mkoa wa simiyu · ufugaji ni shughuli kuu ya pili ya kiuchumi katika mkoa wa simiyu. mkoa una jumla...
TRANSCRIPT
1
MKUU WA MKOA
MH ANTHONY J MTAKA
KATIBU TAWALA MKOA
NDG. JUMANNE A SAGINI
MKOA WA
SIMIYU
UTANGULIZI
Mkoa wa Simiyu ulianzishwa kwa Tangazo la Serikali (GN) Na. 72 la tarehe 02 Machi, 2012, unapatikana Kaskazini mwa Tanza-
nia, Kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria. Mkoa upo kati ya longitudo 33°03” na 34°01” Mashariki ya mstari wa Griniwichi na
latitudi 02°01” hadi 04°00” Kusini mwa Ikweta. Aidha, kwa upande wa Kaskazini, Mkoa wa Simiyu unapakana na Mkoa wa Ma-
ra, Mashariki Mikoa ya Singida na Manyara, Kusini Mkoa wa Shinyanga na Tabora na upande wa Magharibi Mkoa wa Mwanza.
ENEO LA UTAWALA
Mkoa wa Simiyu una eneo la Kilomita za mraba 23,807.70.
Kati ya hizo Km za mraba 11,479.10 zinafaa kwa shughuli za
Kilimo na Ufugaji, Kilomita za mraba 11,723.60 ni eneo la
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Mapori ya Akiba ya Maswa,
Kijereshi na Mwiba, Hifadhi za Jumuiya za Wanyama Pori
(WMAs) Makao. Aidha, Kilometa za mraba 605 ni eneo la
maji ya Ziwa Victoria.
Mkoa una Wilaya 5 za kiutawala ambazo ni Bariadi, Busega,
Itilima , Maswa na Meatu. Aidha, Mkoa una Halmashauri 6,
majimbo 7 ya uchaguzi, Tarafa 16, Kata 130, Vijiji 471, Mitaa
92 na Vitongoji 2,659.
Ufugaji
Ufugaji ni shughuli kuu ya pili ya kiuchumi katika Mkoa wa Simiyu. Mkoa una jumla ya ng'ombe wa asili wapatao
1,568,715 mbuzi 946,649 kondoo 480,788na kuku 2,923,351.
Wanyama wengine ni nguruwe 7936, bata 17,795, punda
4,356 na mbwa 35,006.
Ng’ombe wa kienyeji wanaopatikana Simiyu
Shughuli za Uvuvi na Kilimo cha Pamba Mkoani Simiyu
SHUGHULI KUU ZA UCHUMI
Kilimo:- Kilimo na Ufugaji ni shughuli kuu za kiuchumi
zinazofanywa na wakazi wa Mkoa wa Simiyu. Eneo la Km za
mraba 11,479.10 sawa na asilimia 48.2 ya eneo lote la Mkoa
linafaa kwa kilimo na ufugaji. Kilimo na ufugaji inachangia
asilimia 75 ya pato la Mkoa na zaidi ya asilimia 80 ya wakazi
wa Mkoa huu ni wakulima na wafugaji.
Viwanda na Biashara
Mkoa una viwanda vya kati 14 vya kuchambua pamba na
kusindika mafuta ya pamba na alizeti. Viwanda hivi vinafanya
kazi wakati wa msimu wa zao la pamba.
Ufugaji wa Nyuki Mkoa una jumla ya vikundi 91 vya ufugaji nyuki vyenye
wanachama 2,589 na mizinga 4, 790 yenye uwezo wa kuzalisha
lita 61,500 za asali na kilo 4,690 za nta kwa mwaka.
Madini ya chumvi Chumvi inapatikana katika maeneo ya Mito-Minane na
Mwagotolo katika kijiji cha Lukale, Wilaya ya Meatu. Madini
haya huuzwa ndani na nje ya mkoa.
Mazao ya Biashara
Mazao ya biashara yanayolimwa Mkoa wa Simiyu ni pamba
(inazalishwa kwa asilimia 47 ya pamba yote inayozalishwa
nchini),. Mazao mengine ni alizeti, dengu na choroko.
Mazao ya chakula
Mazao makuu ya chakula ni mahindi, mtama, uwele, mpunga,
viazi vitamu, mihogo, dengu,maharage na jamii nyingine ya
mikunde.
Uvuvi
Shughuli za uvuvi zinafanyika katika Wilaya ya Busega
ambayo ina eneo la Ziwa Victoria lenye km za mraba 605 na
inatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya wilaya, mkoa na
Taifa kwa ujumla.
IDADI YA WATU
Kutokana na Sensa ya Taifa ya Watu na Makazi ya mwaka
2012; Mkoa ulikuwa na jumla ya watu 1, 584,157 kati ya hao
Wanaume walikuwa 759,891 na Wanawake 824,266. Wastani
wa ongezeko la i d a d i y a watu ni asilimia 1.8 kwa
mwaka, na wastani wa watu katika kaya ni 6.9. Aidha, hadi
kufikia Desemba, 2015 Mkoa unakisiwa kuwa na wakazi
wapatao 1,671,250, Wanawake wakiwa 869,582 na Wanaume
801,668.
2
HUDUMA ZA JAMII
ELIMU
Elimu ya Msingi:- Mkoa una jumla ya shule za Msingi 523
zenye madarasa ya awali, kati ya hizo 514 ni za Serikali na 9 ni
za binafsi na Taasisi za dini. Shule hizi zinazohudumiwa na
jumla ya walimu 6912 kati ya walimu 9448 wanaohitajika.
Elimu ya Sekondari:- Mkoa una shule za sekondari 148, kati
ya hizo 140 ni za Serikali na 8 ni za binafsi na Taasisi za dini.
Shule hizi zinahudumiwa na walimu 2,330 kati ya walimu 4317
wanaohitajika.
Vyuo:- Mkoa una vyuo vya ualimu 3 vinavyomilikiwa na watu
binafsi, vyuo 2 vya maendeleo ya Jamii na 1 cha ufundi stadi .
Elimu ya juu:- Mkoa una Chuo Kikuu Huria kinachotoa
mafunzo mbalimbali ya elimu ya juu.
AFYA:
Mkoa una zahanati 191, vituo vya afya 14 na hospitali 4
zinazomilikiwa na serikali, watu binafsi na Taasisi za dini.
