annuur 1179.pdf

20
ISSN 0856 - 3861 Na. 1179 SHAABAN 1436, IJUMAA , MEI 29-JUNI 4, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu facebook: [email protected] AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST Wasiwasi watanda.... Shule za Kiislamu kufutwa Kundecha awataka Waislam kuwa macho Je, ni kufanyia kazi wasiwasi wa Mungai? Kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda inatisha! Mh. Selasini katimiza wajibu wake Ukristo wake, haukubali mambo hayo Siku zitakapodhihirishwa Siri Kila Mchunga ataulizwa… SHEIKH Msellem. Soma Uk. 20 RAIS Dkt. Shein. Waziri Mkuu Pinda. RAIS Kikwete. Apania kuua Waislamu kijiji kizima lakini… Hajashitakiwa kwa tuhuma za ugaidi Hata katika ule utaratibu wetu wa kawaida… Waliokamatwa Arusha walikuwa Waarabu Mheshimiwa Mbunge alikosea… Askofu ‘hawezi kuwa gaidi’! Uk. 10 Allah Ameonya mwenye kwenda kuhiji asivunjiwe heshima, yaani atukuzwe(Al-Maaidah:2). Kwa mapenzi ya Allah, huyu amepewa cheo maalum cha "Al-Hajj au HAJJAT". Waislamu hatuna budi tuipende sana Hijja Muda unakwisha! Gharama zote kwa Hijja ni Dola 4,500. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,300. Karibuni Ahlu Sunna Wal Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0765462022;0782804480; 0717224437. Zanzibar:0777468018;0777458075;0777845010. (11) "MWENYE KUHIJI" NI KIPENZI CHA ALLAH!

Upload: annurtanzania

Post on 08-Nov-2015

1.110 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • ISSN 0856 - 3861 Na. 1179 SHAABAN 1436, IJUMAA , MEI 29-JUNI 4, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

    Sauti ya Waislamufacebook: [email protected]

    AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST

    Wasiwasi watanda....

    Shule za Kiislamu kufutwaKundecha awataka Waislam kuwa machoJe, ni kufanyia kazi wasiwasi wa Mungai? Kauli ya Waziri Mkuu

    Mizengo Pinda inatisha!Mh. Selasini katimiza wajibu wakeUkristo wake, haukubali mambo hayo

    Siku zitakapodhihirishwa SiriKila Mchunga ataulizwa

    SHEIKH Msellem.

    Soma Uk. 20

    RAIS Dkt. Shein.

    Waziri Mkuu Pinda. RAIS Kikwete.

    Apania kuua Waislamu kijiji kizima lakiniHajashitakiwa kwa tuhuma za ugaidiHata katika ule utaratibu wetu wa kawaidaWaliokamatwa Arusha walikuwa Waarabu

    Mheshimiwa Mbunge alikosea

    Askofu hawezi kuwa gaidi!Uk. 10

    Allah Ameonya mwenye kwenda kuhiji asivunjiwe heshima, yaani atukuzwe(Al-Maaidah:2). Kwa mapenzi ya Allah, huyu amepewa cheo maalum cha "Al-Hajj au HAJJAT". Waislamu hatuna budi tuipende sana Hijja Muda unakwisha! Gharama zote kwa Hijja ni Dola 4,500. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,300. Karibuni Ahlu Sunna Wal Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0765462022;0782804480; 0717224437.Zanzibar:0777468018;0777458075;0777845010.

    (11) "MWENYE KUHIJI" NI KIPENZI CHA ALLAH!

  • 2 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 29- JUNI 4, 2015AN-NUUR

    S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.

    www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected] zetu zipo: Manzese Tip Top

    Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

    Tahariri/Habari

    Kauli ya Waziri Mkuu Pinda inakatisha tamaaK WA h a k i k a k i l a aliyesikiliza swali na Mbunge wa Mji Mkongwe ( C U F ) , M u h a m m e d I b r a h i m S a n ya k wa M h e s h i m i wa Wa z i r i Mkuu wiki iliyopita na utangulizi wa Waziri Mkuu katika jibu lake, lazima atajiuliza maswali mengi ambayo hayana majibu.

    Swali la Mh. Sanya lilikuwa wazi sana na lenye kugusa suala zito la kuvunjwa haki za kiraia, kisheria na kikatiba, za Masheikh wanaoshikiliwa kwa zaidi ya mwaka sasa kwa tuhuma za ugaidi. Baada ya kutoa maelezo marefu na kuuliza swali, bado Mh. Sanya alitakiwa na Mheshimiwa Spika kufafanua zaidi alikuwa akikusudia watuhumiwa g a n i a m b a p o S a n y a alisema wazi kuwa, hao ni Masheikh wa UAMSHO wa n a o s h i k i l i wa k wa tuhuma za ugaidi.

    Sasa sikiliza j ibu la Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda:

    Mheshimiwa Spika, ni bahati mbaya tu kwamba swali halipo wazi sana, i l i tuweze kujua hasa k inachota futwa n in i . Ningeshukuru sana kama ningejua Masheikh hawa nani , wanatuhumiwa kwa makosa yapi , na pengine kwa sasa wapo katika hatua ya upepelezi, w a m e s h a f i k i s h w a mahakamani, ili niweze kuwa na uhakika kwamba kinachotafutwa hapa ni katika stage (hatua) gani ya mchakato katika suala hilo ambalo linawakabili.

    Si mara ya kwanza suala la Masheikh hawa k u f i k i s h wa B u n g e n i Dodoma. Lishazungumzwa s a n a w a h e s h i m i w a Wabunge wakihoji mambo ya msingi kuhusiana na watuhumiwa hao. Na mambo yanayohojiwa ni manne. Moja, ni madai ya watuhumiwa hao kuwa

    walifanyiwa vitendo vya kinyama na kudhalilisha, kinyume kabisa na sheria, katiba, haki za binadamu, na ubinadamu wenyewe. Pili, kunyimwa matibabu stahiki baada ya kuumizwa walipofanyiwa ukatili huo. Tatu, kushikiliwa kwa muda mrefu bila kesi yao kuzungumzwa huku wakinyimwa haki ya dhamana. Nne, wanahoji, k wa n i n i wa k a m a t we na kuletwa mahakama za Tanzania Bara wakati Zanzibar ni nchi na ina mahakama zake.

    Wiki hii, wakati Bunge hili la Katiba likiendelea, Mbunge wa Viti Maalum ( C H A D E M A ) M h . Maryam Salum Msabaha alizungumzia suala hili hili na hoja ni hizi hizi. Kwamba kama watu wana kesi ya kujibu, si izungumzwe basi kama ushahidi upo utolewe ijulikane moja kuwa wamehukumiwa?

    Katika madai haya ya kufanyiwa vitendo vya kinyama na kudhalilisha, yaliwahi kutolewa majibu na maelezo ya kejeli na kwa hakika ya dharau, jeuri na kibri ndani ya Bunge. Ikidaiwa kuwa utafanyika uchunguzi isi je kuwa wanaodai kudhalilishwa, w a l i c h o f a n y i w a n i kamchezo walikozoeya!

    Sasa leo tena, baada ya maelezo marefu ya M h e s h i m i w a S a n y a , Waziri Mkuu anasema, hajui ni Masheikh gani, w a n a t u h u m i w a k w a makosa yapi na hajui nini kinatafutwa! Kwa hakika hii inakatisha tamaa kabisa.

    W a p o w a b u n g e , wanasheria, wasomi na wananchi wa kawaida, a m b a o w a m e k u w a wakihoji kwamba, kama Zanzibar ni nchi, kwa nini Masheikh wakamatwe kimya kimya na kupelekwa Bara? Imekuwa kama zile Rendition za Marekani (Extraordinary rendition / irregular rendition- the government sponsored

    k i d n a p p i n g a n d extrajudicial transfer of a person from one country to another).

    Lakini pia wanahoji, hata kama wanatuhumiwa kwa shutuma nzito kama h iyo ya uga id i , kwa nini wadhalilishwe na kufanyiwa vitendo vya ki-firauni kama wenyewe walivyodai kufanyiwa n a k u t o a u s h a h i d i mahakamani?

    Hata hivyo, la kusikitisha na kushangaza kabisa ni kuwa, pamoja na kilio cha watuhumiwa hao, pamoja na hoja za wananchi, pamoja na ushahidi wa kutisha unaowasilishwa

    mahakamani ukionyesha hali mbaya za watuhumiwa hao kutokana na vitendo walivyofanyiwa, wenye r a i a wa o k i m ya a a ! ! ! Wenye wapiga kura wao ambao wanawataraj ia Wazanzibari na Waislamu wafuasi wa Masheikh hao, wawapigie kura mwaka huu wabaki Ikulu au wenye tamaa ya kuingia, waingie, kimyaa!!!

    F a r a j a p e k e e k w a Masheikh wetu hawa imebaki katika Imani yao kwamba ipo SIKU ya Hukumu. Yupo Hakimu wa M a h a k i m u A l i ye Muadilifu. Na Yupo Maliki yaumiddiin.

    Lakini tukumbushe tu jambo moja na hii ni kwa mujibu ya amri ya Fadhakkir.

    Sisi sote ni wachunga. Na kila mchunga ataulizwa kwa vile alivyovichunga.

    Raha ya mamlaka haiishii tu kwa kukimbizwa na vingora huku wengine wakipisha njia wewe peke yako upite.

    Kuna na kuulizwa juu ya hawa wanaokupisha njia ukipitishwa mbio utadhani kila mtu unayemuona ni adui yako.

    Vipi uliwachunga. Vipi uliwatendea. Na siku hiyo, hakuna vingora vya kukupitisha mbio katika Siratwa.

    Na ambao uwapatao msiba husema: hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye tutarejea (2:156).

    H i v y o n d i v y o a l i v y o a n z a k u s e m a Sheikh Walid Alhad, Imamu Mkuu wa Msikiti wa Kichangani wakati akitoa taarifa za msiba wa ndugu yake Omary Alhad.

    Imam Alhad ambaye ni kaka wa marehemu, alisema mdogo wake Sheikh Omary alikuwa Muhadhiri wa Msikiti wa Kichangani, uliopo Magomeni jijini Dar es Salaam.

    Sheikh Omary alifariki siku ya Jumatano katika H o s p i t a l i y a Ta i f a Muhimbili jijini Dar es Saalam ambako alikuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda mrefu.

    Marehemu alizikwa Alhamisi wiki hii (jana) k a t i k a m a k a b u r i ya Mwinyi Mkuu Jijini Dar es salaam baada ya swala ya Alasir.

    Marehemu ameacha mjane na watoto wawili.

    Akielezea kwa ufupi wasifu wa mdogo wake, Sheikh Walid Alhad a l i s e m a m a r e h e m u alizaliwa mwaka 1970 jijini Dar es Salaam na kusoma shule ya msingi, Ilala Mchanganyiko Dar es Salaam, ambapo baadae alijiunga na shule ya sekondari ya al Haramain jijini ambako alihitimu kidato cha nne.

    Sheikh Omary Alhad hatunayeNa Azza Ally Ahmed

    Al-Marhum Sheikh Omary Alhad.

    Imam huyo alisema, Sheikh Alhad baadae alijiunga na hapo hapo Alharamain na masomo ya Dini.

    A i d h a , a l i s e m a Sheikh Omar Alhad, a l i t a f u t a e l i m u ya Dini na kupata darsa kwa Masheikh wengi, baadhi yao wakiwa ni baba yake mzazi Sheikh Alhad Omary, Sheikh Mohamed Ali Buhury na Sheikh Ahmed Khaidary.

    Hao ni baadhi tu ya Masheikh ambao walimpa elimu ya dini marhum Omary Alhad.

    Sheikh Omar Alhad katika harakati zake za kuhudumia jamii, alianzisha taasisi ya kusaidia kina mama na watoto mbalimbali wenye matatizo.

    S h e i k h W a l i d alisema mdogo wake hakuwahi kufanya kazi nyengine katika uhai wake isipokuwa kazi ya Daawa na kusaidia jamii hadi mwisho wa uhai

    wake. A l i k u w a n i

    mwanaharakati katika masuala ya dini na aliipenda kazi yake.

    Alijitoa kwa moyo wake wote kuitetea na kueneza dini ya Allah.

    Tumempoteza mtu muhimu sana miongoni mwa Wahadhiri walio kuwa na upeo mkubwa wa masuala ya dini.

    A l i s e m a S h e i k h Walid huku uso wake akionekana kujawa na huzuni kubwa.

    N a y e I m a m wa M a s j i d N u u r , Magomeni, Ustadh Amir Hangali, alisema alimfahamu Sheikh Omary Alhad kutokana na kujihusisha sana na kuitetea dini na weledi wake katika maswala ya dini.

    Alisema alikuwa ni mtu wa harakati na alikuwa Khatibu maarufu hasa katika Msikiti wa Kichangani.

    I m a m u h u y o aliwaasa Waislamu kujiandaa na siku ambayo ni lazima kila mtu aipitie katika maisha yake na kwamba mauti sio hiyari ni jambo la lazima kwa kila mtu.

    Alisema ni jambo jema kwa Waislamu kujenga mazoea ya kujiandaa na zawadi pekee ya kwenda nayo ni amali iliyo njema.

    A l i s e m a h i l o l i t a w e z e k a n a k w a Waislamu kuacha mambo ambayo hayampendezi Mwenyezi Mungu kwa safari hiyo.

  • 3 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 29- JUNI 4, 2015Habari

    Shule za Kiislamu kufutwaJ a m b o l a k u t i s h a zaidi linakuja, ndivyo walivyoambiwa Waislamu na Amir wa Shura ya Maimam na Baraza Kuu, Sheikh Mussa Kundecha.

    Jambo lenyewe ni kuwa upo mpango unakuja wa kufuta shule za Kidini au kuzifanya ziwe binafsi kwa maana ya kuwa zisajili wanafunzi wa dini zote.

    S h e i k h K u n d e c h a alitoa tahadhari hiyo kwa Waislamu katika kongamano lililofanyika k a t i k a M s i k i t i w a Magomeni, Kichangani, Ijumaa iliyopita.

    Ilikuwa ni baada ya kutoa taarifa juu ya kadhia ya kukamatwa ovyo Masheikh na Walimu wa Madrasa kwa kisingizio c h a k u p a m b a n a n a ugaidi, Sheikh Kundecha aliwataka Waislamu kukaa macho na kuwa makini kwani kuna balaa jingine linakuja.

    Hapo ndio akafichua kuwa, Shule za Kiislamu a m b a z o h u c h u k u a wanafunzi Waislamu pekee, (au zile za Kikristo a m b a z o h u c h u k u a Wakristo tu) huenda zisiwepo tena na wamiliki wake kutakiwa kuingiza watu wa dini nyingine.

    H a b a r i z a i d i zinafahamisha kuwa upo Muswada wa Sheria ya Elimu, ambapo hata kabla ya kupitishwa kuwa sheria, kuna baadhi ya taasisi za Kiislamu zimenyimwa usajili huku wahusika wakiambiwa kuwa hata waliokwishapewa leseni watanyanganywa.

    Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya vikao vya taasisi za Kiislamu v inavyoendelea h iv i sasa juu ya jambo hilo, baadhi ya maofisa wa Wizara ya E l imu na M a f u n z o ya U f u n d i wamefahamisha kuwa tayari yameshatolewa maelekezo kwa Wakaguzi wa El imu wa Mikoa kukusanya Leseni za Shule hizo za Kidini, ili zisajiliwe upya kama binafsi.

    Hata hivyo, baadhi ya Wakaguzi walioulizwa juu ya jambo hili, walisema kuwa bado hawajapata maelekezo yoyote.

    H a d i t u n a k w e n d a mitamboni, juhudi za mwandish i kumpata Afisa kutoka Ofisi ya Usajili, aliyedai kuwa lesen i z i takusanywa na mpya hazi tolewi , hazikufanikiwa.

    Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa taasisi za Kiislamu wamekiri kunyimwa leseni na kuambiwa kuwa hakuna s a b a b u y a k u p e w a wakati zoezi lililopo ni kukusanywa zilizokwisha kutolewa.

    Kwa uapnde mwingine,

    Na Mwandishi Wetu

    SHEIKH Kundecha akiongea Waislamu katika kongamano lililofanyika katika Msikiti wa Kichangani, Magomeni Jijini Dar es Salaam Ijumaa iliyopita.

    b a a d h i y a v i o n g o z i waliokuwa wakifuatilia suala hili na kufanya warsha wiki iliyoipita, wamearifu kuwa hoja zinazotolewa na baadhi ya watumishi katika ofisi ya Usajili ni kuwa zinazotakiwa ni seminari za watu wachache za kufundishia watu wa kutumikia makanisa au misikiti, sio kuwa na shule yenye wanafunzi zaidi ya 300 na wanaosoma masomo mengine zaidi ya yale ya dini husika ya kumfanya mwanafunzi kuwa Padiri au Sheikh.

    K w a m u j i b u w a Muswada wa Sheria ya El imu ul iopo mezani hivi sasa, ipo Mamlaka itakayoitwa Basic And Secondary Educat ion A u t h o r i t y a m b a y o i t a t a k i w a k u o n d o a vikwazo vote kwa mtoto yoyote kupata elimu bora.

    Kwa hiyo, kwa mujibu wa uchambuzi wa baadhi ya wataalamu walioupitia muswada huo, kama watu wataona shule yako ya Msikitini/Kanisani, ni Bora ila kipengele cha Dini kinamzuiya mtoto wa dini nyingine kusoma, basi Mamlaka hiyo, inaweza kuingilia kati kuondoa kikwazo hicho.

    Kama jambo hili litapita, itakuwa pigo jingine la karne kwa Wais lamu katika zile jitihada zao za kujikwamua kielimu.

    I l ikuwa wakat i wa ukoloni ambapo kutokana na wakoloni kufungamana na Ukristo, walikuwa wakichukua kodi kutoka k w a Wa t a n g a n y i k a , Waislamu na Wakristo, lakini wakitoa ruhusa na ruzuku kwa Watanganyika Wakrsito pekeee kuwa na shule.

    H a t a b a a d a y a kupatikana uhuru, bado serikali ilikuwa ikitoa pesa kwa shule za Wakristo

    pekee.Kwa wakati ule, baada

    ya Waislamu kupiga kelele wakilalamikia mfumo na utarat ibu huo wa kidhalimu na kibaguzi, na kuona ser ikal i ya kikoloni na Tanganyika huru, haijali, walianzisha juhudi za kujenga shule zao kwa harambee, lakini pia wakiendelea kupigania kile kilicho haki yao katika Hazina ya Taifa.

    Hata hivyo, juhudi za Waislamu zilikumbana na P i g o l a k wa n z a kutoka kwa Mwalimu Nyerere ambaye alitaifisha shule.

    Kutokana na propaganda iliyopigwa katika siasa hizo za kutaifisha shule, M w a l i m u N y e r e r e alionekana kama shujaa na msamaria mwema asiye mbaguzi aliyetaka na Waislamu wasome.

    Lakini ukweli wa jambo lenyewe ilikuwa hatua na mkakati wa kuwarejesha nyuma Waislamu.

    Moja, iliuwa ule moyo wa Waislamu wa kujizatiti na kuwa na moyo wa kujiletea maendeleo.

    Pili, zile nafasi chache zilizokuwa zikipatikana kuwapa fursa watoto wa Ki is lamu kusoma ziliporwa.

    Waislamu walifungiwa tena milango ya kusoma kama ilivyokuwa wakati wa mkoloni.

    Hii ni kutokana na sababu kwamba baada ya shule kutai f ishwa zikiwemo zile za Kikristo, bado uongozi wa shule zote hizo pamoja na maofisa walioteuwa nani asome, zilibaki mikononi mwa Wakristo, na inajulikana ni kwa namna gani Waislamu walidhulumika katika utaratibu huo.

    Hata hivyo, pamoja na baadhi ya shule za Kikristo nazo kutaifishwa, bado

    kulikuwa na nyingine zilizokuwa za seminary a m b a p o w a k i s o m a Wa k r i s t o p e k e e n a wakichaguliwa kuingia shule za serikali za kidato cha tano na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au kupata scholarship za serikali.

    K a t i k a m u d a w o t e wa Mwalimu Nyerere kama Rais, haikupata kuandikishwa shule ya seminary ya Kiislamu.

    Na namna ya kuwazuiya Waislamu ilikuwa ukiomba tasjila unaambiwa uende Bakwata. Ukifika Bakwata i l ishapewa maelekezo ikatae.

    I l i k u w a k i p i n d i al ipokuwa Waziri wa Elimu ni Marehemu Prof. Kighoma Ali Malima, aliyefungua mlango baada ya kusema kuwa hapakuwa na sheria inayowalazimisha Waislamu wasiandikishe shule ila chini ya Bakwata.

    Pa m o j a n a j u h u d i zinazoendelea Waislamu kutaka serikali yao itende h a k i k wa r a i a wa k e wote, kwa miaka ya hivi karibuni pamekuwa na mwamko mkubwa na kujitolea kukubwa kwa Waislamu katika kujenga na kuendesha shule na vyuo.

    A w a l i W a i s l a m u walipoanza juhudi hizi mwishoni mwa miaka ya 1980, serikali ilitoa kauli kuwa shule za seminari hazitatambulika.

    Na kwamba, kinyume n a i l i v y o k u wa h u k o nyuma ambapo, watoto wa Kikristo kutoka seminari za Kikristo walikuwa wakichaguliwa kidato cha tano shule za serikali, sasa itakuwa hawachaguliwi tena.

    H a t a h i v y o , h i y o haikuwakatisha tamaa Waislamu. Na kwa bahati nzuri, kimya kimya serikali

    yenyewe haikutekeleza azma yake hiyo ambayo kwa kila sura, ilikuwa ikionyesha kuwalenga Waislamu.

    Takriban sasa kila msikiti una shule ya Awali na mingine Awali na Msingi huku taasisi nyingi za Kiislamu zikianzisha shule za sekondari na vyuo.

    Kwa mujibu wa tahadhari na taarifa iliyotolewa na Amir Kundecha, ni kuwa shule hizi za Waislamu sasa basi.

    I t a k u wa s a s a b a s i kwa sababu hata kama w a t a k u w e p o , l a k i n i watakuwa ni wachache sana katika Waislamu ambao watakubali Zakka na Sadaka zao zitumike kujengea na kuendeshea s h u l e z a M i s i k i t i zinazosomesha Waislamu na wasio Waislamu.

    K a t i k a m o j a y a M i h a d h a r a y a k e , Marehemu Sheikh Ilunga Hassan Kapungu aliwahi kueleza hofu aliyokuwa nayo aliyekuwa Waziri wa El imu wakat i ule M h e s h i m i wa J o s e p h Mungai.

    Ilunga akiwa ofisini Waziri Mungai akifuatilia usajili wa shule yao moja ya Kiislamu kule Mwanza, Joseph Mungai alisema, anashindwa kujua hali itakuwaje miaka 50 ijayo wakati ambapo watoto wa Waislamu watakuwa wamesoma sawa na watoto wa Kikristo.

    I l i k u w a n i k a t i k a m a z u n g u m z o y a kawaida ambapo Mungai al imwonyesha I lunga m a j a l a d a m e n g i n a kumwambia kuwa yote yale yalikuwa ni maombi ya Waislamu wanataka kusajili shule.

    Mheshimiwa Waziri, Wa i s l a m u w e n y e w e h a wa n a u we z o n d i o wanahangaika kujenga.

    Alisema Ilunga kama kumwambia mheshimiwa asiwe na wasiwasi maana nguvu na kasi ya Waislamu haiwezi kushindana na ile ya Wakristo.

    Sawa. Leo mnahangaika n a k u j e n g a . I t a f i k a m a h a l i m n a e n d e s h a . L e o s i s i t u m e s o m a , n y i n y i h a m j a s o m a , lakini miaka 50 i jayo, watoto wenu watakuwa wa m e s o m a n a w e t u watakuwa wamesoma, hali itakuwaje.

    Alisema Sheikh Ilunga ( M u n g u A m r e h e m u ) akimnukuu aliyekuwa Waziri wa Elimu (mwaka 2000-2005) Joseph Mungai.

    A m b a c h o p e n g i n e inabidi Waislamu wajiulize: Mkakati huu na nia hii ya kufuta shule za Kidini na badala yake kuwa Binafsi, je ni katika kukabiliana na hofu aliyokuwa nayo Joseph Mungai?

  • 4 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 29- JUNI 4, 2015Makala

    WAKATI vyama vingi vinaanzishwa tena hapa Zanzibar, vilianza na matumaini makubwa kutoka kwa wananchi baada ya kuchoshwa na ukiritimba wa chama k i m o j a . M a t u m a i n i makubwa yalitegemewa kupatikana kutokana n a c h a m a t a w a l a k w a m b a k i l i k u w a tayari kujisahihisha na makosa yao ya nyuma na kutandika na kuonyesha njia na mwelekeo mpya wa kuongoza Taifa badala ya uchu wa kutawala. Sababu zozote zile naziwe katika kuleta na hatimae kukubali mfumo wa vyama vingi mategemeo ya mabadiliko yalitarajiwa k u we p o n a k u we p o kwa kiwango kikubwa p a m o j a n a k u s a h a u yaliyopita, ijapokuwa wengi wal ioathi r ika wa m e s a m e h e l a k i n i hawakusahau.

    Hali haikuwa hivyo, bali ilikuwa kunyume chake. Chuki, ubagizi ulizidi kushamiri na kupaliliwa. Miaka ishirini na tatu katika uhai wa taifa ni kidogo mno, ni kama jana au juzi tu ilipoanza enzi ya Dr. Salmini bin Amour Komandoo, enzi ya upandikizi fitna, chuki na ubaguzi baina ya Wapemba na Waunguja kwa sababu tu Wapemba wamekikataa Chama cha Mapinduzi.

    S a l m i n A m o u r aliwaondoa Wapemba wote katika nafasi za uongozi katika serikali, alimbakisha Shajak tu. CCM ilianza kuwabagua na inaendelea kuwabagua Wazanzibari na kuwaweka kat ika mafungu na madaraja. Hawa ni Waswahili na hawa ni Waarabu. Hawa ni Wapemba na hawa ni Waunguja. Hawa ni Weupe na hawa ni Weusi. Hawa ni Wazanzibari halisi na hawa si Wazanzibari halisi. Hawa ni wenzetu na hawa si wenzetu. Imekuwa i k i t u m i a m i s i n g i ya makundi iliyoyajenga na kutunga lugha za kibaguzi kwa kundi moja dhidi ya jengine.

    Hiyo ndio CCM. Mpaka leo CCM imekuwa ikifanya unyanyasaji na mateso kadhaa wa kadhaa hata ya kisaikologia kwa msingi wa makundi hayo. Kufanya wengine ni wenye nchi na wengine ni wahamiaji tu Nani aliesahau kauli ya Komandoo kat ika mkutano wa Kibanda maiti akijitutumua kwa kusema

    Vitimbi vya CCMNa Salma Alghaythiya,

    Wapemba weshasoma sasa zamu ya wenzao Waunguja, kauli ambayo ilitafsiriwa kwa vitendo kuwanyima Wapemba nafasi za Masomo ndani na nje.

    Hivo nani kasahau kauli ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi aliposema hawa Wapemba ni vijibwa vya santuri wanaiga sauti za mabwana zao yaani leo wapemba si watu na Wapemba hawana haki ya kutoa mawazo yao?.

    Kauli nyingi za dharau na kejeli zilitolewa hata kufika hadi kusemwa Mpemba kuingia Ikulu ni sawa na mbwa kuingia msikitini. CCM kama kingalikuwa ni chama cha kuongoza nchi, sio kutawala, basi kingefanya utafiti wa kina kujua sababu ya Wapemba k u i k a t a a C C M i l i kufahamu. Lakini CCM ni chama cha kutawala h a t a b i l a ya k u p a t a r idhaa ya wananchi . Lakini maskini ni chama ambacho kimeshapoteza dira na mwelekeo. Haya yalisemwa zamani na aliekuwa Katibu Mkuu wa CCM Horace Kolimba.

    Vishindo vya CCM v i l i t u m i a n g u v u z a dola bi la hata kujal i Katiba wala sheria za nchi. Vyama vya siasa ambavyo viliruhusiwa kufungua matawi pamoja na kufanya mikutano ili kuweza kunadi sera zao

    na kuweza kukubalika hii ikiwa ni haki yao chini ya sheria, lakini haikuwa hivyo pale chama cha CUF kilipofungua tawi na kuperushwa bendera Shumba Mjini (Pemba). Alitokea Mkuu wa wilaya Feruzi na kupeleka askari wa FFU ili kuteremsha bendera ya chama cha CUF. Nguvu za kupita mpaka zilitumika na jeshi la polisi lilitumika na walitumia risasi na kuua pamoja na kujeruhi. Nani amesahau mauaji ya kijana Awadh hapo Mtendeni.

    Hatuwezi kusahau watu waliouawa katika maandamano ya amani k u p i n g a m t o k e o ya uchaguzi yaliyofanya CUF. Wengi walijeruhiwa na kuwa na vilema vya m a i s h a n a w e n g i n e kukimbilia Kenya baada kusakwa kwa mabunduki, nini wameandamana.

    Sote tunakumbuka pale Maaalim Seif pamoja na viongozi wenzake wa CUF akina Juma Duni, Maulid Makame, Mloo na wengineo walifunguliwa kesi (za nyaraka za siri, uchochezi na uhaini) ili kuzuia na kuwafumba midomo katika kuikosoa CCM na kutokubaliana na sera za CCM. Sasa hii leo si ajabu kuona kesi inayomkabili Mansour baada ya kuikosoa CCM na sera zake.

    Vitimbi hivi vya CCM

    ni vingi na si vigeni katika siasa za Zanzibar. Ubao wa Kisonge umekuwa ukitumika tokea enzi kuchochea fitna ,chuki na mgawanyiko. Leo Kisonge i n a t a m k a Wa p e m b a wende kwao, Wapemba wahame, Wapemba na Warabu wahame, Unguja

    tumepindua. Hivo hizi nazo siasa au ni kuishiwa?

