uchambuzi wa kiisimujamii wa majina ya koo za …repository.out.ac.tz/2125/1/tasnifu ya shahadada ya...

109
UCHAMBUZI WA KIISIMUJAMII WA MAJINA YA KOO ZA KISUKUMA: MFANO KUTOKA WILAYA YA MISUNGWI LETICIA BUSSUNGU KALEKWA TASNIFU ILIYOWASILISHWA IKIWA NI SEHEMU YA MASHARTI YA KUPATIWA SHAHADA YA UZAMILI YA KISWAHILI YA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA 2018

Upload: others

Post on 11-Jan-2020

16 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

UCHAMBUZI WA KIISIMUJAMII WA MAJINA YA KOO ZA KISUKUMA:

MFANO KUTOKA WILAYA YA MISUNGWI

LETICIA BUSSUNGU KALEKWA

TASNIFU ILIYOWASILISHWA IKIWA NI SEHEMU YA MASHARTI YA

KUPATIWA SHAHADA YA UZAMILI YA KISWAHILI YA CHUO KIKUU

HURIA CHA TANZANIA

2018

ii

UTHIBITISHO

Aliyetia saini hapo chini anathibitisha kuwa ameisoma tasnifu hii yenye mada:

―Uchambuzi wa Kiisimujamii Katika Majina ya Koo za Kisukuma: Mfano Wilaya

ya Misungwi‖ na amekubali kuwa imefikia kiwango kinachotakiwa na inafaa

kuwasilishwa kwa ajili ya utahini wa shahada ya Uzamili ya Kiswahili ya Chuo Kikuu

Huria cha Tanzania.

………………………………………………

Dkt. Bibiana S. Komunte

(Msimamizi)

………………………….…………………..

Tarehe

iii

HAKIMILIKI

Hairuhusiwi kuiga au kunakili kwa namna yoyote ile tasnifu hii kwa ajili yoyote kama

vile kielektroniki, kurudufu nakala, kurekodi au njia yoyote nyingine bila ya idhini ya

mwandishi au Chuo kikuu Huria cha Tanzania.

iv

TAMKO

Mimi, Leticia Bussungu Kalekwa, nathibitisha kuwa hii ni kazi yangu halisi na

haijawahi kuwasilishwa katika chuo kikuu kingine chochote kwa ajili ya kutunukiwa

shahada hii au nyingine yoyote.

…………………………

Sahihi

………………………….

Tarehe

v

TABARUKU

Tasnifu hii naitabarukia mume wangu mpendwa Mussa Daudi, ambaye alinihimiza na

kunitia moyo kila mara maisha yalipokuwa magumu kama mawe. Aidha alistahimili

upweke na ukiwa ulioathiri hali ya kawaida katika harakati yote ya masomo yangu.

Vilevile, naitabarukia wazazi wangu wapendwa Mzee Julius Nyaga na mama Auleria

Bussungu walionilea na kunifunza thamani ya mtoto wa kike kupata elimu. Baba na

Mama Mungu awape maisha marefu.

vi

SHUKRANI

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa uwezo wa kutimiza ndoto yangu ya

kupata shahada ya uzamili katika Kiswahili. Ninawashukuru wahadhiri wote wa Idara

ya Isimu kwa kazi yao nzuri kupitia nasaha zao.

Aidha.Ninamshukuru Dkt. Bibiana Shauri Komunte kwa mwongozo mzuri wa

kunijenga hadi kukamilisha kazi hii. Mungu amjalie afya njema katika maisha yake.

Pia ninawashukuru Dkt. Anna Kishe, Dkt. Hanna Simpasa, Prof James Mdee, Dkt.

Zelda Elisifa, Dkt. Hadija Jilala, na Dkt. Nestory Ligembe walionipa ushauri na

maelekezo ili nifanikishe kazi hii.

Pia Ninawashukuru marafiki zangu Said H. Said, Johnbosco B. Joseph, Vedastus

Ambrose, Mary Kanichi, na Lucas Jeremiah kwa kunihimiza ili nisife moyo japo

maisha yalikuwa yamechukua mkondo tofauti. Ninawashukuru wote waliofanikisha

utafiti huu.

Mwisho lakini si mwisho kabisa, Ninamshukuru sana Mjomba wangu George

Bussungu kwa kunitia moyo katika muda wote wa masomo yangu. Mwisho kabisa

lakini wa kwanza kwa umuhimu, ninamshukuru sana Mume wangu na wanangu

wapendwa Janeth, Justine, na Japhet kwa uvumilivu na staha yao wakati wote wa

masomo yangu.

vii

IKISIRI

Utafiti huu ulilenga kuchambua kiisimujamii majina ya koo za kisukuma wilayani

Misungwi katika mkoa wa Mwanza. Katika kutimiza azima hii, malengo mahususi

yalikuwa kwanza, kufafanua jinsi majina ya kisukuma yanavyotofautisha jinsi ya

wanajamii na kuchambua jinsi Nyanja za kiisimujamii zinavyosababisha majina ya

koo hizo. Mikabala ya maelezo na takwimu imetumika. Mbinu za utafiti zilizotumika

ni usaili na hojaji. Sampuli makusudi imetumika. Eneo la utafiti ni Wilaya ya

Misungwi katika mkoa wa Mwanza. Data zimekusanywa kwa maswali dodoso, na

usaili .Matokeo ya utafiti wa lengo mahususi la kwanza yamebainisha majina

kutofautisha jinsi za wanajamii hawa lakini yanafanana kimaana, ijapokuwa

yanatofautiana kifonolojia kutokana na kitamkwa (fonimu) kimoja au silabi moja

inayounda maneno ya majina hayo. Mfano ―Kabula,‖ ni mwanamke wakati

―Mabula‖ ni mwamme, lakini yote mawili yanamaanisha ―Mvua‖. Kwahiyo, silabi

$ka$ na $ma$ ndiyo hutofautisha jinsi hizi mbili.Aidha utafiti umedhihirisha kuwa,

nyanja za kiisimujamii zinazotofautisha majina ya koo za kisukuma kisemantiki na

kiisimujamii kama hapo juu, ilihali Kiisimu jamii yanazingatia matukio, ukoo mahali

alipozaliwa, na baada ya kuzaliwa mtu. Mfano, ―Bulugu‖ au ―Malugu‖ hutokana na

vita(vurugu). Kiukoo, jina ―Ng‘hwashi‖ inamaanisha ukoo wa wavuvi ili hali

―Ngwandu‖ inamaanisha aliyezaliwa chini ya Mbuyu.Utafiti umehitimisha kuwa ,

majina ya koo za kisukuma yanafanana kimaana, lakini yanatofautiana kifonolojia

kuhusu jinsi. Aidha, majina ya koo za kisukuma yamegawanyika katika vigezo vya

kisemantiki na kiisimujamii.

viii

YALIYOMO

UTHIBITISHO ............................................................................................................ ii

HAKIMILIKI .............................................................................................................. iii

TAMKO ....................................................................................................................... iv

TABARUKU ................................................................................................................. v

SHUKRANI ................................................................................................................. vi

IKISIRI ....................................................................................................................... vii

ORODHA YA MAJEDWALI .................................................................................. xii

ORODHA YA VIAMBATISHO ............................................................................. xiv

ORODHA YA VIFUPISHO ...................................................................................... xv

SURA YA KWANZA ................................................................................................. 1

UTANGULIZI WA JUMLA ...................................................................................... 1

1.1 Utangulizi......................................................................................................... 1

1.2 Usuli wa Lugha ya Kisukuma .......................................................................... 1

1.2.1 Eneo la Lugha ya Kisukuma ............................................................................... 1

1.2.2 Shughuli za Kiuchumi katika Jamii ya Wasukuma ......................................... 3

1.2.3 Mfumo wa Kijamii wa Wasukuma .................................................................. 3

1.3 Usuli wa Tatizo ................................................................................................ 3

1.4 Tatizo la Utafiti ................................................................................................ 8

1.5 Malengo ya Utafiti ......................................................................................... 10

1.5.1 Lengo Kuu ..................................................................................................... 10

1.5.2 Malengo Mahsusi ........................................................................................... 10

1.5.3 Maswali ya Utafiti ......................................................................................... 11

1.6 Umuhimu wa Utafiti ...................................................................................... 11

ix

1.6.1 Kitaaluma ....................................................................................................... 11

1.6.2 Kiutamaduni................................................................................................... 11

1.6.3 Kitaifa ............................................................................................................ 12

1.7 Mawanda ya Utafiti ....................................................................................... 12

1.8 Hitimisho ....................................................................................................... 12

SURA YA PILI ........................................................................................................... 13

MAPITIO YA KAZI TANGULIZI .......................................................................... 13

2.1 Utangulizi....................................................................................................... 13

2.2 Dhana ya Maana ............................................................................................ 13

2.3 Dhana ya Isimujamii ...................................................................................... 16

2.4 Dhana ya Majina kwa Ujumla ....................................................................... 18

2.4.1 Majina kwa Ujumla ....................................................................................... 23

2.5 Mkabala wa Nadharia .................................................................................... 29

2.6 Sababu za Kiisimujamii za Majina ................................................................ 30

2.7 Kiunzi cha Nadharia ...................................................................................... 30

2.8 Hitimisho ....................................................................................................... 35

SURA YA TATU ........................................................................................................ 36

MBINU ZA UTAFITI ................................................................................................ 36

3.1 Utangulizi....................................................................................................... 36

3.2 Muundo wa Utafiti ......................................................................................... 36

3.3 Eneo la Utafiti ................................................................................................ 37

3.4 Kundi Lengwa................................................................................................ 38

3.5 Sampuli .......................................................................................................... 39

3.5.1 Usampulishaji ................................................................................................ 39

x

3.6 Mbinu za Utafiti ............................................................................................. 40

3.6.1 Mbinu za ukusanyaji wa data......................................................................... 40

3.6.2 Mbinu ya Usaili ............................................................................................. 40

3.6.3 Mbinu ya Hojaji ............................................................................................. 41

3.7 Mikabala ya Uchambuaji Data ...................................................................... 41

3.8 Maadili ya Utafiti ........................................................................................... 42

3.9 Mipaka ya Utafiti ........................................................................................... 42

3.10 Hitimisho ....................................................................................................... 42

SURA YA NNE .......................................................................................................... 43

UWASILISHAJI NA UCHAMBUZI WA MATOKEO YA UTAFITI ................ 43

4.1 Utangulizi....................................................................................................... 43

4.2 Nyanja Zinazosababisha Majina ya Koo za Kisukuma ................................. 43

4.2.1 Mgawanyo wa Majina kwa Kigezo cha Kisemantiki .................................... 43

4.2.1.1 Majina ya Koo Yaliyotokana na Mwonekano wa Maumbile ........................ 44

4.2.1.2 Majina Yanayotokana na Sehemu za Makazi ................................................ 46

4.2.1.3 Majina ya Koo Yanayotokana na Vitu .......................................................... 47

4.3 Mgawanyo wa Majina ya Koo kwa Kigezo cha Kiisimujamii ...................... 50

4.3.1 Majina Yaliyotokana na Matukio .................................................................. 51

4.3.1.1 Matukio Yanavyohusiana na Jinsi Mtoto Alipozaliwa na Baada

ya Kuzaliwa ................................................................................................... 52

4.3.1.2 Matukio Yaliyotokana na Mahali pa Kuzaliwa ............................................. 57

4.3.1.4 Majina Yanayotokana na Vipindi vya Misimu .............................................. 59

4.3.1.5 Majina Yanayotokana na Matendo ya Watu .................................................. 61

4.3.3 Majina ya Koo Yaliyotokana na Shughuli, Ujuzi wa Kiufundi ..................... 64

xi

4.3.4 Majina ya Koo Yaliyotokana na Vitu ............................................................ 64

4.3.5 Majina Yaliyotokana na Mimea .................................................................... 65

4.3.6 Majina Yaliyotofautisha Jinsi ........................................................................ 66

4.3.7 Majina Yanayotokana Baada ya Kuzaliwa Watoto Mapacha ....................... 67

4.3.8 Majina Yanayotokana na Chimbuko la Ukoo................................................ 69

4.3.9 Majina yanayotokana na Jina la Mungu ........................................................ 70

4.3.10 Hitimisho ....................................................................................................... 71

SURA YA TANO ....................................................................................................... 72

MUHTASARI HITIMISHO NA MAPENDEKEZO ............................................. 72

5.1 Utangulizi....................................................................................................... 72

5.2 Muhtasari wa Utafiti ...................................................................................... 72

5.3 Muhtasari wa Matokeo ya Utafiti .................................................................. 73

5.3.1 Majina ya Koo Yanayotofautisha Jinsi .......................................................... 73

5.3.2 Nyanja Zinazosababisha Kutumia Majina ya Koo ........................................ 74

5.3.3 Athari Zinazojitokeza Katika Kutopewa Majina ya Koo za Kisukuma ........ 75

5.4 Hitimisho ....................................................................................................... 76

5.5 Mapendekezo ................................................................................................. 77

5.6 Tafiti Fuatishi ................................................................................................. 77

MAREJEO .................................................................................................................. 79

VIAMBATISHO ........................................................................................................ 86

xii

ORODHA YA MAJEDWALI

Jedwali Na. 4.1: Majina ya Koo Maliyotokana na Mwonekano wa Maumbile ........... 45

Jedwali Na. 4.2: Majina ya Koo Yanayotokana na Makazi ......................................... 47

Jedwali Na. 4.3: Majina ya Koo Yaliyotokana na Vitu ............................................... 48

Jedwali Na. 4.4: Matukio Yaliyohusiana na Jinsi Mtoto Alipozaliwa na Baada ya

Kuzaliwa ............................................................................................ 53

Jedwali Na. 4.5: Majina Yanavyohusiana na Jinsi Mtoto Alipozaliwa na Baada ya

Kuzaliwa ............................................................................................ 54

Jedwali Na. 4.6: Majina Yaliyotokana na Mahali pa Kuzaliwa................................... 57

Jedwali Na. 4.7: Majina Yanatokana na Maradhi/Hali ................................................ 58

Jedwali Na. 4.8: Majina Yanayotokana na Misimu ..................................................... 60

Jedwali Na. 4.9: Majina Yanayotokana na Misimu ..................................................... 60

Jedwali Na. 4.10: Majina Yanayotokana na Matendo ya Watu ................................... 61

Jedwali Na. 4.11: Majina Yanaytokana na Matendo ya Watu ..................................... 62

Jedwali Na. 4.12: Majina ya Koo yaliyotokana na Tabia za Watu, Sitiari

Wanyama na Ndege ......................................................................... 62

Jedwali Na. 4.13: Majina ya Koo Yaliyotokana na Tabia za Watu, Sitiari za

Wanyama na Ndege ........................................................................ 63

Jedwali Na. 4.14: Majina ya Koo Yaliyotokana na Tabia za Watu, Sitiari za

Wanyama na Ndege ........................................................................ 63

Jedwali Na. 4.15: Majina ya Koo Yaliyotokana na Shughuli za Kiufundi .................. 64

Jedwali Na. 4.16: Majina Yanayotokana na Hali ya Vitu ............................................ 64

Jedwali Na. 4.17: Majina Yanayotokana na Hali ya Vitu ............................................ 65

Jedwali Na. 4.18: Majina Yaliyotokana na Mimea ...................................................... 65

xiii

Jedwali Na. 4.19: Majina Yanayotokana na Mimea .................................................... 66

Jedwali Na. 4.20: Majina Yanayotofautisha Jinsi ........................................................ 67

Jedwali Na. 4.21: Majina Yanayotokana Baada ya Kuzaliwa Watoto Mapacha ......... 68

Jedwali Na. 4.22: Majina Yanayotokana na Chimbuko la Koo ................................... 69

Jedwali Na. 4.23: Majina Yanayotokana na MUNGU ................................................ 70

xiv

ORODHA YA VIAMBATISHO

Kiambatisho I: Hojaji kwa watafitiwa ........................................................................ 86

Kiambatisho II: Research Quationnaire ...................................................................... 87

xv

ORODHA YA VIFUPISHO

Dkt Daktari

Prof Profesa

TUKI Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili

ME- Mwanaume

KE- Mwanamke

1

SURA YA KWANZA

UTANGULIZI WA JUMLA

1.1 Utangulizi

Utafiti huu ulihusu Uchambuzi wa kiisimujamii na maana za majina ya koo za

kisukuma. Mfano wilaya ya Misungwi - Mwanza. Utafiti ulimakinika zaidi katika

kuonesha uchambuzi wa kiisimujamii katika uteuzi wa majina ya koo za kisukuma.

Sehemu hii inazungumzia usuli wa lugha ya kisukuma kwa ujumla wake, vipengele

vilivyomakinika ni pamoja na eneo la kijiografia katika jamii ya wasukuma, shughuli

za kiuchumi katika jamii ya wasukuma, usuli wa tatizo, tatizo la utafiti, malengo ya

utafiti, maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti, mawanda ya utafiti, mipaka ya utafiti

na hitimisho.

1.2 Usuli wa Lugha ya Kisukuma

Katika kipengele hiki cha usuli wa lugha ya kisukuma, ulielezea eneo la lugha ya

kisukuma, shughuli za kiuchumi katika jamii ya wasukuma, na mfumo wakijamii wa

wasukuma.

1.2.1 Eneo la Lugha ya Kisukuma

Kisukuma ni lugha ya kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na wasukuma.

Mwaka 2006 idadi ya wazungumzaji wa lugha ya kisukuma ilihesabiwa kuwa watu

5,430,000( ). Kufuatana na uainishaji lugha za kibantu ya Malcon Guthrie, kisukuma

iko kundi la f 20, inafanana na lugha ya Kinyamwezi. Jina ‗wasukuma‘ lina maana ya

watu wa kaskazini lakini maana hii haikuwakilisha maana halisi ambayo watu wengi

huitafsiri. Kwa mfano Wasukuma hutumia alama ya utambulisho (dira), kwa eneo

2

fulani kwa viashirio vya makabila, kama vile jina ‗kiiya‘, kumaanisha mashariki

ambako ni mawio ya jua.

Huu ni utambulisho ambao haukufananishwa ama kuitwa eneo la unyamwezi lakini

zaidi ya mpanuko wake ni upande wa ‗kusini‘. Neno hili hutumiwa sana na kabila la

wanyamwezi ili kutambulisha eneo la wasukuma, ili hali wasukuma nao husema

‗‘dakama‘‘. Upande mwingine ambao unapewa alama ya utambulisho ni ‗‘ushashi‘‘,

ikimaanisha upande wa kabila la washashi. Neno hili la washashi linamaanisha

mkusanyiko wa makabila ya mkoa wa Mara. Aidha neno hili (shashi) lilimaanisha

kabila la Wakurya ambapo mpanuko wake unakomea hapo. Isitoshe, eneo zima la

upande huo humaanisha upande wa kaskazini. Upande wa mwisho kutambulisha ni

‗‘ngw‘eli‘‘. Neno hili halikupewa kabila, badala yake linawakilisha upande wa

magharibi ambako ni machweo ya jua. Wasukuma wenyewe hulirejelea jina hili

(Wasukuma) kama ‗‘Basuguma‘‘ kwa wingi na ―Nsuguma‘‘ kwa umoja.

Wasukuma huishi eneo la kaskazini magharibi mwa Tanzania, karibu na mwambao

wa kusini wa ziwa Victoria na maeneo mbalimbali ya utawala ya wilaya ya Ilemela na

Nyamagana mkoani Mwanza, mkoa wa Simiyu, kusini magharibi mwa mkoa wa Mara

na mkoa wa Shinyanga.

Eneo la kaskazini la makazi yao ni mbuga maarufu ya Wanyama ya Serengeti.

Familia za wasukuma nyingi sana wamehamia maeneo ya kusini ya Tanzsania

kuelekea mkoa wa Rukwa ambao baadae umegawanywa na kuzaa mkoa wa Katavi,

na kuishi katika eneo la kabila la Wapimbwe.

3

1.2.2 Shughuli za Kiuchumi katika Jamii ya Wasukuma

Shughuli kuu za kiuchumi kwa Wasukuma ni kilimo, uvuvi, ufugaji na biashara.

Pamba ndio zao kuu la biashara kwa Wasukuma, pia mazao mengine kama mpunga,

mahindi, choroko, viazi, dengu, matunda (kisiwani Ukerewe) na alizeti (Simiyu)

hulimwa Usukumani. Wasukuma pia ni wafanyabiashara, madini mbalimbali kama

vile dhahabu na almasi huchimbwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mwanza,

Shinyanga na Geita, madini haya yanasababisha shughuli za kiuchumi kwa

Wasukuma.

Wasukuma pia wanajihusisha sana na kilimo cha mazao ya nafaka na mifugo ya aina

mbalimbali maeneo ya Shinyanga wanalima mazao ya nafaka kama mahindi na

mpunga. Idadi ya watu inaongezeka kwa kasi na hivyo pia kuongezeka kwa wakulima

wa mbogamboga.

1.2.3 Mfumo wa Kijamii wa Wasukuma

Jamii ya Wasukuma ina mfumo wao wa kiutamaduni hususani katika masuala

yanayohusiana na ndoa. Mwanaume anapotaka kuoa anatakiwa atume mshenga aende

kuposa kwao mwanamke aliyempenda. Mshenga ataeleza nia ya kufika pale, atakuwa

ameelezwa na familia ya mwanaume ni lini siku ya kuja kupanga mahari. Baada ya

kuelewana mahari itakayotolewa, kuna namna mbili za kuchukua mahari, itategemea

na utayari wa watoa mahari, inaweza kuwa siku hiyohiyo ya posa au siku nyingine

itakayopangwa.

1.3 Usuli wa Tatizo

TUKI (2004) Kamusi ya Kiswahili sanifu, inaeleza; jina ni neno linalomtaja mtu au

kitu. Kwa kawaida jina linalotolewa kwa mtu huweza kuwa la kupanga, yaani jina

4

analopachikwa mtu kwa kuhusishwa na maumbile au tabia yake, majina ya aina hii

aghalabu huwa ni ya muda mfupi ingawa wakati mwingine yanaweza kuwa kama jina

lake halisi. Aghalabu majina hubeba maana ambazo huwa na mtazamo wa kidini,

majina hayo kwa kawaida yanatolewa ili kuonesha fikra na tajiriba za watu katika

jamii husika.