Hospitali ya Somanda ni Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa.
Mkoa unatekeleza mpango wa utoaji elimu ya kinga kwa
magonjwa mbalimbali yakiwemo Malaria, Kifua Kikuu
UKIMWI.
MAJI
Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika
mkoa ni wastani wa asilimia 46 ambapo mijini na asilimia 46.6
na vijijini ni asilimia 46. Serikali inaendelea kuboresha hali ya
upatikanaji wa maji safi na salama katika mkoa kupitia
programu ya maendeleo ya sekta ya maji. Aidha Serikali
inaendelea na mpango wa kuleta maji kutoka ziwa Victoria
katika miji ya Makao Makuu ya Wilaya.
FURSA UWEKEZAJI
Mkoa unazalisha asilimia 47 ya pamba ya Tanzania hivyo una
fursa kubwa ya uwekezaji katika viwanda vya kusokota nyuzi,
kutengeneza nguo na viwanda vya kutengeneza vitu
vitokanavyo na pamba kama mafuta, bandeji, pamba za
hospitali na pamba za masikioni. Aidha, Mkoa una idadi kubwa
ya ng‟ombe hivyo kuna fursa za viwanda vya kusindika mazao
ya ngo‟ombe kama maziwa, nyama na ngozi.
MALIASILI NA UTALII
Shughuli za Utalii na uwindaji wa Kitalii zinafanyika katika
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Pori la Akiba la Maswa na
Hifadhi za Jumuiya ya Wanyamapori (WMA) Makao.
Halmashauri zinazozunguka Pori la Akiba la Maswa zinapewa
asilimia 25 ya ruzuku inayotokana na uwindaji huo.
MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO
Mkoa una mtandao wa barabara zenye urefu wa kilomita
4,730.95 ambazo zimegawanyika katika makundi yafuatayo:-
Barabara kuu Km 334.72, barabara za Mkoa Km 532.30,
barabara za Wilaya Km 2420.5 na barabara za Vijijini
1451.53; kati ya hizi Km 141.76 zina kiwango cha lami, Km
2453.59 kiwango cha changarawe na Km 2134.7 za kiwango
cha udongo. Kwa upande wa Mawasiliano, Mkoa
umeunganishwa na mitandao ya simu ya Airtel, Vodacom,
Tigo, Halotel na TTCL, huduma ya mawasiliano inapatikana
Mijini na Vijijini.
Daraja la Mto Simiyu linalotenganisha Wilaya ya Meatu na
Itilima
UTAMADUNI NA MICHEZO
Mila na desturi za wakazi wa Mkoa wa Simiyu kwa asilimia
kubwa ni za kabila la Wasukuma kwa kuwa ndilo kabila kuu.
Makabila mengine ni wataturu na wahadzabe wanaopatikana
katika wilaya ya Meatu karibu na Ziwa Eyasi.
Ngoma za asili katika Mkoa huu ni Mbina ambazo huchezwa
wakati wa msimu wa mavuno na huitimishwa tarehe 31 Mei ya
kila mwaka. Pia wenyeji (Wasukuma) wanapenda kushiriki
katika michezo mbalimbali ikiwemo mashindano ya mbio za
baiskeli na riadha.
Twiga katika Pori la Akiba la Maswa
Ujenzi wa Jengo la wagonjwa wa nje
Hospitali ya Mkoa (OPD)
Sehemu ya Ngoma ya Asili (Mbina) maarufu katika Mkoa wa
Simiyu
3
Mkuu wa Wilaya
Mhe. Festo Kiswaga
HALMASHAURI YA WILAYA
BARIADI Mkurugenzi Mtendaji (W)
Ndg. Abdallah Malela
UTANGULIZI Wilaya ya Bariadi iko kati ya nyuzi 2015’ na 3010’ kusini mwa Ikweta na nyuzi 33040‟ hadi 350 10’ mashariki ya Greenwich.
Wilaya hii inaundwa na Halmashauri mbili; Halmashauri ya mji Bariadi na Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na ina jimbo 1 la
uchaguzi (jimbo la Bariadi).
JIOGRAFIA
Halmashauri ya Wilaya Bariadi inapakana na Wilaya ya Busega
kwa upande wa magharibi, Mkoa wa Mara upande wa kaskazini,
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Pori la Akiba la Maswa upande
wa mashariki, Wilaya ya Maswa na Itilima upande wa kusini.
ENEO Halmashauri ina eneo la ukubwa wa Km za mraba 5,091.21 kati
ya hizo, Km 1,096.21 ni ardhi yenye udongo unaofaa kwa
shughuli za kilimo na ufugaji, Km 790 ni eneo la Pori la Akiba la
Maswa na Km 3,160 ni Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na eneo la
Km 45 ni maji, misitu na milima.
ENEO LA TAWALA Halmashauri ina tarafa 3 ambazo ni Mhango, Dutwa na Nkololo,
kata 21, vijiji 84 na vitongoji 555.
IDADI YA WATU: Kulingana na sensa ya Taifa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012,
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ilikuwa na jumla ya watu
267,296 kati yao wanawake 139,426 na wanaume ni 127,870 na
ongezeko la asilimia 3 ya idadi ya watu kwa mwaka. Wastani wa
idadi ya watu kwa kaya ni 6.9.
SHUGHULI ZA KIUCHUMI: Katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi shughuli kuu za
kiuchumi ni Kilimo, Ufugaji na biashara ndogo ndogo.
Mifugo Halmashauri ina jumla ya ng‟ombe 262,835, mbuzi 113,013,
kondoo 54,328 na kuku 373,738. Asilimia kubwa ya wafugaji wa
wanafuga kienyeji.
Kilimo Zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Bariadi wanategemea kilimo. Halmashauri ina eneo la hekta
185,729 linalofaa kwa kilimo kati ya hizo, hekta 102,151 ndizo
zinatumika kwa kilimo na eneo la hekta 63,348 linafaa kwa
kilimo cha umwagiliaji. Mazao makuu ya chakula yanayolimwa
ni mtama, mahindi, mpunga, viazi vitamu na mihogo. Mazao ya
biashara yanayolimwa ni pamba, alizeti, dengu na choroko.
