao ndio waliokuwa wanamiliki biashara za mifugo kutoka Chad.

I m e e l e z w a k w a m b a kitoweo pekee kilichopo ni nyama ya nguruwe ambayo ni kidogo sana kutokana na nguruwe kufugwa kwa uchache na wenyeji.

Kwa sasa kuna upungufu m k u b w a w a n y a m a k w a s a b a b u w a f u g a j i wamekimbilia msituni na wakati wanapochinja mifugo yao, bei huwa ghali sana.

“Tuna mashaka makubwa sana kwasababu iwapo upungufu huu utaendelea kidogo tu, tutakufa kwa njaa,” alinukuliwa akisema

Kuondoka Waislamu Afrika ya Kati kwaleta njaa N a d e g e K o d o , m a m a aliyekuwa akitafuta bidhaa za nyumbani.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la Oxfam na Action Contre la Faim, usambazaji wa b i d h a a z a m a j u m b a n i B a n g u i k u t o k a k w a wafanyabiashara wakubwa wa jumla ambao walikuwa wakiingiza bidhaa nchini humo, umepungua sana kufuatia wafanyabiashara hao kuondoka na inakisiwa w a m e b a k i k u m i t u , ambao muda wowote nao wataondoka iwapo hali ya usalama haitaimarishwa.

“Tayari kuna uhaba mkubwa wa chakula Jamhuri ya Afrika ya Kati na hali inatarajiwa kuendela kuwa mbaya zaidi,” alisema Steve Cockburn, Meneja wa Kanda wa Oxfam.

K u f u a t i a h a l i h i y o , mashirika hayo yameonya kuwa chakula kinapungua kwa kiasi kubwa nchini humo na kwamba bei za vyakula huenda zikapanda mara dufu na kuna uhaba mkubwa.

U m o j a w a M a t a i f a unakadiria kuwa zaidi ya asilimia tisini ya raia wa nchi hiyo, wanaishi kwa kula mlo mmoja kwa siku na kwamba hali hiyo huenda ikawa mbaya zaidi.

“Shirika la World Food Programme lina malori 27 yaliyobeba mahindi na mchele lakini yamekwama katika mpaka wa Cameroon huku madereva wakikataa kuendelea na safari.

Sasa shirika hilo linapanga kusafirisha kwa ndege tani 90 za chakula kwa siku kutoka Cameroon mwezi ujao na gharama yake ikiwa ni zaidi ya mara tano ya gharama ya kusafirisha kwa malori. Hatuna namna nyingine," alisema mfanyakazi mmoja wa WFP, Alexis Masciarelli.

Taifa hilo limegawanyika zaidi kufuatia vita vilivyoanza mwaka uliopita kati ya Wakristo ambao ni wengi nchini humo na Waislamu kufuatia mapinduzi ya serikali.

Maelfu ya Waislamu tayari wametoroka nchini humo na kutafuta hifadhi katika mataifa jirani ya Cameroon na Chad.

W a i s l a m u w e n g i waliofukuzwa na Wakristo wal ikuwa wakichangia s e h e m u k u b wa k a t i k a uchumi wa taifa hilo.

U m o j a w a M a t a i f a u m e s e m a k u wa i k i wa imesalia chini ya mwezi mmoja kabla ya msimu wa kilimo, zaidi ya asilimia tisini na sita ya wakulima hawana mbegu.

Ghasia zinazoendelea zimezuia vyakula kuingizwa nchini humo na r ipot i

zinasema kuwa mamia ya malori yaliyosheheni chakula yamekwama katika mpakani mwa nchi hiyo na Cameroon, kwa sababu madereva wengi ambao ni Waislamu, wana wasiwasi wa kushambuliwa.

Shirika hilo la Oxfam, limesema kuwa endapo raia waliosalia hawatapewa ulinzi wa kutosha, hali nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati huenda ikawa mbaya zaidi.

Shirika la Medecins Sans Frontiers (MSF) limesema siku za hivi karibuni limewatibu watu 100 majeraha ya risasi na mapanga katika kambi iliyopo jirani na uwanja wa ndege wa Bangui ambako kuna wakimbizi 100,000.

“Watu wanakuja hapa bila pua, masikio, chuchu,” al isema Lindis Hurum, msimamizi miradi wa MSF

Mahakama ya Kimataifa

ya Makosa ya Jinai ilisema Ijumaa iliyopita kwamba i n a k u s u d i a k u f u n g u a mashataka ya awali kutokana na kuwepo uwezekano mkubwa wa makosa ya kivita katika machafuko hayo.

U m o j a w a M a t a i f a umesema kuwa zaidi ya watu 2,000 wameuliwa na zaidi ya elfu 800,000 wamekimbia nchi, huku nusu ya watu hao wakitoka mji wa Bangui.

KHARTOUMBalozi mdogo wa Marekani nchini Sudan, Joseph D. Stafford, amefutwa kazi ghafla mara tu baada ya kusilimu na kuingia katika dini tukufu ya Kiislamu.

H a t a h i v y o m s e m a j i wa ubalozi wa Marekani mjini Khartoum, amedai kuwa balozi huyo aliamua kujiuzulu yeye mwenyewe na kuachia nyadhifa zote za kisiasa.

Habari zilizochapishwa na World Bulletin, zimeeleza kuwa Bw. Joseph D Stafford, alijiuzulu nafasi yake baada ya kuamua kusilimu na kuwa Muislamu.

Lakini vyanzo vya vyombo vya habari nchini Sudan vimesema kuwa Balozi huyo wa Marekani alilazimishwa kujiuzulu baada tu baada ya kubainika taarifa zake za kusilimu.

S t a f f o r d m w e n y e w e ameieleza Idara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuwa a m e a m u a k u j i u z u l u kwasababu zake binafsi, lakini vyanzo vya habari nchini Sudan vimedai kuwa balozi huyo alilazimishwa kujiuzulu baada ya kuamua

Marekani yamtimua balozi baada ya kusilimu

kusilimu.Vyanzio hiyo vilibainisha

k wa m b a B w . S t a f f o r d alikuwa akirekodiwa kila al ipokuwa anatembelea Makao Makuu ya Ansar al-Sunnah nchini Sudan, ziara ambazo ziliweza kuanzisha uhusiano wa karibu na idadi

kubwa ya viongozi wa dini ya Kiislamu kufuatia ziara za mara kwa mara za balozi huyo.

I d a r a ya M a m b o ya Nje ya Marekani haijatoa maelelzo yeyote kuthibitisha ama kukanusha habari za kusilimu na kuacha kazi Bw. Joseph Stafford.

Mara baada ya kujiuzulu, Bw. Stafford aliandika habari katika jarida la Sudan Tribune akisema, "Mke wangu na mimi tumekuwa na bahati ya kukutana na watu wengi wazuri hapa Sudan, ambao tulikuwa na nia na lengo muhimu la kuimaridha jamii zao.

“Siku zote tutawakumbuka na nchi yenu nzuri , na natambua kuwa mtaendelea kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kufikia maisha bora, kama mnavyosema kila siku 'Fi Kulu Harakah Baraka' kila hatua ina Baraka zake.”

M a r e k a n i h a i j a wa h i kuteua balozi kamili katika Ubalozi wake wa Khartoum nchini Sudan tangu mwaka 1998 na kwa muda wote huo, shughuli zote za kibalozi n c h i n i h u m o z i l i k u wa zikisimamiwa na balozi mdogo (charge d’affaires).

Aliyekuwa Balozi mdogo wa Marekani nchini Sudan, Joseph D. Stafford.

WAISLAMU nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wakihama nchi hiyo kuelekea nchi jirani za Chad na Cameroon.

Page 6: ANNUUR 1112

6 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 14-20, 2014Makala

“DAD, do you believe in heaven?” Hilo ni swali ambalo kijana mdogo Jeffrey siku moja alimuuliza baba yake wakati wakiwa katika matembezi na kupunga upepo ufukweni (beach).

Swali hili kwa lugha na msamiati wa Kiislamu ni sawa na kumuuliza je, unaamini kuwa kuna Pepo?

Muundo wa swal i u k i l i n g a n i s h w a n a umri wake wakati huo, ulidhihirisha jambo moja: kuwa ni mdadisi na mtu wa ‘logic’ na haikushangaza wengi alipokuja kuwa profesa wa hesabu akiwa muhadhiri katika Chuo Kikuu cha Kansas.

Dr. Jeffrey Lang ni P r o f e s a w a h e s a b u katika Chuo Kikuu cha Kansas (University of Kansas), moja ya vyuo vikuu vikubwa sana katika Marekani. Safari yake ya kutafuta dini ya haki inaanzia Januari 30, 1954, alipozaliwa katika familia ya Kikatoliki huko Bridgeport, Connecticut.

Katika miaka 18 ya kwanza ya maisha yake aliitumia katika shule za Kikatoliki (Catholic schools) , hata hivyo, masomo katika shule hizo, yalimwacha na maswali mengi badala ya kupata majibu na kwa hakika kumchanganya zaidi kuhusu dhana ya Mungu na uhusiano wake na binadamu au viumbe kwa ujumla.

“Kama kuna Mungu, na huyu Mungu ni Mungu wa upendo na mwenye h u r u m a , k w a n i n i anawaacha baadhi ya watu wanaishi maisha ya tabu hapa duniani, magonjwa, njaa na hata kuonewa na wanadamu wenzao (kama wal ivyokuwa Wa m a r e k a n i We u s i w a k i b a g u l i w a n a kuonewa na Wazungu wa Marekani). Kwa nini asituchukue tukaishi huko mbinguni tukaepukana na tabu za dunia hii? Kwa nini aumbe watu ili wataabike?”

Anasema, maswal i kama haya, yaligonga akili yake kila siku na hakupata majibu.

A n a s e m a , a k i w a sekondari-Notre Dam Boys High, alikuwa akihoji sana juu ya Mungu na wakati mwingine kukataa majawabu aliyokuwa akipewa na walimu na wachungaji akisema kuwa hayana mantiki wala hayakubaliani na akili ya

Profesa Jeffrey-kutoka Ukatoliki hadi Uislamu

Jeffrey Lang ni Profesa wa hesabu katika Chuo Kikuu cha Kansas (University of Kansas)

kawaida.Kadir i a l ivyofanya

mjadala na Mchungaji wa shule (school Priest), wazazi wake na wanafunzi wake, hawakuweza kabisa kutosheleza kiu yake ya kumjua Mungu. Kwa hiyo, kwa mshangao wa mchungaji na wazazi, akatangaza kuwa yeye sasa haamini juu ya M u n g u . Wa k a t i h u o alikuwa na umri wa miaka 18. Na akabaki hivyo kwa miaka 10. Kwa maana mpaka alipokuwa na umri wa miaka 28, alikuwa haamini juu ya kuwepo kwa Mungu wala alikuwa hashughuliki na kwenda kanisani s i Jumapil i , Krisimasi, Pasaka wala mwaka mpya.

Akiwa anafundisha katika Chuo Kikuu cha San Francisco (University of San Francisco), alikutana na mwanafunzi Muislamu a k i i t w a M a h m o u d Qandeel akiwa mmoja wa wa n a f u n z i wa k e

akiwafundisha hesabu. Alijikuta akiwa karibu sana na mwanafunzi huyu na kuwa marafiki hasa kutokana na mwenendo wake. Urafiki wa Profesa na mwanafunzi wake ukapelekea urafiki kuingia katika familia zao.

Hata hivyo, katika muda wote walipoanza urafiki wa kifamilia, kila familia hizi mbili zilipokutana, dini haikuwa kabisa moja ya mada katika mazungumzo yao. Hata hivyo, baadae kabisa familia ya Kiislamu ya mwanafunzi wake, walimzawadia Dr. Jeffrey Lang Qur’an.

Japo hakuwa na hamu ya dini, lakini akaona ngoja tu asome kama kitabu kingine chochote.

“You cannot simply read the Qur’an, not if you take it seriously. You either have surrendered to it already or you fight it. It attacks t e n a c i o u s l y , d i r e c t l y , personal ly ; i t debates , cr it ic izes , shames, and

challenges. From the outset it draws the line of battle, and I was on the other side.”

H a y o n i m a e l e z o yake baada ya kuipitia Qur’an kidogo. Anasema, ukiisoma Qur’an, utakuta ikikushambulia (kama unafanya mambo yasiyo kubalika), ikijadiliana na wewe juu ya mambo mbalimbali, ikikulaumu, ik ikupa changamoto n a n a s a h a , n a h a t a kukuaibisha kwa matendo yako.

Kwa hiyo anasema, alijikuta akiwa vitani na Qur’an. Anapambana nayo.

“ I wa s a t a s e ve r e disadvantage, for it became clear that the Author knew me better than I knew myself.”

Hata hivyo anasema kuwa alijikuta akizidiwa nguvu kwani ilielekea kana kwamba mwandishi wa Qur’an alikuwa akimjua vizuri pamoja na maswali yake yote aliyokuwa nayo kichwani.

Hivyo, kila akisoma, anakuta swali lililokuwa kichwani linajibiwa kabla hajauliza.

“The Qur’an was always way ahead of my thinking; it was erasing barriers I had built years ago and was addressing my queries. I was being led, working my way into a corner that contained only one choice.”

D r . J e f f r e y L a n g anasema, Qur’an ilikuwa muda wote imetangulia fikra na mawazo yake na kila akisoma ilikuwa ikiondoa vikwazo na kutosheleza kiu yake ya mambo yaliyokuwa yakimtatiza kwa muda mrefu. Mwisho anasema, alijikuta amewekwa katika kibano ambapo, hana jingine ila kusalimu amri. Alikuwa hana namna nyingine ila kusilimu.