Salapion (2011) anaeleza kwamba majina hususani ya asili, pamoja na kuwa na

maana, baada ya kuja kwa dini za kigeni zilizoletwa na wakoloni, majina haya

waliyaita ya kishenzi, ni majina ambayo hayahusiani na dini za Mungu. Athari ya ujio

wa wageni hususani katika masuala ya majina yameikumba pia jamii ya kisukuma.

Kwani hapo awali kabla ya ujio wa wageni jamii hii ilikuwa na utamaduni wake

katika kutumia majina ya koo. Baada ya ujio wa wageni na dini zao hususani dini ya

kiislamu na kikristo matumizi ya majina ya koo yalianza kupungua kwa kiasi kikubwa

na badala yake majina ya kigeni yalichukua nafasi. Hii ni kwa sababu watu wengi

walichukua hatua ya kutumia majina mapya yaliyotolewa na wageni wakiamini

kwamba haya ndio majina ya kistaarabu. Kwa hiyo matumizi ya majina ya koo

yalibaki katika shughuli maalumu kama vile zinazohusu sherehe za kimila.

Muzere (2000) anaeleza kwamba majina ya kiafrika hususani ya watu huwa na kazi

mbalimbali, yanaweza kuhusiana na shughuli au kuoanisha asili ya watu wanaoishi

katika sehemu fulani, wakati mwingine majina hayo huonyesha kumbukumbu ya

matukio makubwa yaliotokea katika jamii, matukio yanaweza kuwa ya kiutamaduni,

kwa mfano matukio yanayotokea katika kipindi cha kuzaliwa kwa mtoto. Vilevile

majina yanaweza kuelezea maumbile, mwonekano, tabia au sifa za mtoto aliyezaliwa.

Katika kuonesha msisitizo wa maelezo yake Muzere( Keshatajwa) anatoa mfano

5

katika jamii za wafugaji kwa kudai kwamba, katika jamii hizo majina huwa

yanatolewa kutegemea matukio ambayo yanahusiana na shughuli za ufugaji kama vile

vita vya utekaji wa mifugo, uwindaji, kuvamiwa na wafugaji wengine au wanyama

wakali na uhamasishaji unaohusiana na shughuli za ufugaji.

Muzere (Keshatajwa) anaendelea kueleza kwamba jamii za kiafrika zina tamaduni

mbalimbali zenye mvuto na heshima kubwa ambazo huunganishwa na maumbile,

matukio ya kibaiolojia na maafa. Hivyo majina mengi ya kiafrika hususan ya watu

yanatokana na matukio kama vile ya ukame, magonjwa, wadudu waharibifu wa

mazao, mafuriko na vipindi mbalimbali visivyo na neema. Anazidi kueleza kwamba

wakati mwingine majina yanaweza kutolewa kutokana na sababu za kimazingira

kama vile vipindi vya majira ya mwaka na wakati wa neema ya chakula katika jamii.

Hivyo mtoto aliyezaliwa anaweza kupewa jina kutokana na tukio lililopo katika jamii

kwa kipindi hicho.

Mutembei (2009) naye anaeleza suala la majina kwa kujikita katika majina ambayo

yaliibuka baada ya kuja kwa ugonjwa wa UKIMWI. Maswali anayojiuliza ni kwamba

sababu zipi zinazowafanya watu kutoa majina katika vitu, hali au tukio? Je majina

hayo yanakuwa na maana? Je majina hayo yanakuwa kama kielelezo kwa yale

yatakayotokea? Mtaalamu huyu anatoa majibu na anaeleza kwamba majina

yanayotolewa kimsingi yanakuwa na msukumo ambao unawafanya watu kuweza

kutoa majina hayo.

Kwa hakika maswali yaliyoulizwa na Mutembei pamoja na majibu aliyoyatoa ndio

kiini cha sababu iliyowasukuma wataalamu kadhaa kutoka ndani na nje ya Tanzania

6

kumakinika zaidi katika kuchunguza kipengele cha majina. Katika tafiti zao,

wataalamu walioshughulikia suala hili (Omari; 1970, Muzale; 1998, Rubanza;2000,

Chotsman ;2003, Manyasa ;2009, Baitain; 2010, Buberwa ;2010, na Salapion; 2011),

walichunguza zaidi majina ya watu na maeneo. Schotsma (2003) na Buberwa (2010)

wao walijikita katika kushughulikia majina yanayotokana na maeneo. Kwa upande

mwingine tafiti hazijashughulikia suala la majina ya koo. Kadhalika kuna tafiti

kuhusiana na majina hususani ya watu zilizofanywa katika jamii ya Wasukuma. utafiti

huu unachambua kiisimujamii majina ya koo katika jamii ya Wasukuma kwa

kuchambua zaidi maana ya majina ya koo za Wasukuma.

Kapinga (1983:36) anasema kuwa,

“Jina ni neno linalotaja kitu fulaniili kutofautisha na kukipambanisha miongoni

mwa vitu vingine” .

Aidha, Bakiza (2010) wanadai kuwa Jina ni neno linalotumika kutambulisha mtu,

mnyama, kitu, jambo, mahali au kitu.

Rugemalira, (2005) kwa upande wake alichunguza majina ya sehemu katika jamii ya

Runyambo.Katika utafiti wake alimakinika zaidi katika kuchunguza mbinu za

kimofolojia zinazotumika katika kuunda majina ya maeneo. Matokeo ya utafiti wake

yalibaini kuundwa kwa majina katika jamii hiyo kwa kuzingatia utaratibu maalumu

wa kimofolojia. Kulingana na maoni ya Rugemalira(keshatajwa), majina ya mahali ya

warunyambo yanaviambishi maalumu kama nya-na ru-a kumaanisha ‗enye‘ sifa

fulani au enye kumilikiwa kwa mfano:

Nya-isozi ‗enye vilima‘

7

Omu-rusaka ‗kichakani‘

Ru-a-cikoona ‗enye kunguru‘

Nya-rubaare ‗enye changarawe‘

Ru-a-nkende ‗enye nyani‘

Aidha, mifano hii inaonessha kuwa majina ya mahali ya kirunyambo yana maana. Pia

ni wazi kuwa yanawakilisha maumbile ya kawaida kama vile vilima, changarawe na

vichaka. Majina ya wanyama kama vile kunguru na nyani. Uchunguzi huu unaipa

nguvu hoja ya uchunguzi mwingine unaohusu majina ya mahali yakisukuma kwa

kusudi la kutalii maana na sababu za kiisimujamii. Schotsman (2003) kwa upande

wake alifanya utafiti kuhusu maeneo katika mkoa wa Dar es Salaam.

Katika uchunguzi wake alijikita katika kuangalia majina ya vituo vya daladala katika

mkoa wa Dar es Salaam. Lengo la uchunguzi lilikuwa ni kubaini maana na vigezo

viivyotumika katika kutoa majina ya vituo hivyo. Matokeo ya utafiti wake yalibaini

kwamba majina hayo yalitolewa kwa kuzingatia vigezo tofautitofauti. Kwa mfano

kwa kuzingatia majengo yaliyopatikana katika maeneo husika kama vile shule,

misikiti na makanisa, majina ya watu kwa mfano kituo cha kwa mwalimu, majina ya

mimea/ miti kwa mfano kituo cha ‗Ubungo‘ kimetokana na mti wa mbungo ambao

ulikuwepo katika eneo hilo.

Pia Buberwa (2010) alifanya utafiti wake mkoa wa Kagera, hususani katika katika

wilaya ya Bukoba, alimakinika katika kuchunguza majina ya maeneo katika jamii ya

wahaya. Lengo la utafiti wake lilikuwa ni kubaini maana na sababu za kiisimujamii

katika utoaji wa majina hayo kwa jamii ya wahaya. Matokeo ya utafiti wake yalibaini

8

kwamba majina ya maeneo katika jamii hiyo yanatokana na vigezo mbalimbali kama

vile maliasili zinazopatikana katika maeneo hayo. Kwa mfano milima na mchanga.

Jina kama ‗‘Mishenye‖ maana yake mchanga, sababu ya kutumia jina hilo ni kutokana

na sehemu husika kuwa na mchanga mwingi. Baadhi ya majina katika jamii hiyo

yanatokana na tabia mbalimbali, kwa mfano ‗mugajwale‘ maana yake ni uvivu.

Kwa ujumla tafiti zilizofanywa wataalamu mbalimbali zimebainisha majina

yanayotumika katika jamii mbalimbali huzingatia sababu na matukio muhimu

yanayojitokeza katika jamii na maana zake inaeleweka huwa zaidi na jamiilugha ya

watumiaji wa majina hayo

1.4 Tatizo la Utafiti

Majina ya watu katika wilaya ya Misungwi yana tatizo la kukosa ubayana wa maana

ya kutumiwa kwake na waongeaji wa jamiilugha ya Kisukuma wa eneo hili. Baadhi

ya Waongeaji wa lugha hii wanaoishi katika maeneo haya huwaita watoto wao sasa

hivi majina kutokana na mazoea kwa kwa kuyasikia tu majina bila kuelewa kuwa

zipo sababu za msingi za kiisimujamii ambazo zinachagiza wanajamiilugha wa

Kisukuma wa Misungwi kutumia majina fulani fulani ya koo hizo. Aidha majina ya

Kisukuma yana asili ya kubainisha jinsi ya Kike na ya Kiume. Hata hivyo, kadiri

muda unavyozidi kwenda wazungumzaji wa lugha ya Kisukuma wa Misungwi na

wengine wa wilaya zingine wanachanganya kuita majinawatoto wao bila kujali

umuhimu huu. Kwa mfano, Ingawa jina ―Mabula‖ na ―Kabula‖ kisemantiki

humaanisha ―mvua‖, matumizi ya silabi $ka$ katika jina ―kabula‖ na silabi $ ma $

Katika jina ―Mabula‖ yalikuwa na msingi wa kubainisha tofauti za Kijinsi (kabula

9

ikiwa ni jina la mwanamke na Mabula ikiwa jina la Mwanamme); wanajamiilugha

hii sasa hivi wameanza kupuuza msingi huu ambao ulikuwa na maana yake katika

Jamii hii.

Hadi sasa, ni vigumu sana kutofautisha kijinsi baina ya Mabula Mhe. Mbunge wa

Ilemela (ambaye ni mwanamke), na Mabula Mhe. Mbuge wa Nyamagana (ambaye ni

Mwanamume) kwa kusikia majina yao, bali msikilaji lazima awe anawafahamu hawa

Waheshimiwa Wabunge toka zamani na kwa majimbo yao, au kwa kuzingatia

majina yao ya Kwanza ambayo ni ya kidini( Angelina, na Stanslaus). Swala hili pia

linaweza kusababisha hata ugomvi kwa baadhi ya watu pale inapotokea mwanamme

mmoja kuitwa jina la kike kwa makusudi na mzungumzaji yeyote kama mwenye jina

atakuwa na kasumba za mfumo dume, kwani yeye atajihisi kutukanwa.

Tatizo lingine ni kuwa, umuhimu wa kubainisha koo mbalimbali kwa kuzingatia

matukio, na mahali alipozaliwa mtu, na baada ya kuzaliwa umeanza kutoweka.

Hatimaye utambulisho wa koo za kisukuma kama vile koo za kichifu, au koo za

kiuvuvi, mahali na wakati alipozaliwa mtu umeanza kutoweka. Mfano, kutokana na

tukio la vita yalikuwepo majina kama ―Bulugu‖(kwa mwananamke) au ―Malugu‖

(kwa mwanamume).

Aidha, kiukoo,jina ―Ng‘hwashi‖ ilikuwa na maana ya ukoo wa wavuvi, na mahali

alipozaliwa mtu kulikuwepo jina kama ―Ngwandu‖ likimaanisha aliyezaliwa chini

ya Mbuyu. Matumizi ya majina kiuokooo yalikuwa na msingi wa kubainisha bayana

koo fulanifulani ili koo za jamiilugha ya Kisukuma zisije zikamezwa na koo zingine,

hata ndugu kujikuta kutofahamiana na ukoo kutoweka.

10

Ikumbukwe kwamba hata kwa mataifa ya ughaibuni, majina hutumika kama kigezo

cha kutofautisha jinsi. Kwa mfano, kwa Wakristo wengi ambao huabudu katika dini

iliyoletwa Afrika kutoka ughaibuni, yapo majina yanayobainisha jinsi ya Kike na

mengine hubainisha jinsi ya Kiume. Mfano, Fransiska-mwanamke, na Fransis –

Mwanamme. Vivyo hivyo kwa wale wanaoabudu kupitia dini ya Kiisilamu. Mfano,

Amina-mwanamke na Abdala-Mwanamme. Utambulisho huu basi una umuhimu wa

kwa jamiilugha ya Kisukuma, bali hata kwa jamii lugha zingine nje ya bara la Afrika,

Kwahiyo, kuna hatari kubwa sana kwa kuita ya majina watoto bila usipozingatia

vigezo vya kiisimujamii na vile vya kisemanti kikwani huweza kuwa tishio la

kutoweka kwa utambulisho bayana wa koo za jamiilugha za Kisukuma.

Kutokana na matatizo haya, utafiti huu utachambua majina haya kwa kuzingatia

vigezo vya kiisimujamiina kisemantiki ili kuwezesha jamiilugha hii na jamiilugha

zingine kuelewa bayana mdhumuni ya kuitwa majina haya katika jamiilugha ya

Kisukuma. Aidha kwa njia hiyo, lugha ya Kisukuma itaweza kudumu katika misingi

ya kijamii na kuimarisha uwepo wa koo za jamii lugha hii.

1.5 Malengo ya Utafiti

1.5.1 Lengo Kuu

Uchambuzi wa kiisimujamii wa majina ya koo za kisukuma.

1.5.2 Malengo Mahsusi

(i) Kufafanua jinsi majina ya koo za kisukuma yanavyotofautisha jinsi ya

Wanajamii.

(ii) Kuchambua nyanja za kiisimujamii zizosababisha kutumia majina ya koo za

kisukuma.

11

1.5.3 Maswali ya Utafiti

(i) Je majina ya koo ya kisukuma yanatofautishaje jinsi ya wanajamiilugha ya

Kisukuma?

(ii) Je, sababu zipi za kiisimujamii zinazochangia watoto (watu) kuitwa majina ya

koo za kisukuma?

1.6 Umuhimu wa Utafiti

Mulokozi (2005) anasema bado tunahitaji maandishi mengi zaidi yanayotokana na

utafiti wa uwandani, utafiti huu utasaidia kukusanya data na kuzihifadhi katika

maandishi, kuna mambo mengi yamehifadhiwa vichwani mwa watu kama sehemu ya

kutunza kumbukumbu, utunzaji wa kumbukumbu wa namna hii siyo thabiti, kwani

wakati wowote data hizo huweza kupotea kwa kusahaulika kutokana na maradhi au

kifo.Utafiti huu una mchango katika nyanja ya kitaaluma, kiutamaduni Kama

inavyojibainishwa katika sehemu ifuatayo;

1.6.1 Kitaaluma

Utafiti umesaidia watu kutambua majina ya koo na kufahamika na watu wengi tofauti

na wasukuma ndani na nje ya nchi. Umesaidia katika kutoa mchango wa kitaaluma

hususani katika taaluma ya isimujamii, matokeo ya utafiti huu yatakuwa marejeo

muhimu kwa walimu, wanafunzi na watafiti wanaoshughulikia vipengele vingine

katika kisukuma. Vilevile matokeo ya utafiti huu umesaidia kwa upande wa watafiti

wengine watakaoshughulikia kipengele cha majina katika lugha nyingine.

1.6.2 Kiutamaduni

Utafiti umesaidia kuonesha utamaduni wa Wasukuma, kuhifadhi utamaduni wa jamii

ya wasukuma katika maandishi ikiwa mojawapo ya lugha za kibantu.

12

1.6.3 Kitaifa

Utafiti huu una umuhimu mkubwa sana kwa taifa kwani umesaidia kufafanua majina

ya koo ya wasukuma, ambao yanaelekea kupotea kutokana na majilio ya wageni

pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia.

1.7 Mawanda ya Utafiti

Utafiti huu ulimakinika katika taaluma ya isimujamii. Aidha, katika taaluma hiyo ya

isimujamii, ulijikita zaidi katika kuchunguza kipengele cha majina ya koo za

kisukuma hususani katika uchambuzi wa kiisimujamii na maana za majina ya koo za

kisukuma.

1.8 Hitimisho

Sehemu hii ilizungumzia usuli wa lugha ya kisukuma, usuli wa tatizo na tatizo la

utafiti, malengo ya utafiti, maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti, mawanda ya utafiti,

na mipaka ya utafiti

13

SURA YA PILI

MAPITIO YA KAZI TANGULIZI

2.1 Utangulizi

TUKI (2013) Mapitio ni makala yanayoeleza mawazo ya mtu juu ya kitabu au

maandishi fulani yaliyosemwa. Sehemu hii inahusu mapitio ya machapisho

mbalimbali yanayohusiana na mada ya utafiti pamoja na nadharia inayotumika katika

utafiti. Sehemu hii imeanza kwa kuelezea dhana ya maana na ufafanuzi wake, dhana

ya isimujamii pamoja na kuelezea historia malengo yake, dhana ya majina kwa

ujumla, nadharia ya utafiti, sababu za kiisimujamii za majina ya kisukuma, na

hitimisho.

2.2 Dhana ya Maana

Dhana ya maana ni telezi, kutokana na utelezi, huo wataalamu mbalimbali wameweza

kuifasiri maana ya maana kama ifuatavyo, maana ya maana ni fahiwa ya neno au kirai

ama dhana, matumizi au kitajwa. TUKI (1990), inaelezea kuwa maana ya maana ni

tafsiri ya kitu au jambo, maelezo ya kufanya jambo lieleweke waziwazi. Kamusi ya

Kiswahili sanifu (2004). Maana ya maana ni kile ambacho neno au tungo huashiria

kutokana na nadharia, matumizi au kitajwa, Massamba (2004). Kwa ujumla maana ya

maana ni tafsiri anayokuwa nayo msemaji au msikilizaji. Kwa kawaida maana huwezi

kuiona bali huwa katika ubongo wa mtu anaye itafsiri maana, Mnata (2014).

Hivyo dhana ya maana ni ya kidhahania kwa sababu maana haina muundo thabiti

kama vile viambajengo vingine vya lugha vya kifonolojia, kimofolojia, au kisintaksia.

Maana hutegemea pia dhamira ya mtoa ujumbe na fasili ya mpokea ujumbe.

14

Kwa watu wa kawaida hutumia neno maana kumaanisha vitu mbalimbali. Kwa

mfano, utawasikia wakitumia katika mazungumzo tungo kama ifuatavyo;

―Una maana gani kuchelewa hivi? Nieleze maana ya kumpiga mwenzio. Hakualikwa

maana akilewa hugombana. Akinywa pombe huwa hana maana. Nini maana ya

“sharobaro”? Mradi huu una maana kubwa kwa nchi yetu. Nguo nyekundu

inamaanisha upendo. Ukimwona kikongwe ana macho mekundu, ina maana kwamba

ni mchwawi. Kitambaa cheupe kinamaanisha amani. Asiyejua maana haambiwi

maana”[Resani]

Lyons (1984) anadai maana ni seti ya mawazo. Anaendelea kufafanua kwamba

mawazo hayo kimsingi yanawakilishwa na alama ambazo zinatumika na jamii husika

katika kuwakilisha matukio mbalimbali. Alama za lugha kwa kawaida huwa

zinahusisha mtumiaji wa alama, alama yenyewe na kile kinachowakilishwa na alama.

Hymes (1964) anaendela kufafanua kwamba maana ambayo inabebwa ndani ya alama

huwa inaeleweka kwa urahisi zaidi na wazawa wa lugha husika. Hymes (1964:33)

anaonyesha kuwa ishara za lugha kuhusu vipengele vitatu ambavyo ni mtumiaji

ishara, ishara yenyewe na maana yake. Hymes anashikilia kuwa maana ya ishara

hufahamika vyema na mtumiaji asili wa lugha. Pia hutegemea matukio ya kijamii

katika jamii fulani ambapo lugha hiyo hutumiwa.

Maoni ya Malinowski (1923) yanakaribiana na ya Hymes anadai lugha ni sharti

ieleweke kama namna ya amali muhimu katika utendaji. Matokeo ya uchunguzi huu

yanaunga mkono mwelekeo huu wa dhana ya maana. Austin (1962) na Searle (1969)

katika nadharia yao ya ‗Speech Act Theory‘ wanasema dhana hii ya maana katika

15

lugha ni tata. Hivyo maana za wazi za maneno haya ni sawasawa na matumizi ya

kawaida huku maana halisi ni za kuhusishwa tu.

Kwa upande mwingine Herriot (1971) anaeleza kuwa dhana ya maana inaweza kuwa

na fasili nyingi lakini maana fulani irejelee asasi fulani ya kijamii katika muktadha

ambapo lugha hutumiwa. Anaongeza kuwa msamiati wa lugha ni orodha changamano

ya mawazo, maslahi ya kijamii pamoja na matukio ya kijamii yanayohusu jamii hiyo.

Kulingana na jinsi wanavyochanganua maana, Verma na Krishnaswamy (1989)

wanaonyesha kuwa ni muhimu kuhusisha nadharia ya vitendo wakati wa kuchanganua

dhana ya maana kwa lugha ya kawaida. Hii inamaanisha kuwa uchanganuzi wa maana

unafaa kuhusu asili, matumizi na matokeo ya ishara hizi katika muktadha wa

matumizi.

Massamba (2009) anaungana na Hymes kwa kudai kwamba maana kwa kawaida

huwa inahusisha kile ambacho neno au tungo huashiria kutokana na dhana, matumizi

na kitajwa. Ogden na Richard (1966) wanaungana na Lyons (1984) kwa kuhusisha

mambo matatu katika kuelezea maana ya maana. Mambo hayo ni alama, dhana, na

maana yenyewe. Wanaendelea kufafanua kwamba alama ndio msingi unaosababisha

kupatikana kwa dhana ya kitu au jambo lolote liwalo.

