serikali ya mapinduzi zanzibar wizara ya mifugo na uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa...

97
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuvi SERA YA MIFUGO ZANZIBAR 2011

Upload: others

Post on 17-Jan-2020

20 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Wizara ya Mifugo na Uvuvi

SERA YA MIFUGO ZANZIBAR

2011

Page 2: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

ii

YALIYOMO…………………………………………………………………….................

DIBAJI…………………………………………………………………………………......

TAFSIRI YA VIFUPISHO KWA KISWAHILI……………………………………………

FASILI………………………………………………………………………………………

ii

v

vi

1. SURA YA 1: UTANGULIZI JUMLA…………………………………………... 1

1.1. Usuli……………………………………………………………………………… 1

1.1 Sura ya Taifa……………………………………………………………………...

1.2 Haja ya Kuandaa Sera ya Mifugo………………………………………………... 1

1.2.1 Uhusiano kati ya Sera ya Mifugo na Sera za Maendeleo, Mipango na Sekta

nyingine……....................................................

2. SURA YA 2: UCHAMBUZI WA SEKTA YA MIFUGO ZANZIBAR…… 4

2.1. Uchambuzi wa Hali Halisi………………………………………………………. 4

2.1.1 Hesabu ya mifugo………………………………………………………………... 4

2.1.2. Kiwango cha uzalishaji………………………………………………………….. 4

2.1.3. Mwenendo wa uzalishaji……………………………………………………….. 4

2.1.4. Bidhaa muhimu zinazoweza kuongezewa thamani……………………………. 5

2.1.5. Tija ya mifugo isiyo ya kawaida………………………………………………… 5

2.1.6. Ustawi wa wanyama na maendeleo……………………………………………… 6

2.1.7. Uzalishaji na matumizi ya bayogesi……………………………………………... 6

2.1.8. Fursa za masoko…………………………………………………. 6

2.1.9. Magonjwa ya Yanayoweza Kuambukiza Binadamu na Wanyama (Zoomotiki) 6

2.1.10. Magonjwa ya Wanyama Yanayovuuka Mipaka………………………………. 7

2.1.11. Utoaji wa huduma za maabara…………………………………………………… 7

2.1.12. Utoaji wa huduma za mifugo na elimu kwa wafugaji…………………………… 7

2.1.13 Biashara ya mifugo………………………………………………………………. 7

2.1.14 Utoaji wa huduma za fedha…………………………………………………….. 7

2.1.15. Ubia kati ya Sekta ya umma na binafsi…………………………………………. 8

2.1.16. Maendeleo ya rasilimali watu……………………………………………………. 8

2.1.17. Misaada ya pembejeo……………………………………………………………. 8

2.1.18. Mchango wa mifugo katika pato la taifa………………………………………… 8

2.1.19. Mchango wa mifugo katika uchumi wa familia…………………………………. 8

2.1.20. Utafiti waMifugo………………………………………………………………… 9

2.1.21 Usalama wa chakula na lishe…………………………………………………….. 9

Page 3: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

iii

2.2. Vikwazo dhidi ya maendeleo ya mifugo…………………………………... 9

2.3 Fursa kwa ajili ya maendeleo ya mifugo………………………………………… 11

3. SURA YA 3 : MAPITIO YA SERA ZINAZOHUSIANA NA MIFUGO…… 12

3.1. Maelezo ya Jumla………………………………………………………………... 12

3.1.1. Sera ya Sekta ya Kilimo…………………………………………………………. 12

3.1.2. Sera ya Chakula na Lishe………………………………………………………... 12

3.1.3. Sera ya Misitu……………………………………………………………………. 12

3.1.4. Sera ya Maji………………………………….…………………………………... 12

3.1.5. Sera ya Ardhi …………………………………………………………………… 13

3.1.6. Sera ya Mazingira ……………………………………………........................… 13

3.1.7. Sera ya Biashara Ndogo na Kati………………………..………................. 13

3.1.8. Sera ya Biashara ……………………………………………................................ 13

3.1.9. Sera ya Viwanda ……………………………………………................................ 13

3.1.10. Sera ya Uwekezaji ……………………………………………............................. 14

3.1.11. Sera ya Afya ……………………………...……………...................................... 14

3.1.12. Sera ya Elimu ……………………...……………………..................................... 14

3.1.13. Mpango wa Taifa wa Kudhibiti VVU na UKIMWI Zanzibar…………………... 14

3.1.14. Sera ya Ajira ……...……………………………………...................................... 14

3.1.15. Sera nyengine za kisekta na mipango inayohusiana na maendeleo ya sekta ya

mifugo……………………………………………………………………………

14

14

4 SURA YA 4: MKAKATI WA SERA…………………………………………. 15

4.1. Maelezo ya Jumla ……………………………...……………............................... 15

4.1.1. Dira ……………………………………………................................................... 15

4.1.2. Dhamira ……………………………………………............................................ 15

4.1.3. Madhumuni……………………………...……………......................................... 15

4.1.3.1 Lengo Kuu ……………………………...…………….......................................... 15

4.1.3.2. Malengo Mahsusi ………………………………..…………................................ 15

5. SURA YA 5: MAENEO YA SERA…………………………………………... 17

5.1 Maelezo ya Jumla …………………………………………….............................. 17

5.1.1.. Uzalishaji wa wanyama ……………………………………………..................... 17

5.1.1.1. Kuku ……………………………………………................................................ 18

Page 4: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

iv

5.1.1.2. Kondoo na mbuzi …………………………………………….............................. 19

5.1.1.3 Ng'ombe wa maziwa …………………………………………….......................... 20

5.1.1.4 Ng'ombe wa nyama ……………………………………………........................... 20

5.1.1.5 Ufugaji wa wanyama bora ……………………………………………................. 21

5.1.1.6 Chakula cha wanyama na malisho ………………………………………………. 22

5.1.1.7 Uhakika wa chakula ……………………………………………........................... 23

5.1.1.8 Ufugaji wa kilimo hai……………………………………………………………. 24

5.1.1.9 Mifugo na mazao ya mifugo yanayoweza kuongezewa thamani na masoko….... 25

5.1.2 Afya ya wanyama …………………………………………….............................. 25

5.1.2.1 Huduma za afya ya wanyama……………………………………………………. 25

5.1.2.2 Magonjwa Yanayoenezwa na kupe ……...……………………………….……... 26

5.1.2.3 Magonjwa ya Wanyama Yanayovuuka Mipaka……………………………… 27

5.1.2.4. Magonjwa ya Zonotiki na Uhakika wa Chakula………………………………... 28

5.1.2.5. Huduma za Uchunguzi wa Mifugo ……………………………………………… 28

5.1.2.6. Ustawi wa wanyama …………………………………………….......................... 28

5.1.3. Wanyama rafiki na Wasiofugwa sana…………………………………………... 29

5.1.3.1. Wanyama rafiki na wa Mapambo………………………………………………. 29

5.1.3.2. Wanyama Wasiofugwa …………………………………………….............. 30

5.1.4. Utafiti wa Mifugo …………………………………………….............................. 31

5.1.5. Maendeleo ya Rasilimali

watu…………………………………..………………..

31

5.1.6 Huduma za elimu za mifugo na mafunzo kwa

wakulima………………………………………..

32

5.1.7. Huduma za taarifa za mifugo…………………………………………………….. 33

5.1.8 Masuala mtambuka na kisekta…………………………………………………… 34

5.1.8.1 Misaada kwa wajasiriamali wa mifugo………………………………………….. 34

5.1.8.2 Rasilimali ardhi ……………………………………………................................. 35

5.1.8.3 Maendeleo ya miundombinu ya mifugo…………………………………………. 36

5.1.8.4 Rasilimali maji……………………...…………………….................................... 36

5.1.8.5 Wanyama wanaotumika kwa kazi…………………………...………………….. 37

5.1.8.6. Wizi wa mifugo ……………………………………………................................. 38

5.1.8.7. Uzalishaji na matumizi ya bayogesi……………………………………............... 38

5.1.8.8. Huduma za fedha kwa ajili ya maendeleo ya mifugo……………………………. 39

5.1.8.9. Wanawake na mifugo……………………………………………......................... 39

Page 5: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

v

5.1.8.10. Ajira ya vijana na mifugo………………………………………………….......... 40

5.1.8.11. Ajira ya watoto na mifugo……………………………………………................. 41

5.1.8.12. Usimamizi wa majanga ya mifugo…………………………......………............... 42

5.1.8.13. VVU/ UKIMWI na mifugo……………………………………………................ 43

5.1.8.14. Mifugo na Utunzaji wa mazingira......................................................................... 43

5.1.8.15. Mifugo na mabadiliko ya tabianchi…………………………………….............. 44

5.1.8.16. Ushiriki wa sekta ya umma na binafsi…………………………........................... 45

6. SURA YA 6: MIUUNDO YA KITAASISI NA UDHIBITI………………. 47

6.1. Miundo ya kitaasisi ………………………………………………...................... 47

6.2. Kazi na majukumu ya taasisi…………………………………………………... 48

6.2.1. Wizara ya Mifugo na Uvuvi (WMU)………………………………………......... 48

6.2.2. Wizara ya Kilimo na Maliasili (WKM)………………………………………… 49

6.2.3. Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati (WANMN)……………………… 49

6.2.4. Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko (WBVM)……………………............. 49

6.2.5. Wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendele ya Vijana, Wanawake na Watoto

(WUJMVWW)……………………………………………………………………

49

6.2.6. Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika (WKUWKU)… 49

6.2.7. Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (ORMBLM)…................. 50

6.2.8. Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais - OMKR (Idara ya Mazingira; Tume ya

UKIMWI Zanzibar-ZAC)……………………………………………………

50

6.2.9. Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo (ORFUMM)……… 50

6.2.10. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali (WEMA)……………………….…… 50

6.2.11. Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Idara ya Kukabiliana na Maafa). (OMPR-

DDM)……………………………………………………………………………..

50

6.2.12. Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo (WHUUM)………………… 50

6.2.13. Wizara ya Afya (WA) ………………………………………………................... 51

6.2.14. Wizara ya Mawasiliano na Miundombinu (WMM)…………………………….. 51

6.2.15 Taasisi Zisizo za Kiserikali ……………………..……………………………….. 51

6.2.16. Jumuia za kikanda na kimataifa………………………………………………… 51

6.2.17. Washirika wa Maendeleo ……………………………………………………….. 51

6.2.18 Sekta Binafsi ……………………………………………………………….......... 51

6.3. Mifumo ya Kisheria na

Usimamizi……………………………………………….

52

Page 6: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

vi

6.4. Uwezo wa kitaasisi kwa ajili ya utekelezaji wa Sera ya Mifugo Zanzibar ……. 52

7 SURA YA 7: UFUATILIAJI NA TATHMINI……………………………... 54

7.1. Maelezo ya Jumla…………………………………………………………........... 54

7.2. Malengo ya Ufuatiliaji na Tathimini……………………………………………. 54

7.3 Mkabala wa Ufuatiliaji na Tathimini wa Sera ya Mifugo Zanzibar…………… 54

7.4 Muundo wa Kitaasisi wa Ufuatiliaji na Tathimini ……………………………… 55

Page 7: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

vii

DIBAJI

Kuongezeka kwa kasi ya ukuaji wa uchumi katika mifugo na sekta nyengine

zinazohusiana nazo ni suala muhimu la kisera linalopewa kipaumbele katika kuleta

maendeleo endelevu ya familia masikini hapa Zanzibar.Ongezeko hilo la ukuaji wa

uchumi linaoana na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Muda Mrefu (Dira ya 2020) na

Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Zanzibar (MKUZA II). Uzinduzi

wa Sera mpya ya Mifugo Zanzibar unakwenda sambamba na Lengo la Maendeleo ya

Milenia la kupunguza umaskini.

Zanzibar imejaaliwa kua na rasilimali za kutosha za miti na wanyama zinazoweza

kutumika kama msingi wa maisha kwa familia za vijijini zinazofikia karibu asilimia 60 ya

idadi ya watu wote (ZSGRP, 2007). Hata hivyo, katika kipindi kirefu, visiwa hivi

vimekabiliwa na upungufu wa raslimali ardhi, teknolojia sahihi na raslimali fedha ambazo

kwa pamoja zinachangia katika kupunguza kasi ya ukuaji wa sekta ya kilimo (ikiwemo

mifugo), licha ya juhudi kubwa zinazochukuliwa na serikali na Washirika wake wa

Maendeleo katika kukabiliana na changamoto hizo.

Wizara ya zamani ya Kilimo, Mifugo na Mazingira kupitia Programu zake zinazofadhiliwa

na IFAD za kusaidia Huduma za Kilimo Zanzibar/Programu ya Maendeleo ya Sekta ya

Kilimo – Mifugo zilitoa kandarasi kwa Jumuia ya Ustawi na Maendeleo ya Mifugo

kufanya mapitio ya sera mbalimbali pamoja na miundo ya vyombo vya usimamizi

vilivyopo hivi sasa ambavyo kwa namna moja au nyengine vinaweza kuathiri uzalishaji

wa mifugo na maendeleo ya afya ya wanyama hapa Zanzibar. Wakati wa kipindi cha

mchakato wa tathmini hiyo, taarifa muhimu zilizokusanywa kutoka kwa wadau

mbalimbali zilikua msingi wa uandaaji wa sera hii ya kwanza kamilifu ya mifugo kuwahi

kutayarishwa katika visiwa hivi. Kwa hakika, Sera ya Mifugo Zanzibar imechukua nafasi

ya changamoto zile za sekta ndogo ya mifugo zilizofafanuliwa katika sera ya zamani (Sera

ya Sekta ya Kilimo, 2002). Aidha, Sera hiyo ya zamani ilitayarishwa kutokana na

midahalo ya kina ya muda mrefu yaliyolenga katika kuiandaa sekta ya mifugo kuchukua

sura ya kibiashara ili iweze kutoa faida inayotokana na fursa ya kuongezeka kwa mahitaji

ya bidhaa za mifugo ikiwa ni pamoja na ile ya soko la utalii.

Sera ya Mifugo Zanzibar ni ya aina yake hasa kutokana na michango ya kitaalamu na

Page 8: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

viii

kimaadili iliyotolewa na wadau tafauti kutoka ngazi za awali, kitaifa, kikanda na kimataifa.

Wakati wa mchakato wa midahalo ya utayarishaji wa sera hii, kaya, wakulima,

wafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo

kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa. Aidha, michango illikusanywa kupitia

warsha mbalimbali za wadau wa sekta binafsi na umma pamoja na mikutano ya

mashauriano. Wahusika wengine ambao walitoa michango mujimu ni pamoja na Kamati

ya Kisekta ya Usimamizi (MSC), Wizara za Serikali, Jumuia za Kiraia (CSOs) vyombo

vya usimamizi na maandiko mbalimbali ya sera. Taarifa zilizomo katika waraka huu

zinatarajiwa kwamba zitasaidia kuandaa mipango, mikakati na baadae kuwezesha kubuni

mipango ya maendeleo ya sekta ya Mifugo. Aidha, inatarajiwa kwamba wadau wote na

jamii kwa ujumla itaweza kupata fursa ya kuyasoma na kuyaelewa masuala yote

yaliyofafanuliwa katika kitabu hiki.

Mwisho, ninachukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa kazi ya heshima

iliyoandaliwa na Timu ya Kitaalamu ya Sera ya ZALWEDA, Kamati ya Sera ya

ZALWEDA, Kamati ya Kisekta ya Usimamizi na Timu ya Ushauri wa Kitaalamu kutoka

Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na

Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine ambavyo kwa pamoja viliwezesha kufanikisha utoaji wa

kitabu hiki.

Asante.

.................................................. ....

Said Ali Mbarouk

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Zanzibar

Page 9: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

ix

TAFSIRI YA KISWAHILI YA VIFUPISHO VYA KIINGEREZA

AHPC Vituo vya Utabibu na Uzalishaji wa Wanyama

AI Upandishaji kwa Sindano

AIDS UKIMWI

ASDP-L Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo - Mifugo

ASSP Programu ya Huduma za Msaada wa Kilimo

AU Jumuia ya Afrika

BQ Chambavu

CBPP Homa ya Mapafu kwa Ng’ombe

CCPP Homa ya Mapafu kwa Mbuzi

CMO-DMD Ofisi ya Waziri Kiongozi - Idara ya Kukabiliana na Maafa

CSOs Jumuia za Kiraia

DAP Idara ya Uzalishaji wa Wanyama

DoE Idara ya Mazingira

DPs Washirika wa Maendeleo

DVS Idara ya Huduma za Utabiba wa Mifugo

EAC Jumuia ya Afrika Mashariki

ECF Matukwi

EPZ Ukanda wa Kiuchumi

FAO Shirika la Chakula na Kilimo Ulimwenguni

FFS Mashamba Darasa ya Wakulima

FMD Ugonjwa wa Miguu na Midomo

FVPO Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais

FYM Mbolea ya Samadi

GDP Pato la Taifa

HIV VVU

IAEA Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki

IFAD Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo

LES Huduma za Elimu kwa wakulima na Mifugo

LPCC Kamati ya Uratibu wa Sera ya Mifugo

LSD Ugonjwa wa Ngozi

LSPs Watoaji wa Huduma za Mifugo

M & E Ufuatiliaji na Tathmini

Page 10: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

x

MACEMP Mradi wa Usimamizi wa Mazingira ya Pwani na Baharini

MANR Wizara ya Kilimo na Maliasili

MIC Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano

MDGs Malengo ya Maendeleo ya Milenia

MICTS Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo

MLDF Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi-Tanzania Bara

MLEEC-DC Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika - Idara ya

Ushirika

MLF Wizara ya Mifugo na Uvuvi - Zanzibar

MLHWE Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati

MOH Wizara ya Afya

MSC Kamati ya Kisekta ya Usimamizi

POFEDP Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo

MSWYWCD Wizara ya Ustawi wa Jamii,Vijana,Maendeleo ya Wanawake na Watoto

MTIM Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko

NCL Mifugo Isiyo ya Kawaida

ND Mahepe/Magwa

NGOs Jumuia Zisizo za Kiserikali

NPHC Sensa yaTaifa ya Idadi ya Watu na Makazi

OIE Shirika la Afya ya Wanyama Ulimwenguni

PLHAs Watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi na UKIMWI

POCRC Ofisi ya Rais, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi

PRIDE Uendelezaji wa Juhudi za Vijijini na Maendeleo ya Biashara

RVF Homa ya Bonde la Ufa

SACAS Vyama vya Akiba na Mikopo

SACCOS Ushirika wa Akiba na Mikopo

SADC Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika

SMEs Biashara Ndogo ndogo na za Kati

SUA Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine

SVPO-DDM Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Idara ya Kukabiliana na Maafa)

SWAP Mkabala Mkuu wa Kisekta

SWOC Uwezo,Udhaifu, Fursa na Changamoto

T & V Mafunzo na Ziara

Page 11: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

xi

TADinfo Mfumo wa Taarifa za Maradhi ya Wanyama Yanayovuuka Mipaka

Magonjwa

yanayovuuka

mipaka

Maradhi ya Wanyama Yanayovuuka Mipaka

TB Kifua Kikuu

TBDs Maradhi Yanayotokana na Kupe

TNA Tathmini ya Mahitaji ya Mafunzo

UAES Mfumo Shirikishi wa Elimu kwa wakulima katika Kilimo

URT Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

VIC Kituo cha Uchunguzi wa Maradhi ya Mifugo

WHO Shirika la Afya Ulimwenguni

ZAC Tume ya UKIMWI Zanzibar

ZALWEDA Jumuia ya Ustawi na Maendeleo ya Mifugo

ZFDCB Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar

ZFSNP Sera ya Uhakika wa Chakula na Lishe

ZLP Sera ya Mifugo Zanzibar

ZLRB Bodi ya Usimamizi wa Mifugo Zanzibar

ZNCCIA Jumuia ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima

ZPC Kamati ya Sera ya ZALWEDA

ZPTT Timu ya Kitaalamu ya Sera ya ZALWEDA

ZSGRP Mpango wa Kupunguza Umasikini Zanzibar – MKUZA

FASILI

Kwa madhumuni ya waraka huu, istilahi zifuatazo zimefasiriwa kama ifuatavyo:

Kilimo - Ni eneo lolote linalofanywa shughuli za kibinaadamu

zinazohusiana na mazao, mifugo, uvuvi na misitu.

Mnyama - Ni kiumbe hai chenye au kisichokua na uti wa mgongo mbali na

binaadamu.

Kabila ya wanyama - Ni neno linalotumika kuelezea kabila la wanyama wa majumbani

au wanaofugwa

Chakula cha - Ni vyakula vya asili au mchanyanyiko vinavyolishwa wanyama

Page 12: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

xii

mifugo wa majumbani au wanaofugwa

Upandishaji kwa

Sindano

-

Ni mbinu ya kukusanya shahawa kutoka kwa wanyama dume,

kuzichakatua na kisha kuziingiza mbegu hizo kwenye njia ya

uzazi ya wanyama jike kwa kutumia vifaa maalumu.

Bayofueli

-

Inafasiliwa kama ni nishati inayotokana na mabaki ya vitu vya

kibayolojia vilivyorundikana kwa muda mfupi na inatafautishwa

na nishati inayotokana na mabaki ya vitu vya kibayolojia

vilivyorundikana kwa muda mrefu.

Bayogesi - Ni gesi inayozalishwa kutokana na viumbe hai vya kibayolojia

ambayo hufanyika panapokuwa na ukosefu wa hewa ya oksijini.

Bayogesi inatokana na vitu vya bayoojeniki na ni aina ya

bayofueli.

Bayo usalama - Katika kilimo bayo usalama ni kupunguza hatari ya vimelea vya

maambukizi

Bayoteknolojia - Hii inajulikana kama ni matumizi ya mfumo wa kibayolojia kama

bidhaa au kwa madhumuni ya kuzalisha bidhaa.

Bivalvu - Inahusisha viumbe wanaotokana na jamii ya chaza, kombe n.k.

Viumbe hivi vina magamba yanayofunga na kufunguka.

Chambavu - Ni ugonjwa unaowaathiri wanyama kama ng’ombe

unaosababishwa na baktiria. Ugonjwa huu unawakumba

wanyama kutokana na kula chakula kilichoathiriwa na baktiria

wa ugonjwa huu. Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na mnyama

kuvimba ulimi na koo, na sehemu ya nyama iliyoathirika hupiga

weusi.

Kuku wa Nyama - Ni aina ya kuku au bata mzinga ambao hufugwa kwa ajili ya

nyama.

Koksidia - Ni ugonjwa mkali unaowaathiri wanyama hasa katika sehemu za

utumbo na husababisha mnyama kuharisha damu

Homa ya Mapafu

kwa Ng’ombe

- Ni ugonjwa mbaya sugu wa ng’ombe unaosababishwa na baktiria

anaeitwa Mycoplasma mycoides. Dalili za ugonjwa huu mnyama

hupumua kwa tabu na homa ya mapafu

Homa ya Mapafu

ya mbuzi

- Ni ugonjwa wa mbuzi unaofanana na Ugonjwa wa Homa ya

Mapafu ya Ng’ombe.

Page 13: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

xiii

Upandishaji wa

wanyama wenye

vinasaba tafauti

- Istilahi hii inafasiliwa kama ni kuwapandishia wanyama wa

mbegu au koo mbili tafauti kwa njia ya kiasili au kwa

kupandikiza

Krasteshia - Ni kundi kubwa la athropodi linalojumuisha takriban makundi

52,000 ambayo ni pamoja na jamii nyingi za wanyama kama vile

kaa, kamba, kamba wa maji baridi, uduvi, chaza.

Ng’ombe wa

Maziwa

- Ng’ombe wanaofugwa kwa kuzalisha maziwa

Magonjwa yenye

athari za kiuchumi

-

Ni maradhi ambayo husababisha hasara za kiuchumi ikiwa ni

pamoja na vibuma/matukwi, mahepe/magwa, uvimbe wa kiwele,

chambavu, homa ya mapafu, Gumburo na maradhi mengine

ambayo yametangazwa na OIE.

Magonjwa yenye

athari za kiafya

kwa umma

- Ni maradhi yanayosababisha hatari za kiafya kwa umma kama

vile kifua kikuu cha ng’ombe, kichaa cha mbwa, uvimbe wa

kiwele, mafua ya ndege, kimeta. Uvimbe wa kibofu cha mkojo na

maradhi mengineyo ambayo yamefafanulliwa na OIE na WHO

Wanyama

wanaotumika kwa

kazi

-

Ni wanyama maalumu wa kufuga ambao hupewa mafunzo ili

kufanya kazi

Matukwi/vibuma

(ECF)

- Ni maradhi mabaya yanayowaathiri ng’ombe yanayoenezwa na

kupe

Uhaulishaji wa

kiinitete (embryo)

-

Ni mbinu ya uhamishaji wa kiinitete kutoka kwa mnyama jike

(mchangiaji) kwenda kwa mwengine (mpokeaji) kwa lengo la

kuzalisha ndama

Michirizi ya mto - Ni sehemu ambazo maji safi ya mito na chemchem huingia

katika bahari na kuchanganyika na maji ya chumvi. Aina

mbalimbali za ndege, samaki, na wanyama pori hufanya maskani

yao katika sehemu hizi.

Huduma za Elimu

kwa Wafugajii

- Ni uhaulishaji wa teknolojia kutoka kwa wataalamu wa mifugo

kwenda kwa wafugaji. Aidha, wataalamu wa mifugo ni pamoja

na wafugaji wenye uwezo wa kutoa huduma kama hizi kwa watu

wengine.

Samadi - Ni mchanganyiko wa mkojo na kinyesi cha wanyama ambao

hutumika kama mbolea ya asili

Page 14: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

xiv

Manyoya - Ni nywelenywele au mbawa zinazoota katika ngozi ya wanyama

jamii ya ndege.

Ugonjwa wa Miguu

na Midomo (FMD)

- Ni ugonjwa unaoambukizwa na virusi ambao huwaathiri

wanyama wenye kwato mbili na dalili zake ni vidonda vya

malengelenge mdomoni, miguuni na maeneo mengine ya mwili

pamoja na ngozi laini

Vinasaba - Ni sifa za kibayolojia ambazo hurithiwa kutoka kizazi kimoja

kwenda kingine.

Serikali - Ni Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Gumboro - Ni ugonjwa unaosababiswa na virusi unaowaathiri vifaranga

chini ya umri wa wiki 8.

Ngozi - Ni ngozi zinazopatikana kutoka kwa wanyama wakubwa

wanaofugwa kama vile ng’ombe na nyati

Kwato - Ni gamba nene na gumu la ncha ya mguu wa mnyama kama vile

ng’ombe , kondoo, mbuzi n.k

Pembe - Ni chipukizi la mfupa lililofunikwa na ngozi ngumu kichwani

kwa wanyama kama vile ng’ombe, mbuzi n.k.

Uzalishaji

Maziwa

- Ni uzalishaji wa maziwa katika kiwele cha wanyama kwa ajili ya

ndama.

Lagoni ( wangwa) - ni umbo la maji ambalo lina chumvi au maji yenye chumvi

chumvi ambalo hutenganishwa kutoka kina kirefu cha bahari na

fungu au uwazi wa matumbawe au maumbo yenye kufanana

nayo

Kuku wa mayai - Ni kuku ambao hufugwa kwa ajili ya kuzalisha mayai

Mifugo - Ni Wanyama wanaofugwa wakiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo,

kuku, sungura n.k.

