utokezo al-badaa
DESCRIPTION
Maudhui ya Utokezo (Badaa’) yanazingatiwa kuwa ni kati ya masuala ya falsafa ya Kitawhidi ambayo yamechochea utafiti wenye wigo mpana baina ya maulamaa wa elimu ya falsafa, hiyo ni kutokana na yanayopatikana humo miongoni mwa masuala ya kina na ya muhimu.TRANSCRIPT
UTOKEZO(AL-BADAA)
Kimeandikwa na:
Sayyid Abdul-Karim al-Bahbahani
Kimetarjumiwa na:
Abdul-Karim J. Nkusui
©Haki ya kunakili imehifadhiwa na:
AL-ITRAH FOUNDATION
ISBN: 978 - 9987 - 512 - 26 - 3
Kimeandikwa na:
Sayyid Abdul-Karim al-Bahbahani
Kimetarjumiwa na:Abdul-Karim J. Nkusui
Kimepangwa katika Kompyuta na:
Hajat Pili Rajab
Toleo la kwanza: Julai, 2009
Nakala: 1000
Kimetolewa na kuchapishwa na:
Alitrah Foundation
S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania
Simu: +255 22 2110640
Simu/Nukushi: +255 22 2127555
Barua Pepe: [email protected]
Tovuti: www.alitrah.org
Katika mtandao: www.alitrah.info
YALIYOMO
1. Al – badau katika Qur’an tukufu............................................................2
2. Kauli za Maulama wa Shia ithna ashariyah juu ya Al-badau.................7
3. Nafasi ya itikadi na malezi yenye kujenga ya Al-badau......................10
4. Maswali juu ya itikadi ya Al-badau.......................................................13
5. Hitimisho...............................................................................................15
NENO LA MCHAPISHAJI
Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjumi ya kitabu cha Kiarabu
kiitwacho, al-Badaa’. Sisi tumekiita, Utokezo.
Kitabu hiki ni matokeo ya kazi ya kielimu iliyofanywa na mwanachuoni
wa Kiislamu, Sayyid Abdul-Karim al-Bahbahani.
Kumekuwepo na kutokuafikiana katika miji yetu ya Kiislamu, hususanmiongoni mwa wanavyuoni kuhusu usahihi wa itikadi ya Badaa’ - yaaniutokezo wa jambo fulani kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Baadhi wanase-ma kwamba itikadi hii ni sahihi na wengine wanasema si sahihi. Baadhi yawanavyuoni wamekwenda mbali zaidi hadi kufikia kuwaita Waislamuwenzao wanaoitakidi juu ya Utokezo (Badaa’) kuwa ni washirikina aumakafiri.
Lakini je, Badaa’ haina asili katika dini? Ukweli ni kwamba ina asili kati-ka dini kama utakavyoona katika kitabu hiki.
Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo
makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na
upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za
watu. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imea-
mua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni
yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa
Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii.
Tunamshukuru ndugu yetu, Abdul-Karim J. Nkusui kwa kukubali jukumu
hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote
walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa
kwake.
Mchapishaji:Al-Itrah FoundationS. L. P. 19701Dar-es-Salaam, Tanzania.
NENO LA JUMUIYA
Hakika mirathi ya AHLUL-BAYT ambayo imehifadhiwa na kambi yao na
wafuasi wao dhidi ya upotovu inaonyesha kambi iliyokusanya aina mbal-
imbali za taaluma za kiislamu.
Kambi hii imeweza kulea nafsi mbalimbali zilizo tayari kunywa kutoka
kwenye chemchemu hiyo, na kuupa umma wa kiislamu wanachuoni
wakubwa wenye kufuata nyayo za ujumbe wa Ahlul-Bayt.
Wanachuoni waliyokusanya vidodosa na maswali mbalimbali ya madhe-
hebu na mitazamo tofauti ya kifikra kuanzia ndani ya desturi ya kiislamu
hadi nje ya desturi hiyo, huku wao wakitoa majibu na utatuzi makini juu
ya maswali hayo ndani ya karne zote.
Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt imefanya hima kutetea tukufu za
ujumbe wa Uislamu na ukweli wake ambao umechafuliwa na makundi,
madhehebu na wanaharakati mbalimbali wenye chuki na uislamu.
Jumuiya imefuata nyayo za Ahlul-Bayt na za wafuasi wa kambi yao njema
ambayo imefanya hima kujibu madai yenye kuendelea na daima ikajaribu
kubaki ndani ya msitari wa mapambano kwa kiwango kinachohitajika
ndani ya kila zama.
Hakika uzoefu ambao umehifadhiwa ndani ya vitabu vya wanachuoni wa
kambi ya Ahlul-Bayt katika dhamira hii ni vya aina ya pekee, kwa sababu
una nguzo ya kielimu inayotegemea akili na hoja, huku ukijiepusha na
matamanio na uzalendo uliokatazwa.
Unazungumza na wasomi na wanaharakati wenye fani maalumu
mazungumzo ambayo yanaituliza akili na yanapokewa na maumbile sala-
F
ma.
Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa
watafuta ukweli hatua mpya ya uzoefu wa thamani katika ulingo wa
mazungumzo na maswali na kujibu hoja za utata zilizotolewa zama zilizo-
pita au zinazotolewa leo kwa njia ya Tovuti, na hasa kwa kupewa nguvu na
baadhi ya nchi zenye chuki dhidi ya uislamu na waislamu.
Jumuiya imejiepusha na udadisi uliokatazwa na ni yenye kuhangaikia
kuzidadisi akili zenye kufikiria na nafsi zenye kutafuta haki ili ziweze
kufikia kwenye haki ambayo inatolewa na kambi ya Ahlul-Bayt ulimwen-
gu mzima, ndani ya zama ambazo akili inaerevuka na nafsi na roho zina-
boreka kwa kasi ya pekee.
