toleo la 20 january—march banana investments ltd · ckht huandaa mafunzo ya awali, “orientation...
TRANSCRIPT
HALIUZWI
Toleo la 20 January—March
TOLEO NAMBA 20 HALIUZWI JANUARY— MARCH
Banana Investments Ltd.
2 HALIUZWI
Toleo la 20 January—March
Hili ni toleo la kwanza kutoka baada ya wahariri
kupatiwa mafunzo ya uandishi wa makala kwa
hiyo litakua na mabadiliko kidogo ambayo
tumeyafanya baada ya kupata utaalam zaidi.
Pia tunapenda kuchukua nafasi hii kuwatangazia
wasomaji wa jarida hili ikiwa ni pamoja na wasam-
bazaji wa bidhaa za BIL, wateja pamoja na marafiki
wote kwamba tunapokea makala mbalimbali kutoka
sehemu zote kwa hiyo wote wanaoweza kuandika
watume kwenye email ifuatayo: ba-
[email protected] au [email protected]. Pia
wanaweza kutuma kwa kupitia magari wa wasam-
bazaji au S L P 10123 Arusha. Kila makala ita-
kayochapwa mwandishi atapewa motisha ya kiasi
kidogo cha fedha ili aweze kuandika makala nyingi
zaidi.
Wote mnakaribishwa.
RAHA: BONGE LA LADHA KWA
BEI NAFUU.
KAMATI YA WAHARIRI YALIYOMO
Augustine S. Minja - Mwenyekiti 0715 451004
Beatha Anthony - Katibu 0717 350971
Philbert A. Mhindi - Mjumbe 0713 139052
Gerald Lyimo - Mjumbe 0754 380105
1. WAHARIRI WAPATA MAFUNZO YA UANDISHI WA HABARI ...2
2. PROMOTION YA TAJIRIKA NA RAHA YAFIKIA TAMATI……...3
3. MABORESHO KATIKA HUDUMA YA WATEJA…………….……3
4. MTANDAO WA USAMBAZAJI WA RAHA NCHINI TANZANIA..4
5. KIJUE CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA……………….…5
6. BANANA FOUNDATION WADHAMINI MAFUNZO YA VION-
GOZI WA SACCOS………………………………………….……….5
7. Y’S MEN TANZANIA WAFANIKISHA VUKA BODA BASH…....6
8. AJIRA MPYA, NGUVU MPYA KAMPUNI YA BANANA……......7
9. MATUKIO YA KUGAWA ZAWADI ZA TAJIRIKA NA RAHA…..8
WAHARIRI WA MBIU YA BANANA WAFANYIWA MAFUNZO
YA UBORESHAJI WA UASHISHI WA MAKALA
Baadhi ya washiriki wa Semina wakiwa ukumbini tayari kwa
kuanza masomo.
Mnano tarehe 12/10/2010 kampuni iliandaa semmina ya siku
moja kwa ajili ya kuwanoa wahariri wa Mbiu ya Banana.
Semina hii iliyoshirikisha wahariri kutoka mashirika mbalim-
bali wakiwepo AMCF na TCCIA iliendeshwa na wakufunzi
kutoka chuo cha Uandishi wa habari cha Arusha. Katika
mambo yaliyofundishwa kwenye hiyo semina ni pamoja na
upangiliaji wa
makala, jinsi ya kuandika makala bora na pia jinsi ya kupitia
makala.
SALAMU ZA MHARIRI
3 HALIUZWI
Toleo la 20 January—March
Akampuni yaboresha huduma kwa watejaKutokana na kampuni kujali na kuwathamini wateja wetu, imeanzisha huduma
bora kwa wateja kwa saa 24 kwa njia ya simu:Huduma hii itakuwa kwaajili ya kuhakikisha kwamba wateja wanapata
yafuatayo:-
Kujibu maswali mbalimbali ya wateja.
Kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bila kukosa.
Kupata maoni na mahitaji mbalimbali kutoka kwa wanywaji/wateja.
Huduma hii itakuwa kwa kutumia meseji au kupiga simu na majibu yake yaweza kuwa ni kwa meseji au kupigiwa simu
na mteja atajibiwa hapo hapo au baadae. Namba za simu kwaajili ya huduma hii ni ; 0759 270508 na 0682 802283
WATEJA KWETU NI WAFALME, TUPO TAYARI KUWAHUDUMIAWATEJA KWETU NI WAFALME, TUPO TAYARI KUWAHUDUMIAWATEJA KWETU NI WAFALME, TUPO TAYARI KUWAHUDUMIAWATEJA KWETU NI WAFALME, TUPO TAYARI KUWAHUDUMIA
MABORESHO KATIKA HUDUMA KWA WATEJA.
