idara ya mifugo na uvuvi 1.0 utangulizi 1.1 watumishi ...ifakaratc.go.tz/storage/app/media/mifugo...

12
1 IDARA YA MIFUGO NA UVUVI 1.0 UTANGULIZI Idara ya Mifugo na Uvuvi ina jukumu la kusimamia maendeleo ya Sekta za Mifugo na Uvuvi katika Halmashauri. 1.1 WATUMISHI Idara ya Mifugo na Uvuvi ina jumla ya watumishi 10 kati ya hao watumishi 8 ni wa Mifugo na watumishi 2 ni wa Uvuvi kama mchanganuo unavyoonesha katika jedwali hapa chini: 1.2.SEKTA YA MIFUGO Sekta ya Mifugo inatekeleza shughuli kwa mujibu wa muundo ufuatao a) Huduma za Mifugo (Veterinary Services) . i) Kuratibu na kusimamia udhibiti wa magonjwa ya mifugo. ii) Kusimamia utoaji wa huduma za afya ya wanyama pamoja na kuwawezesha watoa huduma za afya ya wanyama katika kutoa huduma kama vile Tiba na Chanjo kwa mujibu wa Sheria, Taratibu na Kanuni. iii) Kusimamia ukaguzi wa nyama na usafi wa machinjio. iv) Kusimamia na kudhibiti uingizaji na utoaji wa wanyama na mazao yake ndani ya Halmashauri. v) Kusimamia utoaji wa huduma za afya ya wanyama pamoja na kuwawezesha watoa huduma za afya ya wanyama katika kutoa huduma kama vile Tiba na Chanjo kwa mujibu wa Sheria, Taratibu na Kanuni. vi) Kupanga program za muda mfupi,wa kati na mrefu katika kudhibiti magonjwa ya wanyama. vii) Kusimamia uingizaji na usambazaji wa pembejeo za Mifugo. viii) Kukusanya na kuchambua taarifa za magonjwa ya wanyama kwa ajili ya matumizi mbalimbali. ix) Kusimamia utekelezaji wa sheria za Magonjwa ya Wanyama, sheria ya Veternari na kanuni zake na Sheria ndogo za Mifugo b) Huduma za Ugani (Livestock Extension Services) i) Kusimamia uendeshaji wa shughuli za huduma za ugani katika Halmashauri. ii) Kuandaa orodha ya watoa huduma binafsi zikiwemo NGO’s na kuwawezesha kutoa huduma za ugani. iii) Kukusanya na kuchambua takwimu za Mifugo katika ngazi za kata na Halmashauri. iv) Kuwasaidia maafisa ugani kufanya kazi na vikundi vya wafugaji ili waweze kufikia malengo. KITENGO OFISI KUU KATA/VIJIJI Mifugo 3 5 Uvuvi 1 1 JUMLA 4 6

Upload: others

Post on 10-Jan-2020

27 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

1

IDARA YA MIFUGO NA UVUVI

1.0 UTANGULIZI

Idara ya Mifugo na Uvuvi ina jukumu la kusimamia maendeleo ya Sekta za Mifugo na Uvuvi katika

Halmashauri.

1.1 WATUMISHI

Idara ya Mifugo na Uvuvi ina jumla ya watumishi 10 kati ya hao watumishi 8 ni wa Mifugo na

watumishi 2 ni wa Uvuvi kama mchanganuo unavyoonesha katika jedwali hapa chini:

1.2.SEKTA YA MIFUGO

Sekta ya Mifugo inatekeleza shughuli kwa mujibu wa muundo ufuatao

a) Huduma za Mifugo (Veterinary Services) .

i) Kuratibu na kusimamia udhibiti wa magonjwa ya mifugo.

ii) Kusimamia utoaji wa huduma za afya ya wanyama pamoja na kuwawezesha watoa

huduma za afya ya wanyama katika kutoa huduma kama vile Tiba na Chanjo kwa mujibu

wa Sheria, Taratibu na Kanuni.

iii) Kusimamia ukaguzi wa nyama na usafi wa machinjio.

iv) Kusimamia na kudhibiti uingizaji na utoaji wa wanyama na mazao yake ndani ya

Halmashauri.

