mnyunyiziaji mwongozo wa mfukoni · mwongozo wa mfukoni wa mnyunyiziaji 1 1. vifaa bbinafsi vya...

28
Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni JANUARI 2014

Upload: others

Post on 12-Sep-2019

16 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni

JANUARI 2014

Page 2: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

Chapisho rejea: Were, Allan, Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji dawa ya ukoko majumbani. Bethesda, MD: Mradi wa Afrika wa Kunyunyizia Dawa ya Ukoko Majumbani, Mpango wa Rais wa Malaria, Januari 2014.

Na. ya Mkataba: GHN-1-00-09-00013-00

Na. la Agizo: AID-OAA-TO-14-00035

UONDOAJI LAWAMA Maoni ya mwandishi yaonekanayo katika chapisho hili hayaakisi maoni ya Shirika la Kimataifa la Maendeleo la watu wa Marekani au Serikali ya Marekani.

Picha ya Juu: Haijulikani

Abt Associates4550 Montgomery Avenue Suite 800 North - Bethesda, Maryland 20814T. 301.347.5000 - F. 301.913.9061www.abtassociates.com

Chapisho hili lilitolewa kwa mapitio na Shirika la Kimataifa la Misaada na Maendeleo la watu wa Marekani. Limetayarishwa na Allan Were.

Page 3: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

1 Vifaa vya Kinga (PPE) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 1

2 Mkoba . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 2

3 Afya & Uzima . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 3

4 Tahadhari za Kiusalama . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 4

5 Huduma ya Kwanza . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 5

6 Maadili ya Mnyunyiziaji kwenye Kaya . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 6

7 Usalama wa Kaya au katika Kaya . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 7

8 Maandalizi ya Nyumba kabla ya kupiga dawa . . . . . . . . . . . . . . . . 8

9 Kuchanganya Dawa ya Kuua Wadudu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 10

10 Mbinu za Unyunyiziaji . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 12

11 Kunyunyizia Dari . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 14

12 Kunyunyizia Mtaambaa panya . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15

13 Unapotumia pampu ya unyunyijiaji , kuwa makini na zingatia

Yafuatayo na uripoti madhara yoyote kwa Kiongozi wa Timu

yako au Msimamizi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 16

14 Baada ya Kunyunyizia Nyumba . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .17

15 Ushughulikiaji Mabaki ya Dawa ya Kuua Wadudu & Taka zilizochanganyika na dawa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 18

16 Usafi Mwisho wa Kazi ya Siku . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 19

17 Utumiaji Sahihi wa Vifaa vya Unyunyiziaji . . . . . . . . . . . . . . . . 20

18 Malengo ya Utendajikazi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 21

Jedwali la Yaliyomo

Page 4: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia
Page 5: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1

1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE)

■■ Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia.

■■ Hii inajumuisha: • Ovaroli • Kofia ngumu yenye miwani ya kukinga uso • Kichujio cha Vumbi • Glovu • Buti za Raba

VIDOKEZO:■■ Vaa ovaroli nje ya buti.■■ Vaa glovu nje ya mikono ya ovaroli.■■ Mtaarifu Kiongozi wa Kundi lako maramoja ikiwa

mojawapo ya vazi la kinga ulilopokea halikutoshi vizuri, au limeharibika (k.m., limechanika)

Page 6: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

2 Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji

■■ Mkoba utumike kubebea vifaa vifuatavyot tu (vifaa hivi huenda vikatofautiana kulingana na nchi yako): • Dawa ya kuua wadudu • Vifungashio vitupu au

chupa tupu • Taulo • Kadi na fomu za unyunyiziaji • Kalamu

VIDOKEZO:■■ Usibebe vifaa vyovyote vya binafsi ndani ya mkoba.■■ Weka mkoba mahali unapoweza kuuona na chini ya udhibiti

wako nyakati zote za kazi.■■ Rejesha mkoba kwenye ghala la kuhifadhia mwisho wa kazi

ya siku.

