zaka na sadaka (ibada na sadaka)

120
ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA) Azania Front Cathedral 9-16-23 January, 2011 Na Mwl. Mgisa Mtebe 0713 497 654

Upload: theodore-todd

Post on 01-Jan-2016

305 views

Category:

Documents


17 download

DESCRIPTION

ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA). Azania Front Cathedral 9-16-23 January, 2011 Na Mwl . Mgisa Mtebe 0713 497 654. KUSUDI LA MUNGU KWA KANISA. IBADA NA SADAKA Waebrania 7:1-10. KUSUDI LA MUNGU KWA KANISA. Waebrania 7:1-10 - PowerPoint PPT Presentation

TRANSCRIPT

Page 1: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA(IBADA NA SADAKA)

Azania Front Cathedral9-16-23 January, 2011

Na Mwl. Mgisa Mtebe

0713 497 654

Page 2: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

KUSUDI LA MUNGU KWA KANISA

IBADA NA SADAKAWaebrania 7:1-10

Page 3: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

KUSUDI LA MUNGU KWA KANISA

Waebrania 7:1-101 Kwa kuwa huyu Melkizedeki alikuwa Mfalme wa Salemu na

Kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Abrahamu akirudi katika kuwapiga na

kuwashinda hao wafalme; naye Melkizedeki akambariki,

Page 4: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

KUSUDI LA MUNGU KWA KANISA

Waebrania 7:1-102 na Abrahamu akampa

Melkizedeki “sehemu moja ya kumi (Zaka)” ya kila kitu. Jina hilo Melkizedeki maana yake,

“Mfalme wa haki,” pia “Mfalme wa Salemu” maana yake

“Mfalme wa amani (Salama).”

Page 5: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

KUSUDI LA MUNGU KWA KANISA

Waebrania 7:1-103 (Huyo Melkizedeki, Mfalme wa Salem; )Hana Baba na wala hana

mama; hana ukoo, hana mwanzo wala mwisho wa siku

zake, ni kama Mwana wa Mungu; na yeye adumu kuhani

milele.

Page 6: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

KUSUDI LA MUNGU KWA KANISA

Waebrania 7:1-104 Tazama jinsi alivyokuwa mkuu!

Hata Abrahamu, baba yetu mkuu, alimpa moja ya kumi

(Zaka) ya nyara zake zote alizoziteka kule vitani, alipokuwa akipigana na wale wafalme, kwa

ajili ya Lutu, mpwa wake.

Page 7: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

KUSUDI LA MUNGU KWA KANISA

Waebrania 7:1-105 Basi sheria inawaagiza wana wa

Lawi, wale ambao hufanyika makuhani, hupokea sehemu moja ya kumi kutoka watu

ambao ni ndugu zao (yaani yale makabila 11 mengine, katika

watoto 12 wa Yakobo)

Page 8: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

KUSUDI LA MUNGU KWA KANISA

Waebrania 7:1-106 Huyu Melkizedeki, ingawa hakufuatia ukoo wake kutoka kwa Lawi, lakini alipokea moja ya kumi kutoka kwa Abrahamu na kumbariki yeye aliyekuwa

na zile ahadi (yaani Abrahamu).

Page 9: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

KUSUDI LA MUNGU KWA KANISA

Waebrania 7:1-107 Wala hakuna shaka kwamba

mdogo hubarikiwa na aliye mkuu kuliko yeye (Kwamba Melkizedeki, ni Mkuu kuliko

Ibrahim).

Page 10: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

KUSUDI LA MUNGU KWA KANISA

Waebrania 7:1-108 Kwa upande mmoja, sehemu

moja ya kumi (yaani Zaka) hupokelewa na wanadamu ambao hupatikana na kufa

(yaani Walawi au Makuhani) …

Page 11: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

KUSUDI LA MUNGU KWA KANISA

Waebrania 7:1-108 … lakini kwa upande mwingine

(Zaka, yaani sehemu ya kumi), pia hupokelewa na Mungu, Yeye ambaye hushuhudiwa kuwa yu hai (Yaani Mungu).

