10, february 16, swahili - wordpress.com · mambo muhimu katika toleo hili: hekalu 2 mafundisho ya...

9
EGWEBO katika AUA Namba. 10 FEBRUARI 2016 1 Mambo Muhimu KATIKA TOLEO HILI: Hekalu 2 Mafundisho ya Hekalu 4 Hukumu ya Upelelezi 5 Kristo Hekaluni 6 Makala ya Watoto 7 EGWEBO kwa ajili yako 8 Kongamano kuhusu Roho ya Unabii 9 “Mafundisho ya hekalu, ikiwa ni pamoja na mafundisho ya hukumu ya upelelezi, na imani kuwa Ellen White alivuviwa na Mungu, ni ya kipekee kwa Waadventista Wasabato. Kama Kristo hakuanza huduma ya hukumu ya upelelezi mbinguni mwaka wa 1844, na kama Ellen White hakuwa mjumbe mteule wa Mungu, kanisa la Waadventista Wasabato wangepoteza mafundisho mawili yanayowabainisha kama kikundi la kinabii, lililoteuliwa na Mungu ili kuandaa njia kwa ajili ya ujio wa pili wa Kriso” (R. W. Olson, 101 Questions on the Sanctuary and on Ellen White, 6). Ili kuwasilisha mpango wake wa wokovu kwa wanadamu, Mungu aliwaamuru wajenge hekalu takatifu. Hii ilikuwa iwe mahali ambapo angeweza kuja na kukaa kati yao. Maelezo yote ya hekalu hili, ikiwa ni pamoja na huduma zake za kila siku na kila mwaka, ilikuwa mfano wa lile hekalu takatifu lililoko kwenye makao makuu ya ulimwengu wa Mungu mbinguni. Hakuna mada katika biblia iliyo kubwa kuliko hadithi ya ukombozi—jinsi Mungu, kwa upendo wake usio na mipaka, anawaokoa wanadamu kutoka kwa uovu na kuwapa nafasi ya kuishi milele. Watu wa Mungu wanavyozidi kujifunza neno lake, ndivyo wanavyozidi kuona upendo wake wa ajabu na gharama yake. Kwenye kurasa za Biblia wanamwona Mungu akiweka mpango sio tu kurejesha picha yake ndani yao, lakini pia kuifanya vitendo katika maisha yao. Wanachofanya wateule wa Mungu— iwe ni katika ibada, kazi, maisha yao ya kifamilia, wanachosema, kusikia au kuona na hata katika njia zao za kula — haya yote yanachangia kwa wao kukubali au kukataa upendo wa Mungu. Hivyo ndivyo ilivyo kwenye hekalu. Mpango wa Mungu wa kuwarejesha watu wake wa thamani wawe watu wa mfano wake unapatikana pale. “Yesu ndiye mkombozi wetu leo. Anatuombea kwenye pahali patakatifu sana pa hekalu la kule mbinguni, na atatusamehe dhambi zetu. Jambo hili linaleta tofauti mkubwa kwetu duniani ikiwa tunamtegemea Mungu bila shaka, kama juu ya msingi dhabiti, au kama tunatafuta na kujipa haki sisi wenyewe kabla ya kumjia. Tuache ubinafsi na tuangaze macho yetu kwa mwana kondoo wa Mungu, aondoaye dhambi za ulimwengu” (RH, Aprili 22, 1884). Swali kuu ni hili, je, wewe uko wapi katika mpango wa Mungu wa wokovu? Je, una imani kabisa katika uwezo wake kukuokoa, au unajitegemea kwa sehemu zingine? Usiruhusu hata wazo lije akilini mwako kwamba unaweza kupata wokovu kwa uzuri wako wewe mwenyewe. “Pata ukombozi upatikanao katika Kristo Yesu” (2 Tim 2:10) kwa unyenyekevu wazi wa imani yako. Mpate mwokozi wako kwenye hekalu na umfuate yeye tu. Mruhusu Kristo akubadilishe wewe kutoka moyoni na kukufanya mtu afaaye uzima wa milele pamoja na Uungu, malaika wake, na wote waliokombolewa.

