zanzibar daima online

33
“ZANZIBAR YASONGA MBELE, KATU HATURUDI TULIPOTOKA” Toleo #01 Agosti 09 - 22 /2013 Zanzibar Kwanza Zanzibar ni Salama 05 Kamati ya Maridhiano ina ridhaa ya Wazanzibari. 14 Si haki kusema SUK imeshindwa kazi. 18

Upload: hassan-mussa-khamis

Post on 28-Oct-2015

3.500 views

Category:

Documents


7 download

DESCRIPTION

Jarida la kila wiki mbiliToleo la kwanza la Zanzibar Daima Online liko hewani kuanzia leo. Miongoni mwa stori na makala zilizomo:1. Zanzibar ni salama: Kauli ya SMZ baada ya mashambulizi ya tindikali dhidi ya wasichana wawili wa Uingereza2. Rais wa Zanzibar arudi kwenye umakamu wa rais wa Muungano: Msimamo wa Taasisi ya Wasomi wa Kizanzibari, ZIRPP3. Yataka moyo kuwa Moyo 4. Kamati ya Maridhiano ina ridhaa ya Wazanzibari5. Zanzibar Hairudi Ilikotoka - Mahojiano na Mansoor Yussuf Himid 6. Si Haki kusema SUK imeshindwa kazi7. Waume zetu wamewafunga, familia hazina muongozo - Mahojiano na familia za masheikh wa UamshoNa mengi mengine. Ni jarida la bure la mtandaoni. Tembelea Mzalendo.net na ZanzibarDaima.net kwa kusoma hayo na mengine tele juu ya Zanzibar.

TRANSCRIPT

1

“ZANZIBARYASONGA MBELE, KATU HATURUDI

TULIPOTOKA”

Toleo #01 Agosti 09 - 22 /2013

Zanz

ibar

Kw

anza

Zanzibar ni Salama 05

Kamati ya Maridhiano ina ridhaa ya Wazanzibari. 14

Si haki kusema SUK imeshindwa kazi. 18

ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 20132

YALIYOMO

05 “Zanzibar ni pahali salama na wageni

wenyewe wanaokuja wanaliona hilo. Tu-

nachukulia suala hili la kusikitisha kuwa

ni la bahati mbaya na halina uhusiano

wowote na hisia za kidini wala za wenyeji

dhidi ya wageni.“.

08 “Sasa inabidi tuondokane na hapo.

Tuwe na wanasiasa ambao wako taya-

ri kuwa na mizani, wako tayari kukemea

hata wenzao, wako tayari kuwakosoa

wenzao, kwa kutizama maslahi ya nchi na

kizazi chetu” - Mansoor Yussuf Himid

12 Pamoja na kuwa tuna mwaka wa tatu

sasa tangu iundwe serikali ya Umoja wa

Kitaifa, bado nchi imendelea kugawaika,

upande mmoja ukiamini kuwa ndio we-

nye haki ya kutawala na mshirika wake ni

mkaribishwa tu.

16 Cha kushangaza ni kwamba hatusikii

sauti zozote za kuwatetea. Labda kwa sa-

babu wao ni masheikh na si wanasiasa.

Labda wangekuwa wanasiasa tungewa-

ona wana harakati wakiwasiliana na Ju-

muiya za Kimataifa na kuzizindua kuhusu

janga lilowafika Masheikh hao.

UCHAMBUZI

22 K Gwiji: Msitutishe kwa chui wa

karatasi

23 A Omar: Si mbili wala si tatu ni

Mkataba

25 R Omar: Zanzibar ndani ya Afrika

Mashariki

26 Familia hazina Viongozi Kuhusu kesi haikufikia pahala pazuri, kwani kisheria kesi miezi minne inatakiwa iwe imeendeshwa mtu kama ana kosa ahukumiwe, hana aachiwe. Lakini mpaka sasa hatu-jui vipi wanakwenda mahkamani. Tunahisi kama wanakwenda ‘Day Out’ tu. Wanakwenda kutembea na kurudushwa ndani. Tumeambiwa wao wamekata rufaa, iko Bara. Tumekwenda siku ya kwanza, siku ya pili, tuliambiwa tutaitwa baada ya wiki mbili. Mpaka leo hatujaona jambo lolote.” - MKE WA SHEIKH ABDALLA SAID ALI

ZANZIBAR DAIMA // Toleo #01 // AGOSTI 09 -22 / 2013

20 SALIM SAID: Ramadhani mwaka huu ilikuwa na viroja

28 TUFUNGUE KITABUKatika sahafu hii ya TUFUN-GUE KITABU tutakuwa tu-nawaletea uhakiki na uchambuzi wa vitabu na maandishi mbalimbali yaliyo-andikwa na Wazanzibari au kuhusu Zanzibar

30 YATAKA MOYO KUWA MOYO.Ndiyo maana wale wenye kuweka masilahi yao mbele badala ya taifa, wajuwe kwamba kinachowashinda wao ni kutokuwa na moyo alionao Mzee Moyo, maana inataka moyo hasa mtu...

05 BARUA Naupenda Mji Mkongwe na mara kwa mara huwa nakwenda huko na rafiki yangu kwa ajili ya kuny-wa na chakula cha jioni, chakula cha mchana au kutembelea duka la vileo..

3

UJUMBE WA BODI YA

WAHARIRI

UTOTONI mwetu, siku kama ya leo ya Idi, ilikuwa ni siku ya furaha kubwa. Wengi tuki-usubiri mwezi uandame, na

tulikuwa wa kwanza kupiga: “Koron-go mwezi!“, huku tukirukaruka kwa furaha. Usiku wake tulikuwa hatulali kwa mshawasha na hamasa za kutaka asubuhi ifungue macho.

Ni kweli kwamba utotoni mwetu hatukuwa miongoni mwa walioshinda na saumu mchana kutwa wala hatuku-wa miongoni mwa waliokuwa wakisi-mama usiku kucha kuswali na kuso-ma Qur’an, lakini sisi ndio tuliokuwa na furaha kuliko wazee wetu walikuwa wakijikurubisha kwa Mola wao mwezi mzima wa Ramadhani. Sisi tulifurahia Sikukuu na mambo yake: vyakula, nguo mpya, zawadi na kutoa mkono wa Barakatil Idi vijumbani ili tupewe Sikukuu yetu. Hali bado ingali hivi hivi kwenye miji na vijiji vya Zanzibar.

Nasi, timu ya Zanzibar Daima Online, tuna furaha ya kuipa Zanzibar na Wazanzibari wote mkono wetu wa Idi. Tumeamua pia kukupeni Sikukuu yenu: hili jarida jipya la Zanzibar Daima Online, kwa kifupi ZDOnline.

Hili ni jarida lenu nyote Wazanzibari. Ni jarida lililo huru lisilofungamana na chama chochote cha siasa. Tutakuwa tunalitoa bure kila baada ya wiki mbili.

Azma yetu ni kulitoa kila wiki.

Kwa hivyo siku ya leo ni siku adhimu. Ni siku adhimu kwa kila hali. Pamoja na kuwa ni siku ya kuitukuza Idd el Fitr siku hii pia ni siku ambayo Zanzibar inajaribu tena kuwa na chombo huru cha kupashana habari na kupeana rai na maoni. Kadhalika hii ni mara ya kwanza kuwa na jarida la mtandaoni.

Bila ya shaka tutazizungumza, kuz-ijadili na kuzichambua siasa. Lakini hatutoishia hapo. Tutaupigia mbizi utamaduni wetu, tutavipekua vitabu vya waandishi wetu Wakizanzibari, tutakumbushana historia yetu ya jinsi wazee wetu na mabibi na mababu zetu walivyokuwa wakiishi na jinsi walivy-okuwa wakijiburudisha.

Zanzibar imezaa magwiji wengi wa da-raja na hadhi ya kimataifa. Baadhi yao wanatukuzwa nchi za nje lakini huku kwao hawajulikani. Wengine wana-julikana lakini wanasahauliwa. Jarida la ZDOnline litawabeba na kuwaenzi wote. Lengo la kwanza – na yumkini la pekee la jarida hili – ni kulifanya liwe jukwaa la mawasiliano miongoni mwa Wazan-zibari na kati ya Zanzibar na ulim-wengu. Makusudio ni kuiwasilisha na kuiwakilisha Zanzibar kwa mtazamo wa Kizanzibari, na sio kinyume chake.

Tunaamini kuwa Wazanzibari wanap-enda wajisemee wenyewe juu ya hisia na matakwa yao, khofu na matarajio yao, na hata juu ya nguvu na udhaifu wao. Imani kuu ya waanzilishi wa jarida hili ni Uzanzibari, ambao ni fakhari kwa kila Mzanzibari anayeishi ndani ya mipaka ya Zanzibar au nje yake.

Kwa hivyo, kazi kubwa ya gazeti hili ni kusimamia na kuendeleza msimamo wa Wazanzibari. Msimamo wenyewe ni kwamba nchi yao ya Zanzibar ilikuwepo, ipo na itakuwepo milele. Tunaamini pia kwamba Uzanzibari ni utambulisho ulio hai na kwamba Wazanzibari wenyewe wanajivunia na kuulilia utambulisho huo.

Ndani ya jarida hili msomaji anakutana na habari, makala, mahojiano, cham-buzi zinazohusiana na Zanzibar na ambazo zinaakisi msimamo tuliougu-sia hapo juu. Kulitoa jarida hili ndio mkono wetu wa Idi ndogo kwa Zanzibar na Wazanzi-bari. Lakini, kinyume na ilivyo desturi, mkono huu utaendelea kutolewa hata baada ya Iddi kumalizika. Tunawaom-ba muupokee mkono huu, msiung’ate wala msiukate, na tusaidiane kwa pamoja kuipaza sauti ya Zanzibar.

Zanzibar Daima!

Barakatil Id Zanzibar

Zanzibar DaimaWasiliana NasiSahafu za JaridaMHARIRI MKUU: Ahmed [email protected]

MHARIRI MSAIDIZI: Mohammed [email protected]

MHARIRI MSANIFU: Hassan Khamishassan.zanzibarimage.com

WaandishiMauwa [email protected]

Jabir [email protected]

Othman [email protected] [email protected] S [email protected]

MatangazoKwa matangazo, tafadhali wasiliana nasi kuupitia: Hassan Khamis+44 7588550153 [email protected]

BaruaTafadhali tuandikie maoni yako kupitia barua pepe:[email protected] hili huchapishwa na: Zanzibar Daima Collective233 Convent Way - Southall - MiddlesexUB2 5UHUnited Kingdom

Nonnstr. 2553119 BonnGermany

ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 20134

5

Kufuatia mashambulizi dhidi ya wasichana wa Kiingereza, SMZ yatoa kauli

Zanzibar ni salama – Waziri Said• Asema Z’bar imekuwa na utamaduni wa mchanganyiko karne kadhaa

• Si mashambulizi ya kidini, ni uhalifu wa kawaida

• Aonya vyombo vya habari dhidi ya upotoshaji

ZDOnline, BonnSerikali ya Zanzibar imesema kwamba Zanzibar inaendelea kuwa sehemu salama kwa wageni na wenyeji wa makabila, dini na mataifa yote na kwamba hakuna chochote kinachoashiria uwepo wa makundi ya siasa kali za kidini au chuki dhidi ya wageni.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Utalii, Utamaduni na Habari wa Zanzibar, Said Ali Mbarouk, katika mazungumzo maalum na Zanzibar Daima Online kwa njia ya simu kufuatia mashambulizi ya tindikali dhidi ya wasichana wawili raia wa Uingereza yaliyotoke Mjini Zanzibar usiku wa Jumatano (7 Agosti) siku moja kabla ya mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani katika nchi hiyo yenye wakaazi wengi Waislamu na iliyo moja ya vivutio vikuu vya utalii duniani.

“Zanzibar ni pahali salama na wageni wenyewe wanaokuja wanaliona hilo. Tunachukulia suala hili la kusikitisha kuwa ni la bahati mbaya na halina uhusiano wowote na hisia za kidini wala za wenyeji dhidi ya wageni,“ alisema Waziri Said, akipinga vikali baadhi ya taarifa zilizokuwa zimeanza kuchapishwa na vyombo mbalimbali vya habari vya nje ya Zanzibar, ambavyo

vilifanya haraka ya kuhusisha mashambulizi hayo na udini na chuki dhidi ya wageni.

Katika toleo lake la mtandaoni la siku ya Alhamisi, siku moja tu ya mkasa huo kutokea, gazeti la Mirror la Uingereza lilichapisha maoni kadhaa kutoka nchini humo, ambayo yalionesha hisia kali miongoni mwa wachangiaji dhidi ya Zanzibar.

Moja ya maoni hayo yanasomeka: “Nadhani yalikuwa ni mashambulizi ya kupangwa. Wasichana hao wawili walikuwa kwenye ziara ya kufundisha na kuwaelimisha wanawake na watoto wa Kiislamu kitu ambacho wanaume wa Kiislamu hawakipendi.“

Waziri Said amesema kwamba licha ya ukweli kwamba Zanzibar ni nchi inayokaliwa na asilimia 99 ya Waislamu, bado ni taifa ambalo limezoea mchanganyiko wa kidini, kikabila na kitamaduni, na kwamba lina uzoefu wa kupokea wageni “kwa zaidi ya miaka 2000 ya historia yake. Hapa ni nyumbani pia pa Wahindu, Wakristo, Mabudhdha, na hata wasio

na dini kwa miaka yote hiyo na kamwe dini halijawahi kuwa suala la kuwagawa wala kuwachonganisha watu,“ aliongeza Waziri Said.

Wasichana hao wawili, Katie Gee na Kirstie Trup, wote wakiwa na umri wa miaka 18, wote wakiwa raia wa Kiingereza wenye asili ya Kiyahudi, na wote walimu wa kujitolea kisiwani Unguja, walimwagiwa kitu kinachoaminika kuwa tindikali wakati wakitembea katika mitaa ya Mji Mkongwe, majira ya saa mbili usiku, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis, ambaye alisema tayari polisi visiwani humo imeshaanzisha uchunguzi juu ya mkasa huo.

“Polisi imeanzisha msako na tunawaomba wananchi kutoa ushirikiano katika kuwatambua washambuliaji hao,” alisema Kamanda Mkadam, ambaye pia ni naibu kamishna wa polisi Zanzibar.

Mara tu baada ya mashambulizi hayo, Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na vyombo vya usalama, mashirika ya

utalii na ndege, iliwasafirisha Katie na Kirstie kwenda Dar es Salaam, ambako walipatiwa matibabu ya dharura katika Hospitali ya Aga Khan na baadaye kupangiwa safari ya kurudi nyumbani.

Kampuni ya usafiri ya i-to-i Travel ya Uingereza iliyoandaa ziara ya masomo ya wasichana hao ilithibitisha kwamba walitarajiwa kurudi nyumbani siku ya Alhamisi usiku, kwa mujibu wa gazeti la Mirror la Uingereza.

Kabla ya wasichana hao kusafirishwa kurudi nyumbani, Rais Jakaya Kikwete aliwatembelea Hospitalini ya Aga Khan jijini Dar es Salaam walikolazwa kwa muda, na ambako alielezea masikitiko yake na kuahidi kufanya kila awezalo kuhakikisha washambuliaji wanatiwa mkononi.

“Ni tukio la aibu ambalo linaharibu heshima ya nchi yetu. Naviamuru vyombo vya usalama kuharakisha uchunguzi na kuwakamata wanaoshukiwa kuhusika na mashambulizi haya,” alisema Rais Kikwete.

Mapema, Ofisi ya Mambo ya Kigeni ya Uingereza ilisema kwenye taarifa yake kuhusu tukio hilo kwamba inatoa msaada wa ushauri kwa raia wake hao wawili, na wakati huo huo “kuwasiliana na serikali ya Tanzania” juu ya suala zima.

Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe ambako ndiko lilikotokea tukio hilo, Ismail Jussa, alisema kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari kwamba mashambulizi hayo yalikuwa na madhara ya moja kwa moja kwa utalii,

ambao ni uti wa mgongo wa uchumi wa Zanzibar.

