mwl . mgisa mtebe +255-713-497-654 mgisamtebe
DESCRIPTION
IMANI YA USHINDI USHINDI JUU YA DHAMBI NA UASI. ‘ Hatua za Kumwezesha Mtu wa Mungu Kuishi Maisha Matakatifu. ’. Mwl . Mgisa Mtebe +255-713-497-654 www.mgisamtebe.org. HATUA ZA IMANI YA USHINDI. Malengo ; - PowerPoint PPT PresentationTRANSCRIPT
Mwl. Mgisa Mtebe
+255-713-497-654
www.mgisamtebe.org
IMANI YA USHINDIUSHINDI JUU YA
DHAMBI NA UASI.‘Hatua za Kumwezesha Mtu wa
Mungu Kuishi Maisha Matakatifu.’
HATUA ZA IMANI YA USHINDI
Malengo; Kumfundisha mtu wa Mungu
kutoka katika udhaifu na utumwa wa kushindwa na dhambi katika maisha yake
ya Wokovu (Kuokoka).
IMANI YA USHINDI
USHINDI DHIDI YA DHAMBI
Warumi 8:5-11
KANUNI ZA KIROHOWarumi 8:5-11
5 Kwa maana wale wanaoishi kwa kuufuata mwili huziweka nia zao katika vitu vya mwili,
lakini wale wanaoishi kwa kufuata Roho, huziweka nia zao katika mambo ya Roho.
KANUNI ZA KIROHOWarumi 8:5-11
6 Kwa maana kuwa na nia ya mwili ni mauti, bali kuwa na nia inayoongozwa na Roho ni uzima na amani. 7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui na Mungu, kwa maana haiitii sheria ya Mungu,
wala haiwezi kuitii.
KANUNI ZA KIROHOWarumi 8:5-11
8 Wale wanaotawaliwa na mwili, hawawezi kumpendeza Mungu. 9 Lakini ninyi, hamtawaliwi na mwili, bali na Roho, ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu.
Mtu ye yote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo.
KANUNI ZA KIROHOWarumi 8:5-11
10 Lakini kama Kristo anakaa ndani yenu, miili yenu
imekufa kwa sababu ya dhambi, lakini roho zenu zi
hai kwa sababu ya haki.
KANUNI ZA KIROHO
Warumi 8:5-1111 Nanyi ikiwa Roho wa Mungu
aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu anakaa ndani yenu, Yeye aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataihuisha pia miili
yenu ambayo hufa, kwa njia ya Roho Wake akaaye ndani yenu.
HATUA ZA IMANI YA USHINDI
1Yohana 5:1-41 ‘Kila mtu anayeamini kwamba, Yesu Kristo ni
Mwana wa Mungu, amezaliwa na Mungu…’
(Zab 82:6, Yoh 10:34-36)
HATUA ZA IMANI YA USHINDI
1Yohana 5:1-44 “Kwa maana, kila kitu kilichozaliwa na Mungu,
huushinda ulimwengu, na huku ndiko kushinda,
kuushindako ulimwengu, ni hiyo Imani yetu.”
2Petro 1:3-43 Kwa kuwa Uweza wake wa uungu umetupatia (au nguvu zake za uungu zimetupatia)
mambo yote tunayohitaji kwa ajili ya maisha na utakatifu, kwa
kumjua Yeye aliyetuita kwa utukufu Wake na wema Wake
mwenyewe.
KANUNI ZA MAISHA YA USHINDI
2Petro 1:3-44 Kwa sababu hiyo, Mungu
ametukirimia ahadi zake kuu na za thamani, ili kwa kupitia hizo tupate kuwa washiriki wa tabia
za uungu, tukiokolewa na uharibifu (au upotovu) ulioko duniani kwa sababu ya tamaa.
KUTEMBEA KWA IMANI
IMANI YA USHINDI
Ndani ya kila mtoto wa Mungu, kuna Sura na Mfano
wa Mungu, (yaani asili ya Mungu) ambayo inakupa asili
ya ushindi ndani yako, dhidi ya kila upinzani wa adui shetani
maishani mwako.
UTU MPYA WA KRISTO
Roho zetu zina uwezo wa Ki-Mungu wa kutawala miili yetu
katika maisha ya Utakatifu, ni ile hali ya kukosea kujiona, ndicho kitu kinachozima utendaji kazi
wa Nguvu za Mungu unaowezesha ushindi huo.
KANUNI ZA KIROHO1Yoh 5:4, Rum 8:37
Pamoja na kwamba Neno la Mungu linatuahidi Ushindi wa Yesu msalabani, kuwa ushindi wetu sisi tuaminio; lakini bado waumini wengi tunaishi maisha
ya utumwa juu ya dhambi.
UTU MPYA WA KRISTO
Warumi 8:5-12Ikiwa roho zetu zina uwezo wa Ki-
Mungu wa kutawala miili yetu katika maisha ya Utakatifu, ni
kitu gani basi kinazima utendaji kazi wa Nguvu za Mungu
unaowezesha ushindi huo?
USHINDI JUU YA DHAMBI1Yohana 5:4, Mathayo 17:19-21
Imani ni uhakika wa kazi ya Yesu msalabani. Ukikosea kujiona,
utakosea kujiwaza; na utakosea kuongea. Makosa hayo,
yatazima utendaji kazi wa nguvu za Mungu unaohusika na
kukusaidia kushinda.
KANUNI ZA KIROHO
KUSTAHILISHWAPASIPO KUSTAHILI
Warumi 5:17-19Warumi 6:5-6, 11-14
KANUNI ZA KIROHOWarumi 5:17-19
18 … kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta hukumu
kwa watu wote, vivyo hivyo pia kwa tendo la mtu mmoja
la haki watu wote wamehesabiwa haki.
KANUNI ZA KIROHOWarumi 5:17-19
19 Kwa maana kama vile kwa kutokutii yule mtu mmoja,
watu wote walifanywa wenye dhambi, vivyo hivyo kwa kutii kwa mtu mmoja
wengi wamefanywa wenye haki.
KANUNI ZA KIROHOWarumi 5:17-19
17 Kwa maana ikiwa kwa kosa la mtu mmoja, mauti
ilitawala kupitia huyo mtu mmoja, zaidi sana wale wanaopokea wingi wa neema ya Mungu na
kuhesabiwa haki [wokovu], …
KANUNI ZA KIROHOWarumi 5:17-19
17 … wale wanaopokea wingi wa neema ya Mungu na
kuhesabiwa haki [wokovu], watatawala katika uzima
kwa njia ya huyo mtu mmoja, yaani, Yesu Kristo.
USHINDI JUU YA DHAMBIWarumi 5:17-19
Torati Neema
Kosa la Mtu 1, Tendo la Mtu 1, Wote ni Wote ni ‘Wakosaji’ ‘Wenye-Haki’(Wenye Dhambi) (Watakatifu)
USHINDI JUU YA DHAMBIWaefeso 2:8-10
9 Si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. 10 Kwa
maana sisi ni kazi ya mikono ya Mungu, tulioumbwa
katika Kristo Yesu (utakatifu) …
USHINDI JUU YA DHAMBIWaefeso 2:8-10
10 … tulioumbwa katika Kristo Yesu, ili tupate
kutenda matendo mema, ambayo Mungu alitangulia
kuyaandaa tupate kuishi katika hayo.
USHINDI JUU YA DHAMBIWaefeso 2:8-10
Matendo mema yaliumbwa kwa ajili ya watakatifu
(wenye-haki); ndo kusema, kutenda mema wakati uko
upande wa Wakosaji, haikufanyi Mwenye haki
mbele za Mungu.
USHINDI JUU YA DHAMBIWaefeso 2:8-10
Matendo mema yaliumbwa kwa ajili ya watakatifu
(wenye-haki); ndo kusema, kutenda mema wakati uko
upande wa Wakosaji, haikufanyi Mwenye haki
mbele za Mungu.
USHINDI JUU YA DHAMBIWaefeso 2:8-10Ndio kusema;
Kufanya Makosa wakati uko upande wa Wenye-Haki,
haikufanyi ‘Mwenye Dhambi’ mbele za Mungu.
USHINDI JUU YA DHAMBIWarumi 5:17-19
Torati Neema Upande wa Upande wa ‘Wakosaji’ ‘Wenye-Haki’
Matendo mema ‘Makosa’ Hayakuingizi HayakuondoiKtk Stahili/Haki. ktk Stahili/Haki.
USHINDI JUU YA DHAMBIWarumi 5:17-19
Torati Neema Upande wa Upande wa ‘Wakosaji’ ‘Wenye-Haki’
Matendo mema ‘Makosa’ Hayakuingizi Hayakuondoi ktk Utakatifu. ktk Utakatifu.
USHINDI JUU YA DHAMBI
Hatua ya kwanza;Warumi 6:5-6, 11-14
11 kujihesabuni mfu katika dhambi lakini mlio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu;
Yaani “Mtakatifu”
KANUNI ZA KIROHOWarumi 6:5-6, 11-14
4. MATOKEO; 14 Kwa maana dhambi
haitakuwa na mamlaka juu yenu, kwa sababu hampo
chini ya sheria, bali chini ya neema.
KANUNI ZA KIROHO
Warumi 6:5-6, 11-14 Hii ndio kusema;
Dhambi itakuwa na mamlaka juu yenu, endapo
mtajihesabu mpo chini ya sheria (torati), na si chini ya
neema.… (ajionavyo mtu nafsini mwake)
KUTEMBEA NA NGUVU ZA MUNGU
Mawazo ya UshindiMithali 23:7
‘ajionavyo mtu nafsini mwake (kwenye mawazo yake)
ndivyo alivyo (atakavyokuwa)’
KUTEMBEA NA NGUVU ZA MUNGU
Macho ya RohoniMithali 24:14
‘Basi utaijua hekima kuwa tamu kwa nafsi yako, ikiwa
umekwisha kuiona (kuipata) ndipo itakapokuja thawabu
yako, wala hutalikosa tarajio lako’
KANUNI ZA KIROHO
Waebrania 11:1, 6 1 Imani ni kuwa na hakika
wa mambo yasiyoonekana
(kabla ya kuona katika ulimwengu wa mwili).
USHINDI JUU YA DHAMBIWarumi 5:17-19
Torati Neema
Upande wa Upande wa Wote ni Wote ni ‘Wakosaji’ ‘Wenye-Haki’(Wenye Dhambi) (Watakatifu)
USHINDI JUU YA DHAMBI1Yohana 5:4, Mathayo 17:19-21
Imani ni uhakika wa kazi ya Yesu msalabani. Ukikosea kujiona,
utakosea kujiwaza; na utakosea kuongea. Makosa hayo,
yatazima utendaji kazi wa nguvu za Mungu unaohusika na
kukusaidia kushinda.
KANUNI ZA KIROHO
Warumi 6:5-6, 11-14 Hii ndio kusema;
Njia ya kuvunja ‘sheria ya dhambi’ (kimwili) ni kutembea kwa Imani
kwamba wewe ni Kiumbe Kipya.
