eclea.net: equipping church leaders east africa: home · web viewufunuo 11 hulitazama kanisa katika...

165
Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved. HUDUMA YA KIMATAIFA YA KUWAIMARISHA WACHUNGAJI THEOLOJIA YA KI-BIBLIA na Jonathan M. Menn B.A., University of Wisconsin-Madison, 1974 J.D., Cornell Law School, 1977 M.Div., Trinity Evangelical Divinity School, 2007 Equipping Church Leaders-East Africa 3701 N. Gillett St., Appleton, WI 54914 (920) 731-5523 [email protected] www.eclea.net December 2009; revised February 2011. Theolojia ya Ki-Biblia ni mkondo wa maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji wa nchi na mwanadamu katika Mwanzo, kupitia anguko la mwanadamu na matokeo yake, na historia ya ukombozi wa Mungu kwa mwanadamu, hata utimilifu wa mbingu mpya na nchi mpya katika Ufunuo. Biblia inaeleza ksimulizi

Upload: others

Post on 22-Oct-2020

15 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

HUDUMA YA KIMATAIFA YA KUWAIMARISHA WACHUNGAJI

THEOLOJIA YA KI-BIBLIA

na

Jonathan M. Menn

B.A., University of Wisconsin-Madison, 1974

J.D., Cornell Law School, 1977

M.Div., Trinity Evangelical Divinity School, 2007

Equipping Church Leaders-East Africa

3701 N. Gillett St., Appleton, WI 54914

(920) 731-5523

[email protected]

www.eclea.net

December 2009; revised February 2011.

Theolojia ya Ki-Biblia ni mkondo wa maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji wa nchi na mwanadamu katika Mwanzo, kupitia anguko la mwanadamu na matokeo yake, na historia ya ukombozi wa Mungu kwa mwanadamu, hata utimilifu wa mbingu mpya na nchi mpya katika Ufunuo. Biblia inaeleza ksimulizi inayofungamana, huku Yesu Kristo akiwa ndiye moyo wake. Theolojia ya Ki-Biblia huangalia dhana kuu ambazo zinazopitia katika Biblia nzima, zinazolenga juu ya uhusiano wa Mungu na mwanadamu. Pia huonyesha jinsi Kristo na kanisa ndio utimilizo wa maagano, ahadi, unabii, na taasisi zilizoanzishwa katika Agano la Kale. Ramani za nyakati, na Dibaji zimeambatanishwa kama nyenzo za kusaidia.

ORODHA YA YALIYOMO

THEOLOJIA YA KI-BIBLIA: UTANGULIZI…………………………………………………………..........................3

I. Tabia ya Theolojia ya Ki-Biblia …………………………………………………………………….............................3

A. Maelezo ya Theolojia ya Ki-Biblia……………………………………………………………..….....…………………..3

B. Fikira za Theolojia yaKi-Biblia ………………………………………………………………...….…………………..3

II. Mtazamo wa Mkondo wa simulizi na Dhana za Theolojia ya Ki-Biblia….……………………................................4

A. Msingi wa mkondo wa simulizi za Biblia …………………………………………………………...…………………..4

B. Dhana ya Theolojia ya Ki-Biblia …..………………………………………………………………..…………………..4

MSINGI WA SIMULIZI YA MKONDO WA BIBLIA ………………………………………….…...............................5

I. Uumbaji (Mwanzo 1-2)………………………………………………………..................................................................5

A. Simulizi ya mkondo wa Biblia huanzia na Mungu (Mwa 1:1) ………………………………………...........................6

B. Mungu aliumba kila kitu bila kutumia chochote …………………..………………………………..............................6

C. Mungu alimuumba mwanadamu ili atawale viumbe vingine vyote (Mwa 1:26-28) …………………………………..6

II. Anguko la Mwanadamu Katika Dhambi na Matokeo Yake (Mwanzo 3-11:26)……………….…………………..7

A. Uhusiano kati ya uwepo wa Mungu na dhambi …….……………………………………………….............................7

B. Adamu naHawa watenda dhambi na kufukuzwa kutoka bustani ya Edeni (Mwanzo 3)……………………………...9

C. Matokeo ya Anguko—kutoka kwa Kaini hadi Mnara wa Babeli (Mwanzo 4-11:26)…………….…………………..12

III. Tukio la Ukombozi—Mungu aita Watu Kwa Ajili Yake Mwenyewe (Mwa 11:27-Ufu 20)……………………..14

A. Mwanzo mpya wa Mungu—Kutoka Ibrahimu hadi Yusufu (Mwa 11:27-50:26)…………………………………….14

B. Kuanza kwa taifa la Israeli—Kutoka Misri kwenda nchi ya ahadi (Kutoka-Kumbu-kumbu)…................................16

C. Israeli ndani ya hiyo nchi (Yoshua-1 Samueli 7)……………………………………………………..........................18

D. Israeli kama ufalme ulioungana (1 Samueli 8-1 Wafalme 11; 1 Nyakati 1-2 Nyakati 9;

Zaburi-Wimbo ulio bora)…………………………………………………………………………………………18

E. Israeli kama ufalme uliogawanyika (1 Wafalme 12-2 Wafalme 17; 2 Nyakati 10-31; Isaya na Mika

[utabiri kwa Israeli na Yuda]; Yoeli [utabiri kwa Yuda]; Hosea na Amosi

[utabiri kwa Israeli]; Obadia [utabiri kwa Edomu]; Yona [utabiri kwa Ninawi])………….………………….19

F. Kuwepo, kushuka, na kuanguka, kwa ufalme wa Kusini (2 Wafalme 18-25; 2 Nyak 32-36:21;

Isaya-Danieli; Nahumu-Zefania)………………………………………………………………………….……19

G. Kurejeshwa kwa ufalme wa Kusini (2 Nyak 36:22-Esta; Hagai-Malaki)…………………………………….……...21

H. Kutimia kwa mpango wa Mungu wa ukombozi katika Yesu Kristo (Mathayo-Ufunuo 20)………………………...21

I. Ufunuo wa Yesu wa Masiha wa kweli ufalme wa Mungu, na kanisa……………………………..……………….....22

IV. Mbingu Mpya na Nchi Mpya (Ufunuo 21-22)…………………………………………..……………………….…24

DHANA MBILI ZA KI-BIBLIA KUHUSU UHUSIANO WA MUNGU NA MWANADAMU.…………………....24

I. Hekalu na Nchi: Maskani ya Mungu na Mwanadamu……………………………………………………………...24

A. Bustani ya Edeni (Mwanzo 2-3; ona pia Ezek 28:13-16)………………………………….………………………....25

B. Hema ya kukutania (Kutoka 25-31, 35-40)……………………………………………………………...……………26

C. Hekalu (2 Sam 7:1-17; 1 Waf 6; 8:1-11; 1 Nyak 17:1-15; 22:1-16; 28:1-29:9; 2 Nyak 3-5)……..............................27

D. Maono ya Ezekiel ya Hekalu Jipya (Ezek 40-48)……………………………………………………………………..29

E. Yesu ndiye hekalu la kweli……………………………………………………………………………….....................33

F. Kama kiwakilishi cha Yesu kionekanacho duniani, kanisa ni “Hekalu” la Mungu duniani ………........................36

G. Ufunuo wa Mbingu Mpya na Nchi Mpya (Ufunuo 21-22)………… ……………………………………………….38

II. Uhusiano wa Mungu na Watu Wake Kuhusu Ndoa……………………………………………………………......42

A. Mwa 2:23-24 (mwanamke kuumbwa rasmi kwa ajili ya mwanaume;mwanaume kuwaacha babaye na

mamaye na kuunganishwa na mkewe na kuwa “mwili moja” naye) ni mfano unaoelezea uhusiano

ambao Mungu anautaka kwa watu.…………………………..………………………………………………...42

B. Katika AK kiungo cha ndoa kati ya Mungu na watu wake kiliwekwa, lakini Israeli hakuwa mwaminifu.………..42

C. Katika AK kiungo cha ndoa kati ya Mungu na watu wake kiliwekwa, lakini Israeli hakuwa mwaminifu……….41

D. Katika Ufunuo, picha ya Ki-Biblia kuhusu uhusiano wa kindoa kati ya Mungu na watu wake huja

kutimilika katika Kristo, bibi arusi (Kanisa), na Nchi Mpya…………………………………………………..45

KRISTO NA KANISA KAMA UTIMILIZO WA AK……………….……….……………………………………….46

I. Biblia Kimsingi ni Kumhusu Yesu Kristo—Yeye Ndiye Mtu Aliye Kiungo na Dhana Iunganishayo Yote.…....46

A. Zinapotazamwa peke yao, simulizi za AK na nabii zake hazimtaji moja kwa moja Yesu Kristo, bali huwa na

Nguzo ya kusimamia, na hutumia lugha zinazolenga, na kumwelekea mlengwa wa kuibukia taifa la Israeli.…………………………………………………………………………………………………………....47

B. Yesu na waandishi wa AJ wote walitumia AK kumhusu Yesu na kwa Injili..……………………………………....47

II. Agano la Ibrahimu, la Daudi, na Jipya Yalielekea Kwake na Kutimilizwa Katika Kristo na Kanisa.………..48

A. Agano la Ibrahimu limetimizwa katika Kristo na Kanisa…………………….………………..…………………….48

B. Agano la Daudi limetimizwa katika Kristo na Kanisa…………………………………..…….……………………...51

C. Agano Jipya limetimizwa katika Kristo na Kanisa………………………………………….………………………..55

III. Yesu Atimiza Maana na Kusudio la Israeli Kama Taifa, na Taasisi Zote za Israeli: Sikukuu zake;

Mifumo ya Dhabihu; Ukuhani; Sheria, na Sabato…………………………………………………………...56

A. Yesu ndiye Israeli mpya, wa kweli, na mwaminifu…………………………………………………………………...57

B. Yesu atabiriwa kuwa ndiye “Mtumishi wa Bwana.”………………………………………………………………….59

C. Katika Yesu, ahadi za AK za marejezo kwa Israeli zinatimizwa.……………………………………………………..60

D. Yesu alitimiliza na kubadilisha siku kuu za Kiyahudi, mifumo ya dhabihu, na ukuhani……………………….….64

E. Yesu alitimiza na kubadilisha Sheria ya AK na Sabato.……………………………………………………………...75

IV. Kwa vile Kanisa Liko “Katika Kristo,” Kanisa ndilo Israeli Mpya, wa Kweli na wa Kiroho.………………...80

A. Neema ya kimwili na ya kiroho, uteuzi, na imani katika AK.….………………...…………………………………..80

B. Aina mbili za uteuzi —wa kimwili na wa kiroho—huonyesha jinsi Maagano ya Ibrahimu, Musa na

Agano Jipya yanavyooana.……………………………………………………………………………………...80

C. Aina mbili za uteuzi—ya kimwili na ya kiroho—huonyesha kwamba Israeli ya AK ilikuwa taifa la

kimwili ambalo “ni mabaki tu” yaliyookolewa kiroho.………………………………………………………...81

D. Uhusiano kati ya Israeli ya AK na kanisa.……………………………………………………………………………82

E. Yesu alilikataa taifa la Israeli kama chombo cha kuujengea ufalme wa Mungu, na kutoa jukumu hilo

kwa wafuasi wake mwenyewe, kanisa.……..…………………………………………………………………...84

F. Kanisa ndio watu wapya, wa kweli, wa Mungu—Israeli wa kiroho………………………………………………….85

G. Kanisa ni jumuisho la “Mtumishi wa Bwana,” kama vile Yesu kibinafsi alivyokuwa “Mtumishi wa

Bwana” (Isa 42:1-9; 49:1-6; 50:4-9; 52:13-53:12)……………………………………… ……………..88

H. Kama Israeli mpya, wa kweli, kanisa linakabiliwa na mitihani ile ile ya uamini fu ambao Israeli ya AK

ya kimwili ilikumbana nayo……………………………………………………………………………………..89

NUKUU ZILIKOTOLEWA……………………………………………………………………………………………..89

DIBAJI 1— VIFUPISHO KWA UCHACHE VYA VITABU VYA BIBLIA ………………………………………..95

DIBAJI 2— MIPANGILIO YA MUDA WA HISTORIA YA BIBLIA …………………………………………...…98

DIBAJI 3— MPANGILIO WA MUDA WA WAFALME NA MANABII WA ISRAELI NA YUDA.…...............100

DIBAJI 4— NABII ZA KIMASIHI CHACHE NA KUTIMIZWA KWAKE...........................................................102

DIBAJI 5— RAMANI ZA HIMAYA ZA ASHURU, BABELI, NA UAJEMI………………...…………………....103

DIBAJI 6— RAMANI YA HIMAYA YA RUMI & MAJIMBO YAKE……………………………………………104

DIBAJI 7— RAMANI YA KANAANI: SEHEMU 12 ZA MAKABILA…………………………………………....104

DIBAJI 8— RAMANI YA UFALME ULIOUNGANA WA ISRAELI…………………………………………….105

DIBAJI 9— RAMANI YA FALME ZILIZOGAWANYIKANA ZA YUDA NA ISRAELI………………………105

DIBAJI 10— RAMANI YA ISRAELI NYAKATI ZA AGANO JIPYA……………………………………………106

THEOLOJIA YA KI-BIBLIA: UTANGULIZI

I. Tabia ya Theolojia ya Ki-Biblia.

A. Maelezo ya Theolojia ya Ki-Biblia.

1. Theolojia ya Ki-Biblia (TK) ni masomo yahusuyo kuweka bayana mkondo wa simulizi za Biblia kuanzia mwanzoni (Mwanzo) hadi mwisho (Ufunuo). Ni “kutafuta unganiko la ndani la Biblia” (Bartholomew 2005: 84).

2. Theolojia ya Ki-Biblia “Hufuatia hatua za ufunuo tangu neno la kwanza la Mungu kwa mwanadamu kupitia kupambanuliwa kwa utukufu kamili wa Kristo. Huchunguza hatua mbali mbali za historia ya Biblia na mahusiano kati yao. Kwa hiyo, hutoa msingi wa kuelewa jinsi vifungu vya sehemu moja ya Biblia vinavyohusiana na vifungu vingine vyote. Tafsiri iliyo safi ya Biblia hutegemeana na yapatikanayo katika [TK].” (Goldsworthy 1991: 32)

3. Kwa vile inajihusisha kuelezea kiunganisho cha ndani cha Biblia kwa namna yake yenyewe, ni “ya kujieleza na ya kihistoria kiasi kwamba tafsiri ya kitheolojia na theolojia ya ki-mfumo haiwezi kuwa hivyo” (Bartholomew 2005: 86).

B. Fikira za Theolojia ya Ki-Biblia.

1. Biblia inaelezea simulizi inayoshikamana, na Yesu Kristo ndiye moyo wa simulizi hiyo (Luka 24:25-27, 44-47; Yoh 5:39). Kila kitabu cha Biblia kinachangia kitu fulani kwenye simulizi hiyo, na ujumla wa simulizi nzima hutoa mpangilio ambao kila kitabu kilichomo kinaweza kutafsiriwa vizuri zaidi.

