file · web viewmtu anaweza jenga nyumba mzuri sana, lakini baada ya miaka michache...

16
Kanisa la ukweli‘‘Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, hata malango ya kuzimu hayataweza kulishinda” (Mathayo 16:18). Tunaishi katika dunia ambayo kila kitu kinaharibika. Mtu anaweza jenga nyumba mzuri sana, lakini baada ya miaka michache nyumba hii haitaonekana kuwa vizuri kama vile ilivyokuwa wakati ilijengwa. Na ikiwa mwenye nyumba hachungi nyumba yake vizuri, ataona kwamba baada ya miaka michache nyumba inaweza kuanguka kabisa. Hivi ndivyo maisha yanaendelea hapa ulimwenguni. Hili ni jambo la kutuhuzunisha sana. Wakati tunawaza juu ya mambo kama haya, tunajiuliza, “Je, kuna kitu chochote ambacho hakitaangamiza bali kitasimama milele? Je, kuna kitu ambacho hata kama dunia yote itaangamika, bado kitasimama? Jibu la swali hili ni, “Ndiyo.” Katika mstari huu Yesu Kristo anaongea kuhusu kitu kimoja ambacho hakitaangamika kamwe, bali kitaendelea milele na milele. Kitu hiki kimejengwa juu ya msingi ambaye ni Yesu Kristo mwenyewe na ni kanisa lake. Hii ndiyo maana ya maneno haya ya Yesu Kristo, ‘‘Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, hata malango ya kuzimu hayataweza kulishinda” (Mathayo 16:18). Kuna mambo matatu ambayo tunapata katika mstari huu. 1. Kwanza, kuna mjengo: “Kanisa langu.” 2. Pili, kuna mjenga. Yesu alisema, “Nitalijenga kanisa langu.” 3. Tatu, kuna msingi. Yesu alisema, “Juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu.” 4. Nne, kuna maadui: “Mlango ya kuzimu.” 5. Tano, kuna hakikisho ya ushidi: “Mlango ya kuzimu hayataweza kulishinda.” Ninaomba kwamba wote ambao watasoma maneno ya sura hii watabarikiwa na watajichunguza kuona kwamba wao kweli ni washiriki wa kanisa la Yesu Kristo. Ninakusihi, usome maneno haya na uangalifu sana na omba kwamba Mungu atakusaidia kuyafahamu. 1. Kwanza, kuna mjengo katika mstari huu. Yesu Kristo alisema, “Nitalijenga kanisa langu.” Je, kanisi hili ni nini? Hili ni swali muhimu sana. Kuna wengi ambao wanadai wao ni wakristo ambao hawafahamu kanisa ni nini, na kwa hivyo wamechanganyikiwa sana. Wakati Yesu Kristo anaongea kuhusu kanisa katika mstari huu Yeye hamaanishi mjengo wa mawe au mbao au mabati. Pia, Yesu hamaanishi kanisa la kianglikana au kibaptisti au kanisa lingine la aina hii. Wakati Yesu anaongea kuhusu kanisa hamaanishi lile kanisa ambalo linaonekana. Kanisa ambalo Yesu anamaanisha hapa ni wale watu ambao wameokoka kwa ukweli. Kanisa hili ni wale watu ambao wametubu dhambi zao na wamemwamini Yesu Kristo na kwa hivyo sasa ni viumbe vipya. Watu hawa

Upload: phamnga

Post on 06-Feb-2018

248 views

Category:

Documents


6 download

TRANSCRIPT

Page 1: file · Web viewMtu anaweza jenga nyumba mzuri sana, lakini baada ya miaka michache nyumba hii haitaonekana kuwa vizuri kama vile ilivyokuwa wakati ilijengwa

Kanisa la ukweli‘‘Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, hata malango ya kuzimu hayataweza kulishinda” (Mathayo 16:18).Tunaishi katika dunia ambayo kila kitu kinaharibika. Mtu anaweza jenga nyumba mzuri sana, lakini baada ya miaka michache nyumba hii haitaonekana kuwa vizuri kama vile ilivyokuwa wakati ilijengwa. Na ikiwa mwenye nyumba hachungi nyumba yake vizuri, ataona kwamba baada ya miaka michache nyumba inaweza kuanguka kabisa. Hivi ndivyo maisha yanaendelea hapa ulimwenguni.Hili ni jambo la kutuhuzunisha sana. Wakati tunawaza juu ya mambo kama haya, tunajiuliza, “Je, kuna kitu chochote ambacho hakitaangamiza bali kitasimama milele? Je, kuna kitu ambacho hata kama dunia yote itaangamika, bado kitasimama? Jibu la swali hili ni, “Ndiyo.” Katika mstari huu Yesu Kristo anaongea kuhusu kitu kimoja ambacho hakitaangamika kamwe, bali kitaendelea milele na milele. Kitu hiki kimejengwa juu ya msingi ambaye ni Yesu Kristo mwenyewe na ni kanisa lake. Hii ndiyo maana ya maneno haya ya Yesu Kristo, ‘‘Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, hata malango ya kuzimu hayataweza kulishinda” (Mathayo 16:18).Kuna mambo matatu ambayo tunapata katika mstari huu.1. Kwanza, kuna mjengo: “Kanisa langu.”2. Pili, kuna mjenga. Yesu alisema, “Nitalijenga kanisa langu.”3. Tatu, kuna msingi. Yesu alisema, “Juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu.”4. Nne, kuna maadui: “Mlango ya kuzimu.”5. Tano, kuna hakikisho ya ushidi: “Mlango ya kuzimu hayataweza kulishinda.”Ninaomba kwamba wote ambao watasoma maneno ya sura hii watabarikiwa na watajichunguza kuona kwamba wao kweli ni washiriki wa kanisa la Yesu Kristo. Ninakusihi, usome maneno hayana uangalifu sana na omba kwamba Mungu atakusaidia kuyafahamu.1. Kwanza, kuna mjengo katika mstari huu.Yesu Kristo alisema, “Nitalijenga kanisa langu.” Je, kanisi hili ni nini? Hili ni swali muhimu sana. Kuna wengi ambao wanadai wao ni wakristo ambao hawafahamu kanisa ni nini, na kwa hivyo wamechanganyikiwa sana. Wakati Yesu Kristo anaongea kuhusu kanisa katika mstari huu Yeye hamaanishi mjengo wa mawe au mbao au mabati. Pia, Yesu hamaanishi kanisa la kianglikana au kibaptisti au kanisa lingine la aina hii. Wakati Yesu anaongea kuhusu kanisa hamaanishi lile kanisa ambalo linaonekana.Kanisa ambalo Yesu anamaanisha hapa ni wale watu ambao wameokoka kwa ukweli. Kanisa hili ni wale watu ambao wametubu dhambi zao na wamemwamini Yesu Kristo na kwa hivyo sasa ni viumbe vipya. Watu hawa ni wateule wa Mungu na wamepokea neema kutoka kwa Mungu. Wao wameoshwa katika damu ya Yesu Kristo na wanavaa haki ya Yesu Kristo. Wao wameokoka kwa sababu wanamwamini Yesu Kristo pekee; wao wamezaliwa mara ya pili na wametakaswa na Roho Mtakatifu. Hawa ni watu ambao wanaishi kila mahali ulimwenguni. Wao sasa ni mwili wa Yesu Kristo; wao ni mfugo wa Kristo; wao sasa ni bibi yake Yesu Kristo. Hili ni kanisa ambalo Yesu anamaanisha katika mstari huu.Wakati tunaangalia mambo hapa ulimwenguni, tunaona makanisa mengi: kianglikana, kibaptisti, na mengine; lakini hawa wote ni washiriki wa kanisa moja: kanisa la Yesu Kristo hapa ulimwenguni. Watu wa kanisa hili wanamsifu Mungu wao kwa njia tofauti tofauti, na kila kanisa ni ya aina tofauti tofauti. Lakini moyoni wako pamoja: wote wanamwamini Yesu Kristo, wote wanampenda na kumtumikia Mungu, na wote wanamsifu kwa mioyo yao yote.Biblia inatufundisha kwamba wale wote ambao wameokoka kupitia kwa imani ndani ya Kristo wanaweza hudhuria na kushirikiana na makanisa tofauti tofauti, lakini pia wao wako washiriki wa kanisamoja, yaani lile kanisa ambalo linakusanya watu wote wa Mungu duniani kote. Haijalishi ni kanisa gani wanahudhuria kila wiki, wote ni watu wa Mungu ambao wameokoka kupitia kwa

