annuur 1171a

20
ISSN 0856 - 3861 Na. 1171 JAMADIUL AKHER 1436, IJUMAA , APRILI 3 - 9, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu facebook: [email protected] AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST Mtume(saw) amesema, “…Mahujaji wanalipwa kwa kila walichokitumia katika Hija, shilingi moja kwa milioni moja.” Mali ya Muislamu huongezeka anapohiji! Unapata duniani na unafanikiwa Akhera. Wahi sasa kuja kulipa uitakase mali yako. Muda unakwisha! Gharama zote kwa Hijja ni Dola 4,500. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,300. Karibuni Ahlu Sunna Wal Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0765462022;0782804480; 0717224437. (5) TAJIRIKA KWA KUHIJI! Wawakilishi nusura wazipige Barazani Watambiana ucha Mungu, ubabe wa kisiasa PICHANI juu ni siasa za Zanzibar wakijeruhiana wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya mambo ya kisiasa. Picha chini mitutu ya vifaru vya Saudi Arabia vikielekezwa Yemen. Nchi zote hizo za Kiarabu. Siasa za mabeberu Iraq na Yemen Mashabiki wa Abu Baghdad mnasimama wapi! Kama Iraq ni tatizo la Shia kuzuiya Khilafah… Yemen napo Waarabu wanachopigania nini? Kwaheri Mahakama ya Kadhi Ni matokeo ya Kambi ya Maaskofu Dodoma Alisema kweli Mtwangi. Waislamu wajifunze Soma Uk. 2 Soma Uk. 10 Lipo Jinamizi Tutafute ulipo mzizi wa fitna Vijana hawa wanakwenda wapi? Haya yanafanyika bila serikali kujua? Soma Uk.7 Zanzibar watishiana Albadiri

Upload: zanzibariyetu

Post on 02-Oct-2015

3.887 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • ISSN 0856 - 3861 Na. 1171 JAMADIUL AKHER 1436, IJUMAA , APRILI 3 - 9, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

    Sauti ya Waislamufacebook: [email protected]

    AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST

    Mtume(saw) amesema, Mahujaj i wanalipwa kwa kila walichokitumia katika Hija, shilingi moja kwa milioni moja. Mali ya Muislamu huongezeka anapohiji! Unapata duniani na unafanikiwa Akhera. Wahi sasa kuja kulipa uitakase mali yako. Muda unakwisha! Gharama zote kwa Hijja ni Dola 4,500. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,300. Karibuni Ahlu Sunna Wal Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0765462022;0782804480; 0717224437.

    (5) TAJIRIKA KWA KUHIJI!

    Wawakilishi nusura wazipige BarazaniWatambiana ucha Mungu, ubabe wa kisiasa

    PICHANI juu ni siasa za Zanzibar wakijeruhiana wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya mambo ya kisiasa. Picha chini mitutu ya vifaru vya Saudi Arabia vikielekezwa Yemen. Nchi zote hizo za Kiarabu.

    Siasa za mabeberu Iraq na Yemen

    Mashabiki wa Abu Baghdad mnasimama wapi!Kama Iraq ni tatizo la Shia kuzuiya KhilafahYemen napo Waarabu wanachopigania nini?

    Kwaheri Mahakama ya KadhiNi matokeo ya Kambi ya Maaskofu DodomaAlisema kweli Mtwangi. Waislamu wajifunze

    Soma Uk. 2

    Soma Uk. 10

    Lipo JinamiziTutafute ulipo mzizi wa fitnaVijana hawa wanakwenda wapi?Haya yanafanyika bila serikali kujua?

    Soma Uk.7

    Zanzibar watishiana Albadiri

  • 2 AN-NUURJAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 3-9, 2015AN-NUUR

    S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.

    www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected] zetu zipo: Manzese Tip Top

    Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

    Tahariri

    TAMAA ya Waislamu k wa m b a s i k u m o j a wa n a we z a k u wa n a Mahakama yao ya Kadhi nchini, chombo ambacho kingekuwa suluhu ya hitilafu nyingi katika kutekeleza majukumu yao ya msingi ya kiibada na kimaadili, sasa ifikie kikomo.

    Pamoja na kwamba wapo watu ambao bado wa n a d h a n i k wa m b a masuala au matatizo ya Waislamu yanaweza kutatul iwa ndani ya mfumo wa sasa wa serikali yetu na vyombo vyake vya kimamlaka, lakini ukweli ni kwamba historia inadhihirisha kwamba katu haiwezekani jamii ya Waislamu kutimiziwa au kukubaliwa haja zao za kiimani ndani ya himaya ya watu waliofura chuki, ambao wengi wao ndio waliopo katika nafasi nyeti za maamuzi.

    Mwandishi mashuhuri wa makala, Mzee wetu Bw. Shaaban Khalid Mtwangi, siku za nyuma aliwahi kuandika makala yake kuhusu Mahakama ya Kadhi katika gazeti hili, akisema katu haiwezekani Mahakama ya Kadhi ikaanzishwa nchini kwa kuwa, i l i Mahakama h i y o i w e z e k u p a t a uhalali wa kuanzishwa n a k u t a m b u l i wa n a sheria ya nchi (katiba), ni lazima kwanza muswada wa kuanzishwa kwake upelekwe Bungeni na kuridhiwa na wabunge walio wengi.

    Kwa msingi huo, Bw. Mtwangi alisema kwa namna ambavyo sura ya Bunge letu ilivyo, a k i m a a n i s h a k u j a a wa b u n g e w e n g i wa imani ya Kikristo, na kwa kuzingatia ukweli kwamba kuna chuki kubwa ya kiimani iliyojificha ndani ya mioyo yao, kamwe h a wa w e z i k u k u b a l i kuupitisha muswada huo hata utakapofikishwa mbele yao.

    M z e e M t w a n g i alihitimisha kwa kusema, Waislamu wanapoteza m u d a w a o k u d a i mahakama hiyo ndani ya mfuno wa sasa wa kimamlaka na kidola

    Kwaheri Mahakama ya KadhiNi matokeo ya Kambi ya Maaskofu DodomaAlisema kweli Mtwangi. Waislamu wajifunze

    na akaona Wais lamu kuendelea kupambana katika mazingira haya kudumu katika matumaini kuwa watakubaliwa kuwa na chombo chao hicho kikatiba, ni kupoteza muda na nguvu za kufanya mambo mengine kwa maslahi ya Waislamu.

    Yeye alishauri kwamba kwanza uwepo mkakati wa kuhakikisha kwamba jamii ya Waislamu, nao wanakuwepo kwa namba inayor idhisha ka t ika v y o m b o v y a k i d o l a n a k i m a m l a k a h a s a Bunge. Hapo wanaweza kupambana uso kwa uso kusimamia heshima na maslahi yao ya kiibada.

    Tukitizama kwa kina alichokuwa akikieleza Mzee Mtwangi ndani ya makala yake hiyo, utagundua kwamba suala la kuanzisha Mahakama ya Kadhi nchini, ni mchezo wa kisiasa na hadaa tupu dhidi ya jamii ya Kiislamu nch in i l ak in i ukwel i wake ni kwamba haiwezi kukubaliwa iwepo.

    Suala hili limekuwa likipigiwa kelele kwa muda mrefu, limewahi hata kuingizwa katika Ilani ya CCM ya mwaka 2005.

    Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda, ambaye ndiye hasa aliyepewa jukumu la kusimamia mchakato wa kuanzishwa mahakama hii kwa upande wa serikali, pamoja na k u j a r i b u k u a n z i s h a mchakato huo kwa kuunda Kamati ya Pamoja ya Viongozi wa Jumuia za Kiislamu na serikali, bado yalifanyika madudu kwa kuanzisha Mahakama ya Kadhi ya Bakwata kule Dodoma.

    M a k a d h i a m b a o hawafahamiki kisheria ( k i k a t i b a ) , a m b a o walipatikana bila utaratibu wa Kiislamu na kibaya zaidi, yote hayo yalifanyika bila kuwepo mawasiliano na Kamati ya Pamoja iliyojumuisha serikali chini ya Waziri Mkuu, ambayo kimsingi ndicho chombo halali kichokubalika na Waislamu na ser ikal i kushughulikia suala hilo kiutaratibu.

    Tunaamini kwamba hadaa hii dhidi ya Waislamu

    ilifanyika huku kwa namna moja au nyingine serikali ikihusika chini ya mwavuli wa Makamu wa Kwanza wa Rais.

    Baadae likaja zoezi la mchakato wa kuwa na Katiba mpya. Waislamu wakaona hiyo ndiyo njia muafaka ya kuwasilisha hoja yao ya kurejeshwa Mahakama ya Kadhi nchini kikatiba.

    S o t e t u l i s h u h u d i a namna ambavyo Tume ya kukusanya maoni ya Katiba Mpya chini ya Jaji Joseph Warioba, ilivyotupilia kwa mbali maoni ya Waislamu juu ya kuhitaji mahakama hiyo, ambayo yameelezewa katika rasimu ya maoni ya wananchi Uk. 203 hadi 206, ambapo imeelezwa kwa upana namna wananchi walivyotoa maoni yao kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi.

    Serikal i kwa kuona hadaa imekithiri, ikaamua kufanya mjadala kati ya Kamati ya Viongozi wa Kiislamu na wajumbe wa Kamati ya Bunge, kuona namna gani wanaweza k u k i d h i v i g e z o v ya kuuwasilisha muswada wa kuingizwa kipengele cha Mahakama ya Kadhi katika Katiba Pendekezwa.

    Tuliona zoezi likifanyika kwa mvutano mkubwa huku Maaskofu na Mapadri wakija juu kupinga hatua hiyo k ias i cha kutoa Matamko kupitia jumuia zao. Baadhi ya Wakristo walipinga sana kukataa hatua hiyo. Hata hivyo serikali kupitia Waziri Mkuu Pinda, iliendelea kusisitiza kuwasilisha Bungeni mswada huo licha ya kuwepo kauli za kuukataa kutoka kwa viongozi wa Kikristo, baadhi ya Wabunge na watu wengi wasiokuwa Waislamu.

    Baadae tukashuhudia Maaskofu kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wakipiga kambi kwa zaidi ya wiki mjini Dodoma, kuhakikisha muswada huo hauingii Bungeni. Tunaambiwa zaidi ya Maaskofu 4O kutoka mikoa yote nchini, walikutana na wabunge katika ukumbi wa Kanisa La Kiinjili la Kilutheli (KKKT) mjini Dodoma kujadiliana suala la muswada wa Mahakama ya Kadhi. Katika mkutano huo Maaskofu walitoa azimio kuwa muswada huo usiwasilishwe Bungeni kwa kuwa kufanya hivyo i n a we z a k u h a t a r i s h a amani i l iyoko nchini . Maaskofu hao wanaounda J u k w a a l a K i k r i s t o Tanzania, waliwasili mjini Dodoma tangu mwishoni m w a w i k i i l i y o p i t a kuhakikisha wakiazimia kuwa wanafanya lobbing kwa wabunge Wakristo, kuhakikisha muswada h u o u l i o k u s u d i w a kuwasilishwa bungeni,

    haufaulu.Sote tumeshuhudia,

    wabunge karibu wote wa Kikristo kwa umoja wao, kila ilipojitokeza hoja juu ya muswada huo, walipinga vikali kiasi cha kusababisha Bunge kuvurugika licha ya Wabunge wachache Wa i s l a m u k u j a r i b u kushinikiza kuingizwa muswada huo Bungeni hapo.

    Hatimaye wiki hii Kambi yao ilifanya kazi yake. Wamefanikiwa kuifanya Serikali ishindwe kuingiza muswada bungeni. Suala la Mahakama ya Kadhi, ambalo lilizua mjadala mkali kwenye Kamati za Bunge la Bunge Maalumu la Katiba, likaundiwa Kamati Ndogo i l iyoongozwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Suluhu Hasan, hoja ikaishia kuondolewa.

    Waziri Mkuu kutaka m u s w a d a u i n g i z w e tena Bungeni ili uweze kuingia katika Katiba Pendekezwa, Lobbing i m e f a n ya k a z i ya k e , zimezuka hoja za chuki na hatimaye muswada umekwama na haujulikani utapelekwa tena au la, na l ini . Tunachoweza kusema ni kama umezikwa rasmi. Kambi ya Maaskofu imefanya kazi yake na imekamilika. Hakuna tena muswada wa Mahakama ya Kadhi.

    Katibu wa Bunge Thomas Kashilila, ameshasema kuwa muswaada huo hautakuwepo kwenye ratiba za Bunge, badala y a k e n a f a s i h i y o itachukuliwa na miswaada m i n g i n e k u j a d i l i wa . Serikali inasema imeamua kuuondoa kutokana na hofu ya kutokea mpasuko nchini.

    Dk. Kashilila alisema h a i j u l i k a n i n i l i n i utawasilishwa bungeni kwa sababu Mkutano wa Bunge ujao unaotarajia kufanyika Mei, utakuwa mahsusi kwa ajili ya bajeti.

    W a z i r i M k u u alivyosema wataangalia na kushauriana kimsingi, alitoa maneno ya busara tu au ilikuwa kauli ya mtu mzima, lakini huu muswada hautakuwapo, alinukuliwa akisema.

    Naibu Spika, Job Ndugai, yeye amenukuliwa akisema muswada huo hauwezi kuletwa bungeni kutokana na hali ilivyo. Bila shaka hali yenyewe ni kutokana na upinzani wa Wakristo.

    Hii ni mara ya pil i tunashuhudia muswada wa Mahakama ya Kadhi ukiondolewa Bungeni katika dakika za majeruhi kutokana na upinzani kutoka kwa baadhi ya wabunge na Maaskofu.

    Tunakumbuka kuwa

    Februari mwaka huu, m u s w a d a h u o p i a uliondolewa Bungeni kwa kile Mwanasheria Mkuu wa Serikali alichokiita, k w a m b a n i k w e n d a kuonana na viongozi wa dini kuwaelemisha juu ya mahakama hiyo, ili uwasilishwe tena kwenye mkutano uliomalizika wiki hii.

    Itoshe sasa kupata funzo kwamba, suala lolote la Waislamu, ambalo kwa namna moja au nyingine litakuwa na muingiliano na ser ika l i , ha l iwezi kukubaliwa kama litapata pingamizi la Kanisa.

    Bado tuna kumbukumbu ya uwezekano wa Tanzania kujiunga na Jumuia ya k iuchumi ya nchi za Kiislamu (OIC), ambapo Waziri wa Mambo ya Nje Bernad Membe alishaeleza Bungeni kwamba halina tatizo wala athari mbaya kwa nchi.