2. Ingawaje Biblia inaelezea simulizi iliyounganika, ufunuo wa Mungu ni hatua kwa hatua—hujifunua kila mahali katika Biblia yote. Kanuni kadhaa muhimu huibuka kutokana na kweli hizi.

a. Andiko halitalipinga Andiko. Vifungu viwili vinavyoonekana vinapingana, vitakuja kuonyesha havipingani pale vitakapochunguzwa kwa umakini zaidi. Kifungu kimoja kinaweza kurekebisha au kuongezea sifa ya kingine, lakini hakitakipinga.

b. Yote mawili- hatua za ukombozi na “kusudi lote la Mungu” (Mdo 20:27) lazima yaangaliwe ili kuelewa kiusahihi kifungu chochote kile. Mafundisho ya “ufunuo wa hatua kwa hatua” hutueleza kwamba hatua za ukombozi lazima zizingatiwe wakati wa kutafakari kifungu chochote kile. Biblia ni muunganiko unaoelezea simulizi ya kisa kilichoungan. Hata hivyo, kweli za Biblia hazifunuliwi zote kwa mkupuo moja, bali hufunuliwa hatua kwa hatua. Maana kamili ya kifungu chochote husika au fundisho la Ki-Biblia laweza lisiwe wazi hadi Biblia nzima iwe imezingatiwa.

c. Agano Jipya linavyolitafsiri Agano la Kale.

(1) Maandishi yoyote ya Ki-Biblia yanapaswa kusomwa ndani ya muundo wa maneno yaliyotumiwa (lugha na mfumo wa maandishi husika) na mazingira ya kihistoria yalipoandikwa mara ya kwanza. Agano Jipya limeandikwa kwa misingi ya Agano la Kale. Miktadha mingi ya Agano Jipya husimamia Agano la Kale. Uelewa wetu wa Agano Jipya hutajirishwa kwa kiwango kikubwa kwa kulielewa Agano la Kale. Wakati huo huo, hatupaswi kulisoma Agano la Kale kama kwamba Jipya halipo. Yote mawili yapo – kutokuendeleza na mwendelezo kati ya Agano la Kale na Agano Jipya. Agano Jipya hujengwa juu ya miktadha ya Agano la Kale, mara nyingi katika namna za kushangaza. Hilo ni kweli zaidi kuhusu jinsi Agano Jipya linavyohusisha unabii wa Agano la Kale.

(2) Lazima tukumbuke kwamba sheria za Agano la Kale, sikukuu, na taratibu nyingine zimetimilizwa na kukamilishwa katika Kristo (Math 5:17; Rum 10:4; 2 Wakor 3:12-16; Wagal 3:23-4:7). Kwa namna nyingi, Israeli ya kimwili ya Agano la kale, sheria zake, sikukuu zake, na taratibu nyingine, zilikuwa “aina,” “vivuli,” au “mifano” ya uhalisi wa Agano Jipya (1 Wakor 10:1-6; Wakol 2:16-17; Waebr 8; 10:1). Kwa hiyo, tunapoiangalia picha nzima, hasa tunapotumia Maandiko, tunapaswa “kuyasoma Maandiko ya Agano la Kale kwa kupitia miwani ya Maandiko ya Agano Jipya” (Lehrer 2006: 177). Kama ilivyosemwa, “Hili Jipya, ni lile la Kale lililotimilika; la Kale ni Jipya lililofunuliwa.”

II. Mtazamo wa Mkondo wa Simulizi na Dhana za Theolojia ya Ki-Biblia.

A. Msingi wa mkondo wa simulizi za Biblia.

1. Katika mtazamo wa kawaida zaidi, Biblia ni simulizi ya uumbaji, historia, na hatima ya ulimwengu na mwanadamu, kama ielezwavyo kimsingi kwa mtazamo wa kitheolojia. Mungu aliumba ulimwengu wa kupendeza sana na wanadamu kuishi kwa furaha, na maisha yaliyotimilika katika ushirika na yeye. Kupitia dhambi zetu tulipoteza ushirika ule na kuleta uovu na uharibifu na mauti duniani. Hata hivyo, Mungu hakutuacha katika dhambi zetu na mauti. Kwa njia ya mpango mahususi uliohusisha kumwita Ibrahimu na taifa la Israeli, aliandaa njia kwa ajili ya kuja ndani ya mwanadamu kwaYesu Kristo ili kuleta msamaha wa dhambi na kurejesha ushirika na yeye. Anakuja tena, kumaliza dhambi kabisa na mauti pasipo kutuangamiza sisi. Atakwenda kutimiliza kurejeshwa kwetu na uhusiano wetu na yeye. Na pia ataifanya upya nchi, hata iwe ya utukufu zaidi ya ilivyoumbwa mara ya kwanza. Katika muundo huo, mkondo wa simulizi hii ungeonekana namna hii: uumbaji (Mwanzo 1-2)=>Anguko na madhara yake (Mwanzo 3-11:26)=>Ukombozi (Mwanzo 11:27-Ufunuo 20)=>Uumbaji mpya (Ufunuo 21-22). Mungu mwenyewe ndiye yote mawili -mtunzi wa simulizi na ndiye mhusika mkuu wake.

2. Biblia ni ufunuo wa Mungu kuhusu jinsi alivyo na mpango wake (Injili) kwa mwanadamu.

a. Kiungo cha katikati cha ufunuo huo—yeye aliye kiungo mtendaji wa uumbaji, njia ya ukombozi, na chanzo na utimilifu wa uumbaji mpya—ni Yesu Kristo (ona 2 Wakor 1:20; Waef 1:9-10; Wafil 2:6-11; Waebr 1:1-3).

b. Kwa hiyo, Agano la Kale ni maandalizi ya Injili, Injlili zile ni udhihirisho wa Injili; Matendo ya Mitume ni upanuzi wa Injlili; Nyaraka ni maelezo ya Injili; na Ufunuo ni utimilifu wa Injili.

3. Biblia ni simulizi ya uhusiano na mwanadamu, tangu uumbaji hadi uumbaji mpya. Wanenaji mbalimbali wameielezea simulizi kwa njia nyingine zinazotofautiana kidogo:

a. “Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi, hadi kuutwaa mwili, kusulubiwa, ufufuo na kupaa; na mwafaka ni hukumu ya mwisho, mbingu na jehanamu” (Sykes 1997: 14).

b. “Theolojia ya Ki-Biblia ni Mungu kuuleta ufalme wake ambamo mahusiano yote yanakuwa yamerejeshwa kwenye ukamilifu” (Goldsworthy 1991: 76).

c. “Watu wa Mungu, katika nafasi ya Mungu, chini ya utawala wa Mungu, wakiishi kwa njia ya ki-Mungu, katika uwepo mtakatifu na wa upendo wa Mungu, kama familia” (Cole 2006: n.p.).

B. Dhana za Theolojia ya Ki-Bibia.

TK yaweza kukabiliwa kwa njia mbali mbali. Mtu moja aweza kuikabili TK kwa kujaribu kuelezea mpangilio mzima wa mtiririko wa mkondo wa simulizi ya Biblia kiutaratibu kuanzia mwanzo hadi mwisho. Ndani ya mtiririko wa mkondo wa simulizi hiyo, dhana na miktadha muhimu hujitokeza mara kwa mara kila mahali katika Biblia, ambayo husaidia kukazia na “kuimarisha upya” mkondo wa simulizi nzima ya Biblia. mwishowe, dhana hizi, na Biblia yenyewe, huhusishwa, na huweza kutimilizwa, katika Yesu Kristo (ona Luka 24:25-27; Yohn 5:39, 46). Baadhi ya dhana muhimu zaidi na miktadha ni:

1. Ahadi na Kutimizwa. Mungu ni mwaminifu kutimiza ahadi zake. Lakini mara zote ahadi zake hutimizwa kwa njia za kushangaza. Utimilifu wa mwisho wa ahadi za Mungu hupatikana katika Yesu Kristo. Kama asemavyo Paulo katika Waef 1:9-10, “Akiisha kutujulisha siri ya mapenzi yake, sawasawa na uradhi wake, alioukusudia katika yeye huyo. Yaani, kuleta madaraka ya wakati mkamilifu atavijumlisha vitu vyote katika Kristo, vitu vya mbinguni na vitu vya duniani pia, naam, katika yeye huyo.”

2. Agano la Mungu. Mungu alifanya Maagano kadhaa (mapatano maalum) kipindi chote cha historia ya Biblia. Maagano makuu ni: Agano la Nuhu (Mwa 8:20-9:17); Agano la Ibrahimu (Mwa 12:1-3; 13:14-17; 15:1-21; 17:1-21; na 22:15-18); Agano la Musa (Kutoka 19-24), pia hujulikana kama Agano la Kale (2 Wakor 3:14; Waeb 8:6, 13); Agano la Daudi (2 Sam 7:8-17; Zab 89:1-4); na Agano Jipya (Yer 31:31-34; 32:40; Ezek 36:22-28; 37:15-28; Luka 22:20; 1 Wakor 11:25; 2 Wakor 3:6; Waebr 8:6-13; 10:15-17). Kwa namna nyingi, mpango mzima wa Mungu wa ukombozi waweza kuonekana kama ni kutenda kazi kwa Agano la Ibrahimu. Kama simulizi ya ukombozi inavyoendelea, Maagano ya Ibrahimu, Musa, na Daudi, yote hupata utimilifu wake katika Agano Jipya, na Agano hilo hupata utimilifu wake katika Kristo na watu wake, na kanisa.

3. Aina husika-Aina-Kinyume; Kivuli- Kitu halisi. Kadiri mpango wa Mungu ulivyoendelea na wakati, kwanza alimwita Ibrahimu, kisha Isaka, kisha Yakobo, ambaye kupitia yeye alianzisha taifa la Israeli, kuwa chombo ambacho kwacho mpango wake ulifanyika uhalisi. Hata hivyo katika mtazamo wa kitheolojia na wa kiroho, mifano yote ya Agano la Kale au taasisi zake—kama vile Madhabahu na Hema, mifumo ya utoaji dhabihu. Sikukuu, Sheria, na Nchi ya Ahadi. Ufalme, Sayuni, Yerusalemu, na Israeli yenyewe—viliwakilisha “vielelezo” au “vivuli” vya kuonekana au vya kidunia, ambavyo vilielekeza kwenye Agano Jipya, na uhalisi wa kiroho wa siku za mbeleni (Wagal 4:21-31; Wakol 2:16-17; Waebr 8:5; 9:15-10:22; 12:18-24). Uhalisi wa kweli ambao aina na vivuli vya Agano la Kale (AK) vilielekeza, viko katika Kristo, kanisa, mbingu, Yerusalemu mpya, na mbingu mpya na nchi mpya.

4. Mkondo wa Mungu wa Uhusiano: Mungu huanzisha na hutenda kwa neema yake, watu wake wanatakiwa kuonyesha mwitikio kwa imani.

a. Mungu siku zote ametafuta watu kwa ajili yake. Hivyo, kauli inayojirudia mara zote katika Biblia nzima (ikitumia maneno tofauti) ni, “Nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu” (ona Mwa 17:8; Kut 6:7; 29:45; Walawi 26:12; Yer 7:23; 11:4; 24:7; 30:22; 31:1, 33; 32:38; Ezek 11:19-20; 14:10-11; 36:28; 37:23, 27; Hos 2:23; Zek 8:8; 13:9; 2 Wakor 6:16; Waebr 8:10; Uf 21:3).

b. Mkondo unaojirudia mara kwa mara katika Biblia nzima kwa ajili ya watu kuwa na uhusiano mzuri na Mungu ni kwamba, Mungu huanzisha, na watu wake huonyesha mwitikio kwa imani (ambayo kimsingi humaanisha “kutumaini na kutii kutoka moyoni”).

(1) Mungu hutenda kwa neema kwa watu; hata katika kuhukumu na kuwaadhibu makosa huonyesha neema yake. Mungu alianza mchakato kwa kumuumba Adamu na Hawa na alizungumza nao katika bustani ya Edeni (Mwa 2:7, 15-25; 3:8). Baada ya Adamu na Hawa kuanguka dhambini, kwa neema Mungu alianzisha mpango wa ukombozi kwa kuahidi mwokozi (Mwa 3:15) na kutoa sadaka ya wanyama ili kuwavika mavazi (Mwa 3:21). Kwa neema, Mungu alimchagua Nuhu na familia yake waokolewe wakati alipoiangamiza dunia yote kwa Gharika Kuu, na Nuhu aliitikia kwa imani (Mwa 6:5-22). Mungu akamchagua Ibrahimu, aliyeitikia kwa imani (Mwa 12:1-5; 15:5-6). Kwa neema yake, Mungu alituma manabii wake kuwaonya Israeli juu ya maafa ya dhambi zake na kuwaita warudi kwenye uaminifu tena. Mwishowe, kwa neema yake, Mungu mwenyewe akafanyika mwili katika mwanadamu aitwaye Yesu Kristokuwaokoa watu wake na dhambi zao na kurejeza mahusiano mazuri kati ya Mungu na wanadamu.

(2) Kwa vile wanadamu kiasili ni wadhambi, hawawezi “kustahili” au “kufanyia kazi” mbinu iwawezeshayo kuwa na mahusiano mazuri na Mungu (Mdo 13:39; Wagal 2:16; 3:11; Waef 2:1-3, 12). Njia pekee ya watu kuwa na mahusiano mazuri na Mungu ni tu kama wataitikia kwa imani kile Mungu, kwa neema yake, alichokifanya kwa ajili yao. Kwa sababu hiyo, muktadha wa imani na uaminifu kwa Mungu—“mwenye haki ataishi kwa imani”—hujirudia kila mahali katika Biblia (Hab 2:4; War 1:17; Gal 3:11; Waebr 10:38; ona pia Yoh 6:27-29; 20:26-29; 1 Yoh 3:23). Bahati mbaya, mkondo umekuwa mara nyingi watu wengi hawaweki imani zao kwa Mungu, ingawaje daima wamekuwako “mabaki wachache waaminifu” ambao wamefanya hivyo (1 Waf 19:11-18; Rum 11:1-5; ona pia Luka 18:8).