Page 2: file · Web viewMtu anaweza jenga nyumba mzuri sana, lakini baada ya miaka michache nyumba hii haitaonekana kuwa vizuri kama vile ilivyokuwa wakati ilijengwa

imani ndani ya Yesu Kristo. Hawa watu wote ni watu tofauti tofauti na wako na uwezo tofauti tofauti, na wamepewa vipawa tofauti tofauti. Lakini wote ni watu wa Mungu ambao wameokoka na wote wanajua kwamba Mungu ni Baba yao na Yesu Kristo ni Mwokozi yao. Wote wanajua kwamba wao wamezaliwa mara ya pili kwa sababu Roho Mtakatifu amewaokoa. Wote wanajua kwamba wao ni sawa mbele ya Mungu, hakuna mmoja ambaye ni mkuu mbele ya Mungu kuliko wengine. Haifai kwa kanisa moja fulani kusema, “Sisi pekee ni watu wa Mungu, na wengine si watu wa Mungu wa kweli.” Wote ambao wameokoka ni watu wa Mungu.Kanisa la Mungu ni la thamani sana kwa Yesu Kristo. Yeye anaahidi kanisa lake kwamba kanisa halitaangamika, bali litaendelea milele. Pia, Yeye anaahidi kanisa lake kwamba Yeye mwenyewe atalilinda kanisa lake na kwamba watu wake wote watavumilia katika imani yao na kuingina mbinguni ile siku Yeye mwenyewe atarudi hapa ulimwenguni. Biblia inatufundisha wazi kwamba Mungu anawapenda watu wake na upendo wa milele. Hapa ulimwenguni kanisa la Mungu linawezadharauliwa na linaweza kuwa kidogo tu lakini mbele ya Mungu, kanisa lake ni la thamana sana; Yeye analipenda sana.Katika Agano la Kale tunasoma kwamba Solomoni alijenga hekalu ambalo lilikuwa kubwa sana na mzuri sana. Tunasoma kwamba hata wanafunzi wa Mungu waliona uzuri wa hekali hili. Lakini kanisa la Mungu hapa ulimwenguni ni la thamani zaidi kuliko hekalu hili. Kanisa la Mungu ni watu wa Mungu ambao wameokolewa na damu ya Yesu Kristo na hii ndiyo sababu kanisa la Mungu ni ya thamana sana moyoni mwake.Ni lazima wote ambao wameokoka wafahamu vizuri ni nini Biblia inatufundisha kuhusu kanisa. Kuna wengi ambaowamechanganyikiwa kuhusu jambo hili. Wakati Biblia inaongea kuhusu kanisa la Mungu, inamaanisha watu wote wa Mungu ambao wameokoka. Watu wa Mungu wote wanahitaji kutumia vipawa vyao kwa kuwafaidisha kanisa la Mungu.Ikiwa wewe bado hujaokoka, basi wewe si mshirika wa kanisa la Mungu. Pengine unahudhuria kanisa kila wiki, pengine umebatizwa na kuwa mkuu katika kanisa lako. Lakini ikiwa wewe hujaokoka, basi wewe si mshirika wa kanisa la Mungu. Ikiwa hii ni hali yako, ninakusihi uje kwake Yesu Kristo leo na kuokoka. Ukimwomba wokovu, basi utapata msamaha wa dhambi zako zote na utakuwa mshirika wa kanisa la Mungu. Hii ni kazi ya mahubiri wote: kuwaalika wote waje kwake Yesu ili wapate wokovu na waweze kuwa washirika wa kanisa la Mungu. Ukitaka kuokoka lazima uwe mshirika wa kanisa la Mungu. Hakuna yeyote ambaye anaweza kuokoka hadi akuwe mshirika wa kanisa la Mungu.2. Pili, katika mstari huu tunasoma kumhusu mjenga wa kanisa. Katika mstari huu, kwanza tunasoma mjengo ambao ni kanisa la Mungu, na pili, tunasoma kumhusu mjenga wa mjengo huu. Yesu Kristo alisema,“nitalijenga kanisa langu.”Biblia inatufundisha kwamba Mungu wa Utatu anapenda sana na kuchunga sana kanisa lake. Pia Biblia inatufundisha kazi ya kuwaokoa wenye dhambi ni kazi ya Mungu wa Utatu. Inatufundisha kwamba Mungu anawachagua wale ambao wataokoka, na kwamba Mungu Roho Mtakatifu atawaokoa wale ambao Mungu Baba amewachagua na kuwafanya wawe washirika wa mwili wa Yesu Kristo. Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu wote Watatu wanafanya kazi pamoja kuwaokoa wenye dhambi. Jambo hili ni la ukweli na sisi sote tunahitaji kulikumbuka kila wakati. Lakini, pia, Biblia inatufundisha kwamba kazi ya kulinda kanisa la Mungu ni kazi maalum ya Bwana wetu Yesu Kristo. Biblia inatufundisha wazi kwamba ni Yesu Kristo ambaye ni Mkombozi na Mwokozi wa kanisa la Mungu. Hii ndiyo sababu Yesu Kristo anasema katika mstari huu,“nitalijenga kanisa langu.” Yaani, Yesu Kristo anasema katika mstari huu kwamba kujenga kanisa la Mungu ni kazi yake maalum.Biblia inatufundisha kwamba ni Yesu Kristo ambaye anawaita watu wa Mungu waondoke dhambi zao na kuokoka na kuingia kanisa la Mungu. Biblia inasema, “Ninyi nyote pia mko miongoni mwa watu waliotiea ili mpate kuwa mali ya Kristo Yesu” (Warumi 1:6).

