tume ya mipango zanzibar - planningznz.go.tzplanningznz.go.tz/doc/new/ufuatiliaji wa mpango wa...

127
TUME YA MIPANGO ZANZIBAR RIPOTI YA UFUATILIAJI WA MPANGO WA MAENDELEO 2018/2019 Agosti, 2019

Upload: others

Post on 15-Feb-2021

4 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • TUME YA MIPANGO ZANZIBAR

    RIPOTI YA UFUATILIAJI WA

    MPANGO WA MAENDELEO

    2018/2019

    Agosti, 2019

  • i

    YALIYOMO

    YALIYOMO .................................................................................................................................... i

    ORODHA YA VIFUPISHO .......................................................................................................... iii

    SURA YA KWANZA: UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MAENDELEO 2018/19

    KIFEDHA ........................................................................................................................................1

    1.1. Utangulizi ......................................................................................................................... 1

    1.2. Uchambuzi wa Kifedha wa Mpango wa Maendeleo Mwaka 2018/19 kwa Kipindi cha

    Julai 2018 - Juni 2019 ...................................................................................................... 1

    1.2.1. Mgawanyo wa Fedha za Maendeleo 2018/19 ........................................................... 1

    1.2.2. Utekelezaji wa Bajeti ya Maendeleo kwa 2018/19 ................................................... 3

    1.2.3. Ulinganisho wa Fedha kwa Mwaka 2016/17 na 2017/18 ......................................... 7

    SURA YA PILI: UTEKELEZAJI WA PROGRAMU NA MIRADI KWA KIPINDI CHA JULAI

    2018 – JUNI 2019 KWA WIZARA ................................................................................................9

    2.1. Ofisi ya Rais, Ikulu na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ......................................... 9

    2.2. Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais .................................................................................. 10

    2.3. Wizara ya Fedha na Mipango......................................................................................... 15

    2.4. Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi ............................................................. 28

    2.5. Wizara ya Biashara na Viwanda .................................................................................... 40

    2.6. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ......................................................................... 43

    2.7. Wizara ya afya ................................................................................................................ 51

    2.8. Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji, na Nishati.................................................................. 61

    2.9. Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji ............................................................. 69

    2.10. Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto ........................................ 79

    2.11. Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora ............................ 85

    2.12. Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale ................................................................. 88

    2.13. Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo ......................................................... 91

    2.14. Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ ............ 94

    SURA YA TATU: HITIMISHO .................................................................................................108

    3.1. Hitimisho ...................................................................................................................... 108

    3.2. Changamoto za Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo Julai 2018 – Juni 2019 ........ 108

    3.3. Mapendekezo katika Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ..................................... 108

  • ii

    KIAMBATISHO NAM 1: ...........................................................................................................110

    KIAMBATISHO NAM 2: ...........................................................................................................120

  • iii

    ORODHA YA VIFUPISHO

    AfDB African Development Bank

    AGOA African Growth and Opportunity Act

    AGRA Alliance for a Green Revolution in Africa

    ARV Antiretroviral

    BADEA Arab Bank for Economic Development in Africa

    BLRC Business Licensing Regulatory Council

    BoQ Bill of Quantity

    BPRA Business and Property Regulatory Authority

    CCM Chama cha Mapinduzi

    CEDAW Convention on the Elimination of All Forms of Discrimination Against

    Women

    DNA Deoxyribonucleic acid

    EDF-EU European Development Funds - European Union

    EMIS Education Management Information System

    EU European Union

    FAO Food and Agriculture Organisation

    GBV Gender Based Violence

    GPE Global Parneship for Education

    HT High Tension

    IFAD International Fund for Agriculture Development

    IMCI Integrated Management of Childhood Illnesses

    IRCH Integrated Reproductive and Child Health

    JICA Japan International Cooperation Agency

    JKU Jeshi la Kujenga Uchumi

    KIST Karume Institute of Science and Technology

    KMKM Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo

    KVZ Kikosi cha Valantia Zanzibar

    LAPA Local Adaptation of Plans of Action

    MIVARF Market Infrustructure, Value Addition and Rural Finance

    MKURABITA Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania

    MKUZA Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Zanzibar

    MoU Memorandum of Understanding

    NESAP North East Special Area Plan

    NGOs Non-Government Organisations

    OPEC Organization of Petroleum Expoting Countries

    ORIO The Facility for Infrustructure Development (Implemented by Nertherland

    Enterprise Agency)

    PPP Public Private Partnership

    SDGs Sustainable Development Goals

  • iv

    SIDA Swedish International Development Cooperation Agency

    SMIDA Small and Medium Industrial Development Authority

    SMZ Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

    SUZA State University of Zanzibar

    SWIOFISH South West Indian Ocean Fisheries Governance and Shared Growth

    Programme

    TASAF Tanzania Social Action Funds

    TB Tuberculosis

    THPS Tanzania Health Promotion Support

    TRA Tanzania Revenue Authority

    TUTU Tusome Tujifunze

    TZS Tanzanian Shilings

    UKIMWI Ukosefu wa Kinga Mwilini

    UN WOMEN United Nations Entity for Gender Equality and Empowermrnt of Women

    UNDAP United Nations Development Assistance Plan

    UNDP United Nations Development Program

    UNESCO United Nations Educational, Scientific and Cultural Organisation

    UNFPA United Nations Population Funds

    UNICEF United Nations Children’s Fund

    USDA-USAID US Department of Agriculture – US Agency for International

    Development

    VFD Virtual Fiscal Device

    VVU Virusi vya UKIMWI

    WHO World Health Organisation

    WUMU Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi

    ZAECA Zanzibar Anti-Corruption and Economic Crimes Authority

    ZAN SDI Zanzibar Special Data Infrustructure

    ZANSASP Zanzibar Non-State Actors Support Programme

    ZARI Zanzibar Agriculture Research Institute

    ZAWA Zanzibar Water Authority

    ZBC Zanzibar Broadcasting Corporation

    ZBS Zanzibar Bureau of Standards

    ZECO Zanzibar Electricity Corporation

    ZIPA Zanzibar Investment Promotion Authority

    ZIToD Zanzibar Institute of Tourism Development

    ZPPDA Zanzibar Public Procurement and Disposal of Public Assets Authority

    ZRB Zanzibar Revenue Board

    ZSTC Zanzibar State Trade Corporation

    ZURA Zanzibar Utility Regulatory Authority

    ZUSP Zanzibar Urban Services Project

  • 1

    SURA YA KWANZA: UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MAENDELEO

    2018/19 KIFEDHA

    1.1. Utangulizi

    Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa mwaka 2018/19 ni muendelezo wa utekelezaji wa

    Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Zanzibar Awamu ya Tatu (MKUZA III).

    MKUZA III unakusudia kuendeleza mageuzi ya kiuchumi na kijamii na kupunguza umasikini

    kwa (i) Kuwezesha ukuaji wa uchumi jumuishi na endelevu; (ii) Kukuza uwezo wa watu; (iii)

    Kutoa huduma bora kwa wote; (iv) Kuweka mazingira endelevu na uhimili wa mabadiliko ya

    tabianchi; na (v) Kushikamana na misingi ya utawala bora.

    1.2. Uchambuzi wa Kifedha wa Mpango wa Maendeleo Mwaka 2018/19 kwa

    Kipindi cha Julai 2018 - Juni 2019

    1.2.1. Mgawanyo wa Fedha za Maendeleo 2018/19

    Kwa mwaka 2018/19 Mpango wa Maendeleo umelenga kutekeleza jumla ya programu 27 na

    miradi 55 (miradi 14 mipya). Jumla ya TZS 613 bilioni zilipangwa kutumika kwa ajili ya

    kugharamia Mpango huo. Kati ya fedha hizo, Serikali ilipanga kutumia TZS 148.8 bilioni sawa

    na asilimia 24.3 ya bajeti ya maendeleo kutoka fedha za ndani ambazo TZS 97.29 bilioni ni kwa

    programu na miradi ya kimkakati, yenye dhima (Commitment) na TZS 51.46 bilioni kwa miradi

    mengineyo. Aidha, jumla ya TZS 464.2 bilioni sawa na asilimia 75.7 zimepangwa kutolewa na

    Washirika wa Maendeleo ambazo TZS 75.6 bilioni ni ruzuku na TZS 388.6 bilioni ni mikopo.

    Bajeti ya Mpango wa Maendeleo wa 2018/19 ni ongezeko la TZS 116.4 bilioni sawa na asilimia

    23.4 ikilinganishwa na bajeti ya maendeleo ya mwaka 2017/18 ya TZS 496.6 bilioni. Mgawanyo

    wa fedha za Maendeleo kwa Mujibu wa Wizara na Taasisi unaonekana katika jadweli namba 1

    hapo chini.

  • 2

    Jaduweli Nam 1: Mgawanyo wa fedha za Programu na Miradi ya Maendeleo 2018/19 kwa

    Mujibu wa Wizara na Taasisi

    Jina la Programu/Mradi

    KilichopangwaTZS (‘000)

    Serikali ya Mapinduzi

    Zanzibar

    Washirika

    wa

    Maendeleo

    Jumla

    Ofisi ya Rais, Ikulu na Mwenyekiti wa Baraza la

    Mapinduzi 1,000 1,000

    Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais 973 14,060 15,033

    Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa

    za Kulevya 500 500

    Wizara ya Fedha na Mipango 20,500 63,708 84,208

    Tume ya Mipango Zanzibar 609 546 1,155

    Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi 5,652 33,733 39,385

    Wizara ya Biashara na Viwanda 4,700 4,700

    Wizara ya Elimu Na Mafunzo ya Amali 5,890 77,552 83,442

    Wizara ya Afya 15,926 32,338 48,264

    Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati 7,800 79,287 87,087

    Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji 42,300 161,570 203,870

    Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake

    na Watoto 370 1,408 1,778

    Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma

    na Utawala Bora 1,050 1,050

    Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale 1,350 1,350

    Kamisheni ya Utalii 1,300 1,300

    Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo 3,800 3,800

    Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa

    na Idara Maalum za SMZ 23,510 23,510

    Ofisi ya Usajili na Vitambulisho 500 500

    Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) 5,000 5,000

    Kikosi cha Valantia 500 500

    Chuo cha Mafunzo 2,100 2,100

    Jeshi la Kujenga Uchumi 2,150 2,150

    Kikosi cha Zimamoto na Uokozi 500 500

    Mkoa wa Mjini Magharibi 770 770

    JUMLA 148,750 464,202 612,952

    Chanzo: Tume ya Mipango Zanzibar, 2018/19

    Kuanzia bajeti ya mwaka wa fedha 2016/17 kumeanzishwa mfuko wa miundombinu ambao unahudumia

    baadhi ya programu na miradi yenye hadhi ya kuimarisha miundombinu. Jumla ya programu na miradi

    kumi na tatu (13) ilipangiwa fedha kutoka katika mfuko huo ambayo iligharimu jumla ya TZS 39.5

    bilioni kwa mwaka wa fedha 2018/19. Jaduweli namba 2 linaonesha miradi iliyopangiwa fedha kutoka

    katika mfuko wa miundombinu (infrastructure funds) na bajeti yake.

  • 3

    Jaduweli Nam 2: Orodha ya Programu na Miradi ya Maendeleo 2018/19 Iliyopangiwa

    Fedha Kutoka Mfuko wa Miundombinu (TZS Milioni)

    Jina la Programu/Mradi Kiasi cha Fedha

    Kilichopangwa

    Kiasi cha Fedha

    Kilichopatikana

    Asilimia

    1. Ujenzi wa Nyumba ya Makamu

    wa Pili wa Rais

    850 819 96

    2. Programu ya Upatikanaji

    Rasilimali Fedha

    1,000 0 0

    3. Kuimarisha Taasisi ya Viwango

    Zanzibar

    2,000 581 29

    4. Uimarishaji wa Elimu Mbadala na

    Amali - Awamu ya Pili

    1,600 82 5

    5. Ujenzi wa Maabara ya Mkemia

    Mkuu

    900 910 101

    6. Kuendeleza Visima vya Ras el

    Khaimah

    4,000 3,610 90

    7. Usambazaji Umeme Vijijini 1,000 0 0

    8. Ujenzi wa barabara ya Chake -

    Wete

    1,000 0 0

    9. Ununuzi wa Land Craft 2,400 0 0

    10. Uwekaji wa Kamera na Vifaa vya

    Ulinzi

    20,000 20,727 104

    11. Ujenzi wa Kiwanda cha Ushoni 1,000 1,000 100

    12. Ujenzi wa Wodi ya Wazazi

    KMKM

    1,500 1,500 100

    13. Kuimarisha Huduma za Uzamiaji

    na Uokozi

    2,200 2,195 100

    JUMLA 39,450 31,424 80

    Chanzo: Wizara ya Fedha na Mipango, 2018/19

    1.2.2. Utekelezaji wa Bajeti ya Maendeleo kwa 2018/19

    Kwa kipindi cha kuanzia Julai 2018 hadi Juni 2019, jumla ya TZS 339 bilioni zilitumika ikiwa ni

    sawa na asilimia 55 ya lengo la TZS 613 bilioni zilizopangwa kwa kutekeleza Mpango wa

    Maendeleo Zanzibar kwa mwaka 2018/19. Kwa upande wa Serikali, jumla ya TZS 102.4 bilioni

    sawa na asilimia 69 ya bajeti yake zimetolewa na kwa upande wa Washirika wa Maendeleo,

    jumla ya TZS 236.3 bilioni sawa na asilimia 51 ya bajeti yake zimetolewa. Jaduweli nam 3

    linaonesha upatikanaji wa fedha za programu na miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha

    2018/19 kutoka Serikalini na Washirika wa Maendeleo kwa mujibu wa Wizara na Taasisi.

