upande 1.0 bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. kama kufanya kazi nje ja mji...

66
Upande 1.0 Bajeti yako Bajeti (Budget) ni muhustari wa njisi wewe (na familia yako) mnavyopata na kutumia pesa. Inaunganisha pesa zinazoingia nyumbani kwako (Kipato/ income) na zile unazotumia (matumizi/expenses). Siyo lazima Bajeti iwe sawa na pesa unazozipata na kuzitumia kutokana na hizi nambari kubadilika. Bajeti yako inapaswa kuwa lengo unalojiwekea ambalo unajitahidi kwenda sambamba nalo. Kwa nini ni muhimu kuwa na bajeti? Inakusaidia kutambua ni wapi utumie pesa zako Inakusaidia kuamua unavyotumia pesa zako katika siku za mbeleni Inakusaidia kutunza pesa zako Inakuweka katika nafasi ya kuzuia pesa zako KIPATO Orodhesha sehemu zote kiapato chako kitatokea kwa mwezi ujao(Hauhitaji kuorodhesha viwango vya pesa baado): _________________________ _________________________ _________________________ _________________________ _________________________ _________________________ _________________________ _________________________ _________________________ _________________________ _________________________ _________________________

Upload: others

Post on 31-Jan-2020

22 views

Category:

Documents


2 download

TRANSCRIPT

Page 1: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

Upande 1.0

Bajeti yako

Bajeti (Budget) ni muhustari wa njisi wewe (na familia yako) mnavyopata na kutumia pesa. Inaunganisha pesa zinazoingia nyumbani kwako (Kipato/

income) na zile unazotumia (matumizi/expenses). Siyo lazima Bajeti iwe sawa na pesa unazozipata na kuzitumia kutokana na hizi nambari kubadilika. Bajeti

yako inapaswa kuwa lengo unalojiwekea ambalo unajitahidi kwenda sambamba nalo.

Kwa nini ni muhimu kuwa na bajeti?

Inakusaidia kutambua ni wapi utumie pesa zako Inakusaidia kuamua unavyotumia pesa zako katika siku za mbeleni

Inakusaidia kutunza pesa zako

Inakuweka katika nafasi ya kuzuia pesa zako

KIPATO

Orodhesha sehemu zote kiapato chako kitatokea kwa mwezi ujao(Hauhitaji kuorodhesha viwango vya pesa baado):

_________________________

_________________________

_________________________

_________________________

_________________________

_________________________

_________________________

_________________________

_________________________

_________________________

_________________________

_________________________

Page 2: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

2

MATUMIZI Matumizi (Expenses) ni vitu vyote vinavyokulazimu kutumia pesa zako. Zipo

aina mbili za matumizi: Fixed Expenses (Matumizi yasiyobadilika) na Flexible Expenses (Matumizi yanayobadilika). Matumizi yasiyobadilika ni yale

yasiyoweza kubadilika mwezi hadi mwezi. Matumizi yanayobadilika ni matumizi yale unayoweza kuyabadilisha ikibidi kufanya hivyo. Viwango vya pesa

unavyotumia katika matumizi yanayobadilika vinaweza kuwa tofauti kila mwezi.

Matumizi yasiyobadilika Tengeneza orodha ya matumizi yasiyobadilika utakayokuwa nayo mwezi

ujao(Hauhitaji kuorodhesha viwango baado). Kumbuka kwamba matumizi yasiyobadilika ni yale yasiyotofautiana mwezi hadi mwezi.

KODI______

___________________

___________________

___________________

___________________

___________________

___________________

___________________

___________________

___________________

___________________

___________________

Page 3: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

3

Matumizi yanayobadilika Tengeneza orodha ya matumizi yanayobadilika unayoweza kuwa nayo

mwezi ujao(Hauhitaji kuorodhesha viwango baado). Kumbuka matumizi

yanayobadilika ni yale unayoweza kuyazuia aidha kwa kutotoa pesa au kwa kutumia pesa kiasi.

MAHITAJI vs. MATAKWA

Ni muhimu kuweza kuelezea tofauti kati ya mahitaji (Needs) na matakwa (Wants). Mahitaji ni kitu ambacho ni LAZIMA uwe nacho. Mifano ya

mahitaji ni umeme, kodi ya nyumba na chakula. Matakwa ni vile vitu ambavyo ungependa kuwa navyo ili kuboresha au kurahisisha maisha. Mifano yake ni kama

kufunga cable au ungo vya TV, soda, na pipi au peremende. Unapokuwa unataka kununua kitu unapaswa kufikiria kama kweli unakihitaji. Hii inaweza kuwa ngumu

lakini utashitushwa na wingi wa vitu ambavyo ungeweza kununua visivyo mahitaji

ya kweli. Kama kitu haukihitaji kweli ni bora ukatunza pesa kwa ajili ya siku za mbeleni. Unapaswa kutumia pesa kwenye mahitaji kabla ya matakwa.

_____CHAKULA______

___________________

___________________

___________________

___________________

___________________

___________________

___________________

___________________

___________________

___________________

___________________

Need ni kitu

ambacho ni lazima uwe

nacho

Want ni kitu ambacho

ungependa kwa ajili ya kuboresha au kurahisisha maisha..

Page 4: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

4

Kazi: Mahitaji na Matakwa yako

Orodha ya Mahitaji:

Mahitaji Ni muhimu kiasi gani

kuwa nacho?

Orodha ya Matakwa:

Matakwa Ni kiasi gani unakitaka?

Page 5: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

5

‘Matakwa’ ambayo sitanunua:

Kutoka kwenye ‘Orodha ya juu’, tambua ambavyo hautanunua mwezi huu.

‘Matakwa’ Nitakayonunua:

Page 6: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

6

Kutoka kwenye ‘Ordha ya juu’tambua baadhi

ya vile utakavyonunua mwezi huu

JILIPE MWENYEWE – AKIBA

Umeweka akiba kama matumizi? Umeiweka wapi,

katika matumiziyasiyobadilika au yanayobadilika? Unapopangilia bajeti yako unatakiwa kuweka baadhi ya akiba

zako kama, atumizi yasiyobadilika. Hizi ni pesa unazojitolea

ahadi mwenyewe ya kuziweka kama akiba kila mwezi. Kujilipa mwenyewe yamanisha kwamba kuweka akiba ndiyo jambo la kwanza kutekeleza

kila mwezi na siyo la mwisho. Bajeti nzuri yapaswa kuwa na kiasi cha kutosha kukidhi matumizi yako ya

kwaida, pesa taslimu kwa ajili ya matumizi ambayo hayakutalajiwa na akiba ya kutosha kwa ajili ya wakati ujao. Miezi Fulani utaweza kuwa na akiba zaidi. Miezi

kadha hutaweza kuweka akiba kabisa. Lakini kila mwezi unapaswa kujaribu kuweka akiba angalau kiasi.

UTUMAJI PESA – KUTUMA PESA NYUMBANI Sasa baada ya kufika Marekani, unaweza kutaka kutuma pesa nyumbani kwa wanafamilia. Hilo ni jambo la kawaida na linaloeleweka. Hata hivyo ni

muhimu usitume pesa zaidi ya uwezo wako. Hii ina maana kwamba baada ya kutambua matumizi yako kwa ujumla na kipato chako, kama kuna pesa

inayosalia, unaweza kuweka katika bajeti unaweza kuongezea pesa ya kutuma nyumbani. Uwe makini usitume pesa zaidi ya uwezo wako. Ukifanya hivyo

unaweza kulipia bili zako au ukose pesa ya kulipia mambo muhimu.

Page 7: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

7

Wakati mwingine, inaweza kuwa ngumu sana kutuma pesa ukiwa ndo

umefika Marekani kwa sababu unaweza ukawa baado hauna kazi, na unaweza kutakiwa kutumia pesa kuanza maisha (mfano kununua nguo, vitu vya ndani ya

nyumba yako…). Katika hali kama hii, wakati mwingine ni bora zaidi usubiri hadi utakapojua kipato na matumizi yako ni kiasi gaini kwa mwezi kabla ya kutuma

pesa nyumbani.

Page 8: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

8

MONTHLY BUDGET WORKSHEET KARATASI YA BAJETI YA MWEZI

INCOME/KIPATO

Monthly Income KIPATO KWA MWEZI

Amount KIASI

Mshahara wako $

Mshahara wa mke

$

Msaada wa pesa wa serikali $

Msaada wa pesa kutoka LFS $

Food Stamps/Msaada wa kulipa chakula

$

Usitawi wa jamii(SSI)

Matunzo ya watoto

Kipato kingine ____________ $

Kipato kingine $

Kipato kwa ujumla $

One Time Income KIPATO CHA WAKATI MMOJA

Amount Kiasi

Msaada wa dharula (Unatolewa na LFS)

$

Pesa ya mapokezi (Inatolewa na LFS)

$

Kipato kwa ujumla $

Page 9: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

9

EXPENSES/MATUMIZI (Inaunganisha kila kitu kutoka kwenye orodha ya

‘Mahitaji’ na ‘Matakwa’ yakununua hapo juu)

Fixed/Yasiyobadilika Matumizi kwa mwezi Kiasi

Kodi ya nyumba

$

Maji/majitaka/mengineyo (Kadilia)

$

Simu(Hudumaza kawaida/siyo masafa marefu)

$

Pesa za usafiri(basi) $

Matunzo ya watoto $

Akiba $

Mengine _______________

$

Mengine _______________

$

Jumla ya matumizi

yasiyobadilika

$

Page 10: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

10

Flexible/Yanayobadilika

Matumizi kwa mwezi

Chakula $

Simu (Masafa marefu) $

Umeme

$

Mavazi

$

Elimu $

Vifaa vya Shule $

Usafi wa mwili (Sabuni, shampoo, dawa ya mswaki..)

$

Huduma za afya (Dawa)

$

Kadi za simu

$

Kutuma pesa nyumbani

$

Kufua

$

Mkopo wa usafiri

$

Mengine ____________

Mengine ____________

Jumla ya matumizi $

Page 11: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

11

Bajeti yako vs. Ukweli wako

KUFUATILIA MATUMIZI YAKO

Mwisho wa kila wiki, utaweza kujumlisha kila ulichokitumia kwenye

chakula, mavazi, burudani, na matumizi ya kila aina. Mwisho wa mwezi utapata jumla ya kiasi ulichokitumia katika kila kitengo na kujaza kwenye

karatasi ya muhtasari wa matumizi kama ifuatavyo hapa chini. Ukiisha rekodi kila unachokitumia kwa wastani wa mwezi, unatakiwa

kuipitia bajeti yako sasa ili uhakikishe kwamba inakubalika. Kama bajeti na matumizi yako haviendi sambamba, utahitaji kubadilisha kimoja wapo au

vyote.

Kodi

Umeme

Utunzaji

Watoto

Akiba

Chakula

Mavazi

Burudani

Wiki1

$

$

$

$

$

$

$

Wiki 2

$

$

$

$

$

$

$

Wiki 3

$

$

$

$

$

$

$

Wiki 4

$

$

$

$

$

$

$

Jumla

$

$

$

$

$

$

$

Page 12: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

12

MAPITIO YA BAJETI vs MATUMIZI Je mpango wa matumizi uko sawa na matumizi halisi? Kama sivyo,

ulitumia kidogo au zaidi ya vile ulivyotarajia? Sababu ni zipi? Ni vipi utaweza kuboresha mipango yako mwezi ujao? Andika baadhi ya majibu ya swali hili

hapo chini:

____________________________________________________ ____

____________________________________________________ ____

KUIMARISHA BAJETI YAKO

Kipato Ni maoni gani kwa ajili ya kuongezea kipato?

____________________________________________________ ____

Utumiaji Ni maoni gani kwa ajili ya kupunguza matumizi?

_______________________________________________________ _

Page 13: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

13

ONGEZA KIPATO CHAKO Njia moja ya kuimarisha bajeti yako na kupata pesa zaidi za akiba au za

kutumia ni kuongeza kipato. Mara huwa ni vigumu kupata kazi inayolipa zaidi.

Pamoja na hayo, huwa kuna vitu tunavyoweza kufanya kuongeza kipato chetu kiana. Zaidi ya njia tulizojifunza darasani, njia za kupunguza matumizi

zinajumlisha:

Tumika masaa zaidi: Ukitumika zaidi ya masaa 40 kwenye kazi

moja unatakiwa kulipwa pesa zaidi ya kiwango chako cha kawaida

kwa saa moja. Hii inaitwa “working overtime-kutumika muda wa

ziada” na boss wako anapaswa kukulipa and your boss 1.5 X ya pesa unazotumikia kawaida. Kawaida kama unapata $8.00 kwa saa

unaweza kulipwa $12.00 kwa saa kwa muda wowote uliotumika juu ya masaa 40.

Mke kufanya kazi: Kipato cha familia yako kitaongezeka sana

kama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu,

nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi nyumbani au ya ziada itarahisisha kulipa bili zako au kuweka akiba ya familia kwa

ajili ya wakati ujao.

