annuur 1182

20
ISSN 0856 - 3861 Na. 1182 RAMADHAN 1436, IJUMAA , JUNI 19 - 25, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected] AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST Tunahitaji afya, uwezo na nafasi ili kutekeleza Nguzo ya Hijja. Tuzitumie leo rasilimali hizi. Hakuna uhakika wa kufika mwakani. Jithibitishe katika Uislamu na uiokoe nafsi yako na Moto. Us.imwendekeze shetani (iblis). Muda unakwisha! Gharama zote kwa Hijja ni Dola 4,500. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,300. Karibuni Ahlu Sunna Wal Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0765462022;0782804480; 0717224437. (13) AFYA, UWEZO NA NAFASI Waislamu Mbeya wavunja rekodi Tamasha lakusanya watu 700 Ni mfano wa Jihad ya mali, nafsi ILIKUWA wakati wa Serikali ya Mkapa na Waziri Mkuu Sumaye ambapo yalitokea mauaji ya raia. Ni vigumu kuhalalisha na kusema kuwa adhabu ya mwananchi kupinga anachoamini ni dhulma, iwe ni kuuliwa kwa risasi. Haya ni mambo ambayo hutokea katika nchi ambazo ukandamizaji ndio staili ya uongozi na katu sio katika Tanzania yetu njema. Najiuliza, Mheshimiwa Sumaye anakuwa na ujasiri wa namna gani naye kujiona kuwa ni mwanasiasa anayefaa kupokewa Zanzibar na kufikiriwa kuungwa Sumaye amesahau mauaji ya Wazanzibari mwaka 2001? Mh. Frederick Sumaye. mkono katika mkakati wake wa kusaka urais wa Jamhuri ya Muungano! (Uk. 9) Elimisheni-Totonji Wapeni wake zenu amani, furaha Imarisheni ndoa na familia zenu Msihangaishwe na propaganda DK. Ahmad Totonji Dk. Muhsin Masoud WANATAMASHA wakiponda na kubeba udongo wa kufyatulia tofali. AKINAMAMA wakibeba mawe katika Tamasha la Ujenzi wa Kituo cha Kiislamu Mbeya.

Upload: zanzibariyetu

Post on 16-Dec-2015

1.095 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • ISSN 0856 - 3861 Na. 1182 RAMADHAN 1436, IJUMAA , JUNI 19 - 25, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

    Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected]

    AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST

    Tunahitaji afya, uwezo na nafasi ili kutekeleza Nguzo ya Hijja. Tuzitumie leo rasilimali hizi. Hakuna uhakika wa kufika mwakani. Jithibitishe katika Uislamu na uiokoe nafsi yako na Moto. Us.imwendekeze shetani (iblis). Muda unakwisha! Gharama zote kwa Hijja ni Dola 4,500. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,300. Karibuni Ahlu Sunna Wal Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0765462022;0782804480; 0717224437.

    (13) AFYA, UWEZO NA NAFASI

    Waislamu Mbeya wavunja rekodiTamasha lakusanya watu 700Ni mfano wa Jihad ya mali, nafsi

    ILIKUWA wakati wa Serikali ya Mkapa na Waziri Mkuu Sumaye ambapo yalitokea mauaji ya raia.

    Ni vigumu kuhalalisha na kusema kuwa adhabu ya mwananchi kupinga anachoamini ni dhulma, iwe ni kuuliwa kwa risasi.

    Haya ni mambo ambayo hutokea katika nchi ambazo ukandamizaji ndio staili ya uongozi na katu sio katika Tanzania yetu njema.

    Najiuliza, Mheshimiwa S u m a ye a n a k u wa n a ujasiri wa namna gani naye kujiona kuwa ni mwanasiasa anayefaa kupokewa Zanzibar na k u f i k i r i wa k u u n g wa

    Sumaye amesahau mauaji ya Wazanzibari mwaka 2001?

    Mh. Frederick Sumaye.mkono katika mkakati wake wa kusaka urais wa Jamhuri ya Muungano! (Uk. 9)

    Elimisheni-TotonjiWapeni wake zenu amani, furahaImarisheni ndoa na familia zenuMsihangaishwe na propaganda

    DK. Ahmad Totonji Dk. Muhsin Masoud

    WANATAMASHA wakiponda na kubeba udongo wa kufyatulia tofali.

    AKINAMAMA wakibeba mawe katika Tamasha la Ujenzi wa Kituo cha Kiislamu Mbeya.

  • 2 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 19-25, 2015AN-NUUR

    S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.

    www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected] zetu zipo: Manzese Tip Top

    Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

    Tahariri/Habari

    RAMADHANI ni mwezi mtukufu, mwezi ambao ndani yake imeteremshwa Q u r a n , a i d h a n d a n i yake kuna usiku wa L AY L AT U L - Q A D I R , usiku ambao ni bora kuliko usiku nyenginezo. Ramadhan ni mwezi a m b a o h u s a m e h e wa watu makosa yao na kukubaliwa maombi yao.

    Tunamshukuru Allah k w a k u t u f a n i k i s h a k u u d i r i k i m we z i wa Ramadhani wa mwaka wa 1436 AH mwafaka na mwaka wa 2015. Mwezi huu unamtaka mja awe kwenye Taqwa, na taqwa ni kitu kimmoja kilicho na upeo wa hali ya juu. Taqwa sio mtu kujifanya mnyonge na huku ana yake. Lakini Taqwa ni kule kumcha Allah na kuyafanya yale yote aliyoyaamrisha Mola pasi kujionyesha wala kujipigia zumari kuwa umo kwenye Taqwa.

    E n y i m l i o a m i n i , M u m e l a z i m i s h w a kufunga (Saumu) kama w a l i v y o l a z i m i s h w a waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu (Al-Baqarah 2:183).

    Hapa ndipo kwenye k a z i k u b wa a m b a p o tunatakiwa kuifanya, kumcha Mungu na kuwa katika unyenyekevu.

    F u n g a n i C h u o kinachomchukua mja kuweza kuj i funza na kujisafisha kwa mwaka mzima na kwa maisha yake. Unaambiwa kuwa kwenye funga usiibe, usisengenye, usifanye unyumba wakati wa funga kwa alio ni halali yako, usile mchana pamoja na makatazo yote ya mabaya, umetakiwa usiyafanye. Hii nikumaanisha kuwa Chuo hichi kikufunze na kikuchukue ndani ya miezi mengine kuwa ni mtu ambaye anafwata yale yote aliyoamrishwa na Allah.

    Tunafahamishwa katika S u r a t u l A h z a b N a wanaume wenye kufunga na wanawake wenye

    Kuukaribisha mwezi wa Ramadhani

    yake ni Pepo. Mwezi wa Ramadhan

    ni mwezi wa machumo, mwezi wa Ramadhan ni msimu, kama mfanya biashara hujikaza achume k w e n y e m s i m u w a biashara na ndipo nasi tunatakiwa tujihimize na tupinde mgongo katika kufanya mema na kusaidia wa l i o k u wa wa h i t a j i . Tunatakiwa tusome Quran kwa wingi, kusali Taraweh na Witri , Kufuturisha waliofunga, Kuwasaidia m a s i k i n i , k u f u t u r u mara tu jua linapozama, kuchelewesha kula daku na kukithirisha katika kufanya mema na kujitenga na yale yalioharamishwa.

    Ramadhani ya mwaka huu katika nchi zilizopo ndani ya Equator na chini yake watakuwa kwenye kipupwe (Winter ) na Wa i s l a m u w e n g i n e o waliokuweko sehemu za juu Tropic of Cancer na kukurubia sehemu za barafu North Pole huko watakuwa kwenye kiangazi (Summer). Wakati

    wa baridi usiku unakuwa mrefu na mchana unakuwa mdogo na nyakati za kiangazi mchana unakuwa mrefu na usiku unakuwa mdogo. Hapa kwa wale watakaofunga kwenye wakati wa kiangazi kuna wanaokaribia kuwa ndani ya saumu kwa masaa baina ya 18-20 wakati wale waliokuwa katika kipupwe hawatozidi masaa 14.

    Hikma kubwa kutokana na Allah ni kuonyesha k u w a t u l i v y o k u w a tunafwata mwezi kama mwezi wala sio mwezi kwa mzunguko wa jua, basi tutakuwa na mapungufu ya siku 11 kila mwaka, na haya yanajalia kuwa katika maisha yako yote utapata kufunga katika miezi ya kiangazi ikiwa mchana mrefu, a idha utapata kufunga siku za kipupwe ikiwa mchana ni mdogo, kinyume chake na miezi ya jua (solar), inegekuwa Ramadhani imejaaliwa iwe kila mwaka January, i n g e k u j a k u w a k u t a w e n g i n e wa n a f u n g a

    maisha kwenye miezi ya kiangazi na wengine maisha wanafunga katika mwezi wa kipupwe.

    Hii ni neema kubwa a l i o t u j a a l i a A l l a h wa l a h a i k u wa k u wa inahitajia kupangwa na kupanguliwa, lakini ni mwenyewe Subhana wa Taala katupangia nasi tumo kwenye kufaidika na funga katika misimu mbalimbali.

    Gazet i l a An-Nuur linawombea Waislamu wa Somali, Iraq, Syria, Phalestina ambao wamo k w e n y e m s u k o s u k o mkubwa wa kupigana wenyewe kwa wenyewe, M we n ye - e n z i - M u n g u awaondoshee fitna hii na vilevile tunamuomba A l l a h a w a l a i n i s h e wafanya biashara ambao w a m e k u w a h a w a n a huruma kwa kupandisha bei bidhaa nao waipate S p i r i t ya R a m a d h a n kwa kuuza biashara zao kwa bei iliyomuwafaka,. Tu n a m u o m b a A l l a h atautakabaliye ibada zetu na tusiwe kati ya wale we n ye k u t o k a t u p u . Ameen.

    kufunga na wanaume wenye kujihifadhi tupu zao na wanawake wenye kujihifadhi tupu zao na wanaume wenye kumtaja ALLAH kwa wingi na wanawake wenye kumtaja ALLAH (kwa wing i ) amewandal ia ALLAH watu hao msamaha na ujira (malipo) uliokuwa mkubwa (kabisa) (Al Ahzab 22:35).

    Sura hii inatoa kielelezo fika juu ya wale wanaume w a t a k a o f u n g a n a wanawake watakaofunga kwaajili ya Allah malipo yao yatakuwa ni kitu gani. Aidha tunafahamishwa kutokana na hadithi hii ya Bwana Mtume SAW:

    Hakika Peponi kuna mlango unaoitwa RAYYAN wataingia (humo) wenye kufunga siku ya kiama na hato ingia (humo) asiyekuwa miongoni mwao (wafungaji) watakapoingia ( w o t e ) u t a f u n g w a (mlango huo) na hatoingia mwengine yeyote (Bukhari na Muslim). Hii ni mmoja ya jaza kwa wale ambao watakuwa wanafunga.

    T u n a f a h a m i s h w a kutokana katika hadithi ndefu kwamba Salman anasimulia alituhutubia mjumbe wa Mwenye-enzi-Mungu mwisho wa mwezi wa Shaabani akasema:

    Umekufikieni mwezi Mtukufu wenye baraka, mwezi ambao ndani yake k u n a L AY L A L AT U L -Q A D I R a m b a y o n i bora kuliko miezi elfu, mwezi ambao amejaalia Mwenyezi Mungu kufunga kwake katika mwezi huo ni fardhi, kusimama usiku ni Sunna (ni kujikurubisha) Mwenye kujikurubisha katika (mwezi) huo kwa jambo (moja) jema huwa kama aliyetekeleza fardhi katika mwezi usiokuwa huo (wa Ramadhani) na ataketekeleza fardhi katika (mwezi) huo huwa kama aliyeteleza fardhi sabini katika mwezi usiokuwa huo. Nao ni mwezi wa subira, na subira malipo

    P.O. BOX 72045, Dar es Salaam, TANZANIA. TEL+255 655 654900, +255 754 208585, +255 713 731 300.

    Email: [email protected], Web: www.tampro.org

    TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA TAMPRO WA MWAKA 2015

    Jumuiya ya Wataalaamu wa Kiislamu Tanzania (TAMPRO) inatoa taarifa ya Mkutano Mkuu wa Kumi na Tano (15) utakaofanyika siku ya Jumamosi na Jumapili, Tarehe 25-26 Julai, 2015, katika Ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondari Shamsiye, Mbweni, Dar es Salaam. Mkutano huo utaanza saa 2:30 asubuhi mpaka 11.00 jioni, in shaa Allah.

    Siku ya Jumamosi kutakuwa na semina elekezi kwa wajumbe wa mkutano na wageni waalikwa kuhusu uendeshaji bora wa NGOs. Pia, siku hiyo kutakuwa na ripoti za matawi, Taarifa ya Utendaji na Fedha 2011 - 2015, Mpango Mkakati wa TAMPRO na salaamu za wageni wa Taasisi mbalimbali.

    Siku ya Jumapili, Mkutano Mkuu utahusika na ajenda zifuatazo: Ufunguzi, kuthibitisha akidi, kupokea ajenda, kuthibitisha kumbukumbu za kikao kilichopita, yatokanayo, uchaguzi mkuu, mengineyo, kufunga mkutano.

    Kwa mujibu wa Katiba Mpya ya TAMPRO 2014, Wajumbe Wote wa Mkutano Mkuu Wanaombwa Kuhudhuria Bila ya Kukosa.

    PAZI MWINYIMVUA

    KATIBU MKUU-TAMPRO

  • 3 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 19-25, 2015Habari

    Lile agizo katika Quran la kupigania Dini kwa mali na nafsi, limefanyiwa kazi mkoani Mbeya wiki iliyopita ambapo Waislamu zaidi ya 700 walikusanyika wakifanya kazi ya ujenzi wa Kituo cha Kiislamu, Ilongo.

    Waislamu hao wakitokea m i k o a y o t e n c h i n i (kasoro Geta) ikiwemo ile ya Visiwani, Zanzibar, walichapa kazi katika tamasha hilo lililoanza Juni 5 hadi 12 huku wakitoa michango yao ya pesa kuendeleza ujenzi.

    Kazi kubwa iliyofanyika ilikuwa kufyatua matofali ambapo hadi tamasha linafungwa zilikuwa tayari zimepatikana tofali 44,000.

    Kazi nyingine ilikuwa kuchimba mis ingi ya nyumba za madarasa, mabweni na ofisi, huku akina mama wakifanya kazi kubwa ya kusomba mawe na kuyajaza katika misingi iliyochimbwa.

    Utaratibu wa matamasha hayo ni kuwa washiriki wanajisafirisha kwa pesa zao huku wakitakiwa kuchangia gharama za chakula halikadhalika kuja na michango ambayo itasaidia kuendeleza ujenzi baada ya tamasha.