Hivi karibuni kampuni yetu ilifanikiwa kufanya promotion kabambe ambayo ilianza mnamo tarehe 21.09.2010 hadi tarehe
09.12.2010.Kwa kipindi chote hicho wanywaji wetu waliweza kujipatia zawadi mbalimbali kama vile Raha ya bure, Fulana maalum
na pesa taslimu kuanzia shilingi 1,000/=, 2,000/= 5,000/= 10,000/= na 20,000/=
Hata hivyo haikuishia hapo tu, Shindano kubwa ilichezeshwa tarehe 12.12.2010 katika eneo la Sanawari maarufu kama stand ya
tax, ambapo washindi 8 walipatikana. Zoezi zima liliendeshwa chini ya usimamizi wa mwakilishi kutoka Bodi ya bahati na nasibu
Ndugu Humud Abdulhusein na waandishi wa habari kutoka sehemu mbalimbali. Washindi waligawanyika katika makundi matatu
ambayo kwa kundi la tatu walizawadiwa baiskeli 5 aina ya phonex, washindi wawili kwa kundi la pili walizawadiwa TV 2 aina SON
ya inchi 21 na Mashindi mmoja kwa nafasi ya kwanza alizawadiwa pikipiki aina ya Toyo 125CC.
ZAWADI HIZO ZILITOLEWA KAMA JEDWALI LINAVYO ONYESHA HAPA
PROMOTION YA TAJIRIKA NA RAHA YAFIKIA TAMATI, WENGI WATAJIRIKA NA VITU MBALIMBALI
DRO
NAM
BA
JINA LA
MSHINDI
ENEO
ZAWADI
SIMU
NAMBA.
980 DEUS FRANSIS NGARANARO BAISKELI 0757145298
1500 GENES JASTIN
MOSHI
OLORIENI BAISKELI 0753299738
1060 JOSEPH UWAWI SASI- DULUTI BAISKELI BOX 99
DULUTI
802 PIUS BENEDICT
MALLYA
MOSHONO BAISKELI 0759206692
514 MAIMU KI-
MARO
BABATI BAISKELI 0787866876
785 NESTO ED-
WARD KIMARO
NJIRO TV 0768614444
1046 DEVOTA LYIMO MIANZINI TV 0782459405
696 JOHN J.SHOO ESSO MOTORCY-
CLE
0753627459
0714439303
Baadhi ya washindi wakipokea zawadi zao maeneo
ya kiwandani.
4 HALIUZWI
Toleo la 20 January—March
Tunawakaribisha wafanyabiashara kujiunga na Kampuni yetu ya Banana Investments Ltd kusambaza kinywaji chetu kwenye mikoa
ambayo RAHA haijafika. Hali ya sasa katika usambazaji wa mvinyo wa Raha upo kama unavyoonyesha hapo juu kwenye Ramani.
5 HALIUZWI
Toleo la 20 January—March
CHUO Kikuu huria cha Tanzania, CKHT, ni chuo ki-
kuu cha umma hapa nchini. Chuo hiki hutoa elimu kwa
njia ya masafa kwa watu wa rika zote ambao hawana
muda wa kuhudhuria masomo darasani muda wote,
hivyo kutoa fursa kwa waajiriwa na wafanya biashara
kujiendeleza katika taaluma mbalimbali katika ngazi
za stashahada ,”certificate”, stashahada , “diploma” na
shahada “degree”. Elimu inayotolewa na Chuo Kiku-
kuu huria cha Tanzania ni elimu yenye ubora na inayo-
kubalika (Quality and affordable education) sawa na
vyuo vikuu vingine duniani Makao makuu ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yako
Dar es Salaam, Sanduku la posta 23409, na tovuti ya
chuo ni www.out.ac.tz. Chuo kina vituo katika mikoa
yote ya Tanzania Bara na Zanzibar. Kuna usemi kuwa
“CKHT kinawafuata wanafunzi popote walipo nchini
Tanzania” na si kinyume chake kama ilivyo kwa vyuo
vikuu vingine. Wanafunzi wanaojiunga na CKHT
husailiwa na Tanzania Commission of Universities,
TCU, sawa na wale wanajiunga na vyuo vikuu vingine
hapa nchini. CKHT huandaa mafunzo ya awali, “orientation pro-
gram”, baada ya wanafunzi kuchaguliwa au kufaulu
kuendelea na elimu ya juu. Mwanafunzi hupata fursa
ya kujifunza taratibu za chuo na maelezo ya kina kuen-
dana na mafunzo aliyochagua. Katika kipindi hiki
mwanafunzi hupewa nafasi ya mwisho kubadilisha aina
ya mafunzo atakayochukua na CKHT.
