annuur 1139aa

16
ISSN 0856 - 3861 Na. 1139 SHAWWAL, IJUMAA , AGOSTI 22-28, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz Muhongo awarushia Waislamu makombo Na hiyo kwa shingo upande baada ya kulalamika Udini huu kama wa polisi Ferguson utaleta balaa Itabidi kulazimisha ‘Sospeter’ wajue Waislam wapo NECTA watuhumiwa kuleta Utanganyika katika mitihani Wabagua Zanzibar katika kanuni zake Ni kinyume na ‘matakwa’ ya muungano Waislamu walalamika kwa Kawambwa Wataka matokeo kidato cha 6 yatenguliwe Dkt. Charles Msonde, Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani Tanzania. WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. Trayvon Martin. Michael Brown. Mansour afungulia mlango wanyonge juu ya dhamana Kumbe hakuna kosa lisilo na dhamana Hata Uamsho ingetumika kanuni hii pia Mtume(saw) amesema, “Kutoa katika Hijja ni sawa na kutoa katika Jihadi, …”. Uwezo wa baadhi yetu ni uwezo wetu. Waislamu ni kama jengo au kiwiliwili kimoja. Tupelekane Hijja na tusaidiane kuisimamisha nguzo ya Hijja! Kadiri tutavyokwenda wengi Hijja, ndivyo na Allah Atavyotupa utukufu na nguvu nchini mwetu. Karibuni Ahlu Sunna wal Jamaa kwa mipango mizuri na huduma bora. Gharama zote ni Dola 4,500. Tafadhali wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0655/0765/0682/0777 - 462022; Zanzibar: 07 77468018/0685366141/0657606708. (15) MATAJIRI WA KIISLAMU!

Upload: zanzibariyetu

Post on 22-Nov-2015

990 views

Category:

Documents


22 download

TRANSCRIPT

  • ISSN 0856 - 3861 Na. 1139 SHAWWAL, IJUMAA , AGOSTI 22-28, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

    Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz

    Muhongo awarushia Waislamu makombo

    Na hiyo kwa shingo upande baada ya kulalamikaUdini huu kama wa polisi Ferguson utaleta balaaItabidi kulazimisha Sospeter wajue Waislam wapo

    NECTA watuhumiwa kuletaUtanganyika katika mitihani

    Wabagua Zanzibar katika kanuni zakeNi kinyume na matakwa ya muunganoWaislamu walalamika kwa KawambwaWataka matokeo kidato cha 6 yatenguliwe

    Dkt. Charles Msonde, Katibu

    Mtendaji Baraza la Mitihani Tanzania.

    WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

    Trayvon Martin.Michael Brown.

    Mansour afungulia mlangowanyonge juu ya dhamana

    Kumbe hakuna kosa lisilo na dhamanaHata Uamsho ingetumika kanuni hii pia

    Mtume(saw) amesema, Kutoa katika Hijja ni sawa na kutoa katika Jihadi, . Uwezo wa baadhi yetu ni uwezo wetu. Waislamu ni kama jengo au kiwiliwili kimoja. Tupelekane Hijja na tusaidiane kuisimamisha nguzo ya Hijja! Kadiri tutavyokwenda wengi Hijja, ndivyo na Allah Atavyotupa utukufu na nguvu nchini mwetu. Karibuni Ahlu Sunna wal Jamaa kwa mipango mizuri na huduma bora. Gharama zote ni Dola 4,500. Tafadhali wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0655/0765/0682/0777 - 462022; Zanzibar: 0777468018/0685366141/0657606708.

    (15) MATAJIRI WA KIISLAMU!

  • 2 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014AN-NUUR

    S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.

    www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected] zetu zipo: Manzese Tip Top

    Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

    Tahariri/Habari

    I L I k u o n y e s h a mshikamano na familia ya Brown, kijana aliyepigwa risasi na kuuwawa na polisi kule Fegurson, Missouri, Sybrina D. Fulton, mama Trayvon Martin, kijana mwingine aliyeuliwa kwa mtindo huo mwaka juzi, aliandika barua ya mkono wa pole na katika kuhitimisha akasema:

    If They Refuse to Hear Us, We Will Make Them Feel Us.

    Hapana shaka ujumbe huu umeelekezwa kwa serikali ya Marekani na vyombo vyake vya Dola na Sheria.

    Katika kutoa ujumbe huo Sybr ina a l i sema kuwa asidhaniwe kuwa analeta uchochezi, lakini anachotaka ni mamlaka husika zizingatie kuwa masaibu yanayowakuta Wa m a r e k a n i We u s i ya kubaguliwa na uhai wa o k u t o t h a m i n i wa , hayakubaliki na hakuna binadamu anayeweza kuyavumilia.

    Kwamba wadhulumiwa na wenye kubaguliwa h a w a w e z i k u k a a t u wakaridhia kuona vitendo v ya k u wa h u j u m u n a kuwanyanyasa vikijirejea mara kwa mara. Akawataka hao wanaoona raha kuuwa watoto wa wenzao halafu wasichukuliwe hatua za kisheria, wafikirie lau ingekuwa ni watoto wao wangejisikiaje.

    Ni katika hali kama hiyo, tunamuuliza Waziri wetu wa Nishati na Madini, kama ingekuwa vijana wote waliochaguliwa kwenda kusoma China wangekuwa Wa i s l a m u w a t u p u , angejisikiaje. Kama nafsi na dhamira yake kama Mkristo inamwonyesha kuwa jambo hilo halifai kufanyiwa Wakristo, kwa nini yeye aliona ni sawa kuchagua vijana wote 10 Wakristo kwenda kusomea utaalamu wa mafuta na

    Watu wasilazimishwekuonyesha kuwa wapo

    Pasipo haki, uadilifu amani haidumugesi!

    Na kwa maana hiyo hiyo, kila aliyepo katika madaraka fulani ya kufanya maamuzi serikalini na katika taasisi za umma, ajiulize, kama inatokea mtu mwingine akatumia madaraka yake kuchagua watu wa dini yake na kuacha wengine kabisa, yeye angejisikiaje.

    J a p o ya we z a k u wa vigumu kujenga hisia hiyo sasa kwa sababu hali halisi imekuwa ya upande mmoja kufaidi kwa muda mrefu, lakini ukweli ni kuwa hakuna anayeridhia hali kama hiyo. Ndio maana Mzee Mtei alikuja juu sana i l ipoteuliwa Tume ya Jaji Warioba, ambapo wajumbe wa Bara wakijumuishwa na wale wa Zanzibar, ilionekana kuwa Waislamu ni wengi. Ile kuwa Mwenyekiti na Makamo wake walikuwa Wakristo, haikuwa na uzito kwa Mzee Mtei. La muhimu aliangalia idadi ya watu wote.

    Hoja ya Mtei ilikuwa k w a m b a j a p o n c h i h i i t u n a s e m a k u w a haiongozwi kwa misingi ya dini, lakini huwezi kukwepa ukweli kwamba dini ina mchango mkubwa katika kuelekeza maamuzi na utendaji wa watu.

    Na wanapokuwa wa dini moja mahali, hapana shaka kile kinachowaunganisha, dini, kitafanya kazi kuliko kabila zao na mambo mengine. Ndio haya ya Wizarani kwa Waziri wetu Muhongo.

    K a m a a l i v y o tahadharisha Bi Sybrina, hebu watu wasilazimishwe kuonyesha kuwa wapo.

    S o t e t u n a t a k a n a tunapigania nchi hii idumu katika amani. Na amani haiwezi kudumu pasipo haki.

    LEO ni harambee ya kukusanya vifaa vya ukarabati wa Shule ya Kiislamu ya Mivumoni iliyoteketea kwa moto mapema wiki iliyopita.

    K i l a M u i s l a m u ametakiwa kufika siku ya Ijumaa (leo) kuswali Msikitini hapo akiwa na kifaa chochote cha ujenzi kulingana na uwezi wake.

    H a r a m b e e h i y o imetangazwa na Imamu wa Msikiti huo Sheikh S u l e i m a n A b d a l l a h , akiongea na Waislamu waliofika Msikiti hapo kwa ajili ya ibada ya swala ya Ijumaa na kujionea athari ya moto uliowaka Msikitini

    Harambee Mtambani leoNa Bakari Mwakangwale hapo.Tunawaita Waislamu

    siku ya Ijumaa (leo) katika kheri unahitajika masaada wa hali na mali, ikiwa una vitabu, Kompyuta, smenti, Nondo, Mbao, Misumari, waya za umeme, swichi au pesa wewe lete, toa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya kurudisha huduma haraka kwa vijana ili waendelee kusoma, h a t u t a r a j i i k u s i t i s h a masomo wakati Waislamu mpo. Alisema Imamu Suleiman.

    I m a m u S u l e i m a n i , alisema gharama za vifaa zinakadiriwa kuwa ni kiasi cha 6m/-, kwa ajili ya vifaa kutokana na athari ya moto huo ulioteketeza sehemu yote ya Shule, iliyopo

    ghorofaya pili.Mpaka sasa uongozi

    wa Msikiti huo umesema, tayari walianza kupokea misaada siku ya pili tu baada ya janga la moto, kutoka kwa Waislamu, Misikit i , viongozi wa Kisiasa na watu binafsi kutoka Serikalini.

    Miongoni mwa Misikiti hiyo ni Masjidi Veteran-Ihsan, wametoa 1.32m/-, Msikiti wa Kigogo (Shia), 1m/-, kwa upande wa vyama wamepokea kiasi cha Tsh. 5,000,000/- kutoka Chadema, ACD wao wametoa mifuko 20, ya saruji pia Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani (NECTA) Dkt. Charles Msonde, amechangia 5,000,000/-, pamoja na kiongozi mmoja kutoka TAMISEMI, katoa 5,000, 000/-.

    KITUO cha Ki tuo cha Kiislamu cha kimisri cha Dar es salaam kwa kushirikiana na umoja wa wanazuoni wa Kiis lamu Tanzania kimefanya kongamano la kidini llilofanyika chuoni hapo mwishoni mwa wiki iliyopita.

    Masheikh mbalimbali waliwasilisha mada katika kongamano hilo lililokuwa na anuani uharamu wa kuua katika sheria ya Kiislamu ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Rais mstaafu Alhaj Mzee Ali Hassan Mwinyi.

    K a b l a y a k u a n z a uwasilishwaji wa mada za Masheikh katika kongamano h i l o , m u o n g o z a j i w a kongamano Sheikh Mohamed al-Amiri Athumani, ambaye ni mwalimu wa Markaz, aliwakaribisha Masheikh wa kimisri na wa kitanzania kuwasilisha mada zao ambapo kongamano lilifunguliwa kwa kusomwa Qurani na Sheikh Elysayed Awadh, ambaye ni mwalimu wa Markaz.

    Miongoni mwa Masheikh waliokaribishwa kuwasilisha mada zao katika kongamano h i lo n i She ikh Khamis Mataka, Katibu Mkuu wa taasisi ya Wanazuoni na Masheikh Tanzania, ambaye alitoa mada kuhusu namna roho ilivyo na thamani kubwa katika Uislamu, ambapo aliwakumbusha watu juu ya uharamu wa kuua katika Qurani na hadithi.

    A i d h a a l i z u n g u m z i a suala hilo kwa mujibu wa Qurani Surat Nisai, ambapo aliegemea katika neno la mwenyezi Mungu Na yeyote atakayemuua muumini kwa makusudi basi malipo yake ni moto wa Jahanam atakaa

    Kongamano lafanyika Markaz ChangombeNa Mwandishi Wetu humo milele na hasira za

    mwenyezi Mungu ni zake na atamuandalia adhabu kubwa.

    Likafuatiwa na neno la makaribisho lililotolewa na Mudir wa Markaz, Sheikh Salah Sayed Hussein Miftah, a m b a y e a l i a n z a k wa kumkaribisha mgeni rasmi Rais mstaafu wa awamu ya pili ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania al-Haji Mzee Ali Hassan Mwinyi, ambaye alilipamba kongamano kwa kufika kwake kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi kupita.

    Akiwasilisha mada yake, Sheikh Mataka alijikita pia katika hadithi ya Mtume (saw) Kila Muislamu kwa Muislamu ni haramu roho yake na mali yake na heshima yake .

    N a y e D k . A b d a l l a h D a r u we s h i , a m b a ye n i mwalimu wa Markaz hiyo ya k imisr i a l iwas i l i sha mada iliyokuwa na anuani kuhifadhi nafsi ya binadamu ni makusudio makubwa ya sheria, ambapo alifafanua kwamba kusudio la sheria ni kuhakikisha maslahi ya binadamu (waja).

    Aidha alibainisha kuwa hayo ndio makusudio ambayo U i s l a m u u m e ya h i f a d h i n a k u b a i n i k a k a t i k a mambo makuu matano na akaichukulia dalili juu ya kuhifadhi nafsi ya binadamu na baadae Sheikh Yahya Mkali kutafsiri mada yake.

    Kwa upande wake Sheikh Suleiman Kilemile, ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, alizungumzia juu ya uharamu wa kuwaua wale wanaoishi kwa mkataba na ahadi katika sheria ya

    Kiislamu.Sheikh Kilemile alitumia

    fursa hiyo kufafanua mada yake juu kuhusu ukubwa wa kosa la kumwaga damu au kuua wale wanaoishi kwa mikabata ya amani katika miji ya Kiislamu kwa njia ya vibali (visa na permit).

    Alisema kuwa huo ni mkataba wa amani hivyo hai fa i kwa mtu yeyote kuuvunja mkataba huo kwa njia ya kumwaga damu au kwa kufanya uadui wowote.

    A l i f a f a n u a h a d i t h i ya Mtume (saw) isemayo yeyote atakayemuua mtu anayeishi kwa mkataba wa amani, huyo hatoisikia harufu ya pepo, kwani harufu yake hupatikana mwendo wa miaka arobaini.

    U l i f i k a w a k a t i w a k u z u n g u m z a S h e i k h Mohamed Iddi Mohamed (Abuu Iddi), ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanazuoni wa Masheikh wa Kiislamu Tanzania na Imamu Mkuu Masjid Mnyamani.

    M a d a y a k e i l i k u w a ni thamani ya uhai katika Uislamu. Alibainisha kwamba uhai ni zawadi toka kwa mwenyezi Mungu mtukufu, hivyo haifai kuifanyia uadui neema hii isipokuwa kwa haki zake au hukumu za mwenyezi Mungu.

    Kongamano hilo lilifikia tamati kwa maneno al-Haji Hassan Mwinyi, ambaya alitilia mkazo juu ya neema ya amani.