v) Kusimamia utoaji wa huduma za afya ya wanyama pamoja na kuwawezesha watoa

huduma za afya ya wanyama katika kutoa huduma kama vile Tiba na Chanjo kwa mujibu

wa Sheria, Taratibu na Kanuni.

vi) Kupanga program za muda mfupi,wa kati na mrefu katika kudhibiti magonjwa ya

wanyama.

vii) Kusimamia uingizaji na usambazaji wa pembejeo za Mifugo.

viii) Kukusanya na kuchambua taarifa za magonjwa ya wanyama kwa ajili ya matumizi

mbalimbali.

ix) Kusimamia utekelezaji wa sheria za Magonjwa ya Wanyama, sheria ya Veternari na

kanuni zake na Sheria ndogo za Mifugo

b) Huduma za Ugani (Livestock Extension Services)

i) Kusimamia uendeshaji wa shughuli za huduma za ugani katika Halmashauri.

ii) Kuandaa orodha ya watoa huduma binafsi zikiwemo NGO’s na kuwawezesha kutoa

huduma za ugani.

iii) Kukusanya na kuchambua takwimu za Mifugo katika ngazi za kata na Halmashauri.

iv) Kuwasaidia maafisa ugani kufanya kazi na vikundi vya wafugaji ili waweze kufikia

malengo.

KITENGO OFISI KUU KATA/VIJIJI

Mifugo 3 5

Uvuvi 1 1

JUMLA 4 6

2

v) Kuandaa vifaa vya kufundishia wafugaji kama vitini, mabango, vijitabu vidogo na

machapisho muhimu kwa ajili ya kutolewa huduma za ugani.

vi) Kiunganishi kati ya watafiti, maafisa ugani, wafugaji na vikundi vya wafugaji katika

programu mbalimbali zinazohusu sekta ya Mifugo.

vii) Kuratibu na kusimamia uhusiano na vikundi vya wafugaji , NGO’S na watoa huduma za

Mifugo katika Halmashauri.

c) Usimamizi wa nyama na ngozi (Meat, Hides and Skins)

i) Kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Nyama na Kanuni zake.

ii) Kuwawezesha sekta binafsi kuwekeza kibiashara katika sekta ndogo ya nyama na ngozi.

iii) Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu matumizi na uhifadhi wa ngozi (Hides and Skin).

iv) Kuangalia uzalishaji, ukusanyaji, usindikaji na mfumo wa masoko wa ngozi (Hides and

Skin).

v) Kupitia mara kwa mara mfumo wa masoko wa nyama na ngozi katika Halmashauri.

d) Uzalishaji na ukaguzi wa maziwa (Dairy)

i) Kuwahamasisha sekta binafsi kuwekeza katika sekta ndogo ya maziwa (uzalishaji na

usindikaji),kuwahamasisha kuunda vikundi vya ukusanyaji,upoozaji na uuzaji wa

maziwa.

ii) Kuratibu na kuhimiza uboreshaji wa kosaafu kwa ng’ombe wa maziwa na wa asili kwa

mujibu wa Sera ya Taifa.

iii) Kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Maziwa na Kanuni zake.

e) Utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa Mifugo ( Livestock identification ,Registration and

Tracebility)

i) Kuandaa na kusimamia ukusanyaji wa takwimu za Mifugo

ii) Kutambua na kusajili mifugo yote iliyopo katika Halmashauri

iii) Kusimamia sheria ya utambuzi, usajili na ufuatiliaji mifugo

f) Uzalishaji wa wanyama wadogo (Small Stocks)

i) Kuandaa mipango ya uboreshaji wa wanyama wadogo

ii) Kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika uzalishaji na masoko ya wanyama wadogo

pamoja na mazao yao

iii) Kupitia mara kwa mara mfumo wa masoko wa wanyama wadogo ndani na nje ya

Halmashauri

g) Mifumo ya ufugaji

i) Kuelimisha wafugaji juu ya matumizi sahihi ya nyanda za malisho na vyakula

vya Mifugo

ii) Kuhamasisha wafugaji juu ya matumizi ya mabaki ya mazao na vyakula vingine

3

iii) Kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza kwenye ufugaji wa kibiashara

iv) Kuelimisha wafugaji juu ya uvunaji wa mifugo na kuanzisha miradi mingine ambayo

