zanzibar daima online, toleo la tano

24
“Kuna watu wana chuki tu na sisi. Kwa sababu ya chuki zao dhidi yetu, wanasema watakavyo juu yetu. Wanatuhusisha na uhalifu unaofanywa wakati sisi tuko gerezani. Inawezekana wanaofanya wanajulikana lakini wanalindwa kwa sababu wa- nazozijua hao wanaowatuma. Ni chuki yao tu hawana ushahidi hata chembe wa kuhusika kwetu.” ‘‘Hatujabadili kauli’’ JARIDA LA KILA MZANZIBARI www.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013 ZANZIBAR DAIMA ONLINE

Upload: hassan-mussa-khamis

Post on 26-Oct-2015

3.403 views

Category:

Documents


0 download

DESCRIPTION

Zanzibar Daima Online, Jarida la kila Mzanzibari litolewalo wiki mara mbili. Jarida la Mtandaoni lenye kusomwa na zaidi ya nchi 27 Ulimwenguni hadi sasa.

TRANSCRIPT

Page 1: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

“Kuna watu wana chuki tu na sisi. Kwa sababu ya chuki zao dhidi yetu, wanasema watakavyo juu yetu. Wanatuhusisha na uhalifu unaofanywa wakati sisi tuko gerezani. Inawezekana wanaofanya wanajulikana lakini wanalindwa kwa sababu wa-nazozijua hao wanaowatuma. Ni chuki yao tu hawana ushahidi hata chembe wa kuhusika kwetu.”

‘‘Hatujabadili kauli’’

JARIDA LA KILA MZANZIBARI www.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

Page 2: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

PAGE

2

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

3

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

2

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

Yaliyomo Graphics

Designer

(Hassan)www.zanzibarimage.com

HKDesigner

MHARIRI MKUUAhmed Rajab

Email: [email protected]

MHARIRI MSAIDIZIMohammed Ghassani

Email: [email protected]

MHARIRI MSANIFUHassan M Khamis

Email: [email protected]

COMMUNICATION MANAGERHassan M Khamis

WAANDISHIJabir Idrissa

Email: [email protected]

Othman MirajiEmail: [email protected]

Hamza RijalEmail: [email protected]

Salim Said SalimEmail: [email protected]

Ally SalehEmail: [email protected]

WASAMBAZAJImzalendo.net

zanzibardaima.netzanzibardaima/facebook

MATANGAZOHassan M Khamis

Simu: +44 7588550153Email: [email protected]

WASIALIANA [email protected]

JARIDA HILI HUCHAPISHWA NAZanzibar Daima Collective

233 Convent WaySouthallUB2 5UH

Nonnstr. 2553119 Bonn

Germany

www.zanzibardaima.net

Zanzibar Daima Online

Timu Yetu

Zanzibar Daima Online Toleo 05 03

18 14 20

1810

NGURUMO LA MKAMA NDUME NIONAVYO

WARAKA KUTOKA BONN BARZA YA JUMBA MARO MKEKA WA MWANA WA ...

Kurasa Makala na taarifa za Uchambuzi wa kina!

14

28

36

12KALAMU YA BIN RAJAB

MICHEZO

HABARI

KAULI YA MWINYI MKUU

Page 3: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

PAGE

4

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

5

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

4

Moja ya mijadala ya tangu dahari ya falsa-fa ya kisiasa ni iwapo

tunaweza kuvitenganisha vitu hivi vitatu: dini, maadili na siasa. Dhana ya kwamba dini haina budi kuungan-ishwa na siasa imekubalika kwa muda mrefu katika nchi zenye mifumo iliokomaa ya demokrasia.

Wazo la kuitenganisha dini na siasa ni wazo jipya na linashadidiwa sana barani Afrika ambako kuna mivu-tano kati ya usasa na ukale.

Kuna njia tatu zinazoweza kuifanya dini iwe na tash-wishi katika siasa. Njia ya kwanza ni ile ya viongozi wa dini kujihusisha moja kwa moja katika siasa. Njia ya pili ni ya kuichanganya dini na siasa kuzifanya ziwe moja, kitu kimoja.

Ya tatu ni kuzifanya siasa au Serikali ziwe chini ya Shari’a au itikadi za kidini, yaani utawala uwe unatii maam-risho ya kidini. Njia hii hu-wataka viongozi wa Serikali wawe wanafuata maamrisho ya kidini. Wawe na uadilifu wa kidini.

Uadilifu aina hiyo unahitajika hasa katika nchi kama zetu ambapo viongozi aghalabu

huwa majambazi, wezi, maf-isadi na wasio na maadili.

Hapa ningependa kuizung-umza ile njia ya kwanza ya kuifanya dini iwe na tash-wishi katika siasa, yaani ile ya viongozi wa kidini kupiga mbizi katika siasa. Hivyo ndivyo walivyokuwa waki-fanya viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam (JUMIKI), kwa ufupi Uamsho.

Viongozi hao wa Uamsho wamekuwa wakijihusisha moja kwa moja katika siasa wakiwa wanayatetea masla-hi ya nchi yao. Matokeo yake ni kwamba harakati zao zimeifanya Serikali iwatie nguvuni Oktoba 16 mwaka jana na iwatumbukize koro-koroni ambako wameselelea hadi sasa. Kesi yao ilikuwa ikitazamiwa isikilizwe Okto-ba 7 katika Mahakama Kuu, Vuga.

Kwa bahati mbaya walip-owasilishwa Mahakamani hawakuwahi hata kufiki-shwa kwenye chumba cha kusikiliziwa kesi kwa sababu Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu, hayuko nchini.

Swali ni kuwa je, ilipopangwa tarehe hii ya leo ilikuwa

haijulikani kwamba Jaji Mkuu atakuwa nje ya nchi?

Kwa mara nyingine masheikh hao wamenyimwa haki ya kesi yao kusikilizwa ili iju-likane kama kweli wana hatia au la. Na kama hawana waachiwe halan; la sivyo haki zao za kibinadamu zitazidi kukiukwa.

Katika toleo hili tuna makala maalum kuwahusu viongozi hao wa Uamsho tulioy-aandika baada ya Zanzibar Daima Online kuzungumza na mmojawao, Sheikh Azzan Khalid Hamdan, aliyeachiwa kwa dhamana ili ende India kutibiwa.

Mashtaka yanayowakabili viongozi hao wa kidini ni mashtaka makubwa. We-nyewe wanaamini kwamba mashtaka yenyewe ni kisin-gizio tu. Wanasema kwamba kosa kubwa walilolifanya mbele ya wakubwa wa Seri-kali ni kupigania Zanzibar irejee kuwa dola kamili.

Pamoja na utetezi huo ju-muiya yao imekuwa ikiende-sha miradi kadhaa ya kijamii, kama kwa mfano ule wa kuwaangalia na kuwatunza mayatima wapatao 1,000 na mwingine wa kuwasaidia watoto wapate masomo

Kesi ya Uamsho itaakhirishwa hadi lini?Na Ahmed Rajab

ndani na nje ya Zanzibar.

Kwa kuwekwa ndani miradi hiyo hivi sasa inazorota na watoto zaidi ya elfu moja wanany-imwa huduma za Uamsho.

Zanzibar Daima Online inawasihi wakubwa wanaohusika wafanye uungwana kesi ya masheikh hawa isikilizwe kwa haraka. Wasipofanya hivyo wataonekana kwamba wanafanya njama za kuwaonea kwa sababu za kisiasa

Sheikh Mussa [mwenye kanzu na kofia] ni miongoni mwa viongozi wa Uamsho wanaoshikiliwa takri-ban mwaka mmoja sasa.

Tahariri

Page 4: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

PAGE

6

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

7

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

6

KIONGOZI MWANDAMIZI WA UAMSHO, SHEIKH AZZAN KHALID HAMDAN

HABARI KUU

UAMSHO:Hatujabadili kauliMiezi 12 baada ya kukamatwa na ku-

funguliwa kesi inayohusu mashta-ka ya uchochezi na kushawishi

fujo, masheikh na viongozi wa Uamsho hawajabadilika.

Viongozi hao walio chini ya mwamvuli wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Ki-islam (JUMIKI) wanaendelea na msimamo wao wa kutaka kuona Zanzibar inarejesha mamlaka yake kamili ya kujiendesha kama dola huru.

“Msimamo wangu mimi na wenzangu ni uleule. Ingawa tuna mwaka mmoja sasa tuko gerezani, tungali na msimamo wetu uleule wa kupigania Zanzibar. Hii ni nchi yetu na tuna haki ya kuitetea kikamilifu,“ anasema Sheikh Azzan Khalid Hamdan, mmoja wa masheikh hao.

Sheikh Azzan ambaye ni Naibu Amir wa Uamsho, ametoa kauli hiyo katika maho-jiano maalum na Zanzibar Daima Online, yaliyofanyika nyumbani kwake Mfenesini, nje kidogo ya mji wa Zanzibar, siku moja kabla ya kiongozi huyo kuondoka nchini kuelekea India kwa matibabu.

Anasema hakuna sababu ya kuoneka-na wao eti wameondoka kwenye malen-go ya kuanzishwa kwa jumuiya hiyo kwa

kuwa hata taasisi ya dini kama hiyo yao, inao wajibu wa kushughulikia maslahi ya wananchi.

“Si sawa jumuiya yetu kuchukuliwa kuwa imekiuka sheria za kuanzishwa kwake. Jumuiya inapaswa kuwa karibu na kujihu-sisha hasa na mas’ala yanayohusu haki ya wananchi,“ alisema Sheikh Azzan akiwa anajibu hoja

inayotolewa mara kwa mara ndani ya Se-rikali na katika mazungumzo ya watu wa kawaida kwamba jumuiya ya Uamsho imevunja sheria kwa kujihusisha na hara-kati za kupigania mustakbali wa Zanzibar.

Anasema yeye na wenzake wanaami-ni kuwa hawajavunja sheria yoyote kwa sababu kama ni hivyo, Serikali ingekwis-haifuta jumuiya hiyo ambayo ilisajiliwa kwa mujibu wa sheria za Zanzibar mwaka 2003.

“Wanajua kwamba hatujavunja sheria yoyote mpaka sasa. Shughuli yetu tume-zifanya kwa mujibu wa sheria. Hawa watu wa Serikali wanajua kuwa tungekuwa ha-tuna uhalali, wangekwishatufuta kwenye usajili. Hawajafika hapo kwa sababu tupo kwenye misingi ya sheria.

Na Waandishi Wetu Habari

Page 5: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

PAGE

8

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

9

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

8

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013 HABARI KUU

Matukio ya uhalifu na ma-tukio ya kutia watu tindikali, wanajua wanatuonea. Wana-jua hatuhusiki. Nasi kwa ki-nywa kipana kabisa, tunase-ma hatuhusiki kwa namna yoyote na matukio haya ya kuchafua watu, ya kujeruhi watu kwa risasi au kwa ku-wamwagia tindikali. Mara zote na kila tunapoyasikia, tunasikitika na kuwalaani kwa nguvu wale wanaoya-tenda,’’ anasema.

Katika hoja kwamba watu wengi ndani ya nchi Zanzi-bar, ndani ya Tanzania na ul-imwenguni wanainasibisha jumuiya yao na makundi ma-baya ya kigaidi kama Al Sha-baab, Al Qa’eda na Boko Ha-ram, anasema ni bahati nzuri hakuna mwenye ushahidi wa mnasaba huo.

’’Kuna watu wana chuki tu na sisi. Kwa sababu ya chuki zao dhidi yetu, wanasema wata-kavyo juu yetu. Wanatuhu-sisha na uhalifu unaofanywa wakati sisi tuko gerezani. Inawezekana wanaofanya wanajulikana lakini wana-lindwa kwa sababu wanazo-zijua hao wanaowatuma. Ni chuki yao tu hawana ushahi-di hata chembe wa kuhusika kwetu.

’’Hata hiyo kesi waliyotufun-gulia, ni chuki tu waliyonayo baadhi ya viongozi. Na ndo maana nasema mimi na wen-zangu tuna ujasiri wa kusema watoe ushahidi wa sisi kuh-usika na matukio hayo... Hii kesi ina mwaka mzima sasa haijasikilizwa. Ni kwa sababu hawana ushahidi,’’ anasema.

Sheikh Azzan na wenzake tisa wamekuwa kwenye ge-reza la Kiinua Miguu, lililopo Kilimani, mjini Zanzibar waki-endelea kusota huko wakati kesi walizofunguliwa hazija-pata kusikilizwa.

Wengine ni Masheikh Mselem bin Ali Mselem, Fa-rid Hadi Ahmed, Suleiman Juma Suleiman, Mussa Juma Mussa, Abdalla Said Madawa, Fikirini Khamis Fikirini, Gharib Said, Khamis Suleiman Ali na Hassan Bakari.

Walikamatwa Oktoba 16 katika maeneo tafauti ya mjini Zanzibar, na siku tatu baadaye ndipo walipelekwa mahakamani kwa mashta-ka ya kula njama ya kutenda jinai. Baadaye mashtaka ya-libadilishwa na kuwa ya ku-shawishi watu kufanya fujo – uchochezi.

Wanatuhumiwa kuvunja Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1968 ambayo in-asimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Kwa sasa wanakabiliwa na kesi mbili ambazo mashtaka yake yanafanana, moja iki-wepo Mahakama ya Wilaya iliyopo Mwanakwerekwe na nyingine mbele ya Mahaka-ma Kuu, Vuga.

Sheikh Farid ndiye kiongozi wa Maimamu wa Zanzibar, ambaye kutoweka kwake kwa siku tatu ambako mas-heikh wenzake walikulala-mikia ndiko chimbuko la kukakamatwa kwao.

Sheikh Farid alitoweka kati-ka mazingira ya kutatanis-ha akiwa eneo la Mombasa Kwa Bakathir usiku wa siku hiyo, na akaibuka siku tatu baadaye majira yaleyale ya usiku na palepale alipokuwa amechukuliwa na watu am-bao hajawahi kuwataja kwa kudai hawafahamu.

