tra saccos limited ya chama .pdfiii) kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya chama. 10...
TRANSCRIPT
CHAMA CHA AKIBA NA MIKOPO
CHA
MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA
TRA SACCOS LIMITED
MASHARTI YA CHAMA
(BY-LAWS)
(Marekebisho ya Mwaka 2012)
S. L. P 63225
DAR-ES-SALAA
I
YALIYOMO Tafsiri ya Maneno ……………………………….. i Sehemu ya Kwanza 1.0 Jina la Chama na utambulisho wake ……… 1 Sehemu ya Pili 2.0 Madhumuni ya Chama ……………………… 2 Sehemu ya Tatu Uanachama 2.0 Kutakua na aina zifuatazo za Uanachama .. 4 3.1 Sifa za Mwanachama ……………………….. 4 3.2 Utaratibu wa Kujiunga ………………………. 5 3.3 Haki na Wajibu wa Mwanachama …………. 6 3.3.1 Haki za Mwanachama ………………….. 6 3.3.2 Wajibu wa Mwanachama ………………. 7 3.4 Kukoma Uanachama ……………………….. 8 3.5 Kusimamishwa/Kufukuzwa Uanachama …. 9 Sehemu ya Nne Kazi za Chama ………………………………….. 11 Sehemu ya Tano Uongozi na Usimamizi wa Chama 5.1 Mkutano Mkuu wa Wanachama ………….. 12 5.2 Bodi ya Chama …………………………….. 12 5.3 Mwenyekiti wa Chama …………………….. 15 5.4 Meneja/Katibu ………………………………. 16 5.5 Kamati ya Usimamizi ………………………. 18 5.6 Uchaguzi wa Bodi na Kamati ya Usimamizi 18 5.7 Sifa za Mgombea …………………………… 19 5.8 Utaratibu wa kuwapata wagombea ……….. 20
II
5.9 Muda wa Uongozi ………………………….. 21 5.10 Kuacha Uongozi ……………………….. 22 Sehemu ya Sita Mikutano ya Chama 6.1 Mkutano Mkuu wa Mwaka ………………… 24 6.2 Mkutano wa Kawaida ……………………… 25 6.3 Mkutano Maalumu …………………………. 26 6.4 Taarifa ya Mikutano ……………………….. 27 6.5 Mahudhurio …………………………………. 27 6.6 Mkutano wa Tawi …………………………… 28 6.7 Dondoo za Mkutano Mkuu ………………… 29 Sehemu ya Saba Mali na Fedha za Chama 7.1 Mali za Chama …………………………….. 30 7.2 Umiliki ………………………………………. 30 7.3 Fedha ………………………………………. 30 7.4 Utunzaji wa fedha …………………………. 31 Sehemu ya Nane Mwongozo wa Mkopo 8.1 Mahitaji ya jumla …………………………… 32 8.2 Mikopo isiyolipika na ifutwayo ……………. 32 8.3 Taarifa ya mikopo …………………………. 33 Sehemu ya Tisa Mgao wa Ziada 9.1 Matengo ……………………………………. 35 Sehemu ya Kumi Kufutwa kwa Chama 10.1 Utaratibu wa kukifuta Chama …………… 36
III
TAFSIRI YA MANENO
Tafsiri ifuatayo ya maana na maneno itatumika katika
Masharti haya na kwa kutilia maanani tafsiri ya maneno
kama yalivyoelekezwa kwenye Sheria ya Vyama vya
Ushirika ya mwaka 2003, isipokuwa pale
itakavyosemwa vinginevyo;
“Bodi” inamaanisha Wajumbe saba waliochaguliwa na
Mkutano Mkuu kusimamia uendeshaji wa shughuli za
kila siku za Chama.
“Chama” inamaanisha Chama cha Akiba na Mikopo
cha Mamlaka ya Mapato Tanzania.
“Daftari la Wanachama” inamaanisha orodha ya
Wanachama kama inavyotolewa kutoka kwenye mfumo
wa Komputa.
“Gawio” inamaanisha kiwango kinacholipwa kwa
Wanachama kwa kuwekeza pindi faida inapopatikana.
“Fedha” inamaanisha Shilingi za Kitanzania.
“Fungamano” inamaanisha hitaji ambalo Wanachama
wote wanataka/wanahitaji.
“Mkutano Mkuu” inamaanisha Mkutano wa
Wanachama wa Chama cha Akiba na Mikopo cha
Mamlaka ya Mapato Tanzania kama ilivyoainishwa
kwenye Sheria ya Ushirika Namba 20 ya mwaka 2003
na Kanuni zake za mwaka 2004.
IV
“Mwanachama” inamaanisha mtu yeyote
atakayekubaliwa na bodi, pamoja na Wanachama wa
Chama cha Akiba na Mikopo cha Mamlaka ya Mapato
Tanzania kuwa Mwanachama na ambaye atakuwa
ametii Katiba na Masharti ya Chama.
“Ruzuku” inamaanisha fedha/mali inayotolewa na
wadau mbalimbali ndani na nje ya Nchi.
“Sheria” inamaanisha sheria ya Vyama vya Ushirika
ya mwaka 2003 (namba 20).
“Tawi” inamaanisha mikoa yote ya Tanzania kama
itambulikavyo na Mamlaka ya Mapato.
“Tozo” inamaanisha malipo yatolewayo na
Mwanachama kama adhabu kwa kutorejesha au
kuchelewesha mkopo.
“Wafanyakazi” inamaanisha watu walioajiriwa na Bodi,
wanaofanya kazi katika Chama cha Akiba na Mikopo
cha Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa niaba ya bodi.
