asili ya madhehebu katika uislamu

Download Asili ya Madhehebu katika Uislamu

If you can't read please download the document

Upload: alitrah-foundation

Post on 28-Mar-2016

5.390 views

Category:

Documents


2.151 download

DESCRIPTION

Suala la madhehebu lilianza kuzungumzwa na Mtukufu Mtume SAW mwenyewe katika hadithi zake tukufu: “Mayahudi walikuwa madhehebu sabini na tatu baada ya Nabii Musa AS, na Wakristo madhehebu sabini na mbili baada ya Nabii Isa AS, na Umma wangu huu utakuwa na madhehebu sabini na moja baada yangu, na (madhehebu) zote (zitaingia) Motoni isipokuwa moja.” Kutokana na kauli hii ya Mtume SAW ni kwamba suala la madhehebu haliwezi kuepukika, lazima madhehebu zitakuwepo bali changamoto moja tu iliyoko katika kauli hii ni kwamba madhehebu zote hizo zitaingia Motoni isipokuwa moja. Suala hapa sasa ni kufanya utafiti ili kujua ni madhehebu ipi hiyo itakayokuwa salama.

TRANSCRIPT

  • Asili ya Madhehebu katika

    Uislamu

    Kimeandikwa na:Isa Rwechungura

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page A

  • BAsili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page B

  • Haki ya kunakili imehifadhiwa na:AL-ITRAH FOUNDATION

    ISBN: 978 - 9987 - 512 - 88 - 1

    Kimeandikwa na:Isa Rwechungura

    Kimehaririwa na: Ramadhani Kanju Shemahimbo

    NaUstadh Abdallah Mohammed

    Kupangwa katika Kompyuta na:Hajat Pili Rajab.

    Toleo la kwanza: Januari, 2010 Nakala: 1000

    Kimetolewa na kuchapishwa na:Alitrah Foundation

    S.L.P. 19701 Dar es Salaam, TanzaniaSimu: +255 22 2110640

    Simu/Nukushi: +255 22 2127555Barua Pepe: [email protected]

    Tovuti: www.alitrah.orgKatika mtandao: www.alitrah.info

    C

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page C

  • Haki ya kunakili imehifadhiwa

    Ni lazima ipatikane idhini ya maandishi kwa Taasisi yoyote ya Kiislamuau Mwislamu anayetaka kuchapisha kitabu hiki kwa shughuli ya Tabligh.

    Idhini ya kufasiri kitabu hiki katika lugha nyingine yaweza kutolewa piakwa masharti ya kutuma nakala yake kwa mtungaji. Kitabu hikikimekusudiwa kwa wasomaji wenye kuzama katika kutafakari mambokwa undani, hali ya kuwa wako tayari kuiona haki na kuikubali, japo hakihiyo inatambuliwa na kukubalika na watu wachache. (Qurani: 6:116)

    Mwenye kupinga kila hoja kwa sababu ya ujinga wake, atabakia kipofuasiyeuona ukweli. - Mtume (s.a.w.w.)

    Saa moja ya kutafuta elimu ni bora mbele ya Mwenyezi Mungu kulikoibada ya miaka sitini. - Mtume (s.a.w.w.)

    Usingizi wa mtu mmoja mwenye elimu ni bora mbele ya MwenyeziMungu kuliko ibada ya usiku mzima ya kundi la wajinga elfu moja. -Mtume (s.a.w.w.)

    Tafuta elimu toka mberekoni hadi kaburini - Mtume (s.a.w.w.)

    Kusikiliza ukweli, sio kila sikio linafaa, kama vile chakula kwa kila ndegesi kimoja na kilekile. - Mshairi wa Kihindi: Rumi

    D

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page D

  • EYaliyomo Utangulizi ...................................................................................................3

    Maelezo juu ya mwandishi wa kitabu hiki na historia fupi ya utafitiwake..........................................................................................................17

    Asili ya Tofauti kati ya Suni na Shia Ithnashari.......................................22

    Utukufu wa Bani Hashim..........................................................................32Bwana Hashim.........................................................................................34Utamaduni wa Maquraishi........................................................................35Bwana Abdul Muttalib..............................................................................36Kisima cha ZamZam.................................................................................38Abraha ataka kuvunja Al-Kaaba..............................................................39 Je, Hao Ahlul Bayt wa Mtume Sa.w.w. ni Nani?....................................53Maneno ya Mtume (s.a.w.w) juu ya Ahlul Bayt wake.............................53Sifa za Ahlul - Bayt wa Mtume (s.a.w.w).................................................56Imam Hasan na Imam Husein (a.s)...........................................................56Bibi Fatma (a.s)................................................................................ .......57Msaada wa Allah kwa Bibi Fatma (a.s) katika shida................................57Ahlul - Bayt waletewa chakula toka Peponi...........................................58Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alikuwa akimheshimu sana Bibi Fatma.........59Kwa nini aliitwa Fatma Zahra?.................................................................60Ahlul Bayt (a.s) katika tukio la Mubahilah .............................................60Kisa cha Imam Hasan Al-Askari Imam wa 11 (a.s)................................63Kisa cha Imam Muhamad Mahdi (A.s) Imam wa 12...............................66Utoto na Ujana wa Imam Mahdi (a.s)......................................................70

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page E

  • FImam Mahdi (a.s) katika kasri (Ikulu) ya Khalifa Mutamid...................73Asili ya elimu za kidunia na maendeleo ya Kisayansi.............................90Jinsi Elimu za Kiislamu zilivyoleta maendelea ya Sayansi huko Ulaya..93Uchanganyaji madawa (Pharamacology)..................................................93Hospital.....................................................................................................93Kemia (Chemistry)...................................................................................93Barabara za kisasa (paved Roads)............................................................94Hisabati (Mathematics).............................................................................94Abdul -Wahid Muhammad Ibn kushd.....................................................100Abu Husein ibn Al-Haitham ..................................................................101Abu ali Al-Husein Ibn Abdullah Ibn Sina............................................ 102Abu Adullah Al-Battani..........................................................................103Jabor Ibn Hayyan ...................................................................................104Abu Rahman Muhammad Al-Biruni...................................................... 105Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abdallah Ibn Idrisi (1099-1166A.D).105Kwa nini Hatusikii majina ya wanasayansi maarufu wa Kiislamu........106Sifa za peke a Ahlul - Bayt wa Mtume (s.a.w.w)...................................106Hotuba (wasia) kamili ya mtume (s.a.w.w) pale Ghadir Khum na ushahidikamili wa tuko hilo ................................................................................108Mwisho wa Khutba ................................................................................126Kwa nini wasia wa Mtume (s.a.w.w) ulipuuzwa?..................................128Hoja za Sunni kuhusu uongozi wa Waislamu baada ya Mtume(s.a.w.w)................................................................................................. 137Jeshi la Usamah bin Zayd.......................................................................143Alipokaribia kufariki Mtume (s.a.w.w) hadi kufa kwake..................... 145Mkutano wa Saqifah ban Saidah ......................................................... 151Demokrasia au Shura?........................................................................... 158Bibi Fatima (a.s.) kunyanganywa Urithi wake Fadak......................... .191Kufutwa zaka ya Khums....................................................................... .193

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page F

  • Utawala wa Umar ibn al- Khattab .........................................................194Kuhusu udhu wa Tayamam.....................................................................197Taraweh kuswaliwa jamaa......................................................................197Umar atoa hukumu bila ujuzi na hivyo akakosolwa na Imam Ali (a.s).200Talaka tatu kwa mpigo...........................................................................202Ndoa ya Muda Maalum (Mutah)...........................................................204Faida ya unyago katika ndoa zetu...........................................................216Wanawake wajane...................................................................................219Kanuni za ndoa ya Mutah......................................................................223Tamko la ndoa (ndoa zote) .................................................................. 223Idhini ya Baba au Babu na mke (Ndoa zote)..........................................224Mashahidi (kwandoa zote)..................................................................... 225Utawala wa Uthman ibn Affan ..............................................................230Waislamu wanamtaka Imam Ali ibn Abu Talib kuwa Khalifa. wao..... 242Sababu za kuuwawa Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s) ................................269Ulul-amr ni Nani? Quran 4:59...............................................................275Muawiyah Anyakua Ukhalifa.................................................................295Muawiya amwachia urithi wa Ukhalifa mwanawe Yazid......................307Je, ili Muislamu Suni inabidi kuamini Nini?..........................................320Dini siyo nadharia popote Dogma bali ni Tauluma ..............................330Deni siyo nadharia potofu DOGMA bali ni Taaluma...........................336Asili ya tofauti katika ibada kati ya Shia na Sunni.................................356

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page G

  • NENO LA MCHAPISHAJI

    Kitabu kilichoko mikononi mwako kinaitwa, Asili ya Madhehebu katikaUislamu, kilichoandikwa na Ndugu Isa Rwechungura kwa lugha yaKiswahili.

    Maudhui kubwa katika kitabu hiki ni kuhusu madhehebu za Kiislamu.Suala la madhehebu limekuwa na bado halieleweki vizuri miongoni mwaWaislamu kiasi kwamba wakati mwingine hufikia kupigana na kuuanakutokana na kuzozana juu ya suala hili.

    Suala la madhehebu lilianza kuzungumzwa na Mtukufu Mtume SAWmwenyewe katika hadithi zake tukufu: Mayahudi walikuwa madhehebusabini na tatu baada ya Nabii Musa AS, na Wakristo madhehebu sabini nambili baada ya Nabii Isa AS, na Umma wangu huu utakuwa na madhehe-bu sabini na moja baada yangu, na (madhehebu) zote (zitaingia) Motoniisipokuwa moja. Kutokana na kauli hii ya Mtume SAW ni kwamba sualala madhehebu haliwezi kuepukika, lazima madhehebu zitakuwepo balichangamoto moja tu iliyoko katika kauli hii ni kwamba madhehebu zotehizo zitaingia Motoni isipokuwa moja. Suala hapa sasa ni kufanya utafitiili kujua ni madhehebu ipi hiyo itakayokuwa salama, na sio kugombanakwa jambo ambalo lilikwishatabiriwa na Bwana Mtume mwenyewe - nahiki ndicho alichofanya mwandishi wa kitabu hiki.

    Wafuasi wa madhehebu nyingine wanaweza kuchambua uthibiti wa kitabuhiki ili kujenga maoni yao wenyewe kuhusu mtazamo mzuri wa mtumwenyewe. Ni muhimu mtu kuelewa hoja za wale ambao hakubaliani nao.Inaweza ikasemwa kwamba wale ambao hawaelewi kabisa mtazamo wamaoni tofauti, hawaelewi kwa ukamilifu mtazamo wa kwao wenyewe.

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page H

  • Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wamaendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, nganoza kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tenakatika akili za watu.

    Shukurani zimuendee mwandishi wa kitabu hiki, tunamwomba AllahMwenye uhai wa milele, amjaalie umri mrefu, amruzuku ilmu na fahamuili aweze kufanya tafiti nyingine zaidi, Insha-Allah.

    Tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadikufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

    Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni changamoto kubwakwa wasomaji wetu.

    Mchapishaji:Al-Itrah FoundationS. L. P. 19701, Dar-es-Salaam.

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page I

  • BISMILLAHIR-RAHMANIR-RAHIYM

    LENGO KUU LA KUANDIKA KITABU HIKI

    Sababu kubwa ya kuandika kitabu hiki ni kuwaeleza Waislamu au mtuyeyote anayetaka kufahamu Uislamu asilia, kuhusu hotuba (Wasia) ndefualiyotoa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mnamo mwezi 18, Mfunguo Tatu,Mwaka 10 A.H. (632 A.D.), mahali paitwapo Ghadir-Khum wakati aki-tokea Hijja yake ya mwisho, miezi mitatu tu kabla hajafariki. Hotuba hiyoambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliitoa mbele ya Masahaba wapatao140,000, inaeleza wazi Uislamu ulivyotakiwa kuendeshwa baada yake,kinyume kabisa na hali halisi iliyofuatia mara tu alipofariki hadi wakatihuu! Jambo la maana ni kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika hotubahiyo alituamrisha Waislamu kila atakayeisikia, ni wajibu kwakekumweleza asiyewahi kuisikia hadi Siku ya Kiyama.

    Kwa hiyo mimi nimetimiza wajibu wangu kwenu na nimeeleza pia histo-ria juu ya sababu zilizosabibisha Wasia huo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)kupuuzwa. Kimsingi naomba ieleweke kuwa mimi simlazimishi aukumshawishi Mwislamu yeyote aipokee hotuba hiyo tukufu. Ni juu ya kilammoja wetu kuamua atakavyo baada ya kusoma kitabu hiki. Yaliyoelezwakatika kitabu hiki ni uchambuzi wa kisayansi na siyo unganganizaji waimani. Hotuba kamili ipo ndani ya kitabu hiki Sura ya 3.

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page J

  • KJINSI YA KUTUMIA KITABU HIKI

    Ili uweze kupata haraka moja kwa moja somo unalotaka, fungua mwishoni- Sura ya 22 ambapo utakuta orodha ya masomo muhimu yaliyomokitabuni na kurasa zake.

    Isa RwechunguraMtungaji

    MAPITIO

    Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

    Ee Allah! Mteremshie baraka zako Bwana wetu na Rasuli wetuMuhammad Mustafa na Dhuria wake uliowatoharisha na ukawateua kuwaviongozi wetu na ukatufaradhisha kuwapenda, kuwatii na kuufuata mwon-gozo wao.

