kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao...

28
kwa utetezi Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU KUWA TAYARI

Upload: others

Post on 31-Aug-2019

45 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

kwa uteteziMwongozo

kwa vijana wanaoishi na VVU

KUWA TAYARI

Page 2: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

ShukraniShukrani ziwaendee wanachama wa Mtandao wa Y+ duniani kote kwa kushirikisha uzoefu wao kama watetezi katika mwongozo huu. Kwa njia ya pekee tunapenda kushukuru mchango mahsusi wa Chimumbwa Mubanga, Kelvin Makura, Phindile Nhleko, Audrey Nosenga, Bakita Khasada, Alexander Stanciu na Cedric Nininahazwe.

Umeandikwa na Kate Iorpenda

Umechorwa na Jane Shepherd

READY+ aims to advance sexual and reproductive health and rights (SRHR), psychological wellbeing, care and treatment with, by and for 30,000 adolescents and young people living with HIV in Mozambique, eSwatini, Tanzania and Zimbabwe. The programme is being implemented by an innovative and multi-disciplinary consortium of youth, SRHR, HIV and communication partners.

READY+ is one of a portfolio of projects being implemented under the READY programme. For more information, visit https://frontlineaids.org/our-work-includes/ready/

Funded by the Embassy of the Kingdom of the Netherlands, Mozambique

Page 3: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU | 3

Kijitabu hiki ni kwa ajili ya vijana wanaoishi na VVU wanaotaka kushirikishwa kwenye kazi za Utetezi. Kijitabu kinauliza maswali muhimu kwa mfano, ni kwa nini unapenda kuwa Mtetezi, na kutaka kujua mambo unayoshughulika nayo. Kinatoa mapendekezo ya njia unazopaswa kutumia, vidokezo muhimu kwa ajili ya kazi yako na maneno ya hamasa kutoka kwa watu kadhaa mashuhuri. Kuna miongozo mingi inayokuelekeza jinsi ya kufanya kazi za utetezi na jinsi ya kuandaa kampeni au shughuli mbalimbali ambazo tutazigusia kwenye mwongozo huu, lakini lengo kuu ni kujifunza zaidi kukuhusu wewe kama mtetezi.

Utangulizi

“Mabadiliko hutokea kwa kuwa watu wa

kawaida hufanya mambo yasiyo ya

kawaida.”

BARACK OBAMA

Page 4: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

Utetezi unamaanisha vitu tofauti kwa watu tofauti.

Ufuatao hapa ni ufafanuzi ufaao uliotolewa na Shirikisho la Kimataifa la Uzazi wa Mpango (International Planned Parenthood Federation).1

“Utetezi ni kazi ya kutambua na kupigania kufanyika kwa mabadiliko. Utetezi hupigania mabadiliko yafanyike katika sheria, sera, taratibu na mifumo ili kuboresha maisha ya watu.”

Utetezi hauishii tu katika kuongeza ufahamu wa jambo fulani, bali ni kujaribu kutafuta mabadiliko katika sera, taratibu, mifumo, miundo, maamuzi na mitazamo ambayo husababisha ubaguzi, kutenga watu au udhalimu.

Kuhamasisha mabadiliko yafanyike

4 | KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU

1. IPPF (2011), Unataka kubadili dunia? Tazama jinsi ya kufanya hivyo: Nyenzo yako ya hatua za mabadiliko.

Nini maana ya Utetezi

Kushawishi watoa maamuzi

Kulinda haki za binadamu

“Nina hasira. Sote tunapaswa kuwa na hasira.

Hasira ina historia ndefu ya kuleta mabadiliko chanya. Ila

nina matumaini pia, kwa sababu naamini kwa dhati kabisa

katika uwezo wa binadamu kujirekebisha na kuwa

bora zaidi.”

CHIMANDA NGOZI ADICHIE

Page 5: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU | 5

Advocacy can happen at different levelsInaweza kuwa ni kazi ya kawaida iliyofanywa ndani ya jamii yako, ikitetea upatikanaji na usambazaji wa huduma au ugawaji wa rasilimali au katika ngazi ya kitaifa au kimataifa ikitaka mabadiliko ya sera au vipaumbele ili kuvutia umakini na uwekezaji. Shughuli zote hizi zinahusiana na hivyo mabadiliko katika ngazi moja yanaweza kuchochea mabadiliko katika ngazi nyingine.

Waandae wengine wachukue hatuaMara nyingi utetezi ni uwezo uliokuwa nao wa kuwaunganisha wengine, kuongeza umakini kwenye jambo fulani na kuwahimiza watu waone umuhimu wa jambo hilo na kuingilia kati ili kubadili mazoea au sheria.

Utetezi unawahusu viongozi na watoa maamuziKuna njia nyingi za kufanya utetezi na sio lazima kutoa hotuba kubwa au taarifa fupifupi zinazohusu masuala ya kidunia. Utetezi unaweza kuwa ni mazungumzo au uwasilishaji wa ushahidi muhimu unaoweza kubadili akili za watu.

Mtetezi ana majukumu gani?Watu unaowalenga katika utetezi wanaweza kuwa ni wale wanaoweza kubadilisha mambo, wanaoweza kubadili vitu, wanaofanya maamuzi katika ngazi mbalimbali- wakiwemo wakuu wa kaya, viongozi wa kijamii au hata marais wa nchi.