1
SEHEMU YA KWANZA
1.0 Jina la Chama na utambulisho wake
a) Jina la Chama “TRA SAVINGS AND
CREDIT COOPERATIVE SOCIETY
LIMITED”.
b) Anuani ya chama
S.L.P 63225, Dar-es-Salaam, Simu namba
+255 2864556 0712–494312/ 0752– 494312/
0684 - 557070
c) Tarehe ya kuandikishwa : 19.07.2006
d) Nambari ya Kuandikishwa: DSR 894.
e) Idadi ya Wanachama waliodhamini 9.
f) Eneo la shughuli za Chama litakuwa:
Tanzania.
g) Makao makuu ya Chama yatakuwa: Ghorofa
ya Tano, Jengo la Mariam, Mtaa wa
Shaurimoyo, Ilala.
h) Fungamanisho:MFANYAKAZI MWAJIRIWA/
MSTAAFU/ALIYEACHA KAZI KATIKA
MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA.
i) Kifupi cha jina itakuwa ni TRA SACCOS
LIMITED.
2
SEHEMU YA PILI
2.0 Madhumuni ya Chama.
Madhumuni ya Chama yatakuwa ni kuinua, kustawisha
na kuboresha hali ya Wanachama wake katika kukidhi
mahitaji mbalimbali ya Kiuchumi na Kijamii kwa kufuata
taratibu za Kidemokrasia, Misingi, Sheria za Vyama vya
Ushirika na Kanuni zake na Masharti ya Chama pamoja
na;
a) Kupokea Hisa, Akiba na Amana kutoka kwa
Wanachama.
b) Kushawishi Wanachama kuweka Akiba na
kununua Hisa kwa kuweka riba juu ya Akiba.
c) Kutoa bidhaa mbalimbali za fedha (financial
products) kwa Wanachama ili waweze kushiriki
zaidi kuimarisha mitaji ya Chama na mitaji yao
binafsi na kuleta mvuto kwa wasio Wanachama
kujiunga na Chama.
d) Kutoa Elimu inayolenga kushawishi na kujenga
tabia ya kuweka Akiba na Amana kwa
Wanachama wake na kuepuka matumizi ya
fedha yasiyo ya lazima miongoni mwa
Wanachama.
e) Kujenga tabia ya kujitegemea kwa Wanachama
wake.
3
f) Kujenga tabia ya uaminifu kati ya Wanachama
wake.
g) Kusaidia maendeleo ya jamii.
h) Kushawishi Watu na Vikundi mbalimbali kujiunga
na Chama.
4
SEHEMU YA TATU
UANACHAMA
3.0 Kutakuwa na aina zifuatazo za Uanachama
a) Wanachama wote waliojiandikisha wakati wa
kuomba kuandikishwa kwa Chama katika daftari
la Chama (Waanzilishi).
b) Wanachama wapya, waliojiunga baada ya
kutimiza masharti ya Chama ambao ni waajiriwa
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
c) Mwanachama ambaye ameamua kuendeleza
Uanachama katika Chama baada ya kustaafu,
kuacha au kuachishwa kazi katika Mamlaka ya
Mapato Tanzania na kuendelea kutoa michango
yake ya kila mwezi.
d) Vikundi vilivyomo ndani ya Mamlaka ya Mapato
Tanzania ambavyo vimesajiliwa kisheria.
3.1 Sifa za Mwanachama.
a) Awe ametimiza umri wa miaka 18.
b) Awe na akili timamu.
c) Awe wa kuaminika na kufahamika na
wanachama wenzake.
d) Awe Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania
5
aliyeajiriwa/aliyestaafu/aliyeacha/kuachishwa
kazi.
e) Awe tayari kushiriki kikamilifu katika shughuli
zote za Chama.
f) Asiwe na shughuli binafsi zinazofanana na
shughuli za Chama.
g) Awe amelipa kiingilio na kununua kima cha chini
cha Hisa.
h) Awe tayari kufuata sheria ya Vyama vya Ushirika
Na. 20 ya Mwaka 2003 na Marekebisho yake
pamoja na Kanuni za Ushirika za Mwaka 2004
na Masharti ya Chama.
3.2 Utaratibu wa Kujiunga
a) Mwombaji atatakiwa ajaze Fomu ya maombi ya
Uanachama inayopatikana ofisini na kutuima
kwa Mwenyekiti.
b) Mwombaji atakubaliwa kuwa Mwanachama
baada ya kupitishwa na wingi wa kura za
Wajumbe wa Bodi waliohudhuria Kikao, lakini
hatakuwa Mwanachama hadi atakapolipa ada ya
kiingilio na kununua kiwango cha chini cha Hisa
kilichokubaliwa na Wanachama.
c) Mwanachama akishathibitishwa na Mkutano
Mkuu jina lake litaorodheshwa kwenye daftari la
Uanachama.
6
3.3 Haki na Wajibu wa Mwanachama
3.3.1 Haki za Mwanachama
a) Kupiga na kupigiwa kura kuwa Kiongozi.
b) Kuhudhuria Mikutano ya Chama.
c) Kusikilizwa na kutoa maoni.
d) Kuomba kuitisha Mkutano Mkuu kwa mujibu wa
Masharti ya Chama na Sheria ya Ushirika Na. 20
ya Mwaka 2003 pamoja na Kanuni zake za
Mwaka 2004.
e) Kushiriki katika shughuli zote za Chama.
f) Kuweka na kutoa Amana, Akiba na Hisa zake
kwa kufuata kanuni za Chama.
g) Kupatiwa Mikopo kwa ajili ya kuongeza tija na
maendeleo ya kijamii.
h) Kuwa Mdhamini wa Mkopo wa Mwanachama
mwingine.
i) Kusoma taarifa za Mikutano ya Chama, Mizania,
Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, katika
ofisi ya Chama katika nyakati za saa za kazi.
j) Kujitoa Uanachama.
k) Kukata rufaa.