Aidha dhana ya kitu inajengeka kichwani mwa mzungumzaji au msikilizaji kutokana

na kuathiriwa na mazingira ya jamii au mtu binafsi. Athari zinazotokana na mazingira

ya kijamii au mtu binafsi ndizo zinazosababisha alama moja kuweza kuwa na maana

zaidi ya moja. Hii ni kutokana na mtazamo wa jamii au mtu binafsi dhidi ya alama

husika.

16

Ogden na Richard (1966) wanaweka bayana ufafanuzi wao kwa kutumia mchoro wa

pembe tatu kama unavyobainishwa hapa

Dhana

Alama………...............................Maana

Kielelezo Na. 2.1: Uhusiano Uliopo kati ya Alama, Dhana na Maana

Chanzo: Ogden na Richard 1966: UK 9-10)

Ufafanuzi wa mchoro huu ni kwamba, upo uhusiano wa karibu kati ya alama na

dhana, na kati ya dhana na maana. Lakini kwa upande mwingine hakuna uhusiano wa

karibu kati ya alama na maana. Maelezo yaliyotolewa na wataalamu yanadhihirisha

kwamba ingawa kuna maelezo tofauti kuhusiana na dhana ya maana, upande

mwingine wanaonekana kukubaliana katika baadhi ya vipengele vinavyohusiana na

dhana ya maana. Kwa mfano Hymes (1964) na Massamba (2009) wanahusisha

kipengele cha kitaja na kitajwa katika fasili zao. Vilevile Katz, Lyons, Ogden na

Richard wanahusisha kipengele cha mawazo katika fafanuzi zao kuhusu dhana ya

maana kama mchoro ulivyojibainisha hapo juu.

2.3 Dhana ya Isimujamii

Wanaisimujamii hawatofautiani kuhusu fasili ya isimujamii. Ttudgill (1983), Hudson

(1985), Wardhaugh (1986), Holmes (1992), Romaine (1994) Coulmans (1997).

Wanasema isimujamii ni taaluma inayotafiti, kuchanganua na kufafanua uhusiano

uliopo baina ya lugha na jamii. Msanjila, Kihore na Massamba (2009), wanaunga

17

mkono maelezo ya wataalamu hapo juu, kwa kuelezea uhusiano uliopo baina ya lugha

na jamii kama pande mbili zinazokamilishana.

Mekacha (2000) anaelezea dhima ya isimujamii kuwa ni kutafiti na kufafanua nafasi

ya lugha katika jamii. Pia isimujamii hutafiti na kufafanua tofauti zilizopo ndani ya

lugha namna zinavyotofautiana na tofauti zilizomo ndani ya jamii. Anaendelea

kusema ingawa isimujamii ina historia ndefu zaidi kifalsafa na kinadharia, lakini

isimujamii kama taaluma inayojitegemea ilianza miaka ya 1950 na 1960. Taaluma hii

ilijikita katika kukabiliana na upungufu wa mkabala wa kiisimu [wa kichomsky]

uliotamalaki wakati huo wa kuchambua lugha bila ya kuzingatia muktadha halisi wa

matumizi na utumiaji wa lugha.

Romaine (2000) anaungana na Mekacha (2000), katika kuelezea historia ya

isimujamii na kudai kwamba ni taaluma ambayo ilianza katika miaka ya 1950,

taaluma ya isimujamii ilianza kupata nguvu na kutambulika zaidi kuanzia miaka ya

1960 hadi 1970. Mbali na kuelezea historia ya isimujamii Romaine (2000) anafafanua

zaidi malengo ya kuanzishwa kwa taaluma ya isimujamii na taaluma ya sosiolojia ili

kuweza kupata taaluma moja ambayo ni isimujamii.

Kulingana na Trudgill (1983) Isimujamii ni taaluma inayochunguza uhusiano uliopo

baina ya lugha na jamii. Hivyo, inahusu lugha na inavyohusiana na mazingira yake ya

kijamii na kitamaduni. Msanjila na wenzake (2009:2) anaongeza kuwa uhusiano wa

lugha na jamii ni sawa na pande mbili za sarafu moja, inamaanisha kuwa pasipo jamii

hakuna lugha.

18

Taaluma hii ya kiisimujamii inayojihusisha na maana na vipengele vya jamii na

kitamaduni katika uundaji wa majina ya Kiruhaya. Inachukuliwa kuwa majina ya

jamii ya mahali kwa Kiruhaya haiwezi kuwa dhana dhahania ambazo hazitaelezwa

bila kurejelea maisha ya kijamii ya Waruhaya. Kwa ujumla maelezo ya wataalamu

hapo juu yanadhihirisha kwamba isimujamii ni taaluma inayojaribu kuonesha

uhusiano uliopo kati ya lugha na mazingira ya kijamii.

2.4 Dhana ya Majina kwa Ujumla

Jina ni alama ya mtu, mahali, au kitu. Latham (1904) Hanks na wengineo (1990).

Wahusika hawakubaliani kuhusu lini binadamu alianza kutumia majina katika historia

ingawa mtindo huu ni wa zamani. Majina huwa na maana ya etimolojia inayoonesha

kuwa awali yalikuwa maneno.

Upewaji wa majina kwa watu ulianzishwa na Mungu ambaye alimpa mtu wa kwanza

jina Adamu lenye maana ya binadamu na huashiria kuwa binadamu wote ni sawa (The

African Bible, 1999). Baada ya kuumba mwanamke, alimpa Adamu jukumu la kumpa

jina. Alimuita Hawa likimaanisha uhai, ishara ya kuwa mwanamke ndiye chanzo cha

uhai katika familia ya binadamu (The African Bible, 1999). Kulingana na Hanks

(1990), wafaransa, wajerumani, na wahispania hawawachagulii watoto majina

kutegemea maana iliyomo kwenye jina, ila huchaguliwa kwa sababu linapendeza au

kwa heshima ya jamaa fulani katika jamii.

Jinsi wakati upitavyo ndiyo majina ya asili ya kibiblia huacha kutumiwa. Kwa mfano,

Latham (1904), anasema kuwa katika karne ya kumi na saba, jina Adamu lilipendwa

sana na watu, na lile la Hawa wa kibiblia lilichukiwa na halikutumiwa na wengi kwani

19

ndiye mwenye asili ya dhambi duniani. Hanks (1990), anaendelea kusema, baadhi ya

majina hutokana na mitume, dini fulani, na hata familia za kifalme kama vile; Charles,

Louis, huko Uropa majina ya wahusika katika vitabu vya Shakespeare yalishawahi

kutumika kama majina ya kuwapa watoto kwa mfano, Rosalind, Olivia, na Perdita.

Hata hivyo athari za majina haya hayakuchukua muda mrefu.

Tamaduni tofauti hutofautiana upeanaji wa majina. Mtoto huweza kupewa jina

kutegemea yaliyompata mama akiwa mjamzito au baada ya kumpata au kupitia

upigaji ramli jambo linaloungwa mkono na Mbiti (1991). Mandende (2009), anaeleza

kuwa katika jamii za kiafrika majina ni sehemu ya utamaduni wao kwa sababu ya

uhusiano mkubwa uliopo kati ya utamaduni unaohusika, majina ya kafrika

yanamchango mkubwa katika jamii, kwani huashiria kinachotokea katika maisha ya

kila siku. Katika jamii lengo la kutoa majina ni kutoa utambulisho wa mtu au kitu.

Kila jamii huwa na utaratibu wake katika kuita majina, hivyo basi, Mandende (2009)

katika utafiti wake juu ya majina ya watu ya Wavhavenda ina utaratibu wake katika

kuita au kutoa majina kwa watoto wao. Anaeleza kuwa jamii huita majina baaada ya

mtoto kuzaliwa hata anapoendelea kuishi na kupita katika hatua moja hadi nyingine

anapewa majina mengine kwa kuzingatia hatua husika, anaendelea kueleza kuwa

majina ya kuzaliwa, hayo hutolewa baada ya mtoto kuzaliwa kwa mfano, Nnwakhulu

likiwa na maana ya mpiganaji (shujaa) mtoto huyu huzaliwa kunakuwepo na mgogoro

ndani ya familia au nyumbani. Vhuthuhawe jina hili hutolewa na jamii wakiamini

kuwa Mungu ndiye aliyesababisha kuzaliwa kwa mtoto huyo.

Katika jamii hii anaeleza kuwa mtoto anapoanza shule hupewa jina jingine ambalo ni

kwa ajili ya masomo, jina hili huitwa jina la kikristo, au la shule kama sifa mojawapo

20

ya wanajamii. Majina ya ndoa, inaelezwa kuwa majina haya yanatolewa wakati binti

anapoolewa kwa kufuata utaratibu wa kiutamaduni, humtambulisha kuwa binti kuwa

ametoka katika kundi la mabinti na kuinngia katika kundi la wanawake, Nyandega,

Nyamasindi, Mususumeli na Phophi.

Majina kutokana na uongozi wa kijadi. Mandende (2009:68), majina haya hutolewa

katika kusimikwa katika uongozi wa kijadi, mfano, Dzulani, jina hili likiwa na maana

ya mkuu (mtawala) wa jumuiya na Gumani likiwa na maana ya simama. Vilevile

majina ya wahenga, matukio ya kisiasa na majina ya kihistoria, mfano Nndwakhulu.

Malengo makuu yakuita majina ya kiafrika ni kupeleka ujumbe kutoka kwa mtu

anayeita kwenda kwa familia na jamii kwa ujumla, Mandende (2009:83).

Rasekh na Ahmadvand (2012) wanaelezea kuwa kutoa jina la kitendo mahsusi katika

lugha, ambacho huonesha thamani, mila, matumaini, uoga na matukio ya kila siku,

katika maisha ya watu. Rasekh na Ahmadvand wakimrejelea Rosenhouse (2002)

wanasema majina huonyesha upendeleo wa mwenye jina hilo pamoja na wanayempa

jina hilo kwa kuangalia vitu halisi katika maisha ya kila siku. Jina analopewa mtoto

hutambulika kama jina la kwanza, nchi za kikiristo jina la kwanza ni jina ambalo

huwatofautisha wanafamilia, mara nyingi jina la kwanza hutolewa kwa mtoto na

wazazi, mababu na miungu.

Kwa mujibu wa Rasekh na Ahmadvand (2012) wanaeleza kuwa majina huwa na

vyanzo mbalimbali kama ifuatavyo, asili kimakazi, mfano jiji, jimbo, nchi ya uzawa

na jina la kabila, kwa kuangalia sifa za ndani na za nje za mtoto au mtu na wakati wa

kuzaliwa mtoto, hapa yaweza kuwa sherehe ya kidini au burudani, majina kutokana na

21

waadhifa, vitu muhimu vinavyozunguka jamii husika na mazingira ya kijiografia

mfano, milima, mito, na tambarare vilevile yapo majina yanayotokana na watu

muhimu.

Manyasa (2009) anaeleza majina ya watu miongoni mwa wasukuma jamii ya nchi ya

Tanzania analichukua swala hili la upaji wa majina ni muhimu sana miongoni mwa

wasukuma wa Tanzania. Analichuguza kwa uwanda mpana wa kianthropolojia huku

akiichanganua kimiundo na kimaana ili kuonyesha uhusiano wake na mazingira ya

jamii. Anaongeza kuwa majina katika lugha sharti yawe na maana zinazohusishwa na

masuala ya kijamii na utamaduni wa watu. Hii inamaanisha kuwa bado kuna nafasi ya

kuchunguza maana na sababu za kiisimu jamii kuhusu lugha zingine zaidi ya

kisukuma.

Bariki (2009) katika tafsiri ya majina ya kiafrika, anasema katika jamii nyingi za

kiafrika majina huwa na historia yake, vilevile majina haya huwa na maana katika

jamii husika, mfano katika majina ya Wayoruba na Waizoni, jina la mtoto hutokana

na mtoto wakati mtoto alipozaliwa, vile vile jamii hizi hutoa majina kulingana na

majina ya siku, mimea na wanyama pori na kuangalia umbo la mwili wa mtoto,

(Bariki: 47).

Anasema katika jamii ya Waakan, majina ya watu hutokana na siku za kuzaliwa yaani

siku za juma, mfano Kwasi, kwa mtoto wa kiume anapozaliwa jumapili. Akosua ni

kwa watoto wa kike. Majina ya familiya ambayo ni majina ya ukoo ambayo hupewa

watoto na baba zao kwa kujadiliana na mama wa watoto mfano wa majina hayo ni

Bosommuru, Basompra, Bosomtwe,na Basompo,.

22

Majina yatokanayo na hali au tukio maalumu wakati wa kuzaliwa kwa mtoto, kwa

mfano inaweza kuwa sherehe ya kidini ya mfano Mumufie, majina yatokanayo na

wadhifa katika vita mfano, Okogyesuo likiwa na maana ya mpiganaji anayejitwalia

mto na Okoforobo likiwa na maana ya mpiganaji anayepanda wakati wa vita na

majina asili ya kitaifa mfano Akuyampon na Dapaa majina haya hutokea wakati wa

kudai uhuru.

Malande (2006) anasema utoaji majina huleta maana kutokana na muktadha uliopo.

Vilevile anaeleza maana ya ziada huleta taswira akilini ambapo katika majina ya asili

hayo ni kutokana na sababu za kibinadamu na sababu za kiasili mfano njaa, umaskini,

vita, majira, shughuli za kijamii, shughuli za kisiasa. Ebeoga (1993), Isabiriye (2000)

na Musere (2000) wanaosema kuwa majina ya watu ni sehemu muhimu katika

utamaduni wa waafrika.

Mbiti (1991), anasema kuwa mtoto angeweza kupewa jina la babu au bibi aliyekwisha

kufariki, Kulikuwa na imani kwamba mtoto huyo angemlanda somo wake kwa kila

njia. Mazoea haya ya kuwapa watoto majina ya mababu zao yana maana ya kiasili ni

njia ya kuwatukuza na kuwakumbuka waliokufa. Aguedze (2000), anasema jamii

nyingine ziliwapa watoto majina ya siku za juma, waliozaliwa desturi iliyofuatwa

Uganda, Ghana, na sehemu zingine za Afrika Magharibi.

Majina mengine hutokana na mizimu ambayo katika ndoto huweza kuelezea jina

ambalo wangependa mtoto fulani apewe kama si hivyo mtoto anayehusika huishia

kufariki. Mbiti (1991), Shillingtoni (1995), Sitati (2000). Madai haya yanaungwa

mkono na King‘ei na Kisovi (2005), ambao wanasema kuwa majina yana maana

23

fulani katika tamaduni nyingi kote duniani yawe ya mahali, nyakati, au watu. Majina

huashiria tabia fulani. Majina huwa ni kielelezo chenye maana ya ndani katika jamii

wasemavyo King‘ei na Kisovu.

Wataalamu mbalimbali katika tafiti mbalimbali za majina kwa ujumla wamedhihirisha

kwamba majina mengi yanayohusiana na sehemu pamoja na majina ya watu huwa

yanabeba maana zinazowakilisha jamii, mtu mmojammoja, uhusiano wa familia au

hata hadhi za watu katika jamii. Kalkanova, (1999), Kadmon (2000) anabainisha

kwamba majina yanayotolewa kwa watu au sehemu huwa yanabeba maana

zinazohusiana na mazingira ya jamii husika.

2.4.1 Majina kwa Ujumla

Waandishi mbalimbali kwa namna tofauti wamezungumzia kipengele cha majina,

miongoni mwa wataalamu ni pamoja na Msanjila, Kihore na Massamba (2009).

Wanaeleza kwamba kila jamii ina lugha yake kuu inayotumiwa na watu wake. Hii ina

maana kwamba hata jina analopewa mtu hutokana na lugha ya jamii husika.

Wanaendelea kuelezea kwamba majina yanayotolewa kwa watu huwa yanabeba

maana zinazotokana na utamaduni wa jamii husika.

Gray (1999), Kalkanova (1999) na Koul (1982) wanakubaliana kwamba jina linaweza

kutumika katika kumuwakilisha mtu au jamii, pia huweza kuonesha uhusiano wa

kijamii pamoja na kutunza hadhi ya jamii. Wanaendelea kufafanua kwamba utumiaji

wa majina huwa unaendana na kanuni, sheria na desturi za jamii husika. Musere

(2000) kwa upande wake anaeleza kwamba watu wengi wanakosa ufahamu kuhusiana

na asili au chimbuko la majina yao ambapo kiasili majina hayo huwa yanabeba maana

24

maalumu. Wakati mwingine maana za majina zinaweza zisiwe wazi kwasababu

majina mengi yametokana na vifupisho vya maneno au jina kuwa na mzizi au

kuchukuliwa kutoka katika lugha za zamani.

Vilevile maana za majina zinaweza kubadilishwa kwa herufi za majina ambapo

mabadiliko hayo yanaweza kufanywa na wazungumzaji ambao pengine kwa

kutokufahamu lugha ambayo majina hayo yamechukuliwa au kutokujua asili na

maana ya majina hayo. Hali hii inaweza kupotea kwa maana za asili za majina hayo

au kutoshabihiana na maana za awali. Anaendelea kusema kwamba katika jamii

nyingi za kiafrika jina linaweza kuonesha jamiilugha ambayo jina hilo limetokana

nayo. Pia jina linaweza kuonesha muundo wa lugha na mchakato wa kifonolojia

unaotumika katika lugha hiyo.

Mphande (2006) anasisitiza maelezo ya Musere (keshatajwa) kwa kudai kwamba

majina yanaweza kuchukua na kukusanya historia ya maisha ya watu ambao

wanapatikana katika eneo fulani. Mbiti (2003) kwa upande wake anazungumzia

majina ya asili ya kiafrika kwa ujumla wake Anadai kwamba majina ya kiasili

wanayopewa watu huwa yanabeba utambulisho wa dini za kiafrika. Anaelezea mtu

anapopewa jina la asili, anadhihirisha ushiriki wake katika dini yake.

Pia anaelezea kwamba majina ya asili maana zake huwa zinaonyesha imani juu ya

kifo kwa maana kwamba mtu aliyekufa atakuja kuzaliwa tena katika familia. Kwa

mujibu wa Mbiti majina ya asili huwa katika utaratibu wa kimzunguko wa

kurithishana ndani ya familia. Pia Msanjila, Kihore na Massamba (2009) wakielezea

majina ya familia wanadai kwamba majina hayo ya familia yanabeba maana ambazo

25

huwa zinafahamika na watumiaji husika wa majina hayo. Vilevile wanafafanua

kwamba majina ya familia huwa na uhusiano na matukio yanayotokea katika jamii

husika kama wanayoeleza:

Majina haya ya familia hubeba maana mbalimbali ambazo kimsingi hueleweka kwa

wana-jamiilugha wenyewe kwa sababu wana-jamiilugha hao wanachukuliwa kuwa

wana maarifa, elimu, na uzoefu wa maisha unaofanana. Maana hizi za majina huwa na

uhusiano na utamaduni wa mzungumzaji, mazingira ya jamii lugha ilipo, majira ya

mwaka, matukio muhimu katika jamii inayohusika, kwa mfano katika jamiilugha ya

kikuyu majina yanahusiana na mazingira, tabia, hali ya hewa na watu waliokufa.

Kwa mfano:

Jedwali Na. 2.1: Majina Yanayobeba Maana Mbalimbali Yanayoeleweka kwa

Wanajamii

JINA MAANA

Wanjira Amezaliwa njiani

Nyaga Ndege (mbuni) anayeaminika kuwa anakimbia sana hasa

anaponyang‘anywa mayai yake au watoto wake

Mwansoko kama alivyonukuliwa na kihore na Chuwa (2004), anazungumzia majina

ya kibiashara katika lugha ya Kiswahili. Anaeleza majina mengi ya kibiashara

yaliibuka yakiwa katika lugha ya Kiswahili, kwasababu watumiaji wengi wa bidhaa

zinazozalishwa viwandani wanatumia Kiswahili kama lugha yao ya mawasiliano.

Anafafanua mbinu mbalimbali zinazotumika katika kubuni majina hayo, mbinu ya

kutumia sifa/tabia za kimaumbile, kuyapa maneno ya kigeni maumbo ya Kiswahili,

kutumia maneno ya kijiografia kwa mfano vibiriti chapa KIBO, jina hili limetumika

26

kwa sababu kiwanda cha vibiriti vya aina hii kipo Moshi karibu na kilele cha Kibo cha

mlima Kilimanjaro na kubuni kinasibu.

Kwa hiyo majina ni kipengele muhimu katika maisha ya mwanadamu, katika nyanja

zote kiuchumi, kisiasa, na kijamii, katika jamii za kiafrika watu wengi hususani wazee

huwa na kawaida ya kurithisha majina yao katika jamii husika. Maelezo haya

yanaungwa mkono na Msanjila, Kihore na Massamba pale wanapoeleza;

“Ikumbukwe kwamba wanafamilia wengine hupewa majina kama hayo hapo juu

lakini wenyewe hawakuzaliwa katika mazingira yaliyoelezwa. Watu kama hao

hupewa majina kama hayo kwa heshima ya ama babu au bibi zao lakini bado maana

za majina hayo hubaki vilevile (UK 53)‖.

Uhakiki wa majina katika lugha za kibantu

Manyasa (2009) anaeleza majina ya watu miongoni mwa wasukuma, jamii ya nchi ya

Tanzania. Analichukua swala hili la upaji wa majina ya muhimu sana miongoni mwa

wasukuma wa Tanzania. Analichunguza kwa uwanda mpana wa Kianthropolojia huku

akiyachanganua kimuundo na kimaana ili kuonesha uhusiano wake na mazingira ya

jamii.

Anaongezea kuwa maneno katika lugha ni sharti yawe na maana zinazohusishwa na

maswala ya kijamii na utamaduni wa watu hao. Hii inamaanisha kuwa bado kuna

nafasi ya kuchunguza maana na sababu za kiisimujamii kuhusu lugha zingine zaidi ya

kisukuma na pia kuhusu njia zingine za uundaji majina ya watu kama vile ilivyo

katika lugha ya kiruhaya.