Katika miaka ya 1980s, kulikuwa na Waislamu wachache sana katika K a m p a s i y a C h u o Kikuu, University of San Francisco. Wanafunzi wa c h a c h e Wa i s l a m u waliokuwa Chuoni hapo, walikuwa wakiswali swala tano katika chumba kidogo ndani ya Kanisa la Chuo. Kichumba hicho amekitaja kama “a small place at the basement of a church.”

Anasema, alijipa moyo, alipiga moyo konde, siku moja akawatembelea wanafunzi Wais lamu wakati wa swala, aliporejea tayari alikuwa ni mmoja wao. Alikuwa ametamka shahada.

Kwa mara ya kwanza aliposwali swala ya jamaa, anasema Imam alikuwa kijana akiitwa Ghassan. Akiwa kavaa kanzu na kofia, kasimama mbele peke yake, huku wengine wakiwa nyuma yake katika mistari iliyonyooka wakimfuta kila anapotoa t a k b i r a ya k u h a m a , anasema alishtuka sana.

Anasema hal i hiyo i l imkumbusha ndoto ambayo alikuwa akiiota mara kwa mara zamani wakati huo akiwa haamini kwamba kuna Mungu. A n a s e m a , a l i k u w a akiota ameingia katika chumba kidogo kuna w a t u w a m e s i m a m a katika mistari , lakini mmoja wao yupo mbele peke yake kavaa kanzu na kofia. Wengine wote wapo kimya, yeye tu ndiye anazungumza, wengine wanamsikiliza.

Anasema, ndoto hii i l ikuwa ikimjia mara kwa mara, japo akiamka alikuwa akijiuliza, nini

Inaendelea Uk. 7

Page 7: ANNUUR 1112

7 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 14-20, 2014Makala

Profesa Jeffrey-kutoka Ukatoliki hadi Uislamu

Inatoka Uk. 6maana yake, lakini mara akipuuza na kuiacha kama ilivyo.

“Hivi naota tena au nipo macho”, anasema alijuliza akiwa ndani ya swala ilipomjia ile picha ya ndoto aliyokuwa akiota zamani ikiwa sawasawa na jinsi watu walivyokuwa katika chumba kile kidogo wakiswali naye akiwa mmoja wao.

Ni kutokana na ndoto hii na historia yake kupitia kwenye Ukatoliki hadi kukanusha Mungu, Dr. Lang anasema, hawezi kusema kuwa amefanya juhudi kubwa sana kutafuta ukweli juu ya Uislamu, ila anamshukuru Mwenyezi Mungu kuwa ndiye pekee a l iyemwongoza hadi kusilimu.

Mtoto kama baba“ B a b a k w a n i n i

tunaswali (Daddy, why do we pray)?”

Hili ni swali ambalo binti wa Dr. Lang aitwaye Jameellah akiwa na miaka minane (8), siku moja alimuuliza baba yake baada ya kumaliza swala ya dhuhuri.

“Sikutarajia kuulizwa swali hili kutoka kwa mtoto wa miaka minane na kwa hiyo sikuwa na jawabu la haraka.”

Anasema Dr. Lang, hata hivyo akisema kuwa swali la binti yake huyo mdogo, linamkumbusha swali la kiudadisi kama hilo ambaye naye alimuuliza baba yake Mzee Lang. Yeye alimuuliza, “unaamini kuwepo kwa Pepo?”

Anasema, swali kama hilo la kimantiki na kitafiti, l inampa fara ja kuwa huenda binti yake huyo akawa msomi wa kiwango cha hali ya juu. Wasomi wa kiwango cha juu kabisa katika fani mbalimbali, ndio wanatakikana katika ulimwengu wa leo kufanya Da’wah na hao ndio watakaouhuisha Uislamu ukarejesha heshma yake.

Baada ya kutafakari kwa muda, a l imj ibu: “Tunaswali kwa sababu M w e n y e z i M u n g u anatutaka tuswali.”

Jameellah akauliza tena, “lakini kwa nini? Kwa nini Mungu atuamrishe kuswali? Swala ina faida gani kwetu?”

Maswali yal ikuwa mazito na uzito wake unakuwa kwamba Dr. Lang alikuwa akipata tabu ni kwa vipi na kwa maelezo gani mepesi atatumia binti yule wa umri mdogo apate

kuelewa.“Binti yangu ninaye

kupenda sana, ni vigumu kueleza kwa mtoto mdogo kama wewe ukaelewa. We endelea tu kuswali swala tano kila siku, nina uhakika itafika siku utaelewa kwa nini tunaswal i . Hata hivyo, ngoja ni jaribu kukufahamisha.”

Huku akimshika kichwa kwa upendo akasema: “’Honey’ Binti yangu, si unaona nakupenda, lakini Mungu ndiye chanzo cha upendo, huruma, ukarimu, hekma, busara na uzuri wa kila kitu kinachotuzunguka katika maisha. Kama unavyoona, jua ndio chanzo cha m w a n g a t u n a o u o n a wakati wa mchana. Lakini Mungu ndiye chanzo cha vyote hivyo na vingine usivyovijua. Kwa hiyo, upendo nilio nao kwako, kwa dada zako na kwa mama yako, unatoka kwa Mungu, ni Mungu kanipa. Tunajua kuwa Mungu ni mkarimu sana kwa kutupa yote mazuri katika maisha yetu.”

“Tunaposwali tunapata hisia za upendo wa Mungu na ukarimu wake kwetu kwa namna ya kipekee kabisa na yenye athari kubwa katika mioyo yetu.”

“Binti yangu, chukua m f a n o h u u : u n a j u a kuwa mama yako na m i m i t u n a k u p e n d a sana na tunafanya kila tuwezalo kukuhudumia, k u k u h u r u m i a n a k u k u l i n d a . L a k i n i t u n a p o k u k u m b a t i a n a k u k u b u s u , b i l a shaka unapata hisia za upendo wa hali ya juu na za ndani kabisa jinsi tunavyokupenda. Ni vivyo hivyo, tunajua Mungu anatupenda sana na ni mkarimu kwetu, lakini tunaposwali, tunapata hisia za ndani kabisa na za kipekee juu ya upendo, huruma na ukarimu wake kwetu.”

Hayo yalikuwa maelezo ya Dr. Lang kwa binti yake Jameellah aliyetaka kujua ni kwa nini tunaswali.

“Does praying make you a better daddy?” Je, swala inakufanya kuwa baba mwema zaidi, inakufanya kuwa baba mzuri zaidi (kwetu na kwa mama?) Jameellah alimuuliza tena

baba yake.Kwa ufupi maelezo

ya Dr. Lang yalikuwa k wa m b a u n a p o m j u a Mungu, ukawa unaswali, unakuwa katika nafasi ya kuona huruma ya Mungu kwako, upendo wa Mungu kwako, neema za Mungu kwako kwa hiyo ukizingatia j insi Mungu anavyokupenda na kukuhurumia, lazima nawe utakuwa na huruma kwa binadamu wenzako ukianzia na watu wa familia yako. Lazima utataka ile huruma ya Mungu kwako nawe umfanyie mkeo na watoto wako.

“ U m e n i e l e w a Jameellah? Je, mimi si baba mwema kwako?”

Jibu la Jameellah lilikuwa kumkumbatia baba yake na kumwambia: “I love you, Daddy! (nakupenda baba yangu.)”

“I love you too, sweetie pie. I love you too.” Alijibu Dr. Jeffrey Lang kurejesha jawabu la upendo kwa binti yake.

Baada ya kusi l imu Dr . Lang ana j i tahidi kufuata Uislamu kama unavyoagiza. Anaswali swala tano na anasema, hakuna sakina, utulivu wa nafsi, burudani na faraja anayopata kama ile anayopata akiswali na kusoma Qur’an.

Anasema, hata asiyejua tafsiri ya Qur’an, akiisoma kwa imani na kwa utulivu, naye hupata utul ivu na sakina kama mtoto mchanga anapokumbatiwa na mama yake.

Dr. Lang ana Shahada ya Uzamili na ya Uzamivu (master’s and doctoral degrees) katika hesabu k u t o k a C h u o K i k u u cha Purdue (Purdue University).

L a n g a n a s e m a , anapenda sana hesabu kwa sababu “Maths is logical. Kwamba hesabu ni logiki. Ni kutafuta ukweli na majibu sahihi na ya wazi yasiyo na utata. Na kwamba, kwake yeye anapokutana na mambo yasiyo na maelezo ya

uhakika wala majibu ya wazi, hupata tabu sana.

Ni kutokana na msingi huu wa ufanyaji kazi wa akili yake, alishindwa kumeza baadhi ya maelezo aliyokuwa akipewa katika maisha yake ya awali katika dini.

Kwa upande mwingine anasema, Uislamu ni dini ya kutumia akili toka kwenye kuamini. Uislamu unakutaka utafakari juu ya maumbile na mambo mbalimbali kutambua ukweli.

Kwa sasa yeye ndiye mshauri wa wanafunzi Waislamu katika Chuo Kikuu anakosomesha na pia wa Chama cha Wanafunzi Waislamu k a t i k a V y u o Vi k u u , M a r e k a n i . A k i w a mwakilishi wao katika m a m b o ya n a y o h i t a j i kuwasiliana na uongozi wa vyuo.

Dr. Jaffrey Lang ameoa mke kutoka Saudi Arabia na ana watoto watatu. Wote mabinti. Ameandika v i t a b u v i n g i j u u ya Uislamu. Kitabu kimoja amekipa jina “Even Angels ask; A journey to Islam in America”.

Kat ika k i tabu h ik i p a m o j a n a m a m b o m e n g i n e a n a h i m i z a utumiaj i wa aki l i na kuhoji. (Imekusanywa na waandishi wa An nuur kutoka vyanzo mbalimbali.)

Tunavurugwa bila kujuaInatoka Uk. 3

kinachoendelea. Bali tulio wengi achilia mbali swala za jamaa hata swala ya mtu akiswali peke mpaka mtu akitoa salamu haelewi amesoma sura gani wala kuwa ameswali rakaa ngapi? Mathalani, miongoni mwa nguzo za swala ni mtu kuwa na “Khushui” (Unyenyekevu) au “Tumanina” (Kutulizana) a k i wa y u p o n d a n i ya swala. Lakini jambo hilo halipatikani kwa watu wengi bali hupatikana kwa mtu anapokuwa yupo kwenye kutizama TV/Runinga. Kwani msanii mwenye kuilingania hadhira hugusa hasa moyo kile kitu inachokipenda. H i v y o h u f u n g u k a n a kupokea chochote k i le kiwe ni cha heri au shari bila ya kuchuja. Leo mtu ili kulithibitisha hili ajifanyie tathimini yeye mwenyewe pindi anapokuwa yupo kwenye swala mawazo yote

na akili itakuwa yapo nje ya swala na inafikia mahali hata hufahamu upo kwenye rakaa ya ngapi na bali utashituliwa na imamu akitoa salamu ndio utakumbuka kwamba ulikuwa upo kwenye swala, na hata kuelewa kuwa imamu a l i soma sura gani baada ya kusoma “Suratul Fatiha”. Lakini jiulize jinsi unavyoweza kueleza kwa ufasaha mara baada kumalizika mpira uliokuwa ukiutizama katika TV/Runinga, na mtu akitokea na kukuuliza ni timu ipi iliyoshinda? Utajibu kwa ufasaha kabisa timu iliyoshinda, mfungaji wa goli, aliyempatia pasi, dakika Fulani na beki au kipa wa adui aliyesababisha makosa yaliyopelekea timu yao kufungwa au jiulize jinsi unavyoweza kuelezea Filamu na wakati mwingine hata hiyo lugha inayozungumzwa huifahamu bali utaweza

kutaja wahusika wakuu na wadogo na kila mtu nafasi au dhima yake i l ikuwa ni ipi. Au hata wanafunzi wengi wanapokuwa mbele ya mwalimu ni tofauti kabisa na wanavyokuwa mbele ya kioo cha TV/Runinga.

Je, kwa muda wa mwaka mzima tumeisoma Qur’an aya ngapi na kuzifanyia kazi?

J e , k wa m u d a wa mwaka mzima kwenye matatizo yetu ambayo yametutokea kwenye Nyanja ya siasa, uchumi, maadili na mizozo yetu nk. Tumeweza kuirejea Qur’an mara ngapi ili kuweza kututatulia matatizo yetu?

Swal i la msingi la kujiuliza wapi tunakwenda na mustakabali wetu dunia na akhera ni upi? Kwa mantiki hiyo ni ukweli halisi kwamba tumeidhara Qur’an na tuko mbali nayo kabisa.

Page 8: ANNUUR 1112

8 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 14-20, 2014Makala

Inaendelea Uk. 9

“SAA hiyo nilikuwa nimepigwa risasi, wakati natolewa kwa uchungu nilikuwa nikililia Laailaha ilallah, laailaha ilallah. Sasa yule jamaa alikuwa kwa strecha (machela ya kubebea wagonjwa), nafikiri naye alikuwa Muislamu kwa sababu nikisema laailaha ilallah, husema Muhammadu r a s u u l u l l a h …n i k a i n g i z w a k w a a m b u l a n c e ( g a r i ya w a g o n j w a ) b a d o nasema laailaaha ilallah aliyekuwa akinipatia first aid (huduma ya kwanza), naye husema Muhammad rasuulullah-ndio jamaa (askari) akauliza ‘nani anasema hiyo? Huyo ni wetu au wa upande gani? Sasa nikashangaa n i k a s i k i a j a m a a wanasema ‘suspect ’ , ‘suspect’ (mtuhumiwa, mtuhumiwa)”.

