mwongozo wa mratibu wa mafunzo ya walimu kazini ngazi ya … · na chuo kikuu kishiriki cha elimu...

60
MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-II Moduli ya Kwanza Uchunguzi wa Muhtasari Ulioboreshwa wa Darasa la I na la II Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule TAASISI YA ELIMU TANZANIA

Upload: others

Post on 17-Sep-2019

36 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-II

Moduli ya Kwanza Uchunguzi wa Muhtasari Ulioboreshwa

wa Darasa la I na la II

Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

TAASISI YA ELIMU TANZANIA

Page 2: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-II

Moduli ya Kwanza Uchunguzi wa Muhtasari Ulioboreshwa

wa Darasa la I na la II

Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

TAASISI YA ELIMU TANZANIA

Page 3: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

@Taasisi ya Elimu Tanzania, 2016

ISBN: 978-9976-61-410-7

Taasisi ya Elimu TanzaniaS.L.P, 35094Dar Es Salaam, Tanzania,

Simu: 255-2773005Nukushi: 255-277 4420Barua pepe: [email protected]: www.tie.go.tz.

Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga, kunakili, kurudufu, kuchapa, kutafsiri kitabu hiki kwa namna yoyote ile bila idhini ya Taasisi ya Elimu Tanzania.

MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-II

Moduli ya Kwanza Uchunguzi wa Muhtasari Ulioboreshwa

wa Darasa la I na la II

Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

TAASISI YA ELIMU TANZANIA

Page 4: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

SHUKURANI

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa kushirikiana na EQUIP-T inatambua na kuthamini michango ya wataalamu wote walioshiriki kuandaa moduli hii. Shukrani za pekee zinatolewa kwa wahadhiri kutoka vyuo vikuu vifuatavyo; Dar es Salaam, Dodoma, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro.

Tunapenda pia kuwashukuru wawezeshaji ambao walipitia na kuboresha moduli hii kutoka katika vyuo vya Ualimu vifuatavyo: Bunda, Butimba, Bustani, Kabanga, Kasulu, Mpwapwa, Ndala, Shinyanga, Tabora na Tarime.

Vile vile tunapenda kuwashukuru wataalamu toka TET and EQUIP-T walioshiriki katika hatua mbalimbali za uandishi na uhariri wa moduli hii.

Dkt. Elia Y. K. KibgaKaimu Mkurugenzi MkuuTaasisi ya Elimu Tanzania

Page 5: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

1Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DIBAJI

Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta ya elimu ili kuleta mageuzi yakiuchumi na kijamii. Lengo la Dira ya Maendeleo ni kuwa na taifa la watu walioelimika na jamii iliyotayari kujifunza ku�kia 2025. Serikali ya Tanzania imethibitisha kwa vitendo kuwa Elimu ni kiambato muhimu katika kupunguza umaskini na kuimarisha maendeleo ya taifa. Kwa muda mrefu serikali imetambua kuwa “Ubora wa elimu yoyote hauwezi kuwa bora kuliko ubora wa mwalimu mwenyewe” hivyo imetilia mkazo mafunzo kazini kwa walimu kupitia mikakati mbalimbali ili kuimarisha umahiri wa walimu katika ufundishaji na ujifunzaji darasani.

Katika kuongeza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji darasani, Taasisi ya Elimu Tanzania kwa kushirikiana na EQUIP-Tanzania, wameandaa moduli hii ambayo imesheheni kazi mbalimbali ambazo waalimu mtazitenda katika vikundi wakati wa mafunzo kwa kutumia mbinu ya Mafunzo ya Walimu Kazini ngazi ya shule. Mbinu hii inatambua umuhimu wa walimu kujifunza pamoja na kubaini changamoto zinazowakabili ili kupata suluhisho la changamoto za ufundishaji na ujifunzaji kwa pamoja.

Moduli hii ya Mafunzo ya Walimu Kazini, imeandaliwa ili kusaidia juhudi za Wizara ya Elimu naMafunzo ya Ufundi kuhakikisha kuwa mbinu fanisi zinatumika darasani wakati wa ufundishaji naujifunzaji. Moduli hii pia inawasaidia walimu kushirikishana uzoefu na umahiri katika ufundishaji na ujifunzaji darasani. Vilevile Moduli inatoa mafunzo ya ziada ikitarajiwa kuwa walimu watakuwawamekwisha pata Mafunzo Kabilishi ya utekelezaji wa Mtaala ulioboreshwa wa kuimarisha ufundishaji wa KKK kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili.

Taasisi ya Elimu Tanzania inatarajia kuwa moduli hii itawasaidia walimu kuimarisha umahiri waufundishaji na ujifunzaji ili kuwasaidia wanafunzi waweze kujenga uwezo unaokusudiwa wakati wa kujifunza.

Changamoto iliyo mbele yetu ni kuhakikisha kuwa tunaonyesha kwa vitendo matokeo mazuriyanayotokana na maudhui ya moduli hii wakati wa ufundishaji na ujifunzaji darasani ili kuimarishaubora wa elimu ya shule ya msingi.

Dkt. Elia Y. K. KibgaKaimu Mkurugenzi MkuuTaasisi ya Elimu Tanzania

Page 6: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

2 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

Maelezo Muhimu kwa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

Mwongozo huu utatumika sanjari na moduli ya kwanza ya mwalimu ili kumsaidia mratibu wa mafunzo kuwa na mpangilio

mzuri wenye kufuata hatua kwa hatua ili kuwafanya walimu washiriki kikamilifu katika kujifunza maudhui ya moduli ya kwanza.

Mwongozo huu umegawanyika katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ambayo ni upande wa kushoto wa mwongozo unabeba maelezo ambayo mratibu wa mafunzo ya walimu kazini ngazi ya

shule atatakiwa kuyafuata wakati wa kuratibu kipindi cha kujifunza maudhui ya moduli. Sehemu ya pili ambayo ni upande wa kulia wa mwongozo unabeba maudhui yaliyo kwenye moduli ya mwalimu

ambayo watayasoma wakati wa kipindi cha kujifunza.

Wakati wa kipindi cha kujifunza, unatakiwa kufuata maelezo yanayokuongoza yaliyo upande wa kushoto wa mwongozo huu

na kuyahusianisha na maudhui yaliyo kwenye moduli ya mwalimu ambayo yapo upande wa kulia wa mwongozo huu kama

yanavyosomeka kwenye moduli ya mwalimu.

