uzalishaji bora wa mahindi -...

9
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Idara ya Sayansi ya Udongo P. O. Box 3001, Morogoro, Tanzania Tel.: +255 23 260 4 649 Uzalishaji bora wa mahindi Matumizi sahihi ya mbolea na mbinu nyingine za kilimo nchini Tanzania

Upload: others

Post on 12-Jul-2020

18 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Uzalishaji bora wa mahindi - ASHCafricasoilhealth.cabi.org/wpcms/wp-content/uploads/2014/05/71-SUA... · 1 Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Idara ya Sayansi ya Udongo P. O. Box

1

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo,Idara ya Sayansi ya UdongoP. O. Box 3001, Morogoro, Tanzania Tel.: +255 23 260 4 649

Uzalishaji bora wa mahindi

Matumizi sahihi ya mbolea na mbinu nyingine za kilimo nchini Tanzania

Page 2: Uzalishaji bora wa mahindi - ASHCafricasoilhealth.cabi.org/wpcms/wp-content/uploads/2014/05/71-SUA... · 1 Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Idara ya Sayansi ya Udongo P. O. Box

2

Andaa mashamba mapema kabla msimu wa kupanda haujaanza ili kupanda kwa wakati unaotakiwa.

Unaweza kufyeka, kung’oa visiki au kulima.

Matumizi ya trekta, power tillers na jembe la kukokotwa na wanyama yanapunguza nguvu kazi kwani vinachimbua udongo na kuufanya kuwa tifutifu. Hii husaidia mizizi ya mimea kupenyeza ardhini kirahisi na udongo kuhifadhi maji.

Kuandaa shamba

Page 3: Uzalishaji bora wa mahindi - ASHCafricasoilhealth.cabi.org/wpcms/wp-content/uploads/2014/05/71-SUA... · 1 Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Idara ya Sayansi ya Udongo P. O. Box

3

Tumia mbegu zilizoboreshwa ili kupata mazao mengi na bora.

Nafasi hizi zote hutoa mimea 44,000 katika heka.

Nafasi ya kupanda mahindi ni 90 sm kwa 30 sm (mbegu moja kwa shimo); 90 sm kwa 25 sm (mbegu moja kwa shimo) au 90 sm kwa 50 sm (mbegu mbili kwa shimo).

Kupanda

Page 4: Uzalishaji bora wa mahindi - ASHCafricasoilhealth.cabi.org/wpcms/wp-content/uploads/2014/05/71-SUA... · 1 Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Idara ya Sayansi ya Udongo P. O. Box

4

Mbolea za kupandia zinawekwa shambani kabla ya kupanda/kusia mbegu kwa kusambaza kwenye eneo husika na kuchanganya na udongo, au kwenye mistari au mashimo ya kupandia.

Zinapowekwa kwenye mashimo ni vyema kufukia mbolea kabla ya kuweka mbegu (kutenganisha mbolea na mbegu).

Aina ya mbolea zakupandia

Idadi ya mifuko ya kilo 50 kwa hektari

Idadi ya mifuko ya kilo 50 kwa ekari

Kiwango kwa kila shimo(kizibo cha soda)

DAP 3 1 ½Minjingu fosfati 2 1½ 1

Minjingu Mazao 4½ 2 1½

Mbolea za kupandia hasa Minjingu Phosphate na Minjingu Mazao zinahitaji hali maalum ya udongo ili ziweze kufanya kazi vizuri.

Kuweka mbolea

Page 5: Uzalishaji bora wa mahindi - ASHCafricasoilhealth.cabi.org/wpcms/wp-content/uploads/2014/05/71-SUA... · 1 Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Idara ya Sayansi ya Udongo P. O. Box

5

Palilia siku 14 hadi 21 baada ya mimea kuota. Magugu hunyonya virutubisho ardhini na yanaweza pia kuhifadhi wadudu na magonjwa.

Palilia kwa kung’oa kwa mkono, kwa mashine au kwa kutumua viua magugu (herbicides) kama inavyoshauriwa.

Palilia mara 2-3, kufuatana na hali ya magugu katika shamba.

Mbolea za kukuzia huwekwa kuzunguka kila shina la mimea au pande mbili au tatu au nne za kila shina.

Kupalilia

Page 6: Uzalishaji bora wa mahindi - ASHCafricasoilhealth.cabi.org/wpcms/wp-content/uploads/2014/05/71-SUA... · 1 Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Idara ya Sayansi ya Udongo P. O. Box

6

Fosfati (Phosphorus): Kupungua kwa kasi ya kukua na mashina kuwa membamba na mmea unakuwa na rangi ya zambarau. Rangi hii inaanzia pembeni mwa majani na kwenyemashina na baadaye husambaa kwenye jani lote.

Potashi (Potassium): Kupungua kasi ya ukuaji wa mimea na kudumaa.

Upungufu ukiwa mkubwa sehemu iliyoathirika inakauka (necrosis). Majani yanakuwa na michirizi ya manjano na vinundu nundu kama migongo ya bati (yellowish streaks and corrugated).

Naitrojeni (Nitrogen): Mmea unakuwa mdogo, mwembamba na hutoa suke dogo. Kama upungufu ni mkubwa sana mmea unaweza usitoe mhindi kabisa.

Dalili ya upungufu wa virutubisho

Page 7: Uzalishaji bora wa mahindi - ASHCafricasoilhealth.cabi.org/wpcms/wp-content/uploads/2014/05/71-SUA... · 1 Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Idara ya Sayansi ya Udongo P. O. Box

7

Maize streak virus, Smut (Fugwe) na Cob rot ni magonjwa yanayoshambulia mahindi.

Vikata shina (Cutworms) na Stalk borerni wadudu wanaoshambulia mahindi.

Tumia dawa na njia zinginezo ili kuzuia magonjwa na wadudu wanaoshambulia mimea.

Magonjwa na wadudu

Page 8: Uzalishaji bora wa mahindi - ASHCafricasoilhealth.cabi.org/wpcms/wp-content/uploads/2014/05/71-SUA... · 1 Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Idara ya Sayansi ya Udongo P. O. Box

8

Mahindi yakishakauka vizuri yanatenganishwa na bua alafu majani ya mhindi kutolewa.

Kausha juani kwa siku 3-4 ili kupunguza unyevunyevu kufikia kiwango kinachofaa kwa kuhifadhi (14%). Ni muhimu mahindi ikauke vizuri ili isioze ikiwekwa ghalani.

Pepeta halafu ondoa mahindi mabovu.

Changanya mahindi safi dawa za kuua wadudu kama vile Actellic Super.

Hifadhi kwa kuweka kwenye gunia na magunia kupangwa ghalani juu ya mbao yasiguse sakafu.

Vuna mahindi wakati kikonyo kimekuwa dhaifu na mahindi yanaangalia chini.

Kuvuna na kuhifadhi

Page 9: Uzalishaji bora wa mahindi - ASHCafricasoilhealth.cabi.org/wpcms/wp-content/uploads/2014/05/71-SUA... · 1 Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Idara ya Sayansi ya Udongo P. O. Box

9

Kufanya kazi kwa pamoja na wadau/wabia kutayarisha taarifa zinazohusu mbinu husishi za afya ya udongo