neno la uzima

28

Click here to load reader

Upload: sera

Post on 09-Jan-2016

124 views

Category:

Documents


33 download

DESCRIPTION

Neno la Uzima. Februari 2013. Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. (1Yh 3:14). Yohane anaandikia jumuia za kikristo alizozianzisha kipindi ambapo zinapitia wakati mgumu. - PowerPoint PPT Presentation

TRANSCRIPT

Page 1: Neno  la  Uzima

Neno la

Uzima

Februari2013

Page 2: Neno  la  Uzima

Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. (1Yh 3:14)

Page 3: Neno  la  Uzima

Yohane anaandikia jumuia za kikristo

alizozianzisha kipindi ambapo zinapitia wakati

mgumu.

Yohane anaandikia jumuia za kikristo

alizozianzisha kipindi ambapo zinapitia wakati

mgumu.

Page 4: Neno  la  Uzima

Mafundisho ya uongo kuhusu imani na maadili yalikuwa yanaanza kuenea, na jamii ya kipagani ambamo wakristo waliishi ilikuwa kati na adui kwa roho

ya Injili.

Page 5: Neno  la  Uzima

Ili kuwasaidia, mtume anaonyesha njia ya pekee: kumpenda ndugu, kuishi sheria ya upendo waliyoipata tangu mwanzoni ambayo, anaona kama

mhutasari wa amri zingine zote.

Page 6: Neno  la  Uzima

Kwa kufanya hivyo watajua ‘maisha’ ni nini. Wataongozwa, yaani kwa undani zaidi na zaidi

katika ushirika na Mungu na watang’amua Mungu-upendo. Na kwa kuwa na mang’amuzi hayo, watathibitishwa katika

imani na kuweza kukabiliana na kila shambulizi, na hasa katika

nyakati za hatari.

Page 7: Neno  la  Uzima

Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. (1Yh 3:14)

Page 8: Neno  la  Uzima

Tunajua...’ Mtume anamaanisha ujuzi utokanao

na mang’amuzi. Ni kama kusema: ‘tumeng’amua,

‘tumegusa kwa mkono wetu’.

Page 9: Neno  la  Uzima

Ni mang’amuzi ambayo wakristo walioinjilishwa na Yohane walifanya tangu mwanzoni mwa uongofu wao.

Tunapoweka katika matendo amri za Mungu, kwa namna ya pekee

amri ya upendo kwa jirani, tunaingia katika maisha ya Mungu.

Page 10: Neno  la  Uzima

Lakini je, wakristo wa leo wanafahamu mang’amuzi haya? Bila shaka wanajua kuwa amri za Mungu zina lengo maalum. Yesu

daima anasisitiza kuwa haitoshi kusikiliza Neno la Mungu; sharti kuliishi (taz. Mt. 5:19; 7:21; 7:26).

Page 11: Neno  la  Uzima

Baadala yake, kisicho dhahiri zaidi kwa wengi, aidha kwa kuwa

hawajui au wana ujuzi wa kinadharia tu bila kuwa na

mang’amuzi, ni uzuri wa maisha ya kikristo ambayo mtume

anayadhihirisha. Tunapoishi amri ya upendo, Mungu anatuchukua, na ishara isiyokosewa ya hili ni ile amani, ile furaha anayotujalia

kuonja tayari hapa duniani.

Page 12: Neno  la  Uzima

Hapo kila kitu kinaangazwa, kila kitu kinakuwa katika ulinganifu. Hakuna tena tofauti kati ya imani na maisha. Imani inakuwa ile nguvu

inayoingiana na kuunganisha matendo yetu yote.

Page 13: Neno  la  Uzima

Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. (1Yh 3:14)

Page 14: Neno  la  Uzima

Hilo Neno la Uzima linatuambia kuwa upendo kwa jirani ni njia ya kifalme inayotuongoza kwa Mungu

Page 15: Neno  la  Uzima

Kwa kuwa sote ni watoto wake, hakuna kilicho cha muhimu kwake zaidi ya upendo kwa jirani yetu. Hatuwezi kumpa furaha kubwa zaidi kuliko

tunapompenda jirani yetu.

Page 16: Neno  la  Uzima

Na kwa kuwa upendo kwa jirani unaleta ushirika na Mungu, ni chemchemi isiyokauka ya mwanga wa ndani, ni kisima cha maisha, cha

matunda ya kiroho, cha upyayusho endelevu.