    Hata hivyo siku chache baadae aliitwa na Kardinal Polycarp Pengo na baada ya hapo al iufyata na ikaonekana kufanya hivyo ni tatizo. Pia tunakumbuka wakati serikali ilipotangaza B u n g e n i k w a m b a imeondoa misamaha ya kodi kwa taasisi za kidini, kwa kuwa misamaha hiyo imekuwa ikitumika vibaya.

    Maana yake ilikuwa ni kwamba misamaha hiyo ilikuwa ikitumiwa na wafanyabishara kukwepa kodi. Lakini pia taasisi za dini pamoja na kwamba zinasamehewa kodi katika kuingiza bidhaa za huduma kwa jamii, lakini huduma hiyo imeendelea kutolewa kwa malipo makubwa sawa na huduma zinazotolewa na taasisi binafsi, mfano mzuri ukiwa ni hospitalini, shule na vyuo.

    Hapo napo Maaskofu walikuja juu na kupinga hatua hiyo ya serikali. Kama kawaida, kwa nguvu waliyo nayo, mara moja serikali ilirejesha msamaha huo.

    Tunachoweza kusema ni kwamba, wenye kutafakari v i z u r i , s a s a h a k u n a kilichosalia kubaini hadaa iliyodumu kwa muda sasa.

    Sasa Waislamu nchini w a s h u g h u l i s h w e n a mambo yao mengine katika Uislamu, lakini ni hakika kwamba wale wanaoendelea kusubiri kuona Mahakama ya K a d h i h a p a n c h i n i , n i ndoto za mchana. Vinginevyo, labda tusubiri hadi hapo Masheikh wetu nao watakapokuwa na nguvu na thamani mbele ya dola kama walivyo Maaskofu, kiasi kwamba wataweza nao kusimamia hoja zao mbele ya serikali na wakasikilizwa.

  • 3 AN-NUURJAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 3-9, 2015Habari

    HALI inazidi kuwa tete Zanzibar ambapo sasa watu wanatishiana kusomeana Albadiri.

    Hayo yalijiri katika k ikao cha Baraza la Wawakil ishi ambapo ilipelekwa hoja binafsi juu ya baadhi ya Wazanzibari kunyimwa vitambulisho vya Ukaazi.

    A l i k u w a M j u m b e mmoja baada ya kuona w e n z a k e w a C C M wanakuja juu kupinga hoja madai ya baadhi ya wanachama wa CUF kunyimwa vitambulisho a l i p o s e m a k u w a anakusudia kuita watoto wa madrasa kusoma Albadiri kuwashitaki CCM kwa Mungu.

    Hiyo ilikuwa baada ya kutokea mvutano m k a l i n d a n i y a Baraza la Wawakilishi kuhusiana na hoja binafsi i l i y o w a s i l i s h w a n a Mwakilishi wa Ole (CUF) Hamad Masoud Hamad ya kuitaka serikali ichukue hatua za kuhakikisha Wa z a n z i b a r i a m b a o hawana vitambulisho vya Mzanzibari na wana sifa, wapewe vitambulisho kabla ya uchaguzi mkuu.

    Mvutano huo ulianza baada ya Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani Hamza Hassan Juma (CCM) kuuchana waraka wa hoja hiyo iliyowasilishwa na wapinzani ambapo baadhi ya Wawakilishi w a l i k a s i r i s h w a n a kitendo hicho na kuanza kusimama na kutaka kupigana kutokana na kitendo cha Mwakilishi huyo.

    K u f u a t i a t a h a r u k i hiyo, Spika wa Baraza hilo Pandu Ameir Kificho, ali lazimika kusit isha shughuli za Baraza kwa muda wa zaidi ya saa moja na baada kurudi tena, hakukuwa na maafikiano ambapo ki la upande ukivutia upande wake wapinzani wakisema w a n a d h u l u m i w a huku upande wa CCM wakisema sheria zipo wa z i we n ye k u t a k a vitambulisho wafuate sheria.

    Kabla ya kuahirishwa kwa kikao hicho, mjumbe wa Baraza hilo kutoka CCM , Issa Haji Gavu ambae pia ni Naibu Wizara wa Miundombinu

    Wawakilishi Zanzibarwatishiana Albadiri

    Na Salma Alghaythiyah

    n a M a w a s i l i a n o n a Mjumbe wa Baraza hilo k u t o k a C U F H a s s a n Hamad kutaka kupigana katika kikao hicho na kurushiana maneno ya jazba na kudharauliana.

    Wakati Gavu akitaka kushikana shati na Hassan huku Hamza aliyechana waraka huo alishikana kwa maneno makali na Mnadhimu na Baraza hilo kwa upande wa upinzani Abdallah Juma Abdallah.

    Baada ya nusu saa, suluhu iliweza kupatikana na wajumbe wote wa Baraza hilo kurejea na Spika kuendeleza kikao huku Spika ak isema kuwa hajafurahishwa hata kidogo kutokana na kitendo kilichotokea katika Baraza hilo.

    Kitendo hiki kwa kweli hakikuwa cha kupendeza n a k i m e l e t a t a s w i r a mbaya kwa wananchi wanaotuangalia, alisema Kificho.

    Aidha Kificho aliwataka wajumbe wa baraza hilo k u wa n a u v u m i l i v u w a k i s i a s a , k u a c h a kutukanana na kutoleana maneno ya kashfa, kwani wana dhamana kubwa kwa wananchi.

    Chanzo cha ugomvi na malumbano hayo ni pale wajumbe wa Baraza hilo wakati wakichangia hoja hiyo kwa jazba na baadhi yao kuchangia michango hiyo kutoka nje ya mada ambapo baadhi yao walionekana kukerwa na dhulma inayoendelea kwa kunyimwa watu v i t a m b u l i s h o h u k u baadhi yao wakiwapeleka viongozi kuwashitaki mbele ya Allah.

    Bi Ashura Sharif Ali kutoka nafasi za wanawake (CUF)aliwataka viongozi k u z i h e s h i m u n a f a s i zao na kujua kwamba wana dhamana kubwa waliopewa na Allah na ipo siku watarudi kwa Mwenye enzi Mungu na wanayoyatenda yote wataulizwa.

    N a p e n d a kuwakumbusha kwamba hapa duniani tumekuja kuishi kama wapita njia tu, bado kuna maisha mengine ya milele, sasa v i o n g o z i m n a o p e wa hizi dhamana mjue haya mnayoyatenda mtakuja kuulizwa na kuhukumiwa mbele ya Allah, alisema kwa uchungu Bi Ashura.

    Akichangia hoja hiyo Bi Kadija Khamis Kona wa (CUF) alisema kwa kuwa hatua zote wameshapitia za kuomba vitambulisho hivyo lakini mamlaka zinazohusika zinafanya kusudi kuwakatalia, basi anasubiri kumaliza vikao vya Baraza arudi nyumbani kwake na kuitisha kisomo cha watoto wa chuoni kumshitakia Mwenyeenzi Mungu juu ya dhulma hiyo.

    N i t a w a k u s a n y a watoto wa chuoni tusome halalbadri kwa sababu anayepaswa kuombwa na kutegemewa ni yeye Mwenyeenzi Mungu tu, alisema Mwakilishi huyo.

    Wa k i c h a n g i a h o j a hiyo, baadhi ya wajumbe walisema Mwenyeenzi Mungu ni wa watu wote na baadhi yao walionesha kubeza visomo hivyo kuwa hata wao wanaweza kusoma kwa kuwa ni miongoni mwa wacha Mungu.

    Mwakil ishi wa Viti Maalum (CCM), Wanu Hafidh Ameri alisema hao wenye kumuelekea Mwenye enzi Mungu, pia nao wana mabaya yao na hawezi kuiunga mkono hoja hiyo kwa sababu Baraza la Wawakilishi halina uwezo wa kuangalia utaratibu wa kisheria ila Baraza kufuata utaratibu wa kisheria na sio kutoa maamuzi na masharti ya kupata vitambulisho kwani suala la kupata vitambulisho hivyo lipo kisheria.

    A l i s e m a , s u a l a l a kupata kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, ni haki ya kikatiba na masharti

    ya kupata kitambulisho hicho yameeleza vizuri katika ibara ya sita ya katiba ya Zanzibar na i b a r a h i y o i n a e l e z a kama mtu hajaridhika katika upatikanaji wa v i t a m b u l i s h o h i v y o kwenda Mahakama Kuu na sio katika Baraza la Wawakilishi.

    Aliyewasilisha hoja hii kama anahisi wanaotoa vitambulisho hivi kuwa hawawajibiki na haki haitendeki, basi aende mahakamani na hakuna haja ya kuishurutisha serikali, alisema Wanu.

    Alimtaka mjumbe huyo aliewasilisha hoja hiyo ni vyema kuwashajihisha w a n a n c h i k u f u a t a utaratibu wa upatikanaji wa vitambulisho hivyo ili kuweza kupatia haki hiyo.

    Mohammed Aboud Mohammed ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, aliwaomba Wawakilishi wasifikishane kwa Mungu kwa kuwa mambo ya kupatikana vitambulisho yana taratibu zake na kuwataka wajumbe wafuate taratibu, kauli ambayo ilidharauliwa na wapinzani kwa kuwa suala hilo serikali imeshindwa kulisimamia huku ofisi yake ikishutumiwa kutoa muongozo kwa masheha wasitoe vitambulisho.

    Mwakilishi wa Jimbo Micheweni (CUF) Subeti Khamis Faki Abdallah Hamad ameunga mkono hoja hiyo na kuitaka serikali kuwachukulia h a t u a z a k i s h e r i a wahusika wa utoaji wa vitambulisho hivyo ambao wanawanyima haki yao hiyo baadhi ya wananchi kwa sababu zisizo na msingi.

    A l i s e m a , s u a l a l a kuwanyima wananchi v i t a m b u l i s h o h i v y o ni mtaji wa chama cha mapinduzi na suala hilo limeingizwa kisiasa zaidi.

    A l i s e m a s u a l a h i lo la kuwakosesha vitambulisho wananchi ni njama ya CCM kuweza

    kungangania kukaa madarakani na kuweza kupata ushindi katika uchaguzi mkuu kwa kuwa asie na kitambulisho hicho hatoweza kupiga kura.

    Aidha, Wawakilishi wa CUF waliwatupia lawama masheha wa shehia (viongozi wa mitaa) kutokana na kuwanyima b a a dh i ya wa n a n c h i vitambulisho hivyo kwa makusudi kutokana na itikadi za kisiasa.

    M w a k i l i s h i w a v i t i m a a l u m S a l m a Mohammed Ali alisema masheha wamepewa agizo maalum la kuwakosesha wananchi vitambulisho hasa wale wenye msimamo tofauti na Chama Cha M a p i n d u z i a m b a p o alisema hana imani na Masheha kwa kuwa wao ndio chanzo cha wananchi kunyimwa haki zao.

    Awali akizungumzia suala hilo Waziri wa Sheria na Kat iba, Abubakar Khamis Bakari alisema sio kwamba wananchi h a w a w e z i k w e n d a mahakamani, lakini tatizo liliopo wananchi hawawezi k u f i k a m a h a k a m a n i kutokana na vikwazo vingi wanavyowekewa na suala la kuambiwa sheria inasema hivi ni mambo ya kuhangaishwa tu wananchi.

    Waziri wa Nchi ofisi ya Rais, Idara Maalum, Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ, Haji Omar Kheir amekanusha k a u l i z a b a a d h i ya wajumbe wa Baraza la Wawakl ishi wal iodai k u wa v i t a m b u l l i s h o vya Mzanzibari Mkaazi vinatolewa kwa sababu ya siasa.

    Huku akijisifu kuwa yeye pia ni mcha Mungu na amekuwa akitoa sadaka na zaka k i la mwaka pamoja na kwenda Hijja ambapo alisema mwaka huu anatarajia kwenda tena kuhiji na umra kwake yeye ni jambo la kawaida.

    K h e r i a l i s e m a v i t a m b u l i s h o h i v y o vinatolewa kwa mujibu wa sheria na kama wajumbe hao wanaona kuwa sheria hiyo ina mapungufu, basi waifanyie marekebisho.

    Waziri huyo alisema k a m a k u n a m t u ananyimwa haki hiyo ya kupata vitambulisho, afuate taratibu za kisheria ili kuweza kupata haki yake hiyo.

  • 4 AN-NUURJAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 3-9, 2015MakalaNa Khalid Gwiji

    KUNA methali isemayo "mwanzo wa moto ni cheche" ikimaanisha kuwa ubaya mkubwa huanza kwa ubaya mdogo na kwamba fujo aghlabu huanza kwa uchokozi. Bila ya shaka shabaha ya methali hii ni kututahadharisha tusidharau matatizo m a d o g o k w a n i y a k i j i l i m b i k i z a yatakuwa rundo la m a t a t i z o n a n d i o huweza kusababisha balaa, maafa au janga la jamii.

    Watu wenye akili na hisia za utu watalaani k w a n g u v u z o t e uharamia uliofanyika kwenye maeneo ya Fuoni Jitimai na Sheli Maili Tano Zanzibar wa kuvamiwa wafuasi wa Chama cha Wananchi - CUF na kuwajeruhi vibaya. Kitendo hiki kwa mazingira yake na kutokea kwake, kinaashiria nia mbaya waliokuwa nayo watu wa s i o i t a k i a m e m a Zanzibar. Bila ya shaka yo yote watendaji wa kitendo hiki kiovu ni watu wasiokuwa na uchungu na Zanzibar wala kufuata silka na maadili yake.

    Matukio haya na mfano wake yanalenga kuturudisha enzi zile za siasa za chuki, fujo, uhasama na mifarakano ambazo tu l i shaapa k u a c h a n a n a z o kupitia Maridhiano na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ambazo zilijengeka juu ya misingi ya kuaminiana na nia njema miongononi mwa viongozi na Wananchi.