(tayari umeshakuwa)
KANUNI ZA KIROHO
Waebrania 11:1, 6
6 “Kwa maana pasipo Imani haiwezekani
kumpendeza Mungu”.
KANUNI ZA KIROHO
Waebrania 10:38
38 “Mwenye haki wangu ataishi kwa Imani, naye
akisisita-sita, Roho yangu haina furaha naye”.
UTU MPYA WA KRISTO
Roho zetu zina uwezo wa Ki-Mungu wa kutawala miili yetu
katika maisha ya Utakatifu, ni ile hali ya kukosea kujiona, ndicho kitu kinachozima utendaji kazi
wa Nguvu za Mungu unaowezesha ushindi huo.
USHINDI JUU YA DHAMBI
Warumi 6:5-6, 11-14
Hatua ya kwanza;Kuelekea ushindi
juu Dhambi.
KANUNI ZA KIROHO
KustahilishwaWarumi 5:17-19
USHINDI JUU YA DHAMBIWarumi 5:17-19
Torati Neema Upande wa Upande wa ‘Wakosaji’ ‘Wenye-Haki’
Matendo mema ‘Makosa’ Hayakuingizi HayakuondoiKtk Stahili/Haki. ktk Stahili/Haki.
USHINDI JUU YA DHAMBIWarumi 5:17-19
Torati Neema Upande wa Upande wa ‘Wakosaji’ ‘Wenye-Haki’
Matendo mema ‘Makosa’ Hayakuingizi Hayakuondoi ktk Utakatifu. ktk Utakatifu.
IMANI YA USHINDI
MAISHA BAADA YA WOKOVU
- Swali Muhimu -
Warumi 5:17-19, Warumi 6:15Eti kwasababu katika Neema
ya Wokovu, tunahesabiwa haki hata kama tumekosea, Je, hii ina maana kwamba, tunaweza kuendelea tu na
maisha ya dhambi na anasa?
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Warumi 5:17-19
Jibu ni Hapana!
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Warumi 5:17-19Na Mungu akijua kwamba, dhana hii ya kustahilishwa, itazaa maswali ya namna hii
ndani ya watu, akaandika yafuatayo, kupitia mkono wa Mtume Paulo, ili tusipotoke.
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILIWarumi 6:15, 1-2
15 Ni nini basi? [Je,] tufanye dhambi [eti] kwasababu hatuwi [hatupo] chini ya
sheria [torati], bali chini ya Neema [wokovu]? Hasha
[hapana kabisa]
Warumi 6:15, 1-21 Tuseme nini basi? Je, tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?
2. Hasha! [hapana kabisa]
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
KANUNI ZA KIROHO
Warumi 6:15, 1-2
2. Hasha! Sisi tulioifia dhambi, tutaishije tena
katika dhambi?
Warumi 5:17-19
Eti kwasababu katika Neema ya Wokovu, tunahesabiwa haki hata kama tumekosea,
haina maana kwamba, tunaweza kuendelea tu na
maisha ya dhambi na anasa!
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Warumi 4:17-3417 Tangu sasa nawaambia hivi,
tena nawasisitiza katika Bwana, kwamba, msienende
[wala msiishi] tena kama watu Mataifa waishivyo, katika ubatili wa mawazo yao.
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Warumi 4:17-3418 Watu hao akili zao
zimetiwa giza na wametengwa mbali na uzima wa Mungu kwa
sababu ya ujinga wao na ugumu wa mioyo yao.
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Warumi 4:17-3419 Wakiisha kufa ganzi,
wamejitia katika mambo ya ufisadi na kupendelea kila
aina ya uchafu, wakiendelea kutamani zaidi.
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Warumi 4:17-3420 Lakini ninyi, hivyo sivyo
mlivyomjifunza Kristo. 21 Kama hivyo ndivyo ilivyo,
ninyi mmemsikia, tena mmefundishwa naye, vile kweli ilivyo katika Yesu.
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Warumi 4:17-34
22 Mlifundishwa kuuvua mwenendo wenu wa
zamani, utu wenu wa kale, ulioharibiwa na tamaa zake
za udanganyifu.
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Warumi 4:17-3423 Mfanywe upya roho ya nia
zenu, 24 mkajivike utu mpya, ulioumbwa sawa
sawa na mfano wa Mungu katika haki yote na
utakatifu.
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Warumi 4:17-3425 Kwa hiyo kila mmoja wenu
avue uongo na kuambiana kweli mtu na jirani yake, kwa maana sisi sote tu
viungo vya mwili mmoja.
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Warumi 4:17-34
26 Mkikasirika, msitende dhambi, wala jua lisichwe mkiwa bado mmekasirika,
27 wala msimpe ibilisi nafasi.
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Warumi 4:17-34
28 Yeye ambaye amekuwa akiiba, asiibe tena, bali afanye kazi zake mwenyewe, ili awe
na kitu cha kuwagawia wahitaji.
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Warumi 4:17-34
29 Maneno mabayamwenu, bali yale yafaayo
kwa ajili ya kuwajenga wengine kulingana na
mahitaji yao, ili yawafae wale wasikiao.
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Warumi 4:17-34
30 Wala msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu,
ambaye kwa huyo mlitiwa muhuri kwa ajili ya siku ya
ukombozi.
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Warumi 4:17-34
31 Ondoeni kabisa uchungu, ghadhabu, hasira, makelele
na masingizio pamoja na kila aina ya uovu.
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Warumi 4:17-34
32 [Msiwe na choyo, bali] Iweni wafadhili [ninyi kwa
ninyi] na wenye kuhurumiana [kama Mungu alivyomtoa Mwanaye kwa
ajili yenu],
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Warumi 4:17-34
32 … [Msiwe na kinyogo, bali] msameheane [ninyi kwa
ninyi], kama vile naye Mungu katika Kristo
alivyowasamehe ninyi [makosa yenu].
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Mungu anatuonyesha kuwa, Eti kwasababu katika Neema
ya Wokovu, tunahesabiwa haki hata kama tumekosea,
haina maana kwamba, tunaweza kuendelea tu na
maisha ya dhambi na anasa!
USHINDI JUU YA DHAMBI
Pamoja na kwamba, Mungu ametupa [ametuhesabia]
Utakatifu wa Kristo, bado kila mtoto wa Mungu anatakiwa kudumisha maisha safi na ya
Utakatifu binafsi katika maisha yake.
USHINDI JUU YA DHAMBI
Hii ina maana kwamba;Kuna Utakatifu wa aina mbili. [1]. Utakatifu wa Kristo, Tuliopewa Bure kwa Neema
[2]. Utakatifu wa mtu, Unatakiwa kudumishwa.
USHINDI JUU YA DHAMBI
Ufunuo 22:10-1211 ... Mwenye haki azidi
kutenda haki na yeye aliye Mtakatifu [1] na aendelee
kuwa Mtakatifu [2].’’
USHINDI JUU YA DHAMBI
Pamoja na kwamba, Mungu ametupa [ametuhesabia]
Utakatifu wa Kristo, bado kila mtoto wa Mungu anatakiwa kudumisha maisha safi na ya
Utakatifu binafsi katika maisha yake.
USHINDI JUU YA DHAMBI
1Petro 1:15-16
Mungu hana ushirika na dhambi; anachukia dhambi
na hapendi kuiona. Ndio maana anasisitiza Utakatifu
katika mwenendo wetu wote.
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
USHINDI JUU YA DHAMBI
Warumi 6:23 Mauti Uzima
Torati NeemaMungu hakuwa Mungu huwa na ‘Uvumilivu’ ‘Uvumilivu’
wowote mkubwajuu ya Dhambi. juu ya dhambi.
Warumi 6:23Mungu wetu habadiliki,
japo Njia za Mungu hubadilika, lakini Mungu bado
ana tabia zake zile zile za kuchukia dhambi na uasi.
USHINDI JUU YA DHAMBI
1Petro 1:15-19
15 Bali kama Yeye aliyewaita alivyo Mtakatifu, ninyi nanyi
iweni Watakatifu katika mwenendo wenu wote, …
USHINDI JUU YA DHAMBI
1Petro 1:15-19
16 kwa maana imeandikwa: “Mtakuwa Watakatifu, kwa kuwa Mimi ni Mtakatifu.”
USHINDI JUU YA DHAMBI
1Petro 1:15-19
17 Nanyi kama mnamwita “Baba,” Yeye ahukumuye kila
mtu kulingana na matendo yake pasipo upendeleo …
USHINDI JUU YA DHAMBI
1Petro 1:15-19
17 … enendeni kwa hofu ya kumcha Mungu wakati wenu wa kukaa hapa duniani kama
wageni [na wapitaji].
USHINDI JUU YA DHAMBI
1Petro 1:15-19
18 Kwa maana mnafahamu kwamba mlikombolewa
kutoka katika mwenendo wenu usiofaa ambao mliurithi
kutoka kwa baba zenu, …
USHINDI JUU YA DHAMBI
1Petro 1:15-19
18 …mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, yaani, kwa
fedha na dhahabu, …
USHINDI JUU YA DHAMBI
1Petro 1:15-19
19 bali mlikombolewa kwa damu ya thamani ya Kristo, kama ile ya Mwana-Kondoo
asiye na dosari wala doa.
USHINDI JUU YA DHAMBI
1Petro 1:15-19
15 [kwahiyo] kama Yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu
katika mwenendo wenu wote
USHINDI JUU YA DHAMBI
1Petro 1:15-16
Mungu hana ushirika na dhambi; anachukia dhambi
na hapendi kuiona. Ndio maana anasisitiza Utakatifu
katika mwenendo wetu wote.
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Ufunuo 22:10-1210 Kisha akaniambia,
“Usiyafunge maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, kwa sababu
wakati umekaribia.
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Ufunuo 22:10-12
11 Atendaye mabaya na aendelee kutenda mabaya, aliye mchafu na aendelee
kuwa mchafu, ...’’
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Ufunuo 22:10-12
11 ... Mwenye haki azidi kutenda haki na yeye aliye
Mtakatifu na aendelee kuwa Mtakatifu.’’
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Ufunuo 22:10-12
12 “Tazama, naja upesi! nikiwa na mshahara wangu,
nami nitamlipa kila mtu sawasawa na alivyotenda.
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
1Wakorintho 6:14-18
Mungu hana ushirika na dhambi; anachukia dhambi
na hapendi kuiona. Ndio maana anasisitiza Utakatifu
katika mwenendo wetu wote.
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
1Wakorintho 6:14-18
‘... Hakuna ushirika kati ya nuru na giza ...’
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Kwahiyo, Eti kwasababu katika Neema, tunakuwa chini
ya mwamvuli wa haki ya Kristo hata kama tumekosea,
haina maana kwamba, tunaweza kuendelea tu na
maisha ya dhambi na anasa!
USHINDI JUU YA DHAMBI
1Wakorintho 6:14-18Katika Agano Jipya, Mungu akikutana na dhambi; ataipa muda wa ‘neema’. Muda wa
‘neema’ ukiisha, Mungu anaihikumu dhambi mara
moja, bila kusita.
