mwongozo wa lugha rahisi wa ripoti ya mwaka ya utekelezaji ... · ipoti ya mwaka ya utekelezaji wa...
TRANSCRIPT
Mwongozo wa Lugha Rahisi wa
Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa
MKUKUTA 2006/07
Mwongozo huu Umeandaliwa na Hakikazi Catalyst kwa niaba ya Wizara ya Fedha na Uchumi.
Desemba 2007
ii
Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA (MAIR) ni moja ya matokeo ya Mfumo wa
Ufuatiliaji wa MKUKUTA. Hivyo ripoti hii ni sehemu ya muundo wa jumla wa utoaji wa
taarifa za wadau mbalimbali wanaojihusisha na utekelezaji wa MKUKUTA. Wadau hao ni
pamoja na Wizara, Idara, na Wakala wa Serikali, Mamlaka za Serikali za Mitaa,na Asasi Zisizo za
Kiserikali.
Ripoti hii inatokana na uchambuzi wa utekelezaji wa kila lengo la MKUKUTA na inatoa picha
ya mafanikio yaliyofikiwa, changamoto, mambo ya kujifunza, na hatua zinazopaswa kuchukuliwa
kwa kila nguzo ya MKUKUTA. Pia ripoti hii inajumuisha hatua iliyopigwa katika michakato na
maboresho mengine, na kuonyesha jinsi yanavyochangia katika kufikiwa kwa matokeo ya MKUKUTA
yanayotarajiwa.
Lengo la ripoti hii ni kuwafahamisha wadau kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa MKUKUTA sanjari
na michakato inayohusiana, ikiwa na lengo la kuchochea mijadala juu ya masuala muhimu, na kusaidia
kuboresha michakato ya mipango, bajeti na utekelezaji.
Msingi wa wazo la kuandaa chapisho hili la lugha rahisi ni lengo la jumla la MAIR 2006/07 liliotajwa
hapo juu. Ili kuwezesha ushiriki wa wadau wengi zaidi wa kada mbali mbali, ilionekana ni lazima
kuandaa chapisho hili kwa lengo la kujenga ufahamu wa pamoja juu ya maendeleo ya utekelezaji wa
MKUKUTA.
Dibaji
iii
Dibaji ............................................................................................................................................. ii Yaliyomo ...................................................................................................................................... iii Ujue MKUKUTA .......................................................................................................................iv Vifupisho .......................................................................................................................................v Utangulizi ......................................................................................................................................vi 1. Ijue MAIR ........................................................................................................................... 1 Masuala Makuu ya MAIR, Madhumuni, Malengo na Matumizi .......................................... 1 Uoanishaji na Kuhusianisha Michakato ya Kitaifa ................................................................... 2 Ripoti Ilivyoandaliwa .................................................................................................................... 2 Mapana ya MAIR ......................................................................................................................... 3 Mapana na Mapungufu ya Mwongozo huu wa Lugha Rahisi ................................................. 3 2. Changamoto za Nguzo na Hatua za Kuchukua ................................................................... 5 Nguzo ya Kwanza – Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini wa Kipato ........................ 5 Nguzo ya Pili –Uboreshaji wa Maisha na Ustawi wa Jamii .................................................... 9 Nguzo ya Tatu – Utawala Bora na Uwajibikaji ....................................................................... 13 3. Mfumo wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA .............................................................................. 18 Chimbuko la Mfumo wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA ........................................................... 18 Sekretarieti ya MKUKUTA ..................................................................................................... 19 Makundi Matatu ya Kiufundi .................................................................................................. 21 Uoanishaji wa Shughuli ............................................................................................................. 22 Shughuli Zinazoendelea ............................................................................................................ 23 Changamoto na Mambo Tuliyojifunza .................................................................................... 24 Hatua za Kuchukua.................................................................................................................... 25 4. Ugharamiaji ....................................................................................................................... 26 Utafutaji na Upangiliaji wa Fedha ............................................................................................ 26 MKUKUTA na Bajeti ya Taifa ................................................................................................. 28 Kuboresha Michakato ya Bajeti na Ugharamiaji ..................................................................... 29 Njia za Kuripoti Bajeti ............................................................................................................... 30 Mapana ya Ripoti ya Bajeti ........................................................................................................ 31 Sera Nyingine Zinazohusiana na Bajeti .................................................................................. 31 5. Muhtasari wa Masuala Makuu na Hatua za Kuchukua ...................................................... 33 6. Viambatisho ...................................................................................................................... 36 Kiambatisho 1: Muundo wa Utekelezaji wa MKUKUTA.................................................... 36 Kiambatisho 2: Mchakato wa Mapitio ya Kisekta .................................................................. 37 Kiambatisho 3: Viunganishi muhimu vya intaneti ................................................................. 38 7. Maana za Maneno Makuu Yaliyotumika (Faharasa) .......................................................... 39 8. Shukrani ........................................................................................................................... 41
Yaliyomo
iv
� Ni Mkakati wa Kitaifa wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini kwa kipindi cha kuanzia
2005/2006 hadi 2009/2010
� Ni uzao wa pili wa Waraka wa Mkakati wa Upunguzaji Umaskini. Uliandaliwa kufuatia mapitio ya
Mkakati wa kwanza wa Upunguzaji Umaskini wa mwaka 2000 yaliyohusisha mashauriano ya wadau
mbali mbali nchini.
� Uliandaliwa na unatekelezwa kwa njia ya mashaurino endelevu yanayohusisha ushiriki mpana wa
wadau wengi.
� Umekusudiwa kuwa muundo wenye kuoanisha mipango, bajeti, utekelezaji, ufuatiliaji na taarifa za
wadau wengi.
� Hupitiwa na Mfumo wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA ambao huongozwa na Mpango Mkuu wa
Ufuatiliaji wa MKUKUTA.
� Huongozwa na Kamati ya Ufundi. Husimamiwa na Sekretarieti. Huendeshwa na makundi matatu
ya Kitaalamu ‘Utafiti na Uchambuzi’, ‘Tafiti na Takwimu za kila siku’ na ‘Mawasiliano’
� Unagharamiwa na Serikali, fedha za ndani na msaada wa Wabia wa Maendeleo sanjari na wadau
wengine wa MKUKUTA.
� Umejikita katika nguzo tatu zenye kulenga matokeo badala ya kuzingatia sekta (Tazama jedwali
lifuatalo kwa maelezo zaidi)
Nguzo ya kwanza: Kukuza Uchumi
na Kupunguza Umaskini wa Kipato
Nguzo ya pili: Uboreshaji wa Maisha
na Ustawi wa Jamii
Nguzo ya tatu: Utawala Bora na
Uwajibikaji
Matokeo ya Jumla Matokeo ya Jumla Matokeo ya Jumla
Ukuaji wa uchumi wenye msingi mpa-na na unaozingatia usawa unafikiwa na kuendelezwa
Kuboreka kwa maisha na ustawi wa jamii msisitizo wa kipekee ukiwa kwa watu maskini zaidi pamoja na wale walio katika mazingira hatarishi.
Kupungua kwa tofauti ya kimatokeo (mfano; elimu, na afya) kwa kuzingatia maeneo ya kijiografia, kipato, umri, jinsia, na makundi mengine
Utawala bora na Utawala wa Sheria
Uwajibikaji wa Viongozi na watumishi wa umma,
Demokrasia na uvumilivu wa kisiasa na kijamii,
Amani, Utulivu wa kisiasa, umoja wa kitaifa na mshikamano wa kijamii.
Malengo Malengo Malengo
Kuhakikisha kunakuwapo usimamizi mzuri wa uchumi
Kuchochea ukuaji wenye msingi mpana na endelevu
Kuongeza upatikanaji wa chakula
Kupunguza umaskini wa kipato kwa wanaume na wanawake vijijini
Kuhakikisha upatikanaji sawa wa elimu bora ya msingi na sekondari kwa wavulana na wasichana, elimu ya kufuta ujinga miongoni mwa wanaume na wanawake, na upanuzi wa elimu ya juu, ufundi na ufundi stadi
Kuboresha maisha, afya na ustawi wa watoto wote na wanawake hususan makundi yaliyo katika maazingira hatarishi
Kuhakikisha kuwa miundo na mifumo ya utawala pamoja na utawala wa sheria ni vya kidemokrasia, shirikishi, uwakilishi, uwajibikaji na ujumuishaji.
Kuhakikisha ugawaji sawa wa rasili-mali za umma – pamoja na kushughu-likia rushwa ipasavyo.
Ujue MKUKUTA
v
Malengo Malengo Malengo
Kupunguza umaskini wa kipato kwa wanaume na wanawake mjiniKutoa nishati ya kuaminika na rahisi kwa watumiaji.
Kuongeza upatikanaji wa maji safi, salama nay a gharama nafuu, usafi, malazi mazuri, na mazingira salama na endelevu; na hivyo kupunguza uathirikaji utokanao na hatari za mazingira.
Kuhakikisha kunakuwapo hifadhi ya uhakika ya kijamii na utoaji wa mahitaji na huduma za msingi kwa wahitaji na walio katika maazingira hatarishi.Kuhakikisha kunakuwepo mfumo wenye ufanisi unaotoa fursa sawa kwa watu wote kupata na kumudu huduma bora za umma.
Kuweka mfumo wa huduma za umma unaofaa kama msingi wa kuboresha utoaji wa huduma na kupunguza umaskini.
Kuhakikisha kwamba haki za maskini na vikundi vilivyo katika mzingira hatarishi zinalindwa na kukuzwa katika mfumo wa haki.
Kupunguza kutengwa na kutovumiliana kisiasa na kijamii.
Kuboresha usalama binafsi na wa mali, kupunguza uhalifu na kuondoa unyanyasaji wa kijinsia na unyanyasaji majumbani.
Kuendeleza na kuimarisha utamaduni wa watu kama utambulisho wa kitaifa.
VifupishoAZISE Asasi Zisizo za Serikali
JAST Mkakati wa Pamoja wa Misaada ( Joint Assistance Strategy for Tanzania)
MAIR Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji MKUKUTA
(MKUKUTA Annual Implementation Report)
MKUKUTA Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini
NACSAP II Mkakati na Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kupambana na Rushwa
PHDR Ripoti ya Umaskini na Maendeleo ya Watu (Poverty and Human Development Report)
PIMA Kadi ya Jamii ya kukusanyia taarifa (Community score cards)
PlanRep Programu ya Kompyuta ya kuandalia mipango na Kutoa taarifa inayotumika
kwenye Serikali za Mitaa. (Planning and Reporting Takwimubase for
local authorities )
RIMKU Ripoti ya Utekelezaji ya MKUKUTA (Programu ya Kompyuta)
SBAS Mfumo wa Bajeti wa Upangiliaji Fedha Kimkakati
(Strategic Budget Allocation System)
UKIMWI Upungufu wa Kinga Mwilini
VVU Virusi Vya UKIMWI
vi
Kijitabu hiki kinaelezea Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA (MAIR) 2006/07
kwa lugha rahisi. Kifupisho MAIR, kinachotokana na maneno ya Kiingereza MKUKUTA
Annual Implementation Report kitatumika kumaanisha ripoti hii.
MKUKUTA uliandaliwa mwaka 2005. MKUKUTA ni Mkakati wa Kitaifa wa Kukuza Uchumi na
Kupunguza Umaskini. Ulikuwa ni matokeo ya ufuatiliaji uliohusisha marudio na mapitio makubwa ya
Waraka wa Mkakati wa Kupunguza Umaskini wa mwaka 2000. MKUKUTA ni Mkakati utakaodumu
kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2005/06 hadi 2009/10.
MKUKUTA umejengwa kwenye nguzo kuu tatu za mikakati. Nguzo ya “Kukuza Uchumi na
Kupunguza umaskini wa Kipato” inahusiana kwa karibu na nguzo ya “ Kuboresha Maisha na Ustawi wa
Jamii” ambapo zote kwa pamoja zinajengwa kwenye msingi wa “Utawala Bora na Uwajibikaji”.
Hata hivyo mafanikio ya utekelezaji wa MKUKUTA hayategemei kuwepo kwa sera nzuri zinazokubalika
na zenye malengo na shabaha zinazoeleweka pekee. Pia unahitajika mfumo bora na wenye ufanisi wa
kufuatilia na kutathmini utekelezaji. Kwa hiyo Mfumo wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA umebuniwa ili
kuubadili mfumo wa awali wa Ufuatiliaji wa Umaskini. Maelezo ya kina ya Mfumo wa Ufuatiliaji wa
MKUKUTA yamebainishwa kwenye Mpango Mkuu wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA.
MAIR ni mojawapo ya matokeo yaliyopendekezwa kwenye Mpango Mkuu wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA.
Lengo kuu ni kuleta pamoja na kuchambua aina mbali mbali za taarifa za ufuatiliaji kwa makusudi ya (a)
kutoa taarifa juu ya kazi zinazofanyika (au kutofanyika) (b) kubainisha changamoto na mambo muhimu
ya kujifunza kutokana na utekelezaji (c) kupendekeza hatua za kuchukua katika siku zijazo. Wazo la
msingi ni kuifanya MAIR iweze kuwafikia wadau wengi ili kuwahimiza na kuwahamasisha wadau hao
kufanya mijadala na midahalo. Hii itasaidia kuboresha michakato ya mipango na utungaji sera kwa siku
zijazo katika maeneo mbali mbali ya kiutawala. Hata hivyo, katika muundo wake, MAIR ni kitabu
kikubwa na kilichoandikwa kitaalam sana kiasi kwamba wasomaji wengi watashindwa kuelewa, hata
kama kingetafsiriwa kwa Kiswahili. Ni kwasababu hiyo ndiyo maana tumeandaa kijitabu hiki cha lugha
rahisi.
Utangulizi
1
Kwenye sura hii tunaeleza kwa ufupi juu ya masuala makuu ya MAIR, madhumuni na
malengo yake na jinsi MAIR ilivyoandaliwa. Kisha tunaelezea mapana ya MAIR na mapana
na mapungufu ya mwongozo huu wa lugha rahisi.
Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA (MAIR) ni moja ya matokeo ya Mfumo wa Ufuatiliaji
wa MKUKUTA. Hivyo ripoti hii ni sehemu ya muundo wa jumla wa utoaji wa taarifa za wadau
mbalimbali wanaojihusisha na utekelezaji wa MKUKUTA. Wadau hao ni pamoja na Wizara, Idara, na
Wakala wa serikali, Mamlaka za Serikali za Mitaa,na Asasi Zisizo za kiserikali.
Masuala makuu ya MAIR ni:• MAIR imejikita zaidi kwenye uchambuzi wa maendeleo ya utekelezaji wa kila lengo, kwa kuzingatia
malengo ya MKUKUTA na kutoa picha halisi ya utekelezaji, changamoto, mambo ya kujifunza na
hatua za kuchukua katika siku zijazo kwa kila nguzo ya MKUKUTA
• MAIR huzingatia kwa karibu uhusiano baina ya makundi makuu ya MKUKUTA
• Inajumuisha maendeleo ya michakato na maboresho yaliyofanywa na Wizara, Serikali za Mitaa na
AZISE na kubainisha mchango wa kila moja katika kufikia matokeo ya MKUKUTA.
• Inatambua kwamba licha ya mchango wa AZISE kutowekwa bayana mara nyingi, sekta hii ina
mchango mkubwa.
• Katika maeneo mengi uandaaji na utoaji wa taarifa hutegemea taarifa na takwimu za malengo ya
utekelezaji. Taarifa hizi zinaweza kuwa za kitakwimu zaidi ama za maelezo kutegemeana na upatikanaji
wa takwimu.
• Utekelezaji wa masuala mtambuka umejumuishwa katika uchambuzi wote wa mafanikio
yaliyopatikana.
1. Ijue MAIR
2
MAIR ina Madhumuni Makuu Mawili• Kuwafahamisha Watanzania na wadau wote kuhusu mafanikio yaliyofikiwa katika utekelezaji wa
MKUKUTA pamoja na michakato inayohusika. Hili linaweza kufanyika moja kwa moja ama kupitia
wawakilishi wa wadau au wananchi kama vile Wabunge.
• Kuchochea mijadala katika masuala ya msingi, na hivyo kusaidia kuhabarisha, kushawishi na
kuboresha mipango, bajeti na utekelezaji wake
Malengo makuu na matumizi ya MAIR• Kupima mafanikio ya vipaumbele vya Serikali kwa ajili ya ukuaji wa uchumi na upunguzaji wa
umaskini kama vilivyoainishwa kwenye MKUKUTA
• Kuwezesha upatikanaji wa taarifa zitakazosaidia kubaini vipaumbele katika sekta mbali mbali na
kubuni mikakati thabiti na endelevu.