7
l) Kumiliki kiasi chochote cha Hisa, ilimradi tu
hataruhusiwa kumiliki zaidi ya asimilia 20 ya
Hisa zote za Chama.
m) Kupatiwa Cheti cha Hisa mara baada ya
kununua Hisa zinazokubalika na Chama.
n) Kuchagua Mrithi.
3.3.2 Wajibu wa Mwanachama
a) Kutii Sheria za Chama, Kanuni na Miongozo
yake kama ilivyokubaliwa na Wanachama wote.
b) Kulipa ada ya kiingilio, kununua Hisa na kulipa
ada zozote zitakazokuwa zimeamuliwa na
Wanachama kwenye Mkutano Mkuu.
c) Kushiriki katika shughuli za kiuchumi za Chama
kama zilivyoainishwa kwenye Sera za Chama.
d) Kuhudhuria Mikutano ya Chama.
e) Kuchagua Viongozi wa Chama.
f) Kutii maamuzi ya Mkutano Mkuu.
g) Kulinda na kutunza Mali za Chama.
h) Kudhamini Chama pale inapohitajika.
i) Kubeba dhamana ikiwa janga lolote litatokea.
Dhamana hiyo kikomo chake ni kiasi cha Hisa
alizonazo kwenye Chama.
8
j) Kuchagua Warithi wao.
k) Kulipa madeni aliyonayo ndani ya Chama kwa
wakati uliopangwa.
l) Kulipa mkopo alioudhamini endapo mkopaji
atashindwa kulipa mkopo wake bila sababu za
msingi.
m) Kuwa na angalau kiwango cha chini cha Hisa
kwa mujibu wa Masharti ya Chama.
n) Kuweka Akiba mara kwa mara.
o) Kutoa taarifa kwenye Uongozi wa Chama iwapo
Mtumishi au Kiongozi anatoa huduma kwa
upendeleo, au anatoa au kupokea rushwa.
3.4 Kukoma Uanachama
Mwanachama atakoma Uanachama kutokana na
miongoni mwa sababu zifuatazo;
a) Kifo.
b) Akiwa na Ugonjwa wa Akili uliothibitika.
c) Akipatikana na hatia ya jinai ambayo
itasababisha afungwe jela.
d) Kutohudhuria Mikutano ya Chama mara tatu
mfululizo bila sababu za msingi.
9
e) Kufukuzwa Uanachama na theluthi mbili (2/3) ya
Wanachama waliohudhuria katika Mkutano
Mkuu wa Chama baada ya kupewa nafasi ya
kujitetea.
f) Kujiuzulu kwa Hiari yake.
g) Kwa sababu zozote zilizomo kwenye Kanuni za
Ushirika za Mwaka 2004 kifungu cha 25.
3.5 Kusimamishwa/Kufukuzwa Uanachama
a) Kwa mujibu wa Masharti ya Chama, Bodi ya
Chama itawasilisha kwenye Mkutano Mkuu
majina ya Wanachama ambao kwa nyakati
tofauti wataonekana kutenda makosa ambayo
yanaenda kinyume na Kanuni na Taratibu za
Chama kama ifuatavyo;
i) Kutoheshimu na kutotekeleza maamuzi
ya Mikutano Mikuu na vikao vya Bodi ya
Chama.
ii) Kutolipa Hisa na ada mbalimbali za
Chama baada ya kupewa muda
uliokubaliwa na Mkutano.
iii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na
kutozingatia maadili ya Chama.
10
iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za
Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,
Kanuni na Sera za Chama.
v) Kubainika kutoa au kupokea rushwa
katika utekelezaji wa shughuli za Chama.
vi) Wizi.
vii) Sababu zozote zilizomo katika kifungu
cha 26 cha Kanuni za Ushirika za Mwaka
2004.
b) Kusimamishwa au kufukuzwa kwa Mwanachama
kutafanywa na Mkutano Mkuu ambapo
Wanachama waliohudhuria wasiopungua theluthi
mbili (2/3) watatoa uamuzi huo baada ya
mhusika kutoa utetezi wake.
Mwanachama aliyejiuzulu au kufukuzwa
Uanachama anaweza kujiunga tena kwa kuomba
upya na taratibu za kujiunga na Chama
zitazingatiwa.
11
SEHEMU YA NNE
KAZI ZA CHAMA
4.1. Kuandikisha Wanachama.
4.1.1. Kuandaa taarifa zifuatazo na kuzituma kwa
Mkaguzi wa nje ndani ya miezi mitatu (3) baada
ya kufunga mwaka wa fedha kwa mujibu wa
Sheria na Kanuni za Ushirika;
a) Hesabu zinazoonyesha mapato na matumizi.
b) Hesabu za mtiririko wa fedha.
c) Urari wa Chama.
4.2. Kuweka wazi taarifa za Hesabu za Chama kila
mwaka kwa Mwanachama yeyote atakayekuwa
anahitaji kupata taarifa juu ya utendaji wa Chama
katika muda wa saa za kazi.
