annuur 1223

Upload: anonymous-x8qgwff

Post on 07-Jul-2018

485 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • 8/18/2019 ANNUUR 1223

    1/20

    ISSN 0856 - 3861 Na. 1223  JAMADUL AAKHER 1437, IJUMAA ,  APRILI 1-7, 2016 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

    Sauti ya Waislamu

    www.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected]

     AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST

    Mtume(saw) amesema kuwa Mwenye kuhijiamedhaminiwa na Allah na ni mgeni wake.Tuyaweke maisha yetu katika udhamini wa Allah. Tulishaitwa sote tangu zama za NabiiIbrahim(as) tukawe wageni wa Allah, nahakuna wito mwengine Gharama zote kwa Hijja2016/1437 ni Dola 4,600. Umra ya Ramadhanini Dola 2,700. Karibuni Ahlu Sunna walJamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora.Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0679895770/

    0688895777; 0765462022; 0712735363.Zanzibar : 0777468018; 0777458075;0777845010; 0777497300.

    (3) HIJJI UDHAMINIWE NA ALLAH!

     MUFTI Abubakar Zubery (wa pili kushoto), akimuombea dua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), hivi karibuni. Kutokakulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum,

     Mshauri Mkuu wa Mufti, Sheikh Abubakar Khalid na Msaidizi wa Sheikhwa Mkoa wa Dar es Salaam, Othman Mkambaku.

    Hapa inahitajika Fat’wa…Mufti kamwombea Dua RC Makonda!

    Kamfkishia yanayowasibu Waislamu?

    Tukumbuke, wema hushinda uovuMwishowe, batili ni yenye kuondokaKwa pamoja tukatae

    “Wazanzibari tulichagua maridhianona kukataa mfarakano. Tulichaguaumoja na kukataa mgawanyiko.Tulichagua upendo na kukataa chuki.Tulichagua matumaini na kukataakhofu. Tulichagua amani na kukataafujo.” - Uk. 4.

    ISMAIL Jussa Ladhu.

    Maalim Bassaleh awe kigezo  Waislamu, Wakristo 

    wamkosa Idrisa  Mimbar zitumikevyema kutoa ujumbe

     MAALIM Ally Bassaleh.

    ANNUUR NEW.indd 1 3/3

  • 8/18/2019 ANNUUR 1223

    2/20

    2  AN-NUUR

    JAMADUL  AAKHER 1437, IJUMAA APRIL I 1-7, 2016Mafundisho ya Qur'an/Uwanja wa Maarifa

    Fethullah-Gulen

    Jee Unajua?

    MASUALA1.“Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana

    na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaenezakutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharinina Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. HakikaMwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni” Suara ipi na aya gani?

     Jawabu: 4:1 (An-Nisaa)2.Kibla cha mwanzo kilikuwa wapi? Jawabu Bayt al Maqdis3.Kuba lijulikanalo kwa Kiengereza Dome of the rock liliopo Jerusalem

    linaitwaje kwa Kiarabu? Jawabu Quba as Sakhrah4.Siku gani inakaririwa sana katika Quran? Jawabu Qiyama5.Sehemu gani katika Qur’an imetajwa kuwa maji ndio chimbuko la

    maisha? Jawabu 21 :306.Mwanamke gani wa pekee jina lake linasomeka kwenye Quran?

     Jawabu Maryam7.Kushuka kwa wahyi wakawanza na wapili kilipita kipindi cha muda

    gani? Jawabu Miaka 2 miezi 68.Sura ipi inaanza bila Bismillahi? Jawabu Tawba9.Sura ipi Bismillahi inajitokeza mara mbili? Jawabu Suratul Naml

    10.T'alaka ni mara mbili. Kisha ni kukaa kwa wema au kuachana kwavizuri. Wala si halali kwenu kuchukua chochote mlicho wapa wake zenu,ila ikiwa wote wawili wakiogopa ya kwamba hawataweza kushikamanana mipaka ya Mwenyezi Mungu. Basi mkiogopa kuwa hawatawezakushikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu hapo itakuwa hapanalawama ikiwa mwanamke atajikomboa. Hii ndiyo mipaka ya MwenyeziMungu; basi msiikiuke. Na watakao ikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu,hao ndio madhaalimu. Aya hii ni yangapi katika Sura ipi? Jawabu 2:229

    JAWABU CHEMSHA BONGO NAMBA: 44

    CHEMSHA BONGO: 45Weka duara kwenye jawabu ilio sawa. Jawabu kamili wiki ijayo.

    MASUALA1.Sura gani na aya ya ngapi? ‘Na kupishana usiku na mchana, na riziki anayo iteremshaMwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwayo akaifufua ardhi baada ya kufa kwake,na mabadiliko ya upepo, ni Ishara kwa watu wenye akili.’2.Sura gani na aya ya ngapi? ’Walio kufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu,Yeye atavipotoa vitendo vyao.’3.Sura gani na aya ya ngapi?’’Na jueni kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu yuko nanyi.Lau angeli kut'iini katika mambo mengi, bila ya shaka mngeli taabika. Lakini MwenyeziMungu amekupendezeeni Imani, na akaipamba katika nyoyo zenu, na amekufanyenimuuchukie ukari, na upotovu, na uasi. Hao ndio walio ongoka”4.Sura gani na aya ya ngapi? ‘’Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!”5.Sura gani na aya ya ngapi? ‘’ Na bila ya shaka tulimtuma Nuhu na Ibrahim, natukaweka katika dhuriya zao Unabii na Kitabu. Basi wapo miongoni mwao walioongoka, na wengi katika wao ni wapotovu. ‘’6.Kuna aya ngapi za Sajda katika Qur’an?7.Jamaa yupi wa Mtume aliotajwa katika Qur’an?8.Sura za Makka ni ngapi?9.Sura za Madina ni ngapi?10.Siku ya Qiyama hali ya watu itakuwaje?

    MWENYEZI Mungundiye mjuzi zaidi wamahali atakapouwekaujumbe wake”. [Al –An-Aam 124]

    Kuzaliwa kwa Uislamu

    na ujumbe wake, katikamji wa Makkah kishakuenea kwake katikapande mbalimbali zaulimwengu, baada yahapo kumejengwa juuya hekma nyingi sanana kama ambavyokunawezekanakuifanyia tathmini ayatukufu:“MwenyeziMungu ndiye mjuzi zaidiwa kupajuwa mahali pakuuweka ujumbe wake.”

    Katika mtizamo nauelewa huu vile vilekunawezekana kufanyiatathmini kwa upandewa elimu inayotatiasili ya binadamu namaendeleo yake na

    mazoea yake na itikadizake . Anthropology – na jiograa na Historianna Ubinadamu na kwaupande wa lugha namahali na baki ya vipeovyengine vya masualahaya. Ndiyo hakikaMwenyezi Mungumtukufu yeye ndiye mjuzisana wa yule ambayeanamchagua kwa ajili yautume wake na kwa ajiliya ujumbe wake na katika

     jamii gani utadhihirikaujumbe wake, na katikaujumla wa mazingiragani ya mapambano yakimataifa, na ya kidinina kibinadamu na baadaya kukia mapambano

    haya, kiwango gani ndipohumpeleka MwenyeziMungu mjumbe mpyana dini mpya. Na sasatutayapekua mambohayo:

    1. Upeo waubinadamu kwa ajiliya ujumbe: Aya hiiinaashiria kwenyekwamba MwenyeziMungu mtukufundiye anayemjuwasana mjumbe ambayeanamchagua na atawekakwake amana yakuukisha ujumbe huu

    wa Mwenyezi Mungu nayule ambaye kunafanyikakuuelekeza ujumbehuu. Na katika zama zaMtume kulikuwa kunawatu ambao wanadhanikwamba Walid binMughera na Urwa binMasoud A-Thaa, niwabora sana kwa kupewaujumbe na wanafaa mno.Na kwa hakika Qur’animetaja rai ya watu hawakwa hawa watu wawilikatika aya nyingine kwakusema: “Na wamesema:Kwanini isingeteremshwahii Qur’an juu ya mtukutoka miji miwiliambayo ni mtukufu”.[A-Zukhruf 31] Qur’anikawa jibu kwa kusema:“Sisi tumegawa kati yaomaisha yao katika uhaiwa dunia”. [Al-Zukhruf32]. Na hapana shakakwamba masuala yote, na

     jambo kubwa mno mfanowa jambo la utume,hakuwezekani kuliachakwa maoni ya huyu auyule. Akiwa MwenyeziMungu mtukufu anajuwana yeye anajuwa hapanashaka yoyote – siri za

     binadamu ambazozimo katika raha ya

     binadamu na moyo wakena analenga kwenyekuzihusisha siri hizo, kwahuyo binadamu, yeyendiye anayejuwa sana

    pasi na shaka yoyote, mtuambaye anafaa sana kwakusimama na jukumuhili. Kwa msingi huu,mtu ambaye anamtukuzayeye Mwenyezi Mungumtukufu kwa ujumbe,ndiye mtu anayefaa sana.

    Kwa hakika kusimamakwa Al-Walid Bin Al-Mughira na wenginekwa kumdogoshaMtume wetu (S.A.W.)na kumwangalia kwakumzingatia kuwa hafaikwa utume kitendohicho kinahesabiwakuwa ni kuchumamadhambi makubwa nawao kwa mtazamo huuwameporomoka katikamtazamo wa MwenyeziMungu mtukufu.Wameshuka kwenyedaraja la chini sana nakwenye cheo duni sana.Na Mwenyezi Mungumtukufu anatuelezaunyonge na uduniambao utawapata watuhawa katika mtiririkowa aya hiyo hiyo(Utawapata wale ambao

    wamefanya maovuuduni kutoka mbeleza Mwenyezi Mungu,adhabu ngumu kwasababu ya yaliyokuwawanayatenda” [Al-Annam124].

    Na Mwenyezi Mungumtukufu anasema:“Mwenyezi Munguanawateuwa kutokanana malaika wajumbe nakutokana na watu”. [Al-Hajj 75]. Hapana juu yetu,isipokuwa kumheshimuna kumtukuza Yuleambaye ameteuliwana Mwenyezi Mungumtukufu. Na kamahaikuwa hivyo, kuoneshakutoridhika kwa namnayoyote ile dhidi ya yuleambaye ameteuliwa

    na Mwenyezi Mungu,kuna kiporomoshacheo cha mtu huyo nakunamfanya awe dunimwenye kudhalilishwana anakuwa ni mwenyekunyimwa msaadana Baraka ambazowanafaidika nazo Mitumena Mawalii na wateule nawenye kukurubishwa.

    Ndiyo mfano wamtu huyu vyovyotekitakavyo kuwa cheochake, atafungamanishwana unyonge na uduni naatanyimwa misaada yoteya Mwenyezi Mungu.Kisha kwa hakikautukufu wa Mtume wetu(s.a.w.) na kufaa kwakena kukubalika kwakehayo yanajulikana nayanakubaliwa katikazama zote na nyakatizote na kwa watu wote.Na umoja na kuwavitabu vya mbinguni vyazamani vimepotoshwakwa hakika wanawazuiawatukufu mifano yamjuzi sana RahmatullahAl-Hindi na mjuzi sanaAl-Jisri wamekuta katikavitabu hivi bishara miamoja na kumi na nnena misemo kuhusukuja kwa Mtume huyumtukufu. Ndiyo kwahakika wamekubaliana

    Manabii wote kwakuzingatia tokea Dawoudna Sulayman na Mussa(a.s.) na kukomelea kwaYahya na Zakaria na Issa(a.s) juu ya bishara yakuja kwa mjumbe huyumtukufu na waliwaelezawatu wao kwambaMtume huyo atakuwani mwenye kukusanyaubora wote wa Mitume(a.s.). Na kwa mazingatiohaya, Mtume (s.a.w.)ndiyo mwenye daraja kwawote. (Itaendelea)

    Suratul An-aam 124

    1.Katika karne ya 6 ikiwa ni mwaka 700 na Waislamu walikuwa tayari wanazohospitali kama zilivyo leo na madaktari na kufanya shughuli zote za kitibabu: hps://www.nlm.nih.gov/exhibition/islamic_medical/islamic_12.html2.Katika karne ya 7 kulikuwa na madaktari bingwa wa Kiisalamu nawalianzisha fani mbalimbali ikiwa kati ya hao ni Ibn Zuhur, Ibn Sina,Al-Kindi, Al-Razi, Ibn Haytham : hps://en.wikipedia.org/wiki/List_of_Muslim_doctors

    3.Ingawa kwa kuwa ni Muislamu hatajwi lakini ndio muasisi wa kutumiazana za kupasulia mgonjwa anapoumwa Abū al-Qāsim Khalaf ibn al-‘Abbāsaz-Zahrāwī (936–1013), inasemekana kuwa alitengeneza aina zisopungua 200ya zana za kupasulia wagonjwa : hps://en.wikipedia.org/wiki/Al-Zahrawi4.Alikuwa Bibi wa Kiengereza Mary Wortley Montagu (1689-1762) ndioaliotoa utaalamu wa Chanjo ya Ndui kutoka kwa magwiji wa Kiislamu hukoUturuki nakuipeleka Uiengereza, kufanya hayo alikabiliana na upinzanimkubwa lakini wapinzani wake walikuja kunyanyua mikono baada yaukweli kudhihiri : hp://www.muslimheritage.com/article/lady-montagu-and-introduction-smallpox-inoculation-england5.Fahamu kuwa huu Ulimwengu wetu unefanyiwa kazi kubwa na wataalamuwa Kiislamu katika maendeleo ikiwa kina Al-Farabi, Ibn Rushd, Al-Khawarizim, pitia mtandao huu uwaone katia ya wengi majina 15 yaliofanyakazi nzito : hp://www.famousscientists.org/famous-muslim-arab-persian-scientists-and-their-inventions/6.Abu Abdallah Mohammad ibn Jabir ibn Sinan al-Raqqi al-Harrani al-Sabial-Baani maarufu Al-Baani na Wazungu humwita Albategnius, Albategniau Albatenius alikuwa mjuzi wa mambo ya nyota na aliweza kutengenezadarubuni yake ya kuangalia sayari aliishi katika miaka ya 858-929 : hp://www.famousscientists.org/al-baani/7.Wajue wanataaluma ya Sayansi ambao walikuwa ni sio wenye kujikitamoja kwa moja katika Sayansi (part-timers) kati ya hao ni Eratosthens 276BC, Nicholas Copernicus 1473-1543, Johannes Kopler 1571 -1630hp://www.famousscientists.org/part-time-scientists/

    B B B A K A A T U A M S S M

     A  A Q I J G L R R L I U U A

    T S A K U H T P D Q A R R R

    al R M H N A U L U A K A A Y

    M  A A T U R F U N B A T T A

     A B R I B B A S D A 2 U U M

    Q  A S L M I N A A 211 :30 M T A A

    D G H F A S S S M 7 :19 I T N S

    I H A U T H H A A 20 :12 E A N Y

    S D M M L I A B S 8 :9 Z W A A

    U A S A A M R A H 6:6 I B M A

    R D I T A A I A K 20 :7 6 A L S

    D D Y A I L Q N A 3 :15 8 J U H

    Q I Y A M A I U A 4 :1 9 N U A

     A O A B C D E F G A 77 :19 M A S

    B P K A Q M C Y H B W F S I

    C Q L S W N E R T U X A X R

    D R M D E B A KJ G L 57 :26 D C T

    E S B F R V S H B A 14 H V Y

    F T D H T C D H N H 86 A T F

    G U C G Y X A J M A Y H B T

    H V V H U Z S K S B Z I F Y

    I W F J I A D K S R Q K R V

     J X B K O Q D J D Y A O T B

    K Y D L G W S H F U 49 :7 D Y G

    L Z F M F ER B G G I 28 D U Y

    M V G N D F C B K O 47 :1 F N R

    N V H V T V V N O P 45 :5 G M S

    ANNUUR NEW.indd 2 3/3

  • 8/18/2019 ANNUUR 1223

    3/20

    3  AN-NUUR

    JAMADUL  AAKHER 1437, IJUMAA APRIL I 1-7, 2016Habari

    SHEIKH mpya wa BAKWATAMkoa wa MorogoroAbdallah Salim Mkang’ambeamesema kazi yake yakwanza atakayoanza nayoni kuhakikisha vijana waKiislamu wanaosoma katikashule za sekondari mkoanihumo wanapata elimu ya dini.