Page 3: file · Web viewMtu anaweza jenga nyumba mzuri sana, lakini baada ya miaka michache nyumba hii haitaonekana kuwa vizuri kama vile ilivyokuwa wakati ilijengwa

Biblia inatufundisha kwamba ni Yesu Kristo ambaye anawapa watu wake uzima. Biblia inasema, “Hakika kama vile Baba awafufuavyo wafu na kuwapa uzima, vivyo hivyo Mwana huwapa uzima wale anaopenda” (Yohana 5:21).Biblia inatufundisha kwamba ni Yesu Kristo ambaye anawaosha watu wake dhambi zao. Biblia inasema, “Kwake Yeye aliyetupenda na ambaye ametuweka huru kutoka katika dhambi zetu kwa damu Yake” (Ufunuo 1:5).Biblia inatufundisha kwamba ni Yesu Kristo ambaye anawapa watu wake amani. Yesu alisema, “Amani nawaachia, amani yangu nawapa, amani hii niwapayo si kama ile ulimwengu utoayo” (Yohana 14:27). Biblia inatufundisha kwamba ni Yesu Kristo ambaye anawapa watu wake uzima wa milele. Yesu alisema, “Nami ninawapa wumma wa milele, hawataangamia kamwe wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka katika mikono Yangu” (Yohana 10:28).Biblia inatufundisha kwamba ni Yesu Kristo ambaye anawapa watu wake kutubu dhambi zao. Biblia inasema, “Mungu alimtukuza akamweka mkono wake wa kuume kuwa kiongoi na Mwokozi ili awape Israeli toba na msamaha wa dhambi” (Matendo ya Mitume 5:31).Biblia inatufundisha kwamba ni Yesu Kristo ambaye anawawezesha watu wake wawe watoto wa Mungu. Biblia inasema, “Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndilo wale waliaminio Jina Lake” (Yohana 1:12).Biblia inatufundisha kwamba ni Yesu Kristo ambaye anawawezesha watu wake wavumilie katika imani yako. Yesu alisema, “Badokitambo kidogo ulimwengu hautaniona tena, ila ninyi mtaniona, kwa kuwa Mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai” (Yohana 14:19).Kwa ufupi, Biblia inatufundisha, “Kwa kuwa ilimpendeza Mungu kwamba ukamilifu Wakke wote wa kiMungu uwe ndaniYake” (Wakolosai 1:19). Biblia inatufundisha kwamba Yeye ni mwaandishi na yule ambaye anamaliza kazi yake ya kutuokoa (Waberania 12:2). Inatufundisha kwamba kila sehemu ya mwili wake (yaani kanisa) unalishwa naye: “Kutoka Kwake, mwili wote huunganishwa na kushikamanaishwa maoja kwa msaada wa kila kiwango, hukua na kujijenga wenyewe katika upendo, wakati kila kiungo kinafanya kazi yake” (Waefeso 4:16). Inatufundisha kwamba ni Yesu Kristo mwenyewe ambaye anawawezesha watu wake kumhudumia Mungu. Inatufundisha kwamba Yesu Kristo atawawezesha watu wake kuvumilia katika maisha yao ya ukristo na kuwapeleka kwa Mungu Baba siku ya mwisho bila dhambi au makosa yoyote. Yeye ni yote kwa watu wa Mungu na ako ndani ya kila mmoja ya watu wa Mungu.Biblia pia inatufundisha ni namna gani Yesu Kristo anafanya haya yote katika kanisa la Mungu. Inatufundisha kwamba anamtuma Roho Mtakatifu kufanya kazi yake katika kanisa lake. Roho Mtakatifu ako ndani ya kila kanisa ambalo ni kanisa la ukweli na anawaongoza watu wa Mungu katika njia ya Yesu Kristo. Ni Yeye ambaye anawaletea watu wa Mungu baraka kutoka kwa Yesu Kristo. Ni Roho Mtakatifu ambaye anawawezesha wenye dhambi kupokea neno la Mungu na kuokoka, ni Yeye ambaye anawaleta wale ambao wanaokoka ndani ya kanisa la Mungu, na ni Yeye ambaye anawatayarisha watu wa Mungu kwa ile siku ambayo Yesu Kristo atarudi kuwachukua wao ili wawe pamoja na Yeye milele. Wale ambao wameokoka bado hawajakamilika lakini bado wako na dhambi ndani yao. Ni kazi ya Roho Mtakatifu kuwakamilisha na kuondoa dhambi zao zote ili waweze kuwa tayari kwa ile siku watakutana na Bwana wao na Mwokozi wao Yesu Kristo.Kwa hivyo tunaona hapa kwamba kazi ya kujena kanisa la Mungu ni kazi ambayo Yesu Kristo mwenyewe anafanya, na kwamba anafanya kazi hii kupitia kwa kazi ya Roho Mtakatifu. Kazi ya kujenga kanisa ni kazi lake, ni Yeye ambaye analijenga kanisa.Wakati Yesu Kristo anafanya kazi hii ya kujenga kanisa lake, anatumia vitu vingi. Kwanza, anatumia mahubiri ya neno la Mungu. Wakati neno la Mungu linahubiriwa, wale ambao hawajaokoka wataokoka, na wale ambao wameokoka wanatakaswa. Pili, Yesu Kristo anatumia neno lake kujenga kanisa lake. Kila mmoja ambaye ameokoka na ni mshirika wa kanisa la

Page 4: file · Web viewMtu anaweza jenga nyumba mzuri sana, lakini baada ya miaka michache nyumba hii haitaonekana kuwa vizuri kama vile ilivyokuwa wakati ilijengwa