Jeshi la Polisi lilimwita na kumhoji atoe ushahidi wa madai yake kuwa alitekwa na watu wa Serikali. Alipofi-ka kituoni Mwembemadema, yalipo makao makuu ya Poli-si Mkoa wa Mjini Magharibi, alishikiliwa na halafu waka-kamatwa masheikh wengine tisa walio ndani mpaka sasa.

Dhamana yao imezuiliwa na Mahakama kutokana na Mkurugenzi wa Mashta-ka Zanzibar (DPP), Ibrahim Mzee, kusema wasitolewe kwa dhamana.

Ila Sheikh Azzan, yeye yuko nje kwa dhamana iliyotolewa na Mahakama Kuu wiki iliyo-pita ili kumwezesha kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya mati-babu.

Ombi lake ambalo lilisikilizwa na kuamuliwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu, lilikuwa ni jitiha-da za mwisho za mawakili wake na masheikh wenzake baada ya kupata maradhi ya vijiwe kwenye figo ambayo yamemzidi gerezani kiasi cha kuanguka na kuzimia mara tano, mara mbili ikiwa ndani ya gereza.

Kabla ya hapo, alikuwa ame-

lazwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, mjini Zanzibar. Mbele ya Jaji Makungu, mawakili waliwa-silisha maelezo ya madaktari ya-liyomthibitisha kuwa ni mgonjwa na hakuna hospitali ndani ya nchi inayoweza kumtibu isipokuwa kupelekwa nchini India.

Sheikh Azzan anatarajia kusafiri wiki hii kwenda India kwa matiba-bu ambayo anajilipia kwani serikali imesema haina uwezo wa kum-peleka haraka hivyo kwa kuwa wapo wagonjwa waliomtangulia ambao wangali wanasubiri kupa-tikana fedha ili wapelekwe nje ya nchi kutibiwa.

Akizungumzia maisha ya gereza-ni, alisema ni ya unyonge mkub-wa, yasiyopendeza na yanayo-sikitisha.

’’Angalau siku hizi kuna afadha-li kidogo. Zile siku 42 za kwanza tulipoingia tu gerezani zilikuwa siku mbaya na ngumu sana. Tuki-ishi katika upweke na udhalilishaji mkubwa. Tulipofika tu tulinyole-wa ndevu. Tukawa tunakaa mbali na watu. Kwa wiki nzima tulikuwa hatukutanishwi. Tumetengwa.

’’Tukiishi katika vyumba vidogo na vya kiza. Afya zetu zimeathirika sana kwa kila mmoja na hali yake. Siku hizi angalau tunapata taarifa za yanayotokea huku nje, tafauti na siku zile tulipoingia,’’ anasema.

Alipoulizwa kama anajua kwa nini wako gerezani, labda ana-jua wana kesi gani, Sheikh Azzan alisema yeye hajui anashtakiwa kwa sababu gani. Anaona hawana kesi yoyote ila wamefungwa kwa sababu viongozi wametaka wa-fungwe.

Sheikh Azzan anasema kwa kuendelea kukaa gerezani, huduma mbalimbali za ku-saidia watu dhalili walizo-kuwa wakizitoa zimezorota. Shughuli zao za kimaisha pia zimekufa na familia zao zimepata pigo kubwa.

’’Tulikuwa tunahudumia wa-toto yatima zaidi ya 1,000 kupitia jumuiya yetu ya Uamsho. Hatujui wanapata vipi huduma sasa. Wengi-ne tukiwasomesha, hatu-jui maendeleo yao. Baadhi wako nje ya Zanzibar, ha-tujui hatma zao. Wakati ule ilikuwa dhima kwetu lakini kwa sababu tumetiwa gere-zani, dhima yote imemuan-gukia Rais Dk. Shein. Yeye anajua kwa nini sisi tuko ge-rezani, yeye ndo Rais anajua sababu.

’’Dk. Shein tunamwambia aliapa, tena kwa kushika Mas’hafu kuwa atakuwa mwadilifu. Sasa tungepen-da aoneshe uadilifu, atende uadilifu. Sisi tunaendelea kukaa gerezani kwa sababu viongozi wa Serikali wame-amua tu tukae ndani, haku-na ushahidi wa kesi yetu. Hawana ushahidi, wangeu-leta na kesi ikaendelea. Kwa hivyo dhima anayo Rais,’’ anasema.

Sheikh Azzan anasema wa-lichokuwa wanakipigania ni lazima kiendelee kupigani-wa na Wazanzibari kwa sa-babu anasema walianzisha kampeni kwa madhumuni ya kuhangaikia maslahi ya Wazanzibari ambayo yame-kuwa yakidhoofishwa na watu wabaya.

Baadhi viongozi wa Uamsho wakijerejeshwa gerezani baada ya kesi yao kuakhirishwa tena mwishoni mwa mwaka jana.

Page 6: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

PAGE

10

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

11

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

10

CCM, Katiba Mpya na Bwana Mandola

Bwana Mandola ni mhusika kwenye filamu ya kijem-be cha kisiasa iliyotolewa na Bollywood mwanzoni mwaka huu wa 2013 kwa jina la Matru Ki Bijlee Ka Mandola.Ni filamu ya vichekesho inayozungumzia watu wata-tu – Harphool Singh Mandola, bintiye aitwaye Bijlee

na dereva wake Hukum Singh Matru. Bwana Mandola ana sifa, au tuseme ila, tatu: ni tajiri mkubwa, ni mlevi mkubwa na ni mwanamapinduzi mkubwa. Lakini hilo la uwanamapinduzi halionekani kwenye haiba yake mpaka kwanza ‘apige maji’ na yamtoshe. Mara tu akishalewa chakari, hapo ndipo Mandola Mwanamapinduzi huibuka ndani yake. Yule tajiri mlafi anayetaka kukigeuza kijiji kizima kilichope-wa jina lake kuwa eneo huru la kiuchumi na kuwafukuza kwa dhuluma wakulima wa kijiji hicho, hutoweka. Mwanzoni mwa mchezo, ni yeye anayewatokea wanakijiji waki-fanya mkutano wa kudai mashamba yao kutoka kwake, na ni yeye anayewahamasisha wafanye mapinduzi ya kumpindua mwenyewe. Lakini wakati wanakijiji wameshahamasika, mwenyewe anapi-tia mlango wa nyuma wa kasri lake, ambako kwa bahati mbaya anatumbukia kwenye bwawa la maji, ulevi unamtoka na sasa Mandola tajiri mlafi anaibuka ndani yake. Anachukua bunduki na kuwaelekeza wanakijiji wanaoelekea kulivamia kasri lake kutwaa haki yao kwa njia ya mapinduzi ya umma. Wanakijiji wote wanakimbia, huku wakijiuliza: “Lakini si ni huyu huyu aliyetuhamasisha tufanye mapinduzi tukatwae haki zetu kwake!?”Kisha Bwana Mandola anamgeukia dereva wake Matru na ku-muuliza kwa nini amemruhusu (yeye Mandola) alewe mpaka kupitiliza, ilhali anajua kuwa tajiri wake huyo akishalewa hupo-teza fahamu na kuwa Mandola mwengine. Ndipo hapo mtaz-amaji anapojua kuwa kumbe kazi ya Matru haikuwa udereva wa gari tu, bali pia kuendesha kiraru cha ulevi wa Bwana Mandola.

Chama cha Mapinduzi (CCM) ni Bwana Mandola. Kinapokuwa ‘kizima’ hakijalewa, ni chama kilichoshika dola na hatamu za uongozi, chenye ulafi wa kutosha kuhalalisha upapiaji wake wa madaraka. Kimefanya hivyo miaka nenda miaka rudi kwa jina la kukubalika na umma kwa mbinu na kiwango kile kile Bwa-na Mandola anachofanya kwenye umiliki wa ardhi ya wanaki-jiji. Ghilba, jeuri na kiburi, kwa kushirikiana na mawakala wake waliomo kwenye asasi na taasisi kilichoziunda chenyewe ku-toka unyayo hadi utosi wa nchi. Lakini CCM ina khulka ya ulevi. Kwa hakika imeshalewa na kule-walewa kwenye madaraka, kiasi cha kwamba baadhi ya wakati andasa za kilevi hupanda kichwani zikaiibua CCM nyengine nda-ni yake – taasisi ya kimapinduzi hasa kama lilivyo jina lake. Kipindi cha mwaka mmoja uliopita andasa hii ya CCM ikampanda mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, ambaye naye akadhuk-uru matarajio ya kimapinduzi kwa kutangaza mchakato wa kue-lekea katiba mpya. Ilikuwa andasa ya kilevi ya Bwana Mandola, maana nani asiyejua kuwa miezi michache tu kabla ya hapo CCM hiyo hiyo ilikuwa imeng’ang’ania kuwa katiba iliyopo ‘yatosha’?Lakini Rais Kikwete akazuka ghafla-bin-vuu akisema vyengine – kwamba katiba hii haitoshi. Panapaswa kuwepo na nyengine. Nchi nzima ikainuka kumpigia makofi na kumpongeza. Bwana Mandola akatunga wimbo na ngoma ya kimapinduzi. Mapinduzi hupinduliwa mtawala. Mtawala hapa ni CCM. Hivyo wimbo wa katiba mpya ulikuwa ni wimbo wa kuipindua CCM.Ikateuliwa Tume ya Jaji Mstaafu Joseph Warioba (pia mwana-CCM) kuusimamia mchakato huo. Lakini, kumbe, kama tu-livyokuja kujua baadaye, jukumu la Tume hii lilitakiwa na CCM liwe ni kama lile la dereva Matru wa Bwana Mandola. Sio tu kuiendesha nchi kuelekea Katiba Mpya, lakini pia kuiendesha Katiba yenyewe kuelekea kwenye matakwa ya CCM. Kumbe Jaji Warioba na wenziwe walikuwa na jukumu la ‘kum-dhibiti’ Bwana Mandola asilewe, ama akilewa asipitilize. Hai-kufanya hivyo. Ikauwacha wimbo wa kimapinduzi kwa jina la katiba mpya ulioanzishwa na mwenyekiti mwenyewe wa CCM

usikike, uakisike na mwangwi wake uaminike kwa umma. Tumejua hivyo baada ya jitihada ambazo zimekuwa zikifanywa tangu pale tume hiyo ilipoitangaza na kuikabidhisha rasimu ya kwanza ya katiba, ambayo miongoni mwa mengi iliyoyapende-keza, lililoikasirisha CCM ni pendekezo la Muundo wa Muunga-no wa Serikali Tatu. Tangu hapo, Bwana Mandola ndani ya CCM amekuja juu kama moto wa kifuu. Hakuna tusi alilowachwa ku-tukanwa Jaji Warioba na wenzake kwenye Tume kwa kuja na pendekezo hilo. Na hata ilipodhihirika wazi kwamba wananchi walio wengi kupi-tia ama kauli zao za moja kwa moja au kupitia vyama vya siasa, makundi ya kijamii au asasi za kiraia zinazowawakilisha, wa-naunga mkono pendekezo la Muundo huo wa Muungano, CCM haikuacha kufanya mbinu na hila. Ya karibuni zaidi ikawa ni hat-ua ya wabunge wa CCM kupitisha Mswaada wa Mabadiliko ya Sheria ya Katiba Mpya, kwa kile kilichoonekana wazi ni mapindi ya mwisho mwisho ya kuinusuru nchi isiingie kwenye Muundo wa Muungano wa Serikali Tatu. Sasa tena Bwana Mandola wa CCM amejikuta akilewa chupa nyengine za ulevi. Za mara hii ni baada ya shinikizo la Zanzibar kupitia upande wa Chama cha Wananchi (CUF) ndani ya Seri-kali ya Umoja wa Kitaifa na kambi ya upinzani Bungeni. Kwam-ba wataishitaki CCM na serikali zake kwa umma kwa kuuteka mchakato wa Katiba Mpya na kuikandamiza Zanzibar. Rais Kikwete ameinuka mwanzoni mwa Oktoba hii akasema ni kweli kuna ulazima wa hili kuangaliwa upya. Huko ni kwenda kinyume na maneno na matarajio ya wana-CCM wenzake, am-bao walishaamini kwamba Rais Kikwete angeliusaini mswada kama ulivyo, na hivyo kukengeuka matakwa ya wananchi wen-gine wengi. Tena Bwana Mandola amebugia ‘murji’. Na bora asileuke tena hadi Katiba mpya ipatikane na Jamhuri mpya zizaliwe, zikifuati-wa na ushirikiano wa haki baina yao.

Na Mohammed Ghassani Ngurumo la Mkama Ndume

Page 7: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

PAGE

12

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

13

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

12

Shirika la Umeme Zanzibar linaandaa ri-poti maalum itakayoelekeza mustakbali wa majenereta 32 yaliyonunuliwa ka-

tika mazingira yenye utata kwa kuwa shirika haliwezi kuyatumia kutokana na gharama zake kuwa kubwa.

Meneja Mkuu wa Shirika hilo, Hassan Ali Mbarouk, amesema wanataka kueleza ni hatua gani ifanywe kwa sasa kwa kuwa si rahisi wao kuchukua uamuzi wa kuyatumia majenereta hayo.

Mbarouk ametoa kauli hiyo baada ya kuuliz-wa sababu ya shirika hilo kulazimika kuanzi-sha mgao wa umeme katika kipindi amba-cho lililazimika kuzima laini kuu ya umeme unaotoka Kidatu, Morogoro ambao unakuja nchini kupitia waya za baharini.

Mbarouk alisema wamelazimika kuzima laini hiyo kwa sababu wangelazimisha kuendelea kutumia, wangesababisha hitilafu kubwa zaidi.

Amesema umeme wa mgao unatolewa kati-ka kipindi ambacho mahitaji yameongezeka kwa megawati tisa kutoka 43 ambazo zina-tolewa kwa kutumia laini ya umeme ya za-mani.