Yana Panfilova, Y+ Steering Group member, speaks on a #WhatWomenWant panel with Ambassador Deborah Birx at the 2016 High Level Meeting on Ending AIDS, New York.

© U

N W

omen

/Rya

n B

row

n

Page 6: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

6 | KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU

Utetezi unatokea katika ngazi tofauti na kwa njia mbalimbali , kwa hiyo ukiwa kama mtetezi kuna majukumu ya aina mbalimbali ambayo unaweza kuwa nayo. Ifuatayo hapa chini ni nyenzo ya msaada inayoonesha baadhi ya majukumu na jinsi yanavyohusiana na malengo yako kama mtetezi, watu unaotaka kuwabadilisha akili na wengine walioathirika na jambo hilo.2

Mtetezi ana majukumu gani?

2. Tearfund (2014), Advocacy guide. https://learn.tearfund.org/en/resources/publications/roots/advocacy_toolkit/

“Dunia nzima inapokaa kimya, hata sauti moja tu

huwa na nguvu.”

MALALA YOUSAFZAI

Page 7: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU | 7

JUKUMU SIFA

Wakilisha Zungumza kwa niaba ya watu

Jadili Fanikisha majadiliano na watoa maamuzi ili kufikia mabadiliko fulani

WezeshaWawezeshe watu wazungumze kwa niaba yao wenyewe

PatanishaWezesha mawasiliano baina ya watu na watoa maamuzi

UnganishaWakutanishe watu ili wazungumze kwa pamoja

ShawishiMshawishi mtoa maamuzi kufanya jambo Fulani mnalo-lipigania

HamasishaWahamasishe watu wachukue hatua ili kumshawishi mtoa maamuzi kufikia jambo Fulani mnalolipigania

ShaurianaShauriana hadi kufikia suluhu ya jambo fulani

MobiliseEncourage people to take action to influence a decision-maker

BargainNegotiate the settlement of something

Mtetezi Walengwa/watoa maamuzi/wenye mamlaka Wanaoathirika na hali ilivyo sasa

Page 8: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

Persuasive

Mtu yeyote ambaye ameathirika na, au mwenye nia na jambo au mwenye tatizo Fulani anaweza kuwa mtetezi. Hakuna mahitaji maalum. Kitu cha msingi ni kuwa na shauku na jambo hilo na tamaa ya kuunga mkono mabadiliko chanya.

Kwa vijana wanaoishi na VVU kunaweza kuwa na dhana kwamba ni lazima ujihusishe kwenye utetezi, na kwamba unawajibika kufanya kazi za utetezi. Huu sio ukweli. Kuishi na VVU hakukufanyi uwe mtetezi.

Kazi ya utetezi ni ya kuunga mkono kazi ya kufanya mabadiliko baada ya kupata taarifa, kujua mlengwa ni nani, kutafuta ushahidi unaohitajika ili kuwashawishi watu wabadilike. Kazi hii inahusisha kukusanya taarifa, kupangilia kazi yako na kutathmini mafanikio.

Kuwa mtetezi kijana kuna faida zake, shauku na nguvu na ubunifu vinaweza kuhamasisha na kutia msukumo lakini kunaweza pia kuwa na changamoto kwa watetezi vijana kutokana na kugombania madaraka, ushawishi na viwango vya uzoefu ambavyo vinaweza kufanya mambo kuwa magumu zaidi.

Watetezi wenye nguvu zaidi ni wale walio na mvuto, wanaozungumza kwa kutumia ujuzi na uzoefu na wenye uhalali, ambao ni sehemu ya jamii wanazoziwakilisha au wenye uzoefu na ujuzi kuhusiana na masuala wanayotaka yabadilishwe. Kuna pia watu ambao wanaweza kushawishi na kuwasilisha ujumbe wenye nguvu.

Je mimi ni mtetezi?

Authentic

8 | KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU

Legitimate

Page 9: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

“Watu walikuwa wakinionea huruma na hali hii ilinifanya

kuwa na hofu na kutojisikia vizuri.”

MTETEZI KIJANA

KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU | 9

Mvuto, uhalali na ushawishi vinatokana na kulichukulia jambo kwa umakini na kuwa na hamu ya kutaka mabadiliko yafanyike. Vitu hivi ni vya muhimu wakati tunapofikiri juu ya kazi zetu kama watetezi. Jambo hili linanihusu? Ni kweli kwamba nataka kufanya mabadiliko?

Nyakati Fulani watu wanaulizwa kuzungumzia mambo ambayo hawana shauku nayo na matokeo yake huwa dhaifu.

Tumia maswali haya kutafakari kuhusu jukumu lako kama mtetezi na jinsi utakavyoupa kipaumbele ujumbe wako. Ikiwa jambo lenyewe sio kipaumbele chako, tafuta mtu mwingine alifanye na usijaribu kufanya kila kitu peke yako.

●● Shauku zangu ni zipi, ni vitu gani

vinavyonihusu zaidi?

●● Ni mambo gani hunifanya nikasirike?

●● Ujasiri wangu upo katika maeneo gani?

●● Watu huniona nikiwa na ujasiri wa aina gani?

●● Ni vitu gani kati ya hivi ninavyopenda

kufanya? Kuunganisha, kuzungumza,

kuandika, kushawishi, kuandaa, kuhamasisha,

kuwasilisha?

●● Ni vitu vitu gani vinanifanya nifanikiwe katika

mambo haya? Nguvu, kushikilia jambo, ubunifu,

uhalali, uwepo, ujuzi, uzoefu?