Page 12: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

KUSUDI LA MUNGU KWA KANISA

Waebrania 7:1-109 (Kwahiyo) Mtu anaweza hata kusema kwamba Lawi, ambaye hupokea sehemu moja ya kumi

(Zaka), naye pia alitoa hiyo sehemu moja ya kumi, kupitia

kwa Abrahamu,

Page 13: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

KUSUDI LA MUNGU KWA KANISA

Waebrania 7:1-1010 kwa sababu, Melkizedeki

alipokutana na Abrahamu, Lawi alikuwa ndani, katika viuno vya baba yake (Yakobo, ambaye pia alikuwa ndani ya Isaka, ambaye pia alikuwa ndani, katika viuno

vya Abrahamu).

Page 14: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

KUSUDI LA MUNGU KWA KANISA

Waebrania 7:1-1010 Kwahiyo, Ibrahimu alipotoa

Zaka ya vitu vyake vyote kwa Melkizedeki, ndio kusema, na

Lawi pia, alitoa Zaka kupitia kwa Ibrahimu, angali bado yu katika kiuno cha babu yake (hata kabla

ya kuzaliwa kwake duniani).

Page 15: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

KUSUDI LA MUNGU KWA KANISA

IBADA NA SADAKAYohana 4:23-24

Page 16: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SIFA NA IBADA KWA MUNGU

KWANINI IBADA ?

Page 17: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SIFA NA IBADA KWA MUNGU

Zaburi 22:3 Wewe U Mtakatifu, nawe

“UNAKETI” juu ya sifa za Israel

“Inhabit” “Unaishi”

Page 18: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SIFA NA IBADA KWA MUNGU

Zab 22:3 IDABA ndio kitu cha kwanza

kabisa katika moyo wa Mungu, kwasababu

MUNGU ANAISHI KATIKA IBADA na SIFA.

Page 19: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SIFA NA IBADA KWA MUNGU

Zaburi 22:3 Wewe U Mtakatifu, nawe

“UNAKETI” juu ya sifa za Israel

“Inhabit” “Unaishi”

Page 20: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

KANISA LA MTU BINAFSIZABURI 150:1-6

6 Kila mwenye pumzi amsifu Bwana, kwa sauti kuu, kwa

zeze, kwa filimbi, kwa zomari, kwa matari, kwa vinubi na kwa

matoazi yavumayo sana.

Page 21: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SIFA NA IBADA KWA MUNGU

Mungu Kuhani Ibada Nchi Adam

Page 22: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Walawi 6:8-1312 Moto ulio juu ya

madhabahu (ibada) lazima uwe unaendelea kuwaka juu ya madhabahu, siku zote, na

kamwe usizimike. (Masaa 24 bila kukatika)

Page 23: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Walawi 6:8-1313 Moto (wa ibada) lazima

uendelee kuwaka juu ya madhabahu mfululizo (Kwa Masaa 24 bila kukatika), na

kamwe usizimike!

Page 24: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Nafasi ya

Sadaka katika Ibada

Page 25: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Kumbukumbu 18:1-51 Makuhani na kabila lote la

Lawi hawatakuwa na mgao wala urithi pamoja na Israeli.

Wataishi kwa sadaka zitolewazo kwa ajili ya BWANA;

na huo ndio urithi wao.

Page 26: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Kumbukumbu 18:1-52 Hawatakuwa na urithi miongoni mwa ndugu zao,

BWANA ndiye urithi wao, kama alivyowaahidi.

Page 27: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Kumbukumbu 18:1-53 Hili ndilo fungu la makuhani kutoka kwa watu watakaotoa

dhabihu ya ng’ombe au kondoo: mguu wa mbele,

mashavu mawili na matumbo.

Page 28: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Kumbukumbu 18:1-54 Mtawapa malimbuko ya

nafaka zenu, divai mpya, mafuta na sufu ya kwanza

kutoka manyoya ya kondoo zenu;

Page 29: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Kumbukumbu 18:1-55 kwa kuwa BWANA Mungu

wenu amewachagua pamoja na wazao wao kutoka makabila

yenu kusimama na kuhudumu katika jina la BWANA siku zote.

