nakala mtandao(online document) · 2020. 11. 26. · nakala mtandao(online document) 5 mhe. dkt....

71
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ________ BUNGE LA KUMI NA MBILI _________ MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KWANZA Kikao cha Nne – Tarehe 13 Novemba, 2020 (Bunge Lilianza Saa 3:00 Asubuhi) (Saa 3.06 Asubuhi Viongozi wa Kitaifa Walianza Kuingia Ukumbini) Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (Mhe. Zubier Ali Maulid) na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) (Mhe. Martin Ngoga) Waliingia Ukumbini Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma) na Jaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (Mhe. Omar Othman Makungu) Waliingia Ukumbini Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi) na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar (Mhe. Hemed Suleiman Abdullah) Waliingia Ukumbini (Hapa Wabunge Walipiga Makofi na Vigelegele) Waziri Mkuu Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa) Aliingia Ukumbini (Hapa Wabunge Walipiga Makofi na Vigelegele)

Upload: others

Post on 05-Feb-2021

16 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    1

    BUNGE LA TANZANIA

    ________

    BUNGE LA KUMI NA MBILI

    _________

    MAJADILIANO YA BUNGE

    MKUTANO WA KWANZA

    Kikao cha Nne – Tarehe 13 Novemba, 2020

    (Bunge Lilianza Saa 3:00 Asubuhi)

    (Saa 3.06 Asubuhi Viongozi wa Kitaifa Walianza KuingiaUkumbini)

    Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (Mhe. Zubier AliMaulid) na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) (Mhe.

    Martin Ngoga) Waliingia Ukumbini

    Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mhe.Prof. Ibrahim Hamis Juma) na Jaji Mkuu wa Serikali yaMapinduzi Zanzibar (Mhe. Omar Othman Makungu)

    Waliingia Ukumbini

    Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti waBaraza la Mapinduzi (Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi) na

    Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar (Mhe. HemedSuleiman Abdullah) Waliingia Ukumbini

    (Hapa Wabunge Walipiga Makofi na Vigelegele)

    Waziri Mkuu Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa) Aliingia Ukumbini

    (Hapa Wabunge Walipiga Makofi na Vigelegele)

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    2

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(Mhe. Samia Suluhu Hassan) akiongozana na Naibu Spika

    wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mhe. Dkt.Tulia Ackson) Waliingia Ukumbini

    (Hapa Wabunge Walipiga Makofi na Vigelegele)

    (Saa 3:51 Asubuhi Bunge Lilisitishwa kwa muda)

    (Saa 4.15 Asubuhi Bunge lilirudia)

    (Hapa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mhe.Dkt. John P. J. Magufuli) akiongozana na Spika wa Bunge laJamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mhe. Job Y. Ndugai)

    Waliingia Ukumbini

    (Hapa Wabunge Walipiga Makofi na Vigelegele)

    D U A

    Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua

    SPIKA: Ahsanteni Waheshimiwa Wabunge, mnawezakukaa.

    Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania - Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, MheshimiwaMakamu wa Rais - Mama Samia Suluhu, Mheshimiwa Rais waZanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi - Dkt. HusseinAli Mwinyi ambaye amekuwa Mbunge mwenzetu kwa miaka20 mfululizo humu ndani, Mheshimiwa Makamu wa Pili waRais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa NaibuSpika, Mheshimiwa Jaji Mkuu, Mheshimiwa Jaji Mkuu Zanzibar,Mheshimiwa Spika Zubeir Ali Maulid kutoka Baraza laWawakilishi na Mheshimiwa Spika Martin Ngoga kutokaBunge la Afrika ya Mashariki ninawakaribisha sana kwa niabaya Waheshimiwa Wabunge. (Makofi)

    Mheshimiwa Rais, tuna wageni wengi sana kamautakavyoona galleries zetu hizo zimejaa, nitawatambulisha

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    3

    mwishoni baada ya hotuba yako, lakini pia kumbi nyingineza Bunge pia nazo zimejaa wageni nje ya ukumbi huu ambaonao wanafuatilia kila kinachoendelea hapa live.

    Nichukue nafasi hii kabla sijatoa taarifa yangu rasmi,niseme kwamba Mheshimiwa Rais jumla ya WaheshimiwaWabunge Kikatiba wa Bunge hili kuwa wanakuwa ni 393 jumlawote, waliopo hivi sasa ni 359. Bado tunasubiri Wabungewatano kutoka Baraza la Wawakilishi na Mheshimiwa Spikaupo hapa, bado tunasubiri Wabunge watano hapa. Halafutunasubiri Mheshimiwa Rais wateule wa kwako kumi;wanawake watano, wanaume watano, pia tunasubiri walewa Viti Maalum kutoka vyama vingine kwa kadriwatakavyokuja. (Makofi)

    Kwa hiyo, jumla yetu tutakuwa 393 pale tunapokuwatupo kamili kabisa full house, kwa sasa ni 359. Katika hao 359tuna Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wabunge wa CUFwatatu, tunapaswa kuwa na Wabunge wa ACT Wazalendowanne, tuna Mbunge wa CHADEMA mpaka sasa hivi nimmoja na tuna Wabunge wa Chama cha Mapinduzi 256.

    Mheshimiwa Rais kati ya hao, Wabunge wa VitiMaalum ni 94, lakini wanawake kwa ujumla wanakuwa 94kujumlisha 24. Ningeomba Wabunge wanawake wote palemlipo hebu msimame angalau Mheshimiwa Rais apate pichaya uwakilishi wa akina mama Bungeni, kila Mbungemwanamke asimame, wengine bado wamekaa naombaWabunge Wanawake wote msimame. (Makofi/Vigelegele)

    Kwa hiyo, Watanzania wanaweza wakaona uwakilishiwa akina mama ulivyo kwa kweli ni mkubwa kabisa,hongereni sana wote, ni moja ya nchi chache zenye uwakilishimkubwa kiasi hiki wa wakina mama katika Ukanda wetu waAfrika. (Makofi)

    Mheshimiwa Rais, pia ningependa niseme kwambakatika Wabunge hawa tulionao hadi hivi sasa, Wabungewapya kati ya 259 ni 206. Naomba Wabunge wapyamsimame pale mlipo, wapya wote. Waandishi wa Habari

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    4

    picha hii ni muhimu sana ya Wabunge wapya, inatoa pichaya demokrasia ya nchi yetu jinsi ambavyo mabadiliko kwawakati mmoja wa miaka mitano huwa ni makubwa sana.Safari hii mpaka sasa hivi Mheshimiwa Rais ni asilimia 61.1mpaka sasa ya Wabunge wapya. Ahsanteni sana mnawezakukaa. (Makofi/Kicheko)

    Waheshimiwa Wabunge, hiyo inatoa picha kwambakukaa hapa ni shughuli, kuendelea kuwepo hapa siyomasihara. Inabidi mumsikilize Mheshimiwa Rais na mzingatieatakayoyaeleza hapa unaweza ukarudi, ahsante sana.(Kicheko)

    Mheshimiwa Rais na Waheshimiwa Wabunge, kwamujibu wa Ibara ya 91(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania na Kanuni za Bunge Kanuni ya 32 ya Kanuni zaKudumu za Bunge, Toleo la Juni, 2020 ningependa kuwajulishakwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli yupo pamojanasi leo hii ili kulihutubia na kulifungua rasmi Bunge jipya laKumi na Mbili ambalo limekaa katika Mkutano wake waKwanza ulioanza tarehe 10 Novemba na tumefanya kazi yakuwaapisha Wabunge wote 359 hadi hivi sasa, tumefanyakazi ya uchaguzi wa kumpata Spika, tumefanya kazi yakumpata Naibu Spika na tumefanya kazi ya kupiga kurakuthibitisha pendekezo la uteuzi wa Waziri Mkuu MheshimiwaKassim Majaliwa Majaliwa. Hizo ndizo kazi zilizopangwa kwaajili ya Bunge hili la mwanzo na zote tumeshazikamilisha,imebakia sasa hotuba yako Mheshimiwa Rais ambayoukiimaliza tutakuwa tunaahairisha Bunge hili hadi wakatiambao nitautaja pale mwishoni. (Makofi)

    Mheshimiwa Rais, kwa heshima na taadhima sasaningeliomba nikukaribishe uhutubie Bunge hili na kupitiakuhutubia Bunge hili basi uhutubie Taifa na Taifa zima kwakweli limejipanga kukusikiliza huko walipo Watanzania nadunia nzima kwa ujumla. (Makofi)

    Mheshimiwa Rais, nakukaribisha sana. (Makofi)

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    5

    MHE. DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI - RAIS WAJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA: Mheshimiwa Spika,mara ya mwisho nilipoingia kwenye ukumbi huu kulifungaBunge la Kumi na Moja tulibahatika kuwa na Marais wetuwastaafu watatu, lakini kama mnavyokumbuka mmoja waMarais wetu Wastaafu wa Awamu ya Tatu ametanguliambele ya haki Mheshimiwa Benjamin William Mkapa. Pianakumbuka wapo pia baadhi ya Wabunge katika Bungelililotangulia na watumishi wengine wa Bunge waliotanguliambele ya haki, basi kwa heshima yao kabla ya kuanza hotubayangu, ninawasihi sote tusimame tumkumbuke MheshimiwaMkapa pamoja na Wabunge wote waliofariki dunia tangukufungwa kwa Bunge la Kumi na Moja.

    (Hapa Wabunge na Wageni Waalikwa Walisimamakuwaombea watu wote walifariki dunia)

    MHE. DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI - RAIS WAJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA: Mwenyezi Munguaiweke roho ya Marehemu Mzee Mkapa pamoja namarehemu wetu wote mahali pema peponi, amina.

    Mheshimiwa Spika, baada ya utangulizi huo, napendaniseme kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania Ibara ya 91(1) imempa dhamana Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania kulifungua rasmi Bunge la Jamhuriya Muungano wa Tanzania, ni kwa sababu hiyo nimekujahapa leo kulihutubia Bunge hili kwa lengo la kutimiza mashartihayo ya Katiba.

    Napenda nianze kwa kumshukuru sana MwenyeziMungu aliyetujaalia neema ya uhai na kutuwezesha kuionasiku ya leo. Aidha, nakupongeza wewe Mheshimiwa SpikaJob Ndugai, Mbunge wa Jimbo la Kongwa kwa kuchaguliwakwa mara nyingine kuliongoza Bunge hili ukiwa Spika,hongera sana. (Makofi)

    Nampongeza pia Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson kwakuchaguliwa tena kwa mara nyingine kuwa Naibu Spika tenamara hii akiwa Mbunge wa kuchaguliwa kutoka Jimbo la

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    6

    Mbeya Mjini, hongera sana Mheshimiwa Dkt. Tulia, huu niuthibitisho kwamba nchi yetu kupitia Serikali inayoongozwana Chama cha Mapinduzi inawaamini sana wanawake.Kama mnavyofahamu Makamu wetu wa Rais MheshimiwaSamia Suluhu Hassan naye ni mwanamama. (Makofi/Vigelegele)

    Aidha, Bunge hili la Kumi na Mbili nalo lina Wabungewengi wanawake kama ulivyotaja. Kwa msingi huo, napendanitumie fursa hii kuwaahidi kuwa Serikali ninayoiongozaitaendelea kuwaamini wanawake katika kushika nafasimbalimbali za uongozi. Wanawake na akina mama oyee.(Makofi)

    WABUNGE WANAWAKE: Oyee.

    MHE. DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI - RAIS WAJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA: Mheshimiwa Spika,napenda pia kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge wotekwa kuchaguliwa kwenu kuwa Wabunge wa Bunge hili laKumi na Mbili. Mmechaguliwa kwa vile wananchi wana imanikuwa mna uwezo wa kuwawakilisha vizuri. Nafahamumichakato ilivyokuwa, Wajumbe na kadhalika. Hivyo,nawasihi sana Waheshimiwa Wabunge msiwaangushewananchi waliowachagua, Watanzania wana imani kubwasana na Bunge hili la Kumi na Mbili. (Makofi/Kicheko)

    Nitumie fursa hii pia kuwashukuru WaheshimiwaWabunge kwa kuridhia na kumpitisha Mheshimiwa KassimMajaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, ahsanteni sana. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, nimekuja kulizindua Bunge hilibaada ya nchi yetu kufanikiwa kumaliza Uchaguzi Mkuuuliofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 kwa uwazi, amani nautulivu mkubwa. Kwa msingi huo, napenda nirudiekuipongeza Tume yetu ya Taifa ya Uchaguzi kwa kusimamiavizuri zoezi la Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kuanziauandikishaji wapiga kura, uchukuaji na urejeshaji fomu zawagombea, usimamizi wa kampeni na pia zoezi la kupiga

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    7

    kura na utoaji wa matokeo mapema. Kwa hakika,tumethibitisha uwezo mkubwa katika kusimamia uchaguzibila kutegemea misaada kutoka nje. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mwenyekiti wa Tumeya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage,Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu HamidMahamoud, Makamishna wa Tume, Mkurugenzi wa UchaguziDkt. Wilson Mahera pamoja na watendaji wote wa Tume,hongereni sana kwa kazi nzuri mliyofanya. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekeenawapongeza kwa jinsi tulivyotumia vizuri fedhamlizotengewa, kama inavyofahamika uchaguzi wa mwakahuu uligharamiwa na Serikali kwa asilimia 100 ambapo kiasicha shilingi bilioni 331 kilitengwa. Hata hivyo mpaka uchaguziumekamilika, Tume imetumia shilingi bilioni 262 tu. Hii ni isharanzuri ya uadilifu mkubwa walionao viongozi na watendaji waTume ya Taifa ya Uchaguzi, hongereni sana. Natoa rai kwataasisi nyingine kuiga mfano mzuri wa Tume hii. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, kwa moyo wa dhati kabisanarudia kuwashukuru viongozi wetu wa dini kwa kutuongozavyema kwa sala na dua katika kipindi chote cha uchaguzina hatimaye tumeweza kumaliza uchaguzi wetu salama.Nawasihi waendelee kuliombea Taifa letu ili libaki katikamikono ya Mwenyezi Mungu. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, narudia pia kuvishukuru vyombovyetu vya ulinzi na usalama kwa kusimamia vizuri amani nautulivu wa nchi yetu na mipaka yetu wakati wote wauchaguzi. Hii ni ishara kuwa vyombo vyetu vya ulinzi nausalama ni imara na vinafanya kazi kwa weledi mkubwa,hongereni sana vyombo vyetu vya ulinzi na usalama. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee kabisanatoa shukrani nyingi kwa Watanzania wenzangu wote kwakushiriki vizuri na kuonesha utulivu mkubwa kwenye uchaguziuliopita kuanzia kwenye zoezi la uandikishaji wapiga kura,wakati wa kampeni, upigaji kura na kupokea matokeo.