    Mwisho alisimama Sheikh Swalah Miftah, Mudir wa Markaz na kuwashukuru wote waliohudhuria kongamano na kumshukuru Rais mstaafu kwa kushajiisha Markazi katika kongamano hilo.

  • 3 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014Habari

    Muhongo awarushia Waislamu makomboTAARIFA za uchunguzi zinaonyesha kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kaongeza watu watano katika orodha ya kwenda kusomea utalamu wa mafuta na gesi, China.

    P r o f . M u h o n g o amechukua hatua hiyo siku kadhaa baada ya hapo awali kuchagua kwa asilimia 100 Wakristo watupu watakaolipiwa na serikali ya China kusoma katika vyuo vikuu vya nchi hiyo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili (Masters) na ile ya Uzamivu (Ph.D) katika utaalamu wa mafuta na gesi.

    Hatua hiyo ya kuwapa Waislamu sifuri (0%), i l izua malalamiko na maswali mengi na joto lake lilivyozidi kupanda, Waziri akaona alipoze kwa maelezo kuwa kaongeza watu watano katika wale kumi aliowateuwa awali wakiwa Wakristo watupu.

    Waliotajwa kuongezwa watakwenda kusomea Shahada ya Uzalimili (MSc) katika mafuta na gesi.

    H a t a h i v y o t a a r i f a ndani ya Wizara hiyo z i n a f a h a m i s h a k u wa wakati wale kumi wa awali watasomeshwa na serikali ya China, hawa alioongeza Mheshimiwa Waziri Muhongo katika kupoza mambo, itabidi Wizara itafute namna ya kuwalipia jambo ambalo h a l i j a f a h a m i k a k u wa Muhongo atapata wapi ba jet i yake, kwa vi le haikuwepo toka awali.

    Wengi wanaonyesha wasiwasi kuwa isije kauli h i y o i m e t o k a k a t i k a kupoza joto hali ikawa ngumu baadae kwa hao waliotupiwa makombo wakakwama njiani hata masomo wasimalize.

    Awali katika orodha iliyotolewa kufaidi msaada huo wa kusomeshwa na serikali ya China walitajwa kuwa ni Erasma Rutachura (PhD), Abel Masanja (MSc), Beatrice Tubuke (MSc), Faustine Matiku (MSc) na Alvin Mulashani (MSc).

    Wengine ni Kunugula Lwakutubi (MSc), Nigel Kimaro (MSc), Ansila Kiusa (MSc.), Hebert Msangi (MSc.) na Victor Mugarula (MSc).

    Hawa wanasomeshwa ili kuja kuwa wataalamu katika mafuta na gesi, rasilimali ambazo zinaonekana kuwa

    Na Mwandishi Wetu

    zitachukua nafasi kubwa sana ya uchumi wa nchi hii kwa siku za hivi karibuni.

    Ni kutokana na uteuzi huu wa awali ambao wengi walioona orodha hiyo walisema wazi kuwa huo ni udini, walihoji kuwa iwapo hivi sasa siasa, sera, mweleko na wito ni kumshirikisha kila mtu, kila mwananchi, mbona inapokuja suala la dini mwelekeo huo unapigwa chenga?

    Au inapozungumzwa kila mwananchi kushiriki katika uchumi wa nchi, Muislamu yeye hayumo?

    Wa t a a l a m u h a w a wanaoandal iwa, ndio wa t a k u j a k u s i m a m i a sekta hii muhimu kwa uchumi wa nchi, sasa unapoandaa watu wa dini moja tu, maana yake ni kuwa unataka wakirudi na kushika nafasi mbalimbali, nao wateuwe na kuajiri wa chini yao walio katika wao, hii maana yake nini? Si ndio udini wanaouzungumzia n a k u u u p i g i a k e l e l e Waislamu?

    Alihoji mtumishi mmoja katika sekta binafsi ambaye hata h ivyo hakutaka kutajwa jina lake gazetini.

    Lakini mtu anapofanya kitu kama hichi, kutumia nafasi ya Uwaziri wake na kutumia dhamana ya uongozi aliyopewa na taifa kufanya ubaguzi na udini kama huu ulio wazi kabisa, lengo lake nini, kama si kutaka kuleta machafuko katika nchi. Aliongeza.

    K a t i k a k u f a f a n u a a l i s e m a k u w a k w a takriban wiki mbili sasa, kumekuwa na machafuko kule Ferguson, J imbo la Missouri, Marekani kutokana na kuuliwa kwa kupigwa risasi kijana wa Kimarekani mwenye asili ya Afrika.

    Anasema, hasira ya watu inakuja baada ya kuwa

    yametokezea matukio kama hayo mengi ambapo wa t u we u s i h u u l i wa na polisi kwa kupigwa r isasi b i la ya sababu za msingi, kinyume na sheria na hakuna hatua wanazochukuliwa polisi wanaofanya jinai hiyo.

    Akasema kuwa, vurugu za sasa kule Ferguson, ni kuwa watu wamefikia mahali wamechoka.

    Wanaona kuwa wao hawathaminiwi kama binadamu, damu yao na uhai wao unaonekana hauna thamani kwa hiyo unaweza kutolewa ovyo tu na isiwe lolote.

    Sasa isidhaniwe na Waislamu wa Tanzania wataendelea kushuhudia ubaguzi na udini kama huu halafu wakae kimya tu, watameza itafika mahali watashiba , ya takuwa hayamezeki t ena , na ikifika hapo wasilaumiwe, w a c h a w i w a t a k u w a ni hawa wanaotumia madaraka yao kuendeleza udini na ubaguzi katika nchi hii. Alimaliza.

    Huyu Trayvon Martin a l i p i g w a r i s a s i n a kuuliwa na Polisi, George

    Zimmerman, usiku wa Februari 26, 2012, kule Sanford, Florida.

    Wakat i huo Mart in alikuwa bado kijana mdogo wa umri wa miaka 17 na mwanafunzi wa sekondari.

    Japo kijana Trayvon h a k u w a n a s i l a h a , mamlaka za k isher ia zilimwachia huru George Zimmerman, kwa madai kuwa alimuuwa Trayvon akiwa katika harakati za kujihami/kujilinda, utadhani kulikuwa na mapambano kati ya kijana huyo na askari mweye silaha.

    Hatua h iyo i l i ibua hasira ambapo yalifanyika maandamano nchi nzima na kupelekea kukamatwa tena George Zimmerman akishitakiwa kwa mauwaji.

    Hata hivyo, ilipofika Julai 13, 2013 aliachiwa tena mahakama ikikariri hoja za awali kuwa hana hatia kwa sababu alikuwa akijihami.

    Hatua hiyo iliibua tena hasira na maandamano makubwa na kuwapa moyo Wamarekani Weusi wakiungwa mkono na raia wenzao Weupe kuwa kuna

    haja ya kuchukua hatua kuhakikisha kuwa mfumo huo usio rasmi wa kibaguzi unangoka.

    Katika salamu zake za rambirambi na kuwafariji wafiwa, Sybrina D. Fulton, ambaye ni mama wa Trayvon Martin, baada ya maelezo marefu ya kuonyesha masikitiko yake , a l imal iz ia kwa kusema kuwa iwapo wenye mamlaka katika serikali ya Marekani hawatataka kuwasilikiza, basi jamii inayobaguliwa itawafaya wahisi na watambue kuwa nao Weusi wapo.

    Alisema, If they refuse to hear us, we will make them feel us.

    Na akaongeza kuwa wala hii isichukuliwe k u w a n i u c h o c h e z i kwani kinacholengwa ni kuwafanya wabaguzi na wanaouwa ovyo watoto wa wenzao, wafikie mahali wafikirie, lau ingekuwa ni watoto wao wanaouliwa wangejisikiaje.

    Wakifikishwa hapo, anasema, hapana shaka haraka watachukua hatua za kurekebisha hali iliyopo.

    Polisi, George ZimmermanBaba yake Michael Brown Mama yake Trayvon Martin

    MAANDAMANO nchini Marekani kupinga mauaji yanayofanywa na polisi dhidi ya watu weusi.

    Mama yake Michael Brown.

  • 4 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014Habari

    NECTA watuhumiwa kuleta Utanganyika katika mitihaniBARAZA la Mitihani nchini (NECTA) limeshutumiwa kuleta ubaguzi kati ya Bara na Visiwani katika utendaji wake.

    Ubaguzi huo umetajwa kuwa ni ule wa kuona kuwa wenye haki kutendewa haki katika mitihani ya Lugha ya Kiarabu na Maarifa ya Uislamu, ni Wazanzibari tu, lakini kwa Bara hawana haki hiyo.

    Ni katika muktadha huo huo, ikakumbushwa kuwa Baraza hilo lilikuwa likiweka utaratibu wa kuwafelisha watoto wa Kiislamu, wakati likiwarahisishia kufaulu wale wa Kikristo.

    Ikafafanuliwa kwa kusema kuwa somo la Islamic Knowledge, lilikuwa likiwekewa alama za juu za ufaulu, wakati lile la Bible, likiwekewa alama za chini.

    Hayo yameelezwa na Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu, likimtaka Wizari ya Elimu na Mafunzo ya Ufudi, kutengua matokeo ya wanafunzi wa Kiislamu wa kidato cha sita kufuatia kuenguliwa masomo ya Dini katika kupanga madaraja ya ufaulu.

    Katika Barua yao kwenda kwa Waziri wa Elimu, Mh. Shukuru Kawambwa, Baraza hilo limesema, zipo sababu za kutosha zenye maslahi na Taifa za kubadilisha matokeo hayo ya wanafunzi ambao wameathirika kwa kuenguliwa kwa masomo hayo.

    Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu linapinga mabadiliko haya na kuomba yatenguliwe. Baraza linaamini kwamba ziko sababu za kutosha na zenye maslahi na Taifa letu za kubadilisha matokeo ya wanafunzi walio athirika na mabadiliko hayo yaliyofanywa na NECTA. Imesema Barua hiyo.

    Barua hiyo imeyatafsiri mabadiliko hayo yaliyofanyika kuwa ni ya kibaguzi kwa sababu yanawabagua watahiniwa wa masomo ya Arabic na Islamic Knowledge kwa misingi ya Zanzibar na Tanganyika, hivyo wakaitaka NECTA iwatendee haki watahiniwa hao kupitia masomo hayo ya Dini.

    Wakuu hao wa Shule za Kiislamu nchini wakasema kinacho wasikitisha zaidi ni kuona kwamba kila mara Baraza la Mit ihani (NECTA) wanafanya maamuzi ambayo yanapelekea kusababisha mgogoro na wadau wake wa dini ya Kiislamu.

    Baraza hilo limemweleza Waziri Kawambwa, sababu za kutaka kutenguliwa kwa matokeo hayo kuwa ni kinyume na sheria za nchi na haioneshi utawala bora pia utaratibu huo utaleta sintofahamu isiyokuwa na msingi kwa wadau wa Baraza la Mitihani hasa wale wa Vyuo Vikuu vya ndani na nje ya nchi.

    Hii ni kwa sababu wanafunzi wawili, mmoja kutoka Tanganyika na mwingine kutoka Zanzibar ambao watakuwa wamesoma KLA na kila mmoja akafaulu sawa na mwingine, yule wa Zanzibar atapewa cheti chenye ufaulu wa juu zaidi, kuliko huyu wa Tanganyika hali hii italishushia Baraza la Mitihani la Tanzania hadhi yake. Imesema Barua hiyo.

    Walimu hao wamesema, Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu,

    Na Bakari Mwakangwale l inashindwa kuelewa mantiki inayotumiwa na wataalamu wa Wizara ya Elimu kuamua lugha gani ya kigeni ina umuhimu katika nchi hii.

    Kwa uelewa wao, wamesema somo la Kifaransa lina watahiniwa wachache kuliko somo la Kiarabu humu nchini, lakini wataalamu wa Wizara ya Elimu wanaendelea kulihesabu somo la Kifaransa katika kupanga madaraja ya matokeo ya mtihani wa kidato cha sita na kuliondoa somo la Kiarabu.

    Somo la Kifaransa lina watahiniwa wachache kuliko somo la Kiarabu humu nchini, lakini wataalamu wako wanaendelea kulihesabu somo hilo katika kupanga madaraja ya matokeo ya mtihani wa kidato cha sita, tunashindwa kuelewa maamuzi haya yanafanywa ili kumfurahisha nani na kumridhisha nani? Imesema na kuhoji barua hiyo.

    B a r a z a h i l o l i m e s e m a , lmesikitishwa na hatua ya Baraza la Mitihani kwa kuyaengua masomo ya Arabic na Islamic Knowledge katika mchakato wa kutoa madaraja ya wanafunzi katika mtihani wa kidato cha sita.

    Baraza hilo limeeleza kwamba ni kawaida kwa Wizara ya Elimu au hata Baraza la Mitihani kuwasiliana na wadau wanapotaka kufanya mabadiliko ili kupata maoni yao au hata kuwapa taarifa tu ili wajiandae pia kufanya maamuzi bora kwa wakati muafaka, lakini kwa hili imekuwa tofauti.

    Wakizungumzia waraka wa Kamishna wa Elimu wa mwaka 2006 na Tahasusi zenye somo la Kiarabu, wamesema waraka huo haujabadilika bado na Baraza la Mitihani limekuwa likitunuku kama somo moja wapo.

    Mheshimiwa, waraka wa Kamishna wa Elimu wa April 1, 2006, haujabadilika mpaka hivi sasa, Baraza la Mitihani limekuwa likitunuku somo la Kiarabu kama somo mojawapo la Lugha katika Shule mbalimbali na miaka tofauti. Imeainisha barua hiyo, iliyotiwa saini na Mwekiti wa Baraza hilo, Mwl. Hamisi Togwa.

    Wakuu hao wa Shule za Kiislamu, katika barua hiyo kwa Waziri Kawambwa, wameain isha na kuchanganua mifano ya watahiniwa wa wakidato cha sita kwa mwaka 2014 kutoka Tanzania Bara walioathiriwa na uamuzi wa kuyaengua masomo hayo.

    Aidha, Baraza hilo la Wakuu wa Shule za Kiislamu, wamemkumbusha Waziri Kawambwa, kuwa huko nyuma kumekuwa na malalamiko kutoka kwa Waislamu, kwamba Baraza la Mit ihani wal ikuwa wakipuuza kwa makusudi kuajiri waratibu wa somo la Arabic na Elimu ya Dini ya Kiislam.