    M k o a wa M wa n z a walipangiwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja na nusu (1,500,000) ambapo wali fanikiwa kuleta ziada ya laki tano kwa maana kuwa walitoa shilingi milioni 2.

    Kwa upande mwingine, Mwanza inatajwa kuleta washiriki wengi katika mikoa ya mbali ambapo i l ikuwa na washir ik i 46 ikipitwa kidogo na Singinda ambao walikuwa 47.

    Hata hivyo Songea ndiyo iliyokuwa na washiriki wengi wakiwa 74 huku Iringa ikifuatia kwa kuwa na washiriki 33.

    Iringa iliongoza pia katika utoaji wa michango ya kifedha na vifaa vya k u f a n y i a k a z i k a m a majembe.

    Wa l i l e t a k i a s i c h a shilingi milioni moja na laki mbili (1,200,000) wakiwa wamevuka lengo la laki tano walizopangiwa kutoa.

    K w a u p a n d e w a U n g u j a n a P e m b a , washiriki walikuwa 16 na walikamilisha michango y a o w a l i y o p a n g i w a ambapo Pemba walitoa shilingi 500,000 na Unguja 500,000.

    Taarifa kutoka Kamati y a M a a n d a l i z i n a

    Waislamu Mbeya wavunja rekodiNa Mwandishi Wetu.Usimamizi wa tamasha hilo imefahamisha kuwa waliohudhuria kutoka Dar es Salaam walikuwa 41 wakipeleka mchamngo wa shilingi 1,200, 000 na kubakisha deni la 1,800,000 kwa kuwa walipangiwa kutoa shilingi milioni 3.

    T a a r i f a z a i d i z i k a f a h a m i s h a k u wa jumla ya fedha taslimu z i l i z o k u s a n y w a i l i kuendeza ujenzi baada ya tamasha, ni kiasi cha shilingi milioni 10,549,500.

    B a d o k u n a m i k o a i n a d a i w a k w a v i l e h a i k u t i m i z a k a s m a w a l i y o p a n g i w a n a inatarajiwa kuwa wakirejea watakusanya na kuituma.

    Ukiacha juhudi kubwa i l iyokuwa ik i fanyika

    kutoa nguvu kazi katika kusimamisha kituo hicho cha Ki is lamu, I longo mkoani Mbeya, washiriki walijumuika pia katika ibada za pamoja ikiwemo kisimamo cha usiku na darsa duara.

    I l i k u w a n i k a t i k a kuhi t imisha tamasha na darsa hizo ambapo washiriki waliazimia kuwa kila mmoja wao ajiendeleze kwa kusoma ili kuujua Uislamu vizuri ikiwa ni pamoja na kusoma Qur an na Tafsiri kwa mazingatio angalau aya 5 kila siku. (Tafsiri yenye tangulizi za Sura ya Sheikh A. S. Farsy.)

    Azimio lingine ni kuwa kila mmoja wao ajitahidi kusoma Hadithi angalau tatu (3) katika Tafsiri ya

    Riadha-s swaalihiin.Tamasha la ujenzi wa

    Kituo cha Kiislamu Ilongo, Mbeya, linatajwa kuvunja rekodi kutokana na ufanisi wake katika maandalizi ambapo kwa mara ya kwanza wanatamasha waliishi katika mazingira bora na rafiki yakiwemo maji ya kutosha na mahali pazuri pa kufanyia ibada na kulala.

    Hii ni kwa sababu wana-Mbeya wal ikamil isha u jenzi wa Msiki t i na kupata mazulia, lakini kubwa zaidi kupata maji ya kutosha yanayotoka katika mfumo wa bomba kutoka kisima kirefu, yakivutwa na machine (pump) na kuhifadhiwa katika matanki.

    K a t i k a m a t a m a s h a

    yaliyotangulia yakiwemo yale ya ujenzi wa Kirinjiko, N ya s a k a , M k u z o n a Shenge juu, washir ik i walifanya kazi katika m a z i n g i r a m a g u m u yakiwemo uhaba wa maji, kutokuwepo mahali pazuri pa kupumzika baada ya kazi ngumu na mapungufu mengi.

    Kwa tamasha la Ilongo, washiriki wameswali na kulala katika msikiti wenye mazulia huku vyoo vikiwa na tailis na hivyo hali ya usafi kuzingatiwa muda wote huku maji yakitiririka katika bomba.

    Ukiacha ujenzi ambao unakwenda kwa awamu, changamoto pekee kubwa inayokikabili kituo cha Ilongo, ni kufikisha umeme baada ya maji kupatikana.

    Kituo kitakapokamilika, kinatarajiwa kuwa na shule ya msingi na sekondari na katika mipango ya muda mrefu kuwa na chuo cha ufundi.

    HAKIKA kila nafsi itaonja mauti. Sisi sote Kwake t u m e t o k a n a K wa k e tutarejea.

    Haya ni maneno ya Mwenyezi Mungu katika Quran kwa wanadamu, kwamba hakuna chochote chenye uhai ambacho kinaweza kuishi milele. Lazima kitakufa.

    Jumatatu wiki hii, Mufti Issa Shaaban Simba alifariki dunia katika hiospitali ya TMJ ya jijini Dar, ambako a l i k u w a a m e l a z w a a k i t i b i w a k u f u a t i a kusumbuliwa na maradhi ya shinikizo la damu na sukari.

    Mufti Simba alizikwa Jumanne wiki hii mkoani Shinyanga ambako pia ndio yaliyokuwa makazi yake kwa muda mrefu.

    Kwa mujibu wa historia fupi iliyotolewa na Sheikh Khamis Mataka, ambaye aliwahi kufanya kazi na Mufti Simba BAKWATA, a l i sema Muf t i S imba alizaliwa mkoani Mwanza mwaka 1936.

    Katika miaka ya 1950 a l i k w e n d a k u s o m a masomo ya dini Zanzibar katika kituo cha Kiislamu kilichokuwa kikubwa na maarufu Afrika Mashariki wakati huo cha Muslim Academy.

    Chuo hiki ki l ikuwa chini ya Sheikh Said Umar

    Sheikh Issa Shaaban SimbaInnalillahi wa inna ilaihir rajiuun Na Mwandishi Wetu

    Abdallah Mwinyi Baraka.Marhum Simba alirejea

    bara mwaka 1964 wakati wa Mapinduzi ya Zanzibar.

    A l i k u wa m i o n g o n i mwa vijana walioajiriwa na i l iyokuwa Jumuia ya Wais lamu Afr ika Mashariki wakati huo ya East Africa Muslim Welfare Society (EAMWS), akiwa mwalimu wa dini.

    Alifanya kazi yake ya ualimu wa dini katika m i k o a y a M w a n z a ,

    Shinyanga, Kagera hadi pale EAMWS ilipovunjwa mwaka 1968 na kuundwa BAKWATA.

    Mwaka huo wa 1998 Sheikh Simba alikuwa akitumikia BAKWATA ambapo mwaka 1970 alikuwa Sheikh wa mkoa wa Shinyanga na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa BAKWATA.

    Mwaka 2002 alipofariki Mufti Sheikh Hemed bin Juma, aliteuliwa kuwa

    Kaimu Mufti wa Tanzania (BAKWATA).

    Mwaka 2003 lichaguliwa rasmi kuwa Mufti ndani ya BAKWATA katika uchaguzi uliowaniwa na Maulamaa kadhaa wakiwemo Prof. Juma Mikidadi, Sheikh Amran Kilemile, Marhum Sheikh Suleiman Gorogosi na wengine.

    Nafasi hiyo aliitumiaka hadi alipofariki Jumatatu wiki hii Juni 2015.

    MUFTI Sheikh Issa Shaaban Simba (kulia). Kushoto ni Sheikh Alhad Mussa.

  • 4 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 19-25, 2015Makala

    H A B A R I ya k i f o c h a Sheikh Mkuu wa Bakwata, M u f t i S h a a b a n b i n Simba zimewahuzunisha Watanzania wengi. Kifo c h a k e s i o p i g o k w a Waislamu peke yao, bali kwa Watanzania wengine nje ya Jumuia ya Waislamu. Huzuni na simanzi hiyo i n a t o k a n a n a u k w e l i kwamba Mufti Shaaban bin Simba alikuwa kiongozi wa Taifa, kwangu namweka daraja moja na akina Rashid Mfaume Kawawa, Hemed bin Jumaa, Julius Nyerere, Abeid Karume, Kardinali Lugambwa na Paul Bomani.

    K w a m d i n i h a w e z i kunielewa ninapowaweka pamoja akina Kawawa, Nyerere, Bomani, Rugambwa, Hemed bin Jumaa na Simba, l a k i n i k w a m z a l e n d o inaeleweka. Tanzania ni taifa moja lakini linalokusanya watu wa aina tofauti. Kuweza kudumu katika umoja ndani ya utofauti, hapo ndipo ulipo umuhimu wa uongozi imara. Tunaziona nchi zingine kama Somalia yenye wananchi wa dini moja, lugha moja n a u t a m a d u n i m m o j a , lakini hawaelewani wala hawasikilizani.

    Nilibahatika kumwona na kumsikiliza mzee Bernard Ntiliya ambaye alikuwako viwanja vya Mnazi mmoja usiku ule wa kuamkia tarehe 09 Desemba 1961 wakati wakoloni walipomkabidhi kat iba Mwalimu Jul ius Nyerere na bendera ya Union Jack ikishuka na kupandishwa bendera ya Tanganyika.

    Mzee Bernard ambaye ana zaidi ya miaka 90 lakini ukimwona utadhani mzee wa miaka 60, anakumbuka kuwa kwenye meza kuu mstari wa mbele walikaa mwakilishi wa Malkia Dwirt of Edinburg, Gavana Richard Turnball, mkuu wa Jeshi la mfalme KAR, Askofu mkuu Laurean Lugambwa, Chifu wa Wagogo Mazengo Salula, Adamu Sappi Mkwawa na wengine hawakumbuki.

    Baadaye nikaiona picha hiyo askari wa Kizungu a n a t e r e m s h a b e n d e r a . Kwenye meza kuu (High table) anaonekana Rugambwa akiwa kijana mbichi, mzee kuliko wote ni Mazengo na Sheikh mmoja ambaye jina lake halielezwi labda mzee Bernard akimwona anaweza kumkumbuka.

    Wazungu walipoamua kuikabidhi Tanganyika kwa kiongozi wa TANU Mwalimu Julius Nyerere, walijua kuwa wanamkabidhi nchi ambayo ni moja lakini ndani yake kuna wingi ndio maana wakawaalika viongozi wa

    Mufti Simba: Taifa limepoteza kiongozi muhimuNa Mwinjilisti Kamara

    Kusupa

    AL-MARHUUM Sheikh Mkuu wa Bakwata, Mufti Shaaban bin Simba (kushoto) akisalimiana na Rais Jakaya Kikwete wakati wa uhai wakeJadi yaani Machifu, viongozi wa dini na makundi yenye nguvu kama vyama vya wafanyakazi.

    K w a m t u m w e l e w a hawezi akaubeza mchango wa viongozi wa dini katika kuifanya Tanzania idumu kama Taifa moja lenye watu tofaut i . CCM inaj inadi na ku j igamba kwamba imedumisha umoja na utulivu. Hiyo ni propaganda ya kisiasa. Lakini ukweli ni kwamba kama viongozi wa madhehebu ya dini mbili za Ukristo na Uislamu walioongoza asasi hizo baada ya kuondoka mkoloni wangeamua kuhubiri shari, chuki na machafuko kama wanavyoelekea kufanya baadhi ya wahubiri wa kizazi cha Utandawazi na mfumo wa soko huria, Tanzania isingekuwa na amani iliyo nayo.

    Inabidi tuwaenzi viongozi wa jadi na viongozi wa dini kwamba walikubali kimsingi kwamba tunaishi ndani ya Tanzania moja, viongozi wa jadi walikubali matokeo hata baada ya serikali ya TANU kuvunja Taasisi ya Uchifu. Hakuna kabila lililoamua kuasi kwasababu walijua kwamba ili Tanzania iendelee kuwa Taifa, kabila moja linalihitaji kabila lingine, vinginevyo wangeurudia utaifa mdogo wa ngazi ya kabila.

    Vivyo hivyo viongozi wa dini walikubali kwamba Tanzania ni ya wote hata wasiokuwa wafuasi wa itikadi zao.

    B i n a f s i n i m e k u w a nikivutiwa na watu wanne katika jamii ya Waislamu wa Tanzania, nitawataja watatu waliotangulia mbele haki, huyu wa nne sitomtaja kwakuwa bado yu ngali hai pamoja nasi.

    Nilikuwa nikivutiwa na mawaidha ya Hayati Sheikh Hemed bin Jumaa ambayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja na Radio Tanzania

    Dar es Salaam (RTD). Siku moja nikiwa nyumbani kwa Masamu (Mkristo wa madhehebu ya kipentekoste), ulifika wakati wa mawaidha, al i fungul ia redio yake taratibu huku akinitizama n a k u t a b a s a m u , n a m i sikuchelewa nikamwambia ongeza sauti ili tumsikilize Sheikh Hemedi leo anasema nini. Ndipo alipocheka na kuniuliza kumbe hata wewe mwinjilisti huwa unamsikiliza Sheikh Hemedi? Akaendelea kusema mimi napenda kumsikiliza huyu Sheikh kwa sababu anaifafanua vizuri Korani katika lugha rahisi kiasi kwamba hata akili ya kawaida inaelewa.

    Nikamwambia huwezi kuamini nikikwambia mimi huwa namsikiliza Redioni na kuna wakati nikitembelea maeneo ya Kinondoni, huwa nakaa pembezoni mwa msikiti anaoswalisha na kusikiliza hotuba yake tangu mwanzo hadi anamaliza.

    Tulitaniana na baadaye tukawa kimya kusikiliza mawaidha yake.

    Mwingine ninayevutiwa naye ni Ustaadh Ilunga. Siku moja nikiwa nimejipumzisha, simu yangu ya kiganjani iliita nikapokea, msemaji akajitambulisha kwamba, akisema:

    Mimi naitwa Sheikh Ilunga, naita kutoka Songea n i k o s a f a r i n i n i t a r u d i Dar es Salaam wiki ijayo. Nimekutana na mwanafunzi wangu mmoja ambaye ulimuuzia kitabu chako cha maisha yako ulipokuwa kifungoni, nimesoma kabla ya kumaliza nimekipenda nimemnyanganya sasa nataka unihakikishie unacho kingine? Nataka nimtume mwanafunzi wangu aje kwako akichukue kwa niaba yangu.