Page 7: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

3Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

MAELEKEZO NA TASWIRA KATIKA MODULI

Kuna picha na michoro mingi katika moduli. Baadhi zinajirudia mara nyingi kwa sababu zinamaanisha jambo mahususi linalotokea. Zifuatazo ni mifano ya taswira mbalimbali ambazo zinapatikana katika moduli pamoja na kile ambacho zinawakilisha:

Jadili na mwenzako: Wakati wote wa kusoma moduli, walimu wataelezwa kufanya kazi pamoja na mwalimu mwingine juu ya maswali au kazi.

Fikiri– Wawili wawili – Shirikishana: Kama ilivyo katika maelezo ya hapo juu, hapa vilevile walimu wanafanya kazi wakiwa wawili wawili. Japokuwa, hapa walimu wanatafakari mmoja mmoja kwanza juu ya swali au tatizo, halafu mwalimu anafanya kazi na mwenzake na mwishoni wanawasilisha katika kundi lote.

Jadiliana katika kikundi: Wakati mwingine walimu wataelekezwa kutafakari au kujadili maswali mbalimbali katika kikundi.

Soma: Katika kila moduli kuna “dhana kuu” ambayo kwa kawaida huwasilishwa kwa kirefu katika maelezo.

Andika: Moduli itawahamasisha walimu kuchukua maelezo na kuandika �kra zao na majibu.

Igizo: Baadhi ya mazoezi yatahitaji walimu kuigiza kazi ya KUFUNDISHA wakati wengine watapaswa kuigiza kama wanafunzi.

Page 8: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

4 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

MAELEKEZO KWA MRATIBU WA MAFUNZO YA WALIMU KAZINI

Kabla ya kuanza moduli hii:

• Andaa vifaa kwa ajili ya kipindi na hakikisha kuwa wewe au walimu wanavileta • Hakikisha kuwa wewe na walimu wenzako mmeisoma kwa umakini kabla ya kuanza kipindi• Tafadhali walimu waandike taarifa zao katika jedwali hapa chini.

Tarehe: Shule: Wilaya: Mkoa:

Muda wa kuanza: Jina la Mratibu wa MWK na Sahihi:

Muda wa kumaliza: Jina la Mwalimu Mkuu na Sahihi:

JINA LA MWALIMU ME / KE SAHIHI: DARASA1

2

3

4

5

6

7

8

WAAMBIE WALIMU:

‘Sasa tutasoma utangulizi wa moduli. Mwalimu mmoja ataanza kusoma kwa sauti aya ya kwanza, kisha atamwita mwalimu mwingine ili asome aya inayofuata.’

Page 9: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

5Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

MODULI YA 1: UCHUNGUZI WA MUHTASARI ULIOBORESHWA WA DARASA LA I NA LA II

MAUDHUI YA MODULITaasisi ya Elimu Tanzania (TET) imeandaa muhtasari ulioboreshwa wa Darasa la I na la II ambao unazingatia umahiri. Umahiri mkuu mmojawapo ni wa Kuhesabu. Umahiri mahsusi uliopo katika umahiri huu ni pamoja na: Dhana ya namba, Matendo katika namba, Uhusiano kati ya vitu halisi na namba, Vipimo, Maumbo na Kukusanya na kuorodhesha vitu. Katika umahiri huu, walimu wanahitaji kuwa na uelewa sahihi wa maudhui na umahiri ambao mwanafunzi anapaswa kuukuza anapo�ka mwisho wa Darasa la I na la II. Vile vile walimu wanapaswa kupambanua ni nini cha kufundisha na kwa wakati gani katika mwaka wa masomo. Moduli hii itawaongoza walimu kwa kupitia muhtasari ulioboreshwa ili waweze kutayarisha maazimio yao ya kazi kwa ajili ya mwaka wa masomo.

DHANA KUU1. Umahiri: Haya ni maarifa, stadi na mwelekeo unaojengeka kwa wanafunzi kwa mwendelezo katika kipindi

chote kuanzia elimu ya msingi, sekondari hadi elimu ya juu pamoja na nje ya mfumo rasmi wa elimu. 2. Malengo ya Ujifunzaji: Haya ni matarajio yanayotegemewa ku�kiwa katika kipindi kilichokusudiwa kama

vile mwisho wa kipindi, muhula au somo. 3. Shughuli za Ujifunzaji: Haya ni matendo ya ujifunzaji ambayo mwanafunzi anayatenda wakati wa somo.

Matendo haya yanaweza kutumika katika utangulizi wa somo, kujenga uelewa au kukazia maarifa. Mfano wa shughuli za ujifunzaji ni pamoja na kuimba, kuhadithia, kufanya kazi katika vikundi, kufanya kazi kibinafsi, na kucheza. Ieleweke kwamba, mwalimu anapoelezea kuhusu dhana Fulani, hii siyo shughuli za ujifunzaji.

4. Azimio la Kazi: Huu ni mpango wa utekelezaji wa muhtasari unaotayarishwa kwa muda maalum, kwa mfano kwa wiki, mwezi, muhula au mwaka. Mpango huu hubainisha ni nini cha kufundisha, namna ya kukifundisha na ni vifaa gani vitumike wakati wa ufundishaji na ujifunzaji.

MUDA WA KUJIFUNZA MODULI HIITumia masaa 4 kwa ajili ya Dhana kuu na Vitendo na masaa 2 ya Kuandaa Somo

MALENGO YA MODULI Hadi mwisho wa moduli hii, mwalimu utakuwa na uwezo wa:

1. Kubaini umuhimu wa ufundishaji na ujifunzaji wa kuhesabu katika madarasa ya mwanzo na malengo ya Mafunzo ya Walimu Kazini (MWK).

2. Kuchambua kwa kina umahiri mkuu wa kuhesabu uliomo katika muhtasari wa Darasa la I na la II wa mwaka 2015 ambao umeboreshwa na kuulinganisha na ule wa mwaka 2005.

3. Kufafanua malengo ya ujifunzaji kwa Darasa la I na la II kwa kutumia muhtasari ulioboreshwa. 4. Kutayarisha maazimio ya kazi kwa ajili ya Kuhesabu Darasa la I na la II.