• Kuchochea mazungumzo na midahalo zaidi miongoni mwa wadau juu ya masuala muhimu ya
kimkakati ikiwemo (a) kuweka na kupanga vipaumbele na utafutaji raslimali; na (b) namna bora ya
kutumia michakato ya mijadala siku za baadaye 1
• Kubaini masuala muhimu pamoja na fursa zilizopo kwa ajili ya kuinua uwekezaji ili kufikia malengo
ya MKUKUTA
• Kuwezesha upatikanaji wa taarifa zitakazosaidia kuboresha mchakato wa kitaifa wa uandaaji wa
bajeti.
Uoanishaji na upangiliaji wa michakato ya kitaifa Pamoja na wadau wakuu, serikali imefanyakazi ya kuoanisha na kupangilia michakato mikuu ya (a)
mipango ya sera na bajeti (b) ufuatiliaji na utoaji taarifa, na (c) kuoanisha mtiririko wa raslimali fedha
kutoka nje ya nchi na malengo na vipaumbele vya Maendeleo ya taifa. Kanuni za kuoanisha na kupangilia
masuala ya ubia kuhusiana na misaada zimeelezwa kwenye nyaraka nyingi 2 . MAIR inazingatia uoanishaji
wa ajenda na hatua iliyokwisha pigwa, changamoto na fursa zilizopo mbele ya safari.
Jinsi ripoti ilivyoandaliwaMaandalizi ya MAIR yamekuwa na changamoto kubwa kutokana na kubadilika kutoka utaratibu wa
kuzingatia sekta wa mfumo wa awali wa Ufuatiliaji wa Umaskini kwenda kwenye utaratibu unaozingatia
matokeo wa Mfumo mpya wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA (. Mabadiliko haya yameongeza mipaka ya
ripoti kwa kiasi kikubwa. Hali kadhalika wadau wanaohusika wameongezeka.
Idara ya Kuondoa Umaskini Wizara ya Fedha na Uchumi inaratibu maandalizi ya MAIR kwa kushirikiana
na wadau wengine wengi. Kamati ya Kiufundi ya MKUKUTA3 inawajibika na kusimamia uandaaji.
Kazi ya kuandaa MAIR ilihusisha kukusanya taarifa kutoka vyanzo mbali mbali (tazama kisanduku 1).
Taarifa hizi zilitoa picha ya jumla, jinsi raslimali zilivyotumika, matokeo, na maendeleo katika masuala
mtambuka.
3
Izingatiwe kuwa ni nchi chache zinazoweza
kuandaa ripoti ya kitaifa inayotoa taarifa za
jumla zinazohsu serikali nzima. Ripoti za
aina hiyo zitakuwa kubwa sana na utakuwa
ni ufujaji mkubwa wa raslimali za umma.
Badala yake ripoti nyingi huzingatia kutoa
taarifa za matokeo. Taarifa hizi zinaelezea
juu ya mabadiliko makubwa na mienendo ya
hali na huwa zinatumika kutoa mwanga na mwelekeo katika uandaaji wa mipango na sera na uwekaji wa
vipaumbele. Inafahamika kwamba hatua muhimu inayofuata nchini Tanzania ni kuimarisha uhusiano
baina ya utengaji wa raslimali, matumizi na utoaji wa taarifa za matokeo.
Mapana ya MAIRTangu ilipoanza, MAIR imekuwa na kiu kubwa ya kutaka kutoa taarifa za utekelezaji wa shughuli
zilizopangwa, matumizi pamoja na matunda yake kwenye matokeo. Hii ingehusisha utoaji wa taarifa za
kina kuhusu mambo ambayo serikali ilipanga kufanya, kiasi cha raslimali kilichopangwa na kutumika,
shughuli zilizotekelezwa na hatua zipi zilichukuliwa. Hata hivyo, MAIR 2007 haijakidhi matarajio yote
haya kutokana na sababu zifuatazo:
• Licha ya bajeti za Wizara, Idara, Wakala na Serikali za Mitaa kufungamanishwa na MKUKUTA
kwa kiasi kikubwa, njia ya sasa ya utoaji ripoti juu ya namna bajeti inavyotumika haijafungamanishwa
kikamilifu na malengo ya kimkakati na matokeo ya MKUKUTA.
• Kukosekana kwa takwimu kwa baadhi ya viashiria ambapo taarifa hazizalishwi mara kwa mara.
• Kwa baadhi ya maeneo kama vile utamaduni, mfumo wa ufuatiliaji bado haujaweka viashiria vya
matokeo. Hata hivyo, kila inapowezekana, shughuli na michakato inayohusika kwenye maeneo hayo
imeripotiwa.
Mapana na Mapungufu ya Mwongozo huu wa Lugha RahisiMAIR huwasilisha muhtasari wa taarifa zilizotolewa kwenye ripoti nyingine nyingi. Nyingi ya
hizi hutolewa kama takwimu zinazothibitisha kiwango cha kufikiwa au kutofikiwa kwa shabaha za
MKUKUTA. Takwimu hizi hutumika kuzalisha na kuhalalisha orodha ya changamoto, mambo ya
kujifunza na mapendekezo kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa.
Mwongozo huu haujaribu kuufupisha takwimu bali unachukulia kwamba takwimu hizo ni sahihi na
kwamba msomaji mwenye kutaka kujua undani wa takwimu hizo anaweza kuzipata kwenye MAIR (au
chanzo kingine ambako MAIR imechukua takwimu hizo).
Mwongozo huu umejikita kwenye orodha ya changamoto, mambo ya kujifunza na mapendekezo ya
hatua zinazopaswa kuchukuliwa. Katika sura inayofuata ya kijitabu hiki, taarifa hizi zimewasilishwa kwa
kila nguzo ya MKUKUTA na katika sura mbili zinazofuata zimewasilishwa kulingana na mfumo wa
kwanza wa ufuatiliaji na tathmini, na kisha masuala ya ugharamiaji.
Kisanduku 1: Vyanzo vya Taarifa za MAIR
• Ripoti ya Umaskini na Maendeleo ya Watu (PHDR)
• Ripoti za Mapitio ya Matumizi ya Umma (PER)
• Taarifa ya Hali ya MKUKUTA (2006)
• Tafiti za Kiuchumi
• Mapitio ya Sekta
• Ripoti za Wizara mbali mbali
4
Sura ya mwisho hujumuisha na kutoa muhtasari wa mawazo kutoka kwenye sura zilizotangulia.
Izingatiwe kwamba mwongozo huu wa lugha rahisi unatoa vidokezo vingi kwa wasomaji wenye kutaka
kufahamu masuala husika kwa kina zaidi. Vidokezo hivi ni pamoja na visanduku vya maelezo, ambavyo
vinatoa maelezo ya kina zaidi kwa baadhi ya mada zinazotajwa kwenye kijitabu hiki.
5
Katika sura hii tunafanya mapitio ya mahitimisho makuu kuhusu changamoto zilizobainishwa,
mambo ya kujifunza na mapendekezo ya hatua za kuchukua kwenye nguzo kuu tatu za
MKUKUTA. Kwa kila nguzo tunaanza kwa kuelezea sehemu za nguzo hiyo. Hii itamsaidia
msomaji kuona kiwango na ugumu wa muundo wa MKUKUTA. Kisha tunaendelea kutazama
changamoto kuu zilizojitokeza na mambo ya kujifunza yaliyoonekana. Kila sehemu inahitimishwa kwa
kueleza mapendekezo ya hatua za kuchukua. Kwa ujumla Maendeleo ya utekelezaji wa MKUKUTA
yamechanganyika. Kuna matokeo mazuri katika baadhi ya maeneo, matokeo mabaya katika maeneo
mengine wakati masuala mengine yamebaki kama yalivyokuwa. Izingatiwe kwamba kumekuwepo tofauti
kati ya mijini na vijijini na baina ya maeneo mbali mbali ya nchi. Watu mbali mbali kutoka sehemu mbali
mbali watakuwa na vipaumbele tofauti. Ziko changamoto nyingi zaidi katika hatua za kuchukua kwa
siku zijazo!
Nguzo ya kwanza – Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini
wa Kipato
Katika sehemu hii kwanza tunaelezea matokeo makuu na malengo ya nguzo halafu tunazungumzia
kwa ufupi juu ya sehemu nyingine za nguzo hii. Hii itasaidia msomaji kupata mapana na mipaka ya
nguzo hii. Kwa vile huu ni mwongozo wa lugha rahisi hatufanyi mapitio ya takwimu ‘kavukavu’ ila
tonasonga mbele na kudokeza juu ya changamnoto kuu zilizojitokeza na mapendekezo ya hatua za
kuchukuliwa.
2. Changamoto za Nguzo na Hatua za Kuchukua
6
Sehemu za Nguzo ya KwanzaNguzo ya kwanza hujumuisha shughuli zinazolenga kukuza uchumi na kupunguza umaskini wa kipato.
Matokeo ya jumla ni kuhakikisha kuwa “Ukuaji wa uchumi mpana na unaozingatia usawa unafikiwa na
kuendelezwa “
Malengo sita ya nguzo ni haya yafuatayo:
• Kuhakikisha kuwa kunakuwapo na usimamizi mzuri wa uchumi
• Kuchochea ukuaji wa uchumi wenye msingi mpana na endelevu
• Kuongeza upatikanaji wa chakula
• Kupunguza umaskini wa kipato kwa wanaume na wanawake vijijini
• Kupunguza umaskini wa kipato kwa wanaume na wanawake mjini
• Kutoa nishati ya uhakika na rahisi kwa watumiaji.
Changamoto Kuu Nane za Nguzo ya KwanzaPamoja na kuwepo Maendeleo mazuri katika kufikia na kuendeleza ukuaji wa Uchumi mpana na wenye
kuzingatia usawa katika miaka miwili iliyopita, bado zimekuwepo changamoto nyingi. Sehemu hii
inaelezea changamoto kuu nane.
Kuharakisha Ukuaji wa UchumiKasi ya ukuaji wa uchumi bado iko chini ya shabaha iliyowekwa kwenye MKUKUTA. Kasi ya sasa ya
ukuaji wa uchumi haiwezi kupunguza umaskini, hususan kwa kuzingatia kasi ya sasa ya ongezeko la
idadi ya watu ya asilimia 3 kwa mwaka. Uharakishaji wa ukuaji wa uchumi unahitajika ili kuongeza wigo
wa raslimali za ndani ya nchi na kuongeza uwezo wa serikali kutoa huduma za umma.
Mahusiano Bora Zaidi ya Uchumi Mkubwa na Ule wa Ngazi za Chini ili Ukuaji Uweze Kuwanufaisha Zaidi Watu Maskini. Changamoto kubwa ni kuona mafanikio katika Uchumi mkuu yakileta Maendeleo endelevu katika ngazi
za chini za jamii. Swali muhimu ni namna gani faida itokanayo na ukuaji inaweza kusambazwa kwa kaya
za watu maskini. Hii itahusisha kutafakari upya mifumo (kama vile sera, ya kisheria, taasisi n.k.) katika
ngazi ya kati, kwa mfano ya serikali za Mitaa (kama halmashauri za wilaya) ili ziweze kuhudumia ngazi
za chini zaidi kama vile ngazi ya jamii.
Uoanishaji Bora Zaidi wa SeraUoanishaji bado unakosekana miongoni na baina ya sekta. Mifano yaweza kuwa Ajira dhidi ya Biashara,
Kazi dhidi ya Ubinafsishaji, Elimu, Uwekezaji, Fedha, na Sera zenye kulenga kuwavutia wawekezaji zaidi
wa kigeni. Ipo haja ya kuzifanyia mapitio sera hizi na nyingine nyingi, sambamba na sheria zinazohusiana
na sera hizo ili ziweze kuoana badala ya kukinzana.
Uongezaji wa Mauzo ya Bidhaa Nje ya NchiUchumi wa Tanzania bado unategemea kiasi kidogo cha bidhaa zinazouzwa nje ya nchi; na mapato
yanayotokana na mauzo ya bidhaa nje ya nchi hayajaongezeka kwa kiwango cha kuridhisha. Hii inaweza
7
kuelezwa kuwa imetokana na kushindwa kubaini fursa zilizoko kwenye soko la kimataifa. Fursa zilizoko
katika soko la nje hazijaweza kutumika ipasavyo. Kwa hiyo serikali inafanya jitihada za kuongeza wigo
wa bidhaa za kuuza nje ya nchi zenye kukidhi viwango vya soko la kimataifa.
Kuna changamoto mahsusi katika kuboresha uuzaji nje wa huduma mbali mbali. Hii inahitaji upanuzi
wa vivutio vya kitalii sanjari na uboreshaji wa miundombinu inayohusika, kama vile viwanja vya ndege,
barabara na reli.
Kiwango kidogo cha mauzo ya bidhaa nje ya nchi na kiwango kikubwa cha bidhaa zinazoingizwa kutoka
nje ya nchi vimesababisha kukosekana kwa mizania ya kibiashara nchini.
Upatikanaji Bora wa NishatiKatika miaka miwili iliyopita Tanzania imekumbwa na uhaba na kutotabirika kwa upatikanaji wa nishati
itokanayo na nguvu ya maji. Kwa hiyo kuna umuhimu wa Kupunguza utegemezi katika nishati itokanayo
na nguvu ya maji kwa kuendeleza vyanzo mbadala vya umeme. Changamoto inayohusiana na hii ni ile ya
kufikisha nishati katika maeneo ya vijijini kwa gharama nafuu.
Kuboresha Zaidi Maendeleo ya Vijijini na Katika KilimoChangamoto ya ukuaji katika Uchumi wa maeneo ya vijijini zina uhusiano wa karibu na zile za sekta ya
kilimo. Hizi ni pamoja na:
• Uzalishaji mdogo wa ardhi na nguvu kazi
• Utegemezi katika maji ya mvua
• Kutoendelezwa kwa fursa za umwagiliaji
• Mtaji mdogo na kutopatikana kwa huduma za kifedha
• Huduma zisizotosheleza za utaalamu wa kilimo
• Miundombinu hafifu ya vijijini ambayo hukwamisha ufanisi wa uhusiiano wa Mjini na vijijini.
• Maambukizi na milipuko ya magonjwa ya mazao na wadudu na magonjwa ya wanyama
• Mmomonyoko wa raslimali asilia sanjari na uharibifu wa mazingira
• Vyama dhaifu vya wazalishaji sambamba na uratibu dhaifu na uhaba wa teknolojia sahihi na rahisi
Mipangilio Mizuri Zaidi ya Soko la AjiraSoko la ajira linakabiliwa na changamoto kutokana na (a) uhuria unaotarajiwa katika ajira kwa nchi
za Afrika Mashariki, na (b) kuwepo kwa utandawazi. Utafiti zaidi unahitajika katika masuala ya ajira,
likiwemo suala la uhaba wa ajira miongoni mwa vijana.
Matumizi Bora na Endelevu ya MaliasiliHayajapatikana mafanikio ya kuridhisha katika utunzaji wa mazingira na maliasili katika maeneo ya
nyanda za juu kusini, misitu ya miombo huko Tabora, na kusini mwa Tanzania kuliko katika maeneo
mengine ya nchi.
8
Matokeo ya Maendeleo ya viwanda vinavyohusisha mazao ya misitu na uendelevu wa maisha si wa
kuridhisha. Hii kwa sehemu imesababishwa na kukosekana kwa fedha za kutosha kunakohusisha
kushindwa kwa kuchochea sekta binafsi kuchangia utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Misitu.
Imebainishwa pia kwamba ongezeko la mapato kutokana na sekta ya maliasili kunatokana na utaifishaji
na uuzaji wa mazao haramu ya maliasili yanayokamatwa.
Hatua za KuchukuliwaHatua zinazopaswa kuchukuliwa zinahusisha kukabiliana na changamoto zilizotajwa hapo juu. Sehemu
hii inaorodhesha baadhi ya hatua muhimu zinazopaswa kuchukuliwa:
Kilimo Sera ya kilimo haina budi kuwa na malengo ya aina mbili. Lengo moja likijikita katika kuinua uzalishaji
mdogo wa kilimo kama sehemu ya mkakati wa kupunguza umaskini. Hii itahusisha kuanzisha shughuli
za mashamba madogo madhubuti, na za muda wote zikijumuisha uzalishaji wa kujikimu na kwa ajili ya
kukidhi soko.