Upload: others

Post on 06-Nov-2020

18 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: 10, February 16, Swahili - WordPress.com · Mambo Muhimu KATIKA TOLEO HILI: Hekalu 2 Mafundisho ya Hekalu 4 Hukumu ya Upelelezi 5 Kristo Hekaluni 6 ... Jambo hili linaleta tofauti

EGWEBO katika AUA Namba. 10 FEBRUARI 2016

1

Mambo Muhimu

KATIKA TOLEO HILI: Hekalu 2 Mafundisho ya Hekalu 4 Hukumu ya Upelelezi 5 Kristo Hekaluni 6 Makala ya Watoto 7 EGWEBO kwa ajili yako 8 Kongamano kuhusu Roho ya Unabii 9

“Mafundisho ya hekalu, ikiwa ni pamoja na mafundisho ya hukumu ya upelelezi, na imani kuwa Ellen White alivuviwa na Mungu, ni ya kipekee kwa Waadventista Wasabato. Kama Kristo hakuanza huduma ya hukumu ya upelelezi mbinguni mwaka wa 1844, na kama Ellen White hakuwa mjumbe mteule wa Mungu, kanisa la Waadventista Wasabato wangepoteza mafundisho mawili yanayowabainisha kama kikundi la kinabii, lililoteuliwa na Mungu ili kuandaa njia kwa ajili ya ujio wa pili wa Kriso” (R. W. Olson, 101 Questions on the Sanctuary and on Ellen White, 6).

Ili kuwasilisha mpango wake wa wokovu kwa wanadamu, Mungu aliwaamuru wajenge hekalu takatifu. Hii ilikuwa iwe mahali ambapo angeweza kuja na kukaa kati yao. Maelezo yote ya hekalu hili, ikiwa ni pamoja na huduma zake za kila siku na kila mwaka, ilikuwa mfano wa lile hekalu takatifu lililoko kwenye makao makuu ya ulimwengu wa Mungu mbinguni.

Hakuna mada katika biblia iliyo kubwa kuliko hadithi ya ukombozi—jinsi Mungu, kwa upendo wake usio na mipaka, anawaokoa wanadamu kutoka kwa uovu na kuwapa nafasi ya kuishi milele. Watu wa Mungu wanavyozidi kujifunza neno lake, ndivyo wanavyozidi kuona upendo wake wa ajabu na gharama yake. Kwenye kurasa za Biblia wanamwona Mungu akiweka mpango sio tu kurejesha picha yake ndani yao, lakini pia kuifanya vitendo katika maisha yao. Wanachofanya wateule wa Mungu— iwe ni katika ibada, kazi, maisha yao ya kifamilia, wanachosema, kusikia au kuona na hata katika njia zao za kula —haya yote yanachangia kwa wao kukubali au kukataa upendo wa Mungu.

Hivyo ndivyo ilivyo kwenye hekalu. Mpango wa Mungu wa kuwarejesha watu wake wa thamani wawe watu wa mfano wake unapatikana pale. “Yesu ndiye mkombozi wetu leo. Anatuombea kwenye pahali patakatifu sana pa hekalu la kule mbinguni, na atatusamehe dhambi zetu. Jambo hili linaleta tofauti mkubwa kwetu duniani ikiwa tunamtegemea Mungu bila shaka, kama juu ya msingi dhabiti, au kama tunatafuta na kujipa haki sisi wenyewe kabla ya kumjia. Tuache ubinafsi na tuangaze macho yetu kwa mwana kondoo wa Mungu, aondoaye dhambi za ulimwengu” (RH, Aprili 22, 1884).

Swali kuu ni hili, je, wewe uko wapi katika mpango wa Mungu wa wokovu? Je, una imani kabisa katika uwezo wake kukuokoa, au unajitegemea kwa sehemu zingine? Usiruhusu hata wazo lije akilini mwako kwamba unaweza kupata wokovu kwa uzuri wako wewe mwenyewe. “Pata ukombozi upatikanao katika Kristo Yesu” (2 Tim 2:10) kwa unyenyekevu wazi wa imani yako. Mpate mwokozi wako kwenye hekalu na umfuate yeye tu. Mruhusu Kristo akubadilishe wewe kutoka moyoni na kukufanya mtu afaaye uzima wa milele pamoja na Uungu, malaika wake, na wote waliokombolewa.