    N i k a m j i b u k i p o nitakuhifadhia ama unaweza kukichukua hicho moja kwa moja nami nitamfidia. Baada ya siku chache alikuja kijana mmoja muungwana akanunua vitabu vyangu v y o t e v i t a t u , M a i s h a yangu Gerezani, Tanzania tunayoitaka na Kumrudisha Mwafrika kwenye asili yake.

    Siku hiyo nikamwambia Ilunga nitafurahi ukija Dar es Salaam tuonane maana ni jana tu nilikuwa nikisikiliza CD yako pale Magomeni mkabala na wanapouza vyakula mama lishe.

    Baada ya siku chache Ustadh Ilunga akanipigia tena akasema:

    M i k o n o n i m wa n g u n i n a c h o k i t a b u c h a k o cha pi l i k i i twacho HII N D I Y O T A N Z A N I A TUNAYOITAKA, ingawa s i j a k i m a l i z a , l a k i n i nimekupigia ili kukwambia naiona objectivity.

    Tangu hapo hatukuonana wala kuongea tena na Ilunga hadi siku moja niliponunua g a z e t i l a A n n u u r n a kusoma habari ya kifo chake nikahuzunika.

    Sheikh Shaaban Simba nilimfahamu kupitia kwa ndugu Mohamed Simba ambaye kwa muda mfupi tulikaa naye nyumba moja kwa mama Zuwena eneo la Mwembechai.

    Huyu Mohamed Simba tuliyeishi nyumba moja hana udugu wa damu na Simba mufti, ila majina tu yanafanana kwani yeye Mohamed ni Mluguru wa Morogoro.

    Kuna wakati Mohamed Simba al ipata matatizo ya mkewe kuhamishwa kutoka nyumba aliyokuwa akiishi, katika misingi ya ubinaadamu nikamhifadhia baadhi ya vyombo vyake

    sebuleni kwani ulikuwa wakati wa mvua.

    Baada ya ndugu Simba k u z u n g u k a m a e n e o mbalimbali na kwa watu m b a l i m b a l i w e n g i n e wakimwelewa na kumsaidia na wengine wakimtolea nje, kuna siku akanijia akiwa amechangamka, akasema bwana Alhamisi nakwenda kuonana tena na Mufti ameniahidi

    N i k a m u u l i z a k a m a wa n a u d u g u a k a s e m a siyo ndugu wa damu bali n i mtu mwelewa, juz i nilimuuzia kitabu chako na leo nimekikuta mezani anaendelea kukisoma.

    N a m i n i k a c h o m e k a n i k a m w a m b i a S i m b a ukifanikiwa kumwona Mufti mwambie ukweli kwamba hivi vitabu tunavichapisha kilalahoi, kama ameguswa atukutanishe na tajiri yeyote anayemjua ili agharamie walau uchapaji wa vitabu 3,000 tu atakuwa ametusaidia sana kupiga hatua mbele.

    Alhamis ilifika ndugu S i m b a a l i t i m i z i w a alichokuwa ameahidiwa na Mufti, akaniambia hata ombi letu amelielewa amekubali kumwendea Bw. Mmoja ingawa haswali kwenye msikiti wake.

    J u m a t a t u s a a 4 . 0 0 za usiku nikiwa kwenye kibaraza kupeana habari n a n i n a o w a f a h a m u baada ya kurudi safari ya Dodoma nikasikia mtu mmoja n is iyemfahamu akimwambia Yusuf muuza chips , una habari mtu mkubwa ametutoka? Huyo akamjibu nimesikia, baadaye n i l i m u u l i z a m k u b w a huyo ni nani ndipo Yusuf akanijibu ni Mufti Shaaban Simba, nikahuzunika sana. Lakini kwakuwa kufa siyo kuadhibiwa bali ni hatua hala l i ya maisha sawa na kuzaliwa, nalazimika kusema kwa Mola wetu ndiko tulikotoka na kwake tutarejea.

    V i f o v y a w a t u t u n a o w a f a h a m u n a kuwapenda, vitukumbushe kuwa zamu yao imepita inayofuata ni zamu yetu sisi tulio hai leo. Kwani maisha ya hapa duniani ni kama tumekopeshwa tu baadaye tunamrejeshea mwenyewe aliyetuwezesha kuwako. Tuhimizane kutendeana haki ili tukauone ufufuo wa wenye haki siku ya kiama.

    Natamani BAKWATA impate Mufti mwingine mwenye kaliba ili aendelee kusimama kama daraja kati ya Waislamu na Watanzania wasiokuwa Waislamu.

  • 5 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 19-25, 2015Habari za KimataifaWABUNGE wasiopungua 100 wa Bunge la Ulaya, akiwemo Naibu Spika wa Bunge hilo Dimitrios Papadimoulis, wameweka saini katika hati inayotaka kusimamishwa mara moja mzingiro unaofanywa na utawala wa Israel dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza.

    M k u u w a K a m a t i i n a y o s h i n i k i z a kuondolewa mzingiro huo, amesema kuwa kutiwa saini kwa hati hiyo, kuna maana kuwa mzingiro huo wa miaka kadhaa sasa si wa kisheria.

    U k a n d a w a G a z a umekuwa ukizingirwa na kuwekwa kifungoni na utawala dhalimu wa Israel tangu mwaka 2006, baada ya Wanarakati wa Kiislamu Palestina H A M A S , k u s h i n d a uchaguzi mkuu wa bunge.

    Wa k a z i 1 , 8 0 0 , 0 0 0 Ukanda huo wanakabiliwa na hali ngumu kutokana na utawala huo kuzuia kila aina ya bidhaa za m s i n g i n a h u d u m a kikiwemo chakula na dawa kuingizwa katika ukanda huo na wakati huo huo, ukanda huo kugeuzwa kuwa uwanja wa majaribio ya silaha za maangamizi za utawala huo ghasibu.

    Siasa za mauaji ya kizazi

    Bunge la Ulaya lawatetea wakazi Gaza Waweka saini kuondolewa mzingiro

    Dimitrios Papadimoulis

    za Wazayuni wa Israel zinatekelezwa katika hali ambayo jamii ya kimataifa, hasa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya, zikiwa

    zimepiga kimya bila ya kuuchukulia utawala huo hatua zozote za kisheria.

    Pamoja na hayo, jinai na ukatili wa utawala huo umefikia kiwango

    ambacho hata waungaji mkono wake wa jadi, wameamua kupaza sauti kutokana na mashinikizo ya walio wengi barani Ulaya.

    Daima fikra za walio we n g i b a r a n i h u m o zimekuwa zikilalamikia j inai zinazotekelezwa na utawala huo dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Palestina, na kuzikosoa vikali serikali zao kwa kutochukua msimamo thabiti dhidi ya utawala huo.

    Hatua ya baadhi ya serikali za Ulaya ya kususia bidhaa zinazotengenezwa Israel na vilevile hatua ya baadhi ya wabunge wa Ulaya ya kutia saini hati ya kuondoa mzingiro wa Ukanda wa Gaza, bila shaka inatokana na mashinikizo ya fikra ya walio wengi barani humo dhidi ya serikali zao.

    Wanaodai kutetea haki za binadamu duniani wanakabiliana kisiasa na suala la jinai za utawala wa kibaguzi wa Israel

    dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds Tukufu, katika hali ambayo jinai na ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na utawala huo, uko wazi kiasi kwamba hauwezi kutathminiwa kisiasa.

    Mzingiro na vikwazo vya miaka minane dhidi ya Ukanda wa Gaza, mauaji ya kila siku ya Wapalestina, mateso ya wafungwa wa Kipalestina na upinzani dhidi ya kurejea wakimbizi wa Kiapalestina katika ardhi zao za jadi, ni mambo ambayo yamewaudhi watetezi wa haki na uadilifu duniani kiasi kwamba hayawezi tena kufumbiwa macho wala kutazamwa kisiasa.

    Hujuma ya siku 50 ya utawala wa Israel h u k o G a z a m w a k a uliopita iliwakasirisha wengi ambapo za id i ya Wapales t ina 2000 waliuliwa katika hujuma hiyo, wengi wao wakiwa ni watoto na wanawake na kuharibiwa nyumba na maisha yao huku wakiwekewa mzingiro (kifungo).

    U k a n d a m i z a j i h u u ni suala lililoweka wazi zaidi utambulisho halisi wa ukatili wa utawala wa Israel mbele ya macho ya walimwengu.

    W I M B I l a k u t o r o k a wanajeshi katika Jeshi la Utawala wa Kizayuni l i m e k u w a j i n a m i z i kubwa kwa utawala huo.

    Gazet i la Kizayuni la Haaretz limefichua kuwa, jeshi la Israel sasa limelazimika kutumia maelfu ya wahalifu sugu na wenye kesi nyingi za jinai, ili kuziba pengo la askari wanaotoroka jeshini.

    Kwa mujibu wa gazeti hilo, hata wahalifu sugu wa makosa ya kijinsia wameanza kutumiwa na jeshi la Israel kuziba pengo hilo.

    Wahalifu hao sugu ni wale waliopatikana na hatia za wizi, kutumia dawa za kulevya, vitendo vya j ina i na uhal i fu mwingine mkubwa.

    Kat ika kipindi cha muongo mmoja uliopita, W a z a y u n i w e n g i wamekuwa wakipelekwa korokoroni za kijeshi

    Jinamizi la kutoroka wanajeshi IsraelWahalifu watumika kuziba pengo

    kutokana na kujaa jela za kijeshi za Israel, ambapo wengi wanaoshikiliwa kwenye jela hizo ni askari wanaotoroka jeshini.

    Kwa mujibu wa takwimu za jeshi la Israel, mwaka 2014 pekee, wanajeshi 1900 wa Kizayuni walitoroka jeshini na 2700 waliacha kazi.

    Hivi sasa utawala wa Kizayuni umedhamiria kuongeza adhabu kali kwa wale wanaotoroka jeshini.

    Jeshi la utawala huo limesema pia kuwa, hivi karibuni wanajeshi watatu wa Israel wal iokuwa wanafanya kazi katika idara mbalimbali za jeshi la utawala huo wamejiua.

    Kiwango cha wanajeshi wa I s rae l wanao j iua kwa mujibu wa jeshi lenyewe la utawala wa Kizayuni, kimeongezeka mara mbili mwaka 2014 huku kazi ya kuendesha j e l a n a k o r o k o r o n i z i n a z o w a s h i k i l i a

    wa n a j e s h i wa I s r a e l wa n a o t o r o k a j e s h i n i ikisababisha hasara kubwa kwa utawala huo wa Kizayuni.

    B a a d a y a I s r a e l kuushambulia kikatili Ukanda wa Gaza kwa muda wa siku 50, kiwango cha wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wanaojiua k i m e o n g e z e k a s a n a , suala ambalo limewatia wasiwasi viongozi wa Israel.

    A i d h a b a a d h i y a wa n a j e s h i wa I s r a e l waliasi amri za maafisa wao wa juu jeshini katika mashambulizi hayo ya siku 50, kiasi kwamba utawala wa Kizayuni ulilazimika kukimbiza wanajeshi wake kwenye mipaka ya Ukanda wa Gaza.

    I m e e l e z w a k u w a Wana jesh i wa I s rae l wanatumikishwa kwa nguvu jeshini na wengi wao wanachukizwa na siasa za

    kijeshi za kupenda kuua watu zinazoendekezwa na wanasiasa wa utawala huo.

    Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa, hatua ya Israel ya kuegemeza s i a s a z a k e k w e n y e matumizi ya nguvu za kijeshi na uvamizi, kuwa ni uthibitisho wa wazi wa muundo wa kigaidi wa utawala wa Kizayuni, muundo ambao daima u m e i w e k a k w e n y e wakati mgumu Israel na ambao umefanywa kuwa dondandugu na kensa iliyoopandikizwa katika

    kitovu cha ulimwengu wa Kiislamu.

    Kuongezeka wimbi la kukimbia jeshini wanajeshi wa Israel pamoja na kuasi amri za maafisa wa juu, ni tishio kwa jeshi la utawala huo.

    Itakumbukwa kuwa jeshi ndio msingi mkuu wa uwepo wa Israel.

    H a t a h i v y o i s h a r a zinaonyesha kuwa hali si nzuri kiasi kwamba utawala huo unalamizika kuwatumia wahal i fu kuziba pengo la askari wake wanaokimbia jeshini.

    BAADHI ya wanajeshi wa Israel.

  • 6 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 19-25, 2015Makala/Tangazo

    Mafundisho ya Quran

    Fethullah-Gulen

    NAKUMBUKA aliposema Bwana wako kuwaambia Malaika: Hakika mimi nitafanya katika ardhi K h a l i f a . Wa k a s e m a : Hivi utamfanya humo atakayeharibu humo, na atakayemwaga damu. [Al-Barah 30]

    Wa l i k u w a m a l a i k a wamejuwa mambo hayo k w a e l i m u m a a l u m u ambayo walipewa na hili linamaanisha kutokezea kwao kwa kipimo fulani juu ya ubao wa kufuta na kuthibitisha kwani katika elimu ya Mwenyezi Mungu, hapatikani kujuwa kwa mwanzo kisha kujuwa kwa mwisho wala kumjuwa mtoto wa tumboni kisha mtu aliyekamilika, wala electron kisha kokwa, na kadhalika, kwa sababu hiyo ni elimu ambayo inazunguka kila kitu katika kitambo hicho hicho.

    Kwa sababu hii, wakati tunaposema maudhui ya kuchukua ahadi na mkataba kwamba Mwenyezi Mungu alichukua ahadi na mkataba katika ulimwengu wa roho au katika mfuko wa uzazi wa mama, haya ni maneno yaliyo sahihi isipokuwa yamepungua na yana mpaka na huenda kungekuwa ni bora sana kusema: Hakika y e y e h a k u a c h a k u wa anaichukua ahadi kwa sababu ulimwengu wetu unabadilika kila wakati.

    Ama kwa upande wake Mwenyezi Mungu mtukufu, mabadiliko si yenye kuja katika haki yake. Na hakika ni kusema: Ifanyeni upya imani yenu kwa Laillaha I l la Al lah Hapana Mola apasaye kuabudiwa a s i y e k u wa M w e n y e z i Mungu. Hakuwezekani kulifahamu hilo isipokuwa wakati tutakapofahamu kuchukuliwa kwa ahadi na mkataba katika ujumla wa elimu yenye kuyazunguka yaliyokwishakuwa na yale yatakayokuwa, na yale yakuwa hivi sasa.