Na lengo la pili ni kutia msukumo na nguvu mpya katika sekta ya kilimo cha kibiashara ili kukuza
uzalishaji. Hii moja kwa moja itaongeza ajira na kupunguza umaskini wa vijijini kwa kuajiri nguvu kazi
na kupitia viwanda vya usindikaji vinavyohusiana na mazao ya kilimo.
Njia nyingine za kuinua uzalishaji wa sekta ya kilimo ni pamoja na kuongeza upatikanaji wa taarifa za
masoko ya bidhaa za kilimo na kuongeza kasi ya mwitikio wa sekta binafsi katika kuzitumia taarifa
hizo.
Juhudi za maksudi zitahitajika katika kuboresha upatikanaji, usambazaji, na wananchi kumudu pembejeo
za kilimo, huduma za ugani, na huduma za kudhibiti wadudu waharibifu na magonjwa. Juhudi pia hazina
budi kuelekezwa katika kuboresha uzalishaji wa mazao ya sekta ya mifugo na kuhakikisha kwamba
kunakuwepo na masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi kwa mazao ya mifugo.
Shughuli Zisizo za Shamba VijijiniShughuli za vijijini zisizo za mashambani hususan kwenye usindikaji na utoaji huduma, hazina budi
kukuzwa kwani ni fursa muhimu katika kuongeza ajira maeneo ya vijijini. Mkakati wa aina hii unaweza
kufanikiwa katika maeneo yenye barabara nzuri, umeme na mawasiliano ya kuaminika.hii inamaanisha
kwamba maeneo yenye sifa hizo ndiko viwanda na masoko ya bidhaa kuweza kuwa na ufanisi na gharama
za uzalishaji zitakuwa chini zaidi.
Viwango vizuri vya elimu na miundombinu ya msingi ndivyo vichocheo muhimu katika kukuza shughuli
za kiuchumi zisizo za mashambani kwenye maeneo ya vijijini. Hivyo serikali haina budi kuhakikisha
kuwa mambo hayo yanaboreshwa.
9
Huduma za FedhaSerikali inapaswa kuongeza kasi ya utekelezaji wa awamu ya pili ya Maboresho ya Sekta ya Fedha. Sekta
hii itaendelea kuchochea ukuaji wa uchumi kwa kutoa huduma za kifedha za kutosha za kna ambazo
watu wengi wanaweza kuzimudu.
NishatiKuna umuhimu wa kuwa na vyanzo mbadala vya nishati. Hili linaweza kufanikishwa kwa kukuza
ushirikiano wa kikanda katika sekta ya nishati, na kwa kutekeleza Mpango Mkuu wa Sekta ya Nishati.
Ajira Kuna uhitaji mkubwa wa kutekeleza Sera ya Maendeleo ya Vijana, Sera ya Ajira ya Taifa, na Sera ya Taifa
ya Hifadhi ya Jamii. Utekelezaji wa sera hizi utasaidia kuongeza fursa za ajira sambamba na kuandaa
mazingira bora zaidi kwa ajili ya ajira binafsi.
Fedha za UmmaHapana budi kuwapo msisitizo (a) katika kufikia na kudumisha kiwango cha kuridhisha cha usimamizi
bora wa fedha na uwajibikaji na (b) kuboresha ukusanyaji, upangiliaji na utumiaji wa raslimali.
Katika ngazi ya kimataifa, kuna umuhimu wa kuhimiza diplomasia ya kiuchumi kwa lengo la (a) kuvutia
masoko na wawekezaji wa nje ya nchi (b) kujadiliana na wahisani juu ya mikopo yenye riba nafuu pamoja
na kushawishi kufutiwa madeni.
Maliasili na MazingiraJuhudi zinahitajika ili:
• Kuboresha usimamizi katika sekta hii
• Kuongeza jitihada za upandaji miti
• Kutekeleza malengo ya ukusanyaji wa maduhuli (mapato)
• Kuimarisha Kitengo cha Usimamizi wa Misitu
• Kuzuia uvunaji haramu wa maliasili
Msaada zaidi unahitajika katika kuwezesha ukusanyaji na uchanganuzi wa taarifa kwa kuzingatia
uendelevu wa mchango wa maliasili kwa
Maendeleo ya Taifa.
Nguzo ya Pili – Uboreshaji wa Maisha na Ustawi wa Jamii
Katika sehemu hii kwanza tunaelezea matokeo makuu na malengo ya nguzo halafu tunazungumzia kwa
ufupi juu ya sehemu nyingine za nguzo hii. Hii itasaidia msomaji kupata mapana na mipaka ya nguzo hii.
Kwa vile huu ni mwongozo wa lugha rahisi hatufanyi mapitio ya takwimu ‘kavukavu’ ila tunasonga mbele
na kudokeza juu ya changamnoto kuu zilizojitokeza na mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa.
10
Sehemu za Nguzo HiiNguzo ya pili ya MKUKUTA inahusu shughuli zinazochochea “Uboreshaji wa Maisha na Ustawi wa
Jamii” . Matokeo ya jumla yatakuwa (a) Kuboreka kwa maisha na ustawi wa jamii msisitizo wa kipekee
ukiwa kwa watu maskini zaidi pamoja na wale walio katika mazingira hatarishi. (b) kupungua kwa tofauti
ya kimatokeo (mfano; elimu, kiwango cha kuishi na afya) kwa kuzingatia maeneo ya kijiografia, kipato,
umri, jinsia, na makundi mengine Malengo matano ya nguzo hii ni:
• Kuhakikisha upatikanaji sawa wa elimu bora ya msingi na sekondari kwa wavulana na wasichana,
elimu ya kufuta ujinga miongoni mwa wanaume na wanawake, na upanuzi wa elimu ya juu, ufundi na
ufundi stadi.
• Kuboresha maisha, afya na ustawi wa watoto wote na wanawake na hasa makundi yaliyo katika
mazingira hatarishi.
• Kuongeza upatikanaji wa maji safi, salama na ya gharama nafuu, usafi, malazi mazuri, na mazingira
salama na endelevu; na hivyo kupunguza uathirikaji utokanao na hatari za mazingira.
• Kuhakikisha kunakuwapo hifadhi ya uhakika ya kijamii na utoaji wa mahitaji na huduma za msingi
kwa wahitaji na walio kwenye mazingira hatarishi.
• Kuhakikisha kunakuwepo na mfumo mzuri kuwezesha upatikanaji wa huduma safi za umma na
zenye gharama nafuu kwa wote
Changamoto kuu sita za nguzo ya piliLicha ya kuwepo Maendeleo mazuri katika kufikia na kuendeleza uboreshaji wa maisha na ustawi
wa jamii katika miaka miwili iliyopita, bado zimekuwepo changamoto nyingi. Sehemu hii inaelezea
changamoto kuu sita.
11
Ubora na Upanuzi wa ElimuNi muhimu kuhakikisha kunakuwa na elimu yenye ubora wa kiwango cha juu katika ngazi zote kadri
mfumo unavyozidi kupanuka. Upanuzi wa elimu unajumuisha kuwepo kwa vyumba vingi zaidi vya
madarasa ili kukabili tatizo la msongamano wa wanafunzi, vifaa na zana za kufundishia, nyumba za
walimu, vyoo, na uwiano unaokubalika wa walimu wenye sifa na wanafunzi.
Jinsia na ElimuBado iko tofauti katika uandikishaji wa wanafunzi katika shule za sekondari na taasisi za elimu ya
juu. Katika hili changamoto kubwa ni kuhakikisha wanafunzi wa kike wanaoandikishwa wanaendelea
na masomo hadi kuhitimu na kuinua viwango vya ufaulu kwa wanafunzi wa kike. Hali hii inaweza
kusababishwa na kukosa uwezo wa kumudu gharama, mahitaji ya soko la ajira na mimba na watoto
wa kike kulazimishwa kuolewa mapema. Sababu hizi huchangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi wa kike
kuacha shule katika maeneo ya mijini na vijijini
AfyaJuhudi zinahitajika (a) kuendeleza chanjo ya Donda koo, Pepopunda, na Homa ya Ini na kuifikia mikoa
yote (b) Kuhakikisha maambukizi mapya ya Kifua Kikuu yanapungua, na (c) kufanya ushauri na upimaji
wa VVU na UKIMWI kuwa endelevu.
Maji na Usafi wa MazingiraKuna umuhimu wa kukarabati, kupanua na kujenga mitandao ya mifumo ya miundombinu ya maji na
usafi wa mazingira. Juhudi za maksudi zinahitajika katika kuhimiza matumizi sahihi ya vyoo na mifumo
ya utupaji wa taka, sambamba na uboreshaji wa makazi holela.
Makundi Yaliyo katika Mazingira HatarishiKunahitajika juhudi katika kushughulikia ongezeko la makundi maalum ya watu walio katika hatari
zaidi ya kuathirika yanayosababishwa na matatizo ya kiafya kama vile magonjwa yanayoenezwa kwa
ngono. Ni muhimu kulenga katika (a) hali ngumu ya maisha inayosababishwa na VVU na UKIMWI
(b) matatizo mahsusi ya familia zinazoongozwa na watoto na wazee.
Wafanyakazi Wenye SifaSekta za elimu , afya na kwenye serikali za Mitaa kuna upungufu wa wafanyakazi wenye ujuzi unaohitajika.
Wafanyakazi wengi waliopo hawajapewa motisha wa kutosha – hususan wale wanaofanyakazi maeneo
ya vijijini na maeneo yasiyokuwa na vivutio vingi.
Mambo TuliyojifunzaMtazamo wa MKUKUTA wa kuzingatia matokeo unawezesha kubainisha mwelekeo mtambuka wa
juhudi nyingi za kimaendeleo
12
Elimu Kuongeza idadi ya walimu wenye sifa zinazotakiwa ni sharti muhimu la kukuza ubora wa elimu.
Hata hivyo sharti hili peke yake halijitoshelezi.
AfyaKumekuwepo na mafanikio katika kupunguza utapiamlo, vifo vya watoto wachanga na walio chini ya
umri wa miaka mitano, na kudumaa. Mafanikio haya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na utoaji wa
chanjo, sanjari na uboreshaji wa lishe.
Maji na NishatiUpatikanaji duni wa huduma za jamii kama vile maji na vyanzo mbadala vya nishati hukwamisha juhudi
za upatikanaji wa elimu katika ngazi ya familia, hususan kwa wanawake. Muda mwingi unaotumika
katika kuchota maji na kutafuta nishati kama vile kuni ungeweza kutumika kwa shughuli nyingine.
Wafanyakazi Wenye SifaMaeneo mengi ya vijijini na yasiyokuwa na vivutio hayana huduma nzuri kwa watumishi, ikiwa ni pamoja
na nyumba za kuishi. Hali hii inawakatisha tamaa wafanyakazi katika sekta ya huduma za jamii wenye
sifa kufanya kazi katika maeneo hayo.
Ushiriki wa JamiiBila ushiriki wa wananchi malengo mengi ya Nguzo ya pili hayatafikiwa. Mchango wa ushiriki wao
katika kupanga, kutoa mchango wa hali na mali katika miradi ya maendeleo ni muhimu sana hivyo
taratibu zinapaswa kuwekwa ili kuongeza ushiriki wao.
Hatua za KuchukuliwaHatua zinazopaswa kuchukuliwa zinahusu namna ya kukabiliana na changamoto zilizotajwa hapo juu.
Sehemu hii inaorodhesha baadhi ya hatua muhimu zinazopaswa kuchukuliwa:
Ushiriki wa Wadau Changamoto zilizoibuliwa kwenye nguzo hii zinaashiria kuhitajika kwa juhudi za maksudi kwa wadau
wote kuchukua hatua zitakazowezesha kufikiwa kwa malengo ya MKUKUTA.
ElimuSerikali itaendelea kuboresha na kupanua elimu kupitia programu zinazolenga kuongeza idadi ya walimu
wenye sifa, na kuongeza ubora wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia ili kuboresha mazingira ya shule.
Pia juhudi hazina budi kuelekezwa katika kuondoa tofauti za kijinsia katika ngazi zote za elimu.
Watumishi Wenye SifaUjengaji uwezo kwa watumishi wa serikali za Mitaa utaendelea kama njia ya kuimarisha usimamizi wa
raslimali za umma katika ngazi hiyo. Kutakuwa na mafunzo kwa njia ya masafa kwa watumishi wa sekta
ya huduma za jamii, hususan wale walioko vijijini na maeneo mengine yasiyokuwa na vivutio.
13
Afya Juhudi za maksudi zinahitajika miongoni mwa wadau wa afya ili kukomesha tatizo la vifo vya kinamama
wazazi. Hii itahusisha (a) Muundo wa Kitaifa wa VVU na UKIMWI unaohusisha sekta nyingi (b)
kupanua utoaji wa dawa za kurefusha maisha
Makundi ya Watu Walio katika Mazingira HatarishiMiongozo na mifumo ya kuyafanya masuala ya watoto yatima na wale walio katika mazingira hatarishi
kuwa mtambuka haina budi kuandaliwa. Miongozo na mifumo hii itapaswa kutumiwa na Wizara, Idara,
Wakala wa Serikali na Wadau wasiokuwa wa Kiserikali. Miongozo hiyo inapaswa kuhusisha ujengaji wa
uwezo wa maofisa husika katika kushughulikia masuala ya watu wenye ulemavu na wazee.
Ugharamiaji wa Huduma za Jamii. Kutakuwa namwendelezo wa juhudi za kuongeza upanuzi na uboreshaji wa huduma za jamii kupitia
ubia wa sekta ya umma na ya binafsi .
Hifadhi ya JamiiKuna umuhimu mkubwa wa kuboresha mipango ya hifadhi ya kijamii kwa makundi yaliyo katika
mazingira hatarishi.
Mazingira Kampeni za utunzaji wa mazingira zinapaswa kupanuliwa ili kuongeza ufahamu wa wadau juu ya hifadhi
ya mazingira.
Nguzo ya Tatu –Utawala Bora na Uwajibikaji
Katika sehemu hii kwanza tunaelezea matokeo makuu na malengo ya nguzo, halafu tunazungumzia kwa
ufupi juu ya sehemu nyingine za nguzo hii. Hii itasaidia msomaji kupata mapana na mipaka ya nguzo hii.
Kwa vile huu ni mwongozo wa lugha rahisi hatufanyi mapitio ya takwimu ‘kavukavu’ ila tunasonga mbele
na kudokeza juu ya changamnoto kuu zilizojitokeza na mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa.
Sehemu za Nguzo HiiNguzo ya tatu ya MKUKUTA inahusu shughuli zinazo lenga kukuza, “ Utawala Bora na Uwajibikaji”.
Matokeo ya jumla ni (a) Utawala bora na Utawala wa Sheria (b) Uwajibikaji wa Viongozi na watumishi
wa umma, (c) Demokrasia na uvumilivu wa kisiasa na kijamii, na (d) Amani, Utulivu wa kisiasa, umoja
wa kitaifa na mshikamano wa kijamii.
Malengo saba kwa nguzo hii ni haya yafuatayo:
• Kuhakikisha kuwa miundo na mifumo ya utawala pamoja na utawala wa sheria ni vya kidemokrasia,
shirikishi, uwakilishi, uwajibikaji na jumuishi
• Kuhakikisha ugawaji sawa wa rasilimali za umma – pamoja na kushughulikia ipasavyo suala la
rushwa
14
• Kuweka mfumo wa huduma za umma unaofaa kama msingi wa kuboresha utoaji wa huduma na
kupunguza umaskini
• Kuhakikisha kwamba haki za maskini na makundi yaliyo katika mazingira hatarishi zinalindwa na
kukuzwa katika mfumo wa haki
• Kupunguza hali ya baadhi ya watu kutengwa na kutovumiliana kisiasa na kijamii
• Kuboresha usalama binafsi na wa mali, kupunguza uhalifu na kuondoa unyanyasaji wa kijinsia na
unyanyasaji majumbani
• Kuendeleza na kuimarisha utamaduni wa watu kama utambulisho wa kitaifa.
Changamoto Kuu Saba za Nguzo ya TatuLicha ya kuwepo mafanikio kuelekea kuboreka kwa utawala na uwajibikaji katika kipindi cha miaka
miwili iliyopita, bado tunakabiliwa na changamoto nyingi. Sehemu ifuatayo inazungumzia changamoto
kuu saba zilizojitokeza.