• Pua za ziada • Zana za kurekebishia

Pampu ya Unyunyiziaji • Kipande cha nguo cha

kuchujia au chujio • Karatasi ya plastiki • Tochi

2. Mkoba

Kila wakati uweke mkoba wako mahali unapoweza kuuona.

Page 7: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 3

3. Afya & Uzima

■■ Pata usingizi mzuri usiku ukijiandaa na kazi kila siku inayofuata.

■■ Pata kifungua kinywa na uje umeshiba kabla ya kuanza kazi.■■ Hakikisha kwamba unakunywa maji au juisi ya kutosha

kabla ya kuripoti kazini.

TAHADHARI:■■ Mtaarifu Kiongozi wa Kundi lako maramoja ukihisi au

kusikia dalili zifuatazo ukiwa kazini: • Kuvuta pumzi kwa taabu • Kuumwa na kichwa • Uchovu

• Kuwashwa machoni • Muwasho kwenye ngozi • Aina nyingine yoyote ya

kujisikia vibaya

Page 8: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

4 Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji

■■ Usile, kunywa, wala kuvuta sigara wakati wa kazi.■■ Kama sehemu yoyote ya mwili wako itakutana na kiuatilifu,

nawa kutumia maji mengi na sabuni na na uripoti tukio hilo hilo kwa Kiongozi wa Kundil lako au Msimamizi.

■■ Ondoa hewa ya mkandamizo kwenye pampu yako unapotembea toka nyumba moja kwenda nyumba nyingine na pale unaposafiri katika jamii.

4. Tahadhari za Kiusalama

Page 9: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 5

Muarifu Kiongozi wa Kundi lakoo au Msimamizi maramoja yafuatayo yakijitokeza:

UVUTAJI HEWA ILIYOCHANGANYIKA NA KIUATILIFU ■■ Toka nje ya nyumba maramoja. ■■ Pumzika kwenye kivuli. ■■ Kiongozi wa Kundi lako au msimamizi ataandaa utaratibu ili

upelekwe kwenye kituo cha afya kwa matibabu zaidi.

MGUSANO NA NGOZI ■■ Vua maramoja nguo zote zilizochafuliwa. ■■ Osha maramoja kwa maji mengi na sabuni.■■ Kama kuwashwa na ngozi kukiendelea, mtaarifu kiongozi

wa Kundi lako au msimamizi, atakayeandaautaratibu ili ufikishwe kwenye kituo cha afya.

MGUSANO NA MACHO ■■ Nawa maramoja kwa maji mengi , ukisafisha chini ya kope za

macho, kwa angalau dakika 15. ■■ Utapelekwa kwenye kituo cha afya kwa uangalizi zaidi.

5. Huduma ya Kwanza

Page 10: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

6 Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji

■■ Kuwa mpole na mkarimu, mwenye heshima unapozungumza na wanajamii.

■■ Waarifu jamaai kwenye Kaya ya kwamba mpango huu wa unyunyiziaji umedhaminiwa na kufadhiliwa na Serikali ya Marekani.

■■ Wajulishe wafahamu kwamba unyunyiziaji utawasaidia kuwalinda wao na familia zao kutokana na ugonjwa wa malaria.

■■ Elezea hatua zitakazochukuliwa ili kutayarisha Kaya zao kwa ajili ya unyunyiziaji.

■■ Omba ruhusa au ridhaa yamkazi ambaye ni mtu mzima kabla ya kuingia nyumba yoyote.

6. Maadili ya Mnyunyiziaji afikapo kwenye Kaya

Page 11: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 7

■■ Kabla ya kunyunyizia, hakikisha kwamba watoto na wanyama wamewekwa angalau mita 10 mbali na nyumba wakati wa uchanganyaji dawa ya kuua wadudu au kiuatilifu na wakat wa unyunyiziaji.

■■ Waarifu wanaopokea huduma kwamba: • Wanatakiwa kusibiri angalau saa 2 kabla ya kuingia ndani

ya nyumba yoyote ambayo imenyunyiziwa, ili kuruhusu kuta kukauka na mvuke wote wa dawa kutuama chini.