Page 30: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

MZUNGUKO WA BARAKA

Mungu Kuhani Nchi Adam

Lawi 6:12-13

Kumb 18:1-5

Malaki 3:7-12 Hagai 1:5-11

Kumb 8:6-18

Lawi 26:3-7

2Kor 9:6-8, 11

Page 31: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Kazi yoyote inayofanywa na kanisa (makuhani) ili Mungu apewe ibada

na utukufu anaostahili, kazi hiyo ikichechemea, kwa namna yoyote,

basi mimi na wewe hatuwezi kubarikiwa katika maisha yetu

wala katika kazi zetu.

Page 32: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Na utaratibu ambao Mungu aliuweka kwa ajili ya kuitunza ofisi

yake duniani (kanisa) ni Watu wake kutuoa sehemu za mali

zetu kwake (Zaka na Sadaka) katika namna ya kuonyesha

heshima na upendo wetu kwake

Page 33: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKAMalaki 3:7-12

7 Tangu siku za baba zenu, mmegeukia mbali na amri

zangu, nanyi hamkuzishika. 8 ‘‘Mnaniibia zaka na dhabihu. 9 Hivyom mko chini ya laana,

ninyi taifa lote, kwa sababu mnaniibia mimi.

Page 34: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Malaki 3:7-1210 Leteni zaka kamili ghalani,

ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, asema

BWANA Mwenye Nguvu;

Page 35: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Malaki 3:7-1210 Nijaribuni katika hili,’’ asema BWANA Mwenye Nguvu, ‘‘nanyi

mwone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na

kuwamwagieni baraka nyingi mpaka mkose nafasi ya kutosha

au la.

Page 36: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKAMalaki 3:7-12

11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala

hataharibu mazao ya ardhi yenu, wala mzabibu wenu

hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake,’’ asema

BWANA Mwenye Nguvu.

Page 37: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

12 ‘‘Ndipo mataifa yote watawaita ninyi,

mliobarikiwa, kwa maana nchi yenu itakuwa ya

kupendeza sana,’’ asema BWANA Mwenye Nguvu.

Page 38: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Kwahiyo, Utaratibu ambao Mungu aliuweka kwa ajili ya kuitunza ofisi

yake duniani (kanisa) ni Watu wake kutuoa sehemu za mali

zetu kwake (Zaka na Sadaka) katika namna ya kuonyesha

heshima na upendo wetu kwake

Page 39: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Malaki 3:7-12

Tunamwibia?

Page 40: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKAMalaki 3:7-12

7 Tangu siku za baba zenu, mmegeukia mbali na amri

zangu, nanyi hamkuzishika. 8 ‘‘Mnaniibia zaka na dhabihu. 9 Hivyom mko chini ya laana,

ninyi taifa lote, kwa sababu mnaniibia mimi.

Page 41: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Kuiba; ni kuchukua mali au kitu kisicho chako (kutokuachilia, mali ya mtu).

Kunyima; ni kuzuia mali au kitu kiilicho chako (kuto-kuachilia, mali yako kwa mtu mwingine)

Page 42: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Uwe mwanagalifu sana na mwaminifu katika mali hii,

kwasababu,

ZAKA sio yako!ZAKA ni ya Mungu!

Zaka ni takatifu!

Page 43: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

10 = 1 + 9

ZAKA + MATUMIZI

(Dhabihu)

Page 44: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

ZAKA Ya Mungu.

Dhabihu Ya Kwako.

Page 45: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

ZAKA Dhabihu

Ya Mungu. Ya Kwako. 1 9

‘Unarudisha’ ‘Unatoa’

Page 46: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Kwanini vitu 10?

Page 47: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Kwanini vitu 10?Katika maisha mahesabu ya

vitu vyote yapo katika tarakimu 10 tu.

Page 48: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

1

7

6

3

54

8

9

2

0

Page 49: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Kwanini vitu 10?Katika mduara, namba kumi

(10) ndiyo inayokamilisha mzunguko kamili.

Page 50: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

1

7

6

3

54

8

9

2

10

Page 51: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Kwanini vitu 10?Pasipo ile namba kumi (10)

seti au duara linakuwa si kamilifu (hakijakamilika).

Page 52: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

1

7

6

3

54

8

9

2

Page 53: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

1

7

6

3

54

8

9

2

10

Page 54: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

9

8

7

65 4

3

2

110

Page 55: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Kwanini vitu 10?Yaani; Mungu ndiye

ukamilifu wa maisha ya Mwanadamu.