    Pia Baraza la Mitihani, wamekuwa wakiweka alama za ufaulu kwa somo la Islamic Knowledge kuwa za juu zaidi ikilinganishwa na somo la Bible Knowledge, ili kuwafelisha Waislamu na kuwarahishia kufaulu Wakristo.

    Ama, mgogoro wa matokeo ya somo la Islamic Knowledge kwa mwaka 2012, pia ni miongoni mwa mambo yaliyo liweka Baraza la Mitihani (NECTA) na Waislamu kuwa katika sintofahamu kubwa.

    Awali, akiongea na An nuur,

    Ofisini kwake kufuatia kuenguliwa huko kwa masomo ya Dini, Kaimu Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt. Charles Msonde, alisema kazi yao ni kutekeleza miongozo ya Serikali (Wizara ya Elimu) pasi ya kukengeuka.

    Pa m o j a n a h i v y o , a l i s e m a changamoto anayoiona na kusikia kwa wadau mbalimbali, ni kufahamu ni ipi michepuo (Combinition) inayotambulika na hususani kwa Waislamu baada ya kuona masomo yao hayajahesabiwa kama sehemu ya ufaulu.

    Ho ja inaku ja kwamba , j e masomo hayo yapo katika michepuo inayotambulika na Wizara ya Elimu? Mtoto alipokwenda kujiunga na kidato cha Tano, alisoma kombi yenye masomo hayo? Alihoji Dkt. Msonde, akijenga hoja yake.

    Alisema, Wakuu wa Shule za Sekondari wameainishiwa masomo ya michepuo yanayotambulika na Wizara ya Elimu ya kitado cha Tano (A-Level), kuwa ni HGE, HGL, HGK, HKL, mengine ni KLF, EGM, PCM, PCB, CBG, pamoja na PGM, ECA, CBA, CBN.

    Hata hivyo alisema, mwanafunzi hakatazwi kusoma masomo ya ziada anayoyapenda kama ni Maarifa ya Uislamu, Arabic, au Divinity na hata kama ni kompyuta Sayansi, na Baraza litayasahihisha na kuyapa madaraja na yatatambulika popote ndani na nje ya nchi.

    Dkt. Msonde, alibainisha kwamba katika usahihishaji changamoto huwa ni katika ukokotoaji kwani hufanywa na mfumo wa Kompyuta ambao tayari upo katika programu (programmed) ya kombinisheni zinazotambulika na Wizara ya Elimu.

    Lakini, alisema pamoja na hali hiyo bado Waislamu na wadau wengine wanayo nafsi ya kushauri kwa sababu wao ni wadau wa elimu na wanahaki ya kusikilizwa.

    Kwa mfano, alisema hoja ya msingi ambayo inaweza kutumika katika hilo ni kutumia idadi ya wanafunzi wanaosoma na kufanyia mtihani masomo hayo na hakutakuwa na sababu ya kuwazuia ikiwa itabainika ipo haja kwani wao ndio wanaohitaji.

    H i i m i c h e p u o i l i y o p o n a i n a y o t a m b u l i k a n a Wi z a r a , imewekwa na wanaadamu na haina

    maana kwamba itakaa milele, hapana imewekwa kwa mahitaji ya watu na kwa wakati husika hivyo inaweza kubadilishwa au kuongezwa mingine.

    Kwa mfano kombinisheni hizi zilitolewa mwaka 2006, lakini hayo yalikuwa ni mahitaj ya watu kwa wakati huo inawezekana sasa watu wanamahitaji mengine zaidi. Alisema Dkt. Msonde.

    A l i s e m a , k wa s a s a wa d a u wanaweza kusema hivi kuna HKL, KLF, lakini kulingana na mahitaji kwa kipindi hiki inaonekana ongezeko la wasomaji wa somo hilo kuwa kubwa hivyo kuna haja ya somo la Arabic kuwa katika mchepua wa Lugha, hivyo pakawa na KLA, LFA au hata HGA kwa kuwa tayari kuna HGK.

    Sasa hoja hii unaijenga wapi, unaweza ukaandika kwa Kamishna wa Elimu katika Wizara ya Elimu, kwa sababu yeye ndiye anayetoa hiyo miongozo na sisi tunatekeleza au kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, lakini hoja hiyo isiwe katika malalamiko, bali iwe katika ushauri kama wadau wa elimu. Alishauri Dkt. Msonde.

    Aidha, Dkt. Msonde, alieleza kwamba hata kama masomo hayo kwa sasa hayapo katika michepuo, lakini Baraza la Mitihani linayagredi kama kawaida na kuyapa maksi kama kawaida na yatakuwa na manufaa kulingana na malengo ya mtahiniwa.

    Akifafanua alisema, Vyuo Vikuu wanapopokea maombi ya kujiunga wao huanza kupitia pasi alizoombea mtahiniwa katika masomo husika, kwani alidai hawafati pointi kutoka Baraza.

    V y u o V i k u u h a v i c h a g u i mtahiniwa kwa sababu ya idadi ya poini za Baraza, wao huchagua mtu kujiunga na Chuo Kikuu kwa kutegemea na kozi aliyoiomba na masomo yanayohusiana na kozi aliyoiomba.

    Katika cheti cha Baraza la mitihani masomo yote aliyofanyia mtihani mtahiniwa yanatolewa ambayo yatakuwa na nguvu ya kuombea kujiunga na Chuo chochote duniani au taasisi yoyote ya elimu. Alidai Dkt. Msonde.

    Ama kuhusu Zanzibar, kuwa wao masomo hayo ya dini yametumika

    Inaendelea Uk. 5

    WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa.

  • 5 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014Habari

    TANGU alipotoweka kijana wake Juni 28 mwaka huu, Bw. Mahat Elmi Hassan, mwenye umri wa miaka 51 hakai mbali na simu yake ya mkononi, akitumaini kupata habari mpya kuhusu mahali alipo kijana wake mkubwa mwenye umri wa miaka 17, Abdi Mahat Elmi.

    Ki jana wangu Abdi alikuwa akifanya kazi kama mwalimu wa madrassa katika eneo la Koreni, katika Kaunti ya Lamu miezi miwili kabla ya kupotea kwake, Hassan aliuambia mtandao wa Sabahi.

    Aliongeza kuwa kupotea kijana wake kulitokea wakati wa msako wa watu wa vikosi vya usalama vya Kenya dhidi ya watuhumiwa wa mashambulio katika Kaunti ya Lamu.

    Katika miezi hiyo miwili, ni mara chache sana siku ilipita bila yeye kupiga simu na kusema anavyoendelea na kuuliza juu ya sisi kurudi nyumbani, alisema Hassan, mkazi wa Garissa.

    Alisema kabla ya kupotea kwake, aliwaambia kwamba maofisa wa polisi walikuwa wakikamata watu pasipo sababu maalumu.

    Walielezea wasiwasi wao kwamba kijana wao anaweza kuwa mwathirika wa ufagiaji wa polisi.

    Bw. Hassan alisema Elmi, alikwenda Kaunti ya Lamu kufanya kazi kama mwalimu wa madrassa kusaidia familia yake maskini.

    Baada ya kupotea kwake, familia hiyo ilikwenda Lamu kumtafuta na kuuliza yeyote anayejua mahali alipo, lakini pasipo mafanikio.

    Kwa sasa nabeba simu hata ninapokwenda kuoga n i k i wa n a m a t u m a i n i kwamba yeye au mtu yeyote atapiga simu kunipa habari nzuri, alisema.

    Elmi siyo kijana pekee ambaye hajulikani alipo katika wiki za hivi karibuni.

    Viongozi wa kisiasa wa ndani na vikundi vya haki za binadamu wanalaumu polisi kwa kupotea watu wasiopungua 21 wakati wa operesheni ya usalama katika mkoa wa Pwani.

    Bw. Hussein Khal id , Mkuregenzi Mtendaji wa asasi ya haki za binadamu ya Haki Afrika, alisema wana hofu kwamba vikosi vya usalama vinaweza kuwa viliwakamata watu ambao hawakurekodiwa katika vitabu au hata kuishia katika mauwaji yanayotokana na

    Familia zataka majibu kuhusu watu 21 wasiojulikana walipo

    Ni baada ya fagiafagia ya usalama Pwanikatika viwango vya ufaulu, alisema ni kanuni ndio zinazo ruhusu hivyo kwa kuwa tayari wao masomo hayo yanatambulika.

    Alisema, kifungu cha 23 cha Baraza la Mitihani k i m e a n i s h a k wa m b a Kamishana wa Elimu anaweza akatoa miongozo na yeye au Baraza la Mit ihani wanatakiwa waifuate.

    L a k i n i k u m b u k a Zanziba ni nchi , ina Waziri wake wa Elimu, ina Katibu Mkuu wake na ina Kamishna wake pia, lakini Baraza la Mitihani (NECTA) sio la Tanzania Bara pekee, ni Taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

    Kwa hiyo, mimi naweza kupokea maelekezo ya Kamishana wa Bara na bado pia naweza kupata maelekezo na miongozo kutoka kwa Kamishina wa Zanzibar. Alisema Dkt. Msonde.

    Hivyo, alisema kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Kamishna wake wa Elimu katika muongozo uliopo NECTA hadi sasa wa mwaka 2012, ambao B a r a z a u n a o u t u m i a , umetoa ufafanuzi wa michepuo ya masomo husika kwa Zanzibar.

    M u o n g o z o h u o umeniambia kwamba, k a t i k a ya l e m a s o m o a m b a y o z a m a n i waliyokuwa wakiyaona ni ya hiyari kwa Zanzibar, sasa yamekuwa ni ya lazima na kunitaka yatambulike kwa hatua zinazofaa kwa muunganisho maaluma. Alisema Dkt. Msonde.

    Alisema, waraka huo wa Kamishana wa Elimu Zanzibar, umeainisha michepuo ya masomo hayo kuwa ni Arabic Kiswahili Islamic Knowledge, Arabic Kiswahili English, Arabic History Kiswahili, Arabic History Geography na Arabic Kiswahili French.

    Akasema, yeye binafsi anaona umefika wakati yakatambulika ik iwa data zitaonyesha kuna ongezeko la watahiniwa wa Masomo hayo na anaweza kushirikiana na wadau wengine kujenga hoja kwa Kamishana na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu kwa manufaa ya Taifa il i kuepusha migongano na wadaui wake.

    NECTA watuhumiwa kuleta UtanganyikaInatoka Uk. 4

    Na Bosire Boniface, Garissa kutumia nguvu nyingi katika vita vinavyoendelea kuhusiana na ugaidi.

    T u m e t h i b i t i s h a kwa hati watu 21 ambao hawajulikani walipo. Sita kati yao hawaonekani huko Lamu tangu kuzinduliwa operesheni ya usalama baada ya mashambulio ya Mpeketoni. Alisema Bw. Khalid.

    Alisema watu wengine ambao hawajulikani walipo waliripotiwa kuonekana kwa mara ya mwisho mwezi Mei katika kaunti za Mombasa, Taveta na Kwale wakati wa operesheni nyingine za usalama.

    Bw. Khalid aliongeza kuwa mashuhuda na wanafamilia wa watu ambao hawajulikani walipo, walisema ndugu zao walionekana kwa mara ya mwisho wakichukuliwa na maofisa wa polisi na kwamba, ndugu wamewasilisha ripoti za watu wasiojulikana waliko kwa mamlaka za eneo na katika taasisi yake.

    F a m i l i a z i n a h o f i a k w a m b a n d u g u z a o wasiojulikana walipo, ama wameuawa au wanashikiliwa kinyume cha sheria. Serikali inatakiwa kuchukua hatua na kueleza watu hao wako wapi kwa kuwa polisi ni watu wa mwisho kuonekana na watu hao. alibainisha Mkurugenzi huyo.

    Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Lamu, Shakila Abdalla, al isema polisi wanawakamata watu bila ya sababu.

    Ni haki ya katiba na haki ya mtu yeyote kuarifiwa makosa yake anapokamatwa na kubainishiwa mahali anapopelekwa, lakini polisi hawataki hata kuwaruhusu waliokamatwa kuwajulisha ndugu zao. Mwakilishi huyo aliuambia mtandao wa Sabahi.

    Alisema kuwa wamefanya mikutano na viongozi wa u s a l a m a k u t a k a k u j u a walipo baadhi ya watu waliokamatwa na polisi kwani ukamataji huo wa kiholela na kutoweka watu hakutaleta matokeo yanayotakiwa ya operesheni ya usalama na badala yake, kutaleta hofu na watu wanaweza kushindwa kushirikiana na polisi.

    K w a u p a n d e w a k e , K a m i s h n a w a K a u n t i ya Lamu, Miiri Njenga, alisema mamlaka zilikuwa zinachunguza madai ya kutoweka watu hao.

    N i t u h u m a n z i t o dhidi ya vikosi vyetu vya usalama ambavyo viko hapa kuwatafuta wahusika wa

    vurugu zinazotokea katika Kaunti, alisema Bw. Njega

    Alidai kuwa wanahitaji ushahidi ambao kwa hakika utabainisha polisi ambao wanahusika na kutoweka kwao.

    Aidha alisema kwamba hawawezi kuthib i t i sha kwamba baadhi ya tuhuma za watu wasio ju l ikana walipo, wanaweza kuhusika katika vurugu na kuamua kukimbia operesheni ya usalama kwenda kaunti au nchi nyingine.

    Kaimu Kamanda wa Polisi wa kaunti ya Mombasa, Sevelino Kubai, alinukuliwa akikanusha kuwepo kwa ufanyaji makosa wowote kwa upande wa pol i s i n a k u s e m a , wa l i k u wa wanachunguza kesi zote za watu wasiojulikana walipo.

    Kamanda Kubai alisema M b u n g e w a M v i t a , A b d u l s wa m a d S h a r i f f N a s s i r n a S e n e t a w a Mombasa, Hassan Omar, wamewasilisha ripoti kuhusu watu wasiojulikana walipo.

    Kamanda huyo alisema kuwa viongozi wanasema watakwenda mahakamani kuwashitaki polisi, wakitaka waelezwe walipo kuhusu watu wasiojulikana walipo, aliiambia Sabahi.

    Tulikuwa tunafanya uchunguzi kuhusu ripoti za madai ya watu wasioonekana. Wakati huohuo, tunawataka viongozi kutoshikilia madai ya uongo kuhusu polisi bila kuwa na ushahidi wa kutosha.

    Madai kwamba polisi wanaweza kuwa wamewaua watu hao wasiojulikana walipo ni ya kufedhehesha. Taarifa za kina za mtu ye y o t e t u l i ye m k a m a t a zimerekodiwa katika kitabu cha kumbukumbu cha polisi. Kama uchunguzi wetu utagundua mmojawapo h a h u s i k i n a u h a l i f u , ataachiwa huru. alisema Kubai.