    Tu n a e l e wa k u wa p a m o j a n a s a b a b u kadhaa za kuzuka kwa matukio haya, sababu kubwa moja wapo ni kuwepo kwa wanasiasa U C H WA R A a m b a o HAWAUZIKI tena katika siasa za hoja na badala yake wanajidanganya kwa kuwekeza kwenye vurugu za kuwahujumu wanachama wa Chama cha Wananchi - CUF, kuchoma moto ofisi za Chama, kupachua bendera nk ambapo k w a o w a o h a y o ndio mtaji. Hawa ni wanasiasa waliozoea k u p a t a u m a a r u f u kwa njia za vurugu, uhasama na mifarakano. Wamekuwa ni sawa na baadhi ya 'WAGANGA WA KIENYEJI' ambao

    Mnaotaka nuru ya maridhiano ififie hamuitakii mema Zanzibar yetu !

    wa Zanzibar na wa Wa z a n z i b a r i k w a kutumika kwa n j ia yo yote inayoweza kuhujumu mshikamano, u m o j a , m a p e n z i , udugu na uvumilivu baina yetu, uliojengeka tokea kuasisiwa kwa

    wanaamini kuwa bila ya migogoro - hawana biashara.

    N i b u s a r a t u k a k u m b u k a n a kuzingat ia eneo la mafanikio la Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kwa pamoja tukaiendeleza kutokana na ukweli kwamba imekuwa na maslahi mapana kwa wote na ni vile vile ni muakilishi na mtetezi wa makundi yote.

    Serikali ya Umoja wa Kitaifa kimsingi ni nyenzo muhimu sana ka t ika u jenz i wa Zanzibar mpya. Imekuja kuzika siasa za chuki, uhasama, vurugu zi l izolenga k u f u k u a m a k a b u r i na visasi na badala yake kuleta mfumo mpya wa mahusiano mema miongoni mwa Wananchi, viongozi na Serikali yao kwa k u y a w e k e a m a u a makaburi. Serikali hii ya pamoja ina eneo kubwa la Mafanikio ambayo ni pamoja na: Kwanza, imeleta mshikamano m i o n g o n i m w a wananchi kwa kuzizika s i a s a z a c h u k i n a uhasama. Pili, ilianzisha ustaarabu mpya na w e n y e u k o m a v u wa k i s i a s a k a t i k a uendeshaji wa siasa za vyama. Matumizi ya

    lugha, kauli mbiu, sanaa (nyimbo na ngoma) hazikuwa za vijembe kama ilivyokuwa huko nyuma. Tatu, imerudisha imani ya wananchi kwa serikali yao baada ya wananchi kujiona na kuamini kuwa serikali h i i i m e t o k a n a n a wao kufuatia kura ya maoni (referendum) waliyoipiga kuunga mkono mfumo huu wa serikali ya pamoja - jambo ambalo limeipa uhalali serikali hii . Nne, imesaidia katika upatikanaji wa huduma (afya na e l imu) na ustawi wa jamii (haki za wataafu na wazee) katika misingi ya usawa. Kwa kiwango kizuri, haki imekuwa ikipatikana kwa kustahiki na sio kwa kutizamwa we ni nani.

    Ta n o , i m e s a i d i a Zanzibar na Wazanzibari kufikiria nje ya chaguzi (beyond elect ions) . K wa m u d a m r e f u , chaguzi zimekuwa ni chombo cha kuwagawa Wa z a n z i b a r i . S U K imesaidia kuonesha kuwa chaguzi si lengo, bali ni nyenzo kuelekea lengo kuu ambalo ni maisha mema, ustawi na maslahi mapana na ya pamoja miongoni mwa wananchi.

    Sita, SUK imesaidia

    k u e n d e l e z a n a kusimamia amani na utulivu. Saba, SUK imesaidia kuengeza wigo wa uvumilivu wa k i s i a s a . N a n e , GNU ilisaidia serikali kutotumia nguvu ya dola dhidi ya wananchi kama ambavyo pia ilisaidia wananchi kutotumia nguvu ya umma dhidi ya serikali. Ilijaribu kuja katika mrengo wa kati na kati wa mazungumzo. Muhimu zaidi, Serikali ya Umoja wa Kitaifa inahitaji kuendelezwa kwa vile hatujawa na d e m o k r a s i a t u l i v u (s table democracy) yenye kuamini juu ya mmoja atoke na mwengine a ingie - demokrasia tulivu ya kupokezana madaraka na mamlaka kwa njia za amani na ustaarabu.

    W i t o w e t u k w a Wazanzibari, ni muhimu sana kuimarisha Umoja w e t u w a P a m o j a , kudumisha amani na utulivu ndani ya nchi yetu na kwamba harakati zote za kuwatafuta na kuwabaini walio nyuma ya uovu huu ziendelee na kuendelezwa na Wazanzibari wote kwa ajili ya kuthamini haki na utu wa wenzetu hawa.

    Aidha, tusikubal i kutumiliwa na maadui

    Maridhiano na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) na kuipa nchi yetu sifa njema na umaarufu duniani.

    Tusitumikie ajenda potofu za baadhi ya wanasiasa na watendaji wa l i o m o n d a n i ya SUK ambao kwa wao siasa ni biashara - na ambao wanaamini kuwa maslahi ya chama ni makubwa zaidi kuliko maslahi ya nchi na taifa na wako tayari kuyabeza maslahi ya nchi pale yanapopingana na yake ya vyama vyao.

    Wengi wa wanasiasa wa aina hii ni wakongwe walioshindwa kufahamu maana na umuhimu wa SUK. Wao wamezoea siasa za kimapinduzi na/au ile za mfumo wa chama kimoja. Mwisho, tunatoa mkono wa pole kwa wananchi wenzetu wazalendo waliojeruhiwa, kwa familia, wafuasi na w a p e n z i w a o n a tunawaombea wapone haraka, insha'Allah.

    M u n g u i b a r i k i Zanzibar.

    M u n g u wa b a r i k i Wazanzibari.

    M u n g u wa b a r i k i Watanzania

    KATIBU Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto) akimjulia hali mmoja wa majeruhi aliyeshambulia katika mkutano wa Chama hicho Unguja hivi karibuni.

  • 5 AN-NUURJAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 3-9, 2015Habari za Kimataifa

    JESHI la Anga la Marekani l i m e t a n g a z a k u w a limefanya majaribio ya kombora kubwa (balistiki) l i n a l o w e z a k u v u k a mabara na kwamba, majaribio hayo ni ujumbe kwa walimwengu kuhusu uwezo wa s i laha za nyuklia wa nchi hiyo.

    Kwa mujibu wa taarifa i l i y o t o l e wa n a J e s h i la Anga la Marekani, kombora la Minuteman-III, lilifanyiwa majaribio mapema Jumatatu katika kituo cha Jeshi la Anga cha Vandenberg huko California.

    Taarifa ya Jeshi la Anga la Marekani imesema kuwa Majaribio hayo ya kombola la balestiki la nyuklia, yanaonesha picha ya wazi kwa walimwengu kuhusu uwezo wa kombora ya Minuteman-III ambalo linaweza kulenga mahala popote.

    Kwa kutilia maanani kwamba Jeshi la Anga la Marekani haliwezi kutumia makombora ya Peace Keeper kwa mujibu wa makubaliano ya silaha ya START II (Strategic Arms

    Marekani yaonyesha jeuri ya NyukliaYafanyia jaribio kombora la Minuteman-III

    RAIS Barack Obama wa Marekani.

    RAIS Hassan Raohani wa Iran.

    Reduction Treaty), kombora la Minuteman-III litakuwa kombora pekee la balestiki linaloweza kuvuka mabara la jeshi la Marekani.

    K o m b o r a h i l o

    linavishwa kichwa cha silaha ya nyuklia aina ya W87, ambacho kina u w e z o m k u b w a w a uharibifu. Majaribio hayo yamefanyika sambamba

    na mazoezi ya kijeshi yanayoendelea kufanywa na majeshi ya shirika la NATO huko Ulaya Mashariki.

    Inaonekana kuwa kwa majaribio ya kombora hilo la nyuklia, jeshi la Anga la Marekani linafuatilia malengo kadhaa.

    Wachambuzi wanaeleza kuwa Marekani inataka kuonesha misuli na uwezo wake wa silaha za nyuklia kwa wapinzani wake wakubwa hususan Urusi.

    Katika kipindi cha miaka kama miwili iliyopita jeshi la Urusi lilifanya majaribio ya makombora ya n a y o we z a k u v u k a mabara (Intercontinental Ballistic Missile au IBM) na hata kurusha makombora kama hayo kwa kutumia nyambizi. Kwa msingi huo Marekani ilikuwa ikinyemelea fursa ya kukabiliana na majaribio hayo ya silaha za nyuklia ya Urusi.

    I m e f a h a m i s h w a kwamba kichocheo cha pili cha majaribia hayo ni kukithiri mivutano baina ya Urusi na NATO huko Ulaya Mashariki, ambako kumezifanya pande hizo mbili kujizatiti kwenye medani ya s i laha na majeshi katika eneo hilo na katika Bahari Nyeusi.

    H i v y o i n a o n e k a n a kuwa Marekani inataka kumuonesha adui yake mkubwa kijeshi, yaani Urusi, kwamba iwapo mgogoro huo utaendelea inaweza kutumia silaha zake za nyuklia.

    Marekani ni miongoni mwa wamiliki wakubwa zaidi wa silaha za nyuklia duniani na ndiyo nchi pekee ambayo hadi sasa imetumia silaha hizo kuua watu wa taifa jingine.

    Nchi hiyo kinyume na ahadi zake za kupunguza maghala yake ya silaha za nyuklia, bado inaonekana kustawisha na kupanua za idi s i laha h izo na kuzifanyia majaribio.

    P i a i n a d a i w a k u z i b o r e s h a z a i d i silaha zake za zamani z a n y u k l i a l i c h a ya harakati za kimataifa za kupunguza silaha hizo, husuan mkataba wa NPT unaosisitiza kupunguzwa na hatimaye kuangamizwa kabisa silaha hizo.

    Washington imetenga bajeti ya dola bil ioni 355 ambazo zitatumika kuboresha mitambo yake ya silaha na kuinua juu kiwango cha majaribio ya silaha za nyuklia.

    A i d h a M a r e k a n i imechukua hatua za kuboresha s i laha na maghala yake ya zana za nyuklia barani Ulaya, yakiwemo mabomu ya nyuklia ya B-61.

    Kwa utarat ibu huo Washington, kinyume na mikataba ya kimataifa ya kuzuia uzal i sha j i wa silaha za nyuklia, inaendelea kuzalisha na kufanyia majaribio silaha za aina hiyo, suala ambalo linakiuka mkataba wa NPT na wakati huo huo kutolalamikiwa na yeyote.

    Wa k a t i M a r e k a n i ikionyesha uwezo wake wa silaha za nyuklia, Tauifa hilo l imekuwa kinara wa kushinikiza mataifa mengine, hasa ya Mashariki ya Kati k u a c h a n a k a b i s a n a mpango huo.

    W i k i i l i y o p i t a mazungumzo ya Iran na kundi la 5+1 kuhusu miradi ya nyuklia yenye malengo ya amani ya Iran, yalisimama mjini L a u s a n n e , U s w i s i kufuatia tofauti na hitilafu zilizopo kati ya pande za mazungumzo hayo.

    Mazungumzo hayo yamesimama baada ya wawakilishi wa kundi la 5+1 kushindwa kuchukua maamuzi magumu juu ya kuondolewa vikwazo dhidi ya Tehran. Licha ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutekeleza masharti ya makubaliano yaliyofikiwa mjini Geneva miaka miwili iliyopita, bado upande wa pi l i umeshindwa kutekeleza ahadi zake, suala ambalo limeendelea kuleta mvutano katika mazungumzo hayo.

    Kwa mufa mrefu Iran, nchi ambayo imeonekana kupiga hatua za haraka za maendeleo ya teknolojia na k i j esh i , imekuwa i k i w e k e wa v i k wa z o vya kiuchumi kufuatia mpango wake kuzalisha nishati ya nyklia na ajili ya matumizi salama na maendeleo ya Iran.

    MSEMAJI wa Rais Vl a d m i r P u t i n wa Urusi, Dmitry Peskov, amesema kuwa hakuna kizuizi chochote cha kisheria kitakachoizuia s e r i k a l i y a U r u s i kupeleka silaha na zana za kijeshi nchini Syria.

    Bw. Peskov, amesisitiza kuwa hakuna kizuizi chochote kitakachoweza kuzuia kuwepo pia mashirikiano ya kijeshi na kiufundi kati ya serikali za Moscow na

    U T A F I T I m p y a umegundua kuwa Ebola, imesababisha a thar i mbaya zaidi kwa watoto wadogo kuliko watu wazima.

    Asilimia 90 ya watoto chini ya mwaka mmoja ambao waliambukizwa walikufa.

    Utafiti huo ulifanywa k wa u s h i r i k i a n o wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na chuo kimoja cha London cha Imperial

    Ebola imeuwa asilimia 90 ya watoto-UtafitiCollege London.

    U t a f i t i u m e o n e s h a k w a m b a j a p o k u w a k iwango cha wato to w a l i o a m b u k i z wa n i k i d o g o k u l i k o wa t u wazima, watoto na watoto wachanga ambao walipata ugonjwa huo walikuwa na nafasi ndogo sana ya kupona.

    V i r u s i h i v y o vinavyosababisha homa kali na kutokwa damu ndani na nje ya mwili,

    vinaua asilimia 90 ya watoto wachanga katika mlipuko wa sasa.

    Utafiti umebainisha zaidi kuwa karibu asilimia 80 ya watoto wa umri kati ya mwaka mmoja na miaka mine, hufa kama walivyogundua wanasayansi.

    Zaidi ya watu 23,000 waliambukizwa virusi vya ebola na zaidi ya 10,000 walifariki dunia.(VOA).

    Urusi wasema hakuna wa kuwazuia kupeleka silaha SyriaDamascus.

    Hayo yanaelezwa katika hali ambapo nchi za Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel, zimeingiwa na hofu kutokana na kuwepo uwezekano mkubwa wa serikali ya Urusi kupeleka nchini Syria mfumo wa kuzuia makombora S-300.

    Msemaji huyo wa Rais wa Urusi alisisitiza kuwa, Moscow hai jakiuka sheria za kimataifa kwa

    kuipelekea serikali ya Syria silaha za kujihami na kujilinda.

    Hivi karibuni Rais Bashar Assad wa Syria, alivieleza vyombo vya habari kwamba kuna makubaliano mapya ya silaha na zana za kijeshi yaliyofikiwa kati ya serikali yake na Urusi na kusisitiza kwamba, m a k u b a l i a n o h a y o yako katika hatua ya utekelezaji. (irib).