• Baada ya masaa mawili kupita , wanauhusiwa kuingia ndani na kufungua milango na madirisha ili kuruhusu hewa safi kuingia.

• Kabla ya watu au wanyama kuruhusiwa kuingia ndani ya nyumba, usafi wa nyumba unatakiwa kufanyika ambao unahusisha kufagikiwa kwa sakafu ya nyumba.

• Wadudu au uchafu wowote uliokutwa ndani unatakiwa kutupwa kwenye choo cha shimo, au kuzikwa ndani ya shimo lenye kina cha sentimita 50. Hii ni kwa ajili ya kuzuia wanyama wafugwao majumbani au kuku kutokula wadudu wadudu wowote waliokufa kutoka kwenye nyumba iliyonyunyiziwa.

• Kuta zilizonyunyiziwa hazitakiwi kusafishwa, kupakwa rangi ,kupigwa lipu au kusiribwa kwa tope.

7. Usalama katika Kaya

Wadudu waliokufa na uchafu vyote vinatakiwa kufukiwakweye shimo lenye kina cha sentimita

Page 12: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

8 Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji

■■ Watahadharishe wakazi wanufaikaji juu ya uwepo wako ili wajitayarishe kwa ajili yako.

■■ Hakikisha kwamba vifaa vyote vya nyumba vinavyoweza kuhamishika vimeondolewa kutoka kwenye nyumba kabla ya kuanza kunyunyizia. Vifaa hivyo vinajumuisha:

• Chakula na vyombo vya kuhifadhia chakula

• Maji na vyombo vya kuhifadhia maji

• Vyombo vya kupikia ■■ Sogeza vifaa au vyombo vikubwa mpaka katikati ya chumba

na uvifunike kwa karatasi ya plastiki. Usinyunyizie vyumba vyovyote vyenye watu ambao hawawezi kutoka nje, kama vile wagonjwa.

■■ Hakikisha milango na madirisha yote yawe yamefungwa unaponyunyizia nyumba.

• Vifaa vilivyoning’inia kweye kuta

• Nguo • Wanasesere au midori • Samani

8. Utayarishaji wa Nyumba kwa ajili ya Unyunyiziaji

Vifaa vyote vya nyumba vinavyoweza kuhamishika vinatakiwa kuhamishwa na kutolewa kutoka kwenye nyumba kabla ya kuanza kunyunyizia.

Page 13: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 9

VITU VINAVYONING’INIZWA UKUTANI, MABANGO, PICHA NA VIFAA VINGINE UKUTANI■■ Uliza ujue kama vifaa vile vimewekwa ukutani moja kwa

moja au la.■■ Nyunyizia juu ya vifaa ambavyo vimewekwa ukutani moja

kwa moja. • Ikiwa hicho kifaa kinaweza kuinuliwa kutoka ukutani,

inafaa pia kunyunyizia upande wake wa chini, na eneo la ukuta lililo nyuma yake.

■■ Ukikutana na vyombo vya ndani ambayo haviwezi kuhamishika viliyo karibu na ukuta, unafaa kuweka bomba katikati mwa ukuta na chombo hicho na kunyunyizia. (Kumbuka kwamba huenda ikawa haiwezekani kudumisha umbali sahihi).

■■ Weka mbali vifaa vyovyote vya nyumba vilivyo nje ya nyumba ambavyo huenda vimewekwa karibu na mtambaa panya.

Page 14: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

10 Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji

■■ Weka pampu kwenye sakafu iliyothabiti nje ya nyumba, mbali na vifaa vyovyote vya nyumbani.

■■ Funika mdomo wa kinyunyiziaji kwa kipande cha nguo cha kuchujia au chujio.

■■ Jaza pampu hadi nusu ya kiwango kamili cha kazi kwa maji safi.