Ni lazima tugusie kuwa mfululizo huu wa tafiti hizi umeandaliwa na
Kamati maalum toka jopo la wanachuoni watukufu, hivyo tunatoa shuku-
rani njema kwa hawa wote na kwa wasomi na wahakiki kwa kila mmoja
miongoni mwao kupitia sehemu ya tafiti hizi na kutoa mchango wao wa
thamani kuhusu tafiti hizi.
Tunategemea na kutaraji kuwa tutakuwa tumetoa kile tunachokiweza kati-
ka juhudi za kutekeleza baadhi ya wajibu tulio nao mbele ya ujumbe wa
Mtukufu Mola wetu Mlezi ambaye alimtuma Mtume Wake na uongofu na
dini ya haki ili aidhihirishe juu kuliko dini zote. Na Mwenyezi Mungu
anatosha kuwa shahidi.
JUMUIYA YA KIMATAIFA YA AHLUL-BAYT
KITENGO CHA UTAMADUNI
G
2
Utokezo (al-Badaa)
AL-BADAU KATIKA
QUR’AN TUKUFU
Maudhui ya Badau yanazingatiwa kuwa ni kati ya masuala ya falsafa ya
kitauhidi ambayo yamechochea utafiti wenye wigo mpana baina ya maula-
maa wa elimu ya falsafa, hiyo ni kutokana na yanayopatikana humo mion-
goni mwa mas’ala ya kina na ya muhimu.
Al-Badau katika lugha: Ina maana ya kudhihiri baada ya kufichikana, na
inatumika katika mijadala ya kawaida katika nyanja za kubadilishana rai,
fikra, maoni, malengo na makusudio. Hivyo husemwa: “Rai yake ilikuwa
hivi kisha akabadili.”
Ni dhahiri kwamba Al-Badau kwa maana hii ni kutotambua jambo mwan-
zo kisha ukalitambua baadaye na yote mawili hayapatikani kwa Mwenyezi
Mungu (s.w.t.) kwa sababu elimu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni ya
dhati ambapo haijatanguliwa na ujahili. Lakini tukichunguza Al-Badau
katika maana yake ya kilugha tunaikuta inaundwa na vitu viwili:
Ujahili wa mwanzo na elimu mpya.
Kubadilika kwa rai, nia na malengo kufuatana na elimu mpya aliyoipata.
Kisha tunaulizana ni kipi kati ya hivi viwili kinapingana na tawhidi? Cha
kwanza au cha pili au vyote viwili?
Je, kuna uwezekano wa kutenganisha baina yake kiasi kwamba tunasal-
imika na aina ya kubadili na kugeuza ambapo hakutokani na ujahili
uliotangulia wala elimu inayokuja baadaye?
Ama kuhusiana na suala la kwanza: Kwa wepesi tunaona kwamba jambo
la kwanza linapingana na tawhidi na hakuna Mwislamu anaekubali kuna-
3
Utokezo (al-Badaa)
sibisha ujahili kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na wala hatuhitaji kuleta
aya wala riwaya juu ya hilo.
Ama suala la pili: Ikiwa mabadiliko yanalazimiana na dhati ya kuwepo
ujahili wa awali na kupatikana kwa elimu baadaye basi hali hii inapingana
na tawhidi pia. Kama ambavyo ujahili unapingana na tawhidi vivyo hivyo
unapingana na kila mabadiliko na mageuzi yanayosababishwa na hilo. Na
ikiwa mabadiliko yana sababu nyingine katika hali hii hayapingani na
tawhidi.
Kubadili rai na mtazamo – mfano - ni kati ya mambo ya lazima ya dhati
kwa ajili ya kudhihiri elimu na kuondoka kwa ujahili, hivyo basi hai-
wezekani kunasibisha ujahili kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Vivyo
hivyo haiwezekani kunasibisha mabadiliko ya rai na mtazamo kwa
Mwenyezi Mungu Mtukufu. Bali dhana ya rai na mtazamo peke yake hai-
wezekani kunasibishwa kwa Mwenyezi Mungu tukiachilia mbali mabadi-
liko na mageuzi kwa sababu dhana hii inategemea maana ya kupata na
kujifunza elimu, na elimu ya Mwenyezi Mungu haipatikani kwa njia ya
kujifunza hadi isemwe kuwa huu ni mtazamo wa Mwenyezi Mungu na rai
yake bali ni elimu ya dhati na inasimama juu ya dhati yake.
Baada ya jawabu la maswali mawili kuwa wazi tunajaribu kutazama
Qur’anTukufu ili tuangalie je, kunapatikana aya inayonasibisha mabadi-
liko au mageuzi katika jambo miongoni mwa mambo au nyanja kati ya
nyanja?
Kuna ambao wanafanya haraka kusema Qur’an inakataa kuwepo mabadi-
liko au mageuzi kwa Mwenyezi Mungu na hiyo ni kutokana na kauli yake
(s.w.t.): “Lakini hutopata mabadiliko katika kawaida ya Mwenyezi
Mungu”1 na kauli yake (s.w.t.): “Na wala hutopata mabadiliko katika
kawaida ya Mwenyezi Mungu.”2
1 Suratu Fatir: 432 Suratul Ahzab: 62
4
Utokezo (al-Badaa)
Ila jawabu hili halitoshelezi kwa sababu uhalisia wa Qur’ani ni jambo
linalotokana na Qur’ani yote na kinachopatikana katika upande mmoja tu
hakiwakilishi isipokuwa nusu ya Qur’ani kwa sababu kinatokana na
upande mmoja tu wa Qur’ani Tukufu.