Page 56: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Unapotoa ZAKA (Sehemu ya Kumi) ya vitu vyako (mali zako),

unathamini na kuheshimu nafasi ya Mungu katika maisha

yako, kwamba;Mungu ndiye ukamilifu wako.

Page 57: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Kwanini vitu 10?Yaani; Mungu ndiye

ukamilifu wa maisha ya Mwanadamu.

Page 58: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Walawi 27:30-3131 Tena Zaka yote ya nchi,

kama ni Zaka ya mbegu, kama ni matunda ya nchi,

ni ya BWANA, na ni TAKATIFU kwa Bwana.

Page 59: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Kwahiyo, uwe mwanagalifu sana na mwaminifu katika fedha na

mali hizi tunazopata; kwasababu …

ZAKA (1/10) yote ni ya Mungu Hivyo, Zaka ni takatifu

Page 60: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

ZAKA Dhabihu

Ya Mungu. Ya Kwako. 1 9

‘Unarudisha’ ‘Unatoa’ (Haibariki) (Inabariki)

Page 61: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Kwa mfano; Mapato yako.

Page 62: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Kwa mfano; Mapato yako.Mshahara 500,000

Page 63: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Kwa mfano; Mapato yako.Mshahara 500,000Marupurupu 160,000

Page 64: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Kwa mfano; Mapato yako.Mshahara 500,000Marupurupu 160,000Kuku/Mayai 130,000

Page 65: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Kwa mfano; Mapato yako.Mshahara 500,000Marupurupu 160,000Kuku/Mayai 130,000Soda 110,000

Page 66: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Kwa mfano; Mapato yako.Mshahara 500,000Marupurupu 160,000Kuku/Mayai 130,000Soda 110,000Mengineyo 100,000

Page 67: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Kwa mfano; Mapato yako.Mshahara 500,000Marupurupu 160,000Kuku/Mayai 130,000Soda 110,000Mengineyo 100,000 JUMLA 1,000,000 .

Page 68: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Zaka yako. Jumla 1,000,000 = 10

Page 69: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Zaka yako. Jumla 1,000,000 = 10

100,000

Page 70: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Walawi 27:30-3130 Tena Zaka yote ya nchi, kama

ni Zaka ya mbegu, kama ni matunda ya nchi, ni ya BWANA,

na ni TAKATIFU kwa Bwana.

Page 71: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Watu wa Mungu wakielewa, nafasi ya sadaka katika maisha yao,

watatoa mali zao kwa heshima na utii, na kwa moyo wa furaha,

katika kuifanya kazi ya Mungu. Na kazi ya Mungu inakwenda vizuri,

nasi sote tunabarikiwa sana.

Page 72: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Kwa kadri kila mtu alivyojaliwa na Mungu, anatakiwa kutoa

matoleo haya kwa heshima na kwa upendo, kwasababu ya ukuu na wema wa Mungu maishani mwetu, ambao

hatuwezi kuulipa.

Page 73: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Aliyejaliwa kidogo, katika hicho hicho kidogo, ampe Mungu iliyo yake; na kwa aliyejaliwa vingi,

katika hivyo vingi, naye pia ampe Mungu sehemu yake,

kwa heshima na upendo.

Page 74: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Walawi 27:30-3131 Na kama mtu akitaka

kukomboa chochote cha Zaka yake, ataongeza sehemu ya

tano (1/5) juu yake. “cha juu”

Page 75: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Zaka yako.

1 X 100,000 = 5

Page 76: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Zaka yako.

1 X 100,000 = 20,000 5

Page 77: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Zaka yako.

100,000 (Zaka) + 20,000 (Riba)

Page 78: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Zaka yako.

100,000 (Zaka) + 20,000 (Riba) 120,000 (Z’Kamili)

Page 79: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

ZAKA HUTOLEWA WAPI?Malaki 3:10-12

Page 80: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Malaki 3:7-1210 Leteni zaka kamili ghalani,

ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, asema

BWANA Mwenye Nguvu;

Page 81: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Malaki 3:7-12

NGUVU YA SADAKA (ZAKA + DHABIHU)

Page 82: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Malaki 3:7-1210 Leteni zaka kamili ghalani,

ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, asema

BWANA Mwenye Nguvu;

Page 83: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Malaki 3:7-1210 Nijaribuni katika hili,’’ asema BWANA Mwenye Nguvu, ‘‘nanyi

mwone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na

kuwamwagieni baraka nyingi mpaka mkose nafasi ya kutosha

au la.