    Hayo ameyasema mwishonimwa juma lililopita mjiniMorogoro muda mfupi mara

     baada ya kumalizika kwauchaguzi Mkuu uliomwekamadarakani kwa kura 34 dhidiya kura mbili za mshindani wakeSheikh Idd Hussein Nyagongo.

    Akifafanua zaidi kuhusu azmayake hiyo, sheikh Mkang’ambealisema hadhani kama kwakushirikiana na Waumini wadini ya Kiislamu mkoani humowatashindwa kusambaza vitabuvya Elimu ya Dini ya Kiislamuwalau 20 kwa kila shule iliyopomkoani humo.

    Bakwata Moro wapata

    Sheikh mpya wa mkoa

    Na Bakari Mwakangwale

    “Nina vipaumbele vyanguvitatu vya kwanza ambavyonaamini tukishirikiana nawenzangu tutaweza kukiamatarajio ya Waislamu waliowengi ambayo ni kuona Barazahaliwi katika sura hii iliyopo,

     bali linabadilika”, alisemaMkang’ambe.

    Kuhusu vipaumbele vingine,sheikh huyo mpya wa Mkoaalivitaja kuwa ni Uchumi naArdhi ambavyo kwa pomojaamesema ni lazima jamii yaWaislamu iamke na kuwekezakatika Ardhi ikiwa itahitajikujikwamua Kiuchumi na

    Kielimu.“Uchumi, Ardhi na Elimu

    ni vitu muhimu sana kwetuWaislamu na hasa katikaulimwengu huu wa Sayansi naTeknolojia ambao maendeleoyoyote yanategemea iwapo unaElimu, Ardhi ama Uchumi kwakiasi gani”, aliongeza.

    Mbali na hayo SheikhMkang’ambe ameahidi kutatuachangamoto mbalimbali mkoanihumo ikiwemo hitilafu zamakundi ya kidini na kijamiiili kurejesha heshima naustawi mzuri wa maendeleo yaWaislamu mkoani Morogoro.

    Kwa upande wa wajumbewa mkutano huo wa mkoawamesema sheikh huyopamoja na mambo mengine,analo jukumu la kuhakikishaanarejesha mali za Waislamuambazo wamedai Barazalimekuwa likikosa pesa za

    kujiendesha ilihali mali zake zikomikononi mwa watu binafsi.Katika uchaguzi huo uliokuwa

    umesimamiwa na NaibuKatibu Mkuu Dini SheikhMohammed Khamisi, BakwataMkoa ilifanikiwa kuwapatamasheikh watano watakaounda

     jopo la maulamaa ambalokwa mujibu wa katiba yaondilo litakalomsaidia sheikhMkang’ambe kufanya maamuzimbalimbali yenye maslahi yakidini na kijamii mkoani humo.

    Wengine ni wajumbe 10wa Halmashauri Kuu yaBakwata mkoa watakaomsaidiaMwenyekiti mpya waHalmashauri hiyo sheikhMwisheh Ismail Mwisheh katikakazi za kila siku za Baraza hilo.

    Wakaribishwa kuswali kanisaniKATIKA kuonyesha moyowa mapenzi kwa wakimbizi,mapadiri Massimo Biancalanina Alessandro Carmignani,wamewakaribisha Waislamukufanya ibada yao ya swalatano katika kanisa.

    Mapadiri hao walikuwatayari kuondosha kila kitundani ya kanisa lao ambachokingekwaza ibada ya

    swala kwa Waislamu, kilawanapokuja kuswali.

    Hata hivyo, Askofu MkuuFausto Tardelli wa Kanisala Vicofaro, Pistoia, Toscananchini Italia, amepiga ruhusahiyo.

    Askofu Mkuu huyo, ametoakauli kali ya kuwakemeaMapadri hao wawili akisemakuwa ukarimu katikakuwahudumia wakimbizi,haihusishi kuchanganyaibada.

    Massimo Biancalani naAlessandro Carmignani

    walitangaza wiki iliyopitakuwaruhusu Waislamukuswali ndani ya Kanisa baada ya Parokia yaokuwakaribisha wakimbizi 18Waislamu.

    Massimo Biancalani alisemawaliondoa vikalio katika altariili kuwasaidia wakimbizi haowa Kiislamu kujihisi waponyumbani.

    “Sioni kuna tatizo gani,tunaweza kuwatia ugumu

    kufanya ibada zao, Mtu yeyoteakitaka kuja kuswali Kanisanianakaribishwa na hata kamawanataka kwenda sehemunyingine wanaruhusiwakufanya hivyo.” Alisema Padrihuyo.

    Lakini Askofu Mkuu FaustoTardelli, alisema mpango huo

    ni hatua ya mbali ambayoinaweza kuhatarisha nakuharibu kuwaunganishawakimbizi hao katika jamii.

    Alisema kuwapa misaadana kuwakaribisha hainamaana kuwapatia nafasiKanisa kufanya ibada zao nakwamba kuna maeneo bora nasahihi zaidi yanapatikana.

    Pamoja na kupinga AskofuMkuu wa Kanisa hilo,Makuhani wa Kanisa hilonao walipinga vikali kauli yaAskofu na kutaka wakimbizihao waendelee kufanya ibada

    zao kanisani hapo na kutakaParokia nyingine ziige mfanowao.

    Ukimbizi ni dharura,kutetea uhai lakini je, Uislamuunasemaje juu ya kuswalindani ya Kanisa?

    Italia ni katika moja ya nchiza Ulaya zenye idadi ndogosana ya Waislamu. Kwamujibu wa makisio ya mwaka2011, idadi ya Waislamukatika nchi hiyo ni kiasi cha

    asilimia 2 tu.Hata hivyo, Msikiti mkuu

    wa nchi hiyo, maarufu, ‘TheMosque of Rome’ (Kitaliano:Moschea di Roma), ulioParioli, ndio msikitimkubwa kuliko misikitiyote, katika Ulaya na nje yanchi za Kiislamu, Urusi na

    India.Msikiti huo una ukubwa

    wa mita za eneo 30,000(30,000 m2) ukiwezakuchukua watu 12,000 kwawakati mmoja.

    Walioshiriki uanzilishina ufadhili wa ujenzi wa

    msikiti huo ni aliyekuwamwanasa Sultan waAfghanistan PrinceMuhammad Hasan namkewe Princess Razia,huku kiasi kikubwa chafedha za ujenzi kikitolewana Mfalme Faisal wa SaudiArabia.

    Mafundi walioandaamichoro ya msikiti

    walikuwa Paolo Portoghesi,Viorio Giglioi na SamiMousawi.

    Aliyekuwa Rais wa ItaliaSandro Pertini, alishirikikuweka jiwe la msingimwaka 1985 pamoja nakuufungua rasmi msikitihuo tarehe 21 Juni, 1995.

    BAADHI ya Masheikh watoa mada wakiwa katika Semina ya walimuwa Madrasa iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha

     Markaz Chang`ombe, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

     Askofu Mkuu Fausto Tardelli apinga

    ANNUUR NEW.indd 3 3/3

  • 8/18/2019 ANNUUR 1223

    4/20

    4  AN-NUUR

    JAMADUL  AAKHER 1437, IJUMAA APRIL I 1-7, 2016Tahariri/Makala

    AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

    Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.www.annuurpapers.co. E-mail: [email protected]

    Ofsi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

    “WAZANZIBARItulichagua maridhianona kukataa mfarakano.Tulichagua umoja nakukataa mgawanyiko.Tulichagua upendona kukataa chuki.Tulichagua matumainina kukataa khofu.Tulichagua amani nakukataa fujo.”

    Tarehe 5 Novemba2009 daima itakumbukwakuwa ni siku ambayonchi yetu iliandikahistoria mpya paleviongozi wawiliwazalendo na mashujaa,Dk. Amani Abeid

    Karume na MaalimSeif Sharif Hamad,walipowaongozaWazanzibari kukiaMARIDHIANO.

    Haikuwa kazi rahisilakini kwa kuongozwana hisia za uzalendo namapenzi kwa nchi yaona wananchi wenzao,Dk. Karume na MaalimSeif waliamua kujitoleakuongoza enzi mpya zasiasa. Walijua kwambakatika vyama vyao viwili,CUF na CCM, wapo watuambao wasingewaungamkono na penginewangeyatumiaMARIDHIANO yalekutaka kuwahujumu

    kisiasa. Na kweli,walikuwapo watu waaina hiyo na wapo hadileo.

    Kwa kutambuakuwa watu waovuwasiopendelea umoja namasikilizano miongonimwa Wazanzibariwatakuja kusema kuwaMARIDHIANO hayoyalikuwa ni maamuziya watu wawili tu, nahayawakilishi matakwaya watu, Dk. Karumealipendekeza kwaMaalim Seif kukubali raiya kufanya kura ya maoniili kupata ridhaa yaWazanzibari kuhusianana mwelekeo huo mpya

    wa siasa na hasa kuhusuhaja ya kuanzishamuundo wa Serikali yaUmoja wa Kitaifa.

    Tarehe 31 Julai 2010ikafanyika kura ya maoniya kwanza katika historiaya Zanzibar. Asilimia66.4 ya Wazanzibariwakapiga kura yaNDIYO kuchaguaMARIDHIANO namuundo wa Serikaliya Umoja wa Kitaifa.Baada ya maamuzi hayoya Wazanzibari, ndipoBaraza la Wawakilishi

    Kwa pamoja tukataeTukumbuke, wema hushinda uovu

    Mwishowe, batili ni yenye kuondoka

    likafanya Marekebisho ya10 ya Katiba ya Zanzibarna kuingiza muundo huondani ya Katiba.

    Maamuzi hayo yaWazanzibari yalikuwana maana kubwa sanakwa nchi yetu na watuwake. Kwa kupiga kuraya NDIYO, Wazanzibaritulichagua maridhianona kukataa mfarakano,tulichagua umoja nakukataa mgawanyiko,tulichagua upendo nakukataa chuki, tulichaguamatumaini na kukataakhofu, tulichagua amani

    na kukataa fujo.Inasikitisha kwambamiaka sita baadaye walewaovu miongoni mwetuambao hawakutakaMARIDHIANO(wakiwemo waleambao kwa dhahiriwalijionesha kuyaungamkono kwa sababu tuwalitaka kulinda ul’wawao kwa kumridhishaRais aliyekuwamadarakani lakinikwa siri wakiyapinga),wameturudisha kulekule kwenye mfarakano,mgawanyiko, chuki,khofu na fujo.

    Lakini pamoja na juhudi hizo ovu za

    kuturudisha tulikotoka,ukweli mmoja unabakikwamba Wazanzibariwengi hawako tayarikurudishwa huko.Wazanzibari wameonafaida ya siasa zaMARIDHIANO, UMOJA,UPENDO, MATUMAININA AMANI.

    Binafsi, bado naaminikwamba MARIDHIANO,UMOJA, UPENDO,MATUMAINI NAAMANI vitashinda.Wazanzibari ni watuwema. Kutokana na

    wema wao, watachaguaWEMA dhidi ya UOVU.

    Kwa sababuhizo basi, NATOANASAHA ZANGUKWA WAZANZIBARIWENZANGU kwambatukatae njama zote zakuturudisha tulikotoka.Katika siku za hivikaribuni kumekuwa nawatu WAOVU ambaowamekuwa wakiandikamaneno ya ovyo na matusikatika mitandao ya kijamii.Wengine ni watu wazimaambao ungetegemea kwaumri wao wangeoneshamfano mwema kwa kizazicha leo. Bahati mbaya, baadhi ya vijana wameingiakwenye mtego wa WAOVUhao na kujibizana naokwa matusi na lughazinazoturudisha kwenyemfarakano, mgawanyiko,chuki na ubaguzi, mamboambayo tukiyakataakupitia kura ya maoni yatarehe 31 Julai, 2010.

    Nawapa NASAHAndugu zangu tukataekuingia katika mtegohuo. Tuoneshe kama SISINI TOFAUTI NA WAO.Tusijibu lugha zao zamatusi, chuki na ubaguzina sisi tukaandika lughaza matusi, chuki naubaguzi. Haitoonekana

    tofauti kati yetu.Tuithamini na kuilindakazi kubwa iliyofanywana Dk. Amani Karumena Maalim Seif SharifHamad.

    TUNAYOPITIASASA NI MAJARIBUTU. TUSIKUBALIKUSHINDWATUKARUDISHWATULIKOTOKA.TUWAONESHEWAOVU KWAMBASISI NI WEMA. NAWEMA SIKU ZOTEHUUSHINDA UOVU.

    RAIS Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Aman Abeid Karume(kushoto) akisalimiana na Maalim Seif. Kulia niIsmail Jussa (kulia).

    Maalim Bassaleh awe kigezoWaislamu, Wakristo wamkosa IdrisaMimbar zitumike vyema kutoa ujumbe

    MAALIM Ali Bassaleh, nimfano mzuri wa kiongoziwa Kiislamu, ambayeanatumia vyemba mimbarkatika siku za Ijumaakukisha ujumbe mahsusikwa Waislamu kulinganana wakati na matukio.

    Toka zama, alikuwana kawaida ya kuandaamada ya hutba ya Ijumaamapema kabla ya siku yaswala. Akipenda kufuatiliataarifa za vyombo vya

    habari vya ndani na njeya nchi, akipenda kusomamagazeti mbalimbali ilikupata na kujua matukiombalimbali yanayokuwayanajiri katika jamii. Zaidi akipenda kusoma vitabumbalimbali.