  • 6 AN-NUURJAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 3-9, 2015Makala

    JIONI ya tarehe 29 Machi 2015, msafara wa wafuasi wa Chama cha Wananchi ( C U F ) w a l i o k u w a wakitoka Makunduchi, kusini Unguja, kuelekea M j i n i M a g h a r i b i , ulishambuliwa njiani na watu wasiojulikana. H i l o n e n o w a t u wasiojuilikana tuliwache hivyo hivyo kwenye alama za mashaka, maana ni mtazamo wangu kwamba ni kinyume chake, yaani ni watu wanaojuilikana na wale wanaopaswa na wenye wajibu wa kujuwa mambo kama haya.

    Kwa mujibu wa mmoja wa watu waliokuwamo kwenye msafara huo gari ya majanjawidi ikiwa katika mwendo wa kasi iliupita msafara wao na kisha kuwarushia watu waliokuwemo katika gari hiyo visu na nondo. Muda mchache uliopita, Katibu Mkuu wa CUF na Makamu wa Kwanza wa Rais , Maalim Seif Sharif Hamad, alikuwa amewaomba watu wote walioshiriki mkutano huo huko Makunduchi, waondoke kwenye msafara mmoja kurudi mj ini . Inaonekana alishakuwa na wasiwasi juu ya kile ambacho kingelitokea na ushauri wake ulilenga, y u m k i n i , k u k i z u w i a kisitokee.

    Siku tano kabla ya h a p o , o f i s i z a C U F jimbo la Dimani, mkoa wa Mj in i Maghar ib i , zikateketezwa kwa moto na watu wasiojuilikana na kusababisha hasara kubwa. Mashuhuda wa tukio hilo, ambalo lilitokea mtaa wa Kisauni saa 8: 00 usiku, wanasema watu hao walifika na gari aina ya Pick-up na kuvunja mlango wa ofisi hizo na kuliripua jengo hilo kwa petroli. Kwa mujibu wa Diwani wa wadi ya Tomondo, Hassan Hussen Yussuf, jengo hilo lilikuwa na vifaa mbalimbali vya thamani na fedha taslimu za malipo ya uchukuaji wa fomu za wagombea walizolipia.

    Kuchomwa kwa ofisi za CUF Dimani kulikuja siku tatu tu baada ya chama hicho kufanya mkutano kwenye eneo la jirani na hapo kwa kile kilichosema ni kumgotoa Mansoor Yussuf Himid, ambaye

    Kauli ya kutolipiza kisasi yahitaji kushereheshwaNa Mohammed Ghassany

    MIONGONI mwa majeruhi wa mkasa wa kushambuliwa na watu wasiojuilikana wakati wakirudi mkutano wa CUF, Makunduchi, tarehe 29 Machi 2015.

    a n a r u d i k u g o m b e a uwakilishi kwa tiketi ya CUF katika jimbo la Kiembesamaki. Mansoor alikuwa mwakilishi wa jimbo hilo hapo kabla kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kabla ya kufukuzwa kutokana na msimamo wake kuelekea Muungano wa Tanzania na nafasi ya Zanzibar kwenye Muungano huo. Kwenye mkutano huo kulizungumziwa kuwepo kwa njama za kuiingiza Zanzibar katika machafuko kabla ya kura ya maoni ya Aprili 30 mwaka huu na kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 25. Wito wa wazungumzaji wa CUF kwenye mkutano huo ilikuwa kutochokozeka n a k u t o o n d o s h w a kwenye mstari.

    M k u t a n o h u o n a o ulitanguliwa na mkutano wa wazee wa CUF kwenye ukumbi wa Salama, Hoteli ya Bwawani Zanzibar, ambako pamoja na mengine mengi, Maalim Seif naye alizungumzia mipango hiyo ya fujo zinazopangwa na zilizokwishafanywa huko nyuma. Na yeye akasogea mbele zaidi kwa kurejelea tamko la kutofukua makaburi lau chama chake kitachukuwa madaraka kamili baada ya uchaguzi wa Oktoba. Kwa hakika, aliwakemea wote waliomo kwenye chama chake, ambao

    wanadhani kwamba ikiwa CUF itaingia madarakani, itakuwa zamu yao ya kutesa.

    M s t a r i wa m a k a l a h i i u n a p i g w a h a p a ambapo nadhani pana haja ya kushereheshwa na sio kutafsiriwa tu. Kusherehesha kwa wasioufahamu vyema msamiati huu na asili yake kuna maana ya kuchambua tafsiri, wakati kutafsiri ni kuhamisha maana kutoka chanzo kimoja kupeleka chengine. Asili ya neno kusherehesha ni kwenye madarasa ya dini, ambako masheikh wa n a o t a f s i r i Q u r a n huchambuwa maana ya kile walichokitafsiri kwa upana na marefu.

    Kwa maoni yangu, kauli za kutochokozeka, kutoondoka kwenye mstari, kutokufufua makaburi na kutolipiza kisasi ni za muhimu sana katika kujenga siasa za Maridhiano visiwani Zanzibar na kulivuta kundi ambalo hadi sasa linayapinga Maridhiano hayo kwa kuwa tu lina wasiwasi juu ya hatima yake, endapo CUF itaingia madarakani. Lakini kwa umuhimu huo huo pia, panahitajika kuchorwa mstari na kuwekwa vituo ili kundi lililokwishaamua kuiangamiza Zanzibar, liujuwe pia ulipo mpaka ka t i ya k i l e wenzao wanachokichukulia kuwa ni uvumilivu lakini wao wakakiona ni ubwege.

    Kwa namna yoyote

    ile, sidhani ikiwa CUF inakusudia kulipa kundi hilo la watu wasiojulikana h u n d i s a f i m k o n o n i mwao ili liijaze litakavyo, kisha liondoke zake bila kuguswa. Sidhani hivyo, maana huko ni kwenda kinyume na hata misingi mikuu ya kuundwa kwa CUF yenyewe, ambayo ni haki za binaadamu na utawala wa sheria. CUF haivuni chochote k w a k u w a p u n g u z i a khofu watu hawa zaidi ya kuwahakikishia kile kinachoitwa impunity, yaani uwezo wa kukwepa sheria. Wanachofahamu wao pale wakiambiwa k w a m b a m a k a b u r i h a y a t a f u k u l i w a n i kuwa wamepewa ruhusa ya kuendelea kupiga, kujeruhi na hata kuua, wakijuwa kuwa hatimaye hakuna mahakama wala jela inayowasubiri. Huo ndio uzoefu wao, maana hawajaanza leo wala jana kuyafanya haya.

    Akili ile ile ya kutia moto mabanda ya skuli n a v i n y e s i k w e n y e visima, ndiyo akili ile ile iliyounda Melody, kisha ikaja na Janjawidi na Mbwa Wakali na Ubaya Ubaya. Madhara yale yale ya miaka ya 90, ndiyo yaliyokuwa ya 2000, 2005 na sasa 2015. Kundi hili, lenye akili hizi, halihitaji kuambiwa kuwa makaburi yake hayatafukuliwa, ikiwa bado linaendelea kuyatenda yale yale . Makaburi yao yanapaswa kufukuliwa na maovu

    yao kuanikwa hadharani na, zaidi kuliko yote, k u f i k i s h w a k w e n y e vyombo vya sheria.

    Zanzibar ijayo baada ya Oktoba 2015 inapaswa kuwa ya kuvumuliana na kushirikiana kuijenga kiuchumi, ki jamii na k i s i a s a , l a k i n i h i l o halipaswi kuwapa watu n a f a s i m w a n y a w a kuichafua salama ya Wazanzibari hivi sasa, k i s h a w a k a t e g e m e a msamaha na kuvumiliwa baadaye.

    Kwa hivyo, ingawa ni sahihi kabisa kujenga moyo wa Maridhiano na kuondosheana wasiwasi kwa wale waliotenda uovu katika zama za ujahili , si sahihi hata kidogo kuwajengea imani waovu wa zama za leo ambazo ni zama za nuru. Hawa ni akina Abu Jahl. Hakuna chochote kitakachowabadilisha na kuwafanya waikumbatie salama ya Wazanzibari w o t e . H a wa l a z i m a waelezwe kinagaubaga kuwa kuna mahakama, kuna jela, na kuna adhabu.

    Wakati tunaji tahidi kuwazuwia vijana wetu wasipande jazba na kuingia kwenye machafuko, kwani nako pia kutakuwa kwa faida ya kundi hilo la watu wasiojuilikana, tunapaswa kuchora mstari na kuweka alama zetu.

    (Makala kwa hisani ya Mohammed Ghassani kwenye zanzibardaima.wordpress.com.)

  • 7 AN-NUURJAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 3-9, 2015MakalaThe Boogeyman ni filamu ya kutisha ya Kimarekani (American supernatural s l a s h e r h o r r o r f i l m ) iliyotolewa mwaka 1980. Ikiongozwa na Ulli Lommel. Wachezaji wakuu (stars) walikuwa Suzanna Love, John Carradine na Ron James.

    Filamu iliwahusu watoto wawili , Willy na Lacey ambao wakishi r ik iana , walimuuwa rafiki wa kiume wa mama yao. Willy alinyata na kuingia chumbani kwa mama yake ambapo alikuwa akifanya mapenzi na rafikiye haramu (kwa maana sio mume wake wala baba wa watoto wake). Kwa kutumia kisu akamuuwa rafiki huyo wa mama yake. Wakati hayo yakifanyika, Lacey alikuwa akitizama kupitia kiyoo.

    Miaka 20 baadae, mpenzi huyo wa mama yao anakuja kulipiza kisasi katika namna ya jinamizi, lililowahangaisha sana watoto hao Lacey na Willy, wakati huo wakiwa watu wazima. I l ikuwa kila siku Lacey na Willy, wanaweweseka kwa kujiwa na mtu kama yule mpenzi w a m a m a y a o a k i w a na kisu mkononi akitaka kuwashambulia. Majinamizi kama haya (Bogeyman au monsters), inakuwa tabu sana kupambana nayo na kuyashinda kwa sababu moja tu muhimu: Sio viumbe halisi.

    Inayodaiwa kuwa vita dhidi ya ugaidi, imejaa ma-bogey men, wengi iwe kwa jina la Boko Haram, Al-Shabaab, IS, Alqaidah, Abubakar Shekau, Abu Baghdad n.k. na kwa maana hiyo, si vita inayotarajiwa kumalizika kwa kutumia p o l i s i , m a k a c h e r o a u jeshi. Itamalizika tu kwa wanaounda majinamizi haya kuacha mchezo wao. Watu hao kila kukicha, wanabuni mbinu mpya ama za kubuni majinamizi mapya au kuyapa u h a i n a k u ya d u m i s h a yaliyopo.

    Oktoba 2008 ilichapishwa habari moja katika vyombo vya habari iliyopewa kichwa cha habari : Beware the Bogey Man: A new low, even for McCain and his ignorant supporters!

    Chini ya kichwa hicho likaelezwa tukio moja katika mkutano wa hadhara wa kampeni kule Minneapolis, a m b a p o J o h n M c C a i n alikuwa katika kampeni za kuwania Urais wa Marekani. Ilikuwa ni katika mkutano huo mwanamke mmoja alieleza wasiwasi wake juu ya Barack Obama akisema kuwa hamwamini kwa sababu amewahi kusoma mahali kuwa Obama ni Mwarabu.

    "I don't trust Obama. I have read about him. He's an Arab."

    Alisema mwanamke huyo katika jitihada za kuonyesha kuwa huenda John McCain akawa Rais bora kuliko Obama.

    Katika kujibu swali la mama huyo, John McCain a l ip ig i l i a msumar i wa ubaguzi na kit isho cha Muarabu na Muislamu. Alisema:

    No, maam. Hes a decent, family man, [a] citizen that I just happen to have disagreements with on fundamental issues and

    Lipo JinamiziNa Omar Msangi

    that's what this campaign is all about."

    Katika namna nyingine ni sawa na kusema: Dont worry, maam, Barack Obama is NOT an Arab. Unlike Arabs, hes a decent, family man.

    Ukitizama namna zote mbili, hapa John McCain anachofanya ni kushindilia tu msumari wa ubaguzi na k i t i sho cha Uarabu n a U i s l a m u . A n a m t o a hofu muuliza swali kwa kusema kuwa Obama ni mtu mstaarabu, sio kama Waarabu/Waislamu.

    Kinachoelezwa na swali la mama muuliza swali ni kuwa jamii ya Kimarekani imejengwa kuogopa kitisho cha Waarabu na Waislamu, na pengine John McCain angeweza kusema lolote kusahih isha kuwa iwe Muarabu, Mzungu, wote ni raia wa Marekani bila kujali asili zao. Au katika muktadha wa dunia, kuwa wote ni binadamu, watu wasipimwe kutokana na asili yao. Lakini hakufanya hivyo. Akamwacha mama h u y o n a w a s i l i k i z a j i wengine katika mkutano huo wakibaki na ujinga wao wa kuogopa kitisho bandia cha Uislamu/Waislamu na hivyo kuendeleza agenda ya ubaguzi na vita dhidi ya ugaidi.

    Taarifa kuu na muhimu kabisa wiki hii katika eneo letu hili la Afrika Mashariki kwa wiki hii, pengine zitakuwa ni zile za kukamatwa wasichana watatu, wakidaiwa kutaka kuvuka mpaka kwenda Somalia kujiunga na Al-Shabaab. Vyombo vya habari vikasherehesha vikidai kuwa wasichana hao Khadi ja Abubakar Abdulkadir , Maryam Said Aboud na Ummul Khayr Sadir Abdulla waliokamatwa katika mji wa El Wak ilikuwa wakaolewe na Mujahidina wa Al-Shabaab na IS. Kati ya wasichana hao, mmoja ni kutoka Zanzibar akitajwa kwa jina la Ummul Khair Sadri Abdallah.

    Taarifa zaidi zikafahamisha k u w a w a s i c h a n a h a o walijikuta katika mtego wa kwenda Somalia-Al Shabaab na kisha IS, kupitia mawasiliano waliyokuwa

    wakifanya na mwanamke mmoja wa Syria, aliye katika IS.

    Katika jambo hili, upo uwezekano wa namna mbili. Moja ni kuwa inawezekana k w e l i w a s i c h a n a h a o walishawishiwa wakafikia k iwango cha kukubal i kwenda kujiunga na Al-Shabaab. Nasema hivyo kwa sababu ipo mifano mingi ya watoto wa Kiislamu kuacha shule na hata walio Vyuo Vikuu baada ya kughilibiwa kuwa kusoma ni kupoteza muda, bali kinachotakiwa ni kwenda Jihad. Lakini hata kama itakuwa hivyo, bado waliofanya kazi hiyo watabaki kuwa mawakala wa mabeberu walioandaliwa na mabeberu kuwafanyia kazi.