ELimu: Kurudi shuleni kukamilisha sekondari ya juu, chuo kikuu au

masomo mengine ni moja ya njia nzuri za kuongeza kipato cha

familia yako.

Misaada ya Serikali: Kama kipato chako kiko chini au unayo familia kubwa kuna uwezekano wa kukubaliwa misaada ya serikali.

Kutokana na kipato chako na ukubwa wa familia yako unaweza kustahili kupewa:

Cash Assistance(Msaada wa pesa taslimu): Kusaidia katika

matumizi ya kila siku Food Stamps Kusaidia kulipia chakula

Rental Assistance kusaidia kulipa kodi ya nyumba Medical Assistance kusaidia kupata bima ya afya ya bure.

Zana za kujaribu:

211 (taarifa kuhusu msaada uwezekanao) Mengine?

Page 14: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

14

KUPUNGUZA MATUMIZI

Inaweza kuwa ngumu kwa watu wengi kuongeza

kipato chao sana. Kwa walio wengi, ni rahisi zaidi kudhibiti kiasi cha pesa wanachotumia kuliko kupata kazi inayolipa

zaidi au kutumika masaa mengi. Zaidi ya njia tulizojifunza darasani, njia za kupunguza matumizi ni:

Tembea na pesa taslimu kidogo tu ili usishikwe

na majaribu ya kutumia. Kula nyumbani au uende na chakula chako badala ya kula nje.

Lipa bili zako kwa wakati ili usilazimike kulipishwa pesa za kuchelewa.

Jihadhari matumizi madogo madogo kama soda, pipi na chipsi.

Tumia kuponi. Nunua vitu vya mnada, lakini uendelee kuhemea.

Hemea kwenye maduka yanye punguzo (Maduka yanayouza vitu dollar moja).

Hemea kulingana na mahitaji yako, siyo na matakwa. Usikubaki kushaurishwa na mtu kununua kitu ambacho hauhitaji.

Kama umenunua au umekubali kitu ambacho hauhitaji kirudishe au usimamishe hiyo huduma.

Uwe makini na bajeti yako iliyoandikwa. Hemea wakati wa bei nzuri kama unafikiria kununua kitu chenye

gharama. Tunza risiti za vitu ulivyonunua ili uweze kuvirudisha ukiwa na

tatizo. Epuka mitego ya matumizi!

Kumbuka kwamba

wakati unapojaribu kuweka akiba ya

pesa hata $1 au $5 kwa siku itageuka

kuwa pesa nyingi

Kumbuka Kutunza

risiti zako!

Page 15: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

15

SPENDING TRAPS/MITEGO YA MATUMIZI

Mitego ya matumizi ni bidhaa au huduma ziishiyazo kukugharimu zaidi ya thamani yake au ambavyo haukutegemea.

Mara nyingi hizi huduma huonekana ni za bei nafuu lakini kabla hujakubaliana na moja wapo unapaswa kuelewa gharama zake

kikweli.

Check-Cashing and Money Orders

Kupewa pesa taslimu za cheki na Hawala za pesa

Maduka yanayotoa pesa taslimu za cheki uliyopewa hutoza pesa nyingi ili

upewe pesa taslimu. Ada inakuwa mara nyingi sawa na asilimia 8% za pesa wanazokupa. Kwa mfano, kama ulikuwa na cheki ya $100 na

ukaipeleka kwenye duka linalotoa pesa taslimu kwa ajili ya cheki utatakiwa kulipa $8 ili kupata pesa zako taslimu.

Credit Card Interest and Fees/Riba na Ada za kadi ya mkopo

Kama tutakavyoyazungumzia baadae, kutumia kadi za mkopo kwa

busara yaweza kuwa muhimu wakati ujao kifedha. Ni rahisi sana kujikuta

kwenye matatizo makubwa kutokana na kadi za mkopo. IKama ni lazima ulipe riba ya kadi yako ya mkopo unaweza kujiingiza kwemye madeni

makubwa ambayo ni vigumu kuyaepuka. Wakati huo huo ni vyema kulipa deni la kadi yako ya mkopo kila mwezi (ili usilazimike kulipa riba).

Na unapaswa kulipa kiwango cha chini. Kama hukufanya hivyo, utalipishwa riba na ada, mara nyingi $15 or $20 kila wakati.

Over Drawing Accounts/Kuchukua pesa zaidi kwenye akaunti

Hii hutokea unapo andika cheki au kujaribu kuchukua pesa kwenye

mashine ya ATM ukiwa hauna pesa zilizosalia kwenye akaunti yako. Ukifanya hivyo, benki itakutoza ada ya juu sana. Mara nyingi ada

inaweza kuwa kubwa zaidi ya cheki uliyoandika.

Payday Loans/Mikopo ya kulipa kwa siku

Mikopo ya kulipa kwa siku ni miongoni mwa mitego ya matumizi mibaya

zaidi. Kama unahitaji pesa angalau siku mbili kabla ya kulipwa, wakopeshaji wa kulipwa kwa siku watakutaka uandike cheki ambayo

hawatachukulia pesa taslimu hadi utakapopokea cheki yako ya malipo. Hata hivyo, kama unahitaji $100 kabla ya siku yako nyingine ya malipo,

Page 16: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

16

watakutaka uandike cheki ya $125. Kwa hiyo kukopa $100 kwa wiki

itakugharimu $25 za ziada! Ni karibu riba ya asilimia 1,300%!

Rent-to-Own/Kodi hadi Umuliki

Maduka ya Kodi hadi umiliki ni mtego mwingine mbaya wa matumizi.

Haya maduka yanakuuzia vifaa vya ndani ambavyo hauna uwezo wa kuvilipia bei yake kwa ujumla. Kila mwezi unatoa sehemu ya malipo.Hata

hivyo, haya maduka yanatoza faida au riba kubwa. Hadi kufikia muda wa

kumiliki kifaa ulichouziwa, utakuwa umelipa kati ya mara 3 hadi 10 zaidi ya thamani yake!

Interest Free Purchases/Mauzo bila riba

Baadhi ya maduka yanatangaza kwamba unaweza kununua kitu, ukalipa

baadae na usilipe riba kwa muda wa miaka miwili. Unapaswa kuwa makini na hizi ahadi kwa sababu utakapotakiwa kulipa riba itakuwa ya

juu sana. Kama utanunua kitu bila riba kwa mwaka mmoja au miwili, unatakiwa kukilipia kwa ujumla katika ule muda ambao hautakiwi kulipa

riba.

Page 17: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

17

Upande 2.0

Shopping/ Grocery Ununuzi/Biashara ya vyakula

THE SUPERMARKET – NI NINI?

NI DUKA KUBWA LINALOUZA VIFAA NA

VYAKULA Maduka mengi yanayouza vyakula Marekani

yanakuwa na sehemu ya vyakula, bucha, sehemu ya kutengeneza mikate, matunda na mbogamboga, na

vyote katika ndani ya duka moja. Unaweza kwenda

kwenye soko kubwa kila unapohitaji – yaliyo mengi yanafungua masaa 24. Katika maeneo mengi,

utakuwa na chaguo la maduka makubwa mawili. Kila moja wapo litakuwa na vyakula vyako vya msingi na vitu kadha wa kadha, vinavyoongezea baadhi ya

vitu maalum na vya asili.

Maduka mengine:

Specialty Stores/Maduka maalum: Zaidi ya maduka makubwa, yapo maduka madogo madogo maalum yanayohusika na aina

chache za vitu mfano kama bucha na masoko ya vitu vya asili.

Small neighborhood markets/Masoko madogo ya mitaani:

Mitaa mingi inakuwa na maduka madogo yanayouza vitu vya

msingi (mikate, maziwa, jibini au chizi). Haya maduka yanafaa lakini yanakuwa na gharama kuliko maduka makubwa.

Specialty Stores/Maduka maalum: Wakati yapo maduka maalum au ya asili yanayouza vitu visivyopatikana katika maduka

makubwa ya kawaida (Masoko ya vitu kutoka asia, maduka ya kiafrika…). Watu wanaojitolea wanaweza kusaidia familia kujua

haya maduka yalipo.

UNDERSTANDING PRICING/KUELEWA BEI

Store brands/Matoleo ya duka: Mara nyingi yanakuwepo

matoleo mengi ya kila bidhaa moja maalum. Maduka makubwa

Page 18: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

18

yaliyo mengi yanakuwa na matoleo yake (mfano Kroger), ambayo

yanakuwa ya bei nafuu kuliko mengine. Matoleo mengine mengi yanafanana katika maduka mengi na yote ya na ubora

unaokubalika na ni salama kwa matumizi.

Buying in bulk/Kununua vitu kwa wingi: Njia nyingine nzuri ya kuweza kuweka akiba ya hela ni kununua vitu kwa wingi. Hii ni

njia bora ya kuweka akiba ya hela kwa sababu unaweza kufaidika na punguzo litokanalo na kununua vitu kwa wingi. Na utahifadhi

vile utakavyovihitaji kwa baadae, hasa hasa unavyovitumia sana, au vitu visivyoharibika haraka.

Maduka makubwa yanauza bidhaa zake kwa njia nyingi. Hata kama alama inasema “Mnada”, unapaswa kuelewa utakachikipata kwa

hela yako. Kwa mfano, maduka makubwa yanakuvuta kwa kutumia

vitu kama “2 for $5”. Ukisoma alama kwa undani inaweza ikawa kwamba unaweza kununua kitu kimoja kwa bei ya mnada. Kingine,

kunaweza kuwa “Nunua moja, pata moja bure”. Hii ina maana kwamba unalipa bei kamili kwa ajili ya kitu cha kwanza halafu

unaongezewa kingine bila malipo.

<Mifano ya vitambulisho>

Page 19: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

19

Coupons/Kuponi: Kuponi ni vipande vidogo vya karatasi vinavyotangaza bidhaa za maduka makubwa. Unazipeleka kwenye

maduka na unazitumia kupata punguzo kwenye bidhaa fulani. Kuponi ni sawa na pesa taslimu. Kwa mfano, kama unayo kuponi

ya dola $1.00 kwenye boxi ya nafaka, muuzaji ataipokea kuponi kama ambavyo ingelikuwa ni pesa taslimu. Ufikapo kaunta, kabidhi

kuponi zako kwa muuzaji, atazikagua na mashine na kasha kukutoza pesa inayobaki kwa ajili ya kitu kile ulichonunua.

Kuponi zinapatikana kwa njia nyingi tofauti.

Tovuti za maduka na eKuponi

Mitandao ya tovuti inayouza kuponi

Gazeti la sunday Vipeperushi vy maduka makubwa vya katikati ya wiki

Tovuti za viwanda au watengenezaji Eneo la kuponi kwenye maduka

Kuponi za risiti (nyuma ya risiti yako) Njia ya posta

Store discount cards/Kadi za punguzo za duka: Kadi ya uaminifu, kadi za zawadi, kadi za pointi, kadi za

heri, kadi ya klabu ni kadi ya karatasi au plastiki, ambayo inafanana na kadi ya mkopo

au kadi ya benki, inamtambulisha mwenyenayo kama mwanachama katika mpango wa

uaminifu. Ni njia ambayo maduka makubwa

yanatumia kukuhamasisheni kuendelea kuhemea kwao. Kwa kutumia hiyo kadi unapata

bei nzuri na punguzo kwa baadhi ya bidhaa. Kujua kama bidhaa zimepunguzwa bei, tazama katika vipeperushi

vya duka au chunguza bei kwenye rafu (note to volunteer: explain how items have a price for use with, and without loyalty card. And

you only get discount when card it presented at each purchase). Kupata kadi ni rahisi na ni bure. Jaza tu fomu ya kujiunga kwenye

meza ya huduma kwa wateja, na utakuwa tayari kuanza kuitumia kadi. Uje na kadi yako kila mara unapokuja kuhemea na

uimuonyeshe muuzaji; lakini usiwe na hofu, unaweza kupewa

Page 20: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

20

nyingine ukiipoteza. Pitisha kadi yako kwenye mashine au

uimukabidhi muuzaji. Punguzo lako litakatwa kwenye malipo yako.

Comparison shopping/kufananisha mahemezi: Ukubwa wa furushi haumanishi bei bora zaidi. Wakati mwingine kununulia pamoja vinatoa

bei nafuu, wakati mwingine vinakuwa na bei ya juu. Njia moja tu ya uhakika ni kufananisha bei za kila kipimo. Kawaida vipimo vinakuwa

katika aunsi au paundi. Maduka mengi yanabandika bei kwenye rafu, hali ambayo inarahisisha ufananishaji. Kitambulisho cha bei kitakuonyesha ni

kiasi gain kila kipimo cha hiyo bidhaa kinauzwa.

Mahemezi na bajeti Hakikisha kwamba mahemezi yanakwenda sambamba ba bajeti yako, (Mahitaji vs Matakwa)

Unayo maelfu ya vyakula ya kuchagua katika duka, kwa hiyo ni rahisi

kujisahau na kununua vingi, kununua vitu unavyovitaka lakini ambavyo huvihitaji, au kusahau kitu ambacho unakihitaji

kweli. Andaa orodha ya vitu utakavyonunua kabla ya kwenda dukani. Kuandaa orodha

inaokoa muda nakusaidiakuhakikisha unanua kile unachokihitaji.

