walimu wa neno la mungu - wordpress.com · kuandaa ujumbe huu maalumu kwa walimu wa neno la mungu...

13
WALIMU WA NENO LA MUNGU: MAMBO MUHIMU UNAPOANDAA SOMO/UJUMBE WA KUFUNDISHA Mwl. Daudi, JL VIJANA NA UTUMISHI

Upload: others

Post on 26-Jul-2020

107 views

Category:

Documents


8 download

TRANSCRIPT

Page 1: WALIMU WA NENO LA MUNGU - WordPress.com · kuandaa ujumbe huu maalumu kwa walimu wa Neno la Mungu pia hata kwa mwamini yeyote ili kufahamishana mambo muhimu unapoandika somo/ujumbe

WALIMU WA NENO LA MUNGU:

MAMBO MUHIMU

UNAPOANDAA

SOMO/UJUMBE

WA

KUFUNDISHA

Mwl. Daudi, JL

VIJANA NA UTUMISHI

Page 2: WALIMU WA NENO LA MUNGU - WordPress.com · kuandaa ujumbe huu maalumu kwa walimu wa Neno la Mungu pia hata kwa mwamini yeyote ili kufahamishana mambo muhimu unapoandika somo/ujumbe

Uk | i

SHUKRANI

Kipekee kabisa, namshukuru Mungu kunitia nguvu kuandika somo hili la kujifunza mambo kadhaa wa kadhaa tunapoandaa somo/ujumbe wa kufundisha. Sifa na utukufu kwa Bwana Yesu Kristo.

Sikuwahi kuwa na wazo kuandika haya yote niliyoandika. Nilipata somo hili baada ya kupangwa kuhudumu katika ibada ya vijana ninapoabudu katika kanisa la Pentecostal Assemblies of God [PAG] KAWE. Mungu ambariki sana mwenyekiti wangu wa vijana Peter M Mabula na vijana wote wa PAG-KAWE. Pia namshukuru sana Mchungaji wangu Elly Botto kunilea kiroho hata sasa.

Pia Mungu akubariki sana wewe ambae utasoma somo hili mpaka mwisho, naamini yako mambo kadhaa ambayo utajifunza. Usisahau kumshirikisha na mwingine Baraka hii ili tuzidi kujenga mwili wa Kristo.

-Mwl. Daudi, JL.

Page 3: WALIMU WA NENO LA MUNGU - WordPress.com · kuandaa ujumbe huu maalumu kwa walimu wa Neno la Mungu pia hata kwa mwamini yeyote ili kufahamishana mambo muhimu unapoandika somo/ujumbe

Uk | ii

UTANGULIZI.

Haleluya! Bwana Yesu asifiwe mtoto wa Mungu. Namshukuru Mungu kwa neema hii ya kuandaa ujumbe huu maalumu kwa walimu wa Neno la Mungu pia hata kwa mwamini yeyote ili kufahamishana mambo muhimu unapoandika somo/ujumbe wa kufundisha. Mtume Paulo katika 1 Wakorintho 8:2 anasema “Mtu akidhani ya kuwa anajua neno, hajui neno lo lote bado, kama impasavyo kujua”. Hakuna mwisho wa kujifunza bali kila siku tunaendelea kujifunza. Maana yangu ni hii, hata kama unajua kuandaa somo/ujumbe ila bado katika haya nitakayozungumza hapa utajifunza jambo fulani la kukusaidia.

Page 4: WALIMU WA NENO LA MUNGU - WordPress.com · kuandaa ujumbe huu maalumu kwa walimu wa Neno la Mungu pia hata kwa mwamini yeyote ili kufahamishana mambo muhimu unapoandika somo/ujumbe

Uk | iii

YALIYOMO

SHUKRANI……………………………………………………………………………...…………..i

UTANGULIZI…………………………………………………………………………...………….ii

USIACHE KUANDIKA!……………………………………………………………….……………1

HATUA ZA KUFUATA UNAPOANDIKA SOMO/UJUMBE……………………………...…………..2

MWISHO………………………………………………………………………………….......……7

Page 5: WALIMU WA NENO LA MUNGU - WordPress.com · kuandaa ujumbe huu maalumu kwa walimu wa Neno la Mungu pia hata kwa mwamini yeyote ili kufahamishana mambo muhimu unapoandika somo/ujumbe

VIJANA NA UTUMISHI

#Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk | 1

Na: Mwl. Daudi, JL

USIACHE KUANDIKA!