    Uwezekano wa pili ni kuwa wasichana hao wapo katika mtego alionasa Sami Osmakac. Wakati mwingine mawakala wanaofanya kazi hii, ikionekana kasi yao ndogo, makachero huingia moja kwa moja na kuwatia walengwa katika uhalifu k i s h a k u wa k a m a t a n a kuwasukumizia tuhuma za ugaidi. Ndiyo yaliyomkuta Sami Osmakac ambaye hivi sasa anatumikia kifungo cha miaka 40 kule Marekani.

    Hivi sasa kuna mikakati ya kuhakikisha kuwa haya mazimwi (bogey men) yanahuishwa na namna ya kuhuishwa ni kama hivi k u p a t i k a n a k wa wa t u k a m a h a o w a k i d a i w a kwenda kujiunga na Al-Shabaab au IS . Namna nyingine ni kupatikana kwa mashambulizi ya kupanga au kutolewa mara kwa mara kwa tahadhari za vitisho kama zile za wiki mbili zilizopita kwamba magaidi wa IS watapiga Mwanza, Dar es Salaam, Nairobi na Kampala.

    Kat ika mato leo yetu ya hivi karibuni, tuliwahi kueleza kukamatwa watu kule Uturuki ambao hufanya kazi ya kunasa watu na kuwapelekwa kwa IS na kwamba mawakala hao hufanya kazi kwa kutumwa na chini ya uangalizi wa vyombo vya kikachero vya Magharibi na hupewa fedha nyingi kwa kila mtu

    wanayemnasa. Lengo ni kuzidi kukoleza kitisho cha bogey man IS.

    Katika kadhia ya Sami Osmakac, makachero wa FBI waliunda mtego ambapo walimnasisha kijana huyo asiye na hatia, na kisha kumtangazia ugaidi ambao lau wasingekuwa wao FBI, kijana huyo asingefanya yote hayo aliyokuja kusingiziwa kufanya.

    Inawezekana pia kwa hawa wasichana wakapatikana makachero mawakala wa mabeberu wakawachezea akili zao na kuwanasisha kama a l ivyonasa Sami Osmakac kisha wakaibuka na taarifa kuwa wanakwenda Somalia kuolewa na Al-Shabaab.

    J o s e p h K i b w e t e r e w a U g a n d a , a l i w e z a kuwaaminisha watu wake kuwa wakijitia katika tanuri la moto Kwa jina la Yesu, wanaibukia upande wa pili wakiwa Mbinguni (Peponi). Mamia ya watu wakajitosa w a k a f a . S a s a y a w e z a vi jana wakat iwa imani hizi za Joseph Kibwetere wakawaona wazazi wao Wa i s l a m u n i m a k a f i r i wakahiyari wakaolewe na Al-Shabaab, bila ya Walii maana walii (mzazi) ashakuwa kafiri!

    K w a v y o v y o t e itakavyokuwa, kama nchi, tunatakiwa tulitizame jambo hili kwamba kwa asili yake, sio la Waislamu wala Al-Shabaab. Ni mitengo na mikakati ya mabeberu katika kujihakikishia utawala na udhibiti wa kidunia- US World Hegemony. Kupitia v i t a d h i d i ya u g a i d i , kinapatikana kisingizio cha kuingia popote kwa hoja ya kuwafuata magaidi au kusaidia nchi inayolengwa kupambana na magaidi. Tukilitizama kwa makengeza kwamba ni tatizo la Ummul K h a i r , t u n a j i z a m i s h a wenyewe katika tope mithili ya Boko Haram, ambalo hatutaweza kutoka hata tukitamani.

    Imani yangu ni kuwa tuna akili pevu za kuyatizama mambo ya dunia hii kwa mtizamo sahihi. Na niseme hapa kuwa katika hili, akina

    James Mbatia na sisi sote, tuziweke pembeni z i le chuki zetu za kidini kama zilivyojitokeza katika ile semina kwa wabunge juu ya Mahakama ya Kadhi. Haya ya Mahakama ya Kadhi ni yetu, tutajua namna ya kuelewena huko mbele ya safari. Lakini hili la ugaidi s i l e t u n a t u k i r u h u s u kuundiwa haya majinamizi, wala tusijidanganye kuwa tutakuwa na uwezo wa kupambana nayo. Tutaumia sote. Nchi i tavurugwa, tutapigwa wala hatutamjua anayetupiga, kama ambavyo hatukuweza kumkamata aliyetupiga kule Westgate n a M a n d e r a , K e n y a . Tumebaki tunaimba Al-Shabaab, Samantha Louise Lewthwaite (White Widow) na danganya toto nyingine kama hizo, utadhani hatuna akili timamu.

    Tukilitizama suala hili kwa sura yake halisi, tutaacha ushabiki wa kulifanya kuwa ni tatizo la ugaidi wa baadhi ya Waislamu, bali ni tatizo la ubeberu na mbinu zake ambapo tusipokuwa makini, sote tutaumia.

    Hivi sasa uta f i t i wa haraka haraka unaonyesha kuwa kuna vijana wengi kule Mwanza hawajulikani w a l i p o . K w a l u g h a mashuhuri miongoni mwa vijana wa Mwanza ni kuwa wa m e k we n d a s h a m b a . Wapo wazazi wanal ia , hawajui watoto wao walipo. Wapo wanawake, hawajui walipo waume zao, mpaka imebidi warejee makwao. Mis ik i t i wanapoibukia n a k w e n d a s h a m b a , inajulikana. Viongozi wao wanaowaghilibu mpaka kutoweka kwenda shamba, wanajulikana.

    Hapa kuna uwezekano wa namna mbili: Moja ni kuwa huenda Shamba ni Somalia/Syria, kwamba wamepenya wamekwenda huko au wapo hapa hapa nchini wakijiandaa kuja kuibuka kama bogey man la mfano wa Boko Haram.

    Kwa mtu binafsi kama a m b a v y o t u m e j i t a h i d i kufanya, inakuwa vigumu sana kujua kwa uhakika, huko shamba wanakokwenda vijana hawa ni wapi. Lakini tunaamini kuwa serikali inaweza kujua na kama nchi tukaweza kujinusuru na balaa linaloweza kujitokeza kama tutachelewa tukaibukiwa na bogey man letu.

    Kinachotutatiza ni kuona sehemu zinazozalisha vijana wanaokwenda shamba zinajulikana na zinazidi kunawiri, lakini kimyaa! Si Masheikh, viongozi wa Kiislamu wala wa serikali wanaoonyesha kujali.

    Inafikia mahali tunakuwa na wasiwasi kuwa isi je ikawa tumefikishwa mbali. Tumekuwa akina Pervez Musharraf wa kuwasaidia mabeberu kuunda vikosi vya bogey men wao katika nchi yetu. Lakini huo ni wasiwasi tu.

    Khadija Abubakar Abdulkadir, Maryam Said Aboud na Ummul Khayr Sadir Abdulla.

  • 8 AN-NUURJAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 3-9, 2015Makala

    Na Ally Nzomkunda

    NABII Swaalih alikuwa ni Mtume katika kabila maarufu ambalo jina lake linatokana na jina la babu yao Thamuud ambaye ni katika ukoo wa Nabii Nuuh. Kwa hivyo jina lake ni Swaalih ibn 'Ubayd ibn Maasih ibn 'Ubayd ibn Haajir ibn Thamuud, ibn 'Aabir ibn Iram, ibn Saam, ibn Nuuh.

    Naye Swaalih na watu wake wa Thamuud ni Wa a r a b u wa l i o k u wa wakiishi Hijr ambayo iko baina ya Hijaaz na Tabuuk (Kaskazini Magharibi ya Madinah) ambako siku moja Mtume alipita wakati wa n a e l e k e a k w e n y e vita vya Tabuuk kama tutakavyoelezea mwisho wa kisa hiki. Hiki ndio kisa chake Nabii Swaalih na watu wake kama tulivyoelezewa katika aya mbalimbali za Qur'an.

    Watu wa Thamuud walikuwa ni watu baada ya Nabii Huud (as) ambao walikuwa wakiabudu masanamu na baada ya kuletewa Nabii Huud (as) na kumkanusha, Allaah (sw) aliwaangamiza.

    Baada ya miaka, watu wa Thamuud wakaibuka na kuwa na nguvu na ufahari. Nao pia waliabudu masanamu, kwa hivyo A l l a a h A k a wa t u m i a mjumbe miongoni mwao naye ni Nabii Swaalih a m b a y e n a y e k a m a kawaida ya Mitume, alikuja na wito uleule wa kuwaita watu katika Tawhiiyd ya Allaah yaani kumuabudu Yeye pekee bila ya kumshirikisha na kitu, na kuwanasihi waache ibada ya masanamu na pia kuwataka watubu kwa Mola wao kwa kufuru wanayoifanya.

    N a k i n a T h a m u d tuliwapelekea ndugu yao Swaalih. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Yeye ndiye aliyekuumbeni k a t i k a a r d h i , n a akakuwekeni humo. Basi mwombeni msamaha, k i sha mtubu kwake . Hakika Mola wangu Mlezi yupo karibu, anaitikia maombi. (Huud: 61)

    Kwa maana kwamba: Amekujaa l ien i kuwa makhalifa baada ya watu wengine (kina 'Aad na

    Kisa cha Nabii Swaaalih sehemu ya Mitumewa nyuma yao) ili mfikiri na mtambue ubaya wao waliotenda, na nyinyi msiwe kama wao, na Akakujaalieni katika hii ardhi na kukuneemesheni neema mbali mbali kama za mashamba na matunda na majumba ya fahari mkastarehe, basi Yeye Pekee ndiye anayestahiki k u a b u d i w a b i l a y a kumshirikisha, vile vile mkabilini Mola wenu kwa kumshukuru na kufanya amali njema wala msjije kumkhalifu amri Zake na kutoka nje ya mipaka kwa kutokumtii, basi rudini kwake kwa kutubia na Yeye Allaah yuko tayari kupokea tawbah zenu.

    Aya ifuatayo inaeleza z a i d i n e e m a h i z o wal izojaal iwa na pia kuonesha ukumbusho wa Swaalih kwa hao watu wa Thamuud kwa kuwaita kwao kwenye dini ya haki.

    Na kwa Thamuud tulimpeleka ndugu yao, Swaalih. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni M w e n y e z i M u n g u . Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Hakika imekwisha kukufikieni Ishara iliyo wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Huyu ni ngamia jike wa Mwenyezi Mungu aliye ni Ishara kwenu. Basi mwachieni ale kwenye ardhi ya Mwenyezi Mungu, wala msimdhuru, isije kukushukieni adhabu chungu. (Al-A'araaf: 73)

    N a k u m b u k e n i a l i v y o k u f a n y e n i wa kushika pahala pa 'Aadi na akakuwekeni vizuri katika nchi, mnajenga majumba ya fakhari katika nyanda zake , na mnachonga majumba katika milima. Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu wala msitende uovu katika nchi kwa ufisadi. (Al-A'araaf: 74)

    Kama zilivyo umma zilizopita zilipojiwa na M i t u m e , wa k a a m i n i wachache miongoni mwao na wengi wakamkanusha.

    Na kwa kina Thamuud tulimtuma ndugu yao Swaal ih kuwaambia : Muabuduni Mwenyezi Mungu. Basi wakawa m a k u n d i m a w i l i yanayogombana. (An-Naml :45)

    W a l i o m k a n u s h a wal imshutumu kuwa anawaletea shari , na k wa m b a l a b d a a k i l i yake haiko sawa kwani hawakumtegemea yeye

    SHEIKH Ally Bassaleh (kushoto), Sheikh Rajab Katimba (katikati) na Sheikh Mohamed Issa (kulia).

    Swaalih ambaye kwao alikuwa ni mtu mwema kabisa, aje kuwakataza k u a c h a w a l i y o k u j a nayo mababu zao na kutaka wamfuate hayo anayotaka yeye Swaalih Wakamwambia;

    Wa k a s e m a : E w e Swaalih! Hakika kabla y a h a y a u l i k u w a u n a t a r a j i w a k h e r i kwetu. Je, unatukataza tusiwaabudu waliyokuwa wakiwaabudu baba zetu? Na hakika sisi tuna shaka na wasiwasi kwa hayo unayotuitia. (Huud: 62)

    Walikuwa na shaka kubwa juu ya yale Swaalih aliyowalingania nayo na kuyaona ni mapya! Swaalih akawajibu:

    Akasema: Enyi watu wangu! Mwaonaje ikiwa ninazo dalili zilizo wazi kutokana na Mola wangu Mlezi, naye akawa kanipa rehema kutoka kwake - je, ni nani atakaye ninusuru kwa Mwenyezi Mungu nikimuasi? Basi nyinyi h a m t a n i z i d i s h i a i l a khasara tu. (Huud:63)

    Akasema: Enyi watu wangu! Mwaonaje ikiwa ninazo dalili zilizo wazi kutokana na Mola wangu Mlezi.

    Dalili za dhahiri zenye uhakika kabisa kwa yale anayowaitia kumuabudu k wa m b a Ye ye n d i ye Mola wa Viumbe wote na Mola wa mbingu na Ardhi na mwenye kupasa kuabudiwa kwa haki.

    Naye akawa kanipa

    rehema kutoka kwake.Rehma kutoka kwa

    Allaah kumchagua yeye na kumpa uongofu na kumfanya Mjumbe Wake Allaah. Aliyemtuma kwao kuwatoa katika upotofu.

    Je, ni nani atakaye ninusuru kwa Mwenyezi Mungu nikimuasi?

    Nikiacha kukuiteni k a t i k a h a k k i y a kumuabudu Allaah Pekee, basi nyinyi hamtoweza kunifaa wala kuninusuru na adhabu yake Allaah atakaponiadhibu, bali itakuwa ni hasara tu na kuangamia kwangu. Vile vile wakamwambia:

    Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa waliorogwa. (Ashura: 153)

    M u j a a h i d k a s e m a ; Wamemaanisha kuwa kaathirika na uchawi. Wafasiri wengi wamefasiri k wa m b a i n a m a a n a ; Huju i unachokisema kutuita katika ibada ya mungu mmoja na kuacha miungu mingine! Hiyo ndio ilikuwa kawaida ya watu wa umma za nyuma, walipojiwa na Mitume yakawa majibu yao ni kuwaambia hao Mitume kuwa ni wachawi! kama alivyoambiwa vile vile Mtume na makafiri wa ki-Quraysh. Vile vile ni kawaida yao nyingine kuwadharau hao Wajumbe wa Allaah kwa vile wao ni binaadamu tu kama wao. Na wakisema:

    Wewe si chochote ila ni

    mtu kama sisi. (Ashura: 154)

    T h a m u d i w a l i w a k a n u s h a Waonyaji. Wakasema: Ati tumfuate binaadamu mmoja katika sisi? Basi hivyo sisi tutakuwa k a t i k a u p o t o f u n a k ichaa! . Ni yeye tu a l iyeteremshiwa huo ukumbusho kati yetu sote? Bali huyu ni mwongo mwenye kiburi! Kesho watajua ni nani huyo mwongo mwenye kiburi. (Al-Qamar : 23-26)

    Kama kweli yeye ni Mtume, basi wametaka miujiza ndio waweze kumuamini.