●● Ni hisia zipi ambazo kazi ya utetezi huweza

kuchechemua? Hasira, kuchanganyikiwa,

msisimko, matumaini?

Page 10: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

Watu wengi wanaoishi na VVU huwashirikisha watu wengine simulizi zao au ushuhuda wao ili kukabiliana na unyanyapaa, kuelimisha au kuwapasha watu habari na kushawishi na kuhamasisha mabadiliko. Kwa vijana uzoefu wao wa kwanza mara nyingi ni wakati wanapoulizwa kuwashirikisha wengine shuhuda zao. Lakini siyo kila mtu anajisikia vizuri kuwashirikisha watu wengine mambo yao, au inaonekana kama siyo jambo sahihi kufanya hivyo. Vijana wasilazimishwe kuwashirikisha watu shuhuda zao kama hawapendi, na wanatakiwa kusaidiwa ili watambue madhara yanayoweza kujitokeza kwa kufanya hivyo. Labda hawajawahi kuwashirikisha watu wengine shuhuda zao kabla au pengine hawajawahi kupata fursa ya kutafakari kwa kina kuhusu matokeo ya kuwashirikisha wengine.

Kwa bahati mbaya, vijana wengi sana wanalazimishwa kufunua hali zao na mara nyingi hii inakuwa ni mara yao ya kwanza kuulizwa hivyo wakiwa watetezi. Hali hii inaweza kusababisha unyanyapaa, ubaguzi na mwonekano usiofaa toka kwa jamii. Ikiwa utaulizwa kutoa ushuhuda wa hali yako ujiridhishe na sababu za kutakiwa kufanya hivyo na ujue matokeo ya kitendo hicho.Tafakari maswali yafuatayo ili ufikie uamuzi sahihi. Fikiri kwa makini maswali unayoweza kuulizwa na iwapo utajisikia vizuri kuyajibu.

●● Je? Ninahitaji kuwashirikisha watu

wengine ushuhuda wangu?

●● Je? Ni watu hawa ndiyo ninaotaka

kuwashirikisha?

●● Je? Ushuhuda wangu utanukuliwa kwenye

vyombo vingine vya habari, kwenye

mtandao wa intaneti ?

●● Ni mambo gani ninayotaka kuwashirikisha

wengine? Labda baadhi tu ya historia

yangu au sehemu ya maisha yangu nikiwa

na VVU?

Kutoa ushuhuda wangu

10 | KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU

Page 11: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU | 11

Haya ni baadhi ya maswali ya kuingilia uhuru wa mtu ambayo vijana wamekuwa wakiulizwa. Fikiria vizuri majibu unayopaswa kutoa, andaa ushuhuda wako, amua kama utajisikia vizuri kuwashirikisha wengine ushuhuda wako.

Uamuzi unaohusu kuwashirikisha watu wengine hali yako ya VVU ni jambo la binafsi. Una haki ya kuamua kama unataka kufunua hali yako ya VVU na ni lini, kwa nani na kwa jinsi gani. Usilazimishwe kufunua hali yako ili ushirikishwe kwenye kazi ya utetezi, na pia shirika lisisambaze taarifa za hali yako ya VVU kwa watu bila ridhaa yako.

Chukua muda kutafakari kwa kina ikiwa unapenda hali yako ya VVU au utambulisho kwamba unaishi na VVU vijulikane kwenye jamii yako, kuna madhara gani na matokeo gani mazuri na misaada utakayopata kwa kufunua taarifa zako.

“Kama unafikiri wewe ni mdogo sana

kufanikisha jambo, hujawahi kulala kitanda

kimoja na mbu!”

WENDY LESKO

Ulipataje maambukizo ya

VVU?

Ulishawahi kuwaambukiza watu

wengine VVU?

Kuna mtu mwingine kwenye familia yako anayeishi na VVU?

Page 12: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

12 | KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU

Sasa tayari umeshafikiri kwa makini mambo ambayo unayamudu na ujasiri unaouleta kwenye kazi ya utetezi na kufikiri jinsi unavyotaka kutumia uzoefu wa kuishi na VVU katika kazi ya utetezi.

Nitanufaika na nini nikiwa Mtetezi?Kuwa mtetezi kunaweza kuwa jambo la kusisimua na lenye kutoa uzoefu wenye nguvu kwa vijana, likifungua fursa za kuwa sehemu ya harakati na matendo ya kuleta mabadiliko. Unatarajia manufaa gani? Kuna baadhi ya mawazo hapa, Je? unaweza kufikiria mengine pia?

●● Fursa ya kukutana na watu mbalimbali wenye hamu na uzoefu unaofanana

●● Kupata ujuzi kuhusu masuala muhimu

●● Kuhamasika na kuwahamasisha wengine

●● Kutafuta washauri wa kusaidia katika mafunzo yako na kukupa ushauri

●● Kujifunza kuhusu jamii yako, kupata undani wa mambo muhimu zaidi

●● Kupata ufahamu wa viwango vya kimataifa, kujifunza kutoka kwa vijana wanaoishi na VVU katika nchi nyingine.