Kabla hatujaona hayo mambo muhimu unapoandika somo/ujumbe wa kufundisha, Natamani ujue kuwa “Mungu anataka tuwe na tabia ya kuandika, Hivyo USIACHE KUANDIKA!”. Wengi tuliookoka hatuna tabia ya kuandika vitu ambavyo Mungu anatufunulia katika maisha yetu badala yake tunasema viko moyoni siwezi kusahau nakumbuka tu!. Mungu akikupa maono, ujumbe, au jambo lolote ukaliona katika ulimwengu wa roho LIANDIKE! Usiseme sitasahau. Maandiko yenyewe ukisoma yanaonyesha hata Mungu wetu HUANDIKA; Ukimpokea Yesu katika maisha yako, Jina lako Mungu huandika katika kitabu cha uzima.

Habakuki 2:2 “Bwana akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apaye kuisoma kama maji”. Sehemu ya jibu la Mungu kwa Habakuki lilikuwa IANDIKE NJOZI. Angalia! Bwana Mungu anataka tuwe na nidhamu ya kuandika, kama Habakuki alivyoambiwa Hata sisi tunapata ujumbe uleule Tuandike njozi zetu. Ngoja nikupeleke andiko lingine uweze kuona tena,

Ufunuo wa Yohana 1:11 “………Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba………..”. Bwana Yesu mwenyewe anamwambia mtume Yohana kuwa HAYA UYAONAYO UYAANDIKE, Sikiliza! Lichukue andiko hili kwako uwe ni wewe unaambiwa Haya uyaonayo uyaandike, je! utachukua hatua ya kuanza kuandika hayo Bwana Yesu anakuonesha katika maisha yako?. Baraka zetu ziko rohoni zote Mungu amekwisha kutubariki tayari[Waefeso 1:3], na tunaanza kuziona kwa macho ya rohoni kwanza maana Bwana Yesu anatuonesha, Sasa ninachokikazia hapa ni kwamba UKIONA ANDIKA!. Mungu atakupa somo/ujumbe iwe kwa ajiri yako au wengine, jambo la muhimu kabisa baada ya kupewa somo/ujumbe ANDIKA. Mungu anataka tusiache kuandika, kila mwamini awe na nidhamu ya kuandika.

Jenga nidhamu ya kuandika kuanzia sasa Hujachelewa mtoto wa Mungu, nunua notebook au diary na peni yako. Usiende kanisani bila notebook na peni yako. Sikiliza! Kuwa na nidhamu ya kuandika kwa mwalimu wa Neno la Mungu ni muhimu zaidi sana tena sana. Nimezungumzia jambo hili USIACHE KUANDIKA kwasababu hatuishii tu kusema sitasahau mbona nakumbuka.

Page 6: WALIMU WA NENO LA MUNGU - WordPress.com · kuandaa ujumbe huu maalumu kwa walimu wa Neno la Mungu pia hata kwa mwamini yeyote ili kufahamishana mambo muhimu unapoandika somo/ujumbe

VIJANA NA UTUMISHI

#Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk | 2

HATUA ZA KUFUATA UNAPOANDIKA SOMO/UJUMBE.