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    8

    Hakuna shaka, uchaguzi wa mwaka huu kwa mara nyingineumethibitisha ulimwengu kuwa sisi watanzania ni wapendaamani, tunajitambua, hatudanganyiki na tumekomaakidemokrasia, ahsanteni sana Watanzania wenzangu.(Makofi)

    Mheshimiwa Spika, masuala yote muhimutuliyoyapanga kuyatekeleza kwenye miaka mitano ijayotumeyaweka kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka2020 hadi 2025 ambayo ina kurasa 303, kwa bahati nzuriWaheshimiwa Wabunge wengi wa Bunge hili wanaifahamuvizuri Ilani hiyo kwa vile wameitumia katika kuomba kura kwawananchi kwenye Uchaguzi Mkuu uliomalizika. Lakinisambamba na masuala hayo yaliyopo kwenye Ilani yetu yaUchaguzi wa mwaka 2020/2025 tunaendelea pia kutekelezana kusimamia mambo yote niliyoyaeleza wakati nikizunduaBunge la Kumi na Moja tarehe 20 Novemba, 2015.

    Mheshimiwa Spika, kama mtakavyokumbuka kwenyehotuba hiyo ya kuzindua Bunge la Kumi na Moja nilielezamambo mengi sana ambayo kimsingi yaliyotoa falsafa bilana vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Tano baadhitumeyatekeleza vizuri yapo ambayo hatujayatekeleza kwaukamilifu na mengine yapo kwenye hatua mbalimbali zautekelezaji. Kwa hiyo, kwenye miaka mitano ijayotutaendelea kusimamia na kutekeleza mambo yoteniliyoyaeleza kwenye hotuba ya kuzindua Bunge la Kumi naMoja, hii ndiyo sababu nimeamua kuigawa tena hotubayangu ya uzinduzi wa Bunge la Kumi na Moja kwenuWaheshimiwa Wabunge il i mkaisome na hatimayeikawaongoze katika kutekeleza majukumu yenu vizuri.(Makofi)

    Mheshimiwa Spika, pamoja na hayo yote naombaMheshimiwa Spika uniruhusu nitaje baadhi ya mambomuhimu tunayoyapa kipaumbele kikubwa katika kipindi chamiaka mitano ijayo.

    Mheshimiwa Spika, jambo la kwanza na muhimututakalolipa kipaumbele kikubwa kwenye miaka mitano ijayo

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    9

    ni kuendelea kulinda na kudumisha tunu za Taifa letu yaaniamani, umoja na mshikamano, uhuru wa nchi yetu,Muungano na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Katika hilonaahidi kushirikiana kwa karibu sana na Rais mpya waZanzibar Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi. Kamwehatutakuwa na mzaha na yeyote mwenye kutakakuhatarisha amani ya nchi yetu, mwenye nia ya kuvurugaumoja na mshikamano wetu na pia mwenye kutaka kutishiauhuru wetu, Muungano pamoja na Mapinduzi Matukufu yaZanzibar. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, napenda pia kutumia fursa hiikumuahidi Mheshimiwa Rais Dkt. Hussein Mwinyi kwambakwenye miaka mitano ijayo Serikali ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania itatoa ushirikiano mkubwa wa kufanya kazi kwakaribu na Serikali ya Zanzibar. (Makofi)

    Kwa kifupi naweza kusema tutafanya kazi kwapamoja kwa lengo la kuleta maendeleo kwa pande zetuzote mbili za Muungano. Katika hilo nampongeza sanaMheshimiwa Rais Dkt. Hussein Mwinyi kwa hotuba nzurialiyoitoa wakati wa kuzindua Baraza la Wawakilishi, kwenyehotuba yake alitoa dira, mwelekeo na kutaja vipaumbelevya Serikali ya Awamu ya Nane ya Zanzibar, hongera sanakwa Mheshimiwa Rais Dkt. Mwinyi kwa hotuba nzuri. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, kupitia Bunge hili napendanimuahidi Mheshimiwa Rais Dkt. Hussein Mwinyi kuwa nitampaushirikiano wa kutosha katika kutekeleza yote aliyoyaahidiwakati wa uzinduzi rasmi la Baraza la Wawakilishi. (Makofi/Vigelegele)

    Mheshimiwa Spika, sambamba na kulinda nakudumisha tunu za nchi yetu, kwenye miaka mitano ijayotutaendelea kuimarisha utawala bora hususani kwakusimamia nidhamu kwenye utumishi wa umma pamoja nakuzidisha mapambano dhidi ya rushwa, wizi, ufisadi naubadhirifu wa mali za umma. Katika miaka mitano iliyopitatuliwachukulia hatua za kinidhamu watumishi 32,555 nakuiwezesha nchi yetu kushika nafasi ya kwanza kati ya nchi

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    10

    35 za Afrika kwa kupambana na rushwa kwa mujibu waTransparency International na pia kushika nafasi ya 28 katiya nchi 136 duniani kwa matumizi mazuri ya fedha za ummakwa mujibu wa utafiti wa Jukwaa la Uchumi la Dunia yaaniWorld Economic Forum wa mwaka 2019. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, hata hivyo watumishi wazembebado wapo, wala rushwa bado wapo na pia wezi nawabadhirifu wa mali za umma bado wapo, kwa hiyo, katikamiaka mitano ijayo tutaendelea kushughulikia matatizo hayo,kwa kifupi niseme utumbuaji majipu utaendelea. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, hata hivyo kwa upande mwinginetutaendelea kuboresha mazingira ya kazi pamoja na maslahiya watumishi wetu wote ili yaendane na hali halisi ya maishaya Watanzania, tutaangalia maslahi yao, kwa hiyo watumishiwasiwe na wasiwasi, wachape kazi. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, kwenye miaka mitano ijayo piatumejipanga kuendeleza jitihada za kukuza uchumi, kamaunavyofahamu katika kipindi cha miaka mitano iliyopitatulijitahidi kusimamia vizuri uchumi wetu ambapo ulikua kwawastani wa asilimia saba kwa mwaka. Aidha, pato ghafi laTaifa limeongezeka kutoka shilingi trilioni 94.349 mwaka 2015hadi kufikia shilingi trilioni 139.9 mwaka 2019. Tulidhibitimfumuko wa bei kutoka asilimia 6.1 mwaka 2015 hadi kufikiawastani wa asilimia 4.4 na kuongeza akiba ya fedha za kigenikutoka Dola za Marekani bilioni 4.4 hadi kufikia dola zaMarekani bilioni 5.2 mwezi Julai, 2020 ambazo zinatuwezeshakununua bidhaa na huduma kwa miezi sita. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, zaidi ya hapo kwenye miakamitano iliyopita tuliongeza mauzo yetu ya nje kutoka Dola zaMarekani bilioni 8.9 mwaka 2015 hadi Dola za Marekani bilioni9.7 mwaka 2019, pia kuvutia uwekezaji wenye thamani yaDola za Marekani bilioni 14.6 sawa na zaidi ya shilingi trilioni30. Aidha, tulifanikiwa kupunguza umaskini wa kipato hadikufikia asilimia 26.4 kwa takwimu za mwaka 2017/2018.Mafanikio haya bila shaka ndiyo yamewezesha mwezi Julai,2020 nchi yetu kutangazwa kuingia katika kundi la nchi za

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    11

    uchumi wa kati kutoka kundi la nchi maskini. Hongereni sanaWatanzania, hongereni sana Waheshimiwa Wabunge.(Makofi)

    Mheshimiwa Spika, kwa mafanikio hayoyamepatikana miaka mitano kabla ya muda uliopangwayaani mwaka 2025, kwa hiyo kwenye miaka mitano ijayotunakusudia kuendeleza mafanikio ya kiuchumiyaliyopatikana na tutahakikisha ukuaji wa uchumiunawanufaisha wananchi hususani kwa kuinua vipato vyao,kupunguza umaskini na tatizo la ajira. Katika hilo tunalengakukuza uchumi wetu kwa wastani angalau asilimia nane kwamwaka na pia kutengeneza ajira mpya zipatazo milioni nane.(Makofi)

    Mheshimiwa Spika, tutaendelea pia kuboresha serazetu za uchumi jumla na sera za fedha (microeconomics andmonitory policies) pia kuhakikisha viashiria vyote vya uchumiikiwemo thamani ya sarafu yetu, mfumuko wa bei pamojana viwango vya riba vinabaki kwenye hali ya utulivu, piatutaongeza jitihada za kuwawezesha wananchi wetukiuchumi kwa kuwapatia mikopo isiyo na riba ama yenyeriba nafuu ikiwemo mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwaHalmashauri zetu. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, pia kupitia mifuko na programumbalimbali zilizoanzishwa na Serikali ambayo kwa idadi zipo18 baadhi ya mifuko hiyo ni Mfuko wa Maendeleo ya Vijana(YDF), Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF), Mfuko waTaifa wa Kuendeleza Wajasiriamali (NEDF), Mfuko wa KutoaMikopo kwa Wajasiriamali Wadogo (SELF-Microfinance Fund),Mfuko wa Kuthamini Mikopo ya Mauzo ya Nje, Mfuko waKilimo Kwanza na kadhalika. Tutaimarisha usimamizi wamifuko hii na kuhakikisha Watanzania wanaifahamu, najuamifuko hii ni mingi ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, hivyo basinakuagiza Mheshimiwa Waziri Mkuu hii ikawe kazi yako yakwanza kushughulikia. Ikiwezekana muangalie uwezekanowa kuiunganisha baadhi ya mifuko ili ifanye kazi kwa tija zaidina kupunguza gharama za uendeshaji. (Makofi)

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    12

    Nataka mifuko hii ikawasaidie wananchi wa kawaidawakiwemo wamachinga, akina baba na akina mama lishepamoja na wajasiriamali wengine wadogo wadogo, kwa hiyokazi yako Mheshimiwa Waziri Mkuu ukaanze na hiyo. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, sambamba na kutoa mikopotutaendelea pia kutekeleza programu mbalimbali za kukuzaujuzi na maarifa ikiwemo maarifa ya ujasiriamali ili kuwapaujuzi na uzoefu wananchi wetu utakaowawezesha kujiajiriama kuajirika ndani na nje ya nchi, tutaendelea piakutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Awamu yaTatu Mzunguko wa Pili tuliouzindua mwezi Februari, 2020ambao utagharimu takribani shilingi trilioni 2.032. Tutahakikishafedha hizo zinawafikia walengwa ambao ni wananchimaskini.

    Mheshimiwa Spika, muhumu zaidi ni kwamba katikakipindi cha miaka mitano ijayo sekta binafsi pia itapewaumuhimu wa pekee sana. Tunataka mtu yeyote atakayetakakuwekeza asisumbuliwe kwa kuwekewa vikwazo vya ainayoyote. Watanzania ni matajiri, lakini baadhi yao wanasitakuwekeza hapa nchini kwa kuogopa kusumbuliwa namaswali yasiyo na msingi, tunahitaji kuwa na mabilioneawengi wa Kitanzania. (Makofi)

    Tunahitaji mabilionea wengi wa Kitanzania wakiwemoWaheshimiwa Wabunge. Nataka Watanzania wote washirikikikamilifu katika kujenga uchumi wa nchi yao sambamba nakuwekeza, Watanzania wahamasishwe kuweka fedhakwenye benki za hapa nchini ili kusaidia benki zetu kufanyabiashara na kuimarisha mzunguko wa fedha na kupunguzariba kwa wakopaji. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge naWatanzania mnaonisikiliza, wakati wa kufanya mambo bilawoga nataka niwaambie Waheshimiwa Wabunge ni sasa,tumechelewa sana! (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, kwenye miaka mitano ijayo piatutafungua milango wa sekta binafsi kufanya majadiliano na

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    13

    Serikali ili kutafuta muafaka wa migogoro ya kibiashara(business disputes) iliyopo kwa faida ya pande zote mbili.Lengo letu ni kuona Tanzania inakuwa mahali pazuri pakufanya biashara duniani.(Makofi)

    Mheshimiwa Spika, katika miaka mitano iliyopitatumefuta tozo 168 ambapo tozo 114 zilihusu kilimo, mifugona uvuvi na tozo nyingine 54 zilihusu biashara. Tutaendeleana utaratibu huo. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, mbali na hatua hizo kwa lengo lakukuza uchumi kupambana na umaskini na pia kukabilianana tatizo la ukosefu wa ajira, tunakusudia kwenye miakamitano ijayo kuweka mkazo mkubwa katika kukuza sekta zetukuu za uchumi na utazlishaji hususani kilimo, ufugaji, uvuvi,viwanda, madini, biashara na utalii. Sekta hizi ndizo zenyekuajiri Watanzania wengi, kwa hiyo, ni wazi tukifanikiwakuzikuza uchumi wetu utakua kwa kasi na hivyo kupunguzamatatizo ya umaskini na ukosefu wa ajira nchini. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, kwa msingi huo kwenye kilimo kwamfano, tunakusudia kuongeza tija na kukifanya kilimo chetukuwa ni kilimo cha kibiashara, lengo ni kujihakikishia usalamawa chakula, upatikanaji wa malighafi za viwandani na piakupata ziada ya kuuza nje. Ili kufanikisha hayo tutahakikishapembejeo na zana bora za kilimo ikiwemo mbegu, mbolea,viuatilifu, dawa na matrekta vinapatikana kwa uhakika nakwa gharama nafuu. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, tutaongeza pia eneo laumwagiliaji kutoka hekta 561,383 hadi hekta milioni 1.2mwaka 2025, hii itasaidia kupunguza utegemezi kwenyemvua. Tataimarisha mifumo ya upatikanaji wa mitaji kwawakulima wadogo na wawekezaji kwa kushirikiana na taasisiza fedha ikiwemo Benki yetu ya Maendeleo ya Kilimo pamojana benki nyingine. Tutashughulikia pia tatizo la upotevu wamazao (post harvesting loss) ikiwemo kwa kukamilisha ujenziwa vihenge na maghala maeneo mbalimbali nchini ambayoyataongeza uwezo wetu wa kuhifadhi mazao kutoka tani190,000 za sasa hadi tani 501,000. Takwimu zinaonesha kuwa

