Transcript

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898

E-mail: [email protected]: www.ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425

PRESIDENTS OFFICE, STATE HOUSE,

1 BARACK OBAMA ROAD,

11400 DAR ES SALAAM.

Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARIYAH: UTEUZI KATIKA TUME YA UTUMISHI WA UMMA NA

TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI (CMA)___________________________________Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Tume ya Utumishi wa Umma na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).

Katika uteuzi huo, Rais amemteua Mhe. DKT. STEPHEN JAMES BWANA, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma na BWANA EDRISSA R. MAVURA, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Bw. Mavura ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu.

Sambamba na uteuzi huu, Rais amewateua Makamishna katika Tume hizo, ambapo Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma ni:(i)Bwana George D. YAMBESI, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

(ii)Alhaj Y. F. MBILA, Katibu Tawala wa Mkoa mstaafu.

(iii)Bwana Mgeni Mwalimu ALLY, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma iliyomaliza muda wake.

(iv)Bibi Adieu H. NYONDO, Mkurugenzi wa Maadili mstaafu.

(v)Bibi Salome S. MOLLEL, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu mstaafu, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali

(vi)Bibi Evelyne ITANISA, Katibu Tawala wa Mkoa mstaafu.

Aidha Makamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ni:

(i)Bwana Paul Herbert Kinemela, Kamishna wa Kazi, Wizara ya Kazi na Ajira

(ii)Bwana Mathias Bazi Kabunduguru, Mkurugenzi wa Uendeshaji Sera, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

(iii)Bwana Njaa Ramadhani Kibwana, Naibu Katibu Mkuu, Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU).

(iv)Bwana Jones Kyaruzi Majura, Naibu Katibu Mkuu, Chama Cha Wafanyakazi wa Sekta ya Biashara na Viwanda (TUICO).

(v)Bwana Jaffari Ally Omari, Mwanasheria Kiwanda cha Sukari TPC, na Kamishna wa Tume iliyomaliza muda wake.

(vi)Bibi Suzane Charles Ndomba, Afisa Sheria wa ATE na Wakili wa Mahakama Kuu.

Uteuzi huu umeanza tarehe 23 Februari, 2015.Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

26 Februari, 2015


Top Related