MSINGI WA SIMULIZI YA MKONDO WA BIBLIA

I. Uumbaji (Mwanzo 1-2).

“Uumbaji si swala tu la vyanzo, bali la kusudi na mahusiano” (Goldsworthy 1991: 92). Katika uumbaji, twamwona Mungu kama chanzo cha kila kitu. Zaidi ya hapo, kama kila kitu kilivyoumbwa mwanzoni, twaona “kila kitu kuwa chema” (Mwa 1:31)—m.y., Mungu, mwanadamu, wanyama, mimea, na maumbile mengine yote kutimiza makusudi ya kuumbwa kwao katika mahusiano mazuri kila kimoja kwa kingine. “Wasomi wamegundua kwamba Sura za mwanzo za kitabu cha Mwanzo . . . zimeandaliwa ili kujibu swali la kwa nini mambo yako jinsi yalivyo. Seti moja ya maswali ambayo sura za mwanzo za kitabu cha Mwanzo ni, ‘Kwa nini wanadamu wako jinsi hii? Kwa nini wanadamu hutafuta maarifa zaidi? Kwa nini wanadamu hutafuta utawala mkubwa zaidi juu ya dunia? Kwa nini daima hujaribu kuvumbua vitu vipya, kutafuta matumizi mapya ya rasilimali za “asili”? Kwa nini wanadamu hupaka rangi, huchonga sanamu, huchora picha, hujenga majengo, hutunga nyimbo na mashairi? Kwa nini wanadamu mara kwa mara na kwa namna tofauti hujihusisha na utamaduni wa kisanii, sayansi, na teknolojia?’ Jawabu la Mwanzo 1 ni kwamba Mungu alimfanya mwanadamu awe hivyo. Mwanadamu ni mfano wa Mungu. Mungu ni Muumbaji na ni Mfalme. Kama mfano wake, mwanadamu hubuni na kutawala.” (Leithart n.d.: n.p.)

A. Simulizi ya mkondo wa Biblia huanzia na Mungu (Mwa 1:1).

1. Mungu pekee ni wa milele na anaishi kwa kujitegemea. Mungu si sehemu ya ulimwengu wala si kinyume chake pia. Kila kitu kilichopo kumwacha Mungu (vitu; malaika; wanadamu, nk) viliumbwa na Mungu, na humtegemea Mungu kwa kuwepo kwao (Mdo17:28; Wakol 1:17; Waebr 1:3). Ukweli huu huonyesha kwamba Mungu wa kweli, wa Ki-Biblia hafanani na “miungu” ya dini nyingine. Mungu si kama wazo la Mashariki (n.k., Wahindu; Wabudha) kwamba Mungu na maumbile yote ni kitu “kimoja” (m.y; muktadha wa muunganiko katika kimoja). Mungu pia si wa dini za kiutamaduni (zikiwamo zile za Mashariki ya Karibu ya kale wakati Biblia ilipoandikwa), ambazo huamini kwamba vitu vilivyokufa vina “roho”, na wanadamu wa kwanza walikuwa kwa sehemu moja ni wanadamu na sehemu nyingine miungu.

2. Mungu peke yake anajitosheleza. Yuko Mungu moja tu, lakini ni mwenye hali isiyoelezeka kabisa, tofauti na kila kitu kingine. Kwa hiyo, ingawaje yuko Mungu moja tu, anaishi katika nafsi tatu (Utatu): Baba; Mwana; na Roho Mtakatifu. Hili ni muhimu. Kama Mungu angekuwa ni wa nafsi moja (kama dhana ya Allah wa Ki-Islam), na si Mungu wa Utatu, Mungu asingekuwa anajitosheleza: m.y., angekuwa anawajibika aviumbe viumbe vingine ili awe na uhusiano navyo. Hata hivyo, Mungu hakuhitaji aumbe chochote (ona Mdo 17:24-26)—tayari alishaumba ulimwengu, alishakuwa na upendo kamili wa kiuhusiano kati ya zile nafsi tatu za Utatu kabla hajaumba ulimwengu. Kwa hiyo, Biblia (tofauti na Qur’an) hutueleza kwamba “Mungu ni upendo” (1 Yoh 4:8).

B. Mungu aliumba kila kitu bila kutumia chochote.

1. Ulimwengu haukuwa na kitu kilichokuweko kabla ambacho kwacho Mungu aliumbia nyota au mimea au wanyama. Badala yake, Mungu alifanya tu kutamka au kutangaza, na ulimwengu ukatokea pasipo kutumia chochote (Mwa 1:1, 3, 6-7, 9, 11, 14-16, 20-21, 24, 26-27). Sehemu nyingine, kote katika AK na AJ, Biblia inakazia kitu hicho hicho (ona Kut 20:11; 31:17; Zab 8:3-5; 33:6; Math 19:4; Yoh 1:3; Mdo 14:15; Rum 11:36; 1 Wakor 8:6; Wakol 1:16; Waebr 11:3; Ufu 4:11).

2. Mwanadamu alikuwa ni tukio la kilele katika uumbaji wa Mungu. Ni wanadamu pekee wanasemekana kuwa wameumbwa “kwa mfano wa Mungu” (Mwa 1:26-27); Mungu akambariki mwanaume na mwanamke (Mwa 1:28); na Mungu akawaambia atakuwa na ushirika nao (Mwa 1:28-30; 2:16-17, 19; 3:8-9). Zaidi ya hapo, wakati kila siku baada ya kuumba vitu visivyo hai, mimea, au wanyama, Mungu aliuita uumbaji wake kuwa “mzuri (njema)” (Mwa 1:4, 10, 12, 18, 21, 25), baada ya kuumba wanadamu, Mungu akaona kwamba uumbaji ule ni “mwema sana” (Mwa 1:31).

3. Tukio la uumbaji la Mwa 2:4-25 ni sambamba au nyongeza ya tukio la kiuumbaji lililoko katika Mwa 1:1-2:3. Tukio la Mwa 2:4-25 hurudi nyuma na kujazia undani wa yaliopo katika Mwa 1:26-27 kuhusiana na jinsi Mungu alivyoumba wanadamu. Wote wawili mwanaume na mwanamke walikuwa sehemu ya mpango wa Mungu tangu mwanzo (ona, Mwa 1:27), ingawaje Mungu alimuumba Adamu kwanza na kisha Hawa baadaye ili awe msaidizi na mwenzi wake (ona Mwa 2:18-25). Hii inaonyesha kwamba tabia na majukumu ya mwanaume na mwanamke kwa kiwango fulani ni nyongeza, siyo ya kubadilishana kabisa (ona 1 Wakor 11:3-15; Waef 5:28-32; 1 Tim 2:11-13), ingawaje ni kwa kiwango gani yanaweza kuwa hivyo bado yanajadiliwa.

4. Wote wawili mwanaume na mwanamke wana mfano wa Mungu. Maana ya msingi ya “mtu” (Kiebrania, adam) ni neno la kiujumla “mwanadamu, watu,” ambalo hujumlisha wote wanaume na wanawake. Hilo linawekwa bayana katika Mwa 1:26, panaposema, “Na tumfanye mtu kwa mfano wetu . . . wakatawale.” Mwa 1:27 likieleza wazi kwamba wote wawili mwanaume na mwanamke wanahusika kiusawa, kwani panasema, “Mungu akaumba mtu [Adamu] kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.” Zaidi, katika Mwa 1:28 Mungu akawabariki “hao” (mwanamume na mwanamke) kiusawa na Mungu alisema “nao”. Katika Mwa 1:29, wakati Mungu anasema “Nimewapa kila mche utoao mbegu,” hiyo “wa” ni uwingi, siyo umoja.

C. Mungu alimuumba mwanadamu ili atawale viumbe vingine vyote (Mwa 1:26-28).

1. Adamu na Hawa wakiishi mbele za Mungu katika bustani ya Eden hutupatia mkondo wa ufalme wa Mungu. “Mkondo wa ufalme wa Mungu ni huu: Mungu huanzisha uumbaji ulio kamili ambao anaupenda na ambao yeye hutawala. Heshima kuu kabisa inatolewa kwa mwanadamu kama sehemu pekee ya uumbaji uliofanywa kwa mfano wa Mungu. Ufalme unamaanisha kwamba kila kitu kilichomo katika uumbaji kishirikiane vizuri, hiyo maana yake, kama Mungu alivyokusudia kiwe, kwa kingine chochote na kwa Mungu mwenyewe.” (Goldsworthy 1991: 99)

2. Adamu na Hawa waliagizwa “Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha dunia” (Mwa 1:26-28). Kwa vile wanadamu wameumbwa kiajabu “kwa mfano wa Mungu,” kwa kuenea duniani wakitii maagizo ya Mungu, watu wangekuwa wanaukuza utukufu wa Mungu, kwa kueneza sura yake, juu ya dunia yote. Hali hiyo ya “dhana ya wajibu wa kutawala” huendelea kuonyesha kwamba walitakiwa kupanua mipaka ya kijiografia ya Edeni hadi ienee dunia nzima. Kwa kupanua Edeni hadi kuenea dunia nzima, Adamu na Hawa na vizazi vyao wangekuwa wanaigeuza dunia kuwa kioo cha mbinguni: m.y; kuifanya dunia nzima kuwa paradiso imfaayo Mungu na mwanadamu, iliyojaa watu watakatifu.

3. Ni kwa kutegemea Neno la Mungu peke yake kwamwezesha mwanadamu kutimiliza ile dhana ya wajibu wa kutawala sawa-sawa. “Pale Adamu alipowapa majina wanyama, alianza mchakato wa uchunguzi, kupanga makundi, na maelezo toshelevu, ambayo ndiyo moyo wa uchunguzi wa maarifa ya kisayansi. Lakini hangeweza kamwe kufanikisha uhusiano wake mwenyewe kwa Mungu au hata kwa ulimwengu kwa kutegemea uchunguzi peke yake. Badala yake, lilikuwa ni Neno la Mungu lililokuja kwa Adamu kumwambia jinsi ya kuhusiana na Mungu na kwa ulimwengu. Ni Neno la Mungu linalomjulisha mwanadamu kwamba awe mwanasayansi na mwenye kuutunza kiupendo ulimwengu, badala ya kufanya uchawi na kuwa mtu mharibifu asukumwaye na kutaka madaraka katika dunia.” (Goldsworthy 1991: 99)

II. Anguko la Mwanadamu Katika Dhambi na Matokeo Yake (Mwanzo 3-11:26).

A. Uhusiano kati ya uwepo wa Mungu na dhambi.

1. Mungu ndiye mkuu juu ya yote, na yuko kazini daima akitimiza mpango wake (ona Ayu 12:13-25; Isa 40:21-26; Mdo 4:27-28; Rum 9:14-24; Ufu 17:14-17). Hii inamaanisha kwamba, kwa namna fulani, Mungu ndiye mmiliki wa uovu, ingawa si kwa namna kwamba ndiye mwanzilishi wa ule uovu wa mwovu (ona Mwa 4:1-7; Isa 10:5-16; Hab 1:1-11; Mdo 2:22-24). Kwa maneno mengine, Mungu huruhusu na huachilia dhambi, si kwa ajili ya ule uovu wake au udhambi wa dhambi yenyewe, bali kwa makusudi ya matokeo yaliyo “ya busara, matakatifu, na yafaayo sana” (Edwards 1984, Freedom, §IX: 76; pia ona, Piper 2000: 107-31). Mungu hivyo husimama katika uhusiano ambao “siyo pacha” nyuma ya wema na uovu: pasipo kuvuruga enzi za ukuu wake, ule “uovu” wa mwovu siku zote hutokana na sababu zinazousababisha, ambapo wema siku zote hutokana na Mungu mwenyewe.

2. Mtu mwingine anaweza kutazama swala la Mungu kuruhusu dhambi na uovu kutokea kwa mantiki ya uhusiano wa jua na giza na baridi. “Kuna tofauti kubwa kwa Mungu kuhusiana na hivyo, kwa ruhusa, yake katika tukio au tendo, ambalo, kwa jinsi lilivyo na sura yake, ni dhambi, (ingawaje tukio hilo bila shaka litafuatana na ruhusa yake,) na kwa yeye kuhusika katika hilo kwa kulizalisha na kuongoza tendo la dhambi; au katika ya yeye kuamuru kitu fulani kiwepo, kwa kutokukizuia, katika mazingira fulani, na kwa yeye kuwa mtendaji au mmiliki astahiliye, kwa kutumika kiuzuri au kiuwezeshwaji. . . . kama kulivyo na utofauti mkubwa kati ya jua kuwa chanzo cha ile nuru na ujoto wa anga, na uangavu wa dhahabu na almasi, kwa uwepo wake na athari njema za kuwepo kwake; na kwa kuhusiana na hiho hilo kunakuja giza na baridi kali, usiku, kwa mwenendo wake, itokeapo linazama kwenye miisho ya dunia. Mwenendo wa jua ni sababisho la aina ya matukio yanayofuatia baadaye; lakini silo sababu halisi, uwezeshwaji, au mzalishaji wa hayo; ingawaje lazima yatokee kutokana na mwenendo wake, katika mazingira hayo: hakuna tena tendo lolote la Ki-Uungu kuwa ndiyo sababu ya uovu wa mapenzi ya kianadamu. Kama jua lingekuwa ndiyo chemchemi ya mambo hayo, kama lilivyo chemchem ya nuru na joto: na kisha kitu chaweza kujadiliwa kutokana na tabia ya ubaridi na giza, kwa kulinganisha na sifa za jua; na pia inaweza kabisa kukubalika kwamba, jua lenyewe ni giza na baridi, na ya kuwa miali yake ni myeusi na yenye ukungu. Lakini kwa kufanyika sababu si kwa vinginevyo zaidi ya kutokuwepo kwake, hakuna kitu kama hicho kiwezacho kuhusishwa, isipokuwa kinyume chake; yawezekana kiusahihi kabisa ukadai, kwamba jua ni angavu na lenye joto kali, ikiwa baridi na giza ni matokeo ya kutokuwepo kwake; na kadiri matokeo haya yanavyounganishwa na kuwajibishwa zaidi mara kwa mara na kutokuwepo kwake, ndivyo inavyotia nguvu zaidi hoja kwamba jua ni chemchemi ya nuru na joto. Kwa hiyo, kama ambavyo dhambi si tunda litokanalo kwa jinsi yoyote ile na utendaji mwema au uvuvio mzuri wa Aliye Juu sana, bali, kinyume chake, hutokana na kuzuilia matendo yake na nguvu, na katika mazingira fulani, hufuatia ulazima wa athari ya utendaji wake; hili si hoja kusema kuwa yeye ni wa dhambi, au utendaji wake ni wa uovu, au una lolote la asili ya uovu; bali kinyume chake, ni kuwa Yeye, na utendaji wake, pamoja ni mzuri na wa utakatifu, na kwamba yeye ni chemchemi ya utakatifu wote. Itakuwa ni hoja ya kustaajabisha, tena sana, kusema wanadamu hawafanyi dhambi, isipokuwa tu pale Mungu anapowaachia wenyewe, na kulazimika kutenda dhambi afanyapo hivyo, kwamba Mungu lazima awe wa asili ya dhambi: ndivyo itakavyokuwa hoja ya kustaajabisha, kwani siku zote ni giza jua linapokuwa limezama, na kamwe hakuwi giza wakati jua likiwapo, hivyo basi, giza lote latokana na jua, na kwamba mduara wake na miale yake lazima iwe myeusi.” (Edwards 1984, Freedom, §IX: 77)

3. Mungu anaweza kuagiza jambo kwa mapenzi yake ya siri (au “ki-mamlaka”) ambayo mapenzi yake yaliyofunuliwa (au “mtazamo” wake unakataza. “Mungu anao uwezo wa kuitazama dunia kwa vioo viwili. Anaweza kuiangalia kupitia kioo cha upeo mwembamba au kupitia kioo cha upeo mpana. Mungu atazamapo tukio lenye kuumiza au lililo ovu kupitia kioo cha upeo mwembamba, huona maafa au dhambi ilivyo yenyewe na huchukizwa na kuhuzunika. ‘Maana mimi sikufurahii kufa kwake afaye, asema Bwana Mungu’ (Ezek. 18:32). Lakini Mungu anapoliangalia tukio lenye kuumiza au lililo ovu kwa kupitia kioo chake chenye upeo mpana, huona maafa, au ile dhambi kuhusisha na kila kitu kilichosababisha na kitakachotokea kutokana nayo. Huona inavyounganika na mpangilio kuelekea umilele. Mpangilio huo, pamoja na sehemu zake zote (nzuri na mbaya) anazotaka ziwe (Zab 115:3).” (Piper 2000: 126) Kwa mfano, Ayubu alielewa kwamba mabaya yote yaliyompata kiuhalisia yalikuwa yamepangwa na kuruhusiwa na Mungu; kwa hiyo alimwelekezea kilio na kumbariki Mungu, ingawaje aliyesababisha moja kwa moja uovu ule alikuwa ni Shetani (Ayu 1:21-22). Mungu aliwatumia Waashuri kwa kuwaadhibu Waisraeli kwa dhambi yao, bali baadaye aliwaadhibu Waashuri kwa kiburi chao (Isa 10:5-19).