“Ni mapema kusema ni nani aliyepo nyuma ya kitendo hichi, lakini jambo moja la wazi ni kuwa yeyote anayehusika amekusudia kuiumiza Zanzibar na Wazanzibari. Kuuhujumu utalii ni kuuhujumu uchumi wa Zanzibar na kuyahujumu maisha ya Wazanzibari,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa siku ya Alhamis.

Chama cha Wananchi (CUF) kililiita

tukio hilo kuwa ni “dalili mbaya kwa nchi ya Zanzibar….linalotishia uchumi wa Visiwa vyetu”, kupitia taarifa yake iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari, ambapo pia Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu na Uenezi wa chama hicho, Salim Bimani, alilitoea wito jeshi la polisi kuchukuwa hatua za haraka, hasa kwa kuwepo rikodi ya matukio ya mashambulizi ya tindikali katika siku za karibuni.

Tukio hili lisiitie Zanzibar nzima lawamaniTanbihi: Makala hii ya Kerry Stokes ilichapishwa na mtandao wa gazeti la Mirror la Uingereza toleo la Alhamis (Agosti 8, 2013). Kerry ali-hamia Zanzibar kutokea Afrika ya Kusini mwezi Januari 2013 na anafanya kazi kwenye hoteli ya nyota tano. Tumeichapisha hapa tena kwa sababu ya umuhimu wake.

Mimi ninaishi Zanzibar na ninatamani ningeliweza kuy-avunganya mazuri yote ya kisiwa hiki kidogo kwenye kipande cha pamba na kuyaweka kisandukuni na kuga-wana na ulimwengu.Hivyo nachukia kuona “nyumba” yangu hii ndogo ikiwa kwenye jin-amizi kama hili.Ninahisi fadhaa kwa wasichana hao walioshambuliwa usiku wa jana Mji Mkongwe na ninaweza kufikiria khofu ambayo lazima ita-kuwa imewajaa.Hata hivyo, nina maswali – na sa-babu pekee nionayo inanifanya niulize ni kwa sababu ya yale niya-onayo kila wakati.Je, wasichana hao walikuwa wa-natembea wapi kwa miguu na kwa nini walikuwa peke yao? Je, walikuwa wamejitanda?Zanzibar ni nchi ambayo ina Wais-lamu wengi lakini ninawaona watalii wengi wakitembea mitaani na viguo vifupi.Bila ya shaka hiyo haiwezi kuwa sababu ya kuwasham-bulia. Lakini watu wanaovaa hivyo huwa hawaoneshi kwamba wana heshima.Na kuna wengine ambao wanabusiana na kupapasana mitaani au kuvuta sigara hadharani – yote hayo ni mam-bo ambayo yanachukiwa. Unaweza kuendesha chombo

cha moto cha maringi mawili bila ya kofia la chuma na kuzungumza na simu yako ya mkononi au kuwa na watu wamejaza mizigo kwenye baiskeli na hakuna atakayeku-tupia jicho. Lakini kama ukionekana unavuta huku un-

aendesha utavutwa mara moja na unaweza kushitakiwa.Kwa wakati huu, mazingira ni magumu zaidi kwa ujumla kwani ndio kwanza tunaondoka kwenye mwezi mtukufu kwa Waislamu wa Ramadhani na kuingia kwenye sikukuu ya Idd.Naupenda Mji Mkongwe na mara kwa mara huwa nakwenda huko na rafiki yangu kwa ajili ya kunywa na chakula cha jioni, chakula cha mchana au kutembelea duka la vileo. Na-jihisi niko salama kuingia kwenye teksi na kutembea dakika 30 kuelekea Mji Mkongwe kuufuata ulipo mkahawa. Najihisi salama ku-

fanya hivyo.Lakini sijawahi kutoka nje baada ya Futari (chakula cha jioni katika mwezi wa Ramad-hani) tangu Ramadhani ianze na bila ya sha-ka nisingeliweza kwenye peke yangu sasa

– ningelikaa kama wiki moja au mbili kwa kisiwa hiki ku-tulia baada ya Idd.Zanzibar si eneo la kuogofya na hakuna tatizo la uhalifu wa kutumia nguvu. Hapa hakuna uhalifu wa aina hiyo. Ikiwa kitu kama hicho kimetokea, ni jambo tafauti.Tukio kama hilo haliitii Zanzibar nzima lawamani.

Na Kerry Stokes

Jina la Nchi

Ibara ya 1(1) ya Rasimu ya Katiba inasema kuwa “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni shirikisho

lenye mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi huru”.

Lakini, kama inavyoonekana hapa, tafsiri sahihi ya Rasimu inaonekana kupendekeza kuwa jina rasmi la nchi ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pendekezo hili linakwenda kinyume na masharti ya Ibara 1(1) ya Rasimu ya Katiba inayoagiza kuwa shirikisho limetokana na Muungano wa nchi mbili, sio moja. PENDEKEZO: Kwa hivyo, inapendekezwa kuwa jina rasmi la nchi liwe Jamhuri za Muungano wa Tanzania au (United Republics of Tanzania). SABABU: Huu ni Muungano wa nchi mbili huru baina ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Mifano mizuri ya kuigwa inayotumika katika nchi zilizokuwa au bado zenye mifumo ya shirikisho ni nchi iliyokuwa ikijuulikana kama Union of Soviet Socialist Republics (USSR); United Arab Emirates (UAE) na United States of America (USA). Kuliweka jina la Tanzania kwa namna hii kutaonyesha kuwa Muungano wetu umetokana na nchi zaidi ya moja na kweli ni nchi yenye kuendeleza mfumo wa shirikisho lenye mamlaka kamili. Tanzania Bara

Ibara ya 2 ya Rasimu ya Katiba inaeleza kuwa “Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara ikijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la Zanzibar ikijumuisha sehemu yake ya

bahari”. Jina la Tanzania Bara kwa madhumuni ya kumaanisha eneo lote la T a n g a n y i k a l i n a k w e n d a kinyume na Ibara 1(1) ya Rasimu ya Katiba i n a y o f a f a n u a kwa uwazi kabisa kuwa Muungano umetokana na Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

PENDEKEZO: Kwa hivyo, inapendekezwa kuwa jina la “Tanzania Bara” kwa kumaanisha Tanganyika lifutwe; na badala yake jina la “Tanganyika” liwekwe ipasavyo.

SABABU: Kutumia jina la Tanzania Bara kutaifanya ndani ya nchi moja kuwepo na Tanzania mbili; na hivyo kuleta mfadhaiko (confusion) usio wa lazima ndani na nje ya nchi. Isitoshe, “Tan-Zan(ia)” ni jina linalowakilisha nchi mbili zilizoungana. Haiwezekani, kwa hivyo, kwa upande mmoja wa Muungano kulitumia jina hilo kivyake; hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa Tanganyika ndilo jina linalotakiwa na wananchi wengi, hasa kutoka upande wa Bara.

Vile vile, matumizi ya jina la Tanzania Bara litaifanya Tanzania kuwa ndio Tanzania Bara na Tanzania Bara kuwa ndio Tanzania; na hivyo kuibakisha nchi hapa hapa ilipo kwa maana ya kuwa Tanganyika ndio Tanzania na Tanzania ndio Tanganyika. Hali hii haiwezi kukubalika tena. Rais wa Zanzibar kuwa Makamu Rais wa Tanzania

Ibara ya 86(1) ya Rasimu ya Katiba imeagiza kuwa “Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa ndiye

Mzaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa jumla”. Kwa bahati mbaya, Rasimu hii ya Katiba h a i k u m r e j e s h e a Rais wa Zanzibar nafasi yake ya awali ya Umakamu wa Rais wa Tanzania

kama kwa mujibu wa Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964.

Itakumbukwa hapa kuwa kabla ya kuweka utaratibu wa Mgombea Mwenza, Rais wa Zanzibar alikuwa ndio Msaidizi Mkuu wa Rais wa Tanzania kwa upande wa Zanzibar; na hivyo kumfanya Rais wa Zanzibar kuwa kiungo muhimu katika uongozi wa kitaifa wa Jamhuri ya Muungano.

Kwa kumuondolea mamlaka hayo, sasa Rais wa Zanzibar si kiungo tena katika uongozi wa Taifa; na amekuwa sio chochote zaidi ya Mjumbe tu katika Baraza la Mawaziri. Huu ni uvunjaji mkubwa wa Makubaliano ya Muungano.

Kwa kuwa Rasimu ya Katiba inapendekeza kuanzishwa kwa mfumo wa serikali tatu, basi inapendekezwa kuwa Marais wa Zanzibar na Tanganyika wote wawe Wasaidizi Makamu Rais wa Tanzania; yaani First Deputy Vice President na Second Deputy Vice President kwa kutegemea upande upi wa Muungano Rais wa Tanzania atatoka.

Utaratibu huu sio tu utawafanya marais wa Tanganyika na Zanzibar kuwa viungo muhimu katika uongozi wa taifa, lakini vile vile utanyanyua hadhi ya marais hawa wawili kiitifaki ndani ya nchi; na hasa zaidi wanaposafiri nje ya nchi.

Rais Zanzibar arudi kwenye Umakamu wa Rais

TANBIHI: Mnamo tarehe 26 Julai 2013, Taasisi ya Utafiti wa Sera za Umma ya Zanzibar (ZIRPP), ambayo ni jukwaa la wasomi wa Kizanzibari, lilichapisha maoni yake juu ya Rasimu ya Katiba ya Jamuri ya Muungano wa Tanzania. Zanzibar Daima Online inakuletea baadhi ya dondoo za mapendekezo yao.

MAONI

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein

ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 20138

MAHOJIANO • MAALUM

“Zanzibar yasonga mbele, hairudi tena ilipotoka”

ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 20138

9ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 2013

Na wengi wetu wanasiasa, tunapaswa kuondosha khofu na kusimama na ukweli, kwa sababu siasa zilizojengeka hapa kwetu, ni kwamba kama hukuwa muhafidhina, hukuwa tayari kuwatukana matusi ya nguoni wapinzani, unaonekana bado hujatimia kwa siasa ya chama chako.

“Haturudi tulikotoka”

DW: Hebu kwa ufupi tupe tathmini yako juu ya serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar. Je, unaona ndoto muliyokuwanayo inafikiwa?

Mansoor: Nashukuru sana. Ni kweli mimi ni miongoni mwa Wazanzibari wengi waliotaka maridhiano katika nchi yetu, na mimi bado naendelea kuwa na matumaini makubwa juu ya ile dhamira hasa ya kuwa na jamii ambayo imeunganika, jamii ambayo inafanya kazi kwa pamoja kujenga nchi yao, jamii ambayo inatafuta matunda ya hatima yao kwa pamoja. Kwa hivyo, bado wengi wetu matumaini tunayo na tunaendelea kuwa nayo. Na ninaamini, pamoja na mitihani ambayo bila ya shaka itaendelea kutokea – kwa maana wapo watu mpaka hii leo na wataendelea kuwapo ambao hawapendelei umoja wa watu miongoni mwao.

DW: Tuzungumzie hili suala kwa mifano halisi. Katika siku za karibuni imekuwa ikitajwa kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa haisimami kama kitu kimoja. Inasimama kwa mujibu wa vyama vilivyounda serikali

hiyo – wale waliotoka Chama cha Mapinduzi wanasimama kama wana-CCM na wale waliotoka Chama cha Wananchi, wanasimama kama CUF kwenye serikali – na sio kama Wazanzibari. Unasemaje kuhusu hili?

Mansoor: Si kweli ndugu yangu. Kwa bahati nzuri sana, namshukuru Mwenyezi Mungu na namshukuru Dk. Shein (Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein), nimewahi kuwa waziri ndani ya serikali hii ya awamu ya saba, na nimeona namna tulivyokuwa tunafanya kazi. Tukifanya kazi kama watu wamoja kwa lengo la kuijenga Zanzibar iliyo moja. Na ninajuwa kuwa Dk. Shein, Maalim Seif Sharif Hamad (Makamu wa Kwanza wa Rais), Balozi Seif Ali Iddi (Makamu wa Pili wa Rais) na wote mule ndani ya serikali, ni watu ambao wanahishimiana; na wakati mimi nipo, niliyaona hayo kwa vitendo.

Lakini tutakuwa wanafiki kama hatukuwa wakweli kusema kwamba kutiririka kwa lengo na dhamira sahihi ya maridhiano kutoka juu kuelekea kujaa

kwenye nyoyo za watu ndani ya vyama vyetu hivi, bado inahitajika kufanywa. Wako watu ndani ya vyama vyote viwili bado wamekuwa wazito kukubali dhana sahihi ya kuleta maridhiano na kukubali kwamba Wazanzibari wote ni sawa – wana haki sawa, wana fursa sawa, kama malengo ya Mapinduzi Matukufu ya Januari 12 yalivyokuwa.

Huo ndio ukweli wenyewe, lakini hayo yalitegemewa; na si mambo tunayoana sisi na wengi wa Wazanzibari kuwa ni ya kutuvunja moyo. Tunaona pia mafanikio na namna tulivyoweza kupata kituo ndani ya nchi yetu.

DW: Naam, tuje hapo katika kuangazia hilo la mafanikio ukiwa kama mmoja wa waasisi wa Maridhiano ya Wazanzibari. Ukiambiwa utaje kwa ufupi mafanikio ya hatua hii ambayo ilichukuliwa – ya Maridhiano na hatimaye Serikali ya Umoja wa Kitaifa – utayataja yapi?

Mansoor: Ndugu yangu, tuache yote, kwa Wazanzibari la muhimu lilikuwa matumaini. Ilikuwa amani

Mwishoni mwa mwezi Julai 2013, mjumbe wa Baraza la Wawakilishi jimbo la Kiembesamaki, Unguja, waziri wa zamani kwenye Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na mmoja wa wajumbe sita wa Kamati ya Maridhiano ya visiwa hivyo, alizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle, Ujerumani, juu ya mustakabali wa Maridhiano na Umoja wa Kitaifa Zanzibar, miaka mitatu baada ya kuundwa kwa serikali inayovikutanisha pamoja vyama hasimu – Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF). Hapa tumeamua kuyachapisha mahojiano hayo kwa hisani kubwa ya Deutsche Welle, kutokana na umuhimu wake.

ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 201310

na utulivu wao. Mambo hayo tuliyakosa kwa miaka mingi sana tangu mwaka 1995. Maana ulikuwa hujuwi ukiamka siku ya pili asubuhi patakuwa na mashaka gani ndani ya nchi hii. Tuache mengine yote, la msingi ni kupata kituo, kupata matumaini kwamba kuna kesho inayoweza kuwa bora zaidi, hilo peke yake linatosha kwa Zanzibar. Bila ya shaka, tulitarajia na tunatarajia mengi zaidi na tutayafanikisha kwa umoja wetu. Na tutaendelea kujenga Zanzibar iliyo bora zaidi. Zanzibar kwa ajili ya Wazanzibari wote.

DW: Unazungumzia kuhusu matumaini. Unazungumzia kuhusu kesho ijayo ambayo inapaswa na imeanza kujengwa. Lakini tumesikia hotuba za viongozi wakubwa wa Zanzibar hivi sasa: Maalim Seif Sharif Hamad kutoka CUF akiwa kama Makamu wa Kwanza wa Rais na Dk. Ali Mohamed Shein akiwa kama Rais wa Zanzibar na pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, wakishutumiana na wakishambuliana hadharani. Kesho hii iko wapi?

Mansoor: Si kweli, ndugu yangu. Unajua kwa miaka mitatu tusitarajie kwamba patakuwa pana Pepo hapa. Mimi ninawasikiliza wote wawili na ninawaona wanafanya jitihada kubwa za kuendeleza ustaarabu wa kisiasa. Wako waliokuwa chini yao, bahati mbaya sana, wamekuwa wachochezi.

Lakini pia ukilinganisha na tulikotoka, kuna ustaarabu ambao unaendelea kujengeka

siku hadi siku. Bila ya shaka, tuna wajibu na sisi kuwasaidia viongozi wetu hawa kuhakikisha kuwa wao wanakuwa ndio washika bendera wa ustaarabu huo ambao tumekuwa tukiutafuta.

