umiliki wa ardhi

2
ARDHI UMILIKI WA ARDHI Utaratibu wa utoaji wa miliki – Halmashauri ya Manispaa ya Temeke. 1. Mahitaji ya umilikishaji wa miliki mhusika/mwombaji miliki anatakiwa awe na vitu vifuatavyo: Ramani ya eneo husika. Uraia. Mkataba wa mauziano/uthibitisho toka kwa mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kama alimilikishwa kienyeji. Aandike barua ya maombi kwa Mkurugenzi wa Manispaa ikipitia kwa Afisa Mtendaji wa Kata kilipo kiwanja hicho na kwa mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo. Muombaji/mhusika atajaza Form No. 19. 2. UMILIKISHWAJI (A) Umilikishwaji wa “Allocation Letter” (miliki). Utaratibu wa kuandaliwa “Allocation Letter unafuata baada ya mhitaji kukamilisha mahitaji yote ya umilikishwaji. Utaratibu huo ni:- Kufungulishwa file la kiwanja hicho. Matumizi ya kiwanja hicho kutolewa na Afisa Mipango Miji. Makadirio ya kodi ya ardhi kuandaliwa na mthamini. Maandalizi ya “Allocation Letter” yanakamilishwa. (B) Utoaji wa Hati miliki Utoaji wa Hati hufanyika baada ya kuandaliwa “Allocation Letter”. Iwapo hakutakuwa na allocation letter hati haiwezi kuandaliwa. Utaratibu wa kuandaa hati ni kama ifuatavyo:- Ushuhuda wa malipo ambayo huandaliwa baada ya mhitaji/mmiliki kulipia ada za Serikali zilizoainishwa kwenye “Allocation Letter”. Maombi ya ramani na maandalizi ya ramani hufanyika (Request for Deed Plan). Mpima huandaa Ramani za Hati na kuzipitisha . Maandalizi ya Hati miliki yanafanyika. Mhusika anasaini Hati miliki kwa kushuhudiwa na wakili au Mwanasheria. Maafisa Ardhi Huandaa Historia ya kiwanja hicho, na kupeleka kwa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya saini na usajili. Mhusika hufuata Hati yake kwa msajili wizara ya ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Upload: lomayani

Post on 01-Oct-2015

444 views

Category:

Documents


1 download

DESCRIPTION

milki ardhi

TRANSCRIPT

  • ARDHI

    UMILIKI WA ARDHI

    Utaratibu wa utoaji wa miliki Halmashauri ya Manispaa ya Temeke. 1. Mahitaji ya umilikishaji wa miliki mhusika/mwombaji miliki

    anatakiwa awe na vitu vifuatavyo:

    Ramani ya eneo husika.

    Uraia.

    Mkataba wa mauziano/uthibitisho toka kwa mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kama alimilikishwa kienyeji.

    Aandike barua ya maombi kwa Mkurugenzi wa Manispaa ikipitia kwa Afisa Mtendaji wa Kata kilipo kiwanja hicho na kwa mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo.

    Muombaji/mhusika atajaza Form No. 19. 2. UMILIKISHWAJI

    (A) Umilikishwaji wa Allocation Letter (miliki). Utaratibu wa kuandaliwa Allocation Letter unafuata baada ya

    mhitaji kukamilisha mahitaji yote ya umilikishwaji. Utaratibu huo ni:-

    Kufungulishwa file la kiwanja hicho.

    Matumizi ya kiwanja hicho kutolewa na Afisa Mipango Miji.

    Makadirio ya kodi ya ardhi kuandaliwa na mthamini.

    Maandalizi ya Allocation Letter yanakamilishwa.

    (B) Utoaji wa Hati miliki

    Utoaji wa Hati hufanyika baada ya kuandaliwa Allocation Letter. Iwapo hakutakuwa na allocation letter hati haiwezi kuandaliwa. Utaratibu wa kuandaa hati ni kama ifuatavyo:-

    Ushuhuda wa malipo ambayo huandaliwa baada ya mhitaji/mmiliki kulipia ada za Serikali zilizoainishwa kwenye Allocation Letter.

    Maombi ya ramani na maandalizi ya ramani hufanyika (Request for Deed Plan).

    Mpima huandaa Ramani za Hati na kuzipitisha .

    Maandalizi ya Hati miliki yanafanyika.

    Mhusika anasaini Hati miliki kwa kushuhudiwa na wakili au Mwanasheria.

    Maafisa Ardhi Huandaa Historia ya kiwanja hicho, na kupeleka kwa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya saini na usajili.

    Mhusika hufuata Hati yake kwa msajili wizara ya ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

  • LESENI ZA MAKAZI

    Utaratibu wa utoaji wa Leseni za Makazi. i. Kujaza fomu ya maombi Serikali za Mtaa. ii. Mhtaji anakuja Manispaa ya Temeke kwa ajili ya kukadiliwa

    kiasi cha kodi anachotakiwa kulipa pamoja na ada ya uandaaji wa leseni.

    iii. Picha kwa ajili ya kuweka kwenye leseni. iv. Utaratibu wa kuandaa leseni unaendelea ambapo

    mhitaji/mmiliki kupewa muda wa kusubiri leseni ambao ni wiki mbili.

    v. Mkazi atachukua leseni yake akiwa na risiti yake ya malipo.

    UHAMISHO WA MILIKI

    Nyaraka zinazohitajika kwa ajili ya uhamisho wa miliki kutoka kwa mtu mmoja (mmiliki wa mwanzo) kwenda kwa mtu mwingine (mmiliki wa pili) ni:- 1. NYARAKA ZA UHAMISHO Huandaliwa na Mwanasheria/Wakili.

    a. Notijication of disposition Land form No. 29 b. Sale Agreement Mkataba wa mauziano. c. Transfer of a right of occupancy Land form No. 35. d. Application for approval of disposition Land form No. 30 e. Commitment bond Huandaliwa kwa kiwanja ambacho

    hakijaendelezwa (hakijajengwa). 2. TAARIFA YA UTHAMINI

    Taarifa ya uthamini ambayo imepitishwa na mthamini wa Manispaa ya Temeke na kupitishwa na Mthamini Mkuu wa Serikali Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

    3. URAIA

    Nakala ya cheti cha kuzaliwa iliyothibitishwa na Wakili au Mwanasheria. Au

    Nakala ya passport iliyothibitishwa na wakili au Mwanasheria. Au

    Affidavit. 4. ADA ZA SERIKALI

    Stump duty fee.

    Consent/Approval fee.

    Registration fee. Ada hii hulipwa kwa miliki zenye Hati Mhitaji anatakiwa akamilikishe vitu hivi vyote ili aweze kupewa kibali. Kibali hutolewa baada ya wiki mbili na Afisa Ardhi Mteule wa Manispaa ya Temeke. Mhitaji/mmiliki baada ya kupata kibali huenda kulipia Capital Gain Tax TRA kwa miliki zenye hati baada ya kulipa Capital Gain Tax hati zao huenda kusajiliwa kwa msajili wa hati Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kwa miliki zenye barua ya toleo au Allocation letter huandaliwa hati kwa jina la mmiliki mpya.