HUDUMA ZA JAMII
ELIMU
Halmashauri ina jumla ya Shule za Msingi 73 zenye madarasa ya
awali na zinamilikiwa na serikali, shule za sekondari 23 kati ya
hizo 22 zinamilikiwa na Serikali na 1 ni ya mtu binafsi.
AFYA
Halmashauri ina zahanati 25, na vituo 2 vya afya
vinavyomilikiwa na Serikali, watu binafsi, na Taasisi za
Dini. Wilaya haina Hospitali ila wananchi wanapata huduma
katika Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa. (Somanda).
MAJI
Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika
Halmashauri ni asilimia 42.
Kisima cha maji kijiji cha Mwauchumu
MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO
Halmashauri ina jumla ya Km 727.6 za barabara. Kati ya
hizo Km 296.6 ni za Wilaya na Km 429.1 ni za Vijiji.
Halmashauri inapata huduma za mawasiliano ya simu
kupitia makampuni ya Vodacom, Airtel, Tigo, Halotel na
TTCL.
MALIASILI NA UTALII
Zaidi ya asilimia 41.8 ya eneo la Halmashauri ya wilaya ni
Hifadhi ya Taifa Serengeti na asilimia 8.4 ni Pori la Akiba
la Maswa. Hii inatoa fursa kubwa ya utalii na uwindaji wa
kitalii kuzunguka maeneo hayo.
UTAMADUNI
Wenyeji wa Halmashauri hii (Wasukuma) wana tamaduni
tofauti zikiwemo kucheza ngoma ya asili (Mbina), ngoma
hii huchezwa wakati wa msimu wa mavuno na mashindano
ya mbio za baiskeli. Pia wanaendeleza Utamaduni wa
kichifu (Utemi) .
FURSA ZA UWEKEZAJI
Kutokana na Wilaya kuwa na idadi kubwa ya Mifugo na zao
la Pamba, zipo fursa za uwekezaji katika kuongeza thamani
ya Bidhaa ya mazao yanayotokana na Pamba pamoja na
mifugo.
4
HALMASHAURI YA MJI
BARIADI Mkurugenzi wa Mji
Ndg. Melkzedek Humbe
UTANGULIZI
Halmashauri ya Mji wa Bariadi ilianzishwa kwa tangazo la Serikali namba 278 la tarehe 24 Agosti, 2012. Halmashauri hii
iligawanywa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, na ndipo yalipo makao makuu ya Mkoa.
ENEO LA HALMASHAURI
Halmashauri hii ina ukubwa wa Km za mraba 876.71 ambazo
zinatumika kwa shughuli za kilimo, makazi ,biashara na
shughuli nyingine.
ENEO LA UTAWALA
Halmashauri hii ina Tarafa 3, Kata 10 na mitaa 92 na ni
sehemu ya jimbo la Uchaguzi la Bariadi.
IDADI YA WATU
Kutokana na Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, idadi
ya wakazi wa mji wa Bariadi ni 155,620. Kati yao wanawake
ni 81,772 na wanaume ni 73,848.
SHUGHULI ZA KIUCHUMI
Shughuli za kiuchumi katika Mji wa Bariadi ni Biashara,
Viwanda vidogo, Kilimo, Ufugaji na Ushirika.
Kilimo:- Halmashauri ina eneo lenye jumla ya hekta 87,671
ambapo hekta 77,850 zinafaa kwa kilimo. Mazao ya chakula
yanayolimwa ni pamoja na mahindi,mpunga, mtama, viazi
vitamu na mikunde. Mazao ya biashara ni Pamba, Alizeti,
mbaazi, choroko na dengu.
Sehemu ya shamba la Pamba na marobotaya pamba
Biashara:-Mji wa Bariadi una wafanyabiasha wadogo na
wakubwa wanaotoa huduma mbalimbali katika sekta ya
usafirishaji, viwanda vidogo, visima vya mafuta na huduma
nyingine za jamii. Takribani asilimia 95 ya wanyabiashara
katika mji wa Bariadi ni Wanyantuzu (wenyeji).
Ufugaji:- Ufugaji ni Shughuli kubwa ya kiuchumi
inayofanywa na wananchi wa mji wa Bariadi. Kutokana na
sensa ya mifugo iliyofanyika mwezi Aprili 2016 Halmashauri
ina jumla ya Ng‟ombe 66,699, , Mbuzi 40,302, Kondoo
23,575, Nguruwe 1,326 Kuku 102,901, Bata 9,345, Punda
306, Mbwa 8,968, paka 5,198 na Kanga 685
Viwanda:- Mji wa Bariadi una viwanda vitatu vya
kuchambua Pamba, ambavyo ni Nsagali Co. Ltd, NGS
Investment Co. Ltd na Vitreces Investment Co. Ltd.
Viwanda hivi vinamilikiwa na watu binafsi.
HUDUMA ZA JAMII
AFYA Halmashauri ya Mji Bariadi ina zahanati 18, kati ya hizo 8 ni za
serikali, 1 ni ya Jeshi la Magereza na 9 zinamilikiwa na watu
binafsi na Taasisi za Dini. Aidha, vipo vituo 2 vya afya vi-
navyomilikiwa na serikali na Hospitali 1 ambayo ni hospitali
Teule ya Mkoa .
ELIMU Halmashauri ina jumla ya shule 40 za Msingi zenye madarsa ya
awali, kati ya hizo 38 ni za Serikali na 2 ni za binafsi. Shule za
sekondari zipo 16 kati ya hizo 14 ni za Serikali na 2 ni za bi-
nafsi. Aidha, kuna Chuo kimoja cha Ualimu kinachomilikiwa
na mtu binafsi, chuo 1 cha Maendeleo ya Jamii kina-
chomilikiwa na Serikali na Chuo Kikuu Huria.
MAJI Upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika Mji wa
Bariadi ni asilimia 42.5.Vyanzo vya maji ni visima vifupi 240
na visima virefu 27.
MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO
Barabara:- Halmashauri ina mtandao wa barabara zenye
jumla ya km 398.55, kati ya hizo barabara za lami ni Km 6.66
changarawe Km 37.1 na za udongo Km 357.35.
Halmashauri ipo katika mradi wa uboreshaji miundombinu
katika miji (ULGSP) ambapo Km 4.85 zinaendelea kujengwa
kwa ufadhili wa Benki ya Dunia. Barabara hizi
zitakapokamilika zitakuwa na taa za barabarani, sehemu ya
watembea kwa miguu, mifereji na maegesho ya magari
kuzunguka soko.