Page 2: 10, February 16, Swahili - WordPress.com · Mambo Muhimu KATIKA TOLEO HILI: Hekalu 2 Mafundisho ya Hekalu 4 Hukumu ya Upelelezi 5 Kristo Hekaluni 6 ... Jambo hili linaleta tofauti

EGWEBO katika AUA Namba. 10 FEBRUARI 2016

2

Maandiko ambayo juu ya mengine yote yalikuwa msingi na nguzo kuu ya Imani ya Waadventista yalikuwa na tamko hili, “Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa (Danieli 8:14). Haya yalikuwa maneno yaliyojulikana sana na waumini waliokuwa wanangoja ujio wa Bwana. Kwa midomo ya maelfu, unabii huu ulisemwa kwa furaha mara kwa mara kama msemo wa imani yao. Wote kwa mtazamo wao walihisi kuwa matukio ya wakati huo yalikuwa yanaashiria matumaini yao makubwa karibu. Siku hizi za kinabii zilikuwa zimetabiriwa kuisha katika msimu wa vuli wa mwaka wa 1844. Kama wakristo wengine wa wakati huo, Waadventista waliamini kuwa, dunia, au sehemu fulani kwayo ilikuwa patakatifu, na kwamba utakaso wa patakatifu ilikuwa usafishaji wa dunia kwa moto wa siku kuu ya mwisho. Hili walielewa lingetokea katika ujio wa pili wa Kristo. Hivyo hitimisho kwamba Kristo atarudi duniani katika

mwaka wa 1844.

Lakini wakati huo ukafika, na Bwana hakuja. Waumini walijua kwamba neno la Mungu haliwezi kusema uwongo; tafsiri yao ya unabii, lazima ndilo lenye makosa; lakini ni wapi penye makosa? Wengi wao wakaanza

kusema kuwa siku zile 2300 hazikuisha mwaka wa 1844. Hawakuwa na sababu yoyote kuhusu ujumbe huu isipokuwa kwamba Kristo hakuja kwa wakati huo waliomtarajia. Walisema kwamba, kama siku hizo 2300 za kinabii zilimalizika mwaka wa 1844, basi Kristo angekuwa amekuja kusafisha patakatifu (ambayo walidhani ni dunia) kwa moto; na kwa vile yeye hakuja, basi siku hizo hazikuwa zimekwisha.

Ingawa Waadventista wengi walitelekeza hesabu zao za awali za vipindi vya kinabii, na kukanusha usahihi wa kikundi, wachache wao walibaki na imani hiyo kwa mwongozo wa maandiko na ushahidi maalum wa Roho

Mtakatifu. Waliamini kuwa, katika masomo yao ya maandiko walipata kanuni maalum, na kwamba ilikuwa wajibu wao kutegemea ukweli waliokwisha pata tayari, na kuendelea na utafiti wa Biblia. Kwa maombi ya dhati, walipitia tena msimamo wao wa awali, na kusoma maandiko tena wakitafuta makosa yao. Hili liliwapelekea kuchunguza zaidi somo la hekalu takatifu.

Hekalu la Duniani na la Mbinguni

Katika unchunguzi wao, walijifunza kwamba hekalu takatifu la duniani, liliyojengwa na Musa kwa agizo la Mungu, lilikuwa kwa mfano wa lile aliloonyeshwa mlimani. Hekalu “ambayo ndiyo mfano wa wakati huu uliopo sasa; wakati huo sadaka na dhabihu zinatolewa” sehemu zake mbili takatifu “zilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni” na kwamba Kristo, kuhani wetu mkuu, “mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu.”; na kwamba “Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu” (Waebrania 9:9, 23; 8:2; 9:24).

Hekalu la mbinguni, ambapo Yesu anahudumu kwa niaba yetu, ndiyo patakatifu asili ambayo hekalu takatifu lililojengwa na Musa lilikuwa nakala. Kama vile hekalu la mbinguni, lile la duniani lilikuwa na sehemu mbili takatifu, sanduku la agano la Bwana, madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, na vyombo vingine vya huduma. Katika njozi takatifu, mtume Yohana aliruhusiwa kuingia mbinguni, na pale aliona vinara saba vya dhahabu, na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, na wakati “hekalu la Mungu liloko mbinguni lilifunguliwa” aliliona pia “sanduku la agano la Bwana” (Ufunuo 4:5; 8:3; 11:19).

HEKALU The Story of Redemption, 375-378

Ellen G. White

Page 3: 10, February 16, Swahili - WordPress.com · Mambo Muhimu KATIKA TOLEO HILI: Hekalu 2 Mafundisho ya Hekalu 4 Hukumu ya Upelelezi 5 Kristo Hekaluni 6 ... Jambo hili linaleta tofauti

EGWEBO katika AUA Namba. 10 FEBRUARI 2016

3

Wale waliokuwa wakitafuta ukweli walipata ushahidi usiopingika wa kuwepo kwa hekalu mbinguni. Musa alijenga hekalu la duniani kwa mfano wa lile aliloonyeshwa. Paulo alikiri kwamba mfano huo ulikuwa ule wa hekalu la kweli lililo mbinguni (Waebrania 8:2, 5). Yohana pia alishuhudia ya kwamba aliliona mbinguni.