itawaongezea kipato

v) Kusimamia sheria ya nyanda za malisho na rasilimali za vyakula vya Mifugo

2.0 TAKWIMU ZA MIFUGO

AINA YA MIFUGO IDADI YA MIFUGO

Ng’ombe 7,030

Ng’ombe wa maziwa 1,028

Mbuzi 2,309

Kondoo 2,108

Kuku 24,215

Nguruwe 7,087

Bata 768

Sungura 124

Kanga 103

Punda 4

Mbwa 3561

Paka 982

Chanzo: Idara ya mifugo , December 2016

3.0 MIUNDO MBINU YA MIFUGO

Idadi ya miundo mbinu katika Halmashauri ni kama inavyoonekana katika jedwali lifuatalo hapa chini.:-

S/N MIUNDOMBINU ILIYOPO INAYOFANYA

KAZI

MBOVU

1 Machinjio 1 Iko hatua ya

mwisho ya

ujenzi

0

2 Machinjio ndogo

(Slaughter slabs)

2 2 0

3 Maduka ya kuuzia

nyama

64 62 2

4

4.0 WASAMBAZAJI WA PEMBEJEO ZA MIFUGO

NA JINA LA DUKA ENEO LILIPO

1 Divine Agrovet Ifakara Mjini

2 Divine Agrovet Kibaoni

3 Ephraimu Agrovet Ifakara Mjini

4 Malugu Agrovet Ifakara Mjini

lkjh

1.3. SEKTA YA UVUVI

1.3.1.SERA YA UVUVI

Sera ya Uvuvi inasisitiza Kusimamia uhifadhi, na usimamizi endelevu wa rasilimali za Uvuvi kwa

manufa ya kizazi cha sasa na kinachokuja. Shughuli ya uvuvi inachangia takribani 25% ya kipato cha

wakazi wa Ifakara.Pamoja na ajira na kipato faida zingine za Uvuvi ni kuongeza uhakika wa chakula na

lishe katika Jamii.

1.3.2. MAJUKUMU YA SEKTA.

Majukumu ya Sekta ya Uvuvi ni pamoja na;

Kusimamia matumizi na utekelezaji wa Sera ya Uvuvi (1987),Sheria ya Uvuvi Na.22 (2003) na

Kanuni za Uvuvi (2007).

Kushauri matumizi ya zana na teknolojia za kisasa za Uvuvi endelevu.

Kuhamasisha Ufugaji wa Samaki ili kupunguza utegemezi kwenye maji ya asili na kongeza

kipato cha kaya.

Kudhibiti uvuvi haramu kwenye mito na mabwawa ya asili.

Kukusanya mapato ya Serikali

Kukusanya na kuandaa takwimu za uvuvi kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Kuhakiki usafi na ubora wa samaki.

Kuboresha mazao ya samaki,matumizi na uhakika wa masoko

Kuandaa taarifa za kazi za kitengo za mwezi, robo na mwaka.

1.3.3.RASILIMALI ZA UVUVI

5

Shughuli za uvuvi zinafanyika kwenye Mito na Mabwawa ya asili, pia kuna shughuli za Ufugaji wa

Samaki ambazo zinafanyika kwenye mabwawa ya kuchimba.

MITO

Ndani ya eneo la Halmashauri ya Mji Ifakara kuna jumla ya Mito ya Kudumu 2 na mito ya msimu 6.

Mito hii ya msimu baadhi ilikuwa inatirirsha maji mwaka mzima lakini kutokana na uharibifu

unaofanywa na shughuli za kibinadamu pamoja na mabadiliko ya tabianchi sasa inakuwa na maji kipindi

cha Masika tu.

Jedwali : Mito ya kudumu na msimu.

NA KATA MITO YA KUDUMU MITO YA MSIMU

1. Ifakara Kilombero -

2. Lumemo Lumemo Doko

Kihogosi

3. Kibaoni Lungongole

Kikwawila

Kilama

Matawale

JUMLA 2 6

Chanzo; Idara ya Mifugo na Uvuvi Machi, 2017.

MABWAWA

Kuna jumla ya Mabwawa 89 kati ya hayo 52 ni mabwawa ya asili na 37 ni mabwawa ya kuchimbwa

yanayohusika na ufugaji na uzalishaji wa samaki.