    Kufukuza kiongozi kama Hassan Nassor Moyo na wengine waliofukuzwa kabla yake, inaonyeza wazi kwamba meli inakwenda mrama na kuf i l i s ika kisiasa na kutovumilia na kuheshimu mawazo ya wengine. CCM inataka watu wote waimbe wimbo huo huo mmoja.

    Bado CCM iko katika us ing iz i wa manane na kuota ati Mwarabu atarudi. Hivyo Mwarabu gani ataerudi kutawala Zanzibar. Ikiwa Mwarabu atarudi, basi ni katika kuitikia maombi ya msaada unaoombwa na viongozi wa CCM na Serikali. Leo Rais Kikwete, kesho Spika Makinda, akifatiwa na Benard Membe, Lukuvi na akina Shamhuna na Dr. Makame wakibeba mikoba yao kuelekea Arabuni. Ndio hao hao ak ina William wakirudi huku kuwalani Waarabu na kuwapa chambi malenga wa matus i kutukana Warabu.

    C C M i n a e n d e l a k u w a p i g a m a f u n g u W a z a n z i b a r i i l i wachukiane, wahasimiane na wapigane. Huku ndio kupoteza dira na kuishiwa kisiasa. Vijana wa leo ambao wana malengo ya kujikwamua na hali duni ya maisha na kiu ya kutaka mabadiliko na maendeleo. Hawawezi k u c h e z a n y i m b o ya Mwarabu atarudi.

    SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Anne Makinda (kshoto) akiwa katika moja ya ziara nchini Oman.

  • 5 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 29- JUNI 4, 2015Habari/Matangazo

    S h i r i k a K u u l a Kijasusi la Marekani CIA, limelaumiwa kwa kuwa chanzo c h a u g a i d i n a ki le k inachoi twa m i s i m a m o m i k a l i ya k i d i n i i n a y o s h u h u d i w a nchini Kenya.

    Kwa muj ibu wa toleo la leo (juzi) la gazeti la kila siku la People Daily la nchini Kenya, afisa wa serikali ya Kenya ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema mradi wa CIA wa kuwaunga mkono

    MALAYSIA na Indonesia zimekubali kuwaruhusu maelfu ya wakimbizi wa Kiislamu wa wahamiaji wa jamii ya Rohingya kutoka Myanmar na wale kutoka Bangladesh kuingia katika nchi hizo.

    W a k i m b i z i h a o wamekwama baharini kwa siku kadhaa sasa.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Malaysia Anifah Amas, alisema nchi yake na Indonesia zimekubaliana kuendelea kutoa misaada ya k i b i n a d a m u k wa wahamiaji haramu 7,000 ambao bado wamekwama b a h a r i n i n a k u wa p a makazi ya muda, huku mchakato wa kuwapa makazi na kuwarejesha makwao ukishughulikiwa kwa kipindi cha mwaka moja ujao na jumuiya ya kimataifa.

    Anifah ameonya kuwa Malaysia na Indonesia h a z i n a r a s l i m a l i z a k u t o s h a k u wa s a i d i a wahamiaji hao na kuutaka ulimwengu kushirikiana nao kuwasaidia wahamiaji h a o n a k u o n g e z a kuwa nchi hizo mbili hazitajishughulisha katika kuwatafuta na kuwaokoa wahamiaji hao baharini bali zitawasaidia tu wale watakaofika katika fukwe zao.

    K wa u p a n d e wa k e Myanmar imeonekana k u l e g e z a s e r a z a k e za kibaguzi dhidi ya Waislamu, kwa kusema iko tayari pia kuwasaidia wahamia j i hao huku shinikizo kutoka kwa jumuiya ya kimataifa zikizidi kutaka wahamiaji hao kupokea misaada kutoka kwa Thailand, Malaysia na Indonesia.

    W a i s l a m u h a o wamelazimika kukimbia makazi yao kutokana na kuuliwa na wafuasi wa dini ya Budha, ambao ndio wengi katika nchi hiyo.

    M ya n m a r i m e s e m a inat iwa was iwas i na hali ya wahamiaji hao wanaohangaika baharini na inafuatilia kwa karibu matukio hayo.

    Wengi wa wahamiaji hao waliokwana ni wa kutoka jamii ya Rohingya ambao hawatambuliki rasmi na serikali ya Myanmar w a n a o w a c h u k u l i k a wahamiaji kutoka Bengali, huku wakidharauliwa pakubwa na makundi mengine nchini humo.

    Indonesia, Malaysia kupokea wakimbizi WaislamuMakaburi ya halaiki yagunduliwa

    MMOJA wa wahamiaji wa jamii ya Rohingya kutoka Myanmar aliyenusurika kifo.

    Mawaziri wa mambo ya nje wa Thailand, Malaysia na Indonesia wamekutana mjini Kuala Lumpur, kujadili tatizo hilo la kukwama wahamia j i hao baharini , ambao hakuna taifa linaloridhia kuwahifadhi.

    Myanmar hata hivyo imeususia mkutano huo kwa kusema haingependa kulifanya suala hilo kuwa la kimataifa.

    Wa k a t i h u o h u o , wavuvi nchini Indonesia wamewaokoa wahamiaji 370 wiki hii waliokuwa wamekwama kwa boti

    mbili katika jimbo la Aceh. Mkuu wa Shirika la

    Uokozi la mji wa Langsa Khairul Nova, amesema wahamiaji hao kutoka j a m i i y a R o h i n g y a walikuwa wameishiwa maji mwilini, wana njaa na wamedhoofika sana.

    Uokozi huo unakuja siku moja tu baada ya jeshi la Indonesia kuwataka wavuvi kutowasaidia wahamiaji waliokwama majini.

    Idadi ya wahamiaji waliokolewa katika jimbo hilo la Aceh mwezi huu imefikia 1,800.

    Shirika la umoja wa mataifa la kushughulikia w a k i m b i z i U N H C R l inakadir ia kiasi cha wahamiaji 2,000 huenda bado wamekwama majini kat i ya Myanmar na Bangladesh

    Katika tukio jingine, makaburi yasiyopungua 3 0 y a n a y o s a d i k i w a k u wa n a v i w i l i w i l i vya wahamiaji kutoka Myanmar na Bangladesh yamegunduliwa katika jimbo la Kaskazini mwa Malaysia la Perlis.

    Kwa mujibu wa gazeti la Star, miili ipatayo 100

    ilipatikana kwenye kaburi moja la umati siku ya Ijumaa.

    Wa z i r i wa M a m b o ya Ndani wa Malaysia, Zahid Hamidi, amesema m a k a b u r i h a y o yamepatikana kwenye kambi 17 zilizohamwa z a k u h i f a d h i w a t u wanaosafirishwa kwa njia ya magendo.

    Makaburi kadhaa ya umati pia yamegunduliwa nchini Thailand katika njia inayotumiwa na Waislamu wa Rohingya wanaokimbia mateso nchini Myanmar.

    Hii ni mara ya kwanza kwa makabur i kama hayo kugunduliwa nchini Malaysia.

    Wa k a t i h u o h u o Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch, limekosoa vikali sheria mpya ya idadi ya watu iliyosainiwa na Rais wa Myanmar Thein Sein.

    Shirika hilo limesema kuwa sheria hiyo inalenga jamii ya wachache ya Waislamu wa kabila la Rohingya.

    Sheria hiyo iliyosainiwa Mei 19 mwaka huu, pamoja n a m a m b o m e n g i n e inaruhusu serikali za m a j i m b o k u a n z i s h a mpango wa uzazi wa mpangilio ili kupunguza ongezeko la kizazi.

    Serikali ya Myanmar haiwatambui Waislamu wa Rohingya kuwa ni raia wa nchi hiyo, ikisisitiza kuwa ni wahamiaji haramu licha ya kuishi nchini humo kwa karne kadhaa.

    (ABNA).

    CIA chanzo cha ugaidi Kenya 'Mujahidina' katika vita vya Afghanistan vya muongo wa 80, n d i o c h a n z o c h a misimamo mikali ya kidini.

    L a w a m a h i z o z i m e t o l e w a k w a sababu baadhi ya Wakenya walioshiriki kat ika v i ta h ivyo dhidi ya Shirikisho la Sovieti, walirudi nyumbani na kupanda mbegu za misimamo mikali ya kidini na k u e n e z a u g a i d i unaoshuhudiwa hivi sasa nchini humo.

    G a z e t i h i l o

    l i n a d o k e z a k u wa vijana wanaojiunga na Al Shabab hivi sasa wamechochewa na wale walioshiriki katika mradi wa CIA nchini Afghanistan.

    Gazeti hilo linafichua kuwa Sheikh Abubakr Shariff, maarufu kama Makaburi aliyeuawa Mombasa Januar i 2014, alishiriki katika vita hivyo bega kwa bega na 'Mujahidina' wal iopata himaya y a C I A n c h i n i Afghanistan.

    A i d h a P e o p l e Dai ly l imeandika

    k u w a w a l i o e n d a Afghanistan walipata mamilioni ya dola na kwamba wengine walipitia Dubai kabla ya kujiunga na mradi huo wa CIA, ambao m b e g u z a k e s a s a zimechipukia Kenya.

    G a z e t i h i l o p i a l i m e a n d i k a k u wa i n a w e z e k a n a Masheikhe waliouawa akiwemo 'Makaburi' waliuliwa na maafisa wa CIA kwani shirika hilo la ki jasusi la Marekani limekuwa likifuatilia nyendo zao.

  • 6 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 29- JUNI 4, 2015MAKALA H A T U K U K A A kutimiza hata wastani w a m i e z i m i t a t u , tukaaabiwa kuwa sisi sasa tuna kesi ya ugaidi. S i j u i k e s h o k u t wa tutakuja kuambiwaa tuna kesi ya uhaini. Lakini ikiwa ni kwa madai yetu sisi kudai hishma ya nchi yetu, na haki sawa baina ya nchi hizi mbili, madai y e t u m h e s h i m i w a hatuwezi kuyageuka, hata watuite sisi nani. Watuite magaidi, watuite wahaini, watafute na jina jingine lolote lile, bado tutabakia kuwa tunadai madai yetu haya.

    M h e s h i m i w a ( H a k i m u ) ninayatanguliza haya makusudi i l i angalau upate picha, wakati faili hili unalo, upate ile picha yenyewe.

    Wengi wetu wamekuja k u c h u k u l i wa k a t i k a majumba yao saa nane za usiku. Wengine mpaka kuvunjiwa milango yao na kusafirishwa kuletwa huku Tanganyika (Tanzania Bara). Kwa NDUGU ZETU tunaoambiwa wa DAMU na WANATUPENDA.

    Ki l ichotokea baada ya hapo ni mahojiano ya kishenzi. Ya kikatili. U n a we z a u k a o n a n i maneno mazito, lakini mheshimiwa hicho ndio kilichojiri.

    Huwezi ukamchukua mtu mwenye heshma m f a n o k a m a S h e i k h Msellem Bin Ally kiongozi wa Jumuiya na Taasisi ya Kiislamu, wakati huo huo ni Mfasiri wa Quran Tu k u f u , t a f s i r i ya k e inaendeshwa katika redio Afrika Mashariki nzima, na watu wanaisikiliza watu dunia nzima, leo u n a m c h u k u a S h e i k h kama huyo unamhoji uchi wa mnyama! Na sote takribani tumehojiwa u c h i w a m n y a m a . Mbali ya kuwa Sheikh kama huyo hujatosheka, unamtundika na pingu kama alivyozaliwa, eti unamhoji. Ushenzi gani huo na ukat i l i gani . Mheshimiwa nataka uione hiyo picha ilivyokwenda ili uone kuwa kesi hii ina mashinikizo maalum ya kisiasa. Ni kama sisi tupo katika detention maalum. Tunazuiwa tu.

    Unamsikia sasa hivi mwakilishi wa DPP a n a v y o z u n g u m z a . Wa n a s u b i r i r e k o d i

    Kila mchunga ataulizwaSiku zitakapodhihirishwa Siri

    y a m a h a k a m a . Mheshimiwa h icho anachokizungumza y e y e , t a y a r i k i m e s h a t o l e w a m a a m u z i , y a a n i maamuzi ya mahakama ya mwanzo, ya ombi l e t u t u l i l o p e l e k a , yametolewa mwezi wa kumi na mbili (mwaka jana 2014) mheshimiwa.

    Mwezi wa kumi na mbili mpaka leo, ni miezi mitano, anasubiri rekodi. Mheshimiwa unapata picha hapa. Ya kuwa hapa kuna usanii unachezwa. Na kama maneno makali, sisi hatukusema maneno makali Tumedai hishma ya nchi yetu.

    Na hii si mara ya kwanza, watu waliodai ( m a d a i h a ya ) h a t a gazeti la hivi karibuni l a M w a n a n c h i Mheshimiwa Hassan Nassor Moyo anasema madai haya yalianza toka mwaka wa 1970

    lilipokuja jopo zima la serikali ya Zanzibar kuja hapa. Baada ya kufika hapa likiongozwa na Rais wa Zanzibar mwenyewe na Baraza lake zima, wanadai haki sawa na heshima kamili. Lakini Kwa bahati mbaya, huyo anayeambiwa alikuwa Baba wa Taifa, akawaambia wakati haujafika.

    Sie sio wa mwanzo kuletwa hapa. Hata Mwanasheria Mkuu, Dourado alichukuliwa akaletwa magereza huku akafungwa huku. Kwa nini? Anadai hishma ya Zanzibar. Mheshimiwa Ali Muhsin aliletwa hapa hapa naye. Ni mlolongo w a u d h a l i l i s h a j i . W a n a d h a l i l i s h w a Wazanzibari. Kutolewa katika nchi yao, na kuletwa katika nchi hii ya Tanganyika na k u f a n y i wa m a m b o yasiyoingia akilini.

    W a z a n z i b a r i

    w a l i o t o l e w a k u l e wanakaribia 50 sasa hivi. Kila anayeonekana, h u y u a n a c h u k i z a , a n a c h u k u l i w a t u . Wachache tunaojuana. Wengi wetu hatujuani. Tumekuja kujuana hapa.

    M a d a i y e t u makubwa, sis i ni Wazanzibari. Zanzibar kuna Rais. Rais wetu wa Zanzibar apewe heshma yake kama Rais wa Zanzibar. Tuna Rais, tuna DPP, tuna Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Mwanzo, tuna Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Mkoa, tuna Mahakama K u u Z a n z i b a r . N a Mahakama Kuu iliyopo h a p a , h a i n a h a d h i k u z i d i M a h a k a m a Kuu ya Zanzibar. Ile Mahakama Kuu, hii Mahakama Kuu. Hadhi sawa. Kuletwa hapa ni kudhalilishwa na hata kunyanyaswa wake zetu na watoto wetu na jamaa

    zetu. Utamchukuaje mtu kumpeleka nchi nyingine? Mmejigeuza nyie Wamarekani?