Mimi ukiniuliza, naendelea kuwa matumaini na wote – Maalim Seif Sharif Hamad na Dk. Ali Mohamed Shein. Na naamini ni watu wastaarabu na waungwana. Lakini na sisi tulio chini yao, ambao tumekuwa ndio wakorofi wa kuchochea na kujenga mazingira ya ajabu ajabu, tunapaswa kujirekebisha pia ili kuwa na moyo wa dhati.

Na wengi wetu wanasiasa, tunapaswa kuondosha khofu na kusimama na ukweli, kwa sababu siasa zilizojengeka hapa kwetu, ni kwamba kama hukuwa muhafidhina, hukuwa tayari kuwatukana matusi ya nguoni wapinzani, unaonekana bado hujatimia kwa siasa ya chama chako.

Sasa inabidi tuondokane na hapo. Tuwe na wanasiasa ambao wako tayari kuwa na mizani, wako tayari kukemea hata wenzao, wako tayari kuwakosoa wenzao, kwa kutizama maslahi ya nchi na kizazi chetu zaidi.

Hayo ndiyo tunapaswa kuyajenga na kuwasaidia viongozi wetu hawa. Lakini bado pamoja na hayo yaliyojitokeza ya hapa na pale, tunaendelea kuwa na matumaini. Wazanzibari wameshakubali hali iliyopo. Wameshakubali Maridhiano. Wameshakubali kujenga taifa lililo moja.

Hawawezi tena kuondoshwa kwenye misingi hiyo, japokuwa wapo watu wanaofanya kazi. Ndio nikasema tuwache unafiki, lazima tuwe wakweli, lakini pia bado tuna matumaini makubwa.

DW: Unapoiangalia Zanzibar ya miaka mitano au kumi ijayo, unaiona Zanzibar ya aina gani?

Mansoor: Naiona Zanzibar yenye neema, iliyobadilika kwa fikra. Nilikuwa nazungumza na mwenzangu mmoja juu ya hali tuliyonayo, hasa huu mjadala wa Muungano, akaniambia tunahitaji kuwa na mapinduzi ya fikra. Fikra mpya. Kwa maana, Marehemu Mzee Karume – Mungu amlaze mahali pema na wenziwe – wametuletea Mapinduzi na Uhuru wetu, sisi tunapaswa kuyaongezea nguvu yale. Kuwa na mabadiliko ya fikra, mapinduzi ya fikra mpya.

Kwa hivyo, mimi naiona Zanzibar yenye vijana wenye fikra mpya, wasiofungwa na historia zao potofu, wasiofungwa na itikadi za ajabu ajabu. Wazanzibari walio tayari kutazama mbele na kuiona Zanzibar iliyo bora.

DW: Na je, huoni Zanzibar ambayo imerudi nyuma katika siku za kabla ya Maridhiano, kwa hivi hali inavyokwenda sasa?

Mansoor: Ndugu yangu, mimi siioni. Hatukubali. Wazanzibari walio wengi hawako tayari kurudi tulikotoka. Hivi sasa watu wanafikiria matumbo yao. Matumaini ya maisha yao na ya kizazi chao. Wanafikiria kusonga mbele.

11ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 2013

Watu wenye siasa potofu, wanaotaka kuleta ubaguzi, kutugawa Wazanzibari, kuleta uhafidhina, kueneza chuki, hawana nafasi tena kwenye siasa za Zanzibar. Na, inshallah, Mwenyezi Mungu atuongoze kwenye njia ya kusonga mbele. Wazanzibari hatuwezi kukubali tena. Haturudi kule tulikotoka. Tutapambana nao wale watu ambao wanataka kuturejesha nyuma.

Na ukitizama hali halisi ilivyo, pamoja na mitihani hiyo, bado watu wanaelewa kwamba wakivuuka mipaka fulani, Wazanzibari wenyewe, jumuiya ya madola, wanaotusaidia – kwa maana ya washirika

wa maendeleo – hawatakubali hata kidogo kwamba tumetoka kote huko tulikotoka, na sasa waturudishe nyuma. Na Mzanzibari gani hivi sasa utamshawishi kurudi tulikotoka? Si rahisi ndugu yangu!

DW: Kwa maa ya kusema kwamba hakuna kurudi nyuma, kuna kusonga mbele sasa!?

Mansoor: Sadakta! Ni kusonga mbele tu kwa Zanzibar iliyo bora zaidi. Na hilo haliishi ndani ya mwaka mmoja, miwili au mitatu; ni kazi ya mwaka nenda mwaka rudi, muongo mmoja hadi mwengine. Tutaendelea hivyo hivyo.

Mansoor Yussuf HimidMANSOOR Yussuf Himid ni mwanasiasa na

mfanyabiashara aliyezaliwa tarehe 3 Novemba 1967 kisiwani Unguja. Alisomea masomo yake

ya ya msingi na sekondari nchini India kati ya mwaka 1976 na 1987. Kabla ya kuzivaa rasmi siasa mwaka 2000 alipoteuliwa mjumbe kwenye Baraza la Wawakilishi, Mansoor alikuwa akijihusisha sana kwenye biashara ya hoteli.

Katika uchaguzi wa 2005 alichaguliwa mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) nafasi ambayo ameishikilia hadi sasa.

Mansoor ni mwanachama mkereketwa wa CCM aliyeshikilia nafasi za juu za chama hicho. Amewahi kuwa mjumbe wa Kamati Tendaji Taifa (NEC) na Mweka Hazina wa Chama kwa upande wa Zanzibar kati ya mwaka 2002 na 2012.

Nje ya CCM, Mansoor ameshika nyadhifa mbalimbali za uwaziri katika Baraza la Mawaziri la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kwanza kutoka mwaka 2000 hadi 2004, alikuwa Naibu Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, halafu kati ya 2004 na 2010 alikuwa Waziri kamili kwenye wizara hiyohiyo. Baadaye kuanzia 2010 hadi 2012 alikuwa Waziri wa Kilimo na Rasilimali.

Mansoor alihudumu kama mjumbe wa Baraza la Biashara la Zanzibar baina ya mwaka 2002 hadi 2012.

Moja ya mambo yanayomtafautisha kiongozi huyu, ambaye ni mtoto wa Mkuu wa kwanza wa Jeshi la Zanzibar baada ya Mapinduzi, Brigadea Jenerali Yussuf Himid, ni kuthubutu kwake kusema anachokiamini na kukisimamia. Kwa mfano, amekuwa akisimama

kidete kuhusu suala la Maridhiano ya Wazanzibari na Umoja wa Kitaifa. Akiwa mmoja wa wajumbe sita wa Kamati ya Maridhiano, alishiriki kikamilifu kuyaanzisha hayo maridhiano mwaka 2009.

Wajumbe wengine wa Kamati hiyo ni mwenyekiti wake Hassan Nassor Moyo (CCM), Eddie Riyami (CCM), Abubakar Khamis Bakari (CUF), Ismail Jussa Ladhu (CUF) na Salim Bimani (CUF).

Aidha, Mansoor amekuwa miongoni mwa Wazanzibari walio katika safu ya mbele kuutetea muundo wa Muungano utaoipa Zanzibar mamlaka yake kamili. Yote hayo yamemfanya ang’are machoni mwa Wazanzibari na awe kipenzi chao.

ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 201312

BARZA YA JUMBA MARO

Anafaidika nani Zanzibar ikigawanyika?

Na Ally Saleh

Mambo mengi yamekuwa yakitokezea kwetu Zanzibar katika kipindi cha hivi karibuni na kwa ujumla wake mambo hayo yanaashiria mgawanyiko katika jamii. Hatuuhitaji mgawanyiko huo. Tunachohitaji kwa wakati huu ni umoja na mshikamano. Hayo mawili tu ndiyo yatayoweza

kutuvusha na mengi ya mambo makubwa ambayo ni pamoja na uwepo wa Zanzibar yenyewe. Baadhi yetu tulikuwa tukiamini kuwa kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kungelikuwa chachu ya kusakafia umoja wa Wazanzibari.

Lakini hali inayojitokeza hivi sasa inaonyesha kinyume chake kabisa.

Mgawanyiko wa Zanzibar uliviathiri visiwa hivi katika zama za kupigania uhuru, ambapo pamoja na mbinu za kikoloni za wagawe uwatawale, sisi tukaongeza kuni katika moto tusioujua kwa kujigawa wenyewe kwa wenyewe.

Tuliikubali dini lakini tuliuachia hasa ukabila na umaeneo utugawe. Uundwaji wa vyama vyetu ukawa na mnuko huo wa ukabila na umaeneo na kwa hivyo tukajizonga katika makundi na mapande, mambo ambayo yalisababisha kuibuka kwa chuki ambayo mpaka leo imekita mizizi katika jamii.

Hali hiyo ilitufanya tugawike tulipopokea Uhuru wa Disemba 1963 na tugawika tena yalipotokea Mapinduzi ya Januari 1964 na

mgawiko huo ni dhahiri katika macho yetu na matendo yetu hadi leo.

Kwa bahati, Mapinduzi kwa muda

mrefu yamesimamia utaratibu mzima wa nchi. Tatizo ni kwamba Mapinduzi yalishindwa kuundoa mgawanyiko ambao uliendelea kuila nchi chini kwa chini, ingawa katika baadhi ya mambo wazi wazi.

Nchi ilijengeka kwa matabaka: mali ilikwapuliwa bila ya fidia;

elimu, ajira na vyeo vilitolewa kwa ubaguzi; watu walikamatwa wakati mwengine kama mbuzi na ndio maana haikuwa ajabu kwamba kulikuwa na majaribio kadhaa ya

kuipindua serikali. Majaribio hayo yaliitwa ni ya wapinga maendeleo lakini leo tukiyatafakari y a l i y o t o k e a tunaweza kusema kuwa kwa kweli hao walikuwa wazalendo wal iokandamizwa na sio wapinga maendeleo.

Kwa muda mrefu Serikali ya Zanzibar iliendeshwa kwa fimbo ya chuma na Rais wa Kwanza Abeid Karume

na hata katika kipindi cha Rais Aboud Jumbe pamoja na kwamba anastahili sifa kwa Katiba ya 1979. Muda wote huo umapinduzi uliendelea kuigawa nchi, maana kwa kiasi kikubwa waliopata haki za kiraia walikuwa ni wa kundi moja.

13ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 2013

Kutokana na mgawanyiko, ambao hata katika upigaji kura hadi leo unaonyesha unaigawa Zanzibar karibu nusu kwa nusu, kupatikana kwa Katiba ya 1984 bado pia hakukuweza kulitanzua tatizo hilo kwa sababu nchi bado haikuwa ikiongozwa kwa ukuu wa katiba na fursa ya kila mwananchi kushiriki katika uendeshaji wa nchi ilikuwa imebanwa.

Kundi kubwa la Wazanzibari ambalo halikupatiwa fursa ya kushiriki katika siasa za nchi liliona milango imefunguliwa pale Sheria ya Vyama vya Siasa ilipoanzishwa mwaka 1992.

Katika muda mfupi Chama cha Wananchi (CUF) kiliundwa na kuwa na ushindani mkubwa sana dhidi ya chama kikongwe cha CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 1995. Kilionyesha kuwa kinaungwa mkono na nusu ya umma. Matokeo ya uchaguzi huo yalizusha ubishi kama uliozuka katika chaguzi za 1961 na 1963.

Kwa kuwa bado jamii ilikuwa imegawika dhana ya kuwa si kila Mzanzibari ana haki ya kutawala iliendelea 1995, 2000 na 2005. Mgawanyiko ulizidi kuzamisha mizizi kuwa si wote wala si vyama vyote vyenye haki ya kutawala. Ni watu maalumu na chama maalumu waliokuwa na haki hiyo.

Nchi iligawika kwa kumwaga damu, kutoa wakimbizi, kulazimisha watu kuihama nchi yao na kuzaa kizazi cha chuki na hasira. Hayo yaliendelea hadi Novemba 4, 2009, pale viongozi wawili Dk. Amani Karume na Maalim Seif Shariff Hamad waliposema “yatosha“.

Kauli zao za kutaka mgawanyiko umalizwe zikaungwa mkono kwa mabadiliko ya Katiba ya

2010 ambayo yalipigwa muhuri mkubwa na Kura ya Maoni ya asilimia 66. Lakini kumbe nia ya kubadilika haikuwa thabiti miongoni mwa kundi dogo la watawala.

Kwa hivyo, pamoja na kuwa tuna mwaka wa tatu sasa tangu iundwe Serikali ya Umoja wa Kitaifa, bado nchi imeendelea kugawika, upande mmoja ukiamini ndio kuwa ndio wenye haki ya kutawala na mshirika wake ni mkaribishwa tu.

Washirika wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa hawaonyeshi kuwa wanafanya kazi kwa kushirikiana. Hivyo ndivyo tunavyooona tulio nje ya Serikali. Tunaona pia kwamba washirika hao hawaheshimiani. Kwa mgawanyiko uliopo mimi kwa hakika si miongoni mwa watakaosema kuwa Serikali hii imepata mafanikio makubwa ya kiuchumi.

Dalili za mgawanyiko mwingine mkubwa ambao unaweza kuipeleka Zanzibar pabaya tunaziona katika harakati za kuipatia nchi Katiba mpya. Tunaona kuwa kila upande umeshikilia mtizamo na msimamo wake bila ya kushirikiana na kuyaweka mbele maslahi ya Zanzibar. Miongoni mwa wenye msimamo mkali usiotaka kubadilika ni watu wanaoonyeshakuwa hawajali ikiwa itakayoumia itakuwa ni Zanzibar ilimradi wanayoyataka yawe.

Upande mmoja unadai kuwa Zanzibar inahitaji mamlaka na nguvu zaidi ili uweze kujisimamia vyema kiuchumi na hivyo kutononesha Wazanzibari kwa kufanya kwa uhuru mambo ambayo kwa sasa hayawezi kufanywa kwa sababu ya uwezo huo kuwemo ndani ya Serikali ya

Muungano.

Pia upande huo unadai usawa au angalau basi uwiano na heshima kama mshirika kamili wa Muungano huu ambao kwa miaka yake 49 umeundiwa Tume 43 mbali ya mikutano kadhaa ya kujadili Kero za Muungano.

Msimamo wa upande wa pili ni kuwa kila kitu kinakwenda sawa sawa na kama kuna haja basi ni kufanya mabadiliko tu ili Muungano ubakie kama ulivyo hivi sasa. Upande huo hauoni sababu ya mabadiliko ya muundo na wala haja ya kuipatia mamlaka zaidi Zanzibar maana yaliopo yanatosha.

Kwa sababu hiyo mgawanyiko wa Zanzibar umefikia pabaya zaidi maana wanapingana hata katika maslahi ya Zanzibar na hatari kubwa zaidi ni kuwa mgawanyiko huu umefufua fikra, dhana na mitizamo yote ya miaka ya nyuma.

Sasa cha kujiuiliza mpaka lini Wazanzibari wataendelea kugawanyika na kujigawa? Je, ni lini watatambua kuwa mgawanyiko huu una hasara kubwa kwao?

Mimi huwa najiuliza hivi kweli kuna mtu anawagawa Wazanzibari au ni wenyewe ndio wanaojigawa? Na ni kweli kuwa Wazanzibari wanajigawa wenyewe?

Vyovyote iwavyo, ni muhimu kulikabili suala hili sasa. La sivyo, Zanzibar inakwenda, na itakapokwenda haitarudi kesho, keshokutwa hata muhudi. Chaguo ni letu.

ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 201314

MAKALA MAALUM

Kamati ya Maridhiano ina ridhaa ya Wazanzibari Hata hivyo, sikutegemea majibu yale kutoka kwa kiongozi aliye mkuu wa nchi na kinara wa serikali ya pamoja kati ya CCM na CUF. Nilijiuliza, ina maana Rais anatwambia hajui kuwa kuna maridhiano ya ki-siasa Zanzibar? Kama hilo halijui, basi hata hajui kama kuna serikali ya Umoja wa Kitaifa, ambayo anaiongoza yeye mwenyewe? Ikiwa hilo analijua, basi hafahamu serikali hiyo imetokana na mchakato gani hadi pakafikiwa hali ya kuirekebisha Katiba ya nchi na kufanywa kura ya maoni? Au alikuwa ana-jisuta alipotamka Bwawani siku alipotangazwa mshindi wa uchaguzi wa Urais 2010 kwamba anatekeleza matakwa ya Wazanzibari juu ya hali ya kisiasa iliokuweko visiwani?