12
SEHEMU YA TANO
UONGOZI NA USIMAMIZI WA CHAMA
5.1 Mkutano Mkuu wa Wanachama
Kutakuwa na Mkutano Mkuu wa Wanachama wote
ambao ndicho chombo cha juu cha maamuzi juu ya
utendaji wa shughuli za Chama. Kwa mujibu wa
Sheria ya Ushirika ya Mwaka 2003 na Kanuni zake
za Mwaka 2004, Mkutano Mkuu utachagua Bodi ya
Chama yenye Wajumbe wasiopungua watano na
wasiozidi tisa ili kuendesha na kusimamia shughuli
za kila siku za Chama.
5.2 Bodi ya Chama
Kutakuwa na Bodi yenye wajumbe saba (7). Bodi
itachagua Wajumbe watatu miongoni mwao kuwa
Wajumbe wa Kamati ya Mikopo.
Kazi za Bodi:
a) Kusimamia shughuli za Chama kidemokrasia
kwa kutilia maanani mipango na njia za
kushirikiana baina ya Wanachama.
b) Kufanikisha mahitaji ya kiuchumi na kijamii
ya Wanachama.
c) Kutoa elimu ya Ushirika kwa Wanachama.
13
d) Kuandaa miongozo sahihi ya fedha za
Chama zitakazosaidia kuwepo na taarifa
sahihi za mahesabu ya Chama.
e) Kuandaa Sera muhimu za Chama, kama vile
Sera ya Mikopo na kuwasilisha kwenye
Mkutano Mkuu kwa ajili ya kuidhinishwa.
f) Kuhakikisha hesabu za Chama zinaandaliwa
na kupitiwa na Mkaguzi wa Nje kwa mujibu
wa Sheria ya Ushirika, Kanuni za Ushirika na
Masharti ya Chama.
g) Kuwasilisha kwenye Mkutano Mkuu wa
Chama hesabu zilizokaguliwa na Mkaguzi
wa Nje.
h) Kuandaa makisio ya mapato na matumizi ya
Chama kwa mwaka unaofuata na
kuwasilisha kwenye Mkutano Mkuu kwa ajili
ya kuidhinishwa.
i) Kuwezesha ukaguzi wa vitabu kwa wakaguzi
wa ndani na nje kama walivyoidhinishwa na
Mkutano Mkuu na kwa mujibu wa Sheria ya
Ushirika.
j) Kuhakikisha mikopo inaainisha dhumuni la
mkopo husika.
14
k) Kuhakikisha Sera za Chama na Mikataba
inatolewa kwa kuzingatia shughuli za
Chama.
l) Kuandaa mikataba na miongozo ya kazi na
masuala yahusuyo Wafanyakazi.
m) Kuajiri Meneja/Katibu na Wafanyakazi
wengine wa Chama kwa mikataba endelevu
ya kila baada ya miaka mitatu.
n) Kumsimamisha Mjumbe yeyote wa Bodi
asiyetii matakwa ya Sheria na Masharti
akisubiri maamuzi ya Mkutano Mkuu.
o) Kuhakikisha ufunguzi na kuendesha akaunti
ya Chama.
p) Kutunza kitabu cha Rejista ya Wanachama.
q) Kutunza kitabu cha Rejista ya mahudhurio ya
Wajumbe wa Bodi
r) Kutunza dondoo za Mikutano ya Chama.
s) Kuandaa mipango endelevu ya Chama,
mpango wa biashara na kuhakikisha
utekelezaji wake kwa kipindi husika.
t) Kuandaa miongozo ya uongozi wa ndani ya
Chama na namna ya kutoa ripoti.
15
u) Kuhakikisha ina uwezo wa kujua kazi za kila
siku za Meneja/Katibu na Wafanyakazi pia
kusimamia akaunti ya chama.
v) Kusaini cheki za Chama.
5.3 Mwenyekiti wa Chama
Mwenyekiti wa Chama atakuwa na majukumu
yafuatayo:
a) Kuwa msemaji Mkuu wa Chama.
b) Kuongoza Mikutano Mikuu ya Chama
(isipokuwa Mkutano Mkuu Maalum
ulioitishwa na Mrajisi na Kamati ya
Usimamizi).
c) Kuongoza vikao vya Bodi.
d) Kuweka sahihi pamoja na Katibu kwenye
Mikataba kwa niaba ya Chama kwa
kuzingatia matakwa ya Sheria na Kanuni za
Vyama vya Ushirika.
e) Kuwakilisha Chama katika Taasisi/Asasi
mbalimbali ndani na nje ya Nchi.
16
5.4 Meneja/Katibu
Kutakuwepo Meneja ambaye ataajiriwa na Bodi na
atakuwa na kazi zifuatazo:
a) Kusaidia Majukumu ya Mwenyekiti.
b) Kusimamia kazi za kila siku za Chama
zinazofanywa na Wafanyakazi wengine.
c) Kuandaa malipo ya Mishahara ya
Wafanyakazi na kuwasilisha kwa Bodi kwa
ajili ya kuidhinishwa.
d) Kutoa taarifa za utendaji wa shughuli za
Chama kwa Bodi.
e) Kuandaa au kuhakikisha inaandaliwa taarifa
ya maendeleo ya Chama, hesabu za Chama
za kila mwezi na taarifa nyinginezo muhimu
ambazo zitasaidia Bodi kulinganisha makisio
ya mwaka na matumizi yaliyotumika na pia
kutoa maamuzi sahihi.
f) Kuandaa Hesabu za chama za mwisho wa
mwaka na kuziwakilisha kwa Bodi pamoja na
kwa Mkaguzi wa Nje.
g) Kuhakikisha vitabu vinaandikwa kwa usahihi
na kuhakikisha mali za kudumu zinarekodiwa
kwenye vitabu husika.