4. Uovu wote ambao Mungu anauruhusu na anauagiza hatima yake hutumika au kuleta wema mkubwa zaidi kwa uumbaji wenyewe. Paulo alisema “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.” (Rum 8:28). “Hakuna mantiki yoyote kufikiria, kwamba anaweza kukichukia kitu kama kilivyo, na kukiona tu kuwa kiovu, na bado ikawa ni mapenzi yake kitokee, akijua maafa yake yote. . . . Wanadamu hupenda dhambi kama dhambi, kwa hiyo ndio waanzilishi na watendaji wake: wanaipenda kama dhambi, na kwa makusudio mabaya na matokeo mabaya. Mungu hakusudii dhambi kama dhambi, au kwa kusudio la kitu chochote cha ubaya; ingawaje huwa ni furaha yake kuagiza mambo, ambayo, kwa kuyaruhusu, dhambi itakuja kutendeka, kwa makusudio ya uzuri au wema mkubwa zaidi, ambao kwa kutimia kwake yatakuwa ndio lengo. Kule kukubali kuachia mambo ili uovu uweze kutendeka, kama uovu: na kama ndivyo, basi hakuna sababu kwa nini asiweze kiuzuri tu kuuzuia uovu kama uovu, na kuuadhibu kama ulivyo.” (Edwards 1984, Freedom, §IX: 78-79; (pia ona, Piper 2000: 107-31; Edwards, Remarks, ch. 3: 525-43). Kwa mfano, Yusufu aliuzwa utumwani na ndugu zake lakini baadaye aliwaambia, “Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo.” (Mwa 50:20). Huenda mfano mkubwa zaidi kuliko yote ni kusulubiwa kwa Kristo. Yuda, Herodi, Pilato, na watu wengine wasiomcha Mungu walimsaliti, kumlaani, na kumsulubisha Kristo asiyekuwa na dhambi, na bado alikuwa ndiye Mungu aliyeagiza tukio hilo lifanyike kama njia ya kuleta masamaha ya dhambi, mabadiliko ya maisha, na upatanisho wa mwanadamu kwa Mungu (Mdo 2:22-23; 4:27-28).

5. Kwa vile Mungu ndiye wema mkuu zaidi ya wote uwezekanao kuweko, dhambi na uovu ni vya lazima ili hali zote za Uungu na tabia za Mungu ziweze kufunuliwa vizuri. “Ni jambo jema na zuri kabisa kwa utukufu wa Ki-Ungu kung’ara; na kwa sababu hiyo hiyo, ni vyema kwamba uangavu huo wa utukufu wa Mungu uwe kamili; yaani, sehemu zote za utukufu wake zing’are, kwamba uzuri wote uwe kimlingano unaangaza, kwamba mhusika awe na sura halisi ya Mungu. Si vyema kwamba utukufu moja udhihirishwe kupita kiasi, na mwingine usiwepo kabisa; maana hapo, kule kung’ara hakutaleta uhalisia. Kwa sababu hiyo hiyo si sahihi moja udhihirishwe kupita kiasi, na mwingine kidogo sana. Ni vyema sana ule uangavu wa Mungu utoe majibu ya unyofu wake wenyewe; kwamba ile enzi ya kiutukufu iwajibike kwa utukufu halisi na ulio muhimu, kwa sababu hiyo hiyo ni vyema na bora kabisa kwa Mungu kujitukuza mwenyewe kabisa. Kwa hiyo ni lazima, kwamba ukuu wa Mungu usioneneka, mamlaka yake na enzi yake ya kutisha, haki yake, na utakatifu, udhihirishwe. . . . Kama isingelikuwa ni vyema kwamba Mungu aagize na kuruhusu na kuiadhibu dhambi, kusingekuwa na udhihirisho wa utakatifu wa Mungu katika kuchukia dhambi, au katika kuonyesha lile alipendalo, katika upaji wake, katika uchaji mbele zake. Kusingekuwa na udhihirisho wowote wa neema ya Mungu au ucha Mungu wa kweli, kama kusingekuwa na dhambi za kusamehewa, hakuna maafa ya kuokolewa kwayo. . . . Huwa tunajali kidogo mno kiasi gani hisia ya wema inavyoinuliwa kutumia hisia ya uovu, kwa yote mawili – kihamasa na kiasili. Na kama ilivyo lazima kuwe na uovu, kwa sababu kuonekana kwa utukufu wa Mungu kusingelikuwepo na kusingekamilika, kama uovu usingalikuwepo, kwa hiyo uovu ni wa lazima, ili kufikia kiwango cha juu kabisa cha furaha ya kiumbe, na kukamilika mawasiliano ya Mungu, ambayo kwayo aliuumba ulimwengu, kwa sababu furaha ya kiumbe hujumuishwa katika kumjua Mungu, na hisia ya upendo wake. Na ikiwa kumjua yeye kutakuwa hakujakamilika, furaha ya kiumbe lazima iwe haina uwiano kimlingano.” (Edwards 1986, Remarks, ch. 3: 528; ona pia, Piper 1997: n.p.; Erlandson 1991: n.p.; Edwards 1984, The End: 94-121; Piper 2003a: 17-50; Piper 2003b:17-35)

B. Adamu na Hawa watenda dhambi na kufukuzwa kutoka bustani ya Edeni (Mwanzo 3).

1. Biblia inaweka bayana kwamba Shetani “alianguka” kabla ya dhambi ya Adamu na Hawa, kwa vile Shetani ndiye aliyewajaribu Adamun a Hawa na kuwadanganya kuhusu sababu na matokeo ya kula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya (fananisha, Mwa 2:16-17 na Mwa 3:1-4). Kwa hiyo, Yesu alimwita Shetani yote mawili, “muuaji tangu mwanzo” na “mwongo na baba wa huo” (Yoh 8:44-45).

2. “Ujuzi wa mema na mabaya” (Mwa 2:17) huwakilisha uhuru wa kimaadili na kujitawala.

a. Ule “mti wa ujuzi wa mema na mabaya” haukuwa mti wa kiuchawi ambao ulizaa ujuzi wa mema na mabaya kwa kila mtu aliyeula. “Inaelekea sana kwamba Mungu aliuandaa huo mti kama uwigo wa mpaka, kama njia ya kuonyesha tofauti kati ya mema na mabaya. Kwa maneno mengine, uchaguzi wa Adamu na Hawa haukuwa kati ya kutokujua na kujua mema na mabaya, bali katika kubakia wema na wenyewe kuwa wabaya. Sura ya mtihani ilikuwa kwamba lolote watakalolichagua, watakuja kujua mema na mabaya. Walikuwa viumbe vya kimaadili ambavyo vingejua yaliyo sahihi na yasiyo sahihi kwa kutumia mwitikio wao binafsi kwa Mungu.” (Goldsworthy 1991: 98) Kama wangefaulu mtihani huo, kule kumtegemea na kumtii Mungu kungeliuthibitisha wema wao, na wangelilijua hilo. Kama wangelishindwa mtihani huo, kutomtegemea na kutokumtii Mungu kungeliwageuza kuwa watu wenye uovu kwenye kiini kabisa cha uanadamu wao, na wangelilijua hilo pia.

b. Katika vifungu Fulani vya AK (2 Sam 4:17; 1 Waf 3:9) maneno “mema na mabaya” huzungumzia kimsingi uwezo wa kuchukua hatua kisheria. Kwa hiyo, kilichokuwa kimekatazwa kwa mwanadamu kilikuwa ni ule uwezo wa kuamua nini kiwe kwa ajili ya manufaa yake na nini kisiwe hivyo. Mungu hakutoa maamuzi ya aina hiyo kwa mwanadamu, kwa sababu ni Mungu pekee ndiye ajuaye yote, mwenye hekima yote, na mwenye upendo wote. Kwa hiyo, ni Mungu pekee anaweza kufanya uamuzi sahihi na wenye upendo kwa ajili ya manufaa ya mwanadamu ya kweli, wakati wote. Mwanadamu atendapo katika hali ya kujitawala mwenyewe, hujiweka nafsi yake mwenyewe kuwa mhimili wa kati kwa miongozo yake ya kimaadili na hujiamulia nini chema na nini kibaya. Hivyo hujaribu kuwa “kama Mungu” (ona Mwa 3:5, 22). Hata hivyo, kwa vile mwanadamu hajui yote, hana hekima yote, na hana upendo wote, juhudi zake za kuwa kama Mungu ni dhahiri zitashindwa. Badala yake, ataishia kutenda zaidi kama “mungu wa dunia hii” (2 Wakor 4:4), na matokeo yanayofanana nayo.

3. Shetani alimwingia nyoka na kumdanganya Hawa (Yoh 8:44; 2 Wakor 11:3; Ufu 12:9). Adamu alikuwapo pamoja naye na, yeye pasipo kudanganywa, alikubali kumfuata mkewe katika dhambi (Mwa 3:6; 1 Tim 2:14). Hilo laweza kuwa sababu kwa nini dhambi ya Adamu ni kubwa zaidi, na kwa nini matokeo yaliyowajia wanadamu wote baadaye husemekana kutokana na dhambi ya Adamu (ona Rum 5:12-14, 17-21; 1 Wakor 15:21-22).

4. Mbinu ya Shetani ni kielelezo cha majaribu yanayotukabili.

a. Alimjia Hawa kwanza. Huo ulikuwa ni ujanja wa juhudi za kujaribu kumdanganya mtu ambaye hakupokea maagizo moja kwa moja kutoka kwa Mungu, na kumgonganisha mtu moja na mwingine

b. Alilenga jambo pekee ambalo Mungu alikuwa amelikataza. Licha ya Mungu kutoa mahitaji yote kwa wingi mkuu, kwa kule kukazia kitu pekee ambacho hawakutakiwa kukifanya, Shetani ndipo kama matokeo yake alipandikiza wazo ambalo limepotoka au lililokengeuka kuhusu uhalisi katika akili zao.

c. Alitafuta kuingiza mashaka kwenye kweli ya Neno la Mungu (3:1). Kwa kuuliza “ati Mungu [kweli] alisema, ‘msile matunda ya miti yote ya bustani?’” Shetani alitafuta kuingiza mashaka na kupandikiza kuchanganyikiwa kuhusu kile ambacho alikitaka Mungu.

d. Alidanganya na kuligeuza Neno la Mungu (3:4). La kushangaza, ukweli mmoja ndio Shetani aliushambulia kuhusiana na ghadhabu ya Mungu na madhara ya dhambi. Kama ilivyokuwa kwa Adamu na Hawa, tunakabiliwa na uamuzi: nani tumwamini? Kwa mbinu za Shetani (na za kidunia), Neno la Mungu halikubaliwi tena kama kweli inayojieleza yenyewe, bali limefanywa kuwa ngazi ya neno la kiumbe. Yote mawili–Mungu na Neno lake huonekana kuwa na mamlaka ya chini zaidi ambayo lazima yapimwe na mamlaka iliyo juu zaidi. Kwa mara nyingine, ujanja wa nyoka: haupendekezi wanadamu wamwachie Mungu enzi yake mwenyewe, bali wao wenyewe tu waangalie na kutathmini madai ya Mungu kuhusu kweli. Matokeo ya mwisho yalikuwa sawa tu na kumweka Shetani awe Bwana, lakini hayo hufanyika pasipo mwanadamu kuelewa.” (Goldsworthy 1991: 104)

e. Ailzijumuisha sifa za Mungu mwenyewe (3:5). Kimsingi, Shetani alikuwa anasema kwamba Mungu alikuwa hana upendo kwa kuwazuia Adamu na Hawa vitu vya kula, na alikuwa hana upendo kwa kuvitaka viumbe vyake kumtegemea yeye kwa maarifa ya mema na mabaya, badala ya kufanya maamuzi hayo wenyewe.

f. Alichochea kiburi cha kianadamu. Shetani alimwahidi Hawa kwamba kwa kumuasi Mungu angelikuwa na uzima (“hakika hutakufa”), maarifa (“na macho yako yatafumbuka”), furaha kutokana na hali ya kuinuka (“utakuwa kama Mungu”), na ukuu wa kujitawa kimaadili (“kujua mema na mabaya”). Kinyume chake, hata hivyo, kwa Adamu na Hawa kufanya maamuzi kwa njia yao wenyewe (m.y., kujitawala kimaadili) ni sura ya kifo kwa sababu ni kutengwa mbali na Mungu. Kwa hiyo, kiini cha dhambi yao kilikuwa kutokuamini (m.y., kukosa imani na tumaini kwa Mungu, kunakodhihirishwa kwa kumtii Mungu). Hata tangu mwanzo, mpango wa Mungu ulikuwa kwamba watu wamwangalie yeye na kumtumaini yeye kwa ajili ya kweli kuhusu nini ni chema na nini kibaya, na kwa vipi tunatakiwa kuishi maisha yetu—m.y., “mwenye haki ataishi kwa imani” (Hab 2:4; Rum 1:17; Wgal 3:11; Waeb 10:38).