Na Baraka Mwinyi

KWA muda mrefu sasa nimekuwa nikitafakari na kujiuliza maswali mengi

baada ya kuisikia kauli ya Rais wetu, Dk. Ali Mohamed Shein, kwamba haitambui Kamati ya Maridhiano. Tume hii ya watu sita ikiongozwa na mwanasiasa mkongwe na aliyetoa mchango mkubwa katika kupigania uhuru wa Visiwa hivi, Mzee Hassan Nassor Moyo, ina jumla ya w a j u m b e sita, watatu k u t o k a Chama cha M a p i n d u z i (CCM) na w a t a t u k u t o k a Chama cha W a n a n c h i (CUF).

Kamati hii n d i y o iliyofanikisha k u p a t i k a n a m a r i d h i a n o y a l i o l e t a serikali hii ya Umoja wa Kitaifa na kuondoa uhasama wa kisiasa uliozuka tangu baada ya uchaguzi wa 1995. Kwa hakika kamati hii ni chombo cha kulisukuma gurudumu la mabadiliko Viswani.

Aliyeiunda kamati hiyo alikuwa Rais mstaafu Amani Abeid Karume

lakini uamuzi hasa ulikuwa wa umma kupitia ile kura ya maoni ambayo matokeo yake yalionyesha kwamba asilimia 66 ya Wazanzibari waliopiga kura walikiidhinisha hiki wanachojivunia leo. Kuwa na maoni au misimamo tafauti baina ya vyama au hata ndani ya vyama ni jambo la kawaida katika siasa. Aghalabu hoja tafauti na maoni yanayokinzana huzaa maamuzi ambayo hatimaye huwaridhisha walengwa ambao si

w e n g i n e

bali ni jamii. Hivyo ndivyo demokrasia inavyofanya kazi.

Lakini kuna mambo huwa ni misingi ya hiyo demokrasia, na misingi huwa hairuhusu kudhalilishwa, japo yaweza kujadiliwa. Kwa Zanzibar, Kamati ya Maridhiano ni msingi

mmoja mkubwa wa demokrasia yetu, iaminikayo ipo leo. Kwa hivyo ilitushangaza wengine pale Rais Shein ‘alipochochewa’ kuutikisa na kuudhalilisha msingi huu..Alianza siku aliyorejea kutoka China mwezi Juni. Katika mkutano wake na waandishi wa habari, aliulizwa na mwandishi aliyetaka kujua kama kweli Rais ameipa Kamati ya Maridhiano ‘baraka zake’. Mwandishi huyo alidai kwamba

hivyo ndivyo Kamati hiyo ilivyodai.

Jibu la Dk. Shein lilikuwa la kusikitisha. Alisema kwamba

haijui siku iliyoundwa Kamati hiyo wala

u t a r a t i b u wake na k w a m b a w a u l i z w e w e n y e w e wanamjua aliyeiunda.

Ilionyesha k w a m b a swali hilo alililoulizwa Shein na m e n g i n e yaliyofutia yalipangwa k w a

sababu majibu yaliibua vicheko vya kejeli kutoka kwa baadhi ya waandishi habari, wapambe na hata mwandishi aliyeuliza suala hilo, huku akiitikia “sawa sawa” kwa kila anachokisisitiza Rais. Mwezi mmoja baadaye, Rais Shein akayarejelea yaleyale kwenye mkutano wa

15ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 2013

Kamati ya Maridhiano ina ridhaa ya Wazanzibari hadhara wa Kibandamaiti.

Ya waandishi katika mkutano huo yalinikereketa lakini hayakunishangaza hasa unapofikiria utendaji wao hao waliokuwa wakifurahi - kitaaluma, kiuandishi, na hata kielimu. Leo bahati moja mbaya ya Zanzibar yetu ni kuwa kila mtu anaweza kujiita mwandishi. Sukuma twende bora tu halitoti na vigogo wanafurahi.

Hata hivyo, sikutegemea majibu yale kutoka kwa kiongozi aliye mkuu wa nchi na kinara wa serikali ya pamoja kati ya CCM na CUF. Nilijiuliza, ina maana Rais anatwambia hajui kuwa kuna maridhiano ya kisiasa Zanzibar? Kama hilo halijui, basi hata hajui kama kuna serikali ya Umoja wa Kitaifa, ambayo anaiongoza yeye mwenyewe? Ikiwa hilo analijua, basi hafahamu serikali hiyo imetokana na mchakato gani hadi pakafikiwa hali ya kuirekebisha Katiba ya nchi na kufanywa kura ya maoni? Au alikuwa anajisuta alipotamka Bwawani siku ya alipotangazwa mshindi wa uchaguzi wa Urais 2010 kwamba anatekeleza matakwa ya Wazanzibari juu ya hali ya kisiasa iliokuweko visiwani?

Kwenye siasa kuna tafauti kati ya mwanasiasa anayeingia madarakani kwa kubebwa na nguvu fulani kwa sababu ya maslahi fulani na yule anayeingia madarakani kwa ridhaa ya umma akijuwa kwamba ni kujiamini kwake na kuamini anachokipigania ndiko kulikompa ridhaa ya wananchi. Huyu wa pili huwa hatetereki, lakini wa kwanza ni rahisi kusema hili leo na kesho kusema jengine, kwani nyuma yake huwa kuna mikono inayomsukuma njia ya kupita. Si yeye mwenye kuamua njia ipi apite. Natamani sana Rais Shein awe kwenye kundi la pili. Nasema natamani. Lakini wengi wa viongozi wetu wana upungufu mkubwa wa kuweza kusoma nyakati na alama zake. Kuna wengi waliochukulia

kuwa kauli zake ni sawa na kumbeza mwanasiasa Mzee Moyo, mtu ambaye kwa ujasiri ameweka kando masilahi ya chama chake na yake binafsi na amesimama kidete kupigania marekebisho kwa kuamini kwamba tulikuwa tumepoteza dira na huko tulikokuwa tukielekea kwenda siko tulikoazimia kwenda.

Kwa kauli zake Rais Shein pia amekuwa akimkebehi aliyemtangulia madarakani, Rais Amani Abeid Karume, ambaye wengi wanafahamu alivyomuachia nchi iliyokuwa imeungana kwa kiwango kikubwa. Amani na mshikamano uliopo hivi sasa Zanzibar, licha ya changamoto za hapa na pale, kwa sehemu kubwa ni mafanikio ya Kamati hii ya Maridhiano. Na Kamati hii sasa pia inachangia katika suala la mustakbali wa Zanzibar wakati huu wa mchakato wa kupata katiba mpya Tanzania, ambapo jambo kubwa kwa mtazamo wa wengi ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Wenye macho wanaona kwamba sehemu kubwa ya jitihada za Mzee Moyo na kamati yake ni muendelezo wa pale alipoanzia na kupaacha Rais wa zamani, Alhaji Aboud Jumbe, katika kupigania haki ya Zanzibar katika Muungano utakaokuwa wa heshima kwa pande zote mbili. Yeye Mzee Jumbe alianzisha harakati hizo baada ya kung’amua kwamba mtangulizi wake, Mzee Abeid Karume, alikuwa amezidiwa nguvu kwenye masuala mengi yaliyougeuza Muungano wa hiyari kuwa chaka la utumwa.

Almuradi kauli ya Dk. Shein inalirudisha kikaangoni suala zima la maadili ya kisiasa na uwajibikaji kwa nchi. Kusema kwamba haitambui Kamati hiyo si muhimu sana. Muhimu hasa ni msimamo wa Wazanzibari kuhusu hatima yao. Wazanzibari, kwa wengi wao, walipoamua katika kura ya maoni

walifanya hivyo kwa kuweka kando vyama na itikadi zao za kisiasa. Kama alivyosema Mzee Moyo, vyama vimekuja baadaye, lakini kwanza ni nchi na itabakia daima kuwa hivyo, hapo hapo ilipo.

Kama nchi nyingi nyengine, Zanzibar imefika ilipofika sasa baada ya safari ndefu. Ukiitazama iliyokuwa Urusi ya zamani, Yugoslavia na nchi nyengine, kote wakubwa wakiamini mabadiliko ni mwiko. Walisahau kuwa mabadiliko ni mchakato na hutokea wakati wake unapofika. Wakati huo ukifika huwa hakuna nguvu ya kulizuwia wimbi la mabadiliko. Waliowekwa na umma huondolewa na umma. Hivyo kutambuliwa na kutotambuliwa kwa Kamati ya Maridhiano na kiongozi au viongozi fulani si muhimu, almuradi inatambuliwa na umma. Kwa Zanzibar hilo halina mjadala, kamati imepata ridhaa ya umma inaoutumikia. Nikinukuu maneno ya Mwenyekiti Mao Tse Tung wa China: “The people and the people alone are the force in the making of history”. (Ni watu na watu peke yao ndiyo nguvu ya kuandikia historia.)Historia ya kutaka mabadiliko imeandikwa na Wazanzibari na ni Wazanzibari watakaoleta mabadiliko. Wazanzibari wanajua nani ameteuliwa na nani na kwa madhumuni gani. Wao wameitambua Kamati ya Maridhiano, kwani Visiwa vyao vipo hapa vilipo kisiasa kutokana na uamuzi wao wa kuyakubali maridhiano yaliyoekewa msingi na wao wenyewe - Umma. Kwa hivyo la msingi ndilo hilo kwamba Kamati ya Maridhiano inatambuliwa na Wazanzibari na ndiyo inayoonekana kupigania maslahi yao, si kwa kuegemea CCM wala kuegemea CUF. Na la watu ni la Mungu, ndipo mwenyewe Mzee Moyo alisema: “Tumetambuliwa na Mwenyezi Mungu”. Hilo pekee latosha.

ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 201316

XXX • XXXKALAMU YA AHMED

Kuna kimya kinachonishangaza. Nacho ni cha ‘wanaharakati’ wa

Kizanzibari walioziba midomo yao kuhusu madhila yanayowakuta wale waliokuwa wakiwaita “mashekhe wetu wa Uamsho”.

Tangu mashekhe hao 10 waanze kukamatwa Oktoba 16, 2012 mpaka leo kesi yao haijatajwa mahakamani. Hadi sasa wamesomewa tu mashtaka dhidi yao, mashtaka ambayo yanahusika na vurugu zilizotokea Zanzibar Mei mwaka jana.

Washtakiwa hao walifikishwa mara ya mwisho mahakamani Julai 3 mwaka huu na wanatarajiwa kupandishwa tena mahakamani Julai 18.

Washtakiwa wenyewe ni Farid Hadi Ahmed, Msellem Ali Msellem, Mussa Juma Issa, Azan Khalid Hamdani, Suleiman Juma Suleiman, Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakari Suleiman, Ghalib Ahmada Omar, Abdalla Said Ali na Fikirini Majaliwa Fikirini.

Mashtaka yanayowakabili ni

kuchochea vurugu, kuharibu mali za umma na za watu binafsi zenye thamani ya shilingi milioni 500, kufanya vurugu katika eneo la Magogoni na kuhatarisha usalama wa taifa la Zanzibar.

Wanashtakiwa pia kuhusu kadhia ya Farid Hadi Ahmed aliyetoweka Oktoba 16, 2012. Shekhe huyo aliibuka siku nne baadaye akidai kwamba alitekwa nyara na watu waliovaa barkoa waliojitambulisha kuwa ni polisi. Serikali imelikanusha dai hilo. Mashekhe hao wamefungiwa kwenye gereza la Kiinua Miguu wakiwa chini ya ulinzi mkali. Kama wiki mbili za mwanzo baada ya kutiwa nguvuni wakidhalilishwa kwa kunyimwa hata nafasi ya kubadili nguo au ya kuonana na familia zao.

Tena kila mtuhumiwa alikuwa akiwekwa katika chumba cha peke yake. Tunavyosikia ni kwamba siku hizi wameondoshewa madhila hayo ingawa bado mazingira yao si ya kuridhisha.

Cha kushangaza ni kwamba hatusikii sauti zozote zenye kuwatetea. Labda kwa sababu wao ni mashekhe na si wanasiasa.

Labda wangekuwa wanasiasa tungewaona wanaharakati, kwa mfano, wakiwasiliana na jumuiya za kimataifa za haki za binadamu na kuzizindua kuhusu janga lililowafika mashekhe hao.

Labda madevu ya hao mashekhe yanawatia hofu wanaharakati, wanachelea wasije wakashtumiwa kuwa wanawatetea ‘magaidi’ maana siku hizi kwa wakubwa wa dunia hii madevu, Uislamu na utetezi wa haki ni mchanganyiko wa hatari.

Na si kwa hao wakubwa tu bali hata kwa baadhi ya taasisi, magazeti, na wanasiasa wa Tanzania Bara ambao bila ya ushahidi wowote wameihusisha Uamsho na vitendo vya kigaidi.

Juu ya yote hayo, kuna sababu halali za kuwatetea. Sababu kubwa ni kazi walioifanya ya ‘kuwaamsha’ Wazanzibari wenzao wautambue utaifa wao na waachane na chuki na uhasama uliokuwepo baina yao kwa muda mrefu.

Jengine jema walilolifanya ni

La Uamsho na ukimya wetu

TANBIHI: Hii ni sehemu ya makala “Ya Malala, Taliban na Uamsho” yalioandikwa na AHMED RAJAB kwenye gazeti la Raia Mwema la tarehe 17 Julai 2013. Zanzibar Daima Online imeichapisha sehemu hii kutokana na umuhimu wake.

“Cha kushangaza ni kwamba hatusikii sauti zozote zenye kuwatetea. Labda kwa sababu wao ni mashekhe na si wanasiasa. Labda wangekuwa wanasiasa tungewaona wanaharakati, kwa mfano, wakiwasiliana na jumuiya za kimataifa za haki za binadamu na kuzizindua kuhusu janga lililowafika mashekhe hao. Lab-da madevu ya hao mashekhe yanawatia hofu wanaharakati, wanachelea wasije wakashtumiwa kuwa wa-nawatetea ‘magaidi’ maana siku hizi kwa wakubwa wa dunia hii madevu, Uislamu na utetezi wa haki ni mchanganyiko wa hatari.”

17

XXX • XXX

ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 2013

kuwahimiza vijana wa Kizanzibari warudi kwenye maadili ya Kiislamu badala ya kujihusisha na vitendo vinavyoleta madhara katika jamii kama vile vya kubugia mihadarati na uasherati.

Pengine kuna wanaharakati wenye kujuta, wenye kuona kwamba walipoteza nguvu zao walipokuwa wakiwaunga mkono hao mashekhe. Wale waliokuwa na majazba waliokuwa wakiota kwamba siku moja nchi yao itaamka ghafla ionekane na sura nyingine sasa itawabidi waote ndoto nyingine.

Sina dhamira ya kuingilia kesi inayowakabili washtakiwa hao. Hiyo ni kazi ya mahakama na ya mawakili.

Dhamiri yangu ni kukizungumzia hiki kimya kilichotanda kama wingu juu ya kesi hii. Na zaidi nataka kugusia haki wanayonyimwa washtakiwa ya kuachiwa kwa dhamana huku kesi ikiwa inaendelea. Kucheleweshwa

kusikilizwa kwa kesi hiyo ni adha kubwa kwa washtakiwa.

Inavyoonyesha ni kama serikali imeamua kuwatia adabu ingawa hawakupatikana na hatia.

Ikiwa dhana hiyo ni sahihi basi serikali itakuwa imeamua hivyo kwa sababu za kisiasa. Serikali inazidi kujifaragua ikiamini kwamba kuwatia adabu viongozi wenye muelekeo wa Kiislamu hakutowakera wakubwa wa dunia hii.