    Alhamdulilahi nimekipata na kukisoma kitabu hiki: ASILI YA MADHE-HEBU KATIKA UISLAMU. Namshukuru Allah (s.w.t.) kwa kumweze-sha ndugu yetu Isa Hamisi Rwechungura kukiandika kitabu hiki, na kutu-tanabaisha watu wa dini zote kwa ujumla kutokana na ukweli kwambaMungu ni mmoja na kwa hiyo dini inapaswa kuwa moja tu. Kwa upandemwingine, Waislamu wa wakati huu, kwa kukosa elimu ya dini ya kutosha,tumeichukulia dini kimzaha tu, kwa misingi ya kurithi imani mbali mbaliambazo baadhi yake ni upotofu.

    Hata hivyo siku hizi wapo Waislamu wengine ambao wanaitumia dini kwamanufaa yao ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Ndugu zetu hao hatuna hajaya kuwaeleza kwa sababu wao wanaishi kwa ajili ya dunia tu, na hawaonifaida kubwa za kiroho ambazo wangezipata huko akhera.Ama kwa wale ambao, kwa nia njema kabisa, wanayo shauku ya kutaka

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page K

  • Lkujua ukweli wa dini, kwa misingi ya mafunzo sahihi, lakini wanashindwakuupata ukweli kutokana na wingi wa dini na madhehebu, na kila dini aumadhehebu inadai ndiyo ya kweli, basi kitabu hiki kitawapa mwangazamkubwa na kuwafikisha kwenye Uislamu wa kweli, ili mradi wazingatiehoja zilizomo na wasiwe na jazba au ushabiki, iwapo hoja hizi zitatofau-tiana na itikadi zao. Jambo la msingi ni kuufikia ukweli kwa ajili ya kumtiiMwenyezi Mungu.

    Zaidi ya hayo ningependa kumshauri msomaji wa kitabu hiki, kabla yakuanza kukisoma, azingatie yafuatayo ili aweze kupata faida iliyokusudi-wa.

    1. Kujua faida na umuhimu wa dini

    Ni lazima binadamu yeyote atambue kuwa ameumbwa na MwenyeziMungu, na kwamba anatakiwa kuishi duniani chini ya amri au mamlaka yaMuumba wake. Isitoshe ni lazima kila mtu afahamu kuwa kuna maisha yaduniani ambayo ni mafupi sana, na kisha kuna maisha ya akhera yasiyo namwisho. Ubora wa maisha ya akhera utategemea utiifu kwa MwenyeziMungu hapa duniani. Kwa hiyo mtu yeyote ambaye anajenga imani poto-fu za dini na kuzitumikia uhai wake wote hapa duniani, hatapata chochotehuko akhera ila kuangamia tu! Kwa maana hiyo, dini ya kweli lazimaijengeke juu ya hoja imara za kisayansi na siyo katika misingi ya kurithitoka kwa babu zetu, au kujenga imani tu isiyoweza kuthibitika kimantiki.

    2. Jukumu la kuitafuta dini ya kweli ni la kila mtu peke yake.

    Ni jukumu la kila mtu kutafuta dini ya kweli ili aweze kutimiza wajibuwake wa kumtii Mwenyezi Mungu. Mbele ya Mwenyezi Mungu kila mtuatahukumiwa peke yake kwa sababu ya kupewa akili. Maana yake nikwamba hakuna mtu atakayedai kuwa alipotezwa na wazazi wake au kion-gozi wake wa dini au kundi fulani la watu.

    Nikifafanua zaidi ni kwamba binadamu tumepiga hatua kubwa katika

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page L

  • Msayansi na teknolojia kwa sababu ya kutumia akili. Tunatakiwa tutumieakili hiyo hiyo kutambua dini ya kweli, la sivyo tutahukumiwa. Lazimatutambue tofauti kati ya binadamu na mnyama, nayo ni akili. Huwezikumpeleka ngombe mahakamani kwa kula mazao yako shambani kwaningombe hana akili. Badala yake atashitakiwa yule mmiliki wa ngombehuyo. Kwa hiyo iwapo binadamu atatarajia msamaha kwa yeye kutotumiaakili aliyopewa, atakuwa anajilinganisha na mnyama, na hilo halitakubali-ka mbele ya Mwenyezi Mungu.

    3. Kujua kuwa Mungu ni mmoja na Uislamu ni mmoja tu

    Baada ya maelezo hayo juu ya umuhimu na ukweli wa dini kwa maisha yaduniani na akhera, ni muhimi kwa Mwislamu mwaminifu, kutambua kuwakwa kadri ya mafunzo sahihi ya dini, Uislamu ni mmoja tu ingawa zipomadhehebu nyingi za kiislamu zinazotofautiana kimatendo (hukumu zadini). Kwa hiyo kwa msaada wa kitabu hiki tutaona kuwa Uislamu nimmoja tu kwa manabii wote; na kwamba hivi sasa ingawa kuna madhehe-bu nyingi, ni madhehebu moja tu ya kweli mbele ya Mwenyezi Mungu.Ukweli huu unatokana na sababu zifuatazo:

    (a) Uislamu ni ukweli. Dini ya Uislamu ni ya kweli na ukweli wa jambololote lile hauwezi kuwa zaidi ya mmoja. Kitu kimoja hakiwezi kutofau-tiana.

    Uislamu ulifundishwa na mwenyewe Mtume (s.a.w.w) na kwa hiyo asinge-fundisha kitu kimoja kinachotofautiana kama ilivyo wakati huu katikaUislamu. Kwa hiyo lazima iwepo madhehebu moja tu sahihi miongonimwa migawanyiko hii kama tutakavyoona mbele kwa ushahidi wa mafun-zo ya dini, ya kutegemewa. Kibusara ni kwamba haiwezekani nchi mojaikawa na sheria tofauti kwa raia wake watokao mikoa mbalimbali ya nchihiyo.(b) Kazi ya Mtume na vitabu ni kutuondolea mifarakano katika dini:Tunaposoma Qurani tukufu tunagundua kwamba hawa Mitume na vitabuvyao wameletwa ili kutuondolea sisi binadamu mifarakano, na iwapo tuta-

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page M

  • farakana tuweze kupambanua ukweli uko wapi. Hebu tuone Aya ifuatayo:

    Wanadamu wote walikuwa taifa moja (limwaminilo Allah tu lakinibaadaye walihitilafiana), hivyo Allah akawapelekea manabii, kuwawabashiri na waonyaji, na pamoja nao akateremsha Kitabu na ukweliili kuhukumu baina ya wanadamu katika yale waliyohitilafiana.........(Qurani 2:213).

    Bila shaka tunaona wazi kwamba, kuwa na madhehebu mengi zinazoto-fautiana kiitikadi na kimatendo, kunaleta mifarakano, jambo ambalo nikinyume na makusudio ya kuletwa Uislamu. Kwa hiyo wingi wa madhe-hebu sio Uislamu bali Uislamu ni madhehebu moja tu kama ushahidi zaidiutakavyobainisha ndani ya kitabu hiki.

    (c) Ushahidi wa Qur`ani juu ya Uislamu mmoja tu

    Tukisoma Qur`ani Tukufu tunazikuta Aya zionyeshazo wazi kuwa Uislamuni mmoja tu.

    Na hakika hii ndiyo Njia yangu iliyonyooka, basi ifuateni (hii tu) walamsizifuate njia nyingine na mkafarakana na njia yake (hii), AllahAnakuusieni haya ili mpate kuchelea (maovu). (Qurani 6:153).

    N

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page N

  • OHakika wale walioigawa dini yao na wakawa makundi makundi(wewe Mtume wetu Muhammad) huna chochote kwao; hakika jambolao liko kwa Allah (tu), kisha (siku ya Kiyama) Atawaambiawaliyokuwa wakiyatenda........ (Qurani 6:159 ).

    Kauli ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika Hadithi ni Uislamu mmoja tu.Anakaririwa Mtume (s.a.w.w.) akisema:

    Umma wa Nabii Isa uligawanyika makundi 71 baada yake.Umma wa Nabii Musa uligawanyika makundi 72 baada yake.Umma wangu baada yangu utagawanyika makundi 73. Wotewataangamia (motoni) ila kundi moja tu. - Rejea: Sahih Muslim,Juzuu ya 8 Ukurasa wa 7, Sahih Bukhari na Sahih Tirmidh.

    Kwa hiyo basi, kutokana na hoja zote hizi, si rahisi kwa Mwislamu yeyotemwaminifu kudai hivi hivi tu bila hoja thabiti, kwamba madhehebu yakendiyo sahihi katika Uislamu. Kwa kuwa Uislamu wetu unategemea yaletuliyorithi kwa babu zetu bila kutumia akili zetu na kufanya utafiti, inamaana tungewakuta wazazi wetu ni Wakristo na sisi tungekuwa Wakristo.Kwa hiyo umuhimu wa kuchunguza imani zetu za kurithi bado upo. Hivyobasi kama tutazingatia yaliyoandikwa na ndugu yetu Isa H. Rwechungurana kuyafuata, tutafaidika na pia kuongoka - Inshaallah.

    Jambo la maana katika utafiti huu, ni muhimu tutumie sana akili bila kujaliutetezi wa madhehebu uliyowakuta nayo wazazi wako, au madhehebuyenye wafuasi wengi zaidi, au madhehebu yenye watu mashuhuri, n.k.Hayo hayatatusaidia kuufikia uongofu unaotakiwa.

    Mwisho namwomba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Amjaalie ndugu yetu IsaRwechungura kheri, baraka, na amfungulie milango ya elimu ili azidikutuelimisha.

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page O

  • Na sisi sote Mwenyezi Mungu atujaalie usikivu mwema wa kutuwezeshakuyaelewa mafunzo haya ya haki na kuyatumia kufikia ukweli wa dini yaMwenyezi Mungu ambao ni Uislamu mmoja tu - Amin.

    Na Baraka za Allah zimshukie Mtume Wake (Muhammad) na Maimamuwatukufu watokanao na Kizazi chake kitukufu na Awateremshie amani nautulivu kwa wingi.

    Dhikiri U.M.KiondoDar es salaam - T.I.C. (Mwenyekiti) 4th Jamadiul Awwal 1419 A.H. / 27th August 1998.

    P

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page P

  • 2A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page 2

  • 3A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    UTANGULIZIKwa jina la Mwenyezi Mungu,

    Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

    Namwomba Mwenyezi Mungu amteremshie baraka njema za mileleBwana wetu Muhammad na watu wa Familia yake ambao walitoharishwakikamilifu kwa kadri ya Hakika si mengineyo Mwenyezi Munguanataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, nakuwatakasa kabisa kabisa. (Qurani 33:33); pamoja na maswahabawaaminifu walioshikamana na mwendo wa Mtume (s.a.w.w) - Amin.

    Ndugu zangu, namshukuru Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuniwezeshakukamilisha kazi hii ambayo ni wajibu kwa kila Mwislamu. Kama tulivy-otangulia kusoma kuwa ni muhimu kila mmoja wetu achunguze upyaimani na itikadi yake ya kidini, ili afikie dini moja ya kweli mbele yaMwenyezi Mungu, kuliko kubakia kujivunia madhehebu mbali mbali.Kwa msingi huo nilijaaliwa kufanya utafiti kwa miaka 16 kwa kusomavitabu mbalimbali hasa vile vya Historia sahihi ya Uislamu. Niliyoyakutakatika vitabu hivyo, yalinitia simanzi moyoni kwa muda mrefu, kwa kuonajinsi ambavyo Waislamu kwa miaka mingi tumekuwa tunaendelezautamaduni wa kiislamu lakini Uislamu wenyewe upo mbali na sisi.

    Nasema hivi kwa sababu tumetangulia kuona kuwa sisi binadamu tuna-paswa kuishi hapa duniani chini ya amri za Muumba wetu wakati wote.Pale tunapoachana na amri hizo au tunapoacha amri hizi na kuanza kuch-agua tunayotaka, na kuacha tusiyoyataka, hiyo si dini tena. Hali hiyondiyo tuliyonayo wakati huu katika Uislamu wetu. Kwa sababu tutambuekuwa maana ya neno Islam ni kujitoa nafsi yako yote kumtii MwenyeziMungu. Utiifu wa nusu nusu sio Uislamu unaotakiwa.

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page 3

  • 4A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    Isitoshe kama hivi leo Mtume (s.a.w.w.) angekuwa hai tunamwona, vipiangetuamrisha jambo lolote lile kisha tukatae kumtii? Lakini pamoja nakwamba hatuko naye tena, mafunzo yake na amri zake kwetu zipo nazimehifadhiwa katika vitabu vya Hadithi. Inasikitisha kuona Waislamutunapuuzia amri muhimu za Mtume (s.a.w.w.) zilizo katika vitabu tunavy-odai kuwa vinatuongoza! Kwa hiyo yale nitakayobainisha hapa siyomageni kwa wale wenye ujuzi wa dini.

    Ningependa tutambue ukweli kwamba Uislamu ulianza karne kumi nanne zilizopita. Katika muda huo mrefu, ni matukio mengi yametokea.Mtu yeyote asiye na ujuzi wa matukio hayo, hana haki yoyote yakupinga au kuunga mkono hoja zilizomo humu. Kama ambavyo mimisiwezi kuingia kwenye ndege kwa nia ya kujifanya rubani wakati sina ujuziwa kazi hiyo. Kwa maana hiyo, nakaribisha mjadala kwa wasomaji wakitabu hiki, ambao wana mawazo tofauti, mradi mawazo hayo yawe yame-toka katika vitabu vinavyotegemewa. Kama zipo hoja za msingi zaidi yahizi, nitakuwa tayari kuzijadili. Vinginevyo siko tayari kupoteza mudakatika kujibu au kujadili hoja kinyume na msimamo huu; kwani itakuwa nikukiuka misingi ya utafiti. Nina maana kwamba anayetaka tujadili hojahizi au kunipinga, itabidi kwanza athibitishe elimu yake ya Historia sahihiya Uislamu kama inamtosha kujadili hoja hizi.

