kusujudu juu ya udongo

54
Mfululizo wa Masuala ya Kifikihi as - Sujuud ‘Ala ‘l-’Ardh ‘Alaa Dhaw’i ‘l-Kitaab wa ‘s-Sunnah KUSUJUDU JUU YA UDONGO KWA MUJIBU WA KITABU NA SUNNA Kimeandikwa na: Sheikh Ja’far Subhani Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba Selemani Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page A

Upload: alitrah-foundation

Post on 07-Mar-2016

436 views

Category:

Documents


1 download

DESCRIPTION

Kusujudu juu ya udongo ni suala ambalo wanachuo wetu wamehitalifiana; ndani ya madhehebu moja na kati ya madhehebu. Kwa hiyo hii sio hitilafu ya madhehebu, bali ni hitilafi ya wanachuo wa madhehebu zote wamehitilafiana juu ya suala hili. Lakini bahati mbaya Waislamu wengi hawaitambui hitilafu hii kwa usahihi na hivyo kuongelea katika dhana na kusababisha mizozo isiyokuwa na maana. Kutokana na hali hii Sheikh wetu, Jafar Subhani amelifanyia utafiti wa kina suala hili na kuweka wazi asaili ya hitilafu hii, kisha akamuachia msomaji mwenyewe kutoa uamuzi.

TRANSCRIPT

Page 1: Kusujudu juu ya udongo

Mfululizo wa Masuala ya Kifikihi

as - Sujuud ‘Ala ‘l-’Ardh‘Alaa Dhaw’i ‘l-Kitaab wa ‘s-Sunnah

KUSUJUDU JUU YAUDONGO

KWA MUJIBU WA KITABU NA SUNNA

Kimeandikwa na:Sheikh Ja’far Subhani

Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba Selemani

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page A

Page 2: Kusujudu juu ya udongo

'Haki ya kunakili imehifadhiwa na:AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 9987 - 427 - 48 - 0

Kimeandikwa na:Sheikh Jafar Subhani

Kimetarjumiwa na:Ustadh Lubumba

Kimehaririwa na:Ustadh Abdallah Mohamed

Kimepangwa katika Kompyuta na:Ukhti Pili Rajab

Toleo la kwanza: Machi, 2008Nakala: 1000

Kimetolewa na kuchapishwa na:Al-Itrah Foundation

P. O. Box 19701, Dar-es-Salaam, TanzaniaSimu: +255 22 2110640

Simu/Fax: +255 22 2127555Email: [email protected]: www.alitrah.orgOnline: www.alitrah.info

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page B

Page 3: Kusujudu juu ya udongo

YALIYOMOKusujudu juu ya udongo kwa mujibu wa kitabu na Sunna...............2

Kusujudu juu ya udongo.................................................................. 4

Tofauti za wanazuoni wa sheria kuhusu sharti za kitu cha kusujudujuu yake.............................................................................................5

Tofauti kati ya msujudiwa na kisujudio..........................................10

�Sijda� Kilugha (ya kiarabu).............................................................11

Siri ya kuachwa wazi paji la uso katika sijda.................................13

Suna ya Mtume katika kusujudu zama zake na baada yake.............16

Kipindi cha mwanzo: kusujudu juu ya ardhi....................................17

Kupoza changarawe ili kusujudu juuyake................................................................................................. 19

Amri ya kufikisha udongo kwenye paji...........................................20

Amri ya kuondoa kilemba kwenye paji la uso................................22

Mwenendo wa Mtume katika kusujudu...........................................23

Mwenendo wa maswahaba na Tabiina katika kusujudu..................25

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page C

Page 4: Kusujudu juu ya udongo

D

Hatua ya pili:Kuruhusiwa kusujudu juu ya khumra na mkeka.............................27

Hatua ya Tatu:Kusujudu juu ya nguo kwa udhuru..................................................30

Matokeo ya uchunguzi.....................................................................33

Ni ipi siri ya kuchukua kipande cha udongo Tohara.......................35

Mwisho wa Safari............................................................................39

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page D

Page 5: Kusujudu juu ya udongo

E

Neno la mchapishaji

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabukwa jina la: "Al-Sujuud Alal-Ardh" Sisi tumekiita: "Kusujudu juuya udongo."

Kitabu hiki, "Kusujudu juu ya udongo" ni matokea ya utafiti wakielimu uliofanywa na Mwanachuoni wa Kiislamu, Sheikh JafarSubhani.

Sheria ya Kiislamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika na kila jambohuku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanayompata mwanadamukatika sekta zote za maisha yake.

Wanachouni wa Kiislamu kama kawaida ya wanadamu wamehiti-lafiana katika hukumu ndogo ndogo katika matendo ya ibada, lakinikama ilivyo, tofauti ndogo kati ya wanachuo kwa wafuasi inakuwani mlima wa tofauti na kusababisha zongo lisilo na maana. Mamboambayo wanachuo wetu wamehitilafiana si katika asili au misingi yadini, na isitoshe ni mambo machache sana ukilinganisha na yaletunayokubaliana nayo.

Kusujudu juu ya udongo ni suala ambalo wanachuo wetu wamehi-talifiana; ndani ya madhehebu moja na kati ya madhehebu. Kwahiyo hii sio hitilafu ya madhehebu, bali ni hitilafi ya wanachuo wamadhehebu zote wamehitilafiana juu ya suala hili. Lakini bahatimbaya Waislamu wengi hawaitambui hitilafu hii kwa usahihi nahivyo kuongelea katika dhana na kusababisha mizozo isiyokuwa namaana. Kutokana na hali hii Sheikh wetu, Jafar Subhani amelifanyia

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page E

Page 6: Kusujudu juu ya udongo

utafiti wa kina suala hili na kuweka wazi asaili ya hitilafu hii, kishaakamuachia msomaji mwenyewe kutoa uamuzi.

Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maen-deleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukwelihuu, Taasisi yetu ya ’Al-Itrah Foundation’ imeona ikitoe kitabu hikikwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yale yale yakuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ilikuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii.

Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemani (Lipumba)kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vileviletunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyinginehadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

Mchapishaji:Al-Itrah FoundationS. L. P. 19701Dar-es-Salaam, Tanzania.Simu: +255 22 2110640

F

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page F

Page 7: Kusujudu juu ya udongo

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 1

Page 8: Kusujudu juu ya udongo

2

Kusujudu juu ya udongo

KUSUJUDU JUU YA UDONGOKWA MUJIBU WA KITABU NA SUNNA

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehma, Mwenye kurehemu

Kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu mlezi wa ulimwengu.Rehma na Amani zimfikie mbora wa viumbe na hitimisho la mitumeWake, pia kizazi chake kitakatifu ambacho ndio kasha la elimu yakena hazina ya mafunzo yake.

Hakika Uislamu ni imani na sheria. Imani ni kuamini MwenyeziMungu, Mitume wake na Siku ya Mwisho. Na sheria ni hukumu zaMwenyezi Mungu ambazo zina jukumu la kumpa mwanadamumaisha bora na kumhakikishia mafanikio ya dunia na akhera.

Sheria ya kiisilamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika na kila jambohuku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanayompata mwanadamukatika sekta zote za maisha yake, hivyo Mwenyezi Mungu akasema:

“Leo nimewakamilishia dini yenu na kuwatimizieni neemayangu na nimewapendeleeni Uislamu uwe dini yenu.”1

1 Al-Maida:3.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 2

Page 9: Kusujudu juu ya udongo

3

Kusujudu juu ya udongo

Isipokuwa kuna masuala madogo madogo ambayo wanavyuoni washeria wametofautiana kwa sababu ya kutofautiana kwao kuhusuriwaya ambazo zimenasibishwa kwa Mtume. Jambo ambalo lime-pelekea kutofautiana kuhusu masuala madogo madogo ya sheria.

Kwa kuwa ukweli hutokana na uchunguzi basi hakika katikamtiririko wa masomo haya tumejaribu kuliweka swala hili juu yameza ya uchunguzi, kwani huenda ikawa ndio njia ya kuunganishamtazamo na kupiga hatua katika uwanja huu.

Kwani tofauti iliyopo si katika asili na misingi ya dini hata ipelekeekuwa na uadui na chuki, bali tofauti iliyopo ni kuhusu riwaya zili-zonasibishwa na Mtume, nalo ni jambo dogo ukilinganisha namambo mengi ambayo tunaafikiana kati ya madhehebu za Kiislamu.

Na muongozo wetu katika njia hii ni kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote kwapamoja wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya MwenyeziMungu iliyo juu yenu, mlipokuwa maadui na akaziunganishanyoyo zenu, hivyo kwa neema Zake mkawa ndugu.” (al-Imran;3:103).

Sheikh Jafar SubhanyTaasisi ya Imamu Sadiq (a.s.)Qum

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 3

Page 10: Kusujudu juu ya udongo

4

Kusujudu juu ya udongo

KUSUJUDU JUU YA UDOGO

Kati ya alama dhahiri zaidi za utumwa, unyenyekevu na udhalili wakiumbe kwa muumba Wake ni kusujudu. Kupitia kusujudumuuminu hutilia nguvu utumwa wake kwa Mwenyeezi Mungu. NaMuumba aliyetukuka humkadiria mja Wake udhalili na utiifu nahumtiririshia mwenye kusujudu mtiririko wa fadhila Zake na hisaniYake kubwa. Kwa ajili hiyo imepokewa ndani ya baadhi ya riwayakuwa: �Ndani ya sijda ndipo mja awapo karibu mno na MolaWake�.

Kati ya ibada zote, Swala ndio ngazi pekee inayomtofautishamuumini dhidi ya kafiri, huku kusujudu kukiwa ni nguzo miongonimwa nguzo zake, basi hakuna alama ya dhahiri mno katika kudhi-hirisha unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu kuliko kusujudu juu yaudongo, mchanga na changarawe, hii ni kutokana na unyenyekevuwa dhahiri na bayana unaopatikana hapo kuliko ule unaotokana nakusujudu juu ya mkeka na kirago, ukiachia mbali ule unaotokana nakusujudu juu ya mavazi ya kifahari, matandiko, dhahabu na fedha.Japokuwa katika hali zote hizo ni kusujudu, lakini utumwa unadhi-hirika mno katika fungu la mwanzo kwa kiwango kisichoweza kud-hihiri katika fungu lingine.

Shia Imamia hulazimika kusujudu juu ya udongo safarini na nyum-bani, na wala hawana mbadala ila kile kiotacho toka aridhini kwasharti kisiwe chenye kuliwa wala kuvaliwa, wala hawaoni ni sahihikatika hali ya kuswali, kusujudu juu ya kile kisichokuwa udongowala kisichoota toka aridhini kwa kufuata Sunna iliyothibiti kwawingi toka kwa Mtukufu Mtume na kizazi chake na maswahaba

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 4

Page 11: Kusujudu juu ya udongo

5

Kusujudu juu ya udongo

zake.Itadhihiri - ndani ya uchunguzi - kuwa kulazimika kusujudu juu yaudongo au kilichoota toka aridhini ilikuwa ndio Sunna ya maswaha-ba na kitendo cha kuacha Sunna hiyo kilizuka zama za baadaye.