Mawasiliano:- Mji wa Bariadi unapata huduma ya
mawasiliano kupitia makampuni ya simu ya Vodacom, Airtel,
Tigo, Halotel na Zantel. Usikivu na upatikanaji wake ni mzuri .
HUDUMA ZA FEDHA
Taasisi zinazotoa huduma ya fedha katika Mji wa Bariadi ni
Benki ya NMB,CRDB na Benki ya Posta. Pia zipo huduma za
fedha kwa kupitia mitandao ya simu ambayo ni M-Pesa, Tigo-
Pesa na Airtel money.
Mkuu wa Wilaya
Mhe. Festo Kiswaga
5
Mkuu wa Wilaya
Mh. Benson Kilangi
HALMASHAURI YA WILAYA
ITILIMA Mkurugenzi Mtendaji (W)
Ndg. Mariano E Mwanyigu
UTANGULIZI Wilaya ya Itilima kwa upande wa Kaskazini inapakana na Wilaya ya Bariadi, Kusini Wilaya ya Meatu na Maswa, Magharibi
Wilaya ya Busega na Mashariki inapakana na Mkoa wa Arusha. Wilaya ina ukubwa wa Km za Mraba 2,647.7 ambapo Km2
1,938.7 sawa na 73.2% zinatumika kwa shughuli za kiuchumi, makazi na miundombinu, Km2 640 sawa na 24.17% ni Pori la akiba
la Maswa, Km2 69 sawa na 2.61% ni maeneo ya Mto Simiyu, vilima, misitu ya asili (ngitile) na mabonde.
ENEO LA UTAWALA
Wilaya ina Tarafa 4 ambazo ni Kanadi, Bumera, Itilima na
Kinang‟weli, Kata 22, Vijiji 102 na Vitongoji 597. Pia ina jimbo
moja la uchaguzi (Jimbo la Itilima).
IDADI YA WATU Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012,
Wilaya ilikuwa na jumla ya wakazi wapatao 313,900 kati yao
wanawake ni 165,398 na wanaume ni 148,502. Jumla ya Kaya ni
43,597, wastani wa idadi ya watu katika kaya ni 7. Ongezeko la
watu ni 1.8% kwa mwaka hivyo Kwa mwaka 2016 idadi ya watu
inakadiriwa kuwa 342,247.
SHUGHULI ZA KIUCHUMI NA UZALISHAJI
Uchumi wa Itilima unategemea zaidi kilimo na ufugaji.
KILIMO
Kilimo huchangia asilimia 85-95 ya pato la Wilaya. Eneo
linalofaa kwa kilimo ni hekta 193,170 na linalolimwa ni hekta
163,447. Zaidi ya asilimia 75 ya wakazi wa wilaya hii ni
wakulima.
Mazao makuu ya chakula:- ni mahindi, mtama, mpunga, viazi
vitamu, muhogo, maharage na kunde. Pia mazao ya mboga
mboga kama kabichi hulimwa katika baadhi ya maeneo
Mazao ya Biashara:- Pamba, ni zao kuu la biashara, mazao
mengine ni karanga, alizeti, dengu, mbaazi na choroko.
Wilaya imepiga hatua katika matumizi ya zana bora za kilimo
ambapo trekta kubwa zipo 80, ndogo 28, plau 13,031,
mikokoteni 1,188, majembe ya kupalilia 2,100, rippers 3,
majembe ya kupandia 5 na maksai 54,706. Elimu inaendelea
kutolewa ili kuongeza idadi ya wakulima wanaotumia zana bora
za kilimo.
MIFUGO
Wilaya ina zaidi ya ng‟ombe 296,322, kondoo 48,177, mbuzi
100,220, nguruwe 1,063, kuku 201,243, bata 4,843, mbwa
13,752 na punda 89. Shughuli za ufugaji hufanyika
sambamba na kilimo. Eneo la ardhi linalofaa kwa malisho ya
mifugo ni Km za mraba 1,938.7 sawa na hekta 193,870.
Mkulima akiwa katika Shamba la Pamba
Mkulima akilima shamba kwa trekta
Mkulima wa mbogamboga (Aina ya kabichi) katika kijiji cha
Mwabuki .
6
MAENDELEO YA JAMII
Wilaya imesajili vikundi vya wajasiriamali 544 katika mwaka wa
fedha 2015/2016, vikundi hivi vinapewa Mikopo yenye riba na-
fuu ya 10% ya mapato ya ndani ya fedha zinazotengwa katika
bajeti ya Halmashauri. Pia kuna vikundi 41 vinavyojishughulisha
na “Village Community Bank” (VICOBA) kwa lengo la kujiletea
maendeleo.
ELIMU
Elimu ya Msingi:- Wilaya ina jumla ya shule 87 za msingi
zenye madarasa ya awali zinazomilikiwa na serikali. Shule hizi
zina jumla ya wanafunzi 78,688 kati yao wavulana ni 38,127 na
wasichana ni 40,561 na zinahudumiwa na walimu wapato 1,262
kati ya wlimu 1,608 wanaohitajika.
Jengo la darasa katika shule ya msingi Mwakimisha.
Elimu ya Sekondari;- Wilaya ina Shule 30 za sekondari, kati ya
hizo 29 ni za serikali na 1 ni ya Taasisi ya dini. Shule hizi
zinahudumiwa na walimu wapato 502 kati ya walimu 1,160
wanaohitajika.
AFYA
Wilaya ina jumla ya zahanti 29 kati hizo 26 ni za serikali na 3
zinamilikiwa na watu binafsi na Taasisi za dini, kuna vituo
vya afya 3, wilaya haina hospitali hivyo wananchi wanapata
huduma za Rufaa katika Hospitali Teule ya Mkoa (Somanda).
Wananchi wakipata huduma ya maji safi katika kijiji cha
Zanzui
MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO
Wilaya ina mtandao wa barabara zenye urefu wa Km 692.3,
kati ya hizo Km 53.68 ni barabara za Mkoa, Km 227.9 ni
barabara za Wilaya (collector roads), Km 390.72 ni barabara
za Vijiji (feeder roads) na Km 20 ni barabara za vituo vya
biashara (urban roads). Barabara zote ni za kiwango cha
changarawe na udongo. Wilaya ina huduma ya mawasiliano
ya simu za mkononi ya mitandao ya Tigo, Airtel, Vodacom,
Halotel na TTCL.