Kuna upande mwingine umenasibisha mabadiliko na mageuzi kwa
Mwenyezi Mungu Mtukufu mfano kauli yake (s.w.t.): “Mwenyezi Mungu
hufuta ayatakayo na huimarisha (anayoyataka) na asili ya hukumu
iko kwake.”3 Na kauli yake (s.w.t.): “Hakika Mwenyezi Mungu
habadilishi yaliyoko kwa watu hadi wabadilishe yaliyoko katika nafsi
zao.” 4
Aya ya kwanza inaonyesha kwamba Mwenyezi Mungu anafuta na
kuthibitisha na katika hilo kunaashiria mabadiliko na mageuzi.
Ama Aya ya pili imeweka wazi kwamba Mwenyezi Mungu anabadilisha
hali za watu pindi wanapobadilisha yaliyopo katika nafsi zao. Hivyo hali
ya kidini na kisiasa ya watu ni makadirio ya kiungu yanakubali mabadiliko
pindi watu wanapoamua kubadilisha hali zao za kinafsi na kiutamaduni
kutoka katika shirki kwenda kwenye imani, na kutoka kwenye upotovu
kwenda kwenye uongofu. Hivyo kuna makadirio ya aina mbili, makadirio
ya kiungu katika hali ya watu katika utii na makadirio ya kiungu katika hali
zao katika maasi. Wanapochagua utiifu anawapitishia makadirio ya mwan-
zo, na wanapochagua uasi anawapitishia makadirio ya pili. Na aina hii Aya
na riwaya zimeonyesha kuathiri baadhi ya vitendo katika riziki, vifo na
balaa.
Na haya hayakatai yeyote kati ya Waislamu bali ikhitilafu inatokea katika
uelewa wa badau ilipochukuliwa kwa maana yake ya kilugha inayopin-
gana na tawhidi, na ikhitilafu inaisha inapogundulika kuwa makusudio
3 Suratu Raad: 394 Suratu Raad: 11
5
Utokezo (al-Badaa)
yake ni maana ya kiistilahi isiyolazimu kunasibisha ujahili kwa Mwenyezi
Mungu (s.w.t.). Hakika makusudio ya badau kwa Ahlul–Bait (a.s.) ni
kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anamkadiria mja wake kulingana na
hali fulani kisha Mwenyezi Mungu anabadilisha makadirio yake kutokana
na hali mpya inayodhihiri kwa mja kutokana na amali fulani anayoifanya,
pamoja na kutambua Kwake tangu awali mambo yote mawili na hali zote
mbili. Na lau wangefahamu maana hii wangetambua kuwa ni kati ya
mambo ambayo Waislamu wanaafikiana juu yake na ikhitilafu ipo katika
matamshi tu.
Amesema kweli Allammah as-Sayid Abdul-Husein Sharaf Diyn alipose-
ma: “Ikhitilafu katika mas’ala haya baina yetu na Ahlus-Sunna ni ya
matamshi tu.”
Kisha amesema: “Aking’ang’ania asiyekuwa sisi tutamtaka arejee katika
hukumu yake, hivyo abadilishe tamko la badau kama anavyotaka lakini
amuogope Mwenyezi Mungu kwa ndugu yake muumini.”5
Na kabla yake alishaandika Sheikh Al-Mufiyd: “Ama kutamka tamko la
badau, hakika nimelifahamu kupitia yaliyopokewa baina ya mja na
Mwenyezi Mungu Mtukufu na lau kusingepokewa ambayo najua usahihi
wake basi nisingekubali kutamka. Kama ambavyo lau nisingepokea kwam-
ba Mwenyezi Mungu anakasirika na anaridhika, anapenda na kuchukia
basi nisingesema hayo. Ninasema kwa maana ambayo haipingwi na akili
na hakuna ikhitilafu baina yangu na Waislamu wote katika mlango huu,
bali amekhalifu aliyewapinga katika tamko bila ya kupinga maana yake, na
nimeshaeleza sababu yangu ya kusema hayo kwa kifupi, na huu ndio msi-
mamo wa Mashia wote na kila aliyewakhalifu katika madhehebu anapinga
niliyoyaeleza kwa jina tu bila ya kupinga maana yake na wala hayaridhii.”6
5 Ajiwibatul-Masa’ail Jarullah Uk: 796 Awaailul Maqalaat Uk: 92 - 93
6
Utokezo (al-Badaa)
Na kabla yake amesema Imamu Swadiq (a.s.) katika tafsiri ya kauli yake
(s.w.t.): “Mwenyezi Mungu anafuta ayatakayo na huimarisha anay-
otaka na asili ya hukmu iko kwake.” Kila jambo analolitaka basi liko
katika elimu yake kabla ya kulifanya, hakuna kitu kinachodhihiri ila kil-
ishakuwa katika elimu yake. “Hakika Mwenyezi Mungu hakidhihiri kitu
kwake ambako kunatokana na kutotambua.”7
Na amesema (a.s.): “Mwenye kudai kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu
linadhihiri kwake jambo asilolijua basi jitengeni naye.”8
Kisha nguvu ya hoja za Shia katika mas’ala ya badau ni mambo matatu:
Kauli yake (s.w.t.): “Mwenyezi Mungu anafuta ayatakayo na kuimar-
isha ayatakayo na asili ya hukumu iko kwake.”9 Na kauli yake (s.w.t.):
“Humuomba Yeye kila kilichomo mbinguni na ardhini kila siku Yeye
yumo katika mambo.”10
Kufanana mas’ala ya kufuta (nasikh) katika sharia, na badau ni nasikh
katika maumbile, na nasikh ni badau ya kisharia, kama ambavyo waislamu
wamethibitisha nasikh katika sharia kama vile kubadili kibla toka
Masjidul-Aqsaa kuelekea Al-Ka’aba tukufu na hakukhalifu yeyote kati yao
hilo, na hajazingatia yeyote kuwa hilo linakhalifu elimu ya milele ya
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) wala hailazimu kuthibiti ujahili wa mwanzo,
vivyo hivyo katika badau na kubadilika katika hukumu za maumbile bila
ya kulazimu ujahili wa mwanzo wala haikhalifu elimu ya Mwenyezi
Mungu ya milele, kama yeyote atapinga badau basi upinzani wake pia
utapinga nasikh na atakayoyataja katika mas’ala ya nasikh basi tunaweza
kuyajibu pia katika mlango wa badau bila ya tofauti yeyote baina ya
mambo hayo mawili.