    Alisema ukosoaji wa kikosi cha polisi kushughulikia operesheni ya usalama ulikuwa ni jaribio la kuzuia mchakato na kwamba, hawawezi kuzuiwa na madai ambayo lengo lake ni kuharibu au kuchelewesha vita dhidi ya uhalifu.

    W a k a t i h u o h u o , Wafuatiliaji wa Haki za Binadamu (HRW) Jumatatu wiki hii walisema Kitengo cha Polisi cha Kuzuia Ugaidi Kenya (ATPU), kilihusika kwa kufanya matukio ya mauaji kinyume cha sheria na kitendo cha kufanya watu wasijulikane walipo.

    Disko marufuku KiwengwaWA Z I R I w a H a b a r i , U t a m a d u n i , U t a l i i n a Michezo Zanzibar, Saidi Ali Mbaruok, amepiga marufuku shughuli zote za kupiga disko katika eneo la Kiwengwa hadi pale Serikali ya Wilaya itapotoa maelekezo maalumu ya kupigwa disko hilo kwa utaratibu unaofaa.

    Agizo hilo amelitoa hivi karibuni huko Kiwengwa, Mkoa wa Kaskazini A Wilaya ya Kaskazini B Unguja, katika Ofisi ya U m o j a wa M a e n d e l e o wa Kijiji cha Kiwengwa, wakati alipokuwa akifanya mazungumzo na wamiliki wa mabaa, mikahawa, kumbi za starehe juu ya kukithiri wa upigwaji wa magoma kucha.

    Waziri Mbaruok alisema, amelazimika kuzifunga shughuli zote za upigaji madisko usiku kutokana na kutokuwa na utaratibu mzuri wa upigaji ngoma hizo usiku, hali ambayo imesababisha wageni wa kitalii na wenyeji kuchukia hali hiyo kwa kukosa usingizi na kusumbuliwa wagonjwa.

    A m e s e m a , h a l i h i y o haiwezekani kuonekana inaendelea kwani inapoteza muelekeo na mstakabali mwema wa nchi na raia kwa ujumla.

    Nimepokea u jumbe kwamba watalii wamefika kusema wanaondoka na kutafutiwa sehemu nyengine wakapunzike kutokana na zogo kuwa jingi la madisko, hili haliwezekani liendelee, alinukuliwa akisema Waziri huyo.

    A i d h a a l i s e m a h a i w e z e k a n i k u o n a utamaduni wa burudani unavurugwa, jambo ambalo ni kosa kufanya hivyo na kwenda kinyume na taratibu na silka zao.

    Kuanzia leo napiga marufuku mpaka Sheha wa Shehia hii aridhie, hata kama kuna kibali kwani Sheha ndiye anayejua hali za raia wake, kuna wagonja na wenye maradhi ya kuhitaji kupumzika au la, hatutaki kuona masuala yasio na utaratibu.

    Mimi kazi yangu ni kuutangaza utalii sio utalii uharibiwe, tufahamu kuwa utalii Zanzibar ndio uchumi unaotegemewa kwa sasa kwa hivyo tuulinde, aliongeza Waziri Said.

    Hata hivyo Waziri huyo alichukizwa na vitendo vya uwasharati vilivyotapakaa katika kijiji hicho, kujengwa mabaa karibu na nyumba za ibada hivyo kumwagiza M k u u w a W i l a y a kulishughulikia.

    Nao wakazi wa Kiwengwa, Othumani Mnyan ja na Mtumwa Rash id i , k i la mmoja kwa maoni yake walisema Kiwengwa hivi sasa imepoteza muelekeo kwani watoto wao wanaishia katika madisko na kukosa masomo, jambo ambalo ni hatari kwao.

  • 6 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014Habari

    Mansour afungulia mlangowanyonge juu ya dhamana

    KUMBE hakuna kosa lisilo na dhamana. Kanuni au sheria hiyo ndiyo iliyomtoa rumande Mansour Himid.

    Kwa mujibu wa maelezo yal iyotolewa mahakamani , hata kama kuna kosa linatajwa kuwa halina dhamana, lakini Mahakama Kuu imepewa uwezo wa kutengua kifungu hicho kwa jinsi itakavyolitathmini kosa na mtuhumiwa.

    Hayo yalibainishwa katika maelezo ya Jaji Mwampashe kabla ya dhamana kutolewa kwa Bwana Mansour Himid.

    Katika Mahakama ya Mkoa, Vuga, aliyekuwa Waziri wa zamani wa serikali ya Mapinduzi (SMZ), Mansour Yussuf Himid, a l ipewa dhamana ambapo kesi yake imeahirishwa mpaka Agosti 28 mwaka huu baada ya kuahirishwa na Hakimu Khamis Ramadhani.

    Awali kesi i l ipofikishwa mahakamani, Mansour alinyimwa dhamana kwa maelezo kuwa moja ya kosa analotuhumiwa halina dhamana.

    Ombi la Mansour kutaka kupatiwa dhamana linatokana na kushitakiwa kwa makosa matatu, la kwanza likiwa ni kumiliki silaha, kinyume cha sheria.

    Mwendesha Mashitaka Raya akisaidiwa na Maulid Ali litaja tuhuma nyingine zinazomkabili Mansoor kuwa ni kupatikana na risasi 295 kinyume cha kifungu cha 6 (3) na 34 (1) (2) sheria namba 7 ya Zanzibar ya mwaka 1964, na kosa la tatu ni kupatikana na marisau (risasi za shotgun) 112 kinyume cha kifungu cha 34 (1)(2) sheria ya risasi na silaha namba 2 ya mwaka 1991.

    Raya alipinga ombi la dhamana la mshitakiwa Mansour kutokana na tuhuma ya kumiliki risasi nyingi kinyume cha sheria ya Zanzibar kwamba, halina dhamana.

    Hata hivyo, katika hatua hii ya pili, ilielezwa mahakamani hapo kuwa Mansour anapatiwa dhamana kutokana na maelekezo kutoka Mahakama Kuu.

    Hakimu Khamis Ramadhani alitoa dhamana hiyo baada ya kutakiwa kusimamia maamuzi ya kupatiwa dhamana yaliyotolewa na Mahakama Kuu chini ya Jaji Abraham Mwampashe.

    Hatua hiyo ilifuatia kusikilizwa k w a o m b i l a d h a m a n a lililowasilishwa Mahakamani hapo na mawakili wanaomtetea Mansour.

    Jaji Abraham Mwampashe, akitoa dhamana hiyo, alisema kuwa Mahakama imeangalia hoja za kisheria zilizotolewa na pande zote mbili na kisha kufikia uamuzi wa kutoa dhamana.

    Alisema, kutokana na kifungu cha sheria cha (150) kifungu kidogo cha nne(4) sheria No (7 ) ya mwaka (2004) sheria ya Zanzibar, kinaipa Mahakama

    Na Mwandishi Wetu

    Bwana Mansour Himid.Kuu uwezo wa kutoa dhamana kwa mtuhumiwa ikiwa itaridhika

    na hoja zilizowasilishwa.Hakuna kosa lolote lisilokuwa

    na dhamana, kifungu kidogo cha nne (4) kiko wazi kimeeleza Mahakama Kuu ina uwezo wa kutengua makosa yote yaliokuwa hayana dhamana ikiwa itajiridhisha kama yalivyoorodheshwa katika kifungu kidogo cha kwanza. Alisema Mwampashe.

    Kwa kuzingatia matakwa hayo ya kisheria alisema kuwa alitizama faida na hasara za mtuhumiwa kuwepo rumande na kuwa nje, akaona kuwa bora awe nje.

    Na hiyo ni kwa kuzingatia gaharama kwa upande wa serikali halikadhalika hasara na usumbufu kwa mshitakiwa.

    Akifafanua zaidi al isema kuwa mtuhumiwa hana historia ya uhalifu, na kwamba ana majukumu ya kuendesha biashara zake ambazo kuna faida ya ajira kwa vijana walioajiriwa hapo katika vitega uchumi vyake.

    Akaongeza kuwa Mahakama haiwezi kumyima mtu dhamana bila ya kuambiwa sababu ya msingi kwamba kuwepo kwake nje kunawezaje kuathiri mwenendo mzima wa kesi yake.

    Wakati huo huo Jaji Mwampashe amesema kuwa kumnyima mtu dhamana itakuwa dhulma hasa itakapotokea kuwa baadae anashinda kesi au kesi kufutwa.

    A l i y e k u w a r u m a n d e atakuwa amedhulumiwa na waliokuwa wakimtegemea watakuwa pia wamedhulumiwa n a k u t i wa k a t i k a h a s a r a ikiwemo kukosa huduma muhimu kutoka kwa ndugu wanayemtegemea.

    Ni kutokana na maelezo haya ya Jaji Mwampashe watu mbalimbali wametoa maoni yao kuwa Mahakama Kuu ikifanya kazi zake vyema na kwa kuzingatia maslahi ya nchi na watu wake, huenda mlango huu uliofunguliwa katika kesi hii ya Mansour, ukawasaidia wengi.

    Kwamba si wote wanaojua kama kuna uzingatiaji hata wa kibinadamu tu, jambo ambalo kama likifanyika huenda hata kesi kama zile za Masheikh wa Uamsho zisingechukua muda mrefu kwa watuhumiwa wake kukaa ndani kwa zaidi ya miaka miwili, ambapo baadhi ya kesi zao zimefutwa.

    Awali Jeshi la Polisi lilimkamata na kumshikilia Mansour kwa tuhuma za kukutwa na silaha.

    Silaha hizo zilitajwa kuwa ni bunduki moja aina shotgun yenye risasi 112 pamoja na bastola aina ya beretta aliokuwa na risasi 295.

    Polisi ilidai kuwa licha ya silaha hizo kumilikiwa kihalali na Mansour, lakini kisheria hazikutakiwa ziwe na risasi nyingi kiasi hicho kama zilivyokutwa nyumbani kwa Mansour.

    Ilielezwa kuwa kwa mujibu wa sheria ya Zanzibar, silaha aina ya bastola ilitakiwa isizidi risasi 25 na bunduki aina ya shotgun isizidi risasi 20.

    MAHAFALI ya wanafunzi wa Kiislamu wa shule za msingi jijini Dar es Salaam, yamefanyika katika shule Kinondoni Muslim Secondary School mwishoni mwa wiki iliyopita.

    Mahafali hayo yalifanyika chini ya usimamizi wa Jumuiya ya Walimu wa Somo la Maarifa ya Uislam Mashuleni ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mbunge wa Temeke Bw. Abbas Mtemvu.

    Akisoma risala ya walimu katika mahafali hayo mbele ya mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Saidi Makongoro, alisema Jumuiya yao inayojulikana kama Muslim Education Teachers Association (MUETA) ilianzishwa mwaka 2006.

    Katika nasaha zake Bw. Abasi Zuberi Mtemvu, al iwataka wanafunzi hao kusonga mbele katika safari ya kujielimisha kwani elimu haina mwisho.

    Mimi mwenyewe hapa nasoma shahada yangu huko Marekani, u n a t a k i w a u w e k e d h i m a mwenyewe kwamba, Mwenyezi

    Mtemvu awataka wahitimu kusonga mbele safari ya elimuNa Abdulkarim Msengakamba

    Mungu anijalie nifikie elimu ya juu na Mungu atawajalia mtafika hadi vyuo vikuu. Mbunge huyo aliwatia moyo wahitimu.

    Aidha aliwahimiza wazazi kuwapenda watoto wao, kwa kuhakikisha wanasoma kwa bidii

    na wawafuatilie kuhakikisha wanapata elimu iliyo bora na sio bora elimu.

    Na kwamba katika kutafuta elimu, pasiwe na kubagua, zisomwe elimu nzote, hakuna ya dunia na Akhera.

    MWENYEKITI wa Jumuiya ya Walimu wa somo la Maarifa ya Uislamu mashuleni, Saidi Makongoro, akimkabidhi risala mgeni rasmi Mbunge wa Temeke, Mh. Abbas Mtemvu.

  • 7 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014Makala

    ALIYEKUWA Rais wa tatu wa Marekani, Thomas Jefferson, aliwahi kusema: He who knows nothing is closer to the truth than he whose mind is filled with falsehoods and errors.

    Ufupi wa maneno msemo huu una maana kuwa bora mtu ubaki hulijui jambo kwa sababu utafanya juhudi kuli jua, au hata kama hukufanya juhudi, lakini ikitokea ukafahamishwa, utajua ukweli. Lakini kama ulikuwa umejazwa taarifa za uwongo na potofu, halafu ukafanya ndiyo elimu yako juu ya jambo hilo, itakuwa vigumu sana kutoa uwongo huo na kujaza mahali pake taarifa sahihi.

    Yupo msomaji mmoja katuma ujumbe ambao pengine ingekuwa vyema kuwashirikisha wasomaji wengine kat ika kuutafakar i . Anasema:

    An nuur taarifa zenu zinasikitisha. Mnashangaa ISIS kuuwa watu kwa kukata vichwa makafiri. Kuna hadithi Mtume Muhammad (s.a.w) alichinja Wayahudi mia saba mpaka akachimba mitaro ya damu kama mvua. Sasa naye Mtume wetu Muhammad s.a.w unataka useme alikuwa hana huruma? (0713 033 978)

    Huyu labda aseme ni Adolf Alois Hitler. Sio Mtume (s.a.w). Ifikirie Madina ya wakati ule na idadi ya Wayahudi waliokuwepo, halafu linganisha na madai haya ya mito ya damu kama mvua!

    Inawezekana anachozungumzia hapa ni tukio la Banu Qurayzah. Lakini hata kama ni kisa hicho cha Banu Qurayzah, bado huu utakuwa ni uwongo na upotoshaji mkubwa kwa sababu Mtume (s.a.w) na Maswahaba zake hawakuwahi kuuwa Myahudi si kutoka Banu Qurayzah, Banu Nadhr, wala Banu Qaynuqa, kwa sababu ya Uyahudi (ukafiri) wao.

    Mambo manne ya kuzingatia hapa. Moja ni kuwa hata kama unazungumzia Banu Qurayzah, lakini bila kueleza muktadha wake (context), ambao ni vita ya Ahzab, na walichofanya makabila mbalimbali ya Kiyahud, kabla na mara baada ya vita hiyo, unajenga picha kuwa Waislamu waliwakamata na kuwauwa kwa sababu ya Uyahudi au ukafiri wao kama wanavyofanya ISIS.

