neno la uzima

19
NENO LA UZIMA Mei 2012

Upload: flint

Post on 10-Jan-2016

79 views

Category:

Documents


3 download

DESCRIPTION

NENO LA UZIMA. Mei 2012. "Nimekuja kuwasha moto duniani; na ukiwa umekwisha washwa, ni nini nitakalo zaidi!” (Lk 12:49). Katika maandishi ya kiyahudi moto unaashiria neno la Mungu lililotamkwa na nabii. Lakini pia linaashiria hukumu ya Mungu anayetakasa watu wake kwa kupita kati yao. - PowerPoint PPT Presentation

TRANSCRIPT

Page 1: NENO LA UZIMA

NENO LA UZIMA NENO LA UZIMA

Mei 2012Mei 2012

Page 2: NENO LA UZIMA

"Nimekuja kuwasha moto duniani; na ukiwa umekwisha washwa, ni nini nitakalo zaidi!”

(Lk 12:49).

Page 3: NENO LA UZIMA

Katika maandishi ya kiyahudi moto

unaashiria neno la Mungu

lililotamkwa na nabii. Lakini pia

linaashiria hukumu ya

Mungu anayetakasa

watu wake kwa kupita kati

yao..

Page 4: NENO LA UZIMA

Tunaweza kusema hivyo kwa neno la Yesu: linajenga, na kwa wakati huo huo linabomoa kila kisicho thabiti, kila kinachotakiwa kushuka, kila kilicho batili, na kuacha tu

ukweli ukisimama.

Page 5: NENO LA UZIMA

Yohani Mbatizaji alisema:

“Atawabatizeni kwa Roho

Mtakatifu na moto” (Lk 3:16), akitabiri ubatizo

wa Kikristo uliozinduliwa siku

ya Pentekoste kwa kushuka

Roho Mtakatifu na kuonekana

ndimi za moto (rej Mdo 2:3).

Page 6: NENO LA UZIMA

Hii ni kazi maalum ya

Yesu: kuwasha moto duniani, kuleta Roho Mtakatifu na

nguvu zake za kufanya upya na

kutakasa.Huo ndio utume wa Yesu: kutupa

moto duniani, kuleta Roho Mtakatifu pamoja na

nguvu yake ya kufanya yote upya na ya kutakasa.

Page 7: NENO LA UZIMA

"Nimekuja kuwasha moto duniani; na ukiwa umekwisha washwa, ni nini nitakalo zaidi!”

(Lk 12:49).

Page 8: NENO LA UZIMA

Yesu anatupatia Roho. Lakini Roho Mtakatifu anafanyaje kazi?

Page 9: NENO LA UZIMA

Anatujaza upendo na anataka tutunze moto huu wa upendo ukiwaka mioyoni mwetu.

Page 10: NENO LA UZIMA

Je, ni aina gani ya upendo? Si wa kiulimwengu, upendo usio na kikomo. Ni upendo wa kiinjili.

Unaopenda wote kama Baba wa mbinguni anayewaangazia jua lake waovu na wema na

kuwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki, wakiwemo adui (rej Mt 5:45).

Page 11: NENO LA UZIMA

Ni upendo usiosubiri wengine wachukue hatua ya kwanza, bali unakuwa daima

wa kwanza kupenda.

Page 12: NENO LA UZIMA

Ni upendo unaojifanya mmoja na kila mmoja: unateseka na kufurahi pamoja nao, ukishiriki hofu na matumaini

yao. Na ikibidi, unagusika, kwa matendo. Kwa hiyo siyo tu upendo wa kihisia unaoelezwa kwa maneno matupu.

Page 13: NENO LA UZIMA

Ni upendo unaoongozwa na Kristo ndani ya jirani, kwa kuzingatia maneno yake: ‘Ulinitendea mimi” (Mt

25:40).Ni upendo unaopelekea upendano.

Page 14: NENO LA UZIMA

Kwa kuwa upendo huu unaonekana, ni udhihirisho wa maisha yetu ya kiinjili, unasisitiza na kushuhudia neno

- ushuhuda tunaoweza na tunaotakiwa kutoa ili kuinjilisha.

Page 15: NENO LA UZIMA

"Nimekuja kuwasha moto duniani; na ukiwa umekwisha washwa, ni nini nitakalo zaidi!”

(Lk 12:49).

Page 16: NENO LA UZIMA

Upendo ni kama moto – cha muhimu ni kuutunza.

Page 17: NENO LA UZIMA

Na moto lazima uunguze kitu daima. Na zaidi ya yote lazima uunguze ubinafsi wetu, na

unafanikiwa kwa kuwa kwa kupenda tunaelekea nje yetu: aidha kuelekea Mungu kwa kufanya

mapenzi yake, au jirani kwa kuwasaidia.

Page 18: NENO LA UZIMA

Hata moto mdogo, ukiwashwa unaweza kuwa mlipuko – ule mlipuko wa upendo, amani na

undugu wa wote ambao Yesu alileta duniani.

Page 19: NENO LA UZIMA

"Nimekuja kuwasha moto duniani; na ukiwa umekwisha washwa, ni nini nitakalo zaidi!”

(Lk 12:49).