7.Bihrul Anuwari Juz: 4 uk: 121 Hadith Na.: 63
8 " " " " : 30 9.Suratu Rad: 39
10. Suratu Rahman: 29
7
Utokezo (al-Badaa)
Mushkeli katika badau ni kukariri mushkeli waliotoa mayahudi juu
nasikh katika sharia, ambapo wao wanaona ubatili wa hilo na
kutowezekana kunasibisha nasikh kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu,
kama ambavyo wamejibu maulamaa wa Kiislamu kwa mushkeli huu
na kuthibitisha kwao uwezekano wa nasikh katika sharia bila kulazimu
upungufu wowote katika uungu wake mtukufu inawezekana kutumiwa
katika nasikh katika ulimwengu wa kimaumbile na mamlaka.
Kitendo huathtiri katika maisha ya mwanadamu, na huu ni ukweli wa
Qur’ani uliothibiti kwa kuongezea yaliyopo katika Sunna za Nabii
(s.a.w.w.) kwa kutilia mkazo, nayo ni kwamba amali za mwanadamu
imani, shiriki, utii, maasi wema kwa wazazi wawili na kuwaasi kwao,
kuwasaidia mafakiri, kutoa, kuunga udugu na kuukata n.k kunaathiri kati-
ka riziki, baraka, kurefusha umri na furaha. Na mambo haya Qur’ani imey-
ataja mara nyingi na Sunna zinaunga mkono mara nyingi na Qur’ani
imeyafupisha kwa kusema: “Hakika Mwenyezi Mungu habadilishi
yaliyopo kwa watu hadi wabadilishe yaliyopo katika nafsi zao.”
Na ambaye anapinga badau lazima atambue kwamba upinzani wake
unapelekea kupinga mfano wa ukweli huu ulio wazi, na ikiwa anauamini
basi atambue ya kuwa haya anayoyaamini ndio ambayo Shia wanayoyaita
al-Badau.
KAULI ZA MAULAMAA WA SHIA
KATIKA BADAU
Hii ndio maana ya badau ambayo maulamaa wa Shia waliotangulia na
waliokuja baadae wametilia mkazo. Sheikh Mufiyd anasema: “Kauli ya
Shia katika al-badau njia yake ni ya kusikiwa na wala sio ya kutafakari, na
makusudio yake sio kubadili rai na kutambua jambo lililokuwa
limefichikana kwake, vitendo vya Mwenyezi Mungu vyote viko dhahiri
kwa viumbe vyake kabla hata ya kuvimba, navyo vinatambulikana Kwake
8
Utokezo (al-Badaa)
na bado vingali vinatambulika.”11
Sheikh Tusi amesema: “Al-Badau katika lugha ni kudhihiri, hivyo
husemwa umedhihri kwetu uzio wa mji na imetudhihirikia rai …”
Ama likinasibishwa tamko hili kwa Mwenyezi Mungu humo kuna ambayo
hayafai kunasibishwa Kwake; Ama ambayo yanafaa ni ambayo yanakusu-
dia nasikh (kufuta) na kunasibisha hayo Kwake kuna wigo mpana, katika
upande huu yanachukuliwa yote yaliyopokelewa kutoka kwa wakweli
miongoni mwa habari zenye maana ya kunasibisha badau kwa Mwenyezi
Mungu bila ya kunasibisha yasiyofaa kwake miongoni mwa kutambua
baada ya kutotambua, na wajihi wa kuyasema hayo ni kwamba ikiwa
yanayoonyesha nasikh inayodhihiri kwa mkalafu ambayo hayakuwa
dhahiri kwao na kupata kwao elimu baada ya kutokuwa nayo, hayo huitwa
“Al–badau.”12
Na amesema As-Sayyid Abdallah Shubar: “Al-Badau ina maana nyingi,
baadhi yake zinajuzu na zingine hazijuzu nayo ni - kwa fatiha na madda
-aghlab hutumika katika lugha kwa maana ya kudhihiri kitu baada ya
kufichikana na kupata elimu kwayo baada ya kutojua.
Na umma umeafikiana kukanusha hayo kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ila
yale ambayo hayachupi mpaka Kwake, na mwenye kunasibisha hayo kwa
Shia basi ameshawazulia uongo na Shia wako mbali nao.”13
As-Sayyid Abdul-Husein Sharaf Diyn amesema: “Na matokeo wanayose-
ma Shia hapa ni kwamba Mwenyezi Mungu anapunguza riziki na
kuongeza humo, vivyo hivyo katika vifo, afya maradhi furaha, matatizo,
mitihani, balaa, imani ukafiri n.k. kama ilivyosema kauli Yake tukufu:
“Mwenyezi Mungu hufuta atakayo na kuimarisha ayatakayo na asili
11 Taswihihul-Itiqaadatil Imamiyah Uk; 66 chapa ya Darul Mufiyd12 Maswabihu Durar Juz: 1 Uk: 3313 Udstul–Usul Juz: 2 Uk: 29
9
Utokezo (al-Badaa)
ya hukumu iko kwake.”14 Na huu ndio mtazamo wa Umar bin Khattab
na Ibnu Mas’ud, Abi Wail na Qatadah. Na amepokea Jabir kutoka kwa
Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na wengi wa Salaf wanaomba na
kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu awajaalie wawe wema na wala wasi-
we waovu, na yamepokewa hayo kwa tawaatur kutoka kwa Maimamu
wetu katika dua zao zilizopokelewa, na imepokewa katika Sunna kwamba
sadaka kwa namna yake, wema kwa wazazi wawili, kufanya wema, haya
yanabadili uovu kuwa wema na yanaongeza umri.