Alisema kumebainika hitilafu ya nguzo katika laini ya umeme unaotumia nguvu za maji un-aotoka Kidatu na kwa hivyo ni muhimu kutoa umeme kwa mgao mpaka hitilafu iliyobaini-ka Septemba 25 mwaka huu, itakapokami-lika kuondolewa. Mgao utakoma Oktoba 18, alisema.

Mbarouk alisema miundombinu iliyochakaa inayofika kwenye minara mikubwa inayo-beba nyaya za umeme ndio chanzo cha ku-

tokea hitilafu hiyo.

Kampuni ya Calpatar ya nchini India iliyofan-ya kazi tangu awali ndiyo inayotengeneza hitilafu iliyotokea na kwa gharama ya mkan-darasi huyo. Hakutaja gharama ya kazi hiyo. “Tumelazimika kuzima umeme katika laini mpya na kurudia umeme wa zamani ambao uwezo wake ni mdogo megawati 42 wakati Zanzibar inatumia megawati 52 kutokana na uhaba huo imelazimika kuzima baadhi ya maeneo ili kuweza kutumika kiwango hicho kidogo,” alisema.

Alisema Shirika la Umeme lingelazimisha kutumia umeme unaohitajika Zanzibar wa

megawati 52 kwa waya mkongwe ingetokea hatari ya kuripuka kama iliyotokea mwaka 2009 ambapo waya uliripuka na kusababisha umeme kukosekana kwa miezi mitatu mfulu-lizo katika kisiwa cha Unguja.

Waya unaosafirisha umeme baharini ulifung-wa kupitia mradi mkubwa wa shirika la misaa-da la Millennium Challenge Corporation (MCC) chini ya ufadhili wa Serikali ya Marekani. Kazi ya kuufunga waya mpya ilikamilika mwishoni mwa mwaka jana. Katika wakati ambao umeme ilikuwa tatizo kutokana na kazi hiyo, ilitarajiwa kuwa maje-nereta yaliyonunuliwa kwa gharama kubwa, yangetumika kuzalisha umeme.

“Hatuwezi kusema kitu kuhusu majenereta ambayo yapo kituo chetu cha Mtoni, lakini tu-naandaa ripoti na ikikamilika tutatoa tamko rasmi nini kifanyike kuhusu majenereta hayo,” alisisitiza. Mbarouk alisema shirika lina changamoto nyingi ikiwemo ya namna ya kudhibiti tatizo sugu la wananchi kujiungia umeme kinyume cha taratibu na kuchimba mchanga kwenye maeneo zilipo nguzo zilizoshikilia laini yenye umeme mkubwa.

Alisema watumiaji wa umeme wakilipa bili zao kwa wakati na wakitumia umeme kwa uangalifu, watatoa mchango mkubwa kuli-wezesha shirika kujiendesha vizuri.

''Majenereta yale balaa''Na Maua Mohammed

Kituo kikuu cha umeme cha Mtoni Unguja ambacho mradi wake uliofadhiliwa na Shirika la Millennium Challenge (MCC) la Marekani ulizinduliwa na Raiswa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, kikiambiwa kwamba kingelichukuwa umeme wa kilowati 100. [Picha kwa hisani ya Ramadhan Othman, Ikulu Zanzibar].

Habari

Page 8: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

PAGE

14

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

15

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

14

fanuzi wa maelezo hayo, imani inabaki kuwa jambo hilo ni kweli na kweli tupu.

Mapema wiki iliyopita, mtu mmoja aliyekuwa ndani ya gari aina ya pick-up alisita na gari eneo la Darajani, karibu na duka la Sahara. Akatupa kitu. Mwenye duka karibu na hapo akashtukia. Akaki-fuata kilichotupwa. Akakuta kitu cha ajabu, na kuhisi ni bomu. Akakiinua na kukitupia barabarani.

Haikuchukua muda uka-tokea mlipuko mdogo. Gari ile inatajwa namba zake za usajili. Hazikuniridhisa usa-hihi wake, sizitaji hapa. Lakini walioshuhudia wanasema wamekabidhi Polisi. Hakuna uchunguzi uliofanywa. Wale waliotoa taarifa hawajaelez-wa kama kuna uchunguzi

unafanywa. Hakuna ofisa anayetaka kusemea taarifa hii. Huu ndio uzembe.

Kama si uzembe wa maku-sudi, ni nini basi? Polisi wetu wameamua kuendekeza ujinga usio tija hata ndogo. Wanavumilia vitendo vya kihuni vinavyofanywa na wahuni waliotumwa na wa-huni bila ya kutambua kuwa mwisho wa uovu huo ni janga kwa nchi.

Mpaka sasa Jeshi la Polisi linabaki na idadi ya watu 15 waliowashika baada ya tukio la 13 Septemba la kum-wagiwa tindikali Padri Joseph Mwang’amba, aliyekuwa ametoka tu duka la huduma ya mawasiliano ya kimtan-dao la Sunshine, Mlandege, mbele ya Benki ya Exim am-bayo inalindwa na polisi.

Lakini badala ya kufanya uchunguzi wa kitaalamu – mpaka sasa hakuna taarifa zozote za maendeleo ya uchunguzi huo zilizokwisha-tolewa na hakuna mtu aliye-fikishwa mbele ya mahkama kushitakiwa – zinakuja ta-arifa za kusikitisha kuhusu namna Jeshi la Polisi linavyo-endesha operesheni za ku-saka waovu wa tindikali.

Wanavamia maduka ya dawa za binadamu na mifugo. Kuna madai kuwa wauzaji wananyanyaswa na kudhalil-ishwa. Askari wanachukua tindikali na chochote wana-chokidhania ni kimiminika. Wanaamuru duka lifungwe. Wiki nzima wanazuia wenye duka kufungua. Wanazuia biashara.

Mkuu wa Jeshi la

Polisi, Said Mwema

“Hoja hapa ni kwamba Kamishna Mussa amekurupuka. Ni hatari kukuta mtendaji wa hadhi yake anayepaswa kuzungumza jambo kwa kudurusu utafiti, anakurupuka. Kauli zake zinazingatiwa, na baadhi ya wasiokuwa makini wanazinukuu kwa kujenga hoja ya tatizo lisilokuwepo.”

Mhariri katika gazeti moja anaruhusu kuchapisha habari

inayotokana na nukuu ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa. Ofisa huyu wa Jeshi la Polisi amesema ndani ya Zanzibar kuna vi-jana waliojisajili kwa ajili ya kwenda kutumikia kikundi cha magaidi cha Al Shabaab.

Kamishna Mussa anasema vi-jana hao wamo kati ya vijana 15 waliokamatwa na kuhu-sishwa na matukio ya uhalifu wa tindikali yaliyoshika kasi nchini. Eti anasema walishi-kwa wakati wakijiandaa kush-iriki vita vya Jihad katika moja ya nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.

Maelezo ya Kamishna Mussa yametumika katika kujenga hoja ya kuwepo hofu ya us-

alama eneo hili la Afrika ku-tokana na vitendo vya kigaidi vikiwemo vinavyohusisha matumizi ya tindikali. Gazeti linatumia mazingira hayo yasiyo sawa, kuikandamiza Zanzibar. Inatajwa kama nchi yenye vitimbi vinavyotishia usalama wa wenyeji na wa-geni.

Na hapa ndipo ninapoliona tatizo. Gazeti linajenga hoja kwa kutumia maelezo yaliyo-tolewa kiwepesi sana na mtu mwenye hadhi kubwa katika moja ya taasisi zenye jukumu muhimu la kulinda usalama wa raia na mali zao. Polisi ndio wenye wajibu wa kulinda usalama wa ndani wa nchi.

Naona Kamishna Mussa ame-sema maneno mazito, bila ya kuwa amefikiri yatakuwa na athari gani kwa nchi. Haku-

fanya utafiti na wala maneno yake hayaoneshi kama ana-tambua wajibu wake kama kiongozi wa taasisi yenye wa-jibu wa kusimamia ulinzi wa ndani ya nchi. Maelezo yake ni mepesi yasiyochukulika katika uzito huo.

Hoja hapa ni kwamba Ka-mishna Mussa amekurupuka. Ni hatari kukuta mtendaji wa hadhi yake anayepaswa ku-zungumza jambo kwa ku-durusu utafiti, anakurupuka. Kauli zake zinazingatiwa, na baadhi ya wasiokuwa makini wanazinukuu kwa kujenga hoja ya tatizo lisilokuwepo.

Ila wangapi wanajua kama ilivyo hali halisi? Watu wengi wanachukua maelezo ya viongozi katika taasisi za kiserikali na kuziamini kuwa ni sahihi. Kusipotolewa ufa-

Huyu kiranja wa Polisi hakika amepotea

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Said Mwema, Waziri wa Mambo ya Ndani,

Emmanuel Nchimbi, na Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa.

Na Jabir Idrissa Kauli ya Mwinyi Mkuu

Page 9: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

PAGE

16

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

17

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

16

Mmoja wa wamiliki wa mad-uka yaliyoguswa na operesh-eni ya kinyonyaji, ameniambia amekula hasara kwa kuamri-wa kufunga duka kwa muda huo. “Nilikuwa na miadi ya kuuza dawa za Sh. 3,000,000 katika moja ya siku ambapo tumelazimishwa kufunga duka. Ni nani atakayetulipa hasara hii,” analalamika.

Uvamizi kama huo wa mad-uka ulitendwa kwenye skuli za sekondari za Lumumba na Vikokotoni ambako askari waliovalia kivita, kama vile wanamtafuta jambazi sugu au mtuhumiwa wa ugai-di, walijitoma hadi katika maabara na wakachukua vimiminika vyote walivyovi-kuta. Matokeo yake, polisi wamejikuta wamebeba hadi maji yaliyotengwa kwa ajili ya kupunguza nguvu ya tindikali.

Hivihivi Kamishna anajikuta ameinua chupa iliyoandikwa “Distilled Water.” Mbele ya waandishi wa habari anawa-onesha chupa hii na wapi-gapicha, waliopo wanafyatua flashi zao. Aibu iliyoje kwa Polisi.

Baada ya uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kulalamika kuhusu operesh-eni hiyo, ndipo vimiminika vilivyochukuliwa maabara za skuli, vikarudishwa.

Zinapatikana taarifa kuwa Polisi wanachanganya mam-bo mawili yasiyofananika. Wanatafuta wahusika wa uovu wa tindikali, kumbe

papo hapo wanaendelea kunyanyasa vijana waliokuwa mstari wa mbele katika Ju-muiya ya Uamsho na Mihad-hara ya Kiislam (JUMIKI) kwa ufupi Uamsho.

Inaonekana Kamishna Mussa na Polisi yake, pamoja na wale wanaomuamrisha, ha-wajaridhika na kuwakandam-iza masheikh wa Uamsho. Ile kuwakamata tangu Oktoba mwaka jana, na mpaka leo kuwasweka gereza kuu la Kiinuamiguu lililopo Kilimani, bila ya kuitolea ushahidi hata wa kubahatisha kesi wali-yowafungulia, haiwatoshi waheshimiwa.Wamekuwa wakitisha wau-mini wa misikiti mbalimbali inayoonekana kusaidia hara-kati zilizokuwa zikifanywa na Uamsho kabla na baada ya kukamatwa kwa masheikh ambao ni viongozi wakuu wa jumuiya hii iliyosajiliwa kishe-ria mwaka 2003.

Taarifa nilizopokea Jumapili zinasema bado wanamshi-kilia kwenye kituo kikuu cha Muembemadema kijana waliyemkamata wiki iliyopita. Hapo ndipo yalipo makao makuu ya Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi. Tayari kijana huyo mkaazi wa Muembetan-ga, mjini Zanzibar, anahusish-wa na tukio la tindikali dhidi ya Padri Mwang’amba.

Polisi wanamtumia kijana ambaye alikuwa karibu na Uamsho kuwachagua wale wanaoonekana kuhangaikia shughuli za jumuiya hiyo. Nia

ni kuwapa kesi. Vyote hivyo ni vitisho na vitendo vya dhahiri vya kukandamiza raia.

Kauli na misimamo mikali ya Kamishna Mussa vina ma-tokeo mabaya kwa wananchi. Akishasema, wasaidizi wake wanatii kwa kutekeleza kila anachoelekeza.

Ajuwe hiyo si njia nzuri ya kutafuta wahalifu wanao-tenda matukio yanayoleta hofu nchini. Siku zote chuki haijengi. Inabomoa. Uhalifu utaendelea tu iwapo Ka-mishna hajaelekeza wasaidizi wake kuwashika wale wanao-husika kuutenda.

Uhalifu hautakwisha kwa kukamata watu wasiohusika. Kwa hakika kitendo cha ku-wavumilia wanaojulikana kuhalifu ndicho kinacholea uhalifu, na hilo ni jambo baya katika jamii. Inajulikana pasi-po shaka kuwa watu wanao-panga na kutekeleza uhalifu wa tindikali, hawajakamatwa.

Kama hawajakamatwa, wa-taendelea kutenda uhalifu. Uhalifu huo ukiendelea, ma-tokeo yake ni hasara kwa nchi. Ni fadhaa kwa wananchi. Ni kutia hofu wageni wa-naoitamani Zanzibar kuto-kana na vivutio vyake.

Kama maskhara vile, lakini huko ni kuzuia watalii kuja kwetu. Watalii kwetu ni uchu-mi, tunaudhoofisha uchumi kwa kulinda wahalifu wa tindikali na wengineo.

