qasida ya kumsifu mtume - allamah rizvi · pdf fileallamah sayyid saeed akhtar rizvi tafsiri...

13
QASIDA YA KUMSIFU MTUME (S.A.W.W.) NA AHLUL ~ BAYT WAKE (A.S.) Na: Sheikh Abdullah Saleh al-Farsi Tafsiri na Maelezo kwa Kiingereza Na: Rai’sul~Mubaligheen Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi Tafsiri kwa Kiswahili Na: Dr. Mohamed Kanju Kimetolewa na Kuchapishwa na: BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA S.L.P. 20033 DAR ES SALAAM TANZANIA www.allamahrizvi.com

Upload: vuongthu

Post on 12-Feb-2018

405 views

Category:

Documents


48 download

TRANSCRIPT

Page 1: QASIDA YA KUMSIFU MTUME - Allamah Rizvi · PDF fileAllamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi Tafsiri kwa Kiswahili Na: Dr. Mohamed Kanju Kimetolewa na Kuchapishwa na: BILAL MUSLIM MISSION

QASIDA YA KUMSIFU MTUME (S.A.W.W.) NA AHLUL ~ BAYT WAKE

(A.S.)

Na: Sheikh Abdullah Saleh al-Farsi

Tafsiri na Maelezo kwa Kiingereza Na: Rai’sul~Mubaligheen

Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi

Tafsiri kwa Kiswahili Na: Dr. Mohamed Kanju

Kimetolewa na Kuchapishwa na:

BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA

S.L.P. 20033 DAR ES SALAAM

TANZANIA

www.allamahrizvi.com

Page 2: QASIDA YA KUMSIFU MTUME - Allamah Rizvi · PDF fileAllamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi Tafsiri kwa Kiswahili Na: Dr. Mohamed Kanju Kimetolewa na Kuchapishwa na: BILAL MUSLIM MISSION

Haki ya kunakili imehifadhiwa na: Bilal Muslim Mission of Tanzania

ISBN 9987 620 30 2

Toleo la kwanza: Rabiul Awwal, 1423 / Mei, 2003 Idadi: Nakala 2000

kimechapishwa na Kimetolewa na:

BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA

S.L.P. 20033 DAR ES SALAAM

TANZANIA

www.allamahrizvi.com

Page 3: QASIDA YA KUMSIFU MTUME - Allamah Rizvi · PDF fileAllamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi Tafsiri kwa Kiswahili Na: Dr. Mohamed Kanju Kimetolewa na Kuchapishwa na: BILAL MUSLIM MISSION

YALIYOMO 1. Dibaji ................................................................................... 2. Utangulizi ............................................................................. 3. Barua ya Kiarabu ................................................................ 4. Qasida ya Kiarabu ............................................................... 5. Tafsiri ya barua ya kuambatanisha ........................................ 6. Tafsiri ya Qasida ya kumsifu Mtume (s.a.w.w.) na

Ahlul ~ Bayt wake (a.s.) ..........................................

www.allamahrizvi.com

Page 4: QASIDA YA KUMSIFU MTUME - Allamah Rizvi · PDF fileAllamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi Tafsiri kwa Kiswahili Na: Dr. Mohamed Kanju Kimetolewa na Kuchapishwa na: BILAL MUSLIM MISSION

DIBAJI

Tunamshukuru Allah (s.w.t.) na kwa baraka za Mtukufu

Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul~Bayt (a.s.) kwa kutujalia kuweza kufanikisha juhudi zetu hizi katika kuchapisha kitabu hiki “Qasida ya

Kumsifu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul~Bayt wake (a.s.)”. Maandishi haya yaliyopo mikononi mwako ni tafsiri ya barua

na qasida ya kiarabu iliyoandikwa na Marhum Sheikh Abdallah

Saleh al-Farsi aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar. Utasoma katika utangulizi wa Marhum Rais’ul~Mubaligheen

Ayatullah Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi ndani ya kitabu hiki

anaeleza kwamba mwaka wa 1975, Marhum Bwana Hussein

Allarakhya Rahim aliyekuwa Hakimu wa Zanzibar, alimpa kitabu

ambacho ndani yake maandishi haya yaliyoandikwa na Marhum Sheikh al-Farsi, Marhum Allamah Rizvi alichukua kitabu na

akakiweka ndani ya Maktaba yake “Kutub Khana Riyaz Ma’arif ” mji

wa Gopalpur, India.