    Wakati huo akiwaMasjid Idrisa, alikuwaakiandaa hutba yakekwa kuzingatia matukioyaliyojiri nchini kwakunasibisha na nafasiya Waislamu, iwe nikwa kuzingatia maslahiau madhara au kutoatahadhari, kuonya,kukemea au kuchukuahatua.

    Baada ya kuandaahutba yake kulinganana matukio, pamojana kwamba ataitoakwa waumini kupitiakipaza sauti cha Msikiti(Masjid Idrisa, Kariakoo),Maalim Bassaleh alikuwaamezoea kuichapahutba yake na nakalazake kusambazwa kwaWaislamu.

     Jambo hilo liliwasaidiawaumini kuwekakumbukumbu na kupatarejea ya somo la hutbalililotolewa kila walipohitajikufanya hivyo. Mwenendowake huo wa kupenda

    kutoa waadhi au hutba kwauhakika na kwa kunukuumachapisho na vitabumbalimbali, watu wa Dares Salaam wakampachika jina la utani, “Mzee wakunukuu.”

    Kwa kifupi tunawezakusema kuwa, MaalimBassaleh alikuwa anajuakujiandaa na kuiandaahutba yenyewe. Hataanaposimama mimbarini,Msikiti ulikuwa ukijaahadi nje kiasi kwamba,hata wasiokuwa Waislamu

    siku za Ijumaa walikuwawakipenda kusikilizahutba zake nje ya Msikiti,wakitaka kujua Maalimanakuja na somo ganiIjumaa hiyo.

    Tuchukue fursa hiikuwakumbusha Maimam,Masheikh na Makhatibuwetu kwamba, hutba yaIjumaa, hutba za sikukuu zaEid ni somo zito linalohitajimaandalizi makubwa

    kabla ya kuwasilisha kwawaumini.

    Hutba inahitaji iandaliwekiasi cha kuwafanyawatu wahamasike nakushawishika kujifunzakwayo. Somo la hutbalinahitaji utaalamwa muwasilishaji nauwasilishwaji, somo lahutba liendane na maishaya Waislamu kwa wakatihusika.

    Tuweke tu wazi kwambakatika misikiti mingi,hutba za Ijumaa zimekuwazinafanywa mithili ya zimamoto. Yaani zinatolewakwa ajili ya kutimiza tuwajibu Swala ya Ijumaaipite. Hakuna maandaliziya kutosha, somo linakinahimapema, haliwavutiiwasikilizaji, wala halitoiujumbe wa wiki kwawaumini.

    Tufahamu kwamba swalaya Ijumaa ndio mkutanowa ibada unawakusanyaWaislamu wengi zaidi kwapamoja kila wiki kulikoswala nyingine.

    Swala ya Ijumaa ni nafasimuhimu ya kuwakishiaWaislamu ujumbe mahsusikutokana na wingi waokatika swala. Hutba nzurini kichocheo cha kuwafanyaWaislamu kufurika zaidiMisikitini, wakiwa na

    hakika ya kupata elimuna ufahamu wa dini yao,maisha yao, maadili yaokupitia hutba.

    Hutba ni darasa kwawasiojua, ni ukumbushokwa walio sahau, hutbahuweza kuongoa watuna kuhamasika kufanyaibada na kumkurubia zaidiMwenyezi Mungu.

    Kulipua kuhutubu,kunapunguza ushawishi wakujifunza waumini. Lakinipia tunaidhalilisha diniyetu na hata Masheikh naMaimam wetu kiufahamu.

    ANNUUR NEW.indd 4 3/3

  • 8/18/2019 ANNUUR 1223

    5/20

    5  AN-NUUR

    JAMADUL  AAKHER 1437, IJUMAA APRIL I 1-7, 2016HABARI ZA KIMATAIFA

    MGOMBEA uteuzi kwa tiketiya chama cha Democratickwa ajili ya kinyang'anyiro

    cha uchaguzi wa rais nchiniMarekani, Bernie Sanders,amekosoa vikali matamshiyanayotolewa na mgombeachama cha Republican, DonaldTrump dhidi ya Waislamu,akisema mashambulizi dhidiya Waislamu kwa kutumiakisingizio cha matukio kamayale ya hivi majuzi yaliyotokeamjini Brussels yanakasirishana yanapingana na katiba yaMarekani.

    Bernie Sanders amesemaDonald Trump anayemilikivilabu vya kamari na bilioneaanayezusha mjadala mkubwa,anafanya mchezo wa kuigizawa televisheni na kwamba,

    anatumia matukio ya Brusselskama kisingizio cha kuchocheachuki dhidi ya Waislamu.

    Sanders amesisitiza kuwa,matamshi na mwenendo huounaeneza hofu na woga katika

     jamii ya Marekani.

    Matamshi ya Trump kuhusu Waislamu yanakeraKampeni za urais zadaiwa zinaiaibisha Marekani

    BERNIE Sanders, Mgombea uteuzi kwa tiketi ya chama cha Democratickwa ajili ya kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais nchini Marekani.

    Mgombea huyo wa tiketi yachama cha Domocratic alisemakuwa, kundi la kigaidi la Daeshni genge ovu lililofanya uhalifuna jinai dhidi ya binadamu hukoUfaransa, Marekani na Ubelgijilakini mapambano dhidi yakundi hilo hayapasi kukiukakatiba ya Marekani.

    Bw. Sanders alisema haipasikuwapa watu kama Trump fusraya kutumia matukio kama yaUbelgiji kwa ajili ya kutumiavibaya matukio ya kusikitishakama yale ya Brussels kuhujumuWaislamu wote duniani.

    Wakati Bw. Sandersakimlaumu Trump kwa kauli

    zake za chuki na ubaguzi dhidiya Waislamu, hivi karibunimgombea wa kiti cha raiskupitia chama cha Republican,Ted Cruz, amefuata nyayo zaTrump baada ya kupendekezakufanyika msako mkali dhidiya wafuasi wa dini ya Kiislamu,kwa kile alichokiita kuwa msakohuo una lengo la kuwazuia

    ‘wasiingie kwenye kundi lawenye misimamo iliyofurutuada’.

    Cruz aliyasema hayo saachache baada ya kutokeamashambulizi ya kigaidi katika

     jiji la Brussels Ubelgiji, matamshiambayo yamewaghadhabishaviongozi wa kidini na wateteziwa haki za binadamu nchiniMarekani.

    Kadhalika mwanasiasa huyoambaye anaonekana kufuatanyayo za mgombea mwenzakewa chama cha Republican,Donald Trump, alisema kunahaja ya kuimarisha usalamakatika mipaka ya nchi hiyo ili

    kuzia wale aliyowataja kuwawatu wenye misimamo mikali.Baraza la Mahusiano

    ya Kiislamu la Marekanilimeelezea kusikitishwa kwakena matamshi ya chuki yamwanasiasa huyo wa chamaRepublican na kusema kuwa,kauli za aina hiyo hazitakuwana matokeo mengine zaidi ya

    kuzidisha ubaguzi wa kidinina chuki dhidi ya Waislamu naUislamu duniani.

    Nihad Awad, MkurugenziMkuu wa Baraza hilo alisemamatamshi ya Cruz ni sawa nayale yanayotolewa na Trump nakwamba, yanakanyaga uhuruwa kuabudu na kuhatarishamaisha ya jamii ya Waislamunchini Marekani.

    Viongozi wa Kiislamunchini Marekani wamesemakuwa maneno ya chuki dhidiya Uislamu yanayotolewana wanasiasa wa chama chaRepublican, ndiyo sababuya kuongezeka hujumana mashambulizi dhidi yaWaislamu nchini humo.

    Taarifa iliyotolewa hivikaribuni na viongozi wa

     jumuiya za Waislamu nchiniMarekani mjini Washingtonilimtaka Trump, kuwaombaradhi Waislamu kutokana namatamshi yake ya hivi karibuniyaliyojaa chuki dhidi yao.

    Hivi karibuni Waziri waMambo ya Nje wa Marekani

     John Kerry amekiri kuwepoutovu wa nidhamu katikakampeni za uchaguzi wa raisnchini humo na kusema jambohilo linasababisha Marekanikuaibika kimataifa.

    Katika mahojiano natelevisheni ya CBS, Kerryalinukuliwa akisema, "Kilamahala ninapoenda, kilakiongozi ninayekutana

    naye, wananiuliza ni ninikinachoanedelea Marekani.Hawawezi kuaminiyanayojiri na naweza kusemawameshangazwa."

    irib.MASHINDANO ya kitaifaya kuhifadhi Qur’an nchiniSingapore yanatarajiwakufanyika wiki ijayo siku yaJumamosi na Jumapili Aprili2-3.

    Makundi matatu yanatarajiwakushiriki ambayo ni ni ya umriwa miaka 7 mpaka 12, miaka 13mpaka 18 na miaka 19 mpaka 25.

    Washiriki haowatashindanishwakwa kuzingatia namnawalivyohifadhi (hifz).Matamshi,(Tajweed) na ufasaha

    (fasahah).Imeelezwa kuwa lengo lamashindano hayo ni kuibuavipaji vipya katika uwanjawa usomaji wa Qur’an nakuhamasisha kuhifadhi Qur’an.

    Lengo jingine ni kuifanya jamii kuwa na utamaduni wakuhifadhi Qur’an na pia kupatavijana watakaoiwakilishaSingapore katika mashindano yaKimataifa.

    Mashindano hayo yatafanyikakatika Msikiti wa Darul Amanna washindi watapata vyeti napesa taslim. Ahbaabur.blogspot.

    Mashindanokuhifadhi Qur’ankufanyika

    Singapore

    TAASISI ya kwanza ya kibenkiinayofuata kanuni za Kiislamuinatarajiwa kuanza kufanya kazimwishoni mwa mwezi huu katikamji wa Kazan nchini Urusi.

    Mmoja wa waanzilishi wa taasisihiyo alisema kuwa taasisi hiyo

    inayoitwa The partinership BankingCentre, itafanya kazi kama kampunitanzu ya Tatagroprombank.

    Taasisi hiyo inayofanya kazina watu binafsi na makampunimbalimbali, itakuwa na lengo lakupitishia uwekezaji wa Kiislamukatika nchi ya Urusi na pia kusainimakubaliano ya kikazi na Benki yaMaendeleo ya Kiislamu ya IslamicDevelopment Bank.

    Fursa hii imeingia nchini Urusi baada ya kupitishwa sheria mpyakatika Bunge la Duma Januarimwaka huu, inayoruhusu mfumowa kibenki unaoweza kuzingatiataratibu za kidini.ABNA.

    Benki ya kwanza ya Kiislamukufunguliwa Urusi

    MAHAKAMA Kuu nchiniBangladesh imelikataana kulifutilia mbaliombi lililowasilishwa nawanaharakati wasio egemeadini la kutaka Uislamu isiwedini ya kitaifa

     Jopo maalum la Majaji watatuwa Mahakama hiyo limetupiliambali ombi hilo muda mfupi

     baada ya kesi hiyo kufunguliwana bila ya kuruhusu kutolewaushahidi wowote.

    Ombi hilo ambalo kwa

    Ombi kutaka Uislamu usiwe

    dini ya taifa Bangladesh lafutwamara ya kwanza liliwasilishwamiaka 28 iliyopita, limezushamaandamano nchi nzima yamakundi ya Kiislamu katika nchihiyo masikini.

    Bangladesh ilitangazwa rasmikuwa nchi isiyoendeshwa kidini

     baada ya vita vya kudai uhurukutoka Pakistan mwaka 1971.

    Wasioegemea dini wamekuwawakidai kwamba kutumika kwaUislamu kama dini ya kitaifakunakwenda kinyume na sheriaya nchi isiyotambua dini.ABNA

    ANNUUR NEW.indd 5 3/3

  • 8/18/2019 ANNUUR 1223

    6/20

    6  AN-NUUR

    JAMADUL  AAKHER 1437, IJUMAA APRIL I 1-7, 2016Hoja ya Juma Kilaghai

    KUNA namna nyingisana chakulaunachokula kinaweza

    kukugeuka nakuwa ndiye adui yakoanayekumaliza. Kwa mfano,vyakula vilivyochakatwa,na hasa nafaka ikiwa nipamoja na sukari, huchocheamfuro, au inammation kwaKiingereza, ndani ya mwili.Tati zinaonyesha kuwamagonjwa mengi sana yakimfumo chimbuko lake nimfuro. Mfano wa mfuro niule uvimbe unaoupata paleunapojigonga kwenye paji lauso au unapojikwaa kwenyedole gumba la mguu hukuukiwa hujavaa viatu. Aina hii yauvimbe unajitokeza hata katikaseli ndani ya mwili. Aghalabu

    hali hii hutokea pale kinga zamwili zinapoamka kupambanakwa kuhisi kuwa kuna kitishokimeingia ndani ya mwili.

    Mfuro unaotokea pale kingaza mwili zinapopambanana vimelea mbali mbali vyamaradhi siyo tatizo sana kwasababu unakuwa ni wa muda.Tatizo ni pale mfuro unapokuwaendelevu. Kwa bahati mbaya haliya mfuro endelevu inatukabilikaribu watu wote kutokana naulaji wetu. Sehemu kubwa yalishe yetu inatokana na vyakulavilivyochakatwa, na sehemukubwa ya hivyo vyakula ni vilevya nafaka na mafuta ya mbegu.Vyakula hivi vinapoingia

    mwilini mfumo wa kinga zamwili hudhani kwamba kuna‘adui’ kaingia na unajikusanyakufanya mashambulizi.

    Kwa sababu wangauliochakatwa na mafuta yakupikia ya mbegu vimekuwandiyo vyakula vyetu vikuu,tofauti ikiwa ni mapishi tu, inamaana kuwa asubuhi, mchanana usiku, mifumo ya kingazetu za mwili iko katika hali yavita; na muda wote huo mwiliunakabiliwa na mfuro.

    Mfuro endelevuunasababishaje maradhi? Ili uwena siha njema, vitu mbalimbalivilivyomo ndani ya seli za mwiliwako na vile vilivyoko nje ya selihizo vinatakiwa viwe katika hali

    ya uwiano fulani muda wote.Kitaalamu uwiano huu huitwahomeostatis. Mambo yanaanzakuharibika pale uwiano huuunapoanza kuvurugika.

