je, ujumbe wa injili ni nini? - wordpress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri...

72
JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? Yaliyomo 1.Ujumbe wa Injili katika Biblia 2. Mungu ni Mwumbaji wa haki 3. Mwanadamu ni mwenye dhambi 4. Bwana Yesu Kristo ni Mwokozi 5. Imani na Toba 6. Ufalme wa Mungu 7. Msalaba wa Kristo Yesu ndiyo msingi 8. Nguvu za ujumbe wa injili Utangulizi Je, Ujumbe wa Injili ya Yesu Kristo ni gani? Unaposoma swali hili, labda utajieleza kwamba hili ni swali ambalo kila mkristo anaweza kulijibu. Huenda pia unawaza kwamba hakuna haja ya kuandika kitabu kizima kuhusu jambo hili. Labda unawaza kwamba kumwuliza mkristo swali hili ni kama kumwuliza seremala kwamba nyundo ni nini? Ujumbe wa injili ya Kristo ndiyo msingi wa ukristo. Huu ndio ujumbe ambao makanisa yote yamejengwa juu yake. Huu ndiyo ujumbe ambao kila mkristo anafaa kushuhudia na huu ndio ujumbe ambao tunamwomba Mungu kwamba wengi wataupokea na kuokoka. Je, ni wakristo wangapi ambao wanafahamu jambo hili? Je, utamjibu nini mtu ambaye anakuuliza kwamba, je ni ujumbe gani ambao ninyi wakristo mnahubiri mara kwa mara? Je, ni nini kizuri kuhusu ujumbe huu? Ukweli ni kwamba utawasikia wakristo wengi wakijibu kwa maneno ambayo hayaambatni na mafundisho ya Biblia kuhusu ujumbe wa Injili ya Kristo Yesu. Huenda wengi watajibu kwamba: “Ujumbe wa Injili ni kwamba Mungu atakusamehe dhambi zako ikiwa utamwamini.” Ama huenda watasema: “Ujumbe wa Biblia ni kwamba Mungu anakupenda na ana mpango mzuri juu ya maisha yako. Au kwamba ujumbe wa injili ni kwamba wewe ni mtoto wa Mungu na

Upload: others

Post on 11-Sep-2020

16 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? Yaliyomo 1.Ujumbe wa Injili katika Biblia 2. Mungu ni Mwumbaji wa haki 3. Mwanadamu ni mwenye dhambi 4. Bwana Yesu Kristo ni Mwokozi 5. Imani na Toba 6. Ufalme wa Mungu 7. Msalaba wa Kristo Yesu ndiyo msingi 8. Nguvu za ujumbe wa injili Utangulizi Je, Ujumbe wa Injili ya Yesu Kristo ni gani? Unaposoma swali hili, labda utajieleza kwamba hili ni swali ambalo kila mkristo anaweza kulijibu. Huenda pia unawaza kwamba hakuna haja ya kuandika kitabu kizima kuhusu jambo hili. Labda unawaza kwamba kumwuliza mkristo swali hili ni kama kumwuliza seremala kwamba nyundo ni nini? Ujumbe wa injili ya Kristo ndiyo msingi wa ukristo. Huu ndio ujumbe ambao makanisa yote yamejengwa juu yake. Huu ndiyo ujumbe ambao kila mkristo anafaa kushuhudia na huu ndio ujumbe ambao tunamwomba Mungu kwamba wengi wataupokea na kuokoka. Je, ni wakristo wangapi ambao wanafahamu jambo hili? Je, utamjibu nini mtu ambaye anakuuliza kwamba, je ni ujumbe gani ambao ninyi wakristo mnahubiri mara kwa mara? Je, ni nini kizuri kuhusu ujumbe huu? Ukweli ni kwamba utawasikia wakristo wengi wakijibu kwa maneno ambayo hayaambatni na mafundisho ya Biblia kuhusu ujumbe wa Injili ya Kristo Yesu. Huenda wengi watajibu kwamba: “Ujumbe wa Injili ni kwamba Mungu atakusamehe dhambi zako ikiwa utamwamini.” Ama huenda watasema: “Ujumbe wa Biblia ni kwamba Mungu anakupenda na ana mpango mzuri juu ya maisha yako. Au kwamba ujumbe wa injili ni kwamba wewe ni mtoto wa Mungu na

Page 2: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

Mungu anataka watoto wake wafanikiwa na wawe matajiri katika maisha haya.” Wengine wanajua kwamba ujumbe wa injili unahusu kifo cha Bwana Yesu Kristo na kufufuka kwake lakini hawajui jinsi kifo cha Yesu Kristo na ujumbe wa injili vinahusianaje. Swali ni je, ni namna gani kifo cha Yesu Kristo na kufufuka kwake ni msingi wa ujumbe wa injili? Ukweli ni kwamba wakristo wengi huwa hawakubaliani juu ya jambo hili kulingana na jinsi wanavyolifafanua. Kuna wengi ambao wanaamini kwamba Biblia ni ya kweli na kwamba ni neno la Mungu. Wanaamini kwamba Bwana Yesu Kristo alikufa msalabani na alifufuka kutoka kwa wafu. Wao wanaamini kwamba wanadamu ni wenye dhambi na kwamba wanahitaji kuokoka na kuishi maisha yao kulingana na neno la Mungu. Mafundisho kuhusu ujumbe wa injili, ni mafundisho ambayo huleta mijadala mingi sana miongoni mwa wakristo na hata wale ambao hawajaokoka. Tunaweza kuandika au kuzungumza kuhusu mambo kama kuhubiri, kuwafundisha wengine, kuwashauri, serikali ya kanisa na muziki katika kanisa, na katika majadiliano haya hutapata mabishano mengi miongoni mwa wakristo. Lakini tunapozungumza kuhusu ujumbe wa injili, tutapata kutoelewana kwingi hapa. Kuna mtu mmoja ambaye aliulizwa, je, ujumbe wa injili ni upi? Alijibu, “ninawaza kwamba ni, Yesu Kristo alikuja na akaishi hapa ulimwenguni. Baadaye akafa na akafufuliwa kutoka kwa wafu. Pia inahusu Kristo kurejesha vitu vyote katika hali nzuri. Kazi hii inafanyika wazi katika maisha ya wale ambao wameokoka. Pia kuna siku ambapo kazi hii itakamilishwa. Ujumbe wa injili unahusu kuja kwa ufalme wa Kristo.” Kuhusu mawazo haya, mimi na baadhi ya wenzangu tuliwaza kwamba mawazo haya ya yalipungukiwa kwa sehemu fulani. Kwa mfano, yeye hakueleza ni kwa nini Kristo alikufa na kufufuka. Pia hakutaja dhambi hitaji kuu la mwandamu ambalo ni wokovu kutoka kwa ghadhabu ya Mungu?

Page 3: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

Wakati tulisema hii, watu wengine walituuliza mbona mnasema huyu mtu jibu lake limepungukiwa ujumbe wa injili. Je, si pia Kristo Yesu mwenyewe alizungumza kuhusu ufalme wa mbinguni kama tu vile mtu huyu anasema? Lakini kulikuwa na wengine ambao walifurahishwa na mjadala huu kuona kwamba wakristo wanajiuliza maswali ambayo yanahusu jambo lile ambalo wote wanaamini. Kwa njia moja ni jambo zuri sana kuona kwamba wakristo wanahojiana kuhusu ujumbe wa injili ni upi. Hii inaonyesha kwamba wao wanalichukulia jambo hili kwa makini sana. Litakuwa jambo la hatari sana ikiwa wakristo hawajali chochote kuhusu ujumbe wa injili. Pia ninawaza kwamba, wakristo wengi wamechanginyikiwa katika jambo hili na ndio sababu wako na misimamo tofauti tofauti. Unapoona jinsi wanazungumza, ukweli ni kwamba wakristo hatukubaliana kuhusu ujumbe wa injili ni upi hata wale ambao msimamo ni wa Biblia pekee. Ikiwa utawauliza wakristo wengi kuhusu jambo hili kuhusu ujumbe wa injili ya Kristo Yesu, utapata majibu tofauti tofauti. Hata unaposikiliza mahubiri ya wachungaji wengi, pia utaona kwamba wanatofautiana katika mahubiri yao kuhusu jambo hili. Pia unaweza kusoma vitabu vingi sana ambavyo vimeandikwa na wachungaji wengi wazuri, lakini pia utaona kwamba kuhusu jambo hili, wanalizungumzia tofauti tofauti. Kwa mfano kuna mmoja ambaye aliandika: “Habari njema ni kwamba, Mungu anataka kukuonyesha upendo wake. Anataka kujaza maisha yako na mambo mapya ikiwa wewe uko tayari kuondoa yale ya kale. Anza kuwaza mambo makubwa sana na acha kuwaza juu ya mambo mabaya ambayo yanakufanya usiendelee.” Ni lazima tufahamu kwamba huu si ujumbe injili. Haya ni mawazo ya mwanadamu mmoja ambaye amechanganyikiwa.

Page 4: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

Mwingine alisema, “Ujumbe wa injili ni kwamba Kristo alikufa kwa ajili yetu na wale wote ambao wanamwamini, hatia ya dhambi zao imeondolewa kutoka kwao. Wale ambao wameokoka, watakapofika mbinguni watasema kwamba, Kristo alikufa kwa niaba yangu. Huu ndio ujumbe wa injili.” Ni lazima tufahamu kwamba ujumbe wake umepungukiwa kwa sehemu fulani na kwamba huu sio ujumbe kamili wa Injili. Mwingine naye alisema kwamba, “Ujumbe wa Kristo ni ujumbe ambao umebadilisha ulimwengu. 'Kuna mabadiliko ambayo Mungu anatekeleza katika ulimwengu huu. Mabadiliko haya yanafanyika kwa kupatanishwa na kuleta amani. Mungu anaendelea kuupanua Ufalme wake kwa kuwapa watu wake tumaini na upendo. Ufalme huu umewafikia maskini, wadhaifu, wenye uvumilivu na wale ambao wamedharauliwa sana. Ni wakati wa kubadilisha mawazo yako. Mambo yote yahahusu mabadiliko ambayo Mungu analeta. Wakati wa maisha mapya ni sasa.' Ni lazima mniamini kwa haya na umfuate yale ambayo ninawaambia. Mwamini ujumbe wa injili ya Kristo ili mweze kuishi kulingana na ujumbe na mweze kuhusishwa katika mabadiliko haya.” Ni lazima tena tufahamu kwamba huyu haelewi kabisa ujumbe wa injili ni nini. Mwingine naye alisema, “ujumbe wa injili ni kwamba Mungu anakupenda haijalishi umefanya nini, unaishi wapi au umefanya makosa mangapi. Yeye anakupenda na hii ndio sababu anakutafuta kutoka katika dhambi zako.” Ni lazima tufahamu kwamba huu si ujumbe wa injili kamili. Mwingine naye alisema, “Ujumbe wa injili unahusu kutangaza kwamba Yesu Kristo alisulibiwa na Yeye ndiye Kristo ambaye alifufuka na Yeye ndiye Bwana wa kweli wa ulimwengu wote.” Ni lazima tuelewe kwamba huu si jumbe kamili. Haya ni mahubiri ya baadhi ya watu tofauti tofauti ambayo hata leo tunayasikia. Jambo la kuhuzunisha kwamba watu kama hawa

Page 5: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

hawaelewi ujumbe wa injili ni gani na wanafundisha ule ujumbe ambao umepungukiwa na ukweli kulingana na Biblia. Kwa hivyo unaona kile ninamaanisha wakati ninasema kwamba wakristo wengi wamechanganyikiwa kuhusu jambo hili la ujumbe wa injili. Ikiwa ungekuwa hujawahi kusikia lolote kuhusu dini ya ukristo, je, ungewaza nini kutokana na yale ambayo yamesemwa? Ninajua kwamba utasema wakristo wana ujumbe mzuri sana na hili ni kweli. Lakini hungeelewa vyema kabisa kuhusu jambo hili kutokana na yale yamezungumzwa. Je, habari njema ni kwamba tu Mungu ananipenda na kwamba ninahitaji kubadilika? Je, ni kwamba tu Yesu Kristo ni mfano mzuri kwako ambaye anakufundisha kuhusu maisha ya upendo na huruma? Katika haya yote lazima tuwaze kuhusu dhambi na msamaha wa dhambi. Wakristo wengi wanasema kwamba habari njema inahusu kifo cha Kristo Yesu na kuna wale ambao wanakataa jambo hili. Nia yangu katika utangulizi si kukueleza au kukushawishi kuchagua wazo gani zuri na lile baya. Lakini ninaomba kwamba baada ya kusoma kitabu hiki utakuwa umefahamu ukweli. Kile ninataka kukuonyesha katika utangulizi ni kwamba wakati watu wanaulizwa, Je, ujumbe wa injili ni nini, ni majibu gani wanatoa. Katika kitabu hiki, ninataka kukupatia jibu la swali hili kwamba Ujumbe wa injili ni nini ambalo linatoka katika Biblia. Ninataka tujifundishe kutoka kwa Biblia, je, ujumbe wa injili ni nini? Wakati ninafanya hii, ninaomba mambo yafuatayo. 1. Ikiwa wewe ni mkristo, ninaomba kwamba mafundisho ambayo ninafundisha katika kitabu hiki yatafanya moyo wako ujae na furaha na sifa kwa Bwana Yesu Kristo kwa sababu ya yale ambayo amekufanyia. Ikiwa watu hawafahamu vyema ujumbe wa injili, basi hawataweza kumwabudu Mungu kulingana na mapenzi yake na neno Lake. Watu wakikosa kufahamu ujumbe wa injili huwa watoe macho yao kwa Mungu na kuanza kujiona kwamba wao wanaweza

Page 6: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

kufanya kila kitu wenyewe. Jambo hili linafanya kazi ya Kristo msalabani iwe kana kwamba haijalishi kamwe. Jinsi mtu anavyofahamu vyema ujumbe wa injili, ndivyo atamheshimu na kumwabudu Mungu jinsi alivyo na yale ambayo ametufanyia katika Kristo Yesu: “Tazama jinsi kilivyo kina cha utajiri wa hekima na maarifa ya Mungu! Tazama jinsi ambavyo hukumu zake hazichunguziki na ambavyo njia zake zisivyotafutikana!” (Warumi 11:33). Paulo alisema haya kwa sababu moyo wake wote ulikuwa umejawa na ujumbe wa injili. 2. Ninaomba kwamba kitabu hiki kikusaidie kuwa na ujasiri wakati unazungumza na wengine kuhusu Kristo Yesu. Nimeona wakristo wengi ambao wanasisita kuzungumza kuhusu Kristo na marafiki wao na watu wa jamii zao. Wao huwa wana uoga kwa sababu wanawaza wataulizwa maswali mengi ambayo hawana majibu yake. Ukweli ni kwamba hakuna mtu ambaye ana majibu yote kuhusu kila kitu. Lakini wakati huo huo, unaweza kuyajibu mengine. Ninaomba kwamba kitabu hiki kitakusaida kuwa na ujasiri huo. 3. Ninaomba kwamba utafahamu umuhimu wa ujumbe huu wa injili katika maisha ya kanisa lote na kwamba utafanya kazi kwa bidii kuona kwamba ujumbe huu unahubiriwa kwa wote; ujumbe huu unaimbwa kwa nyimbo, unaomba kulingana na ujumbe huu, ujumbe huu unafundishwa na kusambazwa na kusikika katika kila sehemu ya maisha ya kanisa ambalo unahudhuria. Ni kupitia kwa kanisa, watu watafahamu na kusikia ujumbe kutoka kwa Mungu. Hili litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu wa milele wa kuokoka ulimwengu (Waefeso 3:7-12). 4. Ninaomba kwamba kitabu hiki, kikusaidie kuhusu jinsi unavyowaza juu ya ujumbe wa injili. Ujumbe wa injili ni ujumbe ambao huwa unabadilisha maisha yote ya mwanadamu. Jambo la kuhuzunisha ni kwamba miongoni mwa wakristo kuna wale ambao

Page 7: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

wanaishi maisha yao kwa njia ambayo inaweza kuwazuia wengine wasiokeko. Kwa hivyo ni ombi langu kwamba kitabu hiki kitawasaida wengi kufahamu ukweli wa ujumbe huu wa injili. Kila wakati mkristo ni mtu ambaye anajaribiwa kuishi maisha yake kinyume na neno la Mungu. Lakini hata kama mambo yako hivi, tunafaa kuishi maisha yetu kwa ushuhuda kwamba ujumbe huu wa injili ni wa kweli na una nguvu. Ni lazima tusisitize kuhusu mambo haya. Hili ndilo kusudi la kitabu hiki. Pia ninaomba kwamba ikiwa wewe msomaji ambaye hajaokoka, kitabu hiki kitakusaidia na kukufanya uanze kuwaza sana kuhusu ujumbe wa injili ya Kristo Yesu. Huu ndio ujumbe ambao ndio msingi wa maisha yetu ya ukristo na ni huu ujumbe ambao hata yule ambaye hajaokoka anahitaji kuuamini. Hufai kuupuza ujumbe huu kwa sababu hii ndio sauti ya Mungu. Huu ndio ujumbe wa injili. Kwa kuamini ujumbe ni kuepuka hukumu wa Mungu. Huu ndio ujumbe ambao tunafaa kuwatangazia wote. Sura ya kwanza Ujumbe wa Injili katika Biblia Ni lazima kila wakati tuwe tayari kutoa jibu la swali hili; je ujumbe ambao tunahubiri tunautoa wapi? Kwa wale wote ambao wanaamini katika Biblia, jibu la swali hili ni rahisi sana: tunapata ujumbe wetu kutoka kwa Biblia. Ukweli kwamba ujumbe ambao tunauhubiri unatoka katika Biblia si jambo ambalo wengi watakubaliana nalo. Kuna wale ambao wanadai kwamba wao ni wakristo na ni wahubiri, lakini hawakubaliani na ukweli huu. Kuna wale ambao wanasema kwamba kufahamu kwa kweli kuhusu ujumbe wa injili hakutoki tu katika Biblia, bali katika desturi za dini ya kikristo. Yaani ikiwa kanisa limeamini katika jambo fulani kwa muda mrefu sana, basi tunafaa kukubali kwamba huo ni ukweli hata kama hautoki katika Biblia. Wengine wanasema kwamba tunajua ukweli kwa kuwaza juu ya

Page 8: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

jambo. Wanasema kwamba ikiwa tutakua katika mawazo yetu, basi tutajifahamu, tutafahamu ulimwengu na tutamfahamu Mungu. Pia wengine wanasema kwamba tunafaa kutafuta ukweli kutokana na yale ambayo tumeyapitia. Kwa kawaida ni kwamba huwa mwanadamu anawaza kuhusu Mungu si kutokana na mafundisho ya Biblia bali kutokana na jinsi anavyowaza mwenyewe. Unapozingatia mambo haya yote, utaona kwamba hakuna lolote la kweli. Ikiwa tutafauata destiru za wanadamu, basi ni wazi kwamba tutakuwa tunafuata mawazo ya wanadamu. Ikiwa tutategemea yale ambayo tumeyapitia, ni wazi kwamba tutakuwa tunajidanganya. Je, tunafaa kufanya nini ili tujue ukweli wa ujumbe wa injili ya Kristo Yesu? Ukweli ni kwamba Mungu amezungumza nasi kupitia kwa neno lake, yaani Biblia. Pia kile ambacho Mungu amezungumza katika Biblia ni cha kweli na kwamba tunafaa kuamini kwa mioyo yetu yote: “Kila andiko lililovuviwa na Mungu lafaa kwa mafundisho kwa kuwaonya watu makosa yao, kuwaongoza na kuwafundisha katika haki” (2 Timotheo 3:16). Pia mfalme Daudi aliandika, “Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu, neno la Bwana ni kamili. Yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia Kwake.” (Zaburi 18:30). Kwa hivyo ikiwa tunataka kujua kile ambacho Mungu amesema kuhusu Kristo Yesu na kuhusu ujumbe wa injili, basi tunafaa kuisoma Biblia na kuitii. Je, tutasoma wapi katika Biblia ili tufahamu ujumbe wa injili kwa wazi kabisa? Je, tutasoma wapi katika Biblia ikiwa tunataka kujua maana ya neno hili injili? Njia moja tunaweza kutumia ni kutazama jinsi neno injili lilivyotumika katika Biblia haswa katika Agano Jipya. Lakini tukitumia njia hii, kwa ukweli hatutafahamu maana ya injili kamili kwa sababu kuna mahali katika Agano Jipya ambamo mtu fulani alihubiri injili bila kutumia neno injili. Kwa mfano katika Matendo ya Mitume 2, Petro alihubiri habari njema bila kutumia neno injili. Pia Yohana alitumia neno hili mara

Page 9: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

moja katika maandishi yake yote ingawa katika maandishi haya yote anatueleza injili ni nini (Ufunuo 14:6). Tuzingatie ujumbe huu wa injili kwa kutazama jinsi wakristo wa kale walivyofundisha kuhusu maisha, kifo na kufufuka kwa Kristo Yesu. Tunaposoma vitabu ambavyo vimeandikwa na mitume wa Kristo, tunaona kwamba wao wanazungumza kuhusu yale walijifundisha kutoka kwa Kristo Yesu kuhusu ujumbe wa injili. Pia tutatazama jinsi mitume na wakristo wa kwanza walivyohubiri ujumbe huu. Pia tutaona maswali na ukweli ambao wakristo hawa walizingatia katika kazi yao ya kuhubiri ujumbe wa injili kuhusu Kristo Yesu. Ujumbe wa injili katika Warumi 1-4 Katika barua hii ya Warumi, tunapata mafundisho ya wazi kabisa kuhusu ujumbe wa injili. Paulo aliandika barua hii kwa sababu alitaka wasikilizaji wake wamjue, wajue huduma yake na haswa ujumbe ambao alikuwa akihubiri. Alitaka wajue kwamba ujumbe ambao alikuwa anahubiri ndio ujumbe ambao walikuwa wameuamini. Anaanza barua hii kwa kusema, “Mimi siionei haya Injili ya Kristo kwa maana ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aminiye” (Warumi 1:16). Baadaye katika sura nne za kwanza, Paulo anafafanua ujumbe wa injili ya Kristo. Wakati alikuwa anafanya hili, alizungumza kuhusu mambo fulani ya muhimu sana kuhusu ujumbe huu wa injili ya Kristo. Mambo ambayo aliyazungumza hapa, yanajitokeza mara kwa mara katika barua hii yote. Kwanza tutazame mafundisho ya Paulo katika sura nne za kwanza za kitabu cha Warumi. 1. Alifundisha kwamba wanadamu wote wanahitajika kuajibika mbele za Mungu. Baada ya utangulizi katika Warumi 1:1-7, Paulo anaanza kufafanua ujumbe wa injili ni nini kwa kusema kwamba, “ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni” (mstari wa 18). Kwa maneno haya, Paulo alikuwa anadhihirisha kwamba mwanadamu hakujiumba wala

