taarifa ya mkutano mkuu wa mwaka wa tatu ......2 taarifa ya mkutano mkuu wa mwaka wa tatu wa...

7
1 Jenga Afya Tokomeza Umasikini

Upload: others

Post on 03-Jan-2021

36 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1: TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TATU ......2 TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TATU WA WANAHISA WA JATU PLC Taarifa inatolewa kwamba mkutano mkuu wa mwaka wa tatu wa wanahisa,

1Jenga Afya Tokomeza Umasikini

Page 2: TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TATU ......2 TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TATU WA WANAHISA WA JATU PLC Taarifa inatolewa kwamba mkutano mkuu wa mwaka wa tatu wa wanahisa,

2 Jenga Afya Tokomeza Umasikini

TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TATU WA WANAHISA WA JATU PLC

Taarifa inatolewa kwamba mkutano mkuu wa mwaka wa tatu wa wanahisa, wakulima pamoja na wageni waalikwa uliositishwa tarehe 28/04/2020 baada ya kuibuka kwa ugonjwa wa virusi vya ko-rona utafanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 14 Novemba, 2020 katika ukumbi wa VIP Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza, Dar es Salaam. Ajenda zitakazojadiliwa ni kama ifuatavyo;

1. Kufungua mkutano

2. Kuthibitisha Akidi

3. Kuthibitisha Ajenda

4. Yatokanayo na Mkutano mkuu wa pili wa wanahisa wa JATU PLC uliofanyika tarehe 27 Aprili 2019

5. Taarifa ya Mchakato wa kuingia soko la hisa la Dar es Salaam (DSE)

6. Ripoti ya kilimo kwa msimu wa mwaka 2020/2021

7. Kuzindua miradi mipya ya kilimo

8. Huduma ya Uwakala wa bidhaa za JATU

9. Taarifa fupi ya bodi

10. Taarifa ya kifedha iliyofanyiwa ukaguzi ya mwaka unaoishia tarehe 31 Desemba 2019

11. Gawio la hisa kwa mwaka 2019

12. Mapendekezo kutoka kwa wanahisa

13. Masuala mengine kwa ridhaa ya mwenyekiti

14. Maamuzi ya mahali na tarehe, kwa kikao kijacho

15. Kufunga kikao

Kwa niaba ya bodi

Mohamed Issa SimbanoKatibu 28/09/2020.

Page 3: TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TATU ......2 TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TATU WA WANAHISA WA JATU PLC Taarifa inatolewa kwamba mkutano mkuu wa mwaka wa tatu wa wanahisa,

3Jenga Afya Tokomeza Umasikini

MAHUDHURIO

WAKURUGENZI1. EVA DAMAS KAPINGA-MWENYEKITI2. PETER ISARE GASAYA- MKURUGENZI MKUU3. MARIAM SAID MRUTU-MJUMBE4. CHARLES MWITA GICHOGO-MJUMBE5. NICHOLAUS HILMARY FUIME-MJUMBE6. AMINIEL ELIMRINGI MARO - MJUMBE7. ESTHER PHILEMON KIUYA-MJUMBE8. CLAUDIA SIMON ALBOGASTI-MJUMBE

KATIBUMOHAMED ISSA SIMBANO

WAGENI WAALIKWAWASHAURI WAELEKEZI WA BIASHARA, FEDHA NA UWEKEZAJI (ARCH FINANCIAL LTD)

WANAHISA WALIOHUDHURIA WENYEWE (250) WALIOTUMA WAWAKILISHI (12)

MUHTASARI NA MAAZIMIO YA MKUTANO MKUU WA PILI WA WANAHISA UNAOISHIA 2018

Page 4: TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TATU ......2 TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TATU WA WANAHISA WA JATU PLC Taarifa inatolewa kwamba mkutano mkuu wa mwaka wa tatu wa wanahisa,

4 Jenga Afya Tokomeza Umasikini

KUFUNGUA MKUTANOKabla ya ufunguzi wa kikao mwenyekiti alithibitisha kuwa kwa sasa akidi imetimia hivyo tunaweza anza mkutano na baada ya salamu mkutano ulifunguliwa rasmi saa tatu na nusu (3:30) asubui baada ya ufunguzi mwenyekiti aliomba mjumbe mmoja kutuongoza kwa sala, ili tuweze pata baraka kwa yale tutakayoenda jadili katika mkutano wetu.

KUPITISHWA KWA AJENDAMara baada ya kufungua kikao wanahisa walipata wasaa wa kupitisha ajenda zilizo mbele yao kabla ya kuan-za kuzijadili, ajenda zilikubaliwa na wanahisa wote kisha mwenyekiti aliendelea na kikao.