    Wewe si chochote ila ni mtu kama sisi. Basi lete Ishara ukiwa wewe n i miongoni mwa wasemao kweli. (Ashu'araa: 154)

    N a b i i S w a l i h akajitenga nao kwani alikwishakata tamaa nao:

    B a s i S w a a l i h akawaacha na akasema: E n y i wa t u wa n g u ! Nilikufikishieni Ujumbe wa Mola wangu Mlezi, na nikakunasihini, lakini nyinyi hamwapendi wenye kunasihi. (Al-A'araaf: 79)

    Ishara au Miujiza waliyotaka kutoka kwa Nabii Swaalih ni ngamia kama tutakavyoona: (Kisa kinaendelea ...)

  • 9 AN-NUURJAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 3-9, 2015Makala

    Inaendelea Uk. 12

    MACHI 24, 2015 Mtandao wa Kupashana Habari - Marekani na Ulaya wanaona vita kama nyenzo ya kuweka mamlaka na kudhibiti rasilimali ghali za nchi za Kiarabu na Kiislamu. Marekani yenye hulka ya kujiona na washirika wao wa Ulaya wanakosa hisia ya hatia kwa wahanga wa uharibifu na uteketezaji wa miaka kumi ya kuzikalia na kuziharibu Irak na A f g h a n i s t a n . K u i n u a mahitaji ya dhamira ya binadamu, wananchi katika nchi za Kiarabu wanaziona nchi hizi ni za kishenzi zaidi kuliko watangulizi wao wa Vita vya Msalaba vya karne ya 12.

    Kutojiweza kukiungana na ubinafsi kichaa, hufanya wa t a wa l a wa n c h i z a K i a r a b u z i n a z o z a l i s h a mafuta kuridhika na kufuata maagizo ya nchi za Magharibi licha ya changamoto za ndani na fitina katika tawala zao. Tamaa na ulazima wa kufanya maovu na kushindwa kwa uongozi wa kimaadili na kifikra, umeweka hatarini hali ya sasa na ya baadaye ya dunia yote ya Kiarabu na Kiislamu. Ukiangalia kwa karibu kinachopita akilini, ghadhabu na mauaji ya kidhehebu kila siku na kugeuza jamii ziwe za kijeshi vimeinua taswira potofu.

    Kwa kutojali kimaadili na kifikra viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu wamechoka na wanangoja na kungoja nini kitatokea baada ya hapa, bila ubunifu na fikra mpya kwa ulimwengu wa udadisi na uhalisia. Utumiaji vita wa kupanga na ukatili unaotokana na hali hiyo, imekuwa ndiyo sura ya kawaida ya dunia ya Kiarabu na Kiislamu. Wanasubiri muujiza utokee hivi hivi tu. Kupenda anasa na kulea hali ya kivita kumevuruga utamaduni asilia wa nchi za Kiarabu na mfumo wake wa hisia. Labda utajiri mpito wa fedha za mauzo ya mafuta umeleta mafanikio na imeondoa hisia ya hofu na aibu kwa kuwapa uwezo wa kudiriki kufanya uhalifu wowote dhidi ya heshima ya binadamu na wananchi. Mapambano ni kati ya ubabe wa tawala zinazoungwa mkono na nchi za Magharibi na harakati ya kutaka mabadiliko ya kisiasa miongoni mwa raia wa nchi za Kiarabu. Kila mahali watu wanapigana. Kwa karne yote, Waarabu wameshindwa katika vita hivyo. Viongozi wanaonekana kujikita katika jahiliya mpya isiyofahamika katika historia ya binadamu. K a m a m t u a k i u l i z a , wanapigana kwa ajili gani?

    Ni nani hasa washenzi - Nchi za Magharibi au Waislamu?Na Mahboob A. Khawaja

    WAPIGANAJI nchini Yemen wakiwa na silaha zao.Hakuna uhusiano wa mantiki katika vita inayosimamiwa na Marekani dhidi ya ISIL au Iran kuendesha Shiite kundi Al-Badr na wengine kufanya uhalifu dhidi ya waumini wa ki-Sunni au wa ki-Shia walio wachache. Hakuna maadili katika vita ya mawakala. Matendo yote ya kushambulia yanaamrishwa kwa makusudi kutokana na nia za wanaowatuma.

    Dunia ya Kiarabu na Kiislamu imeangukia katika ukatili wa kisiasa na tope la kudidimia. Mtu kuua mtu mwingine, na hakuna kujiuliza kwanini. Viongozi na watu wanaonekana kuwa katika ukurasa huo huo wa umwagaji wa damu, kuzorota kwa usalama na kupumulia mashine katika eneo la zama za kutatanisha linaloangukia kusikojulikana. Hawaamini katika chochote kile kana kwamba dunia imezubaa, kana kwamba hakuna Mungu na maisha hayana tena lengo tukufu la amani, uelewano na kuishi pamoja. Wapanga mikakati ya vita wa nchi za Magharibi ni sababu muhimu katika kuwafikisha kwenye hali hii potofu kimaadili na mlingano wa kibinadamu. Katika karne ya 21 yenye maendeleo ya juu kimaarifa, hekima na ufahamu, watu wanaka katika ujinga na kiburi cha kutokufahamu ubaya wa fikra zake. Utawala wa kidhalilmu wa nchi za Kiarabu na Kiislamu ukisukumwa na taswira yake yenyewe kufanya vita iliyopangwa na uchokozi d h i d i ya h a r a k a t i ya kimapinduzi ya wananchi wa Syria, Irak, Yemen, Misri, Libya na Bahrain. Baada ya miaka mitano, jumuiya ya kimataifa ni mtazamaji tu akiangalia uhalifu wa kutisha wa wachache dhidi ya wengi.

    Hakuna mamlaka ya dunia iliyopo tayari kuwalinda waathirika wa umwagaji

    damu unaoendelea. Hakuna sheria ya kimataifa kukataza machafuko. Viongozi wengi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu wanakosa uwezo wa kufikiria hali ya baadaye ya kisiasa yenye tija na kuelewa kusudi la maisha ya binadamu na vipaumbele vyake ndani ya wigo wa dunia hai na ulimwengu hai ambako kuna uwajibikaji makini wa mtu kuhusiana na wakati na mahali. Ni kwa njia gani ukatili huu wa kutengenezwa na hali ya machafuko kutasimamishwa na binadamu aokolewa kutoka janga la umwagaji d a m u k i m a d h e h e b u uliokolezwa kisiasa uliofikia pabaya sana na ni vigumu hata kufikiria matokeo yake?

    Ingekuwa wanamwamini Mungu, ubinadamu na madhumuni ya maisha ndani ya uwajibikaji unaoeleweka, Dunia ingeweza kuwa mahali pema zaidi kwa wote kuishi kwa amani. Mgawanyiko ya kuchukiza ya kidhehebu na mauaji ya wa-Sunni, wa-Shia, Wakristo na jamii nyingine za walio wachache katika nchi za Kiarabu imefikia kiwango cha kutisha na janga lisilopimika. Hivi jumuiya ya kimataifa inayojua nini kinatokea inataka kuona nchi za Kiarabu kujitengenezea yenyewe mwisho wake kikat i l i? Kumwua kwa makusudi binadamu mmoja ni kama kuua binadamu wote. Mabwana vita wa dunia wanawakilisha ukatili kimawazo usioweza kuona upande wa kibinadamu wa dhamira iliyo hai. William T. Hathaway ("Marekani inashambuliwa!") ambaye pia ni mwandishi wa Dunia ya Maumivu na profesa mshiriki wa elimu kuhusu nchi za bara la Amerika, Chuo Kikuu cha Oldenburg, Ujerumani, amejaribu kufafanua jinsi Marekani na Uingereza wameifikisha dunia katika

    kilele cha mauaji katika nchi za Kiarabu za Mashariki ya Kati:

    "Marekani na Uingereza zimefanya maovu kama hayo katika Irak, Syria, Lebanon, Libya, Indonesia na Afghanistan. Tulipindua ser ikal i zao, tukaweka madikteta, tukadhoofisha uchumi wao - yote i l i kuimarisha maslahi yetu ya kibiashara. Katika kila nchi ambako sasa kuna ugaidi, tulianza kwa kuwanyanyasa. Marekani inashambuliwa kwa sababu tu ilitangulia kushambulia. Haishangazi kuwa wanatuchukia. Fikiria tungejisikiaje kama nchi ya kigeni ingekuwa inatufanyia hivi. Tungejibu mapigo kwa njia yoyote ile tunayoweza ...... Kama watu wangefahamu hili - wangejua jinsi ilivyo rahisi kusimamisha ugaidi - wasingetaka kupigana vita hivi. Ndiyo maana vyombo vya habari vinapuuza madai ya al- Qaeda. Viongozi wa nchi za Magharibi hawataki watu waone kuwa nia halisi ya vita si kusitisha ugaidi ila kudhibiti raslimali za eneo hlo. Kusema kweli wanautaka ugaidi kwa sababu unawapa kisingizio wanachohitaji - tishio la adui mwovu."

    Ni nani hasa washenzi, n c h i z a M a g h a r i b i a u Waislamu?

    "Ilikuwa chini ya ushawishi wa Waarabu na Machotara walioinua utamaduni na siyo katika karne ya kumi na tano, ambako zama mpya za ustaarabu zilianza. Hispania si Italia, i l ikuwa ndiyo Ulaya ilipovamiwa upya ... Inawezekana kabisa kuwa kama siyo kwa mchango wa Waarabu, utamaduni w a k i s a s a w a U l a y a usingeanza kabisa; ni jambo la uhakika kabisa kwamba isingekuwa wao, isingekuwa n a m w e l e k e o a m b a o umetuwezesha kuvuka hatua zote za mabadiliko

    hadi hapa. Kwani licha ya kwamba hakuna eneo hata moja la kukua kwa Ulaya ambako mchango muhimu wa utamaduni wa Kiislamu hauonekani, hakuna ambako hilo liko wazi na muhimu kama katika kuzaliwa kwa mamlaka ambayo ni kielelezo mahsusi cha dunia ya kisasa na mwanzo mkuu wa ushindi wake." (Robert Briffault, profesa wa Chuo Kikuu cha) Cambridge, 'Uasisi wa Binadamu,' London. 1919

    Waarabu waliwahi kuwa waanika njia ya ustaarabu endelevu uliojikita katika elimu uliodumu kwa miaka 800 - kipindi kirefu zaidi cha kuongoza kwa ustaarabu katika historia ya binadamu. Hivi sasa, wasomi wa nchi za kikoloni za zamani na wakaliaj i kwa mabavu wanawaita Waarabu na Waislamu kama watu wa 'siasa kali' na 'washenzi.' Katika muda wote wa karne ya 20 na hadi kuingia karne ya 21, utajiri mafuta ulishindwa kukabiliana na matatizo ya kijamii, kimaadili, kifikra na kisiasa. Badala yake, kuingizwa mkondo wa kijeshi wa ukanda huo, kuongezeka kwa mauaji kunaonyesha mkanganyiko mpana wa kisiasa.

    Uislamu uliwatajirisha Waarabu wakawa viongozi wa utamadunmi wenye kasi ya maendeleo. lakini kukua kwa haraka kutokana na mafuta kumewabadilisha kuwa 'waendesha mbio za ngamia' na walengwa wa vicheko vya kina katika meza za chakula cha jioni katika utamaduni wa Magharibi. Wakati Waarabu wakiwa na bidii ya kimisionari ya "kukataza maovu, na kukar ib i sha b inadamu wote kuyaelekea mema," walifanikiwa sana katika mabadiliko ya kibinadamu, uongozi wa kimaadi l i , m a e n d e l e o ya v i t u n a ustaarabu. Fedha haiwezi kununua hekima, heshima na uadilifu wa kibinadamu. Marehemu Mfalme Abdullah wa Saudia na Sheikh Sabah al-Sabah wa Kuwait wote wawili walikuwa nyororo katika kutoa msaada wa hali na mali kwa George Bush mwaka 2003 wakati wa uvamizi wa Irak na mauaji ya watu takriban mamilioni tatu nchini Irak wakati wa ukaliaji nchi hiyo kwa muda mrefu. Uwongo wa 'vita dhidi ya ugaidi' usingetokea iwapo viongozi wa nchi za Kiarabu - wanaotumiwa m s t a r i w a m b e l e w a Marekani - wangekuwa na mwelekeo chanya wa akili, uwezo wa kufikiri na uadilifu kukinzana na hatua isiyo na mantiki kabisa na ya kikatili katika historia ya binadamu.

  • 10 AN-NUURJAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 3-9, 2015Makala

    Inaendelea Uk. 11

    WA K AT I M a r e k a n i i l i p o t a n g a z a k u w a inawashambulia ISIS, baadhi ya wasomaji wetu walituandama kwa maneno makali wakidai kuwa kile tulichokuwa tukisema juu ya uhusiano wa Abu Baghdad (ISIS) na Marekani, ilikuwa uwongo mtupu. Msingi wa shutuma zao ni kuwa wakati sisi tukijenga h o j a k u wa I S I S n i mawakala wa mabeberu wakitumika katika proxy war ya kuisambaratisha Syria, Iraq na Mashariki ya Kati kwa ujumla, wapo Waislamu walikuwa wakiamini kuwa ISIS walikuwa katika Jihad ya kusimamisha Dola ya Kiislamu/Khilafah (Islamic State) . Sasa i l ipokuwa Marekani inawashambulia ISIS, wakaja na hoja kuwa kama IS wangekuwa mawakala, mamluki na vibaraka wa Marekani, basi isingekuwa tena Marekani iwashambulie IS. Baadhi ya wasomaji hao wakaenda mbali kwa kuja na kashfa na matusi wakisema kuwa sisi ni Mashia na kwamba kwa vile jeshi la Iraq na serikali ya Iraq inadhibitiwa na Mashia, basi Marekani i n a s h i r i k i a n a n a inawasaidia Mashia kuzuia Dola ya Kiislamu kusimama Syria na Iraq.