Mapungufu katika mfumo wa kisheriaChangamoto zinazoukabili mfumo wa kisheria ni pamoja na:
• upungufu wa miundombinu (yaani Ofisi, vifaa vya ofisini, nyumba, vifaa vya mawasiliano) kwa vyombo
vya utekelezaji wa sheria ( yaani jeshi la Polisi, Magereza, Mahakama)
• mishahara isiyokidhi mahitaji jambo linalowafanya wasimamizi wa utekelezaji wa sheria kutumbukia
katika kuchukua rushwa
• uchache wa raslimali watu na ujengaji wa uwezo katika kufanya yale yanayopaswa kufanyika
• kukosekana kwa upanuzi wa magereza na hivyo kusababisha msongamano wa wafungwa
15
• Teknolojia duni katika kupambana na uhalifu mkubwa kama ule wa kimataifa (kama ugaidi, fedha
haramu, Biashara ya dawa za kulevya, uhamiaji haramu, n.k)
Maboresho ya Sekta ya SheriaLicha ya kuwepo mafanikio katika maboresho ya sekta ya sheria bado ziko changamoto katika kuboresha
mfumo wa mahakama. Hizi ni pamoja na:
• Kutafakari upya na kuwianisha ngazi za mishahara kwa watumishi wa sekta ya sheria
• Kuongeza kasi ya mfumo wa uendeshaji wa kesi
• Kuongeza uhuru wa mahakama
• Kuongeza utolewaji wa taarifa kwa wananchi wa kawaida kuhusu muundo na kazi za mfumo wa
mahakama.
Usimamizi wa Upelekaji wa Madaraka, Majukumu na Raslimali kwa WananchiInaziwia vigumu Serikali za Mitaa kumudu usimamizi wa ongezeko la fedha lililosababishwa na
maboresho ya serikali za Mitaa ambapo raslimali nyingi zinapaswa kupelekwa moja kwa moja kwenye
mamlaka za serikali za Mitaa.
Kuna hitaji la haraka kuwianisha upelekaji wa madaraka, majukumu na raslimali kwa wananchi dhidi ya
programu za kuzijengea uwezo mamlaka husika za serikali za mitaa. Hii inapaswa kuhusisha kuongeza
uelewa miongoni mwa watumishi wa serikali kuu na serikali za mitaa kuhusu dhana ya ‘‘Upelekaji wa
Madaraka, Majukumu na Raslimali kwa Wananchi”
Kumekuwepo na uhaba mkubwa wa raslimali katika kufanya ukaguzi wa mahesabu ya fedha za umma.
Maeneo ya vijijini zaidi yameathirka zaidi na uhaba huu kwa vile wakaguzi wa mahesabu wenye sifa
wamekuwa wakigoma kwenda maeneo hayo pale wanapopangiwa kufanya kazi huko.
Usimamizi wa MaliasiliKumekuwa na udhaifu katika kanuni na ushiriki wa wananchi katika kusimamia matumizi ya maliasili.
Hali hii imesababisha kuongeza kwa vitendo vya rushwa. Juhudi zaidi zinahitajika katika kuzishirikisha
asasi zisizo za serikali katika kutekeleza NACSAP II . Suala lenye umuhimu wa kipekee ni utendaji wa
bodi za zabuni chini ya sheria mpya ya manunuzi.
Haki za BinadamuIpo haja ya kujenga uwezo wa watumishi wa haki za binadamu pamoja na kufanya ufuatiliaji wa mara
kwa mara. Wazo la kutumia ubia wa serikali na sekta binafsi linaleta changamoto ya kubainisha AZISE
zinazoaminika katika ngazi ya wilaya. Pia kumekuwepo na ukosefu wa takwimu za kitaifa zinazohusu
masuala ya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili wa majumbani.
Mbao za MatangazoKubandika taarifa kwenye mbao za matangazo hakutoshelezi kwa vile hakuwasukumi wananchi katika
ngazi ya jamii kusoma na kuzichambua taarifa hizo. Mojawapo ya sababu ya hali hii ni mbao nyingi za
16
matangazo kutofikiwa na wananchi walio wengi kwani zinapatikana kwenye makao makuu ya wilaya na
siyo vijijini.
Teknolojia ya Habari na MawasilianoTeknolojia ya kisasa inaweza kutumika vizuri zaidi katika kusambaza taarifa na kuwahamasisha wadau
kuhusiana na jambo Fulani. Maeneo ambako huduma hii inahitajika zaidi ni pamoja na magerezani na
kwenye makambi ya wakimbizi.
Mambo TuliyojifunzaMatumizi hafifu ya taarifa za umma
Wizara, Idara, Wakala wa Serikali na Serikali za Mitaa hutoa taarifa kwa umma lakini bado kumekuwapo
na hamasa ndogo miongoni mwa wananchi katika ngazi ya jamii katika kuzitumia taarifa hizo. Hili
linajidhihirisha zaidi kutokana na taarifa zinazotolewa kwa umma na Serikali za Mitaa. Kuna haja ya
kuzirahisisha zaidi taarifa hizi ili ziweze kueleweka kirahisi.
Mambo ambayo jamii inapenda kupatiwa taarifa ni mengi ikiwa ni pamoja na:
• Watu wenye hati za kimila za umiliki wa ardhi katika ngazi ya kaya kwa kuzingatia jinsia
• Mazingira ya kazi ya watumishi wa vyombo vya dola
Vita Dhidi ya RushwaHatua za kuchukuliwa ili kupunguza rushwa zinapaswa kuhusisha:
• Uhamasishaji unaolenga kubadili mitazamo ya watumishi wa umma
• Kuimarisha shughuli za ukaguzi wa taasisi za umma ili kupunguza matumizi mabaya ya raslimali
• Kuimarisha uwezo na utayari wa wananchi kuwa makini katika kufuatilia michakato ya uwajibikaji wa
ofisi za umma
Uoanishaji Masuala yanayohitaji kuoanishwa ni pamoja na:
• Mchakato wa kupeleka madaraka, majukumu na raslimali kwa wananchi ili kuhakikisha uthabiti,
uendelevu na utekelezaji wenye ufanisi.
• Uratibu rasmi wa maboresho mbalimbali (Sekta ya Sheria, Sekta ya Utumishi wa Umma na Programu
za Maboresho ya Serikali za Mitaa n.k.)
• Migongano ya sheria za kisekta
Hatua Zinazopendekezwa KuchukuliwaHatua zinazopaswa kuchukuliwa zinahusisha namna ya kukabiliana na changamoto zilizotajwa hapo
juu. Sehemu hii inaorodhesha baadhi ya hatua muhimu zinazopaswa kuchukuliwa:
Serikali kwa ushirikiano na wadau wengine watapaswa;
• Kuongeza shughuli za uhamasishaji wa jamii juu ya umuhimu na matumizi ya taarifa za umma.
• Kutoa mafunzo zaidi juu ya maadili na uaminifu kwa wataalamu ili kuimarisha utawala bora na
uwajibikaji
17
• Kufanya utafiti wa awali wa viashiria vikuu vya utendaji ili kusaidia ufuatiliaji na tathmini za baadaye
• Kuboresha mazingira na miundombinu ya kazi
• Kushirikisha wadau wasiokuwa wa kiserikali katika kuimarisha uwajibikaji ikiwemo kupitia matumizi
ya mbao za matangazo
• Kuajiri wafanyakazi wapya na kuwapatia mafunzo kazini kila inapohitajika
• Kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani
• Kuboresha miundombinu ya mawasiliano
• Kuweka mfumo uanaoeleweka wa utawala bora, uwajibikaji na uwakilishi.
• Kushirikisha zaidi jamii katika kusimamia maliasili
• Kujenga uwezo wa watumishi wa Serikali za Mitaa katika kusimamia raslimali na utoaji wa huduma.
• Kupanua na kuboresha magereza na kuweka mfumo wa uwekaji wa taarifa za wahalifu
• Kupanua mifumo katika kudhibiti na kufuatilia mipaka ya nchi
• Kupanua na kuimarisha Programu ya Huduma za Jamii na ya Zima moto na Uokoaji katika mikoa
yote
18
Katika sura hii kwanza tunaangalia chimbuko la MKUKUTA kwenye mapitio ya Mfumo wa
awali wa Ufuatiliaji wa Umaskini. Kisha kwa ufupi tunatazama kazi za sasa za Sekretarieti ya
MKUKUTA na Makundi matatu ya Kiufundi. Hii itatupeleka katika kutafakari maendeleo
ya uoanishaji wa shughuli mbalimbali. Sura hii inahitimishwa kwa kutoa fikra juu ya changamoto
zilizobainishwa, mambo ya kujifunza na mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa.
Chimbuko la Mfumo wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA
Mwaka 2001, Serikali iliandaa Mfumo wa Ufuatiliaji Umaskini kwa ajili ya Mkakati wa Kupunguza
Umaskini. Mfumo huo ulipitiwa na kuboreshwa mwaka 2005/06 ili uweze kutumika kufuatilia
MKUKUTA ambao ni mkakati mpana zaidi na wenye kuzingatia matokeo zaidi kuliko Mkakati wa awali
wa Kupunguza Umaskini. Mfumo wa ufuatiliaji uliopitiwa na kuboreshwa uliidhinishwa mwaka 2006
na unajulikana kama Mfumo wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA.Mabadiliko makubwa yaliyojumuishwa
kwenye mfumo mpya ni pamoja na:
• Kuunganishwa kwa kamati za awali za utendaji na kamati ya ufundi na kuwa Kamati moja ya Kiufundi
ya MKUKUTA . Kazi za kamati hii ni (a) kuhakikisha utendaji mzuri wa Mfumo wa Ufuatiliaji wa
MKUKUTA na uandaaji wa taarifa kutoka kwenye Makundi ya Kiufundi (b) kuarifu ngazi mbali
mbali za uwakilishi za serikali (yaani Kamati ya kiufundi ya Makatibu Wakuu wa Wizara, Baraza
3. Mfumo wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA
19
la Mawaziri na Bunge) kuhusu hatua
zinazopigwa pamoja na masuala ya sera
yanayoibuka kutokana na mfumo wa
ufuatiliaji.
• Kubadilika kutoka Makundi manne ya
Kiufundi na kuwa Makundi matatu.
Makundi ya Kiufundi ya ‘utafiti na sensa’
na ‘ Taarifa za kawaida za kila siku za
kiutawala’ yameunganishwa kufuatia
kutambuliwa kwa mchango wa Ofisi ya
Takwimu ya Taifa katika kuhakikisha
kuwa takwimu rasmi zinakuwa bora. Kundi hilo hivi sasa linaitwa ‘Kundi la Kiufundi la Utafiti na
Takwimu za Kawaida za Kila Siku za kiutawala’. Makundi ya Kiufundi ya ‘Utafiti na Uchambuzi’ na
ya ‘Mawasiliano’ yamebakia kama yalivyokuwa, lakini ili kuleta urahisi zaidi, kundi la Mawasiliano
limebatizwa jina jipya la ‘Uenezaji, Uhamasishaji na Ushawishi’
• Kuimarishwa kwa uwianishaji na uhusiano baina ya (a) Matokeo ya ufuatiliaji katika ngazi ya kitaifa
na tathmini (b) Mipango mikakati ya serikali, Bajeti na mifumo ya utoaji ripoti.
Sekretarieti ya MKUKUTA
Sekretarieti ya MKUKUTA ina malengo ya (a) kuhakikisha utendaji mzuri wa jumla wa Mfumo wa
Ufuatiliaji wa MKUKUTA (b) Kuhudumia Kamati ya Kiufundi, Makundi ya Kiufundi, na Kamati
ya Ushauri wa Ufuatiliiaji, na (c) kutumia muundo wa MKUKUTA Kuboresha uhusiano na uratibu
baina ya michakato ya serikali ikiwemo ya upangaji wa mipango, utoaji wa taarifa na uandaaji wa bajeti
ya Wizara, Idara, Wakala wa Serikali na Serikali za Mitaa. Shughuli za hivi karibuni vya Sekretarieti ya
MKUKUTA ni pamoja na kufanya mapitio, uratibu na mashauriano.
Mapitio Mwaka 2005/06, Sekretarieti ya MKUKUTA ilifanya mapitio ya Mfumo wa awali wa Ufuatiliaji wa
Umaskini, na kuandaa Mfumo mpya wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA. Mchakato wa mapitio ulihusisha
mashauriano baina na miongoni mwa wadau wengi wanaohusika na mfumo wa ufuatiliaji.
Kama sehemu ya mchakato huu, Viashiria vya kitaifa pia vilifanyiwa mapitio ili kupanua wigo wake
kutoka kulenga sekta za kipaumbele kwenye Mkakati wa Kupunguza Umaskini, na kuzingatia nguzo
tatu za MKUKUTA. Mchakato huu ulihusisha zaidi mashauriano na Wizara, Idara na Wakala wa
serikali sambamba na wadau wengine. Orodha ya mwisho yenye viashiria 84 katika ngazi ya kitaifa kwa
kiasi kikubwa vinazingatia sekta mbali mbali na vinatambua kuwepo kwa viashiria vingi zaidi kwenye
nyingi ya Wizara, Idara na Wakala wa serikali. Changamoto iliyopo sasa ni kuimarisha usimamizi wa
mfumo wa taarifa za Wizara, Idara, Wakala wa serikali pamoja na Serikali za Mitaa kwa lengo la kuinua
ubora wa taarifa na upatikanaji wa mara kwa mara wa taarifa hizo.
Kisanduku 2: Hali ya Utekelezaji wa Mfumo wa
Ufuatiliaji wa MKUKUTA
Hali ya autekelezaji wa mfumo wa ufuatiliaji wa
MKUKUTA inahusu kipindi cha mwaka 2005/06
na 2006/07. hii ni kwasababu mwaka 2005/06
ulikuwa wa mpito ambapo mfumo wenyewe ulikuwa
ukifanyiwa mapitio; kwa hiyo mambo mengi
yaliyofanyika hayakutolewa taarifa.
20
Uratibu Sekretarieti ya MKUKUTA ilisimamia kupangwa kwa kazi za Makundi matatu ya Kiufundi pamoja
na Kamati ya Ufundi. Kalenda ya mwaka ya mikutano ya kamati zote pamoja na Makundi ya Kiufundi
ilipitishwa mapema mwaka 2006. Sekretarieti ilifanya kazi kwa karibu sana na Makundi ya Kiufundi
ili kuhakikisha kwamba (a) Mikutano ilifanyika, (b) mipango kazi ilikuwa na ubora unaokubalika na (c)
ripoti za utekelezaji zinaandaliwa kwa wakati. Zaidi ya haya, Sekretarieti ilihakikisha fedha kwa ajili ya
Makundi ya Kiufundi zinapatikana na kutumika vizuri.
Mafanikio mengine ni pamoja na kuimarishwa kwa mawasiliano na mitandao baina ya Sekretarieti
na wadau wengine. Jarida lilopo kwenye tovuti www.povertymonitoring.go.tz limesaidia kuimarisha
mawasiliano baina ya sekretarieti na wadau wengine .
Sekretarieti kwa ushirikiano na wizara mbali mbali, zimejumuishwa katika ajenda ya kuoanisha upangaji
wa mipango, upangaji wa bajeti na utoaji wa taarifa kwenye michakato mbali mbali ya serikali. Matokeo
muhimu ya uoanishaji ni pamoja na Mwongozo wa Upangaji wa Kimkakati wa Mipango ya Muda
wa Kati, Uandaaji wa Bajeti na Utoaji wa Taarifa. Mwongozo huu unafafanua uhusiano uliopo kati
ya MKUKUTA, Sera za Kisekta, Mipango Mikakati, Muundo wa Mipango ya Matumizi ya Muda wa
Kati, na kuzisaidia taasisi mbali mbali kupanga, kuandaa bajeti, kufanya ufuatiliaji, na kutoa taarifa kwa
kuzingatia MKUKUTA.
Matrix ya MKUKUTA ilifanyiwa mapitio ili kuimarisha usahihi wa upangaji mipango katika ngazi za
Wizara, Idara na Wakala wa serikali. Mfumo wa Bajeti wa Upangiliaji Fedha Kimkakati (SBAS) pia
ulifanyiwa mapitio ili kwenda sambamba na mfumo mpya uliobainishwa na mwongozo wa mipango,
pamoja na kujumuisha Mikakati ya Nguzo za MKUKUTA. Hii imezirahisishia Wizara, Idara, Wakala
na Serikali za Mitaa kuhusisha hatua mbali mbali zinazochukua na malengo ya MKUKUTA kupitia
mchakato wa uandaaaji wa bajeti.
