ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa ... secondary... · hapo utachukua boda boda kwa...

10
[UMBWE HIGH SCHOOL] 2018 [© Umbwe High School July 2018 - Joining instructions] Page 1 OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI Shule ya Sekondari Umbwe, S. L. P. 718, MOSHI. Tarehe 11.05.2018. Unapojibu tafadhali taja, Kumb. Na. USS/150/VOL.II/145 Simu Na. 0786 748 338 / 0754 748 338 Jina la mwanafunzi: ………………………..……………………………………………………………..………………. S. L. P. ………….… MJI ………………………………..……… MKOA WA ………………………………..………… YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI UMBWE KIDATO CHA TANO MWAKA 2018 0.0. Ninafurahi kukutaarifu kuwa umechaguliwa kujiunga na kidato cha tano (V) tahasusi (combination) ya ECA/CBG/HGE/HGL katika shule hii kwa mwaka wa masomo wa 2018/2019. Shule ya Sekondari Umbwe ipo wilaya ya Moshi vijijini umbali wa km.20 kutoka Moshi mjini. Usafiri wa basi kutoka Moshi mjini unapatikana katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani, panda gari la Kibosho Umbwe nauli ni Tsh. 1000/= na unapaswa kuteremkia kituo kinachoitwa kwa Raphaeli. Hapo utachukua Boda boda kwa nauli ya maelewano kati ya sh. 1000/=(bila mzigo) au 3000/= (pamoja na mzigo). Muhula wa kwanza wa masomo unaanza mwezi July 2018. Unatakiwa kuripoti shuleni siku ya Jumatatu tarehe 02 July 2018, tarehe ya mwisho ya kuripoti shuleni ni tarehe 16 July 2018. Zaidi ya hapo, nafasi yako atapewa mwanafunzi mwingine katika chaguo la pili. Shule yetu ni ya wavulana tu na ni ya bweni, ina michepuo ifuatayo:- i. ECA Economics, Commerce, Accountancy, Basic Applied Mathematics & General Studies. ii. HGE History, Geography, Economics, Basic Applied Mathematics & General Studies. iii. HGL History, Geography, English Language & General Studies iv. CBG Chemistry, Biology, Geography, Basic Applied Mathematics & General Studies. Tafadhali soma kwa makini sana maelekezo / maagizo yafuatayo na ukamilishe mahitaji yote yaliyomo katika barua hii ili uweze kupokelewa shuleni na kuanza masomo bila usumbufu wowote. VIAMBATANISHO MUHIMU: Fomu A ya kukubali kufuata sheria zaote na masharti yote ya shule na mkataba wa kutoshiriki migomo fujo zozote na makosa ya jinai ya aina yoyote shuleni. Fomu B ya mzazi / mlezi ya uthibitisho wa kulipa ada, michango na mahitaji mengine ya shule. Fomu C ya siri inayohusu maelezo binafsi ya mwanafunzi. Fomu ya kupimwa afya na Daktari wa Hospitali ya Wilaya / Mkoa / Rufaa na siyo Zahanati au Kituo cha Afya. Fomu E ya usajili wa mwanafunzi (itajazwa shuleni wakati wa kuripoti).

Upload: lyhanh

Post on 02-Mar-2019

511 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA ... SECONDARY... · Hapo utachukua Boda boda kwa nauli ya maelewano kati ya sh. 1000/=(bila mzigo) au 3000/= (pamoja na mzigo)

[UMBWE HIGH SCHOOL] 2018

[© Umbwe High School – July 2018 - Joining instructions] Page 1

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI

Shule ya Sekondari Umbwe, S. L. P. 718,

MOSHI. Tarehe 11.05.2018.

Unapojibu tafadhali taja, Kumb. Na. USS/150/VOL.II/145

Simu Na. 0786 748 338 / 0754 748 338

Jina la mwanafunzi: ………………………..……………………………………………………………..……………….