    Lak in i p i l i n i kuwa kama ilivyo katika suala la holocost ya Wayahudi, zipo simulizi nyingi za tukio la Banu Quraizah zimeandikwa kwa kunukuliwa kutoka katika simulizi za Kiyahudi lengo likiwa kujenga huruma kwa Wayahudi na wakati huo huo kuupaka matope Uislamu.

    Tatu, tuzingatie kuwa katika zama hizi za kuwatumia Waislamu kupigana kwa niaba ya mabeberu, l inaweza kupenyezwa jambo. Inasemwa tu kuna hadithi inasema.Na kwa bahati mbaya watu wetu sio wasomaji. Elimu yao kwenye CD. Anaibuka mtu na CD/DVD, hiyo ndiyo elimu yake ndiyo fatwa yake. Kisa kama hicho cha Banu Quraizah, kinaweza kunyumbulishwa kikatiwa nakishi nje ya muktadha wake, kikarembwa na kutumiwa na mawakala waliopewa tenda na makafiri ya kutengeneza fanatiki wa Kiislamu wa kuwatumia katika

    Kasema kweli Clinton:Tunao Fanatics wachafuzi wa dini

    Elimu yao CDs za wakala wa proxy war

    BI Hilary Clinton.

    Na Omar Msangi proxy war yao na vita dhidi ya ugaidi (crusade).

    Nne, kwa vile watu sio wasomaji, hata hawana habari kuwa kuna taarifa nyingi za uwongo zikiwemo z i n a z o i t wa h a d i t h i a m b a z o zimeingizwa katika vitabu vya Kiislamu. Sasa ni mpaka usome uwe na mafhum ya ujumla ya Uislamu na misingi ya kufahamu hadithi sahihi na bandia, ndio unaweza kutambua hadithi potofu.

    Lakini nadhani pia kuwa ipo haja kwa Masheikh wetu kuboresha hata mitaala yao. Watoe elimu ya kuwasaidia watu kujitambua na kutambua itikadi na dhana mbalimbali zilizopenyezwa katika dini. Wakati nasoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam palikuwa na somo la DS. Hapo utasomeshwa siasa za kikomunisiti na kibeberu na uchambuzi wake juu ya faida na madhara ya kila moja wapo. Kwa vile nchi yetu ilikuwa ya kijamaa, ukomunisti ndio ulikuwa ukipewa maelezo mazuri zaidi.

    Sasa katika hali hii ya mchafukoge, confusion na ujinga ndani yake, nadhani kuna haya kwa Masheikh wetu kusomesha itikadi na siasa za makundi mbalimbali wakiwemo wanaoitwa Salafi-Takfiri.

    Quran inasema: Mwenyezi Mungu hakukukatazeni kuwafanyia ihsani na uadilifu wale ambao hawakupigana nanyi kwa ajili ya dini wala hawakukufukuzeni katika nchi zenu. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao uadilifu. (60:8)

    Lakini hata katika uwanja wa vita kwa wale ambao imelazimu Waislamu kupigana nao, bado Mtume s.a.w anaweka kanuni za vita ikiwa ni pamoja na kutozifanyia ufedhuli maiti au kuuwa wanawake na watoto na yeyote ambaye hajashika silaha na kuingia katika uwanja wa vita. Na pia ifahamike hapa kuwa hutawajumuisha makafiri wote katika kapu moja. Kwa hiyo hakuna hoja kuwa Mayahudi/makafiri, huko Gaza au Somalia, wanauwa Waislamu, kwa hiyo na wewe unatafuta kafiri wa Tanzania, unamuuwa!

    Sasa Mwenyezi Mungu hawezi kuagiza haya katika Quran tukufu, halafu Mtume wake awe anachinja watu ovyo kwa vile tu ni Mayahudi-kama ISIS wanavyowachinja Yazid na Waislamu (Shia na Suni wasio wakubali) wanaowakuta katika miji wanayoteka.

    Kipo kile kisa mashuhuri kati ya Muislamu na Yahud ambapo Muis lamu mmoja na Yahudi walidhulumiana. Kesi ikafika kwa Mtume s.a.w. Baada ya Mtume kusikiliza pande zote mbili, akaona haki ipo kwa Yahudi. Akampa haki Yahud. Kama ushahidi wa kafiri haukubaliki, hapana shaka Mtume (s.a.w) asingemsikiliza Yahud na kumpa haki yake, kama huyu msomaji anavyosema katika meseji nyingine kuwa:

    Katika Uislamu kafiri hafai kuwa shahidi kutoa tu ushahidi haruhusiwi wewe unatoa taarifa kutoka kwa makafiri mtu anaitwa Michael sijui nani huko sisi Waislamu ushahidi wetu unatoka kwenye Quran na Sunnah. (O713 033 978)

    Hydrogen cyanide (HCN), wakati mwingine ikiitwa prussic acid, ni katika sumu kali zinazojulikana

    duniani. HCN ikiwa hewani katika kiwango cha (concentration) 300 mg/m3 inamuuwa binadamu ndani ya dakika 10. Ikifikia concentration ya 3500 ppm (3200 mg/m3), inamuuwa mtu ndani ya dakika moja tu. Hii ni kwa sababu cyanide ion hukwamisha upumuaji ndani ya cell (cellular respiration) kwa kitendo chake cha kuzuiya ufanyaji kazi wa kimengenya (enzyme) cytochrome c oxidase ndani ya mitochondria.

    Historia ya kuvumbuliwa sumu hii na matumizi yake katika uchimbaji wa madini ya dhahabu na silver ikiwa kama sodium cyanide na potassium cyanide, inawataja wanasayansi Pierre Macquer (1752), Carl Wilhelm Scheele (1782), Claude Louis Berthollet (1787), Joseph Louis Gay-Lussac (1811) na Gay-Lussac (18150).

    Sasa ukiona chupa imeandikwa cynide na tahadhari kuwa ni sumu kali, wewe tizama katika Quran na Sunnah, kama haijaandikwa na kwa vile maelezo hayo yametolewa na akina Joseph Louis, we usijali, kunywa au jipake, maana ushahidi na maelezo ya kafiri hayakubaliki!!!

    Wiki i l iyopita kuna taari fa zilinikera sana kwa jinsi zilivyokuwa zinawatukana Waafrika, lakini pia zikawa zinapewa nafasi kubwa na kukaririwa sana, kutwa kucha katika Aljazeera. Nadhani na katika CNN, BBC na wengine. Habari zenyewe ilikuwa juu ya kuingia kwa ugonjwa wa ebola Nigeria. Wataalamu na mamlaka husika wakatoa taarifa za tahadhari kuwa watu wasile nyama za porini, na hasa nyani kwani inaaminika kuwa kirusi kinachosambaza ugonjwa huo kinatokana na wanyama wa porini. Katika taarifa hiyo, mpasha habari wa Aljazeera, anaonekana akitembelea vilabu vya pombe za kienyeji na mama lishe wanaouza supu na mishikaki ya nyama pori na kuhoji watu juu ya ushauri huo wa kitaalamu kuwa wajiepushe kula nyama pori katika kipindi hiki cha mlipuko wa ebola. Watu hao katika mama ntilie wakiwa na minofu yao ya wanyama pori wakiwemo nyani, tumbili na swala, wakaja juu. Wanasema kuwa wao hawatasikiliza ushauri huo kwa sababu nyama pori imekuwa ikiliwa katika eneo lao toka zama za mababu zao. Hawawezi kuacha urithi wa wakale wao. Mtu mmoja anaonekana akitoa hoja hiyo huku kashikilia fuvu la nyani lililokwishachomwa ananyofoa minofu akila.

    Hapana shaka kurejewa sana kwa taarifa ile ni kama kusema, watizameni hawa na ujinga wao, watizameni Waafrika walivyo wajinga.

    Hoja kama hii ya wa-Nigeria wala nyani, ni sawa na ile ya huyu ndugu yangu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam na mhandisi mtarajiwa. Ile kwamba babu zao walikuwa wakila nyani haitazuiya kupata maambukizi ya ebola iwapo watakutana na tumbili mwenye virusi vya ugonjwa huo. Jaaliya kuwa utafiti huo juu ya ebola na namna unavyoambukizwa umefanywa na John. Hoja kuwa utaalamu huo umetokana na utafiti wa John (kafiri) na hoja kuwa maelezo ya John hayapo katika Quran na Sunnah, haitakuzuiya wewe ukimkumbatia na kushika damu au majimaji kutoka mwili wa mtu mwenye ebola kuambukizwa.

    Morogoro ni katika mikoa ambayo tatizo la homa ya matumbo (typhod) ni kubwa sana. Katika baadhi ya hoteli ukiingia wameweka tangazo kuwa hata kupiga mswaki na kusukutua utumie maji yaliyochemshwa au wanakuwekea maji ya chupa bafuni kwa ajili ya kupigia mswaki.

    Inawezekana aliyefanya utafiti wa

    taifodi na jinsi inavyoambukizwa ni Alexander na maelezo anayotoa yasiwemo kabisa kwenye Quran na Hadithi, maana Qurna ni Kitabu cha Mwongozo, sio kitabu cha sayansi au taaluma nyingine muhimu katika maisha. Mengine katika maisha unasoma na kufanya utafiti mwenyewe au unauliza wajuzi ikiwa hujui. Sasa wewe kachote maji mtoni Morogoro unywe bila ya kuchemsha, maana tahadhari inayotolewa na kafiri juu ya taifodi na kipindupindu haikubaliki katika Uislamu!!!

    We Funded The Wahhabis We Are Fighting Today- Hilary Clinton Confesses .

    Hiyo ni taarifa ambayo ilisambaa sana wiki iliyopita ambapo sehemu ya mazungumzo ya Hilary Clinton, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani wakati wa awamu ya kwanza ya urais wa Barack Obama iliwekwa katika mtandao. Ukifungua: We Funded The Wahhabis We Are Fighting Today, bado utaikuta ambapo Clinton anasema kuwa wao ndio walio waandaa Mujahidina wakapigane na Mrusi kwa niaba yao kwa sababu walijua hiyo itakuwa vita ya muda mrefu na ya gharama kubwa kwa maana ya kuuliwa askari wengi. Wakaone Waislamu wakafe kwa niaba ya askari wa Marekani na kwa malengo ya Marekani. Lakini ili ionekane ni agenda ya Waislamu, waakamua misaada na mafunzo yapitie Pakistan na Saudi Arabia. Muislamu akiona ni makachero na Masheikh wa Pakistan na Saudia, wanao wakusanya na kuwapiga dawah juu ya Jihad Afghanistan, wataamini kuwa hiyo ni Jihad ya kweli. Na ndio hivyo hivyo Saudia na Qatar zinavyotumika katika suala la ISIS hivi leo.

    Akihojiwa hivi karibuni na Fox News Hilary Clinton, anasema:

    We have brilliant idea. We created these mujahideen. We said, lets go to Pakistan create these mujahideen, equip them, we send them missiles and everything. And we were successful. The Soviet left Afghanistan. We said, great, good bye, leaving these trained people who are fanatical in Afghanistan and PakistanSo the people we are fighting today (ISIS), we created them.

    Sasa leo wewe ukisema kuwa huyaamini haya anayosema Clinton kwa sababu hayapo katika Quran na Sunnah na Clinton mwenyewe ni kafiri, haitaondoa ukweli huo.

    Sana sana utakuwa tu unathibitisha yale aliyosema Bi Clinton kuwa miongoni mwetu Waislamu wapo fanatics (mashabiki, walokole wachemkaji wasiotumia akili) na ndio hao wanaotumiwa katika proxy war.

  • 8 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014MakalaNa Omar Msangi

    Inaendelea Uk. 9

    KATIKA miaka ya 1980s wakati nipo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, niliwahi kuhudhuria semina Kuala Lumpur, Malaysia, iliyokuwa imeandaliwa na The International Islamic Federation of Student Organizat ions (IIFSO), kwa pamoja na The International Institute of Islamic Thought (IIIT) wakishirikiana na Vijana wa Harakati za Kiislamu, wakijul ikana kwa j ina la Angkatan Belia Islam Malaysia (ABIM) au Malaysian Islamic Youth Movement.

    Pale Bombay (sasa Mumbai), mji mkuu wa Jimbo la Maharashtra, nilikaa zaidi ya masaa 24 kusubiri kuunganisha ndege, kwa hiyo ikabidi nipelekwe hotelini. Baada ya kupata chakula katika hoteli niliyoshukia, nilitoka kutembea kuangalia mji. Sikufika mbali. Ilibidi nirudi. Sikuweza kuhimili kero ya kuzongwa na ombaomba, akina mama, watoto, wazee mpaka watu wazima wanaume na wazee. Waliowahi kufika India, watanielewa.

    Kwa wakati ule mimi haikunijia akilini kuwa nchi za ughaibuni, nje ya Afrika, nazo zaweza kuwa na kundi la masikini wa kutupwa na ombaomba wa kiwango kile. Wakati huo nilikuwa sijajua kuwa katika India kuna watu wanawekwa katika kapu la untouchable Dalits.

    Pamoja na mambo mengine, katika semina ile, palijadiliwa m a t a t i z o ya n a y o wa k a b i l i Waislamu katika elimu na ikatajwa kuwa tatizo kubwa ni, mtizamo potofu katika elimu na dunia. Kwamba mtizamo kuwa kuna elimu ya dunia na elimu ya akhera, au elimu ya kikafiri na elimu ya dini (ya Kiislamu), limekuwa ni tatizo kubwa na lau Waislamu hawatafanya juhudi kubwa kulitatua, litawaangamiza. Ni katika zama hizo ambapo, tatizo la mgawanyo katika elimu (Crisis of Duality in Education Systems and Disciplines of Knowledge), kwa maana hii ya kuwa na elimu ya madrasa na elimu ya shule kama vitu viwili tofauti, lilizungumzwa sana. Ukiacha kuwa mtizamo huo, unazaa makundi mawili ya Waislamu wanaokinzana, lakini pia huzalisha wasomi Waislamu waliochanganyikiwa na hivyo wanakuwa hawana msaada wowote wa maaana katika jamii ya Wauslamu wala nchi kwa ujumla. Makundi mawili yanayokizana ni lile linaloitakidi kuwa elimu ya manufaa ni ya madrasa (dini) pekee, na kundi la pili, ni lile linalokwenda shule na kuona kuwa hawa wanaobaki katika madrasa na vyuo vya Kiislamu, wakisoma dini, hawana kitu.