Mungu anapaswa kusoma neno la Mungu kilasiku na kuijifunza kwa sababu neno la Mungu ni chakula chao cha kiroho. Tatu, Yesu Kristo anatumia wakristo wengine kujenga kanisa lake. Wakati mtu anaokoka, anapaswa kuwa mshirika wa kanisa moja kwa sababu katika kanisa hili atapata mafundisho ya neno la Mungu na atapata nafasi ya kutumia vipawa vyake. Haya yote Yesu Kristo anatumia kujenga kanisa lake. Haya yote: mahubiri wa neno lake na watu wake, yote ni watumishi wake katika kazi hii ya kujenga kanisa lake. Hii ndiyo sababu Paulo alisema, “Mimi nilipanda mbegu, Apolo akatia maji, lakini Mungu ndiye aliyekuza” (1 Wakorintho 3:7).Wahubiri wa neno la Mungu wanaweza kuhubiri, waanishi wa vitabu wanaweza kuviandika vitabu, lakini ni Yesu Kristo pekee ambaye anajenga kanisa lake. Yeye anatumia mahubiri ya watumishi wake na vitabu vya watumishi wake, lakini kazi ya kulijenga kanisa ni kazi yake. Ikiwa yeye hafanyi kazi hii, wale ambao wanajaribu kulijenga kanisa wanafanya kazi yao bure: “Bwana asipojenga nyumba, wajengao hufanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji, walinzi wakesha bure” (Zaburi 127:1).Wakati tunaona kazi ya Yesu Kristo kujenga kanisa lake, tunaona mambo matatu.(i) Kwanza, Yesu Kristo anatumia hekima yake kujenga kanisa lake. Yeye anapanga kazi yake ya kujenga kanisa lake kwa uangalifu sana.Yeye anafanya kazi hii kama mjenga wa nyumba anafanya kazi yake ya kujenga nyumba ya mawe. Mjenga huyu anachagua kila jiwe na kulitayarisha kwa uangalifu sana na halafu kuweka katika mahali pake katika ukuta. Vilevile, Yesu Kristo anajenga kanisa lake na watu wake ni mawe ambayo anawatumia kulijenga kanisa hili. Na kama vile mjenga wa nyumba anachagua ni jiwe gani atatumia kwa mahali fulani katika ukuta na kutayarisha lile jiwe, Yesu Kristo anachagua ni nani atamtumia kwa kazi fulani katika ufalme wake, na kumtayarisha yule mtu kwa ile kazi. Wakati nyingine, anampa mtu wake fulani vipawa vingi na kumtumia kufanya kazi mingi sana, na wakati nyingine anampa mtu wake fulani vipawa vichache na kumtumia katika kazi ambayo inaonekana kuwa kazi kidogo tu. Haya yote ni hekima ya Yesu Kristo. Yeye ni mjenga wa kanisa lake.(ii) Pili, Yesu Kristo anatumia rehema yake wakati anajenga kanisa lake. Wakati nyingi, Yesu anatumia mtu ambaye haonekani kwamba anafaa kufanya kazi fulani. Pengine mtu fulani alikuwa mlevi na mwenye dhambi mkuu sana. Watu wa dunia wanaweza kuwaza kwamba mtu huyu hawezi kuokoka na kuwa mtumishi mkuu katika Ufalme wa Mungu. Lakini kwa hekima na rehema Yeke, Yesu anaweza kumwokoa na kumtumia sana kujenga kanisa lake. Mara mingi, Yesu Kristo amewaokoa wale ambao walikuwa wenye dhambi wakuu kama mtume Paulo na kuwatumia kwa kazi kuu sana katika Ufalme wake.(iii) Tatu, Yesu Kristo anatumia nguvu zake kujenga kanisa lake. Yesu Kristo ako na maadui mengi hapa ulimwenguni akifanya kazi yake ya kujenga kanisa lake. Watu wa dunia ambao hawajaokoka ni maadui wake; shetani ni adui yake, na pia dhambi ambayo imebaki ndani ya watu wake ambao wameokoka. Kanisa lake hapa ulimwenguni linapata mateso mengi na majaribu mingi hapa ulimwenguni. Lakini miongoni mwa haya mateso na majaribu yote, Yesu Kristo anaendelea kufanya kazi yake ya kujenga kanisa lake. Katika Agano la Kale tunasoma jinsi gani Sulemani alijenga hekaulikatika mji wa Yerusalemu. Tunasoma kwamba yeye alipanga vitu vyote vizuri sana na kwa uangalifu sana, na halafu alijenga hekalu hili. Kazi ya Yesu Kristo ni kazi ya aina hii, lakini ni kazi kubwa sana zaidi na kazi ya Sulemani. Sulemani alijenga hekalu katika mji wa Yerusalemu, Bwana Yesu Kristo anajenga kanisa lake ambalo linapatikana ulimwenguni kote. Kazi hii ya kujenga kanisa lake ni kazi ya nguvu.Ndugu zangu, watu wa dunia hawajali kamwe kazi hii ya kujenga kanisa la Mungu. Watu wa dunia hawajali chochote wakati mwenye dhambi mmoja anaokoka. Hawajali hata kidogo wakati mwenye dhambi huyu anahisi dhambi zake na anatubu dhambi zake. Mambo haya yote ni mambo ya upumbavu kwao. Lakini kwa watu wa Mungu mambo kama wokovu wa kila mwenye dhami ni jambo la kuwafurahisha. Biblia inatufundisha kwamba kanisa la Mungu linaweza kuwa kidogo na kudharauliwa na watu wa dunia, lakini kanisa hili ni kanisa la Mungu na Mungu

Page 5: file · Web viewMtu anaweza jenga nyumba mzuri sana, lakini baada ya miaka michache nyumba hii haitaonekana kuwa vizuri kama vile ilivyokuwa wakati ilijengwa

mwenyewe analijenge. Yesu mara mingi amefanya miujiza mikuu katika kazi yake ya kulinda na kuchunga kanisa lake. Pia Biblia inatufundisha kwamba Bwana Yesu anapanga mambo yote ya ulimwengu kwa ajili ya kanisa lake. Kwa ajili ya kanisa lake, vita kati ya mataifa vimesimamishwa na amani imepewa mataifa haya. Viongozi na wafalme wa mataifa ya ulimwengu wanapanga jinsi watatawala mataifa yao, na wanawaza kwamba wao ni watu wakuu sana. Lakini kuna kazi ingine ambayo inaendelea hapa ulimwenguni, na hawa viongozi na wafalme wa mataifa ni watumishi katika mikono ya Yesu Kristo kwa kazi hii. Kazi hii ni kujenga kanisa la Mungu. Wakati tunasoma Biblia tunasoma chache tu kuhusu viongozi na wafalme wa mataifa, lakini tunasoma mengi sana kuhusu watu wa Mungu. Kwa mfano, katika kitabu cha Mwanzo tunasoma chache sana kuhusu Nimrod, ambaye alikuwa mtu mkuu hapa ulimwenguni, lakini tunasoma sura nyingi kuhusu Abrahamu, ambaye alikuwa mtu wa kawaida tu, lakini alikuwa mtu wa Mungu. Biblia inaongea sanakuhusu watu wa Mungu. Mambo ya dunia hatupati sana katika neno la Mungu, ni mambo ya kanisa la Mungu ambayo tunapata ndani yake.Ndugu zangu, tunapaswa sana kumshukuru Mungu kwamba Yesu Kristo, ambaye ni mjengo wa kanisa lake ni mwenye nguvu zote. Tunapaswa kumshukuru Mungu kwamba kazi hii ya kujenga kanisa la Mungu hapa ulimwenguni si juu ya wahubiri wa neno la Mungu au juu ya wanadamu wengine. Yesu Kristo ataendelea kufanya kazi hii na ataendelea kutumia watu wa dunia, hata kama watu wa dunia hawajui kwamba Yeye anawatumia. Kristo hawezi kushindwa katika kazi hii, ile ambayo ameanza kufanya atakamilika bila shaka.3. Tatu, tuangazie msingi ambao juu yake kanisa la Mungu linajengwa.Yesu Kristo alisema, “Juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu.” Je, msingi huu ni gani? Je, ni mtume Petro? Jibu ni la! Yesu Kristo alikuwa akiongea na Petro na alisema “Juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu.” Yeye hakusema, “Juu ya wewe, Petro, nitalijenga kanisa langu,” bali alisema, “Juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu.” Hapa Yesu anaongea kuhusu yale maneno ambayo Petro alisema. Wakati tunasoma kifungu hiki tunaona kwamba kwanza Kristo aliwauliza wanafunzi wake,“Watu husema Mwana wa Adamu ni nani?” Wanafunzi wake walimjibu, “Baadhi ya watu jusema ni Yohana Mbatizaji, wengine jusema ni Eliya na bado wengine husema, ni Yeremia au mmojawapo wa manabii.” Halafu Yesu aliwauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?” Hapa Petro alimjibu, “Wewe nidwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai” (mstari 16). Ni ukweli huu, kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu aliye hai ambao ni msingi wa kanisa. Msingi wa kanisa ni Yesu Kristo na kazi yake ya Mwokozi wa watu wake na Mwakilishi wa watu wake. Msingi wa kanisa ni Yesu Kristo ambaye aliahidiwa na Mungu Baba, ni Yesu Kristo ambaye alikuja hapa ulimwenguni kukamilishawokovu wa watu wake wote. Huu ni mwamba ambao ni msingi wa kanisa, na kanisa la Mungu linajengwa juu ya mwamba huu. Mandugu zangu, msingi huu uliwekwa kwa gharama kubwa sana. Yesu Kristo alihitaji kuwa mwanadamu kamili na kukaa hapa ulimwenguni. Yeye alihitaji kuteswa na kufa, si kwa ajili ya dhambi zake, bali kwa ajili ya dhambi zetu. Alihitaji kuzikwa na kufufuka kwa ajili ya wokovu wa watu wake. Alihitaji kurudi mbinguni kama mwanadamu na kuketi mkono wa kuume wa Baba baada ya kumaliza kazi yake ya kuwaokoa watu wake kupitia kwa kifo chake. Huu pekee ni msingi wa kanisa la Mungu. Hakuna msingi ingine ambao unaweza kubeba kanisa la Mungu hapa ulimwenguni, Yesu pekee tu anaweza kulibeba kanisa juu yake na kuwa msingi wa kanisa lake.Msingi huu ni wa nguvu sana. Yesu Kristo alibeba dhambi za watu wake wote wakati alikuwa juu ya msalaba. Alibeba dhambi za mawazo yao mabaya, alibeba dhambi za mioyo yao, alibeba dhambi zao ambazo zilionekana wazi na zile ambazo zilifichwa kabisa. Yeye alibeba dhambi zao ambazo walifanya dhidi ya Mungu na dhidi ya wanadamu wengine. Yesu Kristo alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi za watu wake na alizibeba dhambi zao zote. Kwa hivyo yeye anaweza kuwa mwakilishi kwa watu wake wote.Juu ya msingi huu, watu wake wote wanajengwa. Hata kama watu wake wako katika makanisa tofauti tofatui, wote wanasimama juu ya msingi mmoja, ambaye ni Yesu Kristo Mwokozi wao.