MAZINGIRA YA KUJIFUNZIA KATIKA KIPINDI CHA MAFUNZO:1. Panga madawati/meza na viti ili kurahisisha

makusano ya washiriki.2. Kuwa huru kutoa maoni, kuuliza na kujibu maswali.3. Wakati wote uwe tayari kuwasaidia wenzako.4. Kuwa mbunifu na �kiria jinsi mawazo yanayotolewa

yatakavyoweza kutumika katika darasa lako.5. Weka kanuni kwa ajili ya kipindi chenu cha mafunzo

na vipindi vingine vitakavyofuata.

Page 10: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

6 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

UTANGULIZI

WAAMBIE WALIMU:

“Karibuni katika Mafunzo ya Walimu Kazini yanayohusu ujenzi wa umahiri wa kuhesabu kwa Darasa la I na la II. Katika kipindi hiki cha mafunzo tutaangalia kwa undani utendaji bora katika ufundishaji na ujifunzaji wa kuhesabu katika madarasa haya, ambao unaweza kutumika pia katika Darasa la 3. Katika mafunzo haya, tutakutana katika vipindi 13 vya wastani wa saa 4 kwa kila kipindi. Katika kila kipindi, tutaendelea kukutana kwa masaa mengine 2 kwa ajili ya kuandaa somo. Jinsi tutakavyokuwa tunaendelea na mafunzo, tutumie kwa vitendo yale tuliyojifunza katika madarasa yetu. Mafunzo haya yameandaliwa kwa namna itakayowezesha kushirikishana mawazo na kusaidiana wakati wa kujifunza mbinu mpya za ufundishaji na ujifunzaji. Sasa tutaanza kwa kuweka kanuni za kufuata katika vipindi vyetu vya Mafunzo ya Walimu Kazini.”

Page 11: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

7Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

UTANGULIZI

KAZI YA KIKUNDI (DAKIKA 30)\

• Katika kikundi chenu, kubalianeni kanuni zitakazowaongoza katika kipindi cha mafunzo ya umahiri wa kuhesabu kwa ajili ya Mafunzo ya Walimu Kazini.

• Nukuu kanuni hizo katika bango kitita ili kila mmoja aweze kuona na kisha bandika ukutani au ubaoni wakati wote wa kipindi cha mafunzo.

• Vile vileziandike kanuni hizo katika daftari lako kwa ajili ya matumizi ya baadaye• Hizi ndizo kanuni zitakazofuatwa na kila mmoja katika kipindi chote cha Mafunzo ya Walimu Kazini.

Kanuni za Kipindi cha Mafunzo ya Walimu Kazini:

Page 12: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

8 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU- UMUHIMU WA KUJIFUNZA KUHESABU KWA DARASA LA I NA LA II

WAAMBIE WALIMU:

“Sasa tutasoma kwa sauti maudhui muhimu katika matini kwa kupokezana. Baada ya mwalimu wa kwanza kusoma aya ya kwanza, atamwita mwalimu mwingine kwa jina ili asome aya inayofuata. Wakati wa kusoma weka alama zifuatazo: mshangao (!) kwenye jambo lolote ambalo unadhani ni muhimu; kiulizo (?) kuonesha kitu ambacho hukielewi au hukubaliani nacho na duara (o) kuonesha neno jipya.”

Walimu wanaweza kuuliza swali lifuatalo:

“Ni jinsi gani kujifunza kuhesabu kunaimarisha kusoma?”Jibu: Kujifunza kuhesabu hakuna tofauti na kujifunza lugha yeyote mpya. Kwa mfano, kujifunza kusoma na kuandika tarakimu ‘8’ inahitaji matendo ya kwenye ubongo kama ilivyo katika kusoma na kuandika heru� ‘m’. Kwa hiyo kufanyisha kazi misuli hiyo hiyo ya kwenye ubongo, matokeo yake ni kuimarisha ujuzi wa kuhesabu na kusoma. Wanataaluma wamefanya ta�ti nyingi kuhusu matokeo ya kujifunza kuhesabu katika umri mdogo na wameshangaa kugundua matokeo chanya ya uwezo wa mtoto wa kusoma kutokana na kujifunza kuhesabu.

Page 13: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

9Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU –UMUHIMU WA KUJIFUNZA KUHESABU KWA DARASA LA I NA LA II

Umuhimu wa Kujifunza Kuhesabu kwa Wanafunzi wa Darasa la I na II

Zifuatazo zinaweza kuwa nyongeza ya sababu katika orodha yenu za kwa nini ni muhimu kwa wanafunzi kujifunza kuhesabu katika Darasa la I na II:

1. Inahamasisha mafanikio ya baadaye ya mtoto katika masomoMaarifa ya awali ya kuhesabu yanahamasisha kwa kiasi kikubwa mafanikio ya baadaye ya mtoto katika masomo ya hisabati, sayansi na mengine katika shule ya msingi, sekondari na elimu ya juu. Kadhalika inahamasisha mafanikio ya baadaye katika kusoma. Hii ni kwa sababu kuhesabu huimarisha stadi za lugha ya kuongea kama vile msamiati na saru�.

2. Inawafanya wanafunzi kuwa weledi Ubongo ni kama msuli. Jinsi unavyotumika kufanya kazi ndivyo unavyozidi kukua na kuimarika na hivyo huongeza weledi. Uweledi wa Kuhesabu unakuza na kuimarisha misuli ya ubongo kwa wanafunzi wa jinsi zote.

3. Ina manufaa katika maisha ya kila siku. Wanafunzi ambao wanakokotoa kwa haraka na kwa usahihi wana uwezo wa kufanya vizuri katika maisha yao ya kila siku kwa mfano, ununuzi na uuzaji wa bidhaa sokoni au dukani. Vile vile wana uwezo wa kutatua matatizo katika maisha yao ya kila siku kwa kutumia maarifa, stadi na muelekeo wa Kuhesabu. Pia wanapokuwa watu wazima, wanapata fursa zaidi za ajira.

UMUHIMU WA KUSOMA KWA UFASAHA (DAKIKA 35)

1. Mwalimu mmoja aanze kusoma aya ya kwanza kwa sauti na kisha amwite mwalimu mwingine kwa jina ili asome aya inayofuata.