Huyo ni Ali Gitonga a m b a y e a l i w e k w a r u m a n d e k w a w i k i tatu na mateso makali akituhumiwa kwa ugaidi. Katika siku alizokaa ndani,

Mauwaji Msikitini: Makubwa yafichukaUsiombe kuingia anga ya polisi wa ugaidiSheikh aling’olea macho, sehemu za siriMchezo wa danganya toto jinga waendelea

Na Omar Msangi

alihojiwa na kutishwa na makachero wengi

wakiwemo wale wa FBI-Wazungu.

Awali serikali ya Kenya ilikuwa imetangaza kuwa

Al i Gi tonga a l ikuwa mmoja wa magaidi wa Al Shabab waliovamia Westgate Shopping Mall n a k wa m b a a l i k u wa a m e j e r u h i wa k a t i k a mapambano na polisi.

Hata hivyo Ali Gitonga alikuwa kijana dereva aliyekuwa ameajiriwa na tajiri mmoja Nairobi na kwamba siku ya tukio, alikuwa amewapeleka watoto wa tajiri yake katika duka la Nakumatt kufanya manunuzi. Aliposikia risasi zikirindima ndani, i l i b i d i a i n g i e n d a n i k u j a r i b u k u w a o k o a watoto wa tajiri yake na ndio akapigwa risasi na kujeruhiwa na magaidi.

Kama alivyojieleza hapo juu, wakati anatolewa katika ile hali ya uchungu, na akidhani ndio anakufa, a k a wa a n a s h a h a d i a . A s k a r i w a l i p o s i k i a a n a t a m k a “ L a a i l a h ilallah”, wakasema huyu ni gaidi. Serikali ya Kenya ikamtangaza kuwa ni gaidi aliyejeruhiwa. Akasota ndani wiki tatu.

Haya ni baadhi ya mambo ambayo yamefichuka

“ N A A M ! M t a z a m a j i nakuomba umakinike na uniazime masikio yako mawil i , kwani taarifa tutakazokupa sasa zitakushangaza na hata kukufungua macho hata zaidi.”

“ I w a z i e h a l i y a wa n a wa k e k u a c h wa wajane na watoto kuachwa yatima na hata familia kukosa mtu anayetafuta riziki ya kila siku. Kisa na sababu, yeye kuhusishwa na ugaidi. Kinachofuatia ni yeye kufungwa bila ya kufunguliwa mashitaka na hatimaye kuuwawa katika hali ya kutatanisha. Hayo ndiyo masaibu waliyopitia Wakenya (Wais lamu) wengi kwa kuhusishwa na ugaidi. Kwa waliobahatika kuishi, wamesalia kama wa f u n g wa n d a n i ya nchi yao . Haya yote yanatokana na kitengo kinacholaumiwa vikali cha ATPU (Anti Terrorism Police Unit-yaani polisi wa kupambana na ugaidi) miongoni mwa asasi za usalama zinazolaumiwa

Wagigisi wa mauwajikufanya mauwaji kinyama na kuepuka (mkono wa sheria kutokana na) maovu hayo.”

H i v y o n d i v y o m w e n d e s h a k i p i n d i anavyofungua makala ya Jicho Pevu cha televisheni ya KTN, mada ikiwa “Wagigisi wa Mauwaji.”

Mwendesha kipindi katika ufafanuzi wake alisema kuwa wagigisi wa mauwaj i ni watu wanaojifanya kuwa wao ni walinzi wa usalama wa raia (Polisi), lakini hao hao ndio wanaofanya mauwaji ya kutisha na ya kinyama, halafu hakuna hatua zozote wanazochukuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

H u k u a k i w a t a h a d h a r i s h a w a t a z a m a j i k u w a makala hiyo itakuwa na picha za kutisha, hasa

kutokana na maiti za Masheikh waliouliwa kikatili, akafungua mada kwa kueleza masaibu ya Waislamu wa Mombasa katika hiki kinachoitwa vita dhidi ya magaidi.

K i s a c h a k w a n z a kuelezwa ni ki le cha kuul iwa Sheikh Said Mohammed Njiro wa Kiembeni , Mombasa. M a k a l a i n a f u n g u k a kwa kuonyesha chakula kishatengwa mezani . Kama ilivyo kawaida ya wanawake wa Pwani, m k e we S h e i k h S a i d kafunika chakula kwa kawa imeandikwa, “Siringi ni tabia yangu.”

Kwa vile wakati wa dhuhri ulishakaribia, Sheikh Said akamwambia m k e w e k w a m b a a n a k w e n d a k w a n z a msikitini kuswali halafu atakula akirejea. Lakini

Sheikh Said Mohammed N j i r o , h a k u w a h i k u l a c h a k u l a h i c h o kilichoandaliwa na mkewe kipenzi, Rahma Hassan, wala huko msik i t in i hakuwahi kufika.

Askari wa kikosi cha ATPU walimkamata njiani, wakamfunga pingu na kumrejesha nyumbani. Kwa mujibu wa maelezo ya majirani waliokuwa katika eneo la tukio akiwemo msichana Agnes Kanga, ili kuficha ushahidi, polisi walifukuza watu wote walio jirani na eneo hilo. B a a d a ya k u p e k u wa nyumba nzima na kukosa silaha walizodai kuwa zipo katika nyumba hiyo, wal imchukua Sheikh wakamlaza kitandani kwake kifudifudi wakiwa wa m e m f u n g a p i n g u wakampiga risasi sita kichwani.

“Muda mfupi baadae maafisa wa polisi (ATPU) walimlaza Sheikh Said k i tandani mwake na k u m p i g a r i s a s i s i t a kichwani akiwa amelala k i fudi fudi na p ingu mikononi.”

H i v y o n d i v y o anavyosimulia mchunguzi wa KTN kutokana na maelezo aliyopewa na mke wa marehemu pamoja na shemeji yake, Twalha Hassan.

K a t i k a t a a r i f a y a u c h u n g u z i wa K T N wanasema kuwa baada ya kufanya mauwaji hayo, askari hao wa ATPU, wa l i z i d i s h a u n ya m a wao kwa kumkamata m k e n a m t o t o wa k e mdogo eti nao magaidi “kando na kuwa silaha haramu. Silaha ambazo ni za kumbambikizia na kumkamatisha mkononi.”

Akisimulia kisa hicho cha kusikitisha mke wa m a r e h e m u a n a s e m a , yeye binafsi walimpiga sana kabla hawajamuuwa

Inaendelea Uk. 9

KHUBAIB A. Rogo, mtoto wa Marehemu Abdul Rogo.

Page 9: ANNUUR 1112

9 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 14-20, 2014Makala

Inatoka Uk. 8

Inatoka Uk. 8

Inaendelea Uk. 10

Inaendelea Uk. 10

Mauwaji Msikitini: Makubwa yafichukawakati tukifuatilia tukio la kuvamiwa Waislamu waliokuwa masjidi Mussa, Mombasa na watu kadhaa kuuliwa.

Awali katika taarifa zetu tulikuwa tukisema kuwa hakukuwa na picha za kamera zilizo wanasa waliodaiwa kuwa magaidi. Hata hivyo, pamoja na picha nyingi kuharibiwa na kufichwa, lakini jicho la uchunguzi la kituo kimoja cha televisheni, Kenya kimepata picha nyingi zikionyesha tukio hilo, na hasa magaidi hao walivyofanikiwa kutoroka huku jengo likizingirwa na jeshi la Kenya-Kenya Defense Force (KDF). Kama itakavyoonekana katika makala hii huko m b e l e n i , m t a f a r u k u uliotokea baina ya polisi n a wa n a j e s h i k a t i k a operesheni ya Westgate, huenda ndio uliopelekea baadhi ya polisi kutoa picha hizo kwa baadhi ya waandishi wa habari zilizokuwa zimedhibitiwa ili kulipiza kisasi kwa wanajeshi.

Lakini jingine ambalo t u m e l i p a t a k a t i k a ufuatiliaji wetu tukio la Masjid Mussa ni kuwa unyama wa kutisha hadi s a s a u m e s h a f a n y wa dhidi ya Waislamu wa

Wagigisi wa mauwajimumewe.“ Wa l i n i p i g a s a n a

mpaka n ika fura uso ( u s o u k a v i m b a ) . Wakanilazimisha nilale c h i n i . K u l i k u wa n a begi la nguo za mtoto wangu. Walichukua silaha wakatia silaha (katika begi ile) wakanyanyua w a k a n i u l i z a , ‘ w e mama waona hii nini?’ Nikawaambia mimi sijui. Wakanitoa wakaniweka sitting room wakaniambia nikae hapo hapo nisiinuke, nikiinuka wataniuwa…baadae wakanipeleka n d a n i wa k a n i a m b i a t w e n d e u k a o n e , tumemuuwa (mumeo).”

Baada ya kukamilisha o p e r e s h e n i h i y o , tunaambiwa kuwa polisi hao wal i fanya kama walivyozoeya.

“ K u i t a w a a n d i s h i wachache wa magazeti,

r e d i o n a r u n i n g a w a n a o a m i n i k a kutumikia maofisa wa polisi wanaochapisha taarifa bandia na porojo kama wanavyotakiwa z i n a z o c h a p i s h wa n a kitengo hicho na kutumwa kwa wanahabari hao.”

K wa h i y o , k u p i t i a wanahabari hao, polisi w a k a s e m a k u w a wamemuuwa mtuhumiwa wa ugaidi Sheikh Said M o h a m m e d k a t i k a mapambano makali ya kurushiana r isas i na polisi!!!

Mke na mtoto wake kwa muda wa siku sita akawa yupo rumande katika gereza la Shimo la Tewa, kisha akapelekwa

mahakamani akituhumiwa kuwa yeye ni gaidi hatari anayemiliki silaha.

Kutokana na kilio cha mama huyo, Bi Rahma H a s s a n , m a h a k a m a ikampa dhamana, lakini bado akibaki na tuhuma za ugaidi na kukutwa na silaha (silaha ambayo alikamatishwa na polisi).

Mwingine kufikwa na mkasa kama huu ni Sheikh Mohamed Aboud Rogo. Huyu aliuliwa tarehe 27 Agosti, 2012. Akisimulia kisa cha mauwjai yake, Mohammed Ali anasema:

“A g o s t i 2 7 , 2 0 1 2 n d i y o s i k u a m b a y o familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Sheikh Mohammed Aboud Rogo,

hawataisahau kamwe. Siku ambayo kiongozi wa dini aliyekuwa na ufasaha na ustadi wa kusema na kuvutia hadhira, alizimwa kwa mtutu wa bunduki. Je, aliuliwa vipi?”

Maelezo yanatolewa k u wa a l i u l i wa k i a s i mita 200 kutoka kituo cha polisi cha Bamburi. Baada ya yeye kupita eneo fulani kukaribia kituo hicho cha polisi, polisi walikuwa wamepangwa kana kwamba kulikuwa msafara wa Rais. Njia zote zikafungwa. Hakuna gari inayokuja mbele yake wala nyuma yake katika barabara ya Malindi-Mombasa. Hapo ndio watu wanaodaiwa kuwa

ni polisi wa kikosi maalum walijitokeza nje kidogo ya barabara wakamfyatulia risasi.

Maelezo ya mtafiti wa KTN yanasema kuwa waliomuuwa ni watu wa kikosi maalum wanaopewa m a f u n z o k u t o k a Marekani, Uingereza na Israel na kwamba kikosi hicho kina kambi zake Nairobi, ila kukiwa na operesheni kama hiyo, hupewa ndege wakaingia Mombasa wakafanya kazi yao na kurejea Nairobi bi la ya kutambulika. KTN katika Jicho Pevu w a n a s e m a , k a t i k a operesheni chafu kama hizo, Marekani, Uingereza na Israel, hucheza kadi zao kinyumenyume ili wasigundulike.

Wanaoing ia ka t ika orodha hii ni watu wengine sita ambao nao wameuliwa

Kenya katika zile jitihada za serikali hiyo kujisajili kwa Marekani kwamba inapambana na magaidi. Taarifa za uchunguzi zilizokusanywa na kituo cha televisheni KTN, katika kipindi chake maarufu ‘Jicho Pevu’, zinaonyesha kuwa waliomuuwa Sheikh Aboud Rogo ni polisi wa kikosi cha kupambana na magaidi-Anti Terrorism Police Unit (ATPU) na kwamba aliuliwa jirani kabisa na kituo cha polisi cha Bamburi. Na baada ya mauwaji hayo polisi wawili waliomuuwa waliingia katika kituo hicho cha

polisi kurejesha bunduki walizotumia na wengine w a w i l i w a k a e l e k e a baharini.

Mkusanya habari wa KTN baadae aliwahoji w a t o t o w a S h e i k h Rogo, nao wakaeleza jinsi wanavyotishwa na kubambikiziwa tuhuma za ugaidi.

Kijana Khubaib Abdu Rogo anasema, moja ya picha wanazo tumia polisi hao kumtisha ni za Samir Khan. Humwonyesha wakati yupo hai na kisha humwonyesha zile picha za kutisha baada ya kuuliwa. Huyu Samir Khan alitekwa

Mombasa na siku kadhaa baadae, aliokotwa katika msitu wa Tsavo, maiti yake ikiwa imenyofolewa macho na sehemu zake za siri. Walioshuhudia tukio la kutekwa kwake wanasema, alitekwa na polisi wa ATPU mara tu alipovuka kivuko cha Likoni.

“ W a n a n i a m b i a tutakufanya kama huyu.”

Awali polisi walikuwa wamekanusha kabisa kuhusika na kumteka Samir na kisha kumuuwa. Lakini sasa wanatumia picha za Samir baada ya kufanyiwa unyama

kuwatisha watoto wa Sheikh Aboud Rogo.