Baada ya mwanafunzi kusajiliwa, chuo husaidia kutoa
elimu endelevu kwa njia ya majaribio na mitihani kwa
muda wote wa mafunzo. Mwanafunzi hupewa mihta-
sari,“course outlines” za masomo anayochukua pamoja
na vitabu husika, na ana uhuru wa kujisomea kwa wa-
kati wake mwenyewe ndani ya muda wa masomo
uliopangwa. Watu mbalimbali wamefanikiwa kujiendeleza kwa uta-
ratibu huu na kuhitimu mafunzo mbalimbali. Miongoni
mwa wafanyakazi wa Kampuni ya Banana waliofaulu
kupitia CKHT ni pamoja na Bwana Ally A. Massawe,
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala ambaye alitunukiwa
Shahada ya Uzamili ya Biashara na Utawala, “ Master
of Business Administration” na Bi. Betty Mboya,
katibu muhtasi wa kampuni ya Banana, ambaye ame-
hitimu Astashahada ya Biashara na Utawala. Wote
walitunukiwa vyeti vya kuhitimu mwezi October, 2010.
Bi Betty Mboya amefaulu kuendelea kusomea Shahada
ya Biashara na Utawala , “Bachelor of Business Ad-
ministration” kwa mhula ulioanza 13 Novemba, 2010.
KIJUE CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA
Imeandikwa na Betty Mboya.
Faida kubwa za utaratibu wa masomo ya CKHT ni pamoja
na unafuu wa ada ukilinganisha na vyuo vingine, wanafunzi
kupewa fursa ya kujisomea kwa wakati wao nje ya eneo la
chuo na hivyo kuruhusiwa kuendelea kusoma na huku waki-
fanya kazi au biashara kwa wakati mmoja. Wanafunzi wana-
ruhusiwa kufanya mitihani sehemu yoyote nchini bara na
visiwani bila kujali mahali alipojiandikisha. Wahitimu wa
shule za sekondari, kidato cha IV na VI, ambao hawakucha-
guliwa kuendelea na masomo ya juu sasa wanaweza kupata
elimu ya juu kupitia CKHT na kuongeza kwa kiasi kikubwa
idadi ya wahitimu wa elimu ya juu hapa nchini.
BANANA FOUNDATION WADHAMINI MAFUNZO YA
VIONGOZI WA SACCOS.
Na. Beatha Anthony
Banana Foundation ni taasisi isiyo ya kiserikali inayojihu-
sisha na kutoa misaada mbalimbali katika jamii hasa kwa
watu au familia zisizojiweza.
Taasisi hii inapata ruruku zake kutoka Banana Investments
Ltd ambazo zinatumika kutoa misaada mbalimbali. Shughuli
ambazo Banana Foundation inafanya ni pamoja na kusaidia
kuinua kipato cha wanajamii hasahasa wajasiriamali
wadogowadogo. Na hii wanaifanya kupitia kwenye vyama
vya ushirika vya kuweka na kukopa (SACCOS). Mpaka sasa
banana Foundation imeshaingia mkataba na SACCOS za
UDEA, Kijenge RC, TCCIA na Banana. Ili waweze kuwa-
saidia kuinua vyama vyao na kutoa mikopo ya kutosha na
kwa wakati wa wajasiriamali. Msaada unaotolewa na Ba-
nana Foundation ni wa mafunzo mbalimbali ya kujenga
uwezo na sio fedha taslimu.
Ili kuhakikisha kwamba hilo linafanikiwa Banana Founda-
tion wakishirikiana na Benki ya CRDB waliandaa semina ya
siku moja iliyojumuisha viongozi wa SACCOS zote na ku-
toa mafunzo juu ya janga la mikopo ambalo limekua ni ta-
tizo sugu kwa SACCOS nyingi.
Akiendesha mafunzo hayo Bw Seuri kutoka CRDB alisisi-
tiza kwamba viongozi na watendaji wawe makini wakati wa
kutoa mikopo kwani hapo ndio makosa mengi hujitokeza.
Pamoja na hayo pia Banana Foundation hutoa msaada kwa
wanafunzi wanaoishi katika mazingira hatarishi hasa yatima
na wale wanaoishi katika hali duni. Wanafunzi wanaopata
hizi ruzuku ni wale wanaosoma katika shule zilizoko kata ya
Oloirien au wanaoishi Oloirien lakini wanasoma sehemu
nyingine. Pia wanafunzi hao wanatakiwa kuwa na uwezo wa
kimasomo darasani na sio ambao hawafanyi vizuri.