5. Dhambi ya Adamu na Hawa iliwadhuru si wao tu, bali kila mtu katika historia yote.

a. Badala ya kuleta furaha na utoshelevu, Adamu na Hawa walileta hukumu, aibu, hofu, kufarakana na Mungu, uumbaji wote, wao kwa wao, na hatimaye mauti. (Mwa 3:7-19). Adamu na Hawa walitaka kujitawala (m.y., uhuru; kutengwa na Mungu), na wakapata hayo. Hata hivyo, kujitenga huko na Mungu ni sura ya kifo na mauti. Kutokana na kile walichokifanya, Adamu na Hawa kwanza walijikuta na aibu kuhusiana na hali yao ya kuwa uchi (Mwa 3:7-10). Hali yao ya kijinsia ingeliwakumbusha kwamba wao hawakuwa kama Mungu: hawakuwa na uwezo wa kuumba pasipo kutumia chochote (kama Mungu), bali tu waliweza kuzaa. “Hivyo hali yao ya ujinsia ilikuwa iwakumbushe [au ingepaswa iwakumbushe] juu ya uhuru wao na changamoto zake [au ingetoa changamoto] kwa fikira zao za uhuru na hali yao ya kuwa kama Mungu” (Goldsworthy 1991: 105). Kama matokeo ya mkondo ulioanzishwa bustanini, Mungu mara zote huwaachia watu waamue wenyewe njia zao na kisha kubeba madhara yao wenyewe (ona, Kut 16:1-20; Hes 11:18-20, 31-34; Rum 1:24, 26, 28).

b. Adhabu ambayo Mungu aliiagiza (Mwa 3:16-19) kwa mwanaume (kazi inafanyika ngumut) na mwanamke kuzaa watoto kunakuwa kwa uchungu) zote zahusiana na uwajibikazi kimaisha kwa wanaume na wanawake. Zaidi ya hapo, Mwa 3:16b panaonyesha mwanzo wa mgongano wa kindoa na/au mvutano wa madaraka ya kindoa—tangu sasa na kuendelea, uhusiano kati ya waume na wake utakuwa una harufu ya dhambi (ona, k.m., kufuatia kwa mawazo mbali mbali yahusuyo namna ya mwingiliano kati ya “kutamani” na “kutawala” katika 3:16: Busenitz 1986: 203-12; Cassuto 1961: 165-66; Walton 2001: 227-28; Stitzinger 1981: 41-42; Foh 1974-75: 376-83).

c. Dhambi ya Adamu huathiri uumbaji wote. “Uumbaji upo hapo kwa ajili ya manufaa yetu. Unyenyekevu ni uwakilishi wa uumbaji wote ili kwamba Mungu aushughulikie uumbaji kwa msingi wa anavyoshughulika na wanadamu. . . . Mwanadamu aangukapo kwa sababu ya dhambi, uumbaji hufanywa kuanguka pamoja naye.” (Goldsworthy 1991: 96) Zaidi ya hapo, Adamu hupata baadhi ya dawa zake: kama tu jinsi alivyoasi kinyume na utawala wa Mungu, sasa uumbaji wote, ambao anatakiwa kuutawala, utamwasi kinyume naye. “Laana ardhini kusema kweli ni laana kwa Adamu. Mfalme wa dunia sasa hana mtumishi anayemtii ardhini. Uhuru wa kula miti yote katika bustani unabadilishwa na kwa masumbufu kuifanya dunia itoe mkate unaolazimika kila siku. . . . Mwisho wa mwanadamu ni kuipa ardhi mbolea kwa yeye kuurudia mavumbi ambako alitokea.” (Ibid.: 106)

d. Biblia huona watu wote kuwa kama moja na Adamu (“katika Adamu”), Adamu akitenda kama kichwa chetu au mwakilishi wetu (ona, Rum 5:12-19; 1 Wakor 15:21-22; nk., Waeb 7:9-10). Hatimaye, kama matokeo ya dhambi ya Adamu, kizazi chote cha mwanadamu kinapokea: “uhalali” wa kuwa na hatia dunia nzima, kunakoongoza kwenye kuharibika kimaadili dunia nzima (Zab 51:5; Yer 17:9; Rum 3:9; 7:14-25), kunakoongoza kwenye dhambi ya mtu moja moja dunia nzima (Rum 3:10-18, 23), kunakoongoza kwenye hatia ya mtu moja moja. Jinsi kamili ya namna ilivyokuwa na kwa nini na vizazi vya Adamu vimehesabiwa hatia na kuwa na uharibifu mkubwa kutokana na dhambi ya Adamu, ni swala la mjadala. Zifuatazo ni baadhi ya fikira zifikiriwazo:

(1) Biblia siku zote hutazama makundi ya watu kama mtu “moja aliyekamilika” (ona, Yosh 7:10-26; Rum 5:12-19; 1 Wakor 15:21-22). Hii ni sawa na kumtazama Adamu kama mbegu au mzizi wa mti, na uzao wake kama matawi na majani: Vyote ni mti moja; matawi na majani hupokea yote mawili - uzima na sura kutoka kwa ile mbegu na mzizi. Adamu, kama kichwa cha kizazi chote, huzalisha viumbe vilivyoanguka, vyenye uasi, kama vile yeye alivyifanya dhambi. Hali ya Adamu kama kichwa “huhusisha fursa za ndani zaidi kuliko ubaba wa kikawaida. Huhusisha utukuzaji wa kuelezea nini kinamaanisha kuwa mwanadamu [ona, Mwa 5:3; 1 Wakor 15:49]. . . . Ikiwa wahusika wanataka kuasi, je wasimamie wapi ili kufanya hilo? Sioni msingi wowote wa wao kusimamia, hakuna kitovu cha madai yao, uhuru wao binafsi hauko huru, mshabihiano wenye kujitegemea. Mungu ndiye aliyeuumba kama vile alivyowaumba, ndani na kupitia Adamu, kama sehemu ya sifa za Adamu.” (Blocher 1997: 130).

(2) Kwa vile Adamu aliumbwa pasipo dhambi na alikuwa na kila fursa na mazingira yake binafsi, hakukuwa na mtu bora zaidi yake wa kuwakilisha wanadamu katika ujumla wao. Kama mwakilishi wetu, dhambi ya Adamu, na hivyo hata kukosa kwake, kuliwekezwa kwetu (sona, Johnson 1974: 298-316). Hali ilivyo ni kama taifa: “itokeapo mkuu wa nchi akitangaza vita na taifa jingine, watoto wote wanao zaliwa wakati huo wa vita huwa wako vitani na taifa jingine. Katika swala la Adamu, maafa hutenda kazi kwa kina cha ndani zaidi, kwa sababu mshikamano wetu wa ki-Adamu (yaani, uanadamu) ni muhimu zaidi na, kwa vile uhusiano ni kwa Mungu ‘ambaye tunaishi na kuenenda na kuwa na uhalisi ndani yake’.” (Blocher 1997: 129).

(3) Ilikuwa lazima kabisa kwa Mungu kufanya kitu fulani kwa watu wote ili wawe na uharibifu kama matokeo ya dhambi ya Adamu. “Ni kutoa katika yaliyojitokeza, kama ilivyokuwa sahihi na lazima kwa kiwango cha juu sana afanye hivyo, kutoka kwa huyo mwanadamu mwasi, na kanuni zake za kiasili zikiwa zimeachwa zenyewe, kwatosha kumfanya awe mharibifu kabisa na aliyepindana kutenda dhambi kinyume na Mungu” (Edwards, 1984, Original Sin: 219).

e. Matokeo ya anguko, na utu wetu “katika Adamu,”ni kwamba kwa jinsi yetu wenyewe, pasipo Kristo, tunakuwa “wafu katika makosa na dhambi zetu” (Waef 2:1). Hii inamaanisha kwamba kuna upungufu kupita kiasi au uharibifu kuhusiana na kila mtu (pia huitwa nguvu ya dhambi ikaayo ndani) ambayo huathiri kila kitu ndani yetu, kuchanganya hata jinsi tunavyofikiri, kuwaza, kuongea, kutenda, kujisikia, na mahusiano na watu na kwa Mungu. Matokeo ya uharibifu huu ni kuwa, nje ya msaada wa Kristo, tunakuwa: hatuna uwezo kabisa kumjia Kristo na kumwamini yeye (Yoh 6:44, 65; Waef 2:8-9); hatuwezi kabisa hata kuuona ufalme wa Mungu (Yoh 3:3, 5); hatuwezi kabisa kujitoa kwa sheria ya Mungu na kumtii (Rum 8:6- 8); hatuwezi kabisa kuelewa kweli za kiroho kumhusu Mungu (1 Wakor 2:14); hatuwezi kabisa kumpendeza Mungu (Waeb 11:6); tunakuwa watumwa wa dhambi, dunia, mwili, na Ibilisi, hatuna kabisa uzima wowote ule, na tunapaswa ghadhabu ya Mungu na hukumu yake (Rum 6:16-17; Waef 2:1-3) (ona pia Edwards, 1984, Original Sin: 143-233; Owen 1979: passim).

6. Hata katika hukumu yake kwa Adamu na Hawa, Mungu alidhihirisha neema yake.

a. Alitengeneza mavazi ya kuwatosha ya ngozi ya wanyama ili kuwavika Adamu na Hawa (Mwa 3:21).

b. Ingawaje Mungu alimfukuza Adamu na Hawa kutoka bustanini (Mwa 3:22-24), hakuuondolea uwakili wao juu ya hii dunia (k.m., Mwa 2:15 na 3:23). Bila shaka, kufukuzwa kwao kutoka bustanini kulisaidia kukamilika kwa mpango wa Mungu wa mwanadamu kuijaza na kuimiliki dunia (Mwa 1:28).

c. Katika Mwa 3:15 alitoa tamko la kwanza la mpango wake wa wokovu kwa dunia: “Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.” Mtu fulani kati ya uzao wa mwanamke (amekuwa akitajwa kama mzao wa Ibrahimu [Kristo]) atatoa pigo la kichwa na kuleta ushindi kwa Shetani msalabani, wakati Shetani atamponda kisigino, au kumsababisha ateseke. Tamko hili limetekelezeka hatua kwa hatua katika Biblia nzima yote. Bila shaka, tamko hilo, likijumuishwa na swala kwamba Adamu na Hawa wasile kutoka katika mti wa uzima (Mwa 3:22), kuliwahakikishia kuwa wasingeweza kuishi milele wakiwa katika dhambi. Badala yake, kama Mungu alivyofunua hatua kwa hatua mpango wake, wale waishio kwa imani katika Kristo wataweza kula kutoka kwenye mti wa uzima katika nchi mpya milele katika haki (Ufu 22:2).

C. Matokeo ya Anguko—kutoka kwa Kaini hadi Mnara wa Babeli (Mwanzo 4-11:26).

“Baada ya Adamu na Hawa kutenda dhambi, uzao uliowafuatia uliendelea kuitawala dunia. Tatizo halikuwa kama walikuwa hawatawali. Kinyume chake, Mwanzo 4 panaonyesha michango yao katika ubunifu wa muziki, ufuaji vyuma, ufugaji, ustadi wa ujenzi, na siasa (‘Kaini akajenga mji, mst. 17). Tatizo kuu la mwanadamu mwenye dhambi halijawahi kuwa kukataa kwake kuitawala dunia. Tatizo lake kuu ni kwamba huitawala dunia katika namna isiyomcha Mungu. Mwanadamu huyu wa asili ya ki-Adamu hutawala ili kujifanyia jina mwenyewe, siyo kwa kulitukuza jina la Bwana. Wanadamu wadhambi hujaribu kutawala wakati wao wenyewe ni watumwa wa dhambi na Shetani. Mungu aliwaumba Adamu na Hawa ili wajenge nakala ya ule Mji Wake hapa duniani. Wazao wao wakajenga mji uliopotoka wa Mwanadamu.” (Leithart n.d.: n.p.)

1. Kaini na uzao wake (Mwa 4:1-24).

a. Kwa Kaini twaona kuongezeka kwa dhambi: kukufuru (4:3); hasira (4:5); wivu, udanganyifu, na mauaji (4:7-8); uongo (4:9); kujitafutia binafsi na kujihurumia (4:13-14); kukengeuka kutoka kwa Mungu (4:14, 16). Kuongezeka kwa dhambi pia kunaonekana kwamba Kaini siyo tu hakumuua kila mtu, bali alimuua ndugu yake mwenyewe ambaye alikuwa mtu “mwenye haki” (Math 23:35; Waebr 11:4). Pia, hata hivyo, angalia neema ya Mungu kwa Kaini katika kumlinda ili asiuawe na ndugu zake wengine wa kike na wa kiume (Mwa 4:15).

b. Uzao wa baadaye wa Kaini, Lameki (4:18-19, 23-24) apelekea uharibifu kimaadili kuwa kiwango cha chini kabisa: ana kiburi na majivuno; ageuza mgongo wake kwa mpango wa Mungu wa mke moja (Mwa 2:23-24; Math 19:3-6). Wake wengi siyo mpango sahihi wa Mungu. Katika Biblia kuwa na wake wengi mara zote kumeonekana kuwa siyo sahihi, na kuliongoza kuletesha matokeo mabaya. Kwa hiyo, haishangazi kwamba hata aliyeanzisha kuwa na wake zaidi ya moja, Lameki, ni mtu mkali aliyejipatia uhuru wake kamili kutoka kwa Mungu kwa kuua watu kwa visasi vya maswala madogo madogo na kudai haki ya Mungu ya kulipa kisasi (ona Kumb 32:35). Madai yake makali ya kutaka kulipa kisasi kwa wengine “mara sabini na saba” (Mwa 4:24) hupata mkondo mwenza katika kauli ya Kristo kuwa tunatakiwa kuwasamehe wengine “mara sabini na saba” (Math 18:21-22).