9. Uchanganyaji wa Dawa ya Kuua Wadudu au kiuatilifu

Kuchanganya dawa ya kuua wadudu au kiuatilifu

Mchanganyiko wa majimaji

Kifungashio kiyeyukacho

Fungua kifungashio cha nje/chukua kifungashio

cha ndani cha dawa ya kuua wadudu na

uangushe kifungashio hicho kiyeyukacho

ndani ya maji kwenye pampu

Rudisha kifungashio cha nje/pakiti ya nje

ndani ya mkoba wako

Fungua kifuniko cha chupa ya dawa ya kuua wadudu na polepole umwage kiuatilifu kilichomo

kweye chupa ndani ya kinyunyizaji au pampu

Suuza sehemu ya ndani ya chupa tupu ya dawa ya kuua wadudu mara

3 huku ukimwaga mabaki ya dawa ndani

ya kinyunyiziaji au pampu

Rudishia kifuniko cha chupa tupu na

uirudishe ndani ya mkoba wako

Page 15: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 11

■■ Funika mdomo wa kinyunyiziaji au pampu kwa kipande cha nguo cha kuchujia au chujio.

■■ Jaza kinyunyiziaji au pampu kwa maji yaliyosalia.

■■ Funga kifuniko cha kinyunyiziaji au pampu.

■■ Jaza hewa kweye pampu au kinyunyiziaji kwa misuko au mijazo mi 5 kamili.

■■ Inua kinyunyiziaji au pampu kwa mikono yote miwili. Shika mkono mmoja kweye kitako cha pamu kisha utikise kwa nguvu upande hadi upande, mara 10.

■■ Weka kinyunyiziaji au pampu chini sakafuni.■■ Weka mguu wako kwa uthabiti kwenye eneo la mguu

la kinyunyiziaji au pampu na wakati huohuo pampu au kinyunyiziaji kikiwa upande wako wa mbele.

■■ Unapojaza pampu, sikiliza kama kuna uvujaji wa hewa (hewa inayotoka) kutoka kwa kinyunyiziaji. Muarifu Kiongozi wa Kundi lako ikiwa unashuku au unahisi kinyunyiziaji au pampu inavujisha hewa.

Ujazaji hewa kwenye

kinyunyiziaji au pampu

Pampu aina ya Goizper

Pampu aina ya Hudson

Pompa kugeza igihe igipimo cyerekana ko cyageze kuri

psi 55 cyangwa pompa inshuro 55 zuzuye

Jaza hewa kweye pampu mpaka valvu ya usalama ya msukumo wa hewa ianze kuachilia hewa na alama nyekundu inaonekana

Mkao sahihi wakati wa ujazaji hewa kweye pampu.

Page 16: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

12 Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji

■■ Vaa kinyunyiziaji au pampu kwa usahihi, kwa kutumia kamba za begani. Ikiwa unatumia kinyunyiziaji cha aina ya Hudson, hakikisha unaweza kusoma geji ya shinikizo au mkandamizo wa hewa kweye pampu.

■■ Shikilia kifyatuliaji kwa mkono mmoja. Ncha ya pua ya kinyunyiziaji chako yafaa kuwa sentimita 45 mbali na ukuta ukishikilia bomba kwa mlalo kuelekea ukuta (“eneo la kati”). Hii itahakikisha kwamba unafanikisha upana sahihi wa safu wa sentimita 75.

■■ Anza kunyunyizia katika sehemu ya juu ya ukuta (“eneo la juu”), ukisongeza mkono wako kwa mtindo laini au polepole ukipitia “eneo la kati” hadi “eneo la chini”.

10. Mbinu za Unyunyiziaji

Wanyunyiziaji wakijifunzia kinyunyiziaji cha aina ya Goizper.

Page 17: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 13

Pampu ya Goizper

■■ Dumisha kasi iliyo sahihi (mwendo) unaponyunyizia. Kama ulivyofundishwa, kamilisha mita 2 za eneo la ukuta kwa sekunde 5.

■■ Baada ya kukamilisha safu ya kwanza, piga hatua upande wa kulia, na uendelee kunyunyizia kuanzia chini ukielekea juu ya ukuta.