Mwaka wa 1989 alitoa photocopy ya maandishi haya na

akaitafsiri kwa lugha ya Kiingreza na pia akaandika maelezo ili

maneno ya Shaikh al-Farsi na maana yake yaeleweke vizuri.

Mwaka wa1990 mwezi wa Decemba tafsiri ile ya Kiingreza na

maelezo pamojo na asili yake ya Kiarabu ili chapishwa ndani ya

gazeti la “The Light” na tafsiri ya Kiswahili kutoka Kiingreza

iliyotafsiriwa na Sheikh Dhikiri U.M. Kiondo ilichapishwa ndani ya

gazeti la “Sauti ya Bilal”.

Watu wengi wamependekeza kwamba qasida hiyo ichapwe

kama kijitabu, ushauri wao umezingatiwa na Dr. Muhammad Said

Kanju ameitafsiri tena kutoka katika lugha ya Kiingreza na kuiweka katika lugha ya Kiswahili na hivi sasa kitabu hiki tayari kipo

mikononi mwako.

www.allamahrizvi.com

Page 5: QASIDA YA KUMSIFU MTUME - Allamah Rizvi · PDF fileAllamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi Tafsiri kwa Kiswahili Na: Dr. Mohamed Kanju Kimetolewa na Kuchapishwa na: BILAL MUSLIM MISSION

Bilal Muslim Mission inatoa shukurani zake za dhati kwa wale

wote ambao kwa juhudu zao kitabu hiki kinawafikia wasomaji wetu mikononi na wale wote wanaotuunga mkono kwa njia moja au

nyingine katika uchapishaji wa kitabi hiki. Tunamuomba Allah

(s.w.t.) awalipe malipo mema hapa Duniani na ba’adaye huko,

Akhera.

9 Rabiul Awwal 1424 Sayyid Murtaza Rizvi 11 mei 2003 Bilal Muslim Mission

Dar es Salaam

www.allamahrizvi.com

Page 6: QASIDA YA KUMSIFU MTUME - Allamah Rizvi · PDF fileAllamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi Tafsiri kwa Kiswahili Na: Dr. Mohamed Kanju Kimetolewa na Kuchapishwa na: BILAL MUSLIM MISSION

UTANGULIZI Tunachapisha hapa (Qasida) wasifu wa Kiarabu wa Mtukufu Mtume na Ahlul~Bayt wake (Rehema na Amani na iwe juu yawo)

iliyoandikwa na Marehemu Sheikh Abdallah Saleh al-Farsi.

Ilitungwa katika mwaka 1380 Hijiriya sawa na mwaka 1961

Masihiya wakati alipokuwa Kadhi mkuu wa Zanzibar.

Marehemu Sheikh Abdallah Saleh al-Farsi aliwasilisha Kitabu cha ki-Arabu cha maisha ya “Al-Imam Ali bin Abu Talib,

Alayhissalamu” (toleo la Misri) kwa Marhum Al-Haj Hussein

Allarakhya Rahim, O.B.E., ambaye alikuwa ni Hakimu wa Zanzibar

na alikuwa akielewana naye sana. Sheikh alikipata kitabu hicho

kikiwa kimefumwa pamoja na makaratasi meupe mwanzoni. Kisha

alimpata mwandishi wa hati ambaye alinakili barua yake ya

kuambatanisha na qasida katika mwandiko mzuri wa mkono;

Sheikh alisaini barua ya kuambatanisha kwa wino wa bluu (huenda

ni kwa ballpen).

Kitabu ambacho kina maandishi haya kiliwasilishwa kwangu

miaka kumi na tano iliyopita na Marhum Husseni Allarakhya Rahim,

ambacho nilikwenda nacho India na kukiweka katika maktaba

yangu. Miaka miwili iliyopita nilikitoa kitabu hiki kutoka maktaba

yangu na nikayaona maandishi yale na nikataka kuyachapisha

katika jarida la Bilal Muslim Mission, The Light na Sauti ya Bilal.

Karatasi hilo lilikuwa ni jepesi sana na haikuwa rahisi kupata

photocopy nzuri ya maandishi. Hata hivyo, pamoja na shida kubwa

tumeweza kutoa nakala inayosomeka ambayo sasa tunaichapisha

hapa pamoja na tafsiri yake.

Nimeandika maelezo mafupi chini ya kurasa ili kuifafanua zaidi

maneno ya Sheikh na maana yake kueleweka.

