sickle cell disease (seli mundu) - kemri - wellcome...
TRANSCRIPT
DEPARTMENT OF HEALTH SERVICES
Homa ya mifupa (selimundu) ni nini?
Homa ya Mifupa ni hali inayoathiri damu na
wazazi wote wawilli huchangia. Inamaanisha
watu huzaliwa na homa hii, kama vile wanavyori-
thi wazazi
Dalili zake ni zipi ?
Jinsi damu inavyo tembea katika viungo vya mwili,
chembe chembe za damu ya aina ya selimundu
inaweza kukwama mahali popote katika mwili, hapo
ndipo dalili zitajitokeza. Dalili sana sana huanza
kuonekana miezi minne hadi sita baada ya kuzaliwa,
kwa mfano kufura miguu na mikono kwa ghafla.
Maumivu ya mifupa huwa mara kwa mara, katika
sehemu yoyote ya mwili kama vile kwa mikono, mi-
guu, kifua,kiuno na hata kichwa na tumbo. Maumivu
haya huitwa “pain crises”.
Watoto wengine huisi vibaya na wanaweza kujulisha
mlezi wao.
Homa hii inajitokeza kwa kwa jinsi tofauti tofauti.
Watoto wengi mara nyingine wanasikia vyema na
wakati wengine wanjisikia vibaya. Wengine huwa na
dalili chache maishani mwao. Wengine hupata
maumivu makali. Ni ngumu madaktari kujuwa ni
nani ataumwa sana.
Watoto wenye chembe chembe za selimundu huwa
na upungufu wa damu mwilini, na ni kwa sababu
chembechembe zao hizi huwa na Maisha mafupi
baada ya kutengezwa, na husafishwa mara kwa
mara mwilini.
Mtoto huyu huwa na macho meupe kuashiria upun-
gufu wa damu, na pia kuwa na manjano kwa macho
“yellow” mara kwa mara. Rangi ya manjano au
“jaundice” pekee sio shida. Huwa shida tu ikiwa kuna
dalili zingine ama manjano kuzidi kawaida yake.
Jinsi ya kudhibithi selimundu Hakikisha mtoto amemaliza chanjo za klinik
zote za watoto. Ni vizuri pia wapewe yakuzuia homa ya mapafu “pneumonia” wanapo kuwa wakubwa kwa umri Wathiriwa pia wanafaa kupewa vita-min A mara kwa mara
Hakikisha mtoto wako amelala ndani ya neti iliyotibiwa
Hakikisha mtoto anatumia dawa zote anazopewa na daktari.
Hakikisha wanahudhuri kliniki zao za homa ya mifupa au selimundu
Watoto hawa pia wanapewa dawa za kuzuia homa ya mapafu kwa watoto walio chini ya miaka mitano.
Pia watapewa dawa za kuzuia malaria
Wao pia hupewa dawa ya kuongeza damu (Folic Acid).
Hakikisha mtoto anapata lishe bora. Matunda na mboga kama vile Sukuma wiki na mchicha huwa na vitamin and folic acid ya kutosha. Folic Acid inasaidia kujenga damu mwilini na mtoto wa homa ya mifupa anahitaji kujenga damu mpya mwilini.
Tafuta tiba mapema unapopatwa na shida inayo husiana na athari za homa ya mifupa
Usalama wa dawa ya Hydroxyurea kama tiba ya homa ya selimundu Afrika inaendelea kufanyiwa utafiti kwa nchi nyingi vilivile huku Kenya.
Tiba ya pekee ya homa ya selimundu ni ubadilishaji wa uboho au ‘muretso’, ambayo ni hatari na gali mno kwa wagonjwa wengi
Hata kwa kufuata matibabu ya kawaida, watu wanaweza kuishi na homa hii hata kwa miaka themanini (80 years)
Unaweza kuzuia homa ya hii tu ikiwa tu wanaotaka kuoana kwa kupewa ushauri na kupimwa ikiwa wako na hizi chembe chemebe.
Sickle cell disease
(Seli Mundu)
Sickle: Kifaa cha kukatia mimea
Wasiliana: Klinik ya homa ya mifupa -The Sickle Cell Clinic Kilifi County Hospital +245 0721570192 au Meneja wa Uhusiano Mwema na Jamii, - 0723342780 KEMRI/Wellcome Trust Research Programme, S.L.P. 230, Kilifi. Nambari: 0723342780/0738472 281 au 041 7522063
Njia ya kujua hali yako (Diagnosis)
Njia bora ya kutambua homa hii ni kupimwa kipi-
mo kiitwajo“HB – Eletrophoresis” ambayo inawe-
za kufanywa kwa umri wowote, hata siku ile ya
kwanza ya kuzaliwa.