Page 10: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

haendelei kuwepo kwa nguvu zake wala hatoi hesabu ya maisha yake kwake mwenyewe bali kwa Mungu. Anaendelea kusema kwamba ni Mungu ambaye aliumba kila kitu hata mwanadamu. Kwa sababu alituumba, Mungu anatuamuru tumwabudu. Katika mstari wa 21, Paulo anasema kwamba, “kwa maana ingawa walimjua Mungu, hawakumtukuza Yeye kama ndiye Mungu wala hawakumshukuru, bali fikira zao zimekuwa batili na mioyo yao ya ujinga ikatiwa giza.” Kwa maneno haya, Paulo anasema kwamba, kizazi cha mwanadamu kina hatia mbele za Mungu kwa sababu wanadamu hawajamshukuru wala kumwabudu Mungu ipasavyo. Ni jukumu letu kwa sababu tumeumbwa na Mungu, kumheshimu na kumpa utukufu wote; kuishi, kuzungumza, kutenda kwa njia ambayo inadhihirisha mamlaka yake juu yetu. Sisi tumeumbwa na Mungu, sisi ni mali ya Mungu, sisi tunamtegemea Mungu na tunatoa hesabu ya jinsi tunavyoishi maisha yetu Kwake. Hili ndilo jambo la kwanza Paulo anazungumzia wakati anatufafanulia ujumbe wa injili. 2. Alifundisha kwamba shida kubwa ya mwanadamu ni kwamba ameasi dhidi ya Mungu. Anasema kwamba wanadamu wote hawakumheshimu Mungu wala kumshukuru jinsi wanafaa. Mioyo yao ya ujinga ikatiwa giza “na kubadili utukufu wa Mungu aishiye milele kwa sanamu zilizofanywa zifanane na mwanadamu ambaye hufa, ndege, wanyama na viumbe vitambaavyo” (mstari 23). Hili ni jambo baya sana kwamba wanadamu wamemwacha Mungu ambaye aliwaumba na kugeukia sanamu za wanyama na ndege. Wao wameona kwamba wanatosheka kwa kuabudu vitu hivi badala ya kumwabudu Mungu. Hili ni jambo ambalo ni la kumchukiza Mungu kabisa. Hii inadhihirisha dhambi na madhara ya dhambi katika maisha ya mwanadamu. Katika sura tatu ambazo zinafuata, Paulo anasisitiza jambo hili kwamba wanadamu wote ni wenye dhambi machoni pa Mungu.

Page 11: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

Katika sura ya 1 anazungumzia watu Mataifa na katika sura ya 2 anazungumzia Wayahudi. Paulo alijua kwamba Wayahudi walikuwa wanajivuna na kuwadharau watu Mataifa. Katika sura ya 2 anazungumzia Wayahudi ambao walikuwa wanajivuna. Anasema kwamba kama tu watu Mataifa, pia Wayahudi wako na hatia mbele za Mungu na wako chini ya hukumu ya Mungu. Katika sura ya tatu, Paulo anaonyesha wazi kabisa kwamba wanadamu ni wenye hatia mbele za Mungu kwa sababu wametenda dhambi. “Kwa maana tumekwisha kuhakikisha kwa vyo vyote kwamba Wayahudi na watu Mataifa wote wako chini ya nguvu ya dhambi” (Warumi 3:9). Kwa sababu ya dhambi, kila kinywa ni kimya mbele za Mungu na hakuna yeyote ambaye anaweza kujitetea wala kutoa sababu yoyote. Ulimwengu wote, mwafrika, mzungu, kabila hili au lile, wote watasimama mbele za Mungu na kutoa hesabu ya jinsi walivyoishi maisha yao (Warumi 3:19). Unaposoma mambo haya, unaweza kusema kwamba hakuna habari njema katika maneno haya, bali kuna habari mbaya tu. Mambo haya ni mazuri kufahamu kwa sababu haya ndiyo mambo ambayo yanafungua macho yetu kwa ukweli wa maisha yetu kama wanadamu. Ikiwa mtu ataokoka, lazima afahamu vyema hali yake mbele za Mungu. Ni lazima ajue kwamba yeye ni mwenye dhambi na hana uwezo wa kujiokoa na wala hakuna mtu au kitu chochote ambacho kinaweza kumwokoa. 3. Anafundisha kwamba mwanadamu anaweza tu kuokolewa kutoka kwa dhambi zake, kupitia kwa kifo na kufufuka kwa Bwana Yesu Kristo. Baada ya kutuonyesha uovu na dhambi ya mwanadamu mbele za Mungu, Paulo anaendelea na kutuonyesha jinsi mwanadamu anafaa kusamehewa dhambi hii na uovu huu. Sasa Paulo anafundisha kuhusu njia ya wokovu ambayo ni imani ndani ya Kristo Yesu. Katika mstari wa 21, Paulo anasema, “lakini sasa, haki itokayo kwa Mungu imedhihirishwa pasipo sheria.” Kwa ufupi anasema kwamba

Page 12: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

kuna njia ambapo mwanadamu anaweza kuhesabiwa haki mbele za Mungu, yaani anaweza kuondolewa hatia ya dhambi na kuhesabiwa haki badala ya kuhukumiwa. Jambo hili halihusishi kufanya mambo mema au kuishi maisha mazuri. Yaani hatusamehewi dhambi kwa sababu tumefanya mambo mazuri au kwa kujitahidi kuishi maisha mazuri. Je, jambo hili linafanyikaje? Anajibu swali hili kwa wazi kabisa katika Warumi 3:24. Anasema kwamba hata kama tumeasi dhidi ya Mungu na kukosa tumaini lolote, wanadamu “wanahesabiwa haki bure kwa neema Yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu.” Kupitia kwa kifo na kufufuka kwa Bwana Yesu Kristo; na kupitia kwa damu na maisha yake Kristo, wanadamu ambao wanaamini wanaokolewa kutoka kwa hukumu wa Mungu ambayo wanastahili kwa sababu ya dhambi zao. Swali pia ni je, hii ni habari njema kwangu kwa njia gani? Je, ninajumlishwaje katika ahadi hii ya wokovu? Hili ni swali ambalo Paulo analijibu katika kitabu hiki cha Warumi 4. Anafundisha jinsi wanadamu wanaweza kujumlishwa katika mpango huu wa wokovu. Hili ndilo jambo ambalo analizungumzia wazi kabisa katika sura ya 3 na 4. Wokovu ambao Mungu anapeana “hupatikana kwa Yesu Kristo kwa wote wamwaminio” (Warumi 3:22). Je, wokovu huu unakuwaje habari njema kwangu? Je, huwa ninapatikanaje katika wokovu huu? Jibu ni kwamba kwa kumwamini Yesu Kristo pekee. “Lakini kwa mtu ambaye hafanyi kazi na anamtumaini Mungu, Yeye ambaye huwahesabia waovu haki, imani yake inahesabiwa kuwa haki” (Warumi 4:5). Swali manne muhimu sana. Baada ya kutazama mafundisho ya Paulo katika Warumi 1-4, tunaona kwamba sababu za yeye za kuhubiri injili zinapatikana katika maswali haya.

Page 13: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

1. Je, ni nani ambaye alituumba na tutatoa hesabu ya maisha yetu kwa nani? 2. Shida yako kuu ni gani? Yaani ukweli ni kwamba tuko katika shida kuu na ni kwa nini tuko katika shida? 3. Je, Mungu anapeana suluhisho gani kwa shida yetu? Je, Mungu amefanya nini ili kutuokoa? 4. Je, nitafanya nini ili niweze kujumlishwa katika mpango huu wa wokovu? Je, hii inakuwaje habari njema kwangu? Maswali haya manne yanahusu Mungu, mwanadamu, Kristo Yesu na kuitika kwetu juu ya mwito wa wokovu. Paulo anaendelea kufunua ahadi zingine ambazo Mungu ako nazo kwa wale wote ambao wako ndani ya Kristo Yesu. Ahadi hizi ni zinahusu ujumbe wa injili ya Kristo Yesu. Tunafaa kukumbuka kwamba kila ahadi inafahamika na kutimizwa kutoka katika ujumbe huo wa injili. Ahadi hizo zinawajia tu wale ambao wamesamehewa dhambi zao kupitia kwa imani ndani ya Yesu Kristo. Hii ndio sababu wakati Paulo anazungumza kuhusu msingi wa ujumbe wa injili yeye huwa anazingatia mambo haya manne. Ujumbe wa injili katika Agano Jipya lote. Unaposoma Agano Jipya lote, majibu kwa haya maswali manne yote huwa yanajitokeza mara kwa mara. Mitume katika Agano Jipya amazungumza mambo mengi kuhusu ujumbe huu, lakini kile cha kufahamu ni kwamba yote ambayo huwa wanayasema huwa yanatoka katika ujumbe huu wa injili. Hata wale wakristo wa zamani, haya mambo manne waliyazingatia sana katika ujumbe ambao walihubiri. Wao walisisitiza kwamba kila mwanadamu anafaa kuajibika mbele za Mungu ambaye alimwumba. Kila mwanadamu ametenda dhambi dhidi ya Mungu na anastahili kuhukumiwa. Lakini katika Kristo Yesu, Mungu anatupatia wokovu wa bure na kile tunafaa kukifanya ni kutubu dhambi zetu na kumwamini Kristo Yesu. Ujumbe wa injili unazungumzia mambo haya manne: Mungu, Mwanadamu, Yesu Kristo na kuitika kwetu kwa ujumbe wa injili.

Page 14: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

Tutazame kifungu katika Agano Jipya ambapo ujumbe wa Kristo Yesu umezungumziwa. “” (1 Wakorintho 15:1-5). Hata katika haya, tunaona kwamba Paulo anazungumza kuhusu hatari ambayo mwanadamu ako ndani. Wanadamu wamepotea katika dhambi na wanahitaji kuu ambalo ni wokovu. Wokovu ambao wanahitaji ni ule ambao Kristo alikufia msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, alizikwa na alifufuka. Tunapata wokovu huu kwa kuamini neno la Mungu ambalo tunalikisia likihubiriwa. Hata katika mahubiri ambayo yako katika kitabu cha Matendo ya Mitume, ujumbe huu muhimu wa Biblia unatangazwa wazi kabisa. Wakati Paulo aliwahubiri watu siku ya Pentekote, walipomwuliza swali hili, “Ndugu zetu tufanye nini,” Petro aliwaajibu, “Tubuni mkabatizwe kwa jina la Yesu Kristo ili mpate kusamehewa dhambi zenu” (Matendo ya Mitume 2:38). Kila mwanadamu anahitaji Mungu amsamehe dhambi zake na asimhukumu hata kama hivyo ndivyo anastahili. Kifo na kufufuka kwa Kristo Yesu ndiko kunamwezesha mwanadamu kupokea wokovu huu. Mwanadamu anafaa kuupokea ujumbe huu kwa kutubu na kumwamini Kristo Yesu. Baada ya kuokoka, Kristo anaamuru kwamba tubatizwe. “Lakini kwa njia hii Mungu alitimiza kile ambacho alikuwa ametabiri kwa vinywa vya manabii Wake wote, kwamba Kristo atateswa. Tubuni basi mkamgeukie Mungu, ili dhambi zenu zifutwe, ili zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwepo kwake Bwana” (Matendo ya Mitume 3:18-19). Mwanadamu anahitaji kusamehewa dhambi zake na wala si kuhukumiwa na Mungu hata kama hivyo ndivyo anavyostahili. Ndipo tuweze kupata msamaha huu, Kristo alikufa na akafufuka. Kile mwanadamu anahitaji kufanya ni kutubu na kumwamini Kristo Yesu. “Sisi ni mashahidi wa mambo yote aliyoyafanya katika Uyahudi na Yerusalemu. Wakamwua kwa kumtundika msalabani. Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu siku ya tatu na kumwezesha kuonekana na watu. Hakuonekana kwa watu wote, lakini kwetu sisi

Page 15: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

tuliochaguliwa na Mungu kuwa mashahidi, ambao tulikula na kunywa naye baada kufufuka kwake kutoka kwa wafu. Naye alituamuru kuhubiri kwa watu wote na kushuhudia kwamba Yeye aliyetiwa mafuta na Mungu kuwa hakimu wa walio hai na wafu. Manabii wote walioshuhudia juu yake kwamba kila mtu amwaminiye hupokea msamaha wa dhambi katika jina lake” (Matendo ya mitume 10:39-43). Huwa tunapata msamaha wa dhambi kupitia kwa Kristo Yesu ambaye alisulibiwa msalabani Kalivari kwa ajili ya dhambi zetu. “Kwa hiyo ndugu zangu, nataka ninyi mjue kwamba kwa kupitia huyu Yesu msamaha wa dhambi unatangazwa kwenu. Kwa kumpitia Yeye, kila mtu amwaminiye anahesabiwa haki kwa kila kitu ambacho asingeweza kuhesabiwa haki kwa sheria ya Mose” (Matendo ya Mitume 13:38-39). Pia katika mistari hii tunaona kwamba unazungumza kuhusu Mungu, mwanadamu, Kristo Yesu na jinsi wanadamu anafaa kufanya wakati ameusikia ujumbe wa injili. Kila mwanadamu anahitaji kusamehewa dhambi zake kupitia kwa Kristo Yesu. Kila anayeamini anaokolewa. Kufafanua msingi ya kweli ya Biblia katika njia tofauti tofauti. Mambo haya manne, yaani Mungu, mwanadamu, Yesu Kristo na jinsi wanadamu anafaa wakati ameusikia ujumbe wa injili, ni mambo ambayo yalihubiri na mitume kwa ndani sana. Wao walimaliza muda wa kutosha katika kufundisha mambo haya. Lakini pia kuna wakati ambapo kwa sababu muda mambo haya hayafafanuliwi kwa ndani sana. Wakati Paulo alipozungumza na Wafilisofia wa Areopagus, alianza kwa kuwaeleza kwanza kuhusu Mungu. Unaposoma mahubiri ya Paulo katika Matendo ya Mitume 17, utaona kwamba yeye hakuhubiri habari njema bali yale ambayo alihubiri yanaweza kuonekana kuwa habari mbaya. “Basi sasa kile ambacho mmekuwa mkikiabudu kama kisichojulikana, ndicho ninachowahubiria” (matendo ya mitume 17:23). Baadaye katika

Page 16: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

mistari ya 24-28, anawaeleza kwamba kuna Mungu na kwamba huyu ndiye Mungu ambaye ameumba ulimwengu wote na kwamba huyu Mungu anatuita tumwabudu kwa kweli. Baadaye katika mstari wa 29, Paulo anafafanua dhambi na madhara yake. Anasema kwamba mwanadamu badala ya kumwabudu Mungu ambaye amemumba, yeye amegeukia sanamu. Pia anasema kwamba Mungu atahukumu ulimwengu kwa haki akitumia mtu aliyemchagua, kwake huyu amewahakikishia watu wote kwa kumfufua Yeye kutoka kwa wafu” (mstari wa 31). Unapotazama mahubiri haya, hakuna mahali ambapo ametaja msamaha wa dhambi, msalaba wa Kristo na pia hakuna ahadi ya wokovu. Yeye alizungumza tu kuhusu sheria ya Mungu na kufufuka kwa Kristo kama hakikisho la hukumu ambayo inakuja. Paulo pia hakutaja jina la Kristo. Katika maneno haya yote, Paulo hakuonekana kuwa anahubiri habari njema. Lakini unaposoma mistari ya 32-34, tunaambiwa kwamba wale ambao Paulo alihubiria walitaka tena kumsikia na mwishiwe kuna wale ambao waliamini. Paulo aliwahubiria kwamba kulikuwa na njia ambayo mwenye dhambi anafaa kuokolewa kutoka kwa ghadhabu ya Mungu. Kama tu mitume wengine, Paulo pia alifundisha kuhusu misingi mikuu ya dini ya ukristo. Wakristo wa kwanza misingi hii ndiyo ilikuwa msingi wa mafundisho yao, yaani Mungu, mwanadamu, Kristo Yesu na jinsi mwanadamu anafaa kufanya wakati ameusikia ujumbe wa injili. Ukweli ambao kila mwanadamu anafaa kujua ni kwamba, Mungu ni hakimu na tumetenda dhambi dhidi yake. Lakini Kristo Yesu alikuja hapa ulimwenguni kufa kwa ajili yetu wenye dhambi ili Mungu aweze kutusamehe dhambi ikiwa tutatubu na kumwamini Kristo Yesu. Mungu ndiye mwumba mwenye haki Mawazo mabaya kuhusu Mungu ni nani.

Page 17: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

Watu wengi wako na mawazo tofauti kuhusu Mungu, Yeye ni nani na njia zake na jinsi anavyofanya kazi yake. Kuna wale ambao wanawaza kwamba Mungu hayaelewi mambo mengi kuhusu ambayo yanaendelea katika ulimwengu huu. Wengine wanawaza kwamba sasa hana mamlaka juu ya mambo ambayo yanaendelea humu ulimwenguni. Wengine pia hawaamini kwamba Mungu yupo na kwamba anaishi. Kuna wale ambao wanawaza kwamba wanaweza kumwamuru Mungu kufanya mambo fulani na akayafanya kwa sababu wao wamesema afanye hivyo. Kuna wale ambao wao wanajua Mungu yupo na kwamba wanaweza kuenda kwake wakati wowote na kuomba kile wanataka. Wengine wanasema kwamba Yeye ni mtu mzuri ambaye ni rahisi kuzungumza naye. Wengi wanawaza kwamba Yeye wakati wanazungumza naye, Yeye huwajibu kwa kuwaonyesha mambo fulani fulani au ishara fulani fulani. Kuna wale ambao wao huwaza kwamba Mungu ni mzuri na hahukumu yeyote na hatawahi kumpeleka yeyote jahanum bali atawapeleka wote mbinguni. Wao wanasema kwamba Mungu ni wa upendo sana na kazi yake ni kuwasamehe wenye dhambi. Kuna wale ambao wasoma Biblia hapa na pale na wanajua mambo kadhaaa kuhusu Mungu na kile ambacho amekifanya. Mambo haya yote kumhusu Mungu si ya kweli na hata kama yanaonekana kuwa ya kweli, Mungu hayuko hivi. Hata wale wengi ambao wanadai kunjua na kumwabudu Mungu huwa wanawaza hivi kumhusu Mungu. Ni jambo la kuhuzunisha kwamba hata wale ambao wameokoka, wengi hawamfahamu jinsi wanafaaa kumfahamu kwa sababu wao si waangalifu katika kusoma na kutii Biblia zao. Ikiwa sisi ambao tumeokoka tutaweza kuhubiri injili ya Kristo leo, ni lazima tufahamu Mungu ni nani. Kwa hivyo hapo ndipo tutaanzia; Mungu. Ni lazima kila mkristo atenge muda wa kusoma Biblia ili aweze kufahamu kujifunza yale ambayo Mungu amefunua kwetu

Page 18: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

kuhusu Yeye mwenyewe. Ukweli ni kwamba wakati mtu anahubiri injili, si lazima asemi kila kitu ambacho anakijua kuhusu Mungu ndipo msikilizaji wake apate kuokoka. Kuna mambo ambayo lazima mtu ayafahamu kweli ikiwa ataweza kuelewa ujumbe wa injili. Lazima mtu afahamu kwamba Mungu ndiye aliyeumba kila kitu na kwamba Yeye ni mtakatifu na wa haki. Mungu mwumbaji Katika Mwanzo wa Biblia tunasoma kwamba, “Mungu aliumba mbingu na dunia” (Mwanzo 1:1). Ikiwa mtu hataelewa jambo hili, ni wazi kwamba hataelewa chochote kuhusu dini ya ukristo. Kitabu cha Mwanzo kinaanza kwa kutueleza kuhusu kuumbwa kwa ulimwengu na yale yaliyomo: milima, mabonde, wanyama, samaki, ndege wa angani na wanyama wa baharini, nyota, mwezi na viumbe vote ambavyo viko humu ulimwenguni. Haya yote yalifanyika kutokana na neno lake ambalo alilizungumza. Pia haya yote yakuumbwa kutoka kwa chochote, bali Mungu aliumba na akayafanya yakuwepo. Mungu alizungumza na yakakuwepo; “Iwepo nuru nayo nuru ikawepo” (Mwanzo 1:3). Kuna mistari mingi katika Biblia ambayo inatuonyesha kwamba uumbaji wa kila kitu unadhihirisha utukufu na nguvu za Mungu: “Mbingu zinatangaza utukufu wa Mungu, anga zahubiri kazi ya mikono yake” (Zaburi 19:1). Katika Warumi 1:20 tunasoma kwamba, “Kwa maana tangu kuumbwa kwa ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani, uwezo Wake wa milele na asili Yake ya Uungu, umeonekana waziwazi ukitambuliwa kutokana na yale aliyoyafanya ili wanadamu wasiwe na udhuru.” Hadithi ya kuumbwa kwa kila kitu katika kitabu cha Mwanzo, inaonyesha umuhimu wa vile vitu ambavyo viliumbwa. Wakati wa kuumbwa kwa kila kitu unaonyesha umuhimu wa vitu hivyo. Kwa mfano nuru, bahari, arthi, mwezi, jua, ndege wa angani, samaki na wanyama ndiyo viliumbwa kwanza. Halafu ndipo mwanadamu akaumbwa mwishowe. “Ndipo Mungu anasema, 'Tufanye mtu kwa