Mfugaji - Ni mtu yeyote anayejishughulisha na shughuli za ufugaji wa

wanyama

Sekta ya Mifugo - Ni shughuli zote zinazohusiana na maendeleo ya mifugo

Ufugaji wa jadi - Ni ufugaji wa asili wa wanyama unaofanywa na mtu binafsi

Ugonjwa wa ngozi - Ni ugonjwa unaoathiri mifugo unaosababishwa na virusi na

humfanya mnyama kuwa na vinundunundu mwilini

Maradhi ya kiwele - Ni maradhi yanayoathiri kiwele na kusababisha kuharibika kwa

maziwa

Page 15: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

xv

Bidhaa za maziwa - Ni bidhaa zinazotokana na usarifu wa maziwa kama vile siagi,

mtindi, samli n.k.

Ugonjwa wa

Mahepe/magwa

- Ni maradhi yanayosababishwa na virusi ambayo huathiri jamii ya

ndege. Athari zake ni pamoja na kuathiri mfumo wa fahamu,

upumuaji na chakula

Eneo la malisho - Ni ardhi inayoota au kuoteshwa mimea kwa ajili ya malisho ya

mifugo.

Mnyama rafiki - Ni mnyama yeyote ambae hufugwa kwa ajili ya uwenza na

burudani.

Sera - Ni matamko na mikakati inayolenga kufanikisha malengo

mahsusi

Jamii ya ndege

- Ni aina ya ndege wanaofugwa kwa ajli ya kuzalisha mayai,

nyama au manyoya kwa mfano kuku, bata n.k

Homa ya Bonde la

Ufa

- Ni maradhi yanayosababishwa na virusi kwa wanyama

wanaocheua na binaadamu endapo atatumia bidhaa zilizoathiriwa

na ugonjwa huu. Miongoni mwa dalili zake ni homa kali na

kuharibu mimba

Wanyama

wanaocheua

- Ni aina ya wanyama wenye matumbo yaliyogawika sehemu nne

au tatu ambao hula chakula na kukichachusha kisha kukirejesha

kinywani na baadae kukirejesha tena tumboni. Mfano wa

wanyama hawa ni ng’ombe, mbuzi na ngamia.

Shahawa - Ni mbegu za uzazi za mnyama dume

Shehia - Ni ngazi ya chini ya utawala wa Serikali inayoundwa na

kijiji/mtaa mmoja au zaidi.

Tope za samadi - Ni mabaki ya samadi yanayopatikana baada ya kumengenyua

kinyesi cha mifugo katika mitambo ya bayogesi

Mdau - Ni mtu binafsi, jumuia au taasisi ambayo kwa njia moja au

nyengine ina uhusiano na sekta ya mifugo.

Mnyama mzururaji - Ni mnyama anaeishi bila ya kudhibitiwa

Mkakati - Ni mpango unaoandaliwa ili kutekeleza malengo mahsusi

Maradhi

Yanayotokana na

kupe

-

Ni maradhi yanayoenezwa na kupe

Page 16: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

xvi

Maradhi ya Mifugo

Yanayovuuka

Mipaka

-

Ni maradhi yanayoenea kwa urahisi kupitia mipaka ya nchi moja

na nyengine kwa mfano, mafua ya ndege, kichaa cha mbwa,

mahepe/magwa, Miguu na Midomo n.k.

Zebu (Ng’ombe wa

Asili)

Ni ng’ombe wenye nundu ambao wanastahamili sana katika

mazingira ya nchi za joto

Zonosisi - Ni maradhi yanayoweza kumuambukiza binadamu kutoka kwa

mnyama au kinyume chake.

Page 17: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

1

SURA 1: UTANGULIZI WA JUMLA________________

1.1. Usuli

1.1.1. Sura ya Taifa

Zanzibar inajumuisha visiwa viwili vikuu vya Unguja na Pemba, vilivyozungukwa na

vijisiwa vingi vyingine vidogo vidogo. Zanzibar ina idadi ya watu inayokisiwa kufikia

milioni 1.2 inayoongezeka kwa kasi ya asilimia 3.1 kwa mwaka (Sensa ya Taifa ya Watu

na Makazi (NPHC), 2002). Zanzibar ipo kiasi ya kilomita 40 Mashariki ya mwambao wa

Tanzania Bara na ina jumla ya eneo la kilomita za mraba 2654. Visiwa hivi vina idadi

kubwa zaidi ya watu wanaoishi katika eneo moja katika eneo la Afrika ya Mashariki

(yaani watu 370 kwa kila kilomita moja ya mraba) ikiwa na familia za wafugaji

zinazofikia 36,445 (Sampuli ya Kitaifa ya Sensa ya Kilimo, 2003). Zaidi ya asilimia 99 ya

familia hizo zinaendesha shughuli za kilimo mchanganyiko wa mazao na mifugo. Sekta ya

mifugo imemezwa zaidi na wafugaji wadogo wadogo wa ng'ombe, kuku, bata na mbuzi.

Mifugo ambayo bado haijapewa umuhimu mkubwa ni pamoja na kondoo, mifugo isiyo ya

kawaida na aina nyengine ya ufugaji mbali na kuku.

Kilimo pamoja na uzalishaji wa mifugo bado ni sekta kuu katika uchumi wa Zanzibar kwa

kuwa ni tegemeo la maisha kwa zaidi ya asilimia 40 ya watu wote (ZSGRP, 2007). Hata

hivyo, sekta hii inakabiliwa na changamoto nyingi zinazokwaza ukuaji wake ikiwa ni

pamoja na ukosefu wa uwekezaji, maendeleo duni ya miundombinu ya mifugo na

rasilimali watu. Kama tunataka kuona kuwa lengo kuu la kuzalisha asilimia 50 ya chakula

linafanikiwa (DIRA-2020, 2002), changamoto hizi na nyenginezo zinahitaji

kushughulikiwa ipasavyo katika sera zetu.

1.2. Haja ya Kuandaa Sera ya Mifugo

Kuna haja ya kuandaa Sera mpya ya Mifugo ya Zanzibar ili kuweza kushughulikia ipasvyo

upungufu uliopo katika sera ya sekta ya kilimo (2002). Sera ya sekta ya kilimo

imeshindwa kukabiliana kikamilifu na changamoto za tija ya mifugo isiyo ya kawaida,

ustawi wa wanyama na maendeleo, uzalishaji na matumizi ya nishati ya wanyama, fursa za

masoko, uongezaji thamani wa mazao ya mifugo na huduma za kifedha. Aidha,ili kuweza

kukabiliana na changamoto hizi kikamilifu, sera mpya inakusudia kupambana na

Page 18: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

2

changamoto zinazoibuka na au zilizotoweka ambazo zina athari kubwa kwa maendeleo ya

sekta ya mifugo kama vile magonjwa ya zonotiki na yanayovuuka mipaka, ridhaa kwa

wafugaji, wajasiriamali na biashara ya mifugo ili kuhamasisha uzalishaji na fursa za

masoko. Ili kuweza kupambana na changamoto hizo. Sera hii imeweka kipaumbele katika

masuala yafuatayo: -

1.2.1. Uhusiano kati ya Sera ya Mifugo na Sera za Maendeleo, Mipango na sekta

nyingine

Katika será yeyoyote ya maendeleo suala la uhusiano ni la lazima ili hatua muhimu

zinazochukuliwa ziweze kua endelevu. Kwahivyo, ili kufanikisha utekelezaji wa Sera hii,

waraka huu hauna budi kuoanishwa na sera za uchumi za nchi yetu na kufanya tathmini ya

malengo ya msingi ya kitaifa na kimataifa kama yalivyoainishwa katika MKUZA II, Dira

ya 2020 na Malengo ya Maendeleo ya Milenia. Malengo ya Sera ya Mifugo Zanzibar

yanalingana na malengo ya sera za kitaifa katika kufanikisha utekelezaji wa mikakati

iliyopendekezwa. Aidha, sera hii inazingatia changamoto za kukuza sekta ya mifugo kwa

lengo la kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini. Sera hii inaweka

wazi na kufanyia kazi upungufu uliopo kati ya sera ya mifugo na sera nyingine. Aidha,

sera hii imejitahidi kuhusisha maeneo yote yanayoingiliana katika sera tafauti.

Kuchochea Maendeleo ya Mifugo na kuhifadhi mazingira

Sera hii inachochea maendeleo ya sekta ya mifugo kwa kubuni njia za matumizi ya mbinu

endelevu za uzalishaji. Jambo hili limefafanuliwa vyema katika mikakati iliyopendekezwa

ya kupunguza shinikizo la malisho ya mifugo kwa kuendeleza na kuimarisha mifugo na

matumizi bora ya lishe mbadala kama vile mbolea ya samadi.

Ufugaji wa kisasa

Sera ya Mifugo Zanzibar inasisitiza matumizi ya ubunifu uliopo katika sekta ya maendeleo

ya mifugo kwa kutoa huduma bora za elimu kwa wakulima kama inavyoelezwa katika

MKUZA II. Changamoto za masoko, viwango, uhusiano na sekta ya utalii na usafirishaji

wa bidhaa nje ya nchi zimezingatiwa sambamba na uendelezaji wa viwanda vidogo vya

usindikaji.

Page 19: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

3

Kutilia mkazo biashara ya bidhaa na huduma za mifugo

Lengo la Sera ya Ulegezaji wa Masharti ya Biashara la kuongeza fursa ya sekta binafsi

kushiriki katika uchumi wa taifa linajitokeza ndani ya Sera ya Mifugo Zanzibar kwa

kusisitiza umuhimu wa kuendeleza uwekezaji katika sekta ya mifugo. Utoaji wa vivutio

kwa wajasiriamali wa mifugo (wakiwemo wawekezaji) ni njia ya kuongeza pato la taifa na

uhakika wa chakula. Aidha, changamoto za soko na mtandao wa masoko ya mazao ya

mifugo inafanyiwa kazi ili kuongeza pato la wakulima na taifa.

Kudhibiti Utoaji wa huduma za mifugo

Sera hii inatambua umuhimu wa huduma za mifugo kwa maendeleo ya sekta ya mifugo.

Hata hivyo, taratibu na kanuni zilizofafanuliwa vyema katika utoaji wa huduma

zinahitajika ili kuweza kuwa na maadili bora, kuthibiti viwango vya kitaifa na kimataifa na

kudumisha ustawi wa wanyama. Sera hii inasisitiza umuhimu wa kufanya mapitio ya

sheria zilizopo na kupendekeza taratibu mpya za udhibiti na usimamizi zikiwemo

kuanzisha Bodi ya Udhibiti wa Mifugo Zanzibar itakayokua na lengo la kustawisha

huduma za mifugo lakini wakati huo huo inalinda maadili ya kitaaluma.

Kutunza vinasaba vya asili

Kutokana na kuongezeka kwa vinasaba vipya vyenye lengo la kuongeza tija katika mifugo,

kuna hatari ya mifugo yetu kupoteza sifa muhimu zikiwemo uwezo wa kuishi katika

mazingira yaliopo. Sera hii inakusudia kulinda vinasaba vya asili vilivyopo licha ya haja

ya kuimarisha mifugo yenyewe.

Kuchochea tija katika sekta ya mifugo kwa njia ya kutoa ruzuku Ingawa tija katika

mifugo inaweza kuongezeka kwa njia kadhaa zikiwemo matumizi ya teknolojia ya kisasa,

huduma bora za elimu kwa wakulima na pembejeo, lakini wafugaji hawawezi kununua

pembejeo kwa bei ya soko. Sera ya sasa ya kilimo inasisitiza umuhimu wa kuondolewa

ruzuku ili kutoa nafasi kwa sekta binafsi kushiriki katika sekta hii pamoja na kuipunguzia

mzigo wa fedha Serikali. Hata hivyo, lengo lililokusudiwa bado halijafikiwa kwasababu

wakulima ni maskini mno na kwahivyo hawawezi kununua pembejeo na huduma

zinazotakiwa. Kwa hivyo, ipo haja ya kupata ridhaa.

Page 20: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

4

SURA YA 2: UCHAMBUZI WA SEKTA YA MIFUGO ZANZIBAR_______

2.1. Uchambuzi wa Hali halisi

2.1.1. Hesabu ya Mifugo

Kwa mujibu wa Sampuli ya Taifa ya Sensa ya Kilimo (2003), idadi ya mifugo katika

mwaka 2010 ilikadiriwa kufikia ng’ombe 200,030, mbuzi 107,077, kondoo 369, kuku

1,308,329 na idadi ya mifugo na wanyama wengine wadogo. Wanyama hawa

wanaongezeka kwa kasi ya asilimia 3 kwa mwaka. Kati ya jumla ya idadi ya ng’ombe

wote, kiasi cha asilimia 95 ni wa kienyeji wanaofugwa chini ya mifumo ya kutumia eneo

kubwa na kundi lililobakia linajumuisha ng’ombe chotara na wa asili wanaofugwa chini ya

mifumo ya kutumia eneo dogo. Ufugaji wa kuku ni maarufu zaidi hapa Zanzibar na

asilimia 89 ya kuku ni mifugo ya asili inayofugwa chini ya mifumo huru au kutunzwa.

Inakisiwa kuwa asilimia 91 ya wafugaji wanafuga ng'ombe, asilimia 26 mbuzi, asilimia 70

kuku, asilimia 0.2 kondoo na nguruwe asilimia 0.1 tu. Asilimia 3 ya familia zinazofuga

zinategemea mifugo tu kwa kuendesha maisha yao. Wastani wa wanyama wanaofugwa

kwa kila familia ni ng'ombe 5, mbuzi 6 na kuku 16 (Sampuli ya Taifa ya Sensa ya Kilimo,

2003).

2.1.2. Kiwango cha Uzalishaji

Ukamaji wa maziwa ya ng'ombe wa kienyeji hufikia wastani wa lita 2.13 kwa siku kwa

kila ng'ombe wakati wa msimu wa mvua, lakini hupungua hadi lita 1.5 sawa na asilimia 29

wakati wa msimu wa ukame (Sampuli ya Taifa ya Sensa Kilimo, 2003). Imeripotiwa kuwa

ng’ombe wa kienyeji huweza kutoa maziwa katika kipindi cha siku 100-150 wakati

ng'ombe chotara huweza kutoa maziwa katika kipindi cha siku 280-300 kwa wastani wa

lita 8.8 za maziwa kwa kila ng'ombe kwa siku (mazungumzo binafsi 2008).

Uzalishaji wa maziwa ya mbuzi wa kienyeji ni mdogo mno kiasi ya kusema kuwa

hawazalishi kabisa, ingawa mbuzi wa maziwa huweza kutoa hadi lita 3 za maziwa kwa

siku. Aidha, viwango vya mapacha miongoni mwa mbuzi wa kienyeji ni vya chini, kiasi ya

asilimia 30 tu, ikilinganishwa na mbuzi wa maziwa kinachofikia asilimia 80-90 ,hasa kwa

mbuzi wanaotunzwa vyema.

Kuku wa kienyeji hutaga mayai kwa kiwango cha chini. Huzalisha kati ya mayai 50 na 60

kwa kuku mmoja kwa mwaka. Inavyoonekana kuku wa kienyeji hawawezi kutumika

kuzalisha mayai au nyama kwa ufanisi. Kwa upande mwingine, kuku wa mayai anaweza

Page 21: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

5

kuanza kutaga katika umri mdogo wa wiki 20 na kutoa hadi mayai 320-340 katika maisha

yake. Kuku wa nyama anaweza kufikia uzito wa kilo 2 katika umri mdogo wa wiki 6.

2.1.3. Mwenendo wa uzalishaji

Jedwali 1 hapo chini linaonesha wastani wa uzalishaji wa bidhaa tafauti za chakula na

zisizo za chakula cha mifugo katika kipindi cha miaka tisa. Jedwali hili linafafanua

mwenendo wa uzalishaji wa maziwa ambao umeongezeka mfululizo katika kipindi

kinachohusika ingawa data za mwaka 2007 na 2008 hazikuweza kupatikana. Hata hivyo,

kuna kuongezeka na kupungua kwa uzalishaji wa bidhaa nyingine.

Jeduali: 1. Makadirio ya uzalishaji wa chakula na bidhaa za mifugo zisizo za chakula

Zanzibar (2000 -2008)

Aina Bidhaa 2000 2001 2002 2003 2004 2005 2006 2007 2008

Ngo’mbe Nyama

(tani)

1,604 1,590 1,572 1,594 1,256 1,772 1584 1,766 1,624

Maziwa

(tani)

27,157 26,266 28,955 29,846 28,256 33,206 36,544 - -

Ngozi

(vipande)

11,878 10,830 10,799 9,593 70,466 12,899 13,201 12,563 13,530

Kondoo

na mbuzi

Nyama

(tani)

37.7 37 52.4 47.2 52.6 59.7 56.7 39.9 46.0

Ngozi

(vipande)

2,509 2,463 3,496 3,148 3,509 3,980 3,776 2,661 3,063

Kuku wa

Nyama

Nyama

(tani)

103 189 183.2 160 119 123 739 35 -

Kuku wa

mayai

Mayai

(tani)

575 625 660 721 735 804 786 329 -

Nyama

(tani)

57.2 63.9 67.2 57.5 64.8 37.9 56.0 23.8 -

Chanzo: Wizara ya Kilimo, Mifugo na Mazingira, 2008

Page 22: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

6

2.1.4. Bidhaa muhimu zinazoweza kuongezewa thamani

Maziwa ni moja kati ya bidhaa muhimu ya mifugo hapa Zanzibar. Uzalishaji wa maziwa

unatafautiana baina ya sehemu moja na nyengine kutokana na sababu kadhaa zikiwemo

mfumo unaotumika katika uzalishaji, misimu, umri na kipindi cha ngombe kuzaliana. Kwa

jumla, mifugo bora ya ng'ombe inayofugwa katika kanda za miti na mashamba makubwa

hutoa maziwa kwa wingi hasa wakati wa msimu wa mvua. Msimu huu hupatikana chakula

kingi chenye ubora. Jambo hili husababisha kuongezeka kwa uzalishaji wa maziwa ghafi

ambayo yanapaswa kusindikwa ili kuweza kuutunza ubora wake, kuongezewa thamani na

kurefusha muda wa kuharibika. Bidhaa nyingine muhimu za mifugo ni pamoja na nyama

na mayai. Kuna fursa kubwa katika biashara ya mazao ya mifugo isiyo ya chakula kama

vile ngozi, mifupa, pembe, ng’ombe hai, manyoya nk. Kiasi cha ng'ombe 14,800, mbuzi

3,000 na kuku milioni moja huchinjwa kila mwaka hapa Zanzibar. Ngozi, manyoya,

mifupa na pembe zinaweza kusindikwa na kuuzwa kama mali ghafi au kutumika katika

utengenezaji wa bidhaa kwa ajili ya kuuzwa.

2.1.5. Tija ya mifugo isiyo ya kawaida

Sungura, nguruwe, funo, kanga, njiwa na ndege pori wa aina mbalimbali bado

wanaendelea kutoa mchango mdogo katika uzalishaji wa nyama na mayai kwa ajili ya

matumizi ya ndani. Mifugo hii isiyo ya kawaida inaweza kuzaliana ndani ya kipindi kifupi

ukilinganisha na muda wa mifugo mingine ya kawaida na kuweza kuzalisha kipato

kikubwa. Hivi sasa, muamko mdogo, maarifa duni ya ufugaji, vifaa na utaalamu mdogo

unachangia uzalishaji duni na tija ndogo ya mifugo hii isiyo ya kawaida.

2.1.6. Ustawi wa wanyama na maendeleo

Zanzibar imetunga Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali Wanyama Namba 11 ya 1999 ili

kusimamia maisha ya wanyama. Aidha, kuna Jumuia Zizizo za Kiserikali na watu binafsi

wanaojitolea kustawisha maisha na maendeleo ya wanyama. Licha ya Serikali, jamii,

Jumuia Zisizo za Kiserikali na Mashirika ya Kimataifa kuchukua hatua mbalimbali na

kubuni mipango ya kudhibiti ukatili dhidi ya wanyama, lakini bado wanyama wanaendelea

kukoseshwa matunzo bora ikiwa ni pamoja na kuwekwa katika msongamano, kuchapwa

viboko, kufanyishwa kazi za sulubu, kupakiwa shehena za mizigo na kupewa lishe duni.

Aidha, muamko mdogo wa jamii juu ya haki za wanyama, uvunjaji wa sheria, kasoro za

kijamii na kiutamaduni zinafafanuliwa kama ndio sababu zinazochangia hali hizo.

Page 23: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

7

Mazingira hayo yanasababisha kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa na matumizi mabaya ya

wanyama hapa Zanzibar.

2.1.7. Uzalishaji na matumizi ya bayogesi

Wanyama hasa ng'ombe wanaweza kutumika kuzalisha bayogesi kwa ufanisi kama chanzo

mbadala cha nishati. Nishati hii ni rafiki kwa mazingira na kama itatumika kwa usahihi

inaweza kupunguza gharama za uzalishaji katika makampuni ya biashara ya mifugo.

Teknolojia hii bado ni changa hapa Zanzibar na mitambo 17 ya bayogesi hadi sasa

imefungwa. Ukosefu wa elimu na gharama kubwa za ufungaji wa mitambo ya bayogesi ni

miongoni mwa sababu za kupungua matumizi ya teknolojia ya mitambo ya bayogesi kwa

wafugaji. Ikiwa sababu hizi zitashughulikiwa ipasavyo, wazalishaji wa mifugo wanaweza

kufaidika kwa kufunga mitambo ya bayogesi inayoweza kuongeza kiwango cha kipato na

hali ya maisha.

2.1.8.Fursa za masoko

Masoko kwa ajili ya mazao ya mifugo yamegawika sehemu tatu hapa Zanzibar. Nayo ni

soko la ndani, utalii na nje. Hata hivyo,fursa ya masoko kwa wazalishaji wa mifugo kwa

jumla inakwazwa na uchache na ukosefu wa ubora wa bidhaa, uhifadhi, utunzaji na

usindikaji duni, udhaifu wa vifungashio , ukosefu wa alama za utambulisho wa ubora na

uduni wa usafi wa kiafya na wa kimazingira kwa jumla. Aidha, Usafirishaji wa mazao ya

mifugo kutoka shambani kwenda sokoni unafanywa kwa njia ya baiskeli,gari ya ng’ombe,

motor-baiskeli au gari ndogo.Jambo hili linaendeshwa na ama wazalishaji wenyewe au

watu wa kati ambao hawajali sana utunzaji wa ubora na kuzuia kuharibika kwa maziwa .

Hatua mbalimbali zimechukuliwa kuimarisha uzalishaji, ubora na uongezaji thamani wa

mazao yote ya mifugo.

2.1.9. Maradhi ya Zoonotiki

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Ulimwenguni karibu asilimia 61 ya maradhi yote ni ya

zoonotiki yanayofanya asilimia 75 ya maradhi yote yaliyojitokeza katika miongo iliyopita.

Hivi sasa, katika nchi zinazoendelea, wakazi zaidi wa vijijini wanaishi pamoja na mifugo

yao, wanatumia bidhaa za mifugo bila ya kufanyiwa ukaguzi sahihii na usindikaji. Mambo

haya yanaongeza hatari ya kuambukizwa magonjwa ya zoonotiki. Zanzibar kama zilivyo

Page 24: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

8

nchi nyingine zinazoendelea, watu wengi zaidi wanaishi maeneo ya vijijini na

wanategemea wanyama kwa ajili ya maisha yao. Uwiano kati ya wanyama na binadamu ni

2:01. Uhusiano huu unaongeza hatari ya kuambukizwa magonjwa ya zoonotiki. Magonjwa

haya, hivi sasa yanafanyiwa uchunguzi, lakini, uwezo mdogo wa uchunguzi, chanjo na

huduma za afya ya wanyama unakwaza azma ya utekelezaji wa zoezi hili. Hata hivyo,

uchunguzi wa magonjwa unaendeshwa na wakulima wadogo wa mifugo kwa ajili ya

kutaka kuelewa kiwango cha ukubwa wa magonjwa. Magonjwa maarufu ya zoonotiki

yaliyoripotiwa ni Brucellosis, kifua kikuu, kichaa cha mbwa, kimeta na maambukizo ya

salmonella.

2.1.10. Maradhi ya Wanyama Yanayovuuka Mipaka

Magonjwa yanayovuuka mipaka ni magonjwa yanayotokea katika bara la Afrika na

huathiri uchumi. Ili kuweza kudhibiti magonjwa haya kitaifa, kikanda na kimataifa kwa

ufanisi, hatua madhubuti lazima zichukuliwe. Miongoni mwa maradhi makubwa ya

wanyama yanayovuuka mipaka yalioripotiwa Zanzibar ni pamoja na kichaa cha mbwa,

Ugonjwa wa Miguu na Midomo, Chambavu na Magonjwa ya Ngozi na Magonjwa ya

Newcastle katika kuku. Matukio mengi ya Magonjwa Yanayovuuka Mipaka huripotiwa

kila mwaka na hudhibitiwa kwa chanjo ya kila ugonjwa unaohusika. Mwaka 2010, kati ya

matukio ya maradhi makubwa ya wanyama yanayovuuka mipaka yalioripotiwa ni pamoja

na 5 kichaa cha mbwa, 659 Ugonjwa wa Miguu na Midumo, 79 Chambavu, 198

ugonjwa wa ngozi, 1820 Gumboro, 10,254 ya NCA na 43,241 ya Helminthus. Hata

hivyo, kikwazo kikubwa kinachopunguza kasi ya chanjo kushindwa kuenea katika maeneo

yote ni utaratibu unaowataka wafugaji kulipia huduma.

2.1.11. Utoaji wa huduma za maabara

Huduma za maabara hutolewa na Kituo cha Uchunguzi wa Mifugo ambacho kipo

Maruhubi Zanzibar na maabara ya mifugo ilioko Chakechake, Pemba. Huduma zote za

maabara kama vile za uchambuzi wa mlo, Uchunguzi wa maradhi ya parasitologia na

mikrobayolojia zinafanywa. Hata hivyo, huduma hizi zinakwazwa na uchache wa vifaa,

vitendanishi na wafanyakazi wenye sifa zinazohitajika. Katika miaka iliopita, huduma za

maabara zilitolewa katika vituo vyote vya afya ya wanyama na Uzalishaji hapa Zanzibar.

Vituo hivi vimeacha kutoa huduma hizi kutokana na uhaba wa vifaa na vitendanishi.

Page 25: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

9

2.1.12. Utoaji wa huduma za mifugo na elimu kwa wakulima

Huduma za mifugo na elimu kwa wakulima ni muhimu kwa maendeleo ya sekta ya

mifugo. Huduma hizi hutolewa kwa wafugaji kupitia vituo vya afya ya wanyama na

uzalishaji ambavyo viko katika kila wilaya. Kwa jumla utoaji wa huduma ni duni kutokana

na kuongezeka kwa idadi ya wafugaji. Wakati idadi ya wafanyakazi iko chini, imeripotiwa

kwamba asilimia 26 tu ya familia zenye mifugo ndizo hupata huduma za elimu kwa

wakulima (Sampuli ya Taifa ya Sensa ya Kilimo na Mifugo, 2003)

2.1.13. Biashara ya Mifugo

Zanzibar haizalishi mazao ya kutosha ya mifugo ili kukidhi mahitaji yake ya ndani.