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
1Wakorintho 9:27Kwahiyo, kila siku, nautesa [naudhibiti] mwili wangu, ili
[isije ikatokea kwamba] nikiisha kuwahubiri
wengine, mimi mwenyewe nikawa mtu wa kukataliwa.
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
1Wakorintho 9:27Hii ni picha ya wazi kwamba;
Hata walio chini ya Neema wanaweza kuhukumiwa
adhabu na pia wanaweza kukosa kuingia katika
Ufalme wa Mungu, mbinguni.
KUSTAHILISHWA PASIPO KUSTAHILI
Kwahiyo, pamoja na kwamba, Mungu Baba ametupa
[ametuhesabia] Utakatifu wa Kristo, bado kila mtoto wa
Mungu anatakiwa kudumisha maisha safi na ya Utakatifu binafsi katika maisha yake.
USHINDI JUU YA DHAMBI
IMANI YA USHINDI
USHINDI DHIDI YA DHAMBI
Warumi 8:5-11
KANUNI ZA KIROHOWarumi 8:5-11
5 Kwa maana wale wanaoishi kwa kuufuata mwili huziweka nia zao katika vitu vya mwili,
lakini wale wanaoishi kwa kufuata Roho, huziweka nia zao katika mambo ya Roho.
KANUNI ZA KIROHOWarumi 8:5-11
6 Kwa maana kuwa na nia ya mwili ni mauti, bali kuwa na nia inayoongozwa na Roho ni uzima na amani. 7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui na Mungu, kwa maana haiitii sheria ya Mungu,
wala haiwezi kuitii.
KANUNI ZA KIROHOWarumi 8:5-11
8 Wale wanaotawaliwa na mwili, hawawezi kumpendeza Mungu. 9 Lakini ninyi, hamtawaliwi na mwili, bali na Roho, ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu.
Mtu ye yote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo.
KANUNI ZA KIROHOWarumi 8:5-11
10 Lakini kama Kristo anakaa ndani yenu, miili yenu
imekufa kwa sababu ya dhambi, lakini roho zenu zi
hai kwa sababu ya haki.
KANUNI ZA KIROHO
Warumi 8:5-1111 Nanyi ikiwa Roho wa Mungu
aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu anakaa ndani yenu, Yeye aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataihuisha pia miili
yenu ambayo hufa, kwa njia ya Roho Wake akaaye ndani yenu.
USHINDI JUU YA DHAMBI
Hatua ya kwanza;Warumi 6:5-6, 11-14
11 kujihesabuni mfu katika dhambi lakini mlio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu;
Yaani “Mtakatifu”
KANUNI ZA KIROHO
Warumi 6:5-6, 11-1412 Kwa hiyo, msiruhusu dhambi itawale ndani ya
miili yenu, ipatikanayo na kufa, ili kuwafanya mzitii
tamaa mbaya.
KANUNI ZA KIROHO
Warumi 6:5-6, 11-14 14 Kwa maana dhambi
haitakuwa na mamlaka juu yenu, kwa sababu hampo
chini ya sheria, bali chini ya neema.
HATUA ZA IMANI YA USHINDI
1Yohana 5:1-41 ‘Kila mtu anayeamini kwamba, Yesu Kristo ni
Mwana wa Mungu, amezaliwa na Mungu…’
(Zab 82:6, Yoh 10:34-36)
HATUA ZA IMANI YA USHINDI
1Yohana 5:1-44 “Kwa maana, kila kitu kilichozaliwa na Mungu,
huushinda ulimwengu, na huku ndiko kushinda,
kuushindako ulimwengu, ni hiyo Imani yetu.”
1Yoh 5:4, Rum 8:37
Ndani ya kila mtoto wa Mungu, kuna Sura na Mfano
wa Mungu, (yaani asili ya Mungu) ambayo inakupa asili
ya ushindi ndani yako, dhidi ya kila upinzani wa adui shetani
maishani mwako.
KANUNI ZA KIROHO1Yoh 5:4, Rum 8:37
Pamoja na kwamba Neno la Mungu linatuahidi Ushindi wa Yesu msalabani, kuwa ushindi wetu sisi tuaminio; lakini bado waumini wengi tunaishi maisha
ya utumwa juu ya dhambi.
UTU MPYA WA KRISTO
Warumi 8:5-12 Ikiwa roho zetu zina uwezo wa
Ki-Mungu wa kutawala miili yetu katika maisha ya
Utakatifu, ni kitu gani basi kinazima utendaji kazi wa
Nguvu za Mungu unaowezesha ushindi huo?
KABLA YA DHAMBI (ANGUKO)
Utukufu (Msaada) Mungu Mwili Roho Dunia NafsiShetani
BAADA YA DHAMBI
Msaada Ukakatika Mungu Mwili Roho Dunia Nafsi Shetani
BAADA YA WOKOVU
(Utukufu) Roho Mt. Mungu Mwili Roho Dunia Nafsi Shetani (Rum 8:9-11)
VITA YA MWILI NA ROHO
Utukufu (Msaada) Mungu Mwili Roho Dunia Nafsi Shetani (Rum 8:9-11)
UTU MPYA WA KRISTO
Warumi 8:5-12 Ikiwa roho zetu zina uwezo wa
Ki-Mungu wa kutawala miili yetu katika maisha ya
Utakatifu, ni kitu gani basi kinazima utendaji kazi wa
Nguvu za Mungu unaowezesha ushindi huo?
USHINDI JUU YA DHAMBI1Yohana 5:4, Mathayo 17:19-21
Imani ni uhakika wa kazi ya Yesu msalabani. Hivyo, ukikosea
kujiona, utakosea kujiwaza; na utakosea kuongea. Makosa
hayo, yatazima utendaji kazi wa nguvu za Mungu unaohusika na kukusaidia kushinda dhambi.
KANUNI ZA KIROHO
Warumi 6:5-6, 11-14 Hii ndio kusema;
Dhambi itakuwa na mamlaka juu yenu, endapo
mtajihesabu mpo chini ya sheria (torati), na si chini ya
neema.… (ajionavyo mtu nafsini mwake)
KUTEMBEA NA NGUVU ZA MUNGU
Mawazo ya UshindiMithali 23:7
‘ajionavyo mtu nafsini mwake (kwenye mawazo yake)
ndivyo alivyo (atakavyokuwa)’
KANUNI ZA KIROHO
Warumi 6:5-6, 11-14 Hii ndio kusema;
Njia ya kuvunja ‘sheria ya dhambi’ (kimwili) ni
kutembea kwa Imani kwamba wewe ni Kiumbe
Kipya (tayari umeshakuwa).
KUTEMBEA KWA IMANI
Hatua za Imani Timilifu
Waebrania 11:1
Marko 11:23-24Ulimwengu wa roho
Tumaini Imani “Nita …” mnayapokea “Nime ….” (sasa)
Kuanza IMANI yatakuwa
maombi (baadaye)
Ulimwengu wa mwili
KUTEMBEA KWA IMANIHatua Muhimu ya Kwanza
1. Kupata na Kutumia
Neno la Mungu. Waebrania 11:3 Warumi 10:17
HATUA ZA IMANI YA USHINDI
2. Kuomba kwa Bidii na Nidhamu ili Kuumba. - Maombi ya Kuumba -
Yakobo 5:17-18, 161Wafalme 18:29-45
3. Usikivu kwa Uongozi wa
Roho MtakatifuWarumi 8:16, 26-27
2Tim 3:16-17
KUTEMBEA KWA IMANI
4.Kubadilisha Mtazamo(a)Kuona tofauti (Machoni)(b)Kuwaza tofauti (Fikra)
Waefeso 1:15-19
KUTEMBEA KWA IMANI
KUTEMBEA KWA IMANI
5. Kuamuru na Kutabiri.- Maombi ya Kufungulia -
Marko 11:23-24Ezekieli 37:1-14
KUTEMBEA NA NGUVU ZA MUNGU
Marko 11:23-2423 ‘… ukiuambia mlima huu ng’oka, bila mashaka [kwa
uhakika], huku ukiamini kwamba, hayo uyasemayo,
yametokea [tayari, sasa], basi yatakuwa yako [baadaye].’
KUTEMBEA NA NGUVU ZA MUNGU
Marko 11:23-2424 ‘… Amini Amini
nawaambia, mambo yoyote mwombayo mkisali, aminini
mnayapokea [sasa], nayo yatakuwa yenu [baadaye].’
KUTEMBEA KWA IMANI YA USHINDI
Marko 11:23-24 mnayapokea yatakuwa yenu
(sasa) (baadaye)
Ulimwengu wa Ulimwengu wa kiroho kimwili
KANUNI ZA KIROHO
Mambo Mambo ya ya Kimwili Vs Kiroho (Vitu vinavyo- (Vitu Visivyo- Onekana) Onekana)
KANUNI ZA KIROHOWaebrania 11:3
Utaratibu wa Mungu katika kuleta mabadiliko duniani; ni
kwamba, mambo yanayotakiwa kufanyika katika ulimwengu wa kimwili, sharti yafanyike kwanza
katika ulimwengu wa kiroho.
KANUNI ZA KIROHOEbr 11:3, 1Yoh 5:4
Mtu wa Mungu ukitaka kuleta mabadiliko fulani katika ulimwengu wa mwili, ili
utembee kwa ushindi duniani, ni lazima ujue kuutawala
ulimwengu wa roho kwanza.
KUTEMBEA KWA IMANI Siri ya kutembea kwa imani (uhakika) ipo katika kupata
Neno, utakaloliatamia kwa njia ya maombi, ili kuleta mabadiliko
unayoyahitaji (rohoni), kisha utabiri (baada ya kupata uhakika
(imani) rohoni), ili kuyaumba mambo hayo katika U’mwili.
Imani ya Ushindi
Kama vile Roho Mtakatifu alivyohitaji utumie Neno la
Mungu kwa ajili ya uumbaji wa hitaji lako katika ulimwengu wa roho, vile vile atahitaji utumie
Neno kwa ajili ya uumbaji katika ulimwengu wa mwili.
KUTEMBEA NA NGUVU ZA MUNGU
Marko 11:23-2423 ‘… ukiuambia mlima huu ng’oka, bila mashaka [kwa
uhakika], huku ukiamini kwamba, hayo uyasemayo,
yametokea [tayari, sasa], basi yatakuwa yako [baadaye].’
KUTEMBEA NA NGUVU ZA MUNGU
Ufunuo 5:9-10Katika Agano Jipya, Mungu
ametufanya sisi Makuhani na Wafalme katika Ufalme wake, ili kumiliki na kutawala dunia sawa-sawa na mapenzi yake.
MAMLAKA YA MKRISTO
Ufunuo 5:9-1010 Nawe umewafanya hawa
wawe Ufalme na Makuhani wa kumtumikia Mungu wetu, nao
wanamiliki dunia.’’
KANUNI ZA KIROHO
Kuhani Mfalme Kuwasiliana na Kuamuru na Mungu ili Kutawala Kuumba mambo mambo katika ktk ulimwengu ulimwengu wa roho. wa mwili.
MAMLAKA YA MKRISTO
Ufunuo 5:9-10Mfalme hutawala kwa
Nguvu ya Neno lake.