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    14

    kila mwaka nchi yetu inapoteza wastani wa kati ya asilimia30 na asilimia 40 ya mavuno yake kwa sababu mbalimbaliikiwemo kukosekana kwa miundombinu ya kuhifadhi mazaoyetu. Zaidi ya hapo tunakusudia kuanzisha bidhaa mbalimbaliza huduma za bima ya kilimo na pia kuingia makubaliano yakibiashara na nchi walaji na wanunuzi wa mazao ili kupatasoko la uhakika zaidi. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, mazao ya kimkakati tunayolengakuyapa kiupaumbele kikubwa katika miaka mitano ijayo nipamba, korosho, chai, kahawa, tumbaku, mkonge,michikichi, cocoa, alizeti pamoja na miwa, lakini pia mazaoya chakula. Nchi yetu kwa mwaka inaagiza tani zipatazo800,000 za ngano na kwa ujumla tunatumia wastani wa shilingitrilioni 1.3 kuagiza chakula kutoka nje, hii ni aibu kwa nchikama Tanzania! Hivyo, basi ni lazima tutafute majawabu yasuala hili na hii ndio ikawe kazi ya kwanza ya Waziri wa Kilimonitakayemteua. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, zaidi ya hapo tutaweka mkazomkubwa kwenye kilimo cha mazao ya bustani yaanimatunda, mbogamboga, maua na viungo ambachokinakua kwa kasi kubwa nchini, hivi sasa nchi yetu inashikanafasi ya 20 kwa kuzalisha wa wingi mazao hayo duniani namauzo yetu ya nje yameongezeka kutoka Dola za Kimarekanimilioni 412 mwaka 2015 hadi kufikia Dola za Kimarekani milioni779 mwaka 2019. Hii ndiyo sababu hatuna budi kukiendelezakilimo cha mazao hayo na katika hilo napenda kuliarifu Bungehili kuwa kwenye miaka mitano ijayo tunakusudia kununuandege moja ya mizigo ili kurahisisha usafirishaji wa mazao yabustani, lakini pia minofu ya samaki pamoja na nyama.Wakulima wetu ni lazima watajir ike na shughuliwanazozifanya. Hivyo basi, Mawaziri wa Kilimo, Biashara,Mambo ya Nje na Mabalozi wajipange vizuri katika hili.(Makofi)

    Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mifugo; kamamnavyofahamu nchi yetu inashika nafasi ya pili kwa mifugomingi Barani Afrika. Tuna ng’ombe milioni 33.4, mbuzi milioni21.3, kondoo milioni 5.65, punda 657,389 lakini pia tuna idadi

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    15

    kubwa ya kuku, bata, kanga na kadhalika. Hata hivyo, niukweli usiopingika kwamba sekta hii bado haijanufaisha vyakutosha. Kwa kuzingatia hilo, kwenye miaka mitano ijayotunakusudia kuikuza sekta ya mifugo ili ichangie ukuaji wauchumi na kupunguza matatizo ya umaskini na ukosefu waajira nchini. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, tumepanga kuongeza maeneoya ufugaji kutoka hekta 2,788,901 za sasa hadi hekta milionisita. Tunataka wafugaji wetu wasiteswe na mifugo yao,mifugo ni utajiri. Sambamba na hayo, tutahamasisha ufugajiwa kisasa, tutaongeza vituo vya kuzalisha mbegu bora napia kuongeza uzalishaji wa chakula cha mifugo viwandanikutoka tani 900,000 hadi tani milioni nane. Zaidi ya hapotutakamilisha ujenzi wa machinjio saba unaoendeleamaeneo mbalimbali nchini ambapo kwa pamoja yatakuwana uwezo wa kuchinja ng’ombe 6,700 na mbuzi 11,000 kwasiku. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, ujenzi wa machinjio hayo siyo tuutasaidia kupatikana kwa nyama bora inayouzwa hadikwenye masoko ya kimataifa, bali pia utawezeshaupatikanaji wa ngozi bora kwa ajili ya kutengeneza bidhaaza ngozi. Takwimu zinaonyesha kuwa takribani asilimia 90 yangozi inayozalishwa nchini kwa sasa haina ubora unaohitajikakimataifa na kwa sababu hiyo mojawapo ni uchinjaji wawanyama kienyeji. Kwa hiyo, machinjio yanayojengwayatapunguza tatizo hilo. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kuikaribisha sektabinafsi kuwekeza kwenye viwanda vya kutengeneza bidhaaza mifugo yaani nyama, ngozi, maziwa, kwato na kadhalikana katika hilo tunaahidi kutoa vivutio maalum kwawatakaoweza kuanzisha viwanda vya aina hiyo na viwandahivyo vitasaidia kuinua vipato vya wafugaji wetu na piakuongeza fursa za ajira kwa Watanzania. Na hapa natakaniweke bayana kuwa watendaji wataokwamisha ujenzi waviwanda hivyo tutawashughulikia, kwa sababu saa nyinginetunakuwa na mipango mizuri, Watendaji wa chini

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    16

    wanakwamisha. Ilani ya Uchaguzi sitaki icheleweshwe na mtuyeyote. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, nchi yetu pia imebarikiwa kuwana maeneo mengi yanayofaa kwa shughuli za uvuvi ikiwemoUkanda wa Pwani, Maziwa, Mito na Mabwawa. Hali hiiinaifanya sekta hii kuwa na nafasi ya kutoa mchangomkubwa kwenye kukuza Pato la Taifa na pia kupambana naumaskini na tatizo la ajira. Hata hivyo, kwa sasa mchangowake bado ni mdogo sana. Hivyo basi, kwenye miaka mitanoijayo tunakusudia kuikuza sekta hii ya uvuvi ikiwemokuimarisha shughuli za uvuvi kwenye Bahari Kuu ambakotumekuwa tukipoteza mapato mengi.

    Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa report ya Kamatiya Bunge kuhusu shughuli za uvuvi wa Bahari Kuu ya mwaka2018; shughuli za uvuvi kwenye Bahari Kuu zinaweza kuiingiziaSerikali mapato ya moja kwa moja ya takribani shilingi bilioni352.1 kwa mwaka endapo mifumo, usimamizi na udhibitiingekuwa imara. Samaki wangechakatwa hapa nchini hatahivyo mapato yaliyokuwa yamekusanywa kwa kipindi chamiaka tisa yaani kuanzia 2009 hadi 2017 yalikuwa shilingi bilioni29.79 tu sawa na shilingi bilioni 3.3 kwa mwaka. Kiwango hikicha mapato hakikubaliki. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, hii ndiyo sababu tunataka kwenyemiaka mitano ijayo kuisimamia vizuri shughuli ya uvuvi waBahari Kuu ili Taifa letu linufaike na rasilimali zake kwa kuhusishasekta binafsi. Kwa bahari nzuri, tayari mwaka huu 2020tumetunga sheria mpya ya kusimamia na kuendeleza uvuviwa Bahari Kuu. Aidha, tumepanga kununua meli nane zauvuvi kwa kusihirikiana na Shirika la IFAD. Meli hizo nane, nnezitakuwa upande wa Zanzibar na nne zitakuwa upande waTanzania Bara. Meli hizi zitashiriki katika uvuvi wa Bahari Kuu.(Makofi)

    Mheshimiwa Spika, kama mnavyofahamu suala lauvuvi wa Bahari Kuu ni la Muungano, tunakusudia pia kujengabandari kubwa ya uvuvi itakayotoa ajira zipatazo 30,000 na

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    17

    tutaendelea kuihamasisha sekta binafsi kujenga viwanda vyakuchakata samaki.

    Sambamba na kusimamia Bahari Kuu, tutakuzashughuli za uvuvi kwenye Maziwa yetu Makuu yaani Victoria,Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa pamoja na Mito yetumikubwa, tutahamasisha wavuvi wetu wadogo kujiungakwenye vikundi ili tuweze kuwapatia mitaji, ujuzi, vifaa na zanaza uvuvi, na hali kadhalika tutapitia upya tozo za maeneombalimbali ili kuwapunguzia wavuvi kero na kuvutia uwekezajikwa wavuvi wetu. Tutahamasisha pia watu binafsi kujengamabwawa na kufuga kisasa kwa kutumia vizimba. Sekta yauvuvi ni lazima itoe mchango mkubwa kwenye uchumi wanchi yetu. Wateule wote wa sekta hii ni lazima walisimamiehili. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, ni ndoto kufikiria kwambatutaweza kukuza uchumi au kupambana na umaskini pamojana tatizo la ukosefu wa ajira bila kuendeleza nguvu katikakukuza sekta ya viwanda. Duniani kote sekta ya viwandandiyo muhimili mkuu wa kukuza uchumi, kupambana naumaskini pamoja na matatizo ya ajira. Kwenye miaka mitanoiliyopita tulifanikiwa kujenga viwanda vipya takribani 8,477ambavyo vilitengeneza ajira zipatazo 480,000 ambapo Mkoawa Pwani uliongoza kwa kujenga viwanda vingi.Nawapongeza sana uongozi wa Mkoa wa Pwani. (Makofi)

    Hivyo basi, kwenye miaka mitano ijayo tutaendelezajitihada za kukuza sekta hiyo. Mkazo mkubwa tutauwekakwenye viwanda vyenye kutumia malighafi zinazopatikanakwa wingi hapa nchini yaani mazao ya kilimo, mifugo na uvuvivyenye kuajiri watu wengi na ambavyo bidhaa zakezinatumika kwa wingi hapa nchini kama vile nguo, bidhaaza ngozi, mafuta ya kula, sukari, saruji na kadhalika. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, ili kuvutia uwekezaji kwenye sektaya viwanda tutaendelea kuboresha mazingira ya biasharana uwekezaji ikiwemo kuangalia masuala ya kodi na kuondoavikwazo na urasimu. Pamekuwepo na urasimu nyingi nakusumbuliwa kwa wawekezaji kwa kuzungushwa zungushwa

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    18

    na hivyo kuwafanya wakate tamaa. Mimi nataka mwekezajimwenye fedha zake akija apate kibali ndani ya siku 14.(Makofi)

    Mheshimiwa Spika, na kwa sababu hiyo nimeamuasuala la uwekezaji ikiwa ni pamoja na Kituo cha UwekezajiTanzania (TIC) kulihamishia kutoka Ofisi ya Waziri Mkuukwenda Ofisi ya Rais ili hao wanaokwamisha nikapambanenao mwenyewe. Lakini zaidi ya hapo, tumepanga kujengaUkanda na Kongani yaani clusters za viwanda kila mkoakulingana na mazao na maliasili zinazopatikana huko.(Makofi)

    Mheshimiwa Spika, kwenye miaka mitano iliyopitatumepata mafankio makubwa kwenye sekta ya madini.Mapato yameongezeka kutoka shilingi bilioni 168 mwaka2014/2015 hadi shilingi bilioni 527 mwaka 2019/2010. Mchangowa sekta ya madini kwenye Pato la Taifa umeongezekakutoka asilimia 3.4 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 5.2 mwaka2019. Zaidi ya hapo kwa mara ya kwanza katika historia yanchi yetu, mwaka 2019 sekta ya madini iliongoza kwakutuingizia fedha nyingi za kigeni Dola za Marekani bilioni 2.7.(Makofi)

    Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kulipongeza sanaBunge la Kumi na Moja kwa kutoa mchango mkubwa katikakupatikana kwa mafanikio haya ikiwa ni pamoja na kutungasheria humu Bungeni. Ahsanteni sana WaheshimiwaWabunge. (Makofi)

    Nina imani kuwa, Bunge hili la Kumi na Mbili litafuatanyayo za Bunge la Kumi na Moja na katika hili napendaniliarifu Bunge hili tukufu kuwa kwenye miaka mitano ijayotutaendelea kuimarisha ulinzi na usimamizi wa madini yetukama tulivyofanya kwa kujenga ukuta wa Mirerani kwakuimarisha Sheria zetu ili madini yetu yasitoroshwe na Serikalikukoseshwa mapato. Aidha, tunakusudia kuendelea kufanyamajadiliano na wawekezaji wakubwa kwa kuzingatia mfanowa makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali na Kampuni ya

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    19

    Barrick yaliyowezesha kuundwa kwa Kampuni ya TwigaMinerals Corporation.