2. Wakati wa kusoma weka:• alama ya mshangao(!) katika sehemu ambayo unaona ni muhimu. • alama ya kuuliza (?) katika sehemu ambayo huelewi au hukubaliani nayo. • duara (o) katika maneno ambayo ni mapya kwako.

FIKIRI-JOZISHA -SHIRIKISHA (DAKIKA 15)

• Kaa wawili wawili na mjadili swali lifuatalo: “Kwa nini mna�kiri ni muhimu kufundisha kuhesabu kwa wanafunzi wa Darasa la I na la II?”

• Andika angalau sababu 3 za jibu la swali katika bango kitita au katika daftari lako. • Jadilini majibu yenu katika kundi kubwa.

Page 14: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

10 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

WAAMBIE WALIMU:

“Tunaendelea kusoma matini kwa sauti na kwa kupokezana.”

Page 15: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

11Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

Utangulizi wa Mafunzo ya Walimu Kazini ya Umahiri wa Kuhesabu Darasa la I na la II

Moduli 13 za Mafunzo ya Walimu Kazini za umahiri wa Kuhesabu kwa Darasa la I na la II zimezingatia muhtasari ulioboreshwa wa mwaka 2015. Moduli hizi ni elekezi na zinalandana na moduli za Mafunzo ya Walimu Kazini ngazi ya shule ambazo zilizingatia umahiri wa kusoma na kuandika. Moduli hizi za umahiri wa kuhesabu zinasisitiza yafuatayo:

1. Kujenga dhana ya namba na matendo kwa kutumia njia shirikishi zinazofurahisha na kuleta maana kwa wanafunzi.

2. Kufundisha vipimo, maumbo, na kukusanya, kuchambua na kuorodhesha vitu kwa kutumia njia shirikishi zinazofurahisha na kuleta maana kwa wanafunzi.

3. Kutumia vifaa vya kufundishia na kujifunzia, kuhakiki usahihi wa msamiati katika umahiri wa Kuhesabu na maarifa katika utendaji darasani ambao unafanya kuhesabu kufurahishe na kuleta maana kwa wanafunzi.

4. Kutumia mbinu mbalimbali kama vile nyimbo na michezo katika ufundishaji na ujifunzaji wa kuhesabu ili kufurahisha na kuleta maana kwa wanafunzi.

5. Kutumia simulizi za mafumbo katika ufundishaji na ujifunzaji kuhesabu ili ifurahishe na kuleta maana kwa wanafunzi.

Shabaha ya msingi ya mafunzo ni kukusaidia wewe mwalimu kutayarisha somo ambalo litafanya kuhesabu kufurahishe, kuvutie na kuleta maana kwa wanafunzi.

MAJADILIANO KATIKA KIKUNDI (DAKIKA 10)

1. Ni mawazo gani mapya au muhimu ambayo umeyawekea alama ya mshangao (!)?2. Ni mawazo gani ambayo hayaeleweki uliyoyawekea alama ya kuuliza (?)?3. Ni dhana zipi mpya ulizozungushia duara?

Page 16: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

12 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

VITENDO – MUHTASARI ULIOBORESHWA

WAAMBIE WALIMU:

“Tuanze kwa kuchunguza muhtasari wa Darasa la 1 wa mwaka 2015 katika umahiri wa kuhesabu. Tutumie dakika 15 kusoma kwa sauti na kutafakari maswali yaliyotolewa.”

Page 17: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

13Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

VITENDO – MUHTASARI ULIOBORESHWA

SOMA KWA SAUTI (DAKIKA 30)

1. Mwalimu mmoja aanze kusoma safu mlalo ya kwanza kwa sauti kisha amwite mwalimu mwingine kwa jina ili asome safu mlalo unaofuata.

2. Wakati unasoma weka:• alama ya mshangao(!) katika sehemu ambayo unaona ni muhimu• alama ya kuuliza (?) katika sehemu ambayo huielewi au hukubaliani nayo • duara (o) katika maneno ambayo ni mapya kwako.

1. Kadiri unavyosoma tafakari yafuatayo:

a) Sehemu gani za muhtasari ulioboreshwa ni sawa sawa na za muhtasari wa zamani? b) Sehemu gani za muhtasari ulioboreshwa ni tofauti na za muhtasari wa zamani? c) Ni kitu gani sikielewi katika muhtasari ulioboreshwa? d) Ni kwa namna gani Mafunzo ya Walimu Kazini yatanisaidia kujibu maswali a)-c)?

2. Andika maoni yako katika kisanduku kinachofuata, katika daftari lako au sehemu nyingine.

Maoni yangu kuhusu muhtasari mpya wa Darasa la I

Page 18: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

14 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

VITENDO – MUHTASARI ULIOBORESHWA

WAAMBIE WALIMU:

Kama kuna maswali yaliyoulizwa kuhusu maana ya umahiri mahsusi, malengo ya ujifunzaji, na shughuli za mwanafunzi, unaweza kufafanua kwa kutumia maelezo yafuatayo:

• Umahiri ni maarifa, stadi na mwelekeo unaojengeka kwa wanafunzi kwa mwendelezo katika kipindi chote kuanzia elimu ya msingi, sekondari hadi elimu ya juu pamoja na nje ya mfumo rasmi wa elimu.

• Kwa mfano, umahiri wa kutambua dhana ya namba katika shule ya msingi, kwanza unajikita katika namba nzima, kisha katika sehemu na baadaye katika desimali. Katika madarasa yanayofuata, dhana ya namba inaendelezwa hadi namba halisi, kama vile namba chanya na namba hasi.

• Lengo la Ujifunzaji ni tarajio linalotegemewa ku�kiwa katika kipindi kilichokusudiwa kama vile mwisho wa kipindi, muhula au somo. Kwa mfano, mwanafunzi anapaswa kuweza kuhesabu hadi 100 akiwa Darasa la 1 ili kutambua dhana ya namba. Vile vile anapaswa kuwa na uwezo wa kuhesabu hadi 1000 akiwa katika Darasa la 2 ili pia aweze kutambua dhana ya namba.

• Shughuli za Wanafunzi ni matendo ya ujifunzaji ambayo mwanafunzi anayatenda wakati wa somo. Matendo haya yanaweza kutumika katika utangulizi wa somo, kujenga uelewa au kukazia maarifa. Mfano wa shughuli za ujifunzaji ni pamoja na kuimba, kuhadithia, kufanya kazi katika vikundi, kufanya kazi kibinafsi, na kucheza. Katika shughuli za mwanafunzi, yeye ndiye kitovu cha kufanya kazi.