HUDUMA ZA JAMII
UTAMADUNI
Wenyeji wa wilaya hii ni kabila la Wasukuma (Wanyantuzu),
jina hili lilitokana na muunganiko wa makabila mawili,
Wasukuma na Wanyaturu. Wenyeji hujihusisha na shughuli za
ufugaji wa kiasili, kilimo na shughuli za sanaa zikiwemo Muziki
wa asili, tiba asilia, ngoma, ususi, ufinyanzi, uchongaji na
matambiko. Jengo la kliniki ya mama na mtoto kituo cha afya Luguru
MAJI
Huduma ya maji safi na salama inapatikana kwa wastani wa
asilimia 45.2 ambapo wananchi wanapata maji umbali usiozidi
mita 400. Wilaya ina visima virefu na vifupi vinavyotoa
huduma 118, mabwawa 2, malambo 21 na matenki ya kuvunia
maji ya mvua 48.
7
Mkuu wa Wilaya
Mhe
HALMASHAURI YA WILAYA
MASWA Mkurugenzi Mtendaji (W)
DKT. Fredrick D. Sagamiko
UTANGULIZI
Wilaya ya Maswa inapakana na Wilaya ya Meatu kwa upande Mashariki , Kaskazini na Kaskazini Magharibi
inapakana na Wilaya ya Itilima, Kusini inapakana na Wilaya ya Kishapu (Mkoa wa Shinyanga) na Magharibi
inapakana na Mkoa wa Mwanza.
ENEO LA WILAYA
Wilaya ni Km za mraba 3,398 kati ya hizo Km 2,475 zinafaa kwa
shughuli za kilimo na ufugaji, Km 77 ni hifadhi ya misitu na Km
846 ni miinuko ya mawe, vilima na misitu ya asili (ngitili).
ENEO LA UTAWALA
Kiutawala, Wilaya ina tarafa 3, Kata 36, Mamlaka ya Mji 1 yenye
Vitongoji 40, Vijiji 120, na Vitongoji 510. Aidha, kuna Majimbo
mawili ya uchaguzi, ya Maswa Mashariki na Maswa Magharibi.
IDADI YA WATU
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 idadi ya
watu inakadiriwa kufikia watu 344,125 kati yao wanawake ni
176,723 na wanaume ni 167,402. Kaya zinakadiriwa kufikia
52,942 zenye wastani wa watu 6.5 kwa kaya. Ongezeko la watu
linakadiriwa kuwa asilimia 1.8 kwa mwaka.
SHUGHULI ZA KIUCHUMI
Shughuli kubwa za uchumi kwa Wananchi wa Wilaya ya Maswa
ni kilimo na ufugaji. Shughuli zingine ni uvuvi,ushirika na
viwanda vidogo. Wilaya inategemea mapato yake kwa kiasi
kikubwa kutokana na mazao ya kilimo na mifugo. Kwa mujibu
wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 asilimia 80 ya
wakazi wanashughulika kilimo na ufugaji. Wastani wa pato la
mwananchi kwa mwaka inakadiliwa kuwa Tsh. 324, 843
Miundombinu ya Kilimo cha umwagiliaji katika kijiji
cha Kinamwigulu
FURSA ZA KIUCHUMI
Wilaya ina jumla ya ekari 10,576.5 kwa ajili ya uwekezaji
wa viwanda, shughuli za kilimo na ufugaji katika kata za
Shishiyu, Malampaka na Sukuma. Zipo fursa za kuongeza
thamani ya bidhaa zinazotokana na mazao ya pamba, alizeti
na mifugo.
ENEO LA KILIMO
Wilaya ina kilometa za mraba 3,398 kati ya hizo, Km 2,475
zinafaa kwa shughuli za kilimo na ufugaji na Hekta 52,375
zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji. Mazao ya chakula na
biashara yanayolimwa ni pamoja na Mpunga, Viazi vitamu,
Mahindi, Mtama, Ulezi, karanga na Mihogo. Zao kuu la biashara
ni Pamba, mazao mengine ni alizeti , dengu na choroko.
MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO
Barabara;- Wilaya ya Maswa ina barabara zenye urefu wa
km 1,043.98 , kati ya hizo, km 302.27 ni za changarawe na
km 741.71 ni za udongo. Barabara hizi zinapitika kwa
asilimia 55 kwa mwaka mzima.
RELI;- Wilaya ina kituo kidogo cha reli Inayotoka Mwanza
kuelekea Dar Es Salaam katika mji mdogo wa Malampaka na
kuna kituo kidogo cha usafirishaji wa mizigo na abiria.
UFUGAJI
Idadi ya Mifugo katika Wilaya ni ng‟ombe 403,416 mbuzi
239,498, kondoo 182,284, kuku 1,441,648, punda 847, nguruwe
3405 na mbwa 12,286 . Huduma za kustawisha mifugo
zinatolewa kupitia majosho 44, mabwawa 33, malambo 31 Cliniki
1 ya mifugo na vituo 7 vya kutolea Ushauri wa mifugo. Zaidi ya
ekari 92,418 hurutubishwa kila mwaka kutokana na uzalishaji wa
tani 462,090 za mbolea ya samadi.
VIWANJA VYA NDEGE:-Wilaya ina viwanja vya
ndege vidogo viwili (air strips) ambavyo Vipo Maswa Mjini
na Malya.
SIMU: - Mawasiliano ya simu yanapatikana kwa wastani
wa asilimia 92 kupitia makampuni ya mawasiliano ya TTCL,
Vodacom, Airtel,Halotel na Tigo.
REDIO:- Kuna Stesheni 1 ya Redio Sibuka FM, ambayo
inamilikiwa na mtu binafsi. Wilaya hutumia redio hiyo ku-
tolea matangazo na taarifa mbalimbali muhimu kufikishwa
kwa Wananchi.
8
Sehemu ya Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD) katika
Hospitali ya Wilaya ya Maswa
MAJI:- Asilimia 59.78 ya wananchi wanaoishi vijijini
wanapata huduma ya maji safi na salama. Kwa upande wa
mjini wananchi wanapata maji safi na salama kwa asilimia
83, chanzo kikuu cha maji mjini ni kupitia mradi wa maji wa
kitaifa Maswa.