Sayyid Saeed Akhtar Rizvi Dar es Salaam

Mhubiri Mkuu 1990

www.allamahrizvi.com

Page 7: QASIDA YA KUMSIFU MTUME - Allamah Rizvi · PDF fileAllamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi Tafsiri kwa Kiswahili Na: Dr. Mohamed Kanju Kimetolewa na Kuchapishwa na: BILAL MUSLIM MISSION

www.allamahrizvi.com

Page 8: QASIDA YA KUMSIFU MTUME - Allamah Rizvi · PDF fileAllamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi Tafsiri kwa Kiswahili Na: Dr. Mohamed Kanju Kimetolewa na Kuchapishwa na: BILAL MUSLIM MISSION

www.allamahrizvi.com

Page 9: QASIDA YA KUMSIFU MTUME - Allamah Rizvi · PDF fileAllamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi Tafsiri kwa Kiswahili Na: Dr. Mohamed Kanju Kimetolewa na Kuchapishwa na: BILAL MUSLIM MISSION

TAFSIRI YA BARUA

YA KUAMBATANISHA

Kwa Hakimu na Mstahiki mwandesha Mashitaka

Ash-Sheikh Hussein Allarakhya Rahim. Assalaamu Alaykum wa Rahmatullahi wa Barakatuhu. Amma

Baadu.

Huu ni wasifu mfupi wa Wasii1 (mrithi), Imamu Bwana wetu,

Ali ibn Abi Talib alayhissalaam2 (Amani iwe juu yake); nauwasilisha

kwako kama kumbukumbu (ya mapenzi) ambayo naweka hazina

kwa ajili yako katika moyo wangu na kukiri kwa ulimi wangu mbele

ya Allah, Mwenye Kutukuka, Mtukufu, Mkubwa mno, na mbele ya

Mjumbe wake, Mkarimu, Mwenye rehema na mbele ya Ahlul Bayt

wake watukufu na watoharifu na mbele ya hadhara ya malaika na

watumishi wote wema (wa Allah) kuhusiana na baraka zako kubwa

juu yangu na ukarimu wako mkubwa.

Na ni mbinu ambayo shukurani zangu kwa yale uliyoyafanya

yako kimya, ambapo uzuri wako huzungumza kwa sauti kubwa.

Nimekusudia kuelezea shukurani zangu kwako lakini kipaji changu huwa dhaifu; vyema, ninyi nyote muwe mashahidi kwamba

siwezi kuelezea shukurani zangu.

Na ulimi wangu siku zote utaendelea kusoma du’a kwa ajili

yako; na shukurani hufaa kusifiwa.

Ukarimu wako umepata kwa ajili yako vitu vitatu; mkono wangu, ulimi wangu na dhamiri ya ndani.

Sura yako iko kwenye macho yangu, ukumbusho wako uko

kwenye mdomo wangu na sehemu yako ni katika moyo wangu - vipi utakosekana (kutoka kwangu)?

______________________________

Maelezo: 1. Wasiy: Kilugha maana yake mtekelezaji wa Wasia, wakala aliyeteuliwa, kaimu. Katika sheria za Ki-Islamu humaanisha mtu ambaye ameteuliwa na Mtume kwa ajili ya kumrithi.

2. Lazima ionekane hapo kwamba Marhum Sheikh ameandika kwa usahihi kabisa ALAYHI SSALAAM baada ya jina la kiongozi wa waumini Ali (a.s.),

baadhi ya watu kwa kutokujua kwao hufikiria kwamba usemi huo hauwezi kutumika kwa wengine mbali na Mtume.

www.allamahrizvi.com

Page 10: QASIDA YA KUMSIFU MTUME - Allamah Rizvi · PDF fileAllamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi Tafsiri kwa Kiswahili Na: Dr. Mohamed Kanju Kimetolewa na Kuchapishwa na: BILAL MUSLIM MISSION

Kutoka kwa mtu ambaye anashukuru ukarimu wako mkubwa,

wemana neema juu yake.

Abdullah saleh al-Farsi 18 Dhul Q’dah Al-haram, 1380

14 Mei 1961

www.allamahrizvi.com

Page 11: QASIDA YA KUMSIFU MTUME - Allamah Rizvi · PDF fileAllamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi Tafsiri kwa Kiswahili Na: Dr. Mohamed Kanju Kimetolewa na Kuchapishwa na: BILAL MUSLIM MISSION

TAFSIRI YA

QASIDA YA KUMSIFU MTUME (s.a.w.w.)