Na imesihi kwa Ibnu Abbas kwamba yeye amesema: “Tahadhari hainu-
faishi kitu katika Qadar lakini Mwenyezi Mungu anafuta kwa dua anay-
otaka miongoni mwa Qadar.” Hii ndio badau ambayo wanaisema Shia,
inajuzu kuinasibisha badau kwake kwa uhusiano wa kufanana. Ikhitilafu
katika hili baina yetu na Ahlus-Sunna ni ya matamshi tu, na anayosema
Shia katika badau kwa maana tuliyoitaja wanaisema Waislamu wote.15
Sheikh Agha Bazarak at-Twaharaniy anasema: “Al-Badau maana yake
katika lugha ni kudhihiri rai ambayo haikuwepo na kusahihisha kitu kili-
chojulikana baada ya kutojulikana, lakini haifai kunasibishwa kwa
Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kulazimu kudhihiri rai juu ya kitu amba-
cho hakikuwepo kwa kutokijua Kwake awali au kushindwa Kwake na
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ametakasika na hayo.
Al-Badau wanayoisema Shia ni kwa maana ambayo lazima kila mwislamu
anaitakidi mkabala na wayahudi wanaosema kwamba Mwenyezi Mungu
amemaliza kazi hivyo hakidhihiri kitu chochote kwake: “Mkono wa
Mwenyezi Mungu umefumba” au mwenye kufuata kauli za wayahudi
wenye kudai kwamba Mwenyezi Mungu ameumba vyote vilivyopo mara
moja hivyo hakuna kitu ila alichokiumba awali au alikuwa anaitakidi
mfumo wa ulimwengu kwa kusema kwamba Mwenyezi Mungu ameumba
14 Suratu Raad: 3915 Ajuwibatu Masaail Jarullah Uk: 101 -103
10
Utokezo (al-Badaa)
mfumo wa ulimwengu nao uko nje umevuliwa katika mamlaka yake, mifu-
mo mingine ndio inaoiendesha, ambapo lazima kila mwislamu akanushe
kauli hizi na aitakidi kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu “ kila siku
yuko katika mambo”16
NAFASI YA ITIKADI NA MALEZI YENYE
KUJENGA KATIKA BADAU
Imedhihiri katika yaliyotangulia kwamba al- badau ina maana ya Qur’ani
imeenea baina ya waislamu wote na kwamba Shia hawatofautiani na wais-
lamu wengine isipokuwa katika jina ambalo kwalo linafahamika kosa la
kunasibisha ujahili kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na imebainika kutosi-
hi kunasibisha huku, na kilicho muhimu kwetu sasa ni kueleza upande
mwingine wa utafiti, nao ni umuhimu wa fikra ya badau kuhusu itikadi ya
mwanadamu mwislamu, kwani fikra zinapimwa kwa misingi yake ya kie-
limu na hoja zake za kimantiki na kwa malengo yake na matunda yake kwa
upande mwingine.
Na katika maudhui ya badau inaweza kusemwa kwa njia ya kuuliza: Ikiwa
makadirio ya awali hayatakuwa na kazi bali yatamalizikia kwa kufutwa,
nini faida ya kutoa taarifa juu yake? Na nini matunda yanayopatikana kwa
kuitakidi al-Badau wakati huo?
Jawabu: Hakika kuitakidi al-Badau kunarejea kwenye umuhimu mkubwa
sana katika pande mbili: Upande wa itikadi na upande wa malezi.
Ama upande wa kiitikadi yanatutosha maneno ya Allammah al-Majlisiy
ambapo ameandika anasema: “Hakika wamevuka mpaka katika al-Badau
kwa kuwajibu Wayahudi ambao wanasema: “Hakika Mwenyezi Mungu
amemaliza kazi na utawala.” Na baadhi ya Mu’tazila wanasema: “Hakika
16 Suratu Rahman: 29
11
Utokezo (al-Badaa)
Mwenyezi Mungu ameumba viumbe mara moja kama ilivyo hivi sasa
miongoni mwa madini, mimea, wanyama, wanadamu, na wala kuumbwa
Adamu hakujatangulia kuumbwa watoto wake, na kutangulia ni katika
kudhihiri kwake sio katika kuumbwa kwake na kuwepo kwake, bali
wamechukua makala haya kwa watu wa falsafa wenye kusema kuhusiana
na mfumo wenye kuendesha ulimwengu, na wenye kusema kwamba mam-
laka ya Mwenyezi Mungu hayakuathiri isipokuwa katika uumbaji wa awali
tu, hivyo wao wanamuengua Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika mamlaka
Yake na wananasibisha uendeshaji kwenye mfumo wa ulimwengu na wala
sio kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.” 17
Kwa maana kwamba mkazo wa Maimamu (a.s.) juu ya al-Badau umekuja
ili kubatilisha kila fikra zinazofanya uwezo wa Mwenyezi Mungu na
matakwa Yake (s.w.t.) kuwa na kiwango maalum, na kuthibitisha kuwa ni
uhakika wa jumla kwa pande zote hata katika upande wa Qadar ambayo
anaikadiria Mwenyezi Mungu Mtukufu mwenyewe katika ulimwengu wa
maumbile, uumbaji, uendeshaji na malezi. Na kwamba makadirio ya
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika makadirio hayo, hayamfanyi kuwa ni
mwenye kupokonywa hiari Yake na matakwa Yake kutokana na hayo.