Labda serikali inaamini kwamba balozi za Marekani na Uingereza zitayafumbia macho wanayotendewa mashekhe hao kwa sababu zimekwishatiwa sumu ya Uamsho kusingiziwa ugaidi.

Ndio maana kesi hiyo ikawa inaakhirishwa na kuakhirishwa kwa lengo la kuwaweka ndani tu mashekhe hao. Mara ya mwisho Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar alisema wanasubiri waletewe daftari la kesi kutoka

Mahakama ya Rufaa, Dar es Salaam. Sijui Wazanzibari wenzangu wanapofuturu na aila zao katika mwezi huu Mtukufu kama wanawafikiria wananchi wenzao walio gerezani.

Nijualo ni kwamba ingawa uamuzi ni wa mahakama wengi wenye kuifuatilia kesi hii wanaamini washtakiwa hao wanaendelea kuwekwa ndani kwa sababu hivyo ndivyo watakavyo viongozi wa juu wa serikali ya Zanzibar.

Mara mbili tatu hivi Rais Ali Mohamed Shein mwenyewe amesema hadharani kuwa atawashughulikia wanaochochea fujo. Wakati mwingine huwataja Uamsho.

Zanzibar ya leo ni nchi yenye kuhuzunisha; haisikitishi tu bali inahuzunisha. Ni nchi yenye kutatanisha, wakati mwingine hujikanganya yenyewe. Na viongozi wake? Naona hata haina haja ya kuwaeleza walivyo; bora tulifunike kombe..

La Uamsho na ukimya wetu

Baadhi ya viongozi wa Uamsho katika picha hii iliyopigwa mwanzoni mwa mwaka 2011, wakati huo wakiwa-ongoza waandamanaji kudai nafasi bora zaidi ya Zanzibar kwenye Muungano. Sasa wengi wa viongozi hawa wamewekwa kizuizini na Serikali ya Zanzibar kwa takribani mwaka mzima.

ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 201318

XXX • XXXKAULI YA MWINYI MKUU

Si haki kusema SUK imekwama kaziHakuchukulia kuwa ataonekana anamkandamiza waziri mwanamke; wala hakuona kuwa kuhoji sana kwake mambo kadhaa kutawaudhi wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) kilichompa nguvu ya kugombea na hatimaye kuingia Barazani. Na hicho ndiyo chama alicho Waziri Fatma Ferej. Jussa hakujali yote hayo. Alisimamia hoja. Akaijengea nguvu ili kushawishi Baraza litambue umuhimu wa aliyoyapigania. Kwa namna alivyokuwa amedhamiria hasa kuhoji kwa nia ya kujenga, alithubutu kuahidi kubaki peke yake ikibidi mpaka ajiridhishe

Na Jabir Idrissa

KWA kuzingatia semi za kileo zinazovuma Zanzibar – kama hii

isemayo “Tukiweka pembeni khitilafu zetu tunaweza” – mtu aliye makini kisiasa hawezi kusimama hadharani akasema “Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) imegota.”

Kwa hakika, mtu huyo atakuwa amedanganya. Itakuwa kwanza hakufuzu katika vipimo vyake vya kuitambua nafasi ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa na, pili, kwa mbali atakuwa amejibainisha waziwazi kuwa yu katika wale wasioitakia mema Zanzibar. Na hawa wapo.

Napenda kumuweka darasani kidogo mtu huyu na wengineo ambao wamekuwa wakitapakaza maneno na maandishi kuwa Serikali ya Umoja inayumba, inayumbishwa, inasambaratika, imo matatani au inachungulia kaburini.

Maneno mengi mengi yanatajwa kuitambulisha serikali hii iliyoundwa kufuatana na matakwa ya wananchi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Aanzie kwenye chombo cha kutunga sheria – Baraza la Wawakilishi, linalotumika kuzipaza sauti za Wazanzibari kwa ndimi za wawakilishi waliowachagua majimboni.

Akiliangalia vizuri Baraza hili hatachukua muda mrefu kugundua tofauti kubwa iliyopo wakati wa mijadala inayowasilishwa na Serikali na

vile hali ilivyokuwa katika Baraza la saba.

Kuna mabadiliko makubwa ya kupigiwa mfano. Mijadala

imekuwa mizito zaidi; iliyoshiba na ambayo imekwenda skuli barabara. Siku hizi unaisikia mijadala motomoto bila ya kujali nani amewasilisha kinachojadiliwa.

Nani hakushuhudia namna Ismail Jussa Ladhu alivyomkaba koo mwanamke jasiri, kwa vigezo vya Marekani, Fatma Abdulhabib Ferej, wakati wa kupitisha kasma au mafungu ya fedha zilizopangwa kama bajeti ya mwaka wa fedha wa 2013/14?

Fatma ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye anashughulikia hasa usimamizi wa hifadhi ya mazingira, haki za watu wenye ulemavu, udhibiti wa ugonjwa wa ukimwi na kampeni ya kutokomeza matumizi na biashara ya madawa ya kulevya.

Yule asiyeshuhudia ajute. Kwa kweli ilikuwa ni bahati mbaya sana kwake. Baraza la Wawakilishi, likiwa limekaa kama Kamati ya Matumizi, lililazimika kuahirishwa hadi siku ya pili ili kutimiza mantiki ya hoja ambayo Jussa alikuwa ameiibua.

Mwakilishi huyu kijana msomi wa jimbo la Mji Mkongwe, anakopigia kura Waziri Fatma Ferej, hakuangalia uso wa waziri mhusika kwa masuala aliyokuwa akiyapigia kelele.

Hakuchukulia kuwa ataonekana

19

XXX • XXX

ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 2013

anamkandamiza waziri mwanamke; wala hakuona kuwa kuhoji sana kwake mambo kadhaa kutawaudhi wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) kilichompa nguvu ya kugombea na hatimaye kuingia barazani. Na hicho ndiyo chama alicho Waziri Fatma Ferej.

Jussa hakujali yote hayo. Alisimamia hoja. Akaijengea nguvu ili kushawishi Baraza litambue umuhimu wa aliyoyapigania. Kwa namna alivyokuwa amedhamiria hasa kuhoji kwa nia ya kujenga, alithubutu kuahidi kubaki peke yake ikibidi mpaka ajiridhishe.

Jussa alisema hajali kama wawakilishi wenzake watamuona kuwa king’ang’anizi au mkorofi bali alikuwa anaona kama vile labda hawajamuelewa vizuri. Alikuwa na hoja iliyokuwa na mantiki.

Alitaka fedha zipatazo shilingi milioni 200 zipunguzwe kutoka kwenye fungu la Tume ya Ukimwi Zanzibar (ZAC), ili badala yake zipelekwe kusaidia shughuli za kudhibiti uchafuzi wa mazingira, watu wenye ulemavu na vita dhidi ya madawa ya kulevya.

Jussa alikerwa kuona ZAC inapewa fedha nyingi wakati katika utendaji wake hakujaonekana manufaa makubwa ya kupunguza kiwango cha maambukizi ya virusi vya HIV. Akataka badala yake, fedha hizo zipelekwe kunakoweza kuleta matokeo ya kuonekana.

Hili wala si la kubahatisha. Wakati wa majadiliano ya hotuba yake ya makadirio, waziri mwenyewe alikiri waziwazi kuwa upungufu wa fedha umenyima nafasi ya kutekelezwa miradi mingi ya maeneo hayo, hasahasa mazingira.

Namna hoja zilivyotolewa Jussa akazipangua huku akitaka

uhakikisho zaidi wa Serikali, sijaiona siku nyingi katika Baraza letu.

Walimalizaje? Spika Pandu Ameir Kificho aliridhia ushauri wa Jussa kutaka wizara ikiongozwa na Waziri mwenyewe ikae na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, ofisi kuu kiutendaji kazi za serikali, na Tume ya Ukimwi kuangalia namna gani wazigawe fedha hizo.

Ile ni hali usiyoitarajia kwa mwakilishi kumkaba koo waziri wa chama alicho. Jussa alithubutu. Kwa bahati nzuri, wakati hayo yakitendeka, Jussa alimuona waziri mtendaji makini, na waziri naye alimsifia Jussa kwa ufuatiliaji wake uliotukuka.

Baraza la Wawakilishi limejijengea heshima kubwa siku hizi. Limetumika kuisimamia kikamilifu serikali katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku. Limetuma tume mara tatu ndani ya mwaka mmoja kuchunguza tuhuma za ufisadi Serikalini.

Tume zote zimekuja na ugunduzi makini na wa kutegemewa, ingawa ndani ya vitisho vingi vya wajumbe wake kujaribu kuhongwa ili wasibainishe waliyoyakuta. Walimaliza kazi yao na kuwasilisha ripoti ambazo bado zinaitwa kwa majina yake.

Huo ndio utendaji wa Baraza au Bunge. Unaisimamia kisawasawa serikali na kuikosoa pale ilipokwenda mrama, huku ukiipa ushauri wa kurekebisha mambo kwa ajili ya kusonga mbele. Ni hapa inapolazimu kumtaja kiongozi wa Baraza hili, Pandu Ameir Kificho, kama mtu imara.

Anatoa fursa kwa kila mwakilishi anayetaka kusema na kutoa hoja yake. Kificho amelisaidia Baraza liache kuchekwa likionekana kama

mzigo kwa kodi za wananchi. Sasa, mawaziri wanalihofia Baraza.

Nchi kuwa na chombo imara cha kutunga sheria na kuisimamia serikali, ni hatua kubwa katika ujenzi wa demokrasia na Serikali inayowajibika. Huo ni ushindi mmoja wa Serikali ya Umoja.

Wa pili, pamoja na ukweli kwamba ile sura halisi ya maridhiano haikwenda mbali kutoka Baraza la Mawaziri ambalo ndio limechanganyikana, ilivyo leo si jana.

Lililo muhimu zaidi ni kwamba siku hizi tunazidi kuwaona watendaji kutoka vyama viwili vya CCM na CUF wakishirikiana. Kabla ilikuwa si aghlabu kuwaona wakikaa pamoja seuze kushirikiana. Haikuwa rahisi siku hizo kwa kada wa CUF kujadili jambo kwa amani na kada wa CCM. Zipo dalili za kuwepo watendaji wakorofi waliolenga kuwakorofisha mawaziri wa CUF katika zile sekta wanazoshikilia. Hilo likitarajiwa kwani hatukufikiria kuwa chuki za miaka na miaka zitaweza kuondoshwa katika muda wa miaka miwili wala mitatu. Chuki zimeshamiri Zanzibar na zinahitaji muda kuondoka kabisa. Watendaji kama hao wenye chuki ni miongoni mwa wahafidhina wa CCM ambao haweshi kuitia Serikali katika mtihani. Lakini, kama Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein alivyosema hadharani Serikali yake inafanya kazi vizuri na yeye na wasaidizi wake wawili, naye na mawaziri wake wote wanajadili kila jambo kwa pamoja kwa maslahi ya wananchi.

Hatua iliyopigwa ni ya kutia moyo kwa sababu hakuna aliyetarajia kuwa kila kitu kitabadilika mara moja kwa haraka wakati CCM imeshikilia hatamu na kusababisha kudhoofu kwa mifumo ya uongozi na utendaji kazi serikalini.

ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 201320

SIGNATURE XXXXXXXX PHOTO BY XXXXXXXXX

WARAKA MAALUM

MWEZI Mtukufu wa Ramadhani umemalizika na

umewaachia Wazanzibari mengi ya kujifunza juu ya khatima ya nchi yao katika nyanja mbalimbali, ikiwa pamoja na ya dini.

Misikiti ilifurahika, alhamdulillah, kwa vijana na wazee waliokuwa wakihudhuria darsa,wakisoma Qur’an na wakiomba maghfira. Lakini nje ya misikiti kulikuwa na mengi yaliokuwa tafauti na hali iliyokuwepo Zanzibar katika miaka ya nyuma.

Kwa mfano, watu waliokuwa wakitafuta rizki zao kwa kufanya biashara ndogondogo katika sehemu za Darajani walikunutwa

mikong’oto na kuporwa vitu vyao na askari wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ). Tukio la kinyama la aina hii halikuwahi kushuhudiwa Zanzibar miaka iliyopita.

Baya zaidi ni kwamba uhuni huu wa askari wa vikosi vya SMZ ulifanywa kukebehi maelekezo ya Serikali yenyewe yaliotolewa na Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad. Yeye alielekeza kuwa hao wafanyabiashara waendelee na shughuli zao katika maeneo yanayozunguka soko kuu la Darajani kama ilivyokuwa miaka ya nyuma mpaka utapomalizika mwezi Mtukufu.

Lakini askari hao, bila ya shaka wakiwa wanatekeleza amri ya wakubwa wa vikosi, hawakuheshimu maelekezo ya mmoja wa viongozi wakuu wa nchi.

Kwa ujeuri na kebehi walilivamia eneo hilo kwa siku tatu mfululizo wakiwapiga watu ovyo na wakipora mali za wafanyabiashara. Askari hao walikuwa kama wakiambizana ‘chukua chako mapema’ na walizigeuza mali za wafanyabiashara kuwa kama mali za ngawira. Askari hao walijifunika nyuso zao vitambaa mithili ya ‘Ninja’ na hata wakitoa kauli zilizoashiria kwamba hawakujali maelekezo ya Serikali.

Wapo walioona kwamba hao wafanyabiashara walikuwa hawastahiki kisheria kuwepo eneo hilo. Lakini kumbukumbu zinaonyesha kuwa tokea zama za utawala wa kikoloni na Sultani watu walikuwa huru kufanya biashara sehemu hizo na walikuwa hawatozwi ada yoyote ile, iwe walikuwa wanauza bidhaa za futari, daku au mavazi ya Sikukuu

Na Salim Said Salim

Ramadhani mwaka huu ilikuwa na viroja

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, akiulizia bei za vitoweo kwenye Marikiti Kuu Darajani.

21ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 2013

.Kinachoshangaza na kuonyesha kwamba siku hizi mambo Zanzibar yanafanyika kihuni tu ni kwamba wafanyabiashara hawa walikuwa wanatozwa kodi ya ya kila siku ya kati ya shilingi 500 hadi 1,000 na Baraza la Manispaa. Kodi hiyo ilikuwa ya kuhalalisha kuwepo kwao sehemu hizo. Lakini juu ya kulipa kodi hiyo kuwepo kwao hapo bado kukionekana kuwa sio halali.Ukitafakari kwa undani utaona kitendo hiki cha kuwavamia wafanyabiashara hawa na hata kuwapiga na kuwajeruhi kilikuwa hakina lengo jengine isipokuwa kumkejeli Maalim Seif na kuwakomoa hao wafanyabiashara ambao wengi wao ni wa kisiwa cha Pemba. Hii imeonyesha kwa mara nyengine tena kwamba watu kutoka Pemba bado hawapewi haki wanayostahili katika nchi yao. Kosa lao sio jengine isipokuwa msimamo wao usiouyumba wa kukikataa chama tawala cha CCM na kutaka Zanzibar iwe na mamlaka kamili chini ya Katiba mpya ya Tanzania.

Baadaye Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Mwinyihaji Makame, alisema vijana hao wamedhibitiwa na eneo hilo ni shuwari. Lakini kuna swali linaloibuka hapa. Nalo ni: kwa nini waliotoa amri ya kuyakebehi malekezo ya Maalim Seif na kuwatuma hao wahuni kuwapiga watu ovyo wasishughulikiwe kisheria au angalu kuchukuliwa hatua za nidhamu?Hii ni dosari kubwa kwa nchi inayojigamba kutandika mfumo wa utawala bora.Jengine lililoshuhudiwa katika mwezi Mtukufu, tafauti na siku za nyuma, ni watu kula fawahisha.