Zanzibar Daima Online

Je unajua kuwa Jarida hili linapokea matangazo?

ww

w.z

anzi

bard

aim

a.ne

t

Tel: +44 7588550153 UKWeb: www.zanzibardaima.netEmail: [email protected]: [email protected]

Biashara yako haitouzika haraka kama hujaitangaza kupitia ZDO• Likiwa linasomwa jarida hili zaidi ya nchi 28 duniani hadi sasa kupitia mtandaoni• Zaidi ya watu milioni 2 hulisoma kupitia simu za mkononi na vibao vya kuandikia [ Tablet’s]• Zanzibar Daima Online hutolewa kila wiki 2

Kwa Matangazo yako tafadhali wasiliana nasi kupitia:

Ukitaka ujumbe wako uwafikie watu wengi basi tangaza katika Zanzibar Daima Online.

Page 10: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

PAGE

18

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

19

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

18

Katika miaka ya hamsini hadi sabini Jam-huri ya Watu wa China, chini ya viongozi wake Mwenyekiti Mao Tse-tung na

Waziri Mkuu Chou En-Lai, ilikuwa miongoni mwa nchi zilizosaidia sana harakati za ku-pigania uhuru katika nchi kadhaa za Afrika, ikiwemo Zanzibar. Wachina walifanya hivyo licha ya kuwa wakati huo nchi yao ilikuwa katika hali ngumu ya kutengwa na mataifa mengi ya dunia, hasa yale ya Magharibi.

Kwa kusaidia harakati za kupigania uhuru barani Afrika China ilitegemea kuwa Waafri-ka nao wataiunga mkono ili isiwe nchi yenye kutengwa kidiplomasia duniani. Ilitaka sana itambuliwe kuwa ni mwakilishi pekee na wa halali wa Wachina wote, hivyo iwe mwana-chama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Imelifikia lengo hilo.

Katika historia ya karibuni Wachina wali-tia mguu na kueneza ushawishi wao ka-

tika Afrika ya Mashariki kupitia mlango wa Zanzibar. Kwa kiwango kikubwa ilikuwa ni mwanasiasa wa Kizanzibari, Abdulrahman Babu, aliyewasaidia kwa hilo. Kupitia kwake Wachina walikuwa na sahibu wa kuwafaa, kwani Babu alikuwa akivutiwa na nadharia ya ukomunisti kama walivyokuwa kina Mao na Chou. Ni Babu, baaada ya kuundwa Muungano wa Tanzania, aliyemjulisha Rais wa kwanza wa Tanzania, Julius Nyerere, kwa watawala wa China. Baadaye Nyerere naye aliusifu Ujamaa wa Kichina. Kutoka hapo misaada ya Wachina ikazidi kumiminika Tanzania.

Lakini Wachina wa sasa si kama wale wa miaka ya sabini. Sasa Jamhuri ya Watu wa China ni miongoni mwa madola makuu du-niani, la pili lenye uchumi mkubwa na inat-ambuliwa kote duniani. Hali hiyo inaipelekea nchi hiyo kutaka kuzibadilisha nguvu zake za kibiashara na kiuchumi ziwe pia zinakwenda

Mtu mzima halazimishwi kuvaa kofia, hata msikitini

sambamba na ziwe na ushawishi wa ki-siasa na wa kidiplomasia katika maeneo mablimbali ya dunia. Kwa kufanya hivyo iko hatari kwa Wachina kujisahau na kuvu-ka mipaka. Pia kuna hatari kubwa zaidi ya kuja kuonekana na Waafrika wa kawaida kuwa ni wakoloni wepya, mara hii wao ni wa rangi ya manjano na wale waliondoka walikuwa wa rangi nyeupe.

Waafrika wanawashukuru Wachina kwa msaada wao katika mapambano ya ukom-bozi, lakini hawatawastahamilia hata kidogo pale watakapokuwa wanalinda na kupanua maslahi yao ya kibiashara kuin-gilia siasa za ndani za nchi zao. Malalamiko kama hayo ndiyo ambayo mara nyingi seri-kali za Kiafrika zimekuwa zikitoa dhidi ya nchi za Magharibi.

Kitendo cha karibuni cha Balozi wa China nchini Tanzania, Lu Youaqing, kusimama

juu ya jukwaa na kuuhutubia mkutano wa Chama cha Mapinduzi (CCM) huko Shinyanga - akiwa amevaa kofia ilio sare ya chama hicho na kukipigia debe chama hicho - kilikwenda kinyume na maelekezo anayotakiwa Balozi wa kigeni kuyafuata.

Kwa mujibu wa mkataba wa kimataifa wa Vienna wa mwaka 1961, Balozi wa kigeni hatakiwi kujiingiza katika siasa za ndani za nchi iliyompokea. Yeye ni kiungo kati ya Serikali yake na Serikali inayompokea. Japokuwa mtu anaweza kuhoji kwamba huko China hakuna tafauti baina ya chama kinachotawala cha kikoministi na Serikali hata hivyo Balozi yeyote mzoefu ange-tambua kwamba Tanzania kuna mfumo wa vyama vingi vya siasa na kitendo kama hicho kitawachoma wanachama wa vyama vya upinzani.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo

Na Othman Miraji Waraka kutoka Bonn

Siku Balozi wa China nchini Tanzania, Lu Youqing (kulia), alipopanda jukwaani pamoja na Katibu Mkuu wa Chama

cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, akiwa

amevalia kofia ya chama hicho.

Page 11: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

PAGE

20

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

21

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

20

(CHADEMA) papohapo kilitoa malalamiko, na kilikuwa na kila haki. Wakati huohuo wiz-ara ya Nje huko Dar es salaam haijatafuna maneno. Ilisema Balozi Lu alikiuka Mkataba wa Vienna kwa kujihusisha na siasa za CCM.

Chama cha kisiasa cha nchi fulani kuwa na urafiki na ushirikiano na chama cha kisiasa cha nchi nyingine ni jambo linaloeleweka. Hapa Ujerumani chama cha upinzani cha Social Democratic (SPD) kina ushirikiano na Umoja wa Vyama vya Kisoshalisti Duniani; Chama cha Christian Democratic (CDU) kina ushirikiano na Chama cha Demokrasia na Maendele (CHADEMA) huko Tanzania.

Vivyohivyo, Chama cha kiliberali cha Free Democratic (FDP) kimewaalika mara kad-haa hapa Ujerumani maafisa wa Chama cha Wananchi (CUF) kushiriki katika makonga-mano na warsha. Huo ni uhusiano baina ya chama na chama. Pia hapa Ulaya mabalozi wa kigeni hualikwa katika mikutano mikuu ya vyama, kwani moja ya kazi za mabalozi ni kuarifiwa na kujiarifu juu ya yanayojiri katika nchi waliko. Lakini yanakuwa mengine pale Balozi wa kigeni anapohutubia mkutano wa chama, akivaa sare ya chama hicho na kukipigia debe. Huko ni kwenda mbali, nahisi.

Tulisikia kwamba Balozi huyo ataandikiwa barua na wizara ya nchi za nje ya Tanzania kukumbushwa kwamba amekiuka shuruti za kazi yake. Lakini la ajabu ni kwamba badala ya kukiri kwamba alikosea, Balozi huyo amejitetea na kujitoa kimasomaso kwamba alilazimishwa na mama mmoja ai-vae hiyo kofia. Lakini picha zilionesha Balozi huyo kasimama na kofia imemjaa kichwani,

hana wasiwasi. Mtu mzima halazimishwi kuvaa kofia, hata msikitini. Yawezekana mheshimiwa Balozi alitaka kujipendekeza kwa watu waliomualika, akajisahau. Alifikiri, huenda kwa makosa, kwamba Watanzania watakiona kitendo chake hicho si muhimu na kutokitilia maanani. Yeye kutotilia maa-nani hisia za Watanzania ni aina ya kuud-harau uwezo wa Watanzania katika kumaizi mambo yanayowahusu.

Ushauri nasaha wa bure kutoka kwangu: Balozi Lu Youqing angeomba msamaha kwa Watanzania, kupitia wizara ya nje huko Dar es Salaam. Amekosa na haimsaidii kitu kutoa sababu hii na ile. Watanzania watam-heshimu sana wakisikia kutoka kwake: “Samahani nimeteleza.” Mambo yatakwisha na urafiki utaendelea kama kawaida, tena kwa kasi zaidi, kwa maslahi ya watu wa nchi mbili. Balozi huyo ameingizwa katika kosa na akakubali kuingia, na yote huenda inatokana na ile hamu na uchu wa kutaka kupanua biashara ya nchi yake kwa ghara-ma yeyote ile.

Balozi yeyote wa Kichina asingefanya ki-tendo kama hicho katika nchi yoyote ya Ulaya, licha ya kwamba Wazungu wa-nakwenda mbio kuvutia uwekezaji wa Wachina katika nchi zao. Tujiulize: kwanini? Jambo hili limetokea Shinyanga na uzuri kisa hiki kimezungumziwa. Kinaweza kika-tokea Zanzibar, Balozi wa kigeni akaalikwa na chama chochote cha kisiasa ahutubie umma huku amevaa sare ya chama kilicho-mualika na kukipigia debe. Tukiuwachia mtindo huo uendelee basi tutakuwa tuna-jidharaulisha mbele ya nchi za nje.

Hii ajabu wenzangu, makubwa yamenifika Nagombana na mwenzangu, aniona kama paka Shida ni kudai changu, ni mbaya naoneka ‘Tadai kipande changu, sijali akifutuka Kwa kudai haki yangu, naoneka kama taka Nashushiwa hadhi yangu, na kule nilikotoka Kisa ni kutaka changu, ndipo moto ukawaka ‘Tadai kipande changu, sijali akifutuka

Mimi napata uchungu, hiwaona wafutuka Kwa kuwa ni ndugu zangu, wa kufa wakanizika Nifanye nini wenzangu, jibu kwenu nalitaka ‘Tadai kipande changu, sijali akifutuka

Kama wapigwa sindano, kwa wanavyopapatika Wasema yaso mfano, watu wengi wawacheka Kimewakaa kibano, sasa wanaadhirika ‘Tadai kipande changu, sijali akifutuka Hivi ni ubaya gani, kukataa ushirika Mtu ukaitwa jinni, na utu ukakutoka Nipeni jibu jamani, mwenzenu nahangaika ‘Tadai kipande changu, sijali akifutuka

Simba Mwenda Kimya Zanzibar

Naufutuke

LADH

A YA

TUN

GO

Soma jarida lako la Zanzibar Daima Online kila wiki mbili

Page 12: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

PAGE

22UKURASA

23

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

22

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lina historia ya kuwa chombo kilichowahi kutumiwa na

Wabunge 55 wa Tanzania Bara kudai ku-wepo kwa Serikali ya Tanganyika. Miaka karibuni 20 baadaye, Tume ya Jaji Joseph Warioba imetoa hoja ile ile.

Kabla ya hapo, hoja hiyo ilitolewa na ku-muangusha Rais wa Zanzibar, Mzee Aboud Jumbe, na baadaye iliwaangusha akina Maalim Seif Sharif Hamad na hivi karibuni Mansoor Yussuf Himid.

Kitu kimoja ni wazi. Licha ya kuwa na mi-hanga mingi, hoja hii imeshinda majaribu ya wakati. Ilikuwa sahihi wakati wa Jumbe, wa G55, wa Maalim Seif na sasa wa Man-soor. Ilikuwa sahihi jana kama ilivyo sahihi leo na itakavyokuwa kesho.

Tanzania inahitaji aina ya Muungano we-nye Serikali Tatu ili kuondoa mkanganyiko, manung’uniko yasiyokwisha kutoka kila upande, tume zisizokuwa na maamuzi ya maana, vikao visivyokwisha na vinavyo-poteza raslimali za wananchi walipa kodi, ambao ndio wanaozipa Serikali mamlaka zilizonazo.

Kwa mujibu wa Katiba ya sasa ya Muun-gano, kuna Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano, ambayo pia itashughulikia mambo ya Tanzania Bara ambayo si ya

Muungano, na hivyo Katiba hiyo ya Jam-huri ya Muungano inashughulikia tawala mbili - ya Muungano na ya Tanzania Bara, wakati Katiba ya Zanzibar inashughulikia utawala mmoja.

Mtu yoyote anayejua hesabu ataona kuwa, unapokuwa na tawala mbili ka-tika katiba moja na ukaongeza utawala mwengine mmoja katika katiba nyengine, jumla yake ni kuwa na tawala tatu.

Kwa lugha nyepesi iliyowahi kutumiwa na Marehemu Ali Nabwa (mwandishi maarufu visiwani Zanzibar) “ukiwa na machungwa mawili katika kikapu kimoja na chungwa moja katika kikapu kingine, hayo yanakuwa machungwa matatu, na sio mawili.”

Hivyo ndivyo Makubaliano ya Muunga-no yalivyoashiria, yaani kuwa na mfumo wa shirikisho. Tunajidanganya sisi we-nyewe kuamini kuwa Tanzania Bara haipo kama Serikali, maana kilichofanyika hasa ni kuingiza uongozi wa Serikali (Baraza la Mawaziri) na sheria (Bunge) tu katika Jamhuri ya Muungano na sio kuziua Seri-kali na bunge hilo.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni mwakilishi halali wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambayo mwaka 1964 ilitia saini Mkataba, yaani Makubaliano ya Muunga-

no na mshiriki mwengine wa mkataba huu, yaani Serikali ya Tanganyika.

Kwa maelezo ya Makubalia-no hayo, Jamhuri ya shiriki-sho yenye mamlaka kamili ya mfumo wa Serikali tatu ilianzishwa. Kutokana na hayo basi, Serikali ya Map-induzi Zanzibar haikua chini ya nguvu, taasisi au chombo chochote cha dola, zaidi ya mamlaka yake yenyewe.

Kwa maana hiyo, Zanzibar inatakiwa ibaki dola inayo-jitegemea katika mambo ya-siyomo kwenye Mkataba wa Muungano na pia kama seh-emu ya Jamhuri ya Muunga-no ya Tanzania, kwa mujibu wa maelezo na masharti yali-yowekwa katika Makubalia-no ya Muungano baina ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika. Tanganyika nayo ipo kama sehemu nzima ya Jamhuri ya Muungano, ingawa imeingiz-wa katika Katiba ya Muun-gano.

