madawa ya asili...madawa ya asili katika nchi za tropiki dr. hans martin hirt bindanda m’pia 1....
TRANSCRIPT
MADAWA YA ASILI
KATIKA NCHI ZA TROPIKI
Dr. Hans Martin Hirt
Bindanda M’pia
1. Mimea ya tropiki kama chanzo cha ulinzi wa afya.
Uzalishaji wa madawa na vipodozi.
anamed
Nr. 123
Anamed inalenga kuwasaidia watu
kufikia kiwango kikubwa cha kujitegemea
- kwa kulenga zaidi afya zao. Kwa
kutimiza lengo hili anamed inaendesha
semina na kufanya uchunguzi wa mimea
yenye dawa na utayarishaji wa madawa.
Anamed inalenga kufanya kazi kwa
msingi wa kutunza na kujali mazingira.
Hirt na M’pia, Madawa ya asili katika
nchi za Tropiki.
Toleo la kwanza limechapwa 2005
Haki zote zimehifadhiwa.
© Haki miliki na waandishi
Ni matumaini ya waandishi kuwa taarifa zilizomo katika kitabu hiki ienee kiasi
kiwezekanacho. Sehemu ndogondogo za kitabu hiki zinaweza kunakiliwa kwa lengo
la kuelimishana, ili mradi zitajwe zilikotoka na waandishi wataarifiwe. Hairuhusiwi
sehemu yo yote ya kitabu hiki kunakiliwa kwa ajili ya kuuzwa. Kama unataka
kutengeneza kwa wingi madawa yaliyoandikwa katika kitabu hiki, tafadhali
wasiliana nasi kwanza, kwa sababu tunaendelea kuuboresha mchanganyiko huu wa
madawa kwa njia ya uchunguzi na majaribio.
Kimechapwa na:
Toleo la pili limerudiwa kwa msaada wa Innocent Balagizo (D. R. Congo), Prof
Dr.C. Schäfer na Dr. Keith Lindsey (wote kutoka Ujerumani).
Kitabu hiki kinapatikana pia kwa Kifaransa, Kijerumaji, Kiingereza na Kihispania.
Kwa maelezo ya matoleo zaidi ya anamed, tafadhali angalia ukurasa wa mwisho.
Kwa orodha ya gharama au kuagiza tafadhali angalia toviti (web-site) yetu, au andika
kwa:
anamed (Action for Natural Medicine),
Schafweide 77,
D-71364 Winnenden,
Germany.
Email: [email protected]
Website: www.anamed-edition.com
Tafadhali usiwaandikie anamed Ujerumani kuomba nakala za bure au fedha. Kama
unaishi Afrika, Asia, au America ya kusini, agiza kupitia shirika lako lililoko Ulaya,
ambao watakulipia gharama na kukutumia vitabu.
Kitabu hiki ni kwa watu wote weusi kwa weupe
wapambanao kutafuta amani, haki na afya.
YALIYOMO
DIBAJI 7
UTANGULIZI .................................................................................... 13
SURA YA 1: MADAWA ASILI: MUUNGANO WA MADAWA
YA KIENYEJI NA SAYANSI YA KISASA ............ 18
1.1. HISTORIA YA MADAWA KATIKA TROPIKI YA AFRIKA ......... 18
1.2. DAWA YA KIENYEJI NA ILE YA KISASA ................................... 19
1.3. HOFU YA KUSHIRIKIANA ............................................................. 20
1.4. TOFAUTI ZILIZOPO ........................................................................ 20
1.5. JE, SIRI ZIFICHULIWE? HATARI KWA MADAWA YA KUSINI 21
1.6. HASARA ZA MADAWA YA KUSINI ............................................. 22
1.7. HASARA ZA MADAWA YA KASKAZINI ..................................... 22
1.8. LENGO LETU: “DAWA ZA ASILI.” ............................................... 23
1.9. MADAWA YA ASILI: FURSA KWA KANISA ............................... 26
1.10. MADAWA YA ASILI MAANA YAKE NI KUJIHUSISHA NA
SIASA! ............................................................................................... 27
SURA YA 2: MADAWA YA ASILI MIRADI KATIKA NGAZI
YA KIJIJI .................................................................... 31
2.1. KUFUNDISHA NA KUJIFUNZA ..................................................... 31
2.2. MFANO WA RATIBA YA SEMINA ................................................ 32
2.3. BUSTANI ZA MADAWA ................................................................. 35
2.4. KUKUSANYA MIMEA YA DAWA................................................. 37
2.5. KUKAUSHA NA KUTUNZA MIMEA YA DAWA ......................... 37
2.6. UTUNZAJI WA MADAWA .............................................................. 39
2.7. JUA: MSAADA KWA MADAWA YAKO ....................................... 40
2.8. KIASI NA DOZI ................................................................................ 42
2.9. KUTENGENEZA MIZANI RAHISI LAKINI YA UHAKIKA ......... 43
SURA YA 3: MADAWA YA AINA MBALIMBALI ...................... 47
3.1. MADAWA KWA MATUMIZI YA NDANI ...................................... 47
3.2. DAWA KWA MATUMIZI YA NJE .................................................. 48
3.3. MADAWA KWA MATUMIZI YA NDANI NA NJE ....................... 50
SURA YA 4: OKOA FEDHA NA JITENGENEZEE
MWENYEWE!............................................................ 51
4.1. UTENGENEZAJI WA SABUNI KATIKA NGAZI YA KIJIJI ......... 51
4.2. KUMWAGIA MAJIMOTO NA KUTOKOSA (INFUSIONS &
DECOCTIONS) ................................................................................. 56
4.3. MAFUTA YENYE DAWA ................................................................ 56
4.4. MAFUTA YA (KUJIPAKA) DAWA................................................. 58
4.5. PODA ................................................................................................. 59
4.6. ORS (maji-chumvi) ............................................................................ 62
4.7. JIWE JEUSI ....................................................................................... 64
4.8. DIVAI YA ASALI ............................................................................. 65
4.9. DAWA YA KIKOHOZI (Cough Elixir) ............................................. 66
4.10. MADINI NA VITAMINI ................................................................... 66
4.11. MAZAO KWA MIFUGO NA MATUMIZI YA KILIMO ................. 69
SURA YA 5: MIMEA 15 MUHIMU - KAZI NA ATHARI ZAKE . 72
5.1. Allium sativum: Kitunguu Swaumu .................................................. 73
5.2. Artemisia annua anamed (A3) ............................................................ 75
5.3. Azadirachta indica: Mwarobaini ........................................................ 79
5.4. Capsicum frutescens: Pili-pili ............................................................ 84
5.5. Carica papaya: Papai ......................................................................... 86
5.6. Cassia alata (syn. Senna alata): Ringworm bush ............................... 90
5.7. Cassia occidentalis (syn. Senna occidentalis): Mwingajini ................ 91
5.8. Citrus limon: Limau ........................................................................... 93
5.9. Cymbopogon citratus: Michaichai ...................................................... 94
5.10. Eucalyptus globulus: Mkaratusi (kalafulu) ......................................... 96
5.11. Euphorbia hirta: Mziwaziwa (mwache) ............................................. 97
5.12. Mangifera indica: Mwembe ............................................................. 100
5.13. Moringa oleifera: Mlongelonge ........................................................ 101
5.14. Psidium guajava: Mpera ................................................................... 104
5.15. Zingiber officinalis: Tangawizi ......................................................... 106
SURA YA 6: MIMEA 50 ZAIDI NA MAZAO YA ASILI ............ 107
SURA YA 7: DOKEZO KWA FAMILIA, WAFANYAKAZI
WA AFYA NA HOSPITALI .................................... 141
7.1. KATIKA FAMILIA ......................................................................... 141
7.2. WATUMISHI WA AFYA KIJIJINI ................................................. 145
7.3. KITUO CHA AFYA ........................................................................ 145
7.4. GHALA LA DAWA LA HOSPITALI ............................................. 147
SURA YA 8: CHAGUO LA KWANZA KATIKA TUKIO LA
UGONJWA ............................................................... 149
ORODHA YA MANENEO YA KISAYANSI NA MAELEZO
YAKE ........................................................................ 153
Tunapenda kuwashukuru wote waliochangia katika uandishi wa kitabu hiki:
Waganga wa jadi wa kiafrika, makanisa ya kiprotestanti na katoliki yanayoshirikiana
nasi hadi leo; mchoraji wa Kikongo Mr. Sugha na marafiki zake Gregor Müller,
Bindanda Nkoshi na Dorothea Layer–Stahl kwa mifano yao; Mr. M. D. Tauli wa
Organization Chestcore, Ufilipino kwa picha za mimea, vyuo vikuu katika Kinshasa,
Montpellier, Basel, Tübingen, Antwerp, Gent and Brussels vilivyoturuhusu kutumia
masalia ya vitu vya kale, maktaba na kumbukumbu mbalimbali.
Shukrani maalum kwa P. Winrich Scheffbuch, Mrs. M. Munziger, Mr. Ernst
Kranich, Mrs. U. Kohler kutoka Evangelical Assistance Programme na Mr. E. Vatter
kutoka Oberkirchenrat.
Toleo la pili limefaidi uzoefu wa washiriki wetu kutoka nchi mbalimbali pasipo
kifani: anamed Angola Annecy Ibanda, Margarete Roth
anamed Congo-Bandundu: Bindanda M'pia, Emmanuel Mufundu
anamed Congo-Kinshasha: Konda Ku Mbuta
anamed Congo Sul Kivu: Innocent Balagizi
anamed Congo-Haut Congo: Dieudonné, Umo Bombibambe
anamed Eritrea Nighisti Alazar, Micele Paliaro
anamed Ethiopia Ralph Wiegand, Alemayehu Abebe
anamed Kenya Esther Odhiambo, Walter Opiyo
anamed Mozambique Helene Meyer, Pascoal Cumbane, Dr Murray Louw
anamed Nigéria: Hannelore Bachmann, YMCA - Jos
anamed South Africa Aaron Motlhasedi, Sr. Beatrix Knubela
anamed Sudan South-west: Daniel Gumwel, James Tor, Joseph Chok, Dr Elijah
anamed Sudan South-east: Mary Yangi
anamed Tanzânia: Gideon Kibambai, Peter Mabula
anamed Uganda Kasese Thembo Patrick, Simon Challand
anamed Uganda Katakwi Oduc Naboth, Olokojo Fabiano, Ephraim Osilimo
anamed Uganda Masaka: Henry Seswannyana, Gertrude Najjemba
anamed Uganda Vurra: Samual Mundua, Buzu Venensko
anamed Uganda Kampala: Henry Seswannyana
anamed Ucrânia: Andrij Kyrtchiv
Kwa toleo hili la ki-suahili tunamshukuru Emmanuel Biligeya kwa kazi yake ya
utafsiri na Mchungaji Hezron Shimba na Maike Ettling kuhariri.
Pia tunaishukuru HUYAMU (Idara ya Afya ya kanisa la AICT - Dayosisi ya
Mara & Ukerewe) kwa ushirikiano wa karibu.
Tutafurahi kupokea mawazo yenu, lakini yanayohusu uchanganyaji wa madawa
katika kitabu hiki tu.
Tafadhali yatume kwa: Dr. Hans–Martin Hirt, anamed, Schafweide 77,
D-71364 Winnenden, Germany. Email: [email protected]
Tafadhali usiandike kuomba msaada wa fedha zako binafsi au kwa ajili ya miradi
mbalimbali. Tunapokea barua nyingi za aina hiyo, kiasi kwamba hatuwezi kuzijibu.
SHUKRANI
7
Na Hans – Martin Hirt
Katika miaka yangu sita ya mafunzo kazini katika chaka la Afrika huko Zaire, Afrika
magharibi, nilikuwa na watu ambao hawajawahi hata kukusanya ndoo ndogo ya
takataka. Chochote kiwawezeshacho kuishi ndicho ambacho wangekufa nacho,
mfano kikombe cha bati. Vijana wenye miaka 12 wanatengeneza nyumba zao kwa
kutumia malighafi ya asili pamoja na panga tu. Vyumba ambavyo hudumu kwa
miaka pasipo kuvuja. Katika 1950 wanawake walikuwa bado wanabeba magunia ya
chumvi kwa vichwa vyao njia yote kutoka baharini hadi kijijini kwetu Matamba –
Solo, umbali wa kilometa 600! Nani kati yetu angeweza kuunda mitego ya nyati,
kupanda mnazi? Nani kati yetu hana magonjwa ya meno pasipo kutumia hata siku
moja mswaki au dawa ya meno?
“Dunia ya tatu” ina kila sababu ya kujivunia. Ndiyo pekee inayoonyesha dunia
misingi ya kiasili kabisa ya jinsi ya kulima ardhi hii na kuilinda dhidi ya uharibifu
inaonyesha namna ambayo dunia yetu ingedumu kwa urahisi miaka mingi mamilioni
kadhaa.
Mwanzilishi wa msemo huu, “Dunia ya tatu“, Rais Nehru, hasa alitaka kuelezea
njia ya tatu, njia bora zaidi!
Kwa kweli “Dunia“ ya kibepari “ya kwanza” imeunda ushirikiano na “dunia ya
pili” ya kikommunist zamani ushirika wenye kuitumia dunia yetu bila huruma kama
vile hakuna kesho. Muungano huu, uliokuwa sehemu kubwa kaskazini mwa dunia
yetu, bado unaiendesha “dunia ya tatu”, ambayo kwa sehemu kubwa iko kusini, kwa
ukoloni wa kiuchumi. Kaskazini inaamuru bei ya bidhaa, inaongoza biashara,
masharti ya mikopo, na jinsi ya kulipa mikopo . Kaskazini inaamsha tamaa kwa
wateja kupitia TV za satellite na mtandao wa internet. Zaidi kaskazini inafanya
mabadiliko makubwa sana kwa mazingira ya kusini kwa kusababisha mvua ya
tindikali, kwa kukata miti na kuchimba madini katika misitu ya tropiki, na kwa
kutupia huko mazao ya sumu na takataka za sumu. Utamaduni wote unakuja na
kupita, lakini utamaduni wa kokakola ulioenea ulimwengu mzima ukitoweka, upi
utakaobaki?
Watu wa asili wakati fulani walikuwa wa ufahari wa utamaduni wao na uwezo
wao. Je, bado wanajivunia mambo hayo leo? Mara kwa mara watu kutoka Latin
America, Asia na Afrika wanaililia kaskazini kwa misaada. Nchi za dunia ya tatu
zimekaa katika mtego wa mikopo. Badala ya kutumia na kufaidika kutokana na mali
asili yao, na kutumia pesa kuinua hali yao ya maisha, nyingi kati ya nchi hizi
zinapendelea kununua silaha. Kwa hiyo zinazidi kuwa maskini.
Hakuna kitengo ambacho kinaona matokeo ya wehu huu kama kitengo cha afya.
Hospitali nyingi katika nchi za Afrika zisingeweza kuendelea na kazi bila kupata
madawa ya misaada kutoka nje. Ukichunguza mara moja katika maghala ya madawa
ya hospitali za Afrika utagundua kuwa Waafrika wanatibiwa kwa mtindo wa Ulaya
pekee. Hakuna ugunduzi unaofanywa juu ya utajiri mpana wa ufahamu wa mambo
ya afya upatikanao kwa wingi katika Afrika yenyewe.
DIBAJI
8
Ili kuwatuliza dhamira zao, watu wa kaskazini wanatumia dola milioni chache
kusaidia Afrika. Inaweza kuwa zawadi za makasha ya dawa za kikohozi, ambayo pia
hutokea kulinda ajira huko kaskazini. Njia yenye msaada zaidi ingekuwa kuwasaidia
Waafrika kwa:
Kuthamini walichonacho, na kujifunza upya kile walichokijua tangu mwanzo!
Hii ina maana kusambaza elimu halisi ya asili, badala ya kuingiza bidhaa kutoka
Amerika au Ulaya. Lakini kama watu wote katika maeneo ya tropiki wangetambua
hili, faida na kazi nzuri za bidhaa za viwanda vya kaskazini vingetiwa hatarini.
Ninazumgumzia makampuni yaliyochukua hati miliki kwa jambo ambalo lilijulikana
kuwa ujuzi wa kawaida katika nchi za kusini.
Tunapowauliza watu katika vijiji vya Afrika jinsi wanavyoelezea uzoefu wao wa
umaskini wanasema “sisi ni maskini kwa sababu nyinyi weupe hamtuambii siri zenu,
lakini mnachukua siri zetu na hamtulipi chochote”.
Je huu ni msemo wa kijiji hiki pekee? Hakika hapana! Balozi mshauri wa Zaire
(sasa Democratic Republic of Congo) katika Ujerumani Mr. Ziangba Begu, alikuwa
akipiga ngoma ile ile aliposema, “Nchi za magharibi haziko tayari kusikiliza
matatizo ya washirika wao. Ili kulinda ukuu wa kiufundi na kifedha, zinatunza siri za
mafanikio yake …. Kwa nini wafanyakazi wa maendeleo wanamalizia ujenzi wa
madaraja usiku wakati Waafrika wamelala?”
Sidhani kama shutuma hizi ni za kweli, lakini hisia hizi zinabaki kwa namna
fulani: Misaada mingi ya maendeleo imewafanya Waafrika kujisikia ni wa hali ya
chini.
Hapa siongelei hasira zangu na hasira za wengine dhidi ya shehena tatu zilizojaa
madawa ambayo muda wake wa kutumika umekwisha, yaliyotumwa na shirika la
misaada, wala sio juu ya dawa za kupaka miguu zilizofunguliwa tayari, wala juu ya
chakula cha kupunguza uzito kwa watoto wenye njaa, wala juu ya meno ya bandia
kutokana na watu waliokufa au mito ya silkoni ya kukuzia matiti, au chochote
ambacho kaskazini tajiri imetuma kwa hisani wakati wa miaka yangu sita katika
Zaire.
Hapana, ninaongelea juu ya kupungua kwa staha kunakowaathiri kila mmoja,
mwaka hadi mwaka, wakati ambapo 100% ya madawa yanayohitajika yanapoagizwa
kutoka nje, wakati ambapo ndege zilizojazwa na hayo zinashuka kutoka mbinguni,
mbinguni ambapo Mungu anaishi ambapo inaonekana wazi kuwa “anawapenda
weupe kuliko weusi.”
Kwa bahati nzuri, mashirika mengi yamebadilisha mtazamo. Mengine hata
yanasema na ninadhani yako sawa: “Kutoa misaada katika maendeleo maana yake ni
kufanya kila linalowezekana kuzuia watu kusini wasiwe kama sisi huku Kaskazini!”
Kuna mifano mingi, wengi wamegundua kuwa ibada zetu za Jumapili ambazo mara
nyingi hazina raha na zilizopoa hazifai kupelekwa nchi za nje, na wameomba
washirika katika Latini Amerika kuunda “Thiolojia inayoendana na utamaduni wao.”
Wengine wanajua hatari ya udongo wa Afrika kupata sumu kutokana na madawa ya
kuua wadudu kama ilivyo katika Ulaya na Marekani. Kwa jinsi hiyo baadhi ya
9
misheni zinatuma washauri wa mambo ya kilimo ambao husaidia kiikolojia
kuendeleza kilimo.
Lakini ni nani sasa anaongelea mambo ya madawa kiikolojia? Katika Afrika ni
kama sijaona kabisa mitaala juu ya jambo hili! Ujuzi wetu wa madawa una hatari ya
kukaa milele pasipoonekana. Umefichwa katika kitabu kilichoandikwa kwa Kilatini
kwa manufaa ya kiwanda hicho tu. Zamani lugha ya Kilatini ilitumika kama ngao ya
kulinda walio madarakani. Martin Luther alikishambulia Kilatini cha wanatheolojia
na akawatishia katika kujistawisha. Paracelsus alikumbana na jambo kama hili pia
kwenye Kilatini cha waganga. Alikuwa na hamasa, ya kuwafundisha wanafunzi
wake katika lugha yao!
Kinyume na malengo ya kupata fedha ya maadui zake, Paracelsus aliendeleza
kutegemeana katika madawa, dini na sera za kisiasa. Alikuwa ni mwakilishi
aliyejituma katika sayansi ya uponyaji wa asili, na alifundisha jambo lililomletea
kashfa: nguvu ya mwili kujiponya wenyewe. Ilibidi atoroke kuepuka kufungwa.
Hakimu wa Basel hakufuta hukumu yake ya kukamatwa mpaka June 11, 1993 –
miaka 500 baada ya siku ya kuzaliwa kwake.
Kujificha katika “kilatini cha madawa” kunarahisisha kutengeneza fedha nyingi,
iwe katika makampuni ya nchi mbalimbali au kama mtumishi wa afya katika
hospitali kijijini. Tukirudi tena kwa Paracelsus katika safari zangu huko India ,
Nepal, Zaire, Peru, Romania na Ukraine, sijaona bango lolote lenye kutangaza juu
ya nguvu za mwili kujiponya wenyewe. Kama kiwanda hakiko tayari kutoa siri zake,
inakuwa hata muhimu zaidi kwa pamoja na wananchi wa maeneo ya tropiki,
tugundue na kushiriki siri za asili.
Dini haiwezi kutenganishwa na afya.
Katika hotuba zangu katika vyuo vikuu huko Ujerumani, wanafunzi walitoa hoja,
“Mradi huu wa madawa ya asili ni mzuri sana, lakini kwa nini uunganishwe na
kanisa?” Kwa upande wangu jibu ni rahisi. Katika nchi za tropiki mara nyingi kanisa
ni kitengo pekee ambacho bado kinaruhusiwa kuelezea mawazo mengine, kupinga,
kama Yeremia alivyothubutu kusema, “………pandeni Gileadi enyi watu wa Misri,
mkachukue dawa ya marhamu, mmetumia dawa nyingi bure, hakuna
kitakachowaponya nyinyi,” (Yeremia 46:11). Kama ungekuwa mwakilishi wa
kampuni ya kutengeneza madawa, ukadiriki kutamka mara moja tu kwa sauti mbele
ya wamiliki wa kampuni hilo au wateja wake, unafukuzwa kazi, huenda ungegundua
mara moja jinsi kusini na kaskazini zinavyofanana, katika namna za mamlaka na
uendeshaji.
Ukweli ni kwamba serikali nyingi zimeuachia mfumo wa afya kwa makanisa na
misheni. Lakini hata katika hali mbaya ya makanisa na misheni kujiondoa kwenye
tiba, watu hawaasi. Angalau hilo ndilo jambo nililoliona Zaire: Wagonjwa wanakufa
kimya kimya kwa magonjwa yaliyo rahisi kutibiwa. Tuliangalie swala hili,
magonjwa hayawafanyi watu kuwa na mwamko wa kisiasa bali huwahuzunisha,
huwachosha na kuwakatisha tamaa.
10
Biblia, watu, afya na vitu vya
asili kuwa kitu kimoja
Katika mataifa mengi, kuna mashindano
baina ya mahospitali HOSPITALI YA TAIFA
ina upungufu wa fedha, ni chafu, haipokei
misaada kutoka nje, lakini ina gharama nafuu
sana. HOSPITALI YA KANISA, ni safi, hupata
madawa kutoka nje, lakini kwa sababu ya
gharama za matibabu, haipati watu.
Lengo letu ni kwamba WAKRISTO wawe
katika mfumo wa serikali au kanisa
watengeneze HOSPITALI ZA MADAWA YA
ASILI yaliyo rahisi kwa maskini na ghali kwa
matajiri, iliyo safi, yenye wingi wa madawa ya
asili, mahali ambapo pesa ndogo inayopatikana,
inatumika kuagiza dawa ambazo nafasi yake
haiwezi kuchukuliwa na miti ya madawa,
mahali ambapo pia huduma ya kiroho inatolewa.
Hii ndiyo sababu kitabu hiki kimetolewa bila
kutoa udhuru, katika mazingira ya imani ya
kikristo. Tunajaribu kuyachukua mambo haya
kwa ujumla, kuhudumia akili, mwili na roho,
kuhudumia ardhi, kuheshimu watu kwa jinsi
walivyo, na wao ni kina nani, ikiwa ni pamoja na miti yao ya madawa, uzoefu na
ujuzi wao kwa miti hiyo.
Wakati nilipokutana na mwakilishi mkuu wa madawa ya kienyeji ya kihindi
(ayurveda) huko New Delhi mchana mmoja, alianza kwanza kunifundisha dini,
ungeamini hilo? Masaa mawili! Alisema huu ndio ulikuwa msingi wa ayurveda,
vinginevyo nisingeweza kuelewa nguvu ya uponyaji wa miti.
Matumizi ya vitu vinavyopatikana katika mazingira yetu siyo tu yana msingi wake
katika Biblia, bali pia yako kwenye kiini cha malengo ya Shirika la Afya Duniani
(W.H.O.). Tangu 1977, maazimio mbalimbali ya (W.H.O.) yamekuwa yakihitaji
madawa ya asili yachunguzwe na kutumika. Kutendewa kazi kwa maazimio haya
ndiyo jambo lililobakia. Kwa jinsi hiyo hata nyakati zilizopita kidogo, askofu wa
kiafrika ameomba msaada wa lita 1,000 za dawa ya kikohozi pasipo kujua kuwa mti
wa homa ulio karibu na kanisa lake una kila kitu ambacho viwanda vya madawa
vimechukua na kutumia katika uzalishaji wa bidhaa zake.
Aidha Amerika kusini inaagiza vidonge na vichupa vya dawa na drip kutoka
Ulaya au Marekani pasipo kujua kuwa vitu vingi vinapatikana kutoka katika
“magugu” yanayoota kando ya nyumba.
Hali hii haivumiliki
Ufahamu wa muhimu utaenezwa namna gani? Katika D.R. Kongo, vyuo vikuu vingi
vya serikali vimefungwa kwa miaka mingi sasa. Vitabu vya madawa ya asili
11
vitapatikanaje? Hata vingepatikana wanavijiji wasingevielewa, watumishi wa afya
wasingepata nafasi ya kuvisoma na madaktari wasingeviweza.
Katika nchi za tropiki kwa sababu ya vita, umaskini, bei za bidhaa kuongezeka,
kuongezeka kwa ukiukaji sheria, karibu 80% ya watu wote hawawezi tena kupata
madawa yanayoitwa ya “kisasa”. Lakini pia ujuzi wao juu ya miti yao ya madawa
umepotea. Wazungu wamekuwa wakishutumu kwa miongo mingi, mambo yote ya
kichawi na kishirikina, wakati huo huo wameshutumu pia madawa mazuri kabisa ya
kienyeji ya miti shamba.
Kilichobaki ni balaa ya utupu wa ujuzi wa Afya
Leo kuna matangazo mengi juu ya miti ipi itumike kwa magonjwa yapi na katika
nchi gani – Lakini hata hivyo ni taarifa kwa ufupi au kwa uhitaji wa kisayansi.
Yanakosa maelekezo ya muhimu kabisa kwa wale wanaohitaji kutumia habari hizo.
Mwenzangu ndugu Bindanda M’Pia, na mimi tumeamua, kwa jinsi hiyo, kuandika
kitabu hiki kwa namna tofauti. Hiki ni kitabu kinachotakiwa daima kukaa karibu na
wewe, siyo kitabu rahisi tu kielezacho mambo ya mchanganyiko wa madawa au
kitabu cha gharama kilichofungwa kwa dhahahu. Kwa tahadhari zote tunakuomba
ujali kwamba kitaweza kuelezea tiba mbalimbali zinazotokana na uzoefu. Uzoefu
huu ni wa watu maskini kabisa wasioweza kununua hata asprini, (asprini ni alama ya
“kuwa tajiri” katika nchi nyingi), na pia wale “matajiri,” watu wa kisasa
wanaochagua kwa vyovyote iwezekanavyo kuishi bila kutumia vidonge na sindano,
kwa sababu wanaamini swala hili liko katika kujiamria juu ya usalama wa afya zao.
Kitabu hiki kimesomwa sana na wasomi ambao wana mtazamo wa ukosoaji wa
viwanda vya madawa, na wanaotaka kuwasaidia watu katika kujitegemea, badala ya
kutegemea bidhaa zinazoingizwa kutoka kaskazini. Ambao wanataka watu walio
katika nchi za tropiki,”kuinua vichwa vyao juu sana”.
Ni vizuri kwamba taarifa nyingi zimetunzwa katika vituo vya Kumbukumbu za
kimataifa na katika Internet, na kitabu hiki kimefaidika kutokana na taarifa hizo,
lakini kwa sasa ujuzi wa mambo hayo unatakiwa kusambaa hadi kufika mahali
ambako utafanyiwa kazi. Kwa hiyo katika kitabu hiki, tumepanga kuelezea:
Baadhi ya miti fulani muhimu ya madawa.
Magonjwa na dalili ambazo inaweza kutibu.
Baadhi ya michango kwa ajili ya kutengeneza madawa na maelezo juu ya
matumizi yake
Tahadhari na madhara ya madawa hayo.
Hili toleo la pili limerudiwa kutokana na jinsi ambavyo tumekuwa tukijifunza kwa
kuwa tumekuwa tukiendesha semina zetu katika nchi nyingi za Afrika. Toleo hili
limefaidika kutokana na uzoefu na mlisho nyuma toka kwa watumia madawa,
waganga wa miti shamba, madaktari na wanasayansi, ambao mara nyingi
wanajishughulisha na makundi yao ya anamed (Action for Natural Medicine) katika
maeneo yao.
Tunakilenga kitabu hiki kwa watu walioko nchi za tropiki, wanaopenda kujitolea
kufanya kazi, na kutumia ufuzi na mazoezi kwa faida za marafiki zao, majirani,
hospitali na jumuiya mbalimbali.
12
Watu wanaharibu ghala la asili la madawa kwa:
A. Kutumia magome katika madawa ya kienyeji.
B. Kuchoma mkaa.
C. Kuwasha moto pori.
B
A
C
13
Na Bindanda M`Pia
Kama ungekuwa mwalimu wa shule ya msingi katika nchi za tropiki na
unasumbuliwa na maumivu ya viungo ungetakiwa kutumia pato lote la mwezi (US $
11) kununua dawa ya kupaka kwenye maumivu hayo (50g) katika duka la madawa
mjini! Hii ilinitokea Kinshasa (D.R. Kongo). Kwenye kasha utasoma kwamba kitu
kinachotibu ndani yake ni capsicum frutescens. Kwa bahati mbaya hujui kama
ambavyo mimi sikujua – kwamba hii ni pilipili, mmea ambao katika eneo la tropiki
hustawi karibu kila mbele ya mlango wa nyumba ya mtu. Kwa kutumia pesa hiyo
sasa tunaweza kuzalisha kilo 3 za dawa hiyo katika kijiji chetu.
Leo nchi za “dunia ya tatu” zinajitegemea; watu waliotawaliwa zamani sasa
wanafanya maamuzi yao na wanatatua matatizo yao wenyewe. Hiyo ni nadharia -
vitendo ni tofauti! Atakayetembelea miji na majiji ya nchi hizi ataona hali ifuatayo:
Matangazo mbele ya maduka yakisema “Bidhaa kutoka nje” yaani vitu vya gharama,
vitu vya anasa kwa wateja wa daraja la juu. Vitu vingine vyote vinaitwa “vitu vya
kienyeji”, yaani vya bei rahisi, na thamani ndogo, kiasi kwamba katika kijiji chetu
bidhaa hizi zinaitwa, “ndombe” – nyeusi!
Sababu ya kuvibeza vitu tunavyotengeneza kwa ufundi wetu (na kwa wakati huo
kuwadharau pia wenzetu wenye ujuzi huo) ina mzizi wake huko kaskazini na kusini
pia. Kutoka kaskazini vinakuja vivutio mbalimbali na zawadi za watalii, na
mawakala wa maendeleo wa serikali ambao hutumia sehemu iliyo kubwa ya misaada
“wanayotoa” kwa bidhaa waliyozalisha katika nchi zao. Kusini, ni mwanakijiji wa
kawaida, ambaye ufahamu wake juu ya maendeleo ni kuuza bidhaa wanazozalisha
kijijini hapo katika mji ulio jirani na kununua bidhaa za viwanda kutoka huko mjini,
au vizuri zaidi, kutoka nje.
Mifano ifuatavyo imechukuliwa kutoka kijijini kwetu:
Mifugo bora na yenye afya huchukuliwa na kuuzwa mjini. Kisha wanakijiji
wananunua nyama za kwenye mikopo ambayo ina nyama ya hali ya chini.
Mama hulazimika kuuza unga wa mihogo wenye lishe kwa sababu binti yake
aliye sekondari anapenda kununua biskuti zilizotengenezwa kibiashara,
ambazo hudhuru meno yake.
Ili kununua unga wa maziwa baba anakata miti adimu iliyohifadhiwa kwa
miaka maelfu na anaichoma ili kutengeneza mkaa. Lakini kuwanywesha
watoto wao maziwa ya unga toka Ulaya inahatarisha maisha yao wakati maji
yasiyochemshwa yakitumika kuchanganyia au wakati chupa zinatumika pasipo
kufanyiwa usafi kuua vimelea hatari.
Nta nzuri kabisa ya nyuki hutupwa baada ya asali kuvunjwa. Kisha dawa ya
viatu yenye nta bandia yenye ubora mdogo inaingizwa nchini na kuuzwa kwa
bei ya juu.
Wanakijiji wanalipwa pesa kidogo kwa mafuta yao ya mawese yenye thamani.
Huko mjini yanauzwa tena kwa bei ya juu zaidi na kisha yanauzwa huko
Ulaya ambako mafuta ya gharama kama vile Palmolive na mengine
UTANGULIZI
14
yanatengenezwa kutokana na hayo mawese. Kisha yanasafirishwa hadi Afrika
tena na kuuzwa kwa bei ambayo mtu hawezi kwa sababu yana “mafuta ya
tropiki”.
Karanga zinauzwa nchi za nje ili kutengeneza karanga zilizokaangwa, mafuta
ya karanga, siagi ya karanga, na vipodozi, ambavyo baadaye huingizwa tena
nchini na kuuzwa.
Mtoto mwenye ukosefu wa lishe anategemea kula mayai matatu
yaliyopatikana kwenye kiota cha kuku lakini baba aliyauza ili kununua
kokakola.
Wakati watoto wanacheza mpira wa chungwa bichi, mama yao anachezea
fedha ya familia kununua dawa ya kuongeza afya ya kitoto chake, dawa
iliyotengenezwa kutokana na maji, sukari , rangi ya vyakula isiyo asili na
ladha ya machungwa ya kuunda.
Na kwa jinsi hiyo familia, vijiji, mikoa na taifa vinaendelea kuzama ndani kabisa ya
umaskini.
Jambo la kusikitisha kabisa katika Afrika ni upotezaji wake wa mali asili
Moja ya mali asili hizi ni ujuzi. Ulaya kama
maktaba ikifungwa jamii hupiga yowe. Pamoja
na hayo katika Afrika na sehemu zote za
kusini, maktaba yote imezikwa kwa pamoja na
kila mzee anayefariki.
Kwa miaka sita Dr. Hans-Martin Hirt na
mimi tulifanya kazi kwa ushirikiano wa
shughuli za kitabibu za kanisa katika Zaire,
Afrika Magharibi, katika kijiji cha Natamba-
Solo katika wilaya ya Kwango. Katika mkoa
kuna daktari moja tu kwa watu 100,000, hata
leo mwaka 2001. Watoto wanakufa kwa njaa,
kuharisha na minyoo. Kama matokeo ya
barabara mbaya mfanyabiashara mmoja tu
hufanikiwa kufika kijijini kwetu kununua
mazao ya kilimo; kwa jinsi hiyo watu watawezaje kupata fedha ya kutosha kununua
madawa?
Tumeongelea hali yetu katika semina na mamia ya waganga wa kienyeji, manesi,
wachungaji na wengine. Walitutia moyo kufanya utafiti wa ujuzi wa Afrika huko
Ulaya, ujuzi ambao tumefanikiwa kuugundua tena katika vitabu na majumba ya
kumbukumbu katika vyuo vikuu vya Ulaya huko Gent, Antwerp, Brussels, Basel,
Tübingen, Heidelberg na Montpellier. Taarifa nyingi juu ya mimea ya madawa ya
Waafrika wa eneo la tropiki, zinapatikana Ulaya – kwa kutumia kitabu hiki tunazileta
Afrika.
15
Kitabu hiki hakifichui siri za ndani. Ni uonyeshaji wa Elimu ya zamani.
Michanganyiko mingi ya madawa imehakikishwa kwa majaribio maelfu mengi ya
kisayansi na mipango ya utafiti ya siku hizi ambayo haifahamiki kwa wananchi wa
kawaida.
Ni tiba gani ambayo ungechagua: “ya asili” au “ya kikemia”? Kuna baadhi ya
magonjwa ambayo ni vizuri zaidi kutumia madawa ya kikemia. Kwa swala hili
linajitokeza swali lenye kuhoji kama mgonjwa wa maeneo ya tropiki ataiweza bei
yake. Kuna magonjwa ambayo hata hivyo mimea yenye dawa inafaa zaidi kutolea
tiba. Baadhi ya mimea hii ni adimu sana, kama mbafu (Canarium schweinfurthii) au
ni magumu kuyatengeneza kwa wingi, kama mziwaziwa (Euphorbia hirta), au
inaweza kuvunwa miaka 100 baada ya kupandwa katika maeneo yaliyo magumu
kufika, kama vile miti adimu sana ya tropiki, kiasi kwamba viwanda vya madawa
haviifurahii ingawa matibabu yake ni bora zaidi.
Kwa bahati mbaya baadhi ya mimea ya madawa haifanyiwi uchunguzi kabisa.
Magonjwa ambayo ingeweza kutibu, mfano river blindness, wakati wote
yanawaathiri wale walio maskini sana kiasi cha kutoweza kuhimili bei ya dawa zake.
Kwa mara ya kwanza tuliandika kitabu hiki kwa Kifaransa kwa ajili ya maeneo ya
Afrika yanayoongea Kifaransa. Baadaye tukapokea maombi ya kitabu kuandikwa
kwa Kiingereza na lugha nyingine kutoka Amerika Kusini, Kenya, Uganda na
Kameroon. Kama matokeo ya utafiti na uzoefu wetu, na ujuzi na taarifa za wasomaji
wetu na washiriki katika semina zetu, katika toleo hili tumebadili baadhi ya
michanganyo ya madawa kadhaa na kuweka mimea mipya.
Katika kitabu hiki tunajadili mimea ya madawa ambayo inastawi karibu maeneo
yote ya tropiki. Kimetolewa siyo kwa watu wawezao kuona jua, mchanga na mateso
tu katika nchi hizi bali kwa wale waliojitoa kikamilifu kwa uelewa wa namna
nyingine wa maisha, kifo, utajiri, muda, afya n.k.
“Yule anayeithamini mimea ya tropiki anaonyesha kuwathamini kuwathamini
wakazi wa eneo la tropiki pia!” Dr. J. Courtjoie, mwandishi maarufu wa vitabu vya madawa katika Kongo.
Tumekiandika kitabu hiki kwa lugha rahisi kiasi inavyowezekana. Lengo kuu la
kitabu hiki ni kufundisha wananchi wa kawaida - hapana, kufundishana! Maswali
yanayoweza kujadiliwa, kwa mfano, ni haya: Je, tunaujua mmea huu? Unaitwaje?
Tutauita jina gani baadaye? Je, tunautumia katika namna na kwa magonjwa
yaliyoelezwa katika kitabu hiki? Tunategemea madhara gani? Tunawezaje kuulima,
kuutayarisha na kuutunza?
Uelewa wetu wa “madawa ya asili” ni tofauti na ule wa “madawa ya kienyeji ya
magharibi na kusini.” Kwa mfano unavyoeleza: Mama wa kiafrika anataka kumtibu
mtoto wake ugonjwa wa kuhara. Katika hospitali ndogo aina ya Loperamide
inatumika ili kupunguza kasi ya kuharisha. Mganga wa jadi anaweza kuchomeka
kizibo katika njia ya haja kubwa ya mtoto. “Njia“ zote hizo siyo sahihi. Njia sahihi
ingekuwa kuchanganya vifaa vya asili, maji, chumvi na sukari, kutengeneza maji –
chumvi.
16
Kama hospitali yako inahitaji sukari na chumvi kwa ajili ya majichumvi, usiagize
vitu hivyo toka nchi za nje ambavyo vina takataka nyingi. Bali tengeneza
mchanganyiko huu kwa kutumia kwa wingi uwezavyo kile kinachopatikana katika
mazingira yako, pamoja na msaada wa kifedha toka nchi za nje kama ikihitajika.
Madawa ya asili yanawasaidia watu kuwa na mwamko kwa sababu wao ndio
wanawajibika zaidi kwa maisha yao.
Uzoefu wa kutumia taarifa zilizo katika kijiji chetu huko Zaire ulitufundisha
kwamba madawa ya asili yanawapelekea watu kuishi maisha yenye afya zaidi, yenye
kujithamini na yenye mafanikio zaidi bila hayo maisha kuwalazimisha kuhitaji fedha
zaidi kuliko zamani.
Ukiwa mzungu unatembelea nchi fulani katika tropiki, kitabu hiki kinaweza
kukusaidia kwa magonjwa yako. Au, unafanya kazi katika maeneo ya tropiki? Kama
ni hivyo tunaomba msaada wako katika eneo lako ili kwamba madawa ya asili
yaingizwe mashuleni na vyuo vikuu. Kwa njia hii “madawa ya asili” yatakuwa
“madawa ya darasani”.
Au wewe ni nesi mzungu, mganga au mtengeneza madawa? Ujifanye mtaalamu,
au zaidi yake, wape wenyeji wa eneo hilo nafasi, muda na hata msaada wa kifedha ili
wajifunze juu ya madawa hayo ya kienyeji, jinsi yanavyotumika, na kisha fanya
semina mbalimbali.
Kazi inayotakiwa kufanywa ni kubwa. Kwa kufanya kazi na madawa ya asili kwa
miaka 20, bado tunaendelea kupata mimea ya madawa muhimu na inayotumika
ambayo hakuna taarifa hata moja ya uchunguzi iliyoandikwa katika benki za taarifa
350 dunia nzima.
Tunatia kipau umbele madawa ya asili
na njia za maisha za asili.
Mtu anaweza kujiuliza kama “madawa ya
asili” yanaweza kuchanganywa katika
mfumo wetu wa madawa ya kisasa ya
viwandani. “Tusingependa hivi, badala
yake tunasisitiza kwamba, kinyume chake
ndiyo iwe njia bora. Tunatia kipaumbele
“madawa ya asili” na njia za maisha za
asili - swala ambalo limekuwa la “kisasa”
katika baadhi ya sehemu za Ulaya, na sasa
ni swala linalopamba moto katika nchi za
tropiki vile vile. Kisha tunaangalia dawa
zinazotoka nje, dawa za kibiashara, kutusaidia kwa yale matukio ambayo madawa ya
asili peke yake hayatoshi.
17
Juu: Kamati ya kijiji ikijadili jinsi ya
kuanza kutumia madawa ya asili.
Kati kushoto: Mganga wa “kisasa”
anajadili na mkunga wa jadi juu ya mimea
ya madawa.
Kati kulia: Mtawa akijaribu sigara ya
mpapai (Carica papaya); angalia sura 5.5.
Kushoto: Ni bora zaidi kuzika madawa
ambayo wakati wake wa kutumia ulipita.
18
SURA 1:
1.1. Historia ya madawa katika tropiki ya Afrika
Katika Afrika madawa ya kienyeji yamekuwepo na yamekuwa yakitumika kuliko
vile tunavyoweza kufikiri. Waafrika walijua kujitibu na kujilinda kwa kutumia
mimea hata kabla wakoloni weupe hawajaja na kutambulisha dawa zao za “kisasa”.:
Hata mbinu za upasuaji kama kushona mishipa ya damu zilifanyika. Kujikinga kwa
madawa pia kulikuwepo. Waafrika waliishi kwa miaka milioni 4 hivi katika hali ya
hewa ya hatari sana. Ni lazima tukubali kuwa madawa yaliyokuwepo kabla ya
madawa haya ya “kisasa” yalikuwa maridadi sana.
Ebu fikiri, leo China ina madaktari wapatao 20,000 katika hospitali 597 ambao
wanaganga kwa madawa ya kienyeji. Maswala ya uuguzi huko Asia hayakuteteleka
kwa sababu wamepokezana taarifa toka kizazi hata kizazi kwa njia ya maandishi.
Lakini katika Afrika na sehemu za Amerika kusini elimu ya utamaduni imekuwa
ikisafiri kwa njia ya maneno ya mdomo pekee. Kwa sababu ya maisha ya kuhama
hama, vita baina ya nchi na watu kuhamia mijiji, elimu yote inaendelea kupotea
polepole, na mambo waliyofanya wazee hayathaminiwi tena.
Tiba ya kienyeji inajumuisha kutibu kwa mimea kunakofanywa na waganga wa
miti shamba (katika D. R. Kongo wanaitwa “Kimbuki”), tiba ya kiakili, inayofanywa
na makasisi wa madawa na wenye maarifa (kiganga), na matatizo ya mzimu
yanayotibiwa na waonaji, watabiri (kingunza) wanaotegemea zaidi maono na ndoto.
Elimu hii iliendeleaje? Baadhi ya matabibu wa kienyeji ikiwa ni pamoja na wale
watumiao mimea, wanasisitiza kwamba wanapata “nguvu ya ufahamu” kupitia
mawasiliano na mababu waliokufa, kwa njia ya kuvuviwa na kwa ndoto. Wengine
wanajifunza kutoka kwa kizazi kilichowatangulia, na kwa kuangalia tabia za
wanyama. Kwa mfano punda milia mgonjwa anaweza kutembea mamia ya kilometa
ili kutafuta mmea fulani! Na nyani aliyejeruhiwa anaweza kuishi kwa kula majani
fulani.
Dunia nzima mababu zetu waligundua ukweli kuhusu madawa kwa kutumia
“nadharia ya kufananisha,” kwa kudai kuwa, “KITU KINACHOFANANA
KINATIBU KITU KINACHOFANANA NACHO.” Mababu zetu wa Ulaya
waliamini kuwa kama jinsi jani la mchicha lifananavyo na mshale kwa hiyo ni lazima
litakuwa na chuma ndani yake na litafanya kazi ya kutibu upungufu wa damu.
Mababu zetu wa Kiafrika waliamini kuwa mzizi mwekundu unatibu tatizo la
damu, na kwamba kwa kuwa harage lina sura ya figo basi linatibu matatizo ya figo.
Karibu athari zote za mmea ziligunduliwa kwa njia za majaribio (kujaribu na
kukosea). Kwa mfano watu wengi huko Amerika kusini walipoteza maisha yao kabla
haijajulikana kuwa mranaa (Datura stramonium) ina sumu kali.
MADAWA ASILI
MUUNGANO WA MADAWA YA KIENYEJI NA
SAYANSI YA KISASA
19
Lakini ni Waafrika wangapi watakufa kabla pia hawajajifunza jinsi mmea huu
ulivyo wa hatari? Profesa Kabangu wa Kinshasa amesema: “Hakuna mtu leo
anayetegemewa kuhatarisha maisha yake wakati akifanya majaribio ya athari ya
mmea fulani!”
Kwa dhati tunaamini kwamba kitabu hiki kitakusaidia kuepukana na vifo
vifananavyo na hivyo.
1.2. DAWA YA KIENYEJI NA ILE YA KISASA
Wakoloni wa kwanza waliita dawa ya kiafrika kuwa ni ya “kienyeji,” na hata sasa
Waafrika bado wanaziita dawa za kutoka nje kuwa ni za “kisasa.” Lakini kila watu
wanaoishi, wanatengeneza vitu, wanatenda kufuatana na utamaduni wao! Hii ina
maana, kwa mfano, Aspirin na Penicillin zimekuwa dawa za kienyeji kwa Wazungu.
Hali ya hewa ya Ujerumani ni ya baridi kiasi cha kutoweza kustawisha mpapai,
lakini katika Ujerumani nzima kila duka la madawa lina vidonge vya minyoo au
kutoyeyushwa kwa chakula tumboni, ambavyo vimetengenezwa kwa kuchanganya
unga wa majani ya mpapai pamoja na vitu muhimu kwa ajili ya vidonge. Lakini kama
daktari wa kiafrika akiagiza matumizi ya mmea huu wa Afrika moja kwa moja kwa
Mwafrika, mgonjwa huyu atadhani mganga huyu amechanganyikiwa. Waafrika
wachache wanajua jinsi madawa ya Ulaya yaliyo na mimea ya tropiki!
Dawa ya kienyeji ni nini?
Katika toleo fulani mwaka 1978 Shirika la Afya duniani (WHO) lilielezea madawa
ya kienyeji kama ifuatavyo: “Madawa ya kienyeji ni ujuzi wote, wa njia
zinazoelezeka na zisizoelezeka za uchunguzi, uzuiaji na uondoaji wa hali isiyo
sawa kimwili, kiakili na kijamii, ikitokana hasa na ujuzi wa mtu binafsi na
matokeo yaliyorithishwa toka kizazi hata kizazi.” Hiyo maana inaonyesha kutokueleweka vizuri kulikopo: Kutokana na uzoefu,
Waafrika wamejifunza kutumia maji ya nanasi mbichi kuamsha hamu ya chakula.
Kwa kutumia hiyo maana, kwa hiyo, hii ni ya “kienyeji.” Huko Ulaya hata hivyo,
kwa kufuatia majaribio ya kisayansi, njia hii, ambayo ndiyo ile ile, inatumika, kwa
hiyo inaitwa “ya kisasa.”
Mamilioni ya Waafrika wamefanikiwa kuwa hai hadi leo kwa sababu ya Quinine,
ambayo inapatikana kwa hali zote: kama vidonge, sindano, katika maji ya sukari
(syrup) n.k. Lakini kwa urahisi Quinine inapatikana katika gome la mti wa cinchona.
Miti ya cinchona inastawi katika nchi za tropiki. Kwa jinsi hiyo Quinine ni dawa ya
“kienyeji.” Mmisionari wa Kihispania alijifunza siri ya kazi yake (cinchona) kutoka
kwa mganga wa kienyeji wa India.
Mfano mwingine ni dawa ya belladonna: Imetengenezwa Ulaya na inauzwa katika
mahospitali yote ya Afrika. Ina mchanganyiko wa ua la hatari linalochanua usiku,
(nightshade) ambalo kama jina lilivyo, lilitumiwa na vizazi vingi vilivyopita huko
Ulaya kwa uchawi.
Kwa hiyo, ni lazima tuelezee kila zao la mmea kwa kutumia uwezo wake wa
kutibu uliohakikishwa kama “wa kisasa.” Lakini madawa yote yaliyotengenezwa kwa
20
vitu vya asili kwa wakati huo huo ni ya kienyeji, ya asili ya nchi yaliyomo na
yalikotoka!
Dawa za kienyeji, ni vizuri zikimaanisha:
“Jumla ya shughuli zote, njia, huduma, vitu vya ziada, na jitihada za namna
yoyote (kwa vitu halisi, kiroho au vinginevyo) ambavyo kwa vizazi vingi
vimesaidia watu kujilinda na magonjwa, kuondoa maumivu na kuleta
uponyaji.”
1.3. HOFU YA KUSHIRIKIANA
Maneno yanayotumika kuelezea dawa kama ya “kienyeji au ya “jadi” na ya “kutoka
nje” au ya “kisasa” haina maana ya kila moja kuwa kinyume cha jingine. Hofu isiyo
ya msingi ya baadhi ya watu kuhusu dawa za kienyeji inajenga jambo fulani ambalo
mtu anaweza kuliita “hofu ya ushirikiano.”
Kisa kimoja kinasimulia juu ya askari wa cheo cha juu ambaye aliugua. Kwa vile
hakuamini dawa za kienyeji alikwenda kwenye hospitali ya misheni kuhakikisha
anapata huduma ya “kisasa”. Mganga akasema, “Ndugu inabidi tukupe ganzi ya
kienyeji”. “Oh! Mungu wangu! Na nyinyi pia”! Mgonjwa alisema - kisha akatoroka
hospitalini.
Habari kama hizi zikielezea hofu na kutoelewana kwa watu wenye mitazamo
mbalimbali ya kimatibabu, ingeweza kujaza kitabu. Kufuatia mafundisho yake ya
“kisasa,” juu ya madawa nurse mmoja wa Congo, alijua mimea mingi ya kizungu
inayofaa kwa madawa, lakini hakujua hata mmoja uliostawi katika kijiji chake! Na
daktari wa kizungu atawezaje kupinga madawa ya kienyeji wakati ambapo
anawezeshwa kuishi na kufanya kazi katika nchi za tropiki kwa kutegemea mkwinini
wa jadi na kemikali zitokanazo nao?
Yawezekana sababu kubwa kwa nini waganga na wauguzi hukataa madawa ya
kienyeji ni kweli kuwa kuyakubali kutawabadili kuwa wanafunzi tena, na hata
kujifunza kutoka kwa wagonjwa wao tena, watu wale wale ambao wamekuja
kuwaonyesha umahiri wao wa “kisasa”!
Tutaongelea juu ya “madawa ya kusini” tukianza kuelezea mfumo wa kienyeji
katika nchi za tropiki. Katika kizio chote cha kusini cha dunia, njia za matibabu na
mimea inayotumika inafanana kiasi cha kushangaza! Baadhi ya matabibu katika
Kongo D. R. ambao hawajawahi hata kusoma kitabu walitueleza njia za kutibu
ambazo zinatumika vilevile katika Brazili na Ufilipino. Vivyo hivyo tutauita mfumo
wa uzalishaji madawa ulioendelezwa katika Ulaya na Amerika kaskazini kama
“madawa ya Kaskazini.”
1.4. TOFAUTI ZILIZOPO
Kuna tofauti kubwa kati ya madawa ya Kaskazini na madawa ya kusini kwa namna
mgonjwa anavyotibiwa. Madawa ya kaskazini humchukulia mgonjwa kiupekee.
Katika hospitali hutibiwa na madaktari mabingwa waliofundishwa vizuri. Mafanikio
katika mfumo wa afya yanapimwa kwa viwango maalum, mfano kuna waganga
21
wangapi, fedha kiasi gani, kuna vitanda vingapi hospitalini n.k. vinavyohudumia
wakazi 100,000.
Magonjwa katika kaskazini yanaonekana kusababishwa na mambo kama kemikali
zilizovutwa katika hewa chafu au zilizoliwa kama nyongeza katika vyakula au
kuhifadhi vyakula, ulaji wa sukari nyingi, msongo wa mawazo, matumizi mabaya au
madhara ya madawa.
Kinyume chake, madawa ya kusini yanatia msisitizo katika kumchukulia mgonjwa
kama mwanajamii. Mgonjwa hukaa katika uangalizi wa familia na kijiji. Waganga
mbalimbali wa kienyeji wanaweza kuonwa kwa ajili ya mgonjwa. Wale wenye ujuzi
wa kutibu mara nyingi wana elimu kidogo, lakini wana ufahamu mkubwa wa
mahusiano. Maendeleo mazuri katika afya ya mtu yanapimwa kwa kuongezeka kwa
uhusiano mzuri kati yake na jamii. Hasa sababu za magonjwa zinaonekana kuwa
ukosefu wa chakula, ukosefu wa usafi, pasipo kujali mila, hofu ya roho mbalimbali
(pepo) na mambo kama hayo.
1.5. JE, SIRI ZIFICHULIWE? HATARI KWA MADAWA YA KUSINI
Katika semina nyingi, swali moja limekuwa likiulizwa na waganga wa kienyeji
mwanzoni mwa semina: “Mnategemea sisi tufichue siri zetu? Mtalipa kiasi gani kwa
siri moja?” Wana sababu nzuri ya kuuliza. Katika Ulaya na Marekani zaidi ya bidhaa
za madawa 7,000 zinazotokana na mimea ya dawa ziko katika soko na zinauzwa kwa
zaidi ya dola 3,000,0000,000 za kimarekani kwa mwaka!
Kwa miaka mingi tumekuwa tukikutana katika semina bila fedha yoyote kutumika
kununua siri hizo. Katika madawa ya asili tunaamini kuwa ujuzi wa sayansi
unatakiwa kujulikana kwa kila mtu - kama jinsi upendo kwa mgonjwa ulivyo - na
usilipiwe fedha yoyote. Katika kizazi hiki hati miliki ya ugunduzi ni swala lililo
katika kongamano kali. Mabadilishano ya taarifa juu ya dawa za Mungu hayana
gharama zozote, na inatusaidia wote, wenye hali na viwango vyote, kuwa na ujuzi
zaidi, na hivyo kujitegemea na kutegemeana. Kipaumbele cha viwanda vya madawa
ni kupata faida zaidi kuliko kuokoa maisha.
Tuna haki ya kuweka hoja hii ya upinzani kama kipaumbele chetu ni kinyume cha
lengo hilo. Kwa jinsi hiyo malipo yetu siyo faida, bali kufurahi kuona watu, jumuiya
mbalimbali na mazingira kwa ujumla yakiponywa na kufanywa kuwa kitu kimoja.
Hata hivyo kuna hatari tatu hivi kwenye madawa ya kusini:
1. Waganga wa kienyeji wanazidi kufa na ujuzi wao. Viwanda vinanufaika kwa
zilizotokana na ujuzi wa kienyeji ambao hawakuulipia chochote.
2. Serikali za nchi za tropiki zinaruhusu wengine kunufaika kutokana nazo kwa
kujiunga na shirikisho la biashara la dunia. Kisha mashirika ya huduma ya
kimataifa yanaruhusiwa kumiliki uzalishaji wa madawa kutokana na mimea yao
ya asili, na kuwa na haki pekee ya kuzalisha madawa na kuwauzia tena wale wale
– nchi za tropiki.