KUHAKIKI MIKUTANO MIKUU YA ZIADA NA MKUTANO MKUU WA WANA-HISA UNAOISHIA MWAKA 2017Katika ajenda hii wanahisa walitajiwa jumla ya mikutano mikuu ya ziada, pamoja na mkutano mkuu wa mwaka 2017 ambayo imeshafanyika mpaka kufikia siku ya mkutano mkuu wa pili wa wanahisa wa 2018. Katibu aliwasisitiza wanahisa pamoja na wanachama wote kujiwekea mazoea ya kusoma mihutasari ya vikao ili kujua mwenendo wa kampuni pamoja na kujua maazimiao mbali mbali yanay-opitishwa katika vikao vya wanahisa hasa kwa wale wasio hudhuria vikao na hawatumi wawakilishi wakati utaratibu wa kutuma wawakilishi katika mikutano ya wanahisa tulishawapatia na hii ni haki ya kila mwanahisa kufatilia na kujua mwenendo wa kampuni yake. Hivyo ni vema kila mmoja baada ya kikao hiki kupita ofisini na kupata kopi ya mihtasari yote ya vikao.

MAAZIMIO YATOKANAYO NA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA WANA-HISA UNAOISHIA MWAKA 2017

Ajenda 8.Maazimio- Wanahisa walikubaliana kwa pamoja kuwa gawio la faida lililopatikana kiasi cha fedha za kitanza-nia shilingi 6,325,770/= liongezwe kwenye hisa zao badala ya kupokea fedha taslimu.

Ajenda 9.Maazimio- Kupitishwa kwa makadirio ya bajeti ya fedha za kitanzania shilingi bilioni saba na milioni miatano

Ajenda 10.Maazimio- Kuisajili kampuni ya Jatu Plc katika soko la hisa la Dar es Salaam. -Kupitishwa kwa maazimio ya kuweka ahadi ya kununua hisa za jatu pindi zitakapo ingia soko la hisa kwa kuandika barua ya ahadi ama kujaza fomu. (Commitment letter).

TAARIFA FUPI YA BODIMwenyekiti alisoma taarifa fupi ya utendaji wa bodi ya wajumbe wa Jatu Plc Pamoja na maendeleo ya kam-puni kwa ujumla katika kilimo, viwanda na masoko kwa kipindi cha mwaka mmoja, kwa kuwa tutasomewa taarifa ya hesabu, tutapata sikia faida tuliyopata kwa mwaka huu na sisi kama bodi tulishakaa tayari na kushauriana na watendaji kuwa, kampuni ipo katika ukuaji ni vema gawio likagawiwe kwa kuongezewa hisa kuliko kulipa keshi, hivyo tunaleta kwenu ili tupate kusikia mapendekezo yenu juu ya gawio lenu mtakalo somewa na mhasibu.

Pia mwenyekiti alitoa shukrani za dhati kwa wanahisa kuwa, kwa sasa bodi yake ya mpito inaomba kupumzi-ka ili kupisha uchaguzi wa bodi mpya yenye vigezo kutokana na matakwa kwa kampuni inayoingia kwenye soko la hisa, ambapo lazima bodi iwe na watu wenye fani mbali mbali kulingana na biashara inayofanywa na kampuni. Mfano kuwepo kwa mtalaam wa mambo ya kilimo cha umwagiliaji, mambo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama), Mwanasheria(wakili mzoefu katika mambo ya uongozi na utawala wa makam-puni), mtaalamu wa mambo ya kihasibu na ukaguzi wa mahesabu na mjasiriamali au mfanyabiashara mzoe-fu. Lengo la watalaam hawa ni kutokana na matakwa ya mamlaka ya masoko ya dhamana na mitaji Pamoja na soko la hisa la Dar es salaam kwa kampuni yoyote inayoingia katika soko la hisa, pia ni kwa ajili ya manu-faa ya kuwasaidia watendaji ili kuleta ufanisi zaidi.