Page 19: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale juu ya samaki wa baharini na ndege wa angani, juu ya mifugo, juu ya dunia yote, na juu ya viumbe wote watambao juu ya nchi.' Kwa hiyo Mungu alimwumba mtu kwa mfano wake mwenyewe, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanadamu na mwanamke aliwaumba” (Mwanzo 1:26-27). Ni jambo la kuzingatia sana na kufurahia kwamba Mungu ndiye aliyetuumba na kwamba pia Yeye ameumba kila kitu ambacho kinaonekana ulimwenguni. Ni jambo la uongo kwamba ulimwengu upo kwa sababu ya jambo lingine kando na kwamba uliumbwa na Mungu. Mwanadamu hayuko hapa kwa sababu kwa miaka mingi amekuwa akibadilika kutoka katika mnyama fulani hadi akawa mwanadamu jinsi alivyo sasa. Mwanadamu ameumbwa na Mungu na katika mfano wa Mungu. Kwa sababu hii, kila mwanadamu ana jukumu la kufanya na anaajibika mbele za Mungu. Kuelewa jambo hili ndio msingi wa kufahamu ujumbe wa injili. Ukweli ni kwamba mwanadamu hayuko huru kufanya jinsi anavyotaka. Sisi tumeumbwa na Mungu na kwa hivyo sisi ni wake Mungu. Kwa sababu ni Mungu ambaye ametuumba, Yeye ana mamlaka ya kutueleza kuishi jinsi Yeye anapenda. Katika Bustanini mwa Edeni, alimwambia Adamu ni mti gani ambao alikufa kula matunda yake na gani ambao hakufa kula matunda yake (Mwanzo 2:16-17). Siyo hali kwamba Mungu alikuwa anataka kumjaribu Adamu kuona atafanya nini. Biblia inatufundisha kwamba Mungu ni mwema na hamjaribu yeyote. Mungu alijua nini ilikuwa bora kwa watu wake na aliwapatia sheria ambazo zingewawezesha kuendelea kuishi maisha yao kwa furaha na utulivu. Kuelewa jambo hili, ni kitu cha maana sana ikiwa mtu yeyote anataka kufahamu vyema ujumbe wa injili. Majibu ya Mungu kwa dhambi ni, ujumbe wa injili. Dhambi nayo ni kukataa kuongozwa na

Page 20: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

Mungu. Msingi mkuu wa maisha ya mwanadamu ni kwamba Mungu ndiye aliyemwumba na kwa hivyo yeye ni mali ya Mungu. Mungu Mtakatifu na mwenye haki Ni ukweli kwamba Mungu ni mwenye upendo na Yeye ni Mungu mzuri; pia Yeye ni mwenye huruma na mwenye kuwasamehe wengi. Wakati Mungu alimwomba Mungu kwamba umwonyesha utukufu wake na umweleza Jina Lake, Mungu alimjibu, “Bwana, Bwana, Mungu mwenye huruma na neema, asiye mwepesi wa hasira, mwingi wa upendo na uaminifu, akidumisha upendo kwa maelfu, pia akisamehe uovu, uasi na dhambi, lakini haachi kuadhibu mwenye hatia, huwaadhibu watoto na watoto wao kwa ajili ya dhambi ya baba zao hata katika kizazi cha tatu na cha nne” (Kutoka 34:6-7). Hili ni jambo zuri sana kwamba wakati Mungu anataka kutuonyesha utukufu wake na kutueleza Jina lake, Yeye anasema kwamba ni Mungu asiye mwepesi wa hasira, mwingi wa upendo. Lakini pia anasema kwamba, haachi kuadhibu mwenye hatia. Watu wengi leo wanamjua Mungu kuwa Mungu mwenye wingi wa upendo lakini wanasahau kwamba pia Yeye haachi kuadhibu mwenye hatia. Wanawaza kwamba Mungu huwa haadhibu dhambi bali Yeye huipuuza. Wengi huwa wanakataa kwamba Mungu mwenye upendo hawezi kuwaadhibu watu wake. Katika kitabu hiki, tutaona jinsi upendo wa Mungu na kuadhibu kwake mwenye hati yanavyotekelezwa kupitia kifo cha Bwana Yesu Kristo msalabani. Lakini kabla tufanye hivyo, ni lazima tufahamu kwamba upendo wa Mungu hauondoi utakatifu na haki Yake. Katika Biblia tunaelezwa kwamba ni mwenye haki na mtakatifu: “” (Zaburi 11:7). Pia Zaburi 33:5 inasema kwamba, “” Katika Zaburi 89:14; 97:2, tunasoma kwamba ,“” Mistari hii yote inatuonyesha kwamba Mungu ndiye anatawala kila kitu na Yeye ni Matakatifu na mwenye haki. Kulingana na Biblia, Mungu si Mungu wa upendo na huruma tu, bali pia Yeye ni Mungu mwenye haki na Mtakatifu. Hii inatuonyesha kwamba Mungu huwa hapuuzi tu dhambi na Yeye huwa hajifichi

Page 21: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

kutokana na dhambi, bali Yeye huadhibu dhambi. Kwa sababu watu wengi wanataka kuficha dhambi zao ambazo wanazijua vyema, wao hutaka kujidanganya kwamba Mungu hatawahi kuhukumu dhambi zao na wao wenyewe. Kwa sababu wanajua kwamba wao wamefanya dhambi na kwamba hawako tayari kutubu dhambi zao, wao hudai kwamba Mungu ni wa huruma na upendo tu. Lakini pia wakati huo huo wakati wanakumbana na uovu ambao unatatiza maisha yao, wao hutamani na kuomba kwamba Mungu atahukumu uovu huo. Hawa wale ambao wanataka Mungu apuuze dhambi zao lakini amhukumu mwuaji au mwizi. Wao katika mioyo yao huomba Mungu nisamehe hata kama wao hawako tayari kutubu, na kwa yule ambaye anatatiza maisha yo, wao huomba, “Mungu mhukumu huyu.” Wengi wanataka Mungu ambaye anapuuza dhambi kabisa. Lakini wakati tunasoma Biblia, tunasoma kwamba Mungu ni mwenye haki na ni Mtakatifu, na kwa sababu Yeye yuko hivi, hatapuuza kamwe dhambi au uovu. Yeye atahukumu uovu na dhambi vikali sana. Tunasoma katika Habakuki kwamba, “” (Habakuki 1:13). Kusema kwamba Mungu hahukumu dhambi na uovu, ni kusema kwamba Yeye hatawali kila kitu na kila mahali. Pia ni kukata kuwepo Kwake na kukubali kwamba dhambi ni kitu bora. Watu wengi hawana shida kabisa kuwaza kwamba Mungu ni mwenye upendo na huruma. Wengi wamepata mawazo haya kutoka kwetu wakristo. Lakini ukweli ni kwamba ikiwa mtu yeyote atafahamu utukufu na nguvu za ujumbe wa injili ya Kristo, lazima afahamu kwamba huyu Mungu ambaye ni mwenye huruma na upendo, ni Mungu Mtakatifu na mwenye haki. Huyu Mungu hatawahi kupuuza dhambi wala kuikubali iendelee milele. Mwanadamu ni mtenda dhambi Kuna wengi ambao huwaza kwamba dhambi si kitu kibaya sana. Wao huwaza hivyo kwa sababu wao huwa wanatofautisha dhambi. Kwa mfano wengi huwaza kwamba kuna dhambi kubwa na ile ndogo na kwamba wakati Mungu anashughulika nayo, Yeye huwa

Page 22: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

anaadhibu sana wale ambao wamefanya dhambi kubwa na kupuuza wale ambao wanafanya dhambi kidogo. Biblia inafundisha kwamba dhambi ni zaidi ya kufanya mambo fulani fulani na pia hakuna tofauti ya dhambi kubwa na ndogo, mbele ya Mungu dhambi ni dhambi. Kutenda dhambi ni kuvunja uhusiano na Mungu na ni kumkataa Mungu, ni kuvunja sheria ya Mungu, ni kukata mamlaka ya Mungu ambaye alituumba. Kwa ufupi ni kwamba dhambi ni kuasi dhidi ya Mungu. Je, nini ilifanyika ndipo mwanadamu akajipata kuwa katika dhambi. Mungu alipomwumba mwanadamu na kusudi kwamba wao waishi maisha matakatifu katika furaha kamilifu wakimwabudu, wakimtii Mungu kikamilifu. Wao walikuwa waishi maisha ya kuwa na ushirika na Mungu. Mungu alimwumba mwanamke na mwanamume katika mfano wake kumaanisha kwamba wao walikuwa wawe kama Yeye. Wao walikuwa wawe na uhusiano naye kudhihirisha utukufu wa Mungu katika maisha yao. Hii inamaanisha kwamba mwanadamu alikuwa na jukumu la kufanya. Wanadamu walikuwa wawe wakilishi wa Mungu na wakitawala ulimwengu chini Yake. Mungu aliwaamurisha wanadamu kwamba, “Zaeni na mkaongezeke, mkaijaze tena dunia na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi” (Mwanzo 1:28). Mwanadamu alikuwa atawale juu ya kila kitu na utawala huu ulikuwa unatoka kwa Mungu. Mamlaka haya hayakuwa yao bali yalikuwa yanatoka kwa Mungu. Wakati Adamu na Hawa walikuwa watekeleza majukumu yao, walikuwa wakumbuke kwamba wao walikuwa chini ya mamlaka na utawala wa Mungu. Ni Mungu ambaye aliwaumba na kwa hivyo Yeye ana mamlaka juu yao na kwa hivyo lazima watii yale ambayo anawaamurisha wafanye. Mti ule wa kujua baya na uzuri ulikuwa uwakumbushe kuhusu jambo hili (Mwanzo 3:17). Wakati Adamu na Hawa walitazama mti na kuona matunda yake, walifaa wakumbuke kwamba wao

Page 23: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

hawakuwa na mamlaka yote na kwamba wao ni viumbe ambavyo vinaishi kwa kumtegemea Mungu pekee. Wanadamu ni wafanyikazi na Mungu ndiye Mfalme. Wakati Adamu na Hawa walikula tunda, hawa kukosa tu kutii amri ya Mungu ambayo ilikuwa msile tunda, bali wao walitenda jambo ambalo lilikuwa baya sana machoni pa Mungu. Kula lile tunda, walifanya dhambi kubwa sana machoni pa Mungu. Kwa kufanya hivi, walikataa uongozi wa Mungu juu yao na kutaka kuwa jinsi nyoka alikuwa amewaambia “kama Mungu.” Mungu alikuwa amewapatia kila kitu wakitawale isipokuwa. NI Mungu tu ambaye hawakuwa wamtawale kwa sababu Yeye ni Mungu ambaye amewaumba na ndiye anayetawala. Lakini hata hivyo, Adamu aliona kwamba ni vyema aasi dhidi ya Mungu. Uovu mkuu ambao walifanya, yaani Adamu na Hawa wakati walikosa kumtii Mungu ni kwamba walifanya uamuzi kumkata Mungu kama Mfalme juu yao. Mungu alikuwa amewaambia kwamba siku ile watakula lile tunda, wao walikuwa wakufe. Kwa kusema hivi, Mungu alimaanisha kwamba wao walikuwa wakufe kiroho, uhusiano kati yao Naye ulikuwa ukatike na wao wangefanyika maadui wake badala ya kuwa marafiki wake (Mwanzo 2:17). lakini hata hivyo, wao hawakujali wala kuogopa. Wao walibadalishi furaha yao na Mungu kwa kufuata anasa na kutaka kujitukuza wenyewe. Biblia inafundisha kwamba kukosa kutii Mungu ni dhambi. Dhambi inamaanisha kufanya kinyume na neno la Mungu. Hii haimaanishi kwamba Adamu na Hawa walijaribu sana kufanya mapenzi ya Mungu lakini walikosea kidogo. Hii siyo hali, ukweli ni kwamba wao walijitolea kufanya kinyume na Mungu. Mapenzi na nia yao ilikuwa kinyume kabisa na yale ambayo Mungu alitarajia kutoka kwao, kwa hivyo wao walitenda dhambi. Kwa wazi kabisa na kwa kupenda, walikosa kutii amri ya Mungu na kwa hivyo uhusiano wao Naye ulikatika. Wao walimkata Mungu kuwa Bwana wao.

Page 24: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

Matokeo ya dhambi ya Adamu na Hawa yalikuwa mabaya sana kwao na hata kizazi chao chote na kwa viumbe vyote vya Mungu. Wao wenyewe walifunkuzwa kutoka kwa Bustani ya Edeni. Ardhi sasa hakutoa matunda na chakula jinsi ilivyokuwa ikitoa. Sasa walihitaji kufanya kazi kwa bidii na uchungu mwingi ili waweze kupata chakula chao. Wao sasa walikufa, yaani walikufa kiroho na pia walianza kufa kimwili. Wao hawakufa hapo na hapo, miili yao iliendelea kuishi, lakini maisha ya kioroho na Mungu yalikatizwa hapo na hapo. Uhusiano na ushirika wao na Mungu uliisha hapo na hapo. Si tu Adamu na Hawa ambao walikufa kiroho, lakini pia sisi tulikufa Biblia inafundisha kwamba si tu Adamu na Hawa ambao walianguka dhambi na kufa kiroho, bali inafundisha kwamba wakati wao walianguka dhambini na kufa kiroho, tulianguka pamoja na o na kufa na kufa pamoja nao kiroho. Biblia inafundisha kwamba, “Kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 3:23); “Hakuna mwenye haki, hakuna hata mmoja” (Warumi 3:10). Huu ndio ukweli ambao unapatikana katika ujumbe wa injili. Kwa watu wengi, ujumbe huu ni kinyume na jinsi wanavyojiwazia wao wenyewe. Kwa kawaida wanadamu wengi huwa wanawaza kwamba wao si watu wabaya sana na kwamba wako na mambo fulani fulani ambayo wanaweza kuleta mbele ya Mungu na kukubalika naye kwa msingi wa mambo hayo. Lakini Biblia inafundisha kinyume na mawazo yao, kwani inasema kwamba kila mwanadamu ni mwenye dhambi na kwamba hana chochote ambacho anaweza leta mbele ya Mungu na akubalike kwa ajili ya hicho. Hii ndiyo sababu, ni lazima tufahamu hali halisi ya jinsi tulivyo na hatari kuu ya dhambi zetu. Ikiwa tutawaza kinyume na jinsi Biblia inavyofundisha kuhusu dhambi, bai hatutakuwa tumeelewa ujumbe wa injili ni nini. Nitatoa mifano ifuatayo kukueleza jinsi wakristo wengi wanavyowaza kuhusu dhambi.

Page 25: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

1. Wengi wanawaza kwamba dhambi ni mambo ambayo yanamfanyikia mtu au matendo mabaya. Wengi leo wanafundishwa na kuwaza kwamba Yesu Kristo alikuja hapa ulimwenguni kuokoa watu kutoka kwa uchungu ambao wanakumbana nao, mateso na udhaifu. Haya ni mambo ambayo yametokana na dhambi na ni kweli kwamba ni mambo mabaya na hakuna mtu ambaye anataka kuendelea katika mambo haya. Biblia inafundisha kwamba dhambi ndiyo sababu ambayo ilimfanya Kristo Yesu aje hapa ulimwenguni ili aweze kuwaokoa wengi kutoka katika dhambi hiyo. Kile kila mwanadamu anafaa kujua ni kwamba, amemuasi Mungu na anaenda kinyume na neno lake Mungu. Sisi tumepuuza amri zake na kwa hivyo tumetenda dhambi dhidi yake. Ikiwa mtu yeyote anataka kuokolewa, ni sharti afahamu kwamba, dhambi ni zaidi ya matendo au tabia. Ni kwa sababu ya dhambi wengi watahukumiwa jahanum. 2. Wengi wanawaza kwamba dhambi ni kuvunja uhusiano. Biblia inafundisha kuhusu umuhimu wa uhusiano. Wanadamu wameumbwa waishi katika ushirika na uhusiano mwema na Mungu. Kile kila mwanadamu anafaa kukumbuka ni kwamba uhusiano huu si kama uhusiano mwingine ambao tunakuwa nao na wanadamu wengine. Huu si uhusiano kati ya watu wawili ambao wako sawa, si uhusiano ambamo sheria, hukumu na adhabu hazizingatiwi hata kidogo. Ukweli ni kwamba huu ni uhusiano katika ya Mfalme na watumwa wake. Wakristo wengi wakati wanawaza kuhusu dhambi, wao huwaza kwamba uhusiano huu kati ya Mungu na mwanadamu, ni uhusiano ambao mtu anahitaji tu kusema pole na kukubali msamaha wa Mungu. Wanawaza kwamba huu ni uhusiano kama tu ule kati ya wawili ambapo wanapokoseana, wanaombana pole na maisha yanaendelea. Katika uhusiano wetu na Mungu, wakati mtu anatenda dhambi, yeye huwa anafanya kinyume na Mungu. Na kwamba ya hiyo, yeye huwa anavunja sheria ya Mungu na hukumu na ghadhabu

Page 26: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

ya Mungu huwa inakuwa juu yake. Ndipo Yeye aweze kurudi katika uhusiano na ushirika mwema na Mungu, yeye huwa anahitaji Kuenda kwa Kristo Yesu ambaye alikufa kwa niaba yake msalabani na kuzibeba dhambu zake ikiwa kweli atapata msamaha wa dhambi zake. Biblia inafundisha wazi kwamba dhambi ni kuvunja uhusiano na ushirika na Mungu mwenyewe. Wakati mtu anafanya hivyo, yeye huwa anamkataa Mungu kama Mfalme juu ya maisha yake. Hii si tu kuzini au kuasi hata kama mambo haya ni dhambi. Hii ni kumsaliti Mungu. Ikiwa hatutafahamu dhambi ni nini, basi hatutaweza kufahamu kamwe kwa nini Kristo Yesu alikufa msalabani. 3. Wengi wanawaza kwamba dhambi ni kuwaza vibaya. Wengi ambao wanawaza kwamba wanaweza kujiondolea dhambi wenyewe, ndio huwa wanakuwa na mawazo ya aina hii. Wengi wao ni wale ambao wanachunga katika makanisa makubwa sana ulimwenguni. Kile wao wanafanya ni kuwaambia watu kwamba dhambi zao si mbaya sana na kwamba ni mawazo yao ambayo yanawafanya wakose kuwa na afya mzuri na pesa nyingi. Kwa hivyo wanawaambia watu kwamba ikiwa wao watawaza vizuri na kumwomba Mungu awasaidie basi wao watashinda dhambi. Katika haya yote, wao huwa wanaahidi tu pesa na maisha mazuri. Bwana Yesu Kristo hakufa ili tuwe na maisha mazuri au tuwe na pesa. Shida kubwa sana ambayo mwanadamu ako nayo ni kwamba yeye anajiwazia kuwa mtu mkuu. Hivi ndivyo nyoka alivyo alivyomwambia Hawa wakati alikuwa ana mjaribu. Alimwambia kwamba yeye atakuwa kama Mungu. 4. Wengi wanawaza kwamba dhambi ni dhambi nyingi. Kuna tofauti kati ya kufahamu kwamba wewe uko na hati ya dhambi nyingi na kufahamu kwamba wewe uko na hatia ya dhambi. Watu wengi hawana shida kukubali kwamba wao wametenda dhambi nyingi kwa sababu wao huwa wanawaza na kukumbuka dhambi hizo ambazo wamezitenda.