●● Kujiamini na kujiheshimu

●● Kuleta mabadiliko katika jumuiya yako na dunia kwa ujumla

●● Kupata ujuzi na uzoefu katika Nyanja za mawasiliano, utafiti na kuandika

●● Kuboresha njia za ajira

Kufanya kazi ya Utetezi

Page 13: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU | 13

Mambo ya kukumbuka unapofanya kazi kama Mtetezi

Usikubali kutumiwa visivyoMwonekano wa vijana katika mtazamo wa VVU na sekta pana ya Afya umewavutia vijana wengi zaidi na kuwapa ushiriki wenye manufaa. Hata hivyo bado kuna mashirika mengi, makongamano na mikutano ambayo inatambua kwamba inapaswa kuonekana ikifanya kazi na vijana na bado haifanyi hivyo. Katika hali kama hii, viongozi wa mikutano au mashirika au makongamano huomba uwepo wa vijana kwenye safu ya uongozi, katika picha za video zinazopigwa na katika timu zao lakini hawamaanishi kufanya kazi na vijana kwa usawa kama inavyoonekana.Kama utaambiwa uwe sehemu ya kitu Fulani ukiwa ni kijana mtetezi waulize viongozi wa shirika wakueleze utaratibu wao wa kuwashirikisha vijana na pia uulize kama kuna vijana wengine wanaowakilisha shirika.Hakikisha kuwa hili ni eneo huru la kweli ambapo sauti yako itasikika.

Matumizi ya nguvu na shinikizo kutoka kwa watu wazimaMara nyingi vijana huambiwa washiriki kwenye matukio, mikutano au majadiliano ili kuwakilisha vijana wenzao. Hata hivyo, mara nyingi idadi ya watu wazima kwenye makusanyiko hayo huizidi idadi ya vijana.Hali hii inaweza kuwafanya watu wasiwe na

uhakika, washindwe kujiamini wakati wa kuzungumza, wahisi kama hawasikilizwi au kwamba watu wazima wanawapindua au kudharau mawazo yao. Ni muhimu kukumbuka kwamba ukiwa kijana una uhalali wa kuwawakilisha wenzako, kwamba umepewa nafasi hiyo kwa kuwa uko pale kuzungumza kwa ajili ya jamii yako na watu wengine ambao wanapitia hali kama ya kwako. Usijihisi kama watu wazima wanazuia mawazo yako au vitendo vyako. Unapofanya kazi na shirika toa mapendekezo kwao ili wawashirikishe vijana zaidi ya mmoja, na waeleze jinsi wanavyothibiti matumizi mabovu ya nguvu na kutokuwa na urari na jinsi wanavyohakikisha kuwa vijana wanatoa ushiriki wenye tija.

“Baadhi ya vijana wanatumiwa kama vibaraka na watu

wanaosema ukweli wanaweza kuachwa

kutumika …. (kwenye kazi ya utetezi).”

MTETEZI KIJANA

“Ni lazima niwe hodari, mar a

zote nitasema kile ninachotaka

kusema.”

MTETEZI KIJANA

Page 14: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

14 | KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU

Sema kwa niaba ya wengineUnapopatiwa nafasi na jukwaa la kuzungumzia kuhusu mambo ambayo ni kipaumbele chako, kumbuka kwamba unawawakilisha wengine, watu wenye matarajio na hamu kama yako na pengine watu wanaotaka uwashirikishe uzoefu wako. Kusanya taarifa na maoni kutoka kwa watu hawa ili kuhakikisha una taarifa za kutosha na kwamba wanakuunga mkono katika jukumu hili.

Tambua mipaka yakoSote tuna mipaka, mambo ambayo hatupo tayari kujadili hadharani, mambo ambayo hayapendezi kufanywa. Mambo haya yanaweza kuwa ni pamoja na yale ambayo hutaki kuyasema- hali yako ya VVU, maisha yako binafsi, siasa, dini? Au inaweza kuwa mpaka wa wazi kwa shirika utakalofanya nalo kazi – vyama vya siasa, mashirika ya dini, makampuni ya dawa. Unaweza pia kuwa na mipaka kama vile kutokuwepo kwenye safu ya uongozi labda kuwe na zaidi ya kijana mmoja, safu yenye watu wa jinsia zote na uwakilishi wa umri au rika au kuhusu malipo ya mshahara au msaada unaopewa. Jaribu kufikiri kwa makini kuhusu mipaka yako na uisimamie.

Rahisisha mamboUkiwa mtu unayefanya kazi vizuri ni dhahiri watu watakuhitaji. Mtu aliye na shauku, mwenye mvuto na anayeweza kujieleza vizuri bila shaka ataombwa kuhudhuria mikutano na makongamano yote. Kumbuka kujiuliza maswali ambayo ulijiuliza wakati ukitafakari kuhusu mambo muhimu yanayokuhusu. Usipokee fursa yoyote kwa sababu utasafiri au kuzungumza. Kumbuka kuwa na uhalisi wako na kuzungumza mambo unayoyafahamu na kuyaelewa. Kuna watu wengine ambao wanaweza kuchukua fursa hiyo.

Page 15: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU | 15

Wajue wapinzani wakoUkiwa kama mtetezi bado unaweza kujifunga na mambo yako na hoja zako mwenyewe. Wewe unaweza kuona kama katika jambo Fulani kuna jibu moja tu lakini watu wengine wakaona kwamba huo sio ukweli. Jifunze kuelewa mawazo kinzani, jifunze kuzielewa hoja za wengine, ili ujiandae vizuri kutetea hoja zako na kukubali hoja zako kupingwa na mtazamo wako utakuwa imara zaidi.