    Sababu yake ni kwamba, imenichukua miaka 16 kufanya utafiti huu, kwakusoma vitabu vingi sana, kuliko hivyo nilivyovitaja mwishoni mwakitabu hiki. Isingekuwa busara katika ulimwengu wa wasomi, kutoa hojaau kupinga hoja bila ujuzi wowote wa kutosha. Kwa kuwa nimetaja vitabuambamo zinapatikana habari hizi, ni bora anayetaka kutoa hoja atafutevitabu hivyo au awaulize wanaovifahamu, ili athibitishe hoja nilizotoa nandipo naye atoe hoja zake. Elimu niliyotoa humu ni ya ngazi ya juu sanaukizingatia elimu ya chini sana tuliyonayo Waislamu tulio wengi.Nimejitahidi kuelezea hoja mbali mbali kwa lugha nyepesi, na kwamtiririko bayana kuhusu matukio kadhaa yalivyofuatana, kuanzia miakazaidi ya 500 kabla ya Uislamu wa Nabii Muhammad (s.a.w.w.) hadi mwan-

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page 4

  • 5A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    zo wake mpaka wakati huu. Elimu yote hiyo si rahisi kuipata katika mudamfupi hata kwa mtafiti mwenye bidii sana.

    Mimi nawaheshimu na kuwapongeza mashekhe wetu kwa kuendelea kutoaelimu ya dini katika mazingira duni yatokanayo na kukosa taasisi rasmi zakisasa za kutoa elimu bora ya dini. Uduni wa elimu ya dini siyo kosa lamashekhe bali ni mfumo mbaya wa kukosa chombo imara cha kuongozaWaislamu kwa jumla.

    Hebu tujadili mfano mmoja ambao ni rahisi kila mtu kuelewa. Tuchukuliekuwa hapa Dodoma mjini, mwaka 1995 kulikuwa na Waislamu laki mojana nusu tu, kati ya wakazi wapatao laki tatu hivi. Tuchukulie kuwa kilaMwislamu achange shilingi 100 kila mwezi. Ina maana tutapata shilin-gi milioni 15 kwa mwezi! Hata kama tutapata shilingi milioni saba tukwa kila mmoja wetu kuchanga shilingi hamsini.

    Je, ndugu Waislamu hizo pesa hazitoshi kuwalipa mashekhe wetu misha-hara ya heshima na wakaacha kupiga ramli? Je, pesa hizo hazitoshi kujen-ga misikiti mipya na kuifanyia matengenezo ile ya zamani? Je, pesa hizohazitoshi kujenga mashule ya kisasa ya kutoa elimu zote za dini na dunia?Je, pesa hizo hazitoshi kuanzisha vituo vya ajira kwa vijana wetu wasio nakazi? Je, pesa hizo hazitoshi kuwasaidia mayatima na wajane na wazeewasiojiweza?

    Kwa hiyo Waislamu tukubali kuwa tunao uwezo wa kubadili hali zetu duniza kidini na kidunia iwapo tutapata viongozi waaminifu chini ya uongoziwa chombo chenye uadilifu.

    Nikirejea kwenye hoja ya msingi ni kwamba, kutokana na elimu duni yadini tuliyonayo, ni vizuri tukubali ukweli huo kwa sababu kulitambuatatizo ni nusu ya kulitatua. Haina maana mtu kuitwa wakili wakati hajuisheria! Haina maana mtu kuitwa daktari wakati anawaua wagonjwa kwamatibabu yasiyofaa! Haina maana mtu kuitwa mwalimu wakati hana cho-

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page 5

  • 6A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    chote cha kuwafundisha wenzake! Kwa misingi hiyo hiyo, haina maanayoyote Mwislamu kuitwa Sheikh wakati ambapo hawezi kujibu hojamuhimu za dini. Kushika uongozi kama huo bila ujuzi wa kutosha, nikujibebesha mzigo wa lawama za kuwapotosha watu, kesho huko akhera.Ujuzi wa dini ni taaluma sawa na taaluma nyingine za elimu. Hakunataaluma bila elimu. Hata uchawi wa shetani una elimu zake.

    Kila mara tumewasikia viongozi mbali mbali wakiwataka Waislamu kupa-ta elimu kwa sababu siyo siri tena kwamba Waislamu hatuna elimu! Kwahiyo hatuna sababu ya kujifanya tunayo elimu! Jambo la maana ni kwam-ba tuanze kutafuta njia za kuondoa kasoro hii kwa sababu katika kitabuhiki, tutaona kuwa elimu zote tunazojivunia zilizoleta maendeleo makub-wa zimeletwa na Uislamu. Baada ya utafiti katika historia sahihi ya dunia,hivi sasa hata wazungu wanakubaliana na ukweli huu! Kama Uislamu ndioulioleta elimu duniani, kwa nini leo hii Waislamu tuwe nyuma? Matatizoyaliyotokea hadi tukadidimia kiasi hiki utayakuta humu.

    Inasikitisha kwamba, niliwahi kusikia Sheikh mmoja maarufu katika sem-ina mojawapo ya kidini, akiwahutubia washiriki kwa kuwaogopeshakwamba elimu ya dini ni kubwa sana; na kwa hiyo si rahisi watu kuipatana kuhitimu! Hizi ni mbinu za baadhi ya viongozi wa dini kuficha upun-gufu wao wa elimu, au hata kuficha ukweli iwapo ukweli huo unahatarishamaslahi ya kidunia ya mtu binafsi. Nasema hivi kwa sababu madai yakwamba elimu ya dini ni kubwa sana na ni vigumu kuipata, ni madai yauongo! Mbona watu wamesoma miaka mingi hadi wakaweza kutengenezavyombo vya kuwasafirisha na kutua mwezini? Namna gani watu wamepa-ta uwezo wa kutengeneza bomu la nyuklia? Ni elimu gani kubwa kulikoelimu hizo? Upotofu ulioingia katika Uislamu ni suala la historia na si tati-zo la hukumu za dini.

    Katika kitabu hiki kidogo tutaona vitabu vingi sana vya historia yaUislamu sambamba na historia ya dunia. Je, vitabu hivyo ni vya bandia?Je, ni viongozi wetu wa dini wangapi walionavyo au wanaovifahamu? Je,

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page 6

  • 7A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    kutokijua kitu maana yake ni kwamba kitu hicho hakipo? Kwa kuwaUislamu haukuanzia Afrika Mashariki lazima tusome na kuelewa asiliyake hadi wakati huu.

    Katika ulimwengu wa leo, hakuna elimu iliyojificha labda iwe ni siri yaMwenyezi Mungu. Elimu zipo wazi kwa wenye kuzitafuta. Elimu tunay-oongelea hapa ni ile ya kutosha Mwislamu wa kawaida kufahamu misingiya dini ili awe Mwislamu kamili anayeongozwa na itikadi sahihi zaUislamu.

    Natoa msimamo huu wa kutafuta elimu kutokana na ukweli kwamba, his-toria ya Uislamu ni sambamba na historia ya dunia. Na tunafahamu kuwahuwezi kuifahamu historia ya dunia bila kusoma katika shule za sekondarihadi Chuo Kikuu. Tatizo hili la madhehebu ni tatizo la kihistoria; na kwahiyo ni lazima kutafiti katika historia, ili tuone chanzo chake ni nini. Lakinikama tujuavyo, mashekhe wetu tunaowategemea wakati huu, hawakupataelimu ngazi hiyo, kutokana na ukweli kwamba enzi zao walipata elimu yaokwa mashekhe wenzao mitaani bila kipimo chochote cha viwango. Tatizohili ni la hapa Afrika Mashariki, lakini katika nchi nyingi za Waislamu zili-zoendelea, elimu yote ya dini inatolewa kwa viwango kuanzia Shule zamsingi hadi ngazi ya Chuo Kikuu.

    Nina maana kuwa kwa mfano, unapojifunza lugha ya kiarabu utaanziangazi ya shule ya msingi na ukihitimu unapewa cheti ngazi hiyo. Kishautaingia ngazi ya elimu ya shule za sekondari darasa la kumi na mbili naukihitimu unapewa cheti. Kisha unaingia ngazi ya darasa la kumi na nnena unahitimu na kupata cheti. Mwisho unaingia Chuo Kikuu kwa shahadaya kwanza na ya pili iwapo utahitimu masomo yako. Utaratibu huo wamasomo utamchukua mtu miaka isiyopungua 18 tangu shule ya misingi.Vinginevyo ukianza na elimu ya msingi peke yake, utahitaji vyuo maalu-mu vya lugha ya kiarabu, kwa masomo ya miaka isiyopungua mitano.Au kama utampata Sheikh mwenye ujuzi wa lugha ya kiarabu kwa viwan-go vya kimataifa, aweze kukufundisha binafsi. Mashekhe wenye ujuzi wa

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page 7

  • 8A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    viwango hivyo ni wachache sana hapa kwetu. Lakini hata hapa kwetu,lugha yetu ya kiswahili inafundishwa kwa utaratibu huo! Wala sidhanikuwa kiarabu ni rahisi kuliko kiswahili! Viwango katika elimu yoyote ileni muhimu sana katika ulimwengu wa leo wa wasomi.

    Njia nyingine inayotegemewa hapa kama msingi wa kujifunza kiarabu, nikutumia vitabu vya Fiq-hi vya madhehebu ya Sunni kama: Irshadul-Muslimiin, Safinat Najah, Risalatul-Jamaa na Durarul-Bahiyyah. Vitabuhivi si vya kufundishia lugha. Kwa hiyo kuvitumia, yaani kutumia lughailiyomo, kama njia ya kujifunza kiarabu, ni sawa na mtu asiyejua kiswahili,akaamua kusoma magezeti mengi ya kiswahili kwa matumaini ya kuhitimumoja kwa moja na kufahamu kiswahili, bila kujifunza kwa undani, kanuniza lugha na viwango vyake hatua kwa hatua! Kwa kweli huwezi kutumiakiswahili cha darasa la nne kufahamu masomo ya Chuo Kikuu! Isitoshekiarabu ni lugha ngumu yenye msamiati mpana sana, kiasi kwamba nenomoja laweza kuwa na maana zaidi ya sita, lakini uamuzi sahihi wa matu-mizi yake, hutegemea kanuni nyingine nyingi, kufikia uamuzi kama nenolitumike mahali hapo au lisitumike. Lugha ya kiarabu inajitosheleza hatakatika lugha ya kisayansi kama tutakavyoona mbele katika kitabu hiki.

    Sisi Waislamu wa Afrika Mashariki, iwapo tunataka kupata elimu za juu zadini, hasa somo la historia, tunaweza kupata urahisi kwa kufaidika navitabu vingi vya kiingereza, yaani tafsiri za kiingereza za vitabu maarufuvya Historia ya Uislamu. Vitabu hivyo vimefasiriwa na wajuzi wakuu walugha hizi mbili. Lakini kama tutajaribu kutumia kiarabu cha ngazi ya chinikufafanua elimu za juu, tutaishia kuwapotosha kabisa wale wanaotuonakama viongozi wao. Nasisitiza sana jambo hili ili Waislamu tulio wengitutambue kuwa kuitwa Sheikh ni rahisi sana hasa hapa kwetu, lakinikufahamu dini ni kitu kingine. Kuna kitabu kimoja maarufu kilichoandik-wa na mwanachuoni mmoja maarufu sana huko Tunisia. Mwanachuonihuyo mwanzoni alikuwa Sunni Maalik, lakini alipofanya utafiti akaamuakuwa Ansari Sunna, akatafiti zaidi hatimaye akawa Shia na kwa hiyoakaandika kitabu hicho kueleza aliyoyagudua. Kwa bahati kitabu hicho

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page 8

  • 9A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    kimeshafasiriwa hadi lugha ya kiingereza na kiswahili. Kitabu hichokiitwacho: HATIMAYE NIMEONGOKA, ni muhimu Waislamu wotekukisoma.

    Siku moja nikampa kitabu hicho Sheikh mmoja maarufu nikiwa katikatabligh ili tujadili hoja zilizomo. Yeye alidai nimpe nakala ya kiarabu,nikampa. Mpaka leo hii ni zaidi ya miaka 5 hajanipa jibu wala kugusiasuala hilo wakati ambapo hoja zilizomo ni nzito sana! Mwanzoni nilifikirikuwa anataka kuficha ukweli, lakini siku moja akatutembeleamwanachuoni mmoja toka nchi za nje na ndiye aliyenipatia jibu.Mwanachuoni huyo aliwatembelea mashekhe mbali mbali kwa nia yakuwasalimia. Mwisho wake karibu na kuondoka, alisikika akisema kuwani mashekhe wawili tu aliowaona wanafahamu kiarabu fasaha kwa kanuniza lugha! Bali sisi hatujui siri hiyo! Lakini sijapata kusoma popote palekatika mafunzo ya dini, kwamba Sheikh atabeba dhambi za wafuasi wake!Kwa hiyo Waislamu tujikomboe kwa kutafuta elimu. Tusiwe wafuasi vipo-fu.

