annuur 1144

Download ANNUUR 1144

Post on 26-Dec-2015

817 views

Category:

Documents

0 download

Embed Size (px)

TRANSCRIPT

 • ISSN 0856 - 3861 Na. 1144 DHULQAAD, IJUMAA , SEPTEMBA 26-OKTOBA 2, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

  Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz

  Uk. 16

  M U U N G A N O wa kweli ni wa kuheshimiana, wa kufuata haki na usawa kwa ki la upande.

  SMZ itavuruga amani Zanzibar

  Inarudia yale ya Wareno, MapinduziMakkah walikimbilia kwa mfalme NajashMasheikh Zanzibar nao wakimbilie wapi?

  Mujahidina fekiKifaa cha maadui wa UislamuWatumika kuangamiza Waarabu

  RAIS wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein.

  SHEIKH Mohamed Idd Mohamed.

  Watanzania tujifunze kutoka UK, Scotland

  Kura ya maoni ya wananchi muhimuTusidharauliane kwa ukubwa, udogoWala kwa kejeli za wauza vitunguu

  T u n a p o j a d i l i faida za muungano, tujikite katika uzito wa hoja si kelele za mchele wa Mbeya na tashtiti za dharau kwa wengine.

  Khofu ya j esh i kuchukuwa nchi na tashtiti za kutuita wauza vitunguu, haitasaidia kurejesha umoja tunaoutamani. (Soma uk. 3)

  WAPIGANAJI ISIS katika nchi za Iraq na Syria.

  NIMEHUZUNISHWA sana kwa maneno ya uongo kutoka mdomoni mwa kiongozi wa kidini mwenye cheo cha Upadre.

  Kama Padre anaweza

  Askofu anapokuwa muongowaumini wake watakuwaje!

  Padri Mapunda unampima vipi Kikwete, MkapaMwache Mzee Mwinyi, waulize Kingunge, SlaaIla asante kwa kutuzindua Waislamu usingizini

  k u s e m a u o n g o i l i kufanikisha matakwa yake, je, waumini wafanye nini?

  Hivi kumbe mgogoro wa Somalia wanagombea Ukadhi? (Soma Uk. 6, 7)

  Nafasi ya mwanamke ni kubwa katika jamii ya Kiislamu

 • 2 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 26-OKTOBA 2, 2014AN-NUUR

  S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.

  www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.ukOfisi zetu zipo: Manzese Tip Top

  Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

  Tahariri/Tangazo

  P.O.BOX 55105 , TEL: NO 2450069, Mob: No 0712974428 & 0786457719 Dar Es Salaam.

  UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL

  PRE FORM ONE PROGRAM 22/09/2014 - 28/11/2014

  Program hii itaendeshwa hapa UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL kwa wanafunzi wa Kiislamu wanaojiandaa kujiunga na kidato cha kwanza Januari, 2015.Masomo yafuatayo yatafundishwa:Elimu ya Dini ya Kiislamu, Mathematics, Arabic language na English language ADA: 80,000/= kwa program yote.Jumatatu - Ijumaa kuanzia saa 2:00 asubuhi8:30 mchana.Jumamosi kuanzia saa 2:00 Asubuhi6:30 mchana Masomo yataanza rasmi tarehe 22/09/2014Jiandikishe kuanzia 18/09/2014 ofisi ya Mkuu wa Shule Ubungo Islamic High School kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 8:30 mchana .

  Wahi mapema nafasi hii adhimu Wabillah tawfiiqMKUU WA SHULE

  H I J A H n i m i e z i m a a l u m . N a anayekusudia kufanya Hijah katika (miezi) hiyo , basi as iseme m a n e n o m a c h a f u wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika hiyo Hijjah. N a k h e r i y o y o t e mnayoifanya, Allah huijua. Na chukueni masurufu (ya kutumia njiani, msiombe). Na hakika masurufu bora ni yale yanayomfanya mtu as iombe (kwa kuwa yanamtosha) . N a n i c h e n i M i m i , enyi wenye akili. (Al Baqarah: 197)

  Hakika nyumba ya kwanza waliyowekewa watu kwa ibada ni ile iliyoko Bakka (Makka), i l i y o b a r i k i w a n a yenye uwongofu kwa walimwengu wote. (TMQ 3:96)

  Hija hutukumbusha Waislamu kuj izat i t i vilivyo na majukumu ya Uislamu. Hija ni mafunzo makubwa ya ucha Mungu. Kujifunga vilivyo na kipimo cha halali na haramu katika matendo yetu, kumpinga na kupambana na shetani na kila taratibu na mfumo wake, ili hatimaye kuishi chini ya bendera moja ya Uislamu ili kuhifadhi umoja na udugu.