    Mheshimiwa Spika, nchi yetu imebarikiwa kuwa namadini mbalimbali ikiwemo dhahabu, almasi, Tanzanite,chuma, bati, nickel, copper na kadhalika. Lakini aidha tunagesi za aina mbalimbali kama vile ethane, methane pamojana helium. Kwa taarifa tulizonazo kwa mfano kwenye gesi yahelium ambayo inapatikana kule Rukwa ni tani nyingi sanazilizoko kule za ujazo zikichimbwa zinatosha ku-supply dunianzima kwa miaka 20. (Makofi)

    Kwa hiyo, kama zinaweza zikahudumia dunia kwamiaka 20 huu ni utajiri mwingine tulionao sisi Watanzania. Hiindiyo sababu kila siku nimekuwa nikisema sisi siyo maskini, sisini matajiri, nchi yetu ni tajiri sana. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, lakini kuhusu madini, pia kwenyemiaka mitano ijayo tutaendelea kuimarisha Shirika letu la Taifala Madini yaani STAMICO ili lishiriki kikamilifu kwenye shughuliza madini kuwawezesha wachimbaji wetu wadogo wadogoikiwa ni pamojha na kuwatengea maeneo ya uchimbaji,kuwapatia mafunzo mikopo pamoja na vifaa na katika hilinatambua kuwa wapo baadhi ya watu wamepewa leseniza utafiti na uchimbaji, lakini hawajazifanyia kazi. Tutazifutaleseni zao na maeneo hayo tutawagawia wachimbajiwadogo wadogo. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, wachimbaji wadogo wadogo nimuhimu sana katika kukuza sekta ya madini. Tutaendeleapia kuimarisha masoko ya madini pamoja na kuhamasishaujenzi wa viwanda vya uchenjuaji, uyeyushaji, usafirishaji nautengenezaji wa bidhaa za madini. Tunataka madiniyachimbwe hapa Tanzania, yachenjuliwe hapa Tanzania,yayeyushwe hapa Tanzania kisha bidhaa za madinizitengenezwe hapa Tanzania na ndipo ziuzwe nje ama watukutoka nje waje kununua bidhaa za madini hapa nchini.Tutakuwa tumetengeneza uchumi wa kutosha lakini piatutatengeneza ajira za kutosha kwa Watanzania. Ni imaniyetu kuwa kutokana na hatua tulizopanga kuzichukua, sekta

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    20

    ya madini itaweza kuchangia angalau asilimia 10 ya Pato laTaifa ifikapo mwaka 2025. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, utalii ni sekta nyingine ambayotutaipa mkazo mkubwa kwenye miaka mitano ijayo; sektahii imeajiri takribani watu milioni nne. Kwenye miaka mitanoiliyopita ilikuwa ikitoa mchango mkubwa ambao ulikuwaunaridhisha ambapo idadi ya watalii waliotembelea nchiiliongezeka kutoka watalii 1,137,182 mwaka 2015 hadi watalii1,510,151 mwaka 2019. Mapato nayo yaliongezeka kutokaDola za Marekani bilioni 1.9 mwaka 2015 hadi kufikia Dola zaMarekani bilioni 2.6 mwaka 2019. Nitumie fursa hii kuipongezaHifadhi yetu ya Taifa ya Serengeti kwa kuchaguliwa kuwahifadhi bora Barani Afrika kwa mwaka 2020. Kwenye miakamitano ijayo tumejipanga kuongeza iddai ya watalii hadikufikia milioni tano mwaka 2025 na mapato kutoka Dola zaMarekani bilioni 2.6 za sasa hadi Dola za Marekani bilioni sita.(Makofi)

    Mheshimiwa Spika, hatua tutakazochukua ni pamojana kupanua wigo wa vivutio vya utalii ikiwemo kukuza utaliiwa mikutano na uwindaji wa wanyamapori, kuimarisha utaliiwa fukwe, kujenga miundombinu ya kuwezesha meli za utaliikuzuru nchini na kuongeza kasi ya utangazaji wa vivutio vyetu.Vilevile tutazihamaisha taasisi za watu binafsi kuanzisharanchi, mashamba na bustani za wanyama kamainavyofanyika nchi zingine ili kuzuia ujangili na kukuza utalii,lakini pia kuongeza vipato na fursa za ajira kwa Watanzania.(Makofi)

    Mheshimiwa Spika, katika hilo, napenda kuwaarifuWatanzania kupitia Bunge hili tukufu kuwa tumepunguza beikwa ajili ya kupata wanyama wa mbegu kutoka porini.Mathalani, bei ya nyati wa mbegu imepungua kutoka Dolaza Marekani 1,900 hadi kufikia shilingi 200,000, pofu kutokaDola za Marekani 1,700 hadi shilingi 310,000, swala kutokaDola za Marekani 150 hadi shilingi 90,000; hivyo basi, nawasihiWatanzania hata ninyi Waheshimiwa Wabunge popotewalipo changamkieni fursa hii ya kuanza kufuga wanyamawalioko porini. (Makofi)

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    21

    Mheshimiwa Spika, hii ni fursa pekee, kuna nchimbalimbali zimekuwa zikifanya hivyo, mojawapo ni nchi kamaAfrika ya Kusini na kadhalika. Hii itatufanya Watanzania wotetufaidike na biashara ya wanyamapori, lakini pia watuwataanzisha butcher za wanyamapori na wataanza kuwalabadala ya kula nyama ya pori kuonekana ni adui. Zaidi yahapo, tutaendelea kupitia upya kodi na tozo mbalimbali ilikuzifuta ama kupunguza kodi zenye kero. Kwenye miakamitano iliyopita, tulipunguza ada za leseni za biashara ya utaliikwa Wakala wa Kusafirisha Watalii yenye idadi ya magarichini ya manne kutoka Dola za Kimarekani 2,000 hadi Dolaza Marekani 500 na matokeo yake idadi ya kampuni zaKitanzania zimeongezeka kutoka 643 mwaka 2015 hadikampuni 1,687 mwaka 2020. Tutaendelea na hatua hizo.(Makofi)

    Mheshimiwa Spika, tuna imani, hatua hizi nilizoelezazitatuwezesha kufikia malengo tuliyojiwekea ya kukuzauchumi kwa angalau asilimia nane kwa mwaka na kuinuavipato vya Watanzania, kupunguza umaskini na kutengenezaajira mpya milioni nane. Hata hivyo, najua ili kufikia malengohaya tunategemea sana kupata ushirikiano kutoka sektabinafsi. Kama mnavyofahamu, sekta binafsi ndiyo engine yakujenga uchumi wa kisasa. Hivyo basi, narudia kuikaribishasekta binafsi ya hapa nchini na kutoka nje kuwekeza katikasekta nilizozitaja na ambazo sikuzitaja. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, napenda kuwahakikishia watu wasekta binafsi kuwa Tanzania ni mahali pazuri na sahihi pakuwekeza. Nchi yetu ina amani na utulivu, tumebarikiwa kuwana fursa nyingi za uwekezaji, nchi yetu ipo kwenye eneo lakimkatati, sisi pia ni wanachama wa East Africa Communityna SADC ambazo zina soko la watu takriban milioni 500. Kwahiyo narudia, kuikaribisha sekta binafsi kuwekeza hapa nchini.Kwa bahati nzuri, tangu mwaka jana tumeanza kutetekelezaMpango wetu wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (Blueprintfor Regulatory Reforms to Improve the Business Environmentin Tanzania). Hivyo basi, mazingira ya biashara na uwekezaji,kwenye miaka mitano ijayo yanatarajiwa kuwa bora zaidikuliko miaka mingine yote. (Makofi)

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    22

    Mheshimiwa Spika, ili kukuza uchumi pamoja na sektaya uzalishaji ni lazima tuimarishe miundombinu, hususan yausafiri na nishati ya umeme. Kamwe huwezi kukuza sekta yakilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda, uchimbaji madini na utalii bilakuimarisha miundombinu na huduma za usafiri pamoja naupatikanaji wa huduma za umeme. Kwa hiyo, kamailivyokuwa kwenye miaka mitano iliyopita, tutaendeleakuweka mkazo mkubwa kwenye ujenzi wa miundombinu yausafiri na kuboresha huduma za usafirishaji. Tutakamilishamiradi tuliyoianzisha na kuanza kutekeleza miradi mipya nakatika hilo tumepanga kwenye miaka mitano ijayo,kukamilisha ujenzi wa kilometa 2,500 za barabara za lami nakuanza ujenzi wa barabara za lami zenye urefu wa kilometa6,006. (Makofi)

    Najua Wabunge wengi mmetoa ahadi za barabarakwenye maeneo yenu, ili hatimaye tuweze kufikia lengo letula kuunganisha mikoa na wilaya zote kwa barabara za lami.Barabara hizo zimetajwa kwenye Ilani yetu ya Uchaguzi nazingine zinatokana na ahadi tulizotoa katika kipindi chakampeni. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, tumepanga pia kukamilisha ujenziwa madaraja saba na kuanza madaraja mengine 14likiwemo Daraja la Kigongo – Busisi, Wami na Pangani. Zaidiya hapo, tutaendelea kushughulikia tatizo la msongamanowa magari kwenye miji na majiji yetu, hususan Arusha, Dar esSalaam, Mbeya, Mwanza na hapa Dodoma ambakotumepanga kujenga barabara ya mzunguko ya njia nneyenye urefu wa kilometa 110 ambapo makandarasi wawilitayari wamekwishapatikana na ujenzi utaanza hivi karibuni.(Makofi)

    Mheshimiwa Spika, kwa upande wa usafiri wa reli,tumepanga kuendelea kuimarisha usafiri wa Reli ya Kati naTAZARA. Aidha, tutakamilisha ujenzi wa reli ya kisasa kutokaDar es Salaam - Morogoro hadi Dodoma na kuanza ujenziwa vipande vya reli ya Mwanza – Isaka; Makutopora – Tabora;Tabora – Isaka hadi Tabora – Kigoma na Kaliua – Mpandahadi Kalema. Zaidi ya hapo, tutanunua vichwa vya treni ya

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    23

    njia kuu 39 na kukarabati 31; tutanunua mabehewa ya mizigo800 na kukarabati 690 na pia tutanunua mabehewa 37 yaabiria na kukarabati mabehewa 60. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, kuhusu usafiri wa majini,tumepanga kukamilisha upanuzi wa bandari zetu kuu yaaniDar es Salaam, Bandari ya Tanga na Bandari ya Mtwarapamoja na zilizopo kwenye Maziwa yetu Makuu yaaniVictoria, Tanganyika na Nyasa. Tumepanga pia kununua melimpya ya mizigo kwa ajili ya kutoa huduma katika Bahari yaHindi. Tutakamilisha ujenzi wa meli mpya, kukarabati meli yaMV Butiama na kuanza ujenzi wa meli ya kubeba mabehewa(ferry wagon) Ziwa Victoria. Tutaikarabati MV Liemba na MTSangara pamoja na kuanza ujenzi wa meli mpya ya kubebaabiria 600 na mizigo tani 400 na nyingine kubwa ya kubebamizigo tani 4,000 kwenye Ziwa Tanganyika. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, kuhusu usafiri wa anga, tutajengakiwanja kipya cha Msalato, kikubwa; tutafanya upanuzi naukarabati wa viwanja vya ndege kumi na moja, vikiwepo vyaKigoma, Shinyanga, Sumbawanga, Tabora, Mtwara naSongea pia kujenga kwa kiwango cha lami njia za kutua nakuruka ndege kwenye viwanja vya Iringa, Lake Manyara,Tanga, Musoma, Lindi, Kilwa Masoko, Njombe, Singida Simiyuna kadhalika. Zaidi ya hapo, tutanunua ndege mpya tano,ambapo kama nilivyosema, moja itakuwa ya mizigo. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, ujenzi wa miundombinu hii yausafiri pamoja na uboreshaji wa huduma za usafirishaji sio tuutachochea shughuli za uchumi na uzalishaji, lakini piaitakuwa ni hatua nzuri ya kuelekea kufikia malengo yetu yakuifanya nchi yetu kuwa lango kuu la biashara kwenyeukanda huu; hivyo kuweza kunufaika na nafasi ya kijiografia.Nchi yetu imezungukwa na nchi takribani nane. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, kuhusu sekta ya nishati,tutaendelea kuimarisha miundombinu ya nishati na piakuboresha upatikanaji wa huduma za umeme. Katika hilo,tunakusudia kukamilisha ujenzi wa Bwawa la Kufua Umemela Nyerere litakalozalisha megawati 2,115 na kuanza ujenzi

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    24

    wa miradi mingine mipya ya umeme wa maji katika eneo laRuhudji megawati 358; Rumakali megawati 222; Kikongemegawati 300 na pia umeme wa gesi asilia Mtwaramegawati 300; Somanga Fungu megawati 330, Kinyerezi IIImegawati 600, Kinyerezi IV megawati 300; pamoja na miradimingine midogo midogo. Aidha, tunakusudia kuzalishaumeme megawati 1,100 kwa kutumia nishati jadidifu yaanijua, upepo, na jotoardhi. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, tumepanga pia kukamilisha miradiya kusafirisha umeme wa Msongo wa kilovoti 400 wa Singida– Arusha hadi Namanga na Iringa – Mbeya hadi Tundumaambayo itaunganisha nchi yetu na jirani zetu za Kenya naZambia. Tutatekeleza mingine ya kuunganisha maeneomuhimu ya nchini kwenye Gridi ya Taifa ikiwemo Kigoma.Kwenye miaka mitano iliyopita, tulitekeleza miradi mingi yakusafirisha umeme na hivyo kupunguza matumizi ya umemewa mafuta; na tukaweza kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 719kwa mwaka. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, kuhusu umeme pia kwenye miakamitano ijayo, tumepanga kufikisha umeme kwenye vijiji vyoteambavyo bado havijafikishiwa umeme, ambapo idadi yakehaizidi vijiji 2,384. Kwa sababu kwenye miaka mitano iliyopita,kwa takwimu za hadi jana tumefikisha umeme kwenye vijiji9,884 kutoka vijiji 2,018 mwaka 2016. Nchi yetu ina vijiji 12,280.Miradi hii yote ya umeme itakapokamilika sio tu itatuwezeshatuwe na umeme wa kutosha na kufikisha umeme kwenyemaeneo yote nchini, bali pia itatufanya tuwe na ziada yakuweza kuuza nje, pia itatusaidia kupunguza gharama zaumeme kuliko gharama za sasa hivi. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, sambamba na hayo, kuhusunishati, kwenye miaka mitano ijayo, tutaanza utekelezaji wamiradi ya kielelezo yaani flagship projects ya bomba lamafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tangalenye urefu wa kilometa 1,445. Mradi huu ni mkubwa na niwa kwanza kuwa mkubwa duniani kwa kusafirisha mafutaambayo yako heated kwenye distance kubwa ya kilometa1,444 na kilometa zote 1,115 ni Tanzania, kilometa zingine 300