Mifugo mengi na bidhaa za mifugo zinazotumika hapa Zanzibar ikiwa ni pamoja na sekta

ya utalii zinaagizwa kutoka nje. Mbia mkubwa wa biashara ya mifugo ni Tanzania Bara.

Mwaka 2011, Zanzibar iliagizia ng’ombe7706, mbuzi 2,247, kondoo 255, tani 10,710 za

nyama ya ng'ombe, tani 435,316 za nyama na mayai ya kuku 1,585,360 kutoka Bara. Hadi

sasa, ngozi tu ndio inayosafirishwa kwenda Tanzania Bara. Mwaka 2010, Zanzibar

ilisafirisha vipande vya ngozi 2,793 Tanzania Bara. Hata hivyo, jitihada zinafanywa

kupunguza mwanya wa uzalishaji kwa kuimarisha miundombinu ya uzalishaji na masoko.

2.1.14. Utoaji wa huduma za fedha

Huduma za fedha kwa ajili ya maendeleo ya wajasiriamali wa mifugo ni chache mno. Zipo

baadhi ya taasisi za umma na binafsi zinazotoa huduma za kifedha kwa kiasi kidogo tu.

Taasisi hizi zinajumuisha Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika,

Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake, Changamoto na Pride Tanzania. Aidha, zipo taasisi

chache za kibinafsi na miradi inayotoa ruzuku kama vile Jumuia ya Wafanyabiashara,

Wenye Viwanda na Wakulima na Mradi wa Usimamizi wa Mazingira ya Pwani na

Baharini. Hata hivyo, kuna benki nyingi za kibiashara ikiwa ni pamoja na Barclays,

Benki ya Ushirika na Maendeleo Vijijini, Benki ya Watu wa Zanzibar, Benki ya NMB na

Benki ya Taifa ya Biashara, lakini hakuna benki ya kilimo ambayo kwa makusudi hutoa

mikopo kwa wajasiriamali wa mifugo. Aidha, viwango vya riba katika benki hizi ni

vikubwa mno. Wazalishaji wakiwemo wafugaji hutegemea taasisi zisizo rasmi za fedha

peke yake kama vile SACCOS na UPATU) hasa kwa vikundi vya wanawake.

Page 26: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

10

2.1.15. Ubia kati ya sekta ya Umma na Binafsi

Sera za biashara huria zina lengo la kushirikisha sekta binafsi kikamilifu katika maendeleo

ya kiuchumi. Hivi sasa ushiriki wa sekta binafsi katika biashara ya dawa za mifugo,

vyakula vya kuku, vifaranga na uagiziaji wa bidhaa za mifugo ni mdogo. Kuna

wawekezaji wachache ambao hushiriki katika sekta ya mifugo kama vile kufuga kuku na

uzalishaji wa maziwa. Pamoja na uhamasishaji unaofanywa na Mamlaka ya Uwekezaji

Zanzibar ili kuvutia wawekezaji wa kigeni katika sekta ya mifugo, hadi sasa hakuna

wawekezaji wa kigeni wanaoshiriki katika sekta hii. Sura ya mifugo iliopo hivi sasa

inahitaji kufanyiwa mapitio ili iweze kuakisi uwekezaji, usindikaji wa mazao ya mifugo na

chakula cha wanyama. Uratibu sahihi na ushajiishaji wa sekta binafsi kushiriki katika

maendeleo ya mifugo ni muhimu katika kuongeza nafasi za ajira.

2.1.16. Maendeleo ya rasilimali watu

Wizara imeajiri wafanyakazi 446 kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya mifugo (IKAMA ya

2010-2011). Hata hivyo, karibu asilimia 25 ya wafanyakazi hawa ni wataalamu wa

mifugo (104 sawa na asilimia 23 ya wafanyakazi wamehitimu diploma na wafanyakazi

16 sawa na asilimia 3 wana elimu ya kiwango cha juu ya diploma. Wafanyakazi zaidi

wanahitajika kuimarisha uwezo wa wizara hii kuongeza uzalishaji wa mifugo na tija.

2.1.17. Misaada ya pembejeo

Pembejeo za mifugo ni muhimu kwa maendeleo madhubuti ya sekta ya mifugo. Hivi

sasa, hakuna ruzuku inayotolewa kwa pembejeo za mifugo. Bei za pembejeo hizo ni za

juu sana kwa wafugaji wadogo wadogo kuweza kununua kwa bei ya soko. Matokeo yake,

wafugaji wanazalisha kwa kutumia pembejeo chache tu zinazohitajika. Wafugaji

wanaotumia kiasi cha pembejeo zinazotakiwa, gharama zao za uzalishaji ni kubwa mno.

Hivyo, wazalishaji wa mifugo wa ndani wanashindwa kushindana dhidi ya bidhaa kutoka

nje. Kwa hiyo, jitihada ya kuanzisha utaratibu wa kutoa ruzuku kwa ajili ya maendeleo ya

mifugo ni hatua muhimu itakayochochoea uzalishaji wa ndani wa mifugo na kuongeza

tija.

2.1.18. Mchango wa mifugo katika pato la taifa

Sekta ya mifugo, kama ilivyo katika nchi nyingine zinazoendelea, ni miongoni mwa

vyanzo vikuu vya uchumi wa Zanzibar. Mifugo inatoa mchango muhimu katika familia

Page 27: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

11

na uchumi kwa jumla hapa Zanzibar. Sekta hii inashirikisha zaidi ya familia 36,000

katika uzalishaji wa mifugo na mwaka 2010 ilichangia asilimia 4.7 ya Pato la Taifa. Soko

la ngozi, kwato, manyoya na bidhaa nyenginezo linaweza pia kuongeza mchango katika

sekta ndogo ya mifugo katika uchumi wa taifa. Uimarishaji wa vifaa vya uzalishaji na

pembejeo ikiwa ni pamoja na kuendeleza masoko ya mifugo na mazao yake itachangia

moja kwa moja katika kufikia malengo na shabaha ya MKUZA II.

Hapa Zanzibar uzalishaji wa mifugo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi vijijini na silaha

ya kuifanya nchi kufikia lengo la kuwa na uhakika wa chakula, kupunguza umaskini na

uimarishaji wa jumla wa ustawi wa binadamu. Utoaji na utengenezaji wa ajira zenye

staha katika sekta ya mifugo, hasa kwa wanawake na vijana ni njia kuu ya kuelekea

ukuaji wa kijamii na kiuchumi endelevu na maendeleo vijijini.

2.1.19. Mchango wa mifugo katika uchumi wa familia

Mifugo ni chanzo muhimu cha kujiajiri, chenye kuongeza pato na uhakika wa chakula,

hasa kwa vijana. Karibu asilimia 37.8 kati ya familia 96, 52 zinazotegemea kilimo hapa

Zanzibar zinashiriki katika ufugaji (ukitoa ufugaji wa kuku). Mifugo haifugwi hasa kama

chanzo cha chakula bali inawekwa zaidi kama akiba, hasa wakati wa matatizo ya kifedha.

Shughuli nyingi za kilimo (hasa ufugaji mdogo mdogo wa kuku) unahudumiwa na

wanawake hapa Zanzibar.

Mifugo inatoa mchango muhimu katika uchumi wa familia na jamii hapa Zanzibar.

Wafugaji wadogo wadogo wanaongezeka katika maeneo ya vijijini na kandokando mwa

miji. Mapato ya mwaka yanayotokana na ufugaji wa ng'ombe wa asili ni kiasi cha Sh

120,000 kwa kila mkulima wakati ng’ombe bora ni kiasi cha shilingi 1,200,000. Katika

mwaka 2007, jumla ya Sh 7935000000 na 1810000000 zilichumwa kutokana na kuuza

tani 1,587 na 362 za nyama ya ng’ombe, kondoo na mbuzi kwa kila moja.

2.1.20. Utafiti wa Mifugo

Hivi sasa, hakuna njia sahihi au taasisi maalumu yenye dhamana ya kufanya tafiti. Hata

hivyo, kuna maabara na mashamba yenye idadi ndogo ya watafiti wanaotumiwa kufanya

tafiti. Aidha, kiwango cha chini cha bajeti kinatengwa kwa ajili ya kazi za

utafiti.Halikadhalika, ukosefu wa uratibu kati ya wizara na taasisi za utafiti umepelekea

ushiriki mdogo wa watafiti kutoka taasisi hizo kufanya utafiti wa mifugo hapa Zanzibar.

Page 28: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

12

Katika miaka iliopita, baadhi ya mipango ya utafiti katika sekta ya mifugo ilifanywa

kupitia programu zinazofadhiliwa na wahisani. Ipo haja ya kuimarisha utafiti kwa

kuanzisha taasisi ya utafiti wa mifugo yenye vifaa muhimu na wafanyakazi.

2.1.21. Uhakika wa chakula na lishe

Ingawa maziwa, samaki na vyakula vyengine vya baharini, nyama na mayai vinatoa kalori

kwa wingi, lakini kumbukumbu zinaonesha kuwa kuna matumizi ya viwango vya chini

sana vya kalori (asilimia 4.6, 2.3, 0.5 na 0.1 kwa siku kwa mfuatano). Matumizi haya ya

kiwango cha chini yanasababishwa na watu wengi wa kipato cha chini kukosa uwezo wa

kununua chakula hiki muhimu ingawa kinapatikana katika masoko. Ughali wa bidhaa hizi

ukilinganisha na kipato cha watu wengi wa tabaka la chini inaweza kuwa sababu kuu

inayochangia matumizi ya kiwango cha chini ya kalori. Ukilinganisha mgao wa asilimia ya

mboga na bidhaa za wanyama katika utumiaji wa jumla wa chakula, ni wazi kwamba

bidhaa za mboga zinatumiwa zaidi kuliko za wanyama. Katika mwaka 2007, bidhaa za

mboga zilichangia zaidi ya asilimia 92 ya kalori zote na zaidi ya asilimia 72 ya protini

katika chakula hapa nchini (Mizani ya Chakula Zanzibar, 2007).

2.2. Vikwazo vinavyoathiri Maendeleo ya Mifugo

Licha ya kuongezeka kwa fursa na uwezo kwa mazao ya mifugo kitaifa, kikanda na

kimataifa, lakini kuna mambo mbalimbali yanayokwaza maendeleo ya sekta hii.

Wakati wa mchakato wa utayarishaji wa sera hii, wadau walipata fursa ya kutoa taarifa

muhimu zinazohusiana na changamoto kuu ambazo zinahitaji kupewa kipaumbele

maalumu ili kuendeleza sekta ya mifugo. Changamoto muhimu zilizoelezwa na wakulima,

wafanyabiashara, wasindikaji wa mazao ya mifugo, wafugaji wa wanyama wadogo, walaji

na wadau wengine vinafafanuliwa kwa muhtasari hapa chini:

•Magonjwa na vifo vya wanyama:

Ingawa utokomezaji wa mbungo na Trypanosomosis umefanikiwa kwa kiasi kikubwa,

lakini magonjwa mengine bado yanaendelea kuathiri mifugo hapa Zanzibar. Magonjwa

makubwa yanayoshambulia mifugo yanasababishwa na kupe, hasa Homa ya Afrika ya

Mashariki (ECF) ambayo Inachangia asilimia 89 ya magonjwa yote yanayotokana na kupe

Page 29: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

13

(iliripotiwa mwaka 2007) na homa ya Babesia bovi. Magonjwa mengine ni Chambavu,

Ugonjwa wa Ngozi (LSD), Ugonjwa wa Miguu na Midomo(FMD), bovin mastitis, warm

infestation (asilimia 63 yanawaathiri ng'ombe na asilimia 83.6 mbuzi, kuku asilimia 17),

Ugonjwa wa Newcastle (asilimia 42 ) na Gumboro (asilimia 48) katika makundi ya kuku

wa kibiashara.

• Upungufu na matumizi madogo ya teknolojia: Elimu ndogo ya wafugaji ni

Sababu kuu inayochangia kupungua kwa kasi ya matumizi ya teknolojia mpya ya

uzalishaji,

• Upungufu katika usindikaji wa mazao: Hatua chache zimechukuliwa za usindikaji wa

mazao ya mifugo hapa Zanzibar jambo lililosababisha bidhaa nyingi kuuzwa zikiwa

ghafi kwa bei ya chini,

• Masoko yasiosimamiwa: Hakuna mfumo rasmi wa masoko na makampuni mengi ya

biashara ya mifugo bado ni machanga na hayasimamiwi ipasavyo,

• Wizi wa Mifugo: Wizi wa mifugo ni moja kati ya kikwazo kikuu kinachoathiri

maendeleo ya mifugo ambacho kilitajwa na asilimia 46 ya wadau. Aidha, kuna

ongezeko la wizi wa mazao ya kilimo ambao unakatisha tamaa shughuli za ufugaji,

• Gharama za juu za pembejeo: Bei ya mnyama, dawa na vyakula imeongezeka baina ya

asilimia 92 na 110 kati ya 2005 na 2008 ikilinganishwa na ongezeko la bei za bidhaa

zilizofikia asilimia 43. Hali hii inasababishwa pamoja na sababu nyingine na gharama

kubwa za usafirishaji hasa ukizingatia kwamba pembejeo nyingi zinaagizwa kutoka

Tanzania Bara na nje ya nchi. Aidha, kiwango cha mfumuko wa bei kimeelezwa

kuchangia kiwango cha juu cha ubadilishaji fedha unaosababishwa na mahitaji

makubwa ya fedha za kigeni,

• Huduma na kituo duni cha utafiti: Kwa kawaida utafiti na elimu kwa wakulima

hutengewa fedha kidogo sana. Shughuli za utafiti na elimu kwa wakulima mara nyingi

zinaendeshwa kupitia miradi inayofadhiliwa na wahisani,

• Uchache wa rasilimali: Kuna maeneo makuu manne yanayochangia maendeleo duni

katika sekta ya mifugo hapa Zanzibar unaotokana na uhaba wa rasilimali. Maeneo

yenyewe ni:

Rasilimali fedha: Kwasababu ya kuwepo kwa fursa chache za mikopo, wafugaji

wanaachwa na mitaji midogo ya uwekezaji,

Page 30: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

14

• Raslimali Ardhi: Kwa kuwa Zanzibar ni visiwa vidogo, ufugaji unakabiliwa na uhaba

wa ardhi,

• Rasilimali maji: Uhaba wa malisho unapelekea kutegemea kwa kiasi kikubwa mvua za

msimu kwa ajili ya mazao, ukuaji na uotaji wa malisho,

Rasilimali watu: Kuna idadi ndogo ya wataalamu. (Kiasi cha asilimia 25 ya

wafanyakazi waliopo). Wafanyakazi wengi wa mashambani ni wazee na hivyo

hushindwa kutekeleza kazi za kilimo kwa ufanisi.

• Kilimo hai cha mifugo: Uzalishaji wa bidhaa za wanyama umepata umuhimu mkubwa

katika soko la kimataifa. Jambo hili linasababishwa kwa kiasi kikubwa na kuongezeka

kwa hamu ya mataifa yaliyoendelea juu ya uhakika wa chakula. Kwa kawaida, bidhaa

ambazo zimethibitishwa kuwa hai huhitajiwa sana katika nchi hizi. Nyama, maziwa,

mayai na kuku ni bidhaa tu zenye angalau uwezekano wa kuzalishwa hapa Zanzibar.

Kwa bahati mbaya, kipaumbele kidogo kimewekwa katika utafiti na uzalishaji wa

mazao ya kilimo hai cha mifugo hapa Zanzibar.

• Wizi wa mifugo: kuongezeka kwa matukio ya wizi wa mifugo katika miaka ya hivi

karibuni kumekwaza juhudi za wafugaji za kuendeleza kampuni za ufugaji.

• Miundombinu duni ya mifugo: Hivi sasa, miundombinu mengi ya mifugo kama vile

majosho, machinjio na kliniki za wanyama zimechakaa na hazifanyi kazi. Kuna

majosho mawili tu kati ya tisa yanayofanya kazi.

2.3. Fursa kwa ajili ya maendeleo ya mifugo

Fursa ni mambo ya ziada ambayo yanasaidia kujenga msingi wa Wizara ya Mifugo na

Uvuvi kuweza kufanya kazi kwa ufanisi ili kufufua maendeleo ya mifugo hapa Zanzibar.

Fursa hizi ni pamoja na:

• Maliasili za kutosha ikiwa ni pamoja na maji ya chini ya ardhi.

• Mitandao ya kawaida ya usafirishaji na mawasiliano ya simu ambayo yanawasaidia

wadau wa mifugo kutoa huduma.

• Fursa za upatikanaji wa uhakika wa umeme inatoa huduma bora za uhifadhi wa

mazao ya mifugo na viwanda vidogo.

• Kuongezeka kwa mahitaji ya ndani ya mazao ya mifugo kunakosababishwa na upanuzi

wa soko la utalii na watu wengine wenye kipato cha tabaka la kati.

• Kuna wigo nzuri wa uwekezaji katika usindikaji wa mazao ya mifugo.

Page 31: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

15

• Kuongeza fursa ya uwekezaji katika sekta ya maziwa na nyama ya ng'ombe kufuatilia

ubora na mfumo wa kitaasisi wa kuvutia sekta binafsi kushiriki katika utoaji wa

huduma.

• Upatikanaji wa maeneo ya maweni yenye wingi wa mimea ambayo inaweza kutumika

katika uzalishaji wa mbuzi.

• Kuwepo kwa taasisi za kitaaluma nchini (Zanzibar na Bara) ambazo zinaweza kutumika

kutoa utaalamu wa kuzalisha mifugo.

• Upatikanaji wa jumuia za kiraia za ndani na kimataifa zenye uwezo wa kuchangia

maendeleo ya mifugo.

• Umoja wa Kitaifa, amani na utulivu.

• Upatikanaji wa wahisani ambao wako tayari kusaidia maendeleo ya mifugo.

• Nia na dhamira ya wadau kushiriki katika programu za maendeleo.

• Kuwepo kwa vijana, wanawake na makundi mengine ya pembezoni ambayo yanaweza

kushiriki katika shughuli fulani ya sekta ya mifugo.

• Kwa kuwa Zanzibar ni kisiwa, inaweza kutokomeza na kudhibiti Magonjwa

Yanayovuuka Mipaka na mengine ya zoonotiki.

Page 32: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

16

SURA YA 3: MAPITIO YA SERA ZINAZOHUSIANA NA MIFUGO

.1. Maelezo ya Jumla

Sura hii inatoa ufafanuzi wa sera mbalimbali za kisekta, mikakati na mipango

inayohusiana na sekta ya maendeleo ya mifugo.Sera hii imeainisha na kufanya uchambuzi

wa kina wa mianya ya sera tafauti ambayo ndio msingi wa uandaaji wa sera ya mifugo.

Sekta zenye uhusiano wa moja kwa moja na maendeleo ya mifugo ndizo tu

zilizofafanuliwa. Kwa ujumla, mapitio ya nyaraka hizo yamedhihirisha kwamba masuala

ya mifugo hayakujumuishwa ipasavyo katika sera nyingi zilizopo.

3.1.1. Sera ya Sekta ya Kilimo

Sekta ya kilimo inajumuisha mazao, uvuvi, na ufugaji. Lengo kuu la Sera ya Kilimo ya

mwaka (2002) ni kukuza maendeleo endelevu ya sekta ya kilimo ili iweze kutoa faida za

kiuchumi, kijamii na kimazingira. Umuhimu wa mifugo katika sera hii haukufafanuliwa

vyema. Hata hivyo, changamoto nyimgi zimezingatiwa ikiwa ni pamoja na umuhimu wa

mifugo katika uchumi, matumizi ya mazao ya mifugo, kuongeza mavuno katika mfumo

wa ufugaji wa jadi, biashara ya bidhaa nyama na maendeleo ya maziwa.Lakini kwa

upande mwengine, sera hii haikuweza kuzingatia ipasavyo CHANGAMOTO kama zile

uzalishaji wa mazao ya mifugo isiyo ya kawaida, ustawi wa wanyama na maendeleo ya

uzalishaji,matumizi ya nishati inayotokana na wanyama, fursa ya masoko, kuongeza

thamani, huduma za fedha na ridhaa kama njia ya kuwawezesha wajasiriamali kuweza

kukabiliana na changamoto za ushindani wa soko.

3.1.2. Sera ya Chakula na Lishe.

Sera ya Uhakika wa Chakula na Lishe Zanzibar (ZFSNP, 2008) inatambua umuhimu wa

kilimo ikiwemo mifugo kama shughuli muhimu ya kuongeza kipato kwa jamii za vijijini

na kandokando mwa miji. Kwa upande mwingine, kuongezeka kwa chakula na uhakika wa

lishe hutegemea kwa kiasi kikubwa maendeleo endelevu ya sekta hii. Aidha, lengo kuu la

Page 33: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

17

Sera ya Mifugo Zanzibar ni kuongeza uzalishaji na tija ya mifugo kwa lengo lilelile kama

lilivyoainishwa katika Sera ya Uhakika wa Chakula na Lishe.

3.1.3. Sera ya Misitu

Sera ya Misitu ya mwaka (1996) imejikita zaidi katika eneo la hifadhi ya bayoanuai na

maendeleo ya rasilimali za misitu kwa ajili ya vizazi vijavyo, upandaji wa miti na utoaji

wa elimu kwa umma. Ingawa sera hii imejaribu kuingiza kanuni za mazingira katika

shughuli za usimamizi wa misitu, lakini imekaa kimya katika masuala ya ushiriki wa sekta

ya mifugo katika usimamizi na matumizi ya rasilimali za misitu. ZLP inasaidia uzalishaji

wa miti yenye matumizi anuai (kwa mfano Leucaena na Moringa) kama vyanzo vya

malisho.

3.1.4. Sera ya Maji

Maji ni nyenzo muhimu sana kwa maendeleo ya mifugo, hasa katika kuongeza maziwa,

nyama, mayai na bidhaa nyingine. Lengo kuu la Sera ya Maji ya Taifa ya mwaka (2004) ni

kulinda na kuhifadhi rasilimali maji kwa ajili ya matumizi endelevu. Umuhimu wa sekta

ya kilimo umeeleweka vyema katika sera hii. Hata hivyo, masuala maalumu

yanayohusiana na matumizi ya rasilimali hii kwa ajili ya maendeleo ya mifugo bado

hayajapewa msukumo unaofaa. Sera mpya ya mifugo inatoa fursa ya kuoanisha masuala

ya mifugo na maji.

3.1.5. Sera ya Ardhi

Hivi sasa, Zanzibar haina sera rasmi ya ardhi.Hata hivyo, Mpango wa Taifa wa Matumizi

ya Ardhi (1995) unatambua umuhimu wa kilimo kama ni mtumiaji mkuu wa ardhi.Kilimo

kinatumia asilimia 60 ya jumla ya eneo lote. Maeneo makuu manne ya kilimo ekolojia ni

miti na mashamba makubwa, maweni, mashamba ya serikali au ranchi au maeneo ya

kilimo cha mpunga yamefafanuliwa katika mpango huu. Hata hivyo, mpango huu

hautambui uwezekano wa kupanuka kwa uzalishaji wa mifugo katika maeneo ya maweni.

Sera hii inaweka matumizi makubwa ya ardhi ya maweni kwa ajili ya uzalishaji wa

wanyama wenye kucheua, ufugaji wa kuku na wanyama wengine wasio wa kawaida.

Page 34: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

18

3.1.6. Sera ya Mazingira

Sera ya Mazingira ya mwaka 1992 imepitwa na wakati. Hata hivyo, sera hii imetoa

muongozo wa mfumo wa usimamizi wa mazingira katika vyanzo vya maji, udongo wa

ndani, ukanda wa pwani na maweni kwa ajili ya ulinzi na hifadhi. Mazoea ya binadamu

ikiwa ni pamoja na mbinu duni za uzalishaji wa mazao, ulishaji wa mifugo kupita kiasi

katika eneo moja na ukataji miti inasisitizwa kuwa ndiyo sababu kubwa ya uharibifu wa

mazingira. Hata hivyo, sera hii haijaangalia suala la udhibiti wa idadi ya mifugo katika

kupunguza shinikizo la malisho ya mifugo na uwezekano wa uchafuzi wa hewa kwa

maisha ya binadamu kwa mfano, amonia, methane na gesi nyingine. Sera mpya ya mifugo

inasisitiza juu ya utunzaji wa mifugo kwa kuzingatia ukubwa wa eneo na kuhamasisha

matumizi ya malisho ya asili tafauti na vyakula vya viwandani vyenye naitrojini nyingi

kama vile urea.

3.1.7. Biashara ndogo na kati

Lengo la jumla la sera ya Biashara Ndogo na Kati ya mwaka (2006) ni kujenga mazingira

bora ya kuendeleza biashara ndogo na kati kwa lengo la kuongeza fursa za ajira na mapato.

Sera hii inahusiana moja kwa moja na sekta ya maendeleo ya mifugo hasa ikizingatiwa

kwamba mifugo inaweza kusimama kama biashara inayojitegemea inayoweza kutoa nafasi

ya kujiajiri na hatimae kuongeza pato la familia na taifa.

3.1.8. Sera ya Biashara

Uwezeshaji wa kusimamia shughuli zinazohusiana na biashara hapa Zanzibar umeelezwa

kama lengo kuu la sera ya Taifa ya Biashara (2006). Dhana ya kuimarisha ushiriki wa

sekta binafsi katika biashara ya bidhaa na huduma chini ya sera hii inaoana na lengo kuu la

sera mpya ya mifugo ambayo inaimarisha huduma za kibiashara za mifugo na mazao chini

ya mwevuli wa ubia baina ya sekta ya binafsi na umma. Hata hivyo, msamaha wa kodi na

ushuru wa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje na vyakula (ikiwa ni pamoja na bidhaa za

mifugo) zinakwaza uzalishaji na utumiaji wa bidhaa za mifugo. Uanzishwaji wa Shirika la

Viwango Zanzibar utatoa fursa ya kudhbiti ubora wa pembejeo za mifugo kama vile

chakula cha wanyama, dawa na mazao ya mifugo.

Page 35: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

19

3.1.9. Sera ya Viwanda

Sera ya Viwanda ya Zanzibar ya mwaka (1998) pamoja na mambo mengine,

Inashughulikia masuala muhimu yanayoikabili sekta ya viwanda na kuweka matumizi bora

ya maliasili hasa kilimo, mazao ya baharini na misitu. Hata hivyo, sera hii haikuzingatia

maendeleo ya usindikaji mdogo mdogo wa mazao ya mifugo. Sera hii inashughulikia

masuala ya fursa chache za uwekezaji ambazo zinakatisha tamaa uendelezaji wa sekta ya

kilimo na zinazohusiana nazo ikiwemo mifugo. Sera mpya ya Mifugo inashajiisha

uanzishaji wa viwanda vidogo kwa ajili ya usindikaji na ufungashaji wa mazao ya mifugo

na bidhaa zake.

3.1.10. Sera ya Uwekezaji

Sera ya Uwekezaji ya Zanzibar ya mwaka (2005) inaelekeza kufanya mabadiliko

makubwa ya kimuundo na kitaasisi yenye lengo la kukuza uwekezaji wa sekta binafsi.