NA AHLUL~BAYT WAKE (a.s.)

Na: Sheikh Abdullah Saleh al-Farsi

Ewe Abul Qasim (Muhammad), kushawishi kwangu kwako

kuna sifa zako na qasida.

Kwa elimu ile ambayo ulipewa na Allah bila kuwa na kitabu

kilichoandikwa.

Kwa Ali ambaye wakati macho yake yalikuwa yanauma na

ukaweka mate yako ndani yake, na kuona kwake kukawa na nguvu

kama tai - ilikuwa katika vita (yaani khaybar) ambayo iliandaliwa

chini ya bendera inayoitwa “tai”3. Na Ali ni ndugu wa Mtume ambaye kwamba mapenzi kwake

na utii ni dini ya moyo wangu.

Na ni waziri (wa Mtume), binamu yake mwenye uwezo wa hali

ya juu - na walio wazuri ni mawaziri kutoka miongoni mwa familia.

Alikuwa siku zote anaondoa pazia kwa yakini yake; bali ni jua ambalo juu yake hakuna mfuniko.4

_________________________________

Maelezo:

3.Mistari hii miwili hurejezea kwenye vita vya Khaibari ambako Waislamu

baada ya kushindwa kuiteka ngome ya Qamus kutoka kwa Mayahudi. Kisha Mtume alisema: “Hakika kesho nitampa bendera hii mtu ambaye anampenda Allah na Mjumbe Wake, na ambaye Allah na Mjumbe Wake

wanampenda. Allah atatoa ushindi mikononi mwake.” Masahaba waliupitisha usiku wakijiuliza na kushangaa, ni nani atapewa

bendera. Umar ibn al-Khattab alisema: “Sikupenda amri isipokuwa siku hiyo.” Kesho yake alinyanyua kichwa chake juu ya wengine ili kwamba aonekane na kuitwa. Mtume aliuliza: “Yuko wapi Ali ibn Abi Talib?” Walisema

anaumwa macho. Mtume alimtuma mtu akaitwe. Alipokuja Mtume (s.a.w.w.) aliweka mate yake kwenye macho yake na akamuombea. Mara moja alipona

kama vile alikuwa haumwi. Mtume (s.a.w.w.) alimpa bendera, alikwenda na kuiteka ngome. (Sahih Muslim Toleo la Beirut 1972, juzuu. 4, uk. 1871-1873. Hadithi namba 2405,2406, 2407).

4. Hii hurejezea kwenye msemo mashuhuri wa Ali (a.s.): Kama mapazia

yangeondolewa kwa yakini isingeongezeka.” Alimaanisha kwamba alikuwa na daraja ya juu ya elimu na yakini ya Allah na hakuna nafasi kwa ongezeko zaidi.

www.allamahrizvi.com

Page 12: QASIDA YA KUMSIFU MTUME - Allamah Rizvi · PDF fileAllamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi Tafsiri kwa Kiswahili Na: Dr. Mohamed Kanju Kimetolewa na Kuchapishwa na: BILAL MUSLIM MISSION

Na mama wa Sibtain (yaani, wajukuu wawili; Hasan na

Husein), mke wa Ali; na watoto wake na kwa wale waliofunikwa na Kishani ya (kisaa);5

Na kwa maua mawili6 (yaani, Hasan na Husein), ambayo

harufu yao nzuri ililetwa upesi kutoka kwako na (Fatimah) Zahra; Ulihifadhiwa na wewe kama herufi “Ye” (ي) inavyohifadhiwa na nukta zake mbili;

Mashahidi wawili - si Taif wala Karbala zitanifanya nisahau taadhira zao;

Kuhusiana nazo hakuna mfuasi aliyeheshimu mkataba wako

wa hifadhi, na viongozi walitenda kiulaghai kwenye mkataba wako;

Walibadilisha mapenzi na hifadhi ya jamaa zako wa karibu,7

na wanafiki walionesha ukungu na umande wao (wa ukafiri); Na mioyo yao ikawa migumu juu yake juu ya yule ambaye

amepoteza mbingu, na ardhi ililia na kutoa machozi.8 _____________________________________________________ Maelezo: 5. Hii hurejezea kwenye hadith mashuhuri ya al-Kisaa ambayo Ummul

Muminina Aisha aliisimulia katika njia fupi kabisa inayofaa, anasema: “Mtume alikuja siku moja, na alikuwa na shuka ya rangi ya sufi nyeusi. Kisha akaja al-Hasan bin Ali na Mtume (s.a.w.w.) akamchukuwa ndani ya

shuka. Kisha akaja al-Husein naye vile vile aliingia ndani ya shuka. Kisha akaja Fatima na Mtume (s.a.w.w.) akamfanya naye aingie ndani ya shuka.