Page 27: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

Mara mingi huwa hatuogopeshwi na dhambi za watu kwa sababu tunaziona katika maisha yetu na katika maisha ya wengine kila wakati. Lakini ni jambo la kushitua ni wakati Mungu anatuonyesha wazi dhambi katika maisha yetu na uovu wa dhambi hiyo. Biblia inafundisha kwamba dhambi imo ndani mwetu na iko nasi na si kwamba iko juu yetu. Biblia inafundisha kwamba dhambi imo ndani ya mwanadamu kando na mawazo y6a wengi kwamba dhambi iko juu ya mwanadamu. Kwa kusema hivi wao huwaza kwamba dhambi ni kama kitu ambacho kinaweza kuoshwa na sabuni au maji na kukuondokea. Dhambi imo ndani mwetu na kwa hivyo ni damu tu ya Kristo Yesu ambayo inaweza kutusafisha na siyo maji wala kitu kingine chochote. Paulo anasema kwamba, “Nasi kwa asili tulikuwa wana wa ghadhabu, kama tu mwingine yeyote” (Waefeso 2:3). Warumi 5, inafundisha kwamba wakati Aqdamu alianguka dhambi, pia sisi tulianguka pamoja naye. Bwana Yesu Kristo alifundisha hivi, “Kwa maana ndani ya moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na masingizio” (Mathayo 15:19). Matendo na maneno mabaya ambayo mtu anafanya na kusema yanatokana na moyo wa mtu huyu ambao ni mwovu. Kila sehemu ya mwanadamu imenajisiwa na dhambi na ina tawaliwa na dhambi. Jinsi tulivyo, hisia zetu na mapenzi yetu, haya yote yametawaliwa na dhambi. Hii ndiyo sababu Paulo anasema katika Warumi 8:7 kwamba, “Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui na Mungu, kwa maana haiitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.” Katika mstari huu tunajifunza kwamba dhambi iko katika kila sehemu ya mwili wa mwanadamu. Haitoshi tu kusema kwamba Bwana Yesu Kristo alikuja hapa ulimwenguni kuwaokoa wenye dhambi ikiwa kwa kusema hivi tunamaanisha kwamba alikuja kutuokoa kutoka kwa makosa fulani fulani. Ni hadi wakati tunafahamu vyema kwamba kwa asili sisi ni

Page 28: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

wenye dhambi na kwamba sisi ambao tumeokoka tulikuwa wafu katika makosa na dhambi zetu (Waefeso 2:1,5). 5. Hukumu ya Mungu dhidi ya dhambi Katika Warumi8 3:19 tunasoma kwamba, “Basi tunajua ya kwamba chochote sheria inachosema, inawaambia wale walio chini ya sheria ili kila kinywa kinyamazishwe na ulimwengu wote uwajibike kwa Mungu.” Kile Paulo anasema hapa ni kwamba Wayahudi na watu Mataifa wote wote wametenda dhambi na wako na hatia mbele za Mungu. Anasema, “kila kinywa kinyamazishwe na ulimwengu wote uwajibike kwa Mungu.” Hii inamaanisha kwamba watu watakaposimama mbele za Mungu watakuwa wenye hatia na kustahili ghadhabu ya Mungu mwenye haki. Biblia inafundisha kwamba Mungu ni Mungu mtakatifu na mwenye haki na kwamba hatapuuza dhambi yoyote bali ataihukumu. Katika Warumi 6:23 tunasoma kwamba, “Mshahara wa mauti ni kifo.” Mstari huu unafundisha kwamba hukumu ya dhambi ni kifo. Hiki si kifo tu cha mwili bali zaidi ni kifo cha kiroho. Huku ni kutenganishwa kabisa na Mungu mtakatifu. Nabii Isaya anazungumza kuhusu jambo hili kwa kusema, “Lakini maovu yenu yamewatenga ninyi na Mungu wenu, dhambi zenu zimewaficha ninyi uso wake, ili asikie” (Isaya 59:2). Watu wengi wanazangumza kuhusu mstari huu kana kwamba Mungu ni Mungu ambaye anapuuza dhambi. Mstari huu unafundisha kwamba Mungu anahukumu dhambi kwa njia ya kutisha sana. Tunasoma katika kitabu cha Ufunuo kwamba malaika saba waliambiwa kwamba, “Nendeni, mkayamwage duniani hayo mabakuli saba ya ghadhabu ya Mungu” (Ufunuo 16:1). Kuhus wale ambao hawatakuwa wameokoka, Biblia inasema kwamba, “Ndipo wakawakusanya wafalme pamoja mahali paitwapo kwa Kiebrania. Malaika wa saba akamimia bakuli lake angani na sauti kubwa ikatoka mle hekaluni katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa” (Ufunuo 6:16-17). Wao watamwona Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana na wataogopa kwa

Page 29: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

kuwa “Atalikanyaga shinikizo la mvinyo wa ghadhabu ya Mungu Mwenyezi” (Ufunuo 19:15). Biblia inafundisha kwamba mwisho wa wale ambao wamekataa kuokoka ni jahanum milele. Kitabu cha hukumu kinafafanua mahali hapo kuwa ziwa la moto (Ufunuo 20:10) na Kristo Yesu anasema kwamba humo ni mahali ambapo kuna moto ambao hauzimi (Marko 9:43). Biblia inaeleza kuhusu jahanum kama mahli ambapo kuna mateso na kilio sana lakini ni jambo la kuhuzunisha kwamba wengi ambao wanahubiri kuhusu mahali hapa, wao huzungumza kana kwamba mateso ya huko ni machache na wengi wanaweza kuyavumilia. Ikiwa kweli jahanum ni mahali ambapo mtu anaweza kupavumilia, je kwa nini basi tuhubiri tukiwaonya watu kuhusu mahali humo? 6. Wengi wanawaza kwamba haya mambo ya dhambi ni mambo ambayo yametungwa na wale ambao wanayahubiri. Biblia inazungumza kwa njia ya kutisha sana kuhusu jahanum. Kwa sababu hii wengi wamewaza kwamba haya si mambo ambayo yanafaa kuaminika na kwa wale ambao wameyaamini, huwa wana tukanua kwamba wao ni wazimu. Ukweli ni kwamba huu ndio ujumbe wa Biblia na kwamba haya si mawazo ya mwanadamu yeyote bali ni neno la Mungu ambaye atawahukumu wale ambao wanakataa kuokoka. Sisi ambao tumeokoka huwa tunazungumzia jahanum kwa sababu tunaamini Biblia na ujumbe wa wake kwamba ni ujumbe kutoka kwa Mungu. Tunaamini Biblia wakati inatufundisha kuhusu jahanum na hata wakati mwingine tunalia kwa sababu tunajua kwamba wale ambao tunawapenda huenda wakaingia humo ikiwa hawataokoka kwa kumwamini Kristo Yesu na kazi yake msalabani Kalvari. Huu ndiyo ukweli wa Biblia kwetu wenye dhambi. Hakuna mmoja wetu ambaye ni mwenye haki, hakuna hata mmoja. Kwa sababu ya hii, siku moja kila kinywa kitanyazishwa na ulimwengu wote utasimama mbele ya Mungu katika hukumu. Yesu Kristo ambaye ndiye Mwokozi.

Page 30: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

Hili jina ndilo tumaini ambalo kila mwanadamu ako nalo. Jina hili ndilo liko na nguvu za kuondoa dhambi na kuleta tumanini. Hili Jina liko na nguvu za kubadilisha kila hali. Tunamshukuru Mungu kwa sababu kuwepo kwa habari ya dhambi siyo mwisho wa kila kitu. Ikiwa Biblia ingekoma kwa maneno ya Paulo kwamba kila kinywa kitanyamazishwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, basi hakungekuwa na tumaini lolote kwa mtu yeyote. Kungekuwa tu na kushushwa moyo kwa kila mtu na uoga kwamba liwe liwalo, jahanum ni lazima kwa kila mtu. Lakini tunamshukuru Mungu kwa sababu kuna habari ya tumaini kwa wenye dhambi wote na habari hii ni Kristo Yesu. Kila mwanadamu ni mwenye dhambi ambaye hatima yake ni jahanum katika ziwa la moto lakini Mungu amefanya jambo la ajabu ili aweze kumwokoa mwenye dhambi kutoka katika dhambi zake na arithi ufalme wa mbinguni. Neno la Tumaini Marko anaanza kuandika kwa kusema, “Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu” (Marko 1:1). Marko na wakristo wa kwanza wote walifahamu kwamba kuja kwa Kristo Yesu ilikuwa habari njema ya Mungu kwa ulimwengu ambao ulikuwa umekufa katika dhambi. Kwa kuja kwa Kristo Yesu Mungu alikuwa anasema kwamba mambo sasa yatakuwa mapya. Pia katika kitabu cha Mwanzo, Mungu aliwapatia Adamu na Hawa neno la tumaini hata katika hali mbaya ambayo walikuwamo. Neno hili lilikuwa katika Mwanzo 3:15: “Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na wake, huo atakuponda kichwa, nawe utamgonga kisigino.” Katika maneno haya, Mungu alitaka Adamu na Hawa ambao walikuwa wameanguka katika dhambi wajue kwamba kulikuwa na tumaini kwao la kutoka katika hali ambayo walikuwamo wakati huo. Hapa kuliwa na habari njema hata katika hali mbaya sana. Katika Biblia yote, tunaelezwa jinsi mbegu hii ndogo ya ujumbe huu

Page 31: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

ilivyoendelea kukua. Kwa miaka mingi sana Mungu alikuwa anautayarisha ulimwengu kupitia kwa Sheria na manabii kuhusu mpango wake mkuu wa ushindi dhidi ya shetani kupitia kwa kifo na kufufuka kwa Bwana Yesu Kristo. Alikuwa anaonyesha kwamba hatia na dhambi ya Adamu siku itaondolewa kabisa. Alikuwa anafunua pole pole kwamba kupitia kwa Kristo Yesu shetani na dhambi vitashindwa kabisa na viumbe vyote vya Mungu vitaregeshwa katika hali yake ya utukufu. Hadithi ya Biblia ni ushindi wa Mungu dhidi ya dhambi kupitia kwa Kristo Yesu. Ni hadithi ambayo inahusu jinsi Mungu alibadilisha mambo, jinsi Mungu anavyobadilisha mambo na jinsi Mungu atakavyobadilisha mambo yote siku moja na kuyafanya kuwa kamili milele. Yesu Kristo ni mwanadamu kamili na pia ni Mungu kamili Vitabu vyote vya injili vinaonyesha kwamba Kristo Yesu alikuwa mwanadamu wa kawaida. Mathayo na Luka wanaanza kwa kutueleza kwamba malaika alimjia msichana mmoja ambaye aliitwa Maria na kumweleza kwamba yeye alikuwa amepate miba na kumza mtoto. Maria alimwuliza yule malaika, @Maadam mimi ni bikira, jambo hili litawezekanaje.@ Malaika alimjibu, @Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, nazo nguvu Zake Yeye Aliye Juu zitakufunika kama kivuli, kwa hiyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mtakatifu, naye ataitwa Mwana wa Mungu@ (Luka 1:34-35). Yohana naye anaanza kuandika kwa kusema kwamba, @Hapo mwanzo, alikuwako Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu....Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu@ (Yohana 1:1,14). Haya mambo yote kwamba Yesu Kristo alizaliwa na pia kwamba Yeye ni Mungu, yamekususdiwa kutufundisha kuhusu Yesu ni nani. Biblia inatufundisha kwa wazi kabisa kwamba Yesu kristo ni mwanadamu na pia kwamba Yeye ni Mungu. Hili ni jambo la maana sana kufahamu kwa sababu ni mwanadamu kamili na Mungu ambaye anaweza kuwa Mwokozi. Ikiwa Kristo Yesu alikuwa tu

Page 32: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

mwanadamu katika kila jambo kama sisi hata kuanguka katika dhambi, hangeweza kamwe kutuokoa. Lakini kwa sababu Yeye ni Mwana wa Mungu ambaye hana dhambi yeyote na pia kwamba Yeye ni Mungu, Yeye anauwezo wa kutuokoa kabisa kutoka katika dhambi zetu. Kwa njia hiyo, ni jambo la muhimu sana kwamba Kristo alikuwa kama sisi tu ili aweze kutuwakilisha mbele za Mungu. Waebrania 4:15 tunaosma kwamba, @Kwa kuwa hatuna Kuhani Mkuu anaweza kuchukuliana na sisi katika udhaifu wetu, kwani Yeye mwenyewe alijaribiwa kwa kila namna, kama vile sisi tujaribiwavyo, lakini Yeye hakutenda dhambi.@ Yesu Kristo Mfalme Mesiya Bwana Yesu kristo alipokuwa anaanza huduma wake alihubiri kwamba, @Wakati umewadia, Ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuamini Habari Njema@ (Marko 1:15). Mahubiri ya kristo yalienea kote na umati mkubwa ulianza kusanyika kwake ili uweze kusikia habari njema ambazo alikuwa anaeneza. Je, ni kwa nini umati ulikusanyika kwake? Kupitia kwa manabii na makuhani, kwa miaka mingi Mungu alikuwa ameahidi kwamba kuna wakati ambapo atawaokoa watu wake kutoka kwa dhambi zao. Yeye angeanzisha ufalme wake hapa ulimwenguni. Mungu alikuwa ameahidi kwamba angeanzisha ufalme huu kupitia kwa mtu ambaye angetoka katika koo ya Daudi. Katika 2 Samweli 7:1q1, Mungu aliahidi Daudi kwamba mmoja wa watoto wake angetawala milele. Nabii Isaya aliandika kuhusu huyu mtoto wa akisema, @Kwa maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume, nao utawala utakuwa mabegani mwake. Naye ataitwa: Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa Amani. Kuongezeka kwa utawala wake na amani hakutakuwa na mwisho. Atatawala katika kiti cha enzi cha Daudi na juu ya ufalme wake, akiuthibitisha na kuutegemeza kwa haki na kwa adili, tangu wakati huo na hata milele@ (Isaya 9:6-7).

Page 33: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

Kutokna na haya tunaona ni kwa nini umati ulienda kwake. Ni kwa sababu yule mwokozi ambaye alikuwa ametabiriwa alikuwa sasa amefika. Biblia inaonyesha wazi kabisa kwamba yule mfalme ambaye alikuwa ameahidiwa Daudi ni Kristo Yesu. Luka aliandika, @Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yke. Atamiliki nyumba ya Yakobo milele na ufalme Wake hautakuwa na mwisho@ (Luka 1:32-33). Mathayo alianza kuandika kwa kutupatia ukoo wa Yesu kristo kutoka kwa Abrahamu hata kutoka kwa mfalme Daudi. Katika maandishi ya Mathayo ni wazi kwamba mathayo alikuwa anatuonyesha kwamba Yesu Kristo ni Mfalme. Habari njema ambayo haikutarajiwa Agano Jipya linatuoneysha jinsi Mfalme Yesu alivyoanzisha utawala wa Mungu hapa ulimwenguni. Alifanya hiii kwa kuondoa laana ya dhambi. Ufalme huu ulianza hata kama haukuwa kama ule ambao Wayahudi walikusudia. Wao walitarajia ufalme wa duniani ambao ungewasaidia kuondoa utawala wa Warumi katika nchi yao. Lakini wao hawakumtarajia Mesiya ambaye alikuwa Yesu Kristo. Kristo hakuja kuweka utawala wa duniani bali alikuja akihurbiri na kufundisha; alikuja akiwaponya wagonjwa na kusamahe dhambi; alikuja akiwapea uhai ambao walikuwa wamekufa na alimwambia mkku wa Serikali ya Warumi kwamba, @Ufalme Wangu si wa ulimwengu huu@ (Yohana 18:36). Hii haimaanishi kwamba ufalme wa Mungu haupo katika ulimwengu huu. Kabla ya maneno haya Bwana Yesu kristo alikuwa amemwambia kuhani mkuu kwamba, @Mimi ndimi, nanyi mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa Mungu Mwenye Nguvu, akija na mawingu ya mbinguni@ (Marko 14:62) na katika Ufunuo 21 tunasoma kumhusu Kristo akitawala katika

Page 34: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

ulimwengu na nchi mpya ambazo vimebadilishwa na nguvu zake na kuondolewa katika utawala wa dhambi. Hizi zote ni habari njema. Lakini ukweli ni kwamba bado tuko katika dhambi zetu. Tunahitaji kuondolewa hatia ya dhambi zetu na kupatanishwa na Mungu ikiwa kweli tutaingia mbinguni tutaishi katika mbingu na nchi mpya. Ikiwa dhambi zetu zitabaki juu yetu, basi ni wazi kwamba tutaingia jahanum. Huu ndiyo ukweli wa hali yetu ya sasa. Ni kwa sababu ya ukweli, basi habari njema ni habari mzuri sana kwetu. Bwana Yesu Kristo hakuja tu kuanzisha ufalme wa Mungu hapa ulimwenguni bali pia alikuja kuwaingiza humo wenye dhambi ambao wanatubu dhambi zao na kumwamini Yeye pekee. Alifanya hakikisha hili kwa kufa msalabani kwa nia yetu na kwa ajili ya dhambi zetu. Yeye aliadhibiwa kwa ajili ya dhambi zetu na kwa kufanya haya, Yeye alituhakikishia msamaha wa dhambi. Kwa wale wote ambao wamemwamini Kristo, wao wemefanywa wenye haki mbele za Mungu na sasa wao wataurithi ufalme wa Mungu (Wakolosai 1:12). Mfalme Yesu ambaye aliteseka sana. Wakati Yohana Mbatizaji alimwona Kristo Yesus alisema, @Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu@ (Yohana 1:29). Je, kwa kusema haya Yohana alimaanisha nini? Kwa wayahudi, hili lilikuwa jambo ambalo lilieleweka vyema kabisa kwa sababu liliwakumbusha kuhusu ukombozi wa Mungu kutoka katika nchi ya Misri. Mungu aliwahukumu watu wa Misri kwa kuwatumia mapigo kumi. Lakini hata wakati Mungu alituma mapigo haya, Farao aliendelea kuufanya moyo wake kuwa mugumu zaid na zaidi. Pigo la mwisho ndilo lilikuwa baya zaidi. Mungu aliwaambia watu wa Ijsraeli kwamba malaika angepita katika nchi ya Misri yote na kuwaangamiza wazao wa kwamba wa wanadamu na wanyama. Hukumu hii pia ingejumlisha hata Waisraeli kama hawangefuata maagizo ya Mungu kwao. Kila jamii Mungu alikuwa ameiamuru kwamba imchukue mwana-kondoo ambaye hakuwa na doa lolote na

Page 35: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

wamchinje. Kwa kutumia hisopo walikuwa wapaka milango ya nyumba zao. Mungu aliwaambia kwamba kila wakati ambapo malaika anaona damu hiyo, yeye hangemwua mzaliwa wa kwanza wa nyumba zao. Siku ya Pasaka na mwana-kondoo wa Pasaka ilikuwa ishara kubwa sana kwa sababu wao walijua kwamba deni la dhambi la mtu linaweza kulipwa kwa kifo cha mwingine ambaye hapa alikuwa mwana-kondoo ambaye baadaye katika Agano Jipya ni Kristo Yesu. Jambo hili la mwingine kufa kwa niaba ya wengi ndilo lilikuwa msingi wa dhabihu za Agano la Kale. Siku ya Upatanisho Kuhani mkuu aliiingia katika hekalu mahali ambapo paliitwa Patakatifu pa Patakatifu na damu ya mnyama ambaye alikuwa amechinjwa kama dhabihu ya dhambi za watu wa Israeli. Mwaka baada ya mwaka jambo hili lilifanyika. Wafuasi wa kristo Yesu baada ya muda walifahamu kwamba kazi ya Kristo haikuwa tu kuanzisha ufalme hapa ulimwengu lakini pia ilijumlisha kufa kwa niaba ya watu wake. Walifahamu kwamba Bwana Yesu kristo hakuwa tu Mfalme, bali alikuwa Mfalme ambaye alikumbana na mateso mengi sana. Bwana Yesu kristo mwenyewe alijua kwamba alikuja hapa ulimwenguni kufa kwa ajili ya dhambi za watu wake. Wakati Yesu Kristo alizaliwa, maliaka alisema, @nawe utamwita jina lake Yesu, kwa maana Yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka katika dhambi zao@ (Mathayo 1:21). Luka naye aliandika kwamba, @Wakati ulipokaribia wa Yeye kuchukuliwa mbinguni, alikaza uso wake kwenda Yerusalemu@ (Luka 9:51). Mara kwa mara Yesu kristo mwenyewe alizungumza kuhusu kifo chake. Hata kuna wakati ambapo Petro alijaribu kumkataza na Yesu alimkemea kwa kusema, @Rudi nyuma yangu, Shetani Wewe ni kikwazo kwangu@ (Mathayo 16:23). Bwana Yesu Kristo alijua kwamba Yeye alikuja hapa ulimwenguni kufa kwa ajili ya dhambi za watu wake. Bwana Yseu kristo pia alifahamu umuhimu wa kifo chake. Yeye alisema, @Kwa kuwa hata Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa,

Page 36: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

bali kiutumika na kuutoa uhai Wake kuwa ukombozi kwa ajili ya wengi@ (Marko 10:45). Katika Mathayo 26:27-28, alikula chakula na wanafunzi wake na alichukua kikombe cha divai na kusema, @Kunyweni nyote katika kikombe hiki. Hii ndiyo damu yangu ya agano, ile imwagikayo kwa ajiloi ya wengi kwa ondoleo la dhambi.@ Pia katika Yohana 10:15,18 alisema, @Nami nautoa uhai Wangu kwa ajili ya kondoo...Hakuna mtu aniondoleaye uhai wangu, bali ninautoa kwa hiari yangu mwenyewe.@ Bwana Yesu Kristo alijua kwamba alikuwa anaenda kufa. Kwa sababu ya upendo juu ya watu wake, aliutoa uhai wake. Yeye ndiye Mwana-Kondoo wa Mungu ambaye alichinjwa ili watu wake wapate kusamehewa dhambi zao. Kupitia kwa kufundishwa na Roho Mtakatifu, kanisa la kwanza lilifahamu kile ambacho Kristo Yesu alitekeleza msalabani kalivari. Paulo anaeleza kazi ya Kristo msalabani kwa njia hii, @Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa kufanyika laana kwa ajili yetu, kwa maana aimeandikwa, Amelaaniwa yeye aangikwaye juu ya mti. Alitukomboa ili kwamba baraka aliyopewa Abrahamu ipate kuwafikia watu Mataifa kwa njia ya Kristo Yesu, ili kwa imani tupate kupokea ile ahadi ya Roho.@ Pia Paulo aifafanua kwamba, @Kwa maana Mungu alimfanya Yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu katika Yeye@ (2 Wakorintho 5:21). Petro naye aliandika, @Yeye mwenyewe alichukua dhambi zetu katika mwili wake, juu ya mti, ili kwamba, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tupate kuishi katika haki. Kwa kupigwa kwakr, ninyi mmeponywa@ (1 Petro 2:24). Je, unaona jinsi watumishi hawa wa Mungu walivyofahamu kazi ya Kristo Yesu mslabani kalivari? Wao walijua kwamba wakati Kristo Yesu alikufa msalabani hakufa kwa ajili ya dhambi zake bali kwa ajili ya dhambi zetu. Yeye hakuwa na dhambi yeyote na hakuwahi tenda dhambi. Adhabu ambayo alipata ilikuwa kwa ajili ya watu wake. Wakati alipokuwa mslabani Kalivari, Kristo alizibebe dhambi zote za watu wake.