Kama ambavyo al-Badau imekuja ili kutilia mkazo juu ya hiari ya
mwanadamu na matakwa yake wakati wa kubainisha uwezo wa kiungu,
humo kuna Lauhul-Mahfuudh haikubali mabadiliko, na Lauhu nyingine ni
ya kufuta na kuthibitisha ambayo anayakadiria Mwenyezi Mungu (s.w.t.)
tangu mwanzo wa kuumba, hii inakubali mabadiliko kulingana na anayoy-
afanya mwanadamu miongoni mwa amali katika dunia. Kana kwamba
itikadi ya al-Badau imekuja ili kukamilisha itikadi ya Qadhwaa na Qadar
ili kuondolewa “Ghuluu” kuchupa mpaka na kufifiliza katika itikadi ya
Qadhwaa na Qadar, na isichukuliwe kwa maana ambayo itapokonya hiari
kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kwa mwanadamu. Hivyo hakuna budi
kuikamilisha kwa itikadi ya badau ambayo imekuja kutilia mkazo kwam-
17 Biharul-Anwar Juz: 4, Uk: 129 – 130 chapa ya Tehran
12
Utokezo (al-Badaa)
ba Qadar haifikii kiwango cha kupokonya hiari ya Mwenyezi Mungu wala
haipokonyi hiari ya mwandamu.
Na katika upande wa malezi tunaona kwamba itikadi ya al-Badau ina
athari ya kimalezi yenye kujenga katika maisha ya wanadamu, na
Allammah al-Majlisiy anabainisha athari hii katika kukamilisha maana
yake yaliyopita juu ya sababu za kutilia mkazo Maimamu (a.s.) juu ya al-
Badau, ambapo kwanza anataja faida ya kuitakidi ambazo tumezitaja na
akaongezea kwa kutaja faida ya kimalezi kwa kusema: “Hivyo Maimamu
(a.s.) wakakataza hayo na wakathibitisha kwamba (s.w.t.) kila siku yuko
katika kazi miongoni mwa kuondoa, kuleta kingine, kumfisha mtu na
kumhuisha mwingine, n.k. ili waja wasiache kunyenyekea kwa Mwenyezi
Mungu, kuomba, kutii, kujikurubisha kwake kwa yale yanayofaa katika
mambo ya dunia yao na akhera yao, na ili wataraji wanapotoa sadaka kwa
mafakiri, kuunga udugu, kuwafanyia wema wazazi wawili, kufanya mema
na ihsani kwa yale waliyoahidiwa katika kuongezewa umri na kuongeze-
wa riziki.”
Na katika upande mwingine itikadi ya al-Badau ni kuhamasisha juu ya
uzuri wake katika itikadi ya toba na masharti ya kukubaliwa mbele ya
Mwenyezi Mungu, kama ambavyo toba ina athari nzuri katika kumjenga
mwanadamu, na kwa upande mwingine ni kufunga mianya ya kukata
tamaa na kufungua milango ya matumaini na matarajio na kujenga moyo
wa mageuzi na maandalizi ya mafanikio, vivyo hivyo badau ina athari hii
katika maisha ya mwandamu, bali badau ni dharura kati ya dharura za toba
na vigezo vyake ni katika amali, kwani kati ya dharura za toba ni mwenye
kutubia kuitakidi kwamba kalamu ya Mwenyezi Mungu bado wino wake
haujakauka katika ubao wa kufuta na kuthibitisha, hivyo Mwenyezi
Mungu anaweza kufuta na kuthibitisha anayotaka, anamneemesha
amtakaye na kumfanya amtakaye kuwa muovu kulingana na anavyojipam-
ba mja miongoni mwa tabia njema na amali njema, au kulingana na anavy-
ofanya amali mbaya, na wala matakwa ya Mwenyezi Mungu hayaji bure
bure tu, bila ya kudhibitiwa na hekima. Bali lau mja akitubu na kutekeleza
13
Utokezo (al-Badaa)
ya wajibu na kushikamana na wema anatoka katika kundi la watu waovu
na kuingia katika kundi la waja wema, na kinyume chake pia ni sahihi.
Na katika hayo yote tunaweza kufahamu maana ya maneno ya Maimamu
(a.s.) kwamba: “Hajaabudiwa Mwenyezi Mungu kwa chochote mfano wa
anavyoabudiwa kwa badau.”18 Na wala “Hajatukuzwa Mwenyezi Mungu
mfano wa anavyotukuzwa kwa al-Badau.”19 Na “Mwenyezi Mungu haja-
tuma Nabii hadi achukue kwake ahadi ya mambo matatu: Kukubali ibada
ya Mwenyezi Mungu, kuivua shirki, na kwamba Mwenyezi Mungu hutan-
guliza ayatakayo na huchelewesha ayatakayo.” 20
MASWALI KUHUSU ITIKADI YA BADAU
Hapa tunatoa maswali yanayotaka majibu yenye kutosheleza nayo:
1. Hakika kauli ya al-Badau inasababisha Mwenyezi Mungu kufanya upu-
uzi kwani pamoja na kutambua yatakayotokea kwake miongoni mwa
mabadiliko na kudhihiri, basi kutoa taarifa kwa makadirio ya mwanzo
itakuwa ni upuuzi?