3. Hatari ya tatu inasababishwa na wakazi wa nchi hizo wenyewe. Wakati wa kipindi
cha jua sehemu kubwa ya Afrika inachomwa moto. Watu wanachoma moto
mapori kwa makusudi. Baada ya miaka mingi ardhi inapungua thamani, kwa
22
sababu virutubisho vingi vinapotea katika moshi milele! Kwa jinsi hiyo muda wa
mmea kuishi unapungua.
1.6. HASARA ZA MADAWA YA KUSINI
Katika kiwango cha kijiji, vifaa vya muhimu vya utengenezaji wa madawa mara
nyingi vinapatikana. Hata hivyo matatizo yafuatayo hujitokeza mara kwa mara:
Hakuna maji na sabuni ya kuoshea vyombo na kunawia mikono vizuri.
Hakuna vipimo vya vitu vitumikavyo kutengeneza dawa wala njia maalum ya
kuzitengeneza – kwa sehemu kubwa wivu na ugomvi baina ya hao waganga ndiyo
sababu.
Ni mara chache sana kumekuwa na kanuni maalum ya vipimo vya madawa. Kwa
mimea yenye sumu, ina maana ni tishio la maisha, hasa kwa watoto.
Mara nyingi mgonjwa hajui mmea uliotumika wala madhara yake.
Baadhi ya majina ya kienyeji yanatofautiana toka kijiji kimoja hadi kingine, mimea
mingi hujulikana tu kama “maua.”
Mchanganyiko wa bidhaa za biashara na madawa ya kienyeji vinaweza kuua watu.
Mara nyingine madawa kutoka nje ya nchi yanaweza kutumika bila kuangalia kwa
makini mwisho wa muda wake wa kutumika.
Waganga wengi hata huchanganya njia za madawa ya kisasa (kama sindano) na
uchawi.
1.7. HASARA ZA MADAWA YA KASKAZINI
Septemba 1991, Wazungu 25,000 waliikimbia nchi iliyoitwa Zaire wakati ule.
Uhamaji wa ghafla namna hiyo ulipunguza kwa ghafla kiwango cha upatikanaji wa
madawa ya “kisasa.” Matokeo yake ikawa ni vifo vya maelfu ya wagonjwa
waliotegemea madawa hayo kutoka nje. Katika hali kama hiyo wale ambao wana
madawa ya kutibu hata kiasi fulani cha wagonjwa wana bahati sana, wako katika
nafasi ya kuokoa maisha ya wengi.
Kama unajua madawa yaliyo katika mimea inayostawi kuzunguka nyumba yako,
hutatembea tena km. 10, 50, 100 kufikia kituo cha afya au hospitali wakati ukiwa
mgonjwa! Hata wakati wa misukosuko ya kisiasa, kuna hatari kwamba mahospitali
yasipate madawa. Kwa upande mwingine uoto wa asili ni ghala la madawa
tulilopewa na Mungu, ambalo kama tutalitunza, daima litakuwepo kwa ajili yetu
kutumia.
Madawa ya mitishamba hayana gharama yo yote ukilinganisha na madawa ya
kuagiza toka nje! Hutegemei tena fedha, na wagawaji wa dawa wa mbali. Kama
mkitengeneza madawa ya kunywa na kupaka n.k. nyinyi wenyewe kijijini, watu
wataponyeshwa , wenyeji watapata ajira, pesa itazunguka katika uchumi wa eneo
lenu. Badala ya kuvuja na kwenda kwa matajiri nchini mwenu au walio nchi za nje.
Kwa ufupi kila mmoja ananufaika.
Kama wewe ni daktari au mhudumu wa afya katika hospitali na umejifunza
kutengeneza madawa kutokana na maelekezo ya kitabu hiki, unaweza kuokoa fedha
23
ya kigeni ya kutosha ambayo ingetumika kununua, kusafirisha na kutunza madawa,
kwa nyongeza unaepuka usumbufu na gharama za ushuru wa forodha na kanuni zake
mbalimbali.
Chukua kwa mfano D. R. Kongo: Mgonjwa akija kununua dawa hushangaa jinsi
gharama yake ilivyopanda. (Mnamo mwaka 1993 thamani ya fedha ilishuka kwa
100% kwa juma na ilisababisha magonjwa yasitibike). Mgonjwa siyo tu kwamba
analipia dawa, bali analipia pia madeni ya nchi, madeni ya fedha ambayo hajawahi
kuiona, mara nyingine kwa fedha iliyotumika kununua silaha, na madeni ya benki ya
Dunia inamtaka ayalipe. Hata hivyo madawa ya Kusini mara nyingi hufanya kazi
kwa kubadilishana: Tohara moja kwa mfano, ni kuku mmoja!
Mganga wa kienyeji hutibu mgonjwa kikamilifu na matatizo mengine
yanayomzunguka. Hatibu dalili au ugonjwa kwa pekee (mfano surua, minyoo, kifua
kikuu) bali pamoja na mgonjwa mwenyewe, pia huangalia matatizo mengine kama
kukosa ajira, mazao kutostawi, ugonjwa wa mapenzi, kukosa watoto.
1.8. LENGO LETU: “DAWA ZA ASILI.”
Waafrika wameshangazwa na “wimbi la kijani.” linalofurika katika maduka ya
madawa huko Ulaya . Katika kila duka la madawa huko Ujerumani hukuta mimea
400 na chai (dawa za maji) nyingi za mimea mbalimbali zisizohesabika.
Mungu ametupa bure mimea ya maua 500,000. Karibu mimea 50,000 inatumika
kwa madawa ya kienyeji. Kutokana na WHO karibu mimea 10,000 imefanyiwa
uchunguzi kisayansi na kutolewa maelezo. Hivyo hubakiza idadi ya mimea 40,000
kufanyiwa uchunguzi ! Bado tuna kazi kubwa!
Baada ya majaribio marefu ya jinsi ya kuelezea mitazamo yetu kwa madawa,
tunachagua neno “dawa za asili” ambalo kwa sasa tunalielezea kama ifuatavyo:
“Dawa za asili” ni mchanganyiko wa faida za madawa ya kusini na zile za
madawa ya kaskazini.
Dawa za asili ni za asili kwa sababu, kwanza zimetokana na asili, na pili ni kitu
kilicho wazi na cha asili kufanya jambo kwa kutumia zana zinazopatikana. Hii ina
maana kwamba ili kutumia dawa za asili, waganga wa jadi kutoka eneo la kusini,
wahudumu wa afya, madaktari na watumishi wa maendeleo, wenye ujuzi katika
madawa ya kaskazini, wanatakiwa kujitoa kujifunza kutoka katika namna ya kutibu
na uzoefu wa kila mmoja. Kwa jinsi hii huduma muhimu ya afya, inayoweza kuhimili
kulegalega kwa siasa na uchumi vinaweza kuimarishwa.
Kitabu hiki kimeandikwa kwa lengo hilo. Kupitia matumizi yake, tumeona kuwa
tayari watu binafsi na jamii kwa ujumla wamejitegemea zaidi katika kuzuia na kutibu
maradhi. Mamia wamepata ajira kwa kulima hii mimea ya madawa na kisha
kutengeneza haya madawa. Maelfu ya watu wameweza kutibu malaria, kuhara na
magonjwa mengine. Jambo hili na liendelee - katika ngazi mbalimbali ! Kwa sababu
katika kila nchi huduma ya afya inafanyika katika ngazi zifuatazo:
1. Dawa za nyumbani: Madawa yaliyo katika mfumo wa familia, huko kaskazini,
kwa mfano, matumizi ya chai ya mranaa, kusini matumizi ya mbegu za mpapai.
24
2. Dawa za “ngazi ya wilaya” au za hospitali: Madaktari na wauguzi mbalimbali
huko kaskazini, na madaktari na waganga wa jadi kusini, pamoja na ujuzi wao
maalum.
3. Madawa ya chuo kikuu: Uchunguzi na ufundishaji kuhusu madawa na jinsi ya
kuyatumia.
“Dawa za asili” zinapaswa kutumika katika ngazi zote tatu zilizotajwa hapo juu.
Dawa za nyumbani ndicho kipaumbele, kwa sababu kituo cha afya cha muhimu na
chenye manufaa zaidi ni nyumbani. Wakati wa vita vya wao kwa wao na njaa katika
nchi za tropiki mchango nyeti katika kudumisha afya nzuri katika jamii hufanywa
kwa kuongeza ujuzi na utaalamu zaidi katika ngazi ya familia.
Maendeleo yanayoendelea ya uendelezaji madawa ya hospitali ni hatua ya pili
muhimu, kwa sababu huko pia wagonjwa watanufaika na uwezo wa kuponya wa
madawa ya mimea.
Dawa za asili lazima pia zifike ngazi ya tatu, chuo kikuu, ili kupata jinsi ya kutoka
huko na kuwarudia wananchi. Nchi kama Tanzania, Uganda na Cameroon
zitanufaikaje na kufundisha waganga katika madawa ya magharibi pekee? Matokeo
yake ni kwamba waganga wengi wanahamia nchi zilizoendelea ambazo zina vifaa
vya kisasa mahospitalini na zinalipa mishahara mikubwa. “Pori ni kwa ajili ya
wamissionari, siyo kwa ajili yetu wataalam” niliambiwa na mganga kijana katika
nchi ya Peruvia akiwa katika mji mkuu wa nchi hiyo.
Kwa jinsi neno “dawa za asili” litakavyokuwa lenye kuaminika katika tiba, kwa
vyovyote kazi ya tiba vijijini itakuwa na nafasi ya kuvutia, kwa sababu maduka
mengi ya madawa yatakuwa na madawa mengi bora zaidi kuliko mjini!
WEWE NI MWANASAYANSI!
WEWE NI MWANAMAENDELEO!
Kwa makusudi kabisa hatukuweka dawa za kichawi katika kitabu hiki. Baadhi ya
mimea inatumiwa na wale wanaoitwa waganga ili kumtafuta mwenye hatia wakati
kosa limetendwa. Waganga wababaishaji au wachawi humpa dawa mtu mmoja,
kutoka mmea wenye sumu ili anywe, na mtu mwingine dawa kutoka kwenye mmea
unaofanana na huo lakini usio na sumu. Mtu wa kwanza akifa inatangazwa kuwa
mababu wamepitisha hukumu juu ya mtu huyo kwa hiyo atakuwa ni mwizi. Mambo
kama hayo yanaamsha hofu na kuchukuliwa na vijana kama mambo yaliyopitwa na
wakati na yasiyo ya kisasa, na hii ni sababu moja wapo ya vijana kuhamia mijini.
Madawa ya asili yanaunganisha sayansi, madawa ya mimea na upendo, lakini siyo
uchawi wala viini macho.
Katika Ujerumani, matangazo ya biashara za madawa katika Television wakati
wote yanafuatiwa na sentensi, iliyozoeleka lakini ya muhimu: “Kwa hatari na
madhara ya dawa soma maelezo zilizoko ndani na tafuta ushauri toka kwa mganga au
mtengeneza madawa.” Hata hivyo hizo hatari na madhara hayo hayawezi kuepukwa
hata kwa madawa ya mimea pia. Kila dawa za mimea na zile za kemikali zote zina
madhara mengi. Madhara makuu yanaweza kuonekana kwa mgonjwa mmoja,
yasionekane kwa mgonjwa mwingine, na hata kuwa ya hatari kwa mgonjwa
mwingine. Kwa mfano mmea utumikao kutibu mapigo ya moyo yaliyo chini
25
(hypotension) unaweza kumuua mtu kwa mapigo ya moyo yaliyo juu (hypertension).
Kwa sababu hii hatuwezi kuwajibika na matokeo ya hatari ya kutumia miti shamba.
Kwa maneno mengine: unahusika na wewe mwenyewe ni mwana sayansi. Hii
inahusisha kujifunza daima kutokana na uzoefu wako, na kuwa na mahusiano ya
karibu na waganga wengine, ili kwamba ujifunze kutokana na uzoefu na ujuzi wao.
Waganga wa miti shamba huko Amerika ya kusini wanaitwa “Curiosa” –
wadadisi.
Hii ndiyo maana ya “maendeleo”: Kuwa mdadisi, kuwa tayari kubadilika!
Kwa jinsi hiyo swali la msingi ni: Ni kwa njia gani waganga na wauguzi, ambao
mara nyingi wamefunzwa 100% katika madawa ya kaskazini, watafanya kazi na
waganga wa jadi na wakunga kwa faida ya maskini na watu fukara? Watawezaje
kuwa “wadadisi,” kuwa tayari kiakili kujifunza pamoja?
Tangu mwaka 1985 tumekuwa tukiendesha semina ambazo zimeshirikisha
waganga kutoka sehemu zote mbili . Matokeo ni:
Watu wengi wananufaika: kamati za afya za msingi zinachagua wawakilishi
kuhudhuria semina ambao hutoa taarifa tena kwa wananchi waliowatuma ili
kwamba wote wajifunze mambo mapya.
Waganga wa mahospitalini wanafaidika: Wanapata kujua umuhimu na athari za
madawa ya mimea, na wanaanza kujifunza namna mpya za uuguzi.
Waganga wa jadi wananufaika nayo: wanajifunza jinsi ya kutoa kozi zinazofaa,
jinsi ya kutunza dawa vizuri zaidi, na wanajua hasa elimu ya afya ni nini.
Mabadilishano huwasaidia waganga kutibu magonjwa mengi zaidi kuliko awali.
Wakunga wa jadi wanafaidika: Hawalazimiki tena kufanya kazi yao kinyume cha
sheria, lakini wanaruhusiwa kufanya huduma kwa wajawazito, kuzalisha na kutoa
huduma ya watoto wachanga kwa ubora zaidi. Zaidi ya hayo wanasaidiwa jinsi ya
kufundisha wanafamilia, jinsi ya kusaidia kinamama wajawazito. Siyo hivi tu –
mwanzo mkuu wa maambukizi ya UKIMWI katika Kongo D. R. inatokana na
waganga wa jadi 40,000 wanaozunguka zunguka (wasio na mafunzo)
wamchomao sindano kila ahitajiye kwa kutumia sindano zisizo salama au zenye
usalama kiasi kidogo. Waganga na wakunga wa jadi waliofunzwa wanaweza
kutoa huduma bora zaidi bila kusambaza UKIMWI.
Tamaduni za kitropiki zinafaidika kutokana na kuboreshwa kwa huduma za afya
za jadi.
Watu binafsi wanafaidika: Mtu kujitengenezea dawa siyo tu kwamba inampa ajira
bali pia humjengea fahari.
Hata jamii za vitu vyote vya asili vinafaidika: Kupanda miti yenye madawa siyo tu
kwamba inatuletea dawa bali pia kivuli na mvua, ardhi inapata rutuba, na chakula
na makazi ya wadudu, ndege na wanyama vinapatikana.
Makanisa yanafaidika kwa uzoefu wetu: Siyo tu wakati wa semina bali hata
baadaye, baadhi ya makanisa yamekuwa na mahudhurio mazuri zaidi kwa sababu
afya njema ni wazi kuwa ni faida kwa mwili, akili na roho. Baadhi ya wachungaji
sasa wanashirikisha manufaa ya mimea ya madawa katika mahubiri yao kama
“habari njema.”
26
1.9. MADAWA YA ASILI: FURSA KWA KANISA
Madawa ya asili huyapatia makanisa nafasi nzuri za mambo na kazi. Lakini kuna
matatizo. Kwanza, katika Afrika hospitali nyingi zinaendeshwa na makanisa, chini ya
uongozi wa Askofu aliyeathiriwa na Ulaya, na hata kufundishana na wakati
mwingine kutekwa na mambo ya huko. Yasikitisha kusema, baadhi ya viongozi wa
kanisa - siyo wote - wamekuwa maadui wa utamaduni wao, hata kuwa na hofu juu ya
matibabu yao ya jadi!
Pili, kwa sababu ya kukosekana kwa mimea ya madawa, waganga wengi wa jadi
katika miji mikubwa ya Afrika mfano Kinshasa, wanabadilika na kuanza shughuli
kama vile mambo ya nyota, ulozi, au “uchawi wa maneno.” Kwa sababu ya jambo
hili, dawa za jadi zinaanza kupata sifa mbaya. Dawa za asili hata hivyo, hazina
uhusiano na kuibuka tena kwa ulozi, ambao unaanza kuenea zaidi Ulaya na Amerika
ya Kaskazini.
Katika 1993 kule Kalemia, mashariki mwa Kongo D. R., wanawake 40 walikuwa
karibu kuchomwa moto kama wachawi, wakihusishwa na janga la kipindupindu.
Mauaji haya yalizuiliwa kwa jitihada ya makanisa ya kikristo, kwa kufundisha watu
jinsi huduma za afya ziwezavyo kuzuia kipindupindu. Taarifa kutoka Kenya
zilielezea jinsi watu walivyouwawa kwa mitambiko na sehemu za viungo vya
kutumika kutengenezea madawa. Hii ni changamoto kwa makanisa! Majaribio ya ki-
matibabu yaliyofanywa kwa askari wa Marekani na Urusi wakati wa majaribio ya
silaha za atomiki yalikuwa ya kikatili kwa vyovyote! Changamoto, kwa hiyo, siyo
kwamba ni kuondoa utamaduni wa Kaskazini na kuleta ule wetu wa asili, bali jinsi ya
kuendeleza utamaduni ambao unafurahisha watu, jamii mbalimbali na viumbe vyote.
Tunatakiwa kushinda - lakini namna gani? Sisi ni weusi na weupe, madaktari na
waganga wa jadi, wakristo na wasio wakristo. Uzoefu wetu kutokana na mamia ya
semina ni kama wote tukiusogelea MSALABA ghafla tutakuwa tumekaribiana.
Kama wote tukisimama kuzunguka mpapai kujifunza jinsi ya kutibu vidonda, wote
tunatumia mikono yetu na kusahau hata rangi ya ngozi yetu. Na mbegu za mpapai
zinafukuza minyoo ya tumbo kwa daktari kama zinavyofukuza kwa tumbo la mganga
wa jadi, pasipo kujali kwamba tumbo ni la mkatoliki, la mprotestanti au la mpagani!
Matokeo yake semina juu ya “Utendaji katika madawa ya asili” (Action for
Natural Medicine, anamed), juu ya mimea inayotibu, inayoratibiwa na makanisa,
itaondoa vikwazo vingi! Makanisa mengi katika Afrika wameiomba anamed
kuendesha mikutano na waganga wa jadi na madaktari, pasipo kujali imani yao. Na
wachawi wengi watumiao mitishamba walishangaa sana juu ya uwezo wa kutuliza
maumivu wa ua la Mmarakuja (passionfruit) na mafanikio ya ajabu kabisa ya
mziwaziwa katika kutibu amiba. Angalau magonjwa haya hayahitaji uchawi -hakika
hii ni habari njema kwa kanisa.
Imani ya kikristo na uponyaji vyote viwili ni watoto wa mama mmoja, aitwaye
upendo. Yesu alisema: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.” Paracelsus, baba wa
Sayansi ya tiba, alisema, “Msingi mkuu wa matibabu ni upendo.”
Katika kutibu wagonjwa tumegundua kwamba mara nyingi uhusiano wa mganga
na mgonjwa ni wa muhimu kuliko dawa. Ununuzi wa dawa yo yote siyo lazima
upelekee katika nafuu ya mgonjwa. Kuna mambo mengine ya muhimu ambayo yana
27
mguso katika swala la maisha mema ya mwanadamu, mfano – haki (2. Petro 1:1) na
upendo (1. Kor 13).
Kama ukimwuliza mwafrika kukupa maana ya utamaduni wake unaweza kusikia:
“Sisi ni wale ambao hatujagundua TV wala gari. Hatuna komputa, hatuna
sementi…………..”. Kwa nini badala yake Waafrika wasimshukuru Mungu na
kusema: “Utamaduni wetu umedumu kwa miaka maelfu pamoja na vitisho vingi
mbalimbali. Watu wanaweza kuishi bila kuathiriwa na aina nyingine ya magonjwa.
Hewa yetu, udongo wetu na maji yetu bado viko safi. Hatuwaachi wagonjwa
miongoni mwetu bali tunawahudumia kwa ushirikiano na furaha kama Biblia
inavyosema. Moyo wa furaha ndiyo dawa bora zaidi”.Tusisahau kuwa maelfu ya
wazungu wanakuja katika “dunia ya tatu.” kila mwaka kutafuta mapumziko na faraja,
na makampuni mengi ya biashara huja kutafuta faida nyingi iwezekanavyo kutokana
na utajiri wa asili wa misitu, madini na mimea.
Kanisa lina kazi ya kuhubiri na kuonyesha upendo, hiyo inajumuisha siyo tu
upendo kwa jirani, bali pia kujipenda mwenyewe, utamaduni wako, na mazingira
yako. Kanisa lina nafasi ya kuwasaidia watu kuona fahari ya maisha yao. Mtazamo
huo unaunda msingi wa muhimu ambao mtu anaweza kutumia kujenga stadi na
mambo mbalimbali ambayo yamejazwa na upendo na haki.
Mfumo wa afya wa nchi za viwanda za kaskazini uliojengwa katika kutengeneza
faida kwa wenye hisa, umeathirika. Upendo haupatikani - badala yake kuwa uchoyo
usio na huruma! Hiyo ndiyo sababu ya karibu watu 500,000 waharibu afya zao kwa
madawa ya kuua wadudu kama D.D.T. yatengenezwayo na viwanda vya madawa ya
kutibu mimea? Na hiyo ndiyo sababu ya madawa kwa ajili ya UKIMWI na
magonjwa mengine yanauzwa kwa bei ambayo wagonjwa wengine wa kiafrika
hawawezi kuimudu?
Kama wakristo tunatakiwa kuyalaani mambo haya, lakini pia tufahamu kwamba
mganga wa jadi anaweza kuwakatili vilevile kama mgonjwa atakuwa maskini kiasi
cha kutoweza kulipia matibabu kwa mbuzi.
Mifumo yote miwili hata hivyo ina faida zake. Tuchukue hizi faida za kila upande
na tuanze kufanya kazi kwa pamoja. Tuiite “DAWA ZA ASILI” na tuanze
kushughulika kupiga vita ubaguzi na kutokutenda haki kwa pamoja na jamii za kidini
na za kienyeji.
1.10. MADAWA YA ASILI MAANA YAKE NI KUJIHUSISHA NA SIASA!
Pigo la sabuni lenye madini ya zebaki (mercury) Waafrika wengi na Wamarekani wa kusini pamoja na watu wengine wengi
wamebadilisha miili yao kuwa ghala la madawa, kuwa kama ghala la kuwekea
kemikali. Watu wanakusanya miilini mwao madawa mbalimbali yanayotumika
kuhifadhi vyakula, kuua wadudu, na kubadilisha rangi n.k. ambayo yana madhara
kwa afya zao kiasi kwamba leo wakazi wa maeneo ya miji ya tropiki wana D.D.T.
zaidi katika damu zao kuliko watu wa Ulaya.
Wakati fulani jambo hili litasababisha wazaliwe watoto katika nchi za tropiki
wenye kuathiriwa na madawa kama vile watoto wa Ulaya. Leo watoto 4 kati ya 10
28
wazaliwao Ulaya wameathiriwa na tatizo hili. Kwa hiyo dawa za asili zinahusisha
kujiingiza katika siasa. Mfano mzuri kabisa ni dawa na sabuni za kuchubua ngozi.
Soko la madawa katika tropiki limejawa na vitu vitumikavyo kuchubua ngozi.
Mafuta yenye hydroquinone au beta methason, ambayo tena ni hatari zaidi. Hatari
mbaya zaidi ni katika sabuni yenye kiasi hadi 3% ya chumvi za zebaki. Vitu vyote
hivi vinazuia utengenezaji wa Melanin. Melanin ni chembe za hudhurungi au nyeusi
zinazosababisha ngozi kuwa na rangi hii ya kiafrika (nyeusi) na hivyo kufanya kazi
ya kuchuja miale ya jua. Kama matokeo ya uchafuzi wa hali ya hewa, wote tunapata
shida inayotokana na upungufu wa utando wa hewa ya ozone. Kwa sasa miale ya jua
inazidi kuwa mikali zaidi na zaidi – katika kizio cha kusini cha dunia ni zaidi ya kizio
cha kaskazini. Zamani watu wenye ngozi nyeusi waliweza kufanya kazi karibu uchi
siku nzima kwenye jua kali bila tatizo. Wajukuu wao leo wanapata shida ya
kuunguzwa na jua.
Kwa msaada wa mabaraza ya makanisa katika D.R. Kongo tunawashauri
wanawake wa kiafrika wasiendelee kuchukulia ngozi yao nyeusi kama ishara ya
umaskini, kama ugonjwa unaohitaji tiba. Ni kitendawili gani hiki: Wanawake
wanazitia hatarini afya zao kwa kuondoa rangi nyeusi ya ngozi zao, wakati wazungu
wanafanya kila jitihada kupata chembe hizo nyeusi? Kwa nini tusichukulie hiyo rangi
ya ngozi zetu kama zawadi ya uumbaji? Siyo kwamba kitita cha maua kinapendeza
sababu ya mchanganyiko wa rangi zake? Kwa nini hili liwe tofauti kwa watu?
Tunatakiwa kudai sabuni na manukato yote yanayotokea Ulaya yenye madini ya
zebaki yapigwe marufuku. Huko Ulaya vitu hivi vimepigwa marufuku karibu kuanzia
mwaka 1975. Hata Uingereza haiwezekani kuzinunua (angalau kisheria) lakini
makampuni ya kutengeneza marashi ya Uingereza na Hispania yanatengeneza sabuni
zenye zebaki maalum kwa ajili ya Afrika, au wanauza leseni za kuyatengeneza huku
Afrika. Tangu 1977 WHO imezisihi serikali zote za ulimwengu kutoruhusu matumizi
ya sabuni zenye zebaki. Lakini ni nini hasa kazi ya shirika hilo kama halina nguvu za
kuyapeleka Mahakamani hayo makampuni?
Sabuni hizi hazileti weupe uliosawa kwenye ngozi. Matokeo yake ni kuwa na
madoadoa, na wakati mwingine hata maeneo yaliyo meusi zaidi na mabaka inatokea,
ambayo waganga huita “confetti syndrome”. Hii ni kwa sababu zebaki huingia katika
ngozi kwa kiwango tofauti. Pamoja na hayo mwili mzima unapata sumu ya kudumu.
Mwanamke ambaye wakati wote anatumia sabuni hizi (jambo ambalo kwa bahati
mbaya linatokea zaidi katika D.R. Kongo, Tanzania, Uganda, Madagascar n.k.) ana
kiwango cha zebaki mara 400 zaidi ya yule asiyetumia, vibaya zaidi zebaki
hupenyeza ubongo na kuathiri akili. Zebaki hupenyeza mfuko wa uzazi vilevile;
huchanganyika na oksijeni na kuwekwa katika ubongo wa kitoto kilichoko tumboni.
Mkojo wa kitoto kichanga cha miezi mitatu ilipimwa na kuonekana una mara 140
zaidi ya madini ya zebaki yaliyo katika mwili wa binadamu. Mtoto alikuwa hajawahi
kuoshwa kwa sabuni hiyo, ni mama pekee aliyekuwa ameitumia!
Madhara zaidi ya zebaki ni ya kiakili (kuweweseka, kupotewa akili, tabia ya
kujinyonga), kutetemeka viungo, magonjwa ya figo, ama magonjwa ya ngozi ya
kuambukiza.
29
Uchunguzi wa siku hizi unatufanya tufikirie uhusiano wa vifo kati ya matumizi ya
sabuni hizi na UKIMWI (Ugonjwa ambao katika Afrika unaathiri asilimia kubwa ya
wanawake kuliko ya wanaume).
a) Zebaki huwa ni sumu katika kinga ya mwanadamu kwenye T-lymphocytes.
Inapunguza nguvu za asili za mwanadamu kujikinga na magonjwa kama
UKIMWI.
b) Kama matokeo ya kuwa na ngozi nyepesi zaidi, miale mingi zaidi ya ultra-violet –
B inaingia mwilini, pia inadhoofisha nguvu za mwili kujikinga na maradhi.
Sehemu muhimu ya madawa ya asili ni kuwafundisha wananchi kuiheshimu na
kuitunza ngozi yao nyeusi. Mwanamke mweusi atafanyaje ili ngozi yake ionekane
nzuri zaidi? Dr. Yetunde Mercy kutoka Chuo kikuu Lagos, Nigeria anashauri
matumizi ya sabuni rahisi inayotengenezwa kwa mafuta ya mawese ambayo
inatumika katika kila familia ya kiafrika (angalia sura 4:1:6). Aina hii ya sabuni pia
ina uwezo wa kuua bacteria na haina madhara ya ngozi mengi kama zilivyo sabuni
nyingine zilizotengenezwa viwandani zilizo na triethanolamine! Mwanamke yeyote
wa kiafrika anaweza kujitengenezea sabuni isiyo na madhara, ya kujipaka kwa
kuyeyusha sabuni ya kiwandani na kuiongezea mafuta ya mbegu (sura 4:1:9).
Ujumbe ulio ndani ya bidhaa nyingi katika Afrika ni “weupe ni urembo na ni mali.”
Tunawasihi wachungaji na maaskofu watoe tahadhari juu ya tafsiri hii ya
“maendeleo” na “kwenda na wakati.” Waganga, wauguzi na wanamaendeleo,
tafadhali tuitangaze kauli hii “weusi ni uzuri” katika kuelimisha juu ya afya.
1.11 AWA ZA ASILI : HITAJI LENYE MGUSO
Asili, pamoja na miti na vichaka vyake ni ghala la madawa la aina yake. Lakini
kuzidi kuwepo kwake kunategemea ufahamu wetu juu ya mambo yaliyo mazuri kwa
ajili yake na yanayoweza kuidhuru hiyo asili. Mmoja kati ya miti mitano inayostawi
hapa duniani itatoweka katika kipindi cha miaka kumi. Kwa nini? Kwa sababu kila
mwaka msitu wenye eneo kama la nchi ya Switzerland unaharibiwa na shughuli za
kibiashara: mvua yenye tindikali kutoka kaskazini, takataka zinazoingizwa kutoka
nchi za viwanda, na kutokea moto wa porini unaowashwa kwa malengo ya kuwinda
na kilimo.
Kama mganga wa jadi atadai kugundua mmea unaotibu UKIMWI ataonekana ni
mpuuzi. Kwa upande mwingine hata wanasayansi katika Amerika ya kaskazini
hawajakata tamaa. Kila mwaka Idara ya tiba ya saratani huko Amerika huchagua
mimea 1,500 - mingi ikitoka eneo la tropiki - ili kupima nguvu zake dhidi ya
UKIMWI.
Ebu fikiri kwamba kama mababu zetu wangeua fungus aina ya penicillin! Ndugu
Fleming asingekuwa na bahati ya kugundua penicillin katika mwaka 1928. Sasa ebu
fikiri: Wanasayansi wagundue dawa ya UKIMWI katika miti ya eneo la tropiki,
lakini kwa bahati mbaya mti wa mwisho wa jamii hii umetengenezewa kabati au
umechomwa ili kutengeneza shamba la mihogo. Kupotezwa kwa mmea mmoja kama
huu kungemaanisha kibali cha kifo cha mamilioni ya watu ……………….
Kwa pamoja, mimea ya tropiki inafanya kiwanda kilicho bora zaidi cha kemikali
duniani. Kwa mfano Vinca rosea, mmea wenye maua meupe na mekundu, ambao
30
unastawi mahali popote katika nchi za tropiki kama mapambo, una angalau alkaloids
65, ambazo ni muhimu katika tiba.
Mti mmoja wa Mchikichi ambao tutaupanda leo utawapa watoto wetu miti ya
kujengea nyumba, na nyua. Watapata malighafi ya vikapu, viatu, kamba, mifagio, na
brashi. Mti huu utawapatia mafuta, funza, pombe, sukari na vitamin. Na utaboresha
hali ya hewa duniani kote kwa kuzalisha hewa ya oksijeni kupitia majani yake.
Bila miti hakuna mvua
Bila mvua hakuna mimea ya dawa.
Bila mimea ya dawa maisha yetu yatategemea viwanda ambavyo vinauza mazao yake
kwetu kwa bei ya juu zaidi kadiri inavyowezekana. Viwanda havina jinsi nyingine ya
kufanya kazi: Lengo lake ni kuongeza faida, hata kama jambo hili litamaanisha
kuharibu msingi wake, yaani mazingira. Lakini sisi tuna namna nyingine ya kufanya!
Tunaweza kuchagua kama tunataka kuendelea kuharibu misitu, au kushirikiana kwa
pamoja katika mradi wa ushirikiano:
ANAMED – utendaji katika madawa ya asili!
A) Kutumia sabuni za zebaki
zinakufanya uwe “fanta juu na
chini kokakola.”
B) Vitu vya kuvutia lakini vya
hatari katika duka.
C) Wanaume huko Sudan
wanatayarisha vitu vya
kujipaka kama njia mbadala.
A B
C
31
SURA 2
Katika sura zinazofuata tutatoa ushauri jinsi kuyafanyia kazi madawa ya asili na jinsi
ya kuendesha semina na miradi katika ngazi ya kijiji na jinsi ya kutengeneza
madawa.
Mradi wa “Madawa asili” unaweza kuwa na mafanikio, ikiwa tu:
Kama watu wengi watauhitaji.
Kama utakuwa ni sehemu ya mpango mzima wa maendeleo.
Kamati ya afya ya wakazi wa mahali fulani inatakiwa kutengeneza mpango wake
maalum wa maendeleo.
Swali la msingi kuuliza ni: Ni nini tuwezacho kufanya wenyewe pasipo kuhitaji
misaada?
Kisha kamati iorodheshe mambo 10 ya muhimu. Katika uzoefu wetu mambo kumi
ya msingi ambayo yamekuwa yakitajwa ni haya yafuatayo:
1. Tunahitaji nia ya kikristo.
2. Ni lazima tuepukane na kuzagaa kwa mifugo.
3. Tuanze kupanda miti na tukate tu ile iliyotupanda sisi wenyewe.
4. Tulime vichakani – siyo misituni.
5. Tupange uzazi ili tuwe na watoto wenye Afya na elimu bora.
6. Kazi ile ile kwa wanawake na wanaume. Tusibaguane katika kazi – haya ndiyo
maendeleo.
7. Tujivunie dawa zetu za asili.
8. Usafi unazuia magonjwa – tutumie vyoo na vichanja.
9. Tuwe waaminifu kwa wenzi wetu na waangalifu, ili tuepukane na Ukimwi..
10. Tufanye kazi kwa pamoja – tujitoe kwa ajili ya miradi ya kijiji.
2.1 KUFUNDISHA NA KUJIFUNZA
Mikutano: Lengo la mkutano liwekwe wazi, mfano: kufundishana kuhusu madawa
ya asili. Mmoja achaguliwe kuwa mwenyekiti, ili kuzuia uongeaji wa holela na
kuchagua mmoja mmoja achangie juu ya ufahamu wake, mshiriki mwingine aandike
miniti, kutunza kumbukumbu za taarifa muhimu ambazo zimechangiwa na
majadiliano yoyote yaliyofanyika katika lugha yao. Ni vizuri kuwepo na wakati wa
kujieleza juu ya mada fulani wanayopendelea, ambayo imetangazwa katika kundi
kabla. Haiepukiki kwamba watu watasema matatizo yote yanayohusu afya na
maendeleo. Mambo yaliyo muhimu au yanayogusa wengi yahifadhiwe kwa ajili ya
kujadiliwa katika mikutano mingine, na yaweza yakaletwa kama mada kuu kwenye
mkutano mwingine.
MADAWA YA ASILI
MIRADI KATIKA NGAZI YA KIJIJI
32
KUTAMBULISHA MIMEA: Ni muhimu sana kwamba kila mtu aweze kuitambua
kwa usahihi mimea ya madawa ambayo wanataka kuitumia. Tembeleeni sehemu
inakostawi mimea hiyo. Angalieni kwa makini jinsi inavyofanana, umbo na rangi za
maua yake, majani na mbegu, nusa harufu yake, na hata ladha yake. Usionje kabisa
sehemu ya mmea usiojulikana. Wala, usimeze kabisa utomvu wa mmea usiojua;
unaweza kuwa na sumu.
KUTUNZA MAJANI YA MMEA: Katika kila mmea unaoujua kusanya majani,
maua na mbegu, kandamiza sehemu hizi za mmea kwa juma moja katika daftari, na
uzigundishe kwenye karatasi. Upe jina mmea. Uchore, elezea jinsi ya kuutumia na
kuutayarisha, onyesha hatari zake.
PICHA MBALIMBALI: Kama inawezekana chukua picha ya kila mmea, slides ni
bora zaidi, onyesha picha hizi vijiji vingine. Weka nguvu ya umeme kwenye betri
yenye volt 12, wakati wa mchana kwa kutumia panel ya solar. Wakati wa jioni
onyesha picha za slide kwa kutumia projector ndogo ya kubeba. Solar panel
inatakiwa iwe na volt 12 na karibia watt 6, na betri inatakiwa iwe na volt 12 na kati ya
Ah 3 – 6. Projector zinapatikana kutoka:
Radmar, 1263 – B Rand Road, Des plains, IL 60016, USA.
2.2 Mfano wa ratiba ya semina
Semina za kwanza zilizoendeshwa na Anamed zilikuwa Zaire, ambapo tulifanya
semina 2 hadi 4 ya siku moja moja kwa mwaka katika kanda mbalimbali tulipokuwa
na shughuli za afya. Leo walimu wa Anamed wanazunguka kwenye nchi za tropiki
kufanya semina kwa juma moja hadi mawili. Tunafanya semina katika eneo moja kila
mwaka kwa miaka 3. Baada ya semina ya kwanza washiriki wanategemewa
kuendesha semina wao wenyewe katika maeneo yao, na kufanya kwa vitendo sehemu
kubwa ya yale waliyojifunza. Semina katika mwaka wa pili na wa tatu zina lengo la
kuruhusu wahusika kuleta taarifa juu ya mafanikio na kushindwa kwao, na kuongeza
zaidi ujuzi wao kwa dawa za asili.
Katika muundo wo wote wa semina yako, ni bora wakaribishwe washiriki wenye
kuwakilisha aina mbalimbali za watu wanaoshughulika na madawa au katika ngazi
mbalimbali za uongozi yaani waganga wa jadi, wauguzi, madaktari, wafamasia na
wengine kutoka makanisa na serikalini n.k. Haisaidii kuwa na watu wengi hapo hasa
ikiwa hawana msukumo wa kuyatumia waliyojifunza.
Ni sera nzuri kuwaita waganga wakuu wa mikoa ili kufungua semina. Hii ni njia
bora zaidi ya kupata msaada wa ushirikiano na wale walio katika nafasi za ushawishi.
Kama wewe ni kiongozi wa semina ujue kuwa jinsi wewe unavyotibu magonjwa
yako kwa madawa ya mimea ndivyo watu watakavyotumia madawa ya asili kwa
wingi.
Katika kupanga semina, kumbuka kwamba kujifunza na kufundisha kuzuri
kunahitaji kuwepo kwa mambo mbalimbali. Na katika madawa ya asili kuna nafasi
ya kutosha kufanya hivyo. Hapo chini kuna mifano ya mambo ya kufanya:
Kuimba nyimbo na kutunga nyimbo zako mwenyewe kuhusu madawa ya asili.
33
Michango mbalimbali kutoka kwa walimu na wanasemina juu ya magonjwa na
madawa ya asili yanayojulikana
Kazi za vikundi juu ya Maswala ya kimaendeleo.
Kuzunguka kutafuta mimea na kuitambua kwa jina na kuikusanya.
Kutayarisha na kupanda bustani ya madawa.
Kutayarisha dawa.
Kutengeneza fremu ya “A”, jiko la jua, au mizani.
Kuonyesha picha za slide.
Mchango wa washiriki. Tunapata wapi rejea za madawa ya asili katika Biblia, na
wapi tena katika misemo ya kiafrika.
Huu hapa mfano wa ratiba ya mikutano ya siku tatu:
MKUTANO WA KWANZA
Siku ya kwanza
Saa 2 asubuhi: Maombi; Mithali 17:22 (Mtumishi wa Mungu wa eneo hilo).
Saa 3 asubuhi: Majadiliano: Ni magonjwa gani ya kawaida katika eneo letu.
Mfano minyoo, malaria, maumivu ya viungo? (washiriki wote).
Saa 4 asubuhi: Jinsi ya kuzuia magonjwa – njia za jadi na zile za kisasa
(Muuguzi).
Saa 5 asubuhi: Madawa ya asili ni nini? Sehemu I (angalia sura 1:1 na 1:2)
(mganga au muuguzi).
Saa 8 mchana: Papai – mmea muhimu wa dawa (sura 5:5) (mganga au muuguzi).
Saa 9 mchana: Majadiliano : Tunatumiaje mpapai katika eneo letu? (Mganga wa
jadi).
Saa 10: Utengenezaji wa dawa moja ya kuzuia minyoo na nyingine ya kuua
minyoo na “sabuni ya majani” (kutokana na maelezo ya sura 5:5).
Saa 1 Jioni: Mhadhara juu ya mpango wa uzazi kwa picha za slide.
SIKU YA PILI
Saa 2 asubuhi: Maombi: I Nyakati 16:33, Zaburi 96:12 na Isaya 10: 18 – 19.
Saa 3 asubuhi: Rudia papai; nendeni kuzunguka kwa pamoja na kuhesabu miti ya
mipapai kijijini.
Saa 4 asubuhi: Angalieni mimea ya Artemisia annua.
Saa 5 asubuhi: Mimea inayotumika kutibu malaria (angalia sura 8).
Saa 8 mchana: Utengenezaji wa dawa za mafuta (sura 4:3) (washiriki wote).
Saa 10 mchana: Majadiliano: Tutumie miti aina gani kwa kustawisha misitu?
Saa 1 jioni: Picha za slides za mimea ya madawa - bila maelezo kutoka kwa
walimu, washiriki watoe maoni yao juu ya kila picha.
SIKU YA TATU
Saa 2 asubuhi: Maombi: Matendo 3:16
Saa 3 asubuhi: Wimbo juu ya afya (uliotunga mwenyewe)
Saa 3:30: Nini maana ya madawa ya asili? Sehemu II (angalia sura I).
Saa 4:30
asubuhi
Majadiliano (wanaume): Tufanye nini ili kuzuia watu kukimbia
mjini kwa kukosa kazi vijijii? Majadiliano (wanawake):
34
Tutawezaje kuwalisha watoto chakula bora zaidi kwa kutumia kile
tulichonacho? Tumepata taarifa gani katika somo hili?
Saa 5 asubuhi: Uchaguzi wa watu watakaohusika kuandaa semina nyingine.
Saa 5:30: Maombi ya kuagana.
MKUTANO WA PILI
SIKU YA KWANZA
Saa 2 asubuhi: Wimbo uhusuo afya.
Saa 3 asubuhi: Maombi ; Kutoka 15:26 Ayubu 13:4.
Saa 4 asubuhi: Rudia: Madawa ya tiba na kinga. (washiriki wote wachangie
uzoefu wao).
Saa 5 asubuhi: Ameba - Tumia darubini kuzifanya zionekane na kuzitambua
(Muuguzi).
Saa 8 mchana: Mziwaziwa (sura 5:11) - mmea ulio mzuri kupambana na ameba.
Kutengeneza chai (dawa) kutokana na mmea huu.
Saa 9:30
mchana:
Kutengeneza sabuni (sura 4) (kwa vitendo)
Saa 1 jioni: Kuonyesha picha za slide zihusuzo UKIMWI.
SIKU YA PILI
Saa 2 asubuhi: Maombi – Uaminifu , mila na desturi, na UKIMWI (Zaburi
40:11, Kor 13, Rumi 13:10).
Saa 2:30
asubuhi:
Wimbo uhusiano Ukimwi (uliotungwa na washiriki).
Saa 3:00: Marudio - amoeba, mziwaziwa
Saa 4:00: Malaria - Kinga, huduma /tiba za kisasa (Muuguzi), tiba za jadi
(mganga wa jadi). Kubadilishana uzoefu.
Saa 9:30: Jinsi ya kufanya kama mtu ana homa (sura 7:3). Majadiliano
kati ya wauguzi na waganga wa jadi.
Saa 8 mchana: Tembelea bustani ya mimea ya dawa ya kijiji au anzisha bustani
ya mimea ya dawa.
Saa 9 mchana: Wanawake: Jukumu la mkunga wa jadi Wanaume:
Jinsi ya kupanda na kutumia mkaratusi (sura 4:1)
Saa 10 jioni: Kutengeneza sabuni za urembo na sabuni ngumu (sura 4:1).
Saa 1 jioni: Magonjwa ya ngono - kuzuia kwa njia za kisasa na za jadi.:
Majadiliano katika makundi -Wanaume peke yao na wanawake
peke yao, na baadaye kwa pamoja.
Saa 3 usiku: Kuonyesha picha za slide zilizochukuliwa katika semina ya
kwanza.
SIKU YA TATU
Saa 2:00
asubuhi:
Maombi – jinsi ya kutunza mazingira yetu ya asili (Mwanzo
2:15, Kumb. 20:19, Zaburi 96:12)
Saa 3:00
asubuhi:
Kuharisha – jinsi ya kutengeneza aina mbalimbali za maji
chumvi (angalia sura 4:6).
35
MKUTANO WA TATU
Mkutano wa tatu upangwe na washiriki wa kila kundi wao wenyewe. Hata hivyo
wanaweza kukualika wewe na watu wengine ili waweze kupata msaada zaidi au
mchango. Waumini wa kanisa kwa mfano wanaweza kukutanika ili kujadili somo
hili: “Kanisa na dawa za asili” na wakunga wa jadi, waganga wa jadi, au wauguzi na
madaktari wanaweza kukutana kujadili maswala muhimu ambayo ni mahsusi katika
kundi lao.
Semina pia zinaweza kutolewa kwa makundi maalum, mfano watumishi wa afya
“wa kisasa” kutoka maeneo makubwa, au watumishi wa idara ya madawa katika
mahospitali ya kanisa.
2.3 BUSTANI ZA MADAWA
Tunatengeneza bustani mbili tofauti kwa kazi tofauti tofauti. Moja kwa ajili ya
maonyesho nyingine kwa ajili ya uzalishaji.
1. Bustani ya maonyesho
Bustani hii ni ndogo na inafanya kazi ya kuwasaidia watu kujifunza juu ya mimea
mbalimbali. Bustani hii ni kwa watu wote! Katika hospitali kwa mfano, iwekwe
karibu na lango kufuata uzio wa hospitali ili kwamba kila apitaye aweze kuiona.
Panda jamii moja hadi mbili za kila mmea ambao unajulikana kutumika katika
madawa ya jadi. Weka alama ndogo kwa kila mmea kwa kutumia kwa mfano
vipande vya plastiki visivyotumia au mabati. Katika hizo alama andika majina mawili
ya mimea, la kibotania na la kienyeji, na matumizi yake – tumia wino usioharibiwa
na maji. Panga ratiba ya watazamaji, kila upatapo nafasi. Waonyeshe wageni wako,
karibisha wanafunzi wa shule zilizo karibu na uwaelezee juu ya bustani, na
wakaribishwe watu siku za jumapili baada ya ibada ya asubuhi.
2. Bustani ya uzalishaji Hii bustani ya pili ni kwa ajili ya uzalishaji. Hapa utastawisha ile mimea pekee
unayohitaji kwa ajili ya mpango wako wa madawa ya asili. Bustani kama hiyo hata
hivyo itakuwa ya matunda na mboga. Bustani hii inaweza kuwekewa uzio. Na watu
wanaweza kuingia tu kwa makaribisho.
Anza kwa mimea ya ua wa kuzuia mmonyoko au mimea ya ua yenye kurutubisha
ardhi. Panda hii mimea ya ua katika mistari kwa umbali wa meta tatu kwenye
mteremko na meta tano kwenye tambarare, lakini wakati wote kwa kufuata mistari ya
kontua. Tengeneza ua angalau kwa jamii tatu tofauti za mimea; unaweza
kuchanganya mchaichai, mlongelonge, lesena, calliandara, Cassia spectabilis,
Tephrosia vogelii (kibaazi), mbaazi, n.k. Siha mbegu za miti kwa umbali wa
sentimeta 10 tu (mfano calliandra na lesena) au panda matawi (mfano ya Cassia
spectabilis) kwa ukaribu zaidi, tuseme sentimita 50 hivi.
Mara tu hizi nyua zinapostawi, panda mimea yako ya madawa katikati yake.
Epuka vitalu vya mimea pekee, ni vizuri kupanda katika mchanganyiko, au hata
kuichanganya kama ambavyo inaota porini. Kwa jinsi hii mimea inajitengenezea
kivuli, na hapa inawezekana kupata mavuno wakati wa ukame pia.
36
Chunguza kwa kujaribu na kukosea, kupata hali zinazofaa kwa kila mmea; jua la
moja kwa moja la savanna; nusu ya kivuli kama kwenye vichaka, kivuli kabisa kama
porini udongo kichanga ama tifutifu, maji mengi au kidogo.
Kata hiyo mimea ya ua kwa urefu wa mita 1 wakati wa mwanzo wa kipindi cha
mvua, na changanya katika udongo hayo majani uliyokata ili udongo uwe na rutuba
kila mwaka na kulisha mimea ya dawa.
KUTUNZA MBEGU: Baadhi ya mbegu (mfano: embe, chungwa, limao, papai)
zinahitaji kupandwa mara moja. Nyingine kama za mbogamboga, maua na nafaka
zinahitaji kukaushwa kwa majuma mawili hadi matatu.
Weka kila aina kwenye bahasha ya pekee. Andika jina la mmea na siku ya kuvuna
juu ya bahasha. Tunza bahasha hizi kwenye chombo kilichofungwa kabisa ili kuzuia
wadudu na wanyama wasizishambulie. Ili kuzitunza zikiwa kavu kabisa weka mkaa
mpya uliotayarishwa kwa kupikia, baada tu ya kupoa, katika chombo hicho. Au jaza
10% ya chombo kwa mchele uliokaushwa sana, au 0.5% kwa “silica gel”
(inapatikana kwa wakemia). Silica gel huwa ina chumvi ya cobalt iliyoongezwa,
husababisha iwe ya bluu iwapo kavu, lakini huwa pink ikiwa na unyevu. Silica gel na
mchele vinaweza kukaushwa tena na tena kwa jiko la jua au kwa taratibu kwenye
moto kidogo. Ikiwezekana, tunza hicho chombo ulichotunzia mbegu kavu katika
jokovu. Tunza mbegu zenye sumu mahali wasikofika watoto!
KITALU CHA MITI: Kwa miti mingi mbegu zake huhitaji kupandwa katika
udongo mzuri au mboji katika chombo kidogo (mfano: mifuko ya plastiki, au majani
ya migomba yaliyokunjwa kama kikombe kidogo. Hiki kitalu cha miti kinaweza
kulindwa dhidi ya jua kali, mvua na wadudu. Mimea michanga ikipata nguvu ipande
nje. Kumbuka umbali wa mmea hadi mmea kwa mimea iliyokomaa.
Mimea mingine inaweza kuzalishwa kwa wingi kwa kutumia matawi yake.
Mfano, Cassia spectabilis, (angalia sura 6:12) pia miti yote ambayo imepandwa na
kuchipua kwenye ua wa jirani yako!
KUTAYARISHA MASHIMO YA KUPANDA MITI:
Udongo wenye rutuba sana (wa porini): geuza udongo kwa koleo kisha panda
miche au matawi.
Karibu na nyumbani: Usichimbe shimo refu sana kwa choo chako. Kisha lifunike,
na baada ya miezi mitatu au zaidi, chini yake chimba shimo karibu meta tano. Juu ya
hiyo choo ya zamani, jaza takataka za mimea, kama magamba ya ndizi, majani na
matawi, na udongo kiasi: panda mti wa tunda juu yake mara moja.
Katika Savana yenye rutuba ndogo:
a) Kwa upandaji wa miti: Panda meta moja toka mti hadi mti, chimba kina cha
koleo 1 – 2 chini. Chagua mti ambao hauna umuhimu sana kwa watu, kama
vile Cassia spectabilis (sura 6:12) au Mwarobaini (Azadirachta indica, sura
5:3). Kwa mwingajini, chomeka kijiti cha nusu meta chini kisha kimwagilie
vizuri. Kwa kutumia njia hii, mti mmoja wa mwingajini unaweza kuwa baba
wa msitu wote! Mwarobaini unastawi zaidi kwa kupanda mbegu. Kata nyasi
mara kwa mara kuzunguka miti hiyo, hadi meta tatu kutoka kwenye shina.
37
Wakati wa mwanzo wa kipindi cha ukame, choma moto kuzunguka miti hiyo
kuepusha miti michanga kuteketewa na moto wa porini.
b) Kwa miti ya matunda au madawa: Chimba shimo kama 70×70×70 sm. Jaza
kwa mboji matawi, majani machanga, takataka za mimea za jikoni, majivu n.k.
Funika kwa udongo asilia. Kwa uzoefu wetu miche na matawi ya kupanda
vinaweza kupandwa moja kwa moja juu yake. Mwagilia maji na zuia jua kali
na wanyama wazagaao.
2.4 KUKUSANYA MIMEA YA DAWA
SEHEMU: Pata mimea hiyo toka sehemu iliyo safi, kamwe siyo pembeni mwa
barabara.
WAKATI: Maua na majani yanaweza kuvunwa mara mmea unapoanza kuchanua, ni
wakati ambao mmea una kiasi kikubwa cha dawa. Kama itawezekana, kwa
kuchemsha au kuloweka sehemu ya mmea, tumia majani mabichi au maua mabichi.
Kama hii haiwezekani unatakiwa kuyakausha na kuyatunza. Baadhi ya utayarishaji
wa madawa unahitaji majani mabichi au maua. Mfano, dawa za mafuta na za kupaka.
Mizizi na mboga zinazostawi udongoni (mfano karoti) ni nzuri kuvunwa mwisho wa
kipindi cha mvua. Matunda yana vitamini nyingi zaidi yanapoiva. Kwa sababu za
kitabibu, baadhi ya matunda yanatumika kabla ya kuiva. Mfano: papai kwa vidonda
vyenye kutoa usaha. (angalia sura 5:5).
MATAYARISHO: Mizizi inatakiwa kuoshwa na kusuguliwa vizuri. Ni mara chache
majani yanahitaji kuoshwa, (isipokuwa mijini tu). Tupa majani yote yaliyokufa,
yaliyoshambuliwa na wadudu, mba au ugonjwa wowote.
KULINDA MIMEA: Unapohitaji mmea mzima, chukua uliozeeka, uiache iliyo
michanga. Ukihitaji mizizi, chukua mizizi ya ziada, na uache mingine na mzizi mkuu
bila kuujeruhi! Kama huhitaji mizizi ya mimea, iache mizizi chini ili ichipue mmea
tena. Ukihitaji gamba, chukua sehemu kutoka katika matawi! Usikate gamba kutoka
katika shina. Hii ndiyo tabia mbaya katika madawa ya jadi, na mti utakufa kama
utafanya hivyo. Ukihitaji majani chukua machache tu kutoka tawi lolote. Chukua
majani kutoka matawi yanayoelekea katikati ya mti, kwa sababu ni mara chache
yanatoa matunda. Stawisha na uendelee kulima mimea mingine – wewe na watoto
wako mtayahitaji.
2.5 KUKAUSHA NA KUTUNZA MIMEA YA DAWA
Mara nyingi mimea mibichi ni bora kwa tiba kuliko iliyokaushwa. Kwa hiyo
hakikisha wakati wote una mimea yenye nguvu na afya katika bustani yako ya dawa!
Mara nyingine ni muhimu kukausha mimea yako. Mfano, ukitaka kutengeneza
mafuta, dawa ya kujipaka au sigara ya dawa kutokana na mimea ya dawa.
Wakati mwingine unatakiwa kutunza mimea ya dawa. Mziwaziwa kwa mfano,
haupatikani wakati wa ukame. Kwa hiyo uvunwe na kuhifadhiwa wakati wa kipindi
cha mvua.
38
Kwa kulinda salama na kutumia mimea ya dawa na
miti ya dawa anzisha bustani ya dawa.
39
KUKAUSHA: Kwa vile kitabu hiki kinatumika katika mazingira mbalimbali palipo
na joto na ubaridi, palipo na unyevu na ukame, ni vigumu kutoa maelekezo
yanayoweza kufaa mahali pote. Hata hivyo, kama “sheria ya msingi”, hakikisha
umekausha mmea wako katika namna ambayo utakuwa umekauka kabisa baada ya
siku tatu.
1. Tayarisha mimea yako: Mizizi lazima ioshwe vizuri. Osha mbegu na majani kama
tu machafu, mfano mijini. Maua hayawezi kuoshwa.
2. Kama tu majani yatahitajika, toa vikonyo vyote, kama ni muhimu, pia nyuzi za
majani (mfano: majani ya mpapai). Kata kata majani kama unavyokata mboga kwa
kawaida. Vipande visiwe vikubwa zaidi ya sm 1.
3. Wakati wote kausha maua kivulini. Kausha matunda na mizizi kwenye mwanga
wa jua. Kausha majani kwenye jiko la solar, kama lipo au masaa machache
kwenye jua kali. Majani yakiwa yamepoteza unyevu karibu wote, endelea
kuyakausha kivulini. Sehemu nzuri ya kukaushia ni dalini, chini ya paa ili mradi
sehemu hiyo ni safi.
Wakati wa majira ya mvua, majani yanaweza kuwa bado yana unyevu hata baada
ya siku hizo tatu za ukaushaji. Katika hali hii yaweke katika jiko la jua, lakini acha
mfuniko wazi ili joto lisizidi 50˚.