Amua ni pesa kiasi gain unazoweza kutumia

katika bajeti yako KABLA ya kwenda dukani. Kwa mfano kama unanunua

chakula kila wiki, jua ni kiasi gain unaweza kutumia kwa wiki, na utumie hicho

kiasi tu. Kama hauna pesa kwa ajili ya kila kitu kilichoko kwenye orodha yako,

amua vilivyomuhimu na uvinunue hivyo (vitu kama mkate, maziwa,

mbogamboga, mchele…) na usinunue vitu ambavyo havina umuhimu na

visivyo kwenye ‘orodha yako ya mahitaji’ (Vitu kama soda, pipi).

Jumlisha mahemezi yako kadiri unavyokwenda Mashine ndogo ya mahesabu inaweza kukusaidia kufuatilia ni kiasi gani

cha pesa umetumia kadiri unavyohemea. Jumlisha bei ya kila kitu unapokiweka

kwenye torori au kikapo chako. Utaweza kujua kiurahisi ulizojumlisha kabla kufika kwenye eneo la malipo au mbele ya muuzaji.

Ni MUHIMU SANA kufuatilia mahemezi yote

uliyoyafanya na kadi yako ya chalula (Food Stamp Card) ili uweze kujua ni pesa kiasi gani ulizobaki nazo kwenye

Page 21: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

21

kadi yako!!!!! Hivi unaweza kuvifanya kwa kutunza na kujumlisha risiti zote

za mahemezi ya kadi. Kujua salio kwenye kadi, tazama upande unaofuata hapo chini juu ya kadi ya chakula (Food Stamps).

Kupangilia kabla na kuchukua maamuzi mazuri

Kingine, pangilia mapishi unayotaka yako katika siku chache zijazo na

uorodheshe viuongo utakavyohitaji. Nunua vyakula vya kutosha

vitakavyokufikisha siku ya mahemezi mengine na huku ukihakikisha

kwamba hautumii pesa zaidi ya zile ulizopanga kwenye bajeti yako.

Unaweza kutumia mashine ya mahesabu kujumlisha vitu kadiri

unavyoviweka kwenye torori yako.

Hata kama unayo orodha, unahitaji kuchukua maamuzi kadhaa sokoni.

Inasaidia unapofikiria kama mpishi. Mpishi mzuri anatengeneza orodha ya

viungo, lakini anaangalia nyama na mazao kujua vilivyo vibichi na vinavyouzwa

vizuri zaidi. Kama mapishi fulani yanahitaji kitunguu lakini kikawa siyo kizuri

au hakipo dukani, mpishi atachagua aina nyingine ya kitungu kilicho bora zaidi.

Au kama kuna samaki iliyo mbichi zaidi, mpishi anaweza kuipendelea kuliko ile

iliyoko kwenye orodha ya mahemezi.

FOOD STAMPS/KADI YA CHAKULA Unavyoweza au Usivyoweza kununua na kadi ya Chakula (Food Stamps).

Kwa kutumia kadi yako ya chakula (Food Stamp) unaweza kununua vyakula unatumia kama:

Maziwa na vitu vyote vitokanavyo na maziwa; nyama, samaki, kuku, mayayi na maharage; nafaka,

mchele, tambi na vitu vingine vya mbegu; viungo vyote vinavyotumika kuchoma au kupika;

matundana mbogamboga; vyakula vya baridi kwa

ajili ya matumizi ya nyumbani; barafu na maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu; maziwa ya watoto,

baadhi ya vyakula maalum vya lishe au vya watu wenye kisukari na vyakula asilia au vyakula hai, mbegu za bustani na mazao

ya vyakula vya kupanda nyumbani. Kwa kutumia kadi yako ya chakula (Food Stamp) huwezi kununua

vifuatavyo: Aina yoyote ya vileo, pombe au mvinyu; aina yoyote ya tumbaku; bidhaa zote

zisizo za vyakula kama vitu vya kusafishia, sabuni na bidhaa za karatasi, nepi; madawa kama aspirin, dawa za kikohozi na vitamini, vifaa vya kutunzia

Page 22: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

22

vyakula kama majagi na mitungi ya kupozea, vyakula vya moto vilivyo tayari

kuliwa, na vyakula ambavyo siyo vyakutumiwa na binadamu kama vyakula vya wanyama.

Kwa vitu ambavyo huwezi kununua na kadi yako ya chakula, utapaswa

kulipa pesa taslimu.

Checking balance on Food Stamps/Kuangalia salio kwenye kadi yako

ya chakula: Njia nzuri ya kufuatilia salio la kadi yako ni kufuatilia kwa makini

matumizi yako yote. Unaweza pia kuita namba 1-800 iliyoko upande wa pili wa

kadi kujua salio (japo unaweza kufanya hivyo kama mara 3 tu kwa mwezi).

Inawezekana pia kufuatilia salio lako kwenye mtandao lakini utahitaji kujisajili

na kuwa na jina na ufunguo wa siri. Jina la kadi hapa Colorado ni Quest card.

TAXES ON NON-FOOD ITEMS/USHURU WA BIDHAA ZISIZO

ZA VYAKULA (Vipi vilipavyo ushuru na visivyolipa ushuru) Vitu ambavyo havilipi ushuru ni pamoja na vyakula kwa ajili ya matumizi

ya nyumbani. Mifano, lakini siyo hiyo tu, nyama, kuku, samaki, mikate, nafaka, mbogamboga, matunda, juisi ya matunda au mbogamboga,

maziwa na vitu vitokanavyo na maziwa, kahawa, chai, nazi, pipi, jojo,

viungo, vinywaji baridi, keki, chipsi, vyakula maalum, vyakula vilivyorutubishwa, maziwa ya watoto, vitu vilivyotengenezwa kuwa

vyakula (kwa mfano mafuta ya nguruwe, mafuta yatokanayo na mbogamboga).

Vitu vinavyolipa ushuru hadi asilimia 3.62% ni pamoja na uuzaji na ununuzi wa bidhaa za matibabu kama vitamini na madini vinavyouzwa

kama mbadala vyakula mbadala, vitu vinavyosaidia afya kama aspirin, dawa za kikohozi, dawa za mafua vitu vinavyozuia asidi. Vyakula

mbadala, visaidizi vya afya, na dawa za kunua madukani vinalipa ushuru kwa viwango vya asilimia 3.62%.

Bidhaa za vyakula zisizouzwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu zinalipiwa ushuru katika

viwango vya asilimia 3.62%. Mifano inaweza kuwa vyakula vya wanyama, mbegu kwa ajili ya ndege, na vyakula vingine vya wanyama.

Page 23: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

23

Vitu vinavyochukuliwa kama vyakula chini ya mpango wa serikali kuu wa

Food Stamp lakini ambavyo havikubaliki kama vyakula vinavyoweza kuuzwa na kusamehewa ushuru isipokuwa vikinunuliwa kwa kadi ya

vyakula au vocha au cheki za WIC ni: Maji yenye dioksidi ya kaboni yanayouzwa kwenye mitungi (Kwa mfano

maji yenye viputo vidogo vidogo au maji ya seltzer). Pipi/jojo.

Mbegu na mazao ya kukuza vyakula. Saladi/kachumbari iliyotengenezwa inayohitaji kutiwa baridi, iwe

imetengenezwa na duakani au kwenye ghala, au watengenezaji wanaouza au kuwalanguzia wauzaji.

Salad bars. Sandwichi za baridi

Trei za deli Chakula kilichopikwa au chakula kinachouzwa kwa ajili ya matumizi ya

papo hapo.

Page 24: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

24

Upande 3.0

Banking/Kutumia Benki

UTARATIBU WA KUTUMIA BENKI

Ili kuishi kulingana na bajeti yako na usimamie pesa zako kwa njia iliyo mwafaka kwako, utahitaji kufungua

akaunti katika benki au umoja wa mikopo.

Disadvantages of Using Cash/Kasoro za kutumia pesa taslimu

Kutembea na pesa nyingi na kulipia kila kitu na pesa taslimu yaweza kuwa hatari, usumbufu na ghali sana. Ubaya wa kutumia pesa taslimu ni:

Siyo salama (unsafe) kwa sababu pesa taslimu zikipotea au zikaibiwa, huwezi kuzipata tena.

Ni usumbufu (inconvenient) kwa sababu unalazimika kutembea na pesa nyingi kama una mpango wa kununua kitu cha gharama

na kila unapohitaji pesa zaidi lazima wende nyumbani kuzichukua. Ni gharama (expensive) kwa sababu utapaswa kulipa ili upewe

pesa taslimu badala ya cheki zako na hawala za fedha.

Advantages of Banks and Credit Unions/Faida za Benki na Vyama vya Mikopo

Benki na Vyama vya mikopo ni biashara zinazotoa sehemu zilizo salama na rahisi kutunza pesa. Zinatoa huduma nyingi tofauti zinazofanya usimamizi

wa pesa zako salama na rahisi zaidi kuliko kutumia pesa taslimu. . Benki na vyama vya mikopo viko salama (safe) kwa sababu serikali

ya Marekani inavipa bima karibu vyote. Kwa njia hiyo, kama benki itashindwa

kukurudishia pesa zako, serikali ya Marekani itakulipa.Hii inaitwa bima ya FDIC. Unatakiwa kuhakikisha kwamba kila unayemupa pesa zako anayo hii

aina ya bima. . Benki na vyama vya mikopo ni rahisi (easy) kwa sababu vilivyo

vingi vinayo maeneo mengi unapoweza kuchukulia pesa zako. Cheki zinarahisisha pia kulipia au kununua vitu vya gharama.

Benki na vyama vya mikopo vyaweza kutokuwa na gharama ( cheap) kwa sababu,

ikuchagua iliyo sahihi, hawatakulipisha ukifungua akaunti au ukichukua pesa zako.

Hata kukiwa na ada itakuwa ndogo kuliko kutumia biashara zinazotoa pesa taslimu

kwa ajili ya cheki au kununua hawala za fedha.

Tofauti kati ya Benki na vyama vya mikopo Tofauti kubwa kati ya benki na chama cha kukopa ni vile ambavyo benki

zinajaribu kuzalisha pesa lakini vyama vya kukopa havifanyi hivyo. Hiyo ina

Page 25: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

25

maana kwamba vyama vya kukopa vinatoa huduma kwa gharama nafuu kuliko

benki.

AINA ZA AKAUNTI

Zipo aina tatu za akaunti za benki au za vyama vya mikopo tutakazozungumzia, Checking Accounts/Akaunti matumizi ya kila siku,

Savings Accounts/Akaunti ya Akiba na Mutual Funds/Hazina ya ubia. Kila moja ya hizi akaunti ni tofauti na inapaswa kutumiwa kwa sababu

zilizotofauti. Unaweza hata kutaka zaidi ya akaunti moja. Tutazungumzia hizi akaunti kwa kirefu zaidi.

Akaunti ya matumizi ya kila siku Akaunti ya checking inapaswa kutumiwa kwa ajili ya pesa unazohitaji

kuzifikia kila siku. Pesa utakazotumia kulipa kodi ya nyumba, pesa unazodaiwa, chakula na matumizi mengine zinatakiwa kuwa kwenye akaunti

ya Checking. Akaunti za checking ni bora zaidi kwa matumizi ya kila siku kwa

sababu zinakupa urahisi wa kufikia fedha zako. Unaweza ukapata pesa taslimu kwenye benki au mashine ya ATM au andika cheki kulipa bili.

Kabla ya kuchagua akaunti ya matumizi ya kila siku (checking) unatakiwa kulinganisha:

Minimum Balance/Baki ya chini: Baadhi ya benki na vyama vya mikopo vinalazimisha kuacha kiasi Fulani cha pesa katika akaunti

yako. Ukiwa na pesa kidogo katika akaunti yako wanakutoza ada. Kadiri baki inavyokuwa ndogo inakuwa bora zaidi.

Unatakiwa kuweka pesa za

matumizi ya kila siku katika

akaunti ya checking

account.

Unatakiwa

kuweka pesa usizohitaji katika

akaunti ya akiba. Savings

account.

Kama huwezi kutumia akaunti ya akiba kwa

sababu za kidini au hautahitaji pesa kwa

muda unaweza kufungua akaunti ya

Mutual Fund.

Page 26: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

26

Fees/Ada:

o Annual Fees/Ada za mwaka: Benki tofauti zinatoza viwango tofauti vya pesa kwa ajili ya kufungua akaunti.

Baadhi ya zinatoa huduma hiyo bure wakati zingine zinatoza ada ya mwezi au ya mwaka.

o ATM Fees/Ada za mashine ya ATM: Baadhi ya benki zinatoza ada kwa kutumia mashine zake za ATM. Kama

utajaribu kutumia ATM ya benki nyingine, ada itakuwa kubwa.

o Overdraft Fee/Ovadrafti (Sawa na deni katika akaunti): Kama utajaribu kuchukua pesa nyingi kwenye

akaunti yako zaidi ya zile ulizonazo, benki itakutoza ada ya ovadrafti.