Sera hii imezingatia mipango ya maendeleo ya biashara kwa kuanzisha Ukanda Huru wa

Kiuchumi. Aidha, sera hii inakubaliana na haja ya kuimarisha sekta ya huduma na

kuihusisha na sekta ya utalii. Sera ya Mifugo Zanzibar inatambua fursa bora ya uwezekano

wa ukuaji wa sekta hii pamoja na ujasiriamali, ukuaji wa haraka wa sekta ya utalii na

maendeleo ya sekta ya huduma.Aidha, Sera hii inatoa fursa kwa wakazi wa mijini na

vijijini kufaidika na sekta ya uwekezaji:

3.1.11. Sera ya Afya

Sera ya Afya ya Zanzibar ya mwaka (2002) imetaja mikakati ya kuimarisha na kuendeleza

lishe ya binadamu, hasa kwa wale wenye magonjwa ya muda mrefu, wanawake na watoto.

Ili kufikia lengo hili, sera hii inalenga kuhakikisha kuwa kunakuwepo ugawaji wa vyakula

bora vya kutosha na utunzaji salama. Sera ya Mifugo Zanzibar inasisitiza kuongeza

uzalishaji wa bidhaa zenye lishe ya mifugo ambazo hazina magonjwa ya kuambukiza na

zoonosisi kama vile kifua kikuu, brucellosis, salmonellosis nk

3.1.12. Sera ya Elimu

Sera ya Elimu ya Zanzibar ya mwaka (2006) inatambua umuhimu wa kufundisha

masomo ya kilimo ikiwa ni pamoja na uhifadhi wa udongo, ufugaji, lishe ya binadamu

nk. Aidha, sera hii inasisitiza kuingiza masuala ya masomo ya mifugo katika mafunzo ya

msingi, sekondari na amali.

Page 36: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

20

3.1.13. Mpango wa Taifa wa Kudhibiti VVU na UKIMWI ZANZIBAR

Mbali na hatua za kimkakati za kudhibiti na kuzuia kuenea zaidi kwa ugonjwa huo,

Mpango Mkakati wa VVU/UKIMWI (2004 / 5-2008 / 9) umebainisha maeneo matano

yanayopaswa kuchukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na huduma za afya na misaada kwa

watu wanaoishi na VVU na UKIMWI. Mbali na kuoanisha elimu ya VVU na UKIMWI

katika mfumo wa elimu kwa wakulima wa mifugo,Sera hii pia inasisitiza juu ya

uwezeshaji wa kundi hili maalumu la watu kwa kuwapatia stadi na mitaji ya uwekezaji

kwa ajili ya uzalishaji mkubwa wa mifugo ikiwa ni pamoja na kuku.

3.1.14. Sera ya Ajira

Sera ya Ajira ya Zanzibar ya mwaka (2008) inathamini umuhimu wa kilimo (ikiwa ni

pamoja na mifugo) kama chanzo muhimu cha ajira kwa jamii za vijijini, hasa wanawake

na vijana. Kama ilivyo Sera ya Ajira, Sera ya Mifugo Zanzibar pia inasisitiza uwekezaji

wa sekta binafsi katika uzalishaji na masoko ya bidhaa za asili na zisizo za asili ili

kuongeza mapato ya taifa na fursa za ajira katika sekta hii.

3.1.15.Sera nyengine za kisekta na Mipango inayohusiana na Maendeleo ya Mifugo

Pamoja na sera na mipango iliyotajwa katika sehemu ya 3.1.1 na 3.1.14,zipo sera nyingine

na / au mipango ambayo kwa njia moja au nyengine inasaidia utekelezaji wa sekta ya

mifugo. Hii ni pamoja na fedha, takwimu, ustawi wa jamii, wanawake, ulinzi, utalii,

masoko, mawasiliano ya simu, maendeleo ya jamii na sera za Jumuia Zisizo za Kiserikali.

Hata hivyo, hakuna mifumo jumuishi kwa ajili ya ufuatiliaji wa mianya hiyo. Aidha,

ukosefu wa sera ya masoko ya kilimo unaathiri maendeleo ya sekta ya mifugo.

Page 37: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

21

SURA YA 4 : MKAKATI WA SERA

4.1. MAPITIO

Zanzibar ina lengo la kukifanya kilimo kuwa cha kisasa na kuendeleza mifugo. Dira ya

Maendeleo ya Zanzibar ya 2020 inatilia mkazo kilimo cha kisasa ili kuweza kujitosheleza

kwa chakula na kuwa na uhakika wa chakula.Hatua hiyo itafikiwa kwa njia ya kuongeza

chakula, uzalishaji wa mifugo na kilimo kwa ajili ya kuuza nje ili kuhakikisha kwamba

sekta hii inaweza kutosheleza kwa asilimia 50 au zaidi ya uzalishaji wa chakula nchini, na

kuendeleza njia mbadala ya uzalishaji wa mazao ya biashara kwa ajili ya kuuza nje.

Sera za maendeleo ya taifa, mikakati na mipango ya Zanzibar inaongozwa na mfumo

mkuu wa sera - Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini

Zanzibar (MKUZA II). Mageuzi ya kiuchumi chini ya usimamizi wa mfumo wa MKUZA

II yanalenga katika maeneo mawili: ukuzaji uchumi na maendeleo ya miundombinu.

MKUZA II sambamba na Malengo ya Maendeleo ya Milenia inaelezea kwa kina kuhusu

klasta zote tatu zinazohusiana yaani, kukuza uchumi na kupunguza umaskini, huduma za

jamii na ustawi, na utawala bora na umoja wa kitaifa.Klasta 1 ya MKUZA II inalenga

katika kufikia ukuaji wa juu na uendelevu wa uchumi unaozingatia masikini wenye

malengo mahsusi matatu ambayo ni: kujenga mazingira bora ya ukuaji wa juu wa uchumi

endelevu; kukuza uchumi endelevu unaozingatia maskini na ukuaji wa uchumi wenye

wigo mpana, na kupunguza umaskini wa kipato na kufikia lengo la uhakika wa chakula.

MKUZA II umeweka mfumo wa kufikia Dira ya Maendeleo (Dira ya 2020).

4.1.1. Dira

Dira ya Sera ya Maendeleo ya Mifugo Zanzibar ni kujenga sekta ya mifugo yenye

kusitawi itakayochangia kipato kwa familia,kua na uhakika wa chakula, kuongeza kasi ya

ukuaji wa uchumi wa taifa na kwa kiasi kikubwa kupunguza umaskini ifikapo mwaka

2020.

4.1.2. Dhamira

Dhamira ya Sera ya Mifugo Zanzibar ni kuendeleza ufanisi wa kitaalamu na kuwa na

Page 38: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

22

sekta ya mifugo yenye kulenga biashara inayolinda mazingira na maliasili kwa vizazi vya

sasa na vijavyo.

4.1.3. Madhumuni

4.1.3.1 Lengo Kuu

Lengo kuu la Sera ya Mifugo Zanzibar ni kusimamia utekelezaji wa shughuli mbalimbali

kwa ajili ya maendeleo ya mifugo ambayo hatimae itaimarisha ustawi wa jamii na kuleta

maendeleo endelevu ya uchumi wa taifa na kupunguza umaskini kwa mujibu wa

MKUZA II na Dira 2020.

4.1.3.2. Malengo Mahsusi:

i. Kulinda afya, ustawi na usimamizi wa mifugo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji na tija

katika wigo mpana wa mazingira ya kilimo cha kiikolojia,

ii. Kuimarisha uhakika wa chakula na lishe kwa familia na taifa.

iii. Kuimarisha usimamizi wa mipango jumuishi na matumizi endelevu ya rasilimali za asili

kwa ajili ya uzalishaji wa mifugo.

iv. Kupanua wigo wa bidhaa za wanyama kwa kuanzisha mtandao wa wanyama wasio wa

kawaida wenye thamani.

v. Kuimarisha viwango vya usafi wa zizi na kuongeza thamani ya mazao ya mifugo kwa

ajili ya viwanda vya ndani na soko la nje.

vi. Kuimarisha maendeleo ya rasilimali watu kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya mifugo.

vii. Kuhimiza matumizi ya nishati zinazotokana na wanyama kwa ajili ya usafiri na chanzo

mbadala cha nishati.

viii. Kuingiza masuala ya kila sekta mtambuka katika sekta ya maendeleo ya mifugo.

ix. Kuendeleza ubia baina ya sekta ya umma na binafsi katika maendeleo ya mifugo.

x. Kuimarisha utafiti wa mifugo na huduma za elimu kwa wakulima kwa lengo la

kuongeza uzalishaji na tija.

xi. Kuimarisha uratibu na ushirikiano na taasisi nyingine zenye malengo yanayolingana.

Page 39: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

23

SURA YA 5: MAENEO YA SERA

5.1. Maelezo ya Jumla

Mifugo ni chanzo cha bidhaa za chakula chenye umuhimu yaani, nyama, maziwa na mayai

hutoa virutubisho muhimu kwa afya ya binadamu.Aidha, mifugo hutupatia bidhaa zisizo

za chakula kama vile ngozi, manyoya, sufu, pembe na menginezo kwa ajili ya mavazi na

mapambo. Aidha, bidhaa za mifugo zinaweza kutumika kama chanzo cha nishati

inayotokana na wanyama, mbolea na bayogesi. Sura hii inatoa maelezo ya malengo,

changamoto, matamko na mikakati ya sera kwa kuzingatia kila moja ya maeneo yafuatayo:

5.1.1. Uzalishaji wa wanyama

5.1.1.1. Kuku

Sekta hii ni chanzo muhimu cha chakula, kipato na ajira. Aidha, ni chanzo cha msingi cha

maisha ya zaidi ya asiliia 60 ya familia za vijijini. Halikadhalika, kuku wana matumizi

mengi ya kijamii na kiutamaduni. Pia sekta ya kuku inahusiana na sekta nyingine za

kiuchumi ikiwa ni pamoja na viwanda vya vyakula, hoteli na wauzaji wa pembejeo.

Kutokana na upungufu wa data za kutosha kuhusu uhusiano huo, thamani halisi ya

mchango wa sekta ya kuku kwa uchumi wa nchi bado haujajuilikana, lakini mchango wa

kuku unaweza kuwa juu zaidi ya wastani wa takwimu zinazokadiriwa hivi sasa.

Sekta ya kuku imegawanywa katika mfumo wa uzalishaji wa jadi na wa kibiashara hapa

Zanzibar. Mfumo wa jadi umechukua nafasi kubwa na unachangia kiasi cha asilimia 89 ya

kuku wote.Aina ndogo ndogo ya kuku wa asili ni pamoja na Kuchi, Kishingo, Kuchere na

Kibete. Uzalishaji wa kuku kibiashara unafanyika zaidi katika maeneo ya mijini na

kandokando mwa miji. Kuku maarufu na michanganyiko yao ni pamoja na wa mayai na

wanyama.

Changamoto

Mfumo wa uzalishaji wa kuku kibiashara na kienyeji unakwazwa na magonjwa, lishe duni,

uhaba wa huduma za misaada ya kitaalamu, uwezo mdogo wa kuku kuweza kuzaliana,

elimu ndogo ya masoko na uchanga wa jumuia za wakulima. Aidha, hakuna muundo wa

udhibiti katika utotoaji wa vifaranga na mashamba ya uzalishaji.

Page 40: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

24

Lengo

Kuendeleza sekta ya kuku na kuongeza kasi ya uzalishaji na fursa ya masoko na mifumo

ya kibiashara na ya kienyeji ya ufugaji wa kuku.

Tamko la Sera

Hatua maalumu zitachukuliwa kuimarisha ubora wa kuku na mazao yake ili kukidhi

mahitaji ya ndani, kuongeza mauzo ya nje na kuendeleza ufugaji wa kuku endelevu.

Mikakati ya Sera

Kusaidia na kuongeza huduma za misaada ya kitaalamu na matumizi ya teknolojia

katika uzalishaji wa kuku.

Kukuza, kuainisha, kutathmini na kuteua mifugo ya kuku wa asili.

Kuendeleza na kuimarisha uwezo wa kuku wa asili ili kuongeza uzalishaji wa mifugo

kwa kushirikiana na wadau wengine.

Kuhamasisha uwekezaji katika uzalishaji, usindikaji na masoko ya kuku.

Kuhimiza uanzishwaji wa mashamba bora ya uzalishaji, viwanda vya chakula na

vifaa vya utotoaji.

Kuendeleza na kukuza ufanisi wa mfumo wa habari na taarifa za masoko ya kuku na

vyama vya wakulima wa kuku ili kusitawisha ufanisi wa masoko.

Kuwezesha, kutambua, kuchunguza, kutibu na kudhibiti magonjwa ya kuku kwa

wakati.

Kukuza na kuongeza thamani ya mazao ya kuku katika masoko.

Kuwezesha kufanya mapitio ya mara kwa mara na matumizi ya malisho

yyaliyothibitishwa na viungo vyengine kama vile myco-toxin binders, chakula cha

ukuzaji, vimengenya na acidifiers ili kuimarisha ubora wa vyakula vinavyopatikana

nchini.

Kukuza uwezo wa utotoaji, wazalishaji na wafanyabiashara kwa ajili ya kuongeza

uzalishaji.

5.1.1.2. Kondoo na mbuzi

Ufugaji wa kondoo na mbuzi ni shughuli muhimu ya kiuchumi kwa ajili ya watu

wanaoishi katika maeneo ya maweni. Inakadiriwa kwamba karibu asilimia 10 ya familia

zinazojishughulisha na kilimo hapa Zanzibar zinafuga kondoo na mbuzi.Familia hizi

Page 41: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

25

zinafanya asilimia 26 za ufugaji ambazo kwa pamoja zinamiliki mbuzi 52,324 na kondoo

300. Uwezo wa wanyama hawa kuongezeka na ukuaji wao unakwenda kwa kasi zaidi

kuliko ng’ombe.Kwa hivyo kutokana na gharama ndogo za uendeshaji za wanyama hawa

imekuwa kivutio zaidi kwa wakulima wadogo wadogo.

Changamoto

Licha ya umuhimu wao wa kiuchumi kwa jamii, uzalishaji wa wanyama hawa

unakwazwa na lishe duni, magonjwa, uwezo mdogo wa vinasaba na miundombinu duni

ya masoko.

Lengo:

Kuimarisha uzalishaji wa wanyama hawa kwa kupunguza vikwazo viliopo.

Tamko la Sera

Serikali itaendeleza biashara na uzalishaji endelevu wa kondoo na mbuzi ili kukidhi

mahitaji ya ndani na soko la nje, kuongeza uhakika wa chakula na kipato.

Mikakati ya Sera

Serikali itasaidia na kuimarisha huduma za misaada ya kitaalamu katika uzalishaji wa

kondoo na mbuzi.

Serikali itaendeleza mpango wa hesabu, uainishaji wa makundi ya wanyama hawa,

tathmini na uteuzi wa mifugo ya asili ya wanyama wanaohusika.

Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine itaimarisha uwezo wa vinasaba vya

mifugo vya asili ili kuongeza tija katika mifugo.

Juhudi zitafanywa kuendeleza ubia baina ya sekta ya umma na binafsi ili kuimarisha

usimamizi wa wanyama hawa na mifumo ya masoko.

Serikali itahamasisha uanzishwaji wa vyama vya wafugaji wa kondoo na mbuzi.

5.1.1.3. Ng'ombe wa maziwa

Ng'ombe wa maziwa na wanaofanana nao wameongezeka kwa asilimia 3.5 kutoka 7,908

mwaka 2003 hadi kufikia 8185 mwaka 2011.Wilaya ya Magharibi ina asilimia 46 ya

ng'ombe bora, asilimia 20 wilaya ya Kati, Kaskazini A, Chake Chake na Wete zinafanya

asilimia 28 ya ng'ombe bora wakati wilaya nne zilizobaki zinafanya asilimia 6 tu ya

wanyama hao. Ng'ombe wa maziwa maarufu katika Tanzania ni pamoja na

Page 42: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

26

Friesian, Jersey, Ayrshire, na michanganyiko yao. Vyanzo vya mitamba ya maziwa ni

pamoja na Vitengo vya Kuongeza Mifugo, programu za wafadhili kwa njia ya uagizaji na

upandikizaji wa ng'ombe waliopo ndani. Wastani wa uzalishaji wa maziwa unakadiriwa

kufikia lita 8.8 kwa ng'ombe kwa siku.

Changamoto

Maendeleo ya sekta ya ng’ombe wa maziwa inakwazwa na lishe duni, huduma za msaada

na usambazaji wa maziwa usioridhisha. Vikwazo vingine ni pamoja na uchache wa

huduma za kifedha na mikopo, ukusanyaji na usambazaji duni wa maziwa usiosimamiwa

vyema, vifaa vya usindikaji, matumizi madogo ya maziwa na magonjwa ya mifugo.

Lengo

Kuendeleza sekta ya ng'ombe wa maziwa kwa kuzingatia mambo yote muhimu na huduma

za misaada

Tamko la Sera

Serikali itaendeleza matumizi ya rasilimali zilizopo kwa ajili ya uzalishaji wa maziwa

kibiashara na soko ili kuongeza kipato kwa familia na unywaji wa maziwa na bidhaa za

maziwa kwa kuanzisha mifugo ya wanyama yenye kuzalisha maziwa kitaifa.

Mikakati ya Sera

Kuanzisha mpango wa hesabu, kuainisha makundi ya wanyama, kufanya tathmini na

kuteua mifugo ya maziwa kwa ajili ya kuanzisha ng'ombe wa maziwa kitaifa.

Kukuza vinasaba vya mifugo ya kienyeji kwa kupitia mpango wa uzalishaji

mifugo chotara ili kuongeza tija.

Kuhamasisha matumizi ya upandikizaji (AI) katika mashamba ya umma na

binafsi pale inapowezekana ili kuongeza uwezo wa vinasaba vya mifugo.

Serikali itaendelea na uzalishaji wa mbegu za kiume mpaka wakati sekta

binafsi itapokuwa tayari kuchukua nafasi hii katika shughuli hii muhimu.

Kukuza uzalishaji na matumizi ya maziwa na bidhaa za maziwa.

Kuwezesha wakulima kupata wanyama bora wa maziwa.

Kukuza viwanda vidogo vya maziwa katika maeneo ya vijijini na kandokando mwa

miji, Huduma za elimu kwa wakulima na mfumo wa habari.

Page 43: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

27

Kukuza matumizi ya teknolojia za uzalishaji wa maziwa ambayo itaongeza tija katika

kazi za uzalishaji wa mazao ya mifugo na ardhi.

Serikali itahamasisha na kuendeleza uanzishwaji wa vyama vya maziwa na

kuviimarisha vilivyopo.

5.1.1.4. Ng'ombe wa nyama

Katika mwaka 2003, idadi ya jumla ya mifugo ilikuwa 162,643 kati yao asilimia 95 ni

ng’ombe wenye pembe fupi wa Afrika Mashariki ambao hutumiwa kwa ajili ya uzalishaji

wa nyama. Kundi hili linaundwa na aina ndogo kama vile Mpwapwa na Boran. Asilimia

25 tu ya nyama inayotumiwa inazalishwa hapa Zanzibar na iliyobaki hutoka Tanzania

Bara. Zipo fursa za kunenepesha ng'ombe kwa kutumia wanyama wa kienyeji ikiwa ni

pamoja na ng'ombe wa maziwa.

Changamoto

Hivi sasa, ufugaji wa ngombe wa nyama haufanyiki sana hapa Zanzibar kwa kuwa

unakabiliana na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na uwezo mdogo wa vinasaba vya

mifugo iliyopo, miundombinu duni, kiwango kikubwa cha maambukizi ya magonjwa ya

wanyama, uhaba wa chakula na ardhi, uchanga wa vyama vya wafugaji na uchache wa

huduma za kitaalamu.

Lengo

Kuongeza uzalishaji wa nyama ili kukidhi viwango vya ubora wa soko la ndani na la

utalii, kuongeza mapato ya wafugaji wadogo wadogo, kuimarisha maisha yao na kuwa na

uhakika wa chakula.

Tamko la Sera

Serikali itaendeleza uzalishaji wa kibiashara wa nyama bora ili kukidhi viwango vya

ubora kwa ajili ya masoko ya ndani na kimataifa ili kuongeza mapato ya wakulima wa

mifugo na kustawisha maisha yao.

Mikakati ya Sera

• Kukuza mipango ya feedlot

• Kuendeleza uzalishaji wa nyama ya ng'ombe kwa kutoa

Page 44: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

28

fursa ya kupata mitaji ya uzalishaji.kwa wakulima

• Serikali itaongeza kasi ya kupandisha ng’ombe wenye pembe fupi

wa Afrika ya Mashariki na mifugo mengine ya nyama iliyoainishwa chini ya

ufugaji bora ili kuimarisha uwezo wa vinasaba na kuongeza uzalishaji wa

nyama ili kukidhi mahitaji ya ndani ya soko.

• Kuhimiza wakulima wadogo wadogo kutenga maeneo ya malisho kwa

matumizi endelevu ya rasilimali za malisho zilizopo.

• Kusajili wazalishaji wakubwa wa nyama, machinjio, wasindikaji na maduka

ya nyama.

• Kusaidia na kuendeleza huduma za misaada ya kitaalamu katika

kuendeleza nyama ya ng’ombe.

• Kuhimiza, kukuza na kuanzisha jumuia za wazalishaji na wafanya

biashara ya nyama ya ng’ombe.

• Kwa kushirikiana na wadau wengine serikali itaanzisha utaratibu wa

Kuitambua, kuweka kumbukumbu za mifugo na mfumo wa ufuatiliaji

kwa ajili ya uzalishaji salama wa nyama bora.

• Kusaidia ubia na / makampuni ya nchi zinazoagiza nyama ili kuweza

kupata utaalamu, mitaji na masoko.

5.1.1.5. Ufugaji wa wanyama bora

Ufugaji wa wanyama bora ni jambo muhimu kwa ajili ya kuongeza uzalishaji bora wa

mifugo. Ng'ombe wengi wa kienyeji wana uwezo mdogo wa vinasaba unaopelekea

uzalishaji na tija kuwa ndogo. Hata hivyo, wanyama wa kienyeji wana sifa muhimu ikiwa

ni pamoja na uwezo wa kuhimili mazingira yaliopo. Sifa hizi zinaweza kusaidiwa kwa

kuzighuisha na vinasaba bora ili kupata wanyama bora.

Changamoto:

Hapa Zanzibar huduma za uzalishaji wa wanyama ni ndogo kutokana na uzalishaji na

usambazaji duni wa mifugo, ugawaji duni wa rasilimali bora za vinasaba, uwekaji duni wa

kumbukumbu, utambuzi na uainishaji mifugo, utaalamu, huduma na miundombinu duni ya

uzalishaji.

Page 45: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

29

Lengo:

Kuongeza kasi ya uzalishaji wa vinasaba vya mifugo ya kienyeji kwa lengo la kuongeza

uzalishaji na tija bila kuathiri mbegu za ng’ombe wa kienyeji.

Tamko la Sera:

Juhudi za pamoja zitafanywa na pande zote, sekta ya umma na binafsi ili wakulima

waweze kupata vinasaba bora vya wanyama, huduma za uzalishaji endelevu na kuongeza

uwezo wa mifumo ya uzalishaji.

Mikakati ya Sera:

• Kukuza matumizi ya miradi ya kuweka kumbukumbu na kuanzisha mfumo wa

ukusanyaji wa data kitaifa ya kuzalisha mifugo

• Kuanzisha kitengo kitakachokuwa na dhamana ya kutambua,kusajili na kufuatilia

mifugo,

• Kuandaa na kutekeleza mpango na muongozo wa uzalishaji wa mifugo,

• Kuanzisha mfumo wa uainishaji na taratibu za kutenga maeneo kwa ajili ya mifugo iliopo

kwa kuzingatia ubora wa uzalishaji,

• Kuweka mipaka ya uzalishaji ili kuongeza sifa za vinasaba,

• kuimarisha huduma za kuzalisha wanyama ikiwa ni pamoja na mafunzo kwa watendaji,

• Kushajiisha wajasiriamali binafsi kuwekeza katika uzalishaji wa wanyama,

• Kushawishi na kuanzisha teknolojia ya uzalishaji wa kisasa kama uhimilishaji na

uhamisho wa vinasaba katika uzalishaji wa wanyama kwa sekta binafsi

• Kuhamasisha wakulima wa mifugo kuanzisha 'klabu / vyama vya kuzalisha wanyama.

5.1.1.6. Chakula cha wanyama na malisho

Lishe ni sehemu muhimu ya maisha ya wanyama. Malisho bora hutoa virutubisho muhimu

kwa ajili ya utunzaji wa miili na uzalishaji wa nyama, maziwa, mayai, mbolea na bidhaa

nyingine. Hata hivyo, ugawaji duni, ukosefu wa ubora na gharama kubwa za vyakula ni

changamoto kubwa zinazoikabili sekta ya mifugo hapa Zanzibar.

Changamoto:

Chakula cha wanyama hapa Zanzibar ni adimu, chenye kukosa ubora na gharama kubwa.

Tatizo hili kwa kiasi kikubwa linanasibishwa na ukosefu wa chakula chenye virutubisho,

Page 46: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

30

elimu ndogo juu ya ulishaji na uhifadhi wa chakula cha ngombe. Sababu nyingine ni za

malisho ya msimu, uhaba wa ardhi ya malisho na ukosefu wa udhibiti wa ubora na mfumo

wa ubora juu ya chakula kinachoagizwa kutoka nje.

Lengo:

Kuongeza fursa ya upatikanaji wa chakula bora cha wanyama kwa wafugaji

Tamko la Sera:

Hatua zitachukuliwa kuhakikisha kunakuwepo ufanisi na ubora katika uzalishaji, uhifadhi

na matumizi bora ya rasilimali za chakula kutoka wigo mbalimbali wa kilimo cha kiikolojia

na kuimarisha huduma za maabara ya lishe.

Mikakati ya Sera:

Kupanua wigo wa huduma za elimu kwa wakulima na mafunzo ya wakulima juu ya

uhifadhi na biashara ya malisho ya asili, kuimarisha lishe bora na kusindika taka za

bidhaa.

Kuimarisha mafunzo juu ya kilimo mseto cha nyasi-kunde, kilimo cha mimea lishe

chenye matumizi tafauti kwa njia ya FFS na vifurushi vya vyakula vya ziada.

Kuwezesha matumizi bora ya maeneo ya maweni kwa ufugaji wa wanyama wadogo

wenye kucheua.

Kuongeza uelewa na utaalamu juu ya uimarishwaji wa wanyama wenye

kucheua.

Kuwezesha fursa za mikopo kwa ajili ya uanzishwaji wa viwanda vya kati na vikubwa

vya vyakula vya wanyama.

Kufufua huduma za maabara ya lishe ya wanyama ikijumuisha ajira na mafunzo ya

wataalamu.

Kuhimiza wawekezaji binafsi kushiriki katika biashara ya uzalishaji wa wanyama na

masoko.

Kuingiza mfumo wa udhibiti wa chakula cha wanyama ndani ya Bodi ya Usimamizi wa

Mifugo Zanzibar.

Kufanya utafiti wa zana mbalimbali za kulisha wanyama na mfumo wa kula.

Kukuza matumizi bora ya vinenepishaji wanyama kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa

mifugo na tija.