JitunzeKufanya kazi ya utetezi kunaweza kuonekana kama vile hakuna kazi yoyote inayofanyika. Shauku yako kwa mambo Fulani, kujitoa kwako katika kupinga uonevu kunaweza kukufanya ujisahau mwenyewe na usahau mahitaji yako pia. Hakikisha unakuwa na muda wa kupumzika, kula vizuri na kutafuta watu wa kuzungumza nao, kuwashirikisha katika mambo yako makubwa na madogo na kupokea msaada kutoka kwao. Kazi ya utetezi ni muhimu sana kwa hiyo unatakiwa kuwa katika hali nzuri wakati wote na katika hili kuna wakati unatakiwa kupumzika.

Page 16: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

Mshauri ni mtu anayeweza kukuongoza na kukusaida kujifunza. Washauri hutoa uzoefu wao, huuliza maswali yanayoweza kukufanya ufikiri kwa makini na undani zaidi na kukuchagisha ukue kwa kuthubutu kujaribu mambo mapya na magumu. Washauri wanaweza kutoa msaada mkubwa na msukumo na bado wanapata fursa ya ajabu ya kufanya kazi na wewe pamoja na kujifunza baadhi ya mambo kutoka kwako. Kuna wakati unaweza kuwa mshauri kwa watetezi vijana na kuwashirikisha uzoefu wako na kuwashauri.

“Ulimwengu huu unadai sifa za vijana: sio muda mtu alioishi bali ubora wa akili, hasira ya kutimiza matakwa, ubora wa

mawazo, kuonesha ujasiri dhidi ya woga, hamu ya kupenda

matukio dhidi ya vitu rahisi.”

ROBERT KENNEDY

16 | KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU

Tafuta mshauri

Page 17: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU | 17

Kuna machapisho mengi yanayopatikana ambayo yanaweza kukusaidia kupanga kazi yako ya utetezi hatua kwa hatua. Rejea kuhusu machapisho hayo yameambatanishwa mwishoni mwa kijitabu hiki.

Shirikisho la Kimataifa la Uzazi salama liliandaa nyenzo rahisi yenye hatua 7 ambayo inaweza kuwa yenye manufaa. Pitia kwa makini hatua hizi moja baada ya nyingine.

1. Nini kinachotakiwa kubadilishwa?

2. Nani anaweza kufanya mabadikiko yatokee

3. Ninawezaje kushawishi ili malengo yangu ya utetezi yasaidie kufanya mabadiliko?

4. Nitahakikishaje ushiriki wenye tija wa vijana?

5. Nitashirikiana na nani kufanya kazi hii?

6. Ni vizuizi vipi nitakavyokabiliana navyo? Nitavishindaje vizuizi na hatari zitakazonikabili?

7. Nitafuatiliaje na kupima ubora wa kazi yangu ya utetezi ili kuhakikisha kuna mafanikio?

Unaweza kujifunza zaidi kuhusu hatua hizi kwenye kitabu kiitwacho, ‘Want to change the world? Here’s how …’ (Unataka kuubadili Ulimwengu? Hivi ndivyo…), chenye nyenzo zinazoshirikisha maandalizi, vitu muhimu na mikakati kwa makundi mbalimbali ya watu: www.ippf.org/resource/want-change-world-heres-how-young-people-advocates

Jinsi ya kufanya utetezi

Page 18: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

18 | KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU

●● Ukilenga eneo dogo au ukitaalamisha utakuwa na mafanikio. Watu watapenda kujua mawazo yako na kusikia unachotaka kusema. Usijaribu kuwa mtalaamu wa kila kitu.

●● Ongea na watu wengine ili ujue mada muhimu zilizopo, zungumza na vijana wenzako na ufanye kazi kwa bidii ili uwe mbele ya wengine kwenye jambo unalotaka kusimamia. Kwa mfano, ukiwa kama mtetezi wa vijana hakikisha una taarifa mpya kabisa kuhusu teknolojia mpya za kukabiliana na VVU na fikiria jinsi teknolojia hizo zitakavyowanufaisha vijana wanaoishi na VVU.

●● Ufahamu muktadha wako na jinsi masuala ya kimataifa yanavyoigusa jamii yako. Pengine hii ni njia mpya ya kukabiliana na mambo au ni sera mpya. Hii itamaanisha nini kwenye muktadha wako? Unaweza kuwasaidia watu wakubali kutumia njia mpya au sera mpya kwa kutumia uzoefu wako?

●● Usipitwe na mambo mapya, usikubali ujumbe wako udharaulike (au uonekane kama uliopitwa na wakati). Watu wakikusikia ukirudia kusema mambo yale yale waliyoyazoea wataacha kukusikiliza.

●● Elewa sera za kimataifa ambazo zinaweza kukusaidia, elewa kuhusu haki za vijana na haki za watu wanaoishi na VVU.

Kuwa na hamu na shauku kunaweza kukufanya kuwa mtetezi mwenye nguvu. Kujali sana kuhusu jambo Fulani au kuhamasika na jambo fulani kunakusaidia kujifunza zaidi na kunakuchochea kuendelea na kazi yako. Unapochagua eneo la kutetea tafakari ujue kitu mahsusi unachokipenda na eneo unalotaka kujijengea utaalamu zaidi.