Pia tunakaribisha watu wote wanaoweza kutoa msaada an-
6 HALIUZWI
Toleo la 20 January—March
Y’S MEN TANZANIA WAFADIKISHA VUKA BODA BASH NA: Beatha Anthony
Tamasha la Vuka Boda lililoandaliwa na wanachama wa Y’s
Men wa Arusha kuanzia tarehe 17 mpaka tarehe 20 Decemba
2010. Tamasha hili liliudhuriwa na wanachama kutoka Moshi,
Arusha, Nairobi South, Nairobi Central, Thika, CUEA na
KEMU.
Wanachama wote walifikia shule ya Trust St Patrick iliyopo mae-
neo ya Sakina ambapo walipatiwa malazi pamoja na usafiri kwa
muda wote waliokuwepo hapa Arusha. Katika Tamasha hili
lengo kuu lilikua ni kumpongeza kijana Vincent Gichamba wa
Nairobi Central kwa kuchaguliwa kuwa International Youth Rep-
resentative (IYP) wakati wa Convention iliyofanyika Yokohama
Japan mwezi wa August mwaka huu.
Katika tamasha hili kati ya mambo yaliyofanyika ni pamoja na
kuotesha miti katika maeneo ya moshono, pia kulikuwepo na
mafundisho mbalimbali ya uongozi bora katika viwanja vya ki-
talii vya Lake Duluti na kumalizia kwa kutembele kituo cha utalii
cha Snake Park kilichopo Arusha.
Y’s Men International imekua ikitoa kipaumbele kwa mafunzo
ya uongozi bora kuanzia ngazi ya familia, taifa na mpaka kima-
taifa kwani inaaminika kwamba Viongozi waaminifu na wenye
busara ndio wanaleta maendeleo endelevu.
PAP Hiyasinti Kilasara akielezea jambo wakati wa presenta-
tion katika ukumbi wa Lake Duluti.
Baadhi ya Washiriki wa Vuka Boda Bash wakiwa kwenye picha
ya pamoja maeneo ya Snake Park.
Wanachama wakiskiliza kwa makini baadhi ya mafundisho yali-
yotolewa katika ukumbi wa Duluti.
Kiongozi wa Y’s Yoth arusha akiwa na wanachana kutoka Nai-
robi Centrali walivyotembelea kituo cha utalii cha Meserani
snake park
7 HALIUZWI
Toleo la 20 January—March
Elisante Makyao – Afisa Masoko
Bw. Elisante ana Stashada ya juu
katika maeneleo ya ustawi wa jamii
katika chuo cha Community Devel-
opment Training Institute (CDTI)
Tengeru Arusha mwaka 2010. Pia
ana cheti cha maendeleo ya jamii
katika chuocha CDTI Tengeru cha
mwaka 1992 pamoja na cheti cha elimu ya secondary
kidato cha nne katika shule ya secondari Majengo
moshi mwaka 1985. Ana uzoefu wa miaka zaidi ya
kumi katika taasisi mbalimbali.
AJIRA MPYA, NGUVU MPYA KAMPUNI YA BANANA
KIBWENZO
Zuhura Mmbaga – Accounts Technician
Bi Zuhura ana Diploma in Cooperative
and Accounting katika chuo cha
Moshi University Collage of coopera-
tive and business studies – 2010 pia
ana cheti cha kuhitimu elimu ya juu
katika shule ya secondari Shinyanga
Commercial Institute (SHYCOM) –
2008.
Steven Mvungi – Afisa Masoko Msaidizi Bw. Steven Mvungi ana Cheti cha
Accounts Technician – 2009, ana
Certificate ya Accounts Technician
NBAA pia ana cheti cha elimu ya
juu katika shule ya sekondari Ma-
kumira – 2001 pamoja na cheti cha
elimu ya sekondari kidato cha nne
Lembeni mwaka 1998.
8 HALIUZWI
Toleo la 20 January—March
Makao Makuu Kiwanja Na. 311, Kitalu jj Oloirien Village, P. O. Box 10123, Arusha TANZANIA S i m u : +255754224440,+255272506475 E-mail: [email protected] http:/www.banana.co.tz tz
Dar es Salaam Depot Ubungo Kibangu, S. L. P. 79407, Dar es Salaam TANZANIA Simu: +255 222 774 276, +255 756 707 983 Email: [email protected]
Tanga Depot Barabara ya 4, S. L. P. 5150, Tanga TANZANIA Simu: +255 272 646 134
Email: [email protected].
WASHINDI WA TAJIRIKA NA RAHA WAKIKABIDHIWA ZAWADI ZAO