    Sasa ture jee kwenye maudhui yetu kwa mara nyingine:

    Wa l i k u w a m a l a i k a wametokezea katika ubao wa kufuta na kuthibitisha

    juu ya kwamba binadamu atafanya uharibifu katika ardhi na atazimwaga damu. Kwa sababu hiyo, waliuliza maulizo haya mfano wa vile tunavyosema, wakati t u n a p o w a k a b i l i w a t u waovu: Kwa nini ameumba Mwenyezi Mungu mifano ya watu hawa?

    Na inawezekana kwamba malaika hawakutokezea na hawakuizunguka elimu ya kutoka Manabi i na watu safi na wapenzi wa Mwenyezi Mungu (ambao wanahesabiwa na mbegu zao) wakatoka miongoni mwa watu na kwa sababu hiyo hivi hakusema Mwenyezi Mungu mtukufu kwa kuwajibu: Hakika mimi ninayajuwa sana yale ambayo hamyajui. [Al-Baqarah 30]

    H a k i k a m f a n o w a U k h a l i f a h u u a m b a o ameutoa Mwenyezi Mungu mtukufu kwa binadamu, kama ambavyo tunaweza kuuchukua juu ya msingi wa kwamba Mwenyezi Mungu mtukufu amempa binadamu haki ya kujiingiza kwa kiwango fulani na kwa kiasi fulani katika pande zote za ulimwengu na matukio, kunawezekana kuuchukua Ukhalifa huo vile vile na kuufasiri juu ya nafasi yake kat ika kuchaguliwa na kuathiri katika mahusiano kati ya watu na kati ya mataifa. Mfano wa hali hii ya kipekee na huku kupewa kwa upendeleo, kunamaanisha kumruhusu binadamu katika kufanya na kutenda katika kila kitu ambacho mkono wake unakifikia kwa niaba ya Mwenyezi Mungu na kwa jina lake na hali ya kuwa ni naibu wake. Itakuwa burashi yake na katika kukipaka maji ya dhahabu kitabu cha ulimwengu, na atakuwa mtumishi wa bustani katika bustani la mzunguko wa ardhi, na ni mfanyakazi chini ya maelekezo yake katika mambo yote ya dunia na raia yoyote au fikra yoyote kuhusu kwamba binadamu ni mwenye kumiliki au ni mwenyewe wa hakika wa kitu chochote, inahesabiwa ni kuvuka mpaka na ni ujinga.

    Kwa sababu hiyo, tunakuta kwamba Mwenyezi Mungu mtukufu anasema:

    Hakika mimi nitafanya badala ya kusema Hakika mimi nitaumba, maana ni kwamba yeye katika maudhui ya kuumba kwa kwanza alikishughulikia kitendo cha kuumba si kwa dhati yake, bali kwa upande wa sifa zake, kana kwamba kumfanya kuwa ni Khalifa ni ujenzi na muundaji wa daraja la pili, siyo la asili bali ni kwa niaba, kama mwangaliaji na msimamizi, maana ni kwamba yeye ameuweka kwake Ukhalifa huu si kama

    tabia ya kwanza katika kuumbwa kwake, bali ni kama sifa yenye kupatikana, mwa mtu ambaye anahakikisha katika nafsi yake masharti ya Ukhalifa katika ardhi. Ni jambo lenye uwezekano kwamba moja ya mambo yenye kupatikana nyuma ya kusimama Malaika kwa kuuliza au kwa usahihi zaidi kutaka kujuwa ni kuogopea kuchanganyika mambo yenye kufanywa kwa niaba na yale yenye kufanywa kwa asili. Jambo hili la kujifunza majina, na kile ambacho amefundishwa Adam (a.s.) kinahesabiwa kimo katika nafasi ya kokwa na kimo katika nafasi ya mbegu. Kama zilivyokuwa namna zote za damu na asili mbalimbali z i m e t u m b u k i a k a t i k a mgongo wake, kitakuwa kila ambacho amefundishwa ni kokwa na mbegu ya elimu

    zote na inakuwa kazi na jukumu la kuliendelea kokwa hilo na kulikuza na kulipanua limetupwa mabegani mwa vizazi vijavyo.

    K a m a a m b a v y o k u n a w e z e k a n a k u w a m a f u n d i s h o h a y o yalipatikana kwa wahyi ambao aliupeleka Mwenyezi Mungu kwa Mtume, vile vile kunawezekana kuwa kulipatikana kwa kutoa Mwenyezi Mungu mtukufu raghba ya kujifundisha katika maumbile yake na katika asili yake na kiini chake kwa ajili ya kuyafikia mahitaji yake na kwamba hii raghba na maandalizi ya kiutume ya haraka na makubwa kwa ajili ya kujifundisha ya l i m u o n g o z a k we n ye kujifundisha majina na vile vyenye kuitwa kwa majina hayo vile vile.

    Zaidi ya hapo jee, lilikuwa

    lengo la k i le ambacho alifundishwa Adam (as.) ni kufikia kwenye maarifa haya kwa njia ya lugha yoyote katika lugha? Au kulikuwa katika ujumla wa maangalizo juu ya njia yenye kufikisha kwenye majina na vile vyenye kuitwa kwa majina hayo na katika hayo ni kufika kwa mwenye kumiliki kila kitu? Au kwa kumfundisha mahusiano yaliyopo yaliyo wazi katika hayo na yaliyojificha katika ulimwengu wa vitu? Ni sawa sawa ulikuwa mkusanyiko wa maarifa ya ulimwengu? Au y a l i k u w a m a j i n a ya malaika au majina ya binadamu, na vitu vyenye kuitwa, na makadirio yao na hatma yao.

    (Imenukuliwa kutoka Kitabu: Miyangaza ya Quran katika mbingu ya hisia, cha Muhammad Fethullah Gullen kilichotafsiriwa kwa Kiswahili na Sheikh Suleiman Amran Kilemile)

  • 7 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 19-25, 2015Habari

    Elimisheni-TotonjiMsihangaishwe na propaganda

    WAISLAMU wametakiwa kujikita katika kusomesha na kuwavutia watu katika Uis lamu kutokana na maadili mema, ikiwemo kuwapenda, kuwaenzi na kuwatendea wema wake zao.

    A i d h a , wa m e t a k i wa w a s i h a n g a i s h w e n a propaganda za wenye chuki na Uislamu, bali wahangaike k u h a k i k i s h a k u w a mafundisho ya Uislamu yanasambaa na kuwafikia walimwengu wote.

    Hayo yameelezwa na Dr. Ahmad Totonji ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kongamano la kuukaribisha mwezi wa Ramadhani lililofanyika Jumapili ya wiki iliyopita.

    K o n g a m a n o h i l o lililoandaliwa na Jumuia ya Wanataaluma wa Kiislamu nchini ,TAMPRO, lilifanyika

    Na Mwandishi Wetu

    katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na Benki ya Kiislamu ya Amana.

    Mada Kuu ya Kongamano ilikuwa Ndoa Msingi wa Mafanikio.

    Dk. Totonji kutoka Saudia, ambaye al ikuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo, alisema kuwa ni jambo lililo wazi kwamba kuna chuki dhidi ya Uislamu na kwamba Uislamu unapigwa vita duniani kote.

    Lakini pamoja na hali hiyo, aliwaasa Waislamu k u t o p o t e z a n g u v u kupambana na propaganda zinazoelekezwa kwao, bali watumie fusa waliyo nayo kutoa elimu sahihi ya Uislamu na kuithibitisha kwa vitendo kuwa ndio Uislamu na sio hizo propaganda za wenye

    chuki kama wanavyozua.Msipoteze muda wenu

    kupambana na propaganda zao, kazi yenu iwe ni kutoa e l imu juu ya Uis lamu, wasiokuwa Waislamu wapate nafasi ya kuuelewa Uislamu kwa sheria na kanunia zake na kubaini ukweli. Alisema Dk. Totonji.

    Kwa upande mwingine Dr. Totonji aliwataka Waislamu kuimarisha ndoa na familia zao, ikianzia na mume kuhakikisha anampenda na kumuenzi mkewe.

    Akikazia umuhimu wa nukta hiyo, Dr. Totonji alisema kuwa mwanamume anapofunga ndoa, ajue kuwa wazazi wa binti wamempa mtoto wao wakitaraji kuwa

    atampa amani na furaha.Kwa hiyoni lazima mume

    ahakikishe kuwa mkewe anakuwa katika hali ya furaha na amani muda wote.

    Kat ika mazungumzo mengine nje ya kongamano hilo, Dr. Totonji aliwahi kusema kuwa, pamoja na kuwa mkewe sasa ni mtu mzima, lakini haipiti siku bila kumtamkia mara kadhaa kuwa anampenda-I Love Yo u . N a k u p e n d a m k e wangu.

    A l i s e m a , k a m a u s i p o m p e n d a m k e o , utampenda nani na utatimiza vipi malengo ya ndoa ambayo ni mawada na rehma iwapo huhakikishi kuwa mkeo ana furaha na amani muda wote.

    K w a h i v y o , k a t i k a kukabiliana na propaganda za wanaoupaka Uislamu matope, Waislamu waanze

    kuonyesha uzuri wa Uislamu kwa kuwa mfano bora katika k u wa p e n d a wa k e z a o , kuwapa furaha na amani na hivyo kujenga familia imara yenye furaha.

    Dr. Ahmed Totonji alisema kuwa, Uislamu unawaagiza Wais lamu kuwa kat ika kila kitu wanachokifanya wakifanye kwa uzuri na leo yao isiwe sawa na jana.

    Kwa maana kuwa kila siku wafanye vizuri zaidi katika mambo yao.

    Hii ikiwa na maana kuwa hata kat ika kuonyesha mapenzi kwa mke na kwa familia, mume awe mbunifu kuhakikisha kuwa furaha aliyokuwa nayo mkewe jana, haiwi sawa na ya leo au

    kesho.Kila siku anakuwa na

    furaha zaidi na mwenye kujisika amani zaidi.

    W a k a t i h u o h u o , M k u r u g e n z i M t e n d a j i wa Benki ya Amana Dk. Muhsin Masoud, amesema kumekuwa na mahita j i m a k u b wa ya h u d u m a zinazotolewa na Benki ya Amana kiasi kwamba sasa benki hiyo inaelemewa.

    A m e s e m a , B e n k i ya Amana inayoendeshwa kwa misingi ya sheria za Kiislamu, inazidi kukuwa kwa kasi huku huduma zake zikiwavutia wengi.

    Akizungumza kat ika k o n g a m a n o h i l o l a k u u k a r i b i s h a m w e z i mtukufu wa Ramadhani, Dk. Muhsin Masoud, alisema

    wanakusudia kufungua matawi mengi zaidi hivi karibuni ndani na nje ya nchi ili kukidhi mahitaji makubwa ya wateja wanaotaka huduma za Benki hiyo.

    Amesema, imekuwa ni ndoto ya Amana Benki kuwa bora kwa huduma zake zinazofuata Sharia na maadili, n a k wa m b a wa m e z i d i kujenga mahusiano mema na makundi yote kupitia huduma zao.

    Hivi sasa tawi letu la Tandamti l imeelemewa na wateja na inatulazimu kufungua jingine shule ya uhuru, alisema Mkurugenzi huyo.

    Dr. Maosud akaongeza kwa kusema kuwa kutokana na kuongezeka kwa kasi ya kuhitajika huduma za Benki hiyo, wanatarajia kufungua tawi nchini Uganda.

    Dk. Ahmad Totonji akiongea katika kongamano la kuukaribisha mwezi wa Ramadhan Juni 14, 2015.

    BAADHI ya washiriki wa kongamano la kuukaribisha Mwezi wa Ramadhan wakifuatilia mada kwa makini.

    SEHEMU ya washiriki akinamama katika kongamano la kukaribisha Ramadhan.

  • 8 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 19-25, 2015Makala

    WA S WA H I L I h u s e m a , atafutaye hachoki, akichoka k e s h a p a t a ! . S a d a k t a naukubali msemo huu. Lakini katika kutafuta kuna kupata na kukosa. Na ikiwa kuna kushindana, basi kuna kushinda na kushindwa. Vyovyote ilivyo, kushinda ni kupata, na kushindwa ni kukosa daima.

    Msemo huu ni maarufu sana baina ya Waswahili wa kwetu. Katika siasa za nchi hii umaarufu mkubwa wa msemo huo umezidi kunoga na kupata ladha baada ya chama cha Wananchi CUF kushindwa uchaguzi mara zote. Kushindwa huko, kukautumia usemi huu kuwa kama kipozeo na kiliwazo cha kushindwa!

    Chama cha CUF Zanzibar kilipoteza nafasi ya ushindi katika uchaguzi wa mwaka 1995, 2000, 2005 na 2010. Awamu zote hizo, mgombea pekee alikuwa Maalim Seif Shar i f Hamad ambaye hajapatwa kupingwa tangu muda huo. Kushindwa kuko, lakini kwa bahati mbaya CUF imekuwa ikikataa kabisa kabisa kuwa inashindwa kwenye chaguzi zote hizo. Badala yake, CUF hushikilia kutoa madai haya na yale na visingizio lukuki. Madai ambayo kwa muda wa miaka ishirini sasa, yameanza kukosa ladha. Miongoni mwa madai makuu ya CUF kupoteza uchaguzi ni kudai kuibiwa ushindi au kutopewa uraisi na chama tawala CCM.

    Madai ya CUF hapo awali yalikuwa yakiaminika. Lakini kwa vile kila siku maneno ni yale yale, sasa CUF hata wakisema nini, wanaonekana kama debe tupu tu. Haliachi makelele, ilhali halina kitu ndani. Na CUF kama CUF, ni mfano wa debe tupu, kingi maneno, vitendo hamna! Watashindaje uchaguzi?

    Mwaka 1995, tuseme kweli CUF ilidhulumiwa au tuseme kuibiwa kama tulivyozoea kuambiwa. Lakini mwizi huiba mara moja, akirudi tena kukuibia wewe, mahala pale pale, tena katika mazingira yale yale, ilhali unamuona na unamjua kama anakuja kukuibia , ukamwachia akaiba ukitegemea kuonewa huruma, huu ni uzembe usiostahamilika na ndio m a a n a s a s a w e n g i n e tunasema. Na ni uzembe wa aina hii unaoigharimu CUF kila siku na katika kila uchaguzi. Kuna mengi ya kuikosoa CUF juu ya hili, lakini tusiangalie kukosoana, tuwanie kuangalia wapi tunajikwaa na nini kilikuwa kifanywe ili wasijikwae tena.

    Nina taarifa kutoka kwa kada mmoja mkuu wa CCM (jina kapuni) akisema kwamba CCM Zanzibar hawazidi asilimia 35 ya watu wote au wapiga kura wote iwapo watu wataandikishwa bila ubaguzi, hata CCM ikiandikisha na mamluki, basi asilimia hii ndio kiwango chao chote.