Unapoandika somo/ujumbe wako wa kufundisha ziko hatua kadhaa za kupitia. Nimegawanya hatua hizi sehemu tatu. Kila hatua ndani yake yako mambo muhimu ya kujua unapoandika somo/ujumbe wako. Hebu tuone sasa hatua hizo;

1. FANYA MAOMBI KWANZA KABLA YA KUANDIKA SOMO/UJUMBE WAKO

Kabla hujaanza kuandika somo/ujumbe anza na maombi kwanza. Mkaribishe Roho Mtakatifu. Ziko sababu lukuki za kukutaka uanze na maombi kwanza. Nikukumbushe tu kuwa somo utakaloandika ni Mungu amekufundisha wewe, amekupa wewe ufunuo wa somo hilo Hujajipa wewe wala kujitungia kwa akili zako, Hivyo ni muhimu ufanye maombi kwanza ili katika safari yako ya kuandika huo ujumbe Bwana Yesu awe na wewe!. Hebu tuone maandiko yafuatayo

Wakolosai 3:17 inasema “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu………..”. Kila tufanyalo ikiwemo na kuandaa au kuandika ujumbe, tunafanya kwa jina la Bwana Yesu. Tunapofanya maombi kwa lugha rahisi kabisa tunafanya hilo jambo kwa jina la Bwana Yesu. Hii ni sababu kubwa kabisa kwanini tuanze na maombi kwanza kabla ya kuandika somo/ujumbe. Mambo yote ikiwemo na kuandika ujumbe tunaanza na maombi.

Pia katika 2 Petro 1:21 inasema “Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu”. Unapoandika somo/ujumbe Mungu aliokupa jua kabisa hayo unayoandika yametoka kwa Mungu huku Roho Mtakatifu akikuongoza ni nini uandike. Kumbuka hauandiki mapenzi, mawazo au hekima yako kama unavyoona wewe, Neno la Mungu linasema “ Kwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, Na akili zao wenye akili nitazikataa” (1 Wakorintho 19). Tunapaswa kujua unapoanza na maombi unajiweka chini ya uongozi wa Roho ya Mtakatifu ili ujumbe wako Mungu aandike na wewe maana huandiki ya kwako.

2. BAADA YA MAOMBI, ANZA KUANDIKA SOMO/UJUMBE WAKO.

Kuna miundo [structures] kadhaa wa kadhaa ya kuandika somo lako. Katika miundo yote kuna mtiririko wa kufuata unapoandika somo lako. Ujumbe wako ni lazima uwe na mpangilio, hii itakusaidia wakati unafundisha usiweze kujichanganya.

Page 7: WALIMU WA NENO LA MUNGU - WordPress.com · kuandaa ujumbe huu maalumu kwa walimu wa Neno la Mungu pia hata kwa mwamini yeyote ili kufahamishana mambo muhimu unapoandika somo/ujumbe

VIJANA NA UTUMISHI

#Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk | 3

Yako mambo matano (5) katika muundo wowote ambayo ni muhimu kuzingatia unapoandika somo lako. Unapoandika ujumbe wako, baada ya kumaliza hatua ya kwanza ya maombi, ufuatao ni mtiririko/mpangilio mzuri unaoweza kuufuata;

I. KICHWA CHA SOMO/UJUMBE WAKO.

Hakuna ujumbe usio na kichwa yaani “Title” yake. Kichwa cha somo/ujumbe hutoa picha ya nje ya haraka kwa msikiaji kuelewa hata kabla hujaanza kuzungumza yaliyo ndani kabisa.

Kuna aina mbili za kichwa cha somo/ujumbe;

a) General title. Hiki ni kichwa cha somo kilicho jumla sana kwa maana ya kwamba mwanafunzi hatajua ni wapi somo lako litaegemea. Mfano; Kichwa cha somo ni MAOMBI, kwa haraka mwanafunzi hatajua utafundisha maana ya Maombi tu au utafundisha faida za Maombi n.k. Nasema hivi kwa sababu ndani ya Maombi yako mengi ambayo utaweza kufundisha.

b) Specific title. Hiki ni kichwa cha somo kilicho wazi zaidi au bayana kwa kulenga moja kwa moja ujumbe utakaofundisha. Mwanafunzi anajua dhahiri anachokwenda kujifunza. Mfano; Kichwa cha somo ni FAIDA ZA MAOMBI. Hapa kama Mwalimu wa Neno la Mungu utalenga moja kwa moja faida za Maombi.