• Endapo kuna maswali zaidi, yanukuu na uyachukue katika mafunzo ya ngazi ya kata kupata ufafanuzi zaidi. Waarifu washiriki kuwa utajaribu kutoa ufafanuzi katika kipindi cha mafunzo kinachofuata.

Page 19: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

15Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

VITENDO – MUHTASARI ULIOBORESHWA

KAZI ZA KIKUNDI (DAKIKA 60)

1. Kaa katika jozi kisha gawana umahiri mahsusi. Ikiwa kuna jozi pungufu ya sita, gawanya umahiri mahsusi kwa idadi ya jozi. Umahiri mahsusi wa kuhesabu ulioorodheshwa katika ukurasa wa 27 hadi 45 wa muhtasari wa Darasa la I ni:

7.1 Utambuzi wa dhana ya namba 7.2 Kutumia matendo katika namba 7.3 Kutambua uhusiano wa vitu na namba 7.4 Kutambua vipimo 7.5 Kutambua maumbo 7.6 Kuorodhesha na Kukusanya vitu.

2. Kwa kila umahiri mahsusi, chunguza shughuli za mwanafunzi kwa kina. Shughuli za mwanafunzi ni vitendo anavyopaswa kuvitenda mwanafunzi ili ku�kia lengo la kujifunza.

3. Kwa kuzingatia umahiri mahsusi na shughuli za mwanafunzi, andika lengo la kujifunza kwa ajili ya umahiri huo mahsusi. Malengo ya Kujifunza yanazingatia maudhui mahsusi, darasa mahsusi, yanayopimika na kutumiwa kuweka kumbukumbu za ujifunzaji wa mwanafunzi mwishoni mwa kipindi fulani. Malengo ya ujifunzaji ya mwanafunzi wakati wote yanaanza na: “Mwanafunzi aweze.......” Kwa mfano, “Mwanafunzi aweze kuhesabu hadi 100” au “Mwanafunzi aweze kujumlisha na kupata jumla isiyozidi 100.”

4. Andika malengo manne ya ujifunzaji katika bango kitita kwa ajili ya umahiri mahsusi uliopewa.

5. Jadiliana katika kikundi.

Page 20: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

16 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU – UMAHIRI, LENGO LA UJIFUNZAJI NA SHUGHULI ZA MWANAFUNZI

WAAMBIE WALIMU:

“Sasa tutasoma kwa sauti maudhui muhimu katika matini kwa kupokezana. Baada ya mwalimu wa kwanza kusoma aya ya kwanza, atamwita mwalimu mwingine kwa jina ili asome aya inayofuata. Wakati wa kusoma weka alama kuonesha jambo lolote muhimu. Weka alama ya mshangao (!) kwenye jambo lolote ambalo unadhani ni muhimu. Weka alama ya kiulizo (?) kuonesha kitu ambacho hukielewi au hukukubaliana nacho. Mwisho, weka alama ya duara (o) kuonesha neno jipya.”

Page 21: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

17Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU – UMAHIRI, LENGO LA UJIFUNZAJI NA SHUGHULI ZA MWANAFUNZI

KUSOMA KWA SAUTI (DAKIKA 5)

1. Mwalimu mmoja aanze kusoma safu mlalo ya kwanza kwa sauti kisha amwite mwalimu mwingine kwa jina ili asome safu mlalo unaofuata.

2. Wakati unasoma weka:• alama ya mshangao(!) katika sehemu ambayo unaona ni muhimu• alama ya kuuliza (?) katika sehemu ambayo huielewi au hukubaliani nayo • duara (o) katika maneno ambayo ni mapya kwako.

Katika Umahiri Mkuu wa Kuhesabu katika Muhtasari wa Darasa la I wa mwaka 2015, safu mbili za kwanza utaona Umahiri Mahsusi na Shughuli za Mwanafunzi. Ukisoma maelezo ya Shughuli za Mwanafunzi, utabaini lengo la ujifunzaji ambalo linapaswa ku�kiwa katika somo husika. Tuanze kwa kufafanua dhana, Umahiri, Malengo ya Ujifunzaji na Shughuli za Mwanafunzi.

• Umahiri ni maarifa, stadi na mwelekeo unaojengeka kwa wanafunzi kwa mwendelezo katika kipindi chote kuanzia elimu ya msingi, sekondari hadi elimu ya juu pamoja na nje ya mfumo rasmi wa elimu. Kwa mfano, umahiri wa kutambua dhana ya namba katika shule ya msingi, kwanza unajikita katika namba nzima, kisha katika sehemu na baadaye katika desimali. Katika madarasa yanayofuata, dhana ya namba inaendelezwa hadi namba halisi, kama vile namba chanya na namba hasi.

• Lengo la Ujifunzaji ni tarajio linalotegemewa ku�kiwa katika kipindi kilichokusudiwa kama vile mwisho wa kipindi, muhula au somo. Kwa mfano, mwanafunzi anapaswa kuweza kuhesabu hadi 100 akiwa Darasa la 1 ili kutambua dhana ya namba. Vile vile anapaswa kuwa na uwezo wa kuhesabu hadi 1000 akiwa katika Darasa la 2 ili pia aweze kutambua dhana ya namba.

• Shughuli za Wanafunzi ni matendo ambayo mwanafunzi anayatenda wakati wa mchakato wa ujifunzaji. Matendo haya yanaweza kutumika katika utangulizi wa somo, kujenga uelewa au kukazia maarifa. Mfano wa shughuli za ujifunzaji ni pamoja na kuimba, kuhadithia, kufanya kazi katika vikundi, kufanya kazi kibinafsi, na kucheza. Katika shughuli za mwanafunzi, yeye ndiye kitovu cha kufanya kazi.

Unapochunguza kwa kina kila umahiri mahsusi na shughuli za mwanafunzi katika Darasa la I na la II, utabaini malengo ya ujifunzaji yafuatayo:

Page 22: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

18 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

WAAMBIE WALIMU:

“Tunaendelea kusoma matini kwa sauti na kwa kupokezana.”