Page 6: file · Web viewMtu anaweza jenga nyumba mzuri sana, lakini baada ya miaka michache nyumba hii haitaonekana kuwa vizuri kama vile ilivyokuwa wakati ilijengwa

Wote wanajenga maisha yao ya ukristo juu yake, wote wanapata amani kutoka kwake, wote wanamtumaini na wote wanajua kwamba ile siku yeye atarudi, watakuwa pamoja naye milele. Haya yote wanapata kutoka kwake Kristo ambaye ni msingi wa ukristo wao. Wao wote wanajua kwamba Yesu Kristo ni mwakilishi kati ya wanadamu na Mungu na kwamba Kristo ni Kuhani Mkuu wa watu wake; wote wanajua kwamba ni yeye pekee ambaye anawaahidi watu wake uzima wa milele.Sisi sote tunapaswa kujichunguza kuhusu jambo hili. Je, wewe unasimama juu ya mwamba ambaye ni Yesu Kristo? Je, wokovu wako unatoka kwake? Mungu ameweka msingi huu hapa ulimwenguni ili wenye dhambi wanaweza kusimama juu ya msingi huu. Kuna wengi ambao wanadai wameokoka lakini wakati unaona ni msingi gani wanasimama juu yake, utaona si Yesu Kristo, bali ni kitu kingine. Hawa hawataokoka siku ya mwisho. Yule ambaye ako ndani ya Yesu Kristo, basi yeye pekee ataokoka.Rafiki yangu, hakikisha kwamba wewe umejichunguza vizuri sana kuona kama kweli umeokoka au la. Wewe pekee unaweza kujua kama kweli umeokoka au la, wengine hawawezi kujua jambo hili. Wengine wanaweza kuona kwamba unahudhuria kanisa kila wiki na kwamba unahudhuria Meza ya Bwana, lakini hawawezi kuona kama wewe kweli unamwamini Yesu Kristo pekee kwa wokovu wako. Kumbuka kwamba siku moja sisi sote tutasimama mbele zake na kuhumumiwa. Siku ile dhambi zako zote, haswa zile dhambi ambazo umezificha sana zitafunuliwa. Kwa hivyo usiseme tu kwamba unahudhuria kanisa kila wiki na kwamba wewe ni mkristo. Hakikisha kwamba kweli wewe umeokoka. Bila wokovu, hutapata faida yoyote kuhudhuria kanisa kila wiki na kuhudhuria Meza ya Bwana. Hakikisha kwamba kweli umeokoka.Rafiki yangu, chunguza vizuri msingi wa imani yake kuona kama kweli wewe ni msiriki wa kanisa la kweli au la. Usiseme tu, “Ninahudhuria kanisa kila wiki kwa hivyo mimi ni mshiriki.” Mimi siongei kuhusu kanisa ambalo unahudhuria, bali kanisa la Kweli la Kristo. Je, wewe ni mshiriki wa kanisa hili? Hili ni jambo ambalo wewe pekee tu unaweza kujua. Wengine wanaweza kuona kwamba unahudhuria kanisa kila wiki, lakini hawawezi kuona kama umejenga ukristo wako juu ya Yesu Kristo mwenyewe. Wengine wanaweza kuona wakati unahudhuria meza ya Bwana, lakini hawawezi kuona kama katika moyo wako unashirikiana na Kristo mwenyewe. Lakini siku moja haya mambo yote yatajulikana. Siri yakila mtu itafunuliwa. Pengine unahudhuria kanisa kila wili na unajulikana kuwa mtu wa maombi. Haya ni mambo mazuri. Lakini usikose katika hili jambo la wokovu wako. Hakikisha kwamba imani yako iko ndani ya Yesu Kristo pekee. Bila imani ndani Yake, ukristo wako ni tupu na bila maana au faida. Bila imani ndani ya Yesu huwezi kusimama ile siku ya hukumu. Hakikisha kwamba unamwamini Yesu Kristo pekee kwa wokuvu wako.4. Nne, tuangazie kwamba kanisa la Yesu Kristo hapa ulimwenguni litakumbana na majaribu mengi.Yesu Kristo hapa anaongea kuhusu “malango ya kuzimu” kwa kumaanisha kwamba kanisa lake hapa ulimwenguni litakuwa katika vita wakati wote hapa ulimwenguni na litakumbana na majaribu mengi sana hapa kwa sababu kanisa lake hapa ulimwenguni liko na adui mmoja mkuu: shetani. Hii ndiyo sababu watu wa Mungu wakati wote wamekuwa katika vita. Wao wako na adui mmoja ambaye anachukia sana kanisa la Mungu na yeye anapigana vita na watu wa Mungu kila wakati. Yeye pia hutumia watu wa ulimwengu huu katika vita hivi, ili wale ambao hawajaokoka watachukia watu wa Mungu na kupigana vita nao. Shetani hawezi kuiba urithi wao wa maisha ya milele mbinguni, lakini yeye anaweza kujaribu sana warithi wa mbinguni na hii anaifanya kila wakati.Wakati tunasoma historia ya dunia tunaona kwamba kila wakati watu wa dunia wamesimama dhidi ya watu wa Kristo na kuwatesa. Katika Biblia tunasoma kuwahusu watu kama Farao na Herode, na katika historia tunasoma kuwahusu wafalme wa taifa la Warumi ambao waliwatesa watu wa Mungu na kuwaua wengi wao. Watu wa Mungu wa kila wakati watakuwa na vita hivi dhidi ya shetani na watu wake. Watu wa Mungu hapa ulimwenguni wanaweza kuwa na wakati