27

Uchunguzi wa majina ya mahali katika jamii ya Waruhaya una mwanzo wake. Katika

kazi ya Rubanza (2000) anatalii njia tofauti za miundo ya majina ya watu katika jamii

ya ruhaya na yanayohusiana na maana. Kazi yenyewe inalenga hasa majina ya watu

japo yaliyochanganuliwa yalikuwa machache kutokana na mawanda mapana ya

majina ya watu katika jamii ya waruhaya. Rubanza anayaainisha majina haya

kulingana na maoni mbalimbali ya wanaisimujamii.

Utafiti huo unaonesha kuwa majina ya watu wa ruhaya si maumbo tu yamaneno bali

yanahusishwa na matukio ya kijamii yanayoyapa maana hizo. Hii inaeeleza kuwa

pana haja ya kuchanganua maana pamoja na sababu za kiisimujamii zilizopelekea

kuamuliwa majina hayo katika lugha moja. Muzale (1998) alichunguza vipengele vya

unominishaji kwa lugha ya Kirutara pamoja na nyingine zinazosemwa nyanda za juu

za magharibi mwa Tanzania. Muzare anatumia njia ya uchanganuzi miundo yenye

msingi wa vipengele vya kisemantiki ambavyo ndivyo msingi wa uundaji wa maneno

katika lugha husika. Pia aliona kuwa upaji majina ni jambo la kawaida katika kila

jamii japo kuna tofauti katika mikakati inayotumiwa kurejelea vitu, wanyama, mahali,

matukio ya kawaida.

Kwa ujumla kwa uchunguzi huo ulishughulikia majina ya watu kwa lugha

zilizoteuliwa bali si moja pekee. Hii inamaanisha kuwa kulikuwa na haja ya utafiti wa

vipengele vya majina vya mahali angalau lahaja moja ya kiruhaya kama vile

Kiruhamba. Kihore na wenzake (2008: 88-89) amaainisha majina ya mahali katika

Kiswahili kama nomino za pekee kama vile Musoma, Kigoma, Arusha na Mtwara.

Vinadaiwa kuwa majina ya mahali kama aina moja ya nomino za pekee ni tofauti na

28

nomino zingine za pekee. Hivyo majina ni ya vitu, dhana na viumbe vyenye uhai

ambavyo ni tofauti.

Majina ya mahali yanaelekea kuwa na tofauti kubwa, hasa kama jina Fulani

linatofautishwa na majina mengine. Ilionekana ajabu ule upaji wa majina ya mahali

katika jamii ya waruhaya uliokuwa na misingi kutokana na umaarufu wa sura tofauti

ya mahali hapo kulingana na nguvu uwezo au athari ya tukio lililofanya litumiwe

kurejelewa mahali hapo. Hii inamaanisha kuwa ipo haja ya kuchunguza zaidi

vipengele vinavyotumiwa kutoa majina ya mahali.

Legele (2009) anaeleza kuhusu majina ya mimea kwa lugha ya kividuda inayosemwa

nchini Tanzania. Katika utafiti wake ameweka wazi vipengele fulani vya kiisimu vya

majina ya mimea pale ambapo sifa tata ya habari zilizokusanywa zinaoneshwa. Kazi

hii inachanganua njia mbalimbali za uanishaji wa majina ya mimea kwa lugha ya

kivudunda kuanzia ya kawaida hadi yale magumu. Hata hivyo kazi hii imejikita na

miundo ya maneno kwa kivudunda, majina mengine ya mimea kwa Kiswahili na

lugha nyingine za kibantu.

Baitani (2010) anachunguza mfumo wa miundo ya majina ya watu pamoja na maana

zinazohusishwa nayo katika lugha ya kiruhaya. Utafiti huu unaonesha umuhimu wa

kiisimu katika majina ya jamii ya ruhaya na kilichopelekewa kuamuliwa kwayo.

Baitani anadokeza kuwa majina ya wanyama, wadudu hatari, na mimea hutumiwa

kurejelewa watu, japo yanaashiria sifa mbaya. Hili linamaanisha kuwa lilikuwa na

manufaa katika kuamua vipengele katika upaji majina ya mahali ili kutambua sababu

za kuyaunda katika lugha Fulani ya kibantu kama kiruhaya.

29

Schotsman (2003) alichunguza vipengele vya kijamii na kijografia kuhusu mfumo wa

uchukuzi katika Tanzania ya sasa. Lengo muhimu lilikuwa kubaini vipengele vya

kijamii na kijiografia vinavyotumia kuyapa majina vituo vya mabasi, kata na vitongoji

katika jiji la Dar es Salaam. Shughuli muhimu ilikuwa ni kutambua mahali majina

haya yalipatikana jinsi yalivyopata majina na maana ya majina hayo.

Akijadili majina ya mahali katika kiswahili schotman alionesha kuwa huenda

yaliashiria vitu halisi, shughuli za watu, watu maarufu, maumbile ya kawaida, mimea

na wakazi asilia. Uchunguzi huu ulishughulikia maana ya majina katika kiswahili japo

sababu zilizopelekea kuundwa kwayo hazikupelelezwa kwa kina. Uchunguzi wa

Schotman unamaanisha kuwa ilibidi kuchunguza maana na sababu za kiisimujamii

zinazohusiana na uundaji wa majina ya mahali kwa kutumia majina ya mahali kwa

lugha moja ya Tanzania kama vile kiruhaya.

2.5 Mkabala wa Nadharia

Utafiti huu unaongozwa na nadharia ya Makutano na Mwachano. Nadharia hii

imeasisiwa na Giles (1982). Nadharia hii itapima mshikamano walionao wanajamii

lugha kuhusu utamaduni na lugha yao kwa ujumla kama mbinu ya kupima nguvu ya

utambulisho wa jamii lugha. Pia nadharia hii inasisitiza kwamba ni kazi ya

mwanajamii lugha mwenyewe kuhamasika na kukuza lugha yake na kuitumia ili

iweze kuelezea amali za jamii husika, nadharia hii inajaribu kuelezea kwamba

inapofikia hatua wanajamii lugha wake kukubali kuacha kutumia lugha yake na

badala yake kukubali kutumia lugha nyingine, hapo tunasema kumekuwa na

makutano kwa jamiilugha hizo mbili. Jamiilugha hizo mbili ambazo zinakaribiana

30

kimaeneo kuendelea kutumia lugha hiyo inayodumishwa na kutumiwa kama

utambulisho wa jamii hiyo tunasema ni makutano. Vilevile inapotokea jamii

ikaendelea kutumia na kudumisha lugha yake, mazingira kama hayo yanaonyesha

kwamba kuna mwachano kati ya jamiilugha hizo. Kila jamii lugha inapoendeleza

utambulisho wake kwa kutumia lugha yake tunasema ni mwachano.

2.6 Sababu za Kiisimujamii za Majina

Baitan (2010) anabainisha sababu za kiismujamii za majina katika jamii ya wahaya

kuwa ni matukio na hali mbalimali katika kipindi cha kuzaliwa, imani, migongano ya

kifamilia, wanyama na mimea, umaarufu wa watu na vifo. Kadhalika katika jamii ya

Waruguru utafiti wa Abdul (2013) ulibaini kwamba baadhi ya majina ya koo

yalitolewa kwa wahusika kutokana na matendo, hali na matukio ambayo yalijitokeza

au kufanywa na wazazi husika katika kipindi cha ujauzito na hata kipindi cha

kujifungua. Kwa upande mwingine baadhi ya majina yalitolewa kwa wahusika

kutokana na kushiriki au kuhusika kwao moja kwa moja katika matendo mbalimbali,

shughuli makazi, hali, na matukio yaliyojitokeza katika jamii.

Kwa mujibu wa URT (2012), Mwanza Region Misungwi District Council. Wilaya ya

Misungwi ni wilaya moja ya mkoa wa Mwanza, idadi ya wakazi ya wilaya hiyo

ilihesabiwa kuwa 351,607 waishio humo. Lugha inayozungumzwa ni Kisukuma.

Shughuli za uchumi zinazofanyika katika wilaya ni kilimo, uvuvi, ufugaji na

uchimbaji wa madini.

2.7 Kiunzi cha Nadharia

Kwa mujibu wa Massamba (2004) nadharia ni taratibu kanuni na misingi ambayo

imejengwa katika muundo wa kimawazo kwa madhumuni ya kutumiwa kama kiolezo

31

cha kuelezea jambo. Hali kadhalika TUKI (2004), wanaunga mkono maana hiyo kwa

kusema kwamba nadharia ni mawazo, kutatua au kutekeleza jambo fulani.

Giles na Byren (1982) katika Nadharia yao ya makutano na mwachano wanaeleza

kuwa msingi mkuu wa utambulisho wa jamii unategemea sana wazungumzaji wa

lugha. Hivyo basi, kutokana na mawazo yao wanadhihirisha kuwa utambulisho

wowote wa jamii hutegemea wanajamii wenyewe.

Tabouret na Le page (1986), katika nadharia maelezo yao kuhusu utambulisho

wanadai kuwa, majina ya asili ya watu yanabainisha utambulisho wa mtu anakotoka.

Aidha kutokana na madai yao tunaweza kusema kuwa watu hutumia majina ya asili

kwa lengo la utambulisho kuwa wao ni nani na wanatokea eneo lipi kijiografia.

Tajfel (1986), katika nadharia ya utambulisho wa jamii anafafanua kuwa ni nadharia

inayozingatia vibainishi mbalimbali vya kisaikojamii vinavyofanya kundi fulani la

jamii lijione kuwa liko na kundi lingine la jamii kwa kuendeleza maarifa ya jamii

yake na mazoea ya pamoja ya kundi hilo.

Nadharia ya utambulisho wa jamii kwa kuzingatia mtazamo wa Le page na Tabouret-

Keller (1986), kwa kigezo kuwa katika mtazamo huu, wanazuoni hawa wanaeleza

bayana kuwa majina ya asili ya watu hubainisha utambulisho wa mtumiaji wa jina na

hata kupambanua anatoka katika jamii ipi, hili linajipambanua katika utafiti kwani

majina yaliyopatikana katika uwanda wa utafiti yana utambulisho kwa mtumiaji wa

jina linalo husika.

Hii ni tofauti na wanazuoni wengine kama vile Giles na Byren (1982) kwani

hawajazungumzia majina ya asili ya watu kama utambulisho kwa jamii lengwa.

32

JAMII

LUGHA

Jedwali Na. 2.2: Kiunzi cha Nadharia

Chanzo: Ubunifu wa Mtafiti

Nadharia ya makutano na mwachano imejidhihirisha katika utafiti huu kwa malengo

mahsusi matatu, kwanza katika kufafanua jinsi majina ya koo za kisukuma

yanavyotofautisha jinsi ya wanajamii. Mwachano unajidhihirisha pale fonimu, silabi

zinavyotofautiana. Mfano wa majina ya jinsi yanavyoachana.

Kwa jinsi ya ke jina Kabula na jinsi ya me jina Mabula mwachano upo kwenye

fonimu /k/ na /m/ , jina Kalekwa /ke/ na jina Mlekwa /me/ mwachano upo katika

silabi ka- na fonimu /m/ na upande mwingine ni silabi /m/. Jina Limi /ke/ na Malimi

/me/, mwachano upo mofimu kapa na silabi ma-.Pia majina mengine kama Nyanzala

/ke/ na Mayala /me/ mwachano upo kwenye silabi nya-, nza-,ma-,ya-.

MAJINA

JINSI ATHARI

NYANJA

33

Makutano ya majina yanayofanana kwa jinsi zote , kama vile Kalekwa/ke/ na

Kalekwa/me/, Luja /ke/ na Luja /me/,Shija /ke/ na Shija /me/,Mageni /ke/ na

Mageni/me/, Mhoja /ke/ na Mhoja/me/, Kamuli /ke/ na Kamuli/me/. Pili katika

kuchambua nyanja za kiisimujamii ambazo zinasababisha kutumia majina ya koo za

kisukuma, katika jamii ya kisukuma ili kuonyesha mwachano na makutano katika

nyanja ya kigezo cha kisemantiki majina katika jamii ya wasukuma yanabeba maana

ambazo zinafahamika na kueleweka vyema na wahusika, kama vile jina la Kundi

maana yake ni kitovu, jina Nyanza maana yake eneo lenye maji mengi, jina Nshelo

maana yake jiwe la kusagia, jina Mwanzalima maana yake ni uwazi uliopo katikati ya

meno ya mbele ya mtu.

Katika mwachano kuna majina yenye maana moja lakini othografia na fonolojia yake

ni tofauti, kama vile Lyulu na Nindo maana yake ni pua, Nyango, Lugi na Lwigi

maana yake ni mlango. Mwachano kiisimujamii pia katika majina ya koo za kisukuma

hutokea pale jina moja na lingine kutegemea mazingira husika ya utoaji wa majina

kama vile matukio, mtoto alipozaliwa, baada ya kuzaliwa na mahali pa kuzaliwa. Kwa

mfano: mtoto aliyezaliwa katika tukio la njaa ataitwa Mayala/me/ na Nyanzala /ke/,

tukio la vita ataitwa Bulugu/me/ au Malugu/me/. Tukio la tetemeko la ardhi ataitwa

Nyahinga/me/, tukio la mvua kubwa ataitwa Mabula/me/ na Mbula /ke/. Mtoto

akizaliwa ametanguliza miguu ataitwa Kashinje/ke/ au /me/, Mayila/me/ aliyezaliwa

njiani, Ng‘wandu /me/ amezaliwa chini ya mti wa mbuyu.

Majina ya koo za kisukuma katika nadharia ya makutano ni pale wanapozaliwa

watoto mapacha majina yao yanafanana kama vile Kulwa /ke/ na /me/, Doto/ke/ na

/me/, Shija /me/ na /ke/, Mhoja /ke/ na /me/, Kamuli/ke/ na/me/, Kasanda/me/ na /ke/.

34

Pia mtoto aliyezaliwa ametanguliza miguu anaitwa Kashinje kwa koo za kisukuma.

Katika nadharia ya makutano na mwachano majina mengine ya koo za kisukuma

yanatokana na athari za kijamii. Katika makutano majina ya koo za kisukuma

wanayopewa watoto ni ya bibi au babu, inawezekana yupo hai au alishafariki. Hivyo

basi baadhi ya majina akipewa mtoto huwa yanaathiri tabia ya mtoto anakuwa na tabia

aliyokuwa nayo mwenye jina. Kwa mfano: Kama mwenye jina alikuwa mchoyo naye

atakuwa na tabia hiyo ya uchoyo.

Mwachano wa majina mengine ya koo za kisukuma hutokana na athari ya majina

hayo, Kwa mfano: majina yanayorejelea tabia mbaya katika jamii kama vile ukorofi,

majanga vita ,njaa, tetemeko , kuwa mlevi wa kupindukia na hata wizi.Tabia hizi

huwafanya baadhi ya wazazi kutowapa majina watoto wao ya bibi na babu aliyekuwa

na tabia hizo. Katika kufikia malengo ya utafiti huu, mtafiti ameongozwa na nadharia

ya mwachano na makutano ya Giles (1982) wakati wa kukusanya data kwa haja ya

uchambuzi wa kiisimujamii katika majina ya koo za kisukuma.

Nadharia ya Makutano na Mwachano ya Giles inajaribu kupima mshikamano

walionao wanajamiilugha, kuhusu utamaduni wao wa lugha yao, hii ni nadharia

ambayo inarejelea dhana ya msambao na mwingiliano wa lugha katika uchambuzi wa

kiisimujamii katika majina ya koo za kisukuma. Kwa mujibu wa nadharia hii

inapofikia hatua kwa wanajamii lugha wake hukubali kuacha kutumia lugha yao na

kuanza kutumia lugha ya wanajamii nyingine hapo ndipo tunaposema kunakuwa na

makutano lakini inapotokea jamii lugha mbili zinazokaribiana kimaeneo, kila moja

ikaendelea kutumia na kudumisha lugha yake binafsi basi mazingira kama hayo

35

yanaonyesha kwamba kuna mwachano wa jamiilugha hizo (Msanjila na wenzake,

2011)

2.8 Hitimisho

Sehemu hii imechambua kwa kina mawazo ya wataalamu, kuhusiana na majina kwa

ujumla na tafiti mbalimbali zinazohusu majina zimejadili na nadharia ambayo

itaongoza uchambuzi wa data ya utafiti. Data hizi zitakuwa mwongozo katika utafiti

huu juu ya uchambuzi wa kiisimujamii wa majina ya koo za kisukuma,

utakaokamilishwa na malengo mahususin matatu. Malengo hayo mahsusi yatakuwa

kufafanua jinsi majina ya koo za kisukuma yanavyotofautisha jinsi ya wanajamii,

kuchambua nyanja za kiisimujamii ambazo zinasababisha kutumia majina ya koo za

kisukuma, na kubaini athari ambazo zinaweza kujitokeza katika majina ya koo za

kisukuma.

36

SURA YA TATU

MBINU ZA UTAFITI

3.1 Utangulizi

TUKI (2013) Mbinu ni njia ya kutekelezea jambo. Sehemu hii inashughulika na

mbinu mbalimbali zitakazotumika katika mchakato wa kufanya utafiti, mambo

yanayojadiliwa ni pamoja na eneo la utafiti, mbinu za utafiti, mbinu ya usaili, mbinu

ya hojaji, mbinu ya maktabani, kundi lengwa, sampuli, usampulishaji na mbinu za

uteuzi za sampuli, aina ya usampulishaji, mbinu za ukusanyaji wa data, vifaa na

hitimisho.

3.2 Muundo wa Utafiti

Utaratibu wa utafiti ni njia ya ukusanyaji, uchanganuzi na ufasiri wa data, utafiti huu

utazingatia utaratibu wa nyanjani. Kwa mujibu wake Babble (2005) utafiti wa

nyanjani una manufaa kwa sababu unachunguza maswala ya kijamii yakiwa katika

hali yao ya kimaumbile. Kwa utafiti huu utaratibu wa nyanjani utafaa kwani data

itakayotakiwa itakuwa nyanjani. Pia wahojiwa wa kutoa data ya kutosha watakuwa

nyanjani.

Miruka (2003) anaeleza kwamba utafiti wa nyanjani ni ule wenye hali ya kuingia

katika jamii na lengo la kuikusanya data, maana za kiisimujamii, utaratibu huu

utachaguliwa kwasababu utaambatana na mbinu ya mahojiano, itakayotumiwa na

mtafiti. Mtafiti atapaswa kushirikiana na kuwasiliana na wahojiwa akiwa nyanjani.

Usanifu wa utafiti huu katika sehemu kubwa ni wa maelezo, usanifu wa maelezo

kama ulivyofafanuliwa na Coben (2007) ni kupanga , kutoa sababu na kuzielezea data

37

kama zilivyoelezwa na walengwa wa utafiti. Mtafiti huzipanga kutokana na maudhui

au makundi yanayofanana, mtafiti alikuwa makini katika kueleza, kufafanua,

kuhakiki, kuvumbua, kufanya majaribio. Kutafsiri tasnifu alizozipata kupitia muundo

huu wa utafiti, sehemu ndogo ya utafiti imetumia takwimu kama kielelezo.

3.3 Eneo la Utafiti

Utafiti huu ulifanyika katika sehemu mbili, uwandani na maktabani. Kwa upande wa

uwandani utafiti huu ulifanyika katika wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.Eneo

hili la Misungwi liliteuliwa kwa kuwa sababu mbili. Kwanza, hii ndiyo wilaya

aliyozaliwa kukulia mtafiti wa utafiti huu. Hivyo, mtafiti anakielewa vema zaidi

lahaja ya Kisukuma(Kisumbwa) inayozungumzwa katika wilaya hii kuliko maeneo

mengine wanayoishi wasukuma.

Pili, inasemekana kuwa Wasukuma wa Wilaya ya Misungwi ni miongoni mwa

Wasukuma asilia wenye kuongea Kisukuma asilia ambacho hakijaingiliwa na lugha

ya Kiswahili. Aidha kwa mujibu wa mipaka yake, Kisukuma kinachozungumzwa

Misungwi, hakijavurugwa kwa kuingiliwa na lughajamii zingine. Hivyo eneo hili

lilikuwa kiwakilishi kizuri cha maeneo ya Kisukuma chenye lugha jamii yenye

kudumisha lugha ya Kisukuma na tamaduni zote za asili za Kisukuma. Kielezo cha

3.1 hapa chini kinadhihirisha mahali milipo wilaya ya Misungwi katika ramami ya

Mkoa wa Mwanza.

38

Kielezo Na. 3.1: Ramani ya Mkoa wa Mwanza Ikionesha Mahali Ilipo Wilaya ya

Misungwi

Chanzo:https://en.wikipedia.org/wiki/Misungwi_District#/media/File:Mwanza-Misungwi.svg:

Iliyopakuliwa tarehe 12 Februari, 2018

3.4 Kundi Lengwa

Cooper (1989) na Van (1990) wanafasili kundi lengwa kuwa ni mtu mmoja, kikundi

au elementi ambazo mtafiti amekusudia kuzihusisha katika utafiti wake. Katika utafiti

39

huu kundi lengwa ni wazee wenye umri kati ya miaka 50—70, wanaume ishirini na

wanawake ishirini, sababu ya kuchagua walengwa wenye umri huu na idadi hiyo ni

wale wenye uelewa mkubwa wa tamaduni na uelewa wa majina ya koo.

3.5 Sampuli

Adam (2008) anaeleza kuwa ni vigumu kwa mtafiti kushughulikia idadi kubwa ya

wanajamii wanaohusika katika utafiti hata kama anaona watafitiwa wote ni muhimu.

Mtafiti hutakiwa kuchagua idadi maalumu ya wanajamii wa kushughulikia katika

utafiti wake.

3.5.1 Usampulishaji

Katika uteuzi wa sampuli makusudi, umetumika Kothari (2004) McBurney na

wengineo, Mugenda (2008) wanasema sampuli hii huteuliwa kwa kuchagua aina

fulani ya watu ili kuwakilisha makundi maalumu katika jamii, watafitiwa wanawake

ishirini na wanaume ishirini kuanzia miaka hamsini hadi sabini na kuendelea. Umri

huu unatiliwa maanani kwa sababu ya kuaminika kwamba watu wenye umri mkubwa

wana tajriba ya kutosha kuhusu utamaduni wa jamii ya Wasukuma, majina miambili

yalitarajiwa kukusanywa.