DHANA KUU – UMAHIRI, LENGO LA UJIFUNZAJI NA SHUGHULI ZA MWANAFUNZI

Page 23: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

19Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

Umahiri mahususi

Malengo ya Ujifunzaji Darasa la I Mwanafunzi aweze:

Malengo ya Ujifunzaji Darasa la II Mwanafunzi aweze:

Utambuzi wa dhana ya namba

a. Kubaini namba nzima 1 hadi 9b. Kuhesabu 1 hadi 9 c. Kusoma/kuandika namba 1 hadi 9d. Kulinganisha na kupanga namba

zisizozidi 9 e. Kueleza dhana ya 0 f. Kusoma/kuandika 0g. Kubaini/Kuhesabu 10h. Kusoma/kuandika namba 10i. Kuhesabu kuanzia 11 hadi 100j. Kusoma/kuandika namba kuanzia 11

hadi 100k. Kulinganisha na kupanga namba mbili

au zaidi chini ya 100

a. Kuhesabu hadi 1000b. Kusoma/kuandika hadi 1000c. Kulinganisha na kupanga namba

zisizozidi 1000

Kutumia maten-do katika namba

a. Kujenga dhana ya kujumlisha na alama +

b. Kujenga dhana ya sawa sawa na alama =

c. Kujumlisha kupata jumla isiyozidi 10d. Kujenga dhana ya thamani ya nafasi

katika namba (mamoja, makumi)e. Kujumlisha na kupata jumla isiyozidi

100f. Kujenga dhana ya kutoa na alama −g. Kutoa namba zisizozidi 10h. Kutoa namba ambazo hazizidi 100

a. Kujenga dhana ya thamani ya nafasi katika namba (mamoja, makumi, mamia)

b. Kujumlisha/Kutoa kupata jumla isiyozidi 1000

Kutambua uhusiano kati ya idadi ya vitu na

namba

a. Kuoanisha vitu halisi na namba hadi 10 b. Kujenga dhana ya sehemu 1/2 na 1/4

ya kitu kizima c. Kutambua, kusoma na kuandika 1/2 na

1/4 d. Kutambua noti na sarafu za Tanzaniae. Kujumlisha/Kutoa sarafu kupata jumla

isiyozidi 100

a. Kujenga dhana ya sehemu 1/3 na 2/3 ya kitu kizima

b. Kusoma/kuandika 1/3 na 2/3c. Kutambua noti za shilingi 200,

500 na 1000 d. Kujumlisha/Kutoa fedha kupata

jumla isiyozidi 1000

Kutambua vipimo

a. Kujenga dhana ya vipimo vya wakati kutokana na muda na matukio

b. Kujenga dhana ya umbali (karibu, mbali) na urefu ( ndefu, fupi)

c. Kujenga dhana ya uzito (nzito, nyepesi) d. Kujenga dhana ya ujazo (zaidi, pungufu)

a. Kuelewa wakati kwa kutumia muda mrefu na muda mfupi

b. Kulinganisha urefu ulio sawa c. Kulinganisha umbali ulio usawad. Kulinganisha ujazo ulio sawa

DHANA KUU – UMAHIRI, LENGO LA UJIFUNZAJI NA SHUGHULI ZA MWANAFUNZI

Page 24: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

20 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

WAAMBIE WALIMU:

“Tunaendelea kusoma matini kwa sauti na kwa kupokezana.”

DHANA KUU – UMAHIRI, LENGO LA UJIFUNZAJI NA SHUGHULI ZA MWANAFUNZI

Page 25: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

21Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

Umahiri mahususi

Malengo ya Ujifunzaji Darasa la I Mwanafunzi aweze:

Malengo ya Ujifunzaji Darasa la II Mwanafunzi aweze:

Kutambua maumbo

a. Kubaini maumbo bapa na maumbo yasiyo bapa ya pembe tatu, pembe nne na mduara

b. Kuchora maumbo bapac. Kubaini maumbo yenye ukumbi

a. Kutambua maumbo yenye ukumbi na maumbo bapa ya pembe tatu, pembe nne na mduara ili kujenga dhana ya maumbo.

Kukusanya na kuorodhesha

vitu

a. Kukusanya na kuelezea data kwa kutu-mia lugha kama vile “zaidi,” “ya mwisho,” “kubwa zaidi,” “ ndogo zadi,” “nyingi kama,” idadi kama”

b. Kutambua vitu halisi vinavyoweza kuwa-silishwa

c. Kuwasilisha vitu katika michoro

a. Kujenga dhana ya thamani ya nafasi katika namba (mamoja, makumi, mamia)

b. Kujumlisha/Kutoa kupata jumla isiyozidi 1000

c. Kupanga vitu 12 kulingana na matumizi ya taarifa za kuwakilisha

MAJADILIANO KATIKA KIKUNDI (DAKIKA 10)

1. Ni dhana gani muhimu ambazo umeziwekea alama ya mshangao (!)?2. Ni dhana gani ambazo hujazielewa na hukubaliani nazo ulizoziwekea alama ya kuuliza (?)?3. Ni dhana gani mpya ulizozungushia duara?

DHANA KUU – UMAHIRI, LENGO LA UJIFUNZAJI NA SHUGHULI ZA MWANAFUNZI

Page 26: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

22 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

VITENDO: KUANDAA AZIMIO LA KAZI

WAAMBIE WALIMU:

“Katika kipindi hiki tutaandaa Azimio la Kazi kwa Darasa la 1. Hata hivyo, inawezekana tusiweze kukamilisha kazi hiyo katika kipindi hiki, lakini tunaweza kukamilisha wakati mwingine tutakapokutana. Pia tutarudia zoezi hili kama kikundi tutakapokutana kwa ajili kuandaa Azimio la Kazi kwa Darasa la 2”

Page 27: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

23Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

VITENDO: KUANDAA AZIMIO LA KAZI

KAZI YA KIKUNDI (DAKIKA 60)

Umahiri Mahsusi

Shughuli za Ufundishaji

Mwezi Wiki Idadi ya Vipindi

Rejea Zana za Ufundishaji

Zana za Upimaji

Maoni

Jina la shule : _________________________ Jina la mwalimu: __________________________

Darasa:____________________________ Umahiri mkuu: ____________________________

Muhula:__________________________________________________________________________