Page 17: Neno  la  Uzima

Ni kinga dhidi ya uozo, ugumu, ulegevu ambavyo vinaweza kujikita kati ya wakristo; kwa neno moja inatutoa katika mauti kuingia uzimani’.

Page 18: Neno  la  Uzima

Kinyume chake, upendo ukikosekana, kila kitu kinanyauka na kufa. Tukijua hili tunaelewa kwa nini mitazamo mingine imeenea katika ulimwengu wa sasa: kutokuwa na ari na upeo, udhaifu, kukereka, kutamani kutoroka,

mmomonyoko wa maadili, n.k.

Page 19: Neno  la  Uzima

Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. (1Yh 3:14)

Page 20: Neno  la  Uzima

Ndugu ambao mtume anamaanisha, awali ya yote ni wanajamii yetu. Kama ni

kweli kuwa tunatakiwa kuwapenda wote, ni kweli

pia kuwa upendo wetu unatakiwa kuanzia kwa wale

tunaoishi nao, halafu utaenea katika ulimwengu

wote.

Page 21: Neno  la  Uzima

Tunatakiwa kufikiria kwanza wanafamilia yetu, wafanyakazi wenzetu, wanaparokia yetu, jumuiya yetu au shirika letu la kitawa.

Page 22: Neno  la  Uzima

Upendo wetu kwa jirani hautakuwa halisi na wenye muelekeo sahihi kama hautaanzia hapa. Popote tunapojikuta, tunaitwa kujenga familia ya

wana wa Mungu.

Page 23: Neno  la  Uzima

Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. (1Yh 3:14)

Page 24: Neno  la  Uzima

Neno hili la Uzima linafungua mtazamo mpana sana.

Page 25: Neno  la  Uzima

Linatuhimiza katika safari ya kimungu yenye matokeo yasiyotabirika. Zaidi ya yote linatukumbusha kuwa katika ulimwengu kama wetu, wenye

nadharia ya ushindani, ambamo anayeishi ni mwenye nguvu, mjanja, asiye mnyofu, na wakati mwingine kila kitu kinaonekana kama kimekufa ganzi kutokana na tamaa ya kumiliki vitu na ubinafsi, jibu letu linatakiwa kuwa

upendo kwa jirani.

Page 26: Neno  la  Uzima

Hii ndiyo dawa inayoweza kuuponyesha ulimwengu. Hakika, tunapoishi amri ya upendo, si tu maisha yetu

yanatiwa nguvu, bali, kila kitu kinachotuzunguka kinaguswa.

Ni kama wimbi la joto la kimungu, linaloenea na kukua,

likipenya mahusiano ya mtu mmoja na mwingine, kundi moja na lingine, na kidogo

kidogo kubadili jamii.

Page 27: Neno  la  Uzima

Kwa hiyo tuamue sasa! Ndugu wa kuwapenda kwa jina la Yesu, tunao sote, na tutakua nao daima. Hebu tuwe waaminifu kwa upendo huu.

Hebu tuwasaidie wengine kuwa hivi. Tutaelewa mioyoni mwetu maana ya ushirika na Mungu. Imani itastawi, mashaka yatatoweka, hakutakuwa

tena na kukerwa. Maisha yatajaa sana.

Page 28: Neno  la  Uzima

““Parola di Vita” inatangazwa na Movement of Focolare.Matini hii Imetolewa katika Città Nuova n. 9/1985

Chapa cha Anna Lollo akishirikiana na Fr. Placido D’Omina (Sicily, Italy).Maelezo ya Neno la Uzima inatafsiriwa katika lugha 96 na kilugha

na kuwafikia mamilioni ya watu katika dunia nzimakwa njia ya maandishi, radio, TV na kwa njia ya Tovuti.

Kwa kupata maelezo www.focolare.orgPPS hiyo, katika lugha mbalimbali inatangazwa katika

www.santuariosancalogero.it(na hapo unaweza kupakua)

““Parola di Vita” inatangazwa na Movement of Focolare.Matini hii Imetolewa katika Città Nuova n. 9/1985

Chapa cha Anna Lollo akishirikiana na Fr. Placido D’Omina (Sicily, Italy).Maelezo ya Neno la Uzima inatafsiriwa katika lugha 96 na kilugha

na kuwafikia mamilioni ya watu katika dunia nzimakwa njia ya maandishi, radio, TV na kwa njia ya Tovuti.

Kwa kupata maelezo www.focolare.orgPPS hiyo, katika lugha mbalimbali inatangazwa katika

www.santuariosancalogero.it(na hapo unaweza kupakua)

Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. (1Yh 3:14)