KUTUNZA: Kama unataka kutunza mimea yako ya dawa, huna budi kusimamia
ukavu wake. Jambo hili linaweza kufanywa kwa kutumia kipima unyevu
(hygrometer). Chenyewe pamoja na kiganja kizima cha mimea mikavu ya dawa
viwekwe katika chombo kisichopitisha hewa kwa dakika 15. Jedwali lifuatalo
linaonyesha muda ambao mimea yako itakaa katika chombo hicho wakati wa joto.
Unyevu hewani
unaopimwa kwa
hygrometer
Unyevu wa mmea Mmea utadumu kwa
60% 6% Miezi 4
50% 5% Miezi 6
40% 4% Mwaka 1
Kwa kutumia mbinu hii unaweza pia kujua ni kwa muda gani vyakula vyako
vikavu, kama unga wa muhogo, mahindi na maharage vinaweza kutunzwa na kwa
muda gani mbegu zako zinaweza kutunzwa kabla hazijapoteza uwezo wa kuota.
KUHIFADHI: Huwezi kuhifadhi mimea katika mifuko ya karatasi kwa sababu
wadudu wanaweza kuishambulia na inaweza kupata unyevu. Kama imekaushwa
sana, na imefungwa vyema katika chombo cha glass, plastic au metali inaweza
kutunzwa kwa muda mrefu.
2.6 UTUNZAJI WA MADAWA
Vijidudu vinasubiri kila mahali kushambulia na kuharibu madawa yako.
Vinapatikana katika mikono, vyombo, chupa, katika hewa, katika maji (kama
40
hayakuchemshwa vya kutosha) … kwa ufupi, kila mahali! Tunawezaje sasa kutunza
dawa zetu zenye thamani ya uhakika tuliyojitengenezea majumbani?
Ili kutunza uhalisi na umaridadi wa dawa vifaa vilivyo safi wakati wa kutengeneza
dawa; vifanye kuwa safi kwa kuvichemsha.
Bidhaa inaweza kudumu kwa ubora kama:
Itakuwa kavu sana (mfano: unga (poda)).
Itakuwa na sukari nyingi (mfano: syrup)
Itakuwa na chumvi nyingi (mfano: samaki aliyepakwa chumvi).
Itakuwa na kileo kingi (mfano: tincture)
Haichachi (mfano: mafuta)
Amua mwenyewe unavyotaka kuhifadhi dawa yako. Kwa mafuta tunashauri
mawese ya kujitengenezea, mafuta ya shea (mandingo) au mafuta ya biashara
(madukani). Baadhi ya mafuta yanayotengenezwa nyumbani hayadumu muda mrefu
(kama mafuta ya karanga).
Umande ni tishio kwa aina za unga na mimea iliyokaushwa. Viwanda vinatumia
kemikali kuhifadhi bidhaa, lakini kemikali hizi zinaweza kutuathiri, kwa hiyo
tunapendelea vifaa raslimali tuliyo nayo katika kukausha dawa zetu; kwa nini
usitumie jua!
2.7 JUA: MSAADA KWA MADAWA YAKO
Jua ni la muhimu kwa uhai wote kutoa mwanga na nishati. Tuonyeshe njia mbadala
na njia ile potovu ya kuchoma miti na mafuta . Tutumie nguvu ya jua kama teknolojia
inayotufaa. Na kwa kufanya hiyo tutachangia kulinda mali asili iliyo muhimu sana
kwetu kwa siku zijazo! Tunaweza kunufaika na hii dhana ya ajabu, ya bure, kwa
kutengeneza JIKO LA JUA (angalia picha).
Kwa kupikia na kuokea.
Kwa kukaushia chakula ili kukitunza, mfano, mahindi, karanga, udaga, na
katika mikoa mingine panzi kama senene n.k.
Kwa kuyeyusha masega ili kutenganisha na asali.
Kukausha nguo.
Kuondoa chawa kwenye nguo.
Kuwaua wadudu waliovamia chakula.
Kutengeneza dawa ya kujipaka, wakati wa kuyeyusha vitu (kwa kuweka
chombo ndani ya maji ya moto kwenye jiko la jua).
Katika hospitali, kuua na kuzuia kuzaliana kwa wadudu kwenye vifaa
mbalimbali (sterilization).
Ni rahisi kutengeneza jiko la jua kuliko ambavyo ungedhani. Sehemu yake kuu ni
kasha/sanduku. Linaweza kutengenezwa kwa kutumia vitu mbalimbali: Mbao, bati,
plastiki, udongo wa mfinyanzi au kapu. Ndani ya kasha kunawekwa vitu mbalimbali
vya kutunza joto, kama nyasi, karatasi, pamba, maranda au matambara ya nguo.
Sehemu ya ndani ya kasha inatengenezwa kwa bati lililonyoshwa kuondoa matuta na
41
KAUSHIO LA JUA
a = kioo
b= aluminium foil
c= ubao
d= kopo cheusi
A) Kaushio la Jua: hewa inagia
chini, kupata joto na kukausha
majani au matunda kama
maembe yaliyowekwa kwenye
nyavu.
B) Jiko la jua (solar oven):
Sanduku linalofungwa na vioo.
Mfuniko (ulio na aluminium
foil) unawekwa kufuatana na
jua.
C) Kaushio la jua, Ilitengenezwa na Chuo Kikuu Hohenheim,
Ujerumani. Urefu wake ni mita 18, upana wake ni mita 2, eneo la
kukaushia ni 20 m². Inafaa sana kwa kukausha majani na matunda ki-
biashara.
42
kisha kupakwa rangi nyeusi. Kasha linafunikwa kwa kioo, ni bora vikibebana viwili.
Mwanga wa jua unafyonzwa na uso mweusi ulio ndani ya jiko hilo na vyombo vyeusi
vya kupikia. Miale ya mwanga wa jua inabadilishwa na kuwa joto. Joto linaweza
kufikia 100˚ - 180˚C, kutegemea na ukali wa jua na jinsi jiko lilivyozibwa na kujazwa
vizuia joto kutoka. Kiakisio cha mwanga (maana yake ni kifuniko cha kasha
kilichofunikwa kwa karatasi ya aluminium) kinasaidia kuakisi mwanga wa ziada
katika kasha. Unaweza kutengeneza kasha (jiko) lenye ukubwa wowote kufuatana na
mahitaji yako binafsi. Kama vioo havipatikani unaweza kutumia karatasi za plastiki.
Kwa maelezo zaidi ya utengenezaji angalia katika kitabu cha anamed “Use Water
Hyacinth!” rejea ukurasa 160.
Kama huna chombo cha kukaushia, tumia mfuko wa plastiki usio na rangi, na
kasha linalotosha ndani yake. Weka mimea yako ya dawa ndani ya kasha, na kisha
ndani ya mfuko wa plastiki, weka kwa pamoja kwenye jua. Kwa jinsi hii joto ndani
ya mfuko litafika haraka 80˚C, juu zaidi ya joto linalohitajika kukausha madawa ya
mmea, ambayo yanatakiwa kukaushwa kwa joto lisilozidi 50˚ C. Kwa jinsi hiyo
hakikisha kasha umeliweka wazi kwa kiasi fulani.
KAUSHIO LA JUA: Rejea picha (SOLAR DRIER) Hii ndiyo njia bora na ya haraka ya kukausha mimea ya madawa bila kuharibu viini
maalum vya mimea ambavyo vingeharibiwa na miale ya ultraviolet au joto kali zaidi.
Hewa hupita katika nafasi kati ya ubao unaoteremka uliopakwa rangi nyeusi na kioo
kinachoufunika. Hewa inachemshwa, inakwenda juu na kupitia katika bomba. Mimea
ya dawa inayotakiwa kukaushwa inawekwa kwenye nyavu zilizofungiwa kwenye
hilo bomba.
JINSI YA KUTENGENEZA RANGI NYEUSI YA KUPAKA CHOMBO CHA
JUA
Kama unataka kuhakikisha kuwa rangi nyeusi haina madini yoyote yenye sumu,
unaweza kujitengenezea rangi mwenyewe. Nunua black ferric oxide (inapatikana
kwenye duka la mkemia na gram 5 zinatosha kwa kutengenezea jiko moja.
Ichanganye na varnish ya mbao au chuma isiyo na rangi. Unaweza kujitengenezea
varnish mwenyewe kwa kutumia mafuta ya kawaida au utomvu mzito. (Rejea sura
6:10, elemi). Au, kufanya kipande cha metali kiwe cheusi, weka mbegu za mafuta
(karanga, au mbegu za mbono) katika sufuria. Funika sufuria kwa kifuniko cha metali
kisha chemsha hadi mbegu ziwe mkaa, ni wakati ambapo kifuniko kitakuwa cheusi
pia.
2.8 KIASI NA DOZI
a) Kiasi katika kutengeneza dawa Professa Kabangu anasema, “Dozi ni jambo ambalo hujadiliwa sana na watu ambao
wanadharua madawa ya jadi. Kwa uzoefu wetu siyo tu watu wenye tabia ya kuonea
mashaka bali “watu wa kawaida.” Pia wana mashaka ya kunyweshwa sumu kwa
kunywa kozi zisizo za uhakika zinazotolewa na mganga wa jadi.
Wakati wa kutayarisha madawa, inawezekana hata vijijini kuwa na vipimo halisi.
43
Vijiji vichache vina mizani, lakini kwa dawa nyingi za maji ujazo unaweza
kupimwa kwa uhakika zaidi.
Chupa 1 (bia) ml 700 au 0.7 lita
Kikombe 1 ml 500
Matone 20 ya maji ml 1 au gram 1
Kusema kijiko cha mezani (ml 10- 20) au kijiko cha chai (ml 3 – 10) siyo kipimo
halisi, kwa sababu tu ukubwa wa vijiko unatofautiana kwa hiyo kwa kutengeneza
dawa ni bora zaidi kutumia “kipimo fulani”. Mfano: vijiko 3 vilivyojaa (kama
kipimo) cha kitu fulani (A) kujumlisha vijiko vitatu (kijiko kiwe kipimo) ya (B)
vitafanya uwiano wa moja kwa moja kama kijiko kile kile kimetumika wa A na B.
b) Dozi katika kuelezea madawa.
Majani: Kama tukipendekeza kiganja kilichojaa majani kwa siku kwa mtu mzima,
mtoto tutampa kiasi gani? JIBU: Kwa kiganja kilichojaa tunajua kiasi ambacho
mgonjwa anaweza kukunja katika kiganja chake. Kwa jinsi hiyo kwa mtoto tumia
kiasi ambacho mtoto anaweza kukunjia katika kiganja chake.
Vimiminika: Kama tukipendekeza lita moja kwa siku kwa dawa fulani
tutapendekeza kiasi gani kwa mtoto? Jibu: Fuata mwongozo huu:
DOZI KWA WATOTO, KAMA DOSE YA WAKUBWA NI ML 1,000
UMRI WA MTOTO DOZI
Miezi 6 Ml 100
Mwaka 1 Ml 150
Miaka 2 - 3 Ml 200
Miaka 4 - 5 Ml 250
Miaka 6 – 10 Ml 350
Miaka 11 - 14 Ml 600
Miaka 15 - 16 Ml 800
Miaka 17 na zaidi Ml 1000
Hata hivyo uwe mwangalifu, siyo kila dawa iliyo nzuri kwa watu wazima ni nzuri pia
kwa watoto!
2.9 KUTENGENEZA MIZANI RAHISI LAKINI YA UHAKIKA
Kozi halisi zinaweza tu kutayarishwa na kutumika kwa msaada wa mizani. Siyo tu
waganga wa jadi bali hata zahanati nyingi hawana njia halisi za kupima kati ya gram
1 na 50.
Tuchukulie kwamba katika semina kila mmoja kati ya washiriki 30
anajitengenezea mzani wake.
Vifaa vya kutumia: Unahitaji vitu vyenye uzito halisi kati ya gram 1 na gram 20,
kisu, bisibisi ndogo, kalamu za kuwekea alama zisizofutika (marker pen), gundi
imara, tupa ya chuma na kifaa cha kuanzishia tundu kwa ajili ya parafujo (inaweza
kuwa nyundo na msumari).
44
Zana zinazohitajika kwa mzani (kumbuka vipimo
vyote ni vya makadirio).
a. Kipande 1 cha ubao, chenye sm 3 za mraba na
urefu sm 30, kama inavyoonyeshwa.
b. Parafujo 1, urefu sm 5.
c. Kipande 1 cha ubao, 40×14×3 sm, kama
inavyoonyeshwa.
d. Egemeo 1, upana sm 3, na mikono karibu urefu
sm 10 na 7.5.
e. Parafujo 3, mm 3.5 × 16.
f. Mche wa kuungia metali, au mche wowote wa
metali, sm 33 urefu na kipenyo mm 3.
g. Ubao wa miraba 6 iliyo sawa, sm 2 za mraba, na tundu la mm 3 kupitia katikati
yake (ili kupitisha ule mche wa metali F)
h. Parafujo duara 1, urefu sm 2.
i. Mche wa metali 1, sm 25 urefu na mm 1.6 kipenyo.
j. Parafujo za umeme 2 (kasha ya chocolate) za kuunganishia, kipenyo cha ndan mm
3.
k. Vikombe 3 vya plastic visivyo na vishikio vyenye ujazo wa ml 500, vyenye
vitako vya mviringo ikiwezekana.
l. Kamba ya nailoni mita 2.5, kipenyo mm 1
m. Vikopo 5 vya mikanda ya picha iliyo tupu, hasa yenye rangi nyeupe.
n. Mshumaa wa nyumbani 1.
o. Mfuko wa plastiki uwezao kuzibwa, ukubwa wa 45.
Kutengeneza 1. Chukua vipande A kwa C kama inavyoonyeshwa na parafujo B.
2. Chukua mkono mrefu zaidi wa egemeo D kwenye mhimili A.
3. Tafuta sehemu ya kati hasa ya mche F kwa kukunja kipande cha kamba chenye
urefu wa mche – vipande viwili. Weka alama katikati kwa kutumia kalamu ya
wino usiofutika (markerpen) na kisha weka alama kwa sentimeta moja kila
upande.
4. Kandamiza kibao cha
miraba 6, G kwenye
ule mche, kiunganishe
kwa gundi kwenye ule
mche katikati ya zile
alama mbili
zilizotengenezwa kwa
sm 1 kila upande.
5. Laza mche kwenye
meza, ingiza parafujo
ya duara H ndani ya
kibao cha miraba sita, katikati kabisa na kwa pembe mraba na ule mche wa
metali.
45
6. Tengeneza tundu dogo lenye ukubwa sawa wa kuchukua mche I likiwa kinyume
na parafujo duara uunganishe kwa gundi huu mche katika hiyo nafasi yake kiasi
kwamba iwe pembe mraba na mche F.
7. Pitisha kamba fupi kwenye mduara wa parafujo duara, ifunge kwenye tundu la
mwisho la egemeo.
8. Ingiza viunganishi J kila upande wa mche F kiasi kwamba uzito wa mche
ulingane kila upande.
9. Tayarisha vyombo viwili vya plastiki vya kupima K. Kama unatumia vikombe
ondoa vishikio. Tengeneza matunda katika umbali sawa karibu na sehemu ya juu
kabisa ya vyombo hivi. Kata vipande viwili kutoka kamba L, kata urefu wa sm 60
hivi na ufunge kwenye kila tundu lililo kinyume na jingine. Ninginiza kila
chombo kwenye viunganishi J.
10. Mizani ni lazima kila upande ulingane na mwingine. Kama sivyo, rekebisha kwa
uangalifu nafasi za viunganishi.
11. Katikati kabisa ya kibao cha msingi C, weka wastani unaoonekana, ulionyooka,
kuanzia nyuma hadi mbele. Wakati vipimo vya uzito vikilingana (vyombo)
kionyesho I kitaonyesha kwenye mstari huu.
Kutengeneza mizani rahisi zaidi.
Chukua mbao kwa ajili ya mhimili wa ulalo, ambao utaning’inizwa kwenye chango
kwenye ukuta katikati yake kabisa. Vyombo vya kuwekea vipimo vitawekwa kila
upande wa mhimili. Mche wa kuonyeshea (kipande cha chuma kama vile I)
kinafungwa kwa nyuzi 90˚ katikati kabisa ya ule ubao kiasi kwamba kinaelekea chini.
Nyuma ya hii mizani rahisi, mstari wa wima unachorwa kwenye ukuta kiasi kwamba
upimaji unapokuwa sawa, mstari unafichuka kabisa.
Kutengeneza uzani Kama tuna uzani uliohakikishwa, basi tunaweza kutengeneza uzani mwingine
mwingi. Tunahitaji kutumia vifaa visivyonyonya maji, kiasi kwamba tutakuwa na
uzito ule ule wakati wa ukavu na majira ya unyevunyevu. Ni bora kutumia plastiki na
mishumaa ya kuwasha.
Ni vizuri kutengeneza uzani ufuatao 1×1g, 2×2g, 1×5g, 2×10g, 1×20g. Kwa
kutumia uzani ufuatao tunaweza kupima madawa, mfano majani, hadi kufikia gram
50. Kwa kutumia vikopo vya plastiki vya mikanda ya picha kata kwa vipimo vya
gramu 1, 2 na 5 kwa kufuata uzani halisi. Andika uzito kwenye hivyo vikopo kwa
kutumia rangi isiyofutika (markerpen). Tengeneza uzani kwa gramu 10 na gram 20
kwa kujaza vipande vya mishumaa hadi vifikie uzani halisi pamoja na kile kikopo.
Kisha tena andika kiasi cha uzito juu yake, na uvitunze vyote katika mfuko wa
plastiki O ili visichafuke.
Kutumia vipimio Kipimo ni lazima kitumike katika chumba kisichopitiwa na upepo. Kabla ya kupima
kila siku hakikisha vipimo vyako viko sawa, uvirekebishe kama inabidi. Hii inaweza
kufanyika kwa kuweka vipande vya karatasi kwenye upande wa chombo kilichoinuka
hadi vyote viwe usawa. Weka uzito kwenye chombo kilekile. Weka dawa kwenye
chombo kile kingine, hadi vipimo vilingane tena.
46
VIFAA VYA KUJITENGENEZEA kwa ajili ya madawa ya asili.
Fukizo – maji
(water bath)
Jiko la jua
Mizani
47
SURA 3
Mimea ya madawa mara nyingi ina ladha tofauti (chungu, tamu, ukakasi) kutokana
na viasili vilivyo katika mmea.
Ili kupata dawa viasili hivi vinasindikwa katika kimiminika kwa hiyo njia ya
msingi na iliyozoeleka ya kutengeneza dawa ni:
Mmea + KIMIMINIKA + JOTO = DAWA
Madawa yanayotengenezwa kwa njia hii ni ya aina tatu:
Kwa matumizi ya ndani tu (kunywewa)
Matumizi ya nje tu (kuwekwa kwenye ngozi)
Kwa matumizi ya ndani na nje (zinaweza kunywewa au kupakwa kwenye ngozi)
3.1. MADAWA KWA MATUMIZI YA NDANI
Kumbuka: Mapendekezo yote ya Utunzaji wa dawa yanahusu zaidi hali za maisha ya
kijiji katika maeneo ya Tropiki, kwa kuchukulia kuwa hakuna jokovu.
KUTENGENEZA KWA MAJI YA BARIDI
Ni njia inayotumika kutengeneza viasili vinavyoharibiwa na joto; mfano mbaazi
(Tephrosia): ili kupata dawa bora.
1) Majani: Yakatekate vipande vidogo.
2) Mizizi: Itwange kwa kinu.
3) Tumbukiza vitu hivi katika maji kwa usiku mzima.
Kisha chuja: Hii dawa rahisi inatakiwa kutengenezwa (upya) kila siku.
KUMWAGIA MAJI MOTO (INFUSION): Chemsha maji lita moja na umwagie
kwenye dawa kiasi cha kiganja kimoja. Baada ya dakika 15 – 20 chuja kwa kitambaa
kisafi. Itumie dawa hiyo kwa siku moja.
KUTOKOSA (DECOCTION): Ukitaka kupata dawa kutokea kwenye majani
manene, mizizi au magamba, wakati wote tumia njia hii. Chemsha kiganja kimoja
cha hiyo sehemu ya mmea katika lita moja ya maji kwa karibu dakika 20. Dakika
zihesabiwe kuanzia maji yanapoanza kuchemka. Ni vizuri kutumia chungu cha
udongo au kauli kuliko kikaango chochote cha metali. Tengeneza dawa ya
kuchemsha upya kila siku. Kuongeza sukari hakuongezi thamani ya dawa.
SODA (Maji ya limau): Soda (maji ya limau) ni kinywaji kinachoburudisha na
chenye tiba. Mfano: Kamua limau 2. Ongeza lita moja ya maji ya moto kwenye maji
ya limau na uiongezee sukari kuifanya tamu. Tumia kwa siku moja.
SYRUP (DAWA TAMU): Baadhi ya madawa ya mmea hayana ladha nzuri. Ili
kufanya dawa idumu kwa muda zaidi au iwe na ladha nzuri, unaweza kuifanya tamu.
Kwanza tayarisha dawa ya maji, chuja, kisha ongeza kikombe kimoja cha sukari kwa
kikombe kimoja cha dawa ya maji. Ili kuyeyusha mchanganyiko huu weka kwenye
moto na kisha koroga wakati wote. Dawa hiyo tamu (Syrup) imiminwe kwenye chupa
wakati bado inatokota. Kama una mizani chukua gramu 1.650 za sukari kwa gramu
MADAWA YA AINA MBALIMBALI
48
1.000 za dawa ya maji. Utapata lita mbili za dawa tamu (syrup), iwezayo kutunzwa
kwa siku tatu.
Dawa iliyoanza kuvunda itupwe. Tafadhali kumbuka kuwa sukari haina dawa
ndani yake, isipokuwa kwa shida ya utapiamlo. Kwa kweli kinyume chake ndiyo
kweli: sukari ni hatari kwa meno yako. Sukari inaongezwa kwenye dawa ili tu
kutunza dawa na kuongezea ladha.
TINCTURE (Dawa yenye kileo): Kwa nyongeza kwenye dawa ya mimea, dawa ya
maji ina viwango tofauti vya maji na kileo. Kwa matumizi ya kunywa usitumie kile
kilichogeuzwa asili, lakini bora utumie vinywaji (konyagi na mvinyo) vyenye
asilimia kubwa ya kileo, angalau 20%.
Dawa ya maji (tincture) yenye kemikali: Kemikali zinayeyushwa katika
mchanganyiko wa kileo na maji (mfano: Iodine tincture).
Dawa ya maji (Tincture) ya mimea ya dawa: Kwa kawaida, gram 100 za sehemu
ya mmea inachanganywa na lita moja ya kileo na maji (zaidi hasa 45% au 70%
kileo). Usichemshe, bali mimina katika chupa na utunze kwa utulivu kwenye sehemu
ya uvuguvugu kwa juma moja. Tikisa kila mara, kisha chuja. Kiwango kikubwa cha
kileo ndicho kinaongeza muda wa dawa kudumu zaidi. Katika hali ya hewa ya
kitropiki kama chupa imefungwa kabisa tunapendekeza:
20% kileo: Mwaka 1
30% kileo: Miaka 3.
40% na zaidi Miaka 5.
Kuongeza sukari kunasababisha dawa idumu zaidi.
DAWA YENYE DIVAI: Ni nzuri pia kwa kufuata ukweli kuwa viasili vingi vya
madawa vinayeyuka vizuri katika kileo. Divai nzuri ina kileo (kama 12%), sukari na
vitu vinavyoweka rangi. Weka mimea iliyokaushwa (mfano: kola zilizosagwa) katika
divai ya asali au iliyotengenezwa kwa mzabibu, kisha funga chupa. Itunze kwa juma
moja. Itumie baada ya kuchuja. Kufuatana na kiwango cha kileo (kinachofanya kazi
la kulinda dawa) unaweza kuitumia kwa
mwezi 1 – 6.
ENEMA: Enema huingizwa katika matumbo kupitia mkunduni kwa njia ya mpira
mdogo. Kuna enema kwa ajili ya shida ya kufunga choo na strida ya kuharisha. Kama
mtoto hawezi kunywa maji chumvi (rejea sura 4:6) anaweza kupewa kupitia
mkunduni.
Kwa ujumla, haturuhusu matumizi ya enema za jadi, hasa kwa kuharisha kwa
watoto. Tumekuwa tukiona enema ikifanywa kwa mimea yenye sumu. Kwa jinsi
sumu inanyonywa kwa kupitia ngozi laini za utumbo katika Afrika watoto wengi
wanakufa baada ya kuhudumiwa kwa enema za namna hii.
3.2 . DAWA KWA MATUMIZI YA NJE
MWOGO MAALUM (LOCAL BATH): Huduma itolewayo kwenye sehemu moja
tu ya mwili, ambayo inashirikisha viasili vya dawa za mimea (zaidi sana
49
iliyochemshwa), inaitwa mwogo maalum (local bath). Mfano: mwogo-miguu,
mwogo-paja, mwogo-jicho, mwogo-sikio).
KUBANA (KUHUDUMIA KIDONDA) – Compress: Kati ya madawa yote
yatumikayo nje, kubana ndiyo njia rahisi zaidi. Kwa jipu au uvimbe mmea unawekwa
moja kwa moja kwenye ngozi, na kufungwa kwa kitambaa, kamba au uzi. Kinyume
na ushauri mwingi unaotolewa kaitka vitabu kuhusu madawa ya jadi, tunashauri
kwamba usiweke jani moja kwa moja kutoka mtini au lisilochemshwa kwenye
kidonda au uvimbe wa kuungua. Juu ya majani hayo huwa mamilioni ya vijidudu
(staphylococci, pepopunda, virusi, fungus n.k.) vinavyoweza kudhuru kidonda. Kwa
hiyo wakati wote chemsha jani kabla ya kulitumia kwa nje. Badilisha jani mara tatu
kwa siku.
KUSUKUTUA: Dawa za kusukutua hutumika kusafisha na kutibu mdomo na makoo
(siyo za kumeza). Dawa hizi zikitengenezwa nyumbani zihifadhiwe kwa siku moja
tu.
DAWA YA KUPAKA: Dawa ya kupaka zimetengenezwa zikiwa laini kwa kupaka
kwenye ngozi. Zinatumika kama kufunika ngozi (kama vipodozi) kuhudumia ngozi,
mfano wakati wa matatizo ya fungus, au kusaidia dawa kupenya kwenye sehemu za
misuli kwa ndani. Mfano: Kutibu maumivu ya viungo. Ili kutayarisha dawa ya
kupaka, chemsha mimea ya dawa kwa mafuta ya kula katika fukizo-maji (water
bath), chuja, ongeza nta iliyo yeyushwa (mfano: nta ya nyuki au mshumaa) na uiache
ipoe. Kwa taarifa zaidi angalia sura 4.4 .
Dawa ya namna hii iliyo na maji inaitwa cream; kama ina unga inaitwa paste.
SABUNI: Sabuni ni matokeo ya urejeo wa kikemia kati ya nyongo (mfano: Sodium
hydroxide, NaOH) na mafuta , aidha mafuta ya mbogamboga au ya wanyama. Kama
sabuni ina NaOH kuliko mafuta, inasafisha vizuri lakini inachoma ngozi. Kama ina
mafuta mengi zaidi ya NaOH, sabuni itakuwa na uwezo mdogo wa kusafisha lakini
itakuwa nzuri kwa ngozi (rejea sura 4:1).
Kama, baada ya kuoga, unataka kulinda ngozi yako, tumia mafuta (rejea chini) ili
kulinda viasili vinavyolinda ngozi. Baada ya kuoga watu wengine hujipaka sabuni,
usifanye hivyo.
SABUNI ZENYE DAWA: Sabuni hizi zina dawa aina fulani kwa matumizi ya
hospitali. Yeyusha sabuni iliyosagwa pamoja na maji kidogo katika chombo, ongeza
dawa (mfano: sulphur, mafuta ya mwarobaini, au dawa ya kuua vidudu vya
maambukizo), na uuache mchanganyiko upoe.
Usitumie zile zinazoitwa “sabuni za kuzuia wadudu wasizaliane” (antiseptic soap)
ambazo zina madini ya zebaki, kwa kufanya ngozi kuwa nyeupe. Ni za hatari kwa
ngozi na kwa afya yako.
DAWA YA MAJI (TINCTURE): Divai itengenezwayo kijijini kwa kawaida ni bei
nafuu kuliko vileo vya kiwandani. Katika jadi, divai iliyotengenezwa kutokana na
ndizi, mchele au mahindi huchemshwa na mvuke wake hupoa kwa kupitia mrija
wenye urefu wa meta 10 wa mwanzi. Pima kiasi cha kileo chake kutumia kipima
kileo. Nunua kileo pale tu unapohitaji chenye zaidi ya 70%; kwa kileo chenye nguvu
ya chini ya 70% anaweza kutumia vile vinavyopatikana vijijini.
50
Kwa sababu za usalama, tumia vile vifuatavyo tu:
1) Kama kuzuia vidudu vya maambukizi, kuzuia matumizi mabaya, ongeza tone
moja la shampoo au dawa ya maji ya kuoshea katika lita moja ya kileo. Hii
hutengeneza spirit iliyoharibiwa asili.
2) Kwa kutengeneza dawa ya maji ya mimea kwa matumizi ya nje tu (mfano:
Dawa ya maji ya Cassia alata) Rejea sura 5.
3.3. MADAWA KWA MATUMIZI YA NDANI NA NJE
UNGAUNGA: Ungaunga unaweza kutumika kwa ndani au kwa nje. Gamba, mzizi,
majani, mbegu, mara nyingine mmea mzima hukatwa na kuachwa kukauka,
ikiwezekana kivulini. Ni vizuri kama mmea ukiwa mkavu sana kabla hujautwanga
katika kinu. Funga kipande cha nguo ya nailoni juu ya chujio la kawaida kwa
vishikizo. Chekecha unga kupitia katika nailoni kwa kuusugua kwa kipande cha ubao
au plasitiki chenye kingo zilizonyoka.
Mfano: Unga wa mkaa kwa kuharisha.
DAWA ZA MAFUTA (Medicinal Oil): Tengeneza mafuta kwa kutumia karanga,
ufuta, kokoa, nazi, mchikichi, mwarobaini, shea na mengine kama hayo. Aina hizi za
mafuta ya mimea siyo tu kwamba vina lishe bali pia vina viasili vya dawa hata bila
matengenezo mengine.
a) Matumizi ya ndani: Ni nzuri kwa sababu ina kiwango kikubwa cha vitamini A,
D, na E (rejea sura 4:10). Pia inatumika kwa mafuta ya mbono katika hali ya
kufunga tumbo – kukosa choo.
b) Matumizi ya nje: kama vile matunzo ya ngozi, kuzuia maambukizi au kwa
bawasiri. Pia inatumika kwa vipodozi na kama mafuta ya kuchua.
Mafuta ya wanyama yanatumika mara chache sana vijijini kwa sababu ni adimu
na ghali (tunashauri kutotumia mafuta ya chatu ili kulinda jamii za chatu zisitoweke).
Katika utengenezaji dawa mara nyingi tunatumia mafuta ya mawese, ambayo
yanapatikana wakati wote katika vijiji vingi vya Afrika; kama sivyo, panda
michikichi! Badala ya mawese mekundu (yanayotengenezwa kutokana na matunda
yake) unaweza pia kutumia mafuta yasiyo na rangi yanayotokana na kokwa la
mchikichi.
Kama ukitaka kutumia mawese ya kujitengenzea, ni vizuri yatengenezwe siku ile
ile matunda yanapovunwa, ili kwamba matunda ya mchikichi yasitunzwe mpaka
yavunde (jambo ambalo kwa bahati mbaya hutokea mara nyingi).
Tunapotayarisha mafuta kwa ajili ya matumizi ya nje kutokana na kanuni ya
kutengenezea dawa, jaribu kutumia mafuta ambayo yanapatikana hapa kijijini, kwa
bei rahisi zaidi.
Ili kutengeneza dawa ya mafuta, changanya kipimo kimoja cha majani makavu au
maua, na vipimo kumi vya mafuta. Chemsha mchanganyiko huo kwa saa 1 katika
fukizo maji, ichuje na uiache ipoe.
Mafuta yaliyotengenezwa kwa njia hii yanatumika kutibu upele, maumivu ya
viungo na magonjwa ya ngozi. Kwa vipodozi, mafuta kama hayo ni bora zaidi ya
vipodozi vya madukani, kwa sababu rangi mbalimbali na kemikali za kuhifadhi.
51
SURA YA 4
4.1 UTENGENEZAJI WA SABUNI KATIKA NGAZI YA KIJIJI
1. Kwa mujibu wa hadithi ya kirumi, sabuni ilivumbuliwa katika mlima Sapo. Katika
mlima huu watu walitoa kafara kwa miungu. Baada ya mvua kubwa kunyesha, maji
yalijichanganya na majivu pamoja na mafuta ya wanyama waliotolewa kafara na
kuunda kitu cha kushangaza kilichotiririka kutoka mlimani kuelekea bondeni. Watu
waliokuwa wakifua katika mto Tiber waligundua kwamba kitu hicho kipya
kilirahisisha kazi ya ufuaji. Mchanganyiko wa maji, majivu na mafuta umebadilika na
kuwa sabuni!
2. Usafi na elimu nzuri ya afya ni muhimu na nafuu kuliko (aina nyingi za) madawa.
Kwa hiyo mtu anahitaji sabuni. Lakini itakuwaje kama hata sabuni iliyotengenezwa
kwa gharama nafuu utainunua kwa bei kubwa?
UFUMBUZI A: Kukusanya fedha barani Ulaya, kununua sabuni na kuzituma
Afrika. Katika suala hili, bidhaa itakuwa imeagizwa kutoka ng’ambo, wakati ambapo
zaidi ya 90% ya vitu vinavyochanganywa katika utengenezaji wa sabuni vinapatikana
kwa wingi barani Afrika. Mawese na maji!
UFUMBUZI B: Kuendesha semina ili watu waweze kujitengenezea sabuni katika
Vijiji vyao, bila vifaa vyovyote maalum, kama vile mizani. Nimewahi kufungwa kwa
sababu, eti, kutengeneza sabuni kutasababusha serikali kupoteza mapato ya kodi.
3. Tumeandaa maelezo rahisi kwa ajili ya aina mbali mbali za sabuni. Sabuni hizi
hazina tofauti na sabuni za biashara, iwe kwa muonekano au ubora. Na badala yake,
zina muwasho kdiogo kwa sababu hazihitaji rangi na madawa.
Sabuni yetu ni zao la kikemikali lenye vitu vitatu: maji, mawese na sodium
hydroxide (NaOH), ambayo inapatikana katika mji wowote mkuu wa nchi za tropiki.
Inapatikana katika pakiti za kilo 1, inauzwa ikiwa katika vibonge vidogovidogo kwa
kusafishia (mfano choo). Unaweza ukaipata kwa bei nafuu katika mifuko ya kilo 50
kutoka kwenye viwanda vya kemikali. Unaweza ukapata anwani zao kwenye
kiwanda cha pombe kilicho karibu (viwanda vya pombe hutumia NaOH kwa
kusafisha chupa).
Ili kutengeneza sabuni unahitaji vyombo na vifaa vifuatavyo:
- Sufuria au chungu kimoja (cha mfinyanzi au udongo mwingine).
- Chombo kimoja cha plastiki (lita 5)
- Bakuli kubwa moja (plastiki au mfinyanzi)
- Ubao mdogo mmoja
- Kikombe 1 cha maji (plastiki, kauri au mfinyanzi)
- Kisu kimoja
- Mikopo tupu (tazama chini)
- Maji
OKOA FEDHA NA JITENGENEZEE MWENYEWE!A
52
- Mafuta, pamoja na kwamba maelezo haya yanahusu “mawese” vilevile
unaweza ukatumia: mawese mekundu (red palm oil), mafuta ya kokwa la
mawese, mafuta meupe ya mawese, mawese meupe ya kiwandani (Tazama
sura 6:22) au mafuta ya shea.
Vyombo zaidi vinavyoweza kusaidia ni:
- Kitambaa cha nailon au karatasi la plastiki
- Kasha moja la mbao lililo mraba.
4. Vipimo vya kipima (mara zote vikae wima)
Kama vipimo vya kupimia chukua chombo cho chote cha plastic (kwa mfano
kikombe, kopo n.k.)
Vipimo vyote ni vya ujazo.
5. Tahadhari: Sodium hydroxide ni hatari. Katika semina za vijijini ni lazima
mjadili namna ya kuiweka mbali na mahali wanakofika watoto. Kama mtoto atameza
sodium hydroxide, lazima apewe maziwa mengi au kikombe 1 cha mchanganyiko wa
juisi ya limau/siki na vikombe 20 vya maji; kwa tukio lolote lile lazima apewe maji
mengi.
Sodium hydroxide hushambulia ngozi, kila mara nawa mikono vizuri! Kwa kuwa
hali ya unyevu katika hewa huibadili sodium hgydroxide kuwa kimiminika, ni lazima
ihifadhiwe kwenye vyombo visivyopitisha hewa.
Sodium hydroxide hushambulia aina zote za metali. Kwa hiyo ni bora zaidi
kutumia vyombo vya mfinyanzi vilivyotengenezwa kijijini (na hii itasaidia wakati
huohuo kutoa ajira kwa wenyeji!). Na kama vyombo vya mfinyanzi havipatikani
tumia aina nyingine za vyombo vya kufinyanga au plastiki.
6. Uzalishaji wa sabuni ya kugandisha
a) Chemsha vipimo 7 vya mawese au mafuta ya shea hadi ifikie hatua ya
kimiminika, na chujia kwenye chungu cha mfinyanzi au bakuli la plastiki.
b) Mimina vipimo 5 vya maji baridi kwenye chombo cha plastiki. Ongeza kipimo
1 cha sodium hydroxide kwa UANGALIFU MKUBWA. Mchanganyiko
utakuwa wa moto sana - usiweke mfuniko kwenye chombo. Subiri hadi sodium
hydroxide yote imeyeyuka.
c) AMA: Subiri mpaka mchanganyiko wa sodium hydroxide na mafuta vikaribie
kupoa. Kisha, taratibu, ongeza mchanganyiko wa sodium hydroxide kwenye
mawese, huku ukikoroga harakaharaka bila kusita kwa kutumia ubao. Hii ni
njia nzuri zaidi.
d) AU: Chemsha mafuta kwenye joto la kadri ya 55˚C. Subiri hadi sodium
hydroxide nayo imefikia joto hilo. Kisha changanya vimiminika hivyo viwili,
huku ukikoroga kwa nguvu.
e) Wakati sodium hydroxide yote itakapokuwa imewekwa, koroga sana kadri
uwezavyo. Taratibu sabuni itageuka kuwa laini.
f) Kabla ile namna ya sabuni haijawa ngumu kwa kumwagia, mwaga sabuni
ndani ya boksi la mbao lililotanguliziwa karatasi nyembamba za plastiki.
Baada ya saa 3, sawazisha kwa rula au kitu kingine kilichonyoka, kisha huku
ukigandamiza, ipanguse iwe laini kwa kutumia kitambaa kilicholainishwa.
53
g) Katakata sabuni vipande (saizi ya kuuza). Iweke ikauke katika sehemu yenye
kivuli kwa muda wa miezi 2. (Mfano, katika boksi la karatasi nene kwa ndani
chini ya sehemu iliyoezekwa).
MUHIMU: Ni muhimu kukoroga sana mchanganyiko huu kadri uwezavyo! Ni sawa
na ni bora kuiacha sabuni ikauke kwa muda usiopungua miezi 2, kwa sababu tendo la
kikemikali linalozalisha sabuni bado huendelea kwa kipindi kirefu. Epuka majaribu
ya kuitumia mapema, kwa sababu itakuwa bado na uwezo wa kushambulia ngozi.
7. Sabuni nyekundu – nyeupe – njano:
Mawese huwa na rangi ya njano – nyekundu kutokana na carotene iliyomo. Kwa
sababu hii, na kwa maelezo ya hapo ju, unapata sabuni ya njano. Hii ni rangi halisi na
ya asili ambayo haina madhara yoyote. Ila kama unataka kutumia sabuni hii kufua
nguo nyeupe inahitaji kuharibu carotene.
Fanya hivi kwa kuchemsha mawese kwa uangalifu kwa dakika 30 kwenye moto, hadi
kipande cha karatasi utakachokichovya katika mafuta kitoke bila rangi. Mchakato
huu hutoa moshi mbaya na mafuta yanaweza yakashika moto kwa urahisi, kwa hiyo
vaa miwani na hakikisha kwamba hakuna watoto karibu!
Unaweza ukatengeneza sabuni nyekundu kwa kuongeza kipimo 1 cha mbegu za
bixa orellana (tazama SURA 6.7.) kwenye mawese. Chemsha katika fukizo maji kwa
dakika 30, chuja na endelea na utaratibu kama unavyofanya kwa mafuta
yasiyosafishwa hapo. Rangi ya bixa orellan ina carotene na haina madhara.
8. Jaribio la kwanza (mfano, katika semina) Wakati unajaribu kutengeneza sabuni mara ya kwanza tumia kipimo kidogo tu,
mfano kijiko (cha mti au plastiki)
Mawese - vijiko vya chai 7
Maji vijiko vya chai 5
Sodium hydroxide - kijiko cha chai 1
9. Sabuni za urembo Sabuni hizi haziegemei upande wowote. Zina mafuta yaliyosafi, na ni nzuri kwa
mwili kwa sababu ya tabia yake ya kuufanya kama unapakwa mafuta kila wakati.
Kabla sabuni haijawa ngumu kwa kukoroga, unaweza ukakata kwa maumbo
unayotaka (chemsha cha kukatia au kichovye kwenye mafuta ya taa) au kitu
kinaweza kugandamiziwa juu ya sabuni ili kuweka urembo.
a) Chukua na endelea kama ilivyoelezwa katika (6) juu;
- Mawese vipimo 8
- Maji vipimo 5
- Sodium hydroxide - kipimo 1
b) Au badala yake, tumia:
- Sabuni ya kugandisha (ya biashara au iliyotengenezwa nyumbani) vipimo 4
- Mafuta ya mbogamboga (mawese, mafuta ya karanga) kipimo 1
- Maji kipimo 1
Twanga sabuni, na changanya katika mafuta na maji. Chemsha taratibu hadi sabuni
iyeyuke. Koroga mchanganyiko mpaka upoe, kisha mimina kwenye kifyatulio.
54
10. Sabuni ya asali au cream Tumia maelezo ya (a) kwenye sabuni ya urembo juu, lakini punde vitu hivi vitatu
vinapochanganywa ongeza kipimo 1 cha asali.
11. Sabuni ya manukato
Tengeneza sabuni ya urembo kama ilivyoelezwa hapo juu. Baada ya majuma 8 ni
lazima itengenezwe upya kama ifuatavyo: Twanga sabuni, na kwa vipimo 8 vya unga
wa sabuni, ongeza kipimo 1 au 2 vya maji na yeyusha kwenye joto kidogo. Mara
baada ya sabuni kuyeyuka koroga mchanganyiko huo, na mchanganyiko
utakapokuwa mgumu kukoroga ongeza matone kadhaa ya marashi au kipimo 1 cha
michaichai mikavu na iliyosagwa hadi kuwa unga. Mimina katika vifyatulio.
Usiwe na haraka wala pupa unapotengeneza sabuni za manukato! Kama hutasubiri
kwa majuma 8 kabla ya kuzitoa, sodium hydroxide itaharibu manukato.
12. Cream ya kunyolea
- Majani mabichi yanayonukia
(k.k. mkaratusi, limau, michaichai, lavender) kipimo 1
- Maji kipimo 1
Ongeza maji ya moto, chuja na ongeza:
- asali vipimo 3
- Sabuni ya kugandisha
(yenye muda usiopungua miezi 2) iliyotwangwa vipimo 5
Taratibu chemsha mchanganyiko huu hadi uwe kitu kimoja. Na hii ni nzuri kama
itafanyika kwenye jiko la jua ili kupunguza kiwango cha mvuke. Utakaotoweka,
vinginevyo lazima maji yaongezwe ili kurudisha katika ujazo wa awali. Koroga
hivyo hivyo wakati inaendelea kupoa, hadi ipoe kabisa. Hifadhi katika chombo
kisichopitisha hewa ili kuzuia isikauke. Chombo kinaweza kikawa cha kioo, plastiki
au kauri.
13. Sabuni ngumu (inatumika kuondoa uchafu mgumu)
- Mawese vipimo 6
- Maji vipimo 5
- Sodium hydroxide kipimo 1
Kabla sabuni haijawa ngumu sana, ongeza vipimo 2 vya kaolin iliyochekechwa
vizuri (kaolini ni udongo mweupe wa mfinyanzi, unaopatikana mitoni, katika Afrika
hutumika kupamba kuta). Kama kaolin haupatikani, unaweza vilevile ukatumia
majivu ya kuni yaliyochekechwa vizuri. Iache sabuni miezi mitatu kabla ya kutumia.
14. Sabuni ya unga Ukilinganisha na sabuni ya kugandisha, sabuni ya unga huwa ina mawese kidogo:
- Mawese vipimo 5
- Maji vipimo 4
- Sodium hydroxide kipimo 1
Weka ikauke kwa miezi 2 – 3, kisha itwange na tumia chekecheo lenye matunda
ya wastani ili kupata chenga zenye ukubwa sawa.
55
15. Na kama utapata matatizo….. Iwapo sabuni haikutoka kama ilivyotarajiwa (mfano, kama inaonyesha rangi tofauti
au kama ina muundo wa semolina, ikatekate vipande vidogovidogo siku moja baada
ya kuiandaa, na chemsha vipimo 9 vya sabuni pamoja na kipimo 1 cha maji katika
sufuria mpaka mchanganyiko uyeyuke. Iache ikauke bila kukoroga.
16. Sabuni isiyo na gharama - au nini cha kufanya kama sodium hydroxide
haipatikani. Njia hii, hata hivyo, inahitaji juhudi na kazi kubwa. Tumia: Maganda ya ndizi za
kupikia, magogo ya mapapai au aganda ya mbegu za kakao.
Kausha vitu hivi juani, au kwenye jiko la jua, na vichome. Nadhani si usumbufu sana
kukusanya majivu mikavu kutoka mahali unapopikia mara moja kwa wiki, lakini
majivu ni lazima yatokane na kuni au karatasi ambazo hazikuandikwa, sio jivu la
plastiki au vitu visivyo vya asili. Jaza ndoo ya lita 20 ya plastik kwa lita 10 za majivu
na ongeza lita 15 za maji ya moto. Koroga vizuri. Baada ya dakika 10, chuja kwa
kutumia kitambaa kwenda kwenye ndoo ya plastiki (kazi hii inaweza ikachukua saa
12).
Kwenye majivu yaliyobaki, ongeza tena lita 5 za maji ya moto, koroga kwa dakika
10 halafu chuja. Weka pamoja vile ulivyochuja kwenye chombo cha mfinyanzi.
(Kama utatumia chombo cha metali kitaharibika). Chemsha hadi kibaki kikombe
kimoja tu (200 ml). Ongeza kikombe kimoja cha mawese, halafu chemsha tena kwa
muda mfupi. (Kuwa makini mchanganyiko huu hutoa povu jingi). Mimina kwenye
kifyatulio na acha ikauke.
17. Sabuni iliyotengenezwa kwa mafuta mengine. Faida ya mawese na mafuta ya shea ni kwamba hata katika joto la ndani ya nyumba,
huwa zinakuwa ngumu. Hii hufanya uzalishaji wa sabuni kuwa rahisi; glycerine
ambayo inatokana na utengenezaji wa sabuni haitenganishwi na sabuni bali hubakia
humohumo kwenye sabuni.
Kama utataka kutumia mafuta aina nyingine au shahamu (mfano, mafuta ya
karanga), hapa utengenezaji utakuwa ni mgumu zaidi: Yeyusha gramu 36 za sodium
hydroxide kwenye ml 200 za maji (Uwe mwangalifu), ongeza gramu 200 za shahamu
(shahamu ni mafuta ya wanyama kama nguruwe/mifugo) au mafuta yatokanayo na
mbogamboga; koroga. Ongeza ml 600 za maji ya moto halafu mchanganyiko
uhifadhiwe kwenye joto la 70˚- 80˚C angalau kwa saa 6 (k.k. katika jiko la jua),
koroga kila baada ya dakika 15. Kisha ongeza mchanganyiko wa chumvi ya kawaida
gramu 120 na maji ml 200.
Acha ipoe: Sabuni itatuama juu ya maji.
Mwaga maji, kisha mimina sabuni ndani ya
vifyatulio na ikae kwa mwezi moja hadi tatu
ili ikauke.
Sabuni iliyotengenezwa
nyumbani ni nzuri zaidi kuliko
za kiwandani.
56
4.2 KUMWAGIA MAJIMOTO NA KUTOKOSA
(INFUSIONS & DECOCTIONS)
Kwa maelekezo ya namna ya kutengeneza infusions na decoctions angalia sura ya 3.
Chai kwa ajili ya Mimea na Sura:
Amoeba dysentery Mpera 5.14; mwembe 5:12; mpaipai 5.5; mziwaziwa 5.11
Ugonjwa wa pumu Mkaratusi 5.10; mziwaziwa (mwache) 5.11
Bronchitis Limau 5.8; mkaratusi 5.10.
Kufunga choo Mwingajini 5.7; ringworm bush 5.6.
Kikohozi Mkaratusi 5.10; limau 5.8; mchungwa 6.14, Parachichi 6.38.
Maumivu ya kunyonga (cramps) Mziwaziwa 5.11; mana ya passionfruit 6.37
Kisukari Maharage 6.39; mahindi 6.50; vitunguu maji 6.2
Kuharisha Mziwaziwa na ORS 5.11; mpera na ORS 5.14,
mwembe na ORS 5.12.
Tumbo kujaa hewa Mkaratusi 5.10.
Homa Mchaichai 5.9; kurimbasi 6.35
Bawasiri Mwingajini 5.7; mwembe 5.12; artemisa 5.2.
Hepatitis Mpapai 5.5
Shinikizo la damu Mahindi 6.50; vitunguu maji 6.2; vinka rosea 6.49
Indigestion Kechu 6.40; dawam mchuzi 6.19
Maambukizo ya figo (kidney infection) Mziwaziwa 5.11; mahindi 6.50
Mapigo ya moyo kuwa chini (Low blood pressure) Kahawa 6.16
Malaria Artemisia 5.12, cinchoma 6.13; mtukutu 6.48; mpapai
5.5; mchaichai 5.9.
Kuvimbewa (Oedema) Mahindi 6.50; mwembe 5.12.
Vidonda mdomoni Mwembe 5.12
Upungufu wa vitamin C Limau 5.8; mpera 5.14
Kukosa usingizi Matunda passion 6.37; njugu 6.6.
Maumivu ya koo (sore throat) Mwembe 5.12
Maumivu ya Tumbo Mpera 5.14
4.3 MAFUTA YENYE DAWA
Maelezo: MMEA + MAFUTA + JOTO = MAFUTA YENYE DAWA.
Kwanza tayarisha maji robo au nusu ujazo wa fukizo. Chungu kingine kidogo
kiweke ndani ya hicho kilicho kwenye stovu. Mchanganyiko unachemshiwa kwenye
hiki chungu kidogo. Funika vyungu vyote viwili. Mtindo huu unahakikisha kwamba
joto halipandi na kuvuka 100˚C. Hakikisha kwamba hakuna maji yanayoweza
kuingia katika chungu kidogo hata yatakapoanza kutokota - kama mafuta yaliyo
kwenye chungu cha ndani yataingiliwa na maji, mafuta yatachacha haraka sana.
Majani lazima yawe makavu kabisa, ili kwamba pasiwepo maji yatakayoingia
kwenye mafuta toka kwenye majani.
Tumia mafuta yanayopatikana katika maeneo yenu: mawese, mafuta ya kokwa.ya
mawese, mafuta ya shea, mafuta ya alizeti, mafuta ya karanga, mafuta mengine ya
aina yanayofaa kwa ngozi. Weka mchanganyiko katika fukizo maji na acha maji
57
yatokote kwa dakika 60 hivi. Koroga kila baada ya dakika 15. Chuja na acha ipoe bila
kukoroga. Dawa hii yenye mafuta inahitaji kuhifadhiwa pasipo na jua, joto na hewa.
Kwa hiyo tunza mafuta haya ndani ya vyombo vilivyofungwa vizuri. Vijaze tele ili
kupunguza kiasi cha hewa. Kamwe usichanganye bidhaa ya kale na mpya! Mafuta
yanayotoa harufu ya kuchacha yamwagwe mara moja.
Usijiendekeze kwa bidhaa za kibiashara kwa sabuni ya rangi au manukato yake.
Rangi hizo na madawa yaliyomo vinaweza kukusababishia mzio (allergy). Mafuta na
dawa za kujitengenezea nyumbani kwako bila shaka ni bora kwa afya yako!
Vitu kwa ajili ya maelezo haya vimetokwa katika vipimo vya ujazo (k.m kikombe
cha maji ya kunywa, kopo, kikombe cha chai).
Kiasi kwa upande wa mimea ni kwa ile iliyokauka vizuri na kusagwa na isiwe na
vijidudu.
A) Mafuta ya mtoto (baby oil):
- Michaichai (sura 5.9) kipimo 1
- Mafuta ya mbogamboga vipimo 9
B) Mafuta ya urembo
- Michaichai au majani ya
mlimau au mchungwa vipimo 2
- Mafuta ya mbogamboga vipimo 8
C) Mafuta kwa ajili ya kuchua:
- Majani ya mkaratusi vipimo 2
- Michaichai (sura 5.9) vipimo 2
- Mafuta ya mbogamboga vipimo 8
D) Mafuta kwa ajili ya maumivu ya viungo
- Pilipili kavu iliyotwangwa kipimo 1
- (kama inapatikana) elemi resin (sura 6.10) kipimo 1
- Mafuta ya mbogamboga vipimo 4
Angalia yasiingie machoni! Na usiitumie kutibu watoto wadogowadogo.
Unapochua sehemu ambayo ngozi ni nene sana, ongeza kaolin kidogo ili kuleta
hali ya ujoto zaidi. (Tazama jalada la nyuma).
E) Mafuta kwa aliyevimba mishipa ya sehemu ya haja kubwa (Bawasiri) Tumia mimea ifuatayo – kutegemea na upatikanaji tumia baadhi au yote. Majani
yakatwekatwe na kukaushwa. Tumia baadhi au vyote vifuatavyo:
- Majani ya michaichai (sura 5.9),
majani ya msubili (lazima yakaushwe vizuri 6.3), majani ya mpera (5.14),
majani ya chamomile (6.29), majani ya mkurimbasi (6.35) ,
majani ya artemisia (5.2) jumla vipimo 2
- Mafuta mazuri ya mbogamboga , k.m. mafuta ya shea,
mafuta ya kokwa la mawese, au mafuta ya mzeituni vipimo 10
F) Mafuta kwa ajili ya upele Hapa hatuchemshi, bali tunachanganya tu:
- Mafuta ya taa (yatumikayo kwenye taa) kipimo 1
58
- Mafuta ya mbogamboga kipimo 1
Paka mara tatu kwa siku kwa muda wa siku 2.
Kama hospitali itajua juu ya maelezo haya haihitaji tena kununua benzyl benzoate
ambazo ni ghali au mchanganyiko wa Lindan!
Kwa chawa kichwani, paka kijiko kimoja cha chai cha haya mafuta kwenye
nywele mara mbili kwa siku, lakini isiwe zaidi ya siku 2 hadi 3. Mafuta haya
vilevile yanaangaliwa kama yenye uwezo wa kumsaidia mgonwja
anayesumbuliwa na filaria. Paka kwenye ngozi palipovimba.
4.4 MAFUTA YA (KUJIPAKA) DAWA
Maelezo: MMEA + MAFUTA + JOTO + NTA = MAFUTA YA DAWA
Ili kupata haya mafuta ya dawa, chemsha vitu vilivyotokana na mmea pamoja na
mafuta kwa dakika 60, katika fukizo – maji kama ilivyoelezwa katika sura 4.3.
Usipotumia njia hii mafuta yanaweza kuharibika kutokana na kupata joto kupita
kiasi. Chuja mafuta yakiwa bado na joto. Weka mabaki kwenye rundo moja. Yeyusha
nta na uichuje, changanya mafuta yaliyochujwa (yakiwa bado na joto) na nta
iliyochujwa (ikiwa bado na joto) na kisha koroga taratibu kwa dakika moja.
Mmea ni lazima uwe mkavu kabisa na utwangwe hadi kuwa kama unga.Tumia
mafuta yaliyo bora zaidi kadri inavyowezekana (k.m. mafuta ya mzeituni, mafuta ya
kokwa la mawese ) kwa kuvimba kwa mishipa ya sehemu ya haja kubwa (bawasiri)
na vipodozi. Tumia mafuta ya gharama nafuu kama vile mawese, au mafuta ya
karanga kwa ajili ya mafuta ya kuchua au ya maumivu ya viungo.
Faida ya mawese ni kwamba mafuta ya dawa yaliyotengenezwa kwa mawese
hayawezi kuvunda hata baada ya miaka mitano. Hata hivyo kama mafuta haya
yatatunzwa katika sehemu yenye joto kubwa, yanaweza kuwa yanakwaruza.
Kuyapasha joto kidogo huyafanya kurudia hali yake ya kawaida.