    Kwa kweli hata hizo kanuni muhimu za lugha ya kiarabu, ni wachachewenye kuzifahamu zote. Matokeo yake utaona kuwa tafsiri za Quranizinapotoshwa japo isiwe kwa makusudi. Kwa mfano katika tafsiri yakiswahili ya Qurani ya Marehemu Saleh Farsy, aliifasiri Aya ya udhu(Qurani 5:6) kuonyesha kuwa ni wajibu kuosha miguu kwa maji! Tafsirisahihi ya Aya hiyo tutaijadili kwa upana katika maelezo ya sura za mbeleza kitabu hiki.

    Katika maelezo haya sina maana kuwa Mashekhe wetu hawajuikufundisha na kusoma Qurani! Usomaji wa Qurani una kanuni zakezinazofanana dunia nzima. Tatizo la hapa kwetu ni tafsiri ya Qurani. Kwasababu Qurani haiwezi kufasiriwa kwa kutumia kanuni za lugha pekeyake; bali pia sababu za kushuka Aya kihistoria, lazima zieleweke na zizin-gatiwe. Lakini kutokana na upungufu tulionao hapa kwetu katika somo lahistoria sahihi ya Uislamu, ndiyo maana kuna walakini katika baadhi yatafsiri za Aya za Qurani. Nimetangulia kueleza kuwa itamchukua mtu

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page 9

  • 10

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    miaka kama 18 kujifunza lugha ya kiarabu mpaka ngazi ya Chuo Kikuukatika nchi za kiarabu, kwa mfumo wa kawaida wa elimu ya sekondari.Kama siyo hivyo, itabidi mtu huyo asome walau miaka mitano katika vyuomaalumu vya lugha na dini bila masomo mengine. Siyo rahisi mtukuhitimu ngazi hiyo kwa kusoma mitaani bila viwango.

    Kumbukumbu za historia nitakazoeleza humu zinatoka katika vitabuambavyo vimeandikwa na wanahistoria wa ngazi ya Chuo Kikuu kwalugha ya ngazi hiyo. Ndiyo maana sitarajii kuwa itakuwa rahisi kwamashekhe wetu walio wengi, kufahamu kwa ufasaha, yaliyomo katikavitabu vitakavyotajwa humu kama ushahidi wa kihistoria kuthibitishakumbukumbu hizo. Pengine mashekhe wetu hapa kwetu hawatafurahiaukweli huu nilioeleza humu kuhusu ngazi za elimu ya viwango! Huendawengine wakapinga ili wasionekane hawana elimu ya kutosha! Lakinisuala la msingi ni kwamba, kama kuhitimu lugha ya kiarabu ni rahisihivyo, kwa nini nchi hizo zilizoendelea zaidi ya sisi, wapoteze muda waomrefu kusoma miaka yote hiyo tena kwa viwango maalumu? Au kamakusoma kwa viwango si lazima kwa nini vijengwe vyuo vya taaluma mbalimbali dunia nzima? Kwa nini watu wasihitimu urubani, unahodha, udak-tari au uhandisi, mitaani bila kwenda kusoma katika vyuo maalumu? Jeinaingia akilini?

    Maelezo haya nimeyatoa mapema kupinga madai ya baadhi mashekhewengi, ambao hudai kuwa kitabu cha kufundisha dini lazima kiwe katikalugha ya kiarabu! Lakini Waislamu wengi wa kawaida hawafahamukiarabu. Kwa hiyo Waislamu hao hawawezi kumkosoa Sheikh wao, iwapokiongozi huyo ataongea kiarabu kibovu au kufasiri maneno ya kiarabu kwamakosa! Mfano wake ni sawa na mzungu mgeni, ambaye hawezi kuto-fautisha kati ya kiswahili cha mtoto mdogo wa darasa la kwanza, nakiswahili cha ngazi ya Chuo Kikuu! Lugha usiyoielewa utaiona sawa tumasikioni mwako hata kama inakosewa! Hata hivyo pamoja na kushabikia kiarabu, ukweli ni kwamba wengi wahao viongozi wetu wa dini, ujuzi wao wa kiarabu bado ni wa chini. Mfano

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page 10

  • 11

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    mmoja wa kusikitisha ni kwamba, miaka kama ishirini hivi iliyopita, kati-ka mji mmoja kwenye msikiti mmoja, alitembelea shekhe mmoja ambayealitokea Misri. Wenyeji wake walibaini kuwa kiarabu anachoongea ni changazi ya juu na hakieleweki. Baada ya majadiliano, ulitolewa ushauri kuwaapatikane mtu aliyesomea Misri ili asaidie ukalimani. Mtu huyo ali-patikana na haraka akaletwa msikitini kuokoa jahazi. Baada ya siku mbiliza mtu huyo kutoa msaada wake, iligundulika kwa masikitiko, kuwa mtuhuyo alikuwa Mkristo na alipelekwa Misri zamani kusomea fani ya uhan-disi katika taaluma fulani. Mafunzo yake huko Misri yaliendeshwa katikalugha ya kiarabu fasaha cha ngazi ya Chuo Kikuu, na ndiyo maana ujuziwake wa lugha hiyo ni wa kiwango cha juu. Kwa tabia yetu ya kushabikiakiarabu, siku moja tutafikia kuswalishwa na Mkristo kwa sababu tuanaongea kiarabu!

    Ni muhimu tuelewe pia kwamba, lahaja za kiarabu za nchi mbali mbali zaArabuni zinatofautiana kama ambavyo kiswahili cha Mombasa, Zanzibar,Musoma, Mwanza, Mtwara, Tanga, Zaire na Uganda, kinavyotofautiana.Kwa kweli hata tukishabikia kiarabu, ukweli ni kuwa hata somo la Elimuya Kiislam katika shule zetu za sekondari halifundishwi, kwa kukosa wal-imu. Je, hizo taasisi za kiislamu za kutosha kufundisha kiarabu ngazi hiyoziko wapi? Ni kwa njia gani Waislamu walio wengi watapata elimu yadini? Tutangoja mpaka lini?

    Nimeeleza nyuma kuwa kuna mashekhe wanaojua ukweli lakini wanafichaili kulinda maslahi yao. Lakini wakati naandika kitabu hiki, tayari teknolo-jia ya kompyuta imefikia hatua ambapo zimetengenezwa ComputerProgrammes zenye uwezo wa kufasiri lugha kwenda lugha nyingine tenakwa ngazi ya lugha inayotakiwa! Kwa mfano ukiwa na hotuba ya maan-dishi ya kiingereza, ni kiasi cha kuingiza tu kwenye kompyuta ikakutoleatafsiri ya kifaransa muda huo huo! Je, zikipatikana taratibu programmesza kufasiri kiarabu kwenda kiingereza au kiswahili, ni vipi tutaendeleakuficha hayo yaliyomo katika Sahih Muslim, Sahih Bukhari n.k. Je,wakiyagundua hayo wasio Waislamu na wakayaweka wazi, tutalalamika

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page 11

  • 12

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    kuwa wanatukashifu?

    Lengo langu kuandika kitabu hiki, ni kuwaelimisha Waislamu wotewaelewe Uislamu wetu, na wajenge hoja kwa ujuzi wa dini, kuliko tabiayetu ya miaka mingi ya kurithi badala ya kutumia akili na kuichambuadini. Mwislamu ambaye atahitaji ufafanuzi zaidi atajitokeza na atasaidiwaili aweze kuelewa. Sidhani kama ni kosa kwa Daktari aliyepata ujuzi wakekatika lugha ya kiingereza, kuandika kitabu kuelezea jinsi ya kuepukamagonjwa, katika lugha ya kiswahili kwa faida ya watu wote. Na sidhanikama kuna faida yoyote kwa daktari huyo, kuandika kitabu kama hicho,katika lugha ya kiingereza na kuwataka watu wenye kutaka ufafanuzi, kilamara waje kwake ili awafasirie maelezo yake!

    Hata hivyo natambua ukweli kwamba vitabu vingi vya mafunzo ya dinivimo katika lugha ya kiarabu, lakini bado Waislamu wengi wanawezakufaidika kwa kusoma vitabu vingi vya kiingereza kama mimi. Isitoshemimi nimeweza kujifunza kusoma Qurani kwa kutumia vitabu maalumvya lugha ya kiingereza vyenye maelezo bora zaidi ya hizi Juzu Ammatulizozizoea, ambazo humfanya mwanafunzi achukue zaidi ya miaka 8kuhitimu kusoma Qurani! Mimi ilinichukua mwaka mmoja tu tena bilamwalimu! Elimu inazidi kuwa nyepesi! Katika masuala ya dini tusiwewanafiki wa nafsi zetu. Wengi wetu elimu zetu ni za kurithi kwa mababuna mashekhe wetu na siyo elimu za msingi wowote wa utafiti! Kwa hiyotusione uzito kuachana na baadhi ya elimu potofu tulizopoteza muda mrefukuzipata, na leo tunagundua kuwa kwa hakika elimu hizo hazifai! Mfanomzuri tunaupata kwa wasomi wengi waliomiminika Urusi ya zamani kuso-ma Elimu ya Ukomunisti na Ujamaa. Wasomi hao walihitimu na kupewashahada za juu. Walirejea kwetu na kupewa vyeo vikubwa vya uongozi.Walijaribu kutekeleza elimu yao hiyo kwa vitendo lakini baada ya miakamingi sana, hao wasomi wakagundua kuwa elimu yao hiyo inafurahisha nakutia moyo ukiisoma katika vitabu, lakini kivitendo haiwezekani! Baadayehata huko Urusi ikadhihirika kuwa Ukomunisti na Ujamaa ni nadhariapotofu! Viongozi hao hao waliotetea Ukomunisti kwa miaka mingi, hivi

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page 12

  • 13

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    sasa wamefumbua macho na kukumbatia Ubepari! Elimu zao zote zaUkomunisti na Ujamaa hazina faida yoyote tena!

    Kwa hiyo sisi Waislamu tusione hasara kuachana na elimu za mazoea,iwapo kufanya hivyo kutatuelekeza kufaulu mbele ya Mwenyezi Mungu.Na hilo ndilo lengo la dini kimsingi. Hatufuati dini kutafuta umaarufu tokakwa binadamu wenzetu au kupata faida za kidunia. Uislamu ni kumtiiMwenyezi Mungu na Mtume (s.a.w.w.); lakini utiifu huo tutaufikia kwanjia ya elimu sahihi ya dini.

    Ni vizuri kuchunguza elimu zako kwa makini kwa sababu kwa miakamingi tumefundishwa kuwa Uislamu ndio umeleta Utumwa (slavery); nakwamba, Uislamu ulienezwa kwa upanga! Baada ya miaka mingi ya imanihizo potofu, leo hii vinapatikana vitabu vinavyoeleza ukweli tofauti natulivyoaminishwa miaka mingi iliyopita! Rejea: Slavery - From Islamic &Christian Perspective - cha S.S.A. Rizvi - Canada Uk. 105 -138. Faida ganituendelee kukumbatia elimu potofu zilizopitwa na wakati? Katika dinizote kuna mafunzo mengi potofu yasiyo na ukweli wowote lakinibinadamu na akili zetu tunaendelea kuyakumbatia! Hiyo ni dini au uta-maduni?

    Katika kitabu hiki tutaona kuwa upotofu katika dini unasababishwa naujinga tulionao ambao tumeurithi kwa mababu zetu kwa miaka mingi.Inashangaza kuwaona mashekhe wetu siku hizi wanakazania lugha yakiarabu kama njia pekee ya kujifunza dini wakati ambapo Mtume(s.a.w.w.) anakaririwa akisema kuwa: Tafuteni elimu hata kama itabidikuifuata mpaka China. Tukitafakari maneno hayo tutaona kuwa siku hizohuko China, haikutumika wala kueleweka lugha ya kiarabu! Maana yakeni kwamba mwenye kwenda huko kutafuta elimu, ingemlazimu kujifunzalugha ya Kichina. Je, kuna shekhe yeyote ambaye anaweza kudai kuwaelimu yote niliyotoa humu anayo, ingawa kuna aliyonayo ambayo humuhaimo? Je, niliyoeleza humu hayafai kwa kuwa sikuyaandika katikakiarabu?

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page 13

  • 14

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    Hakuna mtu mwenye ujuzi wa elimu zote isipokuwa Mwenyezi Mungu tu.Mwenye ujuzi wa lugha ya kiarabu na elimu zake, na mjuzi wa lughanyinginezo naye ana elimu zake kutegemea vitabu ambavyo kila mmojaamevitumia kupata elimu. Tabia ya Waislamu wa kawaida kutegemea tumaneno au uamuzi wa shekhe peke yake, ni makosa makubwa kwa sababuanakaririwa Mtume (s.a.w.w.) akisema kuwa: Saa moja ya kutafuta (kuji-funza) elimu ni bora kuliko miaka sitini ya ibada. Vile Vile anakaririwaakisema kuwa: Usingizi wa mtu mmoja mwenye elimu ni bora mbele yaMwenyezi Mungu kuliko ibada ya usiku mzima ya kundi la wajinga elfumoja. Maana yake ni kwamba mwenye elimu ndiye mwenye hakika yakila atendalo.

