QASIDA YA KUMSIFU MTUME (S.A.W.W.) NA AHLUL ~ BAYT WAKE
(A.S.)
Na: Sheikh Abdullah Saleh al-Farsi
Tafsiri na Maelezo kwa Kiingereza Na: Rai’sul~Mubaligheen
Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi
Tafsiri kwa Kiswahili Na: Dr. Mohamed Kanju
Kimetolewa na Kuchapishwa na:
BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
S.L.P. 20033 DAR ES SALAAM
TANZANIA
www.allamahrizvi.com
Haki ya kunakili imehifadhiwa na: Bilal Muslim Mission of Tanzania
ISBN 9987 620 30 2
Toleo la kwanza: Rabiul Awwal, 1423 / Mei, 2003 Idadi: Nakala 2000
kimechapishwa na Kimetolewa na:
BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
S.L.P. 20033 DAR ES SALAAM
TANZANIA
www.allamahrizvi.com
YALIYOMO 1. Dibaji ................................................................................... 2. Utangulizi ............................................................................. 3. Barua ya Kiarabu ................................................................ 4. Qasida ya Kiarabu ............................................................... 5. Tafsiri ya barua ya kuambatanisha ........................................ 6. Tafsiri ya Qasida ya kumsifu Mtume (s.a.w.w.) na
Ahlul ~ Bayt wake (a.s.) ..........................................
www.allamahrizvi.com
DIBAJI
Tunamshukuru Allah (s.w.t.) na kwa baraka za Mtukufu
Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul~Bayt (a.s.) kwa kutujalia kuweza kufanikisha juhudi zetu hizi katika kuchapisha kitabu hiki “Qasida ya
Kumsifu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul~Bayt wake (a.s.)”. Maandishi haya yaliyopo mikononi mwako ni tafsiri ya barua
na qasida ya kiarabu iliyoandikwa na Marhum Sheikh Abdallah
Saleh al-Farsi aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar. Utasoma katika utangulizi wa Marhum Rais’ul~Mubaligheen
Ayatullah Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi ndani ya kitabu hiki
anaeleza kwamba mwaka wa 1975, Marhum Bwana Hussein
Allarakhya Rahim aliyekuwa Hakimu wa Zanzibar, alimpa kitabu
ambacho ndani yake maandishi haya yaliyoandikwa na Marhum Sheikh al-Farsi, Marhum Allamah Rizvi alichukua kitabu na
akakiweka ndani ya Maktaba yake “Kutub Khana Riyaz Ma’arif ” mji
wa Gopalpur, India.
Mwaka wa 1989 alitoa photocopy ya maandishi haya na
akaitafsiri kwa lugha ya Kiingreza na pia akaandika maelezo ili
maneno ya Shaikh al-Farsi na maana yake yaeleweke vizuri.
Mwaka wa1990 mwezi wa Decemba tafsiri ile ya Kiingreza na
maelezo pamojo na asili yake ya Kiarabu ili chapishwa ndani ya
gazeti la “The Light” na tafsiri ya Kiswahili kutoka Kiingreza
iliyotafsiriwa na Sheikh Dhikiri U.M. Kiondo ilichapishwa ndani ya
gazeti la “Sauti ya Bilal”.
Watu wengi wamependekeza kwamba qasida hiyo ichapwe
kama kijitabu, ushauri wao umezingatiwa na Dr. Muhammad Said
Kanju ameitafsiri tena kutoka katika lugha ya Kiingreza na kuiweka katika lugha ya Kiswahili na hivi sasa kitabu hiki tayari kipo
mikononi mwako.
www.allamahrizvi.com
Bilal Muslim Mission inatoa shukurani zake za dhati kwa wale
wote ambao kwa juhudu zao kitabu hiki kinawafikia wasomaji wetu mikononi na wale wote wanaotuunga mkono kwa njia moja au
nyingine katika uchapishaji wa kitabi hiki. Tunamuomba Allah
(s.w.t.) awalipe malipo mema hapa Duniani na ba’adaye huko,
Akhera.
9 Rabiul Awwal 1424 Sayyid Murtaza Rizvi 11 mei 2003 Bilal Muslim Mission
Dar es Salaam
www.allamahrizvi.com
UTANGULIZI Tunachapisha hapa (Qasida) wasifu wa Kiarabu wa Mtukufu Mtume na Ahlul~Bayt wake (Rehema na Amani na iwe juu yawo)
iliyoandikwa na Marehemu Sheikh Abdallah Saleh al-Farsi.