Pengine nitaje hapa tena kisa cha kuuliwa Sheikh Said Mohammed. Huyu aliuliwa Mombasa. Polisi wal imkamata wakat i akielekea msikitini kuswali dhuhri, wakamrejesha nyumbani. Wakapekua wa k i d a i wa n a t a f u t a silaha, walipokosa kitu wakamfunga mikono kwa nyuma wakamlaza k i fudi fudi k i tandani mwake na kisha kumpiga risasi sita kichwani. Taarifa ikadai kuwa aliuliwa akipambana na polisi. (Yote haya ni kwa mujibu wa taarifa za Jicho Pevu-KTN). Na hayo ni baadhi tu ya matukio ya mauwaji ya kutisha waliyofanyiwa Waislamu kabla ya hili la juzi la Masjid Mussa.

Pengine sasa tuangalie lile shambulio la Westgate S h o p p i n g M a l l , i l i tutizame linahusiana vipi na matukio kama haya ya kuvamia misikiti na kushambulia Waislamu.

M p a k a s a s a y a p o maswali mengi ambayo bado hayajapatiwa majibu kufuatia shambulio la kigaidi pale Westgate Shopping Mall, Nairobi. Moja ya maswali hayo ni hili: Kama magaidi waliuliwa, maiti zao ziko

POLISI wa Kenya walipovamia Masjid Mussa, Mombasa

Page 10: ANNUUR 1112

10 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 14-20, 2014Makala

Inatoka Uk. 9

Inaendelea Uk. 12

Inatoka Uk. 9

Mauwaji Msikitini: Makubwa yafichukawapi? Pili, magaidi hao ni akina nani? Tatu, kwa nini polisi wa kawaida na vikosi maalum waliondolewa ghafla na badala yake likaletwa jeshi (KDF)? Kwa nini jeshi halikuingia kuanza mashambulizi bali likasubiri usiku kucha muda ambao unadhaniwa ndio waliotumia magaidi kutoka?

Taarifa ya uchunguzi wa KTN inaonyesha kuwa hadi kufikia jioni ya siku ya shambulio, polisi walikuwa wamefanikiwa kuwaokoa watu wote, kwa hiyo ndani kukabaki magaidi peke yao. Na taarifa hiyo inaonyesha jinsi ndani kulivyokuwa k u p i t i a k a m e r a z a CCTV. Wanaonekana watu (magaidi) wanne tu wakiwa na silaha zao wakirandaranda bila hata ya kuwa na wasiwasi.

M o h a m m e d A l i , mchunguzi na mtayarishaji kipindi wa KTN, anasema kuwa pamoja na mafanikio h a y o , l a k i n i j a m b o lisilokuwa la kawaida na lisilokuwa limetarajiwa likafanyika. Ilitangazwa kuwa jeshi l inaingia kuongoza operesheni. Kilichotokea ni kuwa “walijikuta wakiuwana

wenyewe kwa wenyewe”. Wanajeshi wakauwa na kujeruhi polisi. Mmoja wa Polisi aliyeuliwa ametajwa kwa jina la Martin Munene Kithinji.

Kufuatia hali hiyo, makamanda wa polisi w a l i o n d o a v i k o s i v y a o w a k i l a l a m i k a kudharauliwa. Lakini h a t a wa n a j e s h i n a o , hawakuingia ndani mpaka kesho yake. Taarifa ya KTN kupitia kamera za video walizopata, zinaonyesha m a g a i d i h a o wa n n e

wakiwa ndani bila ya wasiwasi. Ilipofika usiku wanaonekana magaidi wale wakiswal i kwa zamu, anaswali mmoja mmoja huku wengine wakishika zamu. Kisha baada ya hapo wakafanya mawas i l i ano kupi t ia simu na kisha mmoja kutoka nje na kuangalia hali ikoje. Mara wote wakatoka wakatokomea kusikojul ikana. Hiyo ilikuwa ni saa 4 na dakika 54 usiku.

K w a h i y o , u s i k u

u l e K D F , w a l i b a k i wamezingira jengo huku magaidi waliokuwa ndani walishatokomea kusiko julikana.

Taarifa ya Jicho Pevu inasema kuwa ilipofika asubuhi ya Jumapi l i ndio wanajeshi waliingia katika jengo hilo. Lakini na weyewe wakajikuta wakiumizana wenyewe kwa wenyewe.

Taarifa hiyo ya KTN inaonyesha rundo la chupa za ulevi na kisha inawaonyesha wanajeshi

hao wakiingia wakiwa wameshika bunduki , lakini wanapotoka kila mmoja kashika mifuko ya Rambo utadhani wanatoka k u f a n y a m a n u n u z i (shopping). Katika tukio m o j a w a n a o n e k a n a wakielekezana duka la kuingia kupora kwa hiyo wakati wanatoka, kila mmoja anaingia hapo na kuchukua kitu kabla ya kutoka.

K a t i k a k i l e l e c h a operesheni hiyo, wakati wananchi waki j iul iza ilikuwaje jeshi likaitwa na nini kinaendelea ndani ya Westgate, ukaonekana moshi mzito ukitokea duka la Nakumatt. Waziri wa Usalama akasema kuwa hao walikuwa magaidi waliokuwa wamechoma m a g o r o k u t a k a kuwababaisha askari na kwamba moto huo ungezimwa mara moja. Hata hivyo, haukupita muda ikaonekana kuwa h a u k u w a m o t o w a magodoro bali ulikuwa ukiwaka n je sehemu ya j u u ya k u e g e s h a magari na mara jengo likaporomoshwa kutoka ghorofa ya tatu mpaka chini.

Wakati hal i ik izidi kuta t iza , mara “ j ina l a S a m a n t h a L o u i s e

Wagigisi wa mauwajikinyama wakituhumiwa kwa ugaidi. Mmoja wao ni Sheikh Samir Hashim Khan, Imam wa msikiti. Huyu alitekwa na maofisa wa polisi akiwa na Sheikh Mohamed Kassim (kipofu). Walitekwa katika kivuko cha Likoni muda wa saa 6 mchana tarehe 10 Oktoba, 2012. Siku sita baadae mwili wa Sheikh Samir uliokotwa katika msitu wa Tsavo ukiwa na majeraha y a k u t e s w a , m a c h o pamoja na sehemu za siri zikiwa zimenyofolewa. A i d h a , u s o u l i k u wa umeharibika ikidhaniwa kuwa alimwagiwa tindi kali katika kuteswa au baada ya kuuliwa. Hadi makala haya ya Wagigisi wa Mauwaji inakamilika, K a s s i m a l i k u w a hajapatikana, si maiti au japo kusikia yupo wapi.

Pengine nimalizie kwa masaibu yanayowakuta watoto wawili wa kiume wa marehemu Sheikh Aboud

Rogo. Hawa ni Khubaib A Rogo na Dhulkif l i Aboud Rogo. Kat ika maelezo yao vijana hawa wanasema kuwa polisi wamekuwa wakiwajia na kuwasumbua mara kwa mara wakiwatuhumu k u w a w a n a f i c h a silaha na kwamba wao walishakwenda Somalia na kuj i funza ugaidi . Katika kuwatisha huwa wakiwaletea picha ya baba yao na masheikh wengine wa l i o u l i wa n a m i i l i yao kuharibika vibaya, kisha huwaambia kuwa watawafanya kama hao au kuwafanyia vibaya zaidi.

“Waliniwekea bunduki juu ya meza wakaniambia n i i f u n g u e , … w a k a t i wakinitisha, wananiletea picha ya Samir wakati n i mzima na wakat i

w a s h a m c h o m a k w a a s i d i , wa s h a m u u wa , wakasema unaona vile tulimfanya huyu, basi na wewe tutakufanya hivi au kukufanyia unyama zaidi. Baada ya hapo wakaniletea picha ya baba yangu wakati yupo hai, wakaniuliza wamjua huyu, nikawaambia ndio baba yangu, kisha hunionyesha picha wakati washampiga risasi.”

H a y o n i m a e l e z o ya Khubaib akie leza a l i v y o k u wa a k i p a t a wageni mara kwa mara kutoka kikosi cha ATPU wakiongozwa na kamanda wa kikosi hicho Mombasa, Elijah Rop, mara baada ya baba yake kuuliwa na hata sasa.

K h u b a i b a n a s e m a katika mambo ambayo

hatayasahau, ni kauli ya Elijah Rop alipomwambia kuwa wao, ATPU, ndio waliomuuwa baba yake. Kisha akamwambia, naye ak i le ta k idomodomo w a t a m u u w a k a m a walivyomuuwa baba yake.

Khubaib anasema, yeye hajawahi kwenda Somalia na wala hana mpango huo, ila yeye ni Mwana Sunna. Ni Muislamu. Sasa kama atauliwa kwa ajili hiyo, hana la kusikitika. Ila anasema, akiitwa katika kituo chochote cha polisi, hatakwenda. Kama ni kumuuwa waje wamuue mbele ya mama yake, kama walivyomuuwa baba yake mbele ya mkewe (mama yake Khubaib). Mama yake ajue kwamba mwanawe kauliwa na polisi.

M a e l e z o ya m t o t o Dhulkifli nayo ni ya namna hiyo hiyo. Naye anasema ATPU wanamwambia kuwa yeye ni komandoo la magaidi waliohitimu mafunzo Somalia.

K a t i k a t u k i o l a kuvamiwa Masjid Mussa wiki mbili zil izopita, Dhulkifli anaonekana mbele ya msikiti akiwa kashikishwa bendera ya Al Shabab huku polisi wenye silaha wakimzingira.

Kat ika p icha mo ja iliyopigwa kupitia simu ya mkononi , ambayo n i m e i s h u h u d i a n a kuisikiliza, mtoto huyo wa Sheikh Rogo anasikika ak i la lamika kwamba kashikishwa bendera hiyo na polisi.

Na katika mahojiano yake na KTN anasema, afya yake ni mgogoro mtupu, kama anavyoonekana (unene usio wa kawaida).

Kisha anahoji, hivi na mwili huu mazoezi gani ya kijeshi/kigaidi naweza kufanya.

POLISI wa Kenya walipovamia Masjid Mussa, Mombasa

Page 11: ANNUUR 1112

11 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 14-20, 2014Makala/Tangazo

K U J I H U S I S H A n a m a d h - h a b f l a n i imekuwa ni dhana na itikadi inayoshadidiwa miongoni mwa Waislamu walio wengi. Kwa dhana hiyo, imefikia hatua m t u k u w a a m i n i s h a waislamu wasiojitambua na kuufahamu Uislamu sahihi na wale ambao si Wasilamu waamini kwamba bila kuwa na dhehebu katika Uislamu wewe si Muislamu.

Niseme tu kwamba dhana hii ni dhanifu na daima haikubaliki katika Uislamu. Suala la kuwa na dhehebu flani, ni wazo na zao la mtu binafsi (Personal and Private opinions).

M w e n y e z i M u n g u (SWT) na Mtume wake, h a w a k u t u a m r i s h a tujitenge kimakundi kama tulivyojitenga sasa hivi. Kwa kuangalia ubaya wa jambo hili, Mwenyezi Mungu (SWT) hakuacha kutuonya tusifanye hivi pale aliposema ndani ya Qur’an:

“Nyenyekeeni Kwake na mcheni, na simamisheni swala wala msiwe katika washirikina. Katika wale walioitenga dini yao na wakawa makundi, kila k i k u n d i k i n a f u r a h i a kilichonacho” (30:30-31).

Kwa kuirejea aya hiyo na ny ingine ambazo sijazinukuu katika makala haya, hakuna mahala s u a l a l a m a d h e h e b u l imebainishwa. Na si lazima kuwa mfuasi wa Hanafi, Shafi’i, Maliki au Hanbali . Hawa ni wanazuoni na maimamu waliofanya na kuonesha juhudi zao katika dini na hawakuwaamrisha watu watengeneze makundi na kupigana ima kutukanana kama tufanyavyo sisi. Na waliweza kuhitilafiana lakini hawakugombana, kuzomeana, kutukanana, k u k u f u r i s h a n a n a kufanyiana uhasama na uadui kama tufanyavyo sisi leo hii.

Jambo moja la msingi la kufuata s i Shekhe w a l a I m a m F u l a n i , bali ni kuitafuta nj ia iliyobainishwa kwetu kama Waislamu. Mwenyezi Mungu anasema ndani ya Qur’an:

“ S e m a : H i i n d i o n j i a y a n g u , n i n a i t a ( n i n a l i n g a n i a ) k w a M w e n y e z i M u n g u kwa u juzi wa kwel i , mimi (nafanya hivi) na ( k i l a ) wa n a o n i f u a t a . Na Mwenyezi Mungu a m e t a k a s i k a n a k i l a

MadhehebuMohammed Makimu

upungufu, wala mimi s i o m i o n g o n i m w a w a n a o m s h i r i k i s h a ( M w e n y e z i M u n g u ) (12:108).

M w e n y e z i M u n g u (SWT) ametuamrisha tushikamane na kuwa kitu kimoja (3:103). Na ametoa tahadhari kwamba iwapo tusipokuwa pamoja na letu likawa moja kama Waislamu tunaomfuata M t u m e m m o j a n i n i kitatufika.

“Na mtiini Mwenyezi M u n g u n a M t u m e wake wala msizozane (msigombane) , msi je mkaharibikiwa na kupotea nguvu zenu, na vumilieni ( m s t a h a m i l i a n e ) . Bila shaka Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanaovumilia” Qur’an (8:46)

Katika miongoni mwa kauli za Imam Maliki a n a s e m a “ m a w a z o au mtazamo wa mtu yeyote waweza kubalika p a l e ya k i e n d a n a n a Qur’an na Hadithi na yanaweza kupingwa pale yanapokuwa kinyume i s p o k u wa ya h u y u aliyelazwa hapa kaburini. (Akaashiria kaburi la M t u m e M u h a m m a d s.a.w).