    Maneno haya yote yanaonyesha wazi umuhimu wa kila Mwislamu kuji-funza elimu yoyote ile iliyo halali na yenye manufaa, mbali na elimu yadini. Kwa mfano tutaona kuwa katika Qurani kuna elimu nyingi za sayan-si. Kama shekhe amehitimu Qurani mpaka kufasiri, lakini hana elimu yasayansi, ni vipi shekhe huyo ataweza kufasiri aya zinazohusiana na sayan-si? Je, kuna shekhe mwenye kitabu cha sayansi cha kiarabu hapa kwetu?Upungufu huo ndio unaopelekea tafsiri potofu za Aya japo isiwe makusu-di. Tukumbuke kuwa baadhi ya wanasayansi wazungu wanasilimu mara tuwakikuta ukweli wa kisayansi katika Qurani! Sababu yake ni kwambawanatambua kuwa miaka iliyoshuka Qurani elimu hizo hazikuwepo duni-ani.

    Zaidi ya hayo tutambue kuwa, hivi sasa dunia nzima inaimba wimbo waSayansi na Teknolojia. Maana yake ni kwamba katika misingi hiyo, ni laz-ima tufahamu kuwa Sayansi na Teknolojia vimejengeka katika Ukweli.Njia pekee ya kupata ukweli ni kupata elimu sahihi ya jambo linalohusika.Katika karne hii hakuna nafasi tena ya kuamini vitu visivyo na ukweliwowote. Hii ni enzi ya uwazi na ukweli.

    Katika dunia nzima kuna imani nyingi za dini ambazo kimsingi hazinaukweli wowote. Kwa mfano imani za wenyeji wa Jamaica juu ya marehe-

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page 14

  • 15

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    mu Haile Selassie si za kweli. Ukichunguza historia ya Vita Kuu ya Pili yadunia, utakuta maelezo ya wahusika wakuu mbali mbali; na hasara wali-zowatia maadui zao. Lakini ukirejea Encyclopedia of Second World War,utakuta maelezo yenye ukweli tu ambayo mara nyingine ni tofauti na imaniza watu kuhusu matukio fulani ya kivita ya vita hivi.

    Mnamo tarehe 29 Septemba, 1999 saa kumi na mbili na robo asubuhi,Idhaa ya kiswahili ya Sauti ya Ujerumani ilitangaza mahojiano na bwanaMohamed Saidi wa Tanga mwandishi wa kitabu kipya: The Life and Timesof Abdul Wahid Sykes, kuhusiana na waasisi 17 Waislamu waanzilishi wachama cha TANU hapa Tanzania. Ni ajabu jinsi ambavyo hatusikii kabisamajina ya wazee hao mashuhuri kisiasa! Badala yake, historia tunayoisikiani ile ya kuwasifu watu wengine, kinyume na ukweli kwamba Waislamundio viongozi wakuu wa harakati za uhuru Tanzania.

    Maelezo yote haya yanaonyesha kuwa, utafiti wa kielimu ndio pekeeuwezao kumfikisha mtu kwenye ukweli, na siyo tu mazoea au imani zakufuata matakwa ya watu fulani kwa nyakati fulani.

    Ulimwengu wa leo, elimu yoyote ile haitegemei lugha maalumu. Kwamfano Wajapani walipata ujuzi wao wa Sayansi na Teknolojia hukoAmerika na Ulaya Magharibi katika lugha ya kiingereza. Hivi sasaWajapani wanatengeneza gari zima kwa mafunzo ya lugha ya Kijapanikitupu hata jina la msumari! Je, hilo gari halifanyi kazi sawa sawa? Je,ubora wa bidhaa za Japan umepungua? Jambo la msingi ni kwamba lughani njia ya kuipata elimu yoyote ile, kwa hiyo lugha zote zitumike ili watuwapate elimu. Tusitumie kiarabu kuficha ukweli na kuifanya dini kuwangumu hata kwa mambo ya kawaida ya ibada za kila siku. Kwa mfanohapa kwetu kuna misikiti mingi ambayo mashekhe wake hawataki kutoaelimu ya kuosha na kukafini maiti kwa watu wote, ila watu fulani tu wakudumu, kwa sababu kuna ushuru wa kuosha maiti! Utadhani kuosha maitini ajira!Lakini mashekhe hao hao wanatueleza kuwa akizikwa Mwislamu bilakuoshwa, Waislamu wote wa mahali hapo huandikiwa dhambi! Kama ni

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page 15

  • 16

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    wajibu kwa sote, basi ni lazima kila Mwislamu afahamu kufanya kazihiyo! Nimetoa mfano huu kuonyesha kuwa kuna mambo kadhaa tunay-ofichwa waumini wa kawaida. Kimsingi hata huko kumwosha maitiMwislamu mwenzetu kwa kulipwa ni haramu lakini Waislamu hatujui!

    Tusichukulie upungufu mkubwa tulionao hapa kwetu katika elimu ya dinitukadhani kuwa dunia nzima iko hivyo! Katika nchi za India, Pakistan,Bangladesh, Malaysia na Indonesia, utawakuta wasomi wengi wenye sha-hada (Degree) mpaka tatu au tano za dini! Je, wasomi kama hao watakuwasawa na Mashekhe wetu wa mitaani? Ni lazima tutambue na kukubalikasoro hii na tufanye juhudi zote kuiondoa. Vinginevyo tunaweza kuaibi-ka mbele ya wajuzi wa mambo ya dini yetu wasio Waislamu!

    Kwa hiyo msomaji wa kitabu hiki asishangae kwa nini hajawahi kuyasikiahaya atakayoyakuta humu! Elimu ya dini ni kubwa mno kuliko tunavy-oichukulia. Baadhi ya sababu za msingi ni hizo nilizozitaja kwa ufupi.Kama waumini wa kawaida wanafichwa jinsi ya kuosha na kukafini maiti,je, ukweli ambao unaweza kuwaunganisha Waislamu wote na kuwa kitukimoja utapokelewa vipi? Ni viongozi wangapi (mashekhe) wako tayarikupoteza vyeo vyao ili Uislamu uwe mmoja?

    Naomba Mwenyezi Mungu aniepushe na kuwa miongoni mwa walewafichao ukweli (Qurani 2:146) kwa unafiki. Jambo la maana sana kati-ka kitabu hiki, tutachunguza sababu kwa nini sisi Ummat Muhammad(s.a.w.w.) tutagawanyika katika makundi 73 hadi kufikia Siku ya Kiyama,na makundi yote yataangamia motoni kasoro kundi moja tu! Leo hiiWaislamu tunaongezeka na misikiti inajaa, lakini wengi wetu tutaangamia!Kwa nini? Endelea kusoma ufahamu. Rejea: Sahih Muslim, Jz. 8 uk.7kuhusu Waislamu kugawanyika makundi 73.Isa RwechunguraDODOMA - TANZANIA.27 DHUL QAADAH, 1418 A.H.26 MACHI, 1998 A.D.

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:18 PM Page 16

  • 17

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    MAELEZO JUU YA MWANDISHI WA KITABU HIKI NA HISTORIA FUPI YA UTAFITI WAKE

    Mimi ni mzaliwa wa Mkoa wa Kagera, kutoka miongoni mwa Tarafaambazo Waislamu wakazi ni kama asilimia mbili hivi kwa kukisia. Kwauchache wetu huo, tulilazimika kusoma katika shule za Wamisionari wakikristo na hivyo kufundishwa Ukristo kama sehemu ya masomo yetu. Halihiyo ilinifanya kuwa mtafiti mapema sana kuhusu tofauti za Uislamu naUkristo. Baadaye kidogo nilipofikia darasa la tatu, nilihamia shule yaSerikali za mitaa ambako kila mwanafunzi alikuwa huru kujifunza diniyake.

    Shuleni hapo kulikuwepo Madrassa lakini kwa uchache wetu wanafunziWaislamu, pamoja na uchumi duni wa wazazi wetu, mwalimu wetuhakulipwa mshahara wa uhakika na hivyo tukakosa masomo muhimu.Kwa hiyo elimu yangu ya dini sikuipata utotoni bali niliipata kwa kiasikikubwa, kwa jitihada zangu ukubwani kwa kusoma vitabu mbali mbali.

    Lengo langu kueleza haya yote nataka kuonyesha kuwa mtu yeyote aki-weka nia, anaweza kuitafuta na kuipata elimu ya dini bila kujali umri wake.Isitoshe Mtume (s.a.w.w.) alipotuamrisha kutafuta elimu hadi Chinaalikusudia Waislamu wote. Hata hivyo natambua kuwa watakaosomakitabu hiki watapata shauku ya kutaka kujua ni vipi nilipata elimu zote hiziiwapo sikupitia njia za kawaida yaani kuanzia Madrassa na kupitiamashekhe kadha wa kadha kwa miaka mingi kama tulivyozoea.

    Kwa kweli namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia kipaji cha lughaya kiingereza tangu shule ya msingi. Bado ninaamini kuwa iwapo ninge-soma dini kupitia mfumo duni tuliouzoea, nisingeweza kugundua yotehaya. Pamoja na ukweli kwamba ujuzi wa lugha ya kiingereza umedidimiakwa miaka mingi sasa mashuleni, mimi nilijibidisha binafsi kutokana na

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:19 PM Page 17

  • 18

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    mazoea yangu ya kupenda kusoma vitabu mbali mbali. Kwa hiyo katikashule ya msingi nilikuwa miongoni mwa wanafunzi wanaoongoza kwaujuzi wa lugha hiyo. Hiyo ni neema ya Mwenyezi Mungu.

    Nikiwa shule ya sekondari, nilishinda mashindano ya uandishi wa Inshakatika lugha ya kiingereza. Nilipata nafasi ya kwanza miongoni mwawanafunzi 245, walioshiriki mashindano hayo. Shule yetu ilikuwa nisekondari ya Ufundi, ikipokea wastani wa wanafunzi kumi bora zaidi, tokakila mkoa. Siku hizo zilikuwepo shule mbili tu za aina hiyo nchi nzima.

    Baada ya kumaliza masomo na kuanza kazi, nilipata bahati ya kupelekwaIndonesia kwa masomo zaidi, mara mbili miaka ya themanini. Indonesiandiyo nchi yenye Waislamu wengi kuliko zote duniani. Katika safari zakuelekea huko nilipata bahati pia kupitia India, Malaysia na Pakistan nakuwaona Waislamu wa huko wanavyoendesha ibada zao pamoja namtazamo wao juu ya Uislamu. Niligundua kwamba Uislamu wa hapakwetu ni tofauti na huko, kwa sababu kwa mfano, huko Pakistan masomoya dini yanayofundishwa shule za msingi ni ya juu zaidi kuliko hata elimuya mashekhe wetu walio wengi! Mfano mdogo ni kwamba utaona misik-iti mingi hapa kwetu wanazuia mtu kuingiza mkono kwenye birika (reser-voir) la maji, kwa madai kuwa maji yatatenguka udhu! Lakini hata ukire-jea hukumu sahihi za Sunni, utakuta kuwa maji kama hayo hayawezikutenguka udhu kwa sababu hiyo tu! Kiasi fulani cha maji hakiwezi kuten-guka udhu kwa kuingia najisi seuze kuingiza mkono tu.

    Nikiwa huko Indonesia nilipata fursa ya kubadilishana mawazo na wenye-ji wangu na kwa mara ya kwanza nikapata bahati ya kuona vitabu muhimuvinavyoongoza Uislamu kama Sahih Muslim, Sahih Bukhari, SahihTirmidh, Tarikh Tabari n.k. Kwa hakika Mwislamu yeyote asiyewahi kuso-ma vitabu hivyo, afahamu kuwa hajaujua Uislamu, kwa sababu yaliyomohumo ni mazito na ni tofauti na imani zetu za Kurithi tulizopokea tokakwa wazazi wetu au mashekhe wetu bila uchunguzi wowote wa kielimu!

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:19 PM Page 18

  • 19

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    Masomo yangu huko Indonesia yalinishirikisha na wafanyakazi ambaokwa mkataba ulionipeleka huko, wa serikali mbili, walitakiwa pia kujaTanzania kusimamia utekelezaji wake. Walipofika huku kwetu na kutem-belea misikiti yetu, walishangaa kwa mfano walipoona jinsi ambavyo watuhawazingatii kuswali kwa unyenyekevu. Halafu walishangaa utaratibutunaotumia misikitini wa kumkuta mtu anasali ukampiga begani ili aweImam wako! Waliuliza kwamba unapompiga mtu begani unajuaje kamaanasali Swala ipi; yaani inawezekana analipa Swala fulani au anaswaliSunna fulani au ni mtu asiyefahamu kanuni za Swala! Walinieleza kwam-ba huko kwao kuna Chuo maalum cha kufundisha kanuni za Swala kwamwaka mmoja! Sisi hapa tunaona Swala ni kitu kidogo na kwamba kilamtu anajua kuswali au kuswalisha.

    Kutokana na mwangaza huo, mnamo, mwaka 1982 nilijikuta na maswalimengi kichwani kuhusu asili ya madhehebu. Nilisoma vitabu vingi kuto-ka Bilal Muslim Mission-Dar es Salaam kwa miaka mitatu nikapatamwangaza mkubwa sana. Namshukuru sana Hujjatul Islam Seyyid SaeedAkhtar Rizvi kwa kujibu barua zangu zote na kufafanua mambo mengi yadini yaliyonitatiza wakati huo. Alinialika rasmi kutembelea taasisi yakekwa wiki moja na akanipatia vitabu vingi zaidi. Lakini sikuishia hapo baliniliandika barua na kuzituma katika taasisi zaidi ya nane za kiislamu duni-ani, kuomba msaada wa vitabu zaidi hasa juu ya historia ya Uislamu.