  • 4

    Upatikanaji wa fedha kwa programu na miradi ya maendeleo umeambatanishwa katika

    Kiambatisho I, Mgawanyo kwa Wizara na Taasisi na Kiambatisho II, Mgawanyo kwa Maeneo

    Makuu ya Matokeo ya MKUZA III.

    Kwa upande wa Washirika wa Maendeleo, kwa jumla fedha zilizotolewa kwa kipindi cha Julai

    2018 hadi Juni 2019 ni TZS 327.6 bilioni. Kati ya hizo TZS 236.3 bilioni (sawa na asilimia 72.1

    ya fedha zote za Washirika wa Maendeleo) zimetolewa kwa programu na miradi iliyomo kwenye

    Mpango wa Maendeleo 2018/19, TZS 5 bilioni (sawa na asilimia 1.5 ya fedha zote za Washirika

    wa Maendeleo) zimetolewa kwa shughuli za kawaida na TZS 86.3 bilioni (sawa na asilimia 26.4

    ya fedha zote za Washirika wa Maendeleo) zimetolewa kwa miradi ambayo haikupangiwa fedha

    lakini zimeingizwa kwa ajili ya kukamilisha miradi hiyo. Miradi hiyo ni mradi wa ujenzi wa

    uwanja wa Mao Tse Tung na mradi wa E-Government awamu ya pili. Mchanganuo wa fedha

    ambazo hazimo katika Mpango wa Maendeleo wa 2018/19 umeambatanishwa katika

    Kiambatisho III.

  • 5

    Jaduweli Nam 3: Upatikanaji wa Fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Mwaka 2018/19 kutoka Serikalini na Washirika wa

    Maendeleo kwa mujibu wa Wizara na Taasisi. (TZS Milioni)

    Jina la Programu/Mradi Kilichopangwa Kilichopatikana Asilimia Kilichopatikana

    SMZ DP Jumla SMZ DP Jumla SMZ DP Jumla

    Ofisi ya Rais, Ikulu na Mwenyekiti wa

    Baraza la Mapinduzi 1,000 1,000 999 999 100 100

    Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais 973 14,060 15,033 877 5,641 6,518 90 40 43

    Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na

    Udhibiti wa Dawa za Kulevya 500 500 166 166 33 33

    Wizara ya Fedha na Mipango 20,500 63,708 84,208 8,798 36,393 45,191 43 57 54

    Tume ya Mipango Zanzibar 609 546 1,155 425 572 997 70 105 86

    Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na

    Uvuvi 5,652 33,733 39,385 1,483 50,711 52,194 26 150 133

    Wizara ya Biashara na Viwanda 4,700 4,700 1,496 1,496 32 32

    Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali 5,890 77,552 83,442 3,683 46,051 49,734 63 59 60

    Wizara ya Afya 15,926 32,338 48,264 9,274 13,976 23,250 58 43 48

    Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na

    Nishati 7,800 79,287 87,087 5,407 40,601 46,008 69 51 53

    Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na

    Usafirishaji 42,300 161,570 203,870 32,162 38,512 70,674 76 24 35

    Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee,

    Wanawake na Watoto 370 1,408 1,778 200 3,800 4,000 54 270 225

    Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi

    wa Umma na Utawala Bora 1,050 1,050 343 343 33 33

    Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya

    Kale 1,350 1,350 1,050 1,050 78 78

    Kamisheni ya Utalii 1,300 1,300 171 171 13 13

    Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na

    Michezo 3,800 3,800 1,000 1,000 26 26

    Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali

    za Mitaa na Idara Maalum za SMZ 23,510 23,510 23,847 23,847 101 101

    Ofisi ya Usajili na Vitambulisho 500 500 500 500 100 100

  • 6

    Jina la Programu/Mradi Kilichopangwa Kilichopatikana Asilimia Kilichopatikana

    SMZ DP Jumla SMZ DP Jumla SMZ DP Jumla

    Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo

    (KMKM) 5,000 5,000 5,025 5,025 101 101

    Kikosi cha Valantia 500 500 500 500 100 100

    Chuo cha Mafunzo 2,100 2,100 1,760 1,760 84 84

    Jeshi la Kujenga Uchumi 2,150 2,150 2,149 2,149 100 100

    Kikosi cha Zimamoto na Uokozi 500 500 494 494 99 99

    Mkoa wa Mjini Magharibi 770 770 554 554 72 72

    JUMLA KUU 148,750 464,202 612,952 102,363 236,257 338,620 69 51 55

    Chanzo: Tume ya Mipango Zanzibar na Idara ya Fedha za Nje, 2018/19

  • 7

    1.2.3. Ulinganisho wa Fedha kwa Mwaka 2016/17 na 2017/18

    Ulinganisho wa bajeti kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17, mwaka wa fedha 2017/18 na mwaka wa

    fedha 2018/19 umeelezwa katika jaduweli nam 4 hapo chini.

    Jaduweli Nam 4: Ulinganisho wa Bajeti ya Maendeleo kwa Kipindi cha Mwaka wa Fedha 2016/17,

    2017/18 na 2018/19

    2016/17 2017/18 2018/19

    Kiwango cha Bajeti ya Maendeleo

    Jumla ya Bajeti ya Mwaka TZS 842 bilioni TZS 1,087 bilioni TZS 1,315 bilioni

    Bajeti ya Maendeleo TZS 396 bilioni TZS 497 bilioni TZS 613 bilioni

    Asilimia ya Bajeti ya

    Maendeleo

    47 46 47

    Kiasi cha Fedha Kilichopangwa

    Jumla TZS 396 bilioni TZS 497 bilioni TZS 613 bilioni

    Serikali TZS 71 bilioni TZS 116 bilioni TZS 149 bilioni

    Washirika wa

    Maendeleo

    TZS 325 bilioni TZS 381 bilioni TZS 464 bilioni

    Asilimia ya Mchango

    Serikali 18 23.7 24.3

    Washirika wa Maendeleo 82 76.3 75.7

    Mgawanyo wa Fedha kutoka Nje

    Ruzuku TZS 89 bilioni

    (27%)

    TZS 82 bilioni

    (22%)

    TZS 76 bilioni

    (16%)

    Mkopo TZS 236 bilioni

    (73%)

    TZS 298 bilioni

    (78%)

    TZS 389 bilioni

    (84%)

    Kiasi cha fedha Kilichotoka

    Jumla TZS 164 bilioni

    (42%)

    TZS 299 bilioni

    (60%)

    TZS 339 bilioni

    (55%)

    Serikali TZS 51 bilioni

    (71%)

    TZS 105 bilioni

    (90%)

    TZS 102 bilioni

    (69%)

    Washirika wa

    Maendeleo

    TZS 114 bilioni

    (35%)

    TZS 195 bilioni

    (51%)

    TZS 236 bilioni

    (51%)

    Chanzo: Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini, 2019

  • 8

    Mchoro Nam 1: Ulinganisho wa Upatikanaji wa Fedha 2017/18 na 2018/19 kwa Wizara na

    Taasisi

    Chanzo: Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini, 2019

    101

    101

    100

    100

    100

    100

    99

    90

    84

    78

    76

    72

    70

    69

    63

    58

    54

    43

    33

    33

    32

    26

    26

    13

    69

    100

    104

    9

    62

    100

    99

    72

    99

    100

    92

    93

    79

    99

    102

    80

    60

    80

    56

    83

    53

    90

    0 20 40 60 80 100

    Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za…

    Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM)

    Ofisi ya Usajili na Vitambulisho

    Kikosi cha Valantia

    Jeshi la Kujenga Uchumi

    Ofisi ya Rais, Ikulu na Mwenyekiti wa Baraza…

    Kikosi cha Zimamoto na Uokozi

    Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais

    Chuo cha Mafunzo

    Wizara ya Habari, Utalii, Mambo ya Kale

    Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji

    Mkoa wa Mjini Magharibi

    Tume ya Mipango

    Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji, na Nishati

    Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali

    Wizara ya Afya

    Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee,…

    Wizara ya Fedha na Mipango

    Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Udhibiti wa…

    Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa…

    Mahkama Kuu

    Wizara ya Biashara na Viwanda

    Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo

    Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi

    Kamisheni ya Utalii

    JUMLA

    2017/18 2018/19

  • 9

    SURA YA PILI: UTEKELEZAJI WA PROGRAMU NA MIRADI KWA KIPINDI CHA JULAI 2018 – JUNI 2019

    KWA WIZARA

    Sehemu hii inaelezea muhtasari wa utekelezaji wa programu na miradi ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2018/19, Julai

    2018 – Juni 2019 kwa utaratibu wa Wizara/Taasisi na programu au mradi husika.

    2.1. Ofisi ya Rais, Ikulu na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi

    i. Mradi wa Uimarishaji wa Nyumba za Viongozi na Nyumba za Serikali

    Mradi una lengo la kuimarisha makaazi ya Viongozi Wakuu wa Nchi kwa kuzifanyia

    matengenezo pamoja na ujenzi ili kuyaweka katika mazingira mazuri. Kwa mwaka

    2018/19, mradi ulipangiwa TZS 1 bilioni kutoka Serikalini na kupanga kutekeleza

    shughuli zifuatazo: Ujenzi wa nyumba za ghorofa za wafanyakazi wa huduma za Rais

    Dodoma; na ujenzi wa uzio na jiko katika Ikulu ya Chake Chake. Hadi kufikia Juni

    2019, mradi umeingiziwa TZS 999 milioni (asilimia 100) na kutekeleza yafuatayo:

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Ujenzi katika Ikulu ya Chake Chake Asilimia ya ujenzi

    iliyokamilika

    100 100 100

    Kufanya matengenezo katika Ikulu ya

    Migombani

    Asilimia ya matengenezo

    iliyokamilika

    100 100 100

    Kufanya matengenezo katika Ikulu ya

    Bosnia, Maisara

    Asilimia ya matengenezo

    iliyokamilika

    100 92 92

    Ujenzi wa ukuta wa kuzuia

    mmong’onyoka wa udongo katika Ikulu

    ya Mkoani

    Asilimia ya matengenezo

    iliyokamilika

    100 92 92

  • 10

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Ujenzi wa eneo la kuwekea jenereta

    umefanyika katika Ikulu ya Dodoma

    Asilimia ya ujenzi

    iliyokamilika

    100 100 100

    2.2. Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais

    i. Mradi wa Ujenzi wa Nyumba ya Makaazi ya Makamo wa Pili wa Rais Pemba.

    Mradi una lengo la kuimarisha makaazi ya Makamu wa Pili wa Rais ili kuweza kutoa huduma bora. Mradi kwa mwaka 2018/19

    ulipangiwa TZS 850 milioni kutoka Serikalini na kupanga kutekeleza shughuli zifuatazo: Ujenzi wa nyumba ya makazi ya Makamo

    wa Pili wa Rais; ujenzi wa nyumba mbili za wafanyakazi, ujenzi wa kibanda cha askari, ujenzi wa jiko na sehemu ya kulia, ujenzi wa

    kibanda cha jenereta, ujenzi wa sehemu ya kufanyia mazoezi, ujenzi wa sehemu ya kufulia, ujenzi wa nyumba ya ulinzi (mapokezi) na

    ujenzi wa msikiti. Hadi kufikia Juni 2019, mradi uliingiziwa TZS 819 milioni (asilimia 96) na kutekeleza yafuatayo:

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Ujenzi wa nyumba ya makazi ya

    Makamo wa Pili wa Rais, Pagali

    Pemba

    Asilimia ya ujenzi

    iliyokamilika

    100 80 80 Ujenzi wa majengo sita umekamilika hadi

    kuezekwa, ujenzi wa majengo yaliyobakia

    ikiwemo nyumba ya Makamo wa Pili

    unaendelea kwa hatua mbalimbali. Kazi inayoendelea sasa ni kukamilisha uwekaji

    wa maji, umeme na milango

    ii. Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF III).