Mhubiri 8:4‘Neno la Mfalme ni Amri’
Imani ya UshindiBaada ya kuumba jambo
pamoja na Mungu kiroho (kama Makuhani) Mungu atasubiri tufanye sehemu yetu pia ya
kuamuru (kama Wafalme) ili na yeye afanye sehemu yake, ya kuumba jambo hilo kimwili.
KANUNI ZA KIROHO
Mungu Mfalme
Kuhani Mazingira
USHIRIKA WA MUNGU NA MKRISTO
1Wakorintho 9:6, Warumi 8:28
6 ‘Kwa maana sisi tu watenda kazi pamoja na Mungu …’
28 ‘Katika mambo yote, Mungu hufanya kazi pamoja na wale
[watu] wampendao …’
MAMLAKA YA MKRISTO
Mathayo 16:19,1819 Mambo mtakayoyafunga
duniani, yatafungwa mbinguni, na mambo mtakayoyafungua
duniani, ytafunguliwa mbinguni.
MAMLAKA YA MKRISTO
Mfano;Utabiri (Uamuru) wa
Nabii EzekieliEzekieli 37:1-14
MAMLAKA YA MKRISTO
Ezekieli 37:1-14Mungu alihitaji “mwanadamu”
ili aweze kutimiza kusudi lake la kuifufua mifupa (jeshi) ya Israeli, kutoka katika bonde
lililozika wafu wa kivita.
MAMLAKA YA MKRISTO
Ezekieli 37:1-14 Kwahiyo, kuna wakati, ili
Nguvu za Mungu ziingie kazini, kuvunja upinzani (Nguvu ya dhambi), ni lazima mtu wa
Mungu ajifunze kuamuru na kuagiza jambo hilo kufanyika.
MAMLAKA YA MKRISTO
Mathayo 16:19/18:18
Mambo mtakayoyafunga (ninyi) duniani (mwilini)
yatafungwa pia mbinguni (rohoni) …
MAMLAKA YA MKRISTO
Mathayo 16:19/18:18
Mambo mtakayoyafungua (ninyi) duniani (mwilini),
yatakuwa yamefungwa pia mbinguni (rohoni).
MAMLAKA YA MKRISTO
1Kor 3:9, Rum 8:28Sisi ni watenda kazi pamoja na
Mungu duniani; na katika mambo yote, Mungu hufanya
kazi pamoja na wale (watu) wampendao, katika kuwapatia
mema (baraka/ushindi).
MAMLAKA YA MKRISTO
1Kor 3:9 Rum 8:28Mungu anaweza kufanya kila
kitu pasipo msaada wa binadamu, na alishafanya mengi; lakini alichagua tu
kufanya kazi pamoja na sisi.
MAMLAKA YA MKRISTO
Mwanzo 1:26-28 Tufanye mtu kwa sura yetu na kwa mfano wetu, ili (wao
binadamu) ndio waende wakatawale dunia na vyote
viijazavyo.
MAMLAKA YA MKRISTO
Isaya 45:11Haya ndiyo asemayo Bwana
Mwenyezi; niulizeni habari za mambo yajayo, na Kwa habari
ya kazi za mikono yangu, ‘haya niamuruni’.
MAMLAKA YA MKRISTO
Ezekieli 37:1-14Mungu alihitaji “mwanadamu”
ili aweze kutimiza kusudi lake la kuifufua mifupa (jeshi) ya Israeli, kutoka katika bonde
lililozika wafu wa kivita.
Imani ya Ushindi
Kwahiyo, kama vile Roho Mtakatifu alivyohitaji utumie
Neno la Mungu ili kuumba hitaji lako katika ulimwengu wa roho, vile vile Roho atahitaji uachilie
Neno kwa ajili ya uumbaji katika ulimwengu wa mwili.
Imani ya UshindiBaada ya kuumba jambo
pamoja na Mungu kiroho (kama Makuhani) Mungu atasubiri tufanye sehemu yetu pia ya
kuamuru (kama Wafalme) ili na yeye afanye sehemu yake, ya kuumba jambo hilo kimwili.
Imani ya Ushindi
Hii ni kwasababu Mungu ameweka USHIRIKA kati yake na sisi Binadamu, katika kumiliki na kutawala
mambo ya dunia.
Imani ya UshindiMtu wa Mungu asipofanya
sehemu yake, hali hiyo itamzuia Mungu kufanya sehemu yake.
‘Mambo mtakayoyafunga (ninyi) duniani, na Mungu atayafunga mbinguni …’
Mathayo 16:19
Yohana 11:1-39-45Mungu anatuonyesha
kwamba, sisi kama watoto wa Mungu ‘tuna wajibu’ katika utendaji kazi wa
nguvu za Mungu maishani mwetu.
KUAMURU MATOKEO
Wajibu Wetu Pamoja na Mungu;• Shusha Nyavu (Luka 5:4)• Jaza Maji Mabalasi (Yoh 2:7)• Nenda Kanawe (Yoh 9:7)• Liondoeni Jiwe (Yoh 11:29)• Mfungueni Sanda (Yoh
11:44)
KUAMURU MATOKEO
Imani ya UshindiKumbe Mtu wa Mungu
asipofafunga mambo hayo, Mungu atazuilika kuyafunga,
hata kama alitaka kuyafunga. ‘Mbingu ni mbingu za Bwana, bali NCHI (Dunia) amewapa Wanadamu.’ (Zaburi 115:16)
UTU MPYA WA KRISTO
Ili kuvunja nguvu ya dhambi, [kimwili] kwa kutumia Nguvu za Mungu, baada ya toba, mtu wa Mungu atatakiwa kuamuru na kutabiri [Kifalme], mabadiliko anayotamani maishani mwake
katika mwenendo [Kimwili].
UTU MPYA WA KRISTO
Ili kuvunja nguvu ya dhambi, [kimwili] kwa kutumia Nguvu za Mungu, baada ya toba, mtu wa Mungu atatakiwa kuamuru na kutabiri [Kifalme], mabadiliko anayotamani maishani mwake
katika mwenendo [Kimwili].
Imani ya Ushindi
Kama vile Roho Mtakatifu alivyohitaji utumie Neno la
Mungu kwa ajili ya uumbaji wa hitaji lako katika ulimwengu wa roho, vile vile atahitaji utumie
Neno kwa ajili ya uumbaji katika ulimwengu wa mwili.
Hatua za Imani ya Ushindi
(Warumi 10:17)
‘Imani yenye Nguvu ya kuhamisha milima,
huzaliwa kwa Neno la Mungu lililovuviwa.
Hatua za Imani ya Ushindi
Waebrania 4:12‘Neno la Mungu li hai,
tena lina Nguvu’ (ya kutenda hata kuleta
mabadiliko)
Hatua za Imani ya Ushindi
Waebrania 11:3,‘Nasi twajua ya kuwa,
Ulimwengu uliumbwa kwa Neno, hata vitu
vinavyoonekana viliumbwa kwa vitu visivyoonekana.’
Hatua za Imani ya Ushindi
2Timotheo 3:16-17‘Kila andiko/tamko lenye pumzi/uvuvio wa Mungu,
lafaa kwa kuleta mabadiliko ya tabia/mwenendo.’
(mafafanuzi)
Hatua za Imani ya Ushindi
NGUVU YA NENOWaebrania 4:12
“Neno la Mungu li hai tena lina Nguvu”
Hatua za Imani ya Ushindi
2Kor 3:6, Yoh 6:63‘Andiko linauwa, lakini Roho
anahuisha; kwahiyo, Neno langu ni Roho, tena ni
Uzima; kwasababu’
Hatua za Imani ya Ushindi
NGUVU YA NENO
Yohana 6:63‘Roho ndio itiayo uzima (uhai),
kwani mwili (pasipo roho) haufai kitu’
Hatua za Imani ya Ushindi
NGUVU YA NENO
Yohana 6:63‘Maneno yangu ni Roho
nayo ndio Uzima’
Hatua za Imani ya Ushindi
2 Timotheo 3:16-17
Andiko + Pumzi = Neno (Hai)
Herufi + Roho = Nguvu
MAMLAKA YA MKRISTO
Math 16:19, Mark 11:23-24Ili nguvu za Mungu ziingie kazini,
kuvunja upinzani (nguvu ya dhambi), ni lazima mtu wa Mungu ajifunze kutabiri au
kuamuru (kuagiza) jambo hilo kufanyika/kuvunjika.
USHINDI JUU YA DHAMBI
Mathayo 16:19, 18Watu wa Mungu wengi hufeli
kiroho na kimwili kwasababu hawajui
kwamba; Kuna saa ya kuongea na Mungu na kuna saa ya kuongea na milima.
KUTEMBEA NA NGUVU ZA MUNGU
Marko 11:23-2423 ‘… ukiuambia mlima huu ng’oka, bila mashaka [kwa
uhakika], huku ukiamini kwamba, hayo uyasemayo,
yametokea [tayari, sasa], basi yatakuwa yako [baadaye].’
MAMLAKA YA MKRISTO
Math 16:19, Mark 11:23-24Dhambi zote zinasukumwa na
roho wa aina fulani nyuma yake. Ikiwa ni ulevi, zinaa, uongo, kiburi, hasira, wivu,
matusi, magomvi, fitina, n.k;tabia zote hizi ni roho.
MAMLAKA YA MKRISTO
Luka 10:19, Math 16:19Ninawapa amri ya kukanyaga
‘nge’ na ‘nyoka’, na ‘nguvu zote za yule adui’; na
hakuna kitakachowadhuru kabisa.
MAMLAKA YA MKRISTO
Luka 10:19, Math 16:19
‘Nge’ = nguvu ya maumivuKama vile magonjwa,
umasikini na mateso ya kila namna.
MAMLAKA YA MKRISTO
Luka 10:19, Math 16:19
‘Nyoka’ = nguvu ya dhambi na nguvu ya uasi
Kama vile; ulevi, zinaa, uongo, kiburi, hasira, wivu, matusi, magomvi, fitina, n.k
MAMLAKA YA MKRISTO
Luka 10:19, Math 16:19
‘Nguvu zote’ = nguvu za shetani na wakala zake.
Kama vile; uchawi, ulozi, uganga, ushirikina,
matambiko, mila, n.k
MAMLAKA YA MKRISTO
Luka 10:19, Math 16:19Ninawapa amri ya kukanyaga
‘nge’ na ‘nyoka’, na ‘nguvu zote za yule adui’; na
hakuna kitakachowadhuru kabisa.
MAMLAKA YA MKRISTO
Yakobo 4:7, 1Pet 5:8-9Mtiini Mungu, mpingeni
shetani, naye atawakimbia; anazunguka-zunguka kama simaba, akitafuta mtu wa
kummeza, muwe thabiti na kumpinga huyo.
KANUNI ZA KIROHO
Mungu Mfalme
Kuhani Mazingira
MAMLAKA YA MKRISTO
Ufunuo 5:9-10Mfalme hutawala kwa
Nguvu ya Neno lake.