Page 7: file · Web viewMtu anaweza jenga nyumba mzuri sana, lakini baada ya miaka michache nyumba hii haitaonekana kuwa vizuri kama vile ilivyokuwa wakati ilijengwa

ambapo wengi wanasikia neno la Mungu na kuokoka, lakini hii haimaanishi hakuna vita dhidi ya shetani. Sisi watu wa Mungu hatutapata amani hapa ulimwenguni. Tunaweza kuwa na amanimioyoni mwetu, lakini hatutakuwa na amani miongoni mwa watu wa ulimwengu.Kila mmoja ambaye ameokoka atapata kwamba maisha yake ya kila siku ni maisha ya vita dhidi ya shetani na watu wake. Kila mmoja anapaswa kupigana vita hivi. Wakati tunasoma kuhusu maisha ya wale ambao walikuwa hapa ulimwenguni na waliokoka, tunasoma kwamba wao walipigana vita maisha yao yote dhidi ya shetani. Mitume kama Paulo, Yakobo, Petro na Yohana walipata majaribu mengi sana hapa ulimwenguni na maisha yao yote yalikuwa maisha ya vita. Wakati nyingine wao wenyewe waliteswa na wakati nyingine, mali yao ilichukuliwa. Watu wa ulimwengu wote walikuwa maadui yao. Shetani ametumia njia nyingi sana kujaribu kuwazuia wakati walijaribu kufanya kazi yao. Malango ya kuzima yamekuwa dhidi yao maishani mwao mote.Msomaji, mimi ambaye ni mhubiri wa neno la Mungu ninakuambia kwamba ukija kwake Kristo na kuokoka, utapata baraka nyingi sana kutoka kwa Kristo. Ninakuahidi kwamba utapata amani moyoni mwako; utapata rehema na neema kutoka kwa Mungu na utaokolewa kutoka kwa dhambi zako zote. Haya yote ninaweza kukuahidi. Lakini siwezi kukuahidi kwamba utakwa na usalama hapa ulimwenguni, au na shetani. Badala ya kukuahidi usalama hapa ulimwenguni, ninakuonya kwamba baada ya kuokoka, utakuwa na vita na dunia na shetani hadi ile siku utakufa. Ninakualika kuja kwake Kristo ili uokoke, lakini pia ninakuonya kwamba unahitaji kuhesabu gharama ya kuja kwake kwa wokovu. Ikiwa wewe umeokoka, kumbuka kwamba umeingia jeshi la Yesu Kristo na unapaswa kupigana vita na maadui wake wote. Mbinguni ni mbele yako na njia ya kuingia huko si rahasi kwa sababu uko na maadui wengi ambao watajarbu kukuzuia kuingia. Lakini kumbuka kwamba kuna mamilioni ya watu ambao tayari wamepitia njia hii na wao wameshinda maadui wote wa Mungu na kuingia mbinguni salama.Kwa hivyo, usishangae wakati unakumbana na maadui ambao wanajaribu kukuzia katika maisha yako ya ukristo. Kumbuka maneno ya Yesu Kristo mwenyewe: “Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungeliwapenda kama vile unavyopenda waliowake” (Yohana 16). Kumbuka kwamba dunia ni dhidi ya Mungu na neno lake na kwamba shetani ni adui mkuu ya Mungu. Kwa hivyo maisha yote yake ya ukristo utakuwa na vita na wewe unahitaji kuwa mwenye jeshi. Walimwengu walimchukia Yesu Kristo na ikiwa kweli umeokoka, basi walimwengu watakuchukia pia. Mtumishi wa Mungu mkuu Martin Luther alisema,“Kaini anatendelea kumwua Abeli hadi kanisa liko hapa ulimwenguni.”Hakikisha kwamba uko tayari kwa vita hivi. Hakikisha kwamba unavaa silaha ya Mungu kila siku. Watu wa Mungu mamilioni wamevaa silaha hii na wamewashinda maadui wote wa Mungu. Kwa hivyo tunajua kwa hakikia kwamba kila mmoja ambaye atavaa silaha hii kweli atashinda maadui wake wote.Pia, hakikisha kwamba unavumilia wakati unajaribiwa na maadui wa Mungu. Kumbuka kwamba kila kitu ambacho unakumbana nacho hapa ulimwenguni ni kwa faida yako. Mungu atatumia majaribu yako kukutakasa, na kuhakikisha kwamba wewe unakesha badala ya kulala. Anatumi majaribu yako kukunyenyekeza na kukuletea katika uhusiano na Yesu Kristo. Anatumia majaribu yako kukufundisha kuomba na kuwa na upendo wa vitu vya ulimwengu na si ya dunia hii. Sisi sote tukona upendo wa dunia katika mioyo yetu, na majaribu huondoa upendo huu. Wakati tuko na majaribu mengi, tunaomba, “Njoo Bwana Yesu” (Ufunuo 22:20).Usishuswe moyo kwa sababu ye shetani na majaribu. Yule ambaye ako katika vita dhidi ya shetati na dunia ako na hakika kwamba yeye kweli ni mtoto wa Mungu ambaye ameokoka. Ikiwa hatutabeba msalaba wetu, basi hatutapata taji siku ya mwisho. Ikiwa hatutapigana vita na dunia na shetani, basi hatutaingia mbinguni.“Ni heri ninyi watu watakapowashutumu na kunena dhidi yenu mabaya ya aina zote kwa oongo kwa ajili yangu” (Mathayo 5:11).5. Jambo la tano tunapaswa kuangazia hapa ni usalama wa kanisa. Yesu Kristo ambaye ni mjenga wa kanisa lake aliahidi, “Hata malango ya kuzumu hayataweza kulishinda” kanisa lake.

Page 8: file · Web viewMtu anaweza jenga nyumba mzuri sana, lakini baada ya miaka michache nyumba hii haitaonekana kuwa vizuri kama vile ilivyokuwa wakati ilijengwa