17
h) Kuhusika na upokeaji wa Hisa kwa
Wanachama na kutoa Cheti cha Umiliki
i) Kutunza vizuri mali za Chama.
j) Kuwa Katibu wa Mikutano yote ya Chama.
k) Kutunza kitabu cha majina ya Wanachama
na taarifa zao muhimu.
l) Kusaini nyaraka na mikataba ya Chama kwa
niaba ya Chama.
m) Kuandaa mpango mkakati wa Chama na
kuwasilisha kwa Bodi ya Chama kwa ajili ya
kuidhinishwa.
n) Kusimamia utekelezaji wa mpango mkakati
ulioidhinishwa na Mkutano Mkuu.
o) Kutoa mapendekezo ya marekebisho ya
Masharti na Sera za Chama.
p) Kutunza taarifa za Wanachama na
Wafanyakazi wa Chama.
q) Kufanya kazi nyingine zozote kama itakavyo
amuliwa na Bodi.
18
5.5 Kamati ya Usimamizi
Kutakuwa na Kamati ya Usimamizi yenye wajumbe
watatu (3) ambao hawatokani na Wajumbe wa Bodi
ya Chama.
Kazi za Kamati ya Usimamizi:
a) Kuhakikiksha kwamba, Bodi, Kamati na
Wafanyakazi wa Chama wanafuata Sheria,
Masharti na Sera za Chama.
b) Kuhakikisha hesabu za Chama na vitabu
vingine vya Chama ikihusisha vitabu vya
Wanachama na Daftari la Wanachama
vinatunzwa vizuri.
c) Kupokea na kupitia taarifa za Mkaguzi wa
Ndani.
d) Kutoa ushauri kwa Bodi na Wafanyakazi wa
Chama, juu ya utekelezaji bora wa shughuli
za Chama na kutoa taarifa kwenye Mkutano
Mkuu wa Chama.
5.6 Uchaguzi wa Bodi na Kamati ya Usimamizi
a) Uchaguzi wa Bodi utafanyika kwa mujibu wa
kifungu cha 63 (1-6) cha Sheria ya Vyama
vya Ushirika Na.20 ya mwaka 2003 na
19
Kanuni za Vyama vya Ushirika za Mwaka
2004 kifungu cha 78.
b) Kila Mwanachama kwenye Mkutano Mkuu
atakuwa na haki ya kupiga kura moja kwa
kila nafasi ya uongozi.
5.7 Sifa za Mgombea
Mwanachama anayetaka kugombea uongozi katika
Chama itabidi azingatie maadili ya Uongozi kwa mujibu
wa kifungu Na.125 cha Sheria ya Vyama vya Ushirika
Na.20 ya Mwaka 2003.
Sifa za kugombea:
a) Awe na upeo na elimu ya kutosha kuweza
kuongoza Chama kulingana na mabadiliko ya
hali ya uchumi wa nchi.
b) Awe ni mfuatiliaji wa shughuli za Chama kwa
kutekeleza wajibu wake katika Chama na kwa
kuzingatia Sheria ya Vyama vya Ushirika,
Kanuni na Masharti ya Chama.
c) Awe ni mtu mwenye ari ya kutoa mchango wake
wenye nia ya kuendeleza Chama endapo
atachaguliwa kuwa Kiongozi.
d) Awe na ufahamu wa shughuli za Ushirika.
20
e) Awe mwaminifu na si mpenda kupokea wala
kutoa rushwa.
f) Awe ni mtu ambaye hajawahi kuenguliwa katika
uongozi katika Chama chochote cha Ushirika
kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.
g) Awe Mwanachama hai kwa kulipa kiingilio na
Hisa zote zinazotakiwa kwa mujibu wa Masharti
ya Chama.
h) Awe anashiriki kikamilifu katika shughuli za
Chama.
i) Awe ni Mwanachama katika kipindi
kisichopungua mwaka mmoja.
5.8 Utaratibu wa kuwapata Wagombea wa Uongozi
wa Chama
Itakapofika wakati wa uchaguzi Mrajis (Registrar) wa
Vyama vya Ushirika nchini atateua Afisa wa uchaguzi
kusimamia uchaguzi wa viongozi wa Chama kulingana
na maadili ya uongozi kwa mujibu wa kifungu Na.125
cha Sheria ya Vyama vya Ushirika Na.20 ya mwaka
2003.
21
Mwenyekiti wa Chama atatoa tangazo la kufanyika
uchaguzi ambalo litabandikwa katika mbao za
matangazo zilizopo kwenye ofisi za Chama na katika
Matawi yote ya Chama. Tangazo hilo litaeleza tarehe ya
uchaguzi, nafasi zinazogombewa, sifa za Wagombea
katika kila nafasi, tarehe ya kuchukua na kurudisha
fomu za maombi na mahali pa kurudisha fomu hizo
baada ya kujazwa.