    Ilikuwa ni katika kutatua tatizo hilo, wasomi wa Kiislamu walikuja na kitu kilichoitwa Islamization of Knowledge. Hata hivyo, msamiati huu nao ulionekana kuwa una matatizo. Unaposema

    Msiba! MSAUD imefia wapi?Hakuna historia, Civics ya kikafiriVidato bila kuelimika ni balaa tupu

    Islamization of knowledge, unachosema bila kutamka ni kuwa elimu ni ya kikafiri sasa unataka kuisilimisha. Lakini hakuna elimu ya kikafiri, bali kuna mawazo ya kikafiri na mtizamo wa kikafiri. Unapozungumzia civics au sosholojia kwa mfano, hii ni taaluma ya namna jamii zinavyoishi na kuhusiana katika mambo mbalimbali ya kijamii, kisiasa, kisheria, kiuchumi, uongozi na mambo kama hayo. Sasa hayo ni mambo ambayo yapo katika jamii yoyote, iwe ya Kiislamu au ya kikafiri . Kitakachotofautisha ni itikadi na mtizamo. Kama ni Kiislamu, civics (elimu ya uraia) itayatizama mahusiano hayo kwa misingi ya Kiislamu. Kama ni ya kishirikina hivyo hivyo. Kwa hiyo, civics ya Wahindu, itaitizama jamii ya India katika mtizamo wake wa kuwa na ubaguzi- The caste system ambapo utawakuta varnas, Brahmins, Kshatriyas, Vaishyas na Shudras. Wapo pia wale untouchable Dalits.

    Muislamu wa India hawezi kusema kuwa kusoma historia iliyozaa untouchable Dalits a u c i v i c s n a s o s h o l i o j i a ya India inavyoeleza j ins i makundi ya varnas, Brahmins, Kshatriyas, Vaishyas na Shudras, yanavyowiana katika jamii ni ukafiri. Ukafiri ni mfumo huo wa kibaguzi na itikadi iliyouzaa. Na kama hukusoma ukajua hayo matatizo yaliyo katika jamii, na chanzo chake, utaisaidiaje jamii kuepukana na mfumo huo mbaya? Suala ni kuondoa itikadi iliyojenga ushirikina, sio kuacha kusoma kwa hoja kuwa historia ya India ni ukafiri.

    I n a w e z e k a n a c i v i c s inayofundishwa katika shule za Tanzania ikasema kuwa hakuna kuoa mke zaidi ya mmoja. Kuzini sio haramu ilimuradi usipate

    ukimwi au kumtia mimba mtoto wa shule. Civics hiyo hiyo inaweza kukuambia kuwa mtoto wa zinaa ana haki ya kurithi, jambo ambalo ni kinyume na Uislamu. Civics hii inatofautiana vipi na ile tunayosoma katika darsa zetu Misikitini na katika vyuo vya Kiislamu kuwa Maquraishi wa Makkah walikuwa wakiwazika watoto wao wa kike wakiwa hai, mpaka Quran inasema: Waidhaal mauudatu suilat. Bi ayyidh dhanbin qutilat! Au civics hii inayofundisha kuwa Waarabu wa Makka waliwazika watoto wao wa kike wakiwa hai ni ya Kiislamu? Au ni ukafiri nayo pia haifai kufundishwa itolewe ndani ya Quran na vitabu vya Kiislamu?

    Ni hivyo hivyo tunasoma katika Maarifa ya Uislamu, jinsi ukafiri na ushirikina ulivyokuwa umetawala Makkah na Madina watu wakiitakidi kuwa kuna miungu wengi-Mungu wa jua, mungu wa mvua, mpaka tende

    zilitengenezwa miungu watu wakishikwa na njaa wananyofoa mkono wa Mungu wanakula. Katika Quran, Allah anatueleza kuwa Makuraishi walidai kuwa malaika ni watoto wakike wa Mungu. Kisha tunaelezwa kisa cha Qaumu Lut na ubaradhuli wao mpaka wakagharikishwa.

    Swali ni je, kusoma historia hii iliyoelezwa katika Uislamu na ndani ya Quran (kwa maana ya elimu), ni ukafiri? Au historia hii ni Uislamu?

    Sasa kama leo kuna watu wanasema kuwa binadamu katokana na nyani, hawana tofauti na wale waliochonga masanamu wakayaabudu na historia yao ikaelezwa katika Quran. Hili ni somo. Hii ni rekodi na historia ya maisha ya watu na mambo yao. Suala hapa ni kuwajua na kutafuta namna ya kuuokoa ulimwengu na dhana potofu juu ya kuumbwa kwa ulimwengu na vilivyomo.

    Kama nilivyosema, katika Quran tunaelezwa visa vya akina

    Ad, Thamud, watu wa Nuhu, Qaumu Lut, n.k. Hiyo ni historia. Halikadhalika leo tunajifunza juu ya kuja wakoloni Afrika, Wareno, Wajerumani, Waingereza, na jinsi wazee wetu akina Suleiman Mamba, Bushir i , Mkwawa, Mirambo n.k, walivyopambana nao. Hiyo ni historia, sio ukafiri. Lakini ambalo ni la ukweli ni kuwa historia inategemea nani anaandika. Kama kwa mfano Watanganyika hatutaandika historia yetu, tukategemea historia iliyoandikwa na Wazungu waliotutawala, wao hawataandika kuwa walikuja kututawala na kupora mali, watasema walikuja kutuletea ustaarabu. Sasa tatizo hapa sio Mzungu wala historia kuwa ni ukafiri. Tatizo ni wewe uliyekuwa mvivu na labda mjinga usiyejitambua kiasi cha kushindwa kuandika historia yako mwenyewe ukangoja watu wengine ndio wakuandikie.

  • 9 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014MakalaInatoka Uk. 8 Msiba! MSAUD imefia wapi?Mohamed Said (Historian), amezungumzia sana jambo hili akionyesha jinsi historia ya Tanganyika ilivyopotoshwa. Kwamba u le mchango wa wazee wa Ki is lamu kat ika kupigania uhuru wa nchi hii, umetupwa kabisa wala wazee hao kama Sheikh Ramia, Dossa Aziz, Mshume Kiate, Suleiman Takadiri na wengineo, hawatajwi kabisa. Historia ya kupigania uhuru Tanganyika imefanywa ni simulizi za kumsifu Nyerere. Hata wale wazee waliompokea Nyerere Dar es Salaam wakamvua kaptura aliyokuja nayo kutoka Musoma wakamshonea suruali ili awe muungwana kama Waislamu wa Pwani , hakuna mahal i popote wanapotajwa. Sasa hapa Waislamu hawawezi kulaumu historia, wakasema historia hii ni ya kikafiri. Wajilaumu kwa nini mpaka sasa hawajaandika historia sahihi ya nchi hii na kuwafundisha watoto wao. Kwa nini wameruhusu historia ikapotoshwa na wanachukua hatua gani. Kudai kuwa historia ni ukafiri, ni kutangaza ujinga wa kutokujua hata maana ya historia.

    Hakuna fizikia wala uhandisi wa kikafiri

    Jamaa yangu Said Omar Nsigarila aliniambia siku moja kuwa wakati wapo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwalimu wao wa fizikia baada ya kusomesha mada juu ya maumbile ya maji na kanuni zake ikiwemo ile kwamba maji yakiganda huwa mepesi na hivyo huelea juu jambo linalosababisha kuwa katika nchi za baridi wakati wa kipupwe (winter) theluji huelea juu ya bahari na yasiyo ganda hubaki chini jambo linalowezesha samaki na viumbe wengine baharini kuendelea kupata uhai. Mhadhri huyo alipomaliza kusomesha akawa anasema kuwa akina Nsigarila wao hawana tabu katika hili, akimaanisha kuwa Nsigarila (na Waislamu wanaoamini juu ya kuwepo kwa Mungu), wao wataona na kusema kuwa hayo ni kwa ajili ya uwezo wa Mungu Muumba. Na ndio pale Quran inaposema kuwa hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, zipo alama za kuonyesha kuwepo kwa Mungu Muumba na uwezo wake.

    Sasa iwapo Waislamu wataacha fizikia, kemia na elimu zingine zifundishwe kwa mtizamo wa kikafiri, badala ya kusema huo ni uwezo wa Allah mhadhiri akasema, nature is so kind, k a m a y u l e m u h a d h i r i wa Nsigarila, tatizo hapa sio la fizikia. Fizikia itabaki kuwa fizikia wala hakutakuwa na fizikia ya Kiislamu au ya Kikristo.

    K a m a w e w e u n a s o m e a uhandisi, kanuni za uhandisi katika ujenzi iwe ni wa majengo,

    madaraja, au barabara, zitabaki zilezile duniani kote, iwe ni katika nchi ya Kiislamu au ya kikafiri. Ila msomeshaji anaweza kutia maneno yake ya kikafiri na kishirikina lakini sio kubadili kanuni za kiuhandishi za ujenzi. Unajua kwa nini? Kwa sababu katika uhandisi unacheza na udongo (soil analysis), vyuma, kokoto (mawe), saruji, miti na vyote hivyo vimeumbwa na Allah na vikawekewa kanuni fulani ambazo kwa elimu ya fizikia, kemia na hesabu, binadamu anavitia katika matumizi. Kanuni hizi, hazitegemei mtumiaji kuwa ni kafiri au Muislamu. Zitafanya kazi Makkah kama ambavyo zitafanya Vatican. Na wewe ukizikosea hata kama ulikuwa unazitumia kujenga (kukarabati) Msikiti wa Makkah au wa Mtume Madinah, utaporomoka.

    Ukafiri hauwezi kubadili fomula ya photosythesis au kubadili vitu vilivyoko ndani ya cell-mitochondria, ribosome,

    cytoplasm, centriole, lysosome, nucleus, nucleolus, .nk. Hivi ni vitu kaviumba Allah, na elimu ni kuvisoma na kujua namna ya kuvitia katika matumizi ya binadamu. Allah anasema, akitaka jambo kuwa ni kusema kun fayakun. Lakini kajaaliya kupatikana kwa chakula chetu na kuzalishwa kwa oxygen, carbon dioxide na mzunguko wake, upitie mfumo fulani ambao tunausoma shuleni. Kama photosynthesis imeumbwa na Allah kuisoma sio ukafiri. Kama law of floatation inategemea Allah alivyoumba vitu akavipa density tofauti tofauti na akaweka kanuni za mahusiano baina yao katika hali tofauti tofauti (mpaka tunaweza kuunda meli na ndege), kusoma hayo, si ukafiri. Ila msomeshaji anaweza kusomesha kwa mtizamo wake wa kikafiri au wa Kiislamu.

    Il i kutatua tatizo la nani anasomesha na anasomesha katika mtizamo gani, ndio IIIT, wakaja na dhana ya Islamization of Knowledge,

    ambayo kama nilivyosema, baadae ikaonekana kuwa inapeleka ujumbe potofu kwa sababu inajenga dhana kuwa kuna elimu ya kikafiri. Msamiati ukabadilika sasa unaotumika ni Integration of knowledge. Na watu wapo kazini wakiandika vitabu na kutengeneza mitaala. Semina iliyomalizika katika Chuo Kikuu cha Waislamu, Morogoro wiki iliyopita, ilikuwa ni katika kutizama jambo hili na namna ya kulifanikisha katika Tanzania na kanda ya Afrika. Kwengine kama ilivyotolewa mfano wa Indonesia, Waislamu wamepiga hatua kubwa sana ambapo hivi sasa vyuo vikuu wanasomesha fani mbalimbali, wakiwa wametengeneza mitaala na vitabu vya taaluma mbalimbali kwa kuzingatia epistemolojia ya Kiislamu.

    Kwa nini nimesema yote haya na kwa urefu kiasi hiki? Kama ambavyo sikujua kuwa kuna dalits, ombaomba kule India, tunao watu wenye visomo, lakini wanahitaji kuelimishwa.

    Wakati tunasoma Chuo Kikuu Dar es Salaam, ilikuwa ummah wa Kiislamu Tanzania, likitokea jambo, hukaa wakisikiliza Wanafunzi wa Kiislamu Chuo Kikuu-Muslim Students Association of UDMS (MSAUD) wanasemaje juu ya jambo hilo. Na ilikuwa watu wakitoka mjini kuja kuswali Ijumaa katika msikiti wa Chuo Kikuu ili kusikia wasomi wanasemaje katika jambo lililotokea, kwa maana kuwa watal i tolea ufafanuzi na kutoa mwelekeo sahihi kwa Waislamu.

    Jumamosi ya wiki i l iyopita, nil ipokea ujumbe wa maneno (sms) ambao ningependa wasomaji wengine nao wapate faida kutokana na yaliyomo. Unasema:

    Unakataa elimu ya circular (sekula) sio ya kikafiri unatolea mfano biology, physics, chemistry, mbona umeacha civics au hujui kwenye civics kuna masuala ya kupinga ndoa zaidi ya (mke) mmoja, kumuozesha binti akiwa mdogo, yaani early marriage, kuna mambo chungu mzima ya kupinga Uislamu. Kuna history, kuna Kiswahili, kuna geography, hata hiyo physics na biology na chemistry ina mifumo ya ukafiri hata kuiendea elimu yenyewe mfumo wake siyo wa Kiislamu. Ni kweli mimi nakubali ni ukafiri na siyo tu kwa kusikia. Nimesoma kuanzia form one nikaenda form five na six PCM sasa niko civil engineering mwaka wa tatu Mlimani COET (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam). Na hata kama nimesoma nikafika huko, haki lazima izungumzwe watu wafahamu kwamba elimu ya circular ni ukafiri kuna mambo mengi yanapinga Kitabu cha Allah lazima watu waelezwe waelewe. (0713 033 978).

    Sina hakika kwamba huyu ni katika viongozi na wanakamati wa MSAUD au ni mwanajumuiya tu ya MSAUD!

    Nimetaja uwepo wa taasisi ya The International Institute of Islamic Thought (IIIT), ambayo inatizama namna ya kuondoa tatizo la duality katika elimu. Na kwa hakika mpaka sasa wamefanya kazi kubwa sana.

    Waswahili wana msemo wao, mkono husafishwa ukichafuliwa na mtoto, haukatwi. Waislamu wameacha makafiri wanachafua e l i m u , wa o n d o e u c h a f u , s i o kuharamisha elimu na kuikimbia.

    PICHA juu ni kielelezo cha umasikini wa untouchable Dalits, India.