    Kwa maana kama hii, ni wazi kuwa CUF ina wingi

    Kwa mwendu huu....

    CUF kuingia Ikulu, labda ngamia apenye kwenye tundu la sindano

    wa kura na wafuasi. Kauli hii pia inathibitishwa na viongozi wengine wa CCM akiwamo Bi Asha Bakari Makame. Bi Asha, amesema Gombani ya kale mbele ya kadam nasi (Umati wa watu). Akarudi akasema tena katika bunge la katiba kuwa ikiwa CUF walishindwa kutawala 1995 hawatawali tena milele nchi hii. Kauli ya Bi Asha haikuishia hapo, akasema na sababu ya kuwa CUF haitashinda pia pale alipodokeza kuwa, nchi hii tumepindua, hatutoi kwa karatasi! Haya si maneno ya Asha Bakari. Ni ahadi na kauli mbiu ya CCM kwa ujumla wake. Huo ndio msimamo wao. Na kwa hakika wanautekeleza kwa vitendo.

    N i l i p o s e m a C U F wanamalizwa na Uzembe wao, ni l isahau na vi tu v i n g i n e v i w i l i : K u j u a sana na Kujiamini sana kunakotokana na kulewa sifa. Vitu hivi vitatu ndio mizimu inayoisumbua CUF miaka yote na kupelekea kushindwa kat ika k i la uchaguzi ingawa wenyewe w a n a d a i w a m e k u w a wakishinda miaka yote hiyo lakini mwisho wa siku, mshindi ni yule atangazwae na Tume ya Uchaguzi (ZEC) na ikisha kuapishwa.

    Wakati CCM ikiponea chupu chupu uchaguzi wa 1995 na kujifunza kutokana na makosa, CUF ilitumia makosa yale yale kama njia yao ya kujipatia ushindi ka t ika chaguz i z i j azo . Kimaumbile, huwezi kutumia makosa kupatia ushindi wa jambo sahihi. Ni lazima urekebishe makosa yako. Makosa siku zote hukupa mwanga wa ulipojikwaa lakini hayakufikishi popote ukiyafuata.

    CUF imekuwa ikirudia makosa yale yale iliyoyafanya miaka ya nyuma. Makosa yenyewe sio mengi sana kwani miongoni mwa makosa hayo, ni mbinu wazitumiazo CCM kuwashinda CUF. CCM,

    haijatumia mbinu nyingi kuishinda CUF: Wembe wao ni ule ule wa ushindi kwani hawaoni haja ya kubadilisha wakati anyolewaye hajali atanyolewa vipi ndio maana miaka yote hawana mbinu mpya.

    K wa m a d a i ya C U F kwenye mikutano yao ya hadhara husema ,CCM hutumia wakati wa kuhesabu kura kuongeza zao. Wakikosa hapo, huficha visanduku vya kura kwa kutumia vyombo vya usalama na kufanya watakayo huko na mwisho hugeuza matokeo tu: CUF akapewa CCM na ya CCM yakarudi CUF. Siku hizi kumezuka utaratibu wa kuandikisha mamluki kutoka bara na kuongeza idadi ya wapiga kura watakaoibeba CCM. Hili liko wazi na linaonekana na kila mtu na ndio maana wenyewe CUF wamekuwa mstari wa mbele kulisemea. Lakini wapi, kazi bure maana kusema kwao ni sawa na kesha matongo us iku kucha unasoma, asubuhi huna kitu kichwani. Msemo huu unabeba maana licha ya CUF kupiga kelele kupitia Katibu Mkuu wake Maalim Seif pale hoteli ya Serena Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi, CCM wao wanaendeleza yao kama kawaida.

    M a k o s a m a k u b w a wayafanyayo CUF ukiacha yale ya uzembe wa viongozi wakuu wa chama, utayaona kwenye mawakala feki na wasimamizi feki wa chaguzi . Mara kadhaa, tunayaona ya mawakala wa CUF kununuliwa na kuachia visanduku vya kura vikiibiwa. Mara kadhaa, tumona mawakala wa CUF wakiambiwa wakapate chakula cha mchana, na wakiondoka mamluki wa CCM huingizwa wakapiga kura mara mia mia kila mmoja, wakirudi hamna kitu na ndio maana hadi leo hii, baadhi ya fomu za matokeo ya Urais uchaguzi mkuu 2010 dhidi ya mgombea wa

    chama hicho hazikuonekana hadi leo hii.

    Licha ya hayo sidhani kama CUF wamejifunza kitu. Kama ilivyokuwa haijajifunza kitu katika kuchaguwa wagombea wazur i wa Ubunge na Uwakilishi, bado ni yayo kwa yayo. Wanachaguana akina wale wale na kuacha watu ambao wananchi wenyewe wamewataka. Hapa mumelindana ingawa athari ya kulindana kwenu, haipo mbali mtaiona.

    Sidhani kama mliwahi k u f a n ya u t a f i t i d h i d i y a w a g o m b e a g a n i wanakubalika na wanachama wenu majimboni Unguja na Pemba na ndio maana sasa kumekuwa na mtafaruku m k u b w a m a j i m b o n i kutokana na wagombea mliowapelekea wananchi wenu ambao wenyewe hawakuwataka na ndio maana hawakuwachagua kwenye kura za maoni lakini wapi? Mwenye mkono mrefu ndio alae.

    Sijui mnajua kuwa hivi sasa kuna uthibitisho wa kutosha kuwa CCM imeandikisha m a m l u k i k a d h a a n a kuwanyima watu kadhaa haki ya kuandikishwa kupiga kura. CUF hili hawajaliona kuwa tishio kwao. Wana uhakika watashindwa kisha waje watwambie, tumeibiwa ilhali wameshindwa kwa idadi kubwa ya kura mamluki ambao wamepiga kura.

    Wakati CCM ikijiandaa kufa kupona, liwalo na liwe, lakini nchi hawatoi, CUF wanaandaa maandamano makubwa ya kumpongeza Maalim Seif. Sijambo baya lakini mnajua wenzenu CCM wakijifungia ndani w a k i p a n g a m i k a k a t i madhubuti ya kuwamaliza wazembe, walewa sifa na wenye kujiamini bila kuwa u b a v u wa k u j i a m i n i a k i k w e l i . T u m e o n a : wa m e o n g e z a m a j i m b o Unguja na kupunguza Pemba watakavyo. CUF wao wanapiga makofi kwa Maalim kurejesha fomu.

    Wakati CCM wakinadi kuwa hawatoi kwa kura; Viongozi wa juu wa CUF t u n a o w a a m i n i z a i d i , wanaongea maneno yasiyo nafasi hata ndogo kwenye siasa za CCM Zanzibar. Eti wanasema, Bakora ya kuwapiga CCM ni siasa za kistaarabu za CUF na eti, kashata kila ukiikata n d i o i n a z i d i u t a m u . N a d h a n i i k i m a a n i s h a kuwa ukatwaji wa majimbo na hilo likishangiliwa na wananchama waliofurika uwanjani. Kwa nderemo na vifijo wanashangilia wakiona wameambiwa jambo la maana!

    N i o n a v y o , C C M wanachokisema ni kweli kwa sababu kina ushahidi. Hawakutoa 95, 2000, 2005, na 2010. Nina uhakika, kwa viongozi kama hawa wa CUF tul ionao, CUF k u i n g i a m a d a r a k a n i Zanzibar ni sawa na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano. Tusidanganyane. Wa l a t u s i k u b a l i t e n a kudanganywa.

    Tus idanganyike kwa sababu, CUF hata baada ya kuona mambo yote yanayofanywa na CCM kuj ihakik ish ia ushindi wa kishindo ambao kwa hakika upo, bado s iku tu, hawajachukua hatua yoyote. Wao wanaona fahari kupokelewa kwa makundi ya wanachama wa CUF wasio na vitambulisho vya ukaazi wala vya wapiga kura, wakadanganyana kuwa watashinda uchaguzi.

    N a s e m a t e n a tusidanganywe, maadamu CUF ikiwa ndani ya Serikali imeshindwa kuleta ushawishi wa kuundwa Tume huru ya Uchaguzi licha ya ahadi ya Rais mteule kipindi kile Dkt. Shein pale Bwawani kuahidi hilo, hakuna liwalo. Tutaishia kumpokea Maalim Seif kurudisha fomu ya urais tu na kumpokea kifalme huku na kule. Kinachofanyika ni kuchezeana akili kwa kutujaza tamaa za kuku lala lala!

    Tusidanganyane, CUF haitashinda kwa sababu inajua inapojikwaa lakini inaendelea kupita hapo hapo kila siku. Kwa nini isibadili njia kuepuka kujikwaa tena? Itajikwaa tena na tena na mwisho, itaanguka chini. Na mwisho wenyewe hauko mbal i . Ni mwaka huu. Iwapo hawataacha uzembe, wakapunguza kulewa sifa, na wakaacha kuj iamini bila uhakika wa kupata ushindi, tujiandae tena kuwa wakimbizi wa kisiasa kama tulivyofanywa 1995 na 2001. Hakuna liwalo!

    CUF ni lazima mubadilike kwa sasa iwapo kweli muna nia ya kuongoza Zanzibar, v y e n g i n e v y o m s u b i r i kusindikiza wenzenu kwenye sherehe zao za kuapishwa pale uwanja wa Amani huku mkiwa na sare za chama chenu.

    (Imeandikwa na Mhamed Khamisi, University of Iringa (UoI))

    MAALIM Seif Sharif Hamad PROF. Ibrahim Lipumba. MUHAMMED Sanya (MB)

  • 9 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 19-25, 2015Makala

    KAMA Wazanzibar i wanakumbuka madhila w a l i y o p a t i s h w a n a uongozi wa Mheshimiwa B e n j a m i n W i l l i a m Mkapa, basi ni lazima pia jina la Frederick Tluway Sumaye lifuatane nae. Mzee Mkapa alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sumaye akiwa Waziri Mkuu wake ambaye ni msaidizi wake mkuu.

    Waziri Mkuu ni kiongozi mkubwa katika jamhuri ye t u . A n a m a m l a k a makubwa ya kumsaidia rais. Kutambuliwa kwake kama kiongozi mkubwa kupo Sehemu ya Tatu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977.

    Ibara ya 51 inaelezea k u w e p o k w a k e , k u p a t i k a n a k w a k e na uhai wake kushika wadhifa huu. Ibara ya 52, inayotiliwa nguvu na Sheria Na.15 ya mwaka 1984, inaelezea kazi na mamlaka yake.

    Waziri Mkuu ambaye h u t e u l i w a k u t o k a miongoni mwa wabunge wa kuchaguliwa kwenye majimbo, atakuwa na mamlaka ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku kwa siku wa kazi na shughuli za serikali (Kif. 1).

    K i f u n g u c h a ( 2 ) k i n a m t a j a k u w a n i Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni. Na kifungu cha (3) kinaeleza k a t i k a u t e k e l e z a j i madaraka yake, Waziri Mkuu atatekeleza au kusababisha utekelezaji wa jambo lolote au mambo yoyote ambayo Rais ataagiza yatekelezwe.

    Maana yake, makosa yoyote yanayotendeka kiserikali katika utekelezaji wa shughuli zake, yana mchango wa Waziri Mkuu. Kama Mheshimiwa Mzee Mkapa anakumbukwa kwa madhila ambayo ser ika l i a l iyoongoza iliwatendea wananchi, b a s i Wa z i r i M k u u hasalimiki . Anabakia s e h e m u m u h i m u ya kuasisi madhila hayo.

    N a h a p a n d i p o anapoguswa Sumaye k a t i k a ya l e m a b a ya w a l i y o t e n d e w a

    Sumaye amesahau mauwaji ya Wazanzibar mwaka 2001?

    Na Mwadili Ali

    WAZIRI Mkuu mstaafu Frederick Tluway Sumaye

    RAIS Mstaafu, Mzee Benjamin William Mkapa.

    Wa z a n z i b a r i k a t i k a Awamu ya Uongozi wa Mzee Mkapa Novemba 1995 hadi Oktoba 2005. Awamu hii ilitenda mengi ya kushangaza, mengi ya kushtua na mengi ya kuumiza Wazanzibari.

    Serikali ya Mkapa na Waziri Mkuu Sumaye ilijipatia sifa ya kuwa ya kwanza ambapo yalitokea mauaji ya raia. Zaidi ya watu 100 (ingawa serikali inasema watu 23 ndio walithibitishwa na Tume ya B r i g e d i a H a s h i m Mbita), waliuliwa kwa risasi za moto kwa kuwa wal i ingia barabarani kuandamana wakipinga uchafuzi wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2000. Waandamanaji walitii wito wa Chama cha Wananchi (CUF) ambacho kililenga kutoa malalamiko yake ya k u i b i wa k u r a n a kutangazwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa ndio kilishinda uchaguzi Zanzibar.

    Ni vigumu kuhalalisha na kusema kuwa adhabu ya mwananchi kupinga anachoamini ni dhulma, iwe ni kuuliwa kwa risasi. Lakini ukweli ni kuwa wal iul iwa wanawake kwa wanaume. Wengi walikimbia nchi yao. Kwa mara ya kwanza Jamhuri yetu ikazalisha wakimbizi, na kuandika historia mpya katika nchi ambayo ni maarufu kwa kuhifadhi raia wa nchi z inazoizunguka

    zilizovurugwa kwa vita.Haya ni mambo ambayo

    h u t o k e a k a t i k a n c h i ambazo ukandamizaji ndio staili ya uongozi na katu sio katika Tanzania yetu njema.

    Mzee Mkapa akiwa pia Mwenyekiti wa CCM, a l i u n d a k i l i c h o i t wa Baraza la Vyama vya S i a s a , k wa l e n g o l a kuunganisha kimawazo wakuu wa vyama vya siasa vilivyosajiliwa kwa mujibu wa sheria, hayo yakiwa yamekusudiwa kuwa mchango katika ujenzi wa demokrasia shirikishi.

    K w a m b a i n g a w a serikali inajumuisha tu viongozi wa chama kimoja kilichotangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu, lakini kwa Rais ambaye pia ndiye kiongozi wa chama kilichopo madarakani, kukaa na kujadiliana na wenyeviti na makatibu wakuu wa vyama vilivyo nje ya serikali, watapata fursa ya ku jadi l iana masuala yanayohusu mustakabali wa taifa.