NTA: Kwa kutengeneza vipodozi au mafuta ya dawa kwa ajili ya ngozi laini
tumia nta ya nyuki tu. Kwa ajili ya mafuta ya kuchulia au maumivu ya viungo,
unaweza ukatumia nta za madukani; kwa kiasi kidogo cha dawa, mishumaa isiyo na
ranghi inafaa kabisa. Mchanganyiko wa mafuta /nta ni bora zaidi ukilinganisha na
Vaseline, kwa sababu Vaseline haipenyi kwenye ngozi. Kinyume na imani ya wengi,
vaseline ambayo pia huitwa “petroleum jelly’ sio nzuri kwa ngozi yako! Na hii
(Vaseline) ni kama mfuko wa plastiki juu ya ngozi yako; kwa maana hiyo, ni nzuri
kuitumia kabla ya kufanya kazi kama vile kutengeneza baiskeli au magari. Kamwe
usiitumie kama kipodozi kwa ajili ya uso wako!
Tunza mafuta ya dawa sehemu yenye ubaridi iwezekanavyo!
A) Mafuta ya dawa kwa ajili ya watoto (ointment for babies): - Mafuta ya mtoto (baby oil) (Taz. Sura 4.3) vipimo 9
- Nta ya nyuki kipimo 1
Chemsha mafuta na nta - tumia water bath kwa kuchemsha mafuta - halafu
changanya
B) Mafuta ya dawa kwa maumivu ya viungo: - Mafuta ya maumivu ya viungo (Taz. Sura 4.3) vipimo 9
59
- Nta ya nyuki kipimo 1
(Kama nta ya nyuki ni ghali, tumia kipimo 1 cha nta ya mshumaa)
Chemsha mafuta na nta - tumia water bath kwa kuchemsha mafuta - halafu
changanya.
C) Mafuta ya dawa kwa kuvimba mishipa ya sehemu ya haja kubwa (bawasiri). - Mafuta kwa kuvimba mishipa ya sehemu ya
haja kubwa (Taz. Sura 4.3) vipimo 9
- Nta ya nyuki kipimo 1
Chemsha mafuta na nta - tumia water bath kwa kuchemsha mafuta - halafu
changanya.
D) Mafuta ya dawa kwa ajili ya majeraha na kuungua - Vitunguu maji vilivyokatwa katwa,
na kukaushwa kwa siku moja kivulini kipimo 1
- Mafuta mazuri ya mbogamboga vipimo 10
- Asali safi vipimo 10
Chemsha mafuta na vitunguu kwa dakika 30 katika fukizo-maji na chuja. Ili
kuboresha uthabiti, unaweza kuongeza kipimo 1 cha nta ya nyuki iliyoyeyushwa.
Usiongeze zaidi, ya kipimo 1, kwa vile inaweza kupunguza kasi ya jeraha kupona,
kutokana na kupungua kwa kiwango cha oksijen kinachoingia kwenye jeraha.
Halafu ongeza asali na koroga taratibu.
E) Mafuta ya dawa kwa upele Changanya sehemu 1 ya sulphur kwenye sehemu 20 za Vaseline au mafuta ya
nguruwe ili kupata mafuta yenye 5% ya sulphur.
F) Uzuri wa ngozi ya uso
- Nyama ya parachichi lililoiva sana vipimo 6
- Juisi ya limau kipimo 1
Kipimo kimoja kinaweza kuwa kijiko 1 cha chai. Changanya muda wa jioni,
halafu paka usoni au ngozi iliyodhurika, na uioshe asubuhi bila kutumia sabuni.
G) Dawa ya kung’arisha viatu au protective grease - Mafuta ya mbogamboga ya bei rahisi vipimo 7
- Nta ya mshumaa usio na rangi vipimo 3
Chemsha pamoja, na acha ipoe. Hii
inaweza kutumika badala ya Vaseline.
Kwa viatu vyeusi, ongeza kipimo 1
cha mkaa uliotwangwa hadi kuwa kama
poda.
4.5 PODA
A. Poda ya watoto
Tumia mihogo tu, iliyokauka vizuri na iwe
nyeupe kabisa. Ikaushe tena kwa siku moja
kwenye jiko la jua. Itwange na uchekeshe
60
kwa kitambaa cha nailon. Kama huna jiko la jua, kausha kikombe 1 cha unga wa
mhogo taratibu sana kwenye sufuria lako hadi ukauke kabisa na kuwa kahawia
(brown) kidogo. Chekecha moja kwa moja baada ya kuchemsha , kwa kutumia
kitambaa cha nailoni. Kama ukipenda unaweza kuongeza tone moja la marashi kwa
kikombe kimoja cha unga uliochekecha. Tunza kwenye chombo kisichopitisha hewa.
B. Poda ya mkaa
Kuni kutoka kwenye mti, ambao hauna sumu wala utomvu unaojivuta (unaonata)
huchomwa hadi kuwa mkaa, kwa njia zilezile zinazotumika katika nchi za tropiki.
Kwa kuwa kuni mara nyingi ni rasilimali adimu, unaweza ukakata matawi ya katikati
ya mti wa mwembe kwa sababu matawi haya huwa hayatoi matunda. Au badala yake
chemsha maganda ya karanga ndani ya sufuria iliyofunikwa hadi yawe mkaa. Uwe
mwangalifu, kwa sababu unga huu unaweza ukaungua kuwa majivu muda wowote
sababu ya joto. Watoto wakae mbali kabisa. Ukipoa, utwange mkaa huo na
uchekeche kwa kutumia kitambaa cha nailoni. Ili kuua vijidudu kwenye unga wako
uliotengeza kutokana na mti wa mwembe au maganda ya karanga , chemsha unga
wako tena katika sufuria hadi uone chembe nyekundu: sasa vijidudu vyote vitakuwa
vimekufa. Hifadhi kwenye vyombo visivyopitisha hewa.
Unga huu hufyonza sumu na hewa. Kwa hewa tumboni, harufu mbaya mdomoni,
na kuharisha, watu wazima watumie kijiko 1 cha chakula mara 3 kwa siku.
Hata hivyo, kama watoto wanaharisha, kitu muhimu zaidi ni kurudisha maji
yaliyopotea kwa kumpa mtoto ORS, (Taz. Sura 4.6)
Kwa vidonda vinavyonuka na kutoa usaha, unaweza ukaweka katika jeraha, lakini
vidonda ni lazima viwe vya juu tu.
Kama mtu amekula mmea wenye sumu na hospitali /kituo cha afya kiko mbali,
jaribu kumtapisha (kwa kumwekea kidole kooni sehemu ya chini). Na kwa
kuongezea umpe vijiko vingi, ina maana gram 50 -100 za poda ya mkaa pamoja na
chai inayosababisha apate choo) (Taz. Mwingajini sura 5.7). Kama mtu amekunywa
mafuta ya taa, petroli au dizeli, usimtapishe kwa sababu ya uwezekano mkubwa wa
kupatwa na kichomi cha pafu, bali mpeleke mgonjwa kwenye kituo cha afya kilicho
karibu haraka iwezekanavyo. (Taz. pia mbono, sura 6.42).
C. Poda (unga ) yenye madini (Bolus rubra) Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, udongo mwekundu, ambao huitwa
“Itsama” na wenyeji wa huko hupatikana karibu na mito. Kidesturi wanawake
wajawazito hula udongo huu ili kukamilisha mahitaji yao ya madini.
Uchambuzi wa udongo huo ulikuwa kama ifuatavyo:
Calcium mg 2450/kg
Magnesium mg 1400/kg
Chuma mg 1400/kg
Manganese mg 152/kg
Copper mg 16/kg
Zinc mg 18/kg
Cobalt mg 3/kg
Madini mengi sana ajabu!! Sehemu kubwa ya jamii isingeweza kujipatia vidonge
vyenye madini haya vinavyopatikana kwenye maduka ya dawa.
Tunapendekeza kwamba unakausha udongo, unauchekecha na kisha unauchemsha
katika sufuria ili kuua vijidudu vinavyoweza kuwa kwenye udongo.
61
Jinsi ya kutumia:
Watoto wenye upungufu wa damu kijiko kimoja cha chai kwa siku.
Wakinamama wajawazito kijiko kimoja cha chakula kwa siku
Kama ikiwezekana, ili kusaidia utaratibu wa madini kufyonzwa kwenda mwilini,
kunywa pamoja na juisi ya limau saa moja kabla ya mlo.
D. Chumvi yenye madini ya joto.
Kausha kabisa kilo 1 ya chumvi na uisage kuwa unga. Ichanganywe taratibu na mg.
30 za potassium Iodine (Ili kuzuia goitre).
E. Chakula cha mtoto, cha unga Kuanzia umri wa miezi 6 mtoto wako anahitaji chakula ili kuongezea katika maziwa
ya mama. Epukana na matangazo yenye ushawishi na usinunue chakula chochote cha
mtoto dukani!! Chakula cha kutoka shambani daima ni bora! Na kama hakipatikani
(k.m. safarini) hapa kuna pendekezo kwa chakula cha mtoto cha kutengenezea
nyumbani ambacho ni cha kupendeza na chenye lishe bora:
- Vyakula aina ya mbegu (uwele, mchele, mahindi, ngano au mtama na ulezi)
viwe vikavu kabisa (Tumia sun box, vinginevyo oka kwa dakika 20,)
halafu saga gramu 650 au vikombe 3.
- Mikundekunde (maharage ya soya, maharage, njegere, dengu) chemsha kadri
ya dakika 20, kisha kausha kabisa na utwange gramu 350 au vikombe 2.
- Mbegu zenye mafuta (Njugu zisizo na magamba, ufuta gramu 100 au
kikombe 1.
- Majani ya kijani ya mlongelonge yaliyokaushwa (kama yapo) gramu 25 au ¼
kikombe.
- KWA UTAPIAMLO TU
- inaweza kuharibu meno yako! – sukari gramu 50 au ½ kikombe.
Changanya kwa mpangilio uliopo na uhifadhi kwenye chombo kisichopitisha
hewa, kutegemea na kiwango cha ukavu, (Taz. SURA 2.7). Mchanganyiko huu
hudumu kati ya juma 1 na mwaka 1. Kama unga sio mkavu sana vya kutosha, fungi
(mba) hatari huota na huhatarisha afya ya mtoto wako.
Kwa mlo mmoja, chemsha vijiko 2 vya chakula (unga) vilivyojaa kabisa vya
mchanganyiko huu kwa ml 350 za maji (nusu ya chupa ya lita yenye ujazo wa 0.7
lita) au changanya unga na maji ambayo yamechemshwa na yakapoa.
F. Poda (unga) kwa ajili ya meno
1. Kwa matumizi ya kila siku:
- Majani yaliyokaushwa ya mkaratusi kipimo 1
- Chumvi kavu (ya mezani) kipimo 1
Tafuta mti wa mkaratusi ulio katika mazingira safi (k.m. kwenye msitu) na vuna
majani mazuri zaidi ya mita mbili kutoka ardhini; yaoshe, yakaushe na yatwange
vizuri. Chemsha chumvi ndani ya sufuria. Ikiwa bado ya moto, imwage kwenye kinu
kilicho kisafi kabisa, wakati huohuo ukiongeza majani ya mkaratusi yaliyotwangwa.
Twanga pamoja, na chekecha kwa kitambaa cha nailoni. Tunza kwenye chombo
kisichopitisha hewa. Weka kiasi kidogo kwenye mswaki wako.
62
2. Poda kwa meno yanayooza. Changanya kipimo 1 cha chumvi na kipimo 1 cha jivu la kuni lililosafi. Weka kitawi
cha mwarobaini (au kitawi cha mkaratusi) ndani ya huu mchanganyiko na kisha
sugua kwa uangalifu kwenye madoa ya kahawia (brown) yaliyo kwenye meno. Sugua
mara 3 kwa siku. Hii inasaidia tu iwapo madoa ya uozo bado yako juujuu.
4.6 ORS (maji-chumvi)
Kwa matatizo yote ya kuharisha (hata kama yanaambatana na malaria, homa ya
matumbo, bacillary infection etc.) daima mpe mgonjwa ORS! Endelea kumpa
vyakula kama kawaida, ili kuzuia upungufu wa vitamin. Unaweza ukatengeneza
mwenyewe ORS, hakuna haja ya kununua vifurushi ambavyo ni ghali; hata vifurushi
vya bure vya ORS huwafanya watu kuwa tegemezi.
A. Vitu vilivyomo
Kwa mtu anayeharisha, kitu muhimu zaidi ni kurudisha maji yaliyopotea. Kwa
watoto au watu wazima, daima mpe mgonjwa maji haya yenye chumvi (ORS) ya
kutosha.
MAJI (ORS) haya yana vitu vitatu: Maji, sukari,
chumvi.
MAJI: Tumia maji mazuri, kama hakuna maji safi ya chemchemi karibu, tumia
maji yaliyochemshwa . Au pika chai ya majani ya mapera.
SUKARI: Ni vizuri zaidi ukitumia asali. Vinginevyo tumia sukari ya nyumbani
(katika hospitali tumia glucose). Kama huna sukari, au mgonjwa ana kisukari,
unaweza kutumia vitu vifuatavyo badala yake:
a) Kutwanga kiasi cha gramu 10 za ndizi sukari (usichemshe).
b) Viazi vitamu gramu 100 - chemsha dakika 5.
c) Gramu 30 (vijiko vya chai 3 vilivyojaa kabisa vya unga wa ngano, mchele
uliotwangwa au uwele. Chemsha vyote katika maji kwa muda wa kawaida.
CHUMVI: Ikiwezekana tumia chumvi ya kienyeji (iliyotengenezwa kienyeji
kutokana na majivu yaliyopatikana kutoka kwenye kuni zilizochomwa). Hii kwa
namna moja ni nzuri, kwa sababu jivu huwa lina potassium. Vinginevyo tumia
chumvi ya nyumbani (sodium chloride).
POTASSIUM: Ni kitu ambacho hakina budi kuongezwa kama mgonjwa
ataendelea kuharisha kwa siku kadhaa. Hata hivyo, potassium huongezwa kama
mgonjwa ana uwezo wa kukojoa. Potassium husaidia misuli ya utumbo na
matumbo kufanya kazi kwa hali yake ya kawaida. Potassium inapatikana katika
parachichi, ndizi, maboga, maji ya nazi, karoti, soya iliyopikwa, njugu, mchicha
na mboga zenye rangi ya kijani – nyeusi zilizopikwa kwa mvuke.Na kwa watoto
wadogo wanaohitaji potassium, a) wape sehemu ya chakula hicho, au b) wape
chumvi iliyotengenezwa kienyeji, au c) ongeza kijiko1 cha jivu safi (kutokana na
miti au nyasi zisizo na sumu, au majani ya magugu maji Eichhornia crassipes
yaliyokaushwa, ambayo ina potassium kwa wingi) kwenye lita moja ya maji
uliyotumia kutengeneza ORS (Taz. chini). Baada ya dakika chache, chuja maji.
63
Kama kitu kimojawapo ulichotumia (sukari, chumvi, maji) hakikuwa safi
kabisa, chemsha mchanganyiko kwa muda mfupi ili kuua bacteria.
B. Utengenezaji wa ORS nyumbani:
a) Katika lita 1 ya maji, ongeza vijiko vya chakula 4 vya asali au vijiko 2 vya sukari
(gramu 30), na chumvi kijiko 1 cha chai, au
b) Kwenye kikombe 1 (ml 500) cha maji, ongeza asali vijiko vya chakula 2 au kijiko
1 cha sukari, na chumvi kidogo (kiasi cha chumvi unachoweza kushika kati ya
kidole gumba na shahada).
C. Jinsi ya kutumia ORS: Mpe mgonjwa kwa siku: Ml 200 (glasi moja) kwa kila kilogramu ya uzito wa mtoto.
Kama hujui uzito wa mwanao na huwezi kupima mililita, lakini una chupa tupu, na
safi ya vinywaji baridi, jedwali lifuatalo litakusaidia:
Jedwali 4.1. : MATUMIZI YA ORS
UMRI Ukubwa wa chupa
Ml. kwa
siku
Lita 0.33 Lita 0.5 Lita 0.7 Lita 1
Chini ya miezi 6 700 Chupa 2 Chupa 1½ Chupa 1 Chupa ¾
Miezi 6 hadi
miaka 2
1,400 Chupa 4 Chupa 3 Chupa 2 Chupa 1½
Miaka 2 – 5 2,100 Chupa 6 Chupa 4 Chupa 3 Chupa 2
Zaidi ya miaka 7 2,800 Chupa 8 Chupa 6 Chupa 4 Chupa 3
Watu wazima 3,500 Chupa 10 Chupa 7 Chupa 5 Chupa 3½
D. Utengenezaji wa ORS mahospitalini:
Si busara kuagiza kutoka nje vifurushi vya ORS ambavyo vina dozi moja; hospitali
yo yote inaweza kujitengenezea.
Vitu vinavyohitajika kwa lita moja ya maji:
- Sodium chloride (chumvi ya kula) NaCl gramu 3.50
- Potassium chloride KCl gramu 1.50
- Glucose (dextrose) anhydrous gramu 20.00
- Sodium bicarbonate NaHCO3 gramu 2.50
Badala ya gramu 2.5 za sodium bicarbonate unaweza kutumia gramu 3.0 za
trisodium citrate dehydrate.
Kausha kabisa chumvi ya mezani na potassium chloride (k.m. katika jiko la jua),
twanga na halafu chekecha. Changanya chumvi, potassium chloride na bicarbonate,
kisha ongeza glucose (vyote viwe karibu kiasi sawa). Weka kwenye maboksi
yasiyopitisha hewa na kila boksi liwe na dozi 30. Vama hakuna glucose, tumia gramu
30 za sukari (sukari ya miwa) badala ya gramu 20 za glucose. Hii haitapunguza
nguvu ya ORS.
64
E. Tatizo la kuhifadhi Kwa kuwa vyombo visivyopitisha hewa ni vichache katika nchi za tropiki, na mara
chumvi inakuwa na vibonge au unyevunyevu; tumeandaa maelezo yafuatayo katika
pharmacy yetu:
- Potassium chloride gram 33
- Chumvi ya kula gram 100
- Sukari ya miwa (ya dukani) gram 600
- Maji ml 400
Yeyusha potassium chloride, kisha chumvi, halafu sukari (Tilia maanani
mpangilio ulioonyeshwa!) kwenye maji ya mtoto. Chemsha na chuja. Hii ina hata
manufaa ya kiafya kwa kuwa sukari na chumvi, ambavyo wakati mwingine huingiwa
na uchafu au vijidudu wakati wa kutayarisha au wakati wa usafirishaji kwenye
malori, wadudu hao huuwawa unapotumia maji ya moto.
Dozi: Weka vijiko 4 vya chai kwenye 0.7 lita ya maji.
4.7 JIWE JEUSI
Jiwe jeusi hutumiwa baada ya mtu kuumwa na nyoka au wadudu wenye sumu kali,
mfano nge. Nguvu zake ziko katika tabia ya jiwe hili ya kufyonza kiwango kikubwa
cha majimaji. Lina vifereji vingi sana na vifereji hivi vinafyonza kwa njia ya hewa
inayopenya katika vifereji hivyo na kwa njia hiyo kunata kwenye sehemu
ilipowekwa hadi kujazwa hadi mwisho.
Kwa kufanya majaribio, weka jiwe hilo jeusi kwenye ulimi wako; hunyonya majimaji
na kung’ang’ania kwenye ulimi. Lisipoondolewa haraka, huenda hata likasababisha
ulimi kuvuja damu wakati utakapoliondoa baadaye.
Muundo wa jiwe jeusi bado ni siri, kitu ambacho huwafanya baadhi ya wakristo
kutuhumu kuwa ni uchawi. Uwezo wake wa kufyonza sumu nyingi na vitu vingine
vya hatari ambavyo hutokana na kuumwa, umeelezwa katika vitabu vya tiba. Ni
lazima lipachikwe haraka mara baada ya kumwa. (ila
snake serum ina nguvu zaidi, lakini katika vituo vingi
vya afya ama haipatikani au ni ghali mno).
Namna ya kutengeneza jiwe jeusi Chukua sehemu ya katikati ya mfupa wa paja la
ng’ombe; kata kwa msumeno vipande vipande, (ukubwa unaokaribia sm 4 × sm 1.5).
Vichemshe mara mbili kwenye maji safi. Kisha chemsha tena kwenye maji yenye
sabuni au sodium hydroxide ili kuondoa mafuta yote yaliyobakibaki . Chemsha tena
katika maji safi ili kuondoa sabuni. Weka juani ukauke kwa muda wa siku 5 au katika
jiko la jua kwa siku moja. “Jiwe jeusi” ni lazima lishikwe au kubebwa kwa uangalifu
mkubwa: usiliweke katika maji ya moto wala kuliweka mahali joto linapobadilika
kwa haraka, kwa sababu kwa hali hizo vifereji vilivyomo ndani ya jiwe, ambavyo
huleta uwezo wa kufyonza, huharibika mara moja. Liache likauke ama kwa siku 3
juani na kisha ndani ya sufuria kavu juu ya moto au kwa siku moja ndani ya jiko la
jua. “Mawe” haya sasa huonekana kama pembe za ndovu.
Fungasha kila kipande ndani ya karatasi 2 nyembamba za aluminia (aluminium
foil). Weka vipande hivyo kwenye sehemu ile nyekundu sana ya moto wa mkaa
65
katikati , na funika kwa mkaa kidogo uliotwangwa. Kagua kipande kimoja baada ya
dakika 40; linatakiwa kubadilika kuwa jeusi na gumu, kuwa kama makaa ya mawe,
lakini bila kuungua. Kama limetengenezwa kwa njia sahihi, jiwe jeusi hunata kwenye
ulimi. Na kama haling’ang’anii ulimi, linahitaji kurudishwa kwenye moto. Kama jiwe
linavunjika kwa urahisi au hata limekuwa kama majivu meupe, basi jiwe hilo
litakuwa limeungua.
Lakini likiwa jeusi, gumu na linanata kwenye ulimi, litakuwa limekamilika na
tayari kwa kutumika.
Namna ya kutumia jiwe jeusi:
Kuumwa na nyoka: Gandamiza kwenye jeraha hadi jiwe ligusane na majimaji.
Mara jiwe linapogusana na damu, hung’ang’ania kwenye jeraha na haliondoki
hadi sumu yote na uchafu vimefyonzwa . Na hii inaweza ikachukua siku nzima.
Majipu na vijeraha vyenye usaha: Vunja jiwe jeusi kulingana na ukubwa wa jipu/
jeraha. Ligandamizie kwenye jipu/ jeraha hadi ligusane na majimaji ya kwenye
jipu/ jeraha. Jiwe jeusi huondoa kila uchafu, kwenye jipu/ jeraha, hivyo kufanya
sehemu kubwa ya vijidudu kufyonzwa na kuondolewa.
KULIPA NGUVU TENA JIWE JEUSI Baada ya kutumika jiwe jeusi huchemshwa kwenye maji kwa dakika 10, kwanza
kwenye maji ya sabuni, kisha kwa dakika 10 zingine kwenye maji safi. Hii inafanyika
ili kuliondolea uchafu katika vifereji vyake na kulisafisha kabisa jiwe ili kuzuia
maambukizi yoyote kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
4.8 DIVAI YA ASALI
Mvinyo ya asali inatumika kama kitu cha msingi kwa mvinyo zenye dawa na syrups.
Ikitengenezwa vizuri ina kileo 12 – 14%
Asali lita 2.5 sawa na chupa 2 ½ ya lita 1
Maji lita 2.25 sawa na chupa 2 ¼ ya lita 1
Juisi ya matunda lita 0.25 sawa na robo chupa au kikombe 1 cha chai.
Kama asali haipatikani:
Sukari kilo 2
Maji lita 2.75
Juisi ya matunda lita 0.25
Unaweza kutumia juisi kutoka kwenye tunda lolote
k.m. embe, chungwa, limau. Juisi ni muhimu kwa
kuwa hutoa hamira na madini yanayohitajika.
Chemsha mchanganyiko kwa dakika 15, chuja na
mimina kwenye chombo chenye ujazo wa lita 5
(inapendekezwa chombo kiwe cha glasi au plastiki).
Acha mchanganyiko upoe. Ongeza hamira nusu
kijiko cha chai (kuna hamira maalum kwa kazi hii, lakini hamira ya kawaida ya
kuokea inafanya kazi pia).
66
Toboa tundu dogo kwenye mfuniko wa chombo na ingiza mpira mwembamba
wenye uwazi katika (k.m. mipira inayotumika kuongeza maji wagonjwa mahospitali
ni).
Ncha nyingine ya mpira huo inaingizwa kwenye kikombe cha maji kilichojaa. Hii
inasaidia carbon dioxide isiyohitajika kuweza kutoka nje - bila oksijen kuingia ndani
ya chombo na kuharibu mvinyo.
Tunza chombo chenye kinywaji hiki sehemu yenye uvuguvugu na uitikise taratibu
kila siku. Baada ya majuma 2 – 3 utaratibu wa kutengeneza chachu unakamilika.
Chuja mvinyo kutumia kitambaa safi. Tunza mvinyo kwenye chupa isiyoingiza hewa,
kwenye sehemu baridi na isiyo na mwanga.
4.9 DAWA YA KIKOHOZI (Cough Elixir)
Divai ya asali lita 5
Majani ya mkaratusi makavu yaliyotwangwa gramu 250
Changanya na tunza sehemu yenye uvuguvugu, ikiwa imefunikwa bila kukaza sana,
kwa siku 5. Chuja na hifadhi ndani ya chupa isiyoingiza hewa, sehemu yenye ubaridi
na isiyofikiwa mwanga.
Jinsi ya kutumia:
Watu wazima Kijiko 1 cha chai, mara 3 kwa siku.
Watoto (mwaka 1 na kuendelea) Matone 20 – 40 , mara 3 kwa siku.
4.10 MADINI NA VITAMINI
Ni kitu kinachosikitisha sana, kwa sababu tu ya ukosefu wa pesa, watu wengi katika
nchi za tropiki wanaugua au hata kufa kwa njaa. Lakini inakuwa ni vibaya zaidi
wakati ambapo matatizo haya yanatokana na matangazo ya kibiashara
yanayokushawishi kununua bidhaa zinazoelezwa kuwa ni za “kuleta hamu ya
chakula”, juisi za vitamini n.k.
Bidhaa hizi siyo za lazima wala hazistahili. Nyama ni gharama nafuu na
inakuongezea nguvu kuliko dawa ya “sana – vita – liver – extract.”; “Vitamin E”
inapatikana kwa wingi katika majani ya mihogo kuliko katika vidonge vya “paradiso
– impotex.”
Kuna mwanamke mmoja katika kijiji chetu nchini D.R. Kongo ambaye alitumia
ujira wake wa wiki nzima kwa kununua chupa moja ya maji mekundu ya madukani
akiamini yataimarisha damu ya mwanae. Je mama huyu alikuwa ni mwanakijiji wa
kawaida? Ngoja tuangalie pia kidogo katika baadhi ya hospitali za serikali na
makanisa, hata katika miji mikuu. Bajeti zinapangwa kwa ajili ya vitu kama “vidonge
vya vitamini B,” “vitamin E forte,” “haemo-vit-orange” na dawa zingine zenye
majina ya kutamanisha sana.
Watu wanaohusika nadhani wangefanya vizuri zaidi kama wangeweka
machungwa na karanga kwenye makabati ya maduka yao ya dawa!!
1. Vitamin A: Ni muhimu kwa kusaidia macho kuona vizuri . Inapatikana kwenye
matunda na mbogamboga zote zenye rangi nyekundu na rangi ya machungwa:
papai, karoti, nyanya, embe, kwenye mayai na matunda jamii ya nazi. Pia
67
mawese yana vitamin A kwa wingi sana. Katika nchi za Afrika ambapo mawese
hupatikana kwa wingi, ni watu wachache wanaopata upofu. Kwa nchi za
mashariki na kusini mwa Afrika, ambako michikichi ni michache, tunapendekeza
kupanda na kula viazi vitamu vyenye rangi ya njano (chungwa), ili kuepuka
kutumia vidonge vya vitamini A.
2. Vitamin ‘B’ Complex: Ni muhimu kwa watu wanaojihisi kuwa dhaifu na kwa
matatizo ya mishipa ya fahamu. Vitamin hizi ni za muhimu kwa kusaidia
uyeyushaji na ufyonzaji wa carbohydrates (wanga), k.m. sukari na unga. Chakula
kinachopatikana katika maeneo ya vijijini kama vile njugu, soya, maharage,
karanga, nyama, samaki, mboga zenye majani ya kijani, hamira, makapi ya
mpunga na maziwa ya mama ambayo yana kiwango kikubwa cha vitamini hizo.
Kwa hiyo, ni kosa kubwa, kuuza njugu ili kununua biskuti za vitamin ‘B’.
3. Vitamin C: Mfumo wa asili wa ulinzi wa miili yetu ambako huulinda na
maambukizi, hupatikana katika vitamin C. Watoto wenye umri hadi miezi 6
hupata kiasi cha kutosha cha vitamin C kutoka maziwa ya mama zao. Zaidi ya
umri huu ni lazima mtoto ale aina zote za matunda (hasa machungwa, ndimu, na
matunda ya passion), mbogamboga (majani ya kijani, vitunguu maji, viazi vitamu
n.k.). Matunda na mbogamboga ni bora zaidi vikiliwa bila kupikwa, kadri
unapozidi kuvipika vitamini C hupungua zaidi. Tofauti na vitamin A, vitamin C
huwa haihifadhiwi mwilini, kwa hiyo matunda na mbogamboga ni lazima viliwe
kila siku.
4. Vitamin D: Husaidia ukuaji wa mifupa. Vilevile mwili una uwezo wa
kujitengenezea vitamini D kutokana na jua. Mayai na mafuta ya wanyama pia
vina vitamin D.
5. Vitamin E: Inapatikana kwenye majani ya kijani na mafuta ya mbogamboga.
Manufaa yake kwa afya ya binadamu bado hayajafahamika wazi. Katika
matangazo vitamin hii huitwa “vitamin ya rutuba”; lakini, pamoja na hayo,
hakuna mtu hata mmoja ambaye amepata mtoto kwa ajili ya dawa ya Vitamin E.
6. Vitamin K: Husaidia damu kuganda unapopatwa na ajali (k.m. kujikata).
Inapatikana kwenye majani ya kijani na huzalishwa vilevile na baadhi ya vijidudu
vya kwenye utumbo. Kuna desturi moja ambayo haina manufaa na hufanywa na
baadhi ya wodi za wazazi, ya kumpa vitamin K kila mama baada ya kujifungua.
Hii vitamin inastahili tu kwa mjamzit mwenye upungufu wa Vitamin K.
7. Folic acid: Ni ya lazima kwa watu wenye matatizo ya kupungukiwa damu.
Inapatikana kwa kiwango kikubwa katika maini na mboga za majani za kijani.
8. Calcium : Calcium ina jukumu muhimu katika ufanyaji kazi wa seli za mwili,
hasahasa katika misuli na mifupa . Kidonge cha calcium kilichonunuliwa dukani,
kina kiwango kilekile cha calcium (gram 200) kama samaki mkavu gram 10,
unga wa maziwa gram 30, mboga mboga za kijani gram 100, au maharage gram
200.
9. Chuma: Madini ya chuma huiwezesha miili yetu kuzalisha haemoglobin,
ambayo huleta rangi nyekundu katika damu. Kujaribu kutibu upungufu wa damu
68
Vitamins – chaguo ni letu!
A. Kwanza umepewa mifano ya vitamin.
B. Halafu ikupase kuzinunua kwa bunda la noti kutoka duka la madawa.
C. Pale ambapo asili inakupa vitamini hizo bure.
B
A
C
69
kwa kutumia juisi au soda nyekundu, hakuna manufaa yoyote! Ni bora zaidi kula
aina zo zote za mboga za majani. Jaribu kufanya lolote linalowezekana ili kuzuia
magonjwa yanayosababisha upungufu wa damu, k.m. malaria, kuharisha kwa
muda mrefu na safura!
Matumizi ya vikaango na masufuria yaliyotengenezwa kwa chuma halisi ni njia
vilevile inayopendekezwa, lakini sio yaliyotengenezwa kienyeji kutokana na bodi
za magari au mapipa, kwa sababu haya huwa yamechanganywa na baadhi ya
metali zenye sumu.
Ili kukifanya chakula kiwe na madini mengi ya chuma, unaweza ukaweka
misumari yenye kutu (lakini iwe misafi) kwenye sufuria wakati wa kupika. Kwa
njia hii kiasi kidogo sana cha chuma huingia kwenye chakula na hivyo mwilini
(miili yetu inafyonza madini kidogo sana kwa siku moja). Au unaweza kuchoma
msumari mrefu wenye kutu ndani ya chungwa au limau (msumari uwe msafi) na
baada ya siku tatu uchomoe na kula hilo tunda; au kamua juisi na kunywa, juisi
itakuwa na madini ya chuma. (Tindikali iliyomo kwenye tunda hubadili chuma na
kuwa madini yaliyoyeyukia ndani ya tunda).
10. Madini ya joto: Katika maeneo yaliyo mbali na bahari, watu wengi hupatwa na
goitre sababu ya upungufu wa madini ya joto, ambayo sanasana hupatikana kwa
viumbe (samaki) wa baharini. Kwa hali hiyo tunapendekeza kununua ml. 30 za
“lugol 0.1%” kutoka duka la madawa, na halafu weka matone 1 – 10 kwa siku
kwa kila mtu katika chakula ulichokiandaa.
Maelezo kwa duka la madawa: Changanya mg. 100 za madini ya joto na mg
200 za Potassium Iodide, na yeyusha mchanganyiko huu kwenye ml. 100 za maji,
yaliyochemshwa na kuchujwa. Gawanya na tunza kwenye vyombo vya kioo, sio
uya plastiki au metali.
4.11 MAZAO KWA MIFUGO NA MATUMIZI YA KILIMO
A. Matofali ya kulamba kwa mifugo:
Sementi Mifuko (2 kilo 50
kila mfuko)
Udongo mwekundu Toroli 2
Chumvi ya kula kilo 35
Iron Sulphate kilo 2
Copper sulphate kilo 1
Magnesium sulphate gramu 100
Manganese sulphate gramu 100
Matofali ya kulamba hutengenezwa kwa kifyatulio. Kama aina hizo tofauti za
sulphate hazipatikani chukua sementi, udongo mwekundu, na chumvi tu. Kama
hakuna sementi wala kifyatulio, tengeneza mchanyanyiko wa udongo mwekundu,
jivu la kuni na chumvi. Lakini kama hivi navyo havipatikani wape mifugo majivu ya
kuni.
B. Upele na kupe: Kwa chawa au kupe waliong’ang’ania kabisa kwenye ngozi, ama tumia mafuta ya
upele (Taz. Sura 4.3.f). au twanga majani makuukuu ya Tephrosia na (ukiwa umevaa
mipira) paka kwenye ngozi pamoja na maji kidogo au mafuta.
C. Maumivu ya viungo: Taz. Sura 4.3.D.
70
D. Mkaa kwa wanyama wanaoharisha: Taz. Sura 4.5.B.
Mpe gramu 0.1. – 0.5. kwa kila kilo ya uzito wake kila siku. Mkaa wa biashara
hufanya kazi vizuri.
E. Dawa ya viroboto kwa kuku (ndege wafugwao)
Katika nchi za tropiki, hasa wakati msimu wa mvua, kufuga vifaranga ni vigumu
sana. Mara tu vifaranga wanapototolewa, melfu ya viroboto kutoka kwa kuku huanza
kuvishambulia. Viroboto hung’ata na kung’ang’ania eneo linalozunguka macho ya
vifaranga na kuku.
Matokeo yake kuku hutaga mayai kidogo na upande wa vifaranga hupoteza damu,
hudhoofika na baadaye kufa. Viuatilifu vyenye kemikali kama DDT na Lindane ni
vya hatari sana na vinatufanya hatimaye kula sumu pindi tulapo mayai yenye dawa.
Ili kuzuia hali hii,
kuku wapewe majivu ya kuchakurachakura.
viota vyao vitandaziwe majani ya mikaratusi, majani ya tumbaku au
michaichai na pia majivu.
vifaranga wapate nafasi ya kuzungukazunguka kwenye maeneo yenye nyasi.
paka mawese kwenye vichwa vya vifaranga mara 1 – 3 kwa wiki, kwa wiki 3
za kwanza za maisha yao.
Kwa vifaranga vikubwa na kuku, tumia mchanyanyiko wa kipimo 1 cha mawese na
kipimo 1 cha mafuta ya taa. Kwa kukushukuru kuku wako watataga mayai mengi
zaidi.
F. Dawa ya minyoo kwa wanyama
Taz. Sura 5.5; mpapai: Mpe juisi ya papai bichi, (ml. 3 kwa kila kilo 10 za uzito wa
mwili). Halafu endelea kuwapa mbegu za mapapai mara kwa mara. Mbwa wetu
(mwenye kilo 10) aliwahi kula papai zima mara kwa mara. Mbwa vilevile hupendelea
kula michaichai ili kupigana na minyoo. Nguruwe anatakiwa ale papai moja bichi
kila siku.
G. Tiba ya majeraha (kwa wanyama tu)
1. Tiba ya Antiseptic
Mafuta ya mbogamboga yasiyo ghali gramu 140 (kopo 1 dogo)
Nta gram 20 (½ mishumaa)
Commercial creosote gram 5 (kijiko cha chai)
Chemsha mawese na nta, acha vipoe kidogo, ongeza kijiko cha chai cha creosote
na koroga hadi mchanganyiko ubadilike kuwa dawa ya mafuta. Au badala yake,
twanga majani mabichi ya tumbaku au mkaritusi na funga kwenye jeraha.
2. Tiba ya antiseptic kwa wanyama wadogowadogo .
Tumia sukari au kipande cha papai bichi kama ilivyoelezwa kwa binadamu.
Mchanganyiko wa mafuta ya mbogamboga na majani ya mkaratusi (Taz. Sura
5.10) husaidia kuzuia nzi kutua kwenye jeraha.
3. Tiba ya antiseptic kwa mifugo
Kusafisha vidonda, tumia mkaa uliotwangwa na kuchekecha kutokana na majani
ya mkaratusi na majani ya tumbaku, chumvi kidogo au mchanganyiko wa vyote
hivi. Kiasi kidogo sana cha oil ya magari vilevile kinaweza kutumika.
71
H. Upungufu wa madini na vitamin kwa kuku (ndege)
Katika maeneo mengi “kuku wa kisasa” wanapatikana, na hiyo ni nzuri. Lakini mara
nyingine watu watakushawishi kununua chakula “cha kisasa” kwa kuku wako kwa
vile kina madini na protein nyingi zinazohitajika kwa kuku hawa. Usidanganyike kwa
hadithi hizo za ki-biashara – virutubisho vyote vinapatikana katika kijiji chako!
PROTINI:
Kuku na vifaranga wako wanahitaji “nyama” (lakini sio unga wa maziwa, ingawaje
unaweza kuwa umeandikwa katika vitabu). Wakati wa mchana waruhusu kuku
kuzurura ili kujitafutia vijidudu vya kula. Wape majani ya kijani wanayopendelea.
Weka rundo la mchanganyiko wa vitu vinavyooza ndani ya zizi la kuku. Rundo hili
litawavutia nzi na minyoo wengi; vyote hivi ni protini nzuri tu ambayo italiwa na
kuku na vifaranga wako!
VITAMIN:
Mara kwa mara wape aina zote za matunda na mbogamboga; mapapai, maembe, nazi,
vitunguu maji, pilipili kichaa n.k. Matunda yaliyodondoka na yakaanza kuoza
yatupwe kwenye ngome ya kuku.
Unapowalisha mahindi, usiyasage bali uyaloweke (yale tu utakayowapa kwa siku)
usiku kucha kwenye maji. Kisha mwaga maji asubuhi, na uyaache mahindi kwenye
unyevunyevu na kivulini kwa siku zingine 2 – 3 (yaoshe mara mbili kwa siku) hadi
kimea kifikie sm 3. Halafu wape vifaranga mahindi hayo yaliyoota – yana vitami
nyingi mno!
MADINI:
Wawekee kuku majivu kutoka jikoni na vilevile uwachanganyie na uwape
mchanganyiko wa kilo moja ya udongo mwekundu, chumvi gram 100 na gram 100
za chokaa iliyotiwa maji (slaked lime), ambavyo watavifikia muda wowote wakitaka.
Vilevile wape makaka ya mayai, lakini yawe yamechemshwa sana na kutwangwa, au
kuchemshwa katika jiko la jua, ili kuzuia kusambaza magonjwa.
I. Viuatilifu (insecticides) kwa matumizi ya kilimo:
Epuka vuatilifu vyenye kemikali inapowezekana. Hatari ni kwamba, kama wadudu
watakuwa na sumu, hata ndege wanaowala wanakula sumu. Na sio ndege tu
wanaokufa, ambao hudhibiti ongezeko la wadudu na mbu, lakini kemikali hizi
zinaweza pia kuua watu. Mfano E. 605, au kubaki katika mazingira kwa miaka mingi
mfano DDT.
Viuatilifu vinaweza kuzalishwa kutokana na mwarubaini (Azadirachta indica,
Taz. Sura 5.3), tumbaku (Nicotiana tabacum, sura 6.34) na tephroson (Tephrosia
vogelii, sura 6.46). Madhara ya tumbaku na tephrosia ni kwamba wadudu wote
wanauwawa hapo hapo, na mimea iliyonyunyiziwa dawa haiwezi kuliwa hadi wiki
mbili zipite.
Mwarubaini una sumu kidogo na mtu anaweza kula mboga ambayo
imenyunyiziwa dawa ya mwarubaini moja kwa moja, na wadudu wenye manufaa
kama vile nyuki watakaotua kwenye mimea hawafi.
72
SURA YA 5
UTANGULIZI Sura hii ina maelezo ambayo tunayapendekeza sana. Tunawatia moyo kupanda na
kutumia mimea hii 15 ya dawa; ni mimea yenye manufaa na ina matumizi mengi.
Karibu mimea yote hii hutumiwa na viwanda vya madawa barani Ulaya kutengeneza
mazao ya biashara, ambayo wakati mwingine huuzwa barani Afrika kwa bei kubwa.
Ili kuchagua tiba iliyo bora kwa ugonjwa fulani, tafadhali rejea sura ya 8. Katika
sura hiyo mimea na michanganyiko yake vimeelezwa, kwa mjibu wa uzoefu wetu, na
kwa kufuata nguvu za madawa yenyewe.
Kwa kutumia mimea hii, hata familia masikini zinaweza kutengeneza dawa na
kutibu magonjwa fulani wao wenyewe kwa gharama ndogo sana.
Kwa hiyo tunapendekeza uanzishe bustani ya dawa, ambayo ni yako mwenyewe,
ukianza na mimea hii 15. Na utaweza kutumia mimea hiyo chini ya mwaka1 tangu
kusiha au kupanda.
Katika sura hii, tunaorodhesha mimea kwa kufuata alfabeti, na kwa mjibu wa
majina yake ya kilatin, (majina ya kisayansi).
Kwa kila mmea tumetoa:
Maelezo ya kibotania
Baadhi ya vidokezo namna ya kulima
Sehemu za mimea zinazotumika.
Baadhi ya matumizi kutoka nchi zingine, hata hivyo sababu ya upungufu wa
uzoefu na ufahamu, hatuwezi tukayapendekeza.
Maelezo ya kina ya magonjwa ambayo tunajua yanaweza kutibika, na maelezo
ya kina ya utengenezaji na usimamizi wa madawa ambayo tuna uzoefu nayo.
Maelezo ya madhara yanayoweza kutokea.
Wafanyakazi wa afya na wahudumu wanaombwa kutoa maonyo ya wazi na yasiyo
ya mzaha, kwamba michanganyiko hii ya madawa haina maana kuwa ni badala ya
darubini au baadhi ya vifaa vya kitaalamu vinavyotumika kwenye vituo vya afya
kupima magonjwa. Pia michanganyiko hii haina uwezo kamwe wa kutumiwa kama
chanjo.
Michanganyiko hii imekusudiwa kuboresha uhusiano mzuri kati ya wagonjwa na
madaktari na wahudumu wengine wa afya. Maelezo haya yanaongeza kwa kiwango
kikubwa tiba zilizopo mahospitalini, vituo vya afya na majumbani. Lakini
TAFADHALI UWE MWANGALIFU. Baadhi ya mimea iliyoelezewa katika kitabu
hiki pia ni sumu, na inaweza kusababisha matatizo makubwa kama utabadili maelezo,
au kutumia isivyotakiwa.
MIMEA 15 MUHIMU - KAZI NA ATHARI ZAKE
73
5.1 Allium sativum Kitunguu, Swaumu
Maelezo ya kibotania: Familia: Liliaceae Kitunguu swaumu ni zao linalovumilia hali ngumu ya hewa. Huweza kufika urefu wa
sm 30 hadi 90 na kitumba chake huzaa vikonyo kati ya 5 na 15. Asili yake ni sehemu
ya Kaskazini ya dunia na Afrika ya Kusini na sasa vinalimwa pia katika nchi za joto.
UKULIMA
Kitungu swaumu hupendelea udongo wenye rutuba na
laini. Tenganisha vikonyo kwa uangalifu kutoka
kwenye kitunguu, na panda sehemu yenye kivuli kadri
ya sm 5 kwenda ardhini, sm 15 kutoka mstari na sm 30
kutoka mche. Katika hatua za kwanza za ukuaji,
kitunguu swaumu huhitaji maji mengi. Mara mmea
unapoanza kutoa maua, likate ua ili nguvu ya mmea
ielekee kwenye kitunguu (kitumba). Muda wa kuvuna
ni pale majani yanapobadilika kuwa kahawia na
kuanza kunyauka. Viweke vitunguu swaumu vikauke,
kwenye kivuli ambapo kuna mkondo mzuri wa hewa,
na kisha kwa uangalifu pangusa udongo na majani ya
nje (hii ikifanyika katika hali ya unyevu, vikonyo vitaharibika). Tunza kwenye
chombo cha udongo (ili kukinga unyevunyevu).
SEHEMU INAYOTUMIKA: Vikonyo
MATUMIZI KATIKA NCHI MBALIMBALI Kitunguu swaumu ni kiungo muhimu katika chakula kwa sehemu nyingi duniani. Na
katika Misri ya zamani, kililimwa kwa ajili ya miungu!
UTENGENEZAJI WA DAWA ZA KITUNGUU SWAUMU
Asali ya kitunguu swaumu. Jaza jagi la kioo kwa vikonyo vya vitunguu
vilivyomenywa na kukatwakatwa. Halafu mimina asali taratibu ambayo itaingia na
kujaa kwenye mianya iliyo kwenye vikonyo. Weka jagi (gudulia) kwenye sehemu ya
uvuguvugu wa kadri ya 20° C. Kwa muda wa wiki 2 hadi 4, asali itafyonza juisi ya
kitunguu swaumu, na kitunguu kitakuwa tepetepe na kizito. Usichuje, na uitumie
katika muda wa miezi.
Mchanganyiko wa dawa ya kikohozi ya kitunguu swaumu. Twanga kijiko cha
chai kimoja cha vikonyo vya kitunguu swaumu na kiasi kile kile cha sukari au asali.
Tumia hapo hapo, mfano kwa kikohozi.
Mafuta ya kitunguu swaumu. Weka gram 200 za vitunguu swaumu
vilivyomenywa na kupondwapondwa ndani ya gudulia lenye mdomo mpana na
ongeza mafuta ya kutosha ya mzeituni (au mafuta mazuri ya mbogamboga) ili
kufunika. Funga vizuri kabisa gudulia, na likae sehemu yenye ujoto wa kadri ya 20º
kwa siku tatu. Litikise mara chache kila siku. Kisha hifadhi sehemu yenye ubaridi,
bila kuchujwa. Tumia katika muda usiozidi mwezi mmoja.
Dawa ya maji ya kitunguu swaumu. Loweka gram 200 za vitunguu swaumu
vilivyomenywa na kukatwakatwa katika lita moja ya mvinyo kali ya zabibu au
74
alcohol nzuri 40 – 50% kwa siku 14 katika joto la 20º ndani ya chupa yenye mfuniko
uliobana kabisa. Tikisa chupa mara kadhaa kwa siku. Kamua vipande vya kitunguu
swaumu. Dawa hii hudumu hadi mwaka mmoja.
MAPENDEKEZO YA NAMNA YA KUTUMIA
Kula kitunguu swaumu kisichopikwa – hii ni bora zaidi!
Tumia katika mapishi.
Kula Vitunguu swaumu kwa wingi kwa ajili ya kuzuia magonjwa. Kitunguu
swaumu ni mfano mzuri ambao ni halisi, kwamba chakula chako kiwe ndio dawa
yako, na dawa yako kuwa chakula chako. Hata hivyo, hii ni kweli pale tu ambapo
vitaliwa vibichi, kwa kuwa virutubisho vingi huharibika vinapopikwa. Vitunguu
swaumu vibichi huimarisha mfumo wa kinga. Ulaji wa vitunguu swaumu kwa
utaratibu maalum umeonyesha kupunguza matukio ya matatizo ya moyo, saratani,
shinikizo la damu, mafua na kiharusi.
Tunapendekeza sana kwa Waathirika wa UKIMWI kula vitunguu swaumu vibichi
na kuvitumia katika milo ya kila siku, ili kupunguza matukio ya magonjwa mengine.
Kwa sababu kinatumika nje na ndani kama kisafisha mwili, kitunguu ni muhimu
katika tiba ya magonjwa yote ya kuambukiza: Homa ya matumbo, minyoo, kichocho,
malaria, kusafisha damu n.k. Zaidi, vitunguu swaumu vibichi huimarisha uwezo wa
kukumbuka, kupunguza shinikizo la damu na homa, na kina nguvu dhidi ya kuvimba
kwa arteri na kuwa ngumu (Arteriosclerosis).
Vilevile kitunguu swaumu kina anti-viral na anti-fungal properties.
1. Majipu au majipu yasiyo na midomo na warts
Ponda ponda vitunguu swaumu vibichi, halafu weka mseto ulioponda kwenye jipu,
jipu lisilo na mdomo au mara mbili kwa siku kwa kutandaza kwenye jipu. Anza tiba
hii mapema iwezekanavyo.
2. Ameba
Katakata vitunguu swaumu katika vipande vidogovidogo kisha chukua kijiko 1
kikubwa pamoja na chai mara 3 kwa siku (Usitafune, ili kuzuia harufu mbaya).
Endelea na tiba hii kwa siku tano.
3. Malaria
Katakata kitunguu swaumu vipande vidogovidogo sana. Kisha tumia kijiko1 cha
chakula cha vitunguu viulivyokatwakatwa mara 3 kwa siku, na kunywa lita 2 za chai
ya michaichai kwa siku. Endelea na tiba hii kwa siku tano. Tazama pia chini ya
malaria sura 8.
4. Kisukari, shinikizo la damu, kuzuia arteri kuvimba na kuwa ngumu
(Arteriosclerosis).
Kula vitunguu swaumu kwa wingi – vitunguu swaumu na vitunguu maji hupunguza
kiwango cha sukari katika damu, kiwango cha lehemu katika damu na shinikizo la
damu. Au tumia matone 20 ya dawa ya maji ya kitunguu swaumu mara tatu kwa siku,
lakini hii haina manufaa makubwa.
5. Kikohozi, mafua, madonda ya koo na sinusitis a) Kula kikonyo kimoja cha kitunguu swaumu mara tatu kwa siku.
75
b) Tumia kijiko kimoja cha chai cha asali ya kitunguu swaumu kila baada ya saa
chache.
c) Watoto wanaweza kutumia kijiko kimoja cha chai cha mchanganyiko wa dawa ya
kikohozi ya kitunguu swaumu kila baada ya saa chache.
d) Tumia kijiko cha chai kimoja cha mafuta ya kitunguu swaumu mara 6 kwa siku.
6. Mtando mweupe mdomoni (fungus)
Tumia kijiko cha chai kimoja cha kitunguu swaumu au asali ya kitunguu swaumu kila
baada ya saa chache. Kaa nayo mdomoni muda mrefu iwezekanavyo.
7. Maambukizi ya mba ikiwemo athlete’s foot. Funika eneo lililoathirika kwa kutumia ama juisi ya kitunguu swaumu kibichi au
mafuta ya kitunguu swaumu
8. Homa ya matumbo na maambukizi mengine
Kwa matatizo ya homa ya matumbo, kifua kikuu, kipindupindu, malale (sleeping
sickness) na bacillary dysentery, daima ongeza vitunguu swaumu katika tiba yako ya
kawaida.
9. Kuzuia damu kugandaganda (thrombosis)
Vitunguu swaumu huifanya damu kuwa laini na huzuia muundo wa damu kuganda
ambako husababisha thrombosis. Na hii ni muhimu zaidi kwa wagonjwa ambao
wamekuwa vitandani kwa muda mrefu.
10. Kwa watoto wanaoota meno
Sugua fizi kwa kikonyo cha kitunguu swaumu.
ATHARI (SIDE EFFECTS)
Vitunguu swaumu vinaweza kuleta mwasho kwa ngozi, hususani baada ya kutumiwa
kwa muda mrefu. Angalia sana kisiingie machoni.
5.2 Artemisia annua anamed (A3)
Maelezo ya kibotania: Familia: Compositae Jamii za porini za Artemisia annua hustawi katika hali ya hewa ya joto dunia nzima.
Artemisia annua anamed ya mbegu mbili tofauti imetokana na mimea ya asili ya
China na Vietnam. Ina ubora kwa kuwa inastawi katika maeneo ya tropiki, hutoa
majani kwa wingi, na majani haya yana artemisinin kwa wingi, kitu ambacho kina
nguvu sana ya kutibu malaria. Mmea huu wa mbegu mbili tofauti hukua hadi kufikia
urefu wa meta 3, lakini haustahimili theluji na unahitaji ukulima wa uangalifu na
makini sana.
UZURI WA ARTEMISIA ANNUA Kwa sababu vimelea vya malaria vimeanza kuonyesha usugu kwa dawa za madukani,
ambazo zimekuwa zikitumiwa kutibu malaria kwa miaka mingi, madawa haya
yanaonekana kupungua nguvu, na mara kwa mara zimeonekana kushindwa kutibu
malaria. Mmea wa Artemisia annua umekuwa ukitumiwa kwa miaka zaidi ya 2000
na Wachina kwa kutibu homa, na hivi karibuni kabisa kutibu malaria. Tumegundua
mmea huu kuwa na mafanikio katika kutibu malaria kama madawa yale tuliyoyazoea,
76
na bila kuwa na madhara ambayo siyo ya kupendeza. Artemisia annua anamed (A3)
kinaweza kuifanya hospitali, au jamii kupata tiba ya malaria kabisa bila gharama
kinachohitajika tu kufanya kazi kwa bidii na juhudi!
UKULIMA
Mbegu na miche ni midogo midogo sana na miepesi kushituliwa na hali ya hewa.
Inahitaji uangalizi wa hali ya juu. Lazima uandae muda wa kutosha kila siku ikiwemo
Jumamosi na Jumapili.
Kuandaa udongo, changanya sehemu 10 kwa ujazo za udongo uliooza au udongo
mweusi kwa sehemu 10 za ujazo za mchanga. Ongeza sehemu 20 za maji na chemsha
mchanganyiko kwa dakika kama 5 au zaidi kidogo ili kuua mbegu zote za magugu.
Baadaye, kama inapatikana, ongeza sehemu moja ya ujazo ya polystyrene
iliyotwangwatwangwa na plastiki nyeupe inayopatikana kwenye vifurushi vya vifaa
vya umeme, hii hufanya udongo kuwa laini.
Inasaidia sana kutengeneza kitalu kinachobebeka. Hii inaweza ikawa nusu jerry-
can au sahani ya mbao lenye ukingo wa sm 10. Mbegu 1000 zinahitaji meta moja ya
mraba. Jaza sahani udongo wa sm 5 kwa kina. Mwagilia, weka mashimo sehemu ya
chini ya sahani ili kuyawezesha maji ya ziada kutoka. Tawanya mbegu juu ya
udongo. Usizifunike kwa udongo, mbegu zimeshachanganywa na kaolin ambayo
huzifunika kiasi cha kutosha. Artemisia huota ikiwa sehemu yenye mwanga kwahiyo,
weka sahani yako sehemu ya jua la moja kwa moja, Baada ya kati ya siku 4 na 7
majani laini huonekana. Kwa wiki 6 zitakazofuata mwagilia kwa uangalifu mkubwa,
kwa kuyaruhusu maji kuingia kupitia matundu ya pembeni, au kwa kuweka sahani
kwa dakika chache ndani ya sahani kubwa lenye maji ili maji yaingie kwa kupitia
chini. Pandikiza miche inayokuwa pamoja kwa karibukaribu sehemu iliyosafi
kwenye sahani ya mbegu kwa kutumia kikoleo au kibano. Wakati miche inapokuwa
na urefu wa sm 3, hii itakuwa kama wiki sita baada ya kusiha, pandikiza kwenye
vyungu na kisha itakapofikia urefu wa sm 15, kadri ya wiki 10 baada ya kusiha,
pandikiza sehemu za wazi kwenye udongo.
Udongo huo lazima uwe na rutuba na laini
jinsi ulivyo. Kwa hiyo kwanza changanya
udongo na matawi, majani, vijiti n.k.
Weka meta moja ya mraba kwa mmea
moja hadi mitatu. Kama msimu wa kiangazi
umekaribia chini ya miezi minne au mitano,
unaweza kupanda karibu karibu. Msimu wa
kiangazi ni mkali kwa mimea, mimea huanza
kutoa maua, na lazima ivunwe haraka hapo
hapo. Changamoto ni namna ya kuitunza
mimea bila kutoa maua kwa muda mrefu
iwezekanavyo! Mara tu maua ya kwanza
yanapoonekana, vuna majani kutoka kwenye
shina (matawi) ya mmea wote na uyakaushe.