■■ Hakikisha kwamba unatengeneza mwingiliano wa sentimita 5 kwa kila safu inayofuata.

■■ Kila wakati piga dawa kuelekea upande wa kulia mwa eneo litakalonyunyiziwa.

■■ Tikisa kinyunyiziaji au pampu kwa nguvu baada ya kila safu 10 mfululizo.

Dumisha shinikizo au

mkandamizo wa hewa

sahihi

Pampu au Kinyunyiziaji cha Hudson

Kaa ukikagua geji ya shinikizo au mkandamizo wa hewa ili

kuhakikisha kwamba halishuki chini ya 35 psi au chini zaidi

Sitisha kunyunyizia shinikizo likishuka hadi 35 psi

Mtiririko au utokaji wa dawa ya kuua wadudu utazima au

kuacha kutoka wenyewe mara tu shinikizo au mkandamizo wa hewa ndani ya pampu utashuka chini ya kiwango cha chini zaidi

kinachohitajika

Sitisha kunyunyizia mtiririko wa dawa ya kunyunyizia ukijizima

Weka kinyunyiziaji chini sakafuni na uweke upya

shinikizo kwa kupiga pampu mpaka mlango wa usalama

uanze kuachilia shinikizo (na alama nyekundu inaonekana)

Shusha kinyunyiziaji au pampu chini sakafuni na ujaze upya

pampu hadi 55 psi

Page 18: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

14 Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji

11. Kunyunyizia Dari

■■ Nyunyizia dari baada ya kukamilisha kuta zote za nyumba. ■■ Weka ncha ya pua sentimita 45 mbali na eneo, na unyunyizie

kwa mtindo sawia kama ule wa kuta. ■■ Shikilia bomba wima katika urefu wa mikono. ■■ Songa nyuma unaponyunyizia ili kuepuka kugusana na dawa

ya kuua wadudu iliyonyunyiziwa.

Page 19: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 15

12. Kunyunyizia Michirizi au Mtambaa panya■■ Nyunyizia michirizi (mtambaa panya) ikiwa ya mwisho,

baada ya kukamilisha ndani ya nyumba. ■■ Ondoa vifaa vyote vya nyumba kutoka kwenye varanda au

vizuizi vinavyoweza kukuzuia unaponyunyizia. ■■ Elekeza bomba katika mwelekeo wima kama unavyofanya

unaponyunyizia dari. Elekeza pua kwenye mchirizi (mtambaa panya).

■■ Usinyunyizie upande wa nje wa ukuta. ■■ Weka ncha ya pua chini ya mchirizi (mtambaa panya)

unaponyunyizia. ■■ Nyunyizia kwa safu iliyosambamba na ukuta. (Nyunyizia

kwenye ukuta, sio kuelekea, au mbali na ukuta). ■■ Nyunyizia kwa mwenendo/kasi sawia kama unavyofanya

kwenye maeneo mengine.

Mkao unaopendekezwa kwa unyunyiziaji michirizi (mtambaa panya).

Page 20: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

16 Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji

13. Unapotumia Kinyunyiziaji au pampu, zingatia Yafuatayo na uripoti masuala yoyote kwa Kiongozi wa Kundi lako au Msimamizi

■■ Uvujaji Uzibikaji. ■■ Pua zilizochakaa. ■■ Sitisha kunyunyizia mtu yeyote akiingia ndani ya nyumba,

au watu au wanyama wakija ndani ya mita 10 ukiwa unanyunyizia mtambaa panya.

Page 21: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 17

■■ Hakikisha milango na madirisha yote yanasalia yakiwa yamefungwa.

■■ Toa shinikizo au mkandamizo wa hewa kwenye kinyunyiziaji au pamu.

■■ Wakumbushe wakazi katika Kayakuhusu miongozo ya usalama wa nyumbani.

■■ Jaza kadi au fomu za data kama ulivyofundishwa.