Ilikuwa kama vile sio kosa la jinai kwa mujibu wa sheria za Zanzibar kwa mtu kula, kunywa au kuvuta sigara hadharani wakati wa mwezi Mtukufu wa mfungo wa Ramadhani.Watalii nao walionyesha jeuri ya hali ya juu. Mara nyingi walionekana wakitembea na vichupi wakati Zanzibar inayo sheria ya mavazi ambayo hutiliwa mkazo zaidi wakati wa mwezi wa Ramadhani. Lakini watalii hao hawakuguswa kwa sababu wanaingiza fedha za kigeni ambazo zinaonekana kuabudiwa zaidi.Kulikuwako pia vijana wasio Wazanzibari (waliotoka sehemu ya pili ya Muungano) waliokuwa wakipiga nyimbo za Kikristo hata katika eneo la Darajani, kitendo ambacho kilileta bughudha na maudhi makubwa kwa Waislamu. Lakini watu walikuwa wakilalama tu. Wakiogopa kutetea misingi ya dini ya Kiislamu kwa kuwa kila anayetetea misingi hiyo huitwa Muamsho na hubambikiwa kesi ili aoze gerezani.Wananchi wengi walibaki kulalama katika mwezi wa Ramadhani kuwa bei za nguo, hasa za watoto, zilikuwa za juu kabisa kuliko miaka iliyopita. Wakati mamia ya watu walikuwa wakifurika Zanzibar siku za nyuma kununua nguo za Sikukuu safari hii watu wengi walikimbilia Bara kwa vile huko bei ni afueni kuliko Zanzibar hivi sasa.Hiki ni kielelezo chengine cha namna ambavyo Zanzibar inaathirika kiuchumi kutokana na mfumo wa Muungano wa viwango vya kodi Zanzibar kuwa juu zaidi kuliko Bara.Suala hili limelalamikiwa sana na Wazanzibari. Lakini siku zote Serikali ikisema patachukuliwa hatua muwafaka na kulipatia ufumbuzi. Kilichoonekana zaidi ni

porojo na si vitendo.Hata taswira ya mji wakati wa mwezi wa Mfungo ilionekana kuzidi kupoteza haiba yake. Ule utamaduni ulioifanya anga ya Zanzibar ijae vishada haupo tena na urushaji wa vishada Visiwani wakati wa Ramadhani umekwenda arijojo.Hata hivyo, inafurahisha kwamba mashindano ya dini, kama ya kuhifadhi Qur’an, yaliongezeka katika kila pembe ya Visiwa vyetu katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.Inatupasa tutafakari kwa kiasi gani Zanzibar imejifunza katika mwezi huu Mtukufu tulioumaliza. Aidha, tujiulize ni mambo gani inafaa tuyachukulie hatua ili iweze kurudi ile Zanzibar ya zamani iliyovutia na kuwa na haiba ya aina yake katika mwezi huu Mtukufu.Labda ingefaa tuanze kwa kuvifanya viwanja vya sherehe za Sikukuu viwe na mambo yanayostahiki kwa kusherehekea siku hii adhimu na sio kuhanikiza kwa muziki wa disko na michezo ya kuigiza ya kuwafundisha watoto wadogo mambo ya mapenzi. Kwa mfano tuachane na michezo inayowapa mafunzo makubwa kuliko umri wao, kama vile kuonyeshwa mwanamke akipanga njia za kumtoroka mume nyumbani kwa kisingizio kuwa amepata taarifa ya msiba, lakini kumbe ni ujanja wake wa kupata ruhusa ya mume ya kuondoka nyumbani ili akafanye mambo machafu, ya fuska.Idd njema, ya raha na furaha na tusichoke kumuomba Mungu atupe maghfira ili Zanzibar yetu irejee kuwa na sura yake ya zamani ya pahala penye utukufu sio wa ibada tu, bali wa utu na wa kuheshimu haki za binadamu za kuishi na kujitafutia rizki za maisha bila ya kubughudhiwa na Serikali.

ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 201322

XXX • XXXMAONI

Musitutishe kwa chui wa karatasi

Tunapounda Jumuiya au Umoja wa aina yoyote huwa tuna shabaha na vitendo vyetu vyote huwa vina

shabaha hiyo moja, yaani kusudi la kuunda Umoja huo. Vitendo vyetu vizuri ni vile vinavyosaidia kutimiza shabaha hiyo, na vibaya ni vile ambavyo vinapinga kutimizwa kwa shabaha yetu.

Vitendo vyetu vinavyosaidia kutimiza shabaha yetu ya kuirudishia Zanzibar MAMLAKA kamili kitaifa na kimataifa ni vitendo vizuri, na vile ambavyo vinapingana na utimizaji wa shabaha hiyo ni vibaya.

Vitendo vyetu vinavyosaidia kuimarisha umoja wetu wa Wazanzibari bila ya kujali misingi ya kwa mfano tafauti za kidini, itikadi za kisiasa, ukabila na jinsia ni vizuri, lakini vile vinavyopunguza nguvu ya huo Umoja wetu bila ya shaka ni vibaya.

Wengine wanatutisha kwa khofu za chui wa karatasi, kwa kile kinachoitwa ‘Kuvunjika Muungano’ kwa kuwa kwao hilo ni jambo la hatari; lakini sisi tunawaambia Zanzibar kumezwa na kupoteza mamlaka na uwezo wake wa kujiamulia mambo yake kitaifa na kimataifa na kupotea katika ramani

ya dunia ni jambo la hatari zaidi na jambo hilo halikubaliki hata kidogo.

Ndio maana tunasema kwamba sisi Wazanzibari tunapaswa kushiriki kwenye maamuzi yote yanaoihusu nchi yetu kwani sisi ndio raia wake.

Kwa hakika, tunastahiki hasa kuruhusiwa kufanya hivyo na kushajiishwa kufanya mengi zaidi na sio kuzuiwa kwa vitisho hivi na vile. Bila ya shaka, hatuachi kushukuru kwamba kwa mara ya mwanzo sasa, baada ya takriban miaka 50, tumeweza tena kuzipaza sauti zetu kupitia majukwaa ya kitaifa na kimataifa.

Lakini hilo halitoshi. Sasa serikali yetu ya Umoja wa Kitaifa inapaswa kutusikiliza na kuziheshimu sauti zetu Wazanzibari. Na siyo tu kutusikiliza, bali ifanye kazi kama mshirika wetu kwa kuzilinda haki zetu, hasa kupitia Tume ya Katiba. Serikali yetu ifanye kazi kwa kutambua kwamba sisi Wazanzibari tumeamua na tumesema kwamba tunaitaka Zanzibar yenye mamlaka yote kwa maslahi yetu na ya vizazi vyetu. Kufanya hivyo sio tu kwamba kutasaidia kuyarekebisha yaliokosewa na kuondoa dhulma iliyopo, bali pia kutatufaidisha sote.

Aidha Serikali yetu ya Umoja wa Kitaifa inapaswa iutambue msingi wa kila upande na watu wake kuwa na uwezo wa kujiamulia mambo yao wenyewe na kila taifa kuwa na uhuru ndani na nje ni sehemu ya shabaha za kidemokrasia na msingi huo unatiliwa mkazo katika maandiko yote ya haki za binaadamu.

Kwa muda mrefu sana sisi Wazanzibari tumekuwa wahanga wa hicho kinachoitwa ‘Muungano’.

Kwa muda mrefu hatukuwa na sauti katika usimamizi wa mambo yetu wenyewe na hatukuweza kuamua khatima yetu na ya vizazi vyetu.

Robert Nesta Marley (Bob Marley) aliwahi kuimba: “Unaweza kuwadangaya watu baadhi ya watu baadhi ya wakati, lakini huwezi kuwadangaya watu wote wakati wote. Sasa tunaiona nuru, tutasimamia haki zetu!”

Kwa hivyo, serikali yetu ya Umoja wa Kitaifa haiwezi tu kusema kuwa haina maoni yoyote kama serikali linapohusika suala la Muungano, na kwamba inasubiri yale ya Tume ya Katiba. Kuongoza ni kuonyesha njia. Nayo ikiwa taasisi ya uongozi wa nchi, lazima ionyeshe njia. Iwe na maono. Iwe na dira yake.

Aidha, Tume ya Katiba pamoja na Serikali ya Umoja wa Kitaifa lazima zitambue kwamba Katiba ina wajibu wa kuiakisi hali na matakwa ya wananchi. Ikiwa itapuuza ukweli au kuzuia harakati za watu wanaotoa matakwa yao juu ya Katiba yao. Ikifanya hivyo, itatengwa na wananchi na itajikuta inajitawala na kujiongoza yenyewe.

Hebu natujiulize: Nini maana ya kuwa na nchi isiyokuwa na heshima ya utaifa? Ni nini nchi pasipo uchumi? Ni nini nchi pasipo uwezo? Nini nchi pasipo utambulisho? Nini nchi pasipo mamlaka?

Kujitoa kwenye Muungano si suala muhimu kwa Zanzibar, lakini kinachopiganiwa ni kuirudisha mamlaka yake. Kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ndio ndoto ya Wazanzibari walio wengi, ikiwa sio wote.

Na Khaleed Gwiji

23

XXX • XXX

ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 2013

Ama iwe, ndani ya Muungano wa Serikali Mbili au wa Shirikisho

la Serikali Tatu uliopendekezwa katika rasimu ya Katiba, utaratibu wa kumpata Rais wa Muungano hauna budi kuwa juu ya msingi wa kupokezana zamu ili nchi mbili zilizoungana ziwe na usawa na heshima katika suala la uongozi wa juu wa nchi. Wapo baadhi ya viongozi kutoka Bara wanaoubeza utaratibu wa kupokezana zamu za urais wa Muungano kwa hoja kwamba utaratibu huo utapelekea kupata rais asiye makini na asiye na sifa kutoka upande wenye zamu kwa kumzuia mwenye sifa kutoka upande wa pili usio na zamu. Hoja hii si ya msingi na ni hoja ya uongo.

Ni hoja isiyo na msingi kwa sababu hakuna taifa kati ya mataifa haya mawili ya Tanganyika na Zanzibar lenye historia refu kutokea uhuru. Hakuna nchi hata moja kati ya mbili hizi yenye ukosefu wa wasomi na wanasiasa wenye sifa za uzoefu na maarifa ya kutosha kuwa viongozi wakuu wa nchi.

Labda watoaji wa hoja hiyo – ambao mara nyingi huwa aidha wanatokea Bara au wale wenye kuyakandamiza maslahi ya Zanzibar kwenye Muungano wanaotokea Zanzibar kwenyewe – wanakusudia kwamba inaweza ikafika zamu ya Zanzibar kutoa rais, lakini huko Zanzibar kusiwe na mgombea mwenye sifa na mwenye sifa akawa Tanganyika ambayo si zamu yake kutoa Rais. Msingi pekee wa hoja hii ni kutotaka Muungano wa haki na usawa. Wenye kutoa hoja hii ni wale wenye kuwazingatia Wazanzibari kuwa ni watu wasiojua kitu au wanaofaa kuwa wasaidizi tu wa viongozi wa Muungano. Isitoshe, hii ni hoja ya kujifichia tu, kwani utaratibu wa mwanzo wa Muungano uliosema makamu wa kwanza wa rais atakuwa Rais wa Zanzibar unafichua unafiki wa hoja hii.

Ilipofika kipindi cha awamu ya pili, Rais wa Muungano Mzee Ali Hassan alitokea Zanzibar na Rais wa Zanzibar ambaye pia alikuwa Mzanzibari Mzee Idris Abdulwakil, alikuwa Makamu wa Rais wa Muungano.

Msingi wa malalamiko ya upande wa Bara hapa ilikuwa eti Zanzibar ilitoa Rais wa Muungano pamoja na makamu

wake. Hilo liliendelea kuwakera waliokuwa wakitoa malalamiko hayo mpaka Katiba ya Tanzania ilipobadilishwa mwaka 1994 ili Zanzibar isiweze tena kutoa Rais na makamu wake. Badala yake kukawekwa utaratibu wa kuwa na mgombea mwenza ili awe makamu wa Rais. Ili kuwaziba midomo wana-CCM wa Zanzibar na kuwafanya waukubali utaratibu huo, upande wa Bara ulitumia kisingizio cha kwamba utaratibu huo uliwekwa kwa lengo la kumzuia Maalim Seif Sharif Hamad, mgombea urais wa Chama cha Wananchi (CUF), asiwe makamu wa Rais wa Muungano kama angelishinda urais wa Zanzibar.

Hoja iliyotumiwa ni kuwa lau Maalim Seif angelikuwa makamu wa Rais basi baraza la mawaziri lingelikuwa na mpinzani na hata Rais wa Muungano angeliweza kuwa mpinzani pale Rais atokaye chama cha CCM angekuwa na dharura ya kuondoka katika kiti chake.

Upande wa Bara ulipata kichaka hicho na “wauza nchi wa Zanzibar“ wakaridhia kubadilishwa kwa utaratibu wa Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa Rais wa Muungano.

Si Mbili wala Si Tatu, ni MkatabaNa Ahmed Omar

ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 201324

XXX • XXX

Hoja yetu hapa ni kwamba ikiwa Watanganyika hawapendi kuiona Zanzibar inatoa viongozi wawili wakuu wa Muungano kwa wakati mmoja au kwa mfululizo wa vipindi, inakuaje leo wao wenyewe walete hoja ya kutokuwepo ulazima wa kupokezana urais kwa kuchelea kumpata Rais asiye na sifa? Ukweli ni kwamba hata wana-CCM waliopo Zanzibar wanasisitiza kuwa urais wa Muungano uwe ni kwa utaratibu wa zamu baina ya Tanganyika na Zanzibar. Hivi ndivyo maoni yao yalivyokuwa na kwa hili wanaungwa mkono na Wazanzibari wenzao wanaotetea muundo wa Muungano wa Mkataba. Sasa tuje katika msingi hasa wa hoja hii. Pamoja na kwamba upo ulazima wa kupokezana urais wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, suala hilo linajidhihirisha kuwa ni gumu na lisilowezekana kwa kutumia muundo wa Muungano wa serikali mbili zilizopo au ule wa shirikisho la serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba. Kwa utaratibu wa chaguzi, katika kumchagua Rais wa Muungano, atayetoka upande mmoja wenye zamu, ni lazima upande wa pili usimsimamishe mgombea wa urais. Hivyo vyama vyote vitabidi vilazimishwe visiwe na mgombea wao

katika upande huo wa pili wa Muungano. Lakini haitokuwa rahisi kuvishawishi baadhi ya vyama vikubali visisimamishe mgombea wao wa urais katika upande huo wa pili. Na hata ikiwa vyama vyote vitakubali visiwe na mgombea wa urais katika upande mmoja wa Muungano bado kutakuwa na tatizo la uhalali wa Rais atayechaguliwa. Tatizo litazuka kwa sababu upande ambao hauna zamu ya kutoa Rais hautalazimika kuwapigia kura wagombea wa urais kutoka upande wenye zamu ya kutoa Rais. Wanaweza wakahoji kwamba kura hiyo haiwakhusu kwa msingi wa kwamba zamu ya urais ni ya upande mwengine na, hivyo, anapaswa kupata ridhaa ya upande huo wenye zamu tu. Hivyo, suala la upande usio na zamu kutokupiga kura ya kumchagua Rais ambae ndiye Mkuu wa Nchi yao, kunaondosha uhalali wa Rais huyo.

Hivyo basi, utaratibu wa kupokezana urais – pamoja na ukweli kwamba hauepukiki baina ya pande mbili za Muungano – hautekelezeki kwa kutumia Mfumo wa Serikali Mbili zilizopo wala wa Shirikisho la Serikali Tatu uliopendekezwa na Tume ya Jaji Warioba, kwa kuzingatia utaratibu wa kiuchaguzi na misingi ya demokrasia. Vyenginevyo, Rais

wa Serikali ya Shirikisho awe hapatikani kwa kura, bali ridhaa isiyo na msingi wowote ule unaotambulika kwenye hali ya sasa ya siasa za kilimwengu. Kwa maoni yangu, ili kuondosha matatizo na mazongezonge yote hayo, mfumo pekee unaotusibu ni wa kutokuwa na Serikali ya Muungano. Badala yake tuwe na chombo tu kinachoziunganisha nchi zetu mbili. Chombo hicho kinaweza kuwa, kwa mfano, Tume ya Muungano au Kamisheni ya Muungano. Huu ndio Muungano wa MKATABA. Katika muundo huo kila nchi inayohusika itabaki kuwa na Mamlaka yake na taasisi zake, ikiwemo ya urais, bila ya kuingiliana na mwenzake, huku masuala machache ya Muungano yakiratibiwa na chombo hicho cha pamoja. Hivyo basi, utaratibu wa kupokezana urais – pamoja na ukweli kwamba hauepukiki baina ya pande mbili za Muungano – hautekelezeki kwa kutumia Mfumo wa Serikali Mbili zilizopo wala wa Shirikisho la Serikali Tatu uliopendekezwa na Tume ya Jaji Warioba, kwa kuzingatia utaratibu wa kiuchaguzi na misingi ya demokrasia. Vyenginevyo, Rais wa Serikali ya Shirikisho awe hapatikani kwa kura, bali ridhaa isiyo na msingi wowote ule unaotambulika kwenye hali ya sasa ya siasa za kilimwengu.