Kisha akaja Ali (a.s.) na Mtume (s.a.w.w.) akamchukuwa ndani ya shuka. Kisha Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Allah anapenda kuwaondolea uchafu enyi watu wa nyumba! Na kuwasafisheni kwa utakaso kabisa.” (Sahih

Muslim juzuu.4, uk. 1883 - Hadithi Na. 2424). 6. Hii hurejezea kwenye hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) kuhusu al-Hasan na al-

Husein (a.s.): “Wawili hawa ni maua yangu.” 7. Angalia namba. 9 chini. 8. Hii hurejezea kwenye hadithi ijulikanayo sana kwamba mbingu na ardhi

zililia machozi wakati al-Husein alipouliwa kishahidi. Imam Suyuti

anasimulia kutoka kwa ibn Hatim, kutoka kwa Ubaya, kutoka kwa Ibrahim

(R.A.) kwamba alisema: “Mbingu hazikulia wakati ulimwengu ulipoumbwa isipokuwa juu ya watu wawili... Kwa hakika wakati Yahaya ibn Zakariya (a.s.) alipouawa mbingu ikawa nyekundu na ikanyesha mvua ya damu, na

hakika siku ambayo al-Husein ibn Ali (a.s.) alipouawa mbingu ikawa nyekundu.” Ibn Abi Hatim anasimulia kutoka kwa Sayid ibn Ziyad (R.A.)

kwamba alisema: “Wakati al-Husein (a.s.) alipouawa mbingu ilibakia na wekundu kwa muda wa miezi minne.” (Tafsir ad-Durrul Manthur-Qum 1404

A.H. Juzuu. 6, uk. 31)

www.allamahrizvi.com

Page 13: QASIDA YA KUMSIFU MTUME - Allamah Rizvi · PDF fileAllamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi Tafsiri kwa Kiswahili Na: Dr. Mohamed Kanju Kimetolewa na Kuchapishwa na: BILAL MUSLIM MISSION

Enyi Ahlul Bayt wa Mtume, hakika hakuna kinachoweza

kuliwaza moyo wangu.

Enyi Ahlul Bayt wa Mtume! Ninyi ni wema, na kuwatukuza

ninyi ni vyema, na huku ndio kuomboleza kwangu (kwa ajili yenu). “Allah anapenda kuwaondolea uchafu, Enyi Ahlul Bayt! na kuwasafisheni kwa utakaso ulio safi kabisa.”

“Sema: Sikuombeni malipo kwa hili isipokuwa mapenzi kwa

jamaa wangu wa karibu, na ambaye atafanya mema, tutampa zaidi humo; hakika Allah ni Mwingi wa kusamehe mwenye shukurani”9

‘AL-IMAM ALI IBN ABI TALIB ALAYHI SSALAAM’.10

______________________

Maelezo: 9. Lazima ifahamike kwamba Sheikh ametaja mapenzi kwa jamaa wa karibu wa Mtume katika ubeti wake wa kumi na tatu wa Qasida yake, na

ameandika aya ya Qur’an ya Tohora (33:33) na akamalizia kuandika kwake

kwa aya hii ya mapenzi kwa jamaa wa karibu. (42:23). Hii huonyesha wazi kwamba mpaka kufikia mwaka 1961 alikuwa akiamini kwamba aya hii

imefanya mapenzi kwa jamaa wa karibu wa Mtume (s.a.w.w.) kuwa ni wajibu juu ya Waislamu wote. Nashangaa ni kitu gani kimemshawishi katika mwaka 1968 kuandika kinyume cha tafsir chini ya kurasa katika

tarjuma yake ya Qur’an kwa kiswahili. 10. Hili ni jina la kitabu kilichowasilishwa na Sheikh Abdallah Saleh al-Farsi

kwa Hakimu Hussein Allarakhya Rahim.

www.allamahrizvi.com