Unapochagua kicha cha somo lako zingatia mambo yafuatayo;

i. Kiwe kifupi na kueleweka. Kichwa cha somo kisiwe na maneno mengi, mfano; “faida kumi za maombi kwa mwamini maana ni muhimu kudumu katika Maombi”, Hapa kuna maneno yasiyo lazima sana kuweka, fupisha andika “faida kumi za Maombi”.

II. MAANDIKO YA NENO LA MUNGU.

Somo lako lazima liambatane na Neno la Mungu. Mwalimu wa Neno la Mungu huwezi kufundisha mpaka unamaliza somo/ujumbe wako hujasema andiko hata moja!. 1 Wakorintho 15: 3 inasema “Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko”, Unaona andiko hili linachofunua? Mtume Paulo anaposema “…..naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea….” Kwa lugha rahisi anamaanisha kwamba “niliwafundisha ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea” na alichofundisha Mtume Paulo anasema ni “…kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu”, Angalia! Hii ndo ilikuwa kichwa cha ujumbe wake!. Sasa angalia alivyomaliza kusema “……….KAMA YANENAVYO MAANDIKO”, Hapa ndo nilitaka uone, alifundisha kama

Page 8: WALIMU WA NENO LA MUNGU - WordPress.com · kuandaa ujumbe huu maalumu kwa walimu wa Neno la Mungu pia hata kwa mwamini yeyote ili kufahamishana mambo muhimu unapoandika somo/ujumbe

VIJANA NA UTUMISHI

#Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk | 4

maandiko yanavyosema. Sikiliza! Neno la Mungu ndo msingi wa Somo/ujumbe wako. Fundisha somo lako vizuri ila kumbuka iwe kama yanenavyo maandiko. Najua Mwalimu wa Neno la Mungu hupokea mafunuo mengi kutoka kwa Mungu ili kufundisha kanisa la Mungu ila usisahau kuchuja mafunuo yako na Neno la Mungu upate uhakika na sio kupoteza kanisa.

Kipengele hiki ni muhimu sana unapoandika somo/ujumbe wako. Maandiko yamegawanyika sehemu mbili kubwa;

a) Andiko kuu [Main scriptural verses]. Hili ni andiko la msingi lililobeba ujumbe wote unaofundisha. Mara nyingi, kwa mara ya kwanza unapopokea ujumbe kwa Mungu huambatana na andiko fulani, andiko hili huwa ndo andiko kuu linaliloweka msingi wa somo/ujumbe wako. Andiko kuu huweza kuwa zaidi ya moja ila huwa si mengi sana. Mfano; Kama unafundisha kuhusu IMANI andiko kuu huweza kuwa Waebrania 11:1 “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana:

b) Andiko la ziada [Supportive/auxiliary scriptural verses]. Maandiko ya ziada hutoa ufafanuzi wa nyongeza katika ujumbe wako. Kuna wakati Yesu akasema hivi “………chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike (Mathayo 18:16). Si vema sana kutumia andiko kuu moja tu kama msingi wa ujumbe wako, ni vizuri zaidi kuwa na maandiko ya ziada kadhaa ili somo lako lithibitike. Neno la Mungu linaposema “…..kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike” pia tunapata picha hata katika kuandaa ujumbe/somo lako maandiko zaidi ya wawili au matatu ni muhimu ili kuthibitisha ujumbe wako.

III. UTANGULIZI

Somo lako likikosa kipengele hiki cha utangulizi, kuna hatari ya kuanza kufundisha ujumbe wako kwa mpangalio ambao hukukusudia na ukapoteza maana ya ujumbe wako kwa kuwachanganya wanafunzi. Kuandika namna utangulizi wako utakavyokuwa ni hatua muhimu sana ili somo/ujumbe wako ufike kama Mungu alivyokusudia.