    Seli zako za mwili ni kamavisiwa vinavyoelea baharini.Kila seli kwa nje imezungukwana majimaji ambayo ndaniyake kuna vitu vingi muhimukwa utendaji kazi muruwawa mwili, ikiwa ni pamoja naviini-lishe vingi vinavyosubirikuingia ndani ya seli kwa ajiliya kuwezesha shughuli za

    Inawezekana lishe yako ndiyo inayokuua!

    seli kwenda inavyotakiwa.Aidha kila seli ndani ni kama

     bahari yenye visiwa vingi. Vituvinavyoitwa organele, ambavyoni maumbile kadhaa wa kadhaayenye majukumu tofautihuelea kama visiwa kwenyemajimaji yaliyomo ndani yaseli. Majimaji yaliyomo ndaniya seli yana vitu vingi ndani

    yake, ikiwa ni pamoja na viinilishe vilivyoingizwa humokwa minajili ya kuchakatwaili kuzalisha nishati, kufanyaukarabati, kuzimua mazao hatariya pembeni ya mchakato wakuzalisha nishati; na kuundamaumbo mengine ambayo nimuhimu kwa utendaji sawawa mwili. Majimaji haya piahupokea kwa ajili ya kutoa njeya seli, na hatimaye nje ya mwili,uchafu au taka zinazozalishwana organele katika michakatombalimbali.

    Katika ngozi ya kila seli(cell membrane) kuna vipokezi(receptors) ambavyo hufanyakazi ya kuingiza ndani ya seli

    vile vilivyomo kwenye majimajiya nje ya seli vinavyotakiwakungia ndani, na kutoa nje yaseli vile vilivyomo kwenyemajimaji ya ndani ya selivinavyotakiwa kutolewa nje.Mwili unapokumbwa na mfuroutendaji kazi wa hivi vipokezikwenye ngozi ya seli huathirika.Hii ina maana kuwa kazi yakuingiza na kutoa nje ya selivitu mbalimbali haifanyiki kwawepesi na ufanisi unaotakiwa,

     jambo ambalo huvuruga uwianowa vitu hivyo.

    Hali ikiwa hivyo ni rahisi

    sana kupata magonjwa yakimfumo ikiwa ni pamoja nakisukari, shinikizo la damu namagonjwa yanayotokana namlundikano wa uchafu ndaniya seli. Ni rahisi kupata kisukarikwa sababu glukosi ambayoinatakiwa itoke kwenye majimajiyaliyoko nje ya seli na kuingiandani ya seli ili ichakatwe

    kuzalisha nishati haitaingiakwa kasi na ufanisi unaotakiwa.Kwa sababu hii sukariitalundikana kwenye damu nakukusababishia mkusanyiko wadalili zote ambazo kwa pamojani kielelezo cha ugonjwa wakisukari. Aidha ni rahisi kupatashinikizo la damu la juu ladamu kwa sababu kunapokuwana mlundikano wa vituvinavyotakiwa viingie ndani yaseli lakini vimeshindwa, mwilihuongeza shinikizo la damukama njia ya kulazimisha vituhusika vipenye katika ngozi yaseli.

    Baadhi ya magonjwa yamoyo, magonjwa yanayoathiriseli zilizoko nyuma ya jicho,magonjwa ya mishipa ya fahamukatika maeneo mbalimbaliya mwili, na magonjwa yaviungo mbalimbali vya mwiliyanaweza pia kusababishwa namlundikano wa uchafu ndani yaseli.

    Ukiondoa kusababishamfuro, vyakula vya wangauliochakatwa pia husababishamagonjwa kwa njia nyingine.Kwa mujibu wa tati,uchakataji wa glucose (sukari

    kuu inayopatikana baada yakuchakata wanga) huzalishakemikali inayoitwa malonyl-coA. Malonyl-coA hupunguzakwa kiasi kikubwa uwezo wamitochondria (viwanda vyakuzalisha nishati vilivyomondani ya seli) kudhibiti chembechembe zilizobeba umemehasi (high energy electrons)zinazotumika wakati wauzalishaji wa nishati inayotwa

     Adenosine Tri-phosphate (ATP),ambayo ni kwa ajili ya matumiziya baadaye mwilini. Hizi highenergy electrons husababishakuzaliwa kwa kiwango kikubwacha chembe zilizobeba umemechanya zinazoitwa free radicals. Chembe hizi zina uwezo wa

    kubadilisha umbo na utendajikazi wa vinasaba kwenye seli(DNA mutations) na kuharibuvimeng’enya mbalimbali ndaniya mwili!

    Aidha glucose inaweza kuletashida kwenye ini (husababishaugonjwa wa ini bonge, yaani

     fay liver disease), inawezaikasababisha unene uliopea,inaweza kuchochea kisukari chaukubwani, na pia ni chakulakikuu cha seli za saratani.

    Tati zimebaini kuwa baadhiyetu miili yetu huchakata wanga

     bila madhara ukilinganishana wengine. Watu wa aina hiihusemekana wana mifumo

    ya ujenzi na uvunjifu wakemikali ambayo inaendana navyakula vya wanga/nafaka auCARBOHYDRATE TYPE  kwakitaalamu. Njia pekee ya kujuakama wewe ni miongoni mwawaliomo katika kundi hili ausiyo ni kwa njia ya kipimo chakutambua mfumo wako waujenzi na uvunjifu wa kemikalimwilini (metabolic typing test).

    Hata hivyo kabla hujabainiaina ya mfumo ulio nao, njia

     bora kabisa ya kujilinda nikuchukua hatua za kupunguzaulaji wa wanga, hasauliochakatwa, na matumizi yamafuta ya mbegu kwa ajili yakupikia.

    (Juma Killaghai ni mtaalamwa lishe, ni mtaalam wa stadiza tiba na ni Mkemia Mtaftiwa bidhaa zinazotokana naviumbe hai (Organic NaturalProducts Research Chemist).Kwa mawasiliano piga:0754281131/0655281131

     Juma Killaghai ana kibali chaWizara ya Afya na Ustawi wa

     Jamii kwa ajili ya kutoa elimuinayohusu masuala ya siha; na

     pia ana leseni ya Baraza la Tiba Mbadala na Tiba Asilia kwaajili ya kutoa tiba asilia.)

     Mafuta ya mbegu

    ANNUUR NEW.indd 6 3/3

  • 8/18/2019 ANNUUR 1223

    7/20

    7  AN-NUUR

    JAMADUL  AAKHER 1437, IJUMAA APRIL I 1-7, 2016Makala

    WIKI iliyomalizia 20

    Machi 2016 Ulimwenguumeshuhudia chaguzi sikuhiyo katika bara la Afrika.Macho na masikio yaulimwengu yaliangaza zaidiZanzibar si kwa uangalizibali kuhabarisha kilekitakacho tokea.

    Kwa nini Zanzibar?Uchaguzi wa marejeo

    umevuta hisia na mvuto wawaandishi na wachambuzimbalimbali kwa vilekususiwa na waangalizi wotewa ndani na nje, uliosusiwana vyama takriban 10 kati ya14,umegubikwa na mzozowa kisheria juu ya ufutwaji

    na ufanyikaji wa Uchaguzimpya ni miongoni mwamaswali mengi na ambayohuwa kama kitendawilikisicho na mteguzi.Mazingira na mtiririko wamatukio tokea Oktoba 28ulipofutwa uchaguzi waOktoba 25 uliupa uchaguziwa Machi 20 picha ya ainayake kutizamwa kiuandishi(Reporter) zaidi kulikokiuangalizi (Observer).

    Kuelekea siku ya UchaguziWiki moja kuelekea Machi

    20 tulishuhudia matukiokadhaa ya Miripuko katikamaskani ya CCM Kisongena nyumba ya Kamishnawa Polisi, Uchomwaji motowa Nyumba za wananchi,Uchomwaji moto wa Maskaniza CUF, pia tumeshuhudiaukamatwaji wa wafuasina viongozi wa CUFkuhusishwa kwao na matukiokadhaa yaliyotokea. Kubwazaidi lililoibua mjadalamkubwa ni kutekwa kwaMwandishi mahiri wa RadioDW na Mwananchi Bi. SalmaSaid. Mtiririko wa hayo yotepamoja na Uimarishwajimkubwa wa Ulinzi kwenyeviunga vya Zanzibar kulizidikuleta taswira ya kipekeekwa Uchaguzi wa Machi 20.

    Siku ya UchaguziMachi 20 iliwadia

    siku ya upigaji kura kwaUchaguzi ambao uliokuwahauna Kampeni na ambaoulifuatiwa na mtiririkokadhaa wa kadhaa. Vyombotakriban vingi vilijikitakuhabarisha hasa upandewa Pemba kutokana nakuwa na wafuasi wengi waCUF. Taarifa za awali kabisazilianza kutoka kujulisha

    Dkt. Shein na safari ya miaka mitanoNa Mwandishi Maalum

    mahudhurio na muitikiowa wananchi katika vituo

    kadhaa vya wapiga nakuonesha muitikio mdogowa wapiga kura kiasi yawapiga kura chini ya 10 kwasaa 1 kwa upande wa Ungujana wapiga kura 6 kwa saamoja kwa upande wa Pemba.Hii ilikuwa inajidhihirishawazi katika maeneo mengikote Unguja na Pembakwa waandishi mbalimbaliwaliokuwa wanataarifuUchaguzi huo. Hali yaUtulivu na na woga ilitawalasana siku ya Uchaguzi na baadhi ya maeneo ya vituovya kura askari walizidi idadiya wapiga kura. Muitikiomdogo wa wapiga kura nahali ya utulivu na ukimyailizidi kutanda viunga vingivya mitaa yote ya Zanzibar.

    Utoaji wa MatokeoMatokeo yalianza kutoka na

    mara hii tulishuhudia wepesina uharaka wa kuhesabukura kuliko chaguzi zoteZanzibar. Kura Laki tano kwachaguzi zote zilopita Zanzibarhuwa ni kama kaa la motona huchukua zaidi ya masaa48 kuweza kuhisabiwa na

    kuhitimishwa kutangazwa.Mara hii iliichukua Tume

    masaa 16 tu kuja na matokeoya mwisho na kumtangazaDkt Ali Mohammed Sheinndie mshindi wa kiti chaRais wa Zanzibar kwa miakamitano mpaka Machi 2021.Hapana shaka palitarajiwanderemo na viji kuanziaBwawani na kwenyeviunga vyake tokea hapoalipotangazwa majira ya saa4 asubuhi kuwa mshindi.Ila hali ilikuwa tofauti mjiuliendelea kuwa kimyakizito na kuanzia jioni jionindipo palipoanza kuonekanamakundi machache yawafuasi wa CCM wakielekeaKachorora na Kisonge naambao wengi wao ni vijanana kutumbuizwa na muzikiuliokuwepo hapo. Hali katikamitaa mingi ilibaki kimya nayenye simanzi kubwa. Hiiilizidi kuleta taswira ya safarirefu sana ya miaka mitanoya Dkt Shein kuongozaZanzibar. Naam wingu lakwanza zito limetandukalakini, Je safari ya miakamitano na muonekano wawananchi wengi kutokupiga

    kura kunampa Dkt Shienutashi wa kisiasa kuongoza jamii inayoonekana imempiga

    pande?.Safari ya Kiza Kuelekea 2021Baadhi ya wachambuzi na

    waandishi wengi wanaitizamaZanzibar na Tanzania kwaujumla baada ya Machi 20.Hili halihitaji uwe mkwasisana kujua mazingira yaUendeshaji wa Serikali zetuzenye Bajeti tegemezi kwazaidi ya 50%. Hii haihitajiuweledi kujua ni kiasi ganiDkt Shein ataongoza jamiiiliyogawanyika kwa miakamitano na kuweza kuletamaendeleo na kuifanyaZanzibar kuwa Dubaiya Afrika. Hii haihitaji

    Uchambuzi mpana sana kwa jamii iliyotengwa na Jumuiyaza Kimataifa na Ulimwenguinawezaje kukia malengoyake na hapa ikumbukwekuwa Zanzibar asilimiakubwa ya mahitaji yakeyanatoka nje. Hii haihitajiuchambuzi mkubwa kwa nchiinayotegemea zao moja ghatu na isiyo na viwanda vyauzalishaji inaweza kuwa nahali gani baada ya miaka 5.

    HITIMISHOKwa maono ya suala

    la Zanzibar kila upandeunaohusika uweze kuchukuamajukumu yake na kuchukua

    dhamana ya uongozi. Maslahimapana ya Zanzibar naustawi wake yazingatiwe natuache kuweka maslahi yavyama vyetu mbele. Tujadilikwa hoja na kuzingatia kuwahuwezi kuuwa au kutesakra. Kiwiliwili ndichokinachokufa lakini kra namitazamo itaendelea kuwepo.Na pia tusibadili ukweli kuwaUadui maana Mungu aliumbaukweli na uongo daimahaikai juu ya ukweli ni sawavyenye mikangamo tofauti.Ukweli mkangamo wake nimzito daima utakaa juu nakudhihirika. Jamii zinahitajimaendeleo kuliko siasa.Ukishinda uchaguzi kwa haliya Majeshi kuwa katika haliya dharura (Standby) huwezikukaa na kuongoza kwadharura na majeshi yakakaakwa dahrura kwa muda wotewa miaka mitano. Utakuwaumetawala viwiliwili na sionyoyo za wananchi wakona ambao ni nguvu kaziunayotegemea kujenga nchiyako.

    DKT. Ali Mohamed Shein (kushoto) akimbatiana na MaalimSeif Sharif Hamad. (Picha kutoka Maktaba yetu).

    ANNUUR NEW.indd 7 3/3

  • 8/18/2019 ANNUUR 1223

    8/20

    8  AN-NUUR

    JAMADUL  AAKHER 1437, IJUMAA APRIL I 1-7, 2016Makala

    AWALI ya yote hatuna budi

    kumshukuru Muumba kwaneema zisizokuwa na hesabutunazoendelea kunufaika nazo.Rahma na amani zimwendeemtume Muhammad, sahaba zake,aali zake na wote waliofuata,wanaofuata na watakaofuatasunnah yake mpaka siku yakiyama.

    Naam! Wanasema mwenyemacho haambiwi tazama, tuongezekatika msemo huu kwamba hatamwenye masikio pia haambiwisikia. Lakini yapo mazingiraambayo hupelekea mtu kuambiwatazama hata kama ana macho na auanaweza kuambiwa kwa kuulizwakwamba, umesikia hiyo!?

    Kwa wenye akili sa na salamazilizochujwa bila shaka wameona nakwa hakika wengi wao wamebaki

    na maswali yasiyojibika. Ni kuhususakata la marudio ya “uchaguzi”visiwani Zanzibar yaliyofanyikasiku ya Jumapili ya Machi 20,2016. Uchaguzi ambao umerudiwaili yapatikane yaliyokuwayanatakikana, yaliyojicha nyumaya pazia. Yakawa yamefanyikayaliyokusudiwa.

    Watu sasa wanaweza kuulizanamaswali na wasipate majibu. Nuktakubwa ambayo inaweza kuzuautata zaidi ni pale atakapojiulizaraia tu wa kawaida, kwambaimewezekanaje “mwanafunziasiyejua kusoma wala kuandikaakafaulu tena kwa daraja ‘A’?” Nani

    Jitahidini kutenda haki japo ngumu!Na Juma Jumanne

    DKT. Ali Mohamed Shein.mwalimu wa huyu mwanafunzi

    ambaye siku zote anashika mkia!?Watu hudai kwamba ng’ombehanenepi siku ya mnada, lakini hiiya leo ni kali.