    Mpango una lengo la kuziwezesha kaya masikini sana kuongeza kipato, fursa na uwezo wa kugharamia mahitaji muhimu ya

    kibinaadamu hasa chakula, afya na elimu. Mpango huu unakusudia kutekeleza miradi iliyoibuliwa na wananchi katika nyanja mbali

    mbali za elimu, afya, maji safi na ajira za muda. Kwa mwaka 2018/19 mpango ulipangiwa TZS 12.7 bilioni ambazo TZS 40 milioni

    kutoka Serikalini na TZS 12.7 bilioni kutoka kwa Washirika wa Maendeleo (Benki ya Dunia), na kupanga kutekeleza shughuli

    zifuatazo: kuratibu shughuli za programu ya TASAF kati ya Zanzibar na Dar es Salaaam na kufanya malipo kwa kaya masikini na

    kusaidia jamii kutekeleza miradi ya muda. Hadi kufikia Juni 2019, mradi uliingiziwa TZS 5.35 bilioni (asilimia 42) ambapo TZS 25

  • 11

    milioni (asilimia 63) zilitoka Serikalini na TZS 5.3 bilioni (asilimia 42) zilitoka kwa Washirika wa Maendeleo na kutekeleza

    yafuatayo:

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Kufanya malipo kwa kaya

    maskini na kusaidia jamii

    kutekeleza miradi ya muda

    Idadi ya kaya maskini

    zilizopatiwa fedha

    33,632 32,572 96.8 Jumla ya Shehia 233 zimepatiwa

    fedha Unguja na Pemba

    Kulipa fedha za masharti na ajira

    za muda kwa kaya Unguja na

    Pemba

    Idadi ya kaya

    zilizopatiwa fedha

    Unguja

    18,204

    32,347

    177.6

    Idadi ya kaya 17,838 zinazonufaika

    zimelipwa kwa ajili ya malipo ya

    fedha za masharti na 14,509 kwa ajili

    ya kazi za jamii

    Pemba

    14,368

    26,268

    182.8

    Jumla ya kaya 14,044 zimelipwa kwa

    ajili ya malipo ya fedha za masharti na

    wanufaika 12,224 wamelipwa kwenye

    sekta zisizo rasmi

    Kutekeleza mpango wa kuweka

    akiba na kukuza uchumi wa kaya.

    Idadi ya vikundi

    vilivyoweka hakiba

    2,235 2,055 92

    Kufanya ujenzi wa miundombinu

    ya vituo vya kutolea huduma kwa

    jamii Unguja

    Asilimia ya ujenzi

    iliyokamilika

    100 96 96 Ujenzi wa jengo la Kituo cha Afya cha

    Kianga umekamilika, shughuli za

    umaliziaji zinaendelea

    iii. Mradi wa Kujenga Uwezo wa Kukabiliana na Maafa Zanzibar

    Mradi una lengo la kuimarisha uwezo wa Taifa katika kujiandaa na kukabiliana na maafa. Kwa mwaka 2018/19, mradi ulipangiwa

    TZS 106 milioni kutoka kwa Washirika wa Maendeleo (UNDP), na kupanga kutekeleza shughuli zifuatazo: Kuandaa mipango ya

    kukabiliana na maafa katika Wilaya za Chake Chake, Mkoani na Kati; Kutoa mafunzo kwa watoto yatima juu ya kukabiliana na

    maafa; Kutoa elimu ya kukabiliana na maafa katika skuli za maandalizi katika Wilaya za Kati, Magharibi ‘A’, Kaskazini ‘A’,

    Micheweni na Mkoani; na Kuandaa na kurusha hewani vipindi 25 vya redio na sita vya TV juu ya kukabiliana na maafa. Hadi kufikia

    Juni 2019, mradi uliingiziwa TZS 164 milioni (asilimia 155) kutoka kwa Washirika wa Maendeleo na kutekeleza shughuli zifuatazo:

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Kutoa mafunzo kwa Walimu wa elimu ya awali kwa Idadi ya walimu 420 420 100

  • 12

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    skuli za Magharibi ‘A’, wilaya ya Kati na Kaskazini

    ‘B’ na Micheweni na Mkoani kwa Pemba kuhusu

    matumizi ya dawa za DRR

    walioshiriki katika

    mafunzo

    Kuandaa mipango ya kukabiliana na maafa mara tu

    yanapojitokeza (Emergence Preparedness Response

    Plan) kwa upande wa wilaya za Mkoani na Chake

    Chake Pemba na wilaya ya Kati kwa Unguja.

    Idadi ya mipango

    iliyoandaliwa

    3 3 100

    Kufanya mafunzo ya njia za kukabiliana na

    kupunguza maafa katika vituo vinne (4) vya watoto

    na vitatu (3) vya wazee kwa Unguja na Pemba.

    Idadi ya vituo vya jamii

    vilivyopatiwa uelewa

    7 4 57

    iv. Mradi wa Kukuza Uwezo wa Kitaifa wa Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi

    Mradi una lengo la kukuza uwezo wa taasisi mbali mbali za Serikali katika kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi. Kwa mwaka

    2018/19 ulipangiwa TZS 840 milioni ambazo TZS 33 milioni kutoka Serikalini na TZS 807 milioni kutoka kwa Washirika wa

    Maendeleo (Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)) na kupanga kutekeleza shughuli zifuatazo: Kuandaa Mwongozo wa Uingizaji wa

    Masuala ya Mabadiliko ya Tabia Nchi na kujenga uwezo kwa maafisa katika uingizaji wa hatua mahsusi za Mabadiliko ya Tabianchi

    katika Mipango ya sekta; Kukuza uwezo wa kitengo cha Mabadiliko ya Tabianchi na maafisa (Focal persons) kutoka Ofisi ya

    Makamo wa Pili wa Rais, Wizara ya Fedha na Mipango na Tume ya Mipango Zanzibar ili kuweza kusaidia upangaji wa hatua za

    mabadiliko ya tabianchi, upatikanaji wa fedha na ufuatiliaji wa utekelezaji; Kukuza uwezo kwa Serikali za mitaa ili kuweza kuongoza

    maendeleo ya LAPAs na shughuli zake na Kuandaa vikao vya Kamati Kiongozi na Kamati ya Wataalamu. Hadi kufikia Juni 2019,

    mradi uliingiziwa TZS 173 milioni (asilimia 21) ambapo TZS 20 milioni (asilimia 61) zilitoka Serikalini na TZS 153 milioni (asilimia

    19) zilitoka kwa Washirika wa Maendeleo na kutekeleza shughuli zifuatazo:

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Kukuza uwezo wa kitengo cha

    Mabadiliko ya Tabianchi na maafisa

    (Focal persons) kutoka Ofisi ya Makamo

    wa Pili wa Rais, Wizara ya Fedha na

    Mipango na Tume ya Mipango Zanzibar

    Idadi ya maafisa

    waliojengewa uwezo

    5 5 100

  • 13

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    ili kuweza kusaidia upangaji wa hatua za

    mabadiliko ya tabianchi, upatikanaji wa

    fedha na ufuatiliaji wa utekelezaji

    Kuandaa vikao vya Kamati Kiongozi na

    Kamati ya Wataalamu

    Idadi ya vikao vya

    Kamati Kiongozi na

    Kamati ya Wataalamu

    vilivyofanyika

    6 2 33

    Kufanya tathmini ya ripoti za kitaalam za

    washauri elekezi ili kumpata mshauri

    mmoja ambaye ataweza kutoa huduma

    kwa mradi

    Idadi ya vikao vya

    tathmini vilivyofanyika

    5 3 60 Ripoti ya mwisho ya

    tathmini ya kumpata

    mshauri elekezi

    inatayarishwa ili itumwe

    makao makuu ya mradi

    Ivory Coast kwa hatua

    Kuhudhuria mafunzo ya muda mfupi

    nchini Eswatini (zamani Swaziland) juu

    ya uandaaji wa miradi (concept note) ya

    miradi ya mabadiliko ya tabianchi (Green

    Climate Fund)

    Idadi ya wafanyakazi

    waliopatiwa mafunzo 5 5 100

    v. Mradi wa Kuimarisha Usimamizi wa Mazingira, Maliasili na Mabadiliko ya Tabianchi – Zanzibar

    Mradi una lengo la kusaidia katika kufanyia kazi changamoto zilizojitokeza za mazingira na mabadiliko ya tabianchi kwa kukuza

    uwezo kwa taasisi mbali mbali za Zanzibar. Kwa mwaka 2018/19 ulipangiwa TZS 496.5 milioni ambazo TZS 50 milioni kutoka

    Serikalini na TZS 446.5 milioni kutoka kwa Washirika wa Maendeleo (UNDP) na kupanga kutekeleza shughuli zifuatazo: Kuandaa

    vikao vya Kamati Kiongozi na Kamati ya Wataalamu; Kuimarisha uwezo wa taasisi zinazohusika na mabadiliko ya tabianchi; Kukuza

    uwezo katika upatikanaji na usimamizi wa rasilimali fedha. Hadi kufikia Juni 2019, mradi uliingiziwa TZS 13 milioni (asilimia 26)

    kutoka Serikalini na kutekeleza yafuatayo:

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Kutayarisha maandiko (Concept note)

    ya utayarishaji wa miradi ya

    Idadi ya maandiko

    iliyokamilika

    4 0 0 Taratibu za kumpata mshauri elekezi

    ambaye atakuwa Mkufunzi wa

  • 14

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    maendeleo ya kukabiliana na

    mabadiliko ya tabianchi katika sekta

    nne (4) kwa kutumia njia shirikishi

    mafunzo ya uandishi wa maandiko ya

    mradi zinaendelea Idadi ya taasisi

    zitakazojengewa uwezo

    17 0 0

    Kurejesha maeneo yaliyoharibika kwa

    mabadiliko ya tabia nchi kwa kufanya

    utafiti mdogo wa kujua ukubwa wa

    athari na hali halisi iliyoharibika

    pamoja na gharama zinazohitajika

    katika marekebisho

    Idadi ya maeneo

    yaliyofanyiwa uhimili

    wa mabadiliko ya

    tabianchi

    2 1 50 Utafiti wa kimazingira (rapid

    assessment) umefanyika eneo la

    Msuka ambalo limeathirika na

    mmong’onyoko wa fukwe. Utafiti huo

    unaonyesha gharama na hatua za

    kuchukuliwa ili kulirejesha eneo hilo

    katika hali yake ilikuwepo awali.

    Asilimia ya utafiti

    iliyokamilika

    100 100 100

    Kufanya ukarabati wa Idara ya

    Mazingira pamoja na ununuzi wa

    vifaa mbalimbali kwa ajili ya

    kuimarisha utekelezaji wa shughuli za

    mradi

    Asilimia ya ukarabati

    iliyokamilika 100 95 95 Idara ya Mazingira imefanyiwa

    ukarabati na baadhi ya vifaa

    vimenunuliwa

    Kufanya ziara ya kutafuta na

    kuchagua maeneo ambayo

    yatafungwa vifaa vya kusomea habari

    za hali ya hewa

    Idadi ya maeneo

    yaliyofanyiwa ziara

    15 15 100 Maeneo 15 yalitembelewa kwa

    upande wa Unguja na Pemba

    Kufanya ziara ya ukaguzi wa vifaa

    vya kusomea hali ya mvua Idadi ya ziara

    zilizofanyika

    2 1 50 Ziara moja ya kuvikagua vifaa

    vinavyotumika kusomea hali ya mvua

    imefanyika kwa upande wa Unguja na

    moja inatarajiwa kufanyika Pemba

    Kufanya mafunzo ya mabadiliko ya

    Tabianchi na mipango ya matumizi ya

    ardhi kwa watendaji wa Idara ya

    Mipango,miji na vijiji na wadau

    wengine

    Idadi ya watendaji

    waliopatiwa mafunzo 12 12 100 Mafunzo ya siku mbili (2)

    yamefanyika kwa watendaji wa Idara

    ya Mipango,miji na vijiji na wadau

    wengine

    Kufanya mafunzo ya mabadiliko ya

    tabianchi na mipango ya matumizi ya

    ardhi kwa watendaji wa serikali za

    mitaa

    Idadi ya watendaji

    waliopatiwa mafunzo 75 75 100 Mafunzo ya siku tatu (3) yamefanyika.