Ukosefu huo wa dhamira nje-ma ndio uliowafanya wen-

zetu kuongeza na kubangaza vifungu kwenye Katiba kila walipotaka kufanya hivyo, ili kukwepa ukweli na uhalisia kuhusu Muungano.

Kwa mfano, hivi sasa Sehe-mu ya Kwanza ya Katiba hiyo inasomeka kwamba “Tanza-nia ni nchi moja na ni Jam-huri ya Muungano,” ambapo katika asili yake, kwanza nchi hii iliitwa “Jamhuri ya Muun-gano ya Tanganyika na Zan-zibar” na baadaye “Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.”

Ibara ya 2 (1) katika sehemu hiyo hiyo ya kwanza am-bapo zinatajwa nchi mbili zilizounda Jamhuri ya Muun-gano kuwa “Tanzania Bara” na “Tanzania Zanzibar.” “Tan-zania Bara” ni jina jipya lili-lobuniwa kuchukua mahala pa Tanganyika na waliotunga Katiba ya 1977, lakini hili la Tanzania Zanzibar hatujui lili-potokea.

Ibara ya 34 (3) inaeleza kwamba “Mamlaka yote ya Serikali ya Jamhuri ya Muun-gano juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri

ya Muungano, na pia juu ya mambo mengineyo yote yahusuyo Tanzania Bara, yatakua mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.”

Ufafanuzi huu unamaanisha kuwa hata kwa Katiba ya sasa, basi tayari pana Serikali tatu, na kilichopendekezwa na Tume ya Warioba si kigeni wala kisichokuwamo kwenye Katiba iliyopo.

Lakini hali iko kama ilivyo, na kulazimisha kuingia ghara-ma kubwa kuandaa Tume ya Warioba, kwa sababu ya ukosefu wa dhamira njema kwa upande wa watawala kuhusiana na uendeshaji na hatima ya Muungano wetu.

Hili la ukosefu wa dhamira njema linaonekana sasa kue-ndelea kuiandama tena nchi. Ndio maana mchakato wa kupatikana kwa Katiba mpya unaonekana kwenda mrama.

Mwalimu Julius Kambarage Mzee Aboud Jumbe Sheikh Abeid Karume

Muungano: Kinachokosekana ni dhamira njema

Na Riziki Omar Mkeka wa Mwana wa Mwana

Page 13: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

PAGE

24

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

25

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

24

Kilimo cha mboga mboga kina faida zake

Kilimo ni moja kati ya sekta muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, kwa nchi yeyote ile duniani.Mara nyingi unapozungumzia kuhusiana na suala la kilimo, hutoacha kukizungum-

zia kilimo cha mboga mboga kutokana na kuwa na tija sana kwa wakulima wanaojishu-ghulisha nacho.

Zanzibar Daima Online ilibahatika kutembelea maeneo ya Fuoni mjini Zanzibar na kuwa-hoji wakulima mbalimbali wanaojishughulisha na ukulima wa mboga mboga.

“Nilianza kujishughulisha na kilimo cha mboga mboga, mara baada ya kugundua kuwa kilimo hichi kina soko la uhakika, na kinaingiza fedha kwa muda mfupi,” Saidi Juma aliliambia Zanzibar Daima Online.

Saidi Juma ni mmoja wa wakulima walionufaika na kilimo cha mboga mboga, na kazi yake hiyo imemsaidia kutunza familia yake yenye watoto watatu.Alianza kujiingiza katika kilimo hicho miaka tisa iliyopita akiwa peke yake, na baadaye mwaka huu ndipo alipoamua kujiunga na kikundi cha watu wanne ili kuendeleza mradi wao.

Bwana Haji Khatibu ambaye pia ni mshirika wa kikundi cha Saidi juma, amesema eneo lao lina ukubwa wa ekari nane ambapo mazao yanapovunwa kutoka shambani huwain-gizia shilingi laki moja au elfu sabiini kutegemea aina ya mazao.

“Aina ya mazao tunayolima hapa shambani kwetu ni mchicha, nyanya, pilipili boga, mabilingani, bamia, nyanya chungu, figili na vitango, na mazao haya hutuingizia shilingi laki moja au elfu sabiini kwa siku,” alisema Haji Khatibu.

Pamoja na kuwaingizia kiasi hicho cha fedha, kilimo hicho pia kinawapa sehemu ya

chakula kinachopikwa majumbani mwao, na hivyo kuwafanya wasitumie fedha nyingi kununulia mboga hizo sokoni.

Akizungumzia muda wa mavuno Haji amesema huwachukua muda wa miezi mitatu hadi mazao yao yanapokuwa tayari kuvunwa na kusafirishwa kutoka shambani mpaka so-koni.

Licha ya faida nyingi wanazozipata kutokana na kilimo cha mboga mboga bado kuna changamoto nyingi ambazo zinawakumba, na kusababisha wakati mwingine mazao wanayoyavuna yapungue kwa wingi.

Akizungumzia changamoto hizo Hassan Ali Mwinyi, mshirika mwengine wa kikundi hicho, amesema tatizo la uhaba wa mbolea limekuwa likiwaumiza sana kwani husa-babisha miche yao isinawiri vyema.

Mbali na tatizo hilo, Hassan amesema kuwa ukosefu wa dawa za kuulia wadudu husa-babisha mimea yao pamoja na mazao kushambuliwa vikali na wadudu waharibifu.

Aidha amesema uhaba wa zana za kisasa katika kilimo chao huwafanya wapoteze muda mwingi shambani na kufanya kilimo chao kutoku wa na ufanisi mkubwa. Wakulima hao wameitumia fursa ya kuhojiwa na Zanzibar Daima Online kuwashauri vi-jana wanaokaa mitaani bila ya kazi yoyote, kuwa wajikite katika shughuli za kilimo cha mboga mboga kwani ni ajira yenye faida kubwa.

Vile vile wameiomba Serikali iwasaidie zana za kilimo za kisasa ili waweze kulima kwa ubora,sambamba na kuwatembelea mara kwa mara kwenye maeneo yao ili waweze kujua kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.

MAK

ALA

MAA

LUM

Na Khelef Nassor Makala Maalumu

Page 14: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

PAGE

26

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

27

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

26

Haki ya Mungu,kweli nalitote?Na Ally Saleh Barza ya Jumba Maro

Siasa za uhasama na ucho-kozi zimerudi upya Zanzi-bar na kwa kipindi kifupi tu

tokea zirudi tena hali imeanza kuwa tete. Ni wazi tunakoelekea siko; tunaelekea kubaya.

Hili si ajabu kwa Zanzibar lakini halijawahi kuwa ni jambolinalokubalika, maana zikianza siasa kama hizi huishia matumizi ya nguvu na uhasama. Kila mtu hupata hasara, ingawa kwa kiasi kikubwa wapinzani ndio wanao-ishia pabaya zaidi.

Viriri vimeanza kutumika kutoa kauli kali, za vitisho na hata za kibaguzi. Viriri vimetumika kutoa kauli za dharau, kebehi na za kutishia amani na mustakbali wa nchi yetu tuipendayo, Zanzibar.

Kama alivyotanabahisha mwenzangu katika uandishi Mo-hammed Ghassani kuwa hali hii imeanza kuwakumba hata ambao kwa kawaida huwa ni watu wa busara. Kidogo waka-chukulika na siasa za jukwaani, wakateleza.

Ingawa wapo wanaoteleza kwa pande zote mbili za kisiasa, wapo pia ambao ni kawaida yao kutukana au ni maarufu kwa matusi na vijembe.

Mashabiki wao huwa wa-nawashangiria ama kwa vicheko, makofi au kuwatia mori zaidi kwa misemo kama vile “ Wapashe baba” au “Toboa toboa” au hata “Chowea chowea.”

Miongoni mwa wanaoin-gia kwenye viriri wakifunga vibwebwe pia ni wanawake. Wao nao wamo. Tungetege-mea hili lisitokee kwa vile tuna ustaarabu wetu wa wanawake wetu Waki-zanzibari kuona haya, kuji-heshimu na kujistahi.

Hata wakati wa siasa za uhasama wa kikweli kwe-nye miaka ya 50 na 60 wanawake walikuwa waki-jizuia na walitumika zaidi kupoza kuliko kupuliza moto.

Tuliamua kwa makusudi kuzika siasa za chuki na uhasama kwa kuanzisha mfumo wa maridhiano chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa mwaka 2010.

Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya wanasiasa wakuu katika mivutano na misuguano, Maalim Seif Shariff Hamad na Sheikh Amani Karume kusema na nyoyo zao walipoona hatari ya nchi inakoelekea.

Ndipo katika kutimiza dhamira hiyo ya Novemba 5, 2009 pakafanywa Kura ya Maoni Agosti 31, 2010 iliyothibitisha kuwa asilimia 66.4 ya Wazanzibari walichagua kuachana na siasa za uhasama ingawa bado wakitaka siasa za vyama vingi na ushindani ziendelee kwa ajili ya uwepo wa demokrasia ambayo imekua hapa kwe-tu.

Si vyema, si haki, si halali kabisa kwa mtu yoyote ku-puuza maamuzi hayo ya thuluthi mbili ya Wazanzibari. Haikubaliki, haiwezekani na asiachiwe mtu yoyote yule kudharau, kubeza na kuy-apiga buti maamuzi

hayo.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa imetuokoa na mengi tangu iundwe. Tumeona jinsi kwa mara ya kwanza kwa Uchaguzi Mkuu ulivyofanywa kwa salama na amani bila ya hata mtu kufinywa.

Niseme wazi hapa kuwa wafaidika wa kubwa wa utulivu huu ni wananchi ambao wameamua kuwa upande wa siasa za upinzani ambao kwa miaka tokea 1992 zilipoanza siasa za vyama vingi mpaka 2009 ndio waliopigwa, kuteswa, kuonewa na kunyimwa kila aina ya haki.

Wale wa upande wa chama ambacho kimekuwa madarakani hawajui shida ya kuwa mpinzani nchi hii kwa sababu toka 1964 hadi 1992 na kutoka 1992 mpaka 2009 ni wachache mno kati yao waliofinywa ukucha, walioba-guliwa, waliosingiziwa kesi, waliofiri-giswa, kukoseshwa cheo, kubaguliwa

katika masomo na kufanyiwa kila aina ya idhlali.

Hadithi ya madhila haiwezi kabisa kuhadithiwa na yoyote ambaye amekuwa mwanachama wa CCM. Kwa hivyo,kwa fikra zangu ni rahisi kwao kutokuuona umuhimu wa kulinda amani na umoja wa kitaifa. Sisemi kuwa walio chama cha upinzani ha-wawezi kuwa pia ni waharibifu wa amani lakini wa CCM ndio waliobo-bea.

Kama nilivyotangulia kusema pande zote mbili zina wajibu wa kuishika, kuienzi na kuibembeleza amani maana hata katika hiyo miaka ya 1964-1992 na 1992 mpaka 2009 Serikali haikuweza kupiga hatua za wazi na jumuishi za maendeleo maana siasa haikuwa imekaa sawa Ingawa mimi binafsi

Page 15: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

PAGE

28

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

29

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

28

BARZA YA JUMBA MARO

siridhiki na muundo wa Seri-kali ya Umoja wa Kitaifa am-bao unaishia kileleni bila ya kushuka kwenye matawi na mizizi, lakini naona faida kub-wa sana ya kuwepo na kue-ndelezwa kwa mfumo huo. Pengine tunawajibika tuupe nguvu na mashiko zaidi tu.

Kwa hivyo wakati tukipanda viriri vya siasa kufanya siasa ni lazima tutashindana kwa hoja, tutakosoana kwa jazba, tutaonyeshana vidole na kushutumiana wakati mwen-gine, maana hakuna kabisa siasa za kimyakimya au zisizo na nguvu na mikiki.

Lakini kabisa, tena kabisa

isifike tukataka, au tukapenda kurudi katika siasa za chuki na uhasama kwa sabab haku-na atayefaidika. Tukumbuke pia hata hao wapinzani walio-kuwa wakionewa muda wote hawatakubali kuendelea kuonewa sawa na wale am-bao wamekuwa wakifaidi nguvu na fursa za kutawa-la wajuwe kuwa haki ya kutawala ni ya wote.

Fikra zangu basi pamoja na yote isifike kabisa tena kabisa kwa yoyote yule, narudia kwa yoyote yule kusema au kuta-mani kuwa jahazi la Zanzibar litote na tugawane mbao, maana anayesema hivyo au anayeashiria kwa kauli zake

au vitendo ajue kutota Zanzi-bar ni kuipasua Zanzibar tuipendayo, na hatujui itapa-suka vipande vingapi.

Tushindane kwa hoja, nguvu na ujanja lakini tusifanye chochote ambacho kitaipele-kea Zanzibar kutota maana ikitota ni hasara kwetu tu-liopo sasa na vizazi vijavyo. Wallahi, haki ya Mungu tu-pate faida gani Zanzibar ikitota. Tusimruhusu, tusim-kubalie yoyote kutamka hivyo na tumwandame na kum-welewesha kuwa tukitota na janga, na watu walisema mchuma janga hula na wa kwao.

Zanzibar Nakupenda

Baadhi viongozi wa viongozi wa CCM Zanzibar katika moja ya mikutano yao ya hadhara

LIMEDHAMINIWA NA ZANZIBAR DAIMA COLLECTIVE

Page 16: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

PAGE

30

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

31

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

30Na Ahmed Rajab

Umuhimu na hatari za uvumiSiku hizi kila mwenye

kuweza kuandika sen-tensi mbili tatu anajiona

kuwa ni mwandishi. Watu wa aina hiyo huwa hawayajali maadili na miko ya uandishi. Lililo muhimu kwao ni uwezo wao wa kutunga maneno na wa kuandika tahajia za neno, yaani namna ya neno lina-vyopaswa kuandikwa.