    Labda tujaalie kweli kafaulumtihani tumwambie awaelekezawaliofeli, ataweza kutoka mbeleya darasa aelekeze namna“alivyopasua mtihani”. Kwawale walipota bahati ya kusomaelimu ya msingi na sekondari,nadhani watanielewa nikitumianeno ‘mkondo’. Wingi wamikondo hutegemeana na idadi yawanafunzi, lengo likiwa ni kuletaufanisi katika ufundishaji.

    Inapokuja suala la kufanya

    mtihani, kila mkondo huwana kinara wake kwa maana yamwanafunzi bora kuliko wotekwa ufaulu na siyo kwa umri,utanashati, ubabe na mfano wahayo. Pamoja na kuwepo kinarakatika kila mkondo, pia anakuwepokinara wa darasa zima. Inawezakutokea kwamba, mwanafunzianayesoma mkondo ‘A’ akashikanafasi ya kwanza kwenye mkondowake lakini yakitolewa matokeo ya jumla hayupo hata kwenye kumi bora. Na ikitokea wanafunzi wamkondo mwingine hawakufanyamtihani ambao ndio wako vizurikitaaluma, hawa washika mkia ndiowatakaokuwa vinara.

    Kwa picha hii, unawezakuwauliza waliopata daraja ‘A’kwenye uchaguzi wa marudio,kwamba kinachowafanyawashangilie ushindi ni kitu ganihasa!? Lazima tukubali kwamba,yapo baadhi ya mambo hata nafsi

    inakataa kuchangamka kwa sababuya kujua ukweli wake.

    Haya ndiyo maeneo ambayomtu unajifunza jambo kwamba,kweli tunatofautiana. Binafsi siwezi jamani kupata ujasiri nisimame,nitangazwe kwamba nimefaulukwa namna ninavyojifahamuuwezo wangu. Huu wote ni utamuwa dunia. Huku kote huku, nikutojiamini. Watu wenye ujasirikama huu wa kusimamia dhulmaifanyike, hawana yakini na kifohata chembe. Mbona wameondokawenzao mfululizo, hawashtuki tu!?Usadi upi mkubwa kuliko huu?

    Kwa ‘speed’ hii ya kufaulisha

    wasiojua kusoma wala kuandikahatutoki. Tatizo hapa siyomwanafunzi kufaulu hali yakuwa hajui chochote, bali tatizoni yule aliyemuwezesha kufaulu.Mwalimu wa aina hii anautakia ninimustakbali wa elimu kwa kizazicha kesho? Tujaalie kwamba ndiyokapata ajira kabisa, ataelekeza ninikatika jamii!? Hebu tujiongeze.

    Allah Mtukufu anasema; “Hapana kulazimisha katika Dini.Kwani Uwongofu umekwishapambanuka na upotofu. Basi anayemkataa Shet'ani na akamuaminiMwenyezi Mungu bila ya shakaamekamata kishikio madhubuti,kisicho vunjika. Na MwenyeziMungu ni Mwenye kusikia,Mwenye kujua” [2:256].

    Vipi tulazimishane kwenye siasaambazo zimejaa uwongo, hadaa,ulaghai, udhalimu, usadi, ubabena kila aina ya maovu?

    Inauma sana licha ya kuwatulijua ka kwamba hili jambo

    haliwezekani kwa kunukuu vifunguvya sheria. Sheria zenyewe zakutungwa na mwanadamu, ambazokwa asilimia kubwa huongozwana hawaa na utashi binafsi. Kamailivyokuwa kwa masheikh waZanzibar kuletwa bara, na hilivile vile limekwenda kwa mtindohuo huo. Hakuna taratibu zozotezilizofuatwa.

    Hongereni kwa “ushindi mnono,ila tendeni haki” japo ngumukutokana na mlango mlioingilia,lakini jitahidini hivyo hivyo.

    Assalaam ‘AlaykumWarahmatullah Wabarakatuh!

    Juma Jumanne (MANYARA).

    MWAKA wa 2012 TV Imaaniliniomba niendeshe kipindicha historia ya WaislamTanzania. Hii ilitokana namahojiano ambayo nilifanyakatika kipindi kilichoitwa,“Ulimwengu wa Kiislam’’kipindi ambacho kilipendwa nawatazamaji wengi sana.

    Tulitengeneza vipindi kadhaaTanga, Zanzibar na Dar esSalaam kwa kufanya mahojianona watu maarufu na kipindichangu nilikiita “WalioachaAlama katika Historia yaTanzania.’’

    Katika mmoja wa watu

    niliofanyanao mahojianoalikuwa Sheikh Twahir HaydarMwinyimvua. Sheikh Haydarhuenda si wengi katika watuwa leo walimjua lakini yeye nimtu maarufu kwa wenyeji waDar es Salaam kama alivyokuwamaarufu baba yake SheikhHaydar Mwinyimvua, mmojawa watu waliokuwa mstari wambele katika TANU na mkonowa kulia wa Nyerere wakati wakupigania uhuru wa Tanganyika.

    Sheikh Twahir Haydaramefariki tarehe 21 Machi2016 nyumbani kwake

    Taazia: Sheikh Twahir Haydar MwinyimvuaMwananyamala B. SheikhHaydar umri wake woteamefanyakazi Kabidhi Wasiihadi alipostaafu kazi miakamichache iliyopita.

    Msaada wake katikaosi hii ndiyo Waislamuwatamkumbuka daima. Kusajilitaasisi yoyote ya Kiislamunchini petu, ni kitu kigumusana kuanzia mwaka wa 1968pale BAKWATA ilipoundwa nakufanywa ndiyo kila kitu kwaWaislamu. Sheikh Twahir juuya matatizo yote yaliyokuwapo,alijitahidi sana kuwaelekezaWaislamu nini wafanye iliwaweze kusajili taasisi zao. Hiihaikuwa kazi nyepesi kwakekwani juu yake walikuwapowakubwa zake kimadarakaambao walifanya kila juhudikuhakikisha kuwa taasisi zaKiislamu hazipati tasjila.

    Mfano wa karibu sana nipale mwaka wa 1992 Waislamuwalipotaka kusajili Baraza Kuu.Ala kuli hali wakati wa Rais AliHassan Mwinyi angalau mamboyalikuwa mepesi kidogo nakipindi hiki Waislamu wengiwatamkumbuka Sheikh Twahiralivyowasaidia kusajili taasisi

    zao.Nilipofanya mazungumzo

    naye mwezi Septemba 2012 kwaajili ya kipindi cha televisheninilimuomba tutoke katikakazi yake anieleze historia yaEast African Muslim WelfareSociety (EAMWS) baada yakupigwa marufuku na serikaliya Nyerere mwaka wa 1968na Sheikh Hassan bin Amiraliyekuwa Mufti wa Tanganyikakufukuzwa nchini.

    Sheikh Twahir alinielezamengi kuanzia maisha yaoKisutu Dar es Salaam yeyeakiwa kijana mdogo akisoma

    Al Jamiatul Islamiyya MuslimSchool katika miaka ya 1950na baba yake akiwa mmoja wawanachama shupavu wa TANU.

    Alinieleza usuhuba mkubwauliokuwapo baina ya baba yakeSheikh Haydar Mwinyimvua,Sheikh Suleiman Takadir naMwalimu Nyerere. Alinielezakazi na mafanikio yaliyokiwana EAMWS na pigo Uislamuuliopata baada ya kupigwamarufuku.

    Picha alonipa Sheikh Twahir

    Haydar ya viongozi wa EAMWSwaliokuwa wakiratibu shule za

    Kiislamu wakiwa na Waziri waElimu Nesmo Eliufoo ubavunikwa Tewa Said Tewa aliyekuwaMwenyekiti wa EAMWS. Kuliawa pili aliyesimama ni MuftSheikh Hassan bin Amir

    Sheikh Twahir siku ile alinitiachuoni kunisomesha na nilitokana mengi. Hakika Sheikh Twahirukimtoa Mzee Waikela, hakunaaliyekuwa kamzidi katikakuifahamu historia ya EAMWSna shida zilizokuwakutaWaislamu katika miaka ile.

    Bahati mbaya hadi leo vipindivile vyote nilivyofanya TVImaan haijavirusha kwa sababukadhaa kubwa ni kufuatia

    kufungiwa Radio na TV Imaankwa kipindi cha miezi sitakwa kile kilichojulikana kamakukiuka taratibu.

    Mpaka pale siku TVImaan itakaporusha kipindinilichofanya na marehemuSheikh Twahir HaydarMwinyimvua, Waislamututosheke na haya machacheniliyoeleza hapa.

    Tunamuomba Allahamsamehe madhambi yake naamuweke mahali pema peponi.

    Amin Mohamedsaid.com

    ANNUUR NEW.indd 8 3/3

  • 8/18/2019 ANNUUR 1223

    9/20

    9  AN-NUUR

    JAMADUL  AAKHER 1437, IJUMAA APRIL I 1-7, 2016

    ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

    UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL KIRINJIKO ISLAMIC HIGH SCHOOL NYASAKA ISLAMIC HIGH SCHOOL

    Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za Kidato cha Tano kwa shule zifuatazo:

    Ubungo Islamic High School - Dar es Salaam : 0687 820895/0657 350172

    Kirinjiko Islamic High School - Same, Kilimanjaro: 0784 296424/0756 676441

    Nyasaka Isamic High School - Mwanza: 0786 417685/0713 749020

    Shule hizi ni za Kiislamu zenye lengo la kuwapa wanafunzi taaluma ya hali ya juu na malezibora ya Kiislamu. Shule hizi ni za BWENI za mchanganyiko wa wavulana na wasichana.Zipo Combinations zote za SAYANSI,  ARTS na BIASHARA.Muombaji awe na ufaulu wa masomo matatu (3) kwa kiwango cha ‘Credit’  (yaani A, B na C)

    Daraja la III (Division three) au zaidi na Grade D kwenye masomo ya Combination. 

    Mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 02/05/2016.

    Fomu za maombi zinapatikana kwa gharama ya Shilingi 10,000= katika Tovuti:www.ipcorg.tz na katika vituo vifuatavyo:

    NAFASI ZA KIDATO CHA TANO - 2016/2017

    WAHI KURUDISHA FOMU ILI UJIHAKIKISHIE NAFASI

    Bismillahir Rahmaanir Rahiim

     ARUSHA:  Ofisi ya Islamic Education Panel, Jambo

    Plastic, Ghorofa ya 2 mkabala na Msikiti Mkuu

    Bondeni : 0783 438676/0715 438676.

    KILIMANJARO:  Moshi: Msikiti wa Riadha:07673453

    67/0686938077. Same Juhudi Studio mkabala na

    Benki ya NMB Same: 0757 013344. Same: Kirinjiko

    Islamic Secondry School: 0784 296424/0713

    115041. Usangi- Falhum Kibakaya : 0787 142054.

    Ugweno – Simbomu centre Mwl. Hidaya A. Mussa:

    0784 655614

    TANGA:  Twalut Islamic Centre – Mabovu

    Darajani : 0715 894111/0713 014469. Uongofu

    Bookshop: 0784 982525. Korogwe: SHEMEA

    SHOP : 0754 690007/071569008. Mandia Shop

    - Lushoto: 0782257533. Handeni –Mafiga -0782

    105735/0657093983

    MWANZA: Nyasaka Islamic Secondary School : 0717

    417685/0786 417685. Ofisi ya Islamic Education

    Panel – Mtaa wa Rufiji mkabala na Msikiti Al-

    Amin 0785 086 770/0714097362.

    BUKOBA: Ofisi ya Kutaiba Saccos: 0765 748056

    MUSOMA:  Ofisi ya Islamic Ed Panel -Mtaa wa

    Karume,Nyumba Na. 05 : 0765024623/0787868611

    SHINYANGA: Msikiti wa Majengo karibu na Manispaa

    ya Shinyanga Mjini :0655608139/0768895484

    KAHAMA: Ofisi ya Kamati ipo karibu na zahanati ya

    Doctor Dalali: 0754 994738/0782 994738Dar es Salaam: Ubungo Islamic High School :

    0756584625/0657350172/0712 033556. Ofisi ya

    Islamic Ed. Panel –Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin

    : 0655144474/0787119531

    MOROGORO:  Wasiliana na Ramadhani Chale :

    0715704380. Ifakara wasiliana na Mwl. Sharifu:

    0659 158958

    GEITA: Ofisi ya Kamati karibu na mashine ya

    kukobolea mpunga shilabera: 0765 748056

    DODOM A: Hijra Islamic Primary School : 0716

    544757/0718661992

    SINGIDA:  Ofisi ya Islamic Education. Panel – karibu na Nuru snack Hotel : 0786

    425838/0784 928039.

    MANYARA: Ofisi ya Islamic Ed. Panel – Masjid

    Rahma: 0784491196

    KIGOMA:Msikiti wa Mwandiga: 0714717727.

    Kibondo – Islamic Nursery School:

    0766406669. Kasulu: Murubona Isl.SS:

    0714710802/0763 298440

    LINDI:  Wapemba Store: 0784 974041/0783

    488444/0653 705627.MTWARA:  Amana Islamic S.S: 0715465158/0787 231007.SONGEA:  Kwa Kawanga Karibu na Msikitiwa NURU : 0713249264. Mkuzo IslamicHigh School :0654 876317MBEYA:  Ofisi za Islamic Education PanelUhindini – 0785425319. Rexona Videomkabala na Mbeya RETICO: 0713200209/0785425319.Rukwa: Sumbawanga:Jengo la HajiSaid –Shule ya Msingi Kizwike:0757090228/0786 313830

    TABORA: Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784944566/0718 556355. Nzega - Dk. Mbaga-0754 576922/0784576922.IRINGA: Madrastun – Najah: 0714 522 122.PEMBA:  Wete: Wete Islamic School : 0777432331/0712772326.UNGUJA: Madrasatul – Fallah: 0777125074.PANDU BOOKSHOP 0777462056 karibu

    na uwanja wa Lumumba

    MAFIA: Ofisi ya Ust. Yusufu Ally jirani na

    msikiti mkuu : 0773580703.

    Tangazo

    ANNUUR NEW.indd 9 3/3

  • 8/18/2019 ANNUUR 1223

    10/20

    10  AN-NUUR

    JAMADUL  AAKHER 1437, IJUMAA APRIL I 1-7, 2016Makala

    KWA muda wa miezi kadhasasa habari kutoka Marekanizimekuwa zikitawaliwa nakinyang’anyiro cha urais.

    Wagombea wanaowaniatiketi za chama wamekuwawakipambana na kulumbanahuku washabiki wao wakitianangumi na kushikana mashati.Mgombea mmoja anasema“ukinichafulia mkutano wangunami n’tamwaga mboga katikamkutano wako.” Alimradiwatazamaji wengi wamekuwawakichukulia mchakato mzimakama burudani ya aina yake.