  • 15

    2.2.1. Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Udhibiti wa Madawa ya Kulevya

    i. Ujenzi wa Kituo cha Tiba na Marekebisho ya Tabia

    Mradi una lengo la kukiendeleza kituo cha Kidimni ili kiweze kutoa huduma bora kwa

    waathirika wa dawa za kulevya. Kwa mwaka 2018/19 ulipangiwa TZS 500 milioni

    kutoka Serikalini na kupanga kutekeleza shughuli zifuatazo: Kuendelea na ujenzi wa

    kituo cha kurekebisha tabia kwa waathirika wa madawa ya kulevya na ununuzi wa vifaa.

    Hadi Juni 2019, mradi uliingiziwa TZS 166 (asilimia 33) na kutekeleza yafuatayo:

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Kuendelea na ujenzi wa kituo cha

    kurekebisha tabia kwa waathirika wa madawa

    ya kulevya na ununuzi wa vifaa

    Asilimia ya ujenzi

    iliyofikiwa

    100 56 56 Ujenzi umefikia hatua

    ya kukamilisha ghorofa

    ya kwanza na kuendelea

    na ghorofa ya pili

    Asilimia ya vifaa

    vilivyonunuliwa

    100 0 0 Vifaa vitanunuliwa

    baada ya kukamilika

    ujenzi

    2.3. Wizara ya Fedha na Mipango

    i. Programu ya Ujenzi wa Ofisi za Serikali Zanzibar

    Programu ina lengo la kujenga Ofisi za Serikali ili kuweka mazingira bora ya kazi kwa wafanyakazi. Kwa mwaka 2018/19 programu

    ilipangiwa TZS 15 bilioni kutoka Serikalini na kupanga kutekeleza shughuli zifuatazo: Kukamilisha ujenzi wa Ofisi za Wizara ya

    Fedha na Mipango; Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora; na Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee,

    Vijana, Wanawake na Watoto Pemba; Kuanza ujenzi wa Wizara ya Fedha na Mipango Unguja; na Kuanza ujenzi wa Mahkama Kuu,

    Tunguu. Hadi kufikia Juni 2019, mradi uliingiziwa TZS 8.2 bilioni (asilimia 55) na kutekeleza yafuatayo:

  • 16

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Kukamilisha ujenzi wa Wizara

    tatu katika eneo la Gombani

    Pemba

    Asilimia ya ujenzi wa jengo

    iliyokamilika

    100 100 100 Ujenzi umekamilika na jengo

    lishafunguliwa rasmi. Jumla ya

    Wizara sita zimeweza kuingia

    katika majengo hayo badala ya

    wizara tatu.

    Kuanza ujenzi wa Wizara ya

    Fedha na Mipango, Unguja

    Asilimia ya matayarisho

    iliyokamilika

    100 95 95 Mkandarasi ameshapatikana na

    mikataba ya ujenzi

    imewasilishwa kwa Mwanasheria

    Mkuu wa Serikali ili kupata

    ruhusa yakuendelea na ujenzi.

  • 17

    ii. Programu ya Kuimarisha Huduma za Miji (ZUSP)

    Programu ina lengo la kuimarisha upatikanaji wa

    huduma bora za miji ya Zanzibar na uhifadhi wa eneo la

    urithi wa Mji Mkongwe ambalo ni kivutio kwa watalii

    na kulinda historia ya mji wa Zanzibar. Kwa mwaka

    2018/19 programu ilipangiwa TZS 41.9 bilioni kutoka

    kwa Washirika wa Maendeleo (Benki ya Dunia) na

    kupanga kutekeleza shughuli zifuatazo: Kuendelea na

    kazi ya ujenzi wa jaa la taka la Kibele na kutayarisha

    mkakati wa usimamizi wa taka; Kuimarisha mandhari

    ya mji (Green Corridor) katika maeneo ya pembezoni

    mwa barabara ya Malindi-Baraza la Wawakilishi la

    zamani, Mlandege-Maisara na Mkunazini Kariakoo;

    Kuweka taa za barabarani (Street Light) katika maeneo

    ya barabara za Uwanja wa ndege - Mnazimmoja,

    Kwerekwe - Kiembe Samaki na Kinazini - Kariakoo

    mpaka Kilimani; na Kuendelea na kazi ya ujenzi wa

    mitaro katika maeneo mbali mbali ya ng’ambo ya mji.

    Hadi kufikia Juni 2019, mradi uliingiziwa TZS 30.6

    bilioni (asilimia 59) na kutekeleza yafuatayo:

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Kuendelea na kazi ya ujenzi wa

    jaa la taka taka la Kibele na

    kutayarisha mkakati wa

    usimamizi wa taka taka

    Asilimia ya kazi

    iliyofikiwa

    40 16 40 Mkataba umeshasainiwa na mshauri elekezi

    yupo katika eneo la kazi. Utekelezaji wa

    shughuli mbalimbali umeanza ikiwemo

    ukataji wa miamba, ujenzi wa tabaka la

    mwanzo la jaa nakadhalika. Aidha, fidia kwa

    waathirika wa ujenzi wa jaa umefanyika.

    Kuimarisha mandhari ya mji

    (Green Corridor) katika

    Asilimia ya

    matayarisho

    100 100 100 Mshauri Elekezi anaendelea kufanya

    merekebisho ya Upembuzi Yakinifu kwa

  • 18

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    maeneo ya pembezoni mwa

    barabara ya Malindi-Baraza la

    Wawakilishi la zamani,

    Mlandege-Maisara na

    Mkunazini Kariakoo;

    iliyofikiwa mujibu wa maoni yaliyotolewa na wadau.

    Kuweka taa za barabarani

    (Street Light) katika maeneo ya

    barabara za Uwanja wa ndege-

    Mnazimmoja, Kwerekwe-

    Kiembe Samaki na Kinazini-

    Kariakoo mpaka Kilimani kwa

    Unguja; na miji ya Mkoani,

    Chakechake na Wete kwa

    Pemba.

    Asilimia ya

    uchimbaji na

    ulazaji bomba

    (sleeves)

    iliyofikiwa

    100 100 100 Uwekaji wa mabomba kwa upande wa

    Unguja umefikia kilomita 13.5 kati ya 14.3

    na kwa upande wa Pemba umefikia kilomita

    6 kati kilomita 17.4.

    Ujenzi wa msingi wa maji ya

    mvua wa system C unaoanzia

    Mwanakwerekwe, Magogoni

    kupitia Sebleni, Kibanda Maiti,

    Kwa Abbass Hussein na

    kumalizia baharini

    Asilimia ya ujenzi

    iliyokamilika

    100 78 78 Watu 143 wamelipwa fidia ya TZS 2.32

    bilioni ili kupisha eneo ambalo linahitajika ili

    mkandarasi amalizie kazi ya misingi ya maji

    ya mvua kwa maeneo ambayo bado

    hayajamalizika. Jumla ya kilomita 6.3

    zimekamilika ujenzi kati ya 10.6.

    iii. Programu ya Upatikanaji Rasilimali Fedha

    Programu ina lengo la kuimarisha upatikanaji wa rasilimali fedha kwa kuimarisha mapato yatokanayo na kodi na mapato yasiyotokana

    na kodi kupitia utekelezaji wa sheria, miongozo na kanuni za fedha. Kwa mwaka 2018/19, programu ilipangiwa TZS 1.0 bilioni

    kutoka Serikalini na kupanga kununua mashine za kutolea risiti (VFD). Hadi kufikia Juni 2019, programu haijangiziwa fedha, taratibu

    za manunuzi zinaendelea.

    iv. Programu ya Kuimarisha Maendeleo Endelevu (UNDAP II)

    Programu ina lengo la kusaidia, kuratibu, ufuatiliaji na tathmini wa MKUZA III pamoja na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya

    Dunia (SDGs) kwa ajili ya kutoa uelewa wa utekelezaji wa malengo yaliyopangwa ili kupata matokeo yake, na kuhakikisha kwamba

  • 19

    rasilimali zilizopo zinatumika kwa ufanisi mkubwa na kwa manufaa ya watu na taifa kiujumla. Kwa mwaka 2018/19 programu

    ilipangiwa TZS 273.3 milioni ambapo TZS 50 milioni kutoka Serikalini na TZS 223.3 milioni kutoka kwa Washirika wa Maendeleo

    (UNDP) na kupanga kutekeleza shughuli zifuatazo: Ukarabati wa ofisi ya mratibu wa mradi; Kuandaa vikao viwili vya Kamati

    Kiongozi na vinne vya Kamati ya Kitaalamu; Kuandaa mkakati wa mawasiliano (Communication Strategy) wa MKUZA III; Kufanya

    mikutano na taasisi za Serikali kwa ajili ya kuwajengea uelewa wa uingizaji wa MKUZA III pamoja na Malengo ya Maendeleo

    Endelevu katika mipango ya sekta zao; Kuandaa utaratibu wa utekelezaji wa Muongozo wa Mashirikiano ya pamoja na Washirika wa

    Maendeleo; Kufanya uchambuzi na kufuatilia miradi ya UNDP na Washirika wa Maendeleo wengine ili kutambua changamoto

    zilizopo; Kutoa mafunzo kwa maafisa wa idara ya Fedha za Nje katika fani za utafutaji wa misaada, usimamizi wa misaada n.k; na

    Kutayarisha mfumo na sera ya utowaji wa taarifa (Data Dissemination), na kutoa mafunzo ya kutumia Micro data kutoka kwa

    webportal. Hadi kufikia Juni 2019, mradi uliingiziwa TZS 120 milioni (asilimia 54) kutoka kwa Washirika wa Maendeleo na

    kutekeleza yafuatayo:

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Kuandaa vikao viwili vya Kamati

    Kiongozi na vinne vya Kamati ya

    Kitaalamu

    Idadi ya vikao vilivyofanyika 6 2 33

    Kuandaa mkakati wa mawasiliano

    (Communication Strategy) wa MKUZA

    III

    Asilimia ya uandaaji wa mkakati

    iliyokamilika

    100 90 90

    Kufanya mikutano na taasisi za Serikali

    kwa ajili ya kuwajengea uelewa wa

    uingizaji wa MKUZA III pamoja na

    Malengo ya Maendeleo Endelevu katika

    mipango ya sekta zao

    Idadi ya mikutano iliyofanyika 3 3 100

    Idadi ya washiriki waliojengewa

    uwelewa

    165 165 100

    Kuandaa utaratibu wa utekelezaji wa

    Muongozo wa Mashirikiano ya pamoja

    na Washirika wa Maendeleo

    Asilimia ya muongozo wa

    mashirikiano ya pamoja

    100 100 100

    v. Mradi wa Uimarishaji Utawala bora Awamu ya Tatu

    Mradi una lengo la ukuzaji na uimarishaji wa masuala ya kifedha na kiuchumi kwa kujenga ufanisi na usimamizi wa fedha na

    uboreshaji wa mazingira ya kibiashara na unatarajiwa kukamilika mwaka 2019. Kwa mwaka 2018/19 ulipangiwa TZS 7.2 bilioni

  • 20

    ambapo TZS 150 milioni kutoka Serikali na TZS 7.1 bilioni kutoka kwa Washirika wa Maendeleo (Benki ya Maendeleo ya Afrika

    (AfDB)) na kupanga kutekeleza shughuli zifuatazo: Kuandaa vikao vya Kamati Kiongozi na Kamati ya Kitaalamu; Kuandaa

    matangazo manane (8); Kuratibu Mkakati wa Kuzuia Rushwa na kuadhimisha siku ya rushwa kimataifa; Kutoa mafunzo kwa

    Wajumbe wa Kamati ya Fedha ya Baraza la Wawakilishi kuhusu wajibu na majukumu yao; Kuandaa semina kwa Wajumbe wa

    Kamati ya Fedha ya Baraza la Wawakilishi kuhusu ripoti ya Mkaguzi wa hesabu za Serikali kuhusu matumizi ya fedha za umma;

    Kufanya malipo kwa washauri elekezi kwa ajili ya kazi za kuandaa Mpango Mkuu wa Uchumi wa Micheweni (Micheweni Master

    Plan), Sekta ya Uwekezaji na Mapitio ya Fedha za Umma; Kutoa mafunzo kwa maafisa wa Taasisi za Serikali zinazonufaika na mradi

    katika fani mbali mbali; Kununua vifaa mbali mbali vya ofisini kwa taasisi za Serikali ikiwemo vifaa vya kuimarisha huduma za

    kimtandao, jenereta na vifaa vya mfumo wa ulinzi na usalama. Hadi kufikia Juni 2019, TZS 5.1 bilioni (asilimia 72) ziliingizwa na

    Washirika wa Maendeleo na kutekeleza shughuli zifuatazo:

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Kuandaa vikao vya Kamati Kiongozi na

    Kamati ya Kitaalamu

    Idadi ya vikao

    vilivyofanyika

    3 1 33

    Kuandaa matangazo manane (8) Idadi ya matangazo

    waliyotolewa

    8 6 75

    Mafunzo ya muda mfupi, warsha na

    semina kwa kwa taasisi zinazofaidika na

    mradi

    Idadi ya taasisi

    zilizopatiwa mafunzo

    20 18 90 Mafunzo yamefanyika kwa

    ZPPDA, Ofisi ya Mdhibiti na

    Mkaguzi Mkuu wa Serikali,

    Idara ya Mhasibu Mkuu wa

    Serikali, Idara ya Sera za

    Kodi, Wizara ya Biashara na

    viwanda, ZAECA, ZIPA na

    Kitengo cha PPP

    Ununuzi wa vifaa vya ofisi kwa taasisi

    zinazonufaika na mradi

    Asilimia ya vifaa

    vilivyonunuliwa

    100 100 100

    Kuandaa sera ya sekta binafsi na

    Kuendeleza sera ya maendeleo ya sekta

    binafsi pamoja na mkakati

    Asilimia ya maandalizi

    ya sera yaliyofikiwa

    100 100 100 Ripoti ya mwisho ya kazi ya

    kuandaa sera ya sekta binafsi

    pamoja na mkakati

    imeshakamilika.