Page 37: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

Hii ndiyo sababu Bwana Yesu Kristo alilia, @Eloi, Eloi lama sabakthani? Maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mona umeniacha@ (Mathayo 27:46). Mungu Baba ambaye ni Mtakatifu na macho yake hayatazami dhambi hata kidogo, alimwacha Mwanawe kwa sababu dhambi za watu wake zilikuwa zimewekwa juu yake. Yeye alimwaga hasira yake yote jjuu ya Kristo Yesu. Mathay anaandika kwamba kulikuwa na giza katika nchi yote kwa masaa matatu wakati Yesu Kristo alipokuwa juu ya msalaba. Hilo lilikuwa giza la hukumu kwa sababu ya hasira ya Mungu ambayo ilimwaga juu ya Kristo kwa sababu ya dhambi za watu wake ambazo zilikuwa zimewekwa juu yake. Isaya alitabiri juu ya jambo akisema, @Hakika alichukua udhaifu wetu na akajitwika huzuni zetu, hata hivyo tulifikiri amepigwa na Mungu, amepigwa sana naye na kuteswa. Lakini alitobolewa kwa ajili ya makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu, adhabu iliyotuletea sisi amani ilikuwa juu yake, na kwa majeraha yake sisi tumepona@ (Isaya 53:4-5). Kile tunasoma hapa ni kwamba ni sisi ambao tulistahili kufa na wala si Kristo Yesu. Ni sisi ambao tulifaa kuadhibiwa wala si Kristo. Lakini hata hivyo, Yeye alichukua nafasi yetu na akafa kwa ajili yangu. Kwa sababu ya dhambi zangu, Yeye aliumizwa; kwa sababu ya dhambi zangu, Yeye alidhibiwa; kwa sababu ya dhambi zangu, Yeye alihuzunika na ni adhabu hii ambayo imeniletea amani. Kwa kupigwa Kwake mimi nimeponywa na kwa huzuni wake, mimi nimepata furaha. Alikufa ili niishi. Msingi wa Ujumbe wa Injili Ujumbe huu kwamba Kristo Yesu alikufa kwa ajili yetu, ni ujumbe ambao wengi katika ulimwengu huu wanauchukia sana. Watu hawapendi kusikia kwamba kweli Kristo Yesu adhibiwa kwa ajili ya dhambi zao. Ukweli ni kwamba kuondoa ujumbe huu, ni kuondoa msingi mkuu wa ujumbe wa injili. Tunaposoma Biblia, tunaona kwamba kwa kifo chake, Kristo Yesu alitupatanisha na Mungu na pia alishinda shetani na dhambi miongoni mwa mambo mengine. Lakini

Page 38: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

ukweli ni kwamba kifo hiki kilikuwa kwa niaba yetu. Hili ni jambo kuu na hatufai kulipuuza kabisa. Ikiwa tutapuuza jambo hili, basi tutaacha maswali fulani yakiwa hayajibiwa. Kwa mfano, Kwa nini watu walikuwa watoa dhabihu?, Je, umwagaji wa damu ulitimiza nini?, Je, Mungu atawezaje kuwahurumia wenye dhambi, wakati huoo akiendelea kuwa wenye haki?, Je, itamaanisha nini kwamba Mungu anasamehe dhambi na makosa na kuwaondolea hatia watu (Kutoka 34:7). Je, inawekanaje kwamba Mungu mwenye haki na Mtakatifu anawahesabia haki wenye dhambi (Warumi 4:5)? Majibu ya maswali haya yote yanajibu kutokana na kazi ya Yesu Kristo msalabani Kalivari wakati alipokufa kwa ajili ya watu wake. Mungu mwenye haki na Mtakatifu anaweza kuwahesabia haki wenye dhambi kupitia kwa Kristo Yesus. Kupitia kwa kifo cha Bwana Yesu Kristo, hurma na haki viliptanishwa. Laana ya Mungu iliondolewa na kwa huruma tuliokolewa. Kufufuka kwa Bwana Yesu Kristo. Ni habari njema kwamba Mfalme Yesu kristo ambaye alikufa, alifufuka kutoka kwa wafu. Shaka za wanafunzi wa Kristo Yesu baada ya kusulibiwa kwa Yesu ziliondolewa wakati Malaika alipomwambia Maria kwamba, @Kwa nini mnamtafuta aliye hai miongoni mwa wafu? Hayuko hapa, amefufuka!@ (Luka 24:5-6). Ikiwa Kristo hangefufuka, kifo chake hakingekuwa na maana yeyote kwetu. Mambo yote ambayo alikuwa amesaema yangekuwa si ya kweli na sisi wanadamu hatungekuwa na tumaini lolote la kuokolewa kutoka katika dhambi zetu. Lakini Kristo Yesu alipofufuka kutoka kwa wafu, kila jambo ambalo alikuwa amesema lilidhihirika kuwa la hakika na la kweli na hatufai kuwa shaka yoyote juu yake katika jambo lolote. Yesu Kristo alidhihirika kwa mwokozi wa kweli. Katika Warumi 8, tunaelezwa kuhusu kufufuka kwa Kristo Yesu na maana ya kufufuka kwake kwetu wakristo: @Ni nani atakayewashitaki wale ambao Mungu amewachagua? Ni Mungu mwenyewe ndiye mwenye kuwahesabia haki. Ni nani basi

Page 39: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa, naam, zaidi ya hayo, ndiye aliyefufuka kutoka kwa wafu, yuko mkono wa kuume wa Mungu, naye ndiye anayetuombea@ (Warumi 8:33-34). Sasa Bwana Yesu kristo ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba akiwa Mfalme wa ulimwengu wote. Pia ameketi akiwaombea watu wake tunapokuwa katika hali ya kungoja kutudi kwake. Hadi hapa, swali ni hili, je, watu wake ni kina nani? Jinsi mwanadamu anafaa kufanya wakati amesikia ujumbe huu. Mwanadamu anafaa kuamini na kutubu. Tunaposma kitabu cha Marko, Marko anatueleza kwamba huduma wa Kristo ulianza akihubiri, @Wakati umewadia, Ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Habari Njema@ (Marko 1:15). Mungu anatarajia tuamini na tutubu wakati tumesikia habari njema. Katika Agano Jipya lote, tunasoma kuhusu mitume wakiwasihi watu kwamba waamini na kutubu dhambi zao. Bwana Yesu Kristo aliwahimiza wasikilizaji wake kwamba walifaa kuamini na kutubu. Baada ya kuhubir siku ya Pentekote, Petro aliwasihi wasikilizaji kwamba, @Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Yesu Kristo@ (Matendo ya Mitume 2:38). Katika Matendo ya Mitume 20:21, Paulo alisema, @Kama nilivyowashudia Wayahudi na Wayunani kwamba inawapasa kumgeukia Mungu kwa kutubu dhambi na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo.@ Katika Matendo ya Mitume 26:18, anakumbuka jinsi Kristo Yesu mwenyewe alivyomtuma: @Uyafungue macho yao ili wageuke kutoka gizani waingie nuruni na kutoka kwenye nguvu za shetani, wamgeukie Mungu ili wapate msamaha wa dhambi na sehemu miongoni mwa wale waliotakaswakwa kuniamini Mimi.@ Wale ambao ni wa Kristo ishara yao ni kwamba manaishi maisha ya imani na toba. Mkristo ni mtu ambaye anageuka kutoka kwa dhambi zake na kumwamini Bwana Yesu Kristo ili aweze kuokolewa kutoka kwa dhambi zake na ghadhabu ya Mungu. Imani ambayo ni ya kutegemea

Page 40: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

Neno imani limetumika vibaya sana kwa siku nyingi kwa sababu wengi hajui neno hili linamaanishi nini. Ukiwauliza wengi wakueleza neno hili linamaanisha nini, watakueleza mambo mengi ambayo yanaonekana kuwa imani lakini si imani. Wao katika mazungumzo nao utaona kwamba imani yao haiambatani na ukweli wa jinsi mambo yalivyo. Wengi huwaza kwamba imani haina uhusiano wowote na ukweli wa mambo katika ulimwengu huu. Wao huwaza kwamba wanaweza kufanya lolote wanalotaka bila kuzingatia hali ilivyo ulimwenguni. Kwa njia hii wao huwaza kwamba wako na imani. Unaposoma Biblia utapata kwamba imani ni kinyume na mawazo ya watu wengi ambao wanadai kwamba kwamba wao wako na imani na ukweli. Imani si kuamini katika mambo au jambo ambalo huwezi kuhakikisha. Imani ya kweli ni ile ambayo ni ya kutegemea, yaani inahusu mambo ambayo unayafahamu na ni ya hakika. Imani kama hii ni ile ambayo inaamini kwamba Bwana Yesu Kristo alikufa na alifufuka kwa sababu huu ni ukweli ambao tumehakikshiwa kutoka katika Biblia. Hata kama hatujaona na macho yetu, huu ni ukweli ambao Biblia inauhakikisha na tunauamini. Biblia inatufaundisha kuhusu imani hii katika Warumi 4. Hivi ndivyo Biblia inavyomfafanua Abrahamu: “Akitarajia yasiyoweza kutarajiwa, Abrahamu akaamini atakuwa, 'Baba wa mataifa mengi,' kama alivyoahidiwa kwamba, 'Uzao wako utakuwa mwingi mno.' Abrahamu hakuwa dhaifu katika imani hata alipofikiri juu ya mwili wake, ambao ulikuwa kama uliyokufa, kwani umri wake ulikuwa unakaribia miaka mia moja, au alipofikiri juu ya ufu wa tumbo la Sara. Lakini Abrahamu hakusitasita kwa kutokuamini ahadi ya Mungu, bali alitiwa nguvu katika imani yake na kumpa Mungu utukufu, akiwa na hakika kabisa kwamba Mungu alikuwa na uwezo wa kutimiza lile aliloahidi” (Warumi 4:18-21). Hata kama Abrahamu alikuwa anazeeka na mke wake Sara alikuwa pia anaezeeka na pia alikuwa hana uwezo wa kupata mtoto,

Page 41: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

Abrahamu aliendelea kumwamini Mungu. Abrahamu alimwamini Mungu na ahadi zake bila kuumba-umba. Tunaposoma Biblia tunaona kwamba Abrahamu hakuwa mtu ambaye alikuwa amekamilika kwa sababu kuna wakati ambapo alijaribu kujitegemea kwa kumchukua Hagai ambaye alikuwa mfanyi-kazo wake na kulala naye ili apate kuwa na mtoto. Yeye alifanya hivi kwa sababu aliwaza kwamba anamsaidia Mungu kukamilisha ahadi zake. Lakini baadaye Abrahamu alitubu dhambi hii na alimtegemea Mungu tu hadi mwisho. Yeye alimtegemea Mungu pekee na kwa sababu hii Biblia inasema kwamba, “akiwa na hakika kanisa kwamba Mungu alikuwa na uwezo wa kutimiza lile aliloahidi” (Warumi 4:21). Habari njema ya Kristo Yesu inatuamuru tuwe watu kama Abrahamu. Tuwe na imani ndani ya Kristo Yesu, tumtegemee na kumwamini Yeye pekee katika kila jambo ambalo ameahidi kufanya. Imani ambayo inakubali haki Je, inamaanisha nini kumwamini kabisa Kristo Yesu? Hii inamaanisha kwamba tunamwamini kabisa kwa ajili ya kutuokoa kutokana na hukumu ya haki ya Mungu badala ya kuhukumiwa kwa sababu ya hatia yetu. Biblia inafundisha kwamba hitaji kuu la kila mwanadamu ni kuokolewa kutoka kwa hukumu ya Mungu. Wakati Mungu anatangaza hukumu yake, tunahitaji kupatikana kwamba hatia yetu imeondolewa na wala si kuhukumiwa. Huku ndiko kuhesabiwa haki, yaani Mungu anatutangaza kwamba sisi ni wenye haki mbele zake na wala si wenye hatia. Je, tunahesabiwa aje haki? Biblia inafundisha kwamba haki hatuipati kwa kufanya mambo mazuri au kuishi maisha mazuri. Ikiwa kweli Mungu atatuhesabia haki, lazima afanye jambo hili kwa sababu ya mtu mwingine na si kwa sababu yetu. Ni lazima Atafanya jambo hili kwa sababu ya mtu mwingine ambaye atachukua nafasi. Hapa ndipo imani ndani ya Yesu Kristo inapatikana. Wakati tunamwamini Kristo Yesu, huwa tunamtegema Yeye pekee kusimama mbele ya Mungu

Page 42: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

kwa niaba yetu. Yeye anaweza kufanya hivi kwa sababu aliishi maisha matakatifu kabisa na pia alilipa dhambi zetu kwa kifo chake msalabani kalivari. Kwa ufupi ni kwamba tunaamini kwamba Mungu ataondoa hati ya dhambi zetu na kutupatia hati ya Kristo Yesu na atatutangaza kwamba sisi ni wenye haki (Warumi 3:22). Wakati tunamwamini Kristo Yesu kwa ajili ya wokovu wetu, huwa tunaunganishwa naye na wakati huo kunakuwa na kubadilishana. Dhambi zetu zote, uasi wetu wote na uovu wetu uliwekwa juu ya Kristo Yesu na alikufa kwa sababu ya haya (1 Petro 3:18). Wakati huo huo tunapewa utakatifu wa Kristo na kuhesabiwa wenye haki. Wakati huu, Mungu anapotutazama, huwa haoni dhambi zetu bali huwa anaona tu haki ya Kristo juu yetu. Hii ndiyo maana Biblia katika Warumi 4 inasema, “Kwa mtu ambaye hafanyi kazi na anamtumaini Mungu, Yeye ambaye huwahesabia waovu haki, imani yake inahesabiwa kuwa haki..... .Wamebarikiwa wale ambao uovu wao umesamehewa na ambao dhambi zao zimefuatwa” (Warumi 4:5,7). Kile Biblia inatufundisha hapa ni kwamba Mungu anawahesabia haki wenye dhambi (mstari wa 5). Mungu huwa hatuhesabii haki kwa sababu sisi ni wenye haki kwa sababu hakuna hata mmoja ambaye angeweza kuhesabiwa haki. Mungu anawahesabia haki wenye dhambi kwa sababu ya imani. Wakati tunahesabiwa haki na Mungu huwa tunapewa haki ya Kristo. Mungu anaokoa wenye dhambi kwa neema si kwa sababu tumefanya lolote zuri bali kwa sababu ya maisha na kazi ya Kristo Yesu msalabani kwa ajili yetu. Nabii Zekaria alizungumzia jambo hili wakati alizungumzia kuhusu Kuhani Yoshua alipokuwa anapewa mavazi mapya: “Kisha akanionyesha Yoshua kuhani mkuu akiwa amesimama mbele ya malaika wa Bwana, naye shetani amesimama upande wale wa kuume ili amshitaki. Bwana akwambia Shetani, 'Bwana, ambaye ameichagua Yerusalemu, akulemee! Je, mtu huyu siyo kijinga kinachowaka kilichonyakuliwa kwenye moto?' Wakati huu, Yoshua

Page 43: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

alikuwa amevaa nguo chafu alipokuwa amesimama mbele ya malaika. Malika akawaambia wale waliokuwa wamesimama mbele yake, 'Mvueni nguo zake chafu.' Kisha akawaambai Yoshua, 'Tazama, nimeiondoa dhambi yako, nami nitakuvika mavazi ya kitajiro.' Kisha nikisema, 'Mvike kilembe kilicho safi kichwani mwake.' Kwa hiyo wakamvika kilembe safi kichwani na kumvika yale mavazi mengine, wakati malaika wa Bwana akiwa amesimama karibu” (Zekaria 3:1-5). Mavazi hayo mapya hayakuwa na Zekaria. Yale ambayo yalikuwa ya Zekaria ni yale ambayo machafu ndiyo yalikuwa yake. Hayo ndiyo mavazi ambayo shetani aliona na akataka kuleta shutuma juu ya Zekaria. Haki ambayo Yoshua alikuwa nayo haikuwa yake bali alikuwa amepewa na Mungu mwenyewe. Hili ni jambo la kweli kwetu sisi wakristo. Haki ambayo tuko nayo mbele za Mungu sio yetu, tumepewa na Kristo Yesu. Mungu alituona tukiwa katika dhambi na akamtuma Mwana wake Yesu Kristo ili aje na atuokoe kutoka katika dhambi. Sasa kwa sababu Kristo Yesu amekufa, kwa wale ambao tumemwamini, Mungu anapotuona, anaona haki ya Kristo juu yetu. Haoni tena dhambi zetu. Mungu mwenye haki ametoshelezwa na kifo cha Kristo Yesu na kwa sababu ya Kristo ametusamehe sisi. Imani pekee Ikiwa tutaelewa kwamba bila Kristo Yesu, haki Yake na kifo Chake hatuwezi kamwe kuwa wenye haki, basi tutafahamu vyema kwa nini Biblia inasisitiza kwamba wokovu huja kwa imani pekee. Hakuna mtu mwingine au njia nyingine ya kupata wokovu isipokuwa tu kwa imani katika Kristo Yesu. Madini mengine katika ulimwenguni yanakataa kwamba wokovu tunahesabiwa wenye haki kwa imani tu. Madini haya yanafundisha kwamba wokovu huja kwa kuishi maisha mazuri, kwa kutenda mambo mazuri na kwa kujitahidi kwa nguvu zako kumfurahisha Mungu. Hii ni kawaida ya mwanadamu ambaye amekufa katika dhambi. Yeye huwaza kwamba anaweza kujiletea wokovu.

Page 44: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

Mwanadamu huwa anajiwazia kwamba kila kitu kinafanyika kwa nguvu na uwezo wake. Huwa hatutaki kusikia kwamba wokovu wetu unapatikana kwa sababu ya Kristo Yesu. Kila wakati tunataka tujulikane kwamba ni kwa nguvu zetu tumepata jambo fulani. Ukweli ni kwamba wokovu ni kazi ya Mungu kupitia kwa Kristo Yesu. Kwa hivyo yeyote ambaye anataka kuokoka, lazima amwamini Kristo pekee. Wokovu ni zawadi ya neema kutoka kwa Mungu na hatuleti lolote kwa wokovu huu (Wagalatia 2:16). Kumwamini Kristo inamaanisha kabisa kuacha kuamini mambo mengine na kujiamini kwa ajili ya kuhesabiwa haki na Mungu. Je, wewe ni mtu ambaye anajiamini na kuamini katika matendo yako mazuri? Kumbuka kwamba imani inamaanisha kumwamini Kristo pekee katika kila jambo. Je, wewe ni yule ambaye anaamini kwamba moyo wako ni mzuri? Imani inamaanisha kukubali kwamba moyo wako ni mwovu na kumwamini Kristo pekee. Kwa ufupi ni kusema kwamba bila Kristo mimi siko na siwezi kamwe. Ni kusema Bwana Yesu niokoe au nitakufa. Hii ndiyo imani. Toba Ujumbe wa Kristo kwa wasikilizaji wake ulikuwa, “Tubuni na kuiamini Habari Njema” (Marko 1:15). Imani ni kumwamini Kristo na kumtegemea Yeye pekee kwa wokovu. Kutubu ni kugeuka kutoka katika dhambi, kuchukui dhambi na kuamua kwa nguvu za Mungu kuacha dhambi na kumgeukia Mungu kwa imani. Petro aliwahimiza wasikilizaji wake kwamba, “Tubuni basi mkamgeukie Mungu, ili dhambi zenu zifutwe, ili zipate kuja nyakati za kuburudisha kwa kuwepo kwake Bwana” (Matendo ya mitume 3:19). Paulo naye aliwahimiza wasikilizaji, “inawapasa kutubu na kumgeukia Mungu na kuthibitisha toba yao kwa matendo yao” (Matendo ya mitume 26:20). Toba ni ishara ya wale wote ambao wameokolewa na Mungu. Kuna watu ambao wanasema kwamba wamemkubali Kristo Yesu kuwa mwokozi wao na kwa hivyo mimi ni mkristo. Lakini hata hivyo mimi

Page 45: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

siko tayari kumkubali Kristo kama Bwana. Kwa ufupi wao wanadai kwamba kuwa na imani katika Kristo Yesu lakini hawajatubu dhambi. Ikiwa tutafahamu vyema jambo la toba, basi tutaona kwamba huwezi kumkubali kwamba Kristo Yesu halafu amkatae kuwa Yeye ni Bwana. Kukataa kwamba Kristo si Bwana ni kukataa mafundisho ya Biblia kuhusu kutubu: “Nanyi msipotubu, mtaangamia vivyo hivyo” (Luka 13:3). Wakati mitume walisikia habari ya Petro kuhusu kuokoka ka Kornelio, “walimwadhimisha Mungu wakisema, 'Basi, Mungu amewapa hata watu Mataifa toba iletayo uzima wa milele” (Matendo ya Mitume 11:18). Paulo anazungumza kuhusu “toba iletayo wokovu” (2 Wakorintho 7:10). Kumwamini Kristo ni kuamimi katika maneno yake. Ni kuamini kwamba Yeye ndiye Mfalme ambaye alisulibiwa na akafufuka. Ni kuamini kwamba Yeye ameshinda kifo na dhambi na ana nguvu za kuokoa. Je, mtu anawezaje, kuamini haya na kuyategemea na wakati huo huo asema kwamba hakubali kwamba Kristo ni Bwana au Mfalme juu ya maisha yake? Kumwamini Kristo ni kuamini kwamba Yeye ni Mfalme ambaye alishinda dhambi. Kama hatukubali hili, basi ni wazi kwamba mtu hana imani ya kweli. Bwana Yesu Kristo alisema, “Hakuna mtu awezaye kuwatumikia mabwana wawili, kwa kuwa ama atachukia huyu na kumpenda yule mwingine” (Mathayo 6:24). Kumwamini Kristo Yesu ni kumtegemea Yeye pekee. Kutubu si kuwa mkamilifu. Ukweli ni kwamba wakristo si watu ambao wamekamilika. Ninamaanisha kwamba wao ni watu ambao bado wako na dhambi mioyoni mwao. Kutubu dhambi haimaanishi kwamba sasa mtu hatendi dhambi yoyote katika maisha yake yote. Wakristo ni watu ambao bado wako na dhambi mioyoni mwao hata baada ya wao kupewa maisha mapya na Mungu. Wakristo wote tutaendelea kupigana na dhambi hadi wakati tutakufa (Wagalatia 5:17; 1 Yohana