Maimam wote wane wa Fiq-hi wamesema katika kauli zao kwamba “kama Hadithi sahihi itabainika kuliko haya maoni yangu, hivyo basi hiyo itakuwa ndio madhehebu yangu” (Idhaa swah-hal-hadiith fahuwa madh-habii).

H i i i n a m a a n a kwamba hadithi sahihi ikibainika katika mas-ala wanayoyafutu, ndio i takuwa n j ia ya wao kufuata. Si maoni yao tena. Na walihimiza na kusisitiza sana watu wayapime maneno na mitazamo yao kwa uzani wa Qur’an na Sunnah, ikibainika wao kwenda kinyume, watu wasiwafute kwa ushabiki kwa kuwa wanawapenda, bali wayaachilie mbali maneno yao.

Ugonjwa unaowasibu Waislamu wengi sasa hivi ni kuifuata dini kibubusa na kuwa washabiki wa dini. Suala la uma’amuma katika Uislamu linaishia katika swala tu. Na hata katika umaamuma katika swala, ni lazima na wewe unayeswalishwa ujue namna ya kuswali. Sio kwamba anatakiwa kujua

Imam pekee. Kama ilivyo wajibu kwa Imamu kusoma Suratul Fat’ha na kujua taratibu zote za swala, ndivyo hivyo anavyotakiwa kuwa maamuma.

Kwa hiyo, kila Muislamu anawajibu wa kuusoma na kuufahamu Uislamu sahihi kutoka kwenye vyanzo vyake (Qur’an na Sunnah) si kushabikia.

Waislamu walio wengi wamekuwa ni wafuasi wa madhehebu mbalimbali. Mbaya zaidi hakuna lolote wanalojua juu ya huyo wa n a y e m n a s i b i s h a n a dhehebu wanalolifuata. Si Shafii, Hanbali, Maliki wa l a H a n a f i . H a k u n a wanachokifahamu wafuasi wa madhehebu hayo zaidi ya kujua jina tu ima huyu ni Shafii, Maliki, Hanbali au Hanafi. Ukiwauliza kipi unafahamu juu ya yale yaliyozungumzwa na Imam

huyu, hana jibu la msingi. Ndugu zangu kat ika

dini hii i l iyofundishwa na Mitume wote, bado i n a t u t a k a t u i t u m i k i e kama inavyotufundisha. Tuire jee ki la kipengele chake kimatendo. Huu ni muda wa kuacha tofauti zetu kwa kuangali Uislamu unafundisha nini si watu w a n a s e m a j e . I s h i n a Muislamu mwenzako kama ndugu yako, penda yamfike mambo ya kheri kama wewe mwenyewe unavyopenda katika nafsi yako.

N i h i t i m i s h e m a k a l a yangu kwa kuirejea hadithi i l i y o s i m u l i a n a I r b a d bin Sariya katika Sahiht-Tirmidh. Anaeleza kwamba “Siku moja Mtume (s.a.w) alituawaidhi waadhi ambao ulishtua nyoyo za watu baada ya swalat Fajr ambao ulibubujisha watu machozi, na nyoyo zikapatwa khofu,

Mtu mmoja akasema “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu i n a o n e k a n a k a m a h u u waadhi wa kutuaga, ni kitu gani unachotupa kwa sasa? Mtume akasema “Nakuusieni kumcha Mwenyezi Mungu na muwe ni wasikivu na wenye kutii hata kama atakujieni Mhabeshi Mtumwa (madhali anakupeni ujumbe utokao kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake). Kwa wale watakaoishi baada ya kufa kwangu, watashuhudia ikhtilafu nyingi. Mnatakiwa mshikamane (pindi muda huo zikitokea hizo ikhtilafu) na Sunnah zangu na zile za Makhalifa waongofu.

Aliyoyatabir i Mtume ndiyo haya yanatokea sasa. Jambo la msingi ni kuiingiza hadithi hii katika utendaji wa maisha yetu. Hakuna haja ya kuwa mfuasi wa madhehebu fulani wakati dhehebu hilo halipo katika asili ya Uislamu.

“ N a a n a c h o k u p e n i Mtume basi pokeeni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho…….” (Qu.’an 59:7)

([email protected])

CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO KINATANGAZA NAFASI ZA MASOMO KWA NGAZI ZA DIPLOMA NA CERTIFICATE KWA MWAKA WA

MASOMO 2014/2015MASOMO YA TOLEWAYO NI:-1) Diploma and Certificate in Science and Laboratory Technology2) Diploma and Certificate in Journalism3) Diploma and Certificate in Islamic Banking and Finance4) Diploma and Certificate in Procurement and Logistics Management5) Diploma and Certificate in Law and Sharia’h6) Diploma and Certificate in Islamic Studies7) Certificate in Medical Laboratory Technology8) Certificate in Information Technology 9) Certificate in Chinese Language10) Certificate in Sign Language11) Certificate in Arabic Language

SIFA ZA KUJIUNGA:-KWA NGAZI YA DIPLOMA.• MWANAFUNZI ANATAKIWA AWE NA FORM SIX ONE PRINCIPLE PASS NA SUBSIDIARY, SIFA ZA MUOMBAJI ZIENDANE NA KOZI ANAYOOMBA.

AU• AWE NA NTA LEVEL 4 CERTIFICATE YA KOZI INAYOFANANA NA IWE YA CHUO KINACHOTAMBULIKA NA SERIKALI.

KWA NGAZI YA CERTIFICATE.• AWE NA ANGALAU D NNE ZA KIDATO CHA NNE ZINAZOFANANA NA KOZI ANAYOOMBA

AU• AWE NA VETA LEVEL 3 CERTIFICATE INAYOFANANA NA KOZI ANAYOOMBAFORM ZA KUJIUNGA NA CHUO ZINAPATIKANA MUSLIM UNIVERSITY OF MOROGORO AU KATIKA WEBSITE YA CHUO, www.mum.ac.tz AU KUPITIA MAWAKALA WETU.

MASOMO YATAANZA RASMI TAREHE 12/05/2014.

MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 31/03/2014

KWAMAELEZO ZAIDI NA KWA KUPATA ORODHA YA MAWAKALA WALIPO KARIBU YAKO PIGA SIMU AU TUMA UJUMBE MFUPI KWA NAMBA ZIFUATAZO: - 0712277598, 0655003744 AU 0785330002

IMETOLEWA NANAIBU MAKAMU MKUU WA CHUO – TAALUMACHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO

Page 12: ANNUUR 1112

12 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 14-20, 2014Mashairi/Makala

Mauwaji Msikitini: Makubwa yafichuka

Inatoka Uk. 10Lewthwaite, maarufu “White Widow”, likaanza kusikika katika vinywa vya wanahabari na serikali kwamba al ihusika na shambulio hilo. Wakenya walijisahau wakashika hilo.”

KTN inasema kuwa kuletwa jina la Samantha ilikuwa namna nyingine ya “danganya toto jinga” k u wa f a n ya Wa k e n ya wasihoji mambo ya msingi kwani japo mama huyo alishawahi kufika Kenya huko nyuma, lakini madai ya “kushiriki mashambulio hayo ilikuwa ni porojo tupu.”

Kat ika kuhi t imisha kadhia hiyo, Waziri wa Usalama akatangaza kuwa kul ikuwa na magaidi 10 mpaka 15. Naye Rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumanne, siku moja baada ya kutolewa tangazo kuwa operesheni imekamilika, alisema kuwa magaidi wal ioul iwa wal ikuwa watano na 11 walikuwa w a m e k a m a t w a n a kushikiliwa na polisi.

Hata hivyo, picha za kamera za CCTV ambazo hatimaye zilifika mikononi mwa waandishi wa habari, zilionyesha kuwa kulikuwa na magaidi wanne tu.

Lakini jingine la kutaja hapa ni kuwa japo taarifa ya serikali ilitangaza kuwa magaidi 5 wal iul iwa, haikuweza kuonyesha picha za maiti hao. Aidha, hadi leo haikuweza pia kuonyesha hao magaidi 1 1 wa l i o k a m a t wa n a kushikiliwa na polisi.

Kinyume chake, kama ilivyoripotiwa katika gazeti la Daily Nation la Jumatatu iliyopita Februari 10, 2014, ser ikal i sasa inasema magaidi waliouliwa eti toka wakati huo, maiti zao zinashikiliwa na FBI wakizifanyia uchunguzi!!! Ajabu ya mambo!

Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa Jeshi la Kenya, Generali Julius Karangi, anasema:

“ H e r e i t f r o m m e , these fellows were killed on Monday morning. It happened on Saturday. We f inished them on Monday morning and their bodies are with the FBI somewhere.”

S wa l i n i j e , i w e j e magaidi wauliwe na jeshi la Kenya, serikali ishindwe kuonyesha mi i l i yao , lakini muda wote huo toka Septemba mwaka

jana 2013 mpaka leo, ndio inasemwa kuwa mii l i hiyo inachunguzwa na FBI. Kenya haina uwezo wa kuchunguza maiti? Hiyo Jumatatu anayosema Generali Julius, hakukuwa na mtu yoyote ndani kwani watu wote wal ikuwa washaokolewa. Kwa hiyo waliobaki ni magaidi na kwa hiyo hakukuwa na utata wowote kutambua nani waliuliwa.

Ukitizama simulizi hizi, ambazo zimefichuka baada ya kufanyika uchunguzi, zinaacha maswali mengi bi la ya majibu. Kama alivyosema mchunguzi wa KTN, nyingi ya taarifa za Westgate zimekuwa ni “porojo za danganya toto jinga.”

Ndio hapa unaweza kuona kuwa pengine katika kutafuta namna nyingine ya kuendeleza hii danganya toto jinga, lazima matukio kama haya ya Masjid Mussa yatokee ili kuwashibisha Wakenya na walimwengu kuwa ni kweli magaidi wapo na magaidi hawa ni Al Shabab na Waislamu waliopata mafunzo Somalia.

Na katika danganya toto jinga hii, tufahamu kuwa michezo ya ‘entrapment’ i t a f a n y i k a s a n a i l i kuwakamatisha Waislamu na silaha au jambo lolote l i n a l o w e z a k u s a i d i a k u wa p a k a z i a u g a i d i Waislamu na kufunika yale maswali ya ‘Westgate’ yasiyo na majibu.

Kabla ya tukio la Masjid M u s s a , v i p e p e r u s h i vilisambazwa kuhimza watu wahudhurie. Na ili kuhakikisha kunakuja v i j a n a w e n g i , h a t a wazamiaji wa mitaani, i k a t a n g a z w a k u w a kutakuwa na ubwabwa.

Sasa pengine ni suala la kutafiti, nani alitoa kipeperushi hiki? Nani waliandaa ubwabwa huu? Nani alikuwa azungumze? Je, naye alikamatwa? Nani a l iku ja na kupachika bendera za Al Shabab katika msikiti huo?

T a a r i f a y a K T N inaonyesha kuwa serikali ya Kenya inapokea mamilioni ya dola kila mwaka kwa ajili ya kupambana na ugaidi. Sasa lazima Kenya ionyeshe kuwa inafanya kazi . Wala haitakuwa jambo la kushangaza hapo baadae ikigundulika kuwa hata ubwabwa ulioliwa pale Masjid Mussa ulitoka

katika hizi dola kutoka Marekani.

Ambalo kila wakati la kujikumbusha ni kuwa vita hii dhidi ya ugaidi i n a m a l e n g o m a k u u m a w i l i . K w a n z a n i kwa ajili ya kuendeleza agenda ya mabeberu ya kuzitia utumwani nchi mbalimbali duniani ili zipate kudhibitiwa na kuwatumikia mabeberu. Pili, ni kuhujumu Uislamu.

Wanapouliwa Masheikh na vijana wa Kiislamu, Uislamu unahujumiwa kwa kuporwa nguvu kazi yake. Lakini unapowaonyesha magaidi kama wale pale Westgate, eti wanaswali Isha, baada ya kuuwa wa t o t o wa c h a n g a n a wanawake wasio na hatia, unahujumu Uislamu kwa kutangaza kuwa ni dini inayofundisha ukati l i na hivyo unahalalisha hatua zozote zinazoweza kuchukuliwa kuupiga v i t a U i s l a m u . Ta t u , unapofanya njama za ‘entrapment’, unawafanya vijana wa Kiislamu na nguvu kazi ya Waislamu, badala ya kufanya kazi za kimaendeleo kwa ajili ya dini yao na dunia yao, wabaki kila mara ni watu wa kupambana na polisi na kufanya ghasia mitaani.

U n a p o u wa S h e i k h , u n a w a t i a g h a d h a b u Waislamu na hasa vijana, kwa hiyo unawafanywa wawe na msimamo mkali zaidi dhidi ya serikali na hata wasio Waislamu. Wanabaki kuwa watu wa kuongozwa na hasira za kujihami badala ya kukaa kupanga na kufanya mambo ya maendeleo. Matokeo yake ni kuwaingiza katika chambo na ndoano ya ‘Free Islamic Army”, kwa maana ya jeshi la mujahidina lisilo na malengo maalum ya nchi maalum wala kuwa na udhibiti wa serikali yoyote duniani. Wao wakisikia mahali kuna vita wanatafuta h o j a z a k u j i r i d h i s h a (kujidanganya) kuwa ni jihad, wanakwenda.

Kwa mtindo huu ndio linaibuka tatizo jingine la hatari la kuwaangamiza Waislamu: Kutumiwa kama jeshi huru la kimataifa la kupigana “proxy war” ya mabeberu.

N d i o w a l i o k o Afghanistan, Iraq, Libya, Pakistan, Somalia na sasa Syria.

Mhariri samahani, niweke japo pembeni, Nitoe yangu maoni, kwa wananchi nchini, Katiba ninabaini, jadidi mada mezani, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu !

Bunge lile tambueni, la katiba li njiani, Wajumbewe kwa yakini, wiki jana si zamani, Amiri-Jeshi nchini, wote aliwabaini, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu !

Si kwa majina kwa nduni, baadhi nakujuzeni, Wanasiasa kundini, pamwe na wanazuoni, Kadhalika wa kidini, viongozi nao ndani,Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu !

Juma lijalo nadhani, yumkini li hewani, Bilhaki kwa yakini, wengi mwalitumaini, Kwa mengi matumaini, tena yaso na kifani, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu !

Kwa finyu wangu uoni, sina nalotumaini, kutoka humo bungeni, la utendi si uneni, Yanenwayo katibani, matendoni siyaoni, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu !

Mifano nitakupeni, toka ile ya zamani, Kwa ibara katibani, msijedhani nabuni, Tisashara namba 'wani', 'UHURU WA KIIMANI', Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu !

Waminywa huu na nani, uhuru wa kiimani, Katiba au insani, jibu mnalo vichwani, Hapo ina kosa gani, katiba nijulisheni, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu !

Kadhalika rejeeni, moja tatu namba 'wani', 'USAWA WA SHERIANI', haki ya kila insani, Nao waminywa na nani, katiba au insani, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu !

Shekhe pale kizimbani, kupandishwa kulikoni, Mchungaji mitaani, yu 'apeta' ni kwanini, Hapo ina kosa gani, katiba nijulisheni, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu !

Moja nane kwa makini, kifungu 'a' durusuni, Waandishi kitanzini, watiwa sasa kwanini, Mwigamba muulizeni, vyema atakujuzeni, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu !

Pamwe na wenza safuni, walikamatwa kwanini, Japo kesi 'waliwini', wiki ya juzi kotini, Kilichowaminya nini, katiba au insani, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu !

Aidha likumbukeni, 'MWANAHALISI' si geni, 'linasota' kifungoni, hadi leo ni kwanini, 'UHURU WA KIMAONI', wa 'Bongo' u mashakani, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu !

Japo sasa i hewani, kifungoche dhukuruni, Redio yetu 'IMANI', 'ilisota' gerezani, Kwa ghaidhi ya insani, si sheria katibani, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu !

Mwisho nakukumbusheni, cha Njozi mwanazuoni,KITABU kilobaini, mauaji ya insani, Dawamu marufukuni, kwa amri yake 'Beni', Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu !

Usuli au kiini, cha tatizo katibani, Adala na si uneni, ya insani matendoni, Kwa yangu mimi maoni, jipya hasa silioni, Katiba mpya si hoja, hoja ni uadilifu !

Kwa kina tafakarini, kuhusu yangu maoni, Yapimeni 'kwa mizani', si 'kwa alosema nani', Kaditama kwaherini, wa Bara na Visiwani, Kalamu naweka chini, mwisho wa yangu maoni.

ABUU NYAMKOMOGI - MWANZA.

BUNGE LA KATIBA (KATIBA MPYA SI HOJA!)

Page 13: ANNUUR 1112

13 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 14-20, 2014Makala

MWAKA 2013 ulimalizika kwa kali ya aina yake katika medani za siasa hapa nchini Tanzania, hasa baada Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoa Rasimu ya Pili ya Katiba mpya ambayo ina ibara 271.

Katika ripoti ya tume hiyo ambayo ilikabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein, hakuna kitu kilichovuta hisia za watu wengi na kusubiriwa kwa hamu kama suala la mundo wa Muungano wa Tanzania.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Warioba katika hotuba yake fupi aliyoitoa katika viwanja vya Kareemje, alikiri kuwa suala la muundo wa Muungano wa Tanzania ndilo lililoipasua kichwa Tume hiyo.

Kwa kauli yake Tume hiyo ilichukua muda mrefu katika kuyafanyia uchambuzi maoni ya wananchi yaliyokusanywa na Tume hiyo juu ya suala la muundo wa muungano na kulazimika kufanya utafiti zaidi.

Kama hiyo haitoshi katika kujiridhisha juu ya suala la muundo wa muungano, Tume hiyo ililazimika kupitia ripoti za tume na kamati mbalimbali zilizoundwa na kutoa mapendekezo juu ya suala la muungano, kama vile Tume za Jaji Kisanga, Tume ya Amina, Tume ya Shelukindo na nyenginezo.

Jaji Warioba alihitimisha kutoa matokeo ya maoni ya Watanzania juu ya muundo wa muungano ambapo kwa Zanzibar asilimia 0.1 (ambazo ni sawa na watu 25) walipendekeza serikali moja, asilimia 34 walipendekeza serikali mbili na asilimia 60 walipendekeza serikali ya mkataba.

K i n a c h o s h a n g a z a n i kwamba wapo baadhi ya watu ambao kwa fikira zao na wanavyojihisi kuwa wao ni Wazanzibari zaidi kuliko wengine huku wakisema suala la serikali tatu katu asilan, abadan haliwezekani, huku wakiapa kul inda mfumo wa serikali mbili uliopo, ambao umechokwa na Wazanzibari.

K i n a c h o s u m b u a k i l a ukiwafikiria watu hawa unajiuliza masuala mawili mawili, hivi kweli wana udhati wa kuipenda Zanzibar? Ama wanashikilia suala la serikali mbili kuendeleza maslahi yao binafsi na wale wanaowatuma kufanya hivyo?

Wakati Rais Jakaya Kikwete akihitimisha matembezi ya maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi, yaliyoratibiwa na Umoja wa Vijana wa CCM pale katika viwanja vya Maisara, viongozi wa umoja huo walikula yamini kuendelea kulinda mfumo wa serikali mbili.

N i l i k u w a p e m b e n i kusikiliza kwa makini sababu za vijana hao kwanini waseme

Serikali tatu ni hatua ya ukombozi kwa ZanzibarNa Alghaithiyyah,

Zanzibar

tuendelee na serikali mbili, lakini nilikuja kubaini kuwa wao ni makuwadi wa kisiasa ni watumwa wa kundi fulani ambalo linapenda liendelee kuwa madarakani kwa manufaa binafsi kama vile suala la ulua limekuwa teule kwao kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

N a t h u b u t u k u w a i t a makuwadi wa kisiasa kwa sababu ni mambumbu, wenye ufinyu wa mawazo, uwezo na upeo mdogo wa kifikiri, kwa ujumla nilibaini wanaugua maradhi yaitwayo ‘ufinyu wa mawazo’.

Katika ripoti yake Jaji Warioba ameainisha sababu kadhaa za kimantiki na sio zile za kiporojo kwanini Tanzania iwe na mfumo wa serikali tatu na sio mbili kama ilivyo hivi sasa au serikali moja ambayo maoni yake hapa Zanzibar yalitolewa na watu 25 tu, sina shaka hawa ni watu wenye asili ya Tanzania bara.

S i k u w a n a s h a k a kuwa UVCCM na wale w a n a o w a t u m a h a p a Zanzibar wanaugua gonjwa la ‘uoni finyu’, kwani dalili kubwa ya kuugua ugonjwa huu ni kushindwa kutoa sababu za kimantiki ambazo tutazikubali Wazanzibari kwanini tuendelee muundao wa serikali mbali.

I p o h o j a n y e n g i n e inayoendelea kutumiwa na wahafidhina wanaotaka ser ika l i mbi l i nayo n i kutokwenda kinyume na mawazo ya marehemu walioasisi muungano mzee Abeid Amani Karume na Mwalimu Nyerere.

Hi i n i ho ja ya kama wale waliopigiwa mifano katika kur-ani, hawajui wanachokifanya au waliodai kufuata waliyowakuta nayo babu zao wakaambiwa na Kuran, hata kama babu zao

walikuwa wajinga au hawajui kitu? Hivi jamani mpaka lini tukiwa katika karne hii tutaongozwa na fikra za tuliokwisha kuwazika na sasa ni hitma tu juu yao?

Wanasahau kuwa mzee Karume alipokuwa akielezea madhila ya muungano wa serikali mbili aliwahi kutamka kuwa ‘koti likikubana livue’, akimaanisha uwezekano wa kujitoa kwenye muungano wa serikali mbili wenye mizengwe.

K w a u p a n d e w a k e marehemu Nyerere wakati alipokuwa hana jinsi ya kuzima kasi ya wabunge waasi G55 mwaka 1993 w a l i o k u w a w a n a t a k a Tanganyika yao, aliwatuliza kwa kile kilichoelezwa kuwa muelekeo ni kutoka serikali mbili kuelekea moja.

Lakini ni sababu zipi h a s a z i n a z o t u f a n y a t u e n d e l e e k u ya a b u d u , kuyaenzi, kuyanyenyekea na kuyaendeleza mawazo ya wafu?

Wazanzibari wamechoka na mfumo wa serikali mbili kwa sababu hautoi haki, i n a k u w a j e M u u n g a n o ujipanue unavyotaka kuchota mamlaka ya Zanzibar, wakati Zanzibar ikigusa tu wanakuja juu, suala la muungano huu pia limewakera baadhi ya viongozi wa Zanzibar.

Nimepitia kitabu cha Rais wa Pili wa Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi kiitwacho ‘The Partner - Ship’, katika kitabu hicho inaonekana wazi mzee huyo hakuwa muumini wa serikali mbili na amebainisha wazi kuwa katiba ya muda ya mwaka 1965 ilikuwa na vipengele vilivyoeleza Tanzania kuwa nchi ya shirikisho kwamba kuna ser ikal i ya Muungano, serikali ya Zanzibar na serikali ya Tanganyika.

Kilichosababisha Mzee Jumbe kulazimisha kujiuzulu kutokana na msimamo wake wa kujenga hoja za kisheria akisaidiwa na aliyekuwa mwanasheria Bashir Swanzy juu ya kuvurungwa kwa mambo ya muungano wa serikali mbili na Nyerere.

Katika kitabu hicho mzee Jumbe anabainisha wazi kuwa suala la mvurugiko katika muungano wa serikali ni njama za dhahiri za kuwamaliza Wazanzibari n a z i l i a n z a b a a d a ya kupitishwa katiba ya mwaka 1977 inayotumika hadi leo ambayo ilipitishwa na wafuasi wasiotetereka wa Chama Cha Mpainduzi.

Hili la katiba ya mwaka 1977 kutogusia suala la shirikisho pia lilielezwa na aliyekuwa mwanasheria wa serikali ya Muungano Joseph Warioba ambaye alinukuliwa na gazeti la Daily News la Machi 16 mwaka 1982 alipokuwa akijibu hoja za Prof. Srivastava.

Akinukil iwa al isema, “ N i n a wa s i wa s i k u wa Profesa alikuwa akitizama katiba ya mwaka 1977 katika mtazamo wa kishirikisho ambapo ungeweza kuwa na serikali tatu tofauti. Nina hakika waliotunga katiba ya 1977 hawakuwa na mawazo hayo vichwani mwao”.

Lakini pia kilichomponza mzee Jumbe ni unafiki waliokuwa nao Wazanzibari kwamba aliandika barua ambayo ilikuwa iwasilishwe kwa Nyerere kwenye vikao halali, lakini cha kushangaza barua hiyo ilitua mikononi mwa Julius Nyerere wakati yeye mwenyewe ameiacha kwenye kabati la Ikulu ya Zanzibar.

Nyerere kama kawaida yake katika kikao cha NEC wakati anataka kummaliza mzee Jumbe aliisoma barua h i y o m a e n e o a m b a y o yalikuwa na faida kwake, kwamba hakutoa nafasi ya Jumbe kujitetea wala wajumbe wa NEC kupewa n a k a l a z a b a r u a h i y o kuisoma na kukifahamu kile kilichokuwa kidaiwa na Jumbe.

K a m a w a p o w e n y e k u k u m b u k u m b u b a s i wakumbuke katika mwaka 1995 katika viwanja vya Malindi akihutubia mkutano m k u b wa wa h a d h a r a , Dk. Salmin Amour Juma alivyochoshwa na visa vya Nyerere na muuungano kwa ujumla alimfuata Butiyama kumuuliza kama anataka Muungano uendelee au hataki.

Ghadhabu za Dk. Salmin zilikuwa wazi hadi kufikia kusema hakuna cha baba wa taifa wa babu wa taifa. Sishangai UVCCM wakati ule walikuwa ama hawajazaliwa au hawajui kitu lakini basi ata kuisoma historia pia hamtaki.

Kwa upande mwengine w a p o w a n a o h o f i a Wazanzibari watakufa njaa endapo tutatoka katika mfumo wa serikali mbili. Swali, kwani Watanganyika ndio walipewa ufunguo

wa riziki za Wazanzibari? Mbona wanatuuzia mchele wa Kiyela ghali kuliko ule unaotoka Thailand, Pakistan, India na China.

Mbona saruji inayotoka Oman na Urusi rahisi kuliko ya Wazo Hill ama kiwanda cha Tanga Cement. Mbona vitunguu thomu vya India rahisi kuliko vya Tanzania bara. Nguzo ya uchumi wa visiwa duniani ni uingiza bidhaa zaidi ‘importation’ k u l i k o k u s a f i r i s h a ‘exporta t ion’ . Kwanini liwasumbue vichwa enyi wenye mawazo mgando?

Mwanafalsafa Aristotle, alipokuwa akitoa tafsiri ya maana neno ujinga, alisema ujinga ni kutokuwa na habari za undani juu ya kitu fulani ama ‘to be a mere lack of information’, hili ndilo tatizo la UVCCM na CCM kwa ujumla wake.

Dunia imebadilika na hii si jamii ya Wazanzibari ambao wanatosheka na sababu kuambiwa waendelee na mfumo wa serikali mbili eti kwa sababu tu sera na ilani zinaeleza hivyo. Wazanzibari wanafahamu kuwa sera na ilani sio misahafu kutoka kwa Mungu.