  • 10 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014MakalaNa Michael Albert

    "NYUMA ya kila gaidi wanasimama dazeni kadhaa za wanaume na wa n a wa k e , a m b a o b i l a wa o asingeingia katika ugaidi. Wote ni wapiganaji wa maadui, na damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao. Sasa hao ni pamoja na mama wa mashahidi, ambao waliwapeleka jehanam kwa maua na mabusu. Watawafuata wana wao, hakuna haki zaidi ya hiyo. Waende, kama zilivyo nyumba zao ambazo ziliwalea hao nyoka. Vinginevyo, vijoka vingine vidogo vitalelewa humo."-Ayelet Shaked, mbunge wa Israel

    M i m i n i M y a h u d i l a k i n i utambulisho huo haunielezi nilivyo. Nilikuwa Bar Mitzvah-ed, lakini siku hiyo ilimaliza uhusiano wangu wa kidini. Nilibwabwaja aya kadhaa za kukariri za Kiyahudi ambazo kwa yakini sikuwa nazielewa. Nilisherehekea (ibada) kwa sababu tu ilinibidi kufanya hivyo. Familia, na mengine yote.

    Zaidi, mara nyingine, mara moja tu tangu au kuanzia hapo, ambako nimekuwa, binafsi nimekutana na chuki dhidi ya Wayahudi, ana kwa ana. Mzazi wa binti mmoja niliyekuwa natoka naye aliongea kitu cha kuudhi kuhusu Wayahudi kushikilia dunia na karibu ningemzaba vibao. Sina subira nyingi kwa ubaguzi katika hali yoyote, lakini nilishangaa kuwa upuuzi aliokuwa anaongea ulinivuruga akili kwa kiasi ulichofikia. Haikuwa suala la uhusiano wa damu, na kwa hakika halikuwa suala la imani za dini ambazo zilisababisha nilichohisi. Hivyo labda kuyasema 'maswali manne' mara kadhaa kama mtoto kumekuwa na athari ya kitamaduni.

    Hivi mabaki ya utoto wangu ya ushiriki kwa namna fulani katika Uyahudi, kwa mfano kumpenda Rabbi Schankman wa Hekalu Israel hadi nikafikia umri wa miaka 13, kunanifanya mimi, sasa, kuhisi kwa nguvu kuudhiwa na kuchoshwa na matukio ya sasa ya Gaza tofauti na kama nisingefika katika Hekalu mara kadhaa? Sijui, ila sidhani kama suala hilo linabadilisha chochote. Kinacholeta maana ni umwagaji damu wa kut i sha unaotokea Gaza. Hata hivyo kina matukio mengi ya umwagaji damu. Hivi maneno yanaweza kufanya hiki kinachoendelea kuingia katika orodha ya wenye mataji ya uovu?

    Maiti? Ndiyo. Maiti zimejazana. Majengo yaliyovunjwa? Ndiyo. Mirundiko ya mawe na vumbi imejaa na inaongezeka.

    Nilipokuwa ninafikia ukubwani, utumiaji nguvu ulikuwa ni Vietnam. Katikati ya hilo, nilijiuliza jinsi binadamu ambao wamefurahia hata uhuru binafsi kidogo tu na maendeleo, tofauti, kwa mfano, na kupigwa na kufungiwa wakiwa watoto, na kukataliwa elimu na maendeleo ya fahamu zao, wanaweza kuwa hata chembe wasiojali na kujidanganya kama serikali ya nchi yangu ilivyokuwa.

    Ila wakati "kuuangamiza mji ili kuuokoa" kuliweka kiwango cha juu sana cha udhihirishaji wa uovu - siwezi kukwepa kuona hitilafu ya

    Kuua 'nyoka' na nafsi

    kina ya kipengere cha 'kuuokoa.' Wakati huo, na zaidi tangu harakati za wakati huo na athari zake, hata bila kuongeza kingine, kuendeleza vitendo vya kidhalimu kwa sababu za ki-dola au za kutafuta faida kulihitaji madai ya nguvu ya kimaadili. Ila, kwa wa-Israeli, hilo halielekei kuwa kweli.

    Ndiyo, kwa ajili ya utumiaji wa kimataifa wanatengeneza uhalalishaji wa kipuuzi - kimsingi wanasema huu ni ulinzi wetu dhidi ya wao kujilinda wenyewe, Na, ili kuwa wazi, kwa wale wanaosema kuwa Israel ina haki ya kujilindaa, kuna jibu moja tu sahihi. Ndiyo. Inayo.

    Na kinachomaanishwa hapo ni kukwepa kushambuliwa na wanaokaliwa kwa mabavu. Israel inaweza kuondoka Gaza, kuondoa ukaliaji, kuondoa ubaguzi. Hiyo ndiyo njia pekee ya jeshi la ukaliaji - kokote, wakati wowote - kujilinda dhidi ya waliokaliwa kikoloni. Acha kuendeleza uhalifu. Suluhisho ni kuondoka. Kama huelewi hilo, lifikirie kwa njia hii. Fikiria Waingereza waliokuwa Marekani wakipigana na waliochukua ardhi kule kuifanya kuwa koloni lao wawambie, 'hamjui, tuna haki ya kujilinda.' Jibu hapo lingekuwa" ndiyo, mnayo, na haki yenu ya kufanya hivyo inahalalisha kuondoka kwenu, ila siyo kutuelekezea risasi sisi.

    Au ingekuwa vipi kwa ma-Nazi nchini Ufaransa, au labda mfano bora zaidi ni ma-Nazi nchini Poland - jijini Warsaw. Fikiria wangesema, lo! Tuna haki ya kujilinda. Pia jibu lingehitaji kuwa, ndiyo, mnayo, na haki hiyo inahalalisha kuondoka kwenu, na siyo kuangamiza maisha yetu, utamaduni na majengo.

    Ni hivyo pia kwa Marekani katika maeneo ya kingo za kusini mashariki ya Asia (Vietnam, Laos na Cambodia). Na pia kwa Israeli eneo la Gaza. Jilindeni, kwa hali yoyote, kweli, na ili kufanya hivyo, tokeni. Ila hiki sicho ninachotaka kusema katika kihadithi hiki. Ila nataka kuainisha kitu kipya kuhusu matukio hayo, labda yanayohitaji maneno machache.

    Ni kuwa wa-Israeli wanaonekana kuridhika, hasa kwa matumizi ya ndani, na kwa kiwango fulani hata kimataifa, kutokubabaisha ni nini wanachokifanya.

    Bisha hodi - kinachoropoka kifaa cha kurusha kombora darini. Mlio mkubwa, na hospitali iliyo chini yake imeteketea. Usiwe na wasiwasi. Ni 'nyoka wafu' waliokuwa wanatibiwa n a n y o k a w a f u w a l i o k u w a wanawatibu.

    Simu inalia. Badala ya nyumba kuna lundo la matofali na vumbi. Usiwe na wasiwasi. Ni vitoto vya nyoka vilivyokufa na nyoka wafu mama zao. Ni maskani mengine ya nyoka yamegeuzwa jivu. Huree!

    Ni wazi kuwa huu ni uharamia. Kama huoni hilo, sijui ni kwa njia gani naweza kukuwezesha kuelewa hilo. Lakini suala ni kuwa 'tahadhari' hizi unaweza kuziona ni wazimu. Ni mzaha wa kutokujali kuwaambia watu watoke wakati wanapoweza kwenda ni mahali ambapo panafuata katika orodha ya kupigwa. Tahadhari hizo pia zinaonyesha kwa ushahidi wa wazi, usioweza kabisa kupingika, ambao nchi nyingi zinajaribu kuficha, au kutokuwa na hatia ya hilo katika mazingira bora zaidi.

    Ni kuwa, kubisha mlangoni k u t a n g a z a k i l e k i n a c h o k u j a kunaonyesha kuwa wa-Israeli hawapigi majumba na mahospitali na mengineyo katika maisha ya Gaza na kufaulu kwa kukisia, lakini kwa dhamira. Kugonga mlango ni kusema, tunaweza kupiga popote tunapotaka, hadi kufikia vijumba vidogo, kokote tunapoteka, hadi kichembe cha mwisho. Ni kama wanasema, angalia tulichofanya. Mnaona vitoto vimelipuliwa na kuchakazwa? Mnaona hospitali imegeuzwa jivu? Mnaona kituo cha umeme kinatoa tu miali ya moto kukizunguka? Mnaona shule ile, msikiti ule, bustani, ufukwe, vituo vya kujaza maji vyote vimegeuka milundiko ya vumbi na binadamu waliochakazwa? Hiki mnachoona ndicho hasa tulichotaka kufanya. Hakuna uharibifu usiotarajiwa. Kuna uharibifu uliolengwa. Sisi

    wa-Israeli kimsingi tunataka kuua chochote k inachotembea . Na tunataka kuwaambia wale ambao bado wanatembea wakati tukiwa tumekamilisha kazi kuwa tulifanya hivyo, kwa makusudi. Tunajua jinsi ya kushawishi hisia!

    Nilipokuwa nasoma sekondari nilikuwa nakaa hadi usiku wa manane, mara kadhaa, kujaribu kufikiria jinsi mtu anavyoweza kuwa Mjerumani mwema. Ni kwa jinsi gani ambako watu wanaweza kuendelea na shughuli zao za kila siku wakati nchi yao ikiwa inaendesha jehanamu ya kutisha ya ukiukwaji wa haki - kwa jambo hilo, mitambo ya kuulia (hasa Wayahudi). Ila nilielewa baada ya muda. Msukumo wa kutaka kumudu, wa kutaka kustahili nafasi fulani na kutokufikiri kuna njia nyingine, na, kwa watu wengi zaidi, utulivu unaoletwa na kutokujua (kunakolindwa kwa kuuliza maswali machache kama mtu atauliza chochote), na, kwa watu wengi zaidi, woga wa kijinga na hamu ya kiasi iliyokuzwa kwa makusudi, ndiyo yaliyofanikisha. Na nikaona hayo pia katika vita ya Marekani kusini mashariki ya Asia, na kuhusu ushindi wa ubaguzi, na sasa pia, kama tunavyoteketeza mazingira. Hivyo ninalipata hilo.

    Ila kuna makundi ya askari wanaovamia na kutenda hayo. Ni 'brownshirts,' wanaovaa kaki za kahawia. Hii ni ngumu zaidi kueleza. Nilikuwa nadhani labda kulikuwa na hitilafu fulani katika lugha ya Kijerumani - nilokuwa najua hawana vinasaba tofauti na wengine walikuwa, hata hivyo, wakiongea kwa njia tofauti. Halafu nikajifunza kuwa mafunzo yanayozalisha askari, na kwa upungufu kidogo zaidi yale yanayozalisha watu wazima, kimsingi yanalenga kuondoa uwezo wa kufikiri kibinadamu na hisia hiyo. Na kuwa wengi wanaanguka. Hivyo sasa tunao wa-Israeli. Na uwezo wa kujidanganya na ukosa mantiki wa kukataa kilicho wazi, na hata dhamira ya kudhuru ya kifashisti, miongoni mwa watu kwa jumla - hata kama wasingedai kila wakati kuwa na uelewa wa ndani na maalum wa uovu wa ubaguzi - ni wa kushangaza. Inasikitisha kweli. Inachukiza.

    Hata nikiwa nalilia uchungu wa Palestina na kutumainia kuwa watashinda, sehemu yangu pia inajiuliza, wakati vumbi likitulia, hivi wa-Israeli wanaohimiza kufumuliwa kwa miali ya moto Wapalestina na Wapalestina watasema nini miongoni mwao ili waweze kuishi na nafsi zao? Maiti ambazo zinaonekana kabisa kama watu zilikuwa kweli ni nyoka? Au labda nilikuwa, kwa muda mfupi angalau, zimwi? Na wanawaambia nini watoto wao? Ili waweze kuishi na watoto wao. Na ili watoto wao wasiwe mazimwi - mtu unatazamia.

    Na kwa kina zaidi, vipi kwa wa-Marekani wenye historia inayonuka ya kuunga mkono uuaj i huu watajieleza? Na kuwaambia watoto wao? Na nahofia jibu litakuwa hapana kabisa. Kwani kopo la jivu la historia - ambalo ni CNN na New York Times - yataziba hisia ya ukosaji na ukweli kwa njia ya majitaka ambayo wanaripoti.

    (Makala hii Killing Snakes and Self kama ilivyoandikwa na Michael Albert,

    imefasiriwa kwa Kiswahili na Anil Kija)

  • 11 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 2014Makala

    TUKITUPIA jicho yale yanayofanywa na makundi haya itafahamika wazi malengo hasa ya makundi hayo. Kwa mfano, mambo yanayofanywa na Boko Haram Nigeria kama mauaji kuwateka nyara wasichana wa shule na mengine mfano wa hayo, ni matukio ambayo humfanya mtu kwa uchache kutilia shaka kama kweli kundi hilo linapigania Uislamu na haki za Waislamu. Sasa limeibuka kundi Dola la Kiislamu la Iraq na Sham kwa kifupi DAESH. Imekuwa ni jambo la kawaida kusoma au kusikia katika vyombo vya habari juu ya jinai na mauaji ya kutisha yanayofanywa na kundi hili. Kwa hakika kundi hili la kigaidi ambalo licha ya kudai kuwa linafuata mienendo ya jihadi ya kisalafi, lakini kwa hakika ni mfuasi wa fikra potofu za Kiwahabi ambazo ni fikra mgando na zilizopitwa na wakati. Kwa maana kwamba, mitazamo na fikra kama hizi hazina nafasi kabisa katika ulimwengu wa Kiislamu.

    Kundi la Daesh hutumia ukatili, utesaji namauaji ya kutisha ambapo mfano wa jinai hizo ni mauaji ya umati ya raia wasio na hatia nchini Syria, mauaji ambayo hutekelezwa hadharani na kuwajumuisha watoto wadogo, wanawake na vizee. La kusikitisha zaidi ni kwamba, kundi hili la kigaidi linafanya mauaji haya kwa jina la Uislamu na utawasikia wakisoma dua ndefu na kumsabihi Mwenyezi Mungu kabla ya kumchinja mtu au kumpiga risasi.