5.9 Muda wa Uongozi
a) Muda wa Uongozi utakuwa ni miaka tisa (9)
tu.
b) Kama kutatokea nafasi wazi ya uongozi
kabla ya kumalizika muda huo wa miaka tisa
(9) Bodi itateua Mwanachama mwenye sifa
kujaza nafasi hiyo hadi Mkutano Mkuu
utakapothibitisha uteuzi huo kuwa
madarakani katika kipindi kitakachokuwa
kimebakia.
c) Kila baada ya miaka mitatu theluthi moja
(1/3) ya wajumbe wa Bodi itapigiwa kura ya
kuondoka madarakani, mwaka wa sita nusu
(1/2) ya wajumbe ambao walibaki itapigiwa
22
kura ya kuondoka madarakani. Wajumbe
walioondoka madarakani hawataruhusiwa
kugombea hadi miaka mitatu ipite. Katika
mwaka wa tisa nusu (1/2) itakayobakia
itapigiwa kura ya kuondoka madarakani na
hawataruhusiwa kugombea hadi miaka
mitatu kupita. Kuondoka kwa Wajumbe hao
kutaruhusu kufanyika uchaguzi wa kuziba
nafasi zao, hii ni kwa mujibu wa kifungu cha
63(1-6) cha Sheria Na.20 ya mwaka 2003.
5.10 Mjumbe wa Bodi na Kamati ya Usimamizi
ataacha kuwa Mjumbe wa Bodi/Kamati iwapo:
a) Litatokea tukio lolote lililo orodheshwa kwenye
vifungu 3.3 na 3.4 vya Masharti ya Chama.
b) Atafanya biashara inayofanywa na Chama.
c) Atafukuzwa na Mkutano Mkuu kwa vitendo vya
kwenda kinyume na maadili ya uongozi baada
ya kupewa nafasi ya kujitetea.
d) Atajiuzulu kwa hiari kwa kutoa taarifa ya siku
zisizopungua thelathini.
e) Atashindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo bila
ya sababu inayokubaliwa na Bodi.
23
f) Atastaafu baada ya muda wa Uongozi
kukamilika kwa mujibu wa Sheria.
24
SEHEMU YA SITA
MIKUTANO YA CHAMA
Kutakuwa na aina zifuatazo za Mikutano:
a) Mkutano Mkuu wa Mwaka.
b) Mkutano wa Kawaida.
c) Mkutano Maalum.
d) Mkutano wa Tawi.
6.1 Mkutano Mkuu wa Mwaka
a) Maamuzi ya Chama, yatakuwa yanaamuliwa
kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama.
Mkutano mkuu wa Mwaka wa Wanachama
utafanyika ndani ya siku thelathini (30) tangu
baada ya kupokea taarifa ya Ukaguzi wa Chama
toka kwa Mkaguzi wa nje lakini si zaidi ya siku
mia na themanini (180) baada ya mwaka wa
fedha kuisha, Mwanachama yeyote aliyetimiza
matakwa ya Masharti ya Chama na Katiba ya
Chama ana haki ya kuhudhuria.
b) Yatakayo zungumzwa kwenye Mkutano Mkuu ni
pamoja na:
i. Kupokea na kukubali taarifa ya Hesabu
za Chama, ripoti ya Viongozi na Kamati
ya Usimamizi na taarifa nyingine zozote
muhimu.
ii. Kuidhinisha gawio endapo kuna ziada.
25
iii. Kuidhinisha posho kwa Watendaji ambao
hawalipwi mshahara kwa Mujibu wa
Sheria.
iv. Kupokea na kuidhinisha makisio ya
Mapato na Matumizi ya Mwaka wa fedha
unaofuata.
v. Kupokea na kuidhinisha Mpango Mkakati
wa Chama na utekelezaji wake.
vi. Kuidhinisha shughuli zozote ambazo
Bodi ya Chama inadhani zinahitaji
maamuzi ya Wanachama wote.
6.2 Mkutano wa Kawaida
a) Chama kitakuwa na Mkutano wa Kawaida mara
moja kwa Mwaka, na itakuwa kati ya Mwezi
Septemba na Desemba.
b) Yatakayozungumzwa kwenye Mkutano wa
Kawaida ni pamoja na:
i. Kupendekeza Wajumbe wa Bodi kama
ambavyo Sheria na Kanuni za Vyama
vya Ushirika zinavyoelekeza na pia
kuchagua Kamati ya Usimamizi ya
Wajumbe 3 ambao sio Wajumbe wa
Bodi.
26
ii. Kurekebisha Katiba, Masharti na Sera
pale inapohitajika.
iii. Kuchagua, kufukuza au kumwondoa
Mjumbe yeyote wa Bodi.
iv. Kuidhinisha manunuzi au mauzo ya Mali
zinazohamishika na zisizohamishika za
Chama.
v. Kupitia na kukubali Mpango Mkakati wa
Chama.
vi. Kuidhinisha Mikataba na Makubaliano.
c) Bila kuangalia vipengele (a) na (b) hapo juu,
mambo yatakayozungumzwa kwenye Mkutano
wa Kawaida yanaweza kuzungumzwa kwenye
Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama kama
yalivyoelekezwa kifungu 6.1 (b).
6.3 Mkutano Maalumu
a) Mkutano Maalumu unaweza kufanyika pale
ambapo angalau moja ya tatu ya Wanachama
kwa maandishi wataomba kufanya Mkutano
Maalumu wa Chama na lazima watume nakala
kwa Mrajis wa Ushirika.
b) Mrajis au yoyote atakayechaguliwa na Mrajis
anaweza kuongoza Mkutano Maalumu wa
27
Wanachama, sehemu na muda ambao Mrajis
atapanga.
c) Mkutano Maalumu utakuwa na agenda maalum
moja.