Usampulishaji kama anavyoeleza Adamu (2008) ni mbinu, mchakato au kitendo cha

kutafuta walengwa wa utafiti. Naye Kothari (2004) anasema kuwa usampulishaji ni

mpango wa kuchagua sampuli maalumu kutoka katika kundi. Aina ya walengwa ni

wazee wenye umri kati ya miaka hamsini hadi sabini, idadi ya wanawake ni ishirini na

wanaume ni ishirini.

40

3.6 Mbinu za Utafiti

Katika utafiti huu mbinu mbalimbali zilitumika kukusanya data na kuzichambua.

Kothari (1990) anafafanua dhana ya ukusanyaji wa data kama zoezi la awali katika

utafiti ambalo humwezesha mtafiti kupata taarifa alizozikusudia ili kumfikisha

kwenye malengo yake ya utafiti. Aidha mtaalamu huyu anasisitiza kuwa hatua ya

uwasilishaji na uchanganuzi wa data haiwezi kufanyika kabla ya hatua hii ya

ukusanyaji data. Katika utafiti huu mtafiti atatumia mbinu mbili za ukusanyaji wa data

ambazo ni usaili na hojaji.

3.6.1 Mbinu za ukusanyaji wa data

Adam (2008) anaeleza kuwa data ni vielelezo vinavyokubalika ambavyo

vinathibitisha ukweli wa matokeo. Data za msingi (awali) kama anavyoeleza Kothari

(2004) ni zile data ambazo hukusanywa kwa mara ya kwanza, data hizi zimekusanywa

wakati mtafiti yupo uwandani. Data ya upili ni zile ambazo tayari zilishakusanywa na

zilishatumika na zimehifadhiwa.

3.6.2 Mbinu ya Usaili

Mbinu hii inahusisha uwasilishaji wa maswali kwa wasailiwa. Maswali hayo

yalijibiwa kwa njia ya mdomo, kwa wakati huohuo na hatimaye mtafiti alirekodi

majibu hayo katika daftari la kumbukumbu. Kwa mujibu wa Kothari (1990) mbinu hii

inahusu unyumbukaji katika mchakato wa kuuliza maswali na hatimaye husaidia

kuweka bayana istilahi ambazo zinaonekana hazieleweki kwa watu wanaoulizwa

maswali. Pia inasaidia kupata taarifa za ziada na za kina zaidi hususani pale ambapo

majibu ya watu wanaosailiwa yanapokuwa hayaeleweki.

41

Kothari anaendelea kueleza kuwa mbinu hii inamruhusu mtafiti kuuliza maswali ya

ziada. Hivyo basi katika utafiti huu usaili utatumika ili kupata data zinazohusiana na

uchambuzi wa kiisimujamii katika majina ya koo za kisukuma. Pia, katika mbinu hii

mtafiti alitumia zaidi usaili maalumu ambapo wasailiwa waliulizwa maswali ya

msingi ya aina moja na yaliyo katika mpangilio ulio sawa. Maswali ambayo yatalenga

kukusanya taarifa za aina moja katika kundi la watafitiwa yaliandaliwa. Mbinu hii ni

nzuri kwa sababu watafitiwa walikuwa na uwezo wa kujibu maswali sawa na hii

inaongeza ulinganishi katika kujibu maswali (Kothari 1990).

3.6.3 Mbinu ya Hojaji

Hii ni mbinu ambayo mtafiti anakusanya data akiwa ana kwa ana na mtafitiwa. Mtafiti

huuliza maswali na majibu huyarekodi katika daftari la kumbukumbu au kwa kutumia

vifaa vya kurekodia au simu. Manufaa ya mbinu hii mtafiti kupata fursa ya kufafanua

maswali, pale ambapo mtafitiwa hakufahamu, pia mbinu hii inatoa fursa kwa watafiti

waliosoma na wasiosoma kushiriki kutoa taarifa.

Kothari (1990) Hojaji ni mbinu ya utafiti ambapo mtafiti anaandaa maswali yake

yanayolenga kupata taarifa kuhusu jambo fulani. Maswali haya yanaweza kuhitaji

majibu mafupi au marefu kutegemeana na taarifa inayohitajika na anayepewa dodoso

hizo. Mbinu hii itatumiwa ili kusaidia katika kukusanya data ambazo mtafiti anaamini

atazipata kutoka watumiaji wa lugha.

3.7 Mikabala ya Uchambuaji Data

Katika utafiti huu mkabala usio wa kitakwimu, na wa kitakwimu kwa kiasi kidogo

utatumika. Mkabala usio wa kitakwimu mchakato wake unatumia udundulizaji wa

42

data kwa kuchunguza jambo, kufuatilia jambo, na kutafsiri majibu yao, utafiti huu ni

bora kwakuwa unatoa taarifa kamili zinazojitosheleza. Mkabala wa kitakwimu ni aina

ya ukusanyaji data kwa kutumia data nyingi, ni data yoyote ile katika mfumo wa

namba, mtafiti anaweza kutumia swali moja na mahsusi lakini akakusanya sampuli

nyingi.

3.8 Maadili ya Utafiti

Aeker (2002) kama alivyonukuliwa na Adam (2008) wametaja maadili ya utafiti kuwa

ni pamoja na haki ya kuwa na usiri, yaani mtafiti hatatoa siri ya mtafitiwa, pia

ameeleza haki ya mtafitiwa kuhakikishiwa usalama wake, haki ya kujua madhumuni

ya utafiti, haki ya kupata matokeo ya utafiti, haki ya kujibu swali atakalopenda kujibu

na haki ya kukataa kushiriki utafiti. Mtafiti atatambua haki zote hizi na kuzitekeleza

tatizo lolote litakalojitokeza ni juu ya mtafiti mwenyewe.

3.9 Mipaka ya Utafiti

Utafiti huu utachunguza uchambuzi wa kiisimujamii na maana za majina ya koo za

kisukuma. Jumla ya watu arobaini watahusishwa katika utafiti huu, utafiti utafanyika

katika wilaya Misungwi, mkoa wa Mwanza, washiriki wa utafiti watakuwa ni wazee

wa kiume ishirini na wa kike ishirini.

3.10 Hitimisho

Sehemu hii ya tatu ilifafanua utangulizi, muundo wa utafiti, eneo la utafiti ni lipi,

kundi lengwa, sampuli, usampulishaji, na mbinu za utafiti, mikabala ya ukusanyaji

data, maadili ya utafiti, mipaka ya utafiti.

43

SURA YA NNE

UWASILISHAJI NA UCHAMBUZI WA MATOKEO YA UTAFITI

4.1 Utangulizi

Sura hii inahusu uwasilishaji na uchambuzi wa data iliyokusanywa kutoka uwandani,

uchambuzi huu unalenga zaidi katika kukamilisha lengo kuu la utafiti ambao ni

uchambuzi wa kiisimujamii katika majina ya koo za kisukuma. Lengo hili kuu

linakamilishwa na malengo mahsusi matatu ambayo ni kufafanua jinsi majina ya koo

ya kisukuma yanavyotofautisha jinsi ya wanajamii, kuchambua nyanja za kiisimu

ambazo zinasababisha kutumia majina ya koo za kisukuma, na kubaini athari ambazo

zinaweza kujitokeza katika majina ya koo za kisukuma.

Sura ya nne imegawanyika katika sehemu kuu tatu, utangulizi, uwasilishaji,

uchambuzi wa data na hitimisho. Katika kukamilisha lengo kuu la utafiti huu, data

imewasilishwa na kuchanganuliwa kwa kuzingatia malengo mahsusi ambayo ni

kufafanua na kuchambua jinsi majina ya kisukuma yanavyotofautisha jinsi ya

wanajamii na kuelezea sababu za kiisimujamii ambazo hutumika kutumia majina ya

koo za Kisukuma. Data iliwasilishwa na kuchanganuliwa katika makundi tofauti kwa

kuzingatia vigezo na sifa zinazofanana katika majina ya koo. Data imewasilishwa kwa

kutumia majedwali na maelezo.

4.2 Nyanja Zinazosababisha Majina ya Koo za Kisukuma

4.2.1 Mgawanyo wa Majina kwa Kigezo cha Kisemantiki

Mgawanyo wa majina kwa kigezo cha kisemaniki katika jamii ya kisukuma yapo

majina ya kiasili ambayo yanatumika. Miongoni mwa majina hayo ni pamoja na

44

majina ya koo. Majina katika jamii ya wasukuma yanabeba maana ambazo

zinafahamika na kueleweka vyema na wahusika wa majina hayo kulingana na

mazingira na utamaduni wa jamii hiyo. Jina ambalo anapewa mtu linatokana na lugha

ya jamii yake na jina hilo hubeba maana inayotokana na utamaduni na mazingira ya

jamii hiyo. Kimsingi majina ya koo ya wasukuma maana zake zinaeleweka vema kwa

jamii ya wasukuma wenyewe.

Kadhalika uwasilishaji na uchambuzi wa data kwa kuweka majina katika makundi

tofauti kwa kuzingatia kigezo cha maana ya sifa zinazofanana katka majina hayo.

Miongoni mwa makundi hayo ni pamoja na haya yafuatayo, majina ya koo

yaliyotokana na mwonekano wa maumbile, majina yanayo tokana na sehemu ya

makazi, majina yanayotokana na vitu vinavyopatikana katika mazingira ya jamii,

makundi haya yamefafanuliwa na kuwasilishwa .

4.2.1.1 Majina ya Koo Yaliyotokana na Mwonekano wa Maumbile

Haya ni majina yaliyohusiana na mwonekano wa maumbile waliyokuwa nayo

waanzilishi wa koo. Majina haya yalihusisha pia viungo mbalimbali vya mwili wa

binadamu, kwa mfano mikono, misuli na hali ya maumbile kwa ujumla, mfano wa

majina hayo ni kama vile.

Mfano wa majina hapo juu inadhihirisha kwamba baadhi ya majina ya koo za

kisukuma maana zake zinanukuliwa na mwonekano wa maumbile kama vile matumizi

ya viungo vya mwili, pia majina haya yalitolewa kutokana na maumbile ya wazazi,

mababu na mabibi, na maumbile yake mwenye kupewa jina.

45

Jedwali Na. 4.1: Majina ya Koo Maliyotokana na Mwonekano wa Maumbile

Na Jina Maana Jinsi

1 Nkonoki Mkono gani Me

2 Mabundu Kuwa na maumbile ya macho makubwa Me

3 Matu Jina litokanalo na maumbile ya masikio makubwa Me/ke

4 Kundi Jina linaotokana na kitovu Ke

5 Shonongo Mpangilio wa meno ya mtu ambayo hayaruhusu

mdomo kufunga

me/ke

6 Mwanzalima Jina linalotokana na mwanya, au uwazi katikati

meno ya mbele

Me

7 Mazala Jina litokanalo na mtu kuzaliwa na vidole zaidi ya

vitano

Me

Chanzo: Data za Uwandani, 2017

Mfano wa jina la Kundi mara nyingi jina hili limekuwa likitokana na maumbile ya

kitovu kama umbo kubwa la kitovu cha mpewa jina, maumbile ya vitovu vikubwa

yamekuwa yakionekana kwa watoto wadogo sana pale kosa la uondoaji wa kondo la

nyuma linalopelekea mtoto kuwa na kitovu kikubwa, hivyo husababisha kupewa jina

hilo. Nkonoki ni jina linalotokana na maumbile ya mikono, yaweza kuwa kati ya

mkono mmoja una tatizo hivyo ni katika hali ya kujiridhisha ni mkono gani ambao

unarejelewa.

Mabundo ni jina linalotokana na maumbile ya macho kua makubwa, ambayo mwenye

jina hili huenda babu yake alikuwa na maumbile makubwa ya macho, na kwa bahati

nzuri mtoto aliyezaliwa baada ya muda akaonekana kuwa na maumbile makubwa ya

macho hivyo kupelekea kupewa jina la mabundo, Mazala ni jina ambalo anapewa

mtoto mwenye maumbile ya vidole zaidi ya vitano vya mikononi au miguuni, baadhi

46

ya koo zimekuwa zikitafuta njia za kuondoa vidole ongezeki kwa maana kubakiza

vidole vitano tu,na vile ambavyo havipo kwenye mpangilio huondolewa kwa kutumia

uzi baada ya kufungwa, hali ambayo hupelekea kidole hicho kunyauka na hatimaye

kidole hicho kukatika. Mwanzalima ni ule uwazi uliopo katikati ya meno ya mbele

kwa mtu, kwa Kiswahili tunasema ―mwanya‖ baadhi ya watu wamekuwa na mtazamo

tofauti na watu wenye umbile hili la meno, inaonekana watu wenye mwanya

wanapendeza sana wanapokuwa wanatabasamu au wanacheka, na baadhi ya watu

wanajitahidi kuchonga meno ili upatikane uwazi huo.

Mtoto anapozaliwa kuna hali ya kutenganisha meno ambapo unajidhihirisha kuwa

baadaye mtoto huyu atakuwa na mwanya. Shonongo ni hali ya kua na meno yasio na

mpangilio ambayo husababisha mdomo kushindwa kufungika, wana jamii wana

chukulia kama utani kwa jina hili hasa pale watu tofauti wanapokuwa na majina

yanayofanana ya ubatizo wanapotaka kutofautisha yupi wanayemrejea watatumia

zaidi jina la Shonongo.

4.2.1.2 Majina Yanayotokana na Sehemu za Makazi

Majina yanayopatikana katika kundi hili yalikuwa yanasawiri sehemu za makazi

walioishi waanzilishi wa koo husika. Aidha, sehemu hizo zilipewa majina hayo

kutokana na vitu vya kiasili na kiutamaduni. Vilivyopatikana katika makazi ya watu

wenye koo husika. Vitu hivyo vilijumuisha mapango, milima, ziwa, mawe na mizimu.

Baadhi ya majina ya kisukuma maana zake zina nukuliwa na majina ya maeneo

walioishi waanzilishi wa koo hizo. Sehemu hizo zilijumuisha majina ya milima,

majina ya mito, majina ya ziwa na majina ya mizimu. Kwa mfano jina ―Nyanza‖ ni

47

eneo ambalo lina maji mengi, kwa mfano ziwa Victoria, zipo sababu zinazopelekea

kupewa jina hili, wazazi walijihusisha na shughuli za majini, mfano uvuvi, kilimo, na

ufugaji, mwenye jina hili alipenda sana shughuli za kwenye maji, hivyo aliweza

kujulikana kwa jina hilo, likapelekea wajukuu zake waweze kuitwa jina hilo ambalo

lilitoka kwa mwanzilishi, na hapo likapelekea kujulikana kama jina la ukoo.

Jedwali Na. 4.2: Majina ya Koo Yanayotokana na Makazi

Na Majina Maana Jinsi

8 Nyanza Sehemu yenye ziwa Me

9 Ngasamo Mlima Me

10 Nsembi Mchimbaji wa madini migodini Me

11 Mongo Mto Me

12 Shing‘weng‘we Zimwi Me

13 Salawe Maeneo ya machimboni Me

Chanzo: Data za Uwandani, 2017

Jina kama ―mongo‘‘ambalo linamaanisha mto linaweza likawa limesababishwa na

mhusika alikuwa anapenda kuendesha shughuli zake kando na mto hivyo kuzoezwa

kuitwa jina lake kama yeye ni mto. Jina ―Nsembi‘‘ambalo linamaanisha mchimbaji

linaweza likaanza kama utani tu lakini kwa baadae likazoeleka na kuwa kama jina

rasmi kwa mhusika na baadae likaja kutumika kwa wajukuu. Jina kama ―Ngasamo‖ ni

jina linalotokana na mlima ngasamo hivyo kupewa jina la ngasamo kwa sababu ya

kujulikana kama mlima ngasamo.

4.2.1.3 Majina ya Koo Yanayotokana na Vitu

Haya ni majina ambayo maana zake zilisawiri vitu ambavyo vilipatikana katika

mazingira yaliyoizunguka jamii. Majina hayo yanahusisha vitu vilivyopatikana katika

48

sura ya nchi, vya asili na vile vilivyotengenezwa na watu. Vitu vilijumuisha nguo, na

zana mbalimbali. Maelezo haya yameungwa mkono na Msanjila, Kihore, na

Massamba kwa kusema;

Kila jamiilugha huwa ina vitu mbalimbali ambavyo hupatikana mahali hapo tu na

havipatikani mahali pengine popote. Vitu hivyo vyaweza kuwa milima mirefu, ziwa

refu au pana, wanyama wa aina fulani, na kadhalika. Majina ya vitu hivi yanaotolewa

kwa lugha yake ya asili ambako vitu hivyo viko, husaidia kuitambuisha jamiilugha ya

mahali hapo.

Jedwali Na. 4.3: Majina ya Koo Yaliyotokana na Vitu

Na Jina Maana Jinsi

14 Makaranga Karanga Me

15 Mahuma Maporomoko Me

16 Luhungo Ungo Me

17 Nshelo Jiwe la kusagia Me

18 Madirisha Dirisha Me

19 Mashini Mashine Me

20 Sulubali Suluali Me

21 Sungi Zawadi anayobeba mtu kwenda ugenini Ke

22 Bugali Ugali Me

Chanzo: Data za Uwandani, 2017

Majina katika koo za kisukuma baadhi yake yanatokana na vitu, vitu katika koo za

kisukuma vina majina ambayo wanajamii wanapewa, majina kama Nshelo, Luhungo,

49

Madirisha, Mashini, Sulubali, Shitambala, Makaranga, Mahuma, Majina haya ni vitu,

lakini yamekubalika katika koo yatumike, majina haya yalitumika kwa waanzilishi,

imekuwa vigumu kuyaacha kwani kuyaacha ni kupoteza majina ya koo, na

kusababisha kuwasahau kabisa mababu na mabibi ambao walishafariki.

Kwa mfano jina la ―Makaranga‘‘ maana yake karanga, mtu aliyezaliwa wakati wa

uvunaji wa karanga, katika tamaduni za kisukuma, karanga zinapokomaa na kufikia

wakati wa kuvunwa huwa zinang‘olewa na kukusanywa katika mafungu makubwa na

kuwekwa chini ya mti shambani humohumo, ili kurahsisha kuzichambua muda

utakapofika, pia familia ambayo ina bahati ya kulima karanga na kuvuna kwa kiasi

kikubwa sana zaidi ya wanajamii wote kila mwaka familia hiyo itaitwa ―kwa

makaranga‖, mtoto atakayezaliwa kipindi hiki ataitwa Makaranga, jina lingine

―Mahuma‘‘ maana yake ni maporomoko ya maji ,kama vile maji ya mto, maji ya

miamba, au maji yanayotoka sehemu moja kwenda nyingine hasa zenye mwinuko

kuelekea bondeni, baadhi ya watu huwa wanakwenda kufanya matambiko katika

maeneo haya.

Pia wengine hufika kwenye maporomoko hayo kuchota maji kwa imani kuwa maji

hayo yana baraka, mama atayejifungua mtoto karibu kabisa na maporomoko haya

mtoto wake ataitwa Mahuma. Jina la ―Luhungo‖ maana yake ni Ungo wa kupepetea

nafaka aina zote, mfano mchele, mtama, dengu, choroko, mahindi. Vilevile shughuli

za kiuchumi zilizokuwa zinafanywa za kiufundi na mababu za usukaji wa nyungo.

Kumekuwepo na imani za kishirikina kuwa ungo unatumika kama chombo cha usafiri

cha wachawi, kutoka sehemu moja kwenda nyingine ya mbali sana kwa muda mfupi,

Jina jingine ―Bugali‖ hili jina humaanisha ugali jina hili huababishwa na sababu

50

mbalimbali kama vile msimu wa chakula kingi na vile vile inaweza kusababishwa na

wakati mpewa jina akiwa mdogo alikuwa anapenda kulilia ugali hivyo ikapelekea

kuitwa Bugali kama jina lake rasmi hata kama alikuwa na jina jingine rasmi, hilo jina

la Bugali likawa maarufu zaidi. Nshelo‖ ni jina ambalo maana yake ni jiwe la kusagia

nafaka, katika tamaduni za kisukuma jiwe hili lina umbile fulani la kuvutia jiwe hili ni

kwa ajili ya kusaga na kuparaza nafaka, kwa mfano mtama, mchele, na karanga.

Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia matumizi ya mawe haya

yamepungua kutokana na kuwepo kwa mashine za kusagia na kuparaza na hata

kukoboa, mawe haya yamebakiza shughuli chache za kusaga karanga za kuweka

kwenye mboga. Matumizi ya mawe haya yamebaki vijijini, wengine kuyatumia zaidi

katika kusaga dawa za kienyeji.

Na hivyo ni utamaduni uliokuwepo enzi za mababu, jamii inaendelea kuuenzi. Jina

―Sungi‖ ni zawadi anayobeba mtu kupeleka ugenini. Ni utamaduni kwamba

unapoandaa safari lazima uandae zawadi itakayokuwa imefungwa vizuri ambayo

utapokelewa pale utakapokuwa umefika ugenini. ―Mashini‖ ni jina ambalo maana

yake ni mashine ya aina yoyote, kwa mfano ya kusaga, mashine ya kukoboa nafaka,

kukamua nafaka, kufua vyuma, katika jamii ya kisukuma mtu mwenye kufanya kazi

kubwa kwa haraka, mfano kulima wanapendelea kumwita mashini, waanzilishi wa

majina haya walikuwa na sifa hizo.

4.3 Mgawanyo wa Majina ya Koo kwa Kigezo cha Kiisimujamii

Sehemu hii ya utafiti ililenga kukamilisha malengo mahususi la kwanza la utafiti

ambalo ni kuelezea sababu za kiisimujamii ambazo hutumika kutoa majina ya koo za

kisukuma. Hata hivyo sababu za utoaji wa majina katika jamii ya wasukuma zilikuwa

51

zikitofautiana kati ya jina moja na lingine kutegemea mazingira husika ya utoaji wa

majina.