Yesu Kristo hasemi uongo wowote na yeye mwenyewe ameahidi kwamba nguvu zote za jahanum haziwezi kushinda kanisa lake hapa ulimwenguni. Maadui wa Mungu watapiga vita vikali sana dhidi ya kanisa la Mungu hapa ulimwenguni, lakini kanisa halitaanguka au kuangamizwa, bali litasimama; kanisha la Mungu hapa ulimwenguni haliwezi kushindwa. Mijengo yote mingine ya wanadamu wanaanguka na kuangamizwa. Mtu anaweza kujenga nyumba mzuri sana, lakini baada ya miaka 200 au 300 hutaona ile nyumba! Lakini kanisa la Mungu ni la milele na halitaangamizwa.Wakati tunasoma historia ya dunia, tunasoma kwamba taifa fulani fulani walikuwa na nguvu nyingi sana wakati ingine, na ilionekana kwamb taifa moja itakuwa ya milele. Lakini wakati tunaona mambo ya dunia leo tunaona taifa kama ya Babeli na Koreshi na Roma wote wameenda na sasa hawana nguvu yoyote. Taifa hizi zilijengwa na wanadamu na si Mungu na kwa hivyo ziliangamika baada ya miaka michache. Lakini kanisa linajengwa na Mungu na kwa hivyo haliwezi kuangamika, bali litakuwa kwa milele.Miji mikubwa mikubwa kama Ninawe na Babeli na Roma wameangamika. Hata makanisa ya mahali fulani leo hayaonekani. Wakati wa Biblia, miji kama Efeso na Antiokia na Thesalonika ilikuwa na makanisa makubwa; lakini leo hatuyaoni makanisa haya. Haya makinsa sasa yameenda. Wengi wao walienda kwa sababu walikataa kutii neno la Mungu na walianguka dhambini. Wengi wao walianza kuwa na kiburi na majivuno kwa sababu waliwaza kwamba wao ni watu wakuu sana. Wao walisahau kwamba Mungu huchukia kabisa kiburi na majivuno na yale makanisa ambayo yako na kiburi na majivuno yataangamizwa kabisa. Hii ndiyo makanisa mengi kamahawa yaliangamizwa. Makania wengine hawakuendelea kuhubiri injili ya Mungu, bali walianza kuhubiri mambo mengine ambayo yalikuwa mawazo ya wanadamu. Wao walisahau kwamba kazi ya kanisa si kuhubiri mawazo ya kanisa bali ujumbe wa Mungu. Kwa hivyo Mungu aliwahukumu na kuondoa kanisa lao kutoka kwa mji yao.Lakini kanisa la Mungu ambalo ni watu wa Mungu ulimwenguni kote bado linaendelea. Kanisa la Mungu ulimwenguni bado liko, na linaendelea kua. Kanisa la mji fualni linaweza kuondolewa na Mungu, lakini kanisa lake duniani kote litakua na kuendelea kushinda maadui wake wote.Kama kanisa la Kriso katika nchi fulani linateswa na watu wa nchi huo na serikali ya nchi huo, basi Mungu atahakikisha kwamba watu wake wataenda mahali pengine na kukua katika imani yao. Maadui wa Mungu wamejaribu njia nyingi sana kuangamiza kanisa la Mungu hapa ulimwenguni, lakini wameshindwa. Wengi wao wamekufa na kuenda jahanum lakini kanisa la Mungu limeendelea kua hapa ulimwenguni na neno la Mungu bado linahubiriwa kila mahali. Kanisa la Mungu hapa ulimwenguni linaweza kuonekana kuwa dhaifu sana na bila nguvu yoyote; lakini kwa ukweli kanisa hili liko na nguvu za Mungu ndani yake na hii ndiyo sababu litashinda maadui wake wote. Yule ambaye anawatesa watu wa Mungu anawatesa wale ambao Mungu mwenyewe hupenda sana.Ahadi ya Yesu Kristo katika mstari huu ni ya hakika: Yesu Kristo hatakosa kuwa na ushuhuda hapa ulimwenguni. Hata ile wakati ambapo inaonekana kwamba watu wote wa dunia ni waovu na hawataki neno la Mungu, Mungu alikuwa na watu wake hapa ulimwenguni ambao waliwashuhudia walimwengu neno la Mungu. Wakati Ahabu alikuwa mfalme wa Israeli, watu wa nchi hii walikuwa waovu sana. Lakini Mungu bado alikuwa na watu 7,000 ambao walimfuata na mioyo yao yote. Hata leo katika nchi mingi sana inaonekana kwamba hakuna dini ya ukristo kamwe, lakini kwaukweli Mungu ako na watu wake kila mahali ambao wanamtumikia. Shetani anaweza kupiga vita vikali sana na watu wa Mungu na kanisa linaweza onekana kuwa dhaifu sana, lakini malango ya kuzimu hayatashinda kanisa la Mungu.Ahadi katika mstari huu ni kweli kwa kila mmoja ambaye ni mtoto wa Mungu. Watu wa Mungu wengi wameteswa sana na watu wa dunia na shetani na wameonekana kuwa dhaifu kabisa. Wengine kama Daudi na Petro walianguka dhambini na kwa muda kidogo wameacha kumfuata Kristo. Wengine wameogopa sana maadui wao. Lakini mwishowe wote wameshinda maadui

Page 9: file · Web viewMtu anaweza jenga nyumba mzuri sana, lakini baada ya miaka michache nyumba hii haitaonekana kuwa vizuri kama vile ilivyokuwa wakati ilijengwa

wao na kufika nyumbani mwao. Yule ambaye bado ni mtoto atavumilia katika imani yake, na yule ambaye ameokoka miaka mingi pia atavumilia. Yule ambaye imani yake ni dhaifu sana atavumilia, na yule ambaye ako na imani ya nguvu sana atavumilia. Hivi ndivyo maisha yataendelea katika ufalme wa Mungu. Ikiwa mtu ameokoka, basi hakika yeye ataingia mbinguni mwisho, na hakuna yeyote ambaye atamzuia au kumshinda.Kanisa ni mwili wa Kristo, na kanisa hili haliwezi kuangamizwa. Kanisa ni bibi aursi ya Yesu Kristo. Wale ambao wameokoka katika agano lake hawaweza kutenganishwa na Kristo na kanisa lake tena. Kanisa ni mfugo wa Yesu Kristo. Wakati Daudi alikuwa mchungaji wa wanyama, yeye alipigana na simba na alimshinda. Yesu Kristo pia atashida wote ambao wanajaribu kuiba watu wake. Siku ya mwisho, Yesu Kristo atawapeleka watu wake wote kwa Mungu Baba na atasema, “Hakuna hata mmoja aliyepotea” (Yohana 17:12).Kanisa ni ngano la ulimwengu. Mtu anaweza kusift ngano lakini ngano haitaangamizwa. Magugu yanaweza kuangamizwa lakini ngano haiwezi.Kanisa ni jeshi la Yesu Kristo, na Yeye ni mkuu wa jeshi hili. Hakuna hata askari mmoja ambaye atauliwa kirohoni katika vita hivi: wote watawashinda maadui wao. Kwa kawaida wakati jeshi la nchi fulani linaenda kwa vita, kuna wengi ambao wanakufa na hawarudi. Lakiniwatu wa Mungu wote watakuwa salama kwa sababu mkuu wa jeshi ni Yesu Kristo mwenyewe.Shetani anaweza kuweka watu wa Mungu wengine gerezani na anaweza kutesa na kuwaua wengine. Lakini baada ya kuua mwili wa mkristo hakuna ingine anaweza kufanya. Yeye hawezi kuangamiza roho ya mkristo. Shetani anaweza kuwaondoa watu wa Mungu kutoka ulimwengu huu lakini hawezi kuwaondoa kutuka kwa kanisa la Yesu Kristo.Watu wa ulimwengu wanawea piga vita vikali sana dhidi ya watu wa Mungu, lakini wao hawawezi kuzuia neno la Mungu kuhubiriwa. Mfalme mmoja wa nchi ya Warumi ambaye aliitwa Julian alikuwa adui mkuu sana wa watu wa Mungu. Yeye alimwuliza mkristo mmoja, “Anafanya nini sasa yule mtoto wa fundi?” Alimaanisha Yesu Kristo ambaye babake Yosefu alikuwa fundi. Mkristo alimjibu, “Anatengeneza sanduku lako!” Baada ya miezi michache huyu Julian alikufa.Je, ni nini Yesu Kristo anafanya wakati watu wake wanateswa sana na kujaribiwa? Yeye anaendelea kujenga kanisa lake hapa ulimwenguni. Hata wakati kanisa lake linapata majaribu mengi na linaonekana kuwa dhaifu kabisa, bado kazi yake ya kulijenga kanisa lake inaendelea.Ndugu yangu, usiogope kuanza kumtumikia Yesu Kristo na moyo wako wote. Yule ambaye unamtumikia ako na nguvu zote mbingni na ulimwenguni na Yeye atakulinda. Yeye atahakikisha kwamba wewe hutashindwa na kutupwa mbali. Watu wa jamii yako wanaweza kukuzuia katika kazi hii, jirani wako wanaweza kukuchekea, watu wa dunia wanaweza kukudharau. Lakini usiogope. Mamlaka ya jahanum haiwezi kukushinda. Yule ambaye ako ndani yako ako na nguvu sana kuliko yule ambaye ni kinyume yako. Usiogope kwamba kanisa fulani litaangamizwa wakati mchungaji wake anakufa au kumaliza kazi yake na kuenda. Kanisa ni mwili wa Bwana wetu Yesu Kristo na yeye atalilinda kila wakati. Usiwe nawasiwasi kuhusu kanisa la Mungu hapa ulimwenguni. Yesu Kristo atachunga kanisa lake na kulipatia mahitaji lake lote, yeye atahakikisha kwamba malango ya kuzimu hayatashinda kanisa lake. Mambo ya kanisa yanaendelea vizuri, hata kama sisi hatuwezi kuona hii. Falme za ulimwengu yatakuwa falme za Mungu na za Kristo. Yale ambayo tunajifundisha kutokana na mafundisho haya.1. Kwanza, ninataka kukuuliza wewe swali moja: je, wewe ni mshiriki wa kanisa la kweli ya Yesu Kristo? Kwa kuuliza hii, ninamaanisha, je, wewe kweli umeokoka? Hapa mimi siongei kanisa fulani kama la Kianglikana au Kibaptisti. Ninaongea hapa kuhusu lile kanisa ambalo limejengwa juu ya jiwe ambalo ni Yesu Kristo mwenyewe. Ninakuuliza, je, wewe ni mshiriki wa kanisa la Yesu Kristo? Je, wewe umeunganishwa na Yesu Kristo mwenyewe? Je, wewe umepata msamaha wa dhambi zako na kuoshwa katika damu ya Yesu Kristo na kupewa Roho Mtakatifu? Je, Roho Mtakatifu mwenyewe anashuhudia na moyo wako kwamba weke uko moja na Yesu Kristo na yeye ako moja nawe? Ninakusihi na moyo wangu wote: jichunguze vizuri