  Hivi sasa Mahujaji k u t o k a s e h e m u mbalimbali duniani, wanamiminika nchini Saudi Arabia kuitikia mwito wa Mola wao kwa ajili ya ibada ya Hija.

  Kat ika kuamrisha ibada hii, Mwenyezi Mungu anatue leza : N a ( K u m b u k e n i ) tulipoifanya nyumba ya (Al-Kaba) iwe mahali pa kuendewa na watu, na mahala pa amani. Na mahali alipokuwa

  Kila la kheri Mahujaji wetuMuhimu zingatieni lengo

  akis imama Ibrahim pafanyeni pawe pa kusalia. (2:125).

  U k i a c h a m w e z i Mtukufu wa Ramadhani na siku za Eid, kipindi cha Hija kinashuhudiwa d u n i a n i k o t e n a kudhihirisha nuru ya Umma wa Kiislamu. Hivi sasa ni harakati kubwa za mahujaji kwenda Makka kutimiza nguzo ya tano katika Uislamu.

  H a r a k a t i h i z i huchochea hisia za imani na ari ya kushikamana na maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Hata hivyo, tunaona kwamba kwa vile Ibada hii kwa wengi ni ya mara moja katika uhai wao, ni vyema Mahujaji wakaelewa na wakawa na yakini katika mioyo yao kuwa nini wanachokwenda kukifanya huko na kwa malengo gani.

  Halitakuwa jambo zuri mtu akapoteza muda muhimu kwa kutokuelewa nini cha kufanya. Tunafahamu kuwa taasaisi zetu za kusafirisha Mahujaji huwa zinatoa semina ya makusudio na namna ya kutekeleza ibada hiyo kabla ya mahujaji kuondoka nchini. Lakini kuzingatia maelekezo na kuujaza moyo kwa nia ni jambo jingine.

  T u n a c h o p e n d a k u s i s i t i z a h a p a n i kwamba, halitakuwa jambo jema, au kielelezo cha mafanikio ya Hija k wa H u j a j i , i wa p o atakamilisha Hija na asiweze kupata athari ya Hija yenyewe, na akabakia kuwa kama hakuwahi kuhiji.

  Lengo la Hi ja s io kujipatia anwani ya Alhaj au Hajat fulani. Hija kama zilivyo ibada nyingine ina lengo lake maalum na lisipofikiwa

  inakuwa zoezi zima limeishia kuwa utalii. Hija humuandaa mja afikie kilele cha Ucha Mungu, ili awe mfano kwa wengine kwa kuwa tayari kwa moyo, kujitoa, kutoa kwa mali na nafsi, kuihuisha, kuisimamisha na kuilinda dini ya Allah (sw). Mtu anapokuwa katika hija, ni sawa na mtu aliye ndani ya kambi ya mazoezi ya kijeshi ya kuandaa kuwa tayari kuihuisha na kuipigania

  dini ya Allah na kwamba akitoka hapo ataishi maisha yake yote kwa uchamungu wa hali ya juu na kuwa tayari kujitoa kwa kila alicho n a c h o k u u p i g a n i a mfumo wa maisha wa Kiislamu.

  N i i m a n i y e t u kwamba mahujaji wetu wakifunga safari huku wakizingatia lengo ibada yenyewe, watarejea na kuwa kiigizo chema kwa umma na jamii

  kwa ujumla na Uislamu utasonga mbele.