S. L. P. ………….… MJI ………………………………..……… MKOA WA ………………………………..…………

YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI UMBWE KIDATO CHA

TANO MWAKA 2018

0.0. Ninafurahi kukutaarifu kuwa umechaguliwa kujiunga na kidato cha tano (V) tahasusi

(combination) ya ECA/CBG/HGE/HGL katika shule hii kwa mwaka wa masomo wa 2018/2019.

Shule ya Sekondari Umbwe ipo wilaya ya Moshi vijijini umbali wa km.20 kutoka Moshi mjini.

Usafiri wa basi kutoka Moshi mjini unapatikana katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani,

panda gari la Kibosho – Umbwe nauli ni Tsh. 1000/= na unapaswa kuteremkia kituo kinachoitwa

kwa Raphaeli. Hapo utachukua Boda boda kwa nauli ya maelewano kati ya sh. 1000/=(bila

mzigo) au 3000/= (pamoja na mzigo).

Muhula wa kwanza wa masomo unaanza mwezi July 2018. Unatakiwa kuripoti shuleni siku ya

Jumatatu tarehe 02 July 2018, tarehe ya mwisho ya kuripoti shuleni ni tarehe 16 July 2018.

Zaidi ya hapo, nafasi yako atapewa mwanafunzi mwingine katika chaguo la pili.

Shule yetu ni ya wavulana tu na ni ya bweni, ina michepuo ifuatayo:-

i. ECA – Economics, Commerce, Accountancy, Basic Applied Mathematics & General Studies.

ii. HGE – History, Geography, Economics, Basic Applied Mathematics & General Studies.

iii. HGL – History, Geography, English Language & General Studies

iv. CBG – Chemistry, Biology, Geography, Basic Applied Mathematics & General Studies.

Tafadhali soma kwa makini sana maelekezo / maagizo yafuatayo na ukamilishe mahitaji yote yaliyomo

katika barua hii ili uweze kupokelewa shuleni na kuanza masomo bila usumbufu wowote.

VIAMBATANISHO MUHIMU:

Fomu A ya kukubali kufuata sheria zaote na masharti yote ya shule na mkataba wa kutoshiriki

migomo fujo zozote na makosa ya jinai ya aina yoyote shuleni.

Fomu B ya mzazi / mlezi ya uthibitisho wa kulipa ada, michango na mahitaji mengine ya shule.

Fomu C ya siri inayohusu maelezo binafsi ya mwanafunzi.

Fomu ya kupimwa afya na Daktari wa Hospitali ya Wilaya / Mkoa / Rufaa na siyo Zahanati au

Kituo cha Afya.

Fomu E ya usajili wa mwanafunzi (itajazwa shuleni wakati wa kuripoti).

Page 2: OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA ... SECONDARY... · Hapo utachukua Boda boda kwa nauli ya maelewano kati ya sh. 1000/=(bila mzigo) au 3000/= (pamoja na mzigo)

[UMBWE HIGH SCHOOL] 2018

[© Umbwe High School – July 2018 - Joining instructions] Page 2

1.0. Vitu unavyopaswa kuja navyo ni:-

a) Viatu vyeusi vya ngozi jozi mbili (02)

b) Soksi Jozi mbili au zaidi rangi yoyote

c) Viatu vya michezo rangi yoyote

d) Bukta mbili na tisheti mbili za rangi ya kahawia (brown) kwa ajili ya michezo

e) Mkanda mweusi wa ngozi kwa ajili ya kufunga suruali – upana si zaidi ya inchi moja na

nusu na usiwe na chuma kipana / kikubwa cha kufungia na kisiwe na picha au mchoro

wowote.

1.1. (A) ADA NA MICHANGO MINGINE NI KAMA IFUATAVYO:

SN MAELEZO KIASI

1. Karo ya shule kwa mwaka ni 70,000.00

2. Huduma ya kwanza 5,000.00

3. Mchango wa ukarabati 15,000.00

4. Kitambulisho na picha 6,000.00

5. Uboreshaji taaluma kwa mwaka 20,000.00

6. Mitihani ya kujipima (Mock) 20,000.00

7. Wapishi na walinzi wa shule kwa mwaka 30,000.00

8. Nembo ya shule 2,000.00

9. Tahadhari 5,000.00

10. Bima ya afya (CHF) 5,000.00

11. Mafuta ya Kangavu (Generator) 10,000.00

JUMLA 188,000.00

NB: Fedha yote ilipwe kwenye akaunti ya shule 4031200152 NMB. Hatupokei fedha shuleni kabisa. Uje

na slip ya benki (nakala halisi (original) sio photocopy) na iwe na jina la mwanafunzi na kidato

vilivyoandikwa na benki wakati wa kuweka.