    Kinachofanyika kwa sasa niuchaguzi wa awali (primaries)utakaopelekea kufanyikakwa uchaguzi wa urais nchiniMarekani tarehe 8 Novemba2016. Wao hufanya uchaguziwa rais kila baada ya miakaminne. Katiba yao imewekakikomo cha mihula miwili,

    hivyo Rais Obama analazimikakung’atuka na kumpishamwengine atakayechaguliwaHivyo, huu uchaguzi wa awali nimchakato wa kumteua mgombeawa urais kutoka kila chama.Vyama vikuu vinavyojulikanazaidi ni Democratic naRepublican. Utaratibu wao wakuteua wagombea na hata wakumchagua rais ni tofauti nawa hapa Tanzania. Kwa kweli siwote wanaoelewa utaratibu huu.Sitashangaa hata Wamarekaniwenyewe wasipoelewa. Waowanadai kuwa wanaongozadunia katika demokrasi. Lakinicha ajabu ni kuwa mgombea wachama hateuliwi na wanachama,na rais hachaguliwi na wananchimoja kwa moja kama tufanyavyo

    sisi hapa kwetu. Ndio maanawanapofanya uchaguzi basiubalozi wao hapa jijini huwaitawaandishi ili kuwaelimisha nawengine hata hupewa fursa yakwenda Marekani ili waandikemakala za kuusifu mfumo wao.

    Huko Marekani wananchiwatawachagua watuwatakaomchagua rais kwa niabayao. Watachagua kikundi chawapiga kura (electoral college)ambao ndio watakaopiga kuraya kumchagua rais. Hivi sasakinachofanyika ni mchakatowa kuwateua wagombea uraisulioanza tarehe 1 Februari

    Uchaguzi wa Marekani ni demokrasia ya kiini macho

    Na Nizar Visram

    na utakaomalizikia tarehe14 Juni mwaka huu. Uteuzihuu unahusu majimbo 50

    nchini kote. Watu watapigakura kuwachagua wajumbewatakaohudhuria mkutanomkuu wa chama (nominatingconvention) ambao ndioutamchagua mgombea wa uraisatakayepeperusha benderaya chama. Katika hatua hii yakichama hata Wamarekani walioughaibuni nao wanashirikishwa.

    Kwa mfano, chama chaRepublican kitawachaguawajumbe 2,472 watakaohudhuriamkutano mkuu (convention)ambako mgombea urais wachama atateuliwa. Chama hikikilianza na wanachama 17waliotangaza nia ya kugombeatangu Machi mwaka jana. Hii niidadi kubwa ya watia nia ambaohaijapata kutokea huko. Wengi

    wao ni watu wenye nyadhifawakiwa magavana wa mikoa aumaseneta (wabunge). Ila mmojani tofauti. Huyu ni DonaldTrump ambaye si gavana walaseneta bali ni bilionea kutokaNew York ambaye amewekezahata katika Mashariki ya Kati.Hiyo ndio sifa yake ambayoimewavutia Wamarekani wengi.

    Trump si mwanasiasakama wagombea wengine.Yeye ni bilionea anayefanya

     biashara ya kujenga na kuuzamajengo, pamoja na kuendeshamahoteli na vituo vya kamari(casino). Anadai kuwa kwavile amefanikiwa kutajirika,

     basi akiwa rais atahakikishawananchi nao wanatajirika.Lakini kisichosemwa ni kuwa

    kampuni zake zimewahikulisika mara nne. Huo simfano mzuri wa kuigwa. Wengiwanamuona kama ndumilakuwili, kwa vile aliwahikujiunga na Democrat. Aliwahihata kumuwezesha kifedha BiHillary Clinton katika kampenizake mnamo 2008. Trump piaamewahi kuwaunga mkonowanawake waliokuwa wakidaihaki ya kutoa mimba. Sasaanapinga jambo hilo na hatakuishambulia serikali kwakuziwezesha asasi za uzazi wampango (family planning).

    Mwaka 2000 alikuwa akiungamkono mfumo wa bima yamatibabu kwa wananchi woteukisimamiwa na serikali. Leoanadai eti huko ni kuingilia

    uhuru wa raia kujichagulia bima. Yaani anataka makampuniya bima yaruhusiwe kushindanakatika soko huria na kilammoja ajiamulie kujiunga aukutojiunga bila ya kuingiliwana serikali. Aidha, Trumpamekuwa akichochea chukina ubaguzi wa kidini dhidi yaWaislamu wanaoishi Marekanikwa kuwaita “wakuja wasiona haki ya kuishi nchini.”Anasahau kuwa Waislamuwalianza kuingia Marekanikabla ya babu yake kuhamiahuko kutoka Ujerumani. Halafuanasema akiwa rais, Waislamu

    hawataruhusiwa kuingiaMarekani.

    Anazishambulia pia

    China, Mexico na Japan kwakuyalaumu makampuniyanayowekeza huko badala yakuwekeza nyumbani. Hawaanawaita wasaliti waliokosauzalendo. Anasahau kuwakufanya biashara na nchi hizo nakuwekeza huko ni muendelezowa sera ya utandawazi, sera yakibeberu ambayo ina manufaakwa mabepari wa kimataifa.

    Trump anasema akiwa raisatawaua watuhumiwa waugaidi bila ya kuwakishamahakamani. Anasema atauahata familia zao. Huyu ndie raismtarajiwa wa Marekani na serazake za kifashisti.

    Mpinzani mkuu wa Trumpkatika chama cha Republicanni seneta Ted Cruz. Huyu

    huwa anaelezwa kuwa nimwenye siasa za wastani.Kinachosahauliwa ni kuwaCruz naye anaunga mkonomashambulizi zaidi katikaMashariki ya Kati, pamojana upunguzaji wa kodi kwamatajiri.

    Kwa upande wa Democratmgombea seneta Bernie Sandersamewavutia watu wengi,hasa vijana, kutokana na serayake anayoiita “usoshalistiwa kidemocrasia”. Yeyeanazungumzia “mapinduziya kisiasa” lakini tukiangaliazaidi tunaona kuwa msimamokama huo hauwezi kukubaliwaasilani na chama cha Democraticambacho siku zote kimekuwakikitumikia maslahi ya

    kibepari kikishrikiana naRepublican, kwa muda wamiaka 150. Ni kweli vyamahivyo vinatofautiana, lakini sikimsingi. Democratic ni chamrengo wa kulia na Republicanni cha mrengo wa kulia zaidi.Ndio maana hata Sandersakishinda urais itamuwiavigumu kutekeleza ahadi zake.Ni sawa na rais Obama ambayekabla ya kuchaguliwa aliahidikufunga gereza la Guantanamo,lakini jitihada zake zimegongaukuta. Hivi sasa tunaambiwaObama anashindwa kutekelezaahadi zake kwa sababu bunge(Congress) linatawaliwa nachama cha Republican. Lakiniukweli ni kuwa mwaka 2009 na2010 bunge lilikuwa na wingi

    wa Democratic, kina Sandersna wenzake pamoja na raiswao katika ikulu ya WhiteHouse. Hata hivyo hakunahatua walizochukua tofauti naRepublican. Wakati huo uvamiziwa kijeshi katika Mashariki yaKati uliongezeka.

    Kuhusu gharama za kampeni,michango mingi ya Hillary nikutoka makampuni makubwawakati Sanders anategemeawachangiaji wadogo. Wakatimmoja Hillary alikuwaamekusanya dola milioni 29.4na Sandera dola milioni 26.2.Fedha za Hillary zilitoka kwa

    wachangiaji matajiri wachachewaliotoa kima kikubwa, wakatiSanders alisaidiwa na watuwengi waliotoa kima cha chini.Hawa ni “walalahoi” 650,000waliochanga wastani wa dola30 kila mmoja. Sanders piaamechangiwa na vyama vyawafanyakazi na vijana wengi

    wamejitolea kumsaidia katikakampeni zake. Ndio maanaSanders huwa anajisifu kuwayeye anawasemea watu wadogona kumshambulia Hillarykuwa anawakilisha maslahiya makampuni makubwaYeye anadai kuwa huwaanazungumza na wananchiwengi ambao hulalamikakuwa uchumi wa Marekaniumepogoka. Ndio maanaunakuta Marekani ambayoni nchi tajiri pekee dunianiisiyokuwa na mfumo wamatibabu bure kwa wote.Sanders anasema hii ni aibu nachini ya utawala wake ataondoaaibu hii ya kuwaachia watuwakifa kwa sababu hawana pesaza kulipia matibabu.

    Wakati huohuo Sandersanakusudia kuongeza mshaharakima cha chini kianzie dola15 kwa saa. Ameahidi piaelimu bure mpaka ngazi yachuo kikuu. Lakini ni Sandershuyu huyu ambaye akiwakatika bunge aliunga mkonomashambulizi ya kijeshi nchiniIraq na Afghanistan. Katikamiaka yake yote alipokuwambunge amekuwa akiungamkono mashambulizi yaMarekani katika nchi kamaSomalia, Haiti, Bosnia,Liberia, Zaire, Albania, Sudan,Yugoslavia, Yemen na kadhalika.Hivi karibuni aliitaka serikaliikamate mali zote za Urusina akaishauri Saudi Arabiaiendeleze vita katika nchi za

    Kiarabu.Mnamo 2006 alipiga kurakuunga mkono azimio dhidi yaIran. Pia aliunga mkono uvamiziwa Israel nchini Lebanon.Akaunga mkono kuuwekeavikwazo utawala wa Palestinakwa sababu tu wananchiwake walichagua chama chaHamas katika uchaguzi wakidemokrasia. Mwaka 2014akaunga mkono uvamizi namauaji ya Israel huko Gaza.Akaunga mkono mpango waObama wa kuuwa raia wa Syriana Iraq kwa kutumia ndegezisizo na rubani. Alipoulizwaakasema akiwa rais atajaribuasiue raia wengi!

    Kuhusu huu uchaguzi, nivizuri tukaelewa kuwa hakunamgombea wa urais yeyote

    wa Marekani anayetarajiakuchaguliwa au aliyechaguliwa,ambaye anaweza kuthubutukuikosoa Israel. Wana asasi yakizayuni iitwayo AIPAC ambayondio inahakikisha kuwa kila raisau rais mtarajiwa anatangazautii wake kwa Israel

    Ndio maana kabla ya Obamakuchaguliwa kwa muhula wapili aliiangukia AIPAC. Nandivyo kina Trump, Hillaryna Sanders nao wanatarajiwakuiangukia AIPAC iliwaruhusiwe kugombea urais.

    (0713-562181 [email protected])

    ANNUUR NEW.indd 10 3/3

  • 8/18/2019 ANNUUR 1223

    11/20

    11  AN-NUUR

    JAMADUL  AAKHER 1437, IJUMAA APRIL I 1-7, 201611 AN-NUUR

    Makala

    KATIKA elimu ya Sekula, upo

    utaratibu wa kutunukianafalsafa za taaluma kamaUdaktari (PhD) au Uprofesa,kutegemea ukaribu wamuhusika na Chuo Kikuuhusika. Wanaweza kumtunukumtu katika tasnia ya Siasa,Utamaduni na masuaka yakijamii.

    Kumbe, hilo pia lipo kwaupande wa elimu ya Maarifaya Uislamu ambayo huitwaIjaza. Hii ni tunu katika Ilimuau zawadi, ambayo inazingatiauelewa na ufahamu (Weledi)wa muhusika katika mambombalimbali kadiri alivyojaaliwana Allah (sw).

    Anaeleza Sharif Muhdhar bin Abdulrahman Khitami(59), ambaye ni Mkenya,akimuelezea AlmaruhumSheikh Mohammed AbubakarAlbukhur, aliyekuwa Mudirwa Chuo maarufu cha Dini,Maahd Shamsil Maarif, Duga

     Jijini Tanga. Anamtaja SheikhMohammed, kuwa alikuwani mtu wa aina yake katikakuhifadhi mas’ala ya kielimuya Dini kwa ujumla, anasemakwa ujumla katika elimu yaKisekula, hufahamika katikataaluma ya fani mbalimbaliambapo mtu akibobea humo,

    ndipo huitwa Profesa auDokta. Anasema, AlmaruhumMohammed Abubakar, katikafani hizi za Ilimu ya Dini, kamavile Nahau, Swarifa, Balagha,Sirah, Tafsiri, elimu ya Mirathina mengine mengi ambapo kwaujumla wake yapo takribani16, yeye kwa ujumla alikuwaamebobea kwa upande wa piliwa elimu angeweza kuwa niProfesa au Dokta. Na kwambailikuwa hakuna unaewezakumlinganisha naye katika ilimuhizo.

    “Tena Sheikh alikuwa ni mtuwa ajabu, pamoja na bahariya ilimu aliyokuwa nayoilikuwa ukimwambia wewekatika swala fulani sioni mfanowake, anasema hapana yupoSharif Muhammad wa Kenya”,(Marhum kwa sasa) ndiyealikuwa akimtaja kuwa ni zaidi.

    Lakini na huyo wa Kenya,alikuwa akiulizwa naye anasemayupo Muhammed Abubakarwa Tanga (Tanzania) kuwa yeyeni zaidi. Kwa kweli hakuwamjivuni.” Anasema SharifMuhdhar.

    Ni kwa maana hiyo basi,

    Profesa Sheikh Mohammed AbubakarNa Bakari Mwakangwale

     ALMARUHUM Sheikh Mohammed Abubakar Albukhur.

    Sharif Muhdhar, anasemakwamba Baba yake ilimlazimukumtunuku daraja ya elimumaarufu kama Ijaza, Sheikh

    Mohammed Abubakar, nakumvika kilemba maalumambacho asili yake kilirithiwakutoka kwa Mtume Muhammda(s a w).

    Sharif Muhdhar, anafafanuakwa kueleza kwambaalimfahamu Almarhumu SheikhMohammed Abubakar, kupitiakwa Baba yake ambaye alikuwani Sharif Abdulrahman Khitami,ambaye alikuwa ni mwanafunziwake.

    Anahadithia tukio laAlmaruhum Sheikh MohammedAbubakar kutunukiwa kilembahicho kwamba ilikuwa Mei2, 2004, ambapo Mzee wakeAbdulrahman Khitami, alika

     Jijini Tanga akiwa mmoja wawageni waalikwa katika haa yauzinduzi wa Msikiti wa chuo chaMaahd Shamsil Maarif, Duga.

    Katika haa hiyo, Mzee wakeambaye alikuwa ni Sharif naSheikh kutokea nchi ya jiraniya Kenya, ndiye aliyepewaheshima ya kufungua Msikitihuo na ndipo alipofanya tukio lakihistoria kwa kumtunukia kwakumvisha kilemba AlmaruhumShkh. Mohammed Abubakari.