2. Tangu Seti hadi Nuhu (Mwa 4:25-6:8).

a. Moja ya sifa kuu za kitabu cha Mwanzo ni matumizi ya vichwa vinavyofanana katika kutambulisha simulizi na vizazi ambavyo hubadilishana katika Kitabu kizima. “Hivyo hutokea katika 2:4; 5:1; 6:9; 10:1; 11:10, 27; 25:12, 19; 36:1, 9; 37:2. Kitu kinachofanana kote katika vichwa hivi vyote ni neno la Kiebrania [Toledot—ambalo kikawaida hutafsiriwa kama “kizazi (vizazi); uzao; hesabu; orodha; kumbu-kumbu”]. . . . Hivyo vichwa [Toledot] hutenda kazi mbili. Kwanza, huwa kama vichwa vya sura katika vitabu vya kisasa. Baadhi yao hutambulisha sehemu kuu za simulizi, kuonyesha hatua mpya ya kukua kwa mpango. . . . [Pili, hivyo vichwa vya Toledot] hukazia mtazamo wa msomaji kwa mtu maalum na watoto wake aliowazaa. Humwezesha mwandishi wa Mwanzo kufuatilia mema ya mkondo mzima wa familia kuu pasipo kulazimika kufuatilia kwa kina maisha ya ndugu zao wengine.” (Alexander 1993: 258, 259)

b. Kuanzia Mwa 4:25 mpango wa kitabu unageukia mkondo wa Seti. Kwa hiyo, hivyo Toledot vya Adamu, kuanzia Mwa 5:1 hukazia kwa Seti na kIsha kwa wazao fulani wa Seti. Biblia hufanya hilo kwa makusudi, kwa sababu watu inaowakazia ndio kitovu cha kuanikwa wazi kwa simulizi nzima.

c. Hivyo Toledot vya Adamu pia ni muhimu kwa sababu nyingine:baada ya kutaja kizazi cha kila mtu na uzao wake muhimu, mara nyingi hurudia kwa kuhitimisha, “naye akafa” (Mwa 5:5, 8, 11, 14, 17, 20, 27, 31). Hilo husisitiza madhara ya “laana” ambayo ilitokana na dhambi ya Adamu (ona Mwa 2:17; 3:19). Ingawaje watu kabla ya gharika kuu waliishi miaka mingi zaidi kuliko waishivyo leo, kila moja wao alikumbana na mauti kwa sababu kila moja alikuwa ni wa mfano na umbo la Adamu (Mwa 5:3)—m.y., ana dhambi ikaayo ndani. Tofauti moja ni Enoki (Mwa 5:21-24). Si kwamba Enoki hakuwa na dhambi ikaayo ndani (kama watu wengine walivyo, naye alikuwa vivyo). Isipokuwa, kule “kumtwaa” Enoki kulikuwa udhihirisho mwingine wa neema ya Mungu kwa sababu alikuwa “ametembea na Mungu” kama mcha Mungu.

d. Hivyo Toledot za Adamu pia zindhihirisha kuporomoka kwa uanadamu kupitia dhambi. Huanzia na Adam katika hali ya baraka za Mungu (Mwa 5:1), na kumalizikia na huzuni ya Mungu kwamba alimfanya mwanadamu, na uamuzi wake wa kuisafisha dunia kuondosha wanadamu, kwa sababu “kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote” (Mwa 6:5-7). Hata hivyo, mtu moja, Nuhu, alipata neema machoni pa Mungu na kwa yeye likapatikana tumaini kwa wanadamu (Mwa 6:8).

3. Nuhu na Gharika (Mwa 6:9-9:29).

a. Sehemu hii ni moja yenye mlinganisho.Huanzia na hukumu ya Mungu kwa dunia (Mwa 6:11-13), lakini huishia kuweka agano na viumbe vyote vilivyo hai kwamba hataangamiza dunia kwa gharika (Mwa 8:21-9:17). Kwa upande mwingine, sehemu hii huanza na Nuhu kutajwa kama “mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu [ambaye] alikwenda pamoja na Mungu. Mwenye haki, mtu mkamilifu nyakati zake” (Mwa 6:9). Huishia na Nuhu kulewa na kumlaani Kanaani (Mwa 9:20-27). Alama moja ya sifa ya ukweli kuhusu Biblia ni kwamba haionei haya kuelezea dhambi hata za watu ambao ni mshuhuri sana.

b. Simulizi ya gharika, inakwenda sambamba na simulizi za uumbaji wa awali, na huishia “uumbaji ” wa dunia: “Dunia inakaliwa na watu kwa kutenganisha ardhi na maji (Mwa. 8:1-3; pia Mwa. 1:9-10). Viumbe hai vinatolewa ili kuijaza upya dunia (Mwa. 8:17-19; pia Mwa. 1:20-22, 24-25). Siku na majira zarejezwa upya (Mwa. 8:22; pia Mwa. 1:14-18). Wanadamu wabarikiwa na Mungu (Mwa. 9:1; pia Mwa. 1:28a), wanaagizwa ‘Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi.’ (Mwa. 9:1b, 7; pia Mwa. 1:28b), na kupewa mamlaka juu ya wanyama wote (Mwa. 9:2; pia Mwa. 1:28c). Mungu awapa wanadamu—walioumbwa kwa mfano wake (Mwa. 9:6; pia Mwa. 1:26-27)—chakula (Mwa. 9:3; pia Mwa. 1:29-30).” (Williamson 2007: 61) Hata hivyo, kuna tofauti moja muhimu kati ya dunia iliyofanywa upya baada ya gharika, na ile ya uumbvaji wa mwanzo: kuwepo kwa dhambi ya mwanadamu.

4. Agano alilolifanya Mungu na Nuhu (“Agano la Nuhu,” Mwa 8:21-9:17) ni agano la kwanza kutajwa wazi katika Biblia. Katika Agano hili “Mungu alionyesha neema ya rehema zake kwa wanadamu wote, wote –waliokombolewa na wasiokombolewa. . . . Alidhihirisha kutokubali kwa dhambi ya mwanadamu kutopangua mpango wake aliouandaa katika Mwanzo 3:15, kutokubali kwa dhambi ya mwanadamu kutotangua agizo lililotolewa kabla ya anguko la ‘Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi.’” (Busenitz 1999: 182). In Mwa 8:21 Mungu anautazama upungufu wa mwanadamu kama sababu ya rehema zake, kama vile mwanzoni aliuona kama sababu ya hukumu yake (Mwa 6:5-7). Isingalikuwa rehema na neema za Mungu katika kufanya upya agano lake na Nuhu, basi mwanadamu angelikuwa anaelekea kuangamia tena, kama vile ilivyotokea wakati wa gharika kuu. “Umuhimu wa kitheolojia wa Agano la Nuhu ni wa namna angalau mbili. Kwanza kabisa, ni msingi kwa ujasiri wetu wa sasa kwa Mungu kama mhimili. Ni Agano la Nuhu ndilo linalotupatia uhakika kwamba Mungu ataudhibiti utaratibu wa viumbe, licha ya machafuko na fujo zinazoendelea kutishia kulimeza. . . . [Pili] Agano la Nuhu linatoa mpangilio wa theolojia ya Ki-Biblia ambao ndani yake maagano yote ya ki-Ungu yanayofuatia yanatenda kazi.” (Williamson 2007: 67-68)

5. Orodha ya mataifa (Mwa 10:1-32) na Mnara wa Babeli (Mwa 11:1-9).

a. Orodha ya mataifa (Mwa 10:1-32) huenda ilifuatia Mnara wa Babeli (Mwa 11:1-11:9) katika historia, kuanziai misemo ya awali na magawanyiko na kutawanyika kwa mataifa mbali mbali kulingana na lugha zao. Mwandishi wa Mwanzo huenda aliweka habari hii kwanza kwa sababu ya kiuandishi: hufuatilia juu ya historia za Shemu, Hamu, na Yafeti kuanzia mwisho wa Mwanzo 9; huonyesha kwamba, kwa vile watu wote duniani ni wazao wa kutokea kwa Nuhu kupitia Shemu, Hamu, na Yafeti, watu wote ni wa “damu” moja na hatimaye kuwa wa familia moja; hufanya kazi kama utimilizo wa agizo la ki-Ungu katika Mwa 9:1, na huonyesha kwamba kutawanyika kwa mataifa kwaweza bila shaka kutathiminiwa kiuzuri tu kama hasi na pia chanya (m.y., hukumu ya Mungu katika Mwa 11:9).

b. Mnara wa Babeli (Mwa 11:1-9) kwaonyesha upotofu wa watu ulieendelea kinyume na Mungu. Jukumu la awali alilotoa Mungu kwa mwanadamu lilikuwa “kuijaza dunia” (Mwa 1:28). Alirudia agizo hilo kwa Nuhu na wanawe katika Mwa 9:1. Hata hivyo, licha ya hukumu ya Mungu ya Gharika kuu, bado tena wanadamu wakamwasi Mungu kwa dhahiri: Watu wanaamua siyo kuijaza dunia, bali kukaa mahali pamoja. Zaidi ya hayo, wanataka kujenga mnara kufika mbinguni ili kuliinua jina lao wenyewe na kuwa kama Mungu (kwa mara nyingine, kama ile dhambi ya Adamu). Kusema ukweli, “uasi wa Babeli ulikuwa ni uharibifu mbaya zaidi kuliko ule uliosababisha gharika; ulikuwa wa dunia nzima na ulikuwa umepangika. Ule mji, na minara yake ikiwa imefika mbinguni ulikuwa ni mbegu ya yule nyoka kumwangusha Mungu Aliye hai kama mfalme.” (Klooster 1988: 147) Matokeo yake, Mungu“alizichafua lugha zao” na “akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote” (Mwa 11:7-8). Maelezo haya hudhihirisha kiwango cha udhambi wa mwanadamu. Kulingana na msimamo wa kiuandishi, humwachia msomaji kutafuta jawabu la mwanadamu kuendelea na dhambi na uasi kwa Mungu.

6. Vile Toledot vya Shemu (Mwa 11:10-26). Baada ya Babeli, Biblia hukazia mkondo wa Shemu, ambao wote wawili- Nuhu na Mungu walivibariki. Toledot hizo hutupeleka kwa Ibrahimu, ambaye Mungu atamwita ambaye kwa kupitia yeye, Mungu atatekeleza mpango wake kukomboa na kuibariki dunia.

III. Tukio la Ukombozi— Mungu aita Watu Kwa Ajili Yake Mwenyewe (Mwa 11:27-Ufu 20

A. Mwanzo mpya wa Mungu—tangu Ibrahimu hadi Yusufu (Mwa 11:27-50:26).

1. Katika sehemu hii ya historia ya Biblia, Mungu sasa anamchagua mtu moja (Ibrahimu) ili kuanza mpango wake maalum wa ukombozi wa dunia. “Licha ya uasi wa wanadamu, Mungu hauachi mpango wake kwa dunia yake. Kama miaka Elfu mbili kabla ya Yesu, Mungu anauanzisha mpango utakaoleta kuponywa tena kwa dunia. Mpango huu ulioahidiwa una sehemu mbili: kwanza, kutoka katika jmii hii ya watu walio waasi, Mungu atamchagua mtu moja [Ibrahimu]. Mungu atamfanya mtu huyu kuwa taifa kuu na kulipatia taifa hilo nchi na kuwabariki. Pili, Mungu atapanua uwigo wa baraka hizo kwa mataifa yote (Mwa 12:1-3; 18:18).

Sehemu iliyobakia ya kitabu hicho cha Mwanzo hufuatilia miinuko na mabonde ya ahadi hii yenye pande mbili. Ahadi inatolewa siyo tu kwa Ibrahimu bali hata kwa mwanaye Isaka (Mwa 26:3-4) na kwa mwana wa mwana wake Yakobo (Mwa 28:13-15). Hatari nyingi zinahatarisha ahadi ya mpango wa Mungu kadri unavyoendelea: utasa, na kutokuzaa,wafalme wa kigeni na maharimu, mikasa ya kimaumbile, kushambuliwa na watu wanaowazunguka, na kutokuamini kwa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, wenyewe. Kupitia hayo yote, anajionyesha mwenyewe kuwa ‘Mungu Mwenyenzi (Mwa 17:1; Kut. 6:3), Yeye aliye na uwezo wa kutekeleza mpango wake.

Akiwa anakaribia mwisho wa maisha yake, Yakobo anawasafirisha wana wake kumi na mbili na familia zao kwenda Misri ili kuziokoa na njaa. Kisa kinachotia mhimili cha mtoto wake wa kumi na moja, Yusufu, kinaonyesha uaminifu wa Mungu na udhibiti wake wa historia anapoweza kuhifadhi watu ambao kupitia hao atauleta wokovu kwa dunia (Mwa 45:5; 50:20).” (Bartholomew and Goheen n.d.: 2)

2. Mungu afanya Agano na Ibrahimu (“Agano la Ibrahimu,” Mwa 12:1-3; 13:14-17; 15:1-21; 17:1-21; 22:15-18), ambalo linathibitishwa kwa Isaka, mwana wa Ibrahimu (Mwa 26:1-5, 24) na kwa Yakobo, mwana mdogo wa Isaka (Mwa 28:3-4, 13-15; 35:11-12).

a. Agano la Ibrahimu kama lilivyoanzishwa awali, na kisha kuimarika kwa jinsi tofauti katika Mwanzo lina “kamba tatu za ki-ahadi” kimsingi: utekelezaji ki-uzao (m.y., ahadi zihusianazo na “uzao”); mipaka ya kitaifa (m.ya ahadi zinazohusiana na “nchi (ardhi)”); na baraka za dunia nzima ahadi zinazohusiana na baraka kwa watu wengine kupitia uzao wa Ibrahimu) (Williamson 2000: 100-01; pia ona, Kaiser 1978: 86; Essex 1999: 208; Reisinger 1998: 6; Williamson 2007: 82-90 [Williamson anaona maagano mawili yakifanywa na Ibrahimu, la kwanza katika Mwanzo 15 na la pili katika Mwanzo 17, hayo hutenda kazi pamoja kutimiza kusudio moja linalolengwa]). Wakati watu wa Babeli walitaka kufanya jina lao wenyewe liwe kuu (Mwa 11:4), kwa neema yake Mungu atalifanya jina la Ibrahimu kuu na kuibariki dunia kumpitia yeye. (Mwa 12:2-3).

b. Agano hili linajikunjua na kutimilizika kila mahali kote katika AK na AJ (bila shaka, ni kweli, uhalisi wa kiroho na hatima ya utimilifu wake unakutikana tu katika AJ). Agano limetendeka kihistoria kwa kuundwa na kuinuka kwa taifa la Israeli. Hasa baada ya mgawanyiko wa taifa la Israeli na utumwa wake, kutimizwa kwa agano hilo kunatajwa na manabii wakiiita “siku ya Bwana” ijayo. Utimilifu wa mwisho na wa kweli wa Agano unapatikana katika Kristo, kupitia Roho Mtakatifu. Kwa namna nyingi, bila shaka, Agano la Ibrahimu ni uti wa mgongo wa theolojia na ni mchoro wa ramani ya Biblia yote inayobakia. “Kwa hiyo, wakati Yahwe anamkusudia kimsingi Ibrahimu na taifa litakalotokana na yeye, hatimaye kuna kuhusishwa kiupana zaidi: ‘jamaa zote za dunia’ (Mwa 12:3 ESV) ambazo, kupitia Ibrahimu, pia zitabarikiwa. Kwa maneno mengine, mipango ya Mungu kwa Israeli siku zote ilikuwa ikiendana na kusudio lake kuu, mipango kwa jamaa za dunia yote.” (Williamson 2007: 84)

3. Kwa kupitia Yakobo, taifa la Israeli litaanzishwa. Ingawaje Ibrahimu na mkewe Sara walikuwa wazee na hawakuweza kuwa na watoto wao wenyewe, Mungu kimuujiza akawawezesha kupata mimba na kumzaa mwana, Isaka (Mwa 18:1-15; 21:1-8). Hilo lilidhihirisha kwamba Mungu alikuwa anaendesha mambo, kuhakikisha kwamba mpango wake na Agano alilolifanya na Ibrahimu litatimizwa. Wakati mke wa Isaka aitwaye Rebeka alipokuwa na mimba ya watoto mapacha, Bwana alimwambia kwamba, kiuhalisi, mataifa mawili yalikuwa ndani yake na kwamba mwana mkubwa (Esau) atamtumika mdogo (Yakobo) (Mwa 25:21-26). Mungu baadaye alilibadilisha jina la Yakobo kuwa Israeli (Mwa 32:24-32; 35:9-12). Kutoka kwa Yakobo (Israeli) yalipatikana makabila kumi na mbili ya Israeli (Mwa 30:1-24; 35:16-18, 22-27; 41:50-52; 49:1-28).