B. Kila mwanafunzi aje na:

a. Godoro moja lenye kuenea kitanda cha mtu mmoja ( 200 cm x 80 cm)

b. Blanketi zito angalau moja au mbili zitafaa zaidi kwani kuna baridi kali.

c. Shuka mbili za rangi moja ya pink.

d. Taulo moja, foronya mbili na mto wa kulalia.

e. Kandambili jozi moja au mbili.

f. Chandarua kimoja.

g. Track suit rangi nyeusi (black)

h. Shati 2 nyeupe za mikono mirefu na suruali 2 za rangi ya kahawia (brown). (Shati na suruali

zote ziwe mpya kabisa). Uje pia na tai ya rangi ya kahawia (brown) yenye miraba mitatu

myeupe kifuani iliyolalia hivi /// toka kushoto kwenda kulia.

i. Sweta la rangi ya kahawia (brown) lenye shingo ya “V”

MASHONO: Suruali zishonwe vizuri, ziwe na mifuko miwili mbele isiyo ya kuchimba na mmoja

wa nyuma usio wa kubandika, marinda 2 mbele kila upande, ziwe na mkunjo wa

chini (turn-up), luksi za mkanda zisiwe pana, suruali zisibane kwa chini wala

zisiwe peckos. Ni marufuku kabisa kuvaa suruali inayoshika maungo ya mwili

(inayobana). Ukileta itachanwa. Hii ni kwa suruali zote hata za binafsi za

kushindia. Mashono ya suruali yazingatie kuwa inavaliwa kiunoni na sio mlegezo

hata kidogo.

1.2. MAHITAJI MENGINE

i. Sanduku au begi moja imara (usije kabisa na sanduku la chuma / bati -

tranka) na kufuli imara ya kufungia.

ii. Fedha za matumizi kwa mahitaji binafsi ikiwa ni pamoja na fedha za matibabu

kwani shule haina huduma hiyo.

iii. Kijiko, sahani, bakuli na kikombe (ni lazima uje navyo vyote).

iv. Mkebe wa vifaa vya Hisabati (Mathematical seti)

v. Daftari za kutosha (quire 3 au 4 )

vi. Scientific Calculator moja na Mathematical table (four figure) – Kwa

watakaosoma Hisabati tu (BAM).

Page 3: OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA ... SECONDARY... · Hapo utachukua Boda boda kwa nauli ya maelewano kati ya sh. 1000/=(bila mzigo) au 3000/= (pamoja na mzigo)

[UMBWE HIGH SCHOOL] 2018

[© Umbwe High School – July 2018 - Joining instructions] Page 3

vii. Nakala ya cheti cha kuzaliwa na picha passpot size nne zenye background ya

bluu iliyopigwa katika sare ya shule.

viii. Karatasi za chooni (Toilet papers) kumi au zaidi

ix. Saa ya mkononi.

x. Ream moja ya karatasi nyeupe zisizo na mistari – size A4

xi. Ream mbili (2) za karatasi zenye mistari – Ruled papers size A4

xii. Wanafunzi wanaochukua CBG, waje na vifaa vya upasuaji (dissecting kit) kwa

ajili ya masomo ya vitendo (practical).

xiii. Ndoo mbili tupu za lita 20 kila moja.

xiv. Wanafunzi wa HGE na HGL kila mmoja aje na mopper moja yenye mpini na

utambi kwa ajili ya kukaushia maji (usilete kindoo chake), wale wa CBG walete

reki na wale wa ECA kila mmoja alete panga moja.

xv. Vifaa vya usafi – kila mmoja alete Squeezer moja, hard broom moja, soft broom

moja, chelewa mbili na dawa ya chooni (disinfectant) moja ya lita tano.