    Uislamu upi na Mungu yupi anayeruhusu kuuawa nafsi isiyo na hatia yoyote? Je hii ni jihadi ya kutaka kuasisi dola la Kiislamu au ni ugaidi na jinai dhidi ya binadamu? Harakati za kundi la Daesh kwa hakika ni fitna kubwa ya karne. Msiba mkubwa zaidi ni kuwepo watu wanaoshabikia mauaji ya kundi hilo na kuwamiminia sifa lukuki wapiganaji hao wakiwaita kuwa ni mujahidina. Historia ya kundi hilo inarejea nyuma mwaka 2004, yaani wakati Abu Mus'ab Zarqawi alipoasisi mtandao uliokuja kujulikana kwa jina la Jama'at Tawhid wa Jihad huku akiwa kiongozi wake. Baada ya Zarqawi kutangaza utiifu wake kwa Osama bin Laden, mkuu wa zamani wa mtandao wa al-Qaida, kundi hilo liligeuzwa na kuwa tawi la taasisi ya al-Qaida nchini Iraq. Baada ya Marekani kuivamia Iraq, kundi hilo taratibu lilijionyesha kuwa lililokuwa likiendesha jihadi dhidi ya vikosi vya Marekani nchini humo. Ni kutokana na hali hiyo ndio maana vijana wengi waliokuwa wakitaka kupambana na vikosi hivyo

    vamizi, wakajiunga nalo ambapo haraka likageuka na kuwa kundi lenye nguvu la wanamgambo nchini Iraq.

    Mwaka 2006 Zarqawi aliuawa na uongozi wa kundi hilo ukachukuliwa na Abi Hamzah al-Muhajir ambaye alikuwa kiongozi wa mtandao wa al-Qaida nchini humo na mrithi wa Zarqawi mwenyewe. Mwishoni mwa mwaka 2006 kuliundwa kundi la wanamgambo kupitia makundi kadhaa ya Iraq ambalo lilikuja kujulikana kwa jina la 'Daulatul-Islam fil-Iraq huku kiongozi wake mkuu

    Kundi la Daesh; Mujahidina au Magaidi?Na Salum Bendera SWAHIBA wangu mmoja siku zote hupenda kusisitiza

    kwamba, katika ulimwengu wa leo asiye na elimu au weledi na ufahamu wa mambo ya dunia yake basi ataishi kwa taabu na atakuwa mfano wa bendera ambayo hufuata upepo. Tukiachana na ya sahiba wangu hayo, waswahili wana msemo wao mashuhuri usemao: Usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Hivi ndivyo hali ilivyo hii leo katika ulimwengu tunaoishi. Vyombo vya habari vya Magharibi vimehodhi kila kitu; lakini kwani ukweli unaweza kuuficha siku zote? Ghiliba na hadaa za Wamagharibi zimefahamika sasa. Kwa hakika njama za Wamagharibi dhidi ya Uislamu hazikuanza leo wala jana; lakini bila shaka katika siku za hivi karibuni zimeshadidi mno.

    akiwa ni Abu Omar al-Baghdadi. Mwezi April mwaka 2010 vikosi vya Marekani vilimuua Abu Omar al-Baghdadi na Abu Hamzah al-Muhajir katika operesheni ya kijeshi. Ni baada ya hapo ndipo Abu Bakar al-Baghdadi alichukua uongozi wa kundi hilo akimrithi Abu Omar al-Baghdadi. Mwanzoni mwa mwaka 2011 sambamba na kuanza kwa mgogoro na vita nchini Syria, kundi

    linalojulikana kwa jina la 'Jab'hatu Nusra kwa ajili ya Watu wa Sham' ambalo ni tawi la Dola la Kiislamu la Iraq liliundwa nchini humo humo na haraka likageuka kuwa moja ya makundi yanayoendesha vita dhidi ya serikali ya Rais Bashar al-Assad. Hatimaye mwaka 2013 Abubakar al-Baghdadi alitangaza kuyaunganisha pamoja makundi ya, Jab'hatu Nusra na Dola la Kiislamu la Iraq na kuzaliwa

    kundi la 'Daulatul-Islam fil-Iraq wa Sham ' kwa kifupi Daesh (ISIS). Hata hivyo upinzani wa al-Qaeda dhidi ya hatua ya kuyaunganisha pamoja makundi hayo na uungaji mkono kwa Jab'hatu Nusra, uliibua vita kati ya Daesh na kundi la Jab'hatu Nusra nchini Syria, vita ambavyo hadi sasa vimeshapelekea zaidi ya wanamgambo 1000 wa makundi hayo kuuawa.

    Mbali na jinai na mauaji ya kinyama ya DAESH, kundi hili limekuja na mambo ya ajabu ajabu kama Jihad Nikah. Wachambuzi wa mambo wanasema huu ni uzinzi na ukandamizaji kwa jina la jihadi ya ndoa. Magaidi hao wa Kitakfiri hivi karibuni waliamua kufungua ofisi za ndoa kwa shabaha ya kuwarubuni wanawake ili waelekee Syria na Iraq kwa shabaha ya kuwahudumia wanamgambo wa kitakfiri wa kundi la Daesh wanaopigana na serikali za Syria na Iraq. Shirika kutetea haki za binadamu la Human Right Watch (HRW) lilitangaza kuwa, magaidi wa kitakfiri wamefungua ofisi hizo katika mji wa al Bab ulioko katika jimbo la Halab nchini Syria. Wanamgambo wa Daesh wamekuwa wakiwashawishi na kuwarubuni wanawake na wajane kuorodhesha majina na anwani za makazi yao kwa lengo la kwenda kutoa huduma ya ngono kwa wanamgambo wa Daesh. Sasa hawa wanaweza kuitwa mujahidina au ni magaidi wanaotenda jinai kwa jina la Uislamu? Hivi kweli kundi hili limeufahamu Uislamu unavyoapaswa?

    Waislamu tuwe macho na njama za makundi kama haya ambayo si ya Kiislamu, au yameufahamu vibaya Uislamu au pengine yanatumiwa na maadui wa Uislamu kuharibu sura nzuri ya dini hii tukufu.

    Mchezo sasa unaanza kunoga na kuwa hatari zaidi kwa Waislamu

    Kama Osama, ISIS wageuziwa kibaoIla bado wanalindwa wakamilishe kazial-Malik amengoka. Zamu ya Bashar

    Hivi sasa ndege za kivita za Marekani zinafanya mashambulizi yasiyosita ikiwaangamzia wapiganaji wengi wa ISIS.

    Hayo yakijiri, Rais Barack Obama ametangaza kuruhusu kikosi maalum kuingia Iraq/Syria kuwalinda Wamarekani.

    Hatua hiyo inafuat ia tukio lililopigiwa sana zumari la kuuliwa mwandishi wa habari James Foley.

    American fighter jets and drones continued to pound Islamic State militants in Iraq on Wednesday, and military planners weighed the possibility of sending a small number of additional U.S. troops to Baghdad.

    Ndivyo vilivyoripoti vyombo vya habari jana huku zikifuatiwa na picha za video zikionyesha jinsi ndege za Marekani zinavyovurumisha makombora katika maeneo walipo ISIS.

    Hata hivyo, picha inayojitokeza

    ni kuwa bado Marekani haijaridhika kuwa ISIS wamemaliza kazi, kwani hata hayo mashambulizi, yanakuwa ya kiwango fulani, ikiacha kitisho cha ISIS kuonekana kuendelea kuwepo.

    Mashambulizi haya mapya, yalianza baada ya kusambazwa video iliyodaiwa kuwa ilitengenezwa na ISIS wakati wakimkata shingo na kumuuwa James Foley.

    James Foley, mwenye umri wa miaka 40, ni mwandishi wa habari wa Kimarekani akitokea Rochester, New Hampshire.

    Alitoweka akiwa Syria, akiwa

    anafanya kazi na Shirika la Habari la Agence France-Presse (APF), halikadhalika kampuni ya GlobalPost (Boston).

    Akizungumzia suala hilo, Rais Barack Obama aliapa akisema kuwa Marekani itakabiliana na ISIS mpaka iwatokomeze.

    Alisema, hakuna Mungu ambaye anaweza kuvumilia kuona haya yanayofanywa na ISIS.

    The (ISIS) fighters had rampaged across cities and villages, abducted women and children and subjected them

    Inaendelea Uk. 12

  • 12 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 22-28, 201412 MAKALA/Mashairi

    Tumefunga wetu babu, kwa swaumu kutimiza,Twamshukuru WAHABU, kwa hilo sisi kuweza,Kilosalia hesabu, kiama na yetu jaza,MWENI kumsindikiza, ni wetu sote wajibu.

    Thelathini bila tabu, zote tumezitimiza,Kulikoni! ni ajabu, kwa SITA kutoziweza,Thakili kwa la thawabu, MchaMungu kulibeza,MWENI kumsindikiza, ni wetu sote wajibu.

    Kwanini ! li juu jibu, la SITA wengi kubeza,Wallahi hakujaribu, MUHAMMAD nadokeza,SITA shawali ajibu, kuacha kutekeleza.MWENI kumsindikiza, ni wetu sote wajibu.

    Mizaniye kithawabu, mithili ya mwaka jaza,Alotujuza HABIBU, si kwamba ninachombeza,Kwa hadithi mujarabu, swahihi katuhimiza,MWENI kumsindikiza, ni wetu sote wajibu.

    Mabanati, mashababu, kwalo alotuhimiza,Kadhalika mashaibu, pamoja na maajuza,Twapaswa kujiratibu, thuma kulitekeleza,MWENI kumsindikiza, ni wetu sote wajibu.

    Shime japo taratibu, SITA twanze dunduiza,Shawali isijeghibu, bila SITA kutimiza,Kwa sita beti wajibu, wangu nimeutimiza,Kwa SITA asindikizwe, Mgenetu RAMADHANI.

    ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA

    ELIMUElimu tunu adhimu, aali iso kifani,Elimu tunu adhimu, kwa insi si hayawani,Elimu tunu adhimu, kutoka kwa RAHMANI,Elimu tunu adhimu, taadhima kwa insani,Shime tuisharifuni, kikoa tunu adhimu.

    Elimu bora johari, yenye aali thamani,Elimu bora johari, kwayo kufuye sioni,Elimu bora johari, si lulu si marijani,Elimu bora johari, kwayo havioni ndani,Shime tuithaminini, kikoa bora johari.

    Elimu angavu nuru, kwa uoni wa yakini,Elimu angavu nuru, kwa ya akhera yakini,Elimu angavu nuru, kwa ya dunia yakini,Elimu angavu nuru, akhera na duniani,Shime tuitafuteni, kikoa angavu nuru.

    ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.

    MGENI ASINDIKIZWE !

    to torture and rape and killed Muslims, both Sunni and Shia, by the thousands.

    V y o m b o v ya h a b a r i vilimnukuu Obama akisema na kuhitimisha kwa kusema kuwa:

    "No just God would stand for what they did yesterday and what they do every single day. Their ideology is bankrupt."

    A l i s e m a O b a m a akimaanisha kuwa mauwaji n a u k a t i l i u l i o k u w a ukifanywa na ISIS ukifuatiwa n a h i l i l a k u m c h i n j a mwandishi, Foley, hakuna Mungu wa haki anayeweza kulikubali.

    Pigia mstari maneno their ideology is bankrupt. Ideology, inayokusudiwa hapa ni Uislamu kwa vile hawa ISIS wanadai kuwa ni Waislamu wanaopigania k u s i m a m i s h a d o l a ya Kiislamu.

    Ambayo tafsiri yake ni kuwa maadui wa Uislamu wametengeneza Waislamu-I S I S , n a k u w a t u m i a kuutangaza Uislamu kuwa ni itikadi iliyofilisika!!!

    Hayo yakasemwa pia na Waziri wa Mambo ya Nje, John Kerry, akisema:

    Islamic State group is an "Ugly, savage, inexplicable, nihilistic, and valueless evil."

    "ISIL is the face of that evil, a threat to people who want to live in peace, and an ugly insult to the peaceful religion they violate every day with their barbarity."

    Kuweka kibwagizo hiki cha Mungu kinakuja kwa sababu hawa ISIS wanadai k u f a n ya h i v y o k a t i k a harakati zao za kusimamisha ukhalifah.

    Hili ndilo kwa upande mmoja makafiri na maadui wa Uislamu wamefanikiwa katika vita yao dhidi ya Uislamu kwa kuwatumia Waislamu wenyewe.

    Viongozi wa Marekani na kat ika NATO, Hivi sasa wameungana wakiwa n a m s i m a m o m m o j a wakitangaza kuwa dola ya Kiislamu inasimamia ushenzi na ukatili usiokubalika katika ulimwengu wa watu wastaarabu.

    Is l amic Ca l ipha t ea "caliphate of barbarism", al inukuliwa Wazir i wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, akisema huku akishajiisha jumuiya ya kimataifa kuungana kuwapiga vita ISIS na mradi wao wa Khilafah.

    Ya p o m a d a i k u w a huenda mkanda uliotolewa akionekana Foley akichinjwa ni wa kughushi, lakini iwe kwel i au la , bado

    Mchezo sasa unaanza kunoga na kuwa hatari zaidi kwa Waislamu

    ukweli unabaki kuwa ISIS imetumiwa na maadui wa Uislamu kuupaka Uislamu matope na kuwa sababu ya majeshi ya Marekani kurejea Iraq na kufanya ufisadi mwingine Iraq, Syria na nchi za Kiislamu.

    Katika Iraq, tayari ISIS wamewezesha kungolewa madarakani a l iyekuwa Wazir i Mkuu wa Iraq, Nour al-Malik ambaye japo alikuwa akitumiwa na Marekani, lakini kuna baadhi ya mambo yalimshinda kuyakubali.

    ISIS wakapewa uwezo na kuachiwa kukaribia kuingia Baghdad. Hapakuwa na namna, Malik akaondoka.

    Sasa ameingia mtu ambaye tayari ashaongea na wakuu wa Marekani na kuridhiana cha kufanya na hapo ndipo mabomu kutoka angani yakaanza kuwaangukia ISIS, wakiambiwa komeni, hakuna ruhsa kuingia Baghdad.

    Kwa upande mwingine, ISIS wamewezesha Jimbo la Kurdistan kuwa na nguvu ya kupigania kujitawala na sasa wanadhibiti visima vyao vya mafuta nje ya udhibiti wa Baghdad na tayari inaelezwa kuwa wanauza mafuta Marekani na Israel.

    Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanasema kuwa tukio hili la kuuliwa James Foley, limetumiwa kufikia malengo mawili.

    Moja ni kufunika ukweli kuwa ISIS ni mtoto wa kuzaa na kule lewa na Marekani/NATO. Kwamba kwa jinsi Mmarekani huyo alivyochinjwa kikatili, na hasira inayooneka kuibuka kutoka Washington na NATO, inafuta dhana yoyote kuwa kuna mahusiano na

    maelewano kati ya wawili hao.

    Jambo la pili linatajwa k u w a k w a h a s i r a iliyoonyeshwa na