Page 5: TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TATU ......2 TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TATU WA WANAHISA WA JATU PLC Taarifa inatolewa kwamba mkutano mkuu wa mwaka wa tatu wa wanahisa,

5Jenga Afya Tokomeza Umasikini

Hivyo kuanzia sasa wajumbe wa bodi hii ambao ni Eva Damasi Kapinga (Mwenyekiti), Esther Philemon Kiuya (Mjumbe), Claudia Simon Albogasti ( Mjumbe), Charles Mwita Gichogo (Mjumbe), Amininel Elimring Maro (Mjumbe), Mariam Saidi Mrutu (Mjumbe) na Nicholaus Hilmary Fuime (Mjumbe) watatambulika rasmi kama KAMATI YA USIMAMIZI ili kushirikiana na watendaji mpaka itakapo patikana bodi mpya. Niwakaribishe pindi nafasi zitakapo tangazwa tutume maombi ili tuweze endeleza pale sisi tulipoishia kwani kwa kipindi chote tumekua bega kwa bega na watendaji kwenye kipindi cha shida na raha, bila kujali maslahi yetu na pasi kudai malipo yoyote kwani tunatambua kuwa tupo kwa lengo la kuijenga kampuni kwa kusaidiana na watendaji na kwa ambao mtakaochaguliwa tunawasihi na kuwaomba muipeleke kampuni hatua nyingine ya kuingia katika soko la hisa, kwani kwa sasa ni kipaumbele kwetu sote mpaka tuhakikishe tunafikia malengo tuliyojiwekea.

Maazimio:– Kuvunjwa rasmi kwa bodi ya mpito na kuundwa kwa kamati maalum itakayosimamia upatikanaji wa bodi Mpya.

TAARIFA YA KIFEDHA ILIYOFANYIWA UKAGUZI KWA MWAKA UNAOISHIA TAREHE 31 DESEMBA 2018 NA GAWIO LA FAIDAMwenyekiti alimkaribisha Mhasibu ili aweze wasilisha ripoti ya kifedha ambapo wanahisa wali-somewa ripoti yote hasa sehemu muhimu zinazo onesha ukuaji na ufanisi wa kampuni kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo faida iliyopatikana ni fedha za kitanzania shilingi 15,985,735/= ukilin-ganisha na mwaka wa kwanza ambapo faida ilikua shilingi 6,325,770. Baada ya ripoti kusomwa wanahisa walipata wasaa wa kuuliza maswali hususani gawio la faida lililopatikana kama litolewa keshi kwa kila mwanahisa au kila mwanahisa apewe kwa utaratibu wa kuongezewa kwenye hisa kulingana na idadi ya hisa zao kwa kugawanya kwa gawio lililopatikana kwa mwaka husika ili kujua kila mmoja atapata hisa ngapi, madeni ya mawakala ambayo kampuni inadai kutoka kwa mawakala na mkakati wa kampuni kuwabana mawakala ili walipe izo fedha kwa haraka iwezekanavyo, madeni ya watendaji ambao wanamalimbikizo ya mishahara pamoja na posho na namna kampuni inaweza tengeneza vyanzo vingine vya pesa, na mwisho madeni ya wakulima tutafute ufumbuzi ili tuweze yamaliza kwa wakati japo tunatambua kuwa huu ni mwanzo hivyo changamoto hazikosekani.

Mkurugenzi alitoa ufafanuzi kuhusu madeni haya ya wakulima kuwa wakulima hawanunui bidhaa zi-nazozalishwa na kampuni hivyo tunapaswa kujua mfumo wa kampuni sote pamoja na wanachama kuwa soko la kwanza kwa kila tunachokilima kabla ya kuanza kuwaza soko la nje ni sisi wenyewe na ndomana tunafanya kilimo-viwanda na masoko, hivyo mnyororo huu hautakiwi kuishia njiani tu-naanzia shambani- tunahamia -viwandani kisha tunamalizia sokoni, kwani kwa wanachama tulion-ao mpaka sasa takribani kumi na tatu elfu sote tukiamua kula kama ilivyo dhima kuu ya kampuni ya jenga afya tokomeza umasikini hakutakuwa tena na changamoto kama kila mmoja atafanya wajibu wake, kwa upande wa kampuni tutazidi boresha mifumo ya masoko ili kuleta ufanisi zaidi na ndo kazi ya watendaji kuhakikisha hatulali ili wawekezaji wetu wawezepata faida katika uwekezaji wao ndani ya kampuni hata kabla ya gawio la hisa kila anayeshiriki fursa mbali mbali ndani ya kampuni, mfano kilimo cha maharage ndani ya miezi mitatu mkulima awe amevuna na kuiuzia kampuni kisha kupata fedha ya maendeleo na kuzidi kufanya uwekezaji mkubwa zaidi, hii ni furaha kwetu na jamii kwa ujumla kwa kuona maono yetu yanatimia.

Maazimio:- Wanahisa walikubaliana kwa pamoja kuwa gawio la faida lililopatikana kiasi cha shilingi milioni kumi na tano liongezwe kwenye hisa zao badala ya kupokea fedha taslimu.