Page 84: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

ZAKA + DHABIHU

Malaki 3:7-12

Page 85: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

ZAKA + DHABIHU

NITAFUNGUA + KUMWAGA

Malaki 3:7-12

Page 86: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

ZAKA + DHABIHU

KUFUNGUA + KUMWAGA

Malaki 3:7-12

Hagai 1:5-11

Page 87: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

ZAKA + DHABIHU

KUFUNGUA + KUMWAGA (Haibariki) (Inabariki)

Malaki 3:7-12

Page 88: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

NGUVU YA SADAKA

Malaki 3:7-12

1. Kufungua mbingu2. Kumwaga Baraka

Page 89: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

KUTEMBEA NA NGUVU ZA MUNGU

Kwahiyo, Sadaka yako, ina nguvu ya kukufungulia fursa (nafasi)

ambazo kikawaida, usingezipata wewe au kwa juhudi zako. Na pia

sadaka yako ina nguvu ya kukumwagia baraka mbalimbali za kukufanikisha zaidi kimaisha.

Page 90: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKAMalaki 3:7-12

11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala

hataharibu mazao ya ardhi yenu, wala mzabibu wenu

hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake,’’ asema

BWANA Mwenye Nguvu.

Page 91: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

NGUVU YA SADAKA

Malaki 3:7-121. Kufungua mbingu2. Kumwaga Baraka3. Upako wa Kushinda Vita

Page 92: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

KUTEMBEA NA NGUVU ZA MUNGU

Kwahiyo, Sadaka yako, ina nguvu ya kufungulia upako maalumu

(msaada wa Roho Mtakatifu) ili kukuwezesha kuendelea

kupigana na adui zako katika vita vya kiroho tulivyonavyo duniani

na kushinda!

Page 93: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

Malaki 3:7-12

12 ‘‘Ndipo mataifa yote watawaita ninyi,

mliobarikiwa, kwa maana nchi yenu itakuwa ya

kupendeza sana,’’ asema BWANA Mwenye Nguvu.

Page 94: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

NGUVU YA SADAKA

Malaki 3:7-121. Kufungua mbingu2. Kumwaga Baraka3. Upako wa Kushinda Vita4. Kukutofautisha.

Page 95: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

NGUVU YA SADAKA

Kutoka 9: 4, 26Nami nitaweka tofauti kati ya

Wamisri na Waebrania. (Mambo yatakayowapata Wamisri

hayatawapata Waebrania)

Page 96: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

NGUVU YA SADAKA

Mathayo 6:26-33Mnahangaikia Chakula? Mavazi? Waangalieni Ndege na Maua …

Ninyi utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu … hayo mengine

nitawazidishia.

Page 97: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

NGUVU YA SADAKA

Zekaria 8:20-23‘Katika siku hizo, watu 10 wa mataifa mbalimbali, wataushika upindo wa nguo wa Myahudi (Mkristo) mmoja

na kusema, tutakwenda pamoja nawe, kwa maana tumesikia Mungu

yupo pamoja nanyi’

Page 98: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

NGUVU YA SADAKA

Daniel 1:1717 Na katika habari za hao vijana

waliompenda Mungu, Daniel, Shadrack, Meshack, na Abednego,

Mungu aliwapa akili, busara na maarifa; na kuwa bora zaidi, mara 10 kuliko werevu wote, waganga wote

na wachawi wote wa Babeli.

Page 99: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

KUTEMBEA NA NGUVU ZA MUNGU

Kwahiyo, Sadaka yako, ina nguvu ya kukufanya uwe tofauti na

watu wengine, ukawa bora zaidi katika utendaji, akili na maarifa, masomo, afya, uchumi, familia,

ulinzi, n.k. kwa Utukufu wa Mungu wako.

Page 100: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

ZAKA NA SADAKA

Kwa mfano;

Ujenzi wa Nyumba (Hema) ya Mungu Jangwani

Kumb 36:2-7

Page 101: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Kumb 36:2-7 Wajenzi wa hekalu wakamwambia

Musa, watu wameleta sadaka nyingi sana na kuzidi, kuliko

tulivyokuwa tunahitaji. Tumewazui, lakini hawataki, nao

bado wanaleta tu.