Page 47: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

31

5.1.1.7. Uhakika wa chakula

Zanzibar inategemea sana uagizishaji wa bidhaa za vyakula muhimu. Chakula

kinachoagizwa kutoka nje kimefikia asilimia 49 ya mahitaji ya mwaka hapa Zanzibar

(Mizania ya Chakula Zanzibar, 2007).Bidhaa za mifugo zikiwemo nyama, nyama ya kuku

na mayai, chizi, maziwa mgando ni miongoni mwa vyakula muhimu vinavyoagizwa kutoka

Tanzania Bara na nje ya nchi. Usambazaji wa chakula cha wanyama wa asili ni mdogo

kutokana na uzalishaji wa kiwango cha chini hapa Zanzibar. Mifugo kama chanzo cha

chakula haijapewa umuhimu mkubwa, isipokuwa inachukuliwa kama akiba, hasa

inapotokea matatizo ya kifedha. Aidha, kiwango kidogo cha kipato kwa wazanzibari wengi

kimesababisha matumizi ya kiwango cha cha chini cha protini ya wanyama.

Changamoto:

Kuna uhaba wa fursa za upatikanaji wa vyanzo vya chakula vya wanyama kwa mujibu wa

mahitaji ya lishe kwa watu wengi. Mchango wa mazao ya mifugo kwa wazanzibari wa

kawaida katika kutoa kalori ni mdogo sana, nyama ya ng'ombe asilimia 1.8, asilimia 0.1

mayai, nyama ya kuku asilimia 4.4, na maziwa asilimia 4.6 (Mizania ya Chakula Zanzibar,

2007).

Lengo:

Kukuza fursa za upatikanaji wa vyanzo vya chakula cha nyama ili kufikia matumizi ya

kiwango cha juu cha protini

Tamko la Sera

Serikali itachukua hatua madhubuti kuhakikisha kunakuwepo ongezeko la mazao ya mifugo

nchini, kuimarisha ulaji na matumizi ya mazao ya mifugo na shughuli za kuongeza kipato

mbali na kilimo.

Mikakati ya Sera

Kuimarisha fursa za upatikanaji wa vyanzo vya chakula cha nyama kwa watu wote kwa

mujibu wa mahitaji yao ya lishe.

Kushajiisha jamii juu ya matumizi ya bidhaa za asili na zisizo za asili za mifugo.

Kukuza matumizi ya maziwa miongoni mwa jamii kwa jumla kwa kuanzisha siku ya

kunywa maziwa na mpango wa kunyisha maziwa skuli na mingine ya uelimishaji.

Page 48: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

32

Kwa kushirikiana na taasisi zinazohusika, serikali itatoa elimu ya utayarishaji wa

chakula kwa umma.

Kushajiisha familia za vijijini kushiriki katika uzalishaji wa mifugo na shughuli

nyingine za kuongeza kipato.

5.1.1.8. Ufugaji wa kilimo hai

Kilimo hai cha mifugo ni ufugaji ambao unapunguza matumizi ya kemikali za viwandani

kama vile dawa, mbolea za chumvi na dawa za kuulia wadudu katika shamba.Dawa hizo

zinaweza kusababisha madhara kwa mifugo na mazao mingine ya kilimo. Kwa kawaida,

bidhaa ambazo zimethibitishwa kuwa hazina madhara zinahitajika sana na huongezeka

thamani kubwa katika soko. Hadi sasa, hakuna hatua yeyote iliyokwishachukuliwa

kuendeleza uzalishaji wa mazao hai ya mifugo hapa Zanzibar.

Chamgamoto:

Hapa Zanzibar kilimo hai cha mifugo kinakwazwa na ukosefu wa uelewa miongoni mwa

wakulima na wananchi kwa ujumla pamoja na upungufu wa utaalamu kwa ajili ya

maendeleo ya teknolojia.

Lengo

Kukuza mazao ya mifugo hai ili kukidhi mahitaji maalumu ya soko.

Tamko la Sera:

Kwa kushirikiana na sekta binafsi na wadau wengine, Serikali itatoa elimu na taarifa za

masoko na msaada wa kitaalamu katika uzalishaji wa mazao hai ya mifugo.

Mikakati ya Sera:

Kuanzisha na kuwezesha kampeni juu ya kilimo hai cha mifugo na matumizi ya bidhaa

hizo.

Kukuza matumizi ya Mbolea ya Samadi.

Kutoa mafunzo kwa maofisa elimu kwa wakulima na wakulima juu ya kilimo hai cha

mifugo.

Kutoa vifaa na utaalamu unaohitajika kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo na

Page 49: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

33

wengine kwa ajili ya kilimo hai cha mifugo.

5.1.1.9. Mifugo na mazao ya mifugo inayoweza kuongezewa thamani

Hapa Zanzibar, idadi ya hoteli za kitalii ambazo ni soko muhimu kwa bidhaa za mifugo

zinazozalishwa nchini zimeongezeka katika miaka ya karibuni. Hata hivyo, hoteli hizi

zinaagiza bidhaa nyingi zaidi za mifugo isipokuwa za baharini na mara chache mayai.

Bidhaa kubwa za mifugo kama maziwa yanayozalishwa hapa Zanzibar yameshindwa

kujipenyeza katika soko hili kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu

wa ubora na uchache wa maziwa, kutopatikana kwa uhakika na kutokuwepo kwa

ushindani katika bei. Mbali na hoteli za kitalii, wazalishaji wadogo wadogo wa mifugo

hutegemea masoko ya mijini kwa ajili ya bidhaa zao. Kwa muda mfupi ujao, watumiaji

watahitajia bidhaa bora za mifugo hasa zisizo na tishio la magonjwa ya zoonotiki.

Changamoto:

Kuna ongezeko dogo la thamani ya mifugo hapa Zanzibar. Uwezo mdogo wa unenepeshaji

wanyama, kushindwa kuongeza thamani mifugo na mazao ya mifugo na miundombinu

duni ya usindikaji imedhihirika hapa Zanzibar. Aidha, gharama za usindikaji ni kubwa,

udhibiti duni wa ubora, ujuzi mdogo wa ujasiriamali, uchanga wa vyama vya wazalishaji

mifugo na miundombinu duni ya soko.

Lengo

kuongeza thamani ya mifugo ili kupata faida zaidi

Tamko la sera:

Serikali itaongeza thamani ya bidhaa za mifugo zinazozalishwa ndani ya nchi.

Mikakati ya Sera:

Kushajiisha sekta binafsi kuwekeza katika usindikaji na masoko ya mazao ya mifugo.

Kukuza masoko kwa ajili ya mifugo na mazao ya mifugo na kuanzisha hesabu ya

masoko ya mifugo.

Kuendeleza uanzishwaji wa wazalishaji wa mifugo, wafanyabiashara na vyama vya

wasindikaji na mitandao ya kuimarisha fursa za upatikanaji wa soko.

Kuanzisha Sera ya Masoko ya Mifugo kwa haraka kadiri inavyowezekana.

Page 50: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

34

Kuimarisha taratibu za kudhibiti ubora wa mazao ya mifugo.

Kutetea na kufanya mapitio ya ushuru wa forodha kwa ajili ya bidhaa za mifugo na

bidhaa kutoka nchi zisizokuwa wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki ili kupenda

kutumia mazao ya ndani.

Kuhimiza ukarabati na ujenzi wa barabara.

Kuhimiza uanzishwaji wa sekta binafsi na ukusanyaji wa maziwa, vituo vya baridi vya

kuhifadhia mazao ya mifugo, machinjio na vifaa vya kuhifadhia.

Kuhimiza uanzishwaji wa feedlots kwa ajili ya kunenepesha mifugo.

Kutoa elimu juu ya usindikaji wa mazao ya mifugo ikiwa ni pamoja na vifungashio ili

kuimarisha thamani ya soko.

Kuanzisha mfumo wa kuweka chapa ya kibiashara kwa mazao ya mifugo hapa

Zanzibar.

Afya ya Wanyama

5.1.2.1. Huduma za Afya ya Wanyama

Magonjwa ya mifugo ni miongoni mwa vikwazo vikubwa katika maendeleo ya sekta ya

mifugo hapa Zanzibar. Serikali, kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi na sekta binafsi

zimepewa jukumu muhimu la kuzuia, kuondoa na kudhibiti kuenea kwa magonjwa ya

mifugo. Utekelezaji duni wa sheria ya karantini unaiweka Zanzibar katika hatari ya

kuvamiwa na aina mbalimbali za magonjwa ya mifugo na mengine ya zoonotiki.

Changamoto:

Kwa ujumla utoaji wa huduma za afya kwa wanyama katika Zanzibar ni wa kiwango cha

chini unaosababishwa na upungufu wa rasilimali watu wenye sifa zinazohitajika, uhaba wa

vifaa, gharama kubwa za dawa na vifaa, huduma chache za msaada wa kitaalamu na

ushiriki duni wa sekta binafsi.

Lengo:

Kuendeleza utoaji wa huduma za afya kwa mifugo ili kudhibiti magonjwa ya wanyama na

kila inapowezekana kuyatokomeza ili kuongeza uzalishaji na tija.

Tamko la Sera:

Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi na wadau wengine itaimarisha mfumo wa afya

Page 51: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

35

ya wanyama na kupunguza hasara za kiuchumi zinazosababishwa na magonjwa ya mifugo

kwa njia ya kutoa huduma bora na kujenga uwezo wa rasilimali watu.

Mikakati ya Sera:

Kuongeza idadi ya wafanyakazi wenye ujuzi na waliohitimu (katika fani za mifugo na

uzalishaji),

Kuongeza utoaji wa huduma bora za afya ya mifugo,

Kuongeza uchunguzi na udhibiti wa magonjwa yenye athari za kiuchumi na kijamii,

Kuwezesha utaratibu wa msamaha wa kodi na ruzuku ili kupunguza gharama za

pembejeo,

Kuanzisha midahalo na wadau na Washirika wa Maendeleo juu ya masuala ya misaada

ya kitaalamu.

Kuanzisha mipango endelevu kwa ajili ya maandalizi ya kulinda mifugo dhidi ya

magonjwa mapya / yanayojitokeza ya wanyama.

Udhibiti wa magonjwa mapya na yanayojitokeza ya wanyama ili kulinda rasilimali za

mifugo.

5.1.2.2. Magonjwa yanayosababishwa na kupe

Magonjwa yanayosababishwa na kupe ni kikwazo kikubwa kwa mifugo Afrika ya

Mashariki. Magonjwa yanayosababishwa na kupe maarufu hapa Zanzibar ni Homa ya

Mwambao wa Afrika ya Mashariki ambayo inakadiriwa kuua asilimia 60 ya ndama kila

mwaka. Magonjwa mengine yanayosababishwa na kupe kubwa ni Cowdriosis (Heart

water), Anaplasmosis, Babesiosis (Red water) na Ormilo. Mbali na kusafirisha

magonjwa, kupe pia husababisha hasara za kiuchumi kwasababu ya vifo vinavyotokana na

toxicosis, kuharibu ngozi na kupunguza thamani yake katika soko.

Changamoto:

Kuwepo kwa maradhi yanayotokana na kupe katika Zanzibar kunachochewa na gharama

kubwa za dawa, uwezo duni katika kuchukua hatua za kuzuia, ukosefu wa ujuzi wa

kitaalamu, magonjwa kuwa sugu dhidi ya acaricides na kuingia kwa aina mpya ya kupe

kwa njia ya uingizaji wa wanyama hai.

Page 52: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

36

Lengo:

Kudhibiti na kutokomeza magonjwa yanayosababishwa na kupe ili kuchochea uzalishaji

na tija pamoja na kulinda rasilimali ya wanyama

Tamko la Sera:

Serikali kwa kushirikiana na wajasiriamali binafsi, wakulima na wananchi kwa ujumla

itadhibiti magonjwa ya kupe yaliopo na kuzuia uingizwaji wa tishio jipya la maradhi

katika visiwa hivi.

Mikakati ya Sera:

Kushawishi ili kufanya mapitio ya taratibu za kodi na kuanzisha ruzuku ili kupunguza

gharama za dawa za acaricides na pembejeo nyengine za mifugo,

Kufufua malambo na huduma za utiaji dawa katika ngazi ya wilaya,

Kusimamia malisho ya mifugo, udhibiti wa kupe kibayolojia na njia nyengine,

Kukuza matumizi ya tafiti juu ya kudhibit kupe, Homa ya Mwambao wa Afrika ya

Mashariki na Maradhi Yanayotokana na Kupe.

Kuweka taratibu za kudhibiti, kuchunguza na kuharibu acaricides,

Kuzuia uingizaji haramu wa wanyama hai kwa kushirikiana na jamii na taasisi za

usimamizi wa sheria,

Serikali itaimarisha huduma za misaada ya kitaalamu juu ya kupe na udhibiti wa

magonjwa yanayotokana nayo.

5.1.2.3. Magonjwa ya Wanyama Yanayovuka Mipaka

Magonjwa ya Wanyama Yanayovuka Mipaka ni ya kuambukiza ambayo yanawaathiri

wanyama wengi katika maeneo yanayohusika na kuacha athari za kiuchumi. Ili kudhibiti

magonjwa haya kwa ufanisi, hatua za haraka za kitaifa, kikanda na kimataifa zinahitajika

kuchukuliwa. Hatua hizi zinaweza kufikiwa kwa njia ya kuanzisha mfumo wa kutoa taarifa

za tahadhari za mapema, kutambua mapema, kuratibu na kuoanisha mikakati ya udhibiti

wa magonjwa haya. Miongoni mwa taarifa za Magonjwa ya Wanyama Yanayovuka

Mipaka zinazoweza kukusanywa Zanzibar ni pamoja na kichaa cha mbwa, kimeta,

Ugonjwa wa miguu na midomo, Chambavu na Magonjwa ya Ngozi katika ng’ombe na

magonjwa ya mahepe/magwa na Gumboro katika kuku. Baadhi ya Magonjwa ya

Wanyama Yanayovuka Mipaka maarufu katika kanda hii ni pamoja na homa ya mapafu

Page 53: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

37

kwa ng’ombe na homa ya mapafu kwa mbuzi, Homa ya Bonde la Ufa, mafua ya ndege na

Sotoka.

Changamoto:

Maendeleo ya sekta ya mifugo Zanzibar yanakwazwa na udhibiti duni wa Magonjwa ya

Wanyama Yanayovuka Mipaka. Ufahamu mdogo na uchache wa taarifa zinazohusiana na

magonjwa haya, uingizaji haramu wa wanyama, gharama kubwa za chanjo, huduma duni

za afya na maendeleo duni ya miundombinu ya mifugo yanaelezwa kama ni miongoni

mwa sababu ya tatizo hili.

Lengo:

Kutokomeza magonjwa ya mifugo yanayovuuka mipaka na kudhibiti kuingia kwa maradhi

mapya ya Magonjwa ya Wanyama Yanayovuka Mipaka ili kukuza sekta ya mifugo na

kuendeleza masoko ya ndani na nje.

Tamko la Sera:

Serikali itashirikiana na jumuia za wananchi, kikanda na kimataifa kuchukua hatua

madhubuti na endelevu za kudhibiti na kutokomeza Magonjwa ya Wanyama Yanayovuka

Mipaka ikiwa ni pamoja na kuongeza msukumo wa kukabiliana na uingizaji haramu wa

wanyama hai na bidhaa zake.

Mikakati ya Sera:

Kuanzisha kampeni za kujenga muamko na kujiandaa dhidi ya Magonjwa ya

Wanyama Yanayovuka Mipaka,

Kuimarisha mifumo ya karantini za wanyama na maendeleo ya miundombinu katika

maeneo ya kuingia,

Kuifanya Zanzibar kuwa ni ukanda huru wa magonjwa ya wanyama,

Kuweka mfumo wa mtandao wa taarifa za Magonjwa ya Magonjwa ya Wanyama

Yanayovuka Mipaka ya kikanda na kuoanisha na mfumo wa mikakati ya kudhibiti

Magonjwa ya Wanyama Yanayovuka Mipaka Zanzibar na zile za Jumuia ya

Maendeleo Kusini mwa Afrika na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Page 54: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

38

Kuimarisha mazungumzo na sekta binafsi na Washirika wa Maendeleo ili kupata

msaada wa kitaalamu na kifedha kwa ajili ya programmu za kudhibiti na kuzuia

Maradhi ya Wanyama Yanayovuuka Mipaka.

Kudhibiti uingizaji wa wanyama hai, bidhaa za wanyama na kwa kushirikiana na

taasisi nyingine zinazohusika za serikali, jamii na vyombo vya sheria,

5.1.2.4. Magonjwa ya Zoonotiki na Uhakika wa Chakula

Magonjwa ya Zoonotiki ni yale ambayo wanyama na binadamu wanaweza kuambukizana.

Kwa hivyo, magonjwa haya ni tishio kwa afya ya binadamu. Kuishi karibu na wanyama na

kutumia bidhaa ghafi za wanyama ni sababu kubwa inayopelekea mtu kuweza kupata

magonjwa hayo. Mafua ya nguruwe, Kupoteza mimba, kifua kikuu, kichaa cha mbwa,

kimeta na salmonella ni mifano ya magonjwa ya zoonotiki.

Changamoto:

Uwezekano wa uingizwaji wa magonjwa mapya ya zoonotiki Zanzibar ni mkubwa.

Inaeleweka kwamba uelewa mdogo wa taarifa za magonjwa haya na uingizaji haramu wa

wanyama, gharama kubwa za chanjo, huduma duni za usaidizi wa afya, maendeleo duni ya

miundombinu, uhusiano duni baina ya huduma za afya ya umma na mifugo ni sababu ya

tatizo hili.

Lengo:

Kuimarisha utoaji wa afya ya/kwa umma na huduma za uhakika wa chakula ili kulinda

binadamu na wanyama.

Tamko la Sera:

Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine na Washirika wa Maendeleo itadhibiti

magonjwa ya zoonotiki kwa ajili ya usalama wa binadamu na wanyama

Mikakati ya Sera:

Kukuza mbinu bora juu ya taaluma ya afya na hatua za kiusalama kwa ajili ya

wazalishaji wa mifugo na wafanyakazi wasio rasmi.

Kuendeleza kampeni ya kujenga Uelewa juu ya udhibiti wa maradhi ya zoonotiki,

Kuimarisha ushirikiano na Bodi ya Dawa, Vyakula na Vipodozi Zanzibar juu ya

Page 55: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

39

changamoto ya uhakika wa chakula.

Kuimarisha ushirikiano na vitengo vya kitaifa, kikanda na kimataifa vyenye dhamana

ya kushughulikia magonjwa ya zoonotiki.

Kuimarisha shughuli za utafiti juu ya zoonosis, ikiwa ni pamoja na tathmini ya hatari

ya magonjwa ya zoonotiki kupitia michakato yanayohusiana na kazi husika.

Kuimarisha sheria ya usimamizi wa raslimali ya Mifugo No 11 ya 1999 juu ya kudhibiti

magonjwa ya wanyama.

Kuanzisha huduma za ukaguzi wa usafi wa mazizi ili kuzuia kuingia

na kuenea kwa magonjwa ya mifugo.

Serikali itaimarisha huduma za msaada wa kitaalamu kwa ajili ya

afya ya mifugo na uhakika wa chakula ili kuhakikisha ubora na usalama wa vyakula

vya mifugo.

5.1.2.5. Huduma za Uchunguzi wa Mifugo

Maabara za mifugo ni vitengo muhimu katika uchunguzi wa Maradhi Yanayotokana na

Kupe, Maradhi ya Wanyama Yanayovuuka Mipaka, ya Zoonotiki na magonjwa

mengineyo. Hivi sasa, huduma za maabara ya mifugo zinadhibitiwa na Serikali. Hadi sasa,

kuna kituo kimoja cha Uchunguzi wa Mifugo na maabara mbili za uchunguzi wa

magonjwa katika Zanzibar. Vituo hivi vinatoa huduma chache kutokana na uwezo mdogo

wa kifedha na rasilimali watu. Kwa muda mrefu maabara hizi zimekuwa zikifanya kazi

chini ya misaada ya wafadhili.

Changamoto:

Utendaji kazi wa maabara za uchunguzi wa mifugo ni mdogo mno kutokana na uhaba wa

wafanyakazi wenye ujuzi, miundombinu na huduma duni, uhaba wa msaada wa kitaalamu,

pamoja na sekta binafsi kukosa msukumo wa kuekeza katika maabara za mifugo.

Lengo:

Kutekeleza kazi za uchunguzi wa magonjwa na kutoa huduma za maabara ili kuendeleza

uchunguzi wa magonjwa ya wanyama na huduma sahihi za afya za wanyama.

Page 56: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

40

Tamko la Sera:

Serikali kwa kushirikiana na watoaji wa huduma za hifugo, Washirika wa Maendeleo na

wadau wengine itaimarisha uwezo wa uchunguzi wa maabara ili kuweza kufanya

uchunguzi wa maradhi yanayotokana na Kupe, Maradhi ya Wanyama Yanayovuuka

Mipaka, Zoonotiki yaliopo na yatakayozuka pamoja na magonjwa mengine ya wanyama

kwa ufanisi.

Mikakati ya Sera:

Kfufua na kuimarisha kazi za utoaji wa huduma za maabara ya mifugo katika visiwa

vyote ya Unguja na Pemba.

Kufufua na kuimarisha kazi za utoaji wa huduma za maabara za mifugo katika ngazi ya

wilaya na vituo vya karantini.

Kuimarisha mazungumzo na sekta binafsi na Washirika wa Maendeleo ili kuweza

kupata msaada wa kitaalamu na kifedha kwa ajili ya uchunguzi wa mifugo.

Kuimarisha ushirikiano wa maabara nyengine za kitaifa, kikanda na kimataifa.

5.1.2.6. Ustawi wa Wanyama

Kuna ongezelo kubwa la ukiukaji wa haki na unyanyasaji wa wanyama Zanzibar.

Wanyama hawatunzwi ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuwekwa katika

msongamano, kuchapwa viboko, kupakiwa mizigo bila ya kiasi, kufanyishwa kazi

za sulubu na kutopatiwa chakula cha kutosha. Juhudi za serikali zimeelekezwa

katika kudhibiti ukatili dhidi ya wanyama kupitia jamii, Jumuia Zisizo za Kiserikali

na Mashirika ya Kimataifa.

Changamoto:

Ustawi wa wanyama unakwazwa na uelewa duni wa jamii juu ya haki za wanyama,

uzururaji wa wanyama, kanuni zilizopitwa na wakati, utekelezaji duni wa sheria na kasoro

za kijamii na kiutamaduni.

Lengo:

Kuhakikisha kuwa wanyama wanahudumiwa vyema na kusimamiwa na wadau wote ili

kufikia viwango vya ustawi bora wa wanyama

Page 57: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

41

Tamko la Sera:

Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine itachukua hatua za kuzuia ukatili dhidi ya

wanyama.

Mikakati ya Sera:

Kufanya mapitio ya Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Mifugo Namba 11 ya 1999

na kuimarisha.

Kuongeza kasi ya utekelezaji wa sheria zinazohusiana na ustawi wa wanyama,

Kuingiza Changamoto ya ustawi wa wanyama katika vipengele vyote vya huduma ya

mifugo kwa kutumia maafisa elimu kwa wakulima wa mifugo, njia ya shamba darasa,

klabu za upendo kwa wanyama, shamba la Wakulima Wadogo na mtandao wa Skuli ya

Maisha na vyombo vya ulinzi /wasimamizi wa sheria,

Kuanzisha mazizi katika halmashauri za mitaa ili kuepusha uwezekano wa wanyama

kupotea,

Kuhimiza uanzishwaji wa klabu za wanyama katika skuli na jamii pamoja na jumuia za

kidini, kuwasiliana na wanaharakati wa kitaifa na kimataifa wa haki za wanyama juu

ya kuanzishwa kwa ustawi wa wanyama na mipango ya usimamizi wa mafunzo kwa

jamii/umma.

Kuhimiza kampeni za uhamasishaji umma juu ya Changamoto ya ustawi wa wanyama

na faida zake.

Kushirikiana na sekta binafsi, mashirika ya kitaifa na kimataifa katika utekelezaji wa

changamoto ya ustawi wa wanyama.

5.1.3. Wanyama rafiki na wasio wa kawaida

5.1.3.1. Wanyama rafiki na wenye mapambo

Utunzaji wa wanyama rafiki na kundi la wanyama wenye mapambo unazidi kupata

umaarufu si kwa sababu tu ya mahusiano yao ya jadi na binadamu, lakini pia kama

sehemu ya kupata burudani na kuendeleza shughuli za kiuchumi. Wakati wanyama rafiki

wa kufuga kama vile mbwa na paka wanatumiwa kwa ajili ya kujifurahisha, uwindaji,

uelekezaji na usalama, kundi la wanyama pori ikiwa ni pamoja na reptilia, ndege pori,

amfibia, nyani na wanyama wengine wanapata mvuto maalumu kwa watalii wa ndani na

wa kimataifa.

Page 58: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

42

Changamoto:

Maendeleo ya wanyama rafiki na wanyama wa mapambo Zanzibar yanakwazwa na

uchache wa wanyama bora, utunzaji na ujuzi duni wa usimamizi, imani au mitazamo,

utaalamu mdogo, mipango duni ya kukuza uwekezaji na mitaji michache ya uwekezaji.

Lengo

Kuendeleza hatua madhubuti kwa ajili ya maendeleo ya wanyama rafiki na wanyama

wa mapambo kwa faida ya jamii

Tamko la Sera:

Ushirikiano wa karibu kati ya sekta binafsi na serikali utakuzwa ili kusaidia maendeleo ya

wanyama rafiki na kundi la wanyama wa mapambo ili kufikia upeo wa juu wa jamii

kuridhika na kuzalisha zaidi mapato kupitia utalii wa ndani na wa kimataifa

Mikakati ya Sera:

Kutoa utaalamu wa ufugaji kwa wadau wanaohusika na wanyama rafiki na wanyama

wa mapambo kwa ajili ya matumizi ya ndani na ya kibiashara,

Kuwezesha uingizaji unaodhibitika na uzalishaji wa wanyama rafiki na wanyama wa

mapambo, wenye ubora

Kuimarisha kampeni za kujenga uelewa na muamko juu ya umiliki wa wanyama

rafiki wenye kutii amri, udhibiti wa magonjwa na haki za wanyama kwa

kushirikiana na wanaharakati wa haki za wanyama, taasisi za utalii na maliasili,

Kuanzisha majadiliano na wadau na Washirika wa Maendeleo ili kupata msaada wa

kitaalamu na kifedha kwa ajili ya uwekezaji katika biashara ya wanyama katika mazizi

maalum.

5.1.3.2. Wanyama Wasio wa Kawaida

Mifugo isio ya kawaida na ndege inachangia kiasi kidogo katika uzalishaji wa nyama na

mayai kwa ajili ya matumizi ya ndani. Mbali na kuwa ni chanzo muhimu cha chakula,

baadhi ya mifugo isio ya kawaida pia wanajuilikana kutokana na umuhimu wake wa

kijamii na kiutamaduni.

Page 59: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

43

Changamoto

Kuna uelewa mdogo juu ya uwezo wa mifugo isio ya kawaida katika kuchangia kipato

cha familia na uhakika wa chakula. Elimu ndogo ya ufugaji wa mifugo isio ya kawaida na

uhaba wa huduma na uzalishaji duni.