Jawabu: Hakika itakuwa ni upuuzi kama tutajaalia kutokuwepo lengo na
manufaa yanayotarajiwa kutokana na kutoa taarifa ya makadirio ya
mwanzo, na haya ni ambayo hatuwezi kuyathibitisha, hivyo
inawezekana kuwepo lengo na manufaa yanayorejea kwa mja kwa faida
kubwa kutokana na taarifa hiyo.
2. Hakika Nabii au Imamu akitoa taarifa ya kitu kisha ikatokea al-Badau
katika kutokea kwake, ni lazima ategemee katika taarifa yake ya awali
kwenye kitu kinachokuwa ni chanzo (rejea) cha taarifa yake na asili ya
chanzo cha elimu yake, sasa ni kwa jambo gani atategemea Nabii au
Imamu katika taarifa yake ya awali?
18 Usulul-Kafiy Juz: 1, Uk: 14619 Usulul-Kafiy : Jz. 1, Uk. 146 kitabu Tawhid Babul-Badai20 Usulul-Kafiy : Jz. 1, Uk. 146 kitabu Tawhid Babul-Badai
14
Utokezo (al-Badaa)
Jawabu: Inahitaji kubainisha mfano kama lau mwanadamu akila sumu
yenye kuangamiza inayosababisha kifo chake hakika utakapoona tukio hili
unaweza kumpa taarifa ya kutokea kifo chake baada ya masaa, nayo ni
habari ya kweli kulingana na hali halisi isiyo na shaka, na kama mauti
hayakutokea kwa sababu ya kutokea kizuizi kisichotarajiwa kama vile
kutokea tabibu wa kumtibu mwenye ujuzi wa hali ya juu, taarifa hiyo haiwi
ya uongo wala haihesabiwi kuwa ni taarifa isiyo na chanzo, vivyo hivyo
katika taarifa ya mbinguni ambayo inatoa taarifa za kutokea baadhi ya
mambo katika siku zijazo, kwani ni za kweli kulingana na hali ya
kutokuwepo na kizuizi wala hakuna ubaya katika jambo hili isipokuwa
kutotambua Nabii au Imamu kupatikana kwa kizuizi hapo baadae. Hivyo
tuseme kwamba Mwenyezi Mungu amempa Nabii taarifa ya jambo na
hakutaka kumpa taarifa ya kutokea kwa kizuizi baadaye kwa maslahi
yanayohusiana na waja.
3. Hakika kutokea badau inasababisha Nabii au Imam kutuhumiwa kwa
uongo.
Jawabu: Hakika kutuhumiwa Nabii au Imamu kwa uongo ni jambo amba-
lo dhambi yake inamwangukia mwenye kulifanya, na tuhuma kama itato-
ka kwa kafiri basi hii sio ajabu kwake baada ya kukataa kuamini asili ya
tawhidi, utume na marejeo, na kama itatoka kwa muumini tunajaalia kuwa
imani yake itamzuia juu ya hilo, na kama haitamzuia basi hiyo ni dalili ya
udhaifu wa imani yake.
Cha muhimu ni kwamba badau sio sababu ya kimantiki ya kumtuhumu
kwa uongo bali hali nyingi za badau zilikuwa zikiambatana na
yanayosadikisha ukweli, kama ilivyo katika kisa cha Ibrahim (a.s.) pale
alipoamrishwa kumchinja mtoto wake, kwani amri mpya ya fidia ina-
maanisha kusadikisha amri ya awali ya kumchinja Ismail (a.s.) na kama
hiyo taarifa ya awali haikuwa ya kweli basi amri ya kuchinja kondoo
isingekuja ni fidia badala yake, hivyo fidia ni kwa maana ya badala.
15
Utokezo (al-Badaa)
HITIMISHO
Hakika al-Badau kwa maana ya kubadili rai haitokei kwa Mwenyezi
Mungu na wala Shia hawasemi hivyo, bali wanasema kutowezekana hilo
na ukafiri wa mwenye kusema hivyo, na kwamba inalazimu kujiepusha na
anayesema hivyo.21
Ndio, al-Badau inayokubaliwa na ambayo ni wajibu kuitakidi kwayo
imeelezwa na Aya za Qur’ani tukufu: “Mwenyezi Mungu anafuta
ayatakayo na huimarisha anayoyataka na asili ya hukumu iko
kwake.”
Na kufuta huku na kuimarisha kunakuwa wazi na kuthibiti katika anayoy-
adhihirisha Mwenyezi Mungu miongoni mwa mambo kwa ulimi wa Nabii
wake au Walii wake katika dhahiri kwa masilahi yanayohitajia kudhi-
hirishwa, kisha anayafuta na yanakuwa yale yasiyodhihiri mwanzo pamo-
ja na kutambua hilo tangu mwanzo kwa elimu yake. Badau inafanana na
nasikh (kufuta) hukumu za kisharia zilizotangulia kabla ya Nabii
Muhammad (s.a.w.w.) au nasikh ya baadhi ya hukumu ambazo zimekuja
katika sharia ya Nabii wetu (s.a.w.w.) kwa hukumu zilizofuata baadaye.22
Hakika ambaye haamini itikadi hii ya badau basi atakuwa amemuwekea
Mwenyezi Mungu kikomo katika uwezo Wake na matakwa Yake yasiyo na
mpaka, kama ilivyoashiria Qur’ani tukufu juu ya hilo katika itikadi ya
kiyahudi kwa kauli yake: “Wamesema Wayahudi mkono wa Mwenyezi
Mungu umefumba, bali imefumba mikono yao.”23 Na haya ndio
ambayo yameenea kwa baadhi ya makundi ya Kiislamu yasiyokuwa Shia
Ithina Ashariyah.