4. Mungu awapeleka watu wake Misri. Wana wa Yakobo walianza kuishi maisha yasiyofaa kama walivyofanya Wakanaani waliokuwa wanakaa nao (Mwa 34:1-31; 35:22; 38:1-26). Kama hilo lingeendelea, kusingekuwa na Israeli tena. Kwa hiyo, Mungu aliwahifadhi hao wateule wake kwa kuwaondoa kutoka Kanaani kwenda Misri kwa njia ya dhambi ya kaka za Yusufu, na haki ya Yusufu. Mungu pia aliitumia dhambi ya Yuda na mkwewe Tamari kama sehemu ya mpango wake jumla wa ukombozi (ona Mwa 38:12-19; Rut 4:18; Math 1:3). Kisa kumhusu Yusufu (Mwa 37; 39-50) kimsingi kinaonyesha jinsi Israeli walivyoingia Misri, na jinsi Mungu alivyokuwa akishughulikia mpango wake alioutangaza miaka mamia kadhaa nyuma (Mwa 15:13-14) kwa Ibrahimu. Kuwepo kwa Israeli Misri kuliandaa jukwaa kwa ajili ya Mungu kufanya hatua inayofuata katika mpango kabambe wa Mungu, wa kuwatoa.

5. Mungu hutenda katika historia (kikawaida kupitia matukio na matendo ya watu ambayo huonekana kwetu kama “ya kawaida” tu, na wala siyo matukio yapitayo ukawaida) kuhakikisha kwamba mpango wake unatekelezwa. Matukio mengi hutishia kuzuia ahadi za Mungu kuonekama kwamba hazitatimizwa tena. “Umuhimu wa vitisho vizuiavyo kutimizwa hutegemea ukweli kwamba ahadi huelekeza jinsi ya utimilizwaji wake kuweza kufanyika tu kwa kazi isiyo ya kawaida ya Mungu. Si kitu kilicho katika uwezo wa mwanadamu, wala si swala la matukio ya kikawaida.” (Goldsworthy 1991: 121)

6. “Mkondo wa ukinyume” (m.y., Mungu kuchagua wa umri mdogo, walio wadhaifu, wageni) ili kutekeleza mipango yake, inajitokeza kila mahali katika Maandiko. Neema ya Mungu na maamuzi yake ya Ki-Ungu huonyeshwa kila mahali katika sehemu hii: k.m., Seti juu ya Kaini (Mwa 4:25); Isaka juu ya Ishmaili (Mwa 17:18-19; ona Rum 9:6-9); Yakobo juu ya Esau (Mwa 25:23; ona Rum 9:10-13); Efraimu juu ya Manase (Mwa 48:8-21); Yuda juu ya ndugu zake wakubwa (Mwa 49:1-12). Hii inaonyesha kwamba Mungu hajali nguvu, umashuhuri, na utajiri ambao ulimwengu huwa unauthamini, lakini neema yake huchagua “wadogo kama hawa” (ona, Math 25:40, 45). Mungu hudhihirisha mkondo huu huu tena na tena: k.m., Musa juu ya Farao (Kut 2:1-14:31; Waeb 11:25-29); Israeli juu ya mataifa mengine (Kumb 7:7-8); Daudi juu ya ndugu zake wakubwa (1 Sam 16:1-13); Sulemani juu ya ndugu zake wakubwa (1 Waf 1:5-40; 1 Nyak 3:1-5); mwanamke mjane wa Sarepta juu ya wajane wa Israeli (1 Waf 17:9; ona Luka 4:25-26); Naaman Muashuri juu ya wakoma wa Israeli (2 Waf 5:1-14; ona, Luka 4:27). Yesu mwenyewe alikuwa mtu masikini na mtumwa wa wote (Math 20:25-28; Wafil 2:5-8). Kwa hiyo, anatuambia, “bali aliye mkubwa kwenu na awe kama aliye mdogo; na mwenye kuongoza kama yule atumikaye.” (Luka 22:26). Anasema, “Mtu atakaye kuwa wa kwanza, atakuwa wa mwisho kuliko wote” (Mark 9:35; ona pia Mark 10:42-44; Yoh 13:12-16). Anaongeza, “kwa kuwa aliye mdogo miongoni mwenu nyote, huyo ndiye mkubwa” (Luka 9:48). Anahitimisha, “Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.” (Math 18:4; ona pia, Mark 10:14-15).

B. Kuanza kwa taifa la Israeli—Kutoka Misri kwenda nchi ya ahadi (Kutoka-Kumbu-kumbu).

1. Katika hatua hii kuu ya Mungu kwa tukio la ukombozi, Israeli lafanyika taifa, na kupata uhuru wake kutoka utumwani huko Misri, kama matokeo ya uaminifu wa Mungu kwa Agano alilomfanyia Ibrahimu, Isaka, na Yakobo (Kut 2:24).

a. Kipindi cha miaka mia nne chapita kabla ya kurudia mwendelezo wa matukio. “Uzao wa Ibrahimu, sasa ujulikanao kama Israeli (jina ambalo Mungu ampatia Yakobo), unaongezeka idadi katika Misri. Bali mafanikio huleta matatizo ya aina yake yenyewe. Mfalme wa Misri aanza kuona jamii hii ndogo inayoongezeka kama tishio. Ili kuizima hatari inayojitokeza, Farao anawaingiza Israeli katika utumwa. Kitabu cha Kutoka kinaanzia wakati wa kilele cha kukandamizwa kwa Waisraeli katika Misri. Katika mazingira haya ya maumivu mazito na kongwa, Mungu anamchagua Musa kuwakomboa Waisraeli kutokana na utawala wa kikatili wa Misri ili Waisraeli waweze kurudi kwa Mungu. Katika mfululizo wa matukio ya kushangaza, mapigo kumi yanaleta hukumu ya Mungu kwa miungu ya Misri (Kut 12:12), na Israeli inaokolewa kimiujiza kutoka jeshi lenye nguvu la Misri pale walipokuwa wanavuka bahari ya Shamu. Mwishowe Israeli wanafika mahali ambapo wanakutana na Mungu—katika mlm. Sinai. Hapo, Mungu akutana na Israeli kwa jinsi ya kiajabu ya ngurumo na radi na moto. Kwa nini Mungu afanye yote haya kwa Israeli? Mungu anayo kazi kwa ajili yao kuifanya. Wanapaswa kuwa taifa na ufalme watakaotumika kama makuhani. Kazi yao ni kuwa kiungo cha baraka za Mungu kwa mataifa na kufanyika watu walio kielelezo kuwavuta watu wengine wote kwa Mungu (Kut 19:3-6). Huu ndio wito utakaoliunda taifa la Israeli kuanzia hapa na kuendelea: watapaswa kuwa mfano na kielelezo mbele za mataifa wakiufunua ule mpango mzuri wa awali wa Mungu wa muundo kwa maisha ya mwanadamu. Baada ya kuwapa kazi hii, Mungu anawapa sheria kuongoza maisha yao, na watu wa Israeli kuahidi kuishi kama watu wa Mungu walio waaminifu. Kisha Mungu anawaamuru kujenga maskani ambamo atakaa ndani yake. Kuanzia hapa na kuendelea, kila waendapo, Mungu ataishi akionekana kati kati yao.

Katika Mambo ya Walawi twaona jinsi Israeli wanavyopaswa kuishi katika ushirika na Mungu Mtakatifu. Kitabu cha Hesabu kinasimulia safari wa Israeli kutoka Sinai hadi Kanaani. Kwa bahati mbaya, kutokuamini kwa Israeli kunawagharimu kukaa miaka arobaini nyikani kabla ya kuingia Moabi, iliyo kando kabisa mwa nchi ya ahadi. Katika Kumbukumbu la Torati, kiongozi wa Israeli, Musa, anawaelekeza Israeli jinsi wanavyopaswa kuishi watakapoingia katika ile nchi ya ahadi. Israeli wanajiandaa kuingia nchi ya ahadi—wanaapizwa kuwa watu wa Mungu na kuwaonyesha mataifa yawazungukayo, kufahamu Mungu ni nani na hekima ya mpango wa uumbaji wake wa awali kwa maisha ya mwanadamu. Israeli wanavyojipanga tayari kwa kuingia, Musa anakufa na uongozi unahamia kwa Yoshua.” (Bartholomew and Goheen (n.d.: 2-3)

b. Mazungumzo kati ya Mungu na Musa yanaongoza sehemu hii ya Maandiko. Tendo la Mungu kwa niaba ya Israeli kulingana na Agano la Ibrahimu (Kut 2:24). Kwa Mungu kujifunua mwenyewe kwa Musa —“NIKO AMBAYE NIKO” (Kut 3:14)—Mungu kimsingi alikuwa anamwambia Musa kwamba, “Mimi ni wa kipekee, na kuhusu Mimi ni nani, hueleweka kutegemeana na nini nataka kukifanya” (ona, Kut 3:13-22). Sifa za Mungu na Tabia yake husimuliwa kwa dhati zaidi katika Kut 34:6-7. Musa mwenyewe anatawala katika AK, karibu 1/3 yake katika Kutoka. Licha ya mazungumzo ya karibu, ya binafsi, na ya kimuujiza aliyokuwa nayo Musa na Mungu kwa kipindi cha miaka 40, ilikuwa ni ukosefu wa Musa kutowakilisha tabia ya Mungu kikamilifu (wakati Musa alipopiga mwamba pale Meriba, badala ya kuuambia mwamba), ndiko kulikomzuia Musa asiwaingize kabisa Israeli katika nchi ya ahadi (Hes 20:8-13).

2. Kutoka kulikuwa ni tukio la kimaamuzi kwa Israeli ya AK.

a. Kutoka kulikuwa ni tukio la kihistoria, la kimwili ambalo liliwakilisha ukweli wa kiroho utendao kazi kwa watu wote wa Mungu katika historia yote. “Kila mahali katika Agano la Kale, kumiliki nchi kunawakilishwa kama kivuli cha uhalisi wa kuishi kama watu wa Mungu katika ufalme wake. Lakini hakuelezwi mkondo ulio wazi kabisa wa njia ya lazima ambayo kwayo kila mtoto wa Mungu anauingilia ufalme. Kwa sababu hii, uzoefu wa kipekee na usiokosewa wa ukombozi kutoka nguvu nje ya ulimwengu huu ilitakiwa.” (Goldsworthy 1991: 130-31) Kutoka pia ni hatua ya mwanzo ya lazima kukamilisha ahadi ya utaifa uliomo katika Agano la Ibrahimu.

b. Kutoka kulikuwa ni msingi wa Mungu kujifunua mwenyewe kwa Israeli. Mungu anasisitiza kutoka kabla na baada ya amri 10 (Kut 19:4-6; 20:2; Kumb 5:6, 15). Kwa umuhimu mkubwa, katika amri 10, neno la kwanza Mungu alisemalo kwa Israeli ni kuhusu neema yake katika kuwakomboa kutoka kifungoni. Ni baada tu ya hapo inakuja Sheria. Kutoka kulikuwa msingi kwa sikukuu ya Pasaka (Kut 12:1-27). Kulikuwa mara nyingi kukirejewa katika Zaburi (ona Zab 66; 77; 80; 81; 105; 106; 114; 135; 136). Kulitumiwa na manabii kuwaitia Waisraeli kurudi katika uaminifu wa kimaagano na Mungu, au kama onyo, au kutoka kwa Mungu (ona Isa 11:16; Yer 2:6; 7:22, 25; 11:4, 7; 16:14; 23:7; 32:21; 34:13; Hos 2:15; 11:1; 12:9, 13; 13:4; Amos 2:10; 3:1; 9:7; Mika 6:4; 7:15).

3. Agano la Mungu na Musa (“Agano la Musa [la Kale])” (Kut 19-24; ona 2 Wakor 3:14; Waeb 8), na Sheria ya Musa (Kut 20-23; Walawi 11-15; 18-20; 25:23-55; 27; Hes 5; 27:1-14; 36; Kumb 5; 12-13; 20-22; 24-25), mifumo ya dhabihu, hema ya kukutania, Sabato, sikukuu, ukuhani, sikukuu za kidini ambazo zilikuwa sehemu za ndani za Agano (Kut 23; 25-31; 35-40; Walawi 1-9; 16-17; 21-25:22; Hes 3-4; 6-10; 15; 18-19; 28-30; 34-35; Kumb 14-19; 23; 26), zilielezea taifa la Israeli hadi Kristo alipokuja na kuzikamilisha. Kwa njia ya Agano la Musa, Mungu aliitenga Israeli kando na mataifa mengine. Agano la Musa lililipita Agano la Ibrahimu kwa kuhakikishia uhifadhi wa Israeli, taifa lililo kizazi cha Ibrahimu, katika nchi. Pia lilirekebisha jinsi taifa la kimwili la Israeli lilivyotakiwa kuishi ndani ya Agano la Ibrahimu katika nchi. (ona Walawi 26:42). Kwa sababu lilifanya kazi ile, Agano la Musa lilikuwa tofauti ki-umuhimu na lile Agano la Ibrahimu na maagano ya baadaye katika Biblia kwa vile lilisisitiza wajibu wa mwanadamu kwa Agano (Israeli) katika namna ambazo maagano mengine hayafanyi hivyo. “Tabia ya pande mbili inaakisiwa katika muundo wa masharti yake (m.y; ‘Kama mtatii . . . ndipo . . .’ TNIV; pia, ESV) ya Kutoka 19:5-6” (Williamson 2007: 96). Ndipo, baraka na laana za Mungu zilifungamanishwa kiuhalisia moja kwa moja kupitia kutii au kutokutii kwa Israeli zile Sheria za Musa (ona Walawi 26; Kumb 4; 6-9; 11; 27-29). Kupitia njia zile za kiuhalisia, Mungu alikuwa anakusudia kuwafundisha Israeli kanuni ya kiroho kuwa, “Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wenu, ni mtakatifu” (Walawi 19:2; “takatifu” limetajwa mara 152 katika Walawi). Zaidi ya hapo, Agano pamoja na taasisi zilizoundwa kama sehemu zake, liliunda kanuni ambazo watu wadhambi waliweza kumkaribia Mungu kwa njia ya mpatanishi peke yake. Musa alifanyika kama mpatanishi kati ya Mungu na Israeli kule nyikani. Pale Sinai, ukuhani ulianzishwa. Mfumo wake na muundo wa hema ya kukutania pia kimwelekeo ulionyesha mpaka kati ya watu wadhambi na Mungu aliye mtakatifu, ambao wangeweza tu kupatanishwa kupitia dhabihu na ofisi ya mpatanishi na ukuhani.