    Kwa mujibu wa SharifMuhdhar, alisema kwambaMzee wake alitoa maelezoya uzito wa Kilemba hicho

    kwamba asili yake kimetokakwa Mtume Muhammad (S aw), na kufafanua kuwa hatayeye (Sharif AbdulrahmanKhitami) alivishwa na Masharifuwenzake na hao nao walivishwana masharif wenzao, ambaomtiririko wake kilitokea kwaMtume Muhammad (s a w)yaani ni kitendo cha kiasili.

    Sharif Abdulrahman Khitami,alifariki mwaka 2006, nakuzikwa kwao Kenya, ambapoSheikh Mohammed Abibakari,alisari mpaka nchini Kenyana kushirika katika mazishiya Sheikh wake yaliyofanyikakatika Mji wa Lamu.

    Ama kuhusu, maziko yaSheikh Mohammed Abubakar,anasema yamekuwa ni yakihistoria, kwani wenyeji wa

     Jiji hilo, wanasema umekuwani miongoni mwa misibamichache iliyopata kutokea nakuhudhuliwa na watu wengi.Baadhi ya wazee wa Jiji la Tanga,kama Sharif Hussen Hashim,ambaye ni mwenzake na SheikhMohammed Abubakar, katikamaswala ya kielimu, na SheikhSaidi Abdallah Makata, ambaye

    ni raki yake wa karibu naMaruhum, wanaitaja misibaya Masheikh Hemed Albuhur,

    na ule wa Sheikh MohammedBin Ayoub, ambayo ndiyoiliyofananishwa na msiba waSheikh Mohammed Abubakar,kwa wingi wa watu.

    Hata hivyo, Sharif Muhdhar,anasema kwa zama za hivikaribuni baada ya Misiba yaMasheikh hao kwa vijanawa kuanzia miaka ya 1980,unaweza kusema kwambahawajawahi kuona mkusanyikowa msiba wenye watu wengikwa Jiji la Tanga, kama waSheikh Mohammed AbubakarAlburhan.

    Ustadhi Samir Sadiq, ambayekwa sasa ndiye ameshika nafasiya Mudir wa Shamsi Maarif,anafafanua kwa nini maziko yaMudir wake yamehudhuriwa namaelfu ya watu wengi penginezaidi ya Masheikh wake.

    “Kwa kweli mimi msibaniliowahi kuuona sijapata kuonakama huu kwa umri wanguwa akili timamu nikiwa humu Jijini Tanga, msiba niliouonakujaa umma kabla ya huu waSheikh Abibakar, ulikuwani wa Sheikh MohammedAyoub.”

    “Lakini huu wa SheikhMohammed Abibakar,ulikuwa ni umma mkubwa

    zaidi ya Sheikh Ayoub,nadhani labda msiba waSheikh Ayoub, ulikuwa jirani sana na maziko yakeukilinganisha na huu waSheikh Abibakar.

    Hii ni kutokana na kwambaSheikh Abibakar, kasomeshawanafunzi wengi, sasaukichanganya na wanafunziwa Sheikh MohammedAyoub.”

    Sheikh Ayoub, alifarikiusiku wa Jumanne, nakuzikwa Alasiri, siku iliyofatia,hiyo inamaana watu wengiwalichelewa kuzika na wenginehawakuweza kusari kuwahimazishi.

    Hatua ya kuweka mazishi yaSheikh Abibakar, siku moja zaidi

     baada ya kifo chake, ilitoa fursaya kila anaemfahamu, popotealipo alitia nia ya kuka msibanikulingana na nafasi yake kwanialikuwa ni mtu wa watu.

    Hali hii imepelekea kwambakila aliyepata taaa popote alipoalipata wasaa wa kizika, kunawatu wamekuja karibia kila konaya Tanzania na mijini ya Lamu,Nairobi na Mombasa katika nchiya jirani ya Kenya.

    ANNUUR NEW.indd 11 3/3

  • 8/18/2019 ANNUUR 1223

    12/20

    12  AN-NUUR

    JAMADUL  AAKHER 1437, IJUMAA APRIL I 1-7, 201612 Tangazo 

    ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

    Muda wa Kozi ni miaka miwili

    SIFA ZA MUOMBAJI:

    (a) Awe Muislamu.

    (b) Awe amefaulu masomo matatu (3) au zaidi kwa kiwango cha D au zaidi katika Mtihani wa Kidato cha 4.

    (c) Atakayekuwa na ufaulu wa kiwango cha D au zaidi katika masomo ya Lugha ya Kiarabu, Kiingereza,

    Kiswahili na Elimu ya Dini ya Kiislamu atapewa kipaumbele zaidi.

    Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe15 JULAI, 2016.Fomu za maombi zinapatikana kwa gharama ya Shilingi 5,000/= (elfu tano) katika Tovuti:www.ipcorg.tz na katika vituo vifuatavyo:

    KOZI YA UALIMU WA LUGHA YA KIARABU, KIINGEREZA,KISWAHILI NA ELIMU YA DINI YA KIISLAMU NGAZI YA CHETI 2016/2017

    USIKOSE NAFASI HII ADHIMU - WAHI KUCHUKUA FOMU SASA!

    Bismillahir Rahmaanir Rahiim

    KIRINJIKO ISLAMIC TEACHERS’ COLLEGE - SAME, KILIMANJARO

    Kwa maelezo zaidi piga simu: 0787 188964, 0784 267762 na 0654 613080

     ARUSHA: Ofisi ya Islamic Education Panel, Jambo

    Plastic, Ghorofa ya 2 mkabala na Msikiti Mkuu

    Bondeni : 0783 438676/0715 438676.

    KILIMANJARO:  Moshi: Msikiti wa Riadha:07673453

    67/0686938077. Same Juhudi Studio mkabala na

    Benki ya NMB Same: 0757 013344. Same: Kirinjiko

    Islamic Secondry School: 0784 296424/0713

    115041. Usangi- Falhum Kibakaya : 0787 142054.

    Ugweno – Simbomu centre Mwl. Hidaya A. Mussa:

    0784 655614

    TANGA:  Twalut Islamic Centre – Mabovu

    Darajani : 0715 894111/0713 014469. Uongofu

    Bookshop: 0784 982525. Korogwe: SHEMEA

    SHOP : 0754 690007/071569008. Mandia Shop

    - Lushoto: 0782257533. Handeni –Mafiga -0782

    105735/0657093983

    MWANZA: Nyasaka Islamic Secondary School : 0717417685/0786 417685. Ofisi ya Islamic Education

    Panel – Mtaa wa Rufiji mkabala na Msikiti Al-

    Amin 0785 086 770/0714097362.

    BUKOBA: Ofisi ya Kutaiba Saccos: 0765 748056

    MUSOMA:  Ofisi ya Islamic Ed Panel -Mtaa wa

    Karume,Nyumba Na. 05 : 0765024623/0787868611

    SHINYANGA:Msikiti wa Majengo karibu na Manispaa

    ya Shinyanga Mjini :0655608139/0768895484

    KAHAMA: Ofisi ya Kamati ipo karibu na zahanati

    ya Doctor Dalali: 0754 994738/0782 994738

    Dar es Salaam: Ubungo Islamic High School

    : 0756584625/0657350172/0712 033556.

    Ofisi ya Islamic Ed. Panel –Temeke -Msikiti

    wa Nurul Yakin : 0655144474/0787119531

    MOROGORO:  Wasiliana na Ramadhani Chale :

    0715704380. Ifakara wasiliana na Mwl. Sharifu:

    0659 158958

    GEITA: Ofisi ya Kamati karibu na mashine ya

    kukobolea mpunga shilabera: 0765 748056

    DODOMA: Hijra Islamic Primary School : 0716

    544757/0718661992

    SINGIDA:  Ofisi ya Islamic Education. Panel –karibu na Nuru snack Hotel : 0786 425838/0784

    928039.

    MANYARA: Ofisi ya Islamic Ed. Panel – Masjid

    Rahma: 0784491196

    KIGOMA: Msikiti wa Mwandiga: 0714717727.

    Kibondo – Islamic Nursery School: 0766406669.

    Kasulu: Murubona Isl.SS: 0714710802/0763

    298440

    LINDI:  Wapemba Store: 0784 974041/0783

    488444/0653 705627.

    MTWARA:  Amana Islamic S.S: 0715 465158/0787

    231007.

    SONGEA: Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU

    : 0713249264. Mkuzo Islamic High School :0654

    876317

    MBEYA: Ofisi za Islamic Education Panel Uhindini

     – 0785425319. Rexona Video mkabala na Mbeya

    RETICO: 0713 200209/0785425319.

    Rukwa: Sumbawanga:Jengo la Haji Said –Shule ya Msingi Kizwike: 0757090228/0786313830TABORA:  Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784944566/0718 556355. Nzega - Dk. Mbaga-0754

    576922/0784576922.IRINGA: Madrastun – Najah: 0714 522 122.PEMBA:  Wete: Wete Islamic School : 0777

    432331/0712772326.

    UNGUJA: Madrasatul – Fallah: 0777125074.

    PANDU BOOKSHOP 0777462056 karibu na

    uwanja wa Lumumba

    MAFIA: Ofisi ya Ust. Yusufu Ally jirani na msikiti

    mkuu : 0773580703.

    ANNUUR NEW.indd 12 3/3

  • 8/18/2019 ANNUUR 1223

    13/20

    13  AN-NUUR

    JAMADUL  AAKHER 1437, IJUMAA APRIL I 1-7, 2016Safu ya Ben Rijal

    KATIKA makala zetu yaMiti duniani na maisha yetuhadi wiki iliopoita ilikuwatunaizungumzia miti ya

    vyakula zaidi pasina kugusiamiti ya biashara. Katikamakala ya safari hii tutagusiamsu ambao hutoa su nakutengenezewa nguo.

    Kitaalamu Msu huitwaCeiba pentandra ukiwa umokatika jamii ya Malvacea, mtihuu kila mmoja huita kwamajina yake. Hebu tuangaliemajina ya Msu kutokanana lugha mbalimbali :Kiengereza White Silk-CoonTree, Kispeni Ceiba, KifaransaFromager, Wasurinam huitaKankantrie, Kihindi Safedsemal, Kitamil – Ilavam,Bengali Shwet Simul, AshanteTwi and Fanteen - Onyãã,au Onyina na Mandigo waohuita banã, bãnda (Dioula), bantã (Malinké), banti.

    Maelezo ya kivazi cha nguoya su ikielezewa namnaya thamani yake ilivyo «apani ilipigana vita vingivya wenyewe kwa wenyewekuanzia mwishoni mwanusu ya karne ya 15 hadikarne ya 17. Wapiganaji wakipindi hicho walishindanamiongoni mwao kuvaa bidhaa zilizokuwa za kipekeeambazo zingewafanyakuonekana kwamba ni wa

    kipekee. Hususan, viongoziwa vita hivyo, walivaa jinbaori – makoti yaliyovaliwa juu ya ngao wakati wa vita–ili kutambulika. Koti la ranginyekundu lililovaliwa wakatiwa vita ambalo tumeliangaziakatika kipindi hiki, linamuundo unaoonekana waziwa mundu upande wa nyumahuku kwa mbele, likionekanakama muundo wa lango lakuingia kenye hekalu ambalolinaashiria matakwa binafsi

    Miti Duniyani na maisha yetu Msufya wapiganaji ya kutakaulinzi kutoka kwa miungu.

    Kitambaa kilichotengenezwakwa su kilichotoka Ulaya,kilitiwa rangi ambayo ilikuwaghali na huenda kiliwasilinchini Japani kupitia ufanyaji biashara na Wareno. Utumiajiwa vitambaa vyenye thamanikama hivyo pia ulikuwaishara ya kuonyesha nguvu.Pia utagundua hisia ya kutakakutambulika ya wapiganajiwanapokuwa vitani katikaenzi za vita vikali. ‘’ Hakikanguo za su ndio nguoambazo zimetawala dunianina wazalishaji wa su wengiwao hawafaidi mapatoyatokanayo na su.

    Msu hutoa pamba na nimmoja kati ya mti maarufuduniani katika mti ambao siowa chakula. Msu ni maarufutunaweza kusema kulikoya aina yoyote ile ya mitimengineo. Nusu ya viwandavilivyo vya kutengenezeanguo duniani hutumiapamba katika matengenezajiwa nguo. Aidha pambahutumiwa katika utengenezajiwa miripuko, mafuta, chakulakwa ng’ombe na dawa zakupigia meno.

    Misu ya kutengenezwaviwandani imeanzishwaduniani lakini juu ya hayo

     bado su itokanayo katikamiti ya asili huwa na thamnikubwa inagwa mara nyingihuhujumiwa na waduduna kutumiwa kwa dawaza kupambana na haowadudu. Pamba ina pambanakujiweka katika soko namatumizi ya nailoni, na ainanyenginezo. Biashara yaPamba imekuwa ni moja yakutumiwa Watumwa katikakazi ya kuuhisha Misu,katika nchi ya MarekaniWatumwa waliotokea Afrikawalikuwa kwenye mashambaya miti iliopandwa Misuwakiimarisha na Mapinduziya viwanda yalitokana nakushamiri kutokana nakukuwepo kwa Pamba.Katika karne ya 18 na 19Waengereza walikuwa ndiowenye viwanda vingi vyakutengeneza nguo zitokanazona Pamba. Mwana taalumawa Kimerekani Ely Whitneykatika mwaka wa 1793 ndioalioasisi mashine ya kwanzaya kukamulia mbegu zaPamba na kupunguza kazi yamwanadamu kufanya hayo

    na waliokuwa wakifanya kazikubwa walikuwa sio wengine

    ila ni watumwa. Ili kuifanyaMisu iendelee kuzalishamadawa ya kunyunyuziahutumiwa kwa wingi nakuleta madhara, katika ardhiya kilimo duniani kote Misuhuchukua eneo la asilimia3 tu lakini hutumia roboya dawa zinanyunyuziwakuuwa wadudu na hayohuchangia vifo vya watu20,000 kila mwaka katika nchizinazoendelea.

    Miaka kama 7,000 iliopitaMisu ilianza kupandwakatika bonde ua Indussehemu ijulikanayo kama nchiya Pakistan hivi sasa. Baada

    ya hapo ikaanza kupandwakatika nchi za Mexico naPeru. Juu ya hayo wataalamuwameweza kugundua nyuziza Pamba zikiwa ni mabakiyaliotumiwa katika nchi zaPakistan na Mexico kamamiaka 5,000 kabla ya kuzaliwakwa Mtume Issa AS. Misukutoka Pakistan ilianzakuenea na kushamiri katikanchi za Mashariki ikiwaChina, Korea na Japan nakuingia katika bara la Ulayakatika mwaka wa 900.