Jedwali :. Rasilimali za Uvuvi ndani ya Halmashauri ya Mji Ifakara.

MADUKA YA KUUZIA SAMAKI- Yapo maduka manne (4) ya kuuzia samaki

Idadi ya

Wavuvi

Mitumbwi Boti Mialo

264 52 4 6

6

AINA YA SAMAKI

Zipo aina ya samaki zipatazo ishirini zinazopatikana kwenye mito na mabwawa hayo ya asili, zikiwemo

aina mbili za samaki ambazo zinapatikana Mto Kilombero pekee ambazo ni Mbala na Mgundu. Kwa

upande wa ufugaji samaki, zipo aina mbili ya samaki wanaofugwa ambao ni Sato (perege) na Kambale.

AINA ZA UVUVI

Ziko aina tatu za mbinu za uvuvi zinazotumika, ambazo ni pamoja na;

Nyavu

Ndoano

Mitego

UCHAKATAJI WA SAMAKI

Ziko aina kuu tatu za teknolojia ya uchakataji wa samaki;

Kubanika kwa kutumia moshi

Kukaanga

Kugandisha/barafu

UZALISHAJI WA SAMAKI

Halmashauri ya Mji Ifakara kupitia maeneo yake ya Uvuvi, masoko na magenge imekuwa ikinakili

samaki wanaovuliwa na kuuzwa kwenye eneo la Halmashauri.Wapo samaki wanaovuliwa ndani ya eneo

na nje ya eneo la mji na wapo ambao husafirishwa nje ya Halmashauri.Uzalishaji wa samaki kwa mwaka

huwa unapanda na kushuka kutokana na sababu mbalimbali kwa kutegemea hali ya hewa na mabadiliko

na tabianchi, nk.

7

VIKUNDI VYA ULINZI WA RASILIMALI ZA UVUVI (BMUS)

Hakuna Vikundi vya Jumuiya Shirikishi za Wavuvi ( BMUs) kwa sasa, hata hivyo kuna mpango wa

kuanzisha BMUs katika Kata za Lipangalala, Lumemo na Katindiuka.Lakini katika ngazi ya Kijiji ziko

Kamati za Maliasili na Mazingira pamoja na Askari Wanyamapori wa Vijiji (VGS) ambao hushirikiana

na Kitengo cha Uvuvi katika kudhibiti Uvuvi haramu na uharibifu wa Mazingira.

UFUGAJI WA SAMAKI

Ufugaji wa samaki ni teknolojia muhimu sana katika kuboresha lishe, ajira, kuongeza kipato, kuhakikisha

uwepo na usalama wa chakula.Halmashauri ya Mji Ifakara inayo maeneo yenye fursa za uwekezaji kwa

ajili ya kufuga samaki kama inavyooneshwa kwenye majedwali hapo chini.

Jedwali : Idadi ya Mabwawa ya kufugia samaki na maeneo yaliyopo

Na ENEO IDADI YA MABWAWA

1 Kibaoni 4

2 Milola 1

3 Kapolo 3

4 Maendeleo 2

5 TAZARA 2

6 Kilama 16

7 Mlabani 1

8 Kining’ina 6

9 Kikwawila 1

10 Kihogosi 1

Total 37

Chanzo; Idara ya Mifugo na Uvuvi Machi, 2017.

JEDWALI :. MAENEO YENYE FURSA ZA UWEKEZAJI WA KUFUGA SAMAKI- MJI

IFAKARA

Na Kijiji Kata Tarafa Fursa

1 Lumemo Lumemo Ifakara Mto Lumemo

8

2 Kining’ina Michenga Ifakara Mto Lumemo

3 Machipi Michenga Ifakara Mto Lumemo

4 Mahutanga Lumemo Ifakara Mabwawa ya asili (cage culture)

5 Kilama Kibaoni Ifakara Vijito na chemchem

6 Kikwawila (Kapolo) Kibaoni Ifakara Mto Kikwawila

7 Lumemo (Igombati) Lumemo Ifakara Skimu ya Umwagiliaji / mabwawa ya asili

8 Lungongole Kibaoni Ifakara Mabwawa ya asili (cage culture)

9 Mbasa Kibaoni Ifakara Mabwawa ya asili

10 Kihogosi Michenga Ifakara Mto Kihogosi

Chanzo; Idara ya Mifugo na Uvuvi Machi, 2017.