Lengo

Kukuza uzalishaji na matumizi ya nyama za wanyama wasio wa kawaida kwa ajili ya

kuongeza uhakika wa chakula katika familia, kipato na kuongeza ubora wa lishe.

Tamko la Sera:

Mifugo isio ya kawaida itajumuishwa ili iweze kuchangia katika mfuko wa taifa wa nyama

na kuongeza mchango wake katika mapato ya kila mwaka,

Mikakati ya Sera:

Kukuza ushiriki wa wakulima katika uzalishaji wa Mifugo Isiyo ya Kawaida kwa

kushirikiana na taasisi na mashirika yanayohusika,

Kupitia mashamba darasa ya wakulima na vyama vya wakulima vijana,serikali

itaendeleza mbinu bora za uzalishaji wa mifugo isiyo ya kawaida,

Kuanzisha majadiliano na wadau na Washirika wa Maendeleo ili kupata

msaada wa kitaalamu na kifedha kwa ajili ya maendeleo ya mifugo isiyo ya kawaida,

Kuhimiza kampeni za kujenga muamko juu ya kilimo mseto na mifugo isiyo ya

kawaida na matumizi ya bidhaa zao.

5.1.4. Utafiti wa Mifugo

Utafiti ni njia muhimu ya kutathmini nadharia ili kupata matokeo mapya ambayo

yanaweza kutumika kutatua matatizo au kuongeza ustawi wa wanyama. Hapa Zanzibar,

utafiti wa mifugo umekuwa kwa muda mrefu ukifanywa kwa ajili ya kuzalisha

vinasaba bora vya wanyama wa maziwa na nyama ya ng'ombe katika mifugo yetu ya

kienyeji na kuongeza uzalishaji wa maziwa. Baadhi ya tafiti nyingine zimelenga katika

lishe ya mifugo, uzalishaji, fiziolojia, udhibiti na kinga dhidi ya magonjwa. Tafiti zote

hizi zilikusudia kuleta manufaa na kuimarisha utendaji bora kwa wafugaji na nchi kwa

ujumla. Lakini, baadae tafiti za mifugo karibu zote zimesimamishwa kutokana na

Page 60: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

44

kutengewa kiasi kidogo cha fedha za bajeti ya serikali, hali duni za taasisi za utafiti na

miundombinu, uhaba wa wafanyakazi wa utafiti na ukosefu wa motisha kwa watafiti na

ukosefu wa chombo kikuu kinachosimamia utafiti wa mifugo.

Changamoto:

Hali ya miundombinu chakavu kwa ajili ya kufanya utafiti wa mifugo ikiwa ni pamoja na

vifaa duni, idadi ndogo ya wafanyakazi wenye sifa, bajeti ndogo ambayo haiwezi kujenga

mazingira bora kwa ajili ya utafiti. Mbali na hayo hakuna taasisi inayodhibiti na

kusimamia kazi zote za utafiti wa mifugo nchini.

Lengo:

Kufufua kazi za utafiti wa mifugo na kujenga mazingira bora kwa ajili ya kazi za utafiti

nchini.

Tamko la Sera

Serikali kwa kushirikiana na watoa huduma binafsi za mifugo Washirika wa Maendeleo

na wadau wengine itaimarisha tafiti za mifugo ili kuongeza uzalishaji wa mifugo lakini

wakati huo huo mkazo utawekwa katika utunzaji wa mazingira.

Mkakati wa Sera

Kuhimiza uundaji wa chombo huru cha kudhibiti na kusimamia tafiti zote za mifugo

katika nchi.

Kuendeleza uanzishwaji wa viituo vya utafiti wa mifugo Unguja na Pemba na kuweka

maabara za kisasa zenye vifaa na huduma bora.

Kuongeza uwezo wa wataalamu wa utafiti wa mifugo,

Kuimarisha mazungumzo na sekta binafsi na Washirika wa Maendeleo ili kupata

msaada wa kitaalamu na kifedha kwa ajili ya utafiti wa mifugo,

Kuimarisha ushirikiano wa kimaabara wa kitaifa, kikanda na kimataifa.

Kuimarisha mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wote wanaohusika na utafiti wa

mifugo.

Page 61: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

45

5.1.5. Maendeleo ya Rasilimali watu

Hivi sasa sekta ya mifugo inakabiliwa na uhaba wa wafanyakazi wa kitaalamu. Ili

kuongeza uzalishaji wa mifugo na tija pamoja na mambo mengine inahitajika kuwepo

wafanyakazi wa kutosha wenye ujuzi katika nyanja za utafiti wa mifugo, uzalishaji

mifugo, teknolojia ya maziwa, kuku, uongezaji thamani, ufugaji wa wanyama, elimu kwa

wakulima, teknolojia ya maabara, mipango, maendeleo vijijini, utawala na masuala

mengine yanayohusiana nayo.

Changamoto:

Kuna upungufu wa wafanyakazi wenye ujuzi wa kitaalamu kwa ajili ya maendeleo ya

mifugo.

Lengo

Kuongeza kiwango cha wafanyakazi wenye sifa muhimu za kitaalamu kwa ajili ya

maendeleo ya mifugo.

Tamko la Sera

Serikali itaajiri wafanyakazi wapya wataalamu na kuimarisha uwezo wa wafanyakazi

waliopo kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya mifugo.

Mikakati ya Sera

Kuanzisha mahitaji ya rasilimali watu kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya mifugo.

Kufanya Tathmini ya Mahitaji ya Mafunzo kwa ajili ya sekta ya mifugo,

Kuongeza idadi ya wafanyakazi wenye ujuzi na utaalamu kwa ajili ya maendeleo ya

sekta ya mifugo,

Kuongeza idadi ya wafanyakazi wasaidizi wa mifugo wenye sifa, wataalamu mabingwa

wa ufugaji wa wanyama na mtaalamu wa kuku aliyepata mafunzo ya ngazi ya

stashahada kwa kila wadi.

Kuongeza idadi ya wafanyakazi wenye sifa, wataalamu mabingwa wa ufugaji wa

wanyama, mtaalamu wa kuku, ofisa elimu kwa wafugaji aliyepata mafunzo ya ngazi

ya shahada katika kila wilaya.

Page 62: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

46

Kuimarisha ushirikiano na taasisi za maendeleo ya mifugo za kitaifa, kikanda na

kimataifa na kubadilishana wafanyakazi wa kitaalamu.

Kujenga mazingira bora yatakayowafanya wafanyakazi waliopo kuendelea kudumu

kazini.

5.1.6. Huduma za Elimu na Mafunzo kwa Wafugaji

Huduma za elimu kwa wafugaji zinakusudiwa kufikisha elimu ya kisayansi na taarifa za

utafiti kwa wakulima na kinyume chake. Mwanzoni mwa miaka ya 90, elimu kwa

wakulima wa mifugo hapa Zanzibar ilijumuishwa katika huduma moja ya Elimu kwa

wakulima wa Kilimo chini ya wizara iliyokuwa inahusika na kilimo. Mfumo huo

ulitumia mkabala shirikishi katika kutoa taarifa za kitaalamu na elimu kwa wakulima

ikiwa ni pamoja na mafunzo na ziara, vituo/mashamba ya maonesho na mkabala wa

mkulima kwa mkulima. Katika miaka ya hivi karibuni mkabala wa shamba darasa, kwa

mfano, Mashamba Darasa kwa Wakulima yanatumiwa kutoa masomo muhimu kwa ajili

ya kuendeleza elimu kwa wakulima. Hivi sasa, mkabala huu unaimarishwa na

unajumuishwa katika mfumo wa utoaji wa huduma za elimu kwa wafugaji.

Changamoto:

Hivi sasa mfumo wa utoaji huduma za elimu kwa wafugaji ni duni kutokana na uwezo

mdogo wa fedha, uhaba wa wafanyakazi wenye ujuzi wa kitaalamu na vifaa vya kutosha.

Lengo

Kuimarisha mfumo wa utoaji wa huduma za elimu kwa wakulima wa mifugo

Tamko la Sera:

Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi na wadau wengine itaendeleza mfumo

madhubuti unaomlenga mfugaji katika kupata huduma ili kusaidia juhudi za wafugaji

katika kuongeza uzalishaji wa mifugo na tija.

Mikakati ya Sera:

Kuongeza kiwango cha mashamba darasa ya mifugo na kujumuishwa katika kurugenzi

yenye dhamana ya sekta ya maendeleo ya mifugo,

Kujenga ushirikiano imara na wadau, hasa sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali

na vyama vya wakulima ili kushiriki katika utoaji wa huduma za elimu kwa wafugaji,

Page 63: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

47

Kuimarisha uwezo wa maofisa elimu kwa wakulima na maendeleo ya wakulima,

Kufanya mapitio ya mbinu za elimu kwa wakulima ili zifanane na mazingira yaliopo,

Kutoa motisha kwa maofisa elimu kwa wakulima kwa mujibu wa utendaji wao,

Kubuni utaratibu wa kuongeza utaalamu wa wafanyakazi wa afya ya wanyama katika

jamii,

Kuanzisha midahalo na wadau na Washirika wa Maendeleo ili kutoa misaada ya

kitaalamu na kifedha kwa ajili ya kusaidia utoaji wa elimu kwa wafugaji.

5.1.7. Upatikanaji wa Taarifa za Mifugo

Upatikanaji wa taarifa za Mifugo ni muhimu katika kuwaunganisha wafugaji, wataalamu

na watoa huduma. Huduma hizi ni pamoja na ukusanyaji, uhifadhi, utayarishaji na

usambazaji wa teknolojia mpya na matukio yanayohusika kwa kutumia ubunifu huo.

Changamoto:

Kuna mfumo duni wa utoaji taarifa katika sekta ya mifugo. Takwimu nyingi zilizopo

zimepitwa na wakati na haziwasaidii watumiaji. Jambo hili, kwa kiasi kikubwa,

limechangiwa na msaada mdogo wa fedha, vifaa duni, miundombinu mibovu na utaalamu

mdogo.

Lengo

Kuanzisha mfumo madhubuti wa utoaji taarifa katika sekta ya mifugo

Tamko la Sera:

Kitengo cha taarifa za mifugo chenye ubora na rafiki kitaanzishwa ili kuongeza kasi ya

maendeleo ya sekta ya mifugo.

Mikakati ya Sera:

Kuanzisha kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Kuanzisha mfumo wa ukusanyaji wa taarifa za mifugo katika mfumo wa kompyuta,

Kuimarisha ukusanyaji wa mara kwa mara wa takwimu za mifugo na mfumo wa

kuweka kumbukumbu katika ukusanyaji wa data, ukokotoaji, usambazaji na uratibu,

Page 64: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

48

Kuanzisha majadiliano na Washirika wa Maendeleo, sekta binafsi na wadau wengine

wanaohusika ili kutoa msaada wa kitaalamu na kifedha kwa ajili ya huduma za taaria

za mifugo,

Kuwezesha mikutano ya kisekta ya uratibu wa data za mifugo.

Kuanzisha programu za uhamasishaji kwa kushirikiana na jumuia za kiraia na vikundi

vya wafugaji.

Kuandaa na kusambaza taarifa za mifugo na nyenginezo zinazohusiana na masuala ya

mifugo,

Kuanzisha kijarida cha Wizara,

Kushirikiana na taasisi za kitaifa, kikanda na kimataifa katika kutoa tarifa

zinazohusiana na mifugo.

5.1.8. Masuala Mtambuka na Kisekta

5.1.8.1. Msaada kwa Wajasiriamali wa Mifugo

Wafugaji wa Zanzibar hawana fursa zinazotokana na ulinganishaji na ushindani wa

uzalishaji wa mifugo bora ikilinganishwa na wafugaji wa nchi nyengine. Hii inatokana na

ukweli kwamba Zanzibar inakabiliwa na uhaba wa ardhi kwa ajili ya uzalishaji wa mifugo

na chakula cha nafaka (mfano mahindi, ngano na soya) pamoja na mbegu za mafuta

ambazo ni vyanzo vikuu vya utengenezaji wa vyakula vya mifugo. Mbali na sababu hiyo,

wafugaji hao pia hawana fursa ya ushindani kwasababu ya matumizi ya kiwango cha chini

cha teknolojia ya kisasa ya uzalishaji wa mifugo na kiwango duni cha uchumi.

Hivi sasa, bei ya pembejeo za mifugo ni kubwa kwa wafugaji wengi kumudu kuzinunua.

Matokeo yake wafugaji wengi hushindwa kutumia teknolojia sahihi za uzalishaji na

kupelekea tija kuwa ndogo. Zaidi ya hayo, hata kama wafugaji wangetumia teknolojia ya

uzalishaji wa kisasa, kiwango chao cha uzalishaji na bei za pembejeo zisizotolewa ruzuku

zinaendelea kukwaza uzalishaji kuweza kuwa wa ushindani wa kibiashara. Wazalishaji wa

ndani wenyewe hawawezi kushindana kwa bei na ubora dhidi ya bidhaa za nje za mifugo.

Zanzibar inaingiza bidhaa nyingi za mifugo kutoka nje, hasa za kuku kama vile nyama na

mayai. Kwa hiyo, msaada mkubwa kwa wajasiriamali wetu wa mifugo katika pembejeo

unapaswa kutetewa ili kupunguza mzigo wa kifedha kwa wafugaji katika kugharamia

pembejeo za uzalishaji.

Page 65: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

49

Changamoto

Bei za pembejeo za uzalishaji wa mifugo ikiwa ni pamoja na mitambo, vyakula na dawa za

mifugo ni kubwa kulinganisha na bei hizo katika nchi jirani. Bei hizo zinapelekea

kutokuwepo kwa ushindani katika sekta ya mifugo. Hali hii imewafanya wazalishaji wa

ndani kushindwa kuendeleza soko la ushindani. Hivyo, kutokana na ukosefu wa msaada

katika ununuzi wa pembejeo za uzalishaji, wazalishaji wadogo wadogo wa mifugo

hushindwa kuendelea na biashara zao.

Lengo:

Kuwashajiisha wajasiriamali wadogo wadogo wa mifugo kuzalisha kwa wingi kwa

kuwawezesha kununua pembejeo za mifugo ili kukabiliana na ushindani wa soko katika

ngazi za kitaifa na kikanda.

Tamko la Sera

Serikali itachukua juhudi za kusaidia wajasiriamali wa mifugo wa ndani kuweza kupata

pembejeo za uzalishaji wa mifugo kwa bei nafuu.

Mikakati ya Sera:

Kuanzisha utaratibu utakaoweza kusaidia wajasiriamali wa mifugo kununua pembejeo

za mifugo kwa bei nafuu na kufanya mapitio ya kila mwaka ya uzalishaji na mazao ili

kutathmini kiasi cha faida wanayopata wajasiriamali ili iwe kama kigezo cha

kusimamia viwango vya msaada vinavyohitajika.

Kwa kushirikiana na taasisi inayohusika na biashara na masoko, hatua za kupambana

na uingizwaji mkubwa wa bidhaa za mifugo zitachukuliwa.

Kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Mifugo ili kugharamia misaada ya pembejeo kwa

wafugaji na wajasiriamali.

Kutoza ushuru maalumu kwa bidhaa za mifugo kutoka nje ya Jumuiya ya Maendeleo

ya Kusini mwa Afrika na nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki kuweza

kuchangia Mfuko wa Maendeleo ya Mifugo.

Kuweka vivutio maalumu kwa ajili ya uwekezaji katika sekta ya mifugo

kwa mfano, viwanda vya chakula cha mifugo, dawa za mifugo, mashamba ya

uzalishaji, mitambo ya usindikaji na vifaa vya kuhifadhia.

Kukuza matumizi ya rasilimali za jadi zilizoimarishwa au teknolojia rahisi

Page 66: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

50

Kuhimiza uundaji wa jumuiya za wafugaji katika uzalishaji na masoko ya bidhaa za

mifugo kwa lengo la kutetea kupunguza gharama za pembejeo na kuongeza faida.

5.1.8.2. Rasilimali ardhi

Hapa Zanzibar, rasilimali ardhi imegawika katika makundi makubwa mawili, ardhi ya

kilimo na ardhi ya maweni. Ardhi ya kilimo ina udongo wenye kina kirefu na rutuba na

shughuli nyingi za kilimo hufanyika. Ardhi ya maweni haina udongo mwingi, kame na

haihifadhi maji ya kutosha. Zanzibar ni visiwa vidogo, vyenye rasilimali ardhi chache hasa

kwa ajili ya shughuli za mifugo. Mifumo ya umiliki wa ardhi haiko wazi kiasi kwamba

ardhi hiyo inatumiwa na mtu yeyote bila ya utaratibu maalumu na bila ya kuwa na uhakika

wa umiliki.

Changamoto:

Uhaba wa ardhi ya malisho ya mifugo ni moja kati ya vikwazo vinavyozuia maendeleo ya

mifugo hapa Zanzibar. Zaidi ya kuwa na uhaba wa ardhi ya malisho, lakini pia hakuna sera

ya ardhi. Mpango wa Matumizi ya Ardhi uliopo umepitwa na wakati na mfumo wa umiliki

wa ardhi haujafafanuliwa vyema.Jambo hili linasababisha matumizi mabaya ya ardhi.

Lengo

Kuendeleza maeneo ya malisho kwa ajili ya maendeleo sahihi ya mifugo

Tamko la Sera:

Wizara ya Mifugo na Uvuvi itashawishi utayarishaji wa sera ya ardhi ili kuhamasisha

matumizi endelevu kwa ajili ya maendeleo ya mifugo ikiwa ni pamoja na matumizi ya

mfumo wa haraka wa uzalishaji mkubwa kwa kutumia eneo dogo ili kupunguza shinikizo

la ardhi.

Mikakati ya Sera:

Kutetea uandaaji na utekelezaji wa Sera ya Ardhi.

Kuhakikisha kuwa Sera ya Ardhi ya kitaifa inatenga maeneo kwa ajili ya sekta ya

mifugo.

Kufanya mapitio ya maeneo ya kilimo cha kiikolojia ili kushughulikia masuala mapya

(kwa mfano ukuaji wa miji, mabadiliko ya hali ya hewa na rutuba ya udongo),

Page 67: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

51

Kuandaa majadiliano na jamii pamoja na wadau wengine juu ya mgao warasilimali ardhi

na matumizi endelevu kwa ajili ya maendeleo ya mifugo ili kupunguza migogoro.

Kutetea Mpango wa Matumizi ya Ardhi uliopo ili kukidhi mahitaji ya sekta ya Mifugo.

Kuhimiza kilimo mseto (kwa mfano mseto wa mazao ya kilimo / mifugo /samaki /

misitu) kwa ajili ya kupata lishe endelevu,

Kuwezesha kampeni ya kujenga muamko wa matumizi endelevu ya ardhi kwa ajili ya

uzalishaji endelevu wa mifugo.

Kushawishi kufanya mapitio na kutekeleza sheria zinazohusiana na ardhi ikiwa ni

pamoja na sheria za msingi na nyenginezo.

5.1.8.3. Maendeleo ya Miundombinu ya Mifugo

Miundombinu ya mifugo kama vile zahanati, majosho, vituo vya karantini, maabara,

machinjio na mazizi ni muhimu katika maendeleo ya mifugo. Hadi sasa miundombinu

hiyo yote inatolewa na Serikali ingawa sekta binafsi ina jukumu kubwa la kuanzisha na

kuendeleza miundombinu hiyo.

Changamoto:

Uhaba wa miundombinu ambayo ni muhimu kwa ajili ya utoaji wa huduma za mifugo

umeathiri maendeleo ya sekta hii nchini.

Lengo

Kutoa huduma zote muhimu za kusaidia ufugaji kwa maeneo yote nchini ambapo sekta

ya mifugo inachangia sehemu kubwa ya mapato kwa jamii.

Tamko la Sera:

Kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo, Serikali itaweka miundombinu muhimu

kwa ajili ya kutoa huduma za mifugo katika maeneo yote nchini ambayo sekta binafsi na

Serikali za Mitaa zinaona hazipati faida, wakati sekta ya mifugo inachangia sehemu kubwa

ya mapato ya watu katika jamii hiyo.

Page 68: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

52

Mikakati ya Sera:

Kushajiisha sekta binafsi na Serikali za Mitaa kutoa huduma za mifugo kama vile

machinjio, majosho, mazizi, maabara, kliniki na nyenginezo katika maeneo ambayo

sekta ya mifugo inatoa mchango mkubwa wa mapato katika jamii.

Serikali kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo itatoa huduma za mifugo kama

vile machinjio, mazizi, maabara, kliniki katika maeneo ambayo hayana huduma hizo.

Kuwezesha uwekezaji katika miundombinu ya mifugo.

Kuhamasisha jamii za wafugaji kusimamia vyema miundombinu ya mifugo iliyojengwa

na Serikali.

5.1.8.4. Rasilimali Maji

Kuna vyanzo vikuu viwili vya maji hapa Zanzibar, Maji ya chini ya ardhi na juu ya ardhi.

Maji ya chini ya ardhi ni pamoja na visima vifupi, mashimo na chemchem, wakati maji ya

juu ya ardhi inajumuisha vijito, mito, mabwawa, n.k.

Changamoto:

Usambazaji wa maji kwa ajili ya maendeleo ya mifugo ni mdogo kutokana na kiwango cha

chini cha uchimbaji wa visima, uhifadhi duni wa maeneo ya rasilimali maji na usambazaji

usiozingatia usawa.

Lengo

Kuongeza kasi ya usambazaji wa maji kwa ajili ya uzalishaji wa mifugo

Tamko la Sera:

Hatua za pamoja zitakazoshirikisha Serikali,Washirika wa Maendeleo na jamii kwa jumla

zitachukuliwa ili kuendeleza rasilimali maji kwa ajili ya matumizi ya mifugo na

kuimarisha fursa za upatikanaji wa huduma hiyo kwa jamii za wafugaji.

Mikakati ya Sera:

Kuimarisha uwezo wa wafugaji na wajasiriamali juu ya teknolojia sahihi za uvunaji

maji,

Kuanzisha kampeni za kujenga muamko juu ya uvunaji wa maji ya mvua.

Page 69: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

53

Kuimarisha uwezo wa wafugaji na wajasiriamali wa mifugo ili kupunguza upotevu wa

maji na kuhamasisha uhifadhi wa maji kwa kushirikiana na wadau wengine.

Kushawishi mamlaka zinazohusika kupunguza ushuru wa maji kwa ajili ya matumizi ya

mifugo,

Kulinda vyanzo vya maji na maeneo ndani ya eneo la uzalishaji wa mifugo,

Kuchimba visima ili mifugo iweze kupata maji.

5.1.8.5. Wanyama Wanaotumika kwa kazi

Wanyama wanaotumika sana hapa Zanzibar ni punda na ng’ombe. Matumizi ya wanyama

hawa kama chanzo cha nguvukazi ni teknolojia sahihi yenye gharama nafuu na endelevu

kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za vijijini na kandokando mwa miji. Wanyama

hawa wanaweza kutumika katika kazi za kulima, kipando, kusafirisha bidhaa na kupalilia

na hivyo kuokoa nguvu na muda wa kazi kama ingefanywa na binadamu .

Changamoto:

Kuna matumizi mabaya ya wanyama wanaotumika kwa kazi yanayofanywa na wamiliki

ambao unasababishwa na ufugaji duni na usio na huruma.

Lengo

Kuimarisha matumizi ya wanyama hawa kwa kuwawezesha wamiliki kuwatumia kwa

usahihi.

Tamko la Sera:

Serikali itaongeza jitihada za kustawisha afya na ustawi wa wanyama wanaotumika kwa

kazi na hivyo kunyanyua maisha ya jamii.

Mikakati ya Sera:

Kuwaongezea taaluma ya ufugaji wa wanyama hawa wafugaji na wadau wengine katika

maeneo ya vijijini na kandolando mwa miji kwa ajili ya matumizi bora.

Kuanzisha majadiliano na wadau, Washirika wa Maendeleo ili kutoa misaada ya

kitaalamu na kifedha kwa ajili ya uzalishaji wa wanyama hawa na wengine

wanaohusiana nao,

Matumizi ya mbegu bora za ng'ombe kwa ajili ya uzalishaji wa wanyama kazi,

Page 70: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

54

Kufanya utafiti juu ya matumizi sahihi ya ng’ombe dume kwa kuvutia mizigo mizito na

kulimia kwa njia bora za uzalishaji na uchaguzi wa wanyama bora,

Kuiwezesha jamii juu ya matumizi bora ya wanyama kazi

5.1.8.6. Wizi wa Mifugo

Wizi wa mifugo umekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya mifugo. Aidha, kuna

ongezeko la wizi wa mazao ya kilimo ambao unaathiri shughuli za ufugaji. Taasisi zote

zinazohusika na utekelezaji wa sheria zinahitaji kuimarishwa ili kuweza kukabiliana na

wizi huo. Jambo hili linalazimisha kufanya marekebisho ya sheria zilizopo ili kuweza

kushughulikia wizi huo kikamilifu.

Changamoto:

Kuna ongezeko la wizi wa mifugo ambao unakatisha tamaa wafugaji. Suala hili

limepelekea wafugaji wengi kuacha shughuli hiyo na hatimae kuathiri nafasi za

ajira hapa Zanzibar.

Lengo

Kuzuia wizi wa mifugo ili kuhamasisha ufugaji, uwekezaji na kuongeza uzalishaji wa

mazao ya mifugo.

Tamko la Sera:

Wizi wa mifugo utadhibitiwa kwa kushirikiana na serikali za mitaa, vyombo vya

utekelezaji wa sheria na jamii kwa jumla.

Mikakati ya Sera:

• Kufanya mapitio ya sheria zinazohusiana na wizi wa mifugo.

• Kuhamasisha uelewa wa umma juu ya kuzuia wizi wa mifugo,

• Kuvijengea uwezo vyombo vya utekelezaji wa sheria, wafanyakazi wa serikali na

mamlaka za serikali za mitaa juu ya sheria na kanuni zilizopo,

• Kuimarisha hatua za upekuzi wa wanyama katika vizuizi vyote vya uangalizi wa

polisi.

• Kuanzisha mifumo ya utambulisho na ufuatiliaji wanyama.

Page 71: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

55

5.1.8.7 Uzalishaji na matumizi ya bayogesi

Umasikini miongoni mwa maeneo ya vijijini na ongezeko kubwa la bei za nishati (umeme

na mafuta) imesababisha kupanda kwa gharama za maisha. Jambo hili limepelekea

matumizi zaidi ya kuni na uharibifu wa ardhi na hivyo kusababisha uharibifu wa mazingira.

Wanyama wanaweza kutumika kwa ufanisi kuzalisha bayogesi kama chanzo mbadala cha

nishati inayotokana na kinyesi na mikojo ya mifugo. Hata hivyo, chanzo mbadala cha

nishati hii kinaweza kutumika kama nishati ya kupikia, taa, nk. Nishati hii ambayo

haijatumika ipasavyo, kwa kiasi kikubwa itapunguza matumizi ya kuni, mafuta ya taa na

umeme.

Changamoto:

Ukosefu wa elimu juu ya matumizi ya bayogesi na bei kubwa ya ufungaji wa mitambo

inapunguza matumizi ya bayogesi na teknolojia ya nguvu ya jua katika maeneo ya vijijini.