NB: Kama mwanafunzi ana kitambulisho cha Bima ya Afya (NHIF) kitakuwa msaada mkubwa

sana kwake kwa ajili ya matibabu, hivyo akumbuke kuja nacho shuleni.

1.3. MAHITAJI YA TAALUMA

Madaftari:- Kila mwanafunzi siku ya kuripoti aje na madaftari makubwa (counter

bookds quire 3 au 4) za kutosha na begi la kubebea ( mfuko wa Rambo haukubaliki)

Kalamu:- Mwanafunzi aje na kalamu za kutosha (za wino wa bluu / mweusi na

penseli).

Vitabu vya rejea:- Kila mwanafunzi anatakiwa kununua vitabu vya rejea/ziada ili

kumwezesha kupata uwanja mpana zaidi wa kujisomea. (Taz. Orodha

iliyoambatanishwa na barua hii).

Mitihani:- Ipo mitihani ambayo huandaliwa na vyombo tofauti na inalipiwa na

wazazi/walezi wenyewe kama ifuatavyo:-

Mitihani ya Taifa ya kidato cha 6.

Mitihani ya utamirifu (mock) Mkoa wa Kilimanjaro kwa kidato cha 6.

ANGALIZO: Kila mwanafunzi awe na sare zote zilizoagizwa na mahitaji yote katika zoezi la

ukaguzi litakalofanyika shuleni siku ya kuripoti. Usipokamilisha hutapokelewa

kabisa.

2.0. KUHUSU SHULE

2.1. HESHIMA

Wanafunzi wote hawana budi kuonesha heshima popote wanapokuwa ndani au nje ya shule.

Ni lazima kuwaheshimu wanafunzi wenzako wote na kuwatii viongozi wa ngazi zote shuleni.

Wanafunzi hawana budi kupendana kindugu na kuheshimiana wao kwa wao.

Ni lazima wanafunzi kuonesha heshima na adabu kwa majirani na wageni wa shule

Mwanafunzi atasimama wima wakati wa kusalimia walimu, wafanyakazi na watu wazima

Mwanafunzi awepo shuleni muda wote wa masomo.

Kutoka nje ya shule lazima upate kibali cha maandishi cha M/shule, msaidizi/Mwl. wa zamu

Mwanafunzi haruhusiwi kuzurura ovyo maeneo yasiyoruhusiwa awapo shuleni.

Ni kosa kuchelewa kufika shuleni, kutofanya shughuli za usafi, elimu ya kujitegemea n.k.

Mwanafunzi aitike wito na kukimbilia anakoitwa. Ni kosa kubwa kumkimbia anayekuita.

Mwanafunzi awahi shuleni kwa tarehe zilizopangwa mara baada ya likizo/mapumziko ya kati

na kuwasilisha shuleni fomu maalumu inayoonesha tarehe ya kufunga na kufungua shule

ambayo imesainiwa na mzazi / mlezi. Ni kosa kubwa kuchelewa kurejea shuleni bila sababu ya

msingi kutoka kwa mzazi / mlezi.

2.2. MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA

i. RUHUSA: - Ruhusa ya kutokuwepo shuleni kwa siku moja au zaidi itatolewa na Mkuu wa

shule, Makamu wake au Mwalimu aliyekasimiwa madaraka.

ii. MWOMBEZI WA RUHUSA:- Anayekubalika kukuombea ruhusa ni mzazi/mlezi

aliyeandikishwa shuleni na sio mtu mwingine yeyote.

iii. MIPAKA YA SHULE:- Ni marufuku kutoka nje ya mipaka ya shule wakati wote wa

masomo/shughuli zingine bila idhini ya mwalimu husika.

iv. LUGHA RASMI:- Unatakiwa kutumia lugha ya kiingereza tu mahali popote shuleni.