6.4 Taarifa ya Mikutano
a) Taarifa ya Maandishi ya angalau siku ishirini na
moja (21) itatolewa kwa Mkutano Mkuu wa
Mwaka na Mkutano wa Kawaida na taarifa ya
siku saba (7) itatolewa kwa Mkutano Maalum wa
Chama kwa njia ya matangazo, barua au
vinginevyo.
b) Taarifa itaelezea madhumuni ya Mkutano na
agenda za Mkutano zitatumwa kwa kila
Mwanachama.
c) Kushindwa kupata taarifa kwa wakati muafaka
kwa Mwanachama haitakuwa kigezo cha yeye
kuharibu yatakayo zungumzwa kwenye
Mkutano.
6.5 Mahudhurio
a) Mahudhurio yanayohitajika kwa ajili ya Mikutano
ya Wanachama ni asilimia hamsini (50%) ya
Wanachama au Wanachama 50 wa Chama, kwa
idadi yeyote iliyondogo.
28
b) Kama mahudhurio hayatafikiwa Kwa Mikutano
ya Wanachama basi Mkutano huo utaahirishwa
kwa siku saba (7). Kama Mkutano utaahirishwa
na baada ya siku saba kama mahudhurio
hayatatimia basi Mkutano huo utafutwa.
c) Mkutano Maalumu unaoongozwa na Mrajis
utafanyika kwa idadi yoyote ya Wanachama
watakaohudhuria na maamuzi yatakayofikiwa
yatachukuliwa kuwa maamuzi ya Wanachama
wote.
d) Mwenyekiti wa Chama ataendesha Mikutano
yote ya Chama, iwapo Mwenyekiti hayupo,
Makamu wake ataendesha Mikutano na iwapo
wote hawapo kwa muda wa dakika 30,
Mwanachama yeyote katika waliohudhuria
atachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa muda na
ataongoza Mkutano huo.
6.6 Mkutano wa Tawi
6.6.1 Kutakuwa na Mikutano minne ya Tawi (Kila robo
mwaka) ambao utahudhuriwa na Wanachama wote wa
Tawi husika.
Mambo yafuatayo yatajadiliwa kwenye Mkutano wa
Tawi:
a) Kupokea na kupitia taarifa za Bodi ya Chama na
Maazimio ya Mkutano Mkuu kwa utekelezaji.
29
b) Kutoa maoni na kuwasilisha mapendekezo
mbalimbali yanayohusu shughuli za Chama
katika Tawi na kuyapeleka kwenye Bodi ya
Chama ili yajadiliwe kwenye Mikutano Mikuu ya
Chama.
c) Kuchagua Viongozi wa Tawi iwapo waliopo
muda wao umekwisha/wamehama na uchaguzi
huo utasimamiwa na Mwenyekiti wa Chama au
Mjumbe wa Bodi ya Chama.
d) Viongozi wa Tawi wataongoza kwa kipindi cha
miaka miwili.
6.6.2 Taarifa za Mikutano ya Tawi zitatolewa siku 14
kabla ya Mkutano.
6.7 Dondoo za Mkutano Mkuu
a) Mambo yote yatakayozungumzwa na kuamuliwa
kwenye Mkutano Mkuu yataandikwa na
kuhifadhiwa kwenye kitabu maalumu mara
baada ya kuidhinishwa kwenye Mkutano
unaofuata na Mwenyekiti pamoja na Katibu.
b) Nakala ya dondoo baada ya kuidhinishwa
zitatumwa kwa Mrajis.
30
SEHEMU YA SABA
MALI NA FEDHA ZA CHAMA
7.1 Mali za Chama
Mali za Chama zitahusisha mali zote
zinazohamishika na zisizohamishika za Chama
ambazo Chama itazinunua kila inapohitaji.
7.2 Umiliki
Mali za kudumu na nyinginezo za Chama
zitamilikiwa na Chama.
7.3 Fedha
Fedha za Chama zitahusisha:
a) Ada ya viingilio, na uuzwaji wa vitabu.
b) Uuzaji wa Hisa.
c) Akiba na Amana.
d) Ruzuku.
e) Tozo za adhabu.
f) Faida.
g) Bima ya mkopo.
h) Njia nyinginezo halali ambazo Bodi itaona
zinafaa.
31
7.4 Utunzaji wa fedha.
Fedha zote za Chama zitatunzwa katika Benki
itakayo amuliwa na Bodi ya Chama kwa niaba ya
Chama .
7.5 Mwaka wa fedha.
Mwaka wa fedha wa Chama utakuwa kuanzia
Januari 1 mpaka Disemba 31 kila mwaka.
7.6 Upokeaji wa fedha.
Karani/Mtunza Hazina wa Chama ndiye
atakayekuwa na mamlaka ya kupokea na kutoa
risiti za Chama kwa kusimamiwa na ofisa wa
fedha/Mhasibu na Meneja.
32
SEHEMU YA NANE
MWONGOZO WA MKOPO
8.1 Mahitaji ya Jumla ya Mwongozo wa Mkopo
Sera ya Mikopo inaainisha njia zote za namna ya
kutoa na urejeshwaji wa Mikopo, na yafuatayo
yatazingatiwa:
a) Hakuna Mwanachama atakayepatiwa mkopo
mpaka pale atakapokua amenunua Hisa
zinazohitajika na kwa msingi wa Masharti ya
Chama.
b) Hakuna Mkopo utakaotolewa zaidi ya mara
tatu ya AKIBA/AMANA za Mwanachama.
c) Ukomo wa juu wa kukopa kwa Mwanachama
na Chama, vitapangwa kwenye Mkutano
Mkuu wa Chama.
d) Faida na adhabu juu ya Mkopo itakuwa kama
ambavyo imeamuliwa na Mkutano Mkuu na
ambavyo sera ya Chama inaonyesha.
e) Muda wa juu wa kurejesha Mkopo
utaamuliwa na Mkutano Mkuu na ambavyo
Sera za Chama zinavyoonyesha.