Ili kuziwezesha taasisi kutoa ripoti za MKUKUTA, programu ya kompyuta ijulikanayo kama RIMKU,
yaani Ripoti ya Utekelezaji wa MKUKUTA ilitengenezwa. Juhudi zinafanyika kuiboresha na kuioanisha
programu hii na programu nyingine za kompyuta za serikali na hivyo kupunguza sana gharama
zinazohusiana na utoaji wa taarifa.
Shabaha nyingine muhimu inayoratibiwa na sekretarieti ni Zoezi la Kukadiria gharama za
MKUKUTA. Hatua muhimu za kuchukuliwa kwenye sekta za msingi za afya, elimu, maji, barabara,
kilimo, ardhi, nishati na nguvu kazi tayari zimefanyiwa ukadiriaji. Zoezi hili linatarajiwa kufanya
ukadiriaji wa gharama kwa kila mwaka katika kipindi cha zaidi ya miaka mitano.
MashaurianoSekretarieti ya MKUKUTA pia imekuwa ikiratibu maandalizi ya Muundo wa Hifadhi ya Jamii wa
sekta Mbalimbali. Mchakato wa kuandaa muundo huu ni shirikishi ambapo unahusisha wadau wengi
katika maeneo matatu tofauti ya kiutawala.
21
Mapendekezo ya rasimu yalitarajiwa kutumika kama rejea katika hatua ya mwisho ya mashauriano
yaliyopangwa kufanyika kati ya Oktoba na Novemba 2007.
Makundi Matatu ya Kiufundi
Makundi ya Kiufundi ni msingi wa uzalishaji wa taarifa, uchambuzi na mawasiliano ya taarifa kwa
wadau. Makundi haya ni kiungo kati ya utoaji taarifa za jumla wa Serikali za Mitaa na wizara, Idara na
Wakala, na uchambuzi wa matokeo unaotolewa kwenye nyaraka kuu kama vile Ripoti ya Umaskini na
Maendeleo ya Watu, Ripoti ya Hali Halisi na dondoo za Sera .
Kundi la Kiufundi la Utafiti na UchambuziKundi hili linawajibika na uchambuzi wa takwimu na kuratibu matokeo ya tafiti za kitaifa ambazo hutoa
taarifa kwa ajili ya watunga sera na wadau wengine.
Matunda makuu ya kundi hili kwa mwaka 2005 – 07 ni toleo la tatu la Ripoti ya Umaskini na Maendeleo
ya Watu, ambalo lilijumuisha dondoo/vidokezo vya Sera kwa lugha za Kiingereza na Kiswahili . Ripoti
hii ilitoa uchambuzi wa viashiria vikuu katika ngazi ya wilaya kwa mara ya kwanza. Hili liliwezekana
kupitia njia ya kuuchambua Umaskini kupitia taarifa za sensa ya kitaifa na utafiti wa bajeti ya kaya. Kwa
nyongeza, Ripoti ya Umaskini na Maendeleo ya Watu ilitoa picha ya Maendeleo kwa viashiria pamoja na
uchambuzi wa ukuaji wa Uchumi kwa maeneo ya vijijini.
Mwaka 2006, iliandaliwa ripoti ya kwanza ya hali halisi iliyopewa jina la Ripoti ya Halihalisi (2006) .
Ripoti hii iliandaliwa kwa kuzingatia viashiria vya MKUKUTA vilivyoboreshwa. Mafanikio mengine
ni pamoja na uratibu wa Utafiti wa Maoni ya Watu na midahalo ya wazi inayohusu sera ambapo wadau
wanapata fursa ya kujadili matokeo ya tafiti mbali mbali. Tafiti hizi mbali mbali zinafanyika kwa lengo la
kusaidia kuboresha mchakato wa utungaji sera nchini.
Kundi la Kiufundi la Utafiti na Takwimu za Kawaida za Kila Siku za Kiutawala Kundi hili linawajibika na ukusanyaji na uchambuzi wa takwimu zitokanazo na tafiti za kitaifa na
zitokanazo na utendaji wa kila siku wa serikali.
Mwaka 2005/06, makundi mawili ya kitaalam yaliunganishwa ili kuweka majukumu ya usimamizi wa
takwimu chini ya udhibiti wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa kama Sekretarieti. Hivi sasa chini ya Kundi
hili kuna makundi madogo mawili: utafiti na takwimu za kawaida za kila siku. Ofisi ya Waziri Mkuu-
TAMISEMI ni mwenyekiti mwenza wa kundi dogo la takwimu za kila siku kutokana na ukweli kwamba
utawala wa serikali za Mitaa ndio unaozozalisha nyingi ya takwimu hizi.
Kundi Dogo la Takwimu za Kila Siku za KiutawalaKabla ya kuunganishwa na kundi la tafiti, majukumu ya kundi la takwimu za kila siku yalilenga katika
uelimishaji juu ya mfumo wa ufuatiliaji hususan kuhusu takwimu za kila siku. Mchakato huu ulihusisha
kuendesha warsha za kanda na kuendesha mashauriano ya kisekta. Matokeo ya michakato hii yalitumika
22
kuandaa Waraka wa Mkakati wa Mfumo wa Takwimu za Kila Siku. Majukumu mengine ya kundi hili
yaliahirishwa kusubiri uboreshwaji wa makundi ya Kiufundi uliofanyika mapema mwaka 2006.
Kundi la Kiufundi la MawasilianoKundi hili linaongozwa na Idara ya Kuondoa Umaskini na Uwezeshaji katika Wizara ya Fedha na Uchumi
Linajumusha Maafisa Habari kutoka Wizara Mama, Sekta binafsi, Wakala za Wabia wa Maendeleo na
wadau wengine wa sekta ya habari. Hii inachochea mijadala na midahalo miongoni mwa wadau na hivyo
kusaidia utekelezaji wa MKUKUTA.
Kundi hili linatumia mbinu mbali mbali katika kufikisha taarifa kwa wadau wengi. Usambazaji mpana
zaidi wa Mpango Mkuu wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA ulifanyika. Taarifa ya Hali halisi ya Utekelezaji
wa MKUKUTA (2006) ilisambazwa kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
pamoja na wadau wengine. Machapisho mbali mbali yanayohusu Mfumo wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA
yalisambazwa sana wakati wa Maadhimisho ya Miaka 45 ya Uhuru wa Tanganyika.
Ili kufikia wadau wengi zaidi, hususan maeneo ya vijijini, vipindi vya radio na televisheni viliandaliwa ili
kufikisha ujumbe wa MKUKUTA na Malengo ya Millenia ya Maendeleo. Shughuli nyingine ni pamoja
na kusambazwa kwa kalenda za MKUKUTA, na semina kwa Wabunge. Kundi hili pia lilishirikiana kwa
karibu na kundi la Utafiti na Uchambuzi katika kuandaa Utafiti wa Kukusanya Maoni ya Watu.
Uoanishaji wa Kazi
MKUKUTA unaozingatia Nguzo, mtazamo wa matokeo hutegemea mchango wa washiriki kutoka sekta
mbali mbali katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini. Maboresho katika baadhi ya michakato
inayoendelea (hususan Mapitio ya Matumizi ya Umma) hayana budi kufanyika ili kuhakikisha kuwa
juhudi za watu na wadau mbalimbali (hususan Wizara, Idara, Wakala na serikali za Mitaa) zinaratibiwa
na kuoanishwa. Mpangilio mzuri na kwa wakati muafaka wa shughuli na matukio ni muhimu sana.
Mwaka 2006/07 kiliundwa Kikundi Maalumu
Kinachohusisha Wizara mbali mbali kwa ajili
ya Mipango, Bajeti na Utoaji taarifa. Lengo la
kikundi hiki lilikuwa ni kuoanisha taratibu za
serikali za utoaji taarifa, ufuatiliaji na tathmini.
Mafanikio ya kuridhisha yamepatikana katika
ajenda ya uoanishaji wa michakato ya mipango,
bajeti, ufuatiliaji na utoaji taarifa na katika
kuandaa mifumo ya mijadala na midahalo. Mwongozo wa lugha rahisi uliandaliwa na serikali mwaka
2005. Mwongozo huu unaitwa Mwongozo wa Upangaji wa Kimkakati wa Mipango ya Muda wa Kati,
Uandaaji wa Bajeti na Utoaji wa Taarifa. Taratibu za upangaji wa mipango, kuandaa bajeti, kufanya
ufuatiliaji na kutoa taarifa zimebainishwa kwa kina kwenye chapisho hili.
Kisanduku 3: Kikundi Maalumu cha Maofisa
kutoka Wizara mbali mbali cha Mipango, Bajeti
na Taarifa Kinahusisha watumishi kutoka:
• Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa
• Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa
Umma.
• Wizara ya Fedha na Uchumi
23
Kikundi hiki maalumu pia kimeandaa mahitaji ya utendaji katika utoaji ripoti ambayo yamejumuishwa
kwenye Miongozo ya Mipango na Bajeti ya mwaka 2007/08. Mahitaji hayo yanabainisha mlolongo wa
ripoti zilizochambuliwa zaidi, na zinazoeleweka vizuri zaidi na watumiaji, na zisizokinzana na mfumo
wa utoaji taarifa wa MKUKUTA na mifumo mingine ya kitaifa.
Ajenda ya uoanishaji na upangiliaji ina msukumo wa aina tatu:
Kwanza kuandaa na kutumia muundo mmoja kwa ajili ya malipo, mahesabu, utoaji taarifa na tathmini ya
utendaji. Muundo huu unazingatia mifumo iliyopo ya serikali. Lengo ni kuboresha uwazi na kutabirika
kwa misaada kutoka kwa wadau wa maendeleo. Pia mfumo unalenga kuboresha uhakika wa kiwango na
muda wa upatikanaji wa mchango wa wafadhili
Pili ni kushughulikia suala la kukosekana kwa muunganiko baina ya Mipango ya Maendeleo ya Kisekta
na MKUKUTA. Hii inamaanisha kwamba Mipango na Mikakati ya Maendeleo ya Kisekta haina budi
kufanyiwa mapitio ili kuhakikisha (a) inaendana na MKUKUTA, na (b) kunakuwepo muunganiko wa
kimkakati wa upangiliaji wa raslimali na MKUKUTA.
Tatu ni kuoanisha michakato ya kitaifa hususan Mfumo wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA, Mapitio ya
Matumizi ya Umma, na Muundo wa Mipango ya Matumizi ya Muda wa Kati/Miongozo ya Bajeti. Vile
vile ni muhimu kuhusisha Misaada ya Bajeti, Mfuko wa Kusaidia Upunguzaji wa Umaskini, na Juhudi za
Sekta binafsi (PSI). hii haina budi kufanywa kuwa michakato ya kitaifa badala ya sasa inavyojitegemea
na kuonekana kama michakato midogo.
Izingatiwe pia kwamba ili kuwezesha ubadilishanaji mpana zaidi wa taarifa baina na miongoni mwa
nguzo za MKUKUTA, hapana budi kuandaliwa muundo mpya wa mijadala na midahalo. Muundo
huu mpya utaleta pamoja michakato iliyochini ya Misaada ya Bajeti, Mapitio ya Matumizi ya Umma na
MKUKUTA. Sekretarieti mbali mbali zimekuwa zikishirikiana kwa karibu katika kufanikisha ajenda
ya uoanishaji. Matukio muhimu kama ya mikutano ya mashauri ya Mapito ya Matumizi ya Umma na
Wiki ya Sera ya Umaskini hivi sasa yanapangwa na kuandaliwa kwa pamoja.
Shughuli Zinazoendelea
Mwongozo wa Upangaji wa Kimkakati wa Mipango ya Muda wa Kati, Uandaaji wa Bajeti na Utoaji
wa Taarifa unabainisha wazi wazi kazi ya utoaji taarifa za MKUKUTA. Mwongozo huu unaziweka
pamoja taarifa binafsi za utendaji kutoka kwenye Wizara, Idara, Wakala na Serikali za Mitaa huku
zikitoshelezwa na matokeo ya tafiti zinazojitegemea na kazi za uchambuzi mbali mbali. Utoaji wa ripoti
unapaswa kufanywa kwa (a) Ripoti ya Utekelezaji wa MKUKUTA, yaani MAIR itolewayo kila mwaka
(b) Ripoti ya Umaskini na Maendeleo ya Binadamu na Ripoti ya Hali Halisi itolewayo kila baada ya
mwaka mmoja.
Ofisi za serikali zinatoa taarifa za utekelezaji za robo mwaka. Taarifa hizi sasa zitahusishwa na matokeo
ya kila nguzo ya MKUKUTA kupitia Mfumo Mpya wa Utoaji Ripoti za Utekelezaji MKUKUTA
24
(RIMKU), na pia kupitia Mapitio ya Kisekta, Mapitio ya Matumizi ya Umma na Taarifa za ukaguzi wa
mahesabu ya Wizara, Idara, Wakala na serikali za Mitaa.
Serikali imedhamiria kuoanisha mifumo mbali mbali ya utoaji taarifa ili kuimarisha uhusisano wa jumla
na MKUKUTA na baina ya Mipango, Bajeti na mifumo ya utoaji taarifa.
Kuna utafiti unaojitegemea unaoendelea kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini kwenye wizara, idara, na wakala
27. Pamoja na mambo mengine utafiti huu (a) utatoa mwanga juu ya hali ya ufuatiliaji na tathmini
kwenye wizara, idara na wakala kuhusiana na upatikanaji wa vitendea kazi na watumishi wenye ujuzi
unaohitajika (b) utawasaidia watoa maamuzi juu ya namna bora ya kuandaa mfumo wa kisheria wa
ufuatiliaji na tathmini.
Muundo mpya wa mijadala umebuniwa ili kuwezesha mawasiliano miongoni mwa wadau wa nguzo ya
MKUKUTA inayohusika. Hii inaleta pamoja michakato iliyochini ya Misaada ya Bajeti, Mapitio ya
Matumizi ya Umma na MKUKUTA. Sekretarieti tatu zinashirikiana kwa karibu katika kufanikisha
ajenda ya uoanishaji. Matukio muhimu kama ya mikutano ya mashauri ya Mapitio ya Matumizi ya
Umma na Wiki ya Sera ya Umaskini hivi sasa yanapangwa na kuandaliwa kwa pamoja.
Changamoto na Mambo Tuliyojifunza
• Mabadiliko kutoka mfumo wa awali wa Ufuatiliaji wa Umaskini kwenda mfumo mpya wa Ufuatiliaji
wa MKUKUTA yamepanua ajenda ya ufuatiliaji katika (a) ukusanyaji wa taarifa, uchambuzi na
usambazaji wa taarifa (b) raslimali zinazohitajika (miundombinu, fedha na watumishi) (c) usimamizi
wa mfumo.
• Kupanuka kwa viashiria kutoka 84 vya awali kunamaanisha kwamba kazi kubwa na yenye kupangiliwa
vizuri zaidi inapaswa kufanyika.
• Mfumo wa MKUKUTA unaozingatia matokeo unahusisha watu na taasisi nyingi zaidi kuliko
Mkakati wa awali wa Upunguzaji Umaskini. Kwa hali hiyo; unahitajika (a) mfumo madhubuti zaidi
wa Ufuatiliaji na Utoaji taarifa (b) Muunganiko bayana kati ya serikali na wadau wengine muhimu, na
(c) Uimarishaji wa michakato ya uwajibikaji.
• Muunganiko kati ya Mfumo wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA na shughuli nyingine za ufuatiliaji
zinazofanywa na serikali na wadau wengine bado ni dhaifu. Mfumo wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA
haujapata mafanikio makubwa katika kuimarisha mifumo ya takwimu za kila siku na tafiti mbali
mbali katika ngazi ya wizara, idara, wakala na serikali za Mitaa. Bado kuna tofauti kati ya viashiria
vinavyotumika kwa shughuli za MKUKUTA, na pale vinapokuwepo, katika muundo wa utendaji wa
serikali.
• Pamoja na mafanikio hayo makubwa ya Mfumo wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA, bado fedha za
utekelezaji wake unategemea msaada kutoka kwa Wabia wa Maendeleo kupitia mfuko wa pamoja wa
fedha. Hali hii inatishia uendelevu wa mfumo huu.
• Makundi Mahsusi ya Kitaalam yaliundwa upya Aprili 2006. Mafunzo ya utambulisho kwa wajumbe
wa makundi haya yalipangwa na kalenda ya mwaka ya vikao vya makundi haya iliandaliwa na
25
kukubaliwa. Pamoja na haya yote, vikao vinavyopangwa vimekosa mahudhurio ya kuridhisha na hii
imeathiri utekelezaji wa shughuli zilizopangwa. Moja ya sababu za mahudhurio hafifu ni kwamba
kazi za makundi hayo hazikujumuishwa kwenye kazi za kawaida za taasisi wanakotoka wajumbe.