  Tunamuomba Allah ( s w ) a w a w e z e s h e Mahujaji wetu kutekeleza salama na kwa usahihi ibada hii na kufikia daraja ya kutakabaliwa/h a j j - m a b r o o r , p i a tunamuomba Muumba kuwawezesha Waislamu wengine kupata fursa adhimu ya kutekeleza i b a d a h i i k a b l a ya k u o n do k a du n i a n i . Ameen

 • 3 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 26-OKTOBA 2, 2014HabariK U R A z a h a p a n a zilizoshinda leo hazijaja kwa urahisi maana ahadi za kurejesha mamlaka m a k u b w a S c o t l a n d yataifanya nchi hii kuwa na mfumo mpya wa muungano wao. Bwana Alex Salmond namuona ni mwenye kipaji kikubwa na mwenye kujiamini, anajuwa anachokifanya na nina hakika hii ilikuwa ni vita ya mtu mmoja dhidi ya vyama vyote vikuu. Hata wakubwa waliostaafu na kubezwa katika siasa za nchi kama Gordon Brown naye pia alijitumbukiza kuhakikisha hawajitengi na umoja wao. Dunia nzima ilihamia Scotland kuhakikisha no vote inapatikana. Nakumbuka hata Bill Clinton nae aliwasihi kutojitenga kwa vile madhara yake ni makubwa zaidi kwa alliance wa Marekani wanaemtegemea.

  Kura za asilimia 45 ni nyingi ukitazama namna gani alivyoshinda dhidi ya mfumo wa miaka 300 ya umoja wao. Lakini naamini hakufanya tu bila ya mpango maalum wa kuhakikisha madai ya Scotland yanasikika vizuri upande wa pili na pia mabadilko makubwa zaidi ya matarajio ya wengi ya k imamlaka kwao yanapewa nguvu hasa pale wataposhindwa kujitenga. Kwa Waskotish leo, ni ushindi juu yao kwa vile miezi minane inayokuja tutaona namna gani mamlaka makubwa yakielekea Kaskazini kuanzia masula ya fedha, kodi , na hata uwezo wa kupanga sera zao za fedha. Chancelor wa fedha anaporwa mamlaka makubwa ya maamuzi kuelekea devolution ya bunge la scotland huku hata mgao wa fedha kwa Scotland ukiongezeka maradufu kuliko kwa Waingereza wenyewe. Hio ndio gharama ya umoja wao.

  Mustakabli wa Waskochi

  M i r a d i m i k u b w a kubwa kama ya ustawi wa jamii na hata pensioni z i tawanufa isha za id i Waskotish kutokana na mamlaka waliokubaliwa kupewa. Lakini kuna uwezekano mkubwa kwa England nayo kupewa devolution ya bunge lake. Hili halina mjadala, ninaamini katika miezi minane ijayo kilio cha Wa i n g e r e z a k i t a z i d i kukuwa hasa baada ya UKIP kulival ia n juga suala zima la mamlaka makubwa kwa Scotland wakiwa si wapingaji bali wakidai nao usawa kwa bunge lao mahsusi kwa yale yaliokuwa hayamo katika umoja wao. Kwa sasa mamlaka waliopewa Waskotish yatazidisha kelele za devolution kwa England ili kuepusha wabunge Waskot land kuchangia masuala yasio wahusu ambayo kwa sasa yatazidi kuwa makubwa zaidi.

  W a n a o m d h a r a u Alex Salmond hawajui mikakati yake na ya SNP waliyoipanga: kwanza w a t a e n d e l e a k u w a madarakani kwa muda mrefu zaidi, kwa vile asilimia kubwa ya kura walizopata zinaonyesha wataweza kuunda serikali hasa kutokana na ukweli wa kutoiva kwa Labour na Tory katika uundaji wa serikali ya pamoja.

  P i l i w a t a e n d e l e a

  k u y a t u m i a m a m l a k a watakayoongozewa kwa faida ya watu wao na zaidi kwamba wameweza kukidhi ahadi walioitoa ya kuleta kura ya maoni baada ya kuchaguliwa. Hil i kwa upande wa Uingereza chini ya uongozi wa Cameron linawaumiza kichwa kwa vile ahadi yao ya kura ya maoni kwa EU wameshindwa kuitekeleza kwa woga wa kushindwa na hata Labour pia anafahamu changamoto zinazowakabili mbele yao.

  N i l i o y a s o m a k w a wenzetu:-Kwanza ustaarabu walioutumia kuhakisha kampeni zao zinakwenda kisheria na kuheshimiana.

  Pili, uhuru wa maoni ya kila mmoja bila ya kufukuzana, kupandikiziana kesi na kutishana kwa uingiaji wa msituni kupinga ukuwaji wa maon