TOFAUTI ZA WANAZUONI WA SHERIA KUHUSUSHARTI ZA KITU CHA KUSUJUDU JUU YAKE

Waislam wote wameafikiana juu ya wajibu wa kusujudu ndani yaSwala, mara mbili ndani ya kila rakaa moja, pia hawajatofautiana juuya msujudiwa kwani kwa hakika msujudiwa ni Mwenyezi Munguambaye husujudiwa na vile vilivyomo mbinguni na ardhini kwakutaka na kutotaka2

Mbiu ya kila muislamu ni kauli ya Mwenyezi Mungu:“Msilisujudie jua wala mwezi, bali msujudieni MwenyeziMungu aliyeviumba.”3

Ispokuwa wametofautiana juu ya sharti za kitu cha kusujudu juuyake; namaanisha kile anachotumia mwenye kusujudu kuweka pajilake juu yake. Kwa Shia Imamia kwao ni sharti kitu hicho cha kusu-judu juu yake kiwe ni udongo (Ardhi) au kiotacho toka ardhini kisi-choliwa wala kuvaliwa, kama vile mkeka na kirago na kina-chofanana na hivyo.

Madhehebu mengine yamewakhalifu juu ya hilo, na zifuatazo ni

2 Inaashiria kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na viliomo mbinguni na katika ardhivinamsujudia Mwenyezi Mungu tu vikitaka visitake. Na vivuli vyao asubuhina jioni.� Ar-Raadi: 153 Fuswilat: 37

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 5

Page 12: Kusujudu juu ya udongo

6

Kusujudu juu ya udongo

nukuu za maoni tofauti: Sheikh Tusi4 amesema: - Anabainisha maoni ya Wanavyuoni washeria:- Pasipo na dharura haisihi kusujudu ila juu ya udongo au kio-tacho aridhini kisicholiwa wala kuvaliwa kuanzia pamba hadi katani.Wanavyuoni wa kisunni wamekwenda kinyume kuhusu hilo, waowameruhusu kusujudu juu ya pamba, katani, manyoya ya mnyama,sufu na mengineyo- mpaka akasema:- Haisihi kusujudu juu kitu kili-cho mwilini kama vile kunjo la kilemba, sehemu ya joho na ukosi wakanzu, na kauli hii ndio ya Shafi�i na imepokewa toka kwa Ali, IbnuUmar, Ubada bin Swamit, Malik na Ahmad bin Hambali.

Abu Hanifa na wenzake wamesema: �Iwapo atasujudu juu ya ali-chokibeba kama vile nguo iliyo mwilini basi itatosheleza. Na iwapoatasujudu juu ya kisichoachana naye, mfano atandike mkono wakena kusujudu juu yake basi itamtosheleza lakini kufanya hivyo nikaraha, hilo limepokewa toka kwa Al-Hasan Al-Basariyu5.

Al-Allamah Al-Hilli6 amesema - Akibainisha maoni ya Wanavyuonikuhusu kitu cha kusujudu juu yake: �Haisihi kusujudu juu ya kitukisicho udongo wala kisicho mmea wake kama vile ngozi na sufu,hili ni kwa wanavyuoni wetu wote. Wanavyuoni wote wa kisunniwamekubaliana kwa kuruhusu7.

Mashia wamewafuata Maimamu wao katika hilo ambao wao ndiopacha wa kitabu na mwenza wake kwa mujibu wa Hadithi ya vizito4- Ni mwanachuoni wa Kishia wa karne ya tano, ana vitabu na maandishi mbal-imbali. Amezaliwa mwaka 385 na akafariki mwaka 460 A.H., ni mwanafunzi waSheikh Al-Mufid (336-413 Hijiriya) na As-Sayyid As-Sharifu Al-Murtaza (355-436 Hijiriya) Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao.5- Al-Khilafu: 1/357-358, suala la 112-113 kitabu cha Swala.6 - Al-Hasan bin Yusuf bin Al-Mutahhari Al-Hilliy (348-726 A.H.) Na yeye nikiongozi wa Mashia katika karne ya saba na karne ya nane. Hajaonekana katikazama mfano wake ila katika vipindi mahsusi.7 At-Tadhkiratu: 2/434, suala la 100.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 6

Page 13: Kusujudu juu ya udongo

7

Kusujudu juu ya udongo

viwili, hivyo sisi hapa tutakomea kutoa sehemu ndogo tu ya yaleyaliyopokelewa toka kwao kuhusu upande huu:

Amepokea As-Swaduq kwa njia yake toka kwa Hisham bin Al-Hakam kuwa alimuuliza Abu Abdillah: �Nipe habari ni kitu ganiinasihi kusujudu juu yake? Na ni kipi hakisihi kusujudu juu yake?�Akasema: �Haisihi kusujudu ispokuwa juu ya ardhi (udongo) au juuya kilichoota aridhini ila tu kile kinacholiwa au kuvaliwa.�Akamwambia: �Mimi ni fidia kwako, niambie ni kwa sababu ipi?�Akasema: �Kwa sababu kusujudu ni unyenyekevu kwa ajili yaMwenyezi Mungu hivyo haisihi sijda kuwa juu ya kinacholiwa aukuvaliwa kwa sababu watu wa duniani ni watumwa wa yalewanayokula na wanayoyavaa, na mwenye kusujudu, katika kusujudukwake huwa yupo katika ibada ya Mwenyezi Mungu, hivyoanapokuwa katika sijda haipasi aweke paji lake juu ya wanachokitu-mikia watu wa dunia ambao wamehadaika kwa hadaa yake�8

As-Swadiq (a.s.) amesema: �Kila kinachokuwa ni matumizi yamwanadamu katika chakula chake au kinywaji chake au mavaziyake basi haisihi Swala juu yake wala sijda ila tu kile kinachokuwani kutokana na mmea wa ardhi usiokuwa tunda kabla haujakuwanyuzi, ama ukiwa nyuzi haisihi kusujudu juu yake ispokuwa katikahali ya dharura”9.

Hivyo haipasi kuwalaumu Mashia wanapowafuata Maimamu waokwa kushikilia msimamo wa kusujudu juu ya ardhi au kilekioteshwacho na ardhi kisicholiwa wala kuvaliwa. Zaidi ya hapo nikuwa yale waliyopokea masunni katika mada hii yanaunga mkono8 Al-Wasailu: Juz: 3, Mlango 1 kati ya milango ya kitu cha kusujudu juu yake,Hadithi ya 1. Na kuna riwaya nyingine zenye madhumuni kama hayo zotezikionyesha kuwa lengo la kusujudu ambako ndio kujidhalilisha hakupatikani kwakusujudu juu ya kisichokuwa ardhi au kisichoota kisicholiwa wala kuvaliwa,chunguza.9 Al-Wasailu: 3, mlango 1 mlango wa kitu cha kusujudu juu yake, Hadithi ya 11.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 7

Page 14: Kusujudu juu ya udongo

8

Kusujudu juu ya udongo

mtazamo wa Shia na hilo litakudhihirikia ndani ya Hadithi zitaka-zokuja kupitia njia zao na itakubainikia kuwa Sunna ya Mtumeilikuwa ni kusujudu juu ya ardhi kisha ikaja ruhusa ya kusujudu juuya mkeka na kirago tu, na wala haijathibiti ruhusa ya tatu baliiliyothibiti ni kuzuwiliwa kwa ruhusa hiyo ya tatu kama utakavy-oona.

Mwanahadithi An-Nuuriyu ndani ya Al-Mustadrak amepokea kuto-ka kwenye (Daaimul-Islamu) toka kwa Jafar bin Muhammad tokakwa baba yake toka kwa babu zake toka kwa Ali (a.s.) kuwa Mtumewa Mwenyezi Mungu alisema: �Hakika ardhi ina huruma na nyinyimnatayamamu kutokana nayo na mnaswali juu yake katika uhaiwenu na yenyewe kwenu nyinyi ni sitara itoshayo kwa maiti wenu,hayo ni neema ya Mwenyezi Mungu ana kila sifa njema, hivyo kitubora anachosujudu juu yake mwenye kuswali ni ardhi safi.�10

Pia imepokewa toka kwa Jafar bin Muhammad (a.s.) kuwa amese-ma: �Inapasa mwenye kuswali aigusishe ardhi paji lake na awekeuso wake kwenye udongo kwa sababu kufanya hivyo ni kujidhalil-isha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.�11

As-Shaaraniy amesema: �Makusudio ni kudhihirisha unyenyekevukwa kichwa mpaka ardhi iguse uso wake ambao ndio kiungo boramno kati ya viungo vyake, sawa agusishe kwa paji lake au pua yakebali inawezekana kwa wengine ikawa kuweka pua ni bora kwa kuwa(jina pua ndani ya kiarabu) limetokana na majivuno na kiburi, hivyoatakapoiweka aridhini atakuwa kama kwamba amejitoa kwenyekiburi ambacho ni sifa ya Mwenyezi Mungu, kwani hakika hadhara10Mustadrakul-Wasailu: 4 mlango 10 mlango wa kitu cha kusujudu juu yake,Hadithi ya 1.11 Mustadrakul-Wasailu: 4/14, mlango wa 10 mlango wa kitu cha kusujudu juuyake, hadithi ya 2.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 8

Page 15: Kusujudu juu ya udongo

9

Kusujudu juu ya udongo

ya Mwenyezi Mungu ni haramu kuingia mtu mwenye chembe yakiburi angalau ndogo. Hakika hadhara hiyo ndio pepo kubwa ya hal-isi, na Mtume amesema: Hatoingia peponi mtu yeyote mwenyechembe yoyote ya kiburi moyoni mwake.�12

Imamu Al-Maghribiy Al-Maliky Al-Raw�daniy amenukuu kwakuvusha toka kwa Ibnu Abbas: �Mtu yeyote asiyeigusisha ardhi puayake pamoja na paji lake pindi anaposujudu basi Swala yake haisi-hi�13

Kama ilivyo asili ya kitendo cha kiibada ni amri ielekezwayo na mtumahususi, pia sharti zake na kanuni zake ni mambo mengine ambayoni lazima yabainishwe na kufafanuliwa na mfafanuzi na mfikishajiwa sheria, na hapa tunamaanisha Mtukufu Mtume wa MwenyeziMungu kwa sababu yeye ndiye kigezo kwa mujibu wa maelezo yaQur�ani tukufu na ndio mfafanuzi wa kitabu kitukufu na ni wajibukwa waislamu wote wajifunze hukumu za dini yao na vipengele vyasheria yao toka kwake.

Mwenyezi Mungu amesema: “Bila shaka mnao mfano mwemakwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa mwenye kumuogopaMwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na kumtaja MwenyeziMungu sana”14. “Na anachokupeni Mtume basi pokeeni na ana-chokukatazeni basi jiepusheni.”15

12Al-Yawaqiti wal-Jawahiri fi Aqaidil-Akabiri: Abdul-Wahabi bin Ahmad bin AliAl-Answariy Al-Misriy maarufu kwa jina la As-Shaaraniy (Ni kati ya wanavyuonimaarufu wa karne ya kumi): 1/164. Chapa ya kwanza.13 Muhammad bin Muhammad bin Sulaymani Al-maghribiy (Aliyefariki mwaka1049) amekusanya kitabu Al-Fawaidu min Jaamiul-Usulu na Maj’maul-Zawaidi:1/214 namba 1515.14 Al-Ahzab: 2115 Al-Hashri: 2.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 9

Page 16: Kusujudu juu ya udongo

10

Kusujudu juu ya udongo

TOFAUTI KATI YA MSUJUDIWA NAKISUJUDIO

Mara nyingi hudhaniwa kuwa kukazania kusujudu juu ya ardhi aukiotacho toka aridhini ni bidaa; na udongo unaotumika kusujudu juuyake hufikiriwa kuwa ni sanamu, na hawa ndio wasiotofautisha katiya msujudiwa na kisujudio. Na wanadai kuwa jiwe au udongounaowekwa mbele ya mwenye kuswali ni sanamu analoliabudumwenye kuswali kwa kuweka paji lake juu yake.