    Nilipokea vitabu vingi na kuvisoma kwa makini. Mwisho niligunduaukweli kwamba kwa hakika kulitokea fitna kubwa katika Uislamu. Mnamomiaka ya tisini na moja, niliandika makala (pamphlet) na kuiwakilishakama Mada katika semina ya kiislamu iliyofanyika Singida chini ya Bilal,ambayo ilijumuisha Waislamu toka karibu mikoa yote. Mada hiyo ilikuwajuu ya hatari za Waislamu kutofahamu madhehebu yao. Washiriki wa sem-ina waliomba nakala zake wakapewa lakini hapakuwepo uwezo wa kumpakila mmoja.

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:19 PM Page 19

  • 20

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    Baadaye nilirekodi hotuba hiyo katika kanda za kaseti na watu wengiwaliomba wazipate lakini nilishindwa kutosheleza mahitaji yao. Hatahivyo kwa kadri nilivyozidi kupokea na kusoma vitabu zaidi, nilipataushahidi muhimu sana kuhusiana na hoja mbali mbali. Mwisho nikaamuakuipanua hiyo Pamphlet ili iwe kitabu kamili chenye hoja zote muhimu.Kazi hii nimeikamilisha baada ya miaka 16 ya utafiti! Nilitambua ugumuwa Waislamu walio wengi kuweza kupata na kusoma vitabu vyote nilivy-opitia, kwa muda wote huo, ili kupata ukweli wote huu. Ndiyo maana nil-ifikia uamuzi wa kuandika kitabu hiki, ili kurahisisha kazi ya mtu yeyoteatakayetaka kuchunguza ukweli huu.

    Napenda kusisitiza tena kwamba vitabu vingi vya lugha ya kiarabu, hatapale vinapofasiriwa katika kiingereza, utakuta kwamba kiingereza chake nikigumu pia; kwa sababu kiarabu chake pia ni kigumu kama nilivyoelezanyuma. Kitabu kama Nahjul Balaghah utakuta tafsiri yake ya kiingerezaunaisoma na kamusi (Dictionary) pembeni, vinginevyo hutaambulia kitu.Ndiyo maana nasema kuwa namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kipaji chakufahamu kiingereza kuliko ningefahamu kiarabu kwa ngazi ya hapakwetu ambayo haitoshelezi kabisa kielimu.

    Mpaka hapa tumeona kuwa milango ya elimu ipo wazi kwa wenye kuitafu-ta kwa bidii. Sina maana kwamba mimi nimehitimu sana! Kwa kweli badonaendelea kupokea vitabu mbali mbali toka nje, na hapa nchini. Elimu yadini ni kubwa mno, na mjuzi wa yote ni Mwenyezi Mungu. Jambo lamaana ni kwamba kila Mwislamu ajitahidi kupata elimu ya msingi ya diniili imani yake ikamilike. Elimu nyinginezo zaidi ya hapo zitategemea bidiiya mtu. Unapofariki, Malaika hukuuliza maswali ya kupima ukamilifu waimani yako ya Uislamu. Hilo halina msamaha.

    Katika ulimwengu wa Shia, kielimu mimi ni mtu mdogo sana wala sinacheo chochote cha ujuzi wa dini! Nilichofanya hapa ni kuitikia mwito waMtume (s.a.w.w.) kwamba Enezeni mafunzo yangu japokuwa unaifahamuAya moja tu. Katika madhehebu ya Shia Ithnaasheri ngazi za ujuzi wadini ni za juu sana kuliko kijitabu hiki kidogo.

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:19 PM Page 20

  • 21

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    Sababu kubwa ya kueleza ujuzi wangu wa lugha ya kiingereza siyo kujisi-fu bali nataka ieleweke wazi kuwa ujuzi wa lugha yoyote peke yake, hau-toshi kumwezesha mtu kuandika kitabu. Mwandishi wa kitabu chochotekile ni muhimu awe na ujuzi wa uandishi au kipaji cha uandishi. Lazimakitabu kiwavutie waliokusudiwa kukisoma, na maelezo yake yawe namtiririko unaofaa. Matukio yaelezwe kama yalivyofuatana n.k. Mara nyin-gi tunasikia wanafunzi wakilalamika kuwa mwalimu fulani ana elimukubwa lakini hajui kufundisha.

    Njia za kueneza mafunzo ya Mtume (s.a.w.w.) zipo nyingi. Yawezekanamtu akawa na kipaji cha kutoa hotuba za kuwavuta wasikilizaji. Kwa hiyoni vizuri anayetaka kufanya tabligh kwanza aelewe kipaji chake na aen-deleze kipaji hicho. Kwa kweli ujuzi wa lugha ni njia tu ya kupata elimuiliyokusudiwa. Kufikisha elimu hiyo kwa watu wengine, ni suala linalohi-taji kipaji au ujuzi mwingine tofauti. Tabligh ina misingi yake.

    Kwa upande mwingine kama sisi wazazi tunataka vijana wetu wawe namoyo wa kuipenda dini, ni muhimu sana sisi wenyewe tuonyeshe mfanowa kujali dini. Mimi baba yangu alifariki nikiwa na miaka miwili tu.Lakini marehemu mama ambaye hakujua kusoma wala kuandika, alikuwatayari keshafundishwa kuswali Swala tano na marehemu baba! Sikuwahikumuona mama akipitwa na kipindi cha Swala maisha yake yote! Leo hiisisi elimu tuliyonayo pamoja na urahisi wa kuipata elimu zaidi, badohatusali! Je! hao watoto wetu vipi wataipenda dini?

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:19 PM Page 21

  • 22

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    ASILI YA TOFAUTI KATI YASUNNI NA SHIA ITHNASHERI

    Waislamu wote tunakubaliana kuwa katika uhai wote wa Mtume (s.a.w.w.),Uislamu ulikuwa kitu kimoja kwa maana kwamba hayakuwepo madhehe-bu kama tunavyoyaona wakati huu. Wapo mashekhe wanaofundishakwamba kuhitilafiana ni Ijtihad na kwa hiyo ni katika njia ya MwenyeziMungu. Lakini ukichunguza tofauti hizo, utakuta mambo yanayopinganana Qurani na Sunna! Je, hayo nayo ni katika njia ya Mwenyezi Mungu?Maneno yanayodaiwa yalisemwa na Mtume (s.a.w.w.) kwamba:Kuhitilifiana kwa maulamaa ni rehema.

    Kusudio la maneno hayo siyo hilo. Maana yake ni kwamba watakapohiti-lafiana maulamaa, itakuwa ni nafasi nzuri ya kukaa pamoja na kujadilitofauti zao na mwisho kuafikiana. Kuendelea kupingana kwa maulamaasiyo misingi ya Uislamu. Rehema iliyopo hapa ni kule kupanuana mawa-zo kielimu. Lakini iwapo atatokea ulamaa akafanya ijtihad yake akadaikuwa wakati huu wa sayansi na teknolojia, Waislamu hatuna muda wakutosha kuswali Swala tano bali tuanze kuswali Swala tatu tu, je, itafaatukubaliane naye? Pana rehma gani kuachana na Sunna sahihi na Qurani?

    Pengine tusingejali kuchunguza jambo hili iwapo lisingekuwa na madharayoyote kwetu. Kwanza tunafahamu kuwa Waislamu wengi hawalipi uzitosuala la madhehebu. Wengi wetu hatufahamu kwa nini tunaitwa Waislamuwa madhehebu ya Sunni wafuasi wa hukumu za Imam Shafii! Maana yakeni kwamba tunaendeleza Uislamu wa kurithi! Kwa kawaida ni vigumukumpata Mwislamu aliyechagua mwenyewe madhehebu yake kwa akiliyake! Hata Wakristo ni hivyo hivyo. Dini ya mtu au madhehebu yakehutegemea walioleta dini mahali hapo kwa mara ya kwanza! Lakini kwaupande mwingine tutaona kuwa hizi imani za dini za kurithi, zinaambatan-

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:19 PM Page 22

  • 23

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    ishwa na mila potofu kama sehemu ya dini.

    Katika maisha ya makabila mbali mbali utakuta mila fulani zilizounganana dini na kuwa sehemu ya dini! Kadri urithi huu utakavyopitia vizazi kad-haa, ndivyo itakuwa vigumu kutenganisha dini ya kweli, mbali na milaambazo mara nyingi ni potofu. Na hiyo ndiyo sababu kubwa inayofanyaUislamu uonekane mgumu kutokana na Waislamu kulazimika kutekelezayasiyohusiana na dini. Hali hii yadhihirisha kuwa Uislamu tulionao wakatihuu ni mchaganyiko wa dini na utamaduni. Haya yote yaonyesha kuwa,katika kipindi kirefu cha karne 14 za Uislamu wetu huu, dini yetu imepitiamikononi mwa watawala wengi na tamaduni nyingi kiasi kwamba kunakasoro nyingi zilizopenyeza katika mafunzo halisi ya dini na kubadili suraya Uislamu kiasi kikubwa.

    Ukichunguza utaona kuwa hiyo ni sababu mojawapo iliyopelekea kutu-gawanya Waislamu kwa sababu tamaduni za mataifa na makabila mbalimbali zinatofautiana, na hivyo hivyo watu wanatofautiana matendo yao.Bali kama tulivyotangulia kuona, dini ni amri za Mwenyezi Mungu zisi-zobadilika na ndiyo maana hatustahili kabisa kurithi dini. Tunatakiwakuelewa dini kwa kutumia elimu za kutegemewa. Qurani nayoinatukataza imani za dini za kurithi.

    Na wanapoambiwa Njooni katika njia ya Mwenyezi Mungu naMtume husema: Yale tuliyowakuta nayo baba zetu yanatutosha.Vipi! Hata kama baba zao hawakujua kitu na hawakufuata njia yahaki? (Qurani 5:104).

    Qurani inawakemea wale ambao hungangania waliyorithi kwa wazaziwao bila kuyachunguza kujua asili yake ni nini. Aya hii inakubaliana na

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:19 PM Page 23

  • 24

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    ukweli kwamba ibada yoyote anayofanya mtu bila kuielewa binafsi, kwamfano kuswali Swala tano kwa sababu ya kulinda heshima ya marehemubaba yako aliyekuwa anasali kila siku, ili na wewe uonekane mchamungukama baba yako! Swala kama hiyo haipokelewi na Mwenyezi Mungu kwasababu unatakiwa kuswali Swala tano kwa kutambua wajibu wako kwaMwenyezi Mungu tu. Kwa hiyo mtu mwenye kutambua wajibu wake huo,siku zote atajitahidi kuswali kwa kufuata kanuni za Mwenyezi Mungu ilikumridhisha na kukubaliwa Swala zake. Na ili kuzifahamu kanuni zaMwenyezi Mungu, itambidi mhusika atafute elimu. Hebu tuone Quraniinasemaje:

    Vipi! yule mnyenyekevu wakati wa usiku wa manane, akisujudu nakurukuu, akijitayarisha kwa (safari) ya akhera na kutumaini msama-ha wa Mola wake! Sema: Je, wale wenye elimu na wale wasio na elimuni sawa? Ni wale wenye ujuzi ndio wenye kujali. (Qurani 39:9).

    Aya hii yaonyesha kuwa hakuna nafasi ya ujinga katika dini. Kila una-chokifanya ukifanye kwa ujuzi na yakini. Aya zifuatazo zinaonyesha kuwakama mtu alipotezwa na watu wengine, hata hivyo asitegemee msamahakwa sababu itakuwa kinyume na lengo la binadamu kupewa akili. Lazimabinadamu awajibike kwa matumizi mabaya ya akili yake:

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:19 PM Page 24

  • 25

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    (a) Na wote watahudhuria mbele ya Mwenyezi Mungu (ili awalipe);Hapo wanyonge waliopotea kwa ajili ya kuwafuata wakubwa zaowaliojivuna watawaambia: Hakika tulikuwa wafuasi wenu, jemnaweza kutuondolea kitu kidogo hivi katika adhabu ya MwenyeziMungu? Hao wakubwa zao watajibu kuwa, AngalituongozaMwenyezi Mungu bila shaka tungelikuongozeni. Lakini sasa ni mamo-ja kwetu tukitapatapa au tukisubiri hatuna pakukimbilia. (Qurani14:21).

    (b) Wakati wale waliofuatwa (viongozi) watakapowakana wafuasi(wao) huku wakiona adhabu yao (inayowasubiri); (hali ya kuwa) uhu-siano wao (wa kidunia) umekatwa. (Qurani 2:166).

    (c) Na wale wafuasi watasema: Kama tungeweza kurejea (duniani),tungewakana kama walivyotukana. Hivyo Mwenyezi Munguatawaonyesha matendo yao ambayo watayajutia majuto makuu, nahawataondolewa motoni. (Qurani 2:167).

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:19 PM Page 25

  • 26

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    (d) Atasema: Ingia motoni kati ya umma zilizopita kabla yenu mion-goni mwa majini na binadamu; kila umma utakapoingia, utawalaaniwa nyuma yake mpaka wote watakapoingia motoni; wa mwisho waowatasema kuwaambia waliotangulia: Ee Mwenyezi Mungu! hawa(ndio) waliotupoteza kwa hiyo wape adhabu mara mbili motoni. NayeAtasema: Kila mmoja wenu atapata (adhabu) mara mbili ila hamfa-hamu. (Qurani 7 : 38 ).