Mawasiliano kati yako na walimu na wanafunzi wenzako yafanyike kwa lugha ya kiingereza.

v. UMEME:- Mwanafunzi haruhusiwi kabisa kugusa wala kukaribia miundombinu ya umeme

mfano: swichi, soketi, taa, swichi kuu wala mita bila sababu za msingi. Tendo la kuwasha

Page 4: OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA ... SECONDARY... · Hapo utachukua Boda boda kwa nauli ya maelewano kati ya sh. 1000/=(bila mzigo) au 3000/= (pamoja na mzigo)

[UMBWE HIGH SCHOOL] 2018

[© Umbwe High School – July 2018 - Joining instructions] Page 4

taa. Lifanywe mara moja tu sio kubonyeza bonyeza. Nikosa kujiunganishia nyaya za

umeme kwa matumizi yoyote yasiyo rasmi, ukikamatwa utafukuzwa shule mara moja.

Ukihurumiwa, utaleta roll ya waya 1.5 mm mita 100 pamoja na gharama ya fundi.

vi. USAFI BINAFSI:-

Ni lazima mwanafunzi awe msafi na nadhifu wakati wote.

Mwanafunzi haruhusiwi kufuga ndevu, nywele ndefu wala kusuka kwa namna yoyote ile.

Ni marufuku pia kunyoa nywele zote na kubaki na upara. Nywele ziruhusu kijiti cha kiberiti kukaa

bila kudondoka.

Kucha za miguu na mikono sharti ziwe fupi na zisipakwe rangi yoyote.

Sare ya shule ni lazima iwe safi na iliyonyooshwa vizuri. Viatu pia vipakwe rangi yake.

Suruali zitavaliwa kiunoni na sio katikati ya makalio (“kata k”). Mikanda mipana yenye

chuma kubwa sehemu ya kufungia na yenye mapichapicha haikubaliki shuleni.

Ni lazima uoge mwili mzima ili kuzuia harufu mbaya.

Ni marufuku kujipaka / kujipulizia manukato makali wakati wa darasani.

Mwanafunzi haruhusiwi kuvaa mapambo mfano pete, bangili, hereni, mkufu au kidani cha aina yoyote.

Mwanafunzi haruhusiwi kuvaa viatu vya mchuchumio (Raizoni) wala vya wazi (open shoes wala

yeboyebo) wakati wote wa masomo.

Nguo za kushindia zisizidi suruali 3 na mashati matatu tu. Mavazi magumu (jeans) hayakubaliki.

vii. USAFI WA MAZINGIRA

Ni wajibu wako kuliweka eneo la shule, majengo na madarasa katika hali ya usafi. Hairuhusiwi

kuchora chora wala kuandika katika kuta za majengo ya shule.

Kila mwanafunzi atapewa eneo la kuhudumia usafi na miti ya kutunza. Ikitokea mti ukafa kwa

uzembe, utalipishwa.

Uchafu na takataka zitupwe mahali panapostahili.

Ni jukumu la kila mwanafunzi kupendezesha maeneo ya shule yetu ili yavutie.

viii. MWENENDO NA TABIA:

Ni marufuku kabisa kwa wanafunzi kuanzisha magenge/vikundi visivyo rasmi shuleni, mfano vya

kikabila, vya kidini, vya kimikoa/kikanda, vya kimkakati fulani wa kutisha wanafunzi wengine na

kuhukumu. Watakaobainika watafukuzwa shule mara moja.

Ni marufuku kwa mwanafunzi kuvuta sigara, bhangi, kutumia madawa ya kulevya, kunywa pombe,

kwenda katika kumbi za starehe mfano disko, baa ama kuonekana maeneo yanayouzwa vileo

wakati wote uwapo shuleni au nyumbani kwenu.

Ni kosa kutoa matusi au kutumia lugha ya matusi wakati wote ndani na nje ya shule.

Ni kosa kubwa kuiba mali ya mtu mwingine ikiwemo mali ya shule, walimu ama ya mwanafunzi mwenzako.

Ni muhimu kufahamu mipaka yote ya shule na kuzingatia kikamilifu maelekezo juu ya kuwepo

ndani ya mipaka hiyo wakati wote wa uanafunzi wako katika shule hii.

Ni marufuku kwa mwanafunzi kuingia maeneo ya giza ama kificho hapa shuleni au nje ya shule wakati wote.