Page 6: TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TATU ......2 TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TATU WA WANAHISA WA JATU PLC Taarifa inatolewa kwamba mkutano mkuu wa mwaka wa tatu wa wanahisa,

6 Jenga Afya Tokomeza Umasikini

MAPENDEKEZO YA MAKADIRIO YA BAJETI YA MWAKA 2019Kuhusu mapendekezo ya bajeti yaliwasilishwa na Mhasibu ambapo takribani ya jumla ya shilingi bilioni saba na milioni miatano iliwasilishwa kwa wanahisa kwa madhumuni ya kufanikisha mradi wa umwagiliaji na ujenzi wa kiwanda kikubwa cha uzalishaji wa bidhaa ya unga wa DONA na SEMBE wilaya ya Kiteto mkoani Manyara. Baada ya uwasilishwaji mwenyekiti alimkaribisha Mkurugenzi atoe maelezo ya ziada kuhusu umuhimu wa bajeti hii ambapo alisisitiza kwakusema ili kufikia malengo tuliyojiwekea kuhusu kupanua huduma na kuongeza uzalishaji hatunabudi kupata hizi fedha kwani mpaka sasa uhitaji ni mkubwa hivyo kiwanda chetu kinaanza lemewa. Kwa wingi wetu sifikirii kama kuna jambo litakalotushinda kama tukidhamiria kwa kauli moja na hata hii bajeti pendekezwa ya mwaka 2019 tukiamua jiwekea malengo ya kila mwezi kuchangia shilingi ishirini na tano elfu 25,000 tu kila mmoja, ukizidisha kwa wanachama elfu kumi (10,000) tunapata milioni miambili hamsini hii ni kila mwezi 250,000,000 tunauwezo wakufanikisha bilioni saba na kila mwezi tukawa tunakamili-sha miundombinu yetu kwa awamu mpaka kukamilisha mradi mzima wa umwagiliaji na ujenzi wa kiwanda pasi kusubiria mchakato wa soko la hisa.

Maazimio:-Kupitiswa kwa makadirio ya bajeti ya fedha za kitanzania shilingi bilioni saba na milioni miatano. KUISAJILI KAMPUNI YA JATU PLC KATIKA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAMKatika ajenda hii ambayo imekua kipaumbele katika kila mkutano mkuu wa wanahisa iliwekewa msisitizo na Mkurugenzi kuwa mchakato wa kuingia soko la hisa umekua mrefu na wenye kuhitaji fedha tofauti na tulivyo tarajia, hivyo tumeona tuwape mrejesho kuwa bado tunaendelea na zoezi la kuandaa nyaraka muhimu am-bazo ni Waraka wa matarajio(Prospectus), Mpango biashara (Business Plan) na taarifa kuhusu thamani ya kampuni (Valuation Riport) pamoja na kuifanyia KATIBA (MEMART) ya kampuni mabadiliko ili iyendane na matakwa ya kampuni ya umma, nyaraka hizi ni muhimu sana kwani bila hizi hakuna kitakacho endelea, na pia inatubidi tuisaidie kampuni angalau kupata fedha hata kwa mkopo ili kufanikisha mchakato mzima, na hatuwezi kwenda benki kukopa kwaajili ya zoezi hili kwanza benki watatushangaa na haitawezekana.

Hivyo ninaomba kusikia maoni yenu kwa kuwa mchakato wa soko la hisa ni kwa ajili ya manufaa yetu sote na kila mmoja atajivunia pindi mchakato huu utakapo kamilika kwa hiyo nashauri kwa wanachama wakulima kama mjuavyo zoezi la kuweka miundombinu ya umwagiliaji unaenda kuwanufaisha moja kwa moja hasa wakulima wa mahindi na alizeti kwa mkoa wa Manyara tuwe wa kwanza kuchangia zoezi la upatikanaji wahii fedha na kwa nyinyi inabidi kila mmoja ajitahidi hata akakope kwenye vikoba ama popote unapoweza kwen-da, kwa kusema hayo naomba maoni yenu mngependa kuikopesha kampuni kwa kuanza kuchangia kiasi gani?, mfano tukianzia na fedha za kitanzania shilingi lakimbili 200,000/= au lakimbili na nusu 250,000/=?