Page 46: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

2:1). Lakini hata kama kutubu hakumaanishi kwamba mtu anakuwa mkamilifu kabisa kutoka kwa dhambi, ukweli ni kwamba mtu ambaye ametubu haishi maisha ya dhambi au haendelei na tabia ya dhambi. Hii ninamaanisha kwamba yeye haifurahi dhambi kama alivyokuwa akiifurahia wakati alikuwa hajatubu dhambi zake. Mtu ambaye ametubu dhambi, huwa anapigana na dhambi hiyo na kuipinga kwa nguvu za Mungu maishani mwake mwote. Ninajua kwamba wakristo wengi huwa hawaelewi jambo hili la kwa sababu wao wanawaza kwamba ikiwa wanatubu dhambi zao, hii inamaanisha kwamba dhambi itaondoka kabisa katika maisha yao na wao watabaki wakiwa ni watu ambao wamekamilika kabisa. Pia wao huwaza kwamba hawatahi kujaribiwa kamwe na mtu yeyote. Wakati wao wanaona kwamba kweli mambo hayafanyiki jinsi wanavyowaza, wao hushushwa moyo sana na wanaanza kujiuliza kama kweli wao wameokoka. Ni ukweli kwamba wakati Mungu atatuzaa mara ya pili, Yeye hutupatia nguvu za kupigana na kushinda dhambi (1 Wakorintho 10:13). Tutaendelea kupigana na dhambi hadi wakati tutakufa lakini jambo la muhimu kuelewa ni kwamba toba la kweli hali ya moyo ya mtu kuhusu dhambi. Hii ni jinsi mtu anavyoitazama dhambi na kuishughulikia katika maisha yake yote. Kutubu si kubadilisha tabia hapa na pale. Swali ambalo kila mmoja wetu anafaa kujiuliza ni, je, tunachukia dhambi na kupigana nayo au tunaipenda na kuitetea. Mabadiliko ya kweli ni yale ambayo yanaonyesha tunda la toba Wakati mtu anatubu na kumwamini Kristo Yesu, Biblia inafundisha kwamba mtu huyu huwa anapewa maisha mapya ya kiroho. Biblia inasema kuhusu mtu kwamba, “Kwa habari zenu, mlikuwa wafu katika makosa na dhambi zenu.....lakini Mungu, kwa upendo Wake mwingi kwetu sisi, ambaye ni mwingi wa rehema, hata tulipokuwa wafu kwa ajili ya makosa yetu, alitufanya tuwe hai pamoja na Kristo Yesu, yaani mmeokolewa kwa neema” (Waefeso 2:1,4-5). Wakati jambo hili lifanyika, maisha hubadilika. Kubadilika huku si kwa hapo

Page 47: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

na hapo wala si kwa haraka wala si kwa papo hapo. Lakini ukweli ni kwamba maisha hubadilika na tunaanza kuzaa matunda ya wokovu wetu. Biblia inafundisha kwamba wakristo wanafaa kujulikana kuwa watu wa upendo, huruma na wakarimu kama Bwana Yesu Kristo. Mkristo anafaa kuwa watu ambao wanathibitisha “toba yao kwa matendo yao” (Matendo ya Mitume 26:20). Mtu unajulikana kwa matunda yake. Yesu alisema, “Kila mtu hujulikana kwa matunda yake. Kwa maana watu hawachumi tini kwenye miiba wala zabibu kwenye michongoma” (Luka 6:44). Wakati watu wanapewa maisha mapya ya kiroho, wanaanza kufanya mambo ambayo Kristo alifanya. Wanaanza kuishi kama Kristo alivyoishi na kuzaa matunda mema ya wokovu. Kile hatufai kuwaza ni kwamba matunda ya wokovu ndiyo yanafanya tuokoke. Ni jambo la hatari sana kuwaza kwamba kwa sababu kuna ishara fulani za mtu ambaye ameokoka katika maisha yako, basi tunawaza kwamba wokovu wetu umekuja kwa sababu ya ishara hizo na si kwa sababu ya Kristo Yesu. Sisi sote tujichunge kutokana na majaribu haya. Kumbuka kila wakati kwamba matunda ya wokovu ambayo yanaonekana katika maisha yako ni matokeo ya kazi ya Mungu kwako kupitia kwa Kristo Yesu. Kutegemea matendo yako mazuri kwa ajili ya wokovu wako ni kuondoa Kristo katika maisha yako na kuanza kujitegemea mwenyewe. Kufa hivi ni kukataa wokovu. Je, utafanya nini wakati utasimama mbele za Mungu? Wakati utasimama mbele ya Mungu siku ya hukumu, je utamwambi nini ili akuingize katika ufalme Wake? Je, utamwambia kuhusu matendo yako mazuri? Ukweli ni kwamba hata yale ambayo unayaona kwamba ni matendo mazuri, hayawezi kukuingiza humo. Wale ambao wameokoka, wao watakapoulizwa maswali haya, watajibu kwa uople kwamba walimwamini Kristo Yesu pekee kwa ajili ya wokovu wao. Hivi ndivyo watasema: “Mungu usitazame lolote ndani mwangu bali Kristo Yesu pekee. Nihesabie haki si kwa sababu

Page 48: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

ya lolote nimefanya bali kwa sababu kazi ya Kristo Yesu. Yeye aliishi maisha ambayo ningeishi; alikufa kifo ambacho nilistahili kufa; nimeacha kujiamini na kuamini mambo mengine yote na kumwamini Yeye pekee. Mungu nihurumia na unihesabie haki kwa sababu ya Yeye.” Ufalme Kuwa mkristo kunagharimu sana lakini pia kuna zawadi kuu sana (Luka 14:28). Miongoni mwa yale ambayo tunapata wakati tunaokoka ni, msamaha wa dhambi, tunafanywa kuwa wana wa Mungu, tunakuwa na uhusiano na Bwana Yesu Kristo, tunapewa Roho Mtakatifu, tunapewa huru kutoka kwa nguv za dhambi, tunakuwa na ushirika na watu wa Mungu, miili yetu itafufuliwa katika utukufu, tunakuwa mmoja wa ufalme wa Mungu, tutaishi katika nchi na mbingu mpya na tutaishi katika uwepo wa Mungu. Hizi zote ni baraka ambazo Mungu ametubariki nazo wakati tunaokoka. Hii ndiyo sababu Paulo katika maandiko yake alinukku Isaya akisema, @Lakini ni kama ilivyoandikwa, Lile jambo ambalo jicho halijapata kuona, sikio halijapata kuiskia wala halikuingia moyoni lile Mungu alilowaandalia wale wampendao@ (1 Wakorintho 2:9). Maisha ya ukristo haihusu tu kuahakikisha kwamba unaepuka ghadhabu ya Mungu. Bali yanahusu kuwa katika uhusiano na ushirika mwema na Mungu na kutazamia kuishi naye milele katika furaha kamili. Ukristo unahusu kupata kile ambacho hatutawahi kupoteza na kuwa raia wa Ufalme wa milele. Wakati mtu anamwamini Kristo Yesu, maisha yake yote huwa yanabadilika milele. Ninajua kwamba jambo hili halifanyika kwa haraka kwa nje. Biblia inafundisha kwamba wakati huu Mungu huwa ametukomboa kutoka katika ufalme wa giza na kutuingiza katika Ufalme wa Mwana Wake mpendwa (Wakolosai 1:13). Je, Ufalme wa Mungu nini?

Page 49: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

Katika mafundisha ya Agano Jipya, Ufalme wa Mungu ni moja wapo ya mambo ambayo yamezingatiwa sana. Bwana Yesu kristo mwenyewe alifundisha sana kuhusu Ufalme huu. Alisema, @Tununi kwa kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia.@ Paulo naye alikamilisha huduma wake huko Efeso @Akihubiri Ufalme wa Mungu na kufundisha mambo yale yaliyomhusu Bwana Yesu Kristo, kwa ujasiri wote na bila kizuizi chochote@ (matendo ya Mitume 28:31). Mwandishi wa Waebrania aliwahimiza wasikilizaji wake kwa kuwaambia kwamba wale ambao wamemwamini Kristo wamepokea ufalme ule ambao hauwezi kutetemeshwa (Waebrania 12:28). Petro naye aliwahimiza wasikilizaji wake kwamba, @Kwa njia hii, mtajaliwa kwa ukarimu mwingi kuingia katika Ufalme wa milele wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo@ (2 Petro 1:11). Katika kitabu cha Ufuno tunasoma, @Kisha nikasikia sauti kuu mbinguni ikisema, 'Sasa Wokovu na uweza na Ufalme wa Mungu wetu umekuja na mamlaka ya Kristo Wake. Kwa huwa ametupwa chini mstaki wa ndugu zetu, anayewashitaki mbele za Mungu usiku nja mchana@ (Ufunuo 12:10). Je, Ufalme huu ni gani? Je, Ufalme huu ni kanisa? Je, Ufalme huu uko wapi? Je, ni nani ambaye ako katika Ufalme huu? Je, Ufalme huu kila mtu ako ndani mwake? Mungu anatawala juu ya mpnago wake wa wokovu Kwanza ni kwamba Ufalme wa Mungu ni utawala wa Mungu juu ya watu wake wote. Ufalme wa Mungu ni utawala wa Mungu, nguvu za Mungu na mamlaka ya Mungu (Zaburi 145:11,13). Biblia pia inafundisha kwamba Ufalme wa Mungu ni utawala wa Mungu juu ya mpango wake wa wokovu. Huu ni utawala wa upendo ambao Mungu ako nao juu ya watu wake. Ni ukweli kwamba ni Mungu ambaye aliumba kila kitu na kwa kila kila kitu kiko chini ya utawala wake. Lakini wakati Biblia inatumia neno Ufalme wa Mungu huwa inammanisha wale watu ambao Mungu amewaokoa kupitia kwa imani ndani ya Kristo Yesu. Hii ndiyo

Page 50: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

sababu Biblia inazungumza kwamba tumekombolewa kutoka katika ufalme wa giza na kuletwa katika ufalme Mwana wa Mungu (Wakolosai 1:12-13). Biblia pia inafundisha kwamba waovu hawataurithi Ufalme wa Mungu (1 Wakorintho 6:9). Kwa ufupi ni kwamba Ufalme wa Mungu ni utawala, mamlaka na nguvu Zake juu ya mpango wake wa wokovu juu ya wale wote ambao wameokoka kupitia kwa Kristo Yesu. Ufalme ambao unakuja Pili ni kwamba Ufalme wa Mungu uko hapa. Wakati Yesu Kristo alianza huduma wake hapa alisema, @Tubuni kwa maana Ufalme wa Mbinguni u karibu@ (Mathayo 3:2). Kwa miaka mingi Wayahudi walikuwa watarajia na kuomba kuja kwa ufalme. Walikuwa wanatazamia siku ile mabpo Ufalme wa Mungu utakuja ulimwenguni na wao waweze kuokolewa kutoka kwa utawala wa warumi. Katika maneno ya Kristo katika Mathayo 3:2, Yesu alikuwa anwaeleza kwamba kile ambacho mlikuwa mnakingoja, sasa kimefika. Pia katika maneno hayo alikuwa nasema kwamba ufalme huu umefika kwa kufika kwake na kwamba Yeye ndiye Mfalme wa Ufalme huu. Wakati Yesu alishitumiwa na Mafarisay kwamba alikuwa anawafukuza mapepo kwa jina la shetani, Yesu aliwakemea kwa kusema, @Kama Mimi ninatoa pepo wachafu kwa Roho wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umekuja juu yenu@ (Mathayo 12:28). katika mstari huu, Yesu anawahakikishia Mafarisay kwamba Yeye alikuwa anatoa mapepo kkwa nguvu za Mungu. Zaidi alikuwa anawahakikishia kwamba ukombozi ambao ulikuwa umeahidiwa watu wa Mungu ulikuwa umeanza. Ukombozi huu haukuwa wa kuwakomboa kutoka katika utawala wa Warumi bali ulikuwa wa kuwakomboa kutoka kwa nguvu na utawala wa dhambi na shetani. Kuja kwa Kristo Yesu hapa ulimwenguni kulikuwa kwa ajili ya kuangamiza nguvu za dhambi, kifo na shetani. Yesu hakuja hapa tu

Page 51: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

kutuonyesha kwamba Yeye ni Mwumbaji. Alikuja kufanya kila kitu mpya. Katika Agano Jipya tunasoma kuhusu hadithi za Kristo na kazi ambayo alifanya wakati alikuwa hapa ulimwenguni. Kwanza tunasoma kuhusu kuzaliwa kwake, kujaribiwa kwake na shetani katika jangwa, miujiza yake, upendo na huruma wake kwa watu. Zaidi ya haya yote tunauona ushindi wake juu ya msalaba wakati alilia, @Imekwishi.@ Baadaye tunaona ushindi wake juu ya kifo wakati malaika aliposema, @Kwa nini mnamtafuta aliye hai miongoni mwa wafu? Hayuko hapa, amefufuka!@ (Luka 24:5-6). Kwa haya yote, pole pole Kristo anarejesha kiumbe katika utukuf wake. Mfalme mkuu alikuja na yale yote ambayo yalikuwa kizuuizi kwa kuja kwa Ufalme wa Mungu ulimwenguni, yaani dhambi, kifo, jahanum na shetani yaliondolewa na kushindwa kabisa. Hii inamaanisha kwamba baraka zote za ufalme huu ni zetu. Bwana Yesu Kristo aliwaahidi wanafunzi wake kwamba alikuwa ametume mfaraiji ambaye ni Roho Mtakatifu ambaye angewaongoza na kuudhitishia ulimwengu kuhusu dhambi na kukutakasa. Wale wote ambao wameokoka, wameletwa katika jamii ya Mungu na wamepatanishwa na Mungu mwenyewe. Biblia inafundisha kwamba machoni pa Mungu tayari tumeshakalisha fufuliwa na kuketishwa na Kristo Yesu (Waefeso 2:6). Huu ni ukweli ambao ni wa kuwahimiza wote ambao wamekoka kwa kumwamini Kristo Yesu pekee. Watu wote wa Ufalme huu kwa sasa hawajaingia wote Tatu, watu wote wa Ufalme huu kwa sasa hawajaingia ndani wote. Mambo yatakuwa hivi hadi kurudi kwa Bwana Yesu Kristo. Yaani Ufalme huu utakamilika wakati Bwana Yesu atarudi. Bwana Yesu Kristo alishinda nguvu za dhambi, kifo na shetani lakini hii haimaanishi kwamba sasa Ufalme wake hapa ulimwenguni umeshekamilika kabisa. Ndiyo shatani alishindwa lakini bado hajaondolewa katika ulimwengu huu. Dhambi ilishindwa lakini bado

Page 52: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

haikuondolewa katika ulimwengu huu. Ufalme ulianzishwa lakini haujakamilishwa kabisa. Bwana Yesu Kristo alizungumza kuhusu siku ambapo Ufalme huu utakamilishwa kabisa na wote wa Ufalme wataingizwa ndani. Alisema, @Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika Ufalme wake kila kitu kinachosababisha dhambi na watenda maovu wote. Nao watawatupa katika tanuri la moto ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno. Ndipo wenye haki watang'aa kama jua katika Ufalme wa Baba yao. Yeye aliye na masikio na asikie@ (Mathayo 13:41-43). Bwana Yesu Kristo anatazamia siku ile atakinywa kikombe cha divai na watu wake katika Ufalme wake: @Lakini ninawaambai, tangu sasa sitakunywa tena kutoka katika uzao huu wa mzabibu, mpaka siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika Ufalme wa Baba Yangu@ (Mathayo 26:29). Paulo naye aliandika akitazamia kufufuka walio kufa milele (1 Wakorintho 15) na pia aliawambia wakristo wa Efeso kwamba wametiwa muhuri kwa yule Roho Mtakatifu wa ahadi waliyeahidiwa @Yeye ndiye amana ya urithi wetu hadi ukombozi wa milki yake kuwa sifa ya utukufu Wake@ (Waefeso 1:14). Baadaye Biblia inasema kwamba Mungu ametuokoa @ili katika ulimwengu ujao apate kuonyesha wingi wa neema Yake isiyopimika, iliyodhihirisha kwetu kwa wema Wake ndani ya Kristo Yesu@ (Waefeso 2:7); @Nanyi, mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hadi uje ule wokovu ulio tayari kufunuliwa nyakati wa mwisho@ (1 Petro 1:5), @Nao walikubali kwamba walikuwa wageni na wasiokuwa na maskani hapa duniani@ (Waebrania 11:13) hawa walitazamia mji wenye msingi ya kudumu ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu@ (Waebrania 11:10). Tumaini letu kuu wakristo ni kurudi kwa Bwana wetu Yesu Kristo na wakati huo kuukamilisha Ufalem wake ambao alianza alipokuja mara ya kwanza. Huu utakuwa ufalme wa milele. Wakati huo ndipo

Page 53: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

kila kitu katika ulimwengu kikifanywa kuwa kipya. Wakati huo uovu na dhambi vitaondolewa kabisa na milele na haki itadhihiri hapa ulimwenguni milele. Mungu aliahidi kwamba: “Tazama, nitaumba mbingu mpya na dunia mpya. Mambo ya zamani hayatakumbukwa, wala hatakuja akilini. Lakini furahini na kushangilia daima katika hivi nitakavyoumba, kwa kuwa nitaumba Yerusalemu uwe wa kupendeza, nao watu wake wawe furaha. Nani nitaifurahia Yerusalemu na kuwafurahia watu wangu, sauti ya maombolezo na ya kilio haitasikika humo tena” (Isaya 65:17-19). Katika siku hiyo, “Hawatudhuru wala kuharibu juu ya mlima wangu mtakatifu wote, kwa kuwa dunia itajawa na kumjua Bwana kama maji yajazavyo bahari” (Isaya 11:9). Mungu anakusudia kuumba ulimwengu mpya ambamo watu wake wataishi. Ulimwengu ambao hauna dhambi yeyote, kifo au magonjwa. Watu wa Mungu hawatakufa tena wala kulia tena. Hakutakuwa tena na huzuni au kuumia. Mungu mwenyewe atafuta machozi yetu na tutaona uso wake. Je, katika haya yote, utasema nini? Jambo moja ambalo linaweza kutoka katika kinywa cha kila mkristo na ni hili, Bwana Yesu njoo kwa haraka! Kuna wengi ambao baada ya kusikia mambo haya, wao hujieleza kwamba wanaweza kufanya haya yafanyika kwa uwezo wao. Hata kama tunajitahidi kwa juhudi kuleta amani kupitia kwa mashirika tofauti, ukweli ni kwamba hilo halitafanyika kwa sababu ni Kristo Yesu tu ambaye atafanya tuwe na amani ya milele. Ulimwengu mpya na mbingu vitakuwepo wakati Kristo Yesu atakaporudi. Hili ni jambo la muhimu sana kukumbuka kwa sababu ya: 1. Tunalindwa na kujidanganya kuhusu yale ambayo tunaweza kufanya na yale ambayo hatuwezi kufanya. Ni ukweli kwamba sisi wakristo kuna mambo ambayo tunataweza kubadilisha katika jamii na nchi zetu. Wakristo wa hapo awali walifanya mambo mengi

Page 54: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

mazuri katika jamii zao na hata leo wanaendelea kufanya hivyo. Uzuri huu ambao tunafanya unadhihirisha utukufu wa Mungu Baba na wa Bwana wetu Yesu Kristo. 2. Tunajifunza kwamba hadi Kristo Yesu arudi hapa, chochote tunachofanya si kamili na kitakamilishwa wakati Kristo Yesu atakaporudi. Wakristo hawatawahi kuuleta Ufalme wa Mungu hapa. Yerusalemu mpya itatoka mbinguni. Mungu ndiye ataukamilisha Ufalme wake na wala si mkristo yeyote. 3. Kujua kwamba Ufalme huu utakamilishwa wakati Kristo Yesu atarudi ni jambo ambalo linafaa kutufanya tuishi maisha yetu kwa tukimtarajia Kristo Yesu kwa hamu sana. Badala ya kutazamia nguvu za wanadamua, matendo ya wanadamu, mamlaka ya wanadamu hata juhudi zetu wakristo, tunatazama mbinguni na kumtegemea Mungu pekee na kama mtume Yohana, tunalia kwa sauti, @Bwana Yesu Krist njoo kwa haraka. Kwa sababu ni Yeye tu ambaye atafanya kila kitu kiwwe kipya, tunatazamia kurudi kwake kwa hamu sana na wakati huo huo, tunaendelea kuvumilia katika maombi yetu Kwake na upendo wetu kwake unakua zaid na zaidi. Kwa ufupi ni kwamba upendo wetu sana unakuwa kwa Kristo na si kwa sababu tu ya Ufalme. Jinsi tunafaa kupokea ujumbe wa Mfalme Kristo Yesu Kuwa katika Ufalme wa Mungu inategemea jinsi tunavyopokea ujumbe wake Mfalme Kristo Yesu. Bwana Yesu Kristo alisisiza jambo hili sana akisema kwamba kuwa katika Mfalme wake inategemea jinsi anavyopokea ujumbe wa injili. Kwa mfano katika Marko 10:17,21 tunasoma, @Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele? Yesu akamtazama na akampenda, akamwambia, 'Umepungukiwa na kitu kimoja, nenda ukauze kila kitu ulicho nacho uwape maskini hizo fedha, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo unifuate.@ Kile Yesu Kristo alikuwa anamwambia ni kwamba, @wacha kuamini katika utajiri wako na uanze kuniamini Mimi.@ Bwana Yesu Kristo alisema kwamba Mungu atawatanyisha wale

Page 55: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

ambao wameokoka kutoka miongoni mwa wale ambao hawajaokoka. Jambo ambalo litafanya kuwe na kutawanyishwa huko ni jinsi wao wanavyompokea Mfalme Kristo Yesu (Mathayo 25:31-46). Katika Mathayo 25:31-46, wale ambao walimpokea Mfalme Yesu kwa kutii ujumbe wa injili wao wataambiwa, @njoni ninyi mliobarikiwa na Baba Yangu, urithini Ufalme uliondaliwa kwa ajili yenu tangu kuumbwa kwa ulimwengu.@ Wale ambao wanakataa kupokea ujumbe wa Mfalme Yesu, wataambiwa, @ondokeni Kwangu, ninyi mliolaaniwa, nendeni kwenye moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya ibilisi na malaika zake.@ Wale ambao wameokoka, wamewezeshwa kuokoka kwa sababu Kristo Yesu alikufa kwa ajili yao msalabani Kalivari. Yesu Kristo si mfalme tu ambaye alianzisha Ufalme wake hapa kwa upendo na huruma mkuu sana. Bali Yeye ni Mfalme ambaye alikufa msalabani ili awaokoe watu wake kutoka katika dhambi zao. Wayahudi kwa miaki mingi walimsubiri Mesiya ambaye angewaokoa kutoka katika utawala wa Warumi. Pia wao walijua kwamba Mesiya huyu alikuwa ateseke sana na pia kutokana na maandiko walijua atakuwa Mwana wa Mungu (Danieli). Kile hawakufahamu ni kwamba mambo haya yote yalikuwa yanazungumza kuhusu mtu mmoja tu ambaye ni Kristo Yesu. Yesu Kristo alisema wazi kwamba Yeye ndiye alikuwa Mesiya ambaye Wayahudi walisubiri sana na kwamba pia Yeye ndiye alikuwa Mwana wa Mungu ambaye alizungumziwa katika Danieli 7. Alisema, @Kwa kuwa hata Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa Wake kuwa ukombozi kwa ajili ya wengi@ (Marko 10:45). Hii ilidhihirisha wazi kabisa Mwokozi ambaye alikuwa ateseke sana kulingana na Isaya 53:10. Kile Bwana Yesu Kristo alikuwa anasema ni kwamba, Yeye ndiye alikuwa Mesiya ambaye alikuwa atoka katika ukoo wa Daudi, Yeye ndiye alikuwa Mwokozi ambaye alikuwa ateseke sana katika Isaya na kwamba Yeye ndiye alikuwa Mwana wa Adamu katika Danieli.