    Kumbe kuunda baraza ilikuwa ni kiinimacho. Rais Mstaafu Mzee wetu Mkapa hakuwahi kuitisha hata mara moja kikao cha baraza. Viongozi w a v y a m a w a k a w a wanakutana na wenzao wa CCM bila ya Rais na kiongozi wa CCM kuwepo. Ina maana uongozi wa Mkapa, ambao na Sumaye alikuwa msaidizi mkuu,

    haikusimamisha uongozi shirikishi hata kwa njia ya kujadiliana na viongozi wa upinzani na kuchukua mawazo yao kwa ajili ya kusaidia kujenga nchi.

    Hawakufanya hivyo tangu awamu ya kwanza ya uongozi wao. Ndio maana haikushangaza waliporuhusu vyombo vya ulinzi na usalama kukabiliana na wananchi waandamanaji kwa risasi za moto na hatimaye kuleta mauaji ya raia, ambayo pia yalisababisha kuuliwa askari polisi mmoja kituo cha Wete mjini, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

    Sumaye mwenyewe anakumbukwa vizuri k w a k a u l i y a k e y a mwaka 1997 akiwa eneo la Pasua, Moshi mkoani Kilimanjaro aliposema mtu yeyote anayetaka kufanya shughuli zake za biashara au aina nyingine ya uzalishaji mali, bila ya kubughudhiwa na serikali, basi ashabikie CCM.

    Ilikuwa ni kauli mbaya kiutawala kwa sababu ilijenga msingi kuwa kuwa shabiki wa chama cha upinzani ni dhambi, mtu hatafikiriwa kwa jambo lolote la haki.

    N a k w e l i w e n y e nazo waliegemea CCM. Wakatwaa maeneo ya ardhi na viwanja vya wazi, ikiwemo kupora maeneo kutoka kwa wananchi na kuyaendeleza kwa miradi yao ya kiuchumi.

    M a e n e o m e n g i yalichukuliwa; na wale wal io j i t ia u jabar i na uanaume wa shoka kutaka kudhibiti kuporwa ardhi, waliishia kwa kuhujumiwa na makada wa CCM. Ni hapo waliibuka mafisadi wa ardhi ji jini Dar es Salaam na kwenye miji mingine mikoani.

    Ninamuweka Sumaye katika nukta ya kujiuliza anakuwa na ujasiri wa namna gani naye kujiona kuwa ni mwanasiasa a n a y e f a a k u p o k e wa Zanzibar na kufikiriwa kuungwa mkono katika mkakati wake wa kusaka

    urais wa Jamhuri ya Muungano. Lipi anaweza kulitaja linalompa ujasiri huo alilofanya wakati ak iwa Wazir i Mkuu, akiwa Mtanzania aliyekaa m u d a m r e f u z a i d i kwenye wadhifa huo mfululizo tangu jamhuri i l ipoanzishwa mwaka 1964.

    Nimetaja tu utawala bora na uongozi shirikishi kama nguzo muhimu ya katika kumpima mheshimiwa S u m a y e a n a p o f i k a Zanzibar, iwapo chama chao kitamteua kugombea urais kwa uchaguzi wa Oktoba 25. Ni katika uongozi wa wawili hawa, Watanzania walishuhudia serikali ikianzisha sera ya ubinafsishaji na kila kitu kikabinafsishwa.

    Hii ilikuwa sera ambayo Mwalimu Julius Nyerere aliipinga akisema kwamba i t a i f i k i s h a Ta n z a n i a kuuza mpaka magereza. Alisikitika kuona Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) i l iyoenea nchi nzima inabinafsishwa kwa bei poa.

    Nyumba za serikali z i l i u z w a k w a b e i isiyolingana na thamani ya jengo na ardhi lilipo jengo lenyewe. Baadhi ya nyumba walipewa mahawara na ndugu.

    Ni chini ya uongozi wa Mkapa na Sumaye Shirika la Ndege (ATC) lilibinafsishwa na haki ya njia karibu zote za safari kuuzwa kwa Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA). Ni pale msingi ya kuitupa ATC ilijengwa; na kweli kufikia sasa sijui kama lina hata ndege moja nzima ya kutegemewa zaidi ya kutengeneza hasara na kila mwaka.

    V i o n g o z i h a w a , w a l i j i t a h i d i m i a k a m i t a n o y a k w a n z a kujenga miundombinu ya kuchochea ukuaji wa uchumi, lakini, katika miaka mitano ya mwisho wakatumia muda mwingi kubuni na kutekeleza mipango ya kumiliki uchumi binafsi.

    N d i y o m a a n a mpaka leo Watanzania w a n a n u n g u n i k a yanayohusu mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira m k o a n i M b e ya , N e t Group kuingizwa Shirika

    Inaendelea Uk. 13

  • 10 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 19-25, 2015Makala

    MWAKA 1900, karibu asilimia 80 ya Wakristo wote duniani walikuwa w a n a i s h i U l a y a n a Amerika ya Kaskazini. Leo Ukristo umenyauka katika maeneo makubwa ya Ulaya, maskani yake ya jadi, na unainuka Amerika ya Kusini, Afrika na China. Zaidi ya asilimia 60 ya Wakristo duniani sasa wamekusanyika Marekani Kusini, Afrika na Asia. Sehemu ya Ulaya katika Wakristo duniani imeshuka hadi asilimia 26 takriban.

    Kuyeyuka kwa Ukristo katika ardhi yake ya asili barani Ulaya, kunaonekana katika kupungua kwa uzazi na kupungua kwa idadi ya walio Wakristo, k a t i k a k u p u n g u a uanachama wa makanisa na mahudhurio kanisani, kupungua kwa uwezo wa kupata vijana wanaoingia k a t i k a u t u m i s h i wa Kanisa, katika kuongezeka k wa k u p u n g u a k wa imani miongoni mwa Wakristo wa Ulaya, katika mabadiliko makubwa ya kanuni za maisha binafsi hasa kuhusiana na mapenzi, kudhibiti uzazi , kutoa mimba, ndoa na kuishi pamoja bila kuoana. Mfululizo wa tafiti za Eurobarometer t a n g u m w a k a 1 9 7 0 katika nchi muhimu tano (Ufaransa, Ujerumani, U b e l g i j i , U h o l a n z i , Italia) zinaonyesha kuwa mahudhurio kanisani kila wiki yameshuka kutoka kiasi cha asimilia 40 miongo mitatu au minne iliyopita hadi asilimia 15 leo. Nchini Ujerumani, kati ya mwaka 1965 na 1999, wastani wa wanaohudhuria kanisani ilipungua kutoka asilimia 75 hadi pungufu ya asilimia 30 na imeshuka hadi chini ya asilimia 15 leo. Mwaka 1851 takriban asilimia 60 ya watu wa England na Wales walihudhuria misa kanisan i . Hadi k u f i k i a m w i s h o wa karne ya 20, hesabu hiyo ilishuka hadi asilimia 10. Kwa mujibu wa Kanisa la Uingereza, Wakristo 80,000 walihudhuria misa Jumapili katika nchi hiyo mwaka 2013, wakiwa wamepungua kutoka 160,000 mwaka 1968. Takwimu za tafiti tofauti zinaonyesha kuongezeka kwa kupoteza imani miongoni mwa Wakristo katika maeneo kadhaa ya Ulaya. Karibu asilimia

    Ukristo umenyauka UlayaMaelfu wanakimbilia UislamuWengi ni wasomi, WanawakeKanisa la Venice lageuzwa Msikiti

    Na Profesa A. R. Momin yanafungwa, kuuzwa a u k u v u n j w a k i l a mwaka. Yako makanisa takriban 47, 000 nchini Uingereza na maelfu kati yake yamechakaa, hayatengenezeki tena. Ta n g u m w a k a 1 9 6 0 karibu makanisa 10,000 ya m e f u n g wa n c h i n i U i n g e r e z a . M e n g i yamegeuzwa kuwa makazi ya watu, maofisi au kuuzwa kutumiwa na Waislamu. Makanisa ya Methodist yalipungua kutoka 14,000 mwaka 1932 hadi 6,000 hivi sasa na kufungwa kiasi cha makanisa 100 kila mwaka. Kanisa la Huguenot la karne ya 18 mashariki ya London liligeuzwa nyumba ya ibada ya Methodist mwaka 1819, likawa sinagogi la Wayahudi kueleka mwisho wa karne ya 19 na msikiti mwaka 1976.

    Mwaka 2005, akieleza masiki t iko yake kwa kunyauka kwa makanisa Ulaya na Australia, Papa Benedict alisema "Hakuna tena ushahidi wa hitaji la kuwepo Mungu, na pungufu zaidi la Kristo. Yanayoitwa makanisa ya jadi yanaonekana kama yanakufa." Lord William wa Oystermouth, zamani Askofu Mkuu wa Canterbury (Makao Makuu ya Kanisa la Uingereza), alisema mwaka 2013 kuwa Uingereza siyo tena "taifa la waamini," akiongeza kuwa sasa ni nchi ya zama baada ya Ukristo. Na Kanisa la Uingereza limepoteza karibu wafuasi milioni mbili katika miaka miwili iliyopita. Kanisa la Uingereza limekuwa likinyauka katika miongo mitatu iliyopita. Uwiano wa wa-Anglikana nchini humo ulikuwa asilimia 40 mwaka 1983. Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni na NatCen, k i tuo cha utaf i t i wa mielekeo ya watu kijamii nchini humo, Kanisa la Uingereza limepoteza wafuasi karibu milioni mbili katika miaka miwili i l iyopita. Uwiano wa watu wanaojitambulisha kama wanachama wa Kanisa la Uingereza ilipungua kutoka asilimia 21 mwaka 2012 hadi asilimia 17 mwaka 2014. Aliyekuwa Askofu Mkuu wa Canterbury, Lord Carey, ameonya kuwa endapo hatua za haraka hazitachukuliwa, Kanisa Anglikana liko katika kizazi kimoja kabla ya

    The-Blue-Mosque-in-Istanbu.

    4 0 ya Wa f a r a n s a n a asilimia 34 ya wa-Sweden wanakanusha uwepo wa Mungu.

    Kupungua kwa kasi k wa u a n a c h a m a wa Kanisa na uhudhuriaji misa na ongezeko kubwa la gharama za kudumisha majengo ya makanisa vimesababisha kufungwa kwa maelfu ya makanisa ya K i p r o t e s t a n t i n a Kikatoliki yamebadilishwa

    kuwa migahawa, maduka, masoko-duka, majukwaa ya michezo ya kuigiza, mabenki, ofisi, maktaba, mandhari za kukutania na maeneo ya kuuza pombe. Idadi kubwa ya makanisa imeuzwa kwa Waislamu na ma-Sikh (Kalasinga), ambao wameyabadilisha kila mmoja kuwa mahali pake pa ibada. Kati ya mwaka 1990 na 2010, makanisa

    340 yalifungwa nchini Ujerumani, na kati yake 46 yalivunjiliwa mbali. Jijini Hamburg, kanisa moja la ki-Protestanti lilinunuliwa na jumuia ya Kiislamu ya eneo hilo. Inakisiwa kuwa kati ya (majengo ya) makanisa 45,000 nchini Ujerumani kiasi cha 15,000 hivi karibuni yataacha kutumika hivyo.

    N c h i n i U h o l a n z i , kiasi cha makanisa 60 Inaendelea Uk. 11

    Ukristo umenyauka Ulaya

    Kanisa la Venice

  • 11 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 19-25, 201511 AN-NUURMakalaInatoka Uk. 10 Ukristo umenyauka Ulayakuyeyuka. Kwa mujibu wa utafiti wa NatCen, karibu nusu (asilimia 49) ya Waingereza (watu milioni 24.7) walisema hawana imani yoyote ya kidini, ukilinganisha na asilimia 31 mwaka 1983.

    W a i s l a m u n c h i n i Uingereza

    Idadi ya Waislamu wote duniani inakisiwa kuwa takriban bilioni 1.85 hivi sasa. Kwa mujibu wa ripoti ya Pew Forum ya mwaka 2011, Ulaya ni maskani ya Waislamu miliioni 38, ambao ni zaidi ya asilimia 6 ya idadi ya watu. Nchi yenye Waislamu wengi zaidi barani Ulaya ni Ufaransa (mil ioni 6) , Ujerumani (milioni 4),. Uingereza (milioni 2.9) na Hispania (milioni 1.6). Idadi ya Waislamu katika Shirikisho la Russia ni za id i ya mi l ion i 20 . Uislamu unaenea kwa kasi ya kushangaza katika maeneo kadhaa barani Ulaya na Marekani.

    Uislamu sasa ndiyo dini inayoenea kwa haraka zaidi Uingereza. Sensa ya watu ya 2011 ilionyesha kuwa Uislamu ndiyo dini inayokua zaidi Uingereza na kukisia kuwa idadi ya Wa i s l a m u n c h i n i humo ni watu milioni 2.6 (asilimia 4.8 ya watu wote). Utafiti wa mwaka 2015 wa NatCen unaonyesha kuwa idadi ya Waislamu nchini Uingereza kuanzia mwaka 2012 hadi 2014 ilikua kwa takriban watu milioni moja, na kuwa Waislamu sasa ni asilimia 5 ya watu wa Uingereza.

    U t a f i t i wa m wa k a 2013 wa Faith Matters (Mambo ya Imani), jopo la wanazuoni wa dini tofauti, uliainisha kuwa idadi ya Waingereza walioingia katika imani ya Kiislamu inafikia 100,000 na wanaosilimu wapya 5,000 kila mwaka. Utafiti uliofanyika Chuo Kikuu cha Swansea ulionyesha kuwa katika miaka kumi i l iyopita, Waingereza 10 ,000 wal i j iunga na Uislamu, na robo tatu yao wakiwa wanawake. Kati ya Waingereza 5,200 waliojiunga na Uislamu mwaka 2010, zaidi ya nusu ni Wazungu na karibu asilimia 75 ni wanawake. Licha ya picha iliyoenea kila mahali kuwa Uislamu u n a w a k a n d a m i z a wa n a wa k e , r o b o ya wanawake waliosilimu walivutiwa na Uislamu

    kwa sababu wanadhani u n a wa p a wa n a wa k e heshima. Wazungu wa Ulaya ambao wamesilimu n i p a m o j a n a wa t u mashuhuri na wasomi, akiwemo Martin Lings (Abu Bakr Siraj ad-Din), mtunzaji wa zamani wa Maandishi ya Mashariki katika Makumbusho ya Uingereza, Yusuf Islam, mwimbaji wa zamani wa muziki wa pop Cat Stevens, Timothy J. Winter (Shaykh Abdal Hakim Murad) ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Oxford, Yahya Brit, mwana wa M k u r u g e n z i M k u u wa zamani wa Shirika la Habari la Uingereza ( B B C ) , J o e A h m a d Dobson, mwana wa waziri wa zamani Uingereza, Lauren Booth, shemejie Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair, Yvonne Ridley, mwandishi wa habari wa Uingereza ambaye alisilimu mwaka 2003 baada ya kutekwa na wapiganaji wa Taliban nchini Afghanistan. na Angela Collins Telles, mwanamke wa Marekani ambaye alisafiri kupitia M i s r i n a S y r i a n a alifurahishwa na ukarimu na upendo wa watu huko.