HUDUMA ZA JAMII
Vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari
Nyalikungu vilivyojengwa kwa ufadhili wa SEDP II
AFYA:- Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ina jumla ya
vituo vya kutolea huduma ya Afya 46, Zahanati 42 kati hizo
Zahanati 2 zinazomilikiwa na madhehebu ya dini 2 na 2
zinamilikiwa na watu binafsi, vituo vya afya 3 na Hospitali
ya Wilaya.
HUDUMA ZA FEDHA
Wilaya ina jumla ya Taasisi za kifedha 2 zinazo toa
huduma kwa jamii nazo ni NMB na CRDB. Aidha kuna
Taasisi ndogo ndogo za fedha zinazotoa mikopo kwa
Wananchi ambazo ni BAYPOT, FINCA, ABC Bank,
VISION FUND.Wilaya ina jumla ya SACCOS 52
zilizosajiliwa. Tenki la kuhifadhia maji kijiji cha Lalago
Wananchi wakipata huduma ya maji katika kijiji cha
Sangamwalugesha
MAENDELEO YA VIJANA
Wilaya ina Vikundi vya vijana 256 vyenye jumla ya wanachama
2,662.Vikundi hivi hujishughulisha na kilimo, ufugaji, biashara
ndogondogo, ushonaji, ususi, ufinyanzi, ufyatuaji wa tofali, ujenzi
na uselemara, utengenezaji wa chaki pamoja na uendeshaji wa
bodaboda.Vikundi 08 vimeunda SACCOS na hadi sasa
vimepatiwa shilingi 38,000,000 toka Wizara yenye dhamana na
Maendeleo ya vijana.Fedha hizi zimetumika kuanzisha kiwanda
cha kutengeneza chaki zinazotambulika sokoni kwa jina la
„MASWA CHALKS‟ (nyeupe) na „JPM CHALKS‟ (za rangi).
HUDUMA YA UMEME
Huduma ya umeme wa gridi inapatikana katika maeneo ya vijiji
pamoja na makao makuu ya Wilaya. Jumla ya vijiji 67 kati ya
vijiji 120 vimeunganishiwa katika Mpango wa Umeme Vijijini
(REA).
iHUDUMA YA UMEME
Huduma ya umeme wa gridi inapatikana katika maeneo ya
vijiji pamoja na makao makuu ya Wilaya. Jumla ya vijiji 67
kati ya vijiji 120 vimeunganishiwa katika Mpango wa
Umeme Vijijini (REA).
ELIMU:- Wilaya ina jumla ya Shule za Msingi 123, kati
ya hizo shule 2 ni za binafsi na shule 121 ni za serikali,
shule za sekondari ziko 40 kati ya hizo 36 zinamilikiwa na
Serikali na 4 ni za watu binafsi na Taasisi za dini.
Vyuo;- Wilaya ina chuo 1 cha Ualimu kinachomilikiwa na
watu binafsi, chuo cha Maendeleo ya Wananchi 1
(Malampaka FDC) na chuo cha Ufundi Stadi 1 (Binza
VTC) vinavyomilikiwa na serikali.
Chaki zinazozalishwa na kikundi cha Vijana
Wilaya ya Maswa
9
HALMASHAURI YA WILAYA
MEATU
MKUU WA WILAYA
Mh. Dkt.Joseph Chilonga
MKURUGENZI WA WILAYA
Ndg. Fabian Manoza
UTANGULIZI
Wilaya ya Meatu inapatikana katika latitudi 2057 na 409 kusini mwa Ikweta na longitudo 3408 na 34049 Mashariki mwa Grinwich.
Imepakana na wilaya ya Bariadi upande wa kaskazini, Ngorongoro na Karatu upande wa mashariki, Wakati upande wa kusini
inapakana na wilaya za Mbulu na Iramba na wilaya za Maswa na Kishapu zipo upande wa magharibi wa wilaya.
ENEO LA WILAYA
Wilaya ina ukubwa wa kilometa za mraba 8,835. Asilimia 49
ya eneo lote la Wilaya ni hifadhi za wanyamapori ambazo ni
Pori la akiba Maswa, sehemu ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti,
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi za Jumuiya ya
Taifa ya Wanyamapori (WMA) . Eneo lililosalia asilimia 51
linatumika kwa ajili ya makazi, shughuli za kijamii na kiuchumi
ENEO LA UTAWALA
Wilaya hii ilianzishwa Tarehe 01 Julai 1987 baada ya Wilaya ya
Maswa kugawanywa. Makao makuu ya Wilaya ya Meatu yapo
katika Mji wa Mwanhuzi. Wilaya ina Tarafa tatu:- ambazo ni
Kisesa, Kimali na Nyalanja na kata 25 ambazo zina jumla ya
idadi ya vijiji 100 na pia ina majimbo 2 ya uchaguzi ambayo ni
Jimbo la Kisesa na Meatu.
IDADI YA WATU
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012,
Wilaya ilikuwa na jumla ya wakazi wapatao 299,619 kati yao
143,569 ni wanaume na 156,050 ni wanawake. Wastani wa
idadi ya watu katika kaya ni 7.4 na ongezeko la watu ni 1.9%.
Wilaya inakaliwa na kabila la Wasukuma ambalo lina idadi
kubwa ya watu ikilinganishwa na Makabila mengine ambayo
yanapatikana katika Wilaya ya Meatu, makabila hayo ni
Wanyaturu, Wanyiramba, Wanyisanzu na Wahadzabe
SHUGHULI ZA KIUCHUMI
Shughuli za kiuchumi zinazofanywa na Wilaya hii ni Kilimo na
Ufugaji. Shughuli za Uwindaji na upigaji picha za kitalii
unafanyika kwenye Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya
Makao na Pori la Akiba la Maswa. Aidha utengenezaji wa
chumvi unafanyika katika eneo la Ziwa Eyasi Tarafa ya
Nyalanja na biashara ndogondogo.