Chaguo langu

Page 19: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU | 19

Ni muhimu kwamba ujumbe wako uwe na ushahidi usio na mashaka, usiwe wa muda mrefu na uwe sahihi. Kuweza kuwasilisha masuala mubashara kupitia kwenye simulizi na mifano halisi ya maisha ni jambo lenye manufaa makubwa. Ukiwa kama mtetezi kumbuka kwamba unawawakilisha wengine. Hakikisha wengine wanafurahia ujumbe wako na kwamba kupitia ujumbe huo wanatafakari maisha yao. Ujaribishe ujumbe wako kwa watu na uhakikishe ujumbe unaeleweka na maudhui yake yanatekelezeka.

Kupangilia ujumbe wangu

“Usipige kelele, boresha hoja zako.”

DESMOND TUTU

Page 20: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

Hakikisha ushiriki wako katika kazi ya utetezi una lengo zuri na sio kwamba unatumiwa kama kibaraka. Mtazamo wa sasa kwa vijana kuhusu mwitikio wa VVU umemaanisha kuongezeka kwa uhitaji mkubwa wa vijana katika kuwakilisha mashirika, kushiriki kwenye mikutano na programu. Hakikisha unafanya kazi na watu unaowaheshimu na wenye mtazamo unaofanana na wa kwako. Unaweza ukapokea mialiko mingi lakini fikiri kwanza ili ujue ni nani wa kufanya naye kazi.

Ili kujua kama hili ni shirika sahihi la kufanya nalo kazi, zielewe kazi wanazofanya, waulize watu wengine wakupe taarifa zao.

●● Ni shirika linaloheshimika?

●● Kazi zake zinasababisha mabadiliko ?

●● Linawashirikisha vijana katika utendaji wa kazi zake?

●● Watetezi vijana wanasemaje kuhusu shirika hili?

●● Kufanya nao kazi kunaweza kunisaidia kujifunza, kukuza ujuzi wangu na kulisaidia shirika langu?

●● Vijana na wafanyakazi wenzangu wanayo thamini ya kazi ninayofanya?

●● Unaulizwa masuala na maamuzi ambayo unahisi unaweza kutoa mchango wenye tija?

Ni nani wa kufanya naye kazi?

20 | KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU

“Usikubali mambo yenye utata

yakakukwamisha. Kuweni wanaharakati. Shughulika

na vitu visivyopatikana kwa wingi. Itakuwa ni

moja ya buzoefu mkubwa utakaoupata maishani

mwako.”

BILL GATES

Page 21: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

Kulielewa shirika vizuri na kuelewa aina ya watu wanaofanya nalo kazi ni jambo la muhimu .

●● Msimamo wao, maadili yao na mbinu wanazotumia ni zipi?

●● Unataka kudumisha mawasiliano nao kwa muda mrefu?

●● Mikakati yao inakufurahisha?

●● Wamekufafanulia mambo vizuri?

●● Waulize maswali kuhusu jukumu lako. Utafanya nini, watakupa msaada gani, watafuatiliaje ufanisi wa jukumu lako?

●● Wanafanya mambo gani kwa ajili ya vijana?

Kuna machapisho unayoweza kusoma ambayo yanakuelekeza jinsi ya kukusanya ushahidi wako, jinsi ya kufanya uchambuzi wa hali, mambo muhimu ya kutarajia unapoingia katika ubia na nyenzo za kukusanya ushahidi.

Kijitabu hiki kimeandaliwa kwa kuzingatia uzoefu wa vijana ambao ni wanachama wa mtandao wa Y+ wanaofanya kazi kama Watetezi. World Health Organization pia lilichangia hoja zenye nguvu kutokana na uzoefu wa vijana zikieleza jinsi ya kufanya kazi za utetezi na serikali ili kuzihamasisha serikali

kufanya kazi na vijana: WHO (2017) ‘Advocating for Change for Adolescents!’ (Kutetea mabadiliko kwa vijana waliofikia balehe! Mwongozo wa Vitendo kwa ajili ya vijana waliofikia balehe ili kutetea maboresho katika afya na ustawi): www.who.int/pmnch/knowledge/publications/advocacy_toolkit.pdf

“Kila wakati ni fursa ya kujiandaa, kila mtu ni mwanaharakati mtarajiwa,

kila dakika ni nafasi ya kuubadili ulimwengu.”

DOLORES HUERTA

KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU | 21

Advocating for Change for Adolescents!A Practical Toolkit for Young People to Advocate for Improved Adolescent Health and Well-being

May 2017

Page 22: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

22 | KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU

●● Taja tukio unalotaka kuhudhuria na utoe sababu. Hakikisha unafuatilia mambo yaliyojiri hadi kufikia kuandaliwa kwa tukio hilo ili upate ufahamu wa jambo unalokwenda kuzungumzia.

●● Kuwa mwaminifu kila mara. Onesha utaalam wako katika eneo unalozungumzia na uwathibitishie maafisa wanaosimamia tukio kwamba unajua unachokizungumza.

●● Ukikutana na mmoja wa maafisa wa serikali yako kwenye tukio lolote, jitambulishe, omba kupata mawasiliano kwa undani na wafuatilie maafisa husika baada ya tukio ili kujenga mahusiano mazuri nao.

●● Toa kauli thabiti zikifuatiwa na ushahidi ili kuonesha kwamba wewe ni mtaalamu katika eneo lako.

●● Wasiliana na kutoa mrejesho kwenye shirika jingine linalofanya kazi zinazofanana na zako na kwa idara ya serikali kwenye masuala maalum; mawasiliano haya yataboresha uaminifu wako.