    Tathmini ya matumizi ya Fedha za Umma Idadi ya ripoti za

    tathmini ya matumizi

    ya Fedha za Umma

    4 4 100 Mshauri elekezi tayari

    amewasilisha ripoti ya

    mwisho ya kazi hiyo. Na

  • 21

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    kuanza matayarisho ya

    kuwasilisha kwa wadau.

    Kuandaa sekta vipaumbele kwa Zanzibar

    vya ZIPA

    Idadi ya Sekta

    vipaumbele

    zilizotayarishwa

    3 3 100 Mshauri elekezi

    ameshawasilisha rasimu ya

    mwisho ya ripoti ya kazi hiyo.

    Kuandaa Mpango Mkuu wa Micheweni Asilimia ya mpango

    iliyokamilika

    100 30 30 Mshauri elekezi tayari

    amewasilisha ripoti ya awali.

    hatua iliopo ni kukubaliwa na

    wadau ili kukamilisha

    uandaaji wa Micheweni

    Master Plan.

    vi. Mradi wa Uimarishaji Rasilimali za Ndani na Usimamizi wa Mali Asili

    Mradi una lengo la kuimarisha rasilimali za ndani na usimamizi wa maliasili. Mradi unaratibiwa na Wizara ya Fedha na Mipango na

    kunufaisha Taasisi za Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Zanzibar. Kwa mwaka 2018/19,

    mradi ulipangiwa TZS 4.27 bilioni ambapo TZS 100 milioni kutoka Serikalini na TZS 4.2 bilioni kutoka Washirika wa Maendeleo

    (Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)) na kupanga kutekeleza shughuli zifuatazo: Kuandaa vikao vya Kamati Kiongozi na Kamati

    ya Wataalamu; Kuandaa matangazo nane (8); Kuratibu shughuli za Kamati ya Tathmini za ununuzi; Kuimarisha mfumo wa usimamizi

    wa ulipaji kodi wa ZRB na uimarishaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (ZURA); Kununua vifaa vya ofisini

    za Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (ZURA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Bodi ya Mapato ya

    Zanzibar (ZRB); Kutoa mafunzo ya muda mfupi, warsha, semina na ziara za kujifunza kwa Taasisi za Serikali zinazonufaika na

    mradi. Hadi kufikia Juni 2019, mradi uliingiziwa TZS 346 milioni (asilimia 8) kutoka kwa Washirika wa Maendeleo, na kutekeleza

    shughuli zifuatazo:

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Mafunzo ya muda mfupi kwa

    wafanyakazi wa ZRB, ZURA na

    TRA juu ya uimarishaji wa

    mapato ya ndani.

    Idadi ya wafanyakazi

    waliopatiwa mafunzo

    70 65 93

  • 22

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Kuwatafuta washauri elekezi

    kwa kazi kumi (10) tofauti

    zitakazosaidia kuimarisha

    mifumo na hatua mbali mabali za

    kuimarisha ukusanyaji wa

    mapato kwa ZRB

    Asilimia ya

    utekelezaji wa

    utafutaji wa washauri

    elekezi

    100 30 30 Kati ya kazi hizo nane (8) ni za

    huduma na mbili (2) za Vifaa. Kazi

    hizo zimewasilishwa Benki ya

    Maendeleo ya Afrika kupata ridhaa ya

    kuendelea na mchakato wa kuwapata

    wataalamu elekezi

    Ununuzi wa vifaa vya ofisi (ICT

    and office equipment) kwa

    mamlaka ya Mapato TRA-

    Zanzibar na ZURA.

    Asilimia ya ununuzi

    wa vifaa iliyofikiwa

    100 80 80

    Ununuzi wa vifaa vya maabara

    kwa ZURA.

    Asilimia ya

    utekelezaji

    100 90 90

    vii. Mradi wa Kuendeleza Bandari ya Mangapwani

    Mradi una lengo la kuimarisha na kuendeleza mindombinu ya

    barabara, umeme na maji katika eneo la bandari ya mafuta na gesi

    asilia inayokusudiwa kujengwa huko Mangapwani. Kwa mwaka

    2018/2019 mradi ulipangiwa TZS 4.2 bilioni kutoka Serikalini na

    kupanga kutekeleza shughuli zifuatazo: Ujenzi wa barabara ya

    kuingilia katika eneo la mradi; na Uwekaji wa miundombinu ya

    umeme na maji. Hadi kufikia Juni 2019, mradi uliingiziwa TZS

    553 milioni (asilimia 13) na kutekeleza shughuli zifuatazo:

  • 23

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Ujenzi wa barabara ya kuingilia

    katika eneo la mradi

    Asilimia ya ujenzi wa

    barabara iliyofikiwa

    100 100 100 Barabara imesafishwa kuanzia

    barabara kuu mpaka eneo la mradi

    kilomita 3.5

    Uwekaji wa miundombinu ya

    umeme na maji

    Asilimia ya uwekaji wa

    miundombinu ya maji

    iliyofikiwa

    100 100 100

    Asilimia ya uwekaji wa

    miundombinu ya umeme

    iliyofikiwa

    100 100 100

    Ujenzi wa nyumba za makaazi

    kwa waliohamishwa ilikupisha

    mradi

    Asilimia ya ujenzi wa

    nyumba iliyofikiwa

    100 25 25 Ujenzi wa nyumba 31 katika kijiji

    cha Dundua katika Shehia ya

    Kidanzini umefikia hatua ya msingi

    viii. Mradi wa Kuimarisha Demokrasia na Utawala Bora Katika Kuzisaidia Asasi za Kiraia (ZANSASP)

    Mradi una lengo la kuimarisha demokrasia na utawala bora katika kuzisaidia asasi za kiraia katika uwajibikaji, ushirikishwaji na

    utekelezaji wa sera za maendeleo. Kwa mwaka 2018/19, mradi ulipangiwa TZS 250 milioni kutoka kwa Washirika wa Maendeleo

    (Jumuiya ya Ulaya (EU)) na kupanga kutekeleza shughuli zifuatazo: Kuzisaidia asasi za kiraia katika masuala mbali mbali ya

    kimaendeleo ili kutimiza malengo yao; Kusaidia Idara ya Fedha za Nje katika masuala ya usimamizi wa misaada na utekelezaji wa

    mkakati na sera ya misaada; Kuzijengea uwezo asasi za kiraia katika masuala mbali mbali yanayohusu uandaaji wa sera na utekelezaji

    wake; Kuijengea uwezo Idara ya Fedha za Nje katika masuala ya makubaliano ya majadiliano ya misaada na washirika wa maendeleo.

    Hadi kufikia Juni 2019, mradi uliingiziwa TZS 138 milioni (asilimia 55) na kutekeleza shughuli zifuatazo:

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Kuzisaidia asasi za kiraia katika

    masuala mbali mbali ya

    kimaendeleo ili kutimiza

    malengo yao

    Idadi ya asasi ya kiraia

    zilizosaidiwa

    11 11 100

  • 24

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Kuzijengea uwezo asasi za kiraia

    katika masuala mbali mbali

    yanayohusu uandaaji wa sera na

    utekelezaji wake

    Idadi ya asasi ya kiraia

    zilizojengewa uwezo

    11 11 100

    Kusaidia Idara ya Fedha za Nje

    katika masuala ya usimamizi wa

    misaada na utekelezaji wa

    mkakati na sera ya misaada

    Asilimia ya utekelezaji wa

    mkakati wa mkakati wa sera

    ya misaada

    100 100 100

    Kuijengea uwezo Idara ya Fedha

    za Nje katika masuala ya

    makubaliano ya majadiliano ya

    misaada na washirika wa

    maendeleo.

    Idadi ya maafisa

    waliojengewa uwezo

    10 0 0 Kuchelewa kwa uidhinishwaji

    wa fedha kutoka EU kwa muda

    ulopangwa

    2.3.1. Tume ya Mipango Zanzibar

    i. Programu ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA)

    Programu ina lengo la kurahisisha urasimishaji wa rasilimali na biashara zilizo katika mfumo usio rasmi ili kukidhi mahitaji ya

    kisheria na umiliki wa mali ndani ya mfumo wa uchumi wa kisasa. Sekta zinazohusika na mpango huu ni biashara na ardhi. Kwa

    mwaka 2018/19, programu ilipangiwa TZS 300 milioni ambazo TZS 200 milioni kutoka SMZ na TZS 100 milioni kutoka Serikali ya

    Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kupanga kutekeleza yafuatayo: Kushiriki mafunzo elekezi ya MKURABITA kwa maafisa

    usimamizi wa mradi, pamoja na maafisa ardhi na biashara Tanzania Bara; Utoaji wa hati kwa maeneo yaliyotambuliwa ya Nungwi,

    Chwaka, Kiungoni na Chokocho; Kuratibu vikao vya Kamati Kiongozi na Kamati ya Wataalamu; Ununuzi wa vifaa Pemba;

    Urasimishaji wa ardhi maeneo ya Mbweni, Kilimani na Mazizini; Kujenga uwezo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo juu ya

    usimamizi na uendeshaji wa biashara kwa Wilaya ya Kaskazini B Unguja na Mkoani Pemba, Kujenga uwezo kwa wafanyabiashara

    wadogo wadogo juu ya usimamizi na uendeshaji wa biashara kwa Unguja na Pemba; na Kurasimisha ardhi katika maeneo ya

    Kizimbani, Nungwi na Chwaka. Hadi kufikia Juni 2019, mradi uliingiziwa TZS 195 milioni (asilimia 65) ambazo TZS 195 milioni

    (asilimia 98) zilitoka Serikalini na hakuna fedha iliyoingizwa kutoka kwa Washirika wa Maendeleo na kutekeleza yafuatayo:

  • 25

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Utengenezaji wa hati katika

    maeneo yaliyotambuliwa

    Idadi ya hati zilizotayarishwa 2,000

    900 45

    Kutoa mafunzo ya ujasiriamali

    na kuwathibitisha wajasiriamali

    wadogo

    Idadi ya wajasiriamali

    waliopewa mafunzo

    200 200 100 Wilaya zilizopatiwa mafunzo

    ni za Mkoani na Kaskazini

    ‘B’, Wilaya ya Magharibi ‘A’

    na Wete Pemba

    Kufanya urasimishaji wa ardhi Idadi ya viwanja

    vilivyotambuliwa taarifa zake

    2,500 1,160 46 Eneo lililoendelezwa ni la

    kwa Bint Amrani-Mpendae

    Kufanya vikao vya Kamati

    kiongozi na Kamati ya

    Wataalamu

    Idadi ya vikao vilivyofanyika 6 6 100

    ii. Kupunguza Umasikini na Ufuatiliaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu

    Mradi una lengo la kuendeleza uwezo wa wananchi katika kuibua na kutekeleza miradi midogo midogo itakayowawezesha

    kujikwamua na umasikini. Kwa mwaka 2018/19, mradi ulipangiwa TZS 403.3 milioni, ambapo TZS 180 milioni kutoka Serikali na

    TZS 223.3 milioni kutoka kwa Washirika wa Maendeleo (UNDP) na kupanga kutekeleza yafuatayo: Kujenga uelewa kwa wananchi

    wa wilaya ya Mkoani juu ya matokeo ya ripoti ya utafiti wa shehia maskini katika Wilaya hiyo; Kusaidia utekelezaji wa mapendekezo

    yaliyotolewa katika ripoti ya utafiti wa hali ya umasikini katika Wilaya ya Mkoani; Kufanya tafiti ya hali ya umasikini (Poverty