Hili ni tatizo lililo bayana katika jamii nyingi duniani na, kwa bahati mbaya, sisi Wazanzibari hatujaachwa nyuma. Yatazame mitandao yetu ya habari na hutakosa kuyaona maandishi yasiyo na sifa za kiuandishi.

Hakuna uchunguzi wa kina unaofanywa na waandishi wa makala hayo na, kwa hakika, mara nyingi waandi-shi wa aina hiyo huwa wanajikita katika uvumi, upenyenye na unabe waki-andika mambo bila ya kuwa na ithibati yoyote. Kazi yao ni kuvumisha yasiyo ya kweli.

Waandishi hao wanasaidiwa sana na vyombo vipya vya mawasiliano pamoja na majukwaa ya mawasiliano ya kijamii yaliyochomoka siku hizi. Yote hayo ni maendeleo, tena ni maendeleo makubwa yaliyopatikana katika kipindi kifupi.

Kwa kweli, kuwako kwa mawasiliano hayo ya kijamii

pamoja na uandishi huru na uwezo wa wananchi ku-vimudu vyombo vipya vya mawasiliano kwa bei rahisi si neema ndogo. Neema hiyo imesababisha pawepo uwazi zaidi duniani kote. Na hayo ndiyo matunda ya maende-leo niliyoyataja hapo juu.

Taksiri iliyopo katika hii mi-tandao ya habari ya umma ni kwamba mara nyingi inakuwa haina mtu au watu mwenye kuyapima makala na kuamua iwapo yawekwe kwenye mtandao kwa vile yana sifa zote zinazohitajika au yasiwekwe kwa sababu

yanakosa sifa hizo.

Matokeo yake ni kwamba watu hujiandikia watakavyo, wakivumisha uvumi wau-takao. Zinazokosekana ni habari za kuaminika.

Kama tujuavyo kuna aina mbili za habari — zilizo rasmi na zisizo rasmi. Habari zilizo rasmi hupatikana kutoka vy-anzo rasmi, mathalan kutoka serikalini au kwenye vyama vya kisiasa au kutoka kwa wataalamu wa fani mbalim-bali au taasisi fulani.

Habari zisizo rasmi hupa-

tikana kutoka minong’ono na uvumi. Ni maneno yenye kuvumishwa na yanayowa-fanya watu wayafasiri wata-kavyo.

Si hayo tu lakini kuna ha-tari nyingine kwamba kila anayeusikia uvumi aghalabu naye huzidi kuuvumisha na afanyavyo hivyo mara nyingi hutia nakshi zake au huon-geza kasumba mbili tatu.

Juu ya hayo, uvumi unaweza ukawa na faida endapo uta-tumiwa kama nyongeza au ziada ya njia rasmi za ma-wasiliano. Kwanza uvumi huvuma kwa kasi na hivyo

huwafikia watu kwa wepesi zaidi kushinda habari zin-azopatikana kwa njia zilizo rasmi.

Kwa hivyo, ijapokuwa uvumi unaweza kuzusha balaa kwa kupotosha ukweli wa hali halisi ya mambo ilivyo uvumi unaweza ukawa na faida. Kwanza, mara nyingi uvumi huwa japo na chembe cha ukweli. Ndo ikawa tunausikia ule usemi wa kwamba “lisemwalo lipo na kama halipo laja”.

Pia uvumi huwagusa wa-naousikia kwa sababu bin-adamu siku zote tunakuwa

na hamu ya kujua mambo, wengine hupindukia mpaka hiyo hamu ikageuka na kuwa unabe.

Ubaya mkubwa wa uvumi ni kwamba hauwezi kutegeme-wa na mara nyingi unaweza kuzusha mzozano, suita-faham na mtafaruki katika jamii.

Njia hiyo ya kupata habari kwa kutegemea uvumi huzidi kuwa na nguvu katika wakati wa hali ya wasiwasi, na pale habari rasmi zinapokuwa hazipatikani kutoka kwa taa-sisi au vyanzo vinavyohusika.

Hivyo basi minong’ono na uvumi hustawi katika mazin-gira ambamo si rahisi kupata habari rasmi, pale Serikali inapokuwa inakaa kimya bila ya kuieleza jamii nini kinachotokea. Mfano mzuri ni huu tulio nao sasa Zanzibar ambapo hatu-jui nini matokeo ya uchun-guzi uliofanywa kuhusika na mauaji ya Kasisi wa Kikatoliki Evaristus Mushi wa Parokia ya Minara Miwili, Mji Mkon-gwe, Unguja aliyepigwa risasi na kuuliwa Februari mwaka huu.

Hadi leo hatujui nini matokeo ya upelelezi uliofanywa na vyombo vinavyohusika hapa nchini pamoja na ule uliofanywa na Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI)

Na Ahmed Rajab Kalamu ya Bin Rajab

Page 17: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

PAGE

32

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

33

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

32

lililoombwa kuja kuisaidia Polisi ya Tanzania.

Kukosekana habari rasmi kutoka vyombo vya usala-ma vinavyohusika kumewa-sababisha wananchi waan-ze kuvumisha uvumi wa kila aina, pamoja na ule unaom-tia jina baya Marehemu.

Kadhalika, visiwani Zanzibar hivi karibuni kumefanywa uhalifu wa watu kadhaa kumwagiwa tindikali. Polisi bado haijampata yoyote na

hatia ya makosa hayo ya jinai.

Badala yake Polisi ime-kuwa ikivumisha uvumi usio na ithibati wala ushahidi wowote wenye kuvihusisha vitendo hivyo vya uhalifu na ugaidi wa kimataifa.

Wengi wanafikiri kwamba Polisi wamefanya hivyo kwa sababu za kisiasa. Lakini maslahi ya umma haya-tetewi kwa mazingatio ya kisiasa, bali kwa kuujua

ukweli. Katika kesi kama vile za mauaji ya Padre Mushi, za watuhumiwa wa mashambulizi ya tindikali au ya viongozi wa Uamsho vyombo vya habari vinaku-wa na dhima moja na Ma-hakama. Vinakuwa na ubia katika wajibu wao.

Ikiwa upande mmoja utas-hindwa kutekeleza wajibu wake, huenda ukausababi-sha upande mwingine pia kushindwa kutekeleza wa-jibu wake.

Kuripoti uvumi na vijembe au masengenyo si uandi-shi. Na hukumu zikitolewa kwa kutegemea uvumi na vijembe au masengenyo zinakuwa si hukumu za haki. Hivyo, ikiwa vyombo vya habari vitashindwa kufanya kazi zake kwa kuwajibika basi matokeo yake yanawe-za kuwa mabaya sana.Hatari tuliyonayo ni kwam-ba Zanzibar imegeuka na kuwa jamii ya uvumi na uzushi. Tarehe 5 Ok-

toba gazeti moja liliandika kwamba amezaliwa mtoto wa ajabu katika kijiji cha Changani, Kivunge, Wilaya ya Kaskazini ‘A’, Unguja, na tunaamini.

Tunaambiwa kwamba mto-to huyo Fahazal, mwenye umri wa miezi 10, alianza kusema akiwa na miezi mi-wili na tunaamini. Tunaam-biwa akisema kwa kuyataja majina ya Mwenye Enzi Mungu, Mtume Muham-mad (SAW) na matamshi ya

kumtukuza Mungu.

Tunaambiwa kwamba ana-zungumza pia Kiingereza na Kiarabu.

Tunalala na uzushi na tu-naamka na uvumi. Tukitoka nje na kwenda makazini au mabarazani tunausambaza huo uvumi. Kila anayeusikia huo uvumi naye hutaka kuongeza lake na kwa ku-fanya hivyo huzidi kuupoto-sha ukweli.

MATANGAZO

Inawatakia Idd Njema

Zanzibar Daima Online Collective

Page 18: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

PAGE

34

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

35

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

34

DKT SHEIN BALOZI IDDI WAZIRI ABUBAKAR MAALIM SEIF

Ubishi uliotokea ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kuhusu

kama imeshiriki au haikush-iriki kujadili muwada unao-husu Sheria ya Mabadiliko ya Katiba umetanua utata wa mustakbali wa Zanzibar, nchi inayoshikilia kurudi-sha mamlaka yake kamili ya kuiendesha, Zanzibar Daima Online linaripoti.

Hata kama sasa Rais Jakaya Kikwete anaonekana kuin-gilia kati kwa kutaka mswa-da huo urudishwe Bungeni kujadiliwa upya, ili kuhakiki-sha ushiriki wa Zanzibar, hilo haliufichi ukweli ulio wazi.

Misimamo isiyoshikamana ya wasaidizi wakuu wawili wa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, kuhusu suala hilo imeonesha bado kuna kazi ya ziada ya ku-fanywa kwa lengo la kuun-ganisha fikra na mitizamo ya viongozi wa kisiasa bila ya

kujali ya itikadi za kivyama ili kuihakikishia Zanzibar mus-takbali mwema.

Hali hiyo imetokana na kutafautiana kwa kauli kati ya wasaidizi hao wa Rais – Makamu wa Kwanza na Makamu wa Pili – ambao kila mmoja ametoa matam-shi yanayozua ubishi kwa kuwa yamewachanganya wananchi.

Wakati Makamu wa Kwaza, Maalim Seif Shariff Hamad anasema Serikali haikush-irikishwa katika kujadili mapendekezo ya marekebi-sho ya sheria hiyo, au an-galau ushiriki wake ulikuwa wa kiinimacho, Makamu wa Pili, Balozi Seif Ali Iddi, yeye anasema serikali ilishirikish-wa kikamilifu.

Ngoma yote ilianzia kwa Makamu wa Pili, ambaye akiwa katika nafasi yake kama Mbunge wa Kitope, kupitia CCM, aliliambia

Bunge tarehe 6 Septem-ba mjini Dodoma, kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzi-bar ilishirikishwa katika ku-jadili mswada huo.

Balozi Iddi alitoa kauli hiyo baada ya “kutupiwa mpi-ra” na Waziri wa Sheria na Katiba wa Serikali ya Jam-huri ya Muungano, Mathias Chikawe, aliyemtaka aeleze msimamo wake kwa kuwa

yeye ndiye mtendaji mkuu wa Serikali na kiongozi wa shughuli za Serikali katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

Lakini, siku chache baada ya kauli yake hiyo ndani ya Bunge, iliyojenga picha kuwa utaratibu wa kujadiliwa mswada na pande mbili za Muungano ulifuatwa, alijik-uta akisimangwa kwa madai kuwa alilidanganya Bunge kwani Serikali haikushiriki-shwa kikamilifu.Kilichokuja kuonekana ni

ulaghai, kilitajwa na Wa-ziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakary, ambaye alisema kili-chopelekwa SUK na kujadili-wa na hatimaye kutolewa maoni, ni vifungu vinne tu vya mswada wakati Chikawe aliwasilisha bungeni mswa-da wenye vifungu 12, vinane zaidi ya vilivyojadiliwa na SUK.Mapema baada ya Bunge

kupitisha mswada, mwandi-shi wa habari alimuuliza Abubakar kama Serikali il-ishirikishwa katika kujadili mapendekezo ya marekebi-sho ya sheria ya mabadiliko ya katiba. Swali kama hilo pia aliulizwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Othman Masoud Othman.

Abubakar alisema alikuwa ameagiza apatiwe mswada uliowasilishwa bungeni ili kulinganisha na yale “tuli-yoletewa na kuyajadili na kuyatolea maoni.” Alisema

akishapata picha iliyopo, ataeleza umma.

Mwanasheria Mkuu Oth-man yeye wakati huo akiwa safarini nchini China, aliwahi kusema kwa kawaida msi-mamizi wa mswada anaku-wa Waziri, ambaye huishirik-isha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kupata maelezo au maoni ya kitaalamu. Alilenga kuele-

keza kuwa Abubakar ndiye mwenye wajibu wa kueleza kwa ufasaha suala hilo.

Abubakar, akiwa mbele ya umma uliohudhuria mku-tano wa hadhara ulioitishwa na wenyeviti wa vyama vi-tatu vinavyosimamia umoja mpya wa kupinga mswada uliopitishwa na wabunge pekee wa CCM, pamoja na Mwenyekiti wa Tanzania La-bour Party (TLP), Augustine Mrema, alisema wamebaini waziri mwenzake alifanya kazi upya na kuchomeka vi-

fungu vinane zaidi bila ya kurudi kuishirikisha Zanzibar kutoa maoni yake.

Wakati huo, Maalim Seif alishatoa msimamo kwamba Zanzibar haikushirikishwa kwa sababu kilichofanyika ni kuitumia kama kiinimacho, kwa kuwa kilichofikishwa kwao ni “mambo nusunusu” na baadaye mambo men-gine kuchomekwa na Seri-

kali ya Muungano.

“Hatukubali kitu kama hichi. Wamemdanganya Balozi Seif. Hawakumwambia uk-weli wa kilichotokea. Mimi namjua Balozi alichoki-jibu alikuwa ana maana ya mapendekezo nusu wali-yotuletea. Hakujua wen-zake wamemla kichogo… wamemchomekea na akain-gia mtegoni kusema uongo kule bungeni.

“Hatukubali kufanyiwa dhi-haka namna hii. Wajuwe

MABADILIKO YA KATIBA

Zanzibar inawekwa wapi?Na Mwandishi Wetu Mazungumzo Baada ya Habari

Page 19: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

PAGE

36

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

37

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

36

Zanzibar si koloni la Bara. Hii ni nchi na sasa watu we-nyewe wanataka mamlaka kamili ili wafanye mambo yao wanavyoona. Wakilazi-misha sheria hii kwa Rais Kikwete kuisaini, wabunge wetu hawatashiriki Bunge Maalum la Katiba. Wajumbe wetu wa Baraza la Wawakil-ishi nao pia hawatashiriki Bunge la Katiba,” alisema Maalim Seif, katibu mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF).