Wakati wa kukamilika kwa siku 2300, mwaka wa 1844, hakuna hekalu lililokuwepo duniani kwa muda mrefu hata kufikia miaka hiyo; kwa hivyo lazima liwe ni hekalu la mbinguni

linaloangaziwa kwa tamko, “Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu

patakapotakaswa.” Lakini ni jinsi gani patakatifu mbinguni

panaitaji kutakaswa? Tukirejelea maandiko, wanafunzi wa unabii waligundua kwamba, utakaso haukuwa kuondolewa kwa uchafu wa kimwili. Utakaso huo ulikuwa kusafishwa kwa damu ili kuondoa dhambi. Ndio maana mtume anasema: “Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo [damu ya wanyama], lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo [hata damu ya thamani ya Yesu]” (Waebrania 9:23).

Ili kupata maarifa zaidi kuhusu utakaso unaoangaziwa na unabii, ilikuwa muhimu kuelewa huduma ya patakatifu pa mbinguni. Hili lingewezekana tu kwa wao kujifunza huduma ya patakatifu duniani.

Paulo anatangaza kwamba, makuhani waliohudumu humo walifuata “mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni” (Waebrania 8:5).

Utakaso wa Patakatifu/ Hekalu

Jinsi zamani dhambi za watu zingesafishwa kwenye hekalu la duniani kupitia kwa utoaji wa sadaka ya dhambi, ndivyo hasa dhambi zetu zinasafishwa kwenye hekalu la mbinguni kupitia kwa damu ya Yesu Kristo. Na kama vile hekalu la duniani lilitakaswa kwa kuondolewa kwa dhambi zilizokuwa zimelichafua, ndivyo utakaso halisi wa mbinguni unaafikiwa kwa kuondolewa au kufutwa kabisa kwa kumbukumbu ya dhambi. Ndio maana kuna haja ya uchunguzi wa vitabu vya kumbukumbu ili kuamua ni nani, kwa njia ya toba na imani katika Kristo, wanastahili kufaidi kutokana na upatanisho wake. Kwa hiyo, utakaso wa patakatifu unahusisha hukumu ya upelelezi. Kazi hii lazima ikamilike kabla Kristo hajakuja kwa mara ya pili kuwakomboa watu wake, kwa kuwa ajapo, ujira wake u pamoja naye, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo (Ufunuo 22:12).

Hivyo wale ambao walizidi kufanya utafiti kuhusu neno la unabii, waliona kuwa, badala ya Yesu kuja duniani mwaka wa 1844, aliingia kwenye sehemu takatifu zaidi ya hekalu la mbinguni, penye uwepo wa Mungu, kufanya kazi ya upatanisho kwa maandalizi ya kuja kwake.

Page 4: 10, February 16, Swahili - WordPress.com · Mambo Muhimu KATIKA TOLEO HILI: Hekalu 2 Mafundisho ya Hekalu 4 Hukumu ya Upelelezi 5 Kristo Hekaluni 6 ... Jambo hili linaleta tofauti

EGWEBO katika AUA Namba. 10 FEBRUARI 2016

4

Mafundisho ya biblia kuhusu hekalu, yapo katika moyo wa Kiadventista na ina uhusiano mkubwa na maisha na mafundisho ya Ellen White. Akiwa kijana, Ellen Harmon … kama wafuasi wengine wa mafundisho ya Miller, waliamini kanuni ya kutafsiri siku moja kuwa sawa na mwaka katika unabii, kwa hivyo unabii wa siku 2300 wa Danieli 8:14 … ulianza mwaka wa 457 B.C. (kama ilivyotajwa kwa Danieli 9:24-27) na ungekamilika kwa Siku ya Upatanisho, katika msimu wa vuli wa mwaka wa 1844, ndipo hekalu (lililotafsiriwa sana kumaanisha kanisa) lingesafishwa kwa moto katika ujio wa pili wa Kristo. Ilipofika tarehe 22/10/1884, walikuwa na masikitiko makubwa ambapo Kristo hakurudi duniani kama walivyotarajia. Ingawa wafuasi wengi wa mafundisho ya Miller waliona kuwa maoni yao ya awali kuhusu unabii wa siku au miaka 2300 hayakuwa sahihi, Waadventista wachache … kwa kutafakari zaidi na kusoma Biblia wakafikia kuamini kwamba tarehe ya 1844 ilikuwa sahihi ilhali hekalu la kutakaswa ni ile ya mbinguni na wala si duniani kama walivyokuwa wameamini hapo awali.… Kristo alikuwa akihudumu kwenye patakatifu mbinguni tangu kupaa kwake mwaka wa A.D. 31, lakini baada ya unabii wa siku 2300 kukamilika katika siku ya upatanisho, 1844, Yesu alianza huduma katika mahali patakatifu zaidi mbinguni.