    Kanisa la Venice lageuzwa Msikiti kwa muda

    Tamasha la Venice la ki la miaka miwil i l i n a f a n y i k a k u a n z i a Mei 9 hadi Novemba 22 mwaka huu. Venice na maeneo yanayozunguka yana wakazi Waislamu wanaofikia 20,000, lakini haina msikiti. Kanisa la kihistoria la Katoliki, ambalo sasa halitumiki la Santa Maria del la M i s e c o r d i a ( K a n i s a

    la Mtakatifu Maria wa M a t e s o ) , l i l i g e u z wa kuwa msikiti kwa muda kwa matumizi ya watu wanaokuja katika tamasa la Venice pamoja na waumini wa eneo hilo. Ujenzi huo, pamoja na Qibla na jukwaa la muda, ulipangwa na kutekelezwa na Chritp Buchel, mchoraji wa K i s w i s i m we n ye asili ya Iceland. Msikiti ukawa ni moja ya maeneo yaliyotembelewa sana nje ya maeneo ya ndani katika tamasha. Wahusika wa hatua hiyo walidhani kuwa hiyo inaweza kuondoa his ia mbovu kuhusu Uislamu na Waislamu na kusaidia kujenga madaraja ya uelewano na kupatana kati ya watu wanaofika katika tamasha ambao hasa ni Wakristo na jumuia ya Kiislamu eneo hilo. Msikiti huo wa muda ulidhamiriwa kutumika kwa kipindi cha tamasha.

    Kuinuliwa kwa msikiti huo wa muda, kulisabisha kukerwa kwa uongozi wa serikali za mitaa, ambao walitoa amri ya kufungwa kwa msikiti huo kwa msingi kuwa kibali halisi hakikuwa kimetolewa cha kutumia kanisa kama mahali pa Waislamu kufanya ibada. Kilichosababisha hasa uamuzi wa serikali za mitaa ni chuki zenye mizizi ya kina na muonekano k u h u s u U i s l a m u n a Waislamu nchini Italy. Inatoa somo la jinsi baadhi ya mataifa yanavyofuta k u m b u k u m b u y a historia zao na urithi wa kitamaduni. Venice ya zama za umwinyi, ilipitia kipindi kirefu cha uelewano na urafiki kilichodumu takriban miaka elfu moja, kuanzia karne ya tisa hadi

    mwisho wa karneya 18, ya ulimwengu wa Kiislamu. Uwepo wa Venice katika eneo la katikati ya dunia ya M a s h a r i k i n a ya Magharibi na shughuli zake pevu za biashara, ziliupatia mji huo fursa zaidi. Nafasi ya maendeleo ya kiuchumi ya mji huo na utengamano wa jamhuri hiyo kisiasa, ulitegemea sana mahusiano ya nyanja kadhaa ya kibiashara na nchi za Kiislamu, hasa G r a n a d a , M o r o c c o , Misri, Syria, Anatolia na himaya ya Kiislamu ya Kituruki. Biashara na nchi za Kiislamu ilikuwa inaingiza zaidi ya nusu ya mapato ya mji huo. Venice ilikuwa inajulikana kama msambaza j i mkubwa wa bidhaa na viungo vya Mashariki. Ilikuwa inaagiza bidhaa tofauti za starehe kutoka nchi za Kiislamu ikiwa ni pamoja na hariri, vibadilishi rangi za nguo, viungo vya chakula, mafuta ya harufu nzuri , mazulia . vi to , pamba sukari, chachu, vioo na vyuma, ambayo baadaye viliuzwa kwa wateja barani Ulaya. Kwa upande mwingine, mji huo ulipeleka kwa nchi za Kiislamu aina mbalimbali za mali ghafi na bidhaa, ikiwa ni pamoja na mbao, vyuma (hasa dhahabu, fedha, bati, chuma na mercury), nailoni, sufi, mafuta ya mizeituni , matunda yaliyokaushwa, manyoya mazito na asali, ambazo zilitoka Italia kusini, Crete, Cyprus na sehemu nyingine za Ulaya.

    Kutoka karne ya 11 hadi ya 17, vioo na vifaa vya udongo zilizozalishwa katika nchi za Kiislamu ziliuzwa kwa wingi Venice, na kufikishwa katika

    maeneo mengine ya Ulaya. Vifaa vya chakula vya China vilifikishwa Ulaya kupitia Misri ya utawala wa Memluk . Mwaka 1442, sultani wa Misri alimpatia mwakilishi wa Venice Fransesco Foscari vipande 30 vya vifaa vya Kichina vya enzi ya Ming. Wachoraji wa Kiislamu na watengeza vifaa wa Misri na Syria kwa karne kadhaa walikuwa mahiri katika utaalamu wa vioo, mbinu na usanii wa kupendezesha majengo. Walifaulu hasa katika ubadilishaji wa muonekano wa vioo. Kwa karne nyingi usanii wa kutengeneza vioo katika dunia ya Kiislamu haukuwa na mshindani kokote barani Ulaya. Vioo vilivyobadilishwa n a k u r e m b w a vilivyotengenezwa Misri na Syria, vilianza kufika Venice katika karne ya 10, na mara vikaanza kushabikiwa na nyumba za kifalme za Ulaya. Wachoraj i wa Venice waligundua umuhimu w a b i d h a a z a v i o o vilivyorembwa na kuanza kunakili michoro hiyo na maudhui ya bidhaa za vioo za Kiislamu.

    M a l i g h a f i z a kutengeneza vioo, ikiwa ni pamoja na jivu-soda la hali ya juu, madini ya cobalt, chachu ya hali ya juu na vioo vilivyovunjika, vikaanza kuagizwa kutoka Mediterranean Mashariki. Punde utengenezaji wa vioo ukawa shughuli iliyopevuka na Venice i k a w a m a s k a n i y a utengenezaji vioo barani Ulaya.

    Nje ya Hispania na Italia kusini, Venice ndiyo jiji pekee katika Ulaya ambalo liliunda nyanja maridhawa na za moja kwa moja za mawasiliano - kupitia b iashara , mahusiano y a k i d i p l o m a s i a , kubadilishana zawadi n a m a z u n g u m z o ya kitamaduni - na dunia ya Kiislamu. Venice ilikuwa jiji pekee katika Ulaya ambalo lilikuwa linapokea mara kwa mara watu mashuhuri kutoka Misri ya Memluk na himaya ya Ottoman, na wajumbe wa tawala hizo. Wavenetia pia walijenga utamaduni wa kupeleka wafanyabiashara kwenda mashariki ya Mediterranean kujifunza Kiarabu, urari wa hesabu za biashara na mbinu za biashara. Kutokana n a k u j e n g e k a k w a mahusiano ya kibiashara,

    Inaendelea Uk. 13

    Lauren Booth, shemejiye Tonny Tony Blair.

  • 12 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 19-25, 201512 MAKALA

    Profesa Ibrahim Noor Shariff

    Propaganda za udini shuleni Tanzania-7

    Hitimisho-1

    K a m a t u l i v y o e l e z e a mwanzoni, Tanzania ni moja katika nchi nzuri duniani kwa ajili ya ardhi yake na hali ya hewa ilivyo na kwa utajiri wa maliasili iliyonayo. Watu wake wengi pia ni watu wazuri kitabia. Katika hali kama hii, inasikitisha kuona kuwa kuna jambo linaloiharibu Tanzania, nalo ni siasa chafu za baadhi ya wanasiasa. Siasa chafu hizi ni zile zenye kujenga chuki baina ya jamii ziliopo ama kwa misingi ya asili au ya udini. Nchi nyingi duniani zilizopaliliwa siasa za aina hiyo zimemalizikia wananchi kupigana vita wenyewe kwa wenyewe na kuuwana kikatil i kabisa na kuivuruga nchi yao vibaya sana.

    Katika nusu ya pili ya karne ya ishirini mauwaji ya kinyama ya kimbari Ta n z a n i a ya m e t o k e a Zanzibar 1964, na visiwa hivyo vimekula khasara kubwa sana ya kupoteza roho za watu wake na kufuatiliwa na wasomi na wajuzi wa kila aina pamoja na wafanya biashara -- watu wote hawa ndio rasilimali kubwa ya nchi yoyote -- kuihama nchi waipendayo na Zanzibar kufukarika pakubwa sana kwa kunyimwa utajiri wa wajuzi iliyokuwa nao. Tuombe yaliyotendwa Zanzibar yasirejelewe tena na yasitendeke Tanganyika p i a . L a k i n i i l i h i l i liepukwe, lazima mizizi ya fitina iondoshwe, na

    kuiondosha fitina, lazima wenye busara wakemee na kupigania ukweli na haki zitawale badala ya kutawaliwa na batili. Na ili haki itawale, lazima siasa chafu ziondoshwe kuanzia katika majukwaa ya siasa na ya dini hadi katika vitabu vya kusomeshea wanafunzi shuleni.

    Siasa chafu za udini zina khatari kubwa sana. Tumeelezea kwa ufupi vipi wenye siasa kali za udini wanapomsulubu Mwarabu kwa tuhuma zenye ukweli finyu na uwongo mwingi, kuwa lengo khasa si Mwarabu b a l i n i k u u s u l u b u U i s l a m u . K a m a tulivyozungumzia kwa mukhtasari pia, masomo ya taarikh shuleni nayo pia yamejaa nganu zenye ukweli finyu na uwongo mwingi unaotokana na propaganda za chuki. Nganu ya Waarabu na Waswahi l i Wais lamu ni wabaya na Wazungu Wakristo ni wema kwa Waafrika, s i s iasa ya kipropaganda tu, bali pia ni siasa iliyojaa khatari khasa inapojazwa katika bongo za watoto wadogo shuleni. Pia kusomesha kuwa Waafrika siku zote ndio wal ioonewa na kukamatwa na kutiwa utumwani na wasiokuwa Waafrika, na kuwa hakuna Waafrika walioshiriki k a t i k a u k a m a t a j i n a uuzaji wa wanyonge, na kama walikuwepo basi Waafrika hao walikuwa ni Waislamu, ni moja katika hizo nganu za kipaukwa pakawa.

    Dini yangu inaniambia k u w a d h a m b i z a mtu habebeshwi mtu m w i n g i n e . Wa a f r i k a wal io t iwa utumwani na hao wakamataji na wanunuzi wa watumwa wote hatunao tena. Hatuna haki ya kuwanyooshea v i d o l e v y a l a w a m a walioko leo wasiokhusika na ukamataji, uuzaji na umiliki wa watumwa. Walioyatenda hayo wote w a m e f a r i k i z a m a n i sana na hata mifupa yao imeshapotea. Unaweza ukamnyoshea k idole

    c h a k o c h a l a w a m a Mwarabu au Mswahili leo na kumtuhumu kuwa mababu zake waliwahi kuwa na watumwa na inaweza kutokea kwa s u d f a i k a wa k w e l i , l a k i n i k u m b e h u y o unayemnyooshea kidole cha lawama ni kitukuu cha suria wa Kiafrika. Jee Mwarabu huyu naye akikunyooshea wewe kidole chake cha lawama na kukwambia kuwa wakale wenu nyinyi Waafrika ndio mliomkamata bibi yake mkuu na kumwuza utumwani, utamjibu nini?

    Tunge l i sema kuwa n g a n u z a u t u m w a na picha za kuchora w a n a z o s o m e s h e w a wanafunzi Tanzania ni nganu za kuchekesha ingelikuwa lengo lake si kutia chuki katika bongo za vijana na kuwa na athari mbaya sana kwa wanafunzi maishani mwao. Chuki hizo huzaa chuki akilini mwa wanaosomeshwa. Lakini lengo ndilo hilohilo la kupanda na kupalilia hisia za chuki dhidi ya Waislamu.

    Y a l i y o k u w a y a m e k w e p w a , hayasomeshwi shuleni, n i s u r a k a m i l i y a u k h a b i t h i m k u b w a walioufanya Waafrika k a t i k a k u w a k a m a t a wanyonge wa Kiafrika wengineo na kuwauzia kwa wingi Wazungu Wakristo na kujiwekea w e n y e w e w a t u m w a wengine na wachache mno kuwauzia Waswahili na Waarabu. Hatuwezi tena kuuficha ukweli huu wakati wanahistoria wakweli wanatu-andikia na kutuelezea vitabuni na mitandaoni ukhabithi na idadi ya mamilioni ya Waafrika waliowaua na mamilioni waliowatia u t u m w a n i . K a m a tulivyotaja, katika Kongo p e k e ya k e Wa z u n g u Wakristo wamewauwa Waafrika wasiopungua milioni kumi, hivyo basi, waliyoyafanya Waarabu na Waswahili Waislamu n i f i n y u ya u k a t i l i walioufanya Wazungu Wakristo na askari wao wa

    Kizungu na wa Kiafrika. Iwapo kweli Wakristo wenye siasa kali za udini wa n a t a k a k u u e l e z e a ukweli kikamilifu, basi hawawezi kuwanyooshea k i d o l e c h a l a w a m a Waislamu peke yao na kuyaficha waliyoyafanya jamaa zao na waumini wa dini yao. Kufanya hivi kama walivyofanya katika vitabu vya kusomeshea historia Tanzania ni upeo wa unafiki.

    Tusisahau pia kuwa n i v i g u m u s a n a l e o kumjua nani ana wakale waliokuwa watumwa na nani hana kati ya Waislamu. Ukifuatilia haya kwa makini utastaajabu k u g u n d u a k u w a n i miongoni mwa tunaowaita Waarabu na Waswahili ambamo utawakuta pia vizazi vya masuria wa Kiafrika. Sasa, itakuwaje tuwaambie watu hao kuwa tunawalaumu kwa sababu babu zao waliwatia bibi zao wenyewe utumwani na hatimaye kuzaliwa wa o . N i t a t o a m f a n o mwingine. Kuna watu ambao wana madukuduku ya o m a p e v u j u u ya (Marehemu Mzee) Abedi Karume na (marehemu Mwalimu) Julius Nyerere kwa kusababisha vifo vya jamaa zao na adhabu walizoadhibiwa baadhi yao pamoja na jamaa zao. Abedi Karume na Nyerere ni Waafrika, kwa hivyo, jee, Waarabu na wengineo wana haki ya kuwalaumu Waafrika wote kwa sababu Waafrika Abedi Karume na Nyerere na majamadari wao walisababisha vifo vya jamaa zao na wengine kuadhibiwa na kufungwa bure? Au kisasi kilipiziwe w a j u k u u w a A b e d i Karume (ambao mama zao ni Waarabu) na pia watoto na wajukuu wa Nyerere? "Mchezo" huu mbaya wa kisiasa wa kunyoosheana vidole vya lawama kwa ajili ya vitendo vya wakale wetu ni mchezo ambao mwisho wake pia, bila ya shaka, ni mbaya sana. Kama tunavyoelewa, mwenye kuwanyooshea wenziwe kidole chake kimoja cha lawama, vinne

    humwelekea mwen-yewe.Ni kweli kabisa kuwa

    mtu yoyote ana haki ya kumlalamikia yule a l iyemtia utumwani . Lakini Mwafrika wa leo aliyekuwa si mtumwa hana haki ya kumlalamikia Mwarabu wala Mswahili wa leo aliyekuwa hana mtumwa wala wakale w a k e h a w a k u m i l i k i watumwa. Dhambi za mtu habebeshwi mtu mwingine.