Lengo

Kukuza matumizi ya samadi kwa ajili ya teknolojia ya uzalishaji wa bayogesi ili

kuimarisha maisha ya watu wa vijijini na wakati huohuo kuhifadhi mazingira.

Tamko la Sera:

Hatua zitachukuliwa kuhamasisha wafugaji kuzalisha na kutumia bayofueli kama chanzo

mbadala cha nishati.

Mikakati ya Sera:

Kuwezesha kujenga muamko na mafunzo juu ya uzalishaji na matumizi ya bayogesi,

Kuanzisha na kutekeleza mipango kwa ajili ya kukuza matumizi ya bayogesi kama

chanzo mbadala cha nishati kwa kushirikiana na sekta binafsi na wadau wengine.

Kushirikiana na mashirika ya kitaifa, kikanda na kimataifa katika masuala ya bayogesi

5.1.8.8. Huduma za Fedha kwa ajili ya Maendeleo ya Mifugo

Maendeleo ya makampuni ya biashara ya mifugo hutegemea fursa za upatikanaji wa

fedha. Hivi sasa, hakuna hata benki moja maalum ya biashara ambayo inatoa mikopo

kwa ajili ya maendeleo ya sekta hii. Zipo taasisi ndogo chache za fedha zinazotoa

mikopo ya kuendeleza sekta hii lakini hazikidhi mahitaji.

Page 72: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

56

Changamoto:

Hakuna fursa ya upatikanaji wa mitaji maalumu kwa ajili ya uwekezaji wa mifugo

inayotolewa na benki za biashara na mipango ya kukopeshana.

Lengo

Kuwezesha upatikanaji wa fursa za mitaji maalumu kwa wajasiriamali wa sekta ya mifugo

kutoka benki za biashara na taasisi za fedha.

Tamko la Sera:

Serikali itasaidia uanzishwaji wa taasisi madhubuti za fedha na bima kwa ajili ya

uwekezaji katika sekta ya mifugo na kuhamasisha uundaji wa mifuko ya kuweka na

kukopa ili kusaidia maendeleo ya sekta ya mifugo.

Mikakati ya Sera:

Kuhimiza uundaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo na Vyama vya Akiba na Mikopo

kwa wafugaji ili kukidhi mahitaji ya mikopo na kuweka akiba.

Kusaidia uanzishwaji wa benki ya kilimo ili kutoa mikopo ya uwekezaji katika

makampuni ya biashara ya sekta ya mifugo kwa masharti nafuu,

Kukuza uhusiano baina ya jumuia za wadau wa sekta ya mifugo wa ngazi za chini na

taasisi ndogondogo za fedha nchini.

Kupata fedha kutoka vyanzo vya ndani na nje kwa ajili ya programu za maendeleo ya

sekta ya mifugo.

Kusaidia uanzishwaji wa miradi ya bima ya sekta ya mifugo na matumizi ya bima ya

sekta ya mifugo kama dhamana kwa ajili ya kupata mikopo ya benki,

Kuanzisha programu za taarifa za kifedha na usambazaji wa taarifa hizo.

Kushajiisha uanzishwaji wa mpango wa dhamana ya mikopo.

Serikali itashirikiana na taasisi nyengine kuendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa

wafugaji, hasa wanawake na vijana.

5.1.8.9. Wanawake na Mifugo

Wanawake wanachukua nafasi muhimu katika maendeleo ya shughuli mbalimbali za

kilimo na mifugo ikiwa ni pamoja na utafutaji wa kuni, madondo, chaza, kilimo cha

mwani na ufugaji. Hata hivyo, kwasababu ya baadhi ya masuala ya kijamii na kitamaduni,

wanawake humiliki hisa ndogo inayotokana na shughuli za kilimo na ufugaji.

Page 73: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

57

Changamoto:

Kwa ujumla, ushiriki wa wanawake katika uzalishaji wa mifugo ni mdogo kutokana na

ujuzi mdogo wa ujasiriamali wa mifugo, upungufu wa mitaji, fursa chache ya kupata

fedha, ugawaji wa kipato usiozingatia usawa, kunyimwa fursa ya kufanya maamuzi na

kufanyishwa kazi kupita kiasi pamoja na masuala ya jamii na familia.

Lengo

Kuimarisha kiwango cha ushiriki wa wanawake katika uzalishaji wa mifugo

Tamko la Sera:

Serikali itafanya jitihada kuwawezesha wanawake kushiriki katika shughuli za uzalishaji

wa faida katika mifugo, lakini wakati huohuo wanalinda haki zao na kuhamasisha

mgawanyo sawa wa faida za rasilimali za ufugaji na kuondoa vikwazo vya kisheria,

kiuchumi, kijamii na kiutamaduni ili waweze kushiriki.

Mikakati ya Sera:

Kuhamasisha wanawake katika uzalishaji wa mifugo na kupata ujuzi wa ujasiriamali.

Kuongeza ushiriki wa wanawake wazalishaji mifugo katika Shamba Darasa.

Kutetea kampeni za kujenga muamko juu ya haki za wanawake na usawa,

Kutetea shughuli za kuhamasisha jamii, hasa wanaume na serikali za mitaa juu ya

masuala ya jinsia.

Kuongeza fursa za wanawake kupata mikopo, teknolojia ya usindikaji wa bidhaa za

mifugo, miundombinu ya soko, umiliki wa ardhi na rasilimali nyingine za uzalishaji kwa

kushirikiana na taasisi zinazohusika.

5.1.8.10. Ajira ya Vijana na Mifugo

Ukosefu wa ajira kwa vijana na kutotumika ipasavyo katika sekta ya mifugo ni

changamoto inayoikabili jamii hivi sasa. Jambo hili linahusishwa na uhaba wa elimu ya

amali, malipo madogo na mafunzo kwa ajili ya vijana, uwezo mdogo wa kifedha, ardhi na

mali nyingine za uzalishaji pamoja na majukumu ya kijadi yanayohusishwa na jamii, hasa

kwa wanawake vijana.

Page 74: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

58

Changamoto:

Ushiriki mdogo wa vijana katika uzalishaji wa mifugo ni changamoto inayosababishwa

pamoja na mambo mengine na muamko mdogo juu ya fursa zilizopo za kujiajiri katika

sekta ya mifugo.

Lengo:

Kuendeleza usawa wa kijinsia katika ajira zenye staha katika sekta ya mifugo, hasa kwa

vijana

Tamko la Sera:

Serikali itaongeza ushiriki wa vijana katika biashara ya mifugo yenye faida.

Mikakati ya Sera:

Kuhimiza kampeni za kujenga muamko juu ya faida za ajira za uzalishaji wa mifugo

kwa vijana.

Kuhamasisha matumizi ya programu za elimu ya amali katika uzalishaji wa mifugo,

maisha na ujuzi wa ujasiriamali, uhamasishaji na uundaji wa vikundi, uongezaji wa

kipato kwa vijana wa kike na wa kiume kwa misingi ya usawa.

Kuimarisha / kuendeleza taratibu za vijana wa kike na wa kiume kupata fursa ya ardhi

na maliasili, miundombinu, teknolojia ya kuokoa nguvu kazi, masoko, huduma rafiki

za fedha na / mikopo kwa vijana kwa kuzingatia vijana waliokosa fursa ya kupata

huduma za kifedha za benki za kawaida za biashara ,

Kukuza na kuimarisha uwekezaji wa mifugo kwa kuweka vivutio na kuwafanya vijana

kudumu katika uzalishaji wa mifugo na kuzuia uhamaji wao,

Kukuza na kuendeleza uwezo wa vijana katika mchakato mzima wa mzunguko wa

thamani pamoja na faida ya bidhaa hai, kukuza uelewa juu ya uthibitisho wa bidhaa.

Kuongeza ukusanyaji wa fursa za taarifa zinazohusiana na umri na jinsia juu ya ajira na

masuala ya tija katika sekta ya mifugo kwa ajili ya maendeleo ya sera na kuandaa

mpango mkakati,

Kukuza na kuanzisha skuli za wafugaji wadogo wadogo vijana kama njia ya

kushawishi kupata ujuzi kwa ajili ya ajira zenye kuzalisha na endelevu katika sekta ya

mifugo,

Page 75: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

59

Kuteua mtu atakaehusika na ajira na kazi za staha katika wizara husika kushiriki

kikamilifu katika mitandao ya taasisi kwa taasisi kwa ajili ya mkabala jumuishi na

madhubuti wa kukuza ajira kwa vijana katika sekta ya mifugo.

5.1.8.11. Ajira ya watoto na Mifugo

Hapa Zanzibar, sekta ya kilimo (ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa mazao, uvuvi na

mifugo) ni moja ya maeneo makuu yanayosababisha ajira za watoto. Ajira ya watoto

huathiri maendeleo ya skuli na matarajio ya ajira za kipato kwa vijana na watu wazima.

Watoto ni mustakabali wa uchumi wa nchi, na makuzi yao ya kiwiliwili na kiakili ni

muhimu kwa sekta ya uzalishaji wa mifugo yenye nguvu. Baadhi ya ushiriki wa watoto

katika kazi unaweza kusaidia kuwafundisha ujuzi kwa ajili ya maisha ya baadae, hata

hivyo aina nyingine za ajira zinawanyonya watoto (ajira ya watoto) na inaweza kuwa na

madhara kwa afya au kuzorotesha maendeleo yao ya elimu. Elimu ya watoto ni muhimu ili

iweze kukidhi mahitaji ya rasilimali watu wenye ujuzi katika sekta ya mifugo.

Changamoto:

Ajira ya watoto na elimu ndogo inachangia kuweko pengo kubwa kati ya wafanyakazi

wenye ujuzi wa kitaalamu waliopo na idadi inayohitajika kwa ajili ya maendeleo ya sekta

ya mifugo.

Lengo:

Kupunguza ajira ya watoto katika uzalishaji wa mifugo, hasa aina ya ajira yenye madhara

Tamko la sera

Serikali itajenga uwezo wa kukabiliana na tatizo la ajira ya watoto katika mifugo sio tu

kwa kulinda haki za watoto, lakini pia kuimarisha rasilimali watu na matarajio ya ajira

zenye staha kwa vijana.

Mikakati ya Sera:

Kujenga maarifa yenye ubora juu ya ajira kwa watoto katika mifugo na njia mbadala

zinazofaa kwa ajili ya wazalishaji.

Kubuni miradi midogo midogo na kutathmini njia mbadala.

Kuimarisha uwezo wa kukabiliana na tatizo la ajira kwa watoto katika uzalishaji wa

mifugo kwa kujenga msingi wa maarifa na kunyanyua muamko ikiwa ni pamoja na

Page 76: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

60

matumizi ya mkakati wa huduma za elimu kwa wafugaji na njia nyingine kama vile

shamba darasa na shamba la wafugaji wadogo,

Kuendesha mafunzo kwa wafanyakazi wa wizara na taasisi zinazohusika juu ya

masuala ya ajira kwa watoto,

Kukusanya na kubadilishana uzoefu juu ya kuzuia ajira kwa watoto katika uzalishaji wa

mifugo, na hasa juu ya uhusiano wake na ajira za vijana.

Kuteua mtu anaehusika na ajira kwa watoto katika Wizara husika na kushiriki

kikamilifu katika kamati ya uendeshaji wa kitaifa kuhusu ajira kwa watoto.

5.1.8.12. Usimamizi wa Maafa ya Mifugo

Maafa au majanga ni matukio yasiotarajiwa yanayoleta madhara kwa ghafla na

kusababisha kupanguka kwa utaratibu wa maisha na makazi, binadamu,mimea na hata

wanyama kupoteza maisha na mali nyingine. Katika sekta ya mifugo, majanga maarufu

ni: magonjwa ya mripuko kwa wanyama, ukame, moto, mafuriko na wadudu

waharibifu. Mpango wa maandalizi na matumizi ya dharura unapaswa kuwekwa ili

kushughulikia maafa. Mipango kama hiyo ni pamoja na mifumo ya kutoa tahadhari za

mapema, kuwasaidia waliopata maafa na programu za kutoa fidia.

Changamoto:

Maendeleo ya sekta ya mifugo Zanzibar yanaweza kukumbwa na hatari ya ukame, moto

na magonjwa ya kuambukizwa kwa wanyama na maradhi ya zonotiki.

Lengo:

Kuendeleza uzalishaji wa mifugo na mazao yake kwa wafugaji kwa kupunguza kiwango

cha hatari kinachosababishwa na majanga ya asili (majanga na maafa)

Tamko la Sera:

Serikali itachukua hatua endelevu kuimarisha uwezo wa taasisi na uelewa wa jamii juu ya

majanga na mipango ya maandalizi dhidi ya hatari ya magonjwa na majanga mengine.

Mikakati ya Sera:

Kuanzisha majadiliano na wadau na Washirika wa Maendeleo ili kutoa misaada ya

Page 77: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

61

kitaalamu na kifedha kwa ajili ya uanzishwaji wa mifumo ya tahadhari ya mapema,

Kuandaa na kutekeleza mipango endelevu kwa ajili ya kulinda mifugo na binadamu

dhidi ya athari za magonjwa ya mifugo na majanga mengine.

Kuendeleza kampeni na kujenga muamko kwa kutumia vyombo vya habari kuiandaa

jamii kupambana na majanga.

Kuanzisha mifumo ya kuwekea bima ya mifugo.

Kushirikiana na wadau wengine katika utoaji wa mafunzo ya utaalamu, vifaa, misaada

ya kifedha ili kupunguza madhara ya majanga kwa wanyama na kaya zilizoathirika.

Kuingiza masuala ya kijinsia katika programu na taratibu zote ili wafugaji

wahudumiwe kwa misingi ya usawa katika mchakato wa kupata fidia.

Kutoa mafunzo ya kijinsia kwa viongozi wanaofanya kazi juu ya masuala ya kutoa

fidia,

Kubuni programu za kusaidia wanawake na vijana katika kudai fidia.

5.1.8.13. VVU, UKIMWI na Mifugo

Watu wanaoishi katika mazingira magumu wanakosa njia za kukabiliana na majanga kwa

wakati na uwezo binafsi wa kuzalisha kipato. Watu kama hawa wapo duniani kote

kutokana na sababu kadhaa ikiwa ni pamoja na VVU na UKIMWI, mabadiliko ya

kiuchumi, majanga ya asili, upungufu wa chakula n.k. Miongoni mwa watu hawa ni

wazee, watoto, yatima, watu wanaoishi na VVU na UKIMWI na watu wenye ulemavu.

Changamoto:

Sekta ya mifugo hutoa fursa ya maisha kwa familia zilizoathiriwa na VVU & UKIMWI

kwa kuwashirikisha katika shughuli za uzalishaji wa mifugo ambazo si ngumu

ikilinganishwa na kilimo cha mazao na kazi nyingine za maisha vijijini. Maofisa elimu

kwa wafugaji kimsingi wanafanya kazi na jamii za vijijini ili kuimarisha uhakika wa

chakula na kustawisha maisha ya kijijini. Hata hivyo, wafanyakazi hawa bado

hawajatumika kikamilifu katika kukabiliana na VVU na UKIMWI katika maeneo yao

husika.

Page 78: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

62

Lengo

Kuongeza uwezo wa maofisa elimu kwa wafugaji kushiriki katika kuingiza masuala ya

chakula katika mipango na programu za kudhibiti VVU / UKIMWI.

Tamko la Sera:

Serikali itatumia maofisa elimu kwa wafugaji wanaofanya kazi na jamii ya vijijini

kuingiza masuala ya VVU na UKIMWI wakati wakifanya kazi zao.

Mikakati ya Sera:

Kuimarisha uwezo wa maofisa elimu kwa wafugaji juu ya taaluma kuhusu VVU &

UKIMWI,

Kukuza kampeni za kujenga muamko kwa njia ya vyombo vya habari na kupunguza

unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na VVU na UKIMWI,

Kutoa elimu juu ya maambukizi ya VVU na UKIMWI kwa jamii za vijijini

zinazoshiriki katika uzalishaji wa mifugo.

Kubuni na kutekeleza miradi midogo midogo kuhusu uzalishaji wa mifugo kwa

familia za watu wanaoishi na VVU na UKIMWI ili nao waweze kufanya kazi za

uzalishaji zenye kukimu maisha yao.

Kuingiza masuala ya VVU na UKIMWI katika wizara inayohusika na mambo ya

mifugo.

5.1.8.14. Mifugo na Mazingira

Kutokana na ukosefu wa matumizi bora na usimamizi wa maliasili, uzalishaji wa mifugo

hapa Zanzibar unaweza kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na uharibifu wa mazingira

ya asili au unaosababishwa na binadamu.

Masuala ya kimazingira yanajumuisha ardhi, maji, hewa, uoto, wanyama na binadamu

ambao wanahitajika ili kuendeleza ufugaji.

Changamoto

Ufugaji mbaya wa wanyama husababisha majanga ya kimazingira kama vile

mmong’onyoko wa ardhi, ukataji misitu, uharibifu wa vyanzo vya maji, uchafuzi wa

mazingira na magonjwa yanayotokana na wanyama

Page 79: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

63

Lengo

Kuendeleza ufugaji bora kwa mazingira endelevu.

Tamko la sera

Serikali itaandaa mazingira bora ya ufugaji wanyama kwa ajili ya uzalishaji endelevu wa

mifugo.

Mikakati ya Sera

Kuingiza masuala ya uzalishaji wa mifugo kwa mujibu wa viwango vya kimazingira

vilivyopendekezwa.

Kuanzisha programu za mafunzo na uhamasishaji katika usimamizi wa maliasili.

Kuanzisha programu za uhamasishaji na mafunzo juu ya usimamizi wa taka taka za

wanyama.

Kutoa misaada ya kifedha na kitaalamu ili kuziwezesha kamati za usimamizi wa

mazingira katika ngazi mbali mbali.

Kuendeleza ufugaji bora, misaada na teknolojia sahihi kwa wafugaji ili kupunguza

uchafuzi wa mazingira.

5.1.8.15 Mifugo na Mabadiliko ya Tabia nchi

Shughuli za kilimo duniani (ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa mifugo) inashikilia nafasi ya

tano kwa utoaji wa jumla wa gesi chafu na hivyo kuchangia mabadiliko ya tabia nchi.

Madhara ya mabadiliko ya tabia nchi yanaweza kubainika kutokana na kuongezeka kwa

joto, kupungua kwa mvua, unyevu na wingi na ubora wa chakula kwa ajili ya mifugo na

binadamu. Mabadiliko haya yanaathiri hewa safi na kusababisha mabadiliko ya mwenendo

wa maradhi ya kuambukiza miongoni mwa wanyama na binadamu.

Changamoto

Uzalishaji mkubwa wa mifugo katika eneo kubwa hupelekea uchafuzi wa hewa katika

maeneo ya uzalishaji, kuchangia mabadiliko ya tabia nchi, kuongezeka maambukizo ya

maradhi miongoni mwa wanyama na baina ya wanyama na binadamu.

Page 80: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

64

Lengo

Kuhamasisha uzalishaji mkubwa wa mifugo katika eneo dogo ambao utapunguza madhara

ya uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.

Tamko la Sera

Serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya mifugo, itaendeleza uzalishaji mkubwa

wa mifugo kwa kutumia eneo dogo na teknolojia rafiki kwa mazingira ili kuzuia

mabadiliko ya tabia nchi.

Mikakati ya Sera

Kuendeleza matumizi ya takataka za wanyama katika uzalishaji wa gesi inayotokana

na vinyesi vya wanyama (bayogesi)

Kuendeleza udhibiti sahihi wa takataka za viwandani na za wanyama.

Kuhamasisha matumizi ya wanyama wanaozaa sana ambao wanapatikana katika

mazingira yetu ya ndani.

Kuendeleza taratibu sahihi za ufugaji zitakazopunguza ongezeko la uchafuzi wa hewa

na mazingira kwa jumla, harufu mbaya inayotokana na mbolea na uwezekano wa

uchafuzi wa maji ya juu ya ardhi

Kuendeleza utekelezaji wa kilimo mseto (mazao na mifugo) ambacho kitapunguza

kiwango cha hewa ukaa katika mazingira.

Kuendeleza matumizi ya teknolojia rafiki kwa mazingira.

5.1.8.16 Ushiriki wa Sekta ya Umma na ya Binafsi

Sekta ya Maendeleo ya Mifugo inaendeshwa kwa ubia baina ya Serikali na Sekta binafsi.

Mchango wa Sekta ya Umma kwa maendeleo ya mifugo ni pamoja na utoaji wa huduma

za matibabu ya mifugo , teknolojia sahihi, huduma za elimu kwa wafugaji, uratibu na

uwekaji wa mazingira bora kwa ajili ya uwekezaji wa mifugo. Sekta binafsi

inashirikishwa katika uzalishaji, usindikaji, utafutaji wa masoko na utoaji wa huduma.

Kuna wajasiriamali wachache makini ambao wanashiriki kwa kiwango kikubwa katika

shughuli za mifugo kwa ajili ya kuendesha maisha yao. Ushirikiano baina ya sekta

binafsi na umma katika maendeleo ya mifugo ni muhimu katika kuongeza

uzalishaji na fursa za ajira.

Page 81: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

65

Changamoto

Wadau wakubwa ushiriki wao katika kuendeleza sekta ya mifugo ni mdogo

.

Lengo

Kukuza ushiriki wa wadau wakubwa katika sekta ya maendeleo ya mifugo.

Tamko la sera

Serikali itaendelea kuhamasisha sekta binafsi kushiriki katika utoaji wa huduma za mifugo

na uzalishaji mkubwa wa bidhaa za mifugo kwa kuekeza katika shughuli za mifugo ili

kutengeneza ajira na kuongeza Pato la Taifa.

Mikakati ya Sera:

Kuendeleza majadiliano baina ya wawekezaji (wafugaji) wa sekta binafsi na taasisi za

umma kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika sekta ya mifugo

Kuandaa sera ya uwekezaji katika sekta ya mifugo ili kuendeleza uwekezaji kwa ajili ya

maendeleo ya sekta hii kama vile viwanda vya chakula, utotoaji vifaranga, vifaa vya

usindikaji, bidhaa za mifugo, uhifadhi wa bidhaa n.k.

Kuweka vivutio kwa ajili ya uwekezaji katika sekta ya mifugo.

Kuimarisha kilimo cha mkataba katika sekta ya mifugo

Kuendeleza uanzishaji wa jumuiya madhubuti ya wazalishaji mifugo na masoko ya

bidhaa za mifugo.

Kukuza biashara na uwekezaji katika sekta ya mifugo kwa kutumia vyombo vya habari,

maonesho ya ndani na kimataifa, na kutetea wahusika kila itakapowezekana.

Page 82: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

66

SURA YA 6: MIUNDO YA KITAASISI NA UDHIBITI

6.1 MIUNDO YA KITAASISI

Wizara ya Mifugo na Uvuvi (WMU) imepewa jukumu la kuongoza na kusimamia

maendeleo ya sekta ya mifugo Zanzibar. Katika suala hili, jukumu kubwa la WMU ni

kuandaa mazingira bora ya kisera yatakayowashajiisha wadau mbali mbali (serikali na

watu binafsi) kushiriki katika kuendeleza sekta hii. WMU ni chombo chenye wajibu wa

jumla wa utekelezaji wa Sera ya Mifugo, lakini jukumu la wadau wengine katika

kufanikisha malengo ya sera hii pia linatambuliwa.

Utekelezaji wa sera hii utahitaji kuratibiwa katika ngazi ya Kitaifa, Mkoa, Wilaya, Wadi

na Shehia. Utaratibu wa utekelezaji wa sera utawekwa ili kuunganisha na kuratibu wadau

mbalimbali. Maofisa wa maendeleo ya mifugo na uvuvi wa wilaya wamepewa jukumu la

uwakala na kuratibu masuala ya utaalamu katika maeneo yao. Katika ngazi ya taifa,

WMU itasimamia utekelezaji wa sera hii pamoja kuunganisha juhudi za wadau ili

kushiriki kikamilifu katika kuendeleza sekta ya mifugo.

Wakati wa uandaaji wa sera hii, uchambuzi yakinifu wa kitaasisi ulifanyika kwa kutumia

mkabala unaotathmini ubora, udhaifu, fursa na changamoto kwa lengo la kuchunguza

uwezo wa taifa wa kusaidia utekelezaji wa Sera ya Mifugo. Kulikua na makubaliano

ya jumla kwamba moyo wa kisiasa uliopo hivi sasa, muundo sahihi wa kitaasisi, uwezo

wa kitaalamu na kifedha na uwezo wa watendaji ni mambo ya msingi katika kufanikisha

utekelezaji wa sera hii.

6.2 Kazi na Wajibu wa Tasisi

Utekelezaji wa Sera ya Mifugo utahusisha kwa kiasi kikubwa taasisi za wadau (Serikali

na binafsi) zinazofanya kazi katika ngazi tafauti. Taasisi muhimu zitakazosaidia

utekelezaji wa sera hii ni pamoja na:-

Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Wizara ya Kilimo na Maliasili

Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati

Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko

Page 83: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

67

Wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya wanawake na Watoto

Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi kiuchumi na Ushirika

Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais (Idara ya Mazingira na Tume ya UKIMWI

Zanzibar).

Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi

Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali

Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais (Idara ya Maafa)

Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano

Wizara ya Afya

Sekta binafsi (zikiwemo Jumuia ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima na

Jumuia za Kiraia)

Jumuia za Kikanda na za Kimataifa.

6.2.1 Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

WMU imepewa mamlaka ya kisheria ya utekelezaji wa Sera ya Mifugo. Wizara hii ni

msimamizi mkuu wa maendeleo ya sekta ya mifugo. Aidha, WMU ina wajibu wa kuandaa

mazingira bora yatakayowavutia wadau kuweza kushiriki kikamilifu katika sekta hii.

Halikadhalika, Wizara imepewa jukumu la kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa sera hii

kwa jumla katika ngazi ya taifa, wilaya na shehia pamoja na kusimamia maadili ya

kitaaluma. Ili kufikia malengo yaliyowekwa, Sera ya Mifugo inapendekeza kuanzishwa

kwa bodi ya ushauri na udhibiti ambayo itafanya kazi kwa karibu na Idara zinazohusiana

na Uzalishaji Wanyama na Utabibu wa Mifugo.

6.2.11 Kamati ya Uratibu wa Sera ya Mifugo

Kamati ya Uratibu wa Sera ya Mifugo imepewa wajibu wa kuratibu shughuli za wadau

katika mchakato wa utekelezaji wa Sera ya Mifugo. Kamati itafanya kazi ya ushauri kwa

ajili ya utekelezaji wenye mafanikio wa Sekta ya Mifugo. Kamati hii itaundwa na

Wakurugenzi wanaohusika na masuala ya sekta ya mifugo katika Wizara na sekta binafsi

zifuatazo:-

Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Wizara ya Kilimo na Maliasili

Page 84: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

68

Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko

Wizara ya kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika

Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi

Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi, na Mipango ya Maendeleo

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Idara ya Kukabiliana na Maafa).

Wizara ya Afya

Sekta binafsi

Mkurugenzi anaehusika na sera chini ya wizara yenye dhamana ya mifugo atakua

mwenyekiti wakati mkurugenzi mwenye dhamana ya Uzalishaji Wanyama katika wizara

hiyo hiyo atakua mkuu wa sekretarieti. Kamati hii itakua ikikutana kila kipindi cha robo

mwaka.