Page 10: file · Web viewMtu anaweza jenga nyumba mzuri sana, lakini baada ya miaka michache nyumba hii haitaonekana kuwa vizuri kama vile ilivyokuwa wakati ilijengwa

sana kulinagana na swali hili. Usiseme tu, “Mimi ni mkristo, nilibatizwa na ninahudhuria kanisa kila wiki.” Ninakuuliza, je, umeokoka na kupata msamaha wa dhambi zako zote?Swali hili ni la muhimu sana. Kumbuka kwamba ni wale tu ambao wako washirika wa kanisa la kweli ambao wataingia mbinguni. Ni wale tu ambao wameokoka ambao watakuwa pamoja na Yesu Kristo milele. Jichunguze sana. Usijidanganye na mwishowe kupotea nafsi yako na kuenda jahanum. Unaishi katika nchi ambayo iko na mafundisho ya Biblia na iko na makanisa mengi. Usiende jahanum baada ya kuishi katika nchi kama hii.2. Pili, ninataka kukualika. Ninataka kuongea na wote ambao bado hawajaokoka. Ninakuambia, “Njoo kwake Kristo na unganana kanisa lake la kweli leo. Kuja leo na unganana na Yesu Kristo mwenyewe ili upate kuokoka. Njoo kwake Yesu Kristo leo na pata msamaha wa dhambi zako zote. Je, ni kwa nini unabaki ndani ya dhambi zako? Je,ni kwa nini unangoja hadi siku ingine? Pengine hutapata nafasi ya kuja kwake tena! Biblia inakuambia kwamba siku ya kuokoka ni leo, kwa hivyo usingoje! Je, ni kwa nini unagoja hadi kesho? Njoo kwake Kristo leo kwa sababu kila kitu kiko tayari. Ukija kwake utapata rehema. Ukija kwake hakika utaingia mbinguni. Ukija kwake, malaika mbinguni watafurahi na Yesu Kristo atakupokea kwa furaha na kukukaribisha katika jamii yake.” Ninakualika kama vile Noa alivyowaalika watu wa siku zake, “Ingieni safina na mtaokolewa kutoka kwa gharika.” Vilevile ninakuambia, “Njoo kwake Kristo na utaokolewa kutoka kwa hukumu ya dhambi zako.Usiendelee kushika dunia hii na vitu vyake. Biblia inakuambia wazi kwamba siku moja dunia hii na vitu vyake vyote vitaangamika. Siku ya Yesu kurudi na kufanya mambo yote mapya ni karibu sana sasa. Usibaki katika dhambi zako. Njoo kwake leo na utaokoka.Pengine unawaza, “Lakini mimi niko na dhambi nyingi sana, ninawezaje kuja kwake Kristo?” Ikiwa hii ni hali yako basi jua kwamba Yesu Kristo bado anaweza kukupokea.Hii ndiyo njia ya kuja kwake Yesu. Kuja kama tu wewe ulivyo na dhambi zako zote, kuja kama yule ambaye ako na njaa kwa wokovu. Ukija kwake kuwa kama tu mwenye dhambi ambaye anataka kusamehewa na kuoshwa, Kristo atakupokea, yeye hatakufukuza. Utapata kwake msamaha wa dhambi zako zote.3. Tatu, ninataka kuwahimiza wale ambao tayari wameokoka. Ninakuhimiza, ishi maisha matakatifu ndugu yangu. Wewe umeitwa na Yesu Kristo katika ufalme wake, ishi yale maisha ambayo yanastahili wale ambao ni watu wa Mungu. Hakikisha kwamba taa yako inashine mbele za watu wote, ili watu wa dunia waweze kupata faida kutoka kwa maisha yako. Uwambie wengien wewe sasa ni mtu wa Kristo na unamtumikia kwa moyo wako wote. Uwe kama waraka ambao umeandikwa na Mungu ili watu wote wajue ujumbe wa Mungu ni nini. Hakikisha kwamba wote wajue kwamba wanapaswa kuokoka, na bila kuokoka hawataingia mbinguni kamwe.Pia, ninakusihi, ishi maisha ya ujasiri. Usiogope kukiri Kristo Yesu mbele za watu wote. Kila mahali ambapo uko, hakikisha kwamba unamkiri Yesu Kristo. Je, ni kwa nini unahisi aibu? Yeye hakusikia aibu kwa ajili yako wakati alikufa msalabani kwa dhambi zako. Yeye akotayari kukubali wewe mbele za Mungu Baba mbinguni, je ni kwa nini utasikia aibu kumkiri mbele za watu wa dunia? Uwe mjasiri. Mwenye jeshi hawezi kupiga vita kama yeye anasikia aibu kwa silaha zake. Yule ambaye ameokoka hapaswi kuwa na aibu kumkiri Kristo.Pia, ninakusihi, ishi maisha ya furaha. Kumbuka kwamba wewe uko na tumaini la kuwenda mbinguni na kukaa huko milele. Kumbuka kwamba Mwokozi wako, Yesu Kristo, ako karibu sana kurudi, na tunapaswa kumtarajia na moyo wetu wote. Ile siku Yesu atarudi, itakuwa wakati mema sana. Kwa wale ambao wameokoka siku ile itakuwa siku ya baraka, na kwa wale ambao hawajaokoka siku ile itakuwa siku ya hukumu. Hakikisha kwamba unaishi maisha yako kwa kutarajia ile siku ya Yesu Kristo. Usichoke kuongoja ile siku. Kumbuka kwamba Mwokozi wako Yesu Kristo amekuamrisha kwamba unahitaji kukesha na kuomba.Muda ambayo imebaki ni mfupi tu sasa. Ile siku Yesu Kristo atarudi kanisa lake litaonekana kuwa mzuri sana, bila makosa au dhambi au hatia. Watu wake wote watakuwa wamekamilika na watakuwa tayari kwa kurudi kwake. Siku ile Mwokozi na watu wake wote watafurahia na ulimwengu wote utashuhuda kwamba kweli alifanya vizuri kujenga kanisa lake.