    Z a n z i b a r k u n a M a h a k a m a .tushitakiwe Zanzibar. Z a n z i b a r s i s i tumekuwa tukihojiwa. Tumeshaitwa na majopo ya viongozi tofauti, wakiwemo Makamishna na wengineo, kutuhoji, lakini wal ikuwa ni w a t u w a s t a a r a b u . Tunashangaa kuletwa hapa tunahojiwa na watu uchi wa mnyama. Unajiuliza kulikoni?

    H i v i t u s e m e ndivyo alivyoamrisha M h e s h i m i w a R a i s K i k w e t e w a f a n y e h a o m a o f i s a w a P o l i s i ? N d i v y o w a l i v y o a m r i s h w a hivyo!

    (Sehemu ya maelezo yaliyotolewa na Sheikh Farid Had Mahakamani jijini Dar es Salaam)

    SHEIKH Msellem Ali Msellem.

  • 7 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 29- JUNI 4, 2015Makala

    Profesa Ibrahim Noor Shariff

    Propaganda za udini shuleni Tanzania-4

    B A A D A ya k u o n e s h a ubaya wote tuliouonesha wanaosingiziwa Waislamu, sasa angalia mfano wa vile Ukristo na Wakristo wal ivyochorwa kat ika kitabu kiitwacho History for Secondary Schools, Form Two mlango wa 7 chini ya anuani ya Abolition of Slave Trade yaani Kupigwa Marufuku Biashara ya Utumwa, ukurasa wa 84:

    Katika vitabu vya historia Tanzania v ina sehemu nyingi ambazo wakoloni na wamishinari wanasifiwa kwa ku jenga shule na mengineyo na kukhusu utumwa hawakutajwa sana ila kusifiwa sana katika k u u o n d o s h a u t u m wa . Hawakutajwa kabisa vile walivyowauwa millioni kumi ya Waafrika katika Kongo (Congo) na wengine kukatwa mikono na kuadhibiwa vikali sana kwa namna nyinginezo za kikatili. Kama nilivyosema, propaganda si lazima uone katika yaliyozungumzwa na yaliyochorwa, bali pia huwemo pale yanapokuwa hayatajwi kwa uovu wao pale panapohitajiwa kutajwa. Kwa mfano, ukiangalia utaona kuwa wamewasifu wakoloni wa Kizungu kwa kuondosha biashara ya utumwa bila ya kuelezea chochoke kukhusu yale aliyoyafanya Sayyid Said katika mamlaka zake ya l i y o s a i d i a p a k u b wa kupiga marufuku biashara ya utumwa.

    Sayyid Said na biashara ya utumwa

    Propaganda za wenye siasa kali za udini hazitaki kuangalia ukweli wa biashara ya utumwa. La muhimu kwao ni kuonesha vipi Waislamu, na Waislamu peke yao ndio waliokuwa wabaya kuliko watu wote duniani. Kwa mfano, ukisoma khabari walizoziandika kukhusu Sayyid Said bin Sultan aliyetawala Zanzibar na upwa wa Afrika Masharika katika nusu ya kwanza ya

    Karne ya 19, utaona ni maovu matupu wanayoyaelezea. Hawataji kabisa kuwa Sayyid Said aliandikiana mkataba na Serikali ya Kiingereza tarehe 22 September 1822 kushirikiana katika kuzuia biashara ya utumwa na kuwapa rukhsa Waingereza y a k u p a n d a c h o m b o c h o c h o t e c h a r a i a wa Zanzibar wanaodhaniwa w a n a f a n y a b i a s h a r a ovu hiyo ya kuwauzia binadamu Wakristo. Kwani Sayyid Said na Waingereza walielewa vizuri sana namna walivyokuwa wakiteswa wa t u m wa wa K i a f r i k a katika nchi zilizomilikiwa na Wazungu Wakristo.

    Kulikuja wakati Wafaransa walikuwa tayari kuipiga v i ta Dola ya Zanzibar kwa sababu ya kuzuiliwa Wafaransa hata kuwachukua vibarua kwa ghi lba i l i baadaye kuwatia utumwani. Sayyid Said aliung'amua ujanja wao Wafaransa. Yote haya yalitokea kitambo kabla ya huo mkataba wa 1873 uliofikiwa na Sayyid Barghash. Katika kitabu chake kiitwacho "History of Zanzibar from the Middle Ages to 1856," Sir John Gray (aliyekuwa Jaji Mkuu Zanzibar) anatuelezea mengi juu ya juhudi alizozichukua Sayyid Said katika kuwazuilia wafanya biashara ya utumwa kutoka nchi za Wakristo, kununua binadamu katika mamlaka zake. Ifuatao ni tafsiri ya mmoja katika mifano hiyo:

    Tafsiri: [] mnamo mwaka 1851, wakati baba yake akiwa tena Oman [] Khalid alikuwa tena anakaimu kuiongoza Zanzibar. Kabla ya kuondoka, Sayyid Said

    a l impa mwanawe amri kali ya kuzuia uvunjwaji wowote wa mikataba ya biashara ya utumwa na Uingereza kwa namna yoyote iliyoyumkinika. Baada ya Sultani kuondoka, jahazi kubwa la mfanyabiashara wa Kifaransa liliwasili kisiwani humo, hapana shaka kwa dhamira ya kuwaandikisha wafanyakazi huru kwa ajili ya mashamba huko Bourbon (Reunion). Jaribio la kuyapa aina fulani ya uhalali malipo yaliyofanyika hapo kwa kumpa mmliki watumwa bakhshishi kwa kila mtumwa aliyeshiriki kwa dhamira hii. Baada ya kulipwa bakhshishi, mmiliki alitoa tangazo rasmi lenye maneno yafuatayo, Mtu huyu al ikuwa mtumwa wangu. Ninamwacha huru. Ana uhuru wa kuhudumu kwa mfanyabiashara wa Kifaransa au mwengine yeyote, ikiwa ataku-baliana na masharti yaliyowekwa. Masharti yanayotajwa hapa ni kwamba mtumwa huyo alipaswa kufanya kazi kwa tajiri wake wa Kifaransa kwa miaka mitano na baada ya hapo ana uhuru wa kwenda atakako .

    Ameongeza Gray na haya yafuatayo:

    Tafsiri: Sio tu kwamba Khalid alipiga marufuku kwa nguvu kali aina yoyote ya makubaliano kama hayo, bali pia alipeleka boti kwenye jahazi la Kifaransa, ambalo aliamini kuwa l i l ikuwa limechukua watumwa kumi na mbili ambao walikuwa wa k i p e l e k wa B o u r b o n bila ya ridhaa zao. Bwana

    Belligny, Balozi wa Ufaransa, ghafla alifoka. Akapeleka malalamiko rasmi Muscati. Ikisha akaelekea mwenyewe B o u r b o n , a k i t a n g a z a kwamba hatorejea mpaka khatua fulani zichukuliwe na Serikali ya Jamhuri ya Ufaransa kulipiza kisasi cha kile anachoamini kuwa ni dharau dhidi ya bendera [Dola] ya Ufaransa.

    Hii ilikuwa ndiyo kadiri iliyofika Zanzibar chini ya utawala wa Sayyid Said kat ika kuzuia biashara ya utumwa hata kabla ya kutawala Sayyid Barghash, na kuna mengi mengineyo ya kweli ambayo hayatajwi na wenye propaganda zao za chuki za udini dhidi ya Waislamu.

    P i l i , W a p o r t u g i z i hawakuwa na uhusiano mzuri na Dola ya Zanzibar b a a d a ya Wa a r a b u n a Waswahili kupigana nao na kuwafurusha mpaka Msumbiji. Wala Waportugizi hawakuwa na haja ya kununua watumwa kwa wafanya biashara kutoka katika Dola ya Zanzibar, kwani walikuwa wakikamatiwa na kuuziwa b inadamu wengi kutokana na Wayao na makabila mengineyo ya Kiafrika yenye nguvu yalioko Msumbiji, Angola na kwingineko. Ukhabithi mkubwa sana ulifanywa na baadhi ya Waafrika katika kuwahujumu, kuwauwa wengi, kuwakamata idadi kubwa na kuwatia utumwani mateka wa Kiaafrika. Kwa hivyo, hawakusafirishwa watumwa kutoka Zanzibar kupelekwa nchi za nje baada ya 1822. Na kabla ya hapo, kulikuwa ni muda mfupi tu kulipotendwa hayo. Kwa hivyo hao wenye kudai kuwa Zanzibar ilikuwa kituo kikuu cha biashara ya utumwa baina ya Afrika na nchi za Mashariki, si maneno ya yaliyoeleza ukweli sawasawa.

    Kama kweli wanataka kutuelezea ukweli sawasawa, basi watueleze yanayokhusu biashara hiyo kikamilifu. Watueleze ukhabithi wa Waafrika katika kuwakamata Waafrika wengine waliokuwa hawana nguvu. Watueleze nani waliokuwa wanahitajia watumwa wengi na sababu z a k e . Wa t u e l e z e p i a waliwachukua watumwa wangapi na kuwapeleka wapi. Watuambie, bila ya kificho, hali za hao watumwa wa Kiafrika zilivyokuwa, na khalafu hali za vizazi vyao ziko katika hali gani leo kila mahala duniani.

    Siasa za chuki ni siasa za kuangamiza. Kubomoa ni rahisi, kujenga ndiyo kazi. Hakuna Wazanzibari huko Zanzibar ambao wanauelewa ukweli, wakawaendea hao mapadiri walioko makanisani Zanzibar na kuwaambia kuwa wanayowazungumzia watalii na wengineo wenye kuzuru Kanisa la Kimoto kuwa nusu ya ukweli wanaouelezea humalizikia kuwa ni uwongo na ni makosa kwa Mungu na kwa binadamu pia? Hakuna Mzanzibar i anayeweza kuwakabili na kuwaelezea kuwa huo uchache wa ukweli wanaouzungumza kulimalizikia kunyooshewa Waarabu peke yao vidole vya lawama na hati-maye katika mavamizi ya 1964 ikawa ndiyo moja katika sababu za kuuliwa idadi isiyojulikana ya Wazanzibari kwa ukhabithi m k u b w a s a n a ? K u w a jukumu la fitina zimo juu ya vichwa vyao pia. Hakuna Mzanzibar i anayeweza kuwaambia hao wenye kupandikiza siasa kali za udini kuwa fitina za kuulisha watu ni dhambi kubwa ambayo wadhulumiwa watakuja kulipiwa mbele ya Hakii? Haitoshi kujidai wanaelezea ya ukweli na ilihali hawafanyi hivyo, nusu ya ukweli huweza kuwa ni uwongo. Kuzungumzia kuwa Kwa Kimoto kulikuwa na soko la utumwa na watumwa wakifanywa hivi na vile na wafanyaji hayo walikuwa ni Waislamu, Waswahili au Waarabu na waliowakomboa ni Wakristo au Wazungu ni kutuelezea nusu ya ukweli ulivyokuwa, na kwa hivyo ni ya uwongo w a n a y o y a t a p a k a z a u l i m w e n g u n i k a m a tunavyoona.

    Na nchi za Ghuba (Yemeni, Omani, Amarati, Bahareni na Kuweit) ambako tunazugwa kuwa walipelekwa watumwa wa Kiafrika kwa mamilioni, idadi ya Waarabu wenyewe haifiki milioni arubaini hii leo, na idadi ya wenye asili za Kiafrika hadi hii leo ni ndogo sana. Waarabu hawakuwa na mahitaji ya kuwatumilia w a t u m w a k u w a l i m i a m a s h a m b a m a k u b w a walokuwa hawanayo kama walivyohitajia Wazungu katika nchi walizozimiliki, khasa zile zilioko Amerika, kwa sababu nchi zao Waarabu ni za jangwa zisizokuwa na maji ya kutosheleza wala ardhi za rutuba ila chache tu. Hakukuwa na haja ya kumpeleka mtumwa katika jangwa kulima; alime nini jangwani?

  • 8 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 29- JUNI 4, 2015Tangazo

    ISLAMIC PROPAGATION CENTREORODHA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2015/2016 KATIKA SHULE ZA IPC

    I. KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL.-SAME -KILIMANJARO

    A.WAVULANANA JINA KAMILI TAHASUSI1 MOHAMED OMARI MOHAMMED PCB2 YAHYA KHALFAN KABOZA PCB3 FADHILI ADAM ALLY CBG4 IBRAHIM HASSAN KIBONA EGM5 NASSIB BAKARI LULELA HKL6 ISSA SALIMU CBG7 ABDALLAH HUSSEIN MSUYA PCB8 RAMADHAN HAMIS MBOZU HGL9 SULEIMAN MAJALIWA KYONDA HGL10 SOUD SULEIMAN SALUM PCB11 HAMIM RAJABU NKYA ECA12 AHMED R.SALUM PCB13 HAMAD ALLY PCB14 IBRAHIM HAJI MWEVURA HGE15 SWALEHE ABEID SWALEHE ECA16 JUMA SAIDI RAMADHAN PCM17 ABDALLAH AYUB ABDALLAH PCB18 MOHAMMED KARIM MUHAMMED EGM19 HUSSEIN RAMADHAN HOTI HGL20 JUMA SALIM MRUMA PCB21 IDDY BAKARI MSUYA HKL22 ALLY MWINDADI BAULEY CBG23 HUSSEIN ABEID HGK24 HARUN HASSAN MUHAMMED PCB25 ALLY BAKARI MWICHANDE PCM26 IBRAHIM TAINADA NGOMUO PCB27 HUSSEIN ABBY MDEE PCM28 MUHAMMED TWALIB KATULLA PCB29 ALFAN IBRAHIM. CBG30 AKIDA NYALUKE HGK31 LUQMAN J.KOOSA PCB32 KASIMU SAIDI JUMA CBG33 MOHAMMED .I.KARATA PCB34 BANDARI ISMAILI CBG35 ABDULHAKIM HASHIM KOMBO HGE36 ALLY ATHUMANI ALLY CBM37 MUHAMMED YAHYA MBWERA CBG38 MADUA ALLY BARUTI CBG39 TWAHA RASHID TWAHA CBG40 HASSAN ALLY HIZZA PCB41 OMARY SWALEHE OMARY PCB42 HAMADI .A .HAMADI PCB43 RAJAB HALID NYONI PCM44 SULEIMAN S.MSANGI. KLA45 ABUUBAKAR.A.ISSA PCM46 SULEIMAN S.ABDULRAHMAAN HGE47 ABDALLAH. B.MVUNGI EGM48 RASHID IDD TWAHIRU PCB49 ALLY MOHAMMED SAMIJI PCB50 ABBAS KHALID UPUNDA HGL51 YUSUFU SUDI ZUBERI PCBB.WASICHANANa. JINA KAMILI TAHASUSI01 SAMIRA SAIDI MKONGE HKL02 KHADIJA H HAMADI ECA03 JASMIN A.MIKONGO ECA04 SAIDINA M MCHOMVU CBG05 ZUHRA NASSORO HAMAD HKL06 RADHIA ALLY HASSAN HGE07 CAROLINE PROSPER CBG08 SABRINA ALLY ABOUD PCB09 SUMAIYA ISMAILI MTORO CBG10 SHEILA SALUM LUYEKO ECA11 AISHA SALUM KLA12 SALMA ABDULRHMAN SALEHE PCB13 MARIYAM MAKAME NYANGE PCB14 SHAZMA HAMIDU KIMARO ECA15 AISHA MAHMOUD PCB16 HAWA HAIDAR HEMED PCB17 SAADA ABDALLAH RASHID EGM18 AMINA ABDALLAH KILUVIA HGE19 SOFIA YUSUF CBG20 RUQAIYA AMRI SULEIMAN PCB21 HADIJA MOHAMMED EGM22 HAMIDA MALIKI MKINDI CBG23 NASRA MUHSIN SAIDI PCB24 MARIAM HAMIS SHIMBO ECA25 SOPHIA HARUNI MBALAMO ECA26 SAUDA RASHIDI MVUNGI HKL27 MARIAM K. ALLY HKL28 JOHARI HENRY ELIBARIKI CBG29 SHARIFA HUSSEIN KIBAURA HGL30 ZAWADI .H. KIBINDU EGM31 RAYA ISSA NASSOR PCB32 FATMA KHAMIS MBANO PCB33 AZIZA SHAZIL HGL34 HUSNA HAMISI NGULYAVYANGU PCB35 ELISIAMINA MSHANA. PCB36 SHEKHA RASHID SAID PCB