Matawi na mashina yaliyobaki yanafanywa
kuwa mbolea.
77
Kutoka kwenye mimea iliyo hai, unaweza ukachukua vipande kwa kukata,
ukapanda mimea zaidi na hata wagonjwa zaidi kutibiwa, na mimea hii inaweza
kusambazwa kutoka mwaka mmoja hadi unaofuata. Tunapendekeza kwamba
uchukue vipande vya kukata kila mwezi, na kuvipanda katika sehemu tofauti tofauti.
Kwa njia hii kuna uwezekano mdogo wa mimea yako kutoa maua kwa wakati moja.
Na vilevile, utajifunza ni wapi mimea inastawi vizuri zaidi.
Kwa kichukua vijiti kuna njia tatu:
Njia ya kwanza: Kata matawi katika vipande vifupivifupi kwa kutumia wembe. Mmea „mama“ lazima
uwe wenye afya na wenye umri wa miezi 2 – 4. Usiwe unakaribia kutoa maua (vijito
vyote vitakuwa vinatoa maua moja kwa moja).
Kila kijito kiwe na vikonyo viwili.Ondoa majani yote ya sehemu ya chini.
Kwenye katawi ka pembeni usiondoe majani yake.
Chukua chombo cha aina yo yote na ukijaze na maji. Funga gunia an wavu juu
yake. Ingiza vipande vifupivifupi kwenye gunia au wavu – sehemu ya chini iwe
majini.
Unaweza kuongeza virutubisho vya aina yo yote kwenye maji. Maji yakianza
kunuka vibaya, yabadilishwe. Weka chombo juani. Baada ya wiki 2-4 vijito huanza
kupata mizizi.
Njia ya pili:
Andaa kitalu kama ilivyoelezwa juu. Weka vipande vifupivifupi ardhini (vilazwe
kidogo ili kurahisisha uotaji wa mizizi). Weka kitalu mahali penye mwanga na jua.
Njia ya tatu: Mmea ukifikia urefu wa sm 50 vitawi vyote vya chini vikatwe nusu kwa kutumia
wembe. Kunja vitawi palipokatwa na uviweke ardhini. Weka jiwe juu yake ile vitawi
vibaki vilivyowekwa. Baada ya wiki nne mizizi itkuwa imeota. Ondoa vijiti kwenye
mmea „mama“ na uvihamishie mahali pengine.
Kutoka mmea mmoja tu, kadri ya miezi miwili kabla ya kuanza kwa msimu wa
mvua unaweza ukapata vipande vya kupanda hadi 1000! Kama kila mmea wa vijiti
hivi utazaa mmea wenye urefu wa meta moja, kila mmea utatoa angalau 200g za maji
yaliyokaushwa. Kutoka kwenye mimea 1000 tunaweza tukapata kilo 200. Wakati kila
tiba ya malaria inahitaji kama gram 35, hii itatosha kwa wagonjwa 5,714 ambao ni
watu wazima – na hii ni kutoka kwa mmea “mama” mmoja tu!
SEHEMU ZINAZOTUMIKA: Majani, kwa majani mabichi, uzito unaotakiwa ni
mara tano zaidi.
MAPENDEKEZO YA JINSI YA KUTUMIA
1. Malaria Kufuatana na dozi zilizotolewa ndani ya jedwali chini, tengeneza infusion kwa
kumimina maji ya moto kwenye majani makavu ya A3, acha yapoe kwa dakika 15
halafu chuja. Gawanya chai itakayopatikana kwa sehemu 4 zilizosawa, na kunywa
kila baada ya saa 6 (maana yake utakunywa mara 4 kwa siku) (Unahitaji kipimo
kizuri! – au gram 5 ni kiasi ambacho kinatosha kabisa, kikibanwa vizuri, katika mm
35 za kikaratasi chembamba cha plastiki). Unaweza kutumia gram 25 za majani
mabichi badala ya gram 5 za majani makavu.
78
Dozi ya Artemisia annua (chai) kwa kutibu malaria
Umri Ujazo wa chai Majani makavu uzito
Watu wazima Lita 1 gram 5
Watoto zaidi ya mika 13 ml 500 gram 4
Watoto zaidi ya miaka 11 ml 500 gram 3
Watoto zaidi ya miaka 7 ml 500 gram 2
Mpe dozi hii kwa siku 7. Kama katika eneo lenu, homa karibia hurudi katika muda
wa wiki 3, kuna mambo mawili katika tiba. La kwanza ni kutumia chai ya Artemisia
kwa jumla ya siku 12. Na la pili ni kutumia chai ya Artemisia kwa siku 7, na katika
siku ya tatu ya tiba kunywa vidonge 3 vya Fansidar (SP) au dawa nyingine ya malaria
inayotumika. Chai ya Artemisia inaweza kufanywa tamu kwa kuweka sukari au asali.
Wajawazito wasitumie chai ya Artemisia, hasa hasa miezi ya kwanza ya ujauzito.
Watoto wadogo wapewe chai ya Artemisia chini ya usimamizi na ushauri wa daktari.
DOKEZO: Unaweza kuifanya chai hii kuwa na nguvu zaidi kwa kusaga majani makavu kabla ya
kumimina maji ya moto juu yake. Uache mchanganyiko utulie kwa dakika 15.
Usichuje, ila tikisa na kunywa mchanganyiko wote.
2. Bawasiri (Haemorrhoids) Tokosa kwa kuchemsha kijiko 1 cha chai (kiasi cha gram1.5) cha majani kwa lita
moja ya maji kwa muda wa dakika 10. (Tazama tofauti kutoka maelezo namba moja
juu). Acha utulie kwa dakika zingine 10, chuja na kunywa kwa vipindi kwa siku
moja.
3. Kuvimba kwa utumbo mkubwa (Colitis)
Fuata mchanganyiko No. 2, lakini tumia gram 5 za majani makavu. Tiba itolewe kwa
muda wa wiki tatu na sio zaidi.
4. UKIMWI Wagonjwa wa Ukimwi wana upungufu wa kinga ya cellular na kinga ya humoral
iliyo juu. Artemisinin huongeza kinga ya cellular na kupunguza kinga ya humoral na
tayari ni dhahiri kwa matumizi kwa wagonjwa wa UKIMWI. Kwa hiyo,
tunapendekeza kwamba wagonjwa wa UKIMWI wanywe chai ya mchanganyiko
namba moja, kwa kutumia gram 5 kwa siku kwa kipindi cha mwezi mmoja, au gram
moja kwa siku kwa kipindi cha miaka kadhaa
5. Kichocho
Maelezo ni kama yale ya malaria.
6. Magonjwa ya macho na conjunctivitis macho mekundu)
Tengeneza chai kama ilivyoelezwa kwa bawasri juu. Chuja kwa karatasi, na loweka
vitambaa viwili visafi kwenye chai uliyochuja. Badala ya kupoa, weka kitambaa
kimoja kwa dakika 10 kwa kila jicho na kitambaa chake.
7. Mtando mweupe mdomoni (Candida) Daima tafuna majani safi ya Artemisia kabla ya mlo. Unapokwenda kulala, weka
majani kadhaa mdomoni kwenye mashavu.
79
8. Kikohozi, mafua na sinusitis Vuta mvuke kutoka kwa chai ya moto ya Artemisia kwa dakika kumi mara tatu kwa
siku. Kama ikiwezekana, chai isiwe na joto kali wakati wa kuvuta mvuke.
9. Majipu
Kwa jipu lililo wazi, osha majani kidogo na yachemshe katika maji kidogo kwa
dakika 20. Twanga na weka kwenye jipu. Kwa majipu yaliyoziba: Weka majani
mabichi yaliyotwangwa, mara mbili kila siku.
Kama dawa ya kuzuia magugu
Jaribu kusambaza majani ya Artemisia kwenye ardhi – yanaweza kuzuia kuota kwa
magugu.
10. Kutengeneza kinywaji cha afya cha kuburudisha! Chukua ml 50 za chai ya Artemisia iliyotengenezwa kama ilivyoelezwa kwenye
mchanganyiko No.2 juu, ongeza ml 950 za maji baridi, juisi ya limau mbili na gramu
50 sukari. Koroga vizuri. Kinywaji hiki na mbadala mzuri wa soda ya dukani.
ATHARI Kwa matumizi ya kunywa, kwa kufuata dozi sahihi, hakuna madhara yanayoeleweka.
Kwa matumizi ya nje inaweza kusababisha kuwashwa.
5.3 Azadirachta indica Mwarobaini
Maelezo ya kibotania: Familia: Meliaceae Mti wa mwarobaini ni wa kijani na hukua hadi kufikia urefu wa meta 25 hadi 30. Na
kwa kawaida huanza kutoa matunda
baada ya miaka 3 hadi 5, na hufikia
kiwango cha juu cha uzaaji baada ya
miaka 10. Katika hali ya hewa iliyo
nzuri, mti mmoja utatoa kiasi cha kilo 50
za matunda kwa mwaka na kilo 350 za
majani ya kijani. Kilo 50 za matunda
hutoa kilo 30 za mbegu ambazo zina
uwezo wa kutoa mafuta kilo 6 na
mashudu kilo 24. Mti wa mwarobaini
huishi kati ya miaka 100 na 200 na
huweza kufikia urefu wa meta 30 na
upana wa meta 20.
Mwarobaini mara nyingi hutumiwa
kwa kuimarisha misitu na ni mzuri kwa
mbao za kujengea, sababu
haushambuliwi na mchwa. Mti huu
ambao hukua haraka hupatikana barani Afrika, Asia na Amerika kusini.
Mbegu kavu za kutokana na matunda husagwa na kukamuliwa ili kupata mafuta.
Katika majaribio kwa wanyama mafuta ya mwarobaini na mashudu yalionyesha
80
kuwa na nguvu ya antidiabetic, antibiotic (mfano dhidi ya kifua kikuu), antiviral,
diuretic, spermicidal effects. Vilevile yana nguvu dhidi ya protozoans (malaria,
malale). Yanapunguza homa na huzuia mzio (anti-allergic).
Kwa matumizi ya kilimo, vinatilifu hutengenezwa mbegu au majani (Tazama
chini). Wadudu wanaotua katika mafuta au mashudu ya mwarobaini hawafi hapo
hapo, tofauti, kwa mfano, baada ya kutumia kinatilifu cha tephrosia au tumbaku
(Tazama sura 4.11) lakini huharibiwa tu ule utaratibu wao wa maisha na kufa katika
muda wa siku chache. Na kwa wadudu wengine, vinatilifu vya mwarobaini hutumika
kama kifukuza wadudu, hivyo wadudu hukaa mbali. Mimea iliyopuliziwa dawa ya
mwarobaini ni mara chache hutokea ikashambuliwa na wadudu. (Hata litokeapo
balaa la nzige miti ya mwarobaini hubaki salama).
UKULIMA
Mwarobaini ni bora zaidi ukapandwa kutokana na mbegu zake. Chagua mbegu nzuri
– mbegu zitaota iwapo tu hazizidi umri wa miezi mitatu. Weka mbegu juu ya gazeti
lililolazwa juu ya plastiki kivulini, na uzinyunyizie maji kila siku ili zikae na
unyevunyevu. Badilisha gazeti kila baada ya siku mbili. Baada ya siku 4 – 7 mbegu
hupasuka na kuanza kutoa. Panda kwenye mchanganyiko wa udongo 50% na samadi
ya ng’ombe iliyooza vizuri ndani ya mifuko ya plastiki. Upande miche kwenye
sehemu ulizozitarajia baada ya miezi mitatu.
Kupanda miti kutokana na matawi: Chukua kitawi kidogo na majani yake (cha
mwishoni) na kichomeke kwenye udongo wenye unyevunyevu.
Miti hii inaweza kupandwa kwenye miteremko ya milima, ardhi isiyo na rutuba,
pembeni ya barabara au sehemu yenye mawe yasiyoenda chini sana.
Mwarobaini unastawi katika nyanda za chini na vilevile katika nyanda za juu,
kwenye mchanga, mawe mawe au hata udongo tifutifu. Inastawi vizuri katika hali ya
hewa ya unyevu wa muda mrefu, lakini miti hii inaweza kuhimili vipindi virefu vya
ukame.
Mwarobaini una uwezo wa kustawi katika ardhi yenye tindikali (acid) ambapo pia
utasaidia kupunguza acid kwa majani yale yanayoanguka na kuoza.
SEHEMU ZINAZOTUMIKA
Majani, mbegu, vitawi, mafuta ya mbegu.
Ili kupata mafuta ya mwarobaini, twanga mbegu kavu, kisha ongeza maji kidogo
ili kupata kama ujiuji mzito. Baada ya kufinyanga kwa muda mfupi, mafuta huanza
kuvuja.
MATUMIZI KATIKA NCHI NYINGINE. India: Mafuta yanatumika kwa wenye minyoo (kwa ndani) na pombe ya majani kwa
malaria na maumivu ya viungo. Nchini India pia watu huoga kwenye maji ya moto
ambamo majani ya mwarobaini yalikuwa yamelowekwa, ili kutibu aina zote za
maambukizi ya ngozi. Kazi ya mwarobaini kama dawa ya malaria imerekodiwa
katika vitabu vya Ayurveda kuwa imekuwa ikitumika tangu mwaka 2000 BC (miaka
2000 kabla ya Kristo). Jina lake katika Ki-suahili lina maana arobaini, sababu ya
madai kwamba unaweza kutibu magonjwa mengi sana . Nchini Uingereza dawa ya
meno ya mwarobaini iko madukani.
81
Nchini Congo (Kinshasa) na Angola, mmea ufananao na mwarobaini Melia
azedarach (Tazama 6.31) mara kwa mara huitwa mwarobaini ki-makosa. Mmea huu
ni mzuri, huweka matunda baada ya mwaka mmoja tu; na kwa ishara namba 5-10
chini, ama ni mzuri au ni bora kabisa. Hata hivyo, kwa viashirio
1- 4, Melia azedarach ni vizuri uepukwe kwa sababu una sumu zaidi. Baadhi ya
tofauti kati ya miti hii miwili ni:
Mwarobaini
(Azadirachta indica) Melia
(Melia azedarach)
Mbegu Ndefu Duara
Maua Meupe Pinki hadi violet
Majani Pinnate Bipinnate (branched)
MAPENDEKEZO YA JINSI YA KUTUMIA
MUHIMU: Katika maelezo yote haya, tunapoongelea jani, tuna maana ya jani moja
dogo tu. Hivyo, picha katika ukurasa wa inaonyesha majani 10 kwa mujibu wa
maelezo yetu.
1. Malaria
Mimina lita moja ya maji ya moto kwenye majani 40 mabichi, au gram 5 za majani
makavu na kunywa chai yake kwa siku moja. Isitumiwe na wamama wajawazito.
2. Kuzuia meno kuoza. Sugua meno yako kwa kitawi kidogo cha mwarobaini mara mbili kwa siku. Njia hii
sio tu kwamba inasafisha meno, lakini pia ina – kufuatana na baadhi ya vitu
vilivyomo kwenye gamba la mwarobaini – nguvu ya kushambulia bacteria
wanaoozesha meno.
3. Sleeping sickness (Trypanosomiasis) (Malale)
Toa tiba ya kawaida kwa kunywa chai ya majani ya mwarobaini kila siku (Tazama
maelezo No. 1 juu)
4. Chawa wa kichwani Osha nywele zako kila siku. Tumia kimoja kati ya vifuatavyo:
i) Weka gram 10 za majani makavu ya mwarobaini ndani ya ml 100 za kileo
(pombe) (45%, mfano gin au vodka) kwa siku 7. Chuja, na tumia kama lotion ya
nywele mara tatu kwa siku muda wa siku tano.
ii) Paka matone kidogo ya mafuta ya mwarobaini kwenye nywele, mara tatu kwa
siku, muda wa siku tano.
iii) Twanga mbegu kidogo za mwarobaini ili kutengeneza kitu kama uji mzito. Kila
jioni, baada ya kuosha nywele paka kama kijiko kimoja cha chai kwenye nywele
na uziache na dawa hivyo hivyo hadi kesho yake jioni.
5. Matatizo ya ngozi Mwarobaini ina nguvu ya kutibu magonjwa yaliyo mengi ya ngozi kama vile acne,
magonjwa yaletwayo na mba (fungus), psoriasis, upele (scabies) na eczema.
Mwarobaini unaweza kutumika pia kutibu matatizo ya mzio (allergy).
Unaweza:
82
Kuoga: Kijadi watu wa India walioga kwenye maji ya moto yakiwemo majani
ya mwarobaini.
Dawa ya mafuta ya kutengeneza: Chukua gram 100 za mafuta ya
kujitengenezea (ya dawa) na ongeza gram 10 za mafuta ya mwarobaini.
Tengeneza dawa ya maji: Loweka gram 20 za majani makavu kwenye ml 100
za kileo 70% (kilicho au ambacho hakikuharibiwa tabia uasili). Baada ya wiki
moja, chuja huo mchanganyiko. Punde kabla ya kutumia, changanya kijiko 1
cha chai cha dawa hii ya maji kwa kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya
mbogamboga na paka kwenye sehemu iliyoathirika.
a) Athlete’s foot: Ama sugua kwa majani eneo lililoathirika au kwa dawa ya
maji/mchanganyiko wa mafuta.
b) Tiba ya ngozi kwa ndui au tetekuwanga: Mafuta ya mwarobaini au dawa ya
maji ya mwarobaini inaweza ikatoa tiba ya anti-viral kwa ndui na tetekuwanga.
Hii ni kwa sababu ina uwezo wa kuzuia virus kuendelea kusambaa.
c) Warts: Paka mafuta moja kwa moja kwenye ngozi.
d) Scabies (aina fulani ya upele): Kuna njia nyingi za kufanya
i) Twanga majani na maji kidogo hadi yalainike, na kisha paka kwenye sehemu
iliyoathirika.
ii) Paka mafuta ya mwarobaini sehemu iliyoathirika.
iii) Saga hadi kuwa ujiuji mchanganyiko wa majani mabichi ya mwarobaini na
dawam mchuzi kwa uwiano wa 4-1 kwa uzito (au kiganja kimoja cha majani
ya mwarobaini kwa kipande cha dawam mchuzi ½ ya urefu wa kidole cha
shahada). Paka mwili mzima na uache ikauke.
e) Scrofula, indolent ulcers, ringworm, psoriasis.
Tumia mafuta ya mwarobaini. Kama yana nguvu sana changanya na mafuta ya
mbogamboga. Badala yake: Chemsha majani kidogo katika maji ya kutosha kwa
dakika 15, na kisha laza majani yakiwa bado na joto juu ya kidonda kwa dakika
15 asubuhi na jioni. Baadhi wanapendekeza pia tiba hii kwa vidonda vya wakoma,
lakini fuata ushauri wa daktari.
f) Majeraha ya kuungua yenye maambukizi
Chemsha kiganja kimoja cha majani mabichi kwenye lita moja ya maji kwa
dakika 20, chuja ikiwa bado ya moto (kuzuia maambukizi), poza, na itumie
papohapo kusafisha kidonda. Tengeneza na tumia chai hii kwa njia hii mara tatu
kwa siku. Mgonjwa akae ndani ya chandarua ili kuepuka maambukizi mapya.
g) Majipu: Kama majipu hayajatoa midomo, dawa ya kubandikiza ya majani inaweza
ikatumika. Kwa majipu yaliyo wazi, ulcers na eczema majani lazima yachemshwe
vizuri katika maji kidogo kabla ya kutumiwa kama dawa ya kubandika.
h) Fungus za mdomoni (candida)
Changanya sehemu moja ya mafuta ya mwarobaini kwa sehemu tisa za vitu
vifuatavyo:
Kwa candida ya mdomoni: asali
Kwa candida ya ukeni: mafuta ya mbogamboga au yoghurt.
Kwa candida ya ngozi: mafuta ya mbono au mafuta yoyote ya mbogamboga.
83
Tumia mchanganyiko huu kupaka eneo lililoathirika.
6. Kuhara na kuhara damu: Kwa siku tayarisha chai ya majani ya mwarobaini kwa kuchemsha majani 40
mabichi na yaliyo safi kwenye kikombe kikubwa cha maji kwa dakika tano. Watu
wazima wanywe chai hii kwa siku moja, huku wakinywa maji ya aina nyingine
kwa wingi. Endelea na tiba hii kwa siku tatu. Daima ongeza ORS (Tazama sura
4.6).
7. Kilimo: Vinatilifu kutokana na matunda Vuna matunda yaliyoiva, ondoa mnofu, osha mbegu na uzikaushe kabisa juani.
Tunza kwenye gunia linalopitisha hewa. Kwa kudhibiti maradhi, twanga kikombe
kimoja cha mbegu na uziweke ndani ya lita moja ya maji kwa saa sita. Chuja na
pulizia, au nyunyizia mchanganyiko huo kwenye mimea ya shambani siku hiyo
hiyo, kwa sababu haidumu muda mrefu. Rudia tena kuweka dawa baada ya siku
sita. Ili kuzuia maradhi kwa mazao yako, tumia mchanganyiko ufuatao (chukua
nusu kikombe cha mbegu kwa lita moja ya maji) kwa mimea yako kila wiki.
8. Kinatilifu kutokana na majani Kama hakuna matunda, chukua kilo moja ya majani mabichi na chemsha kwa
dakika 10 ndani ya lita 5 ya maji, acha ipoe kwa saa 3, chuja na tumia.
9. Dawa ya kupulizia wadudu
Maelezo kwa mchanganyiko wa kupulizia ndani ya nyumba: Saga gram 100 za
mbegu kavu za mwarobaini, hadi kuwa unga, mimina ml. 500 za kileo –kikali (au,
kama hakipo, mafuta ya taa) juu yake, hifadhi ndani ya chombo kilichofungwa
vizuri kabisa kwa siku 10. Kisha chuja mara mbili kwa kutumia karatasi (paper
strainer) na jaza kwenye bomba la kupulizia.
10. Kama dawa ya kuhifadhi chakula
Kwa vyakula kama vile mpunga, maharage au mahindi changanya vitawi
vidogovidogo pamoja na majani gram 250 za majani makavu, changanya na kilo
moja ya majivu makavu na weka mchanganyiko huu katika kilo 50 za chakula
ulichokihifadhi. Osha chakula kabla ya kutumia.
11. Dawa ya kufukiza (au insectifuge) Ili kufukuza wadudu kutoka ndani ya nyumba, weka majani ya mwarobaini
kwenye mkaa wa moto (unaowaka).
12. Kwa kupiga vita nematodes (minyoo wenye madhara wasioonekana waishio
ardhini) Weka majani kidogo ya mwarobaini pamoja na miche au mbegu kwenye mashimo
uliyoandaa kwa kupanda.
ATHARI: Baada ya matumizi ya ndani (kunywa) ya muda mrefu, hali ya kusikia moto
(irritation) kwenye maini au mafigo inaweza kutokea. Kwa sababu ya uzoefu mdogo
kwa mmea huu, matumizi ya kunywa hayapendekezwi kwa wajawazito.
84
5.4 Capsicum frutescens Pili-pili
Maelezo ya kibotania: Familia: Solanaceae Mmea huu hufikia urefu wa meta 2. Matunda yake ni madogomadogo, sm 1-2 urefu
na sm 0.5 upana. Huanza kwa kuwa kijani,
na huwa nyekundu kabisa zinapoiva.
Dawa iliyopo inaitwa capsaicine.
UKULIMA
Hupendelea ardhi yenye rutuba na tifutifu
na iwe juani. Huhitaji joto la chini
lisilopungua 18-21º C. Bora ikapandwa
kutokana na mbegu (kusiha), kwa
kusambaza gram moja kwa meta moja ya
mraba. Panda kwa nafasi sm 40 katika
mistari sm 60 mbali kutoka mche. Vuna
baada ya miezi minne.
SEHEMU ZINAZOTUMIWA: Matunda, majani.
MATUMIZI KATIKA NCHI ZINGINE Sehemu mbalimbali duniani pilipili
hutumika kutibu maumivu ya viungo.
Katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo
inatumika zaidi kwa maumivu ya meno na
tumbo. Visiwa vya Hawaii inajulikana
sana kwa tabia ya kushambuliwa bacteria (bactericidal properties). Nchini
Cameroon na Kusini mwa bahari ya Pacific, pilipili inatumika kienyeji kwa
magonjwa ya ngozi.
MAPENDEKEZO JINSI YA KUTUMIA
Pilipili, pamoja na mapapai, ni mojawapo ya vitu vyenye nguvu na kwa hiyo kufanya
ni dawa zinazouzwa sana za mimea. Nchini Uswisi unakuta kuna aina kama sita
tofauti za mafuta ya dawa kwa maumivu ya kuvimba kwa viungo (rheumatic
arthritis) zikiwa na dawa itokanayo na Capsicum frutescens. Mafuta yatokanayo na
majani na matunda yanaonyesha uwezo wa kusafisha tumbo, mfano, dhidi ya
schistosoma mansoni, kimelea kisababishacho kichocho.
Na inadhaniwa kwamba Wathailand, ambao chakula chao huwa na kiasi kikubwa
cha pilipili, mara chache sana hushambuliwa na matatizo ya moyo sababu ya
fibrinolytic action (huyeyusha damu inayoganda ) ya kimeng’enya (enzyme)
capasaicien.
1. Maumivu ya viungo (baridi yabisi/ rheumatism); kuteguka, maumivu ya
misuli, kuvimba kwa viungo (arthritis), maumivu ya kiuno, na kuuma kwa
mshipa wa nyuma wa paja.
Nyumbani: Twanga kijiko kimoja kikubwa cha pilipili mbichi au kavu na kijiko
kimoja kikubwa cha mafuta ya mbogamboga. Mchue mgonjwa kwa mchanganyiko
85
huu kwa nguvu sana hadi asikie maumivu. Na uendelee kuviweka viungo katika hali
ya joto.
Mahospitalini: Tazama sura 4.3 “Mafuta kwa maumivu ya viungo” na sura 4.4.
“Mafuta ya dawa kwa maumivu ya viungo,” Tazama vilevile picha ya jalada.
2. Aina ya kisukari cha miguu (diabetic feet) Tumia maelezo namba 1 juu, lakini tibu miguu kwa uangalifu mkubwa. Usichubue
ngozi.
3. Maumivu ya miguu
Changanya vitu vifuatavyo:
Pilipili (iliyosagwa) kijiko 1 cha mezani.
Unga (mfano, wa muhogo) kijiko 1 cha mezani.
Mafuta ya mbogamboga vijiko 3 vya mezani.
Koroga ili kupata ujiuji. Halafu sambazia kwenye kipande cha nguo na kisha fungia
kwenye sehemu ya miguu iliyoathirika. Ili kuepuka kuwashwa ondoa kitambaa baada
ya saa 12 – 24.
4. Tumbo kujaa hewa (flatulence) na bawasiri (haemorrhoids)
Ongeza pilipili katika chakula chako. Ndiyo, hata kwa matatizo ya bawasiri! Sababu
ni kwamba bawasiri mara kwa mara huzidi sana kwa sababu ya fungus katika
matumbo, na hawa fungus huuawa na pilipili.
5. Magonjwa ya ngozi, mkanda wa jeshi (herpes zoster)
Tumia mafuta ya pilipili au dawa ya mafuta ya pilipili kwa kiasi ambacho mgonjwa
atakuwa bado ana uwezo wa kuvumilia maumivu.
6. Kupunguza uchungu wakati wa kujifungua Mama hupewa tunda moja la pilipili, la kuweka katikati ya meno wakati wa
kujifungua. Mawazo yake yatahama kabisa kutoka eneo la tumbo na kuhamia
mdomo.
7. Nywele kutoka (hair loss) Tumia madini (udongo unaoponya, sura 4.5)! Ili kuboresha mzunguko wa damu
kwenye ngozi ya kichwani, kaa kwenye kiti na lazia kichwa nyuma; msaidizi achue
ngozi ya kichwa kwa uangalifu kwa kutumia mafuta ya maumivu ya viungo (sura
4.3) na yaoshwe na kuondolewa baada ya dakika 30. Angalia sana mafuta haya
yasiingie machoni, yafunike!
8. Uhifadhi (preservation) Kwa dawa za mafuta pilipili hufanya kazi kama natural preservative.
ATHARI: Tahadhari! Capsaicine ni kitu chenye uwezo mkubwa wa kushambulia ngozi kati ya
mimea mingi. Daima nawa mikono yako mara baada ya kutengeneza au kutumia
dawa yenye Capsicum frutescens. Epuka kugusa macho, pua, sehemu za siri au
vidonda na majeraha. Capsaicine inaweza ikasababisha upofu kama itaingia
machoni. Unapotoa dawa, hakikisha kwamba unamtarifu kila mtu aliye karibu.
86
5.5 Carica papaya Papai
Maelezo ya kibotania: Familia: Caricaceae
Papai ni tunda la jadi na
mmea wa dawa. Hurefuka
hadi kufikia meta 7 kwenda
juu. Mpapai umetokea nchi za
tropiki za Amerika na sasa
unapatikana katika maeneo ya
joto duniani kote, ambapo
ardhi ina rutuba ya kutosha.
UKULIMA Kuna mapapai ya kiume
(hayazai matunda) na ya kike.
Weka mbegu 3 kwa pamoja
katika shimo na baadaye
ondoa miche ya kiume. Papai
moja la kiume linatosha kwa
mapapai 10 – 20 ya kike.
Panda pamoja na vitu vinavyooza au mbolea iliyooza. Panda mapapai mengine kila
miaka 4 -5 kabla hayajarefuka sana kiasi cha kushindwa kuyafikia matunda kwa
urahisi.
SEHEMU ZINAZOTUMIKA: Matunda mabichi na yaliyoiva, mbegu, maua,
majani, mizizi.
MATUMIZI KATIKA NCHI NYINGINE Mpapai wenyewe tu ni duka la madawa. Maelezo juu ya matumizi yake katika
maeneo mbalimbali yanaweza yakajaza kwa urahisi kitabu. Hapa kuna mifano
machache: Barani Ulaya na Asia papai linatumika kutibu minyoo na kuhara damu.
Barani Afrika, kikohozi, kuhara damu, malaria, kisonono, kifua na matatizo ya ini.
America, maw worm, amoeba na pumu. Juisi ya papai bichi imesajiliwa ndani ya
United States Pharmacopoeia 1985 kwa matumizi ya majeraha yaliyoingia hadi
kwenye mfupa.
NAMNA YA KUTUMIA Sehemu zote za mmea zina vitu vyenye thamani ya dawa, kama vile flavonoids,
antibiotics, fungicides, vitamini, na vimeng’enya. Kimeng’enya papaine kinajulikana
kimsingi kama kiua – minyoo; kinapatikana katika sehemu zote za mmea, hususani
katika mbegu za tunda lililoiva au kwenye mnofu wa tunda bichi.
1. Kusafisha majeraha machafu
Safisha vidonda vichafu kwa “maji yaliyodondoshewa juisi ya papai bichi”: Maji
yaliyochemshwa yakapoa pamoja na matone kidogo ya papai bichi ambalo bado liko
mtini. Ili kupata utomvu (juisi) kwanza osha tunda vizuri kabisa, kisha chana chale
kuelekea chini kwa papai hilo bichi. Kinga matone ya utomvu mweupe kwa kijiko au
87
kikombe kisafi. Kisu na kijiko vitakavyotumika visiwe na kutu, kwa sababu kutu
huharibu papaine.
2. Minyoo Papaine hufanya kazi kwa ujumla, lakini kwa viwango tofauti, kwa kuondoa aina
mbalimbali za minyoo ya tumboni, na hata tegu. Utomvu (latex) hugemwa kwa
kukata chale kwenye tunda bichi ambalo bado liko mtini.
DOZI YA UTOMVU WA PAPAI BICHI KATIKA KUTIBU MINYOO
UMRI (MIAKA) IDADI YA VIJIKO VYA CHAI
Miezi 6 – hadi mwaka 1
Mwaka 1 – 3
Miaka 4 – 6
Miaka 7 – 13
Miaka 14 na kuendelea
½
1
2
3
4
Dawa hii hutolewa mara moja, nyakati za asubuhi kabla ya kula chochote, pamoja na
dawa ya kuharisha (kulainisha choo) (mfano, tazama 5.6). Tiba ya minyoo inaweza
kutolewa hata kama mgonjwa anaharisha. Papaine haiondoi minyoo yote, kwa hiyo
tunapendekeza kurudiwa kwa tiba hiyo baada ya wiki moja kama hatua ya tahadhari.
3. Kama dawa ya kuzuia minyoo na ameba Tafuna kipande cha jani la papai (ukubwa: sm 5 × sm 5) kila siku, au kula kijiko cha
mezani kimoja cha mbegu. Minyoo huonekana kuchukia zaidi ladha hiyo hata kuliko
binadamu na minyoo watatoka! (Mfanyakazi mmoja wa kike huko mashariki ya
Congo – Kinshasa, ambaye mara kwa mara alikuwa akisumbuliwa na ameba, aliweza
tu kuendelea na shughuli zake kwa sababu ya tiba hii!).
4. Upungufu wa Vitamini A, B, na C. Kula kwa wingi mapapai yaliyoiva ili kuimarisha kiwango cha vitamin; vitamin A
kwa kusaidia macho kuona, vitamin B kwa mishipa ya fahamu, vitamin C kusaidia
mfumo wa kinga dhidi ya maambukizi.
5. Matatizo madogo ya kuhara kunatolewa na ameba (amoebic dysentery)
a) Mizizi na majani inajitosheleza yenyewe bila kuongeza chochote: Osha vizuri
na katakata kiganja kimoja cha majani ya mpapai. Ongeza lita moja ya maji,
chemsha kwa dakika 5 na acha ipoe kwa robo saa. Chuja na kunywa kwa siku
moja, Au
b) Tafuna kijiko kimoja cha chai cha mbegu za papai mara 3 kwa siku kwa siku 7.
6. Kuhara damu kwa ameba (severe amoeba dysentery)
a) Tazama sura 5.11 Euphorbia hirta, matumizi namba 2 yaliyopendekezwa .
Tumekwisha tumia tiba hii kwa mafanikio kwa maelfu ya wagonjwa. Au
b) Madaktari wanaofanya kazi na Anamed wamepata matokeo mazuri, kwa
kuwapa wagonjwa kijiko cha mezani cha mbegu za mapapai zilizosagwa mara
3 kwa siku, kwa siku 7.
88
7. Malaria (matatizo madogo madogo) Mimina lita moja ya maji ya moto kwenye majani mabichi ya mpapai yatoshayo
kiganja kimoja. Chuja baada ya dakika 15. Watu wazima wanywe kwa siku moja,
watoto wadogo, kwa mjibu wa umri wao. Isitumiwe na wajawazito.
8. Kuvimbewa Papaine ni kimeng’enya ambacho husaidia kuyeyusha chakula. Pamoja na chakula,
ama tumia matone machache ya utomvu wa papai, au kipande kidogo cha jani la
mpapai, au tafuna mbegu tatu za mpapai.
9. Kikohozi Chimba kiganja kimoja cha mizizi ya mpapai (sio mzizi mkuu), osha vizuri na
chemsha kwa dakika 15 pamoja na lita moja ya maji. Chuja. Namna ya kutumia:
Watu wazima: kikombe 1 mara tatu kwa siku, watoto wadogo, itategemea na uzito
wao.
10. Matatizo ya ini, homa ya manjano, manjano ya ngozi na macho
kunakosababishwa na nyongo katika damu. Kileo chochote kile ni marufuku! Kula matunda mengi! Kisha pia, ama
a) kula kwa mpangilio, mapapai mabichi yaliyopikwa kama mboga au
b) chemsha kiganja kimoja cha mizizi ndani ya lita moja ya maji kwa dakika 10,
acha hivyo kwa dakika 15 na kunywa kwa siku moja, au
c) kila siku kunywa kinywaji kilichotengenezwa kwa kumimina lita moja ya maji ya
moto kwenye kiganja kimoja cha maua ya mpapai wa kiume au gamba la mpapai.
11. Maambukizi kwenye njia ya mkojo:
Tafuna kijiko kimoja cha mezani cha mbegu safi za papai lilioiva, mara tatu kwa
siku, kwa siku 7- 14. Hata hivyo, tiba hii haitoshelezi kutibu magonjwa ya ngono.
12. Kusumbuliwa na pumu Ili kuleta unafuu kwa matatizo ya pumu, vuta majani makavu ya mpapai kwenye kiko
au yaliyofungwa katika karatasi kama sigara, au choma majani karibu na kitanda
chako na vuta moshi.
13. Vidonda vyenye vijidudu Maji yenye kileo yaliyotokana na majani yana nguvu ya kuua bacteria, hasa hasa
staphylococci – wadudu hawa mara kwa mara hupatikana kwenye ngozi ambayo
yameingiliwa na bacteria. Changanya:
Majani ya mpapai makavu na yaliyosagwa na safi gram 10
Kileo kilichoondolewa uasili 70% ml 100
Baada ya wiki moja, kamua na chuja. Dondoshea kwenye kidonda mara kwa mara
kwa siku nzima. Pia tafuna kijiko 1 cha mezani cha mbegu za papai mara 3 kwa siku,
kwa siku 3.
14. Majipu yaliyo wazi, vidonda vyenye vijidudu, au majeraha madogo madogo
yanayotoa usaha
Osha papai bichi lililo bado mtini kwa kitambaa na maji ya moto. Safisha kisu,
kiweke kwenye maji ya moto, halafu kata kipande kidogo cha papai unene wa kidole
89
kidogo cha mtoto. Laza kipande hicho kwenye kidonda na funga kitambaa kisafi.
Kiache kwa saa 4. Kama kinaleta maumivu makali, kitoe mapema.
Endelea na tiba hii mara 4 kwa siku, kwa siku kadhaa hadi usaha umeacha
kuonekana. Badilisha na tiba hii kwa asali/sukari kama tiba iliyoelezwa sura ya 6.33.
Baada ya kila tiba ya asali/sukari, weka kipande cha papai bichi; kwa maana hiyo
unaacha tunda kwenye mti wake.
15. Majeraha makubwa yanayotoa usaha Osha kidonda mara kadhaa kila siku kwa “maji yaliyowekewa utomvu wa mapapai.”
Tazama maelezo namba moja juu. Pia tafuna kijiko kimoja cha mezani cha mbegu za
papai mara 3 kwa siku, kwa siku 3. Mgonjwa lazima aende kwenye kituo cha afya
kilicho karibu! Usikifunge kidonda, na mgonjwa alale katika chandarua.
16. Maambukizi ya mba
a) Majimaji ya matunda mabichi (utomvu) yana nguvu ya kutibu mba (mfano,
ugonjwa wa mabaka kichwani). Changanya matone 10 ya utomvu kwa kijiko
kimoja cha mezani cha mafuta ya mboga mboga. Sugua sehemu zilizoathirika kwa
mchanganyiko huu mara 3 kwa siku. Tayarisha mchanganyiko mwingine kila
siku.
b) Ongeza majani ya Cassia alata (ringworm bush) kwenye mchanganyiko huu
(Tazama sura 5.6, mapendekezo namba 2)
17. Minyoo wa Guinea (Guinea worms)
Kwa pamoja twanga vitu vifuatavyo kwenye chombo kisafi:
Utomvu wa papai matone 10
Nyamanyama kutoka kwenye mrama mbichi
wa Thorn Apples (Datura stramonium,
tazama sura 6.20) kijiko 1 cha chai
Chumvi (iliyosalama kwa kuchemshwa) Nusu kijiko
Paka eneo lililoathiriwa mara tatu kwa siku kwa siku 2 – 3, ukiandaa mchanganyiko
mpya kila unapotaka kupaka. Uzoefu wetu nchini Sudan ni kwamba katika siku ya
tatu mnyoo anakuwa amepooza na anaondolewa kwa urahisi.
18. Kufanya nyama ngumu kuwa laini
Viwanda hutumia papaine kufanya nyama kuwa laini. Kwa matumizi ya nyumbani
nyama ngumu hufungwa kwenye jani bichi la mpapai usiku kucha.
19. Sabuni mbadala Wakati sabuni inazidi kupanda bei kila wiki, isingekuwa bora mtu “kustawisha”
sabuni yake mwenyewe? Miti ya mapapai inatupa sabuni bure: paka mikono na mwili
kwa majani yaliyotwangwa – lakini usiharibu mpapai wa jirani yako!
ATHARI Matumizi ya ndani: (kunywa) papaine inaweza sababisha tumbo kuuma.
Matumizi ya nje: mzio unaweza kutokea kwa kuitumia kwa kipindi kirefu. Epuka
majimaji ya papai (utomvu) kugusa au kuingia machoni.
90
5.6 Cassia alata (syn. Senna alata) Ringworm bush
Maelezo ya kibotania: Familia: Caesalpiniaceae Mmea huu asili yake ni Amerika ya kusini na umeenea katika maeneo yote ya nchi za
joto. Hukua hadi meta 2 – 3 kwa urefu, na majani makubwa yenye manyoya
manyoya. Maua huonekana kama mshumaa. Tunda limeumbika kama mkunde
ulionyoka na unafikia sm 25 kwa urefu. Cassia alata hufunga majani yake wakati wa
giza (kama hakuna mwanga): ujaribu kwa kuweka ndoo iliyogeuzwa kwenye tawi
kwa dakika 30.
UKULIMA
Cassia alata hustawi katika
nyanda za chini, kwenye
udongo ambao una mboji kwa
wingi. Panda kwa kusiha moja
kwa moja udongoni.
SEHEMU
ZINAZOTUMIKA: Majani, mizizi
MATUMIZI KATIKA NCHI
ZINGINE:
Nchini New Guinea, Cassia
alata inatumika kama dawa ya
kuharisha na ya fungus, nchini
Philippines inatumika kwa
ugonjwa wa ngozi aina ya
impetigo na maambukizi
mengine ya ngozi. Huko Mali
ina jukumu la kutibu upele aina
ya scabies, nchini Congo
inatumika kama dawa ya
kitulizo. Nchini Senegal mmea
unatumika kwa minyoo aina ya
maw worms, maambukizi ya
mba na vilevile kama dawa ya kuharisha. Wa Ivory Coast hutumia kama dawa ya
minyoo, na watu wa Congo pia kwa ukoma.
MAPENDEKEZO YA JINSI YA KUTUMIA Katika maeneo ya nchi za joto, mmea huu unafahamika sana kwa nguvu zake za
madawa; nchini New Guinea wamefikia hatua ya kuuita “mmea duka la madawa”
miongoni mwa vitu vingine, ina tindikali ya njano ya chrisophane, ambayo
imefahamika kwa miaka 100 barani Ulaya kwa nguvu zake dhidi ya mba (fungus).
Cassia alata huwashambulia staphylococi, bacteria ambao mara nyingi hupatikana
kwenye vidonda vyenye vijidudu. Uwezo wake wa kufanya mtu aharishe vilevile
umethibitishwa kabisa.
91
1. Shida ya kufunga choo (constipation) Mimina kikombe 1 cha maji ya mto kwenye kijiko 1 cha chai cha majani makavu au
gamba la mzizi, chuja baada ya dakika 10. Kunywa kabla ya kwenda kulala; itafanya
kazi baada ya saa 8. Pia kunywa lita 3 za maji kila siku.
2. Maambukizi ya mba, impetigo, mabaka ya kichwani, upele (scabies),
psoriasis:
Mchanganyiko mzuri ni kama ifuatavyo: Twanga majani katika kinu ili kupata aina
fulani ya “manyoya kijani ya pamba” Changanya na kiasi kilekile cha mafuta ya
mbono (kama hayapo, mawese au mafuta mengine yoyote ya mbogamboga), paka
eneo lililoathirika mara 2-3 kwa siku. Dawa hii hudumu kwa siku moja tu na
kuharibika.
Kwa maambukizi ya mba na impetigo, ongeza matone 10 ya majimaji ya papai
(utomvu), kama yanapatikana (tazama sura 5.5.).
3. Madonda yenye maambukizi
Changanya pamoja:
Majani makavu ya Cassia alata, yaliyotwangwa gram 10
Kileo kilichoondolewa uasili 98% ml 70
Maji ya moto ml 30
Au
Majani makavu ya Cassia alata, yaliyotwangwa kikombe 1
Spiriti (mfano, pombe, cognac, kileo kadri ya 50 % chupa 1
Acha kwa wiki moja, chuja na tumia kama dawa ya kusafisha kidonda.
Majeraha makubwa yanahitaji tiba za hospitali.
ATHARI
Epuka kunywa dawa hii kwa muda mrefu, na usinywe wakati wa ujauzito au
kunyonyesha.
5.7 Cassia occidentalis (syn. Senna occidentalis) Mwingajini
Maelezo ya kibotania: Familia: Caesalpiniaceae
Kamti kafupi meta 0.8. – 1.5 urefu. Majani yake yako pinnate na yanaota kwa
kufuatana, maua yake ni njano. Maganda yake ya mbegu yana urefu wa sm 15,
yamepinda kidogo na huwa na mbegu 10 – 20. Unapatikana sehemu za nchi za
tropiki katika maeneo ya vijijini.
UKULIMA Cassia occidentalis huhitaji ardhi yenye mboji kwa wingi. Siha moja kwa moja
udongoni na mwagilia maji.
SEHEMU ZINAZOTUMIKA: Majani, mizizi, mbegu
MATUMIZI KATIKA NCHI ZINGINE Nchini Sudan, Cassia occidentalis inatumika kwa magonjwa ya ngozi; Philippines
inatumika kwa watu waliofunga choo na wenye shinikizo la juu la damu; nchini
92
Congo inatumika kwa
kutibu bawasiri na
kisonono. Wazulu wa
Afrika Kusini wanatumia
mti huu kama dawa ya
minyoo; katika Jamhuri
ya Afrika ya kati, Benin
na Ivory Coast inatumika
kama dawa ya malaria,
matatizo ya ini, na
kisonono. Huko Burkina
Faso mbegu zilizosagwa
zinanywewa kwa ajili ya
minyoo aina ya Guinea
worms. Katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo
utomvu wa mizizi
husaidia kupanua njia ya
uzazi wakati wa
kujifungua (oxytocicum).
Sumu iliyo katika mbegu
hupotea zinapokaangwa.
Siku za nyuma, Cassia
occidentalis ilitumika
katika hospitali za kikoloni kutibu homa ya manjano na blackwater fever.
1. Mapendekezo ya matumizi
Chemsha kijiko 1 cha chai cha majani makavu na glasi moja ya maji, acha ikae kwa
dakika 15, kisha chuja. Kunywa kabla ya kwenda kulala. Kwa tatizo la kufunga choo
kunywa lita 3 za maji kila siku.
2. Kuvimba mwili sababu ya majimaji (oedema)
Chemsha kijiko 1 cha mezani cha majani makavu au mizizi katika lita 1 ya maji kaw
dakika 15. Chuja na kunywa kidogokidogo wakati wa siku moja.
3. Magonjwa ya ngozi
Ponda ponda kiganja kimoja cha majani mabichi, sambaza majani yaliyotwangwa
kwenye ngozi na funika kwa kitambaa kisafi. Badilisha mara mbili kwa siku.
4. Badala ya Kahawa
Oka kwa moto mbegu; usioke kwa muda mrefu sana na tayarisha “kahawa” kwa
kuchemsha gram 30 ndani ya lita moja ya maji. Chuja.
ATHARI
Dawa itokanayo na majani ya kunywa: Ukizidisha dozi inaweza sababisha tumbo
kusokota. Usitumie dawa hii zaidi ya wiki 1 – 2, wala isitumiwe na wajawazito au
wanyonyeshao.
93
5.8 Citrus limon Limau
Maelezo ya kibotania: Familia: Rutaceae Ni mti mdogo kadri ya meta 6 – 9.
UKULIMA: Inahitaji udongo mwepesi, hasa tifutifu ya mchanga na mfinyanzi. Panda mbegu moja
kwa moja pale ambapo mti unataka uwe. Hutoa matunda kati ya miaka 2 – 6.
SEHEMU ZINAZOTUMIKA: Majani,
matunda mabichi na yaliyoiva, maganda (mafuta
ambayo ni mepesi kutoweka yanapatikana kwa
wingi katika maganda).
MATUMIZI KATIKA NCHI ZINGINE
Barani Ulaya kinywaji cha moto cha juisi ya
limau hutengenezwa kwa ajili ya homa, ili
kuongeza utoaji wa jasho. Huko Asia majimaji ya
majani machanga hutumika kwa masikio yenye
maambukizi, na chai ya maganda inatumika kwa
kichefuchefu. Nchini Ivory Coast chai kwa ajili
ya kikohozi na mafua hutengenezwa kutokana na
majani machanga.
MAPENDEKEZOYA MATUMIZI
1. Kikohozi:
Chemsha viganja 2 vya majani machanga (makavu au mabichi) na lita moja ya maji.
Chuja na kunywa kidogo kidogo kwa siku.
2. Matatizo za kifua Katakata kiganja kimoja cha maganda ya limau. Ongeza lita 1 ya maji ya moto na
acha hivyo kwa dakika 15, kisha chuja. Watu wazima: kunywa kwa siku moja.
Watoto wadogo, kwa mjibu wa uzito wa mwili.
3. Upungufu wa Vitamin C Kila siku, kula angalau limau 1, danzi 1, machungwa 2 au machenza 5.
4. Homa Kuliko kunywa aspirin ni bora zaidi kuimarisha mfumo wa kinga! Mara tatu kwa siku
kunywa juisi ya limau kikombe kimoja kikubwa kwenye maji ya moto (ml 500).
Usichemshe juisi, utaharibu vitamin C.
5. Mafua Minya kipande cha ganda la limau na vuta mafuta mafuta mepesi yatakayotoka
kwenye ganda.
6. Vidonda kwenye midomo au mdomoni (Herpes labialis) Ugonjwa huu hufanya vidonda vidogovidogo kwenye midomo au mdomoni. Mara
kadhaa kwa siku, minya ganda la limau mpya (au chungwa au chenza) ama:
a) Moja kwa moja kwenye vidonda au
b) Kwenye kipande cha plastiki chembamba, ambacho utakiweka kwenye vidonda.
94
Kama kinauma sana, ongeza tone la mafuta ya mbogamboga.
ATHARI
Angalia isiguse machoni. Watoto wadogo na watu wanaoumwa matumbo wanaweza
wakaumizwa na dawa hii kwa kuumwa matumbo kama wataitumia kwa kiwango
kikubwa.
5.9 Cymbopogon citratus Michaichai
Maelezo ya kibotania: Familia: Poaceae
Majani hufikia hadi sm 50 urefu.
UKULIMA
Gawanya mmea uliostawi. Panda sehemu yenye rutuba na tifutifu na kwenye kivuli
kidogo. Yamwagilie maji vizuri katika hatua za awali.
SEHEMU ZINAZOTUMIWA: Majani
MATUMIZI KATIKA NCHI ZINGINE
Katika maeneo yote ya nchi za joto chai hupikwa kwa mchaichai kutibu homa.
Barani Asia mmea huu hutumika kuongeza harufu katika mvinyo na kama kiungo
katika vyakula. Vile vile husaidia kwa maumivu ya meno, kipindupindu na tumbo
kujaa hewa. Pia husaidia kumfanya mtu kukojoa sana. Huko Afrika Magharibi mmea
wote hutumika kwa matatizo ya homa, mafua, kisonono. Mafuta ya mchaichai
hutumika kutia manukato katika sabuni
na marashi.
MAPENDEKEZO YA MATUMIZI
Michaichai haihitaji uangalizi wa hali
ya juu na bora ikapandwa katika kila
bustani. Tunapendekeza kwamba kila
zahanati na hospitali ipande michaichai
kama sehemu ya ua ili kuzia
mmomonyoko wa udongo. Mistari ya
kontua katika bustani za dawa
inapandwa kwa kuchanganya
michaichai na miti.
Michaichai ina myrcene na citral
kwa wingi, vitu vyenye kazi ya kutibu
cramps na kuchochea uyeyushaji wa
chakula. Kunywa chai ya michaichai
kunaongeza kiwango cha mwili
kujisafisha na ukojoaji wa mara kwa
mara ambako kunasaidia kuondoa
pyrogens, ambayo ni mazao ya
microbial yanayosababisha homa kwa
ujumla, unywaji wa maji mengi,
95
unapendekezwa kwa magonjwa mengi, sababu husaidia mwili wote kufanya kazi
vizuri zaidi. Hii ni bora zaidi katika hali ya hewa ya joto ambapo kupungukiwa maji
daima ndio hatari kubwa. Michaichai hutia ladha nzuri katika maji.
1. Matatizo ya kifua, mafua, sinusitis
Chemsha kiganja 1 cha michaichai kwenye lita moja ya maji na vuta mvuke wake.
2. Homa, malaria
Unapokuwa na malaria, kunywa lita 2 za chai ya michaichai. Tengeneza viganja 2
vya michaichai kwa kumwagia maji ya moto lita 2. Kama ni lazima, kwa kuongezea
kunywa chai ya kuzuia malaria, mfano, Artemisia (5.2) au mtukutu (6.48). Kunywa
ikiwa na uvuguvugu na kidogokidogo siku nzima. Watoto wanywe kidogo kufuatana
na uzito wao.
3. Bawasiri (haemorrhoids)
Majani makuukuu yana tannins zaidi kuliko mapya. Kwa hiyo, chemsha kiganja 1
cha majani makuukuu ya mwembe au mkaratusi kwenye lita 2 za maji kwa dakika
15. Kisha ongeza viganja viwili vya michaichai na endelea kuchemsha kwa dakika
zingine mbili. Acha kwa dakika 15, chuja na ongeza maji zaidi vuguvugu, na kisha
oga sehemu za mapaja na kiuno kwa dakika 20.
4. Maumivu ya meno; harufu mbaya mdomoni
Tafuna jani bichi lililosafishwa 2 – 3 kwa siku.
5. Dawa ya kufukuza wadudu
Weka majani mengi kwenye mkaa ndani ya nyumba (juu ya moto mdogo), au panda
mimea hii kwenye vyungu ndani ya nyumba.
6. Mafuta ya watoto na mafuta ya kuchulia: Tazama sura 4.3
7. Dawa ya mafuta kwa ajili ya mwili: Tazama sura 4.4.
8. Dawa ya mafuta kwa bawasiri. Tazama sura 4.4.
9. Utengenezaji wa sabuni: Tazama sura 4.1.
ATHARI: Hakuna zinazoeleweka.
5.10 Eucalyptus globulus Mkaratusi (kalafulu)
Maelezo ya kibotania: Familia: Myrtaceae Urefu meta 30, mti mwembamba, umetokea Australia. Kuna aina 150 zinazotumika
kwa namna mbalimbali (E. globulus, na E. robusta ni “officinalis” katika dawa, E.
citriodora inatumika kwa kuzalisha marashi). Majani ya E. globulus ni marefu na
membamba na hutoa harufu iliyokolea.
UKULIMA Husambazwa kwa mbegu. Panda miche kwenye udongo tifutifu na wenye rutuba
sehemu yenye jua. Unavumilia theluji. Mkaratusi hufanya udongo kuwa na tindikali
zaidi, na matokeo yake ni kwamba mazao hayawezi kustawi karibu na miti hii.
96
SEHEMU ZINAZOTUMIKA: Majani, gamba
MATUMIZI KATIKA NCHI ZINGINE: Barani America na Ulaya chai ya
mkaratusi hutumiwa kwa wenye matatizo ya kifua, kuhara damu na magonjwa ya njia
ya mkojo. Barani Afrika muuke unawutwa kwa ajili ya mafua. Nchini Afrika kusini
inatumika kwenye majipu. Huko Asia ni dawa
ya kikohozi, makamasi, kifua kikuu, pumu na
minyoo.
MAPENDEKEZO YA MATUMIZI Mkaratusi una aina mbalimbali ya mafuta
muhimu. Hasahasa yale yanayofaa ambayo ni
eucalyptol na cireol, yana nguvu ya antiseptic
(kuua wadudu) na expectorant (kulainisha
makohozi). Majani pia yana phenol, dawa
yenye nguvu ya kusafisha vidonda, na tannins
ambayo husaidia mucous membrane katika
kuzuia mashambulizi kutoka kwa bacteria.
1. Kikohozi, magonjwa ya njia ya mkojo,
madonda ya koo.
a) Chai ya mkaratusi: twanga kiganja 1 cha
majani makavu au mabichi na chemsha
pamoja na lita moja ya maji kwa dakika 5.
Chuja na kunywa kidogokidogo kwa siku. Chai hii ni msaada kwa mgonjwa wa
kifua kikuu anapoendelea na tiba ya Hospitali.
b) Syrup ya kikohozi: Mimina ml 250 za maji ya moto kwenye gram 20 za majani
makavu, funika na acha kwa saa moja. Chuja kwenye kikombe 1 cha chai hii
ongeza kikombe kimoja cha sukari, chemsha kidogo na chuja. Watoto wa miaka 7
watumie kijiko1 cha chai mara 3 kwa siku, na wadogo zaidi kwa mjibu wa uzito
wa miili yao. Watoto wakubwa na watu wazima ni bora wanywe chai kuliko
kutumia syrup. Isipewe kwa watoto chini ya miaka miwili.
c) Matone ya kikohozi: Dawa ya maji ya mkaratusi: mimina mchanganyiko wa ml
700, kileo (95%) na ml 300 za maji yaliyochemshwa na kuchujwa kwenye gram
100 za majani makavu ya mkaratusi. Baada ya wiki moja kamua na ondoa majani.
Watu wazima watumie matone 30, (nusu kijiko cha chai) mara 3 kwa siku.
2. Madonda ya koo
Tafuna nusu jani taratibu kwa masaa kadhaa, mara 3 kwa siku.