    Nimetangulia kueleza jinsi ambavyo Uislamu ulikuwa kitu kimoja palemwanzoni katika uhai wa Mtume (s.a.w.w.). Lakini tunaona leo hiiWaislamu dunia nzima tumegawanyika makundi mawili kiitikadi nayo niSHIA NA SUNNI. Duniani Waislamu wote jumla yetu ni bilioni moja.Kati ya idadi hiyo, Waislamu milioni 750 ni madhehebu ya SUNNI, naWaislamu milioni 250 ni madhehebu ya SHIA. Sasa tuchunguze kwa ninikulitokea mfarakano huu miongoni mwetu.Mara tu alipofariki Mtume (s.a.w.w.) kabla hata hajazikwa, kulitokea fiti-na kubwa miongoni mwa Waislamu wa wakati huo walioishi hapo Madina.Kulitokea kundi moja likadai kuwa Mtume (s.a.w.w.) hakuacha wasiakuhusu uongozi wa Waislamu kwa hiyo Waislamu wachague kiongozi waUmma wa Waislamu. Lakini kundi la pili la Waislamu walikataa na kuse-ma kuwa Mtume (s.a.w.w.) katika uhai wake, na katika matukio kadhaa,alieleza wazi Uongozi wa Waislamu baada yake. Kwa ndugu zetu Sunni(au Ahlul Sunna Wal-Jamaa) wanadai kuwa Mtume (s.a.w.w.) hakuachawasia. Tuahirishe kidogo kujadili hoja zao na tuanze na madai ya ShiaIthnasheri ambao tunasisitiza kuwa Mtume (s.a.w.w.) aliacha wasia. Hatahivyo kabla ya kuzama katika mjadala huu, ni vizuri kwanza tupatemwangaza juu ya uhalali wa vitabu vinavyotambuliwa kuwa ni sahihi kwaupande wa madhehebu ya Sunni. Vitabu hivyo idadi yake ni sita ambavyohuitwa Sitat Sihah navyo ni hivi vifuatavyo:Sahih Bukhari.Sahih Muslim. Sahih Tirmidhi.Sunan Ibn Majah.Sunan Abi Daud.

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:19 PM Page 26

  • 27

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    Sunan Nasai.

    Hivi ndivyo vitabu vinavyotegemewa sana na madhehebu ya Sunni baadaya Qurani. Ushahidi mwingi wa kuthibitisha maelezo yaliyomo humu,umetolewa katika vitabu hivyo kwa kiasi kikubwa. Lakini katikaulimwengu wa wasomi wa dini na historia ya dini, kuna vitabu vingi zaidivya kutegemewa kama tutakavyoona mbele Inshallah. Historia ya Uislamuni ndefu sana.

    Kwa Waislamu wenye ujuzi wa historia kidogo ya Nabii Musa (a.s.), NabiiIbrahim (a.s.) na Nabii Isa (a.s.) wanafahamu kuwa Manabii wote haowaliacha warithi wao nyuma yao ili waendeleze dini katika misingi ile ileingawa mazingira ya wakati huo hayakuwawezesha warithi hao kufanyakazi yao kwa ufanisi. Na kwa kuwa Manabii wote wanaongozwa naMwenyezi Mungu, bila shaka uchaguzi huo wa warithi ni wa MwenyeziMungu. Qurani (38:26), (21:73), (3:30), (28:68), (28:5). Nabii Adamalimteua Shiith. Nabii Ibrahim alimteua Ismail. Nabii Yakub alimteuaYusuf. Nabii Musa alimteua Yusha bin Nuun. Nabii Isa alimteua Shamuun.Nabii Muhammad alimteua Imam Ali Ibn Abu Talib.

    Ilimradi sisi Waislamu tunachambua Biblia na kuwaeleza Wakristo kuwadini ilikuwa ni moja kwa Manabii wote, itakuwaje Nabii wetu Muhammad(s.a.w.w.) alifariki bila kuacha wasia juu ya nani awe kiongozi nyumayake? Wakati ambapo Manabii waliomtangulia katika dini ile ile, waliachawarithi wao kwa amri ya Mwenyezi Mungu?

    Tukirejea kwenye Qurani tunaona kuwa Mwenyezi Mungu ameamrishakuandika wasia (Qurani 2:180) na (Qurani 2:240). Kwa maana hiyotutambue kuwa Mtume (s.a.w.w.) alikuwa mstari wa mbele kutekelezaamri zote za Mwenyezi Mungu yaani Qurani. Ilipoteremka amri yakuswali au kuhiji au kufunga Ramadhan, Mtume (s.a.w.w.) alitekelezamara moja. Hakuna wakati ambapo Mtume (s.a.w.w.) alipuuza amri yoy-ote ya Mwenyezi Mungu hata iwe ndogo namna gani. Kwa misingi hiyo nivipi Mtume (s.a.w.w.) angeacha kuandika wasia na hivyo kumuasiMwenyezi Mungu! Tuchambue mambo kibusara.

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:19 PM Page 27

  • 28

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    Uongozi wa Waislamu baada ya Mtume (s.a.w.w.) umeelezwa pia katika Biblia

    Suala hili la uongozi wa Waislamu baada ya Mtume (s.a.w.w.) ni jambozito sana kwa sababu ndilo limetugawanya Waislamu siku ile ile aliyofari-ki Mtume (s.a.w.w.). Ingawa matukio kadhaa ya kihistoria yanaonyeshakuwa njama za kuhujumu wasia wa Mtume (s.a.w.w.) juu ya suala hili, zil-ifanyika mapema kwa kificho kabla hajafariki. Kimsingi ni kwamba, mak-abila fulani ya Waarabu hayakufurahia kuona ukoo wa Mtume (s.a.w.w.)unapata Utume na kisha uongozi baada ya Mtume nao unaendelea kuwakatika ukoo wa Mtume (s.a.w.w.) wa Bani Hashim. Chuki za kijahiliyandilo chimbuko la mgogoro huu wa uongozi baada ya Mtume (s.a.w.w.):

    Hakika dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na waliopewakitabu hawakuhitilafiana ila baada ya kuwajia elimu, kwa sababu yahasadi tu baina yao. Na anayezikataa aya za Mwenyezi Mungu, basihaikia Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu. (3:19);

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:19 PM Page 28

  • 29

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    Watu walikuwa kundi moja, basi Mwenyezi Mungu akawapelekeamanabii watoao habari njema na waonyao, na pamoja naoakateremsha Kitabu kwa haki, ili ahukumu baina ya watu katika yalewaliyohitilafiana. Wala hawakuhitilafiana katika hicho (Kitabu) ilawale waliokipewa baada ya kuwafikia dalili zilizo wazi, kwa sababu yauasi kati yao. Hapo Mwenyezi Mungu akawaongoza walioamini kwayale waliyohitilafiana katika haki kwa idhini Yake, na MwenyeziMungu humuongoza amtakaye kwenye njia iliyonyooka. (2:213)

    Na hawakutengana ila baada ya kuwafikia elimu, kwa sababu ya uasibaina yao na kama isingelikuwa kauli iliyotangulia kutoka kwa Molawako juu ya muda uliowekwa, lazima ingelihukumiwa (sasa hivi). Nakwa hakika wale waliorithishwa Kitabu baada yao wanakitilia shakainayowahangaisha. (42:14)

    Na tukawapa maelezo wazi ya amri, lakini hawakukhitilafiana ilabaada ya kuwafikia elimu, kwa uasi tu baina yao, hakika Mola wakoatahukumu kati yaoSiku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wakihiti-lafiana. (45:17)

    Lakini kwa msimamo wetu Waislamu, kwamba dini ilikuwa moja yaUislamu kwa manabii wote, hebu tuangalie katika Biblia tuone maelezo

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:19 PM Page 29

  • 30

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    kuanzia kwa Nabii Ibrahim (a.s.) hadi mpaka kwa Mtume wetuMuhammad (s.a.w.w.) na kizazi chake (a.s.).

    Nabii Ibrahim (a.s.) aliwazaa watoto wawili yaani Nabii Ishaqa (a.s.) kwaupande wa Wayahudi, na Nabii Ismail (a.s.) kwa upande wa Waarabu.Baada ya Wayahudi kutowatii Mitume, Nabii Isa (a.s.) aliwaeleza kuwaufalme wa Mungu utaondolewa kwao na kupelekwa kwa ndugu zao yaaniWaarabu. Tazama (Kumbukumbu ya Torati. 18:15).

    Kutokana na kizazi cha Nabii Ismail (kwa kufupisha maelezo) ukapatikanaukoo mtukufu wa Bani Hashim kwa vizazi mbali mbali hadi kufikia kuza-liwa Mtume (s.a.w.w.). Kwa hiyo kwa kuzaliwa Mtume Muhammad,ikawa ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa Nabii Ibrahim imetimiaalipomwambia kuwa:

    Ibrahimu akamwambia: Lau kwamba Ishmaeli angeishimbele yako. Mungu akasema, sivyo, lakini Sara mkeoatakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka.Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano lamilele kwa ajili ya uzao wake baada yake. (Bibila; Mwanzo:17:18-19)

    Utabiri huu unaonyesha jinsi ambavyo Mwenyezi Mungu alitimiza ahadiya kubariki kizazi cha Nabii Ibrahim (a.s.) kupitia kwa mwanae NabiiIsihaka (a.s.) kwa kuendeleza kizazi chake hadi kwa Nabii Isa (a.s.).Mwisho Nabii Isa (a.s.) anawaeleza Wayahudi kwamba utukufu wa kabilalao kuendelea kuwa na Manabii umekwisha na utahamia kwa ndugu zaowaarabu yaani kizazi cha kaka yake (baba mmoja) Ismail (a.s.).

    .. Na kwa habari za Ishmail nimekusikia, nimembarika, nita-mzidisha, nami nitamuongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi nawawili, nitamfanya awe taifa kuu. (Biblia: Mwanzo: 17: 20).

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:19 PM Page 30

  • 31

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    Kisha inaelezwa katika Biblia kuwa viongozi kutoka kizazi cha kuanziakwa Nabii Ismail (a.s.) hadi kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.), wataende-lea kutoka kizazi hicho hata baada ya uhai wa Nabii Muhammad (s.a.w.w.):Kwani Bwana Mungu wako amemchagua katika kabila zako zote, asi-mame atumike kwa jina la Bwana, yeye na wanawe milele. (Kumb.Torati 18:5).

    Nabii aliyechaguliwa kwa mataifa yote ni Mtume Muhammad (s.a.w.w.)lakini uongozi wake ni pamoja na wanawe, tena milele! Milele maanayake hadi Siku ya Kiyama. Hapa tutaona kuwa, kwa kadri ya maelezo yamwenyewe Mtume (s.a.w.w.) katika Hadithi na Qurani, watoto wake niAHLUL-BAYT wake waliokusudiwa katika (Qurani 33:33) kamatutakavyoona katika maelezo ya mbele kwa ushahidi kamili. Maana yakeni kwamba utume na ukhalifa vyote vilipangwa kutokana katika ukoomtukufu wa Bani Hashimu.

    Hiyo, ni mipango ya Mwenyezi Mungu kwa sababu angependa angemletaMtume toka kwa Waarabu tu bila kupitia ukoo maalumu unaotokana naNabii Ismail (a.s.) moja kwa moja hadi kwa Nabii Ibrahim (a.s.). Ndiyomaana kabila la Quraish (lenye maana ya wakusanyaji) ni kabila lakizazi cha Nabii Ismail (a.s.). Kabila hilo ndilo lilikuwa na hadhi kubwamiongoni mwa Waarabu kwa sababu ya kazi yao ya heshima ya kuwa wal-inzi wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu yaani Al-KAABA ambayo ilijeng-wa kwa mara ya kwanza na Nabii Ibrahim (a.s.) akisaidiana na mwanae(Nabii Ismail).

    Hakika Mwenyezi Mungu amemchagua Adam na Nuh na kizazi chaIbrahim na kizazi cha Imran juu ya walimwengu. Kizazi cha wao kwawao, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. (3:33-34)

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:19 PM Page 31

  • 32

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    Au wanawahusudu watu kwa yale aliyowapa Mwenyezi Mungu kati-ka fadhila Zake? Basi bila shaka tuliwapa watoto wa Ibrahim Kitabuna hekima, na tukawapa mamlaka makubwa. (4:54)

    Utukufu wa Bani Hashim

    Katika masomo yatakayofuata baadaye, tutapata maelezo juu ya Waarabuwa makabila ya BANI UMAYYAH na BANI ABBAS, wakipinga kwa niniukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w.) uendelee kuwa katika ukoo wa BANIHASHIM. Utukufu wa Bani Hashim unaanzia kabla hata ya Uislamu waMtume (s.a.w.w.). Kumbukumbu za historia zinatueleza kuwa: Baada yaHajira mke wa Nabii Ibrahim (a.s.) kuachwa jangwani pamoja na mwanaeIsmail kwa amri ya Mwenyezi Mungu, mahali hapo kwa miujiza kulitokeachemchem ya maji inayoitwa Zamzam. Kabila moja lililojulikana kamaJarham lilipoona kisima hicho kipya cha maji, liliomba ruhusa ya kuhamiahapo na likakubaliwa na Nabii Ibrahim (a.s.).

    Nabii Ismail (a.s.) alipofikia utu uzima akaoa katika kabila hilo na kupatawatoto 12 ambao mkubwa kabisa akiitwa Cedar (kwa lugha ya Kiyunani).Wana wa Ismail waliogezeka sana. Baada ya kupita vizazi kadhaa alitokeammojawapo katika kizazi hicho aliyeitwa Quraish.