●● Shauriana na vijana wengine unaofanya nao kazi na hakikisha una mamlaka ya kuzungumza kwa niaba yao. Kuzungumza kwa niaba ya kundi kubwa la watu kunaongeza ushawishi kwenye kazi yako ya utetezi.

●● Shirikiana na mashirika ya Kijamii ili wakupe mamlaka ya kuzungumza kwa niaba yao. Jenga ushirikiano na mashirika yenye vipaumbele tofauti na shirika lako lakini ambayo mamlaka yake yanaingiliana au kufungamana na shirika lako.

●● Fahamu vipaumbele vya serikali na jinsi ya kuvifungamanisha na maswali yako.

●● Tumia diplomasia ya uchochezi , pongeza serikali yako kwa kazi nzuri inazofanya na toa mapendekezo chanya kwa changamoto ambazo hazijatatuliwa.

●● Waheshimu watu wote unaokutana nao na kuwaonesha adabu.

●● Kuwa wazi kama , kwa mfano, una mawasiliano na ofisi ya balozi iliyopo New York.

●● Fuatilia, fuatilia na ufuatilie kwa njia zozote zinazowezekana.

●● Kuwa tayari kujibu. Unaweza kutakiwa kuchangia jambo kwa haraka bila kupewa muda wa kutosha kujiandaa.

●● Kuwa tayari kufanya zaidi ya matarajio yako.

WHO (2017) ‘Advocating for Change for Adolescents!’

Page 23: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

Ukiwa ni mtetezi kijana unaweza kupewa jukwaa ili uzungumze au nafasi kwenye vyombo vya habari ili uiwakilishe jamii yako. Jinsi utakavyozungumza na unavyoonekana mbele ya watu ni jambo la muhimu sana. Una nafasi ya kuwa mfano wa kuigwa kwa vijana wengine wanaoishi na VVU kwa jinsi unavyofanya kazi na watu wengine na mtazamo wako katika kazi ya utetezi.

Kumbuka jinsi ilivyo muhimu kuwa katika uhalisia katika kila jambo unalofanya. Waoneshe vijana wengine jinsi unavyofanya kazi kwa uaminifu na uwazi na jinsi unavyofanya chaguzi za aina ya kazi unazotaka kufanya na watu unaofanya nao kazi. Baadhi ya watetezi vijana wanavutiwa na fursa , tuzo za fedha, mwonekano, au kusafiri nje ya nchi. Fikiri uamue sababu zinazokufanya ufanye kazi hii na utafakari jinsi watu wengine watakavyokuona.

Kuwa mshauri wa wengine. Mara nyingi vijana walewale ndiyo wanaotakiwa kuzungumza au kushiriki katika matukio. Mashirika hupenda kuchagua watu wanaowafahamu na kuwamini. Wasaidie vijana wengine wafikie ngazi uliyofikia wewe, wapendekeze,wape rejea, washauri, na wasaidie ili wapate fursa nyingi na kuweka msingi wa kazi za utetezi kwa ajili ya kizazi kijacho. Kuna wakati muda wa ujana utapita na ni muhimu ukaweza kung’atuka na kuwaachia vijana wa wakati huo kuendeleza kazi ya utetezi. Unaweza kuendelea kuwasaidia vijana katika kazi ambayo unaipenda ukiwa kama mshauri.

KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU | 23

Kuwa mfano wa Kuigwa

Page 24: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

Mwongozo ufuatao hapa chini unatoa mchango wa mawazo mazuri ya njia za kupima mafanikio ya kazi yako ya utetezi. Zipo nyenzo na njia za kufuatilia mafanikio uliyofikia. Unaweza kutumia njia nyingine unazozijua kufahamu kama unafanya vizuri au la.

Upimaji wa mafanikio yako

24 | KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU

●● Kuna baadhi ya watu walishawahi kukuambia

ufanye kitu Fulani kwa mara ya pili?

Walihamasika na kukuamini kiasi cha kutaka

ufanye nao kazi tena?

●● Unatumia mitandao ya kijamii? Unaanzisha

mada na mijadala kuhusu mambo Fulani?

●● Unaona mabadiliko yakitokea katika mambo

unayoyaweka maanani? Kuna dalili za

mafanikio?

●● Unatambulika kwa utaalamu wako katika

eneo ambalo una uzoefu nalo?

Weka kumbukumbu ya shughuli zako na namba za mawasiliano, tunza kumbukumbu za mawasiliano yako ili zikusaidie kufuatilia mafanikio yako.

Page 25: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

“Usikate tama ya kuacha kufanya kitu

unachopenda kufanya. Mahali penye upendo na

hamasa sidhani kama unaweza kukosea.”

ELLA FITZGERALD

KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU | 25

Kuwa mtetezi ni jukumu zito ambapo unaweza kusababisha mabadiliko halisi. Uzoefu wako na ujuzi wa masuala unaweza kubadili mioyo na akili. Una fursa ya kupaza sauti kwa niaba ya wengine ambao hawawezi kupata fursa hiyo pia. Au ukapaza sauti kwa niaba ya watu wanaodharaulika au ambao hawajisikii vizuri kuzungumza. Unawajibika katika jukumu hili na ndiyo maana kutafakari kwa kina kujua wajibu wako kama mtetezi na masuala ambayo unayasimamia ili kupata matokeo mazuri ni jambo la muhimu sana. Ni muhimu pia ukawa na uhakika kama wewe ni mtu bora kwa jamii unayoiwakilisha, una uhalali au kuna mtu bora zaidi anayeweza kufanya kazi yako? Umefanya utafiti na kuyaelewa vizuri masuala unayotaka yabadilike? Una ushahidi ? Una ujuzi wa kisasa? Umeshauliza watu wengine kukushirikisha mawazo na maoni yao?