Number of Transaction/Idadi ya shughuli za biashara: Baadhi ya benki

zinaruhusu kuandika cheki au kuchukua pesa mara kadhaa kwa mwezi. Ukiandika

cheki zaidi ya zile unazoruhusiwa basi benki inaweza kukutoza ada ya ziada.

Akaunti ya akiba Akaunti ya akiba ni sehemu ya kuhifadhi pesa kwa ajili ya wakati ujao.

Ukiweka pesa kwenye akaunti ya akiba, benki zinakulipa pesa ambazo

zinajulikana kama riba kwa kipindi chote utakachoacha pesa kwney akaunti.

Hivyo pesa zako zinaongezeka! Zipo aina tofauti za akaunti za akiba. Yapo mambo machache

yakuzingatia unapo amua ni akaunti gaini ya akiba inayokufa zaidi.

The interest rate/Kiwango cha riba: Kumbuka toka somo la 1, unapoweka pesa benki, benki inazitumia zile pesa kwa kipindi

chote zitakuwa kwenye akaunti yako. Benki itakulipa kwa kuiruhusu kutumia pesa zako. Kiwango cha pesa wanazokulipa

kinaitwa riba. Baadhi ya akaunti za akiba zinalipa riba zaidi ya zingine. Unatakiwa kuchagua akaunti inayotoa riba ya juu

unayoweza kupata. Minimum Balance/Baki ya chini: baadhi ya benki au vyama

vya mikopo vinalazimisha kuacha angalau kiasi Fulani cha pesa kwenye akaunti. Ukiwa na pesa kidogo ya zile kwenye akaunti

yako, wanakutoza ada.

Page 27: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

27

o Fees/Ada:

o Annual Fees/Ada za mwaka: Benki tofauti zinatoza viwango tofauti vya pesa kwa ajili ya kufungua akaunti.

Baadhi ya zinatoa huduma hiyo bure wakati zingine zinatoza ada ya mwezi au ya mwaka.

o ATM Fees/Ada ya mashine za ATM: Baadhi ya benki

zinatoza ada kwa kutumia mashine zake za ATM. Kama utajaribu kutumia ATM ya benki nyingine, ada itakuwa

kubwa.

o Overdraft Fee/Ada ya ovadrafti (Sawa na deni katika akaunti): Kama utajaribu kuchukua pesa nyingi kwenye

akaunti yako zaidi ya zile ulizonazo, benki itakutoza ada ya

ovadrafti.

Terms/Mihula: Zipo akaunti ambazo ukiweka hela kwenye akaunti unapaswa kuziacha zikae kwa muda Fulani. Wakati

mwingine inaweza kuwa mwezi mmoja, wakati mwingine mwaka mmoja, wakati mwingine miaka mingi. Ukijaribu kuchukua pesa

zako kabla ya muhula kuisha, wanakutoza ada kubwa sana.

Page 28: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

28

KARATASI YA TAARIFA ZA AKAUNTI ZA BENKI

Hapo chini ni orodha ya akaunti za akiba na matumizi ya kila siku katika benki muhimu San Diego. Kwa kuzingatia kwamba benki inalo tawi katika maeneo unayoishi, ada, viwango vya riba na baki ya chini unatakiwa

uchague akaunti inayokufaa zaidi. Zipo aina nyingi za akaunti zinazopatika San Diego na The International Rescue Committee haiwezi kupendekeza akaunti fulani juu ya zingine, kwa hiyo unatakiwa kuangalia uwezekano

mwingine.

Checking Accounts/Akaunti ya matumizi ya kila siku

Bank Benki

Minimum

Balance Baki ya

chini

Interest

Rate Kiwango

cha riba

Free

Checks per

Month Cheki za

bure kwa

mwezi

Annual Fee

Ada ya mwaka

ATM Fees

Ada ya

ATM

Overdraft

Fee Ada ya

ovadrafti

Number of

Locations Idadi ya

matawi

Page 29: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

29

Page 30: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

30

Savings Accounts/Akaunti ya Akiba

Bank

Benki

Minimum

Balance

Baki ya chini

Interest Rate

Kiwango cha riba

Annual Fee

Ada ya mwaka

ATM Fees

Ada

ya ATM

Overdraft Fee

Ada ya ovadrafti

Number of

Locations

Idadi ya matawi

Page 31: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

31

Mutual Funds/Hazina ya ubia Akaunti za akiba ndiyo njia rahisi ya kuweka akiba ya pesa na kuzifanya pesa zako ziongezeke

kwa ajili ya mahitaji yako ya muda mrefu. Hata kama dini yako haitakuruhusu kukubari riba

itokayo katika akaunti yako ya akiba, pesa zako zitaendelea kuongezeka katika hazina ya ubia.

Kama unazo pesa nyingi katika akaunti yako

akiba unaweza kuamua kuweka kiasi katika hazina ya ubia kwa kuwa zinaweza kuongezeka haraka kuliko katika akaunti ya

akiba. Lakini hili halitokei kila wakati.

Unapowekeza pesa zako katika hazina ya ubia unakuwa umenunua sehemu ndogo ya biashara kubwa sana. Biashara inavyokuwa ndivyo na pesa

zako zinavyoongezeka. Zipo hazina nyingi za ubia unapoweza kuweka pesa zako.s the businesses grow, so does your money. Hazina za ubia zina utata

kuliko akaunti za akiba kwa sababu biashara unayonunua ukifanya vibaya unaweza kupoteza pesa zako.

Kwa sababu zina utata zaidi unatakiwa kupata taarifa zaidi kabla ya

kuweka pesa zako katika hazina za ubia. Kama unahitaji taarifa zaidi uliza case manager wako IRC.

Page 32: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

32

UJUZI WA KUTUMIA BENKI

Opening an Account/Kufungua Akaunti

Kabla ya kufungua aina yoyote ya akaunti katika benki au chama cha mkopo unatika kuhakikisha kwamba hiyo akaunti inakufaa. Unatakiwa

kufahamu yafuatayo: The interest rate/Kiwango cha riba: Kumbuka toka somo la 1,

unapoweka pesa benki, benki inazitumia zile pesa kwa kipindi

chote zitakuwa kwenye akaunti yako. Benki itakulipa kwa kuiruhusu kutumia pesa zako. Kiwango cha pesa wanazokulipa

kinaitwa riba. Baadhi ya akaunti za akiba zinalipa riba zaidi ya zingine. Unatakiwa kuchagua akaunti inayotoa riba ya juu

unayoweza kupata. Minimum balance/Baki ya chini: Kumbuka, baki ya chini ni kiasi

kidogo kabisa cha pesa unachoruhusiwa kuwa nacho benki. Ukienda chini ya kile kiasi, benki itakutoza ada. Kama baki ya chini

ni zaidi ya pesa unazoweza kuacha benki, unatakiwa kutafuta benki au akaunti nyingine.

Fees/Ada: Baadhi ya benki zinatoza ada kufungua akaunti. Zingine zinatoza ada kila mwezi. Kama benki ina ada ya juu

unaweza kuacha kufungua akaunti nao. Number of Transactions/Idadi ya shughuli za biashara:

Baadhi ya benki zinaruhusu kuandika idadi Fulani ya cheki au

kuchukua pesa mara kadhaa kwa mwezi.

Kufungua akaunti unatakiwa kwenda benki na kuzungumza na mfanya kazi

wa benki. Ukienda unavyotakiwa kuwa navyo ni: Namba yako ya Social Security

Vitambulisho vya aina mbili (Angalau kimoja chenye picha yako, baadhi ya benki zinaomba vitambulisho viwili vyenye picha)

Kielelezo cha anwani yako (Hati ya madai ya karibu inatosha)

Page 33: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

33

Kuandika cheki

Unapomwandikia cheki mtu ni sawa na kumpa pesa taslimu. Wanapopeleka cheki yako kwenye benki zao pesa zitachukuliwa moja kwa

moja kutoka kwenye akaunti yako.

The IRC

4535 30th Street #5

San Diego, CA 92116

PAY TO THE

ORDER OF:

Date:

101

$

Dollars

Memo:

[:1234567]: 123456789012 1234

San Diego National Bank

3526 University Ave, San Diego, CA 92117

Benki itaweka

jina na anwani

yako hapa

Unaandika

jina la

unayemlipa

hapa

Benki itaweka

namba ya cheki

hapa. Kila cheki

ina namba

tofauti inayoanza

na 1.

Unaandika tarehe

ya siku ya siku

unapoandika cheki

hapa

Unaweza kuandika

maelezo madogo

kuhusu sababu ya

cheki. Kama unalipa

bili andika namba ya

akaunti ya hiyo bili.

Andika kiasi cha cheki kwa

tarakimu hapa

Unasai

cheki

hapa

Andika kiasi cha cheki

kwa maneno hapa.

Unaweza kuandika senti

kwa kifupi. Kwa mfano

unaweza kuandika 40/100.

Baada ya kuandika kiasi,

chora msitari mwishoni ili

mtu yeyote asibadilishe

ulivyoandika.

Page 34: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

34

Activity/Zoezi: Writing a Check/Kuandika cheki Jaribu kujaza cheki ifuatayo hapo chini kama vile ungelikuwa unahemea

katika duka la Ralph’s na umenutumia $51.50 kwenye chakula.

Your name

123 40th Street

San Diego, CA 92116

PAY TO THE

ORDER OF:

Date:

101

$

Dollars

Memo:

[:1234567]: 123456789012 1234

San Diego National Bank

3526 University Ave, San Diego, CA 92117

Page 35: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

35

Withdrawing Cash/Kuchukua pesa taslimu Unapoandika cheki, unachukua pesa kwenye akaunti

yako kumlipa mtu mwingine. Zipo njia zingine mbili za kuchukua pesa kwenye akaunti yako.Unaweza kwenda

kwenye tawi la benki na kumuomba (teller) mfanyakazi wa benki kuchukua pesa toka kwenye akaunti yako.

Kama hautaki kusubiri kwenye mustari au kama hauwezi kwenda benki unaweza kutumia (Automatic Teller Machine) mashine maalum ya benki.

Zinaitwa pia ATMs. ATMs ni mashine zitakazochukua pesa kutoka kwenye akaunti yako kwa niaba yako. Zipo ATMs katika kila eneo la mji ili ziweze

kufikiwa kiurahisi na haraka kuliko kwenda benki. Matatizo ya ATMs ni kama: Kuwa na urahisi wa kuzifikia pesa zako huweza kupelekea kununua

vitu ambavyo kwa kweli hauhitaji.

Kila ATM inamilikiwa na benki. Kama utatumia ATM ambayo haimilikiwi na benki yako, watakutoza dola $2 au $3 kutumia

mashine. Kama utatumia hizi ATMs sana inaweza kukugharimu pesa nyingi. Unatakiwa kutafuta ATMs zenye maandishi ya jina la

benki yako.

The teller ni

mfanyakazi wa benki na yupo

kujibu maswali yako uliyonayo.

Page 36: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

36

Depositing Money in Your Account/Kuweka pesa kwenye

akaunti yako

Deposit Slips/Stakabadhi za amana Kuweka pesa kwenye akaunti yako unatakiwa kujaza stakabadhi ya amana. Unakabidhi stakabadhi ya

amana kwa mfanyakazi wa benki au ATM pamoja na pesa taslimu au cheki unazoweka. Utakuta stakabadhi nyuma

ya kitabu chako cha cheki pamoja na taarifa zako zikiwa

zimechapwa hapo. Kama hauna zenye taarifa zako, benki itakuwa nazo stakabadhi ambazo hazijajazwa. Kama

unatumia stakabadhi ya amana ambayo haijajazwa, hakikisha unaweka taarifa zako zote ili benki ielewe kamba ni pesa zako!

Subtotal

Less Cash

Back

Checking or Savings Account Number

Date

Deposit (check one): Checking Saving

Name:

Address:

Signature:

X

Checks

Total $

Cash

Andaka namba ya

akaunti yako hapa.

Kama haujui namba

yako, muulize

mfanyakazi wa

benki

Unaweka alama

pembeni ya aina

ya akaunti

unapotaka kuweka

pesa

Unaweka

tarehe ya

siku

unayoweka

pesa

Andika jina

lako, anwani

na usaini hapa.

Andika kiasi cha

kila cheki

unayoweka katika

kila moja ya hizi

boxi

Andika kiasi

cha pesa

taslimu

unazoweka

Weka jumla ya

cheki zote na pesa

taslimu unazoweka

hapa.

Weka

senti

hapa.

Kumbuka, kama hauna uhakika jinsi ya

kujaza fomu, mfanyakazi wa benki

(teller) yupo kujibu maswali yako.

Jumlisha

pesa zote

ulizoweka

Kama unataka

mfanyakzi wa benki

akurudishie pesa,

andika ni kiasi gani

unataka hapa.