C. Israeli ndani ya hiyo nchi (Yoshua-1 Samueli 7).

“Kitabu cha Yoshua kinatueleza jinsi Mungu anavyotimiza ahadi zake kwa Israeli ya kuwapa ile nchi. Bwana anawaongoza Israeli kuiteka nchi na kuwahukumu mataifa maovu yakaayo ndani yake, na kisha anaigawanya nchi kwa zile kabila kumi na mbili. Kitabu kinaishia kwa Yoshua kuwasihi Israeli kudumu waaminifu kama watu wa Mungu. Waamuzi kinaanzia na kutokutii kwa Israeli: wanakataa kupambana na kutokuamini na kuachana na ibada za sanamu katika nchi (Waamuzi 1). Mungu aja na hukumu ya ki-agano na kuwaambia Israeli kuwa sasa itawabidi waishi kati ya Wakanaani (Waamuzi 2). Waamuzi husimulia kisa cha kusikitisha cha jinsi Israeli inavyogeuka kutoka kwa Mungu na kuendelea kugeukia ibada za Wakanaani na mitindo ya kuishi kwao. Mungu mwishowe anawaachia Wakanaani na watu wengine wanaowazunguka kuwatawala na kuwakandamiza mpaka Israeli walipomlilia ili kuwasaidia. Na akawajibu kwa rehema, akiwainulia viongozi wa kijeshi, waitwao waamuzi, ili kuwaokoa. Katika kila mduara wa uasi, hata hivyo, hali inakuwa mbaya zaidi. Kitabu kinaishia na visa viwili vinavyoonyesha uasi wa Israeli na Israeli kulia daima kutaka kuwa na mfalme ili awaokoe na uharibifu huu. (Waamuzi 21:25).” (Bartholomew and Goheen n.d.: 3)

D. Israeli kama ufalme ulioungana (1 Samweli 8-1 Wafalme 11; 1 Nyakati 1-2 Nyakati 9; Zaburi-Wimbo ulio bora).

“Samweli ndiye mwamuzi mkuu wa mwisho, na pia ni kuhani na nabii. Vitabu vya Samweli, vilivyotajwa jina lake, huzungumzia badiliko kubwa ndani ya taifa la Israeli. Israeli wanamtaka Mungu awape mfalme ili wawe kama mataifa mengine (1 Sam. 8:5, 19-20). Kwa hiyo Mungu anamtumia Samueli kumteua Sauli [miaka 1050-1010 KK], na kisha Daudi [1010-970 KK], kama wafalme wa kwanza juu ya watu wake. Sauli ni mfalme aliyeshindwa, lakini Daudi anamtumikia Mungu kama mfalme mwaminifu, akiyashinda mataifa ya kipagani yaliyowazunguka, na kuiimarisha sheria ya Mungu, na kuhamisha makao ya Mungu kuja Yerusalemu. Hapa, kwenye kiini cha taifa, uwepo wa Mungu ni ukumbusho wa kudumu kwa Israeli kwamba Mungu ndiye mfalme wao wa kweli. Sulemani [970-930 KK], mwana wa Daudi na aliyetawala baada yake, analijenga hekalu kama mahali pa kudumu zaidi pa Mungu kukaa na kusikia sifa na sala za watu wake. Licha ya kupewa hekima kuu sana kutoka kwa Mungu, kule kuoa kwa Sulemani wanawake wa kigeni, na tamaa za miradi iliyokuwa inamsukuma sana inamfanya ajulikane kama mtesaji.” (Bartholomew and Goheen n.d.: 3) Daudi ndiye kiungo cha kati cha ufalme ulioungana. Ufalme wake huonyesha sura ya ufalme wa ki-Masiha yenyewe.

1. Kulikuwa na wafalme watarajiwa (Mwa 49:8-10; Kumb17:14-20) na wafalme kinyume (Waamuzi 8:22-23; 1 Sam 8:1-18) hujitokeza katika historia ya Israeli kabla hawajampata mfalwe wao wa kwanza. Hata hivyo, watu hao walimtaka mfalme ili “sisi nasi tufanane na mataifa mengine yote” (1 Sam 8:20). “Hili kiuhakika ni kukataa muundo wa Agano na, kwa hiyo kuukataa utawala wa Mungu (1 Sam 8:4-8)” (Goldsworthy 1991: 165). Huenda, kwa vile siku zote alikusudia kuwatawala kupitia mfalme, Mungu aliwapa haja waliyoitaka.

2. Mungu afanya agano na Daudi (“Agano la Daudi,” 2 Sam 7:8-17; 1 Nyak 17:3-15; ona 2 Sam 23:5; 2 Nyak 6:16; Zab 89:1-4, 28-29). Agano la Daudi linafanyika njia maalum ya Agano la Ibrahimu kuja kutimilizwa. Hata masharti yake yanagusia ahadi alizozifanya Mungu kwa Ibrahimu. Katika Agano hili (2 Sam 7) Mungu amwahidi Daudi: mst. 9—jina kuu (k.m. Mwa 12:2); mst. 10—mahali (k.m. Mwa 12:7; 13:14-17; 15:7, 18; 17:8); mst.11—utulivu kutoka kwa adui (k.m. Mwa 22:17); v. 12— “uzao” (k.m. Mwa 22:18); mist. 12-16—ufalme usio na mwisho na kiti cha enzi (k.m. Mwa 12:3; 13:15; 17:5-7). “Mwendelezo wa agano hili kwa lile agano la Ibrahimu kwaweza kuonekana katika mahitimisho yao. ‘Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu’ hujumuisha kusudio la Mungu katika agano na Ibrahimu na baada yake, na Israeli (Mwa 17:7-8; Walawi 26:12; Yer 7:23; 11:4; 30:22). Sasa ahadi kumhusu mwana wa Daudi, yeye atakayewakilisha wengi, yatolewa kama, ‘nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu’ (2 Sam 7:14). Kwa hiyo, mwana wa Daudi pia ni mwana wa Mungu, na nyumba yake, kiti chake cha enzi na ufalme vitadumu milele (2 Sam 7:16).” (Goldsworthy 1991: 167) Agano hili lilipata utimizwaji wake wa kwanza kwa mwana wa Daudi Sulemani, aliyelijenga hekalu katika Yerusalemu. Hata hivyo, licha ya “kutangulizwa kwa kivuli cha ‘baraka za mataifa’ wakati wa enzi za Daudi - Sulemani, ahadi hii ilisubiri utimizwaji wake wa mwisho. Historia ya kifalme ya Israeli inathibitisha kwa nini hilo liko hivyo. Licha ya wafalme wachache waliokuwa wanarejeza yaliyoharibika, hakuna hata moja wa uzao wa kifalme wa Daudi—kumchanganya na Daudi mwenyewe—aliyetekeleza kikamilifu mwongozo wa muhimu wa mahusiano ya Ki-ungu: mwenendo unaokubalika [ona 1 Waf 2:4; 6:12-13; 8:25; 9:4-9].” (Williamson 2007: 145) Mungu alikuwa ameahidi kubariki mataifa kupitia “uzao” wa Ibrahimu (Mwa 12:3; 22:18). Agano la Daudi huonyesha “ukoo wa kifalme ambamo ule “uzao” wa ushindi unaotarajiwa hatimaye utatokea. . . [lakini kwa sababu ya dhambi katika mlolongo wa Daudi] hatimaye ukategemea ufalme wa ki-Daudi ambaye atakuwa mzao wa Ibrahimu kwa kiwango kitimilifu kuliko vyote, na siyo tu kibayolojia (k.m. Zab. 72).” (Ibid.) Kwa hiyo, Agano la ki-Daudi lilionyesha mbele kumwelekea Yesu Kristo.

3. Fasihi za kihekima (Ayubu, Zaburi, Mithali, Mhubiri, Wimbo ulio bora). Ayubu kwa undani kabisa hutumia dhana ya kiulimwengu ya maumivu na mateso yasiyo haki kama ngazi ya kushughulika na ukuu wa Mungu juu ya mateso ya wanadamu na imani zao kwa Mungu mwenyewe wakiwa katika mtwango wa mateso yenyewe. “Tenzi za sifa [za Daudi], toba, na maelekezo (Zaburi, si zote zilitolewa na Daudi) ni za wakati wake, hata hivyo ni za nyakati zote kwa maelekezi ya kiroho na hivyo ni kitovu cha theolojia ya Ki-Biblia. Vivyo hivyo, hekima (iliyotolewa waziwazi na Mungu: 1 Waf 3:12) ya mwanaye Sulemani husimama pia kwa uzito unaolingana kama kitovu cha mhimili wa kazi za theolojia ya Ki-Biblia, ziitwazo fasihi za Kihekima.” (Yarbrough 1996: 64) Fasihi za kihekima huhusika na kiu na njaa ya maarifa, ufahamu, na uhusiano na Mungu na watu wengineo hapa duniani ambayo yote kwa pamoja yamevurugikwa kwa dhambi.

E. Israeli kama ufalme uliogawanyika (1 Wafalme 12-2 Wafalme17; 2 Nyakati 10-31; Isaya na Mika [vilitabiri kwa Israeli na Yuda]; Yoeli [alitabiri kwa Yuda]; Hosea na Amosi [walitabiri kwa Israeli];

Obadia [Alitabiri kwa Edomu]; Yona [alitabiri kwa Ninawi]).

“Wakati wa utawala wa mwana [wa Sulemani] Rehoboamu, roho ile iliyokuwa inasonga [iliyoanzia kwaSulemani] ikaletesha kugawanyika kwa taifa. Mengi ya makabila yakagawanyikia Kaskazini (Israeli), na kuacha nyuma makabila machache ya Kusini [m.y., Yuda na Benjamini, kujumlisha na baadhi ya watu kutokea makabila ya Kaskazini] (Yuda) [930 KK].

Tangu mwaka huo na kuendelea, sehemu hizo mbili zikawa na wafalme wao binafsi. Vitabu vya 1& 2 Wafalme na 1 & 2 Nyakati huelezea simulizi zao. Simulizi hizo ni kuporomoka kwa uelekeo wa uasi ulioongozwa na wafalme waliokuwa si waaminifu. Badala ya kuwa kielelezo kwa mataifa, watu wa Mungu wanausukumia mbali uvumilivu wa Mungu hadi kufikia kufukuzwa mbali na nchi ile. Mungu akatafuta njia ya kusimamisha njia zao mbaya kwa kuwainulia manabii kuwaonya warudi tena kwenye toba. Eliya na Elisha ndio manabii wajitokezao sana katika 1 & 2 Wafalme. Kupitia manabii hawa, Mungu anaahidi kama Israeli watarejea kwake, Mungu atawapa neema na ataendelea kufanya kati kati yao. Pia anaonya kwamba ikiwa Israeli wataendelea kuasi, atawaletea hukumu na hatimaye kuwapeleka uhamishoni. Kadri hali ya Israeli ianvyoendelea kuwa mbovu zaidi ya kutoponyeka, manabii wanaahidi kuwa Mungu hajashindwa. Kusema ukweli, Anaahidi kwamba atawaletea mfalme baadaye ambaye atauleta ufalme wa amani na haki. Mfalme huyo aliyeahidiwa atawezesha kusudio la Mungu la uumbaji.

Maneno ya manabii hao yaangukia katika masikio yasiyosikia. Kwa hiyo, kwanza, raia wa ufalme wa Kaskazini (722 KK na raia wa ufalme wa Kusini (586 KK.) watekwa uhamishoni na falme zilizokuwa zina nguvu zilizotawala enzi hizo [Israeli kwa Waashuri na Yuda kwa Babeli].” (Bartholomew and Goheen n.d.: 3-4)

F. Kuweko, kushuka, na kuanguka, kwa ufalme wa Kusini (2 Wafalme 18-25; 2 Nyak 32-36:21; Isaya-Danieli; Nahumu-Zefania).

1. Makabila mawili ya Kusini (Yuda) waenda utumwani Babeli. Yuda walifuata nyayo mbaya za wenzao Israeli wa Kaskazini. Kwa hiyo, ikahusuriwa, Yerusalemu ukaharibiwa, na taifa likapelekwa uhamishoni Babeli. “Hali ya uhamisho inawafadhaisha sana Israeli. Nini kilitokea kwa ahadi za Mungu na makusudio yake? Je alizitupilia mbali kabisa? Wakati wa uhamisho huo, Mungu aliendelea kusema nao kupitia manabii kama vile Ezekieli, akielezea ubaya huo umewajia na kuwahakikishia kwamba watarudi tena kwao.” (Bartholomew and Goheen n.d.: 4)

2. Kipindi chote cha historia ya Israeli, hasa wakati wa kipindi cha ufalme uliogawanyikana, na kisha kuendelea hadi wakati wa matengenezo ya ufalme wa Kusini, manabii walifanya sehemu muhimu ya kuwaitia watu warejee kwenye uaminifu kwa Mungu.

a. Manabii wa Mungu walitumia neno la Mungu wakati huo mgumu wa mahusiano ya kiagano kati ya Mungu na watu wake. Kazi kuu ya manabii wa AK haikuwa kutabiri mambo ya baadaye. Badala yake, manabii walinena nyakati hizo ngumu, na wote walikuwa na ujumbe na huduma iliyokuwa ina pande mbili kimsingi: (1) Wanawaonya watu wa Mungu juu ya maafa ya kutofuata njia za Mungu kwa tahadhari za matukio ya hukumu na (2) wanawaitia watu warudi kwenye uaminifu kwa Mungu kwa mausia ya matukio ya matumaini na wokovu. Manabii wote wa AK walihusika na kubadili mienendo ya tabia za watu. Ujumbe wao kiujumla ulikuwa, “Kama hamtafanya hivi, hukumu itawajia; kama mtamfuata Bwana, baraka zitawajia.” Ujumbe wao wa hukumu na wokovu ndio ulio na nguvu kwa vizazi vingi.

b. Kihistoria, mtu anaweza kuona mabadiliko ya msisitizo wa kinabii baada ya utumwa wa Israeli kule Babeli. Kabla ya uhamisho, manabii walielekea kusisitiza ukaidi wa Israeli. Baada ya utumwa msisitizo ukahamia kwenye wajibu wa watu wa Mungu kujiandaa kwa kuujenga kikamilifu ufalme wa Mungu.

3. Kabla ya uhamisho, manabii wakanena kuhusiana na dhana mbali mbali, zikiwamo:

a. Safari mpya. W