Ubunifu, nguvu na shauku ambazo vijana wanaleta kwenye sekta ya VVU na kwenye utetezi kwa pamoja vinaweza kuleta mabadiliko makubwa. Kuwa sehemu ya mabadiliko!

Majumuisho

Page 26: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

26 | KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU

Rejea

GNP+ (2012) GIYPA Roadmap: supporting young people living with HIV to be meaningfully involved in the HIV response (Mwongozo wa ushiriki wa kina kwa vijana wanaoishi na VVU: kuwasaidia vijana wanaoishi na VVU kujihusisha kikamilifu kwenye mwitikio wa VVU)

Kila sura katika mwongozo huu inazungumzia moja ya hatua kuelekea ushiriki wa kina kwa vijana wanaoishi na VVU: 1. Kuelewa maana ya mwitikio wa VVU 2. Kutafuta sababu nzuri za kujihusisha 3. Kuunganisha ushiriki wako na wa shirika lako 4. Kuendeleza na kukuza ushiriki wako 5. Kuona matokeo ya afya bora, heshima na Kinga. www.gnpplus.net/resources/giypa-roadmap/

IPPF (2011) What to change the world? Here’s how … Young people as advocates, your action for change toolkit (Unataka kubadili dunia? Tazama jinsi ya kufanya hivyo: Kijana kama mtetezi, Nyenzo yako ya hatua za mabadiliko)

Nyenzo hii ni kwa ajili ya wanaharakati vijana, wanafunzi na mawakala wa mabadiliko. Inatoa mwongozo wa njia za kupanga, kutekeleza au kuboresha ari ya utetezi kwa haki na afya ya uzazi ya vijana. www.ippf.org/resource/want-change-world-heres-how-young-people-advocates

WHO (2017) Advocating for change for adolescents! A practical toolkit for young people to advocate for improved adolescent health and well-being (Kutetea mabadiliko kwa vijana waliofikia balehe! Nyenzo ya vitendo kwa ajili ya vijana kuwasaidia kuboresha afya na ustawi)

Nyenzo hii iliandaliwa na vijana , kwa ajili ya vijana, ili itumike na mitandao inayoongozwa na vijana na mashirika ambamo vijana wanafanya kazi ili kuibadili dunia kwa kutumia mikakati ya pamoja ya Ushirika kwa ajili ya Mama, Watoto wachanga na Afya ya Watoto na Akina mama waliojifungua. Lengo la nyenzo hii ni kusimamia upangaji,utekelezaji na ufuatiliaji wa mwongozo wa kitaifa wa utekelezaji wenye ufanisi ili kusababisha mabadiliko mahsusi ya sera za kuboresha afya na ustawi wa vijana waliofikia balehe. www.who.int/pmnch/knowledge/publications/advocacy_toolkit.pdf

Page 27: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

“Usikatishwe tamaa kwa kuwa

mwanaharakati kwa sababu watu

wanakuambia kwamba hutafanikiwa

katika malengo yako. Tayari

umeshafanikiwa ikiwa umejitoa

kuwakilisha upatikanaji wa haki au

ukweli au huruma au usawa au upendo.”

DORIS HADDOCK

ATHENA/ GYCA (2015) Vision and Voices (Maono na Sauti)

Vichapisho vya maono na sauti vilitengenezwa na Muungano wa Kimataifa wa Vijana wanaohusika na VVU/ UKIMWI ( GYCA) na Mtandao wa ATHENA kama sehemu ya program ya Kuunganisha. Maelezo yake yamechukuliwa kutokana na ushauri uliopatikana kutoka kwenye mijadala ya kijamii na vikundi maalum vyenye vijana wanaoishi na ambao wameathirika na VVU kutoka Ethiopia, Uganda, Burundi, Bangladesh na Myanmar. www.aidsalliance.org/resources/481-voices-visions-and-priorities

Page 28: kwa utetezi - yplusnetwork.org · wengine ushuhuda wangu? o ninaotaka kuwashirikisha? e e mtandao wa intaneti ? otaka kuwashirikisha wengine? Labda baadhi tu ya historia yangu au

28 | KUWA TAYARI kwa utetezi: Mwongozo kwa vijana wanaoishi na VVU

“Zawadi bora kuliko zote ambayo maisha yanaweza

kumpa mtu ni kumpata fursa ya kufanya kazi

yenye staha, na kuifanya kazi hiyo kwa bidii.”

THEODORE ROOSEVELT

Y+ ni mtandao wa , na kwa ajili ya watu wanaoishi na VVU.

Tupo katika lengo la kuhakikisha kuwa vijana wanaoishi na VVU wanaweza kuchangia katika mwitikio wa VVU.

Tupo tayari kufanya na kushawishi maamuzi chanya yanayoathiri maisha yetu . Wewe je? Unaweza kuungana nasi kupitia sauti za Y+ kwa kutembelea anuani ya www.yplusnetwork.org/blog/ na kufuatana nasi kwenye:

www.yplusnetwork.org

www.facebook.com/YplusNetwork/ https://twitter.com/Yplus_network

www.instagram.com/yplusnetwork/

Mwongozo

kwa vijana wanaoishi na VVUkwa utetezi

KUWA TAYARI