Ilibainika pia kwamba wajumbe wengi wa makundi ya Kiufundi wanaona kazi yao kama ya ushauri
zaidi na siyo utendaji; wanadhani kuwa Sekretarieti itafanya kazi zote. Hali hii imezalisha matarajio
ambayo hayawezi kufikiwa. Inapendekezwa kuwa wajumbe wa makundi haya washirikishwe katika
utendaji wa baadhi ya kazi badala ya kuwa washauri.
Hatua za Kuchukua
• Juhudi zitaendelea kufanyika kuoanisha mfumo wa Ufuatiliaji na tathmini kwenye taasisi za serikali
ili kuhakikisha utoaji taarifa wa kiwango cha juu na utoaji maamuzi ulio bora zaidi
• Kazi za Ufuatiliaji na Tathmini kwenye wizara, idara, wakala wa serikali na serikali za Mitaa
zitabainishwa ili kuzioanisha na Mfumo wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA. Hii itahusisha uandaaji wa
sera ya Ufuatiliaji na Tathmini sanjari na ujengaji uwezo katika ngazi zote.
• Utafiti umefanyika ili kuondoa Mfumo wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA kutoka kwenye utegemezi
wa Mfuko wa Ufadhili na badala yake kuujumlisha kwenye Bajeti ya kitaifa. Serikali itatekeleza
mapendekezo ya utafiti huo hatua kwa hatua.
• Kamati maalum ya pamoja baina ya Serikali na Wabia wa Maendeleo imeundwa ili kubaini masuala
muhimu ikiwa ni pamoja na ugharamiaji na uimarishaji wa Mfumo wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA.
Masuala haya yatashughulikiwa katika kipindi cha mpito ambacho kinaisha mwaka 2012.
26
MKUKUTA unapaswa kugharamiwa na hauna budi kuonekana kwenye bajeti za wadau ili
kuhakikisha kuwa utoaji wa fedha unatabirika na kufanyika kwa wakati. Kwenye sura hii
kwanza tunaangalia (a) namna fedha zinavyopatikana, kupangiliwa kwa ajili ya nguzo mbali
mbali za MKUKUTA (b) jinsi MKUKUTA unavyopatana na bajeti kuu ya kitaifa. Hii inatupeleka
kwenye baadhi ya mawazo kuhusu jinsi michakato ya ugharamiaji na uandaaji bajeti inavyoweza
kuboreshwa. Kisha tunaangalia baadhi ya changamoto kwenye taratibu za kutoa taarifa za bajeti. Sura
hii inahitimishwa kwa kuufanyia mapitio kwa ufupi Mkakati wa pamoja wa Misaada kwa Tanzania na
Sera ya mishahara ya utumishi wa umma.
Utafutaji na Upangiliaji wa Fedha
MKUKUTA unatekelezwa na kugharamiwa na serikali pamoja na wadau wengine nje ya serikali. Si kazi
rahisi kupata taarifa kuhusu michango ya wadau wasiokuwa wa kiserikali, kwa hiyo ripoti hii inajikita
zaidi kwenye hatua zilizochuliwa na serikali.
Mfumo wa bajeti ya Mkakati wa awali wa Upunguzaji Umaskini ulitenga fedha kwa sekta chache tu
za kipaumbele. Bali Mfumo mpya wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA unatambua kwamba wizara, idara,
wakala wa serikali na serikali za Mitaa kwenye sekta zote zinachangia katika juhudi za kukuza uchumi
na kupunguza umaskini. Hali hii imefanya mfumo huu mpya kuwa na mwelekeo wa kutegemea
matokeo ambao unachangiwa na wadau wengi na imechochea hatua za kuwepo kwa juhudi nyingine
zinazokamilishana kama vile Mkakati wa pamoja wa misaada kwa Tanzania. Hii inalenga kufikia
malengo ya MKUKUTA kwa gharama nafuu zaidi.
Kumekuwepo na Maendeleo ya kuridhisha kupitia Mkakati wa pamoja wa Misaada kwa Tanzania
katika kuoanisha misaada ya wahisani na Kupunguza gharama. Michakato ya Kusaidia Bajeti ya jumla
na mapitio ya matumizi ya umma imesaidia kuratibu juhudi za serikali na wadau wa maendeleo katika
kuunga mkono upunguzaji umaskini.
Miongoni mwa mafanikio makubwa yaliyofikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa misaada ya Wabia wa
Maendeleo kwenye bajeti ya kitaifa , na kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato . Ongezeko hili linatokana
na (a) maboresho makubwa yaliyofanywa katika taasisi zinazokusanya mapato ya ndani (b) kuboreka
kwa usimamizi wa fedha. Hali hii imeongeza imani ya Wabia wa Maendeleo kwa Tanzania.
Serikali inaboresha mchakato wa usimamizi wa bajeti (uandaaji na utekelezaji wa bajeti). Kila mwaka
uhusiano baina ya vipaumbele vya MKUKUTA na migawo ya fedha inaboreshwa na kuimarishwa.
Matumizi yanapangiliwa kufuatana na vipaumbele vya nguzo za MKUKUTA. Hii inafanyika kupitia
Mfumo wa Bajeti wa Upangiliaji Fedha Kimkakati (SBAS) katika ngazi ya serikali kuu na kupitia
programu dada ya kompyuta ya Upangaji Mipango na utoaji Ripoti (PlanRep) kwa serikali za Mitaa.
Mfumo wa Bajeti wa Upangiliaji Fedha Kimkakati uilitumika kwenye Sekretarieti za Mikoa wakati wa
4. Mipango ya Ugharamiaji
27
maandalizi ya bajeti ya mwaka 2006/07 . Mifumo hii kwa pamoja inawezesha utengaji wa raslimali kwa
kuzingatia MKUKUTA kwa serikali nzima.
Hatua hii pia imesaidiwa na zoezi la ukadiriaji wa gharama za MKUKUTA na Malengo ya Millenia
ya Maendeleo. Matokeo ya mwanzo ya zoezi hili pamoja na takwimu zinazotokana na nguzo za
MKUKUTA kwa ajili ya mashauriano ya Mapitio ya Matumizi ya Umma, yamesaidia katika kuamua
maeneo ya kutengewa raslimali.
Kukamilika kwa zoezi la ukadiriaji wa gharama za MKUKUTA kutaimarisha juhudi za serikali katika
kuweka vipaumbele na kuunganisha utengaji wa raslimali na MKUKUTA. Sekta nane ambazo tayari
zimekamilisha ukadiriaji wa gharama ni pamoja na afya, elimu, maji, barabara, kilimo, ardhi, kazi na
nishati.
Hata hivyo, pamoja na mafanikio yaliyopatikana, bado changamoto kadhaa zimebakia:
• Kuna umuhimu wa kupima na kujumuisha mchango wa Wadau Wasiokuwa wa Kiserikali kwenye
juhudi za Kupunguza Umaskini. Raslimali za umma zinaweza kutumika vizuri zaidi kwa kujumuisha
hatua zinazochukuliwa na sekta binafsi na asasi za kiraia kwenye mchakato wa uandaaji wa mipango.
Wadau mbali mbali kama vile sekta binafsi, asasi za kiraia, na Wabia wa Maendeleo watahamasishwa
kushirikiana taarifa kuhusu harakati zao za Kupunguza Umaskini wakati wa kuandaa Ripoti ya
Mwaka ya Utekelezaji MKUKUTA itakayofuata. Hii itakuwa hatua ya mwanzo ya ujumuishaji kamili
wa taarifa hizi kwenye mipango ya sekta mbali mbali.
28
• Hakuna raslimali za kutosheleza utekelezaji wa mambo yote yanayopaswa kufanyika. Ukusanyaji
wa raslimali ni suala muhimu sana katika mchakato wa upunguzaji Umaskini. Serikali inapaswa
(a) kutafuta njia za kuongeza mapato ya ndani yatokanayo na kodi na yasiyotokana na kodi (b)
kuwashawishi wadau wa Maendeleo ili waongeze mchango wao kulingana na ahadi zao za kimataifa na
za ndani ya nchi (c) kuongeza kasi ya Kukuza Ubia baina ya Serikali na Sekta binafsi (d) kuhakikisha
kwamba vyanzo vipya vya mapato vinabuniwa.
Ipo haja ya:
• Kuimarisha kutabirika kwa upatikanaji wa raslimali kutoka nje ya nchi
• Kutoa miongozo kuhusiana na vikwazo vya raslimali – hii itapunguza, kama si kuondoa kabisa
maombi yasiyotekelezeka kutoka wizara, idara na wakala wa serikali.
• Kutoa miongozo juu ya kiwango cha maelezo ya kina kinachotakiwa kutolewa na wizara, idara na
wakala wa serikali kwenye mapendekezo ya awali ya bajeti – hii itaepusha kutolewa kwa maelezo ya
kina sana ambayo mara nyingi hukosa muundo wa kimkakati.
• Kuboresha (a) uhusiano baina ya bajeti na nyaraka za programu mbali mbali, na (b) uratibu na
mamlaka kati ya maofisa wa bajeti na programu ndani ya wizara, idara na wakala husika.
MKUKUTA na Bajeti ya Taifa
MKUKUTA unatambua kwamba sekta
zote na wizara, idara na wakala wa serikali
zinachangia katika mchakato wa Kukuza
uchumi na kupunguza Umaskini. Kwa
vile Ukuaji wa Uchumi na Upunguzaji wa
Umaskini vimekuwa nguzo muhimu katika
upangaji wa mipango ya serikali, bajeti
nzima ya serikali inaweza kuelezwa kwamba
ni kwa ajili ya utekelezaji wa MKUKUTA.
Hata hivyo kwa makusudi ya uchambuzi
na upangaji mipango, ni matumizi yale tu
yanayohusiana moja kwa moja na mikakati
ya nguzo za MKUKUTA yanayoainishwa
kuwa matumizi ya MKUKUTA.
Ndani ya Mfumo wa Bajeti wa Upangiliaji Fedha Kimkakati, bajeti iliyopitishwa kutekeleza MKUKUTA
mwaka 2006/07 ilikuwa ni asilimia 48 ya bajeti yote. Asilimia 52 iliyobakia ilikuwa kwa ajili ya miradi na
programu zisizo na uhusiano wa moja kwa moja na MKUKUTA. Mgawanyo wa bajeti iliyotengwa kwa
ajili ya MKUKUTA ulikuwa asilimia 46 kwa nguzo ya kwanza, asilimia 36 nguzo ya pili, na asilimia 18
kwa nguzo ya tatu. mgawanyo huu unashabihiana na lengo la kukuza uchumi na kuongeza kipato cha
watu maskini zaidi.
Kisanduku 4: Machaguo ya Sekta
Matumizi ya kijamii (mfano kwenye elimu na afya)
yanaweza kutazamwa kama uwekezaji kwenye raslimali
watu ambayo ni ya msingi sana katika kuchochea
ukuaji wa Uchumi. Hata hivyo, mapato yanayotokana
na uwekezaji huo siyo ya moja kwa moja na ni ya muda
mrefu. Uchaguzi wa kimkakati hauna budi kufanyika
baina kuelekeza raslimali kwenye sekta za kijamii na
sekta za kiuchumi (mfano fedha na kilimo) ambazo
matunda yake ni ya moja kwa moja na kwa muda
mfupi.
29
Serikali inaendelea kuandaa matumizi halisi kwa mwaka 2006/07. Uchambuzi wa awali unaonyesha
kwamba ugharamiaji wa shughuli za MKUKUTA ulikuwa wa kutosheleza licha ya kuwepo mchepuko
kutoka mafungu yaliyotengwa kwenye bajeti
ya awali. Mchepuko huu ulisababishwa kwa
kiasi kikubwa na serikali kulazimika kupanga
upya mafungu ya fedha ili kukabiliana na
tatizo la umeme katika nusu ya kwanza
ya mwaka wa fedha wa 2o06/07, uhaba
wa chakula, kupanda kwa bei ya mafuta,
kuongezeka kwa riba ya deni la ndani.
Kwa kipindi cha muda wa kati, mkazo utabaki katika kuweka vipaumbele na kutekeleza shughuli za
MKUKUTA zenye matokeo mengi moja baada ya nyingine. Ili kudumisha uthabiti katika vigezo
muhimu vya kiuchumi, bajeti itatenga raslimali zaidi kwa ajili ya shughuli zenye kukuza uchumi wenye
kujali watu maskini zaidi.
Kwa hiyo tunaweza kutegemea bajeti kubwa zaidi kwa ajili ya maendeleo ya miundombinu kwa uwiano
wa ongezeko kwenye huduma za jamii. Tunaweza pia kutarajia mikakati yenye kulenga kupunguza
tofauti baina ya mikoa na yenye kujumuisha masuala mtambuka.
Kuboresha Michakato ya Bajeti na Ugharamiaji Tunahitaji Mkakati mzuri wa kugharamia shughuli za MKUKUTA. Ni muhimu kutenga na kutoa
fedha kwa wakati. Ili kufanikisha hili michakato ya utoaji wa mafungu ya fedha haina budi kuboreshwa.
Hivi sasa shabaha za MKUKUTA zinaweza kufikiwa kwa vile raslimali za kutosha zinatolewa na ipo
mifumo ya kudhibiti ufujaji wa raslimali hizo. Kwa ajili ya shabaha nyingine, kama tulivyoona hapo
juu, serikali itachukua hatua kukusanya raslimali zaidi; na hizi zitatumika kwa busara zaidi kwa ajili ya
malengo yaliyokusudiwa.
Kiwango cha mapato kwa mwaka 2006/07 kiliendana na shabaha za bajeti kwa kiasi kikubwa. Ukusanyaji
mzuri zaidi wa mapato ya ndani ulifanyika sambamba na mambo mengine, kutosheleza utekelezaji wa
hatua za kodi kwa mwaka wa fedha 2006/07.
Kiwango cha matumizi kwa mwaka 2006/07 vile vile kiliendana na shabaha za bajeti. Jumla ya
matumizi kwa mwaka 2006/07 yalikuwa sh. 4,761,700 milioni sawa na asilimia 98 ya makadirio ya
sh. 4,850,588 million, ikilinganishwa na asilimia 94.4 kwa mwaka 2005/06. jumla ya matumizi
kwa uwiano wa pato la ndani lilipungua kutoka asilimia 26.1 mwaka 2005/06, hadi asilimia 25.5
mwaka 2006/07, lakini hii ilibaki kuwa ndani ya mfiko wa shabaha za MKUKUTA. Sababu kubwa
za kushuka huku ni upungufu katika mbinu za kupima msaada wa wahisani uliotolewa moja kwa
moja kwenye miradi.
Kwa vile Ukuaji wa Uchumi na Upunguzaji wa
Umaskini vimekuwa nguzo muhimu katika upangaji
wa mipango ya serikali, bajeti nzima ya serikali
inaweza kuelezwa kwamba ni kwa ajili ya utekelezaji
wa MKUKUTA.
- MAIR (2007)
30
Bado kuna matatizo katika namna mafungu ya fedha yanavyotolewa kwenda kwenye wizara, idara na
wakala wa serikali kwa mwaka. Mpangilio wa utoaji mafungu unatofautiana kati ya wizara na wizara,
kutegemeana na mahitaji na upatikanaji wa raslimali.
Wizara ya fedha imekuwa ikitoa fedha kwenda wizara, idara na wakala wa serikali kila mwezi kwa
kutegemea (a) mpango wa mtiririko wa fedha wa wizara, idara na wakala wa serikali (b) fedha ziliopo
Hazina. Kulikuwa na utoaji mdogo wa fedha ikilinganishwa na makadirio ya mtiririko wa fedha katika
robo ya kwanza ya mwaka 2006/07. Hii ilisababishwa na (a) mapungufu ya Wizara, Idara na Wakala
wa Serikali katika kupanga mtiririko wa
fedha, na (b) uingiaji hafifu wa raslimali
kwenda hazina. Sehemu kubwa ya Bajeti
ya Maendeleo inagharamiwa na Wabia wa
Maendeleo. Makadirio yanaidhinishwa
mapema lakini changamoto inabaki katika
kukabili ucheleweshaji wa na kutotabirika
kwa utoaji wa fedha hizo (tazama kisanduku 5)
Changamoto ya kukadiria uhusiano baina
ya matumizi ya fedha na matokeo halisi
katika ngazi ya jamii. Changamoto hii
inazidi kuwa kubwa inapotokea kuwa
zaidi ya mwaka mmoja unahitajika mpaka
matokeo kuanza kuonekana. Hili ni tatizo
kubwa kwa viashiria vingi vya MKUKUTA
na halina budi kuzingatiwa.