Lakini si lawama juu ya Shia iwapo ufahamu wa mpinzani utakuwafinyu na akawa hajatofautisha kati ya mambo mawili na akadai kuwakisujudio ndio msujudiwa, akalinganisha jambo la mwanatauhidi najambo la mshirikina eti kwa hoja ya ushirikiano wa nje. Akashikiliamuonekano na mtazamo ilihali kipimo ni kuchukua malengo nadhamira ya ndani, kwa sababu kwa muabudu masanamu, sanamu nimuabudiwa na msujudiwa, analiweka mbele yake na anasujudu nakurukuu kwa ajili yake.

Lakini mwanatauhidi ambaye anataka kuonyesha udhalili mpakakiwango cha mwisho yeye ananyenyekea kwa ajili ya MwenyeziMungu na anasujudu kwa ajili Yake anaweka paji lake na uso wakejuu ya udongo, jiwe, mchanga na changarawe kudhihirisha kuwayeye ni sawa na hivyo wakati wa kuthaminisha, akisema: Udongo sichochote mbele ya Mlezi wa walezi.

Ndio, mwenye kusujudu juu ya udongo si mwenye kuuabudu baliyeye anajidhalilisha kwa Mola Wake kwa kusujudu juu yake, naatakayedhania kinyume na hivyo basi yeye amedhoofika kiakili na

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 10

Page 17: Kusujudu juu ya udongo

11

Kusujudu juu ya udongo

hilo litapelekea kuwatilia shaka wote wenye kuswali na kuhukumuushirikina wao, hivyo anayesujudu juu ya busati na kitambaa nakingine lazima awe anakiabudu, kwa utaratibu huu inashangazasana.

Al-Amidiy amepokea toka kwa kiongozi wa waumini (a.s.) kuwaamesema: �Kusujudu kimwili: Ni kuweka sharafu za nyuso juu yaudongo.�16

‘SIJDA’ KILUGHA (YA KIARABU)

Hapana shaka kuwa kusujudu ni kati ya faradhi za sala na makundiyote mawili yamepokea toka kwa Ibnu Abbas kuwa Mtume waMwenyezi Mungu amesema: �Nimeamrishwa kusujudu kwa kutu-mia mifupa saba: Paji la uso, mikono miwili, magoti mawili na vich-wa vya nyayo mbili.�17

Pamoja na hayo ni kuwa ukweli halisi wa sijda ni kuweka paji juu yaardhi, ama vilivyobaki ni sawa na sharti za sijda na hilo linaonyesh-wa na kauli za wanakamusi pale wanapotoa maana ya neno sijdakwani hawataji isipokuwa kuweka paji juu ya ardhi, hivyo ni kamakwamba viungo vingine ni sharti za sijda ambayo muweka sheriaameifaradhisha kisha akaiunganisha na ukweli wake halisi wakilugha na kijamii.

Ibnu Mandhur amenukuu toka kwa Ibnu Sayyidihi amesema:Kitenzi: ??? ???? ????? Sajada, yasujudu, sujudan (Kiarabu) ni ali-

16Ghurarul-hikam wa Duraril-Kalam: 1/107, namba 2234.17Mashekhe wawili wameitoa, Bukhari: 1/206 na Muslim: 1/354.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 11

Page 18: Kusujudu juu ya udongo

12

Kusujudu juu ya udongo

weka paji lake aridhini. Na kundi la watu ni: Sujadu na Sujudu18.

Ibnu Al-Athiri amesema: �Sijda ya Swala ni kuweka paji juu yaardhi na wala hakuna unyenyekevu mkubwa mno kuliko huo�19

Ndani ya kamusi Tajul-urusi min Jawahiril-Qamusi: �Sajada:Alinyenyekea na kati ya unyenyekevu ni sijda ya Swala nayo nikuweka paji juu ya ardhi na wala hakuna unyenyekevu mkubwa mnokuliko huo na jina ni sijda�20.

Maneno haya yaliyothibiti ndani ya vitabu vya lugha toka kwa waan-dishi wa kamusi na mfano wake yanaonyesha kuwa ukweli hasa nasijda halisi ni kuweka paji juu ya ardhi na laiti kama Mtumeasingeamrisha kusujudu kutumia viungo saba basi ingetosha kuwe-ka paji juu ya ardhi, lakini yeye katika kuweka sheria ameongezamambo mengine na wajibu ikawa ni kusujudu kutumia viungo saba.

Ikiwa hali ndio hiyo basi hakuna makosa kitendo cha kuweka pajikuwa na sharti mahususi la pekee lisilohusu viungo vingine, nalo nisharti la kisujudio chake kuwa ni ardhi au kiotacho toka aridhini nawala haisihi kusujudu juu ya kitu kingine, na si viungo vingine.

18 Lisanul-Arabi: 6 neno Sajada.19 An-Nihayatu: 2 neno Sajada.20 Tajul-urusi: 8 neno Sajada.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 12

Page 19: Kusujudu juu ya udongo

13

Kusujudu juu ya udongo

SIRI YA KUACHWA WAZI PAJI LA USOKATIKA SIJIDA

Na linaloonyesha hilo ni wanafiqihi wengi wa kisunni kuona ni laz-ima kuacha wazi paji na si viungo vingine, hivyo laiti kama viungovingine vingekuwa na nafasi kama paji katika ukweli halisi wa sijdabasi hukumu yake ingekuwa kama hukumu ya paji, ilhali ukweli nitofauti.

Ndani ya Muhtasari wa Abul-Qasim Al-Kharaqiy na ufafanuzi wakekuna: �Wala si lazima kwake kugusa msala moja kwa moja kwa cho-chote ila kwa paji, kwa mujibu wa moja kati ya riwaya mbili.� Nakatika riwaya nyingine ni lazima kugusa msala kwa paji bila kizuizi,hilo limetajwa na Abul-Khitabi. Na Athramu amepokea akasema:�Nilimuuliza Aba Abdillah kuhusu kusujudu juu ya kunjo la kilem-ba akajibu: �Haisihi kusujudu juu ya kunjo lake bali kilemba huon-dolewa�, na haya ndio madhehebu ya Shafi.

Khababu amesema: �Tulimlalamikia Mtume kuhusu joto la ardhilinavyounguza vipaji vyetu na viganja vyetu, lakini hakutujali �akaendelea kusimulia mpaka akasema - na kutoka kwa Ali amesema:�Iwapo mmoja wenu anaswali basi aondoe kilemba chake tokakwenye paji lake.� Ameipokea Al-Bayhaqiy21.

Ndani ya Al-Wajiza: �Ni lazima kuacha wazi paji katika kusujudukutokana na riwaya ya Khababu, amesema: �Tulimlalamikia Mtumekuhusu joto la ardhi linavyounguza vipaji na viganja vyetu, lakinihakutujali,� yaani tukaendelea kulalamika. Katika ufafanuzi amese-21As-Sharhu Al-Kabiru ala matni Al-Kharaqiy: 1/557-558 kwenye hamishi ya Al-Mughniy

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 13

Page 20: Kusujudu juu ya udongo

14

Kusujudu juu ya udongo

ma: Wala si lazima kuacha paji lote wazi bali inatosha sehemu tuitakayothibiti jina la paji, hiyo ni kama katika kuweka paji. Na ni laz-ima sehemu itakayoachwa wazi iwe ni ile itakayowekwa juu yaardhi, na iwapo ataiacha sehemu wazi kisha akaweka aridhini sehe-mu nyingine (isiyo wazi) basi haitosihi. Na hakika uwazi unap-atikana pale ambapo kati ya paji na eneo la kusujudia hamnakizuwizi cha kuungana kinachoondoka kwa kuondoka yeye, hivyoiwapo atasujudu juu ya kiungo chake au kunjo la kilemba chakehaitosihi kwa sababu hajagusa eneo la kusujudia kwa paji lake bilakizuizi.

Tuna hadithi ya Khababu na pia amepokea kuwa Mtume alisema:�Gusisha paji lako aridhini.�22

Ibnu Rushdi amesema: �Pia wamekhitilafiana kuhusu je ni shartimkono wa mwenye kusujudu uwe wazi na uwekwe juu ya kile una-chowekwa uso juu yake? Au hilo si sharti lake? Malik amesema:�Hilo ni miongoni mwa sharti la sijda; ameona kuwa ni sharti lakutimia kwake.23 Wengine wakasema: Hilo si miongoni mwa shartila sijda.

Kupitia mlango huu wametofautiana kuhusu kusujudu juu ya kunjoza kilemba na hapa watu wana madhehebu matatu: Wapowanaozuwia, wapo wanaoruhusu, na wapo wanaotofautisha kati yakusujudu juu ya kunjo kubwa la kilemba au dogo, na kutofautishakati ya paji lake kugusa eneo dogo la ardhi au kutokugusa kabisa24.

Al-Qafalu amesema: �Iwapo kwenye paji lake kuna bandeji kwa tati-zo fulani na akasujudu basi inatosha na wala halazimiki kurudia. Na

22 Al-Azizi, Sharhul-Wajizi ijulikanayo kwa jina la As-Sharhul-kabiru: 1 /521.23 Maana yake si sharti la kusihi bali ni sharti la kukamilika.24 -Bidayatul-Mujtahidi:1/139.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 14

Page 21: Kusujudu juu ya udongo

15

Kusujudu juu ya udongo

miongoni mwa Wanavyuoni wetu wapo waliotoa kauli nyinginenayo ni ulazima wa kurudia kwa kupaka juu ya bandeji.�25

Ndani ya fiqihi ya madhehebu manne, Shafi wamesema: �Inadhurukusujudu juu ya kunjo la kilemba na mfano wake kama vile bandejiiwapo litafunika paji lote, na iwapo hatosujudu kwa paji lake lililowazi basi Swala yake itabatilika iwapo tu amefanya makusudi hukuanajua, isipokuwa tu kwa udhuru kama atakapokuwa na jeraha naakakhofu kupata maumivu makali iwapo ataondoa bandeji, basi kati-ka hali kama hii kusujudu kwa paji hilo ni sahihi.�26

Dhahiri ni kuwa siri ya kulazimika kuacha wazi paji ni kugusanishapaji na udongo ili mwenye kuswali afikie kilele cha mwisho chaunyenyekevu na utumwa.

Isipokuwa hawa wamehusisha kuacha wazi paji na kitendo chakutokuwepo kizuizi juu ya paji kizuwiacho kusujudu, kama vilekunjo la kilemba na pande zake na bandeji na wameruhusu kusujudujuu ya zulia au tandiko.

Kwa ajili hiyo wamebatilisha siri na faida ya ulazima wa kuacha pajiwazi, basi hapo ndipo linapowaelekea swali lifuatalo: Ikiwa sijda juuya tandiko na zulia inaruhusiwa basi kuna tofauti gani kati ya kusu-judu juu ya hivyo na juu ya bandeji na kunjo la kilemba? Kwani kut-ofautisha kati ya mambo mawili hayo ni jambo la kushangaza.Kwani kwa hakika bandeji na kilemba hutengenezwa kwa uzi kamatandiko na zulia na kitendo cha kilemba na kunjo zake kubebwa namwenye kuswali kinyume na tandiko na zulia hakulazimishi tofautimadamu kwa madai yao vinashirikiana katika kufanya sijda.