    37 SADA MUHAMMED KISIWA CBG38 JOHA MUHAMMED ATHUMANI KLA39 KHADIJA IBRAHIM IDDY ECA40 SAMIRA SADIKI KGL41 MWANAHAWA OMARI DAUDI ECA42 LULU AMOUR SEIF PCB43 HAMIDA ATHUMANI CBM44 JOKHA ABDULKARIM MOHAMMED PCB45 HADIJA DAUDI CBG46 ASHA OMARI MBARUKU PCB46 SALAMA K.HAMZA CBG46 SWIFATH HASSAN PCB47 BINZUA NASIR MRUTU CBG48 SAUMU RAMADHAN MBANO PCB49 MWAJUMA SALEHE SABO ECA50 ZUBEDA NYANDA SWEYA EGM51 SHAMSA DAUDI UDDY PCB52 BITHUME SHEHA HASSAN PCB53 KHAULAT HAMIS MUSSA PCB54 HAJRA KHAMIS SAID PCB55 AMINA IDD MULLENGA HGE56 KHUSNA .S.KASEKO HGL57 MAHIJA SHABANI ECA58 HALIMA ABDULRAHMAAN MWENDA PCB59 MUNIRA HAMIS ABDALLAH PCB60. FATMA NUHA HGE61 MARYAM YAHYA ECA62 AMINA SAIDI MUSTAFA ECA63 ZAINAB AMEIR RAMADHAN ECA64 SWAUMU. A.ALLY HKL65 ZAINAB ABDILLAAHI MSUYA HKL66 ZEYANA NASSOR CBG67 RUKIA SALUM IBRAHIM EGM68 AISHA ABTWALIB YUSUFU PCM69 ZAINABU ABDILLAH MSUYA HKLII. UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL -DSMA.WAVULANANA. JINA KAMILI TAHASUSI1. OMARI ISSA KIDETE KLA2 HASSAN HAMISI PCB3 HUSSEIN HAMISI ECA4. YUSUF AYOUB ECA5. FARUKI B. MCHALAGANYA CBG6. OMAR ABDUL AZIZ SAID CBG7. IBRAHIM RAMADHANI EGM8 IBRAHIM MTENDA HKL9 WAZIRI JUMA CBG10 RIDHWAN YAHYA ECA11 HUSSEIN SALUM MBAYA CBG12. SELEMAN KAISANGA OMAR KLA13. ABDULKADIR NASSOR MOHAMMED PCM14 SAID HAMDAN HGL15 ABUBAKAR RAMADHAN HAJI PCM16 IDDI ISMAIL MBILINYI HKL17 MUSSA ISHUZA KAWAMBWA EGM18 ISMAIL ALLY KILUA PCB19 FAHMY HAMAD ABDALLAH CBG20 SAID HASSAN SIMA CBG21 ZAKARIA ELIUS MWAJA ECA22 KHAMISI SALIM KIMARO ECA23 ABDUL-RAZAK SEIF PCB24 JABIR MIRAJI MLOSHA HGK25 ISMAIL Y. AMIY CBG26 ZUBERI HAMISI KLA27 ABUBAKARI RAMADHANI SALIM CBG28 ABDALLAH RAMADHAN CBG29. SALUM HASSAN MUTAFUNGWA HGE30 SALUMU HASSAN MUTAFUNGWA HGE31 RAMADHANI A. URASSA ECAB. WASICHANANA. JINA KAMILI TAHASUSI1. AMINA YAHAYA IDDI HKL2. HUSNA SINNA MALTIN PCB3 MCHANGA SAIDI BAKARI ECA4. BI-ULEDI ATHUMANI MAISHA CBG5. ZENA HASSANI MALILO PCB6. JOHARI HUSSEIN ISSA HKL7. ZUHURA SHARIFF JUMA ECA8. SALHA MARSHAL HKL9 MASSAD M. GHARIB HKL10. SAMIRA MBARAKA HEMEDY ECA11. SAWIYA RASHID MTAWALA PCB12. ANZIRAN ATWAI SAID HKL13. ASMA ALLY NASSOR HGE14. LATIPHA BUD MAJANJA PCB15. AMNE SAID HEMEDY EAM16 AMINA YAHYA IDDI HKL17. HAJRA KHAMIS MASOUD PCM18 YUSRA SAID ALLY HGE19 KHADIJA HASSAN ABDULLLAH HKL20 MARIAM SAID IRUNGA EGM21 MWAJUMA KHAMIS MBANO HKL22. HALIMA BILALY MBUYU HGE

    23 ZULFA FADHILI BAKILI CBG24 AISHA MRISHO SAIDI CBG25 AISHA ABOUBAKAR MASOUD PCB24 FATMA M. MWISHEHE CBG25 ARAFA ISMAIL ALLY ECA26 NASRA MOHAMED SALUM CBG27 SABRINA ZUBEIR MZEE PCB28 FATUMA SULEIMAN ALLY CBG29 MARIAM AMANI ISSA HGK30 HAFSWAT MTEPA HKL31 ZAINAB HEMEDY ECA32 ZULEKHA ALI ISSA PCB33 NIHADU ILIYASA NGOKOJA HGE34 AMINA NASIBU ALLY CBG35. FATMA ISSA MTUWA CBG36 SABBAH SLIM HKL37. JOKHA MOHAMMED SEIF PCB38. MARIAM ABDUL-RAHMAN JUMA HGK39. AZIZA SHABAN ECA40 ZABIBU HAMLO NJWAYO HGE41 SOPHIA SAID MGALLAH HGL42 UMMY-KULTHUM J. CHAPONDA HKL43 NAJMA ALLY MOHAMED HKL44 JASMINE YAHYA HKL45 RAYA SEIF OMAR PCB46 SALMA MUJITABA EGM47 ZAKIA FEDASTUS NYAHONGE HGE48 SALMA RASHIDI JUMA HGEIII . NYASAKA -MWANZAA.WAVULANANA. JINA KAMILI TAHASUSI1. CHONGELA SELEMAN CBG2. YUNUS SULEIMAN PCB3. IDDI YAHYA HASSANI HKL4. JUMANNE ATHUMAN MNZAVA PCB5. ABDUL-NASER S. SULEIMAN EGM6. MRISHO RAJAB MRISHO PCB7. OMARI AHMAD BAGIRAMENSHI EGM8. IDDI KASSIM IDDI ECA9. YAAMAN ABBAS HASSAN PCB10. AHMAD S. ABDUL-AZIZ PCM11. ABDULSHAKUR OTHMAN OMARY EGM12. FARID KHASSAN PCB13. KARIM JUMA NSOMBA HGL14 KHARID KHASIM CBG15 KHALIFA MWAMBA HKL16 SHABAN OMARY HGE17. HAMIS IBRAHIM OMARY HGLB.WASICHANANA. JINA KAMILI TAHASUSI1 AZIZA OMARY MGAZA HKL2 HADIJA M MBAROUK CBG3 REHEMA M NGONJI PCB4 HADIJA ABDALLAH LUKAGO HKL5 SWAHIBA ABDALLAH CBG6 AMINA BAONJA MSANGI PCB7 JAMILA KISIJA NTUMBA KLA8 THUWAYBA SULEYMAN NAMBUNGO HKL9 HUSNA SHABANI HAMISI HKL10. HALIMA CHATE AYOUB PCB11. HAULAT RASHID KWANGAYA PCB12. MARYMA ALLY KILIMA PCB13 LUCKY SHABANI PCB14 HAWA HASSAN HUSSEIN PCB15 HAWA SHARIF ABDALLAH HKL16. TUNU ATHUMAN KAKWEKWE EGM17. GLORIA SANGA EGM18 AMINA IDD SALUM KLA19 NYANCHARA HASSAN KITAMA HGE20 HUSNA A MUNISI HGE21. NEEMA ULIMWENGU BANDULILA HGE22 MARIAM RASHID SEIF HGK23 MWAJIBU MAJIDI IGANGULA HKL24 MSEI RAMADHANI NYAGANI HGL25 FATMA HUSSEIN MWAMBA PCB26 AHLAM SULEIMAN NASSOR HGE32 QUDRAT MUSSA RASHID HKL33 SHANI J MTULA CBG34 ZUBEDA AHINDA EGM35 LUCKY SHABANI PCBMUHIMU.1. WALIOCHAGULIWA NA AMBAO HAWAJAPATA MAELEKEZO

    YA KUJIUNGA (JOINING INSTRUCTIONS) WAZIFUATE PALE WALIPOCHUKULIA AU KURUDISHA FOMU.

    2. NAFASI BADO ZIPO KWA SHULE ZOTE TATU NA FOMU ZINAPATIKANA KATIKA VITUO VYA KUUZIA FOMU KOTE NCHINI AU KATIKA TOVUTI WWW.ipc.org.tz

    3. KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU KWA WAKUU WA SHULE

    1. KIRINJIKO ISL.S.S. -07842964242. UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL-06573501723. NYASAKA ISLAMIC S.S.-0786417685.

    WABILLAHI TAWFIIQ.MKURUGENZI.

  • 9 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 29- JUNI 4, 2015Makala

    Mafundisho ya Quran

    Fethullah-Gulen

    MFANO wao ni kama mfano wa mtu ambaye ameuwasha m o t o u l i p o v i o n y e s h a vilivyo pambizoni mwake akauondosha Mwenyezi Mungu mwangaza wao na akawaachia katika viza hawaoni kitu chochote. [Al-Qarah 17]

    A y a h i i t u k u f u , inauswamirisha ulimwengu wa ndani, na inaonyesha kwa mfano wenye kuguswa na wenye kushuhudiwa.

    Kutokana na kuangalia kwamba wanafiki wanaishi k a t i ya Wa i s l a m u n a wanachanganyika nao, kwa sababu hiyo unakuwa mwepes i kwao wakat i mwingi muweko wa nuru ya imani. Isipokuwa unafiki ambao umezama na kubobea kwao katika nyoyo zao na vichwani mwao, unawazuia kufaidika na nuru hii. Ndiyo hawa wanafiki wamegeuka na kuingia kwenye hali

    ambayo hawaoni pamoja na kwamba macho yao yamefunuliwa ama kwa sababu ya kutoshughulika na nuru ya Mwenyezi Mungu ambao anauchukua Mtume mtukufu mkononi mwake au kuudharau mwenge huo au kwa sababu ya kuyaharibu maandalizi ya maumbile yao. Isipokuwa pamoja na hayo inawaelekea nuru ya mwenge ambayo inayachukua macho na badala ya kuiangalia nuru kwa jicho la kuamini, tunawaona wanafanya haraka kwa shaka zao na kuzingazinga k w a o k u i f u t a n g u v u yenye kuchembuka katika roho zao na wanaiondoa taathira yake mpaka tamko (Istaqada) ameuwasha moto linaashiria kwamba wao walikuwa wanafanya mpango wa kuipindua nuru hii na kuigeuza kuwa moto wenye kuunguza badala ya kufaidika nayo katika kuikataa njia.

    A m a m a k a f i r i wa o , hawakuijua imani wala nuru yenye kutokana na imani. Hawakuiona milele na hawakuingia kat ika mazingira yake matakatifu. Kwa sababu hiyo wakati walipohisi makafiri sababu hii au hiyo nuru katika hisia yao tukawatoa wapingaji kat ika wao wali jar ibu k u s h i k a m a n a n a y o n a kuipitisha sehemu ya maisha yao kama waumini wenye Ikhlas i . Hapana shaka kwamba tofauti kati ya nuru

    na kiza na kati ya imani na ukafiri ina mchango mkubwa katika jambo hili . Wale ambao walikuwa wanaona hii huko nyuma mambo mengine, wakati walipoiona nuru hii, waliingia katika ulimwengu unaozungukwa na uzuri wa Uislamu na mvuto wake. Kwa sababu hii wakati tunapolinganisha kati ya ufuataji wa dini wa wale ambao wanasikia kutokana na Uislamu na wanauelewa kwa mara ya kwanza na wanauamini na wanaishi nao na kati ya ufuataji wa dini kwa wale Waislamu ambao wamezaliwa katika nchi za Kiislamu isipokuwa wa c h a c h e k a t i k a wa o , atafahamu kwa sura ya wazi sana usahihi wa yale ambayo tumeyasema hapo juu.

    Wao ni viziwi, wao ni mabubu, wao ni vipofu, kwa sababu hiyo hawarejei. [Al-Baqarah 18]

    Moja kati ya aya mbili h iz i , inafungamana na wa n a f i k i n a n y i n g i n e inafungamana na makafiri. Na kama inavyoonekana hapa kuna kigawanyo cha pamoja kati ya wanafiki na kati ya makafiri katika maudhui ya unganganizi na kutovumilia na kukosekana ulaini katika mwelekeo wa mtazamo na fikra iliyobadili. Kwa sababu hiyo kila moja katika makundi mawili haya linasifiwa kwamba wao ni viziwi, mabubu, vipofu. Is ipokuwa sababu kat i ya makundi hayo mawili zinatofautiana kufuatana na hizo aya mbili. Kwani sababu katika aya ya kwanza inarejea

    kwenye kutorejea kwao kwenye umbile lao la asili, lililotangulia. Ama sababu katika aya nyingine inarejea kwenye kutozitumia akili zao. Na chachu ya pamoja ambayo inawafanya wawe viziwi, mabubu, vipofu na kutoongoka kwao kuelekea kwa Muumbaji mtukufu kwa kukisoma kitabu cha U l i m w e n g u a m b a c h o k i m e w e k wa m b e l e ya macho yao kama maonyesho y a M w e n y e z i M u n g u yenye kupendeza yenye kustaajabisha, na kutosimama kwao kwa kutokifanyia tathmini kitabu hiki ukweli wa kukifanyia tathmini na wala kwa kuuchunguza kwa kina huu ulimwengu na matukio na kuyachunguza na kuchukua mazingatio kutokana na matukio hayo, na kutoyaazima masikio yao kwa kuvisikiliza vitabu vilivyoteremshwa na pia kutoisikiliza sauti ya hisia na dhamira zao. Na lau kwamba wao wangeyafanya haya, wangefanya haraka kama waumini, kwenye k u s h u h u d i a k w a m b a Hapana Mola apasaye k u a b u d i w a k w a h a k i i s i p o k u w a M w e n y e z i Mungu. Maana wangekuwa wamezitumia aki l i zao n a wa m e r e j e a k we n ye maumbile yao ya asili, na wameyapitisha maisha yao kufuatana na katiba na kanuni ya Mwenyezi Mungu na kufuatana na maamrisho yake na makatazo yake. Ndiyo hakika wao ni viziwi kwa sababu wao hawawezi kusikia kila kitu na hali ya kuwa kitu hicho kina mtakasa

    Mwenyezi Mungu mtukufu kwa ulimi wake maalumu na kinamtukuza. Na wao ni mabubu kwa sababu wao hawawezi kuyazungumzia yale ambayo wanayahisi katika vina vya hisia zao na hawawezi kuviweka wazi. Na wao ni vipofu, kwa sababu wao hawazioni njia zenye kufahamisha juu ya kupatikana kwa Mwenyezi Mungu mtukufu na upweke wake.