Wakati Balozi Seif anazidi kuthibitisha kuwa alicho-kisema bungeni ni sahihi, kwa maana ya kwamba SMZ imeshirikishwa kika-milifu kujadili na kuridhia mswada, linaibuka swali: Hivi kwa msimamo wake huo, anamwakilisha nani?

Je, Makamu wa Pili huyu anayetoka CCM anamwa-kilisha Mzanzibari yupi? Ni yuleyule anayemwakilisha Maalim Seif au ni mwengi-ne?

Kwa kuwa Abubakar am-baye ndiye aliyesimamia uchambuzi wa mapende-kezo ya marekebisho ya sheria yaliyotumwa kwake na Chikawe, na kwa kus-hirikiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakay-atolea maoni na kumpele-kea Makamu wa Pili ili aya-wasilishe kwa Waziri Mkuu, na ikabainika sasa kwam-ba timu ya Waziri Chikawe walichomeka vifungu zaidi kinyemela, hapo ndio SMZ imeshirikishwa?

Linakuja swali jipya kwam-ba yupi anastahili kuzinga-tiwa kuwa ametoa msima-mo wa kulinda maslahi ya Zanzibar na Wazanzibari kati ya Makamu wa Pili na Makamu wa Kwanza? Je, maslahi ya Zanzibar yana-lindwa kwa kauli dhaifu au kauli thabiti?

Katika wakati ambapo Wa-zanzibari wanataka kure-jesha hadhi ya nchi yao ili iwe na mamlaka kamili, ki-ongozi imara tu ndiye anay-ewafaa. Kiongozi anayete-tereka au anayefanya kazi kwa kuhofia maslahi yake binafsi, hawafai Wazanzi-bari.

Tanbihi: Hii ni sehemu ya pili ya makala haya ambayo kwa mara ya mwanzo yalichapishwa kwa jina la “Tungo za Bwana Kimbunga: Haji Gora Haji” na yameandikwa na mtaalamu wa lugha ya Kiswahili mzaliwa wa Uholanzi,

PROFESA RIDDER H. SAMSOM, kuelezea kazi za kifasihi za gwiji wa sanaa ya ushairi katika zama hizi visiwani Zanzibar, Haji Gora Haji. Tunayachapisha tena hapa yakiwa yamehari-riwa kidogo kuakisi wakati wa sasa.

SEHEMU YA PILI

Sitiari za Mzee wa Kimbuga:Haji Gora

Nyimbo ya kwanza aliyotunga ilikuwa ni kwa kumjibu

mpinzani wake aliyekuwa akimkejeli na kumwam-bia baada ya kumwacha mkewe kuwa hakuwa na

hekima itoshayo kuishi vyema naye.

Huyo mpinzani wake, marehemu Makame Haji Kitenga alikuwa akim-linganisha na Mduruma,

yaani mmojawapo wa kabila la Wamijikenda, kwa vile unahodha hana na kushona tanga hawezi. Haji Gora akam-jibu:

Najibu mimi najibu, kuimba naweza Jina ulonita Mduruma, mie Peremu limenipendeza Sishindwi na kushona tanga, na wala kuiunga heza Kama unahodha kazi yangu, hakuna moja litalonizoza

Akajiita ‘Peremu’ ambaye wakati ule alikuwa ni mwigizaji maarufu wa filamu za Kihindi. Jina lake hasa alikuwa akiit-wa Premnath, mtu shujaa na mwimbaji aliyependwa na wengi.

Tangu utungo huo wa kwanza Haji Gora hakuwacha tena kutunga. Kila fani ya ushairi ameishughulikia. Akaanza ku-tunga nyimbo za taarab kwa ajili ya klabu mbalimbali, akiendeleza ustadi wake wa ushairi wa kibati unaotungwa papo hapo, na kutunga vitandawili na mashairi na tenzi na riwaya yake Siri ya Giningi.

Umaarufu hasa ameupata diwani yake ya Kimbunga ilipotolewa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili mwaka 1994, na kuiingizwa katika mitaala ya Tanza-nia nzima. Hata njiani wengi humwam-kia kwa kumwita ‘Mzee Kimbunga’.

Huo utungo wake wa kwanza kabisa unaonesha kiini cha sifa ya ushairi wa Mzee Haji. Hali ya ushairi wake ni hali ya kuita na kuitika, kuuliza na kujibu.

Ndiyo ni hali ya kujibizana. Na juu ya hayo, ni hali ya kupingana, kuchoko-zana, kubishana na kusengenyana. Sio umbo tu la ushairi wake unaonesha hali hiyo ya ukinzani, bali dhamira zake na taswira anazotumia zimo katika hali hiyo.

Katika hali hiyo ya – tuseme - kuhalifi-ana, anajijua nafsi yake barabara. Ana-jitambua kuwa si Mduruma wala Mma-sai. Anajiita ‘Peremu’. Kujiita ‘Peremu’ ni zaidi ya kujigamba kuwa ndiye shu-jaa. Ni kujitambua na kujitambulisha awe mtu wa siku hizi, mtu wa sasa.

lngawa karibu tungo zake zote zinaele-za na kuonesha jadi na asili yake, ndiye mtu wa zama hizi za teknolojia, mtu wa jamii ya kisasa. Hakuna mtu anay-emzoza, anayeweza kumshinda katika hiyo jadi yake ya unahodha na kushona tanga, yaani asili yake ya mwambao. Lakini huu ustaarabu na utamaduni wa asili umeunganishwa na maendeleo ya jamii na kutogongana na maisha ya siku hizi.

Kama vile katika utenzi wake wa Visa vya Nabii Suleiman bin Daudi (A.S), watalaam waliofanikiwa kutengeneza ndege na maroketi na Apolo, wameun-

gana na kisa cha Nabii Suleiman ambaye kufuatana na Kuran, alikuwa akiamrisha majini na upepo, na kufuatana na mapokeo kuruka mwenyewe:

Kwa ya angani sehemu Kiumbe binaadamu Ambaye katakadamu Sulemani kusafiri

Katika yake maisha Walio jielemisha Ndio wanaozimsha Ndege kwa hizi dahari

Kwani hizo Repuleni

TUFUNGUE KITABU

Page 20: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

PAGE

38

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

39

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

38

Zino safiri Angani Hazikuweko zamani Zama hizi zimejiri

Maisha yake Nabiya Hao walozingatiya Mola kuwajaaliya Kuzifupisha safari

Kurusha vilothibiti Kuna vyombo tafauti Apolo na maroketi Hupita kwenye sayari

Kupita sehemu hizo Binaadamu wa mwanzo Kikawa ndicho kigezo Ni mtume wa KahariMtume wake Karima Kwa vile kiumbe mwema Miangaza ya rehema Kamshushiya Libari

Vile vile katika matumizi ya lahaja yake Mzee Haji anaweza kutambulika wapi anakotoka, maana anaeleza: “Sishindwi na kushona tanga, na wala kuiunga

heza”. Neno hilo heza ni Kitumbatu am-bacho mara nyingi hudondosha sauti ya nazali, kwa mfano ‘-aza’ kwa ‘-anza’ au hata ‘-fugua’ kwa ‘-fungua’. ‘Henza’ ni ile kamba ya kupandishia na kuterem-shia tanga.

Ushairi wake unamsaidia msikilizaji sana kumtambua yeye mwenyewe

nani. Katika shairi lake la Kiswahili alilomtungia Juma Bhalo, amebaini, tena wazi wazi, vipi anajitambua pamoja na lugha yake:

Iwapo panaridhiwa, warathi wa Kiswahili

Ni hao nilitongowa, ndio wanositahili Vyengine havitakuwa, ni vitendwapo batili Lugha hii Kiswahili, wenyewe ni wa mwambao

Lakini kutambulika huko na kujit-ambulisha kwa njia hii hakuna maana kuwa si mtu wa Ieo, yaani si kwamba haoni dunia ilivyo sasa na yeye ku-ganda katika jadi yake.

Kuhusu zana ya kazi yake, hiyo lugha ya Kiswahili, amemjibu mtaalamu wa Kiswahili, Profesa Tigiti Sengo, kupitia makala yake Kiswahili Asiliya Chahuwika kwa kusema:

Pole pole kugeuza, kwa Kibara kujaziya Kazi twaikokoteza, ni bora kuharakiya Kwa ghafula kukataza, pasiwe anotumiya Hiyo lugha asiliya, izagae duniyani

Si lazima katika ushairi wake Haji Gora atambulike moja kwa moja maana hutumia sana mafumbo na vitandawili. Shairi lake la ‘Kasa’ linamuuliza msom-aji huyo kasa “Vipi tunamsadiki, mnyama au samaki?”

Maswali ya aina hiyo yanatokea mara

nyingi katika ushairi wa Kiswahili, kama vile ile nyimbo maarafu ‘Nilaumu moyo wangu au macho nambieni ‘; au Ati elimu na mali, ni ipi uchaguwayo?’ ama ‘Popo ni mnyama au ndege? ‘, swali watu walilojiuliza wakati wa zama za siasa huko Zanzibar kwa maana ya kueleza kuwa mtu fulani hubadili msimamo wake kila mara.

Hata Muyaka bin Haji al-Ghassany amejiuliza swali kuhusu huyo kasa ali-potunga ‘Munambie ‘Huyu kasa, ni halali,

ni haramu’. Yumkini naye Haji Gora pia anamkusudia mtu mwenye tabia fulani, lakini nadhani jawabu yake imo katika shairi lenyewe na huyo kasa ni sitiari ya wenyeji huko visiwani:

Kiumbe kinapoishi, ni pake mazaliyoni Kwengine habadilishi, wa pwani huzaa pwani Mbona kasa haitoshi, hutagia ufukweni Mkubwa ulalamishi, mnyama au samaki?

ZANZIBAR FAST DISPATCH UK

KWA HUDUMA ZA HARAKA KUPELEKA MIZIGO YAKO

ZANZIBAR KWA NJIA YA NDEGE.

07588550153

MATANGAZO

KWA KUFIKISHA UJUMBE WAKO HARAKA KABISA TUMIA

ZANZIBAR DAIMA ONLINE, JARIDA LA MTANDAONI LENYE WASOMAJI WASIO SAMBAA KWENYE ZAIDI YA

NCHI 37 DUNIANI.ZANZIBAR DAIMA ONLINE,

JARIDA LA KILA WIKI MBILI

TANGAZANA

ZANZIBAR DAIMA

Page 21: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

PAGE

40

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

41

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

40

thanks for everything mom. . I Love You

Min re veliquis ut fugiam, sintion nes minis imi, officii sseritis aut as ea aut laut volorumquis magnatum dolo quist alit re, cullaciis exerescim quo ist aut eum quas es ut apis nulparciet quia di sunt

Mara nyingi huwa hatujiangalii we-nyewe kwanza kabla ya kuwakosoa wen-gine.

Kwa wiki kadhaa sasa kumeibuka mvutano kati ya Serikali ya Jam-huri ya Muungano wa Tanzania na wanachama wen-zake watatu ka-tika Jumuiya ya Af-rika mashariki (EAC), Kenya, Uganda, na Rwanda. Nchi ny-

ingine katika Jumuiya hiyo ni Burundi.

Kikubwa katika mvutano huu ni kutengwa kwa Tan-zania na nchi hizo nne katika mchaka-to wa kuharaki-sha Umoja wa kisia-sa. Hapo mapema Marais Uhuru Ke-nyatta wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda walikutana Momba-sa kuzungumzia juu

ya kuimarisha uhu-siano wa kibiashara baina ya nchi zao, ikiwa ni pamoja na mpango wa ujenzi wa reli kutoka Ke-nya hadi nchi zao na kuitumia bandari ya Mombasa kwa bid-haa zinazoagizwa kutoka n’gambo.

Tanzania ilikuja juu ikataka ielezwe kwanini haikualikwa Mombasa. Inaele-kea haikupata jibu na kama ilipewa basi halikuiridhisha.

Sasa unga umezidi

Sitta analalama na EAC, anasitasita na ya Zanzibar

Wahenga husema “mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mc-hungu”. Huu ni usemi wenye funzo kubwa kwa binadamu .

Samuel Sitta Waziri wa ush-

irikiano wa Afrika Mashariki katika

Serikali ya Tanzania.

Na Mohammed Abdulrahman

kujaa maji. Baada ya kufahamika kwamba mchakato wa kuwa na Umoja wa Kisiasa (Shirikisho la Afrika Mashariki) umepata kasi, hatimaye Waziri wa Tanzania wa Ush-irikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta amesema Tanzania haikubaliani na juhudi za kuharakisha Umoja wa Kisiasa. Awali ilisemekana kuwa Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ambaye hakuhudhuria mkutano wa Mombasa ameuidhinisha mpango huo, lakini Burundi baadaye il-isema haitoidhinisha miradi iliopangwa na nchi hizo tatu na ilioitenga nchi nyingine.

Sasa inasemekana mawaziri kutoka nchi hizo tatu watakutana Oktoba Kigali,Rwanda . Yaliokubaliwa na nchi hizo kama hatua za kutekelezwa kufanikisha azma yao ni :

— Kuondoa vikwazo vya kibiashara na kiuchumi

— Kuzinduliwa kwa ujenzi wa kuitanua bandari ya Mombasa

— Kuanzisha vitambulisho vya pamoja,

Sitta amesema ameshangazwa na hatua ya kuitenga Tanzania. Pia alisema kwamba Tanzania, hairuhusu kitambulisho cha pamoja kutumika katika nchi zote tano wanachama, akisisitiza kuwa raia wa nchi mwanachama anapoingia Tanza-nia lazima taratibu za uhamiaji zifuatwe.

Kadhalika Sitta pia amesema kuwa kuna mambo manne ambayo hayajakamilika na ambayo Tanzania inadai lazima yakamilish-we kwanza nayo kabla ya kuufikia Umoja wa Kisiasa. Nayo ni:

— Ushuru wa forodha,— Soko la pamoja na — Sarafu ya pamoja.