Uzalishaji wa chumvi katika kijiji cha Nyalanja
Uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara
Katika msimu 2015/16 Wilaya iliweka lengo la kuzalisha
jumla ya tani 121,365 za chakula. Katika utekelezaji jumla ya
tani 1,888,217 zilivunwa. Wilaya ya Meatu ni kame kwa
kipindi kirefu cha mwaka. Hivyo wananchi wanahimizwa
kulima mazao yanayostahimili ukame hasa mtama, uwele na
viazi vitamu. Mahindi pia hulimwa katika baaadhi ya maeneo.
Zao kuu la biashara ni Pamba, mazao mengine ya biashara ni
alizeti na vitunguu
UFUGAJI
Ufugaji ni shughuli kuu ya pili Kiuchumi baada ya Kilimo
kwa wananchi wa wilaya ya Meatu.Wilaya inakadiriwa kuwa
na Ng‟ombe 353,389, Mbuzi 385,252, Kondooo 137,297,
Nguruwe 884, Punda 3,114, kuku 457,362 na Bata 3,607.
UVUVI
Uvuvi hufanyika katika kata ya Bukundi, Mwamalole na
Mwabuzo. Shughuli hii hufanyika katika Ziwa Eyasi, Mto
Sibiti, Bwawa la Mwanyahina na Kitangiri. Aina ya samaki
wapatikanao ni perege,kambare,nembe,ningu na kamongo
ambao hutumika kwa ajili ya chakula na biashara.
KILIMO
Eneo la hekta 458,200 kati ya 883,500 ambalo ni eneo lote la
wilaya linafaa kwa kilimo. Eneo linalolimwa ni hekta 159,993
sawa na asilimia 35 za eneo linalofaa kwa kilimo. Eneo
lililobaki (425,300 ha) ni kwa ajili ya mifugo, makazi, hifadhi
ya wanyamapori ya Makao (WMA-Wildlife Management Area)
na Hifadhi ya wanyamapori ya Maswa (Maswa Game
Reserve).
MISITU
Sekta ya misitu imejikita katika utunzaji wa ngitili (Uoto wa
asili) ambapo eneo lenye jumla ya hekta 161,615.4 za ngitili
zilizohifadhiwa. Wilaya imejiwekea utaratibu wa kuanzisha
bustani ya miche ya miti ili kuratibu zoezi la upandaji miti kila
mwaka. Hii inatokana na hali ya kijiografia ya wilaya hii kuwa
kame.Uhamasishaji hufanyika kwa wananchi kutunza uoto wa
asili (ngitili) na kujenga tabia ya kupanda miti kila ifikapo
msimu wa mvua.
10
MALIASILI NA UTALII
Wilaya ya Meatu ina eneo la hifadhi lenye ukubwa wa km za
mraba 3888. Eneo hili linaundwa na pori la akiba la Maswa (Km22094), eneo la hifadhi ya jamii ya Wanyamapori (WMA)
Makao(Km2768.9), Ngitili ya kijiji cha Makao (196.47km2),
Hifadhi ya ya Taifa Serengeti(694km2) na hifadhi ya Ngorongoro(Km2135). Kuwepo kwa maeneo haya yenye wanyama kama
tembo, twiga, simba, nyati n.k kumeongeza uwepo wa fursa za
utalii katika wilaya ya Meatu na kuchangia katika pato la wilaya
na Taifa kwa ujumla
Wanyama pori katika eneo la Hifadhi ya Makao Meatu
MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO
Wilaya ina jumla ya mtandao wa barabara wenye urefu wa Km.
1,032 ambapo urefu huu umegawanywa katika Barabara za
Mkoa (135 Km) ,Barabara za Wilaya (337.94 Km), Barabara za
Mjini (27.45 Km) na Barabara za Vijijini( 542.87 Km). Wilaya
imeunganishwa na barabara za changarawe na zenye tabaka la
udongo. Aidha, Barabara za Mjini Mwanhuzi zenye urefu wa Km
13 zimejengwa kwa kiwango cha lami. Wilaya ina mtandao wa
mawasiliano ya simu ya TTCL, VODACOM, AIRTEL, TIGO na
HALOTEL
Barabara ya lami km 13 mjini Mwanhuzi na ujenzi wa
barabara mpya Katani/Vijijini
ELIMU:-Wilaya hii ina shule za Msingi 111 zenye jumla ya
wanafunzi 59,332 kati yao wavulana ni 27,639 na wasichana
29,693. Mwaka 2016 wilaya iliandikisha jumla ya
wanafunzi 10,931 wa darasa la kwanza, kati yao wavulana
5467 na wasichana 5464 sawa na asilimi 102 ya lengo.
Elimu ya Sekondari:- wilaya ina jumla ya shule 22 za
sekondari kati ya hizo tatu (03) ni za Kidato cha Tano na
Sita.Wilaya pia inasimamia uendeshaji wa madarasa ya
Elimu ya Watu Wazima kwa lengo la kupunguza idadi ya
waisojua kusoma na kuandika kupitia mpango wa Elimu
masafa(ODL) na mpango wa uwiano kati ya elimu ya watu
wazima na jamii (MKEJA).
AFYA Wilaya ina zahanati 52, Vituo vya Afya 3 na Hospitali 1 ya
Wilaya na inatoa elimu ya kinga, chanjo kwa watoto, mama
wajawazito na tiba kwa wananchi. Hali ya upatikanaji wa
vifaa tiba ni asilimia 60.
Huduma za upasuaji Na jengo la hudumu Kwa wazee Hospitali ya wilaya ya Meatu
HUDUMA ZA JAMII
MAJI Hali ya upatikanaji wa maji ni asilimia 34 mjini na asilimia 42.2
vijijini .Vyanzo vikuu vya Maji katika Wilaya ya Meatu ni
Bwawa la Mwanyahina ambalo linahudumia wakazi wa Mjini
Mwanhuzi. Maeneo ya Vijijini vyanzo vikuu ni visima vifupi na
virefu.