    Tutakapokuja kwenye ufupisho wa aya, tutaona kwamba aya inawasifia makafiri kwamba wao hawana akili maana hawazitumii akili zao na hawafikiri na mambo ndiyo yalivyo, kwa sababu lau wangekuwa wanaweza kufikiri au lau wangefikiri njia ambazo zinapelekea kwenye imani kwa wepesi mkubwa sana, kwa ushahidi wa kwamba hawa makafiri wenye kupinga, wenye kuasi ambao walimuudhi Mtume mtukufu (S.A.W.) na maswahaba zake pale Makkah kwa muda wa miaka mingi sana, na wakawapa adhabu wakati walipowajuwa Waislamu baada ya suluhu ya Hudaibiya kuwajua vizuri sana, katika hayo mazingira matulivu, waliacha upingaji wao wa zamani na mtazamo wao uliodumaa wa kale na walijuwa kwamba wao wako juu ya makosa makubwa. Kwa sababu hiyo wanaelekea upande wa haki. Ndiyo kufika makafiri kwenye nukta hii muhimu kunafungamana na kuzamisha kwao fikra na kufanya tathmini kwao. Kwa sababu hiyo tumeiona Quran tukufu inalifupisha jambo lao katika kadhia hii kwa kusema kwamba, wao hawana akili.

    SAHABA mmoja aliwahi kumwomba Mtume (s.a.w.) ampe taarifa kumhusu yeye mwenyewe. Naye akawaambia hivi:

    "Mimi ndiye mtu ambaye Ibrahim (a.s.) aliomba nije, na ambaye Yesu (Nabii 'Isa ibn Maryam) (a.s.) alitangaza habari njema za ujio wangu.

    Usemi huu unadokeza aya zifuatazo za Quran:

    Ewe Mola Mlezi wetu! Wale tee mtume anaye tokana na wao, awasomee aya zako, na awafundishe Kitabu (Chako) na hikima (nyingine) na awatakase (na kila mabaya). Hakika Wewe Ndiwe Mwenye nguvu, Mwenye hikima." (Surat Al-Baqarah, 2:129)

    Na Isa bin Mariamu aliposema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninayethibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria habari njema za kuja Mtume atakayekuja baada yangu; ambaye jina lake litakuwa ni Ahmad ( M u h a m m a d ) ! L a k i n i alipowaletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio dhaahiri!" (Surat As-Saff, 61:6)

    Mjumbe ( s . a .w. ) wa Al lah ( s .w. t . ) a l ikuwa akitazamiwa au akingojewa kuwa atakuja. Manabii

    Nabii aliyekuwa akingojewaZisemavyo Taurati na Zaburi za Mayahudi na Wakristo

    w o t e w a l i o m t a n g u l i a walimwongelea Mtume (s.a.w.) na walitabiri ujio wake.

    Aya ya Qur'an 3:81 inataja waziwazi kuwa Mola (s.w.t.) Alifanya kiaga (convenant) m a a l u m n a M a n a b i i kwamba watamwamini na watamsaidia Mjumbe huyo atakayekuja baada yao na atakayethibitisha ujumbe waliouleta wao:

    N a p a l e M w e n y e z i Mungu Alipochukua ahadi ( k i a g a ) k wa M a n a b i i : Nikisha kukupeni Kitabu na hikima, kisha akakujieni Mtume mwenye kusadikisha mliyonayo, ni juu yenu mumuamini na mumsaidie. A k a s e m a : J e , m m e k i r i na mmekubal i kushika agizo langu juu ya hayo? Wakasema: Tumekubali. Akasema: Basi shuhudieni, na Mimi ni pamoja nanyi katika kushuhudia. (Surat Aali 'Imran, 3:81)

    M a k a l a ya s a s a ( ya Bibl ia za Wakris to) ya Taurati, Injili, na Zaburi,

    mpaka hivi sasa (baada ya kukarabatiwakarabatiwa) zinazomzungumzia Nabii Muhammad (s.a.w.) na hata Maswahaba. Marehemu Husayn Jisri alizitambua jumla ya aya 114 za aina hii. Na akazinukuu katika kitabu chake Risalat Al-Hamidiya. Hapa chini tunanukuu baadhi ya aya hizo (kama Biblia zao Wakristo wenyewe zinavyoandika):

    Kumb. La Taurati 33:2 (Musa) Akasema: (Bwana alitoka Sinai, akawaondokea kutoka Seiri , al iangaza kutoka kilima cha Paran, akaja Meribath-kadeshi. Upande wa mkono wake wa kuume palikuwa na sheria ya moto moto kwao.

    (Tafsiri hii ni ya Biblia ya Kiswahili ya "Bible Societies of Kenya and Tanzania, Union Version, 1952".)

    Tafsiri hii inakanganya makusudi hapo inapotaja ' M e r e b a t h K a d e s h n a kutowataja masahaba au watakatifu 10,000 kama ziandikavyo tafsiri nyingi

    za Kiingereza (na za lugha zingine za kigeni) kama Biblia hii "Authorized King James Version, 1979", ambayo imeandika hivi:

    "Deuteronomy 33:2 And he (Moses) said, The Lord came from Sinai and rose up from Se'ir unto them; he shined forth from mount Paran, and he came with ten thousand saints: from his right hand sent a fiery law for them. "

    Ambayo ta fs i r i yake halisi ya Kiswahili ni kama ifuatavyo:

    "kumbukumbu la Torati 33:2 Naye (Musa) alikuja kutoka Sinai. Akawaondokea kutoka Seiri kuja kwao; Aliangaza kutoka kilima cha Parani, na alikuja na wa t a k a t i f u e l f u k u m i . Kutoka katika mkono wake wa kuume ilikuja sheria motomoto kwa ajili yao."

    A y a h i i y a T o r a t i inaongelea kwa pamoja juu ya Nabii Mu Nabii Isa (Yesu, na Muhammad (a.s.). Kwa mfano ikitaja Sinai, ndiko Nabii Musa (a.s.) alikoongea

    n a M w e n y e z i M u n g u (s.w.t.) akapewa Kitabu cha Taurati (Torati). Inapoitaja Seiri pale ni huko Palestina, ambako Yesu (a.s.) alipokea Wahyi (Ufunuo Kiungu). Na ikitajwa Paran ndiko ambako Mwenyezi Mungu (SWT) Alikojidhihirisha Yeye Mwenyewe kwa walimwengu kwa mara mwisho kwa Wahyi Wake Aliyompelekea Nabii Muhammad (s.a.w).

    Paran ni safu ya milima kule Makka . Imeta jwa katika Taura' Torati ya Biblia katika aya nyingi pamoja na aya hii ifuatayo: 21:19,21, kuwa mahali pale ni jangwani ambako Hajiri (Hagar) alikoachwa na mume wake , lbrahimu (a.s.) ili aishi na mwana wao, Ismail aliyekuwa mwana wa kwanza wa Nabii Ibrahim na mkewe Hajar, na kwa kuwa wote wawili, hususan mwanawe Ismail, walikuwa na kiu sana, Mwenyezi Mungu (SWT) Akamtengenezea kisima cha maji ya Zamzam. Kumbuka Muhammad s.a.w ni kizazi cha Nabii Ismail, wakati Yesu (a.s) ni kizazi cha Ishaq (Isaka au Isaac), na wote wawili-Muhammad na Yesu na baba zao wakuu (wahenga wao), yaani Ismail na Ishaq ni ndugu, kwa kuwa wote ni vizazi vya babu yao mkuu Nabii Ibrahim (a.s).

  • 10 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 29- JUNI 4, 2015Makala

    MWEZI Machi mwaka huu, baadhi ya vyombo vya habari vya Marekani vilitoa habari yenye kichwa cha habari:

    Clarion Project: Fake Terror Expert Ryan Mauro Refuted By Chicago-Area Police.

    Kwa mujibu wa taarifa za gazeti la Chicago (Chicago Tribune), Ryan Mauro katika kipindi chake katika Fox News alikuwa amedai kuwa sehemu moja ijulikanayo kwa jina la Oak Brook, kule Chicago, kulikuwa na kambi ya Mujahidina na Waislamu Siasa Kali, akishangaa ni kwanini magaidi hao hawajachukuliwa hatua wakati wana hatarisha usalama wa Chicago na Marekani kwa ujumla.

    Taarifa hizo ziliwastua wananchi wa eneo hilo ambapo, maofisa wa serikali za miji na mitaa pamoja na wananchi waliwasiliana na Idara ya Polisi kutaka ufafanuzi juu ya taarifa hizo. Kwa vile Idara ya Polisi katika Chicago, katika majalada yake na hata katika uchunguzi wake baada ya kupata taarifa za Fox News, hawakuona kambi hizo za kigaidi, ilibidi watafute taarifa zaidi kutoka FBI.

    The village president and manager contacted me about concerns about it. We started looking at any organization with any kind of connections and couldnt find any.

    Ilisema taarifa ya Mkuu wa Idara ya Polisi, James Kruger, katika eneo la Oak Brook, Chicago, akimaanisha kuwa pamoja na kufanya uchunguzi wa taasisi zote, hawakuweza kugundua hata moja ambayo inaweza kuhusishwa na madai ya Mchungaji Mtaalamu Ryan Mauro wa Clarion Project.

    Katika uchunguzi wao, Polisi wanasema kuwa, kama ni taasisi za Kiislamu ni ile iitwayo North American Islamic Trust, iliyopo 721 Enterprise Drive, Oak Brook halikadhalika Islamic Center of Oakbrook Terrace iliyopo 1S270 Summit Ave., Oakbrook Terrace. Na zote hizo wanazifahamu na hazina matatizo.

    Hata hivyo, kutokana na jinsi kitisho kilivyokuwa kikubwa na kilivyokuwa kimewahamanisha watu wa Chicago, ilibidi Mkuu wa Polisi Bwana James Kruger kutafuta usaidizi kutoka FBI.

    They said it is a legitimate place of business; there are no threats or other concerns in the village. FBI said the Islamic Center of Oak Brook Terrace

    Siasa kali, wachambuzi feki

    MTU huyu angekuwa Muislamu, je, asingeshitakiwa kwa kosa la ugaidi?

    Would This Man Be Charged With Terrorism If He Were Muslim?

    Haya ni maneno ya baadhi ya wananchi wa Marekani, kama yalivyojitokeza katika mitandao ya kijamii. Wananchi hao wamekuwa wakiulizana katika mwezi huu wa Mei kufuatia kisa cha mtu

    Mheshimiwa Mbunge alikoseaAskofu hawezi kuwa gaidi!Na Omar Msangimmoja aliyetaka kuwaangamiza Waislamu wote wa eneo la Islamberg, New York.

    Hili pia ndio swali alilouliza Mbunge wa Vi t i Maalum, kutoka Pemba (CHADEMA), Mheshimiwa Maryam Salum Msabaha pale Bungeni Dodoma.

    Hoja ya Mbunge Maryam ilikuwa juu ya anachoona udhalimu na uonevu wanaofanyiwa Masheikh kutoka Zanzibar waliopachikwa tuhuma za ugaidi.

    Leo nataka niseme tena kwa kinywa kipana. Ingekuwa ni Mapadri na Maaskofu, wamo mle

    ndani, leo kungekuwa na amani Tanzania Bara?

    Hili ndio swali la Mheshimiwa Maryam Msabaha. Ni swali nzuri. Lakini alichosahau Mheshimiwa Mbunge Maryam ni kuwa Askofu au Padri hawezi kutuhumiwa kufanya ugaidi. Hili ni neno kwa watu maalum na kwa malengo maalum ya mabeberu. Na sie huku tunatumikishwa tu. Na mwisho wa yote, kujiangamiza kwa

    is not a concern.Hiyo ilikuwa taarifa ya Idara

    ya Polisi kwa serikali na watu wa Chicago, kwamba hata FBI wamekanusha na kusema kuwa hakuna taasisi yoyote ya Kiislamu ndani ya Chicago ambayo ina tuhuma za ugaidi au kuwa na kambi za kutolea mafunzo ya kijeshi.

    Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa Chicago wanasema kuwa, taarifa hiyo ya FBI, imekuja katika sura hiyo kutokana na namna watu walivyolifuatilia jambo hilo. Hapakuwa na namna ya kutoa taarifa za urongo kwa sababu wasingeweza kuzithibitisha na watu walikuwa wakifuatilia.

    Thank God the FBI didnt see this as an opportunity to manufacture its own terror plot in Oak Brook, like it has in other places.

    N d i v y o w a t u walivyosambaziana taarifa kuwa Ryan Mauro alitoa taarifa ya kitisho cha ugaidi Chicago, wakati haikuwa katika mpango wa FBI kutengeneza kitisho cha ugaidi katika eneo hilo.

    Lilipotokea lile shambulio la bomu katika kanisa la Josefu Mfanyakazi, Arusha, baadhi ya vyombo vya habari vilianza k u s e m a k u wa m u h u s i k a alionekana akiwa amevaa kanzu. Lakini hata tulipoamua kama nchi na kama serikali tufunge mpaka wetu tuwachunguze watu wanaoingia au kutoka kupitia Namanga, basi tuliofanikiwa kuwaona kuwa wanaweza kuwa watuhumiwa wa kuanza nao, walikuwa Waarabu!

    Zimewahi kutolewa kauli huko nyuma, bila kutolewa ushahidi wala watuhumiwa kufikishwa mahakamani, kuwa kuna Waislamu wanapanga kushambulia makanisa na kuuwa viongozi wa Kikristo. Taarifa kama hizo zikapewa umuhimu mkubwa katika vyombo vya habari halikadhalika vyombo vyetu vya usalama.