Page 37: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

37

Activity/Zoezi: Depositing Money/Kuweka pesa Jaribu kujaza stakabadhi ya amana hapo chini kama vile ungelikuwa unaweka cheki mbili, moja ya dola $158.22 na nyingine ya $40.00 katika

akaunti yako ya matumizi ya kila siku. Unataka pia mfanyakazi wa benki akurudishie dola $40 taslimu. Namba yako ya akaunti ni 123456789.

Subtotal

Less Cash

Back

Checking or Savings Account Number

Date

Deposit (check one): Checking Saving

Name:

Address:

Signature:

X

Checks

Total $

Cash

Page 38: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

38

Endorsing Checks/Wekea mkono au sahihi cheki Unapoweka cheki uliyoandikiwa benki, unapaswa kusaini nyuma ili itambue kwamba ilikuwa ni wewe. Hii inaitwa kuwekea kuwekea mkono au

sahihi cheki.

KUWA MAKINI! Cheki ikiisha wekewa sahihi mtu yeyote anaweza

kuibadilisha na pesa taslimu. Kwa hiyo, subiri hadi utakapo kuwa benki

ili uweke sahihi yako!

Tumia kila wakati karamu yenye rangi nyeusi au blu.

Weka sahihi yako pale palipo andikwa “Endorse here”tu.

Weka jina lako vile vile linavyoonekana kwenye ule mustari usemao

“Pay to the Order Of” upande wa mbele wa cheki. Andika namba ya

akaunti chini ya sahihi yako.

Kama unataka kuweka cheki, andika “For Deposit Only” juu ya sahihi

yako na uweke namba ya akaunti yako chini ya sahihi yako.

Kama unataka kuweka sahihi lakini cheki iende kwa mtu mwingine,

andika“Pay to the Order Of” ufuatishe jina la mtu unayetaka ile cheki

iende kwake. Halafu weka jina lako chini yake.

ENDORSE HERE

WEKA SAHIHI YAKO HAPA

________________________________

________________________________

________________________________ Do not write, stamp, or sign below this line. Reserved for

Financial Institution Use.

Page 39: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

39

Balancing Your Checkbook/Kusawazisha kitabu chako cha

hundi

Kama unayo akaunti ya matumizi ya kila siku, kiasi cha pesa katika hiyo

akaunti yako kitabadilika sana kwa kipindi cha mwezi. Unapaswa kufahamu vizuri ni kiasi gani cha pesa ulichonacho kwenye akaunti yako ili uhakikishe

haundiki cheki inayozidi pesa ulizonazo. Kufanya hivyo, unapaswa kufuatilia kwa makini kila

unapochukua pesa kwenye akaunti yako, unapoandika cheki au kuongeza pesa kwenye

akaunti yako. Kufuatilia kiasi cha pesa ulichonacho kwenye akaunti yako inaitwa kusawazisha kitabu

chako cha hundi/cheki.

Kama utaandika cheki/hundi yenye thamani

ya pesa zaidi ya ulizonazo benki, inaitwa kurudishiwa cheki. Ukirudishiwa cheki, benki inakutoza ada ya ziada, inaweza kufunga akaunti yako na

kukuweka kwenye orodha ya ChexSystems. Hii itaathiri kiwango cha kuaminiwa kwenye mikopo na inaweza kusababisha kuwa vigumu kwako

kufungua akaunti na benki nyingine kwa kipindi cha miaka mitano.

Kama kuna tatizo unaposawazisha kitabu

chako cha hundi unaweza kupiga simu benki. Namba

ya simu itakuwa kwenye kadi yako ya ATM au taarifa

yako ya benki.

Page 40: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

40

How To Balance Your Check Book/Jinsi unavyosawazisha

kitabu chako cha hundi Kufuatilia cheki zako, pesa unazoweka na kutoa benki, tumia rejesta ya

cheki inayokuja na cheki zako. Kutumia rejesta ya cheki, fuata hatua zifuatazo:

1) Kama unaandika cheki andika namba za cheki kwanza.

2) Andika tarehe 3) Andika maelezo kwa kifupi ya kile unachokifanyar. Kama ni pesa

unachukua kwenye akaunti yako andika uliyemlipa au ulichozichukulia (kodi, mavazi, chakula). Kama unaongeza pesa

kwenye akaunti yako andika pesa zimetoka wapi (malipo ya kazini, zawadi).

4) Kama umetoa pesa kwenye akaunti yako au kuandika cheki weak kiasi katika mnara wa “malipo/mtoe” (“Payment/Debit”).

5) Kama unaongeza pesa kwenye akaunti yako weka kiasi katika mnara

wa Kuweka/Mkopo (Deposit/Credit). 6) Andika kiasi cha nyongeza au pungufu katika mnara wa wa mwisho.

Toa au ongeza kiasi kwenye baki halafu weka baki mpya kwenye mustari unaofuata.

Number Date Transaction Description Payment/Debit Deposit/Credit Balance

Kama

unarekodi

cheki weka

namba hapa.

Andika neno moja au

mawili ya maelezo ya nani

uliyemwandikia cheki, kwa

nini umechukua au kuweka

pesa kwenye akaunti yako.

Andika kiasi cha pesa

zozote unazoweka kwenye

akaunti yako hapa. Pesa

zinazoingia tu ndizo

zinazowekwa katika huu

mnara.

Andika

tarehe

hapa

Andika kiasi cha pesa

unachotoa kwenye akaunti

yako hapa. Kumbuka kuweka

cheki na pesa taslimu

ulizochukua kwenye ATM au

kupewa na mfanyakazi wa

benki. Pesa zinazotoka tu

ndizo zinazowekwa katika

huu mnara

Andika kiasi cha pesa

ulizonazo kwa sasa kwenye

akaunti yako katika mnara

huu wa rangi ya kijivu.

Halafu andika kiasi cha pesa

unazoongeza au kutoa

kwenye eneo la rangi

nyeupe. Ongeza au toa

hicho kiasi kujua baki yako.

Page 41: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

41

Activity/Zoezi: Balancing Your Checkbook/Kusawazisha

kitabu cha hundi Jaribu kurekodi shughuli za pesa zifuatazo na usawazishe kitabu cha

hundi kifuatacho hapo chini. Tutafanya huu mfano kwa pamoja kama darasa. Chukulia kwamba unaanza na baki ya dola $700.

Novemba 3 uliandika cheki ya mwenye nyumba ya dola $650.00 Novemba 7 ulilipwa cheki ya $530.00

Novemba 10 uliandika cheki (namba 125) ya $48.87 ya Ralph’s.

Number

Date

Transaction Description

Payment/Debit

Deposit/Credit

Balance

Sasa jaribu kufanya mfano huu pekee yako. Unaanza na baki ya $531.13

Desemba 1 ulilipwa $800.00 Desemba 4 unachukua $75 taslimu kutoka benki

Desemba 6 unaandika cheki namba 126 kulipa deni la kadi yako ya mkopo ya dola $122.08

Number Date Transaction Description Payment/Debit Deposit/Credit Balance

$700.00

Page 42: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

42

Upande 4.0

Credit/Mkopo

Katika upande huu tutazungumzia mkopo ni nini, umuhimu wake, kwa nini unauhitaji na jinsi unavyoweza kutumiwa.

BASIC DEFINITION/UFAFANUZI WA MSINGI Mkopo ni mapatano juu ya malipo ya taratibu ambayo kawaida hufanyika

kati ya taasisi za fedha kama benki au kampuni za kadi za mikopo. Hizi kampuni mara nyingi huitwa wakopeshaji kwa sababu zinakopesha pesa. Kwa

kifupi, ni sehemu ambayo mkopeshaji anakupa pesa kwa sasa na kubadilishana pesa kwa baadae. Benki zinafanya hivyo kwa masharti mawili:

1. Wakopeshaji wanaamini kwamba wewe

ni mwaminifu na kwamba utazirudisha pesa;

2. Wakopeshaji watatoza ada kwa kufanya

hivi.

Ili uwe mwaminifu kwa mtazamo wa wakopeshaji unapaswa au

kuendeleza historia ya kukopesha pesa na kuzirudisha baada ya muda. Kadiri unavyozidi kufanya hivi, ndivyo mkopeshaji atakuamini. Wakopeshaji hupanga

ada kwa misingi ya jinsi wanavyoamini wewe ni mwaminifu. Kawaida, wakikuamini zaidi ada inakuwa ndogo.

CREDIT BASICS/MISINGI YA MIKOPO Marekani, mkopo ni muhimu sana. Unatumika kama msingi wa kununua

bidhaa zilizo nyingi na huduma. Mara nyingi watu wanakuwa hawana pesa za kutosha kununua bidhaa Fulani na huduma, kama meza, mashine za kufulia na

kukaushia nguo, magari, nyumba, simu, au matengenezo. Mtu anapaswa kutumia mkopo kununua hizi bidhaa na huduma, ambavyo ni sawa na

kukopesha pesa za kununua bidhaa au huduma kwa wakati huu na kulipa zile pesa kwa baadae.

Kwa mfano, kujenga mkopo ni sawa na

kujenga nyumba—inachukua muda, vinapaswa kufanyika kwa uangalifu, na

vinapaswa kuwa na msingi imara. Unapojengwa vizuri unakuwa imara Sana.

Credit/Mkopo ni

wakati benki au kampuni nyingine

inakukopesha pesa

na kukuamini kwamba

utazirudisha.

Page 43: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

43

HOW IS CREDIT USED/MKOPO UNAVYOTUMIWA Tutazame mfano kama wakunua gari. Mohamed anaamua ni gari gain

anayotaka kununua moja kwa moja kutoka kwa mtu mwingine au kutoka kwa mfanyabiashara. Anafahamu kuwa inauzwa $15,000, lakini hana kiasi hicho

cha pesa. Ili ainunue, Mohamed anapaswa kuzungumza na mkopeshaji ambaye atapaswa kutoa kulipia gari. Hizi pesa anapewa mmiliki wa gari au

muuza magari. Lazima sasa Mohamed arudishe zile pesa kwa mkopeshaji.

Swali ni kama mkopeshaji atazimpa pesa Mohamed? Mkopeshaji ataweza kuamini kwamba Mohamed atarudisha pesa? Swali la kwanza atakalouliza

mkopeshaji ni kama Mohamed aliwahi kuazima pesa kabla. Kama ndiyo, sasa watauliza ni wapi ili wachunguze. Watabaini kama Mohamed alizingatia muda

katika malipo yake au hapana.

Kama Mohamed aliazima pesa mara nyingi na kuzilipa kwa muda sasa

atakuwa ana kitu kinachoitwa “historia nzuri ya mkopo”. Kama hakufanya hivyo, basi atakuwa ana “historia mbaya ya mkopo”. Inaweza kuwa kwamba

Mohamed hajawahi kuazima pesa na hana “historia ya mkopo”. Tutazame yote matatu:

1. Historia nzuri ya mkopo – Katika hali kama hii, mkopeshaji ataelekea

kumpa pesa Mohamed.

2. Historia mbaya ya mkopo – Katika hali kama hii, mkopesahji hatampa pesa Mohamed.

3. Hakuna historia ya mkopo – Katika hali kama hii, mkopeshaji

anaweza kumpa pesa kidogo tu Mohamed ili aweze kujenga historia ya mkopo. Mohamed anaweza kuhitaji kununua gari ndogo.

Hii ndiyo maana mkopo ni muhimu sana. Unaonyesha historia ya kulipa mikopo. Inaweza kuwa nzuri au mbaya. Kama wewe ni mzuri wa kulipa

mikopo yako, mkopo unaweza kuwa mzuri kwa sababu unakuwezesha kuazima pesa. Kama una mkopo mbaya, inaweza kusababisha kuwa ngumu au

kushindikana kuazima pesa.

Different uses of the word Credit

Matumizi mbali mbali ya neo mkopo

Credit Card/Kadi ya mkopo: Kadi ndogo ya plastiki yenye namba

maalum inayotolewa na mkopeshaji ambayo inakuwezesha kuazima

pesa. Zilizozoeleka ni kutoka VISA, Mastercard or Discover.

Page 44: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

44

Credit Agency/Wakala wa mkopo: ni kampuni inayofuatilia historia

ya mkopo. Zinatoa pointi kwa wakopeshaji kuonyesha kwamba una historia nzuri, mbaya au hauna kabisa historia ya mkopo.

Credit Score/Pointi za mkopo: nambari zinazoonyesha jinsi mkopo

ulivyo mzuri au mbaya

Credit Report/Ripoti ya mkopo: Wakala wa mikopo anatoa ripoti na

pointi za mkopo kwa wakopeshaji, ambayo inaunganisha historia ya mkopo.

Kadi za mkopo Ripoti/pointi za mkopo Wakala mikopo

CREDIT SCORE/POINTI ZA MKOPO

Sehemu muhimu ya ripoti ya mkopo itakuwa pointi za mkopo. Pointi

zako za mkopo ni namba inayoonyesha jinsi ulivyo katika kulipa pesa ulizoazima kwa mkopeshaji. Kampuni za kadi za mikopo, benki au vyama vya

mikopo vvote vitatumia namba hii kuamua kama vinaweza kukukopesha pesa.