Mhubiri 8:4‘Neno la Mfalme ni Amri’
UTU MPYA WA KRISTO
Ili kuvunja nguvu ya dhambi, [kimwili] kwa kutumia Nguvu za Mungu, baada ya toba, mtu wa Mungu atatakiwa kuamuru na kutabiri [Kifalme], mabadiliko anayotamani maishani mwake
katika mwenendo [Kimwili].
Hatua za Imani ya Ushindi
6. Kusifu, Kuabudu na
Kushukuru2Nyakati 20:1-30
Matendo 16:13-25-36
Hatua za Imani ya Ushindi
Mungu anajua kwamba; Wewe si mkamilifu, lakini
ameahidi kukukamilisha kwa ukamilifu wake.
Hivyo Jenga tabia ya kumsifu na kumtukuza Mungu kwa ahadi
zake, juu ya kukukamilisha.
Hatua za Imani ya Ushindi
Hili ndilo Neno la Bwana Zerubabeli [kwako] kusema, si kwa uwezo [wako], wala si kwa nguvu [zako], bali ni kwa Roho yangu, asema BWANA.
(Zekaria 4:6)
USHINDI JUU YA DHAMBI
Zaburi 84:1-4-7‘Heri wale wakaa hemani
mwako, wakuhimidi daima; kwasababu huendelea
kutoka nguvu hata nguvu.’
USHINDI JUU YA DHAMBIZaburi 84:1-4-7
‘… wale wanaokaa wakikuhimidi [wakikusifu na kukutukuza] daima; huongezeka kutoka
[kiwango kimoja cha] Nguvu [mpaka kiwango kingine cha]
Nguvu [za Mungu, ili kuwapatia ushindi katika maisha yao].’
KANUNI ZA KIROHO
Zaburi 84:1-4-7Njia mojawapo ya kuvunja ‘sheria ya dhambi’ (kimwili)
ni kutembea kwa Imani kwa kumsifu Mungu kabla
hata ya kuona ushindi katika ulimwengu wa mwili.
Hatua za Imani ya Ushindi
‘Waimbaji na wanamuziki, walipokuwa kama mtu mmoja, wakamsikizisha Mungu sauti za
nyimbo na muziki wa sifa, ndipo nyumba ya Bwana ikajaa wingu la Utukufu na Nguvu za
Mungu. (2Nyakati 5:13-14)
Hatua za Imani ya Ushindi
2Nyakati 5:13-14Kumsifu Mungu kunapofanyika
vizuri [sawasawa] na viwango alivyotaka Mungu, Mungu
hualiachilia Utukufu wake na Nguvu zake, ili kuleta USHINDI
kwa watu wake.
Hatua za Imani ya Ushindi
Kwa Mfano (1);
Mfalme Jehoshephat na Jeshi la Shamu 2Nyakati 20:1-31
Hatua za Imani ya Ushindi
Mfalme Jehoshephat, alipokuwa amezungukwa na
maadui, wamemhusuru pande zote; Hakusubiri kuona ushindi kwanza, ndipo aanze kumsifu
na kumtukuza Mungu, …2Nyakati 20:1-31
Hatua za Imani ya Ushindi
Mfalme Jehoshephat, alianza kuimba sifa na utukufu, kabla hata ya kufika kwenye uwanja wa mapambano; aliitambua
nguvu iliyopo katika kumsifu na kumwabudu Mungu;.
2Nyakati 20:1-31
Hatua za Imani ya Ushindi
Jehoshephat, alijua kwamba, sifa haitoki tu baada ya
ushindi; bali pia, sifa ni silaha mojawapo inayoleta ushindi; hivyo inatakiwa kuachiliwa
kabla/wakati wa mapambano.2Nyakati 20:1-31
Hatua za Imani ya Ushindi
Jehoshephat, akamsifu Mungu sawasawa, ndipo Nguvu za
Mungu zikaachiliwa, na maadui zake wakauana wao kwa wao. Israeli wakashinda ile vita bila kurusha upanga wala mkuki.
2Nyakati 20:1-31
Hatua za Imani ya Ushindi
Na wewe pia, Mungu anajua kwamba, umezungukwa na maadui mbalimbali, [wivu, hasira, wizi, tamaa, zinaa,
kiburi, uongo, umbea n.k.] na wamekuhusuru pande zote,
kama alivyokuwa Jehoshaphat.
Hatua za Imani ya Ushindi
Sasa basi, usisubiri kuona ushindi ndipo uanze kumsifu na kumwabudu Mungu, Hapana,
anza sasa! Sifa ni silaha mojawapo inayoleta ushindi;
hivyo unatakiwa kuachilia sifa, kabla/wakati wa mapambano.
Hatua za Imani ya Ushindi
Kwahiyo, Jifunze kumsifu Mungu sawasawa, ndipo Nguvu
za Mungu zitaachiliwa, na maadui zako [roho za dhambi na uasi] watasambaratishwa kwa Nguvu za Mungu na sio
kwa nguvu zako mwenyewe.
Hatua za Imani ya Ushindi
Hili ndilo Neno la Bwana Zerubabeli [kwako] kusema, si kwa uwezo [wako], wala si kwa nguvu [zako], bali ni kwa Roho yangu, asema BWANA.
(Zekaria 4:6)
Hatua za Imani ya Ushindi
2Nyakati 5:13-14Kumsifu Mungu kunapofanyika
vizuri [sawasawa] na viwango alivyotaka Mungu, Mungu
hualiachilia Utukufu wake na Nguvu zake, ili kuleta USHINDI
kwa watu wake.
Hatua za Imani ya Ushindi
Mfn: Wewe si mkamilifu, lakini Mungu ameahidi kukukamilisha
kwa ukamilifu wake.Hivyo Jenga tabia ya kumsifu na
kumtukuza Mungu kwa ahadi zake, juu ya kukukamilisha.
1Petro 1:15-16
Hatua za Imani ya Ushindi
Kwa Mfano (2);
Paulo na Sila katika Kifungo cha Gereza Matendo 16:16-31
Matendo 16:16-31
Paulo na Sila walijikuta kifungo, wamezuiliwa uhuru wao na
gereza la kirumi. Lakini hawakusubiri wapate uhuru na ushindi, ndipo waanze kumsifu Mungu, Hapana! Walianza sifa
wakiwa bado kifungoni.
Matendo 16:16-31
Panapo usiku wa manane, walipokuwa wakiimba na
kuomba, ndipo Utukufu na Nguvu za Mungu,
zikatetemesha nchi, na milango ya gereza ikafunguka na pingu zilizowafunga, zikawaanguka.
Matendo 16:16-31
Paulo na Sila, hawakumkasirikia Mungu, kwa
vile alivyoacha wakapigwa mijaredi na kufungwa gerezani,
bila hatia; bali waliweka maumivu pembeni na
kujimimina katika sifa na ibada.
Hatua za Imani ya Ushindi
Na wewe pia, Mungu anajua kwamba, umefungwa katika
pingu na magereza ya dhambi na uasi, [wivu, hasira, wizi,
zinaa, kiburi, uongo, n.k.] na umekamatwa pande zote,
kama alivyokuwa Paulo na Sila.
Hatua za Imani ya Ushindi
Sasa basi, usisubiri kuona ushindi ndipo uanze kumsifu na kumwabudu Mungu, Hapana,
anza sasa! Sifa ni silaha mojawapo inayoleta ushindi;
hivyo unatakiwa kuachilia sifa, kabla/wakati wa mapambano.
Hatua za Imani ya Ushindi
Kwahiyo, Jifunze kumsifu Mungu sawasawa, ndipo Nguvu
za Mungu zitaachiliwa, na maadui zako [roho za dhambi na uasi] watasambaratishwa kwa Nguvu za Mungu na sio
kwa nguvu zako mwenyewe.
Hatua za Imani ya Ushindi
Hili ndilo Neno la Bwana Zerubabeli [kwako] kusema, si kwa uwezo [wako], wala si kwa nguvu [zako], bali ni kwa Roho yangu, asema BWANA.
(Zekaria 4:6)
Hatua za Imani ya Ushindi
Mungu anajua kwamba; Wewe si mkamilifu, lakini
ameahidi kukukamilisha kwa ukamilifu wake.
Hivyo Jenga tabia ya kumsifu na kumtukuza Mungu kwa ahadi
zake, juu ya kukukamilisha.
Hatua za Imani ya Ushindi
Matendo 16:16-31Kumsifu Mungu kunapofanyika
vizuri [sawasawa] na viwango alivyotaka Mungu, Mungu
hualiachilia Utukufu wake na Nguvu zake, ili kuleta USHINDI
kwa watu wake.
Hatua za Imani ya Ushindi
Njia;
Namna ya Kumsifu Mungu2Nyakati 20:1-31
Matendo 16:16-31
Hatua za Imani ya Ushindi
(i) Jifunze kuisifia damu ya Yesu. ‘… damu yake yatusafisha na
dhambi zote’ [makosa]. ‘tuna ukombozi kwa damu
yake’ [vifungo].
1Yohana 1:7, Waefeso 1:7
Hatua za Imani ya Ushindi
(ii) Jifunze kumsifia Roho wa Yesu‘Nira/pingu huvunjika kwa
kutiwa mafuta [Roho wa Yesu].’‘Alipo Roho wa Mungu, hapo
pana uhuru [kweli-kweli].’
Isaya 10:27, 2Wakorintho 3:17
Hatua za Imani ya Ushindi
(iii) Jifunze kulisifia Jina la Yesu.‘Jina la Yesu ndilo Jina liotalo majina yote [lenye mamlaka].’‘Kwa Jina la Yesu, kila pepo linatoka [roho, tabia chafu].’
Wafilipi 2:9-11, Marko 16:16-18,
Hatua za Imani ya Ushindi
(iv) Jifunze kulisifia Neno la Yesu.‘Neno la Yesu li hai tena lina
nguvu [ya kuumba na kutenda].’‘Uwatakase kwa ile Kweli,
Neno lako ndio Kweli.’
Waebrania 4:12, Yohana 17:17
Hatua za Imani ya Ushindi
Wewe si mkamilifu, lakini Mungu ameahidi kukukamilisha
kwa ukamilifu wake.Hivyo Jenga tabia ya kumsifu na
kumtukuza Mungu kwa ahadi zake, juu ya kukukamilisha.
1Petro 1:15-16
Hatua za Imani ya Ushindi
(v) Jeshi la Malaika wa Yesu.Silaha nyingine ya ushindi katika mashindano tuliyonayo, ni Jeshi la malaika wa Yesu. Ila hatuwezi kuwasifu malaika, kwani wao, ni wenzetu katika kumsifu Mungu. Ufunuo 4:8-11, Ufunuo 5:11-14
Hatua za Imani ya Ushindi
Kumbuka, Sifa ni silaha mojawapo inayoleta ushindi;
hivyo unatakiwa kuachilia sifa, kabla/wakati wa mapambano.Usisubiri kuona ushindi ndipo
uanze kumsifu na kumwabudu Mungu, Hapana, anza sasa!
Hatua za Imani ya Ushindi
Mungu anajua kwamba; Wewe si mkamilifu, lakini
ameahidi kukukamilisha kwa ukamilifu wake.