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    25

    na kitu zitakuwa nchini Uganda. Mradi wa Kusindika GesiAsilia (LNG) Mkoani Lindi, nao tutahakikisha unaanza kufanyakazi. Zaidi ya hapo, tutaendelea kuhamasisha matumizi yagesi asilia na gesi ya mitungi majumbani, kwenye taasisi naviwanda na magari ili kupunguza uharibifu wa mazingira naathari za mabadiliko ya tabianchi. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, dunia hivi sasa ipo kwenyeMapinduzi ya Nne ya Viwanda yaani The Fourth IndustrialRevoulution) ambayo yanaongozwa na Sekta yaMawasiliano (ICT). Shughuli nyingi duniani, kwa sasazinafanyika kwa kutumia TEHAMA. Hivyo basi, na sisi hatunabudi kuendana na kasi hiyo ya kukua kwa sekta yamawasiliano. Kwa msingi huo, tumepanga, kwenye miakamitano ijayo, pamoja na masuala mengine, kufikishamiundombinu ya Mkongo wa Taifa kwenye maeneo mengiya nchi yetu, hususan wilayani. Tutaongeza wigo wa matumiziya mawasiliano ya kasi yaani broadband kutoka asilimia 45ya sasa hadi asilimia 80 mwaka 2025. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, aidha, tumepanga kuongezawatumiaji wa internet kutoka asilimia 43 ya sasa hadi asimilia80 mwaka 2025 na pia kuboresha matumizi ya simu zamkononi ili kupatikana nchi nzima. Zaidi ya hapo, tutatoavipaumbele kwenye masuala ya utafiti na ubunifu kwenyeTEHAMA, tutawatambua na kuwasajili wataalam wote waTEHAMA; na tunakusudia kuweka anuani za makazi (postalcode) maeneo mbalimbali nchini. Tutaimarisha pia usalamakwenye masuala ya mawasiliano. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, sambamba na kukuza huduma zamawasiliano, tunakusudia kuendelea kuboresha huduma zajamii, hususan afya, elimu na maji. Kuhusu afya, kamamnavyofahamu Waheshimiwa Wabunge, kwenye miakamitano iliyopita tumepata mafanikio makubwa sana ,ikiwemo kujenga vituo vya kutolea huduma za afya zaidi ya1,887; Zahanati 1,198; Vituo vya Afya 487; Hospitali za Wilaya99; Hospitali za Rufaa Mikoa 10; na Hospitali za Rufaa zaKanda tatu. Vilevile, tumepunguza vifo vya akinamamawajawazito kutoka wastani wa vifo 11,000 kwa mwaka

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    26

    mwaka 2015 hadi kufikia wastani wa vifo 3,000 kwa mwakahivi sasa na tunataka vipungue zaidi. Halikadhalika rufaa yakupeleka wagonjwa nje zimepungua kwa asilimia 90 baadaya kuimarisha huduma za kibingwa. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, kwa msingi huo kwenye miakamitano ijayo tunakusudia kuendeleza ujenzi wa miundombinuya kutolea huduma za afya, hususan zahanati, vituo vya afyana Hospitali za Wilaya kwenye maeneo ambako hazipo.Tutaimarisha pia upatikanaji wa dawa, vifaa na vitendanishina kuongeza watumishi wa afya pamoja na kuimarishaMifuko yetu ya Bima ya Afya ili kufikia lengo la kuwawezeshawananchi wote kupata Bima ya Afya. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, wakati wa ugonjwa wa corona,mbali na kumtanguliza mbele Mwenyezi Mungu, tiba za asiliau tiba mbadala nazo zimesaidia sana. Hivyo basi, kwenyemiaka mitano ijayo, tumekusudia kuimarisha Kitengo chaUtafiti wa Tiba Mbadala. Sisi Watanzania hatupaswi kamwekudharau dawa zetu za asili ama tiba mbadala na kwasababu hiyo, matibabu na maduka rasmi ya dawa asiliyataruhusiwa. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, zaidi ya hapo, tutaimarishahuduma za matibabu ya kibingwa na ubingwa bobezi ilikufikia viwango vya kimataifa. Tunataka huduma zote za afyazipatikane hapa hapa nchini, akitaka matibabu ya dawambadala au za asili atibiwe hapa hapa, akitaka za hospitalIatibiwe hapa hapa ili watu waje watibiwe na ikiwezekanawatu kutoka nje waje kutibiwa hapa nchini. Kimsingi, tayariwameanza kuja kutibiwa. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, kwenye elimu, tutaendelea kutoaelimu ya msingi na sekondari bila malipo; tutaongeza bajetiya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ili kuongeza idadiya wanufaika. Aidha, tutaendelea kujenga na kukarabatimiundombinu ya elimu, ikiwemo shule, madarasa, mabweni,maabara, maktaba, ofisi na nyumba za walimu, hostelipamoja na kumbi za mihadhara. (Makofi)

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    27

    Tutahakikisha tunaendelea kuboresha elimuinayotolewa ili iweze kutoa maarifa na ujuzi wa kutosha kwawahitimu wetu. Tutahimiza ufundishaji wa masomo ya sayansina hisabati, hususan kwa wanafunzi wa kike ambaotunakusudia kujenga shule moja ya sekondari kwenye kilamkoa kwa ajili ya kufundisha masomo ya sayansi kwawasichana. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, tutaweka pia mkazo mkubwakwenye elimu ya ufundi na katika hilo, tunalenga kuanzishavituo mahiri vya mafunzo kwa taasisi za elimu ili kuzalishavijana wenye uwezo unaohitajika kitaifa, kikanda nakimataifa ambapo kiasi cha Dola za Marekani milioni 75kimepangwa kutumika. Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaamitabobea katika TEHAMA; Taasisi ya Teknolojia Mwanzaitabobea kwenye masuala ya ngozi; Chuo cha Taifa chaUsafirishaji kitakachobobea katika taaluma za usafiri wa angana Chuo cha Ufundi Arusha kitabobea katika nishati jadidifu.

    Kuhusu maji; mafanikio makubwa sana yamepatikanakwenye miaka mitano iliyopita. Tumetekeleza miradi ipatayo1,422 yenye thamani ya takribani shilingi trilioni 2.2. Hiiimefanya upatikanaji wa maji safi na salama kuongezekakutoka asilimia 47 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 70.1mwaka 2020 kwa vijijini na kwa mijini kutoka asilimia 74 mwaka2015 hadi asilimia 84 mwaka 2020. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, hata hivyo napenda nikiri kwambanilipokuwa kwenye kampeni, moja ya changamoto kubwaniliyoelezwa na wananchi, ilikuwa shida ya maji hususanmaeneo ya vijijini. Kwa msingi huo, kwenye miaka mitano ijayotutajitahidi kuelekeza nguvu zaidi katika kushughulikia sualala maji ikiwemo kuhakikisha kuwa fedha zinazopelekwa vijijinikutekeleza miradi ya maji zinatumika vizuri. Kwa sababu nikweli fedha nyingine zilizokuwa zinapelekwa vijijini zilikuwahazitumiki vizuri na miradi ilikuwa haikamiliki. Nataka kuonamiradi ya maji inayojengwa inakamilika kwa wakati na piawatendaji wawe wabunifu na kuacha kufanya kazi kwamazoea. Mito na maziwa yetu yatumike kikamilifu katikakuwafikishia maji wananchi wa maeneo husika. (Makofi)

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    28

    Mheshimiwa Spika, kwenye miaka mitano ijayo, piatutaimarisha Mfuko wa Taifa wa Maji ili kuuongezea uwezowa kifedha wa kutekeleza miradi ya maji. Tutakamilisha piamiradi mikubwa ikiwemo ya miji 28 itakayogharimu shilingitrilioni 1.2. Upo mradi wa maji wa kutoa maji Ziwa Victoriaunaogharimu takribani shilingi bilioni 600 na mradi mkubwawa maji wa Arusha wenye thamani ya shilingi bilioni 520.

    Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii pia kuwasihiWatanzania kulinda vyanzo vya maji na miundombinuinayojengwa. Nitoe wito pia kwa viongozi wote mkiwemoWaheshimiwa Wabunge, kulifanya suala la kutunza vyanzovya maji na miundombinu yake kuwa ajenda muhimu katikashughuli zetu. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, kwenye miaka mitano ijayotumejipanga pia kuendelea kuimarisha na kukuza uhusianowetu na nchi mbalimbali kwa kuzingatia sera yetu ya mamboya nje inayoweka msisitizo wa diplomasia ya kiuchumi.Tutakuza urafiki na ujirani mwema na pia tutashiriki kikamilifukwenye shughuli za kikanda, kibara na kimataifa hususankwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki na nimefurahi kumwonaMbunge anayewakilisha Bunge letu la Afrika Mashariki na piaJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja waAfrika na Umoja wa Mataifa. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, tutaendelea pia kushirikianakwenye shughuli za kulinda amani. Halikadhalika kwenyemiaka mitano ijayo tutaendeleza jitihada za kukuza nakuimarisha demokrasia, kulinda uhuru na haki ya wananchina vyombo vya habari. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, hata hivyo napenda kukumbushakuwa lengo la demokrasia ni kuleta maendeleo na siyo fujo.Hakuna demokrasia isiyo na mipaka. Aidha, uhuru na hakivinakwenda sambamba na wajibu na hakuna uhuru au hakiisiyo na wajibu. Vyote vinakwenda sambamba. Najuanimeeleweka vizuri. (Makofi)

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    29

    Mheshimiwa Spika, kama nilivyoahidi wakati wakipindi cha kampeni kwenye miaka mitano ijayo tutaendeleakuboresha mazingira ya kufanya biashara kwa wajasiriamaliwadogo yaani machinga, mama lishe, babalishe,waendesha bodaboda, bajaji na kadhalika. Kamamnavyofahamu kwenye miaka mitano iliyopita tulianzishautaratibu wa kutoa vitambulisho maalum kwa wajasiriamaliwetu wadogo. Kwenye miaka mitano ijayo tunakusudiakuviboresha vitambulisho hivyo ikiwemo kuweka picha nataarifa nyingine muhimu, kama ilivyo kwenye Vitambulishovya Taifa au passport. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, hii itawawezeshawafanyabiashara watakaotumia vitambulisho hivyokutambulika, ikiwemo kwenye benki na hivyo, kupata mikopokwa ajili ya kukuza biashara zao. Hii pia itawawezeshawafanyabiashara wetu wadogo wadogo kukua na kutajirika.Hilo ndiyo lengo letu. Tunataka wafanyabiashara wetuwadogo wadogo wawe wanakua na kutajirika na siyo sikuzote wabaki kuwa wafanyabiashara wadogo wadogo.

    Mheshimiwa Spika, kwenye miaka mitano ijayo piatutakuza sekta ya sanaa, michezo na utamaduni ambayoinakua kwa kasi kubwa hivi sasa. Kama nilivyoahidi wakatiwa kampeni, tutaikuza zaidi sekta hii, hususan kwa kuimarishausimamizi wa masuala ya hatimiliki ili wasanii wawezekunufaika na kazi zao. Ninafarijika kuona kuna wasanii ambaoni Wabunge miongoni mwetu humu. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, tutahuisha pia Mfuko waUtamaduni wa Sanaa ili kuwasaidia wasanii wetu ikiwemokupata mafunzo na mikopo. Tutaanza pia kutenga fedhakidogo kidogo kwa ajili ya kuziandaa timu zetu za Taifa. Katikahilo, napenda kutumia fursa hii kuitakia heri timu yetu ya TaifaStars kwenye mechi yao dhidi ya Tunisia baadaye leo, pamojana mwana masumbwi wetu Hassan Mwakinyo ambaye nayeana pambano leo. Watanzania tunataka ushindi, tumechokakushindwa shindwa. (Makofi)

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    30

    Mheshimiwa Spika, kwenye miaka mitano iliyopitatumefanikiwa kuhamishia Makao Makuu ya Serikali hapaDodoma. Viongozi, Wabunge na watumishi wote wa Serikaliwenye kustahili kuhamia Dodoma tayari wameshahamiaDodoma. Kwenye miaka mitano ijayo tutakamilisha ujenzi waofisi na pia kuendelea na ujenzi wa makazi ya watumishi. Zaidiya hapo, tutaendelea kutekeleza miradi ya miundombinuambayo tayari nimeitaja, barabara ya njia nne, uwanja wandege wa Msalato na kadhalika. Tutashughulikia suala laupatikanaji wa maji katika Jij i la Dodoma. Natakaniwahakikishie Wana-Dodoma wote mkiwepo ninyi Wabungena sisi wote na Watanzania, suala la maji tutalitatua harakasana Dodoma. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, masuala mengine ambayotutayapa kipaumbele ni kama ifuatavyo:-

    (i) Tutafanya uendelezaji na uboreshaji wa makazi yawananchi ambapo tutahakikisha vifaa vya ujenzivinapatikana kwa gharama nafuu na mikopo ya ujenziinapatikana kwa riba nafuu; (Makofi)

    (ii) Tutashughulikia pia masuala la mabadiliko yatabianchi;

    (iii) Tutashughulikia masuala ya watu na makundimaalum wakiwemo wazee na watu wenye ulemavu; (Makofi)

    (iv) Tutaendeleza vita dhidi ya biashara haramu yadawa za kulevya. (Makofi)

    (v) Tutaimarisha sekta ya misitu na nyuki, ikiwemo kwakuanzisha viwanda vya mazao ya nyuki ili sekta hiyo itoemchango mkubwa kwenye uchumi wa nchi yetu.Tutahamasisha pia wafugaji wa nyuki. (Makofi)

    (vi) Tutahakikisha wamiliki wa magari wanatoamikataba kwa madereva ili kuipa hadhi inayostahili kazi hiyona kuchochea shughuli za huduma za usafirishaji. (Makofi)

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    31

    Mheshimiwa Spika, nilifurahi jana uliwatambulishahapa madereva akina mama wanaoendesha malori. Nimatumaini yangu na wewe Mheshimiwa Spika utatoa mfanosasa, utaanza kuendeshwa na dereva mwanamke pamojana Naibu Spika. (Makofi/Kicheko)