Inakuwa mahali Fulani kati ya 100 na 900. Pointi zikiwa nyingi, mkopo unakuwa mzuri. Hii hapa ni maana ya pointi za mkopo:

700 to 800: Mkopo ulio bora sana

600 to 700: Mkopo mzuri 550 to 599: Mkopo mbaya

100 to 549: Mkopo mbaya sana

Page 45: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

45

Ukiwa na pointi nzuri za mkopo, benki na biashara zingine zitakukopesha

pesa na kukutoza riba na ada ndogo. Kupata mkopo itakuwa rahisi na bei nafuu.

Kwa hiyo ni vipi wakala wa mikopo anatoa pointi zako za mkopo?

Page 46: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

46

Credit Diagram

Mchoro wa mkopo

Kama mchoro unavyoonyasha, mikopo na kadi za mikopo ripoti mikopo

mizuri. Kwa mara nyingine, njia pekee ya kujenga mkopo wako ni kuazima pesa na kuzilipa!

*Note: Benki yako inaweza kukupa “Kadi” yenye nembo ya Visa. Kutumia hii kadi ni sawa na

kuandika cheki, na pesa inatoka kwenye akaunti yako ya benki. Hii siyo kadi ya mkopo, huwezi

kuazima pesa, na haikusaidii kujenga mkopo.

What Are the Different Kinds of Credit? Ni zipi aina tofauti za mkopo? Unaweza kupata mkopo katika njia tofauti. Aina zilizozoeleka ni:

Credit Cards/Kadi za mikopo

Buying a home/kununua nyumba: Wakopeshaji watakupa rehani ili uweze kununua nyumba. Kawaida unailipa benki kwa

muda wa miaka 30.

Collection

Agencies/Wakala wa

ukusanyaji

Credit

Agencies/Wakala wa mikopo:

TransUnion

Experian Equifax

Utilities/Hudum

a za umma

Gas Electric

Phone Landlord/Rent

Mwenyenyumba/Kodi

Checks credit

Reports only

negative credit

Loans/Miko

po

IOM Loan Car Loan

School Loan Home Loan

Bank Loan

Checks credit

Reports

positive and negative

credit

Credit Cards

Kdai za mikopo

VISA*

Mastercard

Discover Store Cards

(gas, department

store, etc.) Bank Cards

Checks credit

Reports

positive and negative

credit

Other

Mengineyo

Medical Bills

Parking Tickets

Subscriptions

Sometimes

checks credit

Reports only negative credit

Page 47: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

47

Buying a car/Kununua gari: Wakopeshaji watakupa mikopo ya

kununua gari. Buying major appliances/Kununua vifaa muhimu vya ndani:

Wakopeshaji watakupa mikopo ya kununua mashine za kufulia na kukaushia nguo, kipozeo, mashine ya kuosha vyombo na jiko.

College/Shule: Serikali na wakopeshaji watakupa mikopo ya kwenda shule.

Page 48: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

48

Bankruptcy/Taflisi ina

maana kwamba huwezi kulipa deni lako.

Kutangaza kufilisika yamaanisha kwamba

hulazimiki kulipa hili

deni. Pamoja na hayo,

kutangaza kufilisika vitaathiri viwango vyako

vya mkopo kwa muda wa miaka saba. Itakuwa

vigumu sana kuazima pesa yoyote kwa wakati

huu. Pili, maamuzi yote kuhusu hali ya kifedha

yatatoka mikononi mwako na kuwekwa

katika mikono ya hakimu. Tatu, hakimu

atatoa amri ya

kutokuruhusu kusimamia nyingi kati ya mali zako.

THE IMPORTANCE OF CREDIT

UMUHIMU WA MKOPO

Kuwa na mkopo na kujua kuusimamia ni moja

ya ujuzi wa kifedha muhimu zaidi unaoweza kuwa nao. Kama unatumia mkopo kwa hekima inaweza

kukusaidia kuyafikia malengo yako kifedha. Kama utatumia mkopo visivyo unaweza kukuathiri vibaya

wewe na familia yako. Hizi hapa takwimu mbili kukuonyesha jinsi mkopo unavyoweza kuwa mzuri au

mbaya: 68% ya Marekani wanamiliki nyumba zao

(US Census Bureau). Walio wengi kati yao walikopesha pesa kununua nyumba zao.

Miaka 30 ijayo, 38% ya familia za

kimarekani watatangaza kufirisika (zaidi ya mmoja kwa kila watu watatu).

The Benefits of Credit/Faida za mkopo Tayari tumezungumzia faida muhimu za mkopo:

Nyumba, gari, elimu: mkopo unakusaidia

kununua vitu kama nyumba, gari

ambavyo usingeweza kuvilipia kama ungelitakiwa kulipia vyote kwa pamoja.

Kufaa kwake: Badala ya kutembea na pesa taslimu unaweza kununua vitu kwa

kutumia kadi yako. Dharura: Kuwa na mkopo inakupa uwezekano wa kutumia zaidi

kwa wiki au mwezi kuliko uwezo wako wa kawaida. Kama una dharura ya muda mfupi, mkopo unaweza kukusaidia kununua

unachokihitaji, hata kama ulikuwa hauna uwezo wa kukinunua kwa wakati huu. Kwa mfano, kama kipozeo chako kikiharibika au mtu

mmoja katika familia yako akaumwa na akatikiwa kwenda hospitali.

Page 49: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

49

The Dangers of Credit/Hatari za mkopo Tayari tumezungumzia pia hatari kubwa za kutumia mkopo. Moja kati ya wa Marekani watatu watafilisika katika miaka 30 ijayo. Matumizi mabaya ya

mkopo ndiyo chanzo kikubwa cha kufilisika. Hii ni kwa sababu: Watu wengi hawatumii kwa hekima kwa sababu hawatakiwi kulipia

wanavyovitaka papo hapo. Ukiwa na kadi ya mkopo ni rahisi kutumia zaidi ya ulivyotakiwa.

Kununua vitu kwa mkopo leo yamaanisha kwa utatakiwa kulipia

hivyo vitu na kipato chako cha siku zijazo. Kama unanua chakula cha usiku kwa kutumia kadi yako ya mkopo leo unaweza kukilipia

kesho, wiki ijayo, mwezi ujao, hata mwaka kesho. kama unalipa ada na riba inaweza kuwa gharama kubwa. Kama

unanua kitu kwa dola $100 kutumia mkopo na kurudisha pesa kwa muda mrefu unaweza

kuishia kulipa dola $150, $200 au zaidi kwa kitu

ambacho kingekugharimu dolar $100 tu.

How Much Can Buying on Credit Cost? Ni kiasi gani unaweza kununua kwa gharama ya mkopo?

Kama unazo dola $500 kwenye kadi yako ya mkopo na malipo ya chini

ya dola $10 kwa mwezi na riba ya asilimia 18% kwenye kadi yako ya mkopo

itakuchukua miaka 8 kumaliza kulipa unavyoidaiwa. Kwa muda huo utakuwa umelipa dola $440 za riba. Kwa hiyo ulichokinunua kwa dola $500

kilikugharimu $940!

CREDIT REPORTS/RIPOTI ZA MIKOPO

Benki na kampuni zingine hazitakuacha uazime moja

kwa moja pesa kwao. Watawapa mkopo watu wanaofikiria

Familia nyingi za kimarekani zinatumia mkopo kununua wanavyovitaka lakini hawana uwezo navyo. Ni rahisi

kuendelea kununua vitu ambavyo hauna uwezo navyo kwa mkopo hadi utakaposhindwa kulipa mikopo yako.

Hapa ndipo mkopo unapoweza kugeuka jinamizi. Utaratibu mzuri ni kutonunua kamwe kitu ambacho

haukihitaji kweli kwa mkopo labda kama ungekilipia mwezi huo.

Ripoti ya mkopo

inaonyesha ulivyolipia deni la

kadi yako ya mkopo na mikopo mingine.

Page 50: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

50

watarudisha pesa zao tu. Kuamua kama utawalipa hizi kampuni zinaangalia

ulivyoshughulikia mikopo ipindi kilichopita. Hapa ndipo inapotumiwa ripoti yako ya mkopo.

Kama unataka kununua nyumba, kununua gari, kukodi nyumba,

kununua mpango wa simu ya mkononi… kwanza muuzaji atapiga simu kuulizia ripoti yako ya mkopo kutoka kwa wakala wa mikopo. Ripoti ya mkopo ni

muhtasari wa nyakati zote ulizojikopesha pesa katika maisha yako (ukiwa Marekani). Itaorodhesha kiasi ulichojikopesha, kama ulilipa kwa muda na kiasi

unachodaiwa kwa muda huu. Itaonyesha ni mara ngapi ulichelewesha malipo na kama ulichelewa siku 30, 60, 90 au zaidi. Ripoti ya mkopo haitoi rekodi ya

taarifa kuhusu rangi yako, dini yako, historia ya afya yako, utaratibu wa maisha yako, rekodi ya makosa ya jinai, au siasa. Ripoti za mikopo

zinaandaliwa na kampuni tatu za mikopo: Equifax, Experian, and TransUnion. Kampuni zilizokukopesha pesa zinawapa taarifa hizi. Taarifa ya mkopo

inaorodhesha taarifa zitakazomsaidia mtu kuamua kama atakupa mkopo au la.

Taarifa zinazoorodheshwa zinaunganisha:

Identifying information/Taarifa za utambulisho: jina lako, anwani ya sasa na ya zamani, namba ya simu, namba ya Social Security, tarehe ya

kuzaliwa, mwajili wako wa sasa na wa zamani.

Credit information/Taarifa za mkopo: Taarifa kuhusu kadi za mkopo, mikopo ya shule, na mikopo mingine. Kwa mfano, mkopo wa IOM

utaorodheshwa kwenye ripoti yako ya mikopo. Taarifa maalum zinahusu: Malipo yanafanyika kwa muda unaotakiwa? Kama hapana,

yanacheleweshwa siku 30, 60, 90+ au zaidi? Ukikamilisha malipo ya mkopo wa IOM, hili litaonekana katika ripoti yako mikopo pia.

Tarehe uliofunguliwa Tarehe ulipofungwa

Kiasi unachodaiwa

Baki Malipo kwa mwezi

Ukusanyaji (wakati kampuni inayokudai inapoita mawakala wa ukusanyaji kwa sababu haulipi)

Kunyanganywa (kampuni inapokunyanganya kitu ilichokuuzia kwa sababu umeshindwa kulipa)

Ukusanyaji, kunyanganywa na ucheleweshwaji wa malipo unaojirudia ni vitu vibaya sana katika ripoti yako ya mkopo. Vikiwa vingi vitakusababishia ugumu

wa kupata mkopo.

Public record information/Rekodi ya taarifa za serikali: rekodi za kufilisika, nyumba kufungwa, ushuru unaodaiwa au ambao haukulipiwa,

uamuzi wakifedha wa mahakama, na pesa za malezi ya watoto ambazo baado zinadaiwa.

Page 51: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

51

Inquiries/Maulizo: majina ya wale walioomba nakala ya ripoti yako ya mikopo na tarehe walipoyiomba. Kampuni haiwezi kuomba ripoti yako ya

mikopo bila ridhaa yako (kwa maandishi au kwa mdomo). Kwa mfano, kama unafanya maombi ya ripoti yako ya mikopo au ripoti yako ya mikopo

inapovutwa ili upate taarifa kuhusu kununua gari. Maulizo mengi yanweza kuathiri mkopo wako kwa sababu inaonekana unahangaika kupata mkopo.

Credit score/Pointi za mkopo: namba inayotumiwa kutabiri jinsi mtu

anavyoelekea katika kulipa kwake mkopo mpya. Pointi za mkopo zitazungumziwa kwa upana wakati ujao.

How to order your credit report/Namna ya kuomba ripoti ya mkopo:

Checking for mistakes/kuchunguza makosa: Chunguza kwa makini

makosa katika ripoti yako ya mkopo na uhakikishe yanasahihishwa. Kwaida ripoti ya mkopo inaunganishwa na taarifa juu ya namna ya kusahihisha

makosa. Anzia kupiga simu kwa wakala wa mikopo (namba zimeorodheshwa hapo juu). Kwaida inafuata barua inayoelezea/fafanua kosa. Unaweza kuhitaji

kuambatanisha cheki zilizobatilishwa au vielelezo vingine vya malipo. Mfano

Getting Your Report/Kupata ripoti yako

Kwa mjibu wa sheria, wanunuzi wote Marekani wanahaki yakupewa ripoti ya mkopo (1) bure kwa mwaka kutoka kila moja ya ofisi kubwa za mikopo: Trans

Union, Equifax and Experian. Ni rahisi sana kuziomba:

Phone: 1(877)-322-8228

Address: P.O. Box 105281, Atlanta, GA 30348-5281 Web Site: www.Annualcreditreport.com

Au omba ripoti yako ya mkopo kutoka kwa mmoja kati ya mawakala watatu wa

mikopo:

Experian 1-888-EXPERIAN (1-888-397-3742) www.experian.com

Equifax 1-800-685-1111 www.equifax.com Trans Union Corporation 1-800-916-8800 www.transunion.com

Utahitaji kutoa jina lako, namba yako ya social security, tarehe ya kuzaliwa, na

anwani. Unaweza kuomba ripoti zote tatu kwa wakati mmoja, au moja kila miezi nne.