Hivyo Jenga tabia ya kumsifu na kumtukuza Mungu kwa ahadi
zake, juu ya kukukamilisha.
1Petro 1:15-19
15 Bali kama Yeye aliyewaita alivyo Mtakatifu, ninyi nanyi
iweni Watakatifu katika mwenendo wenu wote, …
USHINDI JUU YA DHAMBI
1Petro 1:15-19
16 kwa maana imeandikwa: “Mtakuwa Watakatifu, kwa kuwa Mimi ni Mtakatifu.”
USHINDI JUU YA DHAMBI
Hatua za Imani ya Ushindi
Kwahiyo, Jifunze kumsifu Mungu sawasawa, ndipo Nguvu
za Mungu zitaachiliwa, na maadui zako [roho za dhambi na uasi] watasambaratishwa kwa Nguvu za Mungu na sio
kwa nguvu zako.
USHINDI JUU YA DHAMBI
Zaburi 84:1-4-7‘Heri wale wakaa hemani
mwako, wakuhimidi daima; kwasababu huendelea
kutoka nguvu hata nguvu.’
USHINDI JUU YA DHAMBIZaburi 84:1-4-7
‘… wale wanaokaa wakikuhimidi [wakikusifu na kukutukuza] daima; huongezeka kutoka
[kiwango kimoja cha] Nguvu [mpaka kiwango kingine cha]
Nguvu [za Mungu, ili kuwapatia ushindi katika maisha yao].’
KANUNI ZA KIROHO
Zaburi 84:1-4-7Njia mojawapo ya kuvunja ‘sheria ya dhambi’ (kimwili)
ni kutembea kwa Imani kwa kumsifu Mungu kabla
hata ya kuona ushindi katika ulimwengu wa mwili.
Hatua za Imani ya Ushindi
7. Kufanya Tendo la
Imani.Yakobo 2:17-18, 26
Hatua za Imani ya Ushindi
Yakobo 2:17, 26Kwa maana, kama mwili
pasipo roho imekufa, vivyo hivyo, imani pasipo matendo,
pia imekufa.
Hatua za Imani ya UshindiYakobo 2:17, 26
Baada ya kupata Uhakika (Imani) Mungu atakutaka uiingize imani
yako katika matendo, ili kuachilia NGUVU za Mungu, kuumba
ukamilifu wake katika maisha yako, kwenye Kimwili.
Hatua za Imani ya UShindiYakobo 2:17-18
Njia mojawapo ya kuvunja ‘sheria ya dhambi’ (kimwili) ni kuchukua hatua za kimwili za
kujitenga na kuepuka mazingira hatarishi, yanayoweza
kukuingiza ktk kufanya makosa.
Hatua za Imani ya UshindiYakobo 2:17, 26
Kuna wakatia, Nguvu za Mungu, haziachiliwi katika maisha yetu,
kukamlisha muujiza katika ulimwengu wa mwili tunayo-
isubiria kwa hamu, mpaka tunapochuka hatua za kutenda.
KUTEMBEA KWA IMANI
Kwa Mfano wa Ibrahimu;
Kubadili Majina yao,Abramu – Ibrahim
Sarai – Sara Mwanzo 17:1-22
KUTEMBEA KWA IMANI
Kwa Mfano wa Nabii Eliya;
Kutawanya Mkutano kabla ya ishara yoyote ya
mvua kuonekana1Wafalme 18:41-43
KUTEMBEA KWA IMANI
Kwa Mfano wa Yesu;
Kuamuru Wagonjwa Kutoa Sadaka ya
shukurani kabla ya kuona uponyaji.
Luka 17:11-14-19
KUTEMBEA KWA IMANI
Kwa Mfano wa Mitume;
Kuamuru Kilema Kutembea kabla ya
kuona uponyaji.Matendo 3:1-10-16
KUTEMBEA KWA IMANI
Kwa Mifano Mingine mbalimbali;Kununua nepi na beseni kabla ya
kuona dalili za mimbaKununua suti ya harusi kabla ya
kumpata Bwana ArusiKujenga gereji ya gari kabla ya
kupata gari
Hatua za Imani ya UshindiYakobo 2:17, 26
Kuna wakatia, Nguvu za Mungu, haziachiliwi katika maisha yetu,
kukamlisha muujiza katika ulimwengu wa mwili tunayo-
isubiria kwa hamu, mpaka tunapochuka hatua za kutenda.
Hatua za Imani ya Ushindi
Mfano (1);
Uponyaji wa Kilema Hekaluni, Mlangoni.
Matendo 3:1-10
Hatua za Imani ya UshindiMatendo 3:1-10
Uponyaji wa Kilema huyu, ulishaumbika katika ulimwengu wa roho, na Petro na Yohana,
walishuhudiwa hilo; ndio maana walimwambia asimame na
kutembea.
Hatua za Imani ya UshindiMatendo 3:1-10
Petro alipoona huyu mtu anachelewesha uponyaji wake,
kwa kutofanya kitendo alichoambiwa; Petro alijua
Muujiza huu unaweza kupotea, kwasababu ya kutoamini kwake.
Hatua za Imani ya UshindiMatendo 3:1-10
Ndio maana Petro akalazimika kumkashika mkono na
kumnyanyua na kumtembeza, (aiingize imani katika matendo)
ili kuruhusu utendaji kazi wa Nguvu za Mungu, katika mwilini.
Hatua za Imani ya UshindiMatendo 3:1-10
Kule kujaribu kutembea na kupepesuka kwa huyu kilema,
kuliruhusu Nguvu za Mungu kuanza kazi ya ukamilifu wa
miguu yake, kwasababu, Imani imeingizwa katika matendo.
Hatua za Imani ya UshindiMatendo 3:1-10
Ajabu ni kwamba, Nguvu za Mungu, hazikuachiliwa kukamlisha muujiza ule,
katika ulimwengu wa mwili, mpaka imani ilipoingizwa
katika matendo.
Hatua za Imani ya UshindiMatendo 3:1-10
Na wewe pia, si ajabu umekuwa ukimwamini Mungu akufungue
kutoka katika tatizo la aina fulani [Mfano; dhambi na uasi]; usikae
ukisubiri nguvu za Mungu zija kukutoa hapo, bali chukua hatua.
Hatua za Imani ya UShindiYakobo 2:17-18
Njia mojawapo ya kuvunja ‘sheria ya dhambi’ (kimwili) ni kuchukua hatua za kimwili za
kujitenga na kuepuka mazingira hatarishi, yanayoweza
kukuingiza ktk kufanya makosa.
Hatua za Imani ya Ushindi
Mfano (2);
Kusimamishwa kwa Maji ya Mto Jordan.Joshua 3:1-17
Hatua za Imani ya UshindiJoshua 3:1-17
Wana wa Israeli, walitaka sana kwenda kumalizia safari yao ya kutoka Misri [Utumwani], kwa
kuuvuka mto Jordan, na kuirithi nchi takatifu, iliyojaa maziwa,
asali na unono mwingi.
Hatua za Imani ya UshindiJoshua 3:1-17
Lakini kikwazo kingine, kilikuwa ni namna ya kuuvuka mto
Jordan. Mungu akawaambia, Nguvu zangu zipo tayari
kuwasaidia kuvuka, ili mkairithi nchi ya unono mwingi, lakini …
Hatua za Imani ya UshindiJoshua 3:1-17
‘… Lakini waambie Makuhani, wakanyage maji kwanza, wakiwa wamelibeba lile
sanduku la agano; ndipo na mimi nitaingiza nguvu zangu
kazini, kuzuia maji.
Hatua za Imani ya UshindiJoshua 3:1-17
Joshua akafanya kama Bwana alivyomwagiza, na maji ya mto
Jordan, yakasimama kama mlima upande wa juu. Na wana
wa Israeli, wakavuka mto wakipita mahali pakavu.
Hatua za Imani ya UshindiJoshua 1:1-17
Tunaona wazi kwamba; Nguvu za Mungu,
hazikuachiliwa kukamlisha muujiza ule, katika ulimwengu
wa mwili, mpaka imani yao ilipoingizwa katika matendo.
Hatua za Imani ya UshindiYakobo 2:17, 26
Kuna wakati, Nguvu za Mungu, haziachiliwi katika maisha yetu,
kukamlisha muujiza katika ulimwengu wa mwili tunayo-
isubiria kwa hamu, mpaka tunapochuka hatua za kutenda.
Hatua za Imani ya Ushindi
Joshua 1:1-17, Yakobo 2:17, 26 Na wewe najua kuna maisha unayatamani sana, maisha ya usafi na utakatifu, unaoshinda
kila aina ya dhambi na uasi. Lakini mbele yako kuna tabia na maisha yanayokuzui, kama mto
Jordan kwa wana wa Israeli.
Hatua za Imani ya Ushindi
Joshua 1:1-17, Yakobo 2:17, 26 Nafahamu ya kwamba,
umekuwa ukimwomba Mungu na ukimsubiri Mungu
akufungulie njia ya kushinda majaribu na dhambi
zinazokuzunguka na kukuzui kufikia utakatifu wa kweli …
Hatua za Imani ya Ushindi
Joshua 1:1-17, Yakobo 2:17, 26… wenye kila aina ya baraka na
unono ambao Mungu amekuahidi. Nataka kikwambie kwamba, inawezekana njia ya
kuvuka na kushinda majaribu na dhambi zinazokuzunguka,
inakusubiri wewe na sio Mungu.
Hatua za Imani ya UshindiJoshua 1:1-17
Tumeona wazi kwamba; Nguvu za Mungu,
hazikuachiliwa kukamlisha muujiza ule, katika ulimwengu
wa mwili, mpaka imani yao ilipoingizwa katika matendo.
Hatua za Imani ya UshindiYakobo 2:17, 26
Kuna wakatia, Nguvu za Mungu, haziachiliwi katika maisha yetu,
kukamlisha muujiza katika ulimwengu wa mwili tunayo-
isubiria kwa hamu, mpaka tunapochuka hatua za kutenda.
Hatua za Imani ya UShindiYakobo 2:17-18
Njia mojawapo ya kuvunja ‘sheria ya dhambi’ (kimwili) ni kuchukua hatua za kimwili za
kujitenga na kuepuka mazingira hatarishi, yanayoweza
kukuingiza ktk kufanya makosa.
Hatua za Imani ya UShindiYakobo 2:17-18
Kwa Mfano;Huwezi kukaa unamlilia Mungu
akusaidie usivute sigara tena, wakati unatembea na kiberiti
mfukoni. Utajitia kwenye majaribu mwenyewe.
Hatua za Imani ya UShindiYakobo 2:17-18
Kwa Mfano;Huwezi kukaa unamlilia Mungu
akusaidie usinywe pombe tena, wakati unashinda Baa na
umezungukwa na pombe. Unajitia kwenye majaribu.
Hatua za Imani ya UShindiYakobo 2:17-18
Huwezi kukaa unamlilia Mungu akusaidie usifanye uzinzi tena,
wakati mnashinda wawili wenyewe, nyuma ya mlango uliofungwa. Unajitia kwenye
majaribu wenyewe.