Mwaka: _________________

a. Tafakari mpangilio wa kimantiki wa ku�kia kila lengo la ujifunzaji na jinsi ya kuigawa dhana husika katika juma zima. Kwa mfano, lengo la ujifunzaji “Kuhesabu hadi 100,” linaweza kugawanywa ili ku�kia lengo la “Kuhesabu hadi 20,” “Kuhesabu hadi 30,” “Kuhesabu hadi 50,”na mwisho “Kuhesabu hadi 100” kama njia mojawapo ya kujenga dhana kwa mwendelezo.

b. Kutumia malengo ya ujifunzaji yaliyopo hapo juu ili, kupata nini cha kufundisha na wakati gani wa kukifundisha katika Darasa la I.

c. Kamilisha rasimu ya Azimio la Kazi. Mnaweza kukutana tena kukamilisha Azimio la Kazi.d. Kumbuka kwamba katika mwaka wa masomo kuna siku 4 za somo la Kuhesabu yaani vipindi 8 vya

saa kwa juma. Kuna majuma 40 ya kufundisha kwa mwaka wa masomo. e. Kumbuka kuweka muda wa kutosha kwa ajili ya kufanya marudio na upimaji.f. Mfano ufuatao ni wa Azimio la Kazi unalopaswa kukamilisha.

Page 28: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

24 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU: AZIMIO LA KAZI WAAMBIE WALIMU:

“Kwa vile sasa umepata fursa ya kuandaa Azimio lako la Kazi, tuangalie sampuli ya sehemu za Azimio la Kazi lililokamilishwa.”

Page 29: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

25Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU: AZIMIO LA KAZI

KUSOMA KWA SAUTI (DAKIKA 5)

1. Mwalimu mmoja aanze kusoma safu mlalo ya kwanza kwa sauti kisha amwite mwalimu mwingine kwa jina ili asome safu mlalo unaofuata.

2. Wakati unasoma weka:• alama ya mshangao(!) katika sehemu ambayo unaona ni muhimu• alama ya kuuliza (?) katika sehemu ambayo huielewi au hukubaliani nayo • duara (o) katika maneno ambayo ni mapya kwako.

Katika hatua hii ni dhahiri kwamba, unatambua kuwa kuna tofauti kati ya muhtasari wa Darasa la I na la II wa mwaka 2015 na muhtasari wa 2005. Tofauti zilizopo ni pamoja na ongezeko la mada za vipimo, maumbo na kukusanya vitu na katika kuweka msisitizo mkubwa katika umuhimu wa shughuli mbali mbali ambazo zinavutia na kuleta maana kwa wanafunzi ili waweze kujenga uelewa wa dhana za kihisabati kwa urahisi. Kwa hiyo, ni muhimu kupata mpangilio ambao malengo ya ujifunzaji yata�kiwa katika muda uliopangwa, na kina cha maudhui kitakacho�kiwa darasani. Azimio la Kazi ni jedwali linalotoa mpangilio wa nini cha kufundisha, namna ya kukifundisha na ni wakati gani kifundishwe kwa juma, mwezi, muhula au mwaka mzima wa masomo. Kwa mfano, mtoto anapaswa aweze kuhesabu 1 hadi 100 kabla ya ku�kia hatua ya kujumlisha namba ili kupata jumla isiyozidi 100. Hata hivyo anaweza kuanza kupata dhana ya maumbo katika jometri kabla ya kujua kujumlisha. Kumbuka kwamba katika juma, kuna siku 4 za somo la Kuhesabu yaani vipindi 8 vya dakika thelathini (dk 30) kila kimoja. Kwa ujumla, kuna majuma 40 ya kufundisha katika mwaka wa masomo ambapo maudhui yote kwa kila darasa yanatakiwa kukamilishwa.

Kuwa na Azimio la Kazi linalofanana kwa walimu wote wanaofundisha somo moja katika darasa na shule au wilaya moja inasaidia mwalimu mkuu au viongozi wengine wa elimu kufuatilia maendeleo ya wanafunzi. Vile vile, inarahisisha walimu kushirikiana wanapotengeneza maandalio ya somo ya kila siku.

Mwisho wa moduli hii, utaona mfano wa sehemu za Azimio la Kazi kwa Darasa la I na la II. Unaweza kulitumia kama rejea yako, lakini pia unaweza kulirekebisha kulingana na mahitaji yako.

ANDIKA (DAKIKA 10)Andika maswali au maoni yoyote uliyonayo baada ya kukamilisha zoezi hili na kusoma dhana kuu. Maoni na maswali haya yatashughulikiwa katika kipindi kinachofuata.

MASWALI YANGU & MAONI

Page 30: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

26 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

WAAMBIE WALIMU:

Ni muhimu sana walimu kuwa na uwezo wa kutumia mbinu walizojifunza katika Mafunzo ya Walimu Kazini katika madarasa yao. Kwa sababu hiyo kuna manufaa ya kuandaa masomo katika kikundi kuliko kufanya mtu mmoja mmoja. Tunaposaidiana kupitia mchakato huu wa kuandaa somo, tutaweza kuwa na masomo bora zaidi. Kwa hiyo tutengeni angalau muda wa masaa 2 kwa ajili ya kutayarisha andalio la somo kwa pamoja. Katika mkutano wetu wa kwanza wa kutayarisha andalio la somo, tutakamilisha Azimio la Kazi kwa Darasa la I na la II katika vikundi”

KWA PAMOJA MKUBALIANE SIKU NA MUDA MTAKAOKUTANA KUKAMILISHA SEHEMU YA ANDALIO LA SOMO KATIKA MODULI HII. WAKATI MTAKAPOKUTANA TENA KUFANYIA KAZI SEHEMU HII, ZUNGUKIA WALIMU NA KUONA KAMA WANAHITAJI MSAADA.

KUANDAA SOMO

Page 31: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

27Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUANDAA SOMO

KUANDAA SOMO (MASAA 2)

Ni muhimu sana walimu kuwa na uwezo wa kutumia mbinu walizojifunza katika Mafunzo ya Walimu Kazini ili kuimarisha ujifunzaji wa wanafunzi. Kwa hiyo ni muhimu kutenga angalau masaa 2 kwa ajili ya kutayarisha andalio la somo kwa kushirikiana na walimu wengine.