Baitan (2010) anabainisha sababu za utoaji wa majina katika jamii ya wahaya kuwa ni

matukio na hali mbalimmali katika kipindi cha kuzaliwa, imani, migongano ya

kifamilia, wanyama na mimea, umaarufu wa watu na vifo. Kadhalika katika sehemu

hii data iliwasilishwa na kuchanganuliwa katika makundi tofauti kulingana na vigezo

na sifa zilizofanana kiisimu. Makundi hayo pamoja na, matukio, majina yanayotokana

na kuzaliwa kwa mtoto na baada ya kuzaliwa, majina yanayotokana na mahali pa

kuzaliwa, majina ya koo yanayotokana na sitari za wanyama na ndege, majina

yanayotokana na shughuli za ujenzi, majina yanatokana na maradhi/hali, majina

yanayotokana na hali ya vitu, majina yanayotokana na misimu, majina yanatokana na

mimea, majina yanayotokana na matendo ya watu, majina yanayotokana na jinsi,

majina wanayopewa baada ya kuzaliwa watoto mapacha, majina yanayotokana na

chimbuko la ukoo.

4.3.1 Majina Yaliyotokana na Matukio

Haya ni majina ambayo yalitokana na wahusika kutokana na matukio tofauti

yaliyojitokeza miongoni mwa watumiaji wa majina husika. Kwa kiasi kikubwa

matukio hayo yaliyojitokeza katika matukio yaliyohusiana na jinsi mtoto alivyozaliwa

na baada ya kuzaliwa. Maelezo haya yanaungwa mkono na msanjila, Kihore na

masamba (2009:55-56) kama wanavyoeleza.

Katika kila jamiilugha huwa pia yanatokea matukio mbalimbali makubwa kijamii

ambayo husimuliwa vizazi na vizazi na matukio mbalimbali makubwa kijamii

52

inayohusika. Matukio ya aina hii yanaweza kuwa katika ngazi ya jamiilugha

zitokanazo na makabila mbalimbali au yakawa ni matukio yasiyogusa Taifa kwa

ujumla. Wanaendelea kufafanua kuhusiana na majina ya matukio kwa kutolea mifano

ya majina ya matukio yaliyotokea katika jamii ya wagogo kwa kueleza;

―Majina ya matukio muhimu katika jamiilugha mbalimbali hutegemea jamiilugha

hizo. Tukichukulia tena mfano kutoka jamiilugha ya wagogo, tunapata majina

yanayoelezea matukio ya njaa yaliyosababisha watu wengi kupoteza maisha;

Chonyamagulu-tukio la njaa lililodhoofisha miguu ya watu kiasi cha kuwafanya

washindwe kutembea. Ilitokea mwaka 1860 Chonya maana yake ni ―kunyonya‖ na

magulu ni ―miguu‖ Magubika tukio la njaa lililofanya watu wafunike vyungu vya

kupikia chakula kwasababu hakukuwa na cha kupika. Njaa hii ilitokea miaka ya

1888 na 1889. Gubika maana yake ni funika.

Buberwa (2010) katika kuzungumzia majina ya matukio anadai kwamba, majina

yanayojitokeza katika kundi hili kimsingi yanatokana na matukio kama vile vifo,

sherehe, vita, kuhama na kuzaliwa. Anazidi kufafanua kwa kutoa mifano ya majina ya

matukio katika jamii ya Wahaya kama vile.

―Kifamutima maana yake ―kufa moyo‖, Uwepo wa jina hilo ni kutokana na watu

kupoteza ubinadamu wao kutokana na mtoto wa mtawala kuuwawa katika kijiji hicho.

4.3.1.1 Matukio Yanavyohusiana na Jinsi Mtoto Alipozaliwa na Baada ya

Kuzaliwa

Majina yaliyo katika kundi hili yalikuwa yakitotolewa kwa wahusika kutokana namna

walivyoonekana walivyozaliwa pamoja na matukio yaliyokuwa yanatokea baada ya

53

kuzaliwa. Majina haya yalijumuisha jinsi alivyozaliwa, kipindi anazaliwa kulikuwa na

na hali gani. Majina ni kama ifuatavyo;

Jedwali Na. 4.4: Matukio Yaliyohusiana na Jinsi Mtoto Alipozaliwa na Baada ya

Kuzaliwa

Na Jina Sababu za kiisimujamii

23 Kashinje alizaliwa ametanguliza miguu

24 Makoye alizaliwa wakati wa matatizo

25 Mihayo alizaliwa kipindi cha migogoro ya wazazi

26 Ndebile alizaliwa njiti, hakutimiza miezi tisa tumboni

27 Nhabi Kipindi yupo tumboni baba yake alifariki dunia

28 Ng‘waigwa Alipozaliwa, mama yake alifukuzwa na mume wake

29 Katikaza Wazazi wake weupe ,lakini yeye akazaliwa mweusi

30 Ng‘wendamkono Mama yake wakati anaumwa uchungu alikuwa uchi

kashikilia nguo mkononi.

31 Bugumba Mtoto aliyezaliwa baada ya wazazi wake kuzushiwa

wao ni tasa

32 Mpejiwa Mama yake alifukuzwa nyumbani kipindi ana mimba

33 Mpelwa Mama yake aliachwa na mme wake kipindi ana mimba

34 Matogoro Alizaliwa vichakani

35 Gado Alizaliwa na uzito mdogo

36 Dalahile Mama yake alidharauriwa sana ukweni

Chanzo: Data za Uwandani, 2017

Majina yaliyo katika kundi hili yalikuwa yakitotolewa kwa wahusika kutokana namna

walivyoonekana walivyozaliwa pamoja na matukio yaliyokuwa yanatokea baada ya

kuzaliwa. Majina haya yalijumuisha jinsi alivyozaliwa, kipindi anazaliwa kulikuwa na

54

na hali gani. Majina ni kama ifuatavyo; Maduka, Mashamba, Mabuga, Manho,

Maroha, Nsonzi, Ng‘wenheleja nk.

Jedwali Na. 4.5: Majina Yanavyohusiana na Jinsi Mtoto Alipozaliwa na Baada

ya Kuzaliwa

Chanzo: Data za Uwandani, 2017

Kashinje ni mtoto aliyezaliwa ametanguliza miguu, katika jamii ya kisukuma mtoto

wa namna hii anatabiriwa kuwa ni mkosi kwake, wamwita ―nsebu‖ maana yake ni

wamoto, mkosi kwa jamii pia, Kama ni mwanaume kila atakapooa mke atakufa, na

hata akioa mwingine vivyo hivyo atakufa, wote atakaooa watakufa, na upande wa

mwanamke akiolewa na mwanaume huyo atakufa hata akiolewa na mwingine

mwanaume huyo atakufa.

Japo binadamu ni lazima afe lakini kwa mtoto wa kuzaliwa ametanguliza miguu hali

inakuwa tofauti kila anayemuoa au kuolewa panakuwa na mfululizo wa kufa. Mkosi

kwa jamii panatokea ukosefu wa mvua kwa jamii. Jamii ya kisukuma ina utaratibu wa

37 Ndemi Alizaliwa machungani

38 Madoshi Mtu mwenye majivuno

39 Mwakami alizaliwa kwenye mwaka wa shida

40 Ng‘wenheleja Alisababisha kitu fulani baada ya kuzaliwa

41 Marosha Mtoto aliyezaliwa baada ya wenzake kuwa wanakufa

hivyo na huyo alitegemewa atakufa

42 Nsonzi Mtoto anayezaliwa goigoi

43 Manho Amezaliwa ametanguliza matako

44. Mabuga Alizaliwa kwenye maeneo ya udongo mweusi

45 Maduka Mtoto aliyezaliwa kutokana na mama alivyokuwa

mjamzito kupenda kwenda madukani

46 Mashamba Amezaliwa shambani.

55

tambiko kwa mtoto atakayezaliwa ametanguliza miguu, pia ni vizuri mama akawa

wazi kama amejifungua kwa namna hii, ili jamii ifanye tambiko. Kuna imani kwamba

mtoto huyu huwa ni mkubwa wa watoto mapacha.

Utaratibu wa tambiko unakuwa kama ifuatavyo, mtoto aliyezaliwa kwa namna hii

hatakiwi kunyoa nywele, hatatoka nje, na wazazi wake wanapokuwa wanafanya usafi

ndani ni marufuku kutoa uchafu nje, utakusanya ndani hadi pale tambiko

litakapotimia, hawa wazazi wanatakiwa watafute chakula cha kutosha kwa ajili ya

sherehe hiyo ya tambiko, pia zitafutwe zawadi watakazopewa wale wafanya tambiko

wa jamii, zawadi hizo ni kama vile vitenge, sufuria na shuka.

Baada ya kukamilisha kupata mahitaji haya, basi watu wanaalikwa kwenye sherehe

hiyo ya tambiko, mbuzi au kondoo atakayekuwa kitoeo hatachinjwa, kitakachofanyika

baba na mama waliyemzaa yule ―Kashinje‖ watakaa mlangoni huku wamemkalia

Yule kondoo au mbuzi , miguu ya wazazi hawa lazima iingiliane huku wakimniga

huyo mnyama hadi kufa , wakati huohuo lugha inayotumika hapo ni ya matusi

makubwa makubwa ya nguoni, hata ile hadhira inayoshuhudia ni lazima nayo

izungumze lugha ya matusi, kwa mtu mgeni akishiriki katika shughuli hizi ataona aibu

kubwa na hata sahau maishani mwake. Chakula kikipikwa wazazi watapewa kidogo

wale chakula hicho lugha ni ileile ya matusi hadi sherehe kuisha, huku chakula kikiwa

kimewekewa dawa na hadhira nayo inatazama.

Baada ya hapo watapewa chakula cha kutosha na hadhira nayo itakula chakula

ikiendelea na lugha ileile, baada ya tambiko mtoto atanyolewa nywele na waganga

waliokuja kufanya tambiko, waganga watapewa zawadi zao, na uchafu uliokuwa

56

unakusanywa ndani nao utazolewa na kumwaga. Ikumbuke kuwa akizaliwa mtoto wa

aina hii kwa bahati mbaya akafariki wakamzika bila kusema amezaliwa katika hali hii,

itanyesha mvua ndogo sana lakini itakuwa na radi kubwa ambayo radi hiyo itafukuwa

pale alipozikwa mtoto huyo, taratibu za tambiko inabidi zifanyike.

Kutokana na kukomesha tamaduni nyingine asilimia chache imeanza kutambua jambo

hili kwa mtazamo tofauti wa imani, kwa maana inapotokea mtoto amezaliwa

katanguliza miguu wamekuwa wakimpeleka kanisani kuombewa, na hata kama

wazazi huwa hawana tabia ya kusali wanalazimika kuendelea kusali. Jina la

―Makoye‖ mtoto huyu alizaliwa wakati wa matatizo, au ni mtoto aliyezaliwa kwa

shida, au kipindi ana mimba alipata matatizo mengi, au kipindi anajifungua alipata

shida kubwa.

―Mihayo‖ ni jina lenye maana maneno mengi ambayo si mazuri, kwa maana ya

migogoro kati ya pande mbili huenda ikawa wazazi kwa wazazi, au jamii na wazazi

Jina kama ―Mabuga‘‘ lina maanisha mbuga hivyo yawezekena mpewa jina alizaliwa

wakati mama yake yuko mbugani anachunga au anafanya kazi yoyote huko mbugani

hivyo kupelekea kuitwa jina la mbuga. Jina ―Manho‘‘ hutokana na kuzaliwa mtoto

akiwa ametanguliza matako hivyo kupelekea kuitwa jina hilo.Jina ―Maduka‖

linalomaanisha duka linaweza kusababishwa na kwamba mama yake alimzaa akiwa

ameenda kuuza duka au tabia ya mama mzazi kupendelea kwenda madukani kipindi

akiwa mimba.Jina ―Ng‘wenheleja‖ ni jina ambalo linamaanisha kisababishi huenda

baada ya mtoto kuzaliwa alisababisha kitu kizuri au kibaya kutokea kwa mfano baada

ya mtoto kuzaliwa njaa ikatokea kwasababu mama alipo mzaa mtoto alishindwa

57

kwenda shambani hivyo kupelekea kushindwa kupata mavuno mazuri. Pia ridhiki

fulani ambalo lilikuwa linapelekwa mahali fulani hasa ndugu mara ridhiki ile ikakoma

itaonekana ni kisababishi cha kukoma kwa ridhiki hiyo.

4.3.1.2 Matukio Yaliyotokana na Mahali pa Kuzaliwa

Haya ni majina ambayo yalitolewa kwa waanzilishi wa koo kutokana na mahali

walipozaliwa. Sehemu hizo ni pamoja na zile zilizojumuisha maeneo mbalimbali

njiani na mashambani, mifano ya majina hayo imeonyeshwa kama ifuatavyo,

Jedwali Na. 4.6: Majina Yaliyotokana na Mahali pa Kuzaliwa

Na Jina Sababu za kiisimujamii

47 Mabala Alizaliwa sehemu isiyo na makazi

48 Malale Alizaliwa shambani

49 Mayila Alizaliwa barabarani/njiani

50 Malago Amezaliwa lakini baba yake hajulikani ni nani

51 Mapalala Alizaliwa kipindi mvua kubwa ilinyesha ambayo ilizoa takataka

52 Simenzi Alizaliwa safarini

53 Ng‘wandu Alizaliwa chini ya mbuyu

54 Matogoro Alizaliwa mashambani

55 Mhindi Alizaliwa jioni

56 Malambo Alizaliwa karibu na bwawa

57 Buhemba Mtoto aliyezaliwa kwa mganga wa jadi

58 Mahoja Hali ya mtu kutolewa mizimu

59 Bukombe Alizaliwa siku ambayo mahari inatolewa kwa mmoja katika

familia

Chanzo: Data za UwandaniM 2017

58

Haya ni majina ambayo yalitolewa kwa waanzilishi wa koo kutokana na mahali

walipozaliwa. Sehemu hizo ni pamoja na zile zilizojumuisha maeneo mbalimbali

njiani na mashambani, mifano ya majina hayo Ng‘wandu, Mayila, Mhindi, Giti,

Bukombe, Buhemba, Malambo.

Jina ―Ng‘wandu‘‘ linamaanisha mbuyu, kwa hiyo yule aliyezaliwa chini ya mbuyu,

ilipelekea kupewa jina la Ng‘wandu yaani mbuyu. Jina ―Mayila‖ linamaanisha

barabara au njia Yule aliyepewa jina hilo alizaliwa njiani, hivyo ilipelekea kuitwa jina

la Mayila. Jina ―Buhemba‘‘ ambalo hutokana na mtoto ambaye alizaliwa kwa mganga

wa kienyeji, yawezekana wazazi wa huyo mtoto aliyepewa hilo jina walichelewa

kuzaa hivyo iliwapelekea kwenda kwa mganga wa kienyeji na kupewa dawa hizo za

kiasili na kupata mtoto huyo na kupelekea kumwita mtoto waliyempata jina la

Buhemba.Jina ―Giti‖ lina maanisha giza, hili jina hupewa watoto ambao huzaliwa

kipindi cha giza totoro.Jina ―Mhindi‖ ambalo linamaanisha jioni,watoto ambao

huzaliwa kipindi cha jioni huitwa jina hilo la Mhindi.

4.3.1.3 Matukio Yanayotokana na Maradhi au Hali

Ni majina ambayo kutolewa kwake kuliambatana na maradhi au hali zilizojitokeza

kwa wazazi katika kipindi cha ujauzito.

Jedwali Na. 4.7: Majina Yanatokana na Maradhi/Hali

Na Jina Sababu za kiisimujamii.

60 Buhala ` Aliyezaliwa kama anakichaa

61 Bugonzwa Aliyezaliwa kipindi cha mlipuko wa magonjwa.

62 Lusalo Mama alipokuwa mjazito alipata kifafa

63 Masalago Mama alipokuwa mjamzito aliugua akapelekwa kwa

waganga wa kienyeji akachanjwa chale nyingi

64 Buhele Ni jina linalotokana na ugonjwa wa upele

Chanzo: Data za Uwandani, 2017

59

Majina haya mfano Buhala ni jina ambalo maana yake inajikita zaidi katika hali ya

ukichaa, mpewa jina anaweza kuwa kipindi mama yake mjamzito alikumbana na hali

kama hiyo, au tukio lolote lililofanyika wakati wa kuzaliwa kwake linaloendana na

ukichaa. Pia jina Lusalo maana yake ni ugonjwa anaweza akaupata mtu unaokuwa

kama kifafa, inawezekana kabisa mama alipokuwa mjamzito alipata kifafa cha

mimba, au tukio lolote lililofanywa na mtu mwenye hali ya ugonjwa huu wakati

anazaliwa.

Masalago ni jina pia ambalo mama anapokuwa mjamzito aliugua sana na kupelekwa

kwa waganga wa kienyeji, akachanjwa chale nyingi sana, japo ilimpelekea kupona. Ni

kama tukio lenye kumbukumbu kubwa kwa mzazi. Buhele ni ugonjwa wa upele,

ambapo anaweza kuwa mama alipata ugonjwa wa upele wakati ana mimba au mtoto

mwenyewe alizaliwa akiwa na ugonjwa wa upele.

4.3.1.4 Majina Yanayotokana na Vipindi vya Misimu

Haya ni majina ambayo yaliendana na misimu ya kuzaliwa kwa mtoto. Misimu hiyo

ilijumuisha mavuno, mvua, na hali ya maisha kwa ujumla, baadhi ya majina hayo ni

kama ifuatavyo:

Majina haya yanayotokana na misimu kwa maana ya hali fulani au wakati fulani

mtoto alipozaliwa, majina kama vile Mhindi, huashiria majira ya jioni, kwasababu za

kiisimujamii mtoto huyu atapewa jina hilo la Mhindi. Jina la Bujiku kwa maana ya

usiku, mtoto huyu amezaliwa usiku ni lazima awe wa jinsi ya kiume, japo watoto

wengi wanazaliwa usiku haina maana kwamba watoto wote watakaozaliwa usiku

wataitwa Bujiku, itategemea na mahitaji ya wazazi kumpa mtoto jina hili.

60

Jedwali Na. 4.8: Majina Yanayotokana na Misimu

Na Jina Sababu za kiisimujamii

65 Mhindi Alizaliwa kipindi cha jioni

66 Bujiku Alizaliwa usiku

67 Limi Alizaliwa mchana

68 Makingo Alizaliwa alfajili

69 Dilu Alizaliwa asubuhi

70 Malimi Alizaliwa mchana

71 Nzumbi Alizaliwa kipindi cha mvua zinazonyesha kwa muda

mrefu zenye manyunyu na hali ya kuwepo wingu zito

72 Mayala Alizaliwa kipindi cha njaa

73 Mabula Alizaliwa kipindi cha mvua

74 Nyanzala Alizaliwa kipindi cha njaa

75 Nungula Alizaliwa kipindi cha joto

76 Misoji Alizaliwa wakati wazazi wapo kwenye majonzi

77 Manumbu Alizaliwa wakati wa msimu wa viazi

Chanzo: Data za Uwandani, 2017

Jedwali Na. 4.9: Majina Yanayotokana na Misimu

78 Maliwa Alizaliwa wakati wa msimu wa uvunaji wa mihogo.

79 Mageni Alizaliwa wakati wa ujio wa wakoloni au mgeni alipokuja

nyumbani.

80 Mhangwa Alizaliwa na kutabiriwa maneno ya kimila ambayo kwa baadae

yatakuja kujidhihirisha kwa vitendo ambavyo binadamu huyo

atakuwa anavifanya katika kipindi chake cha maisha

81 Mpina Alizaliwa baadae wazazi wake wote wakafariki

82 Magembe Alizaliwa kipindi cha msimu wa kilimo

Chanzo: Data za Uwandani, 2017

61

Limi maana yake jua. Jina hili anapewa mtoto wa kike, hili jua inaweza kuwa mchana

ambapo jua linawaka sana. Hata kabla ya wazazi kuchagua jina la magharibi ama la

kidini kwa watoto wao, mwana huyo tayari huwa na jina. Majina kama Makingo,

Dilu, Nzumbi, Mayala, Mabula. Nyanzala na mengineyo yote hayo yanatolewa

kulingana na msimu uliopo.

4.3.1.5 Majina Yanayotokana na Matendo ya Watu

Ni majina ambayo yalitokana na matendo yaliyofanywa na waanzilishi wa koo husika.

Baadhi ya matendo hayo ni kama vile ukali, ubishi, uvivu, ni kama ifuatavyo:

Jedwali Na. 4.10: Majina Yanayotokana na Matendo ya Watu

Na Jina Sababu za kiisimujamii

83 Ntemi Inatokana na mtawala au kipindi cha utawala yaani mtemi

84 Nimi Inamaanisha mkulima.

85 Ngokolo Mtu mvivu.

86 Shimba Mtu jasiri kama samba

87 Madata Mtu mbishi, mtu anayetatanisha mambo.

88 Mayunga Ni mtu anaependa kuzurura.

89 Nele Ni mtu anaependa utani.

90 Ntagambi Ni mtu anaetafuta kwa bidii.

91 Shitwala Ni jina analopewa mtu mwenye mazoea ya kupeleka kitu

(taarifa) sehemu mbalmbali.

92 Kitwanga Hutokana na mhusika kuwa na tabia ya kutwanga.

93

Nsabi

Jina analopewa mtu kutokana na hali ya utajiri wake.

94 Nogu Jina analopewa mtu kwa maana ya utiifu wake wepesi wake

wa kukubali jambo fulani.