Njia za Kuripoti BajetiUtoaji wa ripoti za bajeti na za uwazi vimekuwa vikiboreka kwa muda sasa nchini Tanzania.
Bajeti ya taifa huzingatia viwango vya Kimataifa vya Takwimu za za Fedha za Serikali. Mahitaji ya utoaji
taarifa yaliwekwa kwenye Sheria ya Fedha za Umma ya mwaka 2001. hii husaidiwa na miongozo ya
taratibu za mahesabu ya fedha za serikali.
MKUKUTA hutumia Mfumo wa Bajeti wa Upangiliaji Fedha Kimkakati (SBAS) katika kubainisha
namna unavyotumia raslimali. Hii inamaanisha kwamba takwimu za bajeti za MKUKUTA zinapaswa
kubadilishwa ili kuendana na mfumo wa kimataifa wa Takwimu za Fedha za Serikali. Ili kurahisisha
mambo, serikali inaandaa mfumo wa MKUKUTA wa uchambuzi wa matokeo ya utekelezaji wa bajeti.
Hii itaripotiwa kupitia Mapitio ya Utekelezaji wa Bajeti .
Hivi sasa uhusiano wa sera na utekelezaji wa bajeti hupimwa kwa (a) kulinganisha migawo ya SBAS na
matumizi halisi (b) kwa kuangalia matokeo yake kwenye umaskini kwa kutumia Mfumo wa Ufuatiliaji
wa MKUKUTA. Njia nyingine za kuripoti zinazotumika ni pamoja na:
Kisanduku 5: Utolewaji Usio wa Uhakika wa
Mafungu ya Fedha
Mwaka 2005/06 Wizara ya Kilimo, na Usalama wa
Chakula na Ushirika ilipokea asilimia 47 tu ya bajeti
yote ya Maendeleo, asilimia 12 kati ya hiyo ilitolewa
kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa upande
mwingine ilipokea asilimia 32 kwa mwaka huo huo,
asilimia 22 kati ya kiasi hicho kilikuwa kwa kipindi
cha nusu ya kwanza ya mwaka.
Hata hivyo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
mafungu yaliyopokelewa yalikuwa asilimia 81 ya bajeti
yote iliyoidhinishwa kwa mwaka huo na asilimia43
ilitolewa katika nusu ya kwanza ya mwaka.
31
• Ripoti ya utekelezaji ya robo mwaka inayochapishwa kwenye tovuti ya Wizara ya Fedha . Ripoti hizi
hutoa muundo wa jumla wa kifedha.
• Wizara pia hutoa ripoti za kila mwezi kwa kutumia Mfumo wa jumuishi wa Usimamizi wa Fedha.
Ripoti hizi huwa na taarifa kuhusu fedha zilizoahidiwa na kutolewa.
Pamoja na taarifa hizi kutolewa kwa wakati, kufikika, kueleweka na kuwa zenye manufaa, bado hazina
budi kurekebishwa ili kutoa mtazamo wa programu na muundo wa MKUKUTA.
Mapana ya Ripoti ya BajetiMapitio ya Utekelezaji wa Bajeti yanahusisha fedha za serikali kwa misingi ya fedha taslimu, lakini
(a) hayahusishi fedha zinazopelekwa na Wabia wa Maendeleo moja kwa moja kwenye miradi (b)
yanachukulia fedha zinazopelekwa kwenye serikali za Mitaa kama matumizi. Mfumo wa sasa unashindwa
kushughulikia ugumu uliopo katika ngazi ya wilaya kutokana na kuwepo vyanzo mbali mbali vya
ugharamiaji wa programu katika ngazi hiyo.
Ugumu huu kwenye mchakato wa bajeti unahitaji marekebisho katika mtiririko wa fedha na kuhakikisha
kuwa mfumo unabaki kuwa wa uwazi. Kwa hiyo, katika mwaka unaofuata wa utekelezaji wa MKUKUTA,
mifumo ya uainishaji na utoaji taarifa itaanzishwa ili kurahisisha ukusanyaji na utoaji taarifa jumuishi
za fedha.
Ili kufanikisha mchakato huu, wadau mbali mbali hususan wabia wa maendeleo na taasisi zinazonufaika
zitapaswa kuanza kutumia mifumo jumuishi ya ugharamiaji na utoaji wa taarifa.
Serikali inatambua umuhimu wa kuripoti matumizi ya MKUKUTA kila wakati. Kwa ushirikiano wa
karibu na wadau wengine, serikali inaandaa mwongozo utakaotumika na Wizara, Idara na Wakala wa
Serikali kwa kutoa ripoti za (a) MKUKUTA (b) uhusiano wa Mfumo Jumuishi wa Usimamizi wa Fedha
na Mfumo wa Bajeti wa upangiliaji fedha Kimkakati.
Changamoto kubwa ni kupanga na kusimamia utoaji ripoti juu ya nguzo za MKUKUTA pamoja na
shabaha zake. Takwimu zinapatikana kwenye mfumo jumuishi wa usimamizi wa fedha, lakini kuzihusisha
takwimu hizi na Mfumo wa Bajeti wa upangiliaji fedha Kimkakati unabaki kuwa changamoto. Serikali
inaandaa njia itakayo: (a) wezesha ubadilishanaji wa taarifa wenye ufanisi zaidi baina ya zana, na (b)
uchambuzi wa matokeo ya utekelezaji wa bajeti kufanyika kwa wakati.
Sera Nyingine Zinazohusiana na BajetiSerikali ya Tanzania ilianza kutumia Mkakati wa Pamoja wa Misaada ( JAST) mwezi Desemba 2006.
kwa kuzingatia Mkakati huu, Wabia wa Maendeleo wanaohusika kwa kushirikiana kwa karibu na
serikali wameandaa Mwongozo wa Pamoja wa uandaaji wa Programu ambao umefungamana kikamilifu
na malengo ya MKUKUTA.
32
Kwa kuzingatia Mkakati wa Pamoja wa
Misaada kwa Tanzania na Mwongozo wa
Pamoja wa Uandaaji wa Programu, serikali
itashughulikia tatizo la kutotabirika kwa
misaada kutoka nje ya nchi. Itafanya hili
kwa kufanya uchambuzi wa pamoja na
Wabia wa Maendeleo kuhusu njia mbadala
za matumizi na fedha kutoka nje ya nchi.
Hii italeta maafikiano ya wazi juu mkakati
wa muda wa kati na mipango ya matumizi
kabla ya mzunguko wa bajeti ya 2008/09
. hatua hii itachochea kuongezeka kwa
misaada na hivyo kuharakisha ukuaji wa
uchumi na kupungua kwa umaskini.
Tume ya Rais ya Mishahara ya Watumishi wa Umma ilikabidhi ripoti yake Desemba 2006. hii ililenga
kwenye sera ya serikali ya muda wa kati kuhusu kiwango cha ajira ya serikali na uhusiano wake na
bajeti. Serikali inayapitia mapendekezo ya tume kwa kulinganisha na vipaumbele vya utekelezaji wa
MKUKUTA na uwezekano wa kuyatekeleza kwa kuzingatia hali halisi ya bajeti. Matokeo yake itakuwa
ni kutungwa kwa sera ya muda wa kati kuhusu mishahara ya watumishi wa Umma.
Kisanduku 6: Mkakati wa Pamoja wa Misaada kwa
Tanzania (JAST)
JAST ni matokeo ya mashauriano yenye wigo mpana
yaliyoongozwa na serikali kati ya wabia wa maendeleo
na taasisi zisizo za kiserikali. Mkakati huu una
akisi nafasi ya serikali katika kuoanisha msaada wa
wahisani. Malengo makuu ya JAST ni (a) kupunguza
zaidi gharama za uhamishaji fedha (b) kukuza umiliki
wa kitaifa na nafasi ya serikali katika kuongoza ajenda
ya maendeleo.
33
Kwa ufupi, hatua zinazopendekezwa na MAIR zinalenga katika mchakato. Wito wa MAIR ni
juu ya kuwepo kwa mawasiliano bora zaidi yatakayowezesha kuwepo kwa uratibu ulio mzuri
zaidi. Hali hii itathibitisha uhalali wa ongezeko la raslimali kwa ajili ya MKUKUTA.
• Mawasiliano bora zaidi yanahitaji mfumo bora wa ubadilishanaji taarifa na kuwepo kwa mijadala
miongoni na baina ya wadau. Pia inamaanisha kuwepo kwa ushiriki bora zaidi wa asasi zisizo za
kiserikali katika hatua mbali mbali za mchakato wa maendeleo.
• Uratibu mzuri zaidi wa kazi utatokana na kuwepo kwa mawasiliano mazuri zaidi. Kazi iliyo mbele ni
kuhakikisha kuwa wadau wote wanafanya kazi kwa kulingana na muundo wa MKUKUTA wa bajeti,
mipango, ufuatiliaji na utoaji wa taarifa. Mchakato huu utatekelezwa na makundi madhubuti ya kila
nguzo ya MKUKUTA na yale yanayojumuisha wadau kutoka nguzo zote tatu katika ngazi mbalimbali
nchini. Hali kadhalika, mifumo mbali mbali ya takwimu za kompyuta itasaidia kuwezesha mchakato
huu. Kazi muhimu ya usimamizi itafanywa na Kamati maalumu ya Mipango, Bajeti, na Utoaji Taarifa
inayoundwa na wajumbe kutoka Wizara mbali mbali.
• Kuongeza raslimali kwa ajili ya MKUKUTA kutahalalishwa na kuhimizwa na kuwepo kwa uratibu
na ulinganifu mzuri zaidi wa mfumo wa utendaji kazi. Michango mingi ya Wabia wa Maendeleo
itaweza kushabihiana na taratibu za sasa za bajeti ya serikali.Ushiriki wa sekta binafsi utahimizwa
zaidi (hususan kupitia Ubia baina ya Sekta ya Umma na sekta Binafsi)
Sehemu fupi fupi zifuatazo zinatazama hatua zilizopendekezwa kuchukuliwa kwa ajili ya nguzo tatu
za MKUKUTA na kisha masuala ya ugharamiaji, ufuatiliaji na tathmini. Sehemu Hii inajaribu kujazia
nyama kwenye mifupa hapo juu.
5. Muhtasari wa Masuala Makuu na Hatua za Kuchukua
34
Nguzo ya Kwanza: Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini
Hatua za kuchukuliwa katika nguzo hii ni pamoja na:
• Miundombinu ya kiuchumi inaweza kuwa kigezo muhimu zaidi katika kuchochea ukuaji wa uchumi.
Inapunguza gharama za uzalishaji, hususan kwa wazalishaji wadogo na wa kati na wasindikaji wa
bidhaa za kilimo. Katika kuongeza misaada, uwekezaji katika miundombinu huchukua nafasi kubwa
zaidi.
• Kuna umuhimu mkubwa wa kuongeza uzalishaji katika kilimo na kukuza zaidi usindikaji wa mazao
ya kilimo. Hili litahusisha kupunguza au kuondosha vikwazo kama vile upatikanaji hafifu wa huduma
za mikopo na fedha.
• Tatizo la uhaba wa nishati lililolikumba taifa hivi karibuni limethibitisha umuhimu wa nishati kwa
maendeleo. Ni muhimu kutafiti na kubaini vyanzo mbadala vya nishati – kulingana na lengo la sita la
MKUKUTA.
• Juhudi za kuboresha mtandao wa barabara za vijijini si za kuridhisha. Juhudi za kuongeza raslimali na
utekelezaji hazina budi kuwa sehemu ya mchakato wa mjadala wa sekta wa kila mwaka.
• Mishtuko na majanga kama ukame na kupanda kwa bei ya mafuta ulimwenguni hivi karibuni
yamethibitisha kuwa uchumi bado uko katika hali tete. Mbadala wa vyanzo vya nishati, na mazao ya
kuuza nje na akiba ya kutosha ya chakula ni masuala muhimu katika kuimarisha uchumi ili uweze
kuhimili vishindo hivyo.
Nguzo ya Pili: Uboreshaji wa Maisha na Ustawi wa Jamii
Hatua za kuchukuliwa katika nguzo hii ni pamoja na:
• Tatizo la VVU na UKIMWI limerudisha nyuma mafanikio kwenye viashiria vinavyohusiana na
sekta ya afya kama vile kupungua kwa vifo vya kina mama wakati wa kujifungua. Pamoja na juhudi
kubwa iliyofanywa bado vifo hivi vimeongezeka kutoka 529 hadi 578 kwa kila vizazi hai 1000. Hii ni
changamoto ambayo haiwezi kupuuzwa. Ili kuikabili changamoto hii, hatuna budi kuongeza juhudi
na kubuni mikakati mipya.
• Mahusiano yasiyofaa baina ya marika yameleta changamoto kubwa pia.. Kuna haja ya kuongeza
hatua zinazochukuliwa kuwalinda na kuwatunza watu na makundi ya watu walio katika mazingira
hatarishi.
• Makazi holela, hususan maeneo ya mijini yamekuwa ni tishio kwa mazingira. Hali hii inaibua haja
ya kubuni hatua za haraka za kulikabili tatizo hili ikiwa ni pamoja na kuyaboresha na kuyahalalisha
makazi hayo yasiyopangwa.
• Kumekuwepo na ongezeko la mzigo kwa wazee na pia ongezeko kubwa la watoto yatima sambamba
na watoto kutoka katika familia fukara zaidi. Makundi haya yanahitaji namna fulani ya hifadhi ya
kijamii. Mahitaji ya fedha kwa makundi haya ni makubwa kwa hiyo ipo haja ya kubainisha walengwa.
Tafiti zinahitajika ili kusaidia kufahamu uwezo na ufanisi wa hatua za hifadhi ya kijamii.
• Maendeleo ya baadaye ya taifa yatategemea sana uwepo wa wasomi waliofuzu vizuri katika fani mbali
mbali (hususan katika elimu na afya). Changamoto kubwa hapa ni ugharamiaji wa maendeleo ya
raslimali watu inayohitajika ili kuboresha huduma za jamii. Hili siyo tu kwamba linalazimisha kuwepo
35
kwa mfumo endelevu wa ulipaji kodi, bali pia linaleta msukumo wa madai ya ongezeko la mishahara
ya watumishi wa umma.
Nguzo ya Tatu: Utawala Bora na Uwajibikaji
Hatua za kuchukuliwa katika nguzo hii ni pamoja na:
• Uwezo mdogo wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutenga mafungu, na kusimamia matumizi ya
raslimali, unalazimu hatua zaidi za kuimarisha uwezo wake.
• Ukaguzi wa mahesabu chini ya serikali za mitaa unahitaji kujengewa uwezo na kuimarishwa zaidi.
Hitaji hili linazidi kuwa muhimu kufuatia hatua za hivi karibuni za upelekaji wa madaraka, majukumu
na raslimali kwa wananchi.
• Hakuna uhakika kwamba uwekaji wa taarifa kwenye mbao za matangazo unaofanywa na serikali za
mitaa katika ngazi mbali mbali umeweza kuongeza ubora wa upatikanaji na matumizi ya taarifa hizo
miongoni mwa jamii.
Ufuatiliaji wa MKUKUTA
Hatua za kuchukuliwa katika nguzo hii ni pamoja na:
• Kuna haja ya kuboresha mfumo wa taarifa za utendaji kwenye Wizara, Idara na Wakala wa serikali
pamoja na sekta nyinginezo.
• Wadau wote wanapaswa kufanya juhudi za maksudi kubuni mfumo ulioratibiwa vizuri wa ukusanyaji,
uchambuzi na utumiaji wa taarifa
Ugharamiaji wa MKUKUTA
Hatua za kuchukuliwa katika nguzo hii ni pamoja na:
• Kuna umuhimu wa kuoanisha mipango mikakati ya Wizara, Idara na Wakala wa serikali na
MKUKUTA ili raslimali ziweze kuelekezwa kulingana na mipango iliyowekwa.
• Raslimali za kugharamia MKUKUTA hazitoshelezi. Hii inailazimu serikali (a) Kuongeza mapato ya
ndani (b) Wabia wa Maendeleo kuongeza na kulinganisha utoaji wa misaada
• Kuna umuhimu wa kuwepo ufanisi katika (a) kuhusianisha raslimali na matokeo yanayotarajiwa (b)
utoaji wa taarifa za matokeo. Hii inahitaji uboreshaji zaidi wa mfumo wa utoaji taarifa.