    Ni mara kadhaa jeshi la polisi limetangaza kuyalinda makanisa ama siku za Jumapili au katika Sikukuu kama za Krismasi. Lakini yote hayo yanakuja katika mazingira yanayotoa sura kuwa watuhumiwa wanaohofiwa ni Waislamu.

    Hili ndio tatizo. Kuendesha propaganda za kupandikiza chuki

    Inaendelea Uk. 11

    Inaendelea Uk. 11

    Robert R. Doggart

  • 11 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 29- JUNI 4, 201511 AN-NUURMakala

    Siasa kali, wachambuzi fekiInatoka Uk. 10kinyume kabisa na hali halisi ya wananchi tunavyoishi mitaani. Na kwa bahati mbaya, vyombo vyetu vya habari, na hata vya usalama na baadhi ya wanasiasa wetu, wamekuwa wakihusika katika propaganda hii chafu.

    Iliwahi kutolewa habari katika moja ya magazeti ya kila wiki hapa nchini kuwa Masheikh wa UAMSHO, walikuwa wameandaa kikosi na kukodi boti maalum, kuleta kikosi hicho Dar es Salaam ili kusaidia kikosi cha Waislamu wa Dar es Salaam kuchoma makanisa Mbagala.

    Pamoja na kuwa wanaotupiwa tuhuma hizi za ugaidi ni Masheikh wa UAMSHO, lakini tuhuma kubwa zaidi ni, kwanza kwa Serikali ya Zanzibar na Vikosi vyake. Kwamba, wao wanaruhusu Masheikh wa UAMSHO wanakusanya kikosi cha magaidi, mpaka wanakodi boti ya kuleta kikosi hicho Dar es Salaam, wao hawana habari!!! Mpaka leo hatujasikia kesi iliyofunguliwa dhidi ya mwenye boti aliyekodiwa kuleta magaidi Dar es Salaam, wala SMZ kutoa kauli kuwa taarifa zile zilikuwa urongo mtupu!

    L a k i n i m t u h u m i w a n a mshutumiwa mwingine ni serikali ya Dar es Salaam, kuanzia Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, boti ilikotia nanga (Mbweni) kushusha magaidi, Mkuu wa Mkoa na vyombo vya usalama vilivyo chini yake. Taarifa zilisema kuwa boti ya kukodi ilishusha magaidi Mbweni kisha wakapanda daladala hadi Tandika.

    Kama ilivyokuwa kwa wale wakuu wa serikali na Polisi katika Chicago, tulitarajia kuwa watu hao wa serikali ya Dar es Salaam, wangelifuatilia suala hilo na kutoa taarifa, ama ya kuthibitisha na kueleza hatua walizochukua au kukanusha ili kuwatoa wananchi hofu ya kitisho cha Masheikh wa UAMSHO walioletwa Dar es Salaam kusaidia harakati za kuchoma moto makanisa!

    Hilo halikufanyika. Kimyaa! Badala yake wanasiasa wetu na polisi wetu, walibaki kutoa kauli kama zile zile za gazeti na akina Mchungaji Ryan Mauro, kwamba kuna Waislamu wanapanga kuchoma moto makanisa na kuuwa viongozi wa Kikristo.

    Kwa tuhuma nzito kiasi hicho,

    unadhani Mkristo atamfikiria vipi Muislamu wa nchi hii!

    Kwa hiyo, leo unapozungumzia habari za Sheikh Msellem, Mtanzania wa Bara, awe Muislamu au Mkristo, anamtizama kwa jicho na sura iliyopakwa na gazeti lile kuwa ni gaidi aliyeandaa kikosi cha magaidi kuja Dar es Salaam kusaidia uchomaji Makanisa na kuuwa viongozi wa Kikristo!

    Kwa hiyo, wewe ukisema, Sheikh Msellem anadhulumiwa, hawezi kupata huruma ya Watanzania wenzake Wakristo wala Waislamu wenzake (walio wengi).

    Hili ndilo tatizo lililowazalisha akina Robert R. Doggart kule Marekani. Na kwa bahati mbaya, kwa vile akina Robert wana matawi ya makanisa yao huku, wametuletea mikakati na chuki zao hizo hizo. Lakini kwa bahati mbaya tena, tena hii mbaya zaidi, akina Robert walio katika FBI, ndio hao hao tumewachukua kuwa ni wataalamu wetu katika Counter Terrorism zao walizobuni kwa malengo yao na kutupatia vikosi na vitendea kazi.

    K u l e C h i c a g o Wa i s l a m u walimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa wakati akina Ryan wakipika propaganda zao, FBI haikuwa na mpango wa kufanya Sting Operation au mkakati wowote wa Entrapment katika eneo la Oak Brook.

    Kitendo cha serikali ya Zanzibar na ya Dar es Salaam, kukaa kimya, bila kusema chochote juu ya tuhuma kuwa Masheikh wa UAMSHO walikodi boti ya magaidi kuja Dar es Salaam kusaidia zoezi la kuchoma moto makanisa, inatufanya tuwe na wasiwasi kuwa kuna mambo mazito yanaendelea katika kushikiliwa Masheikh hawa, ambayo si rahisi kwa mwananchi wa kawaida kuyajua.

    Kule Chicago ilikuwa bahati nzuri kwa Waislamu wa Oak Brook. Wakamshukuru Mungu kwa kusema:

    Thank God the FBI didnt see this as an opportunity to manufacture its own terror plot in Oak Brook, like it has in other places.

    Katika hil i la akina Sheikh Msellem, yaelekea kuwa tofauti. Ndio maana pengine hata Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda anaomba ufafanuzi Mzee Sanya amwambie, Masheikh hao kina nani na wanakabiliwa na tuhuma gani!

    Askofu hawezi kuwa gaidi!Inatoka Uk. 10mikono yetu kama inavyotokota Kenya na Nigeria.Katika kesi ya New York, Bwana mmoja Mkristo siasa kali, akitajwa kwa jina la Robert R. Doggart alitangaza kuwa anakusudia kuwaangamiza Waislamu wote wa Islamberg pamoja na kuchoma moto misikiti yao na kubomoa nyumba zao. Islamberg, ni eneo linalokaliwa na Waislamu wengi katika Jimbo la New York, Marekani.

    Kat ika kuonyesha kuwa hakukosea na kwamba kweli kadhamiria kuwaangamiza Waislamu kama akipata fursa, Robert alipofikishwa mahakamani, hakuleta lugha za kuzunguka wala kujitetea. Alitamka wazi mbele ya mahakama kuwa anakusudia kufanya jinai hiyo.

    Robert R. Doggart admitted to plotting to kill residents in Islamberg, a Muslim area in the state of New York.

    N d i v y o i l i v y o r i p o t i w a ikionyesha hali i l ivyokuwa mahakamani katikati ya mwezi huu, na hivyo kuifanya kesi hiyo kuwa nyepesi na iliyochukua muda mfupi.

    Robert R. Doggart (63) ambaye mwaka jana 2014 aligombea ubunge katika Bunge la Congress, akitaka kuwawakilisha wakazi wa Tennessee, alikamatwa Aprili 10, baada ya kusambaza habari za dhamira yake ya kutaka kwenda kuwaangamiza Waislamu na

    kuchoma Misikiti yao. Doggart alitangaza kufanya mashambulizi hayo akishirikiana na Wakristo wenzake siasa kali (right-wing militia- OAF)

    We will burn down their buildings (and) if anyone attempts to, uh, harm us in any way, our stand gunner will take them down from 350 yards away. The standoff gunner would be me.

    Were gonna be carrying an M4 with 500 rounds of ammunition, light armour piercing, a pistol with three extra magazines, and a machete.

    And if it gets down to the machete, we will cut them to shreds.

    Hiyo ni kauli ya Doggart

    akieleza jinsi yeye na wenzake watakavyowauwa Waislamu wa Islamberg, New York, kuchoma majengo na Misikiti yao, na aina ya silaha watakazotumia.

    Pamoja na uzito wa kesi hii, lakini inaonekana kupita kimya kimya kwa sababu, kwanza vyombo vya usalama, FBI, na wengine, hawajaifanya kuwa ni habari. Uzoefu unaonyesha kuwa inapokuwa ni jambo limemuhusu Muislamu, hata likiwa dogo kiasi gani au hata ikiwa ni katika zile sting Operation zao, basi itaitishwa Press Conference, ambapo wanausalama watatoa taar i fa juu ya j ambo h i lo linalomuhusu Muislamu.

    Hata hivyo, kwa hili la Robert na siasa kali wenzake Wakristo l a k u a n g a m i z a Wa i s l a m u

    Inaendelea Uk. 16

    WANAODAIWA kujifunza ugaidi marekani

  • 12 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 29- JUNI 4, 201512 Tangazo/MASHAIRI

    SUMU YA HARAKATI ! Kalamu nimeishika, kutoa yangu indhari, Lengo ipate kufika, Bara nako Zanzibari, Kwa kila anohusika, na haya ajihadhari, Umimi, mali na vyeo, ni sumu ya harakati. Mambo haya kwa hakika, chimbuko la nyingi shari, Sahali kubanangika, umma kwa kuyakhitari, Aula kuyaepuka, mambo haya ni hatari, Umimi, mali na vyeo, ni sumu ya harakati.

    Umimi ebu kumbuka, ya ibilisi fakhari, Baidi 'livyomuweka, na rehema za Qahari, Kwa sijida kukiuka, kisa umbole la nari, Umimi, mali na vyeo, ni sumu ya harakati.

    Ruwazaye kuishika, twahisi ni ufakhari, Kumbe ni kujahilika, na za dunia ghururi, Nadra kumkinika, sote kuwa Maamiri, Umimi, mali na vyeo, ni sumu ya harakati. Kulikoni kuutaka, kila mtu Uamiri !Hata nyumbayo mulika, mu wangapi Maamiri ?U wahidu kwa hakika, upinge au ukiri,Umimi, mali na vyeo, ni sumu ya harakati. Fulusi mbele kuweka, jengo kutaliathiri, Malengo tuloyaweka, sahali kuyahajiri, Kwa mwake ndani kusaka, ghawazi na utajiri, Umimi, mali na vyeo, ni sumu ya harakati. Uluwa pia kutaka, kwa sasa tumekithiri, Kwa hili twahangaika, huku na kule twajiri, Kwa mioyo kutoridhika, jengo kutalidamiri, Umimi, mali na vyeo, ni sumu ya harakati. Haya tusipoepuka, wenyewe twajisihiri, Tujaribu kuridhika, bado tawili safari, Kwa hili kulikiuka, hatutafika dahari, Umimi, mali na vyeo, hilaki ya harakati. ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.

    1. Naanza kuwasabahi, ndugu zangu IslamuNimekuja asubuhi, nipatieni kalamuIli nipate kuwahi, niwemo katika zamuMasikini paka wangu, amefariki dunia

    2. Paka niliyempenda, sasa ameshafarikiNilimuona kakonda, kumbe yu katika dhikiAlishikwa na vidonda, mwili hautamanikiMasikini paka wangu, amefariki dunia

    3. Mwenzenu nina majonzi, kwani nimeondokewaTena ni kubwa simanzi, fadhaa imeningiaPaka wangu ni kipenzi, sote tulimzoweaMasikini paka wangu, amefariki dunia

    4. Paka sifa alipata, hapa mtaani kwetuKila unapomkuta, katulia kama mtuNa wala hana matata, paka ni mpenda watuMasikini paka wangu, amefariki dunia

    5. Paka halikuwa jizi, kama yalivyo mengineKuiba vilivyo wazi, avitafune tafuneAli paka msikizi, tapata wapi mwengineMasikini paka wangu, amefariki dunia

    6. Kwa kuwinda usiseme, paka huyu ni hodariPanya wake kwa waume, wote akiwavinjariNyumba ilikuwa kame, kaimaliza hatariMasikini paka wangu, amefariki dunia

    7. Mwengine nileteeni, msiifanye ajiziAkizowea nyumbani, atanifanyia kaziFanyeni hima jamani, mi ukiwa siuwezi Masikini paka wangu, amefariki dunia

    8. Nairejesha kalamu, yatosha niliyonenaNani wakumlaumu, ni shani ya MaulanaHakuna kinachodumu, mauti yametubanaMasikini paka wangu, amefariki dunia

    Mtunzi:Zainab Hamisi Mtima

    Mbweni, Zanzibar Tel:- 0777 357 031

    MASKINI PAKA WANGU

    Waislamu wote nchini mnaalikwa kuhudhuria Tamasha la Ujenzi wa Kituo cha Kiislamu Ilongo Mbeya litakalofanyika kuanzia tarehe 05, 12 Juni, 2015.

    Shime Waislamu tujitahidi kuhudhuria kwa wingi. Wasio na wasaa wa kuhudhuria wachangie fedha na vifaa vya ujenzi.

    Tukumbuke, tukifanya hivyo tutakuwa tumefanya biashara na Allah (s.w) kwa mafanikio ya hapa duniani na malipo ya Pepo Quran (61:10-13)

    Usafiri / Gharama: Kutokana na Miundombinu ya barabara kwa sasa kila mkoa utaratibu safari ya Mbeya kupitia Maamir wa Mikoa

    Kwa kupitia Dar es Salaam nauli ni Tshs. 70,000/- kwenda na kurudi Dar. Kuripoti Dar es Salam ni tarehe 04/06/2015 (0689665045/0713 992395).

    Kipindi hiki Mkoa wa Mbeya una baridi, hivyo wanatamasha waje na nguo za kuzuia baridi.

    Wabillah TawfiiqAMIR TAIFA

    TAMASHA LA KITAIFAILONGO MBEYA

    05 12 JUNI , 2015

  • 13 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 29- JUNI 4, 2015MAKALA

    BAADA ya kuandika makala kuhusu mazingatio kutokana n a m a j a n g a a m b a p o nilieleza jinsi Maskeikh wanavyodhalilishwa na kunyimwa haki zao za kimsingi kama raia, nilipata ujumbe wa simu kutoka kwa msomaji kama ifuatavyo:

    Sms kutoka kwa vijana wa Kisalafi Mwanakwerekwe, tunawaambia gazei la An nuur ya kuwa hakuna uadilifu kwa kuwatetea makhawarij (..... wa motoni) Mashekhe uchwara wa Uamsho.

    Pale ambapo nimeacha dashi ni kwamba sikuweza kuyanakili maneno halisi k u t o k a n a n a u k u b w a w a m a n e n o y e n y e w e (wametukana). Utashangaa, mtu anajiita Muislamu safi, salafi anayejibashiria Pepo, lakini anakuwa na kinywa cha kumtukana binadamu mwenzake, s i kwambii Muislamu!!!

    Sasa n imeonelea leo niandike kuhusu hawa Khawarij ni nani ili wasomaji waepukane na kasumba i n a y o e n e z wa n a wa t u wanaojiita Salafi. Kwa kweli fikra hii ni potofu sana na kama utaisoma makala hii kwa utulivu basi utaona ni Kundi gani hasa lenye hizo fikra za ki-Khawarij.