3. Homa, tiba ya msaada kwa malaria
Chemsha kiganja 1 cha majani na lita 2 za maji kwa dakika 5. Kunywa ikiwa moto,
kidogo kidogo kwa siku moja. Matokeo ni kuongeza na kusaidia mwili kupambana
na vijidudu au sababu zingine zinazoleta homa.
4. Tiba ya msaada kwa kisukari na magonjwa za njia mkojo. Fuata maelezo namba 3 juu. Kukojoa mara kwa mara ni tokeo mojawapo. Na kwa
wagonjwa baadhi wa kisukari kiwango cha sukari katika damu hupungua. Hata
hivyo, tumia tiba hii kwa siku chache tu.
97
5. Mafua, maumivu ya viungo. Mafuta ya mkaratusi: chemsha kiganja 1 cha majani makavu ya mkaratusi
yaliyosagwa kwenye ml 100 za mafuta ya mbogamboga katika fukizo maji kwa saa
moja. Chuja, sugua kifuani kwa nguvu kwa mafuta hayo.
6. Kwa kusafisha vidonda: Ili kusafisha kidonda, tumia mchanganyiko wa maelezo namba 5 (chuja kabla ya
kutumia) kwenye kidonda. Au chemsha kijiko 1 cha mezani cha majani makavu
yaliyokatwakatwa na ml 100 za maji kwa dakika 15, chuja na tumia kwa kuosha
vidonda. Tengeneza mpya kila unapotaka kusafisha kidonda.
7. Pumu, matatizo ya kifua
Twanga kiganja 1 cha majani mabichi au makavu na kisha chemsha katika lita 1 ya
maji. Vuta mvuke wake kwa dakika 15 ikiwa bado moto, huku kichwa na chungu
vikiwa vimefunikwa kwa kitambaa kizito.
8. Usafi wa meno
Tumia katawi kadogo kama mswaki
9. Nzi na mbu
Ili kufukuza wadudu
a) Tengeneza mafuta ya mbu: Changanya gram 100 ya majani makavu
yaliyotwangwa na mafuta ya mbogamboa nusu lita. Chemsha kwa saa moja
katika fukizo maji na kisha chuja. Mafuta haya hudumu hata mwaka mzima.
b) Au, rahisi zaidi, jisugulie majani mabichi mwili mzima au choma majani makavu
ndani ya nyumba.
ATHARI: Kwa sababu ya nguvu zake, matumizi ya kunywa hayapendekezwi kwa
watoto chini ya miaka 2. Watu wazima waitumie kwa siku chache.
5.11 Euphorbia hirta Mziwaziwa (mwache)
Maelezo ya kibotania: Familia: Euphorbiaceae
Mmea wa kawaida katika nchi za tropiki, mara nyingi hupatikana vijijini, urefu sm 30
– 40, wakati mwingine hutambaa ardhini, jani huota kinyume na jingine, katika
vitawi vifupi. Mmea huu una vinywele vya njano , vigumu na vidogovidogo sana.
Utomvu ni mweupe, maua yake ambayo ni madogomadogo ni ya kijani na yako
kwenye vitawi vifupi. Tunda lina mbegu 3 zenye rangi nyekundu, kahawia, iko na
kingo tatu na urefu mm 0.8.
UKULIMA Husambazwa kwa mbegu. Mmea huu hupendelea udongo mkavu wa kichanga ambao
una mchanganyiko wa mabaki ya mimea na iwe juani.
SEHEMU ZINAZOTUMIKA: Mimea wote. Wakati wa kuvuna, kata mmea kwa
mkasi, ili mizizi ibaki ardhini, vinginevyo utamaliza mimea yote katika eneo lako na
usibakiwe na kitu!
98
MATUMIZI KATIKA NCHI ZINGINE Katika nchi za Senegal, Mali, Burundi, Benin na D.R. Congo mmea huu hutumika
kutibu sana kuhara na kuhara damu; nchi Niger kwa pumu; Nigeria kwa tatizo la
kufunga choo na kuvimba matumbo (enteritis). Huko Afrika Magharibi mmea huu
vilevile unajulikana sana kwa uwezo wake kuchochea utoaji wa maziwa kwa mama.
Barani Asia mziwaziwa unatumiwa sana kwa pumu, na magonjwa ya njia ya hewa.
Indian Pharmacopoeia inapendekeza mmea huu utumike kwa minyoo kutibu watoto
wa kuchochea utoaji wa Maziwa kwa wanawake; utomvu wake kwa tumbo
linalosokota na kuondoa uvimbe (warts). Mmea huu umesajiliwa katika Afrikan
Pharmacopoeia (OAU, 1985). Kama ingekuwa rahisi kuulima pengine ungetumika
kwa malengo ya tiba huko Ulaya pia – lakini mmea huu hauwezi ukastawishwa
katika maeneo makubwa!
Katika mji wa Kasai, huko D. R. Congo, mmea huu huitwa “Dawa ya mtoto wa
jicho.” Wakati mtoto wa jicho anapokuwa katika hatua za awali, watu huweka tone 1
la utomvu katika jicho mara tatu kwa siku, na matokeo yake ni mazuri. Hata hivyo,
hatujui athari za tiba hii. Ukitumia tiba hii, hakikisha mmea umeoshwa vizuri, ili
kuepuka kuambukiza jicho na vijidudu vingine.
Katika majaribio ya kisayansi kwa wanyama dawa kutoka katika E. hirta
ilionyesha mafanikio yafuatayo: kuondoa wasisi (anxiolytic), kupunguza maumivu
(analgesic), kuondoa uvimbe na ni kitulizo.
Vilevile ilionyesha kuwa na uwezo kwa
matatizo ya kuharisha (hata kama hii
ilisababishwa na kemikali).
MAPENDEKEZO YA MATUMIZI Mziwaziwa uko katika familia ya
Euphorbiaceae, ambayo mimea mingi ni
ya muhimu, na baadhi ya mimea ina sumu
sana na/au inasababisha kansa
(carcinogenic). Kwa sababu hii ni lazima
uwe na uhakika kabisa kwamba una mmea
sahihi. Utumie mmea ukiwa bado mbichi,
kwa sababu wakati wa ukaushaji sehemu
kubwa ya nguvu hupotea. Tofauti na
mimea mingine mingi, kwa upande wa E.
hirta unachukua kiasi kilekile cha uzito cha
mmea mkavu sawa na unapotumia mmea
mbichi.
1. Kuhara damu kunakoletwa na
Ameba (amoebic dysentery)
Chemsha gram 15 – 30 (kiganja 1
kilichojaa) cha mmea mbichi na uliooshwa
(au mmea mkavu) kwa chupa moja ya maji, dakika 15. Chuja na kunywa
kidogokidogo kwa siku nzima. Rudia tiba kwa siku 8 mfululizo. Vilevile kunywa
ORS (Tazama sura 4.6).
99
2. Kuhara kukali kwa ameba (severe amoebic dysentery) bacillary dysentery. Kwa magonjwa makali, osha na changanya:
Mziwaziwa (mmea wote) kiganja 1 kilichojaa
Majani ya mpapai kiganja 1 kilichojaa
Majani ya mwembe machanga, ya kijani kiganja 1 kilichojaa
Majani ya mpera kiganja 1 kilichojaa
Chemsha kwa dakika 15 katika lita moja ya maji, kisha chuja. Kunywa
kidogokidogo kwa siku nzima. Kiwango cha kunywa kwa watoto, tazama sura 2.6.
Watu wazima na watoto wote ni lazima wanywe ORS daima (Tazama 4.6.).
Endelea kunywa chai hii kwa siku 8, hata kama dalili za ugonjwa zitapotea baada
ya siku 2, na hii kwa uzoefu wetu hutokea mara kwa mara.
Mchanganyiko huu umeisaidia anamed kuokoa maisha ya watu wengi hasa katika
matatizo ambapo watu:
wenye magonjwa ya amoeba walikuwa wakisumbuliwa sana na tumbo baada
ya kutumia dawa ya Metronidazol/Flagyl na kwa hiyo wakaacha kutumia dawa
hii ya “kisasa” ya tiba.
wenye bacillary dysentery iliyosababishwa na wadudu ambao walikuwa
hawauwawi na antibiotics karibu zote.
Mimea yote iliyotajwa hapo juu ina nguvu dhidi ya ameba kwa hiyo inaweza
kutumiwa kipekee.
Kwa wagonjwa wenye kichefuchefu, au kwa watoto, usiongeze majani ya mpapai
(yana ladha mbaya) kwa siku za kwanza.
3. Magonjwa ya njia ya mkojo, magonjwa ya figo, kuhara, matatizo ya tumbo
(intestinal cramps)
Kunywa dawa ya kumwagia maji ya moto kutoka mchanganyiko namba 1, ila haitibu
kisonono! Kama tahadhari, usitumie kwa zaidi ya siku 8. Kwa matatizo ya kuharisha
daima tumia ORS (Tazama sura 4.6).
4. Minyoo ya kwenye utumbo
Osha na changanya
Mziwaziwa, mmea wote bila mizizi kiganja 1 kilichojaa
Majani ya mpapai kiganja 1 kilichojaa
Chemsha kwa dakika 15 katika lita 1 ya maji, kisha chuja. Kunywa kidogokidogo
kwa siku nzima. Kama mtoto atakataa kutumia chai hii, tengeneza kwa kutumia
Mziwaziwa pekee kiganja kimoja. Tiba nyingine yenye mafanikio ni utomvu wa
papai (Tazama sura 5.5.)
5. Pumu
a) Vuta majani makavu yaliyosokotwa kama sigara, au
b) Weka kichwa chako juu ya kiganja 1 cha majani haya wakati wa usiku, au
c) Tumia mchanganyiko namba 1 juu
6. Hali ya wasiwasi, fadhaa, cramps
Tumia mchanganyiko namba 1 juu.
7. Uvimbe (warts)
Tumia utomvu mweupe wa baadhi ya miti kwenye warts.
100
ATHARI: Hazijulikani. Kwa matatizo ya ameba au bacillary dysentery na pumu, E.
Hirta. daima ndio chaguo la kwanza kwa sababu ina nguvu sana. Lakini usizidishe
dozi iliyopendekezwa.
5.12 Mangifera indic Mwembe
Maelezo ya kibotania: Familiae: Anacardiaceae Mti unafikia urefu wa meta 25, huota maeneo yote ya tropiki.
UKULIMA Mwembe hustawi katika maeneo ya joto na nyanda za chini. Panda katika vyombo
vya plastiki mbegu, na panda mahali unapotaka katika umbali wa meta 8 kutoka mti
hadi mti. Miti hutoa matunda baada ya miaka 4 – 6.
SEHEMU ZINAZOTUMIKA: Majani
machanga, gamba, maua, matunda, mbegu.
Ili kuyalinda maisha ya mti, chukua
magamba kutoka kwenye matawi tu (na
iwe kutoka upande mmoja tu). Kamwe
usitoe gamba kwenye shina.
MATUMIZI KATIKA NCHI ZINGINE Nchini Australia chai iliyotengenezwa kwa
majani inanywewa kwa ajili ya kuhara kwa
ameba (amoebic dysentery). Huko Mali na
Niger gamba na majani vinatumika kutibu
vidonda vya koo, meno kuuma, upungufu
wa vitamin C na homa, nchini Senegal
utomvu katika majani inajulikana kama
dawa kwa magonjwa ya akili. Katika nchi
ya Ivory Coast majani yanatumika kwa
matatizo ya kifua, pumu na michubuko.
MAPENDEKEZO YA MATUMIZI
Majani ya mwembe yana tannins 10% - vitu ambavyo vina jukumu kubwa kwa
kuzuia kuharisha. Zaidi ni flavonoids ambazo zinaongeza ukojoaji nazo zinapatikana.
1. Kuharisha; amoebic dysentery Chukua gram 30 (kiganja 1) majani mabichi na machanga, chemsha pamoja na lita
moja ya maji kwa dakika 30, chuja na kunywa kidogokidogo kwa siku nzima.
Changanya na Mziwaziwa kwa utendaji kazi mzuri zaidi, Tazama aya 5.11.
2. Tatizo la kufunga choo
Kula maembe yaliyoiva kwa wingi sana.
3. Kikohozi, matatizo ya kifua
Chukua gram 30 (kiganja 1) za majani machanga na chemsha katika lita moja ya maji
kwa dakika 10. Chuja na kunywa kidogokidogo kwa siku nzima.
101
4. Homa Tumia mchanganyiko namba 3, ila kunywa lita 2 – 3 za maji. Kunywa kwa siku
nzima kidogokidogo. Hii huongeza uwezo wa mwili kujisafisha na kukojoa mara kwa
mara na vyote viwili vinasaidia kuondoa pyrogens. i.e. ni mazao ya microbial
ambayo husababisha homa.
5. Bawasiri (haemorrhoids)
Chukua viganja 5 vya majani makuukuu na chemsha katika lita 5 za maji kwa dakika
30. Chuja na tumia mtokoso huu kwa kuoga sehemu za mapaja.
6. Donda koo Tayarisha mchanganyiko namba 2, jisukutue kwa ½ kikombe cha mchanganyiko huu
kila baada ya saa moja.
7. Kuvimba fizi, upungufu wa vitamin C
Fizi zinaweza zikavimba kwa sababu ya upungufu wa vitamin C. Ili kuzuia, kula
matunda kwa wingi! Kama hayapo, tafuna majani 3 machanga ya mwembe kila siku,
yana vitamin C kwa wingi na pia tannins.
8. Minyoo
a) Kausha kabisa kokwa moja la embe, halafu oka na twanga. Chemsha unga na
chupa moja ya maji. Gawanya mara mbili na kunywa siku hiyo hiyo, au
b) Weka kiganja kimoja cha maua yaliyotwangwa katika 0.7 ya lita ya maji na acha
hivyohivyo usiku kucha. Chuja; kunywa kwa sehemu mbili kesho yake na yote
iishe.
Hata hivyo, tunapendelea tiba ya mpapai (sura 5.5.) au Mziwaziwa (sura 5.11).
ATHARI Majani makuukuu ya mwembe yana sumu, usiyatumie kwa kunywa wala kutafuna.
5.13 Moringa oleifera Mlongelonge
Maelezo ya kibotania: Familia: Moringaceae
Moringa oleifera ni mti mdogo unaokuwa haraka na hupukutisha majani, hufikia hata
meta 12 kwa urefu unapokomaa . Una asili ya India. Ni mti laini, gamba lake ni
jepesi na mizizi yake huenda chini sana. Hukua vizuri penye joto kati ya 26º C -
40ºC, kiwango cha mvua kwa mwaka zaidi ya mm 500 na mwinuko chini ya meta
1000. Unavumilia ukame. Siyo jamii ya mikundemikunde.
UKULIMA
Mti huu hukua haraka kutokana na mbegu au vitawi, hata katika ardhi isiyo na
rutuba. Hupendelea ardhi tifutifu na ya kichanga. Kadri mti unavyokua, unavyozidi
kukatwa ndivyo utakavyotoa majani zaidi.
SEHEMU ZINAZOTUMIKA: Majani, maganda ya mbegu, mbegu, gamba, mizizi,
maua, mafuta, utomvu.
102
MAPENDEKEZO YA JINSI YA KUTUMIA
1. Majani na magamba: kwa Utapiamlo
Panda mti wa mlongelonge nje ya dirisha la jikoni. Majani yana chanzo cha vitamin
A, B, C. Yana madini kwa wingi, hasa calcium, chuma na phosphorus na protein
nyingi.
Yana chuma mara 3 zaidi ya
mchicha na mara 4 zaidi vitamin A
ukilinganisha na karoti. Katika mradi
uliofanyika Senegal majani
yameonekana kusaidia sana wagonjwa
wa Utapiamlo, hasahasa miongoni mwa
watoto.
Yanaweza yakaliwa mabichi, au
yanaweza yakakusanywa
yanapokomaa, kukaushwa, kutwangwa
na kuhifadhiwa. Yanaweza pia
yakavunwa wakati wa kiangazi,
ambapo mboga za majani nyingine
huwa ni haba.
Kukausha majani: Vuna, kausha kwa
siku tatu, kama inawezekana kivulini.
Ukikaushia juani vitamin A hupotea;
yatwange na hifadhi kwenye magudulia
yasiyopitisha hewa. Ikiwezekana pima
kiwango cha unyevu kwa hygrometer,
ili ujue ni kwa muda gani unaweza kuyahifadhi.
Unga huu wa majani unaweza kuongezwa katika wali, makande na kwa kweli ni
katika chakula chochote. Kwa watoto wenye Utapiamlo na matatizo mengine ya
kiafya, kijiko 1 kiongezwe katika milo yao mara 3 kwa siku.
Maganda na mbegu pia yanaliwa. Yakatwe vipande vidogo vidogo na kupikwa na
kuliwa kama maharage machanga. Yanapokuwa yamekomaa, yachemshe na komba
mbegu na nyama ya ndani. Yanapokuwa makubwa na yamekomaa, tumia mbegu tu
ambazo huitwa njugu za mlongelonge. Zikaange katika mafuta na kula kama
Karanga.
- Mizizi ina ladha kama mlonge.
- Maua ya mlongelonge ni chanzo cha asali nzuri.
2. Mafuta: Kwa Utapiamlo na matumizi katika vipodozi Mbegu ya mlongelonge ina gamba laini, kwa hiyo mafuta yanaweza yakapatikana
kwa kutumia mikono kwa screw press (pia inajulikana kama “spindle” au “bridge”
press).
Kwanza mbegu inapondwa, yanaongezwa maji 10% kwa ujazo, inafuatwa na
uchemshaji kidogo kwenye moto kidogo kwa dakika 10 – 15, uwe mwangalifu
usiunguze mbegu.
103
Jaribio moja kama hilo lilitoa lita 2.6 za mafuta, kutoka kwenye kilo 11 za
makokwa.
Mara njia nzuri za kukamua mafuta zitakapogunduliwa, huenda ufanisi ukafikia
65%.
Mafuta ya mlongelonge yanaweza yakatumiwa:
a) Kwa kupikia; yana lishe kama mafuta ya mzeituni.
Hayachachi upesi, na ni mazuri kwa salad.
b) Kwa kulainisha mitambo laini.
c) Kwa kutengenezea sabuni.
d) Ni kitu cha msingi kwa vipodozi.
e) Kwenye taa
3. Matumizi kwa magonjwa mengine
Hatuna uzoefu sisi binafsi kwa dawa ya mlongelonge. Kwa mjibu wa maelezo, hata
hivyo, sehemu nyingi za mmea huu, ikiwemo mizizi, gamba, shina, majani, maua na
maganda yakiwa na mbegu zake, vinatumika kama dawa katika nchi nyingi.
a) Majani yanatibu kuharisha, upungufu wa damu na madonda.
b) Kwa kisukari, chai iliyotokana na majani hunywewa mara kadhaa kwa siku.
c) Vilevile mafuta ya mbegu za mlongelonge yanasaidia kwa waliovimba viungo
(gout), tumbo kuvurugika (stomach disorders) na maumivu ya viungo.
d) Mizizi ni michungu na inaongeza nguvu mwilini na kwenye mapafu. Inaweza
kukufanya kuongeza kukojoa na kuboresha damu. Ni nzuri kwa kutibu uvimbe,
majeraha ya kifuani, magonjwa ya kifua, bawasiri na kukosa hamu ya chakula.
e) Magonjwa ya ngozi yanaweza yakatibiwa kwa dawa nzito kama uji kutoka
kwenye mbegu.
4. Matumizi ya kusafisha maji Mbegu ni bora zikaachwa zikomae zikiwa mtini na zivunwe zikiwa kavu. Ganda la
juu na gamba la mbegu yanaondoka kwa urahisi, na kuacha mbegu nyeupe za ndani.
Hizi zinatwangwa kwa kutumia mwichi na kinu. Kiasi cha mbegu kinachohitajika
kutibu maji ya mtoni kinategemea na uchafu uliomo katika maji hayo. Watumiaji
huzoea haraka mahitaji yanayobadilika ya maji yao kwa kuwa kiwango cha uchafu
hubadilika kufuatana na msimu.
Ili kutibu maji lita 20 (wastani wa ndoo kubwa) mbegu kama 10 zinahitajika
(mbegu moja inaweza kusafisha lita 2 za maji). Ongeza kiasi kidogo cha maji kwenye
mbegu ulizoponda ili kupata ujiuji mzito. Weka katika chupa safi - chupa ya soda
ndio inafaa zaidi. Ongeza kikombe 1 (ml 200) cha maji na tikisa kwa dakika 5. Tendo
hili huziamsha kemikali zilizo katika mbegu zilizopondwa.
Chuja mchanganyiko huu kwa kutumia kitambaa cheupe cha pamba kwenda
kwenye ndoo ya lita 20 ya maji unayotaka kuyatibu. Koroga haraka haraka kwa
dakika 2, halafu endelea kukoroga taratibu kwa dakika 10 – 15. Wakati wa kipindi
hiki cha kukoroga taratibu, mbegu za mlongelonge hushikana pamoja, vipunje
vidogovidogo na bacteria kuwa vibonge vikubwa ambavyo huzama na kutuana
kwenye kitako cha ndoo. Baada ya siku moja hadi mbili maji safi yanaweza
yakaondolewa.
104
Mchakato huu utaondoa 90-90% ya bacteria ambao wamenata kwenye vibonge
vya mlongelonge, na pia kuyasafisha maji. Hata hivyo, kama maji yamechafuliwa
sana, baadhi ya vidudu vyenye madhara kwa binadamu vinaweza visiondolewe. Kwa
maji ya kunywa tiba zaidi ya maji inapendekezwa, ama kwa kuchemsha (ikiwezekana
katika jiko la sola) au kuchujwa kwa chujio rahisi ya mchanga (simple sand filter).
MUHIMU: Mbegu za mlongelonge zinaweza zikatumika kwanza kukamuliwa
mafuta. Na mashudu yaliyobaki, ambayo yanaweza kukaushwa na kuhifadhiwa, yana
nguvu ileile kama mbegu kwa kutibu maji.
UHIFADHI: Mbegu zilizokaushwa (ondoa zilizoharibika rangi) na unga vinaweza vikatunzwa.
Hata hivyo dawa ni lazima itengenezwe mpya kila unapotaka kutumia.
5. Matumizi katika kilimo
a) Kilimo cha misitu: Mlongelonge ni muhimu sana kwa kuzuia upepo na ua – hukua
tena haraka baada ya kukatwa. Kwa kweli, kuukata mti mara kwa mara
kutaongeza uzaaji wa majani. Ua labda ndio njia nzuri ya kuyaweka pamoja
manufaa ya mlongelonge mfano, uzalishaji wa majani, kuni, kivuli, kizuia upepo,
kuzuia mmomonyoko wa udongo, kugawanya mashamba.
b) Chakula cha ng’ombe na mbolea: Majani na mashudu.
5.14 Psidium guajava Mpera
Maelezo ya kibotania: Familia: Myrtaceae
Ni mti mdogo urefu meta 3 – 5. Majani yake ni magumu na hunukia vizuri.
Kutegemea na aina matunda yake ni duara au yana umbo la yai na yana nyamanyama
nyekundu au nyeupe ambayo ni tamu.
UKULIMA
Hayavumilii theluji. Huhitaji mvua zaidi ya meta moja kwa mwaka, au kumwagiliwa,
na ardhi yenye rutuba. Hutoa maua baada ya mwaka mmoja. Husambaa kwa mbegu.
SEHEMU ZINAZOTUMIWA: Majani machanga, matunda na mizizi.
MATUMIZI KATIKA NCHI ZINGINE
Barani Ulaya na Asia chai iliyotengenezwa kutokana na majani inajulikana kama
dawa ya kuharisha, nchini Misri na Hongkong kwa kikohozi, Senegal kwa kufanya
hedhi itoke kawaida, nchini Hawaii kwa maambukizi ya bacteria.
MAPENDEKEZO YA JINSI YA KUTUMIA Majani ya Mpera yana vitu vingi ambavyo kusaidia wagonjwa wanaoharisha: tannins,
ambayo ina nguvu ya kulinda mucous membranes: flavonoids ambayo ina nguvu ya
antispasmodic na antibiotic; na mafuta mepesi ambayo yanasafisha mwili.
1. Kuharisha kwa watu wazima na maumivu ya tumbo a) Rahisi zaidi, kula mapera kadhaa mabichi, au
105
b) Tengeneza chai ya mpera: chukua kiganja kimoja cha majani ya mpera (kiasi
ambacho mgonjwa anaweza shikilia ndani ya kiganja chake) na ongeza lita
moja ya maji. Chemsha kwa dakika 20 katika chombo kilichofunikwa, na kisha
chuja. Ongeza maji mengine hadi yafikie lita moja tena. Kunywa kidogokidogo
kwa siku nzima.
2. Kuharisha kwa watoto, na kuharisha kukali kwa watu wazima
Katika lita moja ya chai ya mpera (Tazama maelezo namba 1) ongeza vijiko 4 vya
mezani vya asali au vijiko viwili vya mezani vilivyojaa sukari, na chumvi kijiko 1
cha chai. Kama hakuna majani ya mpera, chukua maji, chumvi na sukari tu.
Dozi: Kila siku, mpe mtoto ml 200 (glass moja) kwa kila kilo ya uzito wa mwili.
Kama hujui uzito wa mtoto, mpe, chini ya miezi 6: ml 700; miezi 6 hadi miaka 2: ml
1,400, miaka 2 – 5: ml 2,100; zaidi ya miaka 7: ml 2,800, na watu wazima: ml 3,500.
3. Kiseyeye (upungufu wa vitamin C)
Kula matunda mengi yaliyoiva sana.
4. Kuhara damu kwa amoeba Kwa kuhara kuliko nafuu, fuata maelezo 1 b juu.
Kwa kuhara kubaya sana, tengeneza chai kwa kuchanganya na mimea mingine
(Tazama sura 5.11.2)
5. Kikohozi Fuata maelezo 1b, au tafuna jani moja
changa la mpera mara 5 kwa siku.
6. Kisukari
Wakati mwingine matumizi ya chai ya
mapera au juisi yanaweza
yakapunguza kiwango cha sukari
katika damu. Fuata maelezo 1 b.
Kachunguze matokeo katika maabara.
7. Vidonda vinavyovuja damu
Chemsha viganja 2 vya majani
mabichi kwa lita moja ya maji hadi
ibaki kikombe 1 (ml 500) cha
mchanganyiko huu. Chuja na tumia kwa kuosha vidonda.
8. Majipu yaliyowazi Osha kiganja kimoja cha majani mabichi, twanga na ongeza kijiko kimoja cha chai
cha chumvi na cha sukari. Chemsha katika sufuria bila maji, mpaka mchanganyiko
uwe wa kahawia (sio mweusi).
9. Kusafisha sehemu za siri (wanawake) Tumia mtokoso (dawa ya kutokosa) wenye uvuguvugu wa majani ya mapera baada
ya kujifungua.
ATHARI: Hazifahamiki
106
5.15 Zingiber officinale Tangawizi
Maelezo ya kibotania: Familia: Zingiberaceae Ina asili ya nchi za tropiki za Asia. Tangawizi inaweza ikafikia urefu wa meta moja,
huota kutokana na rhizome. Rhizome ina mafuta mepesi ambayo husisimua mishipa
ya fahamu, kuzifanya makini kwa ujoto na hivyo kuleta hisia ya joto.
UKULIMA: Tangawizi inachukuliwa kama zao la mwaka au la miaka miwili hadi
kukomaa. Hustawi vizuri katika tifutifu na wenye nitrogen kwa wingi na inahitaji jua
au kivuli kidogo. Unaweza ukasambaza tangawizi kwa kugawanya rhizome
mwanzoni mwa msimu wa mvua.
UTENGENEZAJI WA DAWA ZA TANGAWIZI Poda (unga) ya mizizi ya tangawizi: inatengenezwa
kwa kuosha, kukausha, kutwanga na kuchekecha
rhizome. Ikitwangwa vizuri, kijiko cha chai kilichojaa
wima hupimwa 1.5 g.
Tincture ya tangawizi: Osha na menya mizizi, chukua
gram 25 tangawizi safi iliyokatwakatwa, ongeza kileo
80% ili kufikisha ujazo wa ml 100, acha kwa wiki moja,
na kamua.
Mafuta ya tangawizi: Chemsha gram 10 za Tangawizi
zilizooshwa, kukaushwa na kukatwakatwa, kwenye gram
50 za mafuta ya mbogamboga kwa dakika 60 katika
fukizo maji, kamua na ondoa mabaki.
MAPENDEKEZO YA JINSI YA KUTUMIA:
1. Travel sickness. Tumia kijiko 1 cha chai cha unga wa
tangawizi dakika 30 kabla ya kuondoka.
2. Kuzuia kutapika kabla ya operesheni. Tumia kijiko 1 – 2 vya unga wa tangawizi
dakika 30 kabla ya operesheni.
3. Kuzuia kichefuchefu na kutapika wakati wa ujauzito. Tumia nusu kijiko cha
chai cha unga wa tangawizi mara 3 kwa siku.
4. Bacillary dysentery. Tumia gram 45 za tangawizi, kidogokidogo kwa siku nzima.
5. Hookworms. Tumia tangawizi mbichi gram 60 mara 2 – 3 kwa siku. Kwa watoto
wadogo, changanya na asali kidogo.
6. Kikohozi, kifua, kuvimbewa. Kunywa matone 10 – 20 ya tangawizi tincture 3 – 4
kwa siku.
7. Maumivu ya viungo (Rheumatism). Fuata mchanganyiko namba 6. Na kwa
kuongezea tumia mafuta ya tangawizi ya kienyeji.
8. Majeraha. Tumia tincture ya tangawizi kama dawa ya kuua wadudu kwa
majeraha madogomadogo.
9. Malaria isiyo kali. Kula kiganja kimoja cha tangawizi mbichi kila siku, au
chemsha kiganja kimoja kwa dakika kumi. Usichuje, bali kula kila kitu mpaka
homa itakapotoweka. Kwa homa kali, tumia mtukutu (Vernonia amygdalina, sura
6.49) au Artemisia annua (sura 5.2).
107
SURA YA 6
Mimea iliyoelezwa katika sura ya 5 hutumika zaidi; na pia ni mimea ambayo ni
muhimu kwa ye yote anayependa kutumia madawa ya asili. Katika maeneo ya tropiki
kuna mimea ya dawa. Baadhi ni:
Ile iliyotajwa mar chache katika vitabu vya ki-pharmacia (mfano: Kalanchoe)
Ile inayojulikana kama viungo (mfano pilipili).
Ile inayojulikana kama sumu (mfano: mranaa - Datura Stramonium)
Ile inayotumika kwa malengo ya manukato (mfano tururu)
Ile inatumika kama chakula (mf. Machungwa, makaranga)
Ile inayotumika kutibu ardhi au kuzuia mmonyoko wa udongo (mf.
Mchongoma)
Katika sura hii, tutaelezea baadhi ya mimea hiyo. Pia tumeunganisha baadhi ya
vitu vya asili vilivyo muhimu ambavyo wakati huo huo si mimea hasa na inabaki
kuwa asili (mf. asali, sukari, chumvi)
Mwonekano katika sura hii ni tofauti na ile ya sura ya tano. Katika sura hii ya 6
tumepigia mistari matibabu ambayo hasa tuliyoshauri, ama kwa sababu tulitumia
matibabu hayo sisi wenyewe, au kwa sababu matibabu hayo yanakubalika katika
vitabu vya madawa. Lakini siku zote “ACHA UZOEFU WAKO UWE
MWONGOZO WAKO.”
6.1. Adansonia digitata Mbuyu Familia: Bombaceae
Mti huu hupandwa mara chache sana. Hustawi
katika maeneo makavu kabisa na huweza kuishi
maelfu ya miaka. Mti huu una viasili ambavyo
hufaa kwa magonjwa ya moyo, kuhara, pumu,
homa na shinikizo la damu.
MATUMIZI KATIKA TROPIKI KWA
UJUMLA: Tunda lake huliwa na hutumika
kutengeneza juisi. Hutumika kutibu homa na
kuongeza utoaji wa jasho. Toka mwaka 1884, gome
limekuwa likitumika huko Ulaya mbadala badala ya
magome ya miti itumikayo kutengenezea dawa
kama kwinini kutibu homa.
Kutibu kuharisha kwa watoto: Chukua gramu 20
za nyama ya ndani ya tunda na chemsha katika
maji. Mbegu zina mafuta ambayo hutumika kwa
kupikia na vipodozi. Majani machanga yanaweza
kupikwa na kuliwa kama mchicha, au kukaushwa,
kusagwa na kutumika katika mchuzi. Mbegu nyeusi zinaweza kukaangwa,
kuandaliwa na kuliwa kama Karanga.
MIMEA 50 ZAIDI NA MAZAO YA ASILI
108
6.2. Allium cepa Kitunguu maji Familia: Amaryllidaceae
Ni mmea wa msimu mmoja na aina mbalimbali ikitofautiana katika rangi. Asili yake
Asia. Mashina yake hustawi zaidi katika hali ya joto, hii ndiyo sababu katika Afrika,
vitunguu hupandwa mwanzoni mwa kiangazi.
ASIA: Hutumika kwa kikohozi, vidonda vya koo, shinikizo la damu, dawa ya
kuongeza mkojo.
AFRIKA MASHARIKI: Hutumika kwa ajili ya homa. Jamii za Waarabu huweka
vitunguu kwenye majipu. Vitunguu swaumu hutumika kwa ugonjwa ule ule kwa dozi
ya chini.
1. Upungufu wa vitamin (Upungufu wa vitamini A,B, na C)
Changanya vitunguu katika mlo wako wa kila siku. Vitunguu vinaweza kuliwa
katika umri wowote. Ikiwezekana kula vitunguu vikiwa vipya na vibichi.
2. Kuongeza kumbukumbu: Kula vitunguu vingi vibichi mara kwa mara au zaidi
vitunguu swaumu.
3. Kikohozi na madonda ya koo: Changanya ½
kikombe cha vitunguu vilivyokatwa katwa na ½
kikombe cha maji, koroga, kunywa kwa siku
nzima.
4. Maambukizi ya utumbo: Kula vitunguu vibichi
vingi vilivyo katwa katwa.
5. Shinikizo la damu, maambukizo katika njia ya
mkojo (UTI), kisukari: wakati wote kula ½
kikombe cha vitunguu vilivyo katwa katwa kwa
siku nzima. Usisahau kwenda katika kituo cha
afya kwa uchunguzi wa afya yako.
6. Maambukizo ya mba (fungus), majipu: Twanga
½ kiganja cha kitunguu kilicho- katwa na
pangusa kidonda, au eneo lililoathirika kwa maji
ya kitunguu; au weka ½ kitunguu kwenye jipu na
funga eneo hilo kwa kitambaa. Tiba hii hufaa,
ingawa kikonyo cha kitunguu swaumu
kilichokatwa, kwa vyovyote, kina nguvu zaidi,
lakini huwasha zaidi.
7. Maumivu ya sikio au linalotoa usaha: Chukua
kiganja 1 cha vitunguu vilivyokatwa vizuri,
weka katika kipande cha kitambaa cha pamba
chepesi. Tumia kitambaa hiki kugandamiza juu na nyuma ya sikio. Tunza hali hii
kwa kufunga kitambaa kuzunguka kichwa; kutunza joto; badilisha kitunguu
asubuhi na jioni.
ATHARI: Kwa watu wenye mzio au kwa kutumia muda mrefu, mwasho wa ngozi
unaweza kutokea. Kuzuia kukutana na macho.
109
6.3. Aloe vera (syn. Aloe barbadensis) Aloe ferox and Aloe arborescens Msubili
Familia: Liliaceae
Msubili hutengeneza (huotesha) matawi kutoka katika shina.
Mimea ya madawa inayostawi kwa miaka mingi, matawi machanga huwa na madoa
meupe na kuwa maua ya rangi ya njano inayongaa.
Aloe ferox: Kinyume na Aloe vera, ni kijiti chenye shina moja, hukuwa na kufikia
kimo cha mita 2 – 3, maua yake ni njano, rangi ya machungwa, au nyekundu.
Aloe arborescens: Ina shina refu ambalo matawi yake huota kufuata urefu wake.
KIULIMWENGU: Utomvu wa njano upatikanao kwa
kuchanja tawi hutumika kama dawa ya kulainisha choo
(aloin).
Gel isiyo na rangi iliyo ndani sehemu ya ndani ya
jani ina tabia ya anti-allergic na anti-inflammatory.
Inatumika kwa sehemu zilizoungua, fizi zilizougua ,
ukurutu, na kwa kufunga vidonda na diabetic ulcers
(vidonda ndugu).
Nchini Uganda chai iliyotengenezwa kutokana na
majani inatumika kwa maumivu ya tumbo (gastritis):
Kiganja kimoja cha majani, yaliyokatwa vizuri, katika
lita moja ya maji ya moto.
1. Kutengeneza dawa ya kuharisha: Osha jani kwa maji
ya moto likiwa bado kwenye shina, kausha na likate.
Weka kwenye kikombe, likiwa limekatwa katikati hadi chini. Baada ya dakika 15
pima utomvu uliopatikana na changanya na sukari kipimo mara tatu zaidi. Kausha
mchanganyiko wa “Aloe sugar” juani, ndani ya chandarua.
Watu wazima watumie gram 3 wakati wa jioni kama dawa ya kuharisha, lakini sio
wakati wa ujauzito, na wala sio kwa matumizi ya muda mrefu.
2. Kuungua: Kata na osha vizuri jani la mmea. Safisha kisu kikali na kukiweka
kwenye maji ya moto. Kata sehemu za pembeni na za mwisho za jani, na kisha
kata sehemu ya katikati ili kupata sehemu kubwa ya ndani ya jani. Paka sehemu
yenye utomvu ya jani (“aloe gel”) kwenye sehemu yote iliyoungua. Fanya hivyo
mara nne kwa siku. Mgonjwa akae ndani ya chandarua ili kuzuia inzi. Tiba hii
kwa majeraha ya kuungua hutoa matokeo bora kuliko hata Vaseline gauze ya
kawaida.
3. Vidonda, ulcers na diabetic ulcers: Fuata mchanganyiko namba 2. Kila baada ya
tiba, tumia kipande kidogo cha papai bichi, asali au sukari kama ilivyoelezwa
katika sura 5.5. na 6.30.
4. Conjunctivitis: Kwa macho mekundu, fuata mchanganyiko namba 2. Weka jani
juu ya jicho kwa dakika 5, mara 4 kwa siku.
5. Nywele kutoka: Chukua aloe gel kutoka kwenye jani. Changanya kijiko kimoja
cha mezani kwa kiini cha yai bichi na chua nywele kila jioni kwa kutumia
mchanganyiko huu. Au tumia aloe gel peke yake.
6. Vidonda vya magonjwa ya zinaa: Tibu mara 3 kwa siku kwa kufuata
mchanganyiko namba 2. Halafu kunywa antibiotics.
110
6.4. Amaranthus gracilis Mchicha
Familia: Amarantaceae
Kuna aina nyingi mbalimbali za mchicha, lakini zote
zinafanana kitabia.. Ni zao la mwaka, na ni mmea wenye
lishe, na hustawi vizuri kwenye ardhi yenye naitrojen
kwa wingi. Majani yake yana vitamin C kwa wingi,
chuma na protini na ni mboga nzuri sana. Mbegu vilevile
zina lishe ya hali ya juu na protini kwa wingi.
KATIKA TROPIKI
Majani yanatumika kama mboga na kutibu upungufu wa
Vitamin C na upungufu wa damu.
Mchicha usichukuliwe tu kama magugu, lakini
uthaminiwe na kulimwa zaidi; panapokuwa na nafasi
tupu shambani (mfano: kati ya mhogo na mhogo) siha
mchicha.
6.5. Ananas comosus Nanasi Familiae: Bromeliaceae
Nanasi lina kimengenya kiitwacho “bromiline,” ambacho hupunguza inflammation.
Nanasi lililoiva lina vitamini C kwa wingi.
1. Oedema na inflammation kwa nje: Funga kipande cha nanasi bichi kwenye
oedema au sehemu iliyovimba (mfano, kwa kitambaa chembamba.)
2. Amenorrhea (kutokuingia hedhini), magonjwa ya njia ya mkojo, dawa ya
kuongeza mkojo na kwa minyoo; changanya kiasi cha gram 500 cha nanasi
mbichi kwa 0.7 ya lita ya maji, chemsha pamoja, na kunywa kidogokidogo kwa
siku nzima. Kama ni lazima rudia kwa siku kadhaa.
3. Upungufu wa Vitamin C na homa: Kunywa juisi nyingi ya nanasi zilizoiva ili
kusaidia mfumo wa kinga wa mwili wako. Juisi za matunda yafuatayo nazo zina
vitamin C kwa wingi pia: limau,
machungwa, papai, machenza,
matunda damu.
4. Kuvimbewa: Juisi ya nanasi
mbichi ni ya kufaa sana na
inasaidia.
5. Kama papaine ya papai, bromeline
nayo hufanya nyama ngumu kuwa
laini. Funga nyama ngumu ndani
ya ganda la nanasi mbichi usiku
kucha. Angalia juisi ya nanasi
isiguse macho. Juisi ya nanasi
mbichi haipendekezwi kutumiwa na wajawazito au wagonjwa wenye vidonda vya
tumbo.
111
6.6. Arachis hypogaea Karanga Familia: Papilionnaceae
Mmea una urefu wa sm 20 – 30, matunda hukomalia
ardhini.
KATIKA TROPIKI
Karanga zina protini na vitamin kwa wingi. Protini
iliyomo katika maziwa ya unga ni sawa na karanga
zilizokaushwa, lakini, katika maeneo ya tropiki,
protini huwa ni mara kumi zaidi. Mafuta yana lishe
pia, na yanaweza yakakamuliwa katika maeneo ya
vijijini kwa kutumia mashine rahisi. Ingawaje
hayadumu kwa muda mrefu.
Kukosa usingizi: Kunywa dawa ya kumwagia maji ya
moto kikombe kimoja cha maji ya moto kwenye
kiganja kimoja cha majani ya Karanga.
6.7. Bixa orellana (lipstick tree) Annatto
Familiae: Bixaceae
Bixa ni kimti kinachokua haraka katika maeneo ya
tropiki; mbegu zake ni nyekundu zilizokoka. Rangi
hii (annatto, terra indica) ina carotinoids, haina
madhara yoyote na inatumika duniani kote kwa
kuweka rangi kwenye jibini, mtindi, mandazi, nyanya
zilizopikwa kiwandani, lipstick, nywele, pamba na
hariri.
AMERIKA YA KUSINI
Rangi inatumika kwa kulinda ngozi dhidi ya jua
wakati wa safari ndefu.
1. Kusafisha vidonda (PHILIPPINES): Chemsha
vijiko 10 vya mbegu za Bixa (nzuri ni zile
utakazochukua kwenye maganda yanayokaribia
kupasuka) katika vijiko 10 vya maji, chuja, na
ongeza kijiko 1 cha juisi ya kitunguu swaumu kipya.
2. Kuungua: Chemsha vipimo 10 vya mafuta ya mbogamboga kwa kipimo 1 cha
mbegu safi za bixa; chemsha kwa dakika 10 katika joto la 100º na chuja.
3. Tunatumia Bixa kuweka rangi katika sabuni (Tazama sura 4.1.7.) na dawa ya
mafuta, kwa kuongeza mbegu mpya katika mafuta yanayochemka.
Michanganyiko ya maji inaweza kuwekewa rangi nyekundu kama ifuatavyo:
Acha gram 100 mbegu na gram 0.5. NaOH (Sodium hydroxide) katika ml 200 za
maji kwa saa 6, chuja na ongeza maji kadri unavyotaka. Au: kutengeneza wino
mwekundu, ongeza gram 20 kwenye mchanganyiko huu (kama dawa ya
kuhifadhi). Hii inafaa pia kwa kunyesha wino kalamu za highlighter!
112
6.8. Brassica oleracea Kabeji Familia: Brassicaceae
Mboga yenye chuma kwa wingi;
inaweza kuliwa mbichi au
imepikwa. Utomvu wa kabeji
mbichi una kitu chenye uwezo
wa kuzuia vidonda (anti-
ulcerous) ambacho hutunza
sehemu laini ya (mucous
membrane) tumbo – DR.
KONGO – KIVU, ULAYA:
Mboga huliwa kwa kutibu
upungufu wa vitamin C na
huliwa mbichi kwa vidonda vya
tumboni. Majani mapya
hutumiwa kutibu magonjwa ya ngozi, hasa eczema ambayo haijulikani chanzo.
6.9. Cajanus cajan Mbaazi Familia: Fabaceae
Ni mmea wenye jamii ya mikunde
mikunde, urefu wake ni meta 2, maua
yake ni njano na yana urefu wa kadri
ya sm 1.5. Ganda lake lina nywele
nywele sm 4 – 7 urefu na lina mbegu
2 – 7. Majani yake ni mbolea nzuri.
Hukua katika maeneo ya tropiki
kuanzia usawa wa bahari hadi
mwinuko wa meta 2,400. Ni mmea
unaofaa sana.
Kwa kuzuia mmonyoko wa udongo:
Kwa sababu hii panda mbaazi kwa
kukingama Mteremko, kufuata mistari
ya kontua . Panda sm 20 kutoka mmea
hadi mmea, katika mistari meta 3 – 5
mbalimbali. Kati ya mistari hii lima
mazao ya chakula na mimea ya dawa.
ASIA: Hutumika katika majipu
yanapokuwa katika hatua za awali,
mseto wa ndizi mbichi na mbegu za
mbaazi unawekwa katika sehemu
iliyoathirika na kufungwa kwa kitambaa kisafi.
AFRIKA: Mmea wa kufunika ardhi: Mbegu zina protini kwa wingi, na zinaweza
kuliwa. Ziloweke kwa saa kadhaa, zitwange na kisha ama kanga au pika kwa mvuke.
Mbaazi ambazo hazijakomaa zinaweza kuchemshwa na kuliwa kama mboga.
113
6.10. Canarium Schweinfurthii Mbafu Familiae: Burseraceae
Mti mkubwa wa porini wenye gome
lenye nyufa. Tunda lake kama mzeituni,
likipikwa na kuwekewa chumvi ni laini.
Mara baada ya kukata katika gamba,
utomvu unaonata na laini (“elemi),
hujitokeza, wenye harufu kali kama
terpenes.
AFRIKA: Elemi inatumika katika tochi,
au inawashwa moja kwa moja kama
mbadala kwa mshumaa. Katika
makanisa ya Catholic hutumika kama
ubani. Kwa dawa hutumika katika dawa
ya mafuta na mafuta ya maumivu ya
viungo na kuvimba viungo. (Tazama
sura 4.3) na upele (scabies). Nchini
Congo dawa ya kutokosa ya gamba la
mti hutumika kwa maumivu ya tumbo,
maumivu ya baada ya kujifungua na
kondo la nyuma kuchelewa kutoka.
ULAYA: Utengenezaji wa “elemi
depuratum” chemsha utomvu taratibu, chuja kwa nguo na tunza kwenye chombo
kisichopitisha hewa. Hutumiwa katika plasta ili kuchochea ngozi kuweza kufanya
kazi. Hutumika katika useremala kutengeneza varnish. Varnish ya kawaida ni mafuta
ya mbono, mbegu za kitani, au ufuta kama hii ni ghali sana. Changanya (ujazo)
kipimo kimoja cha elemi na vipimo 2 vya nta
(mshumaa) kwenye vipimo 7 vya dizeli, chemsha
katika oven ya sola (kamwe usichemshie kwenye
moto!) na chuja ikiwa moto. Kwa matumizi ya
nje, oil ya injini inatumika badala ya dizeli.
6.11. Cannabis sativa Bangi Familia:
Cannabaceae
Mmea wa porini unaopatikana duniani kote. Ncha
za mmea wa kike huvunwa na kutumiwa. Joto la
kukaushia lisizidi 50ºC.
AFRIKA: Bangi mara nyingi huvutwa na watu
wenye magonjwa ya akili au masikini sana.
Inatumika kama dawa kuondoa – maumivu na
“kuwa mtu wa juu.” Kwa kawaida ukulima wa
114
bangi na biashara vinapigwa marufuku.
KATIKA TROPIKI: Kama morphine, bangi iko katika opioid analgesics. Kama
hakuna opiods za biashara, au kama ni ghali sana kwa wagonjwa wenye kansa au
UKIMWI bangi inaweza ikawapunguzia maumivu – lakini hakikisha unazitaarifu
mamlaka zinazohusika kwanza. Kabila la Wagenia nchini D. R. Kongo hutumia chai
iliyotengenezwa kwa majani. Kuosha na kusuuza ukeni kama mtoto njiti anatarajiwa
kuzaliwa.
Kutapika kwa wagonjwa wa kansa na UKIMWI, maumivu makali, psychotic crying:
Mpe sigara ya bangi. Hufanya kazi, karibia hapo hapo, hukolea zaidi baada ya dakika
30 na hutoka baada ya saa 3. Au badala yake chai ya bangi au tincure inaweza
kutumika. Hizi huchukua karibu saa moja kufanya kazi, lakini nguvu yake hukaa
kadri ya saa 8.
ATHARI: Athari ni pamoja na kichefuchefu, kupoteza kumbukumbu kidogo,
wasiwasi, kufunga choo na schizophrenia.
6.12. Cassia spectabilis Familia: Caesalpiniaceae
Ingawaje huu mti hautumiki sana kwa
shughuli za tiba, tumeuingiza hapa kwa
sababu ya thamani kubwa kama “Ua
unaoishi,” kwa kustawisha misitu na
kuzuia mmomonyoko katika bustani za
dawa. Hujiotesha katika misitu ya nchi
za tropiki, una maua makubwa ya
njano sana, umbo lake linafanana na
maua ya mti horse chestnut tree wa
Ulaya.
Kwa kukata vitawi vyenye urefu
kama wa meta moja unaweza
kuanzisha pori jipya.
Chini ya matawi ya mti huu kilimo
kinaweza kufanyika. Ili kuzuia
mmomonyoko, weka vitawi hivyo sm
50 kwa kina ardhini, ukiacha kati ya
mti na mti sm 20. Mwanzo wa msimu
wa mvua, kata ua hadi urefu wa meta 1,
na fukia matawi udongoni kama
mbolea.
Maambukizi ya mba (fungal infections)
kama Cassia alata (ringworm bush, Tazama sura 5.6) haipatikani, tumia Cassia
sptectabilis badala yake.
115
6.13. Cinchona officinalis
Familia: Rubiaceae
Aina mbalimbali ziko katika Cinchona
officinalis, mfano, Cinchona succiruba,
mti ambao hufikia urefu wa meta 24
kwenda juu. Miti ya Cinchona, ambayo
ina asili ya Andes, huota mahali popote
katika maeneo ya tropiki, na hustawi vizuri
kwenye mwinuko kati ya meta 1,000 na 2,
400. Gamba la Cinchona huvunwa ama
kwa kukata miti yenye umri wa miaka 8 na
kuondoa gamba, au kwa kukata vipande
vyembamba vya gamba wakati mti ukikua.
Majeraha ya mti yanafunikwa kwa
mfinyanzi au moss. Gamba lililovunwa
linakaushwa juani.
Miti ya Cinchona iliyo porini imekuwa
ikiteketezwa kwa ukataji usiodhibitiwa.
Kama una bahati ya kuishi katika maeneo
yenye mwinuko sahihi kwa upandaji wa Cinchona, panda miti hata 3 katika bustani
yako. Gamba la Cinchona limekuwa likitumiwa kwa zaidi ya miaka mia tatu kutibu
homa na malaria.
Kutegemea na aina, gamba lina asilimia kati ya 1 na 3 quinine, na kadri ya
asilimia 4 quinine na alkaloids zingine. Kwa uzalishaji wa kiwandani, quinine
ambayo ina nguvu ya kutibu malaria, inatengenezwa kuwa vidonge (dozi ya kila siku
kwa watu wazima: gram 1 – 2) . Quinidine inatumika kwa wagonjwa ambao
magonjwa yao yanaambatana na moyo (mapigo ya moyo yanakwenda haraka sana).
1. Malaria: Kama chaguo la kwanza, tumia Artemisia annua (Tazama sura 5.2), kwa
kuwa ina madhara kidogo. Tumia cinchona iwapo tu Artemisia annua haifanyi
kazi. Chemsha gram 10 au vijiko vya chai vitatu vilivyojaa kabisa vya gamba la
cinchona lililosagwa vizuri katika lita 1 ya maji kwa dakika 10, chuja na kunywa
kidogokidogo kwa zaidi ya saa 24. Hii ni sawa na kama mg 350 za quinine.
Watoto wapewe kidogo kutegemea uzito wa miili yao.
2. Kama ungependa kuwapa wageni wako “soda” chemsha gram 1 au ¼ kijiko cha
chai cha gamba la cinchona kwenye kikombe 1 cha maji kwa dakika 10. Ongeza
juisi na ganda lililokunwa la limau 3, chemsha tena kidogo na chuja. Sasa ongeza
gram 300 au vikombe 2 vya sukari na lita 3 na maji baridi. Tumia ikiwa imepoa.
3. Lotion ya nywele: Chua nywele kwa kutumia mchanganyiko namba 1 juu.
ATHARI
Ikitumiwa kwa ndani: kuumwa kichwa, kutapika au kuharisha. Huchochea mtu
kujifungua, kwa hiyo usitumie mchanganyiko namba 1 kama kuna hatari ya mimba
kutoka. Kama ikitumiwa kwa kipindi kirefu, kuharibika kwa kiini tete, macho
kuharibika na hata kutokusikia kunaweza kujitokeza.
116
6.14. Citrus sinensis Chungwa Familia: Rutaceae
Mti hukua hadi meta 5 urefu, na
maua meupe yenye harufu nzuri.
Matunda hubadilika kuwa njano au
orenji yanapoiva. Ganda lina
mafuta yaliyo muhimu sana. Juisi
ina tindikali, sukari na vitamin C.
KIULIMWENGU: Ganda linaleta
hamu ya chakula na kusaidia
kuyeyusha chakula. Kata kata
ganda. Chemsha vijiko 10 vya
mezani katika lita moja ya maji
kwa dakika 2, kamua na kunywa
kwa siku nzima.
AFRIKA: Kwa pumu, kikohozi,
kuumwa kichwa (migraine):
Chemsha kiganja 1 cha majani katika lita 1 ya maji kwa dakika 2 na kunywa siku
moja. Kwa madonda ya midomo au mdomoni, fuata mchanganyiko uleule kama wa
limau; sura 5.8.
6.15. Cocos nucifera Nazi
Familia: Palmae
Nazi ni mmea wenye chakula
chenye lishe. Wakati wa vita ya II ya
dunia, Askari wa kiingereza barani
Afrika walitumia juisi ya nazi badala
ya glucose (ina 5% glucose safi –
lakini hili siyo pendekezo!)
AFRIKA: Juisi humwagwa mbali
mara nyingi . Baada ya kuongeza
chumvi kidogo inaweza ikatumika
kama kinywaji cha kuongeza maji
kwa watoto wanaoharisha (kama
Oral Rehydration solution). D. R.
Congo inatumika kama lotion ya
nywele na ngozi pia.
117
6.16. Coffea sp Kahawa Familia: Rubiaceae
Katika nyanda za chini aina ya “robusta”
hulimwa, katika nyanda za juu “Arabica.”
Aina mpya “arabusta” hustawi vizuri
katika safu za miinuko.
KIULIMWENGU: Kahawa hunywewa:
a) Kwa aina fulani ya maumivu makali ya
kichwa (migraine)
b) Kichefuchefu
c) Kwa kuamsha, kuchochea na
d) Katika kiasi kikubwa, lakini ikiwa na
maji mengi, kama dawa ya kuongeza mkojo.
Isitumiwe na watu wenye vidonda tumboni. Kahawa huongeza kiwango cha mapigo
ya moyo.
6.17. Cola acuminate, cola nitida Ugongolia Familia: Sterculiaceae
Miti hii inapatikana Afrika Magharibi. Karanga zake zina kadri ya 2% catechine –
caffeine (colanine). Mapigo ya moyo yanazidi na mkojo unaongezeka kwa kiwango
cha chini ukilinganisha na kahawa (Baadhi ya Waafrika hawawezi kunywa kahawa,
lakini kiasi kilekile cha caffeine kilicho katika ugongolia hakiwaletei matatizo
yoyote!).
Karanga mbichi lazima
zitunzwe kwenye ardhi yenye
unyevu au mchanga. Karanga
hukaushwa kwa kukatwa
katwa vipande vyembamba na
kuzikausha kwa saa 24 katika
joto la 80ºC. Kuzioka
zikatwekatwe vipande na
kuokwa kama kahawa.
ULAYA: Kichocheo chenye
nguvu
Kwa kuumwa kichwa (migraine), kuharisha, neuralgia na kutumiwa kama kichocheo
au cardiotonic.Tumia gram 1 – 4 karanga kavu, zilizotwangwa kila siku.
Kwa huzuni, kukosa hamu ya chakula, na kwa kuondoa majonzi: Tumia Karanga 1
kila siku.
118
6.18. Cucurbita maxima Boga Familia: Cucurbitaceae
Mmea unaotambaa, ni wa mara moja kwa
mwaka.
KIULIMWENGU: Boga, mbegu na majani
ni chakula bora. Mbegu zina nguvu ya
kutibu minyoo na prostatitis (Kuvimba kwa
tezi za kiume, ambacho husababisha ugumu
wa kukojoa hasa kwa wanaume wazee).
1. Kwa tegu: Tumia gram 100 (au vijiko 20
vya mezani) mbegu mbichi zilizosagwa
pamoja na dawa ya kuharisha kabla ya
kula. Dawa ya kuharisha ni muhimu
sana, kwa sababu minyoo hafi, ila
hupooza. Kama dawa ya asili ya kusaba
bisha kuharisha, kula mapapai au
maembe mengi yaliyoiva sana.