14. Baada ya Kunyunyizia Nyumba

Page 22: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

18 Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji

■■ Rejesha vifungashioi au chupa zote za dawa ya kuua wadudu ambazo hazikutumiwa kwa Kiongozi wa Kundi au Mtunzaji Ghala mwisho wa kazi kila siku. Hakikisha kwamba dawa yote ya kuua wadudu unayorejesha kwenye ghala inarekodiwa.

■■ Mtaarifu Kiongozi wa Kundi ikiwa una mabaki ya dawa iliyochanganywa ya kuua wadudu katika kinyunyiziaji au pampu yako mwishoni mwa siku.

■■ Mwaga dawa yote iliyochanganywa ya kuua wadudu ambayo imerejeshwa kwenye eneo la operesheni au kambi ndani ya pipa nambari 1.

TAKA ZILILOCHAFULIWA■■ Zifuatazo zinasemekana kuwa zimechafuliwa:

• Vipakiti au vifungashio vitupu au chupa tupu zilizotumiwa za dawa ya kuua wadudu

• Vichujio vya vumbi vilivyotumiwa • Kabidhi vichuji vya vumbi vyote vilivyotumika kwa

Kiongozi wa Kundi na Mtunzaji Ghala mwishoni mwa siku. Mtunzaji Ghala atarekodi vichujio vya vumbi vyote zilizotumiwa na na kurejeshwa.

15. Kushughulikia Mabaki ya Dawa ya Kuua Wadudu & Taka za viuatilifu au dawa ya kuua wadudu

Page 23: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 19

■■ Vaa vifaa vya kinga vyote unapoosha pampu ukifuata utaratibu wa kusuuza pampu (mara tatu) kwa muendelezo.

■■ Vua mavazi yako ya juu au ovaroli na ukabidhi ili yafuliwe. ■■ Kabidhi PPE zilizosalia na vifaa vingine kwa Kiongozi wa

Kundi au Mtunzaji Ghala. ■■ Oga mwili mzima, ukitumia sabuni, katika eneo teule la

kuogea katika eneo la kambi.

16. Usafi Mwishoni mwa Siku ya Kazi

Vaa mavazi yako ya kujikinga unapofanya utaratibu wa kusuuza mara tatu.

Page 24: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

20 Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji

■■ Tumia vifaa vyote uvyopatiwa kwa uangalifu. ■■ Tumia kifaa tu kwa madhumuni yaliyokusudiwa. ■■ Utumiaji mbaya na utelekezaji wa mali ya mradi waweza

pelekea kupewa adhabu. ■■ Utumiajii mbaya au usio sahihi wa mali na vifaa vya mradi

vilivyowekwa chini ya uangaliziwako huenda ukapelekea kupewa adhabu.

17. Matumizi Muafaka ya Vifaa vya Unyunyiziaji

Vinyunyiziaji au Pampu zikiwa vimewekwa sahihi ili kukauka katika shimo maalum la maji taka .

Page 25: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 21

■■ Unatakiwa kujua idadi wastani ya majengo unayotarajiwa kunyunyizia kila siku. Ikiwa hauna uhakika na idadi, muulize Kiongozi wa Kundi lako.

■■ Idadi yangu lengwa ya majengo ya kunyunyiziwa ya kila siku ni ____ .

■■ Unatakiwa kujua wastani wa idadi ya majengo ambayo kila kipakiti (au chupa) ya dawa ya kuua wadudu inatarajiwa kunyunyizia.

■■ Kila kipakiti (au chupa) cha dawa ya kuua wadudu inatarajiwa kukamilisha wastani wa majengo ____.

18. Malengo ya Ufanisi wa Kazi

Page 26: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

22 Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji

Kumbuka, mchango wako unasaidia kulinda jamii kutokana na malaria!

Page 27: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia

Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 23

Page 28: Mnyunyiziaji Mwongozo wa Mfukoni · Mwongozo wa Mfukoni wa Mnyunyiziaji 1 1. Vifaa Bbinafsi vya Kujikinga (PPE) Kila wakati vaa mavazi kamili ya Kinga kabla ya kuanza kunyunyizia