25

XXX • XXX

ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 2013

MKEKA WA • MWANA WA MWANA

Zanzibar isimame wenyewe ndani ya Afrika ya Mashariki

TANBIHI: Makala hii imeandikwa kutokana na hotuba ya Mbunge RIZIKI OMAR JUMA (CUF Wanawake) aliyoitoa kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2010, ukiwa mwaka wake wa mwisho wa kuwa Msemaji wa Kambi ya Upinzani juu ya Masuala ya Muungano. Zanzibar Daima Online imeamua kuichapisha tena kwa sababu ya umuhimu wa yale yaliyozungumzwa ndani yake licha ya miaka mingi kupita. Hotuba hii na

Khofu ambayo inajengeka kwa mkabala huu wa Serikali ya Muungano kuelekea Zanzibar inaweza ku-waathiri washirika wengine wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao wanaweza nao kukhofia jaala za mamlaka yao kama wataingia kwenye ushirikiano wa ndani zaidi na nchi ambayo imezoea kujifanya ‘Kaka Mkubwa’ na kuwachukulia majirani zake kama watoto wadogo ambao hawawezi kujisimamia wenyewe

Na Riziki Omar

NI jukumu la kila upande kwenye Muungano wa Tanzania kuuangalia

upande mwingine wa pili kwa jicho la urafiki, udugu, huruma na upendo. Kwamba wetu ni Muungano wa washirika na wala sio Muungano wa wapinzani. Ni Muungano wa marafiki uliotokana na ridhaa zao wenyewe na wala si Muungano wa wababe wa kivita ambapo mmoja alimshinda mwenzake na kumuweka chini ya himaya yake kwa lengo la kumdhibiti asije akanyanyuka tena.

Sisi, Wazanzibari, tunatambua kwamba kwetu ni kuungana sio kutawaliana, kwa hivyo hatuna na wala hatutakiwi tuwe na ushindani na ukinzani wa kudhibitiana na kuwekana katika wakati mgumu.

Sote, Tanganyika na Zanzibar, tunapigania khatima ya pamoja, ambayo ni kuliona eneo hili la Afrika ya Mashariki likipiga hatua za kimaendeleo ya kiuchumi, ya kisiasa na ya kijamii ambayo yatakuwa kioo cha kuwavutia wengine wa Bara

letu la Afrika.

Ndio maana tungependa kuweka msimamo wetu juu ya nafasi ya Zanzibar iliyo kwenye Muungano ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mambo matatu ndiyo yanayoleta utata: kwanza, maeneo yaliyoorodheshwa kuwa ya mahusiano kwenye Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni 17, ambapo kati ya hayo ni manne tu ndiyo mambo

ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kwa yale yaliyobaki 13, Zanzibar ina mamlaka yake kamili juu ya mambo hayo kwa mujibu wa Makubaliano ya Muungano na hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Ibara ya 102.

Pili, uhusiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaingia katika kigawe cha mahusiano ya kimataifa, ambalo lenyewe si jambo la Muungano.

ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 201326

Na, tatu, hata itokezee kwamba Jumuiya hii inaingia katika kigawe cha Mambo ya Nje, ambalo ni jambo la Muungano, basi bado Serikali ya Muungano haina uhalali wa kuiwakilisha Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, angalau katika yale mambo ambayo si ya Muungano.

Khofu kubwa iliyojengeka Zanzibar ni kwamba, mwenendo wa kulazimishana unaonekana kuchukuliwa kwenye kasi ya kuelekea Shirikisho utaishia kwenye kuzusha mfumo wa Serikali Moja kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maana ikiwa tutaendelea hivi na kukichukua kila cha Zanzibar na kukiwakilisha chini ya mwamvuli wa Muungano, hatimaye hapatabakia na chochote cha Zanzibar. Jumuiya hii ya Afrika Mashariki inathibitisha hilo.

Ripoti ya Kituo cha Katiba cha Afrika Mashariki chenye makao makuu Kampala ilionya kwamba nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanapaswa kujifunza makosa makubwa yanayofanyika ndani ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiwa kweli wanataka Jumuiya hii idumu na iimarike.

Miongoni mwa makosa yaliyotajwa na ripoti hiyo ni ukweli kwamba hisia na mawazo ya upande mmoja wa Muungano hazipewi nafasi katika kuuendesha na kuutawala Muungano wenyewe.

Tabia hii ya kuyachukulia mambo kifichoficho au kwa kuyavungavunga ni mbaya sana kwenye ushirikiano wa pande zaidi ya moja. Unapokosekana uwazi wa kutosha katika mahusiano, shaka na dhana mbaya ndio huchukua nafasi badala ya nia njema na kuaminiana.

Kutokuipa nafasi Zanzibar kama Zanzibar ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ni tatizo jengine linalosubiri kuchipuka kwenye siasa za nje na mashirikiano ya kimataifa za Tanzania.

Kwa upande mmoja, Wazanzibari wanataka kuiona nafasi yao wenyewe ndani ya Jumuiya ili waweze kusimamia vyema maslahi yao kwa yale mambo yasiyo ya Muungano.

Kwa upande mwingine, siasa za Muungano kuelekea Zanzibar zinazosimamiwa na Serikali ya Muungano haziruhusu kuiona Zanzibar inajenga mashirikiano yake yenyewe nje ya mipaka ya Tanzania hata kwa yale mambo yasiyo ya Muungano huku ikieleweka kwamba hata unapoangalia Katiba ya Jamhuri ya Muungano, ushirikiano wa kimataifa si jambo la Muungano.

Khofu ambayo inajengeka kwa mkabala huu wa Serikali ya Muungano kuelekea Zanzibar inaweza kuwaathiri washirika wengine wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao wanaweza nao kukhofia jaala za mamlaka yao kama wataingia kwenye ushirikiano wa ndani zaidi

na nchi ambayo imezoea kujifanya ‘Kaka Mkubwa’ na kuwachukulia majirani zake kama watoto wadogo ambao hawawezi kujisimamia wenyewe.

Inaweza kufahamika kwamba kuna khofu pia kwa upande wa Serikali ya Muungano, ambao unaona hatua yoyote ile ya Zanzibar kutumia haki yake ya kuingia kwenye mashirikiano ya kimataifa kutaathiri mamlaka ya Serikali yenyewe ya Muungano; na hivyo kuhatarisha au kuuvunja kabisa Muungano wenyewe.

Ndiyo hoja iliyotumiwa wakati ule Zanzibar ilipolazimishwa kujitoa kwenye Jumuiya ya Nchi za Kiislam (OIC), hoja ambayo imeshafafanuliwa na wasomi, wanasiasa na wataalamu kadha kwamba ilikuwa potofu.

Kuwepo kwa khofu hii isiyo na msingi kwa upande wa Serikali ya Muungano kunaathiri sana mfumo wa Muungano, maana ule msingi wa ukweli na ridhaa ya khiyari wa Muungano unakosekana.

Msingi huo ni mapenzi na kuaminiana. Tunapofika pahala sisi wenyewe tukiwa kwenye Muungano hatuaminiani na badala yake tunategana mitego na kuviziana, tujuwe kwamba tumefika katika kilele cha udhaifu wa Muungano huo. Na ndoto ya Jumuiya pana ya Afrika ya Mashariki tumeiua wenyewe.

27ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 2013

Nawauza muvaao, hijabu za Ramadhani Mashungi muyashushao, shoti hamuonekani Wachaji wa leo leo, mabanati wa peponi Ya nani mavazi hayo, hebu nami nijuvyani!

Binti niwauzao, wajijua kwa yakini Vikumbo tupiganao, mwaka mzima njiani Ya wazi maungo yao, kwa vitopu na vimini Na mapicha watumao, wa wazi humu netini!

Mwaka mzima ambao, watembea mitaani ‘Mewakaba zao nguo, zimeganda miilini Viereje hivi leo, mwazamia hijabuni Ya nani hijabu hiyo, kwa siku za Ramadhani?

Kama mwezi ndio huo, zake siku thalathini Punde twawa hatunao, wendavye hatuuoni Ni vipi heshima yao, ni hadi tena mwakani?

Na ikiwa kama siyo, hijabu mwajitandani?

Naona yayo kwa yayo, mufanyayo ni utani Ikiwa munamo nyoyo, sitara hamuamini Ikija saumu mbiyo, ndipo mwenda kabatini Mwakumbuka shungi leo, ndio yambwe ni imani?

Hiyo siyo thamma siyo, dada zangu si imani Na wala hishima siyo, kwa mwezi wa Ramadhani Hilo lenu ni jojeyo, mwamjojea Manani Lau imani munayo, kila siku ivaeni!

Mohammed Kh. Ghassani BonnUjerumani

MWAMVALIA NANI

Mungu nakushitakia, mja wako madhulumu Sina pa kuelekea, ila kwako ya karimu Nguvu zishaniishia, taabani mahmumu Yarabi nisaidia, l’ondoke hili dhalimu

Yarabi nisaidia, londoke hili dhalimu Lipotee baidia, linisahau dawamu Likitaka nirudia, ulipofuwe uyunu Likome kunidamia, na kunyonya yangu damu

Likome kunidamia, na kunyonya yangu damu Mjao nateketea, kwa dude hili dhalimu

Hadhi yangu ‘shapotea, siyo tena ya kadimu Rabi lipoteze njia, lileweshe kwa naumu

Rabi lipoteze njia, ulilevye kwa naumu Macho siweze fumbua, lishindwe kunihujumu Nipate jitutumua, kujenga yangu kaumu Na mbele kuendelea, bila ya lolo dhalimu

Hamad Hamad CopenhagenDenmark

RABBI LILISE DHALIMU

LADHA YA BETI

ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 201328

JAMII

TANBIHI: Ukiwa unakaribia mwaka mzima tangu serikali kuwakamata viongozi ya Jumuiya ya Uamsho na Mi-hadhara ya Kiislamu (JUMIKI), maarufu kama Uamsho, familia za viongozi hao zimeupitisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa mara ya kwanza wakati “vichwa vya familia” hizo vikiwa vinataabika kwenye gereza la Kiinua Miguu, mjini Zanzibar.

Waume zetu wamewachukua, familia hazina mwongozo

Zanzibar Daima Online (ZDOnline) ilizitembelea baadhi ya familia hizo, na kuzungumza na wake na wazazi wa viongozi hao kujua hali zao. Kwa sababu zao wenyewe, wake wa viongozi hao hawakutaka watajwe majina yao, na ZDOnline inaheshimu matakwa yao. Kwa jumla, familia zote zilizungumzia kitu kimoja kuhusu hali za maisha ndani ya nyumba zao, hisia za watoto kuwa mbali na baba zao, changamoto wanazokabiliana nazo wakati waume wakiwa ndani, na hata matarajio na khofu zao kwa hatima ya baadaye. Kwa msingi huo, ZDOnline inachapisha moja ya mahojiano hayo, ambapo mke wa Sheikh Abdullah Said Ali (Katibu Mkuu wa JUMIKI) ndiye mzungumzaji mkuu.

ZDOnline: Mama, je hali yako binafsi na maisha kwa jumla yanakwendaje hapa nyumbani?

Mke wa Sheikh Abdullah: Alhamdulillah, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kuhusu maisha na hasa kwa mwezi Mtukufu huu wa Ramadhani Mwenyezi Mungu kaleta neema yake. Ametuonesha ukubwa Wake. Pamoja na kuwa waume zetu hawapo, lakini hatuna shida ya chakula, nguo za watoto na matatizo mengine madogo madogo.

29ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 2013

ZDOnline: Mama, je hali yako binafsi na maisha kwa jumla yanakwendaje hapa nyumbani?

Mke wa Sheikh Abdullah: Alhamdulillah, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kuhusu maisha na hasa kwa mwezi Mtukufu huu wa Ramadhani Mwenyezi Mungu kaleta neema yake. Ametuonesha ukubwa Wake. Pamoja na kuwa waume zetu hawapo, lakini hatuna shida ya chakula, nguo za watoto na matatizo mengine madogo madogo. Ama kwa kweli, Waislamu wenzetu, ndugu, marafiki, wanajitolea kutuletea misaada ya chakula na nguo kama vile mwenzetu alipokuwepo au hata zaidi ya vile alipokuwepo mwenzetu [mume wake, Sheikh Abdullah, Katibu Mkuu wa Uamsho].

ZDOnline: Hilo ni jambo la kushukuru sana, bila ya shaka. Lakini je, kuna changamoto zozote ambazo mmekabiliana nazo, hasa ndani ya mwezi huu wa Ramadhani, kwa kutokuwepo kwa mume wako nyumbani?

Mke wa Sheikh Abdullah: Changamoto kubwa inayotukabili ni huko kutokuwapo kwake. Kwa sababu mume ni mhimili mkuu katika nyumba, ndiye anayeongoza kila jambo. Bila ya mume, mambo mengi yanakuwa hayafanyi kazi kwa sababu yeye ndio kiongozi kama ilivyosema Qur’an: “Ar-Rijaalu Qawwamuuna ‘alaan Nisaai”

Sasa waume hawapo. Kwa hivyo, kuna masuala chungu nzima

ambayo hatuwezi kuyakabili peke yetu.

Sisi wake za Maamiri hatujui kitu chochote. Kila kitu tumezoea kufanyiwa. Tuna jukumu, hasa la ulezi. Hili linatupa shida, tukiwa bila waume zetu. Tukiangalia mazingira ya sasa ni magumu katika nyumba, hasa kwa watoto ambao wanasoma na wanahitaji kushughulikiwa.

ZDOnline: Je, mmewasiliana na Sheikh Abdullah katika siku za karibuni?

Mke wa Sheikh Abdulla: Tumeweza kwenda kumuona gerezani. Tumepangiwa kila wiki mara moja, lakini inatupa usumbufu kwani kila mtu ana familia yake: ana ndugu, baba, mama yake, lakini hawaruhusiwi kuwaona. Na sasa tuna mtihani mkubwa zaidi, tumeekewa aende mke tu na aende na kitambulisho au paspoti.

Hili nalo lina mtihani kuwa ende mke tu. Watoto wanamtamani baba yao, ana wazee, ana jamaa zake. Wengine basi hata kumuona wasiende? Hii inatukosesha faraja.

ZDOnline: Kwani kwa mnavyojua nyinyi kama familia, kesi ya Sheikh Abdullah na wenzake inaendeleaje?