Page 52: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

52

wa barua ya kuwatumia wakala wa mikopo kwa ajili ya kusahihisha makosa

inapatikana katika kiambatanisho. Kama wakala wa mikopo hatasahihisha kosa na baado wewe unaamini lipo kosa, wapigie simu wakopeshaji moja kwa

moja na uwaombe wawatumie mawakala wakuripoti mikopo taarifa sahihi. Tuangalie mfano wa ripoti ya mikopo katika kiambatanisho tuone

inavyofanana.

The Cost of Buying a Home/Gharama ya kununua nyumba:

MALIPO KWA MWEZI KWA REHANI YA MIAKA 30 ISIYOBADILIKA

Mortgage/ Rehani ni mkopo mkubwa unaotumika kununua nyumba. Unatunza pesa

kwa ajili ya malipo ya kwanza, benki inakununulia nyumba, halafu unailipa benki

taratibu, kawaida kwa miaka 30.

Tutazame jinsi viwango vya riba ulivyonavyo kwenye rehani yako

vinavyoweza kuathiri malipo yako kwa mwezi…

Kumbuka: Hii chati haiunganishi ada ya umiliki wa nyumba inayoweza kuombwa kwenye

nyumba za condos

Loan

Amounts Kiasi cha

mkopo

Interest Rates/Viwango vya riba

5.5% 6% 6.5% 7% 7.5% 8% 8.5% 9% 9.5%

$20,000 $114 $120 $126 $133 $140 $147 $154 $161 $168

$40,000 $227 $240 $253 $266 $280 $294 $308 $322 $336

$60,000 $341 $360 $380 $399 $420 $440 $461 $483 $505

$80,000 $454 $480 $506 $532 $559 $587 $615 $644 $673

$100,000 $568 $600 $632 $665 $699 $734 $769 $805 $841

$150,000 $852 $1049 $1261

$200,000 $1136 $1398 $1682

$250,000 $1419 $1748 $2102

$300,000 $1703 $2098 $2523

$350,000 $1987 $2447 $2943

$400,000 $2271 $2797 $3363

$450,000 $2555 $3147 $3784

$500,000 $2839 $3496 $4204

$800,000 $4542 $5594 $6727

$2,000,000 (2 MILLION!)

$11,356 $13,984 $16817

Page 53: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

53

Kama unavyoona, kiwango cha riba kinavyokuwa kidogo, malipo kwa mwezi kwa ajili ya rehani yako ndivyo yanavyokuwa madogo. Pointi za mkopo

wako zikiwa nzuri, kiwango chako cha riba kitakuwa kidogo!

Page 54: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

54

Zaidi ya kuangalia pointi zako za mkopo, uanpokwenda

kununua nyumba,

mkopeshaji/dalali atakuuliza maswali ili atambue kama

unakubalika kupewa mkopo: Kipato chako ni kiasi

gani? Historia yako ya kazi iko je?

Una historia ya mkopo? Unalipa madeni yako kwa

muda? Una akiba ya pesa

kwenye akaunti yako ya benki kwa ajili ya malipo

ya kwanza na gharama za kufunga? (kawaida

malipo ya kwanza ni kati

ya asilimia 5-20% ya bei ya kununua)

Una madeni gani kwa wakati huu?

Utayaweza malipo ya mwezi? Malipo

yanategemeana na kiasi cha mkopo, riba, na

muda wa malipo (kawaida miaka 30).

Wanaweza pia kuongeza ada ya umiliki wa

nyumba.

Tutazame mfano wa tofauti katika kupata mkopo wa nyumba kwa watu

watatu.

Azra anakwenda benki. Anataka kununua nyumba.

Mfanyakazi wa benki anavuta ripoti yake ya mkopo kutoka

kwa wakala wa mkopo na anakuta kwamba pointi zake

zinakaribia 800. Pointi zake za mkopo zinaonyesha kwamba anaweza

kuwa kivutio kwa mkopeshaji na anaweza kupata mkopo kwa riba ndogo ya asilimia

(5.5%). Kwa sababu anazo pointi nyingi za mkopo, itakuwa rahisi

sana kuweka pamoja fomu

za mkopo na dalali hatozi ada kubwa. Bila kuchukua

muda mrefu, Azra anaweza kuhamia nyumba yake mpya!

Pili Kalel anakwenda benki ile.

Anataka kununua nyumba. Pointi zake za mkopo siyo nzuri kama za Azra lakini siyo

mbaya sana. Ziko kati ya 600-700. Anaweza kupata mkopo lakini riba itakuwa

kubwa na mkopo hautakuwa rahisi. Labda atalazimika kutoa nakala za karatasi

anazopokelea mshahara na taarifa za benki. Labda wadhamini watahitaji kuitwa.

Inaomba mambo ya ziada kuhakikisha

kwamba ataulipa mkopo. Kwa sababu ni kazi nyingi, pamoja na riba ya juu sana,

benki itatoza ada kubwa na itachukua muda mrefu kabla hajahamia kwenye

nyumba yake mpya.

Tatu, Ibrahim anakwenda benki ile ile. Anataka kununua nyumba. Mfanyakazi wa benki anavuta ripoti yake ya mkopo na anagundua

kwamba pointi zake ni 300 na ana taarifa ya kulisika kwenye ripoti yake. Ni mara chache amefanya malipo yake kwa muda, na malipo

mengi yalicheleweshwa kwa zaidi ya siku 90. Mfanyakazi wa benki hawezi kumpa mkopo kwa sababu mkopo wake ni mbaya sana!

Atatakiwa kumaliza miaka mingi akiboresha mkopo wake kabla ya kununua nyumba. Tutazama njia za kujenga na kuboresha mkopo.

Page 55: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

55

HOW TO GET A GOOD (OR BETTER) CREDIT SCORE

NAMNA YA KUPATA POINTI NZURI ZA MKOPO

Kama unavyoweza kuelezea, kuwa na ripoti nzuri ya mkopo yaweza kuwa muhimu sana kwa

ajili ya malengo yako ya muda mrefu. Utatakiwa kujifunza namna ya kusimamia mkopo wako ili,

wakati ukiwa mwafaka, unaweza kuazima pesa za shule, gari au hata nyumba. Hizi hapa hatua

muhimu zaidi unazoweza kuchukua kujenga au kuimarisha pointi zako za mkopo.

Lipa madeni yako kwa wakati kila mara. Hata kama unalipa

kiwango cha chini ni muhimu sana ulipe angalau hicho kiasi kwa

wakati. Hii ni pamoja na deni la kadi yako ya mkopo, malipo ya mkopo, malipo kwa ajili ya huduma za umma, na kodi ya nyumba.

Deni la International Organization of Migration (IOM) mkopo wa nauli ya ndege iliyokuleta Amerika.

Ideas for paying your bills on time/Mawazo ya kulipa deni kwa wakati

: Weka alama kwenye kalenda ni lini unapaswa kulipa deni kila

mwezi Lipa madeni moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yako ya

matumizi ya kila siku kila mwezi (lakini kumbuka kuhakikisha kuna pesa za kutosha kulipa deni kwenye akaunti yako).

Mafuta ya gari, umeme, simu, bima na makampuni mengine mara nyingi yanaruhusu wateja wake kulipa kwa njia hii.

Ukienda nje ya mji, fanya mpango wa kulipa madeni kwa

wakati (lipa kabla ya muda, nk.) Ukipata taarifa juu ya malipo yaliyochelewa, ni muhimu sana

kulipa deni papo!

Make More Than Your Minimum Payments/Lipa zaidi ya kima cha chini cha malipo. Ukilipa kima cha chini tu

itakuchukuwa miaka mingi kulipia ulivyonunua.

Spend wisely/Tumia kwa makini. Nunua ulivyo na uwezo navyo tu. Ni rahisi sana kuweka kitu kwenye mkopo kama hauna uwezo

nacho kwa sasa. Lakini kumbuka, kadiri vitu vinavyokaa muda mrefu kwenye kadi yako ya mkopo ndivyo unavyolipa riba kubwa

na ndivyo vitu ulivyonunua vinavyopanda bei. Kama leo hauna

Kumbuka, pointi za mkopo

zinavyokuwa nyingi, ndivyo inavyokuwa rahisi

kupata mkopo mbeleni. Unapokopesha pesa utalipa riba ndogo.

Page 56: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

56

uwezo wa dola $50 kwa ajili ya kitu, huenda kesho usipate dola

$75 kwa ajili ya kitu kile kile!

Use Credit/Tumia mkopo. Kutokopesha pesa haikusaidii kupata pointi nzuri za mkopo kwa sababu makampuni hayatajua cha

kutegemea. Hii haina maana kwamba utatakiwa kutumia pesa usizokuwa nazo.

Increasing

Your Credit Score

Kuongeza pointi zako za

mkopo

Decreasing

Your Credit Score

Kupunguza pointi zako za

mkopo Kulipa madeni kwa muda kila mwezi Kudai kiasi kikubwa kinachowezekana

Kutumia pesa kwenye mahitaji na

mikopo kabla ya kutumia kwenye matakwa.

Kutokulipa madeni

Kutumia mkopo kwa uangalifu Kuchelewa kulipa madeni Kulipa baki yote kwenye kadi za mkopo kila mwezi

Kutangaza kufilisika

Kutumia kadi za mkopo kwenye mahemezi pale unapokuwa na pesa

taslimu zinazotosha mahemezi hayo

Kupunguza deni

Caution/Tahadhari: Kaa mbali na makampuni yanayorekebisha

mokpo “Credit Repair”!

Page 57: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

57

CREDIT CARDS/KADI ZA

MKOPO Kuwa na kadi ya mkopo ndiyo aina ya

mkopo ya kawaida watu wanayotumia. Zipo taarifa za msingi kuhusu kadi za mkopo

unazohitaji kujua kabla ya kufikiria kujisajiri kupata moja.

CHOOSING A CREDIT CARD

KUCHAGUA KADI YA MKOPO Unapofikiria kuhusu kujisajiri kupata kadi

ya mkopo unatakiwa kuhakikisha unajua unachokubali. Baadhi ya kadi za mkopo zinatoza ada na riba za juu

zaidi ya zingine. Kwa hiyo unatakiwa kulinganisha angalau mbili kabla ya

kuweka sahihi.

Nyumba ya kila kadi ya mkopo inayouzwa ipo boxi yenye taarifa

muhimu kuhusu kadi ya mkopo. Unatakiwa kuzisoma hizi taarifa kwa

makini ili upate moja yenye riba

ndogo, isiyolipisha ada na inayotoa kipindi kirefu cha uvumilivu.

Ukielewa sheria na taratibu za kadi ya mkopo unaweza kuepuka kulipa ada na gharama zingine.

Credit Limit/Mpaka wa mkopo

Kuwa na kadi ya mkopo yamaanisha kukubaliwa kuazima kiasi Fulani cha

pesa wakati wowote. Hii inaitwa mpaka wa mkopo wako. Wakati wowote unapolipa unachodaiwa unaruhusiwa kukopesha kadi ule mpaka wa mkopo

wako tena. Kwa hiyo, mpaka wa mkopo wako ulikuwa ni dola $1,000

na ulikuwa unadaiwa dola $500 unaweza kuazima zingine dola $500.

Ukilipa dola $500 ulizokuwa

unadaiwa unaweza sasa kuazima dola $1000 kamili. Lakini ukitumia

zaidi ya mpaka wa mkopo wako unavyokuruhusu, unapaswa kulipa

ada kuvuka ule mpaka wako.

Islam and Credit

Cards/Uislamu na kadi za mkopo “Kwa waislamu,

inawezekana kuwa na kadi ya mkopo, lakini hatua kali

zinapaswa kuchukuliwa kuepuka

kuchelewa kulipa baki yote kwa ujumla,” ili kutokusababisha

riba. “ (Kutoka Muslim-investor.com)

Remember/Kumbuka: Jaribu kulipa baki yako kwa ujumla kila mwezi. Lakini,

bila kujali lolote, lipia kadi yako ya mkopo kima chako cha chini. Ukisahau kulipa

kima chako cha chini, kampuni ya kadi za mikopo itakutoza ada ya kuchelewa na

riba ya ziada. Hii inaongeza gharama zaidi. Kama una matatizo ya kulipa

madeni yako, wapigie simu wakopeshaji

wako kabla ya kushindwa malipo.

Page 58: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

58

Kwa mfano: Mpaka wa mkopo wako ni dola $1,000. Ukinunua gari

lilotumika kwa gharama ya dola $1,200 na kadi yako ya mkopo. Taarifa yako ya benki inayofuata itaonyesha ada ya kuvuka mpaka. Hii inaweza kuwa

dolahis $30, $40, au $50! Utatakiwa kulipa hii ada kila mwezi utakaokuwa umevuka mpaka wa mkopo wako.