8.2 Mikopo isiyolipika na ifutwayo.
a) Endapo mkopo au kiasi cha mkopo utakuwa
haujalipwa kwa siku zaidi ya tisini (90) kama
ambavyo ilikuwa imekubaliwa kwenye fomu
ya marejesho, Chama kitafuta mkopo kwa
Akiba na Amana za muhusika zilizowekwa
33
kama dhamana na itaendelea kukusanya
mali yoyote iliyowekwa kama dhamana.
b) Endapo kiasi chochote kitakuwa hakijalipwa
kwa zaidi ya mwaka mmoja, mkopo huo
utafutwa kwa kupunguza akaunti ya madeni
mabaya/hatari.
c) Malipo yeyote yatakayopatikana baada ya
mkopo kufutwa, yatapokelewa kama faida ya
ziada na itapelekwa kwenye tengo la lazima.
d) Chama kitatenga matengo ya mikopo
iliyocheleweshwa kama ifuatavyo:
i. Siku 0 – 30 mkopo uliocheleweshwa =
1% ya mkopo na ufuatiliaji wa hali ya juu.
ii. Siku 31 – 180 mkopo uliocheleweshwa =
30% ya kiasi cha mkopo unaodaiwa.
iii. Siku 181 – 365 mkopo uliocheleweshwa
= 50% ya kiasi cha mkopo unaodaiwa.
iv. Zaidi ya siku 365 = 100% ya mkopo
unaodaiwa.
Mkopo unaodaiwa kwenye tengo hili utapatikana
kwa kutoa kiasi chote cha mkopo unaodaiwa
kwa Akiba na Amana zilizowekwa na
Mwanachama kama dhamana ya mkopo huo.
34
8.3 Taarifa ya mikopo
Chama kitaandaa na kutoa taarifa za shughuli za
mikopo. Taarifa hiyo itahusisha pamoja na
mambo mengine:
a) Jina la Mwanachama.
b) Tarehe mkopo ulipochukuliwa.
c) Kiasi alichokopa na kiasi anachodaiwa.
d) Namna ya marejesho na riba juu yake.
e) Kiasi ambacho kinadaiwa/kilichopitisha muda
wa marejesho.
f) Majina ya Wadhamini na Dhamana
zilizowekwa.
Taarifa itakaguliwa na kusainiwa na
Katibu/Meneja na kuidhinishwa na Kamati ya
Mikopo.
35
SEHEMU YA TISA
MGAO WA ZIADA
9.1 Matengo
Ziada itakayopatikana mara baada ya Taarifa ya
fedha za Chama kupitiwa na Mkaguzi wa nje na
kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Chama, salio
la ziada litagawanywa kama ifuatavyo:
a) 20% ya ziada itapelekwa kwenye tengo la
lazima.
b) 15% ya ziada itapelekwa kwenye tengo la
madeni mabaya ilimradi tengo hilo lisizidi
asilimia 15% ya madeni yote za Chama.
c) 15% ya ziada itapelekwa kwenye tengo la
kukombolea Hisa ilimradi tengo hilo lisizidi
asilimia 15% ya Hisa zote za Chama.
d) 10% ya ziada itapelekwa kwenye tengo la
Elimu ya Ushirika na mafunzo mbalimbali.
e) Kiasi kinachobaki kitagawiwa kama ambavyo
Mkutano Mkuu utakavyoamua.
36
SEHEMU YA KUMI
KUFUTWA KWA CHAMA.
10.1 Utaratibu ufuatao utatumika kukifuta Chama:
a) Chama kinaweza kufutwa kwa maombi ya
zaidi ya robo tatu ya Wanachama kwenye
Mkutano Maalumu ulioitishwa kwa ajili ya
hitaji hilo na dondoo za Mkutano huo
zitatumwa kwa Mrajis na Wanachama.
b) Baada ya kukamilisha njia za kufuta
uandikishwaji wa Chama, Mrajis atatoa
taarifa ikiwataka wale wote wanaokidai
Chama watoe taarifa kwake au kwa Mfilisi wa
Chama ndani ya mwezi mmoja.
c) Mufilisi atachukua jukumu la kumiliki vitabu
vya Chama ili kuweza kukifuta Chama.
d) Mufilisi ataendelea kushughulikia kuwajua
wanaokidai na wanaodaiwa na Chama tangu
suala la kufuta uandikishwaji wa Chama
uanze na pia atahakikisha anafahamu kiasi
walichochangia Wanachama waliopo na
waliopita katika mtaji wa Chama.
e) Mufilisi atatoa taarifa kwa Mrajis kama
ambavyo Mrajis atataka ikionesha hatua
aliyofikia katika kukifuta Chama.
f) Kiasi chochote cha fedha kitakachopatikana
katika shughuli ya kukifuta Chama kitawekwa
Benki ambayo Mrajis ataamua.
g) Mufilisi baada ya kukusanya madeni ya
Chama na kutoa matumizi ya kukifuta
37
Chama na kujua kiasi walichochangia
Wanachama wa zamani na waliopo katika
mtaji wa Chama na mara baada ya kulipa
wanaokidai Chama, atakifuta Chama na
kuwakilisha taarifa kwa Mrajis.
h) Mrajis atapanga muda wa Mufilisi
kukamilisha kazi.