Pia ikumbukwe kuwa fedha hizi mnaikopesha kampuni ili kufanikisha mchakato wa soko la hisa na kama mchakato utaenda vizuri na baada ya kufanikisha kuingia sokoni na kupata kiasi cha fedha tunachotarajia kukusanya kupitia soko la hisa tutawarejeshea fedha hizo kila mmoja anayeshiriki mradi wa kilimo cha um-wagiliaji awamu ya kwanza mkoa wa Manyara. Kwa kuongezea Mkurugenzi alitoa, mfano halisi wa mchanga-nuo wa gharama kwa taasisi moja ambayo ilikua na mchakato wa kuingia soko la hisa ili kukusanya kiasi cha bilioni saba na milioni miatano kama malengo ya kampuni ya Jatu yalivyo kwa sasa na kutoa mchanganuo wa gharama walizotumia hiyo taasisi mpaka kufanikisha zoezi nzima ambapo jumla ya gharama ilikadiriwa kufikia kiasi cha fedha za kitanzania shilingi milioni miatano, kisha aliwashirikisha wanahisa wa Jatu, ili kus-hauri na kupendekeza namna ya kufanikisha zoezi lililo mbele yake pamoja na watendaji.

Maazimio:- • Wanahisa walipitisha kiasi cha fedha za kitanzania shilingi lakimbili kwa wakulima wanaoshiriki mradi wa umwagiliaji wilaya ya Kiteto-Manyara kuchangia shilingi lakimbili (200,000/=) kwa eka moja. (Itare-jeshwa) • Kwa anayemiliki hisa za jatu (mwanahisa) kuchangia shilingi elfu thelathini tu(30,000/=) na; • Kwa wale wanaomiliki mashamba ya mpunga mkoa wa Morogoro watachangia kiasi cha shilingi (20,000/=).

Page 7: TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TATU ......2 TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TATU WA WANAHISA WA JATU PLC Taarifa inatolewa kwamba mkutano mkuu wa mwaka wa tatu wa wanahisa,

7Jenga Afya Tokomeza Umasikini

MAPENDEKEZO KUTOKA KWA WANAHISAHapakuwa na mapendekezo kutoka kwa wanahisa yaliyowasilishwa ofisini.

MASUALA MENGINEYO KWA RIDHAA YA MWENYEKITIMwenyekiti aliwaomba wanahisa kwa kuwa mengi tumeshajadili ningeomba tuendelee ili kwenda na muda.

MAAMUZI YA MAHALI NA TAREHE YA KIKAO KIJACHOMwenyekiti alimkaribisha katibu ili kuwapa wanahisa mahali na tarehe ya kikao kijacho ambapo katibu aliwaambia wanahisa kuwa tutawafahamisha eneo na tarehe kabla ya siku 21 kwa kikao kijacho ili kila mmoja wetu aweze jua mapema, kwa kawaida mwaka wetu wa mkutano mkuu huwa ni mwezi wa NNE kila mwaka ambapo kwa mkutano ujao itakuwa mwezi wa nne mwaka 2020.

KUFUNGA KIKAO Kabla ya kufunga kikao mwenyekiti na mkurugenzi walitoa neno la shukrani kwa wanahisa wote, kisha kumakaribisha mjumbe mmoja kutufungia kwa sala na baada ya sala kikao kiliahirishwa rasmi saa 11:30 jioni, mpaka pale mkutano mkuu wa tatu wa wanahisa utakapotangazwa.

MAAZIMIO YATOKANAYO NA MKUTANO MKUU WA PILI WA WANAHISA UNAOISHIA MWAKA 2018Ajenda 8. • Wanahisa walipitisha gawio la faida lililopatikana kiasi cha shilingi milioni sita liongezwe kwenye hisa zao badala ya kupokea fedha taslimu.Ajenda 9. • Kupitishwa kwa makadirio ya bajeti ya fedha za kitanzania shilingi bilioni saba na milioni miatanoAjenda 10. • Wanahisa walipitisha kiasi cha fedha za kitanzania shilingi lakimbili kwa wakulima wana-oshiriki mradi wa umwagiliaji wilaya ya Kiteto-Manyara kuchangia shilingi lakimbili (200,000/=) kwa eka moja. (Itarejeshwa) • Kwa anayemiliki hisa za jatu (mwanahisa) kuchangia shilingi elfu thelathini tu (30,000/=) na; • Kwa wale wanaomiliki mashamba ya mpunga mkoa wa Morogoro watachangia kiasi cha shilingi (20,000/=).Ajenda 06. • Kupokewa kwa ripoti ya bodi na kupitishwa kwa maazimio ya kuvunjwa kwa bodi ya mpito na kuundwa kwa kamati maalum (KAMATI YA USIMAMIZI) itakayosimamia upatikanaji wa bodi mpya.

Mwenyekiti wa bodi, Katibu wa bodi,

Eva Damas Kapinga. Mohamed Issa Simbano.