Page 102: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Kumb 36:2-7 Tunaomba wewe Baba, labda

watakusikia; Ndipo Musa akatoa amri, kwamba watu wasilete tena matoleo kwa ajili ujenzi wa hema

ya ibada, kwasababu walikuwa wameleta vingi sana na kuzidi.

Page 103: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Kumb 36:2-7 … Hivyo watu wakazuiliwa kuleta

zaidi, 7 kwa sababu vitu vilivyokuwa vimeletwa, tayari

vilikuwa vimetosha, na hata kuzidi sana, kwa ajili ya kuifanya kazi

yote.

Page 104: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Watu wa Mungu waliomheshimu Mungu,

walitoa mali zao, kuliko hata bajeti iliyokuwa inahitajika

kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mungu kule jangwani.

Page 105: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

Kwahiyo …

Watu wa Mungu wakielewa, nafasi ya sadaka katika maisha yao,

watatoa mali zao kwa heshima na utii, na kwa moyo wa furaha,

katika kuifanya kazi ya Mungu. Na kazi ya Mungu itakwenda vizuri, nasi sote tunabarikiwa sana.

Page 106: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Huu ndio utaratibu ambao Mungu aliuweka kwa ajili ya kuitunza ofisi yake duniani

(kanisa).Malaki 3:10-12

Page 107: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Na Mungu anawapenda, wale wanatoa mali zao kwa heshima na utii, na kwa moyo wa furaha,

katika kuifanya kazi yake. 2 Wakorintho 9:6-7

Page 108: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

IBADA NA UTOAJI

2 Wakorintho 9:6-8, 11

6 Kumbukeni kwamba: Ye yote apandaye kwa uchache pia atavuna kwa uchache, naye apandaye kwa ukarimu pia

atavuna kwa ukarimu.

Page 109: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

IBADA NA UTOAJI

2 Wakorintho 9:6-8, 11

7 Kila mtu atoe kama anavyokusudia moyoni mwake,

si kwa uchoyo au kwa kulazimishwa, kwa maana

Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu.

Page 110: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

IBADA NA UTOAJI

2 Wakorintho 9:6-8, 11

8 Naye Mungu aweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili katika mambo yote kila wakati, mwe

na kila kitu mnachohitaji, ili mweze kushiriki kwa wingi

katika kila kazi njema. …

Page 111: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Kwa mfano; Mapato yako.Mshahara 500,000Kodi - 60,000 440,000Pension - 50,000 390,000

Page 112: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Kwa mfano; Mapato yako.Baki 390,000Mkopo - 100,000 290,000

Page 113: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Kwa mfano; Mapato yako. Mshahara 290,000Posho 140,000Mayai 140,000Soda 130,000Mengineyo 100,000

Page 114: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Kwa mfano; Mapato yako. Jumla 800,000

Page 115: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Kwa mfano; Mapato yako. Jumla 800,000 10

Page 116: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

SADAKA NA IBADA KWA MUNGU

Kwa mfano; Mapato yako. Jumla 800,000 = 80,000 10

Page 117: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

Ibada na Utoaji

Mwisho!

Page 118: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

Mafundisho Mengine

Mwalimu Mgisa Mtebe ana Vitabu vingine, CD na DVD za Mafundisho

ya Neno la Mungu, yanayoweza kukujenga na kukuimarisha sana

kiroho, ili uwe na maisha ya ushindi na yenye mafaniko mazuri.

Page 119: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

Mafundisho Mengine

Vitabu vingine, CD na DVD za Mafundisho vya Mwalimu Mgisa

Mtebe, yanapatikana katika duka la Vitabu vya Kikristo la

Azania Front Cathedral Luther House, Sokoine Drive

Dar es Salaam.

Page 120: ZAKA NA SADAKA (IBADA NA SADAKA)

Kwa mawasiliano zaidi,

Mwl. Mgisa Mtebe (Christ Rabbon Ministry)

P. O. Box 837,Dar es Salaam, Tanzania.

+255 713 497 654+255 784 497 654

[email protected]