    Sisi tulisema kuwa mashambulizi ya Marekani hayalengi kuwamaliza I S , w a l a M a r e k a n i haiwashambulii IS, bali inachofanya Marekani ni kutumia kisingizio cha kuwashambulia IS kupiga na kuharibu miundo mbinu na viwanda vya Syria , kama mkakati wa kumdhoofisha na h a t i m a ye k u m n g o a Bashar Assad. Lakini pia IS kuingia Iraq, ni namna ya kukuza mgogoro wa Shia na Sunni (Waislamu) na kuacha wauwane wenyewe kwa wenyewe. IS kuwepo Iraq na tangazo n a M a r e k a n i k u w a inapeleka jeshi kuwapiga, n i k i s ing iz io tu cha kurejesha na kubakisha jeshi la Marekani katika nchi hiyo ikizingatiwa k u wa i l i s h a t a n g a z a kuondoka. Na hadi sasa wakati Marekani ikidai kuwa inawapiga IS, bado

    Siasa za mabeberu Iraq na YemenMashabiki wa Abu Baghdad mnasimama wapi!Kama Iraq ni tatizo la Shia kuzuiya KhilafahYemen napo Waarabu wanachopigania nini?

    Na Omar Msangi

    Marekani inawapelekea silaha IS na usaidizi wa kila namna kama ambavyo imekuwa ikifichuliwa

    na hata na jeshi la Iraq linalodaiwa kusaidiwa na Marekani kuwapiga IS.

    Pa m o j a n a u k we l i

    huo, bado waliokuwa wakitukashifu kuwa ni Mashia na tunaungana na Mashia (Jeshi la Iraq)

    likisaidiwa na Marekani kuzuiya Dola ya Kiislamu, Iraq na Syria, walibaki na msimamo wao wakisubiri D o l a y a K i i s l a m u kusimama Iraq na Syria chini ya ISIS.

    Katika Yemen, kundi linalojulikana kwa jina la Ansar Allah (anr allh - "Supporters of God"), maarufu kwa j ina la Houthis (al-thiyyn), l ik i tokana na j ina la kiongozi wao wa awali Hussein Badreddin al-H o u t h i , a m b a o n i Mashia wa dhehebu la Zaidi Shia, wamemtimua madarakani Rais wa nchi hiyo Abdrabbuh Mansour Hadi.

    L a b d a t u u l i z e , kwa wale waliokuwa wakisema kuwa Marekani i n a wa s a i d i a M a s h i a kuzuiya kusimama Dola ya Kiislamu ya Abu Baghdad, katika mgogoro huu wa Yemen wapo upande gani. Je, wapo upande wa Saudia Arabia na Israel wanaowapiga Houthi au wapo upande wa Houthi. Na je, wanachotafuta Israel, Marekani na Saudia Arabia, ni kuzuia Ushia kusimama Yemen? Kama utasema ni kuzuiya Ushia k u c h u k u a m a d a r a k a Yemen, mbona katika Iraq ni Mashia na Marekani wanaowapiga IS . Na je, mbona katika Syria ni Masuni walioungana na Marekani na Israel kuwapiga Mashia?

    Hivi sasa Saudi Arabia ik isaidiana na Israel (Israeli Fighter Jets Join Saudi Arabia in War on Yemen), inawashambulia wapiganaji wa Houthi. L a k i n i k wa u p a n d e mwingine pia Marekani japo haijapeleka jeshi, lakini imetangaza kuwa inaisaidia Saudia Arabia na muungano unaoundwa na nchi za Kiarabu kuwapiga Mashia wa Houthi. Jingine ni kuwa wakati Marekani inaendelea kuwapiga Masuni wanaodaiwa k u wa n i A l - Q a i d a h , haiwapigi Houthi. Lakini la ziada ambalo limejitokeza ni kuwa wakati Marekani inasaidiana na Israel, Saudi Arabia na muungano wa nchi za Kiarabu kuwapiga Houthi , kwa mlango wa nyuma ina ta fu ta kuwasiliana na Houthi waliomtimua Rais wa Yemen na kuwahakikishia

    Picha Juu na chini ni wapiganaji wa Yemen waliomuondoa Rais madarakani

    MAKOMBORA ya Saudi Arabia yaliyopo mpakani yakielekezwa Yemen.

  • 11 AN-NUURJAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 3-9, 201511 AN-NUURMakala

    Siasa za mabeberu Iraq na YemenInatoka Uk. 10

    kuwa watakuwa pamoja nao.

    L a s t we e k , O b a m a administration officials were scrambling to contact Houthi leaders and assure them that the United States doesn't consider them an enemy.

    Ndivyo linavyoripoti gazeti la Los Angeles Times.

    We're talking with everybody everybody who will talk with us.

    Los Angeles Times, lilimnukuu Afisa mmoja wa White House akisema.

    (Tazama: Why the U.S. is courting the Houthis taking control in Yemen-By Doyle McManus, LOS ANGELES TIMES)

    Hii tafsiri yake ni kuwa Marekani inataka Houthi wabakie kuwa na nguvu kama walivyo IS kule Syria na Iraq ili Waislamu (Shia na Sunni), waendelee kuuwana katika Yemen.

    Katika Syria, vyovyote u t a k a y o t i z a m a , wanaouwana ni Waarabu wa Syria na Waislamu wa Syria. Katika Iraq, wanaouwana ni Waarabu wananchi wa Iraq, ni Waislamu kwa Waislamu w a n a o u w a n a k a m a ambavyo katika Somalia wanaouwana ni Wasomali kwa Wasomali, Waislamu kwa Waislamu.

    Katika Yemen hivi sasa kuna hatari inayotaka kujitokeza, kwa kuingia Saudia Arabia kijeshi Yemen kuwapiga Houthi ambao inaaminika kuwa wanasaidiwa na Iran, ipo hatar i Hizbul lah kuingia katika mgogoro huo kuwatetea Houthi (Mashia). Lakini ipo hatari pia kwa Iran kuingia. Na hiyo itakuwa ni vita ya Waislamu kwa Waislamu. We ukisema wale Mashia au wale Masuni, haibadili kuwa wanaopigana ni Waislamu na kama ni miji na nchi kuharibika, inayoharibika ni miji na nchi za Waislamu.

    Taarifa kutoka Iraq z inafahamisha kuwa wapiganaji wa Kishia- Iraq Iraqi Militiamen, wanajikusanya kwenda k u p i g a n a Y e m e n k u w a s a i d i a H o u t h i dhidi ya Saudia Arabia na muungano wake wa Waarabu wanaosaidiwa na Marekani na Israel. (Tazama: Iraqi Militiamen Plan To Travel To Yemen To Battle U.S.-Backed Coalition)

    T u m e w a p i g a n a

    kuwashinda ISIS Syria, hivi sasa tunawapiga na kuwaangamiza ISIS ndani ya Iraq, tutawapiga pia Yemen, amesema Abu Kumael, ambaye ni mmoja wa wapiganaji wa

    kundi la Kishia la Iraq likijulikana kwa jina la Peace Brigades.

    Sisi sio wapiga porojo, sio watu wa kusema ovyo, tuko imara na tutawapiga na kuwashinda Wasaudia

    n a wa s h i r i k a wa o , a l i o n g e z a m p i g a n a j i huyo. Kundi jingine la Kishia ambalo linajiandaa kuingia Yemen ni lile la Badr Organization.

    Katika Iraq, wapiganaji

    wa Kishia, wapo pamoja na Marekani wakipigana dhidi ya Islamic State. Sasa katika Yemen, Marekani ipo pamoja na Masuni wa Saudia Arabia na Misri kupigana dhidi ya Mashia, Houthi.

    Kwa upande mwingine litizame hivi: Katika Syria, Marekani inampiga Bashar Assad wakati Iran ikimuunga mkono. Katika Iraq namna yake ni kama Iran ipo pamoja na Saudi Arabia na Marekani kuwapiga IS. Inapokuja katika Yemen, mahesabu yanabadilika. Marekani ipo na Saudia Arabia kuwapiga Houthi na hivyo kuipiga Iran.

    Ni kama alivyojisema aliyekuwa kachero wa CIA katika kikosi cha kupambana na Osama Bin Laden, Michael Scheuer, pale aliposema:

    The thing was ideal when IS was advancing on Baghdad because Sunnis were killing Shias. That's exactly what we need. - Our best hope right now is to get the Sunnis and Shias fighting each other and let them bleed each other white."

    (Tazama: Channel 4 Regrets Letting Ex-CIA Agent Claim Baghdad Massacre Would Have Been 'Ideal')

    Katika vita ya Syria na Iraq, ambapo imekuwa i k i t a n g a z w a k u w a I S wamekuwa wakiuwa Mashia na kuharibu misikiti na taasisi zao, kiongozi wa Hizbullah, Nasrallah alijitahisi sana kuwazuiya wapiganaji wake kujiingiza kwa vita hiyo kwa sababu itakuwa ni kunasa katika mtego wa maadui wa Uislamu na mabeberu wanaotaka kuisambaratisha Mashariki ya Kati. Iran, kama serikali, nayo ilifanya hivyo.

    Inavyoelekea hili la Yemen a m b a p o m j u m u i k o wa Saudi Arabia, Misri, Qatar, Jordan, Bahrein, wakisaidiwa na I srae l na Marekani wanawapiga Houthi, ni katika juhudi mpya za Mabeberu za kuwaingiza Waislamu kwa maana ya Mashia na Sunni, katika vita ya wenyewe kwa weyewe. Kama alivyosema kachero wa CIA Michael Scheuer, wamwage damu zao mpaka wakauke-Our best hope right now is to get the Sunnis and Shias fighting each other and let them bleed each other white."

    Sasa sisi badala ya kukaa kitako na kuangalia namna ya kujinusuru na njama hizi za makafiri, tukae tu na tamaa za fisi kuwa Abu Baghdad anatupigania kusimamisha Khilafah na akitoka huko analeta Khilafah hiyo kwetu!

    Hassan-Nasrallah, kiongozi wa Hezbollah

    PICHA juu na chini ni wapiganaji wa Kishia

  • 12 AN-NUURJAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 3-9, 201512 MAKALA

    ILALA ISLAMIC SECONDARY USAJILI S.2401KIDATO CHA TANO NA KURUDIA MITIHANI

    KWA WASICHANA TUIPO: ILALA-AMANA-MTAA WA ARUSHA: MASJID SHAFII

    SHULE YA BWENI NA KUTWA

    MASOMOMath, Phy, Chem, Bios, Geo, Civ, Eng, Kisw, Commerce,

    B/keeping Islamic, Arabic na Tahfidhul QuranCOMBINATION

    PCM,PCB,CDG,HGL,HGK,HGE,HKA,HEAUFAULU 2014

    KIWILAYA 3/76, KIMKOA 10/191, KITAIFA 118/2322Kwa shule za kiislam KIWILAYA (1) KIMKOA (2) KITAIFA (5)

    Zipo nafasi za kuhamia kidato cha II, III na IV, VMAWASILIANO

    Simu: 0713 007586, 0715 187515, 0714 393822, 0714 381964

    KWA WAVULANA TUIpo Ilala-Bungoni: Masjid Taqwa

    DAR ES SALAAM ISLAMIC SEC.

    MASOMOMath, Phy, Chem, Bios, Geo, Civ, Eng, Kisw, Commerce, B/

    keeping Islamic, Arabic na Tahfidhul Quran

    COMBINATIONPCM,PCB,CDG,HGL,HGK,HGE,HKA,HEA

    UFAULU 2014Kama Ilala Islamic, imetenganishwa toka Ilala Islamic

    Zipo nafasi za kuhamia kidato cha II, III na IV, VMAWASILIANO

    Simu: 0713 007586, 0715 187515, 0714 393822, 0714 381964Ada ni nafuu na inalipwa kwa awamu nne

    MLETE MWANAO APATE ELIMU NA MALEZI BORA

    USAJILI S.4384

    Adayo hupendeleya, wa dinenu wapinzani,Mazuri kuyazuiya, yenu pasi hata soni,Kukuswibuni mabaya, wao ndilo hutamani,UKWELI wa QUR-ANI, si kombo u dhahiriya.

    Daima huwatakiya, yale yanokudhuruni,Ya shururi huridhiya, ninyi yanokufikeni,Ya khairati udhiya, yenu kwao ng'amueni,UKWELI wa QUR-ANI, si kombo u dhahiriya.

    Gaidhi i dhahiriya, kutoka mwao vinywani,Vyanda wanawaumiya, kwa indazo mitimani,Waloficha batiniya, kungaye i kwa MANANI,UKWELI wa QUR-ANI, si kombo u dhahiriya.

    Si kwamba nawazuliya, ishanena QUR-ANI,SURA ya TATU rejeya, si nyingine IMRANI,AYA nawakashifiya, hayo zenye kubaini,UKWELI wa QUR-ANI, si kombo u dhahahiriya.

    MIATU wa THAMANIYA, ASHARA kwa tamakuni,Soma thuma endeleya, hadi MIA ISHIRINI,Humo utajioneya, yote kwa wake ndani,UKWELI wa QUR-ANI, si kombo u dhahiriya.

    ALLAH alotuambiya, si dhahania yakini,Wenyewe mwashuhudiya, yawahusu wao nini!MAHKAMA kugomeya, ya KADHI mahakamani?UKWELI wa QUR-ANI, si kombo u dhahiriya.

    Na hofu wamewatiya, viongozi wa nchini,Si kwa hoja usuliya, kwa pogo yao mizani,Lengo walokusudiya, lipate kuyumkini,UKWELI wa QUR-ANI, si kombo u dhahiriya.

    Nudhumu namaliziya, kwa nyote kukuombeni,Kujifunza kuteteya, kwa pamoja yenu dini,'Wenzenu' huwa pamoya, kwa yao hamuwaoni?UKWELI wa QUR-ANI, si kombo u dhahiriya.

    ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.

    NONGWA YA MAHKAMA YA KADHI

    Mimi nina sikitiko, limenijaa moyoni,Nimepata fadhaiko, wa kufariji nani,Juhudi zangu ni mwiko, wana hawazithamini,Baba nae ni mzazi sifa anastahiki.