Ilitungwa katika mwaka 1380 Hijiriya sawa na mwaka 1961
Masihiya wakati alipokuwa Kadhi mkuu wa Zanzibar.
Marehemu Sheikh Abdallah Saleh al-Farsi aliwasilisha Kitabu cha ki-Arabu cha maisha ya “Al-Imam Ali bin Abu Talib,
Alayhissalamu” (toleo la Misri) kwa Marhum Al-Haj Hussein
Allarakhya Rahim, O.B.E., ambaye alikuwa ni Hakimu wa Zanzibar
na alikuwa akielewana naye sana. Sheikh alikipata kitabu hicho
kikiwa kimefumwa pamoja na makaratasi meupe mwanzoni. Kisha
alimpata mwandishi wa hati ambaye alinakili barua yake ya
kuambatanisha na qasida katika mwandiko mzuri wa mkono;
Sheikh alisaini barua ya kuambatanisha kwa wino wa bluu (huenda
ni kwa ballpen).
Kitabu ambacho kina maandishi haya kiliwasilishwa kwangu
miaka kumi na tano iliyopita na Marhum Husseni Allarakhya Rahim,
ambacho nilikwenda nacho India na kukiweka katika maktaba
yangu. Miaka miwili iliyopita nilikitoa kitabu hiki kutoka maktaba
yangu na nikayaona maandishi yale na nikataka kuyachapisha
katika jarida la Bilal Muslim Mission, The Light na Sauti ya Bilal.
Karatasi hilo lilikuwa ni jepesi sana na haikuwa rahisi kupata
photocopy nzuri ya maandishi. Hata hivyo, pamoja na shida kubwa
tumeweza kutoa nakala inayosomeka ambayo sasa tunaichapisha
hapa pamoja na tafsiri yake.
Nimeandika maelezo mafupi chini ya kurasa ili kuifafanua zaidi
maneno ya Sheikh na maana yake kueleweka.
Sayyid Saeed Akhtar Rizvi Dar es Salaam
Mhubiri Mkuu 1990
www.allamahrizvi.com
www.allamahrizvi.com
www.allamahrizvi.com
TAFSIRI YA BARUA
YA KUAMBATANISHA
Kwa Hakimu na Mstahiki mwandesha Mashitaka
Ash-Sheikh Hussein Allarakhya Rahim. Assalaamu Alaykum wa Rahmatullahi wa Barakatuhu. Amma
Baadu.
Huu ni wasifu mfupi wa Wasii1 (mrithi), Imamu Bwana wetu,
Ali ibn Abi Talib alayhissalaam2 (Amani iwe juu yake); nauwasilisha
kwako kama kumbukumbu (ya mapenzi) ambayo naweka hazina
kwa ajili yako katika moyo wangu na kukiri kwa ulimi wangu mbele
ya Allah, Mwenye Kutukuka, Mtukufu, Mkubwa mno, na mbele ya
Mjumbe wake, Mkarimu, Mwenye rehema na mbele ya Ahlul Bayt
wake watukufu na watoharifu na mbele ya hadhara ya malaika na
watumishi wote wema (wa Allah) kuhusiana na baraka zako kubwa
juu yangu na ukarimu wako mkubwa.
Na ni mbinu ambayo shukurani zangu kwa yale uliyoyafanya
yako kimya, ambapo uzuri wako huzungumza kwa sauti kubwa.
Nimekusudia kuelezea shukurani zangu kwako lakini kipaji changu huwa dhaifu; vyema, ninyi nyote muwe mashahidi kwamba
siwezi kuelezea shukurani zangu.
Na ulimi wangu siku zote utaendelea kusoma du’a kwa ajili
yako; na shukurani hufaa kusifiwa.
Ukarimu wako umepata kwa ajili yako vitu vitatu; mkono wangu, ulimi wangu na dhamiri ya ndani.
Sura yako iko kwenye macho yangu, ukumbusho wako uko
kwenye mdomo wangu na sehemu yako ni katika moyo wangu - vipi utakosekana (kutoka kwangu)?
______________________________
Maelezo: 1. Wasiy: Kilugha maana yake mtekelezaji wa Wasia, wakala aliyeteuliwa, kaimu. Katika sheria za Ki-Islamu humaanisha mtu ambaye ameteuliwa na Mtume kwa ajili ya kumrithi.