95 Nkwabi Mtu anaepewa jina kulingana na jitihada zake za utafutaji wa

kupata ridhiki

96 Ng‘wihambi Mtu mwenye juhudi ya kufanya vitu vikubwa hata kama hana

uwezo

97 Lukanyala Hali ya mimea kunyauka/ kusinyaa

98 Bukwimba Hali ya kuimba

99 Manyenye Mtoto aliezaliwa analialia sana

Chanzo: Data za Uwandani, 2017

62

Jedwali Na. 4.11: Majina Yanaytokana na Matendo ya Watu

100 Luchagula Anapenda kubaguabagua vitu

101 Lutinginya Hali ya kutikisa kitu au mtu

102 Ng‘winamila Mtu anayekaa anajiinamia kwa kufikiri mambo

103 Ng‘humbubanhu Mtu anayekuwa na hamu ya kuishi na watu wengi

Chanzo: Data za Uwandani, 2017

4.3.2 Majina ya Koo Yanayotokana na Sitiari za Wanyama na Ndege

Haya ni majina ambayo yalitolewa kulingana na sifa au tabia ya mhusika kufanana

na sifa au tabia za wanyama au ,ndege. Miongoni mwa tabia hizo ni pamoja na ukali,

ujeuri, ujanja, upole, rangi, maumbile, mfano wa majina hayo ni kama ifuatavyo:

Jedwali Na. 4.12: Majina ya Koo yaliyotokana na Tabia za Watu, Sitiari

Wanyama na Ndege

Na Jina Sababu za kiisimujamii

104 Mbiti Mtu anayefananishwa mlafi kama fisi

105 Shimba Jasiri kama samba

106 Shayayi Mjanja kama sungura

107 Ng‘ombeyapi Ni yule alizaliwa mnene.mweusi, wa kiume

108 Mbogo Kumaanisha mweusi anayefananishwa na mbogo/nyati

109 Susu Anafananishwa na kifaranga cha kuku

110 Nhelegani Ndege anayepiga kelele kama chiriku.

111 Dede Ndege mwenye umbo dogo

112 Nghumbi Mama yake alipenda kula panzi

Chanzo: Data za Uwandani, 2017

63

Jedwali Na. 4.13: Majina ya Koo Yaliyotokana na Tabia za Watu, Sitiari za

Wanyama na Ndege

113 Mhuli Alizaliwa kipindi tembo wanazagaa katika maeneo

waliyokuwepo

114 Sungwa Jina linalotokana na chungu mdudu

115 Manoni Alizaliwa kipindi cha uwindaji wa ndege mashambani

116 Mabuli Jina linalotokana na mnyama mbuzi

117 Maguku Jina linalotokana na mnyama nyani

118 Madulu Alizaliwa kipindi cha pundamilia wengi

119 Nghimbeji Jina analopewa mtu kutokana na nyoka

120 Sawaka Jina linalotokana na nyoka jamii ya chatu

121 Ng‘hoboko Jina linalotokana na nyoka aitwaye koboko

122 Ng‘hele Jina linalotokana na jamii ya njiwa

123 Mhela Mnyama wa porini yaani kifaru

124 Nhiga Jina linatokana na mnyama twiga

125 Manungu Jina linalotokana na nungunungu

126 Ngoko Jina linatokana na ndege kuku

127 Mbata Jina linatokana na ndege bata

128 Zizi/jiji Jina linalotokana na jamii ya ndege wadogowadogo

129 Madelo Alizaliwa kipindi cha samaki zilikuwa nyingi

130 Nyanzobe Mama wakati anaumwa uchungu alibebwa na Punda

Chanzo: Data za Uwandani, 2017

Jedwali Na. 4.14: Majina ya Koo Yaliyotokana na Tabia za Watu, Sitiari za

Wanyama na Ndege

131 Ngoso Mnyama aina ya panya

132 Bung‘ando Mnyama mjanja aitwae sungura

133 Ng‘hungulu Ndege aina ya kunguru

134 Mang‘ombe Jina linalotokana na mnyama aitwaye ng‘ombe

135 Nyamswa Jina lnatokana na mdudu aitwaye mchwa.

Chanzo: Data za Uwandani, 2017

64

4.3.3 Majina ya Koo Yaliyotokana na Shughuli, Ujuzi wa Kiufundi

Hapa ni majina ambayo sababu zake zilitokana na shughuli na ujuzi wa kiufundi

waliokuwa nao waanzilishi wa koo husika katika mazingira walioishi. Miongoni mwa

shughuli ni pamoja na ubebaji wa vitu na shughuli za ujenzi.

Jedwali Na. 4.15: Majina ya Koo Yaliyotokana na Shughuli za Kiufundi

Na Jina Saababu za kiisimujamii

136 Pima Fundi mpimaji wa nyumba

137 Nzengi Mjenzi wa nyumba

138 Chuma Mtu ambaye ana ujuzi wa kutengeza zana za chuma

139 Lugoye Ni zana ya inayotumika ktika ufundi iitwayo kamba

140 Majangito Alizaliwa kipindi mama yake anasomba fito wakati wa ujenzi

Chanzo: Data za Uwandani, 2017

4.3.4 Majina ya Koo Yaliyotokana na Vitu

Haya ni majina ambayo yalitolewa kulingana na vitu ambavyo vilikuwa vinapatikana

kwa wingi katika mazingira yaliyoizunguka jamii hiyo. Vitu ni pamoja na vile

vilivyokuwa vinatengenezwa na binadamu kama vile vyakula, vitu.

Jedwali Na. 4.16: Majina Yanayotokana na Hali ya Vitu

141 Masunga Inatokana na maziwa ya ng‘ombe yaliyomaliza kukamuliwa

142 Masuke Inatokana na maziwa ya mgando halafu yakachekechwa kutoa mafuta

143 Walwa Jina linalotokana na pombe

144 Lufungolo ufunguo wowote wa kufungulia

145 Lyochi Inatokana na moshi.

146 Gululi Amezaliwa kipindi cha ukungu

147 Nchilu Amezaliwa na tabia ya kulialia

148 Busungu Hali ya kupata maumivu makali, mfano uchungu wa kujifungua kwa mwanamke

149 Madirisha Dirisha.

150 Shilugula Mtoto wa mwanzo, yaani kifungua mimba.

151 Buyegi Furaha

152 Nghomba Uji.

153 Malongo Majina yanayotokana na udongo.

154 Shilatu Viatu

155 Maganga Mkojo wa ng‘ombe jike unaotumiwa na wafugaji wa ng‘ombe kusafishia vifaa

vyao

156 Mbasa Jina linalotokana na shoka

Chanzo: Data za Uwandani, 2017

65

Jedwali Na. 4.17: Majina Yanayotokana na Hali ya Vitu

157 Lushu Jina linalotokana na kisu

158 Cheyo Jina linalotokana na ufagio

159 Lushinge Jina linalotokana na sindano

160 Lugembe Jina linatokana na wembe

Chanzo: Data za Uwandani, 2017

4.3.5 Majina Yaliyotokana na Mimea

Ni majina yaliyohusiana na mimea ya aina tofauti iliyokuwa inapatikana katika

mazingira ya jamii husika. Mimea hii ni ile iliyozalisha mazao mbalimbali ya chakula

kama vile mlele, mtana na nafaka nyingine, majina hayo ni kama ifuatavyo:

Jedwali Na. 4.18: Majina Yaliyotokana na Mimea

Na Jina Sababu za kiisimujamii

161 Buluba Mmea yaani pamba.

162 Mchele Jina linalotokana na mpunga.

163 Busiga Jina linalotokana na zao la mtama.

164 Ndulu Jina linalotokana na zao la choroko.

165 Mashili Mimea jamii ya kunde.

166 Magaka Mimea inayotokana na alovera.

167 Bumela Mtama unaolowekwa ili uute kwaajili yakutengeneza

uji au pombe za asili.

168 Limbe Jina linalotokana na matango poli.

Chanzo: Data za Uwandani, 2017

66

Jedwali Na. 4.19: Majina Yanayotokana na Mimea

Na Jina Sababu za kiisimujamii

169 Nyamiji Jina linalo tokana na miti shamba

170 Boyo Nimiti jamii ya mwarobaini

171 Mahushi Ni aina ya miti ambayo hujiotesha bila kupandwa na

baadae kuwa misitu, mtoto hupewa hili kwa maana

atakuwa msaada wa familia

172 Salyungu Tunda litokanalo na jamii ya majani ya maboga

173 Malendi Linatokana na mbogamboga za majani

174 Twege Mlenda

175 Matanga Tunda jamii ya maboga

176 Manala Miti ijulikanayo kama mnyaa

177 Migu Mti wenye jamii ya miiba

178 Manyanya Jina linalotakana na nyanya

179 Shitungulu Jina linalotokana na kitunguu

180 Mponda Miti inayoota porini

181 Bunani Linatokana na mbogamboga za majani

Chanzo: Data za Uwandani, 2017

4.3.6 Majina Yaliyotofautisha Jinsi

Majina yalitolewa kutokana na kutofautisha jinsi, majina haya yalikuwa yanafanana

kimaana lakini ni silabi moja au mbili ambazo zinatofautisha kati ya jina lipi

litatumika katika jinsi ya mwanamke na jina lipi litatumika katika jinsi ya mwanaume.

Majina mengine yanatofautiana kwa fonimu moja, Fonimu hiyo inatofautisha jina lipi

ni la mwanaume au jina lipi ni la mwanamke.

67

Wakati mwingine mofimu kapa inarejelea kutofautisha jinsi, Udogo wa jina, Ukubwa

wa jina, ni sehemu ya kutofautisha jinsi kwenye majina ya koo za kisukuma.

Jedwali Na. 4.20: Majina Yanayotofautisha Jinsi

Na Jina Jinsi Sababu za kiisimujamii.

182 Kabula KE Alizawa kipindi cha mvua.

183 Mabula ME Alizaliwa kipindi cha mvua.

184 Limi KE Alizaliwa kipindi cha jua

185 Malimi ME Alizawa kipndi cha jua

186 Nyanzala KE Alizaliwa kipindi cha njaa

187 Mayala ME Alizaliwa kipindi cha njaa

188 Nyanjige KE Alizaliwa kipindi cha nzige wengi

189 Maige ME Alizaliwa kipindi cha nzige wengi

190 Kalekwa KE Mtoto aliyefiwa na mzazi wake baada ya

kuzaliwa

191 Mlekwa ME Mtoto aliye fiwa na mzazi wake baada ya

kuzaliwa

192 Kahabi KE Ni mtoto anayezaliwa katika hali duni ya

maisha

193 Ng‘habi ME Ni mtoto aliyezaliwa katika hali duni ya maisha.

194 Luja KE Aliyezaliwa kabla yake alifariki

195 Luja ME Aliyezaliwa kabla yake alifariki

196 Mageni KE Alizaliwa wakati wa ujio wa wakoloni

197 Mageni ME Alizaliwa wakati wa ujio wa wakoloni

Chanzo: Data za Uwandani, 2017

4.3.7 Majina Yanayotokana Baada ya Kuzaliwa Watoto Mapacha

Majina haya yalitolewa na waanzilishi namna ambavyo watoto mapacha ambao ni

Kulwa na Doto wamezaliwa, wataofuata baada ya mapacha hao kuna majina maalumu

wanapewa, ni kama fuatavyo:

68

Jedwali Na. 4.21: Majina Yanayotokana Baada ya Kuzaliwa Watoto Mapacha

Na Jina Sababu za kiisimujamii

198 Shija Alizaliwa baada ya kuzaliwa mapacha wawili

199 Mhoja Aliyezaliwa baada ya kuzaliwa Shija

200 Kamuli Alizaliwa baada ya kuzaliwa Mhoja

201 Kasanda Alizaliwa baada ya kuzaliwa Kamuli

Chanzo: Data za Uwandani, 2017

Anaweza kupata ujauzito bali itategemea na asili yake. Imani za kale kuhusu ujauzito.

Baadhi ya mila na desturi. Hasa katika nchi za kiafrika zinaamini kwamba mwanamke

kupata Wasukuma wanaeleza jinsi ya uzaliwaji wa watoto mapacha, mwanamke

yeyote watoto mapacha kunatokana na urithi wa kizazi chake, kuanzia mababu wa

upande mmoja kati ya wanandoa hivyo uzao huo hufuata mkondo kwa miaka na

miaka. Wengi wakipata mapacha huulizwa kama kwenye kizazi chake kuna watoto

mapacha. Akitokea mama akasema hakuna, basi huaminika kwamba lazima upande

wa mwanaume kuna waliowahi kuzaliwa mapacha.

Mwanamke yeyote anaweza kupata ujauzito wenye watoto mapacha hata kama si asili

ya ukoo wake. Wanawake wanaoongoza kwa kushika mimba za mapacha ni wale

ambao wakati wa kulala wanabadili staili mara kwa mara. Mara nyingi inashauriwa

kuwa, mwanamke akishaingia kwenye siku zake za hatari kulingana na mzunguko

wake wa hedhi akutane kimwili na mumewe au mwanaume anayetaka kuzaa naye.

Baada ya tendo la ndoa mwanamke anshauriwa kulala kwa kijigeuzageuza kitandani.

Ikiwa ina maana akiwaa amelala ajigeuze kuangalia juu, kulala kifudifudi kwa usiku

kucha. Mwanamke akifanya hivyo Kwa kijirudiarudia siku kadhaa katika kipindi

hicho cha hatari, hapo uwezekano wa kushika mimba ya mapacha utakuwa mkubwa

sana. Majina haya kutokea kwa watoto mapacha kwa maana ya Doto na Kulwa

69

wakifuatiwa na Shija, Kamuli, Mhoja, na Kasanda. Shija kwa maana ya kubaki

kwamba amebakizwa na watoto mapacha.

4.3.8 Majina Yanayotokana na Chimbuko la Ukoo

Wasukuma inasemekana walikuwa Kongo, wanaume waliuwawa wakabaki

wanawake, wanawake waliulizwa ni kabila gani walisema ni wasukuma, majina yao

yalikuwa kama vile minza, nchama, Nselema, Mwashi, Nkamba, Nkwimba, Ngolo,

Niga. Wanaume walikwisha walibaki wachache ambao hawakutosheleza kuwaoa

wanawake, hivyo ilikuwa akipatikana mmoja anazalisha wanawake kumi au zaidi,

watoto watakaozaliwa watajitambulisha kwa jina na mama, hili linajidhihirisha zaidi

kwenye salamu wanavyouliza‖ Lwembo‖ kwa maana ya chimbuko mama yake

aliitwa nani.

Jedwali Na. 4.22: Majina Yanayotokana na Chimbuko la Koo

Na Jina Sababu za kiisimu jamii

202 Minza Ukoo wa mwanamke aliyeitwa Minza

203 Nchama Ukoo wa Mwanamke aliyeitwa Nchama

205 Nselema Ukoo wa mwanamke aliyeitwa Nselema

206 Ng‘washi Ukoo wa mwanamke aliyeitwa Ng‘washi

207 Nkamba Ukoo wa mwanamke aliyeitwa Nkamba

208 Mhongu Ukoo wa mwanamke aliyeitwa Mhongu

209 Nkwimba Ukoo wa Mwanamke aliyeitwa Nkwimba

210 Ngolo Ukoo wamwanamke aliyeitwa Ngolo

211 Mumba Ukoo mwanamke aliyeitwa Mumba

212 Ng‘wela Ukoo wa mwanamke aliyeitwa Ng‘wela

213 Balega Ukoo wa wasukuma waliotokea Uganda

214 Nseka Ukoo wa mwanamke aliyeitwa Nseka

215 Nkela Ukoo wa mwanamke aliyeitwa Nkela

216 Nkwaya Ukoo wa mwanamke aliyeitwa Nkwaya

Chanzo: Data za Uwandani, 2017

70

Katika majina yanayotokana na chimbuko la ukoo haya majina yanatumika sana kwa

salamu, Wasukuma wanapokutana na kuanza kusalimiana kama hawajawahi kuonana

lazima waulizane LWEMBO kwa maana ya chimbuko lake au asili yake ni nani,

majina kama haya Nkwimba, Minza, Ngolo, Nega, Minza, Nchama, Nselema,

Ng‘washi, Nhongu, Nkwaya, Nkela, Nseka, Ng‘wela na Mumba na huu lwembo

ataulizwa aliye mkubwa kati ya wale wanaosalimiana, kwa maana ya umri yeye

atasema kuwa ni nani, kama Nkwimba basi atasalimiwa kwa salamu ya Nkwimba,

naye pia atauliza kwa Yule anayemsalimu jina la babu au bibi ni nani, hauwezi

ukakuta LWEMBO (chimbuko) linataja jina la mwanaume, majina yote yanayotaja

lwembo ni ya wanawake tu.

4.3.9 Majina yanayotokana na Jina la Mungu

Majina haya yalitolewa na wazazi kulingana na kutambua uwepo wa Mungu.

Jedwali Na. 4.23: Majina Yanayotokana na MUNGU

Na Jina Sababu ya kisimujamii

217 Sebha Jina la Mungu

218 Welelo Jina la Mungu

Chanzo: Data za Uwandani, 2017

Wasukuma si watu wa kitabu kama waisraeli au waislamu na wakristu, hawakupewa

ufunuo wa pekee wa kinywa cha manabii, sawa kama wanadamu wote, wametumia

majina mengi kadri ya madhanio ya kufikiria kwa wazee juu ya ; ―Uyu‖ ,

―Ng‘wenikili‖ asiyeonekana. Siri ya Mungu inagunduliwa katika ufahamu dhaifu wa

71

mwanadamu, akitofautishwa sana na viumbe. Tena majina mengi wanayotumia

kumhusu Mungu yana kiini chao katika ―viumbe‖ vikubwa mno vinavyoonekana.

Lakini visivyoweza kuchukuliwa wala kutengenezwa wala kuigwa na mikono ya

watu. Majina haya ni kama ―ishara‖ kuu ya ukubwa wa Mungu

Wasukuma wanatumia zaidi majina ya Mungu hasa kama haya: WELELO,

LIWELELO, LIMI, majina haya yanamtaja Mungu katika picha ya ajabu ya viumbe

vyake vikubwa mno yasiyoweza kufinyangwa na mkono wa mtu. Msukuma asiye

Mwisrael anamgundua Mungu katika sura yake ya MUUMBA tu, anamfahamu katika

mifano inayoonekana ya viumbe vyake. Lakini ufahamu huo ingawa ni fupi na wa

msingi tu, unafanana na ufahamu wa kipofu atafutaye kupapasa-paasa, si ujinga, si

upagani hata kidogo, ufahamu huo si wa kubomolewa , ni wa kuchunguza. Si

ufahamu wa neno la Bwana Mwenyewe, ila ni ufahamu wa neno lisilotamkwa kwa

‗misemo‘.

4.3.10 Hitimisho

Majina ya koo za kisukuma yanabeba maana zinazotokana na viumbe, maeneo ya

makazi.tabia za watu na vitu vilivyokuwa vikipatikana na mazingira ya jamii husika.

Pia majina mengine yanadhihirisha kwamba zipo sababu za kiisimujamii katika utoaji

wa majina ya koo za kisukuma.

72

SURA YA TANO

MUHTASARI HITIMISHO NA MAPENDEKEZO

5.1 Utangulizi

Sura hii inatoa muhtasari, hitimisho la matokeo ya utafiti na mapendekezo dhidi ya

tafiti zinazoweza kufanywa hapo baadaye katika lugha ya kisukuma. Utafiti huu

ulijikita katika kufafanua jinsi majina ya koo za kisukuma yanavyotofautisha jinsi ya

wanajamii, kuchambua nyanja za kiisimujamii ambazo zinasababisha kutumia majina

ya koo za kisukuma na kubaini athari ambazo zinaweza kujitokeza katika majina koo

za kisukuma. Sura hii imegawanyika katika sehemu nne. Sehemu ya kwanza ni

utangulizi, sehemu ya pili inaeleza kwa ufupi muhtasari wa kila sura, sehemu ya tatu

inaeleza hitimisho la matokeo ya utafiti, kwa kuhusianisha malengo ya utafiti na

maswalj ya utafiti. Sehemu ya nne inatoa mapendekezo dhidi ya vipengele ambavyo

pia ni muhimu kufanyiwa utafiti zaidi katika lugha ya kisukuma.

5.2 Muhtasari wa Utafiti

Utafiti huu ulilenga kuchunguza majina ya koo ya kisukuma. Lengo kuu la utafiti huu

lilikuwa ni uchambuzi wa kiisimujamii katika majina ya koo za kisukuma. Utafiti huu

una sura tano kama zinavyoelezwa, kwa muhtasari, sura ya kwanza katika utafiti

imehusisha vipengele mbalimbali ambavyo ni utangulizi, usuli wa lugha ya kisukuma,

mfumo wa jamii ya kisukuma, shughuli za kiuchumi katika jamii ya kisukuma, usuli

wa tatizo, tatizo la utafiti, malengo ya utafiti, maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti,

hitimisho. Sura ya pili inahusu mapitio ya kazi tangulizi ambayo pia yamekuwa

msaada kwa upande wa mtafiti katika kujua ni kitu gani ambacho kimefanyiwa katika

eneo hili. Maandiko yaliyotumika katika utafiti huu yamepangwa kwa kuzingatia

73

dhana za msingi zilizojibainisha katika mada ya utafiti utangulizi, dhana ya maana,

dhana ya isimujamii, dhana ya majina kwa ujumla, sura hii imebainisha nadharia ya

utafiti, sababu za kiisimujamii za majina ya koo ya kisukuma, mkabala wa nadharia,

kiunzi cha dhana, na hitimisho.

Sura ya tatu inahusu mbinu za utafiti sura hii imeanza na Utangulizi muundo wa

utafiti, eneo la utafiti, mbinu za utafiti , mbinu za ukusanyaji data, kundi lengwa,

sampuli, mikabala ya ukusanyaji data, maadili ya utafiti, mipaka ya utafiti ,hitimisho.

Sura ya nne inahusu uwasilishaji na uchambuzi wa matokeo ya utafiti. Sura hii pia

imeanza na utangulizi, nyanja zinazosababisha majina ya koo za kisukuma ambazo ni

mgawanyo wa majina kwa kigezo cha kisemantiki na kigezo cha kiisimujamii, majina

yanayotofautisha jinsi na athari zinajitokeza kutopewa majina ya koo za kisukuma na

hitimisho. Kadhalika sura ya tano inajadili kwa muhtasari yaliyozungumziwa katika

kila sura. Sura imeanza na utangulizi, muhtasari wa utafiti, ,muhtasari wa matokeo ya

utafiti, majina ya koo yanavyotofautisha jinsi, nyanja zinazosababisha kutumia

majina koo, athari zinazojitokeza kutopewa majina ya koo. Mapendekezo, tafiti

fuatishi, hitimisho.

5.3 Muhtasari wa Matokeo ya Utafiti

Umehusu majina ya koo yanayotofautisha jinsi, nyanja zinazosababisha kutumia

majina ya koo, na athari zinazojitokeza katika kutopewa majina ya koo.

5.3.1 Majina ya Koo Yanayotofautisha Jinsi

Utafiti huu lengo lake la kwanza lilikuwa kufafanua jnsi majina ya koo za kisukuma

yanavyotofautisha jinsi ya wanajamii. Majina yaliyotoka uwandani yanayotofautisha

74

jinsi yalikuwa yanafanana kimaana. Tofauti imejibainisha kutofautiana kwa fonimu,

au silabi moja, au ukubwa, au udogoshaji wa kitu au Mtu, umoja na wingi wa majina.