1. Tenga muda wa kukutana ili kukamilisha zoezi hili kabla ya kuendelea na hitimisho la kipindi cha mafunzo cha leo.

2. Mtakapokutana kwa ajili ya andalio la somo, kwanza pitieni upya dhana kuu zilizoainishwa katika moduli hii.

3. Katika Vikundi, kamilisheni zoezi la kuandaa Azimio la Kazi kwa Darasa la I na la II. 4. Kabla ya kuanza moduli mpya, una fursa ya kushirikisha wenzako changamoto ulizokabiliana nazo na

mafanikio uliyoyapata katika kukamilisha Azimio la Kazi.

Page 32: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

28 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUFUNGA

WAAMBIE WALIMU:

“Tume�ka mwisho wa moduli yetu, tutumie dakika chache kutafakari somo letu la leo. Jaza fomu kutathmini moduli. Baada ya kukamilisha, nyofoa ukurasa huo unipatie. Tafadhali uwe mkweli katika kutoa majibu yako kwa sababu yatasaidia kuboresha mafunzo ya MWK ngazi ya shule hapo baadaye.”

Kusanya fomu za tathmini zilizokamilishwa na walimu na uwe nazo wakati wa mkutano mwingine katika klasta ya kata. Wakati walimu wanaendelea kujaza fomu za tathmini, tafadhali tafakari kwa ujumla juu ya mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika kipindi cha siku hiyo na jaza fomu inayofuata hapo chini.

MAFANIKO YA JUMLA YA KIPINDI HIKI: CHANGAMOTO ZA JUMLA ZA KIPINDI HIKI:

Shule: ______________________ Wilaya: ___________________ Mkoa:____________________

Tafakuri za Moduli # ________ Mada ya Moduli: _______________________________________

Idadi ya walimu walioshiriki : ________ Mwalimu Mkuu alishiriki : Ndiyo/Hapana

Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini (MWK) alikuwepo kuwezesha: Ndiyo/Hapana

Page 33: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

29Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUFUNGA

ANDIKA MWENYEWE (DAKIKA 15)Tafadhali jaza fomu ifuatayo ili kutathmini moduli ya leo. Baada ya kukamilisha, nyofoa ukurasa huu na umpe Mratibu wako wa Mafunzo ya Walimu Kazini (MWK). Tafadhali kuwa mkweli kwa vile mrejesho wako utasaidia kuboresha MWK ngazi ya shule hapo baadaye.

Jedwali la Kutathmini Mafunzo ya Walimu Kazini (MWK ):Alama 0 :

Sikubaliani kabisa na usemi huu

Alama 1 : Kwa kiasi Sikubaliani

na usemi huu

Alama 2 : Nakubaliana kwa

kiasi na usemi huu.

Alama 3 : Nakubaliana kabisa

na usemi huu.

Jedwali la Kutathmini MWK :

Shule: ______________________ Wilaya: ___________________ Mkoa:_____________________

Tathmini ya Moduli: ________ Mada ya Moduli: ______________________________________

Idadi ya walimu walioshiriki: ________ Mwalimu Mkuu alishiriki: Ndiyo/Hapana

Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini (MWK) alikuwepo kuwezesha: Ndiyo/Hapana

Soma semi zifuatazo kasha weka alama ya vema katika kisanduku husika kuonesha jibu lako:

0 1 2 3

1. Dhana muhimu ya moduli ya leo ilikuwa inaeleweka. Najisikia kuwa nimeelewa vizuri mada zote.

2. Moduli hii ina mikakati mingi mizuri na yenye manufaa ambayo nitaitumia darasani kwangu.

3. Muda uliotumika kukamilisha moduli hii unatosha. Sikujisikia kwamba ni muda mrefu sana.

4. Moduli hii iliibua mjadala wa kufurahisha sana na tafakuri ya hali ya juu

5. Mratibu wa MWK amejiandaa vyema (amesoma vizuri moduli na ameandaa zana na vifaa vyote vya kujifunzia) kwa kipindi.

6. Mratibu wa MWK amesimamia vizuri majadiliano (anajua jinsi ya kuwafanya washiriki wajieleze na namna ya kupata majibu).

7. Mratibu wa MWK ameweza kusimamia makundi (anahakikisha kuwa walimu wanatoa ushirikiano, wanashirikiana na wana hamasa).

8. Mratibu wa MWK ameweza kuwahamasisha washiriki (anafuatilia kujua wal-iokosa vipindi au kuchelewa na kutukumbusha umuhimu wa mafunzo haya).

1. Malizia kipindi kwa kupanga tarehe na muda wa kukutana kwa ajili ya kuanza moduli mpya.

Page 34: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru

30 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

AZIMIO LA KAZI

Kuna shughuli kuu nne za wanafunzi ambazo zimependekezwa kwa kila juma. Unaweza kupanga namna ya kutumia vipindi vyako viwili vya dakika 30 kila kimoja kwa siku. Vipindi vya dakika 30 mara mbili kwa siku vinatoa muda wa kutosha wa kushirikisha wanafunzi kufanya kazi katika vikundi au katika jozi. Shughuli za wanafunzi zimeainishwa kama ifuatavyo: Kuimba nyimbo, Kusimulia hadithi, Kufanya Kazi katika vikundi, jozi na binafsi, Kucheza michezo na Sanaa. Shughuli za wanafunzi zilizoainishwa hapa Zinawajengea Umahiri na zimekusudiwa kutoa muda kwa wanafunzi kufanya mazoezi na kujenga umahiri husika. Shughuli za wanafunzi zilizopendekezwa hapa zimeelezwa kwa undani katika moduli za Mafunzo ya Walimu Kazini. Vifuatavyo ni Kioleo na mfano wa Azimio la Kazi kwa Darasa la I na la II vilivyotolewa na Taasisi ya Elimu Tanzania.

Umahiri Mahsusi

Shughuli za Ufundishaji

Mwezi Wiki Idadi ya Vipindi

Rejea Zana za Ufundishaji

Zana za Upimaji

Maoni

Jina la shule : _________________________ Jina la mwalimu: __________________________

Darasa:____________________________ Umahiri mkuu: ____________________________

Muhula:__________________________________________________________________________

Mwaka: _________________

Page 35: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 36: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 37: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 38: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 39: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 40: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 41: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 42: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 43: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 44: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 45: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 46: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 47: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 48: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 49: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 50: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 51: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 52: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 53: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 54: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 55: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 56: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 57: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 58: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 59: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru
Page 60: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa pamoja na wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro. Tunapenda pia kuwashukuru