    Profile) kwa shehia/maeneo ya Wilaya ya Micheweni; Kutoa mafunzo juu ya uibuaji na uandaaji wa miradi midogo midogo ya

    maendeleo na mikakati ya kujikwamua na umasikini katika Mikoa mitano; Kusaidia uingizaji wa malengo ya SDGs katika masuala ya

    umasikini, mazingira, jinsia na mabadiliko ya tabianchi katika mfumo wa ugatuzi; Kuendeleza uwezo kwa taasisi za Serikali za Mitaa

    na Serikali kuu jinsi ya kuandaa na kutekeleza mikakati ya mabadiliko ya tabianchi na jinsia itakayozingatia upunguzaji wa umasikini;

    Kusaidia taasisi za Serikali katika kuratibu na kusimamia utekelezaji na ufuatiliaji wa MKUZA III na SDGs; Kufanya mapitio ya Dira

    ya Maendeleo ya 2020 na uandaaji wa Dira mpya ya Maendeleo ya Zanzibar. Hadi kufikia Juni 2019, mradi uliingiziwa TZS 140

    milioni (asilimia 78) kutoka Serikalini na hakuna fedha kutoka kwa Washirika wa Maendeleo na kutekeleza yafuatayo:

  • 26

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Kujenga uelewa kwa wananchi wa

    wilaya ya Mkoani juu ya matokeo ya

    ripoti ya utafiti wa shehia masikini

    Idadi ya shehia

    zilizopatiwa uelewa

    12 12 100 Wananchi wamepatiwa uelewa juu

    ya matokeo ya utafiti wa shehia

    masikini uliofanyika katika shehia

    12 za Wilaya ya Mkoani – Pemba

    Kufanya utafiti kuhusiana na

    umaskini kutokana na taarifa za

    Utafiti wa Mapato na Matumizi ya

    Kaya Zanzibar wa 2014/15 Wilaya

    ya Micheweni na Mkoani

    Idadi ya tafiti

    zilizofanyika

    2 1 50 Utafiti wa hali ya umasikini katika

    shehia 12 za wilaya ya Mkoani

    umekamilika

    Kutoa mafunzo juu ya uibuaji na

    uandaaji wa miradi midogo midogo

    ya maendeleo na mikakati ya

    kujikwamua na umasikini katika

    Mikoa mitano

    Idadi ya Mikoa

    itakayopatiwa

    Mafunzo

    3 2 67 Mafunzo juu ya uibuaji na

    uandaaji wa miradi midogo

    midogo ya Maendeleo

    yamefanyika katika Mikoa ya

    Kaskazini Unguja na Kusini

    Pemba.

    Kutoa mafunzo kwa maafisa wa

    Tume ya Mipango juu ya uchambuzi

    wa hali ya umasikini

    Idadi ya wafanyakazi

    waliopatiwa mafunzo

    32 32 100

    iii. Kuoainisha Masuala ya Idadi ya Watu katika Afya ya Uzazi, Jinsia na Kupunguza Umasikini

    Mradi una lengo la kuratibu utekelezaji wa Sera ya Idadi ya Watu kwa kuoanisha masuala ya afya ya uzazi, jinsia na umasikini katika

    mipango ya maendeleo. Kwa mwaka 2018/2019, mradi ulipangiwa TZS 252 milioni ambapo TZS 29 milioni kutoka Serikali na TZS

    223 milioni kutoka kwa Washirika wa Maendeleo (Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Idadi ya Watu

    (UNFPA)) na kupanga kutekeleza shughuli zifuatazo: Kuandaa vikao vya kamati ya kitaalamu kwa kila robo ya mwaka; Kuandaa

    vikao vya Kamati za Masheha kuhusu daftari la shehia; Kutoa mafunzo kwa masheha na wasaidizi wao juu ya ujazaji wa daftari la

    shehia; Kuimarisha taarifa za msingi za vizazi na vifo katika ngazi ya Shehia kupitia daftari la Shehia na Mfumo wa Usajili wa Vizazi

    na Vifo; Uimarishaji wa utumizi wa nyenzo za mipango katika kuripoti taarifa za maendeleo endelevu ya dunia (SDGs); Kushiriki

    maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani na kuandaa ripoti ya hali ya idadi ya watu; Uandaaji na usimamiaji wa Sera ya Idadi ya

    Watu Zanzibar. Hadi kufikia Juni 2019, mradi uliingiziwa TZS 582 milioni (asilimia 231) ambazo TZS 10 milioni (asilimia 34)

    zilitoka Serikalini na TZS 572 milioni (asilimia 257) zilitoka kwa Washirika wa Maendeleo na kutekeleza yafuatayo:

  • 27

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Kufanya ufuatiliaji wa daftari la Shehia Idadi ya Shehia

    zilizotembelewa

    38 36 95

    Kutoa uwelewa juu ya ujazaji wa taarifa

    katika daftari la Shehia

    Idadi ya vipindi TV na redio 2 1 50

    Kutoa mafunzo kwa Masheha na wasaidizi

    wao juu ya ujazaji wa daftari la Shehia.

    Idadi ya Masheha waliopatiwa

    mafunzo

    162 21 13

    Kuchapisha daftari la Shehia Idadi ya madaftari

    yaliyochapishwa

    895 735 82

    Kufanya vikao vya robo mwaka kwa

    watekelezaji wa miradi ya UNFPA

    Idadi ya vikao vilivyofanyika 4 1 25

    iv. Mradi wa Kuendeleza Tafiti na Ubunifu

    Mradi una lengo la kuinua matumizi ya matokeo ya tafiti kwa maendeleo ya Zanzibar ili kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi

    na teknolojia. Kwa mwaka wa 2018/19, mradi ulipangiwa TZS 200 milioni kutoka Serikalini na kupanga kuratibu utekelezaji wa tafiti

    zilivyoainishwa katika kitabu cha Agenda za utafiti Zanzibar. Hadi Juni 2019, TZS 80 milioni (asilimia 40) ziliingizwa na kutekeleza

    yafuatayo:

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Kufanya uchambuzi wa maombi ya

    tafiti zilizowasilishwa kwa ajili ya

    kupatiwa fedha za kufanyia tafiti hizo

    Asilimia ya maombi

    yaliyofanyiwa

    uchambuzi

    100 100 100 Jumla ya maombi 12

    yaliwasilishwa, kati ya hayo

    maombi ya tafiti 5 yamepita kwa

    ajili ya kupatiwa ufadhili.

    Kuratibu utafiti wa mchango wa

    Wazanzibar wanoishi nje ya nchi

    (Diaspora).

    Asilimia ya utekelezaji 100 95 95 Uwasilishaji wa rasimu ya awali

    ya utafiti kwa wadau mbali

    mbali umefanyika

    Kuratibu utafiti wa usarifu wa zao la

    mwani.

    Asilimia ya Utekelezaji 100 95 95 Uwasilishaji wa rasimu ya awali

    ya utafiti kwa wadau mbali

    mbali umefanyika

  • 28

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Kuratibu utafiti juu ya chanzo cha

    vifo vya watoto.

    Asilimia ya Utekelezaji 100 90 90 Jumla ya watoto 3000 chini ya

    miaka 5 wamefanyiwa

    uchunguzi wa afya zao

    2.4. Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi

    i. Programu ya Kuendeleza Miundo Mbinu ya Mifugo na Wafugaji Wadogowadogo

    Programu ina lengo la kuimarisha miundombinu ya uzalishaji na masoko ya mifugo na bidhaa zake ili kuongeza kiwango cha

    uzalishaji na tija kwa wafugaji wadogo wadogo. Aidha, programu inakusudia kuimarisha miundombinu ya kufanyia kazi za utafiti wa

    mashamba ya mifugo sambamba na kuwapatia elimu wafugaji wadogo wadogo juu ya uzalishaji bora. Kwa mwaka 2018/19,

    programu ilipangiwa TZS 856 milioni kutoka Serikalini na kupanga kutekeleza shughuli zifuatazo: Kujenga karantini ya mifugo

    Nziwengi-Gando Pemba na kumalizia karantini ya Donge-Muanda; Kufanya utafiti wa uzalishaji wa ng'ombe wa maziwa na kuku wa

    kienyeji na ukaguzi; Ununuzi wa chanjo za maradhi ya mahepe ya kuku na maradhi ya vibuma na matengenezo ya mitambo ya

    biogas; Kutoa mafunzo kwa wafugaji 240 wa ng'ombe wa maziwa katika Wilaya sita za Unguja na wafugaji wa kuku wa kienyeji 160

    Wilaya ya Kaskazini A, B na Kusini Unguja na Micheweni Pemba pamoja na kuchapisha vipeperushi. Hadi kufikia Juni 2019, mradi

    uliingiziwa TZS 658 milioni (asilimia 77) na kutekeleza yafuatayo:

    Shughuli iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    halisi

    Asilimia ya

    Utelezaji

    Maelezo

    Kufanya malipo ya mazao ya

    wakulima

    Idadi ya wakulima

    waliolipwa

    40 40 100

    Uongozi na ufuatiliaji wa shughuli

    za miradi

    Idadi ya miradi

    iliyofatiliwa na

    kutekelezwa

    2 2 100

    Kukarabati ofisi ya watendaji wa

    mradi Maruhubi

    Ujenzi wa ofisi ya

    watendaji Maruhubi

    1 1 100

    Kukamilisha ujenzi wa karantini

    ya mifugo Gando Pemba kwa

    kulipa fidia wakulima 40

    waliopisha ujenzi wa uzio kwenye

    Ujenzi wa karantini ya

    mifugo Gando Pemba

    1 1 100

    Idadi ya wakulima

    waliolipwa fidia

    40 40 100

  • 29

    Shughuli iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    halisi

    Asilimia ya

    Utelezaji

    Maelezo

    karantini

    Kujenga matangi mawili ya maji

    Pangeni

    Idadi ya matangi yaliyo

    jengwa

    2 2 100

    Kukamilika kwa kituo cha Afya

    cha Mifugo na Uzalishaji-Fuoni

    Idadi ya kituo cha afya

    kilichokamilika

    1 1 100

    ii. Programu ya Kusaidia Kilimo na Uhakika wa Chakula

    Programu ina lengo la kuongeza ubora wa mbegu za mpunga na utumiaji wa teknolojia ya kisasa itakayopelekea kuongezeka kwa

    uzalishaji wa zao hilo na kuongeza kipato kwa wakulima na kuwa na uhakika wa chakula. Kwa mwaka 2018/19, programu ilipangiwa

    TZS 4.78 bilioni ambazo TZS 80 milioni kutoka Serikalini na TZS 4.7 bilioni kutoka kwa Washirika wa Maendeleo (Benki ya Dunia)

    na kupanga kutekeleza shughuli zifuatazo: Ununuzi wa mbegu na kutoa mafunzo ya vitendo kwa wakulima 1,500 juu ya taaluma bora

    ya uzalishaji; Kuweka mfumo endelevu wa uzalishaji na usambazaji mbegu; Kutoa mafunzo ya uendeshaji na usimamizi kwa jumuiya

    za umwagiliaji; Kutoa mafunzo ya kusimamia na kuendesha miundombinu ya umwagiliaji kwa mafundi na maafisa ugani; Kuanzisha

    mashamba darasa 200 ya kilimo shadidi na kutoa mafunzo kwa wakulima 1,500 wa Unguja na Pemba; Kutoa mafunzo juu ya mbinu

    bora za uzalishaji wa mpunga kwa maafisa ugani 80; Kununua pembejeo kwa ajili ya Mpango wa Ruzuku; Kuandaa ziara za

    kimafunzo kwa Jumuiya za Umwagiliaji na wakulima wa Unguja na Pemba. Hadi kufikia Juni 2019, mradi uliingiziwa TZS 1.8

    bilioni (asilimia 37) ambazo TZS 25 milioni (asilimia 31) zilitoka Serikalini na TZS 1.7 bilioni (asilimia 37) zilitoka kwa Washirika

    wa Maendeleo na kutekeleza yafuatayo:

  • 30

    Shughuli iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Kufanya ziara ya mafunzo kwa

    wakulima

    Idadi ya wakulima

    walioshiriki kwenye

    mafunzo

    112 112 100 Ziara za mafunzo zimefanyika

    mkoani Morogoro na baina ya

    Unguja na Pemba.

    Kutoa mafunzo ya matumizi ya vifaa

    vya kisasa vya upimaji ardhi (modern

    surveying equipment) kwa maafisa

    umwagiliaji, Unguja na Pemba.