Hatua za Imani ya UShindiYakobo 2:17-18
Huwezi kukaa unamlilia Mungu akusaidie usifanye maovu tena, wakati unashinda na
marafiki wanaoishi maishi ya uovu, uasi na anasa. Lazima
utatumbukia tu katika maanguko.
Hatua za Imani ya UshindiHuwezi kukaa unamlilia Mungu akusaidie usipate mke au mume
mtarajiwa wa ajabu-ajabu, wakati unaukakasi wa kwenda
kanisani au makusanyiko ya watakatifu. Lazima utatumbukia tu kwa wayebusi na wagirigashi.
Hatua za Imani ya UShindiYakobo 2:17-18
Njia mojawapo ya kuvunja ‘sheria ya dhambi’ (kimwili) ni kuchukua hatua za kimwili za
kujitenga na kuepuka mazingira hatarishi, yanayoweza
kukuingiza ktk kufanya makosa.
Hatua za Imani ya Ushindi
Mithali 1:10 ‘Mwanagu, wenye
dhambi wakikushawishi, wewe usikubali.’
Hatua za Imani ya Ushindi
2Wakorintho 6:14-1814 ‘Msifungiwe nira [vifungo] pamoja na wasio amini, kwa jinsi isivyo sawasawa [i.e. ipo jinsi iliyo sawasawa ya kuishi
na wasio amini], ...’
Hatua za Imani ya Ushindi
2Wakorintho 6:14-1814 … ‘Kwa maana, pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru
na giza?
Hatua za Imani ya Ushindi
2Wakorintho 6:14-1815 ‘Tena pana ulinganifu gani
kati ya Kristo na Beliari [Ufisadi, Uchafu]? Au, yeye aaminiye, ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?
[Hawana sehemu]
Hatua za Imani ya Ushindi
2Wakorintho 6:14-1816 ‘Tena pana mapatano gani
kati ya hekalu la Mungu [mwili wako] na sanamu [ushetani]?
Kwa maana sisi [tuliookoka] tu hekalu la Mungu aliye hai, …’
Hatua za Imani ya Ushindi
2Wakorintho 6:14-1816 … ‘Kama Mungu alivyo-sema, ya kwamba, Nitakaa
ndani yako, na kati yao nitatembea; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa
watu wangu.
Hatua za Imani ya Ushindi
2Wakorintho 6:14-1817 ‘Kwahiyo, tokeni kati yao,
mkatebgwe nao, asema Bwana; msiguse kitu kilicho
kichafu, nami nitawakaribisha’.
Hatua za Imani ya Ushindi
2Wakorintho 6:14-1818 ‘[Ndipo] Nitakuwa Baba
kwenu, nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na
wa kike, Asema BWANA MWENYEZI
Hatua za Imani ya UshindiYakobo 2:17, 26
Kuna wakatia, Nguvu za Mungu, haziachiliwi katika maisha yetu,
kukamlisha muujiza katika ulimwengu wa mwili tunayo-
isubiria kwa hamu, mpaka tunapochuka hatua za kutenda.
Hatua za Imani ya UShindiYakobo 2:17-18
Njia mojawapo ya kuvunja ‘sheria ya dhambi’ (kimwili) ni kuchukua hatua za kimwili za
kujitenga na kuepuka mazingira hatarishi, yanayoweza
kukuingiza ktk kufanya makosa.
Hatua za Imani ya Ushindi
Njia za Kujiepusha na Vishawishi;①Weka Mipaka (Stop) Aamua na
Usiivuke mipaka hiyo tena.②Tafuta Marafiki wazuri, na
badilisha mtindo wa maisha.③Inapobidi, Kimbia [Ondoka,
Usiende tena, kwa muda mrefu].
Hatua za Imani ya UShindiMathayo 5:29
Jicho lako la kuume, likikukosesha, ling’oe na kulitupa mbali nawe; kwa
maana ni bora kupoteza kiungo kimoja, kuliko kwenda jehanum
ukiwa na mwili mzima wenye viungo kamili.
Hatua za Imani ya UShindiYakobo 2:17-18
Njia mojawapo ya kuvunja ‘sheria ya dhambi’ (kimwili) ni kuchukua hatua za kimwili za
kujitenga na kuepuka mazingira hatarishi, yanayoweza
kukuingiza ktk kufanya makosa.
Hatua za Imani ya Ushindi
Mfano (3);
Jaribu la Yusufu na Mke wa Waziri Mkuu [Potifa]
Mwanzo 39:1-20 (12)
Hatua za Imani ya UshindiMwanzo 39:1-20
Kwa jinsi Yusufu, alivyokuwa mzuri wa sura na umbo, mke wa Potifa, akamtamani na kumtaka kulala naye kwa uzinzi. Akafanya hivyo siku nyingi, siku kwa siku, lakini Yusufu hakumpa nafasi,
wala kuongea naye.
Hatua za Imani ya UShindiMwanzo 39:1-20
Japo jaribu lilikuwa zito, lakini Yusufu hakuweza kujiepusha na mazingira yale kwasababu ndiko
alipokuwa amepangiwa kama eneo lake la kazi, yeye kama mtumwa tu na si mwajiriwa
ambaye angeweza kuacha kazi.
Hatua za Imani ya Ushindi
Mwanzo 39:1-20Jaribu hili kwa Yusufu halikuwa
rahisi, kwasababu;1. Hakuweza kujiepusha kwani ndiko alipokuwa amepangiwa
kama eneo lake la kazi.
Hatua za Imani ya Ushindi
Mwanzo 39:1-20Jaribu hili kwa Yusufu halikuwa
rahisi, kwasababu;2. Yeye Yusufu alikuwa MTUMWA, mtu maskini,
asiye na matumaini ya kuja kutoka na kuwa mtu huru
tena.
Hatua za Imani ya Ushindi
Mwanzo 39:1-20Jaribu hili kwa Yusufu halikuwa
rahisi, kwasababu;3. Hakupendwa na House-girl,
alipendwa na MKE WA WAZIRI MKUU, maarufu,
mzuri na tajiri Namba Mbili, katika Misri yote.
Hatua za Imani ya Ushindi
Jaribu hili kwa Yusufu halikuwa rahisi, kwasababu;
4. Yusufu alikuwa Mseja (Bachelor) yaani hana ndoa, (na kiafya ni mzima) hivyo
hana binadamu wa kumtenda kosa la kutoka nje ya ndoa.
Hatua za Imani ya Ushindi
Mwanzo 39:1-20Jaribu hili kwa Yusufu halikuwa
rahisi, kwasababu;5. Walikuwa wamebaki wao wawili tu katika chumba cha
ndani cha Mkuu wa Nchi.(Siri Kuu – Salama)
Hatua za Imani ya UshindiMwanzo 39:1-20
Jaribu hili kwa Yusufu halikuwa rahisi, kwasababu;
6. Yusufu angeweza kujitetea kwamba, Kosa si lake; kwamba si yeye aliyemtaka mke wa mtu,
bali ni mke wa mtu kamtaka Yusufu.
Hatua za Imani ya Ushindi
Mwanzo 39:1-20Jaribu hili kwa Yusufu halikuwa
rahisi, kwasababu;7. Yusufu alitishiwa kupigiwa
kelele za ‘ubakaji’, tena ‘ubakaji’ kwa mke wa Waziri Mkuu. Alijua ni Kifo kinakuja!
Hatua za Imani ya UshindiMwanzo 39:1-20
Kwa wengine wasio na hofu ya Mungu, kwasababu ya umaskini na ukame wa ‘kimapenzi’ katika
maisha yao, si ajabu wangesema;
‘Ooh! Mungu anipe nini sasa …Baraka zenyewe si ndio hizi !!!’
Hatua za Imani ya UshindiMwanzo 39:1-20
Lakini pamoja na ‘fursa’ zote hizo, Yusufu alisema ‘Nitamtendaje Mungu wangu, dhambi kubwa
namna hii?’ Kumbe Yusufu, alitambua nafasi ya Mungu;
Japo hana mke wa kumtubia, lakini alijua ana Mungu wa
Kumtubia.
Hatua za Imani ya UshindiMwanzo 39:1-20
Biblia inasema, Yusufu akakimbia na kusema kama Shad, Mesh na Abed, kwamba; ‘liwalo na liwe,
‘Siwezi kumtenda Mungu wangu, dhambi kubwa namna
hii?’ Yusufu, alitambua nafasi ya Mungu, katika maisha yake’.
Hatua za Imani ya UshindiDanieli 3:1-20
Shad, Mesh na Abed wakasema, ‘Mungu anaweza kutuokoa na
mkono wako ee Mfalme na huu moto pia. Lakini tukifa, na
tufie mikononi mwa Mungu wetu kuliko kumtenda dhambi
hii’.
Hatua za Imani ya UshindiMwanzo 39:1-20Biblia inasema;
Yusufu ‘akatimua mbio’
akisema; ‘liwalo na liwe, ‘Siwezi kumtenda Mungu wangu,
dhambi kubwa namna hii?’
Hatua za Imani ya UShindiMathayo 5:29
Jicho lako la kuume, likikukosesha, ling’oe na kulitupa mbali nawe; kwa
maana ni bora kupoteza kiungo kimoja, kuliko kwenda jehanum
ukiwa na mwili mzima wenye viungo kamili.
Hatua za Imani ya UShindi
Mwanzo 39:1-20Huwezi kukaa unamlilia Mungu
akusaidie usifanye uzinzi tena, wakati unakubali kutengeneza mazingira ya kushikwa-shikwa,
wakati eti unajidai kukemea kimoyo-moyo!
Hatua za Imani ya UShindi
Mwanzo 39:1-20Kuna dhambi za kukemea na
kuna dhambi za kukimbia.Huwezi kuwa gangwe mbele ya
dhambi ukamshinda Samsoni na Mfale Sulemani.
Kimbia wewe, acha utani!
Hatua za Imani ya UShindi
Mwanzo 39:1-20Itakusaidia nini wewe kuupata
ulimwengu wote, unapata hasara ya roho yako? Halafu
unakufa na unakwenda jehanum ya moto?(Mathayo 16:26)
Hatua za Imani ya UShindi
“Kwani, atafaika nini mtu, akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake?Au Mtu atatoa nini badada ya
nafsi yake?”Mathayo 16:26
Hatua za Imani ya UShindi
32 Kwa maana mlistahimili mashindano makubwa ya
maumivu 33 pindi mlipoteswa kwa mashutumu na dhiki, na pindi mliposhirikiana na wale
waliotendewa hayo, … (Waebrania 10:34)
Hatua za Imani ya UShindi… mliwaonea huruma wale
waliokuwa katika vifungo, tena mkakubali kwa furaha,
kunyang’anywa mali zenu, mkijua kwamba, nafsini mwenu,
mna mali iliyo njema zaidi, idumuyo. (Waebrania 10:34)
Hatua za Imani ya UShindi‘… Kwa kitambo kidogo,
mmehuzunishwa kwa majaribu ya aina mbalimbali, ila kwa sasa
mnafurahi sana … Kujaribiwa kwa imani yenu, kwasababu ina
thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo. (1Petro 1:5-7)
Hatua za Imani ya UShindi4 ‘Hamjafanya vita [na dhambi
hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi. 5 Tena mmeyasahau yale maonyo. Basi usizimie moyo, ukikemewa naye
6 yeye ambaye Bwana humpenda, humwadhibu.