    Kila nikijitahidi, sifa sipewi kwa nini,Mbona hamna miadi,nyinyi ni watoto gani,Au mwafanya kusudi, mnitoe duniani,Baba nae ni mzazi, sifa anastahiki.

    Zote mwelekeza sifa kwa mama mzazi,Baba mi mmenibeza, hamjali yangu kazi,Leo nawabembeleza, au niachie ngazi,Baba nae ni mzazi, sifa anastahiki.

    Mimi kwenu kama baba, nawajibika kwa mengi,Jukumu langu ni kubwa, na tena ni la msingi,Si tu kuleta ubwabwa, mkafaidi mitungi,Baba nae ni mzazi, sifa anastahiki.

    Mtume katuhimiza, kuwashukuru wazazi,Hakuna alo m-beza, na kuweka pingamizi,Japo mama ni wa kwanza, ila baba ni farazi,Baba nae ni mzazi, sifa anastahiki.

    Shime tuwapeni sifa, mababa zetu jamani,Wamelijenga taifa, malipo yao kwa nani,Tusisubiri wakafa, wakaenda kuzimuni,Baba nae ni mzazi, sifa anastahiki.

    Hayo tukiyatimiza, tutapunguza majonzi,Nyoyo tutazisuuza, na kuondosha simanzi,Mababa watatutunza, na kuboresha malezi,Baba nae ni mzazi, sifa anastahiki.

    Sasa ninahitimisha, wasia wangu jamani,Yatosha nilokumbusha, wanangu tekelezeni,Dharau kutozidisha, wazee tutaabani,Baba nae ni mzazi, sifa anastahiki.

    Zainab Mtima, Mbweni- Zanzibar. 0717 165 602

    SHAIRI LA BABA

    Ni nani hasa washenzi - Nchi za Magharibi au Waislamu?Inatoka Uk. 9W a a r a b u w a l i u n d a utamaduni wenye undani wa elimu na kuonyesha njia ya kuvumiliana, unaojumuisha watu wa mataifa mbalimbali, imani na lugha -hivyo kutoa msukumo wa maendeleo ya kila kitu kutoka hisabati na unajimu, sayansi ya tiba, ushairi na mawazo ya hali ya baadaye ya ustaarabu duniani, elimu, sheria na haki , ubunifu majengo u n a o s t a h i m i l i n g u v u ya uvutano, hadi kufikia maktaba ya kisayansi na mengi zaidi.

    Dunia ya Kiarabu na Kiislamu ilishindwa kutoa kiongozi yeyote mwenye upeo na uadilifu kifikra i l i k u e n d a n a n a h a l i inayobadi l ika duniani na masuala magumu ya kimataifa karne ya 21.

    Wakati Waarabu wakiwa wanaongoza katika Imani ('Emaan') na maadili ya k i b i n a d a m u , wa l i i n u a utamaduni wa aina yake unaokubal i to faut i za kiimani na tamaduni tofauti za kijamii na kujenga kupitia msingi wa umoja wa imani ya Kiislamu kustawisha kuishi kwa amani na maendeleo ya binadamu. Ukiorodhesha uvumbuzi na michango ya wasomi wa Kiislamu, hayahesabiki. Je, unajua wanasayansi wengine au wanazuoni ambao michango yao ilitumika katika vitabu v ya k u f u n d i s h i a k wa karne sita katika vyuo vya tiba barani Ulaya? Fikiria Muhammad Hussein bin Ali Sina na Kanuni za Msingi za Tiba. Wazungu walibadili jina lake kuwa Avicenna hivyo hakuna mtu angejua kwamba alikuwa mwanazuoni wa Kiislamu. Inasemekana Ibn Sina pekee aligundua na kuwezesha kuthibitishwa dawa za aina 36 zinazoendelea kutumika hadi sasa. (Angalia tungo ya Marai Rosa Menocal - Enzi Kuu ya Kuvumiliana: Pambo la Dunia: Jinsi Waislamu, Wayahudi na Wakristo Walivyounda Utamaduni wa Kuvumiliana katika Hispania ya Kimwinyi, i l i y o c h a p i s h wa 2 0 0 3 ) . Anaeleza kuwa "mafunzo ya historia, kama mafunzo ya dini, mara nyingi hupuuza mifano ya kuvumiliana.

    Miaka elfu moja iliyopita katika Peninsula ya Iberia (Ulaya Kusini), mwelekeo wenye hisia za kimaendeleo wa U i s l a m u u l i k u wa umejenga utamaduni wa hali ya juu zaidi barani Ulaya .... Huko Cordoba, maktaba yake ilikuwa na vitabu 400,000 wakati ambapo maktaba kubwa katika eneo la Ukristo wa Kilatini barani Ulaya haikuwa na zaidi ya vitabu 400. "

    Kushusha mapipa ya mabomu kila siku nchini Syria, ulipuaji wa mabomu ya kutegwa kwa gari jijini Baghdad, uasi wa ki-Shia wa Houthi unaofadhiliwa na Iran nchini Yemen, mapambano ya n a y o s a b a b i s h a v i f o vingi katika mitaa ya Cairo na Tripoli - mamilioni wanaondolewa na kufutika kila sekunde kana kwamba s i b inadamu. Yote h i i inaonyesha utamaduni ulioparaganyika wa nchi za Kiarabu wenye mwenendo wa k u t i s h a u s i o w e z a kurudishwa nyuma. Hali ya baadaye inatiwa giza na nguvu za uovu. Utumiaji

    silaha na chuki vinazamisha kwa haraka upana wa jamii za Kiarabu na Kiislamu katika mawimbi ya vifo na kuvunjiliwa mbali kwa jamii. Takwimu za mauaji ya kila siku hujenga kiwewe k a t i k a v y o m b o v ya habari kinachoendana na alichosema Samuel H u n t i n g t o n ( m a d a y a " M t a f a r u k u w a Ustaarabu," katika jarida la Mambo ya Nje nchini Marekani mwaka 1993), akidai kuwa "Uislamu una mipaka ya damu."

    (Dk. Mahboub A. K h a wa j a n i m t a f i t i wa u s a l a m a , a m a n i na kutatua migogoro duniani na ulinganishi wa tamaduni za Magharibi na Kiislamu, na ntunzi wa machapisho kadhaa ikiwa ni pamoja na kitabu cha hivi karibuni, "Amani ya Dunia na Usuluhishi wa Migogoro: Binadamu na Watu Wanapotafuta Fikra Mpya," kilichotolewa na Lambert Academic P u b l i s h i n g n c h i n i Ujerumani, Mei 2012.)

  • 13 AN-NUURJAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 3-9, 2015HABARI

    KATIBU Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amehudhuria mazishi ya Hemed Salum Hemed (38) aliyefariki katika ajali ya barabarani i l i y o t o k e a wa k a t i akirudi katika mkutano wa hadhara wa chama h i c h o u l i o f a n y i k a Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.

    Marehemu ambaye ni mkaazi wa Kinuni, Wilaya ya Magharibi U n g u j a a l i s wa l i wa katika Msikiti Ngamia, Kilimahewa na kuzikwa Kianga, mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

    Aidha, Maalim Seif a l i w a t e m b e l e a n a kuwawafariji baadhi ya wafuasi wa chama hicho waliojeruhiwa na watu wasiojulikana wakati walipokuwa wakirudi katika mkutano huo walipofika eneo la Fuoni.

    Tukio la kujeruhiwa wafuasi 24 wa chama cha CUF waliokuwa w a k i t o k e a k a t i k a mkutano wa hadhara huko Makunduchi , a m b a o we n g i wa o walikuwa ni vijana, lilitokea hivi karibuni k u f u a t i a v i j a n a waliokuwa katika gari eneo la Fuoni Taveta wakiwa na mapanga, n o n d o n a m a w e kuwarushia mawe

    Kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu wa CUF Bi. Pavu Juma, alisema baadhi ya majeruhi hao walipata majeraha makubwa na wamelazwa kat ika hospi ta l i ya Mnazimmoja na wengine wamesafirishwa hadi Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

    M a p e m a akiwatembelea baadhi ya m a j e r u h i h u k o M w e m b e m a k u m b i , Kat ibu Mkuu huyo w a C U F , M h e . Maal im Se i f Shar i f Hamad, alisema watu waliowajeruhi wafuasi wa CUF wamefanya hivyo baada ya chama chao kukosa sera za kuwaeleza Wananchi na sasa wameamua k u f a n y a h u j u m a a m b a z o a m e s e m a hazitowasaidia.

    Maalim Seif ahudhuria mazishiAwapa pole walioshambuliwaAwasihi CUF kuwa watulivu

    Na Khamis Haji (OMKR)

    KATIBU Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (wa tatu kutoka kulia), akihudhuria mazishi ya Hemed Salum Hemed (38) aliyefariki katika ajali ya barabarani iliyotokea wakati akirudi katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja hivi karibuni.

    Alirejea wito wake wa kuwataka wanachama na wafuasi wa CUF wawe watulivu na kwamba, chama hicho kinafuatilia kwa karibu hujuma zote zinazofanywa dhidi yao.

    A w a l i M a a l i m Seif Sharif Hamad, aliwanasihi wanachama w a c h a m a h i c h o kushikilia msimamo wao wa kuendesha siasa za kistaarabu na kuacha k u f i k i r i a k u l i p i z a kisasi kufuatia hujuma zinazofanywa dhidi ya chama hicho.

    A l i s e m a l e n g o kubwa la hujuma hizo, zikiwemo kuchomwa moto kwa ofisi za chama hicho ni kutaka kukitoa chama katika malengo yake ya kupigania haki za wananchi na kwamba, njama hizo hazitoweza kufanikiwa.

    Nakunasihini sana wanachama wa CUF msichokozeke, hawa wanaofanya hujuma hizi wana lengo la kututoa katika malengo yetu ya kupigania haki, lakini nakuombeni musiuingie mtego huo, alisisitiza Maalim Seif.

    Maalim Seif alitoa nasaha hizo wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika viwanja vya Jamhuri, jimbo la Makunduchi.

    Alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi w a M a k u n d u c h i k wa m wa m k o wa o waliouonyesha katika kukiunga mkono chama hicho, ambapo jumla ya wanachama wapya 5 8 4 wa l i j i u n g a n a CUF katika mkutano huo, miongoni mwao wakiwemo makada wa Chama Cha Mapinduzi.

    A l i s e m a h a t u a h i y o i n a dh i h i r i s h a jinsi wanachama wa CUF katika maeneo m b a l i m b a l i n c h i n i w a n a v y o w e z a kuungana kwa aj i l i ya kutetea haki zao bila ya kujali maeneo wanayotoka.

    A k i z u n g u m z i a mipango ya chama hicho, Maalim Seif, alisema chama kinakusudia kuleta mabadiliko kwa kujenga uchumi imara ambapo kila mwananchi ataweza kunufaika na

    rasilimali zilizopo. Z a n z i b a r i n a z o

    ras i l imal i na fursa nyingi za kiuchumi lakini bado hazijatumika ipasavyo kuwanufaisha wananchi wa kipato cha chini, endapo CUF kitashika hatamu za dola, kitaziibua fursa hizo na kuwafanya vijana wengi kuweza kupata ajira katika sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, uvuvi, biashara, utalii na viwanda vidogo vidogo. Alifafanua Katibu Mkuu huyo.

    K u h u s u k a t i b a i n a y o p e n d e k e z wa , Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar alisema Serikali bado haijawahi kukaa na kutoa msimamo juu ya kat iba h iyo , na kufafanua kuwa hakuna msimamo wa serikali juu ya jambo hilo.

    A l i s e m a m a wa z o y a n a y o e n d e l e a kutolewa kuhusiana na katiba hiyo, yanabakia kuwa misimamo ya vyama na siyo msimamo w a s e r i k a l i k a m a inavyodaiwa na baadhi

    ya viongozi wa kisiasa. M i m i n i k i w a

    Makamu wa Kwanza wa Rais, kama Serikali h a t u j a w a h i k u k a a k w e n y e B a r a z a l a Mapinduzi wala kikao chochote cha kiserikali k u j a d i l i a u k u t o a msimamo kuhusu katiba inayopendekezwa, sasa inakuwaje wengine wanasema msimamo wa serikali ni huu, alihoji Maalim Seif.

    Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa C U F Z a n z i b a r , Nassor Ahmed Mazrui, alisema mwaka 2015 ni mwaka wa wana CUF kufanya maamuzi ya kukiweka chama hicho madarakani kwa kukiwezesha kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu ujao.

    K a t i k a m k u t a n o h u o , w a z e e w a C U F M a k u n d u c h i walimkabidhi Maalim Seif, ufunguo maalum kwa ajili ya kuifungua Z a n z i b a r a m b a y o w a m e d a i k u w a imekwama kwa zaidi ya nusu karne sasa.

    Kabla ya kuhutubia mkutano huo, Katibu Mkuu huyo alifanya ziara ya kutembelea barza na matawi ya CUF na kupata fursa ya kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika matawi na barza hizo, z ik iwemo mbi l i za akinamama.

    Katika ziara hiyo, Maalim Seif ambaye aliambana na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, aliwahimiza wanachama wa barza hizo kuanzisha matawi kamili kutoka na idadi kubwa ya wanachama waliyonayo.

    M i o n g o n i m w a b a r z a n a m a t a w i yal iyozinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi ni pamoja na Barza ya Kizimkazi Dimbani , Barza ya Ukawa ya Nganani, Barza ya Ismail Jussa ya Kitundani, Fatma Ferej Madete Barza na Tawi la CUF Shakani.

    Wanachama wapya waliojiunga na CUF kutoka CCM ni pamoja na aliyekuwa mjumbe wa Baraza la Wazazi Wilaya ya Kusini Bw. Yahya Mkongoa Ali na aliyekuwa mhamasishaji wa CCM katika eneo hilo Bi. Kihamba Ali Ronge.

  • 14 AN-NUURJAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 3-9, 2015Makala

    Na Ben Rijal

    Na Ben Rijal

    MAKALA hii itamuangalia Mwanasayansi, mjuzi wa elimu ya nyota na hesabati Al-Sabi Thabit ibn Qurra al-Harrani alioishi kutika mwaka wa 826 hadi 901. Thabit ibn Qurra alikuwa a k i f a h a m u l u g h a y a Kiyunani vilivyo na ufahamu wake huo ulimuwezesha kuzitafsiri kazi mbalimbali zilizoandikwa na Wayunani.

    Thabit ibn Qurra alikuwa ni mjuzi wa hesabati na elimu ya nyota. Aidha akiheshimika na uele