    Idadi ya maafisa

    waliopatiwa mafunzo

    20 20 100 Maafisa umwagiliaji 20 (7

    wanawake na 13 wanaume)

    wamepatiwa mafunzo ya utumiaji

    wa vifaa vya upimaji vya kisasa

    (Total station na GPS).

    Kutoa mafunzo ya matumizi ya

    software za uandaaji wa michoro na

    ramani kwa wahandisi wa

    umwagiliaji, Unguja na Pemba.

    Idadi ya wahandisi

    waliopatiwa mafunzo

    10 10 100 Wahandisi wamejifunza matumizi ya

    design software (AutoCad Civil 3D

    na spreadsheet), kuandaa michoro na

    ramani za miundombinu ya

    umwagiliaji.

    Kuendeleza miundombinu ya

    umwagiliaji maji kwa baadhi ya

    maeneo yaliyokusudiwa

    Idadi ya skimu

    zilizoekewa

    miundombinu ya

    umwagiliaji maji

    9 2 22 Ujenzi wa miundombinu katika

    skimu za Mtwango na Kwalempona

    unaendelea, Mtwango ujenzi

    umefikia asilimia 75 na

    Kwalempona asilimia 55

    Upitiaji wa michoro na ramani

    pamoja utayarishaji wa Kabrasha la

    Zabuni kwa skimu saba (7)

    (Kibondemzungu, Koani,

    Mchangani, Bandamaji, Machigini,

    Dobi na Ole) umekamilika na zabuni

    ya ujenzi imeshatangazwa.

    Idadi ya visima

    vilivyochimbwa

    6 6 100 Visima sita (6) kwa ajili ya

    umwagiliaji vimechimbwa katika

    mabonde ya Kibondemzungu, Koani,

    Bandamaji, Machigini, Dobi na Ole.

    Idadi ya skimu

    zilizoungwa umeme

    7 7 100 Kazi ya uungaji umeme katika skimu

    za Kibondemzungu, Koani,

    Mchangani, Bandamaji, Machigini,

    Dobi na Ole imekamilika.

    Idadi ya vibanda vya 6 3 50 Ujenzi wa vibanda vya pampu

  • 31

    Shughuli iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    pampu zilizojengwa unaendelea katika skimu za

    Machigini, Dobi na Ole.

    Kutoa mafunzo ya kilimo shadidi

    (SRI) kupitia mashamba ya maonesho

    Idadi ya wakulima

    waliopatiwa Mafunzo

    1500 1500 100

    Idadi ya mashamba ya

    maonesho

    yalioanzishwa

    200 50 25 Idadi haikufikia lengo kwa vile

    ujenzi wa miundombinu ya

    umwagiliaji haujakamilika.

    Kutoa ruzuku ya pembejeo za mpunga

    kwa wakulima katika maeneo ya

    umwagiliaji, Unguja na Pemba.

    Idadi ya tani za mbegu

    zilizotolewa ruzuku

    kwa wakulima.

    12 8.3 69

    Kuzalisha mbegu bora za mpunga Kilogramu za mbegu

    daraja la msingi

    zilizozalishwa

    400 400 100 Mbegu za msingi aina ya SARO

    (kilo 200) na SUPA BC (kilo 200)

    zimezalishwa kwa mashirikiano na

    Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (ZARI)

    Tani za mbegu

    zilizothibitishwa

    zilizozalishwa

    15 12.1 81 Mbegu aina ya SUPA BC

    imezalishwa kupitia wakulima wa

    mkataba.

    Kuzalisha kilo 400 za mbegu bora za

    mpunga za daraja la mtafiti (pre-basic

    seeds), aina ya SUPA BC kwa

    kushirikiana na ZARI.

    Kilogramu za mbegu

    daraja la msingi (pre-

    basic seeds)

    zilizozalishwa

    400 0 0 Kazi ya uzalishaji inaendelea na

    tayari mpunga umeshapandikizwa

    katika Bonde la Mwera.

    Kuzalisha tani 1 za mbegu za mpunga

    daraja la msingi kwa kushirikiana na

    Kitengo cha Pembejeo.

    Tani za mbegu daraja

    la msingi

    zilizozalishwa

    1 0 0 Kazi ya uzalishaji inaendelea na

    tayari mpunga umeshapandikizwa

    katika Bonde la Mwera.

    Kuhamasisha matumizi ya mbegu

    bora za mpunga kupitia vyombo vya

    habari.

    Idadi ya vipindi vya

    redio vilivyotangazwa

    6 6 100 Vipindi vimetangazwa kupitia ZBC

    na Coconut FM

    Idadi ya programu za

    TV zilizoonyeshwa

    2 2 100 Programu zimerushwa hewani

    kupitia ZBC.

    Kufanya ziara za siku ya wakulima

    shambani kwa wakulima 230 na

    Maafisa Ugani 8 kuona ubora wa

    mbegu ya SUPA BC na SARO 5.

    Idadi ya wakulima na

    Maafisa Ugani

    walioshiriki katika

    ziara

    238 248 104 Wakulima 240 na Maafisa Ugani

    wanane (8) wameshiriki Siku ya

    Wakulima Shmbani iliofanyika

    katika Bonde la Cheju ambapo

    wamejifunza umuhimu wa kutumia

    mbegu bora za mpunga ili kuongeza

  • 32

    Shughuli iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    uzalishaji.

    Kununua mbegu ya mpunga daraja la

    mtafiti (pre-basic seeds) kilo 60

    kutoka Tanzania Bara.

    Kilogramu za mbegu

    daraja la msingi (pre-

    basic seeds)

    zilizonunuliwa

    60 60 100 Mbegu aina ya SARO 5

    imenunuliwa kutoka Kituo cha

    Utafiti wa Mpunga, KATRIN

    kilichopo Morogoro.

    Kuwapa mafunzo wataalamu wa

    maabara na wakaguzi wa mbegu na

    wataalamu wa maabara.

    Idadi ya wataalamu

    wa maabara na

    wakaguzi waliopatiwa

    mafunzo

    12 12 100 Mafunzo haya ya wiki mbili

    yamefanyika mara mbili katika

    Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa

    mbegu, Morogoro.

    Kuandaa ziara za mafunzo ya kwa

    Jumuiya za Umwagiliaji maji kutoka

    skimu 16 Unguja na Pemba

    Idadi ya skimu

    zilizopatiwa mafunzo

    24 22 91 Washiriki kutoka mabonde 16

    (manane Unguja na manane Pemba)

    wametembelea Chuo cha Kilimo cha

    Kilimanjaro, skimu za umwagiliaji

    za Lower Moshi na Leki Tatu

    ambapo wamejifunza uendeshaji wa

    skimu na namna ya kutanua wigo wa

    vyanzo vya mapato vya Jumuiya.

    Kutoa mafunzo ya mbinu bora za

    uzalishaji wa mpunga kwa Maafisa

    Ugani

    Idadi ya Maafisa

    Ugani waliopatiwa

    mafunzo

    40 40 100 Washiriki wa mafunzo walikuwa

    Wanawake 20 na 20 wanaume.

    Kutoa mafunzo ya mbinu

    mchanganyiko za kudhibiti wadudu na

    maradhi kwa wakulima 240 (120

    Unguja na 120 Pemba).

    Idadi ya wakulima

    waliopatiwa mafunzo

    240 240 100 Mafunzo haya yametolewa kupitia

    Skuli za Wakulima.

    Kulipa fidia kwa wakulima

    watakaoharibikiwa na vipando/mali

    katika mabonde yatayojengwa

    miundombinu.

    Idadi ya wakulima

    waliolipwa fidia

    100 115 115 Pemba wakulima 83 kutoka skimu za

    Kwalempona (8), Machigini (25) na

    Dobi (50), Unguja wakulima 32

    kutoka skimu za Bandamaji (17),

    Kibondemzungu (2), Koani (1) na

    Mchangani (12).

  • 33

    iii. Programu ya Umwagiliaji Maji

    Programu ina lengo la kuendeleza na kuimarisha kilimo cha umwagiliaji maji nchini pamoja na kutoa taaluma ya kiufundi juu ya

    ujenzi na ukarabati wa miundombinu, kushajihisha na kusimamia jumuiya za wakulima katika mabonde ya umwagiliaji maji pamoja

    na kutoa elimu juu ya matumizi bora ya pembejeo za kilimo kwa wakulima. Kwa mwaka 2018/19, programu ilipangiwa TZS 9 bilioni

    ambazo TZS 500 milioni zilipangwa kutoka Serikalini na TZS 8.5 bilioni kutoka kwa Washirika wa Maendeleo (Serikali ya Korea) na

    kupanga kutekeleza shughuli zifuatazo: Ulipaji wa fidia ya mazao kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji maji katika

    mabonde ya Makwararani na Mlemele kwa Pemba, Kinyasini, Kilombero na Chaani kwa Unguja; Kuunga umeme wa laini kubwa

    katika mabonde ya Kibonde Mzungu, Mchangani, Koani na Bandamaji kwa Unguja na Dobi kwa Pemba; Ukarabati wa miundombinu

    ya umwagiliaji maji katika mabonde ya Cheju, Bumbwisudi, Kibokwa, Uzini na Mtwango; na Ujenzi wa miundombinu ya

    umwagiliaji hekta 1,404 katika mabonde ya Cheju (900), Kilombero (100), Kibokwa (194), Chaani (71), Makwararani (78) na

    Mlemela (61). Hadi kufikia Juni 2019, mradi uliingiziwa TZS 43.6 bilioni (asilimia 484) ambapo TZS 500 milioni (asilimia 100)

    zilitoka Serikalini na TZS 43.2 bilioni (asilimia 507) zilitoka kwa Washirika wa Maendeleo na kutekeleza yafuatayo:

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Ujenzi na ukarabati wa

    miundombinu ya umwagiliaji

    maji, katika

    skimu za Mwera, Cheju, Kianga,

    Bumbwisudi na Mtwango kwa

    Unguja na Makombeni na

    Mangwena kwa Pemba

    Ukubwa wa eneo (mita)

    uliofanyiwa ukarabati

    wa miundombinu ya

    umwagiliaji maji

    1,500 550 36 Ukarabati wa mitaro Cheju 400 mita,

    Mwera 50 mita na Bumbwisudi 60 mita.

    Aidha ukarabati wa jengo la ofisi wa

    bonde la Mwera na Mtwango umefanyika.

    Idadi ya visima

    vilivyokarabatiwa

    4 4 100 Matengenezo na ufungaji wa pampu mpya

    katika Bonde la Cheju pamoja na

    matengenezo ya mifumo ya umeme katika

    vibanda 3 vya pampu vya Cheju,

    Mkanyageni na Kirindunda yamefanyika.

    Ulipaji wa fidia wa mazao kwa

    mabonde ya Makwararani na

    Mlemele kwa Pemba na

    Kinyasini, Kilombero, Kibokwa

    na Chaani kwa Unguja kwenye

    mradi wa ujenzi wa miundo

    mbinu ya umwagiliaji maji

    kupitia mkopo wa Exim Bank -

    Idadi ya mabonde

    yaliyolipiwa fidia

    7 2 28 Kazi ya ulipaji wa fidia ya mazao

    imefanyika kwa wakulima 28. Aidha

    mchakato wa ulipaji wa fidia kwa bonde

    la Kinyasini unaendelea ambapo jumla ya

    TZS 438 milioni zilitegemewa kutumika

    katika shughuli hiyo.

  • 34

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Korea

    Kuendeleza kilimo cha

    umwagiliaji maji cha

    mbogamboga katika bonde la

    Machekechuni

    Ukubwa wa eneo

    (hekta) lililoendelezwa

    5 0 0 Kazi hii imeanza kwa uchimbaji wa

    Kisima kwa ajili ya umwagiliaji wa

    mbogamboga

    iv. Programu ya Miundombinu ya Soko, Kuongeza Thamani na Misaada Vijijini (MIVARF)

    Programu ina lengo la kuimarisha miundombinu ya masoko ya kilimo, kuongeza thamani ya bidhaa za kilimo na kuanzisha mfumo wa

    utoaji wa huduma za kifedha vijijini. Kwa mwaka 2018/19, programu ilipangiwa TZS 1.3 bilioni ambazo TZS 300 milioni kutoka

    Serikalini na TZS 950 milioni kutoka kwa Washirika wa Maendeleo (IFAD/AGRA/AfDB) na kupanga kutekeleza shughuli zifuatazo:

    Kulipa fidia kwa nyumba na vipando vilivyoathirika na upitishwaji wa barabara za Mkwajuni – Kivumoni – Mtambwe; Kuwapatia

    mafunzo ya utaalamu na biashara wasarifu wa mazao; Kuzijengea uwezo jumuiya za Wilaya na kijamii kwa kuwapatia mafunzo; na

    Kufanya mikutano na semina. Hadi kufikia Juni 2019, programu iliingiziwa TZS 1.04 bilioni (asilimia 83) ambapo TZS 300 (asilimia

    100) zilitoka Serikalini na TZS 737 (asilimia 78) zilitoka kwa Washirika wa Maendeleo na kutekeleza yafuatayo:

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Kulipa fidia kwa nyumba na

    vipando vilivyoathirika na

    upitishwaji wa barabara za

    Mkwajuni – Kivumoni –

    Mtambwe

    Idadi ya wananchi

    waliolipwa fidia

    1,308 1,308 100

    Kuwajengea uwezo wazalishaji

    na kuwaunganisha na masoko

    Idadi ya mabaraza ya

    wakulima

    10 10 100 Mabaraza yanaendelea na mchakato wa

    kuanzisha chombo kimoja cha wakulima

  • 35

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    yaliyowezeshwa wote wa Zanzibar kitakachoundwa

    kutokana na mabaraza ya wilaya.