2. Kuchochea Maziwa kutoka baada ya
kujifungua: Tumia vijiko 2 vya mezani
vya mbegu mbichi zilizosagwa na maji kwa wingi kwa siku 7 mara mbili kwa siku
(asubuhi na jioni).
3. Prostatitis: Mchanganyiko uleule kama namba 2 juu, tumia kwa mwezi 1 – 2.
6.19. Curcuma longa Dawam mchuzi Familia: Zingiberaceae
Ni mmea, majani 15 kwa sm 40, hutokea kwenye shina (rhizome) lenye umbo la
kiganja. Maua huota kwa kujitegema kutoka
kwenye majani moja kwa moja kutoka
kwenye shina (rhizome), ambalo ni la njano
na lina ladha kama ya tangawizi.
Ili kuhifadhi, kata vipande vyembamba,
acha vikauke, na hifadhi sehemu yenye
ubaridi na kavu.
MATUMIZI DUNIANI KOTE
1. Kwa maumivu na kuvimba kwa viungo
(Baridi Yabisi)
Kula mara 3 kila siku gram 0.5 za unga
wa dawam mchuzi. Hii imethibitishwa
katika kliniki.
2. Kwa tumbo kujaa hewa, kuvimbewa,
hedhi isiyo na utaratibu maalum, na
kuchochea utoaji wa nyongo:
a) Kula gram 1 dawam mchuzi (unga)
mara 3 kwa siku, au
119
b) Twanga gram 3 za dawam mchuzi kavu, au gram 10 za shina (rhizome) bichi,
chemsha katika 0,7 lita ya maji kwa dakika 5, na kunywa kwa siku nzima.
Rudia kwa siku kadhaa au
c) Changanya gram 50 za mizizi mikavu iliyotwangwa ya dawam mchuzi kwa
ml 100 za kileo kizuri 50%, chuja baada ya wiki moja. Dozi kwa watu
wazima: matone 20 mara 3 kila siku.
3. Kwa kikohozi: Tumia gram 6 kavu, au gram 20 za rhizome mbichi; twanga,
chemsha katika 0.7 lita ya maji kwa dakika 5, kunywa wakati wa mchana, na kwa
siku kadhaa. Dawam mchuzi vilevile inatumika kama kitu muhimu katika binzali.
Curcumin ambao inaweza ikapatikana katika dawam mchuzi, inatumika kuweka
rangi katika pamba, hariri, nta , jibini, poda na krimu.
6.20. Datura stramonium Mranaa Familia: Solanaceae
Mmea wenye sumu sana, hufikia urefu wa meta 1, unapatikana katika nchi za Tropiki
kuanzia mwinuko wa meta 0 – 2,000 hupendelea
kuota kwenye kifusi au madampo. Maua yana
urefu kadri ya sm 8, muundo wa tarumbeta meupe
au blue. Mranaa una atropine na anti-spasmodic
alkaloids zingine. Kwa sababu hii hutumika kama
dawa ya kupunguza cramps.
AFRIKA: Majani yalichemshwa na
kutwangwa huwekwa kwenye majeraha ya
kuungua ili kupunguza maumivu. Na hii ifanyike
tu kama jeraha la kuungua ni dogo, kwa sababu ya
hatari ya sumu. Majani lazima yachemshwe ili
kuzuia maambukizo ya bacteria kwenye jeraha.
1. Kuumwa na wadudu: Pangusa sehemu
iliyoathirika ya ngozi kwa utomvu kutoka
kwenye majani (Baadaye nawa mikono).
2. Pumu: Majani huvutwa kama sigara kutibu
pumu. Sigara za pumu zenye nguvu hutengenezwa kama ifuatavyo:
- Majani makavu ya mranaa mg 150
- Majani makavu ya mkaratusi mg 150
- Majani makavu ya mpapai mg 700
Tengeneza sigara kwa karatasi, au tumia kiko.
3. Magonjwa mbalimbali; Tincture ya mranaa (kwa matumizi ya hospitalini tu)
- Mbegu za mranaa, zilizokaushwa (sio zaidi ya joto la 50º C)
- na kupandwa vizuri gram 8
- Plain alcohol 95% ml 45
- Maji yaliyochujwa ml 55
Changanya, baada ya wiki moja kamua na ondoa mbegu. Dawa hii ni sawa na
belladonna iliyoagizwa nje yenye atropine (0.03%) na ni sawa kwa matumizi na dozi
120
(watu wazima, isizidi matone 30 mara 3 kila siku, watoto: Isizidi tone 1/kilo ya uzito
wa mwili mara 3 kila siku).
Matumizi yake:
A. Intestinal spasms, figo au bile colics, kushambuliwa na pumu
Matone 30 kila saa zipitazo 2, sio zaidi ya matone 90 kwa siku.
B. Pumu sugu, madonda ya tumbo: Matone 5 – 10 mara 3 kila siku.
C. Dawa ya awali kabla ya operesheni: Dozi kwa mjibu wa daktari katika hali mbaya
pamoja na chai ya bangi.
D. Parkinson’s disease: Anza na matone 5 mara 3 kwa siku, na ongeza dozi hadi
athari ziwe kubwa kuliko manufaa.
E. Poisoning with organophosphates: Tumia matone 30 (au zaidi, kama ilivyoelezwa
na daktari) kila dakika 30 mpaka kupiga kwa moyo au mishipa kumekuwa
kawaida.
F. Katika kipindi cha msukosuko, kwa mfano vita, unaweza kutafuna mbegu moja
kwa moja badala ya kutumia tincture. Matone 2 ni sawa na mbegu 1, kwa hiyo:
watu wazima: Tumia mbegu zisizozidi 15, mara 3 kwa siku. Hii ina maana, siyo
zaidi ya mbegu 45 kwa siku. Watoto: Mara 3 kwa siku, kiasi cha mbegu 1 kwa
kila kilo 2 za uzito wa mwili.
ATHARI: Datura stramonium ni mmea wenye sumu kali. Dozi inayotumika kwa
matibabu na dozi inayokuwa sumu inakaribiana sana. (K.m. mbegu 10 zinaweza
kuwa dawa, mbegu chache zikiongezwa, tayari zinaweza kuwa sumu)
Alkaloids iliyo katika majani hubadilika wakati wa mchana, lakini mbegu
tulizokusanya zilikuwa na 0.4% alkaloids zisizobadilika, zilikuwa ni
atropine/hyoxyamine. Kwa sababu hii tunatumia mbegu na
sio majani.
6.21. Daucus carota Karoti Familia: Apiaceae
Katika nchi za tropiki, karoti hustawi sana katika nyanda za
juu. Mizizi yake ni chakula (na ni bora zaidi, zikiliwa
mbichi kuliko kupikwa) kwa kuwa zina carotene,
provitamin A (ambayo hugeuzwa mwilini kuwa vitamin A).
KIULIMWENGU: Karoti mbichi zinatumika kuimarisha
tumbo, utumbo na matumbo. Kwa maana hiyo zinafaa kwa
yote: kwa kutibu kuharisha na kwa kutibu shida ya
kutokupata choo (obstipation) - hasa kwa watoto, kwa
tumbo lililojaa hewa na tumbo lililosumbuliwa na Kemikali
kali iliyomo tumboni (gastric acid). Karoti zina nguvu
kidogo kwa minyoo ya safura, hedhi isiyo na utaratibu
maalum, na prostatitis. Kula karoti mbichi kila siku
hupunguza kiwango cha lehemu na kwa hiyo ni hatua ya
kuzuia mishipa kuvimba na kuwa migumu
(arteriosclerosis).
121
6.22. Elaeis guineensis Mchikichi Familia: Palmaceae
Mchikichi una asili ya Afrika, na sasa unapatikana katika nchi zote za tropiki.
Mawese yanapatikana kwa wingi madukani, na yamekuwa sehemu ya milo barani
Afrika kwa karne nyingi sasa. Yanaweza pia yakatengenezwa kutokana na miti yenye
matunda iliyoota porini, lakini upatikanaji wa mawese kwa wingi unatoka kwenye
miti iliyopandwa na kutunzwa . Hustawi vizuri mahala ambapo kuna joto mwaka
mzima, kati ya 25º na 28° C, mvua nyingi na udongo wa ki-mchanga. Kwa hiyo
unaweza ukahitaji kurutubishwa. Katika hali hizi, mchikichi utaanza kuzaa matunda
miaka 3 – 4 baada ya kupanda.
Kutoka kwenye mchikichi, mtu anaweza akazalisha mawese au palm kernel oil.
1. Mawese:
Ili kutengeneza mawese bora, tengeneza siku
ileile mbegu zilipovunwa. Tumia mawese
wekundu kwa kupika, au bora zaidi tumia
matunda mabichi ya chikichi, unapopika kwa
mafuta. Rangi ya nyekundu iliyokolea ni kwa
sababu ya carotene nyingi iliyomo, ambayo pia
huitwa “provitamin A”. Kama utatumia kijiko
kimoja cha chai kwa siku cha mawese,
unaweza ukatupa vidonge vyote vya vitamin A!
Miongoni mwa vitu vingine, vitamin A hulinda
macho. Katika nchi ambazo chikichiki hustawi,
watu wachache hupata upofu!
Usafirishaji wa mawese duniani ni wa pili
tu kwa mafuta ya soya. Kiwango kikubwa
husafirishwa kutoka Afrika kwenda
kutengenezwa upya na kurudishwa tena Afrika
kama “mafuta safi” mawese yasiyo rangi. Kwa
kweli, vitamin zimeondolewa, kwa hiyo mafuta haya ni halisi kwamba “hayana
vitamin” au “hayana lolote.” Yaache kabisa mafuta haya, kama inawezekana
zalisha ya kwako mwenyewe.
Mawese ni muhimu katika utengenezaji wa sabuni, dawa za mafuta, na
vipodozi. Hapa tunapata jina Palmolive!
Kama unataka kweli mawese yasiwe na rangi, labda kutengeneza sabuni
nyeupe, chemsha mawese katika chungu; chemsha sana hadi carotene iharibike
(itolewe) (inakuwa tayari pale ambapo karatasi nyeupe iliyochovywa kwenye
chungu haibadiliki kuwa njano); Lakini kwa makini. Huruka sana, na kuna hatari
kubwa kwa mafuta kushika moto. Vaa miwani, na watoto wakae mbali.
2. Palm kernel oil:
Huzalishwa kwa kuondoa gamba la juu la mbegu, kuzioka ndani ya sufuria,
kuponda ponda mbegu hadi kuwa kama uji mzito, kuongeza maji, kuchemsha na
hatimaye kuengua mafuta ya juu. Mafuta haya lazima yachemshwe tena ili
kuondoa dalili zote za maji. Mafuta haya hayana rangi, na kipodozi kizuri.
Yanatumika kutengeneza chochote, na kama kitu cha msingi kwa kutengeneza
122
suppositories; yeyusha vipimo 6 palm kernel oil na vipimo 4 kama unaishi
maeneo ya baridi, au vipimo 5 (maeneo ya joto) vya nta ya nyuki.
Baada ya kuzalisha palm kernel oil, mabaki, mashudu ya palm kernel oil yana
protini kwa wingi na yanaweza yakapewa mifugo.
6.23. Harungana madagascariensis Mdura
Familia: Hypericaceae
Utomvu wa mmea unaweza kutumiwa kwa
magonjwa ya ngozi, kwa upele (scabies) na kama
haemeostatic (hii ina maana – kuzuia damu kuvuja),
kwa mfano baada ya tohara. Kwa mjibu wa
majaribio ya maabara, mtokoso (dawa ya kutokosa)
kutoka kwenye gamba una nguvu ya kushambulia
tegu, magonjwa ya njia ya mkojo “Trichonomas-
vaginalis” na malaria. Utomvu mwekundu wa mmea
huu unatumika kupaka rangi nguo.
D. R. CONGO: Mbegu hutumika kuharakisha
kujifungua, au kwa kutoa mimba.
AFRIKA MASHARIKI: Mtokoso kutoka kwenye mizizi au gamba, ukitumiwa mara
mbili kwa siku, husimamisha hedhi.
UJERUMANI: Tincture iliyozalishwa kutoka kwenye majani na gamba la mmea
huboresha utoaji wa juisi zinazoyeyusha chakula kutoka kwenye nyongo na
kongosho. Watu wazima watibiwe kwa tincture iliyotengenezwa kwa mg 35 majani
na gamba la mdura kwenye kijiko 1 cha mezani cha kile (45%) mara moja kwa siku.
ATHARI:
Kuhisi mwanga wa jua kwa urahisi sana. Kwa hiyo epuka kukaa juani moja kwa
moja wakati wa tiba.
6.24. Helianthus annuus Alizeti Familia:
Asteraceae
Alizeti sanasana hupandwa kwa madhumuni ya
mapambo. Hustawi vizuri kila mahali katika
maeneo ya tropiki. Mafuta ya hali ya juu
yanaweza yakakamuliwa kutoka kwenye mbegu.
Pamoja na vitu vingine, yanatumika katika
margarine na vipodozi. Mmea ni chakula kizuri
kwa mifugo, na ni mzuri kama mbolea ya asili.
PHILIPPINES: Dawa ya kutokosa (mtokoso)
kutoka kwenye mbegu inaotumika kwa kuumwa
kichwa. KIULIMWENGU: Mbegu zinatumika
kama chakula (zina protini na mafuta, hasahasa
safarini.
123
6.25. Hibiscus sabdariffa Ufuta Familia: Hibisceae
Kimti kinachopatikana Sudan, sasa
kinapatikana katika maeneo yote ya tropiki.
MAENEO YA TROPIKI: Chai kutoka kwenye
maua ya ufuta ina ladha nzuri na chachu
kidogo. Inatumika kama chai ya kuburudisha
na chai ya kifungua kinywa. Ukitumia kiasi
kikubwa cha chai yake, ina nguvu ya kuongeza
mkojo na huleta kuongezeka kwa utoaji wa
nyongo na jasho. Katika majaribio ya kliniki
ufuta ulionyesha tendo la kuchelewesha ukuaji
wa bacteria na kifua kikuu, kwa hiyo, kunywa
chai hii mara kwa mara kwa tiba yoyote
uliyopewa ya kifua kikuu.
ULAYA: Inatumika kuweka rangi nyekundu
ya kuvutia kwenye chai ya dawa ya mmea.
6.26. Ipomoea batatas Viazi vitamu Familia: Convolvulaceae
Mmea wa mwaka wenye maua meupe na bluu. Ni mmea mzuri kwa kufunika udongo
(udongo unaopigwa jua hupungua rutuba – kama ilivyo katika mashamba ya
mihogo). Zao ambalo ni mzizi lina protini kwa wingi sana kuliko mhogo na hivyo
lipewe kipaumbele. Viazi vya njano husaidia kuzuia upofu, hasa kwa watoto, vina
vitamin A kwa wingi sana na majani yake. Majani yake huliwa yamepikwa, yana
vitamini C kwa wingi na chuma, ambayo huyafanya yawe na uwezo wa kupambana
na upungufu wa damu.
MAENEO YA TROPIKI: Viazi vitamu
huliwa lakini, cha kusikitisha majani huliwa
kwa nadra sana kama mboga.
PHILIPPINES: Majani yanatumika kama
dawa ya kuzuia kuharisha.
AMERIKA KUSINI: Dawa inayofahamika
kwa wengi, majani yanatumika kwa uvimbe
(tumours) hasahasa wa kikoromeo.
ASIA: Kwa gastritis, viazi vitamu
vilivyopikwa hukatwakatwa, kukaushwa na
kutwangwatwangwa kuwa unga. Kijiko 1
cha chai kinachukuliwa kwa maji kidogo.
Kwa mjibu wa mchanganyiko mwingine wa
kuzuia kuharisha, viazi vibichi
hukatwakatwa, kukaushwa na kisha
kuchemshwa hadi kuwa mkaa, kusagwa na
unga kutumiwa kwa kumeza.
124
6.27. Kalanchoe pinnata Kineterete Familia: Crassulaceae
Mmea wa mapambo ambao hukua hadi
urefu wa meta 1. Mimea mipya inaweza
kuzalishwa kwa kukata majani na
kuyapanda.
INDIA: Huitwa “Mmea wa ugonjwa wa
kichwa”; dawa nzito kama uji
iliyotengenezwa kwa majani unawekwa
sehemu ya mbele ya kichwa.
MAENEO YA TROPIKI: Kwa
kuungua: Majani yaliyotwangwa
yanachemshwa kwa dakika 20 ndani ya
maji kidogo na kutumiwa kwenye ngozi
iliyoungua kama dawa ya kubandika.
Kwa majeraha: Ponda kiganja kimoja
cha majani yaliyooshwa, ongeza sukari
au asali kijiko 1 cha chai, na chemsha
mchanganyiko hadi ubadilike kuwa
kahawia (caramel – like). Inatumika
kama dawa ya kuweka kwenye kidonda
na iwekwe mpya mara mbili kwa siku.
SENEGAL: Hutengenezwa dawa nzito ya majani kwa ajili ya maumivu ya viungo.
NCHI NYINGI ZA TROPIKI: Kwa magonjwa ya masikio (otitis) kwa kukamua jani
lililochemshwa weka matone kidogo ndani ya sikio linalougua mara 3 kila siku.
6.28. Leucaena glauca Lesena
Familia: Mimosaceae
Mti mdogo, meta 2 – 6 urefu, wenye
majani kama manyoya. Mti ni mzuri kwa
kustawisha msitu, kuni na kutunza majani
ya msitu tofauti na ardhi iliyolimwa.
Kama mbaazi (6.9) tunapendekeza
kupanda lesena ili kuzuia mmomonyoko
wa udongo. Kama miti ya lesena
itapandwa kuzunguka bustani na
mashamba, na matawi yanakatwa na
kuchimbwa udongoni, hapa rutuba ya
ardhi inaimarishwa. Majani yanafanya
kazi kama mbolea ya asili, yanachangia
madini ambayo inaletwa na mti kutoka
mbali udongoni, na kwa sababu mti huu
125
ni mkundekunde, mizizi inatunza nitrogen ndani ya udongo.
PHILLIPPINES: Kwa minyoo ya safura (hookworms) na roundworms. Kausha
mbegu 30 zilizoiva, zisage vizuri na tumia unga kwa kunywa na kikombe kimoja cha
maji ya moto masaa 2 baada ya kifungua kinywa. Watoto watumie kidogo kutegemea
na uzito wao. Sio nzuri kwa watoto chini ya miaka 7.
ATHARI: Matatizo ya tumbo, kuharisha.
6.29. Matricaria chamomilla (syn. M. recutila) Familiae: Asteraceae
Mmea wa mwaka, una harufu kali, na maua madogomadogo yenye vichwa vilivyo
wazi ndani. German chamomile vilevile hustawi katika subtropics na katika nyanda
za juu sana katika maeneo ya tropiki.
Dawa ya kumwagia maji ya moto
(infusion) ya maua ya chamomile
inatumika ndani na nje; na nguvu kwa
tumbo lililojaa hewa; hulainisha tumbo,
huondoa cramps, ni antiseptic na anti –
inflammatory.
1. Inatumika kama chai kwa wagonjwa
wa gastritis au kama dawa ya kuoshea
macho kwa conjunctivitis (macho
mekundu): mimina lita moja ya maji
ya moto kwenye kiganja 1 cha maua.
Kwa kunawa macho, kwanza chuja
chai kwa kutumia karatasi.
2. Kutumika kama dawa ya mafuta kwa
majeraha, kuvimba kwa ngozi (skin-
infection), kuwashwa kwa ngozi kwa
watoto, vidonda vya magonjwa ya
ngono, eczema na bawasiri: Chemsha
gram 100 za maua ya chamomile
katika ml 500 za mafuta ya
mbogamboga katika fukizo – maji
(water-bath) kwa dakika 60, kisha
chuja. Ongeza gram 60 za nta ya nyuki, chemsha kidogo tena, na acha ipoe.
Tumia aina nzuri ya mafuta ya mboga uliyonayo, mfano, mafuta ya mzeituni, shea
butter, palm kernel oil.
3. Ili kuzalisha suppositories kwa ajili ya bawasiri, fuata mchanganyiko namba 2,
lakini badala ya gram 60 za nta ya nyuki, tumia gram 200 za nta ya nyuki, na kwa
mafuta, tumia mafuta magumu kidogo au grisi. Mwaga katika vifyatulio.
126
6.30. Mel: asali
Asali ni mchanganyiko wa aina mbalimbali za sukari, (70 – 80% glucose na
fructose; saccharose chini ya 5%) maji (hayazidi 22%) vitu vyenye harufu nzuri,
rangi na antiobiotics.
Uzalishaji: Licha ya ukweli kwamba asali ina ubora wa hali ya juu sana, katika
maeneo ya tropiki huuzwa kwa bei nafuu sana. Ili kuhakikisha kwamba una asali
yenye ubora sahihi, nunua masega (yaliyokomaa tu, na kufunikwa na nta, na bila
larvae) na jitengenezee asali mwenyewe.
Kama huna vifaa maalum, fanya mseto wa masega, kwa kutumia meat-mincer,
bila kutumia grinding disk. Tengeneza usiku, vinginevyo utajiletea hatari ya
kushambuliwa na nyuki! Sambaza mchanganyiko huu juu ya kipande cha nguo
kilichofungwa juu ya ndoo ya aluminum. Weka ndoo ndani ya sun-box. Kadri joto
litakavyotokea juu, asali na nta vitatiririka kupitia kwenye nguo. Baada ya saa 24,
ondoa asali na pia utando wa nta, ambayo unaweza ukatumia kwa kutengeneza dawa
za mafuta (Tazama sura 4.4.). Mseto unaobaki katika kitambaa cha pamba unaweza
kuchanganywa na maji kwa uwiano wa 1 kwa 1, kuchemshwa na baadaye
kutengenezwa kuwa mvinyo ya asali (Tazama sura 4.7). Mvinyo ya asali inatumika
katika utengenezaji wa syrup za kikohozi na mvinyo zingine za dawa. Kinachobaki
huwekwa katika vikapu vyenye kina kirefu, na kuning’inizwa mtini, hulindwa
kutokana na mvua kwa kufunika na kipande cha bati, na sasa huwa tayari kwa
kufanywa kuwa mzinga mpya wa nyuki.
Tunapendekeza kwamba, inapowezekana, tumia asali badala ya sukari, mfano,
kwenye syrup za dawa, Oral Rehydration Solution (ORS) na katika tiba ya
Utapiamlo.
Katika baadhi ya nchi infusions zilikuwa zikitengenezwa kwa asali safi
iliyopunguzwa nguvu kwa kuchangwya na vitu vingine. Asali inatumika katika kuleta
ladha kwenye tumbaku, na kwa matumizi ya nje katika sabuni, dawa za mafuta,
cream za kunyolea nywele na creams za kulainisha ngozi.
Tunapendekeza kwamba asali itumike kwa njia ya chakula kwa magonjwa ya
moyo, kuharibika kwa ini na kikohozi.(Tazama sura 4.8).
Kwa nje, kwa sababu ya tabia yake ya osmotic and antibiotic properties, asali ni
tiba nzuri kwa majeraha kama ilivyoelezwa na Dr. Efrem kutoka Nigeria katika
“Jenne Afrique” 2/89,”Asali ina bacterial substance inayoitwa inhibine. Kitu hiki
huondoa vimelea kutoka kwenye jeraha. Asali hufyonza maji na hukausha kabisa
jeraha. Katika muda wa wiki chache huwezesha madonda kuanza kupona ambayo
yamekataa kila aina ya tiba kwa kipindi kirefu.”
Kutibu jeraha; kwanza safisha, halafu weka mchanganyiko ulio sawa wa sukari
na asali. Sukari huzuia asali kutiririka. Kwa kuwa ni anti-bacterial, asali huacha
kidonda ikiwa safi. Kidonda ni lazima kitibiwe kwa mchanganyiko wa asali/sukari
mara kadhaa kwa siku, bila kukiosha tena.
Kama utajitengenezea asali mwenyewe, hakikisha kuwa kila kitu ulichotumia ni
safi kabisa. Hapo unaweza ukatumia asali moja kwa moja; vinginevyo ichemshe asali
kwa dakika 10 ili kuua vijidudu – lakini hii husababisha kupotea kwa nguvu zingine
za antiobiotic.
127
6.31. Melia azedarach
Familia: Meliaceae
Melia una uhusiano wa karibu sana na
mwarobaini, Tazama sura 5.3. Ni mti
unaokua haraka, mzuri kwa kutengeneza
pori, hasa katika maeneo ambayo huvamiwa
sana na nzige (mti huu haushambuliwi), au
katika maeneo ambayo mbao
zisizoshambuliwa na mchwa zinahitajika kwa
ujenzi. Maua yake ni bright violet kwa rangi,
majani yake yamegawanyika (branched)
zaidi kuliko mwarobaini, mbegu na matunda,
kinyume na mwarobaini, ni mviringo kabisa.
KATIKA TROPIKI: Chai iliyotengenezwa
kwa majani inatumika kidesturi kwa minyoo
na malaria.
MAREKANI: Gamba lililotwangwa lilitumika kutibu minyoo ya kwenye utumbo
(intestinal worms).
Melia azedarach haujafanyiwa utafiti kama uliofanywa kwa mwarobaini, na hivyo
kwa sababu ya sumu yake, utumike tu kwa shughuli za kilimo kama za mwarobaini,
Tazama sura 5.3.
Insecticidal products: Mazao ya dawa yaliyotengenezwa kutokana na Melia
azedarach yana nguvu kuliko yale yaliyotengenezwa kutokana na mwarobaini.
6.32. Morus nigra Mforsadi Familia: Moraceae
Kimti meta 2 – 3 urefu, majani yake pembeni kama meno ya msumeno. Matunda
yanayoliwa ni kama yai kwa umbo, sm 1.5 –
3 urefu, rangi nyekundu hubadilika kuwa
zambarau yanapoiva. Yana nyamanyama na
ladha tamu yenye uchachu kidogo (kama ile
ya European blackberry).
KATIKA MAENEO YA TROPIKI:
Hulimwa kwa ajili ya matunda, yana vitamin
C kwa wingi. Mforsadi vilevile hulimwa ili
kulisha silkworms (wadudu wa hariri) katika
sericulture (kilimo cha hawa wadudu) .
Katika dawa gamba la mzizi hutumika kama
dawa ya kuharisha na kwa tegu. Yakiliwa
kwa wingi, matunda yana nguvu ya
kukufanya uharishe na yanasaidia kwa
kikohozi. Yanatumika kuweka rangi katika
mvinyo.
128
6.33. Natrium Chloratum Chumvi ya mezani chemical formula: NaCl
Katika tropiki chumvi ni muhimu sana. Kama haipatikani, watu wanaoishi katika
maeneo ya ndani ya Afrika huzalisha chumvi mbadala; huchukua majivu ya kuni,
kuchemsha pamoja na maji, kuchujwa, na kisha kuchemsha maji yaliyochujwa
taratibu hadi vitu vyeupe vituane au kujiunda kwenye chombo.
1. Kama nutrient, mtu mzima huhitaji gram 4 za chumvi kwa siku.
2. Kama dawa hutumika:
a) Katika michanganyiko ya chumvi hutumika kama drip mahospitalini.
b) Chumvi ya madini ya joto (jinsi ya kutengeneza: tazama sura 4.5.D)
c) Kufunga majeraha na vidonda vya kuungua: Chumvi ina tabia ya kuponya:
A. Osha jeraha, ama kwa maji ya mpera yaliyopikwa au kwa mchanganyiko
wa maji ya chumvi (chumvi vijiko 2 vya chai au gram 9 kwa lita 1 ya maji
yaliyochemshwa).Kama jeraha au kuungua ni kidogo na hakuna usaha, asali
inaweza ikatumika kwa tiba (Tazama sura 6.30). Kama jeraha ni ndogo
lakini lina wadudu, fuata ushauri katika sura 5.5 mpapai. Kama jeraha ni
kubwa, mgonjwa anahitaji kusafirishwa kwenye kituo cha afya kilicho
karibu haraka iwezekanavyo.
B. Yeyusha chumvi vijiko 2 vya chai katika lita moja ya maji. Chemsha
kipande cha nguo, kitakachotumika kama bendeji, kwa dakika 20 katika
mchanganyiko huu wa maji na chumvi. Kikipoa, weka kitambaa kwenye
jeraha. Tunza jeraha likiwa na unyevu wakati wote kwa kutumia
mchanganyiko wa maji na chumvi. Rudia utengenezaji wa maji yenye
chumvi kila siku (Tazama pia sura za 6.30 asali na 5.5 mpapai).
Kwa majeraha ya kuungua, epuka dawa za mafuta (ointments). Ni bora
kumimina huu mchanganyiko wa maji na chumvi juu ya jeraha mara
kadhaa kwa siku. Kwa njia hii unaruhusu oksijeni kusafisha kidonda au
jeraha. Tumia chandarua kuzuia maambukizi ya jeraha kutoka kwa nzi.
Tazama pia sura 6.3 Aloe vera.
3. Kwa dawa za mifugo: Mpe gram 50 – 100 kama dawa ya kuongeza mkojo kwa
mifugo.
4. Kama dawa ya kuhifadhia: Kata vipande vidogovidogo vya nyama isiyo na mafuta
mengi au samaki ndogondogo iwezekanavyo, funika na kiwango kilekile cha
chumvi kwa saa 24. Kisha kausha ndani ya sun-box kwa siku 1-2 pamoja na maji
ya chumvi yaliyojitokeza. Tunza nyama iliyokaushwa au samaki kwenye chombo
kisichopitisha hewa. Chumvi inayoganda kutokana na maji ya chumvi ndani ya
sun-box inaweza ikatumika tena; mfano, kutengeneza matofali ya kulamba kwa
wanyama.
129
6.34. Nicotiana tabacum Tumbaku Familia: Solonaceae
Tumbaku ni mojawapo ya mmea
unaofahamika sana kwa kuwa na sumu kwa
wingi duniani. Hakuna mji mkuu wa nchi
hapa duniani, katika tropiki ambao hauna
kiwanda chake cha sigara. Lakini, tafadhali
jizuie kwa gharama yoyote ile majaribu ya
kuvuta sigara. Nicotine ina nguvu ya uraibu
(strongly addictive) na huongeza sana
uwezekano wa kuugua kansa ya mapafu na
matatizo ya njia ya hewa. Dawa
inayofahamika kwa wengi nchini VIETNAM;
majani huliwa kama dawa ya kusababisha
kuharisha na huko PHILIPPINES kama
kitulizo, ambapo dawa ya kutokosa
(mtokoso) kutokana na majani hutumika pia
kwa minyoo. Hata hivyo tunatoa onyo kali dhidi ya michanganyiko hii: Mtokoso
(decoction) wa sigara moja una nguvu ya kutosha kuua mtoto!
Hata hivyo, tunaweza tukanufaika kutokana na nguvu kubwa ya tumbaku kama
kiuatilifu (insecticide) (ingawaje majani ya mwarobaini ni bora kwa sababu yana
sumu kidogo, sura 5.3). Weka kama gram 10 za majani makavu ya tumbaku katika
lita moja ya maji kwa saa 12, chuja na nyunyizia
mboga zako kwa mchanganyiko huu (subira wiki 2
kabla ya kuvuna au mpaka mvua inyeshe). Wanyama
walioshambuliwa na wadudu wanatibiwa kwa kupaka
mchanganyiko huu huu kwenye sehemu iliyoathirika
ya ngozi, au rahisi zaidi sugua sehemu hiyo kwa
majani ya tumbaku. Weka majani kidogo kwenye
viota vya kuku, hasa pale wanaposhambuliwa sana na
viroboto; au badala yake tumia majani ya mwarobaini
au mkaratusi.
6.35. Ocimum basilicum Kurimbasi
Familia: Lamiaceae
Kimti kidogo, cha msimu, hukua karibu na nyumba,
una majani kama msumeno ncha zake, na yenye
harufu nzuri. KATIKA TROPIKI NA ULAYA.
Kurimbasi hutumika kama kiungo katika upishi.
DR. CONGO: Kwa homa na tumbo kujaa hewa
tayarisha dawa ya kumiminia maji (infusion) ya moto:
Mimina lita 1 ya maji ya moto kwenye gram 20 za
mmea mbichi, acha kwa dakika 5, kamua na kunywa
kidogo kidogo wakati wa siku.
130
6.36. Oryza sativa Mpunga Familia: Poaceae
Mmea huu unaweza kukua na kufikia meta
2.”Mpunga mkavu” unalimwa kwenye ardhi ya
kawaida, mfano, Cameroon na Uganda; “Mpunga
maji” hulimwa kwenye mashamba yaliyomwagiliwa
maji na kufunika (hasa Asia). Katika nchi za
mashariki ya Asia mpunga huchukuliwa kama dawa.
ASIA: Kutibu kuharisha kwa watu wazima: Punje za
mchele huokwa vizuri na kusagwa.
Kuharisha kwa watoto: Supu ya unga wa mchele
hufanya kazi vizuri kama hakuna sukari na chumvi ya
kutengenezea ORS.
KATIKA TROPIKI: Makapi ya Mchele ni dawa nzuri
ya kutibu upungufu wa vitamin B1 (beriberi).
Daima tumia mchele “brown” wa kienyeji kuliko
mchele mweupe.
6.37. Passiflora incarnata Matunda damu Familia: Passifloraceae
Passiflora coerulea hutumika pia. Aina zote hizi mbili zina matunda ya njano, saizi
ya mayai. Ni mmea unaotambaa na hufikia hadi urefu wa meta 10. Matunda yana
ladha ya kuvutia. Kwanza mmea huu ulilimwa na wakazi asilia wa America kusini
(wa Aztec), na kisha kusambazwa na wamisionari wa Kihispania. Pale
inapowezekana matunda damu yapandwe kwenye ua, ili ua wako uwe ni chanzo
kizuri cha vitamin! Yana kitulizo kinachoitwa maracugine. Katika maeneo ya
TROPIKI, mizizi inatumika kama dawa ya kuongeza mkojo, kiganja 1 cha mizizi
huchemshwa katika lita 1 ya maji kwa dakika 10, ambayo baadaye hunywa
kidogokidogo kwa siku nzima. Kwa pumu, majani makavu huvutwa kwa kutumia
kiko.
1. Kwa kukosa usingizi, hali ya wasiwasi
na spasms (cramps): Tengeneza tincture
kwa gram 10 za majani makavu ndani ya
ml 100 za kileo (70%). Matumizi yake
matone 30 mara 1 hadi kila siku.
2. Kwa cramps, hali ya wasiwasi, pumu na
kama kitulizo: chemsha kiganja 1 cha
majani machanga kwenye 0.7 ya lita ya
maji kwa dakika 10, kunywa kwa siku.
3. Kwa kukosa usingizi: Chemsha kiganja 1
cha majani, makavu au mabichi, kwenye
kikombe 1 cha maji kwa dakika 10,
chuja na kunywa wakati wa jioni.
131
4. Kwa upungufu wa Vitamin C, kula matunda kwa wingi kwa sababu yana vitamin
C kwa wingi.
6.38. Persea americana Avakado Familia: Lauraceae
Ni mti wenye urefu hadi meta 20. Matunda
yake yana mafuta ambayo ni muhimu kwa
matumizi ya binadamu kutumia kwa mkate;
nyamanyama yake ni bora zaidi kuliko
margarine ya kawaida, ambayo katika
maeneo ya tropiki huwa na madawa mengi ya
kuihifadhi. Ni tunda zuri kwa watu
wanaougua utapiamlo.
D.R. CONGO: Kwa kikohozi: Dawa ya
kutokosa huandaliwa kutokana na majani
machanga (kiganja 1 katika lita moja ya maji).
ASIA: Kwa kuharisha: Majani makavu yenye
kijani – nyeusi huchemshwa katika lita 1 ya
maji kwa dakika 15. Namna ya kutumia: kwa
watu wazima tumia majani gram 20, watoto
wakubwa gram10, na watoto wadogo gram 5. Dawa hii ya kutokosa itumiwe kidogo
kidogo kwa siku nzima (Ushauri: Tumia kwa pamoja na ORS, Tazama sura 4.5).
6.39. Phaseolus vulgaris Maharage Familia: Fabaceae
Mmea huu unapatikana karibu kila sehemu
duniani; kuna aina tofauti 500. Katika nchi
nyingine mbegu tu zinazoliwa, lakini Maharage
mabichi na maganda yake pia ni chakula chenye
thamani.
Matumizi: Kama dawa ya kuongeza mkojo, kwa
gout, maumivu ya kuvimba kwa viungo (baridi
yabisi), magonjwa ya figo na kama hatua ya
kusaidia kwa kisonono: Maharage yaliyo kwenye
maganda yaliyokaushwa (gram 10) hulowekwa
katika lita 1 ya maji usiku kucha, halafu
yanachemshwa baadaye yanachujwa. Kunywa
wakati wa mchana. Kwa wagonjwa wenye
kisukari tiba hii hupunguza kidogo kiwango cha
sukari katika damu. Maharage makavu,
yaliyosagwa yanatumika kama dawa kwenye
weeping eczema, na kama poda kwa mwili.
132
6.40. Piper guineense Kechu Familia: Piperaceae
Mmea unaotambaa katika
maeneo ya misitu ya
mvua ya tropiki. Matunda
makavu yaliyoiva
yanatumika kama kiungo
na kuongeza ladha ya
chakula. Kuna aina kama
700 za pilipili katika
tropiki.
D.R.CONGO: Kama
kiungo na kwa tumbo
linalouma . Kwa
kuvimbewa kinywaji
hutayarishwa, pamoja na Curcuma longa. Kwa maumivu ya mgongo na maumivu ya
kuvimba kwa viungo: Changanya kijiko kikubwa kimoja cha unga wa pilipili (kechu)
kwa kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya mbogamboga, na kisha, kwa dawa hii;
mchue mgonjwa kwa nguvu hapohapo.
AFRIKA: Kwa maumivu ya kuvimba kwa viungo na magonjwa ya zinaa dawa ya
kupika kutokana na mizizi hunywewa; kwa kikohozi dawa kutokosa (decoction)
hutengenezwa kutokana na majani.
6.41. Rauwolfia vomitora Kimusukulu – (Kikongo) Familia: Apocynaceae
Mti mdogo (meta 3 – 4) huota kandokando
ya vijiji na katika ardhi iliyolimwa na
haikupandwa. Matunda yake ni kama red
berries muundo wake. Wakati wa ukoloni
gamba la mzizi lilikuwa malighafi
iliyofahamika sana. Rauwolfia ina alkaloids
nyingi, na baadhi yake ni sumu. Kiwanda
cha madawa hutumia mmea huu kuzalisha
dawa za kitulizo na madawa kwa shinikizo
la damu la kupanda.
1. Poda (unga) ya Rauwolfia: Kupunguza
shinikizo la damu na kama kitulizo kwa
msukosuko, kupotewa akili na psychotic
crying.
Gamba kavu la mzizi lililotwangwa la
Rauwolfia vomitor (katika Asia
Rauwolfia serpentina).
133
Namna ya kutumia: Meza mg100 – 150 mara mbili kila siku. Kwa kuwa ni
vigumu kupima viwango hivi vidogovidogo sana, hospitali zinaweza zikafuata
mchanganyiko huu: Changanya gram 100 za unga wa Rauwolfia kwa gram 900 za
unga mwingine-huu unaweza kuwa maziwa ya unga, sukari, unga wa ngano wa
madukani, au unga wa mahindi mkavu uliochemshwa kidogo na kuanza
kubadilika kuwa brown na kisha kusagwa vizuri. Ni muhimu unga wa
kuchanganya ukawa na saizi ileile ya punje au unga uliyosagwa sawa na poda ya
Rauwolfia. Halafu jaza capsule yenye gram 1, au mifuko ya karatasi
uliyotengenezea nyumbani, kwa gram 1ya mchanganyiko huu. Watu wazima
watumie gram 1 ya mchanganyiko huu mara tatu kwa siku.
2. Upele (scabies) kwenye maeneo madogomadogo tu, mfano, katika mikono tu:
Sugua kwa majani mabichi sehemu iliyoathirika mara 3 kwa siku, kama ni lazima
pamoja na matone kidogo ya mafuta ya mbogamboga.
ATHARI: Ukizidisha dozi inaweza ikasababisha udhaifu wa misuli, wasiwasi na
huzuni (fadhaa). Kwa hiyo, dozi sahihi ni muhimu sana, na huhitaji uzoefu wa hali
ya juu katika matumizi yake. Hata kwa matumizi ya nje ni lazima itumike kwa
kiasi kidogo.
6.42. Ricinus communis Mbono Familia: Euphorbiaceae
Mbono ni mti wenye nguvu
ambao mara nyingi hupatikana
kwenye kifusi au ardhi
iliyolimwa bila kupandwa.
Baada ya kusiha, mti unaweza
kukua hadi kufikia meta 3 – 4,
kwa mwaka mmoja. Sehemu
zote za mmea zina sumu, na
mbegu zina ricin, protini ambayo
ni sumu kabisa. Mbegu
zilizosagwa, mizizi iliyosagwa
au majani mabichi vinatumika
kutibu magonjwa ya ngozi; Kwa
hiyo unaweza ukasugua majani
mabichi kwenye eneo
lililoathirika mara 3 kwa siku.
Mbegu zilizopandwa hadi kuwa
ujiuji kienyeji hutumika katika
majeraha kama dawa ya kuzuia
damu kuvuja na kusafisha jeraha.
Mbegu zisiliwe wala kutumiwa
kwa njia yoyote ile ya mdomo
kwa sababu ni sumu.
134
1. Mafuta ya mbono kwa matumizi ya ndani: Mafuta lazima yakamuliwe kutokana
na mbegu mbichi (cold seeds). Hii inaweza tu kufanyika kwa kutumia vifaa
vyenye pressure ya hali ya juu, kwa hiyo, mafuta lazima yanunuliwe kutoka
maduka ya dawa. Inatumika kimadawa;
a) Kama dawa ya kuharisha. Ina nguvu wakati kufungwa kwa choo kunapofikia
hali mbaya. Namna ya kutumia: Watu wazima; kijiko cha chai 1 hadi 2 mara
mbili kila siku. Watoto ½ hadi kijiko1 cha chai mara mbili kwa siku. Tumia
hadi uanze kuharisha.
b) Kwa matatizo ya kunywa mafuta ya taa, petrol au dizeli. Kwa hali kama hiyo,
kamwe usimtapishe kabisa mgonjwa; ni hatari sana. Namna ya kutumia ni
kama kwa aliyefunga choo, Tazama (a) juu.
2. Mafuta ya mbono kwa matumizi ya nje: Kwa matumizi ya nje, mafuta ya mbono
yanaweza yakatengenezwa nyumbani. Twanga vikombe viwili vya mbegu mbichi
kutokana na mbono lakini usitumie chungu kilekile unachotumia kutwanga
chakula! Hii huzalisha kikombe kimoja cha ujiuji kama peanut butter. Ongeza
kikombe kimoja cha maji na kikombe kimoja cha mafuta ya mbogamboga.
Koroga vyote pamoja katika sufuria, na chemsha kwa muda mrefu utakaofanya
maji yote kutoweka (hii huharibu kile kitu kinacholeta kuganda). Sasa kwa
uangalifu ongeza vikombe 10 vya maji, weka mfuniko kwenye sufuria na
chemsha kwa dakika 10 (hii huharibu sehemu kubwa ya ricin). Mimina kila kitu
ndani ya chupa yenye shingo nyembamba, na ongeza maji moto ya kutosha ili
kujaza chupa. Baada ya siku moja ondoa utando wa mafuta kwa kutumia sindano
(syringe). Mafuta haya yana 30% mafuta ya mbono, na yanaweza kutumiwa:
a) kwa ngozi na kwa usafi na ulinzi wa nywele
b) kwa ugonjwa wa ngozi wa aina ya Neuro-dermatitis.
c) pekee au pamoja na utomvu wa mapapai (sura 5.5) au Cassia alata majani
yake (sura 5.6) unatumika kutibu mba kwenye ngozi na ringworm.
3. INDIA: Mafuta ya mbono yanatengenezwa kama ifuatavyo:chemsha kg 2 za
mbegu katika lita 10 za maji kwa saa moja. Kamua mbegu kutumia 3KW (au
mashine ya kukamua mafuta ya mkono). Acha itulie kwa wiki 1, na kisha mimina
vizuri mafuta na tupa mabaki yaliyo magumu. Mafuta hutumika kwa ulinzi wa
ngozi na nywele na kwa viwango vidogo sana, kuhifadhi mbegu.
4. Kuhifadhi mbegu za mahindi au maharage (hii ina maana kwa mbegu za kupanda
tu), twanga kiganja 1 cha mbegu za mbono, na changanya na kg. 20 za mbegu za
mahindi au maharage.
5. Kwa sababu mbegu za mbono zina sumu kali, unaweza kuzitumia kama sumu ya
panya. Changanya kipimo1 cha karanga kwa kipimo1 cha mbegu za mbono,
twanga pamoja, na weka mchanganyiko huu pale ambako panya hutembelea au
hukaa. TAHADHARI: Weka mbali sana na watoto, na wanyama wengine wote
kama vile kuku au ndege, watakufa wote kama watakula mchanganyiko huu.
135
6.43. Sesamum indicum Ntungo Familia:
Pedaliaceae
Mmea mrefu sm 50 hadi 80, majani marefu
yenye meno meno, kama msumeno, maua
meupe, au yakiwa na madoa ya njano na
zambarau. Tunda ni kama sm 2.5 urefu. Mbegu
zake maarufu kama chakula.
D. R. CONGO: Kinywaji kutokana na majani
kinatumika kwa wagumba wa kiume na wa
kike.
ASIA: Kwa waliofunga choo: Meza vijiko 3
vya chai vya mafuta yake. Kwa maumivu ya
kuvimba kwa viungo, gram 20 za majani
makavu huchemshwa katika 0.7 ya lita ya maji,
kuchujwa na kunywewa kwa siku moja.
6.44. Tagetes erecta Tururu Familia: Asteraceae
Mmea wa mapambo, una asili ya Mexico,
umeenea maeneo yote ya tropiki na Ulaya.
Maua na majani yana harufu ya kipekee.
KIULIMWENGU: Mafuta yake muhimu
hupunguza shinikizo la damu (B.P) na kupanua
bronchia; vile vile yana anti-spasmodic, anti-
inflammatory na sedative effects. Majani
hufanya kazi kama dawa ya kuongeza mkojo
na kuongeza transpiration. Siku hizi
yanatumiwa katika uzalishaji wa manukato ya
biashara. Mbegu zake zina uwezo wa kuua
minyoo na pia kama dawa ya kuharisha. Mmea
wote una nguvu ya kuua nematodes (minyoo
wenye madhara waishio udongoni, ugonjwa wa
kawaida katika nchi za tropiki). Inashauriwa
kusiha tururu bustanini mwisho wa msimu wa
mvua!
ASIA:
1. Kwa kikohozi, bronchitis, kuumwa jino, hedhi isiyo na utaratibu: Mimina
vikombe 2 vya maji ya moto kwenye gram 10 za majani makavu, acha itulie kwa
dakika 20, kamua , kunywa kikombe 1 asubuhi na jioni.
2. Kwa magonjwa ya macho: compress iliyolowanishwa na mchanganyiko huu
hutumika.
136
3. Kwa Kifaduro: Mimea 0.7 lita ya maji ya moto kwenye maua 15, mabichi au
makavu, na kunywa kidogokidogo wakati wa siku moja.
4. Suppurating mammary gland, majipu: Chukua kiganja 1 cha maua kwa kijiko
kimoja cha chai cha chumvi na chemsha kwenye ½ kikombe cha maji. Weka
compress iliyolowanishwa na mchanganyiko huu.
6.45. Tamarindus indica Ukwaju Familia: Caesalpiniaceae
Ni mti mzuri unaovumilia ukame
wenye matawi ya kusambaa, gamba
lake ni grey-black na lina vilima na
vibonde, majani ni kijani isiyokolea
(yenye jozi
9 hadi 12 za vijani). Wakati wa mvua,
maua ni kijivu – njano na yanakuwa
red-veined na hufuatwa na matunda ya
kahawia, yenye mbegu za umbo la figo
ndani ya nyamanyama ya kahawia.
Matunda yana vitamin C kwa wingi, na
huliwa bila kupikwa au kutengeneza
kinywaji. ASIA na AFRIKA: Matunda
mabichi au yaliyokaushwa hutumika
kuongeza uchachu kama limau, juisi au
siki, katika samaki.
Baada ya kuondoa gamba la juu, mbegu
zinaweza zikaliwa hivyo au kuokwa.
Zinaweza zikatumika kutengeneza aina
fulani ya unga, na kama chakula cha
wanyama. Mafuta ya mbegu yanaweza
yakatumika kwenye sabuni.
Mti huu una mfumo wa mizizi uliosambaa na mpana na hivyo ni mzuri kwa kuzuia
mmomonyoko wa udongo. Japokuwa mti una naitrogen, hudondosha majani yenye
tindikali (acid), kwa hiyo siyo mzuri kwa mchanganyiko wa mazao (inter-cropping).
Mbao hutumika kutengeneza mitumbwi, samani, michi na vinu, nguzo za uzio, na
mkaa.
Kimadawa, matunda huliwa kwa waliofunga choo, na hutumika kupunguza homa,
kuponya magonjwa ya kwenye utumbo, kutibu pumu, kuondoa kichefuchefu kwa
wajawazito, na kama kitu kinachowekwa katika dawa kutibu matatizo ya moyo na
kupunguza sukari katika damu. Hutumika kwa nje kama dawa ya kukausha kwa
magonjwa ya ngozi.
137
6.46 Tephrosia vogelii Mbaazi Familia: Papilionaceae
Ki-mti urefu meta 1 – 2, hupatikana vijijini
katika nchi za tropiki. Una rotenone (kitu
ambacho ni chepesi kuhisi joto), kwa hiyo
majani ni lazima yakaushwe kivulini.
Hutumika katika ua kuzuia mmonyoko wa
ardhi. Ng’ombe na Mbuzi huwa hawali miti hii.
D. R. CONGO: Gamba la mzizi husagwa,
huchanganywa na pilipili kichaa na kutumiwa
kwa meno yanayouma.
NCHI ZA TROPIKI: Hutumika kinyume cha
sheria kuwapoozesha samaki ili kurahisisha
uvuaji wake. Mbaazi ina nguvu ya kutibu upele
(scabies): Sugua ngozi kwa majani. Mbaazi
vilevile hutumika kutengeneza kiuatilifu
(insecticide): tayarisha kwa kuloweka kg. 1 ya
majani mabichi yaliyopondwapondwa kwenye
lita 10 za maji kwa saa 8. Acha wiki mbili
zipite kabla ya kuvuna mazao uliyonyunyizia
dawa.
Kutengeneza kiuatilifu cha unga (insecticidal powder) kausha majani yaliyokomaa,
yatwange na yachekeche. Ama peke yake au pamoja na pilipili kichaa ya unga
inaweza ikatumika ndani ya nyumba kufukuza wadudu, lakini tunza vizuri
wasikofika watoto! Gram 100 za majani yaliyokaushwa ya mbaazi huchanganywa na
kg. 50 za mahindi kuyalinda dhidi ya wadudu kwa kipindi cha miezi mitatu. Osha
mahindi kabla ya kuyatumia.
6.47 Tithonia diversifolia Familia:
Asteraceae
Mmea huu huboresha udongo
ulioharibika, na ni wa manufaa zaidi
ambako mmomonyoko wa ardhi
umetokea. Ni mbolea nzuri (green
manure) kwa ardhi yenye upungufu
wa naitrojeni. Hutumika kujenga ua ili
kuzuia mmomonyoko wa ardhi! Hata
hivyo mmea huu ukipandwa ni
vigumu tena kuondoa, hivyo panda
kuzunguka shamba sio shambani .
Kisha fukia matawi yaliyokatwa
kwenye ardhi utakayopanda mazao
yako, ukihakikisha kwamba matawi
138
hayana mbegu, na panda mazao yako haraka iwezekanavyo.
AFRIKA MASHARIKI: Chai iliyotengenezwa kwa majani inatumika kutibu
maumivu ya tumbo na ini, na maumivu ya tumbo wakati wa ujauzito: “Decotion” ya
kutumia nusu au jani moja hutumika kwa siku. D. R. CONGO: Chai iliyotengenezwa
kutokana na majani inatumika kutibu “bacillary dysentery.” Majani yaliyotwangwa
yanatumika kwa dermatitis na ngozi inayowasha.
6.48 Vernonia amygdalina Mtukutu Familiae: Asteraceae
Mti unaokua haraka, meta 3 – 8 urefu, rangi ya majani nyeupe kuelekea bluu kidogo.
Unaweza mti huu ukasambazwa kwa urahisi kwa kutumia vipande vya miti.
UGANDA: Wenyeji huchemsha majani mara 3 kwenye maji na kisha kuyala kama
mchicha. Mmea huu wa muhimu ingawaje mchungu sana hutumika nchini Uganda
kutibu malaria. Baadhi ya wauguzi walituambia kwamba wanapendelea sana kutumia
mtukutu ukilinganisha na quinine au chloroquine kwa sababu wagonjwa wanapata
madhara kidogo (tunaweza tukathibitisha hili).
Tunapendekeza mchanganyiko
ufuatao kwa malaria: chemsha kiganja
1 cha majani au, kwa chai yenye
nguvu, kiganja 1 (gram 15) za gamba
kavu la mzizi, katika lita moja ya maji
kwa dakika 20; chuja na kunywa kwa
siku nzima.
Kwa mjibu wa tiba, mmea huu pia
una nguvu ya kutibu surua, kisukari,
pumu, kuharisha, kifua kikuu, malale,
aina fulani za kansa, minyoo, na
kufunga choo. Wanyama nao hutumia
mtukutu kwa kichocho
(schistosomiasis), matatizo ya
tumboni na parasites.
Kama kwa Mwarobaini (sura 5.3) na
melai (sura 6.31), Vernonia
amygdalina inaweza ikatumika katika
kilimo kuua “nematodes” na majani
kwa kuhifadhi chakula.
NIGERIA : Kutafuna matawi machanga ya mtukutu huzuia meno kuoza. Majimaji ya
majani ya mtukutu yana nguvu ya anti-oxidizing; kwa hiyo unaweza kuwa dawa ya
kuhifadhi ya ki-asili (Natural preservative) ambayo inaweza kuzuia dawa kuchacha.
ATHARI: Mmea una cytotoxic mbili, vernodalin na vernomygdin. Mmea huu wa
kufaa sana huenda ukawa na athari, lakini bado, kumekuwa na utafiti mdogo juu ya
somo hili.
139
6.49 Vinca rosea (syn. Catharanthus roseus) Vinka Familiae: Apocynaceae
Mmea mfupi kadri ya sm 60 urefu. Maua ni meupe na pinki na yana petali 5, kila jani
linaelekea upande wake. Una sumu! Kwa hiyo utumiwe wakati wa hali mbaya tu.
Hupandwa hasa kama mmea wa mapambo, husitawi vizuri kwenye mchanga.
Unaweza ukasambazwa kwa mbegu au vitawi ambavyo havijatoa maua. Majani
yavunwe kabla au wakati mmea unapotoa maua.
Nchini SENEGAL, MALI NA TOGO mmea wote
unatumika kwa kuzuia kuharisha; visiwa vya
COMORO kwa kisonono, NIGER kwa hepatitis,
nchini PHILLIPINES kwa bacterial dysentery.
Katika British pharmacopoeia chai
iliyotengenezwa kwa majani imesajiliwa kama
dawa ya kisukari. Zaidi ya kipindi cha miaka 15,
Vinca rosea imekuwa ikifanyiwa utafiti kuliko
mmea mwingine wa dawa wowote kwa sababu una
aina tofauti 65 za alkaloids. Maisha ya maelfu ya
watoto wanaougua kansa ya damu yamekwisha
okolewa kwa sababu alkaloids 2 ( vincristine na
vinbalastine) zimethibitisha kuwa na uwezo wa
kushambulia aina hii ya kansa kwa watoto.
MATUMIZI ULIMWENGUNI KOTE:
1. Kisukari: Weka gram 5 za majani makavu au
kiganja 1 (kiasi ambacho mgonjwa anaweza
kukuficha kiganjani) cha majani mabichi katika lita 1 ya maji ya moto, chemsha
kidogo kwa dakika 15. Chuja na kunywa kidogokidogo kwa siku moja. Mkojo na
damu ni lazima vipimwe katika kituo cha afya mara kwa mara.
2. Shinikizo la damu: Kausha mizizi ya mti, menya gambalake na twanga gamba
hilo. Chukua kijiko 1 cha chai na chemsha pamoja na vikombe 2 vya maji kwa
dakika 10, chuja na kunywa wakati wa asubuhi au kabla ya kula.
3. Bacillary dysentery
a) Tayarisha mchanganyiko namba 1 kila siku. Mmissionari kutoka Hant – D. R.
Congo alitutaarifu kwamba, wakati wa mlipuko wa bacillary dysentery
ambayo iligoma kupona (ilikuwa sugu) kwa antibiotic, kwa kutumia
mchanganyiko huu, aliweza kuokoa kadri ya asilimia 50% ya watoto
waliougua, ilikuwa na maana maisha ya mamia ya watoto katika eneo hilo
pekee.
b) Tumia mchanganiko wa chai hiyo na chai ya ameba (mziwaziwa na majani ya
mpera – taz. Sura 5.11) kutibu ameba.
4. Kansa: Kama hakuna dawa nyingine (tu!) inayoweza patikana, jaribu
mchanganyiko namba 1. Unaweza kuongeza msubili na mapapai mabichi katika
chai. Kwa nje, tumia kinachoonyesha kuwa na manufaa; kufunga vidonda kwa
msubili, au papai bichi; au kukamulia majani ya vinka yaliyochemshwa kidogo na
ikapondwa pondwa.