    Mheshimiwa Spika, katika hilo suala la maderevainawezekana hata katika Bunge hili ikatungwa sheriamahususi ya kuwalinda madereva wetu wa nchi hii, kwasababu tutashughulikia pia kero mbalimbali za wananchiikiwemo migogoro ya ardhi, mirathi, na kadhalika. Kwenyehili nitawaomba sana Waheshimiwa Wabunge mtusaidiesana katika maeneo yenu. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, hili napenda pia kuwaagizaviongozi wa Serikali kuanzia ngazi za vijiji, kata, tarafa, wilayana mikoa, kuhakikisha wanatenga siku maalum ya kukutanana wananchi kwenye maeneo yao ili kusikiliza kero zao nakuzipatia ufumbuzi. Kero nyingine ni nyepesi sana ambazozinaweza zikatatuliwa hata katika level ya vijiji, lakini wakatimwingine zinasubiri mpaka viongozi wa kitaifa wanapopita.(Makofi)

    Mheshimiwa Spika, kwa ujumla mambotuliyoyapanga kuyatekeleza ni mengi sana, kweli ni mengisana, baadhi nimeyaeleza na yapo mengine mengi ambayoyameelezwa vizuri kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM yenyekurasa 303, lakini kwa sababu ya muda sitaweza kuyaelezayote. Hivyo, basi nawaagiza Mawaziri nitakaowateua,pamoja na watendaji, kuisoma vizuri ilani yetu, kuielewa nakuitafasiri vizuri ilani hiyo katika sera na mipango kazi yautekelezaji kwenye Wizara au Taasisi wanazoziongoza iliitakapofika mwaka 2025 tuweze kuitekeleza kikamilifu ilanihiyo. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, najua pia ili kuweza kutekelezavizuri ilani yetu tutahitaji sana kupata ushirikiano kutokakwenye Bunge hili. Kama mnavyofahamu, Bunge ni kiungomuhimu kati ya Serikali na wananchi. Kwa hiyo, nina uhakikaendapo tutashirikiana vizuri miaka mitano ijayo itakuwa ya

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    32

    maajabu na mafanikio makubwa kwa nchi yetu. Binafsi sinashaka kwamba Bunge hili litatoa ushirikiano wa kutosha kwaSerikali. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, hata hivyo, napenda niwekebayana kuwa ninaposema tunaomba ushirikiano,haimaanishi kwamba tunataka muunge mkono kila kitu, lahasha! Penye kukosoa kosoeni, lakini kwa hoja na kutoamapendekezo ya namna ya kushughulikia. Tunahitajiconstructive criticism na siyo kukosoa kwa lengo la kukosoatu. Katika hilo, kwa upande wetu Serikali tunaahidi kutoaushirikiano wa kutosha kwa Bunge hili ili kuliwezesha kutimizamajukumu yake ipasavyo. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika, tutatoa pia ushirikiano kwa mhimiliwa Mahakama na nimeshukuru sana Mheshimiwa Jaji Mkuuna Majaji wengine wa Mahakama pamoja na Jaji Mkuu waupande wa Zanzibar wote wako hapa ili nao wawezekutimiza majukumu yao ya kusimamia haki nchini. Kamamnavyofahamu Mahakama ni muhimu sana katika kuongozaSerikali, ni muhimu katika kujenga maelewano katika jamii,kudumisha amani na usalama, pia kuchochea shughuli zakiuchumi. (Makofi)

    Kwa mujibu wa Katiba yetu, mimi ni sehemu ya Bungehili. Hivyo, basi, kabla sijahitimisha hotuba yangu, napendakutumia fursa hii kuwashukuru wageni wetu wotewalioungana nasi kwenye tukio hili. Ni vigumu kuwataja wote,lakini pia nataka niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge,mimi niko pamoja nanyi na kamwe sitawaacha. (Makofi)

    Mheshimiwa Spika na Waheshimiwa Wabunge, kwaunyenyekevu mkubwa, baada ya kusema hayo, sasanatamka kwamba nimelifungua rasmi Bunge la Kumi na Mbilila Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

    Mungu libariki Bunge letu, Mungu abariki Wabungewote, Mungu ibariki Tanzania.

    Mheshimiwa Spika, ahsanteni sana. (Makofi)

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    33

    HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA, MHESHIMIWA JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI,WAKATI WA KUFUNGUA RASMI BUNGE LA 12 LA JAMHURI

    YA MUUNGANO WA TANZANIA DODOMA,13 NOVEMBA, 2020 - KAMAILIVYOWASILISHWA MEZANI

    _____________

    Mheshimiwa Spika;Mara ya mwisho nilipoingia kwenye Ukumbi huu KulifungaBunge la 11, tulibahatika kuwa na Marais wetu Wastaafuwatatu. Lakini leo, wapo wawili. Mmoja, MheshimiwaBenjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu,ametangulia mbele za haki. Hivyo basi, kabla ya kuanzahotuba yangu, nawasihi sote tusimame tumkumbuke pamojana wabunge wote waliofariki dunia tangu kufungwa kwaBunge la 11. Mwenyezi Mungu aiweke roho ya MarehemuMzee Mkapa pamoja na marehemu wetu wote mahali pemapeponi. Amina.

    Mheshimiwa Spika;Baada ya utangulizi huo, napende niseme kwamba, Katibaya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 91 Ibarandogo ya kwanza imempa dhamana Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania kulifungua rasmi Bunge la Jamhuriya Muungano wa Tanzania. Ni kwa sababu hiyo, nimekujahapa leo kulihutubia Bunge hili kwa lengo la kutimiza mashartihayo ya Kikatiba.

    Napenda nianze kwa kumshukuru sana Mwenyezi Mungualiyetujalia neema ya uhai na kutuwezesha kuiona siku yaleo. Aidha, nakupongeza wewe, Mheshimiwa Job Ndugai,Mbunge wa Jimbo la Kongwa kwa kuchaguliwa, kwa maranyingine, kuliongoza Bunge hili ukiwa Spika. Hongera sana.Nampongeza pia Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson kwakuchaguliwa kwa mara nyingine kuwa Naibu Spika; tenamara hii akiwa Mbunge wa kuchaguliwa kutoka Jimbo laMbeya Mjini. Hongera sana Mheshimiwa Dkt. Tulia. Huu niuthibitisho kwamba, nchi yetu, kupitia Serikali inayoongozwana Chama Cha Mapinduzi, inawaamini sana wanawake.

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    34

    Kama mnavyofahamu, Makamu wetu wa Rais, MheshimiwaSamia Suluhu Hassan, naye ni mwanamama. Aidha, Bungehili la 12 nalo lina Wabunge wengi wanawake. Kwa msingihuo, napenda nitumie fursa hii kuahidi kuwa, Serikalininayoingoza, itaendelea kuwaamini wanawake katikakushika nafasi mbalimbali za uongozi. Wanawake naakinamama Oyee!!!

    Napenda pia kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge wotekwa kuchaguliwa kwenu kuwa Wabunge wa Bunge hili la12. Mmechaguliwa kwa vile wananchi wana imani kuwa mnauwezo wa kuwawakilisha vizuri. Hivyo basi, nawasihimsiwaangushe wananchi waliowachagua. Watanzaniawana imani kubwa sana na Bunge hili.

    Nitumie fursa hii pia kuwashukuru Waheshimiwa Wabungekwa kuridhia na kumpitisha Mheshimiwa Kassim Majaliwakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Ahsanteni sana.

    Mheshimiwa Spika;Nimekuja kulizindua Bunge hili baada ya nchi yetu kufanikiwakumaliza Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020kwa uwazi amani na utulivu mkubwa. Kwa msingi huo,napenda nirudie kuipongeza Tume yetu ya Taifa ya Uchaguzikwa kusimamia vizuri zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu;kuanzia kwenye uandikishaji wapiga kura; uchukuaji naurejeshaji fomu za wagombea; usimamizi wa kampeni na piazoezi la kupiga kura na utoaji matokeo mapema. Kwa hakika,Tume imedhihirisha uwezo mkubwa katika kusimamiaUchaguzi bila kutegemea misaada kutoka nje. MheshimiwaMwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji MstaafuSemistocles Kaijage; Makamu Mwenyekiti wa Tume, JajiMstaafu Hamid Mahmoud Hamid; Makamishna wa Tume;Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera pamoja naWatendaji wote wa Tume; hongereni sana kwa kazi nzuri.

    Lakini, kwa namna ya pekee, nawapongeza kwa namnamlivyotumia vizuri fedha mlizotengewa. Kamainavyofahamika, Uchaguzi wa Mwaka huu uligharamiwa na

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    35

    Serikali kwa asilimia 100, ambapo kiasi cha shilingi bilioni 331kilitengwa. Hata hivyo, mpaka Uchaguzi umekamilika, Tumeimetumia shilingi bilioni 262 tu. Hii ni ishara ya uadilifu mkubwawalionao Viongozi na Watendaji wa Tume ya Taifa yaUchaguzi. Hongereni sana. Natoa rai kwa Taasisi nyinginekuiga mfano mzuri wa Tume hii.

    Kwa moyo wa dhati kabisa, narudia kuwashukuru Viongoziwetu wa Dini kwa kutuongoza vyema kwa sala na dua katikakipindi chote cha Uchaguzi; na hatimaye tumeweza kumalizaUchaguzi wetu salama. Nawasihi waendelee kuliombea Taifaletu ili libaki katika mikono ya Mwenyezi Mungu.

    Narudia pia kuvishukuru vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalamakwa kusimamia vizuri amani na utulivu wa nchi yetu namipaka yake wakati wote wa Uchaguzi. Hii ni ishara kuwavyombo vyetu vya ulinzi na usalama ni imara na vinafanyakazi kwa ueledi mkubwa. Hongera sana kwa vyombo vyetuvya ulinzi na usalama.

    Kwa namna ya pekee kabisa, natoa shukrani nyingi kwaWatanzania wenzangu wote kwa kushiriki vizuri na kuoneshautulivu mkubwa kwenye Uchaguzi uliopita; kuanzia kwenyezoezi la uandikishaji wapiga kura, wakati wa kampeni, upigajikura na kupokea matokeo. Hakuna shaka, Uchaguzi waMwaka huu, kwa mara nyingine, umeuthibitishia ulimwengukuwa sisi Watanzania ni wapenda amani, tunajitambua,hatudanganyiki na tumekomaa kidemokrasia. Ahsantenisana Watanzania wenzangu.

    Mheshimiwa Spika;Masuala yote muhimu tuliyopanga kutekeleza kwenye miakamitano ijayo, tumeyaweka kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCMya Mwaka 2020 – 2025 ambayo ina kurasa 303. Kwa bahatinzuri, Waheshimiwa Wabunge wengi wa Bunge hil iwanaifahamu vizuri Ilani hiyo kwa vile wameitumia katikakuomba kura kwa wananchi kwenye Uchaguzi Mkuuuliomalizika.

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    36

    Lakini, sambamba na masuala hayo yaliyomo kwenye Ilaniyetu ya Uchaguzi wa mwaka 2020 - 2025, tutaendelea piakutekeleza na kusimamia mambo yote niliyoeleza wakatinikizindua Bunge la 11, tarehe 20 Novemba, 2015.

    Kama mtakavyokumbuka, kwenye Hotuba hiyo ya kuzinduaBunge la 11 nilieleza mambo mengi sana, ambayo, kimsingi,yalitoa falsafa, dira na vipaumbele vya Serikali ya Awamuya Tano. Baadhi tumeyatekeleza vizuri; yapo ambayohatujayatekeleza kwa ukamilifu na mengine yapo kwenyehatua mbalimbali za utekelezaji. Kwa hiyo, kwenye miakamitano ijayo, tutaendelea kusimamia na kutekeleza mamboyote niliyoyaeleza kwenye Hotuba ya Kuzindua Bunge la 11.Hii ndiyo sababu nimeamua kuigawa tena Hotuba yangu yaUzinduzi wa Bunge la 11 kwenu Waheshimiwa Wabunge ilimkaisome na hatimaye ikawaongoze katika kutekelezamajukumu yenu vizuri.

    Hata hivyo, pamoja na hayo yote, naomba MheshimiwaSpika uniruhusu nitaje baadhi ya mambo muhimututakayoyapa kipaumbele kikubwa katika kipindi cha miakamitano ijayo.

    Mheshimiwa Spika;Jambo la kwanza na muhimu tutakalolipa kipaumbelekikubwa kwenye miaka mitano ijayo ni kuendelea kulindana kudumisha tunu za Taifa letu, yaani Amani, Umoja naMshikamano, Uhuru wa Nchi yetu, Muungano na MapinduziMatukufu ya Zanzibar. Na katika hilo, naahidi kushirikiana kwakaribu sana na Rais mpya wa Zanzibar, Mheshimiwa Dkt.Hussein Mwinyi. Kamwe, hatutakuwa na mzaha na yeyotemwenye kutaka kuhatarisha amani ya nchi yetu; mwenyenia ya kuvuruga umoja na mshikamano wetu; na pia mwenyekutaka kutishia Uhuru wetu, Muungano pamoja na MapinduziMatukufu ya Zanzibar.

    Napenda pia kutumia fursa hii kumwahidi Mheshimiwa RaisDkt. Hussein Mwinyi kwamba, kwenye miaka mitano ijayo,Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itatoaushirikiano mkubwa na kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    37

    Zanzibar. Kwa kifupi, naweza kusema, tutafanya kazi kwapamoja kwa lengo la kuleta maendeleo kwa pande zetuzote mbili za Muungano. Na katika hilo, nampongeza sanaMheshimiwa Rais Dkt. Hussein Mwinyi kwa hotuba nzurialiyoitoa wakati wa kuzindua Baraza la Wawakilishi. Kwenyehotuba yake alitoa dira, mwelekeo na kutaja vipaumbelevya Serikali ya Awamu ya Nane ya Zanzibar. Hongera sanakwa Mheshimiwa Rais Dkt. Mwinyi kwa hotuba nzuri. KupitiaBunge hili, napenda nimwahidi Mheshimiwa Rais Dkt. HusseinMwinyi kuwa, nitampa ushirikiano wa kutosha katikakutekeleza yote aliyoahidi wakati wa Uzinduzi Rasmi waBaraza la Wawakilishi.