MAFANIKIO YA IDARA YA MIFUGO/UVUVI

Idara ya Mifugo na Uvuvi imeendelea kutoa ajira kwa Wafugaji,Wavuvi, Wafanyabiashara wa

samaki/nyama, nk. Hata hivyo ufugaji unaendelea kuchangia katika kukuza kipato cha kaya na kuongeza

lishe katika jamii.

Idara imeweka malengo ya kuongeza kasi ya uhamasishaji wa kufuga mifugo/samaki katika maeneo yote

yenye sifa za ufugaji .

Mafanikio ni pamoja na:

Kutoa elimu ya Ufugaji Mifugo/samaki kwenye Kataa 9 zilizopo katika Halmashauri.

Kuanzisha vikundi 4 vya Ufugaji Samaki

Kufanikiwa kufanya Utambuzi na usajili wa mifugo yote

Kudhibiti uvuvi haramu kwa kukamata kokoro/ vyandarua na kuziteketeza.

Kushirikisha jamii kupiga vita uvuvi haramu.

Kutenga fedha kwenye bajeti ya mwaka 2017/2018 kwa ajili ya kuanzisha Kituo cha Kuzalisha

na Kufuga Samaki pamoja na kuanzisha shamba darasa la kuku

Kuendelea kujenga miundo mbinu ya mifugo kama vile machinjio na makaro ya kuchinjia

mifugo

CHANGAMOTO

9

Idadi Ndogo ya Watumishi inayopelekea watumishi kuwa na kazi nyingi hasa kwa upande wa

kitengo cha uvuvi ambapo yupo mtumishi mmoja katika ngazi ya kata

Uhaba wa vitendea kazi kama pikipiki ambazo zingerahisisha shughuli za idara mfano kufanya

doria na kutembelea wafugaji .

Utegemezi wa maji ya asili kwa ajili ya kupata samaki kutokana na mazoea/utamaduni badala ya

kubadilika na kufuga samaki.

Uelewa mdogo wa Teknolojia ya Ufugaji wa Samaki kwa jamii na juu ya ufugaji shadidi ndani ya

eneo la mji

Kuongezeka kwa uvuvi haramu kunakochangiwa na ongezeko la mahitaji na idadi ya watu.

Uvuvi haramu wa kutumia kokoro,nyavu ndogo, vyandarua na uharibifu wa nyumba/mazalia ya

samaki.

Hakuna uhakika wa maji mwaka mzima kwa kuwa mito iliyopo ina kina kirefu kulinganisha na

usawa wa mahali mabwawa yalipo.

MIKAKATI YA KUPAMBANA NA CHANGAMOTO

Kuanzisha mkakati wa kushirikisha jamii kwenye usimamizi wa rasilimali za Uvuvi kwa

kuanzisha Vikundi vya ulinzi wa rasilimali za Jamii za Wavuvi – Beach Management Units

(BMUs)

Kuboresha utendaji wa Kamati za Maliasili na Mazingira za Vijiji (VNRC) na Askari

Wanyamapori wa Vijiji (VGS).

Kufanya Sensa ya Wavuvi,Vyombo na Zana za Uvuvi kwenye maeneo yote ya Uvuvi kila mwaka

Kulinda, kuhifadhi na kuhamasisha matumizi ya busara ya rasilimali za uvuvi.

Kuwezesha, kuhamasisha na kujenga uelewa wa Jamii juu ya Teknolojia ya Ufugaji wa Samaki

na ufugaji wa mifugo wenye tija na unaozingatia uwezo wa maeneo.

Kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo kwenye uvuvi na ufugaji wa samaki ili kuvutia

Wawekezaji kwenye sekta hii.

Kuanzisha na kusimamia Kituo cha Uzalishaji wa Vifaranga bora wa Samaki na Ufugaji wa

Samaki na shamba darasa la kuku

Picha za matukio na miundombinu ya mifugo na uvuvi

Miundombinu:-

10

Mnada wa mifugo

Machinjio, Bucha na usafiri wa kusafirishia nyama

Zoezi la utambuzi na usajili wa mifugo

11

Dc akielezea namna ya kusajili Mifugo..

Zoezi la chanjo dhidi ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa

Miundombinu ya uvuvi

12