6.2.12. Bodi ya Udhibiti wa Mifugo Zanzibar

Inapendekezwa kuundwa kwa Bodi yenye wajibu wa kudhibiti na kusajili watoaji

huduma za mifugo na kutunza maadili ya kitaaluma katika shughuli zinazohusiana na

mifugo. Wajibu wa taasisi hiyo utabakia kama ni taasisi ya kuwezesha utekelezaji wa

masuala ya sera hii kwa mambo yanayohusiana na lishe ,uzalishaji, afya ya wanyama na

huduma za elimu kwa wafugaji wa mifugo ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa

wafugaji. Kazi nyengine muhimu za Idara ya Huduma za Utabibu wa Mifugo na Idara ya

Uzalishaji wa Mifugo ni kuendeleza ustawi wa wanyama, utafiti, taarifa na masoko ya

mifugo.

6.2.2. Wizara ya Kilimo na Mali ya Asili (WKM)

Wizara ya Kilimo na Mali ya Asili ni mdau muhimu katika kufanikisha maendeleo ya

mifugo. Wizara mbili hizi ni sehemu za maisha ya vijijini. Katika mazingira ya vijijini,

shughuli za uzalishaji wa mifugo zinakwenda sambamba na uzalishaji wa mazao ya

kilimo hapa Zanzibar. Kwa msingi huo, maendeleo ya mifugo lazima yaendelezwe

sambamba na kilimo katika mfumo wa kilimo mseto ili kila sekta iweze kufaidika. Aidha,

Wizara hii inapaswa kujumuisha masomo yanayohusiana na mifugo katika Chuo cha

Mafunzo ya Kilimo Kizimbani (KATI).

Page 85: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

69

6.2.3 Wizara ya Ardhi, Nyumba Maji na Nishati (WANMN)

Ardhi na maji ni rasilimali muhimu kwa ajili ya mifugo. Sera ya Mifugo inatambua kuwa

ugawaji bora wa ardhi na utawala ikiwa ni pamoja na Mpango wa Matumizi ya Ardhi ni

vichocheo muhimu kwa uzalishaji wa mifugo na tija.

Wizara ya Ardhi ina nafasi kubwa katika utekelezaji wa Sera ya Mifugo kwa kuwa

inalinda ardhi kwa ajili ya malisho na uwezo wa uzalishaji wa mifugo kwa njia ya

utekelezaji wa sheria ya ardhi. Aidha, Wizara hii imepewa dhamana ya kuwezesha fursa

za upatikanaji wa maji kwa ajili ya matumizi ya mifugo. Wizara hii ni msimamizi mkuu

wa sekta ya nishati na kwa hivyo inaweza kutoa misaada ya kitaalamu katika uendelezaji

wa nishati anuai ikiwa ni pamoja na gesi.

6.2.4 Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko (WBVM)

Sera hii inatambua nafasi ya WBVM katika kusitawisha soko la ndani na nje la bidhaa za

mifugo. Kwa kupitia sera ya Biashara, Sera ya Biashara Ndogondogo na Kati, Mkakati wa

Maendeleo wa Uuzaji Bidhaa Nje, Serikali itaimarisha utekelezaji wa utaratibu huu na

kuendelea kuhamasisha uwekezaji mitaji midogo na mikubwa kwa kushirikisha sekta

binafsi katika maendeleo na ukuaji wa uchumi.

6.2.5 Wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto

(WUJMVWW)

Wizara hii imepewa jukumu la kulinda ustawi wa jamii, haki za vijana, wanawake na

watoto. Wizara hii ina jukumu la kuhamasisha jamii kuhusu masuala ya uzalishaji mali na

ya kijinsia ambayo yote yanatambuliwa kama mambo muhimu katika utekelezaji wa Sera

ya Mifugo.

6.2.6 Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika (WKUWKU)

Wizara hii ina wajibu wa kufanya usajili, kutoa mafunzo na kusimamia maendeleo ya

Jumuiya za kuweka na kukopa na uanzishaji wa vyama vya ushirika katika utekelezaji wa

Sera ya Mifugo. Kuhusu utekelezaji wa Sera hii ya Mifugo, Wizara inategemea kusaidia

kuimarisha vyama vya mifugo kwa kutoa usajili na huduma muhimu za mafunzo na

ukaguzi wa mahesabu kwa ajili ya maendeleo ya chama kinachohusika, wazalishaji,

Page 86: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

70

Ushirika wa Akiba na Mikopo na Vyama vya Akiba na Mikopo. Aidha, Wizara hii

itakuza stadi za wajasiriamali na kutoa misaada ya kifedha.

6.2.7 Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (ORMBLM)

Sera ya Mifugo imeitaka Ofisi hii kuratibu utaratibu wa utekelezaji kutoka ngazi ya Shehia

hadi Wilaya. Wizara hii itaimarisha utekelezaji wa sheria katika kupambana na wizi wa

mifugo, ukiukwaji wa haki za wanyama na kusaidia kudhibiti uingizaji haramu wa

wanyama Zanzibar. Aidha, Wizara hii itasaidia katika uwezeshaji na utunzaji wa sheria na

utengamano ambao utapelekea uhifadhi bora wa mazao ya mifugo na bidhaa za mifugo

kupitia uongozi wa wilaya, Halmashauri za Mitaa na Kamati za Ushauri za Shehia.

6.2.7 Ofisi ya Makamo wa kwanza wa Rais (Idara ya Mazingira, Tume ya

UKIMWI Zanzibar)

Maendeleo endelevu ya mifugo pamoja na mambo mengine yanahitaji uhifadhi bora wa

mazingira ili kuwezesha ukuaji na ustawi wa wanyama. Kwa mujibu wa utekelezaji wa

Sera ya Mifugo. Ofisi hii inatarajiwa kuwa na jukumu muhimu la kuhakikisha kwamba

shughuli za uzalishaji na ustawi wa wanyama haliathiriwi au linaathiriwa na athari za

mazingira. Tume ya UKIMWI Zanzibar inatarajiwa kufanya kazi sambamba na Wizara

yenye jukumu la kusimamia maendeleo ya mifugo ili kuweza kushughulikia masuala ya

VVU na UKIMWI.

6.2.9 Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo (ORFUMM)

Ofisi hii imepewa kazi ya jumla ya usimamizi wa uchumi na fedha katika serikali, pia

inashughulikia moja kwa moja mipango ya kitaifa ya maendeleo, masuala ya bajeti na

matumizi. Aidha, Ofisi ni msimamizi wa programu na sera za kitaifa ikiwa ni pamoja na

Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUZA II) na Dira 2020. Ofisi

hii itakua na jukumu muhimu la utekelezaji wa Sera ya Mifugo kwa kutoa msaada wa

kifedha na kuendeleza uwekezaji katika sekta ya mifugo.

Page 87: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

71

6.2.10 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali (WEMA)

Wizara hii ina wajibu wa kutoa mafunzo ya elimu ya msingi, sekondari, ufundi na amali

nchini kote. Inatarajiwa kuwa ufugaji na masomo yenye kuhusiana nayo yanaweza

kuanzishwa kwa mafanikio katika skuli za msingi, sekondari na vyuo vya amali. Aidha,

Sera ya Mifugo itaongeza matumizi ya taifa ya bidhaa za mifugo kwa kila mtu kwa

kuanzisha kampeni za unywaji wa maziwa katika skuli za maandalizi, msingi na

sekondari.

6.2.11 Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Idara Kukabiliana na Maafa)

Idara hii imepewa jukumu la kuratibu juhudi za taifa za kukabiliana na mazingira ya

kidharura. Idara hii ina kazi muhimu ya kuhakikisha usalama wa jamii dhidi ya maafa

yakiwemo maradhi ya miripuko ya wanyama na binaadamu, mashirikiano na Idara ya

Kukabiliana na Maafa na wadau wengine. Sera ya Mifugo imeandaa mikakati inayoweza

kuwasaidia wafugaji kuweza kukabiliana na hasara zinazosababishwa na majanga.

6.2.12 Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo (WHUUM).

Wizara hii ina jukumu la kusimamia matumizi ya vyombo vya habari na ina wajibu wa

kutoa msaada unaohitajika kwa ajili ya mfumo wa mawasiliano katika jamii. Kwa hivyo

ni muhimu kwa Wizara hii kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kujenga muamko

ili kushughulikia masuala yanayohusiana na ufugaji, udhibiti wa magonjwa ya wanyama

na ustawi wa wanyama. Aidha, Wizara hii ina kazi muhimu za kusaidia utekelezaji wa

Sera ya Mifugo kupitia mkakati mkuu wa mawasiliano ambao utaweka mikabala

itakayotumika katika kuwafikia na kushirikiana na wadau kwa njia ya kufanya uratibu.

Aidha, sekta ya utalii ni mnunuzi muhimu wa bidhaa za mifugo.

6.2.13 Wizara ya Afya (WA)

Wizara ya Afya na WMU zina jukumu la pamoja la udhibiti na uchunguzi wa maradhi ya

zonotiki kwa kutumia (“mkabala mmoja wa tiba”). Kwa kuongezea, Bodi ya Chakula,

Madawa na Vipodozi imepewa jukumu la kusimamia na kudhibiti viwango vya usalama

wa chakula, uingizaji, uhifadhi na matumizi ya bidhaa za mifugo.

Page 88: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

72

6.2.14 Wizara ya Mawasiliano na Miundombinu.

Utoaji wa huduma za mifugo na mazao ya mifugo kwa wakati katika maeneo makuu ya

soko unahitaji njia za mawasiliano na usafiri zenye kuaminika na zenye ufanisi. Hivyo, ni

wajibu wa Wizara hii kuweka miundombinu muhimu kwa mawasiliano ya vijijini na

mtandao wa usafiri. Hii inajumuisha huduma bora za mawasiliano ya simu na mitandao

ya barabara.

6.2.15 Jumuia Zisizo za Kiserikalli

Hivi sasa, kuna idadi kubwa ya jumuia za kiraia, kitaalamu, wazalishaji, mashirika ya dini,

wauzaji wa pembejeo n.k. Taasisi hizi zina jukumu muhimu katika nyanja mbalimbali za

utekelezaji kama vile kutoa huduma za elimu kwa wafugaji na msaada wa kifedha. Sera ya

Mifugo inahimiza ushiriki wa wadau katika ngazi zote za utekelezaji wake.

6.2.15 Jumuia za Kikanda na Kimataifa

Zanzibar inaweza kufaidika na hatua nyingi zilizopo za Kikanda na Kimataifa katika

programu za maendeleo ya sekta ya mifugo kama vile Jumuiya ya Afrika Mashariki,

SADC, Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na Mashirika mengine ya kitaifa. Maeneo

hayo ni pamoja na Usalama wa chakula, magonjwa ya mifugo yanayovuuka mipaka,

Zonosisi na CODEX Alimentarius

6.2.16 Washirika wa Maendeleo

Hivi sasa, kuna idadi kubwa ya washirika wa maendeleo ambao wanachangia sekta ya

maendeleo ya mifugo Zanzibar. Sera ya Mifugo inawashajiisha washirika hawa wa

maendeleo kuendeleza misaada yao katika sekta hii ya mifugo.

6.2.18 Sekta Binafsi

Kuna idadi kubwa ya watu na kampuni binafsi zinazojishughulisha na mifugo kama vile

uzalishaji, kuongeza thamani mazao ya mifugo, utoaji wa dawa za mifugo, usambazaji wa

vyakula vya mifugo, vifaa na vyakula.

6.3 Mfumo wa kisheria na Udhibiti

Mfumo wa kisheria ni muhimu katika utekelezaji wa Sera ya Mifugo. Muundo huu

unaweka mifumo ya uendeshaji, viwango na miongozo kwa mujibu wa sheria na kanuni

Page 89: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

73

zinazosimamia ustawi wa wanyama na binadamu ikiwa ni pamoja na kuwalinda dhidi ya

magonjwa ya kuambukiza na Zonosisi. Licha ya kuwepo kwa miundo iliyotajwa hapo juu

lakini kuna upungufu mkubwa ikiwa ni pamoja na miundo hiyo kupitwa na wakati. Hadi

sasa Sheria ya Rasilimali ya mifugo nambari 11 ya 1999 ndio sheria ya msingi ambayo

inadhibiti maadili ya watu dhidi ya ustawi wa wanyama na maendeleo. Sheria hii imelenga

zaidi katika matibabu na udhibiti wa maradhi. Hata hivyo, masuala muhimu

yanayohusiana na udhibiti wa ubora wa pembejeo, huduma za uzalishaji wa wanyama na

maadili ya kitaaluma ya watoa huduma, ufuatiliaji na usajili wa wanyama pamoja na

kuweka pamoja haki za mifugo kupata rasilimali za maisha (kwa mfano maji na ardhi)

hazijashughulikiwa. Upungufu huo na mwengineo unahitaji kushughulikiwa kwa

mashirikiano baina ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na

Wizara ya Nchi (Ofisi ya Rais) Katiba na Utawala Bora.

Zanzibar inaongozwa na utawala wa sheria wenye mfumo huru wa mahakama ambao una

wajibu wa kushughulikia makosa ya jinai.

Uwezo wa chombo hiki unaweza kuimarishwa kwa juhudi za pamoja kutoka vyama mbali

mbali.Kwa kuzingatia ongezeko kubwa la uvunjaji wa haki za wanyama, Sera ya Mifugo

inapendekeza kuanzishwa kwa Mahakama ya Mifugo na kujumuisha kazi zake katika

mifumo iliyopo ya kisheria.

6.3 Uwezo wa Kitaasisi kwa ajili ya Utekelezaji wa Sera ya Mifugo.

Wakati wa uandaaji wa mchakato wa Sera ya Mifugo, uwezo wa taifa wa utekelezaji wa

sera hii ulichunguzwa kwa kupitia warsha za uchambuzi wa Uwezo,Udhaifu, Fursa na

Changamoto. Mchango mkubwa uliotolewa na washiriki umeonesha kwamba nia ya

kisiasa, mipango ya kitaasisi, data za kitaalamu, rasilimali watu na fedha ni mambo

muhimu ambayo yanaweza kuathiri utekelezaji wa sera hii.

Matokeo yameonesha kuwepo kwa moyo wa kisiasa katika utekelezaji wa sera ya sekta

ya mifugo. Dhana ya uvumilivu wa kisiasa, utawala bora na kuwepo kwa sera

zinazohusiana, miundo na utayari wa Washirika wa Maendeleo kusaidia uchumi wa taifa

unaweza kuchangia maendeleo ya sekta hii. Hata hivyo, udhaifu na changamoto

Page 90: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

74

zilizotajwa zinahitaji kupatiwa ufumbuzi endelevu ili kuwezesha utekelezaji bora wa sera

hii.

Wadau wamegundua udhaifu mwingi unaohusiana na misaada inayotolewa na taasisi kwa

maendeleo ya sekta ya mifugo. Hata hivyo imedhihirika kwamba uwezo wa ndani wa

kuendeleza sekta hii upo. Changamoto moja muhimu iliyoyajwa ni kukuza uhusiano na

wawekezaji (wa ndani na wa nje) na kushajiisha uanzishwaji wa kampuni za mifugo.

Maendeleo ya sekta ya mifugo yamegubikwa na uchache wa teknolojia ya kisasa na

taaluma. Sekta hii itachunguza misaada ya kitaalamu kutoka kwa Washirika wa

Maendeleo. Kuwepo kwa mafunzo ya ndani na taasisi za utafiti imeelezwa kwamba ni

vyanzo muhimu vya utaalamu wa ndani unaohitajika kwa ajili ya maendeleo ya sasa na

ya baadae ya sekta ya mifugo.

Uwezo wa kifedha ni sababu nyengine iliyoibuliwa kama ni udhaifu mkubwa ikiwa ni

pamoja na mgawanyo wa bajeti na vyanzo duni vya mapato. Kwa hakika, kuna uchache

wa fedha zinazotengwa kwa shughuli hizi ambazo haziwezi kukabiliana na changamoto

zinazoongezeka zinazohusiana na uzalishaji wa mifugo.

Mwisho, rasilimali watu imeelezwa kwamba ni sababu nyengine ambayo kwa sasa

inakabiliwa na changamoto ya upotezaji nguvu kazi unaosababishwa na wafanya kazi

kwenda nje ya nchi, tishio la VVU na UKIMWI. Hata hivyo, fursa ya sekta hii kutumia

vituo vya mafunzo ya amali, kubadilishana wataalamu na Washirika wa Maendeleo

inaweza kuongeza maarifa na stadi za nguvu kazi za ndani.

Page 91: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

75

7. SURA YA 7: UFUATILIAJI NA TATHMINI

7.1. MAELEZO YA JUMLA

Utaratibu wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Sera ya Mifugo utafuata na muundo wa ufuatiliaji

wa jumla wa MKUZA II ambao umeweka utaratibu madhubuti wa kitaifa wa kukuza

uchumi na kupunguza umaskini. Utaratibu huu unatoa fursa ya kutumia mkabala mmoja

wa ufuatiliaji na tathmini ya athari ya lengo la muda mrefu la kufikia uhakika wa chakula,

kupunguza umaskini na kuongeza mapato ya taifa kupitia sekta ya mifugo.

Sera hii inahimiza mpango shirikishi wa ufuatiliaji na tathmini unaoelekeza kuratibiwa

hatua zinazochukuliwa na kujenga ushirikiano wa karibu kati ya taasisi za umma na

binafsi na Washirika wa Maendeleo kama ilivyoainishwa katika Sura ya 6. Jambo la

msingi ni kwamba Ufuatiliaji na Tathmini hii inapaswa kuendeleza mpango wa utoaji na

utumiaji wa taarifa zilizopo. Hii itafanya kazi ya kufuatilia kwa kutumia shabaha na

viashiria bora na vingi katika ngazi ya kitaifa, kisekta na wilaya.

7.2. Malengo ya Ufuatiliaji na Tathmini

Ufuatiliaji na Tathmini ya Sera ya Mifugo inalenga katika kuweka mfumo wa ufuatiliaji

wa kina ili kuweza kufikia malengo ya sera hii na pia inatarajiwa kuimarisha utekelezaji

wa mipango ya sera hii. Aidha, Ufuatiliaji na Tathmini ya Sera ya Mifugo unatarajiwa

kutoa utaratibu wa kufuatilia utekelezaji wa mikakati ya sera na kubuni njia ya ugawaji na

matumizi ya rasilimali.

Kwa hivyo, Ufuatiliaji na Tathmini hii utahakikisha kuwa inawekwa mipango bora na

muitiko wenye kulenga shabaha kwa wadau wanaohusika ili waweze kufanya maamuzi

kwa wakati ili kuimarisha utoaji wa huduma.Hii Itasaidia kwa:

Kuimarisha utoaji wa huduma ili kukuza ushiriki bora wa jamii, ubora wa mikakati,

uwazi na uwajibikaji kwa lengo la kuhakikisha kwamba rasilimali zinapatikana na

kutumika kwa ajili ya kufanikisha malengo yaliokusudiwa.

Kujifunza kwa vitendo ili kuimarisha ubora, njia na matokeo ya programu.

Page 92: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

76

Kuimarisha mifumo ya kubadilishana taarifa na utetezi wa sera, programu na rasilimali

zinazosaidia katika kupunguza umaskini.

7.3. Mpango wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Sera ya Mifugo

Mpango wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Sera ya Mifugo utasaidia kuhakikisha kwamba

malengo yaliowekwa katika sera hii yanafikiwa ili hatimae kufikia malengo yaliobuniwa

katika MKUZA II.

Mfumo wa Matokeo ya msingi ya Ufuatiliaji na Tathmini utawekwa ili kua na:

Muundo bora wa kuwasilisha matokeo unaotokana na malengo

yaliyofafanuliwa vyema, malengo mahsusi, matokeo na shughuli zilizofanyika kwa

mujibu wa viashiria vinavyolingana, njia ya ukaguzi na matarajio muhimu.

Mkakati uliofafanuliwa vyema wa Ufuatiliaji na Tathmini kwa ajili ya taratibu za

Sera ya Mifugo, mahitaji ya taarifa, zana na mbinu kwa ajili ya ukusanyaji wa takwimu,

uchambuzi na utoaji wa tarifa.

Mpango mpana wa Ufuatiliaji na Tathmini utakaoweka viashiria vya kufuatilia

vinavyohusiana na ukusanyaji wa takwimu na tarifa.

Mfumo wa sera wa kufuatilia unaotegemea viashiria vilivyokubaliwa kama

vinavyotokana na muundo wa bangokitita la kiashiria cha mfumo wa Mpango Mkuu wa

Ufuatiliaji wa MKUZA II

Upimaji na Tathmini za ndani na nje zitajumuisha tafiti za msingi, tathmini ya

wanufaika, tathmini ya kati, tathmini baada ya tathmini na tathmini ya matokeo.

Mipango na mifumo shirikishi jamii ya ufuatiliaji na uwajibikaji (mfano kadi ya

ushindi wa jamii na tathmini ya madhara ya kijamii). Mbinu na zana

zilizotajwa juu pia zitajumuisha uchakataji, uchambuzi, ukusanyaji wa

data, uwasilishaji ripoti kwa utaratibu wa grafu.

7.4. Muundo wa Kitaasisi wa Ufuatiliaji na Tathmini

Katika utaratibu wa Ufuatiliaji na Tathmini, ushiriki wa wadau wote ikiwa ni pamoja na

Serikali, Jumuia za Kiraia, Sekta Binafsi, Jamii na Washirika wa Maendeleo ni muhimu

katika kupanua wigo wa wadau wanaohusika.

Page 93: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

77

WMU itachukua jukumu la msingi la jumla la utambuzi wa rasilimali na kuanzisha

mifumo ya taarifa na uwekaji kumbukumbu katika ngazi ya kitaifa. Katika ngazi ya

wilaya, maofisa wa mifugo na uvuvi kwa kushirikiana na maofisa wengine wa wilaya

watakua na jukumu muhimu la ufuatiliaji na tathmini ya Sera ya Mifugo. Katika ngazi ya

shehia, maofisa mifugo wasaidizi watakua na jukumu la Ufuatiliaji na Tathmini ya sera hii.

Aidha, uoanishaji wa Ufuatiliaji na Tathmini na utaratibu wa kitaifa wa mipango, bajeti na

utoaji wa taarifa ni muhimu ili kuhakikisha kuwa matokeo ya mfumo wa Ufuatiliaji na

Tathmini yanatumika kuongoza taratibu za kitaifa ikiwa ni pamoja na majadiliano ya sera,

mgao wa rasilimali na ushiriki wa Jumuia Zisizokuwas za Kiserikali. Muundo wa

utekelezaji wa ufuatiliaji na tathmini ya Sera ya Mifugo utakua kama unavyoonekana

katika Kielelezo 1.

Page 94: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

78

Kielelezo 1: Muundo wa Utekelezaji wa Ufuatiliaji na Tathmini wa

Sera ya Mifugo

Mfumo wa Utekelezaji wa Ufuatiliaji na Tathmini

wa Serikali kuu

Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara

ya Mifugo na Uvuvi

Bodi ya Udhibiti

wa Mifugo

Zanzibar

Uratibu wa Sera ya

Mifugo

Idara ya Uzalishaji Wanyama na Idara ya Huduma

za Utabibu wa Wanyama

Sekta

binafsi

Washirika

wa

Maendeleo

Ngazi ya

Jamii

Sekta

nyengine

Jumuia za

kiraia

Ngazi ya

wilaya

Page 95: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

79

Utaratibu wa Ufuatiliaji na Tathmini unaweza kufanikiwa kwa njia ya kutumia misingi

elekezi na viashiria muhimu vya utendaji kazi vilivyowekwa na Mfumo wa Ufuatiliaji wa

maendeleo ya MKUZA II. Aidha, mapendekezo ya viashiria maalumu muhimu ni kama

ilivyoainishwa katika Kielelezo 2. Ufuatiliaji wa viashiria vya utendaji utafanyika kila

mwaka wakati tathmini ya utaratibu wa utekelezaji wa sera hii utafanywa katika kila

kipindi cha miaka 5.

Kielelezo 2 Viashiria vikuu maalumu vya utendaji wa mifugo

Kategoria Kiashiria Ngazi ya familia Ngazi ya Jamii Ngazi ya Taifa

1. Tija:

Uzalishaji

wa

wanyama

Idadi ya

wanyama

waliohamilishwa

Idadi au asilimia

ya wafugaji

wanaotumia

Uhamilishaji

Idadi au asilimia

ya wafugaji

wanaotumia

madume bora

Idadi ya familia

zilizoshajiishwa

juu ya matumizi

ya teknolojia

mpya ya

uzalishaji

Ongezeko la

idadi ya

mashamba

yanayotumia

teknolojia

mpya ya

uzalishaji

Ongezeko la

idadi ya

ng’ombe

chotara.

Ulishaji wa

wanyama

ongezeko la

uzito/ uzito wa

nyama baada ya

kuchinjwa, na

ubora

Ongezeko la

idadi ya

wanyama na

kipato cha

familia

Ongezo la

shughuli za

kuongeza

kipato

Ongezeko la

ufugaji wenye

tija

Page 96: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

80

Kiwango cha

uzaaji wa

ng’ombe na

mbuzi

Mapato

yatokanayo na

mazao ya

mifugo kama

vile

maziwa,mayai

Ongezeko la

kipato kwa

mwaka na kwa

kila mtu

Matumizi ya

bidhaa za

mifugo

Ongeza la Pato

la Taifa.

Afya ya

mnyama

Kupunguza kasi

ya mwenendo

wa maradhi na

vifo

Kuwa na

wanyama wenye

afya bora

Ogezeko la

idadi ya mifugo

Punguzo la bei

za dawa

/uzalishaji

Ongezeko la

uzalishaji wa

kipato

Ongezeko la

uzalishaji

3. Upatikanaji

wa soko

Ongezeko la

uuzaji wa bidha

za mifugo

Ongezeko la

matumizi ya

bidhaa za ndani

za mifugo katika

masoko ya miji

na maeneo ya

utalii.

Ongezeko la

kipato cha

familia

Ongezeko la

shughuli za

uzalishaji wa

kipato.

Kupunguza

uagizaji wa

bidhaa za

mifugo

Page 97: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Wizara ya Mifugo na Uvuviwafanyabiashara, wasindikaji, wafugaji wa wanyama rafiki na watumiaji wa mifugo kutoka wilaya zote za Zanzibar walishirikishwa

81

3. Ongezeko la

thamani

Ongezeko la

uzito

(kunenepesha

wanyama)

ukataji wa

minofu na usafi

Uwiano wa

bidhaa za

maziwa

zilizotayarishwa

na kuzifanya

bidhaa kuwa

anuwai

Uwiano wa

bidhaa nyengine

za ndani za

mifugo (mayai,

ngozi, manyoya,

pembe n.k)

Ongezeko la

mazao ya

nyama na ubora

Kupunguza

upotevu wa

bidhaa za

mifugo baada ya

mavuno

Ongezeko la

kipato cha

familia

Ongezeko la

matumizi ya

bidhaa za ndani

na kuongezeka

kwa ajira

Kupunguza

uagizaji wa

bidhaa za

mifugo kutoka

nje ya nchi na

kuongeza

bidhaa katika

soko la kitalii

na nje.

Tanbihi: Viashiria zaidi vinaweza kuanzishwa wakati wa uandaaji wa programu na miradi

muhimu.