    Su ni muhimu sanakwani mbali ya nguo kunamengi hutenegenezwakutokana na Su, Pamba nambegu zake kati ya hayo nitaulo za kufutia maji baadaya kugoea hutengenezwakutokana na pamba. Tukaekukiria umemaliza kukogana unaharaka unatakakutoka huna taulo ingebidiufanye nini? Aidha bidhaakama karatasi, noti zafedha tutumiazo, nyavu zakuvulia, mabendegi, baadhiya pamba za kutumiwakatika upasuaji, kambahutengenezwa kutokanana Pamba. Aidha nyuzi zaPamba hutumika katika

    utengenezaji wa miripuko,walaji sosej (Sausage) ilesehemu ya juu ya soshejihutokana na nyuzi za pamba.Filamu zinazotengenezwana kutoa picha ni kutokanaMsu na nishati itumiwayona roketi hutumia mafutayanayokamuliwa kutokanana mbegu za Msu. Hatawala Isikrimu (ice cream) nawatafunao ubani ni kati yavitu vinavyotegemea Msukatika matengenezo yake.

    Nchi zinazoongoza

    kusafrisha Pamba kwa wingiduniani kwa maalfu ya Metric

    tani namba mmoja ni China6,532, India 6,423, Marekani3,553, Pakistan 2, 308, Brazil1,524, Uzbekistan 849,Uturuki 697.

    Nchi ya China inaongozakwa uzalishaji wa Pambaduniani lakini nayo ndioinayoongoza ununuwajiwa pamba kwa thamanikubwa, kwa mwaka wa2014 walinunua Pambayenye thamni ya Bilioni 12.8pesa za Kimarekani akiwanikama anayeongoza kwaasilimia 21.8 nchi inayonunuaPamba kwa wingi duniani,

    ikifwatiwa na nchi yaBngladesh Dolari bilioni5.3, Vietnam bilioni dolari4.3, Uturuki Dolari bilioni 3,Hon Kong Dolari bilioni 2.5,Indonesia Dolari bilioni 1.6,Utaliano Dolari bilioni b1.6,Ujerumani Dolari bilioni 1.3,nchi ya Mexico Dolari bilioni1.1.

    Katika orodha niliyoiwekahapo juu nchi ya Vietnamimekuwa ni nchi yenyemahitaji makubwa ya pambana yenye kununua kwa wingiukilinganisha kitakwimu,ikifwatiwa na India, China, Japan na Indonesia. Nchiambazo manunuzi yaoyanapungua ni Hon Kong,Korea ya Kusini, Thailand,Utaliano, Pakistan, Uturuki,Ujerumani na nchi yaMarekani.

    Nchi ya Bangladesh inaviwanda vingi vya nguo nawanatumia vijana, watotona wanawake kuwalipamishahara midogo, lakinikutokana na umasikiniwanakuwa hawana budi jamii ya watu hao kutoingiakatika kazi za viwandani. Jambo la kusikitisha kuwanguo hizo nyingi huuzwakatika nchi za Magharibiambazo zinapinga utumiwajiwa watoto kufanyishwa kazikabla ya kuwa watu wazima.Aidha nchi hizo ndio mstariwa mbele kupinga malipomadogo ya wafanyakaziduniani. Tujiulize hizi nchiza Magharibi ni waokoziwa dunia hii au wachezawatu shere? Jawabu unayo,fwatana na mie wiki ijayo.

    ANNUUR NEW.indd 13 3/3

  • 8/18/2019 ANNUUR 1223

    14/20

    14  AN-NUUR

    JAMADUL  AAKHER 1437, IJUMAA APRIL I 1-7, 2016MAKALA/MASHAIRI

    AMESEMA MwenyeziMungu mtukufu “Ita

    watu katika dini yaMola wako mlezi kwahekima na mawaidhamazuri na jadiliananao kwa yale yaliyomema Zaidi”.

    Amesema ImamuKurtubi katikatafsiri “Mawaidha”na maneno mazuriambayo ameyawekaMwenyezi Mungukuwa ni hoja kwaokatika kitabu chake.Na amesema IbnuKayim /mawaidhamazuri ni kuamrishamema na kukatazamabaya kwa matumainina kwa utisho nakwa umuhimu wamawaidha mazuri .

    Ameweka mlangomzima Imamu Bukharikatika sahihi yakeakasema, hakua Mtume(s.a.w) akiwavamiawatu au kuwarefushiamawaidha iliwasikimbie nakuondoka.

     Juu ya mawaidhaya Mtume (s.a.w)kwa masahaba ilikubadilisha mwenendo,

    imeelezwa kutoka kwaAbdilahi Bin Masudamesema, amesemamtu mmoja eweMtume wa MwenyeziMungu mimi siachi,kuwa ninaiwahiswala kwa namnaanavyorefusha fulanisijapatapo kumuonaMtume (s.a.w) akitoamawaidha makali kwahasira kuliko siku hiyo,na akasema “enyi Watu

     Athari ya mawaidha mazuri katikakubadilisha mwenendo wa jamii

    Na Sheikh KamalAhmed Hassan

    hakika mnakimbizawatu misikitini, basianayeswalisha watu, basi na ashe kwaniwapo miongoni mwaowagonjwa na madhaifuna wenye haja”.

    Hekima, – mjadalakwa njia nzuri nimiongoni mwavitu vya lazima. Nilazima pia kuwampole, kutumia kaulilaini na kuwapendawatu. Hebu tazamamfano huu ulio hai

    katika kubadilishwamwenendo. Kunakijana mmoja alikujakwa Mtume (s.a.w)akasema ewe Mtumewa Mwenyezi Mungu“niruhusu mimikuzini, watu wakapigamayoe.”

    Mtume (s.a.w)akasema nisogezeenikwangu, wakamsogeza

    hadi akakaa mbeleya Mtume (s.a.w)akasema, “jeeunapenda kuziniwamama yako – akasemahapana. akasemana watu hawapendikuziniwa mama zao,akasema jee unapendakuziniwa binti yako?Akasema hapana, vilevile watu hawapendikuziniwa mabinti zao.Akasema je unapendakuziniwa dada yako? Akasema hapana.Akasema na watu

    hawapendi kuziniwadada zao. akawekaMtume (s.a.w) juu yakifua chake akasema:ewe Mwenyezi Mungumfutie madhambiyake na usashe moyowake, na uhifadhi uchiwake.

    wabilah tawfqemail : eg_islamic_

    [email protected]

    NI TAASISI YA KIDINI ILIYOANZISHWA NAKUSAJILIWA KISHERIA MWAKA 2014 MKOANIMOROGORO KWA LENGO LA KUIHAMASISHA

     JAMII YA WAISLAMU KUIKUMBUKA NAKUITEKELEZA NGUZO YA TATU YA ZAKKA.

    PAMOJA NA HAYO TAUZAMO KUPITIAUTOAJI ZAKKA INALENGA KUIUNGANISHA

     JAMII KUWA KITU KIMOJA, KUFUFUA UCHUMIWA KIISLAMU ULIOKUFA NA KUIFANYAQUR’AN NDIYO MUONGOZO SAHIHI KWAUMMA.

    TAYARI TAUZAMO IMEFANIKIWA KUWANA BAYTUL MALL ILIYOKO MTAA WA SIMUKATIKA KATA YA MJI MPYA MANISPAAYA MOROGORO PAMOJA NA KUFUNGUAAKAUNTI KATIKA BANK YA KCB TAWI LA

    MOROGORO NAMBA 3301064116.ILI KUWEZA KUFIKIA MALENGO HAYONA MENGINE, TAASISI INAHITAJI UUNGAJIMKONO KWA HALI NA MALI KUTOKAKWENYE TAASISI NA VIKUNDI MBALIMBALI.

    UNAWEZA KUFIKA OFISINI MAKAOMAKUU MTAA WA SIMU KATA YA MJI MPYAMANISPAA YA MOROGORO AU WASILIANANASI KWA SIMU NAMBARI 0686240494 AU0717337919

    TANGAZO HILI NI KWA HISANI YA MWENYEKITI WA

    TAUZAMO SHEIKH SALEH HUSSEIN S ANGA (BWAWANI).

      TAASISI YA UKUMBUSHO WA ZAKKA

      MOROGORO (TAUZAMO)

    SIKU YA WAJINGA AU WAZUSHI ?

    Nabtadi kualifu, si tungo kuzibananga, Jambo moja kuarifu, si mengi kutangatanga,Si jingine mintarafu, hiyo siku ya wajinga,Sio siku ya wajinga, ya wazushi na warongo!

    Tarehe mosi tengefu, Aprili naipinga,Si siku inosadifu, urongo wanoulonga,Lengolo udanganyifu, kwa kaumu kuikenga,Sio siku ya wajinga, ya wazushi na warongo !

    Wameivika wasifu, eti siku ya wajinga,Wallahi si yake kufu, kwalo mimi nawapinga,U mwingi udanganyifu, katu wala si ujinga,Sio siku ya wajinga, ya wazushi na warongo !

    Kwa tumbi udanganyifu, ndanimwe 'sijejiunga,Ebu basi jikalifu, kutogeuka mshenga,Kwa kupamba upotofu, kadhalika na ujinga,Sio siku ya wajinga, ya wazushi na warongo ! Kumu katika insafu, kwa puya kutozienga,Usimuasi Raufu, kwa longolongo kutunga,Daima kweli sanifu, kukomesha hili janga,Sio siku ya wajinga, ya wazushi na warongo !

    Kwa urongo kurudufu, Jahanamu utatinga,Hamna ndanimwe ufu, wala uhai wa anga,Ikabu zake lufufu, shadidi zitakusonga,Sio siku ya wajinga, ya wazushi na warongo !

    Haya shime kaka Sefu, nawe dada Mwanamanga,Leo sote kwa insafu, tujitanibu kukenga,Tujenge usadikifu, kwa kweli kutwa kulonga,Sio siku ya wajinga, ya wazushi na warongo!

    Tuache ukengeufu, wa puya kutwa kulonga,Ukweli tuusharifu, akhera kwetu ni kinga,Kaditama kualifu, Abuu natia nanga,Sio siku ya wajinga, ya wazushi na warongo!

     ABUU NYAMKOMOGI

    SIKU YA USHAIRI DUNIANI(Maskini Ushairi!)

    Tama nimejishikia, insi nawaajabia,Fani yazidi a, wao washerehekea,Dhamira nakiria, yao sijaing'amua,Maskini ushairi, fani inayojia!

    Sifahamu kwa dunia, wengine watatongoa,Nilonge kwa Tanzania, Bara nilikokulia,Kwa lengo la kuzindua, wala si la kubeua,Maskini ushairi, fani inayojia!

    Hali ninojionea, kwa ya kwangu mizania,Katu si ya kuridhia, wala kutafakharia,Kipi cha kujivunia, Ushairi Tanzania?Maskini ushairi, fani inayojia!

    Weledi umepungua, wa nudhumu Tanzania,Utunzi umekomea, kurasa za nadharia,

    Si kama ilivyokua, zile zama azalia,Maskini ushairi, fani inayojia!

    UKUTA naulizia, i hai imejia?Kama hai kaulia, basi mfu ilia!Nani wa kusimamia, washairi Tanzania?Maskini ushairi, fani inayojia!

    Wito ninawatolea, wote walosherekea,Haya kuyazingatia, pasipo kuyabeua,Mwisho beti nakomea, sita sitaendelea,Maskini ushairi, fani inayojia!

    ABUU NYAMKOMOGI

    ANNUUR NEW.indd 14 3/3

  • 8/18/2019 ANNUUR 1223

    15/20

    15  AN-NUUR

    JAMADUL  AAKHER 1437, IJUMAA APRIL I 1-7, 2016Makala

    SHUKRANI zote zinamstahikiaAllah (sw). Sala na salamuzimkie mtukufu wa daraja,Masahaba wake na wotewanaofuata mwenendo wakempaka siku ya malipo.

    Somo la nne katika mfululizowa masomo haya ya Tawhiid,

    ni taratibu za kukufurishana,yaani ni wakati gani Muislamuataitikadiwa kuwa ni kari.Somo hili ni muhimu sana kwanimakundi yote yaliyochupamipaka na kuanza kugeukakuwa ni makundi ya kihalifukupitia jina la Kiislamu, yalianzakupotea katika suala la kumjuani nani kari na inakuwajempaka unamuitakidi mtu kuwani kari.

    Kipengele nambari sitinina saba katika kitabu chaImam Tahawy kinasema “hatumuitakidi yeyote katikawatu wa kibla,(yaani wafuasiwa Muhammad (saw)) kuwa nikari kwa kufanya madhambi

    makubwa, mpaka aitakidi kuwahiyo dhambi kubwa ni halali,pia hatusemi kuwa dhambihaimdhuru mtu madhaliameamini”.

    Huu ndio mtizamo sahihiwa Kiislamu tofauti na ile yamakundi mawili, moja likiitwaKhawarij ambalo lilikuwa naitikadi kuwa kila Muislamuanayefanya dhambi kubwa nikari. Ametoka kabisa katikaUislamu, na akhera atakaamilele motoni . Hilo ni Kundilililochupa mipaka katikasuala la kukufurishana, waowaliitakidi kuwa Ali (ra) naMuawiyya(ra ) na wafuasi waowote ni makari na waliaminikila mtu ambaye si Khawarij nikari. Waliwakataza wafuasiwao kusema na watu ambaosi Khawarij, kutowaozesha nakutoolewa na wasio Khawarij.Baya Zaidi, walihalalishakumwaga damu ya kilaasiyekuwa Khawarij kwa vilewaliwaona ni makari (lakinitambua pia kuwa katikaUislamu hakuna amri walahukumu ya kuua makari. Mtuatauliwa kutokana na hukumuya kimahakama kutokana nakosa kulingana na shera yaKiislamu.).

    Kundi la Muutazila waowaliamini kuwa dhambikubwa inamuweka mfanyaji

     baina ya Uislamu na Ukari,

    haimfanyi awe kari kikamilifulakini akhera atadumu motonimilele. Muutazila na Khawarijwalihitilaana kuhusu mwenyekufanya dhambi kubwa, dunianinamna yake iko vipi, lakiniwalikubaliana kuwa akherawatadumu milele motoni.

    Kundi la Mur’jia liliaminikuwa Muislamu hata afanyedhambi kubwa kiasi gani,haitomdhuru madhaliameamini yaani kule kuaminitu kunamtosha, na imanihaidhuriwi na madhambi hata

    Tawhiid -4

    yawe kiasi gani. Hili ni Kundi

    lililochupa mipaka katika sualahili, kwa kuamini kuwa dhambihaiathiri imani ya mtu .

    Msimamo wa sahihi waUislamu ni kuwa dhambiinapunguza imani ya mtu naimani inakuwa kwa kufanyamambo mema. Huu ndiyomsimamo wa Uislamu.Lakini Imam Abuu Hanifayeye ana msimamo kuwaimani haiongezeki, na huuni msimamo dhaifu, kwaniaya na hadithi zinaoneshadhahiri kuwa imani inapunguakwa madhambi na inakuwakwa kufanya mema kamatutakavyoona mbele inshaallah.

    Ama Ulamma aliyetoa fatwa

    ya aqida na akijitahidi lakiniakakosea katika fatwa yake, basi hahesabiwi kuwa ni ka