2. Lazima ionekane hapo kwamba Marhum Sheikh ameandika kwa usahihi kabisa ALAYHI SSALAAM baada ya jina la kiongozi wa waumini Ali (a.s.),
baadhi ya watu kwa kutokujua kwao hufikiria kwamba usemi huo hauwezi kutumika kwa wengine mbali na Mtume.
www.allamahrizvi.com
Kutoka kwa mtu ambaye anashukuru ukarimu wako mkubwa,
wemana neema juu yake.
Abdullah saleh al-Farsi 18 Dhul Q’dah Al-haram, 1380
14 Mei 1961
www.allamahrizvi.com
TAFSIRI YA
QASIDA YA KUMSIFU MTUME (s.a.w.w.)
NA AHLUL~BAYT WAKE (a.s.)
Na: Sheikh Abdullah Saleh al-Farsi
Ewe Abul Qasim (Muhammad), kushawishi kwangu kwako
kuna sifa zako na qasida.
Kwa elimu ile ambayo ulipewa na Allah bila kuwa na kitabu
kilichoandikwa.
Kwa Ali ambaye wakati macho yake yalikuwa yanauma na
ukaweka mate yako ndani yake, na kuona kwake kukawa na nguvu
kama tai - ilikuwa katika vita (yaani khaybar) ambayo iliandaliwa
chini ya bendera inayoitwa “tai”3. Na Ali ni ndugu wa Mtume ambaye kwamba mapenzi kwake
na utii ni dini ya moyo wangu.
Na ni waziri (wa Mtume), binamu yake mwenye uwezo wa hali
ya juu - na walio wazuri ni mawaziri kutoka miongoni mwa familia.
Alikuwa siku zote anaondoa pazia kwa yakini yake; bali ni jua ambalo juu yake hakuna mfuniko.4
_________________________________
Maelezo:
3.Mistari hii miwili hurejezea kwenye vita vya Khaibari ambako Waislamu
baada ya kushindwa kuiteka ngome ya Qamus kutoka kwa Mayahudi. Kisha Mtume alisema: “Hakika kesho nitampa bendera hii mtu ambaye anampenda Allah na Mjumbe Wake, na ambaye Allah na Mjumbe Wake
wanampenda. Allah atatoa ushindi mikononi mwake.” Masahaba waliupitisha usiku wakijiuliza na kushangaa, ni nani atapewa
bendera. Umar ibn al-Khattab alisema: “Sikupenda amri isipokuwa siku hiyo.” Kesho yake alinyanyua kichwa chake juu ya wengine ili kwamba aonekane na kuitwa. Mtume aliuliza: “Yuko wapi Ali ibn Abi Talib?” Walisema
anaumwa macho. Mtume alimtuma mtu akaitwe. Alipokuja Mtume (s.a.w.w.) aliweka mate yake kwenye macho yake na akamuombea. Mara moja alipona
kama vile alikuwa haumwi. Mtume (s.a.w.w.) alimpa bendera, alikwenda na kuiteka ngome. (Sahih Muslim Toleo la Beirut 1972, juzuu. 4, uk. 1871-1873. Hadithi namba 2405,2406, 2407).
4. Hii hurejezea kwenye msemo mashuhuri wa Ali (a.s.): Kama mapazia
yangeondolewa kwa yakini isingeongezeka.” Alimaanisha kwamba alikuwa na daraja ya juu ya elimu na yakini ya Allah na hakuna nafasi kwa ongezeko zaidi.
www.allamahrizvi.com
Na mama wa Sibtain (yaani, wajukuu wawili; Hasan na
Husein), mke wa Ali; na watoto wake na kwa wale waliofunikwa na Kishani ya (kisaa);5
Na kwa maua mawili6 (yaani, Hasan na Husein), ambayo
harufu yao nzuri ililetwa upesi kutoka kwako na (Fatimah) Zahra; Ulihifadhiwa na wewe kama herufi “Ye” (ي) inavyohifadhiwa na nukta zake mbili;
Mashahidi wawili - si Taif wala Karbala zitanifanya nisahau taadhira zao;
Kuhusiana nazo hakuna mfuasi aliyeheshimu mkataba wako
wa hifadhi, na viongozi walitenda kiulaghai kwenye mkataba wako;
Walibadilisha mapenzi na hifadhi ya jamaa zako wa karibu,7
na wanafiki walionesha ukungu na umande wao (wa ukafiri); Na mioyo yao ikawa migumu juu yake juu ya yule ambaye
amepoteza mbingu, na ardhi ililia na kutoa machozi.8 _____________________________________________________ Maelezo: 5. Hii hurejezea kwenye hadith mashuhuri ya al-Kisaa ambayo Ummul
Muminina Aisha aliisimulia katika njia fupi kabisa inayofaa, anasema: “Mtume alikuja siku moja, na alikuwa na shuka ya rangi ya sufi nyeusi. Kisha akaja al-Hasan bin Ali na Mtume (s.a.w.w.) akamchukuwa ndani ya
shuka. Kisha akaja al-Husein naye vile vile aliingia ndani ya shuka. Kisha akaja Fatima na Mtume (s.a.w.w.) akamfanya naye aingie ndani ya shuka.