Desemba 1844, Ellen Harmon alipata njozi yake ya kwanza, njozi hiyo ilidhibitisha kuwa Mungu alikuwa amewapa mwanga wa kuwaongoza kuhusu unabii wa siku 2300… Mwezi wa Februari mwaka wa 1845, alionyeshwa kwa njozi nyingine kuwa, baada ya kukamilika kwa siku 2300, Baba na Mwana waliingia mahali patakatifu zaidi pa hekalu ambapo Yesu sasa anahusika na huduma yake ya ukuhani....

Miaka arubaini baada ya masikitiko makuu ya mwaka wa 1844, Ellen White aligundua jinsi “mada ya patakatifu au hekalu ilikuwa funguo lililofungua sababu ya masikito ya mwaka wa

1844” na pia “kufunguliwa kwa mfumo kamili wa ukweli… ukionyesha kwamba mkono wa Mungu uliwaongoza Waadventista huku akifafanua wajibu wao na kudhihirisha msimamo na kazi ya watu wake” (GC 423). Miaka ishirini baadaye, katika mwaka wa 1904, Ellen akakumbuka uongozo wa Mungu kwa mafundisho ya patakatifu katika kipindi cha miaka kadhaa kufuatia 1844 na vikao vingi vya masomo ya Biblia, maombi (mara nyingi usiku mzima) miongoni mwa waanzilishi Wasabato (ikiwa ni pamoja na mumewe James White; Joseph Bates; Stephen Pierce; Hiram Edson; na wengine), ambapo wakati huo akili yake ilikuwa "imefungwa" kutokana na kuelewa maandiko isipokuwa (wakati kundi hilo la watafiti wa Biblia wangekwama), yeye angepewa mwanga kuhusu kifungu hicho walichokuwa wakisoma wakati huo (1SM 206, 207).

Aprili 3, 1847, White alipata maono ambayo yeye alitembelea hekalu la mbinguni, akaona patakatifu na mahali patakatifu zaidi; kwenye patakatifu zaidi, alionyeshwa sanduku la agano, ambalo Yesu alifungua (angalia Ufunuo 11:19), ndani yake kulikuwemo amri kumi za Mungu zikiwa zimezungukwa na utukufu, na amri ya nne ilikuwa inaang’aa zaidi kuliko zile zingine. Aliona kwamba, amri hiyo ya Sabato itakuwa swala kubwa la kuwabainisha watakatifu wa Mungu katika siku za mwisho. Hivyo Sabato ya kibiblia ilikuwa inahusishwa na ujumbe wa hekalu takatifu.

Katika mwaka wa 1858, White alisimulia kile alichoonyeshwa katika njozi zake za awali (ambayo kwa kiasi kikubwa kilirudiwa kwenye njozi ya Pambano Kuu ya tarehe 14 Machi 1858) kuhusu hekalu takatifu (1SG 157-162; angalia LS 162; EW 250-253). Mafundisho hayo ya patakatifu yalipanuliwa (kwenye 1SP [1870] na 4SP [1884]) na yakazidi kukomaa na kuwa kamilifu katika sura kadhaa zilizopangwa taratibu za vitabu vyake kuhusu migogoro ya zama. The Great Controversy (1888, 1911) na Patriarchs and Prophets (1890).