    J a m b o l i n a l o n i s t a a j a b i s h a sana ni kuona Waarabu na Waswahi l i , kama ni ishara ya Uislamu, wanavyohujumiwa vikali sana kupindukia kiasi na wale wenye kuendeleza propaganda za udini na chuki kukhusu utumwa wa Wa a f r i k a ; j a m b o ambalo wachache mno miongoni mwa Waarabu na Waswahili walishiriki. Propaganda zina khatari hata ya kuulisha bure watu wasiokhusika zikiachiliwa ziendelee kutapakazwa k a t i k a m a j u k w a a ya s iasa na shuleni . Tu s i j e t u k a s t a a j a b u kure je lewa maafa ya mauwaj i ya kinyama kama ya l ivyokwisha kutokea Pwani ya Afrika Mashariki katika karne ya 16 na January 1964. Pia, kama tulivyokariri, khatari kubwa zaidi ya vita vya udini huenda vikawakumba Watanzania we n g i i wa p o we n ye kutapakaza propaganda za udini hawatazuiliwa.

    Lakini, safari hii, maafa yatakapoanza, kutakuwa na tafauti kubwa. Kwanza, m a s h a m b u l i o h a y o hayatakuwa Zanzibar p e k e y a k e . B i l a y a shaka yoyote wataingia walioko Tanganyika pia. Wakiuliwa Waislamu, na haya yameshaanza, jua kuwa hautapita muda na Wakrito pia watauliwa. Wakichoma mis ik i t i , jua kuwa na makanisa pia yatachomwa moto. Pakiuliwa majirani wa Kiislamu, jua na majirani Wakristo hawatasalimika. Jee, hao wenye siasa kali za udini huko ndiko wanakotaka kuipeleka Tanzania?

  • 13 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 19-25, 2015MAKALAInatoka Uk. 11k i d i p l o m a s i a n a kitamaduni kati ya Venice na dunia ya Kiislamu, wachoraji na watengeza vifaa wa Kiislamu kutoka Misri na Syria mwanzoni mwa karne ya 14, walianza kutengeneza vifaa vya kuchonga na vya starehe vinavyoendana na ladha za Ulaya. Wafanyabiashara wa Venice wakaanza k u a g i z a v i f a a v y a starehe Misri na Syria vilivyotengenezwa kwa mpangilio maalum aliotoa mteja. Vifaa vya chuma vilivyotolewa maagizo vikitengenezwa na nchi za Kiislamu na kuagizwa na wafanyabiashara wa Venice vikawa na wateja wengi Ulaya katika karne ya 15 na 16 kiasi cha kupewa jina la Venetia-Saracenic.

    M a z u l i a y a l i y o t e n g e n e z w a C a i r o , D a m a s c u s n a Anatolia na kuagizwa na wafanyabiashara wa Venice yalikuwa yanapendwa sana Ulaya. Makanisa na taasisi nyingine za dini z i k a c h u k u a m a z u l i a ya mashariki, ambayo yalitumika kufunika meza kubwa ambako mikutano ilikuwa inafanyika. Hazina ya Kanisa la Mtakatifu Marko la Venice ina vifaa vingi vya Kiislamu vyenye thamani kubwa, ikiwa ni pamoja na zulia la karne ya 16 ambalo lilitolewa kama zawadi na mfalme wa Uajemi, Shah Abbas I kwa maelekezo kuwa litumike kwa kupangilia vifaa vya ibada katika kanisa hilo wakati wa misa.

    Utamaduni wa uwazi wa Venice na ushabiki w a k e w a d u n i a y a Kiislamu vinaonekana kwa dhati katika minara ya ubunifu wa ujenzi ya jiji hilo ambayo inaonyesha uvuvio wa staili za Italia, Ulaya ya zama za kati, Uislamu na zama mpya za Ulaya. Minara ya ubunifu majengo ya Venice, kama Kanisa la Mtakatifu Marko, kasri ya Doge, Palazzo Ducale, mnara wa saa (Torre dell'Orologia) na Kanisa la Mtakatifu Petro Casletto, yana madirisha ya fani ya ubunifu wa K i i s l a m u , v i m a l i z i o n a m a e n e o m a p a n a ya pembeni. Ubunifu majengo wa Venice kwa sehemu kubwa ulichukua ubunifu wa mashariki na dhima yake, ikiwa ni pamoja na upendezeshaji kwa rangi na utumiaji wa vito.

    Kuelekea miaka ya katikati ya karne ya 15, mabadiliko makubwa y a m a j u k u m u k a t i ya watengeza vioo wa Venice na wenzao katika

    Ukristo umenyauka Ulaya

    dunia ya Kiislamu ilianza kuonekana. Wakati fani ya utengenezaji vioo nchini

    Kanisa Torre_dell'orologio_(Venezia)

    Misri na Syria ilianza kupauka, wabunifu na watengenezaji wa Venice

    wa l i p a t a m a e n d e l e o makubwa katika mbinu na mapambo ya vioo. Katika

    karne ya 15, viwanda vya vioo vilijengwa huko Murano. Katika kipindi cha miongo michache Venice ilichukua nafasi ya Cairo na Damascus kama kituo muhimu cha kutengeneza vioo duniani . Kat ika karne ya 16, vifaa vya vioo vya Venice vilianza kuuzwa maeneo tofauti ya Ulaya na pia Misri, Syria na himaya ya Ottoman. Watengenezaji wa vioo wa Venice walichukua mifumo na michoro ya watangulizi hao kwa ajili ya mahitaji ya wateja wao wa soko la nje.

    Wa-Venice wal i fua sarafu za dhahabu mwaka 1284 - labda ndiyo sarafu za kwanza za dhahabu Ulaya - zikiitwa Zecchino, neno linalotokana na Kiarabu, kwa ajili ya biashara na nchi za Kiislamu. Sarafu za aina hii zinaweza kuonekana hata kusini ya Ufaransa hadi mwisho wa karne ya 13. Sarafu hizi za dhahabu zilikuwa na michoro ya Kiislamu na tarehe inayoendana na kalenda ya Kiislamu.

    Katika karne ya 15, Venice i l ikuwa ndiyo maskani ya kuchapisha vitabu barani Ulaya. Tafsiri ya Kilatini ya jumlisho la kazi za Aristotle pamoja na Averroes zilichapishwa Venice maka 1483. Hii i l i f u a t i wa n a t a f s i r i ya Kilatini ya kazi za Avicenna na Alfarabius. Kazi muhimu ya Avicenna ya Al Qanun (Kanuni) i l ichapishwa kwanza kwa tafsiri ya Kilatini jijini Venice mwaka 1595, ambayo ilikuwa ndiyo rejeo muhimu kwa elimu ya tiba katika Vyuo Vikuu kadhaa vya Ulaya hadi karne ya 18.

    ( I m e a n d i k w a n a Profesa A. R. Momin n a k u t a f s i r i wa k wa Kiswahili na Anil Kija)

    Sumaye amesahau mauwaji ya Wazanzibar mwaka 2001?Inatoka Uk. 9l a Umeme (TANESCO) kwa mabavu, na miradi ya Meremeta, Green Finance, Tangold na Mwananchi Goldmine.

    Yot e i l i k u wa mi ra d i iliyobuniwa kwa mtizamo wa kuwa njia ya kuingiza fedha nyingi mifukoni mwa watu na makampuni binafsi hasa inapotajwa kuwa baadhi ya viongozi walihusika katika kuanzisha kampuni iliyomiliki huo mgodi wa makaa ya mawe na wengine wakatajwa katika kashfa ya

    kutwaliwa kwa majengo ya kiwanda cha uchapishaji cha Printpak.

    Kama serikali ya Rais Jakaya Kikwete inalalamikiwa kwa rushwa na ufisadi serikalini, basi mimi, naona misingi yake hasa ilijengwa katika kipindi kilichomtangulia. Alirithi matatizo makubwa ya rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma. Watendaji walionufaika kifisadi na utawala wa wawili hao kabla yake Rais Kikwete, wakaendelea kuchuma mali kupitia nafasi zao.

    Kesi nyingi za ufisadi

    z i l i z o k o m a h a k a m a n i , zikitajwatajwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), m i z i z i ya k u z a l i s h wa kwake ilitokana na uongozi u l i o m t a n g u l i a . K u l e kuimarisha TAKUKURU kwa kuipa mamlaka fulanifulani ilikuwa kiinimacho.

    Wa z a n z i b a r i , k a m a ambavyo hawajapata jambo kwa Bernard Membe na Samuel Sitta, wasijisumbue k a b i s a k w a S u m a y e . Waangal ie kwa macho meupe ni nani katika CCM anayewafaa kama wale

    wenye uzoefu wa uongozi wanaongoza kwa utawala mbaya, ufisadi na chuki dhidi ya maslahi ya Zanzibar katika Muungano.

    Uchaguzi kwao ni serikali mbadala ya Umoja wa Kitaifa ambayo kilichobaki ni kuruhusu ishikwe kikamilifu na CUF kwa kumuingiza Ikulu Maalim Seif Shariff Hamad. Hapo watapata viongozi wenye moyo ambao wamejifunza vya kutosha utatuzi wa matatizo ya msingi yanayosibu Wazanzibari na nchi yao.

  • 14 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 19-25, 2015Makala

    Na Ben Rijal

    Na Ben Rijal

    Fatilia kuandama kwa Mwezi

    UWANJA WA VIJANA - JIONGEZEE MAARIFAMajibu CHEMSHA BONGO namba 10

    1. Taja Sura inayoelezea mwezi wa Ramadhani. Jawabu:Baqara

    2. Vita gani Waislamu walipigana katika mwezi wa Ramadhan. Jawabu: Badri.

    3. Ratio baina ya Waislamu na Makafiri katika vita vya mwanzo waliopigana Waislamu ilikuwa 1:3, 1:6, 2:9. Jawabu: 1:3

    4. Sala gani inayosaliwa katika mwezi wa Ramadhani tu. Jawabu:Tarawehe

    5. Katika mwezi wa Ramadhan kuna milo miwili inatakiwa kuliwa moja jua linapokuchwa na mwengine kabla ya kuingia alfajiri, milo hio ni :, Jawabu: Futari na Daku

    6. Ramadhani una usiku mtukufu unaitwaje? Jawabu: Laylatul Qadr.

    7. Mwezi wa Hijra huandama biana ya na Jawabu: 29 na 30

    8. Kufunga kwa mwezi wa Ramadhan kulifaradhishwa katika mji gani? Jawabu: Makka

    9. Asio balighi ana wajibika kufunga? Ndio au Hapana. Jawabu: Hapana

    10. Ramadhani humtakasa mja .. Jawabu: Kiroho.

    Leo Ijumaa ni tarehe 2 Ramadhani 1436 AH sawa na tarehe 19 Juni 2015.

    Julai 17 mwezi wa Mfungo Mosi utaandama. Kutokea leo hadi Mfungo Mosi tumebakisha siku 28

    B A D R U 1:3 A S D 3 1 F

    A 2 9 O I 3 0 R D 3 0 C

    Q E A O E U P S F Y Z V

    A F N K I R O H O U C B

    R G H A P A N A T I B N A N D I O A A F U O I M

    L A Y L A T U L Q A D R 2:9 N T A R A W E H E P H

    M A K K A S M A D I N A

    F U T A R I N A D A K U

    MASUALA1. Vita vya Badr vilipiganwa mwaka gani wa

    Kiislamu?2. Khalifa wa 3 Syd Uthman bin Affan aliuwawa

    akiwa na umri wa miaka mingapi? 82, 79, 90.3. Baada ya Msikiti wa Makka na Madinah, Msikiti

    gani mwengine mtukufu?4. Mali iliopitia mwaka Muislamu anatakiwa atoe

    kima kipi kama ni Zakka? 1%, 2.5%, 5%.5. Katika Kalenda ya Hijra kuna siku ngapi?6. Kilomita moja ina Milimita ngapi? Milioni 1,

    Milioni 10, Milioni 257. Mto Euphrates na Tigris umehusishwa na

    ustaarabu upi?8. Vita vikuu vya pili vilianza mwaka gani? 9. Mtu gani aliotamka kuwa Mwanadamu ni

    Mnyama wa Siasa (Political animal), Plato, Hagel, Aristotle.

    10. Gazeti la mwanzo duniani lilianzishwa nchi gani? China, USA, England

    Jee Unajua?1. Maji yaliokuwa

    s io sa lama yanauwa watoto wafikao 200 kila saa duniani kote.

    2. T a k w i m u z i n a o n y e s h a k u w a wanawake wanakuwa na umri mrefu kuliko wanaume, wastani wa umri wenye kikomo kwa wanawake ni miaka 69 na kwa wanaume ni miaka 64.

    3. China ndio nchi yenye idadi kubwa ya watu, ikifwatiwa na India. China ina idaidi ya watu

    CHEMSHA BONGO NAMBA: 11Weka duara kwenye jawabulio sawa. Jawabu kamili wiki ijayo.

    M E S O P O T A M I A Z C B N M L H M Z A K 82 A S D C H I N A G 1939

    90 M A D I N A A G H 2AH

    M A F A N I K I O S 1945

    M I L I O N I 1 V 6AH

    A R I S T O T L E J 354 A S D F G H M N O K 360 2.5% S P U I O J F N L 5%

    B A Y T M U Q A D A S

    yaliozikwa kwenye ardhi huchukua roho za watu 24,000 kila mwaka.

    6. Nchi moja peke yake duniani isiokuwa na jeshi wala matumizi ya kijeshi nchi hio ni Iceland.

    7. M a b a r a y a Asia na Paci f ic ndio yanaongoza kwa utapio mlo ikiwa na idadi ifikiayo watu