Kisha akaja Ali (a.s.) na Mtume (s.a.w.w.) akamchukuwa ndani ya shuka. Kisha Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Allah anapenda kuwaondolea uchafu enyi watu wa nyumba! Na kuwasafisheni kwa utakaso kabisa.” (Sahih
Muslim juzuu.4, uk. 1883 - Hadithi Na. 2424). 6. Hii hurejezea kwenye hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) kuhusu al-Hasan na al-
Husein (a.s.): “Wawili hawa ni maua yangu.” 7. Angalia namba. 9 chini. 8. Hii hurejezea kwenye hadithi ijulikanayo sana kwamba mbingu na ardhi
zililia machozi wakati al-Husein alipouliwa kishahidi. Imam Suyuti
anasimulia kutoka kwa ibn Hatim, kutoka kwa Ubaya, kutoka kwa Ibrahim
(R.A.) kwamba alisema: “Mbingu hazikulia wakati ulimwengu ulipoumbwa isipokuwa juu ya watu wawili... Kwa hakika wakati Yahaya ibn Zakariya (a.s.) alipouawa mbingu ikawa nyekundu na ikanyesha mvua ya damu, na
hakika siku ambayo al-Husein ibn Ali (a.s.) alipouawa mbingu ikawa nyekundu.” Ibn Abi Hatim anasimulia kutoka kwa Sayid ibn Ziyad (R.A.)
kwamba alisema: “Wakati al-Husein (a.s.) alipouawa mbingu ilibakia na wekundu kwa muda wa miezi minne.” (Tafsir ad-Durrul Manthur-Qum 1404
A.H. Juzuu. 6, uk. 31)
www.allamahrizvi.com
Enyi Ahlul Bayt wa Mtume, hakika hakuna kinachoweza
kuliwaza moyo wangu.
Enyi Ahlul Bayt wa Mtume! Ninyi ni wema, na kuwatukuza
ninyi ni vyema, na huku ndio kuomboleza kwangu (kwa ajili yenu). “Allah anapenda kuwaondolea uchafu, Enyi Ahlul Bayt! na kuwasafisheni kwa utakaso ulio safi kabisa.”
“Sema: Sikuombeni malipo kwa hili isipokuwa mapenzi kwa
jamaa wangu wa karibu, na ambaye atafanya mema, tutampa zaidi humo; hakika Allah ni Mwingi wa kusamehe mwenye shukurani”9
‘AL-IMAM ALI IBN ABI TALIB ALAYHI SSALAAM’.10
______________________
Maelezo: 9. Lazima ifahamike kwamba Sheikh ametaja mapenzi kwa jamaa wa karibu wa Mtume katika ubeti wake wa kumi na tatu wa Qasida yake, na
ameandika aya ya Qur’an ya Tohora (33:33) na akamalizia kuandika kwake
kwa aya hii ya mapenzi kwa jamaa wa karibu. (42:23). Hii huonyesha wazi kwamba mpaka kufikia mwaka 1961 alikuwa akiamini kwamba aya hii
imefanya mapenzi kwa jamaa wa karibu wa Mtume (s.a.w.w.) kuwa ni wajibu juu ya Waislamu wote. Nashangaa ni kitu gani kimemshawishi katika mwaka 1968 kuandika kinyume cha tafsir chini ya kurasa katika
tarjuma yake ya Qur’an kwa kiswahili. 10. Hili ni jina la kitabu kilichowasilishwa na Sheikh Abdallah Saleh al-Farsi
kwa Hakimu Hussein Allarakhya Rahim.
www.allamahrizvi.com