MAENDELEO YA SEKTA VIJANA Idara ya maendeleo ya jamii kwa kushirikiana na idara ya
ushirika imetoa elimu ya ujasirimali, uanzishwaji na uende-
shaji wa SACCOS kwa vikundi 8 vya vijana. Vikundi hivyo
vimeungana na kutengeneza SACCOS 1 ya vijana ambayo
imekopeshwa kiasi cha Tsh. 31,000,000/= kutoka Wizara
yenye dhamana na Maendeleo ya vijana na kuanzisha ki-
wanda kidogo cha kusindika maziwa ya ng‟ombe wa kien-
yeji yanayotambulika sokoni kwa jina la “MEATU MILK”
UTAMADUNI
Wilaya ina jumla ya makabila matatu ambayo ni watindiga
(wahadzabe), wataturu na kabila kuu wasukuma, makabila yote
haya yamebaki katika asili zao hivyo kuwa kivutio cha utalii wa
utamaduni. Kuna jumla ya Vikundi vya burudani na sanaa 25
ambapo vikundi 6 vimesajiliwa na Baraza la Sanaa Tanzania
(BASATA) ambavyo ni Mshikamano House of Talent, Bomani
Sanaa Group, Nzobe Ngoma Group, Ngoma ya Wataturu, Mshi-
kamano Sanaa Group na Meatu Time Arts Group.
Kabila la Watindiga(Wahadzabe) wakisaga unga na kulia ni Kabila la
wataturu katika ngoma ya Asili inayoitwa “Nyangira”
Maziwa yanayotengenezwa na Kikundi cha Vijana Meatu
11
HALMASHAURI YA WILAYA
BUSEGA
UTANGULIZI
Wilaya ilianzishwa Mwaka 2012 kwa Tangazo la Serikali (G.N) Na 73 la tarehe 02 Machi 2012, Wilaya hii ilianzishwa baada ya
kugawanywa kwa Wilaya ya Magu iliyoko Mkoa wa Mwanza. Kwa upande wa Kaskazini wilaya inapakana na Mkoa wa Mwanza,
Mashariki inapakana na Mkoa wa Mara, kusini inapakana na Wilaya ya Bariadi, Kusini-Magharibi inapakana na Wilaya ya Itilima,
na upande wa Magharibi inapakana na Wilaya ya Magu iliyoko Mkoa wa Mwanza.
ENEO LA KIUTAWALA Wilaya ina Jimbo 1 la uchaguzi, Tarafa 2, Kata 15 na Vijiji 59
vyenye jumla ya Vitongoji 334. Makao makuu yapo katika
Kata ya Nyashimo.
Jengo la ofisi ya Halmashuari linaloendelea kujengwa
IDADI YA WATU Idadi ya watu kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya
mwaka 2012 ni 216,059, kati yao wanaume ni 104,741 na
wanawake ni 111,318, ambapo ukuaji wa ongezeko la watu ni
2% kwa mwaka.
SHUGHULI ZA UCHUMI Shughuli kubwa za kiuchumi katika Wilaya ya Busega ni
Kilimo, Ufugaji na Uvuvi. Wilaya ina jumla ya Hekta
77,293.70 zinazofaa kwa kilimo na ufugaji na kilomita za
mraba 605 ni sehemu ya Ziwa Victoria ambayo inatumika kwa
shughuli za uvuvi.
Kilimo: Katika msimu 2015/2016 jumla ya hekta 36,7776
sawa na asilimia 47.6 za eneo linalofaa kwa kilimo zililimwa
mazao ya chakula na biasahra.
Mazao ya chakula ni pamoja na mahindi, mtama, viazi vitamu
na mihogo, zao kuu la biashara ni pamba.
Ufugaji: Wilaya ina jumla ya ng`ombe 186,054, mbuzi 68,364,
kondoo 35,127, nguruwe 1,258 na kuku 346,459. Eneo
lililotengwa kwa ajili ya malisho ni hekta 150,900.
Uvuvi: shughuli za uvuvi hufanyika katika mialo(Beach
Management Unit) ya Nyamikoma, Nyakaboja na Ihale.
Wilaya ina jumla ya wavuvi 3,926 ambao huvua samaki aina
ya sato na sangara kwa ajili ya kupeleka viwandani na kwenye
masoko ya kawaida ndani na nje ya wilaya hasa soko la
halmashauri ya Mji Bariadi yalipo makao makuu ya Mkoa
MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO Wilaya ina jumla ya kilometa 299.1 za barabara zinazojumuisha
barabara za wilaya Km. 172.9 na barabara za vijiji (Feeder
roads) Km.126.2. Jumla ya Km. 209.37 sawa na asilimia 70 ya
barabara zote za wilaya na vijiji, zinapitika majira yote ya
mwaka. Wilaya ina mawasiliano ya TTCL, Aitel, Vodacom,
Tigo, Halotel na Zantel.
MADINI Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na kampuni ya Twig Gold
mwaka 2011 ilibaini kuwa wilaya ina akiba ya tani milioni 11
za madini aina ya nickel katika mlima wa Ngasamo. Kampuni
ya Red hill nickel Limited imewezeka katika uchimbaji wa
madini hayo na ikokwenye hatua ya tathmini na upembuzi
yakinifu wa mzingira “Social Environmental Impact
Assessment” (SEIA).
HUDUMA ZA JAMII
ELIMU
Elimu ya Msingi: Wilaya ina jumla ya shule za msingi 91
kati ya hizo, 86 ni za serikali na 5 ni za watu binafsi. Shule
zote zina madarasa ya awali na zinahudumiwa na walimu
1,018 kati ya 1,328 wanaohitajika . Elimu ya sekondari: Shule za Sekondari ziko 21 kati ya
hizo 17 ni za Serikali na 4 ni za watu binafsi. Shule zote zina
maabara zilizojengwa kwa nguvu za wananchi na serikali kwa
ajili ya kuwezesha wanafunzi kujifunza masomo ya sayansi
kwa vitendo.
Jengo la Maabara Shule ya Sekondari Mkula.
12
AFYA Wilaya ina vituo 2 vya afya vya serikali vilivyoko kata ya Igalukilo na Nyashimo na Zahanati 20 za serikali
zinazo toa huduma ya afya kwa wananchi . Kuna hospitali 1 ya Mkula inayotoa huduma kwa wananchi na
inamilikiwa na Taasisi ya dini (AIC), ipo katika kata ya Mkula. Halmashauri inatarajia kuingia mkataba na
kuifanya kuwa hospitali teule ya wilaya.
Jengo la Wodi ya mama wajawazito katika zahanati ya Nassa
MAJI
Huduma ya maji safi na salama inapatikana kwa asilimia 38.6 vyazno vikuu vikiwa ni miradi ya maji bomba,
visima vifupi na virefu.
Ujenzi wa Mradi wa maji katika kijiji cha Lukungu