Utangulizi wako unaweza kuanza kwa njia zifuatazo;

i. Mifano ii. Shuhuda

Page 9: WALIMU WA NENO LA MUNGU - WordPress.com · kuandaa ujumbe huu maalumu kwa walimu wa Neno la Mungu pia hata kwa mwamini yeyote ili kufahamishana mambo muhimu unapoandika somo/ujumbe

VIJANA NA UTUMISHI

#Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk | 5

iii. Ufafanuzi wa kichwa cha somo iv. Swali v. Stori fupi.

Andika utangulizi wako vizuri unapoandaa ujumbe wako, usikurupuke unapokuwa madhabahuni.

IV. KIINI CHA SOMO/UJUMBE WAKO

Haleluya! Hapa ndio sehemu ya kufundisha ujumbe wako sasa, andika vizuri kabisa namna utakavyofafanua ujumbe wako. Kama somo lako ni FAIDA ZA MAOMBI elezea kwa mapana hizo faida za maombi katika eneo hili la kiini cha ujumbe. Kwahiyo kiini cha ujumbe wako ni;

i. Uwanja wa kueleza somo/ujumbe Mungu aliokupa ii. Sehemu pekee unayofafanua na kueleza kwa mapana somo lako

Jambo la muhimu katika kipengele hiki unapoandaa ujumbe wako ni kuwa andika bila kuacha vitu vyote ambavyo Mungu anaweka msukumo ndani yako wa kuvieleza.

V. HITIMISHO.

Kipengele hiki kinakupa nafasi ya kuandika namna utakavyohitimisha ujumbe wako. Ukihitimisha vibaya wakati unafundisha ujumbe wako unaweza usilete matokeo Mungu aliyokusudia, Hivyo inakupasa kuandika hitimisho lako wakati unaaandika ujumbe wako. Wewe kama Mwalimu wa Neno la Mungu usiseme nitajua palepale nikiwa madhabahuni, hayo ni makosa. Andaa na andika mapema wakati unaandika ujumbe wako utahitimishaje.

Kuna njia nyingi za kuhitimisha ujumbe wako, baadhi ya hizo ni hizi zifuatazo;

i. Toa majumuisho [giving summarization] ya somo/ujumbe wako ukirudia ka kukazia zile sehemu [points] muhimu zilizokuwa kiini cha somo lako.

ii. Toa swali/maswali kwa wanafunzi iii. Karibisha swali/maswali kutoka kwa wanafunzi. Ukisoma Mathayo 24: 3 “Hata

alipokuwa ameketi katika mlima wa mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia?”. Hata Yesu Kristo kama Mwalimu aliruhusu maswali wanafunzi wake waulize, hata wewe unapohitimisha unaweza kutoa nafasi ya wanafunzi kuuliza maswali.

Page 10: WALIMU WA NENO LA MUNGU - WordPress.com · kuandaa ujumbe huu maalumu kwa walimu wa Neno la Mungu pia hata kwa mwamini yeyote ili kufahamishana mambo muhimu unapoandika somo/ujumbe

VIJANA NA UTUMISHI

#Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk | 6

iv. Kama somo linaendelea, hitimisha kwa kutoa maelezo kwa kifupi kipande kinachofuata cha somo lako.

v. Maombi

Kumbuka! Njia utakayotumia kuhitimisha unaiandika wakati unaandika somo lako.

3. BAADA YA KUMALIZA KUANDIKA SOMO/UJUMBE WAKO MSHUKURU MUNGU KWA MAOMBI.

Baada tu ya kumaliza kuandika ujumbe wako, usifunike notebook au diary yako tu basi ukisuburi kusimama madhabahuni, bali mshukuru Mungu kwa Maombi. Wafilipi 4:6 “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru…………..”, Sikiliza! Usianze kupatwa na woga itakuwaje utakaposimama madhabahuni; bali wewe mshukuru Mungu kwa ujumbe aliokupa na umeweza kuuandika vizuri. Usisahau hili, unapofanya Maombi ya kushukuru pia kabidhi ujumbe wako mikononi kwa Mungu.