Mke wa Sheikh Abdullah: Kesi haikufikia pahala pazuri, kwani

sheria inataka kesi ifanyike kwa miezi minne. Kesi iendeshwe, kama mtu ana kosa ahukumiwe, hana aachiwe. Lakini mpaka sasa hatujui vipi wanakwenda mahkamani. Tunahisi kama wanakwenda ‘Day Out’ (matembezi). Wanakwenda kutembea na kurudishwa ndani. Tumeambiwa wao wamekata rufaa, iko Bara. Tumekwenda siku ya kwanza,

siku ya pili tuliambiwa tutaitwa baada ya wiki mbili. Mpaka leo hatujaona jambo lolote. Hatujui chochote kinachoendelea

ZDOnline: Kama kwa mfano unapata nafasi ya kuzungumza moja kwa moja na taasisi zinazohusika na haki za mume wako, kama mwanaadamu na kama raia, kama vile makundi ya haki za binadamu, mahakama, serikali na wengine, ungewaambiaje? Mke wa Sheikh Abdullah: Watu wa haki za binadamu wanajua kila kitu lakini hakuna hata mtu mmoja aliyechukua hatua yoyote. Mahkama tunataka itende haki. Kama kuna kosa wahukumiwe. Kama hawana kosa, watolewe. Serikali naiambia: mtu asijione kama yuko kwenye uluwa, huu ni mtihani wamepewa mashekhe, tumepewa mtihani sisi wake, kuona je tutaweza kuwasubiria waume zetu? Lakini na wao viongozi waliowatia mashekhe ndani pia wana mtihani mkubwa. Tena ni mtihani mtihani! Waume zetu hawana kosa. Haya ni madai ya Wazanzibari wote wanayoyadai. Sisi tunafanya makongamano, wakati si sheria sauti zetu kusikika hadharani, lakini hatuna budi. Tunayafanya hayo kwa kutetea waume zetu.

ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 201330

TUFUNGUE • KITABU

TUFUNGUE KITABU

TANBIHI: Katika safu hii tutakuwa tunawaletea uhakiki na uchambuzi wa vitabu na maandishi mbalimbali yaliyoandikwa na Wazanzibari na au kuhusu Zanzibar, utamaduni, watu, siasa, imani na mustakabali wake. Tunafungua ukurasa huu kwa uhakiki wa kitabu cha Jumba Maro kilichoandikwa na Ally Saleh na kuchapishwa mwaka 2005 na kampuni ya Readit Books Ltd, kikiwa na nambari ISBN 9987 21 0716. Uchambuzi huu unafanywa na MOHAMMED GHASSANI.

NITANGULIE kusema kuwa mimi ni miongoni mwa wale wanaoamini kuwa dhima kubwa ya mhakiki/

mchambuzi wa kazi ya fasihi ni kuisafirisha kazi hiyo kutoka kwenye kipande chake cha karatasi (au nukuu zake za simulizi) na kuipeleka “watuni”, maana fasihi wenyewe ni watu – ndio inaowalenga, ikawatathmini, ikawaburudisha, ikawafunza, ikawatanabahisha. Ndio

inaowasiliana nao. Mchambuzi/mhakiki, kwa hivyo, ana jukumu la kuwasaidia watu wajione wenyewe kupitia mistari au semi za kazi hiyo ya fasihi.

Basi kama vile ambavyo kazi ya fasihi huweza kusomeka (au kusikika), basi ndivyo pia inavyoweza kupokeleka, kutafsirika na kuchambulika kwa mawanda yoyote ambayo mchambuzi/mhakiki anaweza kujichawanya.

Sababu ni kuwa katika fasihi neno huwa zaidi ya maneno, na kisa huwa zaidi ya mkasa. Yanayosemwa katika fasihi hayabakii kuwa kama yalivyo tu, bali, ili yakifu lengo la kusemwa kwake, lazima yapimwe,

yachambuliwe na yahakikiwe. Ndiyo maana husemwa kuwa kwa kila kipande kimoja cha kazi ya fasihi huweza kuzalishwa maelfu ya kurasa.

Ukweli wa nadharia hii, hata hivyo, haulazimishi kwamba pawe na uwiano wa kimawazo baina ya mbunifu wa kazi ya fasihi na mhakiki/mchambuzi. Kwa hivyo, nitakayoyaona mimi katika Jumba Maro huenda yasiwe kabisa yale aliyoyaona Ally Saleh wakati wa kuiandika kazi yake. Naamini kuwa atanistahmilia kwa mawazo yangu kuhusu mawazo yake. Na kwa ufahamu wa hilo hilo, basi uhakiki na uchambuzi huu usihusishwe naye, bali mimi mwenyewe.

Tuje kwenye kazi yenyewe. Imeitwa Jumba Maro, mkusanyiko wa hadithi fupi fupi kumi na mbili na mashairi yenye idadi hiyo hiyo. Katika Yaliyomo, hadithi hizi zimeorodheshwa kwa mfuatano huu: Bi Sakina, Msafiri, Kutaradadi, Utamu wa Wazimu, Kisa Mkasa, Bwana Uwezo, Nyuma ya Pazia, Jumba Maro, Kigego, Vimbizi, Karamu na Gizani.

Mashairi pia yametangulizwa kwa kila hadithi kwa mfuatano huu: Himaya Zao, Hakika ya Safari, Hangaiko, Huna Moyo Huo, Uso kwa Uso, Hakika ya Mambo, Usiulize Sababu, Mlevi Tapoleuka, Mdomo Mzito, Kesho ni ya Madhulumu, Mjumbe Kaemewa, Giza Nuruni, Nuru Gizani? (Jumba Maro, iii)

31ZANZIBAR DAIMA ONLINE • 9–22 Agosti 2013

Kwa hivyo ni sawa kusema kuwa Ally Saleh hakuwasilisha mbele yetu kitabu cha hadithi fupi fupi tu, bali pia diwani ya ushairi. Kifani, utangulizaji huu wa ushairi kabla ya hadithi umeipamba kazi yenyewe na kuipa upekee katika historia ya uandishi wa Fasihi ya Kiswahili (nakusudia fasihi inayotumia lugha ya Kiswahili kuzungumzia maisha ya Mswahili).

Kwa hakika, hata katika waandishi wa fasihi za lugha nyengine, si wengi sana waliowahi kujitokeza na mbinu hii. Kwa wingi, nakumbuka maandishi ya Ngugi wa Thiong’o ambayo huanza na aya za Biblia (angalia The River Between). Katika Kiswahili, kumbukumbu zangu zinanionyesha kuwa Ally Saleh amekuwa mwandishi wa mwanzo kutumia mbinu hii. Nakubali kusahihishwa ikiwa kumbukumbu zangu haziko sawa.

Lakini utangulizaji huu wa ushairi haubakii kuwa urembo wa kufurahisha macho ya msomaji wa kazi hii tu, bali unakwenda mbali zaidi na kuwa kisaidizi chake cha kuifahamu hadithi inayofuatia. Vipande vya ushairi vilivyotangulizwa kabla ya kila hadithi vinasimama kama ufupisho wa hadithi yenyewe na katika baadhi ya mifano vinakuwa kama changamoto kwa msomaji linalomsisimua aagulie majibu ambayo huenda akayakuta katika hadithi yenyewe.

Katika ukurasa wa 39, kwa mfano, kuna ushairi Uso kwa Uso ambao unaitangulia

hadithi Kisa Mkasa. Kipande cha mwisho cha ushairi huu kinasisimua hivi:

Na siku ayami kupita, mmoja akikataa kusamehe Mwengine akidhani ndio yamekwisha kabisa Loh, kumbe inawezekana kukutana Ama kweli vilima kwa vilima… Nani angedhani uso kwa uso ingekuwa? Ukiisoma hadithi yenyewe ya Kisa Mkasa, utakuta kuwa ni simulizi ya kulipiziana baina ya watendwa na mtenda: visasi vya unyumba ambavyo vinaishia kwa kuvunja heshima na stara ya ndoa ya Zahrani.

Ndivyo pia unavyobashiri ushairi wenyewe, kwamba maisha ni mzunguko, na wanadamu ni ‘waja-kwenenda’, kuna siku moja wale waliotendana na kukimbiana, watakuja kuonana na kutazamana Uso kwa Uso, lakini uso mmoja ukiangalia kwa haya na kujishuku: “Loh, kumbe angali hai!” na mwengine kwa suto na udadisi: “Kwani we’ siye mbaya wangu!”

Kwa wenye uweledi wa sanaa ya ushairi watakubaliana nami kuwa katika baadhi ya sehemu, Ally Saleh amevipa vipande hivi vya ushairi kiwango cha juu zaidi cha tafkira kuliko hadithi zenyewe. Angalia kwa mfano hadithi Msafiri (uk. 10) inayotanguliwa na ushairi Hakika ya Safari unaosomeka hivi:

Safari hakika ni safari

Moyo wako kuujuburi

Siri uiweke kuwa siri

Kushindwa katu usikukiri.

Ujihimu kila mara

Uongozwe na yako ghera

Lisiwepo la kukukera

Hadi kutimu dhamira.

Hatua yako ya kwanza

Mwisho ni kuimaliza

Nchi yako Maliwaza

Hilo hakika timiza. (uk. 9)

Dhati ya shairi hili inamtia moyo msafiri aiandame njia hadi awasili katika nchi yake ya Maliwaza. Lakini katika hadithi yenyewe, Bwan’ Said (huyo msafiri mwenyewe) anashindwa kuinua mguu hapa na hapo, maana ndoto alizooteshwa na mwandishi zinambainishia kuwa, akutakako kwenda hakwendeki.

Itaendelea....…

ZANZIBAR DAIMA • AGOSTI 201332

Na Baraka Mwinyi

KUNA wakati ambapo siasa huwa ni sawa

na mchezo wa karata ambapo kazi ya kubadili mbinu kwa mujibu wa turufu ulizonazo huwa ni sehemu ya mchezo wenyewe. Katika hilo kuna pia kutegea kwa kusubiri wakati mwafaka kuicheza turufu ili ufanikiwe.

Baadhi ya wakati wanasiasa huonekana kuwa watu wasio na msimamo, woga na hata wasaliti. Wapo wanasiasa wenye sifa hizo. Lakini si wote kwani kuna baadhi ya wanasiasa ambao hatimaye historia inapowahukumu, wale waliokuwa na dhana hiyo hujiona imewasuta.

Mbinu ni muhimu kwenye siasa kama ilivyo kwenye mchezo wa karata. Wako wanasiasa walioteleza katika suala hilo la mbinu na mikakati kwa sababu mbalimbali zikiwemo jazba na kutouangalia wakati ikiwa ni mwafaka au la.

Kweli kuna wanasiasa waliokuwa mashujaa kukabiliana na maovu moja kwa moja na kujitoa mhanga kuzuia kasi za maovu hayo na athari zake. Yaani hawakuona njia mbadala isipokuwa

kusabilia maisha y a o ,

ndipo wakasema: “liwalo naliwe”.

Visiwani Zanzibar kuna nyakati inayojulikana kama “Zama za Siasa”. Zama hizo zilikuwa na mihula yake tafauti ya matukio na matokeo. Tukio kubwa lilikuwa kupigania uhuru wa visiwa hivyo. Miongoni mwa waliotoa mchango mkubwa ni Hassan Nassor Moyo, kada wa chama cha Afro Shirazi (ASP) na mwasisi wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (ASPYL).

Moyo alikuwa miongoni mwa watu wa karibu sana wa Rais wa ASP na Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Watu

wa Zanzibar, Sheikh Abeid

Amani Karume. Alikuwa pia kiongozi wa chama kimoja cha wafanyakazi Zanzibar and Pemba Federation of Labour (ZPFL) kabla ya kuteuliwa mjumbe wa Majlis Tashriii yaani Baraza la Kutunga Sheria (LEGCO) wakati wa ukoloni.

Baada ya Mapinduzi Januari 12, 1964 alikuwa miongoni mwa wa mwanzo walioteuliwa wawe memba wa Baraza la Mapinduzi na aliteuliwa pia awe Waziri wa Kazi. Ulipoundwa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar akateuliwa kuwa waziri wa kwanza wa katiba na sheria wa Jamhuri ya Muungano.

Yataka moyo kuwa MoyoMAKALA YA WAANDISHI

33

Baadaye Moyo alirudi nyumbani Zanzibar ambako alishika nyadhifa kadhaa za uwaziri .

Kwa ufupi, huyu ni mtu anayeijua Zanzibar na Tanzania na kubwa zaidi anaujua Muungano nje ndani. Mzee wetu huyu baada ya

mchango wake wakati wa “Zama za Siasa,” sasa amejitokeza tena mstari wa mbele katika enzi hii ya mabadiliko. Katika wakati huu ndipo unapoweza khasa kumpima mwanasiasa mwadilifu na anayejiamini. Na hivyo ndivyo Mzee Moyo alivyo. Aliamua tangu alfajiri kuutumikia umma. Anatumia haki yake ya raia Wakizanzibari kuuhoji Muungano, akiamini mabadiliko yanayohitajika ni yale ya kwenda na wakati, tena kwa lengo la kufungua njia ya kuwa na Muungano imara kwa ridhaa ya pande zote – Muungano utakaofungua njia kwa wengine kuusogelea na

kujiunga nao.

Hata hivyo, la kusikitisha ni kuwa kuna wale wanaojiita wanasiasa katika chama chake mwenyewe cha CCM wanaoubeza na kuukejeli msimamo wake. La kusisimua zaidi ni kwamba Wazanzibari wengi wanamuenzi Mzee Moyo na hawamfanyii kejeli hizo.

Wapo waliojaribu kumtisha na kumtaka yeye na wenzake katika CCM wenye mawazo kama yake warudishe kadi zao za CCM ikiwa wanapingana na msimamo wa chama chao hasa

katika suala la serikali mbili. Mzee Moyo aliwapa changamoto, kwa kuwaambia kwamba anabakia mtiifu kwa CCM lakini katika kuitetea haki ya Zanzibar yuko tayari kurejesha kadi akitakiwa afanye hivyo.

Kwa bahati mbaya, mmoja wa waliojaribu kumtisha Moyo ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM/ Zanzibar, Vuai Ali Vuai. Moyo alimkumbusha Vuai na wenzake kuwa vyama ni vya mpito lakini taifa linabakia milele.

Ole wao wasiojua kusoma nyakati, kwani ingekuwa hivyo basi wanapoiangalia Tanzania wangejiuliza viko wapi vyama vya ASP na TANU, nchini Kenya iko wapi KANU, huko Malawi, Malawi Congress na Zambia i wapi UNIP ya Dr Kenneth Kaunda? Iko wapi iliyokuwa Urusi ya zamani (Muungano wa Jamhuri za Kisovieti) au Yugoslavia ya Marshall Joseph Broz Tito?

Wao pia naamini wakisema, hapa hayawi. Lakini kama wasemavyo wahenga, asiyejua maana haambiwi maana, na akina Vuai bado wamo ndotoni. Mzee Moyo ni mmoja wa wanasiasa adimu sana wenye ujasiri wa kuungama wanapokosea. Kuna kile kisa cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Afrika, Dk. Salim Ahmed Salim, alipogombea mara ya mwanzo

urais wa Tanzania. Wakati huo Mzee Moyo alishirikiana na waliokuwa wakifanya kampeni ya kumpinga na kumwagia sumu. Hatimaye, walifanikiwa kumzuia Dk. Salim asiwe mgombea.

Lakini baadaye, alipotanabahi kuwa alikosea Mzee Moyo alikuwa na moyo na ujasiri wa kumkabili Dk. Salim na kumuomba radhi akisimama kidete kumuunga mkono 2005. Hizo ndizo sifa za uongozi. Sasa Moyo amejitokeza tena bayana bila kificho kutetea masilahi ya Zanzibar katika mfumo wa Muungano. Tafauti ya wakati huo na sasa ni kwamba umma uko nyuma yake, ukiwa na heshima kubwa kuwa na mtu kama huyu. Hakuna shaka yoyote Mzee Moyo ana nafasi yake katika historia ya visiwa vya Zanzibar, kama alivyo Dk. Amani Karume. Kiongozi mwenye busara ni yule anayeungama kuwa amekosea na kujirekebisha kwa manufaa ya wale waliompa imani ya kuwaongoza.

Mzee Moyo ni mmoja kati ya watu wa aina hiyo. Kipaumbele kwake ni uzalendo na mustakbali mwema kwa nchi yake. Ndiyo maana tunawaambia wale wenye kuweka mbele masilahi yao badala ya taifa, watambue kwamba kinachowashinda wao ni kutokuwa na moyo alionao Mzee Moyo, maana inataka moyo wa dhati mtu kuwa Moyo.

Jarida hili hutolewa na Zanzibar Daima Collective, 233 Convent Way - Southall - Middlesex, UB2 5UH, UK.

Nonnstr. 25, 53119 Bonn,Germany