25 -Hil-yatul-ulamai fi maarifati madh�habil-fuqahai:122.26 Al-Fiqhu ala Madhahibul-Arbaa:1/233.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 15

Page 22: Kusujudu juu ya udongo

16

Kusujudu juu ya udongo

Suala hii ni tofauti na pale tutakaposema: Siri ya kuacha wazi paji nikugusanisha uso na ardhi, kwani hapo hakutakuwepo na tofauti katiya bandeji na zulia, na huo ndio mtazamo wa Wanavyuoni wetuwote.

Al-Allamah amesema: �Ni lazima kuchomoza paji wakati wa kusu-judu mpaka juu ya kile kinachosihi kusujudu juu yake.�27

SUNA YA MTUME KATIKA KUSUJUDU, ZAMAZAKE NA BAADA YAKE

Hakika Mtukufu Mtume na maswahaba zake walikuwa wakisujudujuu ya ardhi muda mrefu wakivumilia shida ya joto la ardhi, vumbila udongo na unyevunyevu wa udongo miaka yote, na wala hakunayeyote yule zama hizo aliyesujudu juu ya nguo na kunjo la kilembabali hata juu ya mkeka, kirago na khumra28 wala juu ya tandiko nazulia. Utaratibu wa juu kabisa waliokuwa nao katika kuondoa udhiakwenye paji ulikuwa ni kupoza changarawe kwa viganja vyao kishawanasujudu juu yake.

Baadhi yao walimlalamikia Mtume kuhusu ukali wa joto lakinihakumjibu kwani hakuwa na uwezo wa kubadili amri ya MwenyeziMungu kwa matakwa yake mwenyewe mpaka pale ilipopatikanaruhusa ya kusujudu juu ya khumra29na mkeka, hivyo amri mpyaikawapa wasaa waislamu lakini ndani ya uzio maalumu, kwa mujibuwa hayo waislamu zama hizo walipitiwa na hatua tatu tu na si zaidi:

27 Muntahal-Matlabu: 5/154.28 Mkeka mdogo wa kuswalia.29 Mkeka mdogo wa kuswalia.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 16

Page 23: Kusujudu juu ya udongo

17

Kusujudu juu ya udongo

Wakati ambao ilikuwa ni wajibu kwa waislamu kusujudu juu yaardhi na aina zake mbalimbali kuanzia udongo, mchanga,changarawe na udongo laini na wala hawakuwa na ruhusa yoyote ileya kusujudu juu ya kitu kingine.

Kipindi ambacho ilipatikana ruhusa ya kusujudu juu ya mimea yaardhi kuanzia mkeka, kirago na khumra ikiwa ni kuwarahisishiaamri na kuwaondolea kero na tabu.

Kipindi ambacho iliruhusiwa kusujudu juu ya vazi katika hali yadharura na matatizo.

Na ufuatao ni ufafanuzi wake:

Kipindi cha mwanzo: kusujudu juu ya ardhi

Makundi yote mawili yamepokea toka kwa Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) kuwa alisema: �Nimefanyiwa ardhi tohara na mahala pakusujudia�30. Maana inayoeleweka toka ndani ya Hadithi hii ni kilasehemu ya ardhi ni mahala pa kusujudia na tohara, juu yake hufany-wa sijda na tayamamu, kwa ajili hiyo ardhi hukusudiwa kwa mambomawili: Mara kwa kusujudu na mara nyingine kwa kutayamamu.

Hakika hadithi hii inathibitisha wazi kuwa ardhi, iwe ya udongo aumajabali au changarawe ndio asili katika kusujudu na ndio inayowa-jibika kufanywa mahala pa kusujudia na wala hairuhusiwi kuvukahapo isipokuwa kwa dalili nyingine. 30 Sahih Bukhari:1/91 kitabu cha Tayammam, hadithi ya 2. Sunanil-Bayhaqiy:2/433 mlango: Popote sala itakapokukuta Swali kwani penyewe ni msikiti, na ime-pokewa pia na wengine kati ya waandishi wa Sahihi Sita na vitabu vya Sunna.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 17

Page 24: Kusujudu juu ya udongo

18

Kusujudu juu ya udongo

Ama kutafsiri riwaya hii kuwa ibada na kusujudu kwa ajili yaMwenyezi Mungu haihusishi sehemu maalumu tu na kuacha sehemunyingine bali ardhi yote ni mahala pa kusujudia waislamu, kinyumena wasio waislamu kwani wao wamehusisha ibada na mahekalu namakanisa tu. Maana hii haipingani na maana tuliyoitaja mwanzo,kwani iwapo ardhi yote ni mahala pa kusujudu mwenye kuswali basiinalazimu ardhi yote iwe inafaa kwa ibada, na hapo maana hii iliy-otajwa ni maana muambata ya maana tuliyoitaja mwanzo.

Na kinachoonyesha kuwa hayo ndio makusudio ni kule kutajwa�tohara� baada ya �mahala pa kusujudia� na kuyafanya manenohayo mawili kuwa ni vitendwa vya kitenzi �nimefanyiwa� hivyomatokeo yake ni kuipa ardhi sifa mbili: Yenyewe kuwa ni mahala pakusujudia na kuwa ni tohara, na hili ndilo alilofahamu Al-Jassasuakasema: �Hakika yule aliyeifanya ardhi mahala pa kusujudia ndiyealiyeifanya tohara.�31 Na wengine mfano wake kati ya wafafanuziwa hadithi.

Basi iwapo udongo na changarawe ni tohara basi pia vyenyewe nimahala pa kusujudia mwenye kuswali, hivyo kuwekwa kikomo nihoja mpaka dalili nyingine ionyeshe ruhusa ya kuvuka kikomohicho.

31 Ahkamul-Qur’ani: 2/389 iliyosambazwa Beiruti

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 18

Page 25: Kusujudu juu ya udongo

19

Kusujudu juu ya udongo

Kupoza changarawe ili kusujudu juu yake

2. Toka kwa Jabir bin Abdillah Al-Answariy amesema: �Nilikuwanikiswali pamoja na Mtume (s.a.w.w.) Swala ya adhuhuri basinikachukua fungu la changarawe mkononi mwangu na kuziwekamkono wa pili ili zipowe kisha naziweka kwa ajili ya paji langu ilinisujudu juu yake kwa jinsi joto lilivyokuwa kali32

Al-Bayhaqiy akaongeza kwa kusema: As-Sheikh amesema: �Laitiingeruhusiwa kusujudu juu ya vazi lililo mwilini basi hilo lingekuwani rahisi mno kuliko kupoza changarawe kwa viganja na kuziwekaili kusujudu33.

Tunasema: Laiti ingeruhusiwa kusujudu juu ya nguo yoyote iliyomwilini au iliyo nje ya mwili hilo lingekuwa ni rahisi mno kulikokupoza changarawe na ingewezekana kubeba kitambaa au zulia aumfano wake kwa ajili ya kusujudu juu yake.

3. Anas amepokea akasema: �Tulikuwa tukiswali pamoja naMtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika siku za joto basi kila mmoja wetuhuchukua changarawe mkononi mwake ili kuzipoza na baadae huzi-weka na kusujudu juu yake34.

32 Musnadi Ahmad: 3/327 hadithi ya Jabir. Sunanil-Bayhaqiy: 1/439 mlango wayaliyopokewa kuhusu kuiharakisha Swala kwa ajili ya ukali wa joto.33 Sunanul-Bayhaqiy: 2/105.

34 Sunanul-Kubra: 2/106

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 19

Page 26: Kusujudu juu ya udongo

20

Kusujudu juu ya udongo

4. Toka kwa Khabab bin Al-Arti amesema: �TulimlalamikiaMtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu joto la ardhi linavyounguza vipa-ji na viganja vyetu lakini hakutujibu35. Ibnu Athiri amezungumziamaana ya hadithi hii akasema: �Hakika wao walipomlalamikia yaleyanayowasibu kutokana na joto hilo hakuwapa nafasi ya kusujudujuu ya ncha kona za nguo zao�36

Riwaya hizi zinaonyesha sunna ya Mtume katika swala ilikuwa nikusujudu juu ya ardhi tu mpaka Mtume hakuwapa nafasi waislamuwaache na waende kwenye nguo za mwilini mwao au vitu vya nyuzivilivyo nje ya miili yao, japokuwa Mtume ni mpole na mwenyehuruma kwa waumini lakini aliendelea kuwawajibisha wagusanishevipaji vyao na ardhi hata kama ukali wa joto lake utawaudhi.

Hadithi zinazoamrisha kufikisha udongo kwenye paji zinaonyeshawazi jinsi waislamu walivyokuwa wakisujudu juu ya ardhi na jinsiMtukufu Mtume alivyoshikilia msimamo wa kuweka paji juu yaudongo na wala si juu ya nguo ya mwilini kama vile kunjo la kilem-ba au isiyo mwilini kama vile vitambaa na mazulia. Riwaya hizo ninyingi zaidi ya moja.

Amri ya kufikisha udongo kwenye paji

5- Imepokewa toka kwa Khalid bin Al-Jahaniy amesema: MtukufuMtume (s.a.w.w.) alimwona Suhaybu akisujudu huku akizuwia asi-patwe na udongo, Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: �Ewe Suhaybu,gusisha uso wako udongo�37. Kinachoonekana ni kuwa Suhaybualikuwa anajikinga asipatwe na udongo kwa kusujudu juu ya nguo35 Sunanil-Bayhaqiy: 2/105 mlango: Kuacha wazi paji la uso.36 An-Nihayatu: 2/497, neno � Shaka.�37Al-Mutaqi Al-Hindiy: Kanzul-ummal: 7/465 namba 19810

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 20

Page 27: Kusujudu juu ya udongo

21

Kusujudu juu ya udongo

iliyo mwilini au isiyo mwilini, na kwa uchache ni kusujudu juu yamkeka, kirago na mawe safi. Vyovyote vile itakavyokuwa ni kwam-ba hadithi hii ni ushahidi juu ya ubora wa kusujudu juu ya udongokuliko kusujudu juu ya changarawe kama ilivyotangulia ruhusa yakusujudu juu ya changarawe kinyume na kusujudu juu ya kisi-chokuwa ardhi.

Ummu Salama amepokea kuwa: �Mtume (s.a.w.w.) alimwona kijanawetu anayeitwa Af�lahu akipuliza mahala pa kusujudia,akamwambia: Ewe Af�lahu gusa udongo�38.

Na katika riwaya nyingine: �Ewe Rabahu gusisha uso wako udon-go�39.

Abu Swaleh amepokea akasema: �Niliingia kwa Ummu Salamakisha akaingia mtoto wa kaka yake na kuanza kuswali nyumbanimwake rakaa mbili, aliposujudu akapuliza udongo, hapo UmmuSalama akamwambia: �Ewe mtoto wa kaka yangu usipulize kwanihakika mimi nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.)akimwambia mtumishi wake aliyeitwa Yasari: �Gusisha uso wakoudongo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.�40.

38 Al-Mutaqi Al-Hindiy: Kanzul-ummal:7/459 namba 1977639 Al-Mutaqi Al-Hindiy: Kanzul-Ummal: 7/459 namba 1977740 Al-Mutaqi Al-Hindiy: Kanzul-Ummal: 7/465 Na. 19810. Musnadi Ahmad:6/301.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 21

Page 28: Kusujudu juu ya udongo

22

Kusujudu juu ya udongo

Amri ya kuondoa kilemba kwenye paji la uso

Imepokewa kuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiondoakilemba kwenye paji lake anaposujudu.41

Imepokewa toka kwa Ali kiongozi wa waumini kuwa amesema:Iwapo mmoja wenu anasujudu basi aondoe kilemba kwenye paji ke�inamaanisha ili asisujudu juu ya kunjo la kilemba42.