• Bado kuna changamoto katika kuwashirikisha wadau wengi katika mchakato wa kuandaa Ripoti ya
Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA.
36
Kiambatisho 1: Muundo wa Utekelezaji wa MKUKUTA
Kiambatisho 2 kwa “Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji MKUKUTA 2006/07” Kinahusu “Hali ya
Utekelezaji wa Muundo wa MKUKUTA”. Kinaorodhesha shughuli 16 (tazama hapa chini). Kila moja
ya shughuli hizi imeambatana na kiashiria cha matokeo na jedwali dogo lenye safu za (a) matokeo (b)
malengo (c) hatua zilizochukuliwa (d) Mapendekezo ya hatua za kuchukua. Kiambatisho hiki kinaeleza
kwa mpangilio na kwa kifupi kazi mbali mbali zinazoendelea na kuonyesha kwa ufupi nini kinapaswa
kufanyika ili kufanikiwa katika siku zijazo.
Muundo wa Utekelezaji wa MKUKUTA – Majukumu Makuu
1 Kuoanisha Mipango/Mikakati ya Kisekta na ya Serikali za Mitaa na MKUKUTA
2 Kuoanisha MKUKUTA na Bajeti na Mapitio ya Matumizi ya Umma
3 Imarisha Uwajibikaji na Utoaji Taarifa kwa Sekta na serikali za Mitaa
4 (hakuna)
5 Jumuisha masuala mtambuka kwenye programu na mipango ya Wizara, Idara, Wakala wa Serikali
na Serikali za Mitaa
6 Pitia na kuimarisha Mfumo wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA, na ufuatialiaji na tathmini ya Sekta na
Serikali za Mitaa.
7 Jumuisha MKUKUTA kwenye sera, programu na mipango ya Wadau wasiokuwa wa kiserikali
8 Saidia uoanishaji wa michakato mikuu ya Maendeleo ya kitaifa ( Mapitio ya Matumizi ya Umma,
Muundo wa Matumizi ya Muda wa Kati, MKUKUTA, Mkakati wa Misaada Tanzania, n. k )
9 Tekeleza Mkakati wa Mawasiliano wa MKUKUTA
10 Chukua hatua kuhakikisha kunakuwepo ushirikiano baina ya sekta katika utekelezaji wa
MKUKUTA
11 Fanya mapitio ya Maboresho makuu (Maboresho ya kitaasisi na ya Kimuundo ) na programu mbali
mbali
12 Andaa Mkakati wa Hifadhi ya Jamii na fanya uchambuzi zaidi wa Haki za binadamu, ambacho ni
kiungo muhimu katika umaskini
13 Ongeza utekelezaji wa Nguzo ya ukuaji wa Uchumi
14 Ongeza kasi ya utekelezaji wa MKUKUTA
15 Imarisha Mfumo wa Utoaji Taarifa za MKUKUTA
16 Imarisha Raslimali Watu inayohitajika kwa ajili ya utekelezaji wa MKUKUTA
LGA = Mamlaka ya Serikali za MitaaM&E = ufuatiliaji na TathminiMDA = Wizara, Idara na wakala wa serikaliMMS = Mfumo wa Ufuatiliaji wa MKUKUTAMTEF = Muundo wa Matumizi ya Muda wa KatiNSA = Wadau wasiokuwa wa Kiserikali PER = Mapitio ya Matumizi ya UmmaTAS = Mkakati wa Misaada wa Tanzania
6. Viambatisho
37
Kiambatisho 2: Mchakato wa Mapitio ya Kisekta
Mapitio ya kisekta yalibuniwa ili kusaidia kuhakikisha kwamba sekta zinakuwa na sera, mikakati na
mipango sahihi na kwamba inatekelezwa kwa njia bora zaidi.
Kama sehemu ya mchakato wa MKUKUTA, mapitio ya kisekta hivi sasa yanalenga kupata matokeo
yanayohusiana na ukuaji wa Uchumi na Kupunguza Umaskini. MKUKUTA unatambua umuhimu wa
maboresho na mikakati ya Maendeleo iliyopo ya kisekta. Matokeo ya mapitio ya kisekta yamekuwa
chanzo muhimu sana cha Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji MKUKUTA – MAIR (2007)
Mapitio ya Kisekta yanashughulika na maboresho yanayofanywa na serikali ambapo yanahusisha
wigo mpana wa wadau. Wazo la msingi ni kwamba uwazi, na njia zinazotabirika na kukubalika ndizo
zinazopaswa kutumika katika kuweka malengo ya usimamizi na mifumo ya uwajibikaji. Hii itasaidia
kuibua ushahidi unaohitajika katika kutathmini mafanikio ya sekta husika na kubuni mipango mizuri ya
Maendeleo ya sekta hiyo katika siku zijazo. Mapitio haya hutoa taarifa zinazohitajika kuongoza uwekaji
wa vipaumbele na kuboresha ufanisi na umadhubuti katika kutumia raslimali.
Malengo mahsusi ya mapitio ya kisekta ni pamoja na:
• Kujenga uelewa wa kina juu ya uhusiano maridhawa uliopo baina ya sera, mikakati, mipango, sheria na
kanuni za sekta ndogo mbali mbali
• Kubainisha mafanikio makuu, mapungufu yaliyojitokeza, na changamoto zinazotishia kukwamisha
kufikiwa kwa mabadiliko yaliyotarajiwa katika sekta hiyo
• Kulenga kwenye matatizo na matokeo yake katika upangaji wa mipango na uandaaji wa bajeti kwa
sekta husika na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa.
• Kujadili namna wadau mbali mbali wanavyoweza kuchangia kwenye mijadala ya ufanisi wa sera na
serikali.
• Kujadili jinsi hatua za Maendeleo zinazofikiwa kwenye sekta mbali mbali zinavyoweza kufuatiliwa
kikamilifu sambamba na mwelekeo wa kimatokeo wa MKUKUTA
• Kuwa taarifa zitakazoongoza uandaaji wa miongozo mahsusi ya sera za kisekta na mipango mikakati
Mapitio ya kisekta na programu za maboresho zilizotumika kama chanzo cha MAIR (2007) :
Nguzo ya kwanza: Nguzo ya pili: Nguzo ya tatu:
Ukuaji wa Uchumi Uboreshaji wa Maisha Utawala Bora
na Upunguzaji na Ustawi wa Jamii na Uwajibikaji
wa Umaskini• Mapitio ya sekta ya Usafirishaji
• Mapitio ya sekta ya Nishati
• Mapitio ya sekta ya Kilimo
• Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria
• Programu ya Maboresho ya Utumishi wa
Umma
• Programu ya Maboresho ya Serikali za Mitaa
• Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa
Fedha
• Mkakati wa Taifa wa Mapambano dhidi ya
Rushwa na Mpango kazi
• Mapitio ya sekta ya Mazingira
• Mapitio ya sekta ya Elimu
• Mapitio ya sekta ya Maji
• Mapitio ya sekta ya Afya
38
Kiambatisho 3: Viunganishi Muhimu vya Intaneti
zingatia: [PV] inamaanisha kwamba mwongozo wa lugha rahisi unapatikana kwenye tovuti ya Hakikazi
Catalyst http://www.hakikazi.org/plain_language.htm
Machapisho Mbali Mbali ya Sera Muhimu za Kitaifa ni Pamoja na:Mkakati wa Taifa wa Kuondoa Umaskini (NPES) 1997
www.tzonline.org/pdf/thenationalpovertyeradicationstrategy.pdf
Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025 (1999)
www.tanzania.go.tz/vission_2025f.html
Mkakati wa Misaada wa Tanzania [PV]
www.tzonline.org/pdf/Tanzaniaassistancestrategy.pdf
Waraka wa Mkakati wa Upunguzaji Umaskini (2000) [PV]
www.tzonline.org/pdf/FinalPRSP25.pdf
Mpango Mkuu wa Ufuatiliaji wa Umaskini [PV]
www.tzonline.org/pdf/povertymonitoringmasterplan.pdf
Mkakati wa Taifa wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (2005) [PV]
www.povertymonitoring.go.tz/downloads/new/nsgrptext.pdf
Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (2005) (Kiambatisho)
www.povertymonitoring.go.tz/downloads/new/nsgrpmatrix.pdf
Mpango Mkuu wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA & Taarifa za Viashiria (Sehemu ya 1 &2) (2006)
www.povertymonitoring.go.tz/documents/mkukutamasterplan.pdf
Baadhi ya Ripoti Zinazohusu Ufuatiliaji wa Umaskini:Ripoti ya Maendeleo ya Waraka wa Mkakati wa Upunguzaji Umaskini (PV 2001)
www.mof.go.tz/index.php?option=com_content&task=view&id=172&Itemid=169
Tathmini Shirikishi ya Umaskini Tanzania (PV)
www.repoa.or.tz/content/blogcategory/35/67/
Ripoti ya Umaskini na Maendeleo ya Watu, Ripoti za Hali halisi na dondoo ya Sera
www.repoa.or.tz/content/blogcategory/35/67/
Mawasilisho ya mada mbali mbali za Wiki la Umaskini 2007
www.povertymonitoring.go.tz/Communications_reports.asp
Matokeo ya tafiti na sensa mbali mbali www.nbs.go.tz
Msaada wa Bajeti kwa ajili ya Kupunguza Umaskini (PRBS) www.tzdpg.or.tz/index.php?id=34
Mkakati wa Pamoja wa Misaada kwa Tanzania ( JAST) www.tzdpg.or.tz/index.php?id=8
Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA (MAIR)(2007) www.xxx
39
Tovuti Zenye Taarifa Zinazohusu Ufuatiliaji wa UmaskiniTovuti ya Ufuatiliaji wa Umaskini –ina habari mbali mbali kuhusu hatua za Maendeleo zilizofikiwa na
matokeo ya Mikakati ya Kupunguza Umaskini nchini na Mfumo wa Ufuatiliaji wa Umaskini
www.povertymonitoring.go.tz
Tanzania Mtandaoni -inatoa taarifa nyingi kuhusu masuala mbali mbali ya Maendeleo nchini Tanzania.
www.tzonline.org/
Lango kuu la Maendeleo Tanzania – husambaza taarifa, kubadilishana taarifa, Majadiliano ya kwenye
mtandao www.tanzaniagateway.org/
Taarifa za Kiuchumi na Kijamii – unaweza kupata taarifa sahihi kuhusu masuala mbali mbali ya viashiria
vya Uchumi na kijamii kwa lugha rahisi. www.tsed.org
Maana za Maneno Makuu Yaliyotumika (Faharasa)
Asasi za Kiraia Ma shirika, vyama, taasisi za kijamii, na mitandao mbali mbali kati ya familia na ngazi
ya taifa. Zinahusisha vikundi vya kujitolea na vya hisani, jumuiya za wazazi, vikundi vya wazee, vilabu
vya michezo, vikundi vya sanaa na utamaduni, vyama vya kitaaluma na kitaalamu, taasisi za kidini, vyama
na vikundi vya wafanyakazi
Hifadhi ya jamii ni huduma za ustawi wa jamii zenye kulenga kuwalinda dhidi ya matatizo ya kijamii
kama vile umaskini, uzee, ulemavu, na ukosefu wa ajira. Pia tembelea http://en.wikipedia.org/wiki/
Social_Protection
Huduma za jamii hizi ni huduma zinazotolewa na serikali kwa wananchi, ama moja kwa moja (kupitia
sekta ya umma) au kwa kufadhili sekta binafsi ili iweze kutoa huduma. Miongoni mwa huduma za jamii
ni pamoja na elimu, umeme, afya, majeshi, polisi, usafiri wa umma, simu, mipango miji, maji na huduma
za usafi. Kwa maelezo zaidi tazama http://en.wikipedia.org/wiki/Public_services
Huduma za kifedha ni huduma zinazotolewa na tasnia ya fedha zinazohusisha taasisi nyingi za
usimamizi wa fedha. Miongoni mwa taasisi hizo ni benki, makampuni ya bima, makampuni ya uuzaji wa
hisa, na baadhi ya kampuni za biashara zinazodhaminiwa na serikali.
Masuala mtambuka ni masuala yanayoweza kuathiri na kuathiriwa na sekta mbalimbali. Baadhi ya
masuala mtambuka makuu ni utawala bora, jinsia, mazingira, VVU/UKIMWI, hifadhi ya jamii kwa
makundi ya watu walio katika mazingira hatarishi. Unaweza kupata taarifa zaidi kwenye tovuti http://
www.agriculture.go.tz/Projects/ASDP/Cross-sectoral-issues.htm
Mdau ni mtu anayeweza kuathiri au kuathiriwa na kitendo fulani. Ufanyaji maamuzi mzuri unapaswa
kuzingatia mchango wa wadau wote.
Miundombinu ni pamoja na mifumo ya usafirishaji na mawasiliano, mitandao ya maji na umeme, taasisi
za umma kama shule, posta, na magereza.
Msaada wa Bajeti Ni aina ya msaada ambapo fedha zinatolewa na Wabia wa Maendeleo kusaidia
programu za serikali zikilenga ukuaji wa Uchumi na upunguzaji wa Umaskini. Fedha zinatolewa kwa
serikali husika na kutumika kwa kufuata mifumo yake ya usimamizi wa fedha na uwajibikaji.
Wabia wa Maendeleo Hawa ni wadau wa Maendeleo ya taifa, mbali ya serikali. Mara nyingi msamiati
huu hutumika kumaanisha mashirika ya kimataifa yanayotoa misaada, mikopo, uwekezaji na msaada wa
kiufundi.
40
Ubia baina ya sekta ya umma na ya binafsi (PPP) ni huduma inayoendeshwa na serikali au sekta binafsi
ikigharamiwa kwa ubia wa serikali na kampuni binafsi moja au zaidi. Wakati fulani mapato ya kodi
hutumika kama mtaji wa uwekezaji kwa shughuli zinazofanywa kwa ubia wa serikali na sekta binafsi au
kwa mkataba. Kwa namna nyingine mtaji wa uwekezaji hutolewa na sekta binafsi kwa kupewa msukumo
na serikali chini ya mkataba wa sekta binafsi kutoa huduma husika. Mchango wa serikali kwenye ubia wa
aina hii unaweza kuwa wa hali (kwa kuhamisha raslimali iliyopo)
Ukaguzi wa mahesabu Mchakato wa kutathmini kumbukumbu au mahesabu.
Ukuaji Mpana wa uchumi Ukuaji wa Uchumi ambao unamnufaisha kila mtu (Pia unajulikana kama
ukuaji unaojali watu maskini au ukuaji wa Uchumi wenye kujali usawa)
Uoanishaji wadau hukaa pamoja na kukukubaliana juu ya nadharia na vitendo vya kanuni zinazosimamia
ukuzaji wa uchumi na upunguzaji wa umaskini
Utawala bora unahusisha Uwazi, taasisi zinazowajibika, taratibu za haki za ufanyaji maamuzi,mifumo
ya kidemokrasia ya siasa na mahakama na uwezpo wa asasi hai na huru za kiraia.
Wadau wasio wa Kiserikali ni pamoja na Wabia wa Maendeleo, mashirika ya kijamii, (CBOs), Mashirika
yasiyo ya Kiserikali (NGOs), Taasisi za Kidini (FBOs), Taasisi za Kitaaluma, vyama vya wafanyakazi,
na sekta binafsi
41
ShukuraniWizara ya Fedha na Uchumi inatoa shukrani kwa mchango uliotolewa na wadau waliohusika katika
kutayarisha mwongozo huu wa lugha rahisi wa Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji MKUKUTA
2006/07.
.Michango ya watu na taasisi mbali mbali inatambuliwa, lakini shukrani za pekee ziende kwa timu
ya maofisa wa Wizara ya Fedha na Uchumi. Maofisa hawa walifanya kazi kubwa ya kuwezesha utoaji
wa kijitabu kwa kukipitia mara kwa mara na kutoa maoni ya kina ili kuhakikisha kuwa ni sahihi na
kamilifu.
Pia shukrani za pekee ziende kwa asasi ya kiraia ya Hakikazi Catalyst ambayo
ilijihusisha na utaalamu wa kutayarisha na kuwezesha toleo hili katika lugha za Kiingereza na
Kiswahili.
Kadhalika shukrani ziende kwa Nathan Mpangala kwa katuni zake zinazosisimua. Na kwa kazi ya
usanifu na uchapishaji shukrani ziwaendee Colour Print Tanzania Ltd.