Page 56: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

Katika haya yote, Bwana Yesu Kristo alikuwa zaidi ya Mfalme ambao Wayahudio walisubiri. Yeye alikuwa Mfalme ambaye alikuwa ateseke na afe kwa ajili ya dhambi za watu wake ili watu waweze kuokolewa na wawe wenye haki machoni pa Mungu Baba na awalete katika utukufu wa Ufalme wake. Kwa sababu hii, wale ambao wanaingia katika Ufalme wa kristo ni lazima wawe watu ambao wametubu dhambi zao na kumwamini Kristo na kazi yake ambayo alifanya msalabani Kalivari. Wakati Kristo Yesu anazungumza kuhusu injili ya Ufalme hamaanishi tu kwamba Ufalme umekuja, bali pia anamaanisha kwamba Ufalme umekuja na wewe unaweza kuingia ndani ikiwa utamwamini Yeye pekee. Kwa hivyo kuwa mmoja wa wale ambao wako katika Ufalme huu haimaanishi tu kuishi maisha ya Ufalme huu au kumfuata tu Kristo au kuishi kama vile Kristo Yesu mwenyewe alivyoishi, bali inamaanisha kwamba umekuja kwa Kristo Yesu na umetubu dhambi zako na kumwamini na unategemea Yeye pekee kwa ondolewa la dhambi zako na kupewa msamaha wa dhambi zako. Kuna wengi ambao wanadai kuwa wafuasi wa Kristo lakini ukweli ni kwamba wao si watu wake. Kukiri tu hakukufanyi kuwa mkristo au kujaribu kuishi maisha mazuri. Unafanywa kuwa mkristo kupitia kwa imani ndani ya Kristo Yesu pekee. Mwito wa kuishi kwa ajili ya Kristo Kuwa raia wa Ufalme wa Mungu ni kuishi maisha ya Ufalme huu. Katika Warumi 6, wakristo wote wanahimizwa kwamba waishi maisha matakatifu ya Ufalme kwa sababu wao wamekombolewa kutoka kwa nguvu za shetani na wameletwa katika Ufalme wa Mungu. @Kwa hiyo tulizikwa pamoja Naye kwa njia ya ubatizo katika mauti, ili kama vile Kristo alivyofufuka kutoka kwa wafu kwa utukufu wa Baba, vivyo hivyo sisi nasi pia tupate kuenenda katika upya wa uzima. Kwa maana ikiwa tumeungana Naye katika mauti Yake, bila

Page 57: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

shaka tutaungana Naye katika ufufuo Wake. Kwa maana twajua kwamba utu wetu wa kale ulisulibiwa pamoja Naye ili ule mwili wa dhambi upate kuangamizwa, nasi tusiendelee kuwa tena watumwa wa dhambi. Kwa maana mtu yeyote aliyekufa amewekwa huru mbali na dhambi. Basi ikiwa tulikufa pamoja na Kristo, tunaamini kwamba pia tutaishi pamoja Naye. Kwa maana tunajua kwamba Kristo, akiisha kufufuka kutoka kwa wafu, hatakufa tena, majuti haina tena mamlaka juu Yake. Kifo alichokufa, aliifia dhambi mara moja tu, lakini uzima alio nao anamwishia Mungu. Vivyo hivyo, jihesabuni wafu katika dhambi lakini mlio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu@ (Warumi 6:4-11). Huwa tunaletwa katika Ufalme wa Mungu kwa imani na Roho Mtakatifu huwa anatupatia maisha mapya. Huwa tunafanyika rais wa Ufalme huu na kuanza kumtumikia Mfalme Yesu Kristo. Kwa sababu sasa sisi ni wake, ni jukumu letu kutii Mfalme Yesu Kristo na kuishi maisha yetu kwa njia ambayo inamletea utukufu. Kwa sababu hii Biblia inafundisha kwamba, @msiruhusu dhambi itawale ndani ya miili yenu, ipatikanayo na kufa, ili kuwafanya mzitii tamaa mbaya. Wala msivitoe viungu vya miili yenu vitumike kama vyombo vya uovu vya kutenda dhambi, bali jitoeni kwa Mungu, kama watu waliotolewa kutoka mautini kuingia uzimani. Nanyi vitoeni viungu vya miili yenu Kwake kama vyombo vya haki@ (Warumi 6:12-13). Hadi kurudi kwa Bwana Yesu Kristo, sisi wakristo tutaendelea kuishi katika ulimwengu huu ambamo kuna uovu mwingi. Wakati huo huo Bwana Yesu Kristo anatuamuru tuishi maisha matakatifu ambayo yanamletea utukufu (1 Wathesalonike 2:12). Biblia inatuamuru tung'ae kama nyota katika kizazi hiki kiovu (Wafilipi 2:15). Kwa kusema hivi haimaanishi kwamba tunaokoka kwa kuishi mazuri. Bali ni kwamba baada ya kuokolewa kupitia kwa imani katika Kristo Yesu, tunakuwa chini ya Bwana mpya ambaye ni Yesu Kristo. Katika Ufalme wa Kristo Yesu tunakuwa chini ya sheria mpya na maisha

Page 58: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

mapya na kwa hivyo tunaanza kuishi maisha ya Ufalme wa Kristo Yesu. Biblia inafundisha kwamba katika maisha haya ya hapa ulimwengu maisha ya Ufalme tunayaishi kama kanisa. Je, umewahi waza hivi kuhusu jambo hili? Ni katika kanisa Ufalme wa Mungu unadhihirika wazi kabisa katika ulimwengu huu. Biblia inasema, @Ili kwa njia ya kanisa, hekima yote ya Mungu ipate kujulikana kwa watawala na wenye mamlaka katika ulimwengu wa roho, sawasawa na kusudi Lake la milele katika Kristo Yesu Bwana wetu@ (Waefeso 3:10-11). Mungu amechagua kudhihirsha utukufu wa ujumbe wa injili katika kanisa Lake. Mungu amepanga kwamba katika kanisa Lake, utawala na mamlaka yake vitadhirishwa. Kanisa ni mahali ambapo tunaona Ufalme wa Mungu katika ulimwengu huu. Ikiwa unataka kuona Ufalme wa Mungu ni wa aina gani kabla ya Ufalme huo kukamilshwa na kuona jinsi maisha ya Ufalme yako katika ulimwengu huu, tazama kanisa la Kristo. Katika kanisa tunaona hekima ya Mungu akidhihirishwa. Ni mahali ambapo kuna watu ambao walikuwa maadui wa Mungu na sasa wamepatanishwa Naye kupitia kwa Kristo Yesu. Kanisa ni mahali ambapo Roho Mtakatifu anafanya kazi ya kuwajenga na kuwabadilisha wale ambao wameokoka. Ni mahali ambapo watu wa Mungu hujifunza kupendana, kuvumiliana, kusaidiana, kuhuzunika na kufurahia pamoja na pia kuchungana. Hii haimaanishi kwamba kanisa ni mahali ambapo kuna wale ambao wamekamilika. Bali kanisa ni mahali ambapo watu wake wanaishi maisha ya Ufalme na kuitangazia ulimwengu ujumbe wa injili ambao uleta wokovu. Kuvumilia wakati wa mateso Kwa sababu kanisa linahubiri ujumbe wa injili ambao unaleta wokovu, maisha ya kanisa katika ulimwengu huu ni maisha magumu sana ambayo yamejawa na mateso na shid nyingi sana. Kwa walimwengu, wakristo na dini ya ukristo ni tisho kubwa sana kwao. Katika maisha ya kanisa la kwanza, jumbe kwamba Yesu ni Bwana,

Page 59: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

ulitazamiwa kuwa ujumbe ambao ni wa kukufuru na kukataa mamlaka ya viongozi wa wakati huo. Wakristo wengbi waliuliwa kwa kutangaza ujumbe huu. Leo pia ulimwengu hautaki kusikia maneno haya. Kwa sababu ya kuhubiri ujumbe huu, ulimwengu unatuchukia sana. Katika Biblia tunafundishwa kwamba maisha ya Ufalme ni maisha magugu ya mateso mengi hapa ulimwenguni. Bwana Yesu kristo mwenyewe alisema kwamba wafuasi wake watateswa, kuchekelewa na hata kuuliwa. Lakini hata wakati kuna haya yote, sisi wakristo kwa uvumilivu, tunaendelea na kufanya kazi ya Mungu kwa sababu tunajua kwamba kuna urithi mkuu ambao Mungu ameandalia watu Wake. Ujasiri wa kuendelea kuvumilia tunaupata kutoka kwa Kristo Yesu. Unatoka kwa kujua kwamba mateso yetu ni madogo kulinganishwa na furaha ambayo Mungu ametuandalia katika Ufalme Wake. Pia mateso haya ni muda tu si ya milele. Msalaba wa Kristo Yesu ndiyo msingi wa ukristo wetu Njia ya kuokoka ni kutubu na kumwamini Kristo Yesu na kazi ambayo alifanya msalabani Kalivari. Haitoshi tu kujiita mkristo au kutamani ukristo. Ikiwa mtu anawaza kwamba anaweza kuokoka bila kumwamini Kristo, yeye hataokoka na hata ingia mbinguni. Injili ya uongo Tangu kitambo watu wamekuwa wakijaribu kujiokoa wakitumia njia ambazo wao wanajua ni bora kwao badala ya kusikiliza na kutii ujumbe wa injili. Wao wamekuwa wakijaribu kuona kwamba wanaingia mbinguni bila Kristo na kazi ambgayo alifanya msalabani kalivari. Leo kuna wengi ambao wanajaribu kutumia njia zingine kando na kumwamini Kristo Yesu. Hatari kuu ambayo kanisa la Kristo leo linakumbana nayo ni kwamba wengi wanajaribu wanahubiri injili ambayo msingi wake si Kristo na kazi Yake msalabani Kalivari. Injili ambayo wanahubiri msingi wake ni wao wenyewe na vitu vya

Page 60: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

ulimwengu huu. Wahubiri wengi wanajaribiwa kufanya hivi. Haswa wengi wanawaza kwamba Kristo na kazi yake msalabani Kalivari haitoshi pekee kumwokoa mtu kwa sababu wanawaza msalaba wa Kristo hakushughulikia mambo kama vita vya ulimwengu huu, kunyanyaswa kwa watu, umaskini, ukosefu wa haki kwa watu na mambo kama hayo. Wao wanasema kwa ufupi kwamba msalabaa wa Kristo hashughuliki kamwe na mambo ya hapa ulimwenguni. Huu si ukweli hata kidogo. Mambo haya yote ambayo hawa watu wanayawaza yanatokana na dhambi ambayo imo katika moyo wa mwanadamu na ni jambo la kujidanganya kwamba tunaweza kujitahidi katika kufanya mambo mengine ili kuondoa ubaya katika ulimwengu bila kuzingataia Kristo na msalaba wake. Msalabani kalivari, Kristo Yesu aliangamiza dhambi na ni kazi yake msalabani ambayo inawafanya wengi ambao wanaamini kuungia ufalme wa Mungu. Lakini hata kama huu ndiyo ukweli, bado wengi wanahubiri uongo. Unaposoma katika vitabu vingi ambavyo vimeandikwa na watu fulani fualni, utaona kwamba wao hawazingatii msalaba wa Kristo hata kidogo katika mafundisho yao. Badala ya kufundisha kuhusu msalaba, wao hufundisha kwamba Mungu anataka tuwe na mahali nyingi ya ulimwengu au kwamba Mungu anataka tuwe na afya mzuri. Hawa hupuuza Kristo na kazi ambayo alifanya kwa ajili ya wenye dhambi msalabani kalivari. Aina tatu ya injili ambazo zinahubiriwa Kwa miaka sasa, utaona kwamba zaidi na zaidi wengi ambao wanahubiri, hawahubiri Kristo na msalaba wake. Kuna aina tofauti ya injili ambazo zinahubiriwa sana leo. Kwa mfano wangi wanahubiri kuhusu kupata vitu vikubwa na maisha bora katika ulimwengu huu. Msingi wa mafundisho si Kristo au msalaba wake. Kwa mfano: 1. @Yesu ni Bwana@ si injili.

Page 61: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

Wengi wanahubiri wakisema kwamba ujumbe wa injili ni kwamba Yesu ndiye Bwana. Huu si ujumbe wa Injili. Ujumbe wa injili ni kwamba Bwana Yesu Kristo ambaye anatawala na kwamba anapatanisha ulimwengu wote Kwake na kufanya kila kitu kiwe chini yake. Ni kweli kwamba Yesu Kristo ni Bwana na hili ni jambo la maana sana kuhusu ujumbe wa injili. Biblia inasema kwamba mtu ambaye anakiri kwamba Yesu ni Bwana ataokoka (Warumi 10:9) na katika 1 Wakorintho 12:3, Biblia inasema kwamba ni kupitia kwa Roho Mtakatifu mtu anaweza kuhakikisha ukweli. Kukiri kwamba Yesu ni Bwana si ujumbe wa injili. Msalaba wa Kristo Yesu ndiyo msingi wa ukristo wetu Njia ya kuokoka ni kutubu na kumwamini Kristo Yesu na kazi ambayo alifanya msalabani Kalivari. Haitoshi tu kujiita mkristo au kutamani ukristo. Ikiwa mtu anawaza kwamba anaweza kuokoka bila kumwamini Kristo, yeye hataokoka na hata ingia mbinguni. Injili ya uongo Tangu kitambo watu wamekuwa wakijaribu kujiokoa wakitumia njia ambazo wao wanajua ni bora kwao badala ya kusikiliza na kutii ujumbe wa injili. Wao wamekuwa wakijaribu kuona kwamba wanaingia mbinguni bila Kristo na kazi ambgayo alifanya msalabani kalivari. Leo kuna wengi ambao wanajaribu kutumia njia zingine kando na kumwamini Kristo Yesu. Hatari kuu ambayo kanisa la Kristo leo linakumbana nayo ni kwamba wengi wanajaribu wanahubiri injili ambayo msingi wake si Kristo na kazi Yake msalabani Kalivari. Injili ambayo wanahubiri msingi wake ni wao wenyewe na vitu vya ulimwengu huu. Wahubiri wengi wanajaribiwa kufanya hivi. Haswa wengi wanawaza kwamba Kristo na kazi yake msalabani Kalivari haitoshi pekee kumwokoa mtu kwa sababu wanawaza msalaba wa Kristo hakushughulikia mambo kama vita vya ulimwengu huu, kunyanyaswa kwa watu, umaskini, ukosefu wa haki kwa watu na

Page 62: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

mambo kama hayo. Wao wanasema kwa ufupi kwamba msalabaa wa Kristo hashughuliki kamwe na mambo ya hapa ulimwenguni. Huu si ukweli hata kidogo. Mambo haya yote ambayo hawa watu wanayawaza yanatokana na dhambi ambayo imo katika moyo wa mwanadamu na ni jambo la kujidanganya kwamba tunaweza kujitahidi katika kufanya mambo mengine ili kuondoa ubaya katika ulimwengu bila kuzingataia Kristo na msalaba wake. Msalabani kalivari, Kristo Yesu aliangamiza dhambi na ni kazi yake msalabani ambayo inawafanya wengi ambao wanaamini kuungia ufalme wa Mungu. Lakini hata kama huu ndiyo ukweli, bado wengi wanahubiri uongo. Unaposoma katika vitabu vingi ambavyo vimeandikwa na watu fulani fualni, utaona kwamba wao hawazingatii msalaba wa Kristo hata kidogo katika mafundisho yao. Badala ya kufundisha kuhusu msalaba, wao hufundisha kwamba Mungu anataka tuwe na mahali nyingi ya ulimwengu au kwamba Mungu anataka tuwe na afya mzuri. Hawa hupuuza Kristo na kazi ambayo alifanya kwa ajili ya wenye dhambi msalabani kalivari. Aina tatu ya injili ambazo zinahubiriwa Kwa miaka sasa, utaona kwamba zaidi na zaidi wengi ambao wanahubiri, hawahubiri Kristo na msalaba wake. Kuna aina tofauti ya injili ambazo zinahubiriwa sana leo. Kwa mfano wangi wanahubiri kuhusu kupata vitu vikubwa na maisha bora katika ulimwengu huu. Msingi wa mafundisho si Kristo au msalaba wake. Si kweli kusema kwamba kukiri kwamba Yesu Bwana inamtosha mtu yeyote kuokoka. Katika Agano Jipya tunasoma, @Kwa hiyo Israeli wote na wajue jambo hili kwa uhakika kwamba: Mungu amemfanya huyu Yesu, ambaye ninyi mlisulibisha, kuwa Bwana na Kristo@ (Matendo ya Mitume 2:38). Katika Sentensi hii tunafundishwa kwamba inamaanisha nini kwamba Kristo ni Bwana. Inamaanisha kwamba Bwana Yesu Kristo alikuwa amesulibishwa, akazikwa na akafufuka. Pia ilimaanisha kwamba kifo na kufufuka kwa Bwana

Page 63: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

Yesu Kristo kulihakikisha msahama wa dhambi kwa wale wote ambao wanatubu na kumwamini Bwana Yesu Kristo. Petro hakusema tu kwamba Bwana Yesu Kristo ni Bwana, bali pia alisema kwamba huyu Bwana alikufa kwa ajili ya watu wake ili awaokoke kutoka katika dhambi zao na ghadhabu ya Mungu. Kwa hivyo kusema tu kwamba Yesu ni Bwana, si ujumbe wa injili haswa ikiwa hatutaeleza kwamba Yeye si Bwana tu bali pia ni Mwokozi. Kwa sababu Bwana Yesu Kristo ni Bwana, Yeye ako na mamlaka ya kuhukumu na atakuhukumu dhambi. Kwa mtenda dhambi ambaye amekataa kuokoka, hukumu ya Mungu inawasubiri na hizi si habari nzuri kwa mtenda dhambi. Hii inamaanisha kwamba mwenye dhambi ni adui wa Mungu, na Mungu atamhukumu kwa sababu ya uasi. Ili ujumbe wa injili usiwe ujumbe wa kuogofya, lazima ujumbe huu uonyesha njia ya kupata msamaha wa dhambi zake na kupatanishwa na Yesu kristo ambaye ndiye Bwana. Haya ndiyo mafundisho ya Agano Jipya kwamba Yesu Kristo ni Bwana ambaye alisulibiwa ili wenye dhambi waweze kusamehewa na kuletwa katika Ufalme wa Mungu. Biblia Kristo Yesu kuwa Mwokozi, kukiri kwamba Yeye ni Bwana ni kukiri hukumu kwa wenye dhambi wote. Mahubiri kuhusu kuumbwa kwa kila kitu, kuhusu kuanguka katika dhambi, kuhusu wokovu na kuhusu mnginu na nchi si ujumbe wa injili. Biblia inafundisha kwamba Mungu aliumba kila kitu kikiwa kizuri; mwanadamu alianguka dhambini; Mungu kupitia kwa Kristo Yesu anakomboa watu wake na haya yote yatakamilika wakati Mungu ataondoa dhambi kabisa na madhara yake na kuuweka Ufalme wake hapa milele. Kutoka Mwanzo hadi Ufuno, Biblia inafundisha haya mambo. Ikiwa mtu anafahamu vyema mambo haya, yatamsaidia kuelewa vyema ujumbe wa injili. Shida ku bwa wengi wamefanya ni kwamba wamechukua mafundisho haya na kusisitiza kuhusu kuishi katika nchi mpya na

Page 64: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

mbingu mpya. Mafundisha haya yamechukua nafasi ya mahubiri kuhus Kristo na Kazi yake msalabani. Wala ambao wanahubiri mahaubiri ya aina hii husema, @Ujumbe wa injili ni kwamba hapo mwanzoni Mungu aliumba kila kitu. Mwanzoni kila kitu kilikuwa kizuri lakini mwanadamu aliasi dhidi ya Mungu. Uhusiano na ushirika kati Mungu na mwanadamu ulivunjika na hata uhusiano kati ya mwanadamu na mwanadamu ulikatizwa. Pia mwanadamu aliacha kuwa na uhusiano mwema na ulimwengu. Baada ya mwanadamu kuanguka katika dhambi, Mungu aliahidi kumtuma Mwokozi ambaye angemwokoa mwanadamu na kumptanisha na Mungu tena. Ahadi hii ilianza kutimizwa kutokana na kuja kwa Kristo Yesu hapa ulimwenguni na itakamilishwa wakati Bwana Yesu Kristo atarudi. Mambo katika kifungu ni ya ukweli lakini mambo haya si ujumbe injili. Ukweli kwamba Mungu anaumba kila kitu upya si ujumbe wa injili ikiwa hakuna nafasi ya mtu kuingizwa humo. Ni vyema sana kutumia mpangilio huu kufafanua ujumbe wa injili. Ili tuweze kueleza vyema kuhusu ujumbe injili, ni lazima tueleza vyema kifo na kufufuka kwa Bwana Yesu Kristo na kile Mungu anatarajia mwanadamu afanye baada ya kusikia ujumbe huu. Ikiwa kweli tutawaeleza wengi kwamba anafanya kazi ya kuwakomboa wengi na kuumba kila kitu upya lakini hatusemi ni njia gani Mungu anatumia kufanya haya yote na jinsi mmoja anaweza kuletwa katika ukombozi huu, basi hatutakuwa tumehubiri ujumbe wa injili. Tutakuwa tumeeleza tu yale ambayo yako katika Biblia kwa ufupi na tutakuwa tumewacha wenye dhambi bila tumaini lolote. Ni lazima tuwaeleze kwamba Mungu ako anafanya kila kitu kuwa kipya kupitia kwa kifo na kufufuka kwa Bwana Yesu kristo na kwamba mtu anaweza kuletwa katika ukombozi huu kwa kutubu na kumwamini Kristo Yesu. Kubadilisha tamaduni si ujumbe wa injili.