MAFUNDISHO YA HEKALU TAKATIFU

Richard M. Davidson

The Ellen G. White Encyclopedia, pp. 1130-1131

Page 5: 10, February 16, Swahili - WordPress.com · Mambo Muhimu KATIKA TOLEO HILI: Hekalu 2 Mafundisho ya Hekalu 4 Hukumu ya Upelelezi 5 Kristo Hekaluni 6 ... Jambo hili linaleta tofauti

EGWEBO katika AUA Namba. 10 FEBRUARI 2016

5

Hukumu ya upelelezi inayoendelea kabla ya kuja kwa Yesu kama ilivyoelezwa kwa maandiko yake [Ellen G. White] kwamba inaendelea kwenye patakatifu zaidi pa hekalu la mbinguni na kuwa inahusisha tu kesi ya “waliodai kuwa wakristo.” Kanuni ya hukumu ni “neno la Mungu” (angalia Mhubiri 12:13, 14), na kesi zote zinatathminiwa kulingana na rekodi zinazopatikana kwenye “kitabu cha

uzima” (Ufunuo 20:12), “kitabu cha ukumbusho” (Malaki 3:16), na rekodi ya dhambi za wanadamu (angalia Danieli 7:10). Yesu ndiye

wakili anayetetea watu wake. Hukumu ya upelelezi itakapokamilika, Kristo atakuja, na ujira wake utakuwa pamoja naye, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo” (GC 485).

Mwaka wa 1884 Ellen White alisema yafuatayo kuhusu hukumu ya upelelezi, “hivi karibuni – hakuna ajuaye ni lini – itafikia kesi za wale waliohai” (4SP 315; pia GC 490). Tamko hili linasisitiza maadhimisho ya siku za mwisho. Haikubaliani na uwongo unaosema kwamba, mara tu jina la mtu anayeishi likipelelezwa, mtu huyo hupoteza uhuru wake wa kuchagua. Neema haifungwi kwa mtu yeyote ikiwa bado kuna nafasi ya wao kuokolewa. Uamuzi wa Mungu katika hukumu huonyesha matokeo ya kile alichochagua mtu binafsi. “Nikaona kwamba Yesu [hangesitisha maombezi yake] mpaka kila kesi kuamuliwa” (EW 36). Muda huo wa majaribio utadumu kwa waliohai mpaka hatimaye kufungwa kwake kwa dunia nzima muda mfupi kabla ya Kristo kuja mara ya pili. Lakini hii haipaswi

kuwa sababu ya yeyote kukawia kumkubali Yesu. (angalia Waebrania 3:7-15; 4:6, 7). Ellen White anasema kuwa, “hukumu ya upelelezi unapoendelea mbinguni, dhambi za waumini waliotubu zinapoondolewa hekaluni, lazima kuwe na kazi maalum ya kujitakasa na kuacha dhambi, miongoni mwa watu wa Mungu duniani” (GC 425).

Kusoma zaidi juu ya Hukumu ya Upelelezi: Maelezo Zaidi ya Ellen White kuhusu swala la hukumu ya upelelezi zilichapishwa katika miaka ya 1880 kwenye kitabu The Spirit of Prophecy, volume 4 (1884), aliandika sura nzima juu ya mada hii (4SP 307-315). Maudhui ya sura hiyo yaliandikwa upya na kupanuliwa kwa ajili ya toleo la The Great Controversy mwaka wa 1888 (GC88 479-491) na kubakia kwa maneno yale yale katika toleo la 1911 (GC 479-491). Ufafanuzi mwingine mkubwa ulichapishwa katika Testimonies for the Church, volume 5, kurasa 467-476 (1885), na kwa kiasi kikubwa kufanyiwa marekebisho katika Prophets and Kings, kurasa 582-592 (1917). Taarifa nyingine kuhusu mada hii ilichapishwa katika kitabu cha ibada kiitwacho The Faith I Live By (FLB 206-212). Uandishi wake wa mwisho kuhusu somo hili, ulishughulikia hali inayohitajika kwa wale ambao Kristo atawaidhinisha katika hukumu. Kristo asema: “Wao wana udhaifu wa tabia; wanaweza kuwa walishindwa katika juhudi zao; lakini wao walitubu, na mimi nimewasamehe na kuwakubali” (PK 589).

HUKUMU YA UPELELEZI Alberto R. Timm

The Ellen G. White Encyclopedia, p. 905

Page 6: 10, February 16, Swahili - WordPress.com · Mambo Muhimu KATIKA TOLEO HILI: Hekalu 2 Mafundisho ya Hekalu 4 Hukumu ya Upelelezi 5 Kristo Hekaluni 6 ... Jambo hili linaleta tofauti

EGWEBO katika AUA Namba. 10 FEBRUARI 2016

6

Madhabahu ya sadaka kwa madhumuni ya msamaha ambayo inaweza kutimizwa tu kwa damu ya kondoo. Yesu ndiye mwana kondoo wa kweli wa Mungu “aondoaye dhambi za dunia” (Yohana 1:29).