Unatakiwa kuzingatia kwa umakini maandalio ya mchana na jioni (preparations).

Ni marufuku kutembelea nyumba za walimu wa watumishi bila ruhusa ya mwl. wa zamu.

Ni marufuku kutomasana baina ya wavulana na wavulana, wavulana na wasichana (wowote) ama

wenye jinsia moja mahali popote, njiani au maeneo unayoishi.

Ni mwiko kabisa mwanafunzi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi mwenzake,

Mwalimu, Mtumishi asiye Mwalimu au mtu mwingine yeyote.

Ni kosa kumdharau, kugombana au kumpiga kiranja au kiongozi wa ngazi yoyote shuleni.

Utoro shuleni na utoro wa vipindi vya darasani ni kosa kubwa la kukurejesha nyumbani kwenu.

ANGALIZO:

Uhusiano kati yenu ni wa kaka - kaka, kaka na dada na pia baba/mama na mtoto kwa walimu na watumishi wasio

walimu. Aidha, kuwepo na mipaka ya mazungumzo na mahusiano (Social distance) kati ya wanafunzi na mwalimu au

mtumishi asiyekuwa mwalimu.

Lugha za kujirahisi na zisizo na staha haziruhusiwi. Mavazi, mitindo ya mavazi na mitindo ya uvaaji

isiyozingatia maadili ya Kitanzania ni marufuku hapa shuleni.

NB: ZINGATIA HAYA:

Mwanafunzi haruhusiwi kabisa kuja na simu ya mkononi shuleni. ukija na simu itataifishwa

na wewe kurejeshwa nyumbani kwenu.

Page 5: OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA ... SECONDARY... · Hapo utachukua Boda boda kwa nauli ya maelewano kati ya sh. 1000/=(bila mzigo) au 3000/= (pamoja na mzigo)

[UMBWE HIGH SCHOOL] 2018

[© Umbwe High School – July 2018 - Joining instructions] Page 5

Mwanafunzi asiyefanya mtihani bila sababu ya msingi atapewa adhabu kali na atagharimia utungaji

na usahihishaji wa mtihani mwingine atakaopewa.

ix. MAKOSA MAKUBWA YA KUMFUKUZISHA SHULE MWANAFUNZI:

Wizi, Uasherati, Kuoa. Ulevi wa aina yoyote kupiga au kupigana, kudharau uongozi halali wa

serikali ya wanafunzi, kuanzisha au kushiriki mgomo shuleni, kuharibu kwa makusudi mali

ya umma, kuharibu au kudharau Bendera ya Taifa, picha za Viongozi wa Kitaifa, Wimbo wa

Taifa na kuharibu Fedha za Taifa.

Mwanafunzi akisababisha mimba ataachishwa masomo na kushtakiwa kwa mujibu wa sheria.

Kukataa adhabu ni kosa kubwa la kupelekea kufukuzwa shule.

Kuanzisha magenge/vikundi visivyo rasmi shuleni, mfano vikundi vya kikabila, vya kidini,

vya kimkakati fulani wa kutishia wanafunzi wengine na kuhukumu. Watakaobainika

watafukuzwa shule mara moja.

Kumiliki simu ya mkononi au laini ya simu au kupatikana na vifaa vya kuchajia simu.

3.0. UMUHIMU WA KUJISOMEA: Ni muhimu sana kwa mwanafunzi kujenga tabia ya kujisomea na

kufanya maandalizi ya siku inayofuata. Inashauriwa mwanafunzi atenge muda wa kutosha

kujisomea na kufanya kazi alizopewa na mwalimu wake shuleni.

4.0. JIVUNIE SHULE YAKO: Kila mwanafunzi aipende na ajivunie shule yake. Aidha, kila mzazi /

mlezi aipende na ajivunie shule anayosoma mtoto wake na amtimizie mahitaji yake ili

awawezeshe walimu na watumishi wengine kutoa elimu bora.

5.0. MZAZI/MLEZI KUMBUKA NA KUZINGATIA:

Kila mzazi / mlezi azingatie kuwa jukumu la kumsomesha mtoto wake ni la kwake mwenyewe.