Saleh bin Hayawani As-sabai amesema: �Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)alimwona mtu mmoja akisujudu ubavuni mwake na kilemba chakekikiwa kimefunika paji lake basi Mtukufu Mtume akakiondoakwenye paji lake.�43

Iyadhi bin Abdullah Al-qarashiy amesema: �Siku moja MtukufuMtume (s.a.w.w.) alimwona mtu mmoja akisujudu juu ya kunjo lakilemba kilichoshuka kwenye paji lake, Mtume akamwashiria kwamkono wake: �Ondoa kilemba chako.�44

Riwaya hizi zinadhihirisha kuwa zama hizo waislamu hawakuwa naamri nyingine isipokuwa ni kusujudu juu ya udongo na wala hakuwana ruhusa nyingine isipokuwa kupoza changarawe, na laiti kamakungekuwa na ruhusa nyingine basi wasingefanya hivyo na walaMtume asingeamrisha kugusisha udongo wala kuondoa kilembakwenye paji la uso.

41Tabaqatul-Kubra: 1/151 kama ilivyo kusujudu juu ya ardhi:41.42Muntakhabu Kanzul-ummai iliyochapwa pembezoni mwa Al-Musnadi:3/194.43As-Sunanil-Kubra: 2/10544 As-Sunanil-Kubra: 2/105.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 22

Page 29: Kusujudu juu ya udongo

23

Kusujudu juu ya udongo

Mwenendo wa Mtume katika kusujudu

Kutokana na riwaya nyingi inaonekana Mtume alikuwa akitiliaumuhimu kusujudu juu ya ardhi na zifuatazo ni mfano wa riwayahizo:1-Al-Wailu bin Hajari amesema: �Nilimuona Mtume (s.a.w.w.) ana-posujudu huweka paji lake na pua yake juu ya ardhi.�45

2- Ibnu Abbas amesema: �Hakika Mtukufu Mtume alisujudu juu yajiwe.�46

3- Aisha amesema: �Sikuwahi kumuona Mtume (s.a.w.w.) akikingauso wake na kitu.�47

Ibnu Hajar amesema: �Katika hadithi hii kuna ishara kuwa kugusaardhi bila kizuwizi katika sijda ndio asili kwa sababu kuna sharti lakutojiweza.�48

Hadithi hii inaonyesha ruhusa ya kusujudu juu ya vazi wakati wadharura na kutokuruhusiwa katika hali ya kawaida, na hili ndilolililopokewa toka kwa Maimamu wa Ahlul-baiti, kwani imepokewatoka kwa Uyaynatu Yubaul-Qaswabi amesema: �Nilimwambia AbaAbdillah: Nikiingia msikitini siku yenye joto kali nikichukia kuswalijuu ya changarawe nikitandika nguo yangu, je nisujudu juu yake?

45 Ahkamul-Qur’ani: 3/36. Musnadu Ahmad: 315,317.

46 As-Sunanil-Bayhaqiy: 2/102.

47 Al-Muswanafu:1/397. Kanzul-Ummal: 4/212.

48 Fathul-Bari: 1/414.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 23

Page 30: Kusujudu juu ya udongo

24

Kusujudu juu ya udongo

Akajibu: �Hakuna ubaya.�49

Na Al-Qasim bin Al-Fadhilu amesema: �Nilimuuliza Ridha (a.s):�Mimi ni fidia kwako, Je iwapo mtu anasujudu juu ya kunjo lakilemba chake kutokana na udhia wa joto na baridi.� Akajibu:Hakuna ubaya.”50

Kuna riwaya na hadithi zinazoonyesha Mtukufu Mtume alikuwaakisujudu juu ya udongo na ardhi katika baridi kali na alikuwaakiswali kwenye shuka akijikingia mikono yake na miguu yake dhidiya baridi ya ardhi na wala si paji lake. Na zifuatazo ni riwaya zionye-shazo hilo:

1- Wailu bin Hajar amesema: �Siku moja nilimwona MtukufuMtume (s.a.w.w.) akiswali juu ya kitambaa cheupe na huku akie-pusha mikono na miguu yake dhidi ya baridi ya ardhi kwa kitambaahicho.�51

2- Thabit bin Swamit amepokea kuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)alipokuwa akiswali katika msikiti wa Bani Abdul-Ash�hali aliwekamikono yake juu ya kitambaa alichojivingirishia kujiepusha na bari-di ya mawe.52

3- Abu Huraira amesema: �Mtume (s.a.w.w.) alisujudu siku ya mvuakali kiasi kwamba nikawa naona alama za sijda kwenye paji lake napua yake.�53

49 Al-Wasailu: 3 mlango 4 kati ya milango ya kitu cha kusujudu juu yake, hadithiya 150 Al-Wasailu: 3, mlango wa 4 mlango wa kitu cha kusujudu juu yake, hadithi ya2.51 As-Sunanul-Kubra lil-Bayhaqiy: 2:106.52 Sunani Ibnu Majah: 1/329.53 Maj’maul-Zawaidi: 2/126.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 24

Page 31: Kusujudu juu ya udongo

25

Kusujudu juu ya udongo

Riwaya hizi na mfano wake zinaonyesha kitendo cha MtukufuMtume katika sijda yake siku za mvua na baridi na alikuwa akisu-judu juu ya udongo na wala hakuuepusha uso wake kwa kitu cho-chote, na mara nyingine akiepusha mikono yake bila kuhusisha uso,huku umakini wa wapokezi kuhusu kubainisha kitendo cha Mtumekuepusha mikono yake kwa kitambaa dhidi ya baridi na udongo nawakiwa wameacha kutaja paji kunadhihirisha kuwa yeye hakuwahikuepusha uso wake kwa chochote na laiti kama si hivyo basiwapokezi wangekitaja na wala wasingeghafilika.

MWENENDO WA MASWAHABA NA TABIINAKATIKA KUSUJUDU

Kutokana na riwaya nyingi ni dhahiri kuwa mwenendo wa kundi lamaswahaba ulikuwa ni kusujudu juu ya ardhi.

1- Abu Umayya amesema: Abu Bakr alikuwa akisujudu juu ya ardhihuku akijitandaza nayo.54

2- Abu Ubayda amesema: Ibnu Mas�udi huwa hasujudu au amese-ma: Huwa hasali ila juu ya ardhi.55

3- Mas�ruqu bin Al-Ajdau sahaba wa Ibnu Mas�udi alikuwaharuhusu kusujudu juu ya kisichokuwa ardhi hata ndani ya jahazi naalikuwa akibeba kitu cha kusujudu juu yake ndani ya jahazi.56

54 Al-Muswanafu: 1/39755 Al-Muswanafu: 1/36756At-Tabaqatil-Kubra li-ibnu Saadi: 6/53. Na Al-Muswanafu Abdurazaqi: 2/583.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 25

Page 32: Kusujudu juu ya udongo

26

Kusujudu juu ya udongo

4- Ibrahimu An-Nakhaiy mwanachuoni wa Kufa aliyekuja baada yamaswahaba alikuwa akisimama juu ya busati la matete na kusujudujuu ya ardhi. Mpokezi akasema: Busati la matete ni nini? Akasema:Mkeka.57 Na katika tamko lingine alikuwa akiswali juu ya mkeka nakusujudu juu ya ardhi.

5- Umar bin Abdul-Aziz alikuwa hatosheki na khumra bali alikuwaanaweka udongo juu ya khumra na kusujudu juu yake.58

6- Ur�watu bin Zubair alikuwa akichukia kuswali juu ya kitu kisi-chokuwa ardhi.59

7-Ali bin Abdallah bin Abbas alimuandikia Zurainu kuwa nitumievipande vya mawe ya Mar�wa ili niwe nasujudu juu yake.60

Matokeo ni kuwa kujidhalilisha na kunyenyekea mbele ya utukufuwa Mwenyezi Mungu kwa ubora kunapatikana kwa kuweka paji napua juu ya udongo mkavu na mbichi huku ukisema: Udongo haulin-gani na bwana wa mabwana na udongo ni sawa na mimi, hali hiyohuwezi kuipata kwenye vitu vya viwandani.

Na Allamah Al-Amini ana maneno ya maana sana, na yafuatayo nimaelezo yake:

Na kinachofaa mno kufanyia sijda ambayo si chochote isipokuwa nikujishusha na kujidhalilisha mbele ya utukufu wa Mwenyezi Munguna heshima ya kiburi chake ni ardhi kufanywa mahala pa kusujudia

57 Al-Muswanafu Liabdirazaqi: 1397.58 Fat-hul-Bari:1/410.59 Fat-hul-Bari:1/410.60 Akh-baru Maka lil-Azraqiy

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 26

Page 33: Kusujudu juu ya udongo

27

Kusujudu juu ya udongo

wakati wa kusujudu, huku mwenye kuswali akichafua shavu lakekwa udongo na kuidhalilisha pua yake ili mwenye kusujudu akum-buke udongo wake duni usio na thamani ambao ameumbwakutokana nao, ambao atarudi tena na kutolewa mara nyingine iliawaidhike na awe na kumbukumbu ya uduni wa asili yake ili apatwena unyenyekevu wa kiroho na udhalili wa ndani na mvunjiko wanafsi na kuinuka kwa viuongo kuelekea kwenye utumwa huku aki-achana na ujeuri na ubinafsi, na awe katika ujuzi kuwa kiumbekitokanacho na udongo kinastahiki na kufaa udhalili na uduni nawala si kitu kingine.

Katu kabisa siri hizi hazipatikani ndani ya vitu vya kutengenezwakwa sufi, hariri na mfano wake miongoni mwa mambo ya raha nastarehe ambayo yanamuonyesha mwanadamu ukubwa ndani ya nafsiyake. Vinamuonyesha heshima, utukufu, na cheo cha juu kwake naanapata ujeuri, kiburi na majivuno na hapo kujitoa kwenye udhalilina unyenyekevu.61

HATUA YA PILI

KURUHUSIWA KUSUJUDU JUU YAKHUMRA NA MKEKA

Hadithi na riwaya zilizotangulia zilizothibiti ndani ya Sahihi Sita navitabu vya Musnadi na vingine vya hadithi vinaonyesha jinsi Mtumena maswahaba zake walivyoshikilia msimamo wa kusujudu juu yaardhi na aina zake na wao hawakuacha kusujudu juu yake hata kamamambo yatakuwa magumu na joto likazidi.

61 Siratuna wasunatuna:125-126.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 27

Page 34: Kusujudu juu ya udongo

28

Kusujudu juu ya udongo

Lakini kuna maelezo yanayoonyesha Mtume aliruhusu kusujudu juuya mimea ya ardhi kwa wahyi toka kwa Mwenyezi Mungu, hapolikawa jepesi kwao suala la kusujudu na tabu na usumbufu wa jotona baridi na pale ardhi itakapokuwa imelowana vikaondolewa.