    Khawariji inatokana na neno la Kiarabu, khuruj maana yake ni kutoka. Na Kundi hili lilitoka katika Uislamu kwa kuvunja kiapo cha utiifu kwa Maamiri wa Dola ya Kiislamu na kuacha itikadi sahihi ya Kiislamu na kuwaua viongozi wa Dola ya Kiislamu. Itikadi kuu za Khawariji zilikuwa kama zifuatazo:

    Walikosea kuitafiri Qurani, na waliitafsiri wanavyotaka wao. Walikataa adhabu ya kaburi na walisema kuwa hakuna hodhi la Mtume ( S AW ) h u k o a k h e r a wala hakuna shufaa kwa Waislamu. Walikataa kusali sala ya Ijumaa ila chini ya Imamu wao. Walikubali ndoa bila ya walii. Hii ni kwa sababu waliwaona Waislamu wengi kuwa ni makafiri. Waliwakufurisha Waislamu wengi wakiwemo wale waliopigana vita vya Badri ambao walitabiriwa Pepo na Mtume (SAW). Pia waliwakufurisha, yaani waliwaita makafiri wale wale Masahaba waliokula kiapo cha utiifu chini ya mti ambao Allah (SW) aliwaridhia. Waliitakidi kwamba Ali (RA) na Muawiya (RA) wote ni makafiri na wanastahiki k u u wa wa . Wa l i wa z u i a wafuasi wao kuolewa na Waislamu wengine ila wenye itikadi ya kikhawariji kama wao, kwani wali i takidi kwamba Waislamu wote wasio na itikadi kama wao ni makafiri. Walipigana na Waislamu wenzao na k u w a u a w a k a w a a c h a

    Hatari ya Salafi bandiaChimbuko lake Saudi ArabiaLengo kulinda ufalme, uzayuni

    Na Mussa Ame

    makafiri. Hii ni kwa sababu waliitakidi kuwa Waislamu wenzao wamekufuru na wale Wakristo ni Dhimmi kwa hivyo wakawaua Waislamu w e n z a o w a k a w a a c h a makafiri.

    Imamu Ali (RA) alipigana nao katika vita vya Nahran (656 CE) na alifanikiwa kuwaua wengi wao, lakini baadye khawarij walikula njama ya kumua Ali (RA) na Muawiya (RA) ambapo Khawarij Abdulrahman Ibn Muljam alimuua Ali (RA).

    Wa l i a m i n i k w a m b a M u i s l a m u y e y o t e a t a k a y e f a n y a d h a m b i kubwa, hatosamehewa hata akitubu, na ataingia motoni na hatotoka motoni. Kwa hivi sasa duniani hakuna Kundi lenye sifa hizi kama Mtume(SAW) alizitaja sifa zao kwenye hadithi sahihi j a m b o a m b a l o l i l i m p a ushahidi Imamu Ali (RA) wa kuwaua kwani amri ya kuuliwa makhawariji aliitoa Mtume (SAW) mwenyewe, na yeye Imamu Ali (RA) alimsikia Mtume (SAW) kwa masikio yake

    Katika Sahihi Muslim kuna mlango wa kuwataja makhawarij lakini pia katika vitabu vyengine vya hadithi pia, nitanukuu hadithi za Sahihi Muslim (SM).

    Amesimulia Abiidhari (RA) Amesema Mtume ( S AW ) H a k i k a b a a d a yangu watakuwepo watu wanasoma Qurani lakini h a i t o w a i n g i a m o y o n i mwao, watatoka katika dini kama unavyotoka mshale kwenda katika kiwindwa kisha hawatorudi tena hao ni viumbe waovu(SM 1067 SB 3710).

    Amesimulia Ali (RA) nimemsikia Mtume(SAW) akisema watatokea katika zama za mwisho watu wenye umri mdogo wachache wa kufikiri, watasema maneno kama ya kheri kumbe ni shari, wataisoma Qurani h a i t a f i k a k o o n i k wa o , watatoka katika dini kama mshale unavyopiga shabaha, mtakapowakuta waueni hakika katika kuwaua kwao kuna ujira siku ya kiama(SM 1066 SB3611).

    Amesimulia Abuu Saidi ( R A) a m e s e m a M t u m e (SAW) Hakika katika asili ya mtu huyu kitatoka kizazi kinachosoma Qurani lakini hapiti zaidi ya kwenye koo (hawaifahamu) watawaua Waislamu na kuwaacha wa s h i r i k i n a , wa t a t o k a kwenye dini kama mshale unavyokwenda kwenye s h a b a h a n i n g e wa k u t a

    ningewapiga kipigo cha Adi(SB 2344 SM 1064)

    Ziko hadithi zaidi ya ishirini ambazo ni Muttafaq a layhi z inazowae lezea khawarija na kuwataja sifa zao na kuhalalisha kuwaua. Suala sasa linakuja, jee Mashekhe wa Uamso wana sifa hizi zilizotajwa katika hadithi hizi?.

    Sifa kubwa ya khawarij ni kuitakidi kuwa Waislamu wenzake ni makafiri na huwa ndiyo maadui wao namba moja (badala ya Mayahudi, makafiri khalisi na washirikina wa sampuli zote). Na suala la kujua ni nani mtu wa motoni, hilo anajua Allah (SW) peke yake hata Mtume (SAW) alikuwa hajui. Ndiyo maana katika vita vya Uhud vilipomalizika al iwasema vibaya wale waliongoza vita upande wa makafiri kumbe wengine walikuja kusilimu na wakawa Waislamu wazuri. Angalia kosa alilolifanya Sahaba la kuvujisha siri za kijeshi za Mtume (SAW), lakini Allah (SW) alipomgomba alisema Enyi mlioamnini msiwafanya adui zangu na adui zenu kuwa ni marafiki....(Mumtahina 1). Mtume (SAW) amekataza sana mtu kumwita Muislamu mwenziwe kafiri kwa sababu kama hana ule ukafiri, basi utamrudia yule aliyesema.

    N i m e n u k u u h a d i t h i chache kutoka katika Sahihi Trghyb (ST) ya Imamu Albany. Amesimulia Abii Dhar i (RA) amemsik ia Mtume (SAW) akisema Anayemwita mwenzake kafiri au akamwita adui wa Allah (SW) na hayuko hivyo, basi utamrejea mwenyewe (ukafiri) SB 6045 ST 2772).

    Amesimulia Thabit (RA) .Kumlaani Muislamu ni kama kumuua na anayemrembelea ukafiri muumini, ni kama aliyemuua (ST2776)

    A m a k u m w i t a M w a n a c h u o n i S h e i k h uchwara kwa kwel i n i aibu jambo hili kulifanya Muislamu anayesoma hadithi za Mtume (SAW) labda huwa anasoma haziingii moyoni mwake.

    Amesimulia Abii Hurayra ( R A) a m e s e m a M t u m e (SAW), Inatosha kuwa ni shari akamili kwa mtu kumdogosha ndugu yake Muislamu.(SM 2564).

    Sasa hoja iliyobaki, labla ni kuwa Mashekhe wa Uamsho wanakosoa utawala, kwa maana hiyo wanafanana na khawarij. Jawabu yangu kuhusu hilo ni kuwa hao Mashekhe wa Kisalafi ndiyo waliyoongoza kukosoa tawala

    zao kwa sababu hazikufuata itikadi zao. Kama hoja ni kufungwa jela, Maulamaa wa Kisalafu wanaongoza kwa kukaa sana gerezani, na labda nitoe mifano michache. Imamu Abuu Hanifa (703-767) alipigwa sana na Yazid Ibn Umar mtawala wa ukoo wa Umayya na alifungwa na Khalifa Aboo Jaafar Mansoor mpaka akafa gerezani . Imam Malik (717-801), alikamatwa akafungwa na akapigwa vibaya na Amiri wa Madina wa utawala wa Abbass. Imam Sufyan Thawwry (719- 777 ) alikosoa utawala wa Mnsoor wa ukoo wa Abbas alipelekewa barua ya kuwa Kadhi akaichana na Dola ya Abbass ikamuandama akajificha hadi kufa kwake ndiyo maana hata madhehebu yake hayakuandikwa.

    Imami Shafii (769-800) na Harun Rashid mwaka 805 akatiwa jela halafu akaachiwa. Imam Ahmad Ibn Hambal (778-885) aliwazidi wenzake kwa kukosoa utawala uliokuwa ukifuata falsafa za Muutazila ambao waliamini kwamba Qurani imeumbwa. Lakini Imam Ahmad alipinga hadharani hoja hizo. Akakamatwa na alifungwa miaka miwili na Khalifa Mamoon na alikimbia na kujificha kwa miaka mitano mpaka Khalifa Mutawakki l a l ipoingia madarakani (847-861).

    Ahmad Ibnu Tamymiya (1263-1328) alikosoa utawala na alitiwa ndani mara kadhaa kiasi kwamba muda mwingi aliutumia akiwa jela yeye na mwanafunzi wake Ibnu Jawzy. Sasa jee Mashekhe wa Uamsho wameleta lipi jipya.

    L a k i n i j a m b o l i n a l o s h a n g a z a k a t i k a msimamo wa wale wanaojiita Salafi ni kuwa ufahamu wao uko kinyume na hao Salafi wenyewe kwa sababu msimamo wa Salaf ni kuwa wao hawamtii ukafirini Muislamu kwa sababu tu ya kufanya kosa, mpaka atakapoj i tangaza kuwa amekufuru. Anasema Imam Nawawy katika sherhe ya Sahihi Muslim hadithi ya 56 Kitabu l Iman mlango wa 24 Wamekusanyika watu wa haki yaani Salaf wema kuwa mzinzi, mwizi ,muuaji na wengineo katika watendaji maovu, ukiacha shirki , hawawi makafiri kwa maasi hayo, bali huwa Waislamu il iyopungua imani yao, wakitubu husamehewa, na wakifa hawakutubu hukmu yao iko kwa Allah (SW). Itikadi hiyo ya Salaf wema pia imenakiliwa katika Aqida Tahawiyya Hakuna mtu katika watu wa kibla ambaye ni Muislamu ataitwa kafiri mpaka aoneshe ukafiri wa dhahiri(Aqida tahawiyya Ibnu Aziz Al Izz uk 268).

    Fikra hii imetoka wapi sasa ya kuwaita Maulamaa khawarij na kuwakufurisha Waislamu na kuwafanya

    maadui badala ya makafiri wa kweli? Fikra hii imezuliwa S a u d i A r a b i a w a k a t i Maulamaa wal ipokuwa wanaulaumu utawala wa Kifalme kwa kuegemea zaidi kwa Marekani na Isareli na kuacha misingi halisi ya Kiislamu ambayo ndiyo lengo la kuanzishwa Dola hiyo. Sasa ili kujilinda na lawama, Masheikh wanaoukosoa utawala huo wakapachikwa j i n a l a k h a w a r i j , n a M a u l a m a a wa l i o b o b e a katika Taaluma, wakaitwa makafiri, wakafungwa jela. Ndio unaona Ulamaa kama Said Qutbi akaitwa kafiri, kwawarij. Kitabu cha Fiqhi Sunna kikakatazwa kusomwa kwa sababu kimeandikwa na Sheikh Saidi Sabiq kutoka udugu wa Kiislamu.

    Tabliigh pia kwao wao ni haramu kwa vile inatishia kuwepo kwa utawala wao. Kwa sababu hi i , ndiyo maana utawala wa Saudia ukatoa fedha ili kuuangusha utawala wa Misri uliokuwa na muelekeo wa Kiislamu.

    Kwa i t ikadi yao hi i , basi kila mwanaharakati anayetetea Uislamu kwao ni khawarij na ni gaidi. Ndipo huko vijana mnakopelekwa. Angalieni sana. Kuweni makini. Hizo ni fikra za Kiyahudi. Mnapachikwa nazo mchukie Waislamu wenzenu mgombane nao, muwaitakidi kama makafiri wakati huo huo mnasaidia ukafiri. Na kwa fikra hizi mlizonazo, hamna msimamo wa Salaf wema ila mnafanana zaidi na hao khawarij. Mtume (SAW) amemaliza mambo, anayemrembelea mwenzake ukafiri na hali hanao ule ukafiri, humrejea mwenyewe.

    Makafiri wapo hawana utata wakifa bila kusilimu, basi ni watu wa motoni. Kwa nini basi hamuwalinganii hawa ili wasilimu. Kwanini mjigeuze miungu mhukumu Waislamu na kuwatia motoni, kabla siku ya hukumu, kazi ambayo hata Malaika hawakupewa. Hakuna mtu anayejijua asilimia mia kuwa ni mtu wa Peponi. Tunataraji tu kheri kwa Allah (SW), asi je akatugeuza mioyo yetu. Ndiyo maana dua kubwa aliyokuwa akiomba mwenyewe Mtume (SAW) ni: Yaa Muqalibal qulluub thabit qalby ala dynika .

    S a l a f w a l i k u w a wanyenyekevu mbele ya wenzao, na huo ndiyo uchamungu siyo kujikweza na kudharau watu. Bakari Ibn Abdillahi Al Muzni, alimsikia baba yake Ulamaa wa Salaf akisema, Ingekuwa sipo mimi hapa leo kwenye uwanja wa Arafa, ningesema watu wote wamesamehewa ( Hilyatu talibul ilm- sherhe ya Uthaymin 11/6).

    Hawa ndiyo Salaf, basi tufate nyendo zao.

    Ewe Allah (SW) tusaidie waja wako. Amyn.

  • 14 AN-NUURSHAABAN 1436, IJUMAA MEI 29- JUNI 4, 2015Makala

    Na Ben Rijal

    Na Ben Rijal

    Mchango wa Waislmau katika maendeleo ya Dunia - 12

    Fatilia kuandama kwa Mwezi

    UWANJA WA VIJANA - JIONGEZEE MAARIFACHEMSHA BONGO namba 7

    1. Aya gani katika Quran itajayo Chuma kwa manufaa ya mwanadamu? (2 :148, 57:25, 62 :40) Jawabu: 57:25 (Samahani kwa kosa niliandika 57 :28)

    2. Mamake Mtume Issa Bibi Maryam alipomzaa Mtume Issa alikuwa..(Mjane, Bikra, Mke wa mtu). Jawabu: Bikra

    3. Waislamu wanaamini kuwa Mtume Issa ali(Uwawa, Rufaishwa, Alijiua). Jawabu: Rufaishwa

    4. Anayaongoza Sala kwa Maamuma huitwa (Captain, Imam, Kiongozi) Jawabu: Imam

    5. Katika Quran neno Maisha limetajwa mara (185, 125, 145). Jawabu: 145

    6. Katika Quran neno Mauti limetajwa mara (6,655, 145, 125). Jawabu: 145

    7. Watoto wote wa Mtume Yaqoob ni (24, 11, 12). Jawabu:12

    8. Allah (Mwenye enzi Mungu (Anawashirika, Malaika Hanamshirika) Jawabu: Hanamshirika

    9. Tokeo lipi lilitojwa katika Quran mwaka mmoja kabla ya Hijra? Jawabu: Miraji

    10. Alipofariki mama yake Mtume SAW, Mtume Mohammad SAW alikuwa na umri wa miaka (7,8, 6) Jawabu: 6

    K a t i k a k u m z u n