    Mheshimiwa Spika;Sambamba na kulinda na kudumisha tunu za nchi yetu,kwenye miaka mitano ijayo, tutaendelea kuimarisha utawalabora, hususan kwa kusimamia nidhamu kwenye utumishi waumma pamoja na kuzidisha mapambana dhidi ya rushwa,wizi, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma. Kwenye miakamitano iliyopita, tuliwachukulia hatua za kinidhamu watumishi32,555 na kuiwezesha nchi yetu kushika nafasi ya kwanza katiya nchi 35 za Afrika kwa kupambana na rushwa, kwa mujibuwa Transparency International; na pia kushika nafasi ya 28kati ya nchi 136 duniani kwa matumizi mazuri ya fedha zaumma kwa mujibu wa Utafiti Jukwaa la Dunia (WorldEconomic Forum) wa mwaka 2019.

    Hata hivyo, watumishi wazembe bado wapo; wala rushwabado wapo; na pia wezi na wabadhirifu wa mali ya ummabado wapo. Kwa hiyo, kwenye miaka mitano ijayo,tutaendelea kushughulikia matatizo hayo. Na kwa kifupi,niseme, utumbuaji majipu utaendelea. Hata hivyo, kwaupande mwingine, tutaendelea kuboresha mazingira ya kazipamoja na maslahi ya watumishi wetu wote ili yaendane nahali halisi ya maisha ya Watanzania. Kwa hiyo, watumishiwasiwe na wasiwasi. Waendelee kuchapa kazi.

    Mheshimiwa Spika;Kwenye miaka mitano ijayo pia, tumejipanga kuendelezajitihada za kukuza uchumi. Kama unavyofahamu, katika

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    38

    kipindi cha miaka mitano iliyopita, tulijitahidi kusimamia vizuriuchumi wetu, ambapo ulikua kwa wastani wa asilimia 7 kwamwaka. Aidha, Pato ghafi la Taifa limeongezeka kutokashilingi trilioni 94.349 mwaka 2015 hadi kufikia shilingi trilioni139.9 mwaka 2019; tulidhibiti mfumuko wa bei, kutoka asilimia6.1 mwaka 2015 hadi kufikia wastani wa asilimia 4.4 nakuongeza akiba ya fedha ya kigeni kutoka Dola za Marekanibilioni 4.4 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 5.2 mwezi Julai,2020 ambazo zinatuwezesha kununua bidhaa na hudumakwa miezi 6.

    Zaidi ya hapo, kwenye miaka mitano iliyopita, tuliongezamauzo yetu ya nje kutoka Dola za Marekani bilioni 8.9 mwaka2015 hadi Dola za Marekani bilioni 9.7 mwaka 2019; na piakuvutia uwekezaji wenye thamani ya Dola za Marekani bilioni14.6, sawa na zaidi ya shilingi trilioni 30. Aidha, tulifanikiwakupunguza umasikini wa kipato hadi kufikia asilimia 26.4 kwatakwimu za mwaka 2017/2018. Mafanikio haya, bila shaka,ndiyo yamewezesha, mwezi Julai 2020, nchi yetu kutangazwakuingia kundi la nchi za uchumi wa kati kutoka kundi la nchimasikini. Na mafanikio hayo yamepatikana miaka mitanokabla ya muda uliopangwa, yaani mwaka 2025.

    Kwa hiyo, kwenye miaka mitano ijayo tunakusudiakuendeleza mafanikio ya kiuchumi yaliyopatikana natutahakikisha ukuaji uchumi unawanufaisha wananchi,hususan kwa kuinua vipato vyao, kupunguza umasikini natatizo la ajira. Na katika hilo, tunalenga kukuza uchumi wetukwa wastani wa angalau asilimia 8 kwa mwaka na piakutengeneza ajira mpya zipatazo milioni 8. Tutaendelea piakuboresha sera zetu za uchumi jumla na sera za fedha (yaanimacroeconomic and monetary policies), na pia kuhakikishaviashiria vyote vya uchumi; ikiwemo thamani ya sarafu yetu,mfumko wa bei pamoja na viwango vya riba; vinabakikwenye hali ya utulivu.

    Tutaongeza pia jitihada za kuwawezesha wananchi wetukiuchumi kwa kuwapatia mikopo isiyo na riba ama yenyeriba nafuu, ikiwemo mikopo ya asilimia 10 inayotolewa naHalmashauri zetu; na pia kupitia Mifuko na Programu

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    39

    mbalimbali zilizoanzishwa na Serikali, ambayo kwa idadi zipo18. Baadhi ya Mifuko hiyo ni Mfuko wa Maendeleo ya Vijana(YDF); Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF); Mfuko waTaifa wa Kuendeleza Wajasiriamali (NEDF); Mfuko wa KutoaMikopo kwa Wajasiriamali Wadogo (SELF Microfinance Fund),Mfuko wa Kudhamini Mikopo ya Mauzo ya Nje; Mfuko waKilimo Kwanza. n.k. Tutaimarisha usimamizi wa Mifuko hii nakuhakikisha Watanzania wanaifahamu.

    Najua Mifuko hii mingi ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu; hivyobasi, nakuagiza Mheshimiwa Waziri Mkuu, hii ikawe kazi yakoya kwanza kuishughulikia; ikiwezekana, mwangalieuwezekano wa kuiunganisha baadhi ya mifuko ili ifanye kazikwa tija zaidi na kupunguza gharama za uendeshaji. NatakaMifuko hii ikiwasaidie wananchi wa kawaida, wakiwemomachinga, akina baba na mama lishe pamoja nawajasiriamali wengine wadogo.

    Sambamba na kutoa mikopo, tutaendelea kutekelezaProgram mbalimbali za kukuza ujuzi na maarifa, ikiwemomaarifa ya ujasiriamali, ili kuwapa ujuzi na uzoefu wananchiwetu utakaowawezesha kujiajiri ama kuajirika ndani na njeya nchi. Tutaendelea pia kutekeleza Mpango wa KunusuruKaya Masikini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili tuliouzinduamwezi Februari 2020, ambao utagharimu takriban shilingitrilioni 2.032. Tutahakikisha fedha hizo zinawafikia walengwa,ambao ni wananchi masikini.

    Muhimu zaidi ni kwamba, katika kipindi cha miaka mitanoijayo, sekta binafsi itapewa umuhimu wa pekee sana.Tunataka mtu yeyote atakayetaka kuwekeza asisumbuliwekwa kuwekewa vikwazo vya aina yoyote. Watanzania nimatajiri lakini baadhi yao wanasita kuwekeza hapa nchinikwa kuogopa kusumbuliwa na maswali yasiyo na msingi.Tunahitaji kuwa na Mabilionea wengi wa Kitanzania. NatakaWatanzania wote washiriki kikamilifu katika kujenga uchumiwa nchi yao.

    Sambamba na kuwekeza, Watanzania wahamasishwekuweka fedha kwenye Benki za hapa nchini ili kusaidia benki

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    40

    zetu kufanya biashara na kuimarisha mzunguko wa fedhana kupunguza riba kwa wakopaji. Waheshimiwa Wabungena Watanzania mnaonisikiliza, wakati wa kufanya mambobila woga ni sasa. Kwenye miaka mitano ijayo pia tutafunguamilango kwa sekta binafsi kufanya majadiliano na Serikali ilikutafuta mwafaka ya migogoro ya biashara (businessdisputes) iliyopo kwa faida ya pande zote mbili. Lengo letu nikuona Tanzania inakuwa mahali pazuri pa kufanya biasharaduniani. Kwenye miaka mitano iliyopita, tumefuta tozo 168,ambapo 114 zilihusu kilimo, mifugo na uvuvi na tozo nyingine54 za biashara. Tutaendelea na hatua hizo.

    Mheshimiwa Spika;Mbali na hatua hizo; kwa lengo la kukuza uchumi,kupambana na umasikini, na pia kukabiliana na tatizo laukosefu wa ajira, tunakusudia, kwenye miaka mitano ijayo,kuweka mkazo mkubwa katika kukuza sekta zetu kuu zauchumi na uzalishaji, hususan kilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda,madini, biashara na utalii. Sekta hizi ndizo zenye kuajiriWatanzania wengi. Kwa hiyo, ni wazi, tukifanikiwa kuzikuza,uchumi wetu utakua kwa kasi na hivyo kupunguza matatizoya umasikini na ukosefu wa ajira nchini.

    Kwa msingi huo, kwenye KILIMO, mathalan, tunakusudiakuongeza tija na kukifanya kilimo chetu kuwa cha kibiashara.Lengo ni kujihakikishia usalama wa chakula, upatikanaji wamalighafi za viwandani na pia kupata ziada ya kuuza nje. Ilikufanikisha hayo, tutahakikisha pembejeo na zana bora zakilimo, ikiwemo mbegu, mbolea, viatilifu/dawa na matrekta,vinapatikana kwa uhakika na kwa gharama nafuu.Tutaongeza pia eneo la umwagiliaji kutoka hekta 561,383 hadihekta milioni 1.2 mwaka 2025 ili kupunguza utegemezi kwenyemvua.

    Tutaimarisha mifumo ya upatikanaji wa mitaji kwa wakulimawadogo na wawekezaji kwa kushirikisha taasisi za fedha,ikiwemo Benki yetu ya Maendeleo ya Kilimo pamoja na benkinyingine. Tutashughulikia pia tatizo la upotevu wa mazao(yaani post harvest loss), ikiwemo kwa kukamilisha ujenzi wavihenge na maghala maeneo mbalimabli nchini ambayo

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    41

    yataongeza uwezo wetu wa kuhifadhi mazao kutoka tani190,000 za sasa hadi tani 501,000. Takwimu zinaonesha kuwa,kila mwaka, nchi yetu inapoteza wastani wa kati ya asilimia30 - 40 ya mavuno yake kwa sababu mbalimbali, ikiwemokukosekana kwa miundombinu ya kuhifadhi. Zaidi ya hapo,tunakusudia kuanzisha bidhaa mbalimbali za huduma yaBima ya Kilimo na pia kuingia makubaliano ya kibiashara nanchi walaji na wanunuzi wa mazao ili kupata soko la uhakika.

    Mazao ya kimkakati tunayolenga kuyapa kipaumbelekikubwa ni pamba, korosho, chai, kahawa, tumbaku,mkonge, michikichi, cocoa, alizeti na miwa; lakini pia mazaoya chakula. Nchi yetu kila mwaka inaagiza tani 800,000 zangano na kwa ujumla, tunatumia wastani wa shilingi trilioni1.3 kuagiza chakula kutoka nje. Hii ni aibu kwa nchi kamaTanzania. Hivyo basi, ni lazima tutafute majawabu ya sualahili. Na hii ndiyo ikawe kazi ya kwanza ya Waziri wa Kilimonitakayemteua.

    Lakini, zaidi ya hapo, tutaweka mkazo mkubwa kwenye kilimocha mazao ya bustani (matunda, mbogamboga, maua naviungo), ambacho kinakua kwa kasi kubwa nchini. Hivi sasanchi yetu inashika nafasi ya 20 kwa kuzalisha kwa wingi mazaohayo duniani na mauzo yetu ya nje yameongezeka kutokaDola za Marekani milioni 412 mwaka 2015 hadi kufikia Dolaza Marekani milioni 779 mwaka 2018/2019. Hii ndiyo sababu,hatuna budi kukiendeleza kilimo cha mazao hayo. Na katikahilo, napenda kuriafu Bunge hili Tukufu kuwa, kwenye miakamitano ijayo, tunakusudia kununua ndege moja ya mizigo ilikurahisisha uzafirishaji wa mazao ya bustani, lakini pia minofuya samaki pamoja na nyama. Wakulima wetu ni lazimawatajirike na shughuli wanazozifanya; hivyo basi, Mawaziriwa Kilimo, Biashara, Mambo ya Nje na Mabalozi wajipangevizuri katika hili.

    Kwa upande wa MIFUGO, kama mnavyofahamu, nchi yetuinashika nafasi ya pili kwa wingi wa mifugo Barani Afrika. Tunang’ombe milioni 33.4; mbuzi milioni 21.3; kondoo milioni 5.65;punda 657,389; lakini pia tuna idadi kubwa ya kuku, bata,

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    42

    kanga, n.k. Hata hivyo, ukweli ni kwamba, sekta hii badohaijatunufaisha vya kutosha.

    Kwa kuzingatia hilo, kwenye miaka mitano ijayo, tunakusudiakuikuza sekta ya mifugo ili ichangie ukuaji uchumi nakupunguza matatizo ya umasikini na ukosefu wa ajira nchini.Tutaongeza maeneo ya ufugaji kutoka hekta 2,788,901 zasasa hadi hekta 6,000,000. Tunataka wafugaji wasiteswe namifugo yao. Mifugo ni utajir i. Sambamba na hayo,tutahamasisha ufugaji wa kisasa; tutaongeza vituo vyakuzalisha mbegu bora na pia kuongeza uzalishaji wa chakulacha mifugo viwandani kutoka tani 900,000 hadi tani milioni 8.

    Zaidi ya hapo, tutakamilisha ujenzi wa machinjio sabaunaoendelea maeneo mbalimbali nchini, ambapo, kwapamoja, zitakuwa na uwezo wa kuchinja ng’ombe 6700 nambuzi 11,000 kwa siku. Ujenzi wa machinjio hizo sio tu utasaidiakupatikana kwa nyama bora itakayouzwa hadi kwenyemasoko ya kimataifa bali pia utawezesha upatikanaji wangozi bora kwa ajili ya kutengeneza bidhaa za ngozi. Takwimuzinaonesha kuwa, takriban asilimia 90 ya ngozi inayozalishwanchini kwa sasa haina ubora unaohitajika; na sababumojawapo ni uchinjaji wanyama kienyeji. Kwa hiyo, machinjioyanayojengwa yatapunguza tatizo hilo.

    Nitumie fursa hii, kuikaribisha sekta binafsi kuwekeza kwenyeviwanda vya kutengeneza bidhaa za mifugo (nyama, ngozi,maziwa, kwato, n.k.). Na katika hilo, tunaahidi kutoa vivutiomaalum kwa watakaowekeza kwenye viwanda hivyoambavyo vitasaidia kuinua vipato vya wafugaji wetu na piakuongeza fursa za ajira kwa Watanzania. Na hapa, natakaniweke bayana kuwa, watendaji watakaokwamisha ujenziwa viwanda hivyo tutawashughulikia.