Hawaoni jinsi Zanzibar ilivyokaliwa shingoni kama ngoma ya kimanga haupumui kwa kila kitu si kwa uchumi, siasa, utamaduni, diplomasia. Mbona wanaCCM wenyewe wanalalamika chini kwa chini kulichoka suala la Rais wa Zanzibar kuchaguliwa Dodoma?

Sera ya amani na utulivu si ya CCM, hiyo ni sera yenye uasili wa Wazanzibari tangu zama za kale nashangaa hivi sasa kuwa kufanywa ndio dira. Msingi wa amani na utulivu unatokana na wananchi na sio nguvu za kisiasa.

Angalizo liliopo ambalo linapaswa kungaliwa kwa makini ni kwamba hata Zanzibar iwe na siasa safi kiasi gani, hata iwepo amani na utulivu kiasi gani, bila ya uchumi imara ambao mizizi na mihimili yake imekaliwa na serikali ya muungano ipo siku amani na utulivu huo utatoweka bi la ya kipingamizi.

S u a l a l a u c h u m i n i muhimu na likiwezekana hilo ndipo amani na utulivu utakapodumu lakini kama m n a s i s i t i z a a m a n i n a utulivu mnajilia kuku huku wananchi wakishinda hata kupata kishina cha muhogo hapo litatokezea tatizo.

Tungalie kwa makini majanga yanayotunyemelea ikiwemo lile la kujaliwa kuwa na vijana ambao hawana ajira, na haiwezekani vijana hao kupata ajira endapo uchumi utataendelea kuwa na serikali mbili.

Kwa wale wanaodhani kuwa Wazanzibari wamelala wanakosea, Wazanzibari wanaona mbali, Wazanzibari wanaona mbele na sio kama ng’ombe anayeona mbele haoni mbali.

HAYATI Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Page 14: ANNUUR 1112

14 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 14-20, 2014Makala

H A P A N A S H A K A k i l a a l i y e s o m a a u kusikiliza ile simulizi ya mama wa Kiislamu aliyekuwa Masjid Mussa, Mombasa atasikitika na kupandwa na ghadhabu. Maelezo ya mama huyo tul iyachapisha wiki iliyopita ukurasa wa 3 ikiwa na kichwa cha habari, “Mama aliyekuwepo Masjid Mussa aeleza kilichotokea.”

Baada ya kuelezea kwa urefu kilichojiri na yaliyosemwa na vyombo vya dola vya Kenya, sasa hebu tuanga l i e upande wa pili . Kwa maana ya kutumia jicho pevu kufanya tathmini, uchambuzi na kuona iwapo Waislamu walipatia au kuna tatizo.

Siku kadhaa kabla ya kufanyika muhadhara h u o u l i o l e t a m a a f a makubwa kwa Waislamu, kulisambazwa kipeperushi kuhimiza watu kufika.

Katika sehemu moja k i p e p e r u s h i h i c h o kinasema:

“Alhamdulillah Jihad haiko mbali sasa, na Inshaallah maadam ma-Ikh’wa wameshaanza kuwauwa majasusi, dalili ya kuanza Jihad Kenya zaanza kudhihiri.”

K i s h a k i p e p e r u s h i kikaeleza kuwa vijana wa Jihad wamemuuwa adui wa Uislamu (Ahmed Abdullah Bahshuweiny.)

Juu ya kipeperushi h i c h o i k a c h a p i s h wa p i c h a y a A h m e d Abdullah Bahshuweiny, waliyedai kuwa adui mkubwa wa Waislamu na hivyo ikatajwa kuwa aliuliwa na Mujahidina na kwamba mkusanyiko wa Masjid Mussa siku ya Jumapili, ilikuwa ni katika kujenga umoja wa vijana wanaopenda Jihad na kuweka mikakati na mipango ya kuwauwa makafiri na maadui wa Uislamu.

M o j a y a m a d a z i t a k a z o z u n g u m z wa i k a t a j w a k u w a n i “A h k a m u l - J i h a d ” . Nyingine ni “Hukumu ya Shaheed.”

Kipeperushi kikaandika chini ya picha ya Ahmed Abdullah kuwa “Allah a w a h i f a d h i ( v i j a n a wapenda Jihad) wenye kufanya kazi hi i (ya kuwauwa watu kama Ahmed) na awape nguvu juu ya makafiri.”

I l i k u h a k i k i s h a wanapatikana watu wengi, k i p e p e r u s h i k i k a t o a motisha, kikasema:

Huu ni ujasiri au ujinga

“Vijana wamejitahidi k u p a t i k a n e c h a k u l a cha saa sita kwa kila atakayehudhuria.”

Na kwel i p i lau na ubwabwa kwa wapenda wali mweupe ukapatikana ukivutia vijana na watoto wadogo wengi. Na wote hawa wamekombwa na kuwekwa ndani wakiitwa magaidi ukiacha wale waliouliwa na wengine kuondoka na v i lema kutokana na risasi.

An nuur imejitahidi kupata habari za huyu A h m e d A b d u l l a h Bahshuweiny. Taarifa za ndugu zake wa karibu na marafiki zake zinasema kuwa huyu bwana Ahmed Abdullah Bahshuweiny, ni afisa wa ngazi ya juu wa polisi kituo cha Malindi n a k wa m b a a l i k u wa a k i k a r i b i a k u s t a a f u (taarifa nyingine zinasema alishakuwa katika orodha ya askari wa akiba).

Lakini pia anatajwa k u w a n i M u i s l a m u aliyekuwa aki j i tahidi kutekeleza Uislamu wake wa nguzo tano.

Sifa yake kubwa ni kuwa alikuwa akiwabana sana watu wa unga (madawa ya kulevya) na majambazi walioingia eneo la Malindi.

Watu wa karibu yake wana mawazo kwamba yawezekana aliuliwa na hao watu wa unga na majambazi kulipiza kisasi. Hili linapewa uzito na watu wengi japo hakuna ushahidi.

I l a p o l i s i w a o wameligeuza kuwa ni

Mujahidina waliomuuwa, j a p o h a k u k u w a n a kikundi cha Waislamu w a l i o k i r i k u h u s i k a mpaka kiliposambazwa kipeperushi cha kuita Waislamu Masjid Mussa.

Lakini zipo taarifa za uhakika pia kuwa alikuwa a k i t u m i k i a I d a r a z a Kikachero za FBI na Polisi wa Kupambana na Ugaidi Kenya (ATPU).

Mr Ahmed Bakswein, (61) al iuliwa siku ya Jumanne ya tarehe 28 Januari katika mji wa Malindi.

A l i k u wa n d a n i ya gari yake, watu wawili wal iokuwa na s i laha wakiendesha pikipiki, wakampiga risasi wakati wanapita gari lake.

K w a n a f a s i h i y o ya kufanyia kaz i za u k a c h e r o i d a r a z a ATPU na FBI, inadaiwa kuwa amehusika katika operesheni zilizofanyika k u wa a n d a m a v i j a n a wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Al Shabab katika mji wa Malindi.

K w a m u j i b u w a taarifa ya Kamanda wa Polisi, Malindi, Kiprono Langat Mr Bakswein al ishambuliwa akiwa katika mzunguko (round about) wa barabara ya M a l i n d i - G a r s e n n a kwamba washambuliaji hao walikuwa na bastola.

Kufuatia tukio hilo, kijana mmoja wa Kiislamu aliyetajwa kwa jina la Ali Mohammed a l iu l iwa kwa kupigwa risasi na polisi ikidaiwa kuwa

ni katika waliohusika kumuuwa Ahmed Abdalla Bakshueni.

Anti-terror police unit (ATPU) wanadai kuwa Ali Mohammed Delawa mkazi wa Msambweni, ni katika watu muhimu katika kundi la Al-shabab na Al-Qaeda.

Sasa labda tujiulize: kama wal io i ta darsa na muhadhara ule ni katika waliopanga na kutekeleza mauwaji ya Afisa wa Polisi, Ahmed Abdullah Bahshuweiny; m t u m w e n y e a k i l i t imamu na anaye jua analolifanya, anaweza kufanya mauwaji kama yake halafu akatangaza k a t i k a k i p e p e r u s h i kwamba ndiye aliyehusika na kuitangazia polisi na serikali kwamba atakuwa msikiti fulani siku fulani?

Kama suala ni ujasiri na kwamba haogopi, kwa nini basi baada ya kuuwa asikae hapo na kusubiri polisi waje wamkamate au apambane nao?

Je, alichokusudia mtu huyo au walichokusudia watu hao katika kuita Waislamu Masjid Mussa, na kuwahamasisha kwa pilau; ni kuwaelimisha juu ya Uislamu/Jihad au kuwakamatisha?

V i p i W a i s l a m u waliohudhuria! Wewe m t u a n a k u t a n g a z i a k u wa k a u wa p o l i s i , k wa s a b a b u y o y o t e itakayo kuwa, halafu anakutangazia kuwa uje ili mpange mikakati na kuhamasishana namna

ya kuuwa polisi zaidi n a m a a d u i we n g i n e wa Uislamu: Ukienda utasema hiyo ni akili au ujinga? Utasema uliendea Jihad/Uliitiwa jihad au maangamizi?

Sasa haya ndiyo mambo tunayotahadharishana k w a m b a “ u j i n g a n i mzigo”. Na kutokana na ujinga mwingi, Waislamu wanajikuta wakinaswa kwa wepesi na kujiletea maafa kwa mikono yao wenyewe.

Masj id Mussa pale vijana wabichi, nguvu kazi wanaotegemewa n a f a m i l i a z a o n a Uis lamu wameuliwa. Watoto wadogo kabisa wamejerujiwa. Wanawake wameumizwa na kusota r u m a n d e . Wa i s l a m u wamepata nini? Uislamu umepata nini?

K a m a a s k a r i y u l e alikuwa kauliwa na watu wa biashara za madawa ya kulevya kama wengine wanavyotuhumu, kwa tukio la kipeperushi na Waislamu kuitikia wito wa kipeperushi, sasa wauwaji wa polisi ni Waislamu. Na inawaweka katika mazingira magumu zaidi kutokana na propaganda za kuwatangazia ugaidi.

Y a p o y a l e y a k u w a b a m b i k i z i a Waislamu silaha, mtu unaweza kujitetea na Wa i s l a m u w e n z a k o watasimama nawe na hata wapenda haki duniani kote. Sasa na hili la kuitwa na kipeperushi Muislamu unajitetea vipi?

H e b u t u j i t i z a m e madhaifu yetu na matatizo yetu ya ndani, na hasa hili la elimu na ufinyu wa uelewa mambo. Jazba na mihemko hailipi.

Mtu atakutangaziaje k u wa k a t i k a ‘ J i h a d ’ anayofanya kauwa polisi, na unajua ni kweli kuna polisi kauliwa na watu wanasakwa na Muislamu m w e n z e n u m m o j a kashauliwa kwa sababu hiyo, anakuita ndani ya msikiti muweke mikakati ya kupambana zaidi na polisi, halafu unakwenda!!!

Je, huo utaita ujasiri au ujinga? Hiyo itakuwa jihad au maangamizi?

Ukiyatizama yote haya utaona kuwa makachero wa serikali, wametumia tukio la kuuliwa Ahmed Abdullah Bahshuweiny, kuwanasa Wais lamu, k u f a n ya h u j u m a n a kujenga hoja ya kuendelea kuwabamiza Waislamu.

POLISI wa Kenya walipovamia Masjid Mussa, Mombasa.

Page 15: ANNUUR 1112

15 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 14-20, 2014Makala

WAANDISHI wote wa historia wameshuhudia juu ya Ucha Mungu w a k e , u a d i l i f u n a huruma yake, pamoja na uwezo wake mkubwa wa kuongoza kwa haki na kuibadilisha hali ya umma kutoka katika umasikini uliopindukia na kuiweka katika hali n jema inayoendelea kuzungumziwa mpaka wakati wetu huu.

Huyo si mwengine ila ni Omar bin Abdull Aziz, ambaye baadhi ya wanazuoni wanamuita kuwa ni Khalifa wa tano baada ya wale wanne wakubwa, ambao ni Abuu Bakar, Omar, Othman na Ally (Rehema za Allah ziwe juu yao).

A l i k u w a

Omar Bin Abdul-AzizAliondoa umasikini kwa miaka miwili

Na Rashid Abdallah, MUM

a k i w a t a h a d h a r i s h a magavana wake katika utumiaji wao wa mali na akiwanasihi hata katika utumiaji wa kalamu na mishumaa inayowashwa bila sababu.

Alihakikisha kuwa kila dirham inatumika mahala pake bila ubadhirifu, na kwa njia hii akaweza kuzibadilisha nyuso za huzuni za watu masikini na kuzifanya ziwe za furaha, kwani haukupita muda mrefu tokea pale alipotawala, Wizara ya Mali ya Waislamu (Baytul maal ) ikafur ika kwa wingi wa mali, na Omar akawaandikia magavana wake barua na kuwataka kutekeleza yafuatayo.

“Kila mtu lazima awe na nyumba ya kulala, farasi wa kupanda, vifaa vya nyumbani (furniture), mwenye deni alipiwe deni lake, watumwa na mateka w o t e wa k o m b o l e we , mayatima wadhaminiwe maisha mema, asiyeoa aozeshwe, na ikiwa mali itatosha basi ni vyema, ama isipotosha nijuulisheni nipate kukutumieni mali zaidi ili muweze kutimiza haja za Waislamu”.

A k a t o a a m r i y a

kuwatosheleza maulamaa kwa kila wanachokitaka ili waweze kujishughulisha na kazi ya kuwafundisha watu dini yao.

Ikafika hadi matajiri w a k a t i m w i n g i n e wanatoka na mali yao ya Zaka na hawapati masikini wa kumpa mali hiyo wala hawapati mtu wa kunyoosha mkono wake kupokea mali hiyo.

