mkuu wa majeshi ya rwanda atembelea kiwanda …

3
TOLEO NAMBA 071 | MEI 11, 2021 1 MKUU WA MAJESHI YA RWANDA ATEMBELEA KIWANDA CHA MAJI SUMAJKT Mkuu wa Majeshi ya Rwanda Jenerali Jean Bosco Kazura (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Rajab Mabele, alipofanya ziara katika kiwanda cha maji ya kunywa ya Uhuru Peak kilichopo katika kituo cha uwekezaji cha JWTZ Mgulani JKT jijini Dar es Salaam.

Upload: others

Post on 20-Nov-2021

3 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: MKUU WA MAJESHI YA RWANDA ATEMBELEA KIWANDA …

TOLEO NAMBA 071 | MEI 11, 2021

1

MKUU WA MAJESHI YA RWANDA ATEMBELEA KIWANDA CHA MAJI SUMAJKT

Mkuu wa Majeshi ya Rwanda Jenerali Jean Bosco Kazura (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Rajab Mabele, alipofanya ziara katika kiwanda cha maji ya kunywa ya Uhuru Peak kilichopo katika kituo cha uwekezaji cha JWTZ Mgulani JKT jijini Dar es Salaam.

Page 2: MKUU WA MAJESHI YA RWANDA ATEMBELEA KIWANDA …

TOLEO NAMBA 071 | MEI 11, 2021

2 2

Mkuu wa Majeshi ya Rwanda Jenerali Jean Bosco Kazura (aliyevaa barakoa) akikagua gwaride la mapokezi lililoandaliwa na Kikosi cha JKT Mgulani jijini Dar es Salaam.

M kuu wa Majeshi ya Rwanda Jenerali Jean Bosco Kazura pamoja na ujumbe wake ja-na tarehe 10 Mei 2021 ametembelea ki-wanda cha maji ya kunywa ya Uhuru Peak

(SUMAJKT BOTTLING PLANT) kilichopo katika kituo cha uwekezaji cha JWTZ Mgulani JKT jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Majeshi huyo pamoja ujumbe wake alipokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Rajab Mabele, kwa niaba ya Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Charles Mbuge, ambapo alipatiwa taarifa fupi ya JKT na SUMAJKT na baadae kutembelea kiwanda cha maji ya kunywa ya Uhuru Peak.

Mkuu wa Majeshi ya Rwanda Jenerali Jean Bosco Kazura ameshauri Kampuni za Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kujitanua zaidi kibiashara ndani ya Tanzania na nchi zilizopo katika bara la Afrika.

Jenerali Kazura, ameeleza kuwa lengo kubwa la ziara hiyo ni kubadilishana mawazo na Kujifunza kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa upande wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) hususani kuhusu uchumi.

"Tumekuja hapa kujenga msingi mzuri wa usalama ili

kuweka mazingira mazuri zaidi ya kuendeleza uchumi ndani ya Majeshi yetu" alieleza Jenerali Jean Kazura.

Aidha, Jenerali Jean Kazura aliwaeleza baadhi ya Wakurugenzi wa SUMAJKT waliohudhuria katika ziara ya ugeni huo kuwa kabla ya kufika kiwandani hapo alikutana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo na kusema kuwa wao tayari ni marafiki, hivyo ameagiza Wakurugenzi hao nao kujenga urafiki na maafisa wa Jeshi la Rwanda.

Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) linajishughulisha na Ushonaji nguo za aina mbalimbali, Uzalishaji na Uuzaji wa maji ya kunywa, Ujenzi na Uhandisi, Usambazaji uuzaji wa zana za kilimo, Huduma ya Ulinzi binafsi, Huduma ya Usafi na Unyunyiziaji dawa, Ukusanyaji wa madeni, ushuru na minada, Uzalishaji na usambazaji wa kokoto na matofali.

Vilevile SUMAJKT linajishughulisha na Utengenezaji wa samani za ofisini na nyumbani, uzalishaji wa bidhaa za ngozi, Utoaji wa mizigo bandarini, Usimamizi wa vibarua bandarini, Huduma ya chakula na kumbi, Ufugaji wa samaki kwa njia ya matenki, Viwanda vya kuchakata nafaka, Ufugaji, Kilimo cha mazao ya biashara na chakula.

MKUU WA MAJESHI YA RWANDA ATEMBELEA KIWANDA CHA MAJI SUMAJKT

Page 3: MKUU WA MAJESHI YA RWANDA ATEMBELEA KIWANDA …

TOLEO NAMBA 071 | MEI 11, 2021

Matukio Katika Picha

3

Mkuu wa Majeshi ya Rwanda Jenerali Jean Bosco Kazura (watatu kutoka kulia) akiangalia namna ya uzalisha wa Maji ya Uhuru katika kiwanda hicho kilichopo JKT Mgulani jijini Dar es Salaam, (Kulia kwake) Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT Brigedia Jenerali Rajab Mabele.

Meneja wa Kiwanda cha Maji ya kunywa ya Uhuru Peak (SUMAJKT Bottling Plant) Meja Leah Mtuma (aliyeshika fimbo) akimuelezea Mkuu wa Majeshi ya Rwanda Jenerali Jean Bosco Kazura (aliyevaa barakoa) Uzalishaji wa maji hayo alipotembelea kiwandani hapo, (wakwanza kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT Brigedia Jenerali Rajab Mabele.

Mkuu wa Majeshi ya Rwanda Jenerali Jean Bosco Kazura (katikati) Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Rajab Mabele (wapili kutoka kulia) Balozi wa Rwanda nchini Tanzania (aliyevaa suti) Naibu Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT anaeshughulikia utawala Kanali Absolomon Shausi (wakwanza kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa Isamuhyo JKT Mgulani jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Majeshi ya Rwanda Jenerali Jean Bosco Kazura (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Rajab Mabele (wapili kutoka kulia) Balozi wa Rwanda nchini Tanzania (aliyevaa suti) Naibu Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT anayeshughulikia Oparesheni za Kibiashara Kanali Erasmus Bwegoge (wakwanza kushoto) pamoja na Wakurugenzi mbalimbali wa SUMAJKT nje ya ukumbi wa Isamuhyo Mgulani JKT jijini Dar es Salaam.