Mambo mengine ya kuzingatia;

i. Ombea wanafunzi wako ili wakati unafundisha waweze kuelewa ii. Rudia kusoma ujumbe wako wote

iii. Endelea kuomba mpaka siku ya kusimama madhabahuni utakapofudhisha ujumbe wako.

Page 11: WALIMU WA NENO LA MUNGU - WordPress.com · kuandaa ujumbe huu maalumu kwa walimu wa Neno la Mungu pia hata kwa mwamini yeyote ili kufahamishana mambo muhimu unapoandika somo/ujumbe

VIJANA NA UTUMISHI

#Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk | 7

MWISHO………………

Page 12: WALIMU WA NENO LA MUNGU - WordPress.com · kuandaa ujumbe huu maalumu kwa walimu wa Neno la Mungu pia hata kwa mwamini yeyote ili kufahamishana mambo muhimu unapoandika somo/ujumbe

VIJANA NA UTUMISHI

#Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk | 8

KUHUSU MWL. DAUDI, JL

Mwl. Daudi, JL ni mwalimu wa Neno la Mungu na amekuwa akihubiri na kufanya semina sehemu mbalimbali Tanzania. Amewahi kufanya kazi pamoja na huduma ya vijana mashuleni inayoitwa CASFETA-TAYOMI. . Pia ameshiriki pamoja na CASFETA-TAYOMI kufanya huduma ya kufikia maeneo yasiyofikiwa na injili hasa vijijini ijulikanayo kama OUTREACH MISSION.Pia Mwl Lubeleje ameshiriki sana makongamano ya PASAKA yanayoandaliwa na wanafunzi mashuleni. Amehitimu shahada ya ualimu katika masomo ya Hesabu na Uchumi katika chuo kikuu cha Mzumbe Tanzania. VIJANA NA UTUMISHI ilianza Januari, 2015 mbebaji MAONO akiwa ni Mwl. Daudi, JL ikiwa na lengo la kutengeneza “UWANJA” au PLATFORM maalumu kwa vijana ili kutambua fursa zao za kumtumikia Mungu. Somo hili la “MAMBO MUHIMU UNAPOANDAA SOMO/UJUMBE WA KUFUNDISHA likupe hatua kubwa zaidi ya kukuchochea kufundisha Neno la Mungu, maana baada ya kusoma, ni IMANI yangu umejua vitu vipasavyo unapoandaa somo/ujumbe.

Kwa shuhuda na maoni yako, unaweza kuwasiliana kwa namba +255(0) 764 771 298 au kwa baruapepe [email protected]. Pia tembelea blog ya VIJANA NA UTUMISHI kupitia vijananautumishi.wordpress.com.

Kama unataka kufanya kazi pamoja na VIJANA NA UTUMISHI, una masomo yako yawekwe mtandaoni au kuchapishwa kwenye e-kitabu karibu pia, tumia mawasiliano hapo juu.

Page 13: WALIMU WA NENO LA MUNGU - WordPress.com · kuandaa ujumbe huu maalumu kwa walimu wa Neno la Mungu pia hata kwa mwamini yeyote ili kufahamishana mambo muhimu unapoandika somo/ujumbe

VIJANA NA UTUMISHI

#Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk | 9

JIPATIE e-kitabu cha kwanza kabisa toka VIJANA NA UTUMISHI kinachoitwa JIFUNZE UKUE

KIROHO chenye mkusanyiko wa masomo toka kwa watumishi wa Mungu mbalimbali akiwemo Mwl. Conrad Conwell, Peter M Mabula na wengine wengi.

Kupata e-kitabu tembelea blogu ya VIJANA NA UTUMISHI na uweze kukipakua. Mungu akubariki sana.