Na hii ni kwa sababu U a d i l i f u w a O m a r haukuondoa umasikini tu, bali uliwaletea watu heshima ya nafsi zao, wakawa wanaona haya kunyanyua mikono yao kwa aj i l i ya kupokea mali ya Zakaa au kuwa ombaomba.

Alikuwa akisema;“Wallahi kama haki

haiwezi kusimama na batili kuondoka ila ikatike mikono yangu na viungo vyangu na matumbo yangu, basi nitafanya h i v y o n a m i n i k i w a mwenye furaha”.

Na akasema pia“Wal lahi lau kama

nitaishi nanyi kwa muda wa miaka hamsini, basi sitojishughulisha na jingine isipokuwa kuusimamisha uadilifu.”

H u y o n d i ye O m a r Bin Abdull Aziz, cha kushangaza kama s i kufurahisha hayo yote aliyafanya ndani ya miaka MIWILI TU.

Historia hii ya Omar ni nzuri sana kwa viongozi wa sasa wa Tanzania na hata Duniani haijalishi uwe Muislamu ama siyo Muislamu.

Chakuzingatia ni kuwa aliyeondosha umasikini kwa miaka miwili ni Binaadamu kama wewe.

Siku moja Fatima binti Abdul Malik mke wa Omar bin Abdul Aziz alipoingia chumbani na kumkuta mumewe akiwa juu ya msala akilia.

“Alimuuliza; 'Mume wangu una nini mbona unalia namna hii? Omar akamjibu;

“ Ewe Fatima! Mimi nimepewa jukumu kubwa katika jambo hili. Nawaza juu ya fakiri mwenye njaa na mgonjwa asiyejiweza, n a y u l e a s i y e k u w a n a n g u o y a k u v a a , na yatima asiyekuwa n a w a k u m t a z a m a , aliyedhulumiwa asiyeweza kujitetea, mgeni asiyekuwa na pa kulala na mateka na wazee na vizuka na

wale wenye watoto wengi wasiokuwa na chakula cha kuwatosha na wengine wa mfano wao waliojaa duniani. Nimewaza juu ya hao wote nikatambua kuwa Mwenyezi Mungu a t a n i u l i z a k u h u s u hao siku ya Kiama, na a t a k a y e wa t e t e a h a o dhidi yangu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu M u h a m m a d ( S wa l l a Llaahu ‘alayhi wa sallam). . Nimewaza yote hayo n ikaogopa ho ja i s i j e ikathibiti dhidi yangu siku ya kiama, kwa ajili hiyo ninalia.”

Viongozi wetu wanalia kwa kuwafikiria masikini waliopo Tanzania?

Kule kuneemesha watu wote katika utawala wa Omar ibn Abdul Aaziz, kuliwafanya watu wasiwe na uhitaji, na kufanya Zaka inayokusanywa isiwe na maskini wakupewa, na kwa hivyo zikatumika Zaka kwa mambo ya maendeleo.

N i m a l i z i e k w a k u w a k u m b u s h a aya h i i ya Qur aan , nafikiri itawanufaisha Waislamu na wasiokuwa Waislamu

“ H i y o n y u m b a ya akhera tutawafanyia wale wasiotaka kujitukuza katika ardhi wala (kufanya) u f i s a d i , n a m w i s h o (mwema) utawathibitikia wacha – mungu”. {Al qasas – 83}

Jinsi nilivyoweza kuwa mwanamke wa HijaabInatoka Uk. 16

Mwezi wa Ramadhani ul ipokwisha ni l ipata muda wa kutosha kufikiri na kujiuliza, kwanini navaa hijab katika mwezi wa Ramadhani pekee na sio muda wote? Kuanzia hapo nilianza mwenyewe kujizoesha kuvaa hijab kila nilipotoka nyumbani.

Siku hizi siwezi hata kutoka nje bila kuwa na hijab na sijisikii raha nikiikosa.

Hijab imekuwa sehemu ya maisha yangu na inanipa hamasa na ufahamu mimi ni nani na nini lengo la kuumbwa kwangu hapa duniani.

Nilikuwa nikivaa kama wanavyovaa wanawake wengi wanavyovaa katika mj i . Nimekul ia j i j in i Dar es Salaam. Nilihisi naonekana wa kisasa (up to date) kwa fasheni, lakini nimekuja kutambua

kwamba nilikuwa napiga hatua kwenda nyuma kwa kuendekeza msemo wa kijinga “FREEDOM” lakini uhuru bila nidhamu ni vurugu.

Nil ikuja kugundua kwamba hijab inamweka mwanamke huru dhidi ya dhana ya kuonekana kama chombo cha matamanio na starehe au kuthaminishwa kwa jinsi anavyoonekana, au umbo lake badala ya fikra na weledi wake.

Leo siwezi tena kuwa mtumwa wa utumiwaji. Hijab imenistaarabisha kutoka mtu wa kuiga yasiyowiana na uhalisia, unyanyasaji na kupewa majina machafu na taswira zinazoenezwa na vyombo vya habari.

K u v a a h i j a b kumeonyesha kuwa kuvaa vizuri na kufunika nywele z a n g u , k u m e o n d o a usumbufu wa kimapenzi katika maeneo mengi

ambayo nachanganyika na watu wa jinsia tofauti.

Naz i jua baadhi ya familia au wanawake wanaofuata tamaduni wanalazimishwa kuvaa hijab lakini hii si njia sahihi.

Qur'an imeeleza wazi k wa m b a k a t i k a d i n i hakuna kulazimishana (Q 2:256). Wanawake wanaoamua kuvaa hijab wamekuwa hawafanyi uamuzi huo kirahisi.

H a k i k a wa n a wa k e wengi wanathibitisha k wa m b a wa m e k u wa wakikumbana na upinzani mkubwa kutoka katika f a m i l i a z a o z i we z a Waislamu au zisizokuwa z a K i i s l a m u , p a l e wanapoamua kujistiri.

Duniani kote kumekuwa na mifano kadhaa ya wanawake wakitetea haki yao ya kuvaa hijab.

L a k i n i n a t a k i w a kukumbuka na kufikiri

mara kwa mara kwamba hijab haitakiwi ionekane kama ni nguo tu ya kufunika kichwa changu. Bali ni alama ya utu na sio nguo tu kwa ajili ya kujipendezesha.

Maana yake inapanuka zaidi hadi kuhusu tabia ya n g u . S i we z i wa l a sijawahi kufikiri kwamba imani ya mwanamke kwa Mungu wake mmoja inapimwa kwa vazi lake, lakini sasa natambua raha na uhuru wa kweli ninaopatiwa na Hijab.

Hijab inatulinda kuliko kitu chochote na nina furahia sana kuivaa kuliko ilivyokuwa hapo awali.

Siku ya hijab duniani ni wazo zuri kwasababu wanawake wanawajibika katika hijab. Tunaipenda na tunafanya hivyo kwa ajili ya Allah (SWT). Ni jukumu letu kwa imani yetu, kwa Muumba wetu na bwana wetu.

Inafahamika vyema

kwamba sisi wanawake wa Kiislamu ni viumbe wanaovutia. Mwenyezi M u n g u a n a p e n d a tujihifadhi kwa hijab zetu. Hijab ni ulinzi wetu wa nje dhidi ya uovu wa maisha.

H a k u n a m t u anayetukandamiza na dunia inahitaji kuona kuwa hatuhitaji kuokolewa au kuwekwa huru. Ndio maana msingi huu ni bora kabisa na ninauunga mkono kwa asilimia mia moja na utawasaidia wanawake wasiokuwa Wa i s l a m u k u o n a n i namna gani tunajisikia hasa kwa kuvaa vazi hili tulilolichagua kulivaa.

Nikiwa mwanamke wa Kiislamu ninatambua kuwa vazi hili sio nguo tu ya kuvaa, lina maana nyingi kwetu na tunatumaini litawasukuma wanawake wengine kuelekea katika hali ya kujiweka vizuri wenyewe, Insha Allah.Mrs. Mwanaidi Mohamed Ali.

Page 16: ANNUUR 1112

16 AN-NUURRABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 14-20, 201416 MAKALA

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works LTD, S.L.P. 4605, Dar es Salaam.

AN-NUUR16 RABIUL THAN 1435, IJUMAA FEBRUARI 14-20, 2014

Soma AN-NUUR

kila IjumaaM A K A M U w a K wa n z a wa R a i s wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif H a m a d , a m e s e m a wakati umefika kwa Wizara ya Kat iba na Sheria kuandaa sera itakayozingatia maslahi ya walimu w a m a d r a s a , i l i kuthamini juhudi zao za kuwafundisha watoto.

Maalim amesema, walimu wa madrasa wana kazi kubwa ya kuisaidia jamii katika malezi na kuwajenga wato to k imaadi l i , hivyo hakuna budi kuthaminiwa kwa kazi hiyo ambayo muda w o t e w a m e k u w a w a k i i f a n y a k w a kujitolea.

A k i z u n g u m z a katika hafla ya maulid ya k u z a l i wa k wa Mtume Muhammad (SAW) yaliyoandaliwa n a m a d r a s a t - M u u m i n I s l a m i ya ya Muembeshauri , Maalim Seif amesema hatua hiyo itasaidia kuwapa moyo walimu hao na kuzidisha ari ya kufundisha.

K w a u p a n d e mwengine Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesisitiza suala la umoja na mshikamano miongoni

Wizara ya Elimu yatakiwa kuwa na sera ya madrasa

Wito wa Maalim Seif maulidini AlabamaHazina ya maadili, historia itiliwe mkazo

mwa wananchi , na kuwashauri viongozi wa k i jami i kuacha tabia ya kutoa kauli zinazoweza kuchochea chuki miongoni mwa wanajamii.

Aidha amesisitiza haja kwa wanajamii k u h i m i z a n a n a kukumbushana juu ya kulinda mila, silka, kuuenzi na kuuendeleza utamaduni wa Zanzibar.

A m e f a h a m i s h a kuwa katika kuuenzi utamaduni na silka za Wazanzibari, hakuna b u d i k w a w a z a z i kuwasomesha vizuri watoto wao, ili wajue elimu zote pamoja na historia ya utamaduni wao.

A m e o n y a k u w a iwapo juhudi hizo za kuwaelimisha watoto hazitoungwa mkono na jamii nzima hasa katika ngazi za familia, jamii

itaendelea kushuhudia mporomoko mkubwa wa maadili, ikizingatiwa kuwa sehemu kubwa ya malezi iko katika ngazi ya familia.

Katika kuunga mkono juhudi za madrasa hiyo, Maalim Seif ameahidi kutoa kompyuta mbili pamoja na mifuko ya saruji kwa ajili ya kuiendeleza madrasa hiyo.

M a p e m a a k i s o m a risala ya madrasa hiyo ustadh Baiya Maulid, amesema madrasa hiyo iliyoanzishwa mwaka 1995, kwa sasa inakusudia k u a n z i s h a m i r a d i itakayosaidia kukidhi mahitaji ya kuendeleza madrasa yao.

A m e s e m a t o k e a k u a n z i s h w a k w a madrasa hiyo wameweza kupata mafanikio mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha jengo la madrasa, kuhifadhisha kur’an, pamoja na kukuza mashirikiano baina ya walimu na wazazi.

Hata hivyo wamesema b a d o wa n a k a b i l i wa na changamoto nyingi zikiwemo uchakavu wa vifaa vyao vya ofisi pamoja na kutaka kunyanyua jengo lao.

Hivyo wameiomba s e r i k a l i p a m o j a n a w a h i s a n i w e n g i n e kuweza kuungana nao katika kutatua kero hizo, ili kuwawezesha watoto kusoma katika mazingira mazuri.

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Maalim Seif Sharif Hamad

M W A N A I D I M o h a m m e d A l i ( p i c h a n i ) , n i m w a n a m k e a n a y e j i t a m b u a , a n a y e j i h e s h i m u n a a n a ye t h a m i n i jinsia yake ya kuwa m w a n a m k e n a kujihifadhi.

K u t o k a n a n a kujitambua kwake barabara na kujua thamani yake, Bi . Mwanaidi aliona kuwa anastahili heshma na utu.

Fikara yake inafikia

Jinsi nilivyoweza kuwa mwanamke wa Hijaabkatika vazi la hijab. Vazi la kumstiri, kumthamini na kumletea heshma mwanamke mahali popote awapo.

Ki fuatacho n i k i sa chake juu ya vazi la hijab alichokibainisha katika mtandao wake wa Tmark-turn na Jiko langu Blog. Kisa chake hiki chatosha kuwa somo na funzo kwa wanawake wengine wa Kiislamu na wasiokuwa Waislamu katika suala zima la umuhimu wa vazi la hijab.

Februari mosi ilikuwa

siku ya Hijab duniani. Na hii ni habari yangu jinsi gani nilianza kuvaa hijab.

Nilianza kuvaa hijab mwaka 2011, wakati huo ulikuwa ni katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na hata hivyo, lilikuwa j a m b o l a m a n u f a a zaidi ambalo sikuwahi kulifanya katika maisha yangu.

N i l i k u w a k a t i k a pandembili za shilingi. Kama mwanamke ambaye amezaliwa na kukulelewa katika ‘jamii ya kisasa’ kama walivyo Waislamu

wote, dini mara zote imekuwa ufunguo katika familia yangu, lakini nikuwa navaa hijab katika siku za sherehe za kidini pekee kama sherehe ya ndoa au kwenye Maulid n.k.

Baada ya kuolewa mwaka 2009 nilijaribu kuvaa hijab na jambo la kufurahisha, ni mume wangu ambaye alikuwa kila mara akinieleza kuwa nikivaa hijab naonekana mwanamke mzuri zaidi na mwenye heshima.

Inaendelea Uk. 15