kuna tatizo la ujifunzaji duniani kutafuta ......kuna tatizo la ujifunzaji duniani licha ya...
TRANSCRIPT
WITO WA KUCHUKUA HATU
Ndani ya miaka kumi iliyopita, familia inayoongezeka ya
mashirika ya kiraia imeanzisha tathmini kubwa ya ujuzi
wa watoto kusoma na kuhesabu inayofanyika kwenye
kaya katika nchi tisa barani Asia, Afrika, na Amerika ya
Kusini.
Tofauti na tathmini nyingine kubwa zinazopima matokeo
ya kujifunza, tathmini hizi zinafanyika kwenye kaya na
hufanywa na wananchi wa kawaida. Hii inawapa fursa
watu mbalimbali pamoja na wazazi, kujionea wenyewe
nini watoto wao wanaweza kufanya. Upimaji wa ujuzi
wa watoto kwenye kaya unasaidia kutathmini watoto
WOTE, waliopo nyumbani siku ya utafiti siyo wale tu
walioko shuleni.
Tunaamini kwamba hii ni njia pekee ya kujua kama
watoto WOTE wanapata stadi za msingi za kusoma
na kuhesabu, ambazo huweka msingi muhimu wa
maendeleo ya mtoto shuleni hapo baadaye. Pia ni njia
muafaka ya kuwashirikisha watu wengi kufikiria kwa
pamoja kuhusu ubora wa elimu. Ni pale tu watu wengi
wanapoona kuna tatizo ndipo ufumbuzi unaweza
kupatikana.
KUNA TATIZO LA UJIFUNZAJI DUNIANI Licha ya kuongezeka kwa uandikishaji, takriban watoto milioni 250 hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu, hata
kama wameandikishwa na wanakwenda shule. Duniani kote, vijana wadogo milioni 200 humaliza shule bila kuwa
na stadi za msingi wanazohitaji kufanikiwa maishani.
KUTAFUTA UFUMBUZI WA TATIZO HILI HUANZA NA KULIELEWA TATIZO LENYEWE
1 Hufanywa kwenye kaya, siyo shuleni. Kama lengo
ni kutoa elimu kwa watoto WOTE, basi ni lazima
tathmini ihakikishe kuwa watoto wote wanawakilishwa
kwenye sampuli. Katika nchi nyingi zinazoendelea, hili
haliwezekani kama tathmini inafanyika shuleni.
2 Hufanywa kwa mazungumzo ya mdomo, mtu mmoja
kwa kila mtoto. Matokeo ya tafiti za zamani huficha
ukweli kwamba watoto wengi hawawezi kusoma.
Kuwapima watoto kwa kuhojiana, mtoto mmoja baada
ya mwingine ni njia pekee ya kutambua kama mtoto
anaweza kusoma.
3 Hutumia zana rahisi ambazo ni rahisi kuzitumia. Mara
nyingi tatizo la matokeo duni ya kujifunza halionekani
dhahri. Tathmini hizi huwawezesha wazazi, walimu, na
watu wa kawaida kuelewa matokeo na kuwa sehemu ya
mchakato. Ni pale tu watu wengi wanapoona kuna tatizo
ndipo, ufumbuzi unaweza kujadiliwa na kutekelezwa.
4 Huyafikia maeneo mengi makubwa, ili matokeo yawe
na uwakilishi wa kitaifa na kimkoa. Kukadiria ukubwa
wa eneo la kufikia na mtawanyiko wa tatizo ni muhimu
sana katika kubuni ufumbuzi mwafaka.
TATHMINI ZINAZOFANYIKA KWENYE KAYA
JIUNGE NA HARAKATI HIZINina amini kwamba tathmini zinazofanyika kwenye kaya ni njia pekee ya kupima kujifunza kwa watoto wote.
Ungana nasi kwa kusaini Wito wa Kuchukua Hatua kupitia www.palnetwork.org AU tuma jina lako, shirika na nembo ya shirika lako kwa Hannah-May Wilson kupitia [email protected]
WWW.PALNETWORK.ORG