Page 65: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

Leo kuna wengi ambao wanahubiri kwamba wakristo wanafaa kujitahidi kubadilisha tamaduni ambazo si nzuri. Hili si jambo baya kufanya. Ni vyema ikiwa tutajitahidi kuendelesha madili mema ya uongozi na maisha kulingana na mafundisho ya Biblia. Biblia inatuhimza kwamba tunafaa @tuwatendee watu wote mema, hasa wale wa jamaa ya waaminio@ (Wagalatia 6:10). Bwana Yesu Kristo alituamuru kwamba lazima tuwajali majirani wetu hata wale ambao hawajaokoka (Luka 10:25-37). Pia alisema, @Vivyo hivyo, nuru yenu iangaze mbele ya watu, ili wapate kuona matendo yenu mema wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni@ (Marko 5:16). Kuna wale ambao wanasema kwamba, ikiwa Mungu anafanya kazi ya kuumba kila kitu upya, basi ni jukumu letu kujihusisha na kazi hii kwa kuuleta utawala wa Mungu mahali ambapo tunaishi, katika mataifa ya ulimwengu na katika miji yetu. Wao husema kwamba, @ni lazima tufanye kile tunaona Mungu anafanya.@ Biblia haisisitizi kuhusu kubadilisha tamaduni hata kidogo jinsi wengi wanavyowaza na kusisitiza. Ninasema hivi kwa sababu katika kitabu cha Mwanzo Mungu hakusema kwamba watu walisihi waishi kulingana na tamaduni. Wale wote ambao wanawaza kwamba kwamba wanaweza kuubadilisha ulimwengu kwa minigi ya mafundiosho yao, hawaendi popote na mwishowe watashushwa mioyo. Mabadiliko ambayo ni ya kweli na yanaweza kubadilisha wengi ni yale ambayo msingi wake ni kristo na kazi ambayo alifanya msalabani kalivari. Mungu anawatumia wale ambao amewakomboa kuleta mabadiliko haya. Msamaha wa dhambi na kukombolewa kwa watu wake Mungu yanatekelezwa kupitia kwa msalaba wa Kristo Yesu. Badala ya kuwaleza wengi kwamba wanahitaji kubadili mienendo yao na kuwa na mahali bora pa kuishi humu ulimwengui, tunafaa kwaeleza ujumbe wa injili ya Kristo ambao msingi wake ni kazi ya Kristo msalabani kalivari. Tunafaa kuwaeleza wengi kwamba

Page 66: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

wanahitaji kutubu na kumwamini Kristo ikiwa kweli wanataka kuona mabadiliko yoyote ya kweli katika maisha yao. Wengi wanawaza kwamba ujumbe wa msalaba ni kizuizi na ni upumbavu Wengi wanawaza kwamba ujumbe huu si wa kweli. Hili si jambo ambalo linafaa kutushangaza kwa sababu Biblia inasema, Kwa maana ujumbe wa msalaba kwa wake wanaopotea ni upuzi na kwa wengine ni kizuizi. Lakini hata kama wengi wanauona ujumbe kuwa upuzi na kizuizi, nia yetu wakristo ni kuhubiri ujumbe huu na walimwengu waupokee. Lakini ukweli ni kwamba wengi ambao huwa tunawahubiria, ujumbe huu ni upuzi kwao. Ujumbe huu utafanya wengi wakatae kushirikiana nasi na hata wengi watatutoroka. Watu wa ulimwengu huwa wanatuona kuwa watu ambao ni waimu kwa sababu ya kuzungumza kuhusu wokovu kupitia kwa Kristo ambaye alikufa msalabani. Lakini hata kama tunakumbana na haya yote, Biblia inafundisha kwamba msalaba wa Kristo ndiyo msingi wa ujumbe wa injili. Hatuwezi kubadilisha ujumbe huu na kuanza kuhubiri mambo memngine kwa sababu watu wa ulimwengu huu hawataki kuusikia. Huu ndiyo ujumbe ambao ni habari njema kwetu. Ikiwa tutabadilisha ujumbe huu wa kweli na kuanza kuhubiri mambo mengin, tutakuwa tunahubiri mambo ambayo hayawezi kuwaokoa wenye dhambi. Kwa hivyi hatutakuwa tunahubiri habari njema. Biblia inatufundisha kwamba ikiwa kuna majaribu yoyote ya kutaka tusihubiri ujumbe huu, basi tunafaa kukataa majaribu hayo. Paulo wakati alihubiri ujumbe huu alijua kwamba wengi ambao walikuwa karibu naye hawangeukubali. Lakini hata hivyo hakukata tamaa aliendelea kuuhubiri na alisema, @sisi tunamhubiri Kristo aliyesulibiwa ambaye kwa Wayahudi ni kitu cha kukwaza na kwa Wayunani ni upuzi@ (1 Wakorintho 1:23). Aliendelea kusema, @kwa kuwa niliamua kutokujua kitu chochote wakati nikiwa nanyi

Page 67: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

isipokuwa Yesu Kristo, naye amesulibiwa msalabani@ (1 Wakorintho 2:2). Hii ni kwa sababu Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yasemayo Maandiko@ (1 Wakorintho 15:3). Hili ndilo lilikuwa jambo la maana sana kwake na ndilo lilikuwa jambo ambalo lilimfanya aendelee kwa uvumilivu kuhubiri injili ya Kristo Yesu. Paulo hakujali hata kama wengi walicheka na kudharau ujumbe ambao alihubiri, yeye aliendelea kuhubiri Kristo na kazi yake msalabani kalivari. Hata kama walimwengu watasema huu ni upuzi ukweli ni kwamba, @upumbavu wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya mwanadamu, nao udhaifu wa Mungu una nguvu kuliko nguvu ya mwanadamu@ (1 Wakorintho 1:25). Paulo alihakisha kwamba msalaba wa Kristo ndiyo msingi wa ujumbe wa injili ambao alihubiri. Kwa hivyo tunafaa kufanya kama yeye. Ikiwa tutahubiri jambo lingine kando na msalaba wa Kristo, basi tutakuwa tunahubiri uongo. Nguvu za ujumbe wa injili Nguvu za ujumbe wa injili Ni vyema sana ikiwa tutawaza kuhusu ujumbe wa injili na nguvu za ujumbe huu. Ni vyema sana kujua kile ambacho Mungu ametufanyia sisi wenye dhambi kupitia kwa ujumbe huo. Katika ujumbe huo, tunasoma kuhusu neema kuu ya Mungu kwa kusamehe dhambi zetu sisi; Yeye alimtuma Mwana Wake hapa ulimwenguni ili ateseke na kufe kwa niaba yetu. Katika ujumbe huo tunasoma kwamba Mungu anauanzisha Ufalme wake kupitia kwa Kristo Yesu na kuwaleta wale wote ambao wameokoka na kukombolewa kwa damu ya Kristo Yesukatika nchi mpya na mbingu mpya mahali ambapo hamna dhambi au uovu wowote. Kila mmoja wetu anafaa kuwa na mawazo ambayo yanatawaliwa na utukufu wa Mungu ambao umefunuliwa katika ujumbe wa injili. Ni jambo la kushangaza sana na la aibu kubwa kwamba hata sisi ambao tumeokolewa mara kwa mara mawazo yetu huwa inajawa na mambo ambayo si ya mbinguni bali ni humo duniani. Ujumbe huu

Page 68: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

wa injili ya Kristo Yesu ndio unafaa kuwa ukitawala katika kila sehemu ya maisha yetu; katika nyumba zetu, katika kazini mwetu, miongoni mwa marafiki wetu na popote ambapo tunahusika. Sababu kuu kwa nini mambo yanafanyika hivi, ni kwamba sisi ni wenye dhambi na upendo wa ulimwengu mara kwa mara unatujaribu na kutunasa. Ukweli ni kwamba mambo yatakuwa hivi hadi kurudi kwa Bwana Yesu Kristo. Lakini hata kama mambo ni hivyo, tunajukumu la kupigana na dhambi hii; kupigana na unyonge wa kiroho na mambo yoyote ambayo yanajaribu kuturudisha nyuma katika ukristo wetu. Ombi la kila mmoja wetu linafaa kuwa kwamba tutashikilia ujumbe huu wa Injili ya Kristo na kuudhihirisha katika matendo, hisia, mapenzi, tamaa zetu, mawazo na tabia. Msomaji wangu ninatumaini kwamba hivyo ndivyo wewe pia unataka na kwamba kitbau hiki kimekusaidia sana kujua ni nini Mungu amekufanyia ndani ya Kristo Yesu. Ninataka kukuonyesha jinsi ujumbe huu unaweza kubadilisha maisha yako na kukufanya udhirike kwamba kweli wewe ni Kristo Yesu. Toba na imani Ikiwa wewe hujaokoka, ninaomba kwamba umechukua muda na kuwaza juu ya jumbe huu wa Kristo Yesu na kwamba utafanya kile ambacho Biblia inakusihi ufanye, yaani utubu na umwamini Kristo. Hii inamaanisha kwamba ni lazima kwanza ujitambue kwamba wewe ni mwenye dhambi na kwamba huwezi ukajiokoa na kwamba Kristo Yesu ndiye tumaini lako pekee la kupata wokovu. Kuwa mkristo hakuna chochote ambacho unafaa kulipa. Kile Ujumbe wa injili unasema kuhus mtu yeyote ni kwamba, mtu anafaa kutubu na kumwamini Kristo Yesu. Hii inamaanisha kuamini kwamba huwezi na huna uwezo wowte wa kujiokoa bali ni Kristo pekee ambaye ana uwezo huo. Ukifanya hivi, yaani ikitubu na kuwamini Kristo Yesu, basi utaokoka. Tulia na ufurahie

Page 69: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

Kila mkristo anafaa kutulia na kuwa na furaha katika Kristo Yesu kwa sababu ya wokovu ambao Kristo ametununulia. Kwa sababu ya kuunganishwa na Kristo kwa imani, mkristo anajua kwamba anaweza kupinga na kupinga majaribu ambayo anayapitia. Mkristo anajua kwamba yeye ni Kristo na hakuna mtu au kitu kinaweza kumwondoa katika uhusiano na ushirika huo. Hii ni kwa sababu wokovu wa mkristo si kazi yake bali ni kazi ya Mungu mwenyewe kupitia kwa Kristo Yesu. Shukurani kwa Mungu kwamba kupitia kwa Kristo Yesu, dhambi za mkristo zimesamehewa zote milele. Zaidi ni kwamba hali hii haitawahi kubadilika kamwe liwe liwalo kwa sababu Kristo Yesu alikufa msalabani kwa niaba yangu na kwamba alifufuka na sasa ameketi mkono wa kuume wa Mungu akiniombea. Ikiwa wewe mtu ameokoka, msalaba wa Kristo ni ushuhuda mkuu katika maisha yake kuhusu upendo wa Mungu kwako. Kwa sababu hii, Biblia inasema, @Tuseme nini basi kuhusu haya? Ikiwa Mungu yuko upande wetu, ni nani awezaye kuwa kinyume chetu? Ikkiwa Mungu hakumhurumia Mwanawe, bali alimtoa kwa ajili yetu sote, atakosaje basi kutupatia vitu vyote kwa ukarimu pamoja Naye?@ (Warumi 8:31-32). Penda watu wa Kristo Ujumbe wa injili unafaa kumfanya kila mkristo kupenda mkristo mwenzake. Hii ni kwa sababu hakuna mmoja wetu sisi wakristo ambaye alijiokoa na atakayejileta katika urithi ambao Mungu ametuandalia sisi. Sisi hatujajiokoa. Sisi tunahesabiwa katika urithi wa Mungu kwa sababu tunajua kwamba ni Kristo pekee ambaye ndiye tegemeo letu la kuokoka na kwamba tunaunganishwa Kwake kwa imani. Je, unajua kwamba huu ndiyo ukweli kuhusu dada au ndfugu katika kanisa lako ambaye anakukasirisha? Yeye pia anampenda Kristo kama tu wewe na pia ameokolewa na kusamehewa dhambi zake na Mungu kama tu wewe. Waza juu ya huyu ndugu ambaye hujataka

Page 70: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

chochote kumhusu kwa sababu unawaza kwamba yeye ni mgumu katika mambo yake. Waza juu ya huyu ndugu au dada ambaye uhusiano na ushirika wako naye umevunjika na umeamua hutaki kuutengeneza. Kumbukf kwamba yeye pia anaamini na anampenda Kristo ambaye pia wewe unapenda na kumwamini. Kumbuka pia kwamba huyu Kristo ndiye alikufa kwa ajili yako na kwa ajili yake. Je, wewe unafahamu vyema ujumbe wa injili ya Kristo Yesu kwamba Yeye alikuokoka hata kama hukustahili kuokolewa. Je, jambo hili linachochea uhusiano na ushirika wako na ndugu au dada kwa njia ambayo ni ya kumtukuza Kristo? Je, wewe umewasamehe wale ambao wamekukosea na unawapenda kama tu jinsi Kristo Yesu amekupenda na kukusamehe? Ninaomba kwamba upendo mkuu wa Mungu kwako utazidi kwa ndugu na dada zako katika Kristo Yesu. Shuhudia ujumbe wa injili kwa watu wa uliwengu bila kuwabagua Ujumbe wa injili ambao uliupokea unafaa kuwa umechochea tamaa yako ya kuwaona wengi kimwamini Kristo Yesu. Ikiwa kweli tunafahamu neema ya Mungu kwetu, hatutapuzika hadi tuwaone wengine wakiwa pia wao wamepata neema hiyo. Wakati Kristo alifufuka, aliwaambai wanafunzi wake kwamba, @Ndipo akafungua fahamu zao ili waweze kuyaeleza Maandiko. Akawaambia, 'Haya ndiyo yaliondikwa: Kristo atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka kwa wafu. Toba na msamaha wa dhambi utatamgazwa kupitia Jina Lake, kuanzia Yerusalemu. Ninyi ni mashahidi wa mambo haya@ (Luka 24:46-48). Mpango wa Mungu ni ukombozi wa watu wake na hapa Kristo anaambia kwamba wao watatumika katika kufanya kazi hii. Mungu amekusudia kufanya kazi ya kuwaokoa watu wake akitumia ujumbe wa injili ambao tunahubiri sisi. Hili ni jambo ambalo ni la kunyenyekeza kwetu kwa sababu sisi ni watu wadhaifu ambao hatusatali. Lakini himizo ambalo tunapata hapa ni kwamba Kristo Yesu alisema kwamba sisi tutakuwa mashahidi wake humo

Page 71: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

ulimwenguni. Ni kupitia kwa mahubiri na mafundisho ya neno la Mungu, Mungu atatumia kuokoa wenye dhambi. Je, ni kwa nini malaika ambaye alimtokea Kornelio hakumhubiri injili bali alimwambia akatumaishe Petro alitwe kwake? Jibu ni kwamba Mungu amekusudia kwamba ujumb wa injili utahubiriwa na watu wake ambao wameokoka. Kila mkristo ana jukumu la kuhubiri ulimwengu ujumbe wa injili ambao uneleta wokovu. Hakuna ujumbe mwingine na hakuna njia nyingine kwa watu kuokolewa kutoka katika dhambi zao. Ikiwa marafiki wako, wat5u wa jamii yako na wanyikazi wenzako watakuja siku moja kuokolewa kutoka katika dhambi zao, ni kwa sababu mtu atawazungumza nao ujumbe wa injili ya Kristo Yesu. Hii ndiyo sababu Kristo Yesu alitutuma katika ulimwengu kuhubiri na kufundisha ujumbe huu Wake. Paulo alimaanisha jambo hili wakati aliuliza, @Lakini watamwitaje Yeye ambaye hawamwamini? Nao watawezaje kumwamini Yeye ambaye hawajamsikia? Tena watamsikiaje bila mtu kuwahubiria? (Warumi 10:14). Kuna mambo mengi mazuri ambayo tunaweza kuyafanya sisi wakristo lakini ukweli ni kwamba hayo mambo pia yanaweza kufanywa na wale ambao hawajaokoka. Ikiwa sisi ambao tumeokoka hatutahubiri injili, je ni nani mwingine ambaye atakayeihubiri? Jibu ni, hakuna mwingine. Tangaza ujumbe huu wa injili kwa watu wote. Waza kuhusu ni nini itakayowafanyikia marafiki wako, watu wa jamii yako na hata wale ambao unafanya kazi ano wakati watasimama mbele Mungu wakiwa hawajaokoka. Kumbuka ni nini neema ya Mungu imefanya katika maisha yako na kwamba pia Mungu anaweza kufanya hivyo hivyo katika maisha ya wengine. Omba Mungu kwamba atakupatia ujasiri na Roho Mtakatifu atakuongoza kuhubiri injili. Tazamia kurudi kwa Kristo Yesu Ujumbe wa injili unafaa kutufanya tuwe na tamaa katika kutazamia kurudi kwa Kristo Yesu wakati atakapokamilisha ufalme wake wa

Page 72: JE, UJUMBE WA INJILI NI NINI? - WordPress.com · 2015. 9. 10. · litafanyika kupitia kwa mahubiri ya injili ya Kristo ambayo inaleta nuru kwa kila mtu. Nuru hii ni mpango wa Mungu

milele. Hatutumainii tu kurudi kwa Kristo kwa sababu tunataka kuishi katika ulimwengu ambao hauna dhambia. Hii ni ahadi kubwa ambayo Mungu mwenyewe ametuahidi sisi. Lakini haitoshi tu kutazamia wakati huu kwa njia hiyo tu. Ikiwa tunafahamu vyema ujumbe wa injili, hatutatazamia tu kuishi katika Ufalme, bali tutatazamia kurudi kwa Mfalme mwenyewe Yesu Kristo. Ujumbe wa injili umetufanya tumjue na tumpende Kristo Yesu na kwa hivyo kutamani kuishi pamoja Naye: @Baba, shauku Yangu ni kwamba, wale ulionipa wawe pamoja nami pale nilipo, ili waweze kuuona utukufu ule ulionipa kwa kuwa ulinipenda hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu@ (Yohana 17:24). Kitabu cha Ufuno kinatuonyesha baadhi ya mambo ambayo Mungu ametutayarishia sisi ambao tumeokoka. Ni kidokezo tu lakini tunaonyeshwa ukuu na ushindi na furaha na pumziko na mwishowe wale ambao waliokolewa wakiwa wanamwabudu Yesu Kristo: @Baada ya haya nikatazama na hapo mbele yangu palikuwa na umati mkubwa wa watu ambao hakuna yeyote awezaye kuuhesabu. Kutoka kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo. Walikuwa wamevaa mavazi meupe na wakiwa wameshika matawi ya mitende mikononi mwao. Nao walikuwa wakipiga kelele kwa sauti kubwa wakisema: 'Wokovu una Mungu wetu, Yeye aketiye kwenye kiti cha enzi na Mwana-Kondoo'@ (Ufunuo 7:9-10). Hii ndiyo siku ambayo ujumbe wa injili unatuelekeza. Hata kama tunapitia katika majaribu na mateso ya ulimwengu huu, ujumbe wa injili unatuelekeza mbinguni ambapo Bwana Yesu Kristo Mwana-Kondoo wa Mungu ambaye alisulibiwa kwa ajili yetu na alifufuka kutoka kwa wafu na sasa ameketi mkuu wa kuume wa Mungu akituombea. Ujumbe huu unatuelekeza kwa siku ile ambapo mamilioni ya watu watakuwa wakimwabudu Mwokozi na Mfalme ambaye ni Yesu Kristo.