Utofauti wa fonimu kwa mfano, jina Kabula na Mabula majina haya yanatofautishwa

na /k/ na /m/, ambapo /k/ inatumika kwa jinsi ya mwanamke na /m/ inatumka kwa

jinsi ya mwanaume , ilihali majina haya yana maana ya mvua, pamoja na utofauti wa

fonimu pia kuna utofauti wa ukubwa wa mvua ambao ni (Mabula) na udogo wa mvua

ambao ni (Kabula). Mfano wa majina mengine Mlekwa na Kalekwa maana ya majina

haya ni moja kwa maana ya mtoto aliyefiwa na wazazi wake baada ya kuzaliwa, silabi

m- kwa mwanaume na ka- kwa mwanamke. Utofauti wa umoja na wingi,

umeonekana katika majina kama vile Malimi na Limi, maana ya majina haya ni moja

kwa maana ya Jua, kinachotofautisha ni (Ma-) inawakilisha wingi, linatumika kwa

jinsi ya Mwanaume na Limi (jina lipo kwenye umoja) ambalo linatumika kwa jnsi ya

mwanamke. Vilevile imejidhihirisha baadhi ya majina ya koo hayatofautishi jinsi,

yanatumika kwa jinsi zote mfano wa majina, Mageni, na Luja.

5.3.2 Nyanja Zinazosababisha Kutumia Majina ya Koo

Katika utafiti huu lengo mahsusi la kuchambua nyanja za kiisimujamii ambazo

zinasababisha kutumia majina ya koo za kisukuma, nyanja zimejidhihirisha katika

mgawanyo wa majina kwa kigezo cha kisemantiki na mgawanyo wa majina katika

kigezo cha kiisimujamii.

Katika kigezo cha kisemantiki, katika koo za kisukuma majina yanabeba maana

ambazo zinafahamika na kueleweka vyema kwa wahusika, kwa mfano majina ya koo

yanayotokana na mwonekano wa maumbile, kiuhalisia majina haya yanahusisha

viungo mbalimbali vya mwili wa binadamu mfano wa wa majina Nkonoki maana

75

yake mkono gani, Nkono-maana yake mkono na Ki maana yake gani, Majina kama

Kundi, Mato, Shonongo, Mwanzalima, na Mazala, majina haya yote yanatokana na

mwonekano wa maumbile ya mtu.

Pia majina mengine yenye kigezo cha kisemantiki ni yale yanayotokana na makazi

kama vile, Nyanza, Ngasamo, Mongo, na Nsembi yamebainishwa na watafitiwa.

Maana za majina haya zinatokana na makazi husika, hivyo kuwaezesha wanajamii

kuelewa maana za majina hayo. Majina mengine ni yale yanatokana na maana ya vitu

kama vile Luhungo, Nshelo, Shitambala, Madirisha, Mashini, maana za majina haya

ni za vitu.

Nyanja ya kiisimujamii imeonekana kuchambuliwa data Kwa makundi tofauti

kulingana na vigezo na sifa zilifanana kiisimu. Kama vile matukio, majina

yanayotokana na mahali pa kuzaliwa mtoto, majina yanayotokana na wakati wa

kuzaliwa kwa mtoto na baada ya kuzaliwa, majina yanayotolewa baada ya kuzaliwa

watoto mapacha. Majina yanayotokana na chimbuko la koo, majina yanayotokana na

mimea, majina yanayotokana na maradhi, majina yanayotokana na matendo ya watu.

5.3.3 Athari Zinazojitokeza Katika Kutopewa Majina ya Koo za Kisukuma

Utafiti huu umebaini athari ambazo zinaweza kujitokeza katika kutopewa majina ya

koo za kisukuma kama ifuatavyo, mtoto atakapozaliwa anaweza kuwa analialia sana

mkadhani mgonjwa lakini sivyo, anaweza kupelekwa hospitali lakini hanyamazi kulia

mpaka apewe jina analohitaji, kupoteza kumbukumbu za matukio muhimu, kupoteza

utambulisho wa ukoo, kupotea kwa koo za kisukuma, mtoto anaweza kuwa bubu au

kiziwi ama utaahira. Kwa mtu mzima kuzibiwa ridhiki za maisha, kutodumu katika

76

kazi na migogoro katika ndoa na hata ugumba. Mikosi mikubwa ya kusingiziwa wizi,

kupelekea kufungwa jela.

Majina ya koo za kisukuma wanayopewa watoto mara zote ni ya babu au bibi,

wanaweza kuwa hai au alishafariki. Hivyo baadhi ya majina ya koo akipewa mtoto

yanaathiri tabia alizokuwa nazo mwenye jina, kama alikuwa mchoyo, Mrafi, mkali,

mvivu, mchapakazi, tajiri, aliyependa kuoa wanawake wengi, jasiri, mkimya,

mvumilivu na tabia nyingine zote yanaathiri mwenendo mzima na tabia ya mtoto

atakayepewa jina ,uwezekano wa kuwa na tabia ilele ya mtangulizi wake ni mkubwa.

Wakati mwingine jamii inaweza kushangaa sana na kukuuliza umekosa jina la kumpa

mtoto, ukimpa mtoto jina la mtu aliyekuwa katili, jambazi, mvivu au tabia nyingine

ambazo si rafiki katika jamii.

5.4 Hitimisho

Utafiti huu ulikusudia kuchambua majina ya koo za Kisukuma kiisimujamii. Utafiti

uliongozwa na nadharia ya makutano na mwachano ya Giles ya mwaka 1982.

Nadharia hii imetumika Kama mwega katika uchanganuzi wa data ya utafiti

iliyokusanywa kutoka uwandani, kwani ilisaidia kuonesha mazingira ya makutano na

mwachano. Kati ya lugha kisukuma na lugha nyingine, hususani katika uchambuzi

kiisimujamii katika majina ya koo.

Mazingira ya makutano yamejibainisha Kwa baadhi ya makundi ya majina kwa

mfano, majina ya tabia za watu, majina yaliyotokana ujuzi au shughuli, majina

yaliyotokana na matukio mbalimbali na majina yaliyotokana na mimea. Makundi haya

pia yanajibainisha katika jamiilugha nyingine kwa mfano Wahaya. Vilevile katika

77

jamii ya wasukuma yapo mazingira ya mwachano kwani upo upekee unaojitokeza

hususani katika majina ya koo. Kwa mfano majina Kama vile Masanja, Shija,

Maganga, ni miongoni mwa majina ya koo ambayo ni ya kipekee kwani hayapatikani

katika koo za jamiilugha nyingine.

Kwa kurejea lengo mahsusi la kwanza kuelezea sababu za kiisimujamii ambazo

hutumika kutumia majina ya koo za kisukuma, sababu anuwai kwa mfano matukio

yaliyojitokeza katika jamii, tabia za watu, hali zilizokuwepo miongoni mwa watu,

shughuli mbalimbali za kijamii na uchumi.

Kwa kurejea lengo mahsusi la pili kwamba kuchambua jinsi majina ya kisukuma

yanavyotofautisha jinsi za wanajamii imejidhihirisha kwamba, katika jamii ya

Wasukuma kuna majina yanayofanana kimaana, lakini kuna utofauti wa fonimu moja

au mbili ambazo zinaweza kubainisha kwamba jina hili linatumika kwa jinsi ya kike

au jinsi ya kiume kwa mfano jina Kabula kwa jinsi ya kike na Mabula kwa jinsi ya

kiume, hapo fonimu /k/ na /m/ zimetofautisha jinsi.

5.5 Mapendekezo

Katika utafiti huu mtafiti amegundua vitu vilivyopelea, kutopata data nyingi kwa

sababu ya mwingiliano wa tamaduni, na hata kutoa data zenye mwingiliano wa

tamaduni, wadau kama vile wanataaluma wa isimu, watafiti wa masuala ya isimu

wafanye tafiti nyingi ili kuwepo na kumbukumbu za majina ya koo mbalimbali.

5.6 Tafiti Fuatishi

Imekuwa vigumu kuweza kushughulikia kila kitu kilichohusiana na majina katika

jamii ya wasukuma. Vipo vipengele vingine vya kiisimu ambavyo vipo nje ya

78

mawanda ya utafiti huu ambavyo pia havina budi kufanyiwa uchunguzi, kuna haja ya

utafiti zaidi kuhusiana na maeneo katika jamii ya wasukuma, majina ya wakuu wa koo

katika jamii ya Wasukuma, na majina mengine ya watu yasiyokuwa ya koo za

kisukuma. Tafiti nyingine zinaweza kufanywa kuhusiana na majina mbalimbali ya

vitu vya asili mfano mito, maziwa na milima.

Vipo vipengele vingine kiisimu ambavyo vipo nje ya mawanda ya utafiti huu

ambavyo pia havina budi kufanyiwa uchunguzi. Vile vile tafiti nyingine zinaweza

kufanywa kuhusiana na vipengele vingine vya kiisimu katika lugha ya kisukuma, kwa

mfano fonolojia ya lugha ya kisukuma, mofolojia ya lugha ya kisukuma, na vipengele

mbalimbali vya kisintaksia katika lugha ya kisukuma. Vipengele hivi vikifanyiwa

utafiti wa kina vitaweza kutoa mchango katika kubainisha lugha ya kisukuma.

79

MAREJEO

Agbedor, P. (1001), ―What is in a name‖. Working Papers of the Linguistic Circle of

the. University of Victoria. Ghanaian personal names as information sources.

Accra, Ghana.

Aguedze, I. D. O. (1990) The Principle Underlying the African Religion and

Philosophy. Nairobi. Maillu Publishing House.

Ash, A (2003), (forthcoming), place names in Yuwaalaraay, Yuwaaliyaay and

Gamilaraay Languages of North west New South Wales. Sydney, Australia.

Babble, E. (2005). The Basics of Social Research Third Edition. Toronto: Thomson

Leaning Inc

Bakiza, (2010), Kamusi ya Kiswahili Fasaha, Nairobi: Oxford University Press.

Baitan, B. (2010), Amorpho-semantic Analysis of Ruhaya Person Names

(Unpublished), M.A (linguistics) Dissertation, University of Dar es salaam,

Tanzania.

Bariki, I. (2009). Translating the African Names in Fiction. International Journal of

Current Research in the Humanities, 3(1), 45 – 51.

Bright, W. (1966) Proceedings of the UCLAS Sociolinguistics conference, The

Hague. Retrieved on 21st May, 2017 from: https://www.merriam-webster.

com/dictionary/mouton.

Byrnes, G. (2002), ―A dead sheet covered with meaningless words?‖ Place names and

the Cultural colonization of Tauranga‘, New Zealand Journal of History,

36(1), 18–35

80

Buberwa, A (2010). Investigating sociolinguistic aspects of place names in Ruhaya in

North-Western Tanzania (Unpublished) M.A Dissertation, University of Dar

es salaam, Tanzania.

Cameron, K (1961). English Place Names. London, Batsford

Chambers, J. K. (1995). Sociolinguistics theory: Oxford: Blackwell Publishers

Dijk, T. A (1996). ―Dicourse, power, and Access‖, In Caldaf, R.C and coulthard,

M(eds), Texs and Practices: Reading in critical Discourse Analysis, London,

Routledge.

Dijk, T. A. (2001). “Critical Discouse Analysis”, in Tannen, D. Schiffrin, D and

Hamilton, H (eds). Handbook of Discourse Analysis. Oxford: Blackwell.

Guthrie, M (1948). The classification of Bantu Language, London, Oxford University

Press.

Guthrie, M. (1971). Comparative Bantu, farn borough, New York: Gregg

International Publishers.

Giles, H., and Byrne, J. L (1982), ‖An intergroup Approach to Second Language

Acquasition,‖ Journal of Multilingual and Multicultural Development 3(17)-

40 – 57.

Gray, T. M. (1999). what’s in a name? Some Reflections on the Sociology Anonymity.

New York: Ecco Press.

Hanks, P. (1990). A Dictionary of First Names. New York: Oxford University Press.

Hymes, D. H (1964). Language in Culture and Society, Califonia, University Press.

Hymes, D. (1972). ―Models of Interraction of Language and Social Life‖, in

Gumperz, J and Hymes, D (eds), Directions in Sociolinguistic: The

Ethnography of Communication, New York, Holt, Rinehart and Wiston, Inc.

81

Hymes, D. (1974). Foundation of Sociolinguistics: An ethnographic approach.

Philadelphia: A University of Pennsylvania Press

Hudson, R. A. (1985). Socialinguistics, Cambridge: University of Pennsylvania Press.

Isabiriye, S (2000). Tradition African Names. Retrieved on 16th

May 2016 from:

.http;//wwwnamesite.com/.

Kadmod, N. (2000). Toponymy, The Role, Laws and Language of Geographica

Names. New York: Vantage press.

Kalkanova, T (1999). ―Sociology of Proper Names in Sophia since (1970)

International Journal of the usociology of Language, 135(3), 83-98.

Kapinga, M. C. (1983). SarufiMaumbo ya Kiswahili Sanifu. Dar es Salaam: TUKI

Kihore, Y. M. na Chuwa, R. (2004). Kiswahili katika karne ya ishirini na moja. Dar

es Salaam: TUKI.

King‘ei, K., na Kisovi, C. N. M. (2005). Msingi wa fasihi simulizi. Nairobi: Literature

Bureau.

Kilaini, M. (1990). The Catholic Evangelization of Kagera in North-West Tanzania

Unpublished Ph D thesis, Pontificia Universitas Greoriana, Roma, Italy.

Kothari, C. R. (1990). Research Methodology, Methods and Techniques. New Delhi:

Willey Eastern Limited

Kothari, C. R. (2004). Research Methodology, Methods and Techniques, Second

Edition. New Delhi: New Age International (p) Ltd.

Koul, R. K. (1984). Sociology of Names and Nicknames of India with Special

References to Kashmir, Kashmir: Utpal Publications.

Latham, E. (1904), A Dictionary of Names, Nicknames and Surnames of Persons,

Places and Things. London: Gale Research Company.

82

Legere, K. (2009). Plant Names in the Tanzanian Bantu Language Vidunda. Structure

(some) Etymology in selected proceedings of the 38 Annual conferences

African Linguistics. Arusha, Tanzania.

Lyons, J. (1984). Language and Linguistics, An Introduction. Cambrige: Cambridge

University Press.

Mandende, J. O. M. (2006). ONOMASTICS; Analyisis of the Semantics of

Morphologically, Derived luloogoli personal Names‖ Haikuchapishwa.

Tasnifu kwa ajili ya Shahada ya uzamili katika chuo Kikuu cha Kenyata.

Nairobi, Kenya.

Malande, J. O. M. (2011). what is in a name? Analysis of the semantics of Luoogoli

personal names. New York: Pantheon.

Manyasa, J. (2009). Investigating the Basis of Naming People in Kisukuma

(unpulished), M.A Disertation, University of Dar es salaam, Tanzania.

Massamba, D. P. B. (2004). Kamusi ya Isimu Na falsafa ya lugha. Dar es Salaam:

Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.

Massamba, D. P. B. (2009). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar es Salaam:

TUKI.

Matinde, R. S. (2014). Dafina ya lugha; Isimu na Nadharia, Sekondari, Vyuo vya kati

na Vyuo Vikuu. Mwanza: Serengeti Educationa Publishers (T) Ltd

Mbiti, J. S. (2003). Introduction to Africa Religion. Dar es Salaam: East African

Educational Publishers Ltd.

McBurney, D. H. (2007). Reseach Methods (seventh edition). New York, Thomson

Wadsworth.

Miruka, O. (2003). Studying Oral Literature. Nairobi: Acacia Publishers.

83

Msanjila, Y. P. (2009). Isimujamii, Sekondari na vyuo, Dar es Salaam: TUKI.

Mradi wa lugha za Tanzania, (2009). Atlas ya lugha za Tanzania, Dar es Salaam: Dar

es Salaam University Press.

Msanjila, Y. P. (2006). Nadharia katika Isimujamii, Mjadala unaendelea‖, In Mulika,

27(2), .40-48.

Mulokozi, M. (2005). Miaka 75 ya Taasisi ya Uchunguzi (1930-2005), katika

Madumula J na Kihore,Y (wah) Jarida la taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili,

Dar es Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili

Mutembei, A. K. (2009). UKIMWI katika Fasihi ya Kiswahili 1986-2006, Dar es

Salaam, TUKI.

Muzale, H. R. T. (1998). ‖Linguistic and socio-cultural Aspects of Intarlacustrine

Bantu Namess‖ Journal of the institute of Kiswahili Research, 61(3), 28-49

Muzere, J. (2000). African personal Names, The Great Lakes Areas, Lantham MD:

Scare Crow Press

Ogden, C. K., and Richard, I. R. (1966). Meaning of Meaning, London: Routledge and

Kegan Paul LTD.

Omari, C. K. (1970). ―Person Names in Socio Culture Context‖, University of Dar es

salaam. Journal of the Institutes of Swahili Research, 40(2), 35 – 51.

Palmar, F. (1981). Affecting the Act of Name giving Iran Microthink Institute.Tasnifu

katika Shahada Ya Uzamili katika chuo kikuu cha Isfahani. Imechapishwa.

New York: Cambridge University Press.

Rasekh , A. E. and Ahmadvand, M. (2012). What is in a Name? Berkeley, Ca.:

University of California Press.

84

Rayburn, A. (2010). Place names –The Canadian Encyclopedia-Historical Dominion.

Retrieved on 21st May 2016 from: www.thecanadianencyclopedia.ca/en/

article/dominion.

Reed, A. W. (1975). Place Names of New Zealand. Wellington: New Zealand

University Press.

Resani, M. (2014). Semantiki na Pragmatiki ya Kiswahili. Dar-es-salaam: Karijamer.

Print Technology.

Roden, D. (1974). Some Geographical Implication from the study of Ugandan Places-

Names. East African Geographical Review, 12(4), 77-86.

Romaine, S. (2000). Language in society, an introduction to sociolinguistics. London:

Oxford University Press.

Rubanza, Y.I (2000) The Linguistic creativity of Haya personal Names, Journal of

Institute of Kiswahili Research Volume No.63

Rugemalira, J.M (2005), A Grammar of Runyambo, Language project of Tanzania.

Dar es Salaam: University of Dar es Salaam.

Rye, J. (2006). A Popular Guide to Norkfolk Place names. Guist Bottom: Larks Press.

Salapion, D. (2011). Haja ya kuunda kamusi ya Majina ya Watu ya Asili, Majina ya

watu katika Jamii ya Wahaya, Tasnifu ya M, A, Chuo kikuu cha Dar es

Salaam, (haijachapishwa).

Schotsman, P. (2003). Place names and History in Dar es Salaam, Amsterdam:

Leiden University.

Shillington, K. (1995). History of Africa. London: Macmllan Education Ltd.

Sitati, V. W. (2007) Comprehensive Names Dictionary. Nairobi: Sas Enterprise.

85

Tabouret-keller, R. $., and Le Page, A. (1986). The Mother tongue metaphor. Grazer

linguistics studies” New York: Appleton-Century-Crofts.

Tajfel, H. (1982). Human Group and social categories. Cambridge: Cambridge

University Press.

Trudgill, P. (1983). Sociolinguistics, An introduction to Language and Society,

London: Penguin.

TUKI, (1990). Kamusi ya Ismu na Lugha. Dar es salaam: Oxford University Press.

TUKI, (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Dar es Salaam: East Africa Publications.

United Bible Societies (UBS), (1977). Agano la kale na Agano jipya (The old

testament and the New Testament) in Swahili Dodoma, The Bible Society of

Tanzania, Dar es Salaam, Tanzania.

Wardhaugh, R. (1986). An introduction to Socio-linguistics. Oxford: Basil Blackwell.

86

VIAMBATISHO

Kiambatisho I: Hojaji kwa watafitiwa

1) (a) Je una umri gani?-------------

(b) Jinsi -------------------------------------

(c) Unafanya kazi gani? -------------------

(d) Ulizaliwa wapi? ------------------------------

(e) Lugha yako ya kwanza ni ipi? ----------------

2) Taja majina matano ya ukoo yanayokubalika kutambulisha jamii ya wasukuma

na kisha uelezee asili ya majina hayo.

3) Je, majina ya ukoo yanayotumika katika utambulisho wa wasukuma yanabeba

ujumbe wa ziada kuhusu jamii yao/ ? NDIO/HAPANA.

4) --Kama ndio taja jina na ujumbe wake.

5) Je ni maajina yapi ya kisukuma yanayotofautisha jinsi kwa wasukuma?

6) Je ni namna gani majina ya kisukuma yanatambulisha jamii hiyo?

7) Je kuna uhusiano gani kwenye majina ya kisukuma na matukio?

8) Je ni sababu zipi za kiisimujamii ambazo hutumika kutoa majina ya koo kwa

wasukuma?

9) Je wapo watu wanaojitambulisha kwa majina ya kisukuma wenyewe kwa asili si

wasukuma?

10) Je kuna majina ya ukoo ambayo yanakubalika kwa utambulisho wa wasukuma

lakini watu hawapendi kuyatumia? Kama yapo ni kwanini watu hawapendi

kuyatumia kwa utambulisho.

87

Kiambatisho II: Research Quationnaire

1. (a) How old are you?

(b) Sex

(c) Occupation

(d) Where did you born?

(e) Which is you are mother tongue?

2. Give five accepted clan names used to identify the sukuma people and explain the

orgin of the names.

3. The Sukuma names do they hear extra information about the sukuma community?

True/False. If true list the name and its massage.

4. Which name of Sukuma names are used to distinguish gender in their community?

5. In which ways do the sukuma names give identify of their community?

6. What is the relationship between the sukuma names and the events In their

communit?

7. What are the social-linguistic reasons that are used in giving clan names among

the sukuma people?

8. Are there other people who identify themselves with Sukuma names whereas their

origin is not sukuma?

9. Are there clan names that are accepted in identifying the sukuma but the sukuma

people do not like using them? If there is why do people don‘t like, identifying

themselves with them

88

89

90

91

92

93

94