    Mheshimiwa Spika;Nchi yetu pia imebarikiwa kuwa na maeneo mengiyanayofaa kwa shughuli za uvuvi, ikiwemo Ukanda wa Pwani,Maziwa, mito na mabwawa. Hali hii inafanya sekta hii kuwana nafasi ya kutoa mchango mkubwa kwenye kukuza Patola Taifa na pia kupambana na umasikini na tatizo la ajira.

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    43

    Hata hivyo, kwa sasa, mchango wake bado ni mdogo. Hivyobasi, kwenye miaka mitano ijayo tunakusudia kuikuza sektahii, ikiwemo kuimarisha shughuli za uvuvi kwenye Bahari Kuu,ambako tumekuwa tukipoteza mapato mengi.

    Kwa mujibu wa Ripoti ya Kamati ya Bunge kuhusu Shughuliza Uvuvi wa Bahari Kuu ya Mwaka 2018; shughuli za uvuvikwenye Bahari Kuu zinaweza kuingizia Serikali mapato yamoja kwa moja ya takriban shilingi bilioni 352.1 kwa mwakaendapo mifumo ya usimamizi na udhibiti ingekuwa imara nasamaki wangechakatwa hapa nchini. Hata hivyo, mapatoyaliyokuwa yamekusanywa kwa kipindi cha miaka tisa (2009hadi 2017) yalikuwa shilingi bilioni 29.79, sawa na shilingi bilioni3.3 kwa mwaka. Kiwango hiki cha mapato hakikubaliki.

    Hii ndiyo sababu, tunataka, kwenye miaka mitano ijayo,kuisimamia vizuri shughuli za uvuvi wa Bahari Kuu ili Taifa letulinufaike na rasilimali zake, kwa kuhusisha sekta binafsi. Kwabahati nzuri, tayari, mwaka huu (2020) tumetunga SheriaMpya ya Kusimamia na Kuendeleza ya Uvuvi wa Bahari Kuu.Aidha, tumepanga kununua Meli 8 za Uvuvi kwa kushirikianana Shirika IFAD (4 upande wa Zanzibar na 4 upande waTanzania Bara) ili zishiriki katika uvuvi wa Bahari Kuu. Kamamnavyofahamu, suala la uvuvi wa bahari kuu ni la Muungano.Tunakusudia pia kujenga Bandari kubwa ya Uvuvi itakayotoaajira zipatazo 30,000; na tutaendelea kuihamasisha sektabinafsi kujenga viwanda vya kuchakata samaki.

    Sambamba na kusimamia Bahari Kuu, tutakuza shughuli zauvuvi kwenye Maziwa yetu Makuu (Victoria, Tanganyika naNyasa) pamoja na Mito yetu mikubwa. Tutahamasisha wavuviwetu wadogo kujiunga kwenye vikundi ili tuweze kuwapatiamitaji, ujuzi, vifaa na zana za uvuvi; na halikadhalika tutapitiaupya tozo na maeneo mbalimbali ili kuwapunguzia wavuvikero na kuvutia uwekezaji. Tutahamasisha pia watu binafsikujenga mabwawa na kufuga kisasa kwa kutumia vizimba.Sekta ya uvuvi ni lazima itoe mchango mkubwa kwenyeuchumi wa nchi yetu. Wateule wote wa sekta hii ni lazimawalisimamie hili.

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    44

    Mheshimiwa Spika;Ni ndoto kufikiria kwamba utaweza kukuza uchumi aukupambana na umasikini pamoja na tatizo la ukosefu waajira bila kuelekeza nguvu katika kukuza sekta ya viwanda.Duniani kote, sekta ya viwanda ndiyo mhimili mkuu wa kukuzauchumi, kupambana na umasikini pamoja na matatizo yaajira. Kwenye miaka mitano iliyopita, tulifanikiwa kujengaviwanda vipya takriban 8,477 ambavyo vilitengeneza ajirazipatazo 480,000, ambapo Mkoa wa Pwani uliongoza kwakujenga viwanda vingi. Naupongeza sana uongozi wa Mkoawa Pwani.

    Hivyo basi, kwenye miaka mitano ijayo, tutaendeleza jitihadaza kukuza sekta hiyo. Mkazo mkubwa tutauweka kwenyeviwanda vyenye kutumia malighafi zinazopatikana kwa wingihapa nchini (mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi); vyenye kuajiriwatu wengi; na ambavyo bidhaa zake zinatumika kwa wingihapa nchini (nguo, bidhaa za ngozi, mafuta ya kula, sukari,saruji, n.k.).

    Ili kuvutia uwekezaji kwenye sekta ya viwanda, tutaendeleakuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, ikiwemokuangalia masuala ya kodi na kuondoa vikwazo na urasimu.Pamekuwepo na urasimu mwingi na kusumbuliwa kwawawekezaji kwa kuzungushwa zungushwa na hivyokuwafanya wakate tamaa. Mimi nataka mwekezaji mwenyefedha akija apate kibali ndani ya siku 14. Kwa sababu hiyo,nimeamua suala la uwekezaji ikiwa ni pamoja na Kituo chaUwekezaji Tanzania (TIC) kulihamisha kutoka Ofisi ya WaziriMkuu kwenda Ofisi ya Rais i l i hao wanaokwamishanikapambane nao mimi mwenyewe. Lakini, zaidi ya hapo,tumepanga kujenga Ukanda na Kongani (clusters) zaviwanda kila mkoa kulingana na mazao na maliasilizinazopatikana.

    Mheshimiwa Spika;Kwenye miaka mitano il iyopita tumepata mafanikiomakubwa kwenye sekta ya madini. Mapato yameongezekakutoka shilingi bilioni 168 mwaka 2014/2015 hadi shilingi bilioni527 mwaka 2019/2020. Mchango wa sekta ya madini kwenye

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    45

    Pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 3.4 mwaka 2015hadi kufikia asilimia 5.2 mwaka 2019. Zaidi ya hapo, kwa maraya kwanza, katika historia ya nchi yetu, mwaka 2019, sektaya madini iliongoza kwa kutuingizia fedha nyingi za kigeni,Dola za Marekani bilioni 2.7. Nitumie fursa hii kulipongezaBunge la 11 kwa kutoa mchango mkubwa katika kupatikanakwa mafanikio haya.

    Nina imani kuwa Bunge hili la 12 litafuata nyayo za Bunge la11. Na katika hili, napenda niliarifu Bunge hili Tukufu kuwa,kwenye miaka mitano ijayo, tutaendelea kuimarisha ulinzi nausimamizi wa madini yetu, (kama tulivyofanya kwa kujengaUkuta Mirerani) kwa kuimarisha Sheria zetu ili madini yetuyasitoroshwe na Serikali kukoseshwa mapato. Aidha,tunakusudia kuendelea kufanya majadiliano na wawekezajiwakubwa kwa kuzingatia mfano wa Makubalianoyaliyofikiwa kati ya Serikali na Kampuni ya Barrickyaliyowezesha kuundwa kwa Kampuni ya Twiga MineralsCorporation.

    Nchi yetu imebarikiwa kuwa na madini mbalimbali, ikiwemodhahabu, almasi, Tanzanite, chuma, bati, nickel, copper, n.k.Aidha, tuna gesi aina mbalimbali, kama vile ethane, helium,ambayo hivi karibuni zimepatikana futi za ujazo bilioni 138kwenye Ziwa Rukwa, ambazo zinaweza kuhudumia duniakwa miaka 20. Hii ndiyo sababu, kila siku nimekuwa nikisema,sisi sio masikini; sisi ni matajiri. Nchi yetu ni tajiri sana.

    Lakini, kuhusu madini pia, kwenye miaka mitano ijayo piatutaendelea kuliimarisha Shirika letu la Taifa la Madini(STAMICO) ili lishiriki kikamilifu kwenye shughuli za madini;kuwawezesha wachimbaji wetu wadogo, ikiwa ni pamojana kuwatengea maeneo ya uchimbaji, kuwapatia mafunzo,mikopo pamoja na vifaa. Na katika natambua kuwa, wapobaadhi ya watu wamepewa leseni za utafiti na uchimbajilakini hawajazifanyia kazi; tutazifuta leseni zao, na maeneohayo kuyagawa kwa wachimbaji wengine, hususanwachimbaji wadogo. Wachimbaji wadogo ni muhimu sanakatika kukuza sekta ya madini.

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    46

    Tutaendelea pia kuimarisha masoko ya madini pamoja nakuhamasisha ujenzi wa viwanda vya uchenjuaji, uyeyushaji,usafishaji na utengenezaji wa bidhaa za madini. Tunatakamadini yachimbwe hapa Tanzania, yachenjuliwe,yayeyushwe na kisha bidhaa za bidhaa za madinizitengenezwe hapa hapa Tanzania; na ndipo ziuzwe nje amawatu kutoka nje waje kununua bidhaa za madini hapa nchini.Ni imani yetu kuwa, kutokana na hatua tulizopangakuzichukua sekta ya madini itaweza kuchangia angalauasilimia 10 ya Pato la Taifa ifikapo mwaka 2025.

    Mheshimiwa Spika;Utalii ni sekta nyingine ambayo tutaipa mkazo mkubwakwenye miaka mitano ijayo. Sekta hii imeajiri takriban watumilioni 4. Kwenye miaka mitano iliyopita, ilikua kwa kiwangocha kuridhisha, ambapo idadi ya watalii waliotembeleanchini iliongezeka kutoka watalii 1,137,182 mwaka 2015 hadiwatalii 1,510,151 mwaka 2019. Mapato nayo yaliongezekakutoka Dola za Marekani bilioni 1.9 mwaka 2015 hadi kufikiaDola za Marekani bilioni 2.6 mwaka 2019. Nitumie fursa hiikuipongeza Hifadhi yetu ya Taifa ya Serengeti kwakuchaguliwa kuwa Hifadhi Bora Barani Afrika kwa mwaka2020.

    Kwenye miaka mitano ijayo, tumejipanga kuongeza idadi yawatalii hadi kufikia milioni 5 mwaka 2025 na mapato kutokaDola za Marekani bilioni 2.6 za sasa hadi Dola za Marekanibilioni 6. Hatua tutakazochukua ni pamoja na kupanua wigowa vivutio vya utalii, ikiwemo kukuza utalii wa mikutano nauwindaji wanyamapori; kuimarisha utalii wa fukwe; kujengamiundombinu ya kuwezesha meli za utalii kuzuru nchini nakuongeza kasi ya utangazaji wa vivutio vyetu.

    Vilevile, tutazihamaisha taasisi na watu binafsi kuanzisharanchi, mashamba na bustani za wanyama, kamainavyofanyika nchi nyingine; ili kuzuia ujangili na kukuza utalii;lakini pia kuongeza vipato na fursa za ajira kwa Watanzania.Na katika hilo, napenda kuwaarifu Watanzania, kupitia Bungehili Tukufu kuwa, tumepunguza bei kwa ajili ya kupatawanyama wa mbegu. Mathalan, bei ya nyati wa mbegu

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    47

    imepungua kutoka Dola za Marekani 1,900 hadi kufikia shilingilaki mbili; Pofu kutoka Dola za Marekani 1,700 hadi shilingi310,000 na Swala kutoka Dola za Marekani 150 hadi shilingi90,000. Hivyo basi, nawasihi Watanzania wenzangu, popotewalipo, kuchangamkia fursa hiyo; ambayo itachochea piauanzishaji wa butcher za wanyama pori.

    Zaidi ya hapo, tutaendelea kupitia upya kodi na tozombalimbali ili kuzifuta ama kupunguza kodi zenye kero.Kwenye miaka mitano iliyopita, tulipunguza ada ya leseni yabiashara ya utalii kwa wakala wa kusafirisha watalii yenyeidadi ya magari chini ya manne kutoka Dola za Kimarekani2,000 hadi Dola za Marekani 500 na matokeo yake idadi yakampuni za Kitanzania zimeongezeka kutoka 643 mwaka 2015hadi 1,687 mwaka 2020.

    Mheshimiwa Spika;Tuna imani, hatua hizi nilizoeleza zitatuwezesha kufikiamalengo tuliyojiwekea ya kukuza uchumi kwa angalauasilimia 8 kwa mwaka, kuinua vipato vya Watanzania,kupunguza umasikini na kutengeneza ajira mpya milioni 8.Hata hivyo, najua, ili kufikia malengo haya, tunategemeasana kupata ushirikiano kutoka sekta binafsi. Kamamnavyofahamu, sekta binafsi ndiyo injini ya kujenga uchumiwa kisasa.

    Hivyo basi, narudia kuikaribisha sekta binafsi ya hapa nchinina kutoka nje kuwekeza katika sekta nilizozitaja; na ambazosikuzitaja. Na napenda niwahakikishie watu wa sekta binafsikuwa, Tanzania ni mahali pazuri na sahihi pa kuwekeza. Nchiyetu ina amani na utulivu; tumebarikiwa kuwa na fursa nyingiza uwekezaji; nchi yetu ipo kwenye eneo la kimkatati; sisi piani Wanachama wa jumuiya mbili, EAC na SADC, ambazo zinasoko la watu takriban milioni 500.

    Kwa hiyo narudia, kuikaribisha sekta binafsi kuwekeza hapanchini. Na kwa bahati nzuri, tangu mwaka jana, tumeanzakutetekeleza Mpango wetu wa Kuboresha Mazingira yaBiashara nchini (yaani Blueprint for Regulatory Reforms toImprove the Business Environment in Tanzania). Hivyo basi,

  • NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

    48

    mazingira ya biashara na uwekezaji, kwenye miaka mitanoijayo, yanatarajiwa kuwa bora zaidi.

    Mheshimiwa Spika;Ili kukuza uchumi pamoja na sekta za uzalishaji ni lazimatuimarishe miundombinu, hususan ya usafiri na nishati yaumeme. Kamwe, huwezi kukuza sekta za kilimo, ufugaji, uvuvi,viwanda, uchimbaji madini na utali i bila kuimarishamiundombinu na huduma za usafiri pamoja na upatikanajiwa huduma za umeme. Kwa hiyo, kama ilivyokuwa kwenyemiak