(Waebrania 12:4-6)
Hatua za Imani ya UShindi25 ‘Je! Hamjui ya kuwa wale
washindanano katika michezo, hujizui katika yote? Wao hufanya
hivyo ili wapokee taji iharibikayo, lakini sisi hujizuia na
kushinda, ili tupokee taji isiyoharibika. (1Korintho 9:24-25)
Hatua za Imani ya UShindi
35 ‘… Basi [kama vile Shad, Mesh, Abed na Yusufu]
msiutupe Ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu [kuliko dhahabu ya dunaia ipoteayo]’.
(Waebrania 10:34-35)(1Petro 1:5-7)
Hatua za Imani ya UShindiYakobo 2:17-18
Njia mojawapo ya kuvunja ‘sheria ya dhambi’ (kimwili) ni kuchukua hatua za kimwili za
kujitenga na kuepuka mazingira hatarishi, yanayoweza
kukuingiza ktk kufanya makosa.
Hatua za Ushindi Juu ya Dhambi
Yakobo 2:17, 26Kwa maana, kama mwili
pasipo roho imekufa, vivyo hivyo, imani pasipo matendo,
pia imekufa.
Hatua za Imani Timilifu(1)Kulipata Neno (Warumi 10:17)(2)Kulifanya litokee (Mrk 11:23)(3)Kuthibitisha Uhakika (Rum 4:21)(4)Kubadilisha Mtazamo (Efe 1:18-19)(5)Kuamuru na Kutabiri (Mark 11:23)(6)Kukiri kwa Uhakika (Rum 4:17)(7)Kutenda kwa ujasiri (Mwa 17:1-9)
UTU MPYA WA KRISTO
Ndani ya kila mtoto wa Mungu, kuna Sura na Mfano
wa Mungu, (yaani asili ya Mungu) ambayo inakupa asili
ya ushindi ndani yako, dhidi ya kila upinzani wa adui shetani
maishani mwako.
UTU MPYA WA KRISTO
Roho zetu zina uwezo wa Ki-Mungu wa kutawala miili yetu
katika maisha ya Utakatifu, ni ile hali ya kukosea kujiona, ndicho kitu kinachozima utendaji kazi
wa Nguvu za Mungu unaowezesha ushindi huo.
IMANI YA USHINDI
USHINDI DHIDI YA DHAMBI
Warumi 8:5-11
KANUNI ZA KIROHOWarumi 8:5-11
5 Kwa maana wale wanaoishi kwa kuufuata mwili huziweka nia zao katika vitu vya mwili,
lakini wale wanaoishi kwa kufuata Roho, huziweka nia zao katika mambo ya Roho.
KANUNI ZA KIROHOWarumi 8:5-11
6 Kwa maana kuwa na nia ya mwili ni mauti, bali kuwa na nia inayoongozwa na Roho ni uzima na amani. 7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui na Mungu, kwa maana haiitii sheria ya Mungu,
wala haiwezi kuitii.
KANUNI ZA KIROHOWarumi 8:5-11
8 Wale wanaotawaliwa na mwili, hawawezi kumpendeza Mungu. 9 Lakini ninyi, hamtawaliwi na mwili, bali na Roho, ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu.
Mtu ye yote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo.
KANUNI ZA KIROHOWarumi 8:5-11
10 Lakini kama Kristo anakaa ndani yenu, miili yenu
imekufa kwa sababu ya dhambi, lakini roho zenu zi
hai kwa sababu ya haki.
KANUNI ZA KIROHO
Warumi 8:5-1111 Nanyi ikiwa Roho wa Mungu
aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu anakaa ndani yenu, Yeye aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataihuisha pia miili
yenu ambayo hufa, kwa njia ya Roho Wake akaaye ndani yenu.
USHINDI JUU YA DHAMBI
Hatua ya kwanza;Warumi 6:5-6, 11-14
11 kujihesabuni mfu katika dhambi lakini mlio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu;
Yaani “Mtakatifu”
KANUNI ZA KIROHO
Warumi 6:5-6, 11-1412 Kwa hiyo, msiruhusu dhambi itawale ndani ya
miili yenu, ipatikanayo na kufa, ili kuwafanya mzitii
tamaa mbaya.
KANUNI ZA KIROHO
Warumi 6:5-6, 11-14 14 Kwa maana dhambi
haitakuwa na mamlaka juu yenu, kwa sababu hampo
chini ya sheria, bali chini ya neema.
HATUA ZA IMANI YA USHINDI
1Yohana 5:1-41 ‘Kila mtu anayeamini kwamba, Yesu Kristo ni
Mwana wa Mungu, amezaliwa na Mungu…’
(Zab 82:6, Yoh 10:34-36)
HATUA ZA IMANI YA USHINDI
1Yohana 5:1-44 “Kwa maana, kila kitu kilichozaliwa na Mungu,
huushinda ulimwengu, na huku ndiko kushinda,
kuushindako ulimwengu, ni hiyo Imani yetu.”
1Yoh 5:4, Rum 8:37
Ndani ya kila mtoto wa Mungu, kuna Sura na Mfano
wa Mungu, (yaani asili ya Mungu) ambayo inakupa asili
ya ushindi ndani yako, dhidi ya kila upinzani wa adui shetani
maishani mwako.
KANUNI ZA KIROHO1Yoh 5:4, Rum 8:37
Pamoja na kwamba Neno la Mungu linatuahidi Ushindi wa Yesu msalabani, kuwa ushindi wetu sisi tuaminio; lakini bado waumini wengi tunaishi maisha
ya utumwa juu ya dhambi.
UTU MPYA WA KRISTO
Warumi 8:5-12 Ikiwa roho zetu zina uwezo wa
Ki-Mungu wa kutawala miili yetu katika maisha ya
Utakatifu, ni kitu gani basi kinazima utendaji kazi wa
Nguvu za Mungu unaowezesha ushindi huo?
KABLA YA DHAMBI (ANGUKO)
Utukufu (Msaada) Mungu Mwili Roho Dunia NafsiShetani
BAADA YA DHAMBI
Msaada Ukakatika Mungu Mwili Roho Dunia Nafsi Shetani
BAADA YA WOKOVU
(Utukufu) Roho Mt. Mungu Mwili Roho Dunia Nafsi Shetani (Rum 8:9-11)
VITA YA MWILI NA ROHO
Utukufu (Msaada) Mungu Mwili Roho Dunia Nafsi Shetani (Rum 8:9-11)
UTU MPYA WA KRISTO
Warumi 8:5-12 Ikiwa roho zetu zina uwezo wa
Ki-Mungu wa kutawala miili yetu katika maisha ya
Utakatifu, ni kitu gani basi kinazima utendaji kazi wa
Nguvu za Mungu unaowezesha ushindi huo?
USHINDI JUU YA DHAMBI1Yohana 5:4, Mathayo 17:19-21
Imani ni uhakika wa kazi ya Yesu msalabani. Hivyo, ukikosea
kujiona, utakosea kujiwaza; na utakosea kuongea. Makosa
hayo, yatazima utendaji kazi wa nguvu za Mungu unaohusika na kukusaidia kushinda dhambi.
KANUNI ZA KIROHO
Warumi 6:5-6, 11-14 Hii ndio kusema;
Dhambi itakuwa na mamlaka juu yenu, endapo
mtajihesabu mpo chini ya sheria (torati), na si chini ya
neema.… (ajionavyo mtu nafsini mwake)
UTU MPYA WA KRISTO
Warumi 8:5-12Ikiwa roho zetu zina uwezo wa Ki-
Mungu wa kutawala miili yetu katika maisha ya Utakatifu, ni
kitu gani basi kinazima utendaji kazi wa Nguvu za Mungu
unaowezesha ushindi huo?
KANUNI ZA KIROHO1Yoh 5:4, Rum 8:37
Pamoja na kwamba Neno la Mungu linatuahidi Ushindi wa Yesu msalabani, kuwa ushindi wetu sisi tuaminio; lakini bado waumini wengi tunaishi maisha
ya utumwa juu ya dhambi.
USHINDI JUU YA DHAMBI1Yohana 5:4, Mathayo 17:19-21
Moja ya sababu, kwanini watu wa Mungu wanashindwa na
dhambi, ni kutokana na watu wa Mungu kutozingatia Kanuni za
Sheria ya Roho na Uzima.(Warumi 8:1-2)
USHINDI JUU YA DHAMBISheria ya Roho wa Uzima
(Warumi 8:1-2) 1. Kula Vizuri Kiroho (1Pet 2:2)
Mwili wako unashindana na roho; mwenye nguvu zaidi
[anayelishwa chakula chake zaidi] ndiye atakayemtawala
mwenzake (Gal 5:16-23).
VITA YA MWILI NA ROHO
Utukufu (Msaada) Mungu Mwili Roho Dunia Nafsi Shetani (Rum 8:9-11)
USHINDI JUU YA DHAMBISheria ya Roho wa Uzima
(Warumi 8:1-2)
1. Kula Vizuri Kiroho (1Pet 2:2)2. Epuka Vishawishi (Mith1:10)3. Vunja roho ya Utumwa wa dhambi na matezo. (Isa 52:2)
IMANI YA USHINDI
1Yohana 5:1-41 ‘Kila mtu anayeamini kwamba, Yesu Kristo ni
Mwana wa Mungu, amezaliwa na Mungu…’
(Zab 82:6, Yoh 10:34-36)
IMANI YA USHINDI
1Yohana 5:1-44 Kwa maana, kila kitu kilichozaliwa na Mungu,
huushinda ulimwengu, na huku ndiko kushinda, kuushindako
ulimwengu, ni hiyo Imani yetu.”
IMANI YA USHINDI
Ndani ya kila mtoto wa Mungu, kuna Sura na Mfano
wa Mungu, (yaani asili ya Mungu) ambayo inakupa asili
ya ushindi ndani yako, dhidi ya kila upinzani wa adui shetani
maishani mwako.
NGUVU LA NENO LA MUNGU
Kanuni hizi tulizojifunza, zikusaidie kuzalisha nguvu za Mungu ndani yako, kwasababu, utendani kazi wa mkono wa Mungu maishani
mwako unategemea sana kiwango cha nguvu zake, kinachotenda kazi
ndani yako.
Mafundisho Mengine
Vitabu vingine, CD na DVD za Mafundisho vya Mwalimu Mgisa
Mtebe, yanapatikana katika duka la Vitabu vya Kikristo la
Azania Front Cathedral Luther House, Sokoine Drive
Dar es Salaam.
Kwa mawasiliano zaidi,Mwl. Mgisa Mtebe
(Christ Rabbon Ministry)
P. O. Box 837,Dar es Salaam, Tanzania.
+255 713 497 654+255 783 497 654
www.mgisamtebe.org