140
ATHARI:
Inapotumiwa kwa kipindi kirefu, shinikizo la damu (blood pressure) linaweza kuwa
la chini na maumivu ya tumbo yanaweza kutokea. Vinka isitumiwe kabisa na
wanawake wajawazito, na matumizi yake kamwe yasiwe ya muda mrefu. Kama
madawa mengine yote ya kansa, Vinca rosea yenyewe inaweza ikakuletea kansa.
6.50 Zea mays Mahindi Familia: Poaceae
Mahindi kiasili yalitoka Amerika ya kusini. Sehemu muhimu zaidi ya mmea ni
nywele za mhindi. Nywelenywele hukusanywa kabla ya mbelewele wakati mmea una
maua. Yaweke kivulini na uyaache yakauke
upesi. Yana alkaloid allantoin, na anodyne
(pain-soothing = kutuliza maumivu) ambayo
nguvu yake kwa magonjwa ya kibofu cha
nyongo imethibitishwa.
UFARANSA.: Nywele za mahindi zinatumika
kwa kuongeza mkojo.
GUINEA, ULAYA NA MAREKENI:
Inatumika kwa magonjwa ya njia ya mkojo.
ANGOLA: Kama dawa ya kuongeza mkojo;
ASIA: Kama tiba ya kisukari, oedema na
shinikizo la juu la damu.
1. Kisukari: Chukua gram 15 nywele nywele
kavu za mahindi na chemsha katika lita 1
ya maji kwa dakika 5. Kunywa
kidogokidogo kwa siku nzima.
DOKEZO: Fuata masharti ya milo kwa
kisukari: Punguza matumizi ya chumvi na
usitumie kabisa sukari katika milo ya kila
siku. Changanya na mmea mingine ambayo husaidia kupunguza kiwango cha
sukari katika damu, k.m. kitunguu maji (6.2) au green bean (6.39) (aina ya
maharaghe ambayo inaliwa na maganda yake).
2. Magonjwa ya figo, oedema, shinikizo la damu, na mawe ya figo: Fuata
mchanganyiko kwa ajili ya kisukari. Unaweza ukanywa chai hii kwa zaidi ya
miezi 6 bila kutokea madhara yoyote.
DOKEZO: Kwa vile nywelenywele za mahindi mara nyingine hazipatikana unaweza
kutumia gunzi yake badala yake. Kwa vile nguvu yake ni chini kuliko nywelenywele,
tumia gunzi gr 100 badala ya gr 15 za nywelenywele.
Hakuna madhara yanayofahamika, lakini yakitumiwa kwa muda mrefu lazima
kuchunguzwa katika kituo cha Afya mara kwa mara. Ni muhimu zaidi hasa kwa
wenye kisukari na shinikizo la juu la damu.
141
SURA YA 7
7.1. KATIKA FAMILIA
“Tusiibadili miili yetu kuwa ghala la madawa”
1. Kula vizuri!
Chakula chetu kiwe dawa yetu! Vyakula bora vinajenga nguvu na mfumo wa kinga
ya mwili; ina maana kwamba uwezo wa kupambana na kuzuia maambukizi na
magonjwa unaongezeka. Vyakula visivyo bora hupelekea kupungukiwa lishe, na
kusababisha urahisi wa kuambukizwa magonjwa.
AINA MUHIMU ZA VYAKULA
Kwa kupata nishati
(energy) kirahisi
Mizizi yenye wanga: Mihogo, viazi, taro
Matunda yenye wanga: ndizi, ndizi kuu, mfenesi.
Kwa nishati na protini
bora
Nafaka na mbegu: Ngano, mahindi, mchele,
mawele, mtama
Mkate: Ngano isiyokobolewa ni bora zaidi ukitumia
kuliko mkate wa ngano iliyokobolewa! Viazi
mviringo na viazi vitamu vyote vina protein.
Vyakula vya kushibisha Mbegu za mafuta: boga, tikiti maji, ufuta, alizeti.
Jamii ya kunde: Maharage, karanga, soya, dengu.
Vyenye gamba: Njugu mawe, korosho, kungu
Wanyama: Maziwa, mayai, jibini, samaki, kuku,
nyama yoyote.
Vyakula vyenye wingi
wa virutubisho
Mbogamboga: majani ya mihogo, viazi vitamu na
majani yake, nyanya, karots, mboga, majani
ya Mlonge n.k.
Matunda: Maembe, machungwa, malimau, mapapi,
mapera, passion fruits n.k.
Juisi ya matunda
Kwa ajili ya kinga ya
mwili iliyo imara
Kula vitunguu swaumu vilivyo vibichi
Lima mwenyewe matunda na mbogamboga! Panda miti ya matunda na miti mingine
– maembe, papai, nanasi, migomba, n.k. Panda mlongelonge na kula majani yake.
Watoto wanatakiwa kulishwa mara kadhaa kwa siku kwa chakula cha aina
mbalimbali. Wanahitaji kiasi kidogo kwa mara nyingi. Kama, kwa mfano, wakila
mtama au mihogo tu, watadhurika kwa sababu haitakidhi haja yao ya protini, nguvu,
vitamin na madini. Kunywa maji ya matunda asili – Afrika ina aina nyingi na nzuri
za matunda! Soda na vinywaji vingine vya biashara vina kila aina ya mchanganyiko
DOKEZO KWA FAMILIA, WAFANYAKAZI WA
AFYA NA HOSPITALI
142
na vikolezo vya utamu usio wa asili ambao hauna faida kwa afya yako. Vyakula vya
viwandani vina aina za mafuta na madawa ya kuvitunza vyenye kuleta magonjwa.
Kama kwa vyovyote inawezekana wanyonyesheni watoto wenu kwa maziwa ya
titi la mama – usijaribiwe na matangazo ya ki-biashara ya maziwa ya chupa. Watoto
wanakunywa uchafu na maambukizi kupitia chupa hizo – ambayo husababisha
kuharisha na magonjwa mengine. Jitahidi kujiepusha na vyakula vya watoto vya ki-
biashara vinaharibu tu hali ya uchumi ya kifamilia.
2. Uchumi mzuri wa nyumbani
Kama wewe na familia yako mnazidi kukonda huenda ukawa unasumbuliwa na
magonjwa kama minyoo na kifua kikuu. Lakini mnaweza pia kuwa mnasumbuliwa
na “ugonjwa” mwingine unaoitwa “hali mbaya ya uchumi nyumbani”.
Kwa mfano, kijijini unatakiwa kuuza kilo 20 za karanga zenye maganda ili
kununua kilo 1 ya maziwa ya unga kiwango cha protini katika vitu hivyo viwili viko
sawa, kwa kufuata uzito, iko sawasawa kabisa (270g protein katika kilo 1). Mtu
mzima anaweza kuishi siku 46 kwa kilo 20 za karanga lakini akaishi siku 2 tu kwa
kilo moja ya maziwa ya unga!
Mifano mingine zaidi:
- Unauza machungwa yenye vitamin C nyingi ili kununua chupa ya soda,
ambayo imetengenezwa kwa maji, sukari, na rangi tu.
- Unauza ndizi, ambazo kwa kweli zina vikombe 3 vya sukari ya asili (ilifichika)
ili kununua kikombe kimoja cha sukari dukani.
- Huwezi kupata asali ya kutengenezea, maji chumvi kwa sababu baba
ameitumia yote kutengenezea pombe.
- Kijana anayesoma sekondari hudhani kuwa ana elimu kubwa kiasi kwamba
hawezi kumsaidia mama yake kulima, hata wakati wa likizo. Mwili wa mama
uliofanya kazi zaidi ya uwezo wake hauwezi kutoa maziwa ya kumtosha mtoto
wake; mtoto ataugua itambidi baba auze gunia la karanga lililo salia ili kulipia
gharama za matibabu. Njaa inaanza kuingia kijijini.
Je, umeelewa sasa, kuwa “vitu vyenye kuvutia” havitasaidia familia yako?
3. Chunga maji yako!
Hakikisha maji unayokunywa ni safi. Kutokana na ubora wa maji yako, unaweza
kujenga chujio la mchanga, au unaweza kutumia mbegu za Moringa zilizosagwa
kama ilivyoelezwa katika sura 5:13. Kuchemsha maji, hata katika jiko la jua ndiyo
njia bora zaidi.
Kama watu wakiosha nguo zao, au hata baiskeli na magari, katika maji ambayo
wengine wanayatumia kunywa, basi wanasababisha matatizo!
4. Hifadhi ardhi yako katika ubora na rutuba ya asili.
a) Panda mimea jamii ya mikunde (ambayo kwa asili huweka naitrojeni ardhini).
Mimea jamii ya mikunde ni pamoja na mboga kama maharage na jamii za
Karanga, na miti kama Leucena. Leucena inaweza kupandwa katika kontua ili
kuzuia mmomonyoko wa udongo na kukatwa wakati wote ili kutengeneza ua.
Matawi yanayokatwa yanasaidia kurutubisha ardhi.
143
b) Tengeneza mboji kwa kutumia vitu vyote vyenye asili ya wanyama na mimea.
Maganda ya matunda, majani ya mboga, masalio ya shambani – (lakini epuka
mbegu za magugu). Vinyesi vya kuku na wanyama vitunzwe (siyo karibu sana na
nyumba). Kama vikihifadhiwa katika hali ya uvuguvugu na unyevu, ardhi nyeusi
itapatikana baada ya miezi mitatu, ambayo ikichanganywa katika shamba lako,
kwa taratibu itaingiza virutubisho (naitrojeni na madini) ardhini.
c) Epuka utumiaji wa kemikali za kilimo. Usitumie kabisa, au tumia kiasi kidogo
sana cha mbolea za viwandani au madawa ya kuua wadudu. Vinaharibu maji,
vinaua maisha ya mimea na wanyama visivyo na madhara (mara nyingine vyenye
faida), na kudhuru rutuba ya asili ya ardhi.
5. Vyoo vya kienyeji ni visafi na vinafanya kazi . Vinyesi na mkojo vinabeba maambukizi mengi; chimba shimo, jenga nyumba juu
yake. Shimo lifunikwe muda wote. Weka bomba la hewa chafu; yaani bomba
lisimamishwe (lizibwe juu kwa waya wa mbu) ambalo huchukua hewa chafu kutoka
kwenye shimo, kupitia kwenye sakafu na paa hadi kwenye hewa safi ya nje. Hapo
haitanuka. Shimo likijaa fukia kwa udongo na panda mwembe! Kisha tengeneza tena
choo cha kienyeji kwenye eneo jingine. Kwa kweli vyoo vya kienyeji ni bora kuliko
vyoo vya maji; vinatunza virutubisho kwa upandaji wa baadaye, wakati ambapo vyoo
vya maji vinasababisha uchafuzi wa mito na vijito. Pia vinatumia maji ambayo katika
sehemu nyingi ni mali adimu. Choo kisafi cha kienyeji ni bora mara 1,000 ya vile
vinavyoitwa vyoo vya maji vya kisasa ambavyo ni vichafu kwa ukosefu wa maji!!
6. Utupaji makini wa takataka!
“Mioto ya milele” ambayo mara chache huzima na ambamo taka zote hutupwa, ni
hatari kwa afya. Na haipendezi. Kama vitu fulani, mfano PVC na aluminium
vikichomwa kwa pamoja kwa moto kidogo hewa yenye sumu kali sana iitwayo
dioxins inatokea. Pia, taka zisiachwe kuzagaa ovyo. Vinatoa picha mbaya, vitu
vyenye ncha kali vinaweza kutukata; beteri na vifaa vingine vya umeme vina sumu
na maji ya mvua hujikusanya katika vitu, matairi yaliyozeeka na kutengeneza sehemu
za kuzaliana kwa mbu wa malaria.
a) Matairi, vioo, plastiki, betari kama kuna namna yoyote ya kuvitumia tena au
kuvitengeneza upya vitu hivi fanya hivyo. Kama sivyo, vikusanye pamoja na kila
mwezi uvizike chini sana ardhini; betri zina sumu zaidi. Usipande mboga juu ya
mahali ulipovizika!
b) Karatasi: vikusanye kwa pamoja kwa juma moja kisha kila Jumamosi uzichome
mchana kwa muda mfupi kama dakika 5 hivi. Zika majivu pamoja na plastiki
n.k.
c) Mbao: Zichomwe na upeleke majivu shambani; yana madini.
d) Taka za mimea na wanyama: Ziozeshe utengeneze mboji.
7. Usafi:
Mila ya kiafrika ya kuosha mikono kwa maji na sabuni wakati wote kabla ya kula au
kutayarisha chakula, na baada ya kutoka chooni ni ya muhimu na bora zaidi. Kama
huna sabuni jitengenezee kwa kutumia majani ya mipapai.
144
Kuoga mwili mzima kuanzia kichwani hadi kwenye vidole vya miguu kila jioni
hufanya mwili na kitanda vikae safi.
8. Usafi wa mdomo na meno Kuoza kwa meno siyo tena ugonjwa wa Wazungu. Bali katika nchi za tropiki pia hasa
katika miji mikubwa, watu wengi zaidi wanahangaika na kuoza meno. Soda nyingi
wanazopewa kila mgeni bure ndizo za kulaumu kwa sehemu kubwa. Matunda mazuri
zaidi ya asili na maji ya matunda halisi hayasababishi matatizo kama hayo!
Kuongezeka kwa kiwango cha ulaji wa mikate mieupe pia huchangia kuongezeka
kwa tatizo la kuoza kwa meno. Wakati ambapo mihogo ni rahisi kwa meno, kwa
sababu wanga wa mihogo haubadilishwi na mate kuwa sukari kwa urahisi.
Kama una bahati ya kuishi vijijini, unaweza kuendelea kutumia baadhi ya matawi
(kama mwarobaini, angalia sura 5.3) kwa usafi wa meno. Kama unaishi mjini, tumia
mswaki wako kila baada ya kila mlo, hasa jioni; kama hakuna dawa ya meno usihofu,
kwa sababu jambo kubwa ni usafishaji wa meno, kupiga mswaki.
Badala ya dawa ya meno, unaweza kutumia kiasi kidogo cha chumvi au unaweka
kipande kidogo sana cha sabuni ya jibini (uliyojitengenezea) au sabuni yoyote nzuri
(angalia sura 4) kwenye mswaki wako. Itenge hiyo sabuni kwa kazi hiyo tu. Unaweza
pia kutumia poda ya meno, angalia sura 4.5.
9. Kwa upishi wa ndani, weka dohani! Kama mara nyingi uko katika chumba kilichojaa moshi, uko kwenye hatari kubwa ya
kupata matatizo makubwa ya macho na mapafu. Suluhisho bora kabisa la tatizo ni
kujenga jiko lenye kubana matumizi ya nishati (yaani kutumia kuni chache zaidi)
pamoja na dohani ili kwamba moshi wote utoke nje.
10. Mazoezi na uimara wa mwili.
Watu wengine wana shughuli nyingi zaidi, mfano mwanamke atakiwaye kutembea
kilomita nyingi kwa siku ili kutafuta kuni na maji; wengine wana shughuli ndogo
zaidi. Fanya maamuzi yako mwenyewe kutazama kama familia yako “imeendelea”
au “haijaendelea”! Katika familia “zilizoendelea” mwanamke na mwanamme
wanashirikiana shughuli, kwa hiyo wana mazoezi ya aina moja. Kwa jinsi hii
mwanamke hawi mwembamba na dhaifu zaidi, wala mwanamme hanenepi sana.!
Tunapokuwa imara tunakuwa na kinga ya mwili dhidi ya maradhi.
11. Epuka magonjwa yaambukizwayo kwa ngono na UKIMWI.
Hakuna uhakika kuwa kuna mmea wowote usio na sumu unaoweza kutibu kaswende
au maradhi mengine ya ngono, lakini mimea fulani inaweza kutumika kutuliza dalili
fulani (kama vile kuwashwa). Antibayotiki lazima zitumike, kama hali ya uchumi
inaruhusu. Tumetembelea mbilikimo ambao wamefanikiwa kutibu magonjwa ya
ngono (hata yaliyo sugu kwa antibayotiki) kwa kutumia mimea ya madawa, lakini
kwa uwezekano wa kumdhuru kwa sumu mgonjwa. Kwa dhati kabisa tunawashauri
mtumie njia yoyote ya tiba isiyo na madhara (ya kisasa au ya jadi) iliyochunguzwa
katika maabara.
UKIMWI: Hakuna njia ya kisasa au ya jadi iwezayo kuponya UKIMWI. Ni juu
yako kujiepusha na UKIMWI au maambukizi mengine mabaya.
1. Uwe mwaminifu kwa mwenzako.
145
2. Usitibiwe na “manesi wanaosafiri” (wazururao na kuchoma sindano na kuathiri
watu).
3. Hakikisha nesi hamchanji mtoto wako kwa sindano ile ile au bomba lililokwisha
tumiwa kwa mtoto mwingine (kuna hatari ya maambukizo kama sindano haiku
chemshwa).
4. Zuia upungufu wa damu mwilini ili kuepuka kuongezwa damu wakati wa kuugua,
baada ya ajali au wakati wa kuzaa.
7.2. WATUMISHI WA AFYA KIJIJINI
Kwa kawaida kituo kimoja cha afya au zahanati kinahudumia vijiji 20 – 30 kwenye
haya maeneo ya jirani. Kwa kufikiria bila uhakika, katika kila moja ya vijiji hivi,
kuna mwanamme mmoja (Mhudumu wa afya) na mwanamke mmoja (mkunga wa
jadi) wanaofanya kazi kwa kujitolea (!) ili kuboresha hali ya afya kijijini kwao.
Vifaa vya Mhudumu wa Afya kama huyo ni: Vitambaa vya kufungia, aspirin,
chloroquine (kwa malaria), mebendazole (kwa minyoo), iodine au dawa nyingine za
kusafishia. Wahudumu wa afya wanatakiwa kuwa na ufahamu mkubwa wa madawa
ya kienyeji, na pia wawe na ruhusa ya kuyatumia kwa namna ya kuwajibika. Ifuatayo
ni mifano ya jinsi Mhudumu wa afya wa kijiji anavyoweza kutumia madawa ya asili:
a) Kusafisha vidonda na uvimbe kwa kutumia papai, asali, sukari, au Aloe Vera.
b) Kutumia chai za dawa, angalia sura 4.2.
c) Kuzuia na kutibu kuharisha kwa watoto kwa kuwaonyesha wazazi jinsi ya
kutayarisha maji yenye mchanganyiko wa sukari na chumvi kwa kutumia chombo
cha chumvi, chombo cha sukari na kikombe.
d) Kuwafundisha watoto juu ya njia ya maisha yenye afya , kwa kushirikiana
kutundika matangazo mfano juu ya “Afya” au “Kamwe usitumie sabuni za kuzuia
vijidudu!” (Kwa sababu, katika eneo la tropiki sabuni hizi zina 1 – 3% ya zebaki).
e) Kwa kuwa na bustani ya madawa na kuitumia kwa juhudi zote! Hii inaweza
kutumika kama sehemu ya kufundishia na kama sehemu ya kuzalishia wakati
wote malighafi ya madawa.
7.3. KITUO CHA AFYA
Tafsiri potofu ya dispensary (zahanati): Neno dispensary mara nyingi limeeleweka
vibaya. Linatokana na neno la kilatini “dispensere” likimaanisha kugawanya,
kugawia watu, kutoa msaada, kunywesha. Kwa hiyo hii mara moja inatoa tafsiri isiyo
yenyewe. Yaani ya nyumba ambayo madawa (mara nyingi kutoka nchi za nje)
hugawiwa au kutolewa kwa msaada. Nimeona zahanati nyingi ambapo wagonjwa
wanashughulikiwa kama ofisini: – Mafile yanashughulikiwa zaidi kuliko waki
wenyewe. Nesi mmoja alinionyesha dispensary (zahanati yake) iliyojengwa kwa
namna hiyo: “….hapa katika chumba cha kwanza wagonjwa wanachunguzwa, cha
pili analipia, cha tatu wanadungwa sindano kisha wanatoka kwa mlango wa
nyuma….”.
Wazo potofu juu ya sindano. Sisi Wazungu tumefanya nini katika nchi za tropiki?
Sindano imekuwa na maana sawa na madawa bora ya kimagharibi, tiba bora (ya kiasi
146
chochote) kama hakikisho la kupona haraka. Sasa ni juu ya manesi kupambana na
imani isiyo ya kweli juu ya nguvu ya sindano. Sindano zitolewe tu kama mgonjwa
hajitambui, au kama dawa haipatikani katika hali ya vidonge, au kama suppositories
(mfano chanjo).
Wazo potofu kwamba homa ni ugonjwa: Utoaji wa aspirin ni wa kawaida kabisa
katika vituo vya afya vya kawaida hapa Afrika. Madawa kama aspirin, metamizol au
Paracetamol yanaweza kutuliza dalili za magonjwa (maumivu ya kichwa, homa)
lakini kamwe hayawezi kutibu ugonjwa (aspirin hata siku moja haiwezi kuua vimelea
au vijidudu).
Homa siyo ugonjwa lakini kinyume chake, ni zawadi toka kwa Mungu! Homa
hutuelekeza kujali kuhusu kudhurika kwa mfumo fulani katika uhai wetu, kisha
kutulazimisha kupumzika. Unaweza kulinganisha homa na mwanga mdogo
mwekundu kwenye gari unaoashiria kwa kumaanisha “simama,” kuna tatizo katika
gari!”. Unadhani dereva anaye haribu taa hii ndogo nyekundu kwa nyundo atafurahia
gari lake kwa muda mrefu? Hakika siyo kweli. Lakini mfano huu ni kioo
kinachotuonyesha tabia yetu ya kunywa aspirin kila mara na dawa nyingine kisha
tunaendelea na maisha kama kawaida.
Leo tunajua kuwa homa siyo ishara pekee iliyo nzuri, ishara ya hali ya afya zetu
lakini pia ni silaha muhimu kwa kuchoma vijidudu na kusafirisha masalio yake nje ya
mwili. Lakini utawezaje kuchoma takataka kama mwingine anajitahidi kuuzima
moto? Kwa kweli unadhuru mwili wako (hasa tumbo lako) kama utakunywa vidonge
mara tu utakaposhambuliwa na malaria au baridi ya bisi.
Imeonekana kuwa manesi wenye elimu ya chini ndio walio wepesi kutoa aspirin
kwa wagonjwa.
Joto chini ya 38.5ºC kwa watoto na 39°C kwa watu wazima halihitajiki
kuteremshwa kwa kutumia madawa ya kemikali, kinyume chake kama joto liko chini
tunashauri lipandishwe kwa kutumia chai moto ya mimea ifuatayo (mapera,
mkaratusi, au michaichai).
Kuongezeka kwa kiwango cha kutoa jasho kunaongeza kiwango cha utoaji uchafu
mwilini. Uchafu mwingi hutolewa kwa njia ya jasho kuliko kwa njia ya mkojo!
Kama joto likipanda sana, taulo iliyoloweshwa inaweza kulishusha kama ikiwekwa
juu ya mwili wa mgonjwa. Mpe vidonge kama tu njia hii haisaidii.
Dawa za asili: Inategemea naminifu na ujuzi wa watumishi waliopo kama
wanaruhusiwa kutengeneza madawa wao wenyewe. Jinsi kituo cha afya kilivyo mbali
na bohari la madawa, ndivyo ilivyo bora zaidi kwa manesi kujitengenezea madawa
yao wenyewe, mfano: yale ya maji, ya mafuta ya baridi ya bisi, dawa za mafuta kwa
ajili ya upele. Ni muhimu pia kwamba mikutano ifanywe baina ya waganga wa
kienyeji ikiandaliwa na watumishi wa afya kwa msingi wa utaratibu na kawaida ili
kuondokana na imani juu ya bidhaa zilizoagizwa toka nje, ikiwa ni pamoja na
madawa.
Alama bora ya kuonyesha kituo bora zaidi cha afya siyo idadi kubwa ya wagonjwa
wanaotibiwa kwa mwaka, bali idadi kubwa ya wale wasiotibiwa kwa mwaka ambayo
ni ishara ya afya bora inayotokana na mafundisho mazuri katika semina mbalimbali.
147
7.4. GHALA LA DAWA LA HOSPITALI
A. Nini kizalishwe:
1. Tunza na tengeneza madawa yanayotumika tu: Katika mahospitali mengi nimeona
madawa ya vivutio tu! Tonics (dawa za kutia afya na nguvu – kama zinavyoitwa),
vitamin za maji (vitamin syrup) n.k. Ni upotezaji wa jinsi gani huu wa muda na
fedha! Chunguza pia dawa zako zilizoingizwa toka nje; angalia kiasi cha sukari,
chumvi, maji, na mafuta yaliyomo, vyote kutoka Ulaya? Ninadhani kama 80%!
Kwa kutumia utengengezaji wa dawa ulio katika kitabu hiki mnaweza kupunguza
kwa 50% idadi ya dawa zinazoagizwa kutoka nje, okoa karibu 30% ya fedha yako,
tunzeni mishipa yenu ya fahamu na nguvu muridhike na uzalishaji wa bidhaa za
hali ya juu nyinyi wenyewe!
2. Tengeneza dawa za maji pale tu zinapohitajika. Dawa nyingi za maji zinazidi
kutajirisha watengeneza madawa tu! Watu wazima hawahitaji hizo dawa. Kwa
watoto kidonge kinaweza kugawanywa kabla ya kunyweshwa na kuchanganywa
na maji (au asali) kabla ya kumnywesha, jambo ambalo huokoa karibu 95% ya
gharama. Kwa watu wazima dawa za asili za maji na matone vinatosha, mfano
matone ya dawa ya kikohozi (sura 5:10). Kwa kikohozi kwa watoto, kunywa chai
nyingi au maji inasaidia zaidi kuliko dawa yoyote ya maji ya kikohozi!
Katika hali ya hewa ya tropiki hata dawa hizo zilizochanganywa na maji na sukari
hazitunziki bali zinahitaji vikolezo vya kuzitunza. Uingiaji mwilini wa hivyo
vikolezo unapelekea kuongezeka kwa madhara yake.
3. Tengeneza nzito – ambazo ni gharama kuzisafirisha au kuziagiza kutoka nje. Pia
usitegemee misaada kutoka nje, kwa sababu siku moja hii misaada itakoma au
unaweza kuwa umesahau kutengeneza dawa wewe mwenyewe!
4. Tengeneza inayookoa fedha – bidhaa nyingine ni rahisi kuzalisha, lakini ni
gharama kubwa kununua; mfano: ni bora kutumia chai ya Artemisia, badala ya
vidonge vyenye gharama kubwa vya kutibu malaria, au dawa ya mafuta ya kutibu
bawasiri. Mara nyingine nimeona, kinyume chake, watengeneza madawa ambao
wanazalisha vidonge kwa gharama kubwa lakini vinanunuliwa kwa bei rahisi.
5. Tengeneza iliyo muhimu: Lakini siyo iliyo katika orodha ya “madawa muhimu”
na kwa jinsi hiyo itakuwa ghari. Mahospitali mengi yamekubaliana na ubora na
madawa ya asili baada ya kuona vidonda vilivyooza vikitibiwa kwa kipande
chembamba cha papai bichi. Kisha kuharisha damu kwa (ameba) amiba
kukitibiwa kwa chai iliyotengenezwa kutokana na Euphorbia hirta, malaria kwa
kutumia chai ya Artemisia annua na kuvimba kwa viungo vya mifupa kwa
kutumia dawa ya mafuta ya kutibu baridi ya bisi (iliyotengenezwa kwa pilipili).
B. Madawa yaliyotengenezwa kutokana na mimea hatari Tengeneza kile wengine wasichoweza kutengeneza . Michanganyo mingine ya
madawa lazima itengenezwe katika mahospitali tu; mfano dawa ya maji ya Datura,
unga wa kimusukulu, dawa ya maji ya mbangi. Hizi zinatakiwa kutengenezwa na
wafanyakazi waliofuzu utengenezaji wa madawa katika mahospitali.
148
C. Jinsi ya kutafuta kemikali.
C.1. Sodium Hydroxide
Inauzwa kwa kiasi kidogokidogo katika maduka makubwa kwa ajili ya kusafishia
mifereji na mabomba lakini hakikisha kuwa hakuna kemikali yeyote iliyoongezwa
ndani yake. Kwa kiasi kikubwa uliza kwenye viwanda vya pombe, au jaribu kununua
moja kwa moja toka kwenye kiwanda cha sabuni.
C.2. Kileo (Alcohol): Unaweza kutengeneza kimiminika chenye kama 10% ya kileo (angalia: divai ya asali,
sura 4:8). Mvinyo (gongo) ya mahindi inayotengenezwa vijijini inaweza kuwa na
30% hadi 40% ya kileo, lakini kwa sababu za kiusalama, itumie kwa matumizi ya nje
tu. Ili kupata hadi 70% ya kileo kutoka katika mvinyo ya mahindi unatakiwa
kuichemsha na kupata mvuke wake na kisha kuugeuza kuwa kimiminika tena. Itumie
hii kwa dawa za maji kwa matumizi ya nje ya mwili pekee au kwa dawa ya kusafisha
na kuua vijidudu . Unaweza kupata 95% ya kileo katika mapipa; mfano, kutoka
katika viwanda vya sukari.
C.3. Nta
Ukihitaji kiasi kidogo tumia mishumaa. Nunua kiasi kikubwa kutoka makampuni ya
petroli. Yanauza nta katika mifuko ya kilo 50. Hii ni nta ya kiwandani, lakini
tulipoitumia hakuna aliyedai kupata madhara ya ngozi.
Vinginevyo tumia masega ya nyuki (kwa kuyavuna na kuyatayarisha angalia sura
6:31).Yatumie kwa kutengeneza dawa za mafuta, karatasi zenye nta, mishumaa, rangi
za kupaka, dawa za viatu, varnish.
Nta ya nyuki huondolewa rangi kwa kusambazwa kwenye kipande cha nguo na
kisha kuiweka juani; kwa kufuata mtindo wa kiwandani, ni kwa kutumia chloride of
lime au potassium permanganate lakini sisi huwa hatuiondolei rangi hata mara moja.
Hakuna kabisa haja ya kuiondolea rangi!
kutoka Ukraine:
Mgeni wa kizungu akisaidiwa na tabibu wa kiafrika
149
SURA YA 8
KAMA WEWE NI DAKTARI AU MUUGUZI: Tafadhali angalia uwezo wa tiba
yako kwa kutumia darobini na vifaa vya maabara vilivyopo.
KAMA WEWE NI MGANGA WA JADI: Shirikiana na hospitali ili kuthibitisha
matokeo.
KAMA WEWE NI MGONJWA: Kwa baadhi ya magonjwa, matumizi ya dawa za
mimea yanaweza kukutibu; katika baadhi ya magonjwa, matumizi ziada ya mimea
yanaweza kukusaidia; mtarifu mganga wako juu ya suala hili.
Kwa magonjwa katili kama kifua kikuu, UKIMWI, kansa, magonjwa ya ngono, ni
muhimu kumuona daktari! Tiba bora daima hutolewa kwanza ikifuatwa na tiba ya muhimu zaidi, na kuendelea.
Agitation Mziwaziwa 5.11; raurolfia 6.41; na 7.4b
Arteriosclerosis (arteri
kuvimba na kuwa ngumu)
Kitunguu swaumu 5.1; karoti 6.21
Arthritis Pilipili 5.4; mbafu 6.10; dawam mchuzi 6.19.
Athlete’s foot Kitunguu swaumu 5.1; mwarobaini 5.3.
Baridi yabisi (Rheumatism) Pilipili 5.4; mbafu 6.10; mkaratusi 5.10
Bawasiri Artemisia 5.2; Mwingajini 5.7; embe 5.12; pilipili
5.4; michaichai 5.9 (mafuta ya dawa 4.4)
Bilious troubles Dawam mchuzi 6.19; mfuta 6.25.
Bronchitis Mkaratusi 5.10; michaichai 5.9; limau 5.8; embe
5.12; chumvi 6.33
Chawa kichwani (Mafuta 4.3.F); mwarobaini 5.3.
Choo kufunga Mwingajini 5.7; ringworm bush 5.6; karoti 6.21;
embe 5.12
. tatizo kubwa Mbono 6.43.
Colitis Artemisia 5.2.
Eczema Kabeji 6.8; mwarobaini 5.3; chamomile 6.29;
maharagwe 6.39
Elimu ya afya Sabuni 4.1
Filaria Mafuta ya scabies (upele) 4.3.F
Flatulence Mkaratusi 5.10; pilipili 5.4; dawam mchuzi 6.19.
Gastritis Mperapera 5.14; mshubili 6.3; viazi vitamu 6.26.
Goiter (Mchanganyiko 4.10j)
Guinea worm Papai 5.5
Hedhi
kutokuingia (Amenorrhea)
Nanasi 6.5
maumivu wakati wa hedhi Tururu 6.44
Hepatitis Papai 5.5
CHAGUO LA KWANZA KATIKA TUKIO LA UGONJWA
150
Herpes labialis Limau 5.8; chungwa 6.14.
Hofu (Anxiety) Mziwaziwa 5.11; passion 6.37.
Homa Michaichai 5.9; mkaratusi 5.10; kurimbais 6.35;
mbuyu 6.1 (ushauri 7.3)
Homa ya manjano Papai 5.5.
Homa ya matumbo
(Typhoid)
Kitunguu saumu 5.1; ORS 4.6.
Impetigo Rejea magonjwa ya ngozi
Insect repellant Michaichai 5.9; mkaratusi 5.10
Insecticide Mwarobaini 5.3; mbaazi 6.46; tumbaku 6.34 (ushauri
4.11.I)
Jaundice Papai 5.5
Jipu Papai 5.5; kitunguu maji 6.2
Kansa (Ushauri, vinka 6.49)
Kichefuchefu Tangawizi 5.15; kahawa 6.16
Kichocho (Bilharzia) Artemisia 5.2
Kichwa kuumwa Rejea homa au migraine
Kifaduro Tururu 6.44
Kifua kikuu Mkaratusi 5.10 (supportive)
Kikohozi Mkaratusi 5.10; kitunguu saumu 5.1; limau 5.8;
tangawizi 5.15; kitunguu maji 6.2; ovakado 6.38;
elixir 4.9.
Kisonono (Ushauri 7.1)
Kisukari Mhindi 6.50; kitunguu maji 6.2; kitunguu saumu 5.1;
maharagwe 6.39; Mpira 5.14 kama hakuna mimea
mingine, vinka 6.49.
Kuhara damu:
Light cases: Kitunguu saumu 5.1; Mpira 5.14; tangawizi 5.15;
mwarobaini 5.3.
Bacillary: Mziwaziwa 5.11; vinka 6.49.
Kuhara kwa ameba
Kuharisha kidogo na
kuzuia:
Papai 5.5; Mpera 5.14; Embe 5.12
Kuharisha sana: Mziwaziwa 5.11
Kuharisha Watu wazima Mkaa 4.5; ORS 4.6; Mpira 5.14; mziwaziwa 5.11.
embe 5.12; mwarobaini 5.3
Kuharisha Watoto ORS 4.6; pera 5.14; karoti 6.21; juisi ya nazi 6.15.
Kukosa usingizi Karanga 6.6; passion flower 6.37.
Kupungua uzito (Ushauri 7.1)
Kuumwa na nyoka Jiwe jeusi 4.7.
Kuumwa na wadudu Mranaa 6.20
Kuungua Mshubili 6.3; chumvi 6.33; kiretemete 6.27; kitunguu
maji 6.2; papai 5.5.
Majeraha ya kuungua
yenye vijidudu
Mwarobaini 5.3; papai 5.5.
151
Kuvimbewa Paipai 5.5; nanasi 6.5; kechu 6.40; dawam mchuzi
6.19.
Lactation (kuongeza
maziwa ya mama)
Boga 6.18
Low blood pressure Kahawa 6.16
Lumbago Rejea maumivu ya kuvimba kwa viungo (Baridi
yabisi/ Rheumatism)
Maambukizi ya figo Mahindi 6.50; mziwaziwa 5.11.
Macho mekundu
(Conjunctivitis)
Chamomile 6.29; mshubili 6.3; Artemisia 5.2.
Madawa ya mifugo (Ushauri na michanganyiko 4.10)
Mafua Kitunguu saumu 5.1; limau 5.8; michaichai 5.9;
Artemisia 5.2; mkaratusi 5.10.
Magonjwa ya kusambaa
kwa kujamiiana
Tumia antibiotics. Saidia tiba hii kwa papai 5.5;
mshubili 6.3; mziwaziwa 5.11; (Ushauri 7.1.11)
Magonjwa ya njia ya mkojo Papai 5.5; mziwaziwa 5.11; kitunguu maji 6.2;
Mkaratusi 5.10; vinka 6.49.
Malaria (Ushauri 7.3) kwa mujibu wa homa;
katika joto lolote: Michaichai 5.9; kitunguu saumu5.1)
Hadi 37.5°C Tangawizi 5.15; Mpera 5.14
Hadi 38°C Papai 5.5
Hadi 38.5°C Mwarobaini 5.3; mtukutu 6.48
Hadi 40°C Artemisia 5.2; cinchoma 6.13
Mammary gland infection Tururu 6.44
Matatizo ya tumbo Mpera 5.14
Maumivu ya kunyonga
(Cramps)
Passion 6.37; mziwaziwa 5.11; mramaa 6.20.
Mba (Fungal infection) Kitunguu saumu 5.1; ringworm bush 5.6; papai 5.5;
kitunguu maji 6.2; kabeji 6.8
Meno - kuoza (Caries) Poda ya meno 4.5; mwarobaini 5.3.
kusafisha meno Mwarobaini 5.3; mkaratusi 5.10; (ushauri na
mchanganyiko 7.1d)
Migraine Kahawa 6.16; mgagolia 6.17; chungwa 6.14; mranaa
6.20.
Minyoo, intestinal Papai 5.5; mziwaziwa 5.11; boga 5.19; embe 5.12;
lesena 6.28.
Mkanda wa jeshi (Herpes
zoster)
Pilipili 5.4
Mtando mweupe mdomono
(Candidiasis) Asali na kitunguu saumu 5.1; Artemisia 5.2.
Ngozi kuwasha Kitunguu maji 6.2; kabeji 6.8; mranaa 6.20.
Ngozi – ulinzi (Skin care) Mafuta ya watoto 4.3; mafuta ya dawa ya watoto 4.4.
Nywele kutoka Mshubili 6.3; pilipili 5.4.
Oedema Mahindi 6.50; mwingajini 5.7; nanasi 6.5.
Oral mucous membrane
152
infection Embe 5.12
Parkinson’s disease Mranaa 6.20.
Poisoning Mkaa 4.5B; mbono 6.42; mranaa 6.20.
Prostatitis Boga 6.18; karoti 6.21.
Psoriasis Mwarobaini 5.3; ringworm bush 5.6.
Pumu (Asthma) Mziwaziwa 5.11; mkaratusi 5.10; papai 5.5.
Ringworm Ringworm bush 5.6; Mwarobaini 5.3.
Roundworm Tazama minyoo, intestinal
Safura (Hookworm) Tazama minyoo
Sciatica Pilipili 5.4
Shingles Rejea Herpes zoster
Shinikizo la damu Kitunguu saumu 5.1; mahindi 6.50; kitunguu maji
6.2; vinka 6.49.
Sinusitis Michaichai 5.9; Artemisia 5.2; kitunguu saumu 5.1.
Spasm, intestinal Passion flower 6.37; mranaa 6.20
Sprains Pilipili 5.4
Travel sickness Tangawizi 5.15
Uchungu wa kuzaa Pilipili 5.4
Ugonjwa wa masikio (Otitis) Kinetenete 6.27; kitunguu maji 6.2.
Ugonjwa wa fizi Embe 5.12; mshubili 6.3
UKIMWI (Ushauri 7.1)
Ukosefu wa hamu ya kula Ngongolia 6.17; anchona 6.13
Ulcers Mshubili 6.3.
Upele (Scabies) Mafuta 4.3f; mafuta ya dawa 4.4; ringworm bush 5.6;
mwarobaini 5.3; rauwolfia 6.41.
Upungufu wa damu Jamii ya mchicha 6.4; chuma 4.10; Folic acid 4.10
Upungufu wa Vitamin C Mchicha 6.4; nanasi 6.5; limau 5.8; chungwa 6.4;
mwembe 5.12; matunda damu 6.37; Mpera 5.14
Utapiamlo Mlongelonge 5.13; (ushauri 7.10)
Vidonda Asali 6.30; chumvi 6.33; kinetenete 6.27; papai 5.5;
annatto 6.7; mafuta ya dawa 4.4.D)
Vidonda koo (Tonsillitis) Mkaratusi 5.10; mwembe 5.12
Vidonda vyenye usaha Papai 5.5; kitunguu saumu 5.1; kitunguu maji 6.2.
Warts Kitunguu saumu 5.1; mwarobaini 5.3; mziwaziwa
5.11
153
Abscess (jipu) Mkusanyiko wa usaha chini ya ngozi uliozungukwa na tissue
zilizovimba.
Allergen (Pia huitwa antigen) kitu cha nje ambacho husababisha mzio,
hasa mbelewele, vumbi la ndani ya nyumba na moshi wa sigara
Mzio (allergy) inayosababishwa na allergen. Baadhi ya matukio ya mzio
hutokea hapo hapo, na mengine baadaye.
Amenorrhea Kukosekana kwa hedhi kwa wanawake.
Amoeba dysentery Kuharisha kunakosababishwa na kimelea Entamoeba –
histolytica, ni wa pili kwa malaria ambayo imeenea katika nchi
za tropiki.
Anaemia Upungufu wa chembechembe nyekundu za damu, mgonjwa
hupauka na kuwa dhaifu.
Anaesthetic Dawa ambayo inasababisha kutokuhisi maumivu.
Analgesic Kitu ambacho hupunguza maumivu.
Antiseptic Ni kitu ambacho huzuia maambukizi kwa kuua bacteria.
Anti-spasmodic Kitu ambacho hulegeza maumivu ya kunyonga (cramps).
Arthritis Kuvimba kwa viungo.
Ajurveda Mfumo wa jadi wa dawa za kihindi ambao una maana
“Ufahamu wa namna ya kuishi.”
Bacillary dysentery Pia huitwa shigellosis, ugonjwa mkali wa matumbo ambao
husababisha kuharisha. Husababishwa na kula kinyesi cha
mgonjwa katika vyakula au maji.
Bacillus Jamii ya bacteria ambao huzalisha vijidudu katika familia ya
bacillaceae. Katika aina 33, tatu husababisha ugonjwa.
Beri-beri Ugonjwa wa mishipa ya fahamu ya mikono na miguu
husababishwa na upungufu wa thiamine.
Bile (nyongo) (Pia huitwa gall) Majimaji yanayotolewa na ini, yana rangi
njano-kijani na machungu. Nyongo huhifadhiwa katika kifuko
cha nyongo, na hutolewa wakati mafuta yanapoingia sehemu
ya kwanza ya tumbo mdogo (duodenum), kusaidia katika
uyeyushaji wa mafuta.
Bilharzia (kichocho) Pia huitwa Schistosomiasis. Ugonjwa wa minyo
ohusababishwa na vimelea (schistosoma); mtu anaweza
akaugua kwa kuogelea katika mito au maziwa, yenye vimelea,
au kwa kunywa maji yenye vimelea.
Black water fever Ni madhara makubwa ya kutumia quinine kutibu malaria.
Boil (jipu) Uvimbe wenye usaha chini ya ngozi.
Bronchitis Inflammation of the mucous membrane ya mirija ya hewa
kwenye mapafu.
ORODHA YA MANENEO YA KISAYANSI NA
MAELEZO YAKE
154
Candida Fungus nyeupe ambazo wakati mwingine hutokea midomoni
mwa watoto. Kwa watu wazima ambao wana kinga ndogo
inaweza ikashindikana kudhibitiwa, hivyo kupelekea utando
mweupe mdomoni, ukeni, njia ya chakula au kwenye ngozi.
Carminative Dawa ambayo hutibu msokoto wa tumbo na tumbo kujaa hewa.
Cold sores Malengelenge madogomadogo yanayowasha yaliyo na
majimaji (wakati mwingine husababishwa na virusi vya
herpes).
Colic Maumivu makali ndani ya utumbo.
Colitis Mwako (inflammation) katika utumbo mkubwa (bowel)
Conjunctivitis Kuvimba kwa mucous membrane ya jicho.
Contagious disease Ugonjwa unaoenezwa kutoka mtu mwenye ugonjwa kwenda
kwa mtu mwingine.
Cramp Maumivu ya kunyonga
Delirium Hali ya kuchanganyikiwa kiakili (hasa husababishwa na dawa
au homa kali).
Dermatitis Kuvimba na kuuma kwa ngozi.
Dehydration Upungufu mkubwa wa maji mwilini.
Diabetes (kisukari) Ugonjwa wa kongosho ambao huzuia sukari na wanga
kufyonzwa inavyotakiwa.
Diarrhea (kuharisha) Kinyesi cha mara kwa mara cha majimaji husababishwa na
hofu, wadudu (microbes) au sumu.
Digestion Mchakato wa kuyeyusha chakula kuwa kidogo ambacho
kinaweza kufyonzwa.
Diuretic Kitu ambacho kinaongeza utokaji wa mkojo.
Dysentery Mwako (inflammation) wa utumbo, ambao husababisha
kuharisha sana.
Dysmenorrhea Maumivu wakati wa hedhi
Ebola virus disease Ugonjwa mkali wa virus na wenye homa kali ya ghafla na
kutokwa damu sehemu mbalimbai za mwili, yakiwemo macho.
Unaambukizwa kupitia damu au majimaji ya mgonjwa.
Eczema Ugonjwa wa ngozi unaosababisha wekundu, maumivu makali
na ngozi kuwa na magamba.
Emetic Dawa inayofanya mtu kutapika.
Enema Maji yanayoingizwa kupita njia ya haja kubwa kwa lengo la
kusafisha utumbo.
Enteritis Kuvimba kwa matumbo
Enzyme Protin inayoundwa katika chembechembe hai ambayo husaidia
mabadiliko ya kikemikali.
Expectorant Ni kitu ambacho humsaidia mgonjwa kukohoa makohozi
(mucous) na majimaji mengine kutoka kwenye mapafu.
Filariasis Ugonjwa unaosababishwa na filarial, thread worms wanaoishi
kama vimelea kwa binadamu, wanyama na mimea.
Flavonoid Rangi ya njano kwenye mimea
Furunculosis Ugonjwa mkali wa ngozi unaosababisha majipu majipu.
155
Galenics Ni Sayansi ya kubadilisha kemikali kuwa dawa.
Gall Rejea bile (nyongo).
Gangrene Kuoza na kufa kwa tissue za mwili wakati upelekwaji wa damu
unapokuwa umekatwa.
Gastric Yenye kuhusiana na tumbo.
Genital Yenye kuhusiana na uzazi.
Gonorrhea Ugonjwa wa ngono unaosababishwa na bacteria Neisseria
gonorrhea.
Guinea worm Threadworm hadi meta 1 urefu, huishi chini ya ngozi.
Haemostatic Kitu ambacho huzuia kuvuja damu
Haemorrhoids
(bawasiri)
“Piles” kuungua (kuvimba) kwa mishipa ya damu
inayozunguka njia ya haja kubwa.
Hepatic Yenye kuhusiana na ini.
Hepatitis Kuvimba kwa ini, husababisha ngozi kuwa njano, ini kuwa
kubwa, kukosa hamu ya kula, tumbo kuvurugika, choo chenye
rangi ya mfinyanzi na mkojo kuwa na rangi ya njano sana.
Herpes Ugonjwa unaoletwa na virus; husababisha cold sores kwenye
ngozi na mucous membrane. Aina mbalimbali za virus
hushambulia maeneo ya pua na midomo (herpes labialis), kati
ya kiuno na mapaja (herpes zoster or shingles) na kuzunguka
sehemu za uzazi (herpes genitalis)
Insecticide Inayoua wadudu
Insectifuge Inayofukuza wadudu
Jaundice Ngozi kuwa njano, mucous membrane na
macho,kunasababishwa na bilirubine kuwa nyingi sana
(sehemu ya nyongo) katika damu.
Kwashiorkor Aina ya Utapiamlo unaosababishwa na upungufu wa protein
kwenye chakula
Lactagogue Dawa inayochochea maziwa ya mama kuzalishwa.
Lactation Utokaji wa Maziwa ya mama baada ya kujifungua.
Laxative Dawa inayochochea choo kutoka (kuharisha).
Lesions Vidonda vinavyosababishwa na ugonjwa fulani, mfano candida
au herpes.
Murasmus Kunyong’onyea na kukonda, aina ya Utapiamlo.
Menstrual Yenye kuhusiana na hedhi (utokaji wa damu ya uterine mucous
membrane)
Nephritis Kuvimba kwa figo.
Neuralgia Kutokea na kutoweka kwa maumivu makali kwenye mishipa
ya fahamu, kawaida kichwani au usoni.
Oedema Kuvimba kwa tissue kwa kuwa na majimaji
Oral rehydration “Kurudisha” maji ya mwilini yaliyopotea kwa kunywa
mchanganyiko maalum.
Paralysis Kukosa nguvu katika misuli kwa sababu ya jeraha au ugonjwa
katika mishipa ya fahamu.
156
Parasite Mnyama au mmea ambao huishi kwenye au ndani ya mnyama
au mmea mwingine na kupata chakula chake kutokana na
mnyama huyo.
Pectoral Yenye kuhusiana na kifua au matiti.
Placental retention Kondo la nyuma kushindwa kutoka baada ya kujifungua
Prostatitis Kuvimba kwa tezi za kiume (tezi za kiume ambazo huzunguka
shingo ya kibofu na mfereji wa mkojo)
Psoriasis Ugonjwa wa ngozi unaosababisha ukurutu na ngozi kama
magamba ya samaki
Purgative Kitu kinachofanya utumbo kutoa uchafu.
Pyrogene Kitu cha kibacteria ambacho husababisha homa.
Renal Yenye kuhusiana na figo.
Rheumatism Ugonjwa mkali ambao utaufahamu kwa kuvimba na maumivu
makali kwa kiungo kimoja au zaidi.
Rickettsia Wadudu wadogo ambao sura yao inaunganisha sura ya bacteria
na virusi
Scabies Ugonjwa wa kuambukiza ambao husababisha vigaga na
maumivu. Husababishwa na vijidudu (mites) vidogo.
Schistosomiasis Rejea Bilharzia (kichocho)
Scurvy Ugonjwa unaosababishwa na upungufu wa vitamin C.
Sedative Dawa ya nguvu ya kutuliza.
Shingles Rejea herpes zoster (mkanda wa jeshi)
Sores Vidonda, majeraha au kidonda chochote kilichowazi.
Spasmodic Inahusiana na spasms, mishituko mikali ya vipindi.
Syphilis
(Kaswende)
Ugonjwa unaoletwa na kujamiiana; husababishwa na
Treponema palladium.
Tuberculosis
(Kifua kikuu)
Ugonjwa unaoathiri mapafu na wakati mwingine mifupa,
husababishwa na bacillus, mycobacterium tuberculosis.
Typhoid (Homa ya
matumbo)
Ugonjwa wa gastro-intestinal. Husababishwa na salmonella
typhi, huambukizwa kutokana na maji yasiyo safi.
Typhus Ugonjwa ambao husababishwa na aina ya Rickettsia,
huchukuliwa kutoka wanyama kwenda kwa watu kwa kuumwa
na chawa, viroboto, papasi au vidudu vidogovidogo.
Hujulikana kwa homa kali na mgonjwa kuonekana kuwa
mwenye huzuni kubwa.
Venereal disease Ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya kufanya tendo la ngono.
Vermifuge Dawa ambayo hufukuza parasitic worms.
Volatile oils Mafuta yenye harufu nzuri ambayo hutoweka kwa mvuke
katika hewa.
157
Matoleo mengine ya vitabu vya anamed
“Dawa za asili katika nchi za joto.
I: Mimea ya nchi za joto kama chanzo cha ulinzi wa afya.” Na Hans – Martin Hirt na Bindanda M`Pia.
Kitabu hiki kinapatikana katika Kkiingereza “Natural Medicine in the Tropics”, Kijerumani:
“Natuerliche Medizin in den Tropen,” Kifaransa: “La Médecine Naturelle Tropicale”, Spanish:
“Medicina Natural” and Ukranian.
“Dawa za asili katika nchi za joto II: Uzoefu” Na Hans – Martin Hirt na Keith Lindsay
Kijitabu chenye kurasa 48 kinachoelezea magonjwa ya kawaida na jinsi ya kuyatibu, na maelezo ya
kina ya mimea mitano.
Kitabu muhimu kwa semina ya kwanza katika mada wa asili:
Kinapatikana katika kiingereza, kifaransa kireno na Kisualuli.
Tafsiri katika Lugha nyingine zinaendelea kutayarishwa.
Bango la “Mimea inayoponya katika nchi za joto.” Linapatikana katika kiingereza, kifaransa na kijerumani.
Tumia Water Hyacinth!
Kitabu cha mwongozo wa matumizi ya magugu maji kutoka dunia nzima. Na Keith Lindsay na Hans – Martin Hirt.
Magugu maji ni janga katika nchi zote za joto. Kitabu hiki kinaelezea jinsi Water Hyacinth
inavyoweza kuonekana kama malighafi inayopatikana daima na bure, na inatumika kwa mambo
mengi. Ikiwa ni pamoja na mbolea , chakula cha wanyama, ufundi, samamni, karatasi, usafishaji
maji na kwa nishati. Pia ndani yake kuna mpango wa mtengenezaji wa jiko la jua na ULOG.
Linapatikana katika Kiingereza.
Vikorokoro vya programu ya malaria wa anamed (AMP). Mbegu na taarifa zote unazohitaji ili kupanda na kustawisha Artemisia annua anamed (A3),
kutayarisha chai ya Artemisia na matumizi yake kwa wagonjwa wa malaria. Habari nyingi za
kisayansi juu ya mmea huu zinatolewa pia.
Fomu zinatolewa kwa ajili yako ili kutoa taarifa ya uzoefu wako – kwa anamed.
Nyaraka juu ya mpango wa malaria wa Anamed. Vifurushi vinapatikana katika lugha za kiingereza, kijerumani na kifaransa.
Sabuni zenye zebaki (Mecury): Aibu ya siku hizi. Taarifa inaelezea tatizo la kutumia sabuni na vipodozi vyenye zebaki kwa lengo la kung’arisha
ngozi. Kurasa 15 za taarifa kuu zimefuatiwa na kurasa nyingine 27 zenye taarifa kutoka magazetini,
taarifa za kisayansi na taarifa nyingine muhimu. Anamed inatafuta kuondoa sheria inayoruhusu
uuzaji wa bidhaa za sumu kama hizo dunia nzima.
Kwa taarifa kuhusu bei, au kuagizwa, tafadhali angalia katika toviti yetu , au andika kwa anamed,
Schafweide 77, 71364 Winnenden, Germany.
158
Bindanda M’Pia alizaliwa July, 27, 1963 huko
Matamba – Solo, Zaire.Tangu 1983 hadi 1986
alikuwa mwalimu wa sekondari. Tangu 1986 hadi
1991 aliajiriwa na Kitengo cha Shirikisho la Kitabu
cha Kanisa la Kiprotestanti huko Kwango,
Zaire, ambako alifanya mikutano mbalimbali na
waganga wa kienyeji. Alibadilisha mimea mingi ya
asili kuwa madawa ambayo kwa sasa yanajulikana
sana huko Zaire katika hospitali, kwa kuitikia wito
mbalimbali amekuwa akiwatia moyo na
kuwafundisha watu wengi katika nchi za tropiki jinsi
ya kutengeneza dawa zao wenyewe, na hivyo
kutunza na kushughulikia afya zao wenyewe. Tangu 1991 hadi 1993 alipata
masomo zaidi huko Ufaransa. Kwa wakati huu anajishughulisha na “program
ya madawa ya asili” katika jimbo la Bandundu katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo.
Hans – Martin Hirt alizaliwa huko Winnenden,
Ujerumaji 25 January, 1951. Kufuatia masomo ya
Ufamasia katika Chuo Kikuu cha Heidelberg
alitunukiwa “The Doctor of Pharmacy,”kwa kusomea
“Uimarishaji wa asili wa mfumo wa kinga mwilini,”
kwenye kituo cha Ujerumani cha “Cancer Research
Center”(Utafiti juu ya Saratani) – ambapo katika somo
hilo amekwisha
toa matoleo zaidi ya 30 juu ya uchunguzi wake
kisayansi.
Tangu 1976 hadi 1985 alikuwa Mkuu wa Idara ya
Uchunguzi na Utengenezaji madawa kwenye kituo kikuu cha Ufamasia cha
Wilaya ya Heilbronn. Mwaka 1985 alifanya ziara kwenye mahospitali nchini
Peru, Nepal na India. Tangu 1985 hadi 1991 alikuwa mshauri wa mambo ya
madawa huko Matamba – Solo, Zaire, na tangu 1992 hadi 1994 alikuwa
mshauri wa Kanisa la Kiprotestanti la Ujerumani kwa shughuli za nchi za nje
nchini Zaire. Mwaka 1991 alianzisha “anamed” (Action for Natural Medicines)
ambayo kwayo anaongoza semina juu ya madawa ya asili huko nyumbani na
nchi za nje, ameanzisha vikundi vya anamed katika nchi kadhaa.
159
HATARI KUBWA ZAIDI KATIKA NCHI ZA TROPIKI NI KUPOTEZA
UFAHAMU WA UTAMADUNI WAO.