Birika iliwakilisha ubatizo—Kufa kwa njia yako ya zamani ya maisha na mawazo ya kibinafsi. Ukitoka kwenye maji ya ubatizo, unafufuliwa kama kiumbe kipya katika Kristo Yesu (Warumi 6:3, 4; 2 Wakorintho 5:17).

Meza ya mikate ya wonyesho ilidokeza kuwa Yesu ndiye “mkate wa uzima” (Yohana 6:51). Mkate pia uliashiria neno la Mungu (Yohana 6:51-58). “Lazima tule kwake [Yesu], tumpokee moyoni, ili maisha yake yawe maisha yetu” (DA 389).

Kinara cha dhahabu kilitoa mwanga katika patakatifu. Yesu ndiye “nuru ya ulimwengu” (Yohana 8:12). Mwanga pia uliashiria Roho Mtakatifu, anayetupa mwanga na mwongozo tunaposoma Neno la Mungu. Anatuhakikishia dhambi zetu, haki na hukumu. (Yohana 16:8-11).

Kwenye madhabahu ya uvumba, harufu tamu kamwe haziachi kuchomwa. Kwa njia hiyo hiyo, Yesu anazidi kutuongoza kwa njia sahihi. Kama Mpatanishi, yeye ndiye anayetuombea (Waefeso 5:2; Waebrania 8:1-6; 9:15).

Nyuma ya pazia, kwenye patakatifu zaidi, kulikuwa na sanduku la agano na “makerubi wawili wa utukufu, wakikita kivuli kiti cha rehema” (Waebrania 9:5; Ufunuo 11:19). “kuwakilisha maslahi ambayo jeshi la mbinguni wanatafakari kazi ya wokovu” (GC 415), ambapo Kristo ndiye mwokozi wa ulimwengu (Yohana 4:42).

Vibao viwiili vya mawe viilivyoandikwa sheria ya Mungu viliashiria kuwa sheria ya Mungu ni ya milele kama Mwamba halisi wa wokovu ambaye ni Yesu Kristo (Zaburi 119:97; Mathayo 7:24-27; 22:42).

Kopo la mana liliwakumbusha kuhusu matukio ya kutoka Misiri ambapo watu wa Mungu walikusanya mana kila siku, isipokuwa siku ya Sabato (Kutoka 16). Katika siku ya maandalizi – Ijumaa – Waisraeli walikusanya sehemu mbili. Hivyo mana iliwakumbusha kuhusu utakatifu wa Sabato na Bwana wa Sabato (Kutoka 20:8-11; Marko 2:28).

Fimbo ya Aroni iliyochipuka (Hesabu 16; 17:10) ilikuwa ishara ya daima kuwa watu hawana haki ya kufanya kanuni zao wenyewe au kubadili sheria za Mungu (Mathayo5:17, 18). Kumtegemea Mungu kunaendelea kuunganisha watu wake na chanzo cha uzima (Yohana 14:6; 17:3).

KRISTO HEKALUNI

Page 7: 10, February 16, Swahili - WordPress.com · Mambo Muhimu KATIKA TOLEO HILI: Hekalu 2 Mafundisho ya Hekalu 4 Hukumu ya Upelelezi 5 Kristo Hekaluni 6 ... Jambo hili linaleta tofauti

EGWEBO katika AUA Namba. 10 FEBRUARI 2016

7

Mungu alipowaumba Adamu na Hawa, hawakuwa na kasoro yoyote. Wao walitembea na malaika na walizungumza na Mungu kila siku. Hata wakaona uso wa Mungu! Walimpenda Mungu na walistarehe pamoja naye. Lakini tunajua kwamba hadithi inaacha kuwa ya furaha wakati Shetani, akijifanya nyoka aliwashawishi Adamu na Hawa kumuasi Mungu. Mungu alikuwa amewaonya kwamba wakimuasi na kula tunda alilowakataza, watakufa. Uasi na dhambi huleta mauti.

Adamu na Hawa walipotenda dhambi, walijaribu kujifunika na majani ya mtini.