Itakuwa haina maana yoyote kumleta mtoto wako katika shule hii na kumtelekeza bila kumpatia

mahitaji yake ya msingi na mwisho wa yote utegemee miujiza itokee mwanao afanye vizuri.

Inawezekana, timiza wajibu wako sasa.

TANBIHI: Pamoja na maagizo haya, tafadhali tekeleza yafuatayo:-

Tuandikie tujulishe rasmi kukubali kufuata sheria za shule hii kwa kujaza fomu A

iliyoambatanishwa na uirejeshe siku ya kuripoti shuleni.

Jaza fomu B inayohusu uthibitisho wa kulipa ada na uirejeshe siku ya kuripoti.

Jaza fomu C inayohusu maelezo binafsi ya mwanafunzi (Fomu ya siri) na uiwasilishe kwa mkuu

wa shule siku ya kuripoti.

Jaza fomu D (ripoti ya Daktari) – ijazwe na Hospitali yenye hadhi ya wilaya au mkoa na sio

zahanati au kituo cha afya na pia iletwe siku ya kuripoti.

Fomu E inahusu usajili - Itajazwa na kila mmoja baada ya kuonyesha mahitaji na michango

yote wakati wa kuripoti shuleni.

Hakikisha unaandika jina lako kwa kudarizi katika sare zote, shuka, track suit na blanketi.

6.0. MUHIMU: Mzazi/mlezi unatakiwa kutimiza mahitaji yote uliyoagizwa, Aidha, unatakiwa kulipa

michango yote ya shule ikiwemo ada yote ya mwaka yaani Tsh.70,000/= pamoja na kuleta mahitaji mengine yote kwani itasaidia sana shule kupanga mipango yake. Mwanafunzi ataonesha slip ya malipo ya benki afikapo getini wakati wa kuripoti getini, atakayekosa kukamilisha mahitaji yote hatapokelewa kabisa na atalazimika kurejea nyumbani kwa gharama zake. Tafadhali epuka

usumbufu usio wa lazima kwa mwanao kwa kutekeleza hilo.

7.0. MWISHO: Kwa niaba ya walimu na wafanyakazi wote, nakupongeza kwa kuchaguliwa kujiunga

na shule yetu. Ni Imani yetu kuwa utaitumia vizuri nafasi hii uliyotunukiwa na Taifa.

KARIBU SANA UMBWE SEKONDARI

……………………………………..

Z. E. JAPHET

MKUU WA SHULE

Page 6: OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA ... SECONDARY... · Hapo utachukua Boda boda kwa nauli ya maelewano kati ya sh. 1000/=(bila mzigo) au 3000/= (pamoja na mzigo)

[UMBWE HIGH SCHOOL] 2018

[© Umbwe High School – July 2018 - Joining instructions] Page 6

Page 7: OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA ... SECONDARY... · Hapo utachukua Boda boda kwa nauli ya maelewano kati ya sh. 1000/=(bila mzigo) au 3000/= (pamoja na mzigo)

[UMBWE HIGH SCHOOL] 2018

[© Umbwe High School – July 2018 - Joining instructions] Page 7

Page 8: OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA ... SECONDARY... · Hapo utachukua Boda boda kwa nauli ya maelewano kati ya sh. 1000/=(bila mzigo) au 3000/= (pamoja na mzigo)

[UMBWE HIGH SCHOOL] 2018

[© Umbwe High School – July 2018 - Joining instructions] Page 8

Page 9: OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA ... SECONDARY... · Hapo utachukua Boda boda kwa nauli ya maelewano kati ya sh. 1000/=(bila mzigo) au 3000/= (pamoja na mzigo)

[UMBWE HIGH SCHOOL] 2018

[© Umbwe High School – July 2018 - Joining instructions] Page 9

Page 10: OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA ... SECONDARY... · Hapo utachukua Boda boda kwa nauli ya maelewano kati ya sh. 1000/=(bila mzigo) au 3000/= (pamoja na mzigo)

[UMBWE HIGH SCHOOL] 2018

[© Umbwe High School – July 2018 - Joining instructions] Page 10