Na yafuatayo ni hayo maelezo:1-Anas bin Malik amesema: Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w.) alikuwa akiswali juu ya khumra.62

2- Ibnu Abbas amesema: Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w.) alikuwa akiswalijuu ya khumra. Katika tamko lingine:Nabii alikuwa akiswali juu ya khumra.63

3- Aisha amesema: �Mtukufu Nabii (s.a.w.w.) alikuwa akiswali juuya khumra.�64

4- Ummu Salama amesema: �Mtukufu Mtume wa MwenyeziMungu (s.a.w.w.) alikuwa akiswali juu ya khumra.�65

5- Maymuna amesema: �Mtukufu Mtume anasali juu ya khumra naanasujudu juu yake.�66

6- Ummu Sulaymu amesema: �Mtukufu Mtume wa MwenyeziMungu (s.a.w.w.) alikuwa akiswali juu ya khumra.�67

62 Abunaimil-Is’fihani: Ahk-baru Is’bihani: 2/141.63 Musnadi Ahmad:1/269,303,309,358.64 Musnadi Ahmad: 6/179 na pia mna alimwambia kijakazi wake akiwa msikiti-ni: Niletee khumra.65 Musnadi Ahmad: 6/302-66 Musnadi Ahmad: 6/331-335.67 Musnadi Ahmad: 6/377.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 28

Page 35: Kusujudu juu ya udongo

29

Kusujudu juu ya udongo

7. Abdallah bin Umar amesema: Mtukufu Mtume wa MwenyeziMungu (s.a.w.w.) alikuwa akiswali juu ya khumra.68

Baadhi ya waelekezaji ndani ya msikiti mtukufu walinikosoa palewaliponiona nikiendelea kusujudu juu ya mkeka na kunihoji sababuya kufanya hivyo. Nikamwambia: Hakika Mtukufu Nabii alikuwaakiswali juu ya mikeka.

Akasema: �Hakika Swala ya Mtume juu ya mikeka na virago hailaz-imishi kusujudu juu yake kwani inawezekana akaswali juu ya mkekana akasujudu juu ya kitu kingine.�

Nikamwambia: Hakika kutenganisha kati ya mambo hayo mawilihakulingani na lugha fasaha, kwani hakika kauli: Anaswali juu yamkeka, inamaanisha anasali juu yake katika hali zake zote za Swalakuanzia kisimamo, rukuu na kusujudu na wala si aweke nyayo zakeau magoti yake au mikono yake juu ya mkeka huku kaweka paji lakekwenye kitu kingine. Zaidi ya hapo kuna baadhi ya riwaya zimetam-ka wazi alikuwa akisujudu juu ya mkeka.

1. Abu Said Al-Khiduriy amesema: �Nilikwenda kwa MtukufuMtume nikamkuta anasali juu ya mkeka na akisujudu juu yake.�69

2. Anas bin Malik amesema: �Mtukufu Mtume alikuwa akiswali juuya khumra na akisujudu juu yake.”70

68 Musnadi Ahmad: 2/92-98. 69 Sahih Muslim:2/62, Darul-fikri Beiruti.70 Sahih Ibu Khuzaimati: 2/105, Al-Maktabu Al-Islamiyu chapa ya 2-1412Hijiriyya. Al-Muujamu Al-Awsatu: 8/348. Al-Muujamu Al-Kabiru: 12/292.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 29

Page 36: Kusujudu juu ya udongo

30

Kusujudu juu ya udongo

Ndani ya Hadithi zilizotajwa inabainika ruhusa ya kusujudu juu yaardhi na udongo na baadhi ya vinavyoota aridhini mfano wa mkekauliotengenezwa kwa magome ya mtende.

HATUA YA TATU

KUSUJUDU JUU YA NGUO KWA UDHURU

Tayari umeshazijua hatua mbili zilizopita na laiti kama ipo hatua yatatu basi si nyingine bali ni hatua ya kuruhusu kusujudu juu ya kisi-chokuwa ardhi na kisichoota humo kwa udhuru na dharura. Nainaonyesha kuwa ruhusa hii ilikuja mwisho baada ya hatua hizombili, hiyo ni kama ulivyoona jinsi ambavyo Mtume hakujalimalalamiko ya maswahaba dhidi ya ukali wa joto na ukali wachangarawe huku wakiendelea yeye na maswahaba zake kusujudujuu ya ardhi wakivumilia udhia na joto kali.

Lakini Muumba Mtukufu akaruhusu kusujudu juu ya vazi kwadharura na udhuru kwa lengo la kuondoa tabu. Na zifuatazo ni riwaya kuhusu hili:

Anas bin Malik amesema: �Tulipokuwa tukiswali pamoja naMtukufu Mtume (s.a.w.w.) kila mmoja wetu alikuwa hajimudukuweka paji juu ya ardhi hivyo kila mmoja aliweka vazi lake nakusujudu juu yake.

Na katika tamko lingine: �Tulipokuwa tukiswali pamoja na Mtume(s.a.w.w.) kila mmoja wetu alikuwa akiweka baadhi ya vazi lake kwasababu ya joto kali na iwapo atashindwa mmoja wetu kutuliza pajilake juu ya ardhi hutandika nguo yake.�

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 30

Page 37: Kusujudu juu ya udongo

31

Kusujudu juu ya udongo

Katika tamko la tatu: �Tulipokuwa tukiswali pamoja na MtukufuMtume (s.a.w.w.) baadhi yetu waliweka baadhi ya vazi mahala pakusujudia kwa sababu ya joto kali.”71

Riwaya hii ambayo imenukuliwa na waandishi wa vitabu vya SahihSita, Sunani na Masanidi inadhihirisha ukweli wa baadhi ya riwayazilizopokewa zikikusudia kuruhusu kusujudu juu ya nguo katika haliisiyo ya dharura. Hiyo ni kwa sababu riwaya ya Anas imeeleza iki-husisha ruhusa katika hali ya dharura tu, hivyo yenyewe inakuwa nikihusisho cha makusudio ya riwaya hizi zisizo na sharti.

Na zifuatazo ni baadhi ya hizo riwaya zilizopokewa katika hili:

1-Abdallah bin Muhrizu amepokea toka kwa Abu Huraira kuwa:Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akiswalijuu ya kunjo la kilemba chake.72

Hakika riwaya hii japokuwa inapingana na ile ya katazo la Mtumekuhusu kusujudu juu ya kunjo bado inachukuliwa kuwa ni wakati waudhuru na dharura na hilo limetamkwa wazi na Sheikh Al-Bayhaqiyndani ya Sunnan yake aliposema: �Shekhe amesema: �Ama riwayazilizopokewa toka kwa Mtume (s.a.w.w.) kuhusu hilo la kusujudujuu ya kunjo la kilemba hazithibitishi lolote kuhusu hilo, na sahihimno miongoni mwa yale yaliyopokewa kuhusu hilo ni kauli yaHasani Al-Basriy ambayo ni nukuu toka kwa maswahaba wa Mtume(s.a.w.w.).�73

71 Sahih Bukhari: 1/101. Sahih Muslim: 2/109. Musnad Ahmad: 1/100. As-

Sunanul-Kubra: 2/106.72 Kanzul-Ummal: 8/130 namba 22238.73 Al-Sunnan Al-Kubra: 2/106.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 31

Page 38: Kusujudu juu ya udongo

32

Kusujudu juu ya udongo

Na imepokewa toka kwa Ibnu Rashidi amesema: �NilimwonaMakuhula akisujudu juu ya kilemba chake nikamwambia: Kwa niniunasujudu juu yake? Akasema: Nakinga meno yangu dhidi ya bari-di�.74

2-Riwaya iliyopokewa kutoka kwa Anas: �Tulipokuwa tukiswalipamoja na Mtume mmoja wetu alikuwa akisujudu juu ya nguoyake�.75

Riwaya hii inachukuliwa kuwa ni katika hali ya udhuru kwa kigezocha riwaya tuliyopokea kupitia yeye mwenyewe na aliyoipokeaBukhari kupitia kwake yeye kuwa: �Tulipokuwa tukiswali pamojana Mtume (s.a.w.w.) kila mmoja wetu alikuwa hajimudu kuweka pajijuu ya ardhi kwa sababu ya joto kali hivyo kila mmoja aliweka vazilake na kusujudu juu yake.�76

Na inaungwa mkono na riwaya aliyoipokea An-Nasaiy:�Tulipokuwa tukiswali Adhuhuri nyuma ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) tulisujudu juu ya mavazi yetu ili kujikinga na joto�.77

Na kuna riwaya zisizo na hoja timilifu kiasi kwamba hazionyeshiisipokuwa ni kuwa Mtume aliswali juu ya kirago cha ngozi. Je?

74 Al-Muswanafu li-Abdil-Razaqi:1/400 kama ilivyo ndani ya SiratunaWasunnatuna, na Al-Sijdatu ala Turbati: 93.75 Al-Sunnanu Al-Kubra: 2/106 mlango wa atakayetandika nguo na kusujudu juuyake.

76 Bukhari: 2/64 Kitabu cha sala mlango wa kutandika nguo ndani ya sala kwaajili ya kusujudu.

77 Ibnu Athiir: Jamiul-Usuul: 5/468 namba 3660.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 32

Page 39: Kusujudu juu ya udongo

33

Kusujudu juu ya udongo

Alisujudu juu yake au la. Hakuna dalili ionyeshayo hilo.

3. Toka kwa Al-Mughira bin Shu�ba: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)alikuwa akiswali juu ya mkeka na ngozi yenye manyoya iliyotiwadawa ili isioze.78

Riwaya hii japokuwa ni dhaifu kwa kuwemo Yunus bin Al-Harthi,bado haionyeshi kuwa alisujudu juu yake na wala hakuna mahusianoya lazima kati ya kuswali juu ya ngozi na kusujudu juu yake, na hasangozi inapokuwa kipande kidogo kwani huenda (s.a.w.w.) aliwekapaji lake juu ya ardhi au kiotacho toka aridhini, na hata kama tuki-jaalia kuwepo mahusiano ya lazima bado yenyewe na mfano wakehiyo haziwezi kuzishinda uzito riwaya tulizoorodhesha katika hatuambili zilizopita.

MATOKEO YA UCHUNGUZI

Hakika mwenye kufuatilia riwaya kwa kina ataona jahara kuwasuala la kusujudu ndani ya swala lilipitia hatua mbili au tatu, hivyokatika hatua ya kwanza faradhi ilikuwa ni kusujudu juu ya ardhi nawaislamu hawakuruhusiwa kusujudu juu ya kisichokuwa ardhi, nakatika hatua ya pili ikaja ruhusa ya kusujudu juu ya kinachoota tokaaridhini na nyuma ya hatua hizi mbili hakuna hatua nyingineisipokuwa hatua ya kuruhusiwa kusujudu juu ya nguo kwa udhuru nadharura.

78 Abu Daud: As-Sunnan: mlango wa yaliyopokewa kuhusu kuswali juu ya khum-ra, namba 331.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 33

Page 40: Kusujudu juu ya udongo

34

Kusujudu juu ya udongo

Hivyo maana iyonekanayo toka ndani ya baadhi ya riwaya zina-zoruhusu kusujudu juu ya kirago cha ngozi na mfano wakehuchukuliwa kuwa ni wakati wa dharura. Au hazina dalili kuwaalisujudu juu yake bali makusudio yake ni kuswali juu yake.

Na hapa ndipo inapodhihiri jahara kuwa kitendo cha Shiakung�ang�ania kusujudu juu ya ardhi au kiotacho toka aridhini ndiokile kile kitendo kilicholetwa na Sunna tukufu ya Mtume (s.a.w.w.)na wala hawajakwenda kinyume hata kidogo.

Na sisi tunawaomba kidogo mtazame kwa makini ili muone haki namuache uzushi (bidaa). Katu hakuna dalili inayoruhusu sijda juu yamatandiko, mazulia na mabusati yaliyotengenezwa kwa sufi, many-oya, hariri na mfano wake, na vazi lililomo mwilini, na ndani yaSunna ya Mtume hamna mashiko yoyote yanayoruhusu hilo.