Sababu nyengine aliyoitaja ni kuwa karibu asilimia 84 ya Watanzania walitoa maoni ya kupinga kuharakishwa Umoja wa Kisiasa yaani Shirikisho la Afrika Mashariki .

Ni jambo adhimu kuheshimu matakwa

ya walio wengi, lakini iweje kwa mwana-siasa huyu mkongwe kuliangalia hilo kwa upande mmoja tu.

Demokrasia ni kuheshimu na kutekeleza ya walio wengi na kulinda masilahi ya walio wachache. Maoni ya Wazanzibari nayo je? Kwa miaka 49 sasa kero za Muungano hazikupata ufumbuzi baada ya mambo 11 yaliokubaliwa awali katika Mkataba ulioun-da Muungano sasa kufikia 22 na un-apoyanyambua yanafikia 37. Nasema hivi kwa sababu Gasi Asili na Mafuta tayari ni mambo mawili na Bandari, Posta na Simu ni matatu.

Sitta anajikanganya: Katika sakata hili anaelekea amesahau mapema. Mtazamo wa wale wote waliouunga mkono Muun-gano wa Tanganyika na Zanzibar waka-ti ulipoundwa pamoja na wa wale wote waliokuwa na hisia za uzalendo wa Ki-afrika ulikuwa kwamba Muungano huo ni hatua ya mwanzo kuelekea Shirikisho la Afrika Mashariki.

Bahati mbaya miaka 50 tangu Muungano huu hakuna nchi jirani iliyousogelea. Sitta angejiuliza kwa nini ? Bila shaka jibu limo kwenye maelezo yake , aliposema kwam-ba Tanzania ina uzoefu wa matatizo ka-tika Muungano wake yenyewe na haitaki kwenda haraka kufikia Shirikisho la Afrika Mashariki.

Hivyo ilikuaje Mheshimiwa waziri anasi-mama kidete kulipinga Shirikisho la kisiasa kwa hoja za kulinda mamlaka ya Tanza-nia wakati hoja hizo hizo anazikandamiza zinapodaiwa na Zanzibar?

Sitta ni mtetezi mkubwa wa mfumo huu wa sasa wa serikali mbili na ni mmoja wa wale wanaotajwa kuwa na kiu ya kugom-bea urais wa Tanzania 2015.

Katika mkutano wake na waandishi habari alisema huenda nchi hizo tatu za Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeitenga Tanzania kwa sababu zina ajenda ya siri. Serikali ya Muungano inalalamika kuhu-

Nionavyo

Page 22: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

43

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

su jitihada za Uganda, Ke-nya na Rwanda za kuunda Shirikisho lakini kwa miaka zaidi ya 30 imefunika chini ya busati nafasi ya Zanzi-bar ndani ya Jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki.

Nimalizie kwa matamshi ya Sitta kwamba “Ikiwa viongozi wa Rwanda,

Uganda na Kenya , wame-kubaliana kuandika Ra-simu ya Katiba ya Shiriki-sho la Kisiasa, wanapswa kutambua kuwa Katiba itakayopatikana itakuwa batili kwa sababu haikua-muliwa na wananchi wa nchi husika bali watawala.”

Ninaamini kwa kauli hiyo,

watawala wetu wa Tan-zania watatambua pia kwamba Rasimu ya Katiba ya Tanzania itakuwa ba-tili ikiwa haitapata ridhaa ya walio wengi Zanzibar na Tanganyika. Suala la Muungano haliwezi ku-pata suluhisho maridhawa pindi litaendelea kujadiliwa kichama, wakati hilo ni

suala la kitaifa. Viongozi wa Bara wanapolia na ya kina Museveni, Kenyatta na Kagame hawana budi kutafakari kilio cha muda mrefu cha Wazanzibari kuhusu Muungano.

Tutazame ya historia: Kuna miungano mingi iliyoundwa duniani, lakini

mingi imekufa kama ule wa Kisovieti. Au ule wa Czechoslovakia ambao umegawika na kuwa nchi mbili Cheki na Slovakia. Kila mmoja ina mamlaka yake.

Kuna wanasiasa wetu wanaojigamba kuwa: “Hapa haiwezekani”, wa-

nasahau hata wenzao wa mifano niliyoitaja waki-jigamba hivyo hivyo, lakini hatimaye umma ulip-oamua sasa lazima yab-adilike waliridhia matakwa ya raia, baada ya kuiona hatari ya kuwa vuguvugu la umma linapovuma huwa halizuiliki.

USIIMWAGIE TINDIKALI ZANZIBAR SI UBINADAMU , SI UTU LIMEDHAMINIWA NA ZANZIBAR DAIMA COLLECTIVE

Page 23: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

PAGE

44

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

45

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

44

Naulilia uwanja wa Mnazi Mmoja

“Tusiupe fursa wakati kuja kutuhukumu. Linalo-hitajika nikuhakikisha kiwanja cha Mnazi Mmoja kinarudi katika hadhi yake kama kilivyoipata kuwa.”Kiwanja cha Mnazi

Mmoja kina historia ya muda mrefu in-gawa kwa hivi sasa asilimia isiopungua 25 ya kiwanja hicho kimevamiwa na maji ya chumvi na kush-indikana kwa wana michezo kuzitumia sehemu hizo, seh-emu zilizoathirika ni zile ambazo zamani zilikuwa zikicheze-

wa mchezo wa Krik-eti.

Katika mwaka wa 1999 mwandishi wa makala haya ali-fanya utafiti mdogo kujuwa namna ki-wanja hicho kina-vyotumika pamoja na kile cha Coopers ambacho kwa sasa kinaitwa kiwanja cha Maisara. Katika

utafiti huo ilijionye-sha kuwa sio chini ya timu 8 zinami-liki eneo la kudumu la kuchezea mpira wa miguu katika ki-wanja cha Mnazi Mmoja na kuna timu zisiopungua 20 kwa nyakati tafauti huki-tumia kiwanja hicho mara nyengine huwa katika nyakati za asubuhi, siku za

mwisho wa wiki na siku za mapumziko ambapo skuli huwa zimefungwa.

Kiwanja cha Mnazi Mmoja kiliasisiwa na kutangazwa ras-

mi kuwa ni eneo la wazi mnamo mwaka 1873 pale mfalme Seyyid Barghash bin Said alipotangaza kuwa kiwanja hicho ni Wakfu wa Jamii na kitumiwe na wa-

nanchi kwa ajili ya shughuli za kidini ikiwa pamoja na ku-somwa kwa Mau-lidi, mashindano ya riadhaa, mchezo wa mpira wa miguu pamoja na sherehe za Sikukuu. Kuto-kana na tamko hilo la Mfalme Barghash kiwanja hicho kili-nusurika kujengwa

majengo. Na Balozi mkazi wa Uinger-eza (British Resi-dent) naye alikubali kuwa ni jambo jema kiwanja cha Mnazi Mmoja kibakie kuwa ni eneo la wazi na litumike zaidi kwa michezo, kwa kuwa Balozi huyo na wen-zake wakipenda kwenda kuangalia

“Timu za Malindi, Vikokotoni, Kikwajuni, Ujamaa, Miembeni zilikuwa na viwanja vya ku-dumu hapo Mnazi Mmoja na zikifanya mazoezi ya kila siku hata katika siku za Masika.”

“Katika awamu ya tano ya Dr. Salmin Amour Serikali ilichukua hatu za kuuratibu huu uwanja na kuu-fanya usituwame maji. Matokeo yake ilikuwa kama kutonesha kidon-da kwani kuanzia hapo hadi hii leo kiwanja hicho kimekuwa kinakaa maji kwa wingi na wengine wanafika kusema kuwa kutuwama kwa maji kunatokana na mabadiliko ya tabianchi kitu am-bacho sio kweli.”

mchezo wa Kriketi ukichezwa Mnazi Mmoja mwisho wa wiki.

Katika karne iliyo-fuata Balozi mwen-gine Mkazi kupipi-tia Majlisi Tashrii (Baraza la Kutunga Sheria au Legisla-tive Council “LEG-CO”) alithibitisha na kuliidhinisha tena eneo hilo alipotam-ka kuwa eneo la Mnazi Mmoja lisitu-mike kwa shughuli zozote zile zaidi ya zile zilizoidhinishwa na Sultan Barghash. Maelezo hayo yamo katika gazeti Rasmi la Serikali la mwaka 1903.Ili kuweza kukidu-

misha kiwanja hicho kiwe katika hali ya haiba na kifanyiwe matengenezo mara kwa mara, katika mwaka wa 1924 Balozi mwengine wa Uingereza alise-ma kuwa kiwanja cha Mnazi Mmoja kiwe chini ya uon-gozi wa mji yaani Township Council. Katika mwaka wa 1957 Baraza la Ma-nispaa lilipewa dha-mana na jukumu la utunzaji wa uwanja huo ambao kwa wakati huo ulikuwa ukichezewa mi-chezo miwili mikuu, nayo ni mpira wa miguu na kriketi. Ku-likuwepo na viwanja vinne vya kriketi na

Na Babu Jimba Michezo

Page 24: Zanzibar Daima Online, Toleo la Tano

PAGE

46

Y O U RLO G OH E R E

UKURASA

47

JARIDA LA KILA MZANZIBARIwww.zanzibardaima.net Toleo 05 - 2013

ZANZIBARD A I M AO N L I N E

UKURASA

46

viwanja vitatu vikuu kwa mchezo wa soka na viwanja vyengine vidogovidogo vi-sivyopungua saba. Klabu za soka ambazo zikiutumia zaidi uwanja huo zilikuwa pamoja na Malindi, Vikokotoni, Kik-wajuni, Miembeni, Ujamaa, New Kings, Africa Sport na Hadhrami. Wachezaji maa-rufu kutoka vilabu mbalim-bali walikuzwa vipaji vyao kwenye kiwanja hicho. Mnazi Mmoja ni kiwanja kilichoweza kufikiwa na wachezaji maarufu kutoka nchi mbalimbali duniani akiwemo Len Shackleton

mchezaji soka wa Uinger-eza,. Kwa upande wa wa-chezaji wa kriketi Hanif wa Pakistan, Nat Adcok, T.L. Goddard, H.J. Tayfield, R.J. Westcott na C.B. van Ryneveld wa Afrika ya Kusi-ni nao pia walicheza Mnazi Mmoja.

Watu mbalimbali walivu-tiwa na eneo kubwa kama hilo lililokuwa huru kwa watu kulitumia kwa mi-chezo mbalimbali. Westcott mchezaji kriketi wa Afrika ya Kusini alisema kuwa “Si-japata kuona uwanja un-aotumika kwa kriketi na futboli kwa wakati mmo-ja katika maisha yangu.”

Hanif mchezaji maarufu wa kriketi wa Pakistan katika mchezo wa Test naye ali-wahi kusema haya: “Sikua-mini kuwa nitaweza kuwa-ona wazalendo wa Zanzibar wanacheza kriketi ya hali ya juu. “

Na mlinda mlango maarufu wa timu ya Taifa ya soka ya Uganda kwenye miaka ya 1970 Massagaje yeye alitamka kinaga ubaga bila ya kutafuna maneno kauli ifwatayo “Kwetu Ugan-da hakuna uwanja kama huu wa Mnazi Mmoja na kama ungekuweko, Ugan-da tungekuwa mbele sana kisoka, nawaonea gere

watu wa visiwani kuwa na hazina kama hii.”Timu za Malindi, Vikokotoni, Kikwajuni, Ujamaa, Miem-beni zilikuwa na viwanja vya kudumu hapo Mnazi Mmoja na zikifanya mazoezi ya kila siku hata katika siku za Ma-sika. Vilabu hivyo vikiweza kufanya mazoezi bila ya kuathirika kutokana na njia maalumu zilizotengenezwa chini ya ardhi ambazo zikin-yonya na kuvuta maji na kuyasukuma baharini pasi eneo hilo la Mnazi Mmoja kutwama maji. Jambo la kusikitisha sisi tuliokulia ka-tika miaka ya 60 tunakuwa na kilio nacho ni vile kiwanja

hicho kilivyovamiwa na maji ya chumvi na asilimia 25 ya kiwanja hicho kuwa haki-wezi tena kutumika.

Katika awamu ya tano ya Dr. Salmin Amour Serikali ilichu-kua hatu za kuuratibu huu uwanja na kuufanya usitu-wame maji. Matokeo yake ilikuwa kama kutonesha kidonda kwani kuanzia hapo hadi hii leo kiwanja hicho kimekuwa kinakaa maji kwa wingi na wengine wanafika kusema kuwa kutuwama kwa maji kunatokana na mabadiliko ya tabianchi (Cli-mate change) kitu ambacho sio kweli.

Jambo linalotaka lifanyike kwa haraka ni kuuhami uwanja huu na kuurejeshea haiba yake, ingawa kuliku-wa na fununu kuwa kiwan-ja hicho kilitaka kugeuzwa kuwa sehemu ya maduka ya wafanya biashara kama ilivyonukuliwa katika gazeti la Serikali la Zanzibar leo la tarehe 4 Septemba 2012.

Tusiupe fursa wakati kuja kutuhukumu. Linalohitajika nikuhakikisha kiwanja cha Mnazi Mmoja kinarudi kati-ka hadhi yake kama kili-vyoipata kuwa.

When you want to get your message in front of the audience, BXD Magazine is the first and the best place to go!Wapenzi Wasomaji Wetu,Toleo hili Namba 5 la Zanzibar Daima Online lilikuwa litoke Jumatatu ya tarehe 7 Oktoba 2013, lakini kutokana na matatizo yaliyokuwa nje ya uwezo wetu tulishindwa kulichapisha kwa wakati unaostahiki. Kwa hili tunawaomba radhi sana kwa usumbufu wowote unaoweza kuwa ulitokea kwenu. Tunawashukuru pia kwa kuwa pamoja nasi, huku tukiwaahidi kufanya kila lililo kwenye uwezo wetu ili matatizo kama haya yasitokezee tena.Mhariri Mkuu