    Idadi ya vikundi vya

    wazalishaji na wastaafu

    vilivyopatiwa mafunzo

    40 50 125 Vikundi vimepatiwa mafunzo ya usarifu,

    masoko, uwendeshaji, uongozi, utunzaji

    wa kumbukumbu, masuala ya kifedha na

    mikopo. Idadi iliongezeka kutokana na

    uhitaji wa mafunzo ya huduma za kifedha.

    Idadi ya mikutano ya

    tathmini iliyofanyika

    33 33 100

    Idadi ya mikutano ya

    mapitio ya watoa

    huduma iliyofanyika

    3 2 67 Watoa huduma waliazna kazi Oktoba

    2018, badala ya Julai 2018 kama

    ilivyotarajiwa.

    Idadi ya kamati

    zilizopata mafunzo

    14 14 100 Kamati 10 za vikundi vya usarifu na

    vikundi vinne vya masoko vilipata

    mafunzo yakiwemo: kutayarisha mipango

    biashara, uongozi na uwendeshaji wa

    masoko, kutayarisha miongozo

    mbalimbali ya utendaji, utunzaji

    kumbukumbu na fedha.

    Kuwawezesha vikundi vya

    wazalishaji kushiriki katika

    maonesho ya kilimo ya Kitaifa

    Idadi ya Vikundi

    vilivyoshiriki katika

    maonesho

    12 12 100 Vikundi vinawezeshwa kushiriki

    maonesho ya Nane Nane kwa Unguja, and

    the maonesho ya siku ya chakula Duniani

    kwa Pemba.

    v. Uimarishaji Uvuvi wa Bahari Kuu

    Mradi una lengo la kuanzisha uvuvi wa kina kirefu cha maji ili kuongeza uzalishaji wa samaki utakaopelekea kuongezeka kwa ajira,

    biashara na ukuaji wa uchumi. Kwa mwaka 2018/19, mradi ulipangiwa TZS 10.4 bilioni ambazo TZS 3.7 bilioni kutoka Serikalini na

    TZS 6.8 bilioni kutoka kwa Washirika wa Maendeleo (JICA) na kupanga kutekeleza shughuli zifuatazo: Ujenzi wa soko na diko la

    Malindi; na Kufanya tathmini ya hali ya kimazingira. Hadi kufikia Juni 2019, mradi uliingiziwa TZS 604 (asilimia 9) kutoka kwa

    Washirika wa Maendeleo na kutekeleza shughuli yafuatayo:

  • 36

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Ujenzi wa soko na diko la

    Malindi

    Asilimia ya ujenzi

    iliyofikiwa

    100 0 0 Kazi ya ujenzi haijaanza, lakini

    Mkandarasi ameshapatikana na ameanza

    matayarisho ya ujenzi

    Kufanya tathmini ya hali ya

    kimazingira

    Asilimia ya tathmini

    iliyofikiwa

    100 0 0

    vi. Kuimarisha Ufugaji wa Mazao ya Baharini

    Mradi una lengo la kuongeza uzalishaji kwa kuimarisha ufugaji wa samaki na ulimaji wa mwani kwa wakulima. Aidha, mradi

    unakusudia kusambaza vifaranga vya samaki, vyakula na nyenzo za kuzalishia samaki, pamoja na kufanya tafiti mbali mbali za

    kuongeza uzalishaji. Kwa mwaka 2018/19, mradi ulipangiwa TZS 6.9 bilioni ambazo TZS 200 milioni kutoka Serikalini na TZS 6.7

    bilioni kutoka kwa Washirika wa Maendeleo (FAO/Korea) na kupanga kutekeleza shughuli zifuatazo: Kujenga kituo cha kupokelea

    vifaranga vya samaki, kaa na majongoo ya baharini katika maeneo ya Chokocho – Pemba; Kutotoa vifaranga vya samaki, kaa na

    majongoo ya baharini; Kuanzisha mashamba ya mfano Unguja na Pemba; Kuwajengea uwezo wafugaji wa mazao ya baharini kwa

    kuwapatia mafunzo juu ya mbinu bora za ufugaji wa mazao ya baharini; Kuandaa Mkakati wa kuendeleza kituo baada ya kumaliza

    muda wa mradi. Hadi kufikia Juni 2019, mradi haujaingiziwa fedha lakini umetekeleza yafuatayo:

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Kuanza matayarisho ya kujenga

    kituo cha kupokelea vifaranga

    vya samaki, kaa na majongoo ya

    baharini katika maeneo ya

    Chokocho – Pemba

    Asilimia ya matayarisho

    ya ujenzi iliyofikiwa

    100 20 20 Michoro ya kituo hicho imeanza

    kutayarishwa na Wakala wa Majenzi wa

    Serikali. Itakapokamilika, Wakala hao

    watatafuta Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi

    huo

    Kuzalisha vifaranga vya samaki,

    kaa na majongoo bahari

    Idadi ya vifaranga vya

    kaa vilivyozalishwa

    2,000,000 2,000,000 100 Vifaranga hivyo vinatarajiwa kusambazwa

    kwenye mashamba ya mfano

    Idadi ya vifaranga vya

    majongoo bahari

    vilivyozalishwa

    240,000 240,000 100

    Idadi ya vifaranga vya

    majongoo bahari

    9,000 9,000 100 Vifaranga hivyo vimesambazwa katika

    mashamba ya mfano ya Uzi na Bumbwini

  • 37

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    vilivyosambazwa

    Kuanzisha mashamba ya mfano

    Unguja na Pemba

    Idadi ya mashamba ya

    mfano yaliyoanzishwa

    2 2 100 Mashamba yameanzishwa maeneo ya Uzi

    na Bumbwini

    Kuvijengea uwezo vikundi vya

    wafugaji wa mazao ya baharini

    kwa kuwapatia mafunzo juu ya

    mbinu bora za ufugaji wa mazao

    ya baharini

    Idadi ya vikundi vya

    wafugaji wa mazao ya

    baharini vilivyojengewa

    uwezo

    158 158 100 Unguja vikundi 72 na Pemba vikundi 86

    vii. Mradi wa Usimamizi wa Shughuli za Uvuvi wa Kanda ya Kusini Mashariki mwa Bahari ya Hindi (SWIOFISH)

    Mradi una lengo la kuimarisha ushirikiano wa Kikanda – nchi za ukanda wa Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi, kuimarisha

    usimamizi wa uvuvi maalum uliopewa kipaumbele utakaopelekea kuongezeka kwa kipato kwa jamii inayojishughulisha na uvuvi.

    Kwa mwaka 2018/19, mradi ulipangiwa TZS 2.2 bilioni ambazo TZS 50 milioni kutoka Serikalini na TZS 2.2 bilioni kutoka kwa

    Washirika wa Maendeleo (Benki ya Dunia) na kupanga kutekeleza shughuli zifuatazo: Kuandaa vikao vya Kamati Tendaji na Kamati

    Kiongozi; Kuimarisha Sera na Kanuni za taasisi husika; Kuimarisha tafiti na kujua wingi wa samaki na changamoto zilizopo;

    Kuimarisha mpango wa taarifa za uvuvi kwa mahitaji ya kikanda; Kuimarisha mpango mkuu wa uendeshaji; Kutekeleza programu ya

    kujenga uwezo kwa taasisi husika; Utekelezaji wa mikakati ya kutoa uelewa kwa wadau; Kuwezesha kongamano na NGO's za

    biashara; Kuweka mikakati ya uwekaji wa miundombinu; na Kufanya matumizi mbali mbali ya uendeshaji na ufuatiliaji wa kazi za

    mradi. Hadi kufikia Juni 2019, mradi uliingiziwa TZS 4.2 bilioni (asilimia 195) na kutekeleza yafuatayo:

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    Kufanya doria shirikishi katika

    maeneo ya hifadhi za bahari

    Idadi ya doria shirikishi

    zilizofanyika

    174 174 100 Doria zimebaini kuwa wavuvi 3,839

    hawakuwa na leseni na kulazimika kukata

    leseni.

    Kutoa mafunzo wa upandaji

    mwani katika kina kirefu cha maji

    Idadi ya vijiji

    vilivyopatiwa mafunzo

    48 48 100 Vijiji kutoka Unguja ni 15 na Pemba 33

    Kuimarisha tafiti na kujua wingi

    wa samaki na changamoto

    zilizopo

    Idadi ya tafiti

    zilizofanyika

    4 0 0 Maandiko ya tafiti za jodari 2, uvuvi wa

    miambani moja na hadudi rejea za

    utayarishaji wa andiko la uvuvi wa samaki

  • 38

    Shughuli Iliyopangwa Kiashiria Shabaha Utekelezaji

    Halisi

    Asilimia ya

    Utekelezaji

    Maelezo

    jamii ya dagaa na pweza yamekamilika

    viii. Mradi wa Kudhibiti Sumu Kuvu Inayotokana na Ulaji wa Mahindi na Njugu

    Mradi una lengo la kupunguza athari zitokanazo na sumu kuvu kwenye mahindi na njugu, kuongeza taaluma na kuimarisha

    miundombinu na teknolojia kabla na baada ya mavuno. Kwa mwaka 2018/19, mradi huu ulipangiwa TZS 1.9 bilioni kutoka kwa

    Washirika wa Maendeleo (Benki ya Maendeleo ya Afrika) na kupanga kutekeleza shughuli zifuatazo: Ujenzi wa ghala la kuhifadhia

    chakula Cheju na Ole-Dodeani; Kusaidia upatikanaji wa vifaa vya maabara kwa taasisi ya ZBS na taasisi ya kilimo Kizimbani;

    Kushajihisha jamii juu ya kudhibiti na kujilinda na athari za sumu kuvu; na Kutoa mafunzo kwa wazalishaji, wafanyabiashara na

    waingizaji wa bidhaa za mahindi na njugu. Hadi kufikia Juni 2019, mradi haujaingiziwa fedha hivyo hakuna utekelezaji uliofanyika.

    ix. Mradi wa Uhifadhi wa Misitu kwa Faida za Kiuchumi

    Mradi una lengo la kupunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa, kuimarisha maeneo ya misitu ya hifadhi na

    kupunguza wimbi lisilo endelevu la bidhaa zitokanazo na misitu. Kwa mwaka 2018/19, mradi ulipangiwa TZS 223 milioni kutoka

    kwa Washirika wa Maendeleo (UNDP) na kupanga kutekeleza shughuli zifuatazo: Kuunda kamati zinazoshughulikia uhifadhi wa

    misitu; Kuandaa mikakati mipya ya kukabiliana na usafirishaji haramu wa misitu; Kufanya mapitio ya sera zinazosimamia maliasili na

    misitu; Kufanya mapitio ya bodi ya uhifadhi ya taifa ya misitu; Kulinda, kuhifadhi na kupanda miti maeneo yaliyoharibiwa;

    Kupambana na uvunaji haramu wa paa nunga. Hadi kufikia Juni 2019, mradi uliingiziwa TZS 223 (asilimia 100) fedha ambazo

    amelipwa Mkandarasi kwa ajili ya kutayarisho andiko la mradi. Andiko hilo limekamilika na limewasilishwa Shirika la Umoja wa

    Mataifa la Maendeleo kwa hatua zinazofuata.

    x. Mradi wa Kilimo cha Kushajihisha Ukulima wa Mboga Mboga na Matunda

    Mradi una lengo la kusaidia mnyororo wa thamani wa mazao mbali mbali ikiwemo mboga mboga, matunda na mazao ya biashara.

    Kwa mwaka 2018/19, mradi ulipangiwa TZS 1.8 bil