Ni hizi hapa Sahihi sita zilizochukua dhamana ya kubainisha huku-mu za dini, na hasa swala ambayo ndio nguzo ya dini, lakini ndaniyake hamna hata hadithi moja wala neno moja linaloashiria walakugusia ruhusa ya hilo.

Hivyo kauli ya kuruhusu kusujudu juu ya matandiko na mazulia nakung�ang�ania hilo na kutandaza mabusati misikitini ili kusujudu juuyake kama ilivyozoeleka, suala hilo ni bidaa halisi na jambolililozushwa nje ya sheria, na linapingana na mwenendo waMwenyezi Mungu Mtukufu na Sunna ya Mtukufu Mtume Wake(s.a.w.w.); “…..na wala hamtokuta mabadiliko yoyote katikamwenendo wa Mwenyezi Mungu.”79

79 Siratuna Wasunnatuna: 133-134.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 34

Page 41: Kusujudu juu ya udongo

35

Kusujudu juu ya udongo

= 6 =

NI IPI SIRI YA KUCHUKUA KIPANDE CHAUDONGO TOHARA?

Hapa limebaki swali ambalo mara nyingi hutolewa na ndugu zetuwengi wa kisunni kuhusu sababu ya Shia kuchukua kipande chaudongo tohara safarini na nyumbani na kusujudu juu yake na si kitukingine. Huenda wenye akili duni wakadhani kuwa Shia hukisujudiakipande hicho na wala si kusujudu juu yake, na kuwa wanaabudujiwe na kipande cha udongo, hilo ni kwa sababu masikini hawahawatofautishi kati ya kusujudu juu ya kipande cha udongo na kuk-isujudia.

Vyovyote vile ni kuwa jibu la swali hilo liko dhahiri kwani kilichobora kwa Shia ni kuchukua kipande cha udongo tohara safi ili awena yakini juu ya utohara wake, kipande hicho kichukuliwe ardhiyoyote ile na toka bara lolote lile kati ya pande za ulimwengu nisawa kwao hamna tofauti. Kujali huku ni sawa tu na kile kitendo chamwenye kuswali kujali tohara ya mwili wake, mavazi yake na msalawake.

Ama siri ya kung�ang�ania kuchukua kipande cha udongo ni kwam-ba uhakika wa utohara wa kila ardhi -huwa humo, - na kukifanyamahala pa kusujudia, haupatikani kila eneo miongoni mwa maeneoanayokuwemo muislamu safarini na nyumbani, na itakuwaje awe nauhakika huo ilihali maeneo hayo yanafikiwa na aina tofauti zabinadamu, waislamu na wasio waislamu, washikao misingi ya toharana wasioshika misingi hiyo, hivyo katika hilo kuna taabu kubwainayomfika muislamu katika swala yake, hivyo hana njia ya kuk-wepa kujichukulia kipande cha udongo tohara ili awe na imani na

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 35

Page 42: Kusujudu juu ya udongo

36

Kusujudu juu ya udongo

utohara wa kipande atakachosujudu juu yake wakati wa Swala yakeili kujitahadhari dhidi ya kusujudu juu ya uchafu na najsi na takaambazo katu hazimkurubishi kwa Mwenyezi Mungu; na wala Sunnatukufu hairuhusu kusujudu juu yake, na wala akili timilifu haikubali,hasa baada ya kuwepo mkazo kamilifu wa hali ya juu kuhusu uto-hara wa viungo na mavazi ya mwenye kuswali na kukataza kuswalikatika baadhi ya maeneo yakiwemo: Jalalani, machinjioni, mitaroni,bafuni na maeneo ya ngamia, bali imeamrishwa kutoharisha misiki-ti na kuinukiza manukato.80

Kanuni hii ilikuwa imethibiti kwa watu wema waliotanguliajapokuwa historia ilighafilika kuinukuu kwani imepokewa kuwa:Mwanafunzi mmoja wa maswahaba mwanafiqihi Mas�ruqu bin Al-Ajdau aliyefariki mwaka 62 A.H. alikuwa akitembea na tofali safari-ni tokea Madina na kusujudu juu yake, kama alivyotoa Ibnu AbuShayba ndani ya kitabu chake Al-Muswanafu mlango wa aliyekuwaakibeba kitu ndani ya jahazi na akisujudu juu yake.

Hapo ametoa kwa njia mbili kuwa Mas�ruqu alikuwa akibeba tofalindani ya jahazi na kusujudu juu yake pindi anapokuwa safarini.81

Mpaka hapa imebainika kuwa kitendo cha Shia kukazania kukifanyakipande cha udongo kuwa mahala pa kusujudia si chochote ila tu nikumrahisishia mwenye kuswali awapo safarini na nyumbani kuhofiaasije kukosa ardhi tohara au mkeka tohara na ikawa vigumu kwakekuswali, na jambo hili ni kama kitendo cha muislamu kuhifadhiudongo tohara kwa lengo la kutayamamia.Ama siri ya Shia kushikilia Sunna ya kusujudu juu ya udongo wa

80 Al-Allamatu Al-Amini: Siratuna Wasunatuna:158-159.81 Abu Bakr bin Abu Shayba: Al-Muswanafu: 2/172. Darul-fikra -1409 Hijiriyya.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 36

Page 43: Kusujudu juu ya udongo

37

Kusujudu juu ya udongo

Husein (a.s.) hakika hilo ni miongoni mwa malengo ya juu mno namakusudio ya kina mno, kati ya hayo ni: Pindi mwenye kuswalianapoweka paji lake juu ya udongo huo akumbuke kujitolea kwaImam huyo katika njia ya imani na msingi wa dini na kung�oa ujeurina ufisadi, akiwa yeye mwenyewe na watu wa nyumbani kwake nawateule miongoni mwa maswahaba zake.

Na kwa kuwa kusujudu ndio nguzo kubwa mno ya Swala kamailivyo katika Hadithi: �Katika hali ya sijda ndipo mja awapo karibumno na Mola Wake� hivyo inafaa mno awakumbuke kwa kuwekapaji lake juu ya udongo huu mtakatifu wale ambao walifanya miiliyao fidia kwa ajili ya haki na roho zao zikafikia heshima ya juu iliahofie na kunyenyekea, na alazimike kujishusha na kujiinua kirohohuku akiidharau dunia hii danganyifu na mapambo yake ya kupita.Na huenda haya ndio makusudio ya kuwa kusujudu juu ya udongohuo huondoa vizuwizi saba kama isemavyo hadithi. Hivyo katikakusujudu huko kunakuwa na siri ya kukwea na kupanda toka kwenyeudongo mpaka kwa bwana wa mabwana.82

Allamah Al-Amini amesema: �Sisi tunachukua toka udongo waKarbala vipande ving�aravyo na vidonge tunavyosujudu juu yakekama alivyokuwa akifanya mwanachuoni wa fiq�hi aliyetanguliaMas�ruqu bin Al-Ajdau akibeba kipande toka udongo wa Madina nakusujudu juu yake, na mtu huyu ni mwanafunzi wa ukhalifa wema,mwanachuoni wa Madina na mwalimu wa Sunna ya Mtume(s.a.w.w.),yu mbali na bidaa.

Hivyo katika hilo hamna aina yoyote ya kulazimisha maana au cho-chote kinachopingana na wito wa Qur�ani, au kinachopingana namwenendo wa Mwenyezi Mungu au kutoka nje ya maamuzi ya akili

82 Al-Ardhu wal-Turbatu Al-Husayniyatu: 24.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 37

Page 44: Kusujudu juu ya udongo

38

Kusujudu juu ya udongo

na mantiki. Wala si faradhi kwa Shia kuufanya udongo wa Karbalamahala pa kusujudia, wala si wajibu wa kisharia na dini, na wala sijambo la lazima kimadhehebu, wala hamna yeyote miongoni mwaoaliyetofautisha kati ya ruhusa ya kusujudu juu ya udongo huo na ileya udongo wa eneo lote la ardhi, hilo ni tokea siku ya mwanzo yaudongo huo, kinyume na anavyodai asiyewajua Mashia na rai zao.

Udongo wa Karbala si chochote kwao ila ni ubora wa kiakili na walasi jambo lingine, na ni kuchagua tu kilicho bora kusujudu juu yakekiakili na kimantiki kama ulivyosikia.

Na kuna watu wengi wa madhehebu hii ndani ya safari zaowanachukuwa visivyokuwa udongo wa Karbala miongoni mwa vituvinavyosihi kusujudu juu yake kama vile mkeka tohara na safiwanaoamini utohara wake, au khumra yenye hali kama hiyo nawanasujudu juu yake ndani ya Swala zao.83

Huu ni utambuzi wa jumla kuhusu suala hili la kifiqhi; ama ukamil-ifu wake umeachwa sehemu yake, na katika hilo tumetosheka nayale yaliyoandikwa na Wanavyuoni na wasomi wakubwa wa zamahizi. Miongoni mwao nawataja hawa tu:

1- Al-Muslihu-lkabiru Sheikh Muhammad Husein Kashiful-ghita(1295-1373 A.H.) ndani ya kitabu chake ‘Al-ardhu watur’batul-Huseiniyatu’(Ardhi na udongo wa Husein).

2- Msomi mkubwa Sheikh Abdul-Husein Al-Amini mwandishi wakitabu Al-Ghadir (1320-1390A.H.). Ameandika ujumbe kuhusumaudhui hii na kuchapwa mwisho wa kitabu chake SiratunaWasunnatuna (Mwenendo wetu na Sunna yetu),

83 Siratuna wasunnatuna:116-167 Chapa ya Najaf tukufu.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 38

Page 45: Kusujudu juu ya udongo

39

Kusujudu juu ya udongo

3- As-Sujudu a’lal-ardhi (Kusujudu juu ya ardhi) cha mwanachuoniSheikh Ali Al-Ahmadi na amekifanyia uchunguzi na utafiti bora.

Tuliyoyataja katika suala hili ni matunda ya nuru ya elimu yao.Tunamuomba Mwenyezi Mungu awarehemu Wanavyuoni wetuwaliyotangulia na awahifadhi waliobaki. Hizi ndio riwaya tuli-zokomea na ambazo tumezitoa ndani ya muhtasari huu.

MWISHO WA SAFARI

Tutataja mambo mawili:

1-Kulazimisha itikadi na vitendo juu ya mwenye kuzuru

Katika maajabu ya dunia (Ishi uone maajabu ya dunia) ni kuondole-wa uhuru ndani ya Haram mbili tukufu na mwenyekuzuru kulaz-imishwa itikadi na vitendo maalum ilihali toka karne na karne mwe-nendo ulikuwa ni kumpa mwenyekuzuru Haramu mbili tukufu uhuruwa itikadi na vitendo.

Hakika kutabaruku na kuomba kupitia kwa Mtume (s.a.w.w.) naAhlul-Bait ilikuwa ni Sunna iliyoenea katika karne zilizopita na walahakukuwa na kizuizi chochote; huku Sahih Sita na Masanidi zikiwazimelipokea hilo. Haram mbili Tukufu zilikuwa ni eneo la amanikwa mwenyekuzuru kama alivyotaka Mwenyezi Mungu zenyeweziwe hivyo.