    Wakati huo alikuwepo mtu toka katika kabila la Khuzaa aliyeitwa Hulail.Huyu alikuwa na dhamana ya kutunza Al-Kaaba wakati huo. IkawaQuraish amemwoa binti wa Hulail na huyo Hulail kabla ya kufariki aliusiakuwa dhamana yake ya kutunza Al-Kaaba amemrithisha Quraish. Quraishalianzisha taasisi nyingi mpya kama Dar-un-Nadwa (nyumba ya kukuta-nia), mahali ambapo majadiliano muhimu kama vita au amani yalifanyika.

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:19 PM Page 32

  • 33

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    Misafara ya biashara ilikutana hapo kabla ya kuanza safari zao.

    Quraish alianzisha utaratibu wa Siqayah (kuwapatia maji mahujaji) nautaratibu wa Rifada (kuwalisha mahujaji) siku hizo. Utaratibu huo kwakadri ya Tarikh Tabari uliendelea kwa miaka 500 baada ya kufarikiQuraish. Vile vile ni huyo Quraish aliyefanya matayarisho kuwawezeshamahujaji kulala usiku pale Mash-arul-Haram katika ibada ya Hijja.Alikuwa akimulika bonde hilo kwa taa (mioto) nyingi usiku ili mahujajiwasipate taabu. Ni huyo Quraish aliyejenga upya Al-Kaaba na kuchimbakisima cha kwanza cha maji hapo Makka kwa sababu wakati huo kisimacha Zamzam kilishafukiwa muda mrefu kisijulikane mahali kilipokuwatena. Wanahistoria wanakiri kwamba huyo Quraish alikuwa Mkarimu, shu-jaa na mwenye huruma. Mawazo yake yalikuwa safi na tabia yake yakuvutia. Neno lake liliheshimiwa na kutekelezwa kama dini hata alipok-wishafariki. Watu walizoea baadaye kuzuru kaburi lake huko Hajun mahaliambapo leo panaitwa Jannatul-Maala.

    Quraish alikuwa kiongozi mkuu (chief) wa kabila lake ambalo liliitwa jinahilo hilo kwa heshima yake ya uongozi mwema. Alibeba majukumu yoteyaliyoinua hadhi ya kabila hilo yaani dhamana ya Al-Kaaba (Hijaba), kun-ywesha na kulisha mahujaji yaani (Rifada na Siqaya). Alikuwa mshikabendera ya vita (Liwa) na alikuwa Amiri Jeshi Mkuu wakati wa vita(Qiyada). Hizi ndizo sifa kuu zilizowafanya kabila la Quraish kuheshimi-wa na makabila mengi ya Waarabu.

    Huyu Quraish alipata watoto 6 wa kiume na mtoto mmoja wa kike. Katikawatoto wa kiume Abdud-Dar alikuwa mkubwa zaidi akifuatiwa naMughira (aliyejulikana kama Abd Munaf). Lakini Quraish alimpenda sanaAbdud-Dar na hivyo alipokaribia kufariki alimkabidhi Abdud-Dar majuku-mu yote makuu sita ya kabila la Quraish yaliyotajwa hapo juu.

    Hata hivyo Abdud-Dar hakuwa mwenye uwezo wa kuongoza, wakatiambapo Abd Munaf alionekana mwenye sifa zote za uongozi na hivyo

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:19 PM Page 33

  • 34

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    watu walimtii kama kiongozi wao. Kwa hali hiyo ilibidi Abduddarashirikiane majukumu hayo kwa pamoja na Abd Munaf. Mwisho AbdMunaf alitokea kuwa kiongozi mkuu wa kabila la Quraish.

    Abd Munaf alipata watoto wa kiume 6 nao ni Hashim, Muttalib, Abddus-Shams na Nawfil. Hakukuwepo mgogoro wowote katika uhai wa Abdud-Dar na Abd Munaf. Walipofariki ndipo mgogoro ukaanza miongoni mwawatoto hao kuhusiana na majukumu sita niliyoyataja chini ya dhamana yakabila la Quraish. Ilikaribia kutokea vita katika mgogoro huo, lakinimakubaliano yalifikiwa kwamba majukumu ya Siqaya, Rifada na Qiyadayatekelezwe na watoto wa Abd Munaf; na kwamba majukumu ya Liwa naHijaba yabakie kwa watoto wa Abdud-Dar. Iliamuliwa pia kwambauenyekiti wa Darun-Nadwa watashirikiana pande zote mbili. Na hapoikawa mgogoro umekwisha.

    Bwana Hashim

    Jina la bwana huyu ni maarufu na litaendelea kungara katika historia yaArabuni na Uislamu. Si kwa sababu tu alikuwa babu mkubwa wa Mtume(s.a.w.w.) bali kutokana na mafanikio makubwa aliyoyapata katika uhaiwake. Alikuwa mkarimu mno, mwenye hadhi kubwa ya kuheshimiwa nawote kama kiongozi wa Quraish. Alikuwa akiwalisha mahujaji katikakipindi cha Hijja kwa moyo mkunjufu. Lakini kigezo kikubwa cha heshi-ma yake kuu ni jina hilo la Hashim.

    Wakati fulani kulitokea njaa kubwa sana Uarabuni. Bwana Hashim haku-vumilia kuona mateso kwa wakazi wa Makka. Alichukua utajiri wake woteakaenda Syria akanunua unga na mikate mikavu (mofa) akavileta. Kishaikawa kila siku anachinja ngamia kadhaa kupika supu ya nyama, mikate namofa na kuwalisha watu wote hadi njaa ikaisha. Ni kitendo hicho kili-chomjengea heshima kubwa kwa watu na akawa ameitwa Hashim yaani(anayevunja mikate) ingawa jina lake hasa lilikuwa Amr.

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:19 PM Page 34

  • 35

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    Bwana Hashim ndiye mwanzilishi wa misafara ya biashara ya Maquraishi.Aliingia mikataba ya amani na makabila yote yaliyo katika njia kuu yamisafara, kwa sababu siku hizo kulikuwepo na ujambazi na uporaji wamali za wafanyabiashara. Aliingia pia katika mkataba na Mfalme wa dolaya Byzantine ili kusamehewa ushuru wa aina zote na kodi katika misafaraya biashara ya Maquraishi. Kwa hiyo Maquraishi walianza misafara yabiashara huko Yemen, Syria mpaka Ankara-Uturuki kwa amani. Kutokanana mafanikio aliyoyapata Hashim siku hizo, ndiyo maana katika QuraniMwenyezi Mungu anaelezea tukio hilo kama neema kubwa ya MwenyeziMungu kwa Maquraishi:Kwa ajili ya Maquraish kuzoea, kuzoea safari za Kusi na Kaskazi,

    basi wamuabudu Mola wa Nyumba hii, Anayewalisha wakati wa njaana kuwapa amani wakati wa hofu. (Suratul Quraish).

    Utamaduni wa Maquraishi

    Kulikuwepo na mila ya kutokuwa na matumaini mema iliyoitwa ihtifad.Mila hii ilitumika wakati wa shida ili kulinda heshima ya kabila lao. Iwapofamilia fulani ilikuwa maskini sana na kushindwa kujipatia chakula, famil-ia yote huondoka kwenda jangwani na kupiga hema na kukaa hadi kifokiwamalize wote mmoja mmoja bila siri yao kujulikana kwa watuwengine; na hivyo kulinda heshima yao.

    Bwana Hashim ndiye aliyesimamisha mila hiyo ya kudhalilika na umaski-ni, na badala yake akaweka mikakati ya kuupiga vita umaskini. Alibuniutaratibu wa kumwunganisha maskini mmoja kwa tajiri mmoja ili mradifamilia (wanaomtegemea huyo tajiri na wanaomtegemea maskini) zaoziwe sawa kwa idadi. Kazi ya maskini ni kumsaidia tajiri katika misafaraya biashara. Ziada inayopatikana juu ya mtaji wa tajiri, wagawane sawa; nahivyo umuhimu wa ihtifad hautakuwepo tena. Mpango huo ulipokelewana wote na sio tu uliondoa ufukara, bali pia ulizidisha udugu na mshika-mano miongoni mwao. Matendo hayo yangehalalisha umri mrefu kwaBwana Hashim, lakini ukweli ni kuwa alifariki akiwa mdogo kwa umri wamiaka 25 tu mnamo miaka kama 82 kabla ya kuzaliwa Mtume (s.a.w.w.)

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:19 PM Page 35

  • 36

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    yaani mwaka (488 A.D).

    Bwana Hashim alikuwa kijana mwenye haiba nzuri na hivyo watawala namachifu mbali mbali walitaka aoe binti zao. Lakini alimwoa Salma bintiwa Amr. (kutoka kabila la Adi Bani Najjar) huko Madina. Mke wake huyondiye mama yake Bwana Shaibatul-Hamd (aliyejulikana kama Abdul-Muttalib). Huyu Bwana Abdul-Muttalib alikuwsa mtoto mchanga wakatiBwana Hashim alipofariki.

    Bwana Hashim alipata watoto 5 wa kiume lakini watatu hawakupata uzazi.Kati ya watoto hao, Asad alipata mtoto wa kike tu naye akiitwa Fatima BintAsad - mama yake Imam Ali Ibn Abi Talib. Kwa hiyo ni kutoka kwaBwana Abdul-Muttalib ambapo kizazi cha Hashim kiliendelea baada yake.

    Bwana Abdul-Muttalib

    Bwana Abdul-Muttalib alizaliwa Madina kwa babu yake mzaa mama. Kazizote za Bwana Hashim zilirithiwa na Bwana Muttalib. Bwana Muttalibalikwenda Madina na kumleta bwana Shaibatul-Hamd yaani mjombawake. Waliporejea Makka, wakazi wa pale wakadhani kuwa BwanaMuttalib kamleta mtumwa wake (yaani huyo bwana Shaibatul-Hamd).Kwa hali hiyo ikawa Shaibatul-Hamd ameitwa Abdul-Muttalib kwa maanaya mtumwa wa Muttalib, ingawa Bwana Muttalib aliwaeleza wazi kuwahuyo ni mjomba wake! Hata hivyo likashika jina hilo la Abdul-Muttalib.

    Bwana Muttalib alimpenda sana Abdul-Muttalib lakini Abdus-Shams naNawfil walimchukia. Alipofariki Bwana Muttalib, Abdul-Muttalibalirithishwa majukumu yake yaani kutoa huduma ya maji na chakula kwamahujaji (Siqaya na Rifada). Pamoja na uadui wa wajomba zake wawili,matendo yake mema na sifa za uongozi mwema alizokuwa nazo zilimfanyakupata cheo cha Seyyidul-Batha, yaani, Chifu wa Makka. Kuna baadhiya mashekhe wanaojaribu kueleza kuwa wazazi wa Mtume (s.a.w.w.)hawakuwa Waislamu! Madai hayo si kweli kwa sababu ingawa Waarabu

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:19 PM Page 36

  • 37

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    walikuwa katika ujinga mkubwa wa kiroho wakati huo, ukoo wa BaniHashim waliishi katika misingi ya maadili na sheria za kiislamu (Tawhiid)pamoja na kwamba hakuwepo mtume yeyote. Bila shaka MwenyeziMungu alipanga kuongoza ukoo huu katika usafi wa kiroho, akijua kuwamwisho wake atazaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) mahali hapo.Haiwezekani Mwenyezi Mungu apandikize mbegu bora kwenye shambachafu! Tunafikia uamuzi huu kutokana na maelezo yafuatayo.

    Bwana Abdul-Muttalib aliwazuia watoto wake kunywa pombe. Alikuwaakiingia Pango la Hira Mfungo wa Ramadhan na kutumia muda wa mwezimzima kumkumbuka Mwenyezi Mungu (dhikri) na kuwalisha maskini.Alikuwa pia anaendeleza kazi za baba yake na mjomba wake za kuwalishamahujaji msimu wa Hijja. Hata wanyama na ndege walilishwa mwakamzima toka kwake; na kwa hali hiyo aliitwa pia jina la Mutimut-tayr(Mlisha ndege).

    Baadhi ya hukumu za dini tunazozitumia wakati huu, zilianzia katika uhaiwa Bwana Abdul-Muttalib. Kwa mfano alikuwa wa kwanza kuweka nad-hiri kama tunavyoitumia leo hii na hukumu zake kidini. Alianzisha huku-mu ya kutoa Khumsi (Qurani 8:41) katika njia ya Mwenyezi Mungu.Alizuia ndoa kati ya watu wasiostahili kuoana kama ilivyo sasa hivi.Mwizi alikatwa mkono. Uzinifu ulikatazwa katika kabila lake. Alizuia milaya kuwaua watoto wa kike wanapozaliwa. Alizuia kutufu Al-Kaaba bilanguo yaani uchi. Alipanga kiwango cha fidia kwa mauaji yasiyo yakukusudia, ngamia 100. Hukumu hizi ziliendelea kutumika mara Uislamuulipoanza baadaye yaani baada yake. Ingekuwa hukumu hizi zote hazion-gozwi na Mwenyezi Mungu vipi ziendelee kutumika katika Uislamu?Watu wanaoongozwa na Mwenyezi Mungu hawawezi kuwa makafiri. Historia ya Bwana Abdul-Muttalib ni ndefu mno lakini nitaeleza machachejinsi alivyogundua upya Kisima cha Zamzam kilichojazwa takataka nakupotea muda mrefu kabla ya yeye kuzaliwa. Kisha nitaeleza jaribio lakuishambulia Al-Kaaba lililopangwa na Gavana wa Ethiopia bilamafanikio.

    Asili ya ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd 7/1/2011 12:19 PM Page 37

  • 38

    A s i l i y a M a d h e h e b u k a t i k a U i s l a m u

    Kisim