21 Aqaidul-Imamiyah cha Mudhafar uk: 45 chapa ya pili ya Najaf
22 Aqaidul-Imamiyah cha Mudhafar uk: 45 chapa ya pili ya Najaf
23 Suratul Maida: 64
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA
AL-ITRAH FOUNDATION:
1. Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka
Ishirini na Nne
2. Uharamisho wa Riba
3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza
4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili
5. Hekaya za Bahlul
6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)
7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)
8. Hijab vazi Bora
9. Ukweli wa Shia Ithnaashari
10. Madhambi Makuu
11. Mbingu imenikirimu
12. Abdallah Ibn Saba
13. Khadijatul Kubra
14. Utumwa
15. Umakini katika Swala
16. Misingi ya Maarifa
17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia
18. Bilal wa Afrika
19. Abudharr
20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu
21. Salman Farsi
22. Ammar Yasir
23. Qur'an na Hadithi
24. Elimu ya Nafsi
25. Yajue Madhehebu ya Shia
26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu
27. Al-Wahda
16
Utokezo (al-Badaa)
28. Ponyo kutoka katika Qur'an.
29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii
30. Mashukio ya Akhera
31. Al Amali
32. Dua Indal Ahlul Bayt
33. Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna.
34. Haki za wanawake katika Uislamu
35. Mwenyeezi Mungu na sifa zake
36. Amateka Na Aba'Khalifa
37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s)
38. Adhana.
39 Upendo katika Ukristo na Uislamu
40. Nyuma yaho naje kuyoboka
41. Amavu n’amavuko by’ubushiya
42. Kupaka juu ya khofu
43. Kukusanya swala mbili
44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara
45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya
46. Kusujudu juu ya udongo
47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s)
48. Tarawehe
49. Malumbano baina ya Sunni na Shia
50. Kupunguza Swala safarini
51. Kufungua safarini
52. Umaasumu wa Manabii
53. Qur’an inatoa changamoto
54. as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm
55. Uadilifu wa Masahaba
56. Dua e Kumayl
57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu
58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake
59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata
60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s)
17
Utokezo (al-Badaa)
61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza
62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili
63. Kuzuru Makaburi
64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza
65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili
66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu
67. Tujifunze Misingi Ya Dini
68. Sala ni Nguzo ya Dini
69. Mikesha Ya Peshawar
70. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu
71. Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliy
onyooka
72. Shia asema haya, Sunni asema haya, Wewe wasemaje?
73. Liqaa-u-llaah
74. Muhammad (s) Mtume wa Allah
75. Amani na Jihadi Katika Uislamu
76. Uislamu Ulienea Vipi?
77. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s)
78. Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s)
79. Urejeo (al-Raja’a )
80. Shahidi kwa ajili ya Ubinadamu
81. Kuanzia ndoa hadi kuwa wazazi
82. Myahudi wa Kimataifa
83. Uislamu na dhana
84. Mtoto mwema
85. Adabu za Sokoni
86. Johari za hekima kwa vijana
87. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza
88. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili
89. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu
90. Tawasali
91. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia
92. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu
18
Utokezo (al-Badaa)
93. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi
94. Swala ya maiti na kumlilia maiti
95. Shiya na Hadithi (kinyarwanda)
96. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu
97. Hadithi ya Thaqalain
98. Fatima al-Zahra
99. Tabaruku
100. Sunan an-Nabii
101. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)
100. Idil Ghadiri
102. Mahdi katika sunna
103. Kusalia Nabii (s.a.w)
104. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza
105. Ujumbe - Sehemu ya Pili
106. Ujumbe - Sehemu ya Tatu
107. Ujumbe - Sehemu ya Nne
108. Shiya N’abasahaba
109. Iduwa ya Kumayili
110. Maarifa ya Kiislamu.
111. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza
112. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili
113. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu
114. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne
115. Ukweli uliopotea sehmu ya Tano
19
Utokezo (al-Badaa)
BACK COVER
Maudhui ya Utokezo (Badaa’) yanazingatiwa kuwa ni kati ya masuala ya
falsafa ya Kitawhidi ambayo yamechochea utafiti wenye wigo mpana
baina ya maulamaa wa elimu ya falsafa, hiyo ni kutokana na yanay-
opatikana humo miongoni mwa masuala ya kina na ya muhimu.
Kumekuwepo na kutokuafikiana katika miji yetu ya Kiislamu, hususan
miongoni mwa wanavyuoni kuhusu usahihi wa itikadi ya Badaa’ - yaani
utokezo wa jambo fulani kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Baadhi wanase-
ma kwamba itikadi hii ni sahihi na wengine wanasema si sahihi. Baadhi ya
wanavyuoni wamekwenda mbali zaidi hadi kufikia kuwaita Waislamu
wenzao wanaoitakidi juu ya Utokezo (Badaa’) kuwa ni washirikina au
makafiri .
Lakini je, Badaa’ haina asili katika dini? Ukweli ni kwamba ina asili kati-
ka dini kwani uhalisi wake umeelezwa katika Qur’ani Tukufu, kama
utakavyoona katika kitabu hiki. Hivyo ungana na mwaandishi wa kitabu
hiki, Sayyid Abdul-Karim al-Bahbahani katika utafiti wake huu wa kie-
limu.
Kimetolewa na kuchapishwa na:
Alitrah Foundation
S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania
Simu: +255 22 2110640
Simu/Nukushi: +255 22 2127555
Barua Pepe: [email protected]
Tovuti: www.alitrah.org
Katika mtandao: www.alitrah.info
20
Utokezo (al-Badaa)