Mwenyezi Mungu amesema: “Humo mna dalili zilizo wazi; kati-ka hizo ni mahala aliposimama Ibrahim. Na mwenye kuingia

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 39

Page 46: Kusujudu juu ya udongo

40

Kusujudu juu ya udongo

humo huwa katika amani.”84

Na Mwenyezi Mungu amesema akisimulia dua ya Ibrahimu:

�Na aliposema Ibrahim: ‘Ewe Mola wangu ufanye mji huu uwewa amani”.85

Lakini leo upande huo umekuwa ni kinyume na alivyouombeaIbrahim kwani Shia mwenye kuzuru anayefuata mafunzo ya vitendovya Maimamu wa Ahlul-Bayt haachwi atekeleze ibada zake kwauhuru kamili na wala azungumze chochote anachokiamini, na mfanowa hilo ni kulazimishwa kusujudu juu ya busati la nyuzi nakukatazwa kusujudu juu ya ardhi na udongo.

Na sisi kwa nafasi yetu tunaitolea wito serikali iongozayo katikaardhi za Wahyi iwape uhuru wa kisheria Mahujaji wote iliwatekeleze ibada zao kwa uhuru, kwani hakika hilo linatia nguvumisuli ya umoja na kusaidiana miongoni mwa waislamu bila kujalitofauti zao.

2- Sunna kugeuzwa bidaa

Tayari umeshajua kuwa kusujudu juu ya ardhi au mkeka, kirago namfano wake ni Sunna, na kuwa kusujudu juu ya matandiko, mazuliana mfano wake ni bidaa na hakuna chochote alichoteremshaMwenyezi Mungu kuhusu hilo.

Lakini kinachosikitisha ni Sunna kugeuzwa bidaa na bidaakugeuzwa Sunna, hivyo laiti kama mtu atatenda Sunna misikitini na

84 -Al-Imran; 3: 9785 -Al-Baqara; 2:126

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 40

Page 47: Kusujudu juu ya udongo

41

Kusujudu juu ya udongo

makaburini akasujudu juu ya udongo na mawe basi kitendo chakehiki huitwa bidaa na mtendaji huitwa mtu wa bidaa.

Lakini katika mlango huu si hili tu pekee kwani tunaweza kuonamfano wake ndani ya fiqihi ya madhehebu manne:

1-Sheikh Muhammad bin Abdur-Rahmani Ad-Damashqi amesema:�Sunna katika kaburi ni kusawazisha na ndio rai bora kwa madhehe-bu ya Shafi�i.

Abu Hanifa na Malik wamesema: �Kuweka mwinuko ndio bora kwasababu kusawazisha imekuwa ni alama ya Mashia.�86

Ar-Rafiiy amesema: Hakika Mtume (s.a.w.w.) alisawazisha kaburi lamwanae Ibrahim. Na Qasim bin Muhamad amesema: �Nilionakaburi la Mtume na Abu Bakr na Umar yakiwa yamesawazishwa.

Ibnu Abu Huraira amesema: �Bora hivi sasa ni kuhama toka kwenyekusawazisha kwenda kwenye muinuko kwa sababu kusawazishaimekuwa ni alama ya Mashia na ni bora kuwakhalifu na kumkingamaiti, yeye na ndugu zake dhidi ya kutuhumiwa na bidaa.

Na mfano wa hayo ni haya yaliyonukuliwa toka kwake: Hakika kud-hihirisha Bismillahi kukigeuka na kuwa alama yao basi mustahabuni kuificha ili kuwakhalifu, na akatoa hoja kupitia riwaya iliyopoke-wa kuwa: �Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akisimama lichomozapojeneza ndipo akapewa habari kuwa mayahudi hufanya hivyo basibaada ya hapo akaacha kusimama ili kuwakhalifu.�

86Al-Damash�qiy: Rahmatul-Uma fi-Ikh-tilafil-umati: 1/88 na pia Allamatu Al-Amini ameinukuu ndani ya Al-Ghadiri: 10/209.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 41

Page 48: Kusujudu juu ya udongo

42

Kusujudu juu ya udongo

Na hii hapa ndio sababu aliyotumia kujibu ndani ya kitabu chake naikamvutia Sheikh Abu Muhamad na akaifuata kadhi Ar-Rubaniy.

Lakini wanavyuoni wengi wa kisunni wako katika mtazamo wakwanza, wamesema: Laiti kama tutaacha mambo yaliyothibiti ndaniya Sunna kwa kuwa tu yanalingana na wanayoyafanya watu wabidaa basi hilo litatupelekea kuacha Sunna nyingi.87

2- Al-Imamu Razi amesema: �Al-Bayhaqiy amepokea toka kwa AbuHuraira amesema: �Mtume alikuwa akidhihirisha �BismillahiRahmani Rahimi� ndani ya Swala yake na Ali (Radhi za Allah ziwejuu yake) alikuwa akidhihirisha Bismillahi na hilo limethibiti kwawingi.

Na Ali bin Abu Talib alikuwa akisema: �Ewe ambaye utajo wako nisharafu kwa wenye kukutaja.� Jambo kama hili je inampasa mwenyeakili kwenda mbio kulificha?

Shia wamesema: �Sunna ni kudhihirisha Bismillahi, sawa iwe ndaniya Swala za kudhihirisha au za kunong�ona, na wanavyuoni wote wakisunni wamewakhalifu - mpaka akasema - hakika Ali alikuwaakipindukia katika kudhihirisha Bismillahi hivyo ilipotua dolamikononi mwa Bani Umayyah wenyewe wakapindukia katikakuzuwia kudhihirisha, kwa lengo la kwenda mbio kubatilisha athariza Ali (Radhi za Allah ziwe juu yake).�88

3. Az-Zamakhshari ndani ya Tafsiir yake anapoitafsiri kauli yaMwenyezi Mungu: �Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wakehumtakia rehma Nabii� amesema: Ukiniuliza unasemaje kumtakia

87. Al-Azizi Sharhul-Wajizi: 2/453.88. Ar-Razi: Mafatihul-Ghaibi: 1/205-206.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 42

Page 49: Kusujudu juu ya udongo

43

Kusujudu juu ya udongo

rehma mwingine? Nitasema: Inaruhusiwa kumtakia rehma kilamuumini kwa ushahidi wa kauli ya Mwenyezi Mungu: �Yeye ndiyeambaye huwatakia rehma,� na kauli ya Mwenyezi Mungu: �Watakierehma hakika kuwatakia kwako rehma ni utulivu kwao,� na kauliyake: �Ewe Mwenyezi Mungu wafikishie rehma jamaa wa AbuAufa.�

Lakini wanavyuoni wana ufafanuzi kuhusu hilo nao ni: Ikiwa duahiyo itafuata baada ya ile ya Mtume kama ukasema: Ewe MwenyeziMungu! Mfikishie rehma Mtume na kizazi chake basi hakunamaneno.

Na ama ukimtakia mmoja peke yake miongoni mwa watu wa nyum-bani kwake, kwa namna ile ya kumtakia yeye (Mtume) peke yakebasi kufanya hivyo ni makuruhu kwa sababu jambo hilo limekuwani alama ya utajo wa Mtume na linapelekea kutuhumiwa kuwa niShia89

4- Ndani ya Fat’hul-bari: Wametofautiana kuhusu kumtolea salamuasiye nabii baada ya kuafikiana kuwa ni sheria awapo hai, wapowaliyosema ni sharia bila sharti lolote, na wengine wakasema nisharia kwa kufuatanisha na wala asimtolee peke yake kwa sababukufanya hivyo imekuwa ni alama ya Mashia.

Ameinukuu An-Nawawiy toka kwa Sheikh Abu Muhammad Al-Juwayniy90

Maana yake ni kuwa hajapata kigezo kinachoruhusu kuacha yaleyaliyofanywa kuwa sheria na uislamu ila ni matendo ya Mashia na

89 Al-Kashafu: 2/549.90 Fat’hul-Bari: 14/11.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 43

Page 50: Kusujudu juu ya udongo

44

Kusujudu juu ya udongo

Sunna tukufu za uislamu, na laiti hilo lingesihi basi ingewajibikakwa msemaji aache faradhi na Sunna zote ambazo hufanywa namashia.

�Sema: Kila mmoja anangoja basi ngojeni, na mtajua ni nanimwenye njia iliyo sawa na ni nani aliyeongoka.”91

Imetarujumiwa na Hemedi Lubumba

0715-0171780773-0171780754-017178

91 At-Twaha: 135.

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 44

Page 51: Kusujudu juu ya udongo

45

Kusujudu juu ya udongo

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWANA AL-ITRAH FOUNDATION:

1. Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka kumi na sita

2. Uharamisho wa Riba3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili5. Hekaya za Bahlul6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)8. Hijab vazi Bora9. Ukweli wa Shia Ithnaashari10. Madhambi Makuu11. Mbingu imenikirimu12. Abdallah Ibn Saba13. Khadijatul Kubra14. Utumwa15. Umakini katika Swala16. Misingi ya Maarifa17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia18. Bilal wa Afrika19. Abudharr20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu21. Salman Farsi22. Ammar Yasir23. Qur’an na Hadithi

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 45

Page 52: Kusujudu juu ya udongo

46

Kusujudu juu ya udongo

24. Elimu ya Nafsi25. Yajue Madhehebu ya Shia26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu27. Al-Wahda28. Ponyo kutoka katika Qur’an. 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii30. Mashukio ya Akhera31. Al Amali32. Dua Indal Ahlul Bayt33. Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna.34. Haki za wanawake katika Uislamu35. Mwenyeezi Mungu na sifa zake36. Amateka 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s)38. Adhana.39 Upendo katika Ukristo na Uislamu40. Nyuma yaho naje kuyoboka41. Amavu n�amavuko by�ubushiya42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya swala mbili44. Bismillah ni sehemu ya Qur�ani na husomwa kwa Jahara45. Maulidi46 Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya47. Kufungua Safarini48. Malumbano baina Sunni na Shia

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 46

Page 53: Kusujudu juu ya udongo

47

Kusujudu juu ya udongo

BACK COVER

Sheria ya Kiislamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika na kila jambo hukuikiweka utatuzi wa matatizo yote yanayompata mwanadamu katika sektazote za maisha yake, hivyo Mwenyezi Mungu akasema: "Leo nime-wakamilishieni dini yenu na kuwatimizieni neema Yangu na nime-wapendeleeni Uislamu uwe dini yenu." (5:3).

Isipokuwa kuna masuala madogo madogo ambayo wanazuoni wa sheriawamehitilafiana kwa sababu ya kutofautiana kwao kuhusu riwaya ambazozimenasibishwa kwa Mtume. Jambo ambalo limesababisha kutofautianakuhusu masuala madodo madogo ya sheria.

Kwa kuwa ukweli hutokana na utafiti basi hakika katika mtiririko wamasomo haya mwandishi amejaribu kuliweka swala hili juu ya meza yautafiti, kwani huenda ikawa ndio njia ya kuunganisha mtazamo na kuso-geza hatua katika uwanja huu. Kwani tofauti iliyopo si katika asili namisingi ya dini hata isababishe kuwa na uadui na chuki, bali tofauti iliyoponi kuhusu riwaya zilizonasibishwa na Mtume, nalo ni jambo dogo ukilin-ganisha na mambo mengi ambayo tunaafikiana kati ya madhehebu zaKiislamu. Na mwongozo wetu katika njia hii ni kauli ya MwenyeziMungu: “Na shikamaneni katika kamba ya Mwenyezi Mungu nyote wala msi-farakiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu,mlipokuwa maadui na akaziunganisha nyoyo zenu, hivyo kwa neemaZake mkawa ndugu." (3:103)

Kimetolewa na kuchapishwa na:Al-Itrah Foundation P.O. Box 19701,Dar es Salaam, TanzaniaSimu: +255 22 2110640

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 47

Page 54: Kusujudu juu ya udongo

48

Kusujudu juu ya udongo

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd 7/2/2011 10:52 AM Page 48