Mungu akaja na kuwavika kanzu iliyofanywa kwa ngozi ya wanyama. Hapa ndipo Mungu alianza kuweka mpango wake wa

wokovu. Aliwaeleza kuwa walistahili kufa lakini yeye aliwapenda sana na alikuwa na mpango wa kuwaokoa. Aliwaambia kuwa siku moja, Yesu Masihi, atazaliwa, na kwa kifo chake, kila amwaminiye atapata uzima wa milele (Mwanzo 3:15,Yohana 3:16).

Kabla ya Yesu kuja humu duniani. Wazao wa Adamu na Hawa walitakiwa kutoa sadaka ya mwana-kondoo asiye na dosari wala doa kila mara walipotenda dhambi ili kuondoa dhambi zao. Walitakiwa kukiri dhambi zao na kuomba msamaha huku wakimshika yule mnyama. Kwa njia hii, walikuwa wanamuomba Mungu achukue dhambi zao mbali kutoka kwao na kuziweka juu ya mwana kondoo huyo. Kisha kondoo huyo angeuwawa kwa sababu mshahara wa dhambi ni mauti (Warumi 6:23). Hivi ndivyo dhambi inavyotisha. Wanakondoo wengi wasio na hatia waliuawa wakati watu wakisuburi kuja kwa Masihi.

Yesu alipokuja duniani, alikuwa ndiye mwanakondoo wa kweli, wa Mungu. Yeye hakutenda kosa

lolote, lakini alimwambia Mungu aweke dhambi zetu zote juu yake ili yeye afe badala yetu, na hivyo tuweze kupata uzima wa milele. Alikuwa ni mwana kondoo wa Mungu asiye na doa, dosari wala dhambi. Alikufa ili kuchukua dhambi zetu. Biblia inasema kwamba “alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye” (2 Wakorintho 5:21).

Baada ya kifo cha Yesu, hakuna haja tena ya kutoa sadaka za wanyama. Yesu alilipa bei ya mwisho. Tunachohitaji kufanya ni kukubali wokovu wetu kwa Imani katika Yesu na kuacha dhambi za namna yoyote. Hii ni habari njema sana kwa wote wanaoamini. Je, unaamini?

Tafuta maneno yafuatayo: Yesu, Upendo, Dhambi, Mwanakondoo, Msamaha, Wokovu, Uzima.

O W U

E O O P S

D I D K E E R

S E A N O N I N S

F O R G O V D N E S S

J O K U O D L

M S A M A H A

Y E N O A M

E V A P M I

S O W S B Z

U L M H I U

MAKALA YA WATOTO:

MWANA KONDOO WA MUNGU

R. Mwamakamba na M. Chebichiy

Page 8: 10, February 16, Swahili - WordPress.com · Mambo Muhimu KATIKA TOLEO HILI: Hekalu 2 Mafundisho ya Hekalu 4 Hukumu ya Upelelezi 5 Kristo Hekaluni 6 ... Jambo hili linaleta tofauti

EGWEBO katika AUA Namba. 10 FEBRUARI 2016

8

Ofisi ya Tawi ya Milki ya Ellen G. White katika AUA:

1. Inasaidia watu katika utafiti wao na kuwaongoza sio tu kwa maandishi ya Ellen G. White, bali pia kwa Roho iliyomvuvia

2. Inapanga mipango maalum kuhusu waanzilishi wa kanisa la Waadventista Wasabato na Roho ya Unabii, na kuwahusisha Wasabato wa kisasa barani Africa.

3. Inapanga na kuongoza katika semina kuhusu mada mbali mbali kuhusiana na maandishi ya Ellen G. White, ufafanuzi wao na utekelezaji

Tembelea tovuti yetu:

http://www.aua.ac.ke/index.php/research/whiteestate.html

Ili kupata Mambo Muhimu tafadhali tuma ombi kwa [email protected]

au utupigie simu kwa nambari +254-733-333-451 / 2

EGWEBO KWA AJILI YAKO

VITUO VINGINE VYA UTAFITI BARANI AFRICA:

ECD: University of Eastern Africa, Baraton, Eldoret,

Kenya

SID: Helderberg College,

Cape Town, South Africa

WAD: Babcock University, Ilishan Remo, Ogun State,

Nigeria

[email protected] [email protected] [email protected]

Page 9: 10, February 16, Swahili - WordPress.com · Mambo Muhimu KATIKA TOLEO HILI: Hekalu 2 Mafundisho ya Hekalu 4 Hukumu ya Upelelezi 5 Kristo Hekaluni 6 ... Jambo hili linaleta tofauti

EGWEBO katika AUA Namba. 10 FEBRUARI 2016

9