Interest Rate/Kiwango cha riba Usipolipa kiasi chote cha pesa unazodaiwa mwezi wa kwanza utatozwa

riba juu ya kile unachodaiwa kila mwezi baada ya hapo. Kama utalipa kima cha chini baado utatozwa riba juu kile unachodaiwa ambacho hukulipia. Hii ada

(ambayo inaitwa pia finance fee) inakuwa mara nyingi karibu asilimia 1% au 2% ya kile unachodaiwa kila mwezi. Hii ina maana kwamba riba kwa mwaka

inakuwa kati ya asilimia 12% na 24%. KIwango cha riba kinaitwa pia Annual Percent Rate (APR).

Hata riba za chini zinaweza kugeuka kuwa malipo ya riba za juu (finance

fees)! Kwa mfano: kadi nyingi za mkopo zinatangaza 0% ya riba ya APR. Lakini ukisoma mandishi madogo yaliyochapishwa, mara nyingi utagunduwa

kwamba viwango vya riba vinaweza kubadilika haraka sana. Ukichelewesha malipo mara moja tu kwa ajili ya moja ya kadi/mkopo wako, kiwango cha riba

kinaweza uongezeka hadi asilimia 12%, 18%, hata 24% au zaidi! Kwa hiyo, kwa dola $200 za nguo, ni rahisi kujikuta unatumia dola $36 za ziada kwenye

riba!

Annual Fee/Ada ya mwaka Baadhi ya kadi za mkopo zinakutoza ada kwa kuwa nayo kila mwaka. Kampuni nyingi hazifanyi hivyo. Unapokuwa unatafuta kununua kadi unatakiwa

kuangalia isiyokuwa na ada ya mwaka.

Grace Period/Kipindi cha kuvumiliwa

Hii ni idadi ya siku baada ya kupokea taarifa kwamba kampuni ya kadi ya mkopo itaanza kukutoza riba. Ukilipa kabla ya muda kuisha hautatozwa riba.

Page 59: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

59

Minimum Payments/Malipo ya chini kabisa

Kila mwezi unapaswa kulipa kiasi Fulani kama sehemu ya kile

unachodaiwa. Hichi kinaitwa malipo yako ya chini kabisa na huwa mara nyingi kama dola $20 kila mwezi. Usipolipa hata hicho kiasi kidogo, kampuni

ya kadi za mkopo itakutoza ada ya kuchelewa. Hii ada inaweza kuwa kati ya dola $15 na $30 kila mwezi usipolipa.

Example/Mfano: Baki ya kadi yako ya mkopo ni dola $1,000, kwa riba APR ya asilimia 18%. Malipo yako ya chini kabisa ni dola $30. Ukitoa malipo ya

chini kabisa tu kila mwezi, utalipa kwa ujumla dola $698 za riba kwa muda takribani wa miaka minane! Kama Usipotoa hata malipo ya chini kabisa,

utaishia kuharibu pesa nyingi zaidi katika ada za ucheleweshwaji.

Balance/Baki Baki yako ni kiasi unachodaiwa kwenye kadi yako ya mkopo. Ukilipa kiasi

chote kwa ujumla baki yako itakuwa dola $0. Usipolipa kwa ujumla kiasi chote unachodaiwa baki yako inaweza kuendelea kuongezeka.

CREDIT CARD STATEMENTS/TAARIFA ZA KADI ZA

MKOPO

Kila mwezi utapokea taarifa ya kadi ya mkopo ambayo ni muhtasari wa kila kitu kilichotokea katika akaunti yako. Unatakiwa kuutazama huu

mhutasari na kuhakikisha kwamba unakubaliana na kila kitu kinachojionyesha katika taarifa.

Kama ilivyo benki, makampuni ya kadi za mikopo wakati zinafanya

makosa. Kama utakuta kitu katika taarifa yako na ni kitu ambacho hauna

ku

mb

uku

Kumbuka

kutunza rekodi

zako!

Page 60: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

60

mbu ya kukinunua na kadi yako ya mkopo unatakiwa kuipigia simu kampuni

yako ya kadi ya mkopo papo hapo.

Tutazame mfano wa taarifa ya kadi ya mkopo kwenye kiambatanisho ili tuone inavyofanana taarifa.

Record Keeping/Kutunza rekodi Baada ya kuchunguza taarifa ya kadi yako ya mkopo unatakiwa kuitunza

taarifa yako kwa kufuata ule mtindo wa kutunza nyaraka tuliokufundisha. Kila mwezi weka taarifa yako kwa kufuata mtindo wa kutunza vitu tuliokufundisha.

Hii itakuwasaidia wakati unapokwenda kufuatilia taxes, kuomba mkopo, au ukitaka kuanzisha biashara yako. Ukilazimika kumpa mtu nakala ya taarifa

yako, hakikisha unabaki na karatasi halisi au nakala.

Page 61: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

61

IDENTITY THEFT/WIZI WA UTAMBULISHO Wizi wa utambulisho ni swala zito kabisa. Wizi wa utambulisho ni pale

mtu mwingine anapotumia jina lako, anwani yako, tarehe yako ya kuzaliwa, namba ya social security na/au jina la ubatizo la mama yako katika mambo

yasiyo halali kama kutumia akaunti yako ya benki au kadi ya mkopo kwa jina lako, kupata mikopo, kununua gari, kupata misaada ya kijamii kwa jina lako.

Hili linaweza kuharibu mkopo wako na kuwa ngumu kurekebisha. Haya ni mambo unayotakiwa kufanya kuepuka wizi wa utambulisho:

Chana chana karatasi za maombi ya mkopo, risiti za kadi ya mkopo,

nyaraka zenye taarifa za madeni au za kifedha usizozitaka kabla ya kuviweka kwenye kopo la takataka.

Toa barua zako kwenye sanduku la barua siku ile ile zinapoletwa.

Leta barua zinazokwenda nje kwenye masunduku ya posta ya kukusanyia barua au kwenye ofisi ya posta iliyokaribu. Usiziache katika

masanduku ya barua yasiyo salama.

Kamwe usitoe taarifa zako binafsi kwa njia ya simu labda uwe umpiga simu hiyo mwenyewe.

Kamwe usiache risiti kwenye mashine za benki, etc. Zichanechane wakati

hauzihitaji tena.

Weka kichwani namba yako ya social security na namba zote za siri. Usiziandike popote halafu ukaweka kwenye mkoba wako au pochi.

Saini kwenye kadi kadi zote za mkopo unapozipata au uandike tazama

kitambulisho (“see ID”) badala ya sahihi.

Pitia taarifa za benki za mwezi na utunze risiti zote za kadi za mkopo

Toa kadi za mkopo za ziada na vitambulisho kwenye pochi yako.

Futa kadi zote za mkopo usizozitumia.

Tunza orodha ya kadi zote za mkopo unazozitumia pamoja na namba za

simu za kuita zikipotea

Kadi yako mkopo ikiisha muda wake na usipopokea nyingine mpya kwa njia ya posta, pigia simu kampuni ya kadi za mkopo papo.

Omba ripoti ya mkopo na uyipitie walau mara moja kwa mwaka.

Sahihisha makosa yoyote.

Page 62: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

62

Toa taarifa kwenye kampuni yako ya kadi ya mkopo na benki unapobaadilisha anwani na namba za simu

Ripoti kwenye kampuni kadi za mkopo zilizopotea au kuibiwa papo hapo

Zijue barua na simu zinazoahidi zawadi kupata taarifa zako binafsi.

Zikisikika kuwa nzuri sana kuelekea ukweli, mara nyingi zinakuwa kweli!

Unapopokea ripoti yako ya mkopo unatakiwa kuhakikisha umeichunguza

kwamba haina makosa. Kama kuna kitu chochote usichokubaliana nacho

kwenye ripoti yako ya mkopo, unaweza kujaribu kuomba

kiondolewe. Taarifa zaidi zimetolewa

katika kiambatanisho kuhusu kusahihisha makosa ya mkopo au

zungumza na mkufunzi wako. Kitu bora zaidi ni kujaribu

kuzuia wizi wa utambulisho katika nafasi ya kwanza.

Ukihisi kwamba utambulisho wako umeibiwa, unaweza kuwasiliana na

namba zifuatazo:

Ofisi ya Sheriff iliyoko karibu

Equifax: 1-800-525-6285 Experian: 1-800-397-3742

TransUnion: 1-800-680-7289

Page 63: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

63

IF YOU CANNOT GET CREDIT/KAMA HUWEZI KUPATA

MKOPO Start Building Your Credit/Anza Kujenga mkopo Unatakiwa kujenga mkopo kwa muda. Kama wageni wapya huenda hamkuwa au baado hamjakuwa na historia ya mkopo. Kwa sababu hiyo,

Makampuni ya Kimarekani yajajua mengi juu yenu au jinsi mtakavyowalipa. Kwa hiyo, katika kujiweka salama, yanaweza kuamua kutowakopesha pesa

kabisa. Hili linaweza kusababisha matatizo makubwa unapokuwa unataka kununua gari au nyumba lakini huwezi kupata mkopo.

Kuanza kujenga mkopo unaweza:

Fungua akaunti ya akiba nay a matumizi ya kila siku na uyisimamie

kwa uangalifu.

Jisajili kwa ajili ya kadi ya mkopo ya mafuta ya gari au kitengo cha

duka. Ni rahisi kupata kuliko kadi ya mkopo ya kawaida.

Chukua mkopo mdogo wa gari au vifaa vya ndani na uulipe kwa wakati.

Jisajili kwa ajili ya kadi ya mkopo yenye dhamana.

SECURED CREDIT CARDS/KADI ZA MKOPO ZENYE

DHAMANA Kadi za mkopo zenye dhamana ni nzuri zaidi kwa watu wasio na historia

ya mkopo au wenye historia mbaya ya mkopo. Kadi ya mkopo yenye dhamana

inaomba kutunza pesa kwenye akaunti ya akiba ili kampuni ya kadi za mkopo ijue kwamba italipwa. Kawaida, benki italipa kiasi kidogo cha riba kwenye pesa

uliyoweka benki. Riba utakayotozwa kwenye pesa unayodaiwa kwenye kadi ya mkopo itakuwa kubwa zaidi. Kiwango kidogo unachoweka benki ni kiasi

cha pesa unachotakiwa kukiacha kwenye akaunti ili uweze kuitumia kadi ya mkopo.

Kama ilivyo kadi ya mkopo ya kawaida, unatakiwa kutafuta kadi yenye

ada na riba ndogo. Zifuatazo hapo chini ni orodha ya kadi za mkopo zenye dhamana zipatikanazo California. The International Rescue Committee

haipendekezi kadi yoyote kati ya hizi kuliko nyingine. Huenda zipo kampuni zingine zenye kadi zenye kadi dhamana na unatakiwa kutafuta inayokidhi

vizuri zaidi mahitaji yako.

Page 64: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

64

Bank Benki

Phone Number

Namba ya simu

Annual Fee Ada ya

mwaka

Interest Rate on

Credit Card Riba

kwenye kadi ya

mkopo

Minimum

Deposit Kiasi cha

chini kuweka

benki

Bank of America (800) 732-9194 $29 15%

$250

Washington Mutual (800) 884-1789 $50 14%

$300

US Bank (800) 285-8585 $35 19%

$300

Wells Fargo (800) 642-4720 $18 17.24%

$300

CREDIT CARD STATEMENTS/TAARIFA ZA KADI ZA

MKOPO Kila mwezi utapokea taarifa za kadi ya mkopo ambayo ni mhutasari

wa mambo yaliyofanyika kwenye akaunti yako. Unatakiwa kuutazama huu mhutasari na kuhakikisha kwamba unakubaliana na kila kilichoko katika

taarifa.

Kama ilivyo kwa mabenki, kampuni za kadi za mkopo na zenyewe wakati mwingine hufanya makosa. Kama kuna kitu katika taarifa ambacho

haukununua na kadi yako unatakiwa kuipigia simu kampuni ya mkopo papo hapo.

Record Keeping/Kutunza Rekodi Baada ya kuipitia taarifa ya kadi yako ya mkopo

unatakiwa kuitunza taarifa yako katika jalada lile la nyaraka tulilokupatia. Kila mwezi uweke taarifa yako

katika jalada lile la kutunza nyaraka tuliokupatia. Hili litakusaidia wakati wa kufaili ushuru wako, kufanya

maombi ya mkopo, au kuanzisha biashara yako.

Ukitaka kumpa mtu nakala ya taarifa yako, hakikisha unabaki na karatasi ya asili au nakala.

Kumbuka kutunza rekodi zako!

Page 65: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

65

Page 66: Upande 1.0 Bajeti yakokama watu wazima wote kwenye mji wanafanya kazi. Kama kufanya kazi nje ja mji